Search This Blog

Friday, July 15, 2022

MY X GIRLFRIEND - 3

 







    Simulizi : My X Girlfriend

    Sehemu Ya Tatu (3)





    “UNAENDA WAPI USIKU HUU??”



    Aisha alikutana na swali hilo ambalo alishindwa kulijibu zaidi ya kutumbua tu macho kama mjusi aliyebanwa na mlango.

    “Si naongea na wewe?” aliongea Jack na kumuangalia usoni Aisha. Wakati bado anatumbua macho. Simu yake ikaita tena.



    Alichokifanya ni kumsukuma Jack pembeni na yeye kutoka mule ndani mbio na kumuacha Jack akiwa amepigwa na bumbuwazi.



    Jack hakuamini kuwa kitendo kile kinaweza kutokea kwa mwanamke aliyetokea kumuamini. Hakuyataka machozi ya mapenzi yamtokee ndio maana kipindi kirefu aliishi akiwa hana msichana. Leo hii mwanamke wa kwanza kumuamini ndio amemfanyia mambo kama yale.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alijikuta Jack anaanza kulia na kusababisha kumuamsha mdogo wake na kumfuata pale saebuleni.

    “tatizo nini kaka?” aliuliza Mack baada ya kufika eneo hilo.

    “AISHA” ailiitikia Jack huku analia.



    “amefanya nini?”



    Swali hilo liliongezxa kilio kwa Jack ambaye mpaka wakati huo alipoteza gharama nyingi kwa ajili ya maandalizi ya ndoa yao.



    Mdogo wake alielewa kitu kilichokuwa kinamliza kaka yake. Alimbembeleza usiku kucha bila ya mafanikio.



    Asubuhi ya siku ya pili yake, Aisha alirudi pale nyumbani akiwa na Zakaria. Jack hakuamini kumuona Aisha akiwa na mwanaume waliokuwa wameongozana huku wakiwa wameshikana mikono.



    “Jack, naomba unisamehe sana kwa kile kilichotokea jana. Sio mimi bali ni nguvu ya mapenzi tu niliyokuwa nayo juu ya huyu mtu. Nadhani unakumbuka kuwa kitu kilichonileta Dar ilikua ni kwa ajili ya kumtafuta mpenzi wangu.. huyu ndio Zakaria mwenyewe.”



    Aliongea Aisha huku akimuangalia Jack ambaye alikua tu sebuleni huku akionyesha wazi kuwa alikua na majonzi ya toka usiku wa jana yake.



    “nakushukuru kwa kila ulichonifanyia. Nimekuja kukuaga tu kuwa naenda kuanzisha maisha na mtu nimpendaye kwa dhati. … sina ninachodai humu ndani, zaidi ya nguo ambazo pia sitazichukua. Nawatakia maisha mema.”



    Aaliongea Aisha. Bila kusubiri kujibiwa chochote, aliufungua mlango na kutoka.

    Jack hakuamini kilichotokea. Muda mwengine alijua kuwa labda ni ndoto na kukicha hali itakuwa tofauti.



    Alishindwa kwenda kazini wala kufanya chochote. Hata alipoletewa chakula na mdogo wake, hakikupata nafasi ya kupita kooni kutokana na maumivu aliyokuwa nayo.



    Ule usemi wa kuwa mpende akupendaye na uachane na mtu ambaye haonyeshi upendo ju yako ili uepukane na mateso ya moyo yasio na ulazima ulimuingia Jack na kupiga moyo konde na kuamua kuangalia maisha yake.



    Mapenzi moto moto yaliyopoa kitambo yalipashwa tena moto na kuwa moto zidi ya pale mwanzo kati ya Zakaria na Aisha.



    Wlianza kula nchi na majani yake kutokana na Zakaria kuwa na mali nyingi alizoachiwa na kaka yake ambaye kwa sasa ni marehemu.



    Duka la nguo maeneo ya sinza na la viatu maeneo ya kariakoo ndivyo vilikuwa vitu vikubwa vya ziada vya kuwaingizia kipato cha ziada. Zakaria alimtafutia Aisha kazi pale pale alipokuwa anafanya kazi mwanzo kabla ya kuanza kusimamia miradi ya marehemu kaka yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******************************



    Taarifa na kufa kwa ndoa ya Jack na Aisha iliwasikitishe wengi na kumpa pole sana Jack. Ilikuwa kama picha vile, lakini huo ndio ulikuwa ukweli kwa Jack kupokonywa tonge mdomoni. Ilikua imebaki wiki moja tu ndoa ipite.



    Siku moja akiwa anatoka kazini, alikutana na Aisha njiani. Akaamua kumpita bila kumsalimia.



    “JACK..”



    Ilisikia sauti ya Aisha ikitokea nyuma yake. Akaamua kusimamisha gari yake na kupaki pembeni.

    “jamani, ndio unanipita kama hunijui?” aliongea Aisha huku anatabasamu.



    “sijakuona,.. niambie.” Aliongea Jack huku akinyesha kuwa hakua na tofauti yoyote kati yao.

    “nisubiri dakika mbili, maana nilikuwa pale stationary. Nina mzigo wako nataka kukupa.” Aliongea Aisha huku akionyesha kuwa na furaha kubwa.

    “sawa.” Aliitikia Jack.



    Aisha akatoka mbio na kuingiia stationary aliyokuwepo hapo mwanzo. Alitumia kama dakika kumi mule ndani na kutoka baadae. Alimkuta Jack akiwa pale pale anamsubiri.



    Alivuka bara bara na kumfuata pale alipo.

    “samahani, nimekuweka jamani.” Aliongea Aisha baada ya kurudi eneo lile.

    “poa, .. nakusikiliza wewe.” Aliongea Jack.

    “huu mzigo ni wako. Maana nilikua nataka nikuletee nyumbani kwako, kwa bahati nzuri ndio nimekuona.” Aliongea Aisha baada ya kumkabithi Jack bahasha.



    Jack aliondoa gari na kwenda nyumbani ambapo alimkuta mdogo wake yupo sebuleni anaangalia mpira ambao ulikua unarushwa live mida hiyo.



    Baada ya kula chakula . akakumbuka kuichukua ile bahasha aliyoletewa na Aisha na kuifungua.



    Alipofungua tu, alikutana na kadi iliyorembwa vizuri huku ikiashiria kuwa ulikua mualiko wa harusi. Alipoifungua ndani, aliona majina mawili ambayo aliyajua vizuri. AISHA na ZAKARIA ndio walikua wahusika wa kuu walikuwa wanaoana.



    Taarifa zile zilimuuma kiasi, lakini akapata ujasiri wa kumuita mdogo wake na kumpa ile kadi.

    “sasa ndio anatutambia au?” aliongea Mack kwa hasira.

    “hamna… heshimu tu maamuzi yake.” Aliongea Jack.

    “kwahiyo unaenda au?” aliuliza Mack huku akimuangalia kaka yake usoni ili azisome hisia zake kuwa ameupokeaje ule mualiko.



    “kwakua amenialika na amenisisitizia kuwa nitilie maanani kilichomo ndani, mi nitaenda.” Aliongea Jack kwa ujasiri mkubwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku ya harusi iliwadia na kila mmoja aliyekuwa amepewa kadi alihudhuria ile harusi. Jack na Mack nao walihudhuria harusi ile ilyofana kwa kupata wageni wengi na wafanya biashara mbali mbali.

    Maharusi walitoka ndani na kukaa sehemu waliyotakiwa kukaa. Wakati ratiba ya ndoa inaendelea, Jack alikua makini kufuatilia kila tukio lililokuwa linaendelea. Aisha alianza kulisha keki wageni waalikwa baada ya kumaliza meza kuu zuilizokuwa pale. Alipofika kwa Jack, hakuweza kumuangalia usoni, alijiinamia na kulisha Jack ambaye wakati huo alikua anajitahidi kuonyesha tabasamu lakini ukweli ulibaki moyoni mwake.



    Aisha alipoondoka huku nyuma Jack alibaki anamuangalia Aisha ambaye alitakiwa awe mke wake yeye.



    Ujasiri ulimshinda na kujikuta machozi yanamdondoka. Hakuweza kuvumilia harusi iishe, alimchukua mdogo wake na kuondoka huku ratiba zengine za harusi zikiwa zinaendelea.



    Alirudi nyumbani huku macho yake yakiwa yamelowa machozi. Mack alikuwa mtu pekee aliyekuwa anamtia nguvu na kumfariji Jack kwa ajili maumivu ya mapenzi aliyokuawa nayo moyoni.



    Miezi ikapita huku kumbukumbu za Aisha zikiendelea kuishi ubongoni mwa Jack. Alitumia muda mwingi kumuwaza mtu huyo aliyekuja kumpa kitu alichokikataa katika maisha yake.



    Mack alizidi kumpa moyo kaka yake na kumwambia kuwa kama kweli amechagua moyo wa kupenda, basi atampenda mtu mwengine tofauti na Aisha. Pia alimuambia asisikitike sana kwakua hakujua kuwa mungu atakua amemuepushia gani.



    Kazi ya kuuridhisha moyo kwa kukubali matokeo ni kubwa na inayogharimu sana. Hivyo kuwekeza hisa zako asilimia mia katika moyo wa mtu mwengina ambaye ana lengo tofauti na malengo uliyonanyo wewe ni mateso zaidi ya mtu aliyeamua kukuchoma kisu huku akijitapa kuwa ana ubavu na huwezi mfanya kitu chochote.

    Damu hupooza maumivu, ila kwakua moyo ukiumia hautoi damu, maumivi yake ni makubwa yanayoathiri utendaji kazi wa mwili mzima na kuufanya kuungana nao katika maumivu hayo.



    Maisha ya kubaki wawili bila msichana mule ndani yali wachosha kwa muda mfupi sana. Walishazoea kupikiwa na kufuliwa na Aisha ambaye walimchukulia kama ndugu mara ya kwanza na baadae walitamani kumuoa kabisa. Ila kilichotokea kiliwafanya wasiamini mpaka waliposhuhudia harusi yake live bila chenga.



    Mwaka mmoja ukapita toka ndoa ya Aisha ilipopita, maisha ya furaha yakarudi tena kwa Jack na mdogo wake Mack.



    Ilifika jumapili moja tulivu, Jack aliamua kwenda kufurahi na mdogo wake ufukweni mwa bahari ya hindi.



    Ilikua ni ajabu sana kwa siku hiyo beach kukosa watu wengi. Walipoangalia hali ya hewa kidogo iliwaridhisha kuwa sababu ya watu kutokuwa wengi siku ile.

    Kulikua na mawingu mazito yaliyoashiria mvua kunyesha muda sio mrefu. Lakini hali hiyo ilidumu kwa muda mrefu bila tukio hilo la mvua kunyesha kutokea.



    Wakati wanatembea tembea huku walikila pop cone na crips, walitembea kila mahali huku wakiufurahia upepo ule mwanana.



    Wakiwa wanakatisha katika miti Fulani hivi ambayo ina miba mirefu ambayo inakuwa ya kijani na inapenda kuota sana beach, walisikia sauti ya mtu kwa mbali akiwa analia kwa kwikwi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sauti ile iliwashawishi kuuzunguka ule mti. Walimkuta msichana akiwa amejiinamia huku akiwa analia kwa uchungu. Walitamani kumpita, ila moyo wa Jack ukaona kuwa ulikua unafanya makosa kumpita yule mtu bila kujua tatizo lilikuwa linamfanya alie hadharani.



    “umepatwa na nini dada.”



    Alijikuta Jack anamuuliza yule dada alikua aalia kwa sauti iliyoashiria kuwa jambo lililompata ni kubwa.



    Alichokifanya yule dada ni kuinua sura yake iliyokuwa nyekundu kwa wakati huo huku macho yakiwa yamemvimba kutokana na kilio. Hakujibu chochote, zaidi ya kujiinamia tena na kuendelea kulia kwa kwikwi kama hapo awali.



    ‘kaka, tuondoke. Itakuwa mapenzi tu hayo na si kitu chochote. Ndio maana mimi simuweki mtu moyani kabisa. Yaani sitaki demu na nikimuhitaji basi special kwa game. Hiyo ndio ishu. Maana kujifanya unapenda ndio madhara yake haya. Kila wakati unalia tu na kuumia moyo bila sababu.”

    Aliongea Mack na kumvuta mkono kaka yake ambaye alionyesha kuwa hajaridhika kumuacha yule msichana pale bila kujua amsaidie vipi tatizo lake.



    Walimuacha yule msichana pale na wao wakaendelea kubarizi upepo ule uliozikosha nafsi zao.

    Ilipofika jioni. Waliridhika na kuamua kuingia kwenye gari yao tayari kwa safari ya kurudi nyumbani.



    Walipokuwa njiani , walishangaa kuona foleni kubwa ya magari huku watu wakiwa wamekaa njiani tena wamezunguka kama kuna kitu kama ajali imetokea barabarani pale.

    Kwa sababu gari yao ilikua mbali, wakaamua kubadilisha njia na kutokea mbele kidogo.



    Uwazi wanjia uliwasababisha waone kilichotokea pale. Waliona rangi za nguo zilizokuwa zinafanana kabisa na yule dada waliyekutana nae kule Beach.



    Walipaki gari pembeni na kwenda na wao kushuhudia. Walipigwa na butwaa baada ya kuuona mwiili wa yule dada ambaye ulionyesha kuwa aligongwa na gari kabla ya kifo chake.



    Walisikitika sana hususani Jack. Waliamini itakuwa stress alizokuwa nazo ndio zimesababisha kutokea kwa ajali ile.

    Walirudi nyumbani na kuendelea na shughuli zao.



    Baada ya miezi mitatu, waliamua kujikumbushia tena na kwenda tena Beach. Kutokana na kuwa sio wapenzi sana wa live show zinazokuwa kila mwisho wa wiki kwenye beach hiyo, waliamua kutumia masaa mawili tu hapo Beach na kuamua kurudi nyumbani.



    Wakati wanaliendea gari lao, walimuona msichana mmoja akiwa amelikalia gari lao. Jack alienda mbele ya ile gari iliamuombe asogee pale ili aweze kutoa gari lake.



    Alipomfikia tu yule dada, ghafla moyo ukamlipuka baada ya kumuona yule dada Usoni. Alikua anafanana kabisa na yule dada waliyemkuta amekufa kule barabarani wakiwa wanatoka beach.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alijikuta anashindwa kuongea chochote zaidi ya kumshangaa yule binti bila kumwambia kitu kilichomleta pale. Yule dada alimuangalia kwa pose baada ya kuona anaangaliwa sana na Jack. Macho ya yule dada yalipogangana na Jack, yalimfanya azidi kupigwa na kupigwa na bumbuwazi.

    Alikua anafanana kabisa na yule dada. Mpaka kidoti kilichokuwa pembeni juu kidogo ya midomo yake mizuri iliyokatika kati kati, kilikua kimekaa pale pale kilipokaa kwa yule dada wa awali aliyemuona mwanzo.



    Wakati anajaza mawazo kichwani kwake yasiyokuwa na mtu wa kuyajibu, yule dada aligeuka nyuma na kumuona Mack ambaye aliufungua mlango na kukaa siti ya dereva, alimua kuondoka bila kumjali Jack.



    Jack aliendelea kumsindikiza kwa macho yule dada ambaye hakuamini kabisa kama angeweza kuwa hai tena kutokana na ajali mbaya iliyompata.



    “hata kama duniani wawili wawili,.. hii too much.”



    Alijikuta Jack anaongea maneno hayo huku akimalizia kumfuatilia yule binti kwa macho mpaka alipokata kona ndio macho yake yakaridhika. Alipanda kwenye gari huku fikira juu ya binti yule ambaye hajui kama atamuona tena zikiwa zime mtawala kutokana na kutoamini kuwa ajali iliyompata aliweza kupona tena kwa kuda mfupi na kuwa hai tena.



    “yaani mpaka kidoti?”



    Alijikuta anaongea kwa sauti maneno hayo na kumfanya mdogo wake amuangalie bila ya kuelewa alichokuwa akikimaanisha kaka yake.



    Walifika nyumbani na kuendelea na shughuli nyingine. Kesho yake asubuhi, alienda kazini kama kawaida. Mchana aliona uvivu kurudi nyumbani kwa ajili ya kula kama alivyozoea. Aliamua kuingia kwenye restaurant moja iliyopo sinza kwa ajili ya kupata chakula cha mchana.



    Alipokua anakula, alipigiwa simu na mdogo wake. Aliipokea na kumpa taarifa za yeye kula juu kwa juu. Baada ya hapo akakata simu na kuendelea kula.



    Alipomaliza kula, alilipia na kutoka nje. Simu yake ikaita tena. Wakati anabonyeza kitufe cha kupokelea huku anaendelea kutembea, alijikuta amegongana kikumbo na msichana aliyekuwa amebeba box dogo mkononi.

    Mgongano huo ulimfanya yule dada aliyebeba boksi hilo kuliachia na sahani za udongo zilizokuwa humo ndani zikavunjika.



    “demn… huangalii mbele wakati unatembea?” iliongea sauti ya kike iliyokuwa inakaripia wakati huo. Kwa upole kabisa, Jack alimuangalia huyo dada ikiwezekana waongee ili amlipe kwa hasara aliyoipata katika ajali ile ya maungoni.



    Ghafla akajikuta ameduwaa baada ya kumuona yule msichana pale. Ni yule aliyekutana nae beach mara mbili waluipoenda akiwa na mdogo wake. .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “sorry…. Mi nitalipa hii hasara. We niambie tu ita ni cost shilimgi ngapi?” aliongea Jack kwa upole na kumfanya yula dada kukunjua ndita alizokuwa amezikunja wakati huo.



    “kama utalipa … haina shida, maana sina hata buku hapa useme nirudi tena dukani nikanunue zengine.” Aliongea yule dada kwa sauti ya kawaida.



    “hilo usijali,.. cha muhimu hatukuumia tu,” aliongea Jack huku anatabasamu.

    “ni kweli.” Alijibu yule dada baada ya kumuona Jack anachomoa waleti yake



    “shilingi ngapi hivi vyote vilivyo vunjika?” aliuliza Jack huku akiwa bize kumuangalia huyo dada mwenye uzuri wa sura na umbo.

    “elfu ishirini na nane.” Alijibu yule dada bila kubabaika kuonyesha kuwa ile ndio ilikua fedha halisi aliyoitumia kununulia vile vitu.

    “chukua hizi… usijali.” Aliongea Jack na kumkabithi yule dada noti tano za shilingi elfu kumi kumi.

    “oooh.. thenks.” Alishukuru yule dada na kuzipokea zile hela kwa mikono miwili na kumuachia tabasamu Jack lililomkosha kisawa sawa.



    “milima ndio haikutani kwa sababu haijongei, ila kwa sisi binaadamu hukutana tena sehemu mbali mbali. Sio vibaya tukijuana hata kwa majina dada.” Alijikuta Jack anaongea maneno hayo baada ya kumuona yule dada akiwa na dallili zote za kutaka kuondoka baada ya kupokea zile hela.



    “naitwa ELIZABETH,..ukipenda niite Eliza au Liz nitaitika.” Aliongea huyo dada na kumfanya Jack atabasamu.

    “chukua card yangu ya biashara. Ina jina na mawasiliano yangu kama utapenda tuwasiliane pia.” Aliongea Jack na kumkabidhi business card yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Jackson… nice name.” aliongea yule dada baada ya kuichukua ile kadi na kuisoma kwa sauti sehemu ya jina la Jack na kumuangalia usoni kwa mapozi. Nembo ya benki ya CRADB BANK ilimsisimua yule dada na kumuangalia mtu huyo aliyeonekana kuwa na umri mdogo.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog