Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

I FAIL TO FORGET YOU (NASHINDWA KUKUSAHAU) - 4

 







    Simulizi : I Fail To Forget You

    Sehemu Ya Nne (4)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndege kutoka shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopia Airways) ilikuwa katika anga ya Tanzania ikitokea nchini Afrika Kusini, ratiba ya ndege hiyo ilikuwa itue katika uwanja wa ndege wa KIA (Kilimanjaro International Airport) ambapo baadhi ya abiria wangeweza kushuka na wengine kupanda kuelekea hadi jijini Entebe, Uganda. Mmoja wa abiria waliotakiwa kupanda ni Herieth.

    Baada ya dakika ishirini ndege ilipaa kuelekea Uganda ambapo ratiba ilipangwa itue katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Uganda kilichokuwa kinajulikana kwa jina la Entebe International Airport. Kilikuwa ni kiwanja cha ndege kilichokuwa kilometa chache kutoka ziwa Victoria.

    Alipokuwa kwenye ndege Herieth alikuwa akimfikiria Andrew, alichokuwa akikikumbuka kwa wakati huo ni zawadi ya saa pamoja na busu alilombusu Andrew alipokuwa amelala pale kitandani. Busu hilo lilimtesa sana kila alipokuwa akilikumbuka, alihisi kuwa na mapenzi mazito sana na Andrew ingawa hakuwa akizungumza lolote, alikuwa ni sawasawa na bubu aliyekuwa amepooza.

    Hatimaye ndege iliweza kutua salama katika kiwanja cha ndege cha Entebe na abiria wakaanza kushuka, Herieth alikuwa bado haamini kama kweli alikuwa ameiacha ardhi ya Tanzania na kwa wakati ule alikuwa Uganda. Alikuja kupokelewa na mwenyeji wake kisha safari ya kuelekea shule ya St. Mary’s Kitende ikaanza.



    Ilikuwa ni shule ya wasichana watupu iliyokuwa ikichukua michepuo yote. Herieth alipofika aliweza kupokelewa vizuri na hatimaye akayaanza maisha mapya katika shule hiyo ya St. Mary’s Kitende,alikuwa akichukua mchepuo wa ECA.

    Mapenzi ndiyo yalikuwa yakimchanganya katika kichwa chake, yalichukua nafasi kubwa katika maisha yake. Alipokuwa darasani alionekana kuwa mpole sana, hakuwa ni mtu wa kuzungumza lolote, alibaki kuwa kimya kila wakati. Hilo lilizidi kuwashangaza sana wanafunzi wenzake ambao alikuwa akisoma nao.

    Kwa muda wa miezi miwili tangu alipoanza kusoma katika shule hiyo bado alionekana kuwa mgeni, alikuwa ni mtu wa kujitenga, kila alipokuwa akikaa aliutumia muda huo katika muwaza Andrew.

    Doreen ndiye alikuwa mwanafunzi wa kwanza kuigundua tofauti aliyokuwa nayo Herieth, hakupenda kumuona akiwa katika hali hiyo alichofanya aliamua kumfuata na kumuuliza kama kulikuwa na tatizo.

    “Nini kinachokusumbua?” alimuuliza, hapa ni baada ya kumfuata kantini walipokuwa wakila chakula cha mchana.

    “Hakuna,” alijibu Herieth huku akililazimsha tabasamu katika uso wake.

    “Unanidanganya,” alisema Doreen

    “Hakuna kitu,” alisema Herieth.

    “Mbona sasa unajitenga?”

    “Sijisikii vizuri.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Unaumwa?”

    “Hapana.”

    “Sasa kama huumwi nini tatizo?”

    “Sina tatizo,” alijibu Herieth.

    Doreen alikuwa ni msichana mcheshi sana, alipendwa na wanafunzi wenzake kutokana na uchangamfu wake, alizaliwa Uganda na kukulia Uganda. Alikuwa ni rafiki wa kila mtu.

    Kwa ule muda aliyokuwa na Herieth, alipojaribu kumuuliza baadhi ya maswali na kujibiwa majibu yale, hakutaka kuamini kama kweli hakuwa na tatizo. Alichoamua kukifanya ni kuzidi kuujenga ukaribu zaidi. Alifanikiwa katika hilo, kila siku urafiki ulizidi kujengeka na hatimaye wakawa ni marafiki wakubwa. Kuanzia darasani, bwenini na kila sehemu walionekana kuwa karibu.

    Nyuma ya maisha ya Doreen mbali na kuwa alikuwa akisifika kuwa na tabia nzuri, mcheshi na akipendwa na wanafunzi wenzake pia alikuwa ni msagaji, aliwatumia wanafunzi wenzake katika kufanya nao mchezo huo ambao wengi waliamini walikuwa wakikidhi haja za hisia zao.

    Kila siku aliyokuwa akikaa na Herieth hakuacha kumuuliza kuhusu tatatizo lililokuwa likimsumbua lakini hakuna alichokuwa akiambulia. Alipokuwa bwenini alikuwa akiutumia muda wake mwingi katika kuiandika dayari yake. Doreen alipomuona hakutaka kubaki kimya aliamua kumuuliza.

    “Unaandika nini?” aliuliza Doreen.

    “Hakuna kitu,”alijibu Herieth kisha haraka akaifunga dayari yake, alionekana kuficha kitu fulani.

    “Mbona kama kuna kitu unanificha?” aliuliza Doreen lakini hakuweza kupata jibu lolote.

    Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya Herieth pale shuleni, kila siku alipomaliza vipindi na kurudi bwenini alikuwa ni mtu wa kuandika kwenye dayari yake. Kuna kipindi machozi yalikuwa yakimdondoka, alikuwa akilia na alipoulizwa na wanafunzi wenzake aliwajibu kuwa alikuwa amewakumbuka wazazi wake na hiyo ndiyo ilikuwa sababu iliyomfanya akawa katika hali hiyo.

    “Una email ya wazazi wako?”

    “Ndiyo ninayo ya mama.”

    “Sawa basi chat nao,” alisema Doreen kisha akampatia simu ambayo alikuwa akiiutumia kwa kujificha, sheria za shule hazikuwaruhusu kutumia simu.

    Herieth aliichukua simu kisha akafanya kama alivyoambiwa, aliwatumia wazazi wake ujumbe kuwa alikuwa amewakumbuka. Kwa kuwatumia ujumbe huo ilikuwa kama haitoshi. Moyo wake bado ulikuwa katika maumivu makali sana. Alikuwa akimfikiria Andrew ambapo mpaka kufikia muda huo alikuwa hajui alikuwa katika hali gani.

    ****

    Ilikuwa ni majira ya saa saba za mchana, hali ya hewa ilikuwa shwari katika jiji la Daresalaam, wakazi waishio katika jiji hili walionekana wakiendelea kufanya shughuli zao kama ilivyokuwa kawaida.

    Ndani ya nyumba ya Mzee Antony iliyokuwepo mtaa wa Magomeni Mapipa kulikuwa kuna mazungumzo yanaendelea.

    “Mzigo uko kamili.”

    “Utalipa shilingi ngapi?”

    “Milioni ishirini.”

    “Hiyo hailipi.”

    “Ok fanya ishirini na tano.”

    “Mr. nadhani mzigo mwenyewe umeuona.”

    “Ndiyo uko vizuri sana.”

    “Sasa kwa hicho kiasi mbona kama unataka kunidhulumu kwani sisi tuliahidiana vipi?”

    “Mzee hii ni biashara na biashara ni maelewano, chukua ishirini na nane.”

    “Fanya Thelethini kabisa.”

    “Ok haina tatizo.”

    Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Mzee Antony na wanaume watatu. Mzee Antony alikuwa ameshikilia brufukesi ambayo ilikuwa na madawa ya kulevya na wale wanaume walikuwa wamebeba brufukesi iliyokuwa na pesa, walichoamua kukifanya ni kubadilishana. Kilikuwa ni kitendo cha dakika chache kilichofanyika na hatimaye wale wanaume wakaondoka. Wakati huo Selestine alikuwa akishuhudia kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

    ****

    “Kuna uwezekano wa mwanao kupona,”alisema dokta Masawwe huku akimtazama mama yake Andrew ambaye alikuwa akilia, wakati huo alikuwa ofisini.

    “Dokta unasema?” aliuliza mama Andrew huku akionekana kutoamini kile alichokuwa akiambiwa.

    “Kuna uwezakano wa mwanao kupona,” alirudia kusema tena dokta Masawwe.

    “Dokta ni kweli mwanangu atapona?”

    “Ndiyo ila matibabu yake hayapo hapa Tanzania.”

    “Yako wapi?”

    “Nchini India na nimejaribu kuulizia gharama za matibabu yake kwa kweli sidhani kama utazimudu mama,”alisema dokta maneno yaliyomvunja moyo Mama yake Andrew.

    ****

    Doreen hakutaka kila siku kuendelea kudanganywa na Herieth wakati alimuona kuwa na tatizo, kwa akili ya harakaharaka alipomuangalia aligundua kuwa alikuwa akisumbuliwa na Mapenzi, mapenzi yalikuwa yakimchanganya.

    Alichoamua kukifanya ni kutaka kuiiba dayari ya Herieth ambayo aliamini ilikuwa na mambo mengi ya siri aliyotaka kuyafahamu, alidhamiria kuiiba na kweli alifanya kama alivyopanga. Kile alichokutana nacho ndani ya dayari kilimfanya atokwe na machozi na kumkumbusha simulizi ya maisha yake iliyomsababishia mpaka akawa msagaji.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipokuwa ameifungua dayari na kuanza kuisoma, alikutana na maandishi yaliyoandikwa kwa herufi kubwa I FAIL TO FORGET YOU (NASHINDWA KUKUSAHAU)

    Hakujua yalikuwa na maana gani mpaka pale alipoanza kuisoma, alikutana na kumbukumbu za matukio ambayo yalimfanya aanze kukumbuka mambo fulani yaliyowahi kutokea katika maisha yake. Machozi hayakuwa mbali kwa wakati huo, yalianza kumbubujika mashavuni mwake.

    Alijaribu kuyafuta kwa kutumia viganja vyake lakini hakuweza kuyadhibiti maumivu yaliyokuwa moyoni mwake. Hakutaka tena kuendelea kuisoma ile dayari, aliamua kuirudisha mahali ambapo alikuwa ameitoa.

    “Who is Andrew?” (Andrew ni nani?) lilikuwa ni swali la kwanza ambalo alimuuliza Herieth, wakati huo ulikuwa ni usiku walipokuwa bwenini wamelala, walikuwa wakiishi bweni moja.

    “Where didi you know and who told you about this person?” (Umemfahamu wapi na nani aliyekueleza kuhusu huyu mtu?) aliuliza Herieth huku akijaribu kukumbuka kama kuna siku aliwahi kumueleza mtu yoyote kuhusu habari zile, hakukuwa na mtu ambaye alimueleza.

    “I’ve known him through diary,” (Nimemfahamu kupitia dayari) alisema Doreen.

    Kwa muda wote huo Herieth alikuwa haamini kama Doreen aliweza kufahamu kila kitu kilichokuwa kimetokea, alipanga ibaki kuwa siri yake lakini alihisi kushindwa kufanya hivyo kwani kwa wakati ule tayari rafiki yake alikuwa akifahamu.

    “Tell me the truth do not hide me,” (Niambie ukweli usinifiche) alisema Doreen huku akimtazama Herieth ambaye machozi yalikuwa tayari yameanza kumlengalenga. Haikuchukua muda akaanza kulia machozi, Doreen alipomtazama na yeye akaanza kulia.

    “What truth do you want me to tell you?” (Unataka nikwambie ukweli upi?) aliuliza Herieth huku akiyafuta machozi yake.

    “The truth about Andrew, do you love him?” (Ukweli kuhusu Andrew, unampenda?)

    “Yes, I love him very much.” (Ndiyo, nampenda sana).

    “What happened?” (Ni nini kilitokea?)

    “It’s a long story.” (Ni hadithi ndefu.)

    “Can you tell me?” (Unaweza kunisimulia?)

    “Yeah!” (Ndiyo) alijibu Herieth kisha akaanza kumsimulia kila kitu kilichowahi kutokea katika maisha yake.

    “Mmh!”

    “What?”(Nini?)

    “Really it’s right not to forget.” (Kweli ni haki usimsahau)

    “Really, how about you?” (Kweli, vipi kuhusu wewe?)

    “Even I never found you as you were but in my case it has been a little different,” (Hata mimi yaliwahi kunikuta kama yaliyokukuta wewe lakini kwa upande wangu kuna utofauti kidogo) alisema Doreen kisha akaanza kumsimulia Herieth kile kilichowahi kutokea katika maisha yake.

    ****

    Doreen alizaliwa katika familia ya kitajiri ya Mr. Amos ambaye alikuwa akimiliki kampuni ya usafirishaji Uganda iliyokuwa ikijulikana kwa jina la ATL (Amos Transaport Limited) ilikuwa ni kampuni ambayo ilikuwa ikijihusisha na usafirishaji wa mizigo kutoka nchini Uganda kwenda nchi mbalimbali. Mr. Amos alikuwa ni miongoni mwa matajiri wakubwa Kampala, Uganda.

    Doreen alikuwa ni mtoto wa pekee katika familia hiyo ambapo katika maisha yake yote hakubahatika kumfahamu mama yake mazazi, maisha yake yote alilelewa na Baba yake.

    Alipoanza kukua na kujikuta akiwa na uzuri wa kipekee wanaume hawakuwa mbali, walijitokeza na kuanza kumsumbua, kila mwanaume alitamani kuwa naye kimapenzi.

    “I’ll give you everything you want, love me.” (Nitakupa kila kitu unachokitaka, nipende)

    “Tell me what to give you to love me to be yours?” (Sema unataka nikupe nini ili niwe wako?”

    “I love you very much, I will build you a beautiful house on a small island of the wind.” (Nakupenda sana, nitakujengea nyumba nzuri kwenye kisiwa chenye upepo mwanana)

    Haya yalikuwa ni baadhi ya maneno mazuri ya watoto wa bilionea mkubwa ambao walikuwa wakimpenda Doreen. Kila mmoja alionekana kumpenda sana lakini hakukuwa na mtoto hata mmoja ambaye alifanikiwa kukubaliwa. Kila siku walikuwa ni watu wa kutolewa nje.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Katika mazingira ya kushangaza Doreen alijikuta akiwa katika mahusiano ya kimapenzi na Roy kijana aliyetokea katika familia ya kimasikini sana. Alijikuta akimpenda sana na aliamini Roy ndiye alikuwa mwanaume wa maisha yake ingawa bado walikuwa shule. Walifanya mengi kama wapenzi, waliahidiana ahadi nyingi lakini mapenzi yao hayakuweza kudumu kwasababu ya vita vya kimapenzi vilivyotokea kati ya Roy na wale watoto wa bilionea ambao waliamua kumuua kwa kutumia sumu kali.

    Tangu hapo Doreen hakutaka tena kujihusisha na mapenzi, moyo wake ulihifadhi chuki kali mno dhidi ya wale watoto wa bilionea ambao walishiriki kumuua mpenzi wake Roy.

    Aliamua kuwa msagaji lakini moyoni mwake aliishi na kisasi.

    “I must repay,” (Lazima nitalipa kisasi) alisema Doreen baada ya kumaliza kumsimulia Herieth.

    “So sorry,” (Pole sana) alisema Herieth.

    ****

    “Unaweza kuua?”

    “Ndiyo.”

    “Kweli?”

    “Ndiyo mkuu.”

    “Ulishawahi kuua?”

    “Hapana ila hii ndiyo mara yangu ya kwanza.”

    “Ok inabidi uende kwenye hoteli moja iliyokuwepo maeneo ya Sinza kuna mtu unatakiwa ukamuue.”

    “Sawa mkuu.”

    Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Mzee Antony na Selestine. Mzee Antony alimkabidhi bastola Selestine kwa ajili ya maangamizi, wakati huo yalikuwa ni majira ya usiku.



    Mzee Antony alimuelekeza Selestine hoteli ambayo alitakiwa kufika pamoja na namba ya chumba ambayo alikuwepo mtu huyo ambaye alitakiwa kumuua. Ilikuwa ni maeneo ya Sinza Makaburini ambapo ilikuwepo hoteli hiyo.

    “We muue tu,” alisema Mzee Antony.

    “Sawa Mkuu,” alijibu Selestine.

    Selestine aliamua kwenda mpaka katika hoteli hiyo aliyoelekezwa na Mzee Antony, alipofika ndani ya chumba ambacho alielekezwa alimkuta mzungu mmoja akiwa anafanya mapenzi na mwanamke wa kitanzania.

    “Who are you and what do you want?” (Wewe ni nani na unataka nini?) aliuliza yule mzungu huku akionekana kuogopa mno kwa ujio ule wa Selestine ndani wa chumba chake, alichokumbuka ni kuwa aliufunga mlango wa chumba kile lakini alizidi kushangazwa na ujio wa mtu yule ambaye mpaka kufikia wakati huo hakujua alikuwa na dhamira gani na aliingiaje katika chumba kile.

    “How didi you get in here?” (Umeingiaje humu?) aliuliza swali lingine huku akionekana kuweweseka, wakati huo alikuwa uchi wa mnyama pamoja na yule mwanamke ambaye alikuwa amejifunika kwa kutumia shuka, walikuwa katika uoga wa hali ya juu.

    Selestine hakutaka mazungumzo yoyote wala hakutaka kupoteza muda, alichoamua ni kuitoa bastola yake kisha akaamua kufanya mauaji, aliamua kuwaua wote kwa kuwapiga risasi mbili kila mmoja kisha akatoweka eneo lile.

    Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuua katika maisha yake, lakini hilo halikuonekana kuwa kama tatizo alichokuwa akikiangalia ni pesa alizokuwa akilipwa na Mzee Antony kutokana na kazi ambazo alikuwa akimtuma.

    “Tayari mkuu kazi imeisha nimewaua wote,” alisema Selestine huku akimtazama Mzee Antony ambaye alionekana kutawaliwa na uso wa furaha.

    “Kweli?” aliuliza Mzee Antony.

    “Ndiyo,” alijibu Selestine.

    “Umemuua peke yake?”

    “Hapana nimewaua wote ili kufuta ushahidi.”

    “Vizuri sana, kazi nzuri,” alisema Mzee Antony huku akimpongeza Selestine kwa kazi nzuri ambayo alikuwa ameifanya.

    Mzee Antony alizidi kumtumia Selestine katika kazi zake nyingi za haramu pia hakuacha kumtumia katika mauaji ya wafanyabiashara wenzake aliyokuwa akifanya nao kazi, alikuwa akiwadhulumu mali zao.

    ****

    Hali ya Andrew bado haikuwa nzuri, alizidi kudhoofika mwili wake, alipungua haswaa. Hakuwa Andrew yule tena ambaye alionekana kuwa na afya nzuri, muonekano mzuri, kila kitu kilikuwa kimebadilika kwa wakati huo. Alisikitisha mno, wengi waliomuona hospitalini hapo waliamini kuwa ule ndiyo ulikuwa mwisho wake wa maisha.

    Kwa muda wa miezi takribani sita tangu alipoweza kulazwa katika hospitali ya KCMC hakuna kitu chochote kilichoonekana kubadilika katika ugonjwa wake. Hakuweza kusimama kisha akatembea wala hakuweza kukumbuka lolote japo tayari alikuwa ameshaanza kuzungumza lakini alikuwa akizungumza maneno ambayo hakukuwa na mtu ambaye alielewa kuwa alikuwa akimaanisha nini.

    “Kumbukumbu zake bado hazijarudi,” alisema Dokta Massawe.

    “Kwahiyo Dokta tutafanyaje?” aliuliza Mama Andrew.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hakuna kitu cha kufanya zaidi ya kumuachia Mungu atende miujiza yake hapo,” alisema Dokta Massawe.

    Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa Mama yake Andrew kuanza kukesha usiku kucha kwa ajili ya kufanya maombi, alikuwa akimuombea mwanaye ambaye alikuwa amepooza. Hakuacha pia kila jumapili kwenda kanisani na huko pia alikuwa akimuombea mwanaye aondokane na maradhi aliyokuwa nayo. Aliamini msaada pekee ambao ulikuwa umebakia kwa mwanaye ni Mungu. Mungu ndiye ambaye angeweza kumtibu.

    “Bwana Yesu asifiwe.”

    “Ameen.”

    “Mchungaji nina tatizo.”

    “Tatizo gani tena?”

    “Mwanangu amepooza yupo kitandani anateseka, naomba umfanyie maombi.”

    “Kwa Mungu hakuna kitu kinachoshindikana, amini damu ya Yesu inauwezo wa kumponya mwanao.”

    “Mchungaji mwanangu anateseka.”

    “Usijali lazima tutamfanyia maombi.”

    Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Mama yake Andrew na Mchungaji wa kanisa aliyejulikana kwa jina la Lukacy. Mama Andrew aliamini kwa asilimia kubwa kwamba maombi ya mchungaji huyo yangeweza kumponya mwananye na kumuamsha pale kitandani.

    Mchungaji Lukacy aliianza kazi yake ya kumuombea Andrew, kila siku alikuwa akienda hospitalini kisha akawa akiutumia muda mrefu katika kumuombea Andrew.

    Hakuna kilichokuwa kikibadilisha chochote katika maombi yale, hilo lilizidi kumfanya Mama yake Andrew aanze kutokwa na imani.

    “Mchungaji,” aliita Mama yake Andrew huku akimpa heshima yake Mchungaji Lukacy.

    “Bwana Yesu asifiwe,” alisema Mchungaji.

    “Ameen,” alijibu Mama yake Andrew.

    “Sioni chochote kikibadilika kwa Mwanangu.”

    “Inakubidi uamini kuwa uwezo wa Mungu ni mkubwa sana, amini kuna siku mwanao ataweza kuamka pale kitandani.”

    “Ni siku ipi hiyo?”

    “Amini kuwa ipo damu ya Yesu itatenda miujiza,” alisema Mchungaji.

    Mama yake Andrew tayari alianza kupoteza imani na mchungaji huyo, hakumuamini tena, aliamua kuendelea kutafuta njia mbadala ya kuweza kumsaidia mwanaye lakini kila alilokuwa akilifanya halikuweza kubadili lolote.

    Aliendelea kuhangaika mpaka pale siku moja dokta Massawe alipomuita na kumueleza kuwa kuna uwezekano wa Andrew kupona kabisa na kurudi katika hali yake ya mwanzo kama angeweza kupelekwa katika hospitali ya Apollo Hospital Hyderabad iliyokuwepo India katika mji wa Hyderabad, gharama ya matibabu alizoambiwa ilikuwa ni shilingi milioni themanini za kitanzania.

    Hilo likazidi kumuumiza sana Mama Andrew, hakujua ni kwa jinsi gani ambavyo angeweza kuzipata pesa hizo. Wazo la kuuza nyumba likamjia kichwani mwake.



    Hakutaka kujifikiria mara mbilimbili, alichoamua kukifanya kwa wakati ule ni kutaka kuiuza nyumba yake ili aweze kupata pesa ambazo angeweza kumpeleka mtoto wake nchini India kwa ajili ya matibabu.

    Alianza kutafuta madalali wa nyumba kisha akawaeleza lengo lake la kuuza nyumba yake, kila dalali aliyemfuata na kumueleza kiasi cha pesa ambazo alihitaji aiuze nyumba yake hawakuweza kuelewana.

    Ilikuwa ni nyumba ya kawaida sana na kwa kiasi cha pesa cha shilingi milioni hamsini ambazo alihitaji alipwe hakikuweza kulingana na thamani ya nyumba.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mama wewe ni mgeni wa biashara hii?” aliuliza dalali mmoja baada ya kuambiwa kiasi cha pesa ambazo alitakiwa kuiuza nyumba hiyo yenye vyumba vitatu.

    “Kwanini?” aliuliza Mama Andrew.

    “Yani unasema iuzwe milioni hamsini kwa muonekano huu kweli?” aliuliza yule dalali huku akiinyooshea kidole ile nyumba.

    “Kwani haiwezekani?” aliuliza Mama Andrew huku akionekana kupagawa.

    “Ndiyo haiwezekani,” alijibu dalali.

    “Nina shida sana na ndiyo maana naamua kufanya hivyo sina njia nyingine ya kufanya,” alisema Mama Andrew kwa sauti ya masikitiko sana, hakujua ni nini alitakiwa kufanya kwa wakati huo.

    “Kwa kiasi ulichosema kwa kweli mama huwezi kupata mteja kabisa,” alisema yule dalali wakati huo alikuwa akikikuna kidevu chake kilichokuwa kimejawa na ndevu nyingi sana.

    “Kwahiyo kwa uzoefu wako unahisi ni shilingi ngapi mtu ataweza kuinunua?” aliuliza Mama Andrew kwa sauti ya upole huku akimtazama yule dalali.

    “Labda kwa milioni kumi,” alijibu dalali huku akionekana kujiamini kwa jibu lake lile.

    Mama Andrew alijaribu kuifikiria umbali uliopo kutoka milioni kumi mpaka milioni hamsini. Kiasi cha shilingi milioni Arobaini ndiyo kilikuwa kimepelea. Hakika mawazo yalizidi kumtawala kwani hakuwa akijua ni kwa namna gani ambavyo angeweza kuifidia hiyo milioni arobaini iliyokuwa imepelea.

    “Vipi mama tutafute mteja au?” aliuliza yule dalali.

    “Hapana hiyo pesa haifai,” alijibu Mama Andrew.

    “Sasa mama badala ushukuru nimekwambia hiyo milioni kumi maana ukitafuta dalali mwingine atakwambia milioni tano, kipi bora hapo,” alisema dalali.

    Maneno ya dalali hayakumuingia kabisa Mama Andrew, alichokuwa akikifikiria kwa wakati huo ni kuitafuta hiyo pesa. Wazo lake la kuuza nyumba lilionekana kugonga mwamba kutokana na kiasi ambacho alitarajia kulipwa, kilikuwa ni kiasi kidogo ambacho kiukweli kisingeweza kukidhi shida yake. Alihitaji kumpeleka mwanaye nchini India kimatibabu, hilo ndilo lililokuwa likimuweka katika wakati wa mawazo, hakujua ni nini alitakiwa akifanye.

    Kuna muda akawaza aende kuuza mwili wake kwa wanaume ili aweze kulipwa pesa ambayo ingeweza kumpeleka mwanaye nchini India lakini hilo lilimtisha hapa ni baada ya kuwaza kuwa ni wanaume wangapi angetakiwa kulala nao ili aweze kupata milioni hamsini.

    “Nahisi kuchanganyikiwa,” alijisema kimoyomoyo, hakujua ni nini alitakiwa kufanya.

    Umasikini ndiyo ulikuwa umetawala sehemu kubwa ya maisha yake japo kipindi cha nyuma alikuwa na maisha ya wastani lakini pesa zake zote alizitumia kwa ajili ya ugonjwa wa mwanaye, kupooza kwa Andrew ndiyo kulipelekea mpaka maisha yake kubadilika.

    Hakukata tamaa, aliamua kupambana mpaka mwisho wa pumzi zake katika kuyapigania maisha ya mwanaye. Alichoamua kukifanya ni kwenda kanisani na huko aliomba muda wa kuongea na waumini wenzake, alipopatiwa aliamua kuwasimulia kila kitu kilichokuwa kimetokea katika maisha yake na mwanaye na mwisho akaamua kuwaomba msaada.

    Alipata msaada wa pesa lakini kutokana na michango ambayo ilikuwa ikichangishwa bado haukuweza kufikia kiasi ambacho alihitajika kuwa nacho kwa ajili ya matibabu ya mwanaye kipenzi.

    “Pole sana kwa matatizo yaliyokukuta,” ilisikika sauti ya muumini mmoja mwanaume wa kanisa lile ikimsemesha mama Andrew, wakati huo muda wa ibada ulikuwa umeshapita.

    “Asante sana,” alisema Mama Andrew.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hivi ulisema yule aliyesababisha maradhi ya mwanao uliamua kumchukulia hatua gani za kisheria?” aliuliza yule mwanaume ambaye alionekana kuwa na shahuku ya kutaka kufahamu kila kitu, hata vile visivyojulikana.

    “Nilimripoti polisi lakini hawakuonekana kulifuatilia ila nimeamua kumuachia Mungu naamini yeye ndiye atakayenilipia kwa haya mateso ninayoyapata mimi pamoja na mwanangu,” alisema Mama Andrew huku machozi yakianza kumdondoka, yule mwanaume akapata kazi ya kuanza kumbembeleza.

    “Hapana usilie hiki ni kipindi cha mpito, haya unayoyapitia yana mwisho wake,” alisema yule mwanaume kisha akaanza kumtolea mifano hai kutoka katika biblia aliyokuwa ameishika.

    “Sawa hata mimi naamini hivyo,” alisema Mama Andrew.

    Kila kitu alichokuwa akikifanya kwa ajili ya mwanaye kilikuwa kikishindikana mwisho aliamua kumuachia Mungu, aliamini Mungu ndiye suluhisho la maradhi ya mwanaye aliyekuwa akiteseka kitandani.

    ****

    Herieth na Doreen waliendelea kuwa marafiki wakubwa pale shuleni, walikuwa wakishirikiana mambo mengi sana, waliambiana siri nyingi za maisha yao, mipango yao kila mmoja na hata katika masomo darasani walikuwa wakiongoza. Urafiki wao ulizidi kuwa mkubwa sana siku hadi siku.

    Kutokana na tabia za Doreen alizokuwa nazo za usagaji hakuweza kumuacha salama Herieth ambaye katika maisha yake hakuwahi kukutana kimapenzi na mwanaume yoyote.

    Moyo wake ulijikuta ukiwa katika mapenzi mazito na Andrew lakini mpaka kufikia wakati huo Andrew alikuwa hajui lolote, alikuwa akiendelea kuteseka kitandani.

    “Do you say the truth?” (Unasema kweli?) aliuliza Doreen kwa mshangao mara baada ya kuambiwa na Herieth kuwa katika maisha yake hakuwahi kufanya mapenzi kabisa, alikuwa ni bikra.

    “Yes,” (Ndiyo) alijibu Herieth.

    Kilichofuata mahali hapo ni Doreen kumchojoa nguo Herieth kisha na yeye akachojoa nguo zake, walipomaliza wakaanza kusagana, sauti za miguno ya kimahaba ndiyo iliyokuwa imetawala kwa wakati huo, kila mmoja alikuwa sayari nyingine.



    Waliendelea na mchezo huo wa kusagana huku Herieth akionekana kuupenda zaidi. Hakutaka kushiriki mapenzi na mwanaume yoyote katika maisha yake. Hata kwa upande wa bikra yake iliweza kuvunjwa na mchezo huo wa kusagana.

    Doreen ndiye aliyekuwa kinara, alionekana kuwa mzooefu na mchezo huo, alijua ni nini alitakiwa kufanya ili aweze kumkoleza Herieth mpaka anogewe na utamu wa kusagana.

    ****

    Hali ya Mama Andrew bado haikuwa nzuri, alionekana kuchoka sana, mpaka kufikia wakati huo alikuwa ameshakata tamaa ya kutafuta pesa kwa ajili ya matibabu ya mwanaye. Hakutaka kuumiza tena kichwa chake kitu alichokuwa amekiamua kufanya kwa wakati ule ni kumkabidhi Mungu matatizo yake yote.

    “Mungu naamini wewe sio kipofu kusema hunioni, naamini wewe sio kiziwi kusema hunisikii, nayakabidhi matatizo yangu kwako najua huwezo kuniacha niendelee kuteseka katika dunia hii isiyokuwa na huruma,” yalikuwa ni maneno ya Mama Andrew alipokuwa akifanya maombi.

    Hakukuwa na njia nyingine ya kufanya, aliamini kwa maamuzi yale aliyokuwa ameyachukua ilikuwa ni suluhisho tosha la matatizo yake, aliamini katika jina Mungu ambalo ndilo lingeweza kumponya mwanaye.

    Alitumia pesa nyingi mno katika kulipia matibabu ya mwanaye pamoja na malazi ya pale hospitalini, hilo ndilo lililomuingiza katika dimbwi la umasikini. Hakuwa na biashara yoyote aliyokuwa akiitegemea wala hakuwa na pesa za kuendelea kuyaendeleza maisha yake.

    Awali alighairi kuuza nyumba yake ambayo alidhamiria pesa atakayoipata ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya matibabu ya mwanaye nchini India lakini baada ya umasikini kuzidi kumuandama aliamua kuiuza, aliona hakuwa na sababu nyingine ya kuendelea kuteseka wakati uwezekano wa kuuza nyumba ulikuwepo.

    “Unaiuza bei gani kwani?” lilikuwa ni swala kutoka kwa dalali wa nyumba aliyekuwa akimuuliza Mama Andrew.

    “Milioni tano,” alijibu Mama Andrew huku uso wake ukionekana kuwa na shida lukuki.

    “Mama embu fanya biashara hiyo milioni tano unauza gari au?” aliuliza yule dalali kwa maneno ya kukejeli.

    “Sasa wewe unataka niiuze kwa shilingi ngapi?” aliuliza Mama Andrew huku akionekana kutoelewa kila kitu kilichokuwa kikiendeleakwa wakati huo.

    “Milioni mbili tu!,” alijibu dalali.

    “Milioni mbili!”

    “Ndiyo kwani ndogo?”

    “Mh! Sawa basi mtafute huyo mteja,” alijibu Mama Andrew.

    Yule dalali aliamua kumtafuta mteja kisha nyumba ikaweza kuuzwa. Alimtafuta mteja ambaye aliweza kuinunua nyumba kwa shilingi milioni tano. Shilingi milioni tatu zikawa ni za kwake kisha hiyo milioni mbili ndizo akaweza kumpa Mama Andrew ambaye naye baada ya kupewa pesa hizo aliamua kumlipa kwa kazi yake nzuri ya udalali aliyokuwa ameifanya.

    Maisha yaliendelea huku ile pesa aliyokuwa ameipata mara baada ya kuuza nyumba alikuwa akiitumia katika kuendelea kumuhudumia mwanaye pale hospitalini huku nyingine akiitumia katika upande wa chakula.

    Alikuwa akilala pale pale hospitalini alipokuwa amelazwa mwanaye, alikuwa akilala chini sakafuni. Baridi pamoja na mbu walikuwa wakimshambulia. Hakutaka kujali lolote lile isipokuwa alichokuwa akikijali kwa wakati huo ni uzima wa mtoto wake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ****

    Baada ya kupita miaka miwili hatimaye Herieth alifanikiwa kumaliza kidato cha sita alipokuwa nchini Uganda kisha akapata bahati ya kwenda kusoma chuo kikuu cha Pretoria kilichopo Afrika Kusini. Alifurahi sana, aliamini ndoto yake ya kuja kuwa bilionea kupitia biashara zilikuwa zinakwenda kutimia, alipokuwa katika chuo hicho alikuwa akisomea masomo ya uchumi “Economic”.

    Doreen na yeye alifaulu vizuri na kupata bahati ya kusoma katika chuo kikuu cha Makerere kilichopo nchini Uganda.

    ****

    Selestine hakutaka tena kuendelea kutumiwa na Mzee Antony katika kufanya biashara haramu, moyo wake ulikuwa katika maumivu makali mno, alitumiwa katika kudhulumu mali za watu, kuua na hata wakati mwingine kutumiwa katika kusafirisha madawa ya kulevya na silaha nchi mbalimbali kama vile Afrika kusini, Burundi, Rwanda, Nigeria na nchi za Uarabuni.

    Hakuipenda kazi hiyo hata kidogo, aliamua kuifanya kutokana na shida alizokuwa nazo, aliamini kwa kufanya hivyo angeweza kuishi maisha mazuri lakini tangu alipoanza kufanya kazi hiyo hakuna chochote alichokipata, alitumiwa kuwa kama chambo huku akiendelea kumuingizia pesa nyingi Mzee Antony.

    Kumbukumbu za Andrew zilianza kumrudia Selestine alipokuwa nyumbani kwa Mzee Antony, hakutaka kuamini kama kweli bado Andrew alikuwa ni mzima kwa wakati huo. Hakuacha pia kumkumbuka Herieth msichana ambaye alisababisha mpaka akampiga Andrew na kumsababishia ugonjwa wa kupooza, ilikuwa ni miaka mitatu imepita.

    Alichoamua kukifanya ni kuanza kumtafuta rafiki yake Derick ambaye alipotezana naye kwa muda mrefu, hakujua ni kwa njia gani ambayo angeweza kumpata, tukio lililomjia kichwani kwa wakati huo ni lile tukio la kuibiwa kila kitu siku ile alipokuwa Ubungo, alipoteza kila kitu mpaka namba zake za simu.

    Aliamua kumuibia pesa Mzee Antony kisha akatoroka na kwenda mkoani Kilimanjaro, hakutaka tena kufanya kazi kwa Mzee huyo katili ambaye kitendo cha kumuua binadamu mwenzake kwake haikuwa tatizo hata kidogo, moyo wake ulikuwa tayari kwa lolote ambalo lingeweza kutokea kwa wakati huo.



    Alipokuwa kwenye gari akili yake haikuwa ikiwaza kitu chochote zaidi ya Andrew, aliwaza mambo mengi sana ila kikubwa alichokuwa akikiwaza ni kuhusu kifo cha Andrew, aliamini kwa vyovyote vile ni lazima Andrew alikuwa amepoteza maisha na pia ile kesi yake ilikuwa tayari imeshasahaulika.

    Hakutaka kuamini kuwa bado alikuwa akiendelea kutafutwa na polisi kwa kesi ya mtu ambaye tayari alikuwa ameshapoteza maisha, kwanza ilikuwa ni miaka mitatu imeshapita. Kuna muda moyo wake ulitawaliwa na furaha hapa ni baada ya kuendelea kuwaza mawazo aliyoyafananisha na ukweli.

    “Atakuwa amekufa,” alijiambia moyoni kisha akatabasamu.

    Baada ya kupita masaa kumi na moja hatimaye alifanikiwa kufika katika mkoa wa Kilimanjaro, moshi mjini, hali ya hewa ilikuwa ni ya ubaridi iliyoambatana na upepo wa wastani.

    Aliposhuka kwenye basi aliamua kwenda hotelini ambapo alipanga kukaa huko kwa muda ili aendelee kufanya uchunguzi wake juu ya Andrew ambaye aliamini kuwa tayari alikuwa ameshakufa. Hakutaka kila mtu afahamu kuwa alikuwa tayari amesharudi.

    **** CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzee Antony alikuwa nyumbani kwake, hakutaka kuamini kwa kile kilichokuwa kimetokea, alikuwa ameibiwa pesa na Selestine kijana ambaye aliamua kumsaidia na kufanya naye kazi za haramu zilizokuwa zikimuingizia pesa nyingi mno, alihisi kuchanganyikiwa mno.

    “No haiwezekani, huyu kijana hawezi kunifanyia ukatili huu,” alijisemea huku akionekana kuchanganyikiwa, hakutaka kuamini kama akaunti zake zote za bank zilikuwa zikisoma sifuri, alikuwa ameibiwa.

    Aliamini hakukuwa na mtu mwingine ambaye angeweza kumfanyia ukatili ule zaidi ya Selestine, aliamini kwa vyovyote vile alihusika katika kumuibia pesa zake. Kitendo cha kutokumuona nyumbani kwake na kujaribu kumpigia simu na kutompata hewani kilimthibitishia kile alichokuwa akikiwaza kwa wakati ule.

    “Huyu bwege leo ananiibia mimi?” alijiuliza kisha tabasamu likashika hatamu katika uso wake, alikuwa akitabasamu huku akilini akiwaza ni kwa namna gani ambavyo angeweza kumuadhibu Selestine.

    Moyo wake ulijawa na hasira kali mno na kila alipokuwa akiendelea kumfikiria Selestine alizidi kupandwa na hasira.

    ****

    Alianza kufanya uchunguzi wake alipokuwa katika hoteli ya Keys. Mtu wa kwanza ambaye aliamua kumtafuta alikuwa ni rafiki yake aliyepotezana kwa muda mrefu. Alimtafuta usiku na mchana, kila kona alihangaika kumtafuta mpaka siku moja akafanikiwa kukutana naye. Kitendo cha kufanikiwa kukutana na rafiki yake kwake alikiona kuwa ni ushindi. Kwa wakati huo Derick alikuwa akisoma katika chuo cha MOSHI CO-OPERATIVE UNIVERSITY (MOCU).

    “Siamini kama nimefaniikiwa kukupata rafiki yangu,” alisema Selestine.

    “Hata mimi siamini aisee yani ukaamua kutokomea kabisa kusikojulikana,” alisema Derick huku akionekana kumshangaa rafiki yake huyo.

    “Hapana nilipata matatizo halafu hata namba yako ya simu nilipoteza,” alisema Selestine huku akionekana kutawaliwa na furaha katika uso wake.

    Kila mazungumzo waliyokuwa wakiyazungumza kwa wakati huo yalionekana kuwafurahisha sana, hawakuacha pia kukumbushiana maisha waliyowahi kuishi wakati ule walipokuwa shuleni, wakabaki wakicheka huku kila mmoja wao akionekana kufurahi kukutana na mwenzake.

    “Hivi vipi kuhusu Herieth unataarifa zake zozote?” aliuliza Selestine.

    “Ndiyo ninazo,” alijibu Derick.

    “Yuko wapi sasa hivi?”

    “Yule demu siyo levo yako tena, sasa hivi yuko Afrika kusini anasoma chuo.”

    “Unasema kweli?”

    “Huo ndiyo ukweli kwani vipi?”

    “Hapana nimemkumbuka sana.”

    “Yule mtoto atakuwa amekuloga yani miaka yote hiyo bado unampenda?’”

    “We acha tu,” alijibu Selestine.

    Selestine hakuacha pia kumuulizia Andrew ambaye aliamini kwa asilimia zote kuwa tayari alikuwa ameshakufa. Jibu alilojibiwa na Derick likamuweka katika mshangao wa hali ya juu.

    “Bado anaendelea kuteseka kitandani yani jamaa ameisha ukimtazama utamuonea huruma,” alisema Derick maneno yaliyomuacha Selestine katika mshangao wa hali ya juu.

    “Nini sasa?” aliuliza Derick mara baada ya kumuona Selestine akibadilika na kukumbwa na mshangao.

    “Unataka kuniambia bado yuko hai?” aliuliza Selestine huku akionekana kuyatoa macho yake.

    “Ndiyo,” alijibu Derick.

    Selestine hakutaka kusikia kuwa Andrew bado alikuwa hai, jibu lile likazidi kumuumiza moyo wake.

    ****

    Maisha ya chuo yalionekana kuwa mazuri sana kwa upande wake alipokuwa Afrika kusini katika chuo kikuu cha Pretoria. Uzuri wake haukuweza kufichika, kila mwanaume aliyemtazama alimtazama kwa macho ya matamanio, aliwavutia wanaume wengi sana alipokuwa chuoni hapo. Hakukuwa na mwanaume ambaye alikutana naye kisha akampita bila kumsifia. Hiyo ilikuwa ni moja kati ya changamoto kubwa ambayo alikuwa akipitia.

    Maisha yaliendelea huku moyoni mwake akiuhisi kuhitaji uwepo wa mwanaume, alitamani sana kuwa na mpenzi kama walivyokuwa marafiki zake ambao kila siku walikuwa wakimshauri kumkubalia mwanaume ambaye alikuwa anakuja kumtongoza.

    Mwanaume ambaye aliamua kumkubalia ombi lake na kuwa wapenzi alijulikana kwa jina la Steven Cole huyu alikuwa ni mzungu ambaye alitokea nchini marekani, alikuwa ni mtoto wa bilionea mkubwa sana wa marekani. Hatimaye wakaufungua ukurasa mpya wa mapenzi huku Herieth akionekana kuyafurahia mno. Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kumsahau Andrew mtu ambaye hakuwahi kutembea naye bali yalibaki kuwa mapenzi aliyoyachukulia kuwa yakufikirika, hakutaka kusikia lolote kuhusu Andrew. Ni kama vile aliamua kukifunga kitabu na kukituka katika bahari yenye kina kirefu, ilikuwa ni ngumu mno kukipata tena.

    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog