Simulizi : Queen Of Gorillas ( Malkia Wa Masokwe )
Sehemu Ya Tano (5)
Harrison na mkewe, Angel au Malkia wa Masokwe wanazidi kuoneshana mapenzi makubwa, kila mmoja akiwa na furaha kubwa ndani ya mtima wake. Harrison anaonesha kuwa na furaha zaidi kwani ndoto zake za siku nyingi za kuishi na Malkia wa Masokwe zilikuwa zimetimia.
Baada ya kuhangaika sana akitafuta nafasi ya kumtorosha msichana huyo kutoka ndani ya Msitu wa Tongass alikokuwa analindwa na masokwe, hatimaye anafanikiwa na kukimbia naye hadi nchini Canada.
Wakiwa nchini Canada wanaenda kuishi katika Mji wa Abbotsford. Harrison anafanya kazi kubwa ya
kumbadilisha msichana huyo, anafanikiwa kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu.
Baadaye wanafunga ndoa halali kanisani na kuwa mume na mke. Harrison anamuandikisha mkewe kusomea
kompyuta na yeye anatafuta kazi. Wanaendelea na maisha yao na baada ya muda, Angel anaanza kuhisi dalili zinazowafanya wakubaliane kwenda hospitali. Wanapoenda kupima, wanagundua kuwa Angel amenasa ujauzito.
Upande wa pili, Linda amechachamaa kutaka kuufahamu ukweli juu ya kifo cha Harrison. Baada ya kuhitimu masomo ya Crime Scene Investigation na kutunukiwa shahada yake, anaanza kufanya kazi kwenye kampuni yake
binafsi ya upelelezi akiwa na shauku kubwa ya kuufahamu ukweli uliojificha nyuma ya kifo cha Harrison.
Upelelezi wake unafanikiwa kubaini kuwa aliyekufa hakuwa Harrison na hata mwili uliozikwa haukuwa wa kwake.
Hali hiyo inamchanganya sana na anaapa kutumia mbinu kali alizojifunza chuoni kuendesha upelelezi huo huku akiweka nadhiri kuwa ni lazima ampate Harrison. Anafuatilia nyendo zote za Harrison kwa karibu.
LINDA hakupata usingizi usiku kucha kwani alikuwa akiwaza njia itakayomuwezesha kumpata Harrison kwa gharama yoyote. Bado penzi lake kwa kijana huyo mtanashati halikuwa limekwisha, kila mara alikuwa akimkumbuka na kujipa moyo kuwa lazima ipo siku atafanikiwa kumpata na kukamilisha tendo la kufunga naye ndoa.
Mawazo kwamba huenda Harrison alimkimbia kwa sababu alimpenda zaidi Malkia wa Masokwe, hakutaka kuyapa nafasi katika kichwa chake ingawa mara kwa mara yalikuwa yakimuandama. Alijipa moyo kuwa yeye ni mrembo na ana sifa zote za kumfanya Harrison amuoe kwa ndoa halali.
Mpaka kunaanza kupambazuka, Linda hakuwa amepata hata lepe la usingizi. Jua lilipoanza kuchomoza, alijilazimisha kuamka na kukaa juu ya kitanda, akachukua kitabu chake alichokuwa anakitumia kuandika mambo mbalimbali na kuanza kupitia ukurasa mmoja baada ya mwingine.
Alikuwa akijaribu kutafakari wapi pa kuanzia ili aikamilishe kazi yake. Licha ya kufikiria kwa muda, bado hakupata jibu la haraka, akakifungua kitabu cha Queen of Gorillas na kuanza kupitia kurasa mbalimbali ambazo aliamini zinaweza kuwa na taarifa muhimu zitakazomfanya ampate Harrison.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Katika ukurasa mmoja, alisoma jinsi Harrison alivyofanikiwa kuingia kwa mara ya kwanza kwenye msitu huo. Akagundua kuwa kumbe kuna ofisi za misitu ambazo ndizo zinazotumika kuulinda msitu huo na kutoa vibali kwa ajili ya watu mbalimbali wanaotaka kuingia ndani.
Wazo pekee aliloliona linafaa likawa ni kwenda moja kwa moja mpaka kwenye ofisi hizo akiamini anaweza kupata taarifa zitakazomsaidia kujua mahali alikoelekea Harrison. Kwa kufuata maelekezo yaliyokuwa yameandikwa na Harrison, aliianza safari ya kuelekea mahali zilipo ofisi hizo, akalazimika kutembea umbali mrefu kwa miguu kwani hakukuwa na usafiri wa aina yoyote eneo hilo.
Baada ya kutembea umbali mrefu, hatimaye alifika kwenye geti kubwa la mbao ambalo ndiyo lililokuwa linatumika kama lango kuu la msitu huo. Alipofika alijitambulisha kwa walinzi aliowakuta getini, akaelekezwa mahali ofisi zilipokuwa. Kwa kuwa hapakuwa mbali, alitembea hatua kadhaa akawasili kwenye ofisi iliyokuwa imejengwa kwa mbao na kuezekwa kwa vigae.
Akapokelewa na mzee wa makamo aliyejitambulisha kuwa ndiye Mkuu wa Hifadhi ya Msitu wa Tongass, Ludovick Pharell. Linda lijitambulisha na kuonesha kitambulisho chake cha kazi. Akaeleza kilichomfanya asafiri kutoka Miami mpaka kwenye msitu huo.
Umesema anaitwa nani?
Harrison Harvey, alijibu Linda na mzee Ludovick akaanza kupitia daftari la wageni waliotembelea msitu huo kwa kipindi cha mwaka mzima. Jambo lililomshangaza Linda ni kwamba hakukupatikana taarifa zozote za Harrison kuutembelea msitu huo kwa mwaka huo.
Kutokana na kuendelea kusisitiza sana, Mzee Ludovick aliamua kutoa vitabu vyote vya wageni kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita. Wakaanza kukagua kitabu kimoja baada ya kingine.
Kwa bahati nzuri, walifanikiwa kulipata jina hilo likionesha kuwa Harrison alitembelea msitu huo karibu miaka minne iliyopita. Linda alipoangalia tarehe, aliishiwa nguvu kwani zilionesha kuwa ni kipindi ambacho alikuwa bado hajapata matatizo. Mara ya mwisho, ilionesha kuwa Harrison alitembelea Msitu wa Tongass miezi mitano kabla ya kupata ajali feki.
Kwani hapa hakuna uwezekano wa mtu kuingia kinyemela bila kupitia hapa ofisini kupata kibali?
Uwezekano ni mkubwa na karibu kila mwaka kuna idadi ya watu ambao huingia kinyemela msituni na kufanya mambo yao kisha kutokomea bila sisi kujua. Kama unavyojua huu msitu ni mkubwa sana na umeenda mpaka kwenye mpaka wa Marekani na Canada hivyo inakuwa vigumu kwetu kufuatilia kila kitu, alisema Mzee Ludovick.
Ina maana huu msitu umeingia hadi Canada?
Ndiyo! Na baadhi ya wahamiaji haramu hupitia ndani ya msitu huu kuingia na kutoka nchini Marekani au Canada bila kushtukiwa na maafisa wa uhamiaji.
Baada ya kujibiwa hivyo, kengele ya hatari ililia ndani ya kichwa cha Linda hasa baada ya kugundua kuwa msitu huo ulikuwa ukiziunganisha nchi hizo mbili. Alibaki amepigwa na bumbuwazi kwa dakika kadhaa, akawa amezama kwenye lindi la mawazo akitafakari mambo mengi kwa wakati mmoja.
Baada ya kuwaza sana, Linda alipata wazo la kurudi hadi nyumbani kwao kwanza na kujipanga upya kwani kwa jinsi ilivyoonesha, Harrison alikuwa ametumia akili za hali ya juu kuusuka mpango huo. Kwa shingo upande aliagana na mzee Ludovick na kutoka kwenye ofisi hizo.
Akaawaaga na wale walinzi waliomuonesha ofisi kisha safari ya kurudi Miami ikaanza, alirudi mpaka kwenye mji mdogo wa Tongass ambapo alikata tiketi ya treni na kukaa stesheni kulisubiri.
***
Ujauzito wa Malkia wa Masokwe ulizidi kukua, muda wa kuanza kuhudhuria kliniki ulipowadia, Harrison hakutaka kumwacha aende peke yake. Ikawa kila siku ya kwenda kliniki anaomba ruhusa kazini na kumsindikiza mkewe.
Upendo aliokuwa anaounesha kwa mkewe, ulimfurahisha kila mmoja, wanawake wengi wakawa wanatamani waume zao
wangekuwa na akili kama za Harrison. Njiani alikuwa akimsaidia kubeba mizigo yote ikiwemo mkoba wake. Alikuwa akimdekeza kama mtoto mdogo.
Mwanao ameanza kucheza, hebu msikilize, alisema Angel jioni moja akiwa amekaa na mumewe kwenye bustani nzuri ya maua wakipunga upepo. Harrison alimuinamia mkewe na kusogeza sikio lake kwenye tumbo lake ambalo sasa lilishaanza kuwa kubwa.
Eeeh! Kweli, inaonesha atakuwa mtundu sana huyu, alisema Harrison huku akimbusu mkewe kwa furaha. Mapenzi yalikuwa yakizidi kuongezeka kila uchao, furaha, amani na upendo vikazidi kushamiri.
Ujauzito ulipofikisha miezi minne, Harrison alimuombea ruhusa mkewe ili asimame kufanya kazi mpaka atakapojifungua. Hakutaka mkewe apate shida hata kidogo, ombi hilo lilipokubaliwa, Angel akawa anashinda nyumbani kuendelea kulihudumia tumbo lake.
***
UPENDO, amani, furaha na maelewano vinazidi kushamiri kwenye ndoa ya Harrison na mkewe, Angel au Malkia wa Masokwe. Kila mmoja anafurahia maisha ya ndoa na mapenzi anayoyapata kutoka kwa mwenzake. Harrison
anaonesha kuwa na furaha zaidi kwani ndoto zake za siku nyingi za kuishi na Malkia wa Masokwe zilikuwa zimetimia.
Jinsi alivyohangaika wakati akitafuta nafasi ya kumtorosha msichana huyo kutoka ndani ya Msitu wa Tongass
alikokuwa analindwa na masokwe, inabaki kuwa historia. Mara kwa mara wanakumbushana jinsi Harrison alivyohangaika kumtorosha hadi alipofanikiwa kuondoka naye kuelekea nchini Canada.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kufunga ndoa, Angel ananasa ujauzito na sasa wanasaidiana kuulea, huku Harrison akimtunza mkewe huyo kama mboni ya jicho lake. Mara kwa mara anampeleka kliniki na baadaye anamsimamisha kazi aliyokuwa anafanya. Siku zinazidi kuyoyoma na ujauzito wa Angel unazidi kukua vizuri.
Upande wa pili, Linda anaendelea na upelelezi wa hali ya juu kutaka kuufahamu ukweli juu ya kifo cha Harrison. Baada ya kuhitimu masomo ya Crime Scene Investigation na kutunukiwa shahada yake, anaanza kufanya kazi kwenye
kampuni yake binafsi ya upelelezi akiwa na shauku kubwa ya kuufahamu ukweli uliojificha nyuma ya kifo cha Harrison.
Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda, ndivyo anavyogundua mambo mengi yaliyokuwa yamejificha kuhusu kifo hicho. Anagundua kuwa Harrison hakufa kwenye ajali kama ambavyo kila mtu alikuwa anaamini. Anaendelea na upelelezi wa kina na sasa anakaribia kuujua ukweli wa mahali Harrison alikojificha.
Baada ya kurudi mpaka Miami, Linda aliendelea kutafakari namna ya kumpata Harrison lakini hakupata jibu la haraka. Alijaribu kwenda kwenye idara ya mawasiliano na kuangalia kama namba ya simu ya mkononi ya Harrison ilikuwa ikiendelea kutumika sehemu nyingine lakini hakufanikiwa kupata taarifa zozote muhimu.
Aligundua kuwa siku ya mwisho kwa namba hiyo ya simu kutumika, ilikuwa ni ile ambayo Harrison alipata ajali feki. Linda hakukata tamaa, akaendelea kuumiza kichwa kutafuta njia ambayo itamfanya agundue ukweli wa mahali Harrison alipo.
Kutokana na uchovu wa safari, siku hiyo hakutaka kuendelea na kazi, akarudi nyumbani kupumzika huku akiendelea kutafakari kichwani mwake. Baada ya muda, alipata wazo aliloona linaweza kumsaidia kuujua ukweli.
Aliamini kama kweli Harrison amevuka mpaka na kuingia nchini Canada, lazima taarifa zake za hati ya kusafiria, tarehe ya siku aliyovuka mpaka na sehemu alikoelekea zitakuwepo kwenye idara ya uhamiaji ya nchi hiyo.
Kesho yake akajiandaa na baada ya muda, safari ya kuelekea makao makuu ya idara ya uhamiaji jijini New York ikaanza. Alilazimika kusafiri kwa ndege kutoka jijini Miami mpaka New York. Bila kupoteza muda akaenda moja kwa moja mpaka kwenye ofisi za Idara ya Uhamiaji.
Alipofika alijitambulisha na kueleza shida yake, kwa kuwa alisisitiza kuwa anafanya hivyo kwa sababu za usalama wa nchi, alipewa ushirikiano mkubwa kuliko alivyotegemea. Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Russell Isaacs alimuongoza mpaka kwenye chumba maalum kilichokuwa na kompyuta nyingi zilizounganishwa na mtandao wa internet.
Wakaanza kuangalia taarifa za watu mbalimbali waliokuwa wanatoka na kuingia ndani ya mipaka ya Marekani lakini jina la Harrison halikuonekana. Walifuatilia kumbukumbu za kipindi chote tangu Harrison atoweke lakini hakukuwa na taarifa zozote zilizoonesha kuwa ameingia au kutoka nje ya Marekani.
Au alibadilisha jina?
Hata kama amebadilisha jina lazima angeonekana katika taarifa za watu waliobadilisha majina na kula viapo kwani haiwezekani mtu akabadilisha jina kienyeji halafu akapata hati ya kusafiria, alisema Russell, hali iliyozidi kumchanganya Linda.
Baada ya kushindwa kupata taarifa zozote muhimu za kumsaidia, aliaga na kuondoka, akaenda mpaka Uwanja wa Ndege ambapo alikata tiketi na muda mfupi baadaye, safari ya kurudi Miami ikaanza.
Licha ya vikwazo alivyokuwa anakutana navyo, bado Linda hakukata tamaa, alijiapiza kuwa atatumia mbinu zote anazozijua mpaka afahamu ukweli wa mahali Harrison alipo.
Siku zilizidi kusonga mbele, Linda akawa anaendelea kuumiza kichwa namna atakavyofanikiwa kuufahamu ukweli wa mahali Harrison alipo. Jioni moja wakati akirejea kutoka kazini kwake, alipitia super market kwa ajili ya kujipatia mahitaji muhimu.
Wakati akiendelea kununua bidhaa mbalimbali, alifika kwenye upande ambao vitabu, majarida na magazeti vinapatikana. Katika hali ambayo ilimshangaza, alishtuka kukiona kitabu cha Queen of Gorillas kikiwa miongoni mwa vitabu vinavyouzwa.
Kilichomshtua ni kwamba tangu Harrison atoweke, hakukuwa na mtu aliyekuwa akisimamia kazi zake na kwa kipindi hicho, nakala karibu zote za vitabu zilikuwa zimeshauzwa na kuisha kwenye mzunguko.
Alisogea mpaka kwenye kabati la vioo lililokuwa na vitabu, akafungua na kukitoa, akakitazama kwa muda na kugundua kuwa hakikuwa na tofauti na kile alichokuwa nacho nyumbani kwao. Akajiuliza maswali mengi ambayo yote yalikosa majibu. Akakirudisha mahali pake na kumalizia kufanya manunuzi kisha akaondoka na kurudi kwao.
Alipofika, alikichukua kitabu chake na kuangalia namba za mawasiliano za kampuni iliyohusika na kazi ya kukichapisha kitabu hicho kwa mara ya kwanza. Aliziandika pembeni kisha akainuka na kuelekea sebuleni. Bila kupoteza muda, alipiga simu kwenye makao makuu ya kampuni ya Planet Link Publishers, wachapishaji na wasambazaji wa kitabu hicho.
Baada ya simu kupokelewa, Linda alijitambulisha na kuanza kuhoji maswali kuhusu kukiona kitabu hicho kikiendelea kuuzwa wakati mhusika alishafariki. Pia alitaka kujua fedha za mauzo zinakopelekwa.
Majibu aliyoyapata yaliamsha kitu kipya ndani ya akili yake. Alishangaa sana kusikia kuwa mauzo ya kitabu hicho yanaingizwa kwenye akaunti ya Harrison na kwamba wazo la kukichapisha upya kitabu hicho lilitoka kwa ndugu wa marehemu aishiye Canada ambaye aliwasiliana nao kwa barua pepe (e-mail) na kuwapa maelezo hayo.
Linda aliomba kupewa namba ya akaunti ambayo fedha hizo zilikuwa zikiingizwa kisha akamuomba mtu aliyezungumza naye kutomwambia yeyote mambo yote waliyozungumza kisha akakata simu.
Alishusha pumzi ndefu na kutulia kwa muda, mawazo mengi yakipita ndani ya kichwa chake. Akainuka na kuelekea chumbani kwake ambapo alijifungia mlango na kujitupa kitandani. Wazo pekee alilolipata ni kwenda kwenye makao makuu ya Benki ya Barclays jijini Miami kwa ajili ya kufuatilia taarifa za akaunti ya Harrison.
***
Ujauzito wa Angel ulizidi kukua vizuri bila matatizo yoyote, jambo lililoongeza furaha katika ndoa yao. Kazi aliyokuwa anafanya pamoja na fedha za mauzo ya vitabu vyake kwa pamoja vilimfanya awe na uwezo mzuri kiuchumi hivyo suala la kumtunza na kumhudumia mkewe halikumpa shida.
Miezi ilizidi kukatika, mwezi wa tano ukapita, ukaja wa sita, wa saba, wa nane hatimaye miezi tisa ikatimia. Maandalizi ya kukipokea kiumbe kipya yakaanza kufanyika huku kila mmoja akiwa na hofu kubwa kwani hakuna aliyekuwa na uzoefu na jambo hilo.
Mume wangu, hivi nitafanikiwa kujifungua salama kweli?
Usijali mke wangu, utajifungua salama salmini, si unakumbuka mara ya mwisho daktari alisema kila kitu mwilini mwako kipo sawa? Tena ukichanganya na mazoezi ninayokufanyisha naamini kila kitu kitakuwa sawa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nitafurahi sana kukuzalia mtoto, nakupenda sana mume wangu, alisema Angel na kumkumbatia mumewe, wakawa wanapigana mabusu kwa mahaba mazito.
***
Maisha yanazidi kuwanyookea Harrison na mkewe Angel (Malkia wa Masokwe) ambao sasa wanaishi kwenye ndoa halali nchini Canada katika Mji wa Langley. Kwa kadiri siku zinavyosonga mbele ndivyo wanavyozidi kuoneshana mapenzi ya dhati, kila mmoja akifurahia sana kuwa na mwenzake.
Baada ya kukaa kwenye ndoa kwa muda, Angel ananasa ujauzito na sasa wanasaidiana kuulea na mumewe, huku Harrison akimtunza mkewe huyo kama mboni ya jicho lake. Mara kwa mara anampeleka kliniki na baadaye anamsimamisha kazi aliyokuwa anafanya. Siku zinazidi kuyoyoma na ujauzito wa Angel unazidi kukua vizuri na hatimaye unatimiza miezi tisa.
Upande wa pili, Linda hakubali matokeo, anaendelea na upelelezi wa hali ya juu kutaka kuufahamu ukweli juu ya kifo cha Harrison. Kwa kutumia kampuni yake binafsi ya upelelezi, anafanikiwa kugundua mambo mengi yaliyokuwa yamejificha nyuma ya tukio hilo.
Anagundua kuwa Harrison hakufa kwenye ajali kama ambavyo kila mtu alikuwa anaamini. Anaendelea na upelelezi wa kina na sasa anagundua kuwa akaunti ya
Harrison ilikuwa bado inaendelea kutumika. Anajiapiza kuwa ni lazima afahamu mahali Harrison alikojificha.
Angel akiwa anafanya shughuli ndogondogo nyumbani kwake, tumbo lake likiwa limeongezeka ukubwa maradufu, alianza kuhisi hali iliyomfanya apate woga. Tumbo lilianza kumuuma ghafla, akajikokota kutoka jikoni alikokuwa anaandaa chakula na kuelekea chumbani lakini kabla hajafika, akiwa kwenye korido maumivu yalimzidi.
Akajishikilia ukutani na kukaa chini huku akiugulia maumivu makali, ghafla akasikia kitu kama kisu kikali kimepita katikati ya miguu yake, maji mengi yakaanza kuvuja na kulowanisha nguo zake. Kwa kuwa hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza, hakuelewa ni kitu gani kilichokuwa kinamtokea.
Mu me wa ngu! Na..ku..faaa! Angel aliongea na mumewe kwa njia ya simu kisha akajilaza chini na kutulia kimya. Harrison aliyekuwa njiani akitokea kazini, alishtuka kupita kiasi kutokana na alichoambiwa na mkewe. Hata alipojaribu kupiga tena simu, ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
Akaharakisha kuelekea nyumbani kwake. Alipofika, bila kupoteza muda, moja kwa moja alikimbilia ndani, alichokutana nacho kilimfanya ashikwe na woga kuliko kawaida. Mkewe alikuwa ameanguka chini huku maji mengi yakimchuruzika kutoka katikati ya miguu yake.
Mungu wangu! alisema Harrison huku akiinama na kujaribu kumtingisha mkewe. Mapigo ya moyo yalikuwa yakisikika kwa mbali lakini hakuwa na fahamu. Akalazimika kutoka nje haraka na kwenda kutafuta msaada wa gari la kubebea wagonjwa (Ambulance).
Kwa bahati nzuri, alipopiga namba ya simu ya dharura na kueleza mahali mgonjwa alipo, alipata mwitikio wa haraka, baada ya dakika chache vingora vya gari la kubebea wagonjwa vikawa vinasikika jirani na nyumba yao. Muda mfupi baadaye, gari likapaki nje ya nyumba yao, wauguzi waliokuwa na kitanda maalum cha kubebea wagonjwa wakashuka na kumfuata Harrison.
Yupo ndani, alisema Harrison huku akitangulia kuingia ndani. Wauguzi hao wakamfuata na kwenda moja kwa moja mpaka mahali Angel alipokuwa amelala.
Amebanwa na uchungu na tayari chupa ya uzazi imepasuka, alisema muuguzi mmoja wakati wakisaidiana kumbeba Angel na kumuweka kwenye kitanda maalum, wakatoka mbiombio na kumpeleka mpaka kwenye ambulance na safari ya kuelekea hospitali ikaanza.
Njia nzima Harrison alikuwa akimuomba Mungu wake amsaidie mkewe kujifungua salama kwani hakuna kitu alichokuwa anakisubiri kwa hamu kama mtoto kutoka kwenye tumbo la mwanamke aliyekuwa anampenda kuliko kitu kingine chochote chini ya jua.
Baada ya kufikishwa hospitali, Angel aliteremshwa harakaharaka na kuwekwa juu ya kitanda cha magurudumu, akakimbizwa kwa kasi kuelekea kwenye wodi ya wazazi (maternity).
Inject her with pitressin drip!(Mtundikieni dripu ya maji ya uchungu) alisema daktari mkunga aliyepewa jukumu la kumsaidia Angel kujifungua.
Baada ya kutundikiwa dripu hiyo, Angel alizinduka na kuanza kulalamikia maumivu makali aliyokuwa anayasikia mwili mzima baada ya kuingizwa maji ya uchungu mwilini, hasa tumboni. Manesi na wakunga wakamzunguka, Harrison akazuiwa kuingia kwenye wodi ya wazazi na kila mtu akawa anahaha kujaribu kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Kelele alizokuwa anapiga Angel, zilimfanya Harrison ashindwe kukaa na kutulia, kiti alikiona cha moto, akawa anazunguka huku na kule, mikono ikiwa kichwani. Kila alipomuona daktari au nesi akitoka kwenye wodi aliyokuwa amelazwa mkewe, alikuwa akimfuata na kumuuliza hali ya mgonjwa.
Kuwa na subira kaka, kaa na utulie kila kitu kitakuwa sawa.
Nitatuliaje wakati namsikia mke wangu analia kwa uchungu? Asije akafa nesi.
Hawezi kufa, hayo ni mambo ya kawaida na ndiyo maana wanaume huwa hamruhusiwi kusogelea kwenye wodi za wazazi, nesi alimwambia Harrison huku akimtaka kwenda kukaa sehemu maalum ya kusubiria. Akili za Harrison zilikuwa zimehama kabisa, akawa anamuonea huruma mkewe kutokana na mateso aliyokuwa anayapitia.
Sukuma! Sukuma! Jikaze ukijilegeza utamuua mwanao, sukuma kwa nguvu manesi na wakunga walikuwa wakimuelekeza Angel cha kufanya, baada ya kuhangaika kwa muda, hatimaye Angel alifanikiwa kujifungua salama. Kutokana na kutumia nguvu nyingi, Angel hakuelewa tena kilichoendelea.
Alikuja kuzinduka na kujikuta amelazwa kwenye wodi nyingine, manesi wawili wakiwa pembeni yake. Alipojishika tumboni, aligundua kuwa tumbo lake limepungua ukubwa ingawa alikuwa akisikia maumivu makali kupita kiasi.
Hongera dada! Umejifungua mtoto mzuri.
Nimejifungua mtoto gani? Mwanangu yupo wapi?
Umejifungua mtoto wa kiume, mzuri kama mama yake. Ngoja tukamlete, alisema nesi na kuondoka kuelekea kwenye chumba maalum ambapo mtoto alikuwa amehifadhiwa kwa muda.
Muda mfupi baadaye, mtoto aliletwa na kulazwa pembeni ya mama yake, Angel hakuyaamini macho yake, mtoto alikuwa mzuri ajabu! Halafu alikuwa na mchanganyiko mzuri wa sura kati ya baba yake na mama yake, akajikuta akitokwa na machozi ya furaha.
Manesi wakawa wanamuelekeza namna ya kuanza kumnyonyesha. Angel akawa anacheka wakati akimtazama mwanaye alivyokuwa ananyonya kwa fujo kuonesha kuwa alikuwa na njaa kali.
Muda mfupi baadaye, Harrison alifungua mlango wa wodi aliyokuwa amelazwa mkewe na kuanza kuangaza macho huku na kule. Angel aliwaambia kuwa huyo ndiyo baba mtoto wake, wakampa ishara ya kumuonesha mahali mkewe alipokuwa amelazwa.
Harrison akawa anatembea kwa hofu kubwa kuelekea pale alipoelekezwa. Alipofika, hakuyaamini macho yake kumuona mkewe amelala huku akiwa anamnyonyesha mtoto mchanga. Tabasamu pana lilikuwa limemjaa mkewe, alipomtazama usoni akajikuta akizidi kufurahi.
Mtoto wetu huyu hapa, alisema Angel huku akimuweka vizuri mwanaye, Harrison akainama na kumbusu mkewe kisha akambusu na mtoto huku akimkodolea macho mwanaye ambaye alikuwa amefanana naye kwa kiasi kikubwa. Akamkumbatia mkewe kwa furaha huku naye machozi ya furaha yakimtoka.
***
Kulipopambazuka, Linda alijiandaa na baada ya kumaliza, safari ya kuelekea Miami ikaanza. Alikwenda moja kwa moja kwenye Makao Makuu ya Benki ya Barclays jijini Miami ambapo aliomba kukutana na meneja mkuu.
Baada ya kujitambulisha na kuonesha vitambulisho vyake vya kazi, Linda alieleza kilichompeleka pale. Japokuwa benki hiyo haikuwa na utaratibu wa kutoa taarifa za wateja wake kwa watu wasiohusika, meneja alikubali kumpa taarifa hizo Linda hasa baada ya kusisitiza kuwa anafanya kazi kwa ajili ya taifa la Marekani.
Akaomba kupewa bank statement ya akaunti hiyo na taarifa nyingine muhimu za kuweka au kutoa fedha kwenye akaunti ya Harrison Harvey. Akaambiwa asubiri wakati wafanyakazi wa benki wanalifanyia kazi ombi lake.
***
Harrison anaendelea kujilia mbivu zake baada ya kufanikiwa kulipata penzi la msichana aliyemsumbua kwa kipindi kirefu, Angel (Malkia wa masokwe) ambaye awali alikuwa akiishi kwenye msitu mkubwa wa Tongass, akilindwa na masokwe wengi. Baada ya
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-
kumtorosha, anaenda naye nchini Canada ambako anamfundisha ustaarabu wa kibinadamu na baada ya kubadilika, anatangaza ndoa.
Wanaoana kimyakimya na kuwa mke na mume halali. Wanaishi maisha ya furaha na
upendo mkubwa. Baada ya kukaa kwenye ndoa kwa muda, Angel ananasa ujauzito. Harrison anamlea kama mboni ya jicho lake na hatimaye miezi tisa inatimia.
Angel anashikwa na uchungu ambapo Harrison anamkimbiza hospitali ambako
anajifungua salama mtoto wa kiume, akiwa na mchanganyiko mzuri wa sura ya mama na baba yake. Furaha inazidi maradufu kwenye familia yao, Harrison anaongeza upendo kwa mkewe huku akifurahia sana kuitwa baba.
Upande wa pili, Linda anaendelea na upelelezi wa kina kufuatilia ukweli uliokuwa umejificha nyuma ya maisha ya Harrison. Licha ya watu wote kuamini kuwa tayari kijana
huyo alishakufa, upelelezi wa Linda unamuwezesha kugundua kuwa kumbe hakufa bali ilikuwa ni danganya toto.
Jambo hilo linamuumiza sana moyo wake na sasa amechachamaa kutaka kufahamu ukweli wa mahali Harrison alipo. Anajiapiza kuwa ni lazima ampate mahali kokote alikojificha.
Siamini! Siamini kama na mimi nitakuwa naitwa baba! Natamani mama yangu angelijua hili lakini ndiyo hivyo tena, alisema Harrison huku akijifuta machozi ya furaha, wakaendelea kukumbatiana na mkewe huku wakipigana mabusu motomoto. Angel na mwanaye waliendelea kupewa huduma chini ya uangalizi wa daktari na manesi kwa muda, jioni wakaruhusiwa kurudi nyumbani.
Harrison akatafuta usafiri wa kuwarudisha mkewe na mwanaye nyumbani huku akiwa na furaha isiyoelezeka. Kwa jinsi alivyokuwa anachekacheka ungeweza kudhani akili zinataka kumruka, mtoto alimchanganya mno. Wakiwa kwenye gari, Harrison alimpakata mtoto na kukaa pembeni ya mkewe aliyekuwa amemuegamia begani.
Walipofika nyumbani kwao, Harrison ndiyo alikuwa wa kwanza kuteremka garini, akampeleka mtoto ndani kisha akarudi na kumsaidia mkewe kuingia ndani. Alipomfikisha chumbani alirudi na kumalizia kuteremsha vitu vyote kwenye gari na kumlipa dereva fedha zake.
Nimeandaa zawadi ya jogoo mkubwa kwa ajili yako mke wangu, nataka umle na kummaliza, alisema Harrison huku akianza kuandaa kitoweo cha kuku mkubwa alichokuwa ameandaa maalum kwa ajili ya mkewe. Alishughulikia kila kitu, akawasha moto na kuanza kupika huku mkewe akiendelea kumnyonyesha mtoto wao.
Pilikapilika ziliendelea, Harrison akamuandalia mkewe supu ya kuku mzima na kumuwekea mezani, akamuandalia kila kitu kisha akamsaidia kumbeba mtoto na kumtaka ale.
Nashukuru kwa kunijali mume wangu, kumbe unajua kupika vizuri namna hii, alisema Angel huku akila taratibu. Furaha ilizidi kuongezeka zaidi ndani ya nyumba hiyo, muda mfupi baadaye wafanyakazi wenzake Harrison na wale waliokuwa wanafanya kazi na mkewe wakaanza kuwasili nyumbani hapo wakiwa na zawadi mbalimbali.
Kila aliyekuwa anamuona mtoto, aliwasifu kwani kwa hakika alikuwa mzuri sana. Wengine wakawa wanawatania kuwa wajiandae kukabiliana na kesi nyingi za mabinti kupewa ujauzito na mtoto wao kwani alikuwa handsome kwelikweli. Vicheko vya furaha vilitawala kila sehemu.
Utaratibu wa maisha ya Harrison ukabadilika, akawa analazimika kuwa wa mwisho kulala kila siku na wa kwanza kuamka. Jambo la kwanza kila asubuhi ilikuwa ni kumuandalia mkewe maji ya moto kwa ajili ya kumchua tumbo lake na kuoga kisha kumuogesha mtoto.
Baada ya hapo alikuwa akimuandalia mkewe supu kisha kufua nguo za mtoto alizochafua usiku kucha. Ratiba yake ya kwenda kazini nayo ikabadilika kwani kwa siku tatu za mwanzo aliomba ruhusa kwa ajili ya kuihudumia familia yake, baada ya hapo akawa anaondoka nyumbani majira ya saa nne baada ya kumaliza kazi zote nyumbani.
Upendo wake kwa Angel ndiyo uliomsukuma kufanya yote hayo na kamwe hakuona ugumu wa kufanya hivyo kama walivyo wanaume wengi ambao huwaachia mzigo huo wake zao bila kujali hali za kiafya wanazokuwa nazo wakitoka kujifungua. Baada ya siku kadhaa, wakampa jina mtoto wao ambapo Harrison alipendekeza aitwe Harvey Junior au kwa kifupi Junior, wazo ambalo Angel alikubaliana nalo.
Watu wengi wakaanza kuwaita Harrison na mkewe kwa jina la mama na baba Junior, wakawa wanajisikia fahari kubwa kwani nao sasa walikuwa wazazi, tena wanaopendana pengine kuliko watu wote kwenye mji huo.
Mh! Mama Junior mumeo anakujali mpaka naona wivu, natamani na mimi mume wangu angekuwa ananipenda na kunijali kama wewe! Yaani anafua nepi za mtoto na kumuogesha? Mbona mwenzetu una raha! mwanamke mmoja aliyekuwa anaishi jirani na familia ya Harrison alimwambia Angel asubuhi moja baada ya kumkuta akianika nguo za mwanaye. Angel hakujibu kitu zaidi ya kutabasamu.
Baada ya siku kadhaa,walianza kumpeleka mtoto kliniki ambapo Harrison kama kawaida yake, alikuwa akifanya kazi zote, kuanzia kumbeba mtoto, kumbebea mkewe mkoba wa nguo za mtoto na vitu vingine. Kila walipokuwa wanapita, watu walikuwa
wakimshangaa Harrison huku wengi wakimsifu kwani alikuwa na upendo wa dhati kwa mkewe.
Siku zikawa zinazidi kusonga mbele huku Harvey Junior akizidi kukua vizuri na kuchangamka kila uchao. Uwepo wake ukazidi kuichangamsha nyumba yao kwani mara kwa mara mtoto huyo alikuwa akisikika akilia au kucheka kama wafanyavyo watoto wengi wakiwa bado wadogo.
***
Baada ya wafanyakazi wa Benki ya Barclays jijini Miami kulifanyia kazi ombi la Linda, walikuja na majibu yaliyosababisha msichana huyo mrembo atake kupoteza fahamu. Walimpa taarifa kuwa akaunti hiyo inaendelea kutumika kama kawaida nchini Canada na kwa mara ya kwanza, ilitumika kwenye Mji wa Abbotsford kutoa fedha na baada ya hapo, iliendelea kutumika kwenye mji huo na baadaye ikaonesha kuwa ilitumika Langley.
Mungu wangu! Ina maana Harrison anaendelea na maisha yake kama kawaida? Ooh Lord! Why is this happening to me?
(Ooh Mungu! Kwa nini haya yananitokea?) alisema Harrison akiwa ndani ya ofisi ya meneja mkuu wa benki hiyo.
Kwani vipi afisa? meneja huyo alimuuliza Linda lakini hakujibu kitu zaidi ya kutoa kitambaa kwenye pochi yake ndogo ya bei mbaya na kuanza kujifuta machozi. Hakutaka kuendelea kukaa ndani ya ofisi hiyo, alishukuru kisha akakusanya karatasi alizopewa
na kuziweka kwenye mkoba wake, akatoka mbio huku akiendelea kumwaga machozi kama mtu aliyepokea taarifa za msiba.
Kila aliyemuona alimshangaa kwani haikuwa kawaida kwa msichana mrembo kama yeye, anayeonesha kuwa na kila kitu kwenye
maisha yake kulia hadharani. Alikwenda mpaka kwenye eneo la maegesho na kuingia ndani ya gari lake la kifahari alilokuja nalo. Akajifungia na kulalia kwenye usukani, akawa analia kwa uchungu sana. Alitia huruma.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
My heart is broken! I have never been tired of living like now! Harrison my love, why did you leave me? Why?
(Moyo wangu umevunjika! Sijawahi kuchoka kuishi kama ilivyo sasa! Harrison mpenzi, kwa nini uliniacha? Kwa nini?)
Linda alisema kwa uchungu huku akijipigapiga kichwa kwenye usukani, alilia kwa muda mrefu lakini hakukuwa na mtu wa kumfuta machozi. Kwa unyonge akawasha gari na kuanza kuondoka kurejea nyumbani kwao.
Hata hivyo, licha ya Linda kugundua kuwa Harrison alimkimbia siku ya ndoa yao kwa sababu anazozijua mwenyewe, hakutaka kukata tamaa. Aliamua kupiga moyo konde na kuendelea kumfuatilia ili aujue ukweli. Hakutaka kujali ataumia kiasi gani kuufahamu ukweli, alishakula nadhiri tangu mwanzo kuwa atamfuatilia kwa karibu hadi ajue mwisho wake hivyo hakuwa na la kufanya zaidi ya kuandaa safari ya dharura kwenda Canada.
***
Dunia haina siri, licha ya Harrison kuudanganya ulimwengu kuwa amekufa kwenye ajali ya barabarani, ukweli unakaribia kujulikana. Bila kujua kuwa anafuatiliwa kwa karibu,
Harrison anaendelea kujilia mbivu zake baada ya kufanikiwa kulipata penzi la msichana aliyemsumbua kwa kipindi kirefu, Angel (Malkia wa masokwe).
Harrison amefanikiwa kumnasa msichana huyo ambaye awali alikuwa akiishi kwenye msitu mkubwa wa Tongass, akilindwa na masokwe wengi. Baada ya kumtorosha, anaenda naye nchini Canada ambako anamfundisha ustaarabu wa kibinadamu na baada ya kubadilika, anatangaza ndoa.
Wanaoana kimyakimya na kuwa mke na mume halali. Wanaishi maisha ya furaha na upendo mkubwa. Baada ya kukaa kwenye ndoa kwa muda, Angel ananasa ujauzito.
Harrison anamlea kama mboni ya jicho lake na hatimaye miezi tisa inatimia.
Angel anashikwa na uchungu ambapo Harrison anamkimbiza hospitali ambako anajifungua salama mtoto wa kiume, akiwa na mchanganyiko mzuri wa sura ya mama na
baba yake. Furaha inazidi maradufu kwenye familia yao, Harrison anaongeza upendo kwa mkewe huku akifurahia sana kuitwa baba. Wanampa mtoto wao jina la Harvey Junior.
Upande wa pili, Linda ameshagundua kuwa akaunti ya benki ya Harrison inaendelea kutumika nchini Canada na sasa anajiandaa kusafiri kwa ndege kuelekea nchini humo. Hakati tamaa mpaka ahakikishe amempata Harrison.
Baba na mama, nimewaita jioni ya leo ili niwaambie jambo moja tu kwamba nataka kusafiri kwenda Canada na sijui nitarudi lini. Nafikiri mpaka nitakapokamilisha kazi yangu ndipo nitakaporudi, sitajali muda nitakaoutumia lakini cha msingi mpaka nikamilishe kazi yangu.
Mbona ghafla hivyo mwanangu? Kwani unaenda kufanya kazi gani? aliuliza mama mzazi wa Linda huku akionesha wasiwasi ndani ya moyo wake.
Nakwenda kuendelea na kazi yangu ya upelelezi, kuna jambo moja muhimu sana ambalo inabidi nilifuatilie kwa kina mpaka niujue mwisho wake.
Usituambie kuwa bado unamfuatilia Harrison, alisema mzee Ford huku akiwa na shauku kubwa ya kusikia mwanaye atajibu nini. Japokuwa wote walikuwa wanafahamu jinsi binti yao alivyokuwa anampenda kijana huyo, hawakuwa tayari kuona anazidi kuteseka kumfuatilia mtu asiye na mapenzi kwake.
Linda hakujibu kitu, aliwatazama baba na mama yake kwa zamu kisha akajiinamia chini. Wote walitambua kilichokuwa kinapita ndani ya kichwa chake, wakamsogelea na kumkumbatia kwa pamoja.
Linda mwanangu, hatukukulea uje kuwa hivi, lazima ujifunze kukubaliana na matokeo, haitakuwa na maana yoyote kuendelea kumfuatilia mtu ambaye mara zote amekuwa akiuvunja moyo wako, hayo uliyoyagundua yanatosha, tafadhali usiende.
No! Lazima niufahamu mwisho wa Harrison, ukweli ndiyo kitu pekee kitakachonifanya niishi kwa amani, naombeni mniruhusu.
Lakini Linda, ni ukweli gani tena unaoufuatilia mwanangu? Sote tumeshagundua kuwa Harrison hakufa bali ulikuwa ni mpango wake wa kukwepa kukuoa, hiyo pekee inatosha kukufanya uamini kuwa hakuwa na mapenzi ya dhati kwako, usiendelee kuutesa
moyo wako, utampata tu mwanaume bora, alisema mama Linda huku akiungwa mkono na mumewe, kwa pamoja wakawa wanambembeleza binti yao.
Licha ya kujaribu kutumia ushawishi wao wote, bado Linda hakutaka kubadilisha msimamo wake, alingangania kuwa ni lazima asafiri mpaka Canada kuikamilisha kazi yake. Baada ya wazazi wake kuona binti yao ameshikilia msimamo wake, ilibidi wakubaliane naye kwa shingo upande, wakamruhusu kwenda Canada lakini wakamtaka kuwa mwangalifu na kuendelea kuwasiliana nao mara kwa mara.
Siku mbili baadaye, Linda alikwenda kwenye Uwanja wa Ndege wa Miami, akakata tiketi ya kuelekea Ottawa, Canada kisha akakaa sehemu ya abiria kusubiria ndege. Uchungu aliokuwa nao ndani ya moyo wake ulimfanya muda wote awe anatokwa na machozi. Akakaa kwenye kiti kusubiria ndege huku akiendelea kulia kama mtu aliyepokea taarifa za msiba.
Abiria waliokuwa karibu yake walibaki kumshangaa kwani haikuwa kawaida kumuona binti mrembo kama yeye akilia hadharani, tena bila ya kuwa na mtu wa kumbembeleza. Baada ya kusubiri kwa muda, ndege kubwa ya Shirika la Ndege la Nordic Airways ilianza kupakia abiria kwa safari ya kuelekea nchini Canada.
Linda alikuwa miongoni mwa abiria wa kwanza kupanda kwenye ndege hiyo, akaenda moja kwa moja mpaka kwenye siti yake na kutulia kimya, mawazo machungu yakiendelea kupita ndani ya kichwa chake. Baada ya dakika arobaini kupita, sauti kutoka kwenye vipaza sauti ndani ya ndege hiyo ilianza kusikika ikiwataka abiria wote kufunga mikanda.
Muda mfupi baadaye, ndege kubwa ya Airbus 380, mali ya kampuni ya Nordic Airways ikaanza kusogea taratibu kuelekea kwenye njia za kurukia (run ways). Baada ya muda, injini zote zikawashwa na ndege ikaanza kunguruma kwa nguvu, ikaanza kuondoka kwa kasi na hatimaye ikaiacha ardhi ya Marekani na kupaa angani.
Lazima nimpate Harrison kwa njia yoyote, nataka anitamkie ana kwa ana kwamba hanipendi na hataki kuishi na mimi, najua akiniona lazima atabadilisha msimamo wake kwani bado nampenda sana na naamini na yeye ananipenda ila shetani aliingilia kati tu, Linda aliwaza huku akijifuta machozi, ndege ikapotelea angani.
***
Kwa kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, mtoto wa Harrison na Angel, Harvey Junior alizidi kuchangamka, akawa anakua vizuri akiwa na afya njema, jambo lililozidisha furaha kwa wote wawili.
Mume wangu!
Naam mke wangu.
Kuna jambo nataka kumfanyia mtoto wetu kwa manufaa yake ya baadaye.
Jambo gani kipenzi changu.
Nataka unisaidie kukivua hiki kidani changu shingoni, tukisafishe vizuri kisha tumvalishe ili na yeye kimpe ulinzi kama kilivyofanya kwangu tangu nikiwa mdogo mpaka leo hii nimekuwa mkubwa, alisema Angel huku akikaa vizuri ili mumewe amvue kidani hicho.
Tangu siku ya kwanza Harrison alipomuona Angel kwa karibu, aligundua kuwa alikuwa na kidani hicho shingoni ambacho
kutokana na kuwa na nywele nyingi, hakikuwa kikionekana kwa urahisi. Kuna wakati aliwahi kumhoji alikokipata kidani hicho lakini majibu yake yalionesha kuwa na yeye hakumbuki ila tangu aanze kuwa na akili, alijikuta akiwa amekivaa.
Mara kwa mara Harrison alikuwa akitaka kumvua lakini alikuwa mkali kwa madai kuwa amekuwa akikitumia kama kinga yake kwa kipindi chote cha maisha yake mpaka siku hiyo alipoamua mwenyewe kwa hiyari yake. Harrison alimkubalia, akaanza kazi ya kukifungua.
Kutokana na kukaa miaka mingi mwilini mwake, kazi ya kukivua haikuwa nyepesi mpaka akalazimika kukikata, kikaacha alama kwenye shingo ya Angel. Licha ya kuonekana kuchakaa sana, kidani hicho kwa mbali kilionesha kuwa na maandishi yaliyokuwa yanasomeka kwa shida, Harrison akakishika na kuanza kukichunguza kwa umakini wa hali ya juu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakakubaliana kuwa kabla ya kumvalisha mtoto wao, lazima wakipeleke kwa sonara kikasafishwe na kungarishwa ili kirudie upya wake, kazi ambayo Harrison alitakiwa kuifanya. Kabla ya kuondoka, Harrison aliendelea kumuuliza mkewe maswali mbalimbali kuhusu kidani hicho lakini kama alivyokuwa akimjibu siku zote, hakuwa akikumbuka chochote jinsi kilivyofika mwilini mwake.
Baada ya muda, Harrison alitoka na kwenda kwenye duka la sonara lililokuwa jirani na pale walipokuwa wanaishi. Jambo la kwanza kabla ya kukisafisha, Harrison alimuomba sonara amsaidie kuyasoma maandishi yaliyokuwa kwenye kidani hicho kwa kutumia kifaa maalum. Akaahidi kumpa malipo ya ziada baada ya kuikamilisha kazi hiyo. Sonara akakichukua na kukiweka kwenye mtambo maalum na kuanza kukipitisha taratibu kwa lengo la kuyasoma maandishi hayo.
***
SIRI kubwa iliyokuwa imejificha juu ya maisha ya Harrison ya kuudanganya ulimwengu kuwa amekufa kwenye ajali ya barabarani ili apate muda wa kwenda kuwa na malkia wa masokwe, inakaribia kujulikana. Harrison hajui
kama anafuatiliwa kwa karibu, anaendelea na maisha yake kama kawaida na mkewe kipenzi, wakiwa tayari wamejaliwa kupata mtoto wa kwanza, Harvey Junior.
Kila anapokumbuka jinsi alivyolipigania penzi la msichana huyo ambaye sasa ni mke wake halali, anajikuta akizidi kumpenda na kuahidi kumlinda kwa siku zote za maisha yake. Wanaendeleza maisha yao katika Mji wa Langley nchini Canada.
Upande wa pili, upelelezi wa nguvu unaofanywa na Linda, msichana ambaye Harrison alimkimbia kanisani siku ya harusi yao, amecharuka mno na sasa amekaribia kufahamu mahali Harrison alipo baada ya kugundua kuwa akaunti yake ya benki ilikuwa ikiendelea kutumika kutoka kwenye Mji wa Abbortsford nchini Canada. Anaamua kufunga safari mpaka kwenye mji huo.
Lazima nimpate Harrison kwa njia yoyote, nataka anitamkie ana kwa ana kwamba hanipendi na hataki kuishi na mimi, najua akiniona lazima atabadilisha msimamo wake kwani bado nampenda sana na naamini na yeye ananipenda ila shetani aliingilia kati tu, Linda aliwaza huku akijifuta machozi, ndege ikapotelea angani.
Baada ya kusafiri kwa saa nyingi angani, hatimaye ndege aliyopanda Linda, Airbus 380 mali ya Kampuni ya Nordic Airways iliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ottawa nchini Canada. Mhudumu wa ndege akatoa taarifa kwa abiria wote kuwa kila mmoja afunge mkanda kwani ndege ilikuwa ikijiandaa kutua.
Muda mfupi baadaye, ndege iligusa ardhi ya Canada, ikakimbia kwa kasi mpaka mwisho wa uwanja kisha ikageuza na kuanza kurudi taratibu kuelekea kwenye ofisi za uwanja huo wa kimataifa. Ikasimama kisha ngazi zikateremshwa, abiria wakaanza kushuka mmoja mmoja. Linda alikuwa miongoni mwa abiria hao, akawa anaangaza macho huku na kule kwani hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kufika nchini humo.
Hakutaka kupoteza muda, alipoteremka kwenye ndege tu, alitoka nje ya uwanja wa ndege na kuulizia usafiri wa kuelekea Abbotsford. Dereva teksi mmoja akamuelekeza kuwa ni lazima asafiri kwa mabasi yaendayo kwa kasi ili kufika huko kwa sababu kulikuwa na umbali mrefu kutoka Ottawa.
Linda alikubaliana naye na kumuomba ampeleke na teksi yake mpaka stendi ya mabasi yaendayo kwa kasi. Akaingia ndani ya gari na safari ikaanza. Alipomfikisha stendi, Linda alimlipa fedha zake kisha akateremka na kuelekea kwenye sehemu ya kukatia tiketi. Kabla ya kutoa fedha, aliuliza mambo mawili matatu kuhusu safari yake, alipojibiwa akakata tiketi kisha akaenda kuungana na abiria wengine kusubiri basi lianze safari.
Takribani dakika kumi na tano baadaye, basi liliwasili stendi, abiria wakapanda na safari ya kuelekea Abbotsford ikaanza. Bado mawazo yaliendelea kukisumbua kichwa cha Linda kiasi cha kuona anachelewa kufika. Japokuwa basi hilo lilikuwa likisafiri kwa spidi kubwa, Linda aliona kama linakwenda taratibu, akatamani angekuwa na uwezo apae angani kama ndege ili awahi kufika.
Safari haikuwa nyepesi kwani kulikuwa na umbali mrefu kutoka Ottawa mpaka Abbortsford, Linda akajikuta akipitiwa na usingizi akiwa ndani ya gari. Akiwa usingizini, alianza kuota ndoto za ajabuajabu, hali iliyomfanya awe anashtukashtuka kila mara.
Baada ya safari ndefu, hatimaye basi likawasili Abbortsford. Kwa kuwa muda ulikuwa umekwenda sana, Linda alitafuta hoteli nzuri ya kitalii na kufikia hapo. Akaenda kujipumzisha wakati akifikiria nini cha kufanya na wapi pa kuanzia. Hakutaka mtu yeyote ajue juu ya uwepo wake eneo hilo.
Usiku hakulala, aliendelea kuwaza mambo mengi ndani ya kichwa chake, kitu ambacho hakuweza kukibadilisha mpaka muda huo ilikuwa ni penzi lake kwa Harrison. Kwa kadiri alivyokuwa anakaribia kufahamu ukweli juu ya Harrison, ndivyo hisia zake za mapenzi zilivyokuwa zinazidi kuamka. Akawa anajiapiza kuwa hawezi kuhangaika kiasi hicho halafu akaishia kulikosa penzi la mwanaume wa maisha yake.
Hakutaka kujali Harrison kwa nini alimkimbia au yupo na nani, kitu pekee alichotaka ilikuwa ni kutimiza ndoto yake iliyoyeyuka miaka kadhaa iliyopita ya kuolewa na Harrison. Aliendelea kuwaza mambo mbalimbali huku akiandika vitu muhimu kwenye kitabu chake cha kumbukumbu. Asubuhi kulipopambazuka, aliwahi kuamka na kujiandaa kisha akatoka na kwenda kwenye kituo cha teksi.
Naomba unipeleke kwenye Benki ya Barclays, Tawi la Abbortsford, Linda alimwambia dereva teksi aliyekuwa jirani naye, akaingia ndani ya teksi na safari ikaanza. Iliwachukua dakika kumi tu, wakawa tayari wameshafika. Linda akamlipa dereva fedha zake kisha akaingia ndani ya benki hiyo na kuomba kuonana na meneja mkuu.
Mimi ni afisa upelelezi kutoka nchini Marekani, kuna taarifa muhimu nazifuatilia kuhusu mtuhumiwa mmoja ambaye alitoroka siku nyingi zilizopita na duru za kiintelijensia zinaonesha yupo kwenye mji huu, utambulisho alioutoa Linda ulimfanya meneja wa benki hiyo akae vizuri na kumtegea sikio kwa umakini. Akamuonesha vitambulisho vyake na hati maalum ya kufanya kazi ndani ya Canada ambayo aliitafuta kabla hajasafiri.
Alimueleza meneja huyo kuwa taarifa za kibenki zinaonesha kuwa mtuhumiwa anayetafutwa, anaendelea kutumia akaunti yake kupitia tawi hilo. Linda aliamua kutumia jina la mtuhumiwa kwa Harrison ili iwe rahisi kwake kupata taarifa muhimu kwani alijua kuwa akimtambulisha kama mpenzi wake aliyemkimbia, suala hilo litapoteza uzito.
Aliendelea kueleza mambo kadhaa ambayo yalizidi kumpa picha meneja huyo kuwa ni kweli mtu anayezungumziwa yupo ndani ya mji huo na anatumia akaunti yake kupitia benki hiyo. Kwa kuwa tayari Linda alishaandika tarehe ambayo akaunti ya Harrison ilitumika kwa mara ya kwanza kwenye tawi hilo, meneja hakupata shida.
Alichokifanya ilikuwa ni kumuita mtaalamu wa IT (Information Technology) wa benki hiyo na kumuomba waongozane mpaka kwenye chumba kilichokuwa na kamera za siri zilizotegeshwa kwenye mashine zote za ATM kwenye benki hiyo.
Walipofika ndani ya chumba hicho kikubwa kilichokuwa kimejaa mitambo ya kisasa ya ulinzi, Linda alielekezwa sehemu ya kukaa kisha mtaalamu huyo akaanza kazi akishirikiana na meneja wake.
Unaikumbuka namba ya akaunti yake?
Ndiyo, hii hapa, alisema Linda huku akifunua kitabu chake cha kumbukumbu, wakazitumia namba hizo kufahamu muda ambao ilitumika ili iwe rahisi kunasa picha za mtu aliyeitumia. Mtaalamu wa IT aliendelea kushughulikia mitambo na baada
ya muda, akafanikiwa kuzinasa picha za Harrison zikimuonesha jinsi alivyochukua fedha kwenye mashine ya ATM.
Mungu wangu, ndiyo yeye! Jamani Harrison ni yeye, Linda aliyekuwa amekaa, alikurupuka na kuisogelea kompyuta
aliyokuwa anaitumia mtaalamu yule kufuatilia picha za matukio baada ya kuiona taswira ya Harrison.
Japokuwa alikuwa amebadilika kidogo kwa kufuga nywele ndefu zilizoonesha kukosa matunzo na ndevu, bado Linda aliweza kumtambua vizuri Harrison, mapigo ya moyo wake yakawa yanaenda kwa kasi akiamini sasa kila kitu kitafahamika na lazima atampata Harrison kama alivyokuwa amejiapiza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kufanikiwa kwa hatua hiyo ya kwanza, Linda aliomba ahamishiwe picha hizo kwenye laptop yake kwa ajili ya ushahidi, jambo ambalo lilitekelezwa kisha akaomba kupata bank statement na picha za ushahidi za siku zote ambazo Harrison alitumia tawi hilo la benki.
Katika siku za mwanzo, Harrison alionekana akifika benki kwenye mashine ya ATM na kutoa kiwango fulani cha fedha na kuondoka lakini baada ya kufanya hivyo kwa siku kadhaa, alionekana mtu mwingine kabisa, akiwa na sura tofauti akifika benki na kutoa fedha kwa kutumia akaunti ya Harrison. Kilichozidi kumchanganya Linda, mtu huyo alikuwa akifanana na Harrison umbo la mwili wake na jinsi alivyokuwa akitembea. Utata mwingine ukaibuka.
***
Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu. Maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana, yanapita kama maua yachanuavyo na kunyauka. Wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unapumua, ni vyema basi kufikiria maisha baada ya kifo.
LINDA amechachamaa kumfuatilia Harrison mpaka aujue mwisho wake. Hataki kukubali kuwa mwanaume huyo aliyemkimbia kanisani siku ya harusi yao anampenda msichana mwingine kuliko
anavyompenda yeye. Anaamini alipitiwa na shetani tu ndiyo maana akafanya yote hayo lakini bado anampenda.
Baada ya kugundua kuwa akaunti ya benki ya Harrison inaendelea kutumika kwenye Mji wa Abbotsford, Canada, msichana huyo kutoka familia ya kitajiri anaamua kufunga safari mpaka nchini humo. Anatumia mbinu zote za upelelezi alizojifunza akiwa chuoni ili kuhakikisha anamrejesha Harrison mikononi mwake.
Anaenda mpaka kwenye benki iliyoonesha kuwa akaunti ya Harrison ilitumika. Kwa kutumia picha zilizopigwa na kamera maalum zilizotegeshwa kwenye mashine za ATM, Linda anafanikiwa
kugundua kuwa kumbe Harrison bado alikuwa hai. Hata hivyo, anashangazwa na watu wawili wanaotumia akaunti hiyo. Anaamua kufuatilia kwa kina.
Je, nini kitaendelea?
SONGA NAYO
Kilichozidi kumchanganya Linda, mtu huyo alikuwa akifanana na Harrison umbo la mwili wake na jinsi alivyokuwa akitembea. Utata mwingine ukaibuka. Hata hivyo, hakutaka kuonesha wasiwasi wake mbele ya watu, akatulia na picha zikaendelea
kuhamishiwa kwenye laptop yake mpaka zilipoisha. Akapewa na bank statement kama alivyokuwa ameomba.
Baada ya taratibu zote kukamilika, aliwashukuru meneja wa benki na mtaalamu wa teknolojia ya mawasiliano (IT) ambao walimsaidia sana kutimiza alichokuwa anakitaka. Alipotoka, alirudi moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha hoteli aliyokuwa
amefikia na kujifungia ndani ya chumba chake, akaitoa laptop yake iliyokuwa na picha na taarifa zote muhimu na kuanza kuichunguza kwa jicho la tatu.
Alitaka kufahamu yule mtu mwingine aliyeonekana anaitumia akaunti ya Harrison ni nani na ana uhusiano gani na mpenzi wake huyo. Alizivuta jirani (zoom) picha zote mbili, ile ya Harrison na ile ya mtu mwingine. Picha ya kwanza ilimthibitishia kuwa aliyemuona alikuwa ni Harrison kwani licha ya kuwa na nywele ndefu na ndevu nyingi, bado sura yake haikubadilika.
Kwa uhakika zaidi, alitoa picha yake nyingine aliyokuwa anatembea nayo kwenye mkoba wake, akawa anaifananisha na ile ya kwanza, akajiridhisha kuwa ni kweli alikuwa ni Harrison. Akaanza kuifananisha na ile ya mtu yule ambaye bado alikuwa hajamtambua.
Kila alipojaribu kuvuta kumbukumbu kama alishawahi kumuona wapi, hakupata jibu. Akaanza kumchunguza kiungo kimoja baada ya kingine. Katika hali ambayo hakuitegemea, aligundua kuwa mtu yule alikuwa akifanana kwa kiasi kikubwa na Harrison kwa vitu vingi.
Alifanana naye kuanzia macho, pua, mdomo, masikio na jinsi mwili wake ulivyokuwa umejengeka.
Mbona Harrison hajawahi kuniambia kama ana ndugu yake anayefanana naye kiasi hiki? Yeye alizaliwa peke yake kwa mama yake na hana ndugu yeyote. Huyu ni nani?
Linda alijiuliza maswali mengi ambayo yote yalikosa majibu. Ikabidi ajipe muda wa kutafakari kilichokuwa kinaendelea, akawa anarudiarudia kuitazama ile picha.
Au ni yeye ameamua kubadilisha sura kwa kufanyiwa plastic surgery? wazo jipya liligonga ndani ya kichwa cha Linda, akazidi kuitazama ile picha kwa umakini wa hali ya juu.
Akili zake zikamtuma kuwa lazima yule ni Harrison ila aliamua kubadilisha sura ili iwe vigumu kwa watu waliokuwa wanamfahamu kumtambua.
Kama aliweza kuudanganya ulimwengu kuwa amekufa, unafikiri anaweza kushindwa kujibadili sura ili aendelee kuishi bila kusumbuliwa? Linda alijiuliza maswali yaliyozidi kumpa mwanga wa nini cha kufanya.
Alizidi kuumia moyo wake kuona Harrison alikuwa tayari kupoteza ushahidi wa yeye kuwepo duniani kwa sababu ya mapenzi ya mwanamke aliyelelewa na masokwe. Ndani ya nafsi yake alijiapiza kufanya kila linalowezekana kuhakikisha anampata Harrison na kumrudisha mikononi mwake. Kamwe hakutaka kukubali kushindwa kirahisi kumpoteza mwanaume aliyekuwa anampenda kuliko kitu chochote duniani.
Baada ya kupata uhakika kuwa Harrison atakuwa amebadilisha sura, alianza kazi ya kutafuta vituo vya plastic surgery vilivyokuwa ndani ya Mji wa Abbotsford. Aliamini kwa kutumia mafunzo yake ya kipelelezi aliyoyapitia, lazima atafanikiwa kujua alibadilishwa sura kwenye kituo gani. Aliamini akishakijua kituo hicho na kumpata mtu aliyefanya kazi hiyo, itakuwa rahisi kufahamu anuani ya makazi ya Harrison.
Hakutaka kupoteza muda, alianza kutafuta kwenye intaneti orodha ya kliniki zilizokuwa zinatoa huduma ya kubadilishwa sura (plastic surgery). Aligundua kuwa kulikuwa na kliniki tatu pekee ambazo ndiyo zilizokuwa zinatoa huduma hiyo, Abbotsford Clinic, Facial Surgery Clinic na Albert Stein Sanitarium.
Muda huohuo alinyanyuka akiwa ameshanakili anuani za mahali kliniki hizo zilipo, akabeba laptop yake na kutoka hadi nje, akakodi teksi na kumuelekeza dereva kumzungusha kwenye kliniki hizo.
Alianzia Abbotsford Clinic, alipofika alijitambulisha kuwa yeye ni mpelelezi wa kimataifa kutoka Marekani na amefika hapo kwa ajili ya kumsaka mtuhumiwa ambaye alifanya uhalifu nchini kwake na kutoroka.
Kuna taarifa za kuaminika kuwa amebadilisha sura na sasa ana mwonekano tofauti kabisa. Tafadhali nisaidie kuangalia katika orodha ya watu uliowafanyia plastic surgery na ukinisaidia kumpata nitakupa donge nono, alisema Linda huku akikaa kwenye kiti, mbele ya daktari mzoefu wa kazi hiyo.
Samahani, siwezi kukusaidia kwa sababu ni mwiko kwa taaluma yetu kutoa taarifa za wateja wetu, utanisamehe kwa hilo.
Kwani hujui kwamba kuna sheria zinazoisimamia kazi yako? Nimeshakwambia mimi ni mpelelezi wa kimataifa na hiki ni kitambulisho changu.
Ukishindwa kunipa ushirikiano nitatoa maagizo ukamatwe na kutupwa lupango, alisema Linda huku akionesha kubadilika. Sasa alivaa sura ya kazi na hakutaka masihara hata kidogo.
Baada ya daktari huyo kuona Linda amebadilika, ilibidi atii amri aliyopewa, akafungua kompyuta yake na kuanza kumuonesha Linda orodha ya watu wote waliofanyiwa plastic surgery katika kliniki hiyo. Linda alianza kupitia taarifa za mtu mmoja baada ya mwingine lakini hakuona kama Harrison alikuwepo.
Alipojiridhisha, aliondoka huku akiahidi kuwa atarudi tena endapo atakwama. Akachomoa noti kadhaa na kumpa daktari huyo kisha akaondoka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alitoka nje ambapo alimkuta dereva teksi aliyemleta akiwa anamsubiri. Akaingia na safari ikaanza kuelekea kwenye kliniki ya pili, Facial Surgery Clinic ambapo Linda alitumia mbinu kama alizozitumia awali.
Hata hivyo, alipopewa orodha ya watu waliofanyiwa upasuaji wa kubadilishwa sura kwenye kiliniki hiyo, Harrison hakuwa miongoni mwao. Linda akaanza kukata tamaa kwani matumaini yake yalikuwa yakififia kwa kasi.
Hata hivyo, hakutaka kuishia hapo, aliamua kwenda kuhitimisha kazi yake kwenye kliniki ya mwisho.
Alitoka hadi nje na kuingia ndani ya teksi huku akionesha kuwa na mawazo mengi, akamuelekeza dereva kumpeleka kwenye kliniki ya mwisho, Albert Stein Sanitarium. Alipofika, alijitambulisha mapokezi kisha akapelekwa moja kwa moja kwa Dk. Albert Stein
aliyekuwa akiimiliki kliniki hiyo. Linda alijitambulisha na kutoa kitambulisho chake kisha akaeleza kilichompeleka.
Tofauti na kliniki mbili alizopitia awali, Dk. Stein alionesha ushirikiano wa hali ya juu, akaanza kumuonesha orodha ya watu wote waliofanyiwa upasuaji huo kwenye kliniki yake. Wakati akiendelea kumuonesha, Linda aliona picha ambayo ilimfanya apige kelele.
Ndiyo mwenyewe! Mungu wangu, alisema huku akimtaka Dk. Stein kuivuta kwa karibu picha ya Harrison.
MAPENZI kati ya Harrison na mkewe Angel yanazidi kushamiri, upendo wa dhati unaongezeka kati yao baada ya kupata mtoto wa kwanza, Harvey Junior. Wakati hayo yakiendelea, msichana ambaye Harrison alimkimbia siku ya harusi yao, Linda amechachamaa kumfuatilia Harrison mpaka aujue mwisho wake.
Hataki kukubali kuwa mwanaume huyo anampenda malkia wa masokwe kuliko anavyompenda yeye na ndiyo maana alikuwa tayari kupata shida kwa kipindi kirefu wakati akipigania penzi lake. Linda anaamini Harrison alipitiwa na shetani tu ndiyo maana akafanya yote hayo lakini bado anampenda kwa dhati.
Upelelezi wa kina anaoufanya Linda unamuwezesha kugundua kuwa Harrison yupo kwenye Mji wa Abbotsford, Canada. Msichana huyo kutoka familia ya kitajiri anaamua kufunga safari mpaka nchini humo na baadaye anagundua kuwa kumbe Harrison alibadilisha sura.
Baada ya kugundua jambo hilo, Linda anaanza kupita kwenye kliniki za kubadilishia sura akitafuta maelezo ya kina ya Harrison na mahali alikokuwa anaishi kwa muda huo. Anajiapiza kuwa ni lazima ampate mwanaume huyo na kurejesha penzi lake.
Sonara aliyepewa kazi na Harrison ya kuyasoma maandishi yaliyokuwa yameandikwa kwenye kidani cha Angel, alifanya kazi yake kwa bidii hasa baada ya kuahidiwa kuwa angepewa fedha za ziada kwa kuikamilisha kazi hiyo. Kwa kutumia mashine maalum iliyokuwa na lenzi kali, sonara huyo alifanikiwa kuyasoma maandishi hayo.
Akachukua kalamu na karatasi na kuyaandika huku akijipongeza kwa kufanikiwa kazi aliyopewa bila kutokwa na jasho. Charlote Abdulkarim Charwe, sonara aliyaandika maneno hayo kwenye karatasi dogo kisha akaendelea na kazi ya kukisafisha kidani hicho huku kichwani akiwaza dau aliloahidiwa na mteja wake.
Baada ya muda, Harrison alimfuata sonara huyo na kumuuliza alikuwa amefikia wapi kwenye kazi aliyompa.
Kazi yako tayari bosi, nipe changu, alisema sonara huyo huku akimkabidhi Harrison kikaratasi kilichokuwa na maandishi yale pamoja na kidani ambacho baada ya kusafishwa, sasa kilikuwa kikingaa kama ndiyo kimetoka dukani.
Ahsante sana, alisema Harrison huku akiingiza mkono mfukoni na kutoa kitita cha fedha, akahesabu kiwango alichokuwa amemuahidi na kumpa. Sonara akachekelea mpaka jino la mwisho likaonekana, akaondoka na kurudi nyumbani kwake huku njia nzima akiwa anakisoma kile kikaratasi na kukirudiarudia.
Alishindwa kuelewa majina yale yalikuwa yanamaanisha nini na yalifikaje kwenye kidani cha mkewe kipenzi. Akawa anayatamka huku akiendelea na safari ya kurudi nyumbani.
Charlote Abdulkarim Charwe, Harrison aliendelea kuyakariri majina hayo huku akipanga kwenda kumuuliza vizuri mkewe kama kuna chochote alichokuwa anakifahamu. Baada ya kufika nyumbani, alipokelewa kwa bashasha na mkewe, wakaingia ndani ambapo Harrison kama kawaida yake, alipitiliza chumbani kwenda kumuangalia mwanaye ambaye alikuwa amelala.
Kuna jambo nataka kukuuliza mke wangu kipenzi.
Jambo gani baba?
Kwanza kidani chako hiki hapa, kimeshasafishwa, alisema Harrison huku akikitoa kidani cha mkewe ambacho sasa kilikuwa kinangaa. Mkewe akamshukuru na kumbusu shavuni, akataka kwenda kujaribu kumvalisha mwanaye aliyekuwa amelala lakini mumewe akamzuia.
Hicho kidani kina maandishi ambayo nimeshindwa kuyaelewa.
Maandishi? Yameandikwaje? aliuliza Angel huku akionesha kushtushwa na kilichosemwa na mumewe.
Harrison akatoa kikaratasi kilichokuwa kimeandikwa; Charlote Abdulkarim Charwe na kumuonesha. Akawa anamuuliza kama anafahamu chochote kuhusu majina hayo. Angel hakuonesha kufahamu chochote, na yeye akawa anashangaa yamefikaje kwenye kidani chake. Waliulizana mambo mengi lakini hakuna aliyekuwa na jibu, Harrison akaamua kuendelea kulifuatilia suala hilo.
Kesho yake kulipopambazuka, Harrison aliondoka na kikaratasi kilichokuwa na majina hayo na kwenda kwenye internet cafe iliyokuwa jirani na wanapoishi. Alipofika, alilipia na kukaa kwenye kompyuta, akaliandika lile jina na kuanza kulitafuta mtandaoni.
Majibu aliyoyapata yalionesha kuwa Abdulkarim Charwe ni daktari anayefanya kazi kwenye Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa jijini Geneva, Uswisi. Aliandika maelezo hayo kwenye karatasi kisha akaondoka na kwenda kazini. Njia nzima akawa anaendelea kujiuliza kuhusu uhusiano uliokuwepo kati ya majina hayo, daktari huyo na mkewe.
Jioni aliporudi nyumbani, alimweleza mkewe alichokigundua kuhusu majina hayo, Angel naye akawa anashangaa kwani hakuwa anaelewa chochote.
***
Linda alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kuiona picha ya Harrison akiwa miongoni mwa watu waliofanyiwa upasuaji wa kubadilisha sura (Plastic Surgery) kwenye Kliniki ya Albert Stein Sanitarium. Akamwambia daktari huyo aivute picha yake jirani ili aione vizuri.
Daktari huyo alitii alichoambiwa, akaivuta na kubonyeza sehemu katika kompyuta ambapo picha mbili zilifunguka, moja ikimuonesha Harrison kabla ya kufanyiwa upasuaji huo na nyingine baada ya kufanyiwa.
Alipoifananisha na ile ya kwenye laptop yake, aligundua zinafanana sana, akawa amepata jibu kuwa Harrison alijibadilisha sura, hali iliyomliza sana Linda mpaka daktari akamshangaa. Aliomba kupewa anuani ya makazi ya Harrison ambapo daktari huyo alimpa bila hiyana.
Linda akachomoa burungutu la dola za Kimarekani kwenye mkoba wake na kumpa Dk. Stein, akaaga na kurudi hotelini kwake huku akilia kwa uchungu kama mtu aliyefikishiwa taarifa za msiba. Alipofika, alijifungia chumbani kwake na kuanza kuitazama karatasi iliyokuwa na anuani ya mahali Harrison alipokuwa anaishi, mpaka namba ya nyumba.
Kulipopambazuka tu, Linda aliwahi kuamka na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye mtaa ambao alikuwa anaishi Harrison kwa kutumia maelekezo ambayo aliyapata kwenye kliniki ya Dk. Stein. Kwa kuhofia kuonekana kabla hajamaliza kazi yake, Linda alivaa kofia kubwa iliyoziba sehemu kubwa ya uso wake.
Akabadili mpaka mwendo wake, akatafuta sehemu iliyojificha na kukaa huku macho yake akiyaelekeza kwenye nyumba aliyoelekezwa kuwa ndipo Harrison anapoishi. Alitaka kuhakikisha kwa macho yake kama ni kweli Harrison alikuwa akiishi kwenye nyumba hiyo.
Pia alitaka kujua alikuwa anaishi na nani. Akiwa amejibanza mahali hapo, Linda alishuhudia mlango ukifunguliwa, mapigo yake ya moyo yakawa yanamuenda kwa kasi kubwa.
Alimuona mwanaume ambaye bila wasiwasi alijua kuwa ni Harrison licha ya kubadili sura. Akawa anamtazama kwa makini huku akimfananisha na picha alizotembea nazo, alizochukua kwenye kliniki ya Dk. Stein. Akawa anamuangalia anafanya nini, akamuona akitoka na nguo kwenye beseni na kuanza kuzianika kwenye kamba zilizokuwa nje ya nyumba.
Alipozitazama vizuri nguo alizokuwa akizianika, aligundua kuwa ni za mtoto, wivu mkali ukamchoma moyoni kwani hicho kilikuwa ni kiashiria kuwa tayari Harrison alikuwa na mtoto.
Ina maana amezaa na yule sokwe? Linda alijiuliza huku akijifuta machozi yaliyokuwa yanaulowanisha uso wake. Baada ya kumaliza kuanika nguo, Harrison alirudi ndani. Hakutoka mpaka muda wa kwenda kazini ulipofika ambapo mkewe alimsindikiza. Wakati wanaagana, wakakumbatiana na kumwagiana mvua ya mabusu, huku Linda akishuhudia.
Moyo wake ulimchoma sana, akawa analia kwa uchungu mithili ya mtu aliyepewa taarifa za msiba. Alisubiri mpaka walipomaliza kuagana, mwanamke huyo akarudi ndani na Harrison akaondoka kuelekea kazini. Linda alitoka mafichoni na kuanza kumfuatilia kwa nyuma akitaka kujua anakofanyia kazi. Harrison hakuwa na taarifa yoyote kuwa kuna mtu anamfuata kwa nyuma.
***
Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu. Maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana, yanapita kama maua yachanuavyo na kunyauka. Wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unapumua, ni vyema basi kufikiria maisha baada ya kifo.
UPENDO wa dhati unazidi kushamiri kwenye ndoa ya Harrison na mkewe Angel baada ya Mungu kuwajalia kupata mtoto wa kwanza, Harvey Junior. Kila mmoja anazidisha mapenzi ya dhati kwa mwenzake. Wakati hayo yakiendelea,
msichana ambaye Harrison alimkimbia siku ya harusi yao, Linda amechachamaa kumfuatilia Harrison mpaka aujue mwisho wake.
Bado anaamini kuwa mwanaume huyo anampenda kwa dhati ila alipitiwa na shetani lakini ipo siku atarudi kwenye maisha yake ili watimize ahadi waliyopeana, ya kufunga ndoa. Hataki kukubali kwamba Harrison anampenda malkia wa masokwe kuliko anavyompenda yeye.
Tayari Linda ameshafika kwenye Mji wa Abbotsford, Canada. Msichana huyo kutoka familia ya kitajiri anagundua kuwa kumbe Harrison alibadilisha sura. Anaanza kumfuatilia kwa karibu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya Harrison kugundua kuwa kati ya majina yaliyokuwa kwenye kidani cha mkewe, mawili ya Abdulkarim Charwe yalikuwa ni ya daktari aliyekuwa anafanya kazi kwenye Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa jijini Geneva, Uswisi, hakuishia hapo. Aliamua
kuendelea kufanya utafiti kimyakimya akitaka kubaini uhusiano uliokuwepo kati ya mkewe, Angel, jina la Charlote na daktari huyo.
Aliamini lazima siri kubwa ya historia ya maisha ya mkewe ilikuwa imejificha kwenye majina hayo kwani kwa siku zote tangu
amfahamu Angel, akiwa kwenye Msitu wa Tongass alikokuwa analindwa na masokwe, hakupata bahati ya kumjua ndugu yake yeyote. Akajiapiza kuwa lazima afuatilie kwa kina, hata ikibidi kusafiri mpaka Geneva, Uswisi na kwenda kuonana na daktari huyo.
Kesho yake, aliendelea kufuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zinamhusu daktari huyo mtandaoni, akafanikiwa kuipata picha yake, akiwa kwenye kongamano la madaktari wa magonjwa ya saratani kwenye makao makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) jijini
Geneva. Baada ya kuichunguza kwa makini picha hiyo, alishtuka baada ya kubaini kuwa daktari huyo ambaye alikuwa ni mweusi, alikuwa akifanana vitu vingi na mkewe.
Lazima atakuwa ni ndugu yake, mbona anafanana naye kiasi hiki? alijisemea Harrison na kumuomba mhudumu wa kituo cha intaneti alichokuwa akiifanyia kazi ile, kui-print picha yake kwenye karatasi kwa ajili ya kuondoka nayo. Hakutaka kumshirikisha mkewe kuhusu suala hilo mpaka apate uhakika, akawa anaendelea na uchunguzi wa kimyakimya.
Wakati anatoka kwenye kituo hicho cha intaneti, alishtuka baada ya kumuona msichana aliyevaa kofia kubwa akijificha kwenye magari yaliyokuwa yameegesha nje ya kituo hicho cha intaneti. Alijaribu kumfuatilia lakini hakupata bahati ya kumuona sura kwani alijificha kwenye magari kisha akatokomea kusikojulikana.
Alijiuliza maswali mengi msichana huyo ni nani na kwa nini alikuwa akimfuatilia lakini hakupata majibu. Kilichomshangaza zaidi ni kwamba alikuwa amevaa kofia kubwa iliyomziba sehemu kubwa ya mwili wake. Alibaki na maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu.
Baada ya kutoka, alienda kazini kwake kuendelea na ratiba zake kama kawaida. Jioni akarudi moja kwa moja mpaka nyumbani kwake na kumweleza mkewe juu ya mtu huyo ambaye ilionesha kuwa alikuwa akimfuatilia.
Atakuwa ni nani?
Hata sijui, yaani hapa nimebaki na maswali mengi kweli kichwani.
Kuwa makini mume wangu, si unajua wewe ndiyo kila kitu kwenye maisha yetu? Tunakupenda na kukutegemea.
Usijali mke wangu, nitajitahidi kuwa makini, alisema Harrison kisha wakaendelea na mazungumzo ya kawaida. Hata hivyo,
Harrison hakumwambia chochote kuhusu hatua aliyokuwa ameifikia kwenye utafiti wake aliokuwa anaendelea kuufanya juu ya majina aliyoyakuta kwenye kidani cha mkewe.
Siku hiyo ilipita, kesho yake akawahi kuamka ambapo alimuandalia mkewe maji ya kuoga pamoja na ya mtoto, pamoja na kupika uji kwa ajili ya mwanaye huyo. Akawaamsha na kumuogesha mtoto kisha akafua nguo alizozichafua mtoto huyo usiku. Baada ya kumaliza kazi hizo, alijiandaa na kuondoka kwenda kazini na kumuacha mkewe na mwanaye wanaendelea kupumzika.
Mume wangu ananipenda mpaka naogopa. Hivi ni mwanaume gani anaweza kuwa anamfanyia yote haya mkewe? akija nitamshauri tutafute msichana wa kutusaidia kazi ili siku chache zijazo na mimi nianze kwenda kazini, aliwaza Angel akiwa amejilaza kitandani, akimnyonyesha mwanaye.
Mumewe aliporudi kutoka kazini, alimuandalia chakula na baada ya kula, alimweleza kuwa anataka kuzungumza naye kuhusu malezi ya mtoto wao. Harrison hakuwa na kipingamizi, akakaa mkao wa kumsikiliza mkewe.
Mume wangu.
Naam mke wangu kipenzi.
Najua unanipenda na unampenda pia mtoto wetu kiasi cha kuwa tayari kufanya chochote. Nafarijika sana lakini kuna jambo nataka nikuombe mume wangu.
Ongea tu mke wangu, nakusikiliza.
Nataka tutafute msichana wa kutusaidia kumlea mtoto wetu kwani nataka mume wangu upumzike, kubwa zaidi na mimi nataka nianze kufanya kazi.
Huoni kwamba mtoto wetu bado mdogo? Kwa nini usiendelee kumlea mke wangu?
Napenda kuendelea kukaa nyumbani lakini hali ya maisha inazidi kuwa ngumu mume wangu. Tafadhali niruhusu, alisema Angel,
Harrison akafikiria kwa muda kisha akakubaliana na mkewe. Wakakubaliana kuwa Linda ndiyo afanye kazi ya kumtafuta msichana wa kuwasaidia kazi.
Alifurahi sana mumewe kukubaliana naye, akamkumbatia na kumbusu kimahaba, wakaendelea kuzungumza mambo yao ya kifamilia mpaka muda wa kulala ulipofika.
***
Baada ya kupata uhakika kuwa aliyemuona alikuwa ni Harrison lakini akiwa amejibadilisha sura, Linda alikaa nje ya kituo cha intaneti alichoingia na kumsubiri mpaka aone mwisho wake. Kikubwa alichotaka kufahamu ni mahali alipokuwa anafanyia kazi ili ajipange vizuri namna ya kumnasa na kumrejesha kwenye mikono yake.
Kwa bahati mbaya, alijisahau alipokuwa amejificha mpaka Harrison alipotoka, ikabidi ageuke nyuma haraka na kwenda kujificha kwenye magari yaliyokuwa yamepaki nje ya kituo hicho. Alipoona anamfuata, ilibidi akimbie kwani hakupenda amtambue wakati bado hajakamilisha kazi yake.
Mpango wake wa kumfuatilia mpaka kazini kwake ukawa umeshindikana kwa muda huo lakini hakutaka kukata tamaa. Jioni alitoka hotelini alikokuwa amefikia na kutembea taratibu mpaka kwenye nyumba aliyokuwa anaishi Harrison. Akajipenyeza kimyakimya mpaka kwenye dirisha la nyumba hiyo na kujificha kwenye maua.
Alikaa hapo mpaka aliposikia Harrison akiingia, akatega sikio na kuanza kusikiliza mazungumzo yao. Roho ilimuuma sana alivyokuwa akisikiliza mazungumzo yao kwani walionesha kuwa walikuwa kwenye mapenzi mazito. Licha ya machozi kumtoka, hakutaka kuondoka, aliendelea kuwasikiliza mpaka walipoanza kuzungumza suala la kumtafuta msichana wa kazi.
Aliposikia kuwa wanatafuta mfanyakazi wa kuwasaidia kumlea mtoto wake, alifurahi sana ndani ya moyo wake, akajua hiyo ndiyo nafasi yake ya pekee ya kumrudisha Harrison kwenye mikono yake. Akaondoka kwa kunyata na kurudi hotelini huku akijipanga kuitumia nafasi hiyo kikamilifu.
Kesho yake asubuhi, aliwahi kwenye Kliniki ya Abbotsford Plastic Surgery kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha sura ili akaombe kufanya kazi ndani ya nyumba ya wanafamilia hao.
***
Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu. Maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana, yanapita kama maua yachanuavyo na kunyauka. Wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unapumua, ni vyema basi kufikiria maisha baada ya kifo.
MAHABA ya dhati yanazidi kushamiri kwenye ndoa ya Harrison na mkewe Angel. Mungu anawajalia kupata mtoto wa kwanza wa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kiume, Harvey Junior, jambo linalozidisha mapenzi. Kila mmoja anaifurahia ndoa na hakuna anayejuta kukutana na mwenzake.
Kupitia kidani alichokuwa amekivaa Angel tangu Harrison amfahamu, wanagundua kuwa kuna majina matatu yameandikwa.
Harrison anakipeleka kwa sonara na kugundua kidani kina majina ya Charlote Abdulkarim Charwe. Anaanza kupeleleza ambapo anagundua kuwa ni daktari nchini Uswisi.
Wakati hayo yakiendelea, Linda amechachamaa kumfuatilia Harrison mpaka aujue mwisho wake na sasa ameshajua mpaka anapoishi, anamfuatilia mitaani bila mwenyewe kujua.
Linda akiwa amejificha nyuma ya nyumba ya Harrison na mkewe, aliwasikia wakijadiliana kuhusu kutafuta msichana wa kuwasaidia kazi za ndani ikiwa ni pamoja na kumlea mtoto wao, Harvery Junior. Baada ya kusikia mazungumzo hayo, Linda alianza kushangilia ndani ya moyo wake kwani alijua hiyo ndiyo nafasi pekee ya kupenya na kuingia kwenye familia hiyo.
Hakutaka kupoteza muda, aliondoka eneo hilo kwa kunyata hadi alipofika mbali, akatimua mbio kurudi hotelini alikokuwa amefikia na kuanza kutafakari njia pekee itakayomuwezesha kuingia ndani ya familia ya Harrison kwa urahisi.
Akili ikamjia kuwa na yeye aende kubadilisha sura kisha akaombe kazi ya uhausigeli ili atimize malengo yake. Kesho yake asubuhi, aliwahi kwenye Kliniki ya Abbotsford Plastic Surgery kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha sura ili akaombe kufanya kazi ndani ya nyumba ya wanafamilia hao.
Baada ya kusubiri kwa muda mapokezi, hatimaye Linda alipata nafasi ya kuingia ndani ya chumba cha daktari aliyekuwa anashughulika na kazi ya kufanya upasuaji wa kubadilisha sura. Akazungumza naye na kuahidi kumpa dau nono endapo ataifanya kazi hiyo ndani ya muda mfupi kadiri awezavyo.
Kwa kuwa daktari alishatangaziwa dau, alikubaliana naye. Akavunja ahadi za wagonjwa waliokuwa wanamsubiri na kuingia ndani ya chumba cha upasuaji, akaanza kazi ya kumbadilisha Linda kama mwenyewe alivyokuwa anataka. Alichagua kuwa na mwonekano wa sura kama walivyo wasichana wa Canada.
Baada ya kazi ngumu iliyochukua zaidi ya saa tatu, upasuaji wa kumbadilisha Linda sura ulikuwa umekamilika. Usingeweza kumtambua kuwa ni yeye kwani alikuwa amebadilika kabisa. Hata hivyo, daktari alimuelewesha kuwa endapo atataka kurejea kwenye mwonekano wake wa zamani, alitakiwa kupaka aina fulani ya mafuta ambayo yangeilainisha plastiki iliyokuwa juu ya ngozi ya uso na kuibandua.
Alimshukuru sana na kama alivyokuwa amemuahidi, alimtolea bunda la noti nyingi za Kimarekani. Baada ya taratibu zote kukamilika, Linda alitoka na kuelekea moja kwa moja kwenye maduka ya nguo ambako alichagua mavazi kama waliyokuwa wanavaa wasichana kutoka familia zenye hali duni nchini Canada.
Aliamini wasichana wanaofanya kazi za uhausigeli lazima watoke kwenye familia masikini hivyo ili kutowashtua Harrison na mkewe, ilikuwa ni lazima na yeye afanye kila kinachowezekana kujifanyisha kama anatoka kwenye familia masikini.
Baada ya kufanya manunuzi ya hapa na pale, alirudi hadi hotelini na kubadilisha nguo zake. Vifaa vyake vyote muhimu akavifungia kwenye kabati, akabeba mfuko mdogo wa plastiki uliokuwa na nguo kadhaa pamoja na vitu vingine vidogovidogo kisha akatoka na kuanza kutembea kwa miguu kuelekea kwenye nyumba aliyokuwa anaishi Harrison na familia yake.
Alipokaribia, alianza kupanga mbinu za kuingilia ndani ya nyumba hiyo, akaona ajifanye ana matatizo makubwa kwenye familia yao, hali iliyomlazimu kusafiri mpaka kwenye mji huo kwa ajili ya kutafuta kazi ili apate chochote cha kuisaidia familia yao.
"Ngo! Ngo! Ngo! Ngo!"
"Karibu," sauti ya mwanamke ilisikika kutoka ndani sambamba na kilio cha mtoto mdogo. Alikuwa ni Angel ambaye alikuwa akimbadilisha mwanaye nepi baada ya kuzichafua alizokuwa amevaa. Baada ya kusikia mlango ukigongwa, alimalizia kumbadilisha mwanaye haraka kisha akatoka kumuangalia mtu aliyekuwa anabisha hodi.
"Karibu! Pita ndani," alisema Angel huku akimkaribisha mgeni wake kwa uchangamfu. Licha ya kumchangamkia sana, mgeni alionesha kupooza, macho yake yakiwa mekundu kama mtu aliyekuwa amelia kwa muda mrefu. Akaingia naye ndani mpaka sebuleni ambapo alimuuliza kama anaweza kumsaidia.
"Samahani dada yangu, nina matatizo makubwa mwenzio. Mama yangu amepooza na inatakiwa fedha nyingi kwa ajili ya kwenda kumtibu. Baba yetu alikufa miaka mingi iliyopita na kutuacha mimi, mdogo wangu mmoja na mama yetu. Naomba unipe kazi yoyote ili nipate fedha za kugharamia matibabu ya mama," alidanganya Linda huku akijikamua machozi.
"Ooh! Pole sana mdogo wangu. Hayo yote ni majaribu ya dunia ambayo inabidi upambane kuyashinda," alisema Angel na kumsogelea msichana huyo, akawa anambembeleza kwa kumpigapiga mgongoni.
"Kwani unaitwa nani?" aliuliza Angel huku akiendelea kumbembeleza msichana huyo. Akilini mwake aliamini kuwa ni kweli alikuwa na shida kubwa iliyohitaji msaada ili kuitatua. Hakufikiria hata kidogo kwamba alikuwa akizungumza na mtu aliyekuwa na lengo moja tu, kumpata Harrison na kumrudisha kwenye himaya yake.
"Naitwa Abigail," Linda alidanganya huku akianza kuchunguza mandhari ya sebule ile.
"Kwani unaweza kufanya kazi gani?"
"Yoyote, hata kukusaidia kumlea mtoto na kufanya kazi zote za ndani."
"Tena imekuwa bahati nzuri sana kwa sababu nilikuwa natafuta msichana wa kunisaidia kumlea mwanangu, nataka kuendelea na kazi lakini sikuwa na mtu wa kumuachia mtoto," alisema Angel huku akionesha furaha aliyokuwa nayo kwa kumpata hausigeli kiulaini.
Alimhakikishia kuwa asiwe na wasiwasi kwani kama ni kazi basi ameipata. Akamwambia atajadiliana na mumewe atakaporudi ili wawe wanamlipa mshahara mzuri utakaomuwezesha kumudu kugharamia matibabu ya mama yake kama alivyoeleza.
Linda ambaye sasa alijitambulisha kwa jina la Abigail, akiwa na mwonekano tofauti kabisa wa sura, alimshukuru Angel mpaka akapiga magoti. Akamuahidi kuwa atakuwa mchapa kazi na atajituma kwa kadiri ya uwezo wake wote. Wawili hao waliendelea na mazungumzo ya hapa na pale, Angel akampa msichana huyo mwanaye ili acheze naye wakati wakimsubiri Harrison arudi kazini.
Ilipofika jioni, Harrison alirejea kutoka kazini akiwa na zawadi mbalimbali kwa ajili ya mkewe na mwanaye. Alipoingia ndani tu, mkewe aliinuka na kumvaa mwilini, wakakumbatiana kwa dakika kadhaa huku wakimwagiana mvua ya mabusu kama ilivyokuwa kawaida yao. Baada ya kumaliza kusalimiana na mkewe, Harrison alimbeba mwanaye na kuanza kumrusharusha kwa upendo.
Mkewe akautumia muda huo kumtambulisha kwa mgeni aliyekuwa amekaa pembeni akishuhudia kila kilichokuwa kinaendelea. Akamtambulisha kuwa ndiyo atakuwa mfanyakazi wao wa ndani.
"Mbona kama una wasiwasi sana?" Harrison alimuuliza msichana huyo wakati akisalimiana naye, muda mfupi baada ya kutambulishwa na mkewe. Alishangaa kumuona akitetemeka huku akilengwalengwa na machozi. Hat hivyo, Harrison alidhani ni hofu ya ugeni ndiyo iliyomfanya awe hivyo.
Walikula chakula cha jioni pamoja kisha wakaenda kumuonesha chumba ambacho atakuwa akikitumia. Baada ya hapo wakaagana, Harrison, mkewe na mtoto wao wakaelekea chumbani kwao wakati msichana huyo naye alianza kujiandaa kulala kwenye chumba chake.
"Lazima nimpate Harrison wangu, hata ikibidi kuua nipo tayari," aliwaza Abigail (Linda) akiwa amejilaza kitandani, mawazo mengi yakipita ndani ya kichwa chake.
***
WAKATI mapenzi kati ya Harrison na Angel yakizidi kupamba moto, wakimshukuru Mungu wao kwa kuwaongezea furaha kwa kuwajalia kupata mtoto mzuri wa kiume, Harvey Junior, kumbe Linda anafanya kila liwezekanalo kuingia kwenye maisha yao.
Baada ya kufanikiwa kufahamu nyumba waliyokuwa wanaishi Harrison na mkewe, jioni moja Linda anaenda nyuma ya nyumba hiyo na kusikiliza mazungumzo ya wanandoa hao. Anasikia wakizungumzia kuhusu kutafuta hausigeli.
Baada ya hapo, Linda anakwenda kujibadilisha sura kisha anarudi hotelini anakoingia bila kuonekana, anachukua baadhi ya vitu vyake na kutoka mpaka nyumbani kwa Harrison. Anaingia kwa gia ya uongo na kufanikiwa kupata kazi ya uhausigeli
Walikula chakula cha jioni pamoja kisha wakaenda kumuonesha chumba ambacho atakuwa akikitumia. Baada ya hapo wakaagana, Harrison, mkewe na mtoto wao wakaelekea chumbani kwao wakati msichana huyo naye alianza kujiandaa kulala kwenye chumba chake.
"Lazima nimpate Harrison wangu, hata ikibidi kuua nipo tayari," aliwaza Abigail (Linda) akiwa amejilaza kitandani, mawazo mengi yakipita ndani ya kichwa chake.
Wakiwa chumbani kwao, Angel na Harrison waliendelea na mazungumzo ya hapa na pale huku wakifanyiana michezo ya kimahaba. Harrison akaamua kuutumia muda huo kuwasilisha mpango maalum aliokuwa ameupanga kichwani mwake, akitaka kufahamu ukweli juu ya maisha ya zamani ya mkewe.
"Mke wangu, nataka kusafiri kwenda Geneva, Uswisi. Tunakwenda kikazi pamoja na wafanyakazi wenzangu wawili," alisema Harrison huku akijaribu kumficha mkewe sababu ya safari yake hiyo ya dharura. Angel alishtuka kusikia taarifa hiyo kutoka kwa mumewe kwani tangu waoane, hakuwahi kusafiri na kwenda mbali naye hata kwa siku moja.
"Mh! Kama ni hivyo tuondoke wote, kwani utakaa siku ngapi?"
"Tunakwenda kukaa siku mbili tu mke wangu, hatuwezi kuondoka wote kwa sababu mtoto wetu bado mdogo, isitoshe tunakwenda kikazi," Harrison alijaribu kumuweka sawa mkewe. Angel aliendelea kumng'ang'ania mumewe kwani kwa jinsi alivyokuwa amemzoea, kukaa mbali naye kwa siku mbili aliona ni sawa na mwaka mzima.
Hata hivyo, baada ya kumbembeleza sana, Angel alikubali kubaki ingawa alilia sana usiku huo mpaka mumewe akamuonea huruma. Mpaka usingizi unampitia, alikuwa akiendelea kulia akiwa kwenye kifua cha mumewe ambacho alikilowanisha kwa machozi na kamasi. Harrison alimuonea sana huruma lakini hakuwa na cha kufanya zaidi ya kushikilia msimamo wake kwani alikuwa akitaka kuufahamu ukweli juu ya asili ya mkewe.
Kwa upande wa Linda, baada ya kuwaza kwa muda mrefu, hatimaye usingizi ulimpitia mpaka asubuhi. Kulipopambazuka tu, yeye ndiye alikuwa wa kwanza kuamka, akaanza kufanya usafi nyumba nzima kisha akaandaa kifungua kinywa. Alipomaliza alienda kumuamsha Angel na kumuomba nguo za mtoto alizozichafua ili akazifue.
"Huyu msichana ana bidii sana na kazi, akiendelea hivi atatufaa sana," alisema Harrison baada ya mkewe kumaliza kumtolea nguo za kufua. Mkewe alimuunga mkono ingawa bado hakuwa na furaha kutokana na mumewe kutaka kusafiri.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walipoamka, kazi zote za ndani zilikuwa tayari zimeshafanywa na Linda ambaye wao walikuwa wakimjua kwa jina la Abigail, Harrison akaenda kuoga na kuwahi kuondoka kwa ajili ya kwenda kujiandaa na safari ambayo ilipangwa iwe siku inayofuatia. Baada ya kumaliza kujiandaa, Harrison alimuaga mkewe kisha akaenda kumuaga Abigail.
Wakati wakiagana, Harrison alipatwa na mshtuko wa ajabu baada ya kusikia sauti ya msichana huyo wa kazi kwani aliifananisha na sauti ya mtu aliyekuwa akimfahamu kwa kina ingawa kwa haraka hakuweza kumkumbuka. Licha ya kujitambulisha kuwa yeye ni raia wa nchi hiyo ya Canada, lafudhi ya matamshi yake ilikuwa ikifanana kwa kiasi kikubwa na Wamarekani, jambo lililomfanya Harrison abaki na viulizo vingi kichwani.
"Mbona umeshtuka? Kuna nini?" mkewe aliyekuwa nyuma yake, alimuuliza baada ya kumuona mumewe akishtuka baada ya kuisikia sauti ya mfanyakazi wao wa ndani.
Linda naye baada ya kugundua kuwa alifanya kosa la kushindwa kuibana sauti yake, alijifanya kuendelea na kazi nyingine, akawaacha Harrison na mkewe wakiendelea kuhojiana.
Hata hivyo, Harrison alijivunga na kuonesha kuwa kila kitu kilikuwa sawa. Akaondoka na kumuacha mkewe akiwa na maswali mengi kichwani mwake. Baada ya kufika kazini, Harrison aliomba ruhusa kuwa ana matatizo ya kifamilia hivyo atasafiri kuelekea Geneva kwa siku mbili. Kutokana na uchapakazi wake, alipewa ruhusa kirahisi. Mawazo juu ya sauti aliyoisikia kutoka kwa hausigeli wao ilizidi kumsumbua kichwani.
Akatoka na kwenda benki kutoa kiwango cha fedha ambacho kitamtosha kwenye safari yake hiyo. Pia akatafuta hati mpya ya kusafiria akitumia jina na sura mpya. Kutokana na kutumia ushawishi wa fedha, kila kitu kilienda kama alivyopanga, baada ya muda mfupi tayari akawa na hati ya kusafiria iliyomtambulisha kuwa raia wa Canada.
Hakutaka kupoteza muda, siku hiyohiyo alianza kutafuta hati ya kusafiria, akaenda mpaka kwenye Ubalozi wa Uswisi. Akafanikiwa kupata viza maalum iitwayo Schengen ambayo ingemuwezesha kusafiri kwa zaidi ya nchi 26 za Jumuiya ya Ulaya na nyinginezo.
Alipokamilisha kila kitu, alikwenda mpaka Uwanja wa Ndege wa Abbotsford ambapo alikata tiketi ya kuelekea Geneva siku inayofuata. Akalipia kabisa kisha akaondoka na kurudi nyumbani kwake kuendelea na maandalizi ya safari hiyo.
Alipofika alipokelewa na mkewe ambaye bado alionesha kuwa na majonzi kwani hakuzoea kukaa mbali na mumewe kipenzi.
Hata hivyo, alijitahidi kumfariji mumewe mpaka akamuelewa. Siku hiyo hawakulala mapema, usiku walikuwa wakizungumza mambo mbalimbali kuhusu mipango yao ya maisha ya baadaye na mtoto wao. Baadaye wakapitiwa na usingizi mpaka kesho yake, kulipokucha tu, Angel alimuandaa mumewe kwa ajili ya safari na alipokuwa tayari, alimsindikiza mpaka uwanja wa ndege.
Wakakumbatiana kimahaba kwa muda wa zaidi ya dakika mbili huku Angel akitokwa na machozi, baadaye wakaagana, Harrison akiwa na mkoba wake mdogo, akaanza kuelekea ndani ya uwanja huo ambapo Angel alimsindikiza kwa macho mpaka alipopotea kwenye upeo wa macho yake. Akaondoka na kurudi nyumbani kwake.
***
Baada ya kuwa na uhakika kuwa Harrison amesafiri, Linda aliona hiyo ndiyo nafasi yake pekee ya kutimiza kile alichokuwa amekipanga. Akajiapiza kuwa Harrison atakaporejea, atawakuta mkewe na mwanaye wakiwa maiti. Roho ya ukatili ilishamjaa na alijiapiza kufanya kila linalowezekana kumrudisha Harrison kwenye mikono yake.
Baada ya Angel kuondoka kuelekea uwanja wa ndege kumsindikiza mumewe, huku nyuma Linda alijiandaa na kuondoka haraka kuelekea kwenye duka la madawa na kemikali lililokuwa jirani. Alipofika kwenye duka lililokuwa jirani, aliomba kuuziwa sumu hatari ya Cyanide. Muuzaji akamwambia kuwa sumu hiyo huwa haiuzwi kiholela mpaka awe na maelekezo maalum yaliyoidhinishwa juu ya matumizi yake.
Alipoona anaanza kumuwekea vipingamizi, Linda aliamua kutumia ushawishi wa fedha kama kawaida yake, akatoa noti kadhaa za dola za Kimarekani na kumpa nje ya malipo ya ununuzi wa sumu hiyo. Muuzaji alipoona fedha hizo, alilegeza msimamo wake na kuamua kumuuzia.
Alipopewa tu, alirudi haraka akiwa na kopo hilo la sumu, akaenda kumchukua mtoto ambaye bado alikuwa amelala, akambeba huku mkono mmoja akiwa ameshika kopo lenye sumu, akaanza kukoroga uji huku akijiandaa kuichanganya sumu hiyo kwenye uji wa mtoto.
***
NDOA ya Harrison na Angel, msichana aliyemhangaikia sana kabla ya kumpata na kumuoa, inazidi kushamiri huku upendo, heshima na maelewano vikizidi kuongezeka kila kukicha.
Upande wa pili, msichana ambaye Harrison alimkimbia siku ya harusi yao, Linda ameamua kulivalia njuga suala la
kutoweka kwa mpenzi wake huyo na baada ya kusomea upelelezi kwa kipindi kirefu na kufuzu, anaanza kumfuatilia hatua kwa hatua akitaka kujua yuko wapi na anafanya nini.
Baada ya kuhangaika sana, hatimaye anaugundua ukweli na sasa amefika hadi mahali Harrison alikokimbilia na msichana wake, malkia wa masokwe. Moyo wake unamuuma sana kugundua kuwa kumbe Harrison alimkimbia kwa sababu ya malkia wa masokwe na hakufa kama alivyoudanganya ulimwengu.
Wakati akiendelea kuwafuatilia wanandoa hao, anawasikia wakizungumzia suala la kutafuta msichana wa kazi. Anaitumia nafasi hiyo kuingia upya kwenye maisha ya Harrison ambapo anaenda kujibadilisha sura kisha anakuja
kuomba kazi. Anakubaliwa bila wenyewe kugundua kuwa wamemkaribisha mtu hatari mno ndani kwao. Baada ya muda anaanza kuandaa mipango ya kulipa kisasi.
Baada ya Angel kumfikisha mumewe uwanja wa ndege, wakiwa kwenye geti la nje walikumbatiana kimahaba kwa muda wa zaidi ya dakika mbili, huku Angel akitokwa na machozi, baadaye wakaagana, Harrison akiwa na mkoba wake mdogo, akaanza kuelekea ndani ya uwanja huo. Angel alimsindikiza kwa macho mpaka alipopotea kwenye upeo wa macho yake.
Harrison alitembea huku akigeukageuka nyuma mpaka alipozamia ndani ya uwanja wa ndege, akajipanga sehemu ya lango la ndani la kuingilia kisha utaratibu wa ukaguzi kwa abiria ukaanza kama kawaida. Ilipofika zamu yake, alikaguliwa na kila kitu kikaonekana kipo sawa, akaruhusiwa kuingia mpaka mahali ndege ilipokuwa imeegeshwa.
Akapanda na kwenda kukaa kwenye siti yake. Bado mawazo mengi yalikuwa yakiutesa mtima wake juu ya asili ya Angel. Japokuwa kwa mara ya kwanza alimkuta kwenye Msitu wa Tongass akiwa analelewa na kundi kubwa la masokwe, aliamini hakuna uwezekano wowote wa sokwe kuzaa binadamu hivyo akawa na matumaini makubwa kuwa lazima ataufahamu ukweli wake.
Penzi la dhati alilokuwa nalo kwa Angel ndiyo lililomsukuma kufanya kila linalowezekana ili aijue asili, ndugu na kila kitu kilichokuwa kinamhusu mwanamke huyo ambaye alikuwa akimpenda kuliko kitu kingine chochote kwenye maisha yake.
Aliamini mtu pekee anayeweza kumfumbulia fumbo kubwa lililokuwa limejificha kwenye maisha ya mkewe, ni Abdulkarim Charwe ambaye jina lake alilikuta kwenye kidani cha mkewe ambacho kwa maelezo yake, tangu anapata akili alijikuta tayari anacho mwilini mwake.
Aliamini lazima Abdulkarim Charwe anafahamu ukweli wa maisha ya mkewe na hiyo ndiyo sababu kubwa iliyomfanya apige moyo konde na kusafiri kutoka Abbotsford, Canada yalikokuwa makazi yake na familia yake mpaka Geneva, Uswisi.
Kilichomsukuma kuamini kuwa Abdulkarim anaishi Geneva ni baada ya kulitafuta jina lake kwenye mtandao wa intaneti na kugundua kuwa mtu huyo alikuwa ni daktari katika Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) jijini Geneva, Uswisi.
Wakati mawazo mengi yakizidi kupita ndani ya kichwa chake, alisikia sauti kutoka kwenye vipaza sauti vilivyokuwa ndani ya ndege hiyo ikiwataarifu abiria wote kufunga mikanda kwani ndege ilikuwa ikijiandaa kuruka. Yeye pamoja na abiria wengine wote walitii agizo hilo, ndege ikaanza kujongea taratibu kuelekea kwenye njia za kurukia (runways).
Ikaanza kuongeza kasi huku muungurumo wa injini nao ukizidi kuwa mkubwa, ikaondoka na kuongeza kasi kwa kadiri ilivyokuwa inasonga mbele mpaka ilipoanza kuinuka upande wa mbele. Akajua tayari ndege ilikuwa angani, akawa anamuomba Mungu wake amuwezeshe kukamilisha kazi kubwa iliyokuwa mbele yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kusafiri angani kwa saa nyingi, hatimaye ndege ya Swiss Air aliyokuwa ameipanda Harrison ikawasili jijini Geneva, Uswisi. Baada ya kutua uwanjani, Harrison na abiria wengine waliteremka na kufuata taratibu za kawaida kwenye viwanja vya ndege vya kimataifa.
Baada ya kukamilisha kila kitu, alitoka na kukodi teksi, akamuelewesha dereva kumpeleka kwenye ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani. Safari ikaanza huku Harrison akijaribu kupangilia vizuri maelezo yake ili akifika kwenye ofisi hizo asibabaike. Baada ya muda, teksi iliwasili kwenye jengo refu la kisasa lililokuwa na mandhari ya kuvutia, likiwa limepambwa kwa bustani nzuri za maua pande zote.
Dereva teksi akaliingiza gari mpaka kwenye maegesho na kumwambia Harrison kuwa wamefika, akamlipa fedha zake kisha akateremka na kuanza kutembea kwa hofu kuelekea kwenye lango la kuingilia kwenye ofisi hizo. Alipofika getini, alisimamishwa na walinzi na
kukaguliwa kisha akaulizwa shida yake. Baada ya kujieleza, Harrison alielekezwa aende mpaka sehemu ya mapokezi.
Alipofika hapo, pia alijitambulisha na kueleza kilichompeleka, akaelekezwa kwenda kwenye ofisi ya Inquiries Department ambayo ndiyo ilikuwa ikihusika na maulizo ya taarifa mbalimbali za watumishi wa shirika hilo.
Umesema anaitwa nani?
Abdulkarim Charwe, Harrison alijibu kwa kusitasita wakati akizungumza na mwanamke wa makamo aliyekuwa amekaa nyuma ya
kompyuta ya kisasa. Baada ya kutaja jina hilo, mwanamke huyo wa Kizungu aliandika kitu kwenye kompyuta yake kisha akasubiri kwa sekunde chache.
Baada ya kusoma maelezo fulani, aliteremsha miwani yake na kumtazama Harrison kwa kumkazia macho.
Umesema ni nani yako?
Ni ndugu yangu, alijibu Harrison huku akionesha kutokuwa na uhakika na majibu yake.
***
Baada ya Angel kumsindikiza mumewe mpaka Uwanja wa Ndege, awali alitaka kurudi mpaka nyumbani lakini akiwa njiani alikumbuka
kitu. Alikumbuka kuwa walikubaliana na mumewe kuwa aende kazini kwake na kuzungumza na mabosi wake kuhusu kurejea kazini kabla hata ya kumalizika kwa likizo yake ya uzazi. Aliamini baada ya kumpata msichana wa kazi, Abigail (Linda) sasa atakuwa na uwezo wa kuendelea na kazi bila matatizo.
Alipitia kazini kwake na kuwapa taarifa viongozi wake ambao kwanza walimpongeza kwa kujifungua salama mtoto wa kiume, Harvey Junior lakini pia walimpongeza kwa moyo wa kujituma na kupenda kazi aliokuwa nao kiasi cha kuamua kurejea kazini kabla ya likizo yake ya uzazi kumalizika. Walimkubalia na kuahidi kumuongeza nusu ya mshahara wake kwa moyo wa kujituma aliouonesha.
Baada ya kukamilisha taratibu zote muhimu, alikodi teksi na kurudi mpaka nyumbani kwake. Kabla hata hajaingia ndani, alipokelewa na sauti ya kilio cha mwanaye aliyekuwa akilia kwa nguvu. Hakuna kitu alichokuwa hakipendi kama kumsikia mwanaye huyo akilia bila sababu ya msingi, tena bila kubembelezwa.
Akamlipa dereva fedha zake na kuteremka. Akawa anatembea kwa kasi kuelekea ndani. Alipofika mlangoni, alijaribu kuusukuma mlango lakini ulikuwa umefungwa kwa ndani.
Akagonga kwa nguvu lakini hakuitikiwa, sauti ya mwanaye akilia ikawa inazidi kuongezeka, hali iliyomuumiza moyo wake kupita kiasi. Akawa anaugonga mlango kwa nguvu huku akiliita jina la hausigeli wake. Alipoona kimya, alitoa simu yake ya kiganjani na kuanza kupiga namba ya mfanyakazi huyo, simu ikawa inaita bila kupokelewa.
Alipoona mtoto anazidi kulia kwa sauti kubwa, alianza kutafuta namna ya kuuvunja mlango, akawa anautingisha kwa nguvu lakini kutokana na uimara wa mlango, hakuweza kufanya chochote. Akajikuta na yeye akianza kutokwa na machozi, akaanza kuomba msaada kwa majirani kumsaidia kuvunja mlango kwani hakujua nini kilichomtokea mtoto wake mpaka afikie hatua ya kulia kwa nguvu kiasi kile.
Baada ya kupiga kelele za kuomba msaada, majirani kadhaa walikusanyika na kuanza kumuuliza kulikoni. Wakawa wanamtuliza kuwa asiwe na wasiwasi kwani ni kawaida ya watoto kulia hasa wanapokuwa mbali na mama zao. Licha ya kila mtu kujaribu kumtuliza, bado moyo wake haukutulia, akawaomba majirani wamsaidie kuvunja mlango.
***
WAKATI furaha ya Harrison na mkewe Angel ya kupata mtoto kwenye ndoa yao ikiwa inaendelea, matatizo makubwa yanaanza kuinyemelea familia hiyo. Msichana ambaye Harrison alimkimbia siku ya harusi yao, Linda ameamua kulivalia njuga suala la kutoweka kwa mpenzi wake huyo.
Baada ya kusomea upelelezi kwa kipindi kirefu na kufuzu, anaanza kumfuatilia hatua kwa hatua akitaka kujua yuko wapi na anafanya nini. Hatimaye anaugundua ukweli kuwa mwanaume huyo aliyekuwa anampenda kuliko kitu chochote, hakufa bali alimkimbia na kwenda kumuoa malkia wa masokwe ambaye sasa anaishi naye kama mkewe, akiwa amebadilisha sura na jina.
Moyo wake unamuuma sana na anajiapiza kuhakikisha analipa kisasi kwa kuwapoteza Angel na mwanaye. Anatumia mbinu kali na kufanikiwa kuingia kwenye familia hiyo akiwa kama hausigeli. Harrison anasafiri kwenda Uswisi kuwafuatilia ndugu wa mkewe bila kumwambia ukweli. Akiwa safarini, huku nyuma Linda anataka kuitumia nafasi hiyo kutimiza lengo lake.
Baada ya Harrison kuwasili kwenye Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO), Geneva, Uswisi alijitambulisha mapokezi na kueleza shida yake. Akaelekezwa aende kwenye Idara ya Maulizo (Inquiries Department) ambayo ndiyo ilikuwa ikihusika na maulizo ya taarifa mbalimbali za watumishi wa shirika hilo.
Baada ya kufika kwenye ofisi hiyo, Harrison alijitambulisha tena na kueleza shida yake, mwanamke wa makamo, Mzungu aliyekuwa amekaa nyuma ya kompyuta ya kisasa akajaribu kupekua kompyuta yake na baada ya muda akamgeukia Harrison na kumuuliza uhusiano uliokuwepo kati yake na mtu aliyekuwa anamuulizia.
Harrison alijibu kuwa ni ndugu yake, yule mwanamke akashusha pumzi ndefu na kujiweka vizuri kwenye kiti chake. Akaanza kumueleza kuwa ni kweli kwamba Dk. Abdulkarim Charwe amewahi kufanya kazi kwenye ofisi hizo lakini baadaye walilazimika kumsafirisha na kumrudisha kwao Tanzania kutokana na matatizo ya kiafya yaliyokuwa yanamsumbua.
"Baada ya mkewe na mwanaye mdogo kupata ajali ya ndege na kufa, Charwe alishindwa kuukubali ukweli, muda wote akawa analia mwenyewe kwa huzuni, hali iliyopunguza ufanisi wake kazini," alisema mwanamke huyo wa Kizungu.
Akaendelea kueleza kuwa kutokana na uchungu wa kuipoteza familia yake, Dk. Charwe alianza ulevi wa kupindukia akiamini kuwa anapunguza mawazo lakini haikumsaidia kitu. Baadaye akaanza kuumwa maradhi ya hapa na pale na baada ya kufanyiwa utafiti wa kina, ikabainika kuwa anasumbuliwa na msongo mkali wa mawazo ambao pia ulimsababishia huzuni kali, ‘mental depression'.
"Tulijitahidi kumsaidia kwa kadiri ya uwezo wetu lakini bado alishindwa kuhimili maumivu ya kuipoteza familia yake. Siku moja akiwa chooni, alianguka na kupoteza fahamu. Akakimbizwa hospitali na kutibiwa na madaktari wenye uwezo mkubwa, aliporejewa na fahamu, alipatwa na ‘stroke', akaparalaizi mwili mzima," alisema mwanamke huyo wa Kizungu huku akilengwalengwa na machozi.
Taarifa ile ilikuwa mbaya kwa Harrison kwani alijikuta akigonga mwamba. Hata hivyo, alipata mwanga fulani katika maelezo hayo. Akaanza kumdadisi mambo mbalimbali mwanamke huyo. Maelezo yote aliyokuwa anapewa alikuwa akiyaandika kwenye kitabu chake maalum.
Akatajiwa mpaka kampuni ambayo ndege yake ndiyo waliyosafiria mke wa Dk. Charwe na mwanaye kabla ya kupata ajali na kusababisha wafikwe na mauti. Pia alimuuliza kuhusu sehemu aliyorudishwa daktari huyo baada ya kuparalaizi. Akaambiwa kuwa Charwe alikuwa mwenyeji wa Bukoba, Tanzania na huko ndiko alikorudishwa.
Baada ya kuridhishwa na maelezo aliyopewa, Harrison aliaga na kuondoka huku akiendelea kujiuliza maswali mengi ndani ya kichwa chake. Alishaanza kupata picha ya historia ya mkewe. Aliamini endapo ataendelea kulifuatilia suala hilo kwa karibu, siku si nyingi ataugundua ukweli wa historia ya mkewe, jambo alilokuwa analisubiri kwa hamu kubwa.
Alirudi mpaka kwenye hoteli aliyokuwa amefikia na kuanza kutafakari namna ya kuendelea na uchunguzi wake.
***
Baada ya kufanikiwa kuipata sumu hatari ya Cyanide, Linda ambaye sasa alikuwa akijiita Abigail, alirudi nayo mpaka nyumbani kwa Harrison. Akamchukua mtoto na kuanza kumkorogea uji ambao alipanga kuuchanganya na sumu hiyo.
Akiwa anaendelea kukoroga, alikumbuka maelezo ya muuzaji kuwa sumu hiyo ina uwezo wa kuua ndani ya sekunde chache lakini endapo atahitaji sumu nyingine yenye uwezo wa kuua baada ya siku kadhaa, pia ilikuwa ikipatikana.
Akili ikamcheza haraka, akaona endapo angemkorogea sumu hiyo mtoto kwenye uji, tafsiri yake ni kwamba angekufa kabla hata mama yake hajarudi. Hata hivyo, malengo yake yalikuwa ni kuwaua wote wawili hivyo akajua endapo atarudi na kumkuta mwanaye amekufa, lazima atachanganyikiwa na kujaza watu nyumbani hapo hivyo kukwamisha mpango wake wa kuwaua wote wawili.
Ghafla akapata wazo la kurudi dukani na kwenda kubadilisha sumu ili apewe yenye uwezo wa kuua baada ya siku kadhaa. Baada ya kupata wazo hilo, alienda kumlaza mtoto chumbani kwake, akazima jiko na kuutoa uji jikoni, akatoka mbiombio na kurudi dukani alikouziwa ile sumu.
Kwa bahati mbaya kwake, alipofika dukani, muuzaji aliyemuuzia mara ya kwanza alikuwa ametoka kwenda kupata kifungua kinywa na kumuacha msaidizi wake. Linda alipojaribu kumueleza msaidizi wake kile alichokuwa anakitaka akamwambia amsubiri mwenyewe kwani yeye hakuwa na mamlaka ya kumsaidia. Ilimlazimu Linda kukaa na kumsubiri. Hata hivyo, hakurudi haraka kama alivyotegemea.
Wakati akiendelea kusubiri, upande wa pili Angel alishamaliza mizunguko yake na kurudi nyumbani. Ndipo alipokutana na hali iliyomtia wasiwasi mkubwa baada ya kusikia mwanaye analia kwa nguvu akiwa ndani. Baada ya kuwakusanya majirani , walisaidiana kuuvunja mlango.
Walipofanikiwa tu, Angel ndiyo alikuwa wa kwanza kuingia ndani, akakimbilia mpaka mahali sauti ya mwanaye ilipokuwa inatokea, kwenye chumba cha msichana wao wa kazi. Alipomfikia, alimbeba haraka na kuanza kumuangalia kama yupo salama. Haraka akamtolea ziwa na kuanza kumnyonyesha, mtoto akanyamaza.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Majirani waliingia na walipokuta mtoto yupo salama, waliaga na kuanza kuondoka mmojammoja huku wengine wakimcheka Angel kwa jinsi alivyokuwa na presha na mwanaye.
"Ni mtoto wake wa kwanza ndiyo maana ana presha kiasi hicho, siyo kosa lake," mwanamke mmoja alisema na kuungwa mkono na wenzake. Angel hakujali, akawa anaendelea kumnyonyesha mwanaye huku akizunguka kwenye vyumba vyote kukagua usalama.
Alijiuliza mahali alipokwenda hausigeli wake, tena bila kuaga na kumuacha mtoto akilia peke yake lakini hakupata majibu. Akapanga kuwa akirudi ampe onyo kali na endapo atarudia tena mchezo huo, atajua namna ya kumuadabisha.
Kule dukani, baada ya kusubiri sana, hatimaye muuzaji alirejea na kumkuta Linda akimsubiri. Alipomueleza alichokuwa anakitaka, alimtaka kuongeza fedha kwani sumu aliyokuwa anaitaka yeye ilikuwa ikiuzwa bei kubwa kuliko ile ya awali. Kwa kuwa Linda alidhamiria kweli, alitoa fedha na kuongeza.
Akapewa sumu hiyo ambayo tofauti na ile ya awali, ilikuwa kwenye mfumo wa vidonge vidogo vyenye rangi ya dhahabu. Baada ya kupewa, alitoka haraka na kuanza kukimbia kurudi nyumbani kwani alikuwa na wasiwasi kuwa mtoto atakuwa analia sana. Alipokaribia, alishtuka mno kuona mlango umefunguliwa wakati yeye aliufunga na funguo alikuwa nazo mkononi. Akiwa bado ameduwaa, alishtuka kumuona Angel akitoka huku akiwa amembeba mwanaye aliyekuwa anaendelea kunyonya.
"Ulikuwa wapi?" Angel aliuliza kwa ukali, Abigail (Linda) akawa anajiumauma na kukosa majibu.
***
HARRISON ameiacha familia yake na kusafiri kwenda jijini Geneva, Uswisi kufanya utafiti wa kina kuhusu asili ya mkewe, Angel. Jina la Charlotte Abdulkarim Charwe alilolikuta kwenye kidani cha mkewe ndiyo lililompa mwanga wa wapi pa kuanzia. Baada ya kutafuta mtandaoni, anagundua kuwa Abdulkarim Charwe ni daktari anayefanya
kazi kwenye Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) jijini Geneva, Uswisi.
Baada ya kuondoka, huku nyuma familia yake inaingia kwenye msukosuko mkubwa. Linda ambaye alifanya upasuaji wa kubad
ilisha sura (plastic surgery), anafanikiwa kuingia kwenye familia hiyo akijifanya ni hausigeli.
Baada ya kuingia kwenye familia hiyo, Linda anaanza kufanya mipango ya kumuua Angel na mwanaye kwani
aliwaona kama kikwazo kwenye maisha yake, akawa anaamini kuwa akiwaondoa duniani atapata fursa nzuri ya kuwa na mwanaume wa maisha yake, Harrison. Anataka kuwaua wote wawili kwa sumu.
Baada ya kutoka dukani, Abigail (Linda) alishtuka mno kuona mlango umefunguliwa wakati yeye aliufunga na funguo alikuwa nazo mkononi. Akiwa bado ameduwaa, alishtuka kumuona Angel akitoka huku akiwa amembeba mwanaye aliyekuwa anaendelea kunyonya.
Ulikuwa wapi? Angel aliuliza kwa ukali, Abigail akawa anajiumauma na kukosa majibu.
Nilikuwa nimeenda dukani, najisikia vibaya kwa hiyo niliendaa kununua dawa.
Unaumwa nini na kwa nini hukunipigia simu kunipa taarifa?
Samahani bosi, nisamehe sitarudia tena alisema Abigail huku akipiga magoti mbele ya Angel aliyekuwa amefura kwa hasira. Kutokana na roho yake ya upole na huruma, Angel alimsamehe kirahisi, akamwambia siku nyingine akirudia atamfukuza kazi.
Abigail alijifanya msikivu, akawa anasikiliza kila kitu na kukiri makosa yake. Aliposamehewa, harakaharaka aliingia mpaka chumbani kwake na kujifungia mlango.
Mapigo ya moyo wake yakawa yanamuenda mbio kutokana na hofu aliyokuwa nayo. Alipohakikisha amejifungia na hakuna mtu mwingine anayemuona, alitoa vidonge vya sumu alivyovinunua na kuvificha chini ya godoro, akalala kitandani na kuanza kutafakari nini cha kufanya.
Lazima nikuue Angel! Wewe na mwanao lazima muondoke duniani ili nipate nafasi ya kuishi na mwanaume wa maisha yangu, Harrison! Nampenda sana na nipo tayari kufanya chochote ili nimpate, Abigail aliwaza akiwa amelala kitandani, akawa anaendelea kupanga mikakati ya namna ya kutekeleza mpango wake.
Angel alienda kumtafuta fundi wa kutengeneza mlango, kazi hiyo ilipofanyika akaendelea na shughuli zake za nyumbani huku akiwa amembeba mwanaye. Tayari alishamsamehe Abigail na hakuendelea tena kumfikiria. Muda ukawa unazidi kuyoyoma huku Abigail akiwa bado amejifungia chumbani kwake.
Nikaiweke hii sumu kwenye maji ya kunywa au kwenye vyakula? Abigail alijiuliza kichwani, akapata wazo la kwenda kuiweka sumu hiyo kwenye mboga zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye jokofu pamoja na kwenye maziwa ya mtoto. Alikuwa na uhakika kuwa vyovyote itakavyokuwa, lazima Angel atapika na kula mboga hiyo na vilevile lazima atampa mwanaye maziwa.
Alipopata wazo hilo, harakaharaka aliinuka na kuchukua vidonge viwili vya sumu, akavificha kwenye mfuko wa nguo aliyokuwa ameivaa na kutoka mpaka sebuleni alikomkuta Angel akiendelea na shughuli zake kama kawaida.
Naomba nikusaidie kazi mama.
We nenda kapumzike tu, nitafanya kila kitu mimi mwenyewe, Angel alimjibu hausigeli huyo, akaendelea na shughuli zake za kawaida. Abigail hakutaka kurudi chumbani, akakaa kwenye kochi huku akitafuta nafasi ya kufanya alichokuwa amekipanga.
Hata hivyo, hakupata nafasi hiyo kwa urahisi kwani Angel hakutoka nje hata mara moja wala kuondoka sebuleni hapo mpaka alipomaliza kuandaa chakula. Alipomaliza, alienda chumbani kwake kumuamsha mtoto wake, Abigail akaona hiyo ndiyo nafasi yake ya kutimiza lengo lake.
***
Baada ya Harrison kupata taarifa zote muhimu alizokuwa akizihitaji kuhusu Abdulkarim Charwe, alirudi hotelini na kuanza kutafakari nini cha kufanya. Wazo pekee aliloona linafaa zaidi, ilikuwa ni kwenda mpaka kwenye shirika la ndege ambayo ndiyo mke na mtoto wa Charwe walisafiria kabla ya kupata ajali na kufa.
Alihitaji kufahamu vizuri taarifa zao ikiwa ni pamoja na majina yao kamili, eneo ajali ilipotokea na kama kuna taarifa nyingine zozote zinazoweza kumsaidia. Hakutaka kupoteza muda, akafunga safari mpaka kwenye Shirika la Ndege la Lufthansa ambalo aliambiwa kuwa ndiyo lililokuwa linamiliki ndege ya Herpa Lufthansa Premium iliyopata ajali na kusababisha maafa makubwa.
Baada ya kufika kwenye ofisi za shirika hilo, Harrison alijitambulisha na kueleza shida yake. Bila hiyana, alielekezwa mpaka kwa meneja wa shirika hilo aliyempokea kwa ukarimu na kumueleza kila kitu kuhusiana na ajali hiyo ambayo bado ilikuwa kwenye vichwa vya wengi kutokana na maafa iliyoyasababisha.
Meneja huyo alianza kumueleza upya, akamfafanulia kuwa ndege iliyopata ajali, Herpa Lufthansa Premium ilipoteza uelekeo ikiwa angani baada ya kuzidiwa na ukungu ikiwa safarini kuelekea Geneva, Uswisi.
Kwani ajali yenyewe ilitokea wapi?
Ilitokea kwenye mpaka kati ya Marekani na Canada, kwenye msitu mkubwa wa Tongass, alijibu meneja huyo, kauli iliyomshtua mno Harrison.
Kijana mbona umeshtuka sana? Kuna tatizo?
Ha hapana, alijibu Harrison kwa kubabaika, mshangao alioupata haukujificha. Akaomba kupewa orodha ya wasafiri waliokuwa ndani ya ndege siku hiyo. Meneja huyo akatafuta kwenye kompyuta kisha aka-print na kumpa karatasi lenye majina ya wasafiri wote Harrison.
Wakati anapitia, alikutana na majina mawili ya watu waliokuwa wamekaa siti moja siku hiyo. Macho yake yakaganda hapo, akayatazama majina hayo huku akiwa amekodoa macho, kijasho chembamba kikimtoka.
Anganile Charwe, Charlotte Charwe, Harrison aliyataja majina hayo kwa sauti ya juu, meneja akamfafanulia kuwa hao walikuwa ni mwanamke na mwanaye mdogo aliyekuwa na umri usiozidi miaka mitatu. Akamfafanulia kuwa wote walikufa kwenye ajali hiyo.
Kengele ililia ndani ya kichwa cha Harrison, akajaribu kuunganisha matukio. Kidani alichokikuta kwa mkewe kilikuwa na jina lililosomeka Charlotte Abdulkarim Charwe, jina ambalo ndiyo aliloliona katika orodha ya wasafiri waliokuwa ndani ya ndege siku hiyo. Pia alipotafakari kuwa kwa kipindi hicho Charlotte alikuwa na miaka isiyozidi mitatu, alipatwa na hisia kuwa huenda ndiyo mkewe.
Naweza kupata picha za hawa watu wawili?
Picha zao zipo lakini hazina ubora kwani zilichukuliwa kutoka kwenye nakala ya hati zao za kusafiria.
Naomba nizione hivyohivyo, alisema Harrison akiwa na shauku kubwa ya kuhakikisha kama anachohisi ni cha kweli. Baada ya kupekuapekua kwenye kompyuta yake kwa dakika kadhaa, meneja huyo alizipata na kumuonesha Harrison. Hakuwa amekosea, alichokihisi ndiyo ulikuwa ukweli.
Japokuwa Charlotte alikuwa bado mdogo lakini sura yake haikubadilika sana, Harrison hakuhitaji kuvaa miwani kutambua kuwa Charlotte aliyedhaniwa kufa kwenye ajali ndiyo Angel, mkewe kipenzi. Alishusha pumzi ndefu na baada ya kupata uhakika huo, aliaga na kuondoka huku mawazo mengi yakiendelea kupita ndani ya kichwa chake.
Jambo aliloona linafaa kwa wakati huo, ilikuwa ni kumtafuta mzee Abdulkarim Charwe kwa udi na uvumba mpaka ampate na kumuunganisha na mwanaye. Alirudi hotelini na kuanza kujiandaa kwa safari ya kurudi nyumbani huku akiwa na shauku kubwa ya kumweleza mkewe juu ya utafiti wake na alichokigundua. Hakutaka kulala siku hiyo, akakabidhi chumba na kuondoka kuelekea uwanja wa ndege.
***
BAADA ya Harrison kuiacha familia yake na kusafiri kwenda jijini Geneva, Uswisi kutafuta ukweli juu ya asili ya mkewe, Angel, huku nyuma tatizo kubwa linakaribia kutokea.
Linda, msichana aliyekimbiwa na Harrison siku ya harusi yao, anafanya upasuaji wa kubadilisha sura (plastic surgery) na kuwa na mwonekano wa tofauti kisha anafanikiwa kuingia kwenye familia hiyo akijifanya ni hausigeli. Baada ya kuipata nafasi hiyo, anaanza kuumiza kichwa juu ya namna ya kuisambaratisha familia hiyo.
Anaenda kununua sumu hatari ya Cyanide kwa ajili ya kumuua Angel na mwanaye lakini baada ya kufikiria sana, anaamua kubadilisha sumu hiyo. Anapewa vidonge maalum vya sumu nyingine ambavyo baada ya kuingia ndani ya mwili, humuua mhusika taratibu. Anarudi na vidonge hivyo vya sumu na kuanza kumtegea Angel akizubaa amchanganyie kwenye chakula na hatimaye anafanikiwa.
Baada ya Harrison kupata vielelezo na uthibitisho aliokuwa anautaka jijini Geneva, Uswisi alijiambia ndani ya nafsi yake kuwa jambo pekee linalofaa baada ya kuyafahamu yote hayo, ni kutafuta muda wa kutosha na kufunga safari mpaka nchini Tanzania kumtafuta mzee Abdulkarim Charwe. Alijiapiza kuwa atafanya kila liwezekanalo mpaka ampate mzee huyo na kumuunganisha na mwanaye.
Harakaharaka alirudi Alirudi hotelini na kuanza kujiandaa kwa safari ya kurudi nyumbani huku akiwa na shauku kubwa ya kumweleza mkewe juu ya utafiti wake na alichokigundua. Hakutaka kulala siku hiyo, akakabidhi chumba na kuondoka kuelekea uwanja wa ndege.
"Haloo mke wangu!"
"Haloo baba!"
"Nipo njiani naenda uwanja wa ndege mama, muda si mrefu nitapanda ndege na kurudi nyumbani."
"Oooh! Usiniambie mume wangu? Yaani kwa jinsi nilivyokukumbuka sitakula wala kufanya chochote mpaka utakaporudi mume wangu," alisema Angel kwa furaha, mumewe alipokata simu, alimbeba mwanaye na kwenda naye sebuleni.
Muda huo, tayari Abigail alikuwa ameshafanya alichokikusudia kwa kuchanganya sumu kwenye chakula alichokuwa amekipika Angel na kwenye uji wa mtoto, akawa anasubiri kwa shauku kuona jinsi maadui zake hao wanavyoianza safari ya kifo. Baada ya kufanya ushetani huo, Abigail alirudi kwenye kiti chake na kutulia kimya utadhani hakuna kilichotokea.
Akiwa katika hali hiyo, akamuona Angel akitoka chumbani akiwa na mwanaye, usoni akiwa amejawa na tabasamu pana.
"Mbona umefurahi sana mama?" aliuliza kwa sauti ya kutetemeka.
"Mume wangu kanipigia simu kasema anaelekea uwanja wa ndege, yaani jinsi nilivyommisi sitafanya chochote mpaka atakaporudi," alisema Angel huku akishindwa kuificha furaha yake. Kauli hiyo ilimshtua mno Abigail, akajikaza na kuuliza tena.
"Kwa hiyo hutakula mpaka arudi? Kwa nini usile hata kidogo? Utakaa na njaa kwa muda wote huo?"
"Wala usijali, nitamsubiri tu kwani yeye ni muhimu kuliko hata chakula. Isitoshe kwa usafiri wa ndege hatachukua muda mrefu atakuwa tayari ameshafika."
"Basi njoo nikusaidie kumnywesha mtoto uji wake," alisema Abigail huku akiinuka na kumsogelea Angel ili ampe mtoto lakini akamkatalia. Akamwambia hata yeye hatamnywesha uji wala kufanya chochote mpaka baba yake atakaporudi. Kauli hiyo ilionekana kumvunja nguvu Abigail, akarudi kukaa kwenye kiti chake huku akionesha kuwa na mawazo mengi kichwani.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Angel akawasha runinga na kuanza kuangalia kipindi alichokuwa anakipenda kupitia chaneli maarufu nchini humo ya BET. Akawa anatazama runinga huku shauku ya kumsubiri mumewe ikizidi kuongezeka kwa kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.
Mawazo yalizidi kumtesa Abigail, akawa anajiuliza itakuwaje endapo Harrison akirudi na kutaka kula chakula kile alichokitia sumu pamoja na mkewe? Alijikuta akishindwa kuelewa nini cha kufanya, akainuka na kwenda chumbani kwake kutafakari kwa kina.
"Harrison naye akila si atakufa? Sasa ndiyo nitakuwa nimefanya nini?" alijiuliza Abigail huku akizungukazunguka chumbani kwake. Alitamani utokee muujiza Harrison aahirishe safari yake lakini hilo halikuwezekana. Pia alitamani angekuwa bado hajaichanganya sumu hiyo kwenye chakula ili asubiri mpaka atakapopata nafasi nzuri lakini pia haikuwezekana.
Akawa anaendelea kuzungukazunguka chumbani kwake kama mtu aliyechanganyikiwa. Bado hakupata jibu la nini cha kufanya. Muda ulizidi kuyoyoma akiwa bado anababaika, mara akamsikia Angel akizungumza na simu. Harakaharaka alitoka mpaka sebuleni kwa lengo la kusikiliza alikuwa anazungumza na nani.
Alipogundua kuwa Angel hakuwa anazungumza na mumewe, kidogo hofu ilimshuka, akarudi chumbani kwake kuendelea kupanga nini cha kufanya ili kuepusha hatari kubwa iliyokuwa inataka kumpata Harrison.
"Abigail! Abigail!" aliita Angel, msichana huyo akatoka na kwenda kumsikiliza.
"Pakua chakula uanze kula kwani muda unaenda na kama nilivyokwambia mimi nitamsubiri mume wangu mpaka arudi," alisema Angel huku akimuonesha msichana huyo mahali alipokuwa amehifadhi chakula. Abigail alijishauri kama akubali au la, akaona njia pekee ni kujifanya kama anapakua chakula ili kutomtia wasiwasi Angel kisha kwenda kukitelekeza chumbani kwake.
Harakaharaka akapakua chakula kidogo pamoja na mboga na kwenda nacho chumbani kwake. Kabla hajafika, Angel akamuuliza swali lililomfanya ababaike.
"Umeanza lini tabia ya kwenda kulia chakula chumbani?"
"Leo najisikia vibaya ndiyo maana nimeamua kuja kulia huku chumbani kwangu," alisema Abigail huku akitembea harakaharaka kuelekea chumbani kwake kukwepa kuambiwa kuwa aje kulia sebuleni. Angel alijiuliza maswali kadhaa lakini akaamua kulipuuzia jambo hilo, akawa anaendelea kutazama runinga huku akimsubiri mumewe.
Kule chumbani, Abigail hakukigusa chakula kile zaidi ya kukisukumia chini ya kitanda, akawa anaendelea kuzungukazunguka huku akiongea peke yake kama mwendawazimu.
Baada ya saa kadhaa, Harrison alimpigia simu mkewe na kumtaarifu kuwa tayari alishawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Abbotsford, Canada. Akamwambia aende kumpokea uwanja wa ndege kwani alikuwa na mizigo ya zawadi mbalimbali alizomnunulia.
Harakaharaka Angel akajiandaa pamoja na kumuandaa mtoto wake. Hakutaka kuondoka peke yake, alimwambia Abigail naye ajiandae ili waondoke wote. Awali Abigail alitaka kukataa kwenda ili Angel atakapoondoka aendelee kutafakari nini cha kufanya lakini Angel alipomwambia kuwa kuna mizigo ya kwenda kubeba, hakuwa na cha kufanya zaidi ya kukubali.
Muda mfupi baadaye wakajiandaa na kuondoka kuelekea uwanja wa ndege kwa kutumia teksi ya kukodi. Walipofika, tayari Harrison alikuwa ameshashuka kwenye ndege na kwenda sehemu maalum ya kukaa. Alipowaona mkewe, mwanaye na msichana wa kazi, aliinuka na kwenda kumkumbatia mkewe kimahaba akiwa na mwanaye.
Akawamwagia mvua ya mabusu huku kila mmoja akionesha dhahiri jinsi alivyofurahi. Abigail alikuwa amesimama pembeni huku akionesha kuzama kwenye dimbwi la mawazo na hofu kuu. Walipomaliza, Harrison alisalimiana pia na Abigail kisha wakasaidiana kubeba mizigo na kuipeleka kwenye teksi. Safari ya kurudi nyumbani ikaanza huku Harrison na mkewe wakiwa wamekumbatiana kimahaba pamoja na mtoto wao.
Walipofika nyumbani kwao, Angel alimuandalia mumewe maji ya kuoga na wakati akiendelea kuoga, yeye akaanza kuandaa chakula na kukiweka mezani. Kwa kuwa mwanaye naye alikuwa bado hajanywa uji wake, akamuandalia na kuweka kila kitu mezani.
***
MCHUMA janga hula na wa kwao! Usemi huu wa wahenga unamhusu kijana Harrison. Siku nyingi zilizopita, Harrison alimtoroka Linda kanisani muda mfupi kabla hawajafungishwa ndoa na kutorokea kusikojulikana huku akiudanganya
ulimwengu kwamba amekufa. Sasa siri yake imegundulika kwamba hakufa bali alimkimbia Linda na msichana huyo anajiandaa kulipa kisasi.
Kwa kutumia mbinu za kijasusi, Linda anamfuatilia Harrison hatua kwa hatua mpaka anafanikiwa kujua kuwa kumbe alibadilisha sura na kuishi na malkia wa masokwe kama mume na mke. Linda anaumia sana kuufahamu ukweli huo na kamwe hakubali kushindwa.
Anajibadilisha sura na kuingia kwenye maisha ya Harrison akijifanya hausigeli. Harrison anaposafiri kwenda Geneva, Uswisi, msichana huyo anayetumia jina bandia la Abigail anaamua kukamilisha azma yake ya kumuua Angel pamoja na mwanaye ambao aliwaona kama kikwazo kwenye maisha yake. Anaenda kununua sumu hatari na kuwachanganyia kwenye chakula.
Baada ya kurudi kutoka safari yake ya jijini Geneva, Uswisi, Harrison alilakiwa na mkewe na mwanaye, Harvey Junior pamoja na msichana wao wa kazi, Abigail. Harrison na mkewe wakasalimiana kwa kukumbatiana kimahaba na kumwagiana mvua ya mabusu kisha safari ya kurudi nyumbani ikaanza.
Walipofika nyumbani, harakaharaka Angel alienda kumuandalia mumewe maji ya kuoga na wakati akiendelea kuoga, alianza kuandaa chakula. Baada ya muda mfupi, kila kitu kilikuwa tayari juu ya meza. Kwa kuwa Harvey Junior naye alikuwa bado hajanywa uji wake, mama yake alimuandalia na kwa pamoja wakawa wanasubiri Harrison amalize kuoga ili waungane mezani.
Mbona wewe unakaa mbali? Sogea tule pamoja, Angel alimwambia Abigail aliyekuwa amekaa pembeni kwenye kochi huku akiwa amejishika tama. Abigail alitingisha kichwa tu kuashiria kuwa yeye tayari ameshakula. Muda mfupi baadaye, Harrison alishamaliza kuoga, akaenda kuungana na familia yake mezani.
Tuombe, alisema Angel huku akimtaka kila mmoja kufumba macho, akaanza kukiombea chakula kama ilivyokuwa kawaida yake kila siku. Wakati wakiwa wamefumba macho, Abigail alisimama na kusogea mezani, machozi yakimtoka kama chemchemi ya maji.
Walipomaliza kusali, wote walipigwa na butwaa kumuona Abigail amesimama pembeni ya meza, huku machozi mengi yakiwa yanamtoka.
Mungu wangu nisamehe, alisema Abigail huku akizidi kutokwa na machozi kwa wingi. Nafsi yake ambayo awali ilitawaliwa na ushetani wa kutisha, sasa ilibadilika na kutambua kuwa alichokuwa anakifanya ni dhambi kubwa ambayo kamwe asingeweza kusamehewa na Mungu wake.
Kwani vipi? Abigail kuna tatizo? alisema Harrison huku akiwa amepigwa na butwaa, akasimama na kumsogelea Abigail aliyekuwa akiendelea kulia huku akitamka maneno ya kumuomba radhi Mungu wake.
Wote wakiwa bado wamepigwa na butwaa, walishangaa kumuona Abigail akiinyanyua meza iliyokuwa na vyakula na kuiangusha kwa nguvu, kila kitu kikamwagika chini, kuanzia chakula mpaka uji wa mtoto.
Nakuchukia Angel, nakuchukia sana, nakuchukia malkia wa masokwe, alisema Abigail na kumrukia Angel mwilini, akamdondosha chini na kumkaba shingoni kwa nguvu. Kila mmoja alibaki amepigwa na butwaa, hakuna aliyeelewa kilichokuwa kinaendelea.
Sauti aliyoitoa wakati akitamka maneno hayo na jinsi alivyomtaja Angel kama malkia wa masokwe, viliifanya akili ya Harrison ifunguke haraka na kengele ya hatari ikalia kichwani mwake.
Amejuaje kuwa mke wangu ni malkia wa masokwe? Halafu mbona sauti yake inafanana na ya mtu ninayemfahamu? Harrison alijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu, akawa anababaika kujaribu kukumbuka sauti ile aliisikia wapi. Alishtuliwa kwenye dimbwi la mawazo na sauti ya mkewe aliyekuwa anakoroma kwa nguvu baada ya kukabwa kisawasawa na Abigail.
Kwa kasi ya ajabu, alitumia uanaume wake kumvaa Abigail pale chini alipokuwa amemkaba Angel, akamshika mikono yake na kumtoa kwa nguvu, akamsukumia pembeni kisha akamuinamia mkewe na kuanza kumpa pole.
Nakufa mume wangu, naku..fa, alisema Angel na kukohoa mfululizo, Harrison akawa anamsaidia kupumua huku akimlegeza nguo alizokuwa amezivaa mwilini. Alipogeuza shingo kumtazama Abigail, mapigo ya moyo wake yalimlipuka baada ya kumuona akiwa ameshika kisu kikali cha kukatia mboga, akiwa amemuelekezea mtoto Harvey Junior aliyekuwa akilia kwa sauti kubwa.
Noooo! Abigail, nipo chini ya miguu yako, naomba usimdhuru mwanangu, alisema Harrison kwa sauti ya juu huku akiinua mikono yake kama dalili ya kusalimu amri.
Kwa nini ulinitenda Harrison? Kwa nini? Ulijua sitakupata siyo? Mwanaume muuaji sana wewe, alisema Abigail huku akilia kwa kwikwi kama mtu aliyepokea taarifa za msiba. Bado Harrison alikuwa gizani kwani hakumtambua kwa haraka Abigail ni nani na kwa nini anafanya yote yale.
Kama ulikuwa hunipendi si bora ungeniambia kuliko mateso uliyonisababishia Harrison! Nilikukosea nini mpaka kustahili adhabu kali kiasi hiki? Nilikosea kukupenda? Nilikosea kukukabidhi moyo wangu? alisema Abigail huku akizidi kulia kwa uchungu, kisu akiwa amekielekeza kwenye shingo ya mtoto wa Harrison, Harvey Junior.
Japokuwa Angel alikuwa kwenye maumivu makali baada ya kukabwa kwa nguvu na msichana huyo, alijikakamua na kusimama, naye akapigwa na butwaa kumuona Abigail amemuelekezea kisu mtoto wake huku akizungumza mambo kama mtu aliyekuwa anamfahamu vizuri Harrison. Mtoto Harvey Junior hakuwa akielewa chochote, akawa anawatazama wote kwa zamuzamu.
Angel naye akaanza kulia kumbembeleza Abigail asimdhuru mwanaye, kutokana na jinsi alivyokuwa anamlilia mwanaye kwa uchungu, Abigail aliingiwa na moyo wa huruma. Kwa kasi ya ajabu akakigeuza kisu na kujielekezea tumboni, akawa anataka kujichoma na kujitoa uhai kwani hakuona tena sababu ya kuendelea kuishi.
Kwani wewe ni nani? Naomba uniweke wazi kwani mpaka sasa sijakujua bado.
Unajifanya hunijui? Unajifanya hunijui siyo? Harrison wewe ni muuaji na kamwe sitakusamehe! Nilipanga kuiteketeza familia yako kwa sumu lakini sijui malaika gani amebadili mawazo yangu, najuta kukupenda Harrison, alisema Abigail kwa kilio cha kwikwi,
akaingiza mkono mmoja mfukoni na kutoa kichupa kidogo kilichokuwa na mafuta huku mkono mmoja akiwa bado amejielekezea kisu tumboni.
Akakifungua kile kichupa na kujimimia mafuta kidogo, akaanza kujipaka usoni kwa kutumia mkono mmoja huku ule mwingine ukiwa umekikamata kisu barabaraba. Baada ya kujipaka mafuta yale, alijibandua ngozi ya bandia usoni kwake na kutoa nywele za bandia alizokuwa anazivaa.
Haaaa! Lindaaaa, ni wewe ni sa..m..e..h, Harrison alishindwa kumalizia alichotaka kukisema, kutokana na mshtuko mkubwa alioupata, alidondoka chini kama mzigo, jambo lililoamsha kilio upya kwa mkewe, Angel. Akamkimbilia mumewe pale chini na kuanza kumtingisha.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kuona hivyo, Abigail alikitupa kisu na kusogea mpaka pale Harrison alipokuwa amenguka, huku machozi mengi yakiendelea kumtoka. Akamsukuma Angel kwa nguvu kisha akamuinamia Harrison mpaka chini na kumlalia kifuani, akawa anaendelea kulia kwa uchungu huku maneno ya kimapenzi yakimtoka.
Kuepusha shari, Angel aliinuka na kwenda kumchukua mwanaye. Alijua endapo ataleta ujeuri na Abigail kuamua kumdhuru, hakuna mtu yeyote anayeweza kumsaidia kwani Harrison alikuwa amepoteza fahamu. Wakati Abigail akiendelea kulia kwa uchungu pale chini, akiwa amejikunyata kwenye kifua cha Harrison, Angel alikimbia mpaka nje na kwenda kuomba msaada kwa majirani.
Akawa anapiga kelele za kuomba msaada, muda mfupi baadaye, watu wakajazana nje ya nyumba ya Harrison. Wanaume wakajitosa na kuingia hadi ndani, wakatumia nguvu kumtoa Abigail kwenye kifua cha Harrison na kumkimbiza kwenye hospitali iliyokuwa jirani huku wengine wakimdhibiti msichana huyo asije akaleta madhara makubwa. Bado hakuna aliyekuwa na maelezo kamili ya kilichotokea.
***
HAKUNA marefu yasiyo na ncha. Siri aliyoificha Harrison siku nyingi zilizopita na kuudanganya ulimwengu kuwa amekufa kwenye ajali, hatimaye inafichuka baada ya Linda kuingia kazini kuhakikisha anaufahamu ukweli.
Linda anajisikia vibaya sana kugundua kuwa kumbe Harrison alimkimbia siku ya harusi yao ili apate muda wa kuishi na malkia wa masokwe. Hali hiyo inamfanya awe na hasira na kuwa tayari kufanya lolote kulipiza kisasi.
Bila ya Harrison wala Angel kujua kuwa kumbe Abigail alikuwa amejibadilisha sura, wanampokea nyumbani kwao akiwa kama hausigeli. Msichana huyo anaanza kupanga kufanya ukatili mkubwa wa kuwaangamiza Angel na mwanaye ili apate muda wa kulifaidi penzi la Harrison.
Hata hivyo, mpango wa kuwaua kwa sumu Angel na mwanaye unaingia dosari baada ya Harrison naye kutaka kula chakula kilichowekwa sumu, jambo ambalo Linda hakuwa tayari kuona linatokea. Anaamua kukimwaga chakula hicho na kusababisha kizaazaa kikubwa na baadaye, anaivua sura yake ya bandia na kubaki na sura yake halisi. Harrison anazimia baada ya kugundua kumbe ni Linda.
Kuepusha shari, Angel aliinuka na kwenda kumchukua mwanaye. Alijua endapo ataleta ujeuri na Abigail kuamua kumdhuru, hakuna mtu yeyote anayeweza kumsaidia kwani Harrison alikuwa amepoteza fahamu. Wakati Abigail akiendelea kulia kwa uchungu pale chini, akiwa amejikunyata kwenye kifua cha Harrison, Angel alikimbia mpaka nje na kwenda kuomba msaada kwa majirani.
Akawa anapiga kelele za kuomba msaada, muda mfupi baadaye, watu wakajazana nje ya nyumba ya Harrison. Wanaume wakajitosa na kuingia hadi ndani, wakatumia nguvu kumtoa Abigail kwenye kifua cha Harrison na kumkimbiza kwenye hospitali iliyokuwa jirani huku wengine wakimdhibiti msichana huyo asije akaleta madhara makubwa. Bado hakuna aliyekuwa na maelezo kamili ya kilichotokea.
Harrison alifikishwa hospitalini na kupokelewa na manesi wachangamfu, akapakizwa juu ya kitanda chenye magurudumu na kukimbizwa wodini. Muda mfupi baadaye, alianza kupewa huduma ya kwanza, akatundikiwa dripu na kupewa dawa, baada ya muda mrefu kupita, akapiga chafya na kufumbua macho.
Akawa anashangaa jinsi dripu ilivyokuwa ikitiririka kwenye mishipa yake ya damu.
Akawa anajiuliza pale ni wapi na amefikaje. Nesi aliyekuwa anaendelea kumhudumia, akamwambia kuwa hapo ni hospitalini na amefikishwa baada ya kuanguka na kupoteza fahamu akiwa nyumbani kwake.
Dakika chache baadaye, Harrison akiwa anaendelea kutafakari kilichomtokea, mlango wa wodi aliyokuwa amelazwa ulifunguliwa, akamuona mkewe na mwanaye mdogo wakiingia huku Angel akionesha kuchanganyikiwa mno.
"Jamani mume wangu, pole baba," alisema Angel huku akibubujikwa na machozi, akamuinamia mumewe pale kitandani na kumbusu shavuni huku akiendelea kutokwa na machozi. Harrison alimueleza kuwa ana ahueni kubwa, Angel akakaa pembeni ya kitanda chake huku akiwa amembeba mwanaye, huku akiwa na shauku kubwa ya kufahamu kilichokuwa kinaendelea.
"Kwani kuna nini kinachoendelea mume wangu, mbona mi sielewi chochote?" alihoji Angel huku akimshika mumewe kwa upole kichwani. Harrison alishusha pumzi ndefu na kumtazama mkewe usoni, akashindwa cha kumjibu zaidi ya kumwambia kuwa anampenda sana.
"Najua unanipenda sana mume wangu lakini hebu nitoe wasiwasi."
"Abigail yupo wapi?"
"Tumeenda kumhifadhi kwenye kituo cha polisi cha jirani kule nyumbani."
"Ooh! Mmefanya vizuri, polisi walifika nyumbani?"
"Ndiyo, pia wamechukua na sampuli za vyakula kwani ilibidi niwaelezee kisa kizima."
"Sawa, umefanya vizuri mke wangu, nikitoka hospitali nitakueleza kila kitu," alisema Harrison huku akijinyoosha na kulala vizuri. Nesi alimwambia Angel kuwa mgonjwa anahitaji muda zaidi wa kupumzika. Ikabidi atoke na kwenda kukaa nje ya wodi huku akijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.
Alimtafakari sana Abigail na tukio lililotokea, alijiuliza maswali mengi sana mpaka akaanza kuhisi kichwa chake kinachemka. Alishangaa zaidi baada ya kugundua kuwa kumbe kwa siku zote hizo, Abigail alikuwa amevaa sura ya bandia.
"Atakuwa anataka nini? Inaonekana kuna siri kubwa imejificha hapa! Lazima Harrison aniambie ukweli," aliwaza Angel huku akaikaa vizuri kwenye kiti, nje ya wodi aliyokuwa amelazwa mumewe. Alikaa hapohapo mpaka nesi alipokuja kumwambia kuwa aingie wodini kwani tayari mgonjwa ameshapumzika vya kutosha.
Baada ya kuingia wodini, Angel alianza tena kumdadisi mumewe juu ya kilichotokea. Hata hivyo, Harrison alimsisitiza kuwa asiwe na haraka ya kujua kwani atamueleza kila kitu watakapotoka hospitali.
"Nesi amesema baada ya saa chache nitaruhusiwa, usiwe na wasiwasi mke wangu, nitakueleza kila kitu," alisema Harrison, mkewe ikabidi atulie, wakawa wanazungumza mambo mengine. Baada ya muda, kama nesi alivyomwambia Harrison, aliruhusiwa kutoka hospitalini, mkewe akamsaidia kutembea mpaka nje walikoingia kwenye gari na safari ya kurudi nyumbani ikaanza.
Walipofika nyumbani, Harrison alimuomba mkewe wakafanye taratibu za kumtoa polisi Abigail, wazo ambalo Angel hakulikubali kirahisi. Akawa anasisitiza kuwa msichana huyo ni hatari sana kwenye maisha yao hivyo hatakiwi kuwasogelea tena.
"Hapana mke wangu, nikubalie kisha utagundua kwa nini nimekwambia hivyo," alisema Harrison lakini mkewe bado akawa anashikilia msimamo wake, akamwambia akitaka akubaliane naye, amueleze kila kitu kwanza kisha ataamua kama wakamtoe au la!
Kwa jinsi walivyokuwa wanaishi vizuri, kwa amani na upendo kwa siku zote tangu walipofahamiana, Harrison alikubali kumueleza ukweli wa kila kitu. Akaanza kumsimulia kuanzia jinsi walivyokutana na msichana aitwaye Linda ambaye ndiyo huyo aliyekuwa akijiita Abigail. Akamueleza kila kitu kilivyokuwa mpaka siku aliyomkimbia kanisani.
"Sasa kwa nini ulimkimbia mume wangu? Kumbe ndiyo maana ana hasira kiasi hiki."
"Nisamehe mke wangu na naomba Mungu naye anisamehe kwa hili lakini ukweli ni kwamba wewe ndiyo ulisababisha nimkimbie Linda."
"Mimi? Kwa nini?" alihoji Angel huku akiwa amepigwa na mshangao. Harrison akashusha pumzi ndefu na kumsogelea mkewe, akamueleza kuwa hakuwahi kumpenda Linda hata siku moja ila siku aliyomuona yeye (Angel) kwenye Msitu wa Tongass, alijihisi hali ya tofauti na kujikuta akimpenda kuliko maelezo.
"Upendo wangu wa dhati kwako ndiyo uliosababisha nimtoroke Linda siku ya harusi yetu!
Naomba Mungu anisamehe sana," alisema Harrison huku akianza kulengwalengwa na machozi, mkewe akaenda kumkumbatia na kuanza kumbembeleza.
Akamuuliza jinsi alivyotoroka siku ya ndoa yake na Linda, Harrison akaanza kumuelezea kila kitu. Hakuacha kitu, alieleza jinsi alivyoshirikiana na rafiki yake wa siku nyingi kutengeneza ajali feki ambayo iliwafanya watu wote waamini kama Harrison amekufa kwenye ajali.
Alieleza kila kitu, Angel akajikuta akitokwa na machozi kwani hakuwahi kujua kuwa Harrison alilihangaikia penzi lake kiasi hicho. Wakawa wanabembelezana huku wakijadiliana nini cha kufanya. Kwa pamoja walikubaliana kwenda kumtoa Linda kituo cha polisi na kurudi naye nyumbani hapo ili kila kitu kiwekwe hadharani.
"Niahidi kuwa utaendelea kuwa mume wangu na hutaonesha udhaifu mbele ya Linda," alisema Angel huku akionesha kuwa na wasiwasi kwani kwa jinsi alivyomsimulia, ilionesha kuwa Linda alikuwa akimpenda sana Harrison kiasi cha kuwa tayari kufanya lolote kwa ajili yake.
***
MBIO za sakafuni huishia ukingoni! Hatimaye siri aliyoificha Harrison kwa siku nyingi zilizopita na kuudanganya ulimwengu kuwa amekufa kwenye ajali ili apate nafasi ya kulifuatilia penzi la malkia wa masokwe, inafichuka baada ya Linda kuufahamu ukweli.
Msichana huyo kutoka familia ya kitajiri anajisikia vibaya sana kugundua kuwa kumbe Harrison hakufa na badala yake alimkimbia siku ya harusi yao kwa sababu ya penzi lake kwa malkia wa masokwe. Anapandwa na hasira kali kiasi cha kuwa tayari kufanya jambo lolote ili kulipiza kisasi.
Linda akiwa na mwonekano wa sura na jina tofauti, anaingia kwenye maisha ya Harrison na mkewe akijifanya ni hausigeli bila ya Harrison wala Angel kuujua ukweli. Kutokana na hasira kali, anapanga kuwaua Angel na mwanaye kwa sumu lakini mpango wake unaingia dosari baada ya Harrison naye kutaka kula chakula kilichowekwa sumu. Songombingo kubwa linaibuka.
"Niahidi kuwa utaendelea kuwa mume wangu na hutaonesha udhaifu mbele ya Linda," alisema Angel huku akionesha kuwa na wasiwasi kwani kwa jinsi alivyomsimulia, ilionesha kuwa Linda alikuwa akimpenda sana Harrison kiasi cha kuwa tayari kufanya lolote kwa ajili yake.
"Wala usiwe na wasiwasi mke wangu, mimi ndiyo ninayejua jinsi nilivyolihangaikia penzi lako, sitakuwa tayari kukupoteza," alisema Harrison kwa sauti ya chini, akamkumbatia mkewe na kumbusu kimahaba. Baada ya hapo, waliondoka pamoja na kuelekea kwenye Kituo cha Polisi cha Langley alikokuwa anashikiliwa Linda.
Baada ya kufika kituoni hapo na kueleza shida yao, mkuu wa kituo hicho cha polisi aliwaeleza kuwa majibu kutoka kwa mkemia wa serikali kuhusu sampuli za vyakula vilivyokutwa nyumbani kwa Harrison, zilionesha kuwa na sumu hatari ambayo ingesababisha vifo kwa wote ambao wangekula chakula hicho.
"Kisheria ni kosa la jinai kujaribu kuua kwa hiyo mtuhumiwa hataachiwa, lazima aburuzwe mahakamani ili kujibu mashtaka yanayomkabili," alisema mkuu wa kituo, Bill Curtis, kauli iliyowafanya Harrison na mkewe watazamane. Walishtuka mno kusikia kumbe vyakula walivyokuwa wanataka kula vilikuwa na sumu hatari kiasi hicho.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ina maana Linda alitaka kutuua? Mwanamke muuaji sana huyu."
"Lakini, kama kweli dhumuni lake lilikuwa ni kutuua, kwa nini aliamua kupindua meza na kumwaga vyakula vyote kabla hata hatujaanza kula?" Harrison na mkewe waliulizana maswali ambayo hakuna aliyekuwa na majibu. Kwa kuwa tayari muda ulikuwa umeenda sana, hawakuwa na la kufanya zaidi ya kuondoka kituoni hapo na kurudi nyumbani kwa ajili ya kutafakari kwa kina kilichotokea.
"Mume wangu!"
"Abee mke wangu."
"Unajua Linda ametukosea sana lakini kama maandiko matakatifu yanavyosema, inabidi tumsamehe kwa moyo mkunjufu."
"Ni kweli mke wangu, lakini hilo suala limeshafika kwenye mkono wa sheria, unafikiri itakuwa rahisi kiasi hicho?"
"Hakuna kisichowezekana mume wangu, mtu pekee anayeweza kumuokoa Linda ni wewe, lazima ukaeleze ukweli wa mlolongo wa matukio yote tangu siku uliyomkimbia kanisani ili kumjengea mazingira kwamba wakati anatenda kosa hilo hakuwa akijielewa," alisema Angel, akiwa amemkumbatia mumewe na kulala juu ya kifua chake, wakiwa chumbani kwao.
Harrison alishangazwa sana na moyo wa huruma aliokuwa nao mkewe. Licha ya ubaya wote aliotaka kuwafanyia, bado Angel hakutaka kabisa kumhukumu Linda na akawa mstari wa mbele kuhakikisha anakuwa huru. Harrison na mkewe walizungumza mambo mengi sana usiku huo, Angel akawa anasisitiza kuwa baada ya kufanikisha kumtoa polisi, inatakiwa wakae pamoja na kuelezana kinagaubaga.
"Linda anahitaji kusikia kutoka kwako kama bado unampenda au la! Unafikiri kama ungemweleza tangu mwanzo kuwa humpendi na haupo tayari kuishi naye angehangaika kukufuatilia kiasi hiki? Ukweli ndiyo silaha pekee unayotakiwa kuitumia, nakuamini sana mume wangu," Angel aliendelea kumwambia mumewe maneno ya busara kwa upole mpaka usingizi ulipowapitia.
Kama walivyokubaliana, asubuhi na mapema Harrison alikwenda mpaka kwenye Kituo cha Polisi cha Langley na kuomba kuonana na mkuu wa polisi. Alipoingia ofisini kwake, ilibidi aeleze kinagaubaga juu ya mlolongo wa matukio yaliyotokea mpaka kumsababishia Linda kufanya kitendo hicho.
Hata hivyo, katika maelezo yake, Harrison alikwepa sana kutoa maelezo ya jinsi alivyodanganya kifo chake na namna alivyoishi kwa kipindi chote nchini Canada bila kuwa na vibali halali. Baadhi ya maelezo aliyoona yanaweza kumtia hatiani yeye mwenyewe, aliyaruka. Akajieleza kwa muda mrefu huku mkuu wa kituo cha polisi, Bill Curtis akimsikiliza kwa makini.
Baada ya kumaliza, mkuu wa kituo aliandika maelezo fulani kwenye jalada la kesi ya Linda kisha akamhakikishia Harrison kuwa ampe muda wa saa chache kushughulikia suala hilo na lazima Linda atatolewa mahabusu kwani maelezo aliyoyatoa Harrison ni mazito sana.
Harrison alimshukuru sana na kuondoka, akapitia kwanza kazini kwake kuripoti kwani tangu arejee kutoka Geneva, Uswisi, hakupata muda wa kwenda kutoa taarifa kwamba amesharejea. Baada ya kuripoti kazini, Harrison alirudi nyumbani kwake alikomkuta mkewe anamsubiri kwa shauku. Akamueleza kila kitu kilichoendelea na majibu aliyopewa na mkuu wa kituo cha polisi, Bill Curtis.
"Kwa hiyo tutapataje taarifa kuwa ameachiwa? Inabidi akitoka tu, tumchukue na kuja naye mpaka hapa nyumbani," alisema Angel.
"Nimemuachia mkuu wa kituo namba zangu za simu, amesema atanipigia," Harrison alijibu.
Wakawa wanaendelea kucheza na mtoto wao huku wakipanga mipango mingine ya maisha yao, ikiwa ni pamoja na Harrison kurejea nyumbani kwao na kuwaambia watu wote ukweli wa kila kitu kilivyotokea pamoja na kuomba radhi kwa usumbufu, machungu na huzuni alizowasababishia watu wake wa karibu na mashabiki wake.
Pia walizungumza kuhusu suala la kusafiri mpaka nchini Tanzania kwenda kumtafuta mzee Abdulkarim Charwe, baba mzazi wa Angel. Wakiwa wanaendelea na mazungumzo hayo, simu ya Harrison iliita na alipotazama kwenye ‘skrini', alikutana na namba mpya.
"Haloow! Nani mwenzangu."
"Bila shaka wewe ni Harrison Harvey."
"Ndiyo, hujakosea."
"Unazungumza na mkuu wa Kituo cha Polisi cha Langley."
"Oooh! Kamanda, habari ya kazi."
"Nzuri, unaombwa kufika hapa kituoni mara moja kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kumtoa Linda, vitu vingi vimeshakamilika," alisema mkuu huyo wa polisi kisha simu ikakatwa. Bila kupoteza muda, Harrison na mkewe walijiandaa na kutoka wakiwa sambamba na mtoto wao, wakaenda mpaka kituo cha polisi.
Harrison akapewa baadhi ya nyaraka azisaini kisha wakaambiwa wasubiri kidogo, baada ya takribani dakika kumi, wote wakashuhudia milango ya chuma ikifunguliwa kisha Linda akatolewa na askari wa kike mpaka kaunta, akaandikisha tena baadhi ya maelezo kisha akaachiwa huru.
"Pole sana Linda kwa yaliyokukuta, hizi ni changamoto za maisha," alisema Angel kwa sauti ya upole lakini katika hali ya kushangaza, Linda hakumjibu chochote, akampita na kutoka hadi nje kabisa ya kituo hicho. Harrison alizungumza na mkewe harakaharaka na kumweleza kuwa yeye abaki kimya, kazi ya kumaliza kila kitu ataifanya mwenyewe.
Harrison akamkimbilia Linda na kumuomba amsikilize. Msichana huyo akasimama huku akionesha bado kuwa na kinyongo, akamgeukia Harrison huku akiwa amekunja uso, mwanaume akaanza kumlainisha kwa maneno matamu huku akimsihi arudishe moyo nyuma na kukubali kwenda nao nyumbani ili wakayamalize.
***
Uongo mkubwa alioutumia Harrison na kuwafanya watu wote waamini kwamba amekufa, hatimaye unabainika baada ya Linda kumpeleleza kwa muda mrefu na kufanikiwa kumpata akiwa nchini Canada, akiwa amebadilisha jina na sura.
Msichana huyo kutoka familia ya kitajiri anajisikia vibaya sana kugundua kuwa kumbe Harrison hakufa na badala yake alimkimbia siku ya harusi yao kwa sababu ya penzi lake kwa malkia wa masokwe. Anapandwa na hasira kali kiasi cha kuwa tayari kufanya jambo lolote ili kulipiza kisasi.
Naye anatumia mbinu za hali ya juu kujibadilisha sura na jina kisha anaingia kwenye maisha ya Harrison na mkewe akijifanya ni hausigeli bila mtu yeyote kuujua ukweli. Kutokana na hasira kali, anapanga kuwaua Angel na mwanaye kwa sumu lakini mpango wake unaingia dosari baada ya Harrison naye kutaka kula chakula kilichowekwa sumu.
Vurugu kubwa inaibuka, Linda anamwaga vyakula vyenye sumu na kutaka kumdhuru Angel na mwanaye, Harrison anatumia nguvu kubwa kumdhibiti lakini baadaye anapogundua kuwa ni Linda aliyemkimbia siku ya harusi yao, anapatwa na mshtuko mkubwa unaosababisha aanguke na kupoteza fahamu. Msichana huyo anapelekwa kituo cha polisi lakini baadaye anaachiwa kwa jitihada za Harrison.
Harrison akamkimbilia Linda na kumuomba amsikilize. Msichana huyo akasimama huku akionesha bado kuwa na kinyongo, akamgeukia Harrison huku akiwa amekunja uso, mwanaume akaanza kumlainisha kwa maneno matamu huku akimsihi arudishe moyo nyuma na kukubali kwenda naye nyumbani ili wakayamalize.
"Sitaki! Niache muuaji mkubwa wewe! Nakuchukia, nakuchukia Harrison," alisema Linda kwa sauti kubwa, hali iliyosababisha watu wawageukie na kuwashangaa. Licha ya kumtoa nishai mbele za watu, Harrison bado aliendelea kumbembeleza Linda. Msichana huyo akaanza kuangua kilio kwa nguvu, Harrison akaona huo ndiyo muda muafaka wa kumshinda.
Akamsogelea na kumshika, akawa anambembeleza kwa maneno laini, hali iliyomfanya Linda apunguze sauti, akaendelea kumlaumu kwa kumtesa moyo wake kiasi hicho. Harrison aliamua kujishusha, akawa anakubali makosa lakini akamsisitiza kuwa hiyo haikuwa sehemu muafaka ya kuzungumzia mambo hayo.
Akamsihi atulize moyo wake na kila kitu kitakuwa sawa, Linda akawa anaendelea kulia kwa kwikwi huku akionesha kukubali kuondoka na Harrison pamoja na mkewe, Angel. Kwa kuwa watu wengi walikuwa wameacha shughuli zao na kuwashangaa, Harrison aliita teksi harakaharaka, akamuingiza Linda na kukaa naye huku mkewe aliyekuwa na mwanaye wakikaa mbele.
Wakaondoka eneo hilo na kuwaacha watu wakiwa wamepigwa na butwaa. Kwa kuwa hapakuwa mbali na wanapoishi, baada ya dakika chache waliwasili nyumbani kwao, wakateremka na kuingia ndani, huku muda wote Harrison akiwa makini na Linda asije kusababisha madhara tena. Wakaingia moja kwa moja mpaka sebuleni na kukaa, Harrison akiwa katikati, kushoto akiwa amekaa mkewe na kulia akiwa amekaa Linda. Harrison akauvunja ukimya:
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Najua nimekukosea sana Linda, najua umelia na kuteseka mno kwa kipindi kirefu chanzo kikiwa ni mimi, nahisi hatia kubwa ndani ya nafsi yangu na jambo pekee litakalonifanya nijisikie amani ni kueleza ukweli wa kila kitu kilichotokea tangu siku nilipokukimbia kanisani mpaka leo hii. Nakuomba ukubali kunisikiliza," alisema Harrison kwa sauti ya busara, Linda akatingisha kichwa kuashiria kuwa yupo tayari kumsikiliza.
Harrison akashusha pumzi ndefu na kuanza kueleza kila kitu kilivyokuwa. Alianza kwa kueleza kilichotokea siku ya harusi. Alieleza jinsi ambavyo moyo wake ulikuwa haujamkubali kuwa mkewe na jinsi alivyoamua kumkimbia kanisani.
"Nilikuwa kama nimechanganyikiwa, moyo wangu haukuwa tayari kukupokea wewe kuwa mke wangu wa ndoa lakini nilishindwa kukuambia kwa kuhofia kukuumiza. Nilijua kwa jinsi ulivyokuwa unanipenda, ungeweza hata kujiua kwa ajili yangu, ndiyo maana nikaona njia pekee ni kukukimbia," alisema Harrison huku akilengwalengwa na machozi.
"Baada ya kukukimbia kanisani, nilienda kwa rafiki yangu ambaye alinipa mbinu nyepesi za namna ya kumaliza tatizo hilo, tukaandaa ajali feki na kufanya kila mtu aamini kwamba nimepata ajali na kufa. Nilikuwa sijielewi kwani nilichokuwa nakitaka kwa wakati huo ilikuwa ni kukutana na malkia wa masokwe tu kwani nilikuwa nampenda sana licha ya tofauti kubwa iliyokuwepo kati yangu na yeye.
"Ukweli ni kwamba sikufa kwenye ajali bali tulitafuta maiti na kuivalisha nguo zangu za harusi kisha tukatengeneza mazingira ili ionekane kama kuna ajali mbaya imetokea. Baada ya hapo mimi nikaondoka na kukimbilia kwenye msitu wa Tongass kumfuata kipenzi cha moyo wangu," alisema
Harrison huku akimgeukia mkewe ambaye naye alikuwa amejiinamia, machozi yakimtoka.
Wakakumbatiana huku kila mmoja akitokwa na machozi. Harrison akaendelea kueleza jinsi alivyohangaika na malkia wa masokwe mpaka alipofanikiwa kumtorosha na kukimbilia nchini Canada alikoanza kumfundisha ustaarabu wa kibinadamu mpaka walipofunga ndoa.
"Kwa hiyo mlishafunga ndoa? Ya mkataba au kanisani?" aliuliza Linda kwa sauti ya kilio, akiwa haamini alichokisikia. Harrison alimjibu kuwa walifunga ndoa ya kanisani, Linda akashindwa kujizuia, akawa analia kwa kwikwi huku akisisitiza kuwa bado anampenda.
"Basi na mimi nioe niwe mke wako wa pili, bado nakupenda Harrison nionee huruma. Tangu uliponikimbia sijawahi kuwa na mwanaume mwingine yeyote," alisema Linda huku akiendelea kulia kwa uchungu, Harrison akawa anambembeleza na kumueleza kuwa suala hilo haliwezekani kwani imani ya dini ya Kikristo hairuhusu mwanaume kuoa mke zaidi ya mmoja.
"Wewe bado ni mrembo sana Linda na umri wako siyo mkubwa, utampata mwanaume mwingine utakayempenda kuliko hata ilivyokuwa kwangu na utasahau yote yaliyotokea. Mimi na mke wangu tunakuombea kila la heri upate mume mzuri lakini tafadhali naomba ukubali kunisamehe na kutuacha tuendelee kuishi kwa amani," alisema Harrison kwa sauti ya kubembeleza.
Linda hakutaka kukubaliana na alichokuwa anaambiwa, akawa anaendelea kulia mpaka sauti ikamkauka na macho kuwa mekundu sana. Harrison akaendelea kumbembeleza kwa muda mrefu, jibu la mwisho alilolitoa ni kwamba hawezi kukubali kulikosa penzi lake kirahisi namna hiyo.
"Mimi naondoka kurudi nyumbani kwetu, lakini msimamo wangu ndiyo huo. Sipo tayari kukukosa Harrison, nitafanya chochote mpaka ndoto zangu za miaka mingi zitimie," alisema Linda na kuondoka.
"Sasa unaondoka muda huu unakwenda wapi?"
"Nilikuwa nimefikia hotelini kabla ya kuhamia hapa na nilishalipa kila kitu kwa hiyo msiwe na wasiwasi," alisema Linda huku akiondoka kwa kasi. Harrison na mkewe wakabaki kutazamana huku macho ya kila mmoja yakiwa mekundu kwa kulia.
"Sasa tutafanyeje mume wangu?"
"Yaani hata sielewi cha kufanya. Mimi nafikiri kwa hali ilivyo, inabidi turudi Marekani ili nikawaombe radhi watu wote, wakiwemo wazazi wangu na kuwaeleza ukweli wa kila kitu kama nilivyomweleza Linda kisha baada ya hapo nitaenda kuzungumza na wazazi wa Linda ili wao ndiyo wazungumze na binti yao. Naamini atawasikiliza wazazi wake," alisema Harrison, wazo lililoungwa mkono na Angel.
Kwa kuhofia kuwa Linda anaweza kuwa amechanganya ile sumu kwenye vyakula vingine na maji, Harrison, mkewe na mtoto wao walitoka na kwenda kula hotelini. Walipomaliza kula walirejea ndani kwao na kuendelea na mipango yao ya kurudi Marekani pamoja na safari ya kwenda Tanzania kumfuata baba mzazi wa Angel, Abdulkarim Charwe.
Mipango iliendelea kufanyika mpaka usiku, wakalala huku wakiwa hawana amani kabisa kwani bado walikuwa wa wasiwasi kuwa Linda anaweza kurudi na kufanya lolote ili kutimiza malengo yake.
***
UNAWEZA kuwadanganya watu fulani kwa kipindi fulani lakini huwezi kuwadanganya watu wote kwa kipindi chote, usemi huu wa wanafalsafa wa kale unamhusu Harrison ambaye hatimaye uongo mkubwa alioutumia na kuwafanya watu wote waamini kwamba amekufa, unabainika.
Kijana huyo wa Kimarekani, aliyebobea kwenye masomo ya tabia za wanyama na mimea, aliudanganya ulimwengu kwamba amekufa kwenye ajali mbaya siku ya harusi yake aliyotakiwa kumuoa Linda, msichana ambaye hakuwa chaguo la moyo wake licha ya kwamba alikuwa akitoka kwenye familia ya kitajiri.
Baada ya kumkimbia Linda, Harrison alikimbilia kwenye Msitu wa Tongass alikoanza kupigania penzi la malkia wa masokwe mpaka alipofanikiwa kumtorosha na kukimbilia naye nchini Canada walikooana na kuanza maisha mapya wakiwa kama mume na mke.
Hata hivyo, Linda anaamua kufanya upelezi wa chini kwa chini na hatimaye anagundua kuwa Harrison hakufa bali alibadilisha jina na sura na sasa anaishi na malkia wa masokwe. Anafanikiwa kuingia kwenye
maisha yake akijifanya ni hausigeli na anataka kulipa kisasi kwa kuwaua mke wa Harrison na mwanaye. Muujiza unatokea na anashindwa kutimiza malengo yake. Utata unaendelea.
Kwa kuhofia kuwa Linda anaweza kuwa amechanganya ile sumu kwenye vyakula vingine na maji, Harrison, mkewe na mtoto wao walitoka na kwenda kula hotelini. Walipomaliza kula walirejea ndani kwao na kuendelea na mipango yao
ya kurudi Marekani pamoja na safari ya kwenda Tanzania kumfuata baba mzazi wa Angel, Abdulkarim Charwe.
Mipango iliendelea kufanyika mpaka usiku, wakalala huku wakiwa hawana amani kabisa kwani bado walikuwa na wasiwasi kuwa Linda anaweza kurudi na kufanya lolote ili kutimiza malengo yake ya kulipiza kisasi.
Kulipopambazuka, Harrison na mkewe waliwahi kuamka na kuanza mipango ya kutimiza kila kitu walichokizungumza usiku. Kwa kuwa kila kitu kilikuwa hadharani, Harrison hakuona sababu ya yeye na mkewe kuendelea kuishi kama
wakimbizi nchini Canada, mipango ya kusafiri kurejea nyumbani kwa akina Harrison, Miami nchini Marekani ilianza.
Jambo la kwanza, walikubaliana kuwa kila mmoja akaombe likizo ndefu isiyo na malipo kazini kwake. Wakaongozana
pamoja na kuanzia kazini kwa Angel ambapo aliomba likizo hiyo na kuwashtua viongozi wake. Ilibidi awaeleze kuwa kuna matatizo ya kifamilia ambayo inabidi apate muda wa kutosha kuyashughulikia.
Walipokubaliwa, walienda mpaka kazini kwa akina Harrison, akazungumza na viongozi wake na kuwaeleza malengo yake. Naye hakukubaliwa kirahisi kwani uttendaji kazi wake ulimfanya kuwa tegemeo kazini kwao ndani ya muda mfupi hivyo kuondoka kwake kungesababisha kampuni iyumbe. Hata hivyo, hakuwa na cha kufanya zaidi ya kushikilia msimamo wake, akaruhusiwa kwa shingo upande.
Baada ya hapo, waliondoka na kurudi nyumbani ambako waliwaaga baadhi ya majirani na maandalizi ya safari yakapamba moto. Angel alitafutiwa hati ya kusafiria huku Harrison akiendelea kutumia hati iliyokuwa na jina na sura bandia. Baada ya maandalizi kukamilika, Harrison, mkewe na mtoto wao, Harvey Junior walielekea Uwanja wa Ndege wa Abbotsford.
"Abiria mtakaosafiri na ndege aina ya Douglas DC-6 ya kampuni ya Orca Airways mnaombwa kuanza kuelekea ndani ya ndege," sauti ya mhudumu wa kike ilisikika kwenye vipaza sauti vilivyokuwa kwenye uwanja huo wa kimataifa, abiria wengi waliokuwa ndani ya jengo la uwanja wa ndege, wakainuka na kuanza kusogea kwenye lango la kuingilia sehemu ya ukaguzi kisha kuelekea ndani ya ndege.
Harrison na mkewe nao walikuwa miongoni mwa abiria, wakasaidiana kusogeza mabegi yao makubwa yaliyokuwa na vitu vyao vyote mpaka sehemu ya ukaguzi. Baada ya kukaguliwa, Harrison na mkewe walishikana mikono na kuanza kuelekea mahali ndege ilipokuwa imepaki, wakapanda ngazi na kuingia kwenye ndege hiyo ya kisasa, wakaenda kukaa kwenye siti zao kama tiketi zao zilivyokuwa zinaeleza.
"Kwa heri Canada! Nimekumbuka sana nyumbani, sijui ndugu zangu wakiniona watanipokeaje?" alijiuliza Harrison akiwa amekaa kwenye siti yake na kumsaidia mkewe kumbeba mtoto. Waliendelea kuzungumza mambo mbalimbali na mkewe mpaka waliposikia tangazo la kuwataka kufunga mikanda kuashiria kwamba ndege ilikuwa ikitaka kuondoka.
Muda mfupi baadaye, injini za ndege ziliwashwa na kuanza kutoa muungurumo, ndege ikageuka na kuanza kusogea kuelekea kwenye njia za kurukia, ikawa inaongeza kasi taratibu mpaka ilipokolea mwendo, hatimaye ikapaa na kuiacha ardhi ya Canada.
Baada ya kusafiri kwa saa kadhaa angani, hatimaye ndege aina ya Douglas DC-6 ya kampuni ya Orca Airways iliwasili jijini Miami na kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami. Kwa muda wote huo, Harrison alikuwa akitafakari namna ndugu zake watakavyoipokea taarifa kwamba hakufa. Hakutaka kuchelewa mpaka Linda ndiyo akawaambie ukweli, alitaka kuanika kila kitu kwa kinywa chake mwenyewe.
Baada ya kuteremka kwenye Uwanja wa Ndege wa Miami, akiwa na mwonekano tofauti wa sura na umbo, Harrison alimuongoza mkewe mpaka kwenye Hoteli ya Olympia Heights iliyokuwa jirani kabisa na nyumbani kwao, alikokuwa anaishi mama yake mzazi, Skyler.
Baada ya kufika kwenye hoteli hiyo, Angel akishangaashangaa mazingira ya Miami, Harrison aliwasiliana na mtaalamu wa upasuaji wa kubadilisha sura (plastic surgery) aliyepata namba zake kutoka kwenye kitabu cha
mawasiliano cha Yellow Pages. Akamuelekeza kufika hotelini hapo kwa ajili ya kumfanyia upasuaji mdogo wa kuondoa sura ya bandia ili abaki na sura yake halisi.
Kwa kuwa alimuahidi fedha za kutosha, Daktari Federer aliyebobea kwenye mambo ya ‘plastic surgery' aliacha kazi alizokuwa anazifanya na kufunga safari mpaka kwenye Hoteli ya Olympia Heights na kwenda kuonana na Harrison aliyemweleza kuwa anataka kuivua sura ya bandia.
"Hiyo mbona kazi rahisi sana! Jipake haya mafuta kisha usubiri kidogo nitakuonesha cha kufanya," alisema Daktari Federer huku akimpa Harrison kichupa kilichokuwa na mafuta maalum. Baada ya Harrison kujipaka mafuta hayo usoni, aliingizwa kwenye chumba maalum kilichokuwa na baridi na kulazwa juu ya kitanda maalum.
Akaambiwa afumbe macho mpaka atakapoambiwa afumbue, akatii. Baada ya takribani nusu saa, daktari aliingia kwenye chumba hicho akiwa na vifaa mbalimbali kama mikasi, sindano, nyembe na visu vidogo. Akaanza kazi ya kumbandua ngozi ya bandia Harrison pamoja na nywele, zoezi lililochukua karibu dakika thelathini. Alipomaliza, alimsafisha uso kisha akamwambia akajitazame kwenye kioo kikubwa kilichokuwa ndani ya wodi hiyo.
"Whaoooo! Huyu ndiye Harrison wa siku zote, nimekuwa mzuri kama zamani," alisema Harrison huku akijishika usoni. Akapakwa Mafuta mengine ya kulainisha ngozi kisha akatoka mpaka sehemu ya mapokezi alipomkuta mkewe na mtoto wao wakimsubiri kwa shauku.
"He! Umebadilika mume wangu, kumbe ile sura ya bandia ilikuwa inakuzeesha bure! Cheki ulivyo ‘handsome'," alisema Angel huku akimkumbatia mumewe kimahaba na kumbusu. Harrison alikuwa mwingine kabisa, kama ungemuona saa kadhaa zilizopita, hakika usingeweza kutambua kuwa ni yuleyule kwani alibadilika mno kuanzia nywele mpaka sura.
Baada ya kukamilisha malipo kwa Daktari Federer, wawili hao waliondoka na mtoto wao na safari ya kuelekea nyumbani kwa mama yake Harrison ikaanza. Kwa kadiri walivyokuwa wanakaribia kufika, ndivyo Harrison alivyoanza kubadilika kwani alijisikia uchungu sana kurudi kwenye mazingira aliyokulia baada ya kuwa amemdanganya mpaka mama yake aliyemzaa kwa shida.
Moyoni alijiona mwenye hatia kubwa kwa kuudanganya ulimwengu kwa kipindi chote hicho lakini alipogeuka na kumtazama mkewe aliyekuwa amekaa pembeni yake akimnyonyesha mtoto wao, alijikuta akifarijika na kupiga moyo konde kwamba licha ya kuumiza mioyo ya watu wengi, hatimaye furaha aliyokuwa akiisaka maishani mwake aliipata.
Gari walilopanda likawafikisha mpaka nje ya geti la nyumba ya mama yake Harrison, Skyler, Harrison na mkewe wakateremka na kuanza kusogea taratibu kwenye mlango wa kuingilia ndani.
***
Baada ya kulihangaikia penzi la malkia wa masokwe kwa kipindi kirefu kiasi cha kuudanganya ulimwengu kwamba amekufa, hatimaye ukweli unafahamika kwamba Harrison hakufa kama watu wote walivyokuwa wanaamini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siri hiyo inagunduliwa na Linda ambaye Harrison alimkimbia siku ya harusi yao kwa ajili ya kumfuata malkia wa masokwe kwenye msitu mkubwa wa Tongass. Msichana huyo anaamua kufuatilia kwa kina kilichotokea siku ya harusi yao mpaka Harrison akamkimbia.
Upelelezi wake unamfikisha kwenye Mji wa Abbotsford, Canada ambako anamkuta Harrison akiwa amebadilisha sura na kuishi kinyumba na malkia wa masokwe ambaye sasa alikuwa amestaarabika na kuwa kama binadamu wa kawaida. Roho yake inamuuma sana kugundua kuwa kumbe Harrison alimkimbia kwa sababu ya
msichana huyo, anapanga kulipiza kisasi kikali huku akijiapiza kuwa ni lazima Harrison arudi kwenye mikono yake.
Vurumai kubwa inatokea baada ya Linda kuujua ukweli lakini Harrison anashikilia msimamo wake kwamba mwanamke aliyekuwa anampenda ni Angel. Linda
anaondoka na kutoa vitisho, huku nyuma, Harrison na mkewe wanaamua kurudi nchini Marekani kwani siri yao ilishafichuka.
Wanasafiri kwa ndege mpaka Miami, Marekani nyumbani kwa akina Harrison na tayari wapo nje ya nyumba ya mama yake Harrison, Skyler.
Sijui mama yangu yupo? Sijui akiniona atanipokeaje? Sijui jamii itanielewaje kwa hiki nilichokifanya? Eeeh Mungu nisamehe na unipe ujasiri katika kipindi hiki kigumu," alisema Harrison huku wakizidi kuusogelea mlango wa kuingilia ndani ya nyumba yao, mkewe akiwa nyuma yake pamoja na mtoto wao, Harvey Junior.
Walisimama mlangoni, Harrison akabonyeza kitufe cha kengele, akasubiri kwa sekunde kadhaa kisha wakashuhudia mlango mkubwa ukifunguliwa, msichana aliyeonekana dhahiri kuwa mfanyakazi wa ndani akafungua mlango wa ndani kisha akafungua geti. Akawasalimu Harrison na mkewe kisha akawauliza awasaidie nini.
"Tunaweza kuonana na mwenye nyumba?"
"Nani? Mama? Yupo ndani amepumzika. Nimwambie nyie ni akina nani?"
"Mwambie tu kuna wageni wake," alisema Harrison huku mapigo ya moyo yakizidi kumwenda mbio na miguu yake kuishiwa nguvu. Msichana huyo aliwakaribisha mpaka sebuleni, akaelekea chumbani kwa bosi wake (Skyler) na kumpa taarifa kuwa kuna wageni wake.
Skyler aliamka na kuvaa vizuri nguo zake, akatoka mpaka sebuleni, macho yake yakatua kwa msichana aliyekuwa amembeba mtoto. Alipogeuza shingo yake upande wa pili, macho yalimtoka pima baada ya kumuona mtu ambaye hakutegemea kuja kumuona tena maishani mwake.
"Harrison! Hapanaaa, haiwezekani, jamani mzimu wa Harri…" Skyler alipiga kelele kwa nguvu zilizosikika mpaka kwa majirani lakini kabla hajamalizia alichotaka kukisema, alianguka chini kama mzigo na kupoteza fahamu.
Msichana wa kazi ndiyo aliyekuwa wa kwanza kufika sehemu bosi wake alipoangukia, akifuatiwa na mke wa Harrison, wakainama chini alipoangukia Skyler ambaye sasa alishaanza kuzeeka na kuwa mtu mzima, tofauti na wakati Harrison anamuona kwa mara ya mwisho.
Harrison alibaki amepigwa na butwaa huku machozi yakimtoka, hakutegemea kama mama yake anaweza kushtuka kiasi hicho mpaka kupoteza fahamu. Muda mfupi baadaye, majirani kadhaa waliomsikia Skyler akipiga kelele kwamba ameuona mzimu wa mwanaye, walifika nje ya nyumba hiyo kwa lengo la kutoa msaada.
Kwa kuwa nao walikuwa wakimfahamu Harrison, walipoingia ndani na kumkuta, kila mtu alikimbia nje wakiamini kwamba ni kweli mzimu wa Harrison ulikuwa umewatokea, Harrison na mkewe wakawa na kazi ya ziada ya kuwaelewesha ingawa kazi haikuwa nyepesi.
Baada ya kujieleza sana, baadhi ya majirani wa kiume ambao hawakuwa waoga, waliingia ndani na kusaidiana kumbeba Skyler ambaye hakuwa na fahamu na kumtoa mpaka nje, wakampakiza kwenye gari na kumkimbiza hospitali ili kuokoa maisha yake. Harrison aliongozana nao huku muda wote akiwa amejiinamia, machozi yakimtoka kama chemchemi ya maji.
Bado watu waliendelea kumshangaa, wakiwa wanajiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu kwani kila mtu alikuwa anajua Harrison alikufa siku nyingi zilizopita na kuzikwa. Baada ya kufikishwa hospitali, Skyler alilazwa na kuanza kupewa huduma ya kwanza, akatundikiwa dripu iliyoanza kutiririka kwa kasi kuingia kwenye mishipa yake.
Muda mfupi baadaye, wazazi wa Skyler, mzee Lewis na mkewe walipewa taarifa kuwa mtoto wao wa kipekee, Skyler alikuwa amelazwa kwenye hospitali aliyokuwa akifanyia kazi mzee huyo kabla ya kustaafu. Harakaharaka, wazee hao waliingia ndani ya gari lao huku kila mmoja akiwa na wasiwasi mkubwa juu ya afya ya mtoto wao.
Japokuwa mzee Lewis alikuwa amezeeka, bado alikuwa na uwezo wa kuendesha gari vizuri kwa umakini, wakaelekea mpaka kwenye Hospitali ya Miami na kwenda kuuliza mapokezi. Kwa kuwa wafanyakazi wengi wa hospitali hiyo walikuwa wanamfahamu daktari huyo mstaafu, hakupata shida, muda mfupi baadaye tayari walikuwa kwenye wodi aliyolazwa Skyler.
"Dokta kwani kumetokea nini?" aliuliza mzee Lewis akiwa ameshikana mkono na mkewe. Daktari akawajibu kuwa mgonjwa wao alikuwa amepatwa na mshtuko lakini atakuwa sawa baada ya muda mfupi. Wakatazamana na mkewe kisha daktari akawaomba waende sehemu ya kupumzikia ili madaktari wapate nafasi ya kuendelea kumtibu mgonjwa.
Mzee Lewis na mkewe wakatoka kuelekea kwenye bustani ya maua iliyokuwa nje ya wodi hiyo na kuelekea kwenye viti maalum vilivyokuwa eneo hilo. Wakati wakitembea taratibu, wakijiandaa kukaa, mzee Lewis aliona kitu kilichomshtua moyo wake kuliko kawaida, akamkonyeza mkewe na kumuoneshea kwa kidole.
Mke wa mzee Lewis alipiga kelele kwa nguvu baada ya kuona alichooneshwa na mumewe.
"Harrisoooon! Hapana, siyo yeye, ni mzimu wa…ke," alipiga kelele mama huyo mzee na kujikuta akiishiwa nguvu, mumewe alijaribu kumdaka lakini alishachelewa, mama huyo akaanguka chini kama mzigo na kupoteza fahamu. Manesi waliokuwa jirani, wakakimbilia eneo hilo na kumsaidia kumuinua na kumbeba juu ya kitanda cha magurudumu, akakimbizwa wodini.
Kelele alizopiga mwanamke huyo kabla hajaanguka na kupoteza fahamu, ziliwashtua watu wengi, akiwemo Harrison na mkewe waliokuwa wamekaa eneo hilo wakisubiri mgonjwa wao, Skyler azinduke. Kwa kuwa muda wote Harrison alikuwa ameinama, machozi yakimtoka kutokana na hali iliyompata mama yake mzazi baada ya kumuona, hakuwaona bibi na babu yake wakati wakifika eneo hilo.
Kilichomshtua ni baada ya kusikia jina lake likitajwa, alipoinua macho yake yaliyotandwa na machozi, alimshuhudia mwanamke mzee akianguka huku mwanaume akijaribu kumsaidia. Alipomtazama vizuri mwanaume huyo, alimkumbuka kwa haraka kuwa ni babu yake, moyo ukamlipuka paah!
Harakaharaka aliacha kila alichokuwa anakifanya, akainuka na kuanza kuelekea eneo la tukio, lakini kabla hajafika, manesi tayari walishakuwa wamemuinua mwanamke huyo mzee na kumpakiza kwenye kitanda cha magurudumu.
"Harrison! Ni wewe au naota? Mungu wangu," alisema mzee Lewis huku akitetemeka mwili mzima, akihisi amekutana na mzimu wa mjukuu wake. Harrison alishindwa cha kujibu, machozi yakawa yanamtoka. Akapiga magoti mbele ya babu yake huku akiinua mikono kwa ishara ya kuomba msamaha.
Kwa moyo wa ujasiri, mzee Lewis alimsogelea Harrison na kumpa mkono kisha akamuinua, akamsogeza kifuani kwake na kumkumbatia huku akiwa bado haamini kama ni Harrison kweli au ni mzimu wake. Harrison akawa analia kwa kwikwi huku akitamka maneno ya kumuomba msamaha babu yake na watu wengine wote.
"Kwani nini kilitokea?" alihoji mzee Lewis huku akimtoa Harrison kifauni kwake na kumfuta machozi.
***
Harrison anasababisha mshtuko mkubwa kwa ndugu zake ambao walikuwa wanaamini kuwa alishakufa siku nyingi zilizopita. Wa kwanza kushtuka hadi kupoteza fahamu ni mama yake mzazi, Skyler ambaye baada ya kumuona, anadhani amekutana na mzimu, anaanguka na kupoteza fahamu.
Majirani wanaofika kumpa msaada Skyler baada ya kusikia akipiga kelele, nao wanatoka mbio baada ya kumkuta Harrison akiwa ndani kwani wote walishaamini kwamba amekufa. Hata hivyo, wachache wenye ujasiri wanamhoji kilichotokea, anawaeleza ukweli kisha wanasaidiana kumkimbiza Skyler hospitali.
Mzee Lewis, babu yake Harrison anapopata taarifa za kuanguka kwa mwanaye Skyler, anaondoka na mkewe mpaka hospitali lakini baada ya kufika, anapigwa na butwaa baada ya kumuona Harrison. Anapomuonesha mkewe alichokiona, anapatwa na mshtuko mkubwa, naye anapoteza fahamu.
Wote wanalazwa kwenye hospitali hiyo na mzee Lewis anaanza kumhoji Harrison kilichotokea.
KABLA Harrison hajaanza kumueleza mzee Lewis kilichomtokea maishani, alianza kwa kumtambulisha Angel na mwanaye, mzee huyo akazidi kupigwa na butwaa kwani hakutegemea kuwa tayari Harrison anaweza kuwa ameoa na kuzaa.
Akiwa bado amepigwa na butwaa, Harrison alimuoneshea ishara kuwa wakakae kwenye viti vilivyokuwa pembeni ili amueleze kinagaubaga. Mzee Lewis akiwa bado amepigwa na bumbuwazi, akimshangaa mke wa Harrison na mtoto wake, alisogea mpaka kwenye viti, wote wakakaa.
Harrison alishusha tena pumzi ndefu kisha akaanza kumsimulia mzee Lewis kila kitu kilivyokuwa tangu siku aliyomkimbia Linda kanisani. Mzee huyo alikuwa akishangaa kila kitu, hakuwahi kudhani kwamba Harrison aliyekuwa anamjua, anaweza kudiriki kufanya mambo hayo kwa sababu tu ya mapenzi.
Harrison hakuacha kitu, alieleza kuanzia jinsi walivyoshirikiana na rafiki yake kutengeneza ajali feki, jinsi alivyokimbilia kwenye msitu wa Tongass na yote yaliyofuatia mpaka akafanikiwa kumpata malkia wa masokwe na kwenda naye nchini Canada alikofunga naye ndoa ya kanisani.
"Ulikosea sana Harrison, vipo vya kudanganya lakini siyo kifo. Sisi tulishakuzika ndiyo maana bibi yako na mama yako wamepoteza fahamu baada ya kukuona. Kila mtu anajua kuwa ulikufa kwa ajali na kuzikwa! Umemkosea Mungu na watu wote hasa mashabiki wako wanaokipenda kitabu chako, ulisababisha huzuni kubwa sana nchi nzima," alisema mzee Lewis huku akijifuta machozi.
"Najua kuwa nimefanya dhambi kubwa lakini mimi pia ni binadamu, niliyafanya yote hayo kwa sababu ya penzi langu kwa Angel, nawaomba sana mnisamehe na nitatubu kwa Mungu wangu," alisema Harrison huku naye akilengwalengwa na machozi kisha ukimya ukatawala, kila mmoja akazama kwenye dimbwi la mawazo.
Walikuja kuzinduliwa na nesi aliyewasogelea na kuwapa taarifa kuwa Skyler amerejewa na fahamu. Harakaharaka wote wakainuka na kutaka kukimbilia wodini lakini nesi akamzuia Harrison kwa maelezo kuwa akienda kumuona mgonjwa anaweza kumsababishia mshtuko mwingine, wazo lililoungwa mkono na mzee Lewis.
Wakakubaliana kwamba mzee huyo ndiyo aende kwanza wodini kumjenga mwanaye kisaikolojia kabla ya Harrison kuingia. Harakaharaka akaongozana na nesi hadi kwenye wodi aliyokuwa amelazwa Skyler.
Japokuwa Skyler alikuwa amesharejewa na fahamu, bado alikuwa hakumbuki vizuri kilichosababisha mpaka akafikishwa hospitalini hapo. Alipomuona baba yake, alianza kumuuliza kilichompata. Mzee Lewis akakaa pembeni ya kitanda chake na kuanza kumueleza kila kitu.
Ni hapo ndipo kumbukumbu zilipomrudia Skyler, akawa anamwambia baba yake kuwa amekutana na mzimu wa Harrison. Ilibidi mzee Lewis amuanzie mbali ili kumfanya aamini kwamba alichokiona hakikuwa mzimu bali ni Harrison mwenyewe. Haikuwa kazi nyepesi kwa Skyler kuamini alichokuwa anaambiwa na baba yake, akawa anasisitiza kuwa Harrison alishakufa.
Ilibidi mzee Lewis atoke nje na kwenda kumuita Harrison na mkewe, wakaingia wote wodini na kwenda mpaka kwenye kitanda alichokuwa amelazwa Skyler.
"Harrison! Harr…," alisema Skyler lakini akashindwa kumalizia kauli yake, akawa anaangua kilio kama mtu aliyepewa habari za msiba huku akimng'ang'ania mzee Lewis mwilini kutokana na hofu.
Mzee huyo aliendelea kumueleza kwamba alichokiona hakikuwa mzimu kama alivyokuwa akifikiria awali, akazidi kumsisitiza kwamba Harrison hakufa kama watu wote walivyokuwa wanaamini. Kwa muda wote huo, Harrison alikuwa kimya kabisa, kichwa chake akiwa amekiinamisha chini huku machozi yakimtoka.
Baada ya Skyler kutulia, Harrison alipiga magoti pembeni ya kitanda chake na kuanza kumuomba msamaha mama yake kwa yote yaliyotokea. Alimweleza kuwa hakufa kama watu wote walivyokuwa wanaamini, akaukumbatia mkono wake huku akitokwa na machozi kama chemchemi ya maji.
Skyler bado alikuwa haamini kama ni kweli Harrison hakufa, akawa anamtazama kwa makini huku akijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu. Alishindwa kuelewa nini kilichotokea mpaka watu wote wakaamini kwamba Harrison amekufa wakati siyo kweli. Hata hivyo, mzee Lewis alimwambia kuwa asiwe na wasiwasi kwani akishatoka hospitali ataelezwa kila kitu jinsi kilivyokuwa.
Skyler alishusha pumzi ndefu na kukubali kumsamehe mwanaye, akawageukia Angel na mtoto wake ambao muda wote walikuwa wametulia pembeni ya kitanda. Kabla hata hajauliza, Harrison alimuwahi na kumtambulisha Angel kama mkewe wa ndoa.
"Mungu ametujalia tumepata mtoto, anaitwa Harvey Junior," alisema Harrison huku akimshika mkono mkewe na kumsogeza jirani na mama yake. Japokuwa Skyler alikuwa na hali mbaya kitandani, aliachia tabasamu pana kusikia mtoto wa Harrison amepewa jina kama la kipenzi cha moyo wake, marehemu Harvey.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akataka apewe mtoto ili amshike, Angel akamshusha mgongoni na kumpa Skyler, akajikakamua na kumbeba huku tabasamu likizidi kuchanua usoni kwake. Alipomtazama vizuri usoni, aligundua kuwa mtoto huyo alikuwa akifanana sana na Harrison, akashindwa kujizuia kuonesha furaha yake.
Akambusu kwenye paji la uso kisha akamrudisha kwa mama yake. Wakati wote wakiendelea kufurahi, nesi alikuja kuwapa taarifa kuwa mke wa mzee Lewis aliyekuwa amelazwa kwenye wodi nyingine baada ya kuanguka na kupoteza fahamu, ameshazinduka.
Harakaharaka Harrison na babu yake, mzee Lewis walitoka na kuelekea kwenye wodi aliyokuwa amelazwa, wakamuacha Angel na mtoto wake pembeni ya Skyler. Walipofika, kama ilivyokuwa awali, Harrison alizuiwa kuingia wodini kwa kuhofia anaweza kusababisha mgonjwa akapatwa na mshtuko kwa mara nyingine.
Ikabidi asimame mlangoni wakati mzee Lewis akiingia kumtazama mkewe. Alikwenda moja kwa moja mpaka kwenye kitanda alichokuwa amelazwa, alipomuona tu, alianza kumwambia kuwa amekutana na mzimu wa Harrison. Kama alivyofanya kwa Skyler, mzee Lewis alianza kumuelewesha mkewe kwamba alichokiona siyo mzimu bali ni Harrison.
Akajaribu kumjenga kisaikolojia mpaka akaamini kwamba kumbe Harrison hakufa kama kila mtu alivyokuwa anaelewa. Alipohakikisha mkewe yupo kwenye hali nzuri kisaikolojia, alitoka na kwenda kumchukua Harrison aliyekuwa amejiinamia mlangoni, nje ya wodi aliyolazwa bibi yake. Wakaingia wote mpaka pembeni ya kitanda alicholazwa, akawa anamshangaa Harrison kwa macho ya udadisi.
Mzee Lewis akamwambia kuwa akisharuhusiwa kutoka hospitalini, atamueleza kwa kina kilichotokea, wazo ambalo mwanamke huyo alilikubali. Akawa anaendelea kumshangaa Harrison kama asiyeamini alichokuwa anakiona. Baada ya kuzungumza kidogo, wote walitoka nje kuwapisha manesi waendelee kumhudumia mgonjwa.
Baada ya muda, wagonjwa wote wawili waliruhusiwa kutoka wodini, wakaenda mpaka nyumbani kwa mzee Lewis ambapo Harrison alianza upya kuwaeleza kilichotokea kuanzia siku aliyomkimbia Linda kanisani mpaka siku hiyo. Ilikuwa ni simulizi iliyowatoa wote machozi.
***
KILA anayeufahamu ukweli kwamba kumbe Harrison hakufa kama watu wote walivyokuwa wanaamini, anapatwa na
mshtuko mkubwa na kujiuliza maswali mengi yanayokosa majibu.
Wa kwanza kushtuka hadi kupoteza fahamu ni mama yake mzazi, Skyler ambaye baada ya kumuona Harrison,
anadhani amekutana na mzimu, anaanguka na kupoteza fahamu.
Majirani wanaofika kumpa msaada Skyler baada ya kusikia akipiga kelele, nao wanatoka mbio baada ya kumkuta
Harrison akiwa ndani kwani wote walishaamini kwamba amekufa. Baadaye, bibi yake Harrison naye anapoteza
fahamu baada ya kumuona mjukuu wake. Anaamini amekutana na mzimu.
Wote wanalazwa kwenye hospitali moja na mzee Lewis anaanza kumhoji Harrison kilichotokea. Baada ya kuufahamu
ukweli, anatumia utu uzima wake kuwaelewesha Skyler na mama yake baada ya kurejewa na fahamu. Hali ya taharuki
inaendelea kutanda kila mahali, kila mmoja akiwa haamini anachokisikia.
Baada ya muda, wagonjwa wote wawili, Skyler na mama yake waliruhusiwa kutoka wodini, wakaenda mpaka nyumbani kwa mzee Lewis ambapo Harrison alianza upya kuwaeleza kilichotokea kuanzia siku aliyomkimbia Linda kanisani mpaka siku hiyo. Ilikuwa ni simulizi iliyowatoa wote machozi.
Ulikosea sana Harrison! Sijui tutazificha wapi sura zetu watu wakiufahamu ukweli, lazima watahisi kwamba ulishirikiana na sisi kwenye mpango huo mchafu, alisema Skyler huku akitokwa na machozi. Akaungwa mkono na mzee Lewis ambaye aliwaambia
watu wote kwamba anajisikia vibaya sana kugundua kuwa kumbe Harrison aliwadanganya kwa kipindi chote hicho kwamba amekufa wakati haikuwa kweli.
Nilikwambia hakuna kitu kibaya kama kujichulia kifo, inabidi tumtafute mchungaji ambaye atakuongoza kwenye sala ya toba kisha itabidi uitishe mkutano na waandishi wa habari na kuwaeleza ukweli bila kuficha chochote, watu wote waambiwe ukweli, alisema mzee Lewis, wote wakakubaliana na wazo hilo.
Wakaanza pia kumhoji kuhusu historia ya mkewe na jinsi walivyofanikiwa kumpata mtoto. Harrison alishusha pumzi ndefu na kuwatazama usoni mmoja baada ya mwingine. Akawaeleza kila kitu kuhusu Angel na jinsi alivyofanikiwa kufahamu kwamba asili yake ni nchini Tanzania.
Pia aliwaeleza kila kitu kuhusu Linda na jinsi alivyomfuatilia kimyakimya mpaka alipofanikiwa kuwakuta nchini Canada. Aliwaeleza jinsi Linda alivyojifanya hausigeli na kufanikiwa kuingia kwenye maisha yao na kitendo alichokifanya cha kujaribu kuwaua Angel na mwanaye kwa sumu.
Kila mmoja alipigwa na butwaa, wakawa wanajiuliza kama muujiza usingetokea na Harrison kuamua kurudi haraka nyumbani, nini kingewapata Angel na mwanaye? Kila mmoja kwa imani yake alimshukuru Mungu kwani muda huo wangekuwa wanazungumza habari nyingine.
Linda ana roho mbaya sana, alisema mzee Lewis lakini akapingwa vikali na Skyler na mama yake. Wote walimtetea kwamba hakuwa na roho mbaya kama walivyokuwa wanahisi bali alikuwa akilipigania penzi lake kwa sababu aliamini bado Harrison anampenda.
Ungemwambia ukweli kwamba humpendi wala asingefikia hatua ya kufanya hivyo, ulikosea sana Harrison, unapaswa kumuomba radhi yeye na watu wote uliowakosea, Skyler kwa uchungu na kuungwa mkono na mama yake.
Mjadala uliendelea kwa muda mrefu na mwisho wote wakakubaliana kwamba Linda hakuwa na makosa katika suala hilo, muafaka ukafikiwa kwamba wazazi wa Harrison, mama, bibi na babu yake waongozane mpaka nyumbani kwa wazazi wa Linda na kwenda kuzungumza nao kuhusu suala la Linda.
Hawakutaka kupoteza muda, harakaharaka wakajiandaa na safari ya kuelekea nyumbani kwa akina Linda. Harrison na mkewe ilibidi wabaki nyumbani kwao kwa sababu ya usalama wao.
***
Baada ya mzee Lewis, mkewe na Skyler kufika nyumbani kwa wazazi wa Linda, walishtushwa na umati mkubwa wa watu waliowakuta nje ya nyumba hiyo.
He! Kuna nini tena jamani? Kuna usalama kweli hapa? aliuliza mzee Lewis baada ya kuteremka kwenye gari na familia yake.
Hakuna mtu aliyewajibu, wakaongoza moja kwa moja mpaka kwenye mlango wa kuingilia ndani.
Karibuni! Karibuni sana, alisema baba yake Linda, akawapokea wageni na kuingia nao mpaka ndani ambako waliwakuta baadhi ya watu wakiwa wamekaa sebuleni huku wakiwa na nyuso za huzuni.
Vipi kuna nini mzee mwenzangu, aliuliza mzee Lewis, baba yake Linda akamvutia pembeni na kuanza kumueleza kilichokuwa kinaendelea. Akamwambia kuwa mtoto wao Linda aliyekuwa amesafiri kwa kipindi kirefu, amerejea lakini amekuja na ujumbe wa ajabu unaowafanya watu wote waamini kwamba amerukwa na akili.
Kwani amekuja na ujumbe gani?
Anasema eti Harrison hakufa bali alimkimbia na kwenda kuoana na malkia wa masokwe, nahisi penzi la mjuu wako linamfanya binti yangu awe mwendawazimu, sijui alimpa nini? alisema baba yake Linda kwa uchungu.
Akaendelea kumueleza kuwa watu wote waliokuwa wamekusanyika siku hiyo hapo nyumbani kwake walikuwa ni ndugu zake ambao waliitana kwa lengo la kujadili mustakabali wa Linda na namna ya kumsaidia kwani tangu afike, aligoma kula wala kufanya kitu chochote zaidi ya kuwa analia usiku na mchana akilitaja jina la Harrison.
Ilibidi mzee Lewis amuombe mzee mwenzake watoke nje na kwenda kuzungumza pembeni kwani alihisi endapo angemweleza ukweli palepale mbele za watu, angepata mshtuko mkubwa ambao ungeongeza matatizo kwenye familia hiyo. Baba yake Linda alikubaliana naye, wakatoka mpaka kwenye bustani ya maua na kukaa kwenye viti.
Mzee mwenzangu una kifua?
Kifua ninacho, utu uzima dawa.
Nataka nikupe ukweli wa mambo lakini nakuomba uwe na moyo wa kijasiri kwa sababu wewe ndiyo baba wa familia na kiongozi, alisema mzee Lewis na kushusha pumzi ndefu, baba yake Linda akamhakikishia kwamba hakuna kitakachoharibika.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akaanza kumueleza ukweli kwamba binti yao hakuwa amechanganyikiwa kama walivyokuwa wanadhani bali ni kweli kwamba Harrison hakufa. Akaendelea kueleza kwamba kwa muda huo wakati wanazungumza, Harrison alikuwa nyumbani kwa mama yake, Skyler akiwa na mkewe pamoja na mtoto wao kama Linda alivyokuwa amewaeleza.
Kauli hiyo ilimshangaza sana baba yake Linda, akakodoa macho kama asiyeamini alichokisikia. Mzee Lewis akaendelea kumueleza kila kitu kama alivyohadithiwa na Harrison mwenyewe kuanzia siku aliyomkimbia Linda kanisani na kila kitu kilichoendelea baada ya hapo.
Kijasho chembamba kikawa kinamtoka baba yake Linda. Alijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu lakini mwisho hakuwa na cha kufanya zaidi ya kukubaliana na ukweli. Wakawa wanajadiliana nini cha kufanya kwa sababu mpaka muda huo, Linda alikuwa kwenye hali mbaya sana na mara kwa mara alikuwa akitishia kwamba atajiua.
Baada ya kuambiwa maneno hayo, baba yake Linda alitafakari kwa dakika kadhaa kisha akaona jambo muhimu kwa wakati huo, ni kuzikutanisha familia zote mbili na kujadili kwa kina kuhusu suala hilo. Kwa kuwa tayari nyumbani kwa akina Linda kulikuwa na
watu wengi, alishauri kwamba wamchukue Linda pamoja na mama yake kisha wakalijadili suala hilo nyumbani kwa mama yake Harrison, kila mmoja akiwepo.
***
Kuonekana upya kwa Harrison baada ya kutoweka kwa kipindi kirefu, kunasababisha sintofahamu kubwa huku baadhi ya watu waliomuona wakihisi wamekutana na mzimu. Karibu kila mtu alishaamini kwamba kijana huyo alikufa kwenye ajali ya barabarani na kuzikwa kwenye Makaburi ya Miami Cemetery hivyo kuonekana kwake kunazua maswali mengi.
Mama mzazi wa
Harrison, Skyler aliyekuwa wa kwanza kumuona, anaanguka na kupoteza fahamu akidhani amekutana
na mzimu. Hali hiyo inamtokea pia bibi yake Harrison na majirani kadhaa. Babu yake, mzee Lewis
anamkabili Harrison na kumuuliza kilichotokea ambapo anamueleza kila kitu.
Mzee huyo anabeba jukumu la kuwaelewesha watu wote ukweli juu ya Harrison, anafanya kazi hiyo
nzito na baada ya muda, baadhi ya watu wanaanza kuelewa na kuamini maelezo hayo.
Upande wa pili, Linda amesharejea nyumbani kwao lakini bado hataki kukubaliana na ukweli kwamba
Harrison hampendi bali anampenda mkewe, Angel. Hali hiyo inasababisha ndugu zake waitane kwa ajili ya kikao cha familia kwani anagoma mpaka kula kisa kikiwa ni penzi la Harrison.
Baada ya kuambiwa maneno hayo, baba yake Linda alitafakari kwa dakika kadhaa kisha akaona jambo muhimu kwa wakati huo, ni kuzikutanisha familia zote mbili na kujadili kwa kina kuhusu suala hilo. Kwa kuwa tayari nyumbani kwa akina Linda kulikuwa na watu wengi, alishauri kwamba wamchukue Linda pamoja na mama yake kisha wakalijadili suala hilo nyumbani kwa mama yake Harrison, kila mmoja akiwepo.
Waliondoka kwa kutumia magari mawili tofauti, Linda alipanda gari moja na baba na mama yake wakati mzee Lewis aliondoka na mkewe na Skyler kwa kutumia gari lingine. Njia nzima, Linda alikuwa akiendelea kulia, akiwa amejilaza kwenye kifua cha mama yake aliyekuwa na kazi ya ziada kumbembeleza.
Mzee Lewis, mkewe na Skyler ndiyo walikuwa wa kwanza kufika, wakawaambia Harrison, mkewe na mtoto wao waingie chumbani kwanza mpaka watakapowaita, harakaharaka wakasaidiana kupanga viti na kuiweka sebule katika hali nzuri, tayari kwa kikao.
Muda mfupi baadaye, Linda na wazazi wake waliwasili, wakapokelewa na kupelekwa moja kwa moja sebuleni. Mzee Lewis, mkewe, Skyler na Harrison nao wakatoka na kuungana na wageni sebuleni. Angel aliendelea kubaki chumbani na mwanaye, kikao kikaanza.
Wa kwanza kuzungumza alikuwa ni mzee Lewis aliyetumia busara za hali ya juu kujaribu kumuweka sawa Linda ili aone kwamba kilichotokea ni jambo la kawaida. Alimlaumu Harrison kwa kitendo alichokifanya na kumtaka kabla hawajaendelea mbele, awaombe radhi watu wote waliokuwa kwenye kikao hicho.
Harrison alikubali kutii agizo hilo na kuwaomba radhi wote kwa kilichotokea, akakiri kwamba ni kweli alikosea sana kumkimbia Linda kanisani na baadaye kudanganya kwamba amekufa. Alijitetea kwamba alikuwa hajielewi ndiyo maana akafanya yote hayo.
Baada ya kuomba radhi kwa takribani dakika kumi na tano, kikao kiliendelea. Linda naye akapewa nafasi ya kueleza yaliyokuwa ndani ya moyo wake. Kazi haikuwa nyepesi kwani kila baada ya kuongea kidogo, Linda alikuwa akishindwa kuendelea kutokana na kubanwa na kilio cha kwikwi. Mama yake akawa na kazi ya ziada ya kumtuliza.
"Licha ya yote aliyonifanyia, ba..do na...mpenda sana Harri…son, nata…ka anioe ni..we…." alisema Linda na kushindwa kumalizia alichotaka kukisema, akawa analia kwa kwikwi kiasi cha kuwatoa machozi wote waliokuwa ndani ya nyumba hiyo.
Hata hivyo, ilibidi busara zitumike kuweka mambo sawa, Linda akafafanuliwa kwamba tayari Harrison alishaoa, tena kwa ndoa ya kanisani hivyo asingeweza kumuacha mkewe ambaye amezaa naye wala asingeweza kuoa mke wa pili.
Awali Linda aling'ang'ania sana msimamo wake lakini kwa kadiri alivyokuwa anazidi kupewa nasaha na kuelezwa kwamba kila jambo lina sababu yake, taratibu alianza kuelewa. Akaendelea kupokea nasaha mfululizo kutoka kwa bibi, babu na mama yake Harrison pamoja na wazazi wake ambao kwa pamoja walimueleza kuwa Harrison hakuwa riziki yake na ndiyo maana hayo yote yalitokea.
"Wewe bado ni msichana mrembo ambaye huwezi kukosa mume mzuri wa kukuoa. Isitoshe umesoma sana, familia yako ina uwezo mkubwa wa kiuchumi! Una kila kitu cha muhimu kwa hiyo usiumie sana ndani ya moyo wako. Ukubali ukweli hata kama unaumiza namna gani kisha songa mbele na maisha yako bila Harrison," alisema mzee Lewis na kuungwa mkono na baba yake Linda.
Kikao kiliendelea kwa muda mrefu, Linda akakubali kwa shingo upande kumuacha Harrison aendelee na maisha yake na familia yake lakini akaomba waendelee kuwa marafiki wa kawaida. Baada ya kauli hiyo, watu wote walimpigia makofi na kumshangilia kutokana na ukomavu aliouonesha.
Angel akaenda kuitwa na kuelezwa muafaka uliofikiwa. Naye kwa upande wake alionesha kufurahi sana kwani licha ya kwamba alikuwa anamuonea huruma Linda kwa kilichotokea, alitamani kuona amani inarejea kwenye ndoa yake na kumuombea siku moja apate mume mzuri watakayejenga naye familia.
Kwa furaha, Angel aliwashukuru wote kwa kazi kubwa waliyoifanya kisha wakapatanishwa na Linda, wakakumbatiana kwa zaidi ya dakika mbili huku kila mmoja akitokwa na machozi. Baada ya hapo, wote walioshiriki kazi hiyo walianza kupeana mikono kama ishara ya upatanisho, Linda na Harrison nao wakapeana mikono kuashiria kwamba mambo yote yamekwisha.
"Kazi iliyobaki kama tulivyokubaliana awali ni kwa Harrison kuitisha mkutano na waandishi wa habari kisha kuwaeleza ukweli wote na kuwaomba radhi mashabiki wako na watu wote ambao waliguswa na taarifa za uongo juu ya kifo chako," alisema mzee Lewis, wote wakaliunga mkono wazo hilo.
Waliagana, Linda akaondoka na wazazi wake akiwa kwenye hali tofauti na aliyokuwa nayo wakati akiwasili nyumbani hapo. Huku nyuma, Angel na Harrison walikumbatiana kwa furaha kwani hatimaye, amani ilikuwa imerejea ndani ya ndoa yao baada ya kuhangaika kwa kipindi kirefu.
Harrison alikumbatiana pia na mama yake, Skyler kisha babu na bibi yake ambao wote kwa pamoja walikuwa na furaha ya hali ya juu baada ya Linda kuamua kuukubali ukweli. Mipango ya Harrison kwenda kuzungumza na waandishi wa habari ikaanza kupangwa.
Siku mbili baadaye, Harrison akiwa ameongozana na mkewe, mwanaye, mama yake, bibi na babu yake,
alikwenda mpaka kwenye ofisi za shirika la habari la serikali ambako alikuta waandishi wengi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsubiri kwa shauku kwani walishakuwa na taarifa juu ya azma yake ya kuzungumza na vyombo vya habari baada ya ‘kufufuka'.
Muda mfupi baadaye, picha na sauti ya Harrison vikawa vinasikika na kutazamwa na mamilioni ya Wamarekani. Kila aliyesikia habari hiyo kwamba kumbe Harrison hakufa, alipigwa na butwaa na kushindwa kuamini haraka. Hata hivyo, huo ndiyo ulikuwa ukweli.
"Nawaomba watu wote ambao kwa namna moja au nyingine mliguswa na tukio hilo mnisamehe. Nimeshamuomba msamaha Linda lakini narudia tena, nataka watu wote wajue kwamba nilifanya makosa ambayo mpaka leo nayajutia, namuomba Mungu wangu na watu wote mnisamehe kwa hili," alikaririwa Harrison wakati akiongea na waandishi wa habari.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo, licha ya kuomba msamaha, Harrison na rafiki yake waliyeshirikiana kuandaa ajali feki, walikuwa na kesi ya kujibu mahakamani ambapo pia walitakiwa kueleza mahali walipoipata
maiti waliyoitumia. Baada ya kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali, Harrison, familia yake na ndugu zake walitoka kwenye ukumbi wa mikutano.
Walipofika nje, wote walishtuka baada ya kuwakuta polisi kadhaa wenye silaha wakiwa wanamsubiri Harrison.
Wakamfunga pingu na kuondoka naye mpaka kwenye Kituo cha Polisi cha Miami alikotakiwa kutoa maelezo ya kutosha juu ya mahali alikoipata maiti waliyoitumia kuandaa ajali feki. Alipomtaja rafiki yake waliyeshirikiana kwenye tukio hilo, naye alienda kukamatwa siku hiyohiyo.
***
SIRI aliyoificha Harrison kwa kipindi kirefu inafichuka. Inabainika kwamba kumbe hakufa bali alimkimbia Linda kabla hawajafunga ndoa, kisha akatengeneza ajali feki ambayo ilionesha kwamba amekufa.Akakimbilia kwenye Msitu wa Tongass kumsaka malkia wa masokwe.
Baada ya miaka mingi kupita, akiwa tayari ameshamuoa malkia wa masokwe, anaamua kurejea nyumbani kwao ambapo ujio wake unasababisha kizaazaa kikubwa.
Baadaye anaeleza ukweli na kuwaomba radhi watu wote kwa kilichotokea. Kikao cha kifamilia kinafanyika na kuombana msamaha.
Baadaye Harrison anaitisha mkutano wa waandishi wa habari na kueleza ukweli lakini muda mfupi baada ya kumaliza kueleza kila kitu, anawekwa chini ya ulinzi na askari wenye silaha.
Askari hao wenye silaha wakamfunga pingu na kuondoka naye mpaka kwenye Kituo cha Polisi cha Miami alikotakiwa kutoa maelezo ya kutosha juu ya mahali alikoipata maiti waliyoitumia kuandaa ajali feki, kama alivyoeleza mbele ya waandishi wa habari.
Alipomtaja rafiki yake waliyeshirikiana kwenye tukio hilo, Daktari Rogers ambaye ndiye aliyefanikisha mpango wa kupatikana kwa maiti, naye alienda kukamatwa siku hiyohiyo na kuunganishwa na Harrison, wakawekwa nyuma ya nondo.
Baada ya wote wawili kukamatwa na kupelekwa mpaka kwenye Kituo Kikuu cha Polisi cha Miami, taratibu za kuwaburuza mahakamani zilianza kufanywa haraka iwezekanavyo. Shinikizo kutoka kwa viongozi wa
jeshi la polisi nchini humo lilikuwa kubwa kwani walijua wakiwaachia bila kuwachukulia hatua yoyote, wananchi watawadharau na hadhi yao mbele ya jamii itashuka sana.
Hata hivyo, kwa kuwa mahojiano aliyokuwa akiyafanya Harrison na waandishi wa habari yalionekana na watu wengi, mawakili wengi kutoka pande mbalimbali za nchi hiyo walijitokeza kutaka kumsaidia. Kila
mmoja alijua wakati anafanya kosa hilo, hakuwa sawa kiakili na ndiyo maana alifikia hatua ya kufanya tukio la ajabu kiasi hicho.
Gumzo nchini Marekani likawa ni habari ya Harrison ambapo kila mtu alikuwa akisema lake. Wanaharakati wa haki za wanawake, walikilaani mno kitendo cha Harrison kumkimbia Linda kanisani wakati kila kitu kilishakamilika. Wakasisitiza kwamba alikuwa na nafasi ya kumweleza ukweli kuliko mateso aliyomsababishia.
Hata hivyo, kwa sababu mwenyewe alikiri kufanya makosa na kuwaomba radhi wote aliowakosea akiwemo Linda, baadhi walimsamehe ingawa kuna kundi dogo bado liliendelea kumsakama kwa kitendo alichokifanya.
Harrison aliendelea kutawala kwenye vyombo vya habari, runinga, redio na magazeti vyote vikawa vinazungumzia kwa kina mazungumzo yake aliyoyafanya na waandishi wa habari na hatua ambazo jeshi la polisi lilimchukulia kutokana na alichokifanya. Wazazi na ndugu zake pamoja na ndugu wa Linda walikuwa pamoja na Harrison kwani walikubali kuupokea msamaha wake kwa dhati.
Angel ndiyo alikuwa na hali mbaya zaidi kutokana na kukamatwa kwa mumewe, akawa analia muda wote, hali iliyowapa kazi ya ziada mama yake Harrison, bibi na babu yake. Alikuwa na wasiwasi mkubwa kuwa
huenda mumewe akahukumiwa kifungo kirefu gerezani, jambo ambalo hakuwa tayari kuona linatokea.
Wakawa wanambembeleza na kumweleza kuwa kila kitu kitapita, wote wakawa wanashinda nje ya Kituo Kikuu cha Polisi cha Miami wakijaribu kutafuta njia ya kumuwekea dhamana. Hata hivyo, kutokana na uzito wa kesi iliyokuwa inamkabili, hakupata dhamana kwa urahisi. Siku ya kwanza ikapita wakiwa nyuma ya nondo.
Siku iliyofuata, kesi yao ilisomwa kwa mara ya kwanza mahakamani ambapo Harrison na mwenzake walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matatu; kumuua mtu kisha kutumia maiti yake kuudanganya ulimwengu kwamba ni Harrison, kupanga njama na kufanya udanganyifu.
Timu ya mawakili watano walijipanga kuwatetea Harrison na mwenzake na baada ya kesi hiyo kutajwa, mawakili hao ambao awali walifanya mazungumzo ya kina na Harrison pamoja na mwenzake, Dokta Rogers wakiwa mahabusu.
Kesi ilipoanza kunguruma, mawakili hao walianza kuwatetea wateja wao. Wakaieleza mahakama kwamba hawakumuua mtu yeyote kama mashtaka yao yalivyokuwa yanasema bali maiti waliyoitumia ilichukuliwa kutoka kwenye mochwari ya hospitali ambayo Rogers alikuwa akifanyia kazi.
Mtukufu hakimu, maiti iliyotumika ilikuwa imekaa zaidi ya siku nne ndani ya mochwari na mipango ilishaanza kufanywa ili ikazikwe na manispaa. Hivi hapa ni vithibisho vyake, alisema wakili mmoja huku akiweka mezani cheti cha kifo cha maiti iliyotumika.
Wakili mwingine alieleza kuwa wakati mteja wao anafanya yote hayo, hakuwa sawa kiakili kutokana na kushinikizwa kumuoa mwanamke ambaye hakuwa akimpenda kutoka ndani ya moyo wake. Kesi iliendelea
kuunguruma kwa saa kadhaa huku pande mbili za mawakili wa upande wa serikali na wa upande wa Harrison na mwenzake wakivutana.
Mpaka muda wa mahakama unaisha, tayari Harrison na mwenzake walikuwa wameyapangua mashtaka ya mauaji na kubakiza mashtaka mawili ya kupanga njama na udanganyifu ambayo hata hivyo, kisheria yalikuwa na dhamana. Taratibu zikafanywa na ndugu zao kisha wote wawili wakaachiwa kwa dhamana.
Ilikuwa ni furaha iliyoje kwa Angel na familia nzima ya Harrison. Akakumbatiana na ndugu zake kwa furaha na kurudi hadi nyumbani kusubiri siku nyingine ya mashtaka yao kusomwa. Habari hiyo pia
ilitangazwa sana na vyombo vya habari, jina la Harrison likazidi kuwa maarufu midomoni mwa watu huku mauzo ya kitabu chake cha Queen of Gorillas yakizidi kuongezeka.
Kila mtu alikuwa na hamu ya kukisoma kitabu hicho ambacho kilikuwa kinaelezea jinsi Harrison alivyokutana na malkia wa masokwe kwa mara ya kwanza. Mauzo hayo yalizidi kuitunisha akaunti yake na kumfanya apate fedha nyingi.
Siku zilizidi kusonga mbele, hatimaye tarehe ya kutajwa tena kwa kesi iliyokuwa ikimkabili Harrison iliwadia. Wakaenda tena mahakamani ambapo kesi ilianza kunguruma huku umati mkubwa wa watu wakiwa wamehudhuria mahakamani sambamba na waandishi wa vyombo vya habari.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Katika hali ambayo wengi hawakuitegemea, hakimu alipoisoma kesi hiyo, mwanasheria mkuu wa serikali aliwasilisha hati maalum kutoka kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ya Marekani (DPP), James
Conrad na kuieleza mahakama kuwa baada ya kuupitia mwenendo mzima wa kesi hiyo na mazingira ambayo tukio hilo lilitokea, aliamua kuwafutia mashtaka Harrison na Rogers.
Hakimu akagonga nyundo mezani na shangwe za hapa na pale zikatawala mahakamani, Harrison akawa anakumbatiana na mawakili wake pamoja na ndugu zake na mashabiki wengi waliokuwa wamefurika
mahakamani. Hoihoi, nderemo na vifijo vikatawala eneo lote la mahakama mpaka umati ulipoanza kuondoka kuelekea nyumbani kwa akina Harrison.
Nakupenda sana mume wangu, narudia tena kukuhakikishia kwamba nitakupenda mpaka mwisho wa maisha yangu, alisema Angel huku akitokwa na machozi ya furaha, akakumbatiana na Harrison kimahaba. Watu waliokuwa wamewazunguka wakawa wanashangilia kwa nguvu.
Huo ukawa mwanzo wa maisha mapya ya uhuru wa Harrison na familia yake. Waandishi mbalimbali waliendelea kumtembelea nyumbani kwa mama yake na kumhoji maswali mbalimbali kuhusu ugumu alioupata mpaka alipofanikiwa kumpata malkia wa masokwe. Ilikuwa ni simulizi ya mapenzi iliyomsisimua kila aliyeisikia.
Baada ya wiki moja, Harrison na mkewe walianza maandalizi ya safari ya kwenda Tanzania kumtafuta baba mzazi wa Angel na kuijua vyema asili ya msichana huyo ambaye sasa alikuwa ni mke wake halali, akiwa na baraka zote kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Harrison.
***
Baada ya kuficha siri kwa kipindi kirefu juu ya mahali alipokuwa amejificha, hatimaye siri inafichuka kwamba kumbe Harrison hakufa kama watu wote walivyokuwa wanaamini. Linda ndiyo anakuwa wa kwanza kugundua kuwa kumbe Harrison alitengeneza ajali feki kisha akakimbilia kwenye Msitu wa Tongass kumsaka malkia wa masokwe.
Anaumia sana kuujua ukweli huo na anafuatilia nyendo zake kimyakimya mpaka alipofanikiwa kumkuta nchini Canada. Kufichuka kwa siri hiyo kunazusha tafrani ya hali ya juu. Harrison anarejea nyumbani kwao akiwa na mkewe na mtoto wao na kila anayemuona anahisi amekutana na jini.
Baadaye anaeleza ukweli na kuwaomba radhi watu wote kwa kilichotokea. Kikao cha kifamilia kinafanyika na kuombana msamaha na Linda kisha anaenda kuzungumza na waandishi wa habari kueleza ukweli wa tukio lote. Sakata
linakuwa kubwa kwani Harrison na rafiki yake wananaswa na mkono wa sheria ingawa kwa bahati nzuri, wanatetewa na mawakili wazoefu kisha wanaachiwa huru.
Anaungana tena na familia yake na mipango ya kusafiri mpaka Tanzania kumtafuta baba mzazi wa mkewe, Angel inaanza.
Baada ya wiki moja, Harrison na mkewe walianza maandalizi ya safari ya kwenda Tanzania kumtafuta baba mzazi wa Angel na kuijua vyema asili ya msichana huyo ambaye sasa alikuwa ni mke wake halali, akiwa na baraka zote kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Harrison.
Baada ya maandalizi yote kukamilika, Harrison, mkewe na mtoto wao, Harvey Junior walisindikizwa na ndugu jamaa na marafiki mpaka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami (MIA). Kwa kuwa tayari walishakata tiketi za ndege, waliingia kwenye ukumbi maalum wa kusubiria ndege. Mzee Lewis, mkewe na Skyler, wao hawakutaka kuondoka mpaka wahakikishe Harrison na mkewe wameshapanda ndege.
Wakakaa nao sehemu ya kusubiria ndege mpaka matangazo yalipoanza kusikikia kupitia vipaza sauti vilivyokuwa uwanjani hapo, yakiwataarifu abiria wa ndege namba 876Q, Airbus 380 mali ya Kampuni ya Travelocity kujiandaa kuingia kwenye ndege.
Harrison alikumbatiana na babu yake, bibi yake kisha mama yake mzazi, Skyler ambaye alimpa baraka zote na kumuombea dua katika safari yake.
Naamini Mungu atawasimamia, nawaombea muende salama, mfanikiwe kumpata mzee Charwe kisha mrudi salama kuendelea na maisha yenu ya ndoa, nawapenda sana, alisema Skyler huku akiwakumbatia Harrison na mkewe, Angel. Baada ya kumaliza kuagana na kutakiana heri ya safari, Harrison na mkewe waliingia sehemu ya ukaguzi wa abiria na mizigo uwanjani hapo.
Taratibu zote za kiusalama zilipokamilika, waliruhusiwa kwenda mpaka mahali ndege ilipokuwa imesimama ikisubiri abiria. Harrison akiwa amembeba mwanaye Harvey Junior na kumshika mkono mkewe, Angel, walitembea taratibu mpaka kwenye ngazi, wakapanda na kuingia ndani ya ndege, wakaenda kwenye siti zao na kukaa huku kila mmoja akiwa kimya.
Angel alikuwa akijihisi kama yupo ndotoni kwani tangu alipopata akili zake timamu, hakuwahi kudhani kwamba ana ndugu. Alishaamini kwamba masokwe waliokuwa wakimlea, kumlinda na kumtunza tangu alipokuwa mdogo ndiyo ndugu zake. Mawazo mengi yaliendelea kupita ndani ya kichwa chake, akijiuliza baba yake yukoje, sura yake ikoje na kama anao watoto wengine zaidi yake, wako wapi na wana umri gani.
Wakati mawazo yakiendelea kupita kwenye kichwa cha Angel, Harrison naye alikuwa akiwaza ya kwake. Alimshukuru sana Mungu wake kwa kufanikiwa kulimaliza salama sakata la Linda. Alijiona ni mwenye bahati ya kipekee kwa kufanikiwa kumaliza kila kitu kwa amani.
Sauti laini ya mhudumu wa ndege iliyokuwa ikisikika kupitia vipaza sauti vilivyokuwa ndani ya ndege ikiwahimiza abiria wote kufunga mikanda, ndiyo iliyowazindua wanandoa hao kutoka kwenye dimbwi la mawazo. Harakaharaka Harrison alimsaidia mkewe kumfunga mkanda kisha na yeye akajifunga na kumpakata vizuri mtoto wao, Harvey Junior.
Ndege ikaanza kujongea taratibu kuelekea kwenye njia za kurukia (runways). Baada ya muda mfupi, tayari ilishakuwa imegeuka kuelekea upande wa kurukia, ikawa inaongeza kasi kwa kadiri muda ulivyokuwa unaenda. Ikakimbia kwa kasi mpaka ilipokaribia mwisho wa uwanja, taratibu ikaiacha ardhi ya Miami na kupaa angani, ikapotelea mawinguni.
Harrison na mkewe waliendelea kuzungumza mambo mbalimbali, wakitaniana na kuchekeshana mara kwa mara kama ilivyokuwa kawaida yao. Baada ya takribani saa nane angani, sauti ya mhudumu ilisikika kwa mara nyingine ikiwataka abiria kufunga mikanda kwani ndege ilikuwa ikijiandaa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Wote walifunga mikanda kisha kwa kupitia madirisha madogo ya ndege hiyo, wakawa wanaangalia mandhari ya Jiji la Dar es Salaam. Ndege ikaanza kutua, baada ya dakika kadhaa, tayari ilishasimama na milango ikafunguliwa. Abiria wakaanza kuteremka, wakiwemo Harrison, mkewe na mtoto wao.
Kila kitu kilikuwa kigeni kwao kwani hakuna aliyewahi kufika Tanzania kabla, kwa msaada wa kitabu chenye ramani ya Tanzania kilichotengenezwa maalum kwa ajili ya kuwaongoza watalii, Harrison na mkewe waliondoka uwanjani hapo baada ya taratibu zote za kiusalama kukamilika kisha wakaelekea kwenye Hoteli ya The Southern Sun, katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Dereva teksi aliyewapakiza, alikuwa akiwaelewesha vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na majina ya mitaa na vivutio vingine vilivyopo jijini Dar es Salaam ikiwemo sanamu ya askari iliyopo katikati ya jiji. Wote walifurahia sana kufika Tanzania, nchi ambayo walikuwa wakizisikia sifa zake nzuri kupitia vyombo vya habari.
Siku iliyofuatia, kwa kutumia maelezo yaliyokuwa kwenye kitabu maalum cha watalii, Harrison na mkewe waliwahi kuamka na kukodi teksi iliyowapeleka mpaka Stendi Kuu ya Mabasi ya Mikoani, Ubungo. Kwa kuwa waliwahi, walipouliza kwa wapiga debe kituoni hapo, walielekezwa kwenye basi la Zuberi lililokuwa linakwenda Bukoba.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa bahati nzuri, walifanikiwa kupata siti mbili kwenye basi hilo, wakalipa nauli na kuanza kusubiri muda wa basi kuanza safari. Kila kitu kilikuwa kigeni kwao kuanzia utaratibu uliokuwepo kwenye stendi hiyo, mpangilio wa mabasi, wingi wa abiria na mambo mengine mengi ambayo hawakuwahi kuyaona huko walikotoka.
Baada ya takribani dakika arobaini tangu walipopanda basi, safari ya kuelekea Bukoba ilianza. Wakawa wanaendelea kushangaa mambo mbalimbali waliyokuwa wanayaona njiani. Safari ilipamba moto, wakasafiri kwa kilometa nyingi wakikatisha kwenye mapori, misitu, milima na mabonde.
Baada ya kufika Kahama, ikiwa tayari ni usiku sana, kondakta wa basi walilopanda aliwapa taarifa abiria wote kwamba basi halitaendelea na safari hivyo watalazimika kulala hapo Kahama mpaka alfajiri ya siku ya pili, taarifa ambayo iliwashangaza sana Harrison na mkewe.
Walipohoji zaidi, waliambiwa kuwa kulikuwa na tishio la kutekwa na majambazi kwani tayari ilikuwa ni usiku sana na kipande cha barabara kilichobakia kabla ya kufika Bukoba kilikuwa na msitu mnene ambao ulikuwa ukitumika kama maficho ya majambazi.
Isitoshe barabara ni mbaya sana, hatuwezi kuendelea na safari usiku huu, tusipotekwa na majambazi basi huenda tukapata ajali. Tunafanya hivi kwa sababu ya usalama wa abiria wetu, kondakta aliwafafanulia, ikabidi wakubaliane naye. Kama ilivyokuwa kwa abiria wengine, walilazimika kuteremka kwenda kutafuta vyakula.
Vyakula vingi vilivyokuwa vinauzwa kwenye mji huo vilikuwa vigeni kwao lakini kwa kuwa walikuwa na njaa na hakukuwa na uwezekano wa kupata vyakula walivyovizoea, iliwalazimu kula hivyohivyo. Baada ya kushiba, walirudi kwenye basi na kulala humohumo kama walivyoelezwa na kondakta.
Kutokana na uchovu waliokuwa nao, walipitiwa na usingizi mpaka alfajiri ya siku ya pili. Kulipopambazuka tu, waliendelea na safari kwa kupitia Barabara ya Runzewe na Nyakanazi. Baada ya safari ngumu, hatimaye waliwasili kwenye mji uliokuwa umetawaliwa na uoto wa asili wa rangi ya kijani, ukipambwa na migomba mingi.
Haya tumefika Bukoba jamani, kila mmoja achunge mizigo yake wakati wa kuteremka, kondakta aliwaambia abiria, Harrison na mkewe wakaanza kuweka mizigo yao vizuri huku wakiendelea kushangaa mandhari tulivu na ya kuvutia ya Mji wa Bukoba. Hatimaye basi la Zuberi walilokuwa wamepanda liliwasili kwenye Stendi Kuu ya Bukoba, abiria wote wakateremka, wakiwemo Harrison, mkewe na mtoto wao.
***
Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu. Maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana, yanapita kama maua yachanuavyo na kunyauka. Wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unapumua, ni vyema basi kufikiria maisha baada ya kifo.
Kila siku jiulize: Hivi nikifa leo nitakwenda jehanam au peponi? Kila mmoja wetu analo jibu lake, bila shaka sote tungependa kwenda peponi. Kama hivyo ndivyo, basi tiketi ya kwenda huko ni matendo mema na kujiepusha na uovu. Tukumbuke mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele.
BAADA ya safari ndefu ya hadithi hii ya Queen of Gorillas (Malkia wa Masokwe), hatimaye leo tumefikia sehemu ya mwisho. Tumeona jinsi siri
aliyoificha kijana Harrison kwa kipindi kirefu na kuudanganya ulimwengu kwamba amekufa ilivyofichuka na kuishangaza dunia nzima.
Ukweli unafahamika kwamba kijana huyo hakufa bali alimkimbia Linda kanisani kwani hakutaka kufunga naye ndoa kwa sababu hakuwa
akimpenda kama alivyokuwa akimpenda malkia wa masokwe. Baada ya kila kitu kuwa hadharani, kijana huyo anaomba radhi kwa kila mtu.
Sakata linakuwa kubwa kwani Harrison na rafiki yake wananaswa na mkono wa sheria ingawa kwa bahati nzuri, wanatetewa na mawakili
wazoefu kisha wanaachiwa huru. Harrison na mkewe wanasafiri pamoja na mtoto wao, Harvey Junior mpaka nchini Tanzania.
Lengo lao ni kwenda kumtafuta mzee Abdulkarim Charwe, baba mzazi wa Angel ambaye waliambiwa kwamba anaishi Bukoba, Tanzania. Tayari
wameshawasili nchini Tanzania na kusafiri kwa basi hadi Bukoba.
Baada ya kuwasili mjini Bukoba, Harrison na mkewe walianza kuwauliza wenyeji kama kuna mtu aliyekuwa akimfahamu mzee
Abdulkarim Charwe. Kutokana na umaarufu aliokuwa nao mzee huyo kwa sababu ya historia ya maisha yake aliyokuwa anaipitia, hawakupata shida.
Mnamuulizia yule mzee Charwe aliyekuwaga Ulaya? Twendeni niwapeleke, alisema mwanaume mmoja kwa lafudhi ya Kihaya,
akionekana ametoka shambani, begani akiwa na mkungu wa ndizi na jembe. Akaushusha mzigo wake na kuanza kuwaongoza
Harrison na mkewe mpaka nje kidogo ya mji.
Mnaiona ile nyumba pale? Ndipo anapoishi Charwe lakini sijui kama mtaelewana naye kwani tangu afiwe na mkewe na mwanaye
miaka mingi iliyopita, amekuwa kama kichaa, alisema mwanaume huyo huku akiwaonesha kwa kidole mahali palipokuwa na
kijumba kidogo cha bati, kilichozungukwa na migomba mingi.
Harrison na mkewe walitazamana kama wasioamini walichokisikia na walichokiona. Ilikuwa vigumu kwao kuamini kwamba daktari
mashuhuri aliyefanya kazi mpaka Makao Makuu ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), jijini Geneva, Uswisi ndiyo
alikuwa akiishi kwenye kibanda hicho.
Hata hivyo, walipiga moyo konde na kusonga mbele, wakasogea mpaka kwenye mlango wa kijumba hicho, wakapokelewa na
harufu nzito ya uvundo kutoka ndani. Kila mmoja akashika pua yake.
Harrison alibisha hodi huku mkewe akiwa nyuma yake lakini hawakuitikiwa, ikabidi asukume mlango kwa tahadhari kubwa na
kuingia ndani, walichokutana nacho kiliwasikitisha mno. Mwanaume mzee aliyekuwa na mvi nyingi, mwili wake ukiwa umedhoofika
mno, alikuwa amelala juu ya kitanda huku akionesha kutokuwa na nguvu hata za kuinuka.
Harrison alipojaribu kumsemesha, alifumbua macho na kuanza kuwatazama mmoja baada ya mwingine huku akishangaa ni akina
nani na wamefikaje hapo. Kwa taabu alifumbua mdomo wake na kuwauliza, Harrison akaanza kwa kujitambulisha kisha
akamueleza kuwa walikuwa wakimtafuta mzee Abdulkarim Charwe. Kwa taabu, mzee huyo aliitikia kwamba ni yeye, akamuomba
amsaidie kuamka kitandani na kuegemea ukutani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mnasemaje na mmelijuaje jina langu, alisema mzee huyo huku akimkazia macho Angel kama anayejaribu kukumbuka kitu
kichwani mwake. Harrison akamuuliza kama alikuwa anamfahamu Charlotte Charwe. Swali hilo lilizidi kumshtua mzee huyo,
akazidi kuwakazia macho wote wawili, akashusha pumzi ndefu kisha akamtazama tena Angel.
Machozi yakaanza kumtoka kama anayekumbuka kitu. Akamjibu Harrison kuwa huyo Charlotte alikuwa ni mwanaye wa kipekee
aliyekufa na mkewe, Anganile kwenye ajali ya ndege iliyotokea eneo la Tongass, kwenye mpaka wa Marekani na Canada miaka
mingi iliyopita. Alilia kwa uchungu sana huku bado akiendelea kumtazama Anganile.
Kabla hata hajasema chochote, Harrison alianza kumueleza kwamba mwanaye Charlotte hakufa kwenye ajali hiyo bali aliangukia
kwenye msitu mkubwa wa Tongass na kulelewa na masokwe mpaka yeye alipokutana naye. Akamueleza kwamba msichana
aliyekuwa anamtazama mbele yake ndiyo alikuwa Charlotte, jambo lililomshtua sana mzee huyo aliyekuwa kwenye hatua za
mwisho za uhai wake.
Kwa kuwatazama sura, kweli Angel na mzee huyo walikuwa wamefanana sana, kuanzia macho, pua, mdomo mpaka jinsi sura zao
zilivyoumbika. Akawa analia kwa uchungu huku akiwa amemkumbatia Angel (Charlotte) kwa nguvu. Akamwambia Harrison
kwamba inawezekana Mungu alimuweka hai mpaka muda huo kwa makusudi ili asife mpaka atakapomuona binti yake huyo.
Harrison akamsimulia kila kitu jinsi alivyomuokota msichana huyo msituni, alivyotoroka naye na kuamua kuishi naye kama mume na
mke kwa uhalali. Mzee huyo alifurahi mno, akawapa baraka zote na kuwatakia maisha mema yenye mafanikio na furaha. Akaomba
amshike mjukuu wake, Harvey Junior. Baada ya kumshika kidogo, aliomba apokewe kisha akaomba maji ya kunywa.
Kwa kuwa Angel (Charlotte) alikuwa na chupa ya maji, alimpa baba yake huku akitokwa na machozi. Alipokunywa tu,
alitabasamu kisha akalala na kufumba macho huku akiwa bado ametabasamu, akatulia kimya. Tayari roho na mwili wake
vilishatengana. Harrison na Charlotte wakaanza kulia kwa sauti, kitendo kilichowakusanya majirani wengi.
Msiba ukafanyika kwa mila za watu wa Bukoba na kesho yake, mzee huyo alizikwa nyuma ya nyumba yake, katikati ya migomba
huku kila mmoja akiliona tukio hilo kama muujiza kwamba baada ya kuteseka kwa kipindi kirefu, mzee huyo alikufa muda mfupi
baada ya kumuona binti yake ambaye aliamini ameshakufa.
Harrison na Charlotte walikaa kwa siku arobaini mjini Bukoba, baada ya hapo walienda kulijengea kaburi la mzee Charwe vizuri
kisha wakasafiri na mtoto wao kurejea Miami, Marekani walikowasimulia watu wote walichokutana nacho. Kila mtu aliyesikia
kilichotokea alisikitika sana, mzee Lewis akaitumia nafasi hiyo kumuelezea Harrison historia ya maisha ya baba yake, Harvey.
Alimueleza jinsi alivyokutana na baba yake aliyekuwa akikimbia machafuko yaliyotokea nchini kwao, Liberia baada ya Rais Samuel
Doe kupinduliwa na waasi na kusababisha wananchi waanze kupigana wao kwa wao. Alimsimulia jinsi baba yake alivyojaribu
kutorokea Marekani lakini akaishia kupata ajali mbaya baharini na kuokolewa na wasamaria wema waliompeleka kwenye hospitali
aliyokuwa akifanyia kazi mzee huyo.
Akaeleza kila kitu kilichoendelea, jinsi walivyoishi pamoja kwa amani na upendo na mwisho jinsi kijana huyo alivyoanzisha uhusiano
wa kimapenzi ambao ndiyo ulisababisha Harrison azaliwe. Akamueleza kila kitu mpaka jinsi alivyosababisha kifo cha kijana huyo
kwa bahati mbaya baada ya kugundua ana uhusiano wa kimapenzi na binti yake, Skyler.
Nilishamuomba sana Mungu anisamehe na leo nakuomba na wewe unisamehe kwani halikuwa kusudio langu, alisema mzee huyo
huku akipiga magoti mbele ya Harrison. Kila mmoja aliyekuwa ndani ya nyumba hiyo, alikuwa akilia kwa uchungu kwani ilikuwa ni
historia chungu lakini ambayo ilimsaidia Harrison kuifahamu vyema asili yake.
Kwa moyo mkunjufu, Harrison alikubali kumsamehe mzee huyo na wakakubaliana kufungua ukurasa mpya wa maisha yao.
Wakaanzisha mfuko maalum wa kuwasaidia watu wenye matatizo katika Miji ya Monrovia, Liberia ilipokuwa asili ya baba yake
Harrison, Harvey na mjini Bukoba, ilikokuwa asili ya mkewe, Charlotte.
Wakaendelea kuishi kwa amani, upendo na furaha huku wakisahau yote yaliyopita maishani mwao. Harrison na Charlotte walizidi
kupendana na baada ya miaka mitatu, walibarikiwa kupata mtoto wa pili waliyempa jina la Abdulkarim.
***
Ndugu wasomaji wangu, ninawashukuru sana kwa kuwa nami bega kwa bega tangu mwanzo wa hadithi hii, mkinishauri
na kunikosoa pale nilipokwenda tofauti. Niliyachukua mawazo yenu na kuyafanyia kazi na ndiyo maana nikafanikiwa
kuifikisha hadithi hii hapa ilipofika.
Naamini mmejifunza mengi na kuburudika vya kutosha, yale yaliyo mema yachukueni na kuyafanyia kazi lakini yale
yasiyofaa mbele za Mungu na wanadamu, hampaswi kuyatenda. Ninawaalika tena mjiunge nami Jumatatu katika
Gazeti la Ijumaa Wikienda katika hadithi yangu mpya ambayo nina hakika itakuwa tamu na yenye mafundisho kwenu.
Msichoke kunipa ushauri kwani kufanya hivyo kunanifanya nizidi kukomaa zaidi siku hadi siku. Niwaeleze jambo moja
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
muhimu ambalo hakika nitakuwa sijatenda haki mbele yenu na kwa Mungu pia kama sitalisema. Ukweli ni kwamba
NINAWAPENDA SANA. Mungu awabariki sana. Ahsanteni.
E. J SHIGONGO.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment