Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

JELA NI HAKI YANGU - 5

 







    Simulizi : Jela Ni Haki Yangu

    Sehemu Ya Tano (5)



    Wanajeshi wa Busoga hawakuwa na mda wa kupoteza zaidi ya kurudi nchini kwao kutoa taarifa dhidi ya kile walichokiona .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Furaha ya ajabu ilitanda Kwa baadhi ya viongozi lakini si kwa Robson raisi wa nchi hiyo ambaye hakutaka kuamini hadi alipoomba apelekwe eneo husika , zile habari zilizokuwa zimetawala katika vituo mbalimbali vya redio na luninga vya kutoroka kwa Al- kida na kuuliwa Kwa idadi kubwa ya wanajeshi, iligeuka na kuwa nyingine ,.

    Taarifa hizo hazikuwa tu kwa upande wa Busoga bali hata Tanzania nako kuliwaka moto , wandishi wa habari hawakubaki nyuma achilia mbali vituo vya habari navyo vilielezea tukio hilo , magazeti nayo yalianza kutoka yakiwa na picha mbalimbali na kufanya wananchi wapate amani na furaha kubwa .



    Safari ya kutoka Busoga hadi morogoro vijijini eneo ilipolipukia helkopita haikuwa ya kuchosha wala ya mda mrefu Kwa mheshimiwa Robson alifika hapo akiwa na baadhi ya viongozi wakubwa wa nchi ndani ya ndege yake na kukuta eneo zima limezungukwa na watu hata nafasi ya kuweka miguu ilikosekana , picha zilikuwa zikichukuliwa na kumwa katika mitandao mbali mbali ya kijamii kama whatAAp na kwingineko .



    " napenda kutoa pongezi nyingi na za dhati Kwa jeshi la wananchi ( JWB) jeshi la wananchi Busoga Kwa juhudi walizozionesha za kutokukata tamaa tokea tulipoanza kupambana na magaidi hawa ambao leo hii na mda huu ninapozungumza wanaendelea kuteketea Kwa moto , wanajeshi hawa wameonesha kile ambacho waliamua kukifanya katika maisha yao , siku zote mwanajeshi hapaswi kuwa legelege na wakukata tamaa na niliwahi kutoa ahadi ya kuwaongezewa mishahara yenu na itatekelezwa Kwa nyongeza ya asilimia 20%), na usiku wa leo wanajeshi wote mtapata Chakula cha usiku ikulu ,. Pia ninapenda kutoa pole nyingi na nyingi sana kwa zile familia zilizopoteza wapendwa wao , nchi italazimika kughalamikia mazishi ya wapendwa wetu na kuendelea kutoa mishara kama kawaida Kwa familia hizo hadi miaka yao waliotakiwa kustafu ......." Ilikuwa hotuba ya raisi wa nchi ya Busoga iliyochukua takribani masaa matatu , upande wa Tanzania nako mambo yalikuwa hivyo hivyo mkuu wa nchi nae alikuwa akiongea na wananchi wake kuhusiana na swala hilo .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na aliendelea kuwasisitizia wananchi wake kuwa na amani .

    ******

    Ndani ya helkopita Al- kida wote walikuwa na furaha ya ajabu sana isipokuwa Rambo aliekuwa anaendelea kuugulia maumivu ya risasi aliyokuwa amepigwa mguuni , kidonda cha risasi ya kwanza aliyopigwa mstuni pamoja na machungu ya kupoteza vijana wake ambao alizoea kusafili nao kila alipoelekea somalia na hata lile swala la kutotimiza adhima yake.

    Japo muonekano wa sura ya nje alionekana ana furaha ndani palijaa machungu ya hali ya juu.



    Walifika somalia jimbo la Gedo vijijini mida ya saa kumi na mbili jioni na kupokelewa Kwa furaha ya hali ya juu na viongozi wa kikundi hicho , huku Rambo na Rasi wakikimbizwa ndani ya vyumba vya matibabu .



    Baada ya miaka mitatu

    .

    Hali ya hewa ilikuwa ya utulivu ndani ya nchi ya Busoga , habari za Al- kida zilikuwa zimesahaurika vichwani mwa wananchi wa nchi hiyo , wakiendelea na maisha kama kawaida .

    Upande wa raisi nae hakuwa na wasiwasi tena, aliendelea kuponda raha kama kawaida huku familia yake ikiwa imeshalejea nyumbani hapo, huku binti yake wa kati akiendelea na masomo yake katika Chuo kikuu cha Tanzania alimarufu kama Dar es salaam university akiwa mwaka wa tano na wa mwisho akichukua sheria .



    Tayana Robson alikuwa mwenyewe furaha sana siku ya Jumapili baada ya kutoka kanisani ,kukuta ujumbe wake aliokuwaga amemtumia ama alimuomba rafiki yake kuhudhuria shelehe yake ya kumaliza masomo ahudhulie umejibiwa na ombi lake limekubaliwa , Rafiki huyo walikutania kwenye mtandao wa jamii alimarufu kama Facebook na kuwa marafiki wa mda mrefu hali iliyopekea kupeana hata namba za simu na kutumiana picha ila walikuwa hawajawahi kuonana na hiyo ilikuwa nafasi ya pekee Kwa Tayana kukutana na rafiki Wa Facebook kutoka Jamaica kama alivyojitambulisha Rafiki huyo.





    Japo mda ulikuwa ukiendelea kusonga mbele lakini Rambo alikuwa bado na kinyongo kwa raisi wa Busoga ambaye ni baba yake .mala nyingi alikuwa akikumbukia matukio ya nyuma toka akiwa mdogo , kukatisha masomo baada ya kifo cha mama yake , kulawitiwa na kutupwa polini yote hayo hakuyasahau ilikuwa kama mkanda wa video ukipita katika kichwa chake ,



    " shitiiii!!," alitamka neno hilo kwa hasira huku akipiga ngumi yake katika jiwe na alikuwa ameuma meno kwa hasira baada ya kumaliza mazoezi asubuhi moja , japo palikuwa na mvua lakini mwili wote ulikuwa unavuja jasho " nitampataje??" aliendelea kukihangaisha kichwa chake kimpatie jibu " oyaaaa vipi mbona uko huku" aliuliza Rasi huku akivuta kipande cha gogo na kuketi ,mkononi akiwa na kopa la maji pamoja na mswaki ,akiwa amevaa bkuta ,begani aliweka taulo rangi ya piki .

    " hey mani nakuuliza !?" aliuliza huku akimgusa begani

    " oooh! ,"

    " unaonekana haupo sawa tatizo ni nini!?" Rasi aliendelea kumdadisi kwa kina , Rambo hakuwa na sababu ya kumficha kutokana na urafiki uliokuwa umezaliwa toka mwaka mmoja walipokutana Tanzania kipindi walipotumwa kuja kumuokoa ,

    " simple things man ( vitu rahisi sana mwanaume )" Aliongea huku akinyanyuka eneo hilo , dakika tatu alirudi akiwa na laptop aliwasha na kuanza kumuonesha vitu fulani

    " kwahiyo naweza kumpata hivi !?" aliuliza Rambo akiwa haamini kama anaweza kukutana tena na adui yake alieamini ni namba moja .



    " mtumie mtoto wake huyu hawa wengine ni wakorofi sana "

    " sasa mie sina laptop nitafanya nini !?"

    " nitakupa simu yangu , ufugue account yako baada ya hapo anza kuongea nae japo ni mgumu sana !".CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nguvu ya ushindi iliyokuwa imeanza kupotea ikawa imezaliwa upya Rambo hakupenda kupoteza mda siku hiyo hiyo alianza kumtafuta Tayana binti wa Robson raisi wa nchi ya Busoga kwa kutuma ujumbe wa kuomba urafiki hapo hapo alituma na meseji na kukaa kusubili majibu.



    Hadi wiki ilipita alikuwa hajajibiwa chochote ndipo siku moja alikuta ujumbe wake umejibiwa alifurahi sana hapo hapo alimtumia ujumbe mwingine na huo ukawa mwanzo wa urafiki wao , ili kumvuta vizuri Rambo alikuwa akijitahi kila siku kuwasiliana nae na kumtega tega vimaswali juu ya nchi yao , alijifanya kama haifahamu nchi hiyo na kumdanganya kuwa alikuwa raia wa Jamaica , .

    Upendo huo kutoka kwa Rambo ambaye alijitambulisha kama Mr Jonasi , Tayana alijikuta akimpenda sana na hata ilifikia kipindi cha kutumiana picha ambapo Rambo ama Mr Jonas alikuwa akituma picha alizokuwa amevaa mask ( kinyago ) usoni mwake na kuleta muonekano tofauti kabisa uliopelekea Tayana kutomfahamu hata kidogo .

    Hadi unakatika mwaka wa pili toka urafiki wao uanze Rambo alikuwa ameshapata habari nyingi sana kutoka kwa dada yake Tayana na kilichomfurahisha zaidi ni lile ombi aliloombwa kwenda Busoga katika shelehe yake ya kuhitimu mafunzo yake ya sheria aliyokuwa akiyachukulia Tanzania .

    ******

    Uwaja wa kimataifa wa Busoga ulikuwa umefurika idadi kubwa ya askari pamoja na baadhi ya wanafamilia wa raisi wa nchi hiyo huku nyuso zao zikiwa zimetanda furaha iliyokuwa ikitoka ndani ya mioyo yao , tabasamu na vicheko navyo vilikuwa vikitoka vinywani mwao hakika ilikuwa siku ya furaha sana kwao wakisubili ujio wa ndugu yao ama binti yao mpendwa Tayana aliekuwa akitokea Tanzania baada ya kumaliza masomo yake .



    Wakiwa bado wanaendelea kuongea na kufurahia mala ndege kubwa iliyokuwa imeandikwa ubavuni mwake njina la nchi hiyo maadishi makubwa yaliyonakshiwa na bendela ya nchi hiyo , ilitokea katika mawingu ikitafuta mwelekeo wa kutua huku ikiwa imeanza kushusha tairi , taratibu ilinyosha katika njia yake na kuanza kuseleleka kabla ya kusimama .



    Kila mtu alikuwa na furaha ya ajabu ndani ya ndege hiyo isipokuwa Tayana aliekuwa akigeuza shingo kila sehemu akimtafuta Jonas ama Rambo waliekuwa wameahidiana kukutana Tanzania na safari ya kuelekea Busoga waianze pamoja lakini hadi mda wa kuondoka Tanzania Rambo alikuwa hajaonekana na alikuwa hapatikani, ilibidi Tayana aondoke peke yake tu ila roho ilikuwa ikimuuma sana .



    Taratibu alienda kuchukua mizigo yake na kuanza kutoka huku akiwa ameivuta sura yake huku akitembea taratibu , ndugu zake walimkimbilia Kwa furaha ya ajabu lakini yeye hakuonesha furaha hiyo alikuwa kama mgonjwa " mama vipi mbona hauko sawa !?" aliuliza mama yake wakiwa ndani ya gari aina ya HAMMER wakielekea nyumbani huku misururu mingine ya magari ikiwa mbele na nyuma , askari nao hawakuwa mbali hakika ilikuwa siku ya furaha kwao

    " tintiii, tiniiii!, tintiiii!!" ilikuwa sauti ya ujumbe mfupi katika simu ya Tayana .



    Haraka haraka aliufungua huku akiwa na shauku ya kujua ulikotoka , hakuamini macho yake alianza kutoa machozi huku mikono ikimtetemeka achilia mbali mapigo ya moyo nayo yaliongezeka , kila mtu ndani ya gari hilo walikuwa wakimshangaa sana





    " inatakiwa ukafanye kweli sio kupoteza tena mda unamuua fasta unasepa hakuna kulemba unakuja huku unaendelea kula bata na Asnat binti wa Abubakhar "

    " heeee!, nani alembe Mimi si mpaka poda wala mbana pua utachekishia mapigo yangu lazima nimzamishe mse*** yule " yalikuwa ni mazungzo kati ya Rambo na Rasi usiku mmoja kabla ya safari yake , CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " lakini vipi kuhusu Asnat kakumaindi sana mtoto wa kisomali yule !"

    " aaaaah !!, legeza mshikaji mimi na mademu ni mia na hamsini sina time nae hata kidogo , kwanza potezea habari hiyo ," Rambo hakupendezwa na maongezi yale alinyanyuka kwenye kochi na kuelekea kitandani kwake .



    Usiku mzima hakupata hata lepe la usingizi , mawazo yake yalikuwa juu ya kutekeleza adhima yake , taswila ya mwili wa Robson ukiwa umelala chini hauna uhai ilianza kupita ndani ya fikra zake ,



    " mama , naomba mzimu ya kwenu initangulie katika hilo , mzimu ya baba haina mamlaka tena , najua naenda kufanya baya ambalo ni chukizo kwako , Kwa jamii na hata kwa mungu ila hasitahili kuishi , na haya yote ameyataka mwenyewe , simuamini hata kidogo na nikichelewa yeye ataniua acha nimtangulizeeeee!" yalikuwa ni mawazo katika kichwa cha Rambo usiku huo hadi panapambazuka alikuwa bado macho , talatibu aliziruhusu mbavu zake kutoka katika godoro na kuelekea bafuni baada ya hapo alijumuika na wenzake kupata kifungua kinywa kisha alianza safari ya kuelekea uwanja wa ndege wa somalia akiwa na Rasi pamoja na Brown alieombwa aambatane nae , japo Rambo hakupendenzwa na hilo .



    Saa tatu kamili za asubhi walikuwa ndani ya ndege , wakiwa wametulia katika viti vyao , hawakuwa na maongezi mengi zaidi ya kuwaza kila mtu yake , Rambo aliekuwa amevaa kinyango usoni mwake na kukinakshi na miwani meusi pamoja na suti nyeusi ikiwa imetanguliziwa shati jeupe ndani , huku chini akiwa amepiga kiatu matata cheusi aina ya CLANKS , alikuwa ameamua kutangulia Busoga kabla ya Tayana , alifanya hivyo ili kumpoteza zaidi Tayana nini alichokuwa amedhamilia kukifanya , japo alikuwa akijua fika Tayana keshawaeleza wazazi wake kuhusu ujio wake lakini aliamini hata mtambua kamwe kutokana na mabadiliko aliyokuwa nayo kuanzia sura hadi umbo ambalo lilikuwa limeongezeka kutokana na mazoezi na matunzo mazuri aliyokuwa akipewa kambini hapo .



    Walifika Busoga jioni sana na kuelekea katika moja ya hotel zilizokuwa mjini humo siku mbili kabla ya ujio wa Tayana na kuanza kuzukunguka zunguka mjini humo huku Rambo akipanga jinsi ya kutekeleza mauaji hayo aliyokuwa akiyasubili kwa hamu .

    " twende uwaja wa ndege leo Tayana anakuja "

    " kweli !??"

    " Eeeeeh !?"

    " poa!!"

    Hawakuwa na mda wa kupiteza walishuka ngazi za hotel hiyo na kuchukua Tax iliyowapeleka moja kwa moja Jisangu airport , macho yao yalishanga kukuta umati wa askar na magari ya kifahari , walitafuta sehemu iliyokuwa imejificha na kuketi huku wakiwa wanaona kila kitu , nusa saa ndege aliyikuwa amepanda Tayana ilifika na abilia wote walianza kushuka , Rambo alikuwa akiona kila kitu kuanzia mtu wa kwanza hadi Tayana alipotokezea akiwa hana furaha ,.

    " nakupenda dada ila baba yetu mbaya naenda kumuua , utanisamehe !"



    Aliwaza baada ya kumuona Tayana akipokelewa kwa furaha , na ndugu zake , kabla ya safari kuanza, baada ya dakika tano gari zikiwa zimeondoka hapo ndipo alimpomtumia ujumbe mfupi !.

    ******

    " noooooo!!" Tayana alipayuka neno hilo huku akiendelea kutoa machozi ambayo hakujua yalianzia wapi na kuwashitua sana ndugu zake

    " mama vipi !?" Mama Tayana kama alivyokuwa akifahamika aliuliza Kwa shauku akiwa amemgeukia binti yake

    " Rafiki yangu mpendwa Jonas anakuja !" alionge Kwa furaha iliyokuwa ikisindikizwa na machozi .

    " Jonas !?, Jonas gani !?, isije kuwa unataka kumuacha Yohana !? aliuliza mama mtu akiwa na wasiwasi juu ya rafiki huyo mpya aliepelekea mwanae kutoa machozi .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilibidi Tayana amueleze yote wakiwa humo humo ndani ya gari na alisisitiza kuwa hakuwa mpenzi bali alikuwa Rafiki tu .walifika nyumbani na kupokelewa Kwa furaha ya ajabu huku mji huo wa kiongozi wa nchi ukiwa umefurika watu kutoka nchi tofauti tofauti walioalikwa katika shelehe ya binti yao .

    ******

    Wageni waalikwa walikuwa wamekaa sehemu husika , viongozi kadha wa nchi nao walikuwa eneo lao ndani ya uwaja mkubwa uliokuwa ukitumiwa katika shelehe mbali mbali , familia nayo ilikuwa imekaa sehemu yake iliyokuwa imeandaliwa , taa za rangi mbalimbali zilizidi kupendezesha eneo lote , sipika ndogo a zilizokuwa na uwezo wa kutoa sauti nzuri nazo zilikuwa zimepachik wa kila kona na kuleta radha nzuri zaidi katika shughuli hiyo ambayo ilikuwa ikienda kufanyika mda mfupi tu, pindi mziki ulipopigwa hakika kila mtu alikuwa na furaha sana isipokuwa Tayana ambaye mda wote alikuwa akipepesa macho yake kumtafuta Jonas ama Rambo .



    "Kabla hamjapita lazima tuwakague !" aliongea askari aliekuwa getini , Brown na Rambo hawakutaka kubishana nao walifanya kama walivyamuriwa kisha waliruhusiwa kuingia , wakiwapita askari mbalimbali waliokuwa wametanda eneo lote , Rambo alikuwa haamini kama kweli anaenda kutekeleza lengo lake la mda mrefu kirahisi rahisi , alihisi mwili wote ukitetemeka na miguu kushindwa kupiga hatua , .







    Tayana alinyanyuka sehemu aliyokuwa amekaa na kuanza kutoka nje ya uwanja huo maana hata hamu ya kuendelea kuwa pale ilipotea ghafla aliona aibu kubwa sana kutoka kwa ndugu zake aliekuwa ameshawaeleza ujio wa mgeni wake , hadi mda wa kuanza shughuli ulikuwa umewadia , hakuweza kuyazuia machozi yaliyokuwa yameanza kuyalowanisha machozi yake , taratibu alichuchuma sehemu iliyokuwa na kigiza kiasi lakini kabla hajakaa vizuri eneo hilo , simu yake iliita na jina la Jonas lilijichora katika kioo cha simu yake , alihisi kiwewe kikimpanda na hata vidole vyake vilishindwa kwanza kuipokea .



    "Nimo humu ndani ila kuna mtu amenizuia kupita hapa !"

    " okay nakuja !" hata Rambo hajatamka sababu iliyomsababisha kuzuiwa teyari Tayana alikuwa ameshafika eneo hilo

    " sorry modam sikujua kama hawa ni wageni wako !" askari aliekuwa amewazuia kina Rambo alizungumza kabla ya kuulizwa .

    " usirudie" wote watatu walianza kupiga hatu za kutoka eneo la pili la ukaguzi , akiwa amemshika mkono Rambo aliekuwa bado akitetemeka

    " acha sisi tukae huku "

    " hapana ww ni mmoja wa familia yetu njoo tuungane " " usijali kama kuna kitu kitakachoniladhim mm kuja huko nitakuja " Rambo hakuta kuongea zaidi alivuta kiti na kuketi .



    " Leo ni siku ya furaha sana kwa binti yetu pamoja na sisi tuio...." kabla MC wa shughuli hiyo kumalizia sentesi yake Robson ambaye ni raisi wa nchi hiyo ,na Mgeni rasimi katika shughuli hiyo alitokea na watu wote walinyanyuka , hali iliyopelekea Rambo kupandwa na hasira kama simba aliejeruhiwa pindi alipopita kalibu yake .

    " tunamshukru mwenyezi mungu mwingi wa Rehema kwa kutuwezesha kufika hapa saa hii.." zilikuwa ni salamu za Mgeni rasimi ambazo ziliambatana na pongezi Kwa binti yake, kisha alimkaribisha MC nae amkaribishe mhusika wa tukio

    "Kabla sijazungumza chochote napenda nimuite kaka yangu na rafiki yangu kipenzi Jonas " ilisikika sauti nyororo na nyembaba ikipenya katika masikio ya Rambo hali iliyopelekea woga kwake " be strong man( kuwa jasili )" Brown alitamka hayo baada ya kumuona Rambo akisita sita , maneno hayo yalimpa ujasili wa ajabu taratibu alinyanyuka na kuanza kupiga hatua kuelekeo usawa aliokuepo Tayana , CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Rafiki mda wako wa kufanya kazi umewadia " yalikuwa mawazo ndani ya kichwa chake huku akijifanya kutengeneza koti la suti yake lakini hakuwa na lengo hilo bali alikuwa akikipapasa kisu chake.



    " nitapenda uwasalimie kwanza wazazi wangu " Tayana aliongea huku akipiga hatua kuelekea eneo walilokuepo wazazi wake na nyuma yake alikuwa akifuatwa na Rambo ambaye alikuwa ametuna misuri yake yote , moyo nao ulianza kukunja ngumi , na u kitoa machozi

    " ukipoteza nafasi hii hutokuja kuipata tena wewe ndo utakufa !" ilikuwa sauti ikizungumza ndani ya nafisi yake baada ya kumaliza kushikana mkono na mama Tayana na sasa ilikuwa zamu ya Robson , ambaye alikuwa akitabasamu tabasamu , alinyosha mkono ili asalimiane na Rambo ambaye alikuwa akitetemeka Kwa hasira , aliupokea mkono na kukumbatiana kidogo .

    Robson alihisi kitu chenye ncha kali kikizama tumboni mwake kitendo ambacho Rambo alikifanya Kwa umakini San.

    " aaaaaaaaah!!!, aaaaaaaah!, ilikuwa ni sauti ya maumivu makali , Rambo aliendelea kumshambulia na visu tumboni na kifuani hali iliyopelekea kuanguka chini , hakuna aliethubutu kumsogelea kila mtu alishikwa na gazi ya hakili hadi dakika tatu zinakatika kulikuwa hakuna msaada wowote si Kwa bodgaind wake wala askari hali iliyopelekea Rambo kumtoboa toboa.



    "Ooooh !, puuuuu!, " ilikuwa ni sauti ya maumivu iliyoambatana na kitendo cha kudondaka Kwa mke wa mheshimiwa , hali iliyowashitua watu na baadhi yao walianza kukimbia baada ya kumuona Rambo akilamba damu iliyokuwa imetapakaa kwenye kisu chake huku Robson akiwa ametulia tuli chini na mwili wote kutapakaa damu.



    " nikamateni sasa leo nimemaliza kazi yangu na msihangaike kunipeleka kokote , jela ni haki yangu rasimi kuanzia sasa !" alizungumza huku akivua mask iliyokuwa usoni kwake , nusuru watu wazimie wale woga walianza kukimbia baada ya kumtambua Rambo.



    " umefanya niniiiii Jonas !!!!;aaaah!" zilikuwa ni kelele za Tayana zilizoambatana na vingumi ngumi vya kike kike vikitua katika mwili wa Rambo hali iliyopelekea askari kumkamata Rambo huku viongozi wengine wakimkimbiza hospital mkuu wa nchi hiyo anghalau waweze hata kuokoa uhai wake lakini waliokuwa wameshachelewa .

    " Tayana ntakutetea ili usihusishwe katika haya baba yetu alikuwa mbaya sana " alitamka maneno hayo Rambo alipokuwa akitolewa nje na askari zaidi ya kumi na safari ya kwenda kituo kikuu cha polisi kilianza, hivyo keki ya shelehe ikawa ya msiba uliohudhuliwa na viongozi toka nchi mbalimbali.

    ******

    Jaji mkuu wa nchi ya Busoga alishusha miwani na kuufuta uso wake kwa kiganja cha mkono wake wa kulia mala baada ya kusikia historia ya Rambo , sio yeye tu hata wasikilizaji nao walikuwa hoi wenye mioyo ya biscuit walikuwa wakitoa machozi .

    Zilikuwa zimepita wiki tatu baada ya mazishi ya aliekuwa raisi wa nchi hiyo.



    " je kuna kingine labda hujakisema !?" Jaji Michael aliuliza Kwa sauti ya upole , zile hasira zake za mwanzo zilipotea

    " mheshimiwa jaji inaniuma sana kuona viongozi wakubwa wa nchi wanaingiza madaw ya kulevya , hao hao wanayauza Kwa vijana na kuwaharibia maisha yao , hao hao wanawakamata na kwasotesha jela....." Rambo alishindwa kuendelea chozi la uchungu lilimtoka likiambatana na kukabwa na kilio

    "Msi...m..ka..mat..e..Tay..ana...hana..k.kosa..." alizidi kuongea Kwa kuyakata kata maneno kutokana na kukabwa na kilio huku kamasi nyepesi nyepesi zikichuruzika katika pua zake.

    " hivi mtu akijitolea kumuwekea dhamana inawezekana!!?"

    " mmmmh!!!, sidhani na itakuwa ni ngumu sana maana kwa mdomo wake amekili kumuua na ameomba apewe haki ya kwenda jela!!" ., yalikuwa ni maongezi ya chini chini kati ya watu waliokuwa humo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    " nipelekeni gelezani , na sitaki haki nyingine zaidi ya JELA ambayo NI HAKI YANGU ninayostahili , msiponipeleka leo sirudi tena polisi" alizidi kulalama Rambo pale kizimbani .jaji aligonga nyundo kisha wote walisimama, tangazo likatoka la yeye kurudi baada ya dakika thelasini.



    " Rambo Robsoni mahakama yangu tukufu inakuhukumu kwenda jela Kwa miaka sitini , Kwa kosa la kumshambulia Kwa visu hadi kumuua raisi wa nchi ya Busoga mheshimiwa Robson mnamo tarehe 12\05\2005 Saa 08:17 usiku , nyumbani kwake ikulu" Jaji Michael alimaliza kutoa hukumu , aligonga nyundo kisha alinyanyuka na kuondoka .



    Askari wawili waliokuwa wamevalia sare zao walimtoa Rambo kizimbani huku akiwa na pingu mkononi safari ya kwenda helezani ikaanza akiwa anafurahia ushindi na moyoni hakuwa akijutia yeye kwenda Jela.



    MWISHO.



0 comments:

Post a Comment

Blog