Simulizi : First Year
Sehemu Ya Tatu (3)
Tulitulia kidogo kuweka mambo sawa kabla ndugu Salimu ajaendelea kutupatia kile ambacho kilimsibu katika maisha yake. Ndugu wasomaji hali ile ilikuwa inatisha kiukweli machoni ililihitaji ukomavu sana. Na kama kuna kazi ngumu tangia nikutane nayo kwenye kazi yangu ya uandishi basi hii ilikuwa ngumu si kwa upande wangu, hata ndugu mwandishi mwenzangu alikili wazi wazi kile kilichomkuta ndugu Salimu hakikuwa mkasa wa kawaida.
Alitutupia macho ndugu Salimu kuashiria kuendelea kile alichokuwa anakizungumza. Tulivyovuta umakini tena kwa mara ya nyingi ilikuhakisha tunachukua kila kitu kutoka kwa ndugu yule.
Hatimaye baada ya siku kadhaa tuliweza tena kuonana na Recho punde tu alipolejea tena chuo. Kutoka kwenye msiba kiukweli siku ile ilikuwa tamu sana kwa upande wetu tulitafuta kisehemu baada ya masomo kuzungumza mambo yetu. Kweli kila mtu alionekana yu na furaha sana, tulizungumza mengi tukiekeana ahadi kibao za mapenzi. Kila moja wetu hakutaka kumpoteza mwenzake. Nafikiri uzuri wangu wa muonekanao ulikuwa chachu sana kwenye penzi lile. Unajua ndugu Waandishi katika dunia ya mapenzi haswa wanawake wazuri wanapenda kuwa na wanaume wazuri.
Hili ndio jambo ambalo lililonifanya nipate usumbufu sana pale chuo punde nilipoanza masomo yangu . Uzuri ule wa Recho basi aliona mtu sahihi wa kuanae ni mimi. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Suala la wivu likachukua nafasi naikumbuka vyema siku ile wakati tukiwa kwenye maongezi. Simu yangu iliita nilipokea na kupokea kule hakuwa kwa kawaida nilizungumza kwa muda kidogo. Kabla sijarudisha kinywa changu kuendelea na maongezi na Recho, hakuwa mwingine ambaye alitibua furaha ya Recho muda ule pekee alikuwa Shufaa. Yule dada nilikutana nae kwenye gari wakati nakuja Morogoro baada ya kipindi kirefu hatimaye tulizungumza. Kuzungumza kule niliona inaweza ikawa tabu pale hivyo mazungumzo tulikatisha licha hamu ya dada yule ilikuwa bado imenitawala. Nilikumbuka mengi ila sikutaka kuonesha wazi pale mbele ya Recho.Nilikata simu yangu na kumtazama Recho kwa mara nyingine ila muonekano wake ulitosha kubaini jambo. Nilimtoa wasi wasi hatimaye alinielewa hivyo tukaendelea na maongezi yetu kama kawaida.
Ikiwa jioni kabisa kigiza nacho kilishaanza kuingia kwa hamu aliyokuwa nayo Recho aliniomba twende tukapumzike wote. Na namna yoyote ile nisingweza kukataa ombi lake , nilikubaliana nae ila nilimpigia simu Izack ilikumpa taarifa dakika kadhaa Izack alipokea yangu simu. Punde nilimpatia taarifa ile Izack alibaki tu akicheka, akinitupia maneno ya kunichombeza kabla sijaikata simu kuashiria nimemaliza yale niliyokuwa nataka kuzungumza.
Nilimwangalia Recho namna tulivyokuwa tunatazamana ilikuwa wazi kila mmoja wetu alikuwa anahamu na mwenzake.
Mtazamo ule ulikuwa ni zaidi ya mtazamo kiaibu aibu fulani kilijionesha dhahiri ndani yetu. Tamaa na uchu wa kile tulichokuwa tunaenda kukifanya kili tutawala ndani yetu kila moja.
Kigiza nacho kilikuwa kimeashaanza kuingia hivyo hata sikujua ilikuwaje ila hatimaye tulianza kubadilishana yetu midomo pale pale. Kweli lile zoezi lilkuwa tamu sana ndugu Waandishi ogopa kuwa limbukeni wa mapenzi na kama si kuwa limbukeni wa mapenzi. Basi ogopa kuyafahamu mapenzi ukubwani ni tatizo haswa,na kwa upande wangu lile lilikuwa tatizo sana.
Kile kitendo kilidumu kwa dakika kadhaa kabla masikio yetu hayajasikia hatua za watu zinasogea maeneo yale. Tuliamua kuchukuzana kwenda mahali ambapo akili ya Recho ilishapanga .Alipotoa wazo la kwenda kupunzika , tulitumia nusu saa tu mpaka eneo lile. Njia nzima tukiwa tumeitawala sisi nilishika chake kiuno na yeye alishika changu kama walevi vile tulikokotana mpaka mahali pale.
Tuliandikisha majina pale mapokezi ndani ya logde ile kabla mhudumu kutuonesha mahali kilipo chumba. Nikiwa mara yangu ya pili kwenda sehemu kama zile nilijikuta tu nimezoea hali ile hata habari nilikuwa sipati. Tulikuwa tunaponda raha na Recho kiukweli Recho alikuwa anapesa kweli. Mwanaume nilikuwa nahudumiwa kila kitu na kama ningejua kuwa vya bule vinaponza haki nisingekubali yale yote. Ndugu Waandishi waswahili hawakukosea kabisa kusema mpenda vya bule mwisho wake humtokea puani. Raha zile sikujua kama itafika siku zitanitokea puani kabisa.
Usiku ule ulipita kila moja akionekana bado hajalidhika na kile kilichotokea na hata mipango ya kurudi chuo tena. Kwa siku iliyofata ilikuendelea na masomo haikuwepo, hakuna wazo liloitwa shule tena nikiwa kama nimelogwa vile. Recho alinitawala mpaka basi ule mchezo wake ndio ulikuwa ukinimaliza vibaya hata sikuwa tena nafikiri kitu kingine zaidi ya raha zake. Simu nilizima baada ya kuona kelo kutoka kwa Izack na member wengine wa class. Tulithubutu kukatiza wiki tukiwa pale kama mke na mume kila moja alifaidi mwili wa mwenzake. Kwa upande wangu kitendo kile kama kilikuwa kinanipa mazoezi kwenda kucheza mechi zingine na hapo hamu haikuisha. Pesa tu ndio ilikatisha zoezi lile baada ya wiki na zake mbili siku tutulilejea chuoni. Izack alinilaamu sana kwanini nilizima simu ila nilimpiga kiswahili alinielewa.
Wakati huo uwongo na mimi ulishaanza kunikaa sikumbuki nilijifunza wapi ila, hali ile ilikuja tu nilimuuliza habari class aliniambia tu ameweka mambo sawa nisiwe na hofu.
Wakati huo tiyari nilishaanza kufikiri kumtafuta Shufaa punde tu nilipotulia baada ya kuweka mambo sawa. Nilipiga sana simu yake ila iliita pasipo kupokelewa nilijaribu tena kwa mara nyingine ila hali ilikuwa vile vile. Sikutaka kuahangahika sana nilitulia tuli kwenye changu kitanda huku kichwa changu kikiwa kina fikiria yale yalitokea.
Zilipita siku tatu wakati huo ratiba zangu ziliendelea kama kawaida nakumbuka siku ile ndugu Waandishi. Nikiwa sina hili wala lile wakati huo nipo na Izack tunatoka kwenye kipindi nilishangaa nikishikwa bega na mtu. Nikigeuka kumtazama mtu yule ambaye hakuwa pekee yake sura yake ngumu ilinitisha. Namna macho alivyoyatumbua pamoja na yule mwenzake sikujua moja kwa moja shida yake nini? ila muonekano wake ulijaa shali kabisa. Grafla alianza kunenena maneno ambayo yalinifanya ni ogope. Sikuwahi hata siku moja kugombana na mtu kisa ‘eti mwanamke’ jambo lile lilikuwa geni. Kwa vile hatukutaka kuonesha shali mbele ya ndugu wale ilibidi tuwasikilize kabla hatunyanyua vyetu vinywa kujibizana nao. Jambo ambalo niliona wazi lingeleta mtafaruku pale,ilibidi tuwasikilize kabla hawajamaliza kile nilichoona wazi ni kitisho dhidi yangu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
SURA YASABA
Namna ya ongeaji wao ulinifanya nitafakari sana pindi tu walipomaliza yale maneno na
kutuacha na izack . Nikimpachika maswali mengi iweje? Recho awe na mtu asiniambie na kwanini? amefanya kuniingiza mtoto wa watu kwenye majanga kama yale. Wakati sumu kwenye maisha yangu ulikuwa ugomvi sikupendelea hata kidogo. Namna malezi ya wazazi wangu jambo lile lilikuwa sumu. Niliendelea kumpachika maswali ambayo dhahiri Izack hakuwa na majibu sahihi zaidi ya kumtupia lawama Recho.Kitu ambacho nilikuwa sikubaliani nacho hata kidogo na , pale Izack aliponiambia niachane nae ilikuepusha shali kile kitu mimi hakikuniingia akili kabisa.
Tulipiga hatua kadhaa huku nikiwa bado sikubaliane na hali ile. Niliitoa yangu simu mfukoni kuitafuta namba ya Recho, sikujua ninataka kuongea nae nini? ila niliona kile ninachofanya muda ule ni sahihi. Nilibonyeza kitufe cha kupiga simu punde tu namba yake ilipojitokeza kwenye kioo cha yangu simu. Nilipiga kwa sekunde kadhaa hatimaye ilipokelewa , kitendo cha kupokelewa ile simu laiti ningejua ndugu Waandishi nisingefanya vile kwa muda ule ahhhhh!...ishhhhhhhi!
Hakuwa Recho yule na weza kusema ndugu Waandishi na iweje? Awe yule niliyemzoea mimi muda mfupi kabisa upendo wake, na vipi? kuhusu raha zake na achana na hilo vipi? kuhusu maneno yake kwangu .Recho yule ambaye nilikuwa nikimfahamu mimi aliyekuwa tiyari kunipatia kila kitu siku nne na si kama tatu nilikuwa nae tukiridhishana na kupeana maraha ya ulimwengu mwingine. Maraha yalionifanya hata nisahau kile kilichonileta ndani ya chuo kile ahhh! ndugu Waandishi jambo lile lichoma moyo wangu muda tu lilivyopenya ndani ya masikio yangu.Nilihisi kama naota ndoto! Ndoto mbaya ambayo hakuna mpenzi yoyote katika ulimwengu wa mapenzi angekuwa yu radhi ndani ya fikra zake kuiota.
Najua bado hamjanielewa Waandishi kile ambacho Recho msichana wangu wa kwanza ndani ya ulimwengu wa mambo ya kikubwa alichokisema. Alipoipokea simu ambayo nilipopiga nikiwa sielewi ninachoenda kuzungumza ila nimaumivu makali niliyoyapata, punde baada ya maneno ya wale vijana dhidi yangu .Ijapokuwa walikuwa wanakatisha katisha ila namna ya uzungumzaji wao ulijaa shari dhahiri, ndani ya macho yangu na hata isingekuwa yangu basi ya Izack yaliona vyema jambo lile.
Nadhani wazi hakuwa Recho yule ndugu zangu Waandishi na hapa naomba niwaambia tena, kamwe usimuamini mwanamke katika yako maisha ilo naomba ilieleweke ndugu zangu. Recho si wa kuniambia maneno yale ‘eti yule alikuwa mpenzi wake hivyo amegundua husiano wetu nijichunge sana kutoka na ubabe wa yule kijana’’ Ambaye dhahiri niliona wazi jambo lile halikuniingia hata kidogo kabisa kwanini? aliamua kunifanyia vile Salimu mimi. Kwake alichukulia jambo la kawaida ila kwangu lilikuwa si jambo dogo kabisa linakuwaje? Dogo unajua wanawake wa aina ile wanapenda sana kucheza na mioyo ya watu ndugu Waandishi.
Maneno yale yalinifanya hata nishindwe kuongea na kuikata simu ile huku wazi muonekano wangu ulikuwa umebadilika grafla. Nilipandwa na hasira na hapo maswali yalizidi kuelekea kwa Izack a kama mwanzo alivyokuwa ameshindwa kujibu hata moja wapo ya maswali yangu na hapo hali ilikuwa hivyo hivyo. Ziliongezeka hisia kali za kuachana na Recho zikimtoka izack jambo ambalo nililiona gumu sana upande wangu.
Tulipiga hatua kadhaa mpaka hosteli huku njia nzima nikiwa nimetaliwa na mawazo ya jambo lile. Naweza kusema muda mfupi lilipoteza furaha yangu hata pale nilipofika hosteli nilijikuta na jibwaga kwenye changu kitanda. Na hamu ya kula ilipotea kabisa kwenye wangu mwili unaweza je ? kula ndugu. Hakuna kitu kinachoumiza kama mapenzi miezi miwili tu ilitosha kujua kama katika hii ,duniani kama mapenzi yanaumiza sana japo ya na raha yake ila maumivu yake si masihara hata kidogo. Nilijihisi nimekonda grafla , mwili ukipoteza nguvu kabisa wazi niliona pale kwenye kitanda change. Nikiwa nimetulia kimya , nilishindwa kusoma kama ilivyokuwa kawaida yangu baada ya kutoka class kiukweli nilishindwa kabisa.
Nusu saa zilitosha kuvumilia yale uvumivu ilinishinda nilichukua tena yangu simu nakupiga namba ya Recho. Nilipiga sana haikupokelewa nilijaribu tena kwa mara nyingine haikupokelewa tena nilitulia kidogo. Kabla simu yangu haijaingia ujumbe ambao wazi ulionekana umetoka kwa Recho.
Ndio ulisomeka vyema ndani ya kioo changu ujumbe ule naweza kusema ndugu Waandishi ulikuwa kama ukinipigilia msumali ndani ya moyo wangu.
" NAKUOMBA SALIMU KAA MBALI NA MIMI KABISA SAHAU KAMA ULIWAHI KUONANA NA MTU KAMA MIMI’’
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maandishi yale yalipenya vizuri ndani ya mboni za macho yangu sikuwa ni na amini kama kweli Recho yule ndugu Waandishi. Naweza kusema japo yale maandishi yalijieleza kama vile. Nilihisi uwenda Recho amekosea kabisa sikuwa mimi niliokuwa na stahili ujumbe ule angalau ulikuwa ndani ya kioo cha simu yangu. Niling'ata meno kwa hasira kuonesha jinsi gani nimechukizwa na jambo lile ndani ya akili yangu. Na hata hapo sikujua saa ngapi Izack alitoka ndani mule.
Nakumbuka vizuri tulikuwa wote ndani mule kabla sijajitupia ndani ya kitanda changu.Uchungu ulinipanda mpaka taratibu Machozi yalianza kunitoka. Nililia kama mtoto mdogo mimi kiukweli jambo lile liliuchoma choma moyo wangu nakunisabishia maumivu makali sana upande wangu sikuweza jua nitalizoea vipi jambo lile kwenye yangu akili.Nakili wazi wazi First Year ndio ilikuwa chanzo ya yote kama isingekuwa First Year naweza kusema yale yote yasingenitokea katika maisha yangu yanawezaje kunitokea?
Alivuata pumzi ndefu ndugu yule nakuendelea
Ndugu Waandishi katika maisha naomba mjifunze kitu maisha haswa maisha ya chuo yana changamoto sana haswa First Year ,pale ndipo unapojifunza maisha mapya. Na kama hautokuwa makini unaweza ukajikuta kama mimi hivi. Kuna mengi ambayo yamenisibu leo lazima mtayapata na nawaomba muipelekee jamii bila kuficha yote niyanenayo.
Ndugu yule aliongea kwa uchungu mno wakati huo hisia kali zilikuwa zimenishika juu ya jambo. Nilishika kifaa kile cha kurekodia huku wangu mkono ukiwa unatetemeka vibaya sikujua kwanini inatokea vile. Kwa hakika jambo lile lilikuwa zaidi ya jambo abadani mikono yangu ilijaa jacho grafla.Mwandishi mwenzangu alikuwa yu kimya taratibu akiandika vitu muhimu. Kiukweli hakuna aliyekuwa yu tayari kukatisha mazungumzo yale tulizamilia kufanya kitu, hatukuwa tayari kabisa kupoteza kile alichokuwa anakisema kijana yule.
Sikuwa tayari kuachana na Recho kwa muda ule hata nilipojalibu labda kusahau yale yalitokea nyuma ,nafsi yangu ilikuwa haitaki. Nakumbuka vizuri siku ile nilishindwa kula hata pale Izack aliponibembeleza sana nile chakula kilikuwa hakipiti kabisa mdomoni mwangu. Nilichoweza jua kabla katika hii dunia mapenzi yana nguvu sana na jeraha la penzi kamwe kupona linachelewa. Na hata kama likipona lazima liache kovu ambalo ni gumu!,gumu dhahiri kufutika hapo tiyari nilikubaliana na jambo lile.
Wiki nzima hali yangu haikuwa nzuri na hata mawasiliano na Recho niliyakosa kwasababu sikuwa na mpango wa kuiwasha simu. Na kibaya zaidi mimi na Recho tulikuwa tunasoma madarasa tofauti hivyo bila mawasiliano ilikuwa ngumu kuonana kati yetu.
Nilijikaza hivyo hivyo huku nikitiwa maneno ya kijasiri na Izack, kiugumu ugumu hatimaye hali ile ilianza kupungua. Na mipango yangu kuanza kurejea, nakumbuka ilichukua kama wiki na siku tano na hatimaye hata niliweza kuwasha simu yangu. Ambayo nilikutana na ujumbe nyingi tu ila ujumbe mbazo zilinifanya nizifikilie ilikuwa kutoka nyumbani ambawo ulikuwa wa Baba. Alikuwa akinikumbuka sana na ujumbe wake haukusita kunikumbusha kupambana kwenye masomo yangu kama kawaida yake, na ujumbe mwingine ulikuwa umetoka kwa Shufaaa ujumbe ambao ulinifanya nitabasamu sana hata nilijihisi kama kuna kitu kimeupitia wangu moyo.
Ujumbe ule bado haukunitoka ulikuwa umeandikwa hivi ndugu waandishi
"SALAMU SALIMU NAJUA ULINITAFUTA SANA. ILA HAIKUWA DHAMIRA YANGU KUTOPOKEA SIMU YAKO RAFIKI . NILIKUWA NIMEACHA SIMU YANGU NYUMBANI. MIMI NIKIWA NIMETOKA NA HATA NILIPORUDI NILIKUTAFUTA ILA HAUKUPATIKA SIJUI TATIZO LILIKUWA NINI ? ILA MPENDWA NIMEKUMBUKA SANA NA NIMEKUMBUKA SAFARI ILE YA KUTOKA TANGA.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alimaliza kwa namna ile ujumbe ule ilionifanya kipindi kifupi niyakumbuke yote tuliyafanya ndani ya safari ile. Mwanzo mwisho nilijikuta tu nacheka mwenyewe kama chizi nakuanza kuyatafakari yale kabla ya sekunde kadhaa simu yangu kuanza kuita kuangalia hivi kwenye kioo cha yangu simu sikuamini lile.
Shufaa kama kwenye yangu simu nilivyosevu jina la yule dada lilionekana vizuri juu ya kioo changu cha simu . ikienda sambamba na muito wa simu ulinifanya haraka kubonyeza kitufe cha kupokea yangu simu punde tu nakuiweka kwenye masikio yangu kusikiliza kile cha upande wa pili hama kwa hakika alikuwa Shufaa.
Sauti yake ilipenya kwenye yangu masikio mithiri ya zeze kusaidifu uzuri wa ile sauti ambayo nilisikia kwa mara ya kwanza takribani miezi miwili na nusu na kama si mitatu iliyopita. Haikunipotea kabisa namna ya uongeaji alinifanya ni amini ni yeye mwenyewe kabisa. Nusu saa ilikatika na hata lisaa kasoro kama dakika tano ama sita ndio ilitosha kumaliza maongezi na dada yule, ambaye jinsi maneno yake yalivyokuwa yakitoka kwenye chake kinywa ilionesha wazi alikuwa anamaanisha kile alichukuwa anakizungumza. Japo nilijiona mtu mwenye bahati juu ya kile ila bado akili mwangu hakuniingia.Nitawezaje mimi kuwa na mke wa mtu? naanzia wapi... na ishia wapi? hilo liliniumiza kichwa muda mfupi tu baada kumaliza maongezi yale na Shufaa!!!
Ambaye alinitaamkia wazi ananipenda na atanipa kila kitu pindi tu nitapokuwa nae, sikujuwa nilikubali vipi? lile ombi lake ila nilipoikata yake simu. Mawazo kibao yalianza kunishika nilikumbuka mikwala ya yule jamaa ambaye alikuja kunitishia juu ya Recho. Kwa kawaida tu sidhani kama yule jamaa alikuwa amemuoa Recho ,ila namna ya ujaji wake kwangu haukuwa wa kawaida. Je kwa huyu ambaye nafahamu vyema kuwa ameolewa je itakuwaje? naisitoshe mumewe si mtu wa kawaida mtu mwenye pesa zake. Na mtu mwenye pesa kwenye ulimwengu huu si mwenzako kabisa.
Ndugu Waandishi lile jambo lilinisumbua sana ,niliutafuta ushauri kwa Izack ila mwenzangu alikuwa anaona kawaida. Kwani ashazoe kuwa na wake za watu , jambo lile alichukulia kawaida sana ndugu Waandishi. Naweza kusema katika dunia hii ukiwa na rafiki mlevi basi na wewe utakuwa mlevi itokee sana usiwe hivyo. Basi ile ndio ilinitokea kwangu na laiti ningejua nisinge kubali kuwa na rafiki wa namna hile.
Aah!,hiiii! ndugu Salimu aligumumia kabla ajaendelea kutupatia kile alichokuwa anakisema tulizidisha umakini tena kwa mara nyingi. Tukiwa tunahamu ya kujua kile kilichomtokea kimya kidogo kilitawala kabla ya kuendelea ndugu Salimu kunena.
Baadae nilichukulia kawaida tu kwa mbinu alizonipatia izack niliona suala lile linaweza kuwa gumu kujulikana wakati huo tiyari maisha yalishanza kuwa mazuri sana kwa upande wangu pesa zilianza kucheza tofauti, hata ambavyo Recho alivyokuwa akinihudumia Shufaa alikuwa anapesa mbaya yaani ilikuwa balaha sana hata kunakipindi niliweza kutumia zaidi ya laki kwa siku moja huku visichana ambavyo vipenda pesa viliendelea kujigonga gonga huku nikichagua baadhi yao kuwa navyo kimapenzi huku nikiwapa masharti magumu sana ikiwemo nilikuwa sihitaji mahusiano yangu na wao kujulikana kiukweli mchezo ule ulikuwa mtamu kwa upande wangu hata Recho nilimsahau.
Mwanamke ambaye nilikuwa nikimfikiria ni Shufaa ambaye alikuwa ndio kila kitu muda mfupi tu pindi nilipoanza mahusiano na mke huyo wa mfanya biashara mkubwa.Ubaya ilikuwa kazi sana kupata huduma yake na hata siku nilipopata huduma yake ndugu Waandishi. Ninaweza sema kama kutatokea mwanamke ambaye anajua mapenzi katika maisha yangu basi Shufaa alikuwa zaidi ya wote. Anakila kitu ambacho mwanaume akimpatia hawezi kuchepuka hata kama angekuwa ni bingwa wa michepuko basi hapo angepiga salute. Na kurudisha zipu yake pindi tu afunguapo kwa mwanamke mwingine yule ndio alikuwa shufaa mwanamke aliyejaliwa kila kitu .CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Naikumbuka siku ambayo nilipata fursa ya kuongoza safari ya maraha nikiwa na Shufaa alionekana fundi zaidi yangu. Kiukweli licha ya kukutana na wanawake tofauti kabla sijakutana na Shufaa ila siku ile nilijihisi si lolote si chochote kwake. Dakika tisini za mpambano ule nilikuta na chezea kipigo cha kufaa mtu nakili wazi sikuweza kuendana kasi ya mchezo ule. Ila nilichojua Shufaa alikuwa yuko vizuri kuliko wanawake wote ama kwa hakika ule mchezo kama ningejua mwanzo nisingekubali kubali ,ndugu Waandishi aaaah! lile nalo lilikuwa kosa kwenye maisha yangu.
SURA YA KUMI
Ndio lilikuwa kosa kabisa kwa upande wangu utamu wa mke yule wa mtu ulinifanya nisahau shida zote kwa muda mfupi. Sikuweza kukumbuka kama nyumbani waliniagiza nini nilichojua nikuvizia siku mumewe Shufaa akiwa amesafiri kwenye miradi yake ,mimi kupata nafasi ya kuburudika na mwanamke yule. Ndugu Waandishi naweza kusema waandishi wengi wa fasihi achana na nyinyi waandishi wa habari ,na wazungumzia watu kama kina Shaban Robat au nani huyo Edwin Semzaba na kina Profesa safari. Kwenye fasihi zao nyingi haswa hizi riwaya na tamthiliya wanazungumzia wanawake katika mtazamo tofauti ila ule mtazamo wa mwanamke kama chombo cha starehe hawakukosea kabisa !
Wanakosea vipi? Wakati jambo hili kwangu lilikuwa wazi namna nilivyokuwa nikimtumia Shufaa hakika ilikuwa starehe tosha. Iliyonifanya nisahau yote kiukweli na kujiingiza kwenye dhambi hii ya kuiba mali ya mtu ambaye sikuwa nadhani ipo siku isiyokuwa na jina kama itanitokea puani.
Siku nazo zilikuwa zimeenda sana na hatimaye tulifanya mitihani ya kufungia chuo na kwa bahati nzuri nilifanya vizuri japo si kwa sana. Ila ilikuwa ikilidhisha mbele ya macho yangu na kunipa bichwa ya kuendelea kufanya yale ,ambayo mwanzoni nilikuwa nikayaona yako sawa ila sasa najuta kwanini ilikuwa vile katika maisha yangu.
Kumaliza kule mitihani kulienda sambamba na kufunga chuo ambapo wiki mbili ndio ilikuwa halali yetu katika likizo ile. Hamu ya kurudi nyumbani kumwona Mama ilinijia ila nilivyokuwa nikikumbuka maisha ya nyumbani safari nilianza kuiona noma .Nilijikaza tu baada ya Shufaa kuniambia niende tu kwasababu na yeye baada ya wiki angelikuja kule, hivyo tungepata tena wasaa wakupeana yetu maraha hivyo kutokana na ushawishi wake nilikubaliana nae.
Siku iliyofata baada ya kufunga chuo mipango ya kurudi nyumbani nilifanya na hatimaye saa tisa niliingia ndani ya mkoa wa Tanga.
Kabla ya nusu saa kuingia nyumbani na kupokelewa kwa furaha na Mama na baadhi ya ndugu zangu niliwakuta nyumbani pale furaha iliyokuwepo pale. Kwa muda ule ilikuwa haielezeki Mama alifurahi sana nilimwona wazi Mama yangu ,na kwa vile nilikuwa nikimfahamu vyema hivyo jambo lile nilibaini wazi wazi. Mama yangu alikuwa akinipenda sana akiamini nilikuwa tegemeo lake katika maisha ya familiya yetu na sijui kwanini? nilimuangusha sitaki kukumbuka jambo lile lina nitia uchungu sana kwenye wangu moyo. Natamani hata siku zingerudi nyuma kufuta yale makosa niliyoyafanya lakini hakuna linalowezekana ,majuto ni mjukuu leo hii ninajua ukweli wahenga hawakosea kunena.
Kwa upande wa Baba niliona nae baada ya kutoka kazini nae pia alionesha kufurahi juu ya ujio wangu.
Akiuniliulizia sana maendeleo yangu ya chuo na maisha kwa ujumla ya chuo nilikuwa nikiyaonaje? Kama kawaida yangu uwongo ulichukua nafasi kwenye sehemu hiyo kwa mara nyingine tena .Ilikumwondoa wasi wasi na shaka Baba juu ya maisha yangu ya chuo kutokana Baba alikuwa akiniamini sana hakuonesha hata chembe ya kunitiria shaka. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maisha ya nyumbani siku tatu yalinichocha kwasababu kama kawaida ndani,Msikitini ratiba azikubadilika zilibaki vile vile. Hata pale Shufaa aliponipigia simu baada,ya siku ya tano tangia nifike Tanga akiniomba nitafute hoteli kwa jili ya kufikia ,kwa siku hiyo kabla ajakwenda kuwaona wazazi wake jambo lile lilikuwa gumu sana kulikubali. Japo nilikuwa nina hamu na utamu ule wa mke yule wa mtu ila suala la kutoka nyumbani ndio lilikuwa gumu nitawezaje? kulala nje ya nyumba ile wakati hata siku moja sikuweza kulala nje ya nyumbani kwetu na hata kwenda kwa anko nguvumali mchana tu ilikuwa kazi.
Je kwa siku hiyo ingekuwaje? ila jamani ushawishi wa Shufaaa ulinifanya nifikilie jambo juu ya lile. Na hata sikujua nini kilikuwa kinanisukuma kufanya vile ndugu Waandishi. Chonde chonde duniani hapa kuna wanawake wana ushawishi wahali ya juu unaweza ukafikia hata kugombana na wazazi wako kisa mwanamke jamani lile jambo sijui ilikuwaje? nyie aah!
Uwongo ule uliojengeka baada ya muda mfupi kufikiria juu ya jambo lile hakika ulikuwa mtakatifu sikujua Mama atachomoka vipi? juu ya kile nilichopanga kuzungumza mbele yake kabla ya Mzee ajarudi. Maana yeye angekuwa kipingamizi juu ya kile nilichopanga yote ilikuwa kwa jili ya Shufaa.
Nilijiuliza mara mbili mbili kile nilichonacho kinatosha kweli nilipoona ni kweli kinatosha nilimfata Mama kwa utaratibu kumweleza dhamira yangu. Kwa unyonge na kuonesha nimeguswa na kile nilichokuwa nakitoa ndani ya kinywa changu.Mama alinielewa mapema na hata kunipa ruhusa huku akiniambia nifanye vyovyote kwa jili ya kile , Nilijiona mshindi kwa muda mfupi moyo wangu ulifalijika kwa namna maneno ya Mama yalivyokuwa yakipenya kwenye yangu masikio kuonesha amekubaliana na kile.
Ndugu Waandishi najua amjajua niliamua kufanya nini? juu ya kile ila kile nilichokuwa nikisema kwenye kinywa changu akikustahiri kabisa katika hali ya kawaida. Na hata kama uwongo sio uwongo wa namna ile wa kumsingizia mtu kapata ajari tena mbaya mtu ambaye Mama alifahamu tu kupitia Simu. Ile ilikuwa dhambi kubwa ,nilikubali kuifanya wakati nikifahamu misingi ya dini si ya kwangu mimi dini zote kwamba uwongo ni dhambi tena dhambi kubwa.
Dakika tano tu zilitosha kujianda punde nilipomaliza yale maongezi si kutaka kukaa pale tena. Haraka haraka huku Mama akioneshwa kuguswa na jambo lile, muonekano wake wazi ulionesha kuguswa na uwongo ule. Na hata Mimi sura yangu ilionesha upole ndani ya mboni za macho ya Mama, hivyo kwa namna yoyote asingeweza kutia shaka juu ya kile.
Nilimuwaga Mama na kuianza safari ile ambayo ramani ilishajichora kichwani ni Mkonge hoteli.
Hoteli ya kitalii ambayo nilizoea kuiyona tu kwenye tv,sikuwa na waza kama siku moja na mimi nitapata fursa ya kuwa mahali pale katika yangu maisha. Zali kama lile lilivyotokea moja kwa moja hoteli ile ndio ilikuwa chaguo langu la kwanza.
Baada ya kupiga hatua chache kutoka nyumbani niliitafuta boda boda ilipo mpaka mjini sikutaka anipeleke Mkonge hoteli moja kwa moja, nikihofia anaweza akawa ananijua alafu ikawa tatizo nyumbani. Baada ya kuniacha pale mjini nilichepuka kidogo nalichukua tax hadi mkonge hoteli wakati huo niliendelea kuwasiliana na Shufaa ,katika kila nilichokuwa na kifanya hatua kwa hatua.
Nilingia hotelini huku nikishangaa madhari ya pale yalivutia mno kila pembe ya ile hoteli.
Nilipiga hatua nikiwa na pishana na watu wa aina tofauti tofauti ambao walikuwa wakiendana na hadhi ya mahali pale, wazungu wakichanganyikana waswahili wachache mboni zangu ndio zilikuwa zikikumbana na twasira hizo.
Taratibu mpaka sehemu iliyosomeka MAPOKEZI kwa vile si mara ya kwanza kwenda hotelini mahali pale nilifahamu kuwa taratibu zote hufanyika. Nilijivuta eneo lile nikikaribishwa na tabasamu mwanana la dada ambaye nilifahamu vyema nifanyakazi wa hoteli ile.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliendana vyema na hadhi ya mahali pale naweza kusema hivyo namna alivyokuwa amependeza ilitosha kabisa. Huku nikimpiga jicho la matamanio nilinyanyua changu kinywa na kueleza kile nilichokuwa nakitaka muda mfupi, nilipewa maelekezo na kwa kuwa Shufaa alishanitumia pesa nilipa kabla sijaoneshwa mahali pale ambapo kulikuwa kunavutia mno. Hakika kile chumba kilikuwa kina kila kitu, ambacho unaweza ukasahau shida zote za duniani kibaridi kile ndani ya chumba kile kiliweza ku ukonga moyo wangu vibaya mno.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment