Simulizi : Kisasi Ndani Ya Nafsi Yangu
Sehemu Ya Nne (4)
Ikiwa yafikia saa nne za Asubuhi Anko akiwa ndio anaamka nilimsaidia kumpeleka msalani na kumwogesha kisha kumrudisha ndani na kumvisha nguo, nami nikavaa zangu kisha nikamshika mkono na kutoka.Nilipofika sebleni nikamkutana Asha na Fred wakiwa wamekaa sofani,nikamuweka Anko kwenye kiti nami nikakaa kando yake, usoni nikiwa na tabasamu bandia na kuwasalimia Asha aliitika na kunitaka niwe na amani,nami nikamuitikia kwa kutikisa kichwa kuashiria nimemuelewa.Tukajumuika pamoja na kuandaa kifungua kinywa,mpaka ikawa tayari na kukaa pamoja mezani kwa ajili ya kifungua kinywa,kabda hatujaanza kunywa chai niliwaomba nimchukue Anko Mashaka kwa ajiri ya kupata chai pamoja.Musa alikubali niliinuka na kwenda kumsaidia kunyanyuka, kisha kwenda moja kwa moja mpaka mezani nilimkalisha Kitini nami nikakaa, ghafla Asha aliinuka na kuanza kuniambia.
“Hee! Umetuletea zezeta humu ndani?,
“Hapana dada, Anko Mashaka ana matatizo ya kupooza mwili na sio chizi kama unavyomuona”,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndio chizi sasa, angalia anavyotoka miudenda Kama konokono”Asha alisema,
“Usiseme hivyo Asha kumbuka matatizo kwa mwanadamu tumeumbiwa”Nilimwambia.
“Hapana kwa hali hii ndio maana mkewe kamfukuza “
“Nakuomba umuonee huruma Anko”nilimwambia machozi yakinitoka
“Lazima huondoke hapa sikutaki kabisa na hicho kikalagosi”Alisema bila kutania,
“Okey poa Kama umeamua kunifukuza sawa”nilimjibu Asha pasipo chembe ya masihara
Nilimuona Musa akiwa na majonzi dhidi yangu, alinionea hutuma ingawa sikufahamu sababu iliyomfanya kunyamaza kimya bila kusema chochote, moja kwa moja nikajua nae hakupenda Anko Mashaka kuishi katika nyumba yao, walinitaka mimi na sio Anko nami sikuwa tayari kumuacha akiteketea. Nipo radhi kuteseka kwa ajiri yake.Nikiwa natafakari namna ya kuondoka ghafla Musa akiwa mwenye huzuni aliamua kupingana na dadaye kuhusu jambo hilo,
“Sikiliza dada, nakuomba tumsaidie Fred”Musa alisema,
“Sawa ila tutamsaidia yeye na sio kutuletea mazombi humu ndani”Asha alijibu,
“Huyu ni binadamu kama sisi,yupo hivi kutokana na matatizo yaliyomkuta, hivyo basi anaitaji msaada lazima tumsaidie”,
“Sawa kama wewe upo tayari, kuvalisha, kumfulia na kumpikia huyu chizi”Asha alisema kwa kejeli
“Huduma zote atazifanya mwenyewe, anachoitaji Fred kutoka kwetu makazi tu ndugu yangu” Musa alimwambia ndugu yake.
Wakati wote Musa na dadaye wanagombana juu ya suala la ugonjwa wa Anko Mashaka, Nilikuwa nalia sana, Sikuweza kuelewa kwanini wanamnyanyapaa Anko Mashaka, kwa kweli nilikuwa na maumivu ya moyo yasiyoelezeka nikamuona Musa akisogea karibu yangu na kunibembeleza akinitaka ninyamaze.Kiukweli kauli ya dada yake ilinichanganya sana kumsimanga Anko Mashaka niliona dhahili hakustaili kufanya kitendo kama hicho hata kidogo.Nilibaki nimejiinamia huku machozi yakinitoka, nikapaza sauti yangu na kumwambia....
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
”Rafiki yangu nimekukosea nini dada yako?
“Fred usiwe na wasi wasi mimi ndio niliyekupokea hapa na nitakusaidia sawa”musa alinimbia,
“Lakini nitaishi vipi hapa, wakati dada yako ananichukia kutokana na hali ya Anko Mashaka, nilimwambia
“Usijali nitalimaliza swala hili na kutakuwa sawa”musa aliongea kwa kujiamini,
“Sawa nashukuru Sana”nilimshukuru musa,
“Usijali.
Wakati naongea na Musa,Anko Mashaka alikuwa amekaa pembeni, muda huo akili yake imetulia anasikiliza, alielewa kila kitu ila hakuwa na uwezo wa kuongea,nilipomchunguza vizuri nikamuona Anko Mashaka akiwa amejiinamia chini,Macho yake yakiwa mekundu, ametoka kulia muda mrefu.Musa alimsogelea karibu na kumtaka ahache kulia na kumtaka anywe chai.Nilimuona Anko Mashaka akibadilika ghafla alikuwa kama mtu ambaye haelewi kinachoendelea,alichukua na kikombe cha chai na kuingiza mdomoni, alikula kwa pupa na fujo,Asha aliamua kunawa na kuondoka zake ,alituacha tukiendelea kunywa chai mpaka tulipomaliza niliondoa vyombo mezani kisha tuliendelea kuongea mambo mbalimbali.Anko Mashaka alikuwa kama mtoto kwa vitu alivyokuwa anavifanya alianza kuchekacheka ovyo,akawa anatupa mito ya kiti na vitu mbalimbali mara kachezea television kaacha ambapo nilikwenda karibu yake na kumtuliza lakini haikuwezekana badala yake akaanza kunipiga mabao cha shavu. Musa alipoona hivyo alisogea kisha tukambeba na kumpeleke chumbani na kumtaka atulie, Anko alikubali kutulia nasi tukatoka nje na kumuacha akipumzika, Muda si muda Asha alitoka na kumuaga anakwenda Sokoni, Musa alimkubalia na kumtakia safari njema.
Baada ya nusu saa kupita Asha alirudi na kumtataka Musa waandae chakula cha mchana. Nikiwa pamoja na Musa tuliandaa chakula cha mchana, tulipomaliza tulikiweka mezani kikiwa tayari kwa kuliwa. kama kawaida yangu nilikwenda kumfuata Anko kwa ajili ya chakula na kumleta mezani.Tulipoanza kula tunastaajabu kumuona mwenzetu kachukua tonge la ugali na kujipaka usoni,gafla Asha alitoka na kuondoka kutuacha tukiwa tumebakia mimi,Musa na Anko Mashaka hatukumjali tuliendelea kula mpaka tukamaliza.Nilimpeleka Anko ndani kisha nikarudi kuendelea na kazi nyingine.
*******
Ilikuwa siku ya ijumaa Asha akiwa nje ya nyumba yao,alikuwa anaonekana kuwa ni mtu wa mawazo mengi.nikiwa nafanya usafi nje yeye hakuniona sehemu nilipokuwa nimejificha namuangali.Kisha kama mtu aliyetaka kufanya jambo alichukua hand bagi yake na kutoa simu na kubonyeza tarakimu kadhaa na simu ya upande wa pili ikatoa maelezo badala ya kuita!”Simu unayopiga haipatikani kwa sasa tafadhali jaribu tena baadae.”Nikamuona Asha akikata simu na
Kubonyeza namba zingine na simu upande wa pili ikaanza kuita.
“Hallow Namsoke!”Asha alisikika
“Shoga vipi mbona simu saa hizi, kwema uko?”
“Dah! Poa Sana, Leo nipo nyumbani njoo kama hutojali.kwani nina jambo lililonifanya nikupigie simu muda huu”Asha alimwambia mtu wa upande wa pili
“Mmh! sitaweza kuja shoga, ninasafari ya kwenda kyela leo si unajua yale mambo yetu shoga niambie tu kwenye simu nitakuelewa!”Namsoke alimwambia
“Sawa, kutokana na kero ninayoipata kutoka kwa mjombaye Fred,
“Hee! Nambie umechukua maamuzi gani shoga?”Namsoke alisikika,
“Nimefikiria na kupata wazo juu ya suala hilo”Asha alisema kwa mkato kisha akaangaza kushoto na kulia ili kuangalia kama kuna mtu aliyeshughulika nae, akaona hakuna mtu maeneo yale.
“Naam! Wazo gani?”Simu upande wa pili ilisikika akihoji
“Nakuomba usimwambie mtu nataka kumuua mjombaye Fred”asha aliongea
“Hee! Kwanini shoga unataka kufanya hivyo hujui Kama hiyo ni kesi”Namsoke alimshauri Shoga yake Asha.
“ Naona kama nikimuua matatizo yote yataisha,bora nifanye hivyo mwenyewe na sijamwambia mtu yeyote hata Kaka yangu Musa pia hajui,tena nitamuua wakati Musa na Fred hawapo itakuwa siri yangu mimi na wewe”
“Hapana shoga Mimi sitaki kabisa unishirikishe katika mauaji hayo sawa!”Namsoke alimwambia kisha akakata simu.
Nilimuona Asha akiweweseka pale nje kisha kuiweka simu yake kwenye mkoba wake, aliangaza huku na kule kisha akaingi ndani. Habari za Asha kusema kwamba anataka kumuua Anko Mashaka zilinipa wakati mgumu Sana. Nilizongwa na majonzi,nimechoshwa na maisha yale,siku zimekuwa nyingi sisi tupo pale pale,sikujua maisha yetu huku yaendako kuna masaibu gani.Habari ninazozisikia kwa Asha zilinizidishia unyonge.Lakini moyoni nilikuwa na msimamo mmoja tu lazima nijikaze kiume.Wakati huo bado nimeegemea mlango nawaza,niko mbali sana kimawazo ninamfikiria Anko Mashaka,jinsi anavyoteseka.Shangazi ametufukuza kutoka katika nyumba yetu.Tena tumefukuzwa kwa fedheha ,tukatupiwa nguo nje,majirani wote wapo madirishani.hakuna aliyethubutu hata kutusaidia,nilitamani niende tena kuishi katika nyumba yetu lakini haikuwezekana,tayari shangazi ameshauza nyumba............
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikurupuka ghafla niliposikia sauti ya Asha akinitaka niingie ndani kwa ajiri ya chakula.
Nilijifuta machozi yaliyokuwa yamelowanisha uso wangu na kuingia ndani kuitikia wito wake.Nilikwenda moja kwa moja mpaka chumbani na kumchukua Anko kujumuika nao. Kama kawaida tulikula pamoja kwa amani bila Anko kusumbua,tulipomaliza kula Asha aliaga kuwa anakwenda kwenye matembezi yake.Tulibaki Mimi na Musa tukiwa tumepumzika sebleni,Anko alikuwa kama kawaida yake akaanza kucharuka uchizi ukamwingia, alichukua mito ya sofani na kurusha rusha hovyo, alichukua maji yaliyokuwepo mezani na kuyamwaga,nilimfuata na kumpokonya kisha nikarudisha glasi mezani.Anko akiwa anaendelea kufanya fujo zake Musa hakusema kitu badala yake alimwangalia na kutikisa kichwa kisha kuendelea kuangalia television.
Muda si mrefu Asha alirudi, alipoingia sebleni tu, alimkuta Anko Mashaka akiendelea kuangusha na kushikashika vitu hovyo, nikamwona akimfuata na kumkemea, dakika hiyo hiyo alinifuata niliposimama na kuniambia huku kidole chake kikiwa macho mwangu”Nani amekwambia kumtoa ndani huyu?, mtu mwenyewe unamjua akili hana, angalia sasa alivyoalibu na kumwaga maji hovyo”, Nilinyamaza kimya sikutaka kubishana, maana namjua jinsi gani Asha anavyomchukia, yote sababu ya hali inayomsumbua Anko. Aliendelea kuongea mpaka alipotosheka mwenyewe akanyamaza na kuondoka chumbani kwake huku nikimsikia akimwambia Anko Mashaka “nitakuonesha!” mara moja mawazo yakanijia nikakumbuka Asha alivyokuwa akiongea na Rafikiye kwenye simu, anachomaanisha kumwambia Anko maneno hayo ni ukweli mtupu pale aliposema Anakata kumuua Anko, niliumia sana na kijipa moyo kwa jambo hilo halitaweza kutokea, Asha hawezi kumuua Anko wakati sisi tupo nikajiambia lazima nimlinde Anko Kwa hali na Mali.
Miezi mitatu ilikatika niliona kama miaka miwili.kunapokucha unadhani mchana hautakwisha na kunapokuchwa unadhani jua halitachomoza. Siku zilikuwa ndefu Sana kwangu, zinadorora badala ya kuyoyoma.Hata Musa alituonea huruma kwa mateso tunayoyapata badala ya kutuweka nyumbani kwao kutwa kucha, tukikaa sebuleni pale kutwa nzima.Siku moja Musa akanitaka tukanyooshe miguu kwa kutembea tembea mbali kidogo na nyumbani.Siku hiyo jua lilionesha daliliza uvivu likashindwa kujimwaga kwa sababu ya wingu zito lililotanda angani. Mpaka saa tano tulipotoka, wingu ilo lilikuwa bado limetanda mashariki mpaka magharibi na kuonesha dalili ya mvua.hali ya hewa ilikuwa ya unyevunyevu watu walikuwa wamejifungia majumbani mwao.siku ile hakuna aliyetaka kuoga wala kuanika nguo, watoto kwa vijana tuliowaona njiani walikuwa wamejikunyata kama wagonjwa wa homa. Nyumbani tulimuacha Anko pekee akiwa amelala. Asha hakuwepo nyumbani hivyo nikaona nafasi ya kutoka, ambapo Musa alinipeleka Mjini kyela, nakumbuka siku hiyo tulinunua vitu vingi sana ikiwemo ile suti ya kitenge, viatu vya ngozi na vyakula kwa ajiri ya maitaji nyumbani.
Asha akiwa anashuka kwenye gari, alibisha hodi kisha akasubilia kufunguliwa mlango. akaona kimya,akarudia tena na tena akaona kimya,akakumbuka funguo ya akiba anayotembea nayo.alipekuwa mkoba wake na kutoa funguo kisha akafungua mlango na kuingia ndani.akaangaza kila chumba na kumkuta Anko Pekee akiwa amelala.Asha hakutaka kulaza damu akaona hiyo ndio nafasi pekee kufanya kile alichodhamilia.Kitu alichokuwa anakitaka sasa kimewadia damu ikaanza kumchemka, akaonekana mtu aliyechanganyikiwa.wakati huo Anko Mashaka akiwa bado amelala hakujua ili wa lile.Asha alikwenda mpaka chumbani alipolala Anko, alifungua mlango taratibu huku akinyata kwa mwendo wa kinyonga na kufanikiwa kufungua aliingia ndani moja kwa moja bila woga wowote, mpaka karibu kabisa na kitanda alicholala, alipanda kitandani na kumchoma sindano yenye sumu shingoni.Anko Mashaka alisikia maumivu makali,alipiga ukemi wa hali ya juu,hakuna aliyeusikia ukemi huo ulikuwa umemezwa na mwangwi wa chumba kile. Muda huo huo Anko alitapatapa na kukoloma kisha akakata roho.Asha alimuangalia na alipoakikisha kuwa amekufa , alitoka haraka haraka katika chumba hicho na kuingia chumbani kwake kisha akaenda moja kwa moja msalani na kulitupa bomba la sindano, kisha akajimwagia maji na kujiswafisha kisha akafungua mlango na kutoka ili kuondoa ushahidi wa mauaji hayo bila kugundulika.
Ilikuwa majira ya saa kumi jioni, muda huo tukiwa tunarudi matembezini.tulipoingia tu ndani, nikaenda moja kwa moja mpaka chumbani na kumkutu Anko Mashaka Bado yupo kitandani kama nilivyomuacha.Nilipomuamsha hakuamka, nikasogea na kumtingisha huku nikimwita lakini pia hakuitika nilipomchunguza vizuri nikagundua hali hisiyo ya kawaida.
Mwili wake ukiwa umesinyaa, macho kayafumba nusu, mdomoni akiwa na povuiliamaki na kuchanganyikiwa nikajikuta napiga ukemi mkubwa Musa akaja, mawazo na akiri yangu ikiwa kwa Anko Mashaka. Kijasho chembamba kikaanza kunitoka huku mwili ukitetemeka.Nikafikiria mbona Anko haitiki au Asha amemuua. Nikajiambia hapana Anko Mzima wala hajafa. Niliendelea kumwamsha nikitegemea ataamka lakini haikuwa hivyo, ukweli ulibaki kuwa Anko Mashaka ameshafariki........
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Musa akiwa hajui kinachoendelea ghafla alishtuliwa na sauti ya kilio changu.aliingia chumbani na kunikuta nikilia kwa uchungu, huku nimemkumbatia Anko Mashaka.Alinifuata pale kitandani na kunitaka ninyamaze,Musa alikuwa hajui kilichompata Anko Mashaka,sikuona sababu ya kumficha nilimwambia “Musa Anko amefariki”niliposema hivyo Musa hakuamini masikio yake,nilimuona akiishi nguvu na kukaa chini huku mkono wake ukiwa kifuani,Musa hakukubaliana na Mimi akaamua kuinuka na kumuangali vizuri Anko.Nilimuona Musa akitahamaki, hapo sasa nikajua kweli Anko Mashaka ametutoka, tena muda mrefu uliopita. Maana povu lilikuwa mdomoni mwake na damu zimeganda puani. Musa alipomuangalia juu juu nilimuona akizunguka huku na kule, kama mtu anayetafuta kitu ,nikajua Musa amechanganyikiwa, hakuamini kama kweli Anko amefariki akiwa usingizini.Nilimuona akitoa simu mfukoni mwa suruali yake na kumpigia simu Asha,simu iliita lakini haikupokelewa Musa akaikata na kuirudisha mfukoni mwake.Nilimkumbatia Anko kama Nusu saa mpaka Musa aliponisihi nitoke, kisha akauweka vizuri mwili wa Anko na kuufunika kwa shuka. Tulikatoka sebuleni huku tukiwa hatujui tufanyaje nini kuhusu msiba huo.
Baada ya nusu saa tukiwa tunatafakari jinsi gani tutaweza kuusitiri mwili wa Anko, Asha aliingia, aliponiona nalia na yeye akauliza kilichotokea.sikuwa na nguvu ya kumjibu nilimchukia sana na kumuona kama ndio chanzo cha kifo kile nikifikiria jinsi nilivyomsikia akiongea kwa simu kuusu kumuua Anko moja kwa moja nikajua ndio yeye atakuwa amerudi na kumnyonga Anko au watakuwa wamepanga yeye na musa wanitembeze ili wapate uraisi wa kufanya walichodhamilia niliwaza yote kisha akaondoka nilijifikilia sana mpaka nikajuta kuondoka na kumuacha Anko nyumbani.nilimuona akiinuka alipokuwa amekaa na kunisogelea karibu nakuanza kunifariji. Ilikuwa kazi bure kwake kunibembeleza maana mtu mwenyewe sikubembelezeka niliendelea kulia.
Siku ya pili ilipofika msiba ukawa nyumbani kwa Musa, Ndugu jamaa na marafiki walifika na kushirikiana nasi na kufanikiwa kuzika katika makaburi ya busale. Mwanzo mpaka mwisho wa mazishi hayo sikuwa na Amani hata kidogo, niliwaza na kuwazua kutokana na kifo cha Anko Mashaka.Kipindi chote cha Msiba Asha alikuwa mwenye huzuni mwingi,nami sikuweza kumfuatilia, muonekano wake tu nilijua hakuusika na kifo cha Anko Mashaka. Baada ya mazishi na msiba kuisha nilijiona mtu mwenye mkosi, kila jambo baya unitokea, matatizo yamekuwa mengi kwangu na sasa nimebaki peke yangu.
Baba na Mama wamefariki nikabaki na Anko sasa leo Anko nae Ameniacha nitaishi vipi bila msaada wa ndugu zangu, sina kaka wala dada mtu niliyekuwa namtegemea kwa kila kitu sasa nae ameniacha ndio basi tena.Nimeteseka sana sasa namkabidhi mungu maisha yangu, Hee! Mungu nisaidie
********
Baada ya Mwezi mmoja kupita nilikuwa sijui kinachoendelea kuhusiana na kifo cha Anko Mashaka, nilichukulia kama mapenzi ya mungu kwa kila Mwanadamu.Nilikuwa mtu mwenye mawazo mengi juu ya matatizo yaliyomtokea katika maisha yangu.Siku moja nikiwa nimekaa sebuleni anaangalia television, ghafla nikasikia kama watu wanagombana kutokea chumbani cha pili, nikachungulia kupitia tundu la funguo ndani ya chumba hicho. Sikuamini masikio yangu, nilichokuwa nakisikia kutoka kwenye chumba hicho, kilizidi kunichanganya.Walikuwa Musa na dada yake Asha wanagombana,
“Yaani wewe, unajifanya umekuwa sasa”Asha alimwambia musa
“Hapana dada, Mimi nakwambia ukweli, ulichokifanya sio kitu kizuri”Musa alilalama,
“Wewe unatakaje sasa,nimeshahamua kufanya hivyo”alimjibu
“Inatubidi tumwambie ukweli Kama pesa zake tumezitumia, sasa mpaka Leo mwenyewe
Anangojea pesa zake tumlipe tutazipata wapi, wakati hatuna hata hiyo Biashara yenyewe”Musa alisikika,
“Wewe unasemaje!, naona unataka kunichanganya, umwambie alafu iweje?,
“Tumwambie tuu, labda ataweza kutusamehe”Musa alisema
“Usimwambie kitu, ukimwambia hayo yatakuwa makubwa zaidi, Asha alisisitiza
“Hapana Dada lazima tumwambie “Musa alishikilia msima wake
“Sikiliza Musa usimwambie ndugu yangu, Fred ataishi hapa kwa amani bila matatizo”
“Sawa lakini mwenyewe ananiulizia kila Siku kuhusu pesa zake, amechoka kuishi hapa anataka kuanza maisha yake”Musa alimwambia
“Nakuomba umsihi fred avumilie tukipata pesa zake basi tutamrudishia ili aondoke,maana asije akajua kama mimi ndio niliyemuua Anko Mashaka”Asha alijisahau kuongea,
“Unasemaje dada, yaani wewe ndio umemuua Anko Mashaka? Musa aliuliza kwa mshangao
“Ndio Musa, lakini nakuomba usimwambie, ukimwambia Mimi nitafungwa kaka yangu”
“Hapana dada, kumbe wewe muuaji hee?”Musa alisema huku mwili ukimtetemeka,
“Tafadhali kaka yangu nisamehe”Asha akamsisitiza kakaye,
“Sawa, sitamwambia”
Wakati huo nikiwa nimejiinamia pale mlangoni,nikiwa sijui cha kufanya,nilimuona Musa akiwa anatoka chumbani mwa dada yake na tulikutana uso kwa uso.Alishtuka kuniona pale mlangoni moja kwa moja akajua kwamba nilikuwa nawasikiliza kila kitu walichoongea yeye na dada yake.Musa alinisogelea karibu na kuniuliza ,CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Fred unalia nini?
“Unanifanya Mimi Mtoto mdogo, ujui ulichokifanya”? nilimwambia kwa jazba
“Sijui rafiki yangu niambie,”Musa alinijibu
“Sijui rafiki yangu niambie,”Musa alinijibu
“Yaani, Musa nilikuwa nakuamini sana rafiki yangu, leo umekuja kunisaliti”nilimwambia
“Hapana Fred naomba unielewe, yote yamesababishwa na dada Asha sio mimi”alijitetea,
“Nimekupa wewe pesa zangu, na wewe ukampa dada yako, kwa nini umenifanyia hivi”
Kabla Musa hajanijibu kitu niliondoka na kwenda chumbani, siku hiyo nililia sana, huku nikiwa mtu mwenye mawazo mengi, niliwaza jinsi gani nitalipiza kisasi kwa wabaya wangu. Wakati wote huo, nilijiambia lazima alipize kisasi kuanzia kwa Musa, Asha na Shangazi, hawa wote ndio walioalibu maisha yangu na kusababisha kifo cha Anko Mashaka.Wakati nikiwa kwenye mawazo, nilikuwa sina Amani hata kidogo. Muda wote nilijifungia tu chumbani nikilia.........
Kesho yake kulipokucha asubuhi na mapema,sikutoka kwenda sebuleni nilibaki tu ndani nimejilaza kitandani hata pale wakati wa kunywa chai ulipofika sikwenda kunywa chai badala yake niliendelea kulala.Musa na Asha walipoona kimya,Musa alikuja chumbani na kunikuta nikiwa nimejiinamia kitandani huku nikilia kwa uchungu, aliingia na kunitaka tuongozane tukapate kifungua kinywa, lakini nilikataa na kumwambia “sijisikii kunywa chai” alinilazimisha bila mafanikio,niliushikilia msimamo wangu maana sikutaka kutoka.Alipoona hivyo aliamua kuondoka na kwenda kujumuika na dada yake mezani.Nilijua Musa lazima atamwambia dada yake kuhusiana na hali niliyokuwa nayo.Kweli nilimsikia Musa akianza kumwambia dada yake ,
“Dada jana wakati tunaongea, Fred alitusikia kila kitu”,
“Hee! Unasemaje?”Asha alihamaki
“Ndio hivyo alitusikia kila kitu, Musa alizidi mwambia,
“Ndio hivyo alitusikia kila kitu, Musa alizidi mwambia,
“Sasa tutafanya nini Musa?,
“Mi sijui, amekasilika Kama nini, yaani mpaka sasa hana raha Fred”Musa alisema,
“Mmmmh! Sasa si tutafanyaje
“Mi sijui, kitakachotokea tukubaliane nacho,
“Sawa lakini.....!
Baada ya muda Musa akatoka na kumuacha dadaye pekee akiendelea kunywa chai.Nikiwa mtu mwenye mawazo nikatoka chumbani na kumfuata Asha alipokuwa amekaa, nilipitiliza moja kwa moja mpaka jikoni nikachukua kisu kisha kumfuata Asha Sebuleni, nilipofika pale nikasimama huku kisu nikiwa mikononi mwangu na kukitoa kumuonesha. Asha alipiga ukemi wa gafla nikamdaka na kumziba mdomo huku nikimuelekezea kisu tumboni mwake na kumwambia maneno ambayo yalinitoka kwa uchungu,
“Nakuua Asha kwa kosa lako mwenyewe,
“Kosa gani nimefanya Fred, nisamehee”alijitetea
“Kwa nini unaniomba msamaha,kumbe unajua kosa ulilolifanya hee!”Nilimwambia
“Najua Fred nimekukosea sana. Mimi ndio niliyechukua pesa zako zote, tukazitumia na kununua nyumba kama unataka nyumba chukua”Asha alijitetea na kunishawishi
“Hapana sitoweza kukusamehe, umenisababishia matatizo makubwa sana katika maisha yangu,”nilimwambia
“Najua, Fred mdogo wangu, nisamehee”aliendelea kulia
“Hapana lazima nikuue, wewe ndio uliyemuua Anko Mashaka. Amekukosea kitu gani, mpaka ukaukatisha uhai wake jamani?”Nilisema kwa uchungu huku machozi yakiendelea kunitoka
“Shetani tu aliniingia Fred, nisamee naomba husiniue”
Ghafla nikajikuta namnyanyua na kumuegemeza ukutani.Asha alibaki akitweta, nikiwaza alivyomuua Anko, niliona kama nipo ndotoni, nikiota mateso makubwa niliyoyapata.lakini nilikuwa na hakika kwamba haikuwa ndoto au mauzauza.yalikuwa nateso ya kweli kweli, mateso hayo niliyoyapitia yalinifanya niamini hivyo.Maisha niliyokuwa nikiishi yalikuwa ya shida sana kutokana na wazazi wangu kufariki dunia kiukweli niliumia sana ila sikuwa na jinsi,niliendelea kuteseka kwani maisha yangu yote nilimkabidhi mungu itakavyokuwa na iwe hivyoNikajikuta nikizamisha kisu tumboni mwa Asha na kukitoa kisha kuzamisha tena na tena, mpaka pale nilipolidhika na kumuona ajiwezi nikamsukumia pembeni akadondoka chini kama mzigo. Wakati bado nikiwa nimesimama mapigo ya moyo wangu yakienda kasi. Nikamtupia jicho Asha pale alipodondoka nikamuona akishikilia tumbo lake lililokuwa likiendelea kumwagika damu. Aliweweseka kisha akatulia tuli, na kukata roho.Nilihamaki nilipojiona nikiwa na damu nyingi mwilini mwangu niliingia chumbani na kumuacha Asha pale chini sakafuni.
Wakati nafanya mauaji hayo Musa hakuwepo.hivyo wakati huo ndio alikuwa anarudi alipoingia ndani alimkuta dadaye amelala chini huku damu nyingi zikitapakaa sakafuni. Alipomuangalia vizuri aligundua amechomwa na kisu chenye ncha kali.Musa alichanganyikiwa na kuanza kuniita, lakini sikumuitikia, Badala yake nikatoka kimya kimya na kumfikia nyuma yake. Nilimuona Musa akigeuka nyuma nyumba gafla aliposikia kishindo kikumwa kutoka nyuma yake na kukutana uso kwa uso.Ambapo nilimkamata na kumkaba shingoni kisha kumuegemeza ukutani kisu kile kile kikiwa shingoni mwake.Sikutaka kupoteza muda nikamwambia,. .....
“Yaani wewe umenikosea sana”nilimwambia
“Nisamehe Fred”alijitetea,
“Umenisaliti Musa, nimekukosea nini mpaka umenifanyia hivyo?”Nilimwuliza
“Najua nimekukosea sana, nilikufanyia usaliti kwa kuzitumia pesa zako. Lakini sio Mimi rafiki yangu”,Musa alijiteteaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mimi nimekupa wewe pesa uniwekee, mwenzangu umekuja umezitumia alafu unanidanganya utanirudishia.Sasa naziitaji sasa hivi unirudishie pesa zangu si vinginevyo”nilimwambia
“Please Fred usiniue, nitakurudishia pesa zako”Musa alisema
“Dada yako amemuua Anko Mashaka, nami nimeamua kumuua ili kulipiza kisasi kilichokuwa kinanitatiza ndani ya nafsi yangu” nilimwambia,
“Tafadhali Fred nakuomba tuyamalize”Musa aliniomba msamaha,
“Nakuua….., nilimwambia kwa hasira huku kisu kikiwa shindoni mwake,
Kabla sijamliza kuzungumza hasira zilinikaba mwili ukitetemeka naisi shetani alinivaa nikajikuta nikimchoma kisu Musa kifuani mwake ,ambapo Musa alipiga ukemi mkubwa na alianguka chini kama mzigo kisha kukata roho palepale.Wakati namchoma kisu Musa nilijishangaa sana nikajiisi kama naota nilipotafakari vizuri nakaona haikuwa ndoto bali kweli nikajutia uwamuzi niliochukua,nikajiona mkosaji nisiyekuwa na utu wala huruma kwa Msaada nilioupata kutoka kwa rafiki yangu musa.nilijiinamia pale chini na kuendelea kulia,huku mwili nao ukitetemeka kama niliyemwagiwa maji ya baridi. Hakika nilihujutia uwamuzi wangu, sasa sina wa kumlaumu nafsi yangu hama shetani kwa kufanya mauaji hayo, ya watu wawili kwa siku moja.Wakati nikiwa nimekaa pale sakafuni humu damu nyingi zikiwa zimetapakaa na kulowanisha nguo zangu nilikaa chini na kutafakari namna ya kutoloka haraka iwezekanavyo katika nyumba hiyo.
**********
Upande wa kushoto wa eneo lile,alikuwa amesimama Dada mmoja mwembamba mrefu wa wastani akiwa anapita kando ya nyumba ile,mkononi mwake dada Yule alikuwa amebeba mkoba mweusi.Dada huyo alijulikana mtaani pale kwa jina Mwaija.wakati huo Mwaija akipita njia kandokando ya nyumba hiyo,alisikia sauti za watu zikibishana,alisita kwenda akasimama ili kusikiliza kinachoendele ndipo aliposikia maneno niliyokuwa namwambia Musa,alisogea na kuchungulia ndani kupitia tundu dogo lililokuwa upande ule wa dirisha.Mwaija alihamaki kuona kitendo kile cha mauaji,aliondoka mahali pale na kusogea mbali kidogo kisa alitoa simu kwenye mkoba wake na kubonyeza tarakimu kadhaa na simu upande wa pili ikaitas na kuongea”Hallow! Mwaija hapa naongea,kutoka kijiji cha Sumbi mjini hapa kuna mauaji yametokea kijijini kwetu nyumba namba 14”Mwaija alisema kisha simu upande wa pili ikasikika “Ahsante kwa taarifa!” akakata simu na kuirejesha mkobani mwake na kuendelea na safari zake. Muda si mrefu gari la polisi liliwasili maeneo hayo, kisha askari watatu wakashuka,wote kwa pamoja waliparamia mlango wa nyumba hiyo uliokuwa na nyaya nyingi.Kwa juhudi kubwa waliparamia na kufika juu kabisa ya ukuta ule usiopungua futi sita na nusu,wakachuchumaa pale juu ya ukuta huku mikono yao ikiwa imekamata silaha ndogo ya bastola.Vitendo vyote hivyo vilifanyika bila kelele ndio maana nilipokuwa ndani sikujua kinachoendelea nje ya nyumba hiyo.wakiwa juu ya ukuta wa nyumba hiyo waliruka hadi chini ndani ya uwa wa nyumba hiyo walibimbilika na kulalia tumbu,huku silaha zao wakizielekeza mbele tayari kwa kazi.walipoona kimya hakuna dalili yoyote,walitambaa kwa matumbo na viwiko vya mikono,wakiufuata mlango wa kuingilia ndani na hata walipoufikia mlango,nyumba ikiwa kimya kabisa!.
Sasa wakainuka kwa haraka huku wakiangaza huku na kule huku siraha zao sasa wakizikamata kwa mikono miwili,zikiwa zimeelekezwa juu!mmoja wao alitoa ishara kwa wenzake,bila kuchelewa Askari Yule alirudi nyuma kisha akaukumba mlango hule kwa kishindo bila khiyana mlango ukafunguka kwa kasi na kujibamiza ukutani. Ghafla mawazo yote yalitoweka nikasikia sauti za ving’ola vikilia, kuashiria kuwasili kwa polisi maeneo hayo. Nikiwa sina hili wala lile nikajikuta nimezungukwa na polisi watatu wenye silaha mikononi mwao, sikuwa na jinsi nilijikuta nimenywea kama kuku aliyemwagiwa maji. Polisi wale walipoingia ndani walinikuta nikiwa nimejiinamia na kisu mkononi, damu zimezagaa mwilini mwangu, na maiti mbili zikiwa sakafuni zikivuja damu.walinizunguka na kunitaka niweke mikono juu, sikuwa na jinsi nikasalimu amri na kunyoosha mikono yangu juu.Askari moja mrefu kuliko wenzake akatoa pingu na kunifunga mikononi mwangu, kisha Polisi hao walinichukua bila kuongea neno na kunitoa nje...
Walitoa maiti ya Asha na Musa kisha kuipakia kwenye difenda waliokuja nayo kisha nami kunipakia kwenye gari hiyo hiyo na safari ya kwenda kituoni ikaanza.Muda wote nilikuwa kimya huku machozi yakinitoka.Askari mmoja ambaye ndio dereva aliendesha gari ile kwa kasi huku akiwa makini kwa safari hile akiwai kituoni, aliendesha gari ile kwa kupitia barabara inayoelekea hospitali ya wilaya kyela.baada ya nusa saa tulikuwa nje ya hostitali hiyo.walishuka askari wawili na kuelekea mapokezi, walitoa maelezo na kurudi wakiwa wameongozana na wauguzi wa hospitali hiyo.wauguzi hao walizichua maiti hizo na kuziifadhi hospitalini hapo.Askari hao walipomaliza taratibu za kuifadhi maiti hizo walijipakia tena kwenye gari na safari ya kuelekea kituoni ikaendelea,njia nzima nilikuwa mwenye mawazo lukuki kufuatia tukio lilofanya kumuua Asha na kakaye Musa niliumia sana moyoni ila sikuwa na jinsi maana jambo nimeshalitenda.baada ya mwendo mrefu uliochukua nusa saa nzima hatimaye tuliwasili kituo cha polisi Sumbi.taratibu zikafanyika ikiwemo kuingizwa nyuma ya nondo kusubili hukumu yangu.
*******
Miezi mitatu ikapita, Taratibu za kisheria ziliendelea.hali ya majonzi na wasiwasi niliyokuwa nayo ilichukua muda mfupi kufutika kichwa mwangu. Kama siye Fred ambaye juzi tu alikuwa amepumbaa, unyonge, uzuzu wote ulinitawala sasa umekwisha futika kichwani.leo nimechangamka upya, hali ya matumaini ikajaa tele ndani ya moyo wangu.hata mahabusu wenzangu waliniona tofauti, hali ya uchangamfu imejaa usoni mwangu.Siku moja ilikuwa usiku wa visa nilivyofanya kuwasimulia wenzangu hadithi na soga za kweli na uongo nilijaza homo humo ikajaa msisimko, matukio na vichekesho. siku chache nilizokaa kituoni hapo, mahabusu wote walizoea ghafla na kunipenda,nilijiona mfungwa wa gereza huru ingawa sikuwa huru kama nilivyokuwa uraiani.Hofu ilinitanda nimuonapo Askari anapoingia kwenye chumba hicho,hofu ya dharuba na mateso ya kikatili yanayotokea mahabu hapo.Mbele yangu hakuna ishara wala dalili ya heri ninayoiomba lakini niliona kuna dalili za janga la kuangamiza maisha yangu.Niliogopa lakini nilijikaza na kila wakati niliwafikiria Musa na Asha nilivyowaangamiza.Nilikaa mahabusu kesi ikiwa mahakamani nikisubili kusikilizwa kwa kesi hiyo mahakamani.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*******
Saa mbili asubuhi, lango la mahakama kuu lilifunguliwa.umati wa watu umejaa mbembezoni mwa barabara, mwishoni mwa jingo la mahakama.Askari wamesimama na bunduki mikononi mwao kuwazuia watu kufikia pale ulipo mlango wa kuingilia katika ukumbi wa Mahakama hiyo. Msafara wa washtakiwa uliwasili, Askari waliokuwepo katika msafara huo wakashuka kutoka katika magari yao, bunduki zikiwa mikononi mwao.Ulizi ulikuwa mkali siku hiyo.Mahakama ya wilaya ya kyela, ilisheheni watu siku hiyo, waliokwenda kwa ajiri ya kusikiliza ndugu zao, lakini pia wapo watu waliokuja kusikiliza kesi zao zinavyoendelea.
Nikiwa nimekaa na wastakiwa wenzangu,kesi yangu ilikuwa ya kwanza ikatajwa nami nikaenda kupanda kizimbani huku moyo wangu ukienda kasi.Wakili wa utetezi akasimama na kujitambulisha “Muheshimiwa naitwa Kheri Habibu ,namuwakilisha mshtakiwa”kisha wakili wa serikali akasimama pia na kusema”Muheshimiwa naitwa Kiboja Masanja naiwakilisha serikali,kesi hii imekuja kwa ajiri ya kusikilizwa,leo ndio hukumu inatolewa.
Muheshimiwa alikuwa anaandika yale maelezo kwa makini, kisha baada ya kuandika, akainua uso wake na kusoma kalatasi ya mashtaka,na kuniuliza “Mstakiwa dini yako?”nikajibu “kristo” hakimu akamuambia karani wake “Mpe kitabu cha dini yake na umuapishe” karani mara moja akanyanyua kitabu cha biblia na kunikabidhi,kisha akaanza kuniapisha.Mashaidi wa pande zote mbili walitoa utetezi wao huku akimu akiendelea kuandika kwenye jalada lake kwa urefu,alipomaliza akasema “Ushaidi upande wa mashtaka kuna ushaidi wa kutosha.Katika nyumba hiyo kulipofanyika Mauaji, kulikuwa na kifaa cha kamera inayomuonesha mshakiwa akifanya mauaji hayo,sasa tutaweka tv hapa ili kuonesha ushaidi huo”Hakimu alitoa ruksa viletwe vitu hivyo mara moja,na akageuka kuwaambia Askari,walete vifaa hivyo.Baada ya dakika tano hivi,waya ziliunganishwa,na mara picha yenye ubora wa hali ya juu ilionekana wazi tena bila chenga.Nilionekana nikifanya mauaji hayo.Muheshimiwa hakimu,wakili wa serikali na wakili wa utetezi, tuliokuwa tumekaa pale tuliitazama video ile fupi.Picha za video ile zilinionesha nikimchoma kisu tumboni Asha, baadae Musa akaingi na kumkuta dadaye kwenye umauti kisha nikaonekani nikimfuata Musa pia na kumkaba shingoni, na kumchoma kisu kifuani mwake.Iliishia hapo video ile ikakata kwa namna ya kufikia mwisho wake.
Baada ya kuitazama video ile machozi yalinitoka,nikapoteza matumaini ya kuwa huru.nilimuona hakimu akiandika,kisha akafunua kitabu cha sheria cha mwenendo wa makosa ya jinai,bila shaka labda alikuwa akijiridhisha kutazama kifungu cha sheria.Baada ya kusoma halitoa hukumu.alisoma shitaka lote lilivyo na nilikubali nimetenda kosa ilo,akagusia ushahidi uliotolewa na upande wa mastaka ambao ulikataliwa baada ya hoja za upande wa utetezi kuwa madhubuti.Mwishowe hakimu akasema “Baada ya kuzipitia taarifa zote kwa makini, kwamujibu wa sheria,mahakama yangu imeona mshitakiwa amekili makosa , hakuna ushahidi wa huakika uliokuwepo katika kesi hii!Hivyo natumia kifungu cha sheria cha mwenendo cha makosa ya jinai.Mshtakiwa anaukumiwa kifungo cha miaka kumi na tano gerezani.Nilihamaki ghafla niliposikia hukumu hiyo nikasimama,mikono ikitetemeka,nilitaka kuongea lakini maneno hayakutoka kinywani,yamekwama kooni,uso umebadilika na kusinyaa.Niliinua mikono yangu juu kumshukuru mungu. Baada ya kumalizika kwa kesi hiyo, nikapelekwa katika Magereza mbeya, kuendelea na maisha ya gerezani huku nikiwa na historia katika maisha niliyopitia uraiani......
Nilikaa miaka kadhaa gerezani, nilikuwa nimeshazoea maisha ya gerezani,nikajisikia nipo nyumbani, mawazo yote niliyokuwa nayo yaliyeyuka na kubaki historia kichwani mwangu. Baada ya kuendelea kuishi gerezani kutumikia kifongo changu,huku visa na matukia mbalimbali pamoja na mateso yaliendelea kuniandama nikiwa gerezani.Tulilimishwa mashambani mpaka mikono ikaota usugu mpaka viwiko vyake vikawa vichungu,tukafanyishwa kazi ngumu pamoja na adhabu kwetu zilikuwa si za kuziogopa tena ila mara ya kwanza niliogopa pale nilipokuwa nikitokewa na askari magereza mbele yangu nikajua sasa napigwa,kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo nilivyozidi kuzoea na kuona maisha ya gerezani kuwa ya kawaida sana ikafikia kipindi nikatamani muda usiishe ili niendelee kuishi gerezani maana sikuwa na mahali pa kwenda pale nitakapotolewa.
Niliendelea kutumikia kifungo changu huku nikiwa mtu mwenye heshima kwa kila mtuhumiwa na hata maaskari nao walijua hilo na wengi wao walinionea huruma pale nilipokuwa nikiwasimulia historia ya maisha yangu ilivyokuwa mpaka nikafikia hapo.Wengi waliudhunika ila hawakuwa na msaada wowote kwangu,wangenisaidia vipi wakati wote tupo gerezani kila mtu na kosa lake wapo,waliotenda makosa kama mimi na wakaukumiwa na wapo wasiokuwa na kosa bali waliosingiziwa pia walikuwepo tena wengi sana.Ila hakukuwa na namna ya kusaidiana kwani hata mimi nilikuwa na udhuni sana pale wenzangu walipokuwa wakinisimuliwa kuhusu matatizo yao yaliyowafika mpaka nikaona langu dogo kuliko yao,tukaendelea kuvumilia maisha hayo ya gerezani mpaka pale hukumu ulikalibia kuisha.
hatimaye muda wa miaka kumi na mitano ikawadia, siku moja nikiwa sina hili wa lile, nimekaa na wafungwa wenzangu,aliingia askari Magereza anayeitwa Hafidhi kunitaka nimfuate,nilitoka na kumfuata Askari huyo,kwa mbali nikasikia sauti za watu wakiongea kwa vicheko na furaha,sauti hizo zikitokea kule ofisini ninapoelekea.Askari Hafidhi aligonga kisha mlango ukafunguliwa nikaingia moja kwa moja.Tulimkuta mkuu wa Magereza Bwana Majaliwa Busimba.Nikamsalimu kisha akaniambia,”Fred unajua nilichokuitia?” nilimjibu “hapana sifahamu”akaendelea kuniambia “kuanzia sasa utakuwa na muda mwingi sana wa kufurahi”aliponiambia hivyo moyo wangu ukapiga paa!nikaanza kukumbuka,kumbe leo tarehe 21 mwezi desember,ndio siku ya mwisho kutumikia kifungo changu,niliona kama juzi tu,kumbe miaka kumi na tano imeshahitimu,nikaachia tabasamu na kukakaa vema kumsikiliza.Bwana Majaliwa akaendelea “nimekuita ili kukupa wosia.Ukiona panafuka moshi basi ujue pana moto,na subira yavuta heri ,sasa unatakiwa uchukue kilicho chako na kwenda,sasa upo huru,uende uraiani ukaendelee na maisha yako,uwe mtu mwema kwa wenzako”alipofika hapo akamyamaza na kunitazama usoni akayaona machozi yaliyokuwa yananitoka ,akanipa kalatasi nikasaini. Akaniambia”Fred waweza kwenda sasa!”Nikainuka na kutoka huku nikiwa na furaha.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sikuwa na vitu vingi vya kuchukua ila nifuata nguo zangu nilikuwa nimevaa siku niliyokamatwa.zilikuwa zile zile,shati rangi ya bluu na suruali nyeusi.lakini nguo hizo singuo nzuri tena zilikuwa zimechanika chanika tu.Nilitoka nje ya lile gereza kwa kupitia langu kubwa.nilipofika nje nikasimama,nikaangalia jua lilikua kali mno.nikavuta hewa ya pale niliposimama,ilikuwa hewa safi kuliko mle gerezani haikupatikana hewa hiyo.Nipo huru sasa!nikamkumbuka Anko Mashanka,kumbukumbu za nyuma zikajirudia ndani ya akili yangu huku machozi yakiendelea kunitoka.Nikageuka nyuma na kuliangalia Gereza .Nililitazama kwa chuki na hasira,uchungu ukanijaa moyoni nikawaza jinsi nilivyoteseka.Nikaondoka taratibu pale nilipokuwa nimesimama sijui pa kuelekea,nilitamani kuendelea kuishi gerezani lakini ikawa Haiwezekani lazima nitoke kutafuta maisha mapya.
********
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment