Simulizi : First Year
Sehemu Ya Nne (4)
Nusu saa ilitosha kukaa ndani ya chumba kile kabla ya Shufaa kunipigia simu na kunitaarifu kuwa ameshafika mjini hivyo muda si mrefu, angekuwa eneo lile ambalo kwake lilikuwa sigeni na hata lingekuwa geni kwa umarufu wa eneo lile ilikuwa rahisi kwa dereva yoyote wa tax kufahamu mahali pale hivyo isingekuwa ngumu.
Mapigo ya moyo yalienda kasi kusubili utamu ule nilitamani hata apae, na kwa wakati huo hata zoezi la kukaa peke yangu ndani mule nilishaanza kunichosha.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
SURA YA KUMI NA MOJA
Dakika kumi zilipita na hatimaye simu yangu ilianza kuita na kuonesha vyema yule aliyekuwa akipiga akuwa mwingine bali alikuwa Shufaa. Nilipokea huku nikitoka ndani mule nilishafahamu tiyari alikuwa yu mahali pale. Kweli kile nilichokuwa nafikiria ndio kilikuwa chenyewe, hivyo maongezi haya kuwa mengi nilikata simu na kuelekea mahali kule mmh! Ilikuwa hatari mtoto alikuwa amependeza balaha kiukweli nilisogea mahali pale alipo, jamani Shufaa hata aibu hakuwa anayo alichokifanya pale mapokezi ni noma sana.
Ule mkumbatio aukuwa wa kawaida kabisa namna ulivyofatiwa na mabusu mfululizo ulitufanya tupigwe macho makali na baadhi ya watu walikuwepo eneo lile. Haswa yule mdada wa mapokezi lakini Shufaa hakujali hilo, kitu ambacho kilinifanya nione aibu kwa upande wangu lakini nilijikaza tu kiume. Taratibu tulichukuzana hadi chumba nilichokuwa nimelipia. Haki jamani Shufaa alionekana anahamu na mimi vibaya akunipa hata nafasi punde tulipoingia ndani alinisukumiza kwenye kitanda nikaenda tii!!!. Hadi juu ya kile kitanda kabla ya yeye kuja juu huku akinichezea maeneo yangu ya ikulu kwa namna ya kipekee sana. Sikujua hata ule utundu alikuwa amesomea au ndio masuala ya unyago au raha tu maana zile raha nilizokuwa nazipata hazikuwa za kawaida kabisa.
Hakuna hata moja wenu hapa endapo angezipata raha zile asingekuwa anapiga kelele kama nilivyokuwa nikipiga mimi hapo hata sikutambua kelele zile zinatokea wapi ila nilichojua zile zilikuwa zaidi ya kelele.
Tulicheza ule mchezo mpaka kigiza kiliingia hapo kasi ilipungua sikuwa mimi akuwa Shufaa tulionekana tumelidhika na jambo lile. Wakati huo bado tulikuwa kitandani mule hivyo kimya kilitawala kidogo kabla ya kuanza kuzungumza. Maongezi ambayo kila moja alikuwa analengo la kumsifia mwenzake mwanzo mwisho juu ya penzi lile. Hata hofu si kuwa nayo kabisa, wakati nilitambua kuwa yule alikuwa mke wa mtu na ninachofanya kilikuwa si kitendo sahihi kabisa.
Kwa upande wangu mimi nilizidi tu kupandikiza mzizi wa penzi lile uzuri wake ukichanganya na wangu basi tuliona tunaendana mno. Kumbe ndugu Waandishi ule ulikuwa ni ujinga tena ujinga wa mwisho unawezaje ? Mtu kuwa na mke wa mtu alafu “eti unajipa sifa unaenda nae kweli? unaendana na mali ya mtu. Hii ni sawa na kumwibia mtu kivazi chake cha ndani alafu ukavaa yako suali, huku umechomekea vizuri kuonesha kivazi kile wazi wazi wakati unafahamu fikra kile kivazi si chako. Basi ndio nilikuwa mimi nilikuwa natambua vyema kuwa mke wa mtu ni sumu ,na si sumu tu hata upande wa dini yangu inakataza vikali waumini kumchukua mke wa muumini mwenzio wakati unajua dhahiri juu ya lile kuwa aswiih na adhabu yake ni kali kwa muumba wa ardhi na mbingu ya dunia hii.
Tulitiana ujinga vya kutosha kabla Shufaa kutoa wazo la kwenda kuoga hivyo kama vile nilikuwa nimeoa yeye alikuwa mbele mimi nikiwa nyuma kuelekea sehemu ile ya bafuni. Taratibu tukiwa ndani ya vitaulo vile ambavyo tulipewa kama huduma ndani ya hoteli ile mpaka lilipo bafu ,tulifungua mlango wa bafu lile nakuweka vivazi vyetu pembeni na hapo tena mambo yalikuwa vile vile.Tuliogeshana vya kutosha kama vile mama anavyomuogesha wake mwana utamu ulizidi mno. Sikuwahi hata siku moja kufanya namna vile kwa upande wangu hapo hata wazo la nyumbani halikuwepo nilishakubali yote, kama Mzee hatoelewa kile nilichomwambia Mama shauri yake. Ataongea hata nyamaza sasa nishakuwa mtu mzima mambo ya kunibana bana ndio mwisho nilijisemea ndani ya nafsi yangu wakati bado tukiendelea na zoezi lile la kuogeshana na Shufaa.
Namna ya umaliziaji wakuoga ulikuwa wa aina tofauti kabisa hapo nilishaanza kuona kuwa watu walikuwepo kwenye ndoa wanafaidi sana .Kumbe haikuwa hivyo ni fikra tu potofu zilikuwa zikiniongoza kwa muda ule ata kitu ambacho kilikuwa kibaya kwangu ningekiona kizuri. Shufaa alinipagawisha sana siwezi kuelewa ilikuwa vipi sikuile aah! haikuwa kawaida hata kidogo nakumbuka baada ya kutoka kuoga simu yangu ilianza kuita. Wakati huo giza lilikuwa limeingia kabisa kuonesha muda ulikuwa umeenda na usiku umeingia.
Kioo changu cha simu kilionesha vyema Baba ndio alikuwa anapiga kiukweli baada ya kupokea simu ile nilichojibu pale pindi maneno yake, Mzee kupenya vizuri ndani ya ngome za masikio niliyayona hayakuwa mazuri kwa upande wangu ishiiiii! Sijui ilikuwa nini? Bange au mmh ndugu Waandishi nyie !
Sikuwa mimi yule ambaye nilikuwa hapo mwanzo nikiheshimu kila neno linalomtoka Baba ndani ya kinywa chake, ila kwa siku ile nilikuwa tofauti sana kwa upande wangu maneno makali niliyatoa. Baada ya Baba kuniambia hata kama huyo rafiki yangu ni mgonjwa vile alivyoambiwa na Mama punde tu alipofika nyumbani akitokea kazini ila sikupaswa kulala kule kule, hicho ndio kilikuwa chanzo cha kuyatoa yale maneno ambayo sikujua wapi? yalitoka ila nilichojua nikuikata yangu simu punde tu nilipo bwabwaja yale maneno kwa hasira mno.
Ndugu Waandishi nilizima kabisa simu yangu sikutaka kusikia chochote kutoka nyumbani nilishakubali lolote lile litalotokea sawa tu, Kwa muda ule kiukweli shetani alinitawala hata sikujali litalokwendwa kutokea mbele.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati huo Shufaaa alikuwa kimya tu akinitazama akutaka kutia neno lolote na hata pale nilipomaliza mimi ndio nilikuwa msemaji wa kile hadi tulipomaliza kuvaa. Na kutoka mule ndani ya chumba lengo kubwa ni kwenda kupata chakula ndani ya hoteli ile.
Moja kwa moja tulichukuzana huku tukiwa watu wa furaha sana na hata hapo sikuwa na wazo lolote kama nimetoka kugombana na Baba kisa yote yale, huku nikiwa nimesingizia rafiki yangu ni mgonjwa hivyo kutoka kwangu nyumbani ni kwajili ya ile kumbe haikuwa hivyo kabisa.
Tulifika eneo lile ambalo lilikuwa dhahiri sehemu ya kupata mahitaji ya chakula na vinywaji kwa wateja wote ndani ya hoteli. Eneo lilivutia mno kwa ukaribu tuliweza kuiona bahari ambapo kwa muda ule maji ndio yalikuwa yanajirudisha.
Tulichagua moja wa meza ambayo tuliona panafaa sana kwajili ya kufanya yetu hivyo tuliketi kabla ya dakika tano mhudumu moja ndani ya hoteli kujakutusikiliza. Kwa upande wangu niliagiza kile nilichona kinafaa kula muda ule hata hivyo Shufaa nae aliagiza kama nilivyoagiza mimi ,tukisindikizwa na vinywaji vikali. Wakati huo bia nilishazoea sikumbuki nani alinifundisha ila kwangu ilikuwa kawaida tu hapo tulikula na kunywa vibaya huku tukifanya kile ambacho tulikiona kinafaa.
Wakati nao muda haukuwa nyuma ulitembea vibaya mpaka macho yetu yalipoanza kuingiwa na usingizi , loo! saa sita kumbe ilikuwa imeshaingia. Hivyo tuliamua kuchukuzana na Shufaa tukiwa hoi, tuliburutana hadi kwenye chetu chumba. Moja kwa moja tulijitupia kitadani hapo usingizi haukutuacha ulituchukua tukachukulika.
Si kuwa mimi wala Shufaa aliweza kusikia mlio ule wa simu ambao uliita kwa dakika kadhaa kabla ya kuanza kusikia kwa mbali nikiwa bado usingizini.Nilisita kidogo kumka kelele zile za ile simu ya Shufaa ilinifanya nishindwe kuendelea na usingizi wakati huo bado Shufaa alikuwa kwenye usingizi mzito.
Kiuchovu uchovu nilipapasa kule sauti ya ile simu ilipotokea na kufumbua macho yangu ilikuweza kutambua mpigaji wa ile simu.
Nilikamata ile simu na kufumba mboni zangu ambazo ziliweza kusoma vizuri jina,la yule mpigaji doo!.. MY HUBBY ilisomeka vizuri ndani ya macho yangu. Mikono yangu ikiwa inatetemeka kwa kile nilichokuwa nakiona mwenye mali ndio alikuwa akipiga kuulizia yake mali nilihisi kama ananioa. Yani nilinywea mithili ya panya amuonapo paka awapo kwenye malindo. Nilitetemeka cha kufanya sikukiona nilibaki nimepigwa na butwa wakati muito ule wa simu ulinyamaza kidogo kabla haujaita tena safari nyingine.
Safari hii ulimfanya shufaa kuamka na kuniachia tabasamu huku nikiwa sielewi hata mikono yangu ilipomkabidhi ile simu hadi anamaliza yale maneno. Ambayo nakumbuka yalitawalia na “ilove ilove mume wangu” mimi nilikuwa bado akili yangu haijakaa vyema nilisistushwa na sauti ya Shufaa ikiniuliza kulikoni?
Nilivuta pumzi kama mtu aliyekuwa akifanya mazoezi magumu kisha niliweza kuijibu kile alichokuwa anakizungumza Shufaa ambaye alionekana hana wasi wasi hata kidogo.
SURA YA KUMI NA MBILI
Ukiwa muda umeenda kijua nacho kilishaanza kuwa kikali kuukaribisha mchana wa siku hiyo. Tulichukuzana moja kwenda kuoga, haraka haraka na kuondoka eneo lile kwa miadi ya kuonana siku nyingine kama tukipata nafasi kwa siku nyingine tena.
Tukiachana maeneo fulani hivi , akiwa amenipatia pesa nyingi kwajili ya matumizi kama kawaida yake.
Hapo safari ya kurudi nyumbani ikawadia huku kile kitendo nilichokifanya cha kujibizana na Baba hovyo kikiwa kinanija njia nzima. Kabla hata sijafika eneo lile la nyumbani nilipiga moyo ukonde, nikijikaza liwalo na liwe ndio lilikuwa limenitawala hapo.
Nusu saa zilitosha kufika mitaa ya nyumbani baada ya kuachana na Shufaa. Nilipiga hatua kuelekea ilipo nyumba yetu taratibu, huku nikiigiza kisura cha huruma. Hatua kadhaa nilifikia nje nyumba yetu hapo nilisikia sauti ya Baba ikizungumza jambo. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dhahiri alikuwa akinizungumzuzia mimi huku akionekana amechukizwa mno jambo lile ndani yake. Hasira zote alikuwa akimmalizia Mama kabla ajaiyona taswira yangu muda mfupi baada ya kunyamaza kile alichukuwa akizungumza. Nilijisogeza eneo lile huku nikianza kumtupia Mama salamu kabla sijageukia kwa Baba.Aliyoonekana wazi amechukizwa na jambo lile maana hata salamu alishindwa kuitikia, bali alichojua yeye nikugomba tu kutokana na hali ile huku akinisitizia nimekuwa na tabia mbaya si mimi yule aliyekuwa akinitambua kabla ya kwenda kuanza maisha ya chuo.
Nimekuwa kiburi ninajibu ninavyojisikia mimi na isitoshe kama nitakuwa si vuti bangi hajui? ki Mzee aliongea sana kwa siku hiyo ,nilishindwa kutia neno kwa hasira alizokuwa nazo zingeweza kusababisha kitu kibaya kutokea. Nilitulia nikiwa namsikiliza Mama ambaye alikuwa akinitetea juu ya lile lakini hio haikutosha Mzee aliyeonekana amechukizwa sana. Na yote ilitokana na ile ya kumjibu vibaya pindi alioponipigia simu. Lile lilikuwa kosa ambalo mwanzoni niliona kawaida lakini haikuwa kawaida kama nilivyokuwa na dhani. Kitendo kile kiliondoa uaminifu mbele ya mzazi wangu yule. Kwa upande wa Mama hakuwa akinifikiria vibaya, vyovyote vile na hata pale lilipokuja suala la kile kitu alinipa ruhusa kwa moyo moja huku akioneshwa kuguswa na jambo lile.
Siku hiyo Mzee aliongea sana zaidi ya lisaa mpaka pale alipoona lile alikuwa analisema limefika kwangu na kama si hasira zake kupungua. Taratibu nilimwona akiingia zake chumbani na kutoacha na Mama mahali pale. Nilitulia kimya nikijitahidi kuonesha nimeguswa na maneno yale zaidi.
Kwa unyonge na upole Mama alinipa maneno ya kunifariji na kutamka nimzoe tu Mzee. Kwa sababu ndio kawaida yake ana mambo ya kikoloni sana hivyo nichukulie kawaida tu, huku mwishoni akiniuliza habari za kule nitokako na vipi? hali ya yule rafiki yangu.
Na hapo nakumbuka vyema nilijenga uwongo unafanana vizuri na hali ile, Mama alinielewa kwa mara nyingine na vile alikuwa akinipenda sana chochote nilichokuwa nakiongea alikuwa akinisikiliza sana kwa upande wa mama yangu oooh!.Masikini Mama yangu kwanini nilimfanyia vile wakati alikuwa akinitegemea mimi na kuniamini sana sijui ilikuwa nini uuu!.. aaah !kwanini? mimi Salimu niliamua kufanya yote yale ndugu Waandishi. Kitendo kile kilikuwa akistahili kabisa kumfanya kwa mtu wa namna ile aliyekuwa wazi kunitetea mimi mbele ya Baba.Wakati nilikuwa muovu nisiye stahili hata kile alichokuwa anakifanya, kwa jili ya kwangu mimi niliye jivisha ngozi ya kondoo wakati ni chui mbaya kabisa kwenye macho ya swala kwenye nyikani.
Namna ya uongeaji wa Mama alinifanya nione kwaida ,niliamua kuingia zangu ndani bila wasi wasi wakati Mama aliponiaga anaenda sokoni kununua mahitaji. Na asingeweza kunituma mimi kwa muda ule na kibaya zaidi wale ndugu zangu niliowakuta nilivyo rudi kutoka chuo waliondoka jana yake jioni. Baada ya kupigiwa simu wanahitajika hivyo hakukuwa na mtu mwingine zaidi yetu pale kwanamna yoyote, ilimlazimu Mama aende sokoni kwasababu hakutaka kunituma mimi aliamini kwamuda ule nilikuwa sipo sawa kabisa.
Kitendo kile cha kuingia chumbani kwangu muda mfupi Mama alivyoniaga kwenda sokoni akili yangu aikusoma tena, nilishamkumbuka Shufaa habari za Baba nilishaziweka kando kama alikuwa amemaindi powa tu nilijisemea. Nikitafuta namba ya Shufaa na kuanza kuipiga kwa sekunde kadhaa simu yake ilipokelewa ,sauti nyororo mithiri ya ndege kasuku ilipenya kwenye yangu masikio kuashiria yule niliyokuwa nikizungumza nae alikuwa Shufaaa. Kama kioo cha simu yangu kilivyokuwa kikinionesha kabla sijabonyeza kitufe cha kupiga simu ile. Nilizungumza nae kwa muda mrefu sana, sikujua dakika ngapi nilikuwa nimeutumia kabla ya kukatika ile simu ambayo mzungumzo yetu yalikuwa yametawala kwa kile tulichokuwa tunakifanya usiku wa jana.Tukiendelea kusifiana kwa namna tofauti vikifatiwa na vicheko visiokuwa na idadi dhidi yetu mpaka alipokatika simu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maongezi hayakuwa yameisha kabisa lakini sikuwa najinsi ilibidi nitulie kutafakari yale. Shufaa alinitawala kweli, hata lile wazo la kuwa mke wa mtu kwa wakati huo halikuwa likinijia kabisa niliona kama wakina Recho. Loo!kumbe lile lilikuwa nalo kosa tena kwenye yangu maisha ndugu Waandishi nini sijui? kilikuwa kinanituma mimi uwiiiiii!
Sekunde kadhaa baada ya kukatika ile simu huku nikiwa na tafakari kile mara sauti ya Mama ilipenya vizuri kwa mara nyingine kwenye masikio yangu. Nilitulia tuli mithiri ya maji mtungini kabla sauti ya Mama kupaza tena, safari hii ikitaja jina langu miito miwili ilinifanya niitikie haraka. Nikitoka kitandani nilipokuwa na kuelekea mahali ambapo sauti ya Mama ilikuwa ikitoka hapakuwa kwingine ni kule jikoni hivyo nilielekea kusikiliza wito ule.
Maneno yake yalipenya vizuri ila hayakutosha kunishawishi kile nilichokuwa nacho sikuhitaji kula kwa muda ule ,njaa ilikuwa ainiumi kabisa. Kitendo kile kilimnyima Mama raha akiamini labda maneno yale makali ya Baba ndio yalifanya nishindwe kula kwa wakati ule. Fikra zake zikimtuma kuwa labda niliamua kususa ila ndio ilikuwa vile. Kishingo upande Mama alikubali kile, akinisisitiza baadae nile sikutaka kumvunja moyo nilimwitikia Mama kwa kichwa, nikiwa na ishia kurudi chumbani kwangu.
Siku mbili zilipita nikiwa bado sina mahusiano mazuri na Baba ambaye alionekana amechukizwa sana.Sikutaka kumjali sana mawazo yangu yalikuwa kwa Shufaa ambaye alishaniambia kesho yake atarejea Morogoro. Kitendo kile kilinisumbua sana wazo la kukaaa Tanga likawa limepotea. Siku niliziona ndefu mno kuisha hata zilipokuwa zikiisha niliona bado tu haswa ,kuanzia siku Shufaa alipoondoka kurejea Morogoro na kuniacha ndani ya Tanga. Furaha ilipotea lakini Mama hakuweza kugundua mawazo yake yalikuwa kwa kile ambacho kilitokea siku zilizopita hivyo aliendelea kunisii nisahau. Nilijaribu kuonesha tabasamu muda wote mpaka siku zilivyokatika na kurejea tena chuoni.
Sikutaka kuvuta siku kukaa nyumbani tarehe ile ilipofika moja kwa moja nilingia zangu chuo. Wanachuo wachache ndio walikuwa wamerejea wengi wao waliendelea kuvuta lakini mimi hio aikunipa tabu kuwepo Morogoro ilikuwa furaha tosha. Yote ilitokana mahali pale ilipunguza umbali na kuleta ukaribu ya kuwa na Shufaa na si kingine ndio kilichokuwa kinanifanya nijisikie vile.
Nakumbuka siku hiyo izack alikuwa bado yupo nyumbani kwao, hivyo nilikuwa peke yangu na baadhi ya wazushi wazushi naweza sema hivyo.Maana class yangu na yao ilikuwa tofauti kwa muda ule ,nilisahau kama wao ndio walinipokea ilo sikuliona kabisa.Tabia yangu ilibadilika kweli ndugu Waandishi si kuwa mtu wa watu nilijisahau sana tabia ile ilinifanya hata baadhi watu kujenga bifu na mimi kichini chini haswa wale walikuja kugundua nilikuwa na vishughulikia videmu vyao kimya kimya walinichukia vibaya.
Nakumbuka siku ile kunajamaa alinifata nakuanza kusema mbovu na mimi niliwaka ijapokuwa nilikuwa sina ubavu ila nilijiaminisha, tuliwakiana sana na yule jamaa ambaye hata sikujua ilikuwa ananisubili nirudi tu aje kuniambia yale mambo yake. Niliyoona ya kishamba kwangu
hata sikujua tulimalizana vipi pindi alipokuja kwenye changu chumba lakini lile zogo lilifanya baadhi ya wanachuo ndani ya hosteli wale walikuwa wamewahi siku ile kuja kunyamzisha lile.
Ambalo hata sikujua tulikuwa tunaendea wapi? maana tulikunjana sana na yule jamaa ambaye alionekana wazi wazi alikuwa amechukizwa kwa kiasi kikubwa jambo ambalo sikuwahi kufikiria kama ipo siku nitakunjana na mtu kisa mwanamke.
Lakini sijui ilikuwaje ndugu Waandishi ninaweza kusema ile yote ilikuwa kwajili ya First year mmhhh!,ahhhh! usiombe ndugu Waandishi ya kukute wee! sikia tu hichi ninachokisema mimi yakikuta ndio utakuwa shahidi wa haya hapa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Purukushani zile zilinifanya kwa hasira nimtafute kile kidemu cha yule jamaa muda ule.. ule na kutaka kufahamu alikuwa mahali gani, nilitafuta namba yake kwenye yangu simu haraka haraka na hatimaye ilionekana kwenye yangu srceen . Nilipiga namba ile haikuita sana ilipokelewa upande wa pili sauti ilinifanya niamini niyeye Hadija.
“Uko wapi?”
SURA YA KUMI NA TATU
ndio neno ambalo niliaanza nalo majibu yake kwenye yale maogezi yalinifanya nijione mshindi.Kabla sijaamua kufanya lile jambo ambalo lilikuwa limejengeka baada ya kale ka mzozo aah...hiii! akili zingine sio kabisa sijui kilinisukuma nini kuafanya lile.Ambapo neno naomba “tuonane” ndio lilifatia kutoka kwenye kinywa changu kabla ya maneno mengine ya kutoa maelezo ya kile. Nilichukuwa nakitaka kufanya yote ilikuwa kumkomesha jamaa kuonesha kwamba mimi nilikuwa sifai hata kidogo mbele yake.
Na uzuri kale kademu kalikuwa kanielewa mbaya sikujua ilikuwa sababu ya pesa au uzuri wangu ama nini?. Niliamua kufanya vile kabla sijaikata yangu simu na kuanza kujianda kwajili ya kwenda ile sehemu niliyopanga kuonana nae.
Nilijaianda sikutaka kupoteza muda kwasababu kijua nacho kilikuwa kanaenda kupotea na kukaribisha usiku kama siku zingine zinavyokuwa. Haraka haraka nibadili nguo na kujipulizia uturi ulifanya ninukie, uturi ule ulikuwa hatari mno naweza kusema niliufahamu pindi nilipoletewa na Shufaa siku ile ambayo tulipena maraha kwa mara nyingine. Ndio alinipatia kama zawadi kiukweli ulikuwa mzuri sana ulinifaya niwe tofauti na watu wengine pale chuo na haswa visichana walikuwa wanaupenda sana ile harufu ya utuli wangu .
Nilihakikisha niko powa taratibu nikaufunga wangu mlango kwenye kile chumba cha hosteli,nikianza kutoka hosteli mule ambapo nilikuwa nikipigwa vijicho kila nilipokuwa nikikatiza mule ndani na baadhi ya wanafunzi walikuwa walikuwa wamewahi. Yote ilikuwa purukushani ile iliyotokea muda mfupi na yule jamaa ambaye alikuwa akidai ni achane na Hadija.
Sikutaka kuwajari niligoga hatua nikiacha minong'ono minongo'no nyuma kabla sijachukua boda boda kuelekea mahali pale palipo someka Changarawe lodge. Hakukuwa mbali na chuo dakika kadhaa nilikuwa mahali pale na kuelekea mapokezi na kufanya taratibu za kupata chumba. Na kwabahati nzuri vyumba havikuwa vimeisha kama siku nyingine, huwa vinawahi kuisha kutokana wanachuo wengi hupendelea kufanya mambo yao eneo lile mara nyingi. Kwa muda kama ule moja kwa moja ningeweza kukuta kumeshajaa pingine uwepo wa wanachuo wachache siku ile kwasababu ilikuwa siku ya chuo kufunguliwa ilisaidia kwa kiasi kupata nafasi mahali pale kutimiza hadhima yangu .
Sikutaka kushangaa eneo lile nilipokabidhiwa funguo kwanza nilienda kupakia chakula cha kutosha, nikiwa tiyari nishawasiliana na Hadija nikimtaka awahi kufika. Nikiwa naendelea kufanya makulaji na unywaji eneo lile ambalo lilkuwa kimya kweli niliendelea kufanya yangu. Pombe ilishaanza kuingia kwenye kichwa changu na hapo sikuwa mwenyewe tena yaani tulikuwa kama wawili tunaendesha na kichwa kimoja mithiri ya haya magari ya mizigo ambayo ya nakuwaga na matera mawili likiendesha na kichwa kimoja.
Peleka peleka yake ilikuwa si masihara na hata Hadija alipokuwa amekuja nilikuwa tiyari si Salimu mimi bali alikuwa mwingine hata hivyo muda mchache Hadija nae alikuwa kama mimi. Tulilewa sana, pesa nilikuwa na yao ya kutosha kwenye suala la kutumia pesa kwangu halikuwa tatizo hata kidogo tulitumia mbaya hadi tuliacha simulizi pale kwa mhudumu aliyekuwa anatuhudumia kabla hatujaingia chumbani kufanya yetu.
Huku tukiwa tunakokotana kama malumbesa ya mchele ukweli tulijivuta huku Hadija akiwa hoi tofauti hata na mimi kidogo nilikuwa vizuri mbaya na si unajua tena mlevi huwa anajiamini hata iweje vile ujiona bomba tu. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tulikokotana mpaka pale tulipojitupa ndani ya kitanda kile cha logde ,kikiwa kinaonekana kimezidiwa na uzito ule maana Hadija alikuwa anashepu kama kibonge si kibonge ila alikuwa mtamu. Na kiuzito cha haja ukichanganyisha na wangu wee! ulikuwa si mchezo hatari tupu, tukiwa tunapapasana maeneo fulani ndani ya kitanda kile punde tulipojitupia mmh! sijui pombe ama nini maana ilikuwa raha ajabu hapo tukisindikizwa na miguno ile ya maraha kwa upande wetu uwii! grafla simu ya Hadija ilianza kuita.
Huku bado tukiwa tunapasana kuelekea kwenye mchezo wenyewe namna ya uitaji wa ile simu ilinifanya ni boreke ,wakati huo Hadija alikuwa hoi pombe zilimzidi pia mchezo ule ulimfanya hata asitambue kinaendelea nini maana tiyari alikuwa katika dunia nyingine. Dunia ya maraha na kwa akili zangu za pombe nilitafuta ile simu ilipo nakuanza kusemeshana mbovu na yule mtu aliyekuwa anaongea japo nilikuwa nipo pombe ila sauti ile ilipenya vizuri ndani ya masikio yangu kufanya kuikumbuka vyema ni yule jamaa.
Ambaye nilikuwa nimezinguana naye juu ya Hadija hivyo ile ilikuwa kama bahati ya mimi kuanza kuonesha jeuri yangu huku Hadija akiwa kipombe pombe alikuwa akitoa matusi tu kwa yule jamaa huku akisema "baby!!! baby" nyingi niachane na ile simu tuendelee kufanya yetu.
kwa vile nilikuwa nimepania yule mtu ,Hadija akiwa afahamu lolote na hata kama angekuwa na akili zake za kawaida asingeweza kujua lile lilikuwepo ndani ya kichwa changu. Niliwaka sana mpaka pale jamaa alipoikata simu ."Nitaona!...nitaona" zikiwa nyingi tu sikuzijali mimi nilichofanya nikuzima ile simu wakati matusi yakinitoka mithiri ya unga unapokuwa unatolewa kwenye mashine. Maana mdomo wangu ulijaa fumba la matusi ya aina tofauti mradi kupoza hasira zangu ambazo, kwa namna nilivyokuwa nimpania yule mtu wazi hata asingepiga ningemtafuta wakati nipo na Hadija mahali pale ilimradi kuonesha dharau dhidi yake.
Michezo kama ile alikuwa amenifundisha Izack, dharau za yule jamaa zilinifanya nifanye lile wakati madhara yake si kuya jua mwanzoni na laiti ningekuwa nayajua athari ya lile haki nisingethubutu kufanya vile .Kwanza unawezaje? kufanya kitu ambacho unajua madhara yake ahhh... jibu hapana kwa vyovyote ndungu zangu Waandishi nisingeweza kamwe sijui...sijui! nini? kile kilichonisukuma kufanya vile. Ninachojua akili zangu ndugu kujumlisha kuiga maisha ya marafiki haswa Izack ndio ilikuwa chanzo cha yote.
Niligeuka upande ule alipokuwepo Hadija na kuendelea na mipapaso safari hii ilikuwa ya nguvu ikisindikizwa na vilio vya furaha vya mwanamke yule na kunizidisha mumkari. Ukiongeza pombe zile kali ulifanya jembe langu kulima kweli kwenye shamba lake nilihakikisha na lima vizuri bila kubakisha ungwe yoyote. Hakika si kuwa kama nimempania yule aliyejiita bwana wake hata yeye Hadija nilimperekesha kweli usiku kucha kazi ilikuwa ni ile ile nililima vya kutosha.Hadi kumi usiku nilikuwa bado nipo juu ya shamba lile nikikagua baadhi ya maeneo masumbufu.
Baada ya kumaliza kile nilichokiita ukaguzi kidogo usingizi ulininyemerea, na hatimaye ukanichukua na kuchukulika kweli mpaka asubuhi simu yangu ilipokuwa ikiita nikiwa bado usingizini ,Hadija akiwa hana hata moja .
Kiuvivu uvivu uliojaa uchovu nilifumbua yangu macho na kutafuta mahali simu yangu ilipokuwa na kwabahati nzuri ilikuwa ikita kwenye yangu suruali. Iliyokuwepo karibu na kitanda , taratibu nilitupa wangu mkono kwenye na kuipata.
Kuipata kule kuliendana sambamba na muito ambao ulikuwa bado ukiita , kuliniongeza kasi ya kutaka kujua mpigaji na hata nilipojua mpigaji kidogo nilileta uchangamfu wa haraka kwa muda. Kijua kilikuwa tiyari kimeshatoka ingekuwa ngumu sana kuamini kuwa bado nimelala kwa mpigaji yule ambaye hakuwa mwingine bali alikuwa Shufaa. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hello" ilisika upande wa pili ikifatiwa na maneno matamu ndani ya kinywa cha Shufaa. Kipenya kwenye ngome za masikio yangu, kuleta mabishano wa kile nilichokuwa nikisikia kwenye masikio yangu. Inawezekanaje juu ya kile ndio swali lilikuwepo likinisumbua je ni kweli mumewe hatakuwa na safari hiyo anayosema .Na ukizingatia wakati tulipokuwa Tanga alikuwa mombasa inamaana si mtu wa kutulia nyumbani muda gani anapata fursa wa kulila lake tunda uwiii!ilibidi nijiulize mwenyewe.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment