Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

UPENDO WANGU - 5

 







    Simulizi : Upendo Wangu

    Sehemu Ya Tano (5)





    "Mi nafikiri tumpeleke tu morogoro kwa mama yake,litakalotokea tutajua yupo mikononi mwa mama yake" yohana alishauri

    "Sawa basi fanya hivyo,maana mimi sijai kufika huko"

    " sawa,sasa unachotakiwa saa tano usiku,wewe umlete semeni kituoni mimi mtanikuta pale nawasubili kisha nitampakia semeni kwenye gari litakalokuja nalo kisha tunaondoka"yonaha alisema kwa kirefuCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sawa nimekuele"sauti ya upande wa pili ilisikika kisha simu ikakatwa.

    Yohana alichanganyikiwa kupita maelezo,akajikuta nguvu zikimuishia,akaamua sikusitisha safari ya kazini,alichofanya kwa wakati huo kugeuza nyuma na kuanza safari ya kurudi alipotoka.

    Amina alikuwa mtu mwenye mashaka juu ya alichokifanya kumtorosha dada yake sawa na kujitafutia matatizo yeye,alichokiwaza kwa wakati huo kumpigia simu jeni amuandae dada yake kwa safari ya kurudi morogoro kwa mama yake,Jane alifanya kama alivyoagizwa na amina. Akamfuata semeni mle chumbani kisha akamueleza jinsi alivyoambiwa na amina. Semeni alifurahi kusikia hivyo,furaha yake ilizidi alipomkumbuka mama yake kipenzi,pia kuonana na yohana kipenzi cha moyo wake,hakika semeni alijisika furaha sana mawazo yote aliyokuwa nayo yaliyeyuka kwa furaha ile iliyopitiliza.

    Ilipotimia saa nne na nusu za usiku, amina alikuwa akitoka chumbani kwake,kuelekea kwenye kolido,alipofika katika mlango mkubwa wa kutokea nje alimuona mlinzi yupo getini akiwa na bastora yake aina ya SMG mkononi,amina aliogopa kutoka,alikaa pale mlangoni kama dakika tano akimuangalia mlinzi labda atanyanyuka ila apate upenyo wa kutoroka lakini wapi mlinzi akuinuka kabisa alikaa pale pale,baada ya muda kidogo akamuona mlinzi akielekea maliwatoni,hapo sasa amina akajiandaa kutoka,alipoona mlinzi amezama chooni alichofanya amina alishika viatu vyake mkononi kisha akanyata na kufanikiwa kutoka nje,alimkuta bodaboda akimsubili kwani alikuwa amempigia simu muda mrefu amfuate,amina alijipakia kisha safari ya kuelekea kwa janet ikaanza.

    Ilikuwa saa 12:45 za usiku yohana akiwa kituoni akiwasubuli,baada ya nusu saa tangu yohana kufika pale,sasa aliona gari aina ya Noah lenye namba za usajiri 333 TBC,likiingia kituoni pale na kupaki pembeni kabisa na alipopaki yeye,yohana akiwa pale macho yake na akili yake yote ilikuwa katika gari ile,sasa akiwa makini zaidi alimuona msichana mrefu mwembamba akishuka upande wa dereva kisha akazunguka upande wa nyuma akafungua mlango kisha wakashuka wasichana wawili,yohana akazidi kukaza macho kuangalia pale mlangoni Mara aliwaona wale wasichana wawili walioshuka nyuma na yule aliyetoka upande wa dereva wakija upande alipokaa yeye,moyo ukamuenda kasi,akatamani kushuka ndani ya gari lakini alijipa moyo labda wanapita na safari zao lakini haikuwa hivyo sasa aliwaona wapo jirani kabisa na alipo yeye tena wanakuja upande ule wa dereva alipokaa akaona sasa kazi hipo akajiweka vizuri ili kama ni majambazi akabiliane nao.yohana akiwa na hofu pale ndani ya gari gafra aliona wanatizamana na wale mabinti watatu,yohana akuamini macho yake akaisi anaota maana mpango uliompeleka pale hakuwa nao kichwani kwa wakati hule aliokuwa amechanganyikiwa,mawazo yote yakawa kwa wale wasichana watatu kama sio jambazi basi watakuwa madada poa au wajikanao kama changudoa.

    " habari yako yohana?"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Saa...laa..ma" yohana alijibu kwa hofu uku akiisi kijasho kumtoka

    "Heee hehee! Yohana mbona muoga sana wewe"janet alisema uku akicheka

    "Hatuna muda wa kipoteza,tunaitaji safari ya huyu mwenzetu hapa" amina alisema bila yahana kumtambua

    "Mimi kuna watu nawasubili mperekeni tax ya hapo mbele" yohana alijibu

    " sisi ndio unaotusubili tumefika sasa tunaomba umpereke dada!"

    Moyo wa yohana ukapiga paah! Hakuamini masikio yake akaisi akili yake ikifanya kazi fasta,mawazo yakamjia akaisi kuchanganyikiwa,kisha akawauliza

    "Nyie kina amina au ?

    "Haah heeeh !" Amina akamcheka yohana

    "Ndio sisi na mimi hapa ni semeni"semeni alisema uku akiitoa kofia aina ya kapero kichwani mwake hapo yohana alipomuona ameivua ile kofia, amina nae akafanya hivyo huku akiwa hoi kwa kicheko,hapo sasa yohana akaamini kumbe ndio wao akamwambia semeni aingie garini waondoke. Semeni akajipakia kwenye gari, amina na Jane nao wakarudi katika gari waliyokuja nayo nao kisha wakapanda na kuondoka.

    Kesho yake majira ya asubuhi,amina akiwa bado amejiraza kitandani,gafla simu yake ikawa inaita amina kaipokea

    "Hallow"

    "Mambo vipi amina?"

    "Safi,nambie yohana mmefika salama?"amina aliseme

    "Yes! Nashukuru tumefika salama!"

    "Nimefurahi kusikia hivyo,msalimie sana Dada angu" amina alisema kisha akakata simu

    Wakati amina akiongea na yohana,mama yake alikuwa anafanya usafi kwenye kolido hivyo alimsikia kila kitu amina alivyokuwa anaongea.mama yake amina alichukua simu yake na kumpigia mumewe bahati nzuri au mbaya mzee rashidi hakuwa hewani,akakumbuka kumbe siku hiyo mzee alikuwa na kikao cha dharura akaamua kumuacha mpaka atakaporudi, kisha akaendelea na kazi zake..........



    Siku hiyo mzee rashidi alichelewa kurudi nyumbani,alifika saa kumi jioni alimkuta mkewe akimsubiri kwa hamu kubwa,alipomuona mkewe kwenye hali hiyo akaona sio kawaida yake,mzee rashid alimsogerea kisha akamuuliza ana tatizo gani mpaka akawa kwenye hali hiyo,mama amina hakusita akamsimulia kila kitu mumewe jinsi alivyomsikia binti yake akiongea na yohana.mzee rashidi alikasilika akapata wazo kumtaarifu mzee muba. akaifuata simu ya mezani iliyokuwa jirani yake,na kupiga namba kadhaa kisha kuiweka sikioni,simu upande Wa pili ukasikika

    "Nambie nini kimetokea?" mzee muba aliuliza

    "Semeni ametoroshwa jana usiku kuelekea morogoro kwa mama yake!"

    " heee! Mbwana itakuwaje sasa?

    "Inatakiwa tumfuate huko moro,anaweza akaondoka na huko?

    " basi mi najiandaa nitakuja na manase twende wote"mzee muba alimwambia

    " sawa fanye haraka mimi nitawasubiri kuongozane wote"

    " sawa itakuwa vizuri,sababu mwenzetu unapajua"

    "Tutaulizia tukifika moro,tutapata muelekeo" mzee rashid alisema

    "Sawa ngoja nijiandae"

    "Sawa sawa!"mzee rashid akajibu.

    ***********

    Ilikuwa saa 6:00 asubihi, yohana na semeni walifanikiwa kufika salama,walimkuta mama semeni hayupo,walikaa nje ya nyumba bila wasi wasi, wakimsubili mwenyeji wao. Baada ya saa moja kupita mama semeni alirejea huku mkononi akiwa ameshika jembo,akiashiria ametokea shamba.semeni alipomuona mama yake alimkimbilia kisha wakakumbatiana kwa furaha.mama semeni alishangaa kwa ujio ule wa gafra,ikiwa asubuhi kama ile kuna nini uko,au baba yake kamfukuza maswali yote alijiuliza mama semeni kichwani mwake,akaamua kumsogerea yohana na kisha kumuuliza kilichotokea mpaka asubuhi ile wawe pale.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Yohana nini kimetokea baba?"mama semeni aliuliza

    "Ni story ndefu kidogo mama"yohana alimwambia

    "Niambie baba,kitu gani kimetokea"?

    "Mapenzi mama,nampenda sana semeni ila mzee anataka aolewe na mtu mwingine.

    "Unasemaje?kwa hiyo ulimfuata mwanangu aende kuolewa?"mama semeni alisema kwa hasira

    "Ndio mama nilitumwa na mzee"yohana alijitetea

    "Hata kama kwanini hukunijulisha"mama semeni alizidi kumuandama yohana

    "Nisamehe mama angu,nampenda sana binti yako"

    " mama naomba umdamehe sio kosa lake yohana"amina aliingilia kati

    " sawa acha yapite baba,nimekusamehe karibu tena nyumbani"

    "Asante mama.yohana alijibu akiwa na furaha ndani ya moyo wake.

    "Ondoa shaka,ninawabariki katika maamuzi yenu,

    Semeni alimshika mkono yohana,wakaingia ndani uku kila mmoja akiwa na furaha.

    Baada ya muda semeni alitoka nje na kisha yohana akafata kila mmoja akiwa na tabasamu pana,walipotoka wakakuta mama semeni akiandaa chai ,semeni alimkaribisha kisha wakajumuika pamoja kupata kifungua kinywa,walipomaliza kunywa chai wakawa wanaongea mambo mbalimbali,uku yohana akiwa amelala miguu mwa semeni,mikono na vidole vya semeni vikitarii katika love garden ya yohana iliyokuwa na vichilizi vya majani makavu yaliyokuwa kifuani mwake.

    Baada ya muda wakiwa wamekaa pale nje mama semeni aliwaaga anakwenda kutafuta mboga kwa ajiri ya chakula cha mchana,kabla mama semeni hajafika mbali, aliona magari mawili yakija kwa kasi ya ajabu na kupaki nyumbani kwake,wakatoka vijana wawili na wazee wa makamo wawili,hakuamini macho yake alipomuona mzee rashid,kati ya wazee wale wawili. Mama semeni akiwa anaendelea kuwaangali aliwaona vijana wale wawili wakimtoka na kumvuta yohana kisha wakaanza kumpiga,kati ya vijana wale mmoja alikuwa manase ambaye ndie anayetaka kumuoa semeni ila mama semeni hakumtambua,kuona vile akaakimbilia kutoa taarifa polisi.

    Yohana wakati anaendelea kupigwa na vijana wale wenye vifua vipana,mzee muba alimnyanyua semeni pale chini kisha akamsukuma kwa baba yake semeni akaangikia miguuni mwa baba yake,mzee rashid akaanza kumpiga vibao semeni,kitendo kile kilimuumiza sana yohana akajitutumua pale chini kisha akainuka kuanza kupigana na vijana wale wawili. Yohana alijitaidi kupigana nao kadri ya uwezo wake na kutumia nguvu zake zote,kuwakabiri vilivyo wale vijana.mzee muba alipoona hivyo,aliona kipande cha mti jirani yake akakichukua na kumpiga yohana shingoni,yohana akaanguka chini kama mzigo,wale vijana wakaendelea kumshambulia yohana pale chini akiwa ajitambui kwa kupoteza fahamu huku damu zikiendelea kumtoka puani.

    Mara polisi wakafika wakiwa na mama semeni,bila kuchelewa vijana wale wawili wakawa chini ya ulinzi,mzee rashidi alipowaona askari akamwachia semeni aliyekuwa amemshikilia,semeni alipoona ameachiwa na baba yake alimkimbilia yohana aliyekuwa pale chini wakati huo akiwa amerejewa na fahamu zake ,alimshika kisha kumsaidia kunyanyuka,wakati huo mama semeni akiwa amechanganyikiwa ajui cha kufanya.wakiwa katika taaruki, manase aliyekuwa ameshikiriwa na askari gafra alimsukuma yule askari aliyemshika kisha akachomoa bastora yake iliyokuwa koti lake akaelekeza Kule aliposimama yohana na semeni akiwa tayari kwa kuachia risasi,mama semeni aliona kitendo kile alikimbilia yeye akakaa mbele ya wawili hao,hatimaye manase akaachia risasi iliyokuja moja kwa moja begani mwake na kuanguka chini.askari walipoona hivyo nao wakazitoa siraha zao na kuzikoki tayari kwa mapambano,walipokuwa wanarushiana risasi na watu wale,ikaja risasi iliyompata manase kifuani mwake iliyotokea upande wa pili na kutokea kwenye koti alilokuwa amevaa,maskini manase alianguka chini kama mzigo na kukata roho pale pale.lilikuwa pigo kubwa kwa mzee muba alimkimbilia mwanae pale chini,akaanza kumwamsha bila mafanikio mzee muba akaanza kulia,kilio cha uchungu kumpoteza mwanae mpenz ilikuwa mtihani kwake.semeni nae alimkimbilia mama yake,hakika ilikuwa Siku ya vilio semeni alilia kama mtoto alimnyanyua mama yake kisha kumbusu wala hakujali kuchafuka kwa damu zile zinaendelea kumtoka mama yake.

    Askari walipona hali imetulia,wakawachukua mzee rashid wakamfunga pingu,wakamgeukia mzee muba aliyekuwa bado anaendelea kumlilia mwanae,wakawapakia watuhumiwa wote kwenye gari kisha kuichukua ile maiti nayo waingiingiza kwenye gari na safari ya kuelekea kituoni ikaanza.......





    Yohana alimbeba mama semeni akamuingiza kwenye gari, siti ya nyuma akamtaka semeni kukaa na mama, semeni alifanya hivyo huku akilia kisha safari ya kuelekea hospitali ikaaanza.baada ya mwendo Wa haraka,waliwasili hospitali kilosa,wauguzi walimpokea mgonjwa Mara moja mama semeni akaanza kupatiwa matibabu.

    Mzee rashid na wenzake waliwekwa mahabusu katika gereza la kihonda mjini morogoro,baadae kesi yao ikaendelea na kuamishiwa mjini arusha kwa uchunguzi zaidi.baada ya miezi sita walipandishwa kizimbani katika mahakama ya mwanzo mjini arusha,hakimu aliwasomea washtakiwa makosa yanayowakabili kuuza na kusambaza madawa ya kulevya na kudhuru, kushambulia mwili ,hatimaye siku ya hukumu ikafika mzee rashidi na mzee muba wakaukumiwa miaka miaka kumi jera na faili ya shilingi milioni 20.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa ni Siku ya furaha kubwa sana,siku ambayo nderemo na vifijo zilisikika kila kona ya mtaa Wa matombo hakika ni siku isiyosahaulika yohana alikuwa kanisani akifunga ndoa na mpenzi wake semeni,yohana alifurahi sana kumpata mke ampenda,sasa yohana alikuwa mume halali wa semeni,siku hiyo ndoa ilifungwa kanisani kisha sherehe ilifanyika nyumbani kwa mama semeni,watu walikula na kunywa,amina pia siku hiyo alikuwepo kwa ajiri ya kumpa kampani dada yake kipenzi,baada ya muda kuisha maharusi waliondoka kuelekea kwenye fungate,iliyotayarishwa kwa muda wa wiki moja,amina nae akalejea mjini arusha.

    Baada ya mwaka mmoja semeni akashika ujauzito kisha akajifungua mtoto wa kike aliyempa jina upendo,mtoto huyo akaleta furaha ndani ya familia yao,hasa mama semeni muda mwingi alikuwa akicheza na kufurahi na mjukuu wake kipenzi.furaha yao ilikuwa ya ushindi kwa yohana kumpata semeni ,pia yeye aliona kawaida kuishi maisha ya kijijini.Siku moja yohana na mke wake semeni,wakiwa wamekaa chumbani kwao yohana alimwambia mkewe, leo ninaishi kijijini sikufikiria kama haya yote yatatokea lakini kwa sababu ya upendo wangu kwako ninafurahia maisha,nakupenda na nitaendelea kukupenda sana mke wangu yohana alisema kisha akamkumbatia mkewe.



    Na hapo ndipo MWISHO wa hadithi hii ya UPENDO WANGU, Napenda kukushukuru mpenzi mfuatiliaji wa hadithi hii pia kukukaribisha tena kuendelea kufuatilia hadithi nyingine zinazofuata, usisite kutoa maoni na ushauri.....



    ********.ASANTE SANA*********



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog