Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

SITOISAHAU MBEYA - 2

 





    Simulizi : Sitoisahau Mbeya

    Sehemu Ya Pili (2)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Uwoga wangu wa kukaa pamoja na Evelyne, sasa ulikaribisha urafiki wa dhati kati ya Richard na Evelyne. Richard na Evelyne wakawa wanaelewana sana. Ukaribu ambao niliufurahia sana, kwa kuwa nilijua siku za karibuni tu, Richard atamwita Evelyne



    shemeji yake. Nakumbuka ilikuwa siku ya alhamisi jioni. Kulikuwa na mechi ya mpira wa miguu pale shuleni kwetu, kati ya shule yetu na shule ya Sekondari Pandahill. Kwa bahati mbaya mimi sikuwa mchezaji wa mpira, ingawa niliupenda sana kuutazama mchezo huo. Nilipanga siku hiyo nd'o iwe siku ya kumueleza ukweli Evelyne Gando. Nimueleze ukweli kwamba nilikuwa nampenda.





    Nakumbuka tulikaa pembeni ya uwanja tukiwa

    watatu, mimi, Richard Chali na Evelyne Gando.

    Nilikuwa natamani Richard Chali atoke ili nipasue jipu! Nimueleze Evelyne Gando juu ya hisia zangu zilizojificha moyoni. Hisia nzuri toka kwangu kwenda kwa Evelyne Gando. Kila sekunde nilikuwa namuomba Mungu ili Richard Chali atoke tubaki wawili ili nimueleze Evelyne Gando hisia zangu. Bahati Ilikuwa mbaya kwangu, Richard Chali hakutoka hata kidogo, nilisikitika sana kimoyomoyo.



    Mpira uliisha, matokeo yalikuwa tumewafunga shule ya Pandahili magoli mawili kwa moja. Tulirejea nyumbani Pamoja na Richard huku tukimwacha Evelyne akirejea katika hosteli ya wasichana alikokuwa anaishi. Iliniuma sana siku ile, maana nilijipanga vizuri sana siku ile kumueleza ukweli Evelyne, lakini nilishindwa.

    Usiku wa siku ile sikulala kabisa!



    Nikifumba macho tu nilikuwa namuona Evelyne Gando akiwa amesimama mbele yangu. Nikifumbua macho na kuangalia ukuta, picha ya kuvutia ya Evelyne Gando ilikuwa inajichora pale ukutani. Ukweli mapenzi yangu kwa Evelyne yalinitesa sana. Nilimpenda Evelyne pasi na kifano.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku ile sikulala lakini asubuhi niliamka. Nilijiandaa na kwenda shule. Nilikuwa na furaha sana kwenda shule, kwakuwa nilikuwa naenda kukutana na Evelyne Gando, maana kumuona tu Evelyne nilikuwa naridhika, mwanamke aliyeziteka hisia zangu haraka sana!



    Muda wa kuingia darasani ulipofika, tuliingia darasani nikiwa na Richard Chali. Baada ya kukaa tu kwenye dawati moyo wangu ulikuwa unadunda vibaya sana. Moyo ulikumbuka kitu, haukuwa umemuona mwanamke unayempenda. Na ilikuwa hivyo, hadi mwalimu wa historia anaingia Evelyne hakuwepo darasani. Mwalimu alikuwa anafundisha lakini sikumuelewa hata kidogo. Mwalimu alivyotoka darasani, na mimi nilikuwa nyuma yake, ndio nilitoka nje. Nilianza kurandaranda katika viunga vya shule

    kumtafuta Evelyne, Evelyne Gando mwanamke

    aliyetokea kuziteka hisia zangu. Na kuzipeleka

    atakavyo.



    Nilitafuta katika madarasa mengine, stoo, maofisini kwa walimu mpaka chooni lakini Evelyne Gando sikumuona! Mwishowe nikaamua kwenda kumwangalia Evelyne katika hosteli ya wasichana. Nilihisi labda Evelyne Gando alikuwa anaumwa. Hivyo niliamua kwenda kutafuta hukohuko hosteli kwao! Ngoja nikwambie kitu ...Nilikuwa naenda mahali ambako wanaume hatukuruhusiwa hata kukaribia. Hosteli za kike ilikuwa ni MARUFUKU kwa sisi wanaume kutia pua zetu.

    Mimi sijui niliutoa wapi ujasiri, nilipania siyo tu kusogelea eneo hatari la hosteli bali kuingia hadi ndani. Nilikuwa kama chizi, yaani nilikuwa nafanya kitendo hatari zaidi kufanywa pale shuleni. Kukutwa katika *bweni la wasichana adhabu yake ilikuwa ni kufukuzwa shule!

    Ilikuwa hakuna mjadala.

    Ndio Mkuu wa shule hakuwa na masihara kabisa na kosa hilo. kwa maana hiyo kila hatua niliyokuwa napiga kuelekea katika hosteli ya wasichana, ilimaanisha napiga hatua ili nifukuzwe shule. Kila nilivyokuwa nasogelea hosteli ile ya wasichana nd'o nilikuwa nasogelea kufukuzwa shule!

    Ilikuwa ni hatari sana lakini sikuhofia hata kidogo. Nilifika katika nyumba kubwa yenye vyumba vingi ikiyoitwa hosteli pale shuleni. Ilikuwa nyumba kubwa yenye vyumba vingi sana, nilishindwa kuelewa kipi ni chumba sahihi cha Evelyne Gando. Nilienda katika



    mlango wa chumba cha kwanza, nilikuta kufuli kubwa aina ya solex inaning'inia pale mlangoni, ishara tosha kwamba hakukuwa na mtu ndani ya chumba. Atakuwa vipi mtu ndani ya chumba ilhali mlango ulikuwa umefungwa kwa nje. Niliangalia milango ya vyumba saba vyote havikuwa na mtu. Niliamini hamna watu kwa kuona ishara ileile, ya kufuli mlangoni. Sasa nilikuwa naelekea katika chumba cha nane, nilikuta mlango ukiwa hauna kufuli!

    Ishara kwamba kulikuwa na mtu ndani, au labda iwe amesahau kuufunga. Nilisukuma mlango ule taratibu lakini kwa nguvu kidogo.

    Nilichokutana nacho, nilistuka sana!

    Nilikuwa natazamana na watu wawili ambao sikuwa natamani kuonana nao kabisa wakati ule. Naam, nilikuwa natazamana na Matron wa hosteli ya wasichana pamoja na mkuu wa shule!



    Niliganda pale katika mlango wa hosteli kama sanamu la Michelin. Ghafla nikatoka kwenye usanamu nikarudi katika ubinadamu. Nilipata mstuko mkubwa sana! Mapigo yangu ya moyo yalipiga kwa nguvu mara mbili, Pa..Pa! Pigo la tatu la moyo wangu hata mwenyewe sikulisikia. Nilikuwa nimezimia!



    Sielewi nini kilitokea baada ya hapo, lakini nakiri kuwa siku ile baada ya kuamka ndio niligundua kwamba nilikuwa nampenda sana Evelyne Gando, lakini pia



    niligundua kuwa nilikuwa namuogopa sana mkuu wa shule ya Sekondari Sangu, Mwalimu Bukuku.



    Niliamka toka huko nilikokuwa nimezimia saa nne asubuhi. Nilianguka katika mlango wa hosteli ya wasichana Sangu, niliamka katika hospitali ya mkoa wa Mbeya. Nani alinipeleka? Sikuwa najua. Saa nne asubuhi! Inamaana niliondoka duniani takribani saa nne. Naam, nilizimia saa moja asubuhi, nilizinduka saa nne asubuhi. Nilifumbua macho taratibu nikiwa nimelala kitandani, kwa mbali nilimuona mtu aliyekuwa kasimama pembeni ya kitanda changu nilichokuwa nimelala pale kitandani, nilimtambua vizuri sana mtu huyo, alikuwa anaitwa Evelyne, Evelyne Gando. Baada ya kumuona msichana ninayempenda zaidi hapa duniani. Nilifumbua macho kwa haraka zaidi, kasi tofauti na niliyoanza nayo katika kufungua macho yangu, nia ni kumuona Evelyne Gando.

    Nilimuona!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikutana na Evelyne akiwa analia, nilimuangalia kwa umakini, kuanzia chini, nilipofika katika mkono wake wa kulia macho yangu yaliganda, Evelyne Gando alikuwa na bahasha ya kaki katika mkono huo. Baada ya kuiona bahasha ile niligundua kwanini Evelyne alikuwa analia. Lakini sikujari kabisa. Niliushika mkono wake wa kushoto na kuuvuta taratibu ili



    nimketishe kitandani, nilifanikiwa, Evelyne alikaa. Baada ya Evelyne Gando kukaa kitandani, huku mimi nikiwa nimelala. Sasa nilitafuta neno sahihi la kutamka kwa wakati ule, ndani ya dakika sita sikulipata neno lolote la maana! Nilichoweza kufanya ni kumwangalia tu Evelyne Gando, bado alikuwa anaendelea kulia. Bila kutegemea, nami nilianza kulia. Sikuwa najua Evelyne Gando alikuwa analia nini, wala sikuwa najua mimi mwenyewe nilikuwa nalia nini, labda nililia kwakuwa Evelyne Gando alikuwa analia!



    Huku akiwa analia Evelyne Gando alinipa ile barua aliyokuwa kaishika kwa mkono wake wa kuume, nami bila ajizi nikaipokea, nikanyanyuka kidogo na kuiweka ile bahasha chini ya mto mweupe niliokuwa nimelalia, sikuwa nimeifungua bahasha ile lakini nilikuwa najua kila kitu kilichomo ndani ya bahasha ile. Nilijua Mwalimu mkuu hangeweza kunisamehe kwa kosa la kwenda bila ruhusa katika hosteli ya wasichana, bila shaka yoyote nilijua kuwa ndani ya bahasha ile kuna taarifa ya kufukuzwa shule!

    Mwalimu mkuu Bukuku.



    Ni nani asiyemjua mwalimu huyo mlokole katika Jiji la Mbeya. Mwalimu ambaye alishawahi kumfukuza shule mwanae wa kumzaa mwenyewe, na siku ya pili asubuhi walipokuwa nyumbani kwao alimuuliza mwanae kwanini haendi shule? ilhali ni yeye ndiye aliyemfukuza



    shule jana yake. Ndipo mwanae alimpa barua ya kufukuzwa shule. Mwalimu Bukuku aliisoma barua aliyoiandika mwenyewe kisha akatingisha kichwa, ishara kuwa aliielewa, wakati barua hiyo aliiandika mwenyewe. Mwalimu wa namna hiyo unategemea anisamehe mimi eti kisa nilizimia baada ya kutenda kosa la kuingia katika hosteli ya wasichana?



    Baadae niliitoa ile barua chini ya mto na kuifungua! Na kweli baada ya kuifungua barua ile nilikutana na taarifa hiyohiyo niliyokuwa nahisi. Nilikuwa nimefukuzwa shule! Mkuu wa shule, mwalimu Bukuku hakuwa na huruma kabisa, hakujari kuzimia kwangu. Nikiwa nimeshangaa na barua yangu mkononi, Evelyne Gando alinisimulia jinsi ilivyokuwa sababu ya yeye kutokuja shule, na kilichotokea baada ya mimi kuzimia.

    Taarifa aliyonipa Evelyne Gando ilinisikitisha sana. Kumbe naye alikuwepo katika chumba kile cha hosteli nilichoingia kwa pupa bila kujua kuwa ndani yake kulikuwa na watu hatari sana kwa maendeleo yangu ya shule. Labda kutokana na mstuko na fadhaha wa kukutana na mkuu wa shule pamoja na Matron ndomana mimi sikumuona Evelyne Gando mle ndani ya chumba cha hosteli. Evelyne Gando alinieleza kwamba hakuja shule siku ile kwakuwa alikuwa na tatizo. Alikuwa ameibiwa kiasi kikubwa sana cha pesa. Hivyo Matron aliamua kumwita Mkuu wa shule ili

     CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    waje kusaidiana katika ushauri namna ya kuwezesha pesa yake irudi. Wakati wanajadiliana nini cha kufanya nd'o ghafla mlango ulisukumwa na mimi, nami kutosema chochote zaidi ya kuzimia baada ya kukutana na sura ya Mkuu wa shule akiwa pamoja na Matroni. Cha ajabu Mkuu wa shule hakustuka wala kujari kabisa juu ya kuzimia kwangu. Wakati Matroni anatafuta jinsi ya kunisaidia, Mkuu wa shule alienda ofisini kwake, Evelyne na Matron walihisi labda anaenda kutafuta usafiri ili waweze kunipeleka hospitali, lakini haikuwa hivyo aliporejea Mkuu wa shule alirudi na barua mkononi, na kuitupa katika kifua changu nikiwa nimezimia.

    Ndio, ilikuwa barua ya kufukuzwa shule na hivyo ndivyo nilivyokabidhiwa!



    Matroni kwa kushirikiana na Evelyne Gando walijitahidi kunipa huduma ya kwanza, kisha wao ndio walionipeleka hospitali. Ilikuwa hadithi mbaya sana kwangu. Hadithi yenye wahusika wanne, wahusika wawili kati yao wakiwa na roho nzuri, wahusika hao ni Matron na Evelyne Gando. Huku wahusika wawili wakiwa na roho mbaya sana, wahusika hao ni Mkuu wa shule na rafiki yangu kipenzi Richard Chali.

    Sina haja ya kuelezea roho mbaya ya Mkuu wa shule nadhani wote mnaijua, kumpa barua ya kufukuzwa shule mtu aliyezimia ni roho mbaya sana. Barua hiyo ingeweza kugeuka kuwa barua ya kifo!



    Hebu fikiria mtu unaamka toka katika kuzimia na kukutana na taarifa mbaya, taarifa ya kufukuzwa shule si unaweza kufa kabisa!

    Mtu wa pili mwenye roho mbaya ni Richard Chali. Kwa maelezo aliyonipa Evelyne Gando Richard Chali alikuwa anajua kila kitu juu ya kuzimia kwangu, lakini hakujari kabisa, tena alitabasamu baada ya kupewa taarifa ya kuwa mimi nimezimia, baada ya kukutwa katika hosteli ya wasichana. Niliamini maneno ya wahenga walisema kuna mstari mwembamba sana kati ya uadui na urafiki.



    Mida ya jioni niliruhusiwa kurudi nyumbani. Nilirejea peke yangu nyumbani. Sikuwa na msaidizi, sikuwa na rafiki, sikuwa na ndugu. Wakati Evelyne Gando alikuwa amesharejea shuleni kuendelea na ratiba zingine, maana aliruhusiwa kunipeleka tu hospitali kwa maana hakukuwa na mtu wakufanya hivyo, rafiki yangu, Richard Chali sikumuona kabisa!



    Kumbuka nyumbani hawakuwa na taarifa juu ya kuzimia kwangu. Hilo halikunishangaza sana, kilichonishangaza ni aliyekuwa rafiki yangu kipenzi Richard Chali kutothubutu kabisa kuja kuniangalia.

    Nilifika nyumbani saa moja jioni, sikupata ugumu wowote kumueleza baba yangu kuwa nilikuwa nimefukuzwa shule. Baba alikuwa ananipenda sana mimi na familia yake kwa ujumla, alikuwa anampenda



    sana mama yangu, pia ananipenda mimi na mdogo wangu Christina. Taarifa ya kufukuzwa kwangu shule kwa kosa la kwenda kumwangalia rafiki yangu katika hosteli za wasichana aliipokea kwa upole huku akiniahidi atanitafutia shule nyingine. Suala la kuhamishwa shule baada ya kukutwa katika hosteli ya wasichana labda ingekuwa ya furaha kwa mtu mwengine, maana lilikuwa kosa lenye chembechembe za aibu, lakini kwangu ilikuwa taarifa mbaya sana! Kuhama shule kwangu ilikuwa na maana ya kutenganishwa na msichana niliyempenda sana hapa duniani, Evelyne Gando. Sikuwa natamani kabisa kuwa mbali na Evelyne Gando, lakini sikuwa na jinsi barua ya ya kufukuzwa shule toka kwa mwalimu Bukuku ilinitaka niwe mbali nae msichana huyo niliyempenda zaidi.



    *****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Baada ya wiki mbili nilianza maisha mapya, katika shule mpya kwangu, Shule ya Sekondari Meta. Shule ambayo alikuwa anasoma mdogo wangu Christina. Ukweli ni kwamba sikuwa na furaha kabisa katika shule hii mpya. Wakati wote nilikuwa naiwazia shule ya Sekondari Sangu. Namuwaza Evelyne Gando, sasa hali yangu kimwili ilikuwa mbaya zaidi, nilianza kukonda na kupungua uzito kwa kasi kila siku. Sasa nitaacha vipi kukonda wakati nilikuwa sijamuona



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog