Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

QUEEN OF THE GORILLAS ( MALKIA WA MASOKWE ) - 4

 





    Simulizi : Queen Of Gorillas ( Malkia Wa Masokwe )

    Sehemu Ya Nne (4)





    LINDA, mtoto kutoka familia ya kitajiri, yupo juu ya ghorofa refu la Hospitali ya Oklahoma Medics na anataka kujirusha hadi chini ili afe baada ya kipenzi cha moyo wake, Harrison kumkana kanisani siku ya ndoa



    yao. Linda anatoa sharti moja kuwa mpaka Harrison atakapokubali kumuoa ndiyo atabatilisha uamuzi wake wa kujiua.



    Upande wa pili, vyombo mbalimbali vya habari vinaripoti tukio la ajali mbaya iliyotokea kwenye Daraja la Miami. Mtu anayesadikiwa kuwa ni Harrison, anapata ajali mbaya akiwa anaendesha pikipiki na mwili wake unaokotwa ukielea baharini.



    Habari hizo zinawashtua watu wote waliokuwa wanamfahamu Harrison, wanakimbilia eneo la tukio ambapo ushahidi wa pikipiki aliyokimbia nayo Harrison pamoja na mavazi ya harusi aliyokuwa ameyavaa, unafanya kila mmoja aamini kuwa Harrison amekufa.



    Hakuna anayejua kuwa kila kitu kimetengenezwa na Harrison kwa kushirikiana na rafiki yake Rogers, ambao wanatumia mbinu za hali ya juu kucheza na akili za watu. Akili ya Harrison ipo kwa msichana



    mrembo anayeishi na masokwe ndani ya msitu mkubwa wa Tongass. Ndoto zake ni kumuoa msichana huyo.



    “LINDA, Linda! Kuna habari tumezipata muda si mrefu kumhusu Harrison.”

    “Sitaki habari zozote, namtaka Harrison aje hapa.”

    “Tusikilize kwanza, ni muhimu ukajua kinachoendelea kwani tunaamini ulikuwa unampenda sana Harrison.”

    “Bado nampenda, nimesema hapa siondoki mpaka aletwe,” alisema Linda na kuwakata kauli maafisa usalama wa hospitali ile ambao walikuwa wanataka kumfikishia habari za ajali aliyoipata Harrison.

    “Jamani tufanyeje? Inaonekana hataki kuelewa chochote.”

    “Mi nashauri runinga moja iletwe huku juu haraka iwezekanavyo kabla habari za ajali aliyopata Harrison hazijaisha,” alisema mmoja kati yao, utekelezaji ukafanyika mara moja.

    Runinga ndogo ikaenda kuchukuliwa kutoka kwenye chumba kimoja cha ghorofa ile na kupandishwa mpaka kule juu kabisa alikokuwepo Linda na watu wengine. Waya mrefu ukatumika kuiunganisha kwenye umeme kisha ikawashwa na kuwekwa Kituo cha CNN.

    “Tunaomba uangalie mwenyewe kinachotangazwa,” alisema mmoja kati ya wale maafisa huku akimgeuzia Linda runinga. Kwa muda wote huo, wazazi wake walikuwa wameshapata taarifa za kifo cha Harrison na walikuwa njiani kuelekea eneo la tukio kwenda kuthibitisha kama kweli walichokisikia ni sahihi.

    Baada ya kugeuziwa runinga ile, Linda alishtuka kuliko kawaida kwa alichokuwa anakiona. Ilibidi mwenyewe asogee kutoka kule kwenye ukingo wa ghorofa mpaka jirani na ile runinga, akawa anatazama kilichokuwa kinatangazwa kama asiyeamini macho yake.

    “Whaaat? Harrison amefanya nini? Noooooo!” alisema Linda kwa sauti kubwa huku akianza kuangua kilio kama mtoto mdogo. Maafisa usalama waliitumia nafasi hiyo kikamilifu, wakamzunguka pale alipokuwa amesimama ili asipate tena upenyo wa kukimbilia kwenye ukingo wa lile ghorofa.

    “Noooooo! Harrison hajafa, hap…a…a…a…n,” Linda alishindwa kumalizia kauli yake, akadondoka chini na kupoteza fahamu kwa mara nyingine. Wale maafisa usalama na manesi wakambeba juujuu mpaka kwenye ngazi na kuanza kuteremka naye, wakaingia kwenye lifti na kushuka hadi chini ya jengo lile ambapo alianza kupewa huduma ya kwanza haraka.

    ***

    “Jamani hivi ni kweli Harrison amekufa? Mbona mi siamini?”

    “Yaani inasikitisha sana jamani kwani ndiyo kwanza alikuwa ameanza kupata mafanikio, roho inauma sana.”

    “Au kuna mkono wa mtu? Mbona mi sielewi jinsi haya matukio yanavyotokea?”

    “Mi mwenyewe nahisi kuna mkono wa mtu, haiwezekani bwana harusi amkimbie bibi harusi kanisani halafu akapate ajali mbaya na kufa, lazima kuna jambo hapa,” watu waliokuwa wamekusanyika wakitazama taarifa ya habari kwenye runinga, walikuwa wakijadiliana, kila mmoja akizungumza la kwake.

    Baada ya mwili kuopolewa baharini, ulipelekwa mpaka kwenye Hospitali ya Miami ambapo ulifanyiwa vipimo kadhaa kisha kwenda kuhifadhiwa kwenye chumba cha maiti kusubiri ndugu wa marehemu wawasili.

    Kila aliyeisikia habari ile alipatwa na uchungu usioelezeka kwani ndiyo kwanza nyota ya mafanikio ya Harrison ilikuwa imeanza kung’ara baada ya kuchapisha kitabu cha Malkia wa Masokwe, kilichouza mamilioni ya nakala nchini Marekani na nje ya nchi.

    Ndugu wa Harrison wakiongozwa na mama mzazi wa kijana huyo, Skyler, babu yake, Dk Lewis na mkewe, waliwasili kwenye Hospitali ya Miami wakiwa hawaamini kilichotokea. Skyler ndiyo alikuwa katika hali mbaya zaidi kwani hakuwa na mtoto mwingine yeyote zaidi ya Harrison na hakutaka kuolewa baada ya kipenzi cha moyo wake, Harvey kufariki dunia.

    “Nina mkosi gani mimi mama? Furaha pekee ya maisha yangu nayo imetoweka, nitaishi maisha gani mimiiii?” alilia Skyler kwa huzuni wakati wakiwasili kwenye Hospitali ya Miami.

    “Jikaze mwanangu, yote kazi ya Mungu! Tulimpenda Harrison lakini Mungu kampenda zaidi, ukilia sana utakufuru,” mama Skyler alikuwa akimbembeleza mwanaye. Wakati wakiendelea kuomboleza, wazazi wa Linda nao waliwasili hospitalini pale, mama yake akawa analia kama mwendawazimu. Huzuni kuu ilitanda kila mahali.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya Linda kurejewa na fahamu, alipelekwa mpaka msibani, akawa anaendelea kuomboleza kwa uchungu kuliko watu wote waliofika msibani.

    Baada ya taratibu za kuchukua maiti kukamilika hospitalini pale, mwili ulichukuliwa mpaka nyumbani kwa Dk Lewis ambapo ndipo ndugu walipokubaliana msiba uwekwe. Kampuni ya Oklahoma Funerals iliyopewa kazi ya kusimamia msiba ule, ikapeleka gari la kubebea maiti pamoja na mengine ya kuwabeba ndugu na jamaa wa marehemu.

    Maelfu ya watu walifurika nyumbani kwa Dk Lewis kwenye msiba ule wa kihistoria, idadi ya waliokuwa wanapoteza fahamu kutokana na kumlilia Harrison ikawa inaongezeka kwa kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.

    Vyombo mbalimbali vya habari zikiwemo runinga na redio, vikawa vinatangaza moja kwa moja kila kilichokuwa kinaendelea msibani.

    ***

    Baada ya kushirikiana na rafiki yake, Rogers kutengeneza ajali feki ya kuonesha kwamba amekufa, Harrison alisafiri kwa siri hadi kwenye Msitu wa Tongass akiwa na lengo moja tu, kumpata malkia wa masokwe.

    Tofauti na zamani ambapo kila alipokuwa anawasili Tongass alikuwa akienda kuomba kibali cha kuingia kwenye msitu huo mkubwa, safari hii Harrison aliingia bila kutoa taarifa sehemu yoyote. Mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa malkia wa masokwe yalimchanganya kiasi cha kutoiona hatari iliyokuwa mbele yake iwapo ataingia kichwakichwa ndani ya msitu huo.

    “Samahani sana Linda, najua ulinipenda kwa moyo wako wote lakini ukweli ni kwamba yupo ninayempenda zaidi yako. Najua kumbukumbu za kitendo cha kukukimbia kanisani hazitafutika maishani mwako lakini ilibidi iwe hivyo, samahani kwa yote! Nampenda malkia wa masokwe kuliko wewe,” alijisemea Harisson kimoyomoyo wakati akikatiza kwenye vichaka kuingia ndani ya msitu wa Tongass.

    Kumbukumbu za tukio la ajali waliyoitengeneza na rafiki yake, Rogers bado zilikuwa zikijirudiarudia ndani ya kichwa chake kama filamu ya kutisha. Alikuwa akijiuliza maswali mengi ambayo hakuyapatia majibu lakini kwa kuwa alishaamua kumtafuta malkia wa masokwe kwa nguvu zote, alipiga moyo konde.

    Akiwa anaendelea kujipenyeza kwenye vichaka, Harrison alishtuka kupita kiasi baada ya kusikia matawi ya miti yakitingishika kwa nguvu huku sauti za ajabu zikisikika. Akiwa bado ameduwaa, alishtukia kitu kizito kikimuangukia mgongoni na kumuangusha chini.

    HABARI za ajali mbaya iliyotokea kwenye Daraja la Miami ikimhusisha mwendesha pikipiki aliyegongwa na gari kisha kurushwa hadi baharini, zinasambaa kwa kasi kubwa na kuwafikia watu wengi. Vikosi vya uokoaji wakiwemo askari wa usalama barabarani wanawasili eneo la tukio na baada ya muda, mwili wa mtu aliyepoteza maisha kwenye ajali ile unapatikana.



    Uchunguzi wa awali unawafanya watu wote waamini kuwa aliyekufa kwenye ajali ile ni Harrison kwani mwili wake unakutwa na suti ya harusi huku pikipiki aliyokuwa anaitumia muda mfupi kabla ya ajali ikikutwa eneo la tukio ikiwa haitamaniki. Habari zinaenea kuwa aliyefariki ni Harrison, jambo linalozidi kuzua simanzi kubwa.



    Upande wa pili, Linda, mtoto kutoka familia ya kitajiri, aliyekuwa juu ya ghorofa refu la Hospitali ya Oklahoma Medics akitishia kujirusha mpaka chini ikiwa Harrison hatatafutwa na kuletwa mbele yake, anafikishiwa habari juu ya kifo cha mtu anayedhaniwa kuwa ni Harrison.



    Anapatwa na mshtuko mkubwa na kujikuta akiahirisha alichokuwa anataka kukifanya, anateremshwa kutoka juu ya ghorofa na maafisa usalama waliokuwa wanamlinda asijirushe na kupelekwa hadi nyumbani kwa Dk Lewis, kulipokuwa na msiba wa Harrison. Simanzi kubwa inatawala nchi nzima kutokana na umaarufu aliokuwa nao Harrison baada ya kuchapisha kitabu kilichokuwa kinaitwa Malkia wa Masokwe.



    “MUNGU wangu, sokwe!” alisema Harrison huku akianza kupambana na sokwe mkubwa aliyekuwa amemuangusha chini. Kila alipojaribu kutafuta upenyo wa kukimbia, Harrison alizidi kubanwa pale chini na yule sokwe aliyeonekana kuwa na hasira, ikabidi



    apambane kiume, akaokota gongo kubwa lililokuwa pembeni, akampiga yule sokwe mgongoni na kufanikiwa kupata upenyo wa kutoroka.



    “Kumbe nimeumia?” alisema Harrison huku akizidi kutimua mbio kuelekea ndani kabisa ya msitu. Mkono wake wa kulia ulikuwa ukivuja damu baada ya sokwe yule kumng’ata kwa hasira. Alizidi kutimua mbio huku akijifunga jeraha lake kwa kutumia kitambaa cha mkononi alichokitoa mfukoni mwake.



    Kwa kuwa alikuwa akifahamu uelekeo ambao masokwe waliokuwa wanamlinda malkia wao walizoea kushinda, Harrison alizidi kuchanja mbuga kuelekea upande ule. Safari haikuwa nyepesi kwani aliingilia upande tofauti na ule aliozoea, jambo lililomfanya atumie muda mrefu kujipenyeza kwenye miti iliyokuwa imefungamana.



    Baada ya kutembea kwa miguu kwa takribani saa nne, Harrison alitokezea mahali ambapo alizoea kuweka kambi alipokuwa akifanya utafiti ndani ya Msitu wa Tongass.



    “Sijabeba hema, chakula wala maji, sijui nitaishi vipi huku msituni,” alijisemea Harrison wakati akitafuta sehemu ya kupumzikia. Akakaa chini ya mti mkubwa na kujiegamiza, akawa anahisi uchovu wa hali ya juu. Alipumzika kwa dakika kadhaa kabla ya kuamka na kuanza kutafakari nini cha kufanya.



    “Nisamehe Linda, najua bado unaomboleza kifo changu! Mungu akipenda ipo siku utaujua ukweli kuwa sikufa. Nisamehe kwa yote, nimejaribu kuulazimisha moyo wangu ukupende lakini imeshindikana, nampenda zaidi malkia wa masokwe,” alisema Harrison huku akilengwalengwa na machozi.



    Akawa anazunguka huku na kule kujaribu bahati yake kama atamuona malkia wa masokwe. Alizunguka kwa muda mrefu lakini eneo lote lilikuwa kimya kabisa, giza likaanza kuingia taratibu. Akatafuta sehemu nzuri na kuanza kuisafisha kwa ajili ya kulala.



    Akakusanya kuni kavu na kuwasha moto kwa kutumia kiberiti alichokinunua wakati akikimbilia msituni.



    “Naamini nikiwasha moto hakuna mnyama yeyote mkali anayeweza kunidhuru, hata simba hawawezi kusogea,” alijisemea Harrison huku akihangaika kuwasha moto. Baada ya muda akafanikiwa, akatafuta jiwe kubwa na kulisogeza jirani na moto, akalitumia kama kiti chake.

    ***



    “Harrison mpenzi wangu! Umeniachia kovu ambalo halitafutika kirahisi kwenye moyo wangu, kwa nini usingenioa kwanza ndiyo ufe? Ooh Mungu, kwa nini mimi?”



    “Usilie sana Linda kwani utakuwa unamkufuru Mungu. Yeye ndiyo mwamuzi wa yote, mshukuru kwa kila jambo,” mama mzazi wa Linda alikuwa akimbembeleza mwanaye ambaye alikuwa akilia kwa huzuni kali. Maneno aliyokuwa anayatamka Linda yalizidisha huzuni msibani, akina mama wakawa wanaomboleza kwa huzuni huku wengine wakiwafariji wafiwa.



    Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa mama yake Harrison, Skyler ambaye naye alikuwa akizimia mara kwa mara na kuzinduka. Hakutaka kuamini kama mwanaye wa pekee, kipenzi cha moyo wake alikuwa amefariki dunia.

    “Atazikwa lini?”

    “Kesho mchana.”

    “Sasa mwili wake si utaharibika?”

    “Hauwezi kuharibika, umehifadhiwa kwenye mochwari jirani na hapa nyumbani.”

    “Ataagwa saa ngapi?”



    “Hayo tutajua hiyo kesho lakini kuna uwezekano mkubwa asiagwe kwani sura yake imeharibika vibaya, anatisha.”



    “Daah! Inasikitisha sana, ameondoka akiwa bado kijana mdogo sana,” mzee mmoja wa makamo aliyekuwa akiishi jirani na Dk Lewis, alikuwa akizungumza na mzee mwenzake juu ya taratibu za mazishi ya Harrison. Babu wa marehemu, Dk Lewis akawa anamuelewesha juu ya mipango ya mazishi.



    Habari zilizidi kuenea nchini Marekani kutokana na umaarufu ambao Harrison alikuwa ameanza kuupata. Watu wengi ambao walimfahamu baada ya kusoma kitabu chake cha Malkia wa Masokwe, wakawa wanamiminika kwa wingi kutoka pande mbalimbali za Marekani kushiriki katika msiba ule.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Vyombo mbalimbali vya habari navyo havikuwa nyuma, vikawa vinaripoti hatua kwa hatua juu ya kila kitu kilichokuwa kinaendelea msibani pale. Kama ilivyokuwa imepangwa na wanandugu, kesho yake ilipowadia, taratibu za mazishi zilianza kufanyika.



    Watu wote waliokuwepo msibani wakatengenezewa fulana maalum zilizokuwa na picha na jina la Harrison, akina mama wakatengenezewa kanga maalum zilizokuwa na maandishi yaliyosomeka; Buriani Harrison.



    Ilipofika saa sita za mchana, maiti ilienda kuchukuliwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kilichokuwa jirani na nyumbani kwa Dk Lewis kwa gari maalum, mali ya Kampuni ya Oklahoma Funerals iliyopewa kazi ya kusimamia msiba ule.



    Wakati maiti ikiteremshwa kwa ajili ya kusomewa misa maalum, watu wengi walikuwa wakiendelea kupoteza fahamu kutokana na huzuni waliyokuwa nayo. Kikosi cha Msalaba Mwekundu kilichokuwepo eneo hilo, kilionekana kuanza kuzidiwa uwezo, wafanyakazi wake wakawa wanajituma kwa uwezo wao wote kuwapa huduma ya kwanza watu waliokuwa wanaanguka na kupoteza fahamu.



    Mchungaji Calagher Powel ndiye aliyeongoza misa maalum ya kuuombea mwili wa marehemu. Baada ya misa kuisha, mwili wa marehemu na waombolezaji walisafirishwa kwa magari maalum ya Kampuni ya Oklahoma Funerals mpaka kwenye Makaburi ya Miami Cemetery.



    Mwili ambao kila mmoja aliamini ni wa Harrison, uliwekwa pembeni ya kaburi na taratibu za kawaida za mazishi zikafanyika kisha ukazikwa kwa heshima zote. Baada ya mazishi, waombolezaji walirudishwa nyumbani kwa Dk Lewis, wakaendelea na maombolezo huku wengine wakianza kuondoka mmoja mmoja.



    “Naapa sitaolewa na mwanaume mwingine yeyote kwa ajili ya kumuenzi marehemu Harrison,” alisema Linda akiwa amejilaza miguuni mwa mama yake.

    “Mh! Kwa nini umesema hivyo mwanangu?”



    “ Naamini Harrison alikuwa ananipenda sana lakini alichanganyikiwa dakika za mwisho kabla ya kufunga ndoa. Nimemsamehe kwa yote kwani naamini ni mauti yalikuwa yanamuita ndiyo maana akanikimbiakanisani. Sitaolewa maisha yangu yote.”



    “Usiseme hivyo mwanangu, wewe bado ni msichana mdogo, lazima itafika wakati utahitaji kuwa na mume na watoto, usijiapize.”



    “Nimeshasema mama, hatatokea mtu mwingine yeyote akaziba nafasi ya Harrison kwenye moyo wangu,” Linda alizidi kushikilia msimamo wake. Siku zikawa zinazidi kusonga mbele, waombolezaji wakawa wanazidi kupungua nyumbani kwa Dk Lewis kwa kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.



    PENZI la dhati alilokuwa nalo kijana Harrison kwa malkia wa masokwe linamfanya amkimbie mchumba wake, Linda kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kwenda kwa rafiki yake, Rogers ambapo wanapanga mbinu kabambe ya kuandaa ajali feki.



    Rogers anamsaidia Harrison kutafuta maiti ambayo wanaivalisha nguo za kijana huyo kisha wanaenda mpaka kwenye daraja kubwa la Miami ambapo wanatengeneza mazingira yanayowafanya watu waamini kuwa Harrison amepata ajali mbaya na kufa kisha kutumbukia baharini.



    Hakuna anayeshtukia mchezo huo na habari zinasambaa kwa kasi kubwa zikieleza kuwa Harrison amekufa kwenye ajali hiyo, jambo linaloamsha huzuni kubwa kwa familia yake, ya mchumba wake Linda na kwa mashabiki wake nchini Marekani.



    Wakati taratibu za mazishi zikifanywa, upande wa pili Harrison anakimbilia mpaka kwenye Msitu wa Tongass kwa ajili ya kazi moja tu, kuhakikisha anampata malkia wa masokwe.



    HATIMAYE, baada ya siku saba tangu kutokea kwa kile watu walichoamini kuwa ni kifo cha Harrison, watu wote waliondoka nyumbani kwa Dk Lewis kulipokuwa na msiba isipokuwa ndugu zake wa karibu, Linda na wazazi wake ambao waliendelea kukaa msibani hapo mpaka baada ya wiki mbili.



    Watu wote walipoondoka na kwenda kuendelea na maisha yao, Linda aling’ang’ania kubaki msibani kwa maelezo kuwa ataondoka baada ya siku arobaini.



    “Mbona kila kukicha unazidi kukonda Linda, nini tatizo?”

    “Hamna tatizo, naona ni mabadiliko ya mwili tu.”

    “Mh! Kweli?”

    “Ndiyo mama.”

    “Mimi ni mtu mzima, naelewa jinsi mapenzi yanavyotesa. Najua ulimpenda sana mwanangu Harrison lakini lazima tukubaliane na ukweli kuwa Mungu kampenda zaidi.”

    “Ni kweli mama, yaani mpaka leo bado siamini kama sitamuona tena Harrison kwenye maisha yangu, ameniachia pigo kubwa sana na hiyo ndiyo sababu inayofanya nizidi kudhoofika.”

    “Pole sana, inabidi ujikaze kisabuni, taratibu utaanza kusahau na utampata ambaye ataziba pengo aliloliacha.”

    “Mh! Kiukweli sitaweza kumsahau na wala hatapatikana mtu wa kuziba pengo lake, nilimpenda sana Harrison,” Linda alikuwa akizungumza na mama mzazi wa Harrison, Skyler. Mazungumzo yao yaliendelea kwa muda mrefu, wakazungumza mambo mengi mpaka muda wa kulala ulipofika.



    Siku zilizidi kusonga mbele na hatimaye arobaini ikawadia. Misa ya kumuombea marehemu ikafanyika ambapo mchungaji Calagher Powel aliwaongoza mamia ya watu kusali juu ya kaburi la marehemu. Baada ya misa ya kuhitimisha msiba kuisha, kaburi lilisafishwa



    na kujengewa upya kisha watu wote wakaelekea nyumbani kwa Dk Lewis.

    Wakiwa nyumbani hapo, walikula chakula maalum kilichoandaliwa na familia kama shukrani kwa ushiriki wao kwenye msiba wa Harrison. Baada ya hapo watu wote wakatawanyika kurejea makwao, akiwemo Linda.

    ***



    Baada ya kukaa pembeni ya moto aliouwasha ndani ya msitu wa Tongass kwa muda mrefu, Harrison alienda kujilaza kwenye eneo maalum alilolitengeneza, usingizi mzito ukampitia bila kujali mbu na wadudu wengine waliokuwa wakimfaidi. Alipokuja kushtuka, tayari ilikuwa ni alfajiri ya siku ya pili, akaamka na kuanza kujinyoosha.



    “Lazima nimpate malkia wa masokwe, sitarudi mjini mpaka nihakikishe kimeeleweka, nampenda sana na nipo tayari kumuoa ili aje kuwa mke wangu,” alisema Harrison huku akiendelea kujinyoosha mwili wake ambao karibu kila kiungo kilikuwa kikiuma kutokana na uchovu.



    Jua lilianza kuchomoza upande wa Mashariki wa msitu ule mnene wa Tongass na kulikimbiza giza totoro la usiku, ndege nao wakawa wanaimba nyimbo zao nzuri huku wakiruka kutoka tawi moja la mti kwenda jingine.



    Jua lilipoanza kuchomoza, Harrison alianza tena kazi yake ya kulitafuta kundi kubwa la masokwe lililokuwa likitembea na malkia wao. Alifuata njia alizokuwa anazitumia akiwa ndani ya msitu ule, akaupata uelekeo ambao kundi kubwa la masokwe hupendelea kupita kila asubuhi. Akatafuta sehemu nzuri na kujibanza, akiwa makini kusikiliza huku akiangaza macho huku na kule.



    Baada ya muda, alianza kusikia kelele za matawi ya miti kuvunjika na milio ya masokwe, akakaa mkao wa tahadhari kwani alikuwa akizijua fujo za masokwe wanapogundua kuwa kuna mtu anawafuatilia.



    “Leo nitajitahidi kupambana mpaka nimsogelee jirani malkia wa masokwe, sitajali kama nitaumia,” alijisemea Harrison huku akiwa amejibanza kwenye shina la mti mkubwa. Dakika chache baadaye, tayari lile kundi la masokwe lilikuwa limewasili eneo lile, akawa anajaribu kuangalia katikati yao akiwa na matumaini ya kumuona malkia wa masokwe lakini kazi haikuwa nyepesi.



    “Mungu wangu, nitasalimika kweli?” alisema Harrison baada ya kushtukia jiwe kubwa likivurumishwa na kutua mita chache kutoka pale alipokuwa amejificha. Kabla hajakaa sawa, alishtukia mvua ya mawe makubwa yaliyokuwa yanarushwa na masokwe wale ikimuandama, ikabidi atoke alipokuwa amejificha na kuanza kutimua mbio kuokoa maisha yake.



    Kundi kubwa la masokwe lilianza kumkimbiza, akawa anajaribu kukwepa mawe na fimbo zilizokuwa zinarushwa, ikafika mahali akashindwa kuendelea kukimbia kwani masokwe walikuwa wamemzunguka pande zote, ikabidi asimame akiwa hajui nini hatima yake.



    Katika hali ambayo hakuitegemea, alishangaa kuona yule malkia wa masokwe ambaye siku zote alikuwa akimuona kwa mbali, akijitokeza mbele yake huku akitoa ishara kwa wale masokwe kuacha kumshambulia Harrison. Cha ajabu, masokwe wote walitii, wakatulia na kuanza kumkodolea macho Harrison aliyekuwa akitetemeka kupita kawaida.



    Malkia wa masokwe ambaye kwa mwonekano alikuwa na nywele ndefu zilizoshuka mpaka kiunoni, kucha ndefu kama mnyama na meno yaliyokuwa yamebadilika rangi na kuwa meusi kutokana na kula matunda ya porini na mizizi, alisogea mita chache kutoka pale Harrison alipokuwa amesimama.



    Akawa anamtazama Harrison huku akijifananisha naye, akagundua kuwa alikuwa na tofauti kubwa kati yake na wale masokwe lakini alikuwa akifanana sana na Harrison. Aliendelea kujishangaa huku akimuangalia Harrison, ghafla alianza kukimbia na kupanda juu ya matawi ya miti, wale masokwe wote nao wakamfuata na kuanza kukimbia naye, baada ya muda mfupi, walishatoweka kabisa eneo lile, Harrison akabaki ameduwaa akiwa haelewi kinachoendelea.



    “Mbona ameniangalia na kujifananisha kisha akatimua mbio?” alijiuliza Harrison huku akiugulia maumivu makali aliyoyapata kutokana na kushambuliwa kwa mawe na fimbo na masokwe wale. Sura ya malkia wa masokwe ilikuwa ikijirudiarudia kichwani mwake.



    Japokuwa alikuwa na haiba kama mnyama, bado uzuri na shani za asili alizokuwa nazo, hazikujificha, Harrison akajikuta akizidi kumpenda kiasi cha kujiapiza kufanya lolote mpaka ampate.



    Kutokana na maumivu aliyokuwa akiyahisi, ilibidi arudi mpaka eneo alilolala usiku uliopita, akajilaza chini na kupumzika huku akitafakari atakula nini kwa siku hiyo. Baada ya muda, akili ilimjia kuwa ni lazima akatafute matunda ya porini na maji. Akainuka baada ya kupumzika na kuanza kujikongoja kuelekea ndani kabisa ya Msitu wa Tongass.



    Baada ya muda, alifanikiwa kukusanya matunda mengi ambayo mengine hata hakuwa akiyajua. Kilichomuongoza kujua yapi yana sumu na yapi hayana, ilikuwa ni kuliwa na wadudu na ndege. Yale aliyokuta yameliwa, aliyachuma na yale yaliyokuwa hayajaguswa, aliyaacha kama yalivyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kurudi pale alipoweka makazi yake, alikaa na kuanza kuyala matunda yale. Akiwa katika hali ile, alishtuka baada ya kusikia vishindo vikisogea jirani na pale alipokuwa kutokea vichakani. Akaacha kila alichokuwa anakifanya na kutega masikio kwa makini huku akizungusha kichwa chake huku na kule kutazama ni kitu gani kilichokuwa kinamsogelea.





    HARRISON anaaminika kuwa amekufa kwenye ajali mbaya iliyotokea kwenye Daraja la Miami akiwa anaendesha pikipiki na kugongwa na gari kisha kurushwa hadi baharini. Habari zinasambaa kwa kasi kubwa na kuwafikia watu wengi. Kila mmoja anaamini kuwa ni kweli amekufa.



    Vikosi vya uokoaji wakiwemo askari wa usalama barabarani wanawasili eneo la tukio na baada ya muda, mwili wake unapatikana.

    Uchunguzi wa awali unawafanya watu wote waamini kuwa aliyekufa kwenye ajali ile ni Harrison kwani mwili wake unakutwa na suti ya harusi



    huku pikipiki aliyokuwa anaitumia muda mfupi kabla ya ajali ikikutwa eneo la tukio ikiwa haitamaniki. Simanzi kubwa inatanda.

    Taratibu za mazishi zinafanyika na anaenda kuzikwa kwa heshima zote kwenye makaburi ya Miami. Msiba unafanyika nyumbani kwa Dk. Lewis,



    babu yake Harrison. Baada ya matanga kuisha, watu wote wanatawanyika lakini Linda anakataa kuondoka, anakaa msibani mpaka baada ya siku arobaini.



    Upande wa pili, Harrison ambaye watu wote wanaamini amekufa, yupo kwenye msitu wa Tongass akiendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Penzi la dhati alilokuwa nalo juu yake, linamfanya awe tayari kwa lolote ilimradi ampate.



    BAADA ya kurudi pale alipoweka makazi yake, alikaa na kuanza kuyala matunda yale. Akiwa katika hali ile, alishtuka baada ya kusikia vishindo vikisogea jirani na pale alipokuwa. Akaacha kila alichokuwa anakifanya na kutega masikio kwa makini huku



    akizungusha kichwa chake huku na kule kutazama ni kitu gani kilichokuwa kinamsogelea.

    “Kijana unafanya nini huku porini peke yako?”



    “Shikamoo mzee,” alisema Harrison akionesha kushtushwa sana kumuona mtu ndani ya msitu wa Tongass. Alikuwa ni mwanaume mzee, akiwa na nywele ndefu zenye mvi kichwa kizima. Mkononi alikuwa ameshika silaha za kijadi kuonesha kuwa alikuwa ni mwindaji.



    “Marahaba, nakuuliza unafanya nini peke yako huku? Hujui kama kuna wanyama wakali wanaoweza kukudhuru? Au wewe ni jangili?” yule mtu alizidi kumhoji Harrison, naye akionesha kushtushwa na kitendo cha kumkuta ndani ya msitu ule akiwa peke yake.



    Harrison alimsogelea na kuanza kuzungumza naye kwa upole, akajitambulisha vizuri na kueleza kilichompeleka kule porini.

    “Kuna msichana nimetokea kumpenda lakini anaishi na masokwe.”

    “Anaishi na masokwe? Na yeye ni sokwe?”

    “Hapana, ni binadamu lakini ana tabia kama masokwe.”

    “Alifikaje huku porini?”

    “Hata sijui alifikaje lakini ninachojua anaishi huku msituni.”

    “Sasa ulishawahi kuzungumza naye?”

    “Hapana, wala sijui kama anafahamu kuzungumza kama sisi.”

    “Sasa utamfikishiaje ujumbe?”

    “Nitafanya chochote ilimradi nimpate.”

    “Utakaa siku ngapi huku?”

    “Mpaka nitakapohakikisha nimempata, hata kama ni mwaka mzima.”

    “Unafurahisha sana kijana, yaani huko mjini hakuna wanawake wazuri mpaka uje kuhangaika na viumbe wa ajabu huku porini?”

    “Mzee, we niache tu! Hujui ni kwa kiasi gani nampenda na kumhitaji malkia wa masokwe, nitafanya chochote ili mradi nimpate.”

    “Lakini mbona mimi kila siku nawinda kwenye huu msitu sijawahi kumuona huyo malkia wa masokwe?”

    “Huwezi kumuona kirahisi, analindwa mno na kundi kubwa la masokwe, mi mwenyewe nilimuona kama bahati tu.”

    “Kwa hiyo utakuwa unaishi wapi?”

    “Hata sielewi, hivi unavyoniona sina chochote! Sijui nitalala wapi wala nitakula nini, shida yangu ni malkia wa masokwe tu,” alisema



    Harrison kwa kujiamini, yule mzee akamtazama na kuanza kumuonea huruma.

    “Basi mimi nitakusaidia kujenga japo kibanda cha miti na nyasi kikusitiri, ni hatari kukaa huku porini bila kujihadhari, watu wengi wamekufa kwa kuliwa na wanyama wakali,” alisema yule mzee huku akishusha zana zake za kuwindia chini na kuanza kutafuta sehemu ya kujenga kibanda.



    Kwa kushirikiana na Harrison, walianza kufyeka majani na kukata miti, wakasafisha eneo dogo kisha wakaanza kuchimba mashimo. Baada ya muda, walikuwa tayari wamesimamisha miti mikubwa minne, kazi ikaendelea kwa nguvu. Baada ya saa nyingi, kibanda kidogo cha nyasi na miti kilikuwa tayari kimekamilika.



    “Utakuwa unaendelea kukiboresha taratibu kwa kadiri utakavyokuwa unaishi, nitakuwa nakuja kukutembelea mara kwa mara. “

    “Ahsante sana mzee! Sina cha kukulipa, Mungu atanilipia,” alisema Harrison kwa unyenyekevu.

    “Wala usijali, najua jinsi unavyojisikia na naahidi kuwa msaada kwako mpaka utakapotimiza ndoto zako,” alisema yule mzee huku akichukua zana zake tayari kwa kuondoka. Akamwambia Harrison inabidi naye ajifunze kuwinda kwa ajili ya kupata chakula kwa siku zote ambazo atakaa kule porini.



    Wakati anaondoka, alimwachia mkuki mmoja na sime. Akamwambia kuwa hizo ndiyo zitakuwa silaha zake akitaka kuwinda au kujilinda na wanyama wakali. Harrison alishukuru sana, akamsindikiza kidogo yule mzee na kurudi kwenye kibanda chake. Alishusha pumzi ndefu na kuanza kukitazama kile kibanda.



    Kutokana na uchovu aliokuwa nao, aliingia ndani na kujilaza kwa muda, akapumzika mpaka alipohisi uchovu umeisha. Akatoka nje na kuanza kuangaza macho huku na kule, wazo likamjia la kwenda kutafuta maji kwani tangu afike kwenye msitu huo, hakunywa hata kidogo.



    Alitoka na kuanza kuzunguka huku na kule, baada ya muda akafanikiwa kufika mahali palipokuwa na chemchemi ya maji. Akainama na kuanza kuyanywa kwa fujo kwani alikuwa na kiu kikali. Alipomaliza alirudi kwenye kibanda chake, akalala mpaka kesho yake.



    Alfajiri na mapema, Harrison alishtuliwa kutoka usingizini na milio ya ndege waliokuwa wanaruka kutoka tawi moja la mti kwenda jingine, wakifurahia mapambazuko. Aliamka harakaharaka na kutoka hadi nje ya kibanda chake.



    Akawa anajinyoosha huku akitafakari wapi pa kuanzia kazi ya kumtafuta malkia wa masokwe. Alichukua mkuki aliopewa na yule mzee jana yake na kuanza kuzunguka huku na kule. Baada ya muda, alianza kusikia matawi ya miti yakivunjikavunjika na kusababisha kelele za ajabu.



    Kwa kuwa tayari alishaanza kuzoea, alitambua kuwa ni lile kundi la masokwe linapita. Akajibanza kwenye shina la mti mkubwa na kuanza kutazama kule kundi lile lilipokuwa linatokea.



    Baada ya sekunde chache, lile kundi lilifika pale alipokuwa amejibanza. Harrison kwa mara nyingine akafanikiwa kumuona malkia wa masokwe, aliyekuwa anaruka kwenye matawi kama wale masokwe wengine.



    Harrison alisubiri lile kundi lipite, akaanza kulifuatilia nyumanyuma. Hakutaka kuwashtua wale masokwe wengine, akawa analifuata kwa mbali akitaka kujua huwa linaelekea wapi kila siku.



    Aliendelea kulifuatilia kwa muda mrefu, akawa anapita kwenye majani marefu, vichaka vilivyofungamana na wakati mwingine kupenyeza hadi kwenye miti ya miba. Kazi haikuwa nyepesi lakini kwa kuwa alikuwa na nia ya dhati kufahamu mahali kundi lile lilipokuwa linaelekea, alijikaza.



    Baada ya kutembea kwa saa nyingi, wingu zito lilianza kutanda angani, radi zikawa zinapiga kwa nguvu huku ngurumo kali zikisikika. Manyunyu yalianza kudondoka, yakafuatiwa na mvua kubwa iliyokuwa inapiga na upepo mkali. Harrison alianza kulowana, akawa anatetemeka mwili mzima kwa baridi lakini hakukata tamaa, aliendelea kulifuatilia lile kundi ambalo nalo lilionekana kuchanganywa na mvua ile.







    BAADA ya watu wote kuamini kuwa Harrison alikuwa amekufa kwenye ajali mbaya ya kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami, kijana huyo anakimbilia kwenye msitu mkubwa wa Tongass.



    Penzi la dhati alilokuwa nalo kwa msichana wa ajabu aliyekuwa anaishi porini na kulindwa na kundi kubwa la masokwe, linasababisha amkatae mchumba wake Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa.

    Ndoa hiyo inayeyuka kama theluji iyeyukavyo juani na Linda anapoteza fahamu kanisani. Anapozinduka



    anatishia kujiua lakini baada ya kupata taarifa za kifo cha Harrison, anabadili mawazo yake.

    Baadaye kila mmoja anakubaliana na ukweli kuwa tayari Harrison ameiaga dunia, msiba unapelekwa nyumbani kwa bibi na babu yake, Dk Lewis na mkewe Suzan ambapo taratibu za kawaida zinaendelea na baadaye mwili unaenda kuzikwa kwenye makaburi ya Miami.



    Upande wa pili, Harrison ambaye watu wote wanaamini amekufa, yupo kwenye msitu wa Tongass akiendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Anajiapiza kuwa hatarudi mjini mpaka atakapofanikisha kumpata malkia wa masokwe.





    MVUA kubwa iliendelea kunyesha ikiambatana na upepo na radi kali, Harrison akawa anaendelea kulifuatilia kundi lile la masokwe mpaka aone mwisho wake. Kutokana na mvua ile, mifereji iliyokuwa ndani ya msitu wa Tongass ilifurika maji yaliyokuwa yanakwenda kwa kasi, hali iliyomfanya Harrison apate ugumu kuendelea na kazi yake.



    “Nahisi mwili wote kuishiwa nguvu, itakuwa ni homa nini!” alijisemea Harrison huku akitetemeka mwili mzima. Ilibidi atafute sehemu ya kujificha ili asilowane kwani hali yake ilianza kubadilika na kuwa mbaya.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliingia kwenye shimo kubwa lililokuwa chini ya mti mkubwa, akajikunyata na kujiinamia chini, mvua kubwa ikaendelea kunyesha kwa saa nyingi huku wingu zito likisababisha giza kutanda kila upande.



    Baada ya kunyesha kwa saa nyingi mfululizo, hatimaye mvua ilianza kupungua, lile wingu zito likasambaa angani na kulifukuzia mbali giza lililokuwa limeanza kutanda. Harrison alitoka mahali alipokuwa amejificha na kusimama juu ya kisiki kikubwa cha mti, akawa anatazama huku na kule akiamini ataliona tena lile kundi la masokwe.



    Kilichozidi kummaliza nguvu ni kwamba mvua ile ilisababisha maji mengi kutuama na kuweka madimbwi makubwa kwenye msitu huo. Mifereji mikubwa nayo ilikuwa ikiendelea kutiririsha maji mengi kuelekea sehemu za mabondeni.



    “Mungu wangu, nitarudije kwenye kibanda changu?” alijisemea Harrison huku akiendelea kuangaza macho huku na kule. Licha ya hali ile, alijitahidi kujikaza na kuanza safari ya kurejea kule kwenye makazi yake ya muda.



    Alijipenyeza kwenye vichaka vilivyokuwa vimelowa kwa mvua, akawa anaruka madimbwi makubwa na mifereji kuelekea kwenye makazi yake. Giza nalo likawa limeanza kutanda upya kwani tayari muda ulikuwa umekwenda sana.



    Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kutafuta njia ya kurudia kwenye kibanda chake, hatimaye Harrison alifanikiwa kufika. Kibanda chote kilikuwa kimejaa maji, hali iliyomfanya ashindwe hata kuingia ndani, akatafuta sehemu iliyokuwa na mwinuko kidogo na kukaa, akawa anasubiri maji yapungue ili aingie kwenye kibanda chake.



    Baridi nayo ilizidi kumtesa, akawa anaendelea kutetemeka huku viungo mbalimbali vya mwili wake navyo vikianza kumuuma. Muda ulizidi kwenda lakini maji hayakupungua, ikabidi apande juu ya mti na kutafuta sehemu ambayo angeitumia kama kitanda mpaka asubuhi.



    Usiku hali yake ilizidi kuwa mbaya, akawa anatetemeka mwili mzima huku joto la mwili likianza kupanda kwa kasi. Kutokana na hali ile, hakupata hata lepe la usingizi, mpaka kunapambazuka hali yake ilikuwa ikizidi kuwa mbaya.



    Kwa bahati nzuri, kulipopambazuka jua lilianza kuchomoza kwa mbali, Harrison akajikaza na kuteremka mtini, akatafuta sehemu ambapo kijua kilikuwa kinapenya na kumfikia, akakaa. Jua lilizidi kuchomoza, akawa anazidi kujisogeza ili limpate vizuri zaidi.



    Kwa kadiri muda ulivyokuwa unazidi kusonga mbele, hali ya Harrison kiafya ilizidi kuwa mbaya, homa kali ikawa imechachamaa na kumfanya muda wote ajikunyate huku akitetemeka sana.



    Kutokana na hali ile, Harrison alishindwa hata kuinuka na kuendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Hata aliposikia kelele za matawi ya miti kuvunjika na milio ya masokwe jirani na pale alipokuwa, alishindwa kusimama zaidi ya kugeuza shingo na kuangalia kwa mbali.



    Jioni ilipofika, alijikongoja mpaka ndani ya kibanda chake ambacho sasa hakikuwa na maji, akapanga vitu vyake vizuri na kujilaza juu ya kitanda cha miti na nyasi. Kama ilivyokuwa kwa siku iliyopita, hakupata usingizi hata kidogo, usiku kucha akawa anatetemeka kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.



    Siku ya kwanza ilipita, hali yake ya kiafya ikazidi kuwa mbaya. Kutokana na kukosa dawa, chakula na maji safi ya kunywa, siku ya pili kulipopambazuka Harrison alizidiwa. Akaanza kutapika mfululizo na kuhara, hali iliyoufanya mwili wake kuishiwa na nguvu kabisa.



    “Ooh Mungu wangu, niokoe mimi mwanao kutoka kwenye hili janga, nitakufa peke yangu kwa kukosa msaada huku porini, nipe nguvu ooh Yehova Shalom,” Harrison alinong’ona.



    Hata hivyo haikusaidia chochote kwani aliendelea kutapika na kuhara mlemle ndani ya kibanda chake mpaka akawa hoi bin taaban, kizunguzungu nacho kikazidi kumbana. Ikafika muda akawa hawezi hata kujitingisha pale juu ya kitanda cha miti alipokuwa amejilaza.



    Giza nene likatanda kwenye macho yake na kumfanya apoteze fahamu, akawa haelewi chochote kilichokuwa kinaendelea.

    ***



    “Mamaa! Mamaa!”

    “Nini tena mwanangu? Mbona unatushtua usiku wote huu?”

    “Mama nimeota ndoto mbaya sana.”

    “Ndoto? Kuhusu nini?”

    “Kuhusu mwanangu Harrison.”

    “Aaah! Hayo ni maruweruwe ya kawaida, lazima uchungu wa mwanao uendelee kukusumbua.”

    “Hapana mama, nimemuona kabisa yupo mahali anateseka sana.”

    “Labda bado hajapata sehemu ya kupumzika huko peponi, njoo tufanye maombi maalum Mungu aipokee roho yake,” Suzan,



    alikuwa akizungumza na mwanaye Skyler, mama mzazi wa Harrison usiku wa manane.

    Licha ya mwanamke huyo ambaye sasa umri wake ulikuwa umekwenda sana, kujitahidi kumbembeleza mwanaye Skyler na



    kumfanya aamini kile alichokiota kilikuwa ni ndoto za kawaida tu, bado hakutaka kukubaliana naye.

    Akashikilia msimamo wake kuwa amemuona Harrison akiteseka mahali. Mama yake alimshika mkono, wakafumba macho na



    kuanza kuomba dua maalum kwa ajili ya Harrison. Muda mfupi baadaye, Dk. Lewis naye alishtuka usingizini na kwenda kuungana na mkewe na mtoto wao, Skyler.



    Mpaka kunapambazuka, bado walikuwa wanaendelea na maombi. Jua lilipochomoza, Skyler akamuomba mama yake amsindikize kwenye kaburi ambalo wote walikuwa wanaamini kuwa ndiyo alilozikwa Harrison. Walipofika walipiga magoti huku mikononi mwao wakiwa na Biblia, wakaanza kusali upya.



    Wakiwa wanaendelea kusali, Skyler alianza kuona mambo ambayo yalimfanya apige mayowe kwa nguvu, akiwa kwenye hali ile mara alidondoka chini na kujipigiza kwenye kaburi, akapoteza fahamu. Mama yake akapiga kelele za kuomba msaada ambapo muda mfupi baadaye walinzi wa makaburi walifika na kuwasaidia.



    Wakambeba Skyler juujuu hadi nje, wakasimamisha gari na kumkimbiza hospitali. Baada ya kutundikiwa dripu, Skyler alizinduka, akaanza kupiga kelele kama alivyofanya akiwa kule makaburini.

    “Kwani tatizoni nini mwanangu? Hebu tulia unieleze.”



    “Mama wakati nikiwa nimezama kwenye maombi kule makaburini, nimepata maono kuhusu Harrison. Nimemuona anateseka sana huko aliko, tumbo la uzazi linaniuma sana.”



    BAADA ya watu wote kuamini kuwa Harrison alikuwa amekufa kwenye ajali mbaya ya kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami, kijana huyo anakimbilia kwenye msitu mkubwa wa Tongass. Penzi la dhati alilokuwa nalo kwa msichana wa ajabu aliyekuwa anaishi porini na kulindwa na kundi kubwa la masokwe, linasababisha



    amkatae mchumba wake Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Ndoa hiyo inayeyuka kama theluji iyeyukavyo

    juani na Linda anapoteza fahamu kanisani. Anapozinduka anatishia kujiua lakini baada ya kupata taarifa za kifo cha Harrison,



    anabadili mawazo yake. Baadaye kila mmoja anakubaliana na ukweli kuwa tayari Harrison ameiagadunia, msiba unapelekwa



    nyumbani kwa bibi na babu yake, Dk Lewis na mkewe Suzan ambapo taratibu za kawaida zinaendelea na baadaye mwili unaenda kuzikwa kwenye makaburi ya Miami. Upande wa pili, Harrison ambaye watu wote wanaamini amekufa, yupo kwenye



    msitu wa Tongass akiendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Anajiapiza kuwa hatarudi mjini mpaka atakapofanikisha kumpata malkia wa masokwe. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO… MVUA kubwa iliendelea kunyesha ikiambatana na upepo na radi kali, Harrison akawa anaendelea kulifuatilia kundi lile la masokwe mpaka aone mwisho wake.



    Kutokana na mvua ile, mifereji iliyokuwa ndani ya msitu wa Tongass ilifurika maji yaliyokuwa yanakwenda kwa kasi, hali iliyomfanya Harrison apate ugumu kuendelea na kazi yake. "Nahisi mwili wote kuishiwa nguvu, itakuwa ni homa nini!" alijisemea Harrison huku akitetemeka mwili mzima. Ilibidi atafute sehemu ya kujificha ili asilowane kwani hali yake ilianza kubadilika na



    kuwa mbaya. Aliingia kwenye shimo kubwa lililokuwa chini ya mti mkubwa, akajikunyata na kujiinamia chini, mvua kubwa ikaendelea kunyesha kwa saa nyingi huku wingu zito likisababisha giza kutanda kila upande. Baada ya kunyesha kwa saa nyingi mfululizo, hatimaye mvua ilianza kupungua, lile wingu zito likasambaa angani na kulifukuzia mbali giza lililokuwa limeanza



    kutanda. Harrison alitoka mahali alipokuwa amejifichana kusimama juu ya kisiki kikubwa cha mti, akawa anatazama huku na kule akiamini ataliona tena lile kundi la masokwe. Kilichozidi kummaliza nguvu ni kwamba mvua ile ilisababisha maji mengikutuama na kuweka madimbwi makubwa kwenye msitu huo. Mifereji mikubwa nayo ilikuwa ikiendelea kutiririsha maji



    mengi kuelekea sehemu za mabondeni. "Mungu wangu, nitarudije kwenye kibanda changu?" alijisemea Harrison huku akiendelea kuangaza macho huku na kule. Licha ya hali ile, alijitahidi kujikaza na kuanza safari ya kurejea kule kwenye makazi yake ya muda. Alijipenyeza kwenye vichaka vilivyokuwa vimelowa kwa mvua, akawa anaruka madimbwi makubwa na mifereji



    kuelekea kwenye makazi yake. Giza nalo likawa limeanza kutanda upya kwani tayari muda ulikuwa umekwenda sana. Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kutafuta njia ya kurudia kwenye kibanda chake, hatimaye Harrison alifanikiwa kufika. Kibanda chote kilikuwa kimejaa maji, hali iliyomfanya ashindwe hata kuingia ndani, akatafuta sehemu iliyokuwa na mwinuko kidogo na kukaa,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akawa anasubiri maji yapungue ili aingie kwenye kibanda chake. Baridi nayo ilizidi kumtesa, akawa anaendelea kutetemeka huku viungo mbalimbali vya mwili wake navyo vikianza kumuuma. Muda ulizidi kwenda lakini maji hayakupungua, ikabidi apande juu ya mti na kutafuta sehemu ambayo angeitumia kama kitanda mpaka asubuhi. Usiku hali yake ilizidi kuwa mbaya, akawa



    anatetemeka mwili mzima hukujoto la mwili likianza kupanda kwa kasi. Kutokana na hali ile, hakupata hata lepe la usingizi, mpaka kunapambazuka hali yake ilikuwa ikizidi kuwa mbaya. Kwa bahati nzuri, kulipopambazuka jua lilianza kuchomoza kwa mbali, Harrison akajikaza na kuteremka mtini, akatafuta sehemu ambapo kijua kilikuwa kinapenya na kumfikia, akakaa. Jua



    lilizidi kuchomoza, akawa anazidi kujisogeza ili limpate vizuri zaidi. Kwa kadiri muda ulivyokuwa unazidi kusonga mbele, hali ya Harrison kiafya ilizidi kuwa mbaya, homa kali ikawa imechachamaa na kumfanya muda wote ajikunyate huku akitetemeka sana. Kutokana na hali ile, Harrison alishindwa hata kuinuka na kuendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Hata



    aliposikia kelele za matawi ya miti kuvunjika na milio ya masokwe jirani na pale alipokuwa, alishindwa kusimama zaidi ya kugeuza shingo na kuangalia kwa mbali. Jioni ilipofika, alijikongoja mpaka ndani ya kibanda chake ambacho sasa hakikuwa na



    maji, akapanga vitu vyake vizuri na kujilaza juu ya kitanda cha miti na nyasi. Kama ilivyokuwa kwa siku iliyopita, hakupata usingizi hata kidogo, usiku kucha akawa anatetemeka kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua. Siku ya kwanza ilipita, hali yake



    ya kiafya ikazidi kuwa mbaya. Kutokana na kukosa dawa, chakula na maji safi ya kunywa, siku ya pili kulipopambazuka Harrison alizidiwa. Akaanza kutapika mfululizo na kuhara, hali iliyoufanya mwili wake kuishiwa na nguvu kabisa. "Ooh Mungu wangu,



    niokoe mimi mwanao kutoka kwenye hili janga, nitakufa peke yangu kwa kukosa msaada huku porini, nipe nguvu ooh Yehova Shalom," Harrison alinong'ona. Hata hivyo haikusaidia chochote kwani aliendelea kutapika na kuhara mlemle ndani ya kibanda chake mpaka akawa hoi bin taaban, kizunguzungu nacho kikazidi kumbana. Ikafika muda akawa hawezi hata kujitingisha pale juu



    ya kitanda cha miti alipokuwa amejilaza. Giza nene likatanda kwenye macho yake na kumfanya apoteze fahamu, akawa haelewi chochote kilichokuwa kinaendelea. *** "Mamaa! Mamaa!" "Nini tena mwanangu? Mbona unatushtua usiku wote huu?" "Mama



    nimeota ndoto mbaya sana." "Ndoto? Kuhusu nini?" "Kuhusu mwanangu Harrison." "Aaah! Hayo ni maruweruwe ya kawaida, lazima uchungu wa mwanao uendelee kukusumbua." "Hapana mama, nimemuona kabisa yupo mahali anateseka sana." "Labda bado hajapata sehemu ya kupumzika huko peponi, njoo tufanye maombi maalum Mungu aipokee roho yake," Suzan,



    alikuwa akizungumzana mwanaye Skyler, mama mzazi wa Harrison usiku wa manane. Licha ya mwanamke huyo ambaye sasa umri wake ulikuwa umekwenda sana, kujitahidi kumbembeleza mwanaye Skyler na kumfanya aamini kile alichokiota kilikuwa ni ndoto za kawaida tu, bado hakutaka kukubaliana naye. Akashikilia msimamo wake kuwa amemuona Harrison akiteseka mahali.



    Mama yake alimshika mkono, wakafumba macho na kuanza kuomba dua maalum kwa ajili ya Harrison. Muda mfupi baadaye, Dk. Lewis naye alishtuka usingizini na kwenda kuungana na mkewe na mtoto wao, Skyler. Mpaka kunapambazuka, bado



    walikuwa wanaendelea na maombi. Jua lilipochomoza, Skyler akamuomba mama yake amsindikize kwenye kaburiambalo wote walikuwa wanaamini kuwa ndiyo alilozikwa Harrison. Walipofika walipiga magoti huku mikononi mwao wakiwa na Biblia, wakaanza kusali upya. Wakiwa wanaendelea kusali, Skyler alianza kuona mambo ambayo yalimfanya apige mayowe kwa nguvu,



    akiwa kwenye hali ile mara alidondoka chini na kujipigiza kwenye kaburi, akapoteza fahamu. Mama yake akapiga kelele za kuomba msaada ambapo muda mfupi baadaye walinzi wa makaburi walifika na kuwasaidia. Wakambeba Skyler juujuu hadi nje, wakasimamisha gari na kumkimbiza hospitali. Baada ya kutundikiwa dripu, Skyler alizinduka, akaanza kupiga kelele kama



    alivyofanya akiwa kule makaburini. "Kwani tatizoni nini mwanangu? Hebu tulia unieleze." "Mama wakati nikiwa nimezama kwenye maombi kule makaburini, nimepata maono kuhusu Harrison. Nimemuona anateseka sana huko aliko,tumbo la uzazi linaniuma sana."



    Akiwa porini, Harrison anaendelea na harakati za kumsaka malkia wa masokwe. Mvua na jua vinamuishia mwilini kila siku lakini mwenyewe hajali. Kwa bahati mbaya, anaanza kuugua akiwa ndani ya msitu huo. Anazidiwa na homa kali inayomfanya aishiwe



    nguvu, anakosa msaada na anakata tamaa ya kuendelea kuishi, anabanwa na kizunguzungu kikali na kupoteza fahamu. Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO… Harrison hakuelewa tena kilichoendelea mpaka alipokuja kuzinduka na kujikuta akiwa amelala juu ya kitanda cha ngozi ya mnyama, pembeni yake moto ukiwa unawaka. Alijaribu kukumbuka pale ni wapi lakini hakupata majibu,



    alijaribu kunyanyuka lakini bado mwili wake haukuwa na nguvu, akageuza shingo na kuangalia upande ule kulipokuwa na moto, akagundua kuwa alikuwa ndani ya nyumba ya mtu. “Nimefikaje hapa? Nani kanileta?” alizidi kujiuliza maswali mengi, mara



    akasikia vishindo vya mtu akitembea kuelekea pale alipokuwa amelala. “Unaendeleaje rafiki? Umeshaamka?” alizungumza mwanaume wa makamo ambaye Harrison aliitambua vyema sura na sauti yake. “Niambie hapa ni wapi na nani kanileta.” “Usiwe



    na haraka kijana, nitakuelekeza kila kitu, inuka kwanza unywe dawa mengine yatafuatia baadaye,” alisema yule mwanaume huku akimsaidia Harrison kuinuka pale kitandani na kumuegamiza ukutani. Alikuwa ni yule mwanaume aliyemsaidia kujenga kibanda



    cha miti ndani ya msitu wa Tongass, siku kadhaa zilizopita. Baada ya kumkalisha kitandani, alifunua chungu kikubwa kilichokuwa kinachemka jikoni, akachukua kikombe cha chuma na kukoroga dawa za kienyeji zilizokuwa zinachemka kisha akachota na kumsogezea Harrison. “Ni chungu lakini jikaze unywe ili upone haraka,” alisema yule mwanaume huku naye akikaa pembeni ya



    Harrison, akawa anamhimiza anywe. Ilibidi Harrison ajikaze na kuanza kunywa, japokuwa dawa ilikuwachungu sana lakini alimaliza kikombe chote, jambo lililomfurahisha sana yule mzee. “Safi sana, utapona haraka kuliko nilivyotegemea, una juhudi za kunywa dawa, homa kali ilikuwa imechachamaa, ningechelewa kidogo ungekufa.” “Kwani ilikuwaje?” “Nilikuwa kwenye shughuli



    zangu za uwindaji kama kawaida, si unajua huu msitu kwangu ni kama nyumbani? Nimezaliwa kwenye kijiji hiki na kukulia hapa hivyo kuwinda ni kama jadi yangu.” “Mh! Ikawaje?” “Baada ya kumaliza kuwinda, niliamua kukupitia japo nikuachie na wewe kitoweo kidogo, nikashtushwa na ukimya uliokuwa umetawala kwenye kibanda chako. Nilipofungua mlango ndiyo nikakukuta



    umekauka kitandani ukiwa hujiwezi, nikakubeba haraka na kukuleta mpaka hapa kwangu.” “Ooh! Ahsante sana mzee wangu, Mungu atakulipia, nashukuru sana,” alisema Harrison huku akilengwalengwa na machozi. “Usijali kijana, nilikuahidi tangu siku



    ya kwanza kuwa nitakusaidia mpakandoto zako za kumpata malkia wa masokwe zitakapotimia, pumzika kidogo nikuandalie supu japo urudishe nguvu,” alisema yule mtu, akainuka na kumsaidia Harrison kulala vizuri kisha akatoka nje ya kibandakile cha miti na udongo ambacho kilikuwa kimeezekwa kwa makuti. Baada ya muda alirudi akiwa na bakuli kubwa la bati lililokuwa limejaa



    supu na nyama za porini. “Amka ule,” alisema yule mwanaume ambaye baadaye alijitambulisha kuwa anaitwa Carrick Hondo, raia wa Canada aliyezaliwa pembezoni mwa msitu wa Tongass baada ya wazazi wake kuyakimbia makazi yao miaka mingi iliyopita wakihofia usalama wa maisha yao. Alimsaidia tena Harrison kukaa vizuri, akamsogezea bakuli lililokuwa limejaa supu,



    akaanza kumnywesha na kumlisha nyama. “Nyama ya swala hii, inasaidia sana kurudisha nguvu kwa mgonjwa kama wewe, siku nyingine inabidi nikufundishe majani ambayo yanatibu homa, unaweza kufa porini bila mtu yeyote kukujua.” “Nitashukuru sana, sijaumwa siku nyingi sana, homa ilivyochachamaa nikahisi naelekea kufa.” “Vipi umefikia wapi na kazi yako ya kumsaka



    malkia wa masokwe?” “Nilifikia sehemu nzuri lakini kwa bahati mbaya mvua ikanikatisha. Nilikuwa nalifuatilia kundi la masokwe linalomlinda nikitaka kujua linapoenda kulala, mvua kubwa ndiyo ikaanza kunyesha na kunivurugia mipango yangu yote.” “Usijali, bado una nafasi ya kurudi tena na kufanikisha malengo yako.” “Kwani hapa ni wapi?” “Hiki kijiji nacho kinaitwa Tongass, watu



    wanaoishi hapa wengi ni wawindaji, kipo pembezoni mwa msitu, siyo mbali sana kutoka msituni, ni mwendo wa saa nne tu unakuwa umefika katikati ya msitu.” “Afadhali, nilijua ni sehemu nyingine kabisa, kwa hiyo huku nako ni Marekani?” “Hapana,



    huku ni upande wa Canada, ni mpakani kabisa si unajua huu msitu umeingia hadi Canada?” “Nimefurahi sana kufika huku, japo matatizo ndiyo yaliyonileta. Nataka nikimpata malkia wa masokwe nije kuishi naye huku.” “Litakuwa wazo zuri sana, kijiji kina watu wachache sana, na wewe ukija idadi yetu itazidi kuongezeka,” alisema Hondo huku akiendelea kumnywesha supu Harrison.



    Bakuli zima liliisha, angalau akapata nguvu hata za kuweza kuinuka na kukaa vizuri mwenyewe. Siku ya kwanza ilipita Harrison akiendelea kunywesha dawa za kienyeji, siku ya pili kulipopambazuka, alikuwa na nafuu kubwa ingawa bado mwilihaukuwa



    umerejea kwenye hali ya kawaida. Akawa anaendelea kunywesha dawa na kula vyakula vizuri, zikiwemo nyama za porini. Siku ya tatu alikuwa ameshapona kabisa, akaaga na kuanza safari ya kuelea msituni. Mzee Hondo alimsindikiza na kumuelekeza njia rahisi ambayo itamfikisha moja kwa moja mpaka kwenye kibanda chake. Baada ya kumfikisha mbali, waliagana na Harrison



    akaendelea na safari yake. Baada ya kutembea kwa saa zaidi ya nne, akikatiza kwenye milima na mabonde ndani ya msitu ule uliokuwa na miti iliyoshonana, Harrison alifika kwenye kibanda chake. Kazi ya kwanza aliyoanza kuifanya ni kusafisha kibanda chake kwani wakati alipozidiwa alikuwa akimalizia hajazake zote humohumo. Alipomaliza aliwasha moto na kubanika nyama



    aliyopewa na mzee Hondo,akala na kupumzika kwa muda akitafakari mambo kadhaa kwenye kichwa chake. “Nikimpata maisha yangu yatakuwa mazuri sana, nitahakikisha nambadilisha kila kitu, nampenda sana malkia wa masokwe mpaka nahisi



    kuchanganyikiwa,” alijisemea Harrison akiwa amepumzika pembeni ya moto aliouwasha. Kwa kuwa muda ulikuwa umeenda, ukichanganya na uchovu aliokuwa nao wa kutembea umbali mrefu, aliamua kulala mpaka kesho yake asubuhi. ***







    BAADA ya Harrison kwa kushirikiana na rafiki yake wa siku nyingi, kufanikiwa kuudanganya ulimwengu kuwa amekufa kwenye ajali mbaya ya kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami, Harrison anahamia kwenye Msitu wa Tongass.

    Kinachompeleka huko ni penzi la dhati alilokuwa nalo kwa msichana wa ajabu aliyekuwa anaishi kwenye msitu huo na kulindwa na kundi kubwa la masokwe.



    Penzi lake kwa msichana huyo wa ajabu linasababisha amkatae mchumba wake, Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Ndoa hiyo inayeyuka kabisa baada ya taarifa za kifo cha Harrison kusambaa kwa kasi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akiwa porini, Harrison anaendelea na harakati za kumsaka malkia wa masokwe. Mvua na jua vinamuishia mwilini kila siku lakini mwenyewe hajali. Kwa bahati mbaya, anaanza kuugua akiwa ndani ya msitu huo. Anazidiwa na homa kali inayomfanya aishiwe nguvu, anakosa msaada na anakata tamaa ya kuendelea kuishi, anabanwa na kizunguzungu kikali na kupoteza fahamu.

    Anakuja kuokolewa na mzee mwindaji, Carrick Hondo anayemnywesha dawa za mitishamba mpaka akapona. Baada ya hapo



    anarudi msituni kuendelea na kazi yake.



    KULIPOPAMBAZUKA, kama kawaida Harrison aliamka mapema na kufanya mazoezi mepesi ya mwili kisha kijua kilipoanza kuchomoza, alijiandaa tayari kwa kazi ya kumfuatilia malkia wa masokwe. Alisogea mpaka jirani na mahali kundi kubwa la masokwe lilipokuwa linapita, akatafuta sehemu ya kujificha na kutulia kwa muda.



    Baada ya muda kupita, alianza kusikia kelele za matawi ya miti kuvunjika na milio ya masokwe ikianza kusikika kutoka mbali. Alijiweka tayari huku mkuki wake ukiwa mkononi kwa ajili ya kujihami endapo kundi la masokwe litamshambulia kama ilivyokuwa kwa siku za nyuma.



    Baada ya dakika chache, kundi kubwa la masokwe lilikuwa tayari limeshawasili pale Harrison alipokuwa amejificha, masokwe wakubwa wakawa wanaruka kutoka tawi moja la mti hadi lingine huku wakijitahidi kwa kadiri ya uwezo wao kumkinga malkia wao asidhurike.



    Harrison alisubiri mpaka kundi lote lipite kisha kwa kasi kubwa na yeye akaanza kulifuata kwa nyuma. Akawa anakimbia na kujificha kwenye mashina ya miti akilifuata kundi lile kwa karibu.



    “Kila ninapomuona nahisi kama uzuri wake unaongezeka! Lazima nimuoe,” alisema Harrison huku akizidi kulifuatilia lile kundi la masokwe wakubwa na wengi. Mara kwa mara alifanikiwa kumuona malkia wa masokwe kwa ukaribu, akawa anazidi kuvutiwa naye kutokana na uzuri wa asili aliokuwa nao.



    Wakati akiendelea kulifuatilia lile kundi, masokwe waliokuwa nyuma waligundua kuwa kuna mtu anawafuata kwa lengo la kumdhuru malkia wao, wakaanza kutoa milio ya tahadhari, hali iliyowafanya masokwe wote wasitishe safari yao na kuanza kuangalia kuna jambo gani.



    Harrison alishtukia ameshazungukwa na masokwe wakubwa, wakaanza kumshambulia kwa matawi ya miti, magongo na mawe. Malkia wao ambaye bado alikuwa hajagundua kilichokuwa kinaendelea, alipoona anayepigwa ni Harrison, alitoa mlio mkali uliofanya masokwe wote waache kumshambulia Harrison.



    Akaruka kwenye matawi ya miti kwa kasi kubwa na kushuka hadi pale alipokuwa amesimama Harrison. Akawa anamsogelea taratibu huku akimtazama kwa macho kama anayemshangaa na kumfananisha naye.



    Harrison ambaye tayari alikuwa na majeraha kadhaa mwilini kutokana na kipigo cha masokwe wale, alifurahi sana malkia wa masokwe kumsogelea, akaachia tabasamu pana huku naye akipiga hatua fupifupi kumsogelea.



    Malkia wa masokwe alimtazama Harrison kwa muda mrefu, akawa anamuangalia kiungo kimojakimoja na kujifananisha naye. Japokuwa alikuwa amelelewa na masokwe, bado alitambua kuwa kuna tofauti kubwa kati yake na viumbe wale hivyo alipomuona Harrison, aligundua kuwa anafanana naye kwa vitu vingi.



    Aliendelea kumshangaa Harrison huku lile kundi la masokwe likiwa limewazunguka, akamzunguka hadi nyuma na kuendelea kumchambua kiungo kimojakimoja. Baada ya muda, malkia wa masokwe alitoa mlio kama mnyama kisha akakimbia na kurukia juu ya tawi la mti kama wafanyavyo masokwe, nao wakamfuata na kurukia juu ya matawi, wakaanza kutimua mbio kutokomea kusipojulikana.



    Kwa kuwa Harrison alikuwa amechoka sana, ilibidi akubali kushindwa, akaliacha kundi lile liondoke na yeye akageuza na kuanza kutembea taratibu kurudi kwenye kibanda chake.



    Kimoyomoyo alikuwa akijipongeza kwani kwa mara ya pili alifanikiwa kusogeleana na malkia wa masokwe. Akaamini akiongeza juhudi anaweza kufanikisha azma yake ya kumpata malkia wa masokwe. Alitembea taratibu mpaka kwenye kibanda chake, alipofika kitu cha kwanza alichokifanya ilikuwa ni kuwasha moto na kuanza kuchoma nyama aliyopewa na mzee Hondo.



    Aliichoma vizuri kisha akala na kushushia na maji, usingizi ukampitia kutokana na uchovu aliokuwa nao. Alikuja kushtuka baada ya kusikia kelele za kundi la masokwe likirudi, akakurupuka pale chini alipokuwa amelala na kusimama wima, kelele zikaongezeka kwa kadiri kundi lile lilivyokuwa linazidi kumsogelea.



    Katika hali ambayo hakuitegemea, alimuona malkia wa masokwe akichomoka kutoka katikati ya kundi la masokwe wakubwa na kusogea upande ule aliokuwa amesimama Harrison. Alipomsogelea, alibwaga chini furushi la matunda ya porini jirani na pale alipokuwa amesimama Harrison kisha akakimbia kwa miguu na mikono na kujichanganya tena na kundi la masokwe, muda mfupi baadaye wakawa wametoweka eneo lile.



    Harrison hakuamini kile kilichotokea, akasogea mbele taratibu na kuinama pale malkia wa masokwe alipoliacha furushi lile la matunda, akalifungua ambapo alikuta kuna matunda mbalimbali ya porini, mengine akiwa hajawahi hata kuyaona. Kilichomvutia ni kwamba yote yalikuwa yameiva vizuri, akajikuta mate yakimjaa mdomoni.

    Bila kupoteza muda alianza kuyala moja baada ya jingine huku akiwa na tabasamu pana usoni mwake. Aliamini hayana sumu kwani kama masokwe pamoja na malkia wao walikula bila kudhurika, hata yeye asingeweza kudhurika. Alikula hadi akatosheka, mengine akaenda kuyahifadhi ndani ya kibanda chake.



    Muda ulizidi kuyoyoma kwa kasi na hatimaye giza likaanza kuingia. Harrison aliwasha moto kwa kutumia kuni alizokusanya msituni na kujilaza pembeni. Akawa anaendelea kuchoma nyama taratibu huku akimalizia kuyala matunda aliyopewa na malkia wa masokwe.



    Akiwa anaendelea kuota moto na kuivisha nyama, alisikia vishindo vikitokea kichakani, akakimbilia ndani ya kibanda na kuchukua mkuki aliopewa na mzee Hondo, akajificha nyuma ya mti huku akiwa tayari kwa lolote.



    Katika hali ambayo hakuitegemea, alishtuka kumuona malkia wa masokwe akichomoza kutoka vichakani, safari hii akiwa hajaongozana na masokwe kama ilivyokuwa kawaida yake. Akawa anaangaza macho huku na kule kama anayetafuta kitu.



    Harakaharaka Harrison alichomoka vichakani na kujitokeza, akawa anasogea pale alipokuwa amesimama malkia wa masokwe huku akiwa na tabasamu pana usoni. Wakawa wanatazama usoni kama majogoo yanayotaka kupigana. Mara malkia wa masokwe alitimua mbio na kurudi vichakani, akajificha na kuanza kumchungulia Harrison.



    Muda mfupi baadaye akajitokeza tena na kuanza kumsogelea Harrison, alipomkaribia alikimbia tena na kurukia juu ya tawi la mti. Ilivyoonesha alikuwa anapenda kucheza na Harrison ingawa michezo yake ilikuwa ya kisokwesokwe.



    Kwa kuwa Harrison alikuwa anatafuta namna ya kujenga naye ukaribu, alianza kumuiga alivyokuwa anafanya, naye akawa anakimbia na kujificha kisha kurudi tena, mara akawa anaparamia matawi ya miti kama malkia wa masokwe, jambo lililomfanya aanze kutabasamu.



    Wakaendelea kucheza kwa muda mrefu huku moto ukiendelea kuwaka, walipochoka, Harrison alimsogelea malkia wa masokwe, akamkumbatia kwa nguvu.

    ***







    PENZI lina nguvu kuliko mauti, walinena wahenga. Harrison, kijana msomi anajikuta akiangukia kwenye penzi la msichana aliyekuwa akiishi na masokwe ndani ya msitu wa Tongass. Hajali mazingira anayoishi msichana huyo na tabia zake alizonazo zinazofanana na masokwe.



    Penzi lake kwa msichana huyo wa ajabu linasababisha amkatae mchumba wake, Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Anatoroka kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea.



    Kwa kushirikiana na rafiki yake wa siku nyingi, wanafanikiwa kuudanganya ulimwengu kuwa Harrison amepata ajali mbaya ya kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami, na kufa papo hapo. Taarifa hizo zinasambaa kwa kasi na kila mmoja anaamini ni kweli amekufa.



    Akiwa porini, Harrison anaendelea na harakati za kumsaka malkia wa masokwe. Mvua na jua vinamuishia mwilini kila siku lakini mwenyewe hajali. Kwa bahati mbaya, anaanza kuugua akiwa ndani ya msitu huo mpaka kuwa taabani, anaokolewa na mzee mwindaji, Carrick Hondo anayemnywesha dawa za mitishamba mpaka akapona.



    Baada ya hapo anarudi msituni kuendelea na kazi yake. Anajaribu kujenga mazoea na msichana huyo. Baada ya kuteseka sana, hatimaye ndoto yake inaanza kuelekea kutimia.



    MALKIA wa masokwe alijitoa kwa nguvu mikononi mwa Harrison, akakimbilia kichakani na kujificha. Harrison alimfuata kwani tayari alishaanza kujihisi tofauti alipomkumbatia. Malkia wa masokwe alipoona Harrison anamfuata tena kwa lengo la kumkumbatia, aliparamia matawi ya miti na kutokomea gizani.



    Harrison alijaribu kumfuatilia lakini hakufanikiwa kumpata, akarudi pembeni ya moto alipokuwa amekaa, akawa anatabasamu kwani kwa mara ya kwanza alifanikiwa kucheza na malkia wa masokwe. Alikaa kwa muda mrefu pembeni ya moto akitegemea kumuona tena msichana yule wa ajabu lakini hakurudi.



    Baadaye akaingia ndani ya kibanda chake na kulala. Usingizi haukumchukua haraka, akawa anamuwaza sana malkia wa masokwe na kitendo alichokifanya cha kumfuata pale akiwa peke yake.

    “Inawezekana na yeye ameanza kunipenda?” alijiuliza kimoyomoyo, akaachia tabasamu pana na kujigeuza juu ya kitanda chake cha miti, baada ya muda usingizi ukampitia.



    Kulipopambazuka, aliwahi kuamka na kutoka nje ya kibanda chake, akawa anafanya mazoezi mepesi huku akilisubiri kundi la masokwe lipite. Penzi lake kwa malkia wa masokwe lilikuwa linazidi kuongezeka kila uchao, akawa anamuomba Mungu wake siku moja ndoto zake za kuishi naye zitimie.



    Baada ya muda, kundi la masokwe liliwasili eneo lile, malkia wao akiwa katikati kama kawaida. Harrison alitamani malkia wa masokwe amsogelee lakini haikuwezekana. Lilipopita alianza kulifuatilia kwa nyuma. Tofauti na siku zote, malkia wa masokwe alikuwa akigeuka na kumtazama Harrison mara kwa mara.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kukimbia kwa muda mrefu, hatimaye kundi lile la masokwe lilifika kwenye miti ya matunda, Harrison akajibanza kwenye mti mkubwa uliokuwa jirani. Alikuwa anaogopa kumsogelea hovyo malkia wa masokwe kwani mara zote alizojaribu kufanya hivyo, aliambulia kipigo kikali kutoka kwa masokwe waliokuwa wanamlinda.



    Masokwe waliendelea kula matunda juu ya miti, wakihama kutoka mti mmoja hadi mwingine. Walipotosheka walikusanyana na kuanza safari ya kuondoka huku wakihakikisha malkia wao anapata ulinzi wa kutosha. Harrison alisubiri masokwe waanze kuondoka, na yeye akaanza kuwafuata kwa nyuma huku akikimbia.



    Licha ya kujitahidi kukimbia kwa kasi, Harrison alijikuta akizidiwa na uchovu, akaamua kuliacha kundi lile kubwa liondoke, akatafuta sehemu yenye kivuli na kupumzika. Baada ya muda aliinuka na kuanza kujikongoja kurudi kwenye kibanda chake.



    Baada ya kutembea umbali mrefu, alifika kwenye kibanda chake, akashtuka baada ya kuona kuna furushi limewekwa jirani na mlango wa kuingilia.

    “Nani tena aliyeweka mzigo wake mlangoni?” alijiuliza Harrison huku akitembea kwa tahadhari kuusogelea. Katika hali ambayo hakuamini macho yake, aligundua kuwa ni furushi la matunda mchanganyiko kama ambayo aliletewa jana yake na malkia wa masokwe.



    “Kumbe ananipenda sana? Kila siku ananiletea matunda?” alijisemea Harrison kimoyomoyo huku akitabasamu. Kwa kuwa alikuwa na njaa, alikaa na kuanza kuyafaidi. Mengine aliyahifadhi kwa ajili ya kuyala jioni, akanywa na maji na kujilaza nje ya kibanda chake.



    Muda ulizidi kuyoyoma, jua likawa linazidi kuwa kali. Kwa kuwa nyama aliyopewa na mzee Hondo ilikuwa imeshaisha, alijikuta akipatwa na akili ya kwenda kuwinda ili apate kitoweo. Asingeweza kuendelea kuishi kwa kutegemea kula matunda tu.



    Akachukua mkuki na kisu kikubwa alivyopewa na mzee Hondo na kutoka, akaelekea upande kulipokuwa na chemchemi ya maji kwani aliamini muda ule wa jua kali, wanyama wengi hupenda kwenda kunywa maji. Hakuwahi kuwinda hata mara moja katika maisha yake lakini hakuwa na ujanja.



    Alitembea umbali mrefu mpaka alipofika kwenye chemchemi ndani ya msitu ule wa Tongass, akatafuta sehemu nzuri na kujiweka tayari kwa mawindo. Baada ya muda, aliona kundi la swala wakielekea kunywa maji, akaushika mkuki wake vizuri na kuanza kunyata kusogea mahali kundi lile lilipokuwepo.



    Alipolikaribia, alirusha mkuki wake lakini kwa kuwa hakuwa na uzoefu wa kuwinda, alikosea kulenga shabaha, mkuki ukaenda kuangukia mbali huku wale swala wote wakikimbilia vichakani. Alienda kuuokota mkuki wake, akarudi tena kujificha huku akijipa moyo kuwa lazima atapata kitoweo.



    Baada ya muda, kundi lingine la digidigi lilifika kunywa maji kwenye chemchemu ile, Harrison akanyata hadi karibu na kurusha tena mkuki wake kwa nguvu. Kama ilivyokuwa mwanzo, alikosea shabaha na kusababisha wanyama wale wakimbilie vichakani. Akaenda kuuokota mkuki wake na kurudi tena.



    Alienda kuwakosakosa wanyama mpaka jua lilipoanza kuzama, akaamua kukubali kushindwa. Akanywa maji na kuanza safari ya kurudi kwenye kibanda chake akiwa mikono mitupu. Alitembea kwa muda mrefu mpaka giza lilipoingia, akafanikiwa kufika salama kwenye kibanda chake.



    Kwa kuwa njaa ilikuwa inamuuma, alimalizia matunda aliyokuwa ameyabakiza na kunywa maji, akawasha moto na kukaa pembeni huku mawazo juu ya malkia wa masokwe yakiendelea kukitawala kichwa chake.



    “Leo akija nitamfurahisha mpaka akubali kulala na mimi hadi asubuhi,” aliwaza Harrison huku akiendelea kuweka kuni kwenye moto. Muda ulizidi kuyoyoma bila malkia wa masokwe kutokea.



    Uchovu ulisababisha aanze kuhisi usingizi mzito, akanyanyuka pale alipokuwa amekaa na kujikongoja kuingia ndani ya kibanda chake. Hakukumbuka hata kuubana vizuri mlango, usingizi mzito ukampitia.



    Alikuja kuzinduka usiku wa manane baada ya kuhisi kuna mtu ameingia ndani ya kibanda chake, akatulia kimya akitaka kujua ni nani. Alihisi huenda ni mnyama mkali wa porini anataka kumdhuru, akatulia kimya huku mapigo yake ya moyo yakimwenda mbio kuliko kawaida.



    Akiwa katika hali ile, alishtukia akiguswa mgongoni na mkono wa binadamu, mapigo ya moyo yakawa yanazidi kumwenda mbio, akawa anatetemeka mwili mzima. Kwa ujasiri wa hali ya juu alikurupuka na kusimama wima, hakuamini macho yake baada ya kugundua kuwa aliyekuwa ameingia ndani ya kibanda chake ni malkia wa masokwe.

    ***







    HARRISON, kijana msomi anajikuta akiangukia kwenye penzi la msichana aliyekuwa akiishi na masokwe ndani ya msitu wa Tongass. Licha ya kuwa na mwonekano wa kibinadamu, msichana huyo ana haiba kama za masokwe kwani alilelewa msituni tangu alipokuwa mdogo.



    Penzi la Harrison kwa msichana huyo wa ajabu linasababisha amkatae mchumba wake, Linda siku ya ndoa yao, muda mfupi kabla hawajafunga ndoa kanisani.



    Anamkimbia kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea.

    Kwa kushirikiana na rafiki yake wa siku nyingi, wanafanikiwa kuudanganya ulimwengu kuwa amepata ajali mbaya ya kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami, na kufa papo hapo.



    Taarifa hizo zinasambaa kwa kasi na kila mmoja anaamini ni kweli amekufa kumbe ukweli ni kwamba amemfuata malkia wa masokwe msituni.



    Akiwa msituni, Harrison anaendelea na harakati za kumsaka malkia wa masokwe. Licha ya ugumu anaokutana nao, hakati tamaa na haogopi chochote. Mvua na jua vinamuishia mwilini kila siku lakini mwenyewe hajali. Baada ya kuteseka sana, hatimaye ndoto yake inaanza kuelekea kutimia.



    ALIJARIBU kumsemesha maneno mawili matatu lakini aligundua kuwa malkia wa masokwe hakuwa akifahamu kabisa lugha ya kibinadamu, akawa anatoa miguno na sauti kama wafanyavyo masokwe. Alijaribu kumuelekeza kwa vitendo kuwa apande juu ya kitanda cha miti ili walale pamoja lakini malkia wa masokwe alikuwa mgumu kuelewa.



    Alipoona Harrison anazidi kumng’ang’aniza walale pamoja, malkia wa masokwe alikimbia na kutoka nje ya kibanda, Harrison naye akatoka. Japokuwa ilikuwa ni usiku wa manane, malkia wa masokwe alionesha kuwa na hamu ya kucheza na Harrison kwani alikuwa akikimbia na kuparamia matawi ya miti.



    Harrison hakutaka kuonesha kuwa alikuwa amechoka, na yeye alimfuatisha kila alichokuwa anakifanya, wakawa wanacheza huku mbalamwezi ikiwamulikia. Waliendelea kurukaruka mpaka Harrison akachoka, akafanikiwa kumshika malkia wa masokwe na kumkumbatia kimahaba.



    Kutokana na kuzidiwa na hisia za kimapenzi, Harrison alimbusu malkia wa masokwe shavuni bila kujali uchafu wa ngozi yake. Tofauti na alivyotegemea, malkia wa masokwe alimparua kwa kucha zake ndefu, akachoropoka mikononi na kuanza kukimbia.



    Hakuelewa kupigwa busu maana yake ni nini, akahisi huenda Harrison alikuwa anataka kumdhuru, jambo lililomfanya ajihami.

    Harrison alibaki kuugulia maumivu makali, akajikongoja na kurudi ndani ya kibanda chake, akapanda kitandani na kujilaza. Usingizi haukumjia haraka, aliendelea kumuwaza malkia wa masokwe na mbinu ambazo huenda zingefanikisha ndoto yake ya kumuoa kutimia.



    “Kesho akija nitahakikisha namkata kucha na nywele, lazima nimbadilishe… nataka ajue kuzungumza kama binadamu na awe na tabia za kibinadamu, nitaweza tu,” aliwaza Harrison wakati akiendelea kuugulia maumivu makali.



    Baada ya muda, usingizi ulimpitia. Akalala mpaka asubuhi, akawahi kuamka na kutoka nje ya kibanda chake. Hakuamini macho yake baada ya kumkuta malkia wa masokwe amelala juu ya mti, nje ya kibanda kile. Kwa jinsi ilivyoonesha, alilala usiku mzima palepale juu ya mti.



    Taratibu alitembea mpaka chini ya ule mti, akapanda kwa kunyata mpaka alipofika kwenye tawi ambalo malkia wa masokwe alikuwa amelala. Ghafla alizinduka kutoka usingizini, akataka kurukia kwenye tawi lingine lakini Harrison alimuwahi, akamshika na kushuka naye hadi chini.



    Kitu cha kwanza alichofanya ilikuwa ni kuanza kumkata kucha kwa kutumia kisu kikali alichopewa na Mzee Hondo.

    Kazi haikuwa nyepesi kwani alihisi kama Harrison anataka kumdhuru, akawa anajihami kwa kutishia kumng’ata na kumparua mwilini.



    Baada ya purukushani kubwa, hatimaye alifanikiwa kumkata kucha za mikono yote ambazo zilikuwa ndefu kama mnyama wa porini. Alipomaliza alimkumbatia tena mwilini, safari hii alishindwa kumjeruhi kwa kucha kwani zote zilikuwa zimekatwa.



    “Unaitwa nani?”

    “Mhhh! Arrrgh! Whuuuu,” alinguruma malkia wa masokwe kwa hasira, ikabidi Harrison amuanzishie michezo aliyokuwa anaipenda, akakimbia na kuparamia tawi la mti, malkia wa masokwe naye akamfuata.



    Wakaanza kucheza kwa furaha huku mara kwa mara Harrison akimkumbatia malkia wa masokwe. Wakiwa wanaendelea kucheza, Harrison alishtuka baada ya kusikia kelele kubwa za matawi ya miti kuvunjika na milio ya masokwe.



    Kufumba na kufumbua, kundi kubwa la masokwe waliokuwa wamebeba mawe makubwa, fimbo na magongo liliwasili eneo lile na kukizunguka kibanda cha Harrison. Masokwe walikuwa wanamtafuta malkia wao ambaye alitoweka tangu usiku uliopita.



    “Mungu wangu, leo nimepatikana… nitatoka salama kweli hapa?” alisema Harrison huku akitafuta upenyo wa kukimbilia. Alishangaa kuona malkia wa masokwe anamfuata mwilini na kumshikilia akionesha kwamba hakutaka masokwe wenye hasira wamdhuru.



    Mara malkia wa masokwe alitoa mlio kwa ishara ambayo masokwe waliielewa, wakashusha fimbo na magongo chini huku wale ambao walishajiandaa kuvurumisha mawe makubwa nao wakiyatupa chini. Harakaharaka malkia wa masokwe aliparamia kwenye matawi na kuruka hadi katikati yao, kwa kasi ya ajabu kundi lote likaanza kuondoka eneo lile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Harrison alishusha pumzi ndefu huku akiwa haamini kilichotokea. Alijiuliza maswali mengi ndani ya kichwa chake ambayo yote hakuyapatia majibu, akajisogeza mahali kijua cha asubuhi kilipokuwa kinapenya, akakaa na kuanza kuota jua.



    Muda ulizidi kuyoyoma, baadaye akachukua mkuki wake na kutoka kwenda kuwinda kwani njaa ilikuwa ikimuuma sana na hakuwa na chakula.

    “Leo lazima nipate kitoweo, nitajitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu,” alisema Harrison wakati akitembea katikati ya vichaka kuelekea mahali kulipokuwa na chemchemi.



    Baada ya kutembea kwa umbali mrefu, hatimaye alifika kwenye chemchemi, akatafuta sehemu nzuri na kujificha huku mkuki wake ukiwa mkononi.



    Baada ya muda, kundi la paa liliwasili na kukimbilia kunywa maji, taratibu akaanza kunyata na kusogea huku mkuki wake ukiwa mkononi. Baada ya kusogea, aliinua mkuki na kuurusha kwa nguvu zake zote, ukaenda kumchoma paa mmoja shingoni, akajaribu kukimbia lakini alianguka mita chache mbele huku lile kundi lingine likitawanyika. Akakimbia hadi mahali paa yule alipoangukia, akachomoa kisu na kummalizia huku akiwa haamini kama kweli amefanikiwa kupata kitoweo.



    Kwa jinsi alivyokuwa na njaa, hakutaka kupoteza muda, alimnyanyua na kumbeba begani, akaanza safari ya kurudi kwenye kibanda chake. Alitembea vichakani huku jasho likimvuja kutokana na uzito wa kitoweo chake, baada ya kutembea kwa umbali mrefu akafika.



    Jambo la kwanza lilolifanya ilikuwa ni kuwasha moto kisha akaanza kuandaa kitoweo. Alimchuna ngozi na kumtoa utumbo, akamkatakata na kuanza kumchoma kwenye moto aliouwasha. Akiwa anaendelea kuandaa kitoweo, aliendelea kumfikiria malkia wa masokwe na jinsi alivyofanikiwa kujenga naye ukaribu.



    Japokuwa alikuwa akifahamu kabisa kuwa ni dhambi kufanya mapenzi kabla ya kuoana, alijikuta tamaa ya mwili ikimjaa na kuanza kufikiria kukutana kimwili na malkia wa masokwe. Kila alipokuwa anakikumbuka kifua chake kilichonakshiwa na vifuu vya nazi vilivyochongoka sawia na umbo lake la Kibantu lililositiriwa na kipande kidogo cha kitambaa kikuukuu, alijikuta akisisimka kuliko kawaida.

    “Lazima nimpate, lazima awe mke wangu,” alijisemea Harrison huku akiendelea kuchoma nyama.

    ***





    MVUMILIVU hula mbivu, walinena wahenga. Penzi la malkia wa masokwe, msichana aliyelelewa na masokwe ndani ya msitu wa Tongass linamchanganya kabisa Harrison. Tangu mara ya kwanza alipomuona malkia wa masokwe wakati akiwa kwenye utafiti wake wa tabia za wanyama ndani ya msitu huo, anajikuta akizama penzini kiasi cha kuwa tayari kufanya lolote ilimradi ampate.



    Penzi lake kwa msichana huyo wa ajabu linasababisha amkatae mchumba wake, Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Anatoroka kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea.



    Kwa kushirikiana na rafiki yake wa siku nyingi, wanaandaa mpango maalum wa kuwafanya watu waamini kuwa Harrison amekufa. Wanatengeneza ajali feki inayowafanya watu waamini kuwa amepata ajali mbaya ya kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami.



    Kwa jinsi walivyouandaa mpango huo kwa umakini, kila mtu anaamini kuwa ni kweli kijana huyo msomi amekufa, wanaomboleza kisha wanaenda kuuzika mwili ambao kila mmoja alikuwa anaamini kuwa ni wa Harrison.



    Baada ya hapo anatorokea porini ambako anaendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Hajali ugumu anaokutana nao, akili yake inawaza kitu kimoja tu, penzi la malkia wa masokwe. Jitihada zake zinamuwezesha kuanza kujenga mazoea na malkia wa



    masokwe kiasi cha kuwa wanacheza pamoja michezo ya kisokwe mara kwa mara.



    WAKATI Harrison akiendelea kuchoma nyama pembeni ya kibanda chake, ndani kabisa ya msitu wa Tongass, alisikia vishindo vya mtu akitembea vichakani kuelekea pale alipokuwa. Japokuwa kigiza cha jioni kilikuwa kimeanza kuingia, alipogeuka tu alimtambua malkia wa masokwe mara moja. Akaacha kila alichokuwa anakifanya na kusimama.



    Malkia wa masokwe alitembea taratibu mpaka alipomkaribia Harrison, akasimama mita kadhaa kutoka pale alipokuwepo. Harrison alitabasamu kwa furaha, akamuonesha kwa ishara kuwa asogee jirani na moto kisha akae. Malkia wa masokwe alisita kwa muda, kisha akasogea mpaka pale pembeni ya moto na kukaa.



    Harrison akawa anaendelea kuchoma nyama huku akitumia muda mwingi kumtazama malkia wa masokwe usoni. Alitamani angekuwa na uwezo wa kuzungumza kama binadamu wengine ili amueleze kilichokuwa ndani ya moyo wake lakini haikuwa hivyo.



    Malkia wa masokwe hakuwa akijua lugha yoyote zaidi ya ishara kama wafanyazo masokwe. Akakaa kimya pembeni ya Harrison, akawa anamuangalia jinsi alivyokuwa anachoma nyama. Alipoanza kuivisha, Harrison alikata kipande na kula, kisha akampa na malkia wa masokwe.



    Cha ajabu ni kwamba alishindwa kula nyama, akaishia kuinusa kisha akaitupa chini. Harrison alijaribu kumpa tena lakini bado alifanya vilevile, akavuta kumbukumbu juu ya tabia za masokwe alizojifunza alipokuwa chuoni kwamba wanyama hao hawali kabisa nyama zaidi ya mizizi, matunda na majani ya porini.



    Alikumbuka kuwa ni aina chache sana za sokwe ndiyo hula wanyama wadogo lakini wanapatikana zaidi barani Afrika. Kwa kuwa alikuwa na njaa, aliendelea kula mwenyewe huku malkia wa masokwe akimtazama. Baada ya kula kiwango kikubwa cha nyama, iliyobakia aliibanika kisha akaiingiza ndani ya kibanda chake.



    Akatoka na kuanza kucheza na malkia wa masokwe. Mara kwa mara macho yake yalikuwa yakitua kwenye kifua kibichi cha msichana huyo, hisia za mapenzi zikaanza kumpanda taratibu ingawa alijitahidi kuzizuia. Hakuna kitu ambacho malkia wa masokwe alikuwa anapenda kama kucheza michezo ya kisokwe na Harrison.



    Mara kwa mara alikuwa anapenda wafukuzane kwenye miti na kuparuana na kucha lakini Harrison hakuwa na uwezo huo zaidi ya kuwa anakimbiakimbia na kujificha kwenye miti. Waliendelea kucheza kwa muda mrefu, Harrison akachoka sana hasa ukizingatia kuwa siku hiyo alitembea umbali mrefu kwenda kuwinda.



    “Ngoja nijaribu kumkumbatia na kumbusu, sijui ataelewa?” aliwaza Harrison wakati akimuangalia malkia wa masokwe aliyekuwa anaendelea kurukia matawi ya miti. Baada ya kurukaruka, alimsogelea Harrison aliyekuwa amekaa chini akitaka waendelee kucheza. Alipomkaribia, Harrison alimrukia na kumkumbatia, akambusu shavuni.



    Kama ilivyokuwa kawaida ya malkia wa masokwe, alichoropoka mikononi mwa Harrison na kujaribu kumparua akidhani anataka kumdhuru. Kwa kuwa Harrison alishamkata kucha, hakumjeruhi. Akakimbia na kwenda kwenye tawi la mti, akapanda juu na kuanza kumuangalia Harrison.



    Alimfanyia ishara ya kumuita kwa kutumia mikono yake, malkia wa masokwe akateremka kwenye tawi la mti lakini safari hii hakutaka kumsogelea, akasimama mbali huku akimuangalia kwa macho ya woga. Kwa kuwa tayari ilikuwa ni usiku sana, Harrison alimuoneshea ishara kuwa waingie ndani wakalale lakini malkia wa masokwe akakataa kwa kutingisha kichwa na mabega.



    “Huyu dawa yake ndogo, atanifuata mwenyewe,” alijisemea Harrison kimoyomoyo, akafungua mlango wa kibanda chake na kuingia ndani, akaenda kujilaza huku hisia za mapenzi zikiendelea kumtesa.



    “Angekuwa anaelewa jinsi ninavyoteseka juu yake asingekuwa anakimbia nikimkumbatia na kumbusu,” alijisemea huku akiendelea kuteseka kwa hisia kali za mapenzi alizokuwa nazo. Wakati akiendelea kuwaza, malkia wa masokwe alisukuma mlango, naye akaingia na kusimama kwenye pembe ya kibanda kile.



    Harrison alijifanya hajamuona, akaendelea kujilaza vilevile, baada ya kusimama kwa dakika kadhaa, malkia wa masokwe alisogea na kukaa pembeni ya kitanda, kwa msaada wa mbalamwezi iliyokuwa inapenya mpaka ndani ya kibanda kile, Harrison alianza kuusanifu uzuri wake bila mwenyewe kugundua kuwa alikuwa anatazamwa.



    Aliendelea kumuangalia kiungo kimoja baada ya kingine, kuanzia usoni mpaka kushuka chini. Kwa hakika malkia wa masokwe alikuwa na uzuri wa kipekee unaoweza kumchanganya mwanaume yeyote aliyekamilika.



    Kutokana na kuzidiwa na hisia za kimapenzi, Harrison alijikuta akiinua mkono wake mmoja na kumshika kifuani malkia wa masokwe, akaruka na kusimama, Harrison naye akasimama na kumkumbatia kwa nguvu. Malkia wa masokwe alijaribu kujichoropoa lakini kwa sababu Harrison alimbana ukutani, alishindwa, akabaki anahangaika.



    Kwa mara nyingine Harrison alipeleka mkono wake mmoja kifuani na kumgusa upande wa kulia, malkia wa masokwe akashtuka tena na kuanza kuhema kwa nguvu. Harrison alimbusu shavuni na shingoni, akarudiarudia mara kadhaa mpaka malkia wa masokwe akatulia huku akizidi kuhema kwa nguvu.



    Kwa kutumia mkono mmoja, Harrison aliteremsha suruali yake na kuivua akiwa bado amembana malkia wa masokwe pale ukutani. Alifungua pia vishikizo vya shati lake huku akiendelea kumbusu sehemu mbalimbali, alipomaliza alimbeba malkia wa masokwe na kumbwaga kitandani.



    Kabla hajatimiza alichotaka kukifanya, malkia wa masokwe alipata upenyo, akamsukuma kwa nguvu mpaka ukutani, akainuka na kutoka nje kwa kasi, Harrison alifanikiwa kumdaka mkono, wakawa wanavutana kabla ya malkia wa masokwe kutishia kumng’ata mkono. Harrison alipoona hivyo, alimuachia, akatimua mbio na kutokomea vichakani.

    Harrison aliokota nguo zake na kuzivaa huku akihema kama ametoka kukimbia riadha.



    “Kwanza afadhali amekimbia, kanisani tulifundishwa kuwa ni dhambi kukutana kimwili kabla hamjafunga ndoa na kuhalalishwa mbele za Mungu,” alijisemea Harrison huku akijifuta kijasho chembamba kilichokuwa kinamtoka. Alirudi kitandani na kujilaza, akawa anaendelea kumuwaza malkia wa masokwe.



    “Sijui nifanye nini ili anielewe kuwa nampenda, sitakata tamaa mpaka atakapokuja kuwa mke wangu,” alijisema Harrison. Licha ya kujitahidi kuubembeleza usingizi, Harrison hakulala haraka. Mawazo juu ya malkia wa masokwe yaliendelea kumtesa kwa muda mrefu.

    Akiwa bado anagalagala juu ya kitanda cha miti, alisikia vishindo vya mtu akija, mara akaona mlango ukisukumwa, malkia wa masokwe akaingia tena na kwenda kukaa palepale alipokuwa amekaa awali.

    ***







    LICHA ya aina ya maisha anayoishi msichana wa ajabu ndani ya msitu mkubwa wa Tongass akiwa na tabia kama masokwe, Harrison anajikuta akiangukia kwenye penzi zito la msichana huyo. Hajali watu watamuonaje, anachotaka ni mapenzi tu.

    Hali hiyo inamfanya amkatae mchumba wake, Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Anatoroka kanisani kwa



    kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea. Kwa msaada wa rafiki yake wa siku nyingi, wanaandaa mpango maalum wa kuwafanya watu waamini kuwa Harrison amekufa.



    Wanatengeneza ajali feki inayowafanya watu waamini kuwa amegongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami nchini Marekani.



    Kila mtu anaamini kuwa ni kweli kijana huyo msomi amekufa, wanaomboleza kisha wanaenda kuuzika mwili ambao kila mmoja alikuwa anaamini kuwa ni wa Harrison.



    Baada ya hapo anatorokea porini ambako anaendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Taratibu anaanza kujenga mazoea naye kiasi cha kufikia hatua ya malkia wa masokwe kuwatoroka masokwe na kumfuata Harrison kwenye kibanda chake. Harrison naye anazidi kupandwa na hisia kali za mapenzi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Harrison alijikausha kama hajamuona malkia wa masokwe kwani alijua kuwa akianza kumfanyia vituko tena, anaweza kukimbia kama awali na asirudi tena. Alitulia kimya kitandani, akajifanya macho yake ameyafumba kumbe alikuwa akimtazama malkia wa masokwe kwa wizi.



    “Lazima atapitiwa na usingizi tu,” aliwaza Harrison huku akiendelea kujikausha. Baada ya malkia wa masokwe kukaa pale pembeni ya kitanda kwa muda, alianza kuhisi uchovu mkali, akajisogeza vizuri na kulala kama Harrison alivyokuwa amelala lakini tofauti yao ni kwamba kila mmoja alikuwa amegeukia upande wake huku miguu ya malkia wa masokwe ikiwa kwenye kichwa cha Harrison.



    “Yap, lazima ataingia kwenye mtego tu, leo ndiyo leo asemaye kesho mwongo,” alijisemea Harrison huku akizidi kujikausha pale kitandani. Baada ya kukaa kwa zaidi ya dakika arobaini, alianza kumsikia malkia wa masokwe akikoroma kwa mbali kuashiria kuwa usingizi ulikuwa umeanza kumpitia.



    Kwa tahadhari kubwa aliinuka huku akijitahidi kutosababisha kelele zozote zinazoweza kumshtua malkia wa masokwe. Aliteremka mpaka chini ya kitanda, taratibu akavua suruali yake na shati, akabaki kama alivyoletwa duniani. Kwa msaada wa mbalamwezi alimsogelea malkia wa masokwe pale alipokuwa amelala, akaanza kumpapasa mwili wake kuanzia kichwani kushuka chini.



    Alijitahidi kufanya kila kitu kwa utulivu wa hali ya juu akikwepa kumshitua, alimbusu kwenye mashavu yake huku akizipapasa nywele zake taratibu, akahamia shingoni na kuanza kushuka chini.



    “Tazama ulivyoumbika, nikubalie ombi langu tafadhali… nataka uwe mke wangu wa halali, tujenge familia pamoja, niitwe baba na wewe uitwe mama,” alisema Harrison kwa hisia za hali ya juu. Malkia wa masokwe hakuwa akielewa chochote kutokana na kupitiwa na usingizi mzito.



    Aliendelea kumpapasa mwili wake taratibu, akafika kwenye kifua chake kichanga kilichonakshiwa na michongoma miwili iliyokuwa imesimama wima. Taratibu akaanza kukisanifu huku mapigo yake ya moyo yakizidi kuongezeka kwa kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.



    Alivinjari kwenye michongoma ile kwa zaidi ya dakika ishirini mpaka aliporidhika, akaendelea kushuka chini hadi kwenye kitovu, akaweka kituo hapo na kuanza kucheza nacho. Hakujali uchafu aliokuwa nao msichana huyo wa ajabu, akawa anatalii huku na kule huku akilibusu tumbo lake lililokuwa limejengeka vizuri.



    “Sijawahi kuona msichana mzuri kama huyu, sijui ilikuwaje mpaka akaja kuishi huku porini, angekuwa mjini huyu angewasumbua sana wanaume wakware,” aliendelea kuwaza huku vidole vyake vikiendelea kumpapasa malkia wa masokwe



    hapa na pale. Hakuishia hapo, alizidi kushuka chini ambapo sasa alishindwa kuzizuia hisia zake.

    Akawa anajaribu kumfungua kitambaa kikuukuu alichokuwa amejifunga kiunoni na kujisitiri sehemu muhimu zaidi za mwili



    wake. Hakuweza kufanikiwa kirahisi kwani kilifungwa mafundo mengi na kwa ustadi mkubwa.

    Akaamua kusitisha zoezi lile na kuendelea kwenda chini, akakutana na mapaja yaliyonawiri vizuri, akawa anayabusubusu kwa hisia kali. Alijiuliza maswali mengi ambayo yote hakuyapatia majibu. Alishangaa iweje mtu anayeshindia matunda ya porini na mizizi awe na mwili uliojengeka vizuri kimahaba kiasi kile?



    Aliendelea kufanya utundu wake mpaka alipofika kwenye nyayo za miguu yake. Alipozipapasa aligundua kuwa nyayo zimekuwa ngumu sana, akahisi huenda ni kwa sababu ya kutembea bila viatu. Alipozidi kuzipapasa, aligundua kuwa alikuwa na vipande vingi vya miba na vijiti ambavyo vilikuwa vimeng’ang’ania ngozi yake ya miguuni, akajikuta akimuonea huruma.



    “Kesho nitamtoa miba yote na kuisafisha miguu yake,” alijisemea huku akiianza upya safari ya kutalii mwili wa malkia wa masokwe, safari hii akianzia chini kwenda juu. Alipofika karibu na kiuno, aliweka kituo na kuanza tena kujaribu kufungua kitambaa alichokuwa amejifunga.



    Akiwa anaendelea na zoezi lile, alishtuka kupita kiasi baada ya kusikia kishindo kikubwa juu ya paa la kibanda chake, punde zikaanza kusikika kelele za matawi ya miti kuvunjika na purukushani za hapa na pale kwenye miti iliyokuwa inakizunguka kibanda kile, akajua kundi la masokwe limemfuata malkia wao.



    Alitamani masokwe wamuachie japo dakika chache ili amalizie kufanya kile alichokuwa amekikusudia lakini haikuwezekana, masokwe waliokuwa na hasira walianza kukibomoa kibanda chake huku wengine wakirusha mawe makubwa.



    Kufumba na kufumbua, masokwe watatu wakubwa walivunja mlango na kuingia ndani ya kibanda ambapo walimkuta Harrison akiwa kama alivyozaliwa na malkia wao akiwa amelala kitandani.



    Masokwe wawili walianza kumuadhibu vikali Harrison wakati yule mmoja alimbeba malkia wao. Harrison alijitahidi kujiokoa lakini hakuweza kutokana na nguvu walizokuwa nazo masokwe wale, wakawa wanamtandika makofi mazito huku alama za viganja vyao zikibaki kwenye mwili wa Harrison.



    Purukushani zile zilisababisha malkia wa masokwe azinduke kutoka usingizini, akajikuta tayari amebebwa juujuu na sokwe mkubwa. Japokuwa ilikuwa ni usiku wa manane, malkia wa masokwe aliona jinsi Harrison alivyokuwa anasulubiwa, ikabidi apige yowe kubwa kama ishara ya kuwakataza wale masokwe wasiendelee kumdhuru Harrison.



    Wale masokwe walimuachia Harrison lakini tayari alikuwa amejeruhiwa vibaya, damu zikawa zinamtoka mdomoni na puani huku uso wote ukiwa na alama za viganja vya makofi aliyokuwa anapigwa na masokwe wale.



    Sekunde chache baadaye, kundi lile lilitokomea na malkia wao gizani kwa kasi kubwa, Harrison akatoka nje ya kibanda chake kwa kujikongoja, akapiga magoti na kuanza kulia kwa uchungu kutokana na maumivu aliyokuwa anayahisi. Baada ya hasira kupungua na maumivu kupoa kiasi, alirudi ndani na kujilaza kwenye kitanda ambacho kiliharibiwa upande mmoja na wale masokwe.



    Akalala mpaka asubuhi, kulipopambazuka tu aliamka na kuwasha moto, akabandika maji kwa kutumia kigae alichokiokota njiani siku alipokuwa anatoka kwa mzee Hondo, yalipopata moto akaanza kujichua usoni na sehemu mbalimbali zilizokuwa na majeraha.



    “Nitavumilia mateso na shida zote mpaka nimpate malkia wa masokwe, sitakata tamaa,” alijisemea Harrison huku akiendelea kujichua kwenye majeraha kwa maji ya moto.

    ***





    HARRISON, kijana mdogo aliyekuwa amebobea kwenye masomo ya tabia za wanyama na mimea, anajikuta akiangukia kwenye penzi la msichana wa ajabu ndani ya msitu mkubwa wa Tongass. Msichana huyo mwenye tabia kama masokwe, anamchanganya Harrison kiasi cha kutojali watu watamuonaje au watasemaje, anachotaka ni mapenzi tu kutoka kwake.



    Malkia wa masokwe anamfanya Harrison amkatae mchumba wake, Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Anatoroka kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea. Kwa msaada wa rafiki yake wa siku nyingi, wanaandaa mpango maalum wa kuwafanya watu waamini kuwa Harrison amekufa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wanatengeneza ajali feki inayowafanya watu waamini kuwa amegongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami nchini Marekani. Kila mtu anaamini kuwa ni kweli kijana huyo msomi amekufa, wanaomboleza kisha wanaenda kuuzika mwili ambao kila mmoja alikuwa anaamini kuwa ni wa Harrison.



    Baada ya hapo anatorokea porini ambako anaendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Taratibu anaanza kujenga mazoea naye kiasi cha kufikia hatua ya malkia wa masokwe kuwatoroka masokwe na kumfuata Harrison kwenye kibanda chake.



    Harrison naye anazidi kupandwa na hisia kali za mapenzi na kujikuta akitamani kuvunja amri ya sita na msichana huyo. Ghafla masokwe wanakivamia kibanda chake na kumchukua malkia wao huku wengine wakimtembezea Harrison kichapo.

    HARRISON aliendelea kujiuguza majeraha yake kwa siku tatu mfululizo, hatimaye akapona ingawa alibaki na makovu sehemu mbalimbali za mwili wake. Kwa siku zote hizo, malkia wa masokwe hakumtembelea tena mpaka akaanza kuwa na wasiwasi.

    “Au wale masokwe walimdhuru siku ile?” Harrison aliwaza akiwa amekaa nje ya kibanda chake, akajiapiza kuwa siku inayofuata ataamka mapema na kufuatilia nini kilichomtokea malkia wa masokwe kwani haikuwa kawaida yake.

    Akiwa anaendelea kuwaza, alisikia vishindo vya mtu vikitokea vichakani, alipotazama vizuri aligundua kuwa ni malkia wa masokwe. Tofauti na siku zote, safari hii alionekana kuwa mnyonge sana. Muda wote alikuwa ameinamisha kichwa chake chini huku mwili wake ukiwa umedhoofika.

    “Amepatwa na nini?” alisema huku akimsogelea kwa tahadhari. Malkia wa masokwe alisimama pembeni ya mti na kuuegamia, alionesha kuishiwa nguvu. Harakaharaka Harrison alimsogelea, akagundua kuwa alikuwa ametokwa vidonda vingi mdomoni kuashiria kwamba alikuwa anaumwa.

    “Mungu wangu, nitafanya nini kumsaidia?” aliwaza Harrison huku akijaribu kukumbuka dawa aliyopewa na mzee Hondo siku aliyokuwa anaumwa. Hakukumbuka hata kidogo, akapata wazo kichwani mwake ingawa aligundua kuwa kuna ugumu.

    Alipata wazo la kumpeleka malkia wa masokwe nyumbani kwa mzee Hondo ili akatibiwe kwani kwa jinsi ilivyoonesha, hali yake ilikuwa mbaya sana. Akawa anajiuliza atawezaje kuondoka naye, isitoshe tayari muda ulikuwa umekwenda sana. Bila kupoteza muda alifunga mlango wa kibanda chake na kumshika mkono malkia wa masokwe.

    Wakaondoka na kuianza safari ya kuelekea nyumbani kwa mzee Hondo. Harrison hakujali umbali uliokuwepo na kwamba muda ulishaenda sana, kitu pekee alichokuwa anakiwaza kwa wakati ule ilikuwa ni kuhakikisha malkia wa masokwe anapona.

    Walitembea vichakani kwa muda mrefu, jua likaanza kuzama wakiwa bado ndani ya msitu huo. Mwendo wao ulikuwa wa taratibu sana kwani malkia wa masokwe hakuwa na nguvu kabisa, wakaendelea na safari yao kwa muda mrefu.

    Jua lilipoanza kuzama, malkia wa masokwe alishindwa kuendelea kutembea, akawa anatetemeka mwili mzima huku akitaka kujitoa kutoka kwenye mkono wa Harrison.

    Harrison alimuachia, akainama na kumuoneshea ishara kuwa apande mgongoni. Malkia wa masokwe alipanda kwenye mgongo wa Harrison huku akiendelea kutetemeka, akambeba na safari ikaendelea. Japokuwa alikuwa mzito, Harrison alijikaza, akawa anatembea harakaharaka huku jasho likimtoka.

    Safari iliendelea kwa muda mrefu, giza likaanza kuingia wakiwa bado ndani ya msitu wa Tongass. Ilifika muda Harrison akawa amechoka sana, akatafuta sehemu ya kupumzika, akamshusha malkia wa masokwe na kumkalisha chini. Baada ya kupumzika vya kutosha, akambeba tena na safari ikaendelea.

    Kutokana na jinsi alivyokuwa anaumwa, malkia wa masokwe alipitiwa na usingizi akiwa mgongoni mwa Harrison, safari ikaendelea. Baada ya kutembea umbali mrefu, ikiwa ni tayari usiku sana, hatimaye Harrison alifika nyumbani kwa mzee Hondo.

    Akamshusha malkia wa masokwe na kumlaza chini, akaanza kugonga mlango wa nyumba ya mzee huyo mwindaji. Aligonga kwa muda mrefu bila kuitikiwa, baadaye akasikia mtu akitembea kwa kunyata kusogelea mlango. Akachungulia nje kisha ndiyo akafungua mlango.

    Hiyo ndiyo ilikuwa kawaida ya mzee huyo ambaye muda mwingi alikuwa akijihami. Alipofungua mlango alikutana na Harrison aliyekuwa ameloa jasho mwili mzima.

    “Vipi? Mbona umekuja usiku namna hii halafu unatokwa na jasho jingi? Unaumwa?” aliuliza mzee Hondo kwa mshangao kwani Harrison hakuwa katika hali ya kawaida. Hakumjibu kitu badala yake alimuoneshea mahali alipokuwa amelala malkia wa masokwe.

    Mzee Hondo alirudi ndani na kuwasha taa yake ya karabai, akatoka nje na kumulika pale malkia wa masokwe alipokuwa amelala.

    “Huyu ni nani?”

    “Ndiyo msichana niliyekuwa nakwambia siku zote.”

    “Amepatwa na nini? Mbona mwili wake umechemka hivi?” alihoji mzee Hondo huku akimgusa kwenye paji la uso. Ilibidi Harrison amuelezee kila kitu. Wakasaidiana kumbeba na kumuingiza ndani, akaenda kulazwa kwenye kitanda cha kamba akiwa hajitambui.

    Bila kupoteza muda, mzee Hondo aliwasha moto wa kuni na kubandika chungu kikubwa, akatoka nje na kumwambia Harrison aendelee kuchochea moto. Japokuwa ilikuwa ni usiku sana, baada ya dakika kadhaa mzee Hondo alirudi akiwa na furushi la majani ya porini na mizizi.

    Akachambua harakaharaka na kuweka kwenye chungu cha maji ambacho sasa kilikuwa kinachemka. Waliendelea kusaidiana kuchochea moto mpaka dawa ikachemka. Wakasaidiana kuanza kumnywesha dawa huku nyingine wakimchua nayo mwili mzima.

    Kwa kadiri walivyokuwa wanamnywesha na kumkanda mwili mzima ndivyo hali yake ilivyokuwa inabadilika. Baada ya mwili wake kukolea dawa, alianza kupiga chafya mfululizo kisha akafumbua macho.

    Alianza kuangaza macho huku na kule kama anayejiuliza pale ni wapi, Harrison akamsogelea na kuanza kumpapasa shingoni kwa upole huku mzee Hondo akiendelea na kazi ya kumkanda.

    “Kijana halali yako kusota porini kwa ajili ya huyu msichana, sijawahi kuona mwanamke mwenye sura nzuri kama huyu, tena anaonekana bado mbichi kabisa,” alisema mzee Hondo, Harrison akacheka kwa furaha. Baada ya mzee Hondo kuridhika na hali yake, aliacha kumkanda, wakakaa pembeni ya kitanda chake na kuanza kumtazama.

    “Na wewe mbona una makovu mengi? Nini kilikupata?”

    “Mh! Yaani we acha tu mzee wangu, nilishambuliwa na kundi la masokwe kwa sababu ya huyu mrembo,” alisema Harrison, kauli iliyomfanya mzee Hondo avunjike mbavu kwa kicheko. Wakiwa wanaendelea na mazungumzo ya hapa na pale, walianza kusikia kelele kubwa nje huku matawi ya miti yakivunjikavunjika.

    “Mungu wangu, tumekwisha,” alisema Harrison kwa hofu huku akijificha nyuma ya mzee Hondo.

    “Kwani vipi?”

    “Masokwe wamemfuata malkia wao.”

    “Sasa wamejuaje kuwa umemleta huku wakati ni usiku?”

    “Wana tabia ya kunusa, wamegundua kuwa nimemleta huku kwa kufuatisha harufu ya njia niliyopita naye.”

    “Basi tulia, mimi ndiyo mzee Hondo, nitahakikisha hawatusababishii madhara yoyote,” alisema mzee Hondo, akaingia chumba cha pili na kukusanya zana zake za kuwindia.

    Akatoka na kumwambia Harrison amfuate, wakafungua mlango na kutoka nje.

    “Mungu wangu, mbona wengi hivi?” alisema mzee Hondo kwani awali alidhani ni masokwe wachache ndiyo waliokuja lakini haikuwa hivyo.

    Ikabidi warudi ndani haraka kujipanga upya, Harrison akawa anatetemeka kwa hofu huku mara kwa mara akigeuka na kumuangalia malkia wa masokwe aliyekuwa ametulia kitandani.

    “Hapa inabidi niwaite mbwa wangu wa kuwindia watusaidie kazi,” alisema mzee Hondo, akaanza kupiga miluzi kwa nguvu.

    Baada ya sekunde kadhaa, kundi la mbwa wapatao kumi lilikusanyika mbele ya nyumba ya mzee Hondo. Akatoka na kuwaelekeza mbwa wawafukuze masokwe waliokuwa wanazidi kuongezeka. Mbwa wakaanza kubweka kwa sauti kubwa huku wakikimbilia mahali kundi lile la masokwe lilipokuwa.

    ***





    PENZI la Harrison kwa malkia wa masokwe linazidi kuchanua kila uchao. Kijana huyo aliyekuwa amebobea kwenye masomo ya tabia za wanyama na mimea, kwa mara ya kwanza alimuona malkia wa masokwe wakati akifanya utafiti kwenye msitu huo na kujikuta akiangukia kwenye penzi la msichana wa ajabu.



    Kikwazo kikubwa ni kwamba msichana huyo, licha ya uzuri wa asili aliojaaliwa, alikuwa na tabia kama za masokwe. Hakuwa akijua kuzungumza kama binadamu wengine wala kufanya chochote, alishazoea kuishi kama masokwe.



    Msichana huyo anamfanya Harrison amkatae mchumba wake, Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Anatoroka kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea. Kwa msaada wa rafiki yake wa siku nyingi, wanaandaa mpango maalum wa kuwafanya watu waamini kuwa Harrison amekufa.



    Wanatengeneza ajali feki inayowafanya watu waamini kuwa amegongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami nchini Marekani. Kila mtu anaamini kuwa ni kweli kijana huyo msomi amekufa, wanaomboleza kisha wanaenda kuuzika mwili ambao kila mmoja alikuwa anaamini kuwa ni wa Harrison.



    Baada ya hapo anatorokea porini ambako anaendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe. Taratibu anaanza kujenga mazoea naye kiasi cha kufikia hatua ya msichana huyo kuwatoroka masokwe na kumfuata Harrison kwenye kibanda chake.



    Mazoea yanaongezeka kila uchao, siku moja malkia wa masokwe anamfuata Harrison lakini anaonesha kutokuwa sawa kiafya, mwili wake umechemka na anatetemeka sana. Harrison anaondoka naye hadi nyumbani kwa mzee Hondo anakoanza kupatiwa tiba. Wakiwa wanaendelea, kundi la masokwe linavamia nyumba ya mzee Hondo.



    VITA kali kati ya kundi kubwa la masokwe na mbwa wa mzee Hondo iliendelea kwa dakika kadhaa, eneo lote likachafuka na kugeuka kuwa uwanja wa vita. Harrison ambaye alikuwa akizifahamu vyema vurumai za masokwe, alikuwa akitetemeka kwani alijua baada ya muda, masokwe watahamia kwao.

    Kwa kuwa masokwe walikuwa wengi na wakubwa, waliwashinda mbwa wa mzee Hondo, wakawa wanawarushia mawe makubwa na kuwapiga kwa magongo yaliyowajeruhi vibaya mpaka wote wakakimbia na kutokomea gizani.

    “Mungu wangu, tumekwisha.”

    “Hapa hatuna cha kufanya zaidi ya kuanza kuwaua, tukichelewa watatuua sisi,” alisema mzee Hondo huku akiziweka vizuri silaha zake za kuwindia.

    “Hapana, tusimuue sokwe hata mmoja, tutaanzisha vita kali kwani hawatakubali kuona mwenzao ameuawa.”

    “Sasa tutafanya nini? Tusipojihami watatuua kweli.”

    “Mi nashauri tumtoe malkia wa masokwe mimi nitakimbia naye.”

    “Huwezi kutoka naye, unafikiri utapita wapi wakati wameshatuzunguka,” alisema mzee Hondo huku akimshika mkono Harrison na kumvutia nyuma ya nyumba, kufumba na kufumbua nyumba yote ikavamiwa, masokwe wakavunja milango na kuingia hadi ndani walikomkuta malkia wao amelala kwenye kitanda cha kamba.

    Malkia wa masokwe alishtuka kuona masokwe wamemfuata, akaamua kuwa mpole kwani alikuwa anajua endapo atapingana nao, watasababisha maafa makubwa. Japokuwa alikuwa bado hajapona, alikubali kuondoka, masokwe wakambeba juu kwa juu na kuanza kutimua naye mbio kurudi msituni. Harrison alishindwa kujizuia, akawa anamwaga machozi kwa uchungu kama mtu aliyepewa taarifa za msiba.

    “Bado una nafasi ya kumpata, ukipata tena nafasi toroka naye mpaka mjini, huko hawawezi kukufuata,” alisema mzee Hondo huku akimpigapiga Harrison mgongoni kama ishara ya kumbembeleza.

    Kwa kuwa ilikuwa ni usiku sana, ilibidi Harrison alale palepale kwa mzee Hondo mpaka kulipopambazuka. Mzee Hondo akamfungashia furushi la dawa za mitishamba kwa ajili ya kuendelea kumtibu malkia wa masokwe endapo atakutana naye.

    Akaianza safari ya kurudi kwenye msitu wa Tongass akiwa na furushi lake la dawa. Alitembea kwa unyonge kwani kwa mara nyingine masokwe walimvunja nguvu na kufanikiwa kumchukua malkia wao mikononi mwake.

    ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande wa pili, msichana Linda bado alikuwa na kidonda ndani ya moyo wake ambacho bado kilikuwa hakijapona. Kukimbiwa na Harrison wakiwa kanisani kabla ya kufa katika mazingira ya kutatanisha kama kila mtu alivyokuwa anaamini, kulimfanya muda wote awe kama mgonjwa. Afya yake ikawa inazorota siku hadi siku huku muda mwingi akionesha kuwa na huzuni.

    Licha ya utajiri wa wazazi wake, bado hawakufanikiwa kumrejeshea furaha yake, baba yake akishirikiana na mama yake walifanya kila linalowezekana kumfurahisha lakini hawakufanikiwa.

    “Mbona umejiinamia Linda? Una tatizo?”

    “Roho inaniuma sana baba, bado sijamsahau Harrison.”

    “Najua namna unavyojisikia Linda lakini huna budi kukubaliana na ukweli, ukiwaza sana mwisho utakufuru.”

    “Hapana baba, nampenda sana Harrison mpaka inafika muda na mimi natamani bora nife ili nikaungane naye ahera.”

    “Usifikie huko mwanangu, bila shaka ipo siku utampata mwanaume mwingine atakayekusahaulisha machungu yote.”

    “Lakini baba mimi bado nina wasiwasi mkubwa sana, huenda Harrison aliuawa na watu waliochukia mimi kutaka kuolewa naye. Nahisi lazima kuna hujuma zilifanyika.”

    “Mh! Kwa nini unahisi hivyo mwanangu? Si ilikuwa ni ajali kama zilivyo ajali nyingine?”

    “Roho inaniambia hivyo kwa sababu ya jinsi matukio yalivyoongozana. Najua Harrison alikuwa ananipenda lakini pale aliponikataa kanisani inawezekana kuna kitu kilikuwa nyuma ya pazia. Kwanza alikuja kanisani akiwa amechelewa na inaonesha ni kama alikuwa anafukuzwa na watu.”

    “Yote yanawezekana mwanangu lakini hata ukifuatilia sasa hivi haitakuwa na maana tena.”

    “Hapana baba, lazima nifuatilie ili nijue ni akina nani wapo nyuma ya tukio la kumpoteza kipenzi changu niliyekuwa nampenda kuliko kitu chochote chini ya jua,” Linda na baba yake, mzee Ford walikuwa wakizungumza nje kwenye bustani ya maua.

    Baada ya mazungumzo yale, Linda aliinuka na kwenda chumbani kwake, akajiandaa na baada ya muda akatoka na kuchukua gari lake. Hakumuaga mtu na hata baba yake alipomuuliza mahali alikokuwa anakwenda, Linda alijibu kwa kifupi kwamba anatoka mara moja.

    Aliendesha gari mpaka eneo Harrison alipopata ajali na kufa kama watu wote walivyokuwa wanaamini. Taratibu Linda aliteremka kwenye gari na kutembea kwa hatua fupifupi mpaka eneo lile. Alikuwa analikumbuka vizuri, akaanza kupatazama mahali Harrison alipopatia ajali mpaka kwenye maji alikodondokea.

    “Mh! Mbona kina cha maji siyo kirefu kiasi cha kusababisha mtu afe? Halafu mbona hakuna kona wala chochote kinachoweza kusababisha ajali eneo hili?” Linda alikuwa akijiuliza maswali ambayo yote hakuyapatia majibu. Alizunguka eneo lote, mwisho akaingia kwenye maji na kupima kina chake.

    Kilichozidi kumshangaza ni kwamba hapakuwa na kina kirefu kinachoweza kusababisha kifo cha Harrison. Hata eneo alipopatia ajali bado hapakuonesha alama zozote kwamba mtu anaweza kupata ajali mbaya kiasi kile na kufa. Kengele ya hatari ikalia kwenye kichwa chake.

    “Lazima kuna mchezo ulichezwa hapa, nitafanya kila linalowezekana kuufahamu ukweli, hata kama itanigharimu kiasi gani lakini lazima nihakikishe waliomuua Harrison wangu wanapatikana.

    ***





    KWA kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, Harrison anazidi kuzama kwenye penzi la malkia wa masokwe kiasi cha kuwa tayari kufanya lolote ilimradi ampate. Kwa mara ya kwanza, Harrison aliyekuwa amebobea kwenye masomo ya



    tabia za wanyama na mimea, alimuona malkia wa masokwe wakati akifanya utafiti kwenye msitu huo na kufanikiwa kumpiga picha akiwa katikati ya kundi la masokwe, akajikuta akiangukia kwenye penzi la msichana huyo wa ajabu.



    Kikwazo kikubwa ni kwamba msichana huyo, licha ya uzuri wa asili aliojaaliwa, alikuwa na tabia kama za masokwe. Hakuwa akijua kuzungumza kama binadamu wengine wala kufanya chochote, alishazoea kuishi kama masokwe. Hakuwa na tabia za kibinadamu hata kidogo.



    Kutokana na penzi la msichana huyo, Harrison anamkataa mchumba wake, Linda kanisani muda mfupi kabla ya ndoa yao kufungwa. Anatoroka kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea. Kwa msaada wa rafiki yake wa siku nyingi, wanaandaa mpango maalum wa kuwafanya watu waamini kuwa Harrison amekufa.



    Wanatengeneza ajali feki inayowafanya watu waamini kuwa amegongwa na gari wakati akiendesha pikipiki na kutumbukia baharini kwenye Daraja la Miami nchini Marekani. Baada ya hapo anatorokea porini ambako anaendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe.



    Purukushani kubwa zinaendelea kati yake na kundi la masokwe waliokuwa wanamlinda, hata pale malkia wa masokwe alipokuwa anaumwa, alipojaribu kumsaidia ili apone alijikuta akizusha vurugu kubwa zilizoleta maafa.



    Upande wa pili, Linda bado haamini kama Harrison alikufa kifo cha kawaida na sasa anajiapiza kufanya kila linalowezekana kuujua ukweli.



    BAADA ya Linda kutoka eneo la ajali, alikwenda mpaka nyumbani kwao huku akionesha kuwa na huzuni kali. Alipofika alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwake, akajifungia mlango na kuchukua ‘diary’ yake nyeusi na kuanza kuandika baadhi ya vitu muhimu. Alipomaliza alitoka nje huku bado akionesha kuwa mnyonge.

    “Vipi, mbona unaonekana mnyonge mwanangu kipenzi,” aliuliza mzee Ford, baba mzazi wa Linda. Alishindwa cha kumjibu, akamsogelea na kujilaza kifuani kwa baba yake huku akilengwalengwa na machozi.

    “Niambie mwanangu kinachokusumbua, nitakuwa tayari kukusaidia kwa lolote,” alisema mzee Ford huku akitembea taratibu akiwa amekumbatiana na mwanaye mpaka kwenye bustani ya maua, wakatafuta sehemu tulivu na kukaa, akawa anaendelea kumsisitiza amueleze kinachomsumbua.

    “Baba roho inaniuma sana kwa sababu nahisi kifo cha Harrison hakikuwa mpango wa Mungu bali kuna watu walifanya njama za kumuua.”

    “Kwa nini unaamsha vidonda ambavyo vilishapona mwanangu, hiyo ni kazi ya Mungu na tukiendelea kuzungumzia jambo moja kila siku tutakuwa tunakufuru.”

    “Hapana baba, lazima nifuatilie kwa njia zozote mpaka nifahamu ukweli juu ya watu waliohusika kumuua kipenzi cha roho yangu Harrison.”

    “Sasa unafikiri tutafanya nini mwanangu?”

    “Mi nataka kwenda kutoa ripoti polisi ili uchunguzi wa kina ufanyike upya.”

    “Hiyo itakuwa kazi ngumu mwanangu kwa sababu tayari siku nyingi zimepita tangu ajali ilipotokea. Ingekuwa umehisi hayo kipindi kilekile wakati tukio linatokea, ingekuwa rahisi sana.”

    “Hapana baba, hata kama hutanisaidia mi nitafanya uchunguzi mwenyewe mpaka nibaini ukweli uliyojificha nyuma ya pazia,” alisema Linda huku akiendelea kububujikwa na machozi. Baba yake alikataa kumuunga mkono kwenye hoja hiyo kwa sababu alijua hata kama akiujua ukweli kuwa kuna watu walimuua Harrison, haitakuwa na msaada wowote kwake kwani Harrison hawezi kufufuka kutoka katika wafu.

    Linda alirudi chumbani kwake na kujifungia, akawa anawaza mbinu anazoweza kuzitumia ili kuubaini ukweli. Akili yake ilimtuma kwenda mpaka makao makuu ya polisi, Miami na kuomba kuona ripoti ya uchunguzi uliofanywa eneo la ajali na kitengo cha Crime Scene Investigation (CSI).

    Siku nzima alishinda akiwa hana raha, baba na mama yake wakawa wanajitahidi kumsahaulisha na kumsihi kutoendelea na alichokuwa amekipanga lakini hakutaka kuelewa chochote. Asubuhi ya siku iliyofuatia, Linda aliwahi kuamka na kujiandaa, tayari kwa safari ya kuelekea makao makuu ya polisi.

    Alichagua gari dogo la kifahari aina ya Porsche na kutoka kwenye geti la nyumba yao, akawa anaendesha taratibu huku mawazo yake yote yakimtuma kuhakikisha anafanya kila linalowezekana kuufahamu ukweli juu ya kifo cha Harrison.

    Alipofika kwenye jengo kubwa la Makao Makuu ya Polisi, Miami, Linda alienda kueleza shida yake eneo la mapokezi ambapo alielekezwa kupanda mpaka ghorofa ya saba kwenye kitengo cha Crime Scene Investigation.

    ***

    Baada ya masokwe kufanikiwa kumkomboa malkia wao na kurudi naye porini, Harrison alishindwa kuzificha hisia zake, akawa anamwaga machozi kwa huzuni, hali iliyomfanya mzee Hondo amuonee huruma. Alimpa moyo kwamba bado anayo nafasi ya kutimiza ndoto zake kwani mpaka hapo alipofikia tayari kulikuwa na matumaini makubwa ya kutimiza alichokuwa anakitaka.

    Kwa shingo upande akaianza safari ya kurudi kwenye msitu wa Tongass akiwa na furushi lake la dawa pamoja na chakula cha akiba. Alitembea kwa unyonge akiwa hana raha kabisa. Baada ya kutembea kwa saa nyingi, akipanda milima na kushuka mabonde kwenye msitu mnene wa Tongass, hatimaye alifanikiwa kufika kwenye kibanda chake.

    Alijibwaga chini na kupumzika kwa muda wakati akikitazama kibanda chake ambacho kilikuwa kimeharibiwa na vurugu za masokwe wakati wakimsaka malkia wao. Baada ya kupumzika vya kutosha, alianza kukata miti na nyasi kwa ajili ya kurekebisha sehemu zilizokuwa zimeharibiwa.

    Alipomaliza kukarabati kibanda chake, aliwasha moto na kuanza kuchoma nyama aliyopewa na mzee Hondo kwani alikuwa akisikia njaa kali. Aliwasha moto mkubwa na kukaa pembeni yake huku akiimba nyimbo za mapenzi kujifariji.

    Baadaye alienda kujipumzisha ndani ya kibanda chake kwani alikuwa akihisi uchovu kupindukia. Alipojilaza kwenye tu, usingizi mzito ulimpitia, akawa anaota ndoto za kutisha, hali iliyomfanya awe anaweweseka sana. Alikuja kuzinduka alfajiri baada ya kuhisi kuna mtu amelala pembeni yake.

    Awali alihisi huenda ni mnyama mkali au nyoka mkubwa amelala pembeni yake lakini alipofumbua macho kwa tahadhari kubwa, hakuyaamini macho yake baada ya kumuona malkia wa masokwe akiwa amelala, kijasho chembamba kikiwa kinamtoka.

    Kwa jinsi ilivyoonekana, bado homa kali ilikuwa ikimsumbua kwani haikuwa kawaida yake kutokwa na jasho kiasi kile, tena ikiwa ndiyo kwanza kunaanza kupambazuka. Harrison aliamka haraka na kumsogelea, akawa anampima joto la mwili wake sehemu mbalimbali za mwili. Aligundua kuwa bado anaumwa.

    Akaamka na kuanza kuwasha moto. Kazi haikuwa nyepesi kwani kuni zote zilikuwa zimelowanishwa na umande wa usiku kucha. Baada ya kuhangaika sana, hatimaye alifanikiwa kuwasha moto, bila kupoteza muda akaanza kuchemsha dawa alizotoka nazo kwa mzee Hondo kama alivyoelekezwa.

    Baada ya muda, dawa tayari ilikuwa imechemka vya kutosha, akaanza kumnywesha malkia wa masokwe huku nyingine akimkanda mwili mzima. Baada ya kuendelea kumtibu kwa muda, malkia wa masokwe alianza kupiga chafya mfululizo, joto lake la mwili likaanza kushuka.

    Angalau alipata nguvu na sasa akawa anaweza kurukaruka, tofauti na alivyokuwa awali. Harrison akawa anamtazama kwa hisia huku akijiapiza kuwa atakapopona kabisa, lazima atoroke naye kwenda mjini.

    ***





    PENZI la msichana wa ajabu linamchanganya kabisa Harrison, kijana msomi aliyekuwa amebobea kwenye fani ya tabia za wanyama na mimea. Tatizo ni kwamba msichana huyo, analindwa na kundi kubwa la masokwe kama malkia.



    Kwa mara ya kwanza alimuona malkia wa masokwe wakati akifanya utafiti kwenye msitu huo na kufanikiwa kumpiga picha akiwa katikati ya kundi la masokwe, akaandika kitabu kilichomfanya awe maarufu nchi nzima.



    Licha ya kupata fedha nyingi kupitia kitabu hicho, moyo wake unaangukia kwenye penzi la msichana huyo wa ajabu. Uzuri wa asili aliokuwa nao unamchanganya kabisa Harrison lakini kikwazo kikubwa ni kwamba msichana huyo alikuwa na tabia kama za masokwe. Licha ya yote hayo, Harrison anaweka nadhiri kuwa lazima ampate.



    Penzi hilo linamfanya Harrison amkatae mchumba wake, Linda kanisani. Anatoroka kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea. Baada ya hapo, anashirikiana na rafiki yake wa siku nyingi kuandaa ajali feki inayofanya kila mtu aamini kuwa amekufa.



    Baada ya hapo anatorokea porini ambako anaendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe na taratibu ndoto zake zinaanza kuelekea kutimia. Upande wa pili, Linda bado haamini kama Harrison alikufa kifo cha kawaida na sasa anajiapiza kufanya kila linalowezekana kuujua ukweli. Anajaribu kumweleza baba yake hisia zake lakini anakatishwa tamaa. Anaamua kuutafuta ukweli mwenyewe.



    ALIPOFIKA kwenye jengo kubwa la Makao Makuu ya Polisi, Miami, Linda alienda kueleza shida yake eneo la mapokezi ambapo alielekezwa kupanda mpaka ghorofa ya saba kwenye kitengo cha Crime Scene Investigation.



    “Karibu binti, unaitwa nani na nikusaidie nini?” mzee wa makamo aliyekuwa amekaa kwenye kiti cha kuzunguka, nyuma ya meza kubwa iliyokuwa na kibao kilichosomeka ‘CSI Executive Director’, alimuuliza Linda kwa ukarimu huku akimuonesha sehemu ya kukaa.



    “Ahsante, naitwa Linda Ford, nina shida binafsi tafadhali,” alisema huku akikaa kwenye kiti alichoelekezwa. Bila kupoteza muda, Linda alianza kueleza kilichompeleka pale. Alieleza jinsi mazingira ya kifo cha Harrison yalivyokuwa na yote yaliyofuatia baada ya hapo, mwisho akamalizia kwa kueleza wasiwasi wake juu ya kile alichokihisi kama hujuma.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tukio lilitokea tarehe ngapi?” alihoji yule mzee wa makamo ambaye baadaye Linda aligundua kuwa anaitwa Daniels Wilshere. Linda alitoa kitabu chake cha kumbukumbu na kuanza kukipekua kutafuta tarehe ya siku Harrison aliyoaga dunia. Akamtajia ambapo bila kupoteza muda alinyanyua mkonga wa simu na kutoa maelekezo upande wa pili.



    Dakika chache baadaye, msichana wa umri wa kati aliingia akiwa na faili mkononi, akamsabahi Linda na kuliweka faili mezani. Daniels alilifungua na kuanza kukagua ukurasa mmoja mpaka mwingine kisha akateremsha miwani yake na kumtazama Linda.



    “Nasikitika kukwambia kuwa jalada la tukio hilo lilishafungwa kwani inaonesha ni ajali ya kawaida hivyo sina cha kukusaidia. Ungewahi kipindi kile kazi ingekuwa rahisi lakini umechelewa sana.”



    “Kwani kinachoshindikana na nini mzee wangu? Mi naomba niiangalie tu hiyo ripoti ya ajali, kuanzia mchoro wa ajali yenyewe, vitu vilivyookotwa eneo la tukio na taarifa nyingine muhimu.”



    “Binti, hii kazi haiendeshwi kienyeji kama unavyofikiria, kuna taratibu za kisheria na kimaadili ambazo lazima zifuatwe. Nasikitika kukwambia kuwa sitaweza kukusaidia,” alisema Daniels na kunyanyua mkonga wa simu ya mezani, akazungumza na upande wa pili ambapo sekunde chache baadaye yule msichana aliyelileta faili lile aliingia na kukabidhiwa, akalirudisha alikolitoa.



    Kwa unyonge Linda alisimama na kuaga, akatoka nje ya ofisi huku kichwa chake akiwa amekiinamisha chini. Alitoka mpaka nje alipokuwa ameegesha gari lake la kifahari aina ya Porsche na kuingia ndani yake, akaliondoa taratibu huku kichwani akiwa na mawazo lukuki.



    Aliongoza moja kwa moja mpaka nyumbani kwao, akaegesha gari sehemu yake na kwenda mpaka chumbani kwake, akajifungia na kuanza kulia kwa uchungu. Aliona kama anaonewa kwa kukataliwa alichokuwa anakitaka.



    “Nimepata wazo jipya, alisema Linda huku akiinuka haraka kitandani, akajifuta machozi na kutoka mpaka nje, akaenda kwenye bustani za maua alikomkuta baba yake anajisomea gazeti la The Daily Mail, akakaa pembeni yake na kumuomba kuzungumza naye jambo.



    “Nataka kwenda kusoma.”

    “Mh! Kwa nini usifanye kazi kwanza japo mwaka mmoja ndiyo uende kujiendeleza? Umehitimu shahada yako ya kwanza juzijuzi tu.”

    “Hapana baba, nataka kwenda kusoma, tena haraka iwezekanavyo.”

    “Sawa mwanangu, nilishaahidi kuwa pamoja na wewe kwa kila kitu. Unataka kwenda kusomea nini?”



    “Nataka kwenda kusomea kozi ya upelelezi ya Crime Scene Investigation (CSI).”

    “Lakini si lazima kwanza upitie jeshini ndiyo ukasomee kozi hiyo? Unataka kuwa mpelelezi?”

    “Siyo lazima kupitia jeshini baba, siku hizi sheria zimebadilishwa, mbona kuna wenzangu niliokuwa nasoma nao sekondari wameenda kusomea bila kupitia jeshini?”



    “Kwani lengo lako hasa la kutaka kusomea Crime Scene Investigation ni nini?”

    “Nimeamua tu baba, naomba uniunge mkono tafadhali,” alisema Linda huku akijilaza kwenye kifua cha baba yake, mzee Ford akashusha pumzi ndefu na kumtazama mwanaye. Alishajua kilichokuwa kinamsumbua ndani ya moyo wake, penzi la Harrison lilikuwa limeacha kidonda ambacho kisingeweza kupona kirahisi, ikabidi akubaliane naye.

    ***

    Baada ya kuhakikisha malkia wa masokwe anaendelea vizuri, Harrison alimuoneshea ishara akimtaka arudi kwa masokwe kabla hawajafika na kuanza kuleta vurugu eneo lile. Malkia wa masokwe hakuwa mwepesi kuondoka, muda wote akawa anataka kukaa jirani na Harrison huku akijilazimisha kukimbia huku na kule na kurukia matawi ya miti.



    Tofauti na siku zote, walikaa naye kwa muda mrefu bila kundi la masokwe kumfuata malkia wao, jua lilipokuwa kali, kelele za matawi ya miti kuvunjika na milio ya ajabu ikaanza kusikika. Malkia wa masokwe alipowaona masokwe, hakutaka wamdhuru Harrison, akawakimbilia na kuwazuia kabla hawajakifikia kibanda chake, wakageuza naye na kuanza kurudi walikotoka kwa kasi kubwa.



    Harrison aliwasindikiza kwa macho mpaka walipopotea kwenye upeo wa macho yake. Akashusha pumzi ndefu na kukaa chini, mawazo mengi yakawa yanapita kwenye kichwa chake. Akiwa katika hali ile, alikumbuka jambo, harakaharaka akarudi ndani ya kibanda chake na kuanza kupekua kwenye mifuko ya bukta aliyokuwa ameivaa kwa ndani siku alipowasili kwenye msitu huo.



    “Whaooo, safi sana,” alisema Harrison kwa furaha baada ya kufanikiwa kuipata kadi yake ya ATM ya Benki ya Barclays. Alikuwa na akaunti kwenye benki hiyo ambayo ilikuwa na fedha zake nyingi alizozipata baada ya kuchapisha na kuuza kitabu cha Queen of Gorillas kilichomfanya awe maarufu sana nchini Marekani na kwingineko.



    Aliamini utajiri wake mkubwa bado haujaguswa na mtu yeyote licha ya watu wote kuamini kuwa tayari amekufa. Aliitazama kadi ile ya ATM vizuri, akagundua kuwa haikuwa na tatizo lolote.



    “Nitaishi na malkia wa masokwe sehemu yoyote, hakuna kinachoweza kunishinda mbele ya fedha,” alisema Harrison huku akiibusu kadi ile, akaihifadhi sehemu salama na kuendelea kusubiri apate nafasi ya kutoroka na malkia wa masokwe.

    Muda ulizidi kuyoyoma kwa kasi, hatimaye giza likaanza kuingia. Kama kawaida, Harrison akawasha moto na kuanza kuchoma nyama aliyopewa na mzee Hondo ambayo bado alikuwa nayo ya kutosha.

    ***





    HARRISON bado analihangaikia penzi la malkia wa masokwe. Msichana huyo wa ajabu aliyekuwa anaishi na kulindwa na masokwe kama malkia wao, anamchanganya kabisa Harrison kiasi cha kumfanya awe tayari kufanya lolote ili mradi ampate na kuishi naye kama mkewe.



    Kwa mara ya kwanza, Harrison aliyekuwa amebobea kwenye fani ya uchunguzi wa tabia za wanyama na viumbe wengine, alimuona malkia wa masokwe wakati akifanya utafiti kwenye msitu huo na kufanikiwa kumpiga picha akiwa katikati ya kundi la masokwe, akaandika kitabu kilichomfanya awe maarufu nchi nzima.



    Licha ya kupata fedha nyingi kupitia kitabu hicho, moyo wake unaangukia kwenye penzi la msichana huyo wa ajabu. Uzuri wa asili aliokuwa nao unamchanganya kabisa Harrison lakini kikwazo kikubwa ni kwamba msichana huyo alikuwa na tabia kama za masokwe. Licha ya yote hayo, Harrison anaweka nadhiri kuwa lazima ampate.



    Penzi hilo linamfanya Harrison amkatae mchumba wake, Linda kanisani. Anatoroka kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea. Baada ya hapo, anashirikiana na rafiki yake wa siku nyingi kuandaa ajali feki inayofanya kila mtu aamini kuwa amekufa.



    Baada ya hapo anatorokea porini ambako anaendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe na taratibu ndoto zake zinaanza kuelekea kutimia. Upande wa pili, Linda bado haamini kama Harrison alikufa kifo cha kawaida, anaanza kufuatilia kwa kina kutaka kuujua ukweli. Anapoona hakuna anayemjali, anaamua kwenda kusomea upelelezi ili aifanye kazi ile yeye mwenyewe.



    BAADA ya kukaa pembeni ya moto kwa muda mrefu, Harrison alianza kusikia usingizi, akakusanya vitu vyake vyote na kujikongoja mpaka ndani ya kibanda chake, akajitupa kwenye kitanda cha miti na usingizi ukampitia. Akawa anakoroma kutokana na uchovu wa siku nzima.

    Alikuja kuzinduka alfajiri baada ya kuanza kusikia milio ya ndege waliokuwa wanarukaruka kwenye matawi ya miti kushangilia mwanzo wa siku mpya. Aliamka na kujinyoosha, akatoka nje na kuanza kufanya mazoezi mepesimepesi. Akiwa anaendelea kukimbiakimbia, alisikia vishindo vikitokea kichakani.

    Bila hata kuuliza alijua ni malkia wa masokwe, akajikuta akitabasamu. Malkia wa masokwe ambaye sasa alikuwa ameshapona vizuri, alipomuona Harrison, naye aliachia tabasamu pana, akawa anakimbia na kurukia kwenye matawi ya miti kwa furaha.

    “Leo silazi damu, lazima niondoke naye asubuhi hiihii, mengine nitajua mbele kwa mbele,” alisema Harrison na kurudi ndani ya kibanda chake. Akakusanya kila kitu chake na kuweka vizuri kibanda chake, akapiga magoti na kusali sala fupi akimuomba Mungu wake aifanikishe safari ya kumtorosha malkia wa masokwe kutoka ndani ya Msitu wa Tongass.

    Alipomaliza alisimama na kutoka nje, akamkuta malkia wa masokwe akiwa bado anachezacheza kwenye matawi ya miti. Alimsogelea kwa upole kisha akamshika mkono. Malkia wa masokwe hakuwa mbishi, akaanza kumfuata, Harrison akawa anampitisha katikati ya vichaka, kuelekea upande tofauti na ule ambao kundi la masokwe hupenda kufika.

    Alijikagua mifukoni mwake na kuhakikisha kadi yake ya benki ipo mahali pake, safari ikaendelea huku njia nzima malkia wa masokwe akiendelea na michezo ya hapa na pale, akiwa ameshikwa na Harrison.

    Baada ya kutembea kwa umbali mrefu, Harrison alitafuta mti wenye kivuli kizuri, akakaa chini na malkia wa masokwe na kupumzika. Alikuwa anatamani sana kumweleza nini alichokuwa amekipanga lakini kwa kuwa hakuwa akielewa lugha yoyote ya kibinadamu, ilibidi aendelee kunyamaza.

    Baada ya kupumzika, safari ikaendelea, wakawa wanakatiza kwenye vichaka vilivyoshonana, wakapanda milima na kushuka mabonde mpaka walipofika eneo lililokuwa na hali ya hewa tofauti na kule walikotoka.

    Waliingia kwenye ukanda wa baridi ambapo anga lote lilikuwa limetawaliwa na ukungu huku vilele vya milima na miti mirefu vikiwa vimefunikwa na theluji. Bado hakutaka kumuachia malkia wa masokwe, wakaendelea kutembea kwa umbali mrefu mpaka giza likaanza kuingia.

    Kwa kuhofia kuwa huenda kundi la masokwe likawa linawafuata kwa nyuma kwa lengo la kumkomboa malkia wao, Harrison hakutaka kupumzika, safari ikaendelea usiku kwenye eneo lenye baridi kali. Baada ya kutembea kwa umbali mrefu, malkia wa masokwe alianza kutetemeka kutokana na baridi kali aliyokuwa anaihisi.

    Ilibidi Harrison avue shati lake na kumvalisha, yeye akabaki kifua wazi. Safari ikaendelea. Ilipofika usiku wa manane, hali ya hewa ilizidi kuwa mbaya zaidi, theluji ikawa inadondoka kwa wingi kutoka angani, hali iliyofanya Harisson atafute sehemu ya kujihifadhi na malkia wa masokwe.

    Kutokana na uchovu waliokuwa nao baada ya kutembea umbali mrefu, walipopata sehemu kavu ya kupumzika, malkia wa masokwe alikuwa wa kwanza kulala. Kwa tahadhari, Harrison alimfunga kamba malkia wa masokwe mkononi kisha akajifunga na yeye mkononi. Alifanya vile ili hata kama malkia wa masokwe ataamka kabla yake, asimkimbie.

    Wakalala mpaka alfajiri, Harrison akawa wa kwanza kuamka ambapo alianza kumtingisha malkia wa masokwe ambaye bado alikuwa ameuchapa usingizi. Baada ya kuamka, safari iliendelea huku Harrison akiwa hajui hata upande anaoelekea.

    Alichoamini ni kwamba lazima msitu ule mkubwa ulikuwa na mwisho, hivyo kitu pekee alichokuwa anataka ni kutoka na malkia wa masokwe nje ya msitu, bila kujali watatokea upande gani. Walitembea kwa umbali mrefu, wakavuka eneo lile lenye theluji na kuingia kwenye eneo lililokuwa na miti mifupimifupi iliyoachana.

    “Lazima huku kutakuwa ndiyo mwisho wa msitu, mbona hakuna tena miti mirefu!” alijisemea Harrison huku akizidi kukaza mwendo. Kwa muda huo, malkia wa masokwe hakuwa akiendelea na michezo yake tena kutokana na uchovu aliokuwa anauhisi. Mara kwa mara alikuwa akitaka kupumzika lakini Harrison hakumpa nafasi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kutembea mchana kutwa, njaa na kiu vikiwa vimewabana kisawasawa, Harrison aliamua wapumzike. Kwa bahati nzuri, kulikuwa na chemchemi ya maji jirani na mahali walipopumzika, wakanywa maji na mengine kujimwagia kwenye miili yao ili kupunguza uchovu.

    Wakapumzika kwa dakika kadhaa kisha safari ikaendelea. Giza lilipoanza kuingia, malkia wa masokwe alianza kusumbua akitaka wapumzike palepale, jambo ambalo Harrison hakukubaliana nalo. Ikabidi ambebe mgongoni na safari ikaendelea. Uchovu wa kutembea umbali mrefu ukichanganya na uzito wa kumbeba malkia wa masokwe mgongoni ulimchosha Harrison lakini akapiga moyo konde.

    Baada ya kutembea kwa umbali mrefu, Harrison alitafuta sehemu ya kupumzika, akamshusha malkia wa masokwe ambaye tayari alishapitiwa na usingizi, akamlaza chini vizuri kisha akawa anajinyoosha mwili ili kupunguza uchovu.

    Akiwa anajinyoosha, aliona kitu kilichomfanya afikiche macho yake mara mbili akiwa haamini kama ni kweli. Kwa mbali alianza kuona mwanga wa taa za umeme, kuashiria kuwa tayari walikuwa wameukaribia mji, ingawa hakujua ni mji gani.

    “Ooh! Ahsante Mungu wangu,” alisema Harrison huku akiinua mikono juu kama ishara ya shukrani. Alitamani kuendelea na safari usiku huohuo lakini miguu ilikuwa ikimuuma sana, akaendelea kuangalia upande ule uliokuwa na mji kwa muda mrefu mpaka baadaye alipozidiwa na uchovu.

    Akarudi pale alipomuacha malkia wa masokwe, akalala pembeni yake huku akiwa na matumaini makubwa ya kuufikia mji ule siku inayofuata. Hata usingizi wake ulikuwa wa mang’amung’amu, akawa anashtuka mara kwa mara kabla hata hakujapambazuka. Alfajiri na mapema, aliwahi kuamka na kumuamsha malkia wa masokwe, wakaendelea na safari kuelekea upande ule uliokuwa na mji.

    Saa nane mchana, wakawa wametokezea mahali kwenye mji mdogo.

    “Hapa ni wapi?” Harrison alimuuliza kijana mdogo aliyekuwa anachunga kondoo pembeni kidogo ya mji.

    “Petersburg, Canada,” alijibu yule kijana huku akimkodolea macho malkia wa masokwe.

    ***





    MVUMILIVU hula mbivu, walinena wahenga. Harrison bado anaendelea kulihangaikia penzi la msichana wa ajabu aliyekuwa anaishi na kulindwa na masokwe kama malkia wao. Harrison anachanganyikiwa kabisa kiasi cha kumfanya awe tayari kwa lolote ili mradi ampate na kuishi naye kama mkewe.



    Kwa mara ya kwanza, Harrison aliyekuwa amebobea kwenye fani ya uchunguzi wa tabia za wanyama na viumbe wengine, alimuona malkia wa masokwe wakati akifanya utafiti kwenye msitu huo na kufanikiwa kumpiga picha akiwa katikati ya kundi la masokwe, akaandika kitabu kilichomfanya awe maarufu nchi nzima.



    Licha ya kupata fedha nyingi kupitia kitabu hicho, moyo wake unaangukia kwenye penzi la msichana huyo wa ajabu. Uzuri wa asili aliokuwa nao unamchanganya kabisa Harrison lakini kikwazo kikubwa ni kwamba msichana huyo alikuwa na tabia kama za masokwe. Licha ya yote hayo, Harrison anaweka nadhiri kuwa lazima ampate.



    Penzi hilo linamfanya Harrison amkatae mchumba wake, Linda kanisani. Anatoroka kanisani kwa kutumia pikipiki kubwa na kuwaacha watu wakiwa hawaamini kilichotokea. Baada ya hapo, anashirikiana na rafiki yake wa siku nyingi kuandaa ajali feki inayofanya kila mtu aamini kuwa amekufa. Baada ya hapo anatorokea porini ambako anaendelea na kazi yake ya kumtafuta malkia wa masokwe.



    Baada ya kuhangaika kwa kipindi kirefu, hatimaye anafanikiwa kutoroka na malkia wa masokwe na kutokezea upande wa pili wa msitu huo, kwenye mji mdogo wa Petersburg nchini Canada. Upande wa pili, Linda bado haamini kama Harrison alikufa kifo cha kawaida, anaanza kufuatilia kwa kina kutaka kuujua ukweli.



    "HAPA ni wapi?" Harrison alimuuliza kijana mdogo aliyekuwa anachunga kondoo pembeni kidogo ya mji.

    "Petersburg, Canada," alijibu yule kijana huku akimkodolea macho malkia wa masokwe.

    "Hapa kuna benki jirani?"

    "Hapana, hakuna benki hapa mpaka Abbotsford."

    "Kuna umbali gani kutoka hapa?"

    "Ni mbali lakini kuna treni za umeme. Kituo kipo pale mbele, nyoosha na hii barabara, mpaka mwisho. Mbona huyo hajavaa nguo za heshima?" alisema yule kijana huku akiendelea kumkodolea macho malkia wa masokwe.

    Harrison hakujali, akamshika mkono malkia wa masokwe na kuendelea na safari yake, sasa wakiwa tayari wameshaingia ndani ya mji mdogo wa wafugaji wa Petersburg, upande wa Canada.

    Malkia wa masokwe alikuwa akishangaa kila kitu, hakuwahi kuona nyumba, magari wala pikipiki, akawa na kazi moja tu, kushangaa. Japokuwa watu walikuwa wakiwakodolea macho hasa kutokana na mwonekano wa malkia wa masokwe, Harrison hakujali kitu chochote, akatembea kwa kasi akiwa amemshika malkia wa masokwe mkono mpaka walipofika kwenye kituo kidogo cha treni ya umeme cha Petersburg.

    Kwa bahati nzuri, kituo kile kilikuwa kinapokea kadi za malipo za Mastercard kama ile aliyokuwa nayo Harrison. Akaenda mpaka sehemu ya kukatia tiketi, akamuelekeza mkata tiketi kuwa awape mbili za kuelekea Abbotsford. Shida yake kubwa ilikuwa ni kufika kwenye benki zilizokuwa kwenye mji huo ili atoe fedha kwa ajili ya kumnunulia malkia wa masokwe nguo na kutafuta sehemu ya kujihifadhi.

    Yule mhudumu wa stesheni ile, aliichukua kadi ya Harrison na kuipitisha (swap) kwenye mashine maalum, akapewa tiketi mbili kisha akarudishiwa kadi yake. Harrison akiwa bado amemshikilia malkia wa masokwe, alisogea pembeni na kukaa sehemu maalum iliyotengwa kwa ajili ya abiria kusubiria usafiri. Kila mtu aliyekuwa anapita alikuwa anamshangaa malkia wa masokwe.

    Baada ya kusubiri kwa dakika kadhaa, treni liliwasili kituoni pale, milango ikafunguka na abiria wakaanza kuingia. Harrison alikuwa makini mno na malkia wa masokwe, alihakikisha anamdhibiti ipasavyo. Dakika chache baadaye, safari ya kuelekea kwenye Mji wa Abbotsford ikaanza.

    Ndani ya treni, malkia wa masokwe aliendelea kuwa kituko, kila kitu kilikuwa kigeni kwake. Kwa kuwa ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kusafiri kwa treni ya umeme, njia nzima alikuwa akitapika na kuhangaika, akawa anataka kuruka kupitia dirishani. Harrison hakukata tamaa wala kuchoka, alikuwa akimsaidia malkia wa masokwe kwa kila hatua.

    Baada ya kusafiri kwa saa kadhaa, hatimaye sauti ya mhudumu wa treni ilisikika kutoka kwenye vipaza sauti ndani ya treni ikiwataarifu abiria kuwa tayari walishawasili kwenye Mji wa Abbotsford. Kwa kuwa malkia wa masokwe alikuwa amejichafua sana baada ya kutapika njia nzima, Harrison alikuwa wa kwanza kuteremka. Akamshika malkia wa masokwe mpaka kwenye vyoo vilivyokuwa pembeni kidogo ya stesheni.

    Akamuingiza ndani na kumkalisha kwenye bomba, akafungulia maji na kuanza kumsafisha mwili mzima. Baada ya kumaliza, alivua shati lake na kumpa malkia wa masokwe ajisitiri, wakatoka na kujichanganya na abiria wengine kuelekea katikati ya mji.

    "Ndugu samahani, eti hapa kuna benki yoyote jirani?"

    "Benki gani?"

    "Barclays."

    "Nyoosha na hii barabara mpaka pale kwenye mataa, kata upande wa kushoto utaona ghorofa refu likiwa na maandishi makubwa yanayosomeka Barclays."

    "Ahsante sana," Harrison alimshukuru kijana aliyewaelekeza, akafuata maelekezo akiwa na malkia wa masokwe. Mara kwa mara malkia wa masokwe alikuwa akitaka kumponyoka na kukimbilia mbali na barabara, hasa alipoona magari makubwa yanapita kwa kasi pembeni yao.

    Baada ya kutembea umbali wa mita kadhaa, hatimaye Harrison alifika kwenye benki ya Barclays, tawi la Abbotsford. Alipofika mlangoni, askari waliokuwa wanalinda nje ya benki hiyo walimsimamisha kwa muda na kuanza kumhoji. Kwa mwonekano wa haraka, ungeweza kudhani alikuwa ni mwizi au kibaka kwani alikuwa kifua wazi baada ya kumpa malkia wa masokwe shati lake.

    Alipoonesha kadi yake ya benki, aliruhusiwa kuingia mpaka sehemu maalum kulipokuwa na mashine za ATM (Automatic Teller Machine). Huku kijasho chembamba kikimtoka, Harrison aliisogelea mashine na kuchomeka kadi yake sehemu maalum. Hakupata shida kwani tayari alishakuwa na uzoefu wa namna ya kutumia mashine hizo.

    Kitu cha kwanza alichofanya ilikuwa ni kuangalia salio, akabonyeza kitufe cha kuangalia salio na kusubiri kwa sekunde kadhaa.

    "Whaoooo! Ahsante Mungu," alisema Harrison kwa sauti ya juu na kwenda kumkumbatia malkia wa masokwe baada ya kukuta mamilioni yake aliyoyaacha kwenye akaunti yake bado yapo. Hiyo ndiyo akaunti ambayo aliitumia kuhifadhi fedha alizozipata baada ya kuuza kitabu chake alichokiandika cha Queen of Gorillas kilichompa utajiri wa haraka na umaarufu mkubwa.

    Bila kupoteza muda, aliisogelea tena mashine ya ATM na kubonyeza namba fulani ili itoe kiwango cha fedha ambacho aliamini kitatosha kununulia nguo mpya, za kwake pamoja na malkia wa masokwe, kununulia chakula, kupangisha chumba hotelini na mahitaji mengine muhimu.

    Baada ya muda mfupi, tayari alikuwa na burungutu la fedha mkononi. Kwa kuwa dola za Kimarekani zilikuwa zikitumika sehemu nyingi duniani, hakupata shida kufanya manunuzi. Kitu cha kwanza ilikuwa ni kununua nguo nzuri, akabadilisha akiwa na malkia wa masokwe na kuzivaa ndani ya duka hilo.

    Malkia wa masokwe akawa anachekacheka kwani katika maisha yake hakuwahi kuvaa nguo mpya hata siku moja. Akawa anajitazama kwenye vioo vikubwa ndani ya duka lile. Baada ya kumaliza kununua nguo, Harrison alitoka na malkia wa masokwe hadi kwenye hoteli kubwa iliyokuwa jirani na pale ya Glaciers Peak Motel.

    Kwa kuwa alikuwa na fedha za kutosha, kila kitu kilienda vizuri. Akapangisha chumba na kulipia kwa muda wa wiki nzima. Harrison na malkia wa masokwe wakaelekea mpaka ndani ya chumba chao, ndani ya hoteli ya kifahari ya Glaciers Peak Motel.

    ***





    JITIHADA za dhati alizozionesha Harrison katika kupigania penzi la malkia wa masokwe, zimeanza kuzaa matunda baada ya kufanikiwa kutoroka na msichana huyo kutoka kwenye msitu mkubwa wa Tongass, uliokuwa kwenye mpaka wa Marekani na Canada.

    Anatembea naye kwa siku kadhaa porini mpaka wanapokuja kutokezea upande wa pili wa msitu huo, kwenye mji mdogo wa wafugaji wa



    Petersburg nchini Canada. Wakiwa kwenye mji huo, Harrison anajaribu kuulizia mahali penye benki, kijana mmoja mdogo anamuelekeza kuwa inabidi asafiri kwa treni mpaka mji wa pili uitwao Abbotsford.



    Harrison akiwa amemshika mkono malkia wa masokwe aliyekuwa na mwonekano uliomshangaza kila mtu aliyemuona, anafanikiwa kwenda mpaka stesheni ya treni na kwa bahati nzuri, ananunua tiketi mbili kwa kutumia kadi yake ya benki, muda mfupi baadaye safari ya kuelekea Abbotsford inaanza.



    Baada ya kusafiri kwa saa kadhaa, wanawasili kwenye mji huo uliopo nchini Canada ambapo Harrison anakwenda moja kwa moja benki, kwa bahati nzuri, baada ya kuingiza kadi yake kwenye mashine ya ATM, anagundua kuwa bado fedha zake zote zilikuwa salama kwenye akaunti yake.



    Akatoa kiasi ambacho kilitosha kununulia mavazi mapya, kupanga chumba kwenye hoteli, kula na nyingine ya akiba kwa ajili ya matumizi madogomadogo. Harrison na malkia wa masokwe wakayaanza maisha mapya kwenye Hoteli ya Glaciers Peak, huku msichana huyo akionekana kushangaa kila kitu.



    Upande wa pili, Linda bado haamini kama Harrison alikufa kifo cha kawaida, anaanza kufuatilia kwa kina kutaka kuujua ukweli. Anawaomba wazazi wake apelekwe upya shuleni kusomea masomo ya upelelezi na ujasusi.



    BAADA ya kutoa fedha benki na kununua mavazi mapya, Harrison alienda kupangisha chumba na kulipia kwa muda wa wiki nzima. Akaongozana na malkia wa masokwe mpaka ndani ya chumba chao, ndani ya hoteli ya kifahari ya Glaciers Peak Motel.

    "Nakupenda sana mpenzi wangu, sitaki kukupoteza, nitafanya chochote ilimradi niishi na wewe," alisema Harrison lakini malkia wa masokwe hakuwa anaelewa chochote. Alikuwa ametulia kimya kwenye kiti, akiendelea kushangaa kila kitu alichokiona ndani ya chumba kile.

    Kutokana na jinsi mwili wake ulivyokuwa mchafu, Harrison aliamua kuanza kwa kumsafisha, akamshika mkono na kumpeleka bafuni, akamvua nguo na kumkalisha chini, akafungulia bomba la maji, akaanza kumsugua sehemu mbalimbali za mwili wake huku akimpaka sabuni iliyokuwa inanukia vizuri.

    Kazi haikuwa nyepesi lakini alijitahidi kutumia nguvu zake zote. Alipomaliza kumsafisha mwili mzima, alianza kumsugua meno ambayo yalikuwa yamebadilika rangi kutokana na kula mizizi na matunda ya porini kwa kipindi chote cha maisha yake. Pia kazi haikuwa nyepesi kwani malkia wa masokwe alikuwa akiutafuna mswaki na fizi zake zilikuwa zikitoa damu.

    Alipomaliza, alimpunguza nywele ambazo zilikuwa zinamfanya aonekane kama mnyama wa porini. Akamsugua na miguu yake iliyokuwa imepasukapasuka kutokana na kutembea bila viatu kwa kipindi kirefu. Alipomaliza alimrudisha chumbani na kumlaza kitandani, akachukua mafuta mazuri yanayonukia, aliyoyanunua maalum kwa ajili ya malkia wa masokwe.

    Akaanza kumpaka mwili mzima, mwanzoni malkia wa masokwe alikuwa akileta upinzani lakini baadaye akatulia, Harrison akaendelea kumpaka mwili mzima. Alipomaliza alimbadilisha nguo na kumvalisha nyingine ambazo nazo zilikuwa mpya. Wakapumzika kitandani.

    ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee Ford aliamua kumtimizia mwanaye alichokuwa anakitaka, akaenda kumuandikisha katika chuo cha upelelezi cha Scotland College of Crime Scene Investigation (SCCSI) kilichokuwa jijini London, Uingereza. Kila kitu kilikamilishwa haraka, Linda akapanda ndege na kuelekea jijini London.

    Siku tatu baadaye, alianza masomo huku akijiapiza kufanya juhudi ili aelewe kwa kina namna ya kufanya uchunguzi kitaalamu. Siku zilizidi kusonga mbele, Linda akawa anaendelea na masomo huku akijitahidi kuyazoea mazingira mapya ya nchini Uingereza.

    Kwa kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, Linda alizidi kuwa mahiri kwenye masomo, hali iliyomfanya aanze kupata marafiki wengi. Hata hivyo, bado akili yake ilikuwa ikimuwaza Harrison, uchungu ukawa unazidi kumshika ndani ya moyo wake, akawa anajiapiza kuhakikisha anaujua ukweli juu ya kifo chake.

    Miezi mitatu baadaye, Linda alirudi nyumbani kwao nchini Marekani baada ya chuo chao kufungwa. Akiwa nyumbani kwao, muda mwingi alikuwa akipenda kukaa peke yake huku akionekana kuwa na mawazo mengi.

    Mara kwa mara wazazi wake hasa baba yake alikuwa akimfariji na kumtaka akubaliane na hali halisi. Hata hivyo, haikusaidia kitu kwani mara nyingi alikuwa anashinda ndani akikataa kuonana na marafiki zake.

    Baada ya likizo kuisha, Linda alirudi chuoni kuendelea na masomo, ikawa kila baada ya miezi mitatu kuisha anarudi nyumbani kwao na kupumzika kwa siku kadhaa kisha kurudi tena chuoni. Alifanya hivyo kwa sababu alikuwa hajazoea kukaa mbali na wazazi wake. Suala la nauli halikuwa tatizo kwao kwani baba yake alikuwa na uwezo mkubwa kiuchumi.

    ***

    Siku ya kwanza iliisha, Harrison na malkia wa masokwe wakiwa hotelini, huku msichana huyo akizidi kumzoea Harrison taratibu. Japokuwa hakuwa amevizoea vyakula vya kawaida malkia wa masokwe alilazimika kuanza kula mikate na vyakula vingine alivyofundishwa na Harrison. Mara mojamoja alikuwa akienda kumnunulia matunda kwenye ‘supermarket' iliyokuwa jirani na hoteli ile.

    "Inabidi nimtafutie mwalimu wa kumfundisha lugha, tutaendelea kukaa kama mabubu mpaka lini?" aliwaza Harrison huku akipitia kitabu cha namba za mawasiliano (yellow pages) kilichokuwa ndani ya chumba kile. Akapata jina la mwalimu anayeweza kumsaidia kufanya kazi ile.

    Alimpigia simu na kuomba kukutana naye siku inayofuatia. Kesho yake asubuhi, mwanaume wa makamo aliyekuwa na kichwa chenye mvi nyingi, alifika kwenye Hoteli ya Glaciers Peak Motel na kuomba kuonana na Harrison.

    "Naomba unisaidie kumfundisha mpenzi wangu kusoma, kuandika na kuzungumza kama watu wengine."

    "Kwani ana matatizo gani? Ana mtindio wa ubongo?"

    "Hapana, ameishi sehemu ambayo haina watu, amekaa porini kwa muda mrefu."

    "Utanilipa shilingi ngapi?" alisema yule mzee huku akijaribu kuwasiliana na malkia wa masokwe kwa lugha ya ishara."

    "Nitakupa kiasi chochote utakachohitaji," alisema Harrison huku akimtazama mzee yule alivyokuwa anawasiliana na malkia wa masokwe. Baada ya kufikia makubaliano, Harrison aliongozana na yule mzee mpaka benki iliyokuwa jirani na hoteli ile, akatoa fedha kiasi benki na kumlipa kama malipo ya awali kwa ajili ya kazi ile.

    Kesho yake asubuhi, mzee yule wa makamo ambaye baadaye alijitambulisha kwamba anaitwa mwalimu Gallagher, aliwasili akiwa na vifaa vyake vya kufundishia. Kwa kuwa ilikuwa vigumu kwa malkia wa masokwe kukaa peke yake na mtu ambaye hajamzoea, ilibidi Harrison akae naye, mwalimu akaanza kumfundisha kusoma na kuandika.

    Mwanzo ilikuwa vigumu sana kwani hakuwa anaelewa chochote lakini baada ya kukaa muda mrefu, taratibu alianza kuelewa herufi kadhaa. Akawa anaweza kutamka kama mwalimu Gallagher alivyokuwa anatamka, hali iliyomfanya Harrison afurahi kuliko kawaida.

    Baada ya kumfundisha kwa zaidi ya saa tano mfululizo, mwalimu Gallagher aliaga na kuondoka, akaahidi kurudi kwa ajili ya masomo ya jioni. Huku nyuma Harrison akawa anacheza na malkia wa masokwe huku akiendelea kumfundisha ustaarabu, ikiwa ni pamoja na namna ya kutumia choo anapobanwa na haja.

    Jioni ilipofika, mwalimu Gallagher alirudi tena na Harrison akamchukua malkia wa masokwe na kukaa naye kwa utulivu, tayari kwa awamu ya pili ya masomo. Taratibu malkia wa masokwe akaanza kuingiza neno mojamoja kwenye kichwa chake.

    ***







    BAADA ya kulipigania penzi la malkia wa masokwe kwa kadiri ya uwezo wake wote, hatimaye Harrison anafanikiwa kumnasa msichana huyo na kutoroka naye kutoka kwenye msitu mkubwa wa Tongass, uliokuwa kwenye mpaka wa Marekani na Canada.

    Wanatembea kwa miguu kwa siku kadhaa porini mpaka wanapokuja kutokezea upande wa pili wa msitu huo, kwenye mji mdogo wa wafugaji wa Petersburg nchini Canada. Baada ya hapo, wanasafiri kwa treni ya umeme kuelekea kwenye mji wa pili uitwao Abbotsford.

    Baada ya kusafiri kwa saa kadhaa, wanawasili kwenye mji huo uliopo nchini Canada ambapo



    Harrison anakwenda moja kwa moja benki, kwa bahati nzuri, baada ya kuingiza kadi yake kwenye mashine ya ATM, anagundua kuwa bado fedha zake zote zipo salama kwenye akaunti yake.



    Akatoa kiasi ambacho kilitosha kununulia mavazi mapya, kupanga chumba kwenye hoteli, kula na nyingine ya akiba kwa ajili ya matumizi madogomadogo. Harrison na malkia wa masokwe



    wanayaanza maisha mapya kwenye Hoteli ya Glaciers Peak, huku msichana huyo akionekana kushangaa kila kitu.



    Anamtafuta mwalimu maalum kwa ajili ya kuanza kumfundisha malkia wa masokwe kuzungumza, kusoma na kuandika. Mwalimu Gallagher, anapewa kazi hiyo huku Harrison naye akiendelea kumfundisha ustaarabu msichana huyo.



    Upande wa pili, Linda anaendelea na masomo ya Crime Scene Investigation na anajiapiza kuwa lazima afaulu vizuri kisha aingie mwenyewe kazini kuutafuta ukweli wa kifo cha mpenzi wake,



    Harrison. Bado haamini kama alikufa kifo cha kawaida, anahisi kuna njama zilikuwa nyuma ya tukio hilo.



    JIONI ilipofika, mwalimu Gallagher alirudi tena na Harrison akamchukua malkia wa masokwe na kukaa naye kwa utulivu, tayari kwa awamu ya pili ya masomo. Taratibu malkia wa masokwe akaanza kuingiza neno mojamoja kwenye kichwa chake.



    Kwa muda wa wiki nzima, mwalimu Gallagher na Harrison walikuwa na kazi ya ziada ya kumfundisha lugha malkia wa masokwe. Kwa kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, ndivyo malkia wa masokwe alivyokuwa anazidi kuelewa mambo mbalimbali ya kibinadamu, ikiwemo lugha.



    Mara kwa mara Harrison alikuwa akitoka naye na kumtembeza nje ya hoteli ili kumpunguza ushamba. Siku za mwanzo alikuwa akishangaa kila kitu lakini kwa kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, akaanza kuzoea mazingira. Akapunguza kuwaogopa watu, magari na vitu vingine ambavyo awali vilikuwa vikimtoa ushamba.



    Pia Harrison alikuwa na kazi ya ziada ya kumfundisha ustaarabu kuanzia namna ya kuvaa nguo kila anapoamka asubuhi, jinsi ya kula kwa ustaarabu mezani, jinsi ya kutembea kwa miguu miwili bila kushikashika mikono chini kama wafanyavyo masokwe, kuoga na kulala kwa ustaarabu.



    Siku saba za kwanza zilikuwa za mafanikio makubwa kwa Harrison, akawa na matumaini makubwa kuwa siku chache zijazo malkia wa masokwe atakuwa binadamu aliyekamilika. Kilichokuwa kinamfurahisha zaidi Harrison ni kwamba kwa kadiri malkia wa masokwe alivyokuwa anaishi maisha mazuri, ndivyo alivyozidi kuwa mrembo.



    Ngozi yake ikaanza kuwa nyororo huku yale madoa ya uchafu yaliyokuwa yanaiharibu ngozi yake yakitoweka taratibu, ung’avu wake wa asili ukawa unajionesha dhahiri. Pia nywele zake nazo ziliacha kutoa harufu kama zamani baada ya kuwa anamuosha kwa ‘shampoo’ kila siku. Kucha zake zilizokuwa zimebadilika rangi kwa uchafu nazo zikaanza kupendeza.



    Harrison alipata wazo, akaona kuendelea kuishi hotelini kutamgharimu sana kwani alipanga maisha yake yote kuyahamishia katika mji huo uliochangamka wa Abbotsford, akaona njia pekee ambayo inaweza kumpunguzia matumizi yasiyo ya lazima ni kutafuta nyumba ya kupanga.



    Kwa kuwa hakuwa na mtu mwingine yeyote aliyekuwa anamfahamu kwenye mji ule, aliamua kumtumia mwalimu Gallagher. Baada ya kumwambia nia yake, mzee huyo alimuahidi kumtafutia madalali ambao ndiyo wanaofahamu wapi kuna nyumba za kupanga.



    Kesho yake, kama alivyokuwa amemuahidi, Gallagher alimkutanisha Harrison na dalali wa nyumba, Xavier Simmons. Baada ya mazungumzo na Harrison, Xavier aliomba kupewa muda ili kutafuta nyumba ambayo ingekidhi vigezo alivyovitoa Harrison. Siku mbili baadaye, nyumba ilipatikana katika Mtaa wa Langley, Harrison akapelekwa kwenda kuiona. Ilikuwa ni nyumba nzuri yenye



    kila kitu ndani. Wamiliki wa nyumba hiyo walikuwa wamesafiri kwenda nje ya nchi hivyo hawakutaka nyumba yao ikae bila mtu, wakaamua kutafuta mpangaji ambaye angeitunza mpaka watakaporejea.

    Harrison alifurahi sana, bila hiyana akaenda benki na kutoa kiwango cha fedha kilichokuwa kinatakiwa, akalipa kodi ya mwaka mzima na kuanza kufanya maandalizi ya kuhamia.

    ***



    Linda aliendelea na masomo yake kwa juhudi, hakukosa kuhudhuria vipindi hata siku moja. Hata siku za mwisho wa wiki ambazo wenzake walikuwa wakizitumia kustarehe, yeye alikuwa akishinda maktaba akijisomea. Hakutaka kufanya masihara kwenye masomo hata kidogo, akajiwekea nadhiri kuwa ni lazima afaulu kwa alama za juu.



    Siku zilizidi kusonga mbele, akawa anazidi kupata ujuzi wa namna ya kuendesha kesi zilizokuwa zinahitaji upelelezi wa kutosha. Kila alipokuwa akirudi likizo nyumbani kwao, alikuwa akizidi kubadilika. Hakuwa Linda yule ambaye watu wengi walikuwa wanamfahamu, msichana ‘mayaimayai’ aliyelelewa kitajiri na kupata kila alichokitaka kutoka kwa wazazi wake.



    Sasa alianza kubadilika huku muda mwingi akipenda kujifungia ndani peke yake, akipitia vitabu mbalimbali vilivyokuwa vinahusiana na masomo yake. Hata alipokuwa akitoka na kutembea kupunga upepo, muda mwingi alikuwa mkimya akionesha kuzama kwenye lindi la mawazo. Mara kwa mara alikuwa akilitembelea eneo ambalo Harrison alipata ajali na kufa.



    Wazo pekee lililokuwa ndani ya akili yake, ni kusoma kwa bidii mpaka ahitimu masomo ya Crime Scene Investigation kisha baada ya hapo, alivalie njuga suala la Harrison mpaka aupate ukweli wa nini kilichosababisha kifo chake na utata uliokuwa nyuma ya tukio lile.



    Aliamua kufanya hivyo mwenyewe baada ya kuona msaada alioutegemea kutoka jeshi la polisi hususan kitengo cha Crime Scene Investigation umeshindwa kukidhi kile alichokuwa anakitaka. Akaamua kuingia mwenyewe vitani ili kufahamu kilichomsibu Harrison, mwanaume wa maisha yake ambaye alitokea kumpenda kwa moyo wake wote.

    ***



    Baada ya kukamilisha taratibu zote zilizokuwa zinatakiwa, Harrison alihama kwenye Hoteli ya Glaciers Peak aliyokuwa amefikia na kuhamia makazi mapya, kwenye Mtaa wa Langley.

    Mwalimu Gallagher aliendelea kumfundisha malkia wa masokwe hata baada ya kuhamia makazi mapya, ikawa kila siku anafika mara mbili, asubuhi na jioni kwa ajili ya kuendelea kumfundisha Harrison ambaye kwa kadiri siku zilivyokuwa zinasonga mbele ndivyo alivyokuwa anazidi kuelewa.



    Taratibu akaanza kutamka maneno machache, ikiwa ni pamoja na kumudu kulitamka vizuri jina la Harrison. Akaanza kujua kujieleza ingawa bado ilikuwa kwa shida. Alipohisi njaa alisema, alipobanwa na haja ndogo au kubwa vilevile alikuwa akimwambia Harrison ambaye alikuwa akimpeleka sehemu husika.



    Baada ya Harrison kuridhika na maendeleo aliyokuwa nayo, alianza kupanga mipango ya ndoa. Hakutaka kuvunja amri ya sita na msichana huyo mrembo kabla hajaingia rasmi kwenye ndoa.

    Japokuwa hisia za mapenzi zilikuwa zikimtesa sana, hasa ukizingatia walikuwa wakilala kitanda kimoja, wakati mwingine wakiwa wamekumbatiana, Harrison alijikaza kwa kadiri ya uwezo wake. Akawa anasubiri siku ya kuhalalisha rasmi uhusiano madhabahuni.

    ***

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    MTAFUTAJI hachoki, akichoka ujue amepata. Msemo huu unajidhihirisha kwa Harrison ambaye kwa kipindi kirefu amelipigania penzi la malkia wa masokwe kwa kadiri ya uwezo wake wote hadi akafanikiwa kumnasa msichana huyo



    na kutoroka naye kutoka kwenye msitu mkubwa wa Tongass, uliokuwa kwenye mpaka wa Marekani na Canada.

    Kijana huyo aliyekuwa amebobea kwenye elimu ya viumbe hai, baada ya kumnasa malkia wa masokwe, anatembea



    naye kwa miguu kwa siku kadhaa porini mpaka wanapokuja kutokezea upande wa pili wa msitu huo, kwenye mji mdogo wa wafugaji wa Petersburg nchini Canada. Baada ya hapo, wanasafiri kwa treni ya umeme kuelekea kwenye mji wa pili uitwao Abbotsford.



    Baada ya kuwasili Abbotsford, Harrison na malkia wa masokwe wanayaanza maisha mapya kwenye Hoteli ya Glaciers Peak, huku msichana huyo akionekana kushangaa kila kitu. Anamtafutia mwalimu maalum kwa ajili ya kuanza kumfundisha kuzungumza, kusoma na kuandika.



    Baada ya kukaa hotelini kwa wiki moja huku akifanya kazi ya ziada ya kumfundisha ustaarabu msichana huyo, aliamua kutafuta nyumba ya kupanga, akafanikiwa kuipata na kulipa kodi ya mwaka mzima. Maisha yakawa yanazidi kusonga mbele huku malkia wa masokwe akibadilika taratibu.



    Upande wa pili, Linda anaendelea na masomo ya Crime Scene Investigation na anajiapiza kuwa lazima afaulu vizuri kisha aingie mwenyewe kazini kuutafuta ukweli wa kifo cha mpenzi wake, Harrison. Haamini kama mpenzi wake huyo



    alikufa kifo cha kawaida, anahisi kuna njama zilikuwa nyuma ya tukio hilo na anajiapiza kufanya kila linalowezekana kuufichua ukweli.



    JAPOKUWA hisia za mapenzi zilikuwa zikimtesa sana, hasa ukizingatia walikuwa wakilala kitanda kimoja, wakati mwingine wakiwa wamekumbatiana, Harrison alijikaza kwa kadiri ya uwezo wake. Akawa anasubiri siku ya kuhalalisha rasmi uhusiano wao madhabahuni.



    Malkia wa masokwe aliendelea kufundishwa na mwalimu Gallagher kila siku, kwa kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, akawa anapanuka ufahamu wake, akaanza kuzungumza sentensi fupifupi huku pia akimudu kutaja majina ya vitu mbalimbali kama alivyokuwa anafundishwa.



    Pia alikuwa akizidi kustaarabika, yale mambo aliyokuwa anayafanya muda mfupi baada ya kutoka msituni, sasa hakuwa akiyafanya tena, akawa anaweza kufanya kazi ndogondogo za nyumbani kama kufua na kufanya usafi. Kila siku Harrison alikuwa ni mtu wa furaha, kila alipokuwa anamtazama malkia wa masokwe, alikuwa akitabasamu hasa akikumbuka jinsi alivyoteseka porini.



    Kwa kuwa mpaka muda huo hakuwa akilifahamu jina halisi la malkia wa masokwe, aliamua kumbatiza jina jipya. Akampa jina la Angel. Akawa anamuita kwa jina hilo mara kwa mara mpaka alipoanza kulizoea. Ikawa mtu yeyote akimuuliza jina lake anamwambia anaitwa Angel.



    Siku zilizidi kusonga mbele, Harrison, kwa kuhofia ndugu zake kumtafuta na kugundua ukweli kuwa hakufa, na yeye aliamua kubadilisha jina kwenye nyaraka zake zote. Akajibatiza jina jipya la Alex Wolfgang kisha akaenda kuonana na daktari Albert Stein aliyekuwa anasifika kwa utaalamu wa kuwafanyia watu upasuaji wa kubadilisha sura (plastic surgery).



    “Kwa nini unataka kubadilisha sura? Isije kuwa wewe ni mhalifu unatafuta njia ya kuukimbia mkono wa sheria.”

    “Hapana, kuna sababu binafsi zinazonifanya nibadilishe sura. Nipo tayari kukuelezea lakini niahidi kwamba hutaitoa hii siri yangu,” alisema Harrison huku akijiweka vizuri kwenye kiti.



    Alipohakikishiwa kutunziwa siri, Harrison alimueleza Daktari Stein kila kitu ingawa hakutaka kumueleza kwa undani zaidi akihofia kuharibu mambo.



    “Msichana mwenyewe ndiyo huyu?” aliuliza Daktari Stein huku akimkazia macho malkia wa masokwe ambaye sasa alikuwa akiitwa Angel.

    “Ndiyo huyu, nipo tayari kufanya lolote ilimradi nimuoe.”

    “Lakini hujakosea, msichana mzuri sana huyu, halafu mnapendezana,” alisema Daktari Stein kwa masihara huku akianza kuandaa vifaa vyake tayari kwa kazi.



    Kazi haikuwa nyepesi, ilichukua zaidi ya saa tatu Harrison akiwa ndani ya chumba maalum, daktari akiendelea na kazi yake. Malkia wa masokwe naye alikuwa amekaa na kutulia pembeni, akiangalia jinsi Harrison alivyokuwa anabadilishwa sura.

    Baada ya upasuaji kumalizika, Harrison alisimama na kwenda kujitazama kwenye kioo kikubwa kilichokuwa ukutani, akatabasamu



    kwani alibadilika sana. Isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote kumtambua kirahisi. Baada ya kazi kumalizika, Harrison na malkia wa masokwe walirudi kwenye makazi yao kwenye Mtaa wa Langley.



    Harrison aliendelea na kazi ya kujibadilisha, sasa akahamia kwenye vyeti na nyaraka zake muhimu. Akapanga kwenda kupiga picha za pasipoti ambazo ndiyo angezitumia kwenye nyaraka zake muhimu ikiwa ni pamoja na hati ya kusafiria. Aliamua pia kubadilisha jina ili kuzidi kupoteza ushahidi.



    Akajibatiza jina jipya la Alex Wolfgang ambalo ndiyo alipanga kulitumia kwenye nyaraka zake zote. Alipomaliza zoezi hilo, alipumzika na mchumba wake huku mipango ya ndoa ikianza kukisumbua kichwa chake. Baada ya kazi ya kubadilisha jina na sura kukamilika, hakukuwa na kipingamizi chochote cha kufunga ndoa.



    Kuonesha jinsi alivyokuwa na mapenzi ya dhati kwake, alipanga kwenda kufunga naye ndoa ya kanisani na kuweka kiapo cha maisha. Kwa utaratibu wa dini ya Kikristo, ndoa zilizokuwa zinafungwa kanisani ilikuwa haziwezi kutenganishwa na chochote zaidi



    ya kifo. Hata ikitokea wanandoa wakahitilafiana na kupeana talaka, hakuna aliyekuwa anaruhusiwa kuoa au kuolewa tena.



    “Sidhani kama itakuja kutokea siku nikaachana na Angel wangu, kifo pekee ndiyo kitakachotutenganisha,” alisema Harrison huku akianza kufikiria kumpeleka mchumba wake huyo kanisani akaanze kujifunza mambo ya kiroho.

    Siku kadhaa baadaye, Harrison aliongozana na Angel wake hadi kwenye kanisa lililokuwa jirani na pale walipokuwa wanaishi.



    Wakaomba kuonana na mchungaji ambapo Harrison ambaye sasa alikuwa akijitambulisha kwa jila la Alex, alimweleza mchungaji historia ya maisha ya mchumba wake kisha akaomba msaada aweze kuandikishwa kwenye orodha ya watu ambao walikuwa mbioni kubatizwa.



    Pia aliomba wote wawili wapewe mafunzo ya ndoa na namna ya kuishi wawili, ikiwa ni maandalizi ya kuingia kwenye ndoa halali. Mchungaji alimkubalia, akawataka wote wawili wawe wanahudhuria vipindi vya dini kanisani hapo kila jioni.



    Harrison na mchumba wake wakarudi hadi kwenye makazi yao huku mara kwa mara akijitahidi kumzoesha kuzungumza kwa kawaida. Taratibu wakawa wanaelewana kwenye mazungumzo yao ingawa bado malkia wa masokwe hakuwa na uwezo wa kuzungumza na kuelewa kama watu wengine.



    “Mimi nataka kukuoa wewe uwe mke wangu, tuishi pamoja na tuzae watoto wazuri,” Harrison alikuwa akimwambia mchumba wake huku akijitahidi kumuonesha kwa ishara ili waelewane vizuri. Hakumjibu chochote zaidi ya kuwa anachekacheka tu, hali iliyomfanya Harrison ashindwe kuelewa kama amemuelewa au la.



    “Nitakuwa namwambia hivi kila siku mpaka anielewe, nahitaji aridhie kutoka ndani ya moyo wake, sitaki kumlazimisha,” alisema Harrison. Ikawa anamtamkia maneno yale mara kwa mara huku akimuonesha upendo wa dhati.



    Siku kadhaa baadaye, walianza kuhudhuria vipindi vya dini kanisani. Wakajiwekea ratiba kuwa asubuhi Angel atakuwa anafundishwa na mwalimu Gallagher kama kawaida na jioni wanaongozana kwenda kanisani kuhudhuria mafunzo ya ubatizo na elimu ya ndoa na uhusiano.

    ***







    HARRISON, baada ya kulipigania kwa muda mrefu penzi la malkia wa masokwe, hatimaye anafanikiwa kumnasa na sasa yupo chini ya himaya yake. Amefanikiwa kumtorosha kutoka kwenye mikono ya masokwe kwa tabu kubwa hadi



    alipotoka naye kwenye msitu mkubwa wa Tongass, uliokuwa kwenye mpaka wa Marekani na Canada.

    Baada ya kufanikiwa kumnasa malkia wa masokwe, anatembea naye kwa miguu kwa siku kadhaa porini kisha



    wanatokezea upande wa pili wa msitu huo, nchini Canada. Baada ya hapo, wanasafiri kwa treni ya umeme kuelekea kwenye mji wa pili uitwao Abbotsford.



    Wakiwa kwenye mji huo, wanayaanza maisha mapya kwenye Hoteli ya Glaciers Peak, huku msichana huyo akionekana kushangaa kila kitu. Baadaye anamtafutia mwalimu maalum kwa ajili ya kuanza kumfundisha



    kuzungumza, kusoma na kuandika kisha wanahama hotelini baada ya kupata nyumba ya kupanga.

    Maisha yanazidi kusonga mbele huku malkia wa masokwe akibadilika taratibu na sasa anafikia hatua ya kuanza



    kuzungumza kama binadamu wa kawaida. Anafundishwa ustaarabu na Harrison na kwa kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, malkia wa masokwe anazidi kuwa mrembo. Baadaye wanaanza kusomea mafundisho ya dini kuhusu ndoa na uhusiano ikiwa ni maandalizi ya kuoana.



    Upande wa pili, Linda anaendelea na masomo ya Crime Scene Investigation na anajiapiza kuwa lazima aufahamu ukweli uliokuwa umejificha nyuma ya kifo cha mpenzi wake, Harrison. Haamini kama mpenzi wake huyo alikufa kifo



    cha kawaida, anahisi kuna njama zilikuwa nyuma ya tukio hilo na hiyo ndiyo sababu inayomfanya aingie kazini mwenyewe kuhakikisha anaujua ukweli.



    Harrison na malkia wa masokwe (Angel) waliendelea kuhudhuria mafunzo ya ubatizo na elimu ya uhusiano na ndoa kila siku. Walishaingiza katika ratiba yao ya kila siku, ikawa asubuhi Angel anafundishwa na mwalimu Gallagher elimu ya kidunia na jioni wanaongozana hadi kanisani kufundishwa elimu ya kiroho.

    Siku zilizidi kuyoyoma, Angel akawa na utashi na uelewa kama binadamu wengine. Akaanza kuwa na hisia za mapenzi mazito kwa Harrison hasa kutokana na jinsi alivyokuwa anamdekeza. Siku zote, Harrison ambaye sasa alikuwa akitambulika kwa jina la Alex Wolfgang, hakutaka mchumba wake apatwe na matatizo yoyote.

    Alikuwa akimtunza kama mboni ya jicho lake, muda wote akiwa pembeni yake. Kutokana na kazi kubwa iliyokuwa inafanywa na mwalimu Gallagher, baada ya miezi kadhaa Angel tayari alikuwa na uwezo wa kuzungumza na kuelewa vitu vingi sana. Usingeweza kuamini kwamba huyo ndiye msichana aliyelelewa na masokwe kwa kipindi kirefu katika maisha yake.

    Alistaarabika na sasa akawa hana tofauti na wasichana wengine, kila siku alikuwa akijifunza mambo mapya na kuzidi kuwa bora. Harrison alimzoesha tabia ya kusoma vitabu vyenye maarifa mbalimbali huku muda mwingine wakitazama mikanda ya video iliyokuwa inafundisha mambo mbalimbali ya maisha. Tayari alishasahau maisha ya porini aliyokuwa anaishi na masokwe.

    “Nataka nikuvalishe pete ya uchumba mpenzi wangu, nataka mwaka huu ukiisha tufunge ndoa na kuwa mume na mke halali, nakupenda sana Angel.”

    “Nakupenda pia mpenzi wangu, natamani siku ya kufunga ndoa ifike haraka,” alisema malkia wa masokwe, Harrison akamvutia kifuani kwake na kumkumbatia kimahaba, akawa anambusu sehemu mbalimbali za mwili wake huku Angel naye akimrudishia. Wakaendelea kucheza kimahaba kwa muda mrefu huku kila mmoja akimuonesha mwenzake mapenzi ya dhati.

    “Nilikuwa naisubiri kwa hamu kubwa siku ambayo Angel wangu atazielewa hisia zangu, namshukuru Mungu hatimaye imewadia,” Harrison alijisemea moyoni huku akizichezea nywele za mchumba wake aliyekuwa amejilaza kifuani kwake.

    ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Linda aliendelea na masomo yake kwa juhudi, akikazania kuelewa kwa vitendo namna ya kufanya upelelezi kwenye maeneo ya matukio ya uhalifu (Crime Scene). Kila mwisho wa muhula, Linda alikuwa akiongoza kwenye wastani wa matokeo ya mitihani na majaribio waliyokuwa wanayafanya.

    Kila mmoja alikuwa akitamani kuwa na urafiki naye lakini haiba yake ya kuwa kimya muda wote, ilifanya iwe vigumu kuzoeana na wanachuo wenzake. Mwaka wa kwanza uliisha, Linda akawa anaongoza kwa wastani wa matokeo ya mitihani. Mwaka wa pili nao ulienda vizuri, msichana huyo akiweka rekodi kwa kuongoza masomo ambayo siku zote yalikuwa yakiongozwa na wanaume.

    Mwaka wa tatu kama ilivyo kawaida ya vyuo vingi vya juu, ulikuwa ni mwaka wa kufanya majaribio kwa vitendo (field work). Kutokana na alama za juu alizokuwa anazipata katika mitihani yake, Linda alipata nafasi ya kwenda kufanya majaribio kwa vitendo kwenye mashirika makubwa ya ujasusi ya CIA la Marekani na Scotland Yard la Uingereza.

    Kote alikopita, Linda alikuwa akiweka historia ya ajabu huku sifa yake ya kuwa mkimya muda wote ikimuongezea alama za juu. Baada ya kumaliza mafunzo kwa vitendo, alirejea nyumbani kwao ambapo jambo la kwanza alilomwambia baba yake ni kwamba akishamalizia muhula wa mwisho, anataka kufungua kampuni yake ya upelelezi.

    Kwa kuwa suala la fedha halikuwa tatizo kwa wazazi wake, mzee Ford alimhakikishia kumsaidia kila kitu ili afanikishe azma yake. Akawasiliana na wasaidizi wake ambapo maandalizi yalianza kufanyika. Akatafutiwa ofisi, vyeti vya usajili wa kudumu pamoja na nyaraka nyingine zote zilizokuwa zinatakiwa.

    ***

    Baada ya Harrison kuridhishwa na maendeleo ya malkia wa masokwe (Angel) katika kuelewa elimu ya kidunia na ile ya kiroho, aliamua kumvalisha pete ya uchumba na kuutangaza rasmi uchumba wao hadharani.

    Mchungaji aliyekuwa anawafundisha elimu ya kiroho, alimuelekeza kila kitu kilichokuwa kinatakiwa ili kuufanya uchumba wao uwe mtakatifu ikiwa ni maandalizi ya kuingia kwenye ndoa ya halali.

    Walipokamilisha taratibu zote, Alex (Harrison) na Angel (malkia wa masokwe) walitangazwa rasmi kanisani Jumapili moja mbele ya waumini wengine kuwa wao ni wachumba ambao walikuwa mbioni kufunga ndoa. Kila mtu aliwatakia kila la heri kwani ama kwa hakika walikuwa wakipendana na kupendezana.

    Walidumu kwenye uchumba wao kwa kipindi kirefu, kila siku ikawa mpya kwao kwani walikuwa wakizidisha kupendana. Ikafika mahali wakawa kama mapacha, usingeweza kumuona mmoja bila mwingine kuwepo. Walikuwa wakifuatana kama kumbikumbi.

    “Kwa nini hupendi kukivua hicho kidani chako shingoni? Kwani ulikipata wapi?” Harrison alimuuliza mchumba wake, jioni moja wakiwa wanapunga upepo kwenye bustani nzuri ya maua iliyokuwa jirani na pale walipokuwa wanaishi.

    “Mh! Sikumbuki nilikipata wapi lakini tangu napata akili nilikuwa nacho, huu ndiyo ulinzi wangu ulionifanya nivuke vikwazo vyote maishani mwangu nikiwa salama.”

    “Ooh! Vizuri sana, nikikununulia kingine kizuri utakipenda? Hicho kimeshachakaa sana na tayari kimeanza kukubana shingoni.”

    “Hata ukininunulia kingine nitakuwa navivaa vyote viwili shingoni, nakipenda sana,” alijibu Angel huku akitabasamu, wakakumbatiana na Harrison na kuanza kubusiana sehemu mbalimbali za miili yao.

    Siku zilizidi kusonga mbele, hatimaye siku ya harusi yao ikawa imekaribia. Wakaanza maandalizi ya hapa na pale ikiwa ni pamoja na kununua nguo watakazovaa siku hiyo. Kwa kuhofia watu wasije kuingilia ndoa yao na kukwamisha mpango wao, waliamua kutofanya sherehe zaidi ya kuhalalishwa mbele za Mungu kisha wangesafiri pamoja kwenda sehemu ya mbali kabisa kula fungate pamoja.

    ***





    MIPANGO ya kufunga ndoa kati ya Harrison na mchumba wake, Angel (malkia wa masokwe) imepamba moto. Baada ya kulipigania kwa muda mrefu penzi la msichana huyo mrembo, hatimaye tayari yupo mikononi mwake na sasa anachosubiri ni siku ya kuhalalishwa rasmi madhabahuni.

    Kazi haikuwa nyepesi mpaka kufikia hapo kwani ilimlazimu Harrison kukaa siku nyingi kwenye msitu mkubwa wa Tongass akitafuta njia ya kumtorosha msichana huyo aliyekuwa analindwa na kundi kubwa la masokwe waliokuwa wanamheshimu kama malkia wao.

    Baada ya kuhangaika sana, hatimaye anafanikiwa kumtorosha kutoka kwenye mikono ya masokwe na kuelekea upande wa pili wa msitu huo. Wanatembea siku nyingi porini na kutokezea kwenye Mji wa Petersburg, Canada. Baada ya hapo, wanasafiri kwa treni ya umeme kuelekea kwenye mji wa pili uitwao Abbotsford.

    Wakiwa kwenye mji huo, wanayaanza maisha mapya kwenye Hoteli ya Glaciers Peak, huku msichana huyo akionekana kushangaa kila kitu. Baadaye anamtafutia mwalimu maalum kwa ajili ya kuanza kumfundisha kuzungumza, kusoma na kuandika kisha wanahama hotelini baada ya kupata nyumba ya kupanga.

    Maisha yanazidi kusonga mbele huku malkia wa masokwe akibadilika taratibu na sasa anafikia hatua ya kuanza kuzungumza kama binadamu wa kawaida. Anafundishwa ustaarabu na Harrison na kwa kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, malkia wa masokwe anazidi kuwa mrembo. Baadaye wanaanza kusomea mafundisho ya dini kuhusu ndoa na uhusiano ikiwa ni maandalizi ya kuoana.

    Kwa kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo malkia wa masokwe anavyozidi kubadilika na kuwa na tabia zote kama binadamu wengine. Harrison anabadilisha kabisa mwonekano wake akikwepa kugundulika na ndugu zake ambao wote wanaamini kuwa alishakufa kwenye ajali mbaya ya barabarani. Sasa maandalizi ya ndoa yamepamba moto na wanachosubiri ni siku husika kufika.





    Siku zilizidi kusonga mbele, hatimaye siku ya harusi yao ikawa imekaribia. Wakaendelea na maandalizi ya hapa na pale ikiwa ni pamoja na kununua nguo watakazovaa siku hiyo. Kwa kuhofia watu wasije kuingilia ndoa yao na kukwamisha mpango wao, waliamua kutofanya sherehe zaidi ya kuhalalishwa mbele za Mungu kisha wangesafiri pamoja kwenda sehemu ya mbali kabisa kula fungate pamoja.

    Harrison na mchumba wake Angel waliendelea na maandalizi ya harusi, wakanunua shela zuri kwa ajili ya bibi harusi na suti maridadi kwa ajili ya bwana harusi, pamoja na pete za ndoa za dhahabu. Kwa kuwa akaunti ya Harrison bado ilikuwa na fedha za kutosha alizozipata baada ya kuchapisha na kuuza kitabu chake cha Queen of Gorillas, kila kitu kilienda kama kilivyokuwa kimepangwa.

    Akiwa katika mwonekano mpya wa sura na jina, Harrison alikuwa na matumaini makubwa kuwa hakuna kitu kitakachokwamisha ndoa hiyo. Kilichomfurahisha zaidi ni kwamba alikuwa akimuoa mwanamke aliyekuwa akimpenda kwa dhati kutoka ndani ya moyo wake, akiwa amemhangaikia sana mpaka kufanikiwa kumpata.

    Maandalizi yalizidi kupamba moto, ndoa yao ikawa inatangazwa kanisani kila wiki ili kama kuna mtu yeyote mwenye pingamizi ajitokeze kama ilivyokuwa kawaida kila ndoa zinapotaka kufungwa. Kwa kuwa hakuna aliyekuwa anamfahamu Harrison wala Angel (malkia wa masokwe) kila kitu kilienda kama kilivyopangwa.

    Kama alivyokuwa amepanga tangu mwanzo, Harrison hakutaka kufanya sherehe ya aina yoyote. Alipanga kuwa wataenda kanisani kufunga ndoa kisha baada ya hapo watasafiri kwenda kwenye Visiwa vya Barbados ambako wangekula fungate kwa raha zao bila kubughudhiwa na mtu yeyote.

    Kabla hata hawajafunga ndoa rasmi, tayari Harrison alishafanya ‘booking’ kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Bajans Legacy Apartment iliyokuwa kwenye mji wa pili kwa ukubwa visiwani humo, Speightstown. Alilipia gharama za kuishi kwenye hoteli hiyo iliyokuwa kwenye ufukwe wa Bahari ya Atlantic kwa muda wa mwezi mzima.

    Siku ya harusi ikawadia, Harrison akavaa suti yake maridadi na Angel (malkia wa masokwe) akavaa shela lake lenye hadhi ya kipekee. Kama ndiyo ingekuwa mara ya kwanza kuwaona, ungeweza kudhani wanatoka kwenye familia ya kifalme kwa jinsi walivyokuwa wamependeza. Wapambaji waliokodiwa na Harrison, walifanya kazi yao ipasavyo kwani Angel alibadilika mno. Sasa alikuwa malaika kweli kama jina lake lilivyokuwa.

    Kila Harrison alipokuwa anamtazama, alikuwa akijisikia raha ya ajabu ndani ya moyo wake. Mwalimu Gallagher na mkewe ndiyo waliokuwa wasimamizi wa ndoa hiyo. Baada ya kumaliza kujiandaa, walitoka mpaka nje ambapo magari mawili ya kifahari waliyoyakodi, yalikuwa yakiwasubiri. Bwana harusi akaingia kwenye gari moja na mwalimu Gallagher ambaye naye alikuwa amependeza kisawasawa.

    Bibi harusi akaingia kwenye gari lingine akiwa na mke wa mwalimu wake, safari ya kuelekea kwenye Kanisa la St. Peter Langley ikaanza. Kwa kuwa hapakuwa mbali sana, baada ya muda mfupi wakawa wamewasili. Wakateremka na kuelekea moja kwa moja ndani ya kanisa hilo, huku bendi ya kanisa ikiwatumbuiza kwa muziki laini.

    Hakukuwa na watu wengi waliohudhuria zaidi ya viongozi wa kanisa na waumini wachache waliokuwa wanaishi jirani. Wawili hao walienda moja kwa moja mpaka madhabahuni na kusimama wakiwa wanatazamana. Baada ya taratibu za kawaida za kufungisha ndoa, mchungaji alimuongoza Harrison (Alex) kula kiapo cha ndoa baada ya kumhoji maswali kadhaa.

    “Mimi Alex Wolfgang, nakubali kumuoa Angel kuwa mke wangu wa ndoa, kuanzia leo na kuendelea, katika raha na shida, katika utajiri na umaskini, katika maradhi na uzima mpaka kifo kitakapotutenganisha,” alisema Harrison (Alex) kisha akamvalisha pete ya ndoa, akamsindikiza na busu zito. Watu wote wakashangilia na kupiga makofi.

    Alipomaliza, mchungaji alimgeukia Angel ambapo alimuuliza maswali kadhaa kisha akamuongoza naye kula kiapo cha ndoa. Alipomaliza, alimvalisha pete Harrison kisha wakashikana mikono kwa upendo na kukumbatiana, wakabusiana kimahaba, hali iliyofanya watu wote wasimame na kushangilia kwa nguvu.

    Baada ya hapo walijaza cheti cha ndoa, walipomaliza wakashikana mikono na kuanza kutembea kwa hatua za taratibu kushuka madhabahuni, wakatembea kwa hatua za taratibu mpaka kwenye zulia maalum, wakaongoza moja kwa moja mpaka nje ambako waliingia kwenye gari moja. Wakakumbatiana na kugusanisha ndimi zao, kila mmoja akiwa na furaha isiyoelezeka.

    Kwa kuwa walishajiandaa kwa safari, baada ya kutoka kanisani, walisindikizwa moja kwa moja mpaka Uwanja wa Ndege wa Abbotsford. Wakapanda kwenye ndege kubwa ya Airbus 380 iliyokuwa inaelekea Visiwa vya Barbados. Walitengewa sehemu maalum katika daraja la kwanza (Diplomatic Class).

    Muda mfupi baadaye, ndege ikaanza kujongea taratibu kuelekea kwenye njia za kurukia (run ways). Mwalimu Gallagher, mkewe na watu wachache waliowasindikiza wakawa wanawapungia mikono huku wakiwatakia kila la heri kwenye fungate yao. Taratibu ndege ikaiacha ardhi na kupaa angani.

    “Mbona unalia mke wangu,” Harrison alimuuliza Angel aliyekuwa amejiinamia chini machozi yakimtoka.

    “Nalia kwa furaha mpenzi wangu, sitaki kuamini kama kweli nimekuwa mke wako halali. Umenitoa mbali sana Harrison, yaani hata siamini,” alisema Angel huku akizidi kutokwa na machozi.

    “Usijali kipenzi changu, nilikuahidi kuwa lazima nikuoe na leo nimetimiza ahadi yangu, nakupenda sana mahabuba na kama nilivyoapa kanisani nitakuwa na wewe mpaka kifo kitakapotutenganisha,” alisema Harrison na kumkumbatia mke wake, akawa anamfuta machozi huku akimbusu sehemu mbalimbali za mwili wake.

    Safari iliendelea kwa muda mrefu, hatimaye wakamsikia mhudumu wa ndege akiongea kupitia vipaza sauti vilivyokuwa kwenye ndege, akiwataarifu abiria wote wafunge mikanda yao kwani ndege ilikuwa ikijiandaa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Speightstown kwenye Visiwa vya Barbados.

    Harrison alimsaidia mke wake kumfunga mkanda, na yeye akajifunga na kutulia, ndege ikatua salama uwanjani na baada ya muda, mlango ukafunguliwa na abiria wakaanza kuteremka. Harrison alimbeba mke wake kutoka ndani ya ndege mpaka chini kisha wakaelekea kwenye mlango wa kutokea.

    Mizigo yao ilipitishwa kwenye mtambo maalum hadi upande wa nje, nao wakatoka hadi sehemu ya mapokezi ambapo walikuta gari maalum kutoka Hoteli ya Bajans Legacy likiwasubiri. Harrison hakujali watu waliokuwa wanamtazama alivyombeba mkewe, akamuingiza mpaka ndani ya gari kisha safari ya kuelekea hotelini ikaanza. Njia nzima alikuwa akimwagia mvua ya mabusu.

    ***

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    BAADA ya kulihangaikia penzi la malkia wa masokwe kwa kipindi kirefu, Harrison anafanikiwa kumtorosha msichana huyo, chaguo la moyo wake kutoka kwenye himaya ya masokwe na kwenda naye nchini Canada. Akiwa kwenye Mji wa Abbotsford, Harrison anafanya kazi ya ziada ya kumbadilisha msichana huyo.

    Baada ya kazi kubwa, hatimaye anafanikiwa kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu, pia anamtafutia mwalimu anayemfundisha kuongea, kusoma na kuandika. Baada ya muda, malkia wa masokwe anabadilika kabisa na sasa anakuwa na haiba kama binadamu wengine.

    Kwa pamoja wanaanza kujifunza masomo ya ndoa na mambo ya kiroho na baadaye wanajitambulisha rasmi kama wachumba. Mipango ya ndoa inaanza kupangwa huku kila kitu kikiendeshwa kwa usiri ili ndugu wa Harrison wasishtukie kuwa ndugu yao hakufa.

    Mwisho Harrison na malkia wa masokwe wanafunga ndoa na kuhalalishwa madhabahuni kuwa mume na mke halali. Muda mfupi baada ya kufunga ndoa, wanaondoka pamoja kuelekea kwenye Visiwa vya Barbados wanakoenda kula fungate.

    Upande wa pili, msichana ambaye Harrison alimkimbia kanisani muda mfupi kabla ya kufunga naye ndoa, Linda, haamini kama kweli mpenzi wake huyo alikufa kifo cha kawaida. Hali hiyo inamfanya akasomee upelelezi akiwa na dhamira kubwa ya kuingia mwenyewe kazini kufuatilia ni nini kilichotokea siku ya tukio.



    Mizigo yao ilipitishwa kwenye mtambo maalum hadi upande wa nje, nao wakatoka hadi sehemu ya mapokezi ambapo walikuta gari maalum kutoka Hoteli ya Bajans Legacy likiwasubiri. Harrison hakujali watu waliokuwa wanamtazama alivyombeba mkewe, akamuingiza mpaka ndani ya gari kisha safari ya kuelekea hotelini ikaanza. Njia nzima alikuwa akimwagia mvua ya mabusu.

    Baada ya dakika kadhaa, gari lililowabeba Harrison na mkewe liliwasili kwenye hoteli ya kisasa ya Bajans Legacy Apartment iliyokuwa ufukweni mwa Bahari ya Atlantic. Wahudumu wachangamfu wakaenda kuwapokea mizigo mpaka sehemu ya mapokezi. Harrison akajitambulisha pamoja na mkewe, kwa sababu alishafanya ‘booking’ siku kadhaa nyuma, hakupata shida.

    Wakaongozwa moja kwa moja mpaka kwenye chumba chake kilichokuwa na kila kitu ndani. Wahudumu wakawasaidia kupanga vitu vyao vizuri kisha wakaanza kuwaonesha mazingira ya hoteli ile ambayo ama kwa hakika ilikuwa inavutia.

    “Tutakaa hapa kwa kipindi cha mwezi mzima, nataka tufurahi na kusherehekea pamoja ushindi tulioupata,” alisema Harrison huku akimkumbatia mkewe, akawa anambusu sehemu mbalimbali za mwili wake.

    Waliagiza chakula ambacho kililetwa muda mfupi baadaye, wakala pamoja huku kila mmoja akionekana kuwa na furaha kuliko kawaida. Baada ya kula walitoka na kwenda kupumzika ufukweni huku wakipigwa na upepo mwanana. Ilibidi wabadilishe nguo walizokuwa wamevaa na kuvaa mavazi ya kuogelea (swimming costume).

    “Duh! Mke wangu amejaaliwa uzuri wa asili sijapata kuona. Lazima leo tuingie rasmi kwenye ulimwengu wa mapenzi, najua hajawahi kumjua mwanaume kama nilivyo mimi,” aliwaza Harrison wakati akicheza na mkewe ufukweni. Walikuwa wakikimbia huku na kule na kubebana kama watoto.

    Kwa kadiri walivyokuwa wanazidi kucheza, ndivyo hisia za mapenzi zilivyokuwa zinazidi kuwapanda wote wawili, wakawa wanabusiana kimahaba huku wakinyonyana ndimi mara kwa mara. Baadaye wakaangushana kwenye mchanga wa bahari, wakawa wanatazamana kama majogoo yanayotaka kupigana.

    “Angel!”

    “Abee mume wangu.”

    “Nakupenda sana kipenzi changu, naahidi kukutunza kwa kadiri ya uwezo wangu wote mpaka kifo kitakapotutenganisha.”

    “Ahsante mume wangu, mimi pia naahidi kukupenda na kukuheshimu kwa siku zote za uhai wangu,” alisema Angel huku akimpapasa mumewe kifuani kwa mahaba. Hisia za mapenzi zilipowazidia, walinyanyuka pale mchangani na kuanza kukokotana kuelekea kwenye chumba chao.

    Njia nzima walikuwa wakimwagiana mvua ya mabusu kwa mahaba, wakakokotana mpaka chumbani kwao, Harrison akamuinua mkewe juujuu na kumbwaga juu ya kitanda kikubwa cha kisasa. Wakaanza kupashana miili yao joto kwa ajili ya safari ya kwanza kuelekea kwenye ulimwengu wa mahaba.

    Baada ya takribani dakika kumi na tano, kila mtu alikuwa hajiwezi kwa hisia za kimapenzi. Angel alikuwa akiguna kimahaba wakati Harrison akivinjari sehemu mbalimbali za mwili wake, hali iliyomfanya azidishe utundu. Wote walipokuwa tayari, waliianza safari kwa mara ya kwanza.

    Wakiwa safarini, Angel alikuwa akipiga kelele sana wakati Harrison akitumia nguvu kubwa kuuvunja ukuta imara wa ngome yake kwani hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kusafiri kuelekea kwenye ulimwengu wa huba. Huo ukawa mwanzo wa wawili hao kushiriki tendo la ndoa.

    Mwanzo ulikuwa mgumu sana kwa Angel lakini kwa kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, akawa anazoea huku yale maumivu makali aliyoyahisi mwanzo wa safari yakiisha kabisa. Fungate ilikuwa tamu sana kwa wote wawili, siku zikawa zinakwenda kwa kasi kuliko kawaida huku upendo ukizidi kushamiri kati ya wanandoa hao.

    Baada ya kumaliza muda wao wa kukaa fungate, Harrison na mkewe walifunga safari ya kurudi kwenye makazi yao, Abbotsford nchini Canada. Wakasafirishwa kwa gari maalum la hoteli waliyofikia mpaka kwenye Uwanja wa Ndege wa Speightstown kwenye Visiwa vya Barbados. Safari ya kurejea nyumbani kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Trans Atlantic ikaanza.

    Walifika salama na kuendelea na maisha yao, sasa wakiwa mume na mke halali. Siku zilizidi kusonga mbele, kwa pamoja wakakubaliana kwamba wasifanye haraka kwenye suala zima la kutafuta mtoto mpaka maisha yao yatakapotengemaa.

    Harrison akaanza kutafuta kazi kwani japokuwa alikuwa na fedha za kutosha, hakutaka kukaa nyumbani siku zote. Japokuwa hakuwa na vyeti vyake, lakini ujuzi aliokuwa nao ulisababisha apate kazi haraka kwenye idara ya uchunguzi wa tabia za wanyama na mimea kwenye Mji wa Abbotsford.

    Hakutaka mkewe naye awe mama wa nyumbani, akamtafutia chuo cha mafunzo ya kompyuta. Wakawa wanaondoka pamoja asubuhi mpaka kwenye Chuo cha Langley Computer College ambapo Harrison alikuwa akimuacha mkewe kisha yeye kuelekea kazini kwake. Jioni alikuwa akimpitia na kurudi naye nyumbani, maisha yakawa yanazidi kuwa matamu.

    Kama walivyokuwa wameapa madhabahuni, kila mmoja alizidi kuonesha upendo wa dhati kwa mwenzake, wakawa wanazidi kupendana kwa kadiri siku zilivyokuwa zinasonga mbele na kuwa mfano wa kuigwa kwa watu wote waliokuwa wanawazunguka, kuanzia nyumbani, chuoni kwa Angel mpaka kazini kwa Harrison.

    ***

    Baada ya baba yake kukamilisha mahitaji yote aliyokuwa anayataka ili kufungua kampuni yake binafsi ya upelelezi jijini Miami, Florida, Linda alizidi kuongeza juhudi kwenye masomo yake ya ujasusi, safari hii akiwa na matumaini makubwa ya kutimiza ndoto zake.

    Hatimaye aliingia mwaka wa tatu na wa mwisho wa masomo yake. Kama alivyoanza mwanzo, hakutaka kulegeza kamba hata kidogo, akaendelea kuongeza juhudi mpaka siku ya mwisho aliyohitimu masomo yake. Akatunukiwa shahada ya kwanza ya Crime Scene Investigation. Mahafali yakafanyika chuoni hapo ambapo wazazi wengi ambao vijana wao walikuwa wakihitimu walijumuika nao, wakiwemo mzee Ford (baba yake Linda) na mkewe.

    Baada ya mahafali kumalizika, walisafiri na binti yao mpaka nyumbani kwao, Miami. Linda hakutaka kupumzika hata kidogo, alifikia moja kwa moja kwenye kampuni yake. Siku chache baadaye, kampuni yake ya American Private Investigation Bureau ikazinduliwa rasmi.

    ***

    Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu. Maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana, yanapita kama maua yachanuavyo na kunyauka. Wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unapumua, ni vyema basi kufikiria maisha baada ya kifo.

    Kila siku jiulize: “Hivi nikifa leo nitakwenda jehanam au peponi?” Kila mmoja wetu analo jibu lake, bila shaka sote tungependa kwenda peponi. Kama hivyo ndivyo, basi tiketi ya kwenda huko ni matendo mema na kujiepusha na uovu.

    Tukumbuke mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele.



    MCHUMIA juani hulia kivulini. Harrison aliyesota kwa kipindi kirefu akilihangaikia penzi la malkia wa masokwe, hatimaye anafanikiwa kupata alichokuwa anakitaka. Anamtorosha msichana huyo aliyekuwa analindwa na kundi



    kubwa la masokwe kutoka ndani ya Msitu wa Tongass na kwenda naye nchini Canada.

    Baada ya kufika nchini Canada, kwenye Mji wa Abbotsford, Harrison anafanya kazi ya ziada ya kumbadilisha



    msichana huyo na hatimaye anafanikiwa kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu. Pia anamtafutia mwalimu anayemfundisha kuongea, kusoma na kuandika. Baada ya muda, malkia wa masokwe anabadilika kabisa na sasa anakuwa na haiba kama binadamu wengine.



    Baada ya kuridhishwa na mabadiliko aliyokuwa nayo, Harrison na msichana huyo wanaanza kujifunza masomo ya ndoa na mambo ya kiroho na baadaye wanajitambulisha rasmi kama wachumba. Mipango ya ndoa inaanza kupangwa huku kila kitu kikiendeshwa kwa usiri, hatimaye wanafunga ndoa halali kanisani iliyohudhuriwa na watu muhimu tu.



    Muda mfupi baada ya kufunga ndoa, wanaondoka pamoja kuelekea kwenye Visiwa vya Barbados wanakoenda kula fungate kwa muda wa mwezi mzima. Baada ya kumaliza fungate, wanarejea kwenye makazi yao ambapo Harrison anamuandikisha mkewe kusomea kompyuta na yeye anatafuta kazi.



    Upande wa pili, Linda ameshahitimu masomo ya Crime Scene Investigation na kutunukiwa shahada yake. Baba yake ameshamfanyia mipango yote ya kufungua kampuni binafsi ya upelelezi.



    BAADA ya mahafali kumalizika, walisafiri na binti yao mpaka nyumbani kwao, Miami. Linda hakutaka kupumzika hata kidogo, alifikia moja kwa moja kwenye kampuni yake. Siku chache baadaye, kampuni yake ya American Private Investigation Bureau ikazinduliwa rasmi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Linda akiwa ndiyo mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, aliwaajiri wapelelezi wengine kadhaa pamoja na watu wa kumsaidia kazi, baada ya uzinduzi wa kampuni hiyo uliohudhuriwa na watu wengi mashuhuri nchini Marekani, wakiwemo rafiki za baba yake, Linda alianza rasmi kazi na kama alivyokuwa amejiwekea nadhiri ndani ya moyo wake, jukumu la kwanza lilikuwa ni kufuatilia juu ya kifo cha Harrison.



    Kwa kuwa sasa alikuwa ni mpelelezi aliyekamilika, akiwa amesajiliwa katika bodi ya wataalamu wa Crime Scene Investigation, kila kitu kilikuwa rahisi kwake. Jambo la kwanza alilolifanya ilikuwa ni kwenda mpaka kwenye Daraja la Miami, Florida, mahali Harrison alipopatia ajali.

    Kwa kutumia mbinu za kiintelijensia alizokuwa amejifunza chuoni, alianza kwa kulikagua eneo lote huku akipiga picha kwa kutumia kamera maalum. Alikuwa akichunguza kitu kimoja baada ya kingine, kuanzia urefu wa daraja, kina cha maji chini ya daraja hilo, wingi wa magari yanayopita kwa dakika moja pamoja na taarifa nyingine muhimu.



    Kama alivyokuwa amebaini hata kabla hajaenda kusomea mafunzo hayo, kina cha maji chini ya daraja hilo kilikuwa kifupi sana, hali iliyomfanya aamini kama mtu akitumbukia eneo hilo, hawezi kufa kirahisi. Pia hata urefu wa daraja, kutoka juu mpaka kwenye usawa wa bahari, haukuwa mrefu kiasi cha kutisha.



    Baada ya kufanya uchunguzi wa kina katika eneo hilo uliochukua zaidi ya saa tatu, alirudi ofisini kwake na kuweka vizuri taarifa zake katika ‘database' ya kompyuta yake. Aliandika baadhi ya vitu kwenye kitabu chake maalum kisha akatoka na kuelekea kwenye Kituo Kikuu cha Polisi cha Miami County.



    Alipofika alijitambulisha ikiwa ni pamoja na kutoa kitambulisho chake, akapokelewa kwa unyenyekevu na kuelekezwa ofisi aliyokuwa anataka kuingia. Shida yake kubwa ilikuwa ni kuonana kwa mara nyingine na afisa mkuu wa upelelezi wa kituo hicho, ambaye kipindi cha nyuma alikataa kumpa ushirikiano alipotaka kujua undani wa ajali iliyomuua kipenzi cha moyo wake, Harrison.



    Tofauti na alivyotegemea, alipofika kwenye ofisi iliyokuwa na maandishi makubwa yaliyosomeka Crime Scene Department, alikutana na sura tofauti na ile aliyoikuta miaka kadhaa iliyopita. Safari hii alimkuta kijana ambaye hawakuwa wakipishana naye sana umri, wakasalimiana kisha Linda akajitambulisha. Baada ya utambulisho, Linda alieleza shida iliyompeleka.

    "Mbona tukio lenyewe lilitokea siku nyingi sana? Kwa nini unataka kujua undani wake leo?"



    "Kuna sababu maalum za kiintelijensia, nakuomba unipe msaada ninaouhitaji," alisema Linda kwa msisitizo, akionesha kutokuwa na hata chembe ya masihara.



    Baada ya mazungumzo mafupi, yule afisa alinyanyua mkonga wa simu yake na kupiga namba fulani. Baada ya muda, akaingia msichana nadhifu na kumsabahi Linda kisha akamsogelea bosi wake kumsikiliza. Alimpa maelezo ya kwenda kutafuta faili lililokuwa na maelezo ya ajali hiyo.



    Kwa kuwa Linda alikuwa anakumbuka mpaka tarehe ya siku ya ajali, kazi haikuwa ngumu. Yule msichana akaondoka na kuelekea kwenye chumba maalum mafaili hayo yalipokuwa yanahifadhiwa. Baada ya kupekua kwa zaidi ya nusu saa, alifanikiwa kulipata faili na kulipeleka ofisini kwa bosi wake.



    Faili limepatikana, niambie unataka kujua kitu gani kutoka humu ndani."

    "Kwanza nataka kuona mchoro wa namna ajali ilivyotokea, ramani ya eneo la tukio lilivyokutwa baada ya ajali na kila kitu kilichokuwepo, alama zilizoachwa eneo la tukio, ripoti ya daktari aliyeupima mwili wa marehemu na sehemu alikoenda kuzikwa," alisema Linda kwa msisitizo.



    Kwa kuwa alikuwa akihitaji vitu vingi sana, alikabidhiwa faili zima, akaambiwa kila kitu kilikuwa ndani yake lakini haruhusiwi kuondoka nalo kwa mujibu wa taratibu za kiuchunguzi na kiintelijensia.

    Bila kupoteza muda, Linda alilipokea faili hilo na kuomba apewe muda wa kukaa peke yake kwa ajili ya kulipitia kwa kina na kuangalia kila kitu alichokuwa anakihitaji.



    "Mpeleke chumba cha wageni, nafikiri kuna utulivu wa kutosha," alisema yule afisa akimpa maelekezo msaidizi wake. Linda akatoka na kuongozana na yule msichana mpaka kwenye chumba maalum kilichokuwa kimetengwa kwa ajili ya wageni.

    Akakaa na kushusha pumzi ndefu kabla ya kuanza kulipitia, ukurasa mmoja baada ya mwingine. Baada ya kutulia kwa sekunde kadhaa, huku



    mapigo ya moyo wake yakimuenda kasi kuliko kawaida, alianza kufunua ukurasa wa kwanza uliokuwa na maelezo ya hali ilivyokuwa eneo la tukio.

    Alisoma neno moja baada ya jingine kwa umakini mkubwa, huku akiandika vitu muhimu kwenye kitabu chake. Kwa mujibu wa maelezo yaliyokuwa yameandikwa kwenye faili hilo, ilionesha kuwa Harrison akiwa anaendesha pikipiki, aligongwa na gari kwa nyuma na kuburuzwa mita kadhaa kwenye kingo za daraja, kisha akatupwa mpaka baharini.



    Alipomaliza kusoma ukurasa wa kwanza, alifunua ukurasa wa pili ambao ulikuwa na picha za marehemu kama alivyokutwa eneo la tukio akiwa anaelea baharini, picha ya pikipiki aliyokuwa anaitumia na maelezo mengine muhimu.

    Aliitazama picha ya marehemu ya kwanza, akaitazama ya pili na ya tatu. Katika kitu kilichomshangaza, katika picha zote zilizopigwa, hakukuwa na picha iliyokuwa inamuonesha marehemu usoni.



    "Ina maana ajali hiyo ilisababisha uso wake uharibike kiasi cha kutotambulika?" alijiuliza Linda huku akiendelea kuzitazama picha zile kwa umakini mkubwa. Aligandisha macho yake juu ya picha hizo kwa muda mrefu, akajikuta amezama kwenye dimbwi la mawazo machungu.

    Alipozinduka, alianza kuitazama pikipiki aliyokuwa anaitumia marehemu ambayo nayo ilionekana kubondeka vibaya. Akawa anajiuliza kama iligongwa kutokea nyuma, mbona taa zake hazikuwa zimepasuka na wala hakukuwa na dalili zozote za kugongwa kutokea nyuma?



    Alishusha pumzi ndefu na kuandika baadhi ya vitu katika kitabu chake cheusi. Akafunua ukurasa mwingine ambao ulikuwa na alama zilizokutwa eneo la tukio. Alianza kufuatilia kwa kina kila kitu, katika hali iliyomuacha mdomo wazi, aligundua uwepo wa alama za viatu vya watu wawili tofauti.



    Alizifuatilia kwa makini, zikaonesha kusogea mpaka kwenye kingo za daraja kisha zikageuka na kurudi zilikotokea.

    "Mbona inaonesha kama kuna watu walitupa kitu baharini," alijiuliza Linda huku akiziangalia vizuri zile picha.

    ***





    BAADA ya Harrison kusota kwa kipindi kirefu akilihangaikia penzi la malkia wa masokwe, hatimaye anatimiza ndoto zake. Anafanikiwa kumtorosha msichana huyo aliyekuwa akilindwa na kundi kubwa la masokwe kutoka ndani ya Msitu wa Tongass na kwenda naye nchini Canada.



    Wakiwa katika Mji wa Abbotsford nchini Canada, Harrison anafanya kazi ya ziada kumbadilisha msichana huyo ambapo anafanikiwa kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu. Pia anamtafutia mwalimu wa kumfundisha elimu ya kidunia.



    Baada ya muda, malkia wa masokwe anabadilika kabisa na sasa anakuwa na haiba kama binadamu wengine. Baadaye wanaanza kujifunza mafunzo ya ndoa na uhusiano kisha wanatangaza uchumba. Mipango ya ndoa inaanza kupangwa na hatimaye wanafunga ndoa halali kanisani. Baada ya kufunga ndoa, wanaelekea kula fungate katika Visiwa vya Barbados kisha kurejea Abbortsford.



    Harrison anamuandikisha mkewe kusomea kompyuta na yeye anatafuta kazi. Wanaendelea na maisha yao wakiwa kama mume na mke halali. Upande wa pili, baada ya Linda kuhitimu masomo ya Crime Scene Investigation anaanza kufanya kazi kwenye kampuni yake binafsi ya upelelezi akiwa na ari kubwa ya kuufahamu ukweli nyuma ya kifo cha kipenzi cha moyo wake, Harrison.



    Hatua za awali za upelelezi wake zinamuwezesha kufahamu mambo mengi yaliyokuwa yanaashiria kuwa Harrison hakufa kifo cha kawaida kama watu wengi walivyokuwa wanaelewa. Anajiapiza kuendelea na kazi hiyo mpaka aufahamu ukweli. Anagundua kuwepo kwa alama za viatu za watu wawili tofauti eneo ambalo Harrison alipata ajali.





    Linda alizifuatilia kwa makini alama hizo za viatu, zikaonesha kusogea mpaka kwenye kingo za daraja kisha zikageuka na kurudi zilikotokea.



    “Mbona inaonesha kama kuna watu walitupa kitu baharini,” alijiuliza Linda huku akizitazama vizuri zile picha. Alichokibaini kilimshangaza sana, akarudia tena na tena kuzitazama zile picha, kweli ilionesha kuwa haikuwa ajali ya kawaida. Ilivyoonekana, kuna kitu kilitupwa baharini na watu wawili waliokuwa wanasaidiana, jambo lililozidisha shauku ndani ya moyo wake ya kutaka kuufahamu ukweli.



    Baada ya kugundua jambo hilo, Linda aliendelea kufunua kurasa nyingine za faili lile, akafika kwenye ukurasa uliokuwa na ripoti ya alama za vidole zilizokutwa kwenye pikipiki. Pia katika hali ambayo ilimshangaza, aligundua kuwa pikipiki iliguswa kwenye usukani na zaidi ya mtu mmoja.



    “Lazima kuna jambo hapa, haiwezekani,” alisema Linda huku akiendelea kufuatilia taarifa zote zilizokuwa ndani ya faili lile. Kilichomshangaza zaidi ni kukosekana kwa umakini kwa askari waliofika kuchunguza eneo la ajali kwani kuna vitu vya wazi mno hawakuvifanyia kazi.



    “Kwa nini maafisa wa polisi waliofanya uchunguzi eneo la tukio hawakubaini vitu hivi muhimu ambavyo mimi naviona? Au hawakuwa na elimu ya kutosha kama mimi?” alijiuliza Linda, mwisho akajipa majibu mwenyewe kuwa huenda hawakutilia mashaka tukio hilo na kuona ni la kawaida ndiyo maana hawakujishughulisha zaidi.



    Aliendelea kufunua kurasa nyingine za faili lile ambapo alibaini vitu vingi vilivyozidi kumfanya aamini kuwa lazima kuna njama zilikuwa nyuma ya tukio hilo. Alipomaliza, alishusha pumzi ndefu na kuinuka, akalibeba faili na kulirudisha ofisini ambapo alimshukuru bosi wa kitengo cha Crime Scene Investigation kisha akaagana naye na kuondoka, kichwani akiwa na mawazo lukuki.



    Kwa jinsi alivyokuwa anajisikia, hakutaka kurudi kazini, aliongoza moja kwa moja mpaka nyumbani kwao, akaingia chumbani kwake na kujifungia. Akajitupa kitandani huku machozi yakianza kumtoka na kudondokea kwenye shuka. Mawazo mengi yalikuwa yakipita ndani ya kichwa chake, alijiuliza maswali mengi lakini hakupata majibu.



    Utata alioubaini ulimfanya aumie sana ndani ya mtima wake, akajua kumbe tukio zima halikuwa mipango ya Mungu kama ambavyo watu wote walikuwa wanaamini bali kulikuwa na mkono wa mtu nyuma yake. Hali hiyo iliamsha majonzi upya, akawa anakumbuka maumivu aliyoyapata kuanzia siku aliyopokea taarifa za kifo cha mpenzi wake huyo mpaka siku hiyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sikubali, sikubali nasema, lazima niujue ukweli,” alisema Linda huku akijifuta machozi. Hakuweza kufanya jambo lolote kwa siku hiyo, hata chakula hakula, akaendelea kujifungia chumbani kwake huku akiomboleza. Mama yake alishtushwa na hali hiyo, akaenda kujaribu kumgongea mlango lakini Linda hakufungua mpaka asubuhi ya siku ya pili.



    Kulipopambazuka, Linda aliwahi kuamka kuliko siku zote, akajiandaa na kuchukua vitu vyake muhimu, moja kwa moja akaelekea ofisini kwake ambapo siku hiyo alikuwa wa kwanza kufika. Akaingia na kuanza kupanga namna ya kuendesha oparesheni ngumu na ya hatari ya kutaka kubaini ukweli uliokuwa nyuma ya tukio hilo.



    Alianza kwa kuandika jinsi alivyokuwa anataka mpango mzima ufanyike, jambo la kwanza alitaka kuomba kibali cha kwenda kulifukua kaburi alilozikwa Harrison kwa lengo la kupima vinasaba (DNA) kwenye masalia ya mwili wake kutaka kubaini kama kweli aliyezikwa ni Harrison.



    Pia akapanga kwenda kuonana na mamlaka iliyokuwa inashughulikia kazi ya kuongoza kamera za usalama barabarani kwa lengo la kuangalia siku ya tukio nani na nani walifika eneo hilo na walichokifanya.



    “Naamini nikifanikisha hizi kazi mbili nitapata ukweli wa kinachoendelea,” alisema Linda na kushusha pumzi ndefu. Bila kupoteza muda alienda mpaka makao makuu ya polisi jijini Miami. Akaomba kukutana na mkuu wa kituo kuomba kibali maalum cha kuufukua mwili wa marehemu.



    Alitoka hadi kwenye maegesho ya magari, akaingia ndani ya gari lake la kifahari alilonunuliwa na baba yake kama zawadi wakati anahitimu masomo yake ya Crime Scene Investigation. Akawasha na kuondoka kwa mwendo wa taratibu kuelekea kwenye Makao Makuu ya Polisi, Miami County.



    Alipofika aliomba kuonana na mkuu wa jeshi la polisi kwenye Jimbo la Florida ambapo alijitambulisha na kuonesha vitambulisho vyake, kisha akaeleza shida yake. Kwa kuwa na yeye alikuwa mtaalamu aliyefuzu, alipewa kibali cha kwenda kufukua kaburi la Harrison lakini akaelekezwa kuwa watu wa mwisho wenye mamlaka ya kumruhusu ni Halmashauri ya Jiji la Miami.



    Alipewa fomu maalum ambazo alizijaza kisha zikapigwa mhuri na kuwekwa saini na mkuu wa polisi, akamshukuru na kuaga. Akatoka hadi nje alikokuwa amepaki gari lake na safari ya kuelekea kwenye Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Miami ikaanza.

    Alipofika, alikutana moja kwa moja na Meya wa Jiji la Miami, Collins Duke. Akajitambulisha na kueleza shida yake.



    Bila hiyana, meya huyo aliweka saini yake katika ile fomu maalum aliyopewa na polisi, akamuelekeza kwenda kwenye ofisi za daktari mkuu wa jiji ambaye angempa wataalamu wa afya wa kwenda kusaidiana naye.

    Linda alimshukuru na kutoka nje, akafuata ramani aliyopewa kwenda kwenye ofisi ya daktari mkuu ambayo ilikuwa ghorofa ya chini katika jengo kubwa la Halmashauri ya Jiji la Miami. Aliingia kwenye lifti na kushuka hadi ghorofa ya chini, akakata kona kuelekea upande wa kushoto mpaka alipofika kwenye ofisi ya daktari mkuu.



    Kama kawaida yake, alijitambulisha na kuonesha vielelezo vyote muhimu. Daktari mkuu wa jiji naye akaweka saini kwenye sehemu yake lakini kabla ya kuwateua wataalamu watano wa afya ambao wangeongozana naye hadi kwenye Makaburi ya Miami Cemetery, alimuuliza swali.

    “Ndugu zake wana taarifa ya unachotaka kukifanya?”

    “Hapana, hawana taarifa.”



    “Hatuwezi kukuruhusu mpaka upate idhini kutoka kwa ndugu zake. Fuatilia hilo kwanza ukishakamilisha, uje na mwakilishi yeyote kutoka kwenye familia ya marehemu ndiyo utaongozana na wataalamu kutoka ofisi yangu,” alisema Daktari Adams Phillips, Linda akaahidi kurejea ofisini kwake siku inayofuata akiwa na mwakilishi kutoka familia ya marehemu.



    Alipotoka aliongoza moja kwa moja kwa kutumia gari lake mpaka nyumbani kwa akina Harrison, walikokuwa wanaishi mama wa marehemu, Skyler, babu na bibi yake. Kwa bahati mbaya, alipofika hakumkuta mtu, hali iliyomlazimu kusubiri kwa muda mrefu mpaka jioni.



    Mtu wa kwanza kurejea nyumbani alikuwa ni mama mzazi wa Harrison ambaye alipomuona Linda, alishtuka sana, akamkaribisha ndani huku akiwa na shauku ya kutaka kujua kilichompeleka. Bila kupoteza muda, Linda akaanza kumueleza alichokibaini juu ya kifo cha Harrison na alichokuwa anataka kukifanya.

    ***









    Harrison tayari amefanikiwa kutimiza ndoto yake ya siku nyingi ya kumpata malkia wa masokwe, baada ya kusota kwa kipindi kirefu akilihangaikia penzi lake kwenye Msitu wa Tongass. Amevumilia mateso ya muda mrefu wakati akilipigania penzi la msichana huyo aliyekuwa akilindwa na kundi kubwa la masokwe.



    Baada ya kutoka ndani ya msitu huo, anatoroka naye na kwenda mpaka nchini Canada anakoenda kuishi na msichana huyo katika Mji wa Abbotsford nchini Canada. Harrison anaanza kazi ya kumbadilisha msichana huyo ambapo anafanikiwa kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu. Pia anamtafutia mwalimu wa kumfundisha elimu ya kidunia.



    Malkia wa masokwe anabadilika kabisa na sasa anakuwa na haiba kama binadamu wengine. Baadaye wanatangaza uchumba na mipango ya ndoa inaanza kupangwa. Hatimaye wanafunga ndoa halali kanisani na kuwa mume na mke halali. Harrison anamuandikisha mkewe kusomea kompyuta na yeye anatafuta kazi. Wanaendelea na maisha yao kama kawaida.



    Upande wa pili, baada ya Linda kuhitimu masomo ya Crime Scene Investigation anaanza kufanya kazi kwenye kampuni yake binafsi ya upelelezi akiwa na ari kubwa ya kuufahamu ukweli uliojificha nyuma ya kifo cha kipenzi cha moyo wake, Harrison.



    Upelelezi wake unamuwezesha kufahamu mambo mengi yaliyokuwa yanaashiria kuwa Harrison hakufa kifo cha kawaida kama watu wengi walivyokuwa wanaelewa. Anaendelea na upelelezi ambapo anabaini vitu vingi vilivyokuwa na utata wa hali ya juu. Mwisho akaanza kushughulikia kibali cha kufukua kaburi la Harrison akiwa na nia ya kuchukua vipimo vya DNA.



    Mtu wa kwanza kurejea nyumbani alikuwa ni mama mzazi wa Harrison ambaye alipomuona Linda, alishtuka sana, akamkaribisha ndani huku akiwa na shauku ya kutaka kujua kilichompeleka. Bila kupoteza muda, Linda akaanza kumueleza alichokibaini juu ya kifo cha Harrison na alichokuwa anataka kukifanya.

    “Nahisi Harrison hakufa kwa mipango ya Mungu, lazima kuna mkono wa mtu.”

    “Kwa nini unasema hivyo Linda?”

    “Nimefanya utafiti wa kitaalamu, nimegundua kuwa lazima kuna njama zilifanyika, nahitaji baraka zenu ili niendelee na upelelezi utakaoibua majibu kamili juu ya nini kilichosababisha Harrison akafa.”



    “Hamna shida mama, mimi nakubaliana na wewe kwa roho nyeupe kabisa, nina hamu kubwa ya kuufahamu ukweli,” alisema Skyler huku akilengwalengwa na machozi. Hata alipomueleza kuwa ili kupata kibali cha kufukua mwili wa marehemu (exhumation order) inahitajika aongozane naye hadi kwenye ofisi za Manispaa ya Jiji, Skyler hakuwa na pingamizi.



    Wakakubaliana kuwa asubuhi ya siku inayofuatia, atampitia ili waongozane pamoja kwenda kufuatilia kibali hicho. Linda akaondoka huku akiwa na matumaini makubwa ya kufanikisha kazi kubwa iliyokuwa mbele yake. Alipofika nyumbani kwao, Linda aliwaeleza baba na mama yake kila kitu kilichokuwa kinaendelea.



    Nao wakaahidi kuwa kesho wataungana naye makaburini watakapoenda kuufukua mwili wa Harrison. Baada ya kula chakula cha usiku, Linda alikuwa anaona kama saa hazisogea haraka, akawa anatamani kupambazuke haraka akakamilishe kazi ya kuufukua mwili wa Harrison na kuchukua vipimo vya DNA.



    Kulipopambazuka, Linda ndiyo alikuwa wa kwanza kuamka, akaanza kujiandaa na kuwaamsha wazazi wake ili nao wajiandae. Kila mmoja alipokuwa tayari, waliingia ndani ya gari la familia na kwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa akina Skyler. Wakamchukua na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye ofisi za Halmashauri ya Jiji la Miami.



    Baada ya kukamilisha taratibu zote za kiserikali zilizokuwa zinatakiwa, Linda alikabidhiwa kibali cha kufukua kaburi la Harrison. Wakapewa na wafanyakazi wa halmashauri, gari, vifaa pamoja na daktari kwa ajili ya kuzingatia usalama wa afya zao watakapokuwa wanafanya zoezi hilo.



    Safari ya kuelekea kwenye Makaburi ya Miami Cemetery ikaanza, gari la halmashauri likawa mbele na gari walilopanda Linda, wazazi wake na Skyler likawa linafuata nyuma. Walipofika, walipaki magari yao na kutembea kuelekea kwenye kaburi la Harrison.



    Kazi ya kulifukua ikaanza. Kazi haikuwa nyepesi, ilibidi wafanyakazi hao watumie akili ya ziada kuvunja zege juu ya kaburi hilo, wakafanikiwa kusogeza mfuniko na mmoja kati yao akaingia mpaka ndani ya kaburi na kuchukua mabaki ya mfupa mdogo na nywele.



    Wakati zoezi hilo likiendelea, kwa upande wa Linda alikuwa akijisikia vibaya sana. Picha za siku ya mazishi ya Harrison zilikuwa zikijirudia akilini mwake, hali iliyomfanya alie kwa uchungu sana. Hali ilikuwa hivyohivyo kwa Skyler, alikuwa akilia kwa uchungu sana utafikiri siku hiyo ndiyo mwanaye wa kipekee aliiaga dunia.



    Baba na mama yake Linda wakawa na kazi ya ziada ya kuwatuliza. Zoezi liliendelea, vitu vilivyochukuliwa kaburini vikawekwa kwenye mfuko maalum na kufungwa kitaalamu, kaburi likajengewa upya na mfuniko ukarudishwa mahali pake.



    Baada ya kazi kumalizika, Linda aliwashukuru sana wafanyakazi wale wa halmashauri, wazazi wake pamoja na mama mzazi wa Harrison kwa ushirikiano waliomuonesha. Pia alimuomba Skyler atoe nywele zake kidogo ambazo zingetumika kufananisha vinasaba (DNA) kati ya marehemu na mama yake.



    “Lazima niupate ukweli kwa gharama yoyote,” alisema Linda huku akijifuta machozi, akampa maelekezo daktari aliyeongozana naye alichokuwa anakitaka. Alitoa cheki na kuwapa wale wafanyakazi wa halmashauri kama shukrani kwa kazi waliyoifanya kisha wakaondoka eneo hilo la makaburini.



    Kwa jinsi alivyokuwa anajisikia uchungu, Linda alishindwa kufanya kitu chochote siku hiyo. Hali hiyo ilimtokea pia Skyler ambaye alikuwa akiomboleza kwa uchungu. Kesho yake, Linda akawahi kuamka na kuanza kujiandaa kwa ajili ya kwenda kukutana na yule daktari waliyeongozana naye makaburini.



    “Vipi umefikia wapi?”

    “Mh! Nimeshachukua vipimo vya DNA lakini majibu yanaonesha utata.”

    “Utata? Kwani umegundua nini?”

    “Majibu yanaonesha kutofanana kati ya DNA za mwili tulioufukua kaburini na ya mama yake Harrison.”

    “Mungu wangu, kwa hiyo unataka kusemaje?”

    “Mwili uliozikwa kwenye kaburi hilo siyo wa Harrison,” alisema daktari huyo kwa msisitizo huku akimkabidhi Linda majibu ya vipimo vya DNA.



    Alijikuta akishindwa kuyazuia machozi ya uchungu, akaagana na daktari na kuondoka na majibu yake huku akiendelea kulia. Akaenda mpaka kwenye gari na kuingia. Aliingia kwenye gari lake na kuegamia usukani, machozi yakawa yanazidi kumtoka.



    “Umepatwa na nini Harrison wangu? Kwa nini haya yananitokea mimi? Ina maana hukufa? Kama ni hivyo, uko wapi baba… njoo tutimize ahadi yetu ya kufunga ndoa, njoo Harrison wangu! Sijawahi kuwa na furaha tangu ulipoondoka kwenye maisha yangu, rudi baba…” alisema Linda kwa uchungu huku donge likiwa limemkaba shingoni.



    Alilia kwa muda mrefu sana mpaka macho yakavimba na kuwa mekundu. Aliendelea kulia mpaka akapitiwa na usingizi akiwa ndani ya gari. Alikuja kushtuliwa na mlinzi aliyekuwa anagonga kioo cha gari lake, baada ya kumuona amelala kwa muda mrefu.

    “Una tatizo dada?”



    “Ha.. hapana kaka yangu,” alijibu Linda huku akijinyoosha na kujifikicha macho, akawasha gari na kuondoka kwa mwendo wa kasi. Mlinzi alibaki amepigwa na butwaa kwani kwa kasi aliyoondoka nayo Linda, hakujua kama atafika salama huko aendako.

    Alipoingia kwenye barabara kubwa, Linda alizidi kukanyaga mafuta, gari lake likawa linaenda kwa kasi kubwa iliyowashtua madereva wengine.



    Baadhi ya magari yakawa yanasimama kumpisha kwani alionesha kuchanganyikiwa. Majibu ya DNA aliyopewa, yalimfanya awe kama mwendawazimu.

    ***





    NDOTO za Harrison za kuishi na malkia wa masokwe, hatimaye zimetimia. Baada ya kuhangaika kwa kipindi kirefu akitafuta nafasi ya kumtorosha kwenye Msitu wa Tongass, Harrison anafanikiwa kumpata msichana huyo aliyekuwa akilindwa na kundi kubwa la masokwe.



    Anatoroka naye kutoka ndani ya msitu huo hadi nchini Canada anakoenda kuishi naye katika Mji wa Abbotsford. Harrison anaanza kazi ya kumbadilisha msichana huyo ambapo anafanikiwa kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Msichana huyo anabadilika kabisa na sasa anakuwa na haiba kama binadamu wengine. Baadaye wanafunga ndoa halali kanisani na kuwa mume na mke. Harrison anamuandikisha mkewe kusomea kompyuta na yeye anatafuta kazi. Wanaendelea na maisha yao kama kawaida.



    Upande wa pili, baada ya Linda kuhitimu masomo ya Crime Scene Investigation anaanza kufanya kazi kwenye kampuni yake binafsi ya upelelezi akiwa na shauku kubwa ya kuufahamu ukweli uliojificha nyuma ya kifo cha Harrison.



    Upelelezi wake unaibua mambo mengi ambapo kuna kila dalili zinazoashiria kuwa Harrison hakufa kifo cha kawaida. Uamuzi wa mwisho anaofikia ni kwenda kulifukua kaburi la Harrison kwa ajili ya kuchukua vipimo vya DNA. Anachokibaini kinamliza sana.



    ALIPOINGIA kwenye barabara kubwa, Linda alizidi kukanyaga mafuta, gari lake likawa linaenda kwa kasi kubwa iliyowashtua madereva wengine. Baadhi ya magari yakawa yanasimama kumpisha kwani alionesha kuchanganyikiwa. Majibu ya DNA aliyopewa, yalimfanya awe kama mwendawazimu.

    Kwa bahati nzuri, hakupata ajali licha ya vurugu alizokuwa anazifanya barabarani, breki ya kwanza ikawa ni nyumbani kwao. Bila hata kulisimamisha gari kwenye eneo maalum la maegesho, Linda aliteremka na kukimbilia ndani kwao huku akiangua kilio kama mtoto mdogo.

    "Hee! Kuna nini tena mwanangu? Umepatwa na nini?"

    "Ni bora nife mama, niacheni nife tu, sioni umuhimu wa kuishi."

    "Kwani kuna nini Linda?"

    "Bora nife mimi."

    "Mwanangu hebu tulia kwanza utueleze," mama yake Linda alikuwa akimtuliza mwanaye huku baba yake, mzee Ford naye akionesha kushtushwa na hali aliyokuwa nayo binti yao. Licha ya kubembelezwa sana, Linda hakutaka kusema chochote zaidi ya kuendelea kulia kwa uchungu.

    Katika purukushani za kumtuliza, Linda alijibamiza ukutani na kudondoka chini kama mzigo, akapoteza fahamu. Hali hiyo ilizidi kuwachanganya wazazi wake, harakaharaka wakamkimbiza mpaka nje, wakampakiza kwenye gari na safari ya kuelekea hospitalini ikaanza.

    Kutokana na umaarufu wa baba yake, Linda alipofikishwa hospitalini, alipokelewa harakaharaka na kulazwa juu ya kitanda cha magurudumu, wauguzi zaidi ya wanne wakawa wanasaidiana kukisukuma kitanda kumpeleka wodini.

    "Amepatwa na nini?"

    "Amejigonga ukutani na kupoteza fahamu."

    "Ooh! Poleni sana, atakuwa sawa msijali," daktari aliyempokea Linda alikuwa akizungumza na wazazi wa binti huyo, nje ya wodi aliyolazwa. Jitihada za haraka zikafanyika ambapo alitundikiwa dripu na kuanza kupewa huduma ya kwanza.

    Baada ya kutibiwa kwa saa nyingi, hatimaye Linda alizinduka na kujikuta yupo wodini. Akawa anaangaza macho huku na kule akiwa ni kama anajiuliza pale ni wapi na amefikaje.

    "Mama!"

    "Abee mwanangu."

    "What happened to me?" (Nini kimenitokea?)

    Mama Linda alimuinamia mwanaye na kumshika kwenye paji la uso, akawa anampa pole na kumsihi atulie. Mara akarejewa na kumbukumbu zake na kuanza kulia upya.

    "Harrison mama! Harrison!"

    "Harrison kafanyeje tena mwanangu?"

    "Harrison hakufa mama…"

    "Whaaat?" (Niniii?)

    "Harrison hakufa, kuna mchezo ulifanyika, nimepata ushahidi," alisema Linda huku akilia kwa kwikwi, mama yake akabaki amepigwa na butwaa kutokana na maelezo yale. Harakaharaka alitoka na kwenda kumuita mumewe, mzee Ford aliyekuwa nje ya wodi, wakaongozana hadi ndani kumsikiliza Linda alichokuwa anakisema.

    Bado alieleza vilevile kama alivyomwambia mama yake, safari hii akilia kwa nguvu. Ilibidi daktari aje kumchoma sindano ya usingizi kwani kwa hali aliyokuwa nayo, kulikuwa na hatari kubwa ya kuendelea kujidhuru. Akaendelea kulala huku wazazi wake wakitazamana, wakiwa hawaamini walichokisikia.

    "Unataka kusema Harrison hakufa? Mbona hainiingii akilini?"

    "Mimi mwenyewe hata sielewi, mbona sote tulihudhuria mazishi yake?"

    "Mh! Labda tusubiri azinduke, yeye mwenyewe ndiyo mtu pekee anayeweza kueleza kilichotokea," wazazi wa Linda walikuwa wakijadiliana, wakiwa wamesimama nje ya wodi aliyolazwa mtoto wao.

    Daktari alitoka na kuwaambia kuwa hawatakiwi kumuuliza mgonjwa maswali yoyote mpaka atakapopona kabisa, ushauri ambao waliupokea kwa mikono miwili.

    Dawa ya usingizi ilipopungua nguvu, Linda alishtuka lakini safari hii alikuwa haeleweki alichokuwa anazungumza kutokana na dawa hizo kumlevya. Daktari aliwaruhusu wazazi wake wamchukue na kurudi naye nyumbani lakini akawasisitiza kumuacha apumzike mpaka atakapokuwa sawa.

    Walisaidiana kumshika huku na huku, wakatembea taratibu mpaka nje walikokuwa wamepaki gari lao. Mzee Ford aliwafungulia mlango wa nyuma, Linda na mama yake wakaingia na kukaa na yeye akakaa nyuma ya usukani. Safari ya kuelekea nyumbani kwao ikaanza. Linda alijiegamiza kwenye bega la mama yake, machozi yakawa yanaendelea kumtoka mpaka walipofika kwao.

    Kama walivyoshauriwa na daktari, hakuna aliyemhoji Linda kitu chochote. Walipofika walisaidiana kumteremsha garini na kumpeleka mpaka chumbani kwake. Akaendelea kulala. Kutokana na hali yake ilivyokuwa, mama yake alilazimika kulala naye chumbani kwake mpaka asubuhi.

    "Mama!"

    "Abee mwanangu."

    "Harrison hakufa mama, nimepata uthibitisho."

    "Tuachane na hayo mwanangu, hali yako bado siyo nzuri, ukipona tutaongea kwa kirefu."

    "Nimeshapona mama, nimefanya upelelezi na kugundua kuwa mwili tuliouzika haukuwa wa Harrison, roho inaniuma sana mama."

    "Basi mwanangu, jikaze kila kitu kitakuwa sawa."

    "Siwezi kuwa sawa mama mpaka nijue Harrison alipo, bado nampenda mama."

    "Kwani umejuaje kuwa hakufa," mama Linda aliuliza swali lililomfanya mwanaye aanze kueleza hatua kwa hatua kilichotokea. Maelezo aliyoyatoa yalimfanya mama yake abaki mdomo wazi kwani alikuwa na uthibitisho wa kutosha. Ilibidi akamuite mume wake, wakawa wanajadiliana kwa pamoja juu ya suala hilo.

    Linda alishikilia msimamo wake kuwa lazima amtafute Harrison kwa gharama zozote ili ajue mbivu na mbichi. Licha ya wazazi wake kumkataza, bado alishikilia msimamo wake, akala yamini kuwa ni lazima aifanye kazi hiyo.

    ***







    Wakati Harrison akifurahia kutimia kwa ndoto zake za siku nyingi za kuishi na malkia wa masokwe, hali si shwari kwa aliyekuwa mpenzi wake, Linda. Baada ya Harrison kuhangaika kwa kipindi kirefu akitafuta nafasi ya kumtorosha malkia wa masokwe kwenye Msitu wa Tongass, anafanikiwa kumpata na kutoroka naye kutoka ndani ya msitu huo hadi nchini Canada.



    Baada ya kufika nchini humo, Harrison anaenda kuishi naye katika Mji wa Abbotsford. Harrison anaanza kazi ya kumbadilisha msichana huyo ambapo anafanikiwa kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu.

    Msichana huyo anabadilika kabisa na sasa anakuwa na haiba kama binadamu wengine. Baadaye wanafunga ndoa halali kanisani na kuwa mume na mke. Harrison anamuandikisha mkewe kusomea kompyuta na yeye anatafuta kazi. Wanaendelea na maisha yao kama kawaida.

    Kwa upande wa Linda, baada ya kuamua kwenda kusomea upelelezi, anahitimu na kutunukiwa shahada ya kwanza ya Crime Scene Investigation kisha anaanza kufanya kazi kwenye kampuni yake binafsi ya upelelezi akiwa na shauku kubwa ya kuufahamu ukweli uliojificha nyuma ya kifo cha Harrison.

    Katika upelelezi huo, anagundua mambo mengi ambayo yanaashiria kuwa Harrison hakufa kifo cha kawaida. Uamuzi wa mwisho anaofikia ni kwenda kulifukua kaburi la Harrison kwa ajili ya kuchukua vipimo vya DNA. Anachokibaini kinamliza sana kwani anagundua mwili uliozikwa haukuwa wa Harrison. Anachanganyikiwa kabisa na kuanza kuomboleza tukio hilo upya.



    Kwa siku tatu nzima, Linda hakwenda kazini badala yake akawa anashinda chumbani kwake akiwa amejifungia. Aliendelea kuomboleza baada ya kubaini kuwa kumbe kulikuwa na njama kali nyuma ya tukio la kifo ‘feki’ cha Harrison. Aliendelea kuwaza kwa kina mahali pa kuanzia.

    Siku tatu zilipopita, tayari alikuwa na jibu la nini cha kufanya. Alienda kuwasiliana na jeshi la polisi jimboni Florida na kuomba picha za usalama barabarani zilizochukuliwa na kamera za CCTV kuanzia eneo la tukio. Kutokana na kitengo cha usalama barabarani kuwa na utaratibu maalum wa kuhifadhi picha zote za matukio ya barabarani, kazi haikuwa ngumu kwa Linda.

    Alipofika alijitambulisha na kueleza shida yake ambapo alihojiwa maswali kadhaa kabla ya kuambiwa akasubiri ndani ya chumba maalum. Baada ya takriban dakika ishirini, Linda aliitwa kwenye maktaba maalum ya picha za video na kazi ikaanza.

    Alipewa rekodi nzima ya matukio ya barabarani ya eneo la tukio, kuanzia muda ambao ilisemekana Harrison alipata ajali.

    Kama alivyokuwa amebaini awali, ni kweli alishuhudia magari mawili yakiondoka kwa kasi eneo la tukio baada ya ajali kutokea. Alianza kuyafuatilia, moja baada ya jingine. La kwanza lilionekana kurejea kwenye mitaa ya makazi ya watu jijini Miami na la pili lilionekana kusafiri kwa kasi kubwa kuelekea kaskazini, nje ya jimbo la Florida.

    “Lazima atakuwa kwenye gari hili,” alisema Linda na kumtaka afisa usalama aliyekuwa anamsaidia kazi ile, kulivuta karibu gari hilo na kufuatilia kwa makini upande lilikoelekea.

    “Mungu wangu, ni yeye kweli,” alisema Linda huku akiwa amekodoa macho yake kwenye ‘skrini’ kubwa iliyokuwa ukutani. Ni kweli alikuwa ni Harrison lakini safari hii hakuwa amevaa mavazi ya harusi. Alikuwa amebadilika na kuvaa nguo ambazo Linda hakuwahi kumuona nazohata siku moja, kichwani akiwa amevaa kofia kubwa.

    Linda aliendelea kufuatilia gari hilo kwa makini jinsi lilivyokuwa likichanja mbuga. Alilifuatilia kwa makini mpaka lilipotoka nje ya Jiji la Miami na kuingia kwenye Jiji la Orlando. Akaendelea kulifuatilia kwa makini huku akiandika taarifa muhimu kwenye kitabu chake kidogo. Machozi yalikuwa yakimtoka mara kwa mara, akawa analia na Mungu wake kwa kumsababishia mtihani mgumu kiasi hicho.

    Picha hizo zilimuonesha Harrison alipoenda hadi kwenye kituo cha treni za umeme cha Orlando Metro ambapo alilitelekeza gari alilokuwa analitumia na kwenda kwenye ofisi za stesheni hiyo.

    “Lazima nitampata tu,” alisema Linda huku ndita zikijionesha dhahiri kwenye uso wake, akamshukuru afisa huyo wa kitengo cha usalama barabarani kwa msaada aliompatia kisha akaaga na kuondoka, huku akilini akiwa ameshapata wazo la nini cha kufanya.

    Alipotoka, hakutaka kurudi nyumbani, aliendesha gari lake kwa kasi kubwa kuelekea Jiji la Orlando ambapo alipanga kwenda kufuatilia taarifa za wasafiri wote waliopanda treni, siku ajali feki ya Harrison ilipotokea.

    Kwa kuwa alitaka kuwahi kwenda na kurudi, alilazimika kusafiri kwa kasi kubwa, njia nzima akawa anamlaumu Harrison kwa kitendo alichomfanyia na kumuachia maumivu makali ya mtima kiasi kile.

    Baada ya kusafiri kwa muda mrefu, akinusurika kupata ajali mara kadhaa, hatimaye aliwasili jijini Orlando na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye ofisi za Stesheni ya Orlando Metro. Akaenda kujitambulisha kwa mkuu wa stesheni hiyo na kueleza kilichompeleka.

    Kwa kuwa alieleza kuwa kazi aliyoifuata hapo ni kwa ajili ya usalama wa nchi, alikubaliwa bila kipingamizi na kupelekwa kwenye chumba maalum kilichokuwa na kompyuta nyingi zilizotumika kuhifadhi ‘Database’ za safari zote za treni.

    Linda akaomba kutafutiwa rekodi za wasafiri wote waliosafiri kwa treni, siku Harrison aliyopata ajali feki. Kwa kuwa alikuwa na kumbukumbu nzuri za tarehe na muda Harrison alipowasili kituoni hapo, kazi haikuwa ngumu. Taarifa zote za wasafiri wa muda na siku hiyo zikaanza kuoneshwa ambapo alifuatilia jina moja baada ya jingine kuangalia kama ataliona jina la Harrison.

    Katika kupekuapekua kwake, akakutana na jina la Harrison Harvey ambapo ilionesha kuwa amesafiri siku hiyo kwa treni kuelekea Kituo cha Tongass ambapo ndiyo ilikuwa mwisho wa safari ya treni hiyo. Akashusha pumzi ndefu na kuanza kuandika taarifa muhimu, ikiwa ni pamoja na muda ambao alitegemewa kufikakwenye kituo hicho.

    Wakati akiendelea kuandika, alikumbukakitu kilichomfanya aunganishe matukio kwa urahisi. Alikumbuka kuhusu kitabu kilichoandikwa na Harrison cha Queen of Gorrilas ambacho kilimpatia umaarufu mkubwa nchini Marekani.

    “Aliandika kuwa msichana wa ajabu anayelelewa na masokwe anapatikana kwenye msitu wa Tongass, inamaana aliondoka na kwenda kuendelea na utafiti wake kuhusu msichana huyo? Kwa nini hakutaka kumuaga mtu yeyote,” aliwaza Linda huku machozi yakianza tena kumtoka. Akahisi wivu mkali ndani ya nafsi yake.

    Baada ya kumaliza kuchukua taarifa zote muhimu, alitoka hadi ndani ya gari lake na kukaa kwa muda kuanza kutafakari tafsiri ya matukio aliyokuwa anayagundua kila kukicha.

    Kwa bahati nzuri, alikumbuka kuwa ndani nyumbani kwao ana nakala ya kitabu cha Queen of Gorrilas. Japokuwa tayari alishamaliza kukisoma kitabu hicho, alijiapiza kwenda kukirudia, kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho kwa lengo la kuchunguza vizuri kitu alichokiandika akiamini lazima atapata taarifa zitakazomsaidia kufahamu mahali Harrison alipo.

    ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maisha yalizidi kuwanyookea Harrison na mkewe, kila mmoja akawa anaendelea na kazi huku wakioneshana upendo wa dhati kila kukicha. Jioni moja wakati wakilishana chakula cha usiku kwa mahaba, Angel au malkia wa masokwe, alionesha dalili ambazo zilimshtua mumewe.

    Alianza kulalamika kusikia kichefuchefu kikali kilichosababisha atapike chakula chote alichokula. Harrison akawa na kazi ya ziada ya kumsaidia mkewe ambapo alimpeleka chumbani kulala huku akizoa matapishi yote na kusafisha sakafu.

    “Inabidi kesho twende hospitali mke wangu, inawezekana unaumwa,” alisema Harrison kwa sauti ya upole, wazo lililoungwa mkono na mkewe. Walilala mpaka asubuhi ambapo kulipopambazuka, Harrison alienda kumuombea mkewe ruhusa kazini na yeye akaomba kazini kwake.

    Wakaongozana mpaka Hospitali ya Langley ambapo walikutana na daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake. Angel akaeleza dalili alizokuwa anazihisi, akachukuliwa vipimo kisha wakaambiwa wasubiri majibu.

    ***







    MAISHA yanazidi kusonga mbele kati ya Harrison na mkewe ambao wanaendelea kuifurahia ndoa yao. Harrison anafurahia kutimia kwa ndoto zake za siku nyingi za kuishi na malkia wa masokwe kwani baada ya kuhangaika kwa kipindi kirefu akitafuta nafasi ya kumtorosha msichana huyo, hatimaye anafanikiwa.



    Anamtorosha hadi nchini Canada ambapo baada ya kufika nchini humo, Harrison anaenda kuishi naye katika Mji wa Abbotsford. Anaanza kazi ya kumbadilisha msichana huyo ambapo anafanikiwa kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu.



    Malkia wa masokwe anabadilika kabisa na sasa anakuwa na haiba kama binadamu wengine. Baadaye wanafunga ndoa halali kanisani na kuwa mume na mke. Harrison anamuandikisha mkewe kusomea kompyuta na yeye anatafuta kazi. Wanaendelea na maisha yao na baada ya muda, Angel anaanza kuhisi dalili zinazowafanya wakubaliane kwenda hospitali.



    Upande wa pili, Linda amechachamaa kutaka kuufahamu ukweli juu ya kifo cha Harrison. Baada ya kuhitimu masomo ya Crime Scene Investigation na kutunukiwa shahada yake, anaanza kufanya kazi kwenye kampuni yake binafsi ya upelelezi akiwa na shauku kubwa ya kuufahamu ukweli uliojificha nyuma ya kifo cha Harrison.



    Kwa kadiri anavyoendelea na upelelezi huo, anagundua mambo mengi ambayo yanaashiria kuwa Harrison hakufa kifo cha kawaida. Hata baada ya kuamua kulifukua kaburi lake na kupima DNA, anagundua kuwa mwili uliozikwa haukuwa wa Harrison.



    Anachanganyikiwa na kuanza upya kuomboleza huku akijipanga namna ya kuendelea na kazi hiyo mpaka aufahamu ukweli. Anatumia mbinu kali alizojifunza chuoni kuendesha upelelezi huo huku akijiapiza kuwa ni lazima ampate Harrison.





    Baada ya vipimo kukamilika, daktari aliwaita Harrison na mkewe ofisini kwake ambapo alianza kwa kuwapa hongera.

    "Hongera ya nini daktari?"

    "Mkeo ni mjamzito."

    "Kweli? Oooh! Ahsante Mungu," alisema Harrison kwa furaha huku akiinuka na kumkumbatia mke wake ambaye naye alikuwa amepigwa na butwaa akiwa haamini alichokisikia. Walikumbatiana kwa furaha na kumwagiana mvua ya mabusu, kila mmoja akionesha kufurahishwa sana na majibu yale.

    Daktari aliwapa maelezo ya namna ya kuilea mimba changa ambapo alitoa ushauri kwa Harrison kuhakikisha mkewe hafanyi kazi ngumu zinazoweza kuleta matatizo kwa ujauzito wake. Pia aliwashauri vyakula bora ambavyo mwanamke mjamzito anatakiwa kula ili kumjenga vizuri mtoto tumboni.

    Baada ya darasa refu, Harrison na mkewe walitoka na safari ya kurudi nyumbani ikaanza. Njia nzima Harrison alikuwa akifurahi kuliko kawaida huku akilibusu tumbo la mkewe mara kwa mara bila kujali watu waliokuwa wanawatazama.

    Upendo kwa mkewe uliongezeka maradufu, akawa anamdekeza na kumjali kuliko hata ilivyokuwa mwanzo, hali iliyomfanya Angel awe na furaha kupindukia. Kazi zote za nyumbani sasa alikuwa akizifanya Harrison, kuanzia kufua, kusafisha nyumba na mambo mengine mengi, mkewe alibakia na kazi moja tu, kupika.

    Siku zilizidi kusonga mbele huku amani na upendo wa dhati vikitawala kwenye maisha ya wanandoa hao, ujauzito ukawa unaendelea kukua vizuri bila matatizo yoyote. Harrison alikuwa na shauku kubwa ya kuitwa baba, akawa anamtunza mkewe kama mboni ya jicho.

    ***

    Linda alirudi mpaka nyumbani kwao, kama kawaida yake akapitiliza hadi chumbani kwake ambapo alijifungia na kuanza kutafuta kitabu cha Queen of Gorrilas kilichoandikwa na Harrison. Alipokipata, alianza kusoma ukurasa mmoja baada ya mwingine huku akiandika pembeni vitu vyote muhimu ambavyo aliamini vitamsaidia katika kazi yake ya kumsaka Harrison.

    Jambo ambalo awali hakuwahi kuligundua ni kwamba ndani ya kitabu hicho, Harrison alitumia muda mwingi kumsifia msichana huyo wa ajabu huku akisisitiza kuwa urembo wake haufanani na wa msichana yeyote aliyewahi kukutana naye maishani mwake.

    Wivu ukaanza kufurukuta ndani ya moyo wa Linda, alijisikia vibaya sana kwa jinsi Harrison alivyousifia urembo wa malkia wa masokwe ndani ya kitabu hicho. Kibaya zaidi, Harrison alieleza waziwazi kuwa msichana huyo wa ajabu alikuwa mrembo kuliko hata yeye Linda, jambo lililozidi kumnyong'onyeza.

    "Lazima alikuwa anampenda na ndiyo maana akakataa kuoana na mimi, kwa nini Harrison? Kwani mimi siyo mzuri? Kwani sina mvuto? Mbona niliwakataa wanaume wengi kwa sababu yako Harrison?" alisema Linda huku akibubujikwa na machozi, akasimama na kuanza kujiangalia kwenye kioo huku akiendelea kutokwa na machozi.

    Alijigeuzageuza huku akijiuliza maswali ambayo hakuyapatia majibu. Alikichukua kitabu cha malkia wa masokwe na kuanza kuitazama picha iliyopigwa kwa mbali ya malkia wa masokwe na kuanza kujifananisha nayo.

    "Mbona mimi ni mzuri kuliko huyo malkia wa masokwe? Mbona mimi ni msafi, najua kujitunza na pia nimesoma? Huyo malkia wa masokwe amenizidi nini?" alijiuliza Linda huku akiendelea kububujikwa na machozi, akakaa kitandani na kuendelea kusoma kitabu.

    "Kumbe Msitu wa Tongass upo kwenye mpaka kati ya Marekani na Canada? Lazima niende… nataka Harrison anitamkie mbele ya macho yangu kuwa hanitaki na anampenda huyo nyani wake kuliko mimi," alisema Linda huku akibubujikwa na machozi.

    Kuna wakati alishindwa kuendelea kusoma kutokana na macho yake kuzingirwa na machozi, akakitupa kitabu pembeni na kulala, usingizi ukampitia. Akiwa usingizini alianza kuota ndoto za ajabuajabu, hali iliyomfanya ashtuke na kukaa kitandani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku hiyo nayo alishinda vibaya sana, mpaka giza linaingia, hakuwa amefanya kitu chochote zaidi ya kuendelea kulia kwa uchungu. Hakutaka mtu yeyote aingie ndani ya chumba chake, hata chakula hakikulika siku hiyo.

    Kesho yake asubuhi, aliwaaga wazazi wake kuwa anasafiri kwa siku kadhaa ingawa hakuwa tayari kueleza anakwenda wapi. Jambo pekee alilowaambia ni kwamba anasafiri kikazi akiwa anaendelea na uchunguzi wa suala la Harrison.

    Wazazi wake hawakuwa na la kufanya zaidi ya kumruhusu kwani tangu alipoanza kufuatilia suala hilo, alikuwa ni kama amechanganyikiwa hivyo alitakiwa kupewa uhuru wa kutosha kufanya kazi yake.

    Bila kupoteza muda, alisafiri kwa gari lake la kifahari hadi katika Jiji la Orlando ambako alikwenda mpaka kwenye stesheni ya treni iendayo kwa kasi, safari hii akiwa kama abiria. Alipofika, aliomba kuonana na mkuu wa ‘stesheni' waliyezungumza naye siku moja iliyopita ambapo alimuomba amhifadhie gari lake.

    Alipopata uhakika wa usalama wa gari lake, alikata tiketi ya treni na kusubiri kwa muda mpaka treni lilipowasili. Akaingia na kwenda kwenye siti yake, safari ikaanza. Linda hakubeba vitu vingi zaidi ya mkoba wake muhimu uliokuwa na vitu vichache.

    Safari haikuwa nyepesi kama Linda alivyoifikiria kwani walilazimika kupita majimbo mengi kuelekea Tongass. Mpaka inafika saa kumi jioni, Linda alikuwa bado hajafika. Ilipofika saa kumi na mbili jioni, walianza kuuona mji mdogo wa Tongass uliokuwa umezungukwa na misitu minene.

    Sauti za wahudumu wa treni zikawa zinasikika kwenye vipaza sauti zikiwataarifu abiria kuwa treni lilikuwa limekaribia kuwasili kwenye kituo cha mwisho cha Tongass na kwamba abiria wote walitakiwa kushuka kwani hapo ndiyo mwisho wa safari. Linda akaanza kujiandaa kwa kuteremka.

    Muda mfupi baadaye, treni lilisimama na abiria wachache waliokuwa wamesalia ndani yake, akiwemo Linda wakaanza kuteremka na kuelekea kwenye lango kuu la kutokea. Mji wa Tongass ulikuwa mdogo wenye wakazi wachache. Linda akaongoza mpaka kwenye lango la kutokea na kuanza kuangaza macho huku na kule. Hakujua aelekee wapi baada ya kufika kwenye mji huo.

    Akajaribu kuuliza kwa wenyeji mahali anapoweza kupata nyumba ya kulala wageni ambapo alielekezwa. Kwa kuwa hapakuwa mbali sana kutokea kituoni, alitembea kwa miguu mpaka alipofika. Akalipia chumba na kuingia ndani kupumzika wakati akitafakari wapi pa kuanzia.

    ***



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog