Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

NIMEIPATA FURAHA YANGU - 1

 







    IMEANDIKWA NA : MODEL TEDDY



    *********************************************************************************



    Simulizi : Nimeipata Furaha Yangu

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya mapambano kati ya nuru na giza hatimaye ushindi uliangukia kwa mpambanaji aliyekuwa akifahamika kama giza , kwa kujizolea pointi nyingi zilizomuwezesha kuumiliki muda huo ambao jina jingine ulifahamika kama usiku, mpambanaji huyu alikuwa na furaha sana baada ya kutawaliwa kwa masaa 12 akiwa hana sauti ama nguvu yeyote lakini naye muda wake ulikuwa umewadia wa kijichukulia madaraka.



    Kiumbe huyu aliyekuwa akisifika kwa kusambaza giza na kuleta mtafaruko kwa macho ya viumbe hai naye alizidiwa ujanja na kiumbe mwingine aliyekuwa akitoa mwanga mwangavu na wa kipee ambao hujawahi kutengenezwa na binadamu yeyeto si mwingine bali ni mheshimiwa mbalamwezi ambaye nae alikuwa akisaidiwa na majilani zake akina nyota.



    Kiumbe huyu usiku alikuwa akiendeleza mashambulizi ya kusogeza masaa kadri muda ulivyozidi naye aliendeleza kupachika namba tofauti tofauti na kuzidi kupunguza idadi ya viumbe hai ambao baadhi yao walikuwa wakaidi kuiruhusu miguu yao kuwapeleka majumbani mwao lakini baada ya idadi kubwa ya namba kupita hatimaye viumbe kama binadamu walipungua sana kila eneo la dunia.



    Namba saba au saa saba za usiku alikuwa ndiyo mmiliki halali kwa wakati huo , muda huo ulikuwa umetawaliwa na ukimya ni baadhi tu ya sauti za mijibwa ambayo ilikuwa ibwatua midomo yao na kuleta sauti mbalimbali za mashairi waliyokuwa wakiyaimba , namba saba hakumiliki miziki tu kutoka kwa mijibwa bali alimiliki na midundo ya miziki kutoka kwa mipaka iliyokuwa ikiimba kwa sauti mbalimbali ili mladi tu kuufurahia usiku huo.



    Mbaramwezi na nyota waliendelea kutoa miaga yao iliyopelekea kuwasaidia vijana watatu waliokuwa wamevalia makoti meusi yaliyowaziba vizuri sura zao kutekeleza adhima ya kile walichokuwa wamekidhamiria kwa kusaidiwa na mwanga huo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Vijana hao watatu walikuwa wakifahamika kwa jina la majambazi ambao walivamia duka la nguo na ya vifaa vya umeme katika mtaa wa kongo jijini mwanza na kufanikiwa kupora mali nyingi pamoja na pesa vile vile waliwaua walinzi watatu ambao walikuwa wagumu kuruhusu wizi huo utendeke kwa kuhofia kupoteza ajira zao, hivyo walilazimika kupotezewa uhai wao , milio ya risasi katika masikio ya watu ilikuwa kama miziki katika ukumbi wa muziki ndani ya Coconut hoteli ambapo siku hiyo kulikuwa na bonaza, milio hiyo ilipelekea baadhi ya binadamu kukimbia hovyo ili kuziepusha roho zao , katika watu ambao waliokuwa wakikimbia hovyo walikuwemo wasichana wawili mapacha waliokuwa wakifahamika wa majina ya Rhoda ambaye alikuwa ndiye doto na Rhodina kama kulwa.



    Wasichana hawa walikuwa wamevalia vijinguo vya ajabu ajabu ambavyo havikustahili kuvalika mbele ya macho ya watu , vilikuwa visketi vyepesi na vifupi huku juu wakitupia vitop vilivyokuwa vikiishia katikati ya matumbo yao vikikiruhusu kitovu na kiuno kuwa nje chini walivyaa ndala za kimasai. Mavai hayo yalileta picha ya moja kwa moja kuwa walikuwa wakiuza miili yao alimaarufu kama Changudoa.

    Mbio zao ziliishia katika moja ya jengo la ghorofa lililokuwa halijamalizika kujengwa mtaa wa maduka matatu huku milio ya risasi ikiendelea kupenya katika ngoma za masikio yao.

    Wasichana hawa mapacha waliokuwa wakifanana sana kuanzia unywele wa kichwani hadi kucha la kidole humba , achilia mbali maumbo ya miili yao iliyokuwa ya umbo la namba sita .Walikuwa na nywele nyeusi mithili ya masizi ambazo zilikuwa zimekipendezesha kichwa kilichokuwa na masikio madogo yenye pina nyembamba lakini zilikuwa na uwezo wa kupeleka mawimbi ya sauti vyema.



    Macho mviringo na yenye kusinzia kila muda pua ndefu kama fagio la chelewa nazo zilizidi kuongeza uzuri kwa wasichana hao wenye umri wa miaka 14 tu lakini walikuwa wazuri hatari , shingo ndefu kama ya twiga , vifua vidogo lakini vilibalikiwa chuchu saa sita ambazo zilikuwa na mgomo wa kulala japo wanaume walikuwa wakizilazimisha kufanya vile .

    Nyoga zilizokuwa zimeshikilia hips matata , achilia mbali makalio makubwa kama mito nayo yalizidi kuongeza uzuri kwa mabinti hao kutokana na kufanana huko kwa kila kitu walikuwa tofauti katika kimo ambapo Rhodina alikuwa mfupi na mwenye dipozi matata hata kama analia zilichoreka mashavuni mwake.

    Wakiwa katika jengo hilo huku mioyo yao ikiendelea kutawaliwa na kiumbe woga Rhoda alihisi akipapaswa begani na mtu , kabla hata hajairuhusu shingo yake kugeuka alizibwa mdomo na kiganja cha mtu aliyekuwa akitetemeka kwa uchu!



    "Psiiiii!!!!.......na ..nawewe ukijaribu kupiga kelele natoboa tumbo la...la ..huyu!" Kijana yule aliyekuwa akifahamika kwa jina la Mateso makazi yake yakiwa mtaani aliongea huku akitoa kisu ndani ya suruali yake chafu na kumuonyesha Rhodina huku akiwa hana mdhaha katika kila neno alilokuwa aliongea.



    Machozi ambaye ndiyo haswa alikuwa mfariji kwa mabinti hao alianza kuwafariji kwa kutoka ndani ya macho yao baada ya kusukumwa na moyo ambao ulishindwa kuvumilia.



    lakini mfariji huyo hakuweza kumkataza Mateso kutekeleza adhima yake alianza kumtoa Rhoda nguo ya juu na kupeleka mdomo wake katika chuchu za Rhoda ambaye alikuwa mgumu kuruhusu hilo lakini Mateso alimchana mkono wake kwa kisu kile hali iliyopelekea Rhoda kuachia kilio cha maumivu makali.



    Rhodina hakuweza kuvumilia hayo haraka- haraka aliokota kipande cha nondo na kumpiga nacho kisogoni hali iliyopelekea Mateso kumuachia Rhoda kutokana na maumivu hayo ikawa nafasi kwao kukimbia lakini bahati mbaya Rhodina alijikwaa na kudondoka Mateso akawa amepata nafasi nyingine kwao na safari hiyo alikuwa na hasira sana.





    Haha! Haha!Haha," kilikuwa ni kicheko kutoka kwa Mateso baada ya kumkamata Rhodina ambaye alimpiga na nondo kichwani , kicheko hicho cha Mateso hakikuwa cha furaha tu bali kilichanganyikana na maumivu aliyokuwa akiyoasikia katika jeraha lake la kichwani hata sura yake ijithihilisha meno nayo yaliumana kuashilia kuwa alikuwa na hasira ya maumivu .

    "Ni..sam..ehe ..ka...kaaka," Rhodina alijitajidi kujitetea huku akisindikiza msamaha huo na machozi ambayo alidhani yatamsaidia.

    "Mpu..mbafuuuuuu! Ni..nini ? Yaaani.. paaaa!" Mateso alizungumza kwa hasira huku akimaliza maneno hayo na kofi mwanana lililotua vyema katika mgongo wa Rhodina aliyekuwa ameinama kofi hilo lilimfanya anyanyuke na hiyo ikawa nafasi kwa Mateso kumchania nguo yake kisha alimvamia na kuanza kumuingilia kimwili kwa nguvu .



    "Daaaah!! Ninyi watoto watamu hatali japo mpo wadogo sana nitakuwa nawawinda kila siku , halafu mwambie huyo mwenzako nikimpata naye lazima nimle" alitamka maneno hayo Mateso huku akivuta suruali yake iliyokuwa magotini.

    "Nakesho mje tena !" Mateso aliendelea kutoa maneno ambayo kwake yalikuwa asali lakini kwa Rhodina yalikuwa shubili.



    "Oole dada "Rhoda alitoa neno hilo kwa Rhodina baada ya kurudi eneo hilo kwa mikono yake laini alimfuta machozi aliyoweza kuyaona kwa msaada wa mwanga kutoka kwa mbaramwezi ,

    "Twende dada!" Rhodina alitamka neno hilo huku akiwa anamnyanyua pale chini , pole pole walianza kutembea kuifaata barabara ya nyerere road.



    "Sasa dada Rhodina tutafanyanje?"

    "Kivipi?" Alijibu huku akifunga funga fundo sketi yake iliyokuwa imechanwa vibaya na Mateso .

    "Si hatuna pesa kumbuka juzi jana na hata leo hatujampa pesa atatuua."

    "Mmmmh! Phuuuuuuu!" Rhodina alishusha pumzi ndefu zenye mchoko ndani yake kabla ya kuongea," tutamweleza ukweli!" Alisema Rhodina huku akianza kuondoka maana walikuwa wamesimama kidogo.



    "Atatuelewa kweli?"

    "Itabidi aelewe tu! Mimi sina hamu ya kiendelea na kazi tena twende nyumbani," wote walikubaliana kuondoka mjini na safari ya kuelekea ilemela saba saba usiku huo wa saa nane , kwa miguu huku wakiwa wanaongea story mbalimbali ili tu kujisahaulisha yaliyotokea .



    ******



    Rhodrick alikuwa mtoto wa nne na wa pekee wa kiume katika familia ya Mzee Steven na mkewe Modesita .Mzee huyu alikuwa mwenyeji wa mkoa wa Simiyu ila makazi yake yalikuwa jijini Dar es salaam akiishi masaki.

    Mzee Steven alikuwa mfanyakazi katika benki ya CRDB tawi la vijana kariakoo akiwa kama meneja kuwa meneja hakukumfanya kubweteka na mshahara hivyo alikuwa amewekeza sehemu tofauti tofauti kama vile Mwanza , Mbeya na hata Simiyu alikuwa mfupi kiasi wa kimo na maji ya kunde asiyependa uzembe katika kazi na hata katika masomo kwa watoto wake.

    Umakini huo ulimsaidia kwani mabinti zake wawili walikuwa wamepata kazi nzuri na mmoja alishindwa masoma baada ya kutekwa na starehe za mji ule , alijikuta akipata mimba akiwa kidato cha pili .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Uwepo wa mtoto mmoja wa kiume katika familia hiyo kuliwafanya wazazi hao kumpenda kupita maelezo , hakuwahi kukosa chochote , japo alikuwa anapendwa sana upendo huo hakumfanya kuwa kilaza shuleni nako alikuwa moto wa kuotea mbali.



    Jumamosi moja alikuwa amekaa katika moja ya masofa yaliyokuwemo ndani humo huku akiwa ametazamana na laptop yake , akifatilia habari za mtawala wa zamani wa Mali Makansa Kan Kan Musa , alivutiwa na utwala wake jinsi alivyokuwa akijipatia mali pia hakuishia hapo hapo alifatilia habari za watawala wa Misiri.



    "Duuuh! Hapa hata watungeje swali lazima niue," aliwaza ndani ya akili yake huku akiachia tabasamu.

    " kaaka muda wote huo upo kwenye laptop tu toka asubuhi hadi sasa hivi."

    " Dogo ninamtihani jumatatu tu "

    “Even if( hata kama) " alisema Rebecca huku akiweka vitabu na madaftari yake juu ya kichwa cha kaka yake.

    "Janaaa..jana na leo nimekuomba unielekeze maswali hutaki?" Rebecca aliongea kwa kudeka sana huku akikaaa pembeni mwa Rodrick.

    "Usikute viswali vyenyewe vyepesi," Rodrick alinyanyuka na kuanza kumuelekeza mdogo wake waliokuwa wakipendana.

    "Sasa unataka uende sekondari peke yako".

    “Eeeeh! Utaenda tu zingatia masomo na ushauri wa wazazi,”akamjibu na kuizima talakilishi yake kisha akasogeza vitabu vya mdogo wake na kuanza kumuelekeza kile kilichokuwa kimemkwaza.





    Kama kawaida Mzee Steven hakuacha kumshauri kijana wake hasa hasa upande wa masomo alifanya hivyo baada ya sala za jioni na baada ya Chakula cha usiku

    "Rodrick unatakiwa usome sana ili baadaye uje kuendesha shughuli zangu maana hawa ndugu zako mda si mlefu watakwenda na waume zao sasa ukicheza itakula kwako , kwanza mitihani mnaanza lini?”

    "Jumatatu!"

    "Je umejiandaaje na kumbuka ahadi ya gari endapo utafaulu kwenda kidato cha tano,"

    "Ndio lazima nifaulu tu," walizidi kuongea usiku huo kisha wote waliingia vyumbani kwao , hayo ndo yalikuwa maisha ya familia hiyo.

    Baada ya kufanya mtihani wake Rodrick alifanikiwa kufanya vizuri na kujiunga kidato cha tano na huku alimaliza miaka yake miwili vizuri na kujikuta akifanya vyema zaidi na kufanikiwa kujiunga na Chuo kikuu akisomea shalia .

    "Safi sana kijana unaendelea kunifurahisha , sio kale kangedele Leah !"

    "Dady msamehe tu."

    "Nini? Acha upuuzi tena hii mara ya pili ananijazia wajukuu mpuuzi sana muache akome," aliongea mzee Steven huku akiwa ameanza kuwaka hasira.

    "Lakini Ba..."

    "Hakuna cha lakini kwanza paki hapo niingie kwa rafiki yangu nakuona leo umelewa sijui umeanza lini kunywa pombe !" Aliongea huku akishuka ndani ya gari na kuelekea ndani ya duka lilokua mbele yake.

    Dakika kumi alilejea na safari ya kuelekea sinza iliendelea huku wakiwa wanazungumza , mengi siku hiyo alikuwa anamtembeza kijana wake katika biashara zake kabla ya kuanza masomo ya chuo.

    "Kata kushoto nataka nikaone maendeleo ya Dada yako , toka nimfungulie sijarudi tena."

    "Heeee! Kuna duka huku? Rodrick aliuliza kwa mshangao huku akiwa makini na usukani.

    "ndio Pamela nilimfungulia duka huku alikuwa mtiifu sana daima nampenda mtu wa namna hiyo," walizidi kuhabarishana swala hilo.

    "Paki hapa tu kule hatuwezi kupita."

    Walishuka ndani ya gari aina ya PRADO na kuanza kutembea kuelekea dukani Kwa Pamela

    "Sasa hapa umefanya cha maana hata ukiolewa mmeo atajivunia kuwa na mke mchapa kazi."

    "Ahsante."

    "Naona leo unatembea na asali wetu."

    'Aaaah Pam sipendi bhana."

    "Wewe punguza polojo Pamela hebu leta soda za wageni , makoo yametukaukia sana !" ilibidi mzee huyo akatishe maongezi ya watoto wao

    "Matokeo vip?"

    "Ameua chezea asali wetu," hivyo ndivyo familia hiyo iliyokuwa ikiishi kwa utani utani.



    ******



    Walizidi kutembea usiku huo wakipitia barabara ya airport pole pole huku wakiyapanga maneno ya kumueleza boss wao.

    "Nyie watoto usiku huu mnaelekea wapi?" Aliuliza mwanamme mmoja aliyekuwa ndani ya gari

    " njooni hapa niwasaidie kuwapeleka kwenu " maneno hayo yaliambatana na kitendo cha kushuka ndani ya gari taa ya hatari iliwaka vichwani mwao walianza kukimbia kila mtu njia yake , Rhoda akiwa anakimbia huku akihema kwa nguvu alisitukia ile gari ikiwa tena mbele yake kila alipojalibu kuelekea aliiona mbele yake hali iliyopelekea kupiga kelele lakini. Hakupata msaada wote wote mtisho huo ulipelekea kupoteza fahamu Kwa mda na baada ya dakika kama kumi alizinduka na kujikuta akiwa amelala barabarani pembeni yake alikuepo Rhodina akiwa akikoroma huku umati wa watu ikiwa umewazunguka.

    "Nyie watoto mbona mmelala hapa?" Yalikuwa maswali yaliyojirudia rudia kutoka kwa wananchi hao na kuleta bughudha masikioni mwao , bila kuongea walinyanyuka na kuendelea na safari zao huku wakiwa wamechafu sana na miili yao ikiwauma .

    .

    "Mmmh? Ndo nini kufika saa mbili nyumbani?"

    Mama mchepuko aliwakaribisha Rhoda na Rhodina kwa maneno makali hata kabla ya salamu

    "Tu...tuli...pata ... shikamo ma.." hata kabla Rhoda kumaliza maelezo hayo mama mchepuko alimkatisha .

    "Nipeni kwanza mapato yangu haraka," akasema huku akinyosha mkono wake lakini Rhoda ama Rhodina hawakumpa chochote .

    "Vipi mnanichelewasha!" Alizidi kutapanya maneno tena safari hii yalitoka kwa ukali.

    "Hatukupata chochote !" Rhoda aliyekuwa msemaji zaidi ya Rhodina aliongea akiwa ameikusanya mikono yake chini ya kidevu huku kidole gumba cha mguu wake kikichora chora chini na macho yake yakitazama aridhi , hakutaka kumtazama mama mchepuko aliyekuwa amesimama katikati ya mlango wa kuingia sebuleni na kuziba mlango wote kutokana na unene wake .

    "Acheni masihala siku tatu zote hakuna kitu mnavyokula na kunywa mnajua vinatoka wapi?, Mtajua kwanini naitwa mama mchepuko leteni pesa !" Alizidi kupayuka huku povu mdomoni likimtoka , macho nayo yalitumbuka na kuongeza ukubwa mithili ya tufe, hali iliyozidi kuwa tisha akina Rhoda waliokuwa wamegememea ukuta , bila aibu aliwafuata na kuanza kuwakagua lakini hakupata chochote .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mama tulikutana na jini mbo...." Rhodina aliekuwa mkimya alijikuta akipandwa na hasira na roho ilimuuma sana baada ya kukumbukia masaibu waliyokutana nayo usiku lakini mama huyo hakujali hayo yeye alichokijua ni pesa tu .

    "Mpumbafu nini tena funga kopo lako mbwa mkubwa , na nilishawakataza kuniita mama , na ukome huko huko makaburini ndo aliko mama yenu fyuuuuuuu!," Alizidi kuachia maneno bila kujali.

    "Na kuanzia leo hamtatoka humu , hakuna kula na mtaanza kazi mpya nadhani hamtaweza kuleta mchezo tena " alizidi kufoka wala hakuwa na mda wa kuulizia nguo ya Rhodina ilifanya nini au Rhoda alifanya nini , aliondoka eneo hilo akiwa ametuna Kwa hasira na kufanya kifua chake kivimbe .





    "Mmmmh !" Rhoda aliguna kwanza kabla ya kuongea chochote hali iliyopelekea Rhodina kuhoji.

    " vipi shost!?"

    " nahofia ni wapi tutaenda!,Rhodina unakumbuka jinsi tulivyoteseka mtaani na isitoshe mlinzi hawezi kuturuhusu tutoke nadhani mama atakuwa ameshamweleza "

    Rhoda aliongea huku akiendelea na zoezi la kupaka mafuta

    " daaaaah!, kweli hatari tusubili matokeo mwenzangu"

    Baada ya kumaliza zoezi la kujisafisha walitoka na kuelekea mahali alikokuwa mama mchepuko aliekuwa akiendelea na zoezi la kuwahudumia wateja ndani ya glosery , walipofika tu alitoa ishara kwa wale wanaume

    "Rhoda na Rhodina wasikilizeni hawa vijana msiniangushe mnasikia ?"

    " ndiooo!"

    Wote waliitikia kwa pamoja , hakili zao zilifanya kazi ya haraka sana kutambua mkasa uliokuwa mbele yao , taa nyekudu ziliwaka ndani ya vichwa vyao , kwa kuwa walikuwa hawajawakilisha pesa yeyote Kwa siku tatu Kwa mama huyo ilibidi wakubaliane na lilokuwa mbele yao walihofia kufukuzwa na kuteseka tena mtaani kama mwanzo na hilo hawakutaka litokee tena , manyanyaso ya mtaani Kwa vijana wa kiume waliyaogopa sana ,

    Walipokumbua picha mbalimbali za matukio walioyowahi kukutana nayo miaka ya nyuma waliumia sana hasa hasa tukio la kubakwa na zaidi ya vijana saba kila mmoja na kuvutishwa bagi achilia mbali kuingiliwa kinyume na maumbile wakiwa na miaka tisa tu , tukio hilo lilikuwa likiwasisimua pindi lilipopita vichwani mwao , japo walikuwa wadogo lakini haikutoka kichwani.

    Ilibidi waongozane na vijana hao hadi katika vyumba vyao na mchezo uliokuwa ukiendelea huko ni kufanya mapenzi , baada ya kulizishana na vijana hao dakika kadhaa waliingia wengine nao ikawa hivyo hivyo siku hiyo walijikuta wakilala na wanaume watatu achilia mbali yule Wa usiku , japo wao ndo walikuwa wakihudumia wateja hao malipo yalikuwa yakichukuliwa na mama mchepuko hata bei alizipanga mwenyew Rhoda na Rhodina waliambulia mia tano tu na masimago ya kwani hamli.

    Siku za neema Kwa mama mchepuko alikuwa akipata hata wanaume zaidi ya kumi na tano, wingi wa wateja ulichangiwa na kazi yake ya uuzaji wa pombe hivyo bar mshenzi hiyo haikukata wateja .jingine lililochangia ni uzuri wao , hakuna mwanaume ambaye hakutaka kurudi tena.

    Watoto wale walibebeshwa mzigo mzito usioendana na umri wao , lakini hawakuwa na pa kwenda , hawakuwa na mtu wa kuwasikiliza , wala kuwahurumia , mia tano ndo ilikuwa faraja yao hadi wanafikisha umri wa miaka kumi na nane walikuwa wakitumiwa kama kitega uchumi Kwa mama mchepuko na teyari alikuwa na mafanikio makubwa sana Kwa kupitia kazi hiyo , vilio na machozi vilikuwa havikati machoni mwao , lakini mama mchepuko alikuwa akichekelea na hata mda mwingine alikuwa akijilaumu Kwa nini hakuanza mapema .



    ******



    Mama mchepuko ama Regina jina alilopewa na wazazi wake baada ya kuzaliwa katika kijiji cha shirati mkoani Mara . Alizaliwa katika familia ya kimasikini sana na duni wazazi wake walikuwa wajaruo wa eneo hilo , baba yake alikuwa hana kazi zaidi ya kushinda virabuni akizungusha pombe za kienyeji na aliporudi nyumbani kazi yake ilikuwa ni kusambaza vipigo Kwa mkewe na Kwa watoto wake wawili Regina na Dominic hata kama hawana kosa , ilikuwa ni lazima akute Chakula japo alikuwa haachi chochote ,

    Manyanyaso hayo yalipelekea kumuua mwanae Dominic mbele ya mkewe na binti yake Kwa kumpiga na mwichi kichwani kisha alianza kuwashambulia na wao akiwa na Lego la kuwaua ili kupoteza ushaidi alijikuta akimuua mkewe lakini Regina aliponea chupu chupu baada ya kufanikiwa kufungua mlango na kutoka nje huku akiwa anakimbizwa na baba yake aliekuwa na panga usiku huo , bahati ikawa yake pale baba yake alipoteleza na kuangukia panga lilomchoma tumboni nae akawa amekufa pale pale usiku huo .

    " hamtakiwi kumgusa mtu yeyote aliejinyonga , amejiua ama ameuliwa , kufanya hivyo kunaweza kukuweka matatizoni baada ya uchunguzi kufanyika maana alama zako zitakuepo mmesikiaaa!"

    " ndioooooo!"

    Aliyakumbuka maneno ya mwalimu wake , japo alirudi kuwatazama mama yake na Mdogo wake alijikuta akiogopa sana na kuanza kukimbia hadi barabarani , barabara iliyokuwa ikielekea Tarime usiku huo huo.

    Aliishi tarime hadi alipobahatika kuelewa akiwa na miaka kumi na sita , lakini ndoa hiyo haikudumu Kwa mda kutokana na Mateso aliyokuwa akikumbana nayo , baada ya kuachana na huyo aliolewa tena lakini nako aliachika sababu ilikuwa ni kutozaa , akawa wa kuolewa na kuachika hali hiyo ikambadili tabia , roho chafu ikazaliwa baada ya kuzidiwa na Mateso nae akawa hana huruma ,

    Regina hakuishia hapo tu alianza kuuza bangi na milungi akitoa Tarime na kuzipeleka sirali alifanya kazi hiyo Kwa mda wa miaka mitatu ndio alipokutana na John mwanaume aliekuwa akiuza madawa ya kulevya na kuwa wapenzi wakisambaza unga huo kila kona ya Tanzania huku pesa iliyokuwa inapatikana ilitunzwa benki .

    Siku moja John aliamua kumdhurumu pesa yote baada ya kumchomea Kwa polisi alipokuwa akielekea Sirali hivyo Regina akawa ameenda gerezani Kwa miaka saba , baada ya kutoka hakuwa na mbele wala nyuma isitoshe alikuwa na hasira na pesa zake pia roho mbaya nayo alizidi kuongezeka , akawa tena ameanza kuuza tena bangi akitoa Tarime na musoma na kuzileta mwanza usiku sana , japo alikuwa akiuza bangi kumtafuta John hakuacha hadi alipokuja kungundua kuwa Jhon hakuwa nchini.

    Safari hizo za usiku ndizo zilizochangia kukutana na akina Rhoda stendi ya Buzuruga nyakato mjini mwanza wakiwa na miaka kumi tu usiku mmoja walipokuwa wakibakwa na walizi wa kimasai.





    Kundi kubwa la watu waliokuwa wamevalia mashuka na sime mkononi walionekana wakichekelea tukio lilokuwa likiendelea ,

    Yelo samu yangu aisee!"

    "Hapana yeloo samu yangu akitoka John."



    Yalikuwa ni mazungumzo ya furaha sana na vicheko kati ya wamasai yaliyopenya vizuri ndani ya ngoma za masikio ya mama mchepuko hali iliyopelekea kuingiwa na shauku la kufahamu kipi kilikuwa kikiendelea.



    "Hebu egesha hapo hao wamasai siwaelewi."

    Dereva aliengesha mama mchepuko alishuka CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Eti hapo kunanini?"

    "Aaaah! Si hawa watoto wa mtaani sijui walikula hela ya mmasai sasa wanawabaka!" Aliongea mlinzi mmoja katika eneo hilo la stendi kwa lafudhi ya kisukuma hali iliyopelekea mwanamke huyo kuumia.



    "Nyie mbona mnaraho mbaya!"

    "Aisee yelo polisi huyooooo!"

    Kutokana na mavazi ya kipolisi ambayo mama huyo alikuwa akiyatumia pindi alipokuwa akitoka Tarime ama Musoma kuchukua mizigo yake alifanya hivyo ili asigundulike.



    Kitendo cha wamasai wale kusikia neno hilo wote walitawanyika na kuwaacha akina Rhoda wakiwa watupu huku wakilia.

    "Mbona mko hapa na nyumbani wapi?"

    "Mu..s..omaaaaa!" Rhoda alijibu huku akiendelea kulia kutokana na maumivu aliyokuwa ameyapata.

    "Na hapa?"

    Wote walibaki kimya huku wakiendelea kulia kwa chini chini

    "Haya twendeni."

    "Usitupeleke polisii tuaache tu."

    "Hapana siwapeleki vaeni twende,"



    Wote waliingia ndani ya gari hilo alilokuwa analitumia kuletea mizingo na safari ya kuelekea mabatini alikokuwa akiishi ilianza , mioyo yao ilikuwa ikidunda kwa kasi sana hawakujua kama kweli mama huyo hakuwa askari kutokana na muonekano wa mavazi yake.

    "Eeeeeh! hebu nielezeni kwanini mpo hapa?" Aliuliza baada ya kuwafikisha nyumbani kwake wakiwa tayari wameshaoga na kula kufanya mahojiano usiku huo ili kama kesho angeulizwa kuhusu watoto wale angejua pa kuanzia , kweli hilo lilifanikiwa na akawa amewasistiza endapo mtu angeuliza uhusiano kati yao wangesema alikuwa mama yao mkubwa .



    Mwanzoni aliwalea vizuri sana kama watoto wake lakini upepo ulikuja kubadilika baada ya kukamatiwa mzigo wake uliokuwa na pesa nyingi sana hali iliyopelekea kuishi kama digi digi kutokana na kutafutwa na askari , hakuendelea kukaa Mabatini alihamia Igogo sehemu yenye idadi kubwa ya watu na wenye maisha ya duni sana unaweza ukapaita uswahilini , hakuwa na kazi tena ilibidi aanze kazi ya kuuza pombe ya kienyeji akisaidizana na watoto wale kabla ya kuhamia ilemela.



    Shetani wa mtu ni mtu , ile hali ya upendo aliyokuwa akiitoa kwa watoto wale iliyeyuka kama mshumaa upatao moto na kuzaliwa sumu kali ndani ya moyo wake , shetani akamtumia kuwatumia watoto wale kama njia ya kujipatia riziki kwake , mwanzo alikuwa akiwauza kwa mwanaume mmoja kila siku lakini kadri siku zilivyozidi kidogo alianza kuwauza kwa idadi kubwa ya wanaume na mbaya zaidi hakubagua mkubwa ama mdogo mlevi ama mzima , hali hiyo ilizidi kuongeza idadi ya wateja wa pombe za kienyeji.



    Rhoda na Rhodina walikuwa wakilia sana , muda mwingine walidriki hata kumtukana mungu kwa kitendo cha yeye kuwaleta duniani lakini machozi hayo yenye maumivu na majuto hayakuonwa na mtu .wanaume walevi walikuwa hawakatiki nyumbani kwake na muda mwingine walikuwa wakimsifu kuwa na mabinti wazuri kiasi hicho.



    "Mama mie naumwa tumbo leo siwezi kufanya kazi tumbo linaniuma sana hasa hasa hili la chini!" Rhodina aliongea huku akitoa machozi asubuhi moja, mikono yake yote ikiwa imelikamata tumbo lake na kujikunyata kwa unyonge na kwa maumivu makubwa.



    "Kwa hiyo nani akufanyie kazi zako?” Aliongea kwa ukali huku akiwa ameshika kiuno chake bila kujali.

    "Sijui hata kunyanyuka siwezi."

    "Mmmmh!" Mama mchepuko aliishia kuguna tu na kutoka nje .

    "Sasa wewe utahudumia kila kitu wateja wote uwalidhishe ndugu yako si amejifanya anaumwa sasa kazi kwako," aliongea na Rhoda aliyekuwa bize na kukoroga pombe ndani ya pipa asubuhi hiyo.



    Hivyo Rhoda akawa bize na kazi zote mara ahudumie wateja kimwili asambaze pombe kuosha vyombo usafi wa ndani na n.k, hadi inafikia saa saba alikuwa amechoka nyang'anyang’a .

    "Mama mchepiuiuuu! Leo mke wangu yuko wapi?" Aliuliza kijana mwenye umri wa miaka kumi na tisa lakini alikuwa mwathilika mkubwa wa pombe za kienyeji.

    "Linaumwa hilo," alijibu kwa mkato tena kwa maneno yasiyopendeza kabisa , hakupendezwa na swali hilo maana siku hiyo kulikuwa na wateja wengi sana na hata wengine walikuwa wakiondoka bila kupata huduma ya ngono , hali hiyo ilikuwa ikimuumiza sana maana aliona anapitwa na pesa.

    "Jamani kale kabinti kazuri kweli," mlevi mwingine mzee naye alichangia.

    "Mimi nitakaoa tu."

    "Lakini si umpeleke hospitali."

    "Sina pesa kama hawezi kujitafutia aache afe."

    "Kweli wewe mama mchepuuuuuuu Nitampeleka mimi….. weweeeeeee mlete mke wangu nimpeleke hospitali," kijana wa kwanza alijikuta akiingiwa na huruma.



    Dakika tano Rhoda alitoka akiwa na Rhodina aliyekuwa akitembea huku ameinama kutokana na maumivu ya tumbo.

    "Na muwahi kurudi,"alizungumza akiwa anakerwa sana na kitendo cha kijana yule.

    "Wewe mchepuuu punguza maneno leo nimeoa rasimi," kijana yule aliendelea kutoa maneno ya kilevi kilevi huku akitembea kwa kuyumba yumba.

    Walitembea taratibu sana hadi kilombelo dispersary walifika mapokezi wakaandikisha kila kitu kisha Rhodina akachuliwa vipimo na baada ya vipimo kuchukulia alipewa nafasi ya kukaa nje kwanza akingonja majibu.

    " Rhodina Jackson," daktari aliita haraka Rhoda na yule kijana walimnyanyua Rhodina na kuelekea chumba cha daktari , akiwa bado anatembea akiwa ameinama.

    "Rhodina Jackson una........," daktari aliongea baada ya wote kuingia na kukaaa.

    "Unaaa....., umesema unaishi wapi ?” Daktari alizunguka zunguka kutoka majibu kisha alianza kuwatazama wote kwa zamu.





    Dr malick alizidi kuzungusha zungusha macho yake kwa kila mmoja huku mkono wake wa kulia ukiwa umeshika karatasi ya majibu.

    "Pole binti!"

    "A..sa..ante...," Baada ya Rhodina kujibu Rhoda alijikuta akitoa jibu hilo la mkato mkato huku akinyemelewa na machozi katika kope zake japo alikuwa binti ama mtoto wa miaka kumi na tatu tu dalili ya jambo la hatari kwa dada yake lilianza kujengeka ndani ya kichwa chake kutokana na muonekano wa dakitari yule.

    "Je huyu ni nani yenu?"Akauliza daktari akimtazama kijana yule ambaye alikuwa akiyumba yumba kwenye kiti.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Rafiki tu!"

    "Oky bwana mdogo hebu tupishe kama dakika tatu."

    "Aaaaah! dokta acha hizo mimi hapa ndio nimelipia natakiwa nijue majibu yake," aliongea kijana yule aliyekuwa akifahamika kama Hamis kwa sauti ya kilevi kilevi huku akinyanyuka na kutoka nje moja kwa moja alielekea Igogo hakutaka tena kuendelea kuwa pale maana alijiona kama amedhaarauliwa.



    "Rhodina Jackson ..... majibu yako yanaonesha!....." alisita tena na kumtazama Rhodina aliekuwa amelalia mapaja ya Dada yake huku machozi yakiendelea kutoka taratibu katika macho yake .

    "Rhodina ulishawahi kukutana kimwili na mwanaume?" Aliuliza daktari swali hilo lililowashtua wote, akakosa kidogo raha na kumtazama daktari huyo ambaye alikuwa akimtazama kwa macho makali bila kuyakwepesha.

    “Ulishawahi?”Akarudia kumuuliza.

    "Nd...i...oooo," alijibu kwa sauti ya chini sana.

    “Mmmmh!”Akashusha pumzi ndefu sana na yenye kitu kizido ndani ya moyo wake kabla ya kuzungumza chochote.

    "Sasa inaonekana umeambukizwa magonjwa ya ngono kwa kitaalam tunayaita Sexcually Transmited Infection ama ( STI) kwa kifupi. Magonjwa haya yanasababishwa na kufanya mapenzi bila uangalifu mzuri naweza nikasema ngono zembe !......." alisita kidogo , alivua miwani yake kisha aliendelea.



    "Magonjwa haya yamegawanyika katika makundi matatu lakini tutazungumzia moja tu,..ambalo ndilo wewe limekukumba....maabukizo yake hutokea pale majimaji , mate ama damu ya mtu aliyeambukizwa magonjwa hayo anapokutana kimwili na asiye na maabukizo hivyo inakuwa lahisi mtu huyo kupata magonjwa hayo kwa njia ya kujamiana, kunyonyana ndimi na n.k, magonjwa haya ni kama kisonono , Trikomans na kandida japo yapo mengi tu.

    “Je unafahamu dalili zake,”akawauliza akiwa nawatazama kwa umakini sana.

    “Hapana!!”Wote wakajibu kwa pamoja.



    “Iko hivi…dalili zake kwa mwanamke zipo dalili nyingi sana ila kuu ambazo zinajitokeza kwa haraka ni kama:.

    - kupata maumivu chini ya kitovu au tumbo la chini kama ulivyokuwa ukidai

    - kutokwa na usaha au majimaji yenye harufu mbaya sehemu za siri muda mwingine unaweza kupatwa na muwasho hizo ni chache tu za dalili japo wewe ulikuwa bado hujaathilika sana .

    Chanzo cha magonjwa haya ni kama vile kujihusisha na ngono zembe , kujihusisha na ukahaba na hata kujamiana ukiwa umelewa hivi vyote vinaweza kusababisha wewe kupata magonjwa hayo," dakitari marick aliendelea kuwaelimisha kuhusiana na gonjwa hilo na aliwaomba wamlete na mtu aliyewaambukiza , pia aliwaelekeza namna ya kujikinga na magonjwa hayo na mwisho kabisa alitoa tiba ya awali kwa Rhodina kisha walirejea nyumbani.



    Miezi tisa.



    Hali ya Rhodina ilikuwa imeshatengamana kabisa na alikuwa aliendelea na kazi zake na hicho hicho kipindi walichohama kutoka Igogo hadi Ilemela Sabasaba baada ya mama mchepuko kujenga huko , pia alibadili kazi ya kuuza pombe za kienyeji na kufungua kibar mshenzi nyumbani kwake.



    Mateso kwa mapacha hao hayakupungua hata kidogo mwanzo alikuwa akiwaruhusu kwenda kujiuza mjini lakini baada ya kutoleta pesa za kutosha watoto wale walianza kufungiwa ndani na kuletewa wanaume wa kila namna walivumilia kwa mda mrefu sana hadi walipofikisha umri wa miaka kumi na nane.



    Ilikuwa siku ya krismasi , siku hiyo ilikuwa na wateja wengi sana kwa mama mchepuko toka asubuhi hadi saa tisa Rhodina na Rhoda walikuwa hawajapumzika hata dakika kumi ilikuwa ni bandua bandika ,ikafika hatua Rhodina akachoshwa na hiyo hivyo akamua kukataa kuendelea na kazi hiyo mara baada ya kuwahudumia wanaume saba , hali iliyopelekea mama mchepuko kuanza kumtolea maneno makali sana baada ya kulazimishwa kurudisha pesa za mteja aliyekuwa amelipa pesa nyingi sana siku hiyo.



    "Wewe mwanaharamu unaleta jeuri siyo?" Mama mchepuko aliongea baada ya kuingia chumbani humo.

    "Mwanaharamu mwenyewe kama unaona raha na wewe engesha mk***, umezidi kututumikisha , tazama ni miaka nane bado tu unatunyanyasa ,tunahitaji kuondoka hapa," aliongea Rhodina kwa jaziba huku akitoa machozi ya hasira.



    "Nini wewe mbuzi?"alimaka Regina ama mama mchepuko na kuanza kupiga hatua kumfuata Rhodina aliYekuwa amekaa juu ya kochi chumbani humo , huku akiwa na nguo ya ndani tu ya chini kwa hasira iliyochanganyikana na pombe alimpiga ngumi iliyompeleka hadi chini hiyo ilisababishwa na njaa aliyokuwa nayo , haraka haraka alichukua chupa iliyokuwemo humo aliipasua chini ya kitako na kumfuata Rhodina aliyekuwa bado amelala chali alimchoma na chupa hiyo tumboni kwake kama mala tatu.

    "Nakufaaa… Rhooooooo!" Hakumalizia akawa ametulia pale chini huku mwili wote ukiwa umetapakaa damu.

    "Ukome,” liongea mama mchepuko huku akianza kupiga hatua kutoka chumbani humo

    "Sasa vipi pesa zangu?" Mteja aliyekuwa amekataliwa penzi na Rhodina aliuliza huku akiwa anavaa suruali yake haraka haraka kichwa chake kikiwa kimechanganyikiwa sana.



    "Subili nije " alitoka nje baada ya kama dakika saba alirejea na Rhoda

    "Mtumie huyu."

    "Aaaaaah!, Sina hata hamu tena , niliyekuwa namtaka umemuua basi tena na pesa chukua," aliongea na kuondoka.

    "Mamaa umememuua Rhodina ?"Rhoda aliongea huku akitetemeka hakupata jibu la swali hilo moja kwa moja alianza kukimbia kuelekea chumbani kwa Rhodina hakuamini macho yake baada ya kuingia chumbani mle.



    ******

    Dar es salaam.



    Rodrick Steven alikuwa akiendelea na masomo yake ya Sheria Chuo kikuu na huo alikuwa mwaka wa mwisho , baada ya miezi kadhaa kupita alihitimu masomo yake ya Sheria kisha alianza kusimamia kazi za baba yake zilizokuwa mikoani hasa hasa mwanza hata majibu yalipotoka aliomba afanyie kazi mkoani mwanza akiwa kama mwanasheria .



    Miguu yake yote iliishiwa nguvu hakuweza kupiga hatua mboni za macho nazo zilishindwa kuona kilichokuwa kinaendelea alibaki ameganda mlangoni kama chizi asijue la kufanya kama uchinzi tayari Rhoda alikuwa chinzi dakika kama tatu ndipo alipozinduka na kukimbilia alipokuwa Rhodina .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Rhodinaaaaaa! Rhodinaaaa!” Rhoda alimuita dada yake huku analia kwa haraka sana aliinama na kuichomoa chupa ya bia iliyokuwa bado imo tumboni.

    "R....h..ooooo....d...aaa!”Rhodina aliita kwa sauti ya chini sana huku maneno yake yakitoka kwa shida sana.

    "Dada usifee…dada usife nitabaki na nani mie Rhodinaaaa njoooo!" Alizungumza huku akikiinamisha kichwa chake juu ya kifua cha dada yake na ambaye alikuwa ameyafumba macho yake huku nusu ya mwili wake wote ukitapakaa damu.



    "N..a..ku...p..endaaaaaa.Rhooo..."

    Rhodina hakumalizia sentensi yake akawa ametulia hali iliyopelekea Rhoda kulia sana akiwa anamtikisa kwa nguvu zake zote akidhani labda angeamka lakini haikuwa hivyo.



    "Baba , mama na Dada Rhodina nimewakosea nini hadi mnanifanyia hivi , kwanini mnaondoka wote , nitaishi na nani mimi? Rhodina tulipendana , Rhodina tuliliwazana , Rhodina ulijitolea kubakwa kwa ajili yangu , Rhodinaaaaa njoooo! Usiniache…amkaaaaaaa… amkaaaaaaa… tuliachwa wawili tuuu… leo umeniachaaaaa!"

    Yalikuwa ni maneno yenye maumivu yasiyoelezeka kwa Rhoda hakuamini kama siku moja angekuja kumpoteza pacha mwenzake na ndugu pekee aliyekuwa amesalia katika dunia , alilia sana huku akiwa ameupakata mwili wa Rhodina kilio hicho kilipelekea na yeye kupoteza fahamu hakujua kipi kilikuwa kikiendelea tena, alikuja kuzinduka akiwa hospitali mikono yake ikiwa imefungwa pingu na pembeni alikuwepo askali polisi wa kike.



    "Nimefikaje hapa?" Aliuliza baada ya kurejewa na fahamu.

    "Nyamaza muuaji mkubwa paaaa!" Askari yule alimaka kwa hasira zilizosindikizwa na kofi la shavuni,ambalo lilikuwa kali sana.

    "Sijauaaaa Mimi , oooooh Rhodina mleteni Rhodina wanguuuuu!"

    "Kimya mshenzi sana kama wewe ni shetani basi nambari moja duniani , wanaume walikosa hadi unadriki kumuua dada yako kisa mchumba wake!" Askari yule aliendelea kutoa maneno yaliyomshangaza sana Rhoda.

    "Sikuuu...." alikatizwa.



    "Si ungeenda hata kujiuza vitunguu ama makoroboi , sasa kwa ujinga huo hesabu maisha yako yote jela paaaa!" Alizidi kuongea na kumshushia kipingo cha maana ambacho kilikuwa ni kinyume na kazi yake askari yule hakujua nini kilikuwa chanzo.

    Rhoda alilia sana hakujua nini hatima ya maisha yake.

    "Nataka nikamuone Rhodina askari."

    "Wewe mbwa mkubwa funga kopo lako badala ya kufurahia kitanda kizuri cha mwisho katika maisha yako unalopoka lopoka au unataka nikupeleke selo ukaone utamu?”

    "Ha..pan...a!" Usiku mzima hakupata hata lepe la usingizi muda wote aliutumia kumlilia Rhodina.



    ******

    "Mama mchepuko umeua tafadhali kimbia kabisa."

    "Hana haja ya kukimbia yule mwenziye ndio atakiona cha mtema kuni tayari ameshashika ile chupa na isitoshe uthibitisho wa tukio utaonesha yeye maana hadi sasa bado amemlalia marehemu wewe nenda polisi katoe maelozo kabla hajazinduka."



    Yalikuwa ni mazungumzo kati ya mama mchepuko aliyekuwa akitetemeka kwa hofu na baadhi ya walevi waliokuwepo eneo hilo kweli hakupoteza muda alikodi pikipiki iliyompeleka kituo kidogo ya polisi cha pansiasi.

    "Tukusaidie nini mama?" Mwanaume aliyekuwa amevalia mavazi ya jeshi la polisi alikamuliza mwanamke huyo mara baada ya kufika ofisini hapo.

    "Kuna mtu kamuua dada yake kisa mwanau.....?" Hakumalizia alikatishwa.

    "Maweeeeee…linani hilo?" Askari aliyekuwa zamu alishtuka sana hali iliyopelekea kuongea kilugha.

    "Mama kaa hapa."



    Baada ya kukaaa askari wale walianza kuandika maelezo kisha waliondoka na mama mchepuko hadi nyumbani kwake walikokuta mji mzima umefurika watu na Rhoda akiwa bado ameukumbatia mwili wa ndugu yake huku akiwa bado amepoteza fahamu.



    "Mtoeni huyo muuaji mtieni na pingu kabisa harafu mpelekeni hospitali ya jeshi haraka iwezekanavyo ili atatusaidia kwa hili," alitoa amri mkuu wa msafara huo kweli Rhoda alikimbizwa haraka hospitali ili aje asaidie kesi iliyokuwepo huku mwili wa Rhodina ukichukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya Sekoutoure iliyopo maeneo ya Isamilo ukingonja mazishi , mama mchepuko akiachwa huru kwa siku hiyo.

    "Hivi kweli yule jamaa hawezi kunifatilia?"

    "Hakunaaaaa hebu sogea huku!"

    Yalikuwa ni mazungumzo kati ya mama mchepuko na hawala yake aliyekuwa anempata siku hiyo na pia alishuhudia tukio zima, na ndiyo huyo huyo aliyetoa wazo la kumngeuzia kesi Rhoda

    "Nitakutetea mpenzi.”

    "Kweli "

    "Aaaah! Mimi naijua sheria usinione hivi nilishawahi kufanya kazi mahakamani na isitoshe kuna hakimu ambaye ni rafiki yangu yani wewe furahia maisha tu."

    "Hahahahaha nakupa penzi ambalo hujawahi kupewa mwaaaaaa!" Aliongea mama mchepuko huku akiwa anakidadia kifua cha mwanaume huyo usiku wa siku hiyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kesho wakikuuliza kuhusu kuwafahamu mauaji ya mtoto yule wakane na udai walikuwa wafanyakazi tu, tena subili niongee na afande Juma atatusaidia acha wakafie huko hawana faida yeyote alaaa!" Hakupoteza muda aliichukua simu yake na kumtafuta Afande.

    "Hahahahaha! Usijali wewe ni ndugu yangu hako kachokaraa kamekwisha."

    "Kweli Afande!"

    "Nyie andaeni lakini tano tu na lazima kesho ama keshokutwa atakuwa Butimba."

    "Nitashukru sana Afande".

    "Ndio maana nakupenda," aliongea mama mchepuko baada ya hawala yake kukata simu.



    *****

    "Baby Mimi naondoka mwanza leo hii hii?"

    "Jamani honey mbona hivyo yaani baada ya kunitumia ulivyotaka."

    "Sio hivyo Rose."

    "Ila?"

    "Si unawajua wale akinadada wanaokaa kwa yule mama mwenye groseri iliyoandikwa Mipango, sasa yule mwenye macho ya kusinzia sinzia yule mzuri mzuri a..."

    alikatishwa

    "Andrew usiniambie Rhodina amekufa?" Rose aliyekuwa amelalia miguu ya mpenzi wake huyo alijikuta alinyanyuka huku uso wake ukipoteza tabasamu la hasira alilokuwa nalo mwanzo.

    "Kweli Rhodina amekufa!"

    "My God!(Mungu wangu!) nani kamuua?"

    "Honey ni stori ndefu, niache kwanza niondoke nikifika huko nitakueleza nayahofia maisha yangu mama yule anaweza kunigeuzia kesi," aliongea Andrew huku akiamka na kuanza kukusanya nguo zake.

    "Mbona wewe mwoga hivyo au ndo uliyemua?"

    "Mama mchepukooooooo!" Andrew aliongea huku akitoka ndani na kuanza safari ya kukimbilia Dar es salaam.



    Yalikuwa ni maumivu sana ndani ya moyo wa Rhoda usiku huo alilia sana hadi sauti ilimkwama , machozi nayo yaliisha ndani ya macho yake akawa analia mkavu mkavu , katika kulia sana na kutawaliwa na mawazo mengi fikra yake ilimpeleka miaka ya nyuma sana.



    Rhodina na Rhoda walikuwa watoto pekee katika familia ya mzee Jackson machagu aliyekuwa mwenyeji wa mkoa wa Mara wilayani Tarime kijiji cha mweru , bwana huyu alikuwa mfanyabiashara na mmoja wa viongozi wakubwa wa serikali ( mbunge ).

    Katika kuzaliwa kwao walikuwa peke yao tu yeye na pacha mwenzake , kitu shida kilikuwa historia katika watoto hao , walikula vizuri walivaa vizuri na malezi ya hali ya juu wakiwa na mwaka mmoja na nusu teyari walikuwa wameshapelekwa shule tena yenye gharama ya hali ya juu , japo walikuwa wakiandika vikorokocho lakini vitu hivyo vilikuwa ni furaha kwa wazazi hao , hadi wanafikisha miaka ya kwenda shule maisha ya familia hiyo yalikuwa mzuri sana.



    "Baba nataka hiyo mimi sitaki hiyo!"

    "Aya na wewe Rhodina unataka nini mama?"

    "Mmmmh!"Rhodina aliguna huku akipandisha mabega juu.

    "Hataki dady nipe mimi yake!" Rhoda aliyekuwa muongeaji kuzidi mwenziye alidakia maongezi hayo.

    "Oky twend....."

    Hata hakumalizia fikra zake zilizokuwa zinamfurahisha na kusahau maumivu ya kuondokewa na ndugu yake alikatishwa na askari aliyekuepo.

    "Wewe muuaji amka muda wako wa kusitarehe umekwisha,"

    liongea askari huyo huku akimsukuma Rhoda hakuwa mbishi aliiruhusu miguu yake taratibu kusimama na safari ya kuelekea kituo kikuu cha polisi ilianza , akiwa nyuma ya defender la polisi.

    "Binti unatakiwa uwe mkweli kuhusiana na jambo lililotokea jana je ni kweli ulimuua dada yako ?" Afande Juma aliyekuwa amekabidhiwa kesi hiyo alianza kumhoji Rhoda baada ya kufika kituoni hapo.

    "Sikumuua askari."

    "Hukumuua wakati tulikukuta ukiwa na chupa iliyotumika kufanyia mauaji hayo , yaani kwa akili yako unadriki kunidanganya?"

    "Kwe...li...si...kumuua ka..bisa," Rhoda aliongea huku akianza kulia tena.

    "Kilio chako hakitakusaidia chochote , ni bora unyamaze tu."

    "Nataka nikamuone Rhodina tafadhali."

    "Binti usitupote......" Kabla hajamalizia kuongea aliingia mama mchepuko akiwa na hawala yake.



    "Tena anyongwe kabisa binti huyu ni katili sana paaaaa!" Mama mchepuko aliongea huku akimalizia na kofi kali katika mwili wa Rhoda lililomfanya kulia zaidi , na kumtazama kwa jicho la hasira sana ,lakini hakufanya chochote zaidi ya kuishia kutuna kwa hasira.

    "Mu...ngu...h...yu..uuuupo..!" Rhoda alitamka maneno hayo huku akilia sana , alijiona mkosefu , alijiona hafai chochote , dunia yote ilikuwa imemuacha hakika alichukia kuubwa binadamu alitamani bora angeumbwa hata ngo'mbe ambaye kuchinjwa ni haki yake , kuliko mateso hayo hakuna aliyejali maumivu mabichi ya kuondokewa na dada yake wote walimtenga alilia sana.

    "Wewe unamjua mungu kweli?" Hamis hawala wa mama mchepuko alihoji.

    "Mungu.. Mungu muite sasa ashuke kahaba mzoefu leo anamtaja mumgu hahahaha!! Kweli dunia inavituko hahahaha!" .mama mchepuko nae aliongezea.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ipo siku tu! " Alitamka Rhoda neno hilo ambalo kila mtu alimcheka sana neno hilo lilichangia kumbukumbu ya siku moja akiwa na Rhodina,

    "Rhoda tunateseka ila ipo siku tu na hatuwezi kujua labda huko kukawa na mateso ama furaha cha muhimu ni uvumilivu tu."

    Hakika hazikuwa taratibu za jeshi la polisi kufanya hayo lakini pesa ndio ilikuwa imenunua haki ya Rhoda baada ya mahijiano ya muda mrefu Rhoda alipelekwa mahabusu akigonjea hukumu yake ambayo ilikuwa ikitarajiwa kufanyika muda mfupi sana kutokana na vithibiti vyake kuwa wazi.

    Akiwa mahabusu aliendelea kulia sana hadi ikawa kelo kwa mahabusu wenzie .



    *****





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog