Simulizi: Uliniua Gloria
Sehemu Ya Tano (5)
Fetty alikuwa akitamani kuishi maisha ya raha pamoja na mpenzi wake, Peter ambaye alikuwa akimpa mapenzi motomoto. Uwepo wa Gloria ulionekana kumnyima taha kwa kuona kwamba ingetokea siku ambayo Peter angeweza kumsamehe msichana huyo na kisha kurudiana nae na yeye kuyakosa mapenzi ambayo alikuwa akiyapata katika kipindi hicho. Ukiachana na hilo, Fetty alikuwa ameumia kupita kawaida, kitendo cha msichana Gloria kumsababishia mambo yale Peter ilionekana kumuumiza kupita kawaida.
Japokuwa katika kipindi ambacho yote yalipokuwa yakitokea hakuwa pamoja na Peter lakini moyoni alihisi maumivu makali mno. Katika kila kitu ambacho alikuwa akikifikiria mahali hapo, alijiona kuwa na kila sababu za kumuua msichana huyo kwani aliona endapo angemuacha, mambo yangeweza kuwa mabaya hapo baadae.
“Kwa nini unataka huyo msichana auawe?” Lilikuwa swali la kwanza aliloliuliza mzee Seif.
“Kwa sababu ananiingilia katika mahusiano yangu na mpenzi wangu” Fetty alimjibu baba yake.
“Sasa hilo tu tu ndio unataka ukatishe uhai wake. Kama ni mapenzi, pigania penzi lako usipokonywe” Mzee Seif alimwambia Fetty.
“Si hilo tu baba. Msichana huyu amekuwa katika mipango na kundi la waasi la ZSAG. Na nimesikia kuna mpango wa kuwateketeza matajiri wote ukiwepo wewe” Fetty alimwambia baba yake huku akijifanya kuongea kwa huzuni.
“Unasemaje?”
“Ndio hivyo baba. Amekuwa akifanya mambo kama hayo kwa matajiri wengi, yeye ndiye huwa kiunganishi kikubwa na anafanya kazi kisiri” Fetty alimwambia baba yake.
“Umeyapata wapi yote haya?”
“Dunia haina siri baba. Hata kama utajisaidia usiku wa saa tisa uchochoroni, asubuhi utafuatwa na kuambiwa ukatoe uchafu wako” Fetty alimwambia baba yake maneno ambayo yalimfanya kuwa kimya kwa muda.
Maneno yale yakawa kama sumu moyoni mwa mzee Seif. Ni kweli alikuwa ni tajiri mkubwa mwenye pesa nyingi, alikuwa radhi kufanya kitu chochote kile katika maisha yake lakini mwisho wa siku awe na ulinzi mkubwa wa fedha zake. Hakutaka kufa, hakutaka kuona akiziacha fedha mikononi mwa watu na wakati yeye ndiye aliyezitafuta kwa jasho lake, kila alipokuwa akisikia mtu fulani anataka kukuua, alikuwa akichukua maamuzi ya ghafla bila kukaa chini na kujifikiria.
“Huyo msichana anaishi wapi?” Mzee Seif alimuuliza.
“Bado sijafahamu, ila anafanya kazi katika hoteli ya Paradise 05 na anaitwa Gloria Michael” Fetty alimwambia baba yake.
“Ngoja nilifanyie kazi. Sipendi kuona mtu akiyaingilia maisha yangu” Mzee Seif alimwambia Fetty.
Mzee Seif alionekana kukasirika, katika maisha yake kila siku alikuwa akipenda kujiona akiwa juu tu na wala hakutaka kumuona mtu yeyote akiyaingilia maisha yake. Moyoni alikuwa na hasira na msichana huyo, Gloria ambaye wala hakuwa amemuona au kumsikia siku yoyote au kwa mtu yeyote zaidi ya mtoto wake, Fetty.
Alichokifanya ni kuwaita vijana wake ambao akawapanga vilivyo na kisha kuwapa maagizo juu ya kila kitu ambacho kilitakiwa kufanyika kwa wakati huo. Mchakato ukafanyika na usiku wa siku hiyo vijana watatu walikuwa wamekwenda katika hoteli ya Paradise kwa ajili ya kumtafuta msichana huyo na kisha kukamilisha jambo lao.
Kwa sababu ilikuwa moja ya hoteli kubwa ya kimataifa, walichokifanya ni kuchukua chumba na kisha kutulia chumbani. Mpaka hapo, wakawa wanajiuliza ni wapi pa kuanzia mpaka kumpata msichana huyo ambaye walikuwa na kazi nae. Vijana wale, Ibrahim, Denti na Sumi wakatulia chumbani huku wakijadili ni kipi ambacho kilitakiwa kufanyika baada ya hapo.
“Cha msingi tumuulizieni, au mnahofia?” Denti aliwaambia wenzake.
“Hilo ni wazo zuri pia. Baada ya hapo?” Sumi aliuliza.
“Baada ya hapo ni kumuua tu, au nyie mnaonaje?” Denti alijibu.
“Sawa. Tumuue kwa kipi sasa?”
“Labda risasi” Ibrahim aliingilia.
“Hilo gumu. Hatuhitaji kukamatwa. Cha msingi yatupasa kufanya kitu kimoja tu” Denti aliwaambia.
“Kitu gani?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwanza tujue huyu Gloria anahusika vipi ndani ya hoteli hii. Je ni mlinzi, mhudumu au yupo vipi” Denti alijibu.
“Hakuna tatizo”
Hilo ndilo ambalo walitaka kulifanya kwa wakati huo. Kwanza wakataka kufahamu kazi ambayo alikuwa akiifanya Gloria ndani ya hoteli hiyo hata kabla hawajafanya kile ambacho walitaka kukifanya mahali hapo. Kitu kilichofanyika, Denti akatumiwa na wenzake katika kutekeleza kile ambacho walikuwa wamekiongea. Wakamtaka kuongea na mhudumu mmoja na kisha kumuulizia kuhusu Gloria. Hilo wala halikuwa tatizo, ndani ya saa moja tu, Denti alikuwa meza moja na mmoja wa wahudumu wa hoteli ile, ndani ya mghahawa wa hoteli ile.
“Samahani” Denti alimwambia mhudumu huyo ambaye alimsogelea.
“Unalipwa kiasi gani kwa siku kama malupulupu?” Denti alimuuliza msichana yule ambaye alionekana kumshangaa kwa swali lile.
“Kwacha elfu mbili mpaka elfu mbili mia tano” Mhudumu yule alijibu.
“Sawa. Leo nataka kukupa ofa kama utanijibu maswali yangu. Kila swali nitakupa kwacha mia mbili. Upo tayari?” Denti alimuuliza mhudumu yule aliyejitambulisha kwa jina la Rachel.
“Hakuna tatizo” Rachel alijibu.
“Umeanza kufanya kazi hapa kwa muda gani?” Lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa Denti.
“Miaka miwili” Rachel alijibu, hapo hapo Denti akaingiza mkono wake mfukoni na kutoa kwacha mia mbili na hamsini na kumpa.
“Toka ufanye kazi hapa, unaifurahia kazi yako?” Denti alimuuliza.
“Ndio” Rachel alijibu na Denti kumlipa tena.
“Na kama kuna hoteli inakuhitaji huduma yako, utakuwa tayari kama maslai yatakuwa mazuri zaidi ya hapa?” Denti alimuuliza.
“Nitakubali” Rachel alijibu na kiasi cha makubaliano kuwekwa mezani.
“Toka ufanye kazi hapa, kuna watanzania wangapi wamewahi kufanya kazi hapa?” Denti alimuuliza.
“Walikuwa wengi ila waliondoka. Kwa sasa yupo mmoja tu” Rachel alijibu na kisha kama kawaida yake, Denti akaweka kiasi kile mezani.
“Huyu wa sasa anaitwa nani?”
“Anaitwa Gloria”
“Ninaweza kumuona?”
“Hapana. Ni msichana wa bosi”
“Kwa hiyo kama wa bosi haruhusiwi kuonana na wateja?”
“Inawezekana kama utakuwa na jambo la msingi”
“Kama jambo gani hivi?”
“Kama unataka kuweka oda maalumu kuanzia watu hamsini” Rachel alijibu huku kila alipokuwa akijibu, alikuwa akilipwa.
“Sawa. Nataka kuonana nae. Tunahitaji kufanya mkutano mahali hapa. Nitampataje sasa?” Denti alimuuliza Rachel.
“Ofisini kwake”
“Wapi?”
“Ghorofa ya pili. Ukifika hapo utakuta chumba kimoja kimeandikwa ‘Adminstration’”
“Asante”
“Asante pia”
“Nadhani nimekulipa sawa na makubaliano yetu”
“Yeah! Nashukuru sana” Rachel alijibu na kisha kuondoka mahali hapo.
Denti hakutaka kuendelea kukaa mahali hapo, tayari kile alichokuwa akikitaka alikuwa amekwishakipata alichokifanya ni kurudi chumbani na kisha kuwaambia wenzake kile ambacho kilikuwa kimeendelea kwa mhudumu yule. Kila mtu akaona kwamba walikuwa wamefanikiwa kwa asilimia zaidi ya sitini na kilichobakia ni kufanya utekelezaji tu.
Hawakutaka kumfuata siku hiyo, walichokipanga ni kumfuata siku inayofuatia ambapo huko wangeweza kumuua ndani ya ofisi yake. Wote watatu wakakubaliana na hivyo kumtaarifu mzee Seif kile ambacho kilikuwa kimeendelea.
“Msimuue hapo hotelini” Mzee Seif alisikika akiwaambia.
“Tumuulie wapi sasa?”
“Mpelekeni katika msitu wa Mopani” Mzee Seif alijibu.
“Sawa. Hakuna tatizo” Denti alisema.
Kwa wale wanaoonekana kuchanganyikiwa. Nawasaidia kwa kufafanua.
Kaposhoo amekaa katika nyumba ya Bwana Des kwa muda wa miezi miwili. Amepona na kuondoka huku akiambiwa kwamba Peter ameuawa msituni siku iliyopita na ameuliwa na msichana ambaye ni Gloria.
Kwa upande wa Peter, alipokutana na wale vijana wawili, ilikuwa ni miezi miwili iliyopita kabla ya Kaposhoo kupona. Peter alianza mahusiano na Fetty, mwezi wa kwanza ukapita, kumbuka mwezi huo Kaposhoo alikuwa akiumwa, mwezi wa pili ukaingia ulipofika mwezi wa pili na nusu, ndio Fetty kamwambia baba yake kuhusiana na Gloria huku katika mwezi huo huo ndio Kaposhoo ameruhusiwa kutoka kwa mzee Des. Kwa hiyo ni hadithi moja iliyokuwa na vipindi viwili tofauti, miezi miwili na nusu mbele na miezi miwili na nusu nyuma.
Kwa sasa, miezi inakwenda sawa ila siku zimetofautiana kidogo. Kwa Kaposhoo, siku zipo mbele na ndipo kapewa taarifa kwamba Peter kauawa jana. Hiyo jana ndio siku ambayo vijana wa mzee Seif wamepanga kumchukua Gloria kumpeleka msituni ambapo ndipo Peter alipouawa na Gloria.
Baada ya Peter kuuawa, Gloria ndio anarudi hotelini ambapo leo hii ndio Kaposhoo amekuja kupanga ndani ya hoteli hiyo.
Kutokuelewa mazingira ya hadithi mnanifanya mpaka nielezee mpaka kitakachoendelea kitu ambacho kinatoa hamasa ya hadithi kabisa. Hadithi inaeleweka vizuri ila wengine mmezoea hadithi zile zinazokwenda moja kwa moja. Kwangu, hadithi zinachezwa kwa matukio tofauti, nyakati tofauti lakini baadae matukio yanaunganishwa pamoja na muda unakuwa mmoja. Hadithi za mashuleni kidogo zimetufanya tuzoee hadithi za kwenda moja kwa moja. Kwa sasa, uandishi umekaa kisasa zaidi na ndio maana hata filamu za Marekani ukiziona zinakutamanisha kuziangalia kila siku kutokana na matukio yake kuchanganywa huku na kule lakini mwisho wa siku kuungana.
Ninafanya hivi kama njia mojawapo ya kuonekana mwandishi wa tofauti. Hebu sasa endelea kuisoma ujue nini kilitokea baada ya Gloria kumuua Peter. Maswali yenu, hadithi imekwishajulikana kitakachoendelea, ila kuna kitu kimoja bado hamjakifahamu, kitu ambacho nitawaambia mrudi sehemu ya kwanza kabisa kurudia kuisoma.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mapenzi yao yalikuwa yametimiza miezi miwili na nusu katika kipindi ambacho msichana Fetty alikuwa akitamani sana kumuona Gloria akifa tena mbele ya uso wa mpenzi wake wa zamani, Peter. Kwa fetty, hakuonekana kuwa na wasiwasi na vijana wa mzee wake ambao walikuwa wametumwa katika kutekeleza kila kitu kilichotakiwa kutekelezwa kwa wakati huo.
Bila Gloria kuuawa, Fetty hakuonekana kuwa na raha hata kidogo, alikuwa akitamani kumuona msichana Gloria akionja mauti na ndipo hapo ambapo angekuwa na furaha na kile kilichokuwa kinaendelea katika maisha yake. Fetty alikuwa akimpenda Peter kwa mapenzi ya dhati, hakutaka kabisa kumuona mtu mwingine akiyaingilia mapenzi yale ambayo yalikuwa yamechanua sana.
Kila siku ndoto zake zilikuwa ni kuona akiolewa na Peter, hakutaka kumuachia katika mikono yake, alikuwa akitaka kuwa nae mpaka pale ambapo kifo kingewatenganisha kwa kila mtu kwenda kwenye kaburi lake. Mapenzi ambayo alikuwa akiyapata kutoka kwa peter ndio ambayo yalikuwa yakimuonyeshea ni kwa jinsi gani yalikuwa na thamani, hapo ndipo alipoigundua ile fuaraha ambayo ilikuwa ikizungumziwa na watu wengi walikuwa katika mapenzi.
Masikio ya fetty katika kipindi hicho yalikuwa yakimsikilizia baba yake tu, kila wakati alikuwa akitaka kusikia ni kitu gani ambacho kilikuwa kimeendelea kule walipokwenda kwa ajili ya kumuua Gloria. Mzee seif hakusema kitu chochote, ila kila alipokuwa akiulizwa alisema kwamba kila kitu kilikuwa kwenye mipango yake.
“Mipango kila siku baba” Fetty alimwambia baba yake huku akionekana kushangaa.
“Kuua mtu si jambo dogo binti yangu. Yakupasa kujipanga sana” Mzee Seif alimwambia Fetty.
“Kwa hiyo sasa hivi wamefikia wapi?” Fetty aliuliza.
“Wamekwishafika hotelini”
“Kwa hiyo kazi imebakia moja tu, kumuua?” Fetty aliuliza huku akionekana kutabasamu.
“Ndio”
“Sasa hapo kweli inaweza kuchukua muda mrefu katika kufanikisha hilo baba?” Fetty alimuuliza baba yake, mzee Seif.
“Inategemea. Lakini hebu tuachie kila kitu katika mikono yao, mipango imesukwa na kusukika, hautakiwi kuhofia juu ya hilo” Mzee Seif alimwambia fetty.
Fetty hakuwa na msemo tena, kwa sababu alitakiwa kukiacha kila kitu mikononi mwa vijana wale ambao walikuwa wametumwa kwa ajili ya kutekeleza kila kitu, hakutakiwa kuwa na hofu. Moyoni, alikuwa akitamani kuishi na Peter hata zaidi ya kile kipindi cha miezi miwili na nusu iliyopita, alikuwa akitaka kuishi nae zaidi na zaidi, alikuwa akihitaji kuendelea kuyaona mapenzi yale ambayo alikuwa akipewa.
“Wamesemaje?” Peter alimuuliza Fetty.
“Ndio wanakaribia kutekeleza kila kitu”
“Kwa hiyo watamuua hivi karibuni?”
“Ndio”
“Safi sana. Nitataka kumuua huyo Gloria kwa mikono yangu mwenyewe. Nitaruhusiwa?” Peter alimuuliza Fetty huku akionekana kuwa na hasira na Gloria.
“Bila shaka kipenzi” Fetty alijibu huku akitoa tabasamu pana.
*****
Denti, Sumi na Ibrahim walikuwa wakiendelea na mipango yao kama kawaida. Walikuwa wakitaka kuhakikisha kwamba msichana Gloria anauawa hata kabla ya mambo mengine kuendelea. Mpaka kufikia hatua hiyo tayari walikwishajua kwamba ni kwa namna gani walikuwa na uwezo wa kumfikia Gloria na kisha kumteka kama walivyotaka iwe.
Tayari walikwishaambiwa kwamba walitakiwa kumpeleka Gloria katika msitu wa Mopani mara baada ya kukamilisha kumteka na huko ndipo ambapo wangempigia simu mzee Seif ambaye angefika mahali hapo na kisha kutoa uamuzi juu ya kifo cha aina gani ambacho alitakiwa kuuawa mahali hapo.
“Leo ndio tunakamilisha kila kitu” Denti aliwaambia wenzake.
“Hakuna tatizo. Kwa sababu tumeamka salama asubuhi hii, naamini Mungu amekusudia tufanikishe suala letu” Sumi alimwambia Denti.
“Kwa hiyo unamaanisha tumteke na kisha tumpeleke Mopani?” Ibrahim aliuliza.
“Hayo ndio yalikuwa maelezo ya mzee”
“Baada ya hapo, nini kifuate?”
“Kumpigia simu na kumwambia kwamba kila alichotuambia kilikuwa kimefanikiwa. Hakuna cha zaidi” Denti alimwambia Ibrahim.
“Sawa. Hakuna tatizo. Ila nahisi tunatakiwa kwanza kufanya jambo moja” Ibrahim aliwaambia.
“Jambo gani?”
“Hivi nani amewahi kufanya mapenzi na msichana wa kitanzania?” Ibrahim aliuliza swali ambalo lilimshangaza kila mtu.
“Unamaanisha nini?”
“Swali hamjalijibu. Gumu nini?”
“Mimi sijawahi” Sumi alimwambia Denti.
“Hata mimi sijawahi” Denti alijibu.
“Sasa kama hatujawahi, halafu na hizi tetesi tunazosikia kwamba wanawake wa kitanzania wameongezewa vitu fulani, kwa nini tusichukue nafasi hiyo kufanya mapenzi na huyu Mtanzania?” Ibrahim aliwaambia wenzake.
“Kwa hiyo unamaanisha tumbake?”
“Ndio maana yake. Niliongea vile kupunguza ukali wa maneno” Ibrahim aliwaambia.
“Hilo halina tatizo. Kwa hiyo tumteke, tumbake na kisha kumpigia simu mzee?” Denti aliuliza.
“Yeah! Ikiwezekana iwe hivyo. Au wakati tumempigia simu mzee, sisi tunambaka huku mzee akiwa njiani, nyie mnaonaje?” Ibrahim aliwaambia na kuwauliza.
“Hapo safi. Wazo zuri”
“Hata mimi nimeunga mkono” Sumi aliwaambia.
“Hivyo ndivyo ilivyo. Unaweza kufa ukiwa hujafanya mapenzi na mtanzania na wakati kila siku unasikia wana vitu vya ziada, huyu lazima tufanye nae” Ibrahim aliwaambia wenzake.
Huo ndio uamuzi ambao walikuwa wameuchukua katika kipindi hicho, kitu ambacho walikuwa wakikitaka ni kumteka Gloria, kumpeleka msituni Mopani na kisha kumbaka huku mzee Seif akiwa njiani kuelekea msituni huko kwa ajili ya kumuua Gloria. Hakukuwa na mtu yeyote ambaye aliutilia shaka uamuzi ule, ukaonekana kuwa uamuzi mzuri ambao ulitakiwa kufanyiwa kazi mara moja.
Ilipofika saa nne kamili asubuhi, Sumi akaambiwa kwenda kuandaa gari la kuondokea mahali hapo huku Denti na Ibrahim wakaanza kuelekea katika ofisi ya Gloria ambapo baada ya kuufikia mlango, wakaanza kuugonga na kisha kukaribishwa ndani. Machoni mwao, msichana Gloria alionekana kuwa mrembo sana, uzuri wake ulionekana kumtetemesha kila mmoja, mioyoni mwao, lile wazo la kutaka kumbaka likawa likizidi kushika hatamu zaidi.
“Karibuni” Gloria aliwakaribisha huku akionekana kutoa tabasamu pana.
“Asante” Wakaitikia na kisha kukaa vitini.
Sketi fupi aliyokuwa ameivaa Gloria ikaonekana kuwachanganya sana, mapaja mazuri meupe yalizidi kuwachanganya zaidi na zaidi. Urembo wa Gloria ukawafanya kuamini kwamba wanawake wa Kitanzania walikuwa wazuri sana ambao wala hawakutakiwa kuachwa au kuumizwa mapenzini. Maswali kibao yakaanza kumiminika vichwani mwao juu ya sababu ambayo ilimpelekea mzee Seif kutaka kumuua msichana mrembo namna ile.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tunahitaji chumba cha mikutano” Denti alimwambia Gloria mara baada ya kujitambulisha.
“Huwa tunakodisha kuanzia siku tatu ambapo kwa siku utalazimika kutoa kwacha elfu kumi na tano” Gloria alijibu huku tabasamu likiwa usoni mwake.
“Hakuna tatizo. Tutahitaji kukaa kwa muda wa siku saba pamoja na kuandaliwa vyumba kumi na saba kwa ajili ya wenzetu wa mkutano huo” Denti alimwambia Gloria.
“Hakuna tatizo. Mnaweza kulipia hapa” Gloria aliwaambia.
Alichokifanya Ibrahim ni kusimama na kisha kuufuata mlango na kuufunga. Hali ile ikaonekana kumshtua sana Gloria, muonekano wa Ibrahim ukaonekana kubadilika hasa mara baada ya kuufunga mlango ule. Gloria alitaka kuuliza swali, alipoyapeleka macho yake usoni mwa Denti, nae alikuwa amebadilika pia.
“Nini kinaendelea?” Gloria aliuliza huku wasiwasi ukianza kumuingia moyoni.
“Tumekuja kukuchukua” Denti alimwambia Gloria.
“Kunichukua? Kunipeleka wapi?” Gloria aliuliza huku akionekana kushtuka.
“Kuna sehemu tunataka kwenda nawe. Ila tumeambiwa tukuue endapo utaleta ubishi” Denti alimwambia Gloria huku akiitoa bunduki na kisha kumuonyeshea Gloria.
“Naomba msiniue” Gloria alisema huku akianza kutetemeka.
“Ukionyesha utii na unyenyekevu, hatutokuua ila ukijifanya mbishi, tutamwaga ubongo wako kama tulivyokuwa tukimwaga bongo za watu wengine” Denti alimwambia Gloria.
“Sawa. Sitoleta ubishi” Gloria alimwambia Denti.
“Kitu cha kwanza utakachotakiwa kukifanya, hautakiwi kuonyesha sura ya wasiwasi, yaani utakapoinuka hapo na kuondoka na sisi kuelekea nje, uso wako uwe na tabasamu tu. Umenielewa?” Denti alimwambia Gloria.
“Nimekuelewa” Gloria alijibu huku akitetemeka.
“Sawa. Simama”
Gloria akasimama na kisha kumuamuru kutangulia kutoka nje ya ofisi ile. Muda wote ambao Gloria alipokuwa akipiga hatua, uso wake ulikuwa ukionyesha tabasamu pana, tabasamu ambalo lilikuwa na hali ya wasiwasi. Wafanyakazi wengine hawakuonekana kuhofia kitu kabisa, mpaka wanashuka ngazi kuelekea chini, uso wa Gloria bado ulikuwa ukionyesha tabasamu huku akizungumza na watu wale kana kwamba hawakuwa watu wabaya kwake.
“Ingia ndani ya gari ile” Denti alimwambia Gloria na kisha kupiga hatua, akaingia ndani ya gari lile na kuondoka mahali hapo. Mpaka gari linaondoka, hakukuwa hata na mfanyakazi yeyote ambaye alihisi kitu kibaya, tabasamu alilokuwa akilionyesha Gloria pamoja na kuongea na watu wale katika hali ya kawaida, ilionekana kuwatia kipofu wafanyakazi wote ambao walikuwa wakimwangalia.
“Jamani nimefanya nini?” Gloria aliuliza ndani ya gari huku akianza kulia.
“Utajua mbele ya safari” Ibrahim alimwambia Gloria.
Kaposhoo alikuwa akivuta muda chumbani kwake, bunduki yake ilikuwa mkononi huku akionekana kuwa na hasira kupita kawaida. Siku hiyo alitaka kumuua Gloria pamoja na Bwana Stewart ambao hao wote walikuwa wamehusika katika maisha ya Peter kuwa maisha ya kutangatanga huku na kule mpaka pale alipouawa.
Moyo wake ulikuwa umejawa na hasira kupita kawaida, alikuwa akitaka kuwaua wote wawili kwa kile kitendo ambacho walikuwa wamekifanya. Alikaa nje ya nyumba yao kwa muda wa miezi miwili na nusu pasipo kuonana na baba yake pamoja na rafiki yake, Peter ambaye alikuwa akitamani sana kuonana nae na kumuomba msamaha kwa kile ambacho kilikuwa kimetokea.
Kwa wakati huo alikuwa amekwishachelewa kabisa, hata kabla haaonana na Peter na kumuomba msamaha kwa kila kilichotokea, mtu huyo alikuwa amekwishauawa. Kila alipokuwa akimkumbuka Peter, akiyakumbuka maumivu ambayo alikuwa ameyapata mara baada ya kupigwa risasi akajikuta akipata hasira zaidi za kuwaua watu hao wawili. Huku bunduki ikiwa mkononi mwake na mwili wake ukimtetemeka kwa hasira, hapo ndipo alipokumbuka kwamba alitakiwa kufanya kitu kimoja ambacho kingeonekana kuwa cha muhimu sana kwa wakati huo, kumpigia simu baba yake.
Akainuka kutoka kitandani na moja kwa moja kuifuata simu ya mezani ambayo ilikuwa ndani ya chumba kile na kisha kuanza kubonyeza vitufe vya namba ya baba yake ambayo alikuwa nayo kichwani mwake. Alipomaliza, simu ikaanza kuita na baada ya sekunde chache ikapokelewa.
“Hallow....! Ilisikika sauti ya mzee Mbwana ikiita.
“Hallow baba!” Kaposhoo aliita.
Kitendo cha kuisikia sauti ya baba yake, akajikuta akianza kutokwa na machozi, moyoni alijisikia faraja iliyokuwa na maumivu, maumivu makubwa ambayo kwa upande mwingine yakamletea furaha ambayo ikamsababishia kutokwa na machozi mfululizo. Alimkumbuka sana baba yake, kipindi cha miezi miwili na nusu kuishi bila kumuona baba yake kilikuwa kipindi kirefu sana ambacho wala hakutegemea kama kingeweza kutokea katika maisha yake duniani.
“Kaposhoo.....” Sauti ya mzee Mbwana ilisikika ikiita.
“Ni mimi baba” Kaposhoo aliitikia.
“Mungu wangu! Kuna nini kimetokea? Upo wapi?” Mzee Mbwana aliuliza maswali mawili mfululizo.
“Nipo sehemu fulani nimekuja kukamilisha kazi yangu mara moja” Kaposhoo alimwambia baba yake.
“Kazi gani?”
“Kwa watu walionifanya kupotezana na wewe kwa kipindi hiki kirefu” Kaposhoo alimwambia baba yake.
“Usijali Kaposhoo. Jana tu, yule mbaya wetu ameuawa huko msituni” Mzee Mbwana alimwambia Kaposhoo.
“Mbaya wetu yupi?”
“Peter. Yeye ndiye aliyesababisha haya yote. Peter ameuawa msituni, nadhani alikuwa akitaka kutoroka” Mzee Mbwana alimwambia Peter.
“Kifo chake kimenisikitisha sana baba. Yeye ndiye aliyenifanya leo hii kuwa hapa kwa ajili ya kulipiza kisasi cha kifo chake” Kaposhoo alimwambia baba yake.
“Unamaanisha nini?”
“Peter hakuhusika na kitu chochote kile baba” Kaposhoo alimwambia baba yake.
“Unasemaje?” Mzee Mbwana aliuliza huku sauti yake ikisikika kutokuamini.
“Huo ndio ukweli. Kuna watu walitumwa kwa ajili ya kuniua mimi, na ninadhani hao ndio wamemuua na Peter pia” Kaposhoo alimwambia baba yake.
“Unanichanganya. Watu gani?”
“Mmojawapo ni rafiki yako”
“Rafiki yangu? Yupi?”
“Stewart” Kaposhoo alimwambia baba yake ambaye alikaa kimya kwa muda wa dakika moja nzima.
“Baba...baba...baba” Kaposhoo aliita.
“Umesemaje?”
“Bwana Stewart ndiye alituma watu kwa ajili ya kuniua msituni” Kaposhoo alimwambia baba yake.
“Haiwezekani Kaposhoo. Haiwezekani Stewart kufanya hivyo” Mzee Mbwana alimwambia Kaposhoo.
“Huo ndio ukweli. Wamempakazia Peter kesi nyingi kama kumnyamazisha kwani anafahamu ukweli. Wote wanaamini kwamba nimeuawa ila haikuwa hivyo” Kaposhoo alimwambia baba yake.
“Wewe upo wapi?” Mzee Mbwana alimuuliza Kaposhoo.
“Nimekuja kulipiza kisasi kwa Stewart na msichana wake, Gloria” Kaposhoo alijibu.
“Kwani nae Gloria kahusika?”
“Huyo ndiye alikuwa chanzo wa haya yote. Ni lazima niwaue wote baba” Kaposhoo alimwambia baba yake huku akianza kulia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Stewart ninae huku kwenye mkutano” Mzee Mbwana alimwambia Kaposhoo.
“Mkutano gani?”
“Tumekutana matajiri kwa ajili ya kuchangia fedha za kusaidia watoto yatima na kuutokomeza umasikini” Mzee Mbwana alimwambia Kaposhoo.
“Naanza kwa kumuua Gloria, naomba ufanye juu chini kumteka huyo Stewart ili nikija nije kumalizana nae” Kaposhoo alimwambia baba yake.
“Hakuna tatizo. Lakini kwa nini usiache tu ili niwatume vijana wangu wanifanyie kazi?” Mzee Mbwana aliuliza.
“Hapana baba. Acha niifanye kazi mimi mwenyewe” Kaposhoo alimwambia baba yake.
“Sawa. Ila huyu Stewart, ninae hapa, mpaka kieleweke” Mzee Mbwana alimwambia Kaposhoo na kisha kukata simu.
Kaposhoo hakutaka kuendelea kubaki ndani ya chumba hicho, kama kulia, tayari alikuwa amelia sana na katika kipindi hicho kilikuwa ni kipindi cha kufanya kile ambacho kilimfanya kuwa ndani ya hoteli ile. Akasimama na kisha kuanza kuondoka chumbani hapo huku bunduki yake ikiwa kiunoni mwake.
Kitu ambacho alikuwa akikitaka mahali hapo ni kuonana na Gloria tu na kisha kumuua huku akimsikilizia baba yake kukamilisha mchakato mzima wa kumteka Bwana Stewart na kisha kwenda kumuua kwa mikono yake mwenyewe. Alipofika mapokezi, akaanza kuulizia namna ya kumpata Gloria huku akihakikisha kwamba kofia yake kubwa ya Malboro ikiwa kichwani mwake.
“Toka alipoondoka jana, hajarudi mpaka leo” Msichana wa mapokezi alimwambia Kaposhoo bila ya kumgundua.
“Anaweza kurudi leo?” Kaposhoo aliuliza.
“Mmmh! Mpaka sasa hivi saa kumi na mbili jioni, sidhani kama ataweza kurudi. Kwani una umuhimu nae mkubwa?” Msichana yule alimuuliza.
“Yeah! Nina umuhimu nae mkubwa sana na nitafurahi kama nitaweza kumpata leo hii hii” Kaposhoo alimwambia msichana yule.
“labda uende nyumbani kwake”
“Anaishi wapi?”
“Anaishi Mutaba” msichana yule alijibu.
“Nyumba namba ngapi?”
“Wewe ukifika huko, ukiulizia kwa Stewart, utaonyeshewa” Msichana yule alijibu.
“Sawa” Kaposhoo aliitikia na kuondoka mahali hapo.
Mpaka kufikia hatua hiyo, alikuwa na uhakika wa kumpata Gloria na kisha kukamilisha kile ambacho alikuwa akitaka kukamilisha. Akachukua teksi ambayo ikaanza kumpeleka katika mtaa wa Mutaba. Kichwa chake katika kipindi hicho kilikuwa kikimfikiria Gloria, kadri ambavyo teksi ile ilivyokuwa ikielekea Mutaba na ndivyo ambavyo alikuwa akishikwa na hasira zaidi. Akaitoa bundiki yake iliyokuwa kiunoni na kisha kuanza kuiangalia, ilikuwa imejaa risasi za kutosha, kwa maana hiyo kilichokuwa kimebakia ni matumizi ya risasi hizo katika mwili wa Gloria tu.
Walipofika katika mtaa huo, akaulizia nyumba ya Bwana Stewart, akaelekezwa na kuanza kuelekea katika nyumba hiyo. Alipofika, mlinzi alikuwa getini, Kaposhoo akajitambulisha kwamba alikuwa mmoja wa vijana wa Bwana Stewart, akakaribishwa na kupelekwa katika sehemu ya wageni na kuambiwa asubiri hapo huku mlinzi akienda kumwambia mfanyakazi wa ndani amuite Gloria kwani Bwana Stewart hakuwepo nyumbani muda huo.
“Mwambie nakuja” Sauti ya Gloria ilisikika kutoka ndani akimwambia mfanyakazi.
Kaposhoo alionekana kuwa na presha, kitu ambacho alikuwa akikitaka mahali hapo kilikuwa ni kumuona Gloria na kisha kumuua kama alivyokuwa amepanga. Bunduki yake bado ilikuwa kiunoni na alionekana kuwa na hasira kupita kawaida. Kiu yake kubwa kwa wakati huo ilikuwa ni kumuua Gloria na kisha kuondoka mahali hapo.
Alimsikia Gloria akiwa amemwambia mfanyakazi wa ndani kwa sauti ya juu kwamba angefika pale nje ambapo mgeni wake alikuwa akimsubiria. Wala hazikupita dakika nyingi, Gloria akatokea mahali hapo. Kitu cha kwanza alichokifanya ni kumwangalia mwanaume yule ambaye alikuwa amekaa katika moja ya viti ambavyo vilikuwa katika sehemu maalumu ya kukaa wageni na kufanya mazungumzo na mwenyeji, hakuweza kuuona uso wa mtu huyo kwani alikuwa amekiinamisha kichwa chake na ki kofia ya Malboro tu ambayo alikuwa ameivaa kuonekana kwa juu.
Gloria alionekana kuwa na wasiwasi na mgeni huyo, kitendo cha kutekwa na watu ambao walikuwa wametumwa na mtu aliyefikiria kwamba Peter kilikuwa kimempa wasiwasi mkubwa. Kitu cha kwanza ambacho alikuwa amekifikiria hapo ni kuona kwamba inawezekana Peter hakuwa amekufa jana na alikuwa mahali hapo kwa ajili ya kulipiza kisasi tu.
“Wewe ni nani?” Gloria alimuuliza kaposhoo huku akionekana kuwa na hofu.
Hapo hapo bila kuchelewa, Kaposhoo akauinua uso wake, uso ambao ulikuwa umezibwa na kofia ukaonekana, alikuwa Kaposhoo. Gloria akauhisi mwili wake ukipigwa ganzi, akatulia huku akionekana kuanza kutetemeka. Mtu ambaye alikuwa amefanyiwa mipango ya kuuawa na mwanaume ambaye alikuwa akiishi nae, leo hii alikuwa ndani ya eneo la nyumba yake.
Uso wa Kaposhoo haukuonekana kuwa na amani mahali hapo, alionekana kufika mahali hapo huku akiwa na shari moyoni mwake. Gloria hakutaka kukaa kwenye kiti, alikuwa akitetemeka na kitu ambacho alikuwa akikifikiria akilini mwake kwa wakati ule ni kukimbia tu. Huku hata kabla hajachukua uamuzi huo, akashtukia mdomo wa bunduki aliyoishika Kaposhoo ukimwangalia.
“Umeshtuka?” Kaposhoo alimuuliza Gloria ambaye alionekana kujawa na hofu.
“Kaposhoo” Gloria aliita huku akianza kunyanyua mikono juu kama ishara ya kukubali kuwekwa chini ya ulinzi.
“Usipige kelele, usiulize swali, yaani kwa kifupi, hautakiwi kuufungua mdomo wako” Kaposhoo alimwambia Gloria.
Kaposhoo akasimama kutoka pale alipokuwa amekaa, bunduki ambayo alikuwa ameishika akairudisha kiunoni kwa kuona kwamba Gloria asingeweza kumzidi nguvu endapo angeleta purukushani. Akaanza kupiga hatua kumfuata Gloria, alipomfikia, akamwangalia kwa makini usoni, akajikuta akizidi kujawa na hasira.
“Twende ndani” Kaposhoo alimwambia Gloria ambaye wala hakuonekana kuweka kipingamizi chochote kile.
Mlinzi hakujua kitu kilichokuwa kikiendelea, mbele ya macho yake kila kitu kilionekana kuwa sawa tu. Alimuona Kaposhoo akiwa amesimama mbele ya Gloria na kisha kuanza kuelekea ndani kitu ambacho alijua kwamba kulikuwa na maongezi ambayo walikuwa wakitaka kuongelea ndani kwa muda huo, hivyo akaendelea na shughuli zake kama kawaida.
“Kwa nini umeamua kuyafanya haya Gloria?” Lilikuwa swali la kwanza ambalo aliliuliza Kaposhoo mara baada ya kufika sebuleni na kukaa makochi tofauti, alihakikisha bunduki yake inakaa sawa kiunoni.
“Naomba unisamehe Kaposhoo” Gloria alimwambia Kaposhoo.
“Nikusamehe? Pamoja na maumivu yote uliyosababisha moyoni mwangu, pamoja na maumivu yote uliyosababisha moyoni mwa Peter, pamoja na mauaji uliyoyafanya ya kumuua Peter, leo hii, muda huu unasimama mbele yangu na kuniambia nikusamehe. Nitaanzia wapi kukusamehe wewe kahaba? Nitaanzia wapi kukusamehe wewe muuaji? Toka lini ukaona muuaji akisamehewa?” Kaposhoo alimwambia Gloria na kisha kumuuliza.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Gloria akasimama na kisha kupiga magoti. Akaanza kulia, machozi yalikuwa yakimtoka mfululizo. Kitu ambacho alikuwa akikiamini kwa wakati huo ni kwamba Kaposhoo angeweza kumsamehe kwa yote ambayo alikuwa ameyafanya. Aliyaamini machozi yake kwamba yangeweza kubadilisha kila kitu kilichotaka kutokea mahali pale.
“Nimekosa Kaposhoo. Nilikuwa na tamaa ya fedha, nilikuwa nimezuzuka na fedha nilizokuwa nikiahidiwa kupewa. Naomba unisamehe...naomba unisamehe Kaposhoo” Gloria alisema huku akilia kama mtoto.
“Baada ya kukusamehe utamrudisha Peter duniani? Baada ya kukusamehe utaweza kuirudisha furaha yangu ambayo ilipotea? Sema wewe malaya, utaweza kumrudisha Peter duniani?” Kaposhoo aliuliza kwa sauti ya juu huku akionekana kuwa na hasira sana. Gloria akabaki kimya.
“Mshahara wa dhambi ni mauti, ukiua kwa upanga nawe utauliwa kwa upanga Gloria” Kaposhoo alisema huku akiichomoa bunduki yake kutoka kiunoni mwake.
Kadri alivyokuwa akimwangalia Gloria na ndivyo ambavyo hasira zaidi zilivyokuwa zikimpanda. Hakumpenda Gloria, alikuwa akimchukia sana na alikuwa tayari kwa kitu chochote kile kwa wakati huo. Hakuwa na mawazo yoyote ya kumsamehe Gloria. Alikuwa amemfanyia mambo makubwa na mabaya ambayo hayakuweza kusimulika, kama angemuacha hai Gloria mahali hapo, aliamini kwamba alikuwa akikisaliti kiapo chake ambacho alijiwekea moyoni mwake, mbele ya baba yake na mbele ya mzee Deus.
“NI LAZIMA NIKUUE” Kaposhoo alisema kwa hasira huku akiwa amemnyoonyeshea bunduki Gloria kichwani.
“Naomba unisam....” Gloria alisema lakini hata kabla hajamaliza sentensi yake, milio ya risasi ikasikika sebuleni hapo.
“Paaa....Paaa....Paaa...Paaa...” Milio minne ya risasi ikasikika mahali hapo, damu zikatapakaa, kichwa cha Gloria kilikuwa kimefumuliwa na risasi zile, mwili wake ukadondoka chini na kutulia, risasi zile zilikuwa zimekatisha uhai wake.
Kaposhoo hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kutoka sebuleni pale. Getini, mlinzi hakuonekana, alikuwa amekimbia mara baada ya kusikia milio kadhaa ya risasi ambayo ilitoka sebuleni. Kwa mwendo wa kasi, Kaposhoo akaanza kuelekea katika mtaa wa pili, moyoni, alikuwa akijisikia uhuru, alijiona kama alikuwa kwenye kifungo fulani na katika muda huo alikuwa ameachwa huru.
“Bado huyu mpumbavu mwingine” Kaposhoo alisema huku akiendelea kupiga hatua kuelekea katika mtaa wa pili.
Alijiona kufanya kazi ambayo ilikuwa imempelekea kuingia ndani ya nyumba ile. Japokuwa katika kipindi cha nyuma alikuwa akimpenda sana Gloria lakini katika kipindi hicho alikuwa katika chuki kubwa, chuki ambayo ilimpelekea kummiminia risasi kadhaa Gloria kitu ambacho kwake kilionekana kuwa kama mshahara wa kile alichokuwa amemfanyia.
*****
SIKU MOJA KABLA:
Gloria alikuwa akilia ndani ya gari lakini hakukuwa na mtu yeyote yule ambaye alionekana kukijali kilio chake. Kila mmoja ndani ya gari lile alikuwa na wazo moja tu, kumbaka Gloria huku wakimsubiria mzee Seif ambaye angefika kule walipokuwa na kisha kuchukua uamuzi juu ya msichana huyo.
Sumi hakutaka kuendesha gari kwa mwendo wa kasi, alikuwa akiendesha kwa mwendo wa taratibu sana huku wakizidi kuelekea katika msitu wa Mopani. Kila mmoja ndani ya gari alikuwa na hamu ya kufanya mapenzi na Gloria. Sketi yake fupi ambayo alikuwa ameivaa, mapaja yake manene yaliyonona yalionekana kuwatia tamaa wote watatu kitu ambacho walijiona kuwa na kila sababu ya kufanya mapenzi na msichana huyo. Alichokifanya Denti ni kumpigia simu mzee Seif na kisha kumtaka kufika katika msitu wa Mopani kwa ajili ya kumkabidhi mtu wake ambaye alitaka atweke kwa haraka sana.
“Amesemaje?” Ibrahim alimuuliza Denti mara baada ya kuongea na mzee Seif.
“Anakuja” Denti alijibu.
“Jamani...naomba msiniue. Naombeni msiniue” Gloria aliwaambia vijana wale huku akianza kulia.
“Hatutokuua. Yaani hatutokuua kabisa. Niamini, nakuahidi, hakutokuwa na mtu yeyote ambaye atakuua” Ibrahim alimwambia Gloria.
“Naombeni msiniue” Gloria aliwaambia kwa mara ya pili.
“Hakuna atakayekuua. Sisi hatutoshika bunduki kukua ila huyu bosi wetu ndiye atasimamia shoo yote” Denti alimwambia Gloria.
Gloria hakuona hata dalili kama angeweza kupona, alijua dhahiri kwamba huko mbele ni lazima angeweza kuuawa kama vijana wale walivyokuwa wamemwambia. Hakuwa na kitu kingine cha kuweza kufanya zaidi ya kutumia maungo yake tu. Mapaja yake ambayo yalikuwa wazi kidogo yalionekana kuwachanganya vijana wale kiasi ambacho akaona kwamba ule ndio ulikuwa udhaifu wao na ilikuwa njia ya yeye kunusurika kuuawa.
Alichokifanya, akaanza kujishika huku na kule na kuipandisha sketi yake kisiri. Hakutaka vijana wale wajue lengo lake lakini alikuwa akifanya kila kitu kuhakikisha kwamba vijana wale wajue hakuwa akifanya makusudi. Sketi ile ikazidi kupanda zaidi na zaidi, wote wakaanza kuyaangalia mapaja yale kiwizi. Weupe wa Gloria na kunona kwa mapaja yake kukazifanya suruali zao kuinuka sehemu ya zipu, wote wakaonekana kuwa hoi.
Gloria hakuishia hapo, aliendelea zaidi na zaidi mpaka kufikia hatua ambayo nguo yake ya ndani kuanza kuonekana. Hapo ndipo ilikuwa balaa, kila mikao ambayo walikuwa wakijaribu kukaa ndani ya gari lile kwenye siti zao haikukalika, Gloria akaonekana kuwachanganya kupita kawaida, kila kitu ambacho kilikuwa kikionekana mwilini mwake kilikuwa kama kitu kifeni machoni mwa vijana wale.
“naombeni msiniue” Gloria aliwaambia vijana wale huku akiwa amebadilisha sauti, ilikuwa sauti ya mahaba, sauti ambayo ilipenya katika matundu ya masikio ya vijana wale, ikapiga ngoma za masikio yale, macho yao yalipotua tena kwenye nguo ya ndani ya Gloria, sauti ikapenya mpaka mioyoni mwao, wakawa hoi.
“Daaah! Mtihani sana huu. Ila tatizo ni nini mpaka bosi anataka kukuua mrembo?” Denti alimuuliza Gloria.
“Kwa sababu nilimnyima penzi” Gloria alimjibu Denti.
“Yaani kumnyima penzi tu ndio anataka kukuua. Daaah! Sasa na wewe kwa nini ulimnyima?” Ibrahim alidakia na kuuliza swali.
“Huwa sipendi kuwapa wazee. Mimi nawapenda vijana wenzangu kama nyie” Gloria aliwaambia.
Alichokifanya mahali pale ni kuuchukua mkono wa Denti na kisha kuupeleka kiunoni mwake, akamshikisha mkanda wa nguo yake ya ndani na kisha kuuteremsha ule mkono chini. Denti akaonekana kuchanganyikiwa, nguo ya ndani ya Gloria ambayo ilionekana kuwa kama na vinyavunyavu ikaonekana kumpagawisha sana.
Gloria hakuishia hapo. Alijiona kuwa na kila sababu ya kucheza mchezo wa kijasiri mahali hapo. Alichokifanya ni kuuchukua mkono wa Ibrahim na kuufanya kama alivyomfanyia Denti, wote wawili wakawa wamechanganyikiwa, wakasahau majukumu yao na hivyo kuanza kumtomasatomasa Gloria ambaye alikuwa akijifanya kama kuchanganyikiwa kumbe ilikuwa ni njia moja ya kuwachanganya vijana wale.
Sumi ambaye alikuwa akiendesha gari, akaanza kusikia miguno kutoka nyuma ya gari, akili yake haikutulia, kila wakati alikuwa akishikwa na tamaa ya kuelekea kule nyuma ya gari. Alipoona kwamba miguno imekuwa mingi, akalipaki gari pembeni na kisha kuanza kuwaangalia.
“Tuendelee na safari, mbona umelipaki gari tena?” Denti alimuuliza Sumi ambaye alikuwa akiwaangalia.
“Hivi unafikiri hata gari linaendesheka vizuri kwa hali hii” Sumi aliwaambia.
“Kwa nini lisiendesheke vizuri?”
“Njoo wewe uendeshe uone kama utaweza”
“Kwani halina mafuta?”
“Mafuta yapo”
“Sasa kwa nini haliendesheki?” Denti alimuuliza Sumi ambaye muda mwingi macho yake yalikuwa katikati ya mapaja ya Gloria ambaye alikuwa ameyapanua tu kama njia mojawapo ya kumchanganya mpaka Sumi.
“Nyie mmekaa huku nyuma mnafaidi peke yenu tu hata kunishtua hamnishtui kama mmefikia hatua hiyo” Sumi aliwaambia.
“Acha ujinga Sumi. Endesha gari” Ibrahim alimwambia Sumi.
“Kama unaona kuendesha gari ni kazi nyepesi katika kipindi kama hiki, njoo uendeshe wewe” Sumi alimwambia Ibrahim.
“Mimi sina leseni. Endesha tu” Ibrahim alimwambia Sumi.
“Siwezi. Hali mbaya. Tunaweza hata kupata ajali” Sumi aliwaambia.
Kila mmoja mahali hapo alikuwa amekataa kuendesha gari, mapaja ya Gloria pamoja na nguo yake ya ndani vilikuwa ni vitu ambavyo vilimchanganya kila mmoja mahali pale. Hilo ndilo lilikuwa lengo la Gloria lakini aliona kwamba endapo kusingekuwa na mtu atakayeendesha gari basi asingeweza kufanikisha kile alichokipanga. Alichokifanya ni kumsogelea Sumi, akamnyonya mdomo wake na kumtaka kuendesha gari huku akimuahidi kumpa penzi kubwa zaidi ya wale wengine.
Maneno yale yakamuingia Sumi na kumchanganya kabisa, ahadi ya uongo ambayo alipewa na Gloria ikaonekana kumchanganya sana, akaushikilia usukani na kisha kuendelea na safari tena mara hii ilikuwa ni kwa mwendo wa kasi sana huku akitaka kufika haraka na hivyo kukamilisha kila kitu.
Gari zima likatawaliwa na pepo la ngono, wakasahau wajibu wao, kitu ambacho walikuwa wakikifikiria kwa wakati huo kilikuwa ni kufanya mapenzi na Gloria tu ambaye muda wote nae alikuwa akijifanya kuchanganyikiwa kumbe hakukuwa na kitu chochote kile. Safari iliendelea kwa zaidi ya masaa mawili, wote walikuwa wakiishia kumchezea Gloria lakini kwenye kuivua nguo yake ya ndani alionekana kuleta kipingamizi cha mahaba, kipingamizi ambacho hakukuwa na mtu yeyote alionekana kukielewa zaidi ya kuona kwamba yale yote yalikuwa mahaba.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sasa mbona mmepaki porini?” Gloria aliuliza huku akijifanya kupandwa na pepo la ngono.
“Hapa ndipo bosi amesema tumsubiri” Denti alijibu huku Sumi akiwa amekwishatoka mbele na kuja nyuma, kazi yake ilikuwa ni kushika matiti ya Gloria tu.
“Mmmh! Mbona kunaonekana kama sio salama?”
“Ila hapa ndipo bosi anapotukuta kila anapotutuma kazi tumfanyie” Ibrahim alimwambia Gloria.
“Kwa hiyo nyie mtafurahi kuniona nauawa kwa mtu niliyemnyima penzi na kuamua kutaka kuwapa nyie kwa moyo mmoja?” Gloria aliwauliza.
“Bosi hawezi kukuua” Denti alimwambia Gloria.
“Hawezi kuniua na wakati nyie mmesema anakuja kuniua!”
“Hawezi. Tulikuwa tunakutania tu” Ibrahim alimwambia Gloria.
Wote watatu kitu ambacho walikuwa wakikifikiria mahali hapo kilikuwa ni kufanya mapenzi na Gloria tu ambaye alionekana kuwa mjanja zaidi yao hasa katika kuyatumia maungo yao vizuri. Ndani ya nusu saa, Gloria hakuwa ameivua nguo yake ya ndani japokuwa nguo zake nyingine zote zilikuwa zimetoka mwilini mwake. Kazi yake kubwa ilikuwa ni kuwachezea hapa na pale.
Zilipofika dakika arobaini na tano, muungurumo wa gari ukasikika ukilia, wote wakashtuka, walipoangalia kwa nyuma kupitia kioo cha nyuma, lilikuwa gari la bosi wao, mzee Seif ambaye alikuwa amekwishafika mahali hapo. Wote wakakurupuka na kisha kutoka nje, alichokifanya Gloria ni kuanza kuvaa nguo zake ndani ya gari huku wote wakiwa wametoka garini.
Alipomaliza kuzivaa nguo zake, akaangalia chini ya miguu yake, kulikuwa na bunduki ambayo alikuwa ameiweka Denti kiunoni na alikuwa ameichukua na kuificha chini bila mtu yeyote kufahamu kutokana na pepo la kufanya ngono ambalo lilikuwa limewatawala. Mzee Seif, Fetty na Peter walikuwa wameteremka kutoka garini na walifika hapo huku wakiwa na lengo moja tu, kumuua Gloria ambaye alikuwa na bunduki mkononi bila wao kufahamu.
Kikao cha matajiri kilikuwa kikiendelea ndani ya ukumbi wa hoteli ya Suliviana iliyokuwa pembezoni mwa jiji la Lusaka. Katika kipindi chote hasa mara baada ya kupokea simu kutoka kwa mtoto wake, Kaposhoo, mzee Mbwana hakuwa akimwangalia Bwana Stewart kwa macho mazuri. Uso wake ulionyesha dhahiri kwamba alikuwa na hasira sana na tajiri huyo kiasi ambacho alitamani kumrukia pale pale kikaoni na kumuua.
Moyoni aliumia sana, Bwana Stewart alionekana msaliti na mnafiki mkubwa ambaye alikuwa akimjaza maneno mengi ya kijinga hasa ya kumuonyeshea kwamba Peter ndiye ambaye alikuwa amehusika katika mauaji ya mtoto wake ambaye alikuwa akimpenda sana. Japokuwa mwanzoni alikuwa na umakini mkubwa katika mkutano huo lakini mara baada ya kupokea simu ya mtoto wake, Kaposhoo na kumwambia kwamba Bwana stewart ndiye ambaye alikuwa amehusika katika kila kitu, umakini mkutanoni pale ukaonekana kupotea kabisa.
“Haiwezekani” Mzee Mbwana alisema na kisha kuinuka kutoka kwenye kiti ambacho alikuwa amekaa na kuanza kuelekea nje.
Matajiri wengine ambao walikuwa mahali pale pamoja na waziri mkuu wakaanza kumwangalia mzee Mbwana huku wakionekana kutokufahamu ni kitu gani kilikuwa kikiendelea lakini hawakutaka kumuita na kuuliza kitu chochote kile. Kwa wakati huo mzee Mbwana hakuonekana kuwa makini kabisa, alionekana kukosa amani kabisa, kitendo cha kumwangalia Bwana Stewart mara kwa mara kilionekana kumkasirisha sana.
Alipofika nje, akachukua simu yake na kisha kuwapigia vijana wake. Kitu ambacho alikuwa amekifikiria mahali pale ni kumuua Bwana Stewart tu. Hakutaka kumuona mtu huyo akiendelea kuishi na wakati katika kipindi cha nyuma alikuwa akitaka kumuua mtoto wake.
“Nimesema njooni hapa Suliviana” Mzee Mbwana aliwaambia vijana wake huku akionekana kuwa na hasira.
“Sawa bosi. Ila ulipata habari kwamba yule mbaya wako Peter aliuawa jana?” Sauti ya kijana wake ilisikika simuni.
“Nilipata habari. Fanyeni haraka nawasubiria” Mzee Mbwana alisema na kisha kukata simu.
Majuto yakaanza kumuingia moyoni mwake, akaanza kujiona kuwa mkosefu kwa kile alichotaka kukifanya kila siku, kumuua Peter na wakati hakuwa amehusika katika kitu chochote kile. Kisasi kikubwa kilikuwa moyoni mwake, hakutaka kumuona mtu ambaye alikuwa akitamani kumuua mtoto wake wa pekee akiendelea kuishi, alijiona kuwa na mzigo mkubwa wa kumuua mtu huyo.
Baada ya dakika ishirini, vijana wale wakafika ndani ya hoteli hiyo ambapo akawapokea na kuwapeleka pembeni na kisha kufanya nao maongezi juu ya namna ambavyo mchezo ule ulivyotakiwa kuchezwa na kuhakikisha kwamba Bwana Stewart anauawa bila mtu yeyote yule kugundua.
“Kwa hiyo itakuwaje?” Kijana mmoja aliuliza.
“Nataka mfanye kitu kimoja. Hii ni kama njia mojawapo ya kujitoa mhanga” Mzee Mbwana aliwaambia.
“Njia gani?”
“Nataka mvamie katika ule mkutano unaendelea. Mkiingia ndani, mnamuua na kisha kutoka nje ya chumba kile” Mzee Mbwana aliwaambia.
“Mmmh! Mbona inaonekana kuwa hali ya hatari sana! Hatuwezi kukamatwa?” Kijana yule aliuliza.
“Kama mliweza kuwaua polisi ndani ya nyumba ya wageni ya Sasara mtashindwa kuwaua hawa polisi wachache waliokuwa ndani ya hoteli hii na nyie kukamilisha mambo? Mkiwa makini, hamuwezi kukamatwa. Fanyeni kazi hiyo, mkikamilisha, nitawapa malipo ambayo hamjawahi kulipwa toka mzaliwe” Mzee Mbwana aliwaambia.
“Kwa hiyo twende sasa hivi?”
“Hapana. Dakika thelathini baada ya mimi kuingia ndani ya chumba kile”
“Hakuna tatizo”
Mzee Mbwana hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka na kurudi katika chumba kile cha mkutano huku mkononi akiwa ameshika simu yake kama kuwadanganya watu waliokuwa ndani ya chumba kile kwamba alikuwa ametoka kuongea na mtu simuni.
Kidogo hapo akaonekana kutulia, aliwekea umakini mubwa ndani ya kikao kile huku shauku yake ikiwa ni kutaka kuona kama vijana wake wangeweza kukamilisha kile ambacho walitakiwa kukamilisha. Muda wote macho yake yalikuwa yakiangalia saa yake, dakika zilionekana kwenda taratibu sana zaidi ya siku nyingine, alikuwa akitaka kuona dakika thelathini zikikatika na vijana wake kuingia na kufanya kile walichokuwa wakitakiwa kukifanya.
****
Vijana wanne walikuwa wamejipanga kukabiliana na kile ambacho kilitakiwa kufanyika mahali hapo. Bunduki zao zilikuwa viunoni tayari kwa kufanya kile ambacho kilitakiwa kufanywa mahali hapo. Muda mwingi macho yao yalikuwa katika saa zao, walikuwa wakitaka kukamilisha kila kitu ndani ya muda mchache sana.
Nusu saa ilipoingia, moja kwa moja wakaanza kuelekea ndani ya hoteli ile. Walionekana kuwa makini sana na wote wanne walikuwa wamevalia suti za bei ya juu ili kuwatioa upofu wafanyakazi ndani ya hoteli ile kwamba walikuwa watu wabaya ambao walikuwa wamefika mahali pale kwa ajili ya kufanya mauaji tu. Hakukuonekana kuwa na mfanyakazi yeyote ambaye alionekana kuwatia hofu jambo ambalo liliwafanya kupanda mpaka katika ghorofa iliyokuwa na chumba cha mkutano na kutulia.
Nje ya chumba kile, polisi kama saba walikuwa wamesimama huku wakiwa na bunduki. Usalama mahali pale ulikuwa mkubwa lakini kutokana na muonekano ambao walikuwa nao vijana wale, walionekana kutokuwa watu wabaya kabisa. Polisi walipowaona, wakawasimamisha.
“Mnakwenda wapi?” Polisi mmoja aliwauliza.
“Kwenye chumba cha mkutano” Kijana yule ambaye alionekana kuwa kiongozi alimjibu polisi yule.
“Hapana. Hamtakiwi kwenda kule”
“Kwa nini?”
“Mkutano bado haujakwisha”
“Sawa” Kijana yule aliitikia.
Wakati yeye akiongea na polisi yule, vijana wengine kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwaangalia polisi wengine tu huku wakiwa tayari kwa kuchukua bunduki zao na kisha kuwamiminia risasi mfululizo. Waliwaweka kwenye target zao na kisha kusubiria tu kuanza kazi mahali hapo.
Hawakuwa hapo kwa ajili ya kupoteza muda mpaka mkutano uishe, walichokifanya ni kuchomoa bunduki zao. Lilikuwa ni tendo la ghafla sana ambalo halikuweza kushtukiwa kwa uharaka na polisi waliokuwa mahali pale. Milio ya risasi ikaanza kusikika katika korido ile, polisi wote wakaanguka chini na damu kutapakaa mahali pale. Walichokifanya ni kuufuata mlango wa kuingilia ndani ya chumba kile, walipoufikia, kijana mmoja akaupiga teke na kisha kuingia ndani.
Matajiri wote pamoja na waziri mkuu walikuwa kwenye hofu kubwa isipokuwa mzee Mbwana tu ambaye alikuwa akifahamu kila kitu. Vijana wale hawakutaka kuuliza swali lolote lile, wakaanza kumuangalia kila mmoja usoni, walipomuona Bwana stewart, wakamfuata na kisha kummiminia risasi mfululizo na kisha kutoka ndani ya chumba kile.
Ving’ora vya polisi vikaanza kusikika nje ya hoteli ile, walichokifanya mara baada ya kutoka katika korido ya ghorofa ile ni kupiga chombo ambacho kilikuwa na ishara ya kuonyesha kwamba hoteli ilikuwa ikiteketea moto au kuwa na balaa jingine lolote lile. Watu ambao walikuwa ndani ya vyumba vyao, wakatoka nje na kuanza kukimbia kuelekea nje.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Risasi ambazo zilikuwa zimesikika pamoja na mlio wa hatari ambao bado ulikuwa ukiendelea kulia ukawafanya watu wote kuwa na wasiwasi, zaidi ya watu mia saba ambao walikuwa ndani ya hoteli ile kubwa wakaanza kukimbia kuelekea nje, nao vijana wale wakaanza kukimbia pamoja nao.
Japokuwa polisi walikuwa wametanda nje pamoja na bunduki zao, hawakuonekana kuwa na uhuru wa kufanya chochote kile kwani watu wengi walikuwa wakitoka ndani ya hoteli ile pamoja na wale vijana tena huku wote wakionekana kukimbia kwa hofu kubwa jambo lililowapelekea kuwachanganya polisi wale.
“Ulihakikisha kwamba amekufa?” Kijana mmoja alimuuliza yule aliyempiga risasi Bwana Steart.
“Sikuhakikisha. Ila ninachojua nilimpiga risasi mbili kichwani mwake. Kama alikuwa na bullet proof kichwani nadhani hajafa ila kama hana, jua kwamba kafa” Kijana yule alimjibu mwenzake katika kipindi ambacho walikuwa wakiingia ndani ya gari huku watu wengine wakiendelea kukimbia ovyo. Huo ndio ukawa mwisho wa msaliti na mnafiki, Bwana Stewart ambaye kila siku alikuwa akitamani sana Peter kuonekana mbaya kwa mzee Mbwana ili apate kuuawa.
****
Safari ya kuelekea katika msitu wa Mopani bado ilikuwa ikiendelea. Ni watu watatu tu ndio ambao walikuwa ndani ya gari lile, Peter, mzee Seif pamoja na Fetty. Muda wote ule Peter alionekana kuwa na hasira kupita kawaida, macho yake yalikuwa na kiu kubwa ya kumuona Gloria, msichana ambaye alimuumiza sana moyoni mwake na kumfanya kuwa kama vile alivyokuwa katika kipindi kile.
Peter hakuongea kitu chochote kile, alikuwa kimya garini huku Fetty akiwa ameshikilia usukani. Kwa mze Seif, alionekana kuwa na hasira sana, hakupenda hata siku moja kumuona mtu yeyote akiyaingilia maisha yake. Kitendo cha kuambiwa kwamba msichana Gloria alikuwa nyuma ya kundi la waasi la ZSAG (Zambia Sldiers Against Government) na lengo lake kubwa lilikuwa ni kuhakikisha kwamba anakufa, ilionekana kumuuma sana mzee Seif.
Kwa wakati huo hakutaka kusikia kitu chochote kile, hakutaka kumuona mtu yeyote akimsimamisha juu ya kile ambacho alikuwa akitaka kukifanya mahali pale, moyo wake ulikuwa na kila sababu za kutaka kufanya kile ambacho alikuwa akitaka kufanya mahali pale.
Walichukua muda wa dakika arobaini na ndipo wakaingia ndani ya msitu ule ambapo kama kawaida yake, wakaanza kuelekea katika sehemu ambayo ilikuwa ikitumika kama makutanio yao msituni mule.
“Wale pale” Mzee Seif alisema mara baada ya kuliona gari la vijana wake likiwa limepakiwa pembeni kidogo.
Hata kabla wao hawajashuka kutoka garini, vijana wale wakateremka huku wakionekana kutokuwa kawaida, walionekana kuwa na jambo fulani ambalo walikuwa wakilifanya ndani ya gari. Peter akateremka kutoka garini pamoja na mzee Seif huku Fetty akitakiwa kubaki garini.
“Yupo wapi?” Mzee Seif alimuuliza Denti.
“Ndani ya gari”
“Sasa inakuwaje mnateremka ndani ya gari na kumuacha peke yake. Hebu nipe bunduki yako kwanza nikamuue kule kule” Mzee Seif alimwambia Denti.
Denti akajipapasa kiunoni mwake, hakuwa na bunduki yoyote ile jambo lililompelekea kugundua kwamba kulikuwa na uwezekano kwamba bunduki ile ilikuwa ndani ya gari. Alichokifanya ni kuanza kupiga hatua kurudi ndani ya gari, cha kushangaza kwa kila mtu, mara baada ya denti kuufungua mlango wa gari, mikono yake ikaenda juu kama hali ya kusalimu amri.
Gloria akateremka kutoka garini, mkono wake ulikuwa na bunduki ambayo alikuwa amemnyooshea Denti. Kila mmoja akaonekana kushtuka mahali pale, hakukuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa na bunduki zaidi ya Denti, bunduki ambayo ilikuwa mkononi mwa Gloria.
“Pigeni magoti na mikono kuwa vichwani mwenu” Gloria aliwaambia kwa sauti ya hasira iliyojaa ukali. Hakukuwa na mtu ambaye alipinga hilo, bunduki ambayo aliishika Gloria ilikuwa imempa nguvu.
“Umejifanya mjanja sana kuwakimbia polisi ila jua kwamba kamwe huwezi kunikimbia mimi. Ninakuua leo hii hii hapa polisini kama ulivyotaka kuniua na kisu nyumbani” Gloria alimwambia Peter ambaye alikuwa akitetemeka, kichwa chake kiliona kama kitu kile alikuwa amefanyiwa mchezo na Fetty kumbe haikuwa hivyo.
“Gloria....Gloria....nisamehe mpenzi” peter alimwambia Gloria huku akilia.
“Nikusamehe? Kwanza nani mpenzi wako? Haujui kwamba kila kitu kimepita na kinatakiwa kusahauliwa kati yangu na yako. Nani akusamehe?” Gloria alimwambia Peter na kumuuliza.
Gloria hakutaka kuchelewa, hapo hapo akaanza kummiminia risasi mzee Seif na vijana wake na kisha kubaki yeye na Peter tu. Fetty ambaye alikuwa ndani ya gari alivyoona vile, akaliwasha gari lile na kuondoka mahali hapo.
“Ninakuua Peter. NINAKUUA” Gloria alimwambia Peter kwa hasira.
“Gloria! Kumbuka tulipotoka mpenzi”
“Nani mpenzi wako? Unanikasirisha sana unavyoniita mpenzi. Ninakuua mpumbavu mkubwa wewe” Gloria alimwambia Peter.
“Paaa....paaaa” Ilisikika milio miwili ya risasi mahali pale, Peter akadondoka chini, risasi mbili zilikuwa zimepenya tumboni mwake, alikuwa akiugulia kwa maumivu pale chini. Gloria akamsogelea na kuielekeza bunduki ile kichwani kwa Peter.
“Nakuuaaaaaaa” Gloria alisema kwa sauti huku akijiandaa kufyatua risasi.
“Gloriaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa..........” Peter aliita kwa sauti.
“Paaaaaaaaaaaa.......” Mlio wa risasi ulisikika, risasi ambayo ilipenya kichwani mwa Peter.
******
Peter akashtuka kutoka katika usingizi, jasho lilikuwa likimtoka sana, alikuwa akihema kwa nguvu kupita kawaida. Alionekana dhahiri kuwa na ndoto mbaya, ndoto ambayo ilikuwa imemfanya kuwa na wasiwasi kupita kawaida. Peter akakaa kitako, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakimdunda kupita kawaida. Akaanza kujipapasa kuona kama alikuwa ametonolewa na risasi, alikuwa salama.
“Kumbe ilikuwa ndoto” Peter alijisemea.
Hapo hapo akachukua simu yake kwa lengo la kumpigia Gloria. Macho yake yakatua katika meseji ya mwisho kumwandikia Gloria huku nae Gloria akiwa ametuma meseji ambayo akaanza kuisoma “Nakupenda mpenzi. Najua umeshalala, ila utakapoamka naomba ujue kwamba ninakupenda sana. Mwaaaaaaaa! Hiyo ni kwa ajili yako pekee”
Peter akatoa tabasamu, akaonekana kufurahi mara baada ya kugundua kwamba safari nzima ya kwenda Zambia, kuishi kule na kufanya mambo mengine mpaka kuuawa na Gloria ilikuwa ni ndoto moja ndefu, ndoto ambayo ilikuwa imemchanganya sana na kumuondolea amani. Alichokifanya ni kuanza kumpigia simu Gloria.
“Mpenzi” Peter aliita mara baada ya simu kupokelewa.
“Baby mbona jana umeniacha peke yangu simuni?” Sauti ya Gloria ilisikika.
“Hapana. Nilikuwa nimelala mpenzi. Nilipitiwa na usingizi. Nikwambie kitu” Peter alimwambia Gloria.
“Kitu gani? Usiniambie kwamba hatutofunga ndoa. Nitajiua” Gloria alimwambia Peter.
“Hapana. Kuna kitu kingine” Peter alimwambia Gloria.
“Kitu gani mpenzi?”
“ULINIUA GLORIA” Pater alimwambia Gloria.
“Nilikuua!” Gloria aliuliza kwa mshtuko.
“Ndio. Nimeota ndoto mbaya sana, eti nilisafiri kuelekea Zambia kusoma, kule, ukaniua” Peter alimwambia Gloria huku akianza kucheka.
“Duuh! Hiyo kweli kali. Sasa baada ya kukuua?”
“Ndipo nikashtuka” Peter alijibu.
“Pole sana mpenzi kwa kuwa na njozi mbaya. Nimeamka hapa nataka nijiandae kuja huko” Gloria alimwambia Peter.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sawa. Wewe njoo tu ili tufanye maandalizi mengine ya harusi yetu” Peter alimwambia Gloria na kisha kukata simu.
Muda wote Peter alionekana kuwa na furaha, kitendo cha kuota ndoto mbaya na ya kutisha na kugundua kwamba ile ilikuwa ndoto kilionekana kumfurahisha sana. Alikuwa akimpenda sana Gloria, hakutaka kumpoteza hata mara moja, alikuwa tayari kufanya kitu chochote kile lakini si kumuacha Gloria.
Hiyo ndio jinsi ndoto nzima ilivyokuwa. Baada ya siku thelathini kutimia, harusi kubwa ikafanyika katika kanisa la Praise And Worship na Peter pamoja na Gloria kuwa mume na mke. Katika maisha yote ambayo yaliendelea, ndoto ndefu, ya kutisha na kusisimua ilikuwa ikiendelea kukukumbukwa kichwani mwa Peter. Hakutaka kuisahau ndoto ile kwani ilikuwa moja ya ndoto mbaya ambayo aliwahi kuiota katika maisha yake.
“MmmmH! Ni ndoto mbaya hivyo mpaka nasisimka mpenzi” Gloria alimwambia Peter.
“Ni ndoto na kila siku itaendelea kuwa ndoto tu. Tuachane nayo. Dokta kasemaje kuhusu huo ujauzito?” Peter alimwambia Gloria na kisha kumuuliza.
“Kasema wa kiume” Gloria alijibu huku akitabasamu.
“Safi sana. Jina lake ataitwa Henry. Nimefurahi sana kuwa pamoja nawe. Sahau mambo ya ndoto, sikutaka kukwambia kwa kipindi kile kwa sababu nilitaka kwanza tufunge ndoa” Peter alimwambia Gloria.
“Asante kwa kunijali na asante kwa kunipenda zaidi” Gloria alimwambia Peter na kisha kukumbatiana kitandani pale.
MWISHO.
JE UNAIKUMBUKA SEHEMU YA KWANZA ILIPOISHIA? ITAZAME HAPA KWANI KUANZIA SEHEMU YA PILI MPAKA MWISHO ILIKUWA NDOTO.
Baada ya hapo, wote wakatawanyika na kuyafuata magari yao. Peter hakutaka kumuacha Gloria mikononi mwake, alikuwa amemshikilia vilivyo japokuwa mzee Michael alikuwa akimuita. Wote wakabaki wakiangaliana tu, mapenzi ambayo waliyokuwa nayo mioyoni mwao yalikuwa yakiendelea kuchipuka.
“Ninakupenda sana Gloria” Peter alimwambia Gloria.
“Ninakupenda pia”
Baada ya hapo, Gloria akaingia garini na kuondoka mahali hapo. Muda wote huo Peter alikuwa amesimama tu mpaka pale gari lilipotoka machoni mwake. Akaanza kupiga hatua na kuelekea ndani ambapo akapitiliza hadi chumbani.
Alipofika chumbani, akaanza kuchati na Gloria huku akionekana kuwa na furaha tele. Waliendelea kuchati mpaka saa tisa usiku, muda ambao akapitiwa na usingizi kitandani pale. Ingawa meseji zilikuwa zikiendelea kuingia, Peter alikuwa amekwishalala kitambo kutokana na uchovu mkubwa ambao alikuwa nao siku hiyo.
“Nakupenda mpenzi. Najua umeshalala, ila utakapoamka naomba ujue kwamba ninakupenda sana. Mwaaaaaaaa! Hiyo ni kwa ajili yako pekee” Hiyo ilikuwa ni meseji ya mwisho ambayo Gloria alikuwa amemuandikia Peter ambaye alikuwa amekwishalala.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ASANTENI KWA KUIFUATILIA NDOTO HII YA KUSISIMUA.
0 comments:
Post a Comment