Search This Blog

Friday, July 15, 2022

MY X GIRLFRIEND - 5

 







    Simulizi : My X Girlfriend

    Sehemu Ya Tano (5)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliomba aende huko bandani ambapo alimuona nyoka huyo aliyekuwa ameshauwawa na watu waliowahi kumuona. Baada ya hapo akapelekwa kwenye chumba ambacho mwili wa marehemu ulikuwepo.



    Alipofika aliuona mwili wa mpenzi wake ukiwa umefunikwa gubi gubi. Aliusogolea huku dalili za machozi kuanza tena zilijitokeza wazi kwenye uso wa Jack. Aliufikia mwili wa mchumba wake na kuufunua usoni, hakuweza kuvumilia baada ya kmuona mpenzi wake akiwa amebadilika mpaka rangi kutokana na sumu kali ya yule nyoka. Alilia kwa uchungu sana.

    “ELIZA……amkaaa.. amka eliza wangu, ….amkaaaaaaaaa”



    Alilia mpaka akapoteza fahamu. Watu waliokua pale walimnyanyua na kumpa huduma ya kwanza. Walipoona kuwa hazinduki kwa muda wa masaa matatu, wakaamua kumpeleka hospitalini.

    Huko zilipita siku mbili bila kupata fahamu. Ikabidi wamsaidie kwa kumuwekea life support mashine ili mradi imsaidie kupata hewa safi na kwa haraka.



    Masaa sita baadae, alirejewa na fahamu. Aliangaza huku na huko na kuyasoma mazingira ya pale. Aliuangalia kono wake ambao ulipigwa sindano iliyokua na mpira uliopitisha maji ya dripu. Baada ya dakika tano, alizisikia hatua na kugeuza macho yake kula mlangoni na kumuona nesi ambaye naye alipogonganisha macho yake na Jack aliachia tabasamu na kumsogelea mgonjwa wake.

    “pole sana.” Aliongea yule nesi huku akiendelea kutabasamu.

    “hapa nimefikaje?” aliuliza Jack huku akionyesha wazi kuwa hakua na kumbu kumbu na kitu kilichotokea siku mbili zilizopita.

    “hapa uliletwa ukiwa umezimia baada ya kupewa taarifa za mpenzi wako aliyefariki dunia.” Aliongea yule nesi huku safari hii akiwa na sura ya huzuni wakati anatoa taarifa ile iiyomnyon`gonyesha kabisa Jack.



    Aliruhuswa baada ya kuonekana hana tatizo lingine. Safari ilipeleka mpaka kwa kina Eliza ambapo aliona watu wakiwa katika hatua za mwisho wakiunyanyua mwili tayari kwa kuupeleka makaburini. Hakuweza kusogea pindi walipokua wanamuweka mbele ya hadhira kwa ajili ya kumuangalia kwa mara mwisho marehemu Eliza.



    Alishindwa kabisa kusogea pale kwenye lile tukio na badala yake, alibaki pembeni huku kilio kikichukua nafasi kubwa.



    Baada ya tukio hilo. Maiti ilipelekwa kanisani ambapo hata yeye alihudhuria huku akijitahidi kuizuia sauti, lakini machozi hayakuacha kumbubujika. Baada ya misa hiyo takatifu kwa marehemu. Safari ya kuelekea makaburini ilianza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nyimbo za kumtukuza aliyetoa na kutwaa zikiambatana na zingine zilizowatoa machozi watu wengi waliokuwa karibu na familia ya marehemuziliendelea kuimbwa.

    Hizo nyimbo ziliamsha hisia nyingine na kufanya kilio cha sauti kianze tena kwa Jack. Baada ya mchungaji kumaliza sala yake ya mazishi, watu walianza kuingiza udongo kaburini kama ishara ya kumfukia mwenzetu kama ilivyoandikwa kuwa kila mwenye nafsi basi ataonja umauti. Tumeumbwa kwa udongo na udongo ndio marejeo yetu.



    Tukio la kumfukia marehemu lilimuumiza sana Jack na kujikuta na yeye anajiingiza kaburini na kuwaambia watu wamzike angali hai kwa sababu haoni haja ya kuendelea kuishi bila ya kuwa na Eliza.

    Watu walimtoa na kumtuliza. Ingawaje haikua kazi rahisi. Baada ya watu kumaliza kuzika, walimpa pole Jack na wote wakaondoka na kumuacha akiwa peke yake pale makaburini akilia kwa uchungu.



    Alilia muda mrefu huku akilitaja jina la mpenzi wake huyo aliyetokea kumpenda sana. Wakati anaendelea kulia, kwa mbali alianza kusikia sauti ya mtu akimcheka. Alikasirika na kunyanyuka huku akiangaza huku na huko kuangalia huyo mtu aliyekua anamcheka

    Alinyanyuka na kuifuata hiyo sauti inapotokea.



    Alitafuta sana na baadae akajikuta amejikwaa na kutumbukia kwenye shimo refu ambalo hakujua kina chake. Alipiga kelele na aliposhtuka tu akajikuta anachekwa na mtu aliekua pembeni yake.

    “yaani wewe unaota mpaka unalia jamani.” Aliongea Eliza baada ya kumuona Jack akiwa ameamka kwa kukurupuka na huku akiwa anahema kwa nguvu na usoni akiwa na ishara za machozi.



    “Eliza….. yaani siamini.” Aliongea Jack huku akifikisha macho yake ya usingizi huku akimuangalia Eliza mara mbili mbili. Hakuamini kuwa ile ilikua ni ndoto tu. Ukweli ni kwamba Eliza alikua yupo hai.



    “leo tunaenda wapi baby… si unajua kesho ndio siku ya ndoa yetu?” aliuliza Eliza na kumfanya Jack aamini kua kweli alikua anaota.



    “leo tupumzike tu.. maana kila kitu kipo sawa. Tunasubiri muda tu ufike.” Aliongea Jack na kumfanya Eliza atabasamu.



    “nimekuja mara moja tu kukujulia hali mpenzi wangu asubuhi hii.. pia nimesahau kukuambia kua mama amezifurahia sana zawadi za jana.” Aliongea Eliza na kusimama.



    “okey.. unaenda wapi sasa?.” Aliuliza Jack baada ya kumuona Eliza amesimama.

    “naenda kwa mama… nimeambiwa kua sitakiwi kua karibu na wewe mpaka ndoa ipite.” Aliongea Eliza na kumuangalia Jack ambae muda huo aliamka na kuendea mswaki wake ulipo.

    “poa… nitakupigia simu baadae.. si unajua kua napenda kuisikia sauti yako?” aliongea Jack na kutabasamu.

    “poa.. yaani hii siku nahisi itakua ndefu sana kwangu.” Aliongea Eliza na kumuangalia Jack kwa mapozi.

    “sio kwako tu, hata mimi dear.” Aliongea Jack

    “mi naenda… tutachekiana kwenye simu basi… baadae.” Aliongea Eliza na kuondoka zake.



    Siku hiyo ilikua ndefu sana kama walivyoitabiria kua itakua ndefu. Kila mmoja aitafuta cha kufanya ilimradi aweze kuisukuma siku hiyo angalau iishe mapema kwakua walitamani tukio hilo muhimu katika maisha yao liweze kupita salama.



    Usiku wa siku hiyo. Jack alisali na kuomba mungu amuepushe na ndoto za kutisha na majanga yatokeayo kila siku.



    Siku iliyosubiriwa kwa hamu na Jack kuliko mtu yeyote ilifika. Aliamka mapema sana kujiandaa. Alimuangalia mdogo wake na kucheka baada ya kumuona akiwa na furaha pia kwa kaka yake kuoa siku hiyo.



    Akiwa katika maandalizi ya kujipamba tayari kwa kuelekea kanisani, simu yake iliita. Alipoenda kuangalia ni nani apigaye, aliona namba tupu ambayo hakuifahamu. Aliipokea na kunyamaza ili asikilizie sauti ya upande wa pili.



    “mambo.” Ilikua ni sauti aliyoifahamu kabisa baada ya kusalimia.

    “pouwa tu… niambie.” Alijibu salamu hiyo na kutulia.

    “nahitaji kuonana na wewe siku ya leo.. nina shida kidogo wangu.” Aliongea huyo mtu na kumfanya Jack ashangae kidogo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “hilo swala halitaezekana kwa leo wala siku nyingine.” Aliongea Jack kwa sauti ya dharau kidogo.



    “kwanini Jack?... unisikilize kwanza ni kipi ninachokuitia ndio unikatalie.. kubali wito Jack.” Aliongea huyo mtu kwa sauti ya kubembeleza.



    “sikiliza AISHA…. Leo ni siku muhimu sana katika maisha yangu. Hivyo sihitaji kuitia doa. Kama ulikua hujui, nakujuza sasa hivi kua leo mungu amenijaalia kuwa miongoni wa mabwana harusi watakaofunga ndoa muda si mrefu. Kwa hiyo naomba usitishe mawasiliano kama ilivyokua awali.” Aliongea Jack na kukata simu. Aisha alipopiga tena, jack alikata simu na kuizima kabisa.



    Gari iliyokuja kumchukua bwana harusi iliwasili na kumpeleka salon katika kumpamba na kupigwa mapouder. Baada ya hapo msafara mdogo ukaelekea kanisani.



    Ndoa ilipita baada ya kila mmoja kula kiapo cha kuishi na mwenzake milele kwa shida na raha. Kilichofuata baada ya hapo ni sherehe ya aina yake iliyofana sana na kuhudhuriwa na watu wengi tena wenye nyadhifa mbali mbali kutokana na mahusiano yake na watu wa karibu na benk mbali mbali hapa nchini.



    Zwadi kede kede zilimiminika huku kampuni yake ikimzawadia hati ya nyumba kama mmiliki mpya wa nyumba za kampuni zao.



    Baada ya harusi hiyo kupita. Jack aliona mwenyezi Mungu amemnyooshea mkono na kufanikisha kufikia ndoto zake za kutimiza kile kilichomtesa katika maisha yake.



    Walifurahi sana na kila wakati Jack alikua anaonyesha mapenzi sana juu ya mke wake. Hata Eliza nae alikua msitari wa mbele kuhakikisha kua anamliwaza na kumfanya ajione mwenye furaha na mwenye bahati kila siku yaendayo kwa Mungu.



    Baada ya miezi miwili kupita, Jack alianza kumuona Aisha mara kwa mara ofisini kwake. Hakutaka hata kusalimiana na Aisha kwa kujua kua hakua mwema kwake.



    Mara kwa mara alikataa kuonana nae na kuna wakati mwengine alidiriki mpaka kumjibu hovyo ili mradi tu Aisha aachane na kumfuatilia.



    Siku moja Mack alienda kubarizi upepo wa bahari na mpenzi wake. Huko walikaa kwa muda wa lisaa limoja tu na baadae kuamua kwenda kwenye hotel moja kubwa iliyokua karibu na maeneno hayo kutokana na kutoridhika na mahala hapo walipokua awali.



    Wakiwa wanapiga story huku wakila vitu walivyoagiza, kwa mbali Mack aliona kitu ambacho hakikukitarajia kukiona. Mwanzoni hakuamini , ila kadri sekunde zilivyozidi kusogea, ndipo alianza kuamini macho yake baada ya kumuona shemeji yake maeneo yale akiwa na mtu mwengine.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakulifumbia macho lile swala. Alimuacha mpenzi wake na kuanza kufuatilia ni wapi mshemeji yake alikua anaelekea. Alipomuangalia, Alimuona akiwa ameenda kukaa kwenye meza moja ambayo haikua na watu huku akiwa bado amemkumbata huyo mtu.



    Mack alienda mpaka kwenye ile meza na kusimama mbele yao. Eliza alipoinua macho, alishangaa kumuona shemeji yake akiwa pale.



    “he… shemeji!!” alijikuta Eliza anatamani kupaa kwa aibu iliyomkuta muda huo.

    “unafanya nini hapa??... na huyu jamaa ni nani?” aliuliza Mack huku akionyesha wazi akiwa amekasirika.



    “huyu ni kaka yangu kabisa wa mama mkubwa na mdogo. Na hapa tumekuja kupanga mambo ya familia kwakua kaniambia kua kumetokea mtafaruku kidogo.” Aliongea Eliza huku akijitahidi kujitetea.



    “kama kweli hayo mazungumzo ni ya amani.. kwanini msingezungumzia nyumbani??... kaka anajua kua muda hu upo huku?” aliuliza Mack kwa ukali na kumfanya Eliza achelewe kujibu.

    Hakuendelea kusubiri jibu baada kuona hakuna dalili ya kujibiwa. Alichoamua ni kumpigia simu kaka yake ili amuulize kama ana taartifa za mke wake kuwa hotelini na mwanaume aliyemuita kaka yake.



    Ambulance ilifika eneo hilo na kuichukua maiti ya Aisha baada ya vipimo vya mchoro wa ajali eneo hilo ulio chorwa na mchoraji wa mapolisi. Jack hakuendelea kukaa pale, aliingia katika gari yake na kuelekea nyumbani kwake.



    Alipofika huko hakumuona mke wake. Zaidi alimuona mdogo wake Mack baada ya kumuamsha.

    “vipi.. shemeji yako yupo wapi?” aliongea Jack huku akionyesha wazi kuwa hakua katika hali ya kawaida.

    “katoka muda mrefu. Na hata hajaniaga.” Alijibu Mack na kumuangalia kaka yake ambaye alimgundua kuwa hayupo sawa.



    “napiga simu yake pia haipatikani,…why?” aliongea Jack na kurudi chumbani kwake. Huko alikaa na kuwaza sana.

    Alimuwaza Aisha kuanzia mwanzo toka alipokutana nae mpaka kifo chake ambacho anaamini kuwa kulikua na uwezekano mkubwa kuwa yeye ndio aliye kisababisha.



    Baada ya masaa mawili kupita, simu ya Jack ilianza kuita na kumfanya Jack ashtke kutoka usingizini. Alipoiangalia namba, ilikua ngeni kabisa katika macho yake. Alitafakari kwa muda mpaka simu ikakatika. Baada ya huyo mtu kupiga tena, aliipokea ile simu na kusikiliza upande wa pili.

    “haloo.” Aliongea mtu aliyepiga simu upande wa pili.

    “nani mwenzangu?” aliuliza Jack baada ya kuisikia sauti ngeni masikioni mwake.



    “naitwa Poul. Nakuomba uje hapa sinza kwa Remy.” Aliongea yule mtu aliyejitambulisha kwa jina la Poul.



    “bila shaka sikufahamu, vipi unaniambie tukutane?” aliuliza Jack kwa mshangao.

    “ni kweli hunifahamu. Ila mimi ni msamaria mwema sana na kama mwanaume ambaye najua machungu ya mke. Nimeona bora nikupigie simu ili nikuambie uozo wa mke wako. Hivi sasa ameingia pabovu. Maana huyu jamaa anayetembea nae ni kiwembe hatari.” Aliongea Poul na kumfanya Jack achanganyikiwe.



    “wapo wote muda huu?” aliuliza Jack kwa hamaki.

    “ndio maana nika kwambie uje.” Aliongea yule mtu kwa msisitizo.



    “nakuja sasa hivi.”

    Aliongea Jack na kukata simu. Alitoka mkuku bila hata kumuaga mdogo wake na kwenda kwenye gari yake mbio hadi mahala alipoelekezwa. Alifika na kupaki pembeni gari yake na kuchuku simu yake na kumpigia Pioul.



    “nimeshakuona, nakuja.” Aliongea Poul baada ya kupokea simu ya Jack.



    Kwa mbali jack alimuona mvulana mweusi kidogo aliyepanda hewani akiwa amevalia shati la blue huku akiwa amechomekea mkandas nje akivuka barabara na kuelekea upande aliopaki gari. Alijua kua bila shaka mtu huyo atakua ndio Poul.



    “habari za saa hizi.” Alisalimia Poul baada ya kumfikia Jack ambaye alishatoka nje gari yake baada ya kumuona.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “namshukuru Mungu.” Alijibu Jack na kumuangalia Poul kwa makini.

    “pole na matatizo…. Ila mambo kama haya yana hitaji kifua sana.” Aliongea Poul na kumtazama Jack kwa huruma.



    “kabla sijajua chochote kuhusu mke wangu, umenijuaje na umepata wapi namba yangu?.” Aliuliza Jack huku akiwa amefunga swala mikono yake.



    “mke wako ni rafiki yangu sana. Kwa hiyo kuhusu kukujua wewe na kupata namba yako ni swala jepesi sana.” Aliongea Poul na kumtoa Jack mashakani.



    “ni nani huyo ambaye anatenbea na mke wangu?” hatimaye Jack aliuliza swali lililomfanya Poul ajiinamie kidogo na kumuangalia tena Jack.



    “ni bosi mmoja hivi.. maarufu sana kwa watu wa club na wapenda starehe. Ni Malaya mbwa. Anatambulika kwa jina la Z kubwa au Zakaria kwa jina lake halisi.” Aliongea Poul na kumfaya Jack apigwe na bumbuwazi. Maana jina hilo alishalisikia kutoka kwa marehemu Asha kabla ya kifo chake.

    Pia alishawahi kumuona katika harusi ya Aisha.

    Alipagawa na kushika kichwa. Aliamiini kuwa Zakaria ndio alikua mbaya wake katika mapenzi.

    Huyo ndiye aliyesababisha mpaka Aisha akamkataa katika hatua za mwisho za harusi yake, pia ndio aliyedhulumu penzi la mpenzi wake wa zamani kwa kumnyanyasa kama sio wale waliokula viapo vya kuishi wote milele mpaka kifo.

    Sasa hivi ndio kashika pabaya, maana kamuingilia mpaka kwenye ndoa yake mpya ambayo haina hata mwaka mmoja.



    “wapo wapi?” hatimaye Jack aliuliza swali hilo.

    “nimewaona wakiingia ndani ..nyumbani kwa Zakaria.” Aliongea Poul na kumfanya Jack ashushe pumzi ndefu.

    “nielekeze.”

    Aliongea Jack na Poul aliamua kumuelekeza mpaka anapoishi Zakaria.



    Jack alienda mpaka kwa Zakaria na kufungua mlango wa geti ambalo lilikua wazi wakati huo. Aliingia ndani na kuelekea mlango wa mbao ambao ulitumika katika kuingilia sebuleni.

    Aliufungua mlango huo bila kubisha hodi, hakuweza kuyaamini macho yake pale alipomuona mke wake akiwa katika taulo fupi akiwa amekiegemia kifua cha Zakaria huku wakiwa wanaangalia tv.



    Msindo wa mlango kufunguliwa, ndio uliosababisha wawili hao kugeuka nyuma na kumtazama aliyeingia kwa fujo kwenye nyumba hiyo.

    Eliza alijikuta ameyatoa macho kwa hali ya mshangao. Hakuweza kuamini kama mume wake angeweza kufika pale.

    Jack alishiwa nguvu, ghafla aliikuta anashindwa kufanya chochote zaidi ya kuyatuliza macho yake kwa wawili hao huku hasira zikiwa zinapanda katika kichwa chake. Ghafla machozi ya uchungu yaliyochanganyika na hasira yalianza kumbubujika.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Eliza, what`s wrong with you!!?” alijikuta anaongea Jack huku machozi yanamtoka. Wakati huo Zakaria alinyanyuka na kusimama huku Eliza akiwa amejificha nyuma ya Zakaria.



    Hakuweza kuendaelea kukaa pale, aliamua kuondoka na kurudi zake nyumbani huku analia.

    Masaa matatu baadae, Eliza alirudi nyumbani huku analia. Alimkuta Jack yupo sebuleni huku chupa kibao za pombe zikiwa zimemzunguka zikiwa tupu kuonyesha kua alikua ameshazitumia.

    Alifika mpaka pale alipolala Jack na kumtingisha. Alikuta tayari ameshazima. Wakati anahangaika kumyanyua, mdogo wake aliingia na kumkuta Jack akiwa katika hali ile.



    Walimchukua na kumkimbiza hospitalini.

    Alipata fahamu siku ya pili yake. Maelezo ya daktari yalimsababishie Jack ajute kitendo chake cha kunywa pombe kupita kiasi.



    Hakutaka maelezo wala vikao. Aliamua kumuacha Eliza na yeye akaamua kubaki single kwakua anaamini kua chaguo lake alilopangiwa na Mungu tayari ameshafariki.



    “japo alinitendea mambo ambayo hayawezi kuvumilika, ila alionyesha ni jinsi gani alivyokua na upendo wa dhati kwa mtu ampendaye. Ni msichana ambaye anajua nini maana ya kupenda. Alijua kuwa mimi ndio chaguo lake halisi wakati muda ulishamtupa mkono. Ingawaje alikua MY X GIRLFRIEND, lakini ndio chagua ambalo Mungu ameniwekea. Aisha umekufa na mapenzi yangu. Sihitaji tena kupenda,”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hiyo ndio hadithi ya maisha ya Jack ambaye kwa sasa ameshazeeka. Amelea watoto wa mdogo wake mpaka hivi sasa anaitwa babu kutokana na matunda ya watoto wa mdogo wake. Anaona raha kulea watoto wa mdogo wake na vizazi vyao kuliko wa kake kwa sababu hakuhitaji kabisa swala la kuishi na msichana kwakua alijiwekea nadhiri ndani ya moyo wake kwa Aisha ambaye amekufa na mapenzi yake.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog