Search This Blog

Friday, July 15, 2022

NILIVYOMLIZA MKE WANGU KWA SIKU 366 - 1

 









    IMEANDIKWA NA : NYEMO CHILONGANI



    *********************************************************************************



    Simulizi : Nilivyomliza Mke Wangu Kwa Siku 366

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Nilikuwa kwenye wakati mgumu sana, nadhani wakati mgumu kuliko nyakati zote nilizowahi kupitia katika maisha yangu. Kilichokuwa kikiendelea kati yangu na msichana mrembo, Isabela ndicho kilichonifanya nigombane na mke wangu, Upendo, tena kutemeana maneno kwa sauti ya juu kabisa.

    Alikasirika, ndiyo, hata ningekuwa mimi ningekasirika sana na kama ningekuwa na moyo mwepesi basi ningemuua. Ngoja nikwambie kastori kafupi kuhusu mimi na huyu mrembo Isabela.

    Mara ya kwanza nilikutana naye Dar Free Market, kwa kumwangalia tu, alionekana kuwa msichana wa gharama, sista duu ambaye kwa ujumla, nguo na vitu vingine alivyokuwa navyo siku hiyo ingefika gharama ya shilingi milioni moja.

    Watu walimwangalia kwa matamanio, uzuri wake wa sura hakika ulimchanganya kila mtu, hakuna aliyemfuata ila kwa sababu mimi mwenyewe nilikuwa najiamini, mifuko imejaa, nikapiga hatua kumfuata.

    Watu wote wakanitolea macho, hawakuamini kama kungekuwa na mwanaume aliyekuwa na moyo wa kumfuata na kuzungumza naye, hilo wala sikujali, si nilitaka kuwaonyeshea kwamba watoto wa kike niliwazoea, hivyo nikaamua kufanya hivyo, nilipomfikia tu, nikatoa tabasamu pana, akanirudishia kwa kukunja ndita, sikutishika, nikapiga moyo konde.

    Mimi: Mambo vipi mrembo! CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Isabela: Poa (Akaendelea kufanya mambo yake mengine)

    Dizaini kama hakutaka kuzungumza nami, ila sikutaka kuondoka. Nilikuwa mzoefu sana na watoto wa kike, najua mapozi yao yote yanamaanisha nini na ndiyo maana sikutaka kumuacha kabisa. Nilisimama karibu naye, nami nikajifanya bize kuchagua vitu kumbe akili na mawazo yangu yalikuwa kwake.

    Mimi: Umependeza.....(nilimwambia tena huku nikimwangalia, uso wangu ulikuwa na tabasamu pana)

    Isabela: (Kimyaaaaa)

    Mimi: Umeumbika pia na una uzuri wa ajabu.....

    Isabela: (Kimyaaaa)



    Mimi: Jamaniii! Yaani hata ninavyousifia uumbaji wa Mungu hutaki kuitikia, kweli? Miss, kuna wasichana wengi wanatamani kuwa mzuri kama wewe, wanatamani kuwa na umbo zuri kama wewe, hata weupe huo kuna wengine wanautafuta mpaka madukani. Mungu kakubariki, makusudi yake kuona anakuja mtu kama mimi, nakusifia ili naye aone amefanya kazi nzuri, halafu unakaa kimya! Jamani! Au Mungu kakosea kukupa uzuri huo? (Niliuliza kwa sauti ya chini)

    Isabela: (Akatoa tabasamu la mbali, ninaona Yesss...mtoto anaanza kulainika)

    Mimi: Unaitwa nani Miss?

    Isabela: Claire.

    Mimi: Waooo...jina zuri sana, jina la Kiingereza hilo, la kiume lake ni Clarence....hakika umestahili kuwa na jina hilo Claire (nilimwambia bila kupepesa macho)

    Isabela: Asante.

    Hiyo ndiyo ilikuwa siku yangu ya kwanza kukutana na huyu Isabela, japokuwa alinidanganya jina lake, sikujua hivyo nikamzoea kwa jina hilo la Claire. Siku hiyo nilimganda kama ruba, alipomaliza kufanya manunuzi yake, tukatoka.

    Tulipofika nje, nikaanza kuzugazuga kuona angetumia usafiri gani, aliponiambia kwamba anafuata bajaji, nikamtuliza na kumwambia kwamba nilikuwa na usafiri hivyo ningemfikisha popote anapopataka. Akakubaliana nami, tukapiga hatua na kulifuata gari langu, lilikuwa ni Verrosa nyeusi, tukaingia na kuondoka.

    Tulikuwa tukipiga sana stori, kwa kuwa nilikuwa mtu wa utani sana, nikawa namtania sana, alifurahi mno, tukazoeana kana kwamba tuliwahi kukutana kabla ya siku hiyo.

    Isabela: Naomba tuishie hapa... (aliniambia baada ya kufika Mikocheni B katika Mtaa wa Flamingo, kulikuwa na majengo ya hatariiiiii)

    Mimi: Unaishi wapi kwani?

    Isabela: Hapo mbele, kuna nyumba ina geti jekundu, ndipo ninapoishi...

    Mimi: Na wazazi?

    Isabela: Yaap....

    Mimi: Naweza kwenda kuwaona?

    Isabela: Weeeeee....unataka waniue!

    Mimi: Kwani wakikuua kwa ajili yangu kuna tatizo? (Niliuliza huku nikiachia tabasamu pana)

    Isabela: Hahah! Naomba niondoke...

    Mimi: Ila haujafanya kitu kimoja cha muhimu sana kuliko vyote...

    Isabela: Kitu gani?

    Mimi: Tutawasiliana vipi baada ya hapa?

    Isabela: Ooh! Samahani nilisahau...chukua hii (Akanipa kikaratasi chenye namba yake)

    Mimi: Nashukuru sana...nitakutafuta baadaye....

    Isabela: Sawa...CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mimi: Nakupenda....

    Isabela: Mmh! Asante....(Akaufungua mlango na kuondoka zake, sikutaka kuondoka, nikawa namwangalia umbo lake kwa nyuma, hakuwa na milima mikubwa, umbo lake lilikuwa flat, yaleyale yanayonipagawisha....mwendo wa mapozi ambao nao ulichangia kunipagawisha...alipokata kona, na mimi huyooo....nikasepa zangu).

    **** Kiukweli Isabela alikichanganya kichwa changu, sikuamini kama nilikuwa nimekutana na msichana mrembo kama yeye, wakati mwingine nikawa najiuliza kwamba je, yule niliyekutana naye alikuwa binadamu wa kawaida au malaika.

    Alikuwa mrembo mno. Unaweza usinielewe juu ya uzuri wake kwa kutumia maandishi ila amini kwamba msichana huyo alivutia sana. Sikufanya kazi vizuri, kila nilipogusa hiki, sura yake inanijia kichwani, nilipogusa kile, sura yake hii, yaani kila nilichokifanya, ni Isabela, Isabela, Isabela.

    Japokuwa nilikuwa na namba yake, sikutaka kumtafuta kwenye simu. Unajua wakati mwingine sisi kama wanaume hatutakiwi kuonekana kuwa walaini, yaani mtoto kakupa namba mchana, usiku umemuendea hewani.

    Hiyo haikutakiwa, nilitaka kuleta mapozi kama wao walivyokuwa wanaleta, yaani demu unampa namba Januari, anakupigia March, ili kumuonyeshea kwamba na mimi nilikuwa mtu hatari, mwenye mapozi mengi, nikachunachuna japokuwa mawazo juu yake yaliniandama mno.

    Niliisevu namba yake, nikawa namwangalia kwenye Whatsapp, mara wakati mwingine anabadilisha status na kuandika “I’ve found him” (akinimaanisha amempata), mara A nice man, smart one with nice car, I love him for real (akimaanisha mwanaume mzuri, mtanashati na gari zuri, ninampenda kwa kweli)

    Hizo zilikuwa status zake alizokuwa akiziweka kwenye Whatsapp baada ya kukutana naye, nilichokifanya ni kujiongeza na kuona kwamba inawezekana zile status zilinihusu mimi, sikutaka kuzungumza chochote, nikapotezea.

    Siku ya kwanza ikapita, kukawa kimya, siku ya pili ikapita, nayo kimya, sikutaka kumpigia simu wala nini, nilikuwa navutavuta siku ili animisimisi kwanza. Siku ya saba ilipoingia, nikamcheki kwenye Whatsapp nikaona amebadilisha status na kuandika ‘Please call me now, I am dying because of you, baby boy (Tafadhali nipigie sasa hivi, ninakufa kwa ajili yako mpenzi)



    Kumbuka hakuwa na namba yangu, yeye alinipa kikaratasi chenye namba ila mimi sikumpa kitu chochote. Aliamini kwamba namba yake niliisevu na ndiyo maana aliandika status mbalimbali kama ujumbe kwangu, hivyo nikatabasamu.

    Kesho ambayo ndiyo ilikuwa siku ya nane ilipoingia, nikaamua kumtumia meseji, nikaandika ‘I am a professional doctor, I can heal your wound’ (Mimi ni daktari mwenye uzoefu, naweza kuliponya jeraha lako). Hapohapo akanitumia meseji...

    Isabela: Wewe ni nani?

    Mimi: Daktari wako...

    Isabela: Nani jamani?

    Mimi: Kwani wewe una madaktari wangapi?

    Isabela: Tuna daktari mmoja tu wa familia....

    Mimi: Wa kukuponya kidonda cha moyo wako, wapo wangapi?

    Isabela: Naomba uniambie...

    Mimi: Naitwa Denis....

    Isabela: Yupi?

    Mimi: Wa Dar Free Market......

    Isabela hakutaka kukubali, hapohapo akanipigia simu, alionekana kuchanganyikiwa mno, kumbuka kwamba alisubiri kwa kipindi kirefu nimpigie simu, hakuwa na namba yangu hivyo kitendo cha kuipata, hakutaka kuchelewa, akaniendea hewani...

    Isabela: Nimekukumbuka Denis, nimekukumbuka Love (aliniambia, eti Love, tumeanza muda gani kuwa wapenzi?)

    Mimi: Nimekukumbuka pia.

    Isabela: Upo wapi?

    Mimi: Nyumbani...

    Isabela: Nataka kuja, nataka nije nikuone daktari wangu, nataka nije uyapoze maumivu ya kidonda changu....

    Mimi: Kweli?

    Isabela: Kweli tena! Naomba nije...please mpenzi...

    Mimi: Mmh! Aya njoo mgonjwa wangu....fika mpaka Kijitonyama kwenye Ukumbi wa Heko, nyumba ya nne kutoka hapo.....ina bati la Msouth jekundu, hapohapo, ukipotea, ulizia kwa mwandishi wapi.

    Isabela: Sawa! Nakuja love.

    Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kila kitu. Huyu Isabela hakuwa mke wangu, nilimpenda sana, tena kwa moyo wa dhati, na yeye ndiye aliyenifanya nimchukie mke wangu na kumliza kwa takribani mwaka mzima ambao ni sawa na siku 366. Iliuma, alikuwa mke mwenye kuvumilia mengi, alikasirika, alikumbatia sana mto ila yote hiyo ilikuwa ni kwa sababu ya huyu Isabela....kabla sijaendelea, naomba mke wangu anisamehe...ninaahidi kumpenda milele.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kuna wakati mambo yanaonekana kuwa magumu sana, ila wakati mwingine, mambo yanakuwa mepesi kabisa. Kwa kumwangalia Isabela, ilikuwa kazi kubwa kumpata lakini upande wa pili, alikuwa mwepesi sana, ilikuwa kazi nyepesi kama kumsukuma mlevi kwenye mteremko wa mlima.

    Basi nikakaa zangu home, nacheki video mara nikasikia bajaji ikisimama nje ya nyuma yangu. Nilijua kwamba ndiye yeye hivyo nikajipanga ndani vilivyo, nikaweka mazingira mazuri. Mara simu yangu ikaanza kuita, nilipoangalia jina, lilikuwa lake.

    Isabela: Nimefika baby...

    Mimi: Poa, nakuja, nipe dakika sifuri.

    Nikatoka huku nikiwa nimevaa pensi yangu, nikafungua mlango, ile kumuona tu, mtoto akatoa tabasamu pana, akanisogelea na kunikumbatia kimahaba.

    Mimi: Karibu sana...

    Isabala: Asante mpenzi...nimekumisi Denis wangu...

    Mimi: Nimekumisi pia, unanukia vizuri sana, kama ua waridi....

    Tukaingia ndani, macho yake yalikuwa yakiangalia huku na kule, kwa kifupi alikuwa akiona raha mno, kuwa na mwanaume kama mimi, hakika ilikuwa furaha yake. Basi tukazungumza, alijiweka wazi kwamba hakuwa akiitwa Claire kama alivyoniambia bali alikuwa akiitwa Isabela.

    Isabela: Nisamehe kwa kukudanganya mpenzi...

    Mimi: Usijali, najua wakati mwingine mnakuwa hamtuamini hasa tunapokutana kwa mara ya kwanza, mnahisi sisi ni wachawi na tutawaroga na ndiyo maana mnatupa majina ya uongo, ila usijali kipenzi....

    Isabela: Asante sana.

    Mara zote nimekuwa nikisema wazi kwamba msichana na mvulana hawatakiwi kukaa sehemu moja peke yao, huwa ni hatari sana kwani kama wakikaa hivyo basi jua kwamba hata shetani naye anakuwa around anasubiri muda ufike aanze kufanya yake.

    Sikumjua Isabela vizuri, sikujua historia yake ya kimapenzi lakini huwezi kuamini, uwepo wake ndani ya nyumba yangu ulinifanya kuwa kwenye hali ya tofauti kabisa. Mara tokaanza kugusana hapa na pale, akiniita baby, namwambia nipo hapa, unataka nini kipenzi?

    Sikuwahi kumtongoza ila baada ya dakika kadhaa tukajikuta tukiwa kitandani. Hiyo ndiyo ilikuwa siku ya pili kukutana naye lakini tayari tulilala kitandani na kufanya mambo kama mtu na mke wake.



    Ukaribu wangu na Isabela ukapamba moto, mtoto akawa aambiwi wala hasikii kwangu, alikuwa mahiri wa kupiga simu mpaka anakera, ukikaa kitandani, simu, ukiwa jikoni, simu, sebuleni, simu, yaani hata ukiwa chooni unayakata, unasikia simu inaita, ukienda kuangalia, Isabela.

    Mapenzi yalikuwa machanga, yalimchanganya mno, alitamani nimuoe, niishi naye na kujenga familia pamoja. Sikuwa mchoyo, sikuwa msiri, nikawaambia washikaji zangu wote kwamba kwa sababu nataka kuoa, Isabela ndiye alikuwa mwanamke wangu wa ndoto.

    John: Hahaha! Eti Denis uoe, wewe?

    Mimi: Ndiyo! Kwa nini nisioe?

    Hamisi: Ukioa wewe, haki ya Mungu wote tutaoa.

    Mimi: Halafu washikaji mbona hamniamini nikiwaambia kuhusu kuoa?

    John: Historia inakuharibia...unamkumbuka Stellah?

    Mimi: Hahaha!

    Huyo Stellah alikuwa demu wangu wa ukweli, nilimpenda sana, naye akanipenda kwa mapenzi ya dhati, akaniita majina yote matamu, mara mahabuba, baby, honey, sweetie, yaani majina yote matamu, huyu mtoto aliniita.

    Nilijiwekea future naye, nikamtambulisha kwa wazazi, japokuwa walionekana kumaindi lakini sikujali, sijui kitu gani kilitokea, mara ghafla bin vuu, mimi na Stellah tukawa kama paka na panya. Sasa hiyo stori ndiyo ilionekana kuwa chanzo cha yote hayo, walitaka kunihukumu kupitia stori hiyo.

    John: Ulimpeleka mtu mpaka kwenu, mwisho wa siku, ukala kona, hata kwa huyo Isabela sina wasiwasi, labda mpaka utakapomvisha pete.

    Mimi: Hahaha! Sasa kazi yangu ni kufanya vile visivyowezekana kuwezekana.

    Basi ndio ikawa hivyo, nikawaseti washikaji zangu kwa ajili ya maandalizi ya ishu hiyo. Siku zikaendelea kwenda mbele, baada ya wiki moja, tena huku uhusiano ukiwa umepamba moto, nikamwambia Isabela kwamba twende kijijini kwa wazazi wangu kwa ajili ya kumtambulisha, tupate baraka zote na hatimaye nimuoe.

    Isabela: Siamini kama mambo yangekuwa mepesi namna hii, hatimaye naolewa!

    Mimi: Usijali, nipo kwa ajili ya kukamilisha ndoto yako.



    Kiukweli nilipania, wakati naendelea na uhusiano wa kimapenzi na msichana Isabela, kuna kitu nilianza kugundua. Mtu unaweza ukawa kwenye uhusiano tena kwa userious mkubwa lakini mwisho wa siku uhusiano huo ukaja kuyumba na kuachana kwenye mataa, lakini pia kuna uhusiano ambao inawezekana msiwe serious lakini mkafika mbali kabisa. Kwa mfano mzuri ni mimi na huyu Isabela, kiukweli sikuwa nimejitoa kivile lakini huwezi kuamini kwamba ndiye msichana ambaye alinifanya nijisikie huru na amani moyoni mwangu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya siku kadhaa tukaanza kuelekea kijijini kwetu, njiani, kila mmoja alikuwa na furaha tele, tulizungumza mambo mengi kama wapenzi, tukapanga mipango yetu mingi hapo baadaye kwa kusema kwamba kama inawezekana basi tuwe na watoto wawili tu. Tukakubaliana.

    Mimi: Wawili wanatosha, ila kama maisha yatakuwa poa, tutaongeza wa mwisho, wawe watatu tu.

    Isabela: Sawa! Haina tatizo, cha msingi ni kusimama katika kile tulichokipanga.

    Baada ya saa kadhaa tukaingia katika Kijiji cha Lupiro kilichokuwa mkoani Morogoro. Tukapokelewa kwa shangwe kubwa lakini baada ya ndugu zangu hapo kijijini kumuona Isabela, walionekana kubadilika, hata ile furaha ya kutuona wageni ikapotea.

    Sikujua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea na sikutaka kujali sana, nilichokifanya ni kumchukua Isabela na kwenda naye ndani kisha kuwasubiri wazazi wangu ambao niliambiwa kwamba walikwenda shambani kuwasimamia wakulima waliokuwa wakiendelea na kazi.

    Isabela: Denis mpenzi....

    Mimi: Naam!

    Isabela: Mbona naona mambo yamebadilika...

    Mimi: Kivipi? Usijali, hakuna chochote kibaya...

    Japokuwa nilimwambia hivyo lakini mimi mwenyewe nilikuwa na wasiwasi kibao, hata ndugu waliokuwa wakiingia ndani ya nyumba ile, hawakuonekana kuwa na furaha sana, nikajua kwamba kuna kitu kilikuwa kikiendelea.

    Nilichokifanya, kwa sababu hapo kijijini kulikuwa na msela wangu mmoja aliyeitwa Juma ambaye mara nyingi sana nilimtumia fedha, nikaamua kumtafuta, nikaelekea alipokuwa akiishi, aliponiona, kwa furaha akanifuata na kunisalimia.



    Sikwenda na Isabela, nilikwenda peke yangu kwa kuamini kama kulikuwa na kitu kibaya, basi kwanza niambiwe mimi. Kweli, sikutaka kumficha Juma, nilimwambia ukweli hali niliyoikuta nyumbani hapo.

    Juma: Pole sana kaka.....

    Mimi: Kuna nini?

    Juma: Hivi haukupewa taarifa?

    Mimi: Kwamba?

    Juma: Wazazi wako wamekutafutia mke...

    Mimi: Wamenitafutia mke? Nani?

    Juma: Mtoto wa mzee Mkude, yule Salama....

    Mimi: Juma, hebu kuwa serious, unasemaje?

    Hiyo ndiyo taarifa niliyokutana nayo kijijini, ilinishtua sana, eti wazazi wangu kunitafutia mke, mbona mambo ya kizamani sana. Kiukweli nilishtuka sana, sikutegemea kwa ulimwengu wa sasa hivi, ulimwengu ambao una simu za tachi, watu wanatumia Whatsapp, wanawake wanavaa suruali eti bado kuna wazazi wanawatafutia wake watoto wao.

    Nilimfahamu huyo Salama, alikuwa binti mkubwa wa mzee Mkude, mzee maarufu kwa kunywa pombe hapo kijijini, mzee aliyekuwa akizungumza sana Kiingereza baada ya kupata elimu kutoka kwa wakoloni.

    Hakuwa msichana mzuri hata kidogo, alikuwa mbaya na hakustahili hata kukanyaga mjini. Tangu zamani nilivyokuwa nikifika hapo, alikuwa akiniganda sana, kila nilipokwenda, alikuwa akinifuata, kumbe ndiyo alikuwa akitafuta urafiki kwangu.

    Leo hii, eti kisa wazazi wangu walikuwa marafiki na wazazi wao, wakaamua kuuendeleza urafiki wao kwa watoto wao kuoana, kwa kweli, kwangu lilikuwa suala gumu sana ambalo nisingeweza kukubaliana nalo hata siku moja.

    Juma: Kwa hiyo utafanyaje?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mimi: Siwezi kumuoa Salama, yaani hicho ni kitu kisichowezekana hata kidogo...

    Juma: Mmmh! Na jinsi wazazi wako walivyokuwa watata...sijui.

    Sikutaka kuendelea kukaa mahali hapo, tayari nilichanganyikiwa, maneno yale niliyoambiwa yalinitia hasira sana, sikutaka kukaa kijijini hapo, sikutaka kusubiri mpaka wazazi warudi, kwa sababu nilikuwa na usafiri wangu binafsi, nikapanga niondoke na kurudi Dar es Salaam kwani nisingeweza kukaa na wazazi ambao waliamua kunichagulia mke.

    Bahati mbaya kwangu, niliporudi nyumbani, nikawakuta wakiwa wamerudi kutoka shamba. Sikuwa na furaha, niliwaangalia huku nikionekana kabisa kwamba nina hasira, wao wenyewe walikuwa kama mimi, hasira zao zilikuwa ni kumkuta Isabela mahali hapo.



    Mimi: Naombeni tuondoke...(niliwaambia hata kabla ya salamu)

    Baba: Wewe mtoto, hata salamu!

    Mimi: Nitakusalimia hata baadaye, naombeni tuondoke...

    Walinishangaa, hawakujua kitu gani kilichotokea, hawakujua kama tayari niliambiwa kila kitu. Baba akajaribu kunibembeleza, sikukubali, nilichokisema ni kwamba ilikuwa ni lazima niondoke mahali hapo.

    Isabela: Kuna nini mpenzi?

    Mimi: Tuondoke Isabela, hawa wazee nuksi...

    Isabela: Wamefanyaje tena?

    Mimi: Wewe tuondoke...

    Isabela hakuelewa kilichokuwa kikiendelea, nilishindwa kukaa hapo kijijini na nilichokifanya, siku hiyohiyo tukaondoka. Watu walishangaa, wazazi walishangaa lakini sikutaka kujali. Siku hiyo hali ilionekana kuwa tofauti kabisa, haikuwa kama siku nyingine ambazo nilifika mahali hapo huku nikiwa mwenye furaha ya ajabu, siku hiyo ilikuwa tofauti kabisa.

    Ndani ya gari Isabela aliendelea kuniuliza tatizo lilikuwa nini, sikuwa na cha kumjibu, nilihofia kwamba angejisikia vibaya mno. Nilinyamaza mpaka tunafika Morogoro Mjini ambapo tayari ilikuwa ni saa kumi na mbili jioni, tukachukua chumba katika hoteli moja ya kifahari na kupumzika.

    Isabela: Kuna nini Denis?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mimi: Matatizo ya kifamilia tu mpenzi...

    Isabela: Ambayo sitakiwi kuyafahamu?

    Mimi: Muda ukifika utayafahamu tu.

    Isabela akabaki kimya. Nakumbuka siku hiyo kulikuwa na hali fulani ya kibaridi, tulilala kitandani huku tukiwa tumekumbatiana mpaka kufikia hatua Isabela akaanza kunichokoza chokoza, alianza kwa kunishika hapa na pale, alitaka kuliamsha dude lakini hilo halikuwezekana.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog