Simulizi: Uliniua Gloria
Sehemu Ya Nne (4)
Mzee Mbwana aliendelea kuwa na mawazo mengi huku akiwa na hasira kali, bado alikuwa akihitaji kupokea taarifa kwamba Peter alikuwa ameuawa na si kukamatwa kama walivyokuwa wakitaka polisi. Kitu ambacho alikuwa akikitaka ni Peter kuuawa na si kukamatwa na polisi kama ambavyo serikali ilivyotaka iwe.
Alijua fika kwamba endapo Peter angekamatwa na polisi basi jambo lile lingeweza kuwa gumu kwake, angeingia katika wakati mgumu sana wa kutaka kukamilisha kile alichokuwa akitaka kukikamilisha kwa wakati huo. Masikio yake alikuwa ameyategesha katika simu yake, kitu ambacho alikuwa akitaka kukisikia kutoka kwa vijana wake ni kwamba walikuwa wamekamilisha kila kitu ambacho alitaka kikamilishwe.
Japokuwa alijua fika kwamba mtoto wake, Kaposhoo alikuwa ameuawa lakini mzee Mbwana hakutaka kujifikiria kitu kimoja, kutaka kuuona mwili wa mtoto wake ili kumfanya kuamini zaidi na zaidi na kuwa na uhakika na suala hilo. Alipoona kwamba kulikuwa na ulazima mkubwa wa kufanya hivyo, akaondoka nyumbani na kisha kuelekea katika kituo cha polisi cha Mansansa na kisha kuanza kuwaelezea kile ambacho alikuwa akikihitaji.
“Mnafahamu kwamba mtoto wangu ameuawa?” lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa mzee Mbwana ambaye alionekana kuwa tofauti siku hiyo.
“Tunafahamu mzee” Polisi mmoja kati ya polisi watano waliokuwa zamu kituoni hapo alijibu.
“Ila mwili wake upo wapi?” Mzee Mbwana aliuliza.
“Hata sisi polisi bado tumebaki kwenye wakati mgumu sana. Ni kweli kwamba Peter ndiye aliyemuua Kaposhoo, lakini mwili wa Kaposhoo upo wapi? Cha msingi hapa ni kumkamata Peter kwani atakuwa akifahamu ukweli” Polisi yule alimwambia mzee Mbwana.
“Kwa maelezo ya Peter alisema kwamba alitaka kuuawa wapi?” Mzee Mbwana aliuliza.
“Katika pori la Mwaipompo”
“Huko ndipo pa kuanzia sasa” Mzee Mbwana aliwaambia polisi wale.
Hawakutaka kukaa tena kituoni hapo, walichokifanya ni kuchukua gari lao na kisha safari ya kuelekea katika pori dogo la Mwaipompo kuanza mara moja. Kutokana na maneno ya mzee Mbwana kuonekana kwamba kulikuwa na uwezekano wa mwili wa mtoto wake kuwa huko porini, wakaamua kuelekea huko ili kumridhisha mzee huyo.
Bado heshima yake na utajiri wake ulikuwa ukimpa kiburi sana cha kufanya kila kitu alichokuwa akihitaji kukifanya. Polisi walikuwa wakimheshimu kupita kawaida na kila aliwataka kufanya jambo fulani, walikuwa wakitii na kufanya kile ambacho alikuwa akitaka wakifanye.
“Ila naona kama uongozi umefanya uamuzi kwa kukurupuka” Polisi mmoja aliwaaambia wenzake katika kipindi ambacho walikuwa ndani ya gari wakielekea katika pori la Mwaipompo.
“Kwa nini?”
“Inakuwaje wanatoa amri Peter atafutwe kwa kosa la mauaji na wakati hata mwili wenyewe haujaonekana. Kuna uhakika gani kwamba Kaposhoo ameuawa? Kama ameuawa, mwili wake upo wapi? Haya ni mambo ya msingi sana ambayo uongozi ulitakiwa kujiuliza hata kabla ya kutoa amri ya kutafutwa kwa peter” Polisi huyo aliwaambia wenzake.
“Kwa hiyo wewe una ushauri gani?”
“Unafikiri hapa utashauri nini tena? Uongozi umekwishatoa amri na hatuna budi kutekeleza” Polisi yule aliwaambia wenzake.
“Ila uliloongea ni la muhimu sana. Nadhani hapa kuna kamchezo cha siri ambacho kanaendelea” Polisi mwingine aliingilia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nyie sikilizeni, cha msingi tufanyeni yale ambayo tumeagizwa kuyafanya, ukitaka kuhoji sana, utakuwa ukijisumbua tu na mwisho wa siku unaweza usipate jibu lolote lile” Polisi mwingine aliwaambia.
“Basi sawa. Tufanyeni kile ambacho uongozi umeamua tukifanye” Polisi yule aliwaambia wenzake.
Safari yao bado ilikuwa ikiendelea zaidi huku wote wakiwa na bunduki zao mikononi mwao. Wala hawakuchukua muda mrefu sana wakafika katika mtaa wa Mwaipompo na kisha kukutana na polisi ambao walikuwa mahali hapo kwa ajili ya kuweka ulinzi huku ikiwa imetimia saa tatu asubuhi. Mara baada ya kuongea nao mawili matatu, wakaingia ndani ya pori hilo la Mwaipompo.
Wakaanza kuutafuta mwili wa Kaposhoo porini humo. Kila mmoja alikuwa na bunduki yake mkononi mwake. Walipoona kwamba kutembea kwa makundi haikuwa nzuri, wakajigawa na wengine kwenda katika upande mwingine huku wote wakiwa na lengo moja, kuutafuta mwili wa kaposhoo.
Waliutafuta mwili huo kwa takribani dakika arobaini na tano lakini hawakufanikiwa kuupata mwili huo. Kila mmoja akachoka jambo ambalo liliwapelekea kurudi kituoni huku wakiwa hawajafanikiwa kuuona mwili wa Kaposhoo.
“Imekuwaje?” Mkuu wa kituo aliuliza.
“Patupu”
“Hamjauona mwili wa Kaposhoo?”
“Hapana mkuu. Hatujauona kabisa” Polisi mmoja alijibu.
Tayari hali hiyo nayo ikaonekana kuwachanganya, hawakujua ni kitu gani ambacho walitakiwa kukifanya, kuupata mwili wa Kaposhoo ndicho kingekuwa kitu ambacho kingewapa uhakika kwamba mtu huyo alikuwa ameuawa na hivyo kumtia matatani zaidi Peter.
“Cha msingi apatikane Peter kwanza” Polisi mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa polisi waliokwenda katika pori la Mwaipompo alimwambia mkuu wa kituo.
Kama kuchanganyikiwa katika kipindi hicho walionekana kuchanganyikiwa sana. Umuhimu wa kupatikana kwa Peter bado ulikuwa ukihitajika sana, walitamani kumpata Peter na kisha kumwambia ukweli juu ya mahali ambapo mwili wa Kaposhoo ulipokuwa kwani waliamini kwamba mtu huyo ndiye ambaye alikuwa amefanya mauaji hayo.
“Naongea na nani?” Mkuu wa kituo, Idrisa aliuliza mara baada ya kupokea simu.
“Msamalia mwema” Sauti ya upande wa pili ilijibu.
“Kutoka wapi?”
“Munali”
“Tukusaidie nini?” Mkuu wa kituo aliuliza.
“Tumemuona yule mtu ambaye anatafutwa” Sauti ya upande wa pili ilisikika.
“Nani? Peter?”
“Ndio”
“Upo wapi? Umemuona wapi?” Bwana Idrisa aliuliza huku akionekana kushtuka.
“Huku huku Munali”
“Manali ni kubwa. Wewe umemuonea wapi?”
“Katika nyumba ya wageni ya Sasara” Mpiga simu alijibu.
“Tunakuja. Naomba ufuatilie kila kitakachoendelea. Ikiwezekana hakikisha hatoki” Bwana Idrisa alimwambia mpiga simu.
“Sawa”
Hakukuwa na cha kupoteza mahali hapo, alichokifanya Bwana Idrisa ni kuwaambia polisi kwamba mtu ambaye walikuwa wakimtafuta, Peter alikuwa katika nyumba ya wageni ya Sasara iliyokuwa Munali, walichotakiwa kukifanya ni kuondoka mahali hapo kuelekea huko Sasara.
Polisi wakatoka ndani ya kituo kile huku bundukiwa wakiwa nazo mikononi, wakaingia ndani ya gari na kisha kuelekea Munali huku kila mmoja akiwa na uhakika kwamba Peter alikuwa huko tena ndani ya nyumba ya wageni ya Sasara. Walitumia takribani dakika ishirini, wakaingia Munali na kisha kuanza kuelekea katika sehemu ambayo kulikuwa na nyumba ya wageni ya Munali.
Hata kabla gari halijasimama katika eneo la nyumba hiyo ya wageni, polisi wakaruka kikomandoo huku wengine wakijibinua kisarakasi kama makomandoo na kuanza kusogea katika mlango wa kuingilia ndani ya nyumba ile ya wageni. Watu wote ambao walikuwa wakiwaangalia polisi wale walionekana kushangaa, ushupavu na utundu wa polisi wale wa kuruka sarakasi za chini chini ukaonekana kuwashangaza kupita kawaida kwani hawakuwahi kuwaona wakifanya mambo hayo kabla.
“Kuna mtu tumeambiwa yupo hapa, amechukua chumba” Polisi mmoja alimwambia dada wa mapokezi ambaye alionekana kutetemeka.
“Mtu gani?” Dada yule aliuliza huku bado akiendelea kuwa na wasiwasi.
“Huyu hapa” Polisi yule alijibu huku akitoa picha ya peter na kumuonyeshea.
“Yeah! Huyo mtu aliingia ndani ya jengo hili dakika ishirini zilizopita” Dada yule wa mapokezi alijibu.
“Kwa nini sasa haukutuambia?”
“Nilipomuona, nilijifikiria sana kwamba niliwahi kumuona wapi ila sikukumbuka. Uliponionyeshea picha ndio nimekumbuka sasa” Dada yule alijibu huku akitetemeka.
“Sawa. Yupo ndani?”
“Ndio”
“Chumba kipi?”
“Nilimpa chumba namba 10”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Asante” Polisi yule alisema na kisha wote kuanza kuelekea katika chumba hicho.
Kila mmoja aliona kwamba siku hiyo ndio ingekuwa mwisho wa maisha ya Peter ya kuishi kwa kuwaogopa polisi, tayari waliona kwamba siku hiyo tena muda huo mtu huyo ndio alikuwa akienda kukamatwa. Walipoufikia mlango wa chumba kile, polisi mmoja akachungulia ndani kupitia kwenye kitasa, Peter alionekana kulala ndani ya chumba hicho.
“Yupo”
“Sawa sawa. Fungua mlango” Polisi mmoja alisema na kisha mlango kufunguliwa.
Mlango ulionekana kuwa mgumu kufunguka, ulionekana kufungwa kwa ndani. Kwa sababu walikuwa wakitaka kumkamata bila kutumia nguvu yoyote ile, wakamuita dada wa pale mapokezi na kisha kumwambia apige hodi katika mlango wa chumba kile, dada wa mapokezi hakugoma, akagonga hodi, baada ya muda mlango ukafunguliwa, alikuwa Peter ambaye hakuonekana kuamini kile alichokuwa akikiona mbele yake.
“Upo chini ya ulinzi” Polisi mmoja alimwambia Peter ambaye akaonekana kutokuwa na nguvu, alijiona kukamatwa hata kabla hajaendelea na safari yake ya kuelekea nchini Tanzania. Hapo hapo mlangoni akaamriwa kugeuka kwa ajili ya kupigwa pingu.
****
“Umefikia wapi?” Sauti ya Bwana Stewart ilisikika simuni.
“Nimetuma polisi huyu mpumbavu akamatwe” Mzee Mbwana alimwambia Bwana Stewart.
“Ila nilisikia kama na yeye alitekwa?”
“Ndio alitekwa jana usiku lakini hakufanywa kitu chochote kile, yaani hata kujeruhiwa hakujeruhiwa, mbaya zaidi hata hao waliomteka waliuawa na porisi kule Mwaipompo” Mzee Mbwana alimwambia Bwana Stewart.
“Waliuawa?” Sauti ya Bwana Stewart ilisikika ikiuliza huku akionekana kutokuamini.
“Ndio”
“Shiiiiiit”
“Mbona hivyo tena?”
“Hawa watu nao wajinga sana. Sasa kwa nini wasingemuua huyu muuaji?” Bwana Stewart aliuliza huku akisikika kuwa na hasira.
“Hata mimi mwenyewe nimeshangaa. Ila nadhani ni kwa sababu yeye mwenyewe ni muuaji mwenzao, nadhani walitaka kumgeuka” Mzee Mbwana alimwambia Bwana Stewart.
“Kwa hiyo umeamua nini?”
“Kwanza atafutwe. Nitataka kumuua mimi mwenyewe” Mzee Mbwana alimwambia Bwana Stewart.
“Hilo usijali. Hata mimi pia nitakusaidia mzee mwenzangu” Bwana Stewart alimwambia mzee Mbwana.
“Sawa sawa. Nitakupa taarifa juu ya kila kinachoendelea”
“Hakuna shida”
Bado mzee Mbwana alionekana kuwa na hasira, hakuamini kwamba mpaka katika kipindi hicho hakukuwa na kitu ambacho kilikuwa kimeendelea. Kitu ambacho alikuwa akitaka kusikia wakati huo ni kwamba Peter alikuwa ameuawa na si kukamatwa kama ambavyo polisi walivyokuwa wakitaka.
Baada ya kukaa katika hali hiyo kwa masaa kadhaa, simu yake ikaanza kuita, alipoangalia namba ilikuwa ni kutoka kwa mkuu wa kituo cha polisi cha Mansansa, Bwana Idrisa ambaye alimwambia kwamba Peter alikuwa ameonekana katika mtaa wa Munali ndani ya nyumba ya wageni ya Sasara.
Hiyo ikaonekana kuwa taarifa njema kwa mzee Mbwana. Alichokifanya ni kuwapigia simu vijana wake na kisha kuwataka kuelekea katika mtaa wa Munali haraka iwezekanavyo, aliwapa taadhari kwamba huko kulikuwa na polisi ila kwa sababu hakutaka Peter akamatwe na polisi, akaamuru vijana wake waaue polisi na kisha kumchukua Peter wao.
“Ikiwezekana, ueni polisi wote na kumuua na Peter mwenyewe. Mmenielewa?” Mzee Mbwana aliuliza.
“Tumekuelewa bosi. Ndani ya dakika kadhaa tutakuwa ndani ya eneo la nyumba hiyo ya wageni kwani hatupo mbali na Munali” Sauti ya kijana mmoja ilisikika, kilichofuata, vijana wale wakaanza kuelekea Munali huku nao wakiwa na bunduki mikononi mwao, lengo lilikuwa ni kuua wote, kuanzia polisi mpaka Peter mwenyewe.
Vijana wa mzee Mbwana walikuwa ndani ya gari lao ambalo lilikuwa likiendeshwa kwa kasi na dereva wao. Bunduki zao zilikuwa kiunoni na kila mtu kichwani alikuwa na wazo moja tu kwa wakti huo, kufanya mashambulizi katika kipindi ambacho wangefika katika nyumba ya wageni ya Sasara.
Maagizo ambayo walikuwa wamepewa na mzee Mbwana ndio ambayo yalitakiwa kufanyika tena kwa haraka sana, hawakutakiwa kupuuzia hata kitu kimoja, kama mzee yule alivyosema kwamba waue kuanzia polisi mpaka Peter mwenyewe basi waliona kwamba ilikuwa ni lazima wafanye hivyo.
Kila mmoja alikuwa na hamu ya kufika katika eneo hilo, kila mmoja alikuwa na hamu ya kutaka kufanya mashambulizi kwa polisi na kisha kumuua mtu ambaye aliwafanya kuwa katika hali hiyo kwa kipindi hicho. Hawakutakiwa kumuonea mtu yeyote huruma, walichokuwa wakitaka kukifanya ni kufanya mauaji tu.
Hawakuchukua muda mwingi wakawa wameanza kuingia katika mtaa wa Munali ambapo moja kwa moja wakaelekea katika sehemu ambayo kulikuwa na nyumba ya wageni ya Munali. Walipofika huko, wakaanza kuwaona polisi ambao walikuwa wakiingia ndani ya nyumba ya wageni, wakajua kwamba mahali hapo ndipo kulikuwa sehemu ambayo kwa dakika chache ilibidi igeuzwe na kuwa uwanja wa vita.
“Tuanze kazi?”
“Subiri kwanza” Kiongozi wao alisema.
Walipoona baadhi ya polisi walikuwa wameingia ndani, wakasubiri kwa muda fulani mdogo na ndipo hapo milio ya risasi ikaanza kusikika mahali hapo. Watu ambao walikuwa wamekusanyika katika eneo hilo wakiwaangalia polisi wale waliposikia milio ya bunduki, wakaanza kukimbia, tayari waliona kwamba sehemu hiyo haikuwa na amani hata kidogo.
Yalikuwa ni mashambulizi ya kushtukiza sana, polisi hawakujua kitu chochote kile na wala hawakuwa wamejiandaa, polisi wote ambao walikuwa nje ya nyumba ile ya wageni wakaanguka chini, damu zilikuwa zikiwatoka miilini mwao na baada ya muda wakatulia kabisa.
Kazi ya kuwamaliza polisi wa nje wala haikuwa kubwa kabisa, ilifanyika kwa haraka sana tena kwa mafanikio makubwa kupita kawaida, walipoona kwamba walikuwa wamewamaliza polisi ambao walikuwa nje ya nyumba ile ya wageni, wakaanza kuwafuata wale wa ndani huku kila mmoja akiwa makini.
Ndani ya nyumba ile ya wageni hakukutakiwa kuingiwa ovyo, walikuwa wakiingia kwa mwendo wa kunyata na wa tahadhari sana kwani walikuwa wakiwahofia polisi wale ambao nao walikuwa na bunduki tayari. Hapo ndipo ambapo milio ya risasi ikaanza kusikika kutoka ndani ya nyumba ya wageni, polisi wale ambao walikuwa ndani wakaanza kumiminiana risasi na vijana wa mzee Mbwana ambao walikuwa wameingia ndani ya nyumba ile.
Mapigano yao ya kumiminiana risasi yalichukua muda fulani, polisi wakaonekana kuishiwa risasi, hapo ndipo ambapo wakaanza kushambuliwa mfululizo na baada ya dakika chache tu, hakukuwa na polisi ambaye alikuwa hai. Kila kitu kilipokamilika, vijana wale wakaanza kuelekea kule kulipokuwa na mlango wa kuingilia katika chumba alichokuwa amechukua Peter, walipoufikia, wakaufungua na kuingia ndani, hakukuwa na mtu yeyote yule.
Hali ile ikaonekana kuwachanganya, walichokifanya ni kumtafuta dada wa mapokezi, wakaelekea mpaka katika sehemu ya mapokezi, dada yule alikuwa amelala chini, machozi yalikuwa yakimtoka huku mwili ukimtetemeka kupita kawaida. Wakamuinua na kisha kuanza kumuuliza maswali.
“Peter yupo wapi?” Lilikuwa swali la kwanza lililotoka kwa kijana mmoja ambaye alionekana kuwa na hasira kupita kawaida.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Alikuwa chumbani kwake” Msichana yule wa mapokezi alisema huku akitetemeka.
“Tupeleke” Mwanaume yule alisema na ndipo yule msichana kuanza kuwapeleka katika chumba hicho huku akitetemeka kupita kawaida.
Wakafika mpaka katika mlango wa chumba kile, miili ya polisi ilikuwa imelala chini huku damu zikiwa zimetapakaa, mlango wa kuingilia katika chumba alichokuwa amechukua Peter ulikuwa wazi, walipoingia, hakukuwa na mtu yeyote yule.
“Yupo wapi?” mwanaume yule aliuliza huku bado akiendelea kuwa na hasira, sauti yake ilikuwa ni ya muungurumo fulani iliyojaa utetemeshi.
“Alichukua chumba hiki” Yule dada alisema huku akilia na kutetemeka kupita kawaida.
“Umemficha. Tuambie umemfichia wapi”
“Sijamficha. Alikuwa ndani ya hiki chumba”
“Kama alikuwa ndani ya hiki chumba, yupo wapi sasa?” Mwanaume yule aliuliza kwa sauti ya juu yenye hasira.
“Sijui” Msichana yule alisema huku akizidi kulia.
“Kama hautaki kutuambia ulipomficha, tunakuua” Mwanaume yule alimwambia yule dada ambaye alikuwa akiendelea kulia tu.
Mikwara ilikuwa mingi, mikwara ambayo ilimtaka yule dada wa mapokezi kusema sehemu ambayo alikuwepo Peter, hakusema kitu chochote kile, polisi ambao walikuwa wamegonga ndani ya chumba kile ndio ambao walitakiwa kuulizwa mahali alipokuwa Peter mara baada ya kutaka kumfunga pingu. Walichokifanya wanaume wale ni kuanza kuangalia huku na kule, kila mmoja alikuwa akitafuta Peter ambaye waliamini kwamba alikuwa ndani ya nyumba ile ya wageni.
“Nafikiri ametuacha” Kijana mmoja aliyetoka uani mwa nyumba ile ya wageni aliwaambia wenzake.
“Kwa nini?”
“Nimekuta ngazi kule nyuma”
Vijana wale wakaanza kuelekea huko uani, walipofika huko, ngazi ilikuwa imesimamishwa ukutani huku kukionekana kwamba mtu ambaye walikuwa wakimtafuta hakuwa ndani ya nyumba hiyo ya wageni. Walichokifanya ni kuondoka mahali hapo huku wakionekana kuwa na hasira kwani hawakuwa wamekamilisha kile ambacho walikuwa wameambiwa wakifanye.
“Hata akikimbilia wapi, tutampata tu” Kijana mmoja alisema huku wakiingia ndani ya gari na huku wakipiga risasi hewani, risasi ambazo ziliwafanya watu waliokuwa wamejificha kuendelea kujificha zaidi.
****
Polisi walionekana kufurahia, kila mmoja hakuamini kama wangeweza kumpata Peter kirahisi namna ile. Alichokifanya polisi mmoja ni kumuamuru Peter kugeuka na kisha kutoa pingu yake kwa ajili ya kumfunga Peter. Hata kabla hajachukua hatua hiyo, ghafla milio ya risasi ikaanza kusikika kutoka nje ya nyumba ile ya wageni.
Kila mmoja akaonekana kushtuka, polisi yule ambaye alitaka kumfunga pingu Peter akaacha kufanya hivyo, wote wakatoa bunduki zao na kisha kukaa tayari. Kila mmoja mahali hapo akaonekana kusahau kuhusiana na Peter, walisahau kwamba walikuwa wamefika mahali hapo kwa ajili ya kumkamata Peter, wote wakaonekana kutilia ubize katika suala zima la kutaka kushambuliana na watu ambao walikuwa wakiachia risasi.
“Kaeni pembezoni mwa ukuta” Polisi mmoja aliwaambia wenzake ambao wakakaa pembezoni mwa ukuta.
“Peter yupo wapi?”
“Mmmh! Alikuwa hapa, sijui kaenda wapi” Polisi mwingine alijibu.
Hawakutaka kumfuatilia peter, wakaanza kuweka umakini kutoka nje ya nyumba ile ya wageni. Walikaa mahali hapo huku wakiwa na bunduki zao mpaka katika kipindi ambacho vijana wale walipoanza kushambuliana nao.
Peter alikuwa ametoka mpaka uani mwa nyumba ile ya wageni. Alionekana kuchanganyikiwa kupita kawaida, milio ya risasi ambayo alikuwa akiisikia ilionekana kumchanganya kupita kawaida. Alichokifanya ni kuanza kuangalia huku na kule, lengo lake kwa wakati huo lilikuwa ni kuondoka mahali hapo, aondoke aelekee popote pale lakini hakutaka kujiona akikamatwa kwa mara ya pili au kuuawa.
“Nitafanyaje sasa?” Peter alijiuliza huku akiangalia huku na kule.
Jasho lilikuwa likimtoka, kitu ambacho alikuwa akikitaka mahali hapo ni kuondoka tu. Alipoangalia huku na kule, macho yake yakatua katika ngazi moja ya mbao, alichokifanya ni kuifuata, akaichukua na kuisimamisha. Kwa haraka sana huku milio ya risasi ikizidi kusikika masikioni mwake, akaanza kuipanda na kisha kurukia upande wa pili.
Mitaani hakukuonekana kuwa na mtu yeyote yule, watu wengi walikuwa ndani ya nyumba zao, milio ya risasi ambazo zilikuwa zikiendelea kusikika ziliwafanya kuogopa sana na hivyo kujificha. Peter hakusimama, kilichofuata ni kukimbia mahali hapo, kukimbia kwa mwendo wa kasi kuelekea Chongwe.
Njiani Peter hakutaka kusimama, alikuwa akizidi kukimbia zaidi na zaidi huku jasho likimtiririka na kuonekana kama amemwagiwa ndoo ya maji. Hapo ndipo ambapo akaonekana kukosa amani kabisa, hakuamini kama alikuwa amenusurika kukamatwa na polisi na pia kunusurika kuuawa na watu ambao walikuwa wamevamia ndani ya nyumba ile ya wageni.
Peter alizidi kukimbia mpaka alipoingia Chongwe. Hapo, akaamua kukiendea kibanda kimoja na kisha kutulia. Alikaa ndani ya kibanda hicho huku akionekana kuwa na wasiwasi mwingi, watu ambao walikuwa karibu na kibanda kile walionekana kutokumtambua hivyo walikuwa wakiendelea na kazi zao kama kawaida.
Hapo ndipo ambapo mawazo juu ya Gloria yalipoanza kumjia kichwani mwake, hakuamini kama msichana ambaye alikuwa akipendana nae kwa dhati ndiye ambaye alikuwa amemfanyia mambo yale. Peter alikuwa na uhakika kwamba kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea kilikuwa kikifanywa na Gloria pamoja na mtu aliyekuwa nae.
“Ananitafuta. Kama ananitafuta, ngoja tutafutane” Peter alisema huku akionekana kuwa na hasira.
Peter aliendelea kubaki ndani ya kibanda kile. Wala haukupita muda mrefu sana, vijana wawili wakatokea mahali hapo na kisha kuanza kumwangalia. Peter akaonekana kuwa na wasiwasi, kila alipokuwa akiwaangalia vijana wale alionekana kutokuwaelewa kabisa. Mbaya zaidi, alipowaangalia vizuri, walikuwa wameshika karatasi zenye picha zake mikononi mwao.
“Usikimbie. Ukisema ukimbie tu, utauawa. Watu wa hapa Chongwe si wa kuchezea” Kijana mmoja alimwambia Peter ambaye alionekana kutaka kukimbia.
Peter akawa mpole, akatulia benchini pale alipokuwa. Vijana wale wakamsogelea na kisha kukaa karibu yake huku wakiwa wamemuweka mtu kati. Peter hakujua wale vijana walikuwa ni wakina nani na walitoka mahali gani, kila alipokuwa akiwaangalia alikuwa akishikwa na wasiwasi, moyo wake ulimwambia kwamba vijana wale hawakuwa vijana wa amani maishani mwake.
“Unajua kwamba unamiliki milioni kumi?” Kijana mmoja alimwambia peter.
“Kivipi?” Peter aliuliza huku akitetemeka.
“Yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwako, milioni kumi ndio zawadi yake” Kijana huyo alimwambia Peter.
“Naombeni mnisamehe. Gloria ndiye ambaye amesababisha haya yote, naombeni mnisamehe niondoke zangu kuelekea tanzania” Peter aliwaambia vijana wale.
“Hatuna lengo la kukukamata” kijana mmoja alimwambia Peter.
“Lengo letu kubwa ni kuondoka nawe” Kijana mwingine aliingilia.
“Kuondoka na mie? Kwenda wapi?” Peter aliuliza huku akionekana kushtuka.
“Usijali. Sehemu salama”
“Naombeni mnisamehe”
“Usijali. Huyo Gloria yupo wapi?”
“Sijui. Sijui yupo wapi”
“Ok! Hilo si tatizo. Ungependa kumfanya nini pindi utakapokutana nae?” Kijana mmoja alimuuliza peter.
“Kumuua. Nisipomuua ataniua yeye”
“Hilo si tatizo. Tutakusaidia endapo utatusaiidia kitu kimoja” Kijana mmoja alimwambia Peter.
“Kuwasaidia nini?” Peter aliuliza swali ambalo liliwafanya vijana wale kuangaliana, wakatoa tabasamu pana ambayo yalimfanya Peter kuchanganyikiwa.
Peter akawa mpole, akatulia benchini pale alipokuwa. Vijana wale wakamsogelea na kisha kukaa karibu yake huku wakiwa wamemuweka mtu kati. Peter hakujua wale vijana walikuwa ni wakina nani na walitoka mahali gani, kila alipokuwa akiwaangalia alikuwa akishikwa na wasiwasi, moyo wake ulimwambia kwamba vijana wale hawakuwa vijana wa amani maishani mwake.
“Unajua kwamba unamiliki milioni kumi?” Kijana mmoja alimwambia peter.
“Kivipi?” Peter aliuliza huku akitetemeka.
“Yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwako, milioni kumi ndio zawadi yake” Kijana huyo alimwambia Peter.
“Naombeni mnisamehe. Gloria ndiye ambaye amesababisha haya yote, naombeni mnisamehe niondoke zangu kuelekea tanzania” Peter aliwaambia vijana wale.
“Hatuna lengo la kukukamata” kijana mmoja alimwambia Peter.
“Lengo letu kubwa ni kuondoka nawe” Kijana mwingine aliingilia.
“Kuondoka na mie? Kwenda wapi?” Peter aliuliza huku akionekana kushtuka.
“Usijali. Sehemu salama”
“Naombeni mnisamehe”
“Usijali. Huyo Gloria yupo wapi?”
“Sijui. Sijui yupo wapi”
“Ok! Hilo si tatizo. Ungependa kumfanya nini pindi utakapokutana nae?” Kijana mmoja alimuuliza peter.
“Kumuua. Nisipomuua ataniua yeye”
“Hilo si tatizo. Tutakusaidia endapo utatusaiidia kitu kimoja” Kijana mmoja alimwambia Peter.
“Kuwasaidia nini?” Peter aliuliza swali ambalo liliwafanya vijana wale kuangaliana, wakatoa tabasamu pana ambayo yalimfanya Peter kuchanganyikiwa.
****
Mzee Mbwana alionekana kuchanganyikiwa mara baada ya kupokea simu kutoka kwa vijana wake ambao walimpa taarifa kwamba hawakufanikiwa kumpata Peter ambaye alitoroka ndani ya nyumba ile ya wageni. Uso wake ukatawaliwa na ndita, kile ambacho alikuwa akikisikia mahali hapo kikaonekana kumharibia siku. Akaanza kuuma meno yake kwa hasira.
“Mmeleta uzembe” Mzee Mbwana alisema huku hasira kali zikiendelea kumakata.
“Hapana bosi. Alitoroka hata kabla hatujaingia ndani ya nyumba ile ya wageni” Sauti ya kijana mmoja ilisikika.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sasa alijuaje kama nyie mlikuwa ndani ya nyumba hiyo?”
“Bosi si ulituambia tuue kila tutakayemkuta! Tulianza kwa kuwaua polisi” Kijana yule alisikika akisema.
“Ila pamoja na hayo, mmeleta uzembe mkubwa sana. Kitu ninachokitaka ni kuona huyo mjinga anapatikana haraka iwezekanavyo” Mzee Mbwana alisema huku akiwa na hasira, hakutaka kuendelea kuongea zaidi, alichokifanya ni kukata simu.
Moyo wake ulikuwa kwenye hasira kali kupita kawaida, kitendo cha vijana wake kumkosa Peter kilionekana kumuumiza kupita kawaida, kitu ambacho alikuwa akikitaka sana kwa wakati huo ni kuona Peter anauawa hata kabla hajatiwa mikononi mwa polisi ambao nao walikuwa mstari wa mbele kumtafuta.
Mara baada ya simu kukatwa, mzee Mbwana akatulia katika kochi lake, macho yake yalikuwa yakiangalia darini huku akiendelea kuwa na hasira sana. Kila kitu ambacho alikuwa akikitaka kitokee kwa wakati huo aliona kikiwa kimekwenda ndivyo sivyo. Peter, alikuwa mtu pekee ambaye alimhitaji sana lakini kijana huyo alionekana kuwa na uwezo mkubwa sana wa kuweza kuwakimbia polisi na watu wengine.
“Nitampata tu” Mzee Mbwana alisema na kisha kuinuka mahali hapo.
Kitu cha kwanza alichokifanya ni kuelekea chumbani kwake ambapo huko akachukua simu yake na kisha kumpigia Bwana Stewart na kisha kuanza kuongea nae. Maneno ya Bwana Stewart ndio ambayo yalikuwa yakimtia hasira zaidi za kutaka kumpata Peter popote pale alipokuwa kwa wakati huo.
“Vijana wako wazembe sana. Hivi hawajui kama kadri wanavyozidi kumkosa huyu mpumbavu na ndivyo ambavyo nae atapata nguvu ya kukutafuta na kukuua?” Bwana Stewart alimuuliza mzee Mbwana ambaye akaonekana kuuona umuhimu wa kumpata Peter haraka zaidi.
“Yaani hapo ndio ninaposhangaa kabisa. Mtu yupo ndani ya nyumba ya wageni, sijui wamemkosa vipi” Mzee Mbwana alisema huku akionekana kuwa na hasira sana.
“Kwa hiyo umeamuaje? Kumtafuta na kumuua au kukutafuta wewe na kukuua?” Bwana Stewart alimuuliza mzee Mbwana.
“Kumtafuta na kumuua”
“Kama ni hivyo yakupasa kumtafuta kwa haraka sana. Nimepata tetesi kwamba Peter yupo katika kundi la waasi la ZSAG (Zambia Sldiers Against Government). Na walikuwa wamemtuma kwa ajili ya kumuua mtoto wako na kisha baadae kukua wewe mwenyewe” Bwana Stewart alimwambia mzee Mbwana.
“Unasemaje?”
“Nimekumegea siri. Ni lazima uchunguze na ujue kabisa kwamba unazidi kumkosa huyu kijana, kuna siku atakuja kukuua wewe” Bwana Stewart alimwambia mzee Mbwana maneno ambayo yalionekana kumchanganya kupita kawaida.
“Nitamtafuta”
“Lini sasa?”
“Vijana wangu ndio wanaoniangusha kwa sasa. Ila nitamtafuta tu” Mzee Mbwana alimwambia Bwana Stewart.
“Sawa. Ila kumbuka, unavyochelewa nawe unakarinbia kuuawa” Bwana Stewart alimwambia mzee Mbwana.
“Nitawaharakisha vijana wamuwahi mapema”
“Sawa”
Maneno ya Bwana Stewart yakaonekana kuingia ndani ya kichwa chake, yakaanza kumuogopesha na kumuona Peter ni mtu mbaya ambaye kama asingefanya jambo fulani basi angeweza kuuawa yeye. Alilifahamu kundi la kijeshi la waasi la ZSGA ambalo kila siku lilikuwa na kiu ya kutaka kuuchukua uongozi wa nchi ya Zambia pamoja na kuua matajiri waliokuwa ndani ya nchi hiyo, aliposikia kwamba Peter alikuwa ametumiwa na kundi la waasi la ZSGA akaonekana kutetemeka sana.
Alijua fika kwamba watanzania wengi walikuwa ni watu wa kuongea sana, watu ambao walikuwa wakikubalika katika nchi nyingi za Afrika, watu ambao hawakutakiwa kupewa nafasi hata mara moja katika suala zima la kuongea. Aliwaona watanzania kuwa watu wajanja wajanja ambao walikuwa na ujanja wa kufanya mambo mengi katika maisha yao, alijua fika kwamba kama Peter alikuwa akifanya kazi na ZSGA basi watu hao walikuwa serious katika kumteketeza yeye pamoja na familia yake.
Simu ile ndio ambayo ilionekana kumshtua zaidi jambo ambalo lilimfanya kuwapitgia simu vijana wake kwa kutaka kujua wamefikia wapi katika suala zima la kumtafuta Peter. Japokuwa dakika kadhaa zilizopita alikuwa ameongea nao na kumwambia kwamba wangehakikisha kwamba mtu huyo anapatikana lakini kutokana na maneno ya Bwana Stewart, akaamua kuwapigia simu tena.
“Vipi?”
“Kuhusu nini bosi”
“Kuhusu Peter”
“Si tumekwishakwambia Bossi kwamba kila kitu kitafanyika kama tulivyopanga” Sauti ya kijana wake ilisikika upande mwingine.
“Hapana. Nataka mfanye kazi leo leo, nataka mhakikishe kwamba huyu mtu anauawa leo hii hii, nisipomuua mimi ataniua yeye” Mzee Mbwana aliwaambia huku akionekana kuwa na wasiwasi.
“Hakuna tatizo bosi”
“Unajua mnaniletea utani. Hivi mnajua kwamba Peter anahusika na kundi la ZSGA?” Mzee Mbwana aliuliza huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Hapana”
“Peter anahusika nao, na wana lengo la kutaka kunimaliza mimi mwenyewe” Mzee Mbwana alimwambia kijana wake ambaye akaonekana kutokuelewa vizuri.
“Inakuwaje hapa bosi?”
“Ndio hivyo. Peter anahusika na kundi hilo kwa ajili ya kuniteketeza” Mzee Mbwana alimwambia kijana wake.
“Sidhani. Sidhani kama Peter anaweza kuungana na kundi hilo. Hivi kweli unalifahamu kundi hilo bosi?” Kijana yule aliuliza.
“Sikiliza Bosco. Sitaki maneno maneno. Ninachokitaka ni kuona Peter anakamatwa na kuuawa tu. Basi...hayo mengine yatajulikana akishakuwa kaburini” Mzee Mbwana alimwambia Bosco.
“Sawa bosi” Bosco aliitikia na kisha simu kukatwa.
****
Serikali ya Zambia ilikuwa imechanganyikiwa, mauaji ya polisi ambayo yalitokea katika nyumba ya wageni ya Sasara yalionekana kuichanganya serikali kupita kawaida. Kila mtu mitaani alikuwa akiongea lake jambo ambalo lilionyesha ni kwa jinsi gani suala lile lilikuwa limemshangaza kila mtu nchini Zambia.
Hiyo ndio ilikuwa ni mara ya kwanza nchini Zambia kwa polisi kuuawa kwa wingi katika mashambulizi. Kila mtu ambaye alikuwa amelishuhudia tukio lile alikuwa akiongea lake. Vikao vya dharura vikaitwa na moja kwa moja kumuingiza Peter katika tukio lile kwamba yeye ndiye ambaye alikuwa amehusika katika kila kitu pamoja na kuchonga mchongo mzima wa polisi wengine kuuawa.
Peter akaonekana kama gaidi nchini Zambia, Peter akaonekana mtu wa kutisha ambaye hakutakiwa kusogelewa hata mara moja. Kila mtu ambaye angeweza kumuona Peter alitakiwa kuwasiliana na kituo chochote cha polisi kwani tayari thamani yake ilikuwa imekwishaongezeka na alikwishaandaliwa kesi ya kujibu, kesi ya ugaidi ambayo ilikuwa ikimkabili kwa wakati huo.
Hayo pamoja na mambo mengine ndio ambayo yalikuwa yamejadiliwa katika vikao vya polisi ambavyo vilikuwa vimefanyika katika makao makuu ya polisi, Peter alitakiwa kutafutwa popote pale alipo kwa ajili ya kufikishwa mahakamani na kutakiwa kujibu kesi ya ugaidi ambayo ilikuwa ikimkabili kwa wakati huo.
Taarifa hiyo ikapelekwa mpaka nchini tanzania, watanzania wakatakiwa kufahamu kwamba kulikuwa na mtanzania nchini Zambia ambaye alikuwa amehusika katika ugaidi nchini Zambia. Kila mtanzania ambaye aliisikia habari ile akaonekana kushtuka, haikuwa kutokea kwa mtanzania kuhusika kakatika mambo ya ugaidi kama vile ambavyo Peter alikuwa amehusishwa.
“Hivi huyu Peter ni nani? Mambo yake yananifanya nimkumbuke Savimbi” Jamaa mmoja wa alimwambia mwenzake.
“Hata mimi mwenyewe nashangaa. Mtanzania kuhusishwa na ugaidi! Ni jambo geni sana masikioni mwangu” Jamaa mwingine alimwambia mwenzake.
“Sasa inakuwaje kwa huyu Peter?”
“Hata mimi nashangaa. Nahisi kuna kitu, nahisi kuna watu wapo nyuma yake” Jamaa mwingine alisema.
Kwa kila mtanzania ambaye alikuwa amesikia taarifa ya kijana wa kitanzania, peter kuhusishwa katika ugaidi alionekana kushangaa, lilikuwa jambo gumu kwa Tanzania, nchi ambayo ilikuwa ikisifika kwa amani raia wake kuhusishwa katika ugaidi sehemu yoyote ile. Kamanda wa jeshi la polisi nchini Tanzania akawaita watu mbalimbali katika jeshi lake na kisha kuweka kikao juu ya namna ya kumpata huyo mtanzania ambaye alikuwa amekwenda kuichafua nchi ya Tanzania nchini Zambia.
“Tunatuma wapelelezi wetu kwenda huko haraka iwezekanavyo. Hivi ninavyoongea ninataka wapelelezi wawili wakubwa waelekee huko” Kamanda mkuu wa jeshi la polisi aliwaambia polisi wenzake katika kikao hicho cha dharura.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakukuwa na kilichoendelea zaidi, kilichofanyika ni wapelelezi watatu kuandaliwa na kisha kutakiwa kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya kupeleleza ili kujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea nchini Zambia pamoja na kumtafuta Peter ambaye alionekana kama gaidi katika kipindi hicho.
“Mtakapompata, breki ya kwanza hapa nyumbani. Kwanza tunataka kuonana na mtu wetu, inawezekana kuna jambo limejificha nyuma ya pazia” Kamanda mkuu wa jeshi la polisi nchini Tanzania, Bwana Kimario aliwaambia wapelelezi wa kitanzania ambao walikuwa wakijiandaa kuelekea nchini Zambia.
“Hakuna tatizo mkuu. Tutafanya hivyo” Mpelelezi Michael alimwambia kamanda mkuu.
Miezi miwili na nusu ilikuwa imepita toka Kaposhoo akae nyumbani kwa mzee Desdeus ambaye bado alikuwa akiendelea kumpatia tiba ya mwili wake ambao ulikuwa umepigwa risasi. Kwa Kaposhoo, bado hasira zake kali zilikuwa kwa Bwana Stewart ambaye alijiona kuwa mshindi zaidi ya washindi kutokana na kile ambacho alikuwa amekifanya. Hasira zake hazikuishia kwa mzee huyo tu bali alikuwa akiendeleza chuki mpaka kwa Gloria ambaye kwake kwa wakati huo alionekana kama mwanamke malaya tu.
Tayari alikuwa ameanza kupata nafuu lakini mzee Des hakutaka kumruhusu Kaposhoo kuondoka hapo nyumbani kwake, bado alikuwa kihitaji kumpa tiba zaidi mpaka pale ambapo angejisikia mzima kabisa. Kaposhoo hakuwa na jinsi, akavumilia huku kila siku akiendelea kumuelezea mzee Des kuhusiana na maisha ya mahusiano ambayo alikuwa amepitia.
“Kwa hiyo Gloria ndiye chanzo cha kila kitu?” Mzee Des alimuuliza Kaposhoo.
“Yaani yeye ndiye chanzo cha kila kitu. Sikujua kama kumgeukia Peter kungeweza kusababisha haya yote” Kaposhoo alimwambia mzee des ambaye alionekana kutilia umakini katika kumsikiliza Kaposhoo.
“Pole sana. Sasa kwa nini uliamua kumgeukia Peter na kutembea na msichana wake?” Mzee Des alimuuliza Kaposhoo.
“Ni tamaa. Niliingiwa na tamaa ya kumtamani Gloria” Kaposhoo alimwambia mzee Des.
“Ila haukutakiwa kufanya hivyo”
“Najua ila nilishindwa kabisa kujizuia, nikajikuta nikitembea nae. Ila yule mwanamke ni shetani, tena shetani mkubwa ambaye hatakiwi kuishi katika ulimwengu huu” Kaposhoo alimwambia mzee Des huku akionekana kukasirika.
“Yakupasa umtafute Peter na kisha kumuomba msamaha kwa yote yaliyotokea” Mzee Des alimwambia Kaposhoo.
“Ni lazima nifanye hivyo. Ila baada ya kumuua huyu mwanamke na yule bwana wake” Kaposhoo alimwambia mzee Des.
“Sidhani kama kuna ulazima wa kumuua Gloria hapo” Mzee des alimwambia Kaposhoo.
“Huyu malaya ni lazima afe. Yaani ni lazima iwe hivyo. Nisipomuua huyu malaya, ataweza kumuua Peter kitu ambacho sitaki kitokee kabisa” Kaposhoo alimwambia mzee Des huku akionekana kumaanisha kile alichokuwa akikiongea.
“Kama umeamua hivyo, hakuna tatizo”
“Sawa. Kwanza imekuwaje kipindi kile nilichokwambia uende ukamwangalie Peter?” Kaposhoo alimuuliza Des.
“Kipindi cha mwisho ni kwamba alipewa kesi ya ugaidi. Basi, hakuna kingine” Mzee des alimwambia kaposhoo.
“Kwa hiyo haukuweza hata kumuona?”
“Ndio”
“Kwa sasa hivi yupo wapi?”
“Bado sijajua ila jana nilisikia taarifa ambayo inaweza kuwa mbaya kidogo” Mzee Des alimwambia Kaposhoo ambaye akaonekana kushtuka.
“Taarifa ipi?”
“Wanasema kwamba Peter aliuawa”
“Mungu wangu! Aliuawa? Na nani?”
“Kuna msichana aliuawa. Ila sikujua ni msichana yupi” Mzee Des alimwambia Kaposhoo maneno ambayo yalionekana kumchanganya.
“Nadhani unanitania”
“Huo ndio ukweli. Tena ni msichana wa Kitanzania” Mzee Des alimwambia Kaposhoo.
“Msichana wa Kitanzania! Atakuwa Gloria. Atakuwa Gloria huyo” Kaposhoo alimwambia mzee Des.
“Atakuwa ndiye huyo huyo”
“Siwezi kubaki mahali hapa tena. Ninahitaji kuondoka. Ninahitaji kwenda kuwaua watu hawa. Haiwezekani wamuue Peter. Ni lazima niondoke” Kaposhoo alimwambia mzee Deus huku akisimama kutoka kitini.
“Hakuna tatizo. Utawaua kwa silaha gani?”
“Nitatumia kisu”
“Hapana. Hebu subiri” Mzee Des alimwambia Kaposhoo na kisha kuondoka mahali hapo kuelekea chumbani kwake.
Kaposhoo aliuhisi mwili wake ukitetemeka kupita kawaida, alikuwa akiangalia chini huku meno yake yakigongana gongana tu na kijasho chembamba kikimtoka. Alichokifanya ni kuiwasha televisheni na kisha kuanza kuangalia huku lengo lake likiwa ni kutaka kuiona taarifa ya kifo cha Peter ambaye alikutwa ameuawa.
Alivyotegemea ndicho kile ambacho alikuwa amekutana nacho. Mwili wa peter ulikuwa umekwishafikishwa nchini Tanzania kwa ajili ya kuzikwa. Peter alizidi kuwa na hasira zaidi, alimchukia zaidi Gloria na Bwana Stewart ambao ndio aliwaona kuwa katika kila kitu kilichokuwa kimetokea.
Urafiki ambao alikuwa nao na Peter ulikuwa umekwishapita. Alipanga kumuomba Peter msamaha lakini hata kabla hajafanya hivyo tayari Peter alikuwa amekwishauawa na mwili wake ulikuwa umekwishafika Tanzania na kutarajiwa kuzikwa. Huo ukaonekana kuwa mwisho wa kila kitu, hakutaka kuwasiliana na baba yake mpaka pale ambapo angehakikisha kwamba Gloria na Bwana Stewart wanauawa na ndipo ambapo angeweza kumfuata baba yake na kumwambia kile kilichokuwa kimetokea.
Baada ya dakika kadhaa, mzee Des akarudi mahali hapo huku mkononi akiwa na bunduki yake na kisha kumpatia Kaposhoo ambaye akaichukua na kuanza kuiangalia. Kitendo cha kuigusa bunduki ile kikaonekana kumuongezea hasira zaidi kwa wabaya wake ambao alikuwa akitaka kuwaua kwa kipindi hicho. Akamshukuru mzee Des na kisha kutaka kuondoka mahali hapo.
“Kaposhoo”
“Naam”
“Kuwa makini na bunduki yangu. Kama utaona unahisi huruma, unaweza kuniita nije kuua mimi mwenyewe” Mzee Des alimwambia Kaposhoo.
“Usijali mzee. Sitaki damu za hawa watu zidaiwe mikononi mwako. Nitataka nikamilishe kazi yangu mimi mwenyewe” Kaposhoo alimwambia mzee Des na kisha kuondoka mahali hapo.
*****
Vijana wale wawili bado walikuwa wamekaa na Peter katika benchi lile.Kila wakati Peter alionekana kuwashangaa, hakuwa akiwafahamu kabisa na wala hakuwahi kuwaona hata mara moja. Ni kweli kwamba kwa maisha ambayo alitakiwa kuishi katika kipindi hicho hakutakiwa kumuamini mtu yeyote kwani watu wote kwake nchini Zambia walionekana kuwa maadui zake.
Bado vijana wale walikuwa wakiongea nae huku maneno yao yote wakimtaka kutokuwa na mashaka nao kwani walikuwa ni watu wazuri kwake na ndio maana wala hawakutaka kumkamata na kuondoka nae. Peter akatokea kuwaamini sana kiasi ambacho akaona bora atulie na kuwasikiliza walikuwa wakihitaji nini.
“Tunataka utusaidie kitu kimoja” Kijana mmoja alimwambia Peter.
“Kitu gani?”
“Kutupa utajiri”
“Kuwapeni utajiri? Kivipi?” Peter aliuliza huku akionekana kushtuka.
“Kuna mtu ana milioni mia mbili zetu na tunataka uende ukazichukue” Kijana mmoja alimwambia Peter.
“Mmmh!”
“Mbona unaguna?”
“Naona kama siwaelewi” Peter aliwaambia huku akionekana dhahiri kutokuwaelewa vijana wale.
“Usijali. Utatuelewa. Kuna mzee anafanya biashara ya madini ya almasi na ni wiki iliyopita ndio alikuwa ameingiza madini yenye thamani ya zaidi ya kwacha milioni mia mbili. Tunataka kuziiba hizo fedha na kitu pekee ni kumtumia Mtanzania kama wewe” Kijana yule alimwambia Peter.
“Mmmh!”
“Usijali. Ni kazi nyepesi sana. Unachotakiwa ni kufanya kila tutakachokwambia” Kijana mwingine akaingilia.
“Sawa. Ila kwa nini mnataka kunitumia mimi?”
“Kwa sababu wewe ni Mtanzania”
“Nikiwa mtanzania ndio nini sasa?”
“Mzee yule anawaamini sana watanzania katika kuwa waaminifu sana. Nje ya kila kitu, mzee huyu anauza madawa ya kulevya. Anapenda kuwatumia watanzania kwa sababu ni wajanja” Kijana yule alimwambia Peter.
“Mmmh!”
“Usiogope Peter”
“Sasa nitaingiaje huko?”
“Kazi rahisi sana. Pamoja na hayo yooote...huyu mzee ana binti yake anaitwa Fetty” Kijana yule aliongezea.
“Kwa hiyo?”
“Mchukue huyu msichana. Fanya kila liwezekanalo kuhakikisha anaingia mikononi mwako” Kijana yule alimwambia Peter.
“Nitaanzia wapi?”
“Klabu ya usiku”
“Ooooopssss...nimeokoka jamani”
“Hata sisi tumeokoka pia. Tunasali kwa mchungaji Petreseus ila kwanza tufanye michongo ya hela halafu wokovu baadae” Kijana yule alimwambia Peter.
“Sasa hamuoni kama nitapatikana kirahisi baada ya huyo msichana na baba yake kuniona?” Peter aliuliza.
“Hivi unafikiri kila mtu anayetafutwa wananchi wote wanafahamu? Hakuna kitu kama hicho. Cha msingi wewe fanya kazi yetu, tunakuhakikishia baada ya kupata fedha hizi, keshi yako inafutwa kwa kuwaita mawakili wenye elimu zao” Jamaa yule alimwambia Peter.
“Sawa. Nitajaribu”
“Usiseme utajaribu. Sema utafanya”
“Sawa. Nitafanya” Peter aliwaambia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mzee Seif alikuwa miongoni mwa watu matajiri ambao walikuwa wakimiliki kiasi kikubwa sana cha fedha nchini Zambia. Mzee huyu alikuwa tajiri namba tatu nchini Zambia huku akiwa amewaacha mbali sana mzee Mbwana na Bwana Stewart kwa uwezo wa fedha ambao alikuwa nao.
Mzee Seif alionekana kuwa tofauti na matajiri wengine, yeye, alikuwa akipenda sana kuwa karibu na familia yake, alikuwa akiijali na hata kuwa nayo karibu katika kipindi kingi ambacho anapata nafasi ya kufanya hivyo. Mzee Seif hakuwa na majigambo, alikuwa akipenda kumheshimu kila mtu huku mara nyingi akitoa misaada katika sehemu mbalimbali za dini kama makanisa pamoja na misikitini.
Hakuijali dini yake ya kiislamu ambayo alikuwa nayo, hakujali kitu chochote katika maisha yake, linapotokea suala la kusaidia makanisa, mzee huyu alikuwa mtu wa kwanza kufanya hivyo. Kuhusu kumiliki hoteli pamoja na biashara nyingine, mzee huyu alikuwa akimiliki mali za namna hiyo kwa kiasi kikubwa sana lakini alikuwa akiingiza sana fedha kupitia mashimo yake ya dhahabu yaliyokuwa Kitwe nchini Zambia.
Mzee Seif alikuwa na mashimo zaidi ya matano katika eneo la uchimbaji madini la Kitwe jambo ambalo lilikuwa likimpatia kiasi kikubwa cha fedha. Almasi zilikuwa zikichimbwa kwa wingi sana katika mashimo yake jambo ambalo lilimfanya kuonekana kuwa juu kila siku. Kuhusu masuala ya fedha, mzee Seif hakuonekana kuwa na matumizi mabaya kama matajiri wengine, kwake, fedha hizo alikuwa akiziwekeza kwa watoto wake watatu, Fatuma au Fetty kama alivyokuwa akipenda kujiita, Rahman pamoja na Farida.
Japokuwa mzee Seif alikuwa akijitoa sana katika kusaidia mambo ya dini lakini upande wa nyuma alionekana kuwa mtu mbaya ambaye alikuwa akijihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya. Hiyo ilikuwa ni biashara yake nyingine ambayo ilikuwa ikifanyika kwa siri sana. Si kwamba serikali halikulifahamu hilo, ilikuwa ikifahamu vizuri kabisa lakini kwa sababu alikuwa amejitengenezea heshima kubwa hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akijali.
Madawa yake ya kulevya alikuwa akiyatoa nchini Pakistan na kisha kuyaleta nchini Zambia na kuanza kuyasafirisha katika nchi mbalimbali ikiwepo Tanzania. Biashara hiyo ilikuwa ikizidi kumuingizia sana fedha kiasi ambacho mpaka wakati mwingine alikuwa akijishangaa, fedha hazikuisha, kila siku zilikuwa zikiongezeka zaidi na zaidi.
Mzee Seif alikuwa akiwapenda sana watanzania kwa sababu walikuwa watu wajanja ambao walijua sana kuongea zaidi ya wazambia ambao kwenye kuongea hawakuwa watu wa kujitetea sana. Kuongea sana kwa watanzania pamoja na namna ya ujanja ujanja katika upitishaji madawa ya kulevya mipakani ndio lilikuwa jambo ambalo lilikuwa likimfurahisha sana.
Wafanyakazi wake wengi walikuwa watanzania ambao kwake alikuwa akiwathamini sana na kuwalipa kiasi kikubwa cha fedha. Hakuwa na wasiwasi na watanzania na kila siku alikuwa akijitangaza wazi kwamba alikuwa akipenda sana kufanya biashara na watanzania ambao walikuwa wakimfanya kuwa juu zaidi na zaidi.
Ukiachana na maisha yake hayo, mtoto wake wa kwanza, Fetty alikuwa miongoni mwa mabinti ambao walikuwa na maisha ya juu sana. Alijua fika kwamba baba yake alikuwa na fedha nyingi sana na hata kama angeamua kuzitumia kila siku hakika asingeweza kuzimaliza kabisa. Kazi kubwa kwake ikawa ni kuzitumbua fedha za baba yake kadri alivyoweza.
Alikuwa akinunua magari ya kifahari na kisha kuwagawia marafiki zake kisiri kitendo ambacho baba yake hakukipenda kabisa jambo ambalo lilimpelekea kumlzamisha kutafuta mwanaume wa kumuoa na kila kitu kugharamia yeye mwenyewe. Huo ukaonekana kuwa mtihani mgumu kwa Fetty ambaye mara nyingi alikuwa akipenda sana kwenda klabu, hakuona kwamba kungekuwa na mwanaume ambaye angekuwa na mapenzi ya dhati kwake, wanaume wote ambao walikuwa mbele yake walionekana kuwa miongoni mwa wanaume ambao walikuwa wakipenda kuwa nae kwa sababu tu alikuwa na fedha.
Mapenzi ya dhati, mapenzi ya kupendwa na kupenda kilikuwa ni kitu kigumu sana ambacho aliamini asingeweza kukutana nacho katika maisha yake. Hakuamini kama kungekuwa na mwanaume ambaye angekuwa akimpenda kwa mapenzi ya dhati, mwanaume ambaye kamwe asingejali kama alikuwa na fedha au la.
Pamoja na mambo yote ambayo alikuwa akiyafanya, Fetty alionekana kuwa na ugonjwa wa kupenda ovyo. Kila mwanaume ambaye alikuwa akikatiza mbele yake alikuwa akimpenda kitu kilichowapelekea wanaume wengi kufanya nae mapenzi na kisha kumuacha katika mataa. Jambo hilo halikuweza kumfanya kuwaacha wanaume ambao mara nyingi walikuwa wakigombana wenyewe kwa wenyewe kwa kulilia penzi lake.
Mambo yale ndio ambayo yalionekana kumkera, hakupenda kuwaona watu wakigombana kwa ajili yake, alipenda kuwaona watu wakiishi kwa amani kama ambavyo walitakiwa kuishi. Katika kipindi ambacho alikuwa akiendelea kumtafuta mwanaume ambaye angeonekana kumjali na kumpenda, hapo ndipo alipokuja kusikia kitu kiimoja ambacho kilionekana kumvutia sana.
WANAUME WA KITANZANIA. Sifa kemkem zilikuwa zikitolewa na marafiki zake kwamba wanaume wa kitanzania walikuwa wakiyajua mapenzi, walikuwa wakijua kukaa na mwanamke na kumjali tofauti na wanaume wa Zambia ambao walikuwa wakiangalia zaidi ngono kuliko mapenzi.
Maneno hayo ndio ambayo yalionekana kuubadilisha moyo wa Fetty na kutamani kuwa na mwanaume wa Kitanzania. Alitamani sana kupata mapenzi ya dhati, alikuwa akisikia taarifa tu kutoka kwa wanawake mbalimbali kwamba walikuwa wakipendwa kwa mapenzi ya dhati lakini kamwe kwake hakuwahi kuyaona hayo mapenzi ya dhati.
Alitamani kuyaona mapenzi ya dhati, alitamani kuyajua mapenzi hayo yalikuwa yakifananaje. Kila siku alikuwa mtu wa kukaa chumbani huku akijaribu kufungua taarifa nyingi kuhusiana na wanaume wa Kitanzania. Huku akiwa anahangaika kutaka kuyajua hayo, hapo ndipo alipopata wazo jingine ambalo likamfanya kuanza kuangalia filamu za kibongo.
Akavutiwa na uigizaji wa watanzania, akavutiwa sana na msanii wa maigizo, Steven Kanumba ambaye alikuwa akivuma sana katika kipindi hicho. Kwa muonekano ambao alikuwa akiwaona wanaume wa Kitanzania aligundua kabisa kwamba walikuwa na wanaume ambao walijawa na mapenzi ya dhati, mapenzi ambayo yalikuwa na nguvu ya kumfanya kulia, hakujua kwamba wanaume hao hao wa kitanzania walikuwa wakiwaliza wanawake wa Kitanzania mpaka kufikia hatua ya kutokuyatamani mapenzi.
“Na mimi nataka mwanaume wa Kitanzania” Fetty aliwaambia marafiki zake ambao wakabaki wakicheka tu.
“Sasa mnacheka nini?” Fetty aliwauliza.
“Utawaweza?” Paulina alimuuliza.
“Kwa nini nisiweze?”
“Wanaume wa Kitanzania wana gharama sana japokuwa wana mapenzi ya dhati” Paulina alimwambia Fetty.
“Kivipi?”
“Wanapenda sana shopping, wanapenda sana kupewa fedha kila siku, wanapenda kusikilizwa na kuheshimiwa” Paulina alimwambia fetty.
“Ni hayo tu?”
“Ndio. Hizo ndio sababu zinazonifanya kutotamani kuwa na mwanaume wa Kitanzania, nawapenda sana na ninapenda niwe nao ila kila nikiangalia gharama zao, mmmmh! Siwezi” Paulina alimwambia fetty.
“Kuhusu gharama si tatizo. Mimi nataka kuwa na Mtanzania tu” Fetty aliwaambia.
“Nikutafutie?” Catherine, rafiki yake mwingine alimuuliza.
“Wanapatikana wapi?”
“Wanapatikana kwa wingi Tanzania” Catherine alimwambia Fetty.
“Hebu acha utani, yaani hapa Zambia yote hakuna mwanaume wa kitanzania mpaka uende huko Tanzania?” Fetty alimuuliza Catherine.
“Kama unawataka hakuna tatizo tutaweza kuwapata tu” Catherine alimwambia Fetty ambaye alikuwa makini kumsikiliza.
Hiyo ndio ilikuwa kiu ya Fetty katika kipindi hicho. Alikuwa akitamani sana kuwa na mwanaume wa Kitanzania, alikuwa akitamani sana kuyapata mapenzi ya dhati ambayo marafiki zake wengi walikuwa wakiyazungumzia. Fetty akaonekana kama chizi, kila alipokuwa akikaa alikuwa akiwafikiria wanaume wa kitanzania tu.
Kwenda klabu hakuacha, wanaume wengi wa Zambia walikuwa wakiendelea kujigonga kwake lakini kwa Fetty hakuonekana kuwa na hamu nao, mtu ambaye alikuwa akimtaka katika kipindi hicho alikuwa mtanzania, mmoja wa watu ambao waliaminika kwamba walikuwa na mapenzi ya dhati na mioyo yenye kujali.
“Mambo vipi!” Mwanaume mmoja alimsalimia Fetty kaunta, Fetty akayapeleka macho yake usoni mwa mwanaume huyo.
“Poa” Fetty aliitikia huku akiendelea kunywa pombe pamoja na marafiki zake ambao walikuwa wakimwangalia mwanaume huyo kwa macho ya kumtamani.
“Naweza kukupa kampani?” Mwanaume yule aliuliza.
“Hapana. Marafiki zangu wananitosha sana” Fetty alimwambia mwanaume yule huku akiendelea kunywa pombe.
Mwanaume yule hakuonekana kuridhika, alichokifanya ni kukaa katika kiti cha pembeni huku macho yake yakimwangalia Fetty ambaye alionekana kuwa na mawazo. Mwanaume yule akatoa pochi lake na kisha kumuagiza mwanamke aliyekuwa pale kaunta amletee pombe japokuwa hakuonekana kama mnywaji wa pombe.
“Kiasi gani hii?” Mwanaume yule alimuuliza mhudumu.
“Kwacha mia nane” mwanaume yule alijibu.
“Bei zenu zipo juu kidogo tofauti na kwetu Tanzania” Mwanaume yule alimwambia mhudumu yule.
Fetty akaonekana kushtuka, akayageuza macho yake yaliyojaa mshangao na kumwangalia mwanaume yule. Alisikia vilivyo maneno ambayo aliongea mwanaume yule, akagundua kwamba kumbe alikuwa amemletea maringo mwanaume wa Kitanzania, watu ambao alionekana kuwahitaji kupita kawaida.
Fetty akaanza kujuta, maringo yake yakaonekana kumsababishia hali mbaya, mapenzi ambayo alikuwa akiyahitaji kutoka kwa mwanaume wa kitanzania yakaonekana kuanza kupotea kwa kuwa alikuwa amemletea maringo mmoja wa wanaume wa Kitanzania, Fetty akajisikia aibu lakini pamoja na hayo yote, akajiapiza kumpata mwanaume huyo. Akaupiga moyo konde, akakisogeza kiti chake karibu na mwanaume yule ambaye alionekana kupigwa na mshangao.
Kila kitu kilikuwa kimepangwa na ni Peter ndiye ambaye alikuwa akihitajika kumtafuta huyo msichana ambaye aliambiwa amtafute na kisha kukamilisha kila kitu. Walichokifanya vijana wale ni kumchukua Peter, wakampakiza ndani ya gari lao ambalo lilikuwa hatua chache kutoka katika kibanda kile na kuanza kuondoka mahali hapo.
Muda wote ndani ya gari Peter alionekana kuwa na mawazo, alikuwa akiwafikiria watu wale huku akijiuliza maswali kwamba watu wale walikuwa watu wema kama walivyokuwa wamejitambulisha kwake au walikuwa ni watu wabaya ambao walikuwa wakitaka kumkabidhisha katika vyombo vya dola bila kupata tabu yoyote ile.
Kila alichokuwa akijifikiria mahali hapo hakupata jibu kabisa hali ambayo ikamfanya kutulia kuona ni kitu gani kingeendelea baada ya hapo. Baada ya dakika kadhaa, wakafika katika eneo la nyumba moja kubwa ambayo ilionekana kuwa ya kifahari, geti likafunguliwa na wote kuingia ndani. Peter hakutulia, bado alionekana kutokuwa na amani na watu wale ambao alikuwa nao muda huo.
“Karibu” Mwanaume mmoja alimkaribisha Peter ambaye akatulia katika kochi moja kubwa.
Kilichoendelea mahali hapo ni kumpa maelekezo yote ambayo alitakiwa kupewa, kuambiwa kwamba alitakiwa kuanzisha uhusiana na mtoto wa mzee Seif, Fetty. Akapewa kiasi kidogo cha kuanzia nacho, akapewa picha ya msichana huyo na kuelekezwa mahali ambapo angeweza kupatikana kwa urahisi sana.
“Na vipi kama kuna watu wengine wataniona, hamuoni kama ninaweza kukamatwa?” Peter aliuliza.
“Hautakiwi kuhofia, tutakupa kofia kubwa aina ya Malboro. Halafu ishu ya mtu kutafutwa huwa tunaangalia masikini ila si kwa matajiri” Kijana mwingine, Erick alimwambia Peter.
“Sawa”
Siku hiyo ndio ilikuwa siku ya kuanza kazi ambayo alitakiwa kuifanya. Ilipofika saa nne kamili alikuwa akiingia ndani ya ukumbi wa Casablanca ambapo moja kwa moja akaelekea katika kaunta kwa lengo la kuagiza kinywaji. Macho yake yalipotua usoni mwa msichana ambaye alikuwa pembeni yake, hakuamini, mtu ambaye alikuwa amemfuata ndani ya ukumbi huo ndiye alikuwa yule aliyekuwa pembeni yake.
“Mambo vipi” Peter alimsalimia Fetty ambaye alikuwa pembeni yake.
“Poa” Fetty aliitikia huku akiendelea kunywa pombe pamoja na marafiki zake ambao walikuwa wakimwangalia mwanaume huyo kwa macho ya kumtamani.
“Naweza kukupa kampani?” Peter aliuliza Fetty ambaye hakuonekana kumjali sana.
“Hapana. Marafiki zangu wananitosha sana” Fetty alimwambia Peter huku akiendelea kunywa pombe.
Peter akaonekana kuchoka, tayari akajiona kushindwa kufanikisha kile ambacho alitakiwa kukifanikisha mahali hapo. Msichana ambaye alikuwa ameambiwa kwamba ilikuwa ni lazima kuhakikisha kwamba anaingia mikononi mwake alikuwa pembeni yake lakini mbaya zaidi hakuonekana kumletea shobo kama ambavyo alitaka iwe.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Peter hakutaka kukata tamaa, alijua kwamba mara nyingi mwanzo huwa mgumu, alichokifanya ni kuagiza mzinga mmoja wa pombe kama hatua mojawapo ya kuvuta kasi kwa kile alichotakiwa kukifanya mahali pale.
“Kiasi gani hii?” Peter alimuuliza mhudumu.
“Kwacha mia nane” Mhudumu alijibu.
“Bei zenu zipo juu kidogo tofauti na kwetu Tanzania” Peter alimwambia mhudumu yule.
Peter hakuonekana kujali sana, alichokifanya ni kukishikilia kinywaji kile huku akijifikiria kama alitakiwa kukinywa au la. Japokuwa alikuwa akifanya mengi kwa wakati huo lakini akili yake ilikuwa kwa Fetty ambaye alikuwa pembeni yake tu. Alikuwa akihitaji sana kukamilisha kila mpango ambao alikuwa ameambiwa kuukamilisha na hatimae kuiba kiasi cha fedha cha milioni mia mbili ambacho kilikuwa kimeingizwa na baba wa msichana huyo, mzee Seif.
“Samahani” Fetty alimwambia Peter mara baada ya kumsogelea.
Peter akabaki kimya, kwanza akapigwa na mshangao, hakuonekana kuamini kama msichana yule angeweza kumsogelea na kisha kutaka kuongea nae na wakati dakika kadhaa zilizopita alikuwa amemletea maringo kwa kumuonyeshea kwamba hakuwa akimjali. Peter akaiona hiyo kuwa nafasi, moja ya nafasi ambayo hakutakiwa kuiletea masihala.
Hapo ndipo walipoanza kupiga stori. Peter alionekana kuwa muongeaji mkubwa sana kiasi ambacho kilimfanya Fetty kutokuchoka kabisa. Muda wote Fetty alikuwa akijisikia furaha, hakuamini kwamba mwisho wa siku nae alikuwa amekutana na mwanaume wa kitanzania, mmoja wa wanaume waliokuwa na mapenzi ya dhati kwa wapenzi wao.
Watu wawili waliokuwa na mawazo tofauti wakawa wamekutana na kuendelea kuongea. Kichwa cha Fetty kilikuwa kikifikiria mapenzi tu na wakati kichwa cha Peter kilikuwa kikifikiria wizi zaidi. Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo Fetty akazidi kuvutiwa na Peter kiasi ambacho akalitoa dukuduku lake la moyoni.
“Hakuna tatizo. Ila ninahitaji kupendwa kama nitakavyopenda” Peter alimwambia Fetty huku tayari ikiwa imetimia saa tisa usiku.
Mapenzi yakaanza rasmi, muda mwingi wa mchana Peter alikuwa akijifanya kuwa bize, hakutakiwa kutoka ndani ya nyumba ya vijana wale, Erick na Justo nyakati za mchana kwa kuhofia kuonekana na watu wengine. Muda ambao alikuwa akiruhusiwa kutoka ilikuwa ni usiku tu, kuanzia saa moja na kuendelea.
Fetty akaanza kujisikia huzuni, hakutaka kuonana na mpenzi wake nyakati za usiku tu, alikuwa na hamu ya kuonana nae hata nyakati za mchana ambazo kila siku alikuwa akimwambia kwamba yupo bize na mambo mengine. Maswali mengi yalikuwa yakimiminika kichwani mwa Fetty juu ya mpenzi wake huyo ambaye mpaka katika kipindi hicho walikuwa wametumia muda wa wiki moja kuwa kwenye mapenzi lakini hakuwa akipata majibu ya maswali yake.
Hakujua kama mpenzi wake alikuwa mfanyakazi ambaye alikuwa akikaa ofisini au alikuwa mfanyabiashara kama watanzania wengi walivyokuwa nchini Zambia. Hali ile iliendelea zaidi mpaka pale ambapo Fetty akaona ni lazima atoe dukuduku lake na kuamua kumuuliza Peter kuhusiana na kazi ambayo alikuwa akiifanya.
“Mimi ni mfanyabiashara. Mara nyingi nachukua vitenge kutoka hapa Zambia na kuvipeleka Tanzania” Peter alijibu huku akionekana kutokuwa na wasiwasi hata kidogo.
“Na kwa nini haupendi tuonane mchana mpenzi? Kila nikikupigia simu, upo bize. Yaani ubize mpaka kwa mpenzi wako?” Fetty alimuuliza Peter.
“Kumbuka mimi ni mfanyabiashara mpenzi, bila biashara siwezi kula, bila biashara siwezi kubadilisha mavazi. Yanipasa kuzingatia sana biashara kwanza, mapenzi yapo, nitakupenda mpaka utaona kero mpenzi” Peter alimwambia Fetty.
“Sawa. Ila naomba utenge muda kwa ajili yangu pia. Mambo ya kuonana usiku mpaka usiku wala si mazuri, yaani tunakuwa kama walinzi” Fetty alimwambia Peter.
“Usijali” Peter alijibu.
Kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea katika maisha yake na Fetty yalikuwa ni maigizo tu na wala hakuwa kwenye mapenzi kabisa. Wiki ya pili ikakatika na ya tatu kuingia, mwezi ukaingia, Peter akaanza kujisikia tofauti moyoni mwake. Maigizo ambayo alikuwa akiyaigiza kwa Fetty yakaonekana kupotea na mapenzi ya dhati kuanza kumuingia.
Ukaribu wake na Fetty ukamfanya kuanza kupiga hatua ya kuangukia katika mapenzi ya msichana huyo na mwisho wa siku kujikuta akimsahau mpaka Gloria na kuamua kuwa na msichana huyo. Mpango ambao walikuwa wameupanga Erick na Justo kwamba alitakiwa kufanya uhalifu ukaonekana kusahaulika na hakutaka hata kuusikia kabisa.
Peter hakuonekana kuwa radhi kumuibia mzee Seif na wakati muda wowote kuanzia kipindi kile angekuwa mkwe wake, akaonekana kuyasaliti makubaliano ambayo alikuwa amewekeana na watu wale.
“Umefikia wapi?” Erick alimuuliza Peter.
“Bado bado” Peter alijibu.
“Sasa mpaka lini?”
“Mambo ni hatua kwa hatua. Unajua mambo mengine hautakiwi kukurupuka kwani unaweza kukosa yote” Peter alimwambia Erick.
“Yaani tunaona unachelewa sana, muda tuliokupa unaelekea ukingoni” Justo alimwambia Peter.
“Mnashindwa kuwa waelewa”
“Kivipi?”
“Mambo hayatakiwi kwenda haraka haraka. Kwanza mazoea. Yaani hata kunitambulisha kwa baba yake bado, nyie mnataka niziibe hizo fedha” Peter aliwaambia.
“Kwa hiyo hata kwenda kwao bado?”
“Bado”
“Daah! Kweli ishu itakuwa sawa hii?”
“Hilo msijali”
“Sawa. Hakikisha unafanya kweli kila mtu aondoke na chake, si unajua muda nao ni fedha”
Hakuna noma” Peter aliitikia.
Mapenzi....Mapenzi...Peter hakuonekana kuwa muelewa hata mara moja. Moyo wake ulikuwa kwa msichana Fetty mbaye kwake alionekana kuwa kila kitu kwa wakati huo. Alikuwa akimpenda sana na hakuonekana kuwa tayari kufanya kile ambacho Erick na Justo walitaka akifanye.
Hata katika kipindi ambacho Peter alipelekwa katika nyumba ya mzee Seif, mapokezi mazuri ambayo alikuwa ameonyeshewa na familia hiyo, hakuonekana kuwa radhi kabisa kufanya kile kilichompelekea kuonana na Fetty. Akaendelea kujiwekea kipingamizi kwamba ilikuwa ni bora kupatwa na kitu chochote lakini si kufanya kile alichokuwa ameambiwa akifanye.
“Kuna chochote ambacho unataka kuniambia?” Fetty alimuuliza Peter katika kipindi ambacho walikuwa wamekaa chumbani, nyumbani kwa mzee Seif.
“Hapana” Peter alijibu huku akiwa ameachia tabasamu.
“Ila unaonekana kama unataka kuniambia kitu” Fetty alimwambia Peter.
“Hapana mpenzi”
“Kuwa muwazi”
“Ndio ivyo. Au labda nikuulize swali”
“Swali gani?”
“Upo tayari kuniacha kwa sababu ya fedha?” Peter alimuuliza Fetty.
“Hapana. Mapenzi ni zaidi ya fedha kwangu” Fetty alimwambia Peter.
“Kweli?”
“Ndio”
“Nahitaji kuwa huru kwako mpenzi”
“Najua. Ila unamaanisha nini?”
“Ungependa kuisikia historia yangu?”
“Kama utapenda kufanya hivyo. Nipo tayari”
“Sawa. Ila kabla sijakwambia, upo tayari kunipoteza kwa sababu ya fedha?” Peter alimuuliza fetty huku akionekana kama kutokumuamini.
“Siwezi...siwezi...siwezi Peter” Fetty alimwambia Peter.
“Sawa”
Hapo ndipo ambapo Peter alipoanza kumuelezea Fetty historia ya maisha yake. Alimuanzia toka katika kipindi ambacho alikuwa mdogo, alipokutana na Gloria na kuanza kuelekea shule pamoja mpaka katika kipindi ambacho alipoanza kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na Gloria.
Peter hakuficha kitu chochote kile, aliendelea kuwa muwazi. Alielezea sababu iliyomleta nchini Zambia mpaka pale ambapo Gloria alikuja nchini Zambia na kumfanyia kile alichomfanyia. Alielezea kila kitu tena kwa ufasaha kabisa. Alipomaliza, Fetty alikuwa akitokwa na machozi.
“Usilie mpenzi” Peter alimwambia Fetty.
“Nimeumia mpenzi. Nimeumia kwa kile kinachoendelea katika maisha yako. Kuingizwa katika maisha ambayo hukuyatarajia” Fetty alimwambia Peter huku akilia.
“Kila kitu kimetokea kwa mipango ya Mungu. Ninatafutwa mpenzi na ndio maana sitaki kuonekana mchana” Peter alimwambia fetty.
“Huyo Gloria yupo wapi?”
“Sijajua. Ila nadhani atakuwa na huyo mtu wake” Peter alimjibu Fetty.
“Tutamtafuta mpaka tumpate na tumuue kabla hajakuua wewe” Fetty alimwambia Peter.
“Una uhakika tutafanikiwa?”
“Asilimia mia moja”
“Basi hakuna tatizo”
“Nitamwambia baba. Atatuma vijana wake, tutamuua tu wala usijali. Au ulitaka kumuua kwa mkono wako?” Fetty alimuuliza Peter.
“Kama itawezekana”
“Sawa. Ila kumbuka sifanyi hivi kwa sababu mimi ni muuaji, hapana, nafanya hivi kwa sababu ninataka kuwa na wewe milele na kamwe sitaki kukupoteza. Nisipomuua huyu mpumbavu, atakuja kukuua wewe kitu ambacho sitaki kitokee” Fetty alimwambia Peter.
“Sawa. Kwanza fanya mpango afe na ndio mengine yafuate” Peter alimwambia Fetty.
“Hakuna tatizo. Vijana wa baba watafanya kila kitu” Fetty alimwambia Peter.
*****
Kaposhoo bado alikuwa amechanganyikiwa, hakuamini kama katika kipindi hicho rafiki yake, Peter alikuwa ameuawa na Gloria. Bado moyo wake ulikuwa katika maumivu makali, alikuwa akitaka kumuua Gloria na Bwana Stewart kama sehemu moja ya kulipiza kisasi. Kwa wakati huo, Kaposhoo hakuonekana kuhofia kitu chochote kile, alikuwa akitaka kumuua Gloria na Bwana Stewart tu.
Mara baada ya kutoka nyumbani kwa mzee Des, moja kwa moja akaelekea katika hoteli ya Barbie na kisha kuchukua chumba huku muda wote kichwa chake kikiwa kimefunikwa na kofia kubwa ya Malboro ili asiweze kutambulika na mtu yeyote yule.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Katika kipindi hicho, taarifa bado zilikuwa zikiendelea kutolewa kwamba mwili wa Peter ulikuwa umekutwa katika msitu wa Mopani huku ukiwa umepigwa risasi tatu kifuani. Kadri Peter alivyokuwa akiiona habari ile pamoja na mwili wa Peter moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makubwa, hakuamini kwamba Peter alikuwa amekufa kabla hajatekeleza suala lake la kumuomba msamaha.
Hasira zake zilikuwa kwa wote wawili, hakuona kama watu hao walikuwa wakistahili kuendelea kuishi na wakati walikuwa wameuumiza moyo wake kwa kitendo chao cha kumuua Peter. Kaposhoo aliendelea kukaa ndani ya hoteli ile mpaka ilipofika usiku ambapo akaondoka mahali hapo na kwenda kuchukua chumba katika hoteli ya Paradise 05, hoteli ambayo mara ya mwisho Gloria alikuwa akifanya kazi, hoteli ambayo Bwana Stewart alipokutana na msichana huyo.
Kofia kubwa ya Malboro pamoja na miwani mikubwa ya jua ikaonekana kumsaidia kutokugundulika na wafanyakazi wa hoteli ile jambo ambalo lilimpa urahisi wa kufanikisha kile ambacho alikuwa amekipanga kukifanikisha. Akapewa chumba ndani ya hoteli hiyo, moyoni bado alikuwa na dukuduku kubwa la kutekeleza kile kilichokuwa kimemleta ndani ya hoteli ile, kumuua Gloria na Bwana Stewart ambao piga ua ilikuwa ni lazima waje ndani ya hoteli ile.
“Hizi risasi tano, zinatosha” Kaposhoo alijisemea huku akiziangalia risasi ambazo zilikuwa katika bunduki yake.
Je nini kitaendelea?
Je Fetty na Peter wataweza kufanikisha jambo lao la kumuua Gloria?
Je Kaposhoo ataweza kumuua Gloria na Bwana Stewart?
Dizaini kama unachanganyikiwa hivi.....Usijali, ukiifuatilia kwa makini utaielewa tu.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment