Simulizi : My X Girlfriend
Sehemu Ya Pili (2)
Kipindi chote alichokuwa anaishi pale, Aisha hakuwahi hata siku moja kumuona msichana wa Jack wala kusikia stori juu ya mvulana huyo kuwa na mpenzi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mack hakujificha, alikuwa anakuja nae mpaka pale na muda mwengine walikuwa wanakula chakula pamoja au huwa anaingia jikoni kabisa na kupika. Swali hilo lilimuumiza kichwa kwa muda huku akihofia kumuuliza Jack.
Siku hiyo aliamua kujifunga mkanda na kuamua kumvaa Jack na kuamua kumuuliza swali hilo. Jack alimuangalia Aisha kwa sekunde kadhaa kisha akamjibu.
“ni story ndefu sana, ndio maana mpaka hivi sasa sihitaji kuyashobokea mapenzi.” Aliongea Jack kwa upole na kumuangalia Aisha ambaye walikuwa wote sebuleni wakiangalia picha kutokana na kuwa siku hiyo ilikuwa ni mwisho wa wiki.
“nina muda wa kutosha wa kukusikiliza, usijali kwa hilo.” Aliongea Aisha na kumuangalia Jack ambaye muda huo alikua kama anajifikiria kumuelezea. Baada ya sekunda kadhaa alimuangalia Aisha na kuanza kumpa stori ya maisha yake.
**********************
Jackson Peter alizaliwa hapa Dar-es-salaam katika familia yenye kipato cha juu kiasi. Alimpoteza mama yake baada ya kujfungua tu mdogo wake Mack. Huzuni ilitawala kwao. Baada ya miaka sita baadae, baba yake aliamua kuoa mwanamke mwengine ili amsaidie ulezi wa watoto wake wale wa kiume ambaye mmoja alikua ana miaka kumi na moja ambaye ndio Jack na mwengine akiwa na miaka sita peke yake ambaye ndio Mack.
Walishi kwa furaha kwa kipindi kifupi kutoka kwa mama yao huyo mpya waliyeletewa na baba yao. Baada ya miezi kadhaa kupita, visa na manyanyaso vilianza kutokea kutoka kwa mama yao huyo.
Walivumilia kwa muda na baadae wakaamua kufikisha malalamiko yao kwa baba yao.
Waliilalamika sana bila ya mafanikio. Sana sana waliishia kufokewa na kupigwa wakati mwengine na baba yao wakishitaki chochote wanachofanyiwa na mama yao huyo aliyekuja kuyeyusha furaha na amani kwao.
Miezi ya mateso na manya nyaso yaliendelea kwa kasi kubwa bila mzee wao kuamua lolote iliendelea kwa shida na ukosaji wa haki za msingi kwa watoto hao wawili.
Muda mwengine baba yao aliwaongezea mateso pindi ashitakiwapo makosa yao hata kama hawakufanya kweli.
Miezi sita baadae baba yao alifariki dunia katika mazingira ya kutatanisha. Yule mama yao alirithi mali nyingi za mzee wao kwakua ziliandikwa kwa jina lake, kasoro nyumba moja tu ambayo ilikua na jina la marehemu mama yao.
Mungu akamjaalia Jack baada ya kusoma kwa bidii masomo yake ya biashara na kufanikiwa kuchukua stashahada.
Akapata ajira katika benki ya CRDB ambayo anafanya kazi mpaka sasa hivi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Toka hapo Jackson aliapa kutojihusisha na maswala ya mapenzi kutokana na aliyoyashuhudia kutoka kwa marehemu baba yake.
****************
Baada ya kumuhadithia Aisha stori yake iliyomfanya asimuamini mtu anayeitwa mwanamke katika maisha yake, alinyamaza na kusikiliza mawazo yatakayotolewa na dada yake huyo wa hiyari.
“pole sana, ila si kwamba wanawake wote wapo hivyo. Ni baadhi tu na hasa wanaopenda mteremko kama huyo mama yako wa kambo.” Aliongea Aisha na kumfariji Jack ambaye alikua na hali ya huzuni wakati huo.
Siku hiyo ilipita huku kila mmoja akijua maisha aliyoishi nyuma mwenzake.
Upendo uliopo ndani ulikua mkubwa kila mmoja kumuamini na kumjali mwenzake.
Safari za kwenda matembezi kila week end waliongozana wote watatu. Na hata Jack alipokuwa anaenda shooping kwa ajili ya kununua nguo, basi hakumtenga Aisha na wote walitoka ng`aring`ari kila walipotupia mapigo hayo yaliyokwenda na wakati.
Ni zaidi ya nguvu ya sumaku iliyoshinikizwa na umahiri mkubwa wa Mack katika uchochezi wa hisia za watu. Kufumba na kufumbua Jack na Aisha wakajikuta wapo ndani ya uzio wa mapenzi.
Aisha alikubali kumtua Zakaria baada ya kumtafuta muda mtrefu bila mafanikio. Akaamua kumpa moyo Jack ambaye hajawahi kupenda kabla ila amejawa na uoga na hisia za maumivu kwa vitendo alivyofanyiwa baba yake.
Mapenzi hayo yaliyoanza kwa kasi ya Rocket yalizidi kukua na kupanuka siku hadi siku. Hali hiyo ilimfanya JACK kuandaa part ndogo ya kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake huyo wa kwanza aliyemkubali ukubwani kwa kua hakuhitaji kabisa swala la mapenzi hapo kabla.
Sherehe hiyo ilifana na Aisha alifarijika. Japokuwa hakua na ndugu katika umati wote uliohudhuria pale, ila alijiona yupo juu kwa muitiko wa watu waliohudhuria sherehe yake.
Baada ya zoezi hilo kukamilika, zoezi jengine la kufunga ndoa kabisa ndio likawekwa mezani kwa muda huo.
Mchango uliotolewa na benk anayofanyia kazi na wafanya kazi wenzake ulitosha kabisa kufanya harusi kubwa. Hivyo tarehe ilipangwa na baada ya mwezi mmoja tu basi ndoa ilitakiwa kupita.
Siku zilisogea kwa kasi huku kila mmoja akiwa na hamu ya kuingojea hiyo siku kwa nguvu.
Shooping kwa ajili ya harusi hiyo ilianza mara moja kwa bibi harusi ambaye ndio Aisha kupewa fungu lake la hela kwa ajili ya kununua shela na vitu vingine alivyoviona ni muhimu kwake.
Siku hiyo Aisha alitoka mapema na kuchukua funguo ya gari ndogo mpya aliyopewa kama zawadi na bosi wa benk ya CRDB katika sherehe ya kuvalishwa pete.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alitia gia na kwenda maeneo ya msasani katika madukwa makubwa ya Boutique kwa ajili ya kupata shela zuri kwa ajili ya harusi yake. Alizunguka sana na baadae alirudi jioni bila kununua chochote.
“vipi mke wangu mtarajiwa?.. hujaliona au nikakuchagulie mimi?” aliuliza Mack kiutani akijaribu kumtania shemeji yake.
“sijaona toleo jipya kabisa yaani, naona yote muundo ule ule tuu.. mi nataka siku huyo watu macho yawatoke nikipita tu.” Aliongea Aisha na kumuangalia Jack ambaye muda wote alikua anatabasamu tu.
“sasa watu wakitoka macho si itakuwa vurugu hiyo badala ya sherehe?” aliongea Mack na kumfanya Aisha aanze kumkimbiza huku akichukua mito midogo iliyopo pale sebuleni na kunza kumrushia shemeji yake aliyekua ana vituko visivyoisha.
“acha utani bwana, ninachoongea ni ukweli mtupu. Kama vipi niagizie kutoka nje mume wangu.” Aliongea Aisha kwa kudeka baada ya kucheza kwa dakika kadhaa na Mack.
“sawa, nitaongea na rafiki yangu Awena yupo huko Manchester Uingereza. Atanitumia picha za mashela na bei zake kwenye E-mail yangu halafu utachagua mwenyewe.” Aliongea Jack na kumuangalia Aisha aliyekua na shauku kubwa.
Alimtafuta rafiki yake huyo hewani na baabade akampata na kumuelezea shida yake kupitia e-mail walizokuwa wanatumiana.
Kwa haraka Awena alimtumia rifiki yake huyo picha za mashela kadhaa yaliyomvutia Aisha na kuchagua moja wapo.
Harakati za kuhakikisha kuwa shela hilo linafika nchini zilifanywa na Awena na kupokelewa salama usalimini katika mikono ya Aisha na kuwekwa kabatiki ikisubiriwa tarehe tu.
Vitu vidogo viliyobakia viliandaliwa kwa haraka wakishirikiana wote watatu.
Siku moja Aisha alikua saloon maeneo ya sinza. Wakati anasetiwa nywele, kwa mbali alimuona mtu aliyemfananisha sana.
“shoga hebu nitoe hili dryer,.. kuna mtu nimemfananisha.”
Aliongea Aisha na yule shoga yake akafanya hivyo kama alivyoagizwa.
Aisha alitoka na kumfuatilia yule kaka, alipomuangalia vizuri aligundua kuwa ni yeye kabisa. Mara akamuona anapanda kwenye gari ndogo aina ya starlet na kuondoka.
“HAIWEZEKANI”
Aliongea Aisha na kuchukua funguo ya gari yake na kuanza kuifuatilia ile gari. Aliifuatilia mpaka maeneo ya sayansi kijitonyama.
Gari ilipaki kwenye moja ya geti katika nyumba za pale na yule mtu akashuka. Ndipo Aisha alipomuona vizuri.
“ZAKARIAAAAAAAAAAAAAA”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliita Aisha kwa sauti kubwa huku akishuka kwenye gari yake. Yule mtu naye baada ya kuisikia ile sauti aligeuka nyuma na kukutana na huyo dada aliyemuita.
“AISHA!!!!!!”
Yule kaka nae akalitaja hilo jina ili kuhakikisha kuwa ndiye mwenyewe au alimfananisha.
Bila kusubiri, Aisha alijikuta anamkimbilia mwanaume huyo na kumkumbatia.
Baada ya kukumbatiana kwa muda wa dakika mbili hivi, waliachiana na kuangaliana kwa chati. Kila mmoja alikua haamini macho yake kwa kile alichokiona.
“karibu ndani.” Aliongea Zakaria na kumuangalia Aisha ambaye hakuwa na usemi zaidi ya kumfuata Zakaria aingiapo.
Waliingia mpaka ndani na kwa bahati mbaya umeme haukuwepo pale nyumbani.
“tutafute sehemu nyengine tulivu, hapa hapafai tena.” Aliongea Zakaria na kumuangalia Aisha ambaye alikuwa hana usemi wowote kwa wakati huo.
Walitoka na kwenda sehemu tulivu kwa ajili ya kuongea mawili matatu.
“unajua mpaka muda huu siamini macho yangu kuwa ni wewe ndiye ninayeongea naye?” aliongea Zakaria baada ya kutulia kwa muda mahala hapo walipoweka kambi ya muda mfupi.
“kwanini?” aliuliza Aisha huku uso wake ukiwa umejawa tabasamu.
“unajua nilienda mpaka Morogoro kukutafuta lakini nikakukosa. Nikaambiwa kuwa toka mama yako wa hiyari afariki tu na wewe ukatoweka pale” aliongea Zakaria na kumuangalia Aisha ambaye alikua makini kumsikiliza.
“ni kweli zakaria, niliamua kuja huku mjini kukutafuta wewe mpenzi wangu.” Alifunguka Aisha bila kujali kuwa kwa sasa alikua na mtu mwengine ambaye siku za ndoa yao zilikua zinahesabika.
“kusema ukweli mpaka hivi sasa bado sijachukua uamuzi wa kuwa na mwanamke mwengine japokuwa nilishakata tamaa ya kukutana na wewe tena. Sijui wewe mwenzangu umeshanitoa moyoni?” aliuliza Zakaria huku akijaribu kuonyesha hisia zake juu ya mpenzi wake huyo waliyepotezana muda mrefu sana.
Aisha alipatwa na kitu cha ajabu kilichosoma ubongoni haraka na kumpa maamuzi ya kuivua pete ya uchumba aliyovalishwa na Jack kwa siri hali iliyofanya tukio hilo lisionekane na Zakaria ambaye hakuwa makini sana kumchunguza.
“hata mimi, nimekutafuta bila mafanikio kwa muda mrefu. Japokuwa nilikata tamaa kukutana na wewe tena, ila moyo wangu umekuwa mgumu sana kumkubali mwanaume yeyeto zaidi yako wewe Zakaria”
Alijikuta Aisha anaongea maneno hayo bila kujali kuwa anatengeneza tukio litakalomuumiza mtu asiyekuwa na hatia katika tasnia ya mapenzi. Aliongea maneno hayo na kumtazama Zakaria ambaye muda huo alikuwa ametabasamu huku akoionyesha wazi kuyafurahia maneno yake.
“woooooh… ahsante mungu.” Aliongea maneno hayo Zakaria na kunyanyuka. Akamfuata Aisha alipokaa na kumyanyua. Bila kuchelewa akamkumbatia na kuanza kumpa mabusu yasiyokuwa na idadi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Masaa yalisogea kwa kasi hadi kufikia saa tatu usiku bila ya Aisha kuonekana katika macho ya Jack. Hali ya wasi wasi iliwatanda Mack na kaka yake kwa kuhofia usalama wa Aisha. Kwa mara kadhaa walipiga simu ya Aisha na haikupokelewa. Na baadae haikupatikana kabisa. Hali hiyo ilizidi kuwachanganya sana. Hawakuwa na raha muda wote walipokuwa wamejipanga sebuleni kumsubiri Aisha.
“kwani alivyokuaga kuwa anaenda saluni, hakusema kuwa atapitia sehemu yoyote?” aliuliza Jack huku akionyesha ishara zote za kuchanganyikiwa kutokana na tukio hilo ambalo ni mara ya kwanza kutokea.
“hakuniambia kua atapitia mahala popote, zaidi ya kuniambia kuwa anaenda saluni kuseti nywele zake.” Alijibu Mack
“wewe unapajua huko saloon?”
aliuliza Jack huku akiwa hatulii sehemu moja. Alikuwa anatembea tembea huku akikizunguka kile kiti alichokalia M,ack pasi na kutafuta kitu cha maana alichokuwa anakifuatilia. Kila dakika alitupa macho yake kwenye saa ya ukutani ambayo ilikkuwa inajitahidi kumuhesabia sekunde na dakika ambazo zilimsomea kuwa mpaka wakati huo saa nne juu ya alama ilikuwa imeshagota.
“mambo ya wanawake brother mi nitayajulia wapi?.. sijui ni wapi atakuwa ameenda.” Aliongea mdogo wake Jack na kumfanya kaka yake akae kwenye ngazi ya kuelekea chumbani badala ya kwenye sofa. Tai aliiona inamkaba, aliilegeza kidogo na kuamua kusubiri muda atakaorudi Aisha.
Honi za gari zilizokuwa zikilia muda huo getini ndizo zilizomshtua na kumuamsha Jack pale alipokaa na kwenda nje na kufungua geti. Aliiona gari ya Aisha ikiwa nje, alifungua geti na Aisha aliingiza gari ndani na kwenda kupaki mahala pake.
Baada ya hapo, alishuka na kuingia ndani, alimsalimia shemeji yake na kupitiliza chumbani kwake.
Jack alimfuata Aisha chumbani na kumkuta anasaula nguo kwa ajili ya kulala.
“kimekupata nini mke wangu mpaka unarudi muda huu?” aliuliza Jack baada ya kuingia tu ndani.
“kuna sehemu nilienda, so foleni na ukijumlisha sikuenda muda mrefu ndio maana nimechelewa kurudi.” Alijibu Aisha kwa kujiamini na kuonyesha wazi kuwa haoni kama alikua ana kosa.
“ndio hata kupiga simu angalau kutujulisha basi kwamba utachelewa?” aliongea Jack baada ya kutoridhishwa na jibu la Aisha.
“simu yangu ilikata chaji.” Alijibu Aisha huku akiendelea kuvua nguo zake.
“mbona nilipokupigia simu kwa mara kadhaa ilikua inaita bila yaw ewe kuipokea?”
bado Jack aliendelea kumbana Aisha kwa maswali yalimgusa Aisha kwa wakati huo.
“naomba tulale Jack, maana fikira zako zinafikiria mbali sana. Kwani huniamini?”
Aisha alikwepa kujibu lile swali na kumgeuzia kibao Jack na kumuuliza yeye.
“kukuamini nakuamini, tena asana tu. Ila kitendo ulichokifanya leo sijakifurahia.” Aliongea Jack kwa sauti ya upole kama yeye mwenyewe na muonekano wake ulivyo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“basi, nisamehe mume wangu. Njoo tulale basi.”
Aliongea Aisha na kumfuata Jack alipo na kuanza kumvua shati na tai.
Siku ya pili yake, Jack alienda kazini kama kawaida, huko alipata kazi ambayo ita mlazimu kuchelewa kurudi nyumbani. Alichukua simu yake na kumpa Taarifa hiyo Aisha.
Mishale ya saa mbili usiku, mlio wa simu ya Aisha ulimshtua alipokuwa jikoni anapika na kwenda kuipokea ile simu.
“niambie mpenzi wangu.” Iliongea sauti upande wapili baada ya simu yake kupokelewa.
“safi tu. Mzima wewe?” aliongea Aisha huku akiangaza huku na huko ili ahakikishe usalama kwa kua mdogo wake Jack aliokua nyumbani.
“njoo basi jamani, maana nahisi kitanda kimekuwa kikubwa sana usiku huu.” Aliongea mtu huyo maneno yaliyomshtua kidogo Aisha.
“mpenzi wangu Zakaria, unanipa mtihani mwenzako. Sijawahi hata siku moja kulala nje ya nyumba hii. Unafikiri watanifikiriaje?” aliongea Aisha kwa sauti ndogo lakini iliyosikika vizuri kwenye masikio ya Zakaria.
“we waambie tu ndugu zako kuwa leo unaenda kwa mumeo. Na wakitaka kuniona hata kesho nikiwa nakurudisha wataniona. Kwani kuna tatizo hapo. Njoo bwana.” Aliongea Zakaria na kumfanya Aisha ashushe pumzi.
“ngoja nijaribu.. sijui lakini.” Aliongea Aisha huku akionyesha kutokuwa na jibu sahihi.
“nakuaminia. .. kama kweli unanipenda na nguvu yetu ya mapenzi bado ipo, basi utakuja kwakua tumefanya mengi makubwa na ya kushangaza kuliko hili.” Aliongea Zakaria.
“sawa, nikukute kituoni basi, maana leo sichukui gari.” Aliongea Aisha na kuonyesha kuwa alikua tayari kufanya hivyo.
“poa, nakuja muda huu. Nipe dakika ishirini tu.” Aliongea zakaria na kukata simu.
Aisha aliipua chakula ambacho kilikuwa tayari kimeshaiva. Akaingia bafuni na kuoga. Kwa haraka alichagua nguo zilizomkaa vizuri na kutinga.
Wakati anajipara kwenye dressing table, simu yake ikaita tena.
“nimeshafika tayari.” Aliongea Zakaria baada ya simu yake kupokelewa.
“nakuja, nipe dakika tano tu.” Alijibu Aisha na kuongeza spidi katika kujipamba kwake.
Alitoka sebuleni kwa kunyata. Alifurahi kutomuona shemeji yake sebuleni. Huku akiwa ameshika viatu vyake, aliufikia mlango kwa style hiyo ya kunyata na kuanza kuufungua mlango huo taratibu.
Hamadi!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alichokiona mbele yake hakuamini, alikua Jack yupo mlangoni kama vile alikua anamsubiria yeye amfungulie mlango.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment