Simulizi : Nimeipata Furaha Yangu
Sehemu Ya Pili (2)
Ilikuwa ni siku tulivu sana katika mji wa mwanza mamia ya wakazi wa mwanza walikuwa wamefurika katika viwanja vya mahakama kuu ya mkoa huo iliyopo kamanga , ndani nako watu walikuwa wameshonana wakigonjea hukumu ya binti aliyekuwa akituhumiwa kumuua dada yake . ambayo ilikuwa ikitikisa mji huo.
Minongo'no ya chini chini ilikuwa ikiendelea baada ya Rhoda kufikishwa mahakamani hapo , dakika kumi baada ya Rhoda kuingizwa mahakamani humo akiwa katika ulinzi mkali hakimu aliingia na baada ya kukaa, mwendesha mashitaka alisoma historia fupi ya kesi hiyo .
"Je bi Rhoda unakipi cha kujitetea ili usionekane na tuhuma hii" wakiri aliyekuwa amenunuliwa kumkandamiza Rhoda alimhoji swali Rhoda ambaye alikuwa anaendelea na zoezi la kulia.
"Siku.....aaaah!" Rhoda alishindwa kuongea kutokana na kulia.
"Sidhani kama unaweza kuidanganya mahakama eti hukuua wakati tarehe 25-12-2000 saa kumi na dakika 20 ulitekeleza mauaji ya pacha mwenzio Rhodina kwa kutumia chupa ya bia aina ya safari na vipimo vya daktari vinaonesha wewe ndiyo uliyemuua,"
aliendelea kuongea huku akitoa karatasi za majibu hayo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Noooooooo!, ma...maaaa...mama mchep...." Rhoda hakumalizia sentesi yake hakimu aligonga nyundo akimanisha mahakama itarejea kwa muda mfupi.
.
"Hahaha kweli wewe Hamis noma."
"Mama mchepuko usicheze na mimi aliongea Hamis wakiwa wanaingia ndani ya chumba alichokuwemo hakimu.
"Mkuuu hiki hapa," mama mchepuko alimkabidhi hakimu pay slip bank aliyokuwa amemuwekea laki tano katika akaunti yake.
"Naenda kuchinja tu yule chokora hana maana na isitoshe hana shahidi wakili ama mwanasheria kipi kitaleta usumbufu ?"Aliongea hakimu Marwa akiwa anawatazama wote.
"Nitashukru sana."
"Usijali piteni huku muda wa kurudi umefika," hakimu huyo alitoa maelezo.
" Rhoda Jackson mahakama hii tukufu inakuhukumu kwenda jela maisha kwa kosa la kumuua dada yako mnamo tarehe 25-12-2000 saa kumi na dakika 20 nyumbani kwa kutumia chupa," alimaliza kutoa hukumu hiyo na kuondoka akiacha nderemo na vifinjo kwa watu
"Nipelekeni nikamuage Rhodina," yalikuwa ni makelele ya Rhoda alipokuwa akitolewa ndani ya mahakama hiyo na safari ya kuelekea butimba ikianza moyoni aliumia sana kuona anaenda jela bila kosa.
"Ila haki haijatendeka kabisa?"
"Kiaje Malick?"
"Kesi ilikuwa ya upande mmoja tu hawa mabinti nawafahamu kunakipindi waliwahi kuja kilombelo dispensary wakiwa na tatizo la ugonjwa wa Kandida ."
Wapi sema tu....."
"Dk.Amosi lazima nifatilie kesi hii hapana imenigusa japo pesa imenunua haki yao nipo ladhi kuuza nyumba gari na kila kitu!"
"Sasa wewe umelewa!"
"Hapana !"
Shangwe na ndelemo ziliendelea kutanda kila mahali katika mji wa mwanza kila mtu aliyekuwa haufahamu ukweli juu ya Rhoda alichekelea na kumshukuru hakimu marwa kwa kutekeleza hukumu hiyo ambayo waliamini ilikuwa fundisho kwa baadhi ya watu wenye tabia kama hiyo.
"Yaani nimefurahi sana amestahili adhabu sahihi kabisa."
"Hahaha! Kweli alikuwa akiringa sana sasa wacha akarigie magereza!"
"Mmmmh! Msilolijua ni kama usiku wa giza!" Rose aliyekuwa miongoni mwa watu waliohudhulia kesi hiyo aliongea hivyo na kupelekea baadhi ya machangudoa waliokuwa wakijadili kumcheka ila ukweli aliujua sema aliogopa kuwa shahidi.
Upande wa mama mchepuko na Hamis ambaye sasa alijimilikisha kuwa mume halali wa mama mchepuko siku hiyo walikuwa na sherehe kubwa sana , nyumbani kwao walitoa ofa kwa wateja wao wote .
"Afadhali kesi hii nimeipeleka haraka haraka daaah!" Mama mchepuko aliongea moyoni moyoni akiwa bize na kusambaza vinjwaji.
"Mama mchepuuuuu.. leta na huku halafuuu wako wapi wale mabinti?"
"Wametokaaaaa!" Alijibu kwa mkato kwani hakupendezwa na swali hilo.
Baada ya siku moja mara baada ya hukumu hiyo kuchukua nafasi mwanamke huyo alienda kuchukua mwili wa Rhodina na kuuzika katika makaburi ya lumara.
RHODINA JACKISON
Kuzaliwa
12 | 03 | 1983.
Kufatiki
25 | 12 | 2000.
Yalikuwa maadishi kwenye msaraba katika kaburi la Rhodina , kila mtu aliyekuwa akimfahamu Rhodina hakushindwa kuyazuia machozi kutoka ndani ya macho yake Rose alizima zaidi ya mara tatu pindi alipomfikiria Rhodina na kingine kilichokuwa kikimliza ni jinsi mama mchepuko alivyokuwa akijigaragaza akilia kwa uchungu badia lakini ukweli aliufahamu.
"Sina uwezo wa kumsaidia Rhoda ila mungu yupo!" Yalikuwa maneno yaliyokuwa yakijirudia rudia ndani ya kichwa cha Rose siku hiyo.
Baada ya maziko ya Rhodina walirejea nyumbani kuendelea na maisha kama kawaida na siku hiyo hiyo aliendelea na zoezi la uuzaji wa bia.
"Mama mchepuko leo tu unaendelea na biashara?" Jilani yake aliuliza akiwa na hati hati juu ya mama huyo.
"Kwani yeye mungu yesu mwenyewe alikufa mtume naye hivyo hivyo baba, mama na wengiiiii walishafariki, tuendelee kulia kwani atarudi ? Keshaenda na tumbo lake!" Alitoa maneno hayo bila haya na kumfanya jilani huyo kuondoka bila kuaga .
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa mama mchepuko aliendelea na maisha kama kawaida.
******
Gari la magereza lilianza safari kutoka mahakama kuu ya mwanza likipitia barabara ya mwanza hoteli kisha lilikunja kulia kuikamata barabara ya kinyantta road na kuelekea gereza la Butimba likiwa na wafungwa watatu Rhoda aliyekuwa amehukumiwa maisha na wanawake wawili waliokuwa wamehukumiwa miaka mitatu mitatu kila mmoja.
Rhoda hakuacha kumuita mfariji wake wa miaka yote si mwingine ni machozi alidhani labda alikuwa akipata faraja kuyatoa machozi hayo lakini haikuwa hivyo.
"Nina miaka kumi na nane tu naenda jela tena kifungo cha maisha? Kweli.., kweli…kwanini na mimi nisife tu kuliko kuisi katika nchi hii," Rhoda hakuacha kuwaza na kuwazua.
"Hivi kweli ama naota?" Alizidi kuwaza na safari hiyo alijifinya ili aone kama ilikuwa kweli ama ni ndoto ndefu tu lakini aligundua ilikuwa kweli alilia sana.
"M...mp..e..enzi...Rhodina...umeniacha katika ..m.d..omo...wa....ma...mamba...., n..as..ik..it.ika...hat...aaaaa..sijui..kama...ume...zi...kwa.....au...um..etupwa...., n..ili..penda...nikuone....tena......uki...wa......umefumb.....a.....macho....., la....kin..i ..nimenyimwa....HAKI...hi.yo.., ni..nge..kuo..shaa......ila.....nenda....dada..., ne....nda ..mama..., ipo siku .....tutaona" Rhoda aliendelea kulia huku akitamka maneno hayo yaliyopelekea hata wafungwa wenziye kutoa machozi na kumfuata sehemu aliyokuwa amekaa walianza kumfuata machozi japo hawakujua tatizo lake kiundani ,.
Gari hilo liliendelea na safari lakini lilipokaribia kona ya Butimba ghafla breki zilikatika na kushindwa kukata kona hiyo hali iliyopelekea kuparamiwa na lori la mchanga lilokuwa likitoka nyengezi na kusababisha ajari mbaya sana kwa magari hayo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Madereva wote walifariki hapo hapo askari magereza wawili nao walifia njiani Rhoda aliumia vibaya sana, kwani alipondeka kichwa na hata paja lake la mguu wa kushoto lilivunjika na sehemu mbalimbali za mwili wake ziliumia sana wale wafungwa wenzie hawakuumia hata kidogo.
Haraka haraka wasamalia wema walijitokeza na kuanza kutoa huduma ya kwanza Rhoda alikimbizwa hospitali ya Bugando kwa msaada wa gari la msaraba mwekundu huku akiwa na pingu zake mkononi wale marehemu walipelekwa hospitali ya Butimba wafungwa wale wawili nao walipelekwa gerezani kwa maana hawakuwa wameumia popote pale.
"Inatakiwa apelekwe chumba cha upasuaji haraka sana ili tujaribu kuokoa maisha yake," aliongea nesi aliyekuwa anavuta kitanda alichokuwa amelazwa Rhoda akiwa hajui nini kilikuwa kinaendelea, mara baada ya kumfanyia vipimo vya x-ray ambavyo nilionyesha majibu sahihi.
Dakika tatu zaidi ya madaktari wawili walikuwa katika chumba cha upasuaji , huku nje askari magereza wa wawili wa kike wakigonjea upasuaji huo.
******
"Taarifa zilizotufikia punde ni kwamba gari la magereza lenye namba TM 222 Wz limepata ajari mbaya sana iliyosababishwa na kukatika kwa breki ya gari hilo hivyo likawa limevaana na lori la mchanga lenye namba T 567 DFA,lilokuwa likitoka nyegezi kutokana na mwendo kasi ka Lori hilo , japo dereva wa Lori alijitahidi kulikwepa gari la magereza.
Watu watatu wakufa hapo hapo dereva wa lori na askari magereza wawili wenye no T A. M.109 na T.A.M.234, Emmanuel na Benson, dereva wa lori hilo hakutambulika , na mfungwa mmoja mwanamke aliefahamika kwa jina moja la Rhoda ameumia vibaya yupo Bugando, tutendelea kuwajuza , endelea kusikiliza JEMBE F.M"
Ilikuwa tarifa fupi ya habari iliyopenya vema katika ngoma za masikio ya Dk.Marick aliyekuwa akiongea na mwanasheria katika mgahawa wa Mina mchana hiyo.
"Vipi?" Mathew mwanasheria wa kujitegemea aliuliza baada ya kumuona Dokta Marick kaduwaaa
"Yule binti niliyekuelezea ndie huyo aliepata ajari."
"Duuuh! Twende bugando."
Hata hawakumalizia vyakula walitoka nje na kuingia kwenye gari la Matthew na safari ya kuelekea bugando ilianza kwa mwendo wa kasi sana , kutokana na kuchanganyikiwa Matthew hakuwa makini sana barabarani hivyo alipofika makutano ya barabara ya msoma nyerere road na ile ya bugando alimarufu kama Nata , hakuweza kuliona gari la mafuta lenye namba za usajili T.123 CCB lilokuwa likitoka nyakato hivyo liliivaa gari yao na kusababisha ajari nyingine .
"Vipimo ya x- ray vinasemaje?"
"Viko vizuri upande wa kichwani hana tatizo lolote sema mfupa wa paja ndo umevunjika!" Aliongea Dk. Haruna raia wa Uganda mtaaramu wa mifupa wakiwa ndani ya chumba cha
Dk. Martin .
Kwa kuwa Rhoda hakuumia sana , upande wa kichwani hivyo hata oparesheni yake haikuchukua muda mrefu akawa ametolewa ndani ya chumba cha upasuaji akiwa katika kitanda chenye matairi manne kikisukumwa na manesi wawili huku dripu za maji na damu zikiendelea kuingia ndani ya mwili wake achilia mbali mashine ya kupumulia nayo ilikuwa ikiendelea kufanya kazi yake .
Walikisukuma taratibu kuelekea chumba cha wagonjwa mahututi alimarufu kama ICU , japo alikuwa hajitambui lakini mkono wake wa kushoto ulikuwa umefunganishiwa na pingu kutoka katika kitanda hicho.
"Anaweza kupona kweli?"
"Uhakika wa asilimia mia upo maana tulihofia kichwani lakini madhara makubwa hayajamfika ndani ya wiki tatu atakuwa vizuri sana na hata mfupa wake wa paja utajitengeneza taratibu."
Yalikuwa ni maongezi kati ya Dokta Martin na mmoja wa askari magereza waliokuwa eneo hilo .
Baada ya siku mbili Rhoda alirudiwa na fahamu zake japo alikuwa hajitambua nini kilikuwa kimetokea ndipo askari magereza alipoadhimia kumueleza .
"Mungu kwanini hukuniacha nifeeee tu?"
"Ufe ? Kwa nini?"
"Sina haja ya kuendelea kuishi namna hii."
"Tambua mshahara wa dhambi ni mauti hivyo endelea kuutumikia tu!" Maneno hayo yalizidi kumuumiza sana Rhoda ila hakuwa na jinsi , kama kulia alishalia sana ilibidi aikubali hali hiyo na kukikubali kifungo hicho .
Baada ya miezi mitatu Rhoda alikuwa amepona kabisa hivyo aliagwa hospitali humo na kuelekea moja kwa moja gerezani kuianza safari ya kutumikia kifungo .
******
Gari aina ya Toyota Rav 4 ilibiringita mara tatu kisha ilisimama huku matairi yake yakiwa juu , kila mtu alifumba macho yake wenye mioyo miepesi tayari walikuwa wamesharuhusu macho yao kutoa machozi. Ilikuwa ni ajari mbaya sana kati ya gari hilo alilokuwemo Dk Marick na mwanasheria Matthew .
"Daah! Mwanagu fasta chomoa hiyo wareti tusepe."
"Shwari mwana"
Vijana wawili waliokuwa wa kwanza kujitolea kutoa msaada lakini lengo lao halikuwa hilo , vijana hao walifanikiwa kuondoka na wareti ya Dokta Marick pamoja na simu zao zote .
Kwa kuwa Natta na Bugando hapakuwa mbali dakika tatu gari la wagonjwa mahututi lilifika eneo hilo na kuwachukua Marick na Matthew ambao walikuwa hawajitabui kutokana na kuumia sana .
"Leo ni siku ya ajari duniani?"
"Kwanini !?"
Saa sita tumepokea mmoja yule sijui mfungwa sasa hivi tena kuna machera mbili zimepitishwa zikiwa na watu wawili nasikia mmoja sijui ameletwa akiwa ameshafariki!"
Manesi ambao kazi yao ilikuwa ni kupokea wagonjwa walikuwa wakiongea baada ya kupokea wagonjwa waliokuwa wamepata ajari nao si wengine ni Marick na Matthew .
"Huyu mmoja bado yupo hai apelekwe haraka sana chumba cha upasuaji ila huyu mwingine nasikitika kusema kuwa amefariki," alizungumza Dk. Haruna baada ya kuchukua vipimo , haraka haraka Dokta Marick alipelekwa chumba cha upasuaji ili kujaribu kuokoa uhai wake na mwanasheria Matthew alipelekwa chumba cha kuhifadhia miili ya watu ambao tayari walikuwa wamefariki alimarufu kama Mochwari wakisubili ndugu zake.
"Yaaah! Damu imevujia ubongoni inatakiwa afanyiwe utaratibu wa haraka sana apelekwe muhimbili."
"Why Dk.Martin?( kwanini Dokta Martin)
"Hapa hatuna vifaa vya kuitoa hiyo damu , hata hivyo na mfupa wake wa shingo nao umepata mshtuko kunauwezekano mkubwa wa damu kuvujia humo nayo ni hatari" alizungumza dokta martin baada ya kupata majibu ya X- ray
"But we should do something for him befor we trans him to muhimbili(lakini tunatakiwa tumfanyie chochote kabla ya kwenda muhimbili)" walizidi kujadiliana kabla ya kuingia chumba cha upasuaji ambako manesi walikuwa wakimuandaa dokta Malick.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dakika tano madaktari sita walikizunguka kitanda alichokuwa amelala Dokta Marick akiwa hajui nini kilikuwa kinaendelea mashine ya kupumulia nayo ilikuwa ikifanya kazi yake kawaida . hadi masaa matano walikuwa bado wamo katika chumba hicho wakihangaikia kuzuia damu iliyokuwa ikiingia ndani ya ubongo na kuitoa ambayo tayari ilikuwa imeganda.
"Mama mumeo anaendelea vizuri tu ila inatakiwa kesho asafirishwe."
Aliongea Dokta martin akiwa anamtazama kwa macho ya huruma mke wa Dokta Marick ambaye alikuwa alilia muda wote.
"Kama anaendelea vizuri kwanini mmpeleke muhimbili?" Aliuliza ingali bado analia.
"Aaaah! Hapa kwetu hatuna baadhi ya vifaa hivyo akienda huko atapata matibabu mazuri " ikabidi amwelezee kila kitu hadi alipoelewa na kesho yake asubuhi ya saa nne alisafirishwa hadi muhimbili ambako alipokelewa na madaktari bingwa ila nao walipompima walingundua kuwa alikuwa na tatizo kubwa sana hivyo alilazimika asafirishwe hadi nchini China .
Siku tano alisafirishwa hadi China akiwa na mkewe , na dakitari martini
Hadi inakatika miezi miwili dokta Marick alikuwa hajarudiwa na fahamu hali iliyoendelea kumtesa sana mkewe.
Dokta Marick ambaye alikuwa amezungukwa na kila aina ya vifaa vya kuilinda afya yake zikiwemo mashine ya kupumulia ya chakula , kifaa cha haja , dripu nazo za maji na damu zilikuwa zikiingiza vitu hivyo kupitia katika mishipa yake hakika alikuwa anatisha sana.
Laiti kama angefanikiwa kujiona asingezuia kuyatoa machozi yake sasa ilikuwa imepita miezi tisa akiwa katika hali hiyo ndani ya hospitali ya Changgeny ya Xiamen mjini Taiwan. Japo ilikuwa hospitali kubwa sana yenye sehemu tatu , hospitali chuo cha udaktari , lakini hayo yote hayakumfanya Dokta Marick mtalaamu wa magonjwa ya wanawake kuzinduka hali iliyopelekea mkewe kukata tamaa na alikuwa tayari amedhamiria kumrudisha nyumbani kungonjea kifo.
"Nini tatizo kubwa hasa la mgonjwa huyu? Kma vipimo vyote tumeshafanya damu yote tumetoa na hata vipimo vya leo vinaonesha ubongo wake umepona lakini hazinduki tu?" Aliongea Dokta leeky mtalaamu wa ubongo na raia wa ujerumani kwa lugha ya kichina.
"Hata mie nashindwa kuelewa!"
"Oky hebu nipemeni faili zake zote toka Tanzania kule alikoanzia matibabu," alisema huku akizunguka zunguka ofisini humo ilionesha alikuwa amechanganyikiwa.
"I want to take him back ....( nataka nimrudish....)” mke wa Dokta aliongea huku akiingia ofisi humo bila hata kugonga huku akiwa anapayuka payuka maneno lakini alikatishwa na Dokta Leeky.
"Mama tupe nafasi ya mwisho mumeo atapona mimi sijawahi kushindwa !" Aliongea taratibu huku akimvutia sehemu ya kukaa.
"Hapana Dokta nimechoka kama kulia nimeshalia sana na bado naendelea kutumia gharama kila siku wacha nimrudishe nyumbani !" Maneno hayo hayakuto makavu yalisindikizwa na machozi.
" Leo usiku atakuwa amezinduka!" Aliongea huku akipokea lundo la mafaili .
"Oky mama samahani hebu nipishe kwanza nifanye kazi!" Mke wa Marick hakuwa na mbishi alitoka ofisin humo na kurejea hotelini akiwa na lundo la mawazo.
"Mmeona?” Hamkufanya vipimo vya mishipa ya fahamu kutoka katika uti wa mgongo nadhani hii ndo itakuwa sababu!" Akasema mara baada ya kukagua kila karatasi lililokuwa limeandikwa majibu na vipimo vilivyokuwa vimekuchuliwa huko nyuma
Hakuwa na muda wa kupoteza walielekea moja kwa moja katika wodi aliyokuwemo Marick na kuanza kuchukua vipimo tena hasa hasa upande huo kwa kuwa chumba hicho kilikuwa na kila kitu hawakuwa na sababu ya kumtoa humo.
Masaa matatu teyari majibu yalikuwa nje na tatizo likawa ni hilo hilo kwa kutumia kifaa marumu walianza kuishtua mishipa hiyo wote wakiwa wamejawa na tabasamu la furaha hakika ilikuwa kazi nzito sana lakini baadaye alianza kujitingisha hali iliyozidi kuongeza furaha moyoni mwao.
"Mishipa yake ina damu iliyoganga."
"Hapo lazima ni oparasheni tena?"
"Hapana Dokta Shanuggy na wewe Nunalk, atapewa dawa ya kusafisha mgando wa damu hiyo kwa lisaa limoja!" Dokta Leekly alisema huku akiwa anaandaa dawa hizo alielekea kitandani alichokuwepo Marick na kumtundikia dripu yenye dawa hizo ambazo zilikuwa na uwezo mkubwa sana kuisafisha damu hiyo bila kufanya upasuaji wa aina yeyote.
"Waoooooo!!," wote walitabadamu baada ya kusika taarifa za kufumbua macho kwa Dokta Marick kutoka kwa nesi aliyekuwa na jukumu la kumuangalia hawakuwa na muda wa kupoteza mbio mbio walikimbilia wodini humo.
"Thanks Juses ( asante Jesu ) lilikuwa ni neno kutoka kwa mmoja wa madaktari hao baada ya kumtolea kila kitu ambacho kilikuwa kikimsaidia hivyo akawa anapumua kama kawaida .
Siku tatu baadaye hali yake ilikuwa imetengamaa japo alikuwa na tatizo la kutorejwa na kumbukumbu lakini hilo halikuwa tatizo kubwa sana.
"Usijali mama ataendelea kupata kumbukumbu pole pole japo itachukua muda mrefu kiasi."
" Ahsante sana Dokta" mama Asia ama mke wa Dokta Marick aliongea huku akimkumbatia Dokta Leekly kwa furaha wakiwa katika kiwanja cha ndege kwa safari ya kulejea Tanzania.
******
Rhoda alikuwa amejiinamia muda wote alipokuwa amefikishwa gerezani humo huku machozi yakiendelea kumtoka kumbukumbu za mambo ya nyuma hazikuacha kumsalimia ndani ya kichwa chake japo wafungwa wenzie walikuwa na furaha.
"Rhoda Jackson," sauti ya askari magereza ilipenya ndani ya ngoma za masikio yake hali iliyopelekea kunyanyuka sehemu hiyo na kumfuata askari huyo.
"Shosti unamuona demu huyo?"
"Yupi?"
"Aaaaah! Kule kwenye mlango anaongea na msenge"
"Aaah! Mtoto hatari huyo wangu!"
"Fala nini? Kumuona nione mimi harafu kula ule wewe!"
"Mia mia mkuu," yalikuwa ni mazungumzo kati ya manyapala ndani ya gerezani la wanawake ambao kazi yao ilikuwa ni kufanya mapenzi ya jinsia moja na kila mfungwa mpya na ukileta mgomo utakula kipigo cha kufa mtu hivyo walikuwa wakimjadili Rhoda ambaye alikuwa mfungwa mpya.
Dakika kumi Rhoda alirejea akiwa na mavazi maarumu ya wafungwa hali iliyopelekea kuendelea kulia tena. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nilikuwa naona tu kwenye TV leo nami nimeyavaa mmmmh!".Aliwaza mwenywe.
"Oyaaa njoo fasta!" Mmoja wa wanawake waliokuwa wababe na tena wafungwa wa maisha walimuita Rhoda ambaye alikuwa akitembea pole pole kuelekea eneo la mwanzo ,
"Nyie vipi hebu achaneni na mtu wetu !"Wale manyapala waliongea huku walinyanyuka na kuanza kumfuata Rhoda hali iliyopelekea wale wababe nao wawafuate Rhoda ambaye alikuwa haelewi chochote alibaki amesimama asijue cha kufanya.
"Achaneni na mtu wetu."
"Tabia yenu iishie huko huko."
"Wewe mse*** nini unanijibu hivyo wakati mimi boss wako?".
Majibizano hayo kati ya manyapala na wababe hao , yalikuwa makali sana hadi walijikuta wakipigana lakini ushindi ukawa kwa wababe kisha waliondoka na Rhoda.
"Mimi naitwa Marry nilifungwa toka miaka kumi hapa tena kifungo cha maisha kwa kosa la kumuua mume wangu !" Aliongea marry huku akiwasha sigara na kuanza kuvuta huku akimtazama Rhoda ambaye alikuwa akishanga shanga kila kitu, mara baada ya kutoke eneo walilokuwa wakizozona na manyapala nje kidogo ya jingo hilo.
"Sema tu dogo usijali sisi tutakulinda tu wale ni wasang*** na hapo walikuwa wanataka kukuchezesha mchezo mchafu sana leo hii na laiti ungekataa eeeeh! Hata kukuua wangekuua," mmoja wao aliongea
"Sisi tupo sita wote tuliua wewe je"
"Nilisingiziwa kuua!"
"Hahahaha! Jela hakuna kusingiziwa we sema tu kuwa uliua!"
Walizungumza kwa muda mrefu sana hadi muda wa chakula cha usiku . na huo ukawa mwanzo wa urafiki wao.
Miezi 17 kupita walianza kumshawishi Rhoda kuanza kuvuta bangi na sigara mwanzo alikuwa mgumu lakini baada ya kulishwa maneno alidhamiria kuvuta.
"Hata nikiacha haina maana uraiani sirudi sina ndugu yeyote kufa nitafia huku huku aaaah! kesho naanza!" Yalikuwa ni mawazo ndani ya kichwa cha Rhoda usiku mmoja akiwa amelala katika kipande cha godoro chakavu.
"Rhoda Jackson," askari magereza aliita sauti hiyo ilipenya ndani ya masikio ya Rhoda aliyekuwa bize na kusafisha choo alikiruhusu kichwa chake kugeukia eneo ilikotokea sauti hiyo.
"Abee afande!"
"Kuna mgeni wako!" Askari magereza aliongea huku akiondoka eneo hilo nyuma yake Rhoda naye alikuwa akipiga hatua kuelekea usawa aliokuwa akielekea askari.
"Subiri nakuja!"
"Sawa !" Aliitikia huku akiyaruhusu makario yake kukaa katika moja ya benchi lililokuwepo eneo hilo huku kichwa chake kikiendelea kuwaza na kuwazua kuhusu mgeni huyo maana toka afungwe alikuwa hajawahi kutembelewa na mtu hata mmoja sasa ilikuwa inakaribia miaka miwili.
"Na awe mama mchepuko nitamuua hapa hapa na mimi nikanyong......" kabla hajayaruhusu mawazo yake kufika mwisho alishtukia mlango unafunguliwa na mdada mrefu alionekana ndani ya macho yake.
"Hee! Rose karibu!" Aliongea Rhoda huku akiachia tabasamu.
"Mmmh! Mbona uko hivyo?" Aliuliza Rose akiwa na shauku la kujua
"Kiaje?"
"Umekonda mwili wote upele duuuh !"
"Kawaida tu hebu nielezee vipi Rhodina alikufa kweli ama aliamka tena ?" Lilikuwa ni swali ambalo Rose hakulitarajia na akawa na wakati mgumu sana kujibu.
"Kweli ..ali.kufaaa."
"Mmmmmh!" Rhoda aliishia kushusha pumzi ndefu na kuanza kulia baada ya kuelezwa pia maendeleo makubwa ya mama mchepuko.
"Pole Rhoda pole sana ila mungu ndo anajua."
Waliongea mengi yenye maumivu kwa wote hadi muda wa kuondoka .
Rose hakuta kurejea nyumbani kwake aliamua aende nyakato Mecco anghalau akapoteze mawazo maana hali aliyoiona kutoka kwa Rhoda ilimuumiza sana ule uzuri wake haukuwepo tena alikuwa anechakaa bila mfano.
"Ila mama mchepuko duuuh !" Aliwaza hayo huku akiwa anashuka ndani ya daladala nyakato Mecco na kuelekea kwa rafiki yake Dorce aliyekuwa na salon eneo hilo.
Upande wa Rhoda baada ya kuachana na Rose hali yake ilibadilika ile furaha aliyokuwa nayo asubuhi iliyeyuka kabisa.
"Oyaaa … vipi mbona mnyonge sana?" Marry aliyekuwa rafiki mkubwa wa Rhoda gerezani hapo aliongea huku akikaa chini.
"Kuna rafiki yangu kanisababishia upweke ndani ya moyo wangu" Rose hakumficha kitu
"Hayo madogo sana wewe usiyawaze kwanza shika hii.
Marry alitoa sigara na kumkabidhi Rhoda ambaye aliipokea na kuiwasha kisha aliuruhusu mkono wake kuelekea mdomoni akiwa na lengo la kuvuta .
"Mmmmh! Kula mwanangu vitu hivi ni vizuri vinaondoa mawazo huoni mimi huwa siwazi wazi nikikwama tu nagonga."
"Kweli?" Rhoda aliuliza
"Aaaah ! Vuta bhana!"
Rhoda aliusogeza zaidi mkono wake mdomoni kisha alidumbukiza sigara mdomoni.
*****
Ndege aina ya Legancy 650 yenye uwezo wa kubeba abilia mia tano ilikuwa ikitafuta uelekeo wa kutua katika uwanja wa taifa wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Marick na mkewe mama Asia walikuwa miongoni mwa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo.
Taratibu ilianza kushuka chini huku ikiwa tayari imeshakunjua matairi yake ilielekea barabara yake kwa kasi kabla ya kusimama .
"Baby tumefika nyumbani," Mama Asia aliongea huku akiwa anamfungulia mkanda Dokta Marick aliyekuwa haelewi chochote alimsaidia kunyanyuka na kuanza kutoka nje kuelekea kule iliko mizigo yao.
"Mama Asia tupo wapi hapa?" Lilikuwa ni swali kutoka kwa Marick ambalo lilimfanya mwanamke huyo kuachia tabasamu la kwanza toka mumewe augue.
"Honey tupo airport.”
"Mmmmmh! Sawa!" Alijibu kifupi na kukaa kimya tena , japo mkewe alikuwa akijitahidi kuzungumza naye lakini hakujibiwa tena , siku mbili walisafiri tena kurejea mwanza huku hali ya Marick ikiwa ile ile ya kutopata kumbukumbu.
"Ila Dokta Leekly alinieleza kuwa atapata kumbukumbu tu," mwanamke huyo aliwaza hayo siku sita baada ya kurejea mwanza
Miezi mingine mitatu ilikatika Marick alikuwa hivyo hivyo.
"Mama Asia hivi hapa nilifanya nini?"
" Eeeeeeh!" Mama Asia aliishia kushangaa badala ya kujibu swali hilo , lile zoezi lake la upakaji wa mafuta katika mgongo wa Malick lilikufa na kuhisi nguvu sikimuishia
"Uliumia!" Alijibu kwa mkato huku macho yake yakiwa usoni kwa Marick aliyekuwa akiendelea na zoezi la kushangaa kuvu lake katika mkono lililokuwa limesababishwa na ile ajari ya gari
"Kisa nini?"
"Ajari."
"Lini?"
Ilibidi mkewe aanze kumsimlia kisa chote
"Matthew! Matthew ajari! Ajari! Gari hiloooo! Mamaaaa my God !" Zilikuwa ni kelele kali sana kutoka kwa Dokta Marick huku akifunika uso wake kwa viganja vyake kisha alitulia kama alikuwa amekufa, hali hiyo ilimchanganya sana mkewe alianza kumpepea kwa kipande cha kaka , aliilaumu nafsi yake kwanini alimueleza ukweli , machozi nayo hayakuwa nyuma ghafla Dokta Marick alianza kupepesa macho yake kana kwamba alitaka kuisalimu roho yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
******
Ilikuwa imeshapia miaka mitatu Rodrick akiwa mwanza akiendelea na yake ya uwanasheria huku akisimamia miradi ya baba yake ,kazi hizo zilikuwa zikimpa mafanikio makubwa sana.
Siku moja alikuwa akitoka kazini huku kichwa chake kikiwa na lundo la mawazo ndipo alipoamua kupita bar japo hakuwa na tabia hiyo.
"Aaaah ! Acha nikaangalie hata mpira tu," aliwaza hayo akiwa anatafuta uelekeo wa kupaki gari lake aina ya Mbw.
Alitafuta eneo lilokuwa limejitenga na kuagiza kinywaji taratibu akawa anakunywa huku akitafakari mambo yake.
"Samahani kaka naweza kukaa hapa?" Sauti nyororo ya msichana huyo ndio iliyoyavuruga mawazo ya Rodrick.
"Ooooh! Usijali kaa tu sina muda naondoka mida hii," aliongea Rodrick huku akiwa anamvutia kiti.
"Mmmmh! Nipe kapani kidogo nawasubili wenzangu tafadhali”akasema huku akimtazama Rodrick machoni macho ya kuuliza je umekubaliana na mimi.Lakini Rodrick akashusha pumzi ndefu kabla ya kumjibu chochote.
Mama Asia alizidi kuchanganyikiwa zaidi baada ya kumuona mumewe Dokta Malick akizidi kutoa macho lile zoezi la kumpepea alilisitisha alizunguka chumba kizima huku jasho jembamba likiendelea kulowanisha nguo zake.
"Hodi! Hodiii!" Sauti hiyo ndio iliyoyazindua mawazo ya mke wa Marick haraka sana aliuendea mlango wa chumba hicho lakini alisita na kurudi ndani baada ya kumuona mumewe akizidi kuweweseka. "Tafadhali usiniache baby,"maneno hayo aliyatoa mama Asia huku akimtikisa tikisa Dokta Marick aliyekuwa akikoroma na kutoa povu mdomoni kana kwamba alikuwa mgonjwa wa kifafa. "Ng'oooo!Ng' oooo!" Sauti za kungongwa kwa mlango zilimzindua tena haraka sana alimuachia mumewe na kuelekea mlango. "Ka..kari..bu .shemeji!" "Vipi mbona uko hivyo?" Dokta Amos alizungumza huku akiingia ndani. " Marick! Malick anaumwaaaa njoo!" Dokta Amosi hakupinga wito huo alianza kupiga hatua kumfuata mama Asia chumbani.
"Oky hii ni plesha imepanda nadhani amepatwa na mshtuko wa kitu fulani!" Dokta Amos aliongea huku akiendelea na zoezi la kumpima Dokta Marick , maana karibia kila kitu cha huduma ya kwanza kilikuemo ndani humo.
"Unajisikiaje?" "Mmmmh! Aaaah!" "Niambie mume wangu unajisikiaje?" Japo alikuwa amezinduka lakini hakuwa vizuri kifikira "Muache kwanza atakuwa vizuri tu ."
Dokta Amos alizungumza huku akiondoka nyumbani hapo maana alipita tu kuwsalimia asubuhi hiyo. Baada ya siku mbili Dokta Marick alikuwa kesharejewa na fahamu zake "Nusu nusu nife?" "Aaah! Hapana bhana mungu amesaidia." "Kweli mke wangu," yalikuwa ni mazungumzo yaliyochukua mda mrefu sana kati ya wanandoa hao usiku huo ,
******
Haukupita muda mrefu walitokea wasichana watatu "Karibuni viwajana," Jescal aliyekuwa amekaa na Rodrick aliwakaribisha marafiki zake . " Asante! Naona uko na shemu hatari Jesca hukosei kitu kikali hatari hongera!" Dorce mwenye tabia ya kuongea ongea bila kituo alitupia swali hilo kwa uchokozi huku akituvuta kiti na kukaa.
"Mambo Shemu!" Dorce alitoa salamu hiyo huku akinyosha mkono wake kwa Rodrick mkono huo haukuwa wenyewe bali ulisindiizkwa na kitendo cha kukonyeza jicho lake la kushoto. "Aaaah! Dorce siyo Shemu bhana ni rafiki tu!" Jescal aliyekuwa ameutia mdomo wake superguru ilibidi azibandue na kuongea hayo. "Ooooh! Basi sorry best ila mnaendana ningependa ingekuwa hivyo." "Vipi Rose mbona uko kimya sana?" Ilibidi Jescal abadili mada maana maneno ya Dorce yalianza kumkera hata kabla ya Rose kujieleza mwenyewe Dorce mzee wa talk talk kwa sana alidakia.
"Mmmmh!Hana jipya si anamuwaza yule binti aliefungwa mwaka juzi mwishoni." "Yupi?" "Aaaaah! Acha kuweka pamba katika fikra zako bwana!" "Dorce yule Rhoda," Jescal aliyekuwa kimya ilibidi aliuruhusu mdomo wake kufunguka "Yupi mbona simfahamu jamani?' "Jescal acha kukiruhusu kichwa chako kupoteza poteza kumbukumbu oky sikia wewe kilaza Rhoda ni yule binti aliesemekana kumuua dada yake kule Ilemela sabasaba!" Ilibidi Dorce atoe maelezo kwa Jescal "Eti nini?" Rodrick aliyekuwa kimya muda wote alijikuta akiuliza kwa shauku sana. " kaka yangu yule binti alimuua Dada yake si.." Dorce alikatishwa na Rose "Kaka Rhoda hakuua hata kidogo aliyefanya mauaji hayo alikuwa boss wao kisha akamgeuzia kesi hiyo Rhoda!" "Aisee! Hatari sana eti ila ...ila oky !" Rodrick alijikuta akichanganya changanya maneno kutokana na kuwasha kifaa cha kunasa sauti ndani ya suruali yake . "Mnaweza mkanieleza ilikuwaje?' "Hata mie niliumia?" " Dorce hebu punguza kuongea , " ilibidi Rose aelezee nusu kisa ila baadhi ya vitu hakuviweka wazi . "Je huyo alieshuhudia kifo hicho yuko wapi !?" "Hatujui !" Wote walijibu kwa pamoja na kunyanyuka katika viti vyao wakiwa na lengo la kuondoka maana walianza kumuogopa Rodrick kutokana na maswali yake.
"Jescal tafadhali nieleweni Mimi sio mtu mbaya hata kidogo !" alianza kuongea Rodrick huku akimshika mkono Jescal kumzuia ili asiondoke "Naitwa Rodrick Steven mwanasheria na ni mfanyabishara kazi yangu hiyo ya sheria isiwaogopeshe na wala hamtahusika na lolote tafadhali wasihi wenzio warudi tukae , nakuomba nipo chini ya miguu yako dada yangu niamini mimi ni mtu safi kabisa kazi yangu ni kutetea wanyonge na nimekula kihapo mahakamani nakuomba nielewe fanya utu kama ulivyonisihi mimi mwanzo!"
Maneno hayo yalimfanya Jescal kutulia na kuwatazama wenzie kisha alirudi na kukaa bila kusema chochote na hata wenzie nao walirudi "Weita hebu njoo!" Rodrick aliongeza vinywaji kwa kila mtu.
" Mmmmh !!!, warembo leteni habari , je huyo mama aliyeua yupo wapi?". Rodrick alianzisha tena mazungumzo hayo baada ya wote kutulia. "Mama huyo yupo kwake sabasaba." "Je yule kijana yuko wapi?" "Alielekea Dar toka siku hiyo ila Kwa sasa sijui aliko " Rose aliekuwa ndo msimulizi mzima wa tukio hilo "Nipe namba yake kama hutojali." "Lakini usinitaje tafadhali !" Rose alitoa namba ya Andrew na kumpatia Rodrick.
"Sasa huyo binti yuko gereza gani kweli?" "Butimba na picha yake hii hapa!" Rose alimuonsha picha Rodrick iliyokuwa katika waleti yake enzi za nyuma sana. "Tena kaka mtu aliyemua yuko uraiani anakula maisha simpendi kweli," Dorce aliongea huku wakiwa wanatoka ndani ya bar hiyo ya Green.
"Nashukruni sana dada zangu kama nitapata muda nitafatilia kesi hii" Aliwasha gari na kuondoka kuelekea kwake Buswelu .
"Kaka Rhoda hakufanya mauaji hayo aliefanya mauaji hayo ni boss wao kish......." yalikuwa ni mawazo yaliyokisumbua kichwa cha Rodtick usiku huo. Daaaah ! Sijui niende kumuona ila simjui aaaah! Nitaangalia,” alijikuta akiongea peke yake ndani ya shuka katika kitanda chake kizuri.
*****
"Ila kweli hii sigara haina madhara ?" Rhoda alisita kwanza kuuvuta moshi uliokuwa ukitoka ndani ya sigara hiyo aina ya Embassy. "Aaaah ! Rhoda acha hizo hata kama unamadhara si poa tu unakufa mapema kuliko kukaaa kifungo cha maisha hadi uzeeni wewe vut..." kabla marry hajamalizia sentesi yake alihstukia akishikwa mkono na askari magereza.
"Eeeeeh! Toka lini mnafanya uchafu huuu?" Josephne askari magereza aliekuwa akifahamika kwa jina la pilipili alilobatizwa na wafungwa kutokana na ukali wake aliwakamata. "Tu...samehe... Afande?" Rhoda ndio alikuwa wa kwanza kuomba msamaha. "Aaaah ! Afande kwani kitu gani bhana tupishe tule vitu vyetu!" alisema maneno hayo bila hata woga. "Nini wewe oky leo siwapi adhabu ila kesho Rhoda jiandae kwa safari ya kuelekea gereza la kasungamile !" Aliongea hayo na kuondoka eneo hilo akiwa ameivuta sura yake . "Njooo tuendelee bhana !" "Aaaah mimi sina hamu tena !" Rhoda alimjibu huku akiondoka eneo hilo. "Hahahaha! Hata kama hutavuta ila jua life yote ni huku huku kubadili gereza huwa kawaida kama ulikuwa hujui nenda sengerema ukalime hahahaha!" Marry aliyafyatua maneno hayo bila kujali.
Usiku mzima Rhoda hakupata usingizi hata kidoga japo sheria ya gereza ni kulala saa tisa alasiri lakini hadi inafikia saa kumi na moja siku nyingine hakuwa amepata lepe la usingizi hata kidogo , "Yaaaah Leo wataondoka wafungwa saba wa kike watatu ambao wataelekea musoma na wanne wa kiume ambao wataelekea Shinyanga." "Oky na yule wa kasungamile je?" "Aaah Huyo atasubili kama siku tano kwa sasa hatuna safari ya kuelekea huko!" Yalikuwa maongezi kati ya afande Josephne na mkuu wa gereza bwana Hashimu Rwamba ambayo yalipenya moja kwa moja katika ngoma za masikio ya Rhoda aliyekuwa karibu na eneo hilo asubuhi wakiwa wanalima .
"Yes! Mungu endelea kunipigania duuu! Teh Teh! Teh!" Kilikuwa ni kicheko cha furaha ya ajabu ambayo karibia kila mtu alikisikia. Kutoka kwa Rhoda.
*****
"Hii namba ya nani kweli?" Rodrick alikuwa akiitazama namba ya simu katika kioo cha simu yake. "Oky Andrew wa Dar? Tena nampigia sasa hivi!" Akawaza kisha akaipiga namba ile na simu akaiweka sikioni.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Habari yako ndugu ?" Dakika tatu Rodrick alikuwa akiongea na simu. "Naitwa Rodrick niko mwanza tuliwahi kukutana siku moja ...." Alikatishwa "Rodrick Ngosha?" "Eeeeh! Aaaah! Ndioo! ndiooo!" Rodrick alijikuta mgumu kujibu swali hilo baada ya kutajiwa jina la mtu mwingine lakini baadaye alijikuta akikubali ili apate alichokuwa amedhamiria.
"Duuu! Za siku? Mimi niko zanzibar huku!" Andrew alijikuta akijieleza kila kitu kwa kudhani alikuwa akiongea na Rodrick Ngosha kijana aliyekuwa rafiki yake muda mrefu.
Maelezo hayo yalianza kumpa matumaini Rodrick ya kutaka kujua kisa cha Rhoda binti aliyekuwa akitumikia kifungo cha maisha bila kosa.
"Tena kesho jumapili baada ya kutoka kanisani naelekea huko!"
Saa 4:56asubuhi Rodrick alikuwa akiegesha gari lake aina ya Mbw ndani ya gereza la Butimba alishuka na kuwafuata askari magereza wa kike waliokuwa bize na kuandisha majina ya watu waliokuja kuwaona ndugu zao.
"Kaka taja jina la ndugu yako?" Anaitwaaa ....aaah ...nani Rhoda !" "Rhoda nani? Mfungwa ama mahabusu?" Afande Josephne alimuuliza bila hata kumtazama Rodrick kutokana na chuki kubwa kwa Rhoda iliyowahi kusababishwa na aliyekuwa mpenzi wake kumtaka Rhoda. Japo Rhoda alimtolea nje kitambo lakini afande huyo hakuelewa somo na ni huyo huyo alimchochoea Rhoda kuhamishwa gereza.
"Kwanza huyu mfu.....!' Afande aliyekuwa akichukua watu na kuwapeleka sehemu ya kuongelea na ndugu zao alisita kidogo bada ya kukutanisha macho na Rodrick. "Mfungwa huyo hayupo alipelekwa jana musoma!" "Aaaah! Kweli? Shiti?" "Ndio hivyo kwani nani yako mpaka uumie hivi?" Josephne alizidi kupigilia msumari dhidi ya Rhoda
.
"Oky," alijibu kifupi na kuanza kupiga hatua kuelekea katika gari lake lakini kabla hajalifikia alisikia sauti ya mtu ikimuongelesha. "Bwana mdogo mbona uko mnyonge sana?" "Aaaah! Shikamo mzeee kuna mfungwa nilikuwa nimekuja kumuona sasa nimeelezwa kuwa jana alihamishwa gereza." "Eeeh! Kweli ila huyo wako anaitwa nani?" "Rhoda!" " Rhodaaaa.hebu acha niangalie kwenye orodha yao karatasi bado ninalo " mzee yule alitoa kipande cha karatasi na kuanza kupitia orodha ya wafungwa waliokuwa wameondoshwa siku moja baada.
" Rhoda hakwenda yupo hebu njoo huku," wote wawili walifatana hadi katika chumba kizuri na kisafi ambacho watu hovyo hovyo walikuwa hawakiingii.
"Naitwa Hashimu Rwamba mkuu wa gereza sijui bwana mdogo unaitwa nani?" "Rodrick Steven. " "Oky karibu sana unauhusiano gani na Rhoda?"
Ilibidi Rodrick aelezee kisa chote japo alikuwa akijui vizuri. "Lakini unakibali kutoka mahakani?" "Oooh ! Sina lakini hiyo haina tatizo wacha niongee naye tu." Mkuu wa gereza hakuwa na tatiza alinyanyuka na kuelekea upande walikokuweko wafungwa.
"Viiiiiii!" Sauti za mlango uliokuwa ukilalamika baada ya kufunguriwa ndizo zilizomshitua Rodrick aliyekuwa bize na simu ,macho yake yaligongana na ya binti aliyekuwa amevalia nguo za njano kuanzia sketi hadi kitambaa cha kichwani. Binti huyo alikuwa amekondeana kiasi cha kutisha mwili wote ulikuwa umeota mapele ya kila aina hali hiyo ilidhihilisha maneno ya Rose.
" Rhoda ndo huyu mnaweza mkaongea sasa!" Bwana Hashimu alitoa utambulisho huo kisha alikaa pembeni. " Rhoda naitwa Rodrick Steven mwanasheria kutoka mahakama kuu hapa mwanza , niliguswa na kesi yako je upo tayari kushirikisna na mimi ili haki yako ipatikane ?" Rodrick alianzisha mazungumzo huku macho yake yakiwa yameutazama uso wa Rhoda bila woga.
"Siko tayari niache tu Hina maana tena afande nirudishe ndani," Rhoda aliyatamka maneno hayo huku akinyanyuka na kuanza kuondoka.
****** “Huyu mwanamke mbaya sana na ni zaidi ya shetani," Hamis aliyekuwa mume wa mama mchepuko alijikuta akizungumza peke yake baada ya kuona vitendo vya unyanyasaji kwa watoto wa kike vikishamili ndani humo kila kukicha. Japo mama mchepuko alikuwa ana mafaniko makubwa lakini tabia ya kuuza wasichana haikukatika nyumbani hapo.
"Huyu anaweza kunitesea hata watoto wangu wacha nimripoti polisi" Hamis aliendelea kukiumiza kichwa chake kwa mawazo baada ya kufanikiwa kuipata card ya bank pamoja na namba za siri. "Sasa hapa nakomba kila kitu kisha naamsha shari
"Lakini nikikurupuka hovyo hovyo lazima atanikamata tu sasa cha kufanya naanza kuchota pesa kidogo kidogo zikiisha tu nauwasha moto hahahaha! Hatakuwa na ubavu tena lazima akanyee ndoo mpumbafu sana!" Hamis hakuacha kuwaza jinsi ya kumuangamiza mama mchepuko.
"Na ushenzi zaidi naongeza mapenzi kwake nitakuwa nampa dozi ya kufa mtu hadi asalende." Kweli hamis alianza mkakati wa kuiba pesa kidogo kidogo huku mapenzi yakiendelea mama mchepuko hakuwa akijua chochote kutokana na safari zake za mara kwa mara za kijijini kurubuni wasichana wadogo kwa lengo la kuwatafutia kazi na akiwafikisha mjini anawageuzia kibao ubize huo ulikuwa ushindi wa Hamis kutekeleza adhima yake kiufasaha zaidi.
"Halo hapo ni kituo cha polis?" "Ndioo!" "Kuna gari aina ya Suzuk lenye namba za usajiri T567 BSS linatoka Tarime kuna mtu ana bangi.” "Tiii! Tiiii! Tiii!," simu ilikatwa hali iliyopelekea askari waliokuwa kituoni hapo kujawa na shauku walipojaribu kupiga tena haikupatikana tena ikawaladhimu kuanza kazi hiyo japo hawakuwa na uhakika na taarifa hiyo.
******
"Tafadhali Rodha rudi ukae nakuomba," Rodrick hakuwa na hadhi ya kumbembeleza Rhoda hadi kupiga magoti bila kujali heshima yake na hata pesa zake kitendo hicho kilimuacha hoi mkuu wa gereza bwana Hashim aliyekuwa akiwatazama kama vile walikuwa wakiigiza.
"Nashukru kwa msaada wako ila siko tayar! Rod umechelewa sana tayari mimi ni mfungwa wa maisha pili hata kama nikitoka sina muelekeo wowote ndugu pekee aliyekuwa amebaki tayari ni marehemu niache nimtumikie yeye pole sana," Rhoda aliyafyatua maneno hayo huku akiondoka ndani ya chumba hicho.
Kwa unyonge na aibu kubwa Rodrick aliyatoa magoti yake chini na kurejea kwenye kiti huku akiwa hana raha hata kidogo . "Rodrick!" Sauti hiyo ilimfanya anyanyue shingo yake kutoka katika meza na kumtazama Bwana Hashim "Je upo tayari kuendelea na hiki?" "Mmmmh !" "Usikate tamaa tambua Rhoda ameathilika kisakolojia hivyo unatakiwa uwe mvumilivu sana nenda naye taratibu tu atakuzoea pole!" Yalikuwa maneno kutoka kwa mkuu wa gereza.
Kweli Rhodrick hakukata tamaa akawa anaenda kumtembelea Rhoda kila baada ya siku mbili huku akimpelekea na baadhi ya mahitaji madogo madogo hali hiyo ilimfanya Rhoda kumuamini Rodrick na siku moja kukubali kuzungumza naye.
"Tulizaliwa wawili tu katika tumbo la mama yetu miaka 20 iliyopita ....." Alianza Rhoda kumuhadithia Rhodrick baada ya kuzoeana siku hiyo ilikuwa ya furaha sana kwa Rodrick ambaye alikuwa na kila aina ya vifaa vya kuchukulia habari hiyo.
"Mimi na pacha mwenzangu na mpendwa wangu Rhodina ambaye kwa sasa ni marehemu kwa muda wa miaka miwili baba yangu mzee Jackson alikuwa mfanyabiashara na mbunge wa Tarime miaka mingi iliyopita tuliishi kwa raha na starehe japo tulikuwa wadogo sana lakini tulitambua upendo wa wazazi wetu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Furaha hiyo ilikatika kama umeme baada ya kifo cha wazazi wetu kilichosababishwa na ajari ya gari lao mjini musoma wakiwa katika harakati za kapeni ........." alinyamza kidogo na kumtazama Rodrick aliyekuwa bize na kuandika. "Mmmh ! endelea mama!" "Lilikuwa ni pigo kubwa sana kwetu tukiwa watoto wa miaka sita tu hivyo tukawa tumehamia musoma kijijini kwa bibi baada ya kikao cha ukoo kupendekeza hivyo tukawa tumeyaanza maisha upya ya kijijini na bibi .Bibi alitupenda sana lakini naye hakudumu sana miezi sita tu tukiwa naye alifariki na kutuacha peke yetu.
Mali zote za baba zilichukuliwa na ndugu zake na hata za bibi nazo ziligawanywa maana bibi alikuwa na ng' ombe wengi sana Shangazi Martha akawa amejitolea kutulea hivyo tukawa tumehama musoma kijijini hadi Tarime vijijini tukawa tunaishi na shangazi. Shangazi alituzuia hata kusoma tukawa wa kushinda shambani na kuchunga mifungo na mateso ya hali ya juu sana .Vile vile tulianza kusikia tetesi za sisi kukeketwa kama ujuavyo kabila letu alipokuja kutushirikisha tulikataa maana wazazi wetu pamoja na bibi walikuwa wametuzuia kukataa kwetu ilikuwa kama kuwasha moto...
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment