Search This Blog

Friday, July 15, 2022

FIRST YEAR - 5

 







    Simulizi : First Year

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Majibu nilikosa moyoni nikitamani kucheka juu kile miguu ikiwa nayo tiyari kujiandaa kuruka mdomo ukiwa umeshikwa kigugumizi cha grafla. Yaani maneno yake yalinipa faraja kuanzia pale hadi siku inaisha. Kitendo cha kuikata simu hakika nilijiona hakuna kama mimi bichwa liliongezeka misifa nikiamini mimi mtu mwenye bahati na handsome chuo kizima na niliweza kujiona mimi kidume mbele ya wanaume haswa.

    Kitendo cha kuikata ile simu niligeuka tena,kwenye kitanda wakati bado Hadija alikuwa amelala, tena kwa mbali alikuwa akikwaruza kuonesha bado alikuwa kwenye usingizi mzito sana. Nilitulia pale kitandani kimya nikitafakari yale maneno, mara nilihisi kitu kigumu nimekilalia kwenye mgongo wangu kinaninyima raha.Nilishindwa kuvumilia nilipasa mahali kule hatimaye nilibaini kumbe ilikuwa simu ya Hadija. Nilitoa mahali kule tiyari ikiwa imejiwasha,niliangalia simu hama kwa hakika kile nilichokutana nacho ahhhhhhhh!



    Moyo wangu ulifanya,paa! angalau nilifanya,yote kwa kudhamiria ila zile text zilinitisha sana nilijua wazi jamaa yule ana mpango wa kunifanyia umafia maana halikuwa biti dogo kabisa. Text iliyosomeka maneno ya kwamba "SASA NDIO MWISHO WANGU NIMEZOEA TABIA ILE " ndio ilinitisha zaidi.Pombe zote nilizokunywa jana usiku hazikuwa zinafanya kazi nilikuwa mimi halisi. Mikono yangu ilianza kutetemeka nikiwa nimetumbua macho kwenye kioo cha simu ile mithiri ya fundi saa. Macho yangu yalienda sambamba na mdomo wangu kuwa mzito nikitamani ni mwamshe Hadija ila jambo lile kwa upande wangu niliona zito niligugumia mule ndani ya kitanda furaha yote ilipotea.

    Sasa kichwa kilianza kuongozwa na mawazo ya kufa,kufa tu maana nilishawahi kusikia habari za Mwanachuo kuuliwa kisa mwanamke. Kutoka na mabifu tu yakijinga jinga ile ilinirudia mara kadhaa nikijitahidi kupambana nalo la lilinishinda. Nilianza kujilaumu kwanini niliamua kufanya vile "ona" sasa zilikuwa si chini ya mia zikisindikizwa na uwi!.. uwi! nyingi tu zisiokuwa na idadi. Kabla ya mikono ya Hadija kunipapasa mahali kule nilipokuwa nimegeukia kuonesha alikuwa yu tayari ameamka.

    Mguso ule ulinifanya nishituke, kitu ambacho kilimshitua pia Hadija kabla hatujaanza kuzungumza. Namna hali ilivyokwenda nilitamani sana kumdondoshea lawama msichana yule ila niliona mimi ndio mwenye kosa. Kumhukumu nikufanya kosa lingine kabisa na sikuwa tiyari kuruhusu litokee tena kwa upande wangu.



    Nilichomwambia tu kuwa awe mbali na mimi kwasababu mwanaume wake amepanga kunifanyia kitu mbaya, nilimwelezea alinisikiliza kwa makini lakini alionekana hakulizishwa na kile nilichokuwa nasema.

    Mimi sikujali nilichojua sikuwa na mpango wa kurudia tena kosa kama kufanya nimeshafanya kurudia mara ya pili ni upuuzi tena upuuzi wa kutojali. Sikutaka itokee tena nilimweleza yale nikiwa nimekaza yangu macho kuonesha msisitizo wa maongezi yale nusu saa ilitosha. Kabla hatujajianda kila moja kuitafuta njia yake. Mambo ya kurudi hosteli niliyaona mazito kwa upande wangu machale yalinicheza nikiamini sasa hapa kuwa pazuri hata kidogo.

    Uwepo wa watu wachache kukosekana kwa Izack niliona si vyema kurudi eneo lile kwasababu yule mtu alionekana amedhamiria kufanya kweli .Nilikumbuka nilivyokuwa nikiongea nae usiku wakati nipo pombe jambo lile ndio lilinizidi kunitoa imani na mahali pale ndugu Waandishi. Naweza tena kusema kitu ndugu zangu kama kuna watu wenye roho ngumu basi watu wa aina ya yule jamaa kama sikosei ,alikuwa ni Mkuliya si kwamba wakuliya ni watu wenye roho ngumu naomba nieleweke hapa ndugu zangu Waandishi inasadikia ni watu wenye chembe chembe ya ukatili mno.

    Ilinitisha mno punde tu nilipomsikia Hadija akinisihi niwe mbali na mtu yule, si mtu mzuri kabisa. Japo nilijikaza mbele yake lakini maneno yale yalikuwa kama kupigilia msumali ndani ya gunia la mahindi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilifikiria kwa kina baada ya kutoka mahali pale niliona bora niende Morogoro mjini maana vyovyote vile kesho yake nilitakiwa niwe mahali hapo. Kwajili ya Shufaa kwangu wazo lile lilikuwa sahihi kwa asilimia zote. Niliamua kujisogeza kwenye ile hoteli ambayo mara nyingi tunapenda kwenda na Shufaa ,endapo mumewe anapokuwaga amesafiri na kwa upande mwingine Shufaa anaposhindwa kuja Mzumbe.

    Ni hoteli moja nzuri ilikuwepo mafichoni ndani ya Morogoro mjini ,pale ndipo baadhi ya shida zetu tulikuwa tukimalizia na mke yule wa mtu niliokuwa nikimfanya kama wangu bila wasi wasi wowote.

    Nilifika mapema hotelini pale na kuchukua chumba na kwabahati nzuri nilikipata kile ambacho mara nyingi ndio tulikuwa tunakipenda ndani ya hoteli. Na mara zote huwa tunakiekeaga oda kabla ya kufika hotelini mule.

    Na kwabahati nzuri siku ile ilisha haraka nikiwa peke yangu ndani ya chumba kile kabla ya ujio wa shufaa usiku wa siku ya pili hapo kidogo niliweza kusahau mawazo ya yule jamaa. Yote ilitokana na raha tulikuwa tunapeana na mke yule wa mtu ,karibia wiki nzima kwenye hoteli. Safari hii ikiwa tofauti sana nikilikaa nae sana mpaka nilianza kujishitukia ila Shufaa alinitoa wasi wasi akiniambia mumewe safari ile ingemchukua siku kumi.

    Kidogo ilinitoa hofu kuendelea kula tunda, mawazo tena ya chuo yalipotea mpaka siku ya saba nilivyoachana na Shufaa. Sasa hali ya uwoga ilianza kunirudia tena pindi nilipo ya kumbuka maneno ya Hadija kuhusu yule jamaa. Yalinitisha tena na kuanza kuingia kwenye mawazo juu ya kurudi chuoni mmmh!, wakati bado nafikiria simu yangu ilianza kuiita nilishituka kutoka kwenye dimbwi la mawazo. Na kutoa simu yangu mahali nilipoiweka ahhhh!.. Izack kioo cha simu yangu kilisomeka kuonesha yule mpigaji nilipokea haraka. ila yale maneno ya izack aghhhhh!





    SURA YA KUM NA TANO



    "Huku wapi kijana nasikia uliwahi kurudi chuo kuna nini? wewe mbona kuna boya moja hapa kucha anakuja kuja chumbani kukuulizia kulikoni ndugu"maneno yale ya Izack yalisikika vyema kwenye simu yangu.

    Mapigo ya moyo yalienda kasi sana nilipigwa na butwaa kwa muda kabla sinyanyua mdomo wangu kumjibu Izack alichokuwa anakinena.

    Nilijibu kwa uwoga uwoga nikiwa najiuma uma kiukweki niliogopa sana wazi nilijua yule jamaa alidhamiria kunifanyia kitu mbaya kwa namna yoyote. Jinsi nilivyokuwa naongea Izack alibaini l lakini hakuoneshwa kustushwa. Alichoniomba tu niwahi kurudi chuoni kwasababu masomo yangenza rasmi siku si nyingi, na masuala yale nimwachie yeye atalimaliza tu. Japo nilimkubalia bado uwoga uwoga ulikuwa umenishika kwenye mwili wangu. Niliendelea kuzungumza na Izack kwa muda kidogo kabla sijaelekea stendi ya daladala za Mzumbe.

    Nilifika stendi pale kama kawaida bughudha haziisha maeneo ya stendi, bwana kuna kuwaga na mambo mengi ya kustajabisha sana ndugu Waandishi. Maana wakati nipo mahali pale nikisubilia gari lijae kama kawaida ya magari yaendayo Mzumbe. Kuna jambo lilinishangaza kweli sikuwa mimi tu hata Abiria tulikuwemo kwenye gari lilituacha mdomo wazi. Kwa namna yule kijana alivyokuwa akipokea kipigo kutoka kwa baadhi ya makonda. Ilionekana vyema hali yake isingeweza kuwa nzuri mbeleni punde tu angelitoka kwenye kile kipigo.



    Cha ajabu mwanzoni nilidhani mwizi kumbe haikuwa hivyo inasidikia yule kijana alimpiga moja ya makonda wa gari zinazofanya root zake kihonda na mjini pale. “eti walikuwa wanamfundisha adabu” aache kuonea watu nilitamani kucheka ila nilibana tu moyoni kwangu. Nikiamini kweli duniani kuna watu huwa wanapenda kutumia nguvu kuliko hata busara hekima kwenye kuamua jambo nilisahau kama na mimi ni moja wao.

    Gari nalo lilizidi kuingiwa na abiria na hatimaye dereva aliliruhusu gari kuondoka, tutikiwa tumeachwa na sitofahamu ya kile kitu kilichokuwa kinaendelea juu ya yule kijana.

    Kabla ya kugeuza mada ndani ya gari , kila mtu aliongea lake ilimradi tu alivyokuwa akijisikia na mawazo yake yanampeleka.



    Wakati huo nilikuwa kimya nikichezea simu yangu kwa mbali mawazo yalianza kunishika kadiri dereva alivyokuwa akiupunguza umbali wa eneo lile na Mzumbe, ndivyo kichwa changu kilizidi kupagawa. Nilichanganya tukio la kupigwa yule kijana stendi nikijumlisha na ugomvi uliutokea siku ile ya kwanza tulipofungua chuo na yule jamaa na ujumbe wake alionitumia nikiwa na Hadija Changalawe lodge. Mapigo ya moyo yalienda mbio tena vibaya nikihema mbaya mihemo ambayo ilimtisha hata yule niliyokuwa nimekaa nae karibu alitamani kuniuliza kulikoni? ila alimezea tu. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hatimaye niliingia chuoni nikiwa sijiamini amini haraka nilipiga hatua hadi hosteli wakati huo nilikuwa tiyari nimeshafanya mawasiliano na Izack , nilifahamu vyema Izack atakuwepo yeye kama msaada wangu.



    Vile vile nilivyopanga ndivyo ilivyokuwa nilingia chumbani nikaribishwa na izack aliyekuwa akicheka tu jinsi vile nilivyokuwa Izack alicheka sana alafu akaniambia nisijali tu mtoto mdogo yule awezi kufanya kitu. Ashazoe kupiga piga watu mikwala, wakati demu wake ndio kicheche maneno ya Izack yalinifanya nianze kupata confidence. Na uwoga ulianza kupungua amani kidogo ya moyo wangu ulianza kurejea namna nilivyokuwa nikimwamini Izack chochote alichokuwa anakisema nilikuwa siwezi kukipinga ,nilimwamini kwa kiasi kikubwa mno.

    Siku ilienda vizuri hatimaye jumatatu tulingia darasani kama kawaida tulisoma vipindi vyote.

    Nakumbuka vyema siku ile wakati tunatoka darasani sasa kurejea hosteli macho yangu yalikutana ana kwa ana na yule ndugu, kwenye ile njia ya kuelekea hostel nilistuka lakini sikutaka kuonesha wazi mbele ya Izack .Jamaa alinikunjia sura vibaya kuonesha ana hasira na mimi lakini mimi sikuonesha uwoga niliendelea kuongea na Izack nilichokuwa naongea nae. Sikutaka kushughurika naye tuliendelea kupiga hatua mpaka tuliingia ndani ya chumba chetu.

    Lakini hatukaa sana yule ndugu alikuja na kuingia chumbani kwetu bila ya kupiga hata hodi na kunivaa mia mimi nilipokuwa nimejitupia kitandani.

    Grafla tu Izack nae alimvaa yule jamaaa na kumtoa mahali pale,nikiwa nimefura ajabu maana alivyokuwa amenivamia nilitumia nguvu kujitetea. Yaani vurugu zilizokuwa zinatokea ndani mule kila moja zilimfikia wiki nzima chuoni habari ilikuwa ni hiyo.



    Bifu alikuisha karibia mwezi jamaa alikuwa akiniwinda lakini kilichokuwa kinanisaidia nikuwa na Izack muda wote.

    Nakumbuka siku ile tulipokuwa tonatoka club mimi nikiwa na Witi moja kati ya videmu ambavyo vilikuwa na urafiki na Recho. Nilikichukua tu punde tu tulipozinguana na Recho na kwa upande wake Izack alikuwa na jimaa Rose mwenyewe alikuwa akipenda kumwita hivyo, tukiwa hatuna hili wala hili tumejitanua njia nzima mara grafla .



    Ilikuja gari aina ya toyota mark 2 na kupaki mbele yetu ,katika mwendo wa ajabu ulitofanya kushutushwa kila moja wetu wakati tulijuliza kulikoni?.Mara tulivyamiwa pale pale na jamaa kama wanne hivi walikuwa wamejazia mno japo ulikuwa usiku mnene kama saa saba hivi kama si nane ila miili yao ilivyo niliweza kuibaini. Tulishangaa tu wale wanawake wakiwekwa pembeni jamaa wale wakiendelee kutupakia migumi katika wa miili yetu. Ukweli kile kipigo kilikuwa cha kufa mtu maana nilijitahidi kijitetea kwa upande wangu ila mambo yalikuwa magumu si kwangu mimi hata Izack.Nilikuwa nilizisikia sauti za upigaji wa kelele za maumivu kabla yakipoteza nuru yaani kupoteza fahamu kabisa kwa upande wangu nilizima grafla. Kipigo akikuwa cha kawaida kabisa ndugu waandishi unaweza kufanisha na kile kipigo nilichokishuhudia mwenzi uliopita wakati nipo stendi ya magari ya kuelekea Mzumbe siku ile hakika kilikuwa kipigo cha haja.

    Ameamka!!! daktari nilisikia sauti lie ikipenya ndani ya masikio yangu punde nilipofumbua macho yangu japo kwa tabu. Nikiwa na mipira ndani ya pua yangu niliangalia pembeni hapo niliona mashine ya gesi akiwa ameunganisha na mipira ile pembeni yake pale mwili wangu ulipojilaza juu ya kitanda kile kidogo. Ndani ya chumba kile wakati huo sikuweza kujua nilikuwa mahali gani ila baada ya kuangaza huku na huku hatimaye nilibaini ilikuwa hospitali na yule aliyekuwa akinena yale alikuwa muuguzi wa hospitali ile.



    Nimefikaje? ndio ilikuwa kauli yangu ya kwanza, kinyonge niliweza kutamka. Muda huo huo nilikuwa nikihisi mtu aliyekuwa akiitwa na muuguzi yule kuwa ni daktari. Alikuwa tiyari ameshafika kunitazama wakati huo nilichouliza hata akikujibiwa.

    Lakini nilishangaa mtu yule akiniambia kuwa nitulie kwanza, akitoa ile mipira kwenye pua yangu. Tiyari nilitaka kuamka mahali pale masikini viungo vyangu vilikuwa vizito kunyanyuka, cha ajabu nikiwa nimepungua sana nilijishangaa. Maumivu nayo hayakuwa mbali niliaanza kuyasikia katika upande ule wakushoto wa mbavu zangu. Maumivu makali niliyokuwa nikiyasikia yamkini yalianza kunirudishia kumbukumbu mara ya Mwisho kabla sijafika pale ilitokea nini?. Nilikumbuka kipigo kikali kile kilichotokea siku ile, hapo sasa nikakumbuka nilikuwa na Izack. Yuko wapi? Izack ndio swali lililonijia, niligeuka upande ule wapili lakini sikuweza kumwona mtu. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Daktari yule alitoka na kurudi na kifaa fulani hivi, hata sikujua akiwa sambamba na muuguzi.

    Nilishanga tu akinichoma sindano iliyonifanya maumivu niliyokuwa nikiyasikia kuongezeka maradufu. Kabla ya usingizi kunichukua usingizi ambao hata sikujua nilitumia muda gani kulala ila nilivyostuka macho yangu yalionana sambamba na Shufaa. Aliyekuwa akitokwa na machozi, vile nilivyofumbua macho Shufaa alinishangaa nakuita jina langu kwa sauti ya pole "Salimu" niliitika huku yale maumivu sikuweza kuyasikia kama ilivyokuwa awali. Grafla tu neno “ilikuwaje?” lilifatia kutoka upande wangu na kumwelekezea Shufaa.

    Aliinamia chini kisha kufuta machozi yalikuwa tiyari yanaanza kumdondoka “Vipi Shufaa” niliuliza tena alinua kichwa chake na kuanza kuniambia kuwa ilikuwa hadithi ndefu sana na pale nilipo nilishakaa mwenzi moja tangia nilipoletwa.



    SURA YA MWISHO



    Madaktari wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha yangu maana kile kipigo tulichopokea kutoka kwa wale watu nilikuwa siwajui pindi tunatoka club akikuwa cha kwaida walidhamiria kutuua tu maana shufaa pindi alipokuwa anaongea. Aliniambia kuwa Izack alipoteza maisha pale pale pindi lile tukio linatokea na walishamzika takribani mwenzi. Maneno yaliningia kwenye ngome za masikio yangu hakika yaliniumiza mno maana yalinichoma habari za kifo cha Izack kilinichoma sana. Na vipi? habari zile azikuenea sehemu nyingine maana ile haikuwa kawaida kabisa nilitamani kumuuliza Shufaa kwa muda ule ila alishindwa kuendelea kuongea tu maumivu makali yalianza kunirejea tena.

    Kabla sijasema kitu nilimwona daktari akisogea eneo lile taratibu nilimsikia akiongea na Shufaa maneno ya kumtaka kumpisha eneo lile. Na kama ingewezekana angelejea siku inayofata maana ilikuwa jioni sana kwa muda ule. Hakutaka kupingana na maneno ya daktari yule alichofanya

    aliondoka nakuniacha na maswali kibao ndani ya kichwa changu.Maumivu ya mbavu hayakuacha ijapo sikuwa na tatizo la kidonda chochote ila mbavu na kichwa ndio vilikuwa vinaniletea maumivu makali, ijapokuwa sikuwa daktari niliamini yale ndio matatizo yalikuwa yakinisumbua sana kwa upande wangu.

    Daktari yule aliendelea na vipimo huku akiniuliza hali yangu ninavyojisikia kabla ajaondoka. Nausingiza kunipitia usingizi ulisabisha kuota ndoto mbaya mno nilistuka nikihema juu sikujua kwanini niliota jambo lile ahhhh dah !!!!





    Mihemo ile haikuwa ya kawaida kabisa ilizidi kuongeza maumivu ndani ya mwili wangu maana ile ndoto iliniogopesha mno. Yaani nilikuwa nikiota ujio wa sura ya Mumewe Shufaa mahali pale huku ikiwa imejikunja kuonesha hasira na mimi. Mikono yake akishika vizuri ile bunduki yake kwa ukali akiniuliza maswali ambayo hata kuyakumbuka kwa kipindi hichi siyakumbuki ila ninachokumbuka namna ya ulizaji wake maswali ulinitisha kabisa. Naweza kusema ilikuwa kama fumanizi la mwenye mali kwa mwizi wake maana ndugu yule alivimba mno jambo liliniogopesha sana na kuamka nikiwa na hema kama jibwa koko vile.

    Hali ile ya taharuki iliniongezea maumivu ilinifanya nipige kelele hovyo tu pale kwenye kitanda mikelele ya kuugulia kile ilichukua nafasi kwa muda ule hatasikujua saa ngapi niliweza kunyamaza. Ninachokumbuka kama kuna muda alikuja daktari yule na kunichoma sindano. Sindano ambayo ilinisababishia usingizi mzito sana nakumbuka vyema siku iliyofatia,nilisikia mtu akinitingisha tingisha kuashiria kuniamsha japo nilichelewa kidogo lakini niliweza kuamka nikiwa mzito vibaya. Taswira niliyokutana nayo haikuwa nyingine bali alikuwa ni ya Shufaa sikujua muda gani alifika pale ila ujio wake ulifanya niachie kitabasamu kilichojaa uchungu mbele ya mboni zake wazi wazi juu ya kile nilichokuwa na kisikia hakika hakikuwa sawa hata kidogo wakati huo.

    Hata chanzo sikijua kwanini ilikuwa vile maswali kibao nilikuwa nikijuuliza kabla sijapata kufahamu ukweli wa jambo lile lilikuwa likinitesa karibia mwezi mzima dah!. Ama kweli majuto ni mjukuuu na mwisho wa utamu huwa mchungu wahenga hawakosea hata kidogo. La asiye sikia la mkuu huvunjika guu ni wazi kabisa, nilikuwa nimevunjika guu.

    Mdomo wangu ulikuwa mzito kutamka jina la Shufaa punde tu taswira yake nilipoiyona lakini kabla sijazungumza chochote Shufaa aliniwahi na kuniambia ni amke iliaweze kunipatia kile alichokuwa ameniletea kwajili ya kula. Japo hamu ya kula ilikuwa haipo upande wangu ila nilijitahidi kwa kiasi fulani kuweza kula kile cha kula. Mpaka pale nilipoona sasa nimetosheka ingawa si kula sana ila yamkini kilipita pita hivyo hivyo tu kwenye tumbo langu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kimya kilitawala baada ya lazimisha lazimisha ya kula kwa dakika kadhaa nikibaki kumtumbulia macho tu Shufaa, ambaye machozi yalishaanza kumtoka machozi ambayo yalinifanya hata mimi nilikuwa naumwa kuongeza uchungu zaidi. Kabla ya Shufaa kuendelea kuniambia yale ambayo nilikosa majibu “Sikia Salimu, Izack alikufa kutokana na tukio lile na hakuna yoyote ambaye alikuwa anafahamu zaidi ya mimi na wale wanyama naweza kusema hivyo punde tu lilipotokea hili ujui sababu ilikuwa nini najua mimi. Mume wangu ndio mhusika wa yote” Aliongea Shufaa machozi yakiwa yanamtirika jambo ambalo linishitua zaidi mumewe ndio mhusika kivipi? swali ambalo liliniumiza kwenye kichwa changu kabla sijapata majibu punde shufaa alipoendelea kunena yale mbele yangu.

    Alijikohoza kidogo huku akiwa amebanwa kama na kwikwi ,ngome zangu za masikio zilisikia vyema lile.

    ‘Mume wangu ndio aliyapanga yale baada ya kubaini mimi natoka nawewe kimapenzi habari ambazo nafikiri alizipata kutokana na uchunguzi wake mwenyewe ambao mpaka ninavyokuambia sielewi Salimu. Ilikuwaje lakini nahisi kuna baadhi ya wanachuo wenzako wanahusika juu ya hili”Aliongea tena Shufaa maneno ambayo yalinishanganya hapo nikaanza kumbuka ugomvi na baadhi ya wanafunzi wenzangu kama yule bwana wake Recho na yule Hadija, jamaa ambaye tuliwahi kushikana mashati siku za nyuma na ikabaki Utaona..... utaona tu dah!. Yaani nilichoka jambo ambalo linifanya niinue kinywa changu kutaka kufahamu kwanza pale ni wapi na vipi wazazi wangu wanajua na Shufaa inakuwaje habari za mumewe, ndoa ndio imekufa au la ndugu waandishi.



    Aah aiseeh!!!! ililikuwa pigo takatifu pale hapa kuwa Morogoro ilikuwa ndani ya Mkoa wa Tanga ndani ya Hospitali moja hivi wilayani Muheza aliniambia Shufaa yakuwa punde alipozipata taarifa zile. Ambazo alivujishiwa na Moja ya wale walinifanya jambo lile huku akificha kufahamika na kudai pesa ndefu. Ndipo alipofika haraka eneo lile ambalo nilikuwepo na kuja moja kwa moja kunikuta katika hali mbaya huku mwili wa Izack ukiwa haujulikani ulipo. Baadae aliweza kufahamu Izack alikuwa amefariki. Na pale tulipo hakuna aliyekuwa anafahamu tupo eneo lile maana saka saka ilikuwa kubwa dhidi yake kutoka kwa mumewe alikuwa amedhamiria kumuua kabisa. Maneno yale yaliingia vizuri kwenye ngome za masikio yangu nakuongeza maumivu kutoka kwa kile nilichokuwa nakisikia.

    Maneno yale yalikuwa si machungu tu kwangu kwa Shufaa pia ilikuwa vile vile sikuweza kujua upendo gani alikuwa nao yule mke wa mtu. Lakini nilichokuwa najua mambo ya kuwa na mke wa mtu sasa yalikuwa yamenitokea puani hali yangu haikuwa nzuri hata kidogo.



    Shufaa alizidisha vilio, vilio vilimfanya muuguzi kuja kumtoa eneo lile na kumtaka arudi nyumbani na arejee kwa siku nyingine ahhhhhhhggggg!!!Ndugu waandishi kama ningelijua ile ndio ilikuwa safari yake ya mwisho Shufaa nisingekubali yule muuguzi amruhusu Shufaa kuondoka eneo lile dah!!! Ile ilikuwa ndio mara yangu ya mwisho kuiona sura ile ya yule mke wa mtu.

    Siku ile ilienda haraka na hata siku ya pili ilikuwa vile na hapo hata sikumtia machoni Shufaa. Nilipiga moyo ukonde lakini ilikuwa wapi, wiki ilikata na hata nilianza kupoteza matumaini ya kumwona Shufaa mawazo yalinitawala kuongeza ugonjwa hatimaye mwezi wa pili ulikatika nikiwa kitandani pale. Hali yangu ikiwa dhoofu wakati huo hata nilipojaribu kuulizia habari za Shufaa daktari alinipiga chenga mpaka siku moja katika ya mwezi ule wapili nikiwa bado kitandani daktari alikata shauri na kuniambia ukweli. Yakuwa Shufaa alipoteza maisha tangia siku ile ya mwisho nilionana nae aligongwa na gari wakati akijaribu kuvuka balabala dah! jambo lile liliuchoma sana moyo wangu na kupoteza kabisa furaha yangu kabisa huku nikifiria aibu ile mbele ya wazazi wangu.



    Yale yote yalikuwa ni maneno yalikuwa katika njia ya sauti na vipande vya picha ndani ya mkanda ule, ulisomeka kwa jina la FIRST YEAR (the last page of my life). Mkanda ambao uliwafanya uwatoe machozi na vilio vya kwikwi wanachuo wale wa mwaka walikuwa ndio kwanza wanakaribisha ndani ya chuo kile cha MZUMBE. Ndani ya mkoa wa Morogoro katika siku ile ya kuudhimisha Kumbuku ya kifo cha mwanachuo yule kilichotokea miaka kutokana na Msongo wa mawazo na ugonjwa ule ambao haukuweka wazi pale mwazoni na daktari ila ilibainika alikuwa ameathirika. Hivyo kukosa nguvu mwili kudhoofu punde tu baada ya kuyanena yale aliyokuwa ameyadhamiria kama funzo kwa jamii mbele ya waandishi wale miaka kadhaa iliyopita hakika iliwahuzunisha wote na kubaki kama historia kwa ushujaa alikuwa ameufanya ilijamii iweze kujifunza juu ya lile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    NAAM!!!!HUU NDIO MWISHO WA MKASA HUU, HAKIKA ILIKUWA NI FIRST YEAR. UKWELI NILIANDIKA HUKU NIKIWA NAPATWA NA HISIA KALI WAKATI MWINGINE NIKITOA MACHOZI.WA HIKI NILICHOKUWA NIKIKIANDIKA SHUKRANI ZIWAENDEE WOTE AMBAO TULIKUWA PAMOJA TUKIFATIRIA KAZI HII.



0 comments:

Post a Comment

Blog