Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

DAMU, MABUSU NA MACHOZI - 1

 





    IMEANDIKWA NA : ERIC SHIGONGO



    *********************************************************************************



    Simulizi : Damu, Mabusu Na Machozi

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa muda mrefu sana mvua ilikuwa haijanyesha katika wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani mazao ya watu wengi sana yalikuwa yamekufa mashambani, kulikuwa na dalili zote za kutokea kwa balaa la njaa! Jambo hili lilisababisha watu wengi kuwa na wasiwasi ni wapi wangepata chakula.

    Pamoja na hali hiyo ya wasiwasi, siku hiyo ya Ijumaa baada ya swala ya Ijumaa Kuu wazee wote walikusanyika chini ya mti mkubwa wa mwembe uliopo katika eneo la Kajificheni kulikuwa na mkutano wa hadhara ulioitishwa na mwenyekiti wa mtaa wa Kajificheni! Mkutano huu haukuitishwa kuongelea tishio la njaa lililokuwa likitegemewa! Bali wakazi wa Bagamoyo walitaka kumjadili mtu mmoja hatari katika wilaya yao, huyo hakuwa mwingine bali mzee Wilbord Katobe, mfanyabiashara aliyemiliki vyombo mbalimbali vya uvuvi majini na alikuwa na kiwanda cha kusindika samaki aina ya Kamba na pia alimiliki mashamba makubwa ya nazi na mananasi maeneo ya Kiwangwa huko huko Bagamoyo. Kifupi alikuwa mfanyabiashara tajiri kwa ngazi ya wilaya ya Bagamoyo.

    Ulikuwa ni mkutano kumjadili mzee huyu aliyesifika kwa ukorofi wake, hasa lilipokuja suala la mtoto wake mmoja wa kike! Alishawajeruhi vijana wapatao watatu kwa risasi na mapanga sababu ya binti yake, eti walimtaka mapenzi. Wakazi wa Bagamoyo hawakupenda kabisa vitendo hivyo na siku hiyo ndio ulikuwa mkutano wa kumjadili, wazee walitaka kumuongelea na ikabidi wapeleke mapendekezo yao mkoani baada ya kuona serikali ya wilaya imeshindwa kabisa kumshughulikia, mara kadhaa walisharipoti suala hilo polisi lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake!

    Wananchi walikuwa wamechoka, siku moja kabla ya mkutano huo mzee Katobe alimkamata kijana mmoja aliyesoma Shule ya Msingi Mwanamakuka pamoja na binti yake, alifika nyumbani hapo kufuata kitabu chake cha Kiswahili alichomwazimisha binti wa mzee Katobe ambaye alifikiri kijana huyo alikuja nyumbani kwake kumtaka mtoto wake kimapenzi.

    Alimkamata na kumvutia ndani ya ngome ya nyumba yake kisha kuwaachia mbwa wake kumi na mbili ili wamshambulie, kazi hiyo ilifanyika kikamilifu kijana alipoachiwa nusu saa baadae mwili wake wote ulijaa majeraha ya kuumwa na mbwa, majeraha yake yalivuja damu nyingi mfululizo! Kitendo hicho kiliwakera sana wazee wa mji wa Bagamoyo ndio sababu waliamua kuitisha kikao cha kumjadili mzee Katobe!

    “Haiwezekani, kwani yeye ni nani? Yeye ndiye ana binti peke yake hapa mjini?”

    “Hana nidhamu kabisa mzee huyu, anamchunga mtoto wake kwani yeye ndiye atamwoa?”

    “Aondoke Bagamoyo!”

    “Tutamchukua tu binti yake, hata akimlinda vipi? Huyo ni msichana wetu tu!”

    Watu walizidi kupiga kelele kwenye mkutano huo wakimsubiri mzee Katobe aliyepelekewa taarifa za kikao hicho afike, hata hivyo hakufika na kikao kwa sababu alikidharau, kikawa kimefungwa masaa mawili baadae wazazi wote wakiwa wameazimia kupambana nae kama polisi isingeingilia kati, walidai tabia ya kuwatesa watoto wao ilikuwa imewachosha!

    “Tutapambana nae!” Aliongea mmoja wa wazee.

    “Hakyanani siku atakayoniingiza mimi ndani ya nyumba yake kuniumisha mbwa nitamng’ang’ania mpaka nife nae, haiwezekani, hapa kijijini mbona wapo wazee wengi tu wenye mabinti kwanini hawafanyi hivi, huyu mzee mwendawazimu! We acha tu, ipo siku yake!” Kijana mmoja alilalama.

    Mzee Katobe alitisha, alikuwa mzee katili ambaye hakujali maoni ya watu juu yake, hakujali walimpenda au la! Ukatili wake ulijulikana mkoa nzima wa pwani na hata mkoa wa Dar es Salaam, hakuwa mtu wa kugusika kirahisi wengine walihisi alikuwa na mkono ndani ya Serikali kwa sababu alikuwa na uwezo wa kupindisha sheria pale alipotaka kufanya hivyo na hakuna lililofanyika! Ujeuri wake ulikuwa tishio hata baadhi ya viongozi wa wilaya na mkoa.

    Pamoja na kuishi na mke wake kwa miaka zaidi ya ishirini mzee Katobe alifanikiwa kuzaa mtoto mmoja tu, tena wa kike binti huyu aliitwa Nancy! Alikuwa kipenzi kikubwa cha baba yake, mzee Katobe alikuwa tayari kutumia chochote alichokuwa nacho ili mtoto wake pekee apate elimu bora ambayo ingemwezesha kuziendesha vizuri mali zake mara atakapostaafu kazi kwa sababu ya uzee au kitu chochote.

    “Tulia mwanangu Nancy, wewe ni msichana mzuri na mimi baba yako nina kila kitu hapa nyumbani, usibabaishwe na hawa vijana wa Bagamoyo hawana lolote, wavuvi tu! Watakupa kitu gani hawa? Soma mwanangu, mali yote niliyokuwa nayo mimi ni yako kama hutapata elimu ya kutosha utashindwa kuendesha kazi zangu kesho na keshokutwa mimi na mama yako tukiondoka!” Mzee Katobe alimhusia binti yake.

    “Sawa baba nitajitahidi kufanya yote yatakayokufurahisha wewe mzazi wangu!”

    “Ukimaliza tu darasa la saba, nitakupeleka Uingereza ukasome masomo ya sekondari na hata chuo kikuu, sitaki ukae hapa Bagamoyo!”

    “Sawa baba!” Aliitikia Nancy kwa unyenyekevu mbele ya baba yake, aliamini baba yake alikuwa tajiri kuliko mtu yeyote Bagamoyo, hilo lilimpa majivuno na hali ya kujiamini kupita kiasi.

    Wakati baba yake alitisha kwa ukali na ukorofi binti alitisha kwa uzuri wa sura na mvuto, katika umri wa maiaka kumi na mbili tu Nancy alikuwa tishio wilayani Bagamoyo na mkoa wa Pwani kwa ujumla, sifa zake zilisambaa kama upepo! Umbile lake lilitisha, alikuwa na makalio makubwa yasiyo na maelezo ya kutosheleza, alirithi hali hiyo kutoka kwa mama yake Ashura Mwinyimkuu, mwanamke mwenye mchanganyiko wa Mkwere na Mnyarwanda.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nancy alikuwa na mwili mkubwa uliomfanya aonekane kama binti mwenye umri wa maiak 18 au zaidi na alikuwa na ngozi nyororo yenye rangi ya chokleti! Meno yake yalipangika kisawasawa mdomoni! Alikuwa mwembamba juu lakini mkubwa chini, hii ilimaanisha hata miguu yake pia ilikiwa fiti! Alivutia kumwangalia kwa macho na kushangaa uumbaji wa Mungu, mama yake alikuwa mfupi lakini baba yake alikuwa mrefu na ni kitu hicho ndicho pekee ambacho Nancy alichorithi kutoka kwa baba yake mzee Katobe.

    Mtu yeyote aliyefungua mdomo wake na kusema Nancy alikuwa mzuri hakukosea ni kweli msichana huyo mdogo alivutia, vijana wengi mjini Bagamoyo hata wengine kutoka jijini Dar es Salaam walishajaribu kumfuata wakimtaka kimapenzi lakini hawakufanikiwa, waliishia kupambana na mzee Katobe na kupigwa hata kujeruhiwa kwa mapanga na kukoswakoswa kwa risasi.

    Mzee Katobe alimchunga binti yake kuliko askari alivyomchunga mtuhumiwa wa mauaji! Mambo haya yaliwafanya vijana wengi mjini Bagamoyo wamwogope binti huyo! Waliogopa kufa, maana kuna wakati mzee Katobe aliwahi kutoa vitisho vya kumloga kijana yeyote ambaye angeendelea kumsumbua binti yake kipenzi, Nancy.

    “Aisee huyu mtoto ni mkali?” Mmoja wa vijana alisema.

    “Arooo, cheki! Cheki! Mtoto kajazia idara zote, kaenda juu sekunde mtoto! Aisee huyo anakuja!

    “Wewe, kirusi umeweka katika hiyo listi?”

    “Ebwanae usilete mambo ya matangazo ya Ukimwi hapa, angalia toto liko fiti ….!” Aliendelea kusema kijana mwingine, wote wawili walikuwa wamesimama kwenye njia ya kutoka shule ya msingi Mwanamakuka wakisubiri wanafunzi watoke shuleni, Nancy alikuwa anapita mbele yao akiongozana na kijana mmoja mweusi aliyefunga bandeji usoni na mikononi kama aliyejeruhiwa.

    “Ebwana mie namtokea!”

    “Baba yake unamfahamu lakini? Isitoshe utamtokeaje mtu unayemwona ana boyifrend wake?”

    “Ni mtoto wa nani? Huyo ndiye boyifrendi wake?”

    “Mzee Katobe! Huyo kijana anaitwa Tony sidhani kama ni boyifrendi wake ila mara kwa mara huwa wanaonekana wote”

    “Hivi huyu ndiye Nancy?”

    “Ndiye!”

    “Aisee hapo sitii mguu! Baba yake nuksi ile mbaya, lakini muone anavyotingishika huko nyuma! Ebwanae! Namsifia Mungu kwa uumbaji! Mungu anajua kuchora ramani, lakini ana upendeleo ramani ya huyu binti ni ya uhakika tena selfu kontena, siyo ramani kama yako kibakuli, utafikiri mkate!” Kijana alimtania mwenzake akicheka.

    “Ebwanae mimi utani unaoelekea kwenye ukweli huwa sitaki, Ngovongo ukirudia tena tutagombana!”

    “Samahani mshkaji, nilikuwa naweka msisitizo juu ya ramani za Mungu, sikutegemea ungemaindi.”



    Kadri Nancy alivyozidi kukua ndivyo uzuri na maumbile yake ya nyuma yalivyozidi kuongezeka, cha kushangaza alizidi kukonda juu! Kama ungefanikiwa kuona picha yake ungefikiri ilikuwa ni picha ya kuchora au kutengenezwa kwenye kompyuta, halikuwa jambo rahisi mtu kukubali kuwa umbile lile ulikuwa mwili wake kama si matambala! Akiwa darasa la saba jina lake lilibadilika akawa anaitwa ‘Nyambizi’ akilinganishwa na meli kubwa zisafirizo chini ya maji!

    Nancy alikuwa tishio si kwa sura na uzuri tu bali pia darasani mara kwa mara alishika namba moja darasani mwake hapo ndipo alipowashangaza watu, karibu wanafunzi shule nzima walimtamani lakini hawakufanikiwa kumpata, katika miaka yote saba aliyosoma shule ya msingi Mwanamakuka alishafukuzisha kazi walimu watano waliomwita ofisini na kutaka kumbaka! Huyo ndiyo alikuwa Nancy Nyambizi.

    Alielewana na kijana mmoja tu shuleni kwao, huyo ndiye waliyegombania naye namba darasani, aliitwa Antony Kivembe au Tony! Alikuwa mtoto wa mama mjane mwenye shida pengine kuliko wajane wote wilayani Bagamoyo, alijulikana na watu wengi kwa jina la mama Tony ingawa jina lake halisi aliitwa Irene Ngowika. Mama huyu naye hakuwa na mtoto mwingine zaidi ya Tony! Umaskini uliigubika familia yake, ni mwanae ndiye aliyekwenda nyumban kwao na Nancy kufuata kitabu chake cha Kiswahili na kukamatwa na mzee Katobe kisha kuingizwa ndani na kuumishwa mbwa.

    Nancy alikerwa sana na kitendo hicho, alijifungia ndani na kulia usiku mzima, hakutaka kabisa rafiki yake mpendwa afanyiwe kitu kibaya, alimtegemea Tony sana katika mambo mengi ya masomo kwani alikuwa tofauti na wavulana wengine shuleni, hata siku moja hakuwakuwahi kumtamkia kitu chochote kuhusiana na mapenzi! Siku iliyofuata Nancy aliongea na baba yake na kumweleza ubaya wa kitendo alichokifanya tena akilia machozi.

    “Huyo ndiye hunisaidia mimi katika masomo yangu shuleni! Kwanini umemfanyia hivyo?”

    “Sikufahamu jambo hilo mwanangu, nisamehe!” alijibu mzee Katobe na siku iliyofuata ilibidi dereva atumwe kwenda hadi nyumbani kwao na Tony na kumchukua kisha kumpeleka hospitali ambako alitibiwa na kuweza kuchomwa sindano za chanjo ya kichaa cha mbwa, wiki mbili baadae alikuwa salama salimini na yeye na mama yake walikaribishwa nyumbani kwa mzee Katobe kwa chakula cha jioni kuimarisha zaidi uhusiano wao na tangu siku hiyo mzee Katobe alimruhusu Tony kumtembelea Nancy nyumbani na hata kusoma pamoja.

    “Nisamehe sana Tony! Ni makosa ya baba nipo tayari kuyabeba!” Nancy alimwambia Tony.

    “Hamna shida wewe ni dada yangu Nancy, siwezi kumchukia baba yako, kwani hata mimi namchukulia kama baba yangu, nimekwishamsamehe!”

    “Nashukuru sana kwa hilo!”

    Ukaribu wao uliongezeka maradufu baada ya hapo, mara kwa mara Tony akawa anakwenda nyumbani kwao na Nancy kujisomea nyakati za usiku, walisoma hadi katikati ya usiku bila mzee Katobe na mke wake kuwa na wasiwasi, walimwamini Tony kuliko hata walivyomwamini binti yao Nancy. Usiku walipochoka Tony alilala chumba cha wageni na Nancy alikwenda chumbani kwake na asubuhi waliondoka pamoja kwenda shuleni!

    “Nancy acha!” Tony alisema kwa sauti ya chini, ilikuwa ni tayari saa saba ya usiku, Nancy alikuwa akimvuta ili ampige busu mdomoni, mwili wake ulikuwa ulikuwa ukihisi kitu kisicho cha kawaida ambacho hakuwahi kupambana nacho maishani, zilikuwa ni hisia za mapenzi zilizosambaa mwili mzima.

    “Niache nini Tony? Mimi nakupenda sana, kila binadamu hapa duniani anahitaji kuwa na mpenzi, kwani wewe hufahamu wimbo wa Chaka Chaka usemao Every woman needs love?”

    “Hata kama naufahamu haifai sisi kufanya kitu unachotaka tufanye, sisi bado wadogo sana Nancy, inabidi tusubiri kwanza!”

    “Haiwezekani kusubiri!” Alisema Nancy na kumwangukia Tony kifuani na wote wakaanguka sakafuni, katika kufanya hivyo bahati mbaya alikigonga kiti kimoja kikaanguka chini na kusababisha kelele zilizokwenda hadi chumbani kwa baba yake, Nancy hakujali akiamini mzee Katobe alikuwa usingizini na kwa haraka alivua gauni lake na kumlalia Tony kifuani!

    “Njoo! Njoo! Njoo Tony, usipokubali kufanya ninachotaka nitamwambia baba yangu kuwa ulitaka kunibaka!”

    Kauli hiyo ilifanya mwili wote wa Tony utetemeke, alimwogopa mzee Katobe kuliko kitu kingine chochote ukimwondoa Mungu! Alijua kama Nancy angefungua mdomo wake na kusema maneno hayo, Tony angeuawa kwa risasi. Huku akitetemeka alimwomba Nancy atoke kwanza kifuani ili avue kaptula yake haraka na amtimizie haja yake, kweli Nancy alifanya hivyo na Tony akasimama wima na kufungua vifungo vyote vya kaptula yake na kuteremsha pamoja na nguo yake ya ndani akabaki kama alivyozaliwa.

    “Njoo upesi mwisho baba atakuja!”

    “Sijui, sijawahi kufanya!”

    “Wewe njoo tu nitakuonyesha!”

    Huku akitetemeka Tony alianguka juu ya mwili wa Nancy tayari kwa kufanya alilotakiwa kutenda, alishasahau kuwa ni dhambi! Ghafla akiwa juu ya mwili wa Nancy mlango wa chumbani kwa mzee Katobe ukifunguliwa na mzee Katobe akatokeza na kusimama wima, Tony alihisi haja kubwa na ndogo ikipenya bila amri yake!

    “Unaona sasa?”

    “Nini?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mzee Katobe!”

    “Yuko wapi?”

    “Yule pale mlangoni!” Alijibu Tony akitetemeka mwili mzima kwa hofu, alielewa ambacho kingetokea kama mzee Katobe angemshuhudia akiwa juu ya kifua cha mtoto wake aliyempenda kuliko kitu chochote duniani, ni wazi kifo kingekuwa halali yake, alizidi kutetemeka akiwa amepigwa ganzi bila kujua la kufanya, alimshudia mzee Katobe akitembea kutoka sehemu moja ya chumba kwenda nyingine huku akisonya!

    Tony alibana pumzi yake, hakutaka isikike na taratibu aliporomoka toka kifuani kwa Nancy na kuingia chini ya meza Nancy akimfuata nyuma, hata yeye alikuwa na hofu! Alimuelewa baba yake kwa kina, ingawa asingeuawa kama mwenzake Tony adhabu ambayo angeipata lazima angeisimulia maishani mwake, wakiwa chini ya kiti walimshuhudia mzee Katobe akipita taratibu na kuzima taa iliyokuwepo sebuleni.

    “Hawa watoto bwana hawajui hata gharama ya umeme zilivyokubwa , wanaacha taa zinawaka ovyo!” Alisema mzee Katobe baada ya kuzima taa na kunyoosha moja kwa moja hadi ulipokuwa mlango wa kuingia chumbani kwake, akausukuma na kuingia ndani.

    Tony alishusha pumzi kwa nguvu akiwa chini ya meza, hakuamini kama alikuwa amenusurika na kifo! Hazikuwa juhudi zake bali mpango wa Mungu kumuondolea mzee Katobe wazo la kuangalia chini ya meza, rohoni mwake aliapa kutorudia tena tendo hilo kwani lilikuwa ni hatari kwa maisha yake, akiwaza hilo ghafla alishtukia akiguswa ubavuni.

    “Tony!”

    “Unasemaje?”

    “Tunaendelea!”

    “Nanini?”

    “Unajifanya kuuliza, ina maana umesahau tulikuwa na programu gani kabla ya mzee Katobe hajatokeza toka chumbani?”

    “Nakumbuka lakini hilo si jambo jema Nancy, wewe ni kama dada yangu!”

    “Wewe ndio unaelewa hayo, mimi nataka tucheze tu na kama hutaki swala ni lile lile kuwa nitapiga kelele nimtaarifu baba kwamba unataka kunibaka!”

    “Nancy bado una wazo hilo?”

    “Ndio kama tu hutakubali kufanya ninachotaka! Hutaki?”

    Tony alinyanyuka na kukaa kitako kisha kuinamisha kichwa chake chini akiwaza,alikuwa katika wakati mgumu wa kuchagua maisha au kutenda alichotakiwa kufanya, kwa sababu alipenda kuendelea na maisha, bila kutaka Tony alijikuta akihiari kufanya tendo la ndoa na Nancy, alipovutwa alisogea karibu na alipoamliwa kupanda juu alifanya hivyo kwa kutetemeka. Ilikuwa mara ya kwanza maishani kwake kutakiwa kutimiza wajibu mgumu kama huo, siku zote alilitafsiri tendo la ndoa kama jambo lililotakiwa kusubiri mpaka watu waoane.

    Wote wawili walikuwa wageni wa jambo hilo, hata Nancy pia hakuwahi kukutana na mwanaume maishani mwake, ni maneno ya wanafunzi wenzake shuleni ndio yaliyomsisimua na kumfanya ajikute akitamani kujaribu na mtu pekee wa kufanya naye majaribio alikuwa Tony! Mvulana aliyeishi naye ndani ya nyumba yao ambaye baba yake asingeweza kumfikiria vibaya. Kwa sababu ya ugeni na tendo hilo hakuna walilolifanya wakiwa sakafuni zaidi ya kupapasana na kufanya mambo ambayo waliyaona katika mchezo wa Egoli, kwao hiyo ilitosha kwani walipoachia nusu saa baadaye jasho lilikuwa likiwatoka na kila mmoja akanyanyuka na kuelekea chumbani kwake, walikuwa wameridhika.

    Wakati chumbani Nancy alifurahia kilichotokea, Tony alikuwa akilia machozi, alifanya kitendo ambacho hakukipenda lakini hakuwa na la kufanya zaidi ya kukubali, asubuhi kulipokucha alikuwa mnyonge kupita kiasi, alijisikia mkosaji ndani ya moyo wake hata alipomwamkia mzee Katobe.

    “Mbona unaonekana mnyonge leo?” Mzee Katobe aliuliza.

    “Ninaumwa”

    “Unaumwa nini?”

    “Naumwa kichwa!”

    “Pole, utaweza kwenda shuleni?”

    “Nitaweza baba!”

    “Ok, baadae tutaonana!”

    Shuleni Tony hakuongea kitu na Nancy, alionyesha wazi kuchukizwa na kitendo kilichofanyika usiku na katika maongezi yao hakuficha kilichokuwa moyoni mwake, wakati wanaondoka shule hakutaka kuongozana na Nancy tabia yake ya siku hiyo hata wanafunzi wenzake waliitilia mashaka, wengi walihisi kulikuwa na ugomvi kati yao! Aliondoka shuleni peke yake tena mapema kabla ya wanafunzi wengine hawajaruhusiwa, badala ya kurudi nyumbani kwa mzee Katobe alinyoosha moja kwa moja kwenda nyumbani kwa mama yake eneo la Magomeni mjini Bagamoyo kama kilometa kumi kutoka shuleni kwao.

    Alimkuta mama yake akiendelea na shughuli za nyumbani kama kawaida, hata yeye pia hali ya mwanae ilimshangaza akajikuta akilazimika kumkarisha Tony chini ili aeleze kilichokuwa kikimsumbua! Hakuwa na kitu cha kumwambia mama yake, kamwe asingeweza kufungua mdomo wake na kusema kwa mama yake alifanya tendo la ndoa wakati alielewa siku zote alikemea kitendo hicho na alikiita ni dhambi kubwa sana mpaka pale kilipohalalishwa kanisani.

    “Nieleze nini kinakusumbua mwanangu?”

    “Hakuna kitu chochote!”

    “Wewe ni mwanangu Tony, nilikuzaa mimi, tabia yako lazima niielewe kuna kitu kinakusumbua Tony!”

    “Hakuna kitu mama ila nataka tu kukueleza kwamba sitarudi tena nyumbani kwa mzee Katobe!”

    “We mtoto! Umefanya nini tena? Kwa nini hutaki kurudi? Nani atakulipia ada ya shule? Huelewi kuwa mzee Katobe ameamua kukusomesha mpaka sekondari na hata Chuo Kikuu?”

    “Pamoja na hayo yote mama, sipo tayari kurudi tena nyumbani kwa mzee Katobe!”

    “Lakini kwanini?”

    “Maisha yangu ni kitu cha muhimu sana mama!”

    “Unamaanisha nini Tony?”

    “Kurudi kwa mzee Katobe itakuwa ni sawa na kuuza uhai wangu, iko siku nitarudishwa hapa nikiwa maiti wakati wewe ni mama yangu na mimi ni mtoto wako pekee! Hunipendi mama?”

    “Nakupenda mwanangu!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Basi niache niishi na wewe kama tulivyokuwa tukiishi zamani!”

    “Hata hivyo nahitaji kufahamu kilichotokea!”



    Jioni ya siku hiyo mama yake alitayarisha chakula wakala pamoja na baadae kusali kisha kulala, siku hiyo Tony wala hakushika daftari kusoma kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi kupita kiasi, akiwa kitandani majira ya saa tano za usiku alisikia gari likifunga breki nje ya nyumba yao na muda mfupi baadae mama yake akaingia mbio chumbani kwa Tony huku jasho jingi likimtoka, moyo wake ulikuwa ukidunda kwa kasi kubwa kiasi cha Tony kuusikia.

    Kitendo hicho kilimfanya Tony ambaye hakushtuliwa na breki za gari hilo ashtuke na kunyanyuka kitandani akihema, alianza kufikiria majambazi lakini baadae aliyatoa mawazo hayo kichwani mwake kwani yeye na mama yake hawakuwa na kitu cha kufanya wavamiwe na majambazi.

    “Mama vipi?”

    “Kuna gari nje!”

    “Sasa wasiwasi wa nini? Si ajabu ni gari la majirani!”

    “Hakuna jirani mwenye gari! Ina maana wewe hufahamu? Mimi na wasiwasi!”

    “Wa nini? Majambazi? Tuna nini sisi cha kuvamiwa mama?” Aliuliza Tony akifungua dirisha la chumbani kwake kuchungulia nje.

    Hakuamini alichokiona, ni kweli mama yake alikuwa na haki ya kutetemeka! Moyo wake ulianza kwenda kwa kasi kubwa, hawakuwa majambazi kama ulivyokuwa wasiwasi wa mama yake, mzee Katobe alikuwa amesimama nje ya nyumba yao mbele ya mlango bunduki yake aina ya SMG ikiwa mkononi na akiitumia bunduki hiyo kugonga mlango. Tony alizidi kutetemeka akielewa wazi kuwa, Nancy kwa hasira zake alikuwa ameamua kumsingizia kwamba alimbaka na kilichomleta mzee Katobe nyumbani kwao usiku huo ilikuwa ni kuja kumuua kwa risasi.

    “Nani?”

    “Mzee Katobe, nina uhakika kaja kuniua mimi! Kuna kitu kilitokea jana ambacho nimeshindwa kukueleza kwa sababu wewe ni mzazi wangu!”

    “Kitu gani?”

    “Naona aibu! Ila Nancy alinilazimisha, nisingeweza kufanya kitendo hicho kwa sababu wewe kila siku unaniambia kwamba ni dhambi!”

    “Nini hicho?”

    “Tendo la ndoa!”

    “Mama yangu! Na wewe ulikubali?”

    “Nilipokataa Nancy alitishia kunishtaki kwa baba yake kwamba nimembaka! Ikabidi nikubali, nilichukia sana na ndio maana nikaamua kurudi nyumbani nilijua wazi kama ningeendelea kubaki nyumbani kwa mzee Katobe Nancy angenilazimisha tena tufanye hivyo hatimaye mzee Katobe angegundua na kuniua, naelewa uamuzi wangu wa kurudi hapa umemuudhi sana Nancy na amenisingizia kwa baba yake kwamba nilimbaka na hivyo mzee Katobe amekuja kuniua kwa risasi, sina la kufanya na siwezi kumzuia asifanye hivyo, nasikitika kwamba muda mfupi ujao nitakuwa marehemu, nitakuacha mama!”

    “HODI! HODI! HODI!” Sauti ya mzee Katobe ilisikika huku akiupigapiga kwa kitako cha bunduki mlango wa nyumba yao uliotengenezwa kwa bati.

    Hakuna aliyeitika, Tony na mama yake walikumbatiana huku wakilia, ulikuwa usiku wa huzuni kubwa sana kwao na kwa pamoja walianza kumuomba Mungu abadilishe hatma ya kilichokuwa kikija mbele yao, wakiwa katika maombi hayo ghafla mlango wa nyumba yao uliofungwa kwa msumali uliokunjwa ulifunguka na nyayo za mzee Katobe zikasikika sebuleni. Waliendelea kububujikwa na machozi bila kujua la kufanya.

    “Siwezi kukubali akuue mbele ya macho yangu, nipo tayari kufa mimi lakini wewe ubaki hai!” Mama yake Tony aliongea kwa huzuni.

    Tony na mama yake walikuwa wakitetemeka wakiwa nyuma ya mlango uliokuwa ukigongwa kwa nguvu zote na mzee Katobe, akitumia bunduki yake aina ya SMG huku akiita jina la Tony pamoja na la mama yake! Hakuna aliyeitika wakijua alikuwa amekwenda nyumbani kwao kufanya mauaji.

    “Mama nasikitika nakufa, laiti ningejua nisingekubali kwenda nyumbani kwao na Nancy, najua amenisingizia kwa baba yake kwamba nilimbaka na kwa sababu hiyo mzee Katobe amekuja kuniua!”

    “Hawezi kukuua mwanangu, nitapambana naye labda atuue sote wawili!”

    “Lakini ana bunduki!”

    “Hata kama!”

    Mlango ulizidi kugongwa kwa nguvu lakini hawakudiriki kuitikia wala kuufungua, ghafla ulianza kusukumwa, bahati mbaya sana haukuwa na komeo imara, ulifungwa kwa msumari uliokunjwa! Taratibu ukaanza kuachia, Tony na mama yake hawakuwa na uwezo wa kuzuia tena, walichofanya ni kusogeleana na kukumbatiana wakisubiri lililokuwa likija mbele yao.

    Mlango ulivunjwa na mzee Katobe akaingia hadi ndani bunduki yake ikiwa mkononi, miili yao ilikufa ganzi! Tony aliamini kifo chake kilikuwa kimefika na hata mama yake aliwaza vivyo hivyo, alikuwa tayari kupambana kuzuia mwanae asidhuriwe na katika kufanya hivyo alielewa na yeye angeuawa!

    “Ee Mungu tusaidie!” Walijikuta wakitamka wote kwa pamoja.

    ***

    Nancy alikuwa katika mapenzi mazito na Tony kwa kilichotokea siku moja, lilikuwa ni jambo ambalo hakulitegemea kabisa kwani lilianza kama mchezo, lakini ghafla moyo wake tayari ukawa umetekwa na kumfanya aamini maisha bila Tony yasingewezekana!

    “Nampenda Tony, hilo halina ubishi!” Aliwaza Nancy akitembea kuelekea nyumbani, siku hiyo alikuwa peke yake tofauti na siku zingine zote alizoongozana na Tony.

    Alirudi nyumbani kutoka shuleni akilia, kitendo cha Tony kurejea nyumbani kwao kilimuumiza sana, alielewa yeye ndiye alikuwa chanzo cha tatizo hilo kwa kumshawishi kufanya tendo la ndoa jambo ambalo Tony hakulipendelea, alikuwa na uhakika alishiriki kwa sababu tu alimtishia kumshtaki kwa baba yake kuwa alitaka kumbaka kama tu angekataa kumtimizia shida yake.

    Nyumbani kwao hakutaka kuongea na mtu, baada ya kumsalimia mama yake ambaye alikuwa nyumbani wakati anawasili, Nancy alinyoosha moja kwa moja hadi chumbani kwake akajifungia na kuendelea kulia akimfikiria Tony.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda mfupi baadaye mlango uligongwa na aliposikiliza sauti aliyeongea nje aliitambua, alikuwa mama yake, alinyanyuka taratibu akausogelea mlango na kuufungua, mama yake alipomwangalia usoni aligundua kulikuwa na tatizo.

    “Mbona macho mekundu?”

    “Naumwa!”

    “Unaumwa nini?”

    “Kichwa!”

    “Umekunywa dawa?”

    “Ndiyo!”

    “Dawa gani?”

    “Panado na ningeomba uniache nipumzike mama!”

    “Mwenzako yuko wapi?”

    Badala ya kujibu swali hilo Nancy aliangua kilio mbele ya mama yake na kumhakikishia kabisa kwamba kulikuwa na tatizo lililomsumbua kichwani mwake, badala ya kuondoka mama yake aliketi pembeni mwa kitanda akitaka kufahamu nini kilichotokea kati ya Nancy na Tony.

    “Nini kimetokea? Amekupiga?”

    “Hapana!”

    “Sasa kwanini nilipotaja jina lake ukalia?”

    “Nasikitika kwa sababu Tony ameamua kurudi kwa mama yake, wakati mimi bado namhita-ta-ta-taji...!” Alisema Nancy huku kwikwi ya kulia ikiwa imemkaba.

    “Kwanini ameamua kurudi?”

    “Nilimkosea!”

    “Kosa gani?”

    “Siwezi kusema mama!”

    “Kwanini?”

    “Basi tu, mimi naomba mumfuate nije nimwombe msamaha!”

    “Bahati mbaya nyumbani kwao sikufahamu, baba yako peke yake ndiye anapaelewa! Tumsubiri arudi! Lakini nataka kufahamu umemkosea nini?”

    “Siwezi kusema hata kama kisu kiko shingoni kwangu!” Aliongea Nancy na kumtisha mama yake.

    Mama yake alimfariji kwa kama nusu saa nzima, alipotulia aliondoka chumbani kuelekea jikoni ambako aliendelea na kazi za ndani akisaidiana na wafanyakazi mara kwa mara akienda chumbani kwa Nancy kuhakikisha alikuwa salama, mzee Katobe hakurejea mpaka saa tano za usiku na mkewe kumweleza wazi juu ya jambo lililotokea.

    “Kwa hiyo nikimleta Tony, hutalia tena?” Mzee Katobe aliuliza akiongea na Nancy chumbani kwake.

    “Ndiyo baba!”

    “Ok! Wache nimfuate!” Aliongea mzee Katobe na kuondoka chumbani kwa Nancy kwenda chumbani kwake ambako alichukua bunduki yake aina ya SMG na kutoka hadi nje ambako aliingia ndani ya gari lake na kuliendesha hadi nyumbani kwa mama yake na Tony eneo la Magomeni.

    Alifika na kuanza kugonga mlango lakini hakuna aliyemwitikia, hatimaye akafikia uamuzi wa kuvunja mlango wa bati uliokuwepo ili aingie ndani na hilo likawezekana tena kwa urahisi kwa sababu mlango haukuwa na ugumu wowote, akaingia hadi ndani na kuwakuta Tony na mama yake wakiwa wamekumbatiana.

    “Msiogope ni mimi! Mlifikiri ni majambazi?” Aliuliza mzee Katobe lakini bado hawakumjibu kitu chochote waliendelea kukumbatiana wakisubiri risasi zipenye miilini mwao.

    “Tony! Tony! Tony!” Mzee Katobe aliendelea kuita.

    “Naam!” Tony alijitutumua na kuitika.

    “Kwanini nawagongea hamfungui mlango mpaka nimeuvunja? Basi tutautengeneza tena mlango mwingine!” Aliongea mzee Katobe kwa sauti ya upole.

    Mara moja Tony alielewa kilichomleta mzee Katobe nyumbani hapo hakikuwa kufanya mauaji, kulikuwa na kitu kingine! Hofu aliyokuwa nayo moyoni ilifutika kwa furaha na kujikuta amesimama wima huku akimwomba mama yake pia asimame.

    “Shikamoo baba!”

    “Marahaba hujambo Tony? Mnaogopa sana majambazi au siyo?”

    “Sana! Na hatukufahamu kabisa unaweza kuwa wewe, sisi tulijua ni maharamia wametuvamia!” Aliongea Tony meno yake yakigongana.

    “Hata mimi nilihisi hivyohivyo! Sasa labda nieleze shida iliyonileta na nitaanza kwa kuuliza swali ni kwanini leo hukuja nyumbani mwanangu?” Aliuliza mzee Katobe.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tony alishindwa kulijibu swali hilo haraka, alitulia kwanza akijaribu kutafakari nini alichotakiwa kusema, asingeweza kutoboa siri ya jambo lililofanyika kati yake na Nancy, alikuwa na uhakika mzee Katobe hakuwa na taarifa juu ya ngono iliyotendeka, kama angekuwa na fahamu asingekuwa katika hali aliyokuwa nayo usiku huo.

    “Kwanini umeondoka nyumbani?”

    “Nilikuja kumsalimia mama!”

    “Mbona mwenzako amesema kuna matatizo na anataka akuombe msamaha?”

    “Amesema ni matatizo gani baba?”

    “Hakutaja lakini anakuhitaji na ndio maana nimekufuata!”

    “Lakini mimi nataka kubaki na mama!”

    “Nancy analia sana, anakuhitaji nyumbani upesi tafadhali twende!”

    Moyo wa Tony ghafla ulishikwa na huruma aliposikia Nancy alikuwa akilia mfululizo na alipomwangalia mama yake usoni alipokea ishara ya kumtaka akubali kuondoka, hakutaka kukataa tena ili mradi mama yake alikuwa ameridhia.

    “Sawa twende baba! Mama kwaheri!”

    “Haya nenda mwanangu, ukaishi huko huko na usome shule, unaniona mimi hali yangu ilivyo! Sina uwezo wa kukusaidia lolote, mshukuru Mungu amekupa mzee Katobe akusomeshe!” Aliitikia mama yake wakati Tony na mzee Katobe wakitembea kuelekea nje, hali ilishabadilika hapakuwa na hofu tena na hawakutaka kumwonyesha mzee Katobe jambo walilokuwa wakifikiria kabla hajaingia ndani.

    “Usiwe na wasiwasi mama, nitamsomesha mtoto wako mpaka mwisho ili mradi tu waendelee kuelewana na mwanangu Nancy!”







    Gari lilifika na kuegeshwa tena nyumbani kwa mzee Katobe na wote wawili wakashuka na kuanza kutembea kuelekea ndani, mzee Katobe akiwa mbele Tony akimfuata nyuma, walinyoosha moja kwa moja hadi chumbani kwa Nancy na kuingia ndani! Nancy hakuyaamini macho yake aliruka kutoka kitandani na kumkumbatia Tony huku akilia machozi, mzee Katobe hakutaka kuendelea kukaa ndani ya chumba hicho aliondoka na kuwaacha Nancy na Tony peke yao.

    “Nisamehe Tony! Sikuwa mimi, bali moyo wangu! Nakupenda sana na sijui kama naweza kubadili mawazo, imekuwa ghafla mno lakini siwezi kujizuia”

    “Hata mimi nakupenda Nancy! Lakini tungeweza kusubiri kidogo, ni mapema mno kwetu kuanza mapenzi na isitoshe wewe unamfahamu vizuri baba yako, akielewa mimi na wewe tuna uhusiano huo, mwisho wa maisha yangu utakuwa umefika!”

    “Hawezi kuelewa!”

    “Huwezi kuwa na uhakika Nancy, ni bora suala hili tukalipa muda zaidi! Sasa hivi tuzingatie masomo!”

    “Sawa lakini...” Aliongea Nancy akiwa amemkumbatia Tony na katika hali ya kushangaza Tony alishtukia ulimi wa Nancy ukiingia mdomoni kwake, hakuweza kukataa aliupokea kama alivyotakiwa na dakika chache baadaye walijikuta wakielea katika anga ya mapenzi.

    “.....itabidi tu tuwe wapenzi Nancy!” Tony alikiri na kumshangaza Nancy, msisimko alioupata haukuwa wa kawaida na muda mfupi baadaye waliachana Tony akanyoosha chumbani kwake kulala.

    ****

    Maisha yaliendelea kama kawaida mpaka wakamaliza darasa la saba, mapenzi kati yao yakiwa ni siri kubwa ambayo haikushtukiwa na mzee Katobe wala mkewe na cha kushangaza zaidi mapenzi yalishabadilisha kibao, Tony alikuwa na hali mbaya zaidi kuliko Nancy! Alimpenda kupita kiasi na aligombana na vijana walioonekana kumfuatafuata Nancy wakimtaka mapenzi.

    Ulikuwa ni wivu usio na kipimo, mara kwa mara walikwaruzana sababu ya wanaume! Nancy alikuwa mwaminifu kupita kiasi kwa Tony, hata siku moja hakufikiria kumvunjia heshima! Yote hayo yaliendelea wakati wazazi wao wakiwachukulia kama mtu na dada yake.

    Mwaka ulioufuata walijiunga na shule ya sekondari ya Bagamoyo ambako walisoma pamoja mpaka kidato cha nne, uzuri wa Nancy uliongezeka maradufu! Usumbufu toka kwa walimu na wanafunzi nao pia uliongezeka na kuzidi kumpa wasiwasi Tony, kijana huyu hakujiamini kuna wakati aliona kama hakustahili kuwa na mpenzi kama Nancy kwa sababu ya umasikini wa familia yake kwani watoto wengi wa matajiri walimfuatafuata mpenzi wake.

    “Usiwe na wasiwasi Tony! Siwezi kukusaliti, wewe ni wangu tu mpaka maisha yangu yote!” Hayo ndiyo yalikuwa maneno ya Nancy kwa Tony kila siku.

    “Siamini!”

    Mpaka wanamaliza kidato cha nne na kwenda kidato cha tano na sita katika shule ya Kizunguzi huko Kilosa bado wivu ulimsumbua Tony! Mapenzi yake yalikuwa mazito mno kwa Nancy, kuna wakati alihisi yeye hakupendwa kama alivyopenda.

    Pamoja na wivu huo, Tony alikuwa tishio darasani, tangu darasa la kwanza mpaka anamaliza kidato cha sita hakuwahi kushika namba mbili, kila mtihani alikuwa namba moja mpaka kubandikwa na wanafunzi wenzake jina la ‘mtambo’! Mtihani wa kidato cha sita alifanya miujiza na serikali ikaamua kumpa nafasi ya kusomea udaktari katika chuo kikuu cha Beijing huko China!

    Nancy pia alifaulu vizuri na kupata nafasi ya kujiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa masomo ya Sheria, pamoja na hizi kuwa habari njema kwao zilikuwa za kusikitisha kwani zilimaanisha kuwatenganisha, badala ya kufurahi Tony alikesha akilia kwani alikuwa akitenganishwa na mpenzi wake kwa miaka saba!

    “Usiwe na wasiwasi utanikuta Tony!”

    “Siwezi kuamini, wewe ni mzuri mno Nancy! Wanaume wengine watakuona na utaniacha!”

    “Haiwezekani! Nitakusubiri Tony, nakupenda kwa moyo wangu! Kama ni wanaume mbona kila siku nawaona?”

    “Sawa, lakini miaka saba ni mingi sana Nancy!”

    “Usiwe na wasiwasi mpenzi, amini nakupenda Tony na nitakusubiri, nipo tayari kufanya lolote kukuhakikishia kuwa utanikuta!”

    “Kweli unaweza kufanya lolote?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo!”

    “Kesho twende mlingotini!”

    “Kufanya nini mpenzi?”

    “Kwa mganga ukale yamini!”

    “Yamini ni nini hiyo?”

    “Kiapo! Ili kama ukifanya mapenzi na mtu mwingine kabla sijarudi udhurike”

    “Hiyo tu mbona kitu kidogo, nakupenda sana Tony hata sasa hivi twende!” Aliongea Nancy kwa kujiamini.

    “Hamna tatizo tutakwenda kesho!”

    “Ok!”

    Siku iliyofuata walifanya kama walivyopanga, wakaenda kwa mganga na kueleza shida yao! Kama kawaida mganga alimweleza Nancy madhara ya kitu alichokuwa anataka kukifanya.

    “Binti kama huna uhakika kwamba utavumilia usifanye hiki kitu ni hatari!”

    “Mbona ni kitu kidogo mzee, uamuzi wa kufanya mapenzi ni wa mtu binafsi!” Aliongea Nancy kwa kujiamini na mambo yalifanyika, wakaondoka kwa mganga Tony akiwa ameamini anakwenda China kusoma na atamkuta mpenzi wake.

    “Lakini mbona wewe haukula yamini?”

    “Ah! Mimi ni mwanaume bwana!”

    “Nyie wanaume wajanja sana, si ajabu wewe utakuwa unafanya!”

    “Siwezi!”

    *****

    Wiki mbili baadaye Nancy alimwaga machozi uwanja wa ndege wa Dar es Salaam akimsindikiza Tony, akawa ameondoka na kumwacha Nancy akijiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam, ilikuwa huzuni kubwa sana mioyoni mwao wote wawili.

    Tony alitua Beijing baada ya masaa ishirini na nne na kwenda moja kwa moja chuoni, alikuwa bado akitokwa na machozi! Kumbukumbu za Nancy zilikuwa bado zikimtawala kichwani mwake, miaka saba mbali na mpenzi wake haikuwa kidogo! Ilikuwa ni sawa na mtoto kuanza darasa la kwanza mpaka kumaliza la saba.

    “Ili mradi amekula yamini nitamkuta!” Aliwaza Tony.

    Chuoni alipokelewa na msichana aliyeitwa Mimi, alikuwa mchanganyiko wa Mnaigeria na Mmarekani, Tony alishangazwa na uzuri wa msichana huyo, hakutegemea kukuta msichana mzuri kama huyo katika nchi ya Wachina.

    “You’re beautiful Mimi!”(Wewe ni mzuri Mimi!)

    “You’re handsome as well Tony!”(Wewe ni mzuri pia Tony!)

    Walisoma darasa moja na waliishi bweni moja ingawa vyumba tofauti.

    ****

    Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Nancy alipokelewa na kijana wa Kichaga aliyeitwa Daniel, wengi walimwita Danny. Alikuwa kijana mrefu, mwenye kifua kilichojaa na mikono iliyotuna! Alikuwa na macho malegevu na midomo ya duara, kifupi hakuna mwanamke angemwona Danny akaacha kusisimkwa na mwili!

    “Nancy, kwanini kila siku unalia?”

    “Namkumbuka rafiki yangu wa kiume!”

    “Yuko wapi?”

    “Beijing!”

    “Asiyeko machoni na moyoni mfute! Nitakufanya umsahau”

    “Danny usirudie tena kuniambia hivyo siku nyingine! Tutakosana kabisa!” Alifoka Nancy.

    Nancy na Danny walisoma darasa moja na waliishi bweni moja ingawa vyumba tofauti! Danny aliapa kumpata Nancy kwa njia na kwa gharama yoyote ile.



    Mawasiliano kati ya Tony na Nancy yalikuwa yamekatika kabisa, hakutaka kuwasiliana naye kama njia ya kujisahaulisha, kwa wiki kadhaa alikuwa hajaongea na Nancy! Kwa kufanya hivyo aliamini labda angemwondoa kabisa akilini mwake, siku zote alikuwa karibu sana na Mimi, alishaamua kuwa mpenzi wake hapakuwa na njia yoyote ya kumtenganisha naye tena, hakujali mambo yaliyotokea nyuma wala kiapo ambacho Nancy alikula kwa mganga wa kienyeji, aliamini lazima angepata suluhisho na labda angerudi tena kwa mganga ili kiapo hicho kiondolewe.

    Ni suala la kiapo hicho ndilo lililomsumbua sana Tony, aliamini ndicho kilimfunga Nancy na kumfanya awe mtumwa kwa mwanaume mmoja, lilikuwa ni kosa kubwa sana kumlisha Nancy kiapo hicho kwani asingeweza kuwa na mwanaume mwingine tofauti na yeye wakati tayari alikuwa na msichana mwingine ambaye kwa uhakika ndiye angekuwa mke wake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kinachonisumbua mimi akilini mwangu si kingine ni kiapo alichokula!”

    “Hilo sio tatizo! Ziko dawa Nigeria naweza nikaenda kukuletea, ukimpa akala kiapo chenu kinatoka!”

    “Kweli?”

    “Sina sababu ya kukudanganya, tofauti na hivyo akikutana na mwanaume mwingine bila kiapo kuondolewa atakuwa mwehu au hata kufa kabisa!”

    “Sasa kwanini usiende Nigeria kuniletea hiyo dawa ili ukirudi nami nipange safari ya kwenda Tanzania kumweleza Nancy msimamo wangu baada ya kuwa nimemlisha hiyo dawa utakayoleta?”

    “Inawezekana!”

    “Basi fanya hivyo ili wiki ijayo mimi niende Tanzania!”

    “Nitaondoka kesho!”

    Hivyo ndivyo ilivyokuwa, Mimi alipanda ndege kurejea Nigeria kufuata dawa, alibeba siri kubwa kifuani mwake ambayo Tony hakuielewa, msichana huyu alifikiria mauaji ili kumwondoa mtu waliyegombania naye mwanaume, Nancy! Mpaka wakati huo alikuwa haamini kama kweli alikuwa amempata Tony moja kwa moja, hali haikuonyesha hivyo, alihisi hapakuwepo na mapenzi ya dhati bali Tony alimkubali kwa sababu ya pesa zake, kwa kumwondoa Nancy alikuwa na uhakika Tony angekuwa wake milele.

    Hakwenda Nigeria kama alivyoaga, akiwa Misri alibadilisha ndege na kupanda nyingine iliyompeleka hadi Marekani ambako aliwaona wataalam wa kutengeneza sumu za kuua taratibu na kuwaomba wamuuzie sumu hiyo kwa matumizi yake binafsi! Hawakukataa baada ya kuwashawishi kwa pesa nyingi, akawa ameuziwa sumu hiyo na kuondoka nayo.

    Siku nne baadaye alirejea tena nchini China ambako kabla ya kufika shuleni alinunua unga wa miti shamba na kuuchanganya na sumu aliyokuwa nayo, ilikuwa ni sumu kidogo sana yenye uwezo wa kuua mara iingiapo katika damu ya binadamu, huua chembechembe za damu kidogokidogo na hatimaye kuzimaliza kabisa, mgonjwa hupungua mwili na baadaye hugundulika ana kansa ya damu ama Ukimwi! Sumu hiyo ilitumiwa sehemu mbalimbali kufanya mauaji bila muuaji kugundulika, ilikuwa ni sumu ambayo haijagunduliwa na watu wengi.

    Tony alifurahi kumwona Mimi amerejea na kumkabidhi dawa aliyokuwa amefuata, kilichofuata ni yeye kupanga safari ya kuja Tanzania, ilipangwa siku tatu baadaye! Kwa dawa aliyokuwa nayo alikuwa na uhakika Nancy angekuwa huru kuolewa na mwanaume mwingine, hivyo ndivyo Mimi alivyomweleza, hakumtajia kabisa kwamba ilikuwa ni sumu na kwa kumpa Nancy unga huo wa dawa za kienyeji angekuwa anamuua mtu asiye na hatia! Pamoja na Tony kuamua kumwacha Nancy hakumchukia, asingeweza kufikiria kumuua bali alitaka waachane kwa njia za amani.

    “Hiyo itasaidia sana! Utakachofanya ni kumchanganyia katika chakula bila kumtaarifu, baada ya tu ya kula utaona amebadilika kabisa, wala hataonyesha nia ya kuwa na wewe tena, isitoshe tangu siku hiyo atakuwa na uhuru wa kuwa na mwanaume yeyote amtakaye!”

    “Kweli?”

    “Hakika!”

    “Basi acha kesho kutwa niende Tanzania, nikamalizana naye!”

    Dakika ishirini baadaye wakiwa bado katika maongezi yao tena wote wakiwa kitandani, simu chumba kwa Mimi ambako Tony alikuwa amehamia ili kuzikimbia simu za Nancy iliita, Mimi aliinyanyua na kuipokea, ilitoka idara ya mapokezi ya wageni.

    “Kuna mgeni wako mapokezi!”

    “Mgeni wangu kutoka wapi?”

    “Aha sielewi!”

    “Hajakueleza?”

    “Hajasema ila ni mwanamke! Lazima twende wote, isijekuwa una mwanamke mwingine hapa China!”

    “Twende basi!”

    Wote wawili walinyanyuka kitandani na kuvaa nguo kisha wakaanza kushuka ngazi kuelekea Mapokezi, Hawakumwona mgeni wao mara moja walipofika ikabidi Tony amuulize msichana wa mapokezi ambaye alinyoosha mkono wake na kusonta kwenye kona iliyokuwa pembeni! Nancy alikuwa amekaa hapo na mizigo yake! Tony alishtuka na kutaka kurudi nyuma, jambo lililomshtua Mimi.

    “Kwanini unataka kurudi nyuma?”

    “Ni Nancy!”

    “Sasa ndio umkimbie wakati ulitaka kumfuata Tanzania?”

    “Naogopa!”

    “Unaogopa nini?”

    “Nashindwa nitamweleza nini!”

    “Mbona kitu rahisi, ukishampa ile dawa niliyoleta, yeye mwenyewe atabadilika!”

    “Kweli! Lakini kumbuka tulikuwa tunapendana sana na huyu msichana!”

    “Bwana usiongelee historia, ongea habari zilizopo!”

    “Sasa?”

    “Twende!”

    “Nitakutambulishaje?”

    “Wewe sema mimi ni mwanafunzi mwenzako!”

    Wote wawili walijitokeza na kuanza kutembea kuelekea mahali alipokuwa amekaa Nancy akiwa amejiinamia, walifika na kusimama mbele yake na Tony akamwita jina! Nancy akanyanyua kichwa chake kuangalia juu, macho yake yakapambana na sura ya Tony, hakuamini kama alichokuwa anakiona mbele ya macho yake ndicho kilichomfanya asafiri kutoka Tanzania kwenda Beijing! Aliruka na kumkumbatia Tony aliyeonyesha uso wa kutofurahishwa na ujio wake kwa furaha kubwa.

    “Mbona umekuja bila kunitaarifu?”

    “Nikutaarifu vipi wakati hupokei simu?”

    “Sasa ndio ukaamua kuja tu?”

    “Nilitaka kukupa mshangao au Suprise kwa kimombo!” Aliongea Nancy akitabasamu huku macho yake yakiwa yamemwangalia msichana aliyekuja na Tony.

    “Na huyu ni nani mbona hunitambulishi?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Ni mwanafunzi mwenzangu tunasoma naye!”

    “Anaitwa nani?”

    “Anaitwa Mimi!”

    “Huyu ndiye Mimi?”

    “Kwani unamfahamu?” Badala ya kujibu Tony aliuliza swali.

    “Mbona kachoka namna hii? Au umebabaika kwa sababu ni Mmarekani?”

    “Nimebabaika kitu gani?”

    “Tony! Tony! Tony! Taarifa zako zote ninazo, kumbuka tulikotoka mimi na wewe na usisahau kuwa mimi nilikula yamini kwa mganga wa kienyeji, usifikirie kuniacha Tony, siwezi kuwa na mwanaume mwingine nilishakula kiapo!” Aliongea Nancy kwa ukali.

    “What the shit is she talking about!”(Anaongea upuuzi gani?) Mimi aliuliza akimwangalia Nancy kuanzia juu hadi chini.

    “Hey! You whore, how do you dare call what comes out of my mouth shit?”(Hey! Wee malaya unawezaje kuyaita maneno ninayoyaongea upuuzi?) Nancy aliuliza kwa ukali akimsogelea Mimi, dakika mbili baadaye walikuwa chini Nancy akiwa amekaa juu ya Mimi, ngumi mfululizo zikitua usoni kwake! Watu walifika na kusaidiana na Tony kumwondoa Nancy aliyekuwa akilia kwa hasira.

    Taarifa zilishafika ofisini kwa mlezi wa wanafunzi na Tony, Nancy na Mimi waliitwa kuhojiwa, Tony alimtambua Nancy kama mgeni wake kutoka Tanzania, alipotakiwa kueleza chanzo cha ugomvi alishindwa ndipo Nancy akaeleza kila kitu waziwazi, alilaumiwa kwa kitendo chake cha kupigana mbele ya kadamnasi kilichotafsiriwa kosa kisheria nchini China.

    “Kwa hali aliyonayo Mimi itabidi apelekwe hospitali na lazima taarifa itolewe polisi!” Alisema mlezi wa wanafunzi.

    Simu ilipigwa kituo cha polisi cha chuo kikuu cha Beijing na polisi wakafika na kumchukua Nancy hadi kituoni ambako alihojiwa, alikiri kupigana lakini aliielezea vizuri sababu iliyopelekea yeye kutenda kosa hilo. Sababu yake haikutosha kufanya polisi wamwachie huru akatupwa mahabusu na taarifa za kuwepo kwa Mtanzania mikononi mwa polisi zikapelekwa kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini China.

    Nancy alilia kupita kiasi, hakuamini kama mtu aliyempenda kupindukia angeweza kumtendea jambo hilo, ilikuwa ni kama ndoto! Aliamini baadaye labda baadaye angezinduka na kukuta mambo yakiwa kama yalivyokuwa awali lakini haikuwa hivyo, ukweli uliendelea kuwa ukweli! Alishinda mahabusu hadi jioni bila kumwona Tony, alikumbuka nyumbani, aliwakumbuka wazazi wake na alishindwa kuelewa ni nini angefanya kumsahau Tony na kukiondoa kiapo alichokula ili aweze kuwa huru tena jambo ambalo kwake halikuwa rahisi.

    Alikuwa ameumia tena kupindukia, hakutegemea maishani mwake kumpenda mwanaume tena na hicho ndicho alichouahidi ubongo wake, kamwe asingempenda mwanaume kwa sababu alikuwa ameumizwa na mwanaume, aliwaona viumbe wote wenye jinsia tofauti na yake si binadamu wa kawaida, kwamba hawakuwa na huruma hata kidogo.

    Wakati akiteseka mahabusu, Tony aliyesaidiwa na baba yake Nancy kusoma hadi kufika chuo kikuu, alikuwa amekumbatiwa na Mimi kitandani akimfariji na kumwomba msamaha kwa mambo yaliyotokea! Mimi alikuwa akilia kwa uchungu na kumlaumu Tony kwa kila kitu, mwisho kabisa alimsamehe na kumwomba Tony ampelekee Nancy dawa aliyoileta huko mahabusu alikokuwa ili kuepusha matatizo.

    “Sawa! Ulisema ni ya kuchanganya kwenye chakula?”

    “Ndiyo! Nenda kanunue chakula chochote cha majimaji na uweke ndani yake unga niliokupa, akila tu tayari mambo yatakuwa yamebadilika! Hatakuwa na hasira tena dhidi yangu au yako na baada ya hapo atakuwa huru kufanya lolote maishani mwake, vinginevyo ataendelea kutusumbua maishani mwetu, anaweza hata kuniua!”

    Tony hakusema kitu tena, aliondoka chumbani kwa Mimi na kwenda chumbani kwake ambako aliuchukua unga ulioletwa na Mimi na kushuka nao hadi kwenye mgahawa wa chuo ambako alinunua viazi vilivyosagwa, akamwaga nusu ya unga wa miti aliokuwa nao ndani yake akiamini ni dawa ya kuondoa kiapo cha yamini alichokula Nancy huko Bagamoyo, alikuwa amedhamiria kuachana naye na kuwa na Mimi.

    Hakutaka tena kurudi bwenini, alichofanya ni kuondoka moja kwa moja hadi kituo cha polisi na kuomba kumwona Nancy akidai alikuwa amemletea chakula na alitaka kuongea naye, polisi hawakuwa na tatizo juu ya hilo, walimruhusu akaingia ndani ya kituo na kuonyeshwa chumba maalum ambako Nancy aliungana naye muda mfupi baadaye akilia kwa uchungu.

    “Nisamehe Nancy! Nitabadilika, tunahitaji kuongea juu ya jambo hilo lakini hata hivyo kula kwanza chakula, nitakueleza kila kitu juu ya msimamo wangu, nakupenda Nancy lakini.....!”

    “Lakini kitu gani?”

    “Kula kwanza!”

    “Nitakula kwa sababu nina njaa!”

    “Na mimi pia nataka ushibe kabla sijakueleza ninachotaka kusema!”





    Wafanyakazi wa ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini China, waligubikwa na huzuni, habari kuwa msichana wa Kitanzania alikuwa amepigana katika chuo Kikuu cha Beijing, tena akiwa mgeni zilikuwa zimewasikitisha sana! Ilikuwa ni aibu kubwa kwa nchi ya Tanzania, ukizingatia uhusiano mzuri uliokuwepo kati ya nchi hizo mbili.

    “Tumwambie Balozi?”

    “Hatuwezi kuficha, hili ni jambo kubwa sana na kwa sababu limeshafika polisi ni lazima Balozi ataliona katika taarifa za habari, tutaingia katika matatizo!”

    “Basi nenda wewe ukamwambie!” Imelda, mmoja wa wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China alimwambia mfanyakazi mwenzake aitwaye Kulwa, wote walikuwa ni vijana wa Kitanzania na walisikitishwa sana na kilichotokea.

    “Nenda wewe, si ndiye sekretari wake?”

    “Ina maana unamwogopa Balozi?”

    “Sio hivyo tunafuata protoko!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Imelda alinyanyuka kitini na kuanza kutembea kuelekea ofisini kwa Balozi, alifungua mlango na kuzama ndani wakati anaingia tayari saa ya ukutani ilikuwa ikionyesha saa kumi na moja na nusu kwa majira ya China! Balozi alikuwa nyuma ya meza kubwa, simu ilikuwa masikioni mwake alionekana kupokea maelekezo fulani kutoka nyumbani Tanzania. Imelda aliketi chini kumsubiri, dakika kumi baadaye alirudisha simu mahali pake na kumwamuru Imelda aketi kitini.

    “Vipi binti?”

    “Kuna tatizo mheshimiwa!”

    “Tatizo gani tena?”

    “Tumepigiwa simu kutoka kituo cha Polisi na kutaarifiwa kwamba kuna msichana kutoka Tanzania, aliwasili hapa jana na alikuja kumtembelea mchumba wake ambaye ni mwanafunzi katika chuo kikuu cha Beijing, sasa kilichotokea ni kwamba alimkuta mchumba wake ana mpenzi mwingine na kuamua kufanya vurugu kubwa iliyopelekea msichana ambaye ni mpenzi mpya wa mchumba wake kujeruhiwa vibaya, hivi ninavyoongea na wewe huyo msichana ameshonwa nyuzi kumi usoni na msichana wa Kitanzania yupo mahabusu!”

    “Sasa?” Balozi aliuliza.

    “Unahitajika makao makuu ya polisi Mheshimiwa na kama sio wewe,basi utume mjumbe!”

    “Jamani hamuwezi kuona kuwa ni na kazi nyingi, hiyo simu uliyokuta naongea nayo imetoka Ikulu, kuna ujumbe wa chama cha wafanyabiashara na wenye viwanda nchini Tanzania, TCCIA, wanakuja hapa China kwenye maonyesho ya Februari. Sidhani kama naweza kwenda huko, hebu niitie Mwaibale!” Alisema Balozi akimaanisha msaidizi wake aitwe na Imelda alitoka ofisini haraka na aliporejea aliongozana na Kulwa.

    “Ndio bosi!”

    “Kuna tatizo nafikiri umeshalisikia!”

    “Ndiyo!”

    “Kwa hiyo naomba uniwakilishe makao makuu ya polisi, mimi siwezi kwenda najiandaa kupokea ugeni kutoka Tanzania!”

    “Hakuna tatizo nitakwenda! Si ni lazima nianzie makao makuu?”

    “Ndiyo! Si wito umetoka huko? Au sio Imelda?”

    “Ndiyo hivyo bosi!”

    ***

    Wakati wanaondoka ofisini kwa Balozi na Kulwa kupitiliza hadi nje ya ofisi ambako alipanda ndani ya gari, akiendeshwa na dereva wa Kichina Mr Yu kuelekea makao makuu ya polisi mtaa wa Capital.

    Tayari ilikuwa saa kumi na mbili na dakika kumi na tano za jioni. Ni wakati huo ndio Tony alikuwa akiwasili kituo cha polisi na kuomba aonane na Nancy, mfuko wake wenye chakula kilichouwa ana sumu ambacho yeye aliamini kilikuwa na dawa ya kuondoa Yamini ili kumweka Nancy huru ulikuwa mkononi mwake.

    Hakuelewa hata kidogo kwamba alibeba sumu, angejua asingempatia chakula hicho Nancy! Hakumchukia, alimpenda na alikumbuka wema aliomfanyia, bila yeye maisha yake yasingekuwa hapo alipokuwa!

    Katu asingeweza kumuua mtu aliyemtendea mambo mema katika maisha yake, alichotaka kufanya ni kumwondolea Nancy kiapo cha hatari alichokula ili akitaka kuwa na uhusiano na mwanaume mwingine kusiwe na kizuizi chochote.

    “Kula basi mama!” Tony alizidi kumbembeleza Nancy ili ale chakula, alitaka sana jambo hilo litokee ili Nancy aweze kumchukia na kumwacha ili atafute mwanaume mwingine, hakuelewa ndani ya chakula hicho kulikuwa na sumu mbaya ya kuua taratibu.

    “Nafikiri umenielewa kuwa nitakula kwa sababu nina njaa vinginevyo nisingekula kabisa, umeniudhi sana Tony na sijui baba yangu utamwambia nini siku mkikuta....!” Hakuimaliza sentensi hiyo kwikwi ya kulia ikamkaba tena.

    Kwa dakika kumi na tano nzima, Nancy aliendelea kulia huku Tony akizidi kumbembeleza ili ale chakula, kwikwi ilikuwa imemkaba kooni, asingeweza kufungua mdomo wake na kula chakula ndani yake, alikuwa na hasira kali isiyopimika.

    “Watu wa namna yenu ndio watu huwa wanawaua!” Aliongea Nancy huku akivuta sahani ya chakula karibu yake tayari kwa kula.

    “Samahani mpenzi! Najua nimekukosea lakini uwe tayari kunisamehe, naomba ule ushibe kisha tuanze kuongea!”

    “Sawa Tony lakini....!”

    ****

    Kulwa alikuwa akitoka ofisini kwa kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Beijing, jasho lilikuwa likimtoka! Alikuwa amepewa barua nyingine kwenda nayo kituo cha polisi cha kati, kilichoitwa Central Beijing Police station! Mfumo wa polisi wa China ulikuwa sawasawa kabisa na Bongo, urafiki wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa China, Mwanamapinduzi Mao Tse Tung ulifanya mambo mengi kati ya nchi hizi mbili yafanane.

    “Vipi?” Dereva wake alimuuliza.

    “Ilishakuwa shughuli!”

    “Kwanini?”

    “Yule msichana ana hatia lakini serikali ya China haitaki kumfunga kwa sababu ya uhusiano wa nchi zetu! Ukizingatia suala lenyewe ni la mapenzi na msichana mwenyewe ametendewa kitu kibaya, polisi wameamua tumchukue tumrudishe nyumbani leo usiku!”

    “Afadhali, maana kwa sheria za hapa lazima angekwenda jela sio chini ya miaka mitano!”

    Gari liliondoka makao makuu ya polisi kwa kasi ya ajabu, kuelekea kituo cha polisi cha kati cha Beijing, ilikuwa ni lazima Nancy asafirishwe chini ya uangalizi maalum usiku huo huo kurudi nyumbani Tanzania, kila kitu kilishaandaliwa, saa tatu na nusu ndege ilikuwa inaondoka Beijing kuelekea Hong Kong na baadaye Dubai, Nairobi ambako Nancy angepandishwa katika ndege ya shirika la ndege la Kenya, KQ na kuwasili Dar es Salaam masaa arobaini na nane baadaye.

    Kulwa aliwasili kituoni akiwa na barua na kuingia nayo moja kwa moja ofisini kwa mkuu wa kituo na kumkabidhi! Alipoisoma alielewa kila kitu kwani tayari alishapewa taarifa, alimwita mmoja wa maaskari waliokuwepo mapokezi au Charge room office, CRO kama ilivyoitwa na maaskari na kumwamuru amwite Nancy kutoka mahabusu, askari huyo alinyoosha moja kwa moja mahabusu lakini hakumkuta na kurudi tena hadi mapokezi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Yuko kwenye kile chumba cha kuongea na wageni!” Askari mmoja aliyekuwa mapokezi alisema.

    Bila kuchelewa askari aliyetumwa aliondoka akikimbia kuelekea chumba alichoelekezwa, alipofungua mlango Nancy alikuwa nyuma ya meza akisogeza sahani iliyokuwa na chakula ili ale, alimwonyesha ishara huku akiongea Kichina maneno yaliyokuwa na maana, Nancy aache kwanza kula chakula kwani alikuwa akihitajika na bosi ofisini kwake lakini Nancy hakuelewa alichokuwa akielezwa, alizidi kuvuta sahani yake! Kwa kipindi hicho alimchukia kila mtu.

    “Stop eating dha food!”(Acha kula chakula!) Aliongea Mchina kwa kiingereza chenye lafudhi ya Kichina moja kwa moja.

    “Why?”(Kwanini?) Tony aliuliza.

    “ Dha boss is need her!”(Mkuu anamhitaji!) Mchina aliendelea kuivunjavunja lugha ya wenyewe bila huruma, huku akimvuta Nancy kutoka mahali alipokaa na kuanza kuondoka naye kuelekea ofisini kwa mkuu wa kituo.

    “This is not fair! How can you keep someone without food for more than three hours? Despite being told she hasn’t had anything since moning?”(Hii sio sawa! Unawezaje kumweka mtu bila chakula zaidi ya masaa matatu? Pamoja na kuwa umeambiwa hajala kitu toka asubuhi?) Alilalamika Tony.

    Lengo lake la kumwondolea Nancy kiapo alichokula Bagamoyo lisingetimia bila binti huyo kula chakula alichokuwa amemletea! Hakuelewa chakula alichokuwa ameleta kilikuwa hatari kiasi gani, laiti angejua angemshukuru Mungu kuona Nancy ameondoka bila kukila.

    Ofisini kwa mkuu wa kituo hapakuwa na maongezi marefu, Nancy alitambulishwa kwa Kulwa Mwaibale na kuelezwa ni kwanini kijana huyo kutoka ubalozi wa Tanzania nchni China alikuwa kituoni pia alielezwa adhabu ya kosa alilokuwa ametenda na alitakiwa kuelewa kuwa uhusiano wa Tanzania na China ulikuwa umemsaidia.

    “Siwezi kuondoka, nasema siwezi! Lazima niongee na Tony pengine tunaweza kuelewana” Aliongea Nancy kwa kiswahili akimwambia Kulwa ambaye alimtafsiria mkuu wa kituo nini kilichokuwa kikisemwa.

    “Itabidi uondoke! Hii ni amri na si ombi, tunafanya hivi kukusaidia vinginevyo ungekwenda Jela miaka mitano!”

    “Sitaki! Kama ni jela nipelekeni lakini nisikae mbali na Tony, ninampenda na yeye ananipenda! Amezuzuliwa tu na penzi la yule Malaya, naamini anaweza kubadilika!” aliongea Nancy akilia.

    Hakuna aliyemsikiliza tena, wote walimwona amechanganyikiwa kwani kilichokuwa kikifanyika wakati huo kilikuwa ni kinyume kabisa cha sheria za China ila kilitendeka kwa ajili ya kumsaidia yeye! Mkuu wa kituo aliita askari wawili kutoka mapokezi walioingia muda mfupi baadaye na kuamriwa kumkamata Nancy haraka iwezekanavyo.

    Hilo lilifanyika, akapigwa pingu mikononi na kutolewa kituoni chini ya ulinzi mkali, nje kabla hajapakiwa ndani ya gari la polisi alimwona Tony akiwa amesimama pembeni, roho yake ilimuuma sana! Bado alimpenda Tony haikuwa rahisi hata kidogo kumfuta akilini mwake pamoja na yote yaliyotokea.

    “Love you Tony! And will always do! Please dont do that to me, you know I love you and will never get you out of my mind!”(Nakupenda Tony! Na nitakupenda siku zote! Tafadhali usinifanyie hivyo, unajua nakupenda na sitakutoa akilini mwangu!)

    “I’m sorry Nancy! It’s not me but Mimi, she force me into a relationship that I can not simply pop out at the moment! Anything that happened between you and I is history now, I’m deeply in love with Mimi, you better look for somebody else!”(Samahani Nancy, sio mimi, lakini ni Mimi ndiye amesababisha yote haya, alinilazimisha kuingia kwenye uhusiano ambao hivi sasa si rahisi kwangu kuuacha! Chochote kilichotokea kati yangu mimi na wewe hivi sasa ni historia, ni bora ukatafute mtu mwingine!) Aliongea Tony huku akitabasamu na kumshangaza Nancy, yalikuwa mabadiliko ya ghafla mno na yaliyotendwa na mtu ambaye hakutegemewa.

    “NO!NO!NO!NOOOOO! NO TONY! YOU CANT DO THIS TO ME, I LOVE YOU, I LOVE TONY, WITH ALL MY HEART! THAT MIMI IS JUST ANOTHER LAIR, SHE DOESN’T LOVE YOU, PLEASE REMAIN MY BABY! DO YOU STILL REMEMBER WHAT WE DID AT BAGAMOYO?”(Hapana! Hapana!Hapana!Hapaana Tony, huwezi kunitendea hivyo, nakupenda, nakupenda Tony tena kwa moyo wangu wote, huyo Mimi ni mwongo tu, hakupendi! Tafadhali endelea kuwa wangu, bado unakumbuka tuliyoyafanya Bagamoyo?) Aliongea Nancy huku akilia.



    Dakika zilizotolewa na maaskari ili Tony na Nancy waongee zilikwisha, akaanza kuvutwa hadi kwenye gari ambako mlango ulifunguliwa akaingizwa ndani kwa nguvu huku akilia, maaskari wawili wakaingia na kukaa mmoja kila upande wa Nancy! Lilikuwa jambo la kutia huzuni sana lakini alipochungulia nje kupitia dirishani alimwona Tony akicheka, moyo wa Nancy ulizidi kuuma.

    Kwa nguvu za Kitanzania kabla gari halijaondoka, akiwa amepigwa pingu mikononi, Nancy alijitahidi na kumsukuma askari aliyekuwa mkono wake wa kuume na wote wawili wakaanguka chini.

    “I’m not going!”(Siendi!)

    Pamoja na kukataa Nancy asingeweza kuwashinda maaskari wawili kwa pamoja, alikamatwa tena, akapakiwa ndani ya gari na likaondoka moja kwa moja hadi uwanja wa ndege.

    Wakati wanawasili uwanja wa ndege ilikuwa tayari saa moja na nusu, masaa mawili baadaye Nancy alitakiwa kuondoka chini ya ulinzi wa maaskari wawili wa Kichina! Alikuwa bado akilia na kujaribu kuchukulia mambo yaliyotokea kama ndoto, akiamini labda baadaye angezinduka na kujikuta yuko Tanzania akiongea na Tony katika simu, wakicheka na kufurahi na kukumbushiana ahadi yao ya ndoa baada ya masomo.

    Haikuwa hivyo, kila kitu kilichotokea kiliendelea kuwa kweli na saa tatu na nusu Nancy alikabidhiwa kwa maaskari wengine wawili tofauti na waliomtoa kituoni, akaongozwa hadi ndani ya ndege ambao alikaa katikati ya maaskari wawili akiwa chini ya ulinzi wa kutosha.

    “Why do you treat me like a Terrorist?”(Kwanini mnanichukulia kama gaidi?) Aliwauliza maaskari wakati ndege ikijiandaa kuruka.

    “That is what we have been told to do! You are supposed to reach Tanzania under Maximum security!”(Hivyo ndivyo tulivyoambiwa tufanye, unatakiwa kufika Tanzania chini ya uangalizi wa hali ya juu kiusalama!) Alijibu mmoja wa maaskari.

    Ndege iliiacha China na saa moja na nusu baadaye ilikuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Hong kong, abiria wengine walipanda katika uwanja huo, wakiwemo waafrika kadhaa! Wote walimwangalia Nancy kwa macho ya huruma.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alifika hapo akilia, hata ndege ilipoondoka bado aliendelea! Dubai hadi Nairobi hakuweza kuyazuia machozi yasitiririke, moyo wake ulikuwa umeumia kiasi ambacho binadamu yeyote asingeweza kuvumilia!Hakuna alichouambia moyo wake zaidi ya kutopenda tena, aliahidi kutomruhusu mwanaume kuuteka moyo wake tena.

    “Nitaishi mwenyewe! Sitaki mpenzi tena maishani mwangu, sitapenda tena!” Alijisemea Nancy alipoikanyaga ardhi ya Kenya baada ya kushuka kutoka katika ndege ya China Airways.

    Chini ya ulinzi mkali alipakiwa ndani ya ndege ya shirika la Ndege la Kenya, iliyokuwa ikisafiri kutoka Nairobi kuelekea Dar es Salaam. Alifurahi kufika karibu na nyumbani, mahali kulikokuwa na watu waliompenda ambao angewaeleza matatizo yake na pengine wakampa faraja. Kidonda kilikuwa kikubwa moyoni na hakutegemea kingepona kwa urahisi.

    Nusu saa baadaye ndege iliondoka Nairobi na kutua Dar es Salaam katika muda wa saa moja, uwanja wa ndege badala ya kupokelewa na wazazi wake, Nancy alipokelewa na maaskari, makabidhiano kati ya maaskari wa China na Maaskari wa Tanzania yalifanyika mbele yake huku kamera za waandishi wa habari zikimulika kila upande, kichwani mwake alielewa habari yake ingetawala vyombo vyote vya habari nchini Tanzania siku iliyofuata.

    Maaskari wa China waligeuza na ndege iliyowaleta kurudi Nairobi, Nancy akawa ameingia mikononi mwa askari wa Tanzania na kupelekwa moja kwa moja hadi kituo cha polisi cha kati ambako kwanza kabla hata ya mahojiano alinyang’anywa hati yake ya kusafiria ndipo mahojiano yakaanza, alikataa kuongea chochote mpaka wazazi wake wawepo.

    Ilikuwa tayari ni saa nne asubuhi Simu, ilipigwa nyumbani kwao Nancy huko Bagamoyo! Wazazi wake walipata mshtuko wa ajabu, hawakutegemea kabisa kupata habari hiyo asubuhi. Walichofahamu ni kwamba mtoto wao alikuwa nchini China.

    “Nancy! Yuko kituo cha polisi?”

    “Ndiyo!”

    “Nini kimetokea? Si alikuwa China?”

    “Ndiyo! Lakini amerudishwa nchini!”

    “Kafanya nini?”

    “Mtaelezwa mkifika hapa!”

    “Tunakuja!” Baba yake Nancy alisema.

    Baada ya kukata simu alimsimulia mke wake kila kitu na hawakutaka kupoteza muda, haraka waliingia ndani ya gari lao na kuanza kuendesha kuelekea jijini Dar es Salaam. Masaa mawili baadaye , sababu ya ubovu wa barabara, gari lao lilikuwa likiegeshwa mbele ya kituo cha polisi.

    Walishuka na kutembea kwa haraka kuelekea ndani ambako waliulizia mahali alipokuwa mtoto wao, suala la Nancy lilishapata umaarufu kituo cha polisi, waliambiwa wapande hadi ghorofa ya tatu, ofisini kwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa. Walimkuta Nancy amekaa kwenye benchi akiwa na mizigo yake na akiendelea kulia, alinyanyuka na kuwakumbatia baba na mama yake.

    “Vipi mwanangu?” Mzee Katobe aliuliza.

    “Tony!Tony!Tony baba kani....!” Kwikwi ya kulia ilimkaba Nancy kiasi cha kushindwa kuongea, wazazi wake walishindwa kuelewa ni nini kilichokuwa kimetokea mpaka mtoto wao kuwa katika hali hiyo na hapakuwa na uwezekano wa Nancy kueleza kutokana na hali aliyokuwa nayo, ilibidi mzee Katobe aingie moja kwa moja ofisini kwa mkuu wa Upelelezi Mkoa ili aelezwe kilichotokea, ndani aliambiwa kila kitu kilichotokea nchini China na kutoka akiwa amepandwa na hasira.

    “Tenda wema uende zako usingoje shukrani! Yaani Tony ndiye mtu wa kunifanyia hivi mimi? Sawa tutaona!” Aliongea kwa chuki mzee Katobe.

    “Kwani kimetokea nini?” Mke wake aliuliza.

    “Twendeni, tutaongea kila kitu nyumbani!” Aliongea Mzee Katobe akimnyanyua Nancy kutoka mahali alipoketi, mke wake alisaidia kubeba mizigo na wakashuka ngazi hadi kwenye gari lao.

    Waliondoka mzee Katobe akiendesha kwa kasi hadi Bagamoyo, waliingia saa sita ya usiku! Hawakuwa tayari kumwacha Nancy alale peke yake kwa hali aliyokuwa nayo, kilichofanyika ni mama yake kuhamia chumbani kwa Nancy na kulala naye hadi asubuhi. hakuna kilichofanyika zaidi ya kumfariji mtoto wao na kumfanya achukulie kila kitu kilichotokea kama sehemu ya maisha, walielewa ni kiasi gani iliumizwa lakini ilikuwa ni lazima waungane na mtoto wao katika tatizo alilokuwa nalo.

    Asubuhi hiyo kabla hata ya kunywa chai, gari aina ya Rangrover, muundo wa kisasa liliegesha mbele ya nyumba ya mzee Katobe, kijana mrefu mwenye sura nzuri na mwili uliojaa kama mcheza mpira wa kikapu alishuka na kufunga mlango wa gari lake na kutembea hadi kwenye mlango wa mbele ambako aligonga na kufunguliwa na mzee Katobe.

    “Shikamoo mzee!”

    “Marahaba hujambo mwanangu?”

    “Sijambo baba! Hapa ndio nyumbani kwa mzee Katobe?”

    “Ndiyo! Na mimi mwenyewe ndiye mzee Katobe!”

    “Ahsante mimi naitwa Danny! Ah, ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam!”

    “Ndiyo, nikusaidie nini mwanangu?” Aliuliza mzee Katobe badala ya kumkaribisha Danny ndani ya nyumba.

    “Ah! Nimesoma kwenye gazeti leo asubuhi, juu ya Nancy! Nimesikitika sana na nimelazima kuja kumwona!”

    “Basi karibu ndani!” Mzee Katobe alifungua mlango na Danny akiwa na boksi mikononi mwake aliingia na kuketi kwenye kochi.

    “Huyu bibie anakufahamu?”

    “Sana! Na ni rafiki yangu!”

    “Subiri basi nimwambie!”

    Mzee Katobe aliondoka sebuleni na kumwacha Danny akiwa amekaa peke yake, kichwani mwake alikuwa na mawazo mengi na alimfikiria ana Nancy! Kwake yaliyoandikwa katika gazeti kwamba Nancy alipigana baada ya kusalitiwa na mpenzi wake, yalikuwa ni habari njema! Ulikuwa ni wakati muafaka wa kumpata msichana aliyempenda kuliko mwingine yeyote lakini akamkataa. Akiwa katika fikra hizo mzee Katobe alirejea, uso wake ulionekana kutoka na furaha kama aliyokuwa nayo mwanzo.

    “Kijana!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Naam baba!”

    “Mwenzako hataki hata kukuona! Kifupi anasema hataki kukutana na mwanaume yeyote kwa hivi sasa isipokuwa mimi baba yake! Kwa hiyo naomba uondoke” Aliongea Mzee Katobe bila kumwangalia Danny usoni.

    “Sawa baba lakini naomba basi upokee huu mzigo na umpelekee, mwambia tu asome barua niliyoandika humo ndani ni matumaini yangu anaelewa leo ni siku muhimu kiasi gani katika dunia!”

    “Kwani leo ni tarehe ngapi?” Aliuliza Mzee Katobe akipokea boksi kutoka kwa Danny.

    “Tarehe kumi na nne mwezi wa pili!”

    “Kwani leo kuna sikukuu gani?”

    “Nancy ataelewa baada ya kusoma kadi iliyomo humu ndani na ninaomba umweleze nasubiri majibu yangu!”

    “Sawa!”Mzee Katobe alijibu na kuondoka.

    Danny alibaki kimya akiendelea kusubiri majibu yake kutoka ndani, dakika tano baadaye bado mzee Katobe alikuwa hajarudi! Kwa alichokiandika ndani aliamini lazima Nancy angeungana naye sebuleni na kumwambia alikuwa amekubali kuwa mpenzi wake na ni yeye Danny angekuwa chanzo cha furaha yake tangu siku hiyo.

    Ghafla mlango ulifunguliwa, mzee Katobe akatoka akifuatana na Nancy! Danny akahisi ushindi moyoni mwake, aliona ni fundi wa kuandika maneno ya kutoa nyoka pangoni! Nancy alikuwa amebaba maua mikononi, yalikuwa ni yale ambayo Danny aliyanunua kwa Mama Henjewele asubuhi kabla hajaondoka Dar es Salaam na pia kadi aliyoandika ilikuwa mikononi mwa Nancy, alimfuata mpaka alipokaa! Akaikunjua tena ile kadi na kuanza kuisoma kwa sauti.

    Nancy!

    Naamini upo katika wakati mgumu kupita kiasi, mwanaume uliyempa mategemeo yako yote amekusaliti! Usilie sana Nancy, geuka angalia nyuma bila shaka utaniona mimi, mimi Danny mwanaume ninayekupenda kwa dhati ambaye siku zote nimejitahidi kukufanya uwe wangu lakini haikuwezekana.

    Bila shaka Mungu alipanga haya yatokee ili niweze kukupata, sitaki kusema mengi, sitaki kukuahidi mengi ila ninakuahidi furaha katika maisha yako! Hakika na Mungu anajua sitakuumiza moyo Nancy kama alivyofanya Tony.

    Tafadhali kubali niwe wako, nia yangu si ngono, nia yangu ni kukufanya uwe mwanamke mwenye furaha kuliko mwanamke mwingine yeyote chini ya jua hili la Mungu! Nakubembeleza Nancy, tafadhali kubali uone kama ninayoyasema ni kweli! Hakika hutajutia uamuzi wako wa kunikubali mimi, usimwache Tony achukue furaha yako yote , kwani yeye ni nani? Maisha ni mafupi kuendelea kulia! Ni vyema kuishi kila siku kama vile hakuna kesho, utaliaje wakati yeye anaendelea kufaidi maisha na mwanamke mwingine?

    Tafadhali nikubali, niko chini ya miguu yako.

    Happy Valentine Nancy!



    Nancy alimaliza kuisoma kadi hiyo akilia machozi, mashavu yake yalilowa na blauzi aliyovaa pia ilikuwa chepechepe! Yalikuwa maneno makali na ya kuchoma, yaliyoingia moja kwa moja moyoni mwake na kuupiga ganzi, upande mmoja ulimwambia akubali lakini upande mwingine ukamwambia NO! Wanaume kwake walikuwa ni wanaume tu, rangi nyekundu ilikuwa nyekundu tu, hakuna mtu angeweza kumbadili kutoka kwenye msimamo wake.

    Aliyanyanyua maua aliyokuwa nayo mkononi pamoja na kadi na kumtupia Danny kifuani kwake na kunyanyuka mahali alipokuwa amepiga magoti akisoma kadi, alimwangalia kwa macho makali! Kumbukumbu za siku yeye na mtoto wa masikini aliyebadilika baada ya kupata umaarufu, Tony walipokuwa wakisafiri kwenda Bagamoyo kwa mganga wa kienyeji ambako alikuwa Yamini mbaya kwamba katika maisha yake asingetembea na mwanaume mwingine isipokuwa Tony! Akamwaga machozi.

    “Ninajua utaniacha! Utachukuliwa na wanaume wengine, twende Bagamoyo ukale Yamini kama kweli utanisubiri mpaka nirudi kutoka China!” Yalikuwa ni maneno ya Tony kwa Nancy, yalimiminika kichwani mwake kama filamu! Roho ikazidi kumuuama, hakuna neno kutoka mdomoni kutoka mdomoni kwa mwanaume lingeweza kumbadilisha na kumfanya apende tena.

    “Toka! Toka! Toka nyumbani kwetu, sitaki kuona mwanaume, ondoka na maua yako!” Nancy aliongea kwa sauti huku akilia.

    Danny aliruka kutoka mahali alipokuwa amekaa na kumfikia Nancy, akamkumbatia kwa nguvu na wote wawili wakaanguka hadi chini.

    “Wewee kijana hebu mwachie binti yangu! Unataka kumbaka?” Mama yake Nancy aliongea akijaribu kumvuta Danny.

    Tayari mzee Katobe alishakimbia kwenda chumbani kwake na alipotoka alikuwa na gobole lake lenye midomo miwili.

    “Mwachie!Mwachie nakuambia, nitakuua” Alifoka mzee Katobe.

    Kilichofuata hapo ni mlipuko wa bunduki, chumba kizima kikajaa mwangwi wenye uwezo wa kupasua ngoma ya sikio, mikono ya mama yake Nancy ilikuwa kichwani mwake.

    “Baba Nancy umeua!”

    Damu ilikuwa imetapakaa chumba kizima, naye Danny alikuwa sakafuni akilia kwa maumivu! Risasi ilikuwa imempenya kwenye mguu wake wa kulia chini kidogo ya goti! Mzee Katobe alikuwa akitetemeka kwa hasira, Nancy pia alikuwepo mikono yake ikiwa kichwani na machozi yakimtoka kwa wingi, pamoja na kutompenda Danny alimwonea huruma na kumlaumu baba yake kwa kitendo alichokifanya.

    “Ni hasira!”

    “Hasira yako mbaya sana! Sasa si umeishia Jela mume wangu!” Aliongea mama yake Nancy akimsogelea Danny, alipomfikia alipiga magoti pembeni yake na kuanza kumfunga na khanga sehemu iliyokuwa ikivuja damu.

    “Mama nipelekeni hospitali nikatibiwe!” Danny alilalamika.

    “Danny vipi?”

    “Baba yako amenipiga risasi, hata wewe umeshuhudia! Yote hii ni kwa sababu yako Nancy, nakupenda! Na sitakuchukia hata siku moja!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ingawa siku zote mzee Katobe alimchunga sana binti yake asiwe na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume aligundua umuhimu wa kumtumia Nancy kuyeyusha tatizo lililokuwa limejitokeza, vinginevyo angefia jela, mara moja alikimbia chumbani kwake na akiwa huko alimwita Nancy kwa sauti ya juu naye alimfuata wakimwacha mama peke yake akiendelea kumfunga Danny na khanga ili kuzuia damu zaidi isivuje.

    “Sikiliza mwanangu!” Mzee Katobe alimwambia Nancy.

    “Ndiyo baba!”

    “Hali ni mbaya na ni wewe peke yake unayeweza kusaidia!”

    “Ndiyo! Kusaidiaje?”

    “Huyu kijana anakupenda, pamoja na hasira zangu kumpiga risasi ukimwomba asitoboe siri ya kilichotokea ninafikiri anaweza kukusikiliza!”

    “Mh! Hilo litawezekana kweli?”

    “Linawezekana kabisa! Naomba ukalifanye sasa hivi!”

    Nancy alitoka chumbani bila kuongea chochote na kwenda moja kwa moja hadi mahali alipokuwa mama yake, hali ya Danny ilikuwa mbaya alionyesha kupoteza fahamu! Alimtingisha mara kadhaa akijaribu kumwita lakini hakuitika, muda mfupi baadaye baba yake alifuatia na kukuta akihangaika kumtingisha.

    “Jamani twendeni tumpeleke hospitali!”

    “Mimi naogopa!” Mzee Katobe aliongea, mwili wote ulikuwa ukitetemeka na alionyesha wazi ni kiasi gani alijilaumu kwa kitendo alichokifanya.

    “Basi acha sisi tumpeleke, wewe baki hapa nyumbani maana naona anazidi kuzidiwa!”

    Mzee Katobe alitingisha kichwa kuonyesha hali ya kukubali, hata hivyo aliwasaidia kumbeba hadi kwenye gari lao, wakampakia na kuondoka naye kuelekea hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, njiani kabla hawajafika hospitali Danny alifumbua macho na kumkuta Nancy amekaa pembeni mwake mama yake akiendesha gari kwa kasi.

    “Pole Danny! Naomba umsamehe baba yangu!”

    “Kwa sababu yako naweza kufanya lolote, nakupenda Nancy! Wala sitanii!” Aliongea Danny ingawa kwa taabu.

    Gari liliegeshwa mbele ya jengo la mapokezi dakika kumi baadaye na wauguzi wakasogea wakiwa na kiti cha matairi, Danny aliteremshwa haraka na kukimbiwa chumba cha daktari, wakati anaingia aliweka kidole chake mdomoni kama ishara ya kuwazuia Nancy na mama yake wasiongee lolote, kwa wakati huo hawakuelewa ni kwanini aliwapa ishara hiyo lakini alipoanza kuongea na daktari walielewa maana yake.

    “Nilikuwa natembea huko ufukweni Badeco, wakaja wanaume wawili wakiwa na bastola wakaanza kuninyang’anya kamera yangu pamoja na pesa nilizokuwa nazo! Nilipojaribu kupambana nao ilishindikana wakanipiga risasi mguuni!” Danny aliongea kwa sauti ya chini huku akilia, Nancy na mama yake walibaki mdomo wazi hawakutegemea hayo ndiyo yangekuwa maelezo yake.

    “Aisee pole sana! Unahitaji matibabu ya haraka, kwa kawaida kesi kama hii inabidi upate kwanza fomu ya polisi lakini siwezi kusubiri fomu hiyo ndiyo nianze kukutibu, matibabu yatafanyika na fomu itafuata baadaye!”Aliongea daktari huku akichukua kadi na kuanza kuandika maelezo juu yake.

    “Nina uhakika mfupa umevunjika, kuna milio fulani naisikia ambayo kwa kweli si ya kawaida! Hivyo naomba mmpelekeni chumba cha X-ray akapigwe picha mara moja na majibu niyapate upesi!” Daktari aliwaeleze wauguzi waliokuwepo chumbani na Danny akasukumwa akiwa juu ya kiti cha matairi hadi chumba cha X-ray ambako mguu wa Danny ulipigwa picha, kutoka hapo alipelekwa moja kwa moja wodini na kusubiri majibu yaliyotoka nusu saa baadaye na kuonyesha kweli mfupa wa Danny ulikuwa umevunjika.

    Madaktari walikusanyika na kuijadili hali hiyo, ushauri uliotolewa na daktari bingwa wa mifupa ni Danny kufungwa vyuma kwenye mguu wake uliovunjika ili uungwe kwa urahisi maana kulikuwa vipande kadhaa vilivyosambazwa na risasi iliyopita na kuchimba sakafuni.

    Alichukuliwa kutoka wodini kupelekwa chumba cha upasuaji, Nancy na mama yake wakifuata nyuma! Kabla ya kuingia chumba cha upasuaji, Nancy alipinda shingo yake na kumpiga Danny busu usoni akimshukuru kwa kitendo chake cha kumtetea baba yake alichokifanya.

    “Sijui jinsi ya kukushukuru!”

    “Kitu kimoja tu unaweza kufanya kama shukurani! Ni kukubali kuwa mpenzi wangu, nakupenda Nancy, sijali kuwa baba yako kanipiga risasi ili mradi imetokea wakati nakutafuta wewe! Lakini tofauti na hapo...”

    “Tutaliongelea hilo baadaye nenda kwanza katibiwe!”

    Danny aliingizwa chumba cha upasuaji ambako alikaa kwa karibu masaa mawili, alipotoka alikuwa katika dawa ya usingizi wala hakuweza kuongea lolote, ilikuwa tayari saa kumi na mbili za jioni ni wakati huo ndipo Nancy na mama yake waliamua kurejea nyumbani kwa muda.

    ****

    Walimkuta mzee Katobe akiwa sebuleni amejishika tama kwa mawazo mengi, kichwa chake kilikuwa kimechanganyiki

    wa, aliiona milango ya jela zote Tanzania ikiwa wazi na ikimwita ili aingie! Walipomweleza kilichotokea hospitali, kwamba Danny alisema uongo ili kumtetea hakutaka kuamini! Aliruka juu na kushangilia kwa furaha.

    “Huyu kijana ni wa aina yake, siwezi kumlinganisha na yule Mbweha aliyeko China! Yaani hakusema kuwa nimempiga risasi?”

    “Hajasema!”

    “Nafikiri hakutakuwa na matatizo labda hili gari lake ndio linaweza kuleta usumbufu!”

    “Usumbufu gani?”

    “Si ajabu polisi wanaweza kuuliza limefikaje hapa!”

    “Si tutasema tuliliendesha kutoka ufukweni, hapo kuna tatizo gani?” mama yake Nancy alisema.

    “Bila shaka hakuna shida!”

    Saa moja na nusu ya jioni wote watatu walirejea hospitali na kumkuta Danny akiwa amejilaza kitandani, bado fahamu zake zilikuwa hazijarejea vizuri! Alikuwa akiongea maneno mengi bila kujitambua, dawa za usingizi alizopewa chumba cha upasuaji zilikuwa bado hazijamtoka vizuri! Muda mfupi tu baada ya Nancy na wazazi wake kuwasili, watu watatu waliojitambulisha kama maaskari kanzu walifika kitandani na kumkuta Danny akiendelea kuongea mambo yasiyoeleweka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Yaani Nancy, baba yako amenipiga risasi? Sio mbaya ili mradi nimekupenda na sitamwambia mtu yeyote kwamba mzee Katobe ndiye aliyenifanyia kitendo hiki, nitawadanganya polisi kwamba nilipigwa risasi na majamba…!” Yalikuwa maneno hatari kutoka mdomoni kwa Danny, aliyekuwa bado hajarejewa vizuri na fahamu zake.

    Nancy aliyekuwa jirani kabisa na kitanda alijaribu kuufunika mdomo wa Danny ili asiendelee kusema maneno ambayo yangemtia baba yake katika matatizo, lakini maaskari waliwahi kumwona na kumwamuru aache kufanya kitendo alichokuwa akifanya na mmoja wa maaskari alisogea karibu na kutoa kirekoda kidogo mfukoni kwake akaanza kuyarekodi maongezi yote aliyoyaongea Danny.

    Mzee Katobe alisimama hapo akitetemeka mwili mzima bila kuelewa kitu gani kingetokea, alijuta ni kwanini alikubali kuongozana na mke wake pamoja na mtoto wake kuja wodini! Alifikiria kurudi kinyumenyume na baadaye kutoroka lakini kabla hajafanya hivyo maaskari walianza kuuliza maswali.

    “Bila shaka nyinyi ni ndugu wa huyu mgonjwa au siyo?”

    “Ndiyo!”

    “Mna uhusiano gani na mgonjwa?!”

    “Hatuna undugu ili sisi ndio tumemwokota akiwa amepigwa risasi!” Mama yake Nancy aliongea mzee Katobe akiwa kimya.

    “Mh!”Mmoja wa maaskari aliguna akimwangalia mzee Katobe usoni, alikuwa mzee maarufu sana wilayani Bagamoyo hata maaskari hao walimtambua, ukorofi wake ulijulikana kwa kila mtu.

    “Haiwezekani! Nafikiri mmeyasikia maneno aliyokuwa anayasema huyu mgonjwa!”

    “Huyu amechanganyikiwa anaweza kusema lolote! Ina maana mimi naweza kufanya kitendo anachokisema?”Mzee Katobe aliongea kwa sauti ya ukali kama njia ya kujihami

    “Hapana! Usitutishe mzee, hapa kuna kitu cha kufuatilia!Afande John hebu mfunge pingu huyu mzee twende naye kituoni!” Aliongea askari mwingine na amri yake ilichukua mkondo, mzee Katobe akafungwa pingu na kuanza kusukumwa kwenda nje mke wake akifuata nyuma, Nancy peke yake ndiye alibaki pembeni mwa kitanda cha Danny. Saa nzima baadaye Danny alirejewa na fahamu zake zote na kumwona Nancy pembeni mwa kitanda akilia.

    “Vipi? Mbona unalia?”

    “Baba yangu! Wamemchukua!”

    “Kumpeleka wapi?”

    “Polisi!”

    “Kufanya nini wakati mimi nilishasema nimepigwa risasi na majambazi?”

    “Kuna kitu kimetokea ukiwa usingizini!”

    “Kitu gani?”

    “Ulisema maneno yote ya ukweli!” Alisema Nancy na baadaye kumweleza Danny kila kitu alichokisema.

    Danny alishika mkono wake mdomoni kama ishara ya kuonyesha mshangao, kweli kumbukumbu zilimwijia kwa mbali sana kuwa alitamka maneno hayo lakini akimwambia Nancy na si polisi.

    “Nakumbuka kusema lakini nikikueleza wewe!”

    “Polisi walikuwepo!”

    “Nitawaruka!”

    “Wamerekodi!”

    “Kweli?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo!”



    Mzee Katobe alipofikishwa kituoni alitoa maelezo yake huku akitetemeka na kubabaika na kuwafanya askari wawe na wasiwasi zaidi juu ya tukio hilo, ilibidi atupwe mahabusu na polisi wakamchukua mke wake kwenda nyumbani kufanya upekuzi! Njia nzima mama huyo alikuwa akilia lakini upande mwingine wa moyo wake aliamini nyumbani wasingepata kitu chochote cha kuwasaidia polisi, kama ni bunduki mzee Katobe alikuwa akiimiliki kihalali. Wasiwasi wake ulikuwa ni damu iliyokuwa imetapakaa sakafuni.

    “Kama wataikuta ile damu kwa kweli lazima baba Nancy atakuwa kwenye matatizo, sikumbuki tuliporudi nyumbani kama niliangalia vizuri sebuleni!” Aliwaza mama Nancy akijaribu kukumbuka.

    Walipofika mama yake Nancy alifungua mlango macho yake yakiwa sakafuni, hakuna hata tone la damu! Mzee Katobe alisafisha wakiwa hospitali, furaha ikamjaa moyoni mwake na maaskari zaidi ya watano wakamiminika ndani ya nyumba na kuanza shughuli ya kupekua wakimulika tochi kila mahali, bunduki ilipatikana chumbani walipoomba kitabu cha kumiliki, mama alikifuata mahali kilipokuwa na kuwakabidhi.

    “Ilitumika mara ya mwisho lini?”

    “Mimi sifahamu! Sijaona ikitumika!”

    “Una uhakika?”

    “Ndiyo!”

    Upekuzi uliendelea sebuleni, makochi yalinyanyuliwa na uhamishwa sehemu yalipokuwa! Kwa dakika kumi na nzima maaskari walikuwa sebuleni, wakikaribia kuondoka baada ya kutokupata kitu chochote cha kuwasaidia! Askari mmoja alipiga kelele wote wakageuka na kumwangalia.

    “Vipi?”

    “ Ganda la risasi!” Alisema askari huyo na wote wakamkimbilia!

    “Wee mama unatudanganya?”

    “Ah! Unajua….. Unajua!….!” Mama Nancy alikosa cha kuwaeleza!

    “Sema ukweli?”

    “Kwa kweli sifahamu haya mambo labda muulize mwenyewe!” Aliongea Mama Nancy na baadaye akaanza kulia machozi.

    Ganda la risasi lililopatikana lilitosha kabisa kuunganisha na maelezo ya Danny ili kumtia mzee Katobe hatiani, walirudi kituoni na kutoa taarifa kwa mkuu wa kituo! Hawakuwa na shida tena na mama Nancy hivyo walimwachia aondoke zake, hakukuwa na dhamana yoyote kwa mzee Katobe.

    ****

    Ilikuwa tayari saa sita ya usiku wakati mama Nancy anaondoka kituoni, hakutaka kwenda nyumbani tena wakati huo bali wodini ambako aliamini mtoto wake Nancy alikuwepo na pia alitaka kufahamu hali ya Danny kwa wakati huo, ni yeye peke yake aliyekuwa tegemeo katika tatizo lililokuwa linamkabili mzee Katobe! Kama angesema kweli alipigwa risasi na mzee Katobe basi mume wake angefia jela na huo ndio ungekuwa mwisho wa kila kitu lakini kama angekanusha, ni wazi hata kama polisi wangefanya kitu gani wasingekuwa na uwezo wa kumtia mume wake hatiani lazima mzee Katobe angeachiwa huru.

    Wodini kama alivyokuwa amefikiria alimkuta Nancy akiwa amekaa pembeni mwa kitanda cha Danny, alikuwa akilia machozi.

    “Vipi mwanangu?”

    “Hamna tatizo mama!”

    “Mbona sasa unalia?”

    “Danny amebadilika!”

    “Amebadilika!”

    “Ndiyo!”

    “Kwanini?”

    “Anasema kama siwezi kukubali kufanya naye ngono na mwisho kuwa mke wake, atasema ukweli kuwa baba ndiye alimpiga risasi!” Aliongea Nancy kwa uchungu akijifuta machozi.

    Neno ngono lilikuwa marufuku katika maisha yake, kiapo alichokula kwa mganga bado alikikumbuka! Hakuwa na ruhusa ya kufanya tendo la ndoa na mwanaume mwingine yeyote isipokuwa Tony! Kama angediriki kufanya hivyo lazima angepata madhara na madhara yenyewe aliyakumbuka, ni kufa au kuwa mwendawazimu.

    Ni kweli alimpenda baba yake lakini asingediriki kumvulia Danny nguo yake ya ndani na kufanya naye mapenzi, alikuwa katika wakati mgumu kupita kiasi kufanya maamuzi! Aidha afanye ngono awe mwendawazimu au agome kufanya ngono Danny aseme ukweli juu ya kilichotokea na baba yake, ngome yake na kila kitu kwake apatikane na hatia na kufia jela! Nancy alimwaga machozi mbele ya mama yake.

    “Unasema kweli?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kweli kabisa mama! Ndivyo alivyoniambia!”

    Mama yake Nancy alimgeukia Danny na kumwangalia kwa macho ya huruma kisha kuanza kumuuliza kama yaliyosemwa na Nancy yalikuwa na ukweli wowote, Danny alikiri na kumwambia mama yake Nancy juu ya mapenzi aliyokuwa nayo kwa mtoto wake na hiyo ndiyo ilikuwa nafasi pekee ya kumpata.

    “Baba! Baba! Baba! Nakubembeleza tafadhali, usifanye hivyo!”

    “Kwanini mama? Kwani kuna tatizo gani mimi kuwa na mwanao? Hivi nyinyi hamuoni kama mmeniumiza? Kwa kweli kama Nancy hatakubali kufanya hivyo nitasema ukweli, sidanganyi!” Alimaliza Danny na kugeukia ukutani.

    Nancy aliinamisha kichwa chake chini, alijuta ni kwanini alikula yamini kwa mganga! Alitamani kubadilisha mambo, awe huru na kukubali kufanya ngono na Danny ili kumwokoa baba yake, maisha ya baba yake yalikuwa mikononi mwake!

    “Kesho nitakwenda Mlingotini nikamtafute huyo mganga, nimweleze yote yaliyotokea na kama kuna namna yoyote ya kuniondolea Yamini hii ili niokoe maisha ya baba yangu basi ifanyike kwa gharama yoyote ile!”

    Saa tisa na nusu ya usiku aliondoka hospitalini na kwenda hadi nyumbani, Nancy hakulala! Saa kumi na mbili ya asubuhi bila kumuaga mama yake aliondoka nyumbani akitembea kwa miguu kwenda Mlingotini, bado alikumbuka mahali nyumba ilipokuwa! Jua lilipochomoza tayari alikuwa kijijini Mlingotini, alishangazwa na hali aliyoikuta nyumbani kwa mganga. Nyumba ilikuwa imeanguka na hapakuwa na dalili ya mtu yeyote kuendesha maisha katika eneo hilo.

    Hakuelewa nini cha kufanya, alianguka chini na kulia kwa uchungu! Dunia ilikuwa imembadilikia, kila kitu katika maisha yake kilikuwa kimejisokota kuanzia kwa Tony hadi kwa Danny na baba yake mzazi!

    Akiwa amelala chini aliweza kuona makaburi mawili pembeni yake, akawa na uhakika kuwa pengine mganga wa kienyeji alifariki dunia!

    “Nitafanya nini mimi?”

    Nancy aliendelea kulia akiwa amelala ardhini, mawazo yalimjaa kichwani na alishindwa kuelewa angefanya kitu gani kama mganga aliyemlisha yamini asingepatikana! Alitamani kufa na kuiacha dunia lakini alipofikiria sana aliona hilo halikuwa jibu sahihi la kutatua matatizo yake ukizingatia tayari baba yake mzazi alikuwa mahabusu na alitakiwa kufanya lolote ili atoke.

    “Inavyoonekana Danny hatanii na sijui ni kwanini baba naye alimpiga risasi? Amedhamiria nifanye naye ngono, lakini mimi siwezi mpaka niondolewe yamini!” Aliendelea kuwaza huku akilia.

    Mara ghafla alisikia sauti za wanawake wakiongea nyuma yake, akanyanyuka na kukaa kitako, wanawake watatu walisimama njiani wakiwa na ndoo mikononi mwao jambo lililoashiria walikuwa wakienda kisimani kuteka maji. Walisimama hapo kwa muda bila kusema chochote na Nancy wakiendelea kunong’ona wao kwa wao kwa sauti za chini.

    Baadaye aliwashuhudia wakikatisha njia na kutembea kwenda mahali alipokuwa amekaa.

    “Vipi binti?” Walimuuliza baada ya salamu.

    “Nina shida na mzee aliyekuwa akiishi katika nyumba hii!”

    “Yule mganga?”

    “Ndiyo! Jina lake nimelisahau kidogo!”

    “Mzee Mwinyimkuu!”

    “Ndiyo!”

    “Mbona hayupo muda mrefu!” Aliongea mwanamke mmoja, taarifa hiyo ilimpa matumaini Nancy aliyehisi mganga alishafariki dunia.

    “Kwa hiyo kumbe hajafariki?”

    “Haya makaburi unayoyaona ni ya mke na mtoto wake, walifariki ghafla yeye akadai wachawi wa Bagamoyo wanamchezea akaamua kuhama!”

    “Alihamia wapi?”

    “Tabora!”

    “Mjini?”

    “Hapana! Kijiji kimoja kinaitwa Kisanga!”

    “Una uhakika?”Aliuliza Nancy

    “Uhakika ninao si alikuwa jirani yetu na alituaga wakati wa kuondoka! Kwani una shida gani naye?”

    “Matatizo ndugu yangu!”

    “Matatizo gani?”

    Badala ya kujibu Nancy aliangua kilio tena jambo lililowafanya akinamama hao watamani kudadisi zaidi na zaidi ili kuelewa kilichokuwa kinamsumbua, mara ya kwanza alisita kueleza lakini baadaye alijikuta akilazimika kufungua mdomo wake na kusema ukweli! Wote walishika mikono vichwani mwao na kumsikitikia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Pole sana shoga! Kwanini ulikubali kufanya hivyo?”

    “Mapenzi! Nilimpenda sana mpenzi wangu”

    “Yuko wapi kwa sasa?”



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog