Search This Blog

Friday, July 15, 2022

PLASTIC TEARS - 1

 





    IMEANDIKWA NA : HUSSEIN O. MOLITO



    *********************************************************************************



    Simulizi : Plastic Tears

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gari aina ya pajero inaonekana ikiwa katika mwendo wa kasi usiku wa manane ikielekea katika hospitali ya ocean road. Ndani yake kukiwa na mwanaume ambaye ndio dereva na nyuma ya gari kulikua na mwanamke aliyelala huku akilalamika kwa uchungu sana.



    “usijali mke wangu, vumilia tu.”



    Alisikika mwanaume huyo akimuambia mke wake ambaye hakumsikiliza zaidi ya kulia kwa sauti huku akiendelea kuugulia maumivu.

    Walifika hospitalini hapo na kupokelewa wahudumu waliokuwa nje na kumuweka mgonjwa kwenye kitanda na kwenda naye katika chumba maalum.



    Yule mwanaume alitakiwa abaki nje, na kweli akatii na kumuomba mungu amjaalie mke wake aweze kupona na kutoka salama.



    Saa limoja baadae, mlango ukafunguliwa na dokta aliyekuwa ndani akatoka.

    “vipi hali ya mke wangu dokta?” aliuliza yule mwanaume baada ya kunyanyuka na kumvamia dakitari.

    “hongera, mke wako amejifungua salama mtoto wa kiume.”



    Yale maneno yalimfanya awe kama kichaa kwa jinsi alivyofurahi na kurukaruka . alimshukuru dakitari.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baadae aliruhusiwa kwenda kumuona mke wake. Alipofika alimuona mke wake akiwa ametabasamu na kitoto chao kichanga kabisa kikiwa pembeni yake.



    “ahsante mke wangu.”



    Aliongea kwa furaha na kwenda kumkumbutia mke wake pale kitandani.



    Ni zaidi ya furaha baada ya kuzaliwa mtoto huyo katika familia huiyo yenye uwezo kidogo kifedha. Wazazi wa mtoto huyo ambao wote wanafanya kazi katika shirika la ndege la Fastjet.



    Wazazi na ndugu wa karibu walipigiwa simu usiku ule ule na kupewa taarifa hizo zilizowaacha katika furaha.

    Asubuhi mishale ya saa nne, waliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya ukaguzi na vipimo vyote kukanilika.



    Mtoto huyo aliyewabadilisha majina watu hao badala ya kuitana kwa majina waliyopewa na wazazi wao, sasa hivi kila mtu alimuita mwenzake kwa jilna la mtoto wao huyo waliyempa jina la MAHEER.



    Mtoto huyo aliyekuwa na thamani zaidi ya lulu katika nyumba hiyo alianza ukuaji wake taratibu kabla ya kufikisha miaka mitatu ambapo wazazi wake walimpeleka chekechea katika shule ya Yemen High School.



    Mapenzi juu ya mtoto wao yaliwazidi sana kiasi cha kuajiri wafanya kazi wapatao watatu kwa ajili ya usaidizi wa malezi ya mtoto wao huyo.



    Maheer alipotimiza miaka sita, alihama katika shule ya awali na kuhamia shule ya msingi hapo hapo Yemen.



    Siku moja timu ya shule yao ilienda kushindana na timu ya shule ya msingi kawawa iliyopo luhanga.

    Maheer hakuwa mchezaji, ila alikuwa mshabiki mkubwa wa mpira. Hivyo alienda kuishangilia timu yake huko.



    Gari ya shule yao iliwasili kiwanjani hapo na kuwaacha watoto wa geti kali kuyashangaa mazingira ya uswazi kuazia kigogo mpaka luhanga ambapo shule hiyo ipo.



    Mechi kali ilianza kati ya shule hizo mbili huku zikikamiana sana. Kwa bahati mbaya mchezaji wa timu ya shule ya kawawa aliumia vibaya sana na kupelekwa hospitalini.



    Mechi iliendelea na timu ya shule ya Yemen wakaibuka na ushindi wa magoli matatu kwa mawili.

    Baada ya mechi walielikea hospitali kwenda kumuangali huyo mtoto aliyevunjika kwenye mechi hiyo.

    Walikuta ameshahudumiwa na mguuni alifungwa ogo. Walimpa pole na wengine wakampa fedha. Mtoto aliyemchezea rafu alijitokea na kumuopmba msamaha.

    “usijali, ni sehemu tu ya mchezo.” Alijibu yule mtoto aliyeumia na kuwafanya watu wafurahi kwa maneno yake yaliyoonyesha kuwa hakumuwekea kinyongo mwenzake.



    Maheer alirudi yumbani na kuwaelezea wazazi wake kilichotokea. Wazazi wake walisikitika sana na kumuahidi kuwa wataenda kumuona huyo mtoto hospitalini hapo.



    Siku ya jumamosi, Maheer aliwapeleka wazazi wake kwa mtoto huyo. Walimuona na kumpa zawadi walizomletea. Baada ya hapo walimuaga na kumuahidi kuwa watakuja kumuona tena.

    “samahani jamani, nyie ni ndugu wa huyu mtoto.” Aliuliza nesi mmoja ambaye alikua anawaangalia wagonjwa wa pale.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “hapana.. kwani kuna tatizo?” alijibu mama yake Maheer kwa mshangao kidogo.

    “jamani watu wana roho mbaya sana. Unajua huyu mtoto naweza sema amekuja kutupwa hapa hospitali. Yaani hakuna ndugu wala mzazi aliyekuja hapa kumletea chakula wala kitu chochote. Yaani nawatamani sana ndugu zake hapa waje niwape vidonge vyaoo. Mtoto mzuri kama huyu kumtelekeza maeneo haya?” aliongea yule nesi kwa uchungu sana.

    “mh?,,, sisi tumekuja kumtembelea huyu mtoto kwakua wakati anaumia mchezoni mwanangu alimuona. Alivyotuhadithia tukajikuta tumeguswa na ndio maana tumefunga safari kuja kumuangalia.” Aliongea mama yake Maheer kwa masikitiko .

    “basi ndio hivyo.” Aliongea nesi na kuwasikiliza msimamo wao juu ya kulitatua lile tatizo.

    “mi naona jukumu hilo tulibebe sisi, tutamuhudumia kwa gharama zetu mpaka atakapopona kabisa…. Au sio mke wangu.” Aliongea baba yake Maheer ambaye alikua kimya wakati wote.

    “ni wazo zuri mume wangu.”



    Aliitikia mama yake Maheer na kumfanya nesi atabasamu. Hata alipomuangalia mtoto wake pia alionyesha kulifurahia tukio hilo.



    Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kuanza kuhudumiwa na kula mapochopocho ambayo mtoto wa uswazi huyo hakuwahi kula hapo kabla. Baada ya kupona na kuruhusiwa kurudi nyumbani, walimpeleka mpaka kwao anapoishi. Walikumkuta mlevi mmoja ambaye alikua amejikojolea huku akiwa amelelala hajitambui kabisa.



    “huyu ni nani?” aliuliza mama yake Maheer.

    “ni mjomba wangu.” Alijibu yule mtoto aliyejitambulisha kwao jina la JOAKIM.

    “Ndio unaishi naye?” aliuliza mama yake Maheer huku akionyesha wazi kumshangaa huyo mjomba wake Joakim alivyo.



    “ndio, ila naweza kusema naishi peke yangu kutokana na kuwa sioni faida yake. Zaidi ya yeye kuwa ananichukulia hela zangu za mtaji wa karanga.” Aliongea mtoto huyo na kuwafanya wakina Maheer kushangaa.



    “kwa hiyo wewe unasoma huku unafanya biashara?” aliuliza Maheer kwa mshangao.



    “nisipofanya biashara nitakula nini??.. huyo mlezi wangu mwenyewe mnamuona. Kila siku yeye yuko pombe tu. Na akiamka hapa lazima atawaletea fujo.” Aliongea Joakim na kuwafanya wakina Maheer kupatwa na uoga.



    “acha si twende. Maadamu tumeshapajua hapa, tutakuwa tunakuja kukuachia chochote.” Aliongea Mama yake maheer na kuchukua pochi yake na kutoa kiasi kidogo cha fedha na kumkabidhi Joakim.



    Siku zilienda taratibu sana kwa Maheer baada ya kupita wiki moja bila ya kumuona rafiki yake huyo mpya aliyetokea kumpenda kutoka moyoni na alitamani kuwa miongoni kati ya watakaomuweka Joakim katika hali ya furaha.



    Baada ya wiki mbili kupita, maheer aliwaambia wazazi wake wamchukue Joakim na ikiwezekana waishi nae pale kwakua alikutana nae alipoenda shuleni kwao na kugundua kuwa anapata mateso makubwa kutoka kwa mjomba wake.



    Kutokana na kumpenda sana mtoto wao, walimsikiliza na siku ya pili yake waliamua kwenda kwa kina Joakim ili waangalie wanaweza kumsaidia vipi.



    Walipofika walikuta nyumba imepigwa kufuli na hakukuwa na dalili yoyote ya kuwepo kwa mtu yeyote pale.



    Baada ya kuulizia kwa majirani, walipata majibu yaliyowatia uchungu. Waliambiwa kuwa Joakim yupo hospitalini tena baada ya kupigwa na mjomba wake na kuumia vibaya usiku wa kuamkia jana yake



    Walisikitika sana na walipoelekezwa hospirtali aliyopelekwa, walipanda kwenye gari yao na safari ya kuelekea hospitalini ilianza.

    “watu wengine sio watu kabisa, yaani anadiriki kumpiga mtoto wa dada yake kipigo cha mbwa mwizi?” aliongea baba yake Maheer walipokuwa njiani wakielekea hospitali ya magomeni.



    “yaani roho inavyoniuma!!... ningemkuta huyo mjomba wake pale lazima ningemuitia polisi.” Aliongea mama yake Maheer huku akionyesha dhahiri hasira alizokuwa nazo juu ya mjomba wake Joackim.

    “yaani mimi ningemtwanga kwanza na yeye kabla hao mapolisi hawajafika.” Aliongea baba yake Maheer.



    Wakati safari ya kuelekea magomeni usalama ambapo hiyo hospitali ipo, muda wote huo Maheer alikuwa kimya nyuma ya kiti akijaribu kutathmini uzito wa mateso aliyoyapata rafiki yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dakika ishirini baadae, giri lili wasili hospitalini hapo na kwenda kwenye mabenchi kwa ajili ya kusubiri muda wa kuwaona wagonjwa.



    Muda ulipofika, waliingia wodi waliyoelekezwa na kuanza kumtafuta Joackim. Walimkuta kalala chini kwakua alikosa kitanda. Roho ilizidi kuwauma wazazi wa maheer kwa jinsi hali ilivyokuwa inatisha katika wodi ile iliyojaa walala hoi.



    Walimuona akiwa na bandeji kadhaa kichwani na mkononi akiwa amefungwa P.O,P.

    Walimuonea huruma sana, ukilinganisha na roho nyepesi aliyokuwa nayo mama yake Maheer, machozi yalianza kumbubujika baada ya kumuona mtoto huyo mdogo kabisa aliyekuwa anapata mateso makubwa kushinda umri wake.



    Baba yake Maheer hakuridhika kabisa na huduma za pale, alienda kwa daktari na kuomba uhamisho wa mgonjwa huyo na kumpeleka katika hospitali ambayo aliikatia bima familia yake.



    Walikabidhiwa mgonjwa wao na karatasi za uhamisho.

    Walifika kwenye hospitali hiyo iliyokuwa pembezoni kabisa na bahari ya hindi. Naizungumzia Ocean Road.



    Alipokelewa haraka na kupewa kitanda kwa ajili ya vipimo mbali mbali.

    Walishauriwa wamuache mpaka kesho yake.



    Walimsubiri Maheer arudi kutoka shuleni kama walivyomuahidi na wote wakaenda kumuona Joakim hospitali.



    “unaendeleaje Joakim?” aliongea Maheer baada ya kuruhusiwa kuingia ndani kumuona mgonjwa wao.

    “naendelea vizuri tu.” Aliitikia Joakim huku akiyahangaisha macho yake kuangalia watu waliokuwa pale wakati ule.



    “pole sana rafiki yangu.” Aliongea Maheer na kumshika mkono wa kushoto ambao haukuwa na ogo.



    “nakushukuru sana, nawashukuru pia wazazi wako kwa kunijali….”



    Aliongea maneno hayo na kabla hajaendelea, mara alianza kulia kwa kwiwi. Ilikuwa kama vile maumivu alianza kuyasikia wakati ule. Aliwaangalia wazazi wa Maheer na kumshika mkono mama yake Maheer.



    “ sina mama mie,… naomba nichukue, nifanye kuwa mwanao mama. Nateseka mimi…..nichukue mama na mimi niwe na furaha kama Maheer.”



    Aliongea Joakim huku analia akiwa ameukumbatia ule mkono wa mama yake Maheer kwa mikono yake miwili bila kujali kama bado alikuwa kwenye maumivu.



    Kilio hicho kiliwashinda uvumilivu, wote walionekana kulengwa lengwa na machozi, lakini mama yake Maheer yeye alilia kabisa. Tena alijikuta analia kwa sauti kubwa kuliko Joakim na kumkumbatia pale kitandani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “kuanzia leo wewe ni mwanangu… niite mama nitaitika Joakim.” Aliongea Mama yake Maheer huku akiendelea kulia. Sauti ya kilio cha huzuni kiliwafanya Maheer na baba yake kudondosha machozi bila kutoa sauti.



    Kilio hicho chenye machungu ya mateso aliyoyapata Joakim kilidhihirisha kuwa ni wazi watoto waishio maisha magumu ni wale ambao hawana wazazi na walioachiwa ni watu ambao hawana uchungu nao.



    Walirudi nyumbani na kuendelea kumuhudummia mtoto huyo kama mtoto wao wa kumzaa kabisa.

    Baada ya wiki mbili, aliruhusiwa kurudi nyumbani na kuendelea na matibabu mengine akiwa huko.



    Maheer alifurahi kumpata mtoto mwenzake anayeendana nae kuimri. Walikula pamoja na kulala pamoja.



    Zoezi la uhamisho wa shule lilianza mara moja na kufanikiwa kwa muda mfupi. Baba yake Maheer aliamua kumuhamishia Joakim katika shule yaYemen high school ambapo mwanae anasoma hapo.



    Heshima,utii na uelewa wa haraka ulizidi kumpa maksi mtoto Joakim mbele ya wazazi wa Maheer.



    Familia hiyo iliona matunda ya Joakim kua pale, kwani walimuona mtoto wao akiwa amechangamka na kuwa mjanja kidogo. Pia walipenda tabia ya Joakim ambaye muda wote alikua anamuhusia mwenzake juu ya kuacha michezo na kusoma.



    Kila kitu alicholetewa Maheer, basi na Joakim alikipata au kama kilikua kitu kimoja. Hawakuweka matabaka. Waliwaambia kuwa hiki kitu ni cha kwenu wote.



    Maisha hayo mazuri na ya amani yalimfanya Joakim kunawiri na kuwa mzuri sana. Mavazi mazuri waliyokuwa wananunuliwa yaliwafanya waonekane watoto smart na wenye wazazi wenye kipato cha hali ya juu.



    Siku zilisogea na hatimaye walimaliza elimu yao ya msingi.

    Matokeo yaliyotoka yaliwaruhusu kuendelea na shule. Baba yake maheer akawaandalia wote wawili zawadi kubwa ya laptop kila mmoja wao.



    Watoto hao waliokuwa wanapendana na kufuatana kama mapacha wan je, waliendelea na elimu yao ya sekondari hapo hapo yemen ingawaje walichaguliwa shule tofauti.



    Matokeo mazuri ya Joakim yalitokana na juhudi binafsi aliyokuwa nayo muda mrefu. Hata Maheer nae hakuwa mzembe kutokana na competition aliyokuwa nayo pale nyumbani.



    Waliwakimbiza wenzao kwa kushika nafasi mbili za juu. Yaani kama Maheer akiwa wa kwanza basi Joakim huwa wapili. Na kama Joakim akiwa wa kwanza basi Maheer huwa wapili tena wakiwa wamepishana wastani mdogo tu.



    Wazazi wa Maheer walijisifia na kujivunia watotohao ambao kwa pamoja walitengeneza familia iliyookuwa na furaha kwa muda mrefu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walifanikiwa kuhitimu kidato cha nne bila yoyote kumjua msichana kutokana na sheria kali za hiyo shule iliyokuwa inawatenganisha wasichana madarasa yao na wavulana madarasa yao.



    Hali hiyo iliwafanya kuwa bize na kitu kimoja tu. Nacho ni elimu.

    Walifaulu vizuri sana na kuamua kubadilisha mazingira na kuhamia shule ya S.t Marry iliyopo mbezi beach.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog