Search This Blog

Friday, July 15, 2022

PLASTIC TEARS - 2

 







    Simulizi : Plastic Tears

    Sehemu Ya Pili (2)





    Huko walikutana na wasichana wakiwa wanakaa pamoja na wanaume na kupiga story beneti.

    Kutokana na shule hiyo kuwa siyo ya ki dini kama shule waliyotoka, waliruhusiwa wasichana kusuka na kuweka style mbali mbali za nywele.



    Makusudi ya wasichana wengine waliokuwa wakizibana sketi zao na kuwaonyesha maumbo yao yalizidi kuonekana katika macho yao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mtawanyiko wa combination zao ziliwafanya wasome madarasa tofauti. Ufaulu wa Joackim ulimpeleka PCB na Maheer kwakua alikua mzuri sana katika somo la hisabati basi akapelekwa kombi ya PCM.



    Huko napo waliendelea kuwakimbiza watoto wa huko kila mtu katika darasa lake. Mbali na mitego ya wasichana wa hapo, lakini haikuwa sababu ya wao kunasa katika mitego hiyo. Zaidi walichukulia kama changamoto tu za maendeleo yao.



    Juhudi na maarifa waliyo naye yaliwafanya wafaulu elimu yao na kuchaguliwa katika chuo cha sayansi hapa Dar es salaam.



    Ilikua ni ajabu kwa wavulana wa hivi sasa kuvumilia mpaka kufika chuo bila kufanya mapenzi. Kutokana na misingi ya dini na maisha kwa ujumla, Maheer na Joakim waliweza na waliamini kuwa hivyo vitu vipo na watavikuta huko mbeleni.



    “samahani kaka, kama nakufananisha hivi?”



    Ilisikika sauti ya msichana mrembo aliyekua anawafuatilia wakina Maheer waliokuwa wanatembae katika mazingira ya hapo chuoni.

    Wote waligeuka kwa pamoja na kumtazama huyo dada aliyeongea kutokea nyuma yao. Walikuta na msichana mzuri wa kipemba aliyejitanda vizuri ushungi ulioongeza uzuri wa sura yake. Wote kwa pamoja wakajikuta wanatazamana na kila mmoja akajishuku labda ni yeye aliyefananishwa.



    “Maheer kama sikosei.”

    Aliongea yule dada na kumtupia macho yote Maheer na kumuhakikishia kuwa kweli alikua anamjua kwa kumtajia jina lake.



    “wala hujanifananisha.. ndio mimi.” Aliitikia Maheer huku akivuta taswira ni wapi alishawahi kuonana na binti huyo mzuri.



    “ naitwa AHLAM.”



    Alijitambulisha huyo dada mbele yao. Lakini Maheer bado sura yake ilionyesha kutokumbuka chochote juu ya jina hilo.



    “tulikutana kwenye supermarket kule Tsn maeneo ya upanga njia ya kuelekea muhimbili…. Tuligongana wakati tunachukua pamoja chupa ya Jam?” alielezea Ahlam huku akijaribu kumkumbusha Maheer ambaye mpaka wakati huo tayari Alisha mkumbuka.

    “ulikua na mtoto mdogo wa kike?... nimeshakumbuka,. Mambo.” Aliongea Maheer na kumpa mkono msichana huyo aliyekuwa na uzuri asilia.



    “safi.” Alijibu huyo msichana na kutabasamu.

    “ndio unaingia,.. au na wewe tunaondoka wote muda huu? .” aliendelea kuuliza Maheer.

    “hata mimi natoka muda huu.” Alijibu Ahlam

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walitoka pamoja mpaka kwenye parking ya magari ambapo Maheer na Joakim walipanda kwenye gari yao huku Ahlam akipanda kwenye Kigali chake kidogo cha aina ya starlet

    Kuanzia siku hiyo, urafiki kati ya Ahlam, Maheer na Joakim ukatengenezeka kwa pamoja. Kwakua wote walikua wanaingia muda mmoja chuoni, hawakusita kupitiana. Kuna wakati mwengine walikua wanatumia gari moja tu kwa wote watatu.



    Urafiki wao ulikua na kuwa kama sheria au kawaida yao. Ukimuona Ahlam basi haitopita hata dakika moja lazima utawaona Maheer na Joackim pale.



    Walimaliza masomo yao huku kila mmoja akiwa hajawahi kumuona mpenzi wa mwenzake.



    Hali hiyo ilikua utata hata kwao, maana waliamini kuwa kuna uwezekano jaopokuwa walikuwa pamoja muda mwingi, basi kila mmoja alikua na siri ya mpenzi wake moyoni.



    Siku moja Maheer alikua ana furaha kupita kiasi. Hali hiyo iliwashangaza sana rafiki zake hao. Walimuacha kwa dakika kadhaa. Alipokuwa sawa wakaamua kumuingia ili wajue ni kipi kilichomfurahisha.



    “tuambie ndugu, ni kitu gani kinachokufanya uwe na furaha kiasi hicho?” aliuliuliza Ahlam kwa shauku kubwa.



    “ I AM IN LOVE”



    Aliongea Maheer huku akiruka ruka kwa ulimbukeni wa mapenzi. Hajawahi kupenda hata siku moja. Sasa aliwadhihirishia rafiki zake kuwa alikua ana mahusiano na mtu Fulani.



    “wacha weee.. na nani basi?” aliuliza Joakim kwa furaha na kumuangalia Maheer ambaye muda huo meno yake yote yalikua nje.



    “nimepata msichana mzuri sana.. mfano wa uwa ridi lililokuwa peke yake katika bustani nzuri ya mapenzi lililokuwa linanisubiri mimi tu nije nilichume. Anaitwa Lailati, sidhani kama mnamfahamu.” Aliongea Maheer huku akiwa na furaha isiyokuwa na mfano.



    “duh.. hongera kaka.” Aliongea Ahlam huku akimshika katika bega na kumtuliza kwakua alikua anaruka ruka .



    Baada ya kukaa na kupeana pongezi nyingi, walirudi nyumbani kwao na kumpitisha Ahlam kwao na wao kuendelea na safari yao.



    Usiku ulikua ni kwa ajili ya kuongea tu na simu na kumpa karaha Joakim ambaye usingizi wake ulikua shida kupatikana kutokana na maongezi ya hao wapenzi yaliyodumu muda mrefu.



    Furaha hiyo ya Maheer iliyotawala ghafla kwa wiki mbili tatu ziliwatia maswali wazazi wake na kuamua kumuuliza ni kipi kilichomfanya awe vile.



    “mama, nimetokea kupenda na mtu ninaye mpenda ananipenda pia. Ni mzuri kama wewe mama yangu na isitoshe, pia ni mshika dini.” Aliongea Maheer alipoulizwa swali juu ya furaha yake na mama yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “vizuri…. Una malengo gani na yeye?” aliuliza mama yake huku akijitahidi kuingia na yeye kwenye furaha kama aliyokuwa nayo mwanae.



    “hakuna cha kusubiri mama,..ni kufuata hatua muhimu nichukue jiko jumla jumla.” Aliongea Maheer na kumuangalia mama yake ambaye wakati huo alikua makini kumsikiliza.



    “basi ni jambo la kheri.. inshaallah mungu atufikishe mpaka siku hiyo.” Aliongea mama yake Maheer hayo maneno kama ishara ya kutokua mpinzani katika jambo hilo la kheri.



    “amin.” Aliitikia Maheer hiyo dua.



    “haya na wewe mwanangu.. bado hujapata macho ya kuona?” aliongea mama yake Maheer kwa utani baada ya kumgeukia Joakim ambaye alikua sebuleni na yeye wote wakiangalia tv.



    “inshaallah Mungu atanionyesha na mimi mke wa kuoa… ila kwa sasa bado sijafanikiwa kupata macho kama ya Maheer hapa.” Aliongea Joakim na kufanya wote pale wacheke.



    Siku ya pili yake jioni, Maheer alipigiwa simu na mpenzi wake ambaye alikua na hamu sana ya kumuona siku hiyo.



    “nitakuja na shemeji yako basi umuone.” Aliongea Maheer akimpa taarifa mpenzi wake kua wataenda wawili.



    “sawa.. hamna shida mume wangu mtarajiwa.” Aliongea Lailati kwa sauti laini ya mahaba iliyomfanya Maheer ajisikie raha kuitwa mume mtarajiwa.



    Twende rafiki yangu,.. mida ndio hii.” Aliongea Maheer na Jockim hakusita, aliingia kwenye gari na safari ya kuelekea kwa Lailati ilianza.



    Njiani Maheer hakusita kumwagia sifa rafiki yake huyo anayemuhesabu kama ndugu yake wa damu juu ya uzuri wa mpenzi wake.

    Walifika kwenye nyumba mioja kubwa yenye uzio wa kisasa. Walisimamisha gari na kumpigia simu Lailati.



    “tumishafika my lovely.” Aliongea Maheer.

    “nishawaona .. nakuja my Buu buu.” Aliongea Lailati na kutoka nje baada ya dakika moja. Aliungana nao na wote wakaingia kwenye gari na kuelekea kwenye café moja matata maeneo ya ilala.



    “huyu ni ndugu yangu kabisa, anaitwa Joakim.” Alitambulisha Maheer .

    “sasa mbona ana jina la kikiristo?” aliuliza Lailati kwa mshangao kidogo.



    “usijali kuhusu jina.. utakapoendelea kuingia katika familia yetu…. Utanijua zaidi.” Aliongea Joakim na kumtazama shemeji yake huyo na kuachia tabasamu pana.



    “na huyu ndio mke wetu… anaitwa Lailati.” Aliongea Maheer katika kukamilisha utambulisho wake .



    Walikula na kupiga story mbili tatu huku kila mmoja akipata nafasi ya kumzoea mwenzake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Waliporidhika, walimrudisha Lailati kwao na wao wakarudi nyumbani kwao.

    “unamuonaje shemeji yako.” Aliuliza Maheer walipojitupa kitandani baada ya kuoga.



    “yuko poa sana… ana haki ya kukutia uchizi huu uliokuwa nao.” Aliongea Joakim haku anacheka

    “umeona eeh.” Aliongea Maheer na kucheka.



    Wakati wakiendelea kupiga story, simu ya Maheer ikaita.



    “niambie wangu.” Aliongea Maheer baada ya kugundua kuwa apigaye alikua Ahlam.

    “safi tu… niambie.” Ilisikika sauti lakini ilikua na utofauti katika masikio ya Maheer. Aliijua vizuri sauti ya Ahlam.



    “sorry… naongea na nani?” aliongea Maheer na kuwa makini kuisikiliza ile sauti.



    “mi Ahlam jamani.. leo haunijui, au ume delete number?” aliongea huyo mtu na kujitambulisha jina la Ahlam.



    “we sio Ahlam.. sauti ya Ahlam naijua.”



    Alipoongea tu maneno hayo, simu yake ikakatika. Hakuridhika Maheer, aliamua kungalia mtu aliyempigia. Aliliona jina la Ahlam. Alipopiga tena alikutana na ujumbe wa kutopatikana kwa simu hiyo aliyokuwa anaongea nayo sekunde kadhaa zilizopita.



    Alijaribu mara kadhaa, ila bado ujumbe huo ulijirudia kila alipojaribu kupiga. Aliachana na hiyo simu na kuamua kulala.

    Asubuhi alimpigia simu tena Ahlam. Safari hii siku yake ilipatikana.

    “niambie mine.” Aliongea Ahlam kwa sauti iliyojaa bashasha.

    “safi tu… niambie.” Aliongea Maheer huku akiwa amestaajabu kidogo kwakua aliamini kuwa kama ni kweli aliyepiga simu alikua ni yeye basi ni lazima angemuelezea kitu kilichomfanya apige simu mida ile huku akiwa amebaadilisha sauti.



    “sana usemi.. sijui wewe.” Aliongea Ahlam na kumfanya Maheer atabasamu huku akili yake ikiendelea kulikumbuka tukio la jana yake.

    “jana si ulinipigia simu?” aliuliza Maheer.

    “jana?... juzi bwana ndio tumewaliliana na wewe!.” Aliongea Ahlam huku akiwa hana wasi wasi kabisa.



    “jana usiku kuna mtu alikua anatumia simu yako?” aliuliza Maheer.

    “ndio…. ASPHAA huyo ndio mara nyigi huwa namuachia simu yangu… kwani vipi?” alielizea Ahlam na baadae kumalizia sentensi yake na swali.



    “hakuana tatizo… ila sauti tu ndio niliishangaa sana kwakua lilikua tofauti na wewe.” Aliongea Maheer na kupata uhakika kuwa Ahlam alikua na mdogo wake wanaishi wote kwa sasa.



    “amerudi kutoka huko Kenya?” aliuliza Maheer baada ya kulisikia hilo jina ambalo halikua jipya masikioni mwake kutamkwa na Ahlam.



    “ana wiki tatu now….. ila alikua si mkazi sana wa hapa home kutokana na kutembelea baadhi ya ndugu mbali mbali aliowakumbuka kipindi chote alichokuwa Kenya.” Aliongea Ahlam na kutabasamu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “poa, nilikua nakusalimia tu.” Aliongea Maheer baada ya kuona amepata majibu ya kutosha aliyolala na mawali yake toka usiku wa kuamkia siku hiyo.



    Walipata kifungua kinywa mapema na wakiwa wawili kama wapendavyo toka walipokuwa utotoni. Baada ya kumaliza kunywa chai. Walipasha kwa michezo kadhaa ya game waliyokuwa wanapenda kucheza.



    baada kupotea kwa masaa kadhaa, waliacha kucheza game. Walipanga safari na kutoka kwenda kwenye salon moja ya kiume iliyokuwa kati kati ya jiji na kunyolewa kwenye salon hiyo waliyokuwa wanapenda sana kunyoa hapo.



    Mlio wa sms ulilia pindi tu maheer alipomaliza kunyoa. Aliona namba ngeni. Aliifungua ila sms akaona huyo mtu alikua akimtakia asubuhi njema.

    Akaijibu hiyo sms na kuondoka zao pale saloon.



    Mchana wa siku hiyo, sms nyingine kupitia namba hiyo hiyo ilimtumia sms iliyomkaribisha kupata chakula cha mchana.



    Hiyo sms hakuijibu. Ila ilipofika usiku sms ya usiku mwema ilimshawishi Maheer kumpigia simu huyo mtu ili amjue ni nani.



    “haloo.”

    Sauti nzuri ya binti ilisikika masikioni mwa Maheer.



    “assalaam aliykum.” Alisalimia Maheer.

    “waaleykum salaam.” Aliitikia huyo binti hiyo salamu na kutulia kama alikua anataka kusikia kitu kilichomfanya Maheer kumpigia simu.

    “nani mwenzangu.” Aliuliza Maheer kistaarabu.



    “naitwa Asphaa”



    Alijibu huyo dada na kumfanya Maheer kubaki kimya kwa sekunde kadhaa. Hakujua kwanini mdogo wake Ahlam alichukua namba yake na kumtafuta.



    “mdogo wake Ahlam kama sikosei?” aliuliza Maheer ili kuhakikisha kama mtu anaye muhisi ndie yule aliyepiga simu.



    “ndio mimi Maheer.” Aliongea huyo dada kwa sauti Fulani hivi iliyokuwa na swaga za kipekee kama ya Diva wa kipindi cha ala za roho.



    “okey… tel me.” Aliongea Maheer huku akijisikilizia kutokana na kutokua na maamuzi sahihi juu kile kilichomtokea kwa muda huo.



    “nakutakia usiku mwema . ulale salama na mungu akipenda kesho uamke salama Maheer.” Aliongea Asphaa huku akionyesha wazi kua alikua anatabasamu kama sio kucheka kabisa kutokana na ishara ya sauti yake.



    “ na wewe pia… nakutakia njozi njema.” Aliongea Maheer na kukata simu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alimgeukia Joakim ambaye muda wote alikua kimya akiyasikiliza maongezi hayo.

    “kaka…si mtihani huu?.” Aliongea Maheer baada ya kumuona Joakim akiwa yupo tayari kusikia kitu alichotaka kumuuliza.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog