Simulizi : Machozi Ya Baraka
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya mazishi na msiba kumalizika Mama Juma alikuwa akienda mara kwa mara kumfariji Mume wa marehemu.Hata kupika Mama Juma ndio aliokuwa akiwapikia kila siku mpaka pale Bahati na Baba yake walipozoea mazingira ya kuishi ndani ya nyumba peke yao kazi zote walizifanya kama kawaida, kiukweli walimkumbuka sana Bi Mwasi kwa msaada wake angali yupo hai alikuwa kazi zote anazifanya mwenyewe leo hii kazi hizo hakuna mwanamke wa kuzifanya. Baraka na Babaye walikuwa wamebaki peke yao hawana budi kazi zote kuzifanya, tena Kipindi hicho Baraka na Juma walikuwa nyumbani kusubiri majibu ya kuingia kidato cha pili.
Siku ya Jumatatu majira ya Jioni Baraka akiwa anarudi kutoka nyumbani kwa Rafiki yake Juma njiani alikutana na wanaume wawili wakiwa kwenye pikipiki.Wakati akiendelea na safari yake ,aliwaona wakisimamisha pikipiki yao kandokando ya barabara na mmoja wapo akashuka,Bahati alishtuka Ghafla na kuanza kutetemeka,kijasho chembamba kutililika katika paji lake la uso,akaona sasa mwisho wake umefika. Wakati akiwa katika taharuki wazo likamjia akaona hasilaze damu akachangamka ,haraka haraka akakimbia na kuingia moja kwa moja kwenya Bar iliyo jirani na kijia kile alichokuwa akipita na kujichanganya kwenye meza ya watu waliokuwa hawana hili wala lile wapo tu wakiendelea kuburudika na vinywaji mbalimbali.Baraka aliangaza huku na kule wakati akiwa ndani ya Bar hiyo,mawazo yake labda anaweza kuwaona tena watu hao lakini haikuwa hivyo hakuwaona wala kuwasikia tena, waliokuwa kwenye pikipiki.Alikaa hapo kwa muda kisha akaendelea na safari yake kupitia barabara kuu katu hakuitamani kupitia tena njia hile wala kukatiza kichochoro kingine. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya muda Baraka alifika nyumbani na kumkuta Baba yake akiwa mtu mwenye mawazo tele, alimsalimia na akamsimulia alivyowaona watu hao, Bwana Ahmed alimpa pole na kumtaka kuwa makini na watu mbalimbali kwani wengi wao sio watu wema kwake, pia alimwambia ikiwezekana atokapo shuleni au sehemu yoyote akirejea nyumbani hasiwe peke yake amsubili Juma au mtu mwingine anayemfahamu. Baada ya wiki moja kupita matokea kidato cha pili yalitoka,ilikuwa habari njema wanafunzi wengi walifanya vizuri mitihani yao na kufanikiwa kwa asilimia kubwa kuendelea kidato cha tatu.Baraka na Juma walifurahi sana kutokana na wastani waliopata katika mitihani hiyo,wiki mbili baadae shule zikafunguliwa wanafunzi wakaendelea na masomo kama kawaida.
Wiki hiyo ilikuwa na ahadi kutoka kwa Baba yake Juma kuja Tanzania kuwasalimu, Mzee kimenya ni mfanya kazi katika shirika la kijamii, lenye makazi yake Makadara jijini Nairobi, muda mwingi Bwana Kimenya upendelea kuitembelea familia yake jijini Dar es Salaam.Bwana Kimenya alikuwa na shauku kubwa kutaka kuwaona mke na mtoto wake, siku nyingi zilipita bila kuonana nao, siku zote Bwana Kimenya upendelea kuwasalimu kwa njia ya simu, uongea na mkewe pamoja na mtoto wake. Kilichomkosesha furaha wakati huo kutaka kujua familia yake inaendeleaje kutokana na simu kutopatikana.
**********
Ndege ya shirika la ndege la Kenya Airlines ilizidi kuyakata mawingi ikitokea Jijini Nairobi kuelekea nchini Tanzania.Katika kiti cha nyuma kabisa ndani ya ndege hiyo alikuwa amekaa Bwana Kimenya akionekana mwenye mawazo,alikuwa akielekea Dar es Salaam kuwasalimia familia yake aliyokuwa hajaitembelea kwa kipindi kirefu.Ndani ya ndege hiyo hakuwa na papala hata kidogo,zaidi ya kuendelea kuburudika na mziki uliokuwa ukimliwaza vya kutosha huku akiwaza kwa namna gani ataweza kumwamisha mtoto wake.Baada ya muda Sauti ya mhudumu wa kike wa ndege hiyo ilisikika kwa lugha kadhaa,ikiwapa taarifa abiria waliokuwa wakiitimisha safari yao katika uwanja wa ndege Mwalimu Nyerere(JNIA) pia ikiwakumbusha abiria wote kufunga mikanda.
Baada ya tangazo hilo kusikika,haukupita muda mrefu ambapo ndege hiyo kubwa ya kisasa,iliweza kuinama kwa mbele na baadaye matairi yake madogo yaligusa ardhi na kuanza kuserereka kwa kasi na kisha kusimama kando ya jengo kubwa uwanjani hapo.Abiria wote waliteremka,akiwemo Bwana Kimenya alitoka moja kwa moja mpaka nje ya uwanja huo.Mara moja akafanya utaratibu wa kupata usafiri ,uliomfikisha mpaka nyumbani kwake Buguruni.Mkewe alipomuona akamkimbilia kwa furaha wakakumbatiana,kisha akamsaidia mizigo mumewe na kuingiza ndani .Wakati huo Juma hakuwepo alikuwa amekwenda kujisomea kwa kina Bahati,aliporudi tu alimkuta Babaye ameshafika kutoka safari alimrukia kwa furaha kisha wakasalimiana.Baba yake alifurahi sana kumuona mwanae akiwa katika maendeleo mazuri,alimshukuru mkewe kwa malezi mema muda wa chakula cha usiku ulifika ambapo Mzee Kimenya akajumuika pamoja na familia yake mezani.
Siku hiyo ilikuwa ni siku ya majadiliano kati ya Juma na Baba yake kuhusu kuendelea na masomo yake.Bwana Kimenya alimtaka mwanae aende kusomea nchini Kenya anapofanyia kazi.Lakini Juma akakataa alitaka kusomea Tanzania kama ikishindikana Basi aende huko akiwa na rafikiye Bahati ambaye ni Albino. Baba yake alikataa mtoto wake kuongozana na mtu mwingine hasije akashawishika na watoto wenye tabia chafu, lakini Bi.Mwasi alimsihii mumewe na kuanza kumsimulia historia ya Bahati na maisha aliyopitia mtoto huyo Albino mwenye ulemavu.Bwana Kimenya alijikuta akipata simanzi nzito kutokana na simulizi hiyo, aliona dhahiri Juma na mamaye wanavyomdhamini na kumjali mtoto huyo, alijikuta akikubali na kuunga mkono familia yake kumsaidia mtoto Bahati.Aliwageukia Mke na Mtoto wake na kuwambia “sawa nimekubaliana na ninyi maana napenda wakati wote niwaone katika furaha hivyo basi napenda kuwajulisha kuwa Juma nimemtafutia shule ya kusoma kabisa inayoitwa St.Patrick iliyopo jiji Nairobi,ndipo atakapokwenda kusoma na huyo mwenzake. Bwana Kimenya anaipenda Sana familia yake Kama angeweza kuihamisha familia yake basi angekuwa tayari ameshaihamisha ila kutokana na kazi zake jinsi zinavyokwenda ilishindikana akaamua kuiacha tu nyumbani Tanzania.......
Wiki iliyofuata Bwana kimenya aliongozana na familia yake kwenda nyumbani kwa Bwana Ahmed.Siku hiyo Juma aliona hawafiki haraka kwa furaha aliyokuwa nayo, alitamani aluke ili kuonana na Rafiki yake Baraka kumwambia Furaha hiyo.Hata Baba yake alipokuwa akimwangalia Juma alionekana kuwa na furaha ya wazi juu ya kwenda kusoma nchini Kenya katika shule ya Upili St.Patrick iliyopo katika maeneo ya Makadara jijini Nairobi.Baada ya mwendo uliochukua kama dakika kumi na tano,walifika nyumbani kwa Bwana Ahmed,walimkuta Baraka akiwepo ameketi pekee ,aliwakaribisha huku akiwa na mawazo tele,aliwaza na kuwazua juu ya ugeni huo.Aliwaza kama ni mwema hama washari kutokana na ile sura ngeni kwake, alimwangalia mara mbilimbili Bwana Kimenya alimuona alivyokuwa amefanana kabisa na Rafikiye Juma, akasikia sauti kichwani ikimwambia hasiwe na wasi wasi.Aliwaangalia nyuso zao akaona kila mmoja akiwa kwenye tabasamu muda huo huo Juma aliinuka na kwenda kukaa karibu kabisa na kiti alichokaa Baraka kisha nao walikaribia na kuketi vitini.Baraka kwa adabu aliwasalimia nao kwa unyenyekevu waliitikia na kumuulizia alipo Babaye CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tumekuja kumwona Baba yako sijui kama tumemkuta?”
“Baba yupo ndani amelala, ametoka kazini muda huu”Baraka alijibu
“Kuna jambo muhimu sana tunataka kuzungumza nae”Bwana Kimenya alimwambia
“Sawa basi ngoja nikamwamshe!”Baraka alisema
“Sawa itakuwa vizuri maana mazungumzo yenyewe yanakuhusu wewe, hivyo basi tukaona usiwe peke yako ni muhimu kuwa na mzazi wako”Mama Juma aliongeza
“Sawa ngoja niende”
Baraka aliinuka kutoka kitini na kuelekea kilipo chumba cha Baba yake.Wakati akielekea katika chumba hicho kichwani mwake alikuwa mtu wa mawazo tele, alijiuliza mambo mengi akiwa na shauku ya kutaka kujua kitu gani kinachomuhusu yeye.Aliwaza wanaweza kumchukua na kumsaidia au wanataka kumdanganya baba yake ili wampate kiraisi na kumpeleka kusikojulikana,lakini hajajua kama watu hao wana nia mbaya kwake.Alipofika Mlangoni mwa chumba hicho aligonga baada ya muda mlango wa chumba hicho ukafunguliwa kisha alimwangalia Baba yake na kumwambia kuwa na ugeni nyumbani kwao ,hivyo wanahitaji kumuona.Bwana Ahmed alipata mashaka juu ya ugeni huo,waliangaliana na mwanae kisha akamwambia atangulie yeye atafuata,Baraka alirejea sebuleni kwa hofu.
Muda si mrefu Bwana Ahmed aliwasili kutoka chumbani kujumuika pamoja na wageni sebuleni, alipofika pale alishangaa kumuona Bwana Kimenya.alifurahi sana kwani kipindi cha nyuma kabla Bwana Kimenya hajahamishwa kikazi kwenda Kenya, walikuwa marafiki walioshibana kwa kila kitu.Pale alipoondoka Ndio ikawa tatizo mawasiliano yao yakawa kwa shida, muda mwingi Bwana Kimenya alikuwa alizunguka huku na huko kufanya kazi katika shirika hilo ndio maana hikakosekana muda kuwatembelea na kuwasalimu ndugu na jamaa nyumbani Tanzania.Bwana Kimenya nae alipomuona Bwana Ahmed alisimama na kumpa mkono kisha wakakumbatiana kwa furaha,Bwana Kimenya alimpa pole ya kufiwa na mkewe kuwa yote mipango ya Mungu.Baraka alishangaa kumuona Baba yake akimchangamkia ikionesha akijuana na mgeni huyo ambaye yeye hakuwai kumuona wala kumtambua atokako.
”Bwana Kimenya wanasemaje huku Kenya, vipi kazi zako zinaendaje? Maana muda mrefu ndugu yangu tumepoteana, karibu sana”Bwana Ahmed kumuuliza maswali mfululizo
“Salama kabisa ndugu yangu sijui wewe hapa nyumbani?”
“Nzuri tuambie unatunyima nini huko? Mbwana Ahmed aliuliza
“Hakuna cha maana huko zaidi ya kazi tu”Bwa Kimenya alijibu kwa mzaa
“Naona umetukumbuka sasa”Bwana Ahmed alimwambia
“Yaani nikaamua kuja kukuona kabisa kabla sijaondoka, maana safari wiki hii”
“Aisee! Sie tupo ndugu yangu”
“Pole Sana na matatizo ya msiba “Bwana Kimenya alitoa pole
“Ahsante bwana najua yote mipango ya mungu”
“Ni kweli kabisa, nilikuwa sifahamu Kama mna mtoto mwingine, ndio Mke wangu ameniambia”Bwana Kimenya alisema
“Ni kweli kabisa tumepata mtoto mwingine sasa ni baba anayesoma kidato cha tatu shule moja na Juma”
“Aisee hongera Bwana”
Baraka ndio akapata kuyasikia vema maneno hayo kisha akapata muda wa kuyalingalinisha na maswali yaliyokuwa ndani ya kichwa chake.Akawaza na kuwazua yaliyokuwepo akilini mwake akapata jibu la moja kwa moja kwamba “Kama huyu Bwana kimenya anatokea Kenya, kuna siku ambayo Juma aliwai kuniambia kuwa Baba yake ukaa Kenya mbali na Familia yake na amekuja nyumbani akiwa ameongozana na Juma pamoja na mama yake, ina maana Mzee Kimenya atakuwa Baba Mzazi wa Juma”.Baba yake Juma ni mfanyakazi mzuri katika shirika la kiserikali linalojiusisha na Elimu kwa watoto na haki zao za msingi (Unicelf).
Ndio maana Juma upendelea kuja shuleni na kiasi kikubwa cha pesa elfu mbili au elfu Tatu ya matumizi kwa kila siku, wanafunzi wengi upendalea kuwa rafiki wa Juma kwa ajiri ya kutumia pesa pamoja.Lakini kamwe Juma hakushughulika nao,wala kuwapa nafasi zaidi ya kumpenda na kumdhamini sana Baraka kama ndugu yake wa tumbo moja.
Wakati huo Bwana Ahmed na Bwana Kimenya wakiongea maongezi ya hapa na pale, Juma alimgeukia Baraka na kumfahamisha kwa sauti ya taratibu kwa Bwana kimenya kuwa ni Baba yake mzazi aliyemzaa na Baraka alifurahi kufahamishwa kisha akamwambia “Rafiki yangu kumbe wazazi wetu walikuwa marafiki wa siku nyingi naona hata sisi tumefuata mkumbo wao, maana Bendera ufuata upepo”Juma alifurahi sana kumuona Rafikiye kusema maneno hayo alimkumbatia kwa furaha huku wazazi wao wakiwaangalia.Marafiki hao wakiwa katika furahaJuma alisikika akisema CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Samahani kina Baba vipi kuhusu mazungumzo, mliyokuwa mnataka kuzungumza maana naona maongezi yamebadilika”Juma alisema huku akiwa na shauku ya kutaka kujua Baraka alipokea vipi suala hilo.
“Sawa sawa kabisa kijana, una mawazo mazuri wewe”Bwana Ahmed alisema
“Kabisa! Ngoja sasa nianze mazungumzo yaliyonileta”Bwana Kimenya aliongea
“Haya sasa kazi kwako mie yangu masikio tu kukusikiliza “Juma alimjibu baba yake
“Bwana Ahmed Nia na Madhumuni ya kutuleta hapa ni kwamba, Mke na Mtoto wangu ndio furaha yangu kwa sasa kama unatambua, wanaitaji faraja yangu pia wao ndio walionishika mkono mpaka kufika hapa nyumbani kwako,”Bwana Kimenya aliongea
“Naam! Bwana endelea ninakusikiliza”Bwana Ahmed alisema
“Nimekuja kwa mara nyingine tena nyumbani, safari hii nataka nimchukulie uwamisho mwanangu Juma”Kimenya aliongea kisha akakooa
“Ooooh! Ni vizuri sana Rafiki yangu”Bwana Ahmed alimpongeza kwa uwamuzi huo
“Nashukuru, ila naomba ukubaliane na mie kwa jambo hili ninalokwambia”Bwana Kimenya alizidi kumtia wasi wasi
“Juma anapenda kuongozana na rafikiye Baraka kwenda Kusoma Nchini Kenya maana amekataa katakata kwenda peke yake, anadai akiwa na mwenzake hivyo atafurahi zaidi basi anaomba akubaliwe waende kusoma pamoja”Bwana Ahmed alisema
“Heeee! Juma anataka kwenda kusomea Kenya na Baraka?....
“Ina maana mmejiandaa kila kitu kwa safari? Maana Mimi kwa sasa sina uwezo wa kumgharamia masomo ya huko”Bwana Ahmed aliuliza
“Tumejiandaa vya kutosha ndio maana leo mapema hii tumekuja utupe jibu ili Baraka nae aweze kwenda kubadilisha mwelekeo wa masomo yake, na kuhusu gharama nitaghamia kila kitu mpaka mwisho wa masomo yake“Bwana Kimenya aliongeza
“Nashukuru sana ndugu yangu kwa moyo wa kujitolea, pia nimekubaliana nanyi ili Baraka akaendelee na masomo yake Kenya ila nitamjulisha mwalimu Njaidi ambaye aliyekuwa akimlipia ada ya shuleni”Bwana Ahmed alisema
“Sawa lakini ngoja tumsikilize nae Baraka maneno yake kuhusiana na Safari hiyo”Bwana Kimenya alimgeukia Baraka kisha akamwambia
“Baraka Mwanagu, nadhani umetusikia ili jambo tunaloongea na Baba yako kuhusu kwenda kusomea Nchini Kenya, je upo tayari? Bwana Kimenya alimwuliza
“Ndio nipo tayari kuongozana na Juma kwenda kusoma”Baraka alijibu kwa unyenyekevu
“Sawa kuanzia sasa mavazi, maradhi,na chakula ni juu yangu mpaka pale utakapojiweza kuwa na maisha yako”Bwana Kimenya aliendelea
“Nashukuru sana mume wangu kwa moyo wa kujitolea kumsaidia mtoto huyu“Mama Juma alidakia
“Naomba kitu kimoja ,muwe makini na Baraka maana yeye ni Albino ni mlemavu wa ngozi, akaendelee na masomo yake ya sekondari sio tatizo ila awe katika uangalizi mzuri kutokana na hali yake, hasije akanyanyasika tena mwanangu”Bwana Ahmed alisema
Juma na Baraka walikumbatiana kwa furaha na upendo wa hali ya juu,kisha kwa pamoja wakapeana mikono wakiwa na wazazi wao wakaona sasa ni ndugu walioshibana.Bwana Ahmed alifurahi sana kuona Mwanae Baraka akiwa mwenye furaha akaona ndoto za mwanae zitafika pazuri. Kwenda Kenya kwenye nchi yenye uchumi kibiashara,akaona sasa Muda wa malengo sasa unatimia.Baada ya kukaa pale kwa saa kadha wa kadha ,Bwana Kimenya na Mama Juma waliagana na Bwana Ahmed na kutoka nje , wakaongoza njia kurudi nyumbani huku wakiw a na furaha tele moyoni.
Ilikuwa siku ya jumatatu majira ya mchana Bwana Ahmed na Bwana Kimenya waliongozana mpaka makao makuu ili kufuatilia kibali cha Kuhamia na kuwaamisha watoto hao Kenya.Bwana Kimenya alikuwa na wakati mgumu kuwashawishi wahudumu wanaousiana na mambo hayo ya Passiport,mwisho wake alifanikiwa kumpata mdada mmoja anayejulikana kama Mwanaisha ilimsaidia kwa kiasi kikubwa kukamilisha taratibu zote zinazoitajika.Siku hiyo ndio ilikuwa na mjadala mkubwa kuhusu barua kutoka shule ya sekondari Kibasila walipokuwa wanasoma na kupeleka Shule ya Upili St.Patrick iliyopo makadala jijini Nairobi Nchini Kenya.
Mnamo tarehe tisa mwezi wa kumi na mbili majira ya saa moja Asubuhi,Baraka,Juma na Mzee Kimenya walikuwa uwanja wa ndege wakiagana na Mama Juma na Bwana Ahmed.Baraka alilia sana wala hakuamini kama kweli anakwenda nchi nyingine mpaka pale alipokuja kutulizwa na mama Juma na kumtaka kuwa na amani ,aweze kusoma vizuri huko aendako ili kutimiza ndoto zake.Bwana Ahmed nae aliwahasa Baraka na Juma kuwa na Bidii katika kazi na masomo yao ili waweze kuendana nawanafunzi wa shule waendayo.Muda wa saa mbili ulipofika abiria wote wanaokwenda safari waliambiwa kuwa tayari katika safari hiyo ili kila mmoja awe karibu kabisa na mwenzake.Baraka na Juma walifurahi sana kisha waliongozana kuelekea katika eneo la ndege hizo.Siku hiyo walikuta ndege kutoka shirika la ndege la Emiliate,walipanda ndege hiyo na kuingia ndani kisha kila mmoja akakaa kwenye sehemu yake.
Baada ya muda abiria wote walikuwa yameshaingia katika ndege hiyo tangazo likasikika na kutakiwa kila mmoja afunge mkanda ndege tayari kwa kupaa.Baraka aliangaika kufunga mkanda, Juma alimuona Rafikiye akiwa katika wakati mgumu alimsogelea na kumfunga mkanda,punde ndege ikaanza kupaa kuelekea nchini Kenya.Muda wote ndani ya ndege hiyo kulikuwa nae kimya cha ajabu tena hakuna hata mtu aliyekuwa tayari kuzungumza na mwenzake Baraka alikuwa amelala foofoo yaani hakuwa na habari.Masaa yalipita dakika na sekunde zikapotea na hatimaye siku ikaanza kukatika taratibu ilipofikia majira ya saa kumu na moja za jioni waliwasili jijini Nairobi.Ndege ilipotua watu wote walishuka kisha Bwana Kimenya akawaongoza watoto wake kuelekea kwenye gari tayari kwa kuanza safari nyingine ya kuelekea nyumbani anapoishi.Siku hiyo ilikuwa ya furaha kwao maana gari lilivyokuwa likikatiza barabarani,Baraka na Juma walijisikia fahari macho yao kuwa wazi kuliangalia na kulichunguza uzuri wa jiji la Nairobi,walifurahi sana wakajiona wapo ulaya kwa uzuri wa mji huo, hakika jiji la Nairobi lilikuwa likiwaka na kuvutia.
Walifika katika mtaa wa Eastland wakashuka kwenye tax Bwana Kimenya aliilipia kisha kuwaongoza kuelekea nyuma iliyopo upande wa pili wa barabarani na Bwana Kimenya akatoa ufunguo uliokuwa kwenye mkoba wake na kufungua mlango mkubwa wa nyumba hiyo, Mlango ulifunguka nao wakaingia ndani kumfuata...
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walipofika sebuleni walikaa kwenye viti vilivyopo sebuleni pale na kisha walikaribishwa na mziki mnene uliokuwa umewashwa na Bwana Kimenya baada ya kuingia ili kuwapunguzia uchovu wa safari watoto wake.
Baada ya muda walikuwa wameshakula na kunywa kwani Bwana Kimenya alikuwa na vywakula vyake ndani, alivyovinunua Suparmarket kabla ya kuondoka Tanzania, aliviweka kwenye friji kubwa lililokuwepo sebuleni hapo.Hivyo alivyofika hawakupata shida kutafuta chakula, walipasha moto kisha wakala.
Muda wa kulala ulipofika Bwana Kimenya akawaongoza watoto wake mpaka katika chumba maalum kwa ajiri ya wageni, kabla hajalala aliwaambia kwamba kesho ndio siku ya kwenda kulipoti shuleni kama alivyokuwa ameambiwa na rafiki yake,ambaye ndio mkuu wa shule hiyo ya Upili St.Patrick.Bahati na Juma walilala mnono huku wakiwa na mawazo kuhusu siku hiyo waendapo shule mpya.Asubuhi na mapesa kulipokucha Bwana Ahmed aliwaamsha watoto wake ili wajiandae tayari kwa siku ya kuanza masomo,waliamka na kujiswafi haraka haraka na kuvaa nguo zao tayari kwa kwenda .Bwana Kimenya nae alikuwa tayari akiwasubili walipomaliza mara moja alifunga milango ya nyumba yake vizuri,na safari ya kuelekea shuleni Maeneo ya makadara ilipoanza.Baaada ya muda mfupi walikuwa nje ya shule ya Upili St.Patrick,walipokelewa na dada mmoja wa makamu na kuwaelekeza ilipo ofisi ya mkuu wa shule hiyo iliyokuwa gorofa ya tatu ndani ya jengo hilo. Kimenya alimshukuru Yule dada na alikwenda moja kwa moja alipoelekezwa,walipanda ngazi na watoto wake mpaka juu ya gorofa ya tatu na kumkuta mwenyeji wao mkuu wa shule akiwasubili.Alipomuona tu Bwana Kimenya walisalimiana kisha akamkabidhi makalatasi ambayo ni lipoti maalum kwa ajiri ya uwamisho kutoka shule ya Kibasila waliyokuwa wakisoma watoto wake.Bwana Kimenya akatia saini yake katika makalatasi hayo kisha Juma na Baraka katika shule hiyo ya upili wakiwa kidato cha tatu sasa,walipoingia tu katika darasa hilo tofauti na walivyotarajia wanafunzi walisimama kwa heshima na kumsalimia mkuu wao shule,kisha wakawasalimu wanafunzi wale wageni,Juma na Baraka walikuwa kwenye mshangao wasijue la kuwajibu.
Mzee Kimenya alikuwa kwenye kicheko kikubwa kilichowashtusha Watoto wake kwa pamoja walimwangalia baba yao kwa aibu kisha wakawapungia mikono, darasa zima likalipuka kwa furaha ya ajabu.Juma na Baraka walizidi kushangaa kuwaona wanafunzi hao walikuwa wachache mno, ndani ya darasa walikaa kila mtu na meza yake kama vile wapo kwenye mitihani,walitenganishwa kwa umbali mkubwa sana.Mkuu wa shule aliwataka Juma na Bahati kwenda kukaa kwenye viti ambavyo vililetwa pamoja na meza zake na wanafunzi wawili waliokuwa wameagizwa.Walivileta na kuvipanga sehemu zilizokuwa na uwazi, Juma na Baraka walikwenda kukaa kila mtu na sehemu yake,walijiona ukiwa kukaa mbalimbali maana siku zote walikuwa wamezoea kuwa karibu kama pua na mdomo.
Sasa hapo walikuwa wameachana umbali mkubwa kiasi kwamba waliona taabu ila hawakuwa na jinsi walitulia tuli kila mtu na sehemu yake kusubili kuanza masomo shuleni hapo.Bwana Kimenya alipoona watoto wake wameshapelekwa darasani aliagana nao na kuwataka kuzifuata taratibu za shuleni hapo.Kama kuna jambo ambalo litawasumbua basi wamfuate na kumuuliza mkuu wa shule atawaeleza na kuwajuza kinachotakiwa,aliwaahidi atakuwa kila mwishoni mwa wiki kuja kuwatembelea na kuwaletea mahitaji muhimu nao walikubaliana na baba yao,waliagana na kuwatakia masomo mema kisha akaondoka kuelekea kazini kwake kuripoti.Baraka na Juma waliendelea na masomo katika shule hiyo ya Upili St.Patrick iliyopo maeneo ya makandara jijini Nairobi, kwa furaha na amani tele walijifunza mambo mengi kwa vitendo,wakawa wajuzi wa kila taaluma iliyopo shuleni hapo na nje ya shule.
Bwana kimenya kila mwishoni mwa wiki hupenda kuwatembelea na kuwaletea vitu mbali mbali au huwachukua na kuwatembeza Jiji la Nairobi nzima na kuwanunulia vitu wavipendavyo kisha huwarudisha shuleni.Bahati alikuwa mtu mwenye furaha sana alimshukuru mungu kwa kumpatia mtu wa kumsaidia aliona sasa maisha yake watabadilika na kuwa nafuu kwa ulemavu ,aliokuwa kuwa Albino mwenye ulemavu wa ngozi kumbe siyo sababu ya kuwafanya kushindwa kupata maendeleo mazuri.Muda wote tangu kuanza masomo katika shule hiyo Juma alikuwa haishi kuwa na furaha alionekana wazi kumpenda Baraka alikuwa nae bega kwa bega katu hakuthubutu kumtenga,huo ndiyo ulikuwa urafiki wa kweli kati yake na Rafiki yake kipenzi Baraka.Baada ya miaka miwili kupita Baraka na Juma walihitimisha masomo yao ya kidato cha nne katika shule ya upili St.Patrick.Walipokuwa wamemaliza mitihani yao baada ya wiki moja mbele Bwana Kimenya aliwakatia tiketi na kuwasafirisha kurudi nyumbani Tanzania....
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku ya Jumapili majira ya Asubuhi na mapema waliamka na kujiandaa kwa safari,walikuwa tayari kwa kila kitu huku wakifarijika kwa pamoja kumaliza elimu ya kidato cha nne na sasa wanarudi nyumbani kupumzika.Baada ya kusubili kwa muda Bwana Kimenya alifika shuleni na kuwachukua kisha wakaongozana moja kwa moja mpaka uwanja wa ndege Kenyata.Bwana Kimenya alifanya utaratibu wa usafiri mpaka saa nne asubuhi alikuwa ameshakamilisha kila kitu tayari wakaingia ndani ya ndege na safari ya Tanzania ikaanza.Taratibu ndege ikaanza kuacha ardhi ya kenyata na kupaa angani,ndani ya ndege hiyo walikuwa wamekaa abiria wengi wakiwemo Baraka,Juma na Bwana Kimenya.Ndege ilichanja mawingu angani na kupambana na mvua zilizokuwa zikinyesha kwa taabu.Rubani aliendelea kuendesha kwa ustadi mkubwa ndege hiyo mpaka pale ilipokaa sawa na safari ikaendelea.
*******
Siku zilipita hatimaye miezi ikapotea na miaka miwili ikafikia wakiwa kidato cha sita.Kipindi hicho wakajiunga katika shule ya Kenyatta High School Mwatate,tulipobobea katika masomo ya hisabati,kemia na fizikia.Walisoma shuleni hapo kwa utulivu sana tofauti na kipindi tukiwa shule ya upili pale St.Patrick, hakika ilikuwa raha sana kwa Baraka pale anapoingia mwalimu wa somo la Kiswahili,darasani wote walikaa kimya kumsikiliza Mwalimu tofauti na walivyokuwa upili hakukuwa na masikilizano kati ya mwanafunzi na mwalimu hata pale mwalimu anapofundisha wanafunzi waliendelea kuonyesha ubabe wa hali ya juu.Kuna mwanafunzi mmoja anayeitwa Namsoke,yeye ni mtundu sana darasani hasa kipindi Mwalimu anapotoka darasani upenda kuwatania wenzake bila sababu lakini wengi walishamzoea kwa mambo yake anayoyafanya.
Hata hivyo siku moja wakiwa darasani alikuja mwalimu akiwa anasanifu Kiswahili kwa lafudhi ya Kenya yenye mvuto wa aina yake.Mwalimu huyo aliitwa Mwasongwe akawa anapendeza na kuvutia pale umsikilizapo akiongea na semi na nahau na methali.Mara nyingi uwasomea kwa sauti mashairi ya diwani ya Abdilatif Abdalla ya sauti ya Dhiki.Nilipenda sana Kiswahili japokuwa hatukuwa katika kitengo hiki ila Mwalimu Mwasongwe alijiibia na kutupa ufahamu juu ya umuhimu wa lugha ya Kiswahili. Baraka na Juma hawakuwa wanaelewa undani wa mashairi aliyokuwa anagani waliona kama wanapiga kelele. Lakini mdundo na beti pamoja na mpangilio wa sauti ulikuwa wa aina yake na kunifanya kupendezwa na lugha ya Kiswahili na zaidi walifuatilia katika vitabu mbalimbali pale wapatapo nafasi ya kuingia maktaba ya shuleni hapo.Juma alibaini ilo lakini hakunifuatilia maana yeye hakuwa mpenzi wa lugha yao ya Tanzania.
Mwaka 2006, wakafanikiwa kuufanya mtihani wa kidato cha sita wakaushinda kwa point nyingi tena vizuri sana na kufanikiwa kuingia chuo Kikuu cha Nairobi Mwaka 2007. Kilichopo katika mji wa Nairobi, Kenya, ndicho chuo kikuu cha umma cha pili kwa ukubwa nchini Kenya (baada ya Chuo Kikuu cha Nairobi). Chuo Kikuu cha Kenyatta kimo katika eneo la Kahawa, umbali wa kilomita 20 (maili 12) kutoka mji wa Nairobi, katika barabara kuu ya kuelekea mji wa Thika.Juma yeye hakufanikiwa kufaulu kwa chuo cha Seriakali ,Hasingeweza kuitwa shule yoyote ya serikali .Kwa mara nyingine tena Baba yake Mzee Kimenya akamsaidia kwa matokeo yake,Juma hakuwa na kinyongo moyoni mwake alijionea fahari mafanikio yake mpaka pale alipofikia japokuwa alikuwa na safari ndefu mbele yake.Si jambo dogo kwa mtu aliyekuwa kakokota nanga darasani na kukatiwa tama kuibuka nambari sita katika shule nzima .CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mzee Kimenya alijipa kazi na majukumu ya kumtafutia mtoto wake nafasi katika vyuo kadha wa kadha.Akaandamana na Juma na Baraka toka chuo hii hadi ile.Jinsi walivyoenda kuulizia Chuo Kikuu cha Moi ni chuo kikuu mjini Eldoret, magharibi mwa Kenya. Ni mojawapo wa taasisi saba za elimu ya juu za kitaifa, hiki kilikuwa Chuo cha umaarufu mkubwa.Walipoingia getini Mzee Kimenya alimuhacha nje na kuingia ofisini kuongea chemba na Mkuu wa chuo hiki, baada ya muda alitoka ndani, akawaeleza kwa utulivu watoto wake kwamba wamemkataa,alama zake zilikuwa chini kwa maoni ya Mkuu wa chuo.Wakati huo waliangaika kwa udi na uvumba kumtafutia Juma chuo cha Utabibu lakini ilishindikana.Bwana Kimenya ndipo alipoamua kushikilia msimo wake na kuwasiliana na Mama yake nchini Tanzania ili amtafutie chuo Juma kwani Kenya imeshindikana kutokana na alama zake alizopata.Baada ya wiki kupita Mama yake Juma alipiga simu kwa Mumewe na kumtaarifu kama amefanikiwa kupata chuo cha uuguzi muhimbili kilichopo jijini Dar es Salaam,Juma alifurahi sana pale Mzee Kimenya alipowaambia habari hizo za Juma kufanikiwa kupata chuo kwa ajiri ya kukamilisha ndoto zake kuwa daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto.
Siku mbili tatu zikapita Bwana Kimenya alikuwa akimshughulikia mtoto wake kwa ajiri ya safari ya kurudi Tanzania ili kuanza chuo cha udaktari muhimbili.Baraka alikuwa mtu mwenye mawazo sana hasa kipindi ambacho Juma alitakiwa kuondoka,muda wote Baraka alionekana wazi ukosefu wa amani hata pale Bwana Kimenya alipomuona na kufuata kuzungumza nae lakini Baraka hakudhubutu kusema neno zaidi ya kuuzunika na kupiga moyo konde.Juma alimsihi sana Baraka kuwa na amani kwani yote ni mipango kutoka kwa mwenyezi mungu lakini Baraka hakuelewa aliona kabisa Juma anamkimbia ili abaki peke yake nchini Kenya,
“Baraka Mwanangu nakuomba sana uwe na amani tele moyoni mwako”
“Lakini Baba kwani hapa Kenya hakuna chuo cha kuweza kusoma Juma kwa alama zake alizopata”
“Baraka Mwanangu, nimeangaika usiku na mchana jua ketekete likiwaka utosini kunichoma sikufanikiwa kupata chuo kinachokidhi mahitaji kwa alama alizopata Juma”Mzee Kimenya alijibu
“Kenya nzima jamani kweli Baba au umeamua tu kumrudisha nyumbani Juma”Baraka alidakia
“Hapana ndugu yangu unavyofikilia wewe ni tofauti kabisa najua yote sababu ya uchungu kutengana”Juma alimwambia
“Ni kweli lakini hapa vyuo vipo vingi sana tofauti na Tanzania, mpeleke tu nina imani atapokelewa”Baraka alisema
“Bahati naomba unisikilize nimetembea na kuangaika vyuo karibia vyote wamekataa ufaulu wake ni mdogo mno”
“Sawa haina tatizo nimekuelewa mzee wangu”Baraka alijibu kwa shingo upande
“Hapa msimamo utabaki pale pale kwamba Juma atakwenda kusoma chuo cha udaktari Muhimbili”.....
Ukweli ulijitosheleza kwa Bwana Kimenya kushikilia msimamo wake ni kwamba Juma atakwenda kukaa na kuendelea na masomo yake Tanzania.Baraka hakupendezwa na uwamuzi huo waliochukua Juma na Baba yake. Hakuelewakuelewa kitu gani kilichomfanya Juma kukataa kubaki Kenya kuendelea na masomo yake chuoni.Baraka aliamini Juma anauwezo wa kumshawishi Baba yake amtafutie chuo Kenya ili kuendelea na masomo yake,kama alivyowashawishi wamchukue na yeye ili kwenda kusoma wote Kenya leo hii Juma analilia kurudi Tanzania tena peke yake na Mwenzake Baraka kumuacha Kenya hapo ilikuwa sio bure kuna tatizo tena kubwa sana.Kipindi kifupi kikapita na Juma kuandariwa tayari kwa safari ya kuelekea Tanzania ikawadia.Baraka aliwasindikiza mpaka uwanja wa ndege wa Keny,Juma na baba yake walikuwa tayari ndani ya ndege hiyo,walifunga mikanda pale waliposikia mhudumu ndani ya ndege hiyo akiwataka kuwa tayari kwa safari.
Baadae ya siku mbili tangia Juma na Baba yake kusafiri nchini Tanzania na kumuacha Baraka akiendelea na masomo yake.Wiki moja ikatimia bwana Kimenya akarejea Kenya kuendelea na kazi zake kama kawaida.Baraka alifanikiwa kusoma hadi akahitimu shahada ya uzamifu katika hisabati.Alisoma tena na kuongeza mwaka mwingine tena na tena mpaka Mwaka wa tatu ukawadia chuo kumalizia.Alisoma kwa amani na upendo japokuwa hakufahamu alipofikia kielimu huko chuo cha Muhimbili , alipokwenda kusoma rafiki yake wa ubani Juma, maana mpaka kipindi cha miaka mitatu hakuwa na mawasiliano nae zaidi ya bwana Kimenya pekee.Siku zilipita miezi ikateketea miaka miwili sasa Baraka akaendelea na masoma na kuongeza maarifa na ujuzi juu yake.Likizo ilifika alitakiwa kufanya field.Akaenda katika kampuni moja ambayo huko alifanya kwa ustadi mkubwa sana mpaka viongozi wa kampuni hiyo walimpenda.Hata muda wake ulipokwisha walimtaka hasiondoke ,aendelee kufanya kazi hapo hapo, lakini haikuwezekana chuo kilipofunguliwa alirejea chuoni kuendelea na masomo kwenye chuo cha Ohio state. Hapo alisomo kkwa muda wa miaka miwili na baada ya hapo akatunukiwa shahada ya PhD kwenye chuo hicho, baada ya hapo akafanikiwa kupata kazi katika shirika la udhamirifu Kenya.Baraka alikuwa na furaha kipindi chote hicho alikuwa karibu kabisa na Baba yake aliendelea kuwasiliana nae kwa kipindi kirefu.Mwaka ulipotimia Baraka alikuwa hana furaha kipindi chote alikuwa mtu mwenye mawazo kuhusu kurudi nyumbani Tanzania.Baada ya kuona hakuna ndugu hata mmoja zaidi aliyekuwa akimsaidia,hacha kusaidiwa hata kuwa na mtu wa karibu kusema wametoka wote Tanzania hakuna.Kwani kipindi hicho, Bwana Kimenya alikuwa ameahamishwa na kupelekwa kufanya kazi katika kambi ya wakimbizi Somalia.Baraka alikuwa peke yake Juma na Baba yake hawakuwepo kabisa katika nchi hiyo.
Siku hiyo Bwana kimenya alipoondoka Baraka aliona dhahiri kwamba hapa bado hajaamua la kufanya watu waliomleta na kumsaidia sasa walikuwa wamemuahacha na kumtupia nchini ya watu.Maana kuondoka kwa watu anaowategemea katika nchi ya Kenya ilikuwa tatizo kubwa kwake, kutokana na ulemavu aliokuwa nao hivyo usalama wake ukawa mdogo.Ingawa alikuwa na watu wengi anaofahamiana nao lakini aliona itakuwa tatizo kama ataendelea kubaki peke yake.Japokuwa alikuwa mtu mzima sasa lakini aliona lazima afanye utaratibu ili kurejea nchini kwake Tanzania .Akaamua naye kujichukulia maamuzi magumu kurudi nyumbani Tanzania.Japokuwa Bwana Kimenya alikuwa mbali na Baraka alimuomba alishughulikie kuwasiliana na uongozi wa Kenya ili kupata utaratibu wa kurejea Tanzania.Japokuwa Baraka alikuwa amewekeza nyumbani ,magari na biashara mbalimbali lakini katu haikumzuia kutorudi Tanzani,alifanya kila njia na kwa hali na mali kujitolea ili kuviacha vitu vyake Kenya na kurudi Tanzania na vitu ambavyo vinahamishika kama magari na vifaa vya nyumbani.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kweli Bwana Kimenya aliendelea kuwasiliana na uongozi huo mpaka pale Baraka alipofanikiwa kwa kiasi kikubwa kusafiri na kurudi Tanzania.Siku ya safari iliwadia Baraka alipanda ndege mpaka Tanzania na alifika Uwanja wa ndege na kuwakuta Baba yake Mzee Ahmed,Mama yake Juma na Juma kwa pamoja wakiwa wanamsubili.Baraka alipowaona aligutuka kwa furaha akawakimbilia na kuwakumbatia kwa amani huku akionekana kufurahi zaidi kukutana familia yake.Juma alimsogelea Baraka na kukumbatiana kwa furaha kisha wakapongezana kwa hatua waliyofikia,kisha Baraka akatoka maungoni mwa Juma na kumkumbatia Mama yake Juma huku machozi yakimtoka akamshukuru kwa upendo wake kumuwezesha kwenda kusoma na hatimaye kufika elimu ya juu na sasa amemaliza kilichobaki ni kufanya kazi tu.
Mama Juma alifurahi sana tena akamkumbatia kisha akamwambia “Yote ni maisha mwanangu naamini hizi ni Baraka zako kutoka kwa muumba alitaka ufike huko ulipofika hongera sana Baraka ubarikiwe pia”.Siku mbili zikapita tangia Baraka kufika Tanzania akapata wazo kuzunguka huku na kule kutafuta kazi za kufanya maana sikuweza kukaa tu nyumbani bila kuwa na kibarua cha kufanya.Aliudhunika japo hakuwa na jinsi.Siku moja akiwa nimejiraza ndani simu yake ikaita, Haraka akaipokea na kuiweka sikioni ili kumsikiliza anayeongea upande wa pili, ndipo alipopata uhakika kwa kile alichokuwa akizungumza na mtu huyo.
“Hallow, habari?
“Salama kabisa sijui kwako?
“Salama nadhani naongea na Baraka Ahmed?”
“Yes! Ndio mimi nakusikiliza”
“Naitwa Marijani hapa kutoka kampuni ya St.Peter ya kimara baruti”
“Naam! Nakuelewa
“Kesho naomba ufike ofisini bila kukosa”simu ilisikika
“Sawa ila sijajua wito wa unahusiana na nini?”
“Ni jambo lenye kheri ndani yake ndugu yangu
“Kuna Barua kutoka kwa mkuu wa shule ili kuweza kuzisoma na kuelewa unatakiwa kufika ofisini bila kukosa”
“Nashukuru sana kwa jambo ilo na nimekuelewa nitafika bila kukosa hapo kesho asubuhi na mapema”
“Sawa haina tatizo karibu sana”
“Ahsante”Simu ikakatika.............
Siku hiyo ilikuwa na furaha sana pale Baraka alipofanikiwa kupata fursa ya kuitwa kufanya kazi na kuajiliwa kwenye kampuni mmoja inayojiusisha na masuala ya Biashara na Uchumi.Ilikuwa ni kampuni nzuri sana kwa kusikia tu Baraka aliweza kuitambua pale alipoanza kufanya kazi na kampuni hiyo. Akiwa kama meneja mkuu tawi la Dar es salaam.Katika kampuni hiyo ndio ninapoendelea mpaka sasa kufanya kazi na kuwaongoza wafanyakazi kama uzoefu wake ulivyo. Mpaka sasa hakuna mfanyakazi hata mmoja aliyetokea kumnyanyapaa wala kumdharau kwa ulemavu wake wa ngozi.Baraka siku zote alionekana mtu mwenye furaha tele katika maisha yake, aliendelea kufanya kazi katika kampuni hiyo huku akiwa amepanga nyumba nzima na kuishi pamoja na Baba yake.
Dada yakeTausi akiwa na Mwanae ambaye alimpata baada ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na dereva wa bodaboda mjini Songea huko kwa shangazi alipokuwa akisomea kipindi cha nyuma. Tausi alivyochukuliwa na Shangazi yake alikwenda kusoma mjini songea baada ya kufika kule alikuwa na wakati mgumu kutokana na shule aliyokuwa akisoma kuwa mbali na kitu kilichomfanya kujiingiza kwenye mahusiano na madereva ambaye alikuwa na mazoea nae pale alipokuwa akipanda katika pikipiki yake.
Madereva hao walifanikiwa kumshawishi mpaka akaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na mmoja wa madereva hao.Ikafikia kipindi akawa harudi nyumbani mpaka shangazi yake umtafuta bila mafanikio,mpaka siku mbili au tatu ndio Tausi urejea nyumbani,akiulizwa ulikuwa wapi anajimbu jeuri,mwishowe shangazi alichoka akaamua kumuacha afanye anavyotaka.Wala Tausi hakufanikiwa kumaliza shule aliishia kidato cha tano akapata mimba ya kwanza,shangazi yake hakuwa na namna ya kumsaidia aliamua kuwaeleza wazazi wake nao walikuwa na wakati mgumu kwa mtoto wao kubadilika wakaamua kumwita huyo dereva wa boda boda aliyempa mimba na wakakubaliana kuwa Tausi eande kuishi kwa mwanaume huyo na kuilea mimba hiyo. Tausi alikuwa na wakati mgumu sana kuona ya kwamba shule hawezi kwenda tena alijilaumu ila hakuwa na jinsi alianza maisha kwa mwanaume huyo.Baada ya kuishi kwa miaka miwili baadae alipata mimba ya pili ugonvi ukaanzia hapo, walikuwa hawaelewani na mwanaume huyo.Akirudi amelewa umpiga Tausi na tumbo lake wala hakujali kama alikuwa mjamzito yeye aliendelea kumtesa na kumsababishia maumivu makali lakini tausi katu hakuondoka wala kupiga kelele alivumilia sababu alimpenda sana mwanaume huyo. Dereva huyo akamkimbia na Tausi akarejea kwa baba yake akiwa na kichanga mkononi.Tausi alirudi kwa baba yake mtu mwenye mawazo tele, hakuna aliyejua kitu gani kilimpata Tausi maana muda mwingi alionekana kuwa mtu mwenye mawazo licha ya Kaka yake Baraka kuwa na uwezo kifedha lakini kwake haikuwa kitu.Kama uwezo kifedha wanao na kujenga kaka yake ameshaanza kujenga na mfanyakazi mzuri na miradi mingi wameshawekeza.
Ila mambo hayakuwa hivyo binafsi siku moja baada ya kupata chakula cha jioni Baraka aliamua kuvunja ukimya na kumwambia dada yake awaeleze ukweli kile kilichokuwa kimemsibu lakini Tausi akamjibu “Hamna lolote ni mambo ya kawaida tu kaka angu si unajua maisha ya wanaume wa sasa walivyo full stress”Kabla Tausi ajamalizia kusema baba yake Bwana Ahmed aliamua kumtolea uvivu mtoto wake na kumtaka aseme ukweli uenda wakamsaidia.Lakini Tausi hakudhubutu kusema ukweli kwani alikuwa muoga sana kwa baba yake kwa baba yake ilikuwa kama mkuki alichomoka na kumvaa mtoto wake na kumpa kofi moja zito lililomfanya Tausi kuanguka chini na kuanza kulia. “Nisamehe Baba yote haya niliyataka mwenyewe kwani kipindi nikiwa na yule mwanaume alinitesa na kuninyanyasa sana ikafikia kipindi aliniletea wanaume ndani nikawa sielewi hatma yangu,japo nilimoenda sana ila sikuwa na namna nikafungasha kila kilicho changu nikaondoka na kwenda kwa shangazi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tausi alisema huku akiendelea kulia,Baada ya kufika kwa shangazi nilimueleza tatizo lilinikabili bila kutegemea Shangazi hakukubaliana nami alinifukuza nyumbani kwake na kunipa nauli ili nirudi Dar es Salaam.Kesho yake ndio nikapanda kwenye basi na kurudi huku nyumbani mpaka sasa sielewi kitu gani kilichokuwa kinamsumbua yule mwanaume.Naomba msamaha wako Baba pamoja na kaka Baraka nilijiingiza kwenye matatizo bila mwenyewe kujijua.Baba yake alimsamehe kwa kila kitu alimwambia hasiwe na wasiwasi kwani maisha ndivyo yalivyo.Baraka alimfuata dada yake na kumkumbatia kisha akamtaka hasiwe na mashaka juu ya hilo pale ameshafika na ndipo nyumbani kwake ataishi nae kwa shida na raha,atakapojifunga atampeleka chuo cha veta ili kusomea fani anayoipenda,Tausi alifurahi sana na kumshukuru kaka yake kwa pamoja Tausi,Baraka na Bwana Ahmed walisimama na kukumbatiana kwa furaha na upendo.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment