Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

NISAMEHE GRACE - 3

 





    Simulizi : Nisamehe Grace

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Afande Rama alipogundua Mkuu wa kituo alikuwa anamfahamu Frank kwa kweli alianza kuhanya Maana alikuwa anamjua Afande wake Mkuu kuwa siyo Mtu wa Mchezo. Alikuwa Anajua Mkuu wake wa kituo jinsi alivyokuwa anapinga Mambo ya Rushwa na kuonewa. Hadi Hapo alihisi kazi yake inaweza kuwa Matatani sasa. "Kama nilivyokwambia Kiukweli Mimi Afande Sihusiki na Madawa ya kulevya. Ila CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Mimi nilikuwa na Ugomvi kidogo na Mpenzi wangu Hususani Ndoa yangu hadi kupelekea Mimi kusitisha kuoana. Sasa nilipositisha kumbe Mpenzi wangu hakuwa na Kosa ndipo Yeye alipochukua Jukumu la Kwenda kujiua. Nilipobaini kuwa Mpenzi Wangu Hana Kosa basi niliamua kumfatilia ili kwenda kumzuia Asifanye hivyo. Masikini wa Mungu Sikuweza kumuwahi Mpenzi wangu Maana nilikuta tayari Ameshakufa. Afande Grace kipenzi changu cha Moyo amekufa. Amekufa kabla hata Sijamuona, mimi siyo muuzaji wa Madawa ya kulevya tafadhari naomba unisaidie nikamzike kipenzi changu na kumuomba Msamaha"Aliongea Frank hadi Machozi yalianza kumtoka. Kwa kweli Frank ambacho alikuwa anaamini tayari Mpenzi wake Grace alikuwa ameshakufa kitu ambacho ilikuwa siyo kweli. "Ok nimekuelewa Ndugu yangu Frank, wewe ni mtu Mwadilifu sana mimi nakufahamu. Nakuhaidi hakuna kitu kibaya ambacho kitakupata. Naondoka kuelekea Uwanja wa Ndege kwenda kuchunguza ili nijue ni kweli umekamatwa na Madawa ya kulevya. Nikipata Jibu pia nitaenda hadi Usa river hadi kwa Mchumba wako Grace nikachunguze kweli mpenzi wako amekufa maana huko napajua. Sasa nikipata Majibu ndio nitarudi kuja kukutoa. Na wewe Afande Rama kama nikikuta vitu vipo tofauti na Hivi Basi wewe ndio Utakae Lipa kwa hili maana wewe ndio umethibitisha kuwa huyu Mtu umemkamata akiwa anamadawa ya kulevya. Ina maana kama nitaenda Hadi Uwanja wa Ndege Alafu nikaambiwa hakuna Mtu aliyekamatwa na Madawa ya kulevya. Wewe ndio utakuwa na uhusiano na watu wanaouza madawa ya kulevya na utakuwa umemuwekea huyu Mtu Mfukoni. Hivyo kama utakuwa na uhusiano na hawa wauzaji wa Madawa ya kulevya ambacho kitafuata wewe Kujibu hili shitaka na mwenzako atakuwa Huru"Aliongea Mkuu wa kituo. Alipomaliza Aliondoka na kwenda kupanda kwenye Defender Huku wakiwa na Afande wengine watatu na Safari ya kuelekea Uwanja wa Ndege ilianza. ................................................................. Goodlucky kwa kweli Kila Siku Moyo ulikuwa unamuuma Sana. Kitendo cha kumbaka Grace kwa kweli kilizidi kumtesa Moyoni Mwake. Hakuweza kufanya kazi hata vizuri ilifikia Hadi Usiku alikuwa anaota amemuona Grace akimwijia na Kumlalamikia kwa kile ambacho alikifanya. Kwa kweli hakuwa na jinsi aliamua kujipanga ili kwenda kumuomba Grace Msamaha. Wakati akiwa anawaza atafikaje kwa kina Grace maana alikuwa hafahamu sehemu ambayo alikuwa anakaa Grace na Mpenzi wake simu yake ilianza kuita. Alipoangalia Nani alikuwa Amempigia Aligundua alikuwa Rafiki yake Aisha. Alipoona Namba ya Aisha kwa kweli Mapigo ya Moyo wake yalianza kwenda mbio maana alihisi huenda Aisha alikuwa Amegundua kitu. Hakuwa na Jinsi alipokea Simu na Kusikiliza kuna kitu Gani Aisha alikuwa anahitaji kumwambia. "Tangia nizaliwa sikuwahi kuwaza kama nitakuwa na Rafiki mwenye roho ya kinyama kama wewe. Nashukuru sana Goodluck kwa kutumia picha zangu kama mtego wa kumfanyia unyama rafiki yangu kipenzi Grace. Nasema ni Unyama maana umefanya hadi watu ambae walikuwepo kwenye maandalizi ya ndoa kusitisha. Good ulikuwa umekosa nini hadi kuamua kumbaka Mke wa mtu. Umembaka Grace na kumtoa bikra yake wakati Mumeo alikuwa anajua kama Grace ni Bikra. Achana na Bikra basi maana angesingizia hata imeondoka kwa njia ya Beskeli. Pia kipindi unambaka, Grace alikuwa kwenye siku za hatari hivyo umempa mimba. Hadi hapa Ninapoongea tayari Mume wake Frank ameshaamua kusitisha Kufunga ndoa na Grace na ameenda kujiua na wewe ndio Msababishi. Sasa ulichokifanya rafiki yangu ni kitu cha kinyama. Ninachokushauri Njoo uombe Msamaha mimi nitakuelekeza hadi kwa Grace"Alisikia Sauti ya aisha kisha simu ilikatwa bila hata kumpa jibu Aisha. Kwa kweli yale Maneno ya Aisha yalizidi kumchanganya Goodluck. Kitendo cha kuambiwa kuwa Grace alikuwa na mimba yake na amesababisha mumeo kumuacha alijikuta hadi Machozi yakimtoka. "NISAMEHE GRACE maana nimefikia kufanya hivyo kwa kuwa nakupenda. Ila nimefanya makosa nakuja kukuomba msamaha"Aliongea Goodlucky kimoyomoyo huku akiwa anavaa Viatu kwa kasi ya Ajabu tayari kwa kutaka kuanza Safari ya kuja ARUSHA . Baada ya kuvaa Viatu vyakealitoka Ndani kwake kwa Kasi ya Ajabu na kwenda kupanda Daladala ambayo ilimpeleka hadi Standi ya Moshi. Alipofika Moshi alipanda Coster ambazo zilimpeleka Hadi Arusha Mjini. Tayari Aisha Alishamuelezea Sehemu ambayo atamkuta maana Grace alikuwa anafahamika sana na Dreva Bodaboda. Aliposhuka karibu na Maeneo ya Uwanja wa Ndege Alitafuta Bodaboda na kumwambia ampeleke kwa Grace. Mwendo wa Dakika tano tu kutoka kituo alicho shukia tayari alikuwa Ameshafika kwa kina Grace. Alipofika kwa Kina Grace kwa kweli alijikuta anashangaa maana Hata kabla ya kushuka kwenye pikipiki alimuona Mwanaume akitoka ndani kwa Kasi ya Ajabu na Kwenda kupanda kwenye Gari aina ya IST Kisha kuliondoa kwa kasi. Ile hali ilimfanya kubaki akiwa anashangaa huyu Mtu alikuwa na Tatizo Gani. Kipindi akiwa anatafakari kitu gani kilikuwa kinaendelea alimuona na Aisha akitoka ndani huku Akiita Jina Frank. Hapo ndipo alipokumbuka Mara ya kwanza kumtongoza Grace aliambiwa na Grace kuwa anampenzi wake anaitwa Frank. Hivyo aliposikia Jina Frank moja kwa Moja alibaini kama yule alikuwa Mume wa Grace. Moyo Wake ulizidi kumuuma sana maana kwa kasi ambayo yule Mwanaume alitoka nayo ndani kisha kwenda kupanda Gari yake na Kuliondoa kwa Kasi basi ilimfanya kuhisi kuna kitu hatari kinaendelea. "Aisha Naomba unisamehe Sana kwa hiki ambacho kinaendelea. Tafadhari naomba nionyeshe Grace ili nimuombe Msamaha. Tafadhari naomba unionyeshe Grace ili nimuombe Msamaha maana nimemfanyia kitu cha Kinyama Sana"Aliongea Goodlucky huku akiwa anamfuata Aisha. Aisha aliposikia Sauti ya Goodlucky kwa kweli alishituka sana. Kwa kasi aligeuka na alipomuona Goodlucky alimfuata na Kwenda kumkaba. "Wewe Mbwa umemfanyia Unyama rafiki yangu hadi umepelekea kachukua Maamuzi ya kwenda Kujiua. Nakwambia Kama Grace atakufa lazima nikuue ili mimi CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Nilipize kisasi. Huwezi kutumia Picha Zangu kufanya mambo ya kipumbavu hivi. Twende tukamuokoe Grace anakufa hiyo ndio itakuwa pona pona yako"Aliongea Aisha huku akiwa atatetemeka mbaya. Aisha alipoona Jamaa hamuelewi aliingia ndani na Kuchukua zile Barua ambazo Frank alikuwa anasoma ambazo ziliandikwa na Grace na Kumpa Goodlucky na yeye asome. Goodlucky huku akiwa anatetemeka alifungua vizuri ile Barua na tayari kwa kuanza kuisoma. Alipofungua ile barua alikutana na kibarua kingine ambacho yeye Mwenyewe aliwahi kumwandikia Grace baada ya kumbaka. Kwa kweli alijikuta Anashangaa na kuamini Grace atakuwa na Hasira sana maana hata kile Kibarua alikuwa bado hajakitupa. Aliacha kile Kibarua chake na kuanza kusoma ile barua iliyoandikwa na Grace ambayo ilikuwa inasomeka hivi. "Mpenzi Wangu Frank kwa kweli mimi maisha yangu kwenye hii dunia siwezi kuishi bila wewe. Kwa kuwa nimekueleza kila kitu na Hukutaka kuniami basi mimi bora nijiue kuliko kuendelea kukaa duniani bila ya kuwa na wewe. Nazani Unakumbuka kipindi nakubali ombi lako nilikwambia sitakuwa na Mwanaume tena kwenye hii dunia zaidi yako na endapo nitakukosa wewe basi lazima nijiue. Frank najua hutakufa ila ukiipata hii barua naomba kwanza unisamehe kwa kukufanyia unyama wote huu. Ukisha Nisamehe basi ndipo Uje kunizika nyumbani maana naenda kujiua. Nataka kuibadilisha sherehe ambayo tuliipanga kuwa kilio. Chakula ambacho waliandaa ndugu zangu nataka kitumike kwenye Msiba wangu maana wewe si hutaki harusi tena. Frank tambua kuwa mimi nilibakwa na Rafiki yangu Goodlucky kwa kuniwekea madawa ya kulevya kwenye kinywaji. Hivyo siyo kwamba mimi nilikubali kumvulia nguo goodlucky ila Amenibaka. Nakufa na Mwanangu tumboni kwani alipangiwa kutokuiona hii dunia. Pia naomba tu Umsamehe na Goodlucky maana nahisi hiki ambacho alikifanya hajui madhara yake. Nahisi alinipenda hadi alipitiliza ndio maana alifanya hiki. Nakufa huku nikiwa na Furaha Mpenzi wangu Maana naenda kukusubilia kule Mbinguni. Kama huku Duniani watu wengi wameyapinga Mapenzi yetu basi kule nazani hawatayapinga. Pia Mimi nimeshakusamehe Frank ingawa nilikukuta unafanya mapenzi na Rafiki yangu aisha tena ndani ya nyumba yangu na kitanda changu. Najua umefanya haya kwa hasira ili kulipiza kisasi. Pia nimfurahi sana kufanya mapenzi na Rafiki yangu Hivyo ninachokuomba nafasi yangu kwenye moyo wako achukue Rafiki yangu Aisha"Ile barua iliisha. Kwa kweli ile barua ilimfanya hadi Goodulucky kuanza kutokwa na Machozi. "Ina maana Aisha na wewe ulikamatwa na Grace mnafanya mapenzi na mume wake Frank. Sasa Aisha kwa nini ulifanya hivyo hivi kitu gani hiki ambacho tumfanyia rafiki yetu. Kweli ulikosa Mwanamume mwingine hadi kufikia kufanya Mapenzi na Mume wa rafiki yako tena ndani ya nyumba yake"Aliongea goodlucky kwa Jaziba kidogo huku akiwa anamshangaa Aisha kwa kile ambacho alikisoma kwenye barua. "Hebu acha utaira wako fikilia tutamuokoaje Grace. Mimi nimefanya mapenzi nikiwa sitambui kama huyu ndio mume wake. Unafikili nitakuwa sawa na wewe mnyama uliyembaka. Wewe Dhambi yako hata Mungu hawezi kukusame lakini Mimi mungu atanisamehe maana Anajua sikufanya kusudi. Na wewe ulikosa wanawake wote na uzuri wako uliyonao hadi kufikia kumbaka mke wa mtu ambaye anakaribia kuolewa."Aliongea Aisha. Alichofanya Goodlucky ni kumwambia Waondoke waelekee kwa kina Aisha. Haraka haraka kupitia ile Bodaboda iliyomleta walipanda mishakaki kisha waliondoka. Walipofika kwenye kituoa cha Bodaboda walichukua na pikipiki nyingine kisha walianza Safari ya kuelekea User river kwa kina Aisha. Walipofika kwa kina Aisha walishuhudia Askari wakimkamata Frank na kumpakia kwenye gari. Kilio cha watu pia ndio kilizidi kuwatisha na kuamini kuwa Grace atakuwa Amekufa. Baada ya Gari ya polisi kuondoka ndipo walizidi kushangaa zaidi maana watu waliokuwa wanalia huku wakisema Mwanangu Grace umekufa walianza kushangilia Huku wakiwa Wanakunywa POMBE



     Kwa kweli Baada ya Gari kuondoka na watu ambao walikuwa wanalia kuanza kushangilia huku wakinywa Pombe walifanya Aisha na Goodlucky kubaki wakiwa wanashangaa. Walishindwa kuelewa huu ulikuwa Msiba gani mbona watu wanashangilia na kunywa pombe. Ile hali kwa kweli Goodlucky hakuielewa ilibidi kwenda kumuuliza Mzee mmoja ili kujua kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea pale. "Babau Samahani tumesikia kelele za watu wakilia huku wakiwa wanataja jina la Rafiki yetu Grace kana kwamba amekufa. Nilipofika hapa nimeshuhudia Mtu ambae simjui anakamatwa na Polisi alafu baada ya polisi kuondoka nawaona nyinyi mliokuwa mnalia mnaanza kucheka na kunywa Pombe hebu niambie kitu gani kinaendelea"Aliuliza Goodlucky baada ya kumfikia Mzee Mmoja. "Haha hahahahaha hahaha kijana hapa ni Mjini. Hiyo ilikuwa ni Njia ya kumfunga mpumbavu na kuacha kumfatilia binti ambae hawajaenda sawa. Yeye ni mtoto wa Fukara anamfatilia mtoto wa Tajiri ili amuoe wakati wazazi hawataki. Yani Hapa tulijifanya kama kuna Msiba ili huyu kijana akija aamini kama Grace amekufa. Hicho ndicho tulichoekti na tumefanyikiwa. Hivyo Hakuna Msiba wowote ule zaidi ya kufurahi wala Grace hajafa tena hata wewe chukua pombe kunywaa kijana"Aliongea yule Mzee Maneno yaliyomfanya Goodlucky kubaki akiwa anashangaa. Kwa kweli hakuamini katika Maisha yake kama Kuna watu walikuwa wanafanya vitu vya vituko kama vile. Wakati Goodlucky akiwa anashangaa kile kitu ambacho aliambiwa kweli alimuona Grace akitoka ndani ya nyumba akiwa Mzima kabsa. "Mama lakini kwa nini mmefanya hivyo, mimi nilikuwa nataka frank ajue tu kama nimekufa ila siyo kumfunga. Mama mnamfungaje mtoto wa watu pasipokuwa nakosa"Aliongea Grace baada ya kufunguliwa mlango na Kutoka Nje. "Hivi Mwanangu wewe Ukoje watu tunahangaika kwa ajili yako. Huyu mbwa hakufai ndio maana tunataka tumpoteze kabsa Jela ili asikufatilie tena. Unafikili yeye kujua umekufa ilikuwa ni kisasi sahihi. Anatakiwa kufia Jela huyu ndio utabaki kuwa huru. Mwanangu nafanya hivi kwa kuwa nakupenda sitaki uumie tena. Huruma yako ndio huwa inakuponza wewe. Kweli mtu hakutaki anakufanyia Unyama kama Huu bado unamuonea Huruma. Unamoyo gani wewe Grace utakuja kuuliwa ww mtoto acha huyu Mtoto wa Nguruwe akanyee debe kule"Aliongea mama yake na Grace kisha walimshika Grace na Kurudi nae ndani. Kwa kweli yale Maneno ambayo alikuwa anaongea mama yake na Grace yalimfanya hadi Good pamoja na Aisha kuanza kutokwa na Machozi. Goodlucky hakutaka hata kumtafuta Grace kuongea nae wala kumuomba Msamaha. Ambacho alikipanga ni kufatilia ajue sehemu ambapo Frank alikuwa amepelekwa ili Kumsaidia. Wakiwa na Aisha waliondoka na kwenda hadi kituo cha Polisi cha CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/User river lakini hawakuweza kumuona Frank hali iliyowafanya wabaki wakijiuliza Frank alipelekwa kituo gani cha Polisi. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,;,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Baada ya Mkuu wa kituo kuondoka kuelekea Uwanja wa Ndege kwenda kupeleleza kama kuna mtu alikuwa amekamatwa na Madawa ya kulevya huku afande Rama wasiwasi ulianza kumshika. Alifahamu fika kama Mkuu wake atagundua kama Hakuna mtu ambaye alikuwa amekamatwa na Madawa ya kulevya basi atakuwa kwenye wakati Mgumu sana. Ambacho alikifanya ni kuchukua Simu yake Haraka na Kuwasiliana na Mzee Mambo baba yake na Grace. Baada ya Mzee Mambo Kugundua kuwa Tayari Mkuu wa kituo anakaribia kusanukia Dili ndipo aliamua kumueleza Shawali Mtoto wa Boss ambaye yeye ndio alikuwa anataka Kumuoa Grace. Lile Jambo kwa Shawali lilikuwa ni Jambo Dogo sana ambalo hata halikumsumbua kichwa. Shawali kupitia Mali za baba yake alikuwa anafahamiana na watu wengi sana wakubwa. Hakuna Jambo baya ambalo alikuwa analifanya bila kufanikiwa. Hata alipoambiwa kama kuna Afande mkuu wa kituo cha Majengo anataka kuleta kihelehele wala hakushituka. Alichofanya aliwasiliana na Kamanda mkuu wa Jeshi la Polisi Arusha na kumwambia Kuna kijana anataka afungwe maana anambania ridhiki yake ya kuoa. Alimueleze bayana kuwa amesingiziwa Muhusika wa kuuza madawa ya kulevya ila wakati anakamatwa kesi yake ilikuwa kasababisha mke wake Kujiua. Alimueleza kabsa akikata Simu zitapita dakika kama Arobain tayari milioni tano zitakuwa kwenye Acount yake mkuu kwa ile kazi. Ile kazi aliyopewa Mkuu wa Jeshi la Polisi kwake ilikuwa kazi Rahisi Sana hivyo hakuwa hata na Haraka. Alijua muda wowote anaweza kuwasiliana na Huyu Mkuu wa kituo kisha kumuamuru Muhisika apelekwe mahakami. Pia pale pale alishapanga na Hakimu ambae atasimamia na Hiyo Kesi ili Kuhakikisha Frank anafungwa





    Baada ya Shawali kuongea na yule Mkuu wa jeshi la Polisi tayari alihisi kazi yake imeshaisha. Ni kweli Hadi Hapo Shawali alishamaliza kazi maana kama Mkuu wa Jeshi la Polisi angetoa maagizo mkuu wa kituo cha Majengo Sizani kama angelikuwa na Neno la kuongea tena. Mkuu wa kituo cha Majengo baada ya kuondaka na Vijana watano kuelekea Uwanja wa ndege kwenda kupeleleza walifanikiwa kufika na kila Mtu ambae walikuwa wanamuuliza alikuwa Anajibu kuwa hakuna Tukio kama hilo ambalo limetokea pale Uwanjani. Walipoona wahudumu wa Uwanja wa ndege wamesema hakuna ilibidi Sasa wakaulize kwenye kituo cha Polisi ambacho kipo mle mle Uwanja wa ndege kwa ajili wa kukamata waharifu mbalimbali. Hapo ndio Sasa Mkuu wa kituoa ndio atapata Majibu sahihi. Mwanzo hakutaka kwenda kuwauliza Moja kwa Moja maana alihisi huenda walikuwa Wameshakula deal na Kina Afande Rama. Alienda hadi kituo hicho na kuwaulizia Kama kuna tukio kama hilo limetokea. Wale Afande walimwambia Hukuna Tukio kama lile ambalo limetokea pale uwanja wa Ndege. Kwa kweli hadi Hapo Mkuu wa kituo alibaini kama kweli Frank hakuwa amekamatwa kwa Ajili ya madawa ya kulevya ule Msala alibebeshwa. Kabla ya Kuondoka pale uwanja wa Ndege kwa Hasira alipiga simu kituo cha polisi Majengo na kuwaamuru Askari wamuweke ndani Afande Rama maana yeye ndio atakuwa na Kesi ya Kujibu zidi ya Uuzaji wa Madawa ya kulevya. Alipotoa zile Taarifa sasa ndipo alianza Safari ya kuelekea kwa Kina Grace ili kwenda Kuulizia ajue ni kweli sasa Frank atakuwa Amekamatwa kwa Kosa la kusababisha mke wake kujiua. Mkuu wa kituo cha Polisi alikuwa anamfahamu Sana Grace maama kaka yake Mkubwa na Grace walisoma shule moja sekondari. Hata Grace alikuwa Anamfahamu Mkuu wa kituo cha Majengo na alikuwa wanataniana sana Shemeji maana Mkuu wa kituoa Zaman Alikuwa Anamchukua rafiki yake na Grace Angelina ambae alikuja kufa kwa Ajili ya Gari wakati akiwa ametoka Shuleni Morogoro. Hivyo Mkuu wa kituo kwa kina Grace alikuwa anapafahamu na wasiwasi ulikuwa unamwingia kama kweli Grace atakuwa Amekufa lazima angekuwa ameshapewa taarifa na kaka yake na Grace maana muda siyo Mwingi walikuwa wamewasiliana. Kutoka pale Uwanja wa Ndege hadi User river kwa kina Grace wala hawakuchukua muda Sana. Walipofika aliwaambia vijana wake wamsubiri na yeye ataende Mwenyewe kwenda kuulizia. Alipokaribia na Nyumbani kwa kina Grace kwa kweli alijikuta anasimama Ghafla hasa alipomuona Grace akiwa wanaongea mama yake. Kwa kweli Mkuu wa kituo cha polisi ndio alizidi kuchoka maana hadi hapo alibaini kama Frank Basi alikuwa hana Kosa kabsa. Maana kuhusu Madawa ya kulevya amebaini ni uongo wala hajahusika na kile pia kuhusu kusababisha Grace kufa hata hicho ahusiki maana yeye mwenyewe amemuona kwa macho yake Grace akiwa Mzima. Sasa Mkuu wa kituoa alibaki akiwa anashangaa hiki ni kitu Gani ambacho kinaendelea mbona kama hakieleweki. Wakati akiwa anashangaa ile hali mara simu yake ilianza kuita. Alitoa simu yake kwanza na kuangalia ni Nani yule ambaye alikuwa amempigia. Alipoangalia na Kuona Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha amempigia ilibidi ashituke kidogo. "Afande Joshua kuna Mtuhumiwa mmoja hapo kituoni kwake ameletwa amehusika na usafirishaji wa Madawa ya kulevya hivyo naomba Kessi yake ifatiliwe haraka na Afungwe Mara Moja. Tena wewe Mwenyewe nahitaji hiyo kesi hadi kufikia Siku tatu awe ameshafungwa huyo kijana kama utakuwa unaipenda kazi yako. Haijalishi awe amefanya hilo tukio au hajafanya. Ambacho nakitaka mimi ni Kusikia huyo Kijana Amehukumiwa Siku kazaa na yupo Jera. Pia naomba haraka iwezekanavyo afande Rama uliyeamrisha Afungwe awe Huru mara moja"Aliongea Mkuu wa Jeshi la Polisi na kutaka ile Simu. Kwa kweli yale Maneno ya Mkuu yalimshitua Sana Mkuu wa kituo Joshua. Kwa kweli alishindwa kuelewa kuna kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea Maana ilikuwa siyo kawaida kabsa Mkuu waJeshi la Polisi kufatilia kesi Kama zile



    Kwa kweli ile Simu ambayo Afande Joshua aliipata kutoka kwa mkuu wake wa kazi ilizidi kumchanganya Sana. Alishindwa kuelewa kwa nini huyu Mtu ambaye alikuwa hana kosa lolote alikuwa anaonewa vile. Aliinamisha kichwa chake chini na kufikilia jibu alilopata ilikuwa ni pesa. Bila shaka huu mchezo alihisi kuna Mtu mpambe alikuwa anaucheza huu mchezo. "Kama kufukuzwa kazi acha nifukuzwe tu ila Frank lazima nikutoe huwezi kufungwa wakati hauna hatia. Nazani mkuu wangu ameleweshwa na pesa sasa ngoja nimuonyeshe Mimi kama unatakiwa Usiangalia pesa bali haki ya mtu. Badala ya kumfunga Frank kama Walivyosema mimi naenda kumfunga Afande Rama maana yeye ndio anajiuhusisha na madawa ya kulevya na wala siyo Frank"Aliongea Afande Joshua peke yake kama mtu ambae alikuwa amechanganyikiwa. Kwa kweli alikuwa na haki ya kuchanganyikiwa kama kweli yeye alikuwa mtu mwenye kujali haki za bindamu wengine. "Lakini Mama mimi nahitaji kwenda kumuona Frank nimuombe Msahama maana nahisi hana makosa. Pia mimi niliwaambia nataka Frank ajue kuwa nimekufa tu na wala siyo kumfunga. Lakini sasa mmeenda tofauti na mnahitaji kumfunga mtu ambaye hana hatia. Nahitaji kuonana na frank kumuelezea kila kitu na Kama mtanizuia basi nitajiua kweli. Mimi ndio mwenye kosa nilitakiwa kuhukumiwa. Mama mimi nilibakwa na Kijana lazima kisha alinipa mimba ndio sasa ilifanya mimi Kugombana na frank maana frank alikuwa anajua mimi ni bikra. Nilimuomba Msamaha hakutaka kunielewa na yeye Frank akaamua kunilipizia kisasi kwa kutembea na Rafiki yangu kipenzi aisha. Licha ya kutembea na aisha lakini mimi nilikuwa bado nampenda na kumtaka tuendelee naye kimapenzi lakini aligoma na kusema anaenda kujiua. Kwa kweli niliumia sana ndipo na mimi nilipoamua kuandika barua kama naenda kujiua. Kweli nilikuwa na lengo la Kujiua mama ila nilipofika sehemu nilimkuta mtu anahubiri na kusema kuwa moja ya dhambi isiyokuwa na msamaha ni kujiua. Hayo Mahubiri ndio yaliyonifanya mimi kutojiua. Sasa mama nahitaji kuonana na Frank ili kumuomba Msamaha tena maana bado moyoni nahisi ninamakosa makubwa. Kwa dalili ambayo Frank alikuja nayo naimani ananipenda na atanisame tukaendelea wote kuwa wapenzi"Aliongea Grace kwa sauti ya juu kumwambia Mama yake huku akiwa analia. Yale maneno ambayo aliongea Grace afande Joshua alikuwa anayasikia. Hapo sasa ndio alianza kupata picha ya mchezo jinsi ulivyokuwa. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Siyo afande Joshua tu ambayo alikuwa anayasikiliza yale maelezo. Hata Aisha na Goodlucky walikuwepo pale na wao walikuwa wanasikiliza yale Maneno. "Grace siwezi kukuruhusu ukaenda kumuomba Msamaha yule Masikini asiye na kitu. Kwa nini unamganda yule kapuku. Grace kumbuka haya yote tunafanya kwa ajili ya kufanya maisha yako kuwa Mazuri. Yule mtu hakufai lakini bado unamtaka. Tumeunda mbinu hadi ya kusema kuwa umekufa na tayari ameamini na tumehonga hadi kituoni ili mtu afie huko lakini bado unamtaka huu si ujinga. Grace mwanangu naomba unisikilize kwa makini, kuna mtu tajiri sana na anakupenda mbaya tena yuko tayari kukuoa vile vile huku ukiwa na mimba na kumlea mtoto wako. Yule mtu ni tajiri sana na pia ni mtoto wa tajiri mbaya. Tena umepata zari maana unaolewa na mtoto wa Mwarabu mzee Ramadhani. Sasa mwanangu ukiolewa na Shawali kwanza utatuletea watoto waarabu kwenye ukoo wetu ambae itatufanya hata sisi tuonekane waarabu na pia utakuwa tajiri wa kutupa. Acha kuwaza mawazo Magando mwenangu badilika ni Muda wa kula Raha sisi wazazi wako tunakupenda"Aliongea mama yake na Grace huku akiwa anajitaidi kumfuta Grace machozi ambayo yalikuwa yanamtoka. Yale Maneno ya Mama yake na Grace sasa yalimfanya Afande joshua kuelewa kila kitu. Alibaini hata hili deal la kulazimishwa Frank kufungwa lilikuwa linachezwa na Shawali. Tayari Mkuu wa jeshi la Polisi Arusha alishamwagiwa mapesa ndio maana alikuwa analazimisha kile kitu. Sasa alichofanya Mkuu wa Kituo ni kutoa Simu yake Mfukoni kisha kumpigia Mkuu wa Jeshi la Polisi arusha kumwambia kuwa hawezi kumfunga Frank maana hana hatia na Mtu wa Kufungwa ni Afande Rama Pamoja na Shawali.





    Kwa kweli Afande Joshua Moyo wake Ulikuwa unamuuma Sana. Alishindwa Kuelewa kwa Nini Kijana wa watu Mpole Kama Frank tena Mwalimu ambaye alikuwa anatakiwa Muda ule angekuwa anatoa taaluma Alikuwa Yupo ndani tena bila kosa. Alishindwa kuelewa Mtu Mwenye Cheo kikubwa kama Mkuu wa Jeshi la Polisi Arusha alikuwa anaingia kwenye Rushwa na Kumkandamiza Mtu ambaye wakuonewa Huruma. "Inamaana Lazima Frank atakuwa Anajua kuwa Grace atakuwa amekufa. Masikini wa Mungu mbona inauma Sana, lazima nikamueleze ukweli ili Ajue ni Namna Gani naweza kumsaidia. Anatakiwa Kujua kama Grace Hajafa ili kuweza kupigania haki yake huenda wakarudiana maana Grace Mwenyewe bado anaonekana anampenda Frank" Aliongea Afande Joshua huku akibonyeza batan kazaa za simu yake na kuweka Sikioni. "Mkuu mimi nahisi huyu Kijana Hana Hatia na naenda kumwachia sasa hivi na Kesi hii ya Madawa ya kulevya atahusika Afande Rama. Yeye ndio ataniambia haya Madawa yametoka wapi. Yani inaonyesha wazi kabsa kwamba Frank aliwekewa madawa yale Mfukoni na Afande. Kwanza Mkuu wangu Nashangaa sijui kwa nini unashindwa kufuuata haki unasikiliza Maneno ya pembeni. Labda nisikilize kwa Makini wakati Frank anakamatwa kwao kwa kina Grace alikamatwa kwa kosa la kusababisha mke wake kujiua. Tena walimkamatia Usa River lakini hawakumpeleka kituo hicho cha Polisi bali walimleta Majengo huku wakimbadilishia kesi na kutuhumu anahusika na uuzaji wa Madawa ya kulevya. Alafu kinachoniuma Zaidi frank yeye anajua kuwa Mkewe kafa kweli kumbe Masikini wa Mungu yupo mzima. Hii inaonyesha ni namna Gani Jeshi la kulinda haki za watu linajihusisha kwa kiasi kikubwa na Rushwa. Hivyo Mkuu wangu Samahani mimi Frank naenda kumwachia na Rama ndio atakuwa kwenye kesi nzito ya kushilikiana na Wauzaji wa Madawa ya kulevya"Aliongea Afande Joshua kwa Uchungu mkubwa bila kumwachia hata Nafasi mkuu wake kuweza kuongea. "Afande Joshua naomba Unisikilize kwa Makini kiongozi wangu. Huyu Frank mke wake anahitajika na watu wakubwa. Hayo yote unayoyasema ni yakweli lakini hebu jaribu kufanya kama mimi ninavyotaka. Kama na wewe Hujapata pesa nakufanyia mpango milioni mbili zitaingizwa kwenye acaount mara moja. Huyo Frank wanagombania mwanamke na Shawali mtoto wa tajiri. Hivyo naomba wewe Fanya kama nilivyokwambia huyo Kijana Afungwe mara moja. Kama Unataka Haki basi utakuja Kumuachia Huru baada ya ndoa kupita"Aliongea Mkuuwa Jeshi la Polisi Maneno yaliyomfanya hadi Afande Joshua kushituka na kuanza kutetemeka. "Mkuu kweli mimi ninanjaa ya pesa lakini hata siku moja siwezi kupokea pesa ya Rushwa kumkandamiza binadamu mwenzangu asiyekuwa na hatia. Hivi siku ya mwisho kama nitapokea pesa na kumuhukumu huyu mtu pasipo na hatia Mungu nitaenda kumwambia nini. Mkuu sikutegemea kama mtu mkubwa kama wewe ambae ulitakiwa kupinga vikali vitu kama hivi lakini unaungana na wapumbavu kutetea Ujinga. Sasa mimi siwezi kufanya hicho kitu hata kama nitakuwa nimekufa. Siwezi mkuu wangu kumuhukumu mtu namna hiyooooo"Aliongea Afande Joshua kwa Hasira na kukata Simu yake na kuanza kuondoka sehemu ambayo alikuwa amesimama kwa kasi ya ajabu. Kumbe Wakati akiwa Anaongea yale Maneno kwa Hasira Goodlucky na Aisha na wenyewe tayari walikuwa wamesharudi kwa Grace ili kuja kumuuliza Frank alikuwa amepelekwa kituo Gani cha Polisi. Hivyo walipoona yule Mtu ambaye alikuwa amevalia Mavazi ya kawaida huku akilalamika na kutaja Jina la Frank na kisa ambacho kilikuwa kinahusiana na Cha Frank waliona huenda akawa anajua. Hivyo walichoamua ni kumfuata na kwenda kumuulizia kwa Kina kabsa kama atakuwa anafahamu sehemu ambayo Frank yupo."Za saizi ndugu yangu"Alisalimia Aisha baada ya kumfikia Afande Joshua. "Aaaaahaaa Mwalimu salama afadhali nimekupata na wewe, sasa mbona hivyo mwalimu wenu amekamatwa na nyinyi hamtaki hata kuja kumsaidia kwa nini Jamani"Aliongea joshua. Aisha alipoona yule Mtu akimwambia Mwalimu yeye alibaki akiwa anashangaa maana yeye alikuwa Hamjui afande Joshua. Ila Joshua yeye alikuwa anamfahamu Aisha maana alikuwa anafundisha shule Moja na Frank. "Jamani siyo kwamba hatutaki kuja kumuona Frank ila Sema hatujajua sehemu ambayo yupo frank. Ila Sasa kupitia wewe Sasa tutajua sehemu ambayo yupo"Alijibu Aisha huku akiwa na Hamasa ya kujua Frank Sasa hivi alikuwa anapatikana wapi. Kabla hata ya Afande Joshua hajawajibu kitu Chochote Kina Aisha mara simu yake mfukoni ilianza kuita. Alipotoa ile simu alikuta ni namba ngeni hivyo alipokea"Mkuu Joshua Unaongea na afande Maulisia Kutoka Uwanja wa ndege Hapa Arusha. Baada ya upelelezi wa kutosha kweli tumebaini kuwa kuna Kijana anaitwa Frank alikamatwa na Madawa ya kulevya. Ila sasa wewe ulikosea ulikuja kuulizia leo kama kuna mtu alikamatwa na Madawa hayo. Ila kuna Mtu tulimkata Jana Usiku akiwa anataka kupanda ndege kuelekea Dar. Tulipomkamata tulimfungia ndani hapa Kituoni uwanja wa Ndege hadi Kesho yake ndio walimleta kwenye kituo cha Majengo. Samahani kidogo kwa kushindwa kuelewana Mwanzo. Pia hatukutoa taarifa kmili kwa afande waliokuja kumchukua kama huyo mtu tulimkamata jana usiku"Aliongea Yule Afande na Simu ilikatwa





     Yale Maneno ya Afande Maurisias yalimfanya Afande Joshua kuzidi kuchukia maana alibaina hata kule Uwanja wa Ndege Tayari Rushwa imeshawatembelea. Maana tayari hadi pale Ukweli alikuwa anaufahamu maana Hata Mkuu wa Jeshi la Polisi Arusha alishampa ukweli kama kuna Rushwa hapa inaendelea na anayegawa hizi pesa ni Familia ya Kina Grace ambao walikuwa wanashirikiana na Shawali. Baada ya Afande Maurisias Kukata Simu kutoka Uwanja wa Ndege alichofanya Afande Joshua ni kumpigia Tena na Kumpa ukweli. "Nawewe umeshapokea Rushwa siyo nije kukupitia ukalale Ndani. Najua hakuna mtu ambaye amekamatwa na Madawa ya kulevya hata Jana Usiku. Nimeongea na nyinyi kwa kina na wahudumu wa Uwanja wa ndege nimeongea nae kwa Kina lakini hakuna aliyesema kama Kuna Mtu kakamatwa na Madawa ya kulevya. Leo wewe unanunuliwa tena kutaka kuwaonea wale wasiyokuwa na hatia. Hebu fikilia kama wewe ndio ungelikuwa unatengenezewa kesi kama hiyo ungejisikia. Sasa kwa Taarifa yako hata Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini huu mchezo anaujua kama Huyu Mtu hajahusika na kitu chochote sasa chungu isije kibarua chako kikaota Nyasi. Hivi bado hujapata taarifa kama Afande Rama yupo ndani kwa huo mchezo wa kipumbavu mnaofanya. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Yani nyinyi mliapa kutumikia taifa kwa kulinda haki za inadamu leo mnanunuliwa. Sasa kama nitasikia tena Unanyanyua mdomo kutetea uovu nitahakikisha kazi utakosa pia madawa aliyowekewa frank na wewe utahusika nayo na kwenda gerezan."Aliongea Afande Joshua kwa Sauti ya Kukaza kisha alikata Simu. Muda ule Bado Goodlucky na Aisha walikuwa wanamsubilia yule afande Amalize kuongea na tayari walishajua Yule Afande Ndio anayejua Sehemu ambayo Frank yupo. "Kumbe Hamjui hata Sehemu alipo, Frank kakamatwa leo kapelekwa kituo cha Polisi kusingiziwa Muuzaji wa Madawa ya kulevya hivyo yupo kituoni kwangu. Ila hapa unapoona nimetoka kupeleleza na Frank wala hajahusika na kitu kama kile. Ila anachojua Frank amekatwa kwa kosa la Kusababisha mkewe kufa. Hata pale kituoni anajua Kabsa kama Mkewe wake Kafa kumbe hakuna. Sasa hapa tunatakiwa kushirikiana Kwa Nguvu zote kuhakikisha Frank anatoka jera. Hivi mnaweza Mkawa mnajua kwa nini huyu binti aliamua kufanya kitu kama hiki maana nimemshuhudia kwa macho yangu mzima lakini cha ajabu mume wake anajua amekufa"Aliongea Afande Joshua. Yale Maneno kwa kweli yalizidi kuwaumiza wote wawili Aisha na Goodlucky maana wao ndio walikuwa wamesababisha kwa kiasi kikubwa hata mahusiano ya Frank na Grace kuwa na Misukosuko. Tena Msababisha Mkuu alikuwa ni Goodlucky. Goodlucky baada ya Kumuona Afande anaongea kwa uchungu vile alichofanya alitoa ile barua ambayo Grace aliandika na Kumkabidhi Afande asome ili aelewe Mchezo mzima. Afande Joshua alichukua ile barua na kuanza kuisoma. Alisoma kuanzia Mwanzo hadi Mwisho hadi alipomaliza alibaki akiwa anashangaa tu. Kupitia yale Maneno ya kwenye barua na yale ambayo alikuwa anaongea Grace alianza kupata picha. "Hapa sasa nimeshaanza kuelewa, hii barua kubwa ameandika Grace sasa nahitaji kumuona Aisha ambaye alilala na frank kimakusudi ili frank alipize kisasi. Pia kuna Barua hii ndogo ambayo anaonekana aliandika huyu mtu ambae alimbaka Grace. Tena inaonekana baada ya huyu mtu kumbaka Grace kimakusudi wakati anajua mke wa mtu na anaenda kuolewa ndio alitoa aliandika hii barua.Nikimpata huyu Mtu ambae alimbaka Grace yeye ndio kiini kikuu kilichosababisha hata mambo kama haya yatokee. Ambacho nimekifahamu hapa Frank alikuwa anajua kabsa kama Mke wake ni Bikra. Na kweli Grace alikuwa ni Bikra kama barua hii inavyosema. Sasa baada ya huyu alieandika barua hii kumbaka ndio sasa kitimtim kilianza. Alafu jinsi Mungu alivyowaajabu baada ya huyu mtu kumbaka Grace alisababisha Grace kupata mimba na hii mbimba ndio Sasa ilisambaratisha ndoa maana Kama Frank alikuwa Hajafanya mapenzi na Grace lazima angeshituka pindi aliposikia Grace anamimba. Sasa nahitaji niende kwa Grace sasa hivi nikamjue huyu Mtu aliyefanya Huu Unyama. Ndio Grace anamjua hivyo nikienda lazima nitamfahamu. Huenda ataniambia ni aisha Gani tena ambaye alilala na Frak"Aliongea Afande Joshua bila kujua mtu ambaye alimbaka Grace alikuwa naye pale. Afande Joshua alionekana Mtu mwenye kutumia akili nyingi sana Maana baada ya kusoma ile barua na kuanza kuhusianisha matukio ilikuwa ni vile vile.ITAENDELEA.

    [4/26, 10:32] +255 786 007 307: NISAMEHE GRACE MWANDISHI RAIS WA IRAMBA MAHALI SINGIDA SINGIDA TZA WASSAP NAMBA 0786007307 SEHEMU YA 44 Kwa kweli yale Maneno ya Afande Joshua kusema kuwa anamtafuta mtu ambaye alikuwa amembaka Grace pamoja na Mtu ambaye alilala na Frank yaliwashitua Sana Aisha pamojana na Goodlucky. "Afande haina haja ya kuhangaika kwenda mbali sana kutafuta wahusika wakati tupo hapa. Mimi ndie ambayo nililala na Frank kisha Grace alitukamata ugoni, na Huyu Hapa ndio Goodlucky ambae alikuwa amembaka Grace hivyo waweza kutukamata tu. Grace ni Rafiki yangu Sana na tumesoma chuo komoja. Frank mimi nilikuwa nampenda kuliko maelezo na wakati nakuja kufanya mapenzi sikujua kama mpenzi wake ni Grace huyu ambae mimi ni rafiki yangu. Laiti kama ningejua sidhani kama ningefanya kitu kama hiki"Aliongea Aisha huku hadi Machozi yalianza kumtoka. Kwa kweli yale Maneno ya Aisha yalimshitua Sana Afande Joshua. Maana kwanza alijiuliza kwa nini huyu mtu ananiambia kitu kama hiki huku akiwa kwenye hali ya Uchungu namna hiyo. "Afande ni kweli mimi ndio niliyembaka Grace. Na nilifanya vile kwa kuwa nampenda sana Grace. Kwa kweli Afande naomba Simuliwa tu ila usije ukapenda hata kidogo Grace nilikuwa nampenda kutoka chuo na kila nikimtongoza alikuwa ananikataa. Nimefanya hili tukio ili kuweza kutuliza Moyo wangu kwani nisingeweza kuishi bila ya kufanya kile kitu na Grace. Nilipoona Matangazo kwenye Televisheni kuwa Grace anaolewa ndio nilipanga Mbinu za kuja kufanya nae mapenzi. Mimi ndio niliyemuwekea Madawa ya kulevya kwenye kinywaji na kupoteza Fahamu kisha nilimwingilia bila makubaliano"Aliongea Goodlucky kwa huzuni. Yale Maneno ya Goodlucky yalimpandishia afande Joshua hasira na kumtandika Kofi Goodlucky ikifatiawa na teke ambalo lilimpeleka chini. "Pumbavu nyie watu ndio nilikuwa nawatafuta kabsa, unafikili kunieleza huku ukiwa unalia mimi nitakusamehe. Kwanza hapa unatakiwa kwenda mahakaman tayari kwa kessi mbili. Kesi ya kwanza Unatuhumiwa kwa Kujihusisha na Swala la Uuzaji wa Madawa ya kulevya maana sijajua ulitoa wapi hadi ukamuwekea Grace. Pia kosa la pili unahukumiwa kwa kumbaka Grace"Aliongea Afande Joshua huku akitoa pingu. "Afande ndio maana nimekwambia mimi siogopi kufungwa. Kweli natakiwa kufungwa mimi kwani nimefanya vitu kinyume na sheria. Pia nilifanya vile kwa kuwa nilikuwa nampenda Grace na nilikuwa tayari kwa chochote. Pia wakati nafanya mapenzi sikujua kama Grace alikuwa bikra na ningesabanisha ndoa kuvurugiga kama ningejua kamwe nisingefanya kitu kama kile ndio maana nilipomaliza hilo tukio na kugundua Grace kuwa bikra nilimwandika barua kumuomba Msamaha. Baadae nilipopata taarifa Grace wameachana na Frank ndipo nilikuja kufanya kila mbinu ili Warudiane. Pia Mimi kwa kweli madawa ya kulevya nilikuwa siyajui ila nilipewa na rafiki yangu Afande Rama"Aliongea tena Goodlucky huku akimkabidhi Joshua mikono amfunge pingu. Yale Maneno Good yalimfanya Afande Joshua kusita kidogo kumfunga pingu na kumuuliza Afande rama yupi. Good alipomuelezea kuwa ni Rafiki yake Polisi anafanya kazi kituo cha Polisi Majengo ndio Joshua alibaini ni yule yule aliyemuweka ndani. Hivyo alipata uhakika zaidi kama kweli afande Rama atakuwa amehusika kumuwekea Madawa ya kulevya Frank na yeye hizi biashara anazifanya. "Asante kwa kuisaidia Polisi, sasa kujitetea kwako ndio kutakufanya kuwa huru. Sasa hivi utahusika na kesi ya kumbaka grace tu kama kweli yule Afande ambae nitaenda kukuonyesha kituoni atakuwa ndio yule ambae mimi nimemuweka ndani baaada ya kumfanyia mchezo Frank. Hivyo Sasa Hivi tunelekea kituoni Majengo na utakaa ndani wakati Swala lako la Kesi likiendelea kufanyiwa utafiti. Ila tukifika Kituoni Sitaki kabsa Mtu amwambie Frank kama Grace ni Mzima. Kama Frank akijua hii kitu basi ufanyaji wangu wa kazi utakuwa Mgumu. Ila mnatakiwa kujua Frank mwanamke wake wanagombania na Mtoto wa bosi kama mnavyoelewa. Hivyo maisha yake yapo matatani kuna uwezekano hata wa kuuawa"Aliongea Afande Joshua. "Mimi niko tayari afande wewe nifunge pingu. Hata nikihukumiwa Jera maisha sawa tu maana ni upumbavu wangu na ujinga wa moyo wangu kumpenda mwanamke ambaye tayari alishapendwa. Ila afande Nakuomba tukifika kituoni naomba nimuombe kwanza Msahama Frank ndipo uniweke ndani"Aliongea Good. Afande Joshua alimuelewa Good kisha alimfunga Pingu wakaenda kupanda kwenye gari na Safari ya kuelekea kituo cha Polisi ilianza. Muda wa dakika kumi na tano tayari walishafika kituo cha Polisi Majengo. Walipofika pale cha Ajabu walimkuta afande rama yupo ofisini tayari ndani alishafunguliwa. Wakati akiwa anashangaa Kumuona Afande Rama akiwa ofisin badala ya kwenye sero alimuona Mkuu wa Jeshi la Polisi Arusha akiingia. "Afande Huyu ndio Rafiki yangu Rama ambae alinipa madawa ya kulevya kumuwekea Grace kwenye kinywaji"Aliongea Goodlucky baada tu ya kumuona Rama. Yale Maneno ya Good yalizidi tena kumchanganya Afande Joshua. "Nazani Afande Joshua Sasa hivi husikii hata Order za wakuu wako. Sasa sihitaji upoteze kazi maana wewe ni mtendaji mzuri wa kazi. Ila endelea kufanya kazi hivyo hivyo vizuri lakini Frank muache. Hiyo kesi watu wakubwa Wameishikilia Ndugu yangu Joshua. Mimi nilikuja hapa kumfungulia huyu Afande Rama maana kila Muda nilikuwa nasumbuliwa kupigiwa Simu. Mimi naondoka ila naomba kesho kesi ya frank nisikie Ikisomwa Mahakaman na wewe unatakiwa Kuikamilisha"Aliongea Mkuu wa Jeshi la PolisiCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/





     Kwa kweli yale Maneno ya Mkuu wa Jeshi la Polisi yalizidi kumshangaza Afande Joshua. Kwanza siyo Afande Joshua tu hata Afande Rama pamoja na Aisha na Goodlucky walianza kumshangaa. Maneno ambayo alitakiwa waongee pembeni tena kwa siri maana yeye ndio alikuwa mtu mkubwa na watu walitakiwa kuiga kwao yeye alikuwa anaongea maneno ya Kijinga tena mbele ya watu. Afande joshua alimwangalia Mkuu wake kisha alicheka "Mkuu wangu nahisi siyo bure kuna kitu kinakusumbua kutoka kichwani kwako. Kama hujanywa pombe Asubuhi hii basi itabidi ukapime akili Mkuu wangu. Inamaana mimi natakiwa kuiga utendaji wako wa kazi kutoka kwao leo hii unakuja kuniamrisha nifanye kama nyinyi mnavyotaka wakati mimi nafata haki. Nipo tayari kufa kwa kutetea haki za watu wasio kuwa na hatia. Siwezi kuacha kuifatilia hii kesi na wewe ukizidi kunifatilia basi hili Swala nitalipeleka mbele kabsa maana kuna watu nafahamiana ambao wamekuzidi cheo wewe. Hivyo Mkuu wangu naomba na wewe hii kesi usile Rushwa Rudisha maana itakutokea puani. Tafuta kessi zingine kula rushwa ila siyo hii ambayo Afande Joshua anaisimamia. Wakati namaliza Mafunzo ya upolisi niliapa kuwa nitalitumikia Jeshi la polisi wa kufuata haki na Kulinda haki za binadamu. Hivyo kama hili Somo wewe lilikupita basi rudi Darasani kasome Mkuu wangu. Hivi unajua hii kesi inavyoenda na unafahamu mimi ninae ifatilia ni nani kwa huyu Kijana. Tena umefanya Makosa Afande Kulwa naomba Mkamateni huyu Afande Rama Mrudisheni ndani Asubilie kwenda kusomewe Kessi yake maana upelelezi tayari nimeshaukamilisha na huyu anahusika na uuzaji wa Madawa ya kulevya. Kuna ushaidi unajieleza kwanza amemuwekea Madawa ya kulevya frank kwenye Mfuko wake na Pia alimpa madawa ya kulevya rafiki wake Goodlucky ili Good atumie kumuwekea Grace kwenye kinywaji ambake. Pia naomba na Huyu Goodlucky Mwekeni ndani maana na yeye anakesi ya kubaka inamsubilia"Aliongea Afande Joshua huku akiwa Siliausi mbaya. Yale Maneno ya Afande Joshua yalimshitua kidogo Mkuu wa Jeshi la Polisi hivyo alimwangalia kwa hasira Afande Joshua kisha aliondoka bila kuaga. "Afande nilishakwambia mimi nipo tayari kufungwa. Ila tafadhari sero ambayo mtanipeleka naomba unipeleke ile Sero ambayo Frank yupo. Nahitaji kumlinda Frank maana kwa jinsi nilivyosikiliza Maneno ya Grace wakiongea na Mama yake kama mchezo wa kufungwa utashindikana Basi Frank lazima Afe. Bora nife mimi ila siyo Frank mtu ambaye hana hatia. mimi namfahamu Sana Shawali baba yake Mzee Ramadhani ni Mzee anayejua kufanya mambo ambayo Mungu anayapenda ila siyo Mwanae yule ni mchafu na kunauwezekano Mkubwa wa kuamuua Kabsa Frank. Tena Hata Wewe Mkuu nakuomba kuwa Makini Sana Maana nawasiwasi na huyu Mkuu wako wa kazi kitu chochote kinaweza kukukuta. Hawa huwa hawachelewi kutafuta haki zao ambazo Mungu anazikataa kwa Kuuwa watu"Aliongea Goodlucky kwa Huzini. Yale Maneno ambayo Goodlucky aliyoongea kwa kweli Afande Joshua aliyaona kama kweli yanamana vile. "Sasa mimi nahisi wewe ni Moja ya watu wanaopenda kumuona Frank hafi. Kama umenihaidi utamrinda basi mimi sitakufunga bali nataka ukakae kwenye mlango wa Frank ili Mtu yeyote Asiingie mle. usiruhusu chakula chochote kuingia mle ndani chakula nitaleta mimi. Pia mtu yeyote asikusogelee ukimuona anakuja mwambia aelezee shida mbali. Nauhakika unajua kutumia Bastora hii hapa ndio itakulinda. Sina imani na Askari wangu kama Mkuu wangu ambae anapata pesa za kutosha tu anafanya hivi Je hawa Afande wa kawaida wakimwagiwa pesa si mara moja tutampoteza Frank. Namalizia Upelelezi naomba Wewe ndio ambae utaenda kumlinda Frank ila naomba usimwambie kitu chochote Frank"Aliongea Afande Joshua. Yale Maneo ya Afande kwa kweli yalimfurahisha Goodulucky na kukubali kwa Moyo Mmoja maana muda ule alitaka kufanya mambo mema ya kumshawishi Frank amsamehe pia alitaka kusafisha Jina huenda angesamehewe hata kesi yake ya kumuingilia Grace. Baada ya Kukubaliana Joshua alimpeleka Good kwa Frank na kwenda kumtambulisha kama ndio atakuwa mlinzi wake maana hadi Sasa awaamini kabsa afade. "Afande Umegundua kuwa mimi siyo muhusika wa hili tukio. Tafadhari naomba uniambie basi ni kweli Grace amekufa. Wewe niambie tu mimi roho hainiumi tena. KamaGrace atakuwa amekufa naomba peleleza wapi kazikwa nikamuombe Msamaha. Kwa nini sikuweza kumsikiliza Grace wakati mtu alibakwa siyo kwamba alifanya mapezi kwa kupenda. Hivi ni kweli Huyu aliyembaka mpenzi wangu na Kusababisha majanga kama haya alikuwa anampenda mpenzi wangu kuliko mimi"Aliongea Frank huku akiwa analia. Laiti kama Angejua kama Mtu ambae alimbaka mke wake alikuwa yupo pale Sijui angefanyaje. "Frank upo na Afande Joshua kwa kweli utatoka bila shida yeyote. Nimepeleleza nimebaini wewe uhusiki na Madawa ya kulevya hivyo bado namalizia kitu flani ili wewe utoke usiwe na wasiwasi kabsa. Kuhusu mke wako kwa kweli bado sijajua amekufa au laa maana sijafika kwao"Aliongea Afande Joshua maana hakutaka kumwambia Frank kama mpenzi wake hajafa. "Afande Mpenzi wangu Mimi ameshakufa, mimi mwenyewe nimeshuhudia kwa macho yangu watu wakilia. Ninachotaka fanya haraka nitoke jera ili nikamuombe Grace kwenye kaburi lake msamaha"Aliongea Frank. Kwa kweli yale maneno ya Frank yalikuwa yanaumiza Saa na Afande alibaini akiendelea kuwepo pale mwishowe ataanza kumwelezea Alichofanya alimuaga Frank na kutoka. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Mkuu wa jeshi la polisi alipotoka kwa Afane Joshua alikuwa amevimba mbaya. Aliona huyu mtu kama atamletea utani kazi yake itaenda vibaya. Kitu cha kwanza alichofanya baada ya kutoka kwa Joshua ni kumpigia Shawali Simu na kumuelezea kila kitu kuwa hali ni ngumu. Mwisho wa Maongezi walikubalina Kuwa Shawali atamsaidia kumtumia Vijana wa kazi kwa ajili ya kuwamaliza wote wawili yani Frank na Afande Joshua. Hawakuwa na Njia nyingine hiyo ndio Njia ambayo ingemfanya Mkuu wa jeshi la Polisi kupata milioni za pesa kutoka kwa Shawali pamoja na kufuta Fedheha ambayo aliipata kutoka kwa Afande Joshua. Mkuu wa kituo alishaona hata Ufanyaji wake wa kazi utakuwa Mgumu kama mtu mwenye cheo cha chini atakuwa anamdharau vile





     Wakati Mkuu wa kituo cha Polisi akiwa anaendelea na upelelezi wa Mwisho ili kumwachia Frank na kumtia Kizimbani Afande Rama kule nako kwa Shawali tayari Watu wa kumuua Afande Joshua walishaandaliwa. Tayari Shawali walishamaliza na mkuu wa Wa Jeshi la Polisi kuwa Wataanza kumuua kwanza Afande joshua na baadae kama bado kesi ya Frank itakuwa Ngumu watammalizia na Frank hilo ndio ilikuwa lengo lao. Walitaka kummaliza kabsa afande Joshua maana yule ndio alikuwa Kizuizi kikubwa. Zilipita kama siku tatu tayari Sasa Afande alishakamilisha Upelelezi wake na kwa kuwa upelelezi alikamilisha siku ya Juma mosi na Kesho yake ilikuwa siku ya Juma pili aliamua kusubilia hadi siku ya Juma tatu maana Juma pili huwa mahakama haifanyi kazi. Pamoja na kukamilisha ile kazi yake ya Upelelezi na kuwa na Ushaidi Tosha wa kumpeleka Afande Rama jela ili iwe kama Funzo kwa Afande Wengine upande Wake wa Moyo mwingine ulikuwa unauma sana na Kuhisi mambo ambayo alikuwa amefanya yasiweze kufanikiwa. Afande Joshua alikuwa na Machale aliwaza huenda kuna kitu kibaya kinaweza kumpata kabla ya siku ya kesi. Maana kuna kipindi badala ya kuwa na raha maana tayari alikuwa anaenda kumaliza kesi lakini Moyo wake ulikuwa Unauma sana. Siku ya Juma Mosi Usiku Afande Joshua alichukua karatasi na Kuamua kuandika ujumbe kisha aliweka kwenye Baasha vizuri na juu yake aliandika Kifo Changu. Baada ya kukamilisha ile kazi alienda kuifadhi vizuri uleCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Ujumbe kwenye kabati yake chumbani. Hadi Muda ule zilishapita kama Siku tano tangia Frank akamatwe lakini hakuna Ndugu hata Mmoja ambaye alikuwa anajua kama Frank yupo kituoni. Nyumbani kwa mzee Oska wao walikuwa wanaendelea kujiandaa Juu ya Harusi ya Mwanao. Tena kwa Jinsi baba yake na Grace alivyo na Roho mbaya kila alipokuwa anauliziwa Juu ya Maandalizi ya Harusi alikuwa anasema yanaenda Sawa tu. Tayari Mzee Oska alisha tuma Ng'ombe Wawili kwa mzee Mambo ambao wangetumika kama Mboga na wala Ng'ombe walipofika Mzee mambo aliwapiga Bei. Grace kwa kweli na yeye moyo wake Ulikuwa unauma Sana. Baada ya mama yake kumbana kuwa amsahau Frank alikubali kiusoni tu ili mradi mama wake ampe nafasi ya kutokumbana ili amtafute Frank mwenyewe. Moyo wake Ulikuwa Unauma Sana maana alibaini Fika kuwa Frank atakuwa kwenye wakati Mgumu sana. Baada ya Mama yake Kumuelewa ndipo Sasa alianza kazi ya kumtafuta. Aliulizia vituo vya polisi vyote vilivyopo karibu na User river lakini hakumpata Frank hali iliyomfanya kuwa na Wasiwasi huenda tayari Frank atakuwa ameshahukumiwa na yupo Gerezani. Ilikuwa Siku ya Juma pili muda kama wa saa kumi jioni ambayo ilishabaki siku Moja tu kabla ya Kesi ya Frank kufikishwa Mahakani kuachiwa huru na Rama kufungwa kama Alivyokuwa amepanga Afande Joshua. Ile Siki Afande Joshua aliamua kutoka na Mpenzi wake Suzani pamoja na Mwanao Hawa na Kwenda kwenye Ufukwe kwa ajili ya kuponda Raha. "Mpenzi wangu kwa Mfano nikifa leo huenda kwa kifo cha watu kuniua kuna kitu Gani ambacho utakifanya juu ya kifo changu na mwanangu utamfanyia nini"Alimuuliza Mkewe Afande Joshua huku akiwa amemshikilia. "Kwanza siwezi kufanya kitu maana Najua Huwezi kufa Mpenzi wangu. Pia mpenzi wangu hiyo siyo mada ya kujadili hata kidogo maana mimi nahisi kama ukifa wewe na mimi lazima nife. Ila napendezwe sana na jinsi unavyofanya kazi zako kwa haki maana watu wanakusifu sana. Inawezekana wewe Hujui ila acha mimi nikwambie Ukweli kuna baadhi ya Watu huwa wananiletea hadi zawadi na kuniambia nimepata mume mwenye kujali Utu. Hata mimi namshukuru Mungu na Najivunia Sana kwa kuwa na Mume kama wewe"Aliongea Suzani huku naye akimpapasa mumeo usoni. "Mke wangu kuna kesi flani ya Kijana ambaye hana hatia mimi naifatilia. Kwa Mfano kama nikifa leo maana kesi inafanyika kesho naomba utaenda kwenye kabati yangu utafungua na utakuta barua ambayo...."Aliongea Afande Joshua hata kabla ya Kumalizia Mlio wa Risasi ulisikia kisha Kitu cha baridi alihisi kikipenya kwenye Mgongo wake alipogeuka ili kuangalia nani yule ambaye alimpiga Risasi ni kama aliwapa nafasi zaidi ya Kuhakikisha wanamuua maana walimpiga na Risasi yingine ambayo ilimpeleka chini afande Joshua. "Hawezi kupona hadi Hapa tayari kazi yetu imeshakamilika tena tumeimaliza kirahisi Sana Muda wa kwenda kuchukua Pesa na kuzitumia"Aliongea Kiongozi mmoja wa majambazi na wote walienda kwenye Gari yao na Waliondoka kwenye eneo la tukio kwa kasi. "Mume wangu nani kakupiga Risasi Mume wangu Jamani mume wangu Usife basi"Aliongea Suzani huku akiwa amechanganyikiwa mbaya. Muda ule Afande Joshua alikuwa yupo chini kalala huku akimwangalia mke wake Jinsi ambavyo alikuwa anahangaika. "Suzani unakumbuka kitu ambacho nilikwambia. Mimi kama nilikiona kifo changu hivyo utafanya kama nilivyokwambia. Najua nitakufa lazima ila kabla Sijafa naomba nikimbize kwanza hospitalini ili niendelee kuhudumiwa na utaenda hadi kituoni kwangu Ulizia Kijana Flani anaitwa Goodlucky mwambie amlete Frank hospitali Sehemu ambayo nipo"Aliongea Afande Joshua kwa Shida huku Damu zikiwa zinamtoka.





    Kwa kweli yale Maneno ambayo Afande Joshua aliongea yalizidi kumchanganya Mke wake Suzani na kumfanya azidi kulia. "Mume wangu tafadhali usiongee hivyo maana huwezi kufa, Huwezi kufa mume wangu maana ukifa na wewe hata mimi nitakufa. Sasa tukifa wote ni nani ambae atamlea Hawa. Ndio mimi nakupeleka Hospitalini pamoja na kwenda hadi kituo cha Polisi kwenda kumleta Frank lakini naomba ni promise kama hautakufa"Aliongea Suzani huku akiwa amechanganyikiwa mbaya. Yani yeye alihisi kifo cha Joshua ni yeye Joshua alikuwa anapanga. Inamaana kama Joshua angesema hata kufa yeye alikuwa anaamini kuwa kweli hawezi kufa. "Baba yangu usife tafadhari nakuomba usife Dady kwani nakupenda sana. Bado nakutegemea Dady na watu pia bado wanakutegemea tafadhari usife Dady"Aliongea Mtoto wake na Afande hawa. Kwa kweli hawa alikuwa ni Mtoto mwenye miaka Mitano lakini Mungu alimjalia kuwa na Busara mbaya. Pamoja na kuwa ni Mtoto ambaye alikuwa anasoma awali lakini alikuwa na uwezo wa kuongea na kuelezea mambo utafikili mtu mkubwa. "Mke wangu na Mtoto wangu kipenzi nimewaelewa haya mimi siwezi kufa ila tafadhari ili nisife basi niwaisheni Hospitali"Alionge Afande Joshua kwa shida ili mradi kuwalizisha mkewe na mwanae. Maana bila kusema hicho kitu sizani kama wangefanya kama yeye alivyokuwa anataka. Haraka haraka Suzani alimshika Mumeo na Kumnyanyua kwa shida na walianza kukokotana kupelekwa kwenye Gari. Ingawa Afande Joshua alikuwa amepigwa Risasi lakini Bado alikuwa na uwezo wa kujikaza kiafande huku akiwa ameshikiliwa na mkewe na kufanikiwa kufika kwenye Gari kisha Safari ya kuelekea hosipitalini ilianza. Kutoka pale Ufukweni hadi hospitali walitumia muda wa nusu saa tu tayari frank alishafikishwa kwenye hospitali ya Wiliya majengo naMatibabu yalishanza kufanya. Suzani alikaa nje ya Chumba ambacho alikuwa anatibiwa Mume wake Huku akiwa anasubilia Majibu. Muda wote alikuwa anamuomba mungu mume wake Asife maana alihisi kama mume akifa hata yeye hataweza kuendelea kuishi kwenye Hii dunia. Baada ya Saa kama Moja na Nusu hivi ndio Mlango wa chumba ambacho aliingizwa Afande Joshua Ulifunguliwa. Kwa kasi ya Ajabu Suzani alisimama tayari kwa kupata Majibu kutoka kwa Dactari wake Kuhusu hali ya mumewe. "Dactari niambie Mume wangu kafa, wewe niambie tu kama mume wangu Kafa au bado yupo mzima. Sina wasiwasi wala usinifiche"Aliongea Suzani huku akiwa na Wasiwasi mbaya. "Mama wala usiwe na wasiwasi Mumewe hali yake siyo mbaya na wala hawezi kufa. Muda wa Saa moja ndio utarusiwa kumuona pia ingekuwa vizuri zaidi kama Ungekuja na mtu anaitwa Frank maama ulipomfikisha Mumeo kabla hajapoteza Fahamu alikuwa anasema sana tukwambie Umfuate Frank"Aliongea Dactari. Yale maneno ya Dactari kwa kweli yalimfurahisha Sana Suzani pia alikumbuka kama kweli Mumeo alimpa kazi ya kwenda kumleta Frank. Alichofanya ni kumshika Mtoto wake Mkono na kwenda kupanda kwenye Gari na kuanza kuelekea kituo cha Polisi Majengo. Muda ule Tayari ilikuwa Saa moja kamili Usiku. Alipofika Majengo alimwambia Goodlucky kuwa afande Joshua alikuwa anahitaji kuonana na Frank. Kwa kuwa Goodlucky alikuwa anamfahamu suzani pia taarifa nazo kumbe zilikuwa zimefika Kituoni kama Afande Joshua kapigwa Risasi na yupo hospitalini wala Askari hawakupinga. Walichofanya afande Mmoja akiongozana na Goodlucky walimchukua Frank na kuanza kuelekea Hospitalini. Wakati Frank wakiwa wanaelekea Hospitalini Kumbe Tayari Mkuu wa Jeshi la Polisi alikuwa ameshapata taarifa kuwa Afande Joshua bado Hajafa. Hivyo wakati Frank wakielekea hospitalini Huko nako Shawali na Mkuu wa Jeshi la Polisi walikuwa kwenye mkakati wa kuhakikisha wanammaliza Afande Joshua huko huko Hospitalini NISAMEHE GRACE MWANDISHI RAIS WA IRAMBA MAHALI SINGIDA SINGIDA TZA WASSAP NAMBA 0786007307 SEHEMU YA 48 Mkakati wa kuhakikisha Afande Joshua anakufa ulikuwa unaandalia na Shawali huku wakiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi. Hawakutaka kumwacha Joshua akiwa mzima hadi kesho maana walikuwa wanajua lazima Frank kesho atakuwa huru kisha mtu wao Afande Rama ndio atafungwa. Sasa kama Afande Rama akishikiliwa walikuwa wanahofia siri zao zinaweza kufumbuka maana wao ndio waliomtuma Afande Rama kumuwekea Madawa Frank mfukoni ili kumuuzia kesi ya Madawa ya kulevya. "Lazima Afe na naomba Mjitaidi kuhakikisha huyu Afande anakufa. Kinachotakiwa hapa ni kuondoka kuelekea Kwenye Hospitali ya Majengo. Kama nilivyowaeleza tayari kila kitu nimeshakimaliza na Jinsi ambavyo mtaingia pale hospitalini. Mkifika humo chumbani hakikisheni mnafanya kama nilivyowaambia na Frank msimguse wala kumuua"Aliongea Mkuu wa jeshi la Polisi kwa vijana ambao walikuwa wamepewa kazi yaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ kumuua Afande Joshua. Kilichokuwa kinashangaza Vijana ambao walipangwa kwenda kumuua Afande Joshua walikuwa ni Askari kabsa. "Nahitaji kumuoa Grace jamani. Hicho ndicho ambacho nataka kifanyike. Kama Afande Joshua atakufa hapatakuwa na kipingamizi chochote na mimi lazima nitamuoa Grace" aliongea Shawali. Mwendo wa Gari ambayo alipakiwa Frank kupelekwa kituoni ilikuwa Mwendo kasi wa hatari. Dakika tano tu tayari Gari ilishafika hospitalini na wote Suzani, frank na Goodlucky walishuka kuelekea ndani. Walipofika hospitalini waliambiwa wasubilie kwa muda wa Saa moja ndio wangeruhusiwa kuingia ndani Kumuona Afande Joshua kwani Muda ule bado alikuwa amelala ingawa tayari fahamu zake zilikuwa zimerudi. Saa moja ilipoisha ndipo walingia kwenye chumba ambacho alikuwepo Afande Joshua. Afande Joshua alipomuona Frank kwa kweli alijikuta anatabasamu huku tabasamu lake lilizidiwa na machozi ambayo yalianza kumtoka machoni. " Frank wanataka kuniua ili eti nisikusaidie wewe, sijui hii dunia tunaelekea wapi watu wanajali pesa kuliko utu wa mtu. Frank wewe hakuna kitu kibaya ambacho ulikifanya . Najua nakufa siwezi kuwa Mzima. Afande Mkuu wa jeshi la Polisi wakishirikiana na Shawali ndio wananiua ili eti nisikusaidie wewe. Frank Naomba kwanza Umsamehe yule mtu ambaye alimbaka mke wako maana hata yeye alifanya bila kujua kama Grace alikuwa bikra. Alifanya kwa kuwa alikuwa anampenda kwa dhati Grace na hakuwa na Nguvu za kuishi bila ya Grace moyo wake ulishaapa kufanya mapenzi na Grace ndio maana alitimiza ahadi hiyo. Huyo mtu ukimsamehe ndio ambaye atakusaidia mambo yako kwenda vizuri na mapenzi yako yarudi kama mwanzo na Grace. Naomba mtafuta Grace na Mrudiane kisha mtoto ambaye yupo tumboni kwa Grace umlee tu kama mwanao. Naongea hivyo kwa kuwa mimi nakufa na huyo mtu ndio msaada mkubwa kwako"Aliongea Afande Joshua huku hadi machozi yakimtoka. "Mume wangu kwa nini unataka kunifanya moyo wangu utoke. Utakufaje mume wangu wakati ulinipa ahadi nikulete hospitalini na nimlete Frank. Nimefanya hivyo lakini bado unaniambia unakufa" aliongea Suzani huku na yeye machozi yakiwa yanamtoka. Kwa kweli yale Maneno ya Afande Joshua yalizidi kumchanganya Frank. Maana Frank alikuwa anaamini kuwa Grace amekufa sasa Afande Joshua kusema kuwa warudiane na Grace ilimfanya kushangaa. "Kwanza Afande wewe huwezi kufa niachie niwe haru ili nikulinde. Pia kwa kweli mimi bado sijakuelewa nitarudiana vipi na Grace wakati Grace yeye ameshakufa afande. Grace amekufa na mimi mwenyewe niliona watu wakilia sasa iweje nirudiane naye tena. Au afande na mimi nakufa nitaenda kirudiana naye kaburini nini"Aliuliza Frank. "Frank Grace bado ni mzima na anakupenda sana, grace hajafa na pale watu waliokuwa wanalia ilikuwa ni njama tu za wewe kukupeleka Gerezani"Alionge Afande Joshua na kuanza kumueleza Frank kuanzia Mwanzo hadi mwisho. Alimueleza jinsi msiba wa bandia ulipoanzia na jinsi mbinu zilizopangwa hadi kufika jera. Pia alimuelezea hata kesi yake inavyogombaniwa na watu wakubwa ili kufungwa. Kwa kweli yale maelezo ya joshua yalimfanya Frank alikaa chini kwani hakuamini kama Grace alikuwa mzima "Afande nahitaji kumuona Grace sasa hivi. Ila kabla sijaenda kumuona Grace naomba kwanza uniambie mtu aliyembaka mpenzi wangu nianze naye maana huyo ndio ambae alisababisha hadi haya"Aliongea Frank. "Frank mtu ambaye alimbaka mkewe ni mimi hapa waweza kuniua mimi nipo tayari. Ila hata nisingembaka mkewe bado ungekuwa kwenye matatizo tu maana ile harusi isingefanyikiwa baba yake na Grace walipanga kuja kukuua. Ndio shawali wakishirikiana na mzee mambo walipanga kuja kukuua na walikutumia majambazi walikukosa maana ile siku ndio Grace alikukamata ugoni na Aisha na wewe uliondoka kwa lengo la kwenda kujiua. Pia Grace kwa kweli nilikuwa nampenda sana ndio maana nilishindwa kuvumilia pia sikuwa najua kama grace ni bikra na wewe ulikuwa unalijua hilo. Ila hata mimi mbona umetembea na mpenzi wangu aisha ambaye nilikuwa na mpango wa kumuoa. Ila mimi kutembea na Grace pia imekuwa na Msaada kwako Frank maana nimekuokoa kufa na sasa unamuda wa kujipanga na kurudiana na Grace. Huenda ndio mungu alipanga hivyo huwezi kuzuia"Aliongea Goodluck kumbe tayari aisha alishamwambia kuwa ili Kumshushia Hasira frank wakati anajitambulisha kuwa alimbaka Grace na yeye aseme kuwa wanamahusiano na Aisha. "Frank naomba muelewe huyo kijana maana ndio atakuwa Masaada wako. Yeye ndio ambae alikuwa anakulinda hada kituoni la sivyo ungekuwa kwenye wakati mgumu sana. Mimi sijui kwa kweli sijiamini nahisi kama naweza kufa leo ingawa hizi risasi haziwezi kuniua. Nahisi bado kuna kitu kinaweza kutokea ambacho.."Aliongea Afande Joshua lakini hata kabla hajamaliza kuongea waliingia watu watatu ambao walikuwa na Bunduki. "Afande Joshua ulionywa sana na kuambiwa mwache huyu Mwanaharamu lakini ulikuwa Mgumu. Sasa unaona sasa utamwacha mwanao peke yake na mke wako anaenda kufa kifo cha kinyama. Huyu pia ambaye unamuokoa naye atahukumiwa kifungo cha maisha kwa kesi ya madawa ya kulevya pamoja na kukuua wewe" aliongea Afande Mmoja na kumfuata Afande Joshua kwa kasi. Afande joshua alipotaka kuamka ili kujiokoa lakini hakuwa na nguvu zile maana risasi zilikuwa zimemjeruhi vibaya. Muda ule Frank, Goodlucky pamoja na Suzani walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi."Hivi unafikili naogopa kufa hata nikifa mimi na nyinyi ipo siku mtakuja kufa tu. Nakufa sawa ila bado atapatikana mtu ambaye ataendelea kutete haki za watu wanyonge"Aliongea Afande Joshua kisha alifumba macho na kutulia tayari kwa lolote. Yule afande alipomfikia Afande Joshua alimkita kisu ya tumboni kisha shingoni afande Joshua. Kwa kweli lile tukio liliwachanganya wote kwa pamoja Suzani na Frank lakini tayari watu wengine walishaongezeka na kuwashika vizuri huku wakizibwa midomo kwa sola tape na kufungwa pingu Mikoni. Walipohakikisha wamemuua Afande joshua ndipo sasa walipomchoma frank sindano ya Usingizi na kumuwekea kisu kile Mkononi huku wakimpaka na Damu Mkononi ili kumtupia kesi ya kumuua Afande Joshua kisha walipohakikisha mambo yapo Safi walitoka na Goodlucky pamoja na Suzani ili na wale wakawamalize.



    Kwa kweli ulikuwa ni Mpango kabambe ambao ulikuwa umeandaliwa kuhakikisha kuwa Afande Joshua anakufa na Frank anatupiwa ile Kesi kuwa yeye ndie ambae amemuua Afande Joshua. Kazi ya Kufanyikisha Ule Mpango haikuwa Ngumu Sana kutoka na kuwepo Kwa Dactari Mandewa Dactari ambaye alikuwa anapenda Pesa kuliko maelezo. Dactari Mandewa yeye ndio aliyepewa kazi ya Kuhakikisha zoezi la Frank kukamatwa linaenda sawa. Tayari kila kitu kilishasetiwa kuwa Frank atachomwa sindano ya Usingizi ya Nusu Saa alafu baada ya Nusu saa atazinduka. Hivyo kilichopangwa zikiwa zimebaki Dakika tatu kuzinduka Afande Mandewa tayari atakuwa wapo na Afande wengine ndani na Frank akizinduka Pale pale anakamatwa kisha kesi ya kumuua Afande Joshua inatupiwa kwake. Baada ya Wale Afande Kufanikiwa Kumuua Afande mkuu wa Kituo cha Majengo kisha kumchoma Sindano ya Usingizi Frank waliwakamata Goodlucky na Safari ya kuwapeleka Sehemu ambayo walipanga kwenda kuwaua ilianza. Muda wote kwenye Gari suzani alikuwa analia kila alipokuwa anakumbuka Taswira ya Mume wake akichomwa kisu tumboni na kifuani. Hasira ya Kuua mtu ilikuwa inambana sana ila hakuwa na Ujanja maana pingu alikuwa amefungwa vizuri mikononi huku sola tape naye ikiwa imebanwa vizuri kwenye mdomo wake kuhakikisha kuwa hawezi kupiga kelele. Ile Kazi ilikuwa inafanywa kisiri hata wakati Suzan na Goodlucky wanatolewa pale hospitali walitolewa kisiri tena kwa mlango wa Siri ambayo hayo yote yaliongozwa na Dactari mandewa. Walipotoka nje ya Hospitali walipanda Gari ya Dactari Mandewa ili isije kutiliwa shaka yeyote. Mwendo kama wa Dakika kumi na tano hivi tayari Gari ilishafika sehemu Sahihi ambayo walikuwa wanahitaji kwenda kuwamaliza kina Suzani. "Hatuwezi kuwaua kwa Upanga wala Sumu maana nyinyi hamna kosa hata kidogo ila tatizo mnajua kile ambacho tumekifanya. Siyo wote wanaokufa huwa wanahatia wengine hawana hatia ila wakiona vitu kama hivi wanauawa. Hivyo hili shimo ni shimo zuri ambalo tutawatupia na kufa Pole pole maana hakuna mtu ambaye atakuja kuwapa Msaada. Aliongea Afande Mmoja kisha aliamrisha Goodlucky na Suzani watupiwe kwenye lile shimo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Lilikuwa ni shimo refu sana ambalo mtu akiingia ndani ni vigumu sana kutoka hata akiwa hajafungwa kitu. Sasa mbaya zaidi Wale walitakiwa kuingizwa kwenye lile shimo kisha wanafungwa kamba miguuni na mikononi sola tape inapita mdomoni hivyo ni kweli wangekufa tu. Suzani alijaribu kuwaonesha wale afande kihisia kuwa wasifanye vile lakini hawakuwa na Muda wa kuwasikiliza. Tayari ngazi ilishawekwa kwenye lile shimo kisha Walifunguliwa kamba na kuamrishwa washuke kwenye lile Shimo huku wakiwa wameshikiliwa Bunduki. Hawakuwa na Jinsi maana waliambiwa kama watakataa kufanya vile basi watauawa kwa Bunduki. Waliona Bora waingie kwenye Shimo mungu anaweza kuwasaidia baadae kupata Msaada lakini siyo kufa palepale. Baada ya Suzan na Good kuingia kwenye shimo walienda kufungwa kamba tena kisha Ngazi iliondolewa na wale afande waliondoka na kuwaacha Goodlucky na Suzani kwenye lile shimo. Dactari Mandewa alikuwa yupo Makini sana na Saa kuhakikisha kuwa Kazi aliyopewa inatimia Dakika kumi na tatu zilipobaki tayari alishatoa Taarifa kituo cha Polisi kuwa kuna mtu kavamia Hospitalini na kumuua Afande Joshua. Ila sasa baada ya Kumuua afande Joshua yule amefanyikiwa kumfungia kwenye chumba kile na Ameshindwa kutoka hivyo wawahi. Sasa kwa jinsi mchezo ulivyokuwa unachezwa taarifa Dactari Mandewa hakutoa kituo cha Polisi Majengo ambacho kilikuwa karibu nao maana Kituo kile walikuwa wanajua kama Frank alikuwa ametoka na Afande Mwenzao hivyo isingekuwa rahisi kumuua Afande Joshua wakati alikuwa ni Msaada kwake. Dactari Mandewa alitoa taarifa kwenye makao Makuu ya Polili Arusha na ile Ishu aliambiwa na Mkuu wa jeshi la polisi Arusha. Hivyo Baada ya Taarifa zile kutolewa Mkuu wa Jeshi yeye mwenyewe aliambatana na Askari wengine kwenda kumkamata Frank. Walienda hadi Hosipitali ya Majengo na kukusanya jopo la Madactari kisha walipewa taarifa kuwa kuna muuaji ameingia humu hivyo kafungiwa kwenye chumba na tayari ameshaua. Mambo yote yalikuwa yanafanyika vile ili tu kazi ya kumfunga Frank ifanyikiwe tena afungwe haraka bila hata kuanza kuhangaika kutafuta Ushahidi maana watu wengi watakuwa wameona lile tukio. Baada ya Madactari kukusanywa walienda hadi kwenye chumba kile na Kufungua mlango. Wakati Wanafungua Mlango ndipo na Frank alikuwa anazinduka kwenye Usingizi na kujikuta ametapakaa Damu huku akiwa ameshikilia kisu. "Upo chini ya ulinzi nakuomba Weka kisu yako chini unashitakiwa kwa kesi ya Kumuua Afande Joshua"Ilikuwa ni Sauti ya Mkuu wa Jeshi la Polisi iliyomshitua Frank



     Kwa kweli yale Maneno ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kumwambia Frank kama alikuwa yupo chini ya Ulinzi kwa Tuhuma za kumuua Afande Joshua yalimshitua sana. Ni kweli hata yeye alipojiangalia alikuta Nguo zake zikiwa zimetapakaa Damu huku mkononi akiwa na Kisu ambacho nacho kilikuwa na Damu. Wakati akiwa anashangaa nini ambacho kimetokea hadi amekuwa na kisu huku kikiwa na ndamu ndipo alipokumbuka Afande akiwa anachomeka Kisu kwa Afande Joshua kisha walimfuata na yeye wakamchoma sindano ya Usingizi. "Hapana Ndugu zangu mimi sijahusika kabsa na hili tukio Afande watatu waliingia hapa ndio wamehusika kumuua Afande Joshua ili nikose Msaada. Wao ndio walimpiga Risasi hata kipindi wakiwa na Suzani walipoona hajafa ndio wamemmalizia leo. Afande Joshua mwenyewe amenieleza haya hata na Afande ambaye amemuua Afande Joshua alikuwa analalamika kuwa Afande Joshua kifo hiki kama amejitakia kwani alizuiwa kunisaidia mimi na yeye akaendelea kuniganda. Lakini Afande ungekubali kuachana na Mimi ili nifungwe ona sasa leo umekufa kwa ajili yangu, Ona sasa Mke wako pia Suzani pamoja na Goodlucky wamekamatwa na wanaenda kuuawa kwa ajili yangu"Aliongea Frank kwa Huzuni huku Machozi yakiwa yanatoka. "Naona Kijana umepandwa na uchizi sasa kinachotakiwa wewe ni kufungwa tu. Bado umeua na kuna ushaidi kabsa unaonyesha alafu bado unabisha tena Unasubutu hadi kuwasingizia Askari wangu kuwa wanahusika na hili tukio. Yani Askari ambao wanalinda haki za binadamu leo waje Wahusike na Hiki kitu hebu acha upambaafu Mfungeni hizo Pingu huyu Muuaji haraka sana. Alafu Mwambie yule Afande aliyepewa Jukumu la Kumlinda aje hapa Athibitishe ili huyu Mpumbavu asiendelee kutubishia"Aliongea Mkuu wa Wa Jeshi la Polisi kwa Hasira huku akimpiga na makofi Frank. Askari ambao walikuwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi haraka walienda hadi kwa Frank na kumkamata kisha alifungwa Pingu. Muda ule kwa kweli Frank alikuwa analia tu na kutaja majina ya watu wawili tu. Jina la kwanza ambalo alikuwa analitaja lilikuwa ni Grace na kumlaumu kuwa yeye ndio sababu ya mambo yale na Jina la Pili lilikuwa la Afande Joshua akimlaumu tena kwa nini alimsaidia hadi amepelekea kifo chake kutokea. Baada ya kufungwa Pingu ndipo Mkuu wa Jeshi la Polisi aliamrisha tena Mtu ambaye atakuja kuthibitisha kuwa frank ndio amehusika na kifo cha Afande Joshua aingie. Mlango ulifunguliwa cha Ajabu Frank alizidi kuchoka hasa alipomuona mtu ambaye alikuja kuthibitisha kuwa Frank amemuua Afande Joshua alikuwa ni Afande Rama ambae yeye ndio alimuwekea na Madawa ya kulevya Mfukoni hali iliyomfanya Hadi sasa kuwa jela. "Ni kweli kabsa mimi ndio nilipewa Jukumu la Kumlinda huyu Kijana ndipo alinitoroka kipindi mimi nimeenda kumchukulia chakula. Pia nauhakika hata Tukio la Afande Joshua kushambuliwa kule ufukweni wakiwa na mke wake Frank ndio aliyepanga na Mtendaji mkuu ni Rafiki yake ambaye anaitwa Goodlucky. Hii nimefanikiwa kubaini baada ya kuona barua za Ujumbe mzito ambao walikuwa wanabadilishana namna ya kuweza kumuua Afande Joshua. Yeye alijua kama Afande Joshua ni anaushaidi wa kutosha kuhusu biashara zake za madawa ya kulevya hivyo alizani akimuua kesi yake itakuwa nyepesi sasa sisi polisi tumekuwa imara kulifahamu hili"Aliongea Afande Rama. Muda ule tayari hata waandishi wa habari walikuwepo huku wakichukua picha na video kwa ajili ya kusambaza taarifa. "Afande Rama hicho unachokiongea ni cha Uongo hata hayo maneno unayoongea hadi moyo wako unakulaumu. Wewe Kwanza ulikuwa ndani kwa kosa la kujihusisha na madawa ya kulevya leo umekuwa Huru na unajifanya ulikuwa mlizi wangu. Kweli mimi sijahusika na kitu chochote kile kuhusu kifo cha Afande Joshua. Ila Najua nitafungwa maana mimi sina pesa za kuhonga ili mniache. Ila mungu akifanyikiwa nikamaliza kifungo changu nitakuja kulipa kisasi kuhusu kifo cha Afande Joshua. Lazima nihakikishe namuua Afande aliyemuua Joshua maana namfahamu. Pia nahisi Grace utanisikia maana kuna Waandishi wa habari hapa nateseka hivi kwa ajili yako kwa kweli najuta kukupenda Grace. Pia NISAMEHE GRACE kama huenda kuna kosa nimekufanyia"Aliongea Frank lakini hata kabla hajaelezea Vizuri Mkuu wa Jeshi la Polisi aliamrisha na kuanza kutolewa ndani maana alihisi kwa Maneno ambayo anaongea Frank mwisho watu wataanza Kumuamini. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,;,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Baada ya Aisha kumuacha Goodlucky kituo cha Polisi kwa kazi ya Kumlinda Frank aliyepewa na Afande Joshua yeye alirudi Moja kwa Moja hadi Nyumbani kwake. Kitu ambacho alikipanga ilikuwa Juu ya Kumuona Grace na kumuelezea kila kitu hadi kesi nzito ya Madawa ya kulevya ambayo Frank alitupiwa. Pia alitaka Kumueleza na Mtu ambaye anamsaidia Frank ili Grace naye amuone huyo mtu huenda angekuwa Shaidi. Aisha aliamua kumtafuta Grace kwa kuwa alishafahamu kama Bado alikuwa na Upendo kwa Frank. Kipindi Grace alipokuwa anawalalamikia wazazi wake kwa nini walimfanyia vile Frank ndipo alipogundua Grace bado anampenda Frank na anaweza kurudiana naye. Alitoka nyumbani kwake huku akiwa na Gari ya Frank ya IST Ambaye alienda kuichukua Majengo ambako frank alikuwa ameitelekeza kwa kuhofia foleni. alipofika kwa kina Grace alijitambulisha kama mwalimu mwenzake anafundisha Pamoja amekuja kumuona. Bahati haikuwa upande wake aliambiwa Grace hayupo. Baada ya kuambiwa Grace hayupo aliamua kuchukua namba zake ambae alipewa na Wazazi wake na alipopiga namba ilikuwa haipatikani. Kumbe wazazi wa Grace walikuwa wanamficha tu Grace alikuwa yupo ndani na alikuwa analia tu. Baada ya kupiga simu kwa namba ya Uongo ambae mama yake na Grace alimpa bila mafanikio ndipo aliamua kuaga ili aondoke. Lakini kabla ya kuondoka aliamua kumtajia namba yakeCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Mama yake na Grace ili Grace akija basi ampe amatafute. Sasa wakati Aisha akiwa anataja namba nipo Mfanyakazi wao wa ndani kwa kina Grace ambaye alikuwa anajulikana kwa jina la Rose aliamua na yeye kuchukua zile namba maana Aisha alikuwa anataja kwa Sauti. Yeye alijua kama Mama yake na Grace amesema Grace hayupo ndani wakati alikuwa ndani aliona hata namba hata Mpa. Hivyo yeye aliamua kuchukua zile namba ili kwenda kumpa Grace wawasiliana na yule Dada huenda angejua sehemu ambayo alikuwepo Frank. Aisha alipomaliza kutoa namba aliondoka na kurudi hadi nyumbani kwake kusubilia kama grace atampigia simu. Kutoka saa nane aliporudi nyumbani hadi saa moja Usiku bado alikuwa hajapata simu kutoka kwa Grace. Ile hali kwa kweli ilizidi kumtisha na Kuhisi labda wazazi wake na Grace watakuwa wamejisahau hawajampa Grace namba. Alichoamua ni Kuondoka tena kurudi hadi kwa kina Grace huenda akamuona. Wakati akiwa anatoka ndani kwake ili akapande kwenye Gari ndipo simu yake ilianza kuita. Haraka haraka alitoa simu yake huku akiomba mtu ambaye alimpigia simu awe Grace. Alipotoa simu alikuta namba Ngeni tofauti na ile ya Grace ambayo alikuwa anaitarajia. Huku akiwa anajiandaa kumjibu kwa mkato yule mtu aliyempigia Simu alipokea simu na kumsikiliza. " Aisha ni mimi Rafiki yako Grace, Tafadhari nimepata taarifa ulikuja hapa kwetu na wazazi wangu wakakwambia kuwa sipo wakati nilikuwepo ndani nimejifungia namlilia frank. Tafadhari aisha kama unajua sehemu ambayo Frank yupo naomba unipeleke ili nikaokoe Maisha yake. Frank atahukumiwa jela wakati hana hatia. Namba yako nimepewa na Mfanyakazi wa ndani rose hata namba uliotajiwa na mama yangu ilikuwa ya Uongo"Ilisikika sauti ya Grace kwenye simu iliyomfanya Aisha moyo kuanza kwenda mbio. "Grace Rafiki yangu ni kweli naomba umsamehe frank maana hana hatia na anateseka Gerezani bure. Sasa hivi kule frank alipo amesingiziwa amekamatwa na Madawa ya kulevya. Hivyo nakuomba umsaidia bado siku tatu tu kessi yake isomwe na itakuwa siku ya Juma tatu. Ambacho nakuomba sasa hivi usiwe na wasiwasi kabsa siku ya Juma pili nitakupeleka kwa Afande Joshua yeye ndio anamsadia Frank utaongea naye na wewe utaenda kuthibitisha Mahakamani kuwa frank hana hatia



    Kwa kweli yale Maneno ambayo aisha aliongea yalimfanya Grace kutabasamu na machozi ambayo yalikuwa yanamtoka kumkakuka kwa kasi ya ajabu. "Asante Sana Aisha na nakuomba wazazi wangu usiwaambie kuhusu kitu chochote maana wanataka kumfunga Frank. Ila naomba basi hata leo nitoroke nikamuone Frank wangu Jamani. Huwezi Amini kwa kweli nilikuwa natamani kujiua tu"Aliongea Grace huku akiwa anapapasa kifua chake kujitaidi kuizuia Furaha ambayo alikuwa nayo. "Hapana Grace nakuomba nielewe kile kitu ambacho nimekwambia. Huenda kuna watu wakawa wanakufatilia hivyo wakikuona umejua sehemu ambayo Frank yupo itakuwa hatari tena kwa frank. Sasa hivi Tufanye vitu kimya kimya ili tuje tuwafanyie surprise mahakamani. Pia haya Mambo yote yanapangwa na Shawali ambao wazazi wako wanataka uoelewe. Tena pia tunatakiwa kushukuru mungu uliponifumania na frank maana kumbe hiyo siku Jambazi nao walikuwa wametumwa kuja kummaliza Frank ili harusi yenu isifanyikiwe"Aliongea Aisha maneno ambayo yalizidi kumuumiza Grace. Baada ya kuelewana Grace alikata simu na kurudi ndani kwake huku akiwa na Furaha mbaya. Siku hiyo Usiku aisha alilala kwa raha huku nako Grace alilala kwa furaha ya Hali ya Juu huku akiomba Mungu Siku ya Juma tatu iwahi kufika akamtoe Kifungoni kipenzi chake na Kuridiana. Siku ya Juma pili kama ya saa moja usiku Aisha aliamua kwenda kituo cha Polisi ili kwenda kumuona Afande Joshua kumueleza wakutane na Grace Usiku ili wajadili maana yupo tayari Kumsapoti. Alipofika kituoni kwa kweli alishituka kidogo alipomuona Frank akiwa na Goodluck Afande mmoja na Mwanamke wanaenda kupanda kwenye Gari aina ya mack ii na kuondoka kwa kasi pale kituoni. Ile hali kwa kweli ilimshitua Aisha na kuamua alifatilie lile Gari hadi alipoona limeingia Hospitalini. Kwa kasi ya Ajabu na yeye alipaki Gari nje ya Hospitali na kuingia hospitalini kuwafatilia Frank walikuwa wanaenda wapi. Alipowafatilia na kuona mlango ambao frank waliingia aliamua kurudi nje kwanza kwenda kupaki Gari vizuri ndipo akachunguze kitu gani kilikuwa kinaendelea maana hata simu alipokuwa anampigia Afande Joshua ilikuwa haipatikani. Baada ya kwenda kupaki Gari vizuri kwenye sheli ndipo alirudi kwa kasi ya Ajabu hadi hospitalini. Ila wakati akiwa anaelekea kwenye kile chumba aliwaona Askari wengine ambao waliongozwa na Dactari Mandewa wakiwa wanakiendea kile chumba huku wakiwa wanageuka nyuma hali iliyomshitua Aisha maana wasiwasi wa wale Polisi ilikuwa siyo wa kawaida. Aisha aliamua kubana pembeni kwanza hadi aliwaona wale Askari wakiingia kwenye kile chumba. Baada ya muda wa dakika tano aliwaona tena wakiwa wanatoka huku wakiwa wamewafunga Goodlucky na Suzani pingu. Ile hali ilimshitua Aisha na kuhisi kunataatizo maana wale Polisi hata Mlango waliokuwa wanapitia ulikuwa wa nyuma. Wale Polisi walipoondoka ndipo alienda hadi chumba ambacho waliingie Frank ndipo alikutana na vitu ambavyo vilimshangaza sana. Kwanza alimuona Frank akiwa ametulia tuli kama Amekufa huku na Damu zikiwa zimetapakaa kwenye shati lake. Alipoangalia kwa Afande Joshua ndipo alifumba macho kabsa maana ilikuwa inatisha. "Wamemua Frank na Afande Joshua haiwekezani lazima niwajue nyinyi ni nani na ikiwezekana mkamatwe na Mfungwe"Aliongea Grace na kutoka kwenye kile chumba kwa kasi. Alipotoka kwenye chumba alitoa simu yake na kumpigia Rafiki yake ambaye alikuwa Polisi kituo cha Kambi ya pili na kumpa taarifa anahitaji msaada. Baada ya kupiga simu alitoka hadi nje akawaona Wale Askari wakimpakia good kwenye Gari yao na kuondoka. Yeye pia alipanda kwenye gari na kuwafatilia hadi alipoona wanapaki Gari na kuingia porini. Ndipo na yeye alienda kupaki Gari tafoauti na Sehemu ile na Kurudi tena kuwafatilia. Alifanikiwa hadi kuona wakiweka Ngazi na Kuwaingiza Goodlucky na Suzani kwenye shimo. Aisha alipoona lile tukio alirudi hadi kwenye Gari yake na kuondoka kwa kasi hadi Kambi ya Pili Mkufatilia Rafiki yake Afande ili kuja kuchukua lile tukio ambalo lingekuwa ushaidi tosha. Hadi Muda ule Aisha alikuwa analia kwenye Gari maana aliamini Frank tayari alikuwa ameshakufa. Alipofika kambi ya pili rafiki yake na Aisha ambae alikuwa anajulikana kwa Jina la Sophia tayari na wao walikuwa wameshajiandaa na walikuwa wanamsubilia Aisha aje awapeleke kwenye tukio. Aisha alipofika Kambi ya Pili aliwapakia Sophia na Kwenda hadi kwenye eneo la tukio na Kwenda kuchukua Picha ikiambatana na kuwatoa Frank kwenye lile shimo. "Frank hajafa aisha naomba usiseme hivyo. Frank bado yupo mzima ila amebebeshwa kesi ya kumuua Afande Joshua. Pale Frank amechomwa sindano ya Usingizi na kushikishwa kisu hivyo akishituka atajikuta kwenye mikono ya polisi. Hivyo tunatakiwa kufanya kitu ili kumuokoa Frank"Aliongea Good baada ya kumuona aisha anaongea. Yale Maneno ya Good kwa kweli yalimshitua Aisha na kubaki akijilamu kwa nini hajachunguza huenda angemuokoa Frank kwenye ile kessi. Muda ule Suzani alipofunguliwa yeye alikuwa haongei kitu alikuwa yupo kimya huku machozi yasiyokuwa na kilio yalikuwa yanamtoka. Taswira ya Afande akiwa anamchoma kisu mume wake ilikuwa inamrudia na hasira ya ajabu ilikuwa inamwijia. "Najua haya mambo yote atakuwa amepanga Mkuu wa Jeshi la polisi pamoja na Shawali kwa jinsi tu mlivyonieleza. Hapa tayari tunaushaidi wa kuwafunga hawa watu wote. Kitu ambacho kinatakiwa nyinyi ambae mmetupiwa kwenye shimo msionekane. Na tuache hadi Frank amfunge kama wanavyotaka na baadae sisi tutaanza kesi taratibu. Kama Afande Joshua alikufa kwa ajili ya kutetea haki za watu acheni na mimi nife. Ila nawaomba sasa hivi pigeni moyo wenu konde acheni wafanye wanavyotaka. Tukiingilia njiani hii kesi itatutokea puani na kutupelekea kufa bure maana bado hatujajiandaa"Aliongea Afande Sophia baada ya kupewa maelezo yote hadi jinsi kesi ilivyokuwa ya frank. Baada ya kueelewana mke wake na Afande waliongozana na Goodlucky pamoja na Aisha waliondoka kueleke Moshi. Huko ndiko walijipanga kujificha hadi wabaya wao wote wafungwe. Kesho yake Asubuhi kwa kweli watu walikuwa wamekunyika kwenye Mahakama ya Mkoa wa Arusha kuweza kusikiliza nini Hatima ya Muuzaji wa Madawa ya kulevya Bwana Frank pamoja na kesi yake ya Kumuua Afande Joshua. Muda ule Hadi wazazi wa Frank pia walishapata taarifa jana kupitia televisheni na Walikuwa kituoni huku wakiwa hawaamini kile ambacho walikiona kwenye Taarifa ya Habari. Moja ya watu wengine walioshitushwa Juu ya Tuhuma za ile kesi alikuwa ni Baba yake na Shawali Mzee Ramadhani maana yeye alikuwa anamfahamu Frank maana alikuwa Mtoto wa Rafiki yake. Alimkumbuka Sana kwani Frank aliwahi kwenda na Baba yake Kwenye Kampuni ya Mzee Ramadhani kwenda kunua Gari. Hivyo hata Mzee Ramadhani alikuwa yupo Mahakami kusikiliza ile kesi. Mtu mwingine ambaye alikuwepo kwenye ile kesi alikuwa ni Grace ambae Muda ule alikuwa amechanganyikiwa sana maana Tangia waongee siku ile kwenye simu pamoja na Aisha hawakuongea tena. Hata alipojaribu kumpigia Simu Aisha alikuwa hapatikani. usiku kucha alikuwa amempigia Simu bila mafanikio mwanzo simu ilikuwa inaita bila kupokelewa na baadae ilikuwa haipatikani kabsa. Grace kwa kweli alifika Mahakamani Huki akiwa haamini kabsa kile ambacho alikiona kwenye Tv. Mtu ambaye aliambiwa ndio angeonana naye ili kumsaidia Frank ndio ambae ilisemekana Frank amemua. Saa nne kamili Defender iliingia Mahakami huku ikiwa na Askari kibao kwa ajili ya Kumlinda Frank ambaye ilisemekana alikuwa nyemela wa kutisha. Pamoja na kuwa na kesi ya Madawa ya kulevya aliweza kutoroka kituoni na kwenda kumuua mkuu wa kituo cha polisi majengo afande Joshua. Mahakani Frank alipofika kwa kweli mtu wa kwanza kumuona ilikuwa ni baba yake. "Mwanangu kweli umefanya hichi kitendo. Hapana Frank mimi nakufahamu huwezi kufanya vile huwezi kufanya hivyo Frank"Aliongea baba yake na Frank huku akizidi kulia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Kwa kweli yale Maneno ya baba yake na Frank ambae alikuwa anamwambia mwanae huku akiwa analia yalimfanya Frank kuumia zaidi na machozi yalianza kumtoka. "Kweli baba hicho ulichokisema ni kweli kabsa mimi sijahusika. Ndio maana mimi baba yangu nakupenda maana umeumiza sana Ubongo na kufahamu kuwa mimi sijafanya hiki kitu. Naomba usilie baba yangu Nyamaza mimi sawa nitafungwa ila nitatoka huku nikiwa huru na kumuo Grace wangu. Haya yote..."Aliongea Frank huku machozi yakiwa yanamtoka lakini hata kabla ya Kumaliza kumweleza baba yake Afande walimvuta na Kuondoka kuelekea Mahakani ndani. Yale Maneno ya Frank akiwa anaongea kumbe hata Grace alikuwa anayasikia. Yale maneno ni kama yalitonesha kidonda kwa Grace na kuanza kulia kwa Sauti kabsa maana alishindwa kujizuia. Pia wakati frank akiwa anaongea hata Mzee Ramadhani aliyasikia yale maneno na kuamini Fika kuwa huyu Mtoto hakuwa amefanya kile kitu. Tena alipomuona na Rafiki yake analia ambae alikuwa baba yake na Frank ndio alizidi kumumia zaidi. Alichofanya alitoa Leso mfukoni kwake na kuyafuta Machozi kisha alimfuata Baba yake na Frank. "Mzee Oska mbona unalia Sasa wakati Frank atafungwa hata miezi haishi mimi nitakuwa nimeshamtoa. Najua kabsa mwanao hajafanya hiki kitu lazima kunamchezo unaendelea. Hivyo usiwe na Wasiwasi kabsa. Kama wao wanatumia pesa ili kufanya mambo mabaya na Sisi tutatumia pesa kufanya mambo mazuri. Twende Tuingie Mahakamani tusikilize hukumu ya Mtoto wetu kisha nitakwambia kitu cha kufanya. Ila Tafadhari naomba mahakamini usilie mzee wangu"Aliongea Mzee Ramadhani alipomfikia Baba yake na Frank. Yale Maneno ya Mzee Ramadhani yalimpa Unafuu mzee Oska na waliongozana kuingia ndani. Ndani ya Mahakama kesi ilianza kusomwa tena cha Ajabu kesi zote mbili zilisomwa kwa wakati mmoja wakati kesi ya kumuua Afande Joshua hata siku mbili ilikuwa haijamaliza na ilikuwa inahitajika kufanyiwa uchunguzi. Baada ya kesi zile kusomwa ndipo Frank alipewa muda wa kujitetea. "Sina cha kuongea mbele ya Mahakama hii Tukufu. Ila nashukuru Sana Mkuu wa jeshi la Polisi Arusha kwa kuiandaa hii kesi hadi kuifikisha Hapa. Mwambie na Yule ambaye ananitengenezea hii kesi ipo siku nitatoka na nitamuoa Grace wangu. Pia naombeni na nyinyi ambae mpo mahakamani Mjifunze leo kuwa siyo kila mtu ambaye anafungwa huwa na hatia hapana. Wengine huwa wanaondolewa haki zao na kufungwa pia. Mimi ni Mmojawapo ambae nimeondolewa mpenzi wangu na naenda kufungwa pia. Hakuna kesi ya kweli hata Moja zaidi kesi hizi zote zinatengenezwa. Hakimu mimi nimekubali unihukumu kwenda jera ili kupunguza watu wasiokuwa na hatia wanapotoka kunisaidia kufa ha hatimae kesi zao kutupiwa mimi. Ila tafadhari ambao mnanisikiliza kama mimi nikifungwa naombeni Mkamwambie Grace anisamehe na Aje kituoni kinisalimia kwani nime mmiss Sana. Mwambieni Hakuna mwanamke ninayempenda Duniani kama yeye ingawa napata Matatizo kwa ajili yake lakini siwezi kumwacha"Aliongea Frank mahakani na kushindwa kuendelea Machozi yalianza kumtoka. Yale Maneno ya Frank kwa kweli yalimfanya Grace kuanza kulia kwa sauti mahakamini hali iyomfanya Askari wa Mahakani waende kumtoa. Wakati Frank na Grace wakiwa wanalia huku Shawali alikua akifurahi mbaya na alikuwa anasubilia tu Jaji atoe huku maana hata Jaji wa ile kesi tayari alikuwa amekula milion tano zake kwa ile ksei"Pole sana Frank kwa kufungwa bila hatia ila elewa penzi la Dhati huwa na Misukosuko Mingi. Tafadhari naomba usikate tamaa endelea kunipenda naamini ipo siku haya mambo yote yatakuja kwisha na tutaishi vizuri kama Mume na Mke"Aliongea Grace huku akizidi kulia. kwa kweli Frank alipomuona Grace akiwa anaongea yale Maneno alitamini kuamka na kumkimbilia Akamkumbatie lakini alizuiwa. Kwa Macho yake alimuona Grace akitolewa nje na Afande. Moyoni frank alianza kuyalaumu macho yake kwa nini yamekuwa mazembe kuangalia huenda yangemuona mapema Grace na moyo wake Ungefurahia. Baada ya Grace kutolewa nje Jaji wa ile Kesi alisimama na Kutoa hukumu kwa Frank kuwa ataenda Jera miaka kumi kwa Kosa la kukamatwa na Madawa ya kulevya pamoja na kumuua Afande Joshua



    Baada ya Grace kutolewa nje ya Mahakama baada ya kuanza kulia alienda kukaa nje tena karibu na Defender. Kitu ambacho alikuwa amekipanga ni kwenda kufungwa wote na Frank hakuona Haja ya yeye kwenda Nyumbani wakati Mpenzi wake akiwa anateseka Jera huku yeye akiwa kama msababisha Mkuu. Kesi Mahakamani ilipoisha na Frank Kuhukumiwa Miaka Kumi Alianza kutolewa Nje. Mle Mahakani kwa kweli Mzee Oska alikuwa anamlilia Sana mwanae Frank alijua kamwe hakufanya lile kosa hata kidogo. Grace alimuona Frank akiwa anatolewa Mahakamani na kuanza kupakiwa kwenye Defender tayari kwa kupelekwa Gerezani kwenda kuanza kutumikia Kifungo chake. Alipomuona Frank akiwa anapandishwa na yeye aliondoka mbio na kuanza kupanda mle. "Nasema nifungeni na mimi pamoja na Frank nifungeni. Kama mnauwezo wa kufunga watu ambae hawana hatia kwa nini na mimi msinifunge. Nifungeni siwezi kuishi peke yangu nahitaji kwenda kuishi na Frank. Frank hakuna kosa ambalo amelifanya. Lakini Frank kwa nini Aisha amenidanganya mimi nasema Aisha aliniambia kama ningeonana na Afande Joshua ili tuongee namna ya kukusaidia lakini Mbona sijamuona sasa. Alafu kwa nini na Afande Joshua Afe kwani hakujua kama anatakiwa kuonana na mimi kabla ya kufa ili niweze kukusaidia wewe"Aliongea Grace kama Mtu ambaye alikuwa amechanganyikiwa huku akiwa anahangaika kudandia Gari. Afande Mmoja alikuja kumshika Halima lakini alikutana na Jino moja takatifu hali iliyomfanya mwenyewe kumwachia. "Afande Tafadhari naomba niongee na Mke wangu hata kidogo tu alafu atanielewa ili arudi nyumbani salama. Hizi purukushani anazozileta huku anamimba zinaweza kumletea madhara nipeni Muda kidogo niweze kuongea naye"Aliongea Frank akimwambia Afande Mmoja ambae alikuwa karibu naye. Kweli yule Afande alikuwa mtu mwenye utu sana alimruhusu Frank kushuka kwenye Gari kuongea na Mpenzi wake Grace. Frank aliposhuka kwenye Gari Grace alimkimbilia na kwenda kumkumbatia Kwa Nguvu. "Grace Najua ni kiasi gani unaumia Juu yangu ila naomba usilie maana utakuwa unazuia Baraka za Mungu kuweza kunishukia mimi na kuachiwa huru mapema. Pia kumbuka Grace unaujauzito hivyo pindi unapokuwa na huzuni hata Mtoto tumboni atakuwa na uzuni vilevile kisha utazaa mtoto ambaye atakuwa wa kulia lia ovya. Naomba unielewe watetezi wangu watakuja kunitoa jela na nitakuja kukuoa mapema. Pia naomba umsamehe Goodlucky kwa kitendo ambacho alikufanyia hata yeye alifanya kwa penzi la dhati. Msamehe Goodlucky kwani tayari ameshaomba msamaha maana hata Mungu amesema aombae msamaha husamehewa. Grace nakuomba Mpenzi wangu Usiende na mimi jela wala usiwasumbue hawa afande acha nikafungwe ila nitatoka tu. Kuwa makini mpenzi wangu usikubali kuolewa na mtu yeyote yule"Aliongea Frank kwa huzuni huku Machozi yakiwa yanamtoka na akiwa amemkumbatia Grace. Baada ya maneno yale kweli yalimfariji grace na kuamua kukubali kumwacha Frank akafungwe lakini alimwahidi atapambana kuhakikisha miezi sita haiwezi kupita tayari Frank atakuwa Ameshatoka Jera. Wakati Frank wakiwa wanaongea na Grace huku wakiwa wamekumbatiana Mama yake na Grace pamoja na baba yake walikuwa wanamuona Grace. Ile hali iliwafanya Wazee wale kuchukia mbaya maana waliona watakua na kazi ngumu kuweza kumshawishi Grace kuolewa na shawali. Tena mbaya zaidi Grace alishagundua kuwa wazazi wake walikuwa wanafanya hivyo ili Shawali amuoe Grace. "Mume wangu hapa tuna kazi ngumu, ila lazima Mwanangu aolewe na mtu Tajiri siwezi kukubali hata siku moja. Kuna wazo nimepata mume wangu nahitaji kwenda kwa mtaalamu anifanyie mambo ili Grace amsahau kabsa Frank ndio lazima niende"Aliongea Mama yake na Grace akimwambia Mume wake. Yani HuweziCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Amini mama yake na Grace alikuwa anamchukia Frank mbaya na alikuwa anataka mtoto wake kuolewa na Kijana tajiri Shawali. Tena hata wakati anamwambia mume wake kuwa lazima aende kwa Mtaalamu haadi machozi yalikuwa yanamtoka. Mama yake na Grace alikuwa anamjua mtalaamu ambaye atamfanya binti wake kumsahau frank. Hata yeye alienda kufanyiwa madudu kule ndio maana mzee mambo alikuwa hana neno kwake. Kila kitu ambacho alikuwa anaamua mzee mambo ilikuwa twende tu. Hata nyumba ile aliandika Jina lake maana mzee mambo alishazindikwa hivyo hakuwa na maamuzi yeyote yeye ilikuwa wa kukubali tu. Baada ya kupeana yale Mawazo Mama yake na Grace waliondoka pale mahakani na kuelekea nyumbani. Siku hiyo hiyo alipanga kwenda kwa Mtaalamu ili kumzindika Mwanae amsahau frank.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog