Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

NISAMEHE GRACE - 2

 







    Simulizi : Nisamehe Grace

    Sehemu Ya Pili (2)



    Kwa kweli yale Maamuzi ambayo walichukua Wazazi wake na Grace ya Kumuua Frank yalikuwa ni Magumu sana ila walikuwa Hawana jinsi. Walijua Kama Frank atauawa mwanao atakuwa na Wakati Mgumu lakini huo pia ndio ulikuwa Muda wa Grace kuolewa na Shawali. Maamuzi ya Kumuua Frank yaliungwa CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Mkono na Shawali pia yeye ndio alibeba hata Jukumu la kutafuta watu wa kwenda kummaliza Frank. Aliwatafuta Vijana wenye Uzoefu wa ile kazi ili kuhakikisha Frank anakufa. Baada ya kuwapata wale Vijana alienda kuwakabizi kwa Mzee Mambo baba yake na Grace. Mzee Mambo ndio angewaonesha Mtu ambae alitakiwa kuuawa. Upande Mwingine mzee Mambo moyo wake ulikuwa Unamsuta kidogo kufanya hivyo maana yeye alimuoa Mke wake kwenye familia ya Kimasikini sana lakini wazazi wake hawakupinga. Ila kutokana na kelele za kila siku za Mke wake na Kumtishia kama hatafanikiwa kumuua frank basi wataachana aliamua ukabali tu. Mzee Mambo alikuwa anampenda Sana mke wake hivyo hakutaka hata Siku Moja mke wake kuwa na huzuni hali ambayo ingepelekea kukosekana kwa Furaha ndani. Hadi Muda ule Mzee Mambo anakabidhiwa kazi ya kuwaonyesha wale Vijana mtu wa kumuua ilikuwa imebaki kama miezi miwili tu Frank kuweza kufunga ndoa na Grace. Ambacho alikifanya Mzee Mambo kwanza alikubali kazi ya kuwaonyesha mtu wa kumuua pia aliomba apatiwe Muda maana bado ana mbinu zingine za kumtenganisha Frank na Mwanae. Kama zile Mbinu zikishindikana basi alipanga Kufanya kama alivyotaka Mke wake pamoja na Shawali. Mzee Ramadhani Mwarabu baba yake na Shawali alikuwa ni Mwarabu Tajiri sana ambaye yeye alioa mpare wa Milimani. Mke wake alikuwa anaitwa Rukia na walibahatika kupata Watoto watatu ambae ni Shawali ambae alikuwa chotara yani Sura mbili mchanganyiko pia walikuwa na Mtoto wao Mdogo alikuwa anaitwa Suria ambae alikuwa anasoma Uarabuni pamoja na hadija ambae tayari alikuwa Ameolewa Muscat Oman. Mzee Ramadhani alikuwa anaijua dini kupindukia ila hakujua kama Mwanae alikuwa shetani. Taarifa za Mwanae kuoa binti Mwafrika alikuwa nazo na wala hakumpinga kwa sababu hata yeye alioa Mwafrika ila hakujua kama ndoa ya Mwanae ilikuwa ya kulazimisha na Muda ule walikuwa wanataka hadi kuua mtu. Laiti kama Angejua basi ile ndoa angeipinga Vikali Sana. Baada ya Mzee Mambo kuomba Apewe Muda wa kuhakikisha anatumia mbinu zingine kumfanya mwanae kuachana na Frank na siyo kumua Frank kukubali alianza kufikilia ni Njia Gani aweze kutumia. Usiku ule alimpigia Mwanae Simu na kukutana. Waliongea mambo Mengi Sana ya Kumshawishi Mwanae kuachana na Frank lakini Grace alikuwa Ngangali. Mzee baada ya kuona hata ile mbinu imeshindikana ilibidi kukubali kumtoa Frank Duniani. Ambacho alipanga hatamua Frank Muda ule huenda akapata njia nyingine. Alipanga Kumuua Frank wiki moja kabla ya harusi yake. Hivyo baada ya kuongea na Mwanae alirudi hadi Nyumbani kwake naKumueleza Mke wake kama hakuna njia nyingine ya kuweza kufanikisha Grace kuachana na Frank zaidi ya kumuua. Pia alimuelezea kabsa kuwa watamuua Frank Wiki moja kabla ya ndoa yao ambacho wanatakiwa kufanya Muda huu ni kukubali kinafiki Mwanao kuolewa na Frank hata kama watamuua frank wasije kuhisiwa wao. Kesho yake Asubuhi na Mapema Mzee Mambo walijiandaa na Mke wake kuelekea kwa kina Frank. Lengo walitaka kwenda kumwambia Frank kuwa wapo tayari mwanae kuolewa na yeye. Baada ya kujiandaa waliondoka kuelekea uwanja wa ndege maana ilikuwa Siku ya Juma mosi hivyo Frank na Grace hawakwenda shuleni. Kutoka User liver Hadi Uwanja wa Ndege Ambapo walikuwa wanakaa Frank ilikuwa siyo mbali Sana. Hivyo Muda wa Nusu saa tu tayari walikuwa wameshafika nyumbani kwa kina Frank. Walipofika kwa kweli walikaribishwa vizuri sana na Mwanae. Hata Frank yeye aliwakaribisha vizuri ingawa alijua hawa wanapinga yeye kuweza kumuoa Grace. "Mwanangu Frank kabla hata ya kuongea kitu chochote kwanza natanguliza samahani kwako. Naomba utusamehe sana maana tulitaka kukuondolea kitu ambacho ilikuwa ni halali yako. Hata Mimi wakati Namuoa Mama yake na Grace nilipata Upinzani Mkubwa kutoka kwa wazazi wangu kutokana na Kwao walikuwa Masikini. Ila nilisimama imara kama wewe hatimae nilimuoa Ashura na hadi Sasa naishi nae. Ambacho kimetuleta hapa Mwanangu Frank ni kukutaarifu kuwa Sisi tumekubali Wewe umuoe mtoto wetu. Hivyo kuanzia sasa sisi na wewe tupo pamoja tutashiriki kwa kila kitu kuhusiana na hii ndoa. Hata Harusi haitafanyika kwenu tena bali itafanyika kwetu"Aliongea Baba yake na Grace



    Kwa kweli yale Maneno ambayo aliongea baba yake na Grace yalimfurahisha sana Grace na kwenda kumkumbatia baba yake. Frank nae aliposikia vile alimshukuru sana yule Mzee na Kumshukuru Mungu pia. Laiti kama Angelijua kitu ambacho kilikuwa kimepangwa wala asingethubutu kutoa hata zile shukrani. "Mzee mimi nipo pamoja na nyinyi wala sijawachukia hata siku moja. Nazani Malaika wa Mungu aliwatembelea leo Usiku na kuwaelezea ni Kiasi gani nampenda mwanao na jinsi gani nitakuwa na penzi la dhati kwake. Nashukuru sana Wazazi wangu kwa kulielewa hilo. Lakini Mzee itakuwaje kuhusu Harusi kufanyikia kwenu maana tayari Kadi tulikuwa Tumeshaandaa na tumetoa taarifa kama itafanyika Sanya Juu huko siha"Aliongea Frank huku Uso wake ukiwa Umeenea Furaha ya Ajabu. "Mwanangu Swala la Kadi lisiwaumize sana, ambacho tutafanya tutaandaa kadi zingine nzuri zaidi na tutagawa upya. Pia Matangazo yaHarusi yenu tutarusha kwenye vituo mbalimbali vya Radio vikubwa pamoja na Televishen. Tunahitaji Harusi yenu iwe kubwa Sana na Watanzania Wengi waweza kushuhudia. Kuhusu Gharama za Harusi tutahusika sisi na yale Matangazo yote yatakuwa yanatuhusu Sisi. Muda huu nyie tutawapa kadi za kuwapa Rafiki zenu alafu kazi yote mtatuachia Sisi na wazazi wako Frank"Aliongea Mama yake Na Grace. Yale maneno ya Mama yake na Grace yalimfanya Grace na Frank kuwa na Raha ya Ajabu. Hawakuwa na Jinsi zaidi ya kukubali. Siku hiyo hiyo frank alipiga Simu kwa Wazazi wake na kuwapa taarifa Kuwa Wazazi wake na Grace wamekubali kuunga mkono ndoa yao na wanahitaji kuonana. Baada ya kuwapa Taarifa hizo Grace, Frank na wazazi wake na Grace waliondoka kuelekea User liver nyumbani kwa Mzee Mambo ambapo wangeenda kukutana na Wazazi wake na Frank ambao tayari walikuwa wanajiandaa kuja Usa liver siku hiyo hiyo. Kutoka Sanya Juu kuja Arusha wala siyo mbali sana hivyo Mzee mambo na Frank walipofika User liver hawakukaa sana tayari na wazazi wake na Frank walishafika. Walipofika Walijadiliana mambo mengi sana kuhusu harusi huku Mzee Oska baba yake Frank alihaidi kutoa Ng'ombe Moja pamoja na Gunia moja La mchele kwa ajili ya Harusi ile. Siku hiyo Frank na Grace hawakurudi hata kwao pia wazazi wake na Frank hawakurudi kwao Sanya Juu hivyo wali lala kwa kina Grace. Baba yake na Grace tayari alishamueleza kila kitu Shawali. Hata Sakata la kutoa Matangazo kwenye Radio na Televisheni aliachiwa Shawali. Siku hiyo hiyo Usiku Matangazo mbalimbali yalianza kurushwa kwenye Radio na Tv. Frank na Grace walipoona vile kwa kweli walifurahi sana. Matangazo yalipoanza kurushwa tu Frank na Grace walianza kupata Simu nyingi kutoka kwa Marafi zoa ambao walisoma nao chuo na sekondari huku wakihaidi lazima wafike kwenye hiyo Harusi Maana inaonekana Harusi ya Kifahari sana. Kesho yake Asubuhi Frank waliondoka na Wazazi wake kuelekea kwao Sanya Juu kwa ajili ya Maandalizi kidogo lakini siku hiyo hiyo frank alitakiwa kurudi Arusha kwani kesho yake ilikuwa Juma tatu siku ya shule. Upande Wa Goodlucky Mwanaume ambae alikuwa rafiki mkubwa wa Grace kipindi wanasoma Chuo cha ualimu Mpwapwa kumaliza chuo Aliondoka kuelekea Nyumbani kwao Kilimanjaro. Goodluck yeye aliondoka akiwa na Huzuni Mzito hasa baada ya kukataliwa kabsa na Grace. Licha ya Grace kumkataa lakini aliapa moyoni lazima aje kufanya Mapenzi na Grace hata kama hatamuoa. Hakuwa tayari kumwacha binti mzuri kama Grace kuolewa na mtu mwingine bila yeye kufaidi kitu chochote wakati kuanzia mwaka wa CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/kwanza hadi anamaliza chuo alikuwa rafiki mkubwa wa Grace hadi watu waliamini alikuwa anatoka naye. Hiyo Siku ambayo alikuwa Anaagana na Grace kwa kweli alilia machozi hadi kufikia kumwambia Grace kuwa siku yeyote Mwanaume wake akija kumzingua basi amjulishe atamuoa hata kama akiwa Mzee. Baada ya kuagana na Grace kisha kuondoka alikuwa amechanganyikiwa vibaya mno. Hata simu yake alipoteza Siku hiyo hiyo hali iliyomfanya kuchanganyikiwa zaidi maana namba ya Simu ya Grace hakuwa amekalili. Lakini kwa Upande ule ndio ilikuwa na Faidi kwake Maana huo ndio ulikuwa Muda wa Kumsahau Grace maana alikuwa anateseka sana kimawazo juu ya Grace. Goodlucky alikuwa Anakaa Himo Moshi Kilimanjaro. Baada ya kufika kilimanjaro alimaliza Miezi kazaa hatimae alimsahau Kabsa Grace. Post za Walimu zilipotoka Goodlucky alipata bahati Maana alipangiwa Shule ya Sekondari Makondeko Kufundisha hukohuko Moshi. Siku Moja Goodluck akiwa anaangalia televisheni Ndipo alipokutana na Tangazo ambalo lilikuwa na picha ya Grace na namba zake za Simu huku tangazo lile lilikuwa linahurusu harusi. Kwa kweli Goodluck alipoona tu picha ya Grace alichanganyikiwa sana. Alichofanya alichukua simu yake na Kukopi namba ya Simu ya Grace kisha alimpigia. Tayari Moyo wake ulishamtuma kile ambacho alikuwa anakitaka kufanya mapenzi na Grace kabla ya kuolewa. Baada ya kupiga Simu alimueleza Grace na kukubaliana Kukutana Siku hiyo hiyo ya Juma pili Usa liver. Grace kwanza alifurahi sana kukutana na rafiki yake ambae walikuwa marafiki wa kufa mtu shuleni. Yeye hakujua kabsa lengo ambalo alikuwa nae rafiki yake. Laiti Kama angejua kitu ambacho alikuwa anataka kufanyiwa basi wala asingethubutu hata kukutana na Goodluck. Baada ya Goodlucky kuambiwa na Grace wakutane Usaliver haraka haraka alijiandaa na kutoka. Alipotoka alimtafuta rafiki yake ambae alikuwa Muuzaji mzuri wa Madawa ya kulevya. Baada ya kuonana na rafiki yake alipatiwa dawa ya kulevya kisha Safari ya kuelekea Usa liver kwenda kuonana na Grace ilianza





     Kutoka Pale Makondeko Secondary hadi Moshi Mjini alitumia dakika tano tu. Alipofika Moshi Mjini alipata Gari ambae ilimpeleka hadi Arusha maeneo ya Usa liver. Alipofika Usa liver hakumpa taarifa Grace kuwa Ameshafika. Alimtafuta Rafiki yake kwanza Athumani ambae na yeye alikuwa anafanya kazi Kwenye shirika la Mtu Binafsi. Lengo la Kuonana na Athuman alikuwa anahitaji kumuomba Gari yake ambayo angemaliza kazi ile ambayo alikuwa ameipanga. Athumani hakumnyima Gari lafiki yake maana walikuwa wanashibana mbaya. Baada ya Goodluck kupewa Gari aliondoka na kwenda hadi machame Bar hapo ndipo aliambiwa atamkuta Grace. Kweli alipofika Machame bar Mtu wa kwanza kumuona alikuwa ni Grace. Kwa kweli Goodluck alipomuona Grace ndivyo alizidi kuchanganyikiwa Maana Grace alikuwa amezidi kuwa Mzuri mbaya. Alishuka kwenye Gari na walienda kukumbatiana kwa Furaha. Waliingia hadi Machame bar na kuagiza vunywaji vyao kisha wote walimimina kwenye Glassi na kuanza kunywa huku wakisimulia hadithi mbali mbali za chuoni. "Grace nahitaji kukufanyia Surprise ambayo hutakuja kunisahau kamwe hadi kufa. Naimani hiyo Surprise ambayo nitakufanyia mwenyewe utaipenda maana ni yamuhimu sana kwako. Ambacho nakuomba shika hii hapa Funguo ya Gari kafungue mlango wa gari ingia ndani. Kwenye mbele ya Gari utoana bahasha Moja chukua kisha angalia ndani"Aliongea Goodluck kimwambia Grace. Grace alikuwa anamwamini sana Goodlucky hivyo aliochukua funguo na kuondoka Moja kwa Moja kuelekea kwenye Gari. Alipoondoka tu huo ndio Muda Goodluck aliutumia. Alitoa dawa ya kulevya na kuweka kwenye kinywaji cha Grace. Alipoweka alikichanganya vizuri ili kumfanya Grace asije kuona. "Jamani Goodluck Asante yani nimefurahi sana kwanza ngoja niwasiliane sasa hivi na Aisha maana nimemkumbuka sana"Aliongea Grace huku akikaa kwenye kiti. Ambacho alikuwa amefanya Goodluck alichukua picha ya rafiki kipenzi wa Grace chuoni Aisha na kuweka kwenye bahasha alafu Juu aliandika namba za Aisha. Hivyo hata Grace alipoona alifurahi sana maana aisha nae alikuwa rafiki yake wa Dhati. "Hapana usihangaike kumpigia nataka na yeye tukamfanyia Surprise maana yupo Usa liver hii hii anafundisha. Sema malizia kinywaji kwanza ili tuondoke"Aliongea Goodluck. Grace aliposikia vile kwa kweli alifurahi sana alichofanya alikunywa kinywaji kwa kasi ya ajabu na kumwambi Good waondoke. Alipokunywa kile kinywaji Goodluck alitabasamu maana tayari alimnasa ndege Mjanja kilaini. Kila Goodluck alipokuwa anaangali Mwili wa Grace ndivyo Udenda ulikuwa unamtoka. Alichofanya Goodluck ni kuondoka na Grace hadi kwenye Gari na safari ilianza ya kuelekea sehemu ambayo alikuwa Anaijua Goodluck. Wakiwa kwenye Gari Grace alianza kulalamika kichwa kinamuuama huku akiongea Maneno ya kulewa lewa. Hapo sasa tayari Grace alikuwa hajielewi. Goodlucky alichofanya aliendesha Gari hadi kwenye Guest ambayo alipanga kwenda kufanyia mambo yake. Alipofika alimueleza muhudumu na kumpa chumba huku akimwambia Mtu wake amelewa sana. Alienda kumbeba Grace na kwenda kuingia nae hadi chumbani. Grace alikuwa Amelewa chakali yani alikuwa hajitambui kabsa. Alipomfikisha kitandani hakuwa na Muda wa kuchelewesha zaidi alianza kutoa Nguo yake Moja badala ya Nyingine. Muda wa dakika mbili mbele tayari Grace alikuwa kama alivyozaliwa.



    Baada ya Goodluck kumvua Nguo zote Grace na kufanya mwili wake kuwa uchi hadi alijikuta Goodlucky Mwenyewe akitetemeka. Uzuri ambao aliuona kwa Grace kwa kweli ulikuwa siyo wa Kawaida. Paja ambalo lilikuwa Jeupe na halina hata Upele lilizidi kumchanga sana Frank. Kwa kasi ya Ajabu kama Mtu anaiba kitu kwenye Nyumba ya Mtu Goodluck alivua Nguo zake na kubaki kama alivyozaliwa na Kupanda kwenye Mwili wa Grace na Kuanza Kujihudumia. Ingawa Tunda la Grace lilikuwa Gumu hivi kuweza kuruhusu Mashine ya Good Kupita lakini alijitaidi kuilazimisha kwa kuipaka mate Hadi iliingia. Good hakujua kama Grace hakuwahi kufanya Mapenzi na mtu yeyote hivyo hata wakati anamwingilia Grace alikuwa anatumia Nguvu kama anafanya mapenzi na Mwanamke Mwingine. Baada ya Kumaliza Haja yake na kushuka ndipo Goodluck alipohamaki hasa alipoona Mashine yake ikiwa imetapakaa damu. Alipomwangalia na Grace alikuta Damu zikiwa zinamtoka sehemu yake ya siri. Good kwa kweli alibaki akishangaa maana hakuamini kama angemkuta Grace akiwa kwenye hali ile. Goodlucky alipoona vile kwa kweli alianza kutetemeka hata Muda wa kuoga aliona hana. Alichofanya alichukua shuka akajifuta damu na alianza kutoka chumbani. Kabla hajaufikia hata mlango Moyo wake ulianza kumsuta sana kwa kile ambacho alikuwa amemfanyia Grace. Alichomfanyia Grace ilikuwa kitu cha Kinyama sana na ilikuwa Kama amembaka hivi. Good aliamua kurudi tena hadi Kitandani alimfunika Grace Vizuri kisha alitoa Kalamu yake na kuanza kuandika Ujumbe kwa ajili ya Kumuomba Msamaha Grace. "Grace Naomba Unisamehe sana kwa hiki ambacho nimekifanya. Nimefanya hivi kwa kuwa nilikuwa nakupenda sana Grace. Nahisi unafahamu ni kiasi gani nilikuwa nateseka Juu yako. Najua nimetia Dosari katika mapenzi yako kama mumeo alikuwa anajua kama wewe ni bikra. Naomba unisamehe Sana Grace maana nimekufanyia kosa kubwa Sana. Hii ni Kama nimekubaka hivyo lazima nikuombe Msamaha. Nakutakia Harusi njema Grace na kama Mumeo ataacha kukuoa basi mimi nipo tayari nitakuja kulitekeleza hilo"Alimaliza Good kuandika Sms fupi kisha aliweka kifuani kwa Grace na kuondoka. ................................................................. Frank alipofika nyumbani kwa Wazazi wake waliongea vitu vingi sana kisha alirudi siku hiyo hiyo arusha kwani kesho yake alitakiwa kwenda Shuleni. Alipofika Usa liva alimpigia Sana Grace simu lakini haikupokelewa. Ilibidi aende hadi kwa kina Grace kwenda kuulizia. Majibu aliyopata kuwa Grace alikuwa ametoka kwenda kuonana na rafiki yake ndio yalizidi Kumchanganya Sana. Hadi Muda wa saa kumi na Moja na Nusu bado Frank alikuwa anahangaika kumpigia Simu Grace na Simu yake ilikuwa inaita tu bila kupokelewa. Ile hali kwa kweli ilizidi Kumtia Wasi wasi Frank. Saa Kumi na Mbili kamili Frank aliamua kuondoka na kuelekea kwao walipokuwa wanaishi na Grace. Kichwani alihisi huenda Grace simu yake alikuwa Amesahau nyumbani. Muda wa Saa mbili kamili ndipo Grace alilejewa na Fahamu. Fahamu zilipomrejea kwa kweli alibaki akiwa CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Anashangaa yupo kitandani amelala. Kitu kilichozidi kumchanganya ni baada ya kugundua kuwa alikuwa amelala sehemu ambayo ilikuw ngeni sana kwake. Alipotaka kuamka ili akae na kukumbuka zaidi ndipo alizidi kuchanganyikiwa hasa aliposikia maumivu makali huku akijikuta yupo uchi na Nguo zake zilikuwepo pembeni kitandani. Ile hali kwa kweli ilizidi kumchanga sana Grace maana bado alikuwa hajatambua kitu gani kilikuwa kimetokea. Ilibidi ajifunue shuka yake na kujiangalia.alipofunua shuka alijikuta anapiga mayowe alipokutana na damu kwenye ile sehemu alipolala pamoja na kwenye tunda lake. Ile hali kwa kweli ilimshitua sana Grace na kujikaza kwa Nguvu na kuamka pale. Alipoamka ndipo kile kibarau ambacho aliandika Good kilianguka. Haraka haraka Grace alichukua kile kibarua na kuanza kukisoma huku akiwa anatetemeka. Kila alipokuwa anazidi kusoma kile Sms ndio alikuwa anazidi kuchanganyikiwa. "Hapana Goodluck usifanye hivyo, tafadhari naomba usinitoe bikra yangu maana hii nimemwandalia Mpenzi wangu Frak kama zawadi yake. Nakuomba basi usifanye hivyo Good maana nitaonekana siyo Mwaminifu kwa Frank. Tafadhari naomba uniache kwanza Frank akaitoe ipo siku na wewe nitakuja kufanya mapenzi na wewe Good ila kwa sasa Mwachie Frank maana ndio mwenye haki ya kutoa hii Bikra. Goodlucky nakuomba nirudishie bikra yangu mimi nitamwambia nini Frank tafadhari fanya hivyo"Aliongea Grace huku Machozi yakiwa yanamtoka kama mtoto. Kwa kweli Grace alikuwa amechanganyikiwa Sana maana alishindwa kuelewa ataenda kumueleza nini Mume wake Frank. Frank alivumilia Muda wa Miaka sita bila kufanya mapenzi na Grace leo hii aje kukuta Grace Amefanya Mapenzi na Mtu Mwingine. Kwa kweli Grace alikuwa Amechanganyikiwa na alikuwa analia kama Mtoto Mdogo. Kitendo cha kuingiliwa kimwili bila Ridhaa yake Kisha bikra yake kutolewa ndicho kitu ambacho Kilimfanya kutokwa na Machozi kama Mtoto Mdogo. Alishindwa kuelewa Ataenda Kumwambia Nini Frank Mwanaume ambae alimsubilia kwa Muda Mrefu namna ile. Bora hata kama Angelikuwa Frank kaitoa Kwa Nguvu ingekuwa hafadhari siyo Goodlucky. "Unajua Mwanamke kama bado hutaki kudhaa mapema na mume wako hapendi kutumia Mpira wakati wa tendo la ndoa basi hakikisha ukishamaliza siku zako unahurusiwa kufanya mapenzi kwa Muda wa siku tano hizi zingine za mbele kama Tano hivi unatakiwa umkwepe kwa Namna yeyote ile. Maana hizo ndio Siku ambazo huwa mimba inauwezekano Mkubwa wa kushika"Yalikuwa ni Maneno ya Mkufunzi Anna aliyokumbuka Grace na kufanya ndivyo azidi kuchanganyikiwa zaidi. Grace alikumbuka kuwa ile ilikuwa Siku ya Kumi na Moja ambae ilikuwa hatari sana. Hofu ya kuhisi huenda Mimba ingetunga ilianza kumchanganya kwenye kichwa chake. "Hapana Siwezi kupata mimba haiwezi kutokea bwana. Ila Goodluck kwa hiki ambacho umenifanyia Utakilipa. Lazima nikuue kwa Mkono wangu Haijarishi hata kama ulikuwa Rafiki yangu. Kama Frank akiniacha Jua napanga Kuja kukuua haiwezekani Unikosesha na Mwanaume wangu kisa Starehe zako za Muda Mfupi"Aliongea Grace huku akilia. Grace alijikaza akaamka kitandani na Kuingia Bafuni kujisafisha. Alipooga Haraka haraka alirudi chumbani Guest akavaa Nguo na kuanza kutoka. Muda ule tayari ilikuwa inakimbilia Saa mbili Usiku hivyo Grace hakutaka kupitia hata kwa Wazazi wake Moja kwa Moja alinyoosha Nyumbani kwake ambapo walikuwa wanakaa na Frank. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Baada ya Goodluck Kufanikiwa Kumbaka Grace kisha kumtelekeza Guest alipotoka hakuwa na Muda wa kuendelea kukaa Arusha kabsa. Muda ule hata yeye Moyo wake ulikuwa unamuuma sana kwa kitendo kile ambacho alikuwa Amekifanya. Alijiongelesha Moyoni kuwa atatafuta Muda wa Kumuomba Grace Msamaha. Pia upande Mwingine alikuwa anaomba kwa Mungu yule Mwanaume ambaye alikuwa anamuoa Grace asiwe anajua kama Grace ni Bikra. Maana alijua kama Atajua Grace ni Bikra basi tayari atakuwa ameharibu kabsa ndoa ya Grace. Alipeleka Gari kwa Rafiki yake aliyoazima kisha Alipata Coster Muda ule Usiku na kuondoka kuelekea Moshi ambako alikuwa anaishi kwa Muda ule. Muda wa saa Moja ndio ulitosha kumfikisha Grace nyumbani. Hii ilitokana na Ugumu wa Usafiri siku hiyo kutokana ilikuwa Siku ya Juma pili. Alipofika nyumbani alimkuta Mumeo Frank akiwa Anasoma kitabu Flani cha Hadithi ambacho Hata Grace alikuwa anapenda Kukisoma. Kile kitabu kilikuwa Kimeandikwa na Hussein Tuwa na kilikuwa kinaitwa BIKIRA YANGU. Iilikuwa ni Katabu chenye mikasa ya kutisha ambayo ilikuwa inamkwepesha Mwanamke Angel kutokuvunja bikra yake. Grace alipokiona kile kitabu Kumbukumbu wakati anashituka Kitandani na kukuta ameingiliwa kimwili ilianza kumrudia kichwani. Alikumbuka kuwa hakuwa Bikra tena kama Mwanzo kitendo ambacho kilimfanya Machozi yaanze kumtoka. "Bikra Wangu, Mama watoto wangu karibu, mbona sikuelewi Unakuja huku Ukiwa unalia. Vipi kwani Wazazi Wako wamepinga swala tena la Mimi kukuoa. Hivi Hawajui kama wewe Umehangaika kwa Muda wa miaka Sasa ukitunza bikra yako ili Kuja kunikabidhi Siku ya ndoa yangu"Aliongea Frank akimwambia Grace alipomuona machozi yakiwa yanamtoka. Yale Maneno ya Frank ndio yalizidi kumchoma Grace maana hakuwa na bikra tena. "Hapana Frank Wazazi hawajapinga ila naomba unisamehe Maana nimekuta Miss call nyingi Sana kwenye simu yangu. Niliondoka nikaenda kwa Rafiki yangu Aisha na Simu nilisahau ndani. Ila Hata hivyo Mimi Frank nahisi siyo Mwanamke sahihi kwako"Aliongea Grace na Alizidi kulia zaidi tena kwa SAUTI



    Kwa kweli yale Maneno ambayo aliongea Grace yalimshitua sana Frank. Ilikuwa Vigumu sana kuweza kumuelewa kile ambacho alikiongea Grace. Mwanamke ambaye alikuwa analilia kila Siku kuolewa na Frank leo wazazi wamekubali alafu aje aseme wasitishe. Hata Frank bado alikuwa Hajajua Mpango wa Baba yake na Grace kuwa alikuwa anahitaji kumuua. "Grace Malkia wangu kitu gani ambacho kimekupata hadi Unafikia kusema kuwa wewe siyo Mwanamke Sahihi kwangu"Aliuliza Frank huku akiwa anamshangaa Grace. Lile swali la Frank kama lilizidi kuchoma Moyo wa Grace na kuzidi kulia ziadi. Grace alikuwa anafahamu kuwa Muda ule hakuwa Mke Sahihi kwa Frank. Grace wa Muda ule hakuwa bikra kama Frank ambavyo alikuwa anamjua. Kile kilio cha Grace kwa kweli kilizidi kumshitua Frank na kuamini huenda kuna tatizo ambalo limempata Grace. " Baby hivi unafahamu ni Kiasi gani nakupenda, unapolia wewe ndivyo unazidi kuniumiza mimi. Unafahamu kuwa wewe ndio kila kitu kwangu sasa unapolia mimi nitaliaje" Aliongea Frank huku akiwa anamsogelea Grace. Kwa kweli Grace Alitamani kumueleza Frank kila kitu lakini aliamuua kutulia na kujisemea potelea mbali hata kama akija kugundua kuwa hakuwa bikra alipanga kuisingizia baskeli kuwa ndiyo imemtoa wakati alipokuwa anakimbiza mara kwa mara. "Frank Nakupenda hadi napitiliza nahisi huenda nikawa siyo Mwanamke sahihi kwako kwa haya Mapenzi ambayo tunayo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Ambacho nafahamu mimi watu wanaopendana sana huwahi kusalitiana. Nasikiaga watu wengi husema hasi na hasi siku zote hazigusani, Mimi nakupenda sana na wewe unanipenda sana hivyo nahisi huenda mapenzi yetu baada ya kuoana yawe na hitirafu"Alidanganya Grace. "Grace hicho ambacho unakiwaza hakiwezi tokea hata siku Moja. Mimi nakupenda sana kamwe siwezi kukuacha. Hata Kama ukiniacha basi mimi nitalazimisha kuwa na wewe"Aliongea Frank na kwenda kumkumbatia Grace. Siku hiyo Waliongea mambo mengi Sana huku Frank akijitaidi kumchekesha Grace ili huzuni uishe. Laiti Angejua kitu ambacho alikuwa Amefanyiwa Grace kwa kweli hata Stori zisingekuwa zinapanda. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Baada ya Frank kuondoka kwoa Sanya Juu na Kuwaeleza wazazi wake Juu ya ndoa na Jinsi wazazi wa Grace walivyojirudi Baba yake na Frank alipanga kufanya kitu ambacho Kingeleta heshima kwenye ukoo wao. Baba yake na Frank alikuwa na Utajiri wa kutosha wa Ng'ombe ila hakutaka kuuonyesha ingawala Frank alikuwa analijua hilo. Ambacho alipanga baba yake na Frank ni Kuweza Kumnunulia Mwanae Gari aina ya ST ambae angempa kama zawadi ya kutembelea. Hilo Gari alipanga kumpa Kabla ya Harusi na Siku ya Harusi alipanga Kutoa milioni 50 kwa ajili ya Mwanae kufungulia biashara nyingine. Hicho alikuwa Amekipanga ili kuweza Kumuonesha baba yake na Grace kuwa hata wao walikuwa na mali. Alitaka kuwafundisha siyo kwamba ukiwa na mali lazima uwe na Gari pamoja na nyumba ya kifahari. Alitaka kuwaelewesha mtu anaweza kuwa na Mali lakini akawa anaisha maisha ya kawaida tu. Kesho yake Asubuhi na Mapema Mzee aliondoka na kwenda Hadi Boma Ng'ombe ambako alikuwa Amehifadhi Ngombe zake. Alienda Kuchagua Ng'ombe wakubwa na Kwenda kuuza Maana haikuwa kazi sana kuwapata watu ambae wanahitaji kununua Hizo Ng'ombe. Baada ya Kuuza Ng'ombe Muda wa Saa saba alianza Safari ya kwenda Arusha huku akimtaarifa Mwanae Frank wakutane Arusha Mjini kuna kitu alikuwa anataka kwenda kumnunulia kwa ajili ya Harusi. Alipofika Arusha Mzee tayari alikuwa Ameshaongea na Mzee mwenzake waliokuwa wanafahamiana tangia Zamani na yeye ndio alikuwa anahusika na uuzaji wa Magari. Huyu Mzee hakuwa Mwingine bali ni baba yake na Shawali ambae mwanae Shawali Ndio ambae alikuwa anahitaji Kumuoa Grace. Hata Mpango wa Majambazi ambae yalitakiwa kwenda kumuua Frank yalikuwa yameandaliwa na Shawali





     Baada ya baba yake Kufika Arusha alipokolewa na Mzee Ramadhani kwa Furaha sana. Mzee Ramadhani na Baba yake na Frank urafiki wake ulikuwa Umekomaa Sana kwani ilibidi Mzee Ramadhani yeye Mwenyewe kuacha kazi na Kuja kumpokea Baba yake na Frank. Baada ya Kumpokea Moja kwa Moja aliazisha Safari ya Kuelekea kwenye Jumba lake ambayo walikuwa wanauzia Magari. Njiani Stori mbalimbali zilikuwa zinaendelea hususani ndoa ya Frank. "Nakwambia sitakuunganisha, Hata mimi nitakuwepo na nitatoa zawadi kubwa sana. Kama hiyo Familia inajifanya kwao Matajiri na kukuona Wewe Masikini basi lazima Watakuja kuaibika. Gari Mwanao usimchukulie ST mchukulia IST kabsa maana hizo ndio Gari zinazotesa Sana hapa Arusha. Hata kama utakuwa na Pesa ya ST mimi nitakuuzia kwa bei hiyo hiyo maana huyo Mwanoa ni Mwanangu pia"Aliongea Mzee Ramadhani Maneno yaliyomfanya baba yake na Frak kujivunia kuwa na Rafiki wa Namna ile. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Baada ya Frank kupigiwa Simu na baba yake huku akiambia kuna Surprise anataka kupatiwa Basi alimjulisha na Mpenzi wake Grace ili kwenda Wote. Saa Nne Kamili Wote walikuwa Wameshaomba Ruhusa Shuleni Kwao na walikuwepo Nyumbani Wakijiandaa kwa Ajili ya Safari ya Kwenda kumuona baba yake na Frank alikuwa anataka kwenda Kumpa Surprise gani. Saa saba kamili tayari Walikuwa kwenye Nyumba Kubwa ambayo Wote walikuwa wanafahamu ilikuwa Kampuni ya Mzee Ramadhani ambayo ilikuwa inahusika na Uuzaji wa Magari. Hakuna mtu ambae alikuwa Hamfahamu Mzee Ramadhani Arusha pale kwa utajiri wake. Hadi Frank anapelekwa Pale kwa Kwa Tax ya Kukodi bado hakujua baba yake alikuwa na lengo Gani kumuita kwenye ile Nyumba. Baba yake aliyemzoea kumuona akichunga Ng'ombe Muda wote leo alikuwa yupo kwenye jumba kubwa kama ile ilikuwa ni Kitu Kigeni Sana kwake. Frank hakutaka kujiuliza sana zaidi ya kuingia ndani ya ile nyumba huku wakiwa na Mpenzi wake Grace. Walipoingia Ndani ya ile Nyumba alishangaa Kumuona baba yake akiwa na Mzee Ramadhani wakionyeshana Magari. Ile hali Kwa kweli ilimshitua Frank maana kwanza hakutegemea kama Boss kama yule Kuonana na baba yake na Kuonyesha kitu wakati kumuona tu Mzee Ramadhani ilikuwa Ngumu. Hata yeye aliwahi sana kuja kwenye Jengo hili akiwasindikiza Marafiki zake kuja Kununua pikipiki lakini hata siku Moja hakuwahi kumuona Boss akimuuzia kitu mtu. Hata Style ambayo walikuwa Wanaongea Walionekana walikuwa Wanafahamiana Sana. Siyo Frank tu ambaye alikuwa Anamshangaa baba yake hata Grace pia alikuwa anashangaa Sana. Ilibidi Wasogee hadi wakawafikia na kuwasalimia. Baba yake na Frank alimtambulisha Frank kwa Mzee Ramadhani kuwa ndio Mwanae. "Unaona tena Watapendeza sana kwenye Gari ya IST NA SIYO STpia Bwana Frank Hongera sana kwa kuchangua binti mzuri namna hii. Mimi baba yako ni Rafiki yangu Sana ndio maana hata alipotaka Kununulia Gari yako Kama Zawadi aliamua kunitafuta mimi. Hivyo hata kwenye Harusi yako nitakuwa bega kwa bega na wewe"Aliongea Mzee Ramadhani bila kujua yule binti ambae alikuwa Anasema Mzuri ndio ambae alikuwa anahitajika kuolewa na Mwanae Shawali. Tena Mwanae alikuwa na Mapango Kabambe wa Kumuua Kabsa Frank. Yale Maneno ya Mzee Ramadhani kwa kweli yalizidi kumchanganya Frank maana bado hakuamini kama baba yake alikuwa na Mapango wa Kumnunulia gari alafu walikuwa wanajuana na mtu Tajiri kama huyu. "Mwanangu kabla ya Harusi yako nimemua kukununulia Gari ili Mwanagu Grace asiwe anatembea tena. Sasa hivi kama anaenda kazini hakikisha unamkimbiza kwanza alafu ndio na wewe unaenda kazini. Pia huyu ni Rafiki yangu Mzee Ramadhani wewe ukiwa na shida yeyote Muone huyu usimuogope"Aliongea Baba yake na Frank kisha alitoa Fungua na Kukabidhi Frank kumbe hata Gari tayari walikuwa wameshachagua muda ule walikuwa wanaonyeshana mali mbalimbali mpya tu. Kwa Kweli Grace na Frank bado hawakuamini kama kweli Muda ule walikuwa na Gari ya kutembelea. Frank alimkimbilia baba yake na kukumbatia kwa shukrani. Baada ya Maongezi Mengi hatimae Grace na Frank walienda kupanda Kwenye Gari yao mpya na kutoka nayo. Uzuri Frank alikuwa anajua Kuendesha Gari maana Rafiki yake Ibrahimu kwaoCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ walikuwa na Gari na yeye ndio aliyemfundisha. Bado Grace hakuamini kama wale watu ambae wazazi wake walikuwa wanawadhalau hawana pesa ndio Muda ule walikuwa Wamewanunulia gari kama zawadi. Hata hivyo alijisemea moyoni hawezi kuwaambia wazazi wake Juu ya Gari ambayo walinunulia na baba yake na Frank zaidi alitaka na yeye kuwafanyia Surprise. Alimueleza hata Frank kuwa hili Gari wazazi wake Wasione hadi siku ya Harusi yake. Ilipita kama Mwezi Mmoja hivi Tangu grace na Frank wanunuliwe Gari na Baba yake na Frank. Hadi Muda ule Wazazi wake na Grace walikuwa hawajafahamu kitu chochote. Hata Frank Gari yake alikuwa haitumii sana maana alipanga kuifanyia Surprise. Muda ule Maandalizi ya Harusi ya Frank na Grace yalikuwa yanazidi kupanda chati. Matangazo kwenye Tv ambayo yalikuwa yanashughulikiwa na Shawali ndio ilifanya ile Harusi kuwa Gumzo kila Mtu alikuwa anatamani kushuhudia ile Harusi. Wakati Maandalizi yakiwa yanapamba Moto ya Harusi pia Maandalizi ya Kifo cha Frank yalikuwa yanapamba Moto. Tayari Mzee Mambo alikuwa Ameshawalipa Vijana pesa yote ya Kufanya ile kazi kisha ili kuwapa Mori zaidi aliwapanga kuwaongezea na ingine kama bonus. Pesa yote ya kuwalipa Wale Wauaji ilitoka kwa shawali mtoto wake na Mzee Ramadhani. Wakati Mwanae na Mzee Ramadhani akiwa anafanya maandalizi ya kumuua Frank huku nako baba yake na Shawali Mzee Ramadhani alikuwa anapanga zawadi ambazo angetoa kwenye harusi ya Frank. Kwa kweli hakutaka Kabsa Kumuangusha Rafiki yake kwenye ile Harusi. Tayari Mzee Ramadhani alishatoa nguo za Harusi zote ambazo wangevaa kipindi cha Harusi. Hadi Begi Moja ya nguo kujaa tayari alikuwa ametumia kama milioni Tano hivi. Pamoja na Maandalizi kupamba Moto ila kichwani Kwa Grace kulitawali na Huzuni. Muda wote alikuwa Mtu wa kulia tu Hakuamini uso wake angeliuficha wapi. Ile Siku ambayo Grace alikuwa Amebakwa na Goodlucky ilikuwa si ya hatari kwake hivyo Hadi Muda ule alishajigundua kama alikuwa na mimba ya mwezi Mmoja na Nusu. Grace alishindwa atamwambia nini Mume wake, kitu Gani angetumia kumeleza Mume wake Frank hadi amueleze. Bora Angemkuta siyo Bikra angeisingizia hata Baskeli Swala la Mimba ndio ambalo lilikuwa linampa mtihani Mgumu na Kumfanya Muda wote awe mtu wa kulia TU





    Swala la Grace Kujikuta anamimba lilimfanya kukosa kabsa amani. Alijiona akimkosa Mwanaume ambaye alikuwa anampenda hivi hivi akiwa anamwangalia. Upande Mwingine alitamani akaitoe ile mimba bila mumewe Kujua lakini alijihisi atakuwa Mkosaji Mkubwa kwa Mungu. Hakuwa tayari kuua kiumbe kisichokuwa na hatia yeyote. Kila siku yeye alikuwa anawaza tu ni namna gani Frank atajisikia pindi atakapogundua kuwa yeye hakuwa bikra na alikuwa na mimba ya mtu. Swala la Grace muda wote kuwa mkiya na mwenye Mawazo muda wote yalimfanya Frank Kugundua huenda kuna Tatizo. Frank yeye alihisi huenda Grace alikuwa na Tatizo kutoka kwa Wazazi wake ila alishindwa kumwambia Frank. Frank bado hakuamini kama kweli Grace alikuwa anaumwa kama alivyokuwa anamjibi kila anapomuuliza tatizo ilikuwa ni nini. Muda mwingine Frank alikuwa anamuona Mkewe akiwa analia kabsa. Ile hali kwa kweli ilimfanya Frank kuamua kutafuta sehemu nzuri ambayo angempeleka Grace na kwenda kumbana amuelezee kila kitu. Yeye Frank alihisi lazima Wazazi wake na Grace bado walikuwa wanapanga kupinga yeye asimuoe Grace. Ilikuwa siku ya Juma tatu tulivu ambae zilibaki kama wiki mbili harusi yao kufungwa Frank aliamka asubuhi na kujiandaa pamoja na Mkewe Grace. Frank alimwambia kuna sehemu nzuri alipanga kwenda kumpeleka Grace wakaongee mara ya Mwisho kabla ya kufunga ndoa yao maana wiki moja kabla ya Ndoa Grace alitakiwa Kurudi kwao na Frank alitakiwa kwenda kwao. Hiyo siku wote walijiandaa na kwenda Kupanda Kwenye gari yao Nzuri walionunuliwa na mzee Kishoa baba yake na Frank kama zawadi. Tayari frank alishatafuta Hoteli ya Kifahari ya Morgaline iliyopo Majengo Arusha ndio wangetumia kula Raha zao kwa siku Moja na kumbana Grace hadi amuelezee kitu ambacho kilimfanya kupoteza Furaha namna ile. Wakiwa ndani ya Gari wakielekea Morgaline Mara Grace alimwambia Mumeoa Asimamishe Gari haraka. Aliposimamisha alishuka kwa kasi ya Ajabu na kwenda Pembeni ya barabara na kuanza kutapika. Ile hali ya kutapika kwa kweli ilianza kumchanganya Frank maana ilikuwa mara ya tatu akimuona Grace akitapika. Pia kumbukumbu zilimwijia kipindi alipomuona Grace akiwa anakula udongo kabsa kitu ambacho kilikuwa kigeni sana kwa Grace. Ile tapika tapika ya Grace kwa kweli ilianza kumshitua Frank na kuanza kuhisi huenda Grace tayari alikuwa amemsaliti. Hata hivyo Upande wake mwingine wa moyo ulimpinga vikali maana ulikuwa unaamini kamwe Grace hawezi kufanya vile na Grace hadi muda ule alikuwa bikra. Baada ya Kumaliza kutapika Grace alirudi huku macho yake yakiwa na aibu alipanda kwenye Gari na Safari iliendelea. "Grace Mpenzi wangu una mimba, pia kama una mimba hii mimba nani kakupa"Aliuliza Frank swali ambalo liliufanya Moyo wa Grace kulipuka.



     Kwa kweli lile swali ambalo Frank alimuuliza Grace liliufanya moyo wa Grace kulipukaa paa na kwenda mbio kama vile ameona kitu cha kutisha sana. Grace aliwaza huenda Frank ameshafahamu ukweli kuwa alimsaliti na sasa alikuwa na mimba ya mtu mwingine. "Frank mbona unaniuliza hivyo inamaana huniamini kabsa. Unafikia kuniambia hii mimba ya nani inamaana sasa hivi umeniona mimi malaya"Aliongea Grace kwa hasira kidogo ili kumchokoza Frank kama atakuwa na siri ameijua aitapike yote. "Hapana Grace mpenzi wangu mimi nakupenda sana na pia nakuamini na natambua kama wewe ndio bikra wangu. Ila kuna Vitu mimi vinanishitua sana na kuwaza huenda unamimba ambayo inaweza ikawa ya ajabu kama ya bikra mariamu. Maana mpenzi wangu nimekushuhudia ukitapika sana huku Muda mwingine ulikuwa unakula Udongo na limau. Hii inanifanya niamini utakuwa na mimba mpenzi wangu. Sasa swali ambalo linanisumbua Sana moyo Wangu ni kwamba utakuwaje na mimba wakati wewe ni Bikra au unamimba umepewa na Mungu baba bila ya wewe kujua"Alimjibu Frank Grace kwa utulivu wa hali ya Juu. Kwa kweli yale Maneno yalizidi kumchoma Grace na kufanya kuzidi kulia. Moyoni alifikia kuapa kama Frank akigundua na kumuacha basi yule Aliyempa hii mimba hata kuwa na budi kuendelea kukaa kwenye hii dunia. Grace alihisi Goodluck ndio chanjo cha hii kitu maana isingekuwa yeye kamwe sasa hivi asingekuwa na hali kama hii. Safari iliendelea huku ndani ya Gari CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/wote walikuwa kimya upande wa Frank yeye alikuwa anawaza lazima Wazazi wa Grace watakuwa wamepinga mwanao kuolewa na yeye huku Grace yeye akiwaza ni mbinu gani atumie kumueleza Frank ili kuamini kama yeye siyo msaliti kwake. Tayari sasa walikuwa wameshafika kwenye hotel ya Morgaline ambayo ndio walipanga kwenda kupumzika na kuongea mambo mengi. Baada ya kufika pale walichukua chumba kisha waliweka baadhi ya vitu vyoa na kutoka sehemu ambayo kulikuwa na upepo mzuri walikaa. Wote walikuwa wapo kimya kila Mmoja alikuwa anamtegea mwenzake kuanzisha mazungumzo. Ukimya ule uliwafanya wote kubaini kama kulikuwa na tatizo maana hata siku moja ilikuwa haijawahi kutokea Grace na Frank kuwa sehemu huku wakiwa kimya vile. "Grace wewe ni mpenzi wangu ambae nilipanga nitaishi na wewe milele na milele hilo nazani Mungu amelipokea na tutaenda kuishi wote. Sasa nahitaji uniambie Mpenzi wangu kitu gani kinakusumbua mbona unaonekana haupo sawa. Baby hilo mimi nalifahamu kuwa haupo sawa ndio maana nimeamua kutafuta hotel tuje tutulie tuongee hata kabla ya Harusi yetu. Wewe niambie kila kitu miminipo tayari kukusikiliza mpenzi wangu maana siyo kawaida yako. Kama wazazi wako hawataki mimi nikuoe wewe niambie tu"Aliongea Frank kuvunja ule ukimya. Yale maneno ya Frank kwa kweli yalomfanya Grace kuanza kulia maana alijua kile ambacho ataenda kumueleza frank kinauwezekano mkubwa wa kusambalatisha penzi lake. Aliwaza kichwani ni mwanaume gani anaweza kufunga ndoa na Mwanamke huku akiwa na mimba ya mtu mwingine. Kila alipokuwa anawaza ndivyo alizidi kulia zaidi. Kulia kwa Grace ndio kulimfanya Frank kubaini kuwa Grace alikuwa na kitu kikubwa sana kinamtatiza kichwani mwake. Ilibidi kwanza ambembeleze hadi anyamaze ndio aanze kumuelezea. "Frank moyo wangu unauma sana, frank naomba tafuta Mwanamke mwingine umuoe ila siyo mimi. Frank mimi sasa hivi sikufai, yule Grace ambae ulikuwa unamtegea kuwa naye siyo huyu Frank. Nakuomba mtafute Grace mwingine umuoe wala siyo mimi"Aliongea Grace huku machozi yakiwa yanamtoka. Yale maneno kwa kweli ndio yalizidi kumchanganya Frank maana hakuelewa Grace alikuwa na maana gani hadi kuongea vile. Frank alimwambia tu kuwa hawezi kutafuta Mwanamke mwingi zaidi yake. "Frank naomba uniambie kama hiki ambacho nitakwambia hutaniacha. Frank niambia kama hiki ambacho nitakwambia hutakwenda mbali na mimi na utaendelea na mpango wako wa kunioa" aliongea tena Grace huku Machozi yakiwa yanamtoka. "Grace mpenzi wangu kwa nini unakuwa na Wasiwasi na mimi wakati mwenzako nimeshakusamehe hata kabla ya kuongea"Alimjibu Frank huku akijaribu kumbembeleza Grace. "Frank naomba unisamehe sana kwani siyo Makusudi yangu. Mimi mwenyewe moyo unauma sana hata natamani kujinyonga. Frank unakumbuka ile siku ambayo wewe uliondoka na kutuacha nyumbani na wazazi wangu kisha ww ulielekea kwa wazazi wako Sanya juu. Ile siku kuna rafiki yangu kipenzi sana anaitwa Goodluck alikuja kutembelea. Yule alishawahi kunitongoza mara nyingi sana nilikataa. Basi baada ya kuja Kwetu tulitoka tukaenda bar kunywa vinywaji huku tukipiga stori maana alikuwa ni mmoja wa rafiki yangu sana. Hata tangazo la harusi yetu aliliona na namba alichukulia mle. Wakati tukiwa tunakunywa kumbe mwenzangu alikuja na malengo tofauti. Aliniambia kuna zawadi ameniletea hivyo nikachukue kwenye gari. Mimi niliondoka hadi kwenye gari na kuchukua Baasha kweli nilikuta kuna picha ya rafiki yangu kipenzi Aisha. Kwa kweli nilifurahi sana maana aisha tulikuwa tumeshibana mbaya na namba yake nilikuwa nimeipoteza. Kumbe wakati nilipoenda kuchukua ile picha mwenzangu kwenye kinywaji aliniwekea madawa ya kulevya. Nilipokunywa kile kinywaji aliniambia tuondoke kuelekea kwa aisha maana alidai aisha yupo user liva. Nikiwa ndani ya Gari ndio nilizidiwa na kutokujua kilichoendelea. Nilipokua kushituka nilijikuta goodluck ame... Ame ame ...,ame ameniingilia ame amenibaka. Ndio maana hata muda ule wakati unanipigia Simu sikuwa napokea maana nilikuwa nimepoteza fahamu. Sasa mbaya zaidi baada ya kunibaka hadi sasa amenipa Mimbaaaaaaaaa"Aliongea Grace na kuanza kulia zaidi. Yale maneno ya Grace kwa kweli yalimfanya Frank kushituka na kuamaka kama vile alikuwa ameeona nyoka. Hakujua hata Machozi yalikuwa yametoka wapi alijikuta anaanza kulia tu. "Hapana Grace siwezi kukubali hata siku moja naomba uirudishe bikra yanguu, nasema nataka bikra yangu"Aliongea Frank huku akiwa amechanganyikiwa na kudai kitu kama kweli kilikuwa cha kwake. Yani Muda ule wote walikuwa wanalia kama mtoto mdogo hata wahudumu wa ile hoteli walikuwa Wanamshangaa tu. "Grace ni kweli ambacho ulikiongea kipo sahihi. Wewe sasa hivi siyo Grace yule ambayo nilikuwa namtaka. Ila nashukuru sana kwa kunifanyia hivyo. Miaka sita navulimia kwa ajili yako leo unakuja kuniadhibu hivi kweli. Ni bora basi ungeninyima hiyo Bikra lakini Usingepata hiyo mimba. Hii ni aibu gani Grace. Nashukuru sana Grace kwa ulichonifanyia Mungu atakulipa"aliongea Frank kwa Ujasiri huku akifuta machozi yaliyokuwa yanamtoka na kuanza kuondoka pale hotelini kwa kasi ya Ajabu





    Kitendo cha Grace kusikia yale Maneno ya Frank kuwa yeye hakuwa Grace yule ambaye frank alikuwa anamsubilia yalizidi Kumchanganya Mbaya. Kwa kweli hakuwa tayari kumwacha Frank kuondoka akiwa kwenye hali ile. Haraka haraka na yeye aliamka pale chini na Kumfuata Frank. Alipomfikia Alimshika Mkono huku akimbembeleza Frank asiondoke. "Frank Tafadhari naomba Usifanye hivyo mimi sura yangu nitaiweka wapi. Frank baba sawa nimekubali nimekukosea naomba tafuta adhabu nyingine yeyote ya kuniadhibu ila tu usiniache. Unafikilia mimi nitakuwa Mgeni wa nani frank. Hebu Jaribu kunionea huruma mme wangu, tayari nyumbani maandalizi ya harusi yanaendelea, tayari ndugu na Jamaa wameaanza kuja nyumbani kwenye harusi yetu itakuwaje waambiwe harusi hakuna alafu wajue kuwa mimi nilikusaliti na kutembea na Mwanaume mwingine"Aliongea Grace huku akimvuta Frank asiondoke na machozi yakiwa yanamtoka. "Grace naongea kwa Mara ya Mwisho tena kwa kiswahili ambacho nahisi hata nikimwambia Masai atanielewa. Naongea kwa upole sana na utulivu wa hali ya juu kama mtu yupo ndani ya kaburi anajengea mwana Ndani. Naongea kwa Utaratibu na Unyenyekevu wa hali ya Juu kama Waroma Wanaswali naomba niachie Mimi niondoke hapa. Hivi nitafungaje ndoa na Mwanamke Mwenye mimba alafu siyo yakwangu. Grace nilikuwa nakupenda sana ila sasa hivi nakuchukia kama Mavi. Tayari mimi nilishamwambia CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/kila Rafiki yangu kuwa mke wangu Bikra sasa unafikili itakuaje. Raha ya kuzibua kizipo cha Soda na kuzikilizia mlio wa gesi shiiiiiiiiiii apate mwingine leo mimi nije nipitie sehemu zako za siri ambazo tayari zimekuwa tepetepe kwa kuandaa njia ya kutoka mtoto. Hiyo aibu utapata wewe mimi hainihusu. Inauma Sana ila kama ulivyoniambia kuwa wewe siyo Grace yule ambaye mimi Nilikuwa namzani hivyo Tafadhari wewe Achia tu njia mimi niondoke"Alionge Frank kwa Ujasiri wa hali ya Juu kisha alijitaidi kuondoa mkono wa Grace lakini Grace alikuwa imara hakutaka kumwachia. Muda huo kwa kweli Frank alikuwa Amechanganyikiwa mbaya. "Frank Kumbuka wakati sijakwambia hili neno nilikuomba Msamaha na wewe ulinihaidi kunisamehe. Sasa kama umebadilisha Mawazo mimi siwezi kukuachia nakuomba niue kwanza. Tafadhari niue kwanza Mimi Frank ndipo uondoke hapa"Aliongea Grace huku akizidi kumganda Frank. Yale Maneno ya Grace kwa kweli wala hayakubadilisha Mawazo ya Frank zaidi ya kuzidi kumpa hasira. Alijikaza kujitingisha ili Grace Amuachie lakini Grace alikuwa yupo imara. Kwa hasira ya Hali ya Juu Frank aligeuka na Kumtandika Grace Ngumi kwenye kifua hadi Grace alianza kuyumba kisha alidondoka chini kama Mziko. Ile hali kwa kweli iliwashitua wale wahudumu wa ile hotel na kuamua kukimbia kwenda kumuangalia Grace na Kumzuia Frank asifanye vile. Frank alipoona tayari alishamuweza Grace aliondoka kwa kasi ya Ajabu hadi kwenye Gari yake na kuliondoa Gari kwa kasi. Hata Wahudumu wa ile hoteli walipofika Walimkuta Grace akiwa Amelala chini huku akiwa Ametulia kimya. Mzee Mambo Baba yake na Grace muda ule sasa tayari alikuwa na Jambazi wake na alikuwa anawaelekeza mtu ambaye alitakiwa kwenda kuuawa. Uzuri hakupata taabu maana kuna Jambazi Mmoja alikuwa anamfahamu vizuri Frank hadi sehemu ambayo alikuwa anakaa. Alichofanya Mzee Mambo ni kuwapa tu Bastora ambao wale watu wangetumia kufanya ile kazi. Mzee Mambo hakuwa na Bastora ila ile ya kazi alikuwa Amepata kutoka kwa Mtaalamu Shawali. Baada ya kupewa ila Bastora waliondoka huku wakiafikiana ile kazi inatakiwa kukamilika kesho kutwa saa sita Usiku yani siku tatu mbele.





     Baada ya Grace kupigwa Ngumi na Frank kisha kupoteza Fahamu wahudumu wa ile hotel walilazimika kuchukua gari pale Kwenye ile Hoteli na Kumkimbiza Grace hospitalini. Walipofika Hosipitalini haraka haraka alipokelewa na kupelekwa kwenye chumba cha kufanyiwa matibabu. Hata Walipoulizwa ni nani yao na Amefanyaje walisema kuwa ni Mfanyakazi wa ile hoteli na alijikwaa bahati mbaya na kupigiza kifua. Waliamua Kudanganya ili Wasiulizwe Maswali mengi maana kama wangesema kapigwa lazima ingehitajika kibari kutoka kwa polisi. Muda wa nusu saa mbele Grace alisharudiwa na Fahamu. Aliporudiwa na Fahamu tu mtu wa kwanza kumuulizia alikuwa ni Frank. Kwa kweli Grace alikuwa anahitaji Kumuona Frank kwa Muda ule ule ili aweze kumuomba Msamaha. Muda ule tayari ilikuwa ni Saa saba Mchana hivyo hakutaka kuendelea kukaa pale hospitalini. Dactari walipokuja hawakuwa tayari Kumruhusu Grace kuondoka zaidi ya Kumwambia Apumzike hadi Jioni saa Kumi ndipo angetoka. Wahudumu walimshawishi Grace kwenda kumshitaki Frank polisi au kuachana naye kwani kwa kitendo ambacho Frank alikifanya waliona hafai kabsa. Pamoja na kupewa ushauri huo Grace aliukataa kata kata. Hakuwa tayari kumuacha Frank wala kumshitaki maana aliamini yeye ndie aliyemkosea Frank. Frank alikuwa anakimbiza gari yake aina ya IST kutoka hotel ya Morgaline kuelekea nyumbani kwake huku akiwa amechanganyikiwa mbaya. Kila alipokuwa anakumbuka Maneno ya Grace kumwambia kuwa hakuwa bikra na Muda ule alikuwa na mimba ya Mtu mwingine ndio alizidi kuchanganyikiwa. "Sina Muda wa kuendelea kuwepo kwenye hii Dunia bora nife tu. Grace mimi nitakufa na kukuacha uendelee kuishi maisha mema ila Nashukuru sana kwa kunifanyia unyama kama huo. Ila kabla Sijafa lazima na mimi nikuonyeshe kitu roho yako inapenda. Nataka nife sawa ila kabla ya kufa lazima nilipize kisasi kwako. Lazima nilipize kisasi cha mapenzi ingawa sitafanya na wewe. Lakini Grace Mama kwa nini unanifanyia hivyo Mama yangu. Niambie basi Sweaty wangu kwa nini umenisaliti kinyama hivi. Kweli mimi nipo na wewe miaka Sita bila kukufanyia kitu chochote kumbe mimi ni boya na wenzangu wanagusa kilaini hadi sasa wameamua kukupa na mimba"Aliongea Frank peke yake Kwenye Gari huku akiwa anakimbiza kwa kasi. Muda wa dakika Kumi na Tano tayari alikuwa Amefika nyumbani kwake. Alipofika nyumbani alichukua Nguo zake kama tatu akaweka kwenye Rasketi na Kutoka kwa Haraka kuelekea Shuleni kwao. Huko Shuleni Kwao kulikuwepo na binti alikuwa anaitwa Aisha ambaye alikuwa anampenda sana Frank. Aisha alikuwa yupo tayari kufanya kitu chochote ambacho alikuwa Amepanga Frank ili mradi awe mumewe tu. Hata Aisha aliposikia kuwa Frank alikuwa na Mpenzi lakini bado hakukata tamaa aliendelea kumshawishi Frank akubali hata kufanya nae mapenzi then mambo ya kuoana yangefuata baadae. Yule aisha ambaye walikuwa wanafundisha shule moja na Frank ndio kumbe alikuwa Rafiki kipenzi wa Grace. Na siku ile aliponyweshwa Madawa ya kulevya kisha kubakwa na Goodlucky picha ya Aisha ndio ilitumika kumchanganya Grace. Frank ambacho alikuwa amepanga ni kumshawishi Aisha kukubali kwenda kufanyia mapenzi nyumbani kwake ila hakutaka kumuelezea sababu hasa ya kwenda kufanyia mapenzi kwake. Frank yeye alitaka kwenda kufanyia mapenzi kweke kitanda ambacho walikuwa wanalala na Grace huku akiwa amempigia Grace aje. Akifika ashuhudie frank wakiwa wanafanya mapenzi na Rafiki yake Grace ndicho kisasi ambacho alipanga kulipuka.



    Kutoka nyumbani kwa kina Frank hadi shule ambayo alikuwa anafundisha haikuwa mbali sana. Hivyo Mwendo kama wa dakika tano tu kwa Gari yake tayari alikuwa ameshafika shuleni kwake. Alipofika shuleni hakutaka kuonyesha huzuni ambao alikuwa nao. Aliingia Hadi Ofisini na Uzuri alimkuta Mwalimu Aisha yupo. Hadi Muda ule kwa kweli Aisha alikuwa hajui kama Frank walikuwa na Uhusiano na Rafiki yake kipenzi Grace. Ingawa Frank Kadi za Harusi aliwagawia lakini hakujua yule Grace ambae aliandikwa kwenye lile Jina alikuwa ndio Rafiki yake. Frank alipofika walipiga Stori nyingi na walimu ambae aliwakuta ofisini hata Walipomuuliza mbona alirudi mapema wakati aliaga kuwa hiyo siku hatarudi shuleni aliwadanganya kuwa kule ambako walitaka kwenda amestisha hivyo aliamua kuja tu shuleni.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Baada ya Stori za hapa na pale hatimae Saa nane ilifika na Wanafunzi waliachiwa. Baada ya Wanafunzi kuachiwa ndipo Frank alimfuata Madamu Aisha na Kumwambia kuwa anahitaji ampe lift hadi kwake. Kwa kweli kile kitendo kilimshitua Sana Aisha maana hakuwahi kupewa lift hata siku moja na Frank. Pia kila Mara Aisha alikuwa anambembeleza Frank ampeleka Angalau kwake kupafahamu lakini Frank alikataa. Sasa siku hiyo kupewa vitu viwili kwa pamoja yani kupewa lift pamoja na kupelekwa hadi kwake alihisi ni Moja ya bahati ya Ajabu. Aisha wala hata hakujivuta zaidi ya kulisogelea gari la Frank na kwenda kupanda. "Aisha ni kweli unanipenda kwa dhati kama ulivyokuwa unaniambiaga"Frank alimuuliza Swali Aisha ambalo lilimfanya kushituka sana. Kwa Jinsi Aisha alivyokuwa anamzimia Frank kwa kweli hakutegemea kama ipo siku atakuja kuulizwa vile na Frank. "Frank kwanza naomba uniache nashindwa hata nikuelezeje kwa jinsi tu nilivyojisikia raha leo kunipa lifta na kukubali kwenda kupaona kwangu. Frank mimi nakupenda sana kwa kweli na nipo tayari kwa chochote ambacho unakita. Lakini Frank kwa nini leo unaonekana Mwema Sana kwangu pia unaniuliza Maswali ambayo tayari nahisi tumechelewa maana unakaribia kufunga ndoa bado wiki mbili tu"Aliongea Aisha kwa Mapozi ya hali ya Juu. Furaha ambayo alikuwa nayo Aisha baada ya kuulizwa kama anampenda Frank ilikuwa ya hali ya Juu. "Aisha naweza mimi nikakuoa maana kitu ambacho amenifanyia Mpenzi wangu ambaye nilikuwa nampenda huwezi amini hata nikikuelezeaje. Kiufupi tu nataka ufahamu yule Mwanamke ambaye nilitaka Kufunga nae pingu za Maisha amepewa mimba na Mtu mwingine. Ninavyokwambia kapewa mimba na mtu mwingine namaanisha tangia tuwe na uhusiano sikuwahi kufanya nae Mapenzi. Hata aliponimbia anamimba nilijua siyo ya kwangu. Sasa mbaya zaidi nimemkuta anafanya mapenzi tena na Mtu ndani ya nyumba yangu sasa ambacho mimi nimekiamua nahitaji kuwa na wewe tu. Hiyo ndoa ambayo tulipanga tunaisitisha mara moja alafu tutaenda kufunga ndoa na wewe nyumbani kwetu kilimanjaro. Hivyo kabla ya kuanza kujadili ndoa na wewe nataka unifanyie kitu kimoja. Nahitaji kwanza kulipiza kisasi kwa Grace ndipo nifunge ndoa na wewe. Ambacho nataka kesho nitakuja kukuchukua hadi nyumbani kwangu kisha tuanza kufanya mapenzi. Alafu mimi nitampigia simu yule Mwanamke ili aje nikiwa namwambia nimemsamehe. Akija atakuta tunafanya mapenzi tayari mimi nitakuwa nimelipa kisasi"Aliongea Frank huku akiwa anadanganya. Kwa kweli Ingawa ile ilikuwa ni Kazi Ngumu lakini Aisha alikubali na kumwambia Kesho aje kumchukua. Frank alimpeleka Aisha hadi kwake huku wakipigana Mabusu ya kufa Mtu. Alipofika kwa Aisha frank alikaa kama saa moja kisha aliondoka. Frank alipoenda kwake alimkuta Grace naye amesharudi. Grace alipomuona Frank alimfuata huku akilia na kwenda kumkumbatia huku akimwomba Msamaha. "Grace mimi nimekusamehe kabsa naomba tu utunze hiyo siri. Usimwambie mtu kama hiyo mimba siyo yakwangu"Aliongea Frank kwa Kumdanganya Grace maana yeye tayari alikuwa anajua kile ambacho alikuwa anakitaka. Kwa kweli Grace aliposikia Frank akiongea vile alifurahi sana na kuzidi kumkumbatia zaidi. Hiyo siku kwa kweli Grace na Frank waliongea mambo mengi kuhusu ndoa yao. Laiti kama Grace angejua mawazo ya Frank kwa kweli asingewaza hata ndoa. Kesho yake wote waliamka wakaoga pamoja na kuachana kila mmoja akienda shuleni kwake. Muda wa Saa nne Tayari Frank alikuwa na Aisha kwenye Gari wakienda nyumbani kwa kina Frank kwenda kukamilisha kile kitu ambacho alikuwa amekipanga. Walipofika kwake Frank alimpigia Simu Grace na kumuomba Aje nyumbani kwani kuna kitu cha Muhimu anataka kuongea naye. Frank alijua hadi Grace anaaga shuleni na Kuja nyumbani tayari atawakuta wakiwa wanafanya mpango. Alichokuwa anataka Frank ni Grace kuona tu lile tukio kisha yeye anajiua-



    Grace alipoambiwa na Frank kuwa anatakiwa wakutane nyumbani kuna kitu anaenda kuambiwa wala hakuchelewesha Muda. Hapo hapo alienda kwa Mwalimu wa zamu na Kumuaga kuwa anaenda nyumbani mara Moja. Baada ya kupata Ruhusa kutoka kwa Mwalimu wa Zamu alianza Safari ya Kurudi nyumbani. Moyoni Grace alikuwa anamshukuru Mungu kwa kumsaidia Kumbadilisha Mawazo Frank. Laiti Angelijua kitu ambacho angeenda kukutana nacho kwa Frank Kwa kweli hata asingekubali kwenda. Muda wa Dakika kumi tu tayari Grace alishafika nyumbani. Alipoingia ndani alisikia Vilioa ambavyo Vilimfanya moyo wake kuruka paa. "Baby tafadhari ingiza pole pole mwenzako siyo Mzoefu na haya mambo. Oooooh Frank unaniumiza mpenzi wangu usipige haraka haraka ooooooooh my God nakupenda Frank"Yalikuwa ni Maneno ya Aisha akilalamika kipindi wakiwa wanafanya Mapenzi na Frank. Yale Maneno ya Aisha kwa kweli yalimshitua Sana Grace. Upande Mwingine alihisi Labda Frank alikuwa Anaangalia video ya Ngono. Kwa kasi ya Ajabu Grace aliingia chumbani ambako walikuwa wanalala. Kwa kweli ilikuwa kidogo roho imtoke Grace alipokuta Frank akiwa uchi huku akiwa Amemkunja binti wa watu wakifanya naye Mapenzi. Vile vitu kwa kweli Vilimfanya Grace hadi alianza kuona Kizungu zungu. Mwili wote ulikuwa unamtetemeka Grace na Machozi ya Hasira yalianza kumtoka. Cha ajabu Frank yeye alipomuona Grace ameingia ndio na yeye alionekana kama Amepagawa Vibaya Mno na Penzi la Aisha kwani na yeye lianza kuguna huku akisema aisha nakupenda Sana wewe ndio utakuwa Mke wangu. Kwa kweli yale Maneno ya Frank yalimfanya Grace kupandwa na Hasira na kwenda kumshika Frank na kumvuta kwa nguvu hadi Mashine ya Frank ilitoka kwenye Tunda la Grace. alimvuta Frank alimsukuma pembeni kisha alimfuata yule Mwanamke ambaye alikuwa anafanya mapenzi na Frank ili kumuonesha kazi. Ila anataka kwenda kumshika kwani Aisha na yeye alishaamka ndipo Grace alizidi kushangaa kukuta yule binti ambaye alikuwa anafanya Mapenzi na Frank alikuwa ni Rafiki yake Kipenzi Aisha. Hata Aisha nae kwa kweli hakutegemea kama binti ambae alikuwa Amesimama pale alikuwa ni rafiki yake Kipenzi grace. "Aisha kwa nini unanifanyia hivi Rafiki yangu, Mimi nimekufanyia kosa gani kubwa hadi Unaamua kutembea na Mume wangu tena ndani ya nyumba yangu na kitanda changu. Aisha baada ya kuunda mbinu ya mimi kubakwa na Goodlucky leo hii Umeamua kunionyesha kabsa laivu unalala na Mume wangu tena kwenye chumba Changu. Kweli leo nimeamini kama Rafiki yako ni adui yako"Aliongea Grace huku akiwa anashangaa na Machozi yalikuwa yanamtoka. Muda ule kwa kweli Aisha alikuwa anatetemeka tu hata kuchukua Nguo alishajisahau. Hakutegemea kabsa kama yule mtu ambaye alikuwa anaongea pale alikuwa ni rafiki yake kipenzi wa chuoni Grace . CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Hata pale alihisi labda yule pale alikuwa ni mzimu tu wala hakuwa Grace. Tena Maneno ya Grace kusema kuwa wameunda mpango wa kubakwa na Goodlucky ndio yalimfanya Aisha kuzidi kuchanganyikiwa zaidi. Upande wa Grace kumuona Aisha wakiwa wanafanya mapenzi na Grace alihisi lazima hata picha zile ambazo Goodluck aliweka kwenye bahasha kama mtego wa kumwekea madawa ya kulevya ule mpango walisuka na Aisha ili Frank amuache Grace na Aisha kuwa nae kitu ambacho ilikuwa siyo kweli. Aisha yeye hata wakati anaenda Kwa Grace hakuwa na wazo kama mpenzi wake na Frank atakuwa ni rafiki yake."Grace hicho ndicho kisasi changu ambacho nilikuwa nimepanga kukifanya kwako. Miaka sita nimevumilia nikiwa Najua wewe ni bikra kumbe ulikuwa umenifanya Bwege na ulikuwa Unafanya mapenzi na Watu wengine. Grace nimekuja kulipiza kisasi kisha naenda kujiua, ila NISAMEHE GRACE kwa hiki ambacho nimekufanyia maana naona kimekuuma sana. Hata mimi uliponiambia kuwa Unamimba niliumia hivi hivi. Pia Aisha Naomba unisamehe kwa kukulaghai. Mimi siwezi kuwa na wewe kama nilivyokwambia maana nilikuwa nakudanganya ili niweze kulipa kisasi kwa Grace. Huyu ndio Mwanamke ambaye amepata mimba wakati Mimi bado sijafanya nae mapenzi. Najua Fika kama wewe ni Rafiki yake kipenzi na Grace ndio maana nilifanya hivi ili nilipe kisasi ambacho kitamuuma zaidi Grace"Aliongea Frank na kuanza kutoka mle chumbani kwake akimwacha Grace na Aisha Wakiwa bado Wanaangaliana. Kwa kweli yale Maneno ambayo aliongea Frank yalimfanya Grace taratibu machozi yalianza kumtoka. Hakuamini kama Frank angefanyia unyama kama ule. "Frank tafadhari naomba usinifanyie hivyo Maana mimi nakupenda sana. Tafadhari Frank naomba utambue kuwa mimi sijafanya hicho kitu kwa kukusudia kama wewe ulivyonifanyia. Mimi nilibakwa Frank tena nilibakwa huku nikiwa sijitambue sasa mimi kosa langu hapo ni lipi Frank. Najua umenifanyia kosa kubwa Sana Frank kwa kunifanyia hivi lakini naomba mimi tambua bado nakupenda tena nakupenda Sana mpenzi wangu. Kama hii Mimba ndio tatizo sasa hivi nipo tayari kuitoa ili tu niwe na wewe Mpenzi wangu. Frank Tafadhari Jaribu kuvuta kumbukumbu tulipotoka alafu unisamehe. Hili ndio kosa langu wa kwanza kufanya hivyo Kamwe naomba usinifanyie huu unyama mwenzako nitakufa. Wazazi wangu sasa hivi wapo kwenye maandalizi ya Harusi sasa itakuwaje kama Watapata taarifa kama kuwa wewe umenisaliti na hakuna harusi tena"Aliongea Grace huku akiwa amemshikilia shati frank asiondoke. Yale Maneno ya Grace kwa kweli yalizidi kumchanganya tu Frank maana hakuwa tayari kabsa kurudiana kimapenzi na Grace. Kwa nguvu zake zote Frank alijikakamuua hadi Grace akamwachia kisha alitoka ndani na kwenda kupanda Gari na kuliondoa kwa kasi. Muda ule Frank alishasahau hata kama kuna Mwanamke alikuja nae pale nyumbani kwake. Grace alijitahidi kumuita Frank ili asiondoke lakini hakuna kilichosikilizwa zaidi ya kuachiwa vumbi. "Grace tafadhari naomba unisamehe kwa kweli mimi sikujua kama wewe Grace rafiki yangu kipenzi ndio unamahusiano na Frank. Nimefanya hivyo kwa kuwa nilikuwa nampenda sana Frank ila ningejua kama wewe ndio ulikuwa na uhusiano na wewe kamwe nisingeweza kufanya hivyo"Aliongea Aisha huku akilia maana alijihisi mkosaji mkubwa kwa Rafiki yake. "Aisha naomba usilie maana kwa jinsi Frank alivyojieleza nimegundua wewe huna kosa lolote. Pia siwezi kukulaumu kumpenda Frank kwa kuwa wewe pia ni Mwanamke sahihi na unahisia kama mimi. Ila naomba uniambie wewe ulihusika kwenye mpango wa mimi kubakwa na Goodlucky maana nakumbuka aliniambia nikachukue mzigo kwenye gari yake. Nilipoenda kweli nilikuta kuna picha zako na ndio muda aliyetumia kuniwekea madawa ya kulevya kwenye pombe na kunibaka"Grace alimuuliza Aisha swali huku akiwa anafuta kabsa Machozi hakutaka kabsa kulia kwa muda ule. Lile Swali la Grace kwa kweli lilimshitua aisha kidogo maana hakuwa anajua hata kama Goodluck aliwahi kumbaka Grace. "Grace kwa kweli mimi sijui kitu chochote ambacho kinaendelea. Sawa nakumbuka Goodlucky nilimpa picha kipindi flani tulipoonana lakini mimi sikujua kama alichukuwa kwalengo lile. Hata hizo picha ambazo nilimpa mimi imepita kama mwaka hivi. Ila Grace unataka kuniambia ni Kweli Goodluck ambae alikuwa rafiki yetu shuleni ndio ambae alikufanyia hivi. Ni kweli Goodluck ndio ambae alikubaka na kukupa hii mimba hali iyokufanya kuachana na Frank. Pia huyu Frank ambae upo nae ni huyu Mume ambae ulikuwa unaniambia kipindi tunasoma kuwa unamtunzia bikra yako"Aisha aliongea na kumuuliza Maswali Grace mengi ambayo hayakuwa na Majibu. "Aisha huyu ndio Frank niliyokwambia namtunzia bikra yangu. Pia Goodlucky ndio ambae alinibaka hadi kunipa mimba. Ila Naomba ondoka sasa hivi kamuoke Frank maana anampango wa kujiua. Nenda kamwambia asijiue pia ukikuta kitu chochote kibaya kimenipata naomba umtunze frank wangu na ikiwezekana muoane maana nimegundua hata wewe unampenda sana Frank. Kama ulikuwa tayari kulala hata Frank ili mwanamke wake akija agundue waachane ulikuwa unampenda sana. Tafadhari ondoka kamuokoe Frank maama atakufa"Aliongea Grace. Yale maneno ya Grace ndio yalimkumbusha aisha kweli wakati Frank anatoka alisema anaenda kujiua. Alipokumbuka alitoka nduki ndani ili kwenda kumuokoa Frank. Muda ule Aisha alipanga kwenda kumuelezea kila kitu Frank na kumshawishi frank asimuache Grace maana Grace alibakwa wala hakufanya mapenzi akiwa anajielewa. Aisha alipotoka Grace nae hakuwa na Muda wa kuendelea kukaa ndani kwake kila alipokuwa anaangalia kitanda alikuwa anamuona mpenzi wake Frank wakiwa wanafanya mapenzi na aisha. Alichofanya alichukua Karatasi na kalamu kisha aliandika ujumbe kwa Frank kabla ya kufanya kile ambacho alikiamua kwa Muda ule. Baada ya kumaliza kuandika ule Ujumbe aliweka alitoa na ile barua ambayo Goodlucky aliandika baaada ya kumbaka na kuiweka pamoja. "Mungu baba nahisi mimi nitakuwa mkosaji mkubwa kwenye hii dunia na sipaswi kuendelea kuishi humu. Kweli mimi ni mkosaji maana nimelala na mtu wa nje na kupata mimba kabla ya mpenzi wangu kipenzi sijamkabidhi tunda lake. Sasa Sina umuhimu tena wa kuendelea kuishi kwenye hii dunia kama yule mtu ambaye anafuraha yangu tayari hanitaki. Najua hiki ambacho nakifanya siyo kizuri ila sina jinsi mungu wangu. Naomba usisamehe kwa haya yote mabaya niliyoyatenda na nipokee nakuja kwako Mungu wangu. Mwanagu uliopa tumboni naomba unisamehe kwa kukuua ukiwa upo tumboni wakati ulikuwa na hamu ya kuiona Dunia jinsi ilivyo na Mwanga mzuri. Ila unatakiwa kufa tu Mwanangu maana sikupanga kuja kuzaa na mtu mwingine zaidi ya Frank. Kama Frank angekubali wewe umuite baba basi ningekuzaa Mwanangu. Kwa kuwa Frank hataki wewe uje umuite baba basi acha tufe wote pamoja na mimi"Aliongea Grace kwa huzuni huku machozi yakiwa YANAMTOKA .



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa kweli huzuni ambao alikuwa nao Grace ilikuwa hauna kikomo. Mwanaume ambaye alimsubilia kwa Muda mrefu leo kuja kukataliwa kisa mimba ambayo alipewa kwa kubakwa. Hapo ndipo Grace alipofahamu kuwa Frank hata kama wangeoana huenda angemjali kwenye raha tu na siyo hadi kwenye matatizo. Moyoni alianza kuhisi kuwa Frank kamuonea sana Maana lile lilikuwa kosa la kwanza kwake na hakufanya Makusudi hivyo frank hakutakiwa kumuhukumu kwa Namna hiyo. Baada ya kuandika na kuiweka ile barua Vizuri Grace aliondoka kuelekea Sehemu ambayo alipanga kwenda kuyatoa Maisha yake. ........................................................... Wakati huku Mambo yakiwa hayaeleweki huku tayari mzee Mambo alikuwa Ameshawaelekeza Majabanzi kwenda kuvamia nyumba ya Frank na Kumuua tena Mchana. Nyumbani kwa Mzee Mambo Maandalizi ya kinafiki ya Harusi yalikuwa yanaendelea. Wao hawakuona shida pesa kidogo kupotea ili wakamilishe mpango wa Kumuua Frank. Majambazi walipoenda Nyumbani kwa Frank walimkosa Frank. Hata walipofatilia shuleni kwake wakamkosa pia. Simu ya Mwanae Grace aliyompigia baba yake kumwambia kuwa wasitishe maandalizi ya Harusi kwani hana mpango wa kuolewa na Frank ndio ilimfanya Mzee kuwa na Furaha zaidi. Hata mpango wa kumuua Frank ambaye moyoni ulikuwa unaonekana kazi ngumu kwake aliusitisha. Aliona haina Umuhimu wa kumuua Frank kama Mwanae tayari hataki Frank amuone. Alichofanya aliwapigia Simu Majambazi aliyowatuma na kuwaambia kazi hiyo waache kwani haina haja tena ya Kumuua frank. Hivyo Frank kutengana na Grace ndio ikawa pona pona yake. Baada ya Frank kuondoka nyumbani kwake kwa kasi ya ajabu. Hakuna kitu Kingine chochote ambacho alikuwa anakifikilia zaidi ya kujiua. Wakati yupo kwenye Gari mawazo yalimrudia kipindi wakiwa wanafanya Mapenzi na Aisha. Alikumbuka pia kipindi aisha alipomwangalia kwa macho ya Mshangao pindi aliposema kuwa hampendi kwa dhati ila alikuwa anafanya mapenzi na Aisha ili kulipiza kisasi. Alipokumbuka zaidi alibaini hakumfanyia kitu kizuri Aisha hivyo mpango wake wa kujiua ilibidi asitishe kwanza amuombe Msamaha Aisha ndipo ajiue. Alichoamua ni kwenda nyumbani kwa Aisha kwenda Kumsubilia. Alipofika nyumbani kwa Aisha alikuwa anajua sehemu ambapo funguo zilikuwa zinakaa hivyo alichukua akafungua mlango na kuingia ndani. Mle ndani alikuwa mtu wa kulia tu aliamini kitu ambacho Grace alimfanyia ilikuwa siyo kitu cha kawaida kabsa. Alihisi Grace alimfanyia Unyama mkubwa ambae ulikuwa hauvumiliki. Alikaa kwa Muda kama wa nusu saa ndipo alipomuona Aisha akiwa amerudi. "Frank bado upo mzima kwa nini Frank unataka kujiua ni kweli unataka kujiua au ulikuwa unamdanganya Grace"Aliongea Aisha huku akiwa kama mtu ambae alikuwa Amechanganyikiwa. "Ni kweli aisha nahitaji kufa, nasema nahitaji kufa ili nikaishi mbali kabsa na Grace. Grace kanifanyia kitu cha kinyama sana. Nimekaa miaka sita nikimsubilia yeye kumbe sikujua kama nilikuwa nafanywa taira. Aisha kama isingekuwa nimekukosea wewe tayari hadi Muda huu ningekuwa nimeshakufa. Hivyo nimekusubilia wewe tu nije nikwambie samahani kwa niliyokutendea. Naomba unisamehe Sana Aisha kwa kukutumia kama chambo kulipiza kisasi changu kwa Grace"Aliongea Frank na kuanza kutoka ndani kwa Aisha ili kwenda kujiua. Aisha naye hakuwa tayari kumuona frank akitoka ndani kwake. Alichofanya alimuwahi na kwenda hadi mlangoni na kumzuia asitoke. "Kabla ya wewe kujiua Frank naomba uniue kwanza mimi. Frank nimegundua kweli ulikuwa hauna moyo wa kuishi na Grace. Hata mimi sasa hivi hata ungesema unione tuishi na wewe nisingekubali maana wewe hauna Huruma. Yani Rafiki yangu Grace kabakwa kwa nguvu na Goodlucky tena kwa kuwekewa Madawa ya kulevya lakini wewe hutaki kumsamehe. Frank Grace hakufanya mapenzi huku akiwa anajitambua. Grace alibakwa na Rafiki yake Goodlucky akiwa hajitambui. Hivi Fikilia kama wewe ningekuwekea Madawa ya kulevya kwenye kinywaji. Alafu baadae ujikute upo uchi na tayari ujikute umefanya mapenzi na mimi alafu Grace aje kugundua alafu asikusamehe ungejisikiaje. Nauhakika na Asilimia mia Grace hana kosa na wewe ndio umemkosea sana Grace na unahitajika kwenda kumuomba msamaha. Wewe ndio umemsaliti Grace maana umefanya mapenzi na mimi ukiwa na akili zako. Mwenzako alifanya mapenzi bila yeye kujitambua. Mwanaume gani wewe unakuwa na moyo wa jabari. Baada ya kukaa na kumliwaza mwenzako kwa unyama aliyofanyiwa leo hii unataka kujiua. Unalilia bikra kwani bikra kitu gani, unalilia kitendo cha kuingiza uume wako kwenye uke wa Grace kisha utoke na Damu. Goodlucky mimi namfahamu sana maana alikuwa anampenda sana Grace mbaya. Hata chuoni alikuwa anamlazimisha lakini alikuwa anakataliwa. Sasa kwa Taarifa yako Grace anaenda kujiua na wewe ndio utaenda kuyajibu huko mbinguni. Ila hata hivyo kama na wewe unaenda kujiua basi hakikisha unaniua kwanza mimi ndipo na wewe ujiue maana tayari na mimi umefanya mapenzi na mimi na kunitia janaba. Kaa fikilia kipi kizuri uniue mimi ndipo ukajiue wewe au ukaokoe maisha ya Grace pamoja na kumuomba Msamaha. Maana Grace akifa atakuwa ameua na kitoto tumboni ambacho kilikuwa na hamu ya kuona Mwanga duniani na masabishaji atakuwa wewe"Aliongea Aisha kwa hasira huku hadi machozi yakiwa yanamtoka. Kwa kweli yale maneno ya Aisha yalimmaliza kabsa Frank. Frank alibaini kweli alikuwa hafanyi kitu sahihi maana alikumbuka wakati wakiwa morgaline hotel Grace alishamueleza kuwa hii mimba hakupata kwa kupenda ila alibakwa na Goodluck. "NISAMEHE GRACE tafadhari naomba unisamehe Grace kweli nimegundua mimi ni Mpumbavu. Aisha naomba twende unisindikize nikamuombe Grace Masamaha"Aliongea Frank huku machozi yakiwa yanamtoka. Kwa kasi ya ajabu frank walitoka na aisha kisha walipanda gari na kuanza kurudi nyumbani kwake. Walipofika nyumbani walikuta Milango ipo wazi walipoingia ndani walikuta hakuna mtu. Wakati akiwa anamuita Grace ndipo macho yake frank yalipotua kwenye bahasha flani. Kwa kasi ya ajabu alifungua na kuanza kuisoma. Kila hatua ambayo alikuwa anapitia kuisoma ile bahasha kwa kweli alikuwa anatetemeka huku machozi yakizidi kumtoka. "Hapana haiwezekani, nasema haiwezi tokea kitu kama hiki hata siku moja. Grace hawezi kufa"Aliongea Frank maneno yaliyomfanya aisha kuzidi kushangaa na kutoka ndani kwake nduki alienda kupanda kwenye gari yake na kuliondoa kwa kasi.





    Mwendo kasi ambao alikuwa Anakimbiza Frank Gari ulikuwa siyo wa kawaida kwa gari ndogo kama IST ambayo alinunuliwa na baba yake kwa ajili ya Misele ya hapa na pale. Gari Aina ya IST ni gari mahususi kwa ajili ya kupondea hara mbali mbali na siyo kuzikimbiza namna hiyo. Kwa Muda ule mawazo yale kwa Frank ilikuwa hakuna, alichokuwa anahitaji ni kuwahi Kwa mpenzi wake Grace kwenda kuzuia lile Jambo ambalo alikuwa anaenda kulifanya Grace. Frank alikuwa anakimbiza Gari huku kichwani kwake akiwa ametawaliwa na mambo mengi sana na mazito ambayo yalikuwa vigumu kuyatua kama mtu asipokaa na kupata mawazo kutoka kwa watu ambae wenye busara za kutosha. Kutoka Uwanja wa ndege hadi kufika Majengo kulikuwa hakuna foleni wala Magari ambayo yalikuwa yanakatisha ambayo yangemfanya kuchelewa kufika usa liver ambako alikuwa anaenda. Alipofika Majengo ndio sasa kukawa na foleni ya magari huku sehemu zingine zikimlazimu kusimama kwa Muda magari mengine yapite ili kuweza kuendelea na Safari. Ile hali ya foleni ilipozidi kuongezeka ndio ilimfanya Frank kwenda kupaki Gari akachukua Boda boda kwa lengo impeleke Hadi Nyumbani kwa Grace ili kwenda kumsitisha Grace kile kitu ambacho alikuwa anataka kukifanya. "Kijana tafadhari naomba ongeza Mwendo wa pikipiki. Kama utakimbiza Zaidi nitakulipa mara mbili ongeza Mwendo kijana"Aliongea Frank kwa Buguzi huku akiwa anampiga piga Yule Dreva Mgongoni. Mwendo ambao alikuwa Anakimbiza Dreva ile pikipiki ilikuwa kasi sana lakini Frank ndio kwanza yeye hakuona alizidi kumlalamikia Yule kijana kuwa hawezi kukimbiza Pikipiki ipasavyo. "Frank tafadhari naomba unisamehe naomba unisikilize kwanza ndipo utapata Ukweli wa hiki ambacho kimefanya hadi nikawa hivi. Najua itakuwa Vigumu sana kuweza Kuamini Frank lakini naomba nipe nafasi ya kukueleza kwanza kama hutanielewa na hapo ndipo utanichukulia maamuzi hayo"Alikumbuka Frank moja ya maneno ambayo mpenzi wake Grace alishawahi kumwambia ndio alizidi kuchanganyikiwa zaidi. Kutoka Majengo Arusha hadi Usa liver ni mwendo kama wa dakika kumi hivi kwa gari inayokimbia ila yule Kijana alitumia dakika tano tu tayari alishafika Usa liver. Haraka haraka Frank alishuka akamkabidhi yule kijana pesa yake kisha aliondoka nduki kuelekea kwa kina Grace.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Alipokaribia kwa kina Grace ndipo alihisi miguu yake ikikosa nguvu na radha ya kufika kwa kina Grace ilipungua ghafla. Kile ambacho alikiona kwenye barua ambayo Grace alikuwa Amemwandikia na kuiacha kitandani ndicho ambacho alihisi kimetokea kwa Grace. Kinamama ambao walikuwa wanalia huku na Wazee wengine wakiwa wamekaa kwenye mikeka nje ndio ilimfanya kuamini Tayari mpenzi wake alikuwa Ameshakufa. Huku akiwa anahisi kizungu zungu alizidi kujikaza kutembea kuelekea nyumbani kwa Grace. Ingawa wazazi wake na Grace walikuwa wanamchukia Sana frank lakini bado yeye hakuogopa alizidi kwenda kwenye ile nyumba. "Shemeji Naomba rudi Usifike nyumbani kwa kina Grace Tafadhari. Shemeji utafungwa hapa ninapoongea tayari Grace hayupo tena Duniani hivyo rudi si unajua wazazi wake wanavyokuchukia tafadhari nakuomba rudi"Yalikuwa ni Maneno ya Rafiki yake na Grace akimwambia Frank asifike ndani. Yale Maneno wala Frank hakuyasikia Alimsukuma Rose kisha alianza kukimbia huku Akisema nisame Grace kuelekea kwa kina Grace. Alipofika tu hata kabla ya kuongea kitu chochote alifikia kwenye mikono ya Askari na kukamatwa akapakiwa kwenye Karandika na Safari ya kuelekea kituo cha Polisi ilianza. ******* ******* ***** "Hakuna haja ya kuendelea kuwepo duniani tena maana siwezi kuendelea kuishi huku nikimuona Frank akiwa Mzima. Kwa hiki ambacho amenifanyia Frank kwa kweli bora nife. Lakini kwa nini frank akaniadhibu hivi basi angesubilia niondoke ndipo angenifanyia kitu kama hichi"Aliongea Grace huku akiwa Amechanganyikiwa. Muda ule tayari alishaandika barua kwa Frank na kuiweka kitandani sehemu ambayo ilikuwa rahisi kwa Frank kuweza kuiona. Alipoweka Barua pale kitandani alitoka na kuanza Safari ya kuelekea Kambi ya pil kwa lengo la kwenda kunjinyonga kabisa. Alikuwa amepanga kwenda kujinyonga kwenye shamba la mjomba wake la ndizi ili iwe rahisi ndugu zake kumuona. Pia iwe Vigumu kwa Frank kumfukuzia na kumzuia kufanya lile jambo ambalo tayari alikuwa Ameamua kulifanya kichwani mwake. Muda ule Grace alimchukuia sana Frank kutokana na tabia mbaya ambae alikuwa amemuonyesha hata kama alikuwa amemkosea lakini asingepaswa kumuadhibu kwa kile ambacho alimfanyia tena akiwa anashuhudia kwa macho. Kutoka pale kwao alitembea kwa Mguu hadi barabarani ndipo alikodi pikipiki hadi Kambi ya pili. Alipofika kambi ya pili alianza safari ya kuelekea kwenye shamba la ndizi la Mjomba wake. Kabla hajafika kwenye lile shamba alipita sehemu na kuona mtu akiwa anahubiri injili na watu wengi wamerundikana wakisikiliza na kushangilia. Moja ya Maneno ambayo alikuwa anazungumzia yule mtu pale ilikuwa juu ya watu wanaokata tamaa na maisha kisha wanajiua. Alizungumza kuwa katika Dhambi ambayo mungu Hatoi msamaha ni ile ya kujiua. Aliendelea kusema kuwa mtu yeyote ambae amejiua huyo moja kwa moja ataenda moto hata kama watu watamuombeaje. Yale maneno ya yule mtu ndio yalimfanya Grace kusitisha kwenda kufanya lile jambo na kurud kuelekea kwa wazazi wake huku akiwaza jambo gani afanye ambalo lingemfanya Frank kuamini kama tayari yeye ameshakufa. Kitu ambacho alikuwa Anataka Grace ni kutokuomuon tena Frank kwenye macho yake. Baada ya mawazo ya hapa na pale ndio aliibuka na wazo flani. Alipofika nyumbani kwao kwanza aliwaeleza wazazi wake mkasa wote mwanzo hadi mwisho pia akawaambia na njia ambayo alitaka frank amsahau kabsa. "Kwanza mama nataka utafute watu mchanganyiko wanawake na wanaume. Wanawake watakuwa wanalia na wanaume watakuwa wamekaa kwenye mkeka kushona sanda. Akifika Frank najua lazima atajua kuwa nimeshakufa alafu nyinyi mtamfukuza"Aliongea Grace kuwaambia Wazazi wake. "Nilikwambia kuwa huyu mwanaume hakufai mwanangu wewe ukakataa. Hata kama tukifanya hilo huenda mbeleni atakuja kuupata ukweli. Hapa sisi tutafanya kama ulivyotuambia pia tutatafuta na Askari huyu kijana akamamtwe na kwenda kufia Gerezani"Aliongea Mama yake na Grace huku Mume wake akimuunga mkono. Ingawa Grace alizuia kufanya hivyo lakini wazazi wake wakakataa. Swala la kutafuta watu wa kuekti ule Msiba wa bandia halikuwa Gumu sana kwa watu Maarufu kama Mama Grace. Alishofanya alienda na kuwakuta kinamama wa kichaga wakiwa wanakunywa pombe na wanaume na kuwakusanya. Ili kuwafanya walie zaidi na kazi iende safi aliwapa kila mmoja 5000. Shilingi laki moja ilitosha kabsa kuweza kuwapata watu wa kwenda kumaliza lile tukio. Baada ya kuwapata wale watu alienda hadi kituo cha polisi akaongea na Askari kisha Rushwa ikatembea na Askari wakawa wapo tayari kwa kuja kumkamata. ndio maana Frank alipofika alikamatwa kirahisi na polisi huku akiamini kama kweli Grace alikuwa Amekufa kumbe alikuwa mzima





     Yale Maneno ya Mama yake na Grace kusema kuwa kumwambia Frank kuwa Grace amekufaha haitoshi wanataka hadi polisi wamkamate kisha akafie Jera yalimshitua sana Grace. Alipoona Amewakatalia wazai wake kufanya hivyo lakini Wakagoma aliamua kufanya kitu ambacho kingemfanya Frank kutokukamatwa na Polisi. Kitu cha kwanza alichofanya alimtafuta Rafiki yake Rose ambae hakuwa anakaa mbali na pale kwao. Alipompata alimuelezea mkasa mzima kisha alimpa namba za Frank. Lengo wampigie Frank kupitia simu ya Rose kisha Rose amwambie kuwa Grace amekufa kwa kujiua na Amewambia Wazazi wake yeye ndio amesababisha. Hivyo polisi wanamtafuta na asifike nyumbani kwao. Baada ya Grace kumpa maelezo ya kutosha rafiki yake alimpigia Frank. Bahati mbaya wakati flank anashuka kwenye Gari simu yake aliacha kwenye Gari na walipiga inaita bila kupokelewa. Ila hali kwa kweli ilizidi kumuumiza Grace kwani bado alikuwa anampenda Frank na hakutaka kuona frank anakufa. Walijaribu kurudia kupiga simu hadi walichoka lakini hali ya simu kuita hadi inakata iliendelea kuwa vile vile. Grace alizidi kuchanganyikiwa Zaidi alipowaona hadi Askari wakija na Defender pale nyumbani kwake tayari kwa kuja kumkamata Frank. Yani wazazi wake walimaliza Pesa za kuwahonga wale Askari lengo walitaka Frank Afe kabsa kwani kwanza walikuwa hawataki kabsa kumuona Frank akiwa na mahusiano na Mwanao Grace pili tukio ambalo Frank alimfanyia Mwanao liliwauzi sana . Kufa kwa Frank wao walikuwa wanaamini ndio ulikuwa mwisho wa mahusiano yao na Mwanae. Grace alienda hadi kwa wazazi wake na kuwabembeleza lakini wazazi wake walikataa. Alipoona hana namna ya kuweza kuwabadilisha wazazi wake wamuelewe kile ambacho alikuwa amewaambia ndipo alichukua Jukumu la kumpa kazi nyingine Rose. Alimwambia Rose kuwa akae kwa Nje kama Frank akifika basi amuelezee kuwa tayari Grace Amekufa na kuna askari watamkamata kama ataingia ndani. Rose alikubali yale maneno ambayo aliambiwa na Grace kisha alitoka nje ya uzuio wa ile nyumba na kumsubilia frank ili kuja kumwambia maneno kama alivyoambiwa na Grace. Alipotoka Rose nje wala hakumaliza hata Dakika Tano tayari Frank alikuwa ameshafika. Rose alijitidi kumzui Frank na Kumwambia kuwa Asiingie ndani kwani kuna Askari watamkamata lakini frank alikuwa Mgumu aliingia ndani. Hata alipokamatwa na Polisi Grace alikuwa anaona na huzuni ulimshika na kujikuta akilia na kujilaumu bora angefanya maamuzi mwenyewe kuliko kuwasikiliza wazazi wake. Alitamani kutoka kwenda kumsaidia Frank ambaye alikuwa analia huku akilalamika kuwa hajamuua Grace lakini wazazi wake mlango walikuwa wamefunga kwa nje. Alijitaidi kuongea kwa sauti kuwa wasimkamate Frank kwani hakuna kitu kibaya Ambacho alimfanyia lakini sauti yake hakuna ambaye alisikia kutokana madirisha kuwa na vioo huku juu Gymsang body ilikuwa imeziba vizuri na kufanya sauti isitoke nje. Kwa Macho yake alishuhudia Frank akikamatwa na kupigwa Pingu kisha alipakiwa kwenye Gari Safari ya kuelekea kituo cha polisi ilianza. "Grace Mke wangu unaona sasa umejiua Mwenyewe leo hii unaniacha kwenye matatizo kama haya. NISAMEHE GRACE kwani nilikunyima nafasi ya kusikiliza kile ambacho ulikuwa unataka kuniambia. Ila hata hivyo kwa nini sasa umewaambia wazazi wako kuwa mimi ndio nimehusika kukufanya ukafa. Grace au ndio uliamua kama ukijiua wewe basi na mimi niwepo Gerezani. Kama wewe ndio umeamua nimeamini kama kweli unanipenda Grace. Maana unajua kule Gerezani sitakusaliti kamwe na hatimae nitakukuta huku kaburini. NISAMEHE GRACE na Pumzika mahala pema mke wangu nakupenda sa.."Aliongea Frank huku akiwa analia hata kabla hajamalizia kuongea alinyamazishwa na kofi moja la Afande hali iliyomfanya kuhisi mdomo wake umeongezeka ukubwa. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/.......................................................................................... Alipokamatwa Frank na kuondolewa pale huku Kwa mama Grace msiba wa Uongo ambao ulikuwepo ulibadilika na kuwa Disco ghafla. Wazazi wake na Grace walikuwa na Furaha sana hasa walipohakikisha kuwa Mtu wao ambao walikuwa hawataki kumuona akiwa na Uhusiano na Mwanae amekamatwa. Muda ule tayari walikuwa wameshakodi mziki kwani ulikuwa siyo mbali na nyumbani kwao wakafungulia wale watu ambao walikuwepo kwenye msiba walianza kucheza huku wakinywa bia ambazo Wazazi wake na Grace walikuwa wamenunua. Muda ule bado Grace alikuwa Amefungiwa ndani na kutokana na furaha ambayo walikuwa nao wazazi wake walisahau kama kuna Mwanao walimfungia chumbani ndani. Ili Afande kumpoteza kabsa Frank hawakumpeleka kituo cha polisi cha Usa liver walimpeleka kituo cha Polisi Majengo. Walifanya hivyo kwa kula dili na wazazi wake na Grace. Maana wazazi wake dalili ambayo walikuwa wameiona kwa Mwanae walijua kama Frank ataweka kituo cha polisi cha Usa liver basi Grace angeweza kwenda kufanya lolote na kumtoa tena Frank. "Ndio huyu ambaye anazidi kutuharibia Tanzania yetu pamoja na vijana wetu. Mmefanikiwa kumkamata akiwa na mzigo wote"Aliongea Afande Mmoja ambaye ndio alikuwa mkuu wa kituo pale majengo. Wale Askari tayari walikuwa wameshatoa taarifa kituo cha polisi cha majengo kumbe kuwa kuna mtu wanamfuata uwanja wa ndege amekamatwa na madawa ya kulevya. "Ndio afande tumemkamata pamoja na mzigo ingawa hakuwa na mzigo wa kutosha inaonekana mwingine tayari ameusambaza hapa Arusha na huu mdogo ndio alikuwa anaupeleka dar"Alijibu afande mmoja huku akimsukuma Frank kwenda ndani ya kituo cha polisi. Kwa kweli Frank yeye alibaki akiwa anawashanga tu wale Afande kwani alikuwa hajui kitu gani walikuwa wanazungumzia maana tukio ambalo alikuwa analijua ni kusingiziwa amehusika kusababisha mke wake kujiua. "Huu hapa mzigo ambao tumemkamata nao kisha mwingine atatoa mwenyewe mfukoni alafu kipigo kitafuta hadi ataje mzigo mwingine amesambaza wapi. Maana wakati tunashituliwa na Rai wema tuliambiwa alikuwa na breafcase kabsa ya madawa ya kulevya"Aliongea Afande tena huku akitua kimfuko kimoja cha madawa ya kulevya hali iliyomfanya Frank kuzidi kushanga. "Haya wewe kijana toa hayo madawa mengine kwenye mfuko wako kisha tuambie mzigo mwingine upo wapi kama unataka kubaki salama"Aliongea Afande mkuu huku akiwa amemkazia macho Frank. "Jamani mimi siyo muuzaji wa madawa ya kulevya ndugu zangu. Mimi nimekamatwa hapa kwa kosa la kusababisha mke wangu kujinyonga tafadhari naomba muelewe hivyo. Angalieni mfukoni kwangu hakuna kitu chochote zaidi ya pochi yangu yenye pesa chache"Aliongea Frank kwa huzuni huku akipeleka mikono mfukoni ili kuweza kutoa kila kitu. Alichokuwa Anaamini Frank alikuwa hana kitu kabsa mfukoni kwake. Alipopeleka mikono yake mfukoni ili kutoa mifuko pamoja na pochi yake ya pesa alikutana na vitu laini ndani hali iliyomfanya kushituka. Aliposhika vile vitu ilibidi kuacha kwanza kutoa na kubaki akitafakari kwanza kitu gani alikuwa amekiweka kingine mfukoni. Wakati anatafakari alikutana na ngumi kichwani ya Afande Rama iliyomfanya apige mayowe huku akitoa mikono mfukoni kwake. Alipotoa mikono yake huku akiwa ameshikilia vile vitu kuwaonyesha kuwa kulikuwa hakuna kitu mfukoni kwake alishangaa kuona kuwa alikuwa na vimfuko vya madawa ya kulevya





     "Hapana Afande Jamani mimi sijui haya Madawa nani kaniwekea, ila nakumbuka hata nyinyi mlinikamata kwa kesi ya kusababisha mke wangu kujiua. Sasa haya Maswala ya Madawa ya kulevya yametoka wapi"Aliongea Frank Huku akizidi Kushangaa. Kwa kweli alikuwa na haki ya kushangaa maana picha ambalo alikuwa amechezewa lilikuwa picha lisilo la kawaida kabsa. Ndani ya Saa moja tayari mtu alikuwa amesingiziwa kesi mbili kwanza wakati anakamatwa iliundwa kesi kuwa Kasababisha kipenzi wake Grace kujiua. Alipokamatwa kesi ya kusababisha mtu kujiua ilibadilishwa na Jamaa kupewa kesi ya mtu anayeuza na kusambaza madawa ya kulevya. "Hawa watu Huwa Wajanja Sana, hebu ona hapa anavyopishanisha maneno. Inamaana Unataka kusema kuwa sisi ndio tumekuwekea haya Madawa. Huyu wa kupigwa kabsa maana ametuchukulia sisi Askari Wapumbavu. Kweli anafikia hadi kusema eti Sisi tumemkamata kwa Kosa la Kusababisha mtu Kujiua wakati tumekukamata Uwanja wa Ndege ukitaka kusafiri kuelekea Dar na Madawa ya kulevya. Hebu acha kuekti kijana utakuja kufa hebu tuambie Madawa Mengine umeweka kwa Nani"Aliongea Afande Rama na kisha kuanza kumtwanga Frank Marungu. Kwa kweli Frank alizidi kushangaa na kutokuelewa kitu gani kilikuwa kinaendelea pale. "Jamani Hebu jaribuni kukumbuka mimi nahisi huenda mtakuwa mmechanganya. Mtu ambaye mmemkamata kwa Madawa ya kulevya mkadhani mimi. Labda niwaulize kitu kuna mtu Mwingine mmemkamata kwa ajili ya kosa la kusababisha Mpenzi wake kufa. Kama jibu ni ndio basi huyo ndio atakuwa Muhusika wa Haya Madawa ya kulevya ila mimi nimeletwa Hapa kwa Kosa la kusababisha Mpenzi wangu kufa"Alijaribu tena Kujitetea Frank. Alipoongea vile Frank ni Kama alimpandishia Hasira Afande Rama na kuzidi kumpiga Frank. "Afande Rama nahisi mtu anapokamatwa huwa analetwa kufunzwa wala siyo kupigwa. Mbona bado hata hatujamaliza kuongea na huyu kijana tayari umeanza kumpiga"Mkuu wa kitua alimwambia Afande Rama Maneno yaliyomfanya Rama kushituka. Maana haikuwa kawaida mkuu wa kituo kumzuia Afande Mwenzake kama alikuwa anamwadhibu mtuhumiwa. "Lakini Afande Huyu ni Mkosaji na anakataa kosa anatakiwa kupata adhabu"Alijibu Afande Rama. "Sawa Mkosaji lakini naye anahaki yake anatakiwa kusikilizwa. Maana maelezo ambayo anatoa yapo tofauti kabsa na haya yakwenu"Alijibu Mkuu wa Kituo. Kwa kweli Yale Maneno ya Mkuu wa Kituo yalizidi Kumtia Wasiwasi Afande Rama Maana yeye ndio ambae alikula Dili na Afande wa kituo cha User river.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Hata Madawa ya kulevya ndio yeye aliyemuwekea Frank Mfukoni. "Asante Sana Mkuu wa kituo kwa kulielewa hilo. Labda mimi nikueleze mkuu hapa nahisi kuna mchezo nachezewa. Kwanza Kabla sijafikishwa hapa tayari nimeshabadilishwa kwenye Defender mbili. Defender ya Kwanza ndio ambae ilinikamata nyumbani kwa mpenzi wangu kwa kosa la kusababisha Mpenzi wangu kujiua. Nilipotolewa pale Nyumbani kwa mpenzi wangu nilipokaribia kituo cha Polisi cha usa river nilipakiwa kwenye Defenda nyingine tena. Sasa mimi nataka nimuulize Huyu Afande aniambie ukweli mpenzi wangu Grace bado Mzima au amekufa. Pia Ndugu Mkuu naomba wasiliana na Wahudumu wakuu wa Uwanja wa Ndege uone kama kuna Taarifa zozote zinazosema kama kuna mtu kakamatwa na Madawa ya kulevya"Alijitetea Frank Maneno ambayo yalimfanya Afande Mkuu kweli kuwa na Wasiwasi na yale Maelezo ya Afande Rama. "Kijana mimi nakufahamu kweli wewe si Mwalimu wa Sekondary. Pia Niliona Matangazo yako kwenye Televisheni kana kwamba Unaoa. Sasa hii kazi ya Madawa ya kulevya umeianza lini"Aliongea Mkuu wa kituo. Yale maneno ya mkuu wa kituo kusema kuwa anamfahamu Frank kwa kweli yalimshitua Sana Afande Rama. Mapigo yake ya Moyo yalianza kwenda mbio na kuhisi uongo wake Umekamatika.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog