Search This Blog

Friday, July 15, 2022

MY X GIRLFRIEND - 4

 







    Simulizi : My X Girlfriend

    Sehemu Ya Nne (4)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Waliachana na kila mmoja kushika njia yake. Jack alirudi nyumbani huku akuionyesha wazi kuwa na furaha kuonana tena na yule dada.



    “sijui nisema bahati au mipango ya mungu kunikutanisha mara kwa mara na yule binti.” Aliongea Jack baada ya kumuhadithia mkanda mzima kuanzia mwanzo hadi mwisho toka alipotoka kula mpaka alipomuachia namba huyo binti.



    “labda mungu anakuonyeshea mke mwema.” Aliongea Mack na kumuangalia kaka yake aliyekua amejawa na furaha muda wote.



    “hata mimi naona, maana toka siku ya kwanza nilipomuona mtu kama yeye analia kule beach…… ila nimesahau kumuuliza kama alishawahi kupata ajalia ama vipi?... maana muda mwengine nahofia isije ikawa yule dada ni jini?” aliongea Jack na kumuangalia mdogo wake kama ishara ya kutaka kujua msimamo wake juu ya wazo hilo.



    “hapo hatuwezi kujua,.. maana tulimuona amepata ajali na ilivyokua inaonyesha ni wazi kua kupona ni ngumu,.. now unaonana nae mzima kabisa na hana hata kovu.” Aliongea Mack na kumfanya kaka yake kukaa vizuri na kulegaza tai yake.



    “lakini watu wawili wali bwana… inawezekana wakafanana. Ila wakati mwengine fikira zangu zinakataa watu kufanana vile. Labda wapo mapacha.” Aliongea Jack huku akionyesgha wazi kuwa anazikataa fikiria za kuwa Eliza ni jini.



    Usiku ulipoingia, kila mtu alienda chumbani kwake kwa ajili ya kutuliza akili zake kupitia usingizi. Wakati anajiandaa kulala, Jackson alienda kuoga kwanza. Kutokana na mazoea yake ya kuoga kabla ya kulala ndio usingizi kwake huja vizuri.



    Wakati anaoga, alisikia simu yake ikiita. Alipomaliza kuoga, alichukua simu yake na kukuta missed call tatu za mtu mmoja. Ila namba ilikuja bila jina kuashiria alikua mgeni na hajahifadhiwa kwenye kitabu cha simu ya Jackson.



    Kwakua simu ya Jack huwa na salio wakati wote, hakua na haja ya kuangalia kiasi kilichobaki. Alitwanga moja kwa moja hiyo namba na kukaa kitandani.



    “halloow”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sauti nzuri ya kike iliyochujwa na mawimbi ya mtandao ilisikika sawia katika sikio la Jack.

    Jack alimeza mate kwanza kma ishara ya kuliweka koo lake sawa na kuanza kuongea na huyo dada ambaye hakumtambua ni nani, ila sauti tu ilimshawishi na yeye kuilegeza sauti yake na kuitengenezea swaga zitakazo msaidia na yeye kujibu mashambulizi kwa huyo dada aliyempigia simu.



    “hallo.. mambo?” aliongea Jack kwa sauti ya upole iliyojaa kila aina ya pozi za wanaume wenye sauti nzuri kwenye simu na kumfanya yule dada aheme kwa nguvu . hapo Jack akaona kumbe alikua anaweza na yeye kwenda naye sawa.

    “sorry kwa kukusumbua usiku huu.” Aliendelea kuongea yule dada huku akiyang`ata maneno kwa sawga kama wang`atavyo masisiter duu waongeapo kiingereza.



    “wala hujanisumbua,, ila umenifanya nifurahi kuisikia sauti murua kutoka kwako, ingawaje kwa sasa ningependa kukufahamu wewe ni nani?” aliongea Jack kwa pozi.



    “naitwa LIZ, tulikutana mchana kule kwenye ajali ya vyombo.” Aliongea yule dada huku akiyavuta maneno na kucheka cheka.



    “wooooh, Liz… nimefurahi sana kuisikia sauti yako.” Aliongea Jack na kutabasamu.

    “nimeona sio mbaya kama nikikupa hi… usiku mwema J.” aliongea Eliza huku akitegea kukata simu.

    “nawe pia… uote ndoto njema Liz.”

    Aliongea Jack na kukata simu.

    Japo kua simu ilishakatika, Jack aliendelea kuishika kama vile ameweka loud speacker na alikua anaongea nae kwa jinsi macho yake yalivyoganda kwenye kioo cha simu yake. Akajikuta anatabasamu. Mara kicheko kikubwa kikamtoka.



    “YES!!”

    Alijikuta ana ruka ruka mpaka taulo likamdondoka lakini hakujali kwa furaha aliyo kuwa nayo.



    Asubuhi ilipofika, walianza kuchat kwa sms. Na ilipofika usiku waliongea na kupanga siku ambayo wangeweza kukutana tena.

    Baada ya makubaliano yao, siku iliwadia huku kila mmoja wao bila kukosa alifika tena kwa muda muafaka waliokubaliana.

    “nimefurahi sana kwa jinsi ulivyokua na ahadi za kizungu.: aliongea Jack baada ya kusalimiana na mrembo huyo aliyependeza sana kwa jinsi alivyozipangilia nguo zake. Juu alivaa t-shirt nyeupe iliyombana kisawa sawa na baada ya hapo, chini alivaa kimini cha jinzi cha bluu iliyoiva vizuri. Miwani mikubwa iliyoongeza uzuri wa monekano wake pia ulikua kivutio kingine umtazamapo Liz.



    “hata wewe, maana haikupita hata dakika moja toka nifike hapa na wewe umeshafika.” Aliongea Liz na kutabasamu.

    “agiza basi unachihitaji….. kuwa huru.” Aliongea Jack huku akitabasamu.



    Alimuita muhudumu aliyekua anazunguka karibu yake na kumpa oda zao kasha wakaendelea na maongezi.

    “kuna swali linanitatiza halafu kila siku huwa nasahau kukuuliza.” Aliongea Jack baada ya kukumbuka kitu ambacho kilikua kinamuumiza kichwa juu ya mrembo huyo.

    “uliza tu.” Alijibu Eliza na kumuangalia Jack guku akiendelea kuvunja mifupa ya mbuzi aliyelala pale mbele yao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “umeshaniona mara ngapi kabla ya leo?.” Aliongea Jack na kumuangalia Eliza ambaye nae wakati huo alikua anamuangalia pia.

    “mara moja kama sikosei.” Aliongea Eliza huku akionyesha kuvuta kumbu kumbu juu ya Jack.



    “unakumbuka kule beach kuna siku moja uliegemea gari Fulani hivi. Akaja mtu akawa anakushangaa mpaka ukajishtukia.” Aliongea Jack na kumuangalia Eliza ili aone kama anakumbuka.



    “mh…. Nilivaaje?” aliuliza Eliza huku akionyesha wazi kua hakua na kumbukumbu ya siku hiyo.

    “nakumbuka ulivaa kitopu cha rangi ya papo. Kiliandikwa give me a break.” Aliendelea kufafanua Jack ili aone kama huyo dada ndio huyo au alikua anamfananisha tu.



    “anhaaa… ndio mimi. Ila sikua makini kukutazama. Una kumbu kumbu sana.” Aliongea huyo dada na kumfanya Jack kuingiwa na swali lingine zito kutokana na tukio la ajali alilolishuhudia kwa macho yake.



    “ulishwahi kupata ajali ya gari?” aliuliza Jack huku macho yake akiyatuliza kwenye sura ya Eliza.

    “hapana na mungu aniepushie mbali jamani.” Alijibu Eliza kwa mshtuko kidogo kutokana na kutoritarajia lile swali.



    “samahani kama nimekukwaza kwa swali hilo.” Jack aliyaona mabadiiko hayo na kuamua kumuomba radhi. Maana mshtuko wake ulimfanya akunje sura kidogo kisha akairudisha katika hali ya kawaida.



    “hujanikwaza, ila sikulitarajia swali kama hilo.” Aliongea Eliza katika kumtoa mashaka aliyokua nayo Jack kwa wakati huo.

    “swali hilo nilolilokuuliza nilikua nina maana kubwa. Maana miliishuhudia ajali kwa macho yangu. Na mtu mwenyewe aliyopata hiyo ajali alikua anafanana kila kitu na wewe. Yaani mpaka kidoti cha hapo juu mdomo wako na huyo dada anacho.” Aliongea Jack huku akiweka wazi hisia zake juu ya ufananaji wa kutisha kati ya yule dada aliyepata ajali na mrembo huyo.



    “huyo ni pacha wangu EDINA. Ni kweli alipata ajali na kupoteza Maisha maeneo ya msasani beach.” Aliongea huyo dada na kuhuzunika kidogo kwani bado alikua na kumbukumbu imuumizayo kichwani mwake kwa kufariki kwa pacha yake.



    “pole sana Eliza.” Aliongea Jack baada ya kuona jinsi gani Eliza alivyo nyong`onyea kwa sekunde hizo baada ya kumuambia ukweli juu ya mtu waliyemuona analia huko msasani Beach.



    “nishapoa.. ni kweli tulikua tuna fanana sana. Hata ndugu zetu wengi walikua hawatujui yupi ni Edina na yupi ni Eliza. Ndio hivyo tena alipangalo mungu binaadamu huwezi kulipangua.” Aliongea Eliza na kujitahidi kuwa katika hali ya kawaida kama aliyokua nayo mwanzo.



    “kwenu mlizaliwa wangapi.” Aliendelea kudadisi Jack ili aweze kumjua kiundani msichana huyo.

    “tulikua watatu…. Sisi na mdogo wetu mdogo wa miaka kumi sasa.” Aliongea yule dada na kumuangalia Jack ambaye kwa wakati huo alikua anavuta mrija wa juisi iliyokua pembeni yake.



    “pole sana…. Sisi tupo wawili tu. Mimi na mdogo wangu wa kiume Mack.” Aliongea Jack na kuendelea kula ili huyo dada awe huru kuendelea kula kwani alisimama kula kwa muda akijibu maswali yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “mmekosa dada kama sisi tulivyokosa kaka.” Aliongea Eliza na kutabasamu.

    “unaonaje leo hii ukamuone mdogo wangu nyumbani?” aliuliza Jack huku akionyesha tabasamu lake pana baada ya macho yake kugongana na Eliza.



    “tupange siku nyingine,… utakuja kwetu na mimi nitafika kwako.” Aliongea Eliza na kulipiza tabasamu la Jack.



    “nije kwenu??... kwani unaishi na nani?” aliuliza Jack huku akionyesha wazi kua alikua na ishara zote za uoga.



    “naishi na mama na huyo Nelia mdogo wangu wa mwisho.” Aliongea Eliza na kunywa kinywaji chake kusindikiza mnofu uliokua mdomoni mwake.



    “sasa kwenu hakuna mwanaume?.. akitokea hata panya si makelele nyumba nzima?” aliuliza kiutani Jack

    “umejuaje?.... yaani ni shida.” Aliongea Eliza na kutabasamu.



    Baada ya maongezi yao yalisindikizwa na nyama choma huku vinywaji kadhaa vikiendela kupendezesha meza yao iliyokua na watu wawili tu ila ilikua kama kuna watu sita kwa jinsi chupa kadhaa za vinywaji mbali mbali vikiwa vimesimama katika meza yao.

    Waliachana kila mmoja kivyake baada ya Jack kulipia bili yote na kumpa Eliza kiasi cha shilingi elfu thelathini kama nauli yake ya kurudia.

    Haikua ngumu kwa Jack kumuaga mrembo huyo kwa kumpiga busu la mdomoni baada ya kumkabidhi kiasi hicho cha fedha.



    Kila hatua ailiyopiga katika kumsogelea msichana huyo, jaji alikua mdogo wake. Kwa hatua hiyo aliyoifikia mpaka sasa, alipewa maksi nyingi na Mack.



    Juhudi na ufuatiliaji wa hali ya juu, ndio uliomfanya Jack kukubaliana na moyo wake kua Eliza ndio chaguo halisi la moyo wake. Hata Eliza nae huonyesha dalili zozote za kukubaliana na mawazo ya Jack kwa kile alichoambiwa afanye hata kama muda mwengine alikua anakataa. Ila akilazimishwa mara mbili mara tatu hukubaliana na Jack.



    Alimpeleka nyumbani kwake na kumtambulisha kwa mdogo wake. Eliza alifurahi sana kukutana na shemeji yake huyo asiyeishiwa maneno. Walipata chakula cha mchana pamoja kwa furaha huku Jack akijiona mnene siku hiyo kwakua ndoto zake zilianza kukamilika taratibu.



    Zoezi la kwenda kujianika wazi kwa mzazi wa Eliza wala halikumpa tabu Jack. Alienda kukurtana na mama mkwe wake aliyekua bado anadai kwakua aliwazaa watoto wake hao mapacha akiwa na umri mdogo kabisa.



    Maisha yaliendelea taratibu wakati wapendanao hao wakijiandaa na harusi hiyo matata ambayo kwa Jack anaamini itafuta kumbukumbu mbaya zilizomtokea nyuma.

    Mapenzi hayo motomoto kama ilivyo kawaida kwa penzi changa siku zote huwa lina raha sana.

    Kila mmoja huwa anamuhitaji mwenzake muda wote. Kila mmoja huona usiku mrefu hususani alalapo peke yake. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kila mmoja huona anabanwa kama anaishi na wazazi wake na hua wanatamani wawe huru hata kulala wote chumba kimoja.



    Simu zisizokwisha na sms za mahaba ndio huongeza vanilla katika mapenzi matamu ya ice cream.

    Tabasamu la matumaini huchomoza pindi umuonapo mpenzi wako kwa mbali akiwa anakuja. Hata kama ulikua umeudhika na maudhi ya walimwengu kwa siku hiyo. Basi yeye ndio huwa mahakama na jaji wa kuwa hukumu hao waliokusababishia maudhi. Naye hakuangushi, huwaadhibu hata kwa matusi japokua hawasikii. Na wakati mwengine hudiriki kukuambia umuonyeshe hao watu ili akapambane nao hata kama nguvu zake na hao watu hazilingani.

    Kuifupi hayo ndio mahaba nichekee ambayo huja mwanzo kwa utamu kama kinywaji kilichitiwa sukari ya KK.



    Usiku wa manane unachukuliwa kama ni sehemu ya kuupumzisha mwili baada ya uchovu wa siku nzima. Lakini kwa wapenzi wanaoanza mapenzi mapya, huutumia kwa kuongea huku wakiufurahia utulivu unaowafanya wasikiane vizuri bila kubugudhiwa na ndege wala makelele ya watu waliuopo kwenye pirika pirika mbalimbali.



    Kila mtu hutumia ufundi wa sauti yake ya mahaba ilimradi tu aonekane wa pekee na kumfanya mwenzake ajute kwanini hakujuana na mtu huyo mapema.

    Mtu hukujali kushinda wanavyokujali wazazi wako. Huonyesha mapenzi ya dhati mpaka wewe mwenyewe unajionea wivu.



    Hamu ya kuishi pamoja huja na ndio maana unapoambiwa swala la kuishi nae au kuolewa nae hukubali haraka tena bila kufikiria mara mbili.



    Hayo na mengine mengi ndiyo yanayoendelea kutendeka katika mapenzi ya Jack na Eliza baada ya kutambulishana kila sehemu muhimu na kuamua kuvishana pete ya uchumba huku watu wengi wakihudhuria tukio hilo linalofanyika kwa mara ya pili katika maisha ya Jack.



    Benk ya CRDB haikumtenga kijana wao kwa kuhakikisha wanasheherekea na kuchangia vitu mbali mbali ikiwemo gari ndogo aina ya Starlet kwa mlengwa.



    Sherehe hiyo iliyoacha historia kwa kurushwa hadi kwenye kituo cha televisheni ya taifa TBC kwenye kipindi cha chereko.



    Harusi ilipangwa haraka ili yasije kutokea yale ya nyuma kwakua Jack alishang`atwa na nyuki hata akiguswa na jani, basi moyo wake hushtuka.



    Shela lililokua kabatini alimpimisha mke wake mtarajiwa, lilimkaa sana zaidi ya Aisha ambaye liliagiziwa kutoka uingereza kwa ajili ya harusi yao iliyoishia hewani na kuacha majonzi moyoni mwa Jack.



    Maaandalizi ya harusi yaliendelea huku Jack na Eliza wakiwa hawa ishi pamoja.

    Kila mtu alikua na hamu ya mwenzake. Simu hazikukauka licha ya kuonana kila siku japo mara moja.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zilibaki siku mbili kabla ya ndoa yao. Jack aliamua kuwa toa out mke wake mtarajiwa na mama mkwe wake pamoja na shemeji yake kwenda kuchagua vitu mbali mbali vya ziada baada ya kila kitu kinachohusu harusi kukamilika.



    Siku hiyo aliamka mapema sana na kupitia sheli ambapo aliweka mafuta full tank gari yake na safari ya kwenda kwa kina Eliza ilianza mara moja.

    Kabla hajafika. Alipitia super maket iliyokua karibu na kina Eliza na kununua mikate na bidhaa mbali mbali za Amercan garden ii mradi kuisindikiza asubuhi njema akiwa na familia yake hiyo mpya kabisa. Hakusahau mayai kwakua yeye ni mpenzi sana wa mayai.

    Baada ya shoping ndogo ya kiamsha kinywa, alirudi kwenye gari yake na kutekenya mafuta tayari kwa kuelekea kwa mke wake mtarajiwa ambapo sio mbali na hapo.



    Alifika na kupiga honi kistaarabu kabisa na kufunguliwa na shemeji yake mdogo kabisa mwenye umri wa miaka kumi.



    Aliingiza gari na kwenda kupaki pembeni kidogo na banda la kuku ambalo ndio ulikua mfugo mkubwa waliokuwa wanaufuga toka marehemu baba yake Eliza hajafariki.



    Aliingia ndani na kukaribishwa kwa bashasha na mama yake mkwe na kuingia ndani. Alitulia na kupokelewa mizigo hiyo na Eliza ambaye alikuja na kumpokea kwa mabusu kwanza kabla ya yote.



    Baada ya kuandaliwa mayai na chai, vilisogezwa mezani vitafunwa mbali mbali kwenye meza kuu na wote waliokua humo walianza kuvichangamkia vizuri vitu hivyo vilivyoifaya asubuhi hiyo iwe njema kabisa kwao.



    Baada ya hapo walitulia kwa masaa mawili ambayo yalipotezwa kwa stori na ucheshi wa Jack ambaye alishaizoea familia hiyo.



    Baada ya hapo. Walienda kujiandaa kwa zamu na kutoka wakiwa wamependeza kabisa tayari kwa mtoko huo uliodhaminiwa na Jack.



    Waliongozana na kuingia kwenye gari huku mama mkwe na mdoogo wake Eliza wakiwaachia siti za mbele wapendanao hao.



    Safari iligota njia ya kuelekea msasani na kupaki kwenye duka kubwa la nguo la Mariedo fashion na kungia ndani na kuwaruhusu kila mmoja achague nguo mbili ambazo zitampendeza.



    Baada ya zoezi hilo kukamilika, aliwatoa na kuwapeleka posta katika duka la viatu na kuchagua viatu kadhaa. Walipomaliza, muda wa chakula cha mchana ulifika na wakaingia katika moja ya mgahawa mkubwa huko posta na kupata chakula cha mchana.

    Baada ya hapo, walipitia maeneo ya kamata na kuingia supermarket kwa ajili ya kupata vitu vilivyopungua katika friji na kabati.



    Baada ya hapo, walipelekwa katika eneo tulivu ambalo lilikua likipuliza upepe halisi wa bahari. Walikaa watatu huku mdogo wake Eliza wakimuachia akijiunga na watoto wenzake waliokua hapo wakicheza michezo mbali mbali ikiwemo bembea na kuogelea pia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “nashukuru sana baba kwa kupoteza fedha na muda wako katika kuisimamia furaha yetu ya leo.” Alifunguka mama baada ya kukaa na kuanza kuyasiifia mazingira yao yaliyomvutia kila mtu.

    “usijali mama, ni majukumu yangu kukuhakikishia furaha kwa sababu kunipa mtoto wako tu inaonyesha ni jinsi gani ulivyo niamini na kuonyesha kunipenda. Maana kama ungekataa wewe hata yeye asingeweza kulazimisha kuwa nami hata kama atakua ananipenda kiasi gani” aliongea Jack huku anatabasamu na kumfanya Eliza ajiinamie na kutabasamu chini chini.



    “hakika nimeifurahia sana siku ya leo.. sijui hiyo siku ya ndoa ya mwanangu itakuwaje?” aliongea mama yake Eliza na kumtazama mtoto wake aliyekua anawasikiliza muda wote.





    Baada ya maongezi hayo yaliyoisogeza siku hiyo hadi saa mbili usiku. Jack aliwarudisha nyumbani kwao na y.eye akaenda kwake kujipumzisha.



    Usiku ulipokuwa mkubwa, alishtushwa na sauti ya mlango wake uliokuwa ukigongwa kwa nguvu na sauti ya mdogo wake ikasikika ikimuita. Aliamka na kwenda kufungua mlango huku akiwa amejawa na na usingizi kutokana na uchovu wa siku hiyo. Alipofungua mlango tu, alimuona mdogo wake akiwa na shemeji yake akiwa analia.

    “kuna nini kimetokea?” aliuliza Jack baada ya kumuona shemeji yake akiwa analia.

    “dada… dadaaa”



    Hakuweza kuimalizia kauli yake, zaidi Jack alirudi ndani na kuchukua shati lake haraka na safari ya kuelekea kwa kina Eliza ilianza mara moja ili akashuhudie kilichompata. Aliendesha gari kwa spidi huku akiwa hataki kusikia chochote kutoka kwa shemeji yake huyo na kutaka akashuhudie mwenyewe kwa macho yake hicho kitu kiichompata mpenzi wake usiku huo baada ya masaa machache tu kupita toka walipokua wote pamoja na familia yake.



    Alifika na kusimamisha gari nje ya geti na kushuka haraka huku mdogo wake na shemeji yake wakiwa nyuma wanamfuata. Vilio vilisikika katika nyumba hiyo huku sauti za ubembelezaji zikisikika kwa baadhi ya majirani waliokua hapo nyumbani.



    Alama za uoga na hofu zilimtoka Jack huku kengele ya hatari ikiendelea kutishia amani katika moyo wa Jack. Alizihesabu hatua zake taratibu kuelekea kule sauti hizo zilipokua zinatokea. Aliufungua mlango wa sebuleni na kukuta watu kadhaa wakimbembeleza mama yake Eliza aliyekua analia kwa uchungu. Mama huyo baada ya kuiona tu sura ya mkwe wake mtarajiwa, kilio kiliongezeka na kuamua kumuambia kilichotokea huku akionyesha machungu aliyokua nayo.

    “Eliza wangu baba… Eliza wangu amefariki jamaniiiii… eeh Mungu, mbona kila siku mimi ooooooh….harusi ya mwanangu jamaniii.. mwanangu amka angalau uolewe nikishuhudia ooooooh… Eli..Eliza mwananguuuu.”



    Alilia mama huyo kwa uchungu na kusababisha mpka Jack kuishiwa nguvu na kujikuta uvumilivu umemshinda na yeye akaanza kuangua kilio cha uchungu sana. Alijiona kuwa namkosi sana. Mapenzi yalikua yanamchukia na kila apendapo basi lazima yatokee majanga tena akiwa katika hatua za mwisho katika kutimiza sheria ya ndoa.



    Baadhi ya majirani wa kiume walimtuliza Jack. Alipotulia aliomba aelekezwe ilikuaje mpaka mpenzi wake akafariki dunia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walimwambia kua alipotoka tu safari usiku huo, basi alienda bandani kukagua kuku kwa sababu walikua wanapiga kelele. Alipokua anaangalia tatizo, kumbe alikua nyoka ambaye alikua juu ya banda hilo na kumgonga maeneo ya shingoni na kufariki papo hapo.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog