Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

DUWA LA KUKU - 4

 







    Simulizi : Duwa La Kuku

    Sehemu Ya Nne (4)



    Akilini tukasema; yale yale…..



    ***************



    ‘Oh, kwahiyo..?’ ikawa swali la kuulizana tena, na tukasema kwa vile tumefika pale basi tusubirie tu, ili tujue moja, na baadae tukaenda kumuona docta, docta akatuuliza sisi ni nani kwake, tukamuelezea, na docta hakutaka kutuficha akasema;CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ‘Huyo mzee amefariki…’tukaambiwa.



    ‘Kwa vipi…?’ tukauliza sasa tukichanganyikiwa kabisa, ni kwanini haya yanatokea kwa watu tuliotegemea watatusaidia kwenye hilo tatizo.



    ‘Mzeee kafariki kwa kiharusi,…mshtuko, shinikizo la damu, damu ikavilia kichwani, na kufariki, zaidi  labda mkamuone docta wake aliyempokea.



     ‘Sasa na hayo mauchawi jamaa aliyotuwekea itakuwaje, maana huyo mwalimu wake alisema yeye atatusaidia, nay eye ndio huyo keshafariki..?’ wakaulizana.



    ‘Kama wachawi waliotufanyia hivyo wamefariki , ni nani atafanikisha huo uchawi ina maana mambo hayo nayo yatakufa, kwanini tuogope uchawi na mungu yupo wa kutulinda….’wakajipa moyo hivyo



    ‘Lakini mnakumbuka kauli zao wote wawili ilikuwaje, kuwa hayo mambo yasipoondolewa yataanza kuleta matatizo ndani ya familia zetu..’wakasema na hapo ikawa ni mashaka kwenye nafsi za watu hawa, ikabidi sasa taarifa zifikishwe  kwa waume zao.



    Mama mfadhili akawa wa kwanza kumpiga mume wake simu , alipiga simu ya nyumbani, akijua kuwa mume wake yupo nyumbani, siku hiyo alisema hajisiki vizuri, kwahiyo atapumzika , hataenda kwenye mihangaiko yake ya kila siku, na alipopiga akashangaa aliyepokea ni kijana wake, akamuuliza



    ‘Kwanini unaongea kinyonge hivyo..?’ akamuuliza



    ‘Sijisikii vizuri mama… naona mambo mawili mawili…’akasema



    ‘Kwa vipi,..?’ mama akaulizwa kwa wasiwasi sasa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Hata sijui mama, na alitoka kidogo kununua dawa, alipokua, akawa anaongea ovyoovyo, kama mtu aliyechanganyikiwa, mimi nikaona nimpe zile dawa zake za kichwa, sasa hivi amelala, lakini alikuwa kama kapagawa…’akasema



    ‘Mungu wangu…na wewe umetumia dawa gani, kwanini na wewe usitumie hizo hizo dawa…?’ akamuuliza



    ‘Sasa tukilala wote, ni nani atamsaidia mwenzake,..na ..oh, mama kwani upo wapi, mimi naanza kuingiwa na mashaka kwanini naona watu wa ajabu..’akasema sasa mama naye miguu ikaanza kumuishia nguvu



    ‘Akakata simu na kuwaambia wenzake,



    ‘Jamani mimi naondoka…’akasema



    ‘Unakwenda wapi na wewe..?’ akaulizwa



    ‘Matatizo yameshaanza nyumbani kwangu tena….’akasema



    ‘Oh, ina maana ni kweli, kwangu haitawezekana, mimi namtegemea mungu wangu atatulinda..’akasema yule mama mwenye nyumba ambapo wote walikutania hapo…, lakini hata kabla huyo mwenzake hajaondoka, simu ya huyu mama ikalia.



    ‘Mhh, simu yangu hiyo, hata sikusindikizi, ngoja niisikilize, utatuambia kinachoendelea…’akasema akitoa simu yake kwenye mkoba, na sauti ilikuwa ya askari, ikasema



    ‘Samahani, mama, mume wako kapatwa na ajali, alikuwa kiendesha gari kwenye kazi za kila siku, ghafla akaona kitu mbele yake, kama alivyoniambia maana nilikuwa naye, akajaribu kukiwepa akagonga nguzo ya umeme,  sasa hivi yupo hopsitalini kapoteza fahamu..’akaambiwa



    ‘Ok, hospitali gani..?’ akauliza huyo mama sasa akichukua mkoba wa mwenzake akijua ndio wake



    ‘Mkoba wangu huo mshirika….’mwenzake akasema na simu yake nayo ikaanza kuita…



    ‘Bado mimi, mungu wangu wee…..’ilikuwa sauti ya huyo mama mwingine,  , mama ambaye alinipeleka hospitalini na alisema hivyo, baada ya yeye kusikia simu yake ikiita, na aliogopa hata kuipokea..



    NB: Je itakuwaje sasa.....



    WAZO LA LEO: Wakati mwingine matatizo yanaweza kukutokea kwa mfulululizo ya shida, mpaka unachanganyikiwa, na matatizo hayo yanaweza yakawa yana muelekeo wa jambo ulilolisikia, wewe ulilipuuzia ukasema ni mambo ya kishirikina, lakini sasa yanatokea kama ulivyoambiwa na watu, au mtu fulani, Ni muhimu kuendelea kuwa na imani yako kwa muumba wako, wala usitetereka, kwani mara nyingi,.matatizo haya yanatokea kwa minajili ya kukupima imani yako, Mungu ni mwingi wa rehema, humpima mja wake kumjua imani yake kwake, japokuwa anamfahamu . Kwa ma



    Matatizo yaliingilia familia za wakina mama hao, hasa hao wawili, yule aliyenitoa kijijini, na huyu anayeishi na mdada, ila huyu ninayeishi naye kwasasa hayakuwa makubwa sana, zaidi ya migogoro yao ya kifamilia hasa kati ya baba na mkewe, mkewe alikuwa hataki kabisa mimi niendelee kuishi hapo, hata kurudi kuishi hapo, ilitokea pale wenzake walipomshauri kuwa nirudi kwake niishi kwa muda.



    ‘Mlishakubaliana, aje aishi kwako, huku akitafutiwa chumba, basi wewe endelea kufanya hivyo, nakuomba sana , maana kama unavyosikia, kwangu hakuna amani, mume wangu kawa kama mtu aliyechanganyikiwa..kijana wangu naye haeleweki…’yule mama mfadhili wangu wa kwanza akamwambia mwenzake huyu alipopigiwa simu kuhusu mimi.



    Walikuja wakakutana na kukubaliana aendelee kunivumilia.



    Basi ikakubaliwa hivyo, nikawa naendelea kuishi hapo, lakini kwa makubaliano kuwa niishi hapo kwa muda, lakini alisema hatakubali mimi nikae hadi nijifungulie hapo kwake….



    Tuendelee na kisa chetu…



    ************



    Baada ya tukio hilo, mimi niliendelea kuishi kwa yule mama niliyepelekwa kwake, kwa masharti kuwa nindoke hapo kitakapopatikana chumba, ili nihamie na kuanza maisha yangu mapya, na mtu wa kunitafutia chumba alitakiwa awe mume wa yule mfadhili wangu wa kwanza.



    Siku zikaenda na mimba inakuwa, na hali yangu ilikuwa leo mzima kesho mgonjwa hoi kitandani, na nikiumwa ndio makelele matusi, mimi nipo hapo kwa ajili ya kula na kulala tu,…ikabidi nivumilie hivyo hivyo nitafanya nini.



    Sikuweza kuwalamu wafadhili wangu wa kwanza, kwanini hawanitafutii chumba kwa haraka, kwasababu sikujua kuna tatizo gani huenda bado wanahangaika na matatizo ya familia yao, maana baada ya kutoka siku ile, huyo mama alipopigiwa simu kuwa mume wake kachanganyikiwa, mimi sikuweza kuonana naye tena, nasikia tu, kwa kupitia kwa huyu mama ninayeishi naye kuwa hali ya yule mume imekuwa ya utatanishi.



     Siku moja nikakutana na mdada, nilipokwenda sokoni, tukapata mwanya wa kuongea kidogo, na ndipo akaniuliza nimefikia wapi na mpango wa chumba



    ‘Sinilisikia kuwa wanakutafuti chumba, imefikia wapi…?’ akaniuliza



    'Mimi hata sijui, kila kukicha wanandoa hao wawili, wanakimbilia kwenye shughuli zao, jioni wakikutana ninachosikia ni ugomvi, mama mwenye nyumba analalamika, mimi nitawekwa humo mpaka lini, na mimba ndio hiyo inazidi kukuwa na kila siku siishi kuumwa umwa.



    'Na mzee anasemaje, baba mwenye nyumba?’ akaniuliza



    'Yeye anasisitiza kuwe na mke wake azidi kuwa na subra, kwani hawataweza kunirejesha kule kwa familia ile nyingine kwa hivi sasa kutokana na matatizo yanayoendelea huko, kunipelekea mimi huko kutaizidisha matatizo zaidi, na mpangop wa chumba haujakamilika….’nikasema



    ‘Lakini chumba kiwe ni tatizo kupatikana, mimi hili siamini, nahisi kuna jambo jingine , labda baba yule kutokana na hali yake, na kazi ya kutafuta chumba na kukuhudumia kakabidhiwa yeye..si ndio hivyo..?’ akasema na kuuliza



    ‘Ndio hivyo…’nikasema



    ‘Kwahiyo huyo mama anatakaje, kuwa uondoke, uende wapi, urudi kule au iweje, kama ni hivyo, kwanini yeye asisaidie kutafuta hicho chumba…?’ akaniuliza



    ‘Huyo mama kasema hayo ni mambo ya wanaume waliosababisha hayo yote ,kwahiyo kama ni chumba, waume ndio watafute, ili waweze kuwajibika, wanachoogopa ni kuwa wakitafuta chumba wao, waume wao hawatawajibika ndio makubaliano yao, na zaidi kinachoniuma ni kauli yake tu….’nikasema



    ‘Kauli gani…?’ akauliza



    ‘Hiyo ya kuwa mimi nikizaa shetani, ni nani atahangaika nalo…’nikasema



    ‘Lakini ndivyo alivyosema marehemu au sio, wote wawili hilo walilisema, na hata yule rafiki wa marehemu alilithibitisha hilo, japokuwa yeye ni mganga tu wa miti shamba, lakini si alisema ukiwa na matatizo umpigie simu, atakutafutia dawa…?’ akauliza



    ‘Ndio, lakini huyo mama ninayeishi naye, kasema hataki kuhangaika na mambo ya kishirikina, kama ni shetani, niondoke nalo, nikazalie huko huko…’akasema



    'Hayo waliongea lini…maana majuzi walikutana kwenye kikao chao…?’ akaniuliza



    'Hata wiki haijapita, walizozana kweli, hata usiku sizani kama wamelala kwa amani…maana asubuhi waliamuka kila mtu kanuna, …’akasema



    'Basi hao akina mama  walikutana kwenye kikao chao, wakashauriana kuwa sisi turejeshwe kijijin na kukabidhiwa kwenye familia za hao marehemu maana sasa familia zao hazina amani tena, na tukiendelea kuwepo, matatizo hayataisha…’akasema huyo mdada



    'Aaah mimi hilo sikubali, kama hawanitaki, waniache tu, nitahangaika hapa dar, na najua nitaweza kuishi, lakini sio kunirejesha huko kijijini…’nikasema



    'Haya wakikitupo huko mitaani ndio utaishije, hebu niambie, una mipango gani ya maisha..?’ akaniuliza



    'Mungu mwenyewe atajua, ….’nikasema



    ‘Mungu mwenyewe atajua, ndio mipango yako hiyo, mimi sipendi hata kuongea na wewe, maana huna ubunifu, huna akili ya kufikiria, mungu atajua, ukiwa umekaa hivi hivi tu…’akasema huyo mdada



    ‘Sasa unataka mimi nifanye nini, elimu yangu imeishia hivyo…sina ujuzi zaidi ya kufagia na kusafisha vyombo, na kuomba omba mitaani, nitafanya kazi gani…?’ nikauliza



    'Tatizo wewe….hata nikikushauri jambo ni kama nampigia gita mbuzi, wewe ulivyo, huwezi kuishi na mimi, wewe huwezi  kupambana na mambo ya mitaani…mimi mwenzako ni mjanja, nione hivi hivi tu…’akasema

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    'Mungu atanisaidia, najua mungu anajua fungu langu, kama ni hapo hapo au hata wakinifukuza, ipo siku nitafanikiwa tu, lakini siwezi kufanya mambo nisiyokuwa na ujuzi nayo…’nikasema



    'Mimi ninachokuonea huruma, wewe una mzigo tumboni, na baya zaidi hatujui huo mzigo ulio nao tumboni upoje, ushaambiwa sio mimba ya kawaida, je ukizaa shetani, hebu niambie kutakalika kweli…’akaniambia



    'Mimi sipendi hiyo kauli, kwanini nizaie shetani, …kwani wengine wanazaaje, mbona hospitalini wanasema ni mimba ya kawaida tu…’nikasema.



    'Hiyo ndio kauli yako,mungu anajua, mungu anajua, haya kaa na kauli yako hiyo tuone kama mungu atakusaidia kama wewe mwenyewe hujisaidii,..kiukweli mimi nilikuwa na mpango, lakini kila nikiongea nawe naona ni majanga tu, hutaweza kuniunga mkono, na sana sana, utaniharibia, naogopa kukushirikisha kabisa…’akasema



    'Mpango gani huo…?’ nikamuuliza



    'Niapie hutasema kwa mtu, kama nikikuambia kuhusu huo mpango wangu, maana ni…..’akatulia kama kshtuka jambo, akageuka kuangalia kule sokoni, na mimi nikaangalia huko huko kuwaangalia wenzangu niliokuja nao.



    'Niambie kwanza, ndio niape siwezi kuapa kitu ambacho sikujui, je kama ni dhambi…’nikasema



    'Hawa akina mama si wanajifanya wajanja, hawajui kuwa bado wamekalia bomu….’akasema



    'Bomu gani hilo…?’ nikamuuliza



    'Si yale mazindiko, umesahau, kwani walifanya juhudi gani kuyaondoa, wamepuuza, angalia yule mama kule tulipokuwa awali anavyopata shida, kwanini hawaelewi,…’akasema



    'Si walishahangaika wakaambiwa yameondolewa, na hayo yanayotokea hivi sasa  yawezekana ni mambo ya kawaida tu, mimi hata sijui, …’nikasema



    'Thubutu, kila siku majanga, nimesikia wakiongea, mume wa kule tulipoanzia, siku nyingine anakutwa yupo nje uchi, anaweza akawa anatembea hata hajui anakwenda wapi, usiku amaanuka, anatembea, anafanya kazi, hivi hayo ni mambo ya kawaida…’akasema



    ‘Lakini docta alisema huo ugonjwa upo, na kutibika kwake hakuhitajii haraka, …’nikasema



    ‘Na huyo kijana wao, umesikia vituko vyake…’akasema



    ‘Amekuwaje na yeye…?’ nikauliza



    ‘Hahaha, mimi niliwaambia, huyo kijana wao, ana matatizo, wakaniona namchukia, naingilia mambo ya kifamilia, na unajua mimi walishanichukia mapema hata kabla y ahayo matatizo, kisa namsingizia mtoto wao, eti mambo asiyoyafanya, wanamdekeza sana yule kijana, sasa wameshaanza kuipata joto ya jiwe, watanikumbuka…’akasema



    ‘Amekuwaje kwani…mbona siyajui hayo?’ nikauliza



    ‘Sasa na hilo utasema ni ugonjwa,…hilo sio ugonjwa, pamoja na mengine, mtoto wao ana matatizo, na ukionamtu anakushauri msikilize, yule mama ni mwalimu, msomi mnzuri, lakini sijui kwanini mambo mengine anayafumbia macho, hasa yakihusu mtoto wake..yeye alitekwa na akili kuwa mimi huenda natembea na mume wake, akashindwa kuangalia mambo mengine…’akasema



    ‘Mhh,…sijui kwanini alikuwa akifikiria hivyo, kwanini lakini, mimi wala sikuwa na mawazo hayo…’nikasema



    ‘Hukuwa na mawazo hayo, ushahidi si unao tayari….’akasema akicheka.



    ‘Naona wewe unaleta utani, mimi niliwahi kutembea na mume wake…’nikasema



    ‘Sasa ndio hapo, wangetuliza kichwa, wakaangalia kiundani zaidi, tatizo, sio sisi tu, huenda matatizo hayo yameanzia hata kabla yetu, mzee, kijana,…na ni kweli kuna mamabo yamewekezewa, nayo walitakiwa wayafukue, lakini kwanza wamejiangalia wao wenyewe, mle ndani kuna tatizi zaidi ya tatizo,…’akasema



    ‘Mhh..au wewe unahusika….’nikasema



    ‘Hahaha, watamtafuta mchawi, na hawatampata, maana mchawi keshafariki, yaliyobakia, ni masalio yake, na hayo masalio, watapata shida sana kuyamaliza, ... waache wahangaike, mwisho wa siku watatutafuta, ila mimi sijui kama nitaendelea kuishi na hawa watu…’akasema



    ‘Kwanini wanasema hivyo watatutafuta,…?’ nikauliza



    ‘Hivi unafikiri utaishi na wao milele…na we ngoja tu,…mimi sio mjinga, najua kuishi na watu, kwanza nilipofika hapo kwa madamu, nikafanya utafiti, kuna mtu kanifundisha jambo, mjue mtu unayeishi naye anataka nini…nikamtafit madamu nikajua anataka nini na nini..nikamtafuti mzee, nikajua anapenda nini na nini…mzee wake hata habari na mimi kabisa…hilo nimelifurahia, tatizo ni mama…’akasema



    ‘Lakini si kawaida…mama ndiye mlinzi wa nyumbani…’nikasema



    ‘Sasa huyo mama kuna siki atanitafuta….’akasema



    ‘Utakwenda wapi…?’ nikamuuliza



    ‘Wewe kaa hivyo hivyo, ngoja niondoke, wasije kurudi hao mabosi, madamu wangu nampenda lakini ..unajua kuna kipindi tunakaa naye ananisimulia mambo mengi, ..lakini kuna kipindi haeleweki, kila unachokifanya hakionekani…akiona mume wake akinitupia jicho, basi keshabadilika, ni nani kasema anamtaka mume wake mzee yule..mimi nina mipango yangu, …hahahaha,.’akasema akicheka kwa dharau



    ‘Lakini wewe si ulisema, wanakusifia kuwa wewe ni jembe, unafanya kazi sana,…’nikasema



    ‘Ndio hivyo, kwa hilo, kila mtu ananisifia, sio madamu, hata mzee mwenyewe,  lakini kazi ukimaliza, hawakosie cha kunisema, mara mimi ni muhuni, mara mimi napendelea mambo ya kishirikina, , mara tumeleta matatizo kwenye familia zao, yaani karaha,kashfa, sasa mimi sio mtoto mdogo, nayasikia, yananiuma, mpaka lini…kwa kifupi maisha kaa haya, hayana uhakika, na alishaniambia, siku yoyote atanitimua kama hanijui…’akasema



    ‘Lakini angalau kwako kuna unafuu, sio kama kwangu…yaani kuna muda nafikiria kukimbia, niondoke kabisa, unaweza ukajitahidi kufany akila kitu, lakini watoto wa pale ndani, wale mabinti, wanaharibu, wanachafua, maana wao wanataka kula na kulala, ..ndio maana hawaolewi. Na mama yao anawatetea, sasa hata mimi hali kam hiyo inanikwaza, lakini ndio maisha utafanyaje, hata hivyo, hata mimi nitakimbia, nitaondoka hapo nyumbani…’nikasema



    'Sasa ukimbie na hali kama hiyo uende wapi …?’ akaniuliza akinikagua tumbo



    'Popote,…ipo siku, mungu atanionyesha njia, yaani hata sijui, hakuna anayenionea huruma kazi zote nafanya mimi, nachoka sana, kuna muda nahsi kizungu zungu , kutapika, nakimbia kujificha mpaka hali hiyo inakwisha, najua wakiniona nipo hivyo, itakuwa njia ya kunifukuza, aah, ni shida kwakweli …’nikasema



    'Umeonaeeh,….ndio hayo matatizo yanayonikuta mimi, ila kwako, haaah, unalo….nilikushauri awali uiotoe hiyo mimba ukakataa, sasa kazi unayo…sasa sikiza nikuambie mpango wangu….’akasema



    'Mpango upi huo…usiwe mpango mbaya, mimi sitaki matatizo…?’ nikamuuliza na yeye kwanza akaangalia kule sokoni kama ana mashaka fulani, , halafu akaniangalia na kusema;



    'Unauliza eti mpango gani, …’akasema na kuaniangalia



    ‘Sawa nimekuelewa, niambie sasa…’nikasema



    ‘Nikuambie kitu, hawa watu, hata ufanye kazi kama punda, hata uwe mnyenyekevu kama malaika, hata uwe mtiifu kama …sijui nani, hawatakutahamini kamwe, unanisikia, hawa watu watakutumia, na wewe hivi wanakulipa shilingi ngapi, aheri ya mimi mwisho wa mwezi nakinga japokuwa ni kidogo…’akasema



    'Hawanilipi chochote, wanadai mimi sina mkataba na wao,…mimi hapo nakaa kama nimefadhiliwa tu, kama mgeni, na siku ikifika nitaondoka, yule mama mchungu wa pesa, kila kitu anakupigia mahesabu, na ole wako usirudishe chenji, kwahiyo maisha ninayoishi anayejua ni mungu peke yake….’nikasema



    ‘Sasa sikiliza nikuambie huo mpango, lakini ole wako ufungue domo lako , huu nimeshaufanyia kazi na utafanikiwa, ni wewe tu,….’akasema



    ‘Sawa niambie…’kabla hajaongea mara nikaitwa, na nikiitwa, nawafahamu watu wangu, wanataka niwepo mara moja, ikabidi niachane na huyo mdada, kuwakimbilia watu wenzangu, na mdada akanipungia mkono akisema



    ‘Kwaheri ya kuonana….’akaondoka



    Niliwaendea watu wangu na nilipowafikia tu mama mwenye nyuma akaniuliza



    ‘Ulikuwa wapi muda wote huo,tunakutafuta hatukuoni, ..?’ nikaulizwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Nilikuwa naongea na yule mdada wa kule…’nikasema



    ‘Mumeanza kudanganya tena eeh, sawa, ongeeni tu, na huyo mwenzako ni mjanja njanja, ngoja akudanganye uhadaike, shauri lako…’akasema



    ‘Hakuna kitu kibaya mama, nilikuwa naongea naye tu.



    ‘Sawa ongeeni tu, na nilikuwa sijakuambia, ujiandae, safari yenu ya kwenda huko kijijini inaiva, wewe na yeye mtandoka, sasa kama mlikuwa mnaliongelea hilo mlipange vizuri, safari hii hakuna kurudi nyuma, ukazalie huko kijijini kwenu mlipoyatoa hayo mashetani…’akasema huyo mama



    ‘Mama kwanini unamuambia hivyo….’mtoto wake akasema



    ‘Kwani uwongo mwenyewe anafahamu tumboni kabeba nini, na akijifungulia hapo nyumbani, mtaambukizwa na nyie, na hatujui hilo shetani litakuwaje,…kama ni shetani kweli, si itakuwa ni balaa…’akasema huyo mama



    ‘Mungu anajua,…’mimi nikasema hivyo tu, siku hiyo kiukweli sikuwa na raha kabisa, nikawa kama mgonjwa, kumbe safari imeshapangwa, sasa nitafanya nini…akilini nikajipanga niende kuonana na huyo mdada, niusikie mpango wake, kama ni kutoroka tutoroke wote, sasa sijui tutakwenda kuishi wapi.



    Basi siku hiyo ikapita, na nyingine na siku ya tatu sasa, nikiwa nyumbani, wenzangu walitoka, nilikuwa sijisikii vyema, na nikiwa ndani, mara nikasikia wanzangu wakirudi, na kabla sijatoka nje kuonana nao, mara, wakaja askari,



    ‘Kuna tena jamani…?’ wakaulizwa



    ‘Tunamuhitaji huyu mfanyakazi wenu wa ndani…’akasema



    ‘Kafanya nini…? Huyo mama akauliza



    ‘Atuambie mwenzake yupo wapi, …’wakasema



    ‘Mwenzake yupi…?’ mama akauliza



    ‘Yule mfanyakazi wa yule rafiki yako,….’akasema huyo askari, huku akinikabili mimi, pale nilipo nilihis mwili ukinisha nguvu miguu ikawa kama imekatika kwenye magoti.



    ‘Kafanya nini huyu mfanyakazi …?’ akauliza huyo mama.



    ‘Kaondoka hapo nyumbani, tangia jana, …na kuna kiasi kikubwa cha pesa hakionekani, inaonekana ni yeye kazichukua hizo pesa na vito vya thamani vya huyo mama, na rafiki yake mkubwa ni huyu mfanyakazi wako, tunataka tukamuhoji huyu mfanyakazi wako kituoni…’wakasema hao askari.



    ‘Lakini mna uhakika gani kuwa huyu anajua wapi huyo mwenzake alipokwenda…?’ akauliza huyo mama



    ‘Tuna uhakika, kwa mara ya mwisho , walionekana wakiongea hawa wawili kule sokoni,



    NB: Majanga





    WAZO LA LEO: Tuweni makini kwenye ushauri tunaopewa na watu wengine, kuhusu mikakati ya maisha, tusikubali kwanza, kabla hatujafiria matokeo ya hiyo mikakati, kuna watu wengine ni wepesi wa kubuni na kupanga mambo hata kama ni ya shari, na kuwashikirisha wengine, nia ni kuingiza kipato. Jiulize kwanza kipato hicho ni cha halali kinapatikana kwa njia ya halali, kama kuna mkono wa shari epukana na mipango ya namna hiyo. Tumuome mola wetu atupe njia ya heri, na kupata riziki za halali





    Nilipofika kituoni, nikaanza kuhojiwa tena kwa vitisho, na kuambiwa nitatapelekwa jela, nisipotaja wapi alipo huyo mdada, wakazidi kusema kuwa nisiposma ukweli,  watanifunga, au hata kunitesa, mimi nikaendelea kusema huo ukweli ninaoujua mimi;



    ‘Mimi sijui wapi alipo na hakuwahi kuniambia anakwenda wapi, ni jambo la kushangaza kwangu kusikia kuwa kaondoka,…?’ nikasema



    ‘Je kwa mara ya mwisho mlikutana lini na wapi..?’ nikaulizwa.



    ‘Tulikutana sokoni, tukaongea, lakini hakuwahi kuniambia ana mpango wa kutoroka…’nikasema

    ‘Alikuwambia ana mpango gani…?’ akaniuliza



    ‘Aliniambia ana mpango lakini hawezi kuniambia mimi kwasababu sitauweza….’nikasema



    ‘Kwahiyo kumbe alikuambia ana mpango, si ndio hivyo…?’ akaniuliza



    ‘Ndio….’nikasema



    ‘Mpango gani…?’ akaniuliza kwa hasira



    ‘Hakuwahi kuniambia…’nikasema



     ‘Wewe unasema uwongo, na nimesikia ni tabia yako ya kuficha ukweli, hata kama unaujua huo ukweli, sasa hapa ujue ni wewe mwenyewe kuamua, kusema ukweli, au ukalale jela, unakufahamu jela kulivyo, huko utapambana na watu watukutu, watakufunza adabu, na ukitoka huko hata ukiusema huo ukweli tena hautakusaidia kitu, bora uuseme sasa uwe huru, unajua msema kweli ni mpenzi wa mungu…’nikaambiwa.



    ‘Lakini mimi nimeshawaambia ukweli, mnataka ukweli gani zaidi, niambieni huo ukweli mnaoutaka nyie ni upi, na mkiniweka jela  na hali kama hii, mtakuwa mnanionea bure…’nikasema.



    ‘Utajua wewe mwenyewe huko jela, watu wanajifungulia huko, sembuse, wewe, nakuambia usiposema ukweli, utakuja kujuta,…’akazidi kusema kwa ukali, na mara akaingia jamaa mmoja, usoni, kakunjamana kwa hasira, kifua ni cha wale wainua vyuma, akaniangalia, mpaka nikahisi mwili ukinisisimuka kwa uwoga.



    ‘Unamuona huyu, huyu ndiye atakuuliza maswali, na ukijibu uwongo, atajua jinsi gani ya kukufanya, kama hutatoka hapa huwezi kutembea tena, shauri lako, ulishawahi kuwekewa nyoka mdomoni, um-meze, huyo anayo huyo nyoka, hebu muonyeshe…’akasema na kunizidishia uwoga, na hapo hapo nikahisi kutapika, kichwa kinaniuma , moyo unakwenda mbio.



    Yule jamaa akamtoa nyoka kwenye mfuko wake, na kunielekezea mimi, unajua kuogopa, nilitoa jicho, nikahisi mwili umekufa ganzi,…nilipanua mdomo kupiga yowe, na jamaa akataka kuingiza yule nyoka mdomoni kwangu…halafu akamrudisha huku kanikazia macho.



    ‘Haya upo tayari kusema ukweli…?’ akaniuliza nikawa kimia, maana siwezi hata kuongea, na aliponiona nipo kimia, akasema;



    ‘Haya inuke unakwenda huko ulipokutaka wewe..atakuuliza maswali, na mtamalizana huko,..hutanilaumu kwa chaguo lako…’akasema na mimi nikaganda, siwezi kuongea, siwezi kuinuka.



    ‘Nimekuambia simama….’akasema kwa sauti iliyonifanya nishtuke na kwa haraka nikasimama…hapo nikasema.



    ‘Lakini mimi nimesema ukweli wote.., mama yangu alinifundisha nisiseme uwongo, nyie mnataka niseme kitu gani mnachokitaka..?’ nikauliza.



    ‘Utuambie wapi huyo rafiki yako alipokwenda, au huo mpango aliotaka kukuambia, ni mpango gani…?’ akauliza sasa akiwa kasimama, na mimi nikajibu maneno yale yale kuwa mimi sijui alipokwenda na wala hajawahi kuniambia huo mpango wake.



    Ghafla nilistukia nimeinuliwa juu juu kama katoto na huyo jamaa akiwa kanishikilia shingoni, na sikweza hata kuhema, alivyonishikilia shingoni, na kuniinu juu kwa mkono mmoja tu,..ikawa kama ile ndoto ya majinamisi, nikahisi kichwa kikijaa…masikio yanataka kupasuka…siwezi kuhema…macho yakanitoka..nikajua sasa nakufa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akaniachia na mimi nikaporomoka chini, na kudondokea sakafuni, nikajaribu sasa kuitafuta pumzi, na hata nilipoipata, nikaishia kukohoa, na kuanza kutapika.. nahisi hata mkojo ulipitiliza, na haikupita muda, giza likatanda usoni, na sikuelewa kingine kilichotokea, kwani nilipoteza fahamu, nilipozindukana nikajikuta nipo hospitalini.



    ***************



    Nilipozindukana, sura ya kwanza kuonana nayo, ilikuwa ya yule kijana wa mfadhili wangu wa kwanza, alikuwa kasimama mbele ya kitanda, huku akiniangalia kwa mashaka, kama ana wasiwasi, ni kama kajiiba kuja kuniona, akainama kuniangalia, na akukutana ma macho yangu.



    ‘Oh, umeamuka,..vipi, unajisikiaje…?’ akaniuliza



    ‘Sijambo…’nikasema nikishangaa kumuona huyo kijana hapo.



    ‘Pole, nimesikia yaliyotokea, hivi kweli, hujui wapi huyo mtu alipokwenda, na niambie walikuuliza nini, na wanataka kujua nini…?’ akaniuliza



    ‘Mimi sijui wanasema yule mdada, aliyekuwa akifanyia kazi kwenye katoroka, ..na pesa na vito vya thamani, sasa mimi sijui kaenda wapi, na sikujua kuwa atakuja kufanya hivyo…’nikasema



    ‘Shilingi ngpi..na vito gani hivyo..?’ akaniuliza.



    ‘Mimi sijui shilingi ngapi, na hata hivyo vito sijui ni kitu gani…’nikasema



    ‘Ssshit…’akasema hivyo na kugeuka kutaka kuondoka.



    ‘Mwambie mama yako aje kunisaidia, maana mimi sitaki kwenda jela wataniua…’nikasema



    ‘Mama…unasema nini, mama, aje kukusaidia wewe, hahaha, labda useme aje kukugandamiza, watu hao hawataki hata kukuona, wewe umekuwa ni chanzo, cha matatizo, wewe na mwenzako, …hata mimi kuja hapa nimekuja tu, niliposikia umeletwa hapa, nikawa napita hapo nje, nikaona kwanini nisije kukuona, lakini,….’akasema na kuanza kuondoka.



    ‘Sawa, lakini haya yote sijayataka mimi, na matatizo haya kama ni chanzo, labda ni huyo mdada, na nyie mkachangia kuniingiza kwenye mambo nisiyoyajua, …’nikasema hapo akatulia baadae akageuka na kusema;



    ‘Sikiliza, jaribu sana kujipigania wewe mwenyewe usiwategemee sana hao akina mama, usiwaamini sana ukawaambia kila kitu chako..na…, na usikimbilie kumlaumu mtu, maana kama ni matatizo, unayo, sasa hata ukilalamika, yataondoka hivi hivi kwa kulalamika,.., na hata ukimtupia mtu lawama, kuwa ndio yeye sababu je huyo mtu atakusaidia, jiulize sana hayo. Kwasasahivi dunia ilivyo kila mtu anajali tumbo lake…’akasema



    ‘Lakini hata wakijali matumbo yako , kuma mambo mengine mtu akiwa na na uwezo wa kusaodia, wengine anatakiwa afanye hivyo,..wewe mwambie mama yako, namfahamu yeye ni mtu mnzuri, ..’nikasema



    ‘Ni kweli yeye ni mtu mnzuri, lakini kwa wazuri kwake, wewe hukutaka kuwa mnzuri kwake, ..na…wote hata hao marafiki zake, sasa hivi wanakunyosheeni vidole kuwa nyie ndio sababu ya hayo matatizo…’akasema.



    ‘Lakini sio kweli, mungu anajua mimi sijahusika kwa yote hayo wanayoyasema, wananisingizia tu..’nikasema.



    ‘Mungu anajua sawa,… sasa…hebu niambie, mungu atakusaidia hivi hivi tu…nimeshakushauri tu..mimi naondoka, lakini kumbuka , pambana na matatizi yako usitarajia msaada wa kutoka kwa wengine , hasa hao akina mama, na ukilemaa kwa jinsi nilivyosikia wewe utaenda kufia jela,…’akasema.



    ‘Ni bora nife tu, mama yangu si alishakufa, kwani mimi nina tahamani gani tena…’nikasema.



    ‘Sawa kama ndilo unalolitaka, lisubirie tu linakuja hilo, muda si mrefu.., nina imani wakikupeleka huko jela hutatoka mzima,..na wenzako wataendelea kula nchi, unakumbuka kuna kipindi nilikubembeleza sana uwe mpenzi wangu uliniambia nini,…sasa utanikumbuka kwaheri…’akasema .



    ‘Samahani kabla hujaondoka, nimesikia na wewe una matatizo, unaumwa, unasumbuliwa na nini…?’ nikamuuliza na akasimama kwa muda bila kunijibu halafu akasema.



    ‘Matatizo yangu nayajua mimi mwenyewe, na kama ni mama, kawaambia hilo, …sawa, waache wasema wanayosema, ila kiukweli matatizo yangu chanzo chake ni wao, wazazi wangu…’akasema.



    ‘Kwa vipi, wazazi wako wamekufanya nini..?’ nikamuuliza.



    ‘Wao wakigombana, wakiishi bila kupendana, mimi naumia sana, mimi nawapenda sana wazazi wangu nataka waishi kwa raha, wapendane kama zamani…’akasema.



    ‘Kwani hawapendani, kwanini hawapendani, kama zamani…?’ nikamuuliza.



    ‘Mimi sijui, ningelijua ningafanya kila niwezalo warudie hali yao ya zamani, lakini sijui, na mlipofika nyie mkazidisha matatizo, iliniuma sana, na zaidi nasikia wamegundua kuwa nyie mumesababisha mataizo haya yanayotokea sasa,..niliapa nitafanya nifanyalo mpotee kabisa, lakini nawaonea huruma….’akasema.



    ‘Unaamini hayo kuwa sisi ndio sababu..?’ nikamuuliza.



    ‘Niamini nisiamini, lakini ushahidi upo, niliwahi kumuona yule mdada akifanya mambo ya kishirikiana uchi, niliwaambia siku ile ya kikao..na nilipomgundua ndio akawa ananisema umbea kwa wazazi wangu, wakati nilikuwa najitolea kumsaidia, hata pesa za kujikimu, hana shukurani…’akasema.



    ‘Lakini yaonekana wewe na mdada mlikuwa na jambo lenu wawili…?’ nikasema.



    ‘Kiukweli ilikuwa hivyo,…kama nilivyotaka iwe kwako, unajua ujana tena..lakini yeye, alikuwa mjanja sio kama wewe, nampenda sana kwa hilo, ana kichwa cha kutafuta, kuona mbali sio kama wewe…wewe ni mtu wa mungu mungu tu,…’akasema.



    ‘Kwahiyo hicho alichofanya unaona ndio ujanja..?’ nikamuuliza.



    ‘Hapana mimi siongelei hayo, wizi …hapana, kama kafanya kafanya yeye, sijamsifia kwa hilo, na najua akishikwa ataishia kubaya , lakini hakuwa na tabia hiyo ya wizi, sijui kwanini alifanya hivyo…’akasema.



    ‘Yeye aligundua kitu gani akakusema kwa wazazi wako..?’ nikamuuliza na hapo, ikawa kama nimemfukuza, akasema;



    ‘Kwaheri, fikiria yako, usiwazie ya kwangu maana ya kwangu hayakuhusu na hakuna anayeweza kuyatatua..zaidi yangu na wazazi wangu…’akasema na kutembea kwa haraka kuelekea mlangoni, lakini kabla hajafika mlangoni, mara akaingia mama yake. Akashtuka na kushikwa na butwaa…



    ‘Wewe umefuata nini huku..?’ mama yake akamuuliza.



    ‘Nilikuja hospitalini, kufuatilia kiliniki yangu…’akasema.



    ‘Kliniki yako uko huku …?’ akaulizwa.



    ‘Nilisikia huyu mdada kalazwa hapa, kwa vile namfahamu ndio nikaona nije kumjulia hali..’akasema na hapo mama yake akageuka kuniangalia uso ulikuwa umejaa hasira.



    ‘Achana na hawa watu mwanangu, unajua ni nini walichotufanyia, ..sasa hamueleweki wewe na baba yako, unajua chanzo ni nani, ni hawa watu, ..ni watu wabaya sana, sitaki hata kuwaona, lakini kwa vile nina maswali ya kumuuliza nimeona nije tu, ubinadamu unaniponza,..haya ondoka hapa …’akasema na huyo kijana wake akatoka mbio mbio.



    ***************



    ‘Haya mdada, niliwahi kukuambia kuwa kuna siku utanihitajia, nikakuomba uniambie ukweli ili uwe pamoja na mimi, lakini ukaniona mimi sina maana, unaona dunia inavyokufunza…’akasema.



    Sikusema kitu, nilikaa kimia tu, nikiwazia ni kitu huyu mama alitaka nimuambie nikashindwa kumuambia, ni kuhus mume wake, sasa ningesema nini, kuwa alitaka kunibaka, je ni kweli alitaka kufanya hivyo, mimi sikuwa na uhakika na hilo, na kama ningelimuambia huenda ingelikuwa mwisho wa ndoa, yao, …hapana nilichosema ni sahihi kabisa.



    ‘Sasa niambie huyo rafiki yako kaenda wapi, unaona mlivyo, mnaaminiwa mnakabidhiwa dhamana za watu, maana mtu akiondoka kwenda kazini, na wewe ukabakia na nyumba unakuwa umekabidhiwa dhamana ya kila kitu kilichopo ndani, sasa nyie mnaingiwa na tamaa mnaiba, …niambie ukweli huyo rafiki yako kakimbilia wapi..?’ akaniuliza.



    ‘Mama kiukweli mimi sijui, wewe unanifahamu nilivyo, siwezi kusema uwongo…’nikasema



    ‘Mimi ninavyokufahamu ni kuwa unaweza kuficha ukweli kwa kumuonea mtu mwingine huruma kwa ujinga wako ulio nao, na huyo mtu hawezi hata kukuonea huruma,..ukiogopa kuusema ukweli, sasa huku ni kwingine, huko kuna mateso, hapatakuwepo wa kukuonea huruma, nimekuja hapa kukusikiliza kama unahitajia msaada wangu…’akasema.



    ‘Ndio mama mimi nakutegemea wewe, nimegundua kuwa wewe ni mama mwema unaweza ukanitetea kwa hili, maana ukweli mimi sijui, alipokwenda huyo mtu…’nikasema.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Lakini mlionana naye huko sokoni, au sio..?’ akauliza.



    ‘Ndio…’nikasema



    ‘Ni mara ya ngapi kuonana naye, kabla ya hiyo siku..?’ akaniuliza.



    ‘Mara nyingi tukija sokoni namuona kwa mbali tu, na hatukuwahi kuongea naye kama siku hiyo…’nikasema



    ‘Kwanini siku hiyo mliongea,..?’ akaniuliza.



    ‘Yeye aliponiona aliniita kuwa anataka tuongee…’nikasema.



    ‘Kwahiyo yeye ndio alikuita..sio wewe ulimfuata..?’ akaniuliza.



    ‘Yeye aliponiona alinionyeshea ishara ya mkono, kuwa nimfuate…’nikasema.



    ‘Uliwaambia jamaa zako mliokuwa nao, kuwa umeitwa na mtu ..?’ akaniuliza.



    ‘Ndio, nilimuambia mama, akasema nisichelewe…’nikasema.



    ‘Lakini hakukuuliza ni nani unataka kuongea naye..?’ akaniuliza.



    ‘Hakuniuliza, ila niliporudi baada ya kuongea naye, ndio akaniuliza ni nani niliyekuwa nikiongea naye…’nikasema.



    ‘Mlipokuwa mnaongea naye, mliongea nini na nini..?’ akaniuliza.



    ‘Tuliongea mambo mengi, kuhusu maisha yetu yatakuwaje, tutafanya kazi gani ambayo inaweza kutuingizia, kipato, na baadae ndio akaniambia ana mpango wake, lakini anaogopa kuniambia mimi …’nikasema.



    ‘Kwanini anaogopa kukuambia wewe..?’ akaniuliza.



    ‘Ananiona mimi sio mjanja,…akasema mimi  kauli yangu ni mungu anajua, mungu anajua, nikae na kauli yangu hiyo kama itanisaidia…lakini hakuwahi kuniambia huo mpango wake, akisema haniamini, na kitu kama hicho..’nikasema



    ‘Mimi pamoja na mengine nakuamini, lakini hao walioibiwa hawawezi kukuamini, nimejaribu kuongea nao, wakaona kama na kutetea, mpaka tumeishia kugombana, hata urafiki umemeguka, kisa ni wewe..sisi kabla yenu tulikuwa marafiki wakubwa tunasaidiana, sasa mumekuja nyie, mumeharibu urafiki wetu…’akatulia akiangalia simu yake.



    ‘Sasa utanisaidiaje…maana sina mtu wa kunisaidia zaidi yako wewe…?’ nikamuuliza



    ‘Unajua nikuambie kitu, unachoniuliza kinaniweka njia panda, nikikusaidia wewe, ina maana navunja mahusiano yangu na rafiki yangu, huyo mama aliyeibiwa, na ndivyo alivyoniambia tulipokutana, amesema mtu anayemjali awe upande wake kuhakikisha kwanza anampata huyo mdada, na pili nyie mnaishia jela, …sasa hebu niambie hapo mimi nifanye nini, nikusaidie nivunje urafiki wangu, au nibakie kwa rafiki yangu wewe uende jela…?’ akaniuliza



    ‘Nitaendaje jela wakati mimi sikuiba, na wala sijui huyo rafiki yangu kakimbilia wapi na wala sijui huo mpango wake ulikuwa nini, na kama ningelijua mpango wake ndio huo, ningemkanya, na kumuambia akiiba nitamuambia madamu wake



    ‘Je angelikuambia huo mpango ungalifanya hivyo…?’ akaniuliza



    ‘Kufanyaje…?’ nikauliza.



    ‘Ungelimuambia madamu wake kuwa mwenzako ana mpango wa kuiba..?’ akaniuliza



    ‘Nikuulize wewe mama, mtu kaja kukuambia kuwa ana mpango wa kuiba mahali, je unaweza kwenda kwa hao watu ukawaambia kuwa kuna mtu anataka kuwaibia, je asipoiba, …mimi ningelijitahidi tu kumkanya kuwa asifanye hivyo, na ningelimtisha kuwa nitamuambia madamu wake, najua angeliogopa kufanya hivyo,ila mungu alizuia hilo akijua ungelikuwa ni mtihani kwangu…’nikasema



    Mara simu yake ikalia…akaiangalia, na kusema.



    ‘Haya tunakutana mimi na wenzangu, moja ya ajenda ni hiyo, jinsi gani ya kufanya, na shauri la awali ni kuwa nyie mrejeshwe kijijini, mimi nilijaribu sana kulizuia, na kulichelewesha nia, tupata sehemu ya kukuweka wewe, lakini imeshindikana kutokana na matatizo ya mume wangu, sasa hili limetokea, ajenda sasa sio wewe kupelekwa kijijini tena, bali ni kuhakikisha unapelekwa jela, kama usiposema wapi huyo rafiki yako amekwenda..’akasema



    ‘Lakini mama, ujue mimi nitakwenda jela bila kosa lolote , na hali hii je itakuwaje, na hali hii imetokea nikiwa kwenu, je kama unawahusu watu wa nyumbani kwako,....?’ nikauliza



    ‘Hapo mimi siwezi kusema kitu, na ukizidi kusema kuwa hali hiyo uliyo nayo imetokea kwangu ndio unazidi kuniti hasira,..lakini nikuambie kitu, hiyo hali umejitakia wewe mwenyewe, kama ungenishirikisha, ukaniambi aukweli mapema, nikajua ni kitu gani kinachoendelea isingelifikia hapo…’akasema



    ‘Kwani mimi nilikuwa najua…’nikajitetea



    ‘Ulipojua, ulipohisi kuna hali kama hiyo, unaota sijui, na hata kama kuna tabia ambayo ulihisi sio ya kawaida kwa mume wangu ungeliniambia, mimi ningelijua jinsi gani ya kufanya, na huenda sasa hivi ungelikuwa labda unaishi na huyo bwana, au kungelikuwa na mpango madhubuti wa kuhakikisha kuwa haki yako inapatikana, sasa wewe hukutaka kujisaidia, mimi ningeliwezaje kukusaidia..?’ akaniuliza



    ‘Sawa mungu mwenyewe atajua ,kwa vile mimi nazungumza ukweli, na hayo niliyosema kwa polisi ni  kwako ndio ukweli ulivyo, kama nitapelekwa jela na kufungwa, najua ni mipango ya mungu, yeye anajua zaidi, na kwanini itokee hivyo,  lakini sitachoka kuongea ukweli, na huo niliokuambia ndio ukweli,…kama utanisaidia mungu atakusaidia na wewe…’nikasema na huyo mama akanigeukia na kuniangalia machoni, niliona namna ya huzuni usoni mwake.



    ‘Mhh….huu sasa ni mtihani…’akasema hivyo tu na kuondoka.





    WAZO LA LEO: Ukweli ni silaha kubwa katika maisha yetu, watu wanafikia kusema uwongo ili wafanikiwe mambo yao, wengine wanafikia kusingizia wengine uwongo, kujenga fitina, kisa wao waonekane ni wazuri na wengine ni wabaya, kisa wanataka wafanikiwe kwenye mikakati yao ya maisha, iwe ya ajira, au uongozi, lakini tunasahau kuwa yupo ambaye anatujua sisi zaidi ya tunavyojijua.., je ukisema huo uwongo,labda…ndio ukafanikiwa unaijua kesho yako itakuwaje,..wangapi walipata, lakini hawakuweza kutumia, na wangapi walianza kutumia lakini hawakuweza kufaidi matunda yake…..Tufanyeni mambo tukijua kuna leo na kesho.



    Nikiwa bado hospitalini, akaja mume wa yule mama  aliyeibiwa, akanihoji, alinihoji kwa taratibu tu, na baadae akasema;CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ‘Mtafuteni huyo mdada, huyu hawezi kuwasaidia kitu, hamuoni,….huyu atawasaidia nini kumpata huyo mwizi, muwe mnaelewa,..mnapoteza muda kwa mtu huyu huyu, haya niambieni mumefikia wapi..?’ akawauliza watu wake wakamuelezea, halafu akasema.



    ‘Nataka huyo mdada apatikane, nawapa siku mbili tu..mkishindwa nitaifany amwenyewe…’akasema na kutoa amri kuwa niachwe huru. Hapo nikawa na amani, na baada ya amri hiyo, nilipona haraka kuliko ilivyotarajiwa…na siku napewa ruhusa ya kutoka hospitalini, akaja bint wa kule nilipokuwa nakaa kwa muda huo.



    Alikuwa kabeba begi la nguo, akaja hadi pale nilipokuwa nimesubiria dawa na baada ya hapo niondoke kurudi nyumbani, huyo mdada sijui alijuaje nitatoka, na hakuwahi kuja kuniona kabla, wengine walikuwa wakijitahidi kufika, sikumlaumu kwani nilishamfahamu tabia yake.



    Alipofika na kuniona nasubiria, akaniangalia kwa dharau, ni kawaida yake kuniangalia hivyo, utafikiri yeye ana kwake, au ana maisha yake ya hali ya juu,…yeye na wenzake wanaishi kwa wazazi,..sawa ni wazazi wake ana haki ya kuringa, lakini yeye kazidi, ananichukia sana,  na yeye ni mkubwa tu kuliko mimi , lakini hana mume, nasikia aliolewa akaachika.



    Akanisogelea na kusema;



    ‘Pole na kuumwa, najua umeshapona, vinginevyo utakuwa unadeka tu, …ili uendelewe kuletewa chakula,…’akasemaa



    ‘Ndio nimeshapona namshukuru mungu, na nimeruhusiwa nilikuwa nachukua dawa, nitafute usafiri…’nikasema.



    ‘Sawa endelea kumshukuru, na kumuomba sana, haya kabla hujatafuta usafiri,  …. hapa kuna barua yako kutoka kwa mama, si unajua kusoma wewe…eeh…’akasema akinishikisha mkononi, na mimi kwanza nikasita kuipokea, akanishikiza kwa nguvu, halafu akasema;



    ‘Isome mwenyewe,..maana mjumbe hana kosa au sio..haya soma mpendwa…’akasema huku anacheza mguu chini kwa nyoda na dharau, huku kashika kiuona,…huyu mdada ni katika mabinti wa pale, wanaonichukia sana, yeye tofauti kama wengine, wengine kidogo wana afadhali, lakini huyu kazidi kunichukia sijui kwanini;



    Nikasoma ile barua, iliandikwa hivi;



    ‘Sasa umepona, nimempigia simu docta wa hapo, sasa ni hivi, muda niliokubaliana na mume wangu wa kuishi kwangu umeshapita, sasa kwa wema kabisa, ninakushauri urudi kule ulipotokea, wao ndio walikutoa kijijini na kukuleta hapa mjini, sasa ni wao wajua jinsi gani utaishi,..kwangu sitaki kukuona tena, usije ukaniibia kama mwenzako alivyoiba huko, samahani kwa usumbufu, mimi mama …’



    ‘Sasa mimi nitaende wapi, jamani, si angenipa muda kidogo, ndio nimetoka hospitalini…oh, mbona mtihani huu...?’ nikamuuliza huyu mdada, akabenua mdomo kwa dharau na kuniangalia juu chini, halafu akageuka kuangalia mbele, na kusema;



    ‘Mimi isjui ndivyo nilivyoambiwa, unasikia, usije kunitolea machozi hapa, maana kulia kwako ni wimbo wa taifa, sasa ukalilie huko mbele , sio mbele yangu, ukanitia uchuro…. na begi lako la nguo hilo hapo…umeliona eeh,  mpendwa umesikia, …’akasema akigusa begani, baada ya kuniona nimeduwaa, na mimi sikusema kitu,



    Akatembea hatua moja mbili kama anazihesabu halafu akageuka na kusema , sasa kwa sauto ya kawaida, ili watu wamuone kama tunaagana kwa wema; Anajua kuigiza huyu binti,…kuna muda anaweza kuigiza mtu mwema, utamuona ni katika wema waliofuzu, lakini unayemfahamu tabia yake, hutatamani kukaa naye dakika mbili, …





    ‘Kama kuna kitu kingine kimebakia kule wewe niambie nitakuja kukuletea huko utakapokwenda kuishi…, sawa, pole sana, eeh, halafu nimesahau…’akarudi na kufungua pochi yake, akatoa pesa

    ‘Chukua hii pesa, itakusaidia kujikimu, hapa nimekata nauli yangu, usije kusema umepewa pungufu, unasikia, haya tukijaliwa tutaonana, kwaheri eeh mpendwa, usijali, maisha ndivyo yalivyo, …’akasema na kunikabidhi hizo pesa, na mimi nikawa nimeduwaa tu, hata sijui niende wapi, nilikaa pale hospitalini kama mgonjwa tena, na mdada huyo akaita bajaji na kuondoka zake.



    Nilikaa pale kwa muda mrefu, unajua ni kama mtu kafukuzwa nyumbani kwao, na hajui wapi kwingine pa kwenda, akili imeduwa, haijui hata ifikirie nini, …nikawa nawaza hili na lile, nikamuomba mungu kwa imani zangu zote anionyeshe njia, …mpaka sasa sijui nifanyeje…



    Baadae sana likapita gari, na mara likasimama, alikuwa ni yule mbaba, askari, ambaye ndio walioibiwa, akaniona bado nimekaa hapo hospitalini ndio akaniuliza mbona sijaondoka;



    ‘Mbona bado upo hapa, si nasikia umesharuhusiwa tatizo ni nini tena…?’ akauliza



    ‘Wamesema nisirudi kule tena, wanadai nitawaibia, na mimi sijawahi kuiba maisha mwangu,…na sasa hata sijui nitakwenda wapi..’nikasema huku machozi yakinilenga lenga.



    ‘Oh, sasa hilo ni tatizo jingine, na wewe huna ndugu yoyote hata mmoja hapa Dar…?’ akaniuliza



    ‘Sina, aliyenichukua toka kijijini ni yule mama wa kule, mwenye matatizo na mume wake,..naye hakutaka nikae kwake tena, hata sijui niende wapi tena ..’nikasema.



    ‘Sasa kwanini wanakufanyia hivyo, na hiyo mimba ni ya nani…?’ akaniuliza akinikagua tumbo langu.



    ‘Mimi sijui, ..’nikasema na yeye akaniangalia kwa macho ya mashaka, halafu akasema;



    ‘Wewe hujui,..mbona sikuelewi,…sasa unajua,…hebu ingia ndani ya gari, nikupeleke nyumbani kwangu, nitaongea na mke wangu, najua sasa hivi yupo na hasira sana, lakini tutaona tufanyeje, hawawezi kukufanyia hivyo sio utu…’akasema



    ‘Kwako tena, si ndio huko walipoiba, naogopa kukutana na mkeo, najua ana hasira za kuibiwa nay eye anahis labda nimeshirikiana na huyo mdada, kumbe mimi sijui lolote..’nikasema

    ‘Wewe twende tu…tutajua mbele kwa mbele…’akasema na nikaingia kwenye gar hadi nyumbani kwake.



    Nilipofika tu, aliyetufungulia mlango ni huyo mke wake, aaliponiona aliniangalia kwa uso uliojaa hasira, akageuka na kuingia ndani, hakusema neno. Mimi na begi langu la nguo, nikaingia na kukaa kwenye kiti, nikisubiria maongezi ya wawili hao,…hawa nao wana familia, lakini kwa muda huo watoto wapo shuleni, kwahiyo ndani kulikuwa kimia.



    Wawili hao wakaanza kuongea taratibu, mara sauti zikaanza kuongezeka, mara ikawa sasa ni mshike mshike mwanamke hakubali, na hasikii chochote anachoambiwa na mume wake,..



    ‘Kama umeamua kumleta huyu, haya ngoja mimi niwapishe, maana hata hiyo mimba mpaka sasa haijajulikana ni ya nani huenda ni yako….’akasema huyo mama



    Baadae sana, mume mtu akanijia na kusema;



    ‘Unajua sitaki matatizo, mke wangu ana shinikizo la damu, naogopa ukiendelea kukaa hapa, italeta shida nyingine, sasa ngoja kidogo,…akapiga simu kwa mtu, na akawa anaongea naye;



    ‘Kile chumba bado kipo, hakijapata mtu, eeh, safi kabisa, mimi kitanifaa, kuna binti, ..hana mume…eeh, hana matatizo, hilo nakuhakikishia, sawa, anakuja sasa hivi, hana mizigo yoyote ndio anaanza maisha, hivyo hivyo, ..usijali, tutaongea…’akakata simu



    ‘Oh, afadhali, …kuna chumba, sasa mimi nina rudi kazini,kuna kazi nyingi huko, lakini siwezi kukuacha hapa, mtaishia kubaya na mke wangu, wewe ingia kwenye gari twende…’akasema na mimi nikaingia kwenye gari, hao tukaondoka.



    Wakati tupo kwenye gari, akampigia yule mfadhili wangu wa kwanza, kuwa kapata chumba, na kinafaa mimi nikae huko, wanasema kuhusu kusaidia kulipia kodi, na jinsi gani ya kuishi…



    Mfadhili wangu wa awali, akasema hawataki hata kuniona kwani hivi sasa wanapambana na maisha magumu, yeye alifika nikiwa hospitalini akanieleza kila kitu, na hivi sasa mume wake amekuwa kama kachanganyikiwa, mtoto naye kagundulikana ana matatizo makubwa, kwa hivi  hawezi kubeba mzigo mwingine, keshachoka.



    ‘Oh, mbona inawia ngumu, sawa kwa vile nipo naye nitaona jinsi gani ya kufanya, ila msisahau kuwa nyie ndio mlimchukua huko kijijini, tukifuatilia sheria mnaweza kuwa matatani, unielewe,…hamna shida, mimi nitajitahidi kadri niwezavyo,…hamna shida, sawa shemeji, poleni sana…’akasema na kukata simuCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Tukafika kwenye hiyo nyumba, ilikuwa nyumba ya kawaida tu, ila kuna vyumba vya uwani, vya kawaida tu, na akaongea na mama mmoja, ..huyu mama ndio mwenye nyumba, akaniangalia halafu akasema;



    ‘Sawa mimi sina shida, wanawake ni wazuri maana sitakwua na shida ya usafi, ila sitaki mlevi humu au Malaya, tutakosana…’akasema na kutembea kuelekea kwenye hicho chumba, ..



    ‘Chumba ndio hiki,…unakiona kilivyo, hakina tatizo, …ukitumie na ukiache kama kilivyo, sawa, nimekupa hiki chumba kwasababu ya huyu mtu, kanisaidia sana, …fadhila zake ndizo zimenifanya nikubali, ila kodi sasa itakuwaje…?’ akauliza akimuangalia huyo mbaba.



    ‘Kwanza nitakulipa kodi ya mwezi huu..shilingi ngapi….’akasema akifungua pochi lake, akatia pesa, na huyo mama akazipokea na kuanza kuzihesabu, na kusema;



    ‘Oh, sasa hii si kodi ya mwezi mmoja tu, sio makubaliano yetu  hayo…’akalalamika



    ‘Wewe si unanifahamu, nyingine zitakuja, usijali, ngoja nifike kazini, huyu sasa ni mtu wako, …unanisikia mengine tutaongea…’akasema na kuanza kuondoka, niliogopa hata kumuuliza nitaishije…



    Na mar akarudi tena, sasa akiwa na mifuko mwili na hisi ni ya kilo tano tano, mmoja una unga mwingine mchele, na…mafuta kwenye chupa,……halafu akatoa pesa mfukoni akanikabidhi na kusema;.



    ‘Sasa mimi nimejitahidi hadi hapa,…sikulitegemea hili, cha kushuru ni kuwa sasa.umepata chumba, nimelipia mwezi mmoja, unasikia, utalala vipi, hilo siwezi kuliwazia kwa sasa, tumetoka kuibiwa, si unalewa hasara tuliyoipta, sasa mimi nakucha,…’akasema

    ‘Ahsante nashukuru sana kwa wema wako…’nikasema

    ‘Muhimu kwa hivi sasa,  kama una jamaa unaowafahamu basi watakusaidia zaidi…na, kwa miezi mingine..nitaona jinsi gani ya kufanya, tatizo wewe una mimba,..ok, hilo utajua mwenyewe, sizani kama unaweza kupewa mimba usijue ni ya nani, kwani ulibakwa…?’ akaniuliza



    ‘Hapana, sijabakwa…’nikasema.



    ‘Ulipenda mwenyewe…?’ akauliza.



    ‘Nimekuambia mimi hata sijui mimba imetoka wapi,…hakuwahi kukuelezea mama…maana wao wanajua…’nikasema.



    ‘Hapana, huwa hatoongelei mambo ya watu, mimi na mke wangu, huwa nina sheria zangu, anyway, hilo utajua wewe mwenyewe…’akasema, na kugeuka kuondoka, halafu akageuka tena na kuniuliza.



    ‘Ina maana wewe kweli huna rafiki yoyote wa kiume…?’ akaniuliza akinikagua tumbo.



    ‘Mimi sina tabia hiyo, sina kabisa rafiki wa kiume…’nikasema



    ‘Haya tutaona….basi nitaona jinsi gani ya kukusaidia, ila…usije kusema kwa mke wangu kuwa ni mimi nimekusaidia hadi hapa unasikia,…au kwa yoyote yule, sawa…nitakuja nikipata muda, ila sikuahidi unielewe,…zaidi nitakuwa nawasiliana na huyo mama mwenye nyumba wako, huyo mama ni mtu mwema sana, ananifahamu sana…’akasema na kunitupia jicho….nilihisi namna ya mashaka, wanaume hawaaminiki, lakini nikamuomba mungu apitishie mbali.



    Basi nikachukua vile vitu na kuingie kwenye chumba hakina kitu chochote …zaidi naona kulikuwa na jiko la mchina, na sufuria moja, sijui ni vya nani, nikasema moyoni, hivyo ndio vya kuanzia maisha.



    Huyu mbaba akaondoka na gari lake, nikabakia humo kwenye chumba, kitupu, nikahesabu pesa nilizopewa na huyo mbaba na zile za yule mdada aliyekuja hospitalini, nikaona nitaweza kuishi siku mbili tatu, lakini sasa humo nitalalaje, hakuna godoro,..ila shuka ninayo,…nikafungua lile begi, nikakuta shuka, na khanga zangu, …sio haba, nitaishi.



     Hapo, nikakaa chini kwanza, nikiwaza….na mara moja nikayakumbukia maisha yangu na mama, yalikuwa ya dhiki hivi hivi, lakini tulikuwa na kitanda, hapo machozi yakaanza kunitoka na haikupita muda nikashikwa na usingizi, na mara mama akanitokea



    ‘Mwanagu, usikate tamaa, unakumbuka usia wangu,…usiogope kusema ukweli hata kama utakuumiza wewe au huyo unayemuambia huo ukweli..ukweli uwe ndio silaha yako..na pia usimuamini kila mtu, sio kila akuchekeaye ana nia njema na wewe, cheka naye, lakini akili kichwani mwako, jingine nilikuambia, uwe mbali na wanaume, na usipende kupokea misaada yao, kwani kila wakitoacho kina namna ya ghiliba,..



    Muhimu mwanangu, ishi ukimtegemea mungu wako, kwani kila alilokujalia nalo lina maana yake, usijione upo mpweke, mungu wako yupo nawe kila mahali,usichoke kumuomba...na kumbuka jambo moja,sasa ndio maisha yako yameanza,..subira yako ndiyo itakufikisha kwenye mafanikio,…kamwe usikate tamaa..



    ‘Sasa mama na hizi pesa za huyu mbaba, na vile vitu alivyoninunulia nivirudishe kwake..?’ nikauliza na mara nikazindukana.



     Nikasikia mtu anagonga mlango, nikaitikia karibu,



    ‘Kuna mgeni wako huko nje…’nikasikia yule mama akiniambia, lakini sauti ya mashaka



    ‘Haya nakuja…’nikasema hata sijui ni nani kaja kunitembelea ambaye anajua nimehamia hapo..,



    *****************



     Alikuwa ni yule mama aliyeibiwa, sikumkaribisha ndani, na yeye hakuonekana kutaka kukaa, akasema



    ‘Ndio sehemu mume wangu kakuleta huku, eeh...mume wangu ni wajabu sana, ..hahaha....kwahiyo kakuleta huku muwe mnakutania mara kwa mara nilijua tu kuna kitu kati yako wewe na mume wangu, au sio..?’ akaniuliza.



    ‘Mama , mbona unanishutumu kitu ambacho mimi sikijui, yeye, kanileta huku, wala sijui…’nikasema na yeye akanionyeshea mkono wa kuwa hataki kunisiliza.



    ‘Ila mimi nakuonya tu, nitakuwa nakufuatilia hatua kwa hatua siku nikimkuta mume wangu hapa, mpo naye…utanitambua mimi ni nani…umenisikia, labda mtafute sehemu nyingine, nisiwagundue, lakini nitawafikia tu, siku hiyo ndio hasira zangu zote zitaishia kwako…’akasema na kugeuka kuondoka.



    Na alipoondoka yule mama mwenye nyumba akaja na kuniuliza



    ‘Huyu kajuaje kuwa upo hapa, maana mume wake hakutaka kabisa mkewe ajua kuwa upo hapa, ooh, sasa naona nyie watu mnataka kuniletea balaa kwenye nyumba yangu, kama ni hivyo tutashindwana..’akasema.



    ‘Lakini mama mimi sijui chochote,  hata huyo mume wake kanichukua hospitalini na kunileta hapa, sikujua kama ana lengo lolote baya…’akasema.



    'Lengo lolote baya, kwani hujui kwanini kakuleta hapa...hahaha wajifanya huelewi eeh,,,,'akasema



    'Mimi ninachojua ni usamaria wake mwema tu ...'nikasema



    ‘Kwahiyo wewe na yeye, hamjaelewana chochote kuwa ukae hapa kwa vipi ...?' akaniuliza.



    ‘Kuelewana kwa vipi mama, ..?’ nikauliza.



    ‘Kwani hiyo mimba sio yakwake..?’ akaniuliza



    ‘Hapana..’nikasema bila kuongeza maneno na huyo mama akanikagua kwa macho halafu akasema;



    ‘Ya nani sasa, binti,..hala hala… usije ukawa na matatizo, sitaki matatizo kwenye nyumba yangu, namuheshimu tu huyo askari, kwasababu kanisaidia mambo mengi, vinginevyo nisingelikukubalia wewe, kwasababu huna kazi, je utanilipaje, nikajua huyo askari ni mwenza wako, kumbe tena, huna mahusiano naye,..oh, ngoja nitaongea naye…’akasema



    ‘Mama , kwangu usiwe na wasiwasi sina matatizo na mtu yoyote…, sina tabia mbaya kamwe haya yaliyonikuta ni mitihani tu ya mungu, na wala sijui hata hii mimba imeiingiaje,...’nikasema



    ‘Imeingiaje, kwani mimba zinaiingiaje, usinichekeshe binti, mimi ni mtu mnzima usinifanye mtoto mdogo, ina maana labda ulibakwa au..?’ akaniuliza



    ‘Yaani mama mimi sijui...hata sijui nikueleze vipi unielewe…’nikasema.



    ‘Sawa mimi sina tatizo, ila masharti yangu ni hayo, kukitokea tatizo lolote, wanaume kuja kugombana huku au wake zao kuja kuleta zogo humu, unaondoka,…sawa…’akasema na kuondoka.



    ****************



    Kumbe huyo mama alikuwa na biashara zake , alikuwa anatengeza chapati na kuuza chai, na mara nyingine mama ntilie, na sijui ni kwanini anasema huyo askari alimuokoa hadi biashara zake bado zipo…sikupata muda wa kumdadisi saa maana muda mwingi, alikuwa kwenye shughuli zake na wateja wake.



    Siku iliyofuata nilifika kwa huyi mama anapofanyia shughuli zake nikamuomba nimsaidie atanilipa chochote, atakachoweza na nikashangaa, akanikubalia tu.



    Halafu siku hiyo ikawa ni kama bahati, kukawa na wateja wengi, kiasi kwamba hata huyo mama alishangaa, ikabidi aagize vitu vingine vya kupika na kupika mara mbili, isivyo kawaida yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    'Haijawahi kutokea, yaonekana wewe umekuja na bahati, kesho uje tena…wewe naona unanifaa…’akasema na mimi nikamkubalia kwa furaha nikijua sasa nimepata sehemu ya kujishikiza.



     Basi ikawa hivyo, namfanyia kazi zake, ikifika usiku ananilipa ujira wangu, wiki ikapita, na kila nikienda dukani kununua vitu, naomba maboksi, na mifuko fuko, na hiyo nikatengeneza kitanda, siku zikaenda, maisha yakasonga mbele…



     Kila siku ilikuja na neema zake, nikaja kupata kitanda kilikuwa kinatupwa, nikakiomba, nikampelekea fundi, akanitengenezea vizur tu, huku naendelea kusaidiana na yule mama katika shughuli zake za biashara, akanipenda sana, wateja wakawa wanamiminika…



    Pamoja na hayo yote, tumbo lilikuwa linanisumbua sana, ilikuwa mtoto tumboni hatulii, na zile dalili za kukanguliwa zikawa ndio zinazidi, lakini mimi sikujali vile vitisho kuwa ni dalili za kuwa mtoto huyo atakayezaliwa atakuwa si mtoto wa kawaida, atakuwa na dalili za shetani.



    'Kama nitazaa mtoto mwenye sijui tabia za shetani, basi hata yeye ni kiumbe cha mungu, yeye aliyekiumba atajua jinsi gani ataishi,..ila nakuomba ewe mola wangu, mimi nikiumbe chako dhaifu, nakuomba sana ewe mola wangu nisaidie niyashinde haya majaribu maana mimi sikuomba hili linitokee…’nikawa kila nikiwaza au kutokea na maumivu hayo namuomba mungu wangu hivyo.



     Siku moja nikawa naumwa sana tumbo, yule mama akaniambia nipumzike tu, yeye ataendelea na malipo yatakuwa kama kawaida, basi ikawa hakuna jinsi,lakini sikutaka kwenda kulala kule ndani kwangu, nikatafuta sehemu hapo hapo huyo mama anapofanyia kazi, nikajiliza, sio mbali na hapo, na sehemu  huyo mama anapofanyia shughuli zake. Nilitaka nikijisikia vizuri nimsaidia hata kusoha vyombo.



     Wakati nipo hapo, hali ikazidi kuwa mbaya sana, na wakati napambana na maumivu mara nikasikia huyo mama akiongea na mteja mmoja, cha ajabu niliweza kusikia kwa mbali wanvyoongea, lakini sikuweza hata kujiinua, mwili wote ulikuwa umeishiwa nguvu,  mwili umelegea kabisa siwezi hata kuinua mkono au kutoa sauti, nikawa nasikia maongezi yao, kama ndoto vile, kwa mbali kweli…



    'Mimi nimetokea huko kijijin kwetu nilikuja kutafuta wafadhili, wa ujenzi wa nyumba ya ibada…..’nikasikia hivyo, lakini mengine sikuyasikia,…baadae nikasikia, huyo mama akimuuliza huyo mteja..



    'Ina maana hakuwahi kuwa na mtoto….’sauti ikakatika, na nikajihisi sasa kama napoteza fahamu kabisa, natamani nipige ukelele lakini sikuweza hata kufunua mdomo.



    'Alikuwa naye…., tumemtafuta hapatikani, nasikia, alikuja….  Tujenge…ibada, na kama…..’nikawa nasikia vipande vipande wanavyoongea, mengine sikuyasikia, na sikuweza hata kutafakari, walikuwa wakiongea nini…ila mwishoni nikasikia, hivi;



    'Je akitokea na ikawa yeye hataki hilo jengo, anataka kujenga nyumba yake ya kuishi mtafanya nini…?’ ilikuwa sauti ya huyo mama,  hapo nikasikia vyema, na sauti ya kiume ikasema;



    'Tutamtafutia…….’hapo sauti ikakata,…sasa hapo ndio hali ikawa mbaya kabisa, na nikahisi kupoteza kumbukumbu masikio yakawa hayasikii tena, nikazama kwenye giza na kupoteza fahamu.



     Kumbe kwa bahati nzuri, walivyoniambia baadae, alipita mmoja wa wateja eneo hilo, sijui alikuwa anatafuta nini, ndio, akaniona, akatoa taarifa kwa huyo mama, na walichofanya hapo siwezi kujua, ila walikuja kuniambia walinibeba na kunitoa nje ili nipate hewa, lakini haikusaidia, wakahisi nimekufa,..ila wakajadiliana kuwa nipelekwe hopsitalini.



     Kwa tukio hilo nililazwa karibu wiki, na baadae nikatoka na nilipotoka, nikarudi kwenye chumba changu, na yule mama akawa sasa ndiye ndugu yangu wa karibu…., na tukaanza kuzoeana kiukweli, hata ikafikia hatua nikaanza kumuhadithia baadhi ya maisha yangu, alisikitika sana, mengi ya huko nilipofikia na yaliyotokea kwa hao akina mama, sikumuhadithi, nilimuhadithia, ya nyumbani nilipotokea na kupata taarifa ya kuwa mama kafariki kwa kuchomewa nyumba moto..



    'Wewe, unajua kuna mzee mmoja,..tena siku ile ulipozidiwa ndio alikuja akawa ananihadithia,…umesema kijiji gani, ..ndio huko huko, ..yeye alikuja hapa na karatasi anachangisha pesa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya ibada, nimemzoea tu, kila akifika safari zake za kutoka kijijini anapitia hapa sio mara ya kwanza kuoana naye, lakini hatuna udugu naye kabisa….



    'Sasa nitampataje huyo mzee…?’ nikamuuliza nikiwa na hamasa fulani, japokuwa sikupenda kabisa kurudi huko, lakini kwa vile wametaja eneo, nikawa nimekumbuka eneo la mama, hata hivyo sikuwa na tamaa nalo maana hata kuchomewa nyumba na visasi vinawezekana ni kutokana na eneo hilo.



    'Aliacha karatasi ya kuchangisha watu kwa ajili ya ujenzi wa hiyo nyumba ya ibada, mimi sikutilia maanani, sikjui kama ipo ngoja tukimaliza kazi nitaitafuta, kama ipo au nimefungua wateja vitafunio,…’akasema na tukaendelea na shughuli zetu, tukasahau, siku pili, hata hatukukubuka kuliongelea, ila siku ya tatu, akaja na hiyo karatasi.



    Kweli kwenye ile karatasi kulikuwa na namba ya simu, anasema alimpigia na akamwambia na yeye alikuwa na mipango ya kuja huku dar, wiki ijayo, basi tukasema tusubirie….



     Nikawa namsaidia huyo mama napata ujira wangu, japo kidogo sio haba, na humo humo, nikaanzisha mradi mwingine wa uji, kidogo kidogo nikaanza kuwekeza, nikanunua godoro la bei ndogo, ili nikifungua nipate pa kulala na huyo mtoto nitakayejifungua mungu akipenda.



     Siku moja akaja mbaba mmoja kafuga madevu, alionekana kama kachanganyikiwa vile, akaagiza chain a vitafunioa, na uji,…vitu alivyoagiza, tuliingiwa na wasiwasi huenda asilipe, lakini cha ajabu akaomba apigiwe mahesabu yake, na alipotajiwa ni kiasi gani akalipa, na kuanza kula, taratibu hana haraka.



    Na muda wote alikuwa kainamia vitu vya kula, hakuwa akimuangalia mtu…sasa alipomaliza, akajifuta mdomo na midevu yake, akasimama akitaka kuondoka, ndio akaweza kuniangalia mimi,..muda alikuwa kashika gilasi ya maji, aliomba maji ya kunywa na mimi ndiye nilimpelekea,  aliponiona akashtuka, na kudondosha ile gilasi ya maji ikavunjika…



    ‘Vipi mzee mbona wanivunjia vyombo vyangu…’mama akamuuliza na jamaa akasema.





    'Samahani mama Ntilie, na..na...nataka kuongea na huyu binti....tafadhali...' akasema





    'Wa nini...kuongea naye nini...?' akaulizwa na kabla hajajibiwa akaanza kulia, kulia kweli kweli, na alipotulia akanisogelea na kunipigia magoti....watu kimia, kila mmoja anajiuliza hili na lile kichwani, kunani kwa huyu mzee ambaye anaonekana kama kachanganyikiwa!





    NB: Je ni nani huyu.





    WAZO LA LEO; Sio kila baya lina ubaya, mabaya mengine yanatokea kwa minajili ya kuleta neema fulani ambayo sisi kama wanadamu hatuwezi kuifahamu kwa hapo hapo, na sio kile jema lina wema wote, wema mwingine unaweza ukawa mtego wa kukupeleka kubya, kwahiyo, kila jambo likitokea, shukuru na mkabidhi mola wako, kwani yeye ndiye anajua zaidi.





    Yule mzee aliagiza vitu vingi akawa anakula huku kainama, hakutaka kuinua kichwa, labda hakutaka watu wamuone, na alipomaliza, akaagiza maji ya kunwa, na mimi nakuchukua maji na gilasi nikafika mezani nikamumiminia na kumpa , akaipokea na alipotana kunywa akainua uso akaniangalia,..na mimi muda huo nimesimama mbele yake ili kama anataka maji mengine nimuongezee kwenye gilasi aliyokuwa kaishika!



    Aliponitupia jicho, na macho yake kukutana na yangu, akashtuka, …na ulikuwa mshtuko kweli, sio ule mshituko wa kujificha, mpaka gilasi ya maji aliyokuwa kaishikilia, ikamponyoka, na kudondoka sakafuni ikavunjika, na kila mtu akasikia mlio wa hiyo gilasi ikivunjika, na mama mwenye mgahawa akasema kwa hasira…



    ‘Vipi wewe mzee leo, mbona unavunja vyombo vyangu…’akasema akimuangalia kwa mashaka, na yule jamaa alikuwa bado kaduwaa, akiniangalia mimi..

    Haikutosha akaanza kulia na kusimama, akatoke kwenye meza na kunisogelea, akapiga magoti mbele yangu huku akisema

    ‘Samahani nisamehe…..’ huku akiwa kashikilia miguu yangu, ili nisiondoke…

    Tuendelee na kisa chetu



    ***********



    Kila mtu pale alishikwa na butwaa, ni kwanini huyo mbaba mtu mzima, japokuwa kwa uvaaji wake na jinsi anavyoonekana, alikuwa akionekana kama kachanganyikiwa,, manywele yamevurugika , madevu kayaachia, ya yenyewe yamevurugika, kwa ujumla hakuonekana katika hali ya kawaida, hasa kwa umri kama wake,…CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Sasa analia na haitoshi, anakuja kunipigia magoti, kila mtu alihisi sio bure, yawezekana kukawa jambo kati yangu na huyo mbaba. Lakini kiukweli mimi nilikuwa simfahamu huyo mbaba, na sikumbuki kabisa kukutana na mtu kama huyo kwangu alikuwa mgeni kabisa.



     Yule mama, maana ndio alishakuwa mlezi wangu japokuwa,namlipa kodi, ananilipa mshahara wangu wa kila siku, lakini alishachukua dhamana ya kuwa mimi ni sawa na binti yake, sasa alipoona kile kitendo cha huyo mbaba, haraka  akasimama na kumkabili huyo mzee, lakini alishachelewa huyo mbaba alishapiga magoti, mbele yangu na kunishika miguuni…nilikuwa nimevaa dera refu sana,ikizingatia hali yangu.



    Pale nilipo nilikuwa najisikia vibaya, natamani hata kutapika, moyo ukawa unanienda mbio,...nilitamani aniachie nisije kumdondokea, lakini kila nikijaribu kuinua mgu siwezi jamaa kanishikilia bara bara..



    'Vipi wewe mzee unataka nini  kwa huyu bint yangu, si ameshakupa maji ya kunywa, unataka nini zaidi?...’akamuuliza.



    Jamaa ni kama hasikii akawa kanishikilia na kulaza kichwa cheke miguuni mwangu huku akiinua uso kuniangalia, uso wa huruma huku machozi yakimtoka, mimi nikawa hata sielewe huyo mbaba ana nini kwangu

    Kwa kitendo kile sikuweza kusogeza mguu, maana kanishikilia, nikisogeza mguu nitandondoka, na huku nimeshikilia jagi la maji.



    ‘Wewe mzee vipi, unataka nini, unajua unamfanya binti yangu ashindwe kuwajibika, hii sasa unatuletea vurugu kazini, na tutakuitia polisi…’akaambiwa



    'Ninataka anisamehe…..ndio nitamuachia hu-huu mguu…’akasema



    ‘Akusamehe kwa lipi kwani umemfanyia nini kibaya…?’ mama akamuuliza



    ‘Mi-mi..na-na taka  niongee na ye-ye,  ili aweze kunisamehe..ta-fa-dhali mama ‘n-ti-ti-lie…’akasema sasa akijaribu kugeuza kichwa kumuangalia huyo mama.



    Huyo mama kwanza akanitupia jicho, na halafu kuwatupia macho wateja wake, akainua mkono kuwaashiria wateja kuwa huyo mzee kachanganyikiwa wasimjali.



    'Unasema, akusamehe, kwani ulimkosea nini, muachie awahudumia wateja…unatupotezea muda, hujui ni hasara kwetu…’akaambiwa



    ‘Nitawalipia hiyo hasara lakini ..na-na taka kuongea na –na , na huyu binti,…kwangu ni-ni muhimu , sa-sa-sana…’akasema



    ‘Hapana muachie kwanza,…’yule mama kajaribu kumuondoa huyo jamaa kwenye miguu yangu, lakini alikuwa kashikilia bara bara, na sasa mama akashikwa na mshangao, akajua sasa mzee mzima kazamiria



    ‘Sema sasa kakukosea nini..mtu atakusameheje wakati hakufahamu, na hafahamu kosa lake ni nini..?’ kaulizwa



    'Yeye  mwenyewe anajua,….ndio maana nataka anisamehe,….’akasema akizidi kunishikilia miguuni.



    'Wewe mzee mimi sikujui, na sijawahi kukuona hata siku moja, niachie nifanye kazi …’nikalalamika,



     .

    'Nitakuachia lakini mpaka,ukubali kuwa utanisamehe…..’akasema



    'Nikusamehe nini sasa, kwani ulinikosea nini, mimi sikujui na sijui kosa ulilonifanyia, haya niachie uniambie kosa langu, …’nikasema.



    'Ina maana umenisahau mimi…, mungu wangu sasa hili ni balaa, ..'akasema sasa akazidi kunishikilia, huku analia



    ‘Nisamehe, nisamehe….’akawa anasema hivyo hivyo tu.



     Ikawa sasa ni vurugu, maana wateja wanataka huduma, mzee hataki kuniachia, kang'ang'ania miguu yangu, ikabidi sasa wateja waingilie kati na kumuondoa huyo mzee kwa nguvu, na kitendo hicho kilinifanya mimi niwe kwenye wakati mgumu.



     Lakini wateja walikuwa na nguvu, wakatumia nguvu na kumuondoa miguuni mwangu baada ya kumgonga gonga kidogo mabegani, na juu kwa juu wakambeba na kumtoa nje…na aliponiachilia nikakimbilia sehemu ya haja na kutapika, na nikasubiria mpaka hali ikawa njema ndio nikarudi ndani.



    Nilipofika nikakuta wameshamtoa nje...



    Na hata baada kumtoa nje, bado akawa  analia , kama anavyolia mtoto mdogo…, na kuomba watu wasimfanyie hivyo, maana bila ya mimi kumsamehe akifa ataenda kuangamia..kauli hiyo ikawashtua wengi, na ukazudka mjadala ni kwanini huyo mzee akatoa maneno makali kama hayo. Wengine wakazua visa vya watu kama hao na wakadai maneno mengine ya watu kama hao, yana ukweli ndani yake.



    'Niacheni, nataka nimuombe msamaha, nimemkosea sana  siwezi kuondoka hapa mpaka nipate nafasi ya kuongea naye ili aweze kunisamehe….’akazidi kusisitiza.



     'Basi sikiliza mzee, muache huyo binti afanye kazi yake..unajua hapo yupo kazini,..akishamaliza kazi yake ndio mtaongea naye akujue wewe ni nani na ulimkosea nini, si sawa mzee…’akaambiwa na akazidi kusema.



     'Jaman mnajua ya kesho nyie,…bahati haiji mara mbili, je nikifa kabla hajanisamehe mnataka mimi nikaangamie…’akasema.



    'Mungu atakujalia hutakufa mzee, je usingelimuona leo, mpaka hapo mwenyezimungu keshafahamu dhamira yako njema na ukizidi kumsumbua sasa itakuwa sio busara, utashikwa na kupelekwa milembe, unakufahamu milembe wewe..?’ akauliza

    ‘Mimi sio kichaa, kwanini wanipeleke Milembe, hamjui mimi nina matatizo gani, ….hamjui mimi na huyo binti tuna mahusiano gani, …je kama mimi ni baba yake..’akasema na watu hapo wakasema.



    ‘Aaah, kumbe, ..lakini hata hivyo mzee, subiria kwanza…’akaambiwa.



    ‘’Huyo sio baba yangu, baba yangu alishafariki…’nikasema kujitetea, na watu wakaniambia ninyamaze, kwani nikiongea nitamzidishia ukichaa huyo mzee.



    ***************



     Mzee akakaa hapo nje huku akilia akawa anaimba kama mtoto mdogo,…



    ‘Nisamehe , nisamehe, binti yangu,…nakuomba unisamehe binti yangu…’ basi akalia wewe mpaka akachoka, akawa kimia, tukajua labda kaondoka, watu wanachungulia nje wanamkuta kakaa hapo mlangoni, na kila anayetoka anamkagua kwa macho, na akiona kimia, anatulia huku akiwa kashikilia kichwa ile ya huruma.



     Baadae watu wachache waliokuwa wamebakia wakaanza kumuhoji mama mama mwenye mgahawa



    'Huyu mtu ni nani…mbona hatujawahi kumuona..?’ akaulizwa



    'Hata mimi simfahamu vyema, nimeanza kumfahamu hivi karibuni tu, alianza kuja, kunywa chai hapa, na awali nikajua hataweza kunilipa, kutokana na jinsi alivyo, yupo kama kachanganyikiwa, kama mnavyomuona hivyo, aheri leo ni msafi kidogo, siku nyingine utamkuta varu varu…lakini cha ajabu, akimaliza kula ni lazima alipe, sijui paesa anazipatia wapi,…’basi akatulia kidogo akikanda chapati zake.



    Basi mimi nikamzoea, na kuanza kumtania kuwa yeye ni mume wangu,…wewe,..hapendi kutaniwa hivyo….’akasema



    'Ukimuita hivyo anasemaje…?’ akaulizwa



    'Hapendi, hapendi kutaniwa hivyo, yeye anasema ana mke wake mnzur, hahitaji mke mwingine, mke wake ni mnzuri sana anampenda yeye tu….’akasema



    ‘Hukumuuliza huyo mke wake ni nani na yupo wapi..?’ akaulizwa



    ‘Ukimuuliza hivyo anasema , nisimuingilie maisha yake, mke wake hataki kusemwa kwa watu, maana akijua yeye ni mume wake atajisikia vibaya, kwahiyo nisimuulize zaidi kuhusu mke wake…’akasema huyo mama.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    'Hujamuuliza anaishi wapi, …maana hapo watu wakimuuliza anasema tu, mwambieni anisemehe,..mwambieni anisamehe, imekuwa kama wimbo….?’ Akaulizwa mama



    'Nilimuuliza hilo swali akasema yeye anaishi duniani, potepote pale hapa duniani  ni nyumbani kwake, …’akasema huyo mama.



    ‘Sasa hapo ni mtihani, lakini …sio bure…’wakasema wateja.



    'Huyo kachanganyikiwa, watu kama hao, kuchanganyikiwa kwao, inawezekana alikosana na mke wake, au maswala ya ajira na maisha yakamuwia magumu, akawaza sana mpaka akachanganyikiwa,..ninachojiuliza pesa anapatia wapi, labda akitoka hapa anakuwa omba omba…’akasema huyo mama.



    'Yawezekana huyo binti yako anamfahamu, tuambie bintim, usikatae kwa vile yupo hivyo, kama ni mzazi wako sema, au kama alikufanyia,…maana wengine huwashika wanawake kwa nguvu..’wateja wakanigeukia mimi kwa maswali.



    ‘Ukweli wa mungu, mimi simfahamu huyo mtu, ni mara yangu ya kwanza kuonana naye..huyo kachanganyikiwa tu, au ananifananisha…’nikajitetea.



    'Unajua leo naona mwezi mpya, maana siku zote anakuja hapa anakunywa chai yake na kuondoka, harudi tena mpaka kesho yake,…’akasema



    ‘Sasa leo mnaye mpaka kieleweke…’akasema mteja mmoja



    ‘Tutamuitia polisi…’akasema mama



    ‘Hapana msifanye hivyo, hebu msikilizeni kwanza, huenda akawa na jambo muhimu kwenu, msimzarau tu , kwa vile anaonekana kachanganyikiwa…’wakashauriwa hivyo.



    'Au ndio yeye kampa mimba huyo bint yako, hataki tu kusema ukweli…’mteja mwingine akaropoka



    'Hapana huyu binti yangu hajapewa ujauzito na huyo mzee, nyie hamuoni huyo mzee na binti mdogo kaam huyu wapi na wapi…’akasema huyo mama.



    'Sasa mtuambie mama, bint yako kapewa mimba na nani, maana hilo swali kila siku tunaulizana, tukikuuliza huyo binti kaolewa unasema bado anayetaka alete posa, sasa utaoaje mke na mimb ya watu…’akasema jamaa mwingine.



    'Wewe kama umpenda lete posa, ukipenda boga penda na majani yake, vyote ni vyakula tu, mtoto akikua anaweza kukufaa wewe kuliko huyo wa kumzaa wewe mwenyewe..’akasema huyo mama

    ‘Haya mama Ntilia, ngoja tusubiria hatima ya huyo jamaa, ila msimfukuze mpaka atimize lengo lake, ikibid binti amkubalia tu, kuwa kamsamehe, si inatosha,…’akasema



    ‘Siwezi kukubali tu bila kujua kanikosea nini..’nikadakia mimi niliposikia kauli hiyo.



    ‘Mimi nitakuambia mwenyewe mimi ni nani na kwanini nakuomba unisamehe..tafadhali naomba nipe nafasi niongee, lakini ningeliomba iwe faragha maana yaliyotokea sio vyema kila mtu akayasikia, tafadhali, msinione nipo hivi, lakini wakati mwingine ninakuwa na akili yangu timamu..nawaombeni sana waungwana mnielewe, sitaki kufanya  vurugu….’jamaa akasema sasa akwia kasimama mlangoni.



    Mimi pale milipo, kila nikimuangalia mtu huyu nahisi vibaya, sijui ni kwanini, nahisi kama kutapika, moyo unanienda mbio, lakini alipokuja safari hii hiyo hali ikawa imetulia.







    NB: Jamaa anataka kufunguka, ni nani huyu







    WAZO LA LEO: Pindi kukitokea uhasama kati ya pande mbili, lililo jema ni kuwakutanisha wahusika hasimu ili wao waweze kujieleza na kujitetea wakiwa na msuluhishi kati yao, msuluhisi ambaye hana masilahi na uhasama huo. Ni vabaya sana nyie watu wa pembeni kuhukumu bila ukweli kuwa bayana, nyie wapambe mnaweza mkaja kuhukumiwa siku ya mwisho kwa kupandikiza chuki na fitina, pindi mabaya zaidi yakitokea kati ya wahasimu hao. Kumbukeni fitina ni mbaya sana zaidi ya uchawi.

    Baada ya majadiliano kidogo, mama akaona nipewe nafasi hiyo, mimi nikae faragha na huyo mzee, lakini sehemu ambayo naweza kuonekana ili kama akileta vurugu niweze kusaidiwa, Nilimuangalia yule mzee, , kwasasa akawa anaona aibu hata kuniangalia, sio kama ile awali, ni kama kabadilia, na kule kuona aibu hataki kuniangalia moja kwa moja usoni, kukanifanya nishindwe kumtambua vyema.



    ‘Haya wewe unaweza kuwepo , maana kwa hivi sasa huyu ni binti yako, au sio, sitaki nikae naye faragha tukiwa wawili tu, walimwengu ni wengi wa kuzusha, naogopa sana kwa sasa…” akasema huyo jamaa sasa akiongea vyema sio kama ilivyokuwa awali, ni kama vile mtu anaigiza, kuongea kwake kwasasa sio kama awali alivyokuja akia kama kachanganyikiwa, kama isingelikuwa hayo mavazi na muonekano wake, usingemfikiria vibaya.



    ‘Sawa lakini unaona bado tuna kazi za usafi, maana sisi, siku nzima huwa ni kazi tu, na kazi zetu usafi ni kitu muhimu sana, na wewe sasa unatukwamisha, tumekuheshimu tu kwa vile wewe ni mteja wetu mnzuri…’akasema mama.



    ‘Mimi nitawalipa siku hii nzima, nipo tayari kwa hilo, nipigieni hesabu zenu,…., msijali, hamuwezi kupata hasara kwasababu yangu, najua haya ni kwa masilahi yangu…samahanini sana..’akasema akashika kifuani.



    ‘Pesa utapatia wapi wewe mzee,  au unaomba omba mitaani..?’ huyo mama akamuuliza kwa utani na huyo mzee, hakukasirika akasema kwa uzuri tu



    ‘Pesa sio shida kwangu mama Ntilie,…usinione hivi…’akasema akijikagua huku akitikisa kichwa kwa kusikitika.



    ‘Ukisikia historia yangu utanionea huruma,…hadi nimefikia hii leo naweza kuongea na wewe hivi, namshukuru sana mungu na wanaonifahamu wakiniona hivi naongea na wewe hivi hawataweza kuamini..unajua huko nilipotoka niliondoka siku nyingi hawajui wapi nilipo…’akasema



    ‘Wapi umetokea…?’ akaulizwa



    ‘Huko kwa mke wangu…nilitoka siku moja saa kumi alfajiri nikapotea, hawajui wapi nilipo, niliwahi kuona tangazo,…kwenye gazeti, wakati akili inakuja na kupotea, kuwa natafutwa,..lakini kwa hasira nikalichana lile gazeti, walipiga kipindi sina midevu hii…’akasema.



    ‘Sasa kwanin hunyoi…?’ akaulizwa.



    ‘Ningelinyoa kama nilikuwa najitambua..sijui…kiukweli nahisi nilikuwa sijijui,..unajua hivi sasa nahisi ni mtu mwingine kabisa…’akasema.



    ‘Kwani tatizo lako ni nini…?’ akaulizwa.



    ‘Tatizo langu,!!! ..labda akija mke wangu atawaambia..yeye unajua, tatizo langu limeanzia wapi, ila hajui jinsi ya kunisaidia, mimi nilishajua lakini jinni gani ya kumuelezea ikawa ni vgumu sana ..’akashika kichwa



    ‘Unajua nikuambieni kitu,..hata kwenye njozi, nahisi hivyo, ni kuwa niliwakosea watu wengi sana, na hilo ndio tatizo langu, hakuna zaidi…mengine sawa yawezekana yapo,…ila nahisi , ni hayo niliyowafanyia watu , na ninayemkumbuka kwa haraka ni huyu binti, hasa nilipomuona ndio nikakumbuka,…’akaniangalia kwa aibu.



    ‘Nilipomuona tu nikamtambua, najua yeye ndiye nimemkosea sana, mke wangu nilimkosea lakini yeye alishasema kanisamehe, iliyobakia ni huyu..najua ni huyu tu…baada ya tendo hilo la kunisamehe..akakiri moyoni na vitendoni, nina imani mola anatanirejeshea hali yangu, na kila mara nilikuwa naiota hiyo ndoto na nikionywa kuwa, nispofanya haraka sitapona tena, na tumuwahi kabla hajapata matatizo zaidi ….’akasema.



    ‘Kwenye ndoto ndio unaota hivyo, sio kwa waganga wa kienyeji..?’ akaulizwa.



    ‘Mimi siwajui waganga wa kienyeji, sio kwamba sijawahi kwenda, nakumbuka mke wangu alinipeleka huko kwenye kunihagaikia…lakini nikaja kumtoroka, unajua hata kutoroka kwangu asubuhi siku hiyo sababu kubwa ni hiyo, walipanga wanipeleke kwa mganga wa kienyeji, kuna rafiki yake mke wangu alikuja akamshauri hivyo, mimi alifajiri hakujapambazuka, nikatoroka mapaka leo ndio wanapata taarifa zangu..’akasema.



    ‘Sasa kwanini ukatoroka ukijua kuwa wenzako wanakuhangaikia wewe, ili uje kupona…?’ akaulizwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Mimi sijui kwanini nilifanya hivyo…, ila kuna kitu kiliniambia toroka, huko wanakotaka kukupeleka hutapona, watazidi kukuharibu, dawa ya maradhi yako sio hiyo, dawa ya maradhi yako ni makosa yako mwenyewe, …’akatulia



    ‘Nikijaribu kuuliza ni makosa gani nimeyafanya, basi nikijiuliza hivyo kuna watu , kelele za watu wanalia, …wakuja kunililia, nimewakosea,..sasa kwa vipi ni nani, siwaoni , sioni ..unajua, kichwani tu kelele za vilio, nikisikia hivyo nakiambia, nikijaribu kuzikimbia hizo kelele, lakini wapi, kwahiyo nimekimbia wee…mpaka wapi huko, …nilikwenda mbali sana..’akasema



    ‘Sasa huku uliwezaje kurudi….?’ Akaulizwa

    ‘Hata sijui, nimekua  nikitembea , huku na kule, nalala maporini, majalalani, lakini siachi kumkumbuka mungu, mimi sijawahi kusoma dini, nahisi hili ndio kosa kubwa sana, kama ningelikuwa nimesoma dini, huenda matatizo haya yasingelitokea, nimesoma masomo ya kawaida, nimesoma sana usinione hivi, hadi chuo kikuu…’akasema



    ‘Wewe…?’ mama akauliza kwa mzaha



    ‘Ndio, huamini…’akasema

    ‘Sawa nikiamini aikuamini, haitasiaida kitu, muhimu ni mtu mwingine aje kututhibtishia,…’akasema huyo mama

    ‘Sasa uliambiwa ni makosa yako, hukuambiwa ufanye nini, utubu au ufanya nini…?’ akaulizwa



    ‘Unajua hali hiyo ya kuchanganyikiwa,  inakuja tu, na kupotea, kuna muda nakumbuka kumbuka mambo kuna muda hali inakuwa mbaya, wakati mwingine nahisi kama nipo kwenye njozi, ni kweli kuna muda, niliwahi kuulizia, nitafanyaje kuhusu hayo makosa, sikumbuki jibu, lakin….ikaja hiyo hali kuwa nitubu , kama ni makosa unatakiwaje ufanye nini, ni kutubu au sio , sasa kwa nani….’akatulia



    ‘Kwahiyo ukafanyaje hadi ukafika huku…?’ akaulizwa



    ‘Kufika huku labda niseme ni miujiza ya mungu,..sasa haivi kidogo nimeanza kukumbuka nipo wapi, na kutoka hapa ninaweza hata kwenda nyumbani kwangu, ni mbali kidogo na hapa, ….lakini nitafika tu….’akasema



    ‘Ni mke wako unamkumbuka sasa kwa jina wapi alipo, au sio…?’ akaulizwa hapo akakaa kimia kidogo, halafu akasema;



    ‘Unajua bado, kichwani hakujakaa sawa kabisa, maana sijariskika, nahisi ..lakini nishapona, najua kwa haya mateso, niliyopata nia dhabu tosha, sikuwahi kuambiwa, nifanye nini, ila nahsi hivi ndivyo sahihi, ila jamani nilikuwa nateseka, kichwani kunakuja mambo mengi hili na lile..yaani nikikaa hivi ni kama kuna watu elifu wanaongea kwa pamoja kichwani, wengine wanalia, wengine wanapiga makelele..yaani we acha tu…’akasema



    ‘Pole sana, mungu atakujalia, utapona kabisa, mimi nimeshakusamehe japokuwa sijui kosa ulilonifanyia ni lipi, maana sijawahi kukutana na wewe, sikukumbuki kabisa…’nikasema na yeye akaniangalia kwa makini nikaona kama machozi yakimtoka, kiukweli nilimuonea huruma nikasema;



    ‘Usilie baba yangu, wengi tupo hivyo, tunapitia matatizo, maisha magumu, na ukifikiria sana, unaishia kulia, na hasa ukigundua kuwa wenzako huenda …lakini sitaki niongee zaidia, mimi namuomba mungu kama kuna ulilonifanyia mimi, hata nisipolijua akusamehe tu, ..sina kinyongo na wewe…’nikasema.



    ‘Mungu wangu…hata sijui niseme nini…’akasema.



    ‘Huna haja ya kujiumiza mzee…bint huyu ni mwema, sana, katika misha yangu ya kuhangaika sijawahi kukutana na binti kama huyu , mwenye adabu, anajua kuishi na watu, muaminifu, ..huwezi kuamini, hata kuonja mboga jikoni mpaka aniombe ruhusa, niliona ni mtu wa ajabu sana…’akasema huyo mama.



    ‘Namfahamu sana…’akasema huyo mzee.



    ‘Unamfahamu kwa vipi, unajua unatuweka kwenye mtihani mpaka watu wanatufikiria vibaya wanafikia kuhisi labda, ni  wewe ndiye ulimpa huyu binti hiyo mimba..japokuwa tunajua sio kweli au sio…?’ akaulizwa na hapo akanitizama tumboni, kwa uso wa huruma, akasema;



    ‘Ana mimba, masikini…sikujua hilo…’akasema sasa akinitizama tumboni.



    ‘Wewe si unasema unamfahamu, mbona hujui kuwa ana mimba..?’ akaulizwa.



    ‘Mimi hilo sijui….ooh, yaani labda ..lakini mim isijui kabisa, nisamehe sana …sitaki niongee zaidi hapa, nataka tuongee ukiwa huru…’akasema.



    ‘Kwahiyo hiyo mimba sio ya kwako..’akasema huyo mama kwa utani.



    ‘Wewe mama wewe, huko sasa…hapana, …’akasema akiona aibu





    ‘Niambie ukweli, kama ni wewe ulimbaka au wewe ni baba yake, tuambie maana hata yeye hakufahamu kabisa isije ukawa ni tapeli fulani una mambi yako…?’ mama akauliza hivyo na jamaa akatoa jicho la kushangaa na kusema.



    'Ni hadithi ndefu, na kiukweli hivi unavyoniona na hali niliyo nay oleo ina afadhali, nashangaa hata mimi, najikuta nipo hivi, ile hali ya awali imenitoka, na kama mtu kanivua kofia, kofia niliyoizoea, na kuniacha kichwa, nahisi nipo mtu mwingine kabisa…’akasema.



    ‘Sijakuelewa…’mama akasema.



    ‘Wakati nipo hapo nje, nililia sana, namlilia mola, kuwa nimempata mmojawapo, basi anisaidie huyu niliyempata anisamahe…najua huyu nilimkosea, najua kwa hayo makosa alishawahi kuinua mikono juu na kumlilia yeye, sasa nimeyaona madhambi yangu, anisaidie huyu mtu anisamehe…nililia mpaka macho yanauma.



    Kuna muda nikahisi kama kausingizi…  mara nikahsi kitu kikipiga kichwa, taa..nikasikia nziiiiiii..hujawahi kuhisi hivyo kichwani, mara nikajihisi kama nimetoka usingizi,…naanza kuona watu vyema, nahisi vyema, ..na nilipojiangalia nilivyo nikashtuka, kwanini nimekuwa hivi, unajua nilisimama najikagua kwa muda nikashikwa kichwa manywele mengi, midevu, ohhh, sikuamini, hivi mimi ni nani , na kwanini imekuwa hivi, nikaanza sasa kutafkari, kukumbuka imechukau muda, lakini naanza kukumbuka,…’akasema.



    ‘Mungu mkubwa, kwahiyo kule kuchanganyikiwa ndio kumeondoka hivyo, nahisi mola mwingi wa rehema kasikia kilio chako,…’akaambiwa.



    ‘Lakini sijaamini mpaka nisikie kauli ya huyu mdada, najua kanisamehe moyoni ndio maana ikatokea hivyo, natamani niskie kauli yake kuwa keshanisamehe zaidi ya hapo, katamka na kutamka, lakini bado,ni mpaka asikia kuwa mimi nani nilimfanya nini , hilo la mimba mimi sijui, …, najua siwezi kumlipa kwa hayo niliyomtendea, lakini…mungu anajua jinsi gani nilivyoteseka, muulizeni mke wangu atawaambia ukweli..’akasema



    ‘Sasa mke wako tutamjuaje sisi, maana unasema mke wako mke wako, hutaki hata kututajia jina lake…’akasema huyo mama.



    ‘Atakuja,…naomba simu yako mara moja…’akasema, na huyo mama kwanza akasita kidogo, jamaa akasema



    ‘Usiwe na wasiwasi nimekumbuka namba ya mke wangu, nilikuwa najaribu kuiwazia, sasa nahis ndio hiyo, nipe nimpigie, au wewe nikutajia umpigie kama una mashaka na mimi…’akasema na huyo akampa huyo jamaa simu,



    Jamaa akaanza kubofya hizo namba na kuweka simu sikioni, akasikiliza kwa muda mara, haloo



    Ni mimi mume wako…’akasema



    ‘Ni kweli ni mimi, umenisahau hata sauti yangu jamani…’akasema



    ‘Nipo..nipo..hapa ni wapi…?’ akauliza huyo mama, huyo mama akasema



    ‘Nipe hiyo simu nimuelekeze…’akasema na kupewa akaongea na huyo mke wa jamaa ana kumuelekeza wapi walipo na huko wakasema wanakuja.



    ‘Wanasema wanakuja, sijui nani na nani…’akasema mama



    ‘Oh, mungu mkubwa, …’jamaa akasema huku anafuta machozi,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Unajua niwaambie kitu, bila ya mke wangu kuwepo hapa hili zoezi halitakamlika, nataka aje ashuhudulie kuwa mimi sio yule tena, mimi ni nani, na nilimkosea nini huyu binti, yeye anajua zaidi yangu…kiukweli namuonea huruma sana mke wangu,..kateseka kwa ajili yangu mpaka ikafika sasa hana jinsi, unajua huwezi kujua ugumu wa jambo mpaka uwe nalo, kuishi na mtu aliyechanganyikiwa ndani ya nyumba, ni mtihani…’akasema



    ‘Oh, pole sana, sasa…mimi naona utupe muda, sitaki kukukatili na kwa vile umesema mke wako anakuja na ni bora awepo, unaonaje ukatupa muda, tumalizie hizi kazi au sio,…’akaambiwa



    ‘Sawa, …sasa hivi nahisi nipo binadamu, najua moyoni keshanisamehe ndio maana imekuwa hivyo, …nitawasaidia kazi, ngoja, nipeleke huu uchafu nje…’akasema na kuanza kusaidia kazi za hapo.



     Haikupita muda mara ukaingia ugeni, muda huo tulikuwa tunapanga panga vitu, na kwa vile siku hiyo hatukuwa na kazi za mapishi zaidi, tulikuwa tunafungasha fungasha, na ndio tukaona ugeni wa watu wa dini, wakiwa na mavazi yao, walikuwa kundi, mpaka tukashangaa, kuna nini leo.



    ‘Salamu salamu, amani iwe juu yenu nyote, hamjambo jamani…,’ mmoja wapo akasalamia na mama alikuwa kwa ndani akatoka nje kukutana na ujumbe huo, mimi kwa muda huo nilikuwa namalizia kazi na yule mjamaa alikuwa kapewa kiti kakaa pembeni na muda mwingi alikuwa akinitupia jicho, sasa hivi anafanya kwa kujiiba sio kama asubuhi alikuwa akinitizama , najisikia vibaya sijui kwanini, na hali hiyo inanifanya nasikia hata kutapika.



    ‘Sijui kwanini nilikuwa nikimuangalia nahisi hivyo, hadi nilipotapika, ..na baadae nikamuomba munu kama kuna kitu kanikosea basi amsamehe tu mja wake, maana ni mtu mnzima, hastahili kuadhibiwa hivyo, kiukweli nilimuomba sana mungu amsamehe, sasa sijui nilivyoomba hivyo ina mahusiano na hicho kilichotokea anayejua ni mungu pekee.



    *************



    ‘Jamani wapendwa, mtusamahe kwa kuja bila taarifa kwa siku ya leo, ila taarifa mlikuwa nayo kabla , hatukuwa na jinsi, nyingine ila nikuja hivi hivi,...natumai mliwahi kuongea na kiongozi wetu mmoja, kuwa atakuja kuwatembelea baada ya wiki,..yeye kapatwa na dharura hakuweza kufika..., lakini hatukuona haja ya kutokufika kwa sisi, maana viongozi wengine wapo, ndio sisi …’akasema mmoja wapo.



    ‘Nakumbuka ndio…’akasema huyo mama



    ‘Basi baadhi yetu hapa tumetokea huko kijijini, kama alivyokuambia huyo mzee awali, na katika harakati zetu za kutangaza dini ya mwenyezimungu tukapungukiwa na sehemu ya ibada, huko kijijini kwetu …na katika kuhangaika ndio tukagundua eneo linalofaa, lipo sehemu nzuri tu, tukataka kulinunua, lakini mwenyewe akawa hayupo…’akasema.



    'Mwenye eneo hilo alifahamika, eneo hilo lilikuwa la mama mmoja alikuwa akiishi na binti yake, anafahamika sana kipindi hicho cha uhai wake...'akatulia kidogo



    'Sasa kuna mambo yalitokea, unajua huko vijijini kuna mambo yanakua kwa haraka, imani hizi za kishirikina, kuna mambo mengine vijana wanakuwa hawana kazi, basi yanazuka mambo mengi tu, na baya zaidi, watu wanauwana ovyo, ukiuliza sababu ya msingi hakuna, imani ya kumuogopa mungu haipo tena..



    'Kwa vile watu wanalifahamu hilo eneo ni la nani, ikabidi sisi tuhangaike, ujue, kuna watu walilivamia awali,lakini hawakuweza hata kujenga, wakapata misuko suko, wakakimbia na kuliacha, wakaja wengine hivyo hivyo, mwishowe likaachwa kama lilivyo, ndio sisi sasa tukaingiwa na hamasa nalo,...'akatulia





    ‘Kiongozi wetu akafanya juhudi kubwa kutembelea huku Dar, nia na lengo ni kumpata mumiliki halali wa eneo hilo, maana tulisikia mrithi huyo ni binti wa marehemu huyu mama..., na alichukuliwa huku dar, kuja kufanya kazi za ndani, ..tunasema mrithi maana mama aliyekuwa akilimiliki eneo hilo si ndio kalifariki, watu wahuni walimfanyia kitu kibaya sana, mungu awasahemeh tu, hao watu maana nasikia nao wao wamekumbwa na matatizo makubwa, mungu huwalipa watu hapa duniani, tumuogope sana mungu…’akatulia.



    ‘Sasa nyie mlikuwa wapi mpaka hali hiyo inatokea, nyie si ndio wazee wa huko, tena watu wa dini…?’ wakaulizwa



    ‘Unajua sisi tuna nafasi yetu kama viongozi wa dini, kazi yetu ni kutoa imani kwa watu, na kazi ya ulinzi ni ya serikali, tumejitahidi sana kwa upande wetu, lakini vijana hawataki kuingia kwenye nyumba za ibada, tukiwafuata mitaani, inakuwa kero kwa wengine, na baya zaidi ila hali ya watu kuamini mambo ya ushirikina imeshika kasi, ni kama watu wtunarudi ujingani, hili ni tatizo kubwa sana,….’akasema.



    ‘Ni vyema watu kama nyie mkiwepo…, tunashukuru kwa hilo, kwahiyo mnasemaje sasa….?’ Akaulizwa



    ‘Sasa tulielekezwa hapa na huyo kiongozi wetu, kuwa kuna binti kasema anaishi na wewe, na huenda akawa ndiye huyo tunayemtafuta, kama yupo tumuone, kama ni yeye basi tutapanga siku ya kuja, kama hamna nafasi leo, au kama mna nafasi leo mungu ni mwenye neema, zake, tunaweza kuongea naye, mungu akipenda…’akasema.



    ‘Mhh, kiwezekanacho leo hakiwezi kusubiria, lakini nashangaa leo napata ugeni na wote mnataa kuongea na binti yangu, kuna ugeni mwingine nao unataka kuongea na binti, hatujajua wana nini, sasa nyie tena…’akasema huyo mama.



    ‘Lakini taarifa zetu ulizipata mapema au sio, isije kuja kuazima jamvi akaja mwingine kutaka kuliwahi, sisi tulishakuaambia na eneo hilo sisi tulisha…’kabla hajamaliza mama akasema.



    ‘Wao hawahitajii hilo eneo nijuavyo mimi, wana yao mengine kabisa, …sasa kwa vile hao wengine hawajakamilika, basi ngoja nimuite binti, aje mumuone kwanza isije ikawa sio yeye, nafikiri mkitambulishana itakuwa ni vyema zaidi, au sio…’akasema huyo mama.



    ‘Hewala hilo neno, …’wakasema na mimi nikaitwa kuja kuonana na huo ujumbe.



    Nilitoka nikiwa nimevaa kiheshima, na kiukweli mimi kawaida yangu ni hivyo, huwezi kuniona nimevaa kinyume na maadili yetu, na nilipotoka kuna wazee wawili wakatikisa kichwa kama kukubali, na wengine walibakia kimia.tu wakiniangalia.



    Nikawasalimia kama ada, na wao wakaniitikia, na yule kiongozi wao akaniuliza jina na natokea wapi, nikawaelezea jina na jina la mama na natokea wapi, wakasema;



    ‘Oh mungu mkubwa hatimaye tumekupata..ndio wewe hasa, unafanana sana na marehemu mama yako…’akasema huyo kiongozi wao,



    ‘Ndio huyu sio..?’ akauliza huyo mama



    ‘Ndio yeye, bila shaka…’wakasema



    ‘Sasa muelezeni shida yenu..’akasema huyo mama, na watu wale wakaelezea shida yao, na jinsi gani walivyojpanga, na wapo tayari kunilipa pesa ya eneo hilo, wao walikadria kutokana na bei za huko kijijini, zinajulikana, basi mimi nikawa sina la kusema maana nilichokuwa nikihitajia ndio hicho, kwasababu sikutarajia kabisa.



    ‘Wazee wangu, nawashukuruni sana, maana sikitarajia hilo, mimi nilijua eneo hilo limeshachukuliwa,. Na nilikuwa naogopa kabisa kurudi huko nikijua yatanipata kama yaliyompata mama,  na ujio wenu umenipa faraja kuwa angalau wapo watu wema katika hii dunia, nimepitia machungu mengi sana, sitaki kuelezea, lakini siku zote kama alivyoniusia mama yangu, alinitaka nisikate tamaa na niwe na mtegemea mungu , kwani mungu pake yake ndiye, ataniondolea mizigo hii ya mitihani..’nikasema.



    ‘Sawa kabisa, imani imekuiba binti, endelea hivyo hivyo utafanikiwa hapa duniani na kesho siku ya kiamana,…kwahiyo sasa eeh, umekubaliana na kiwango hicho.au.?’ nikaulizwa.



    ‘Mimi sina zaidi,kama mumeona ni kiwango halali kwa hilo eneo, basi nimeridhia, nyie ndio mnajua na nyie ndio mumelipima,hilo eneo, mimi yote namtegemea mungu tu ni neema zake hizo..’nikasema.



    Basi utaratbu wa nyaraka ukapita, na nikaambiwa kwanza nifunguliwe akaunti ya benki, tutasaidiana na wao,  na malipo yatafanyika huko huko benki, ili hizo pesa ziwe salama na niwe nachukua kwa awalmu nikihitajia, tukakubaliana hivyo, ikabakia sehemu ya kuweka sahihi na kupitia sehemu zote za serikali zinazostahiki ili isije kutokea migogoro baadae, nikawa sasa na mimi tajiri, nilijihisi hivyo moyoni.



    *************CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ugeni ule baadae ukaondoka, ikabakia kesho waje tuongozane kwenda banki kukamilisha mipango yote iliyobakia, na walipoondoka,  mara ukaja ugeni mwingine , gari likasimama nje, …na tukasikia hodi, baada ya muda,



    Wa kwanza kutoka nje alikuwa yule mzee, akasema.



    ‘Huyo anaweza akawa ni  mke wangu…’akasema akiwa na furaha sana usoni.



    NB inatosha kwa leo…nipo kwenye mitihani fulani hivi, lakini nimeona nisiache siki ipite hivi hivi





    WAZO LA LEO: Tusichoke kumuomba mola wetu, kwani mola ni mwingi wa rehema anajua ni lini atatutimizia matakwa yetu kwa wakati gani.



    Yule jamaa aliposikia gari limesimama nje, akatoka mbio mbio uso wake ukionyeha furaha sana, sisi tukabakia ndani tukimaliza kupanga vitu vyetu, na ilichukua muda , jamaa akawa anaongea na huyo mgeni ambaye bafo tulikuwa hatujafahamu ni nani, japo tulihisi huenda akawa ni huyo mke wa huyu jamaa kama ni kweli, ..



    Tulisikia sauti sauti za kuongea lakini hatukuweza kufahamu wanaongea nini hasa, na baadae mlango ukafunguliwa , aliyeingia alikuwa huyo jamaa akiwa na tabasamu tele mdomoni. Aalipofika ndani akasimama na kugeuka nyuma, hamuoni mwenzake, akasita kidogo, lakini akawa anaongea hivi;



    ‘Jamani, natumai muda umefika, najua nimewasumbua sana, na pia nimemsumbua mke wangu, kumbe alikuwa kwenye kikao muhimu cha matatizo ya familia ambayo kisa ni mimi, madeni yamekuwa mengi, matatizo ni mengi kweli kweli, na ..aah, kisa ni mimi, lakini nina imani sasa, kwa vile nitakuwa nimepona natumai hivyo, nitayalipa hayo madeni kwa mikono yangu hii..’akasema akionyesha mikono yake miwili.



    Sasa akawa anaangalia nje, akimsubiria mwenzake lakini kukawa kimia, huyo mwenzake hakuonekana, sisi tukabakia kuangalia mlangoni kwa hamasa, na huyo jamaa alipoona kimia, akaita



    ‘Mke wangu mbona unasita kuingia ndani, ingia, umuone huyo bint, ninayekuambia, ndiye sababu ya kupona kwangu, na ndiye sababu hal zetu zitarejea tena, nina imani hiyo, ingia, mbona …..’akanigeukia na mimi nilikuwa nimesimama nikiangalia huko mlangoni, na huyo anayesema ni mke wake hakuingia mara moja,  ikawa twajiuliza kuna nini tena huko nje mbona huyo mtu haingii. Nikaona niendelee na kazi zangu…nikawaacha, nikiendelea kuingiza vitu sehemu tunapovihifadhia.



    Wakati narudia kuchukua vitu vingine mara nikamuona huyo jamaa akielekea huko nje, kumfuata huyo mke wake, sijui kwanini huyo mke wake, amegomea huko nje,…



    Mara nikasikia huyo jamaa akisema;



     ‘Mke wangu unalia nini, yote hii ni mitihani ya mungu haya yametokea kuwa fundisho kwetu, hasa mimi, kwanini unalia, ingia kwanza tulimalize hili, na nina imani mengine yatakwisha tu kwa mapenzi yake mola, nisamehe sana na nakuomba tuendelee kuwa pamoja, usichukulie hasira, na mimi ni binadamu, kutelekeza kupo, nakuahidi hayo hayatatokea tena…’akasema.



    ;Hayo hayatatokea, ni rahisi kusema hivyo au sio…lakini madhara yake utayalipaje, umwaumiza watu wengi, hadi familia yako,..najua utasema hivyo kwa vile wewe unaitetea nafasi yako, au sio,…aah, sijui kama nitaweza hili na hali irejee tena kama awali,..sijui….’ilikuwa sauti ya kike.



    ‘Mke wangu ulisema umenisamehe, sasa hayo yanakujaje tena…ingia kwanza tuyamalize haya ya hapa, najua baada ya hapa hakutakuwa na matatizo tena, nakuahidi hilo…’akasema huyo mume mtu.



    ‘Sawa, ..nakuja….’akasema



    Baada ya muda nikasikia hodi ya kike, nikajua wawili hao watakuwa wameshaingia ndani. Kwa muda huo nilikuwa kwa ndani nikipanga vitu vizuri, moyoni nilikuwa na hamasa sana nimuone huyo mke wa huyo jamaa yupoje, na yawezekana ni watu wanaojiweza maana kaja na gari…



    Nikawa naharakisha kupanga viitu vyema, ili sije kuwa usumbufu wakati wa kuvichukua, sikutaka kuharibu kazi yangu japokuwa nilikuwa na hamu ya kumuona huyo mke wa huyo jamaa, nikamaliza, na niliskia huyo jamaa akimtambulisha mkewe kwa huyo mama, hapo nikaamini kuwa ni kweli, maana bado tulikuwa tunamtilia mashaka, huenda hata mke hana….



    ‘Huyu ndiye mke wangu, niliwaambia nina mke mnzuri, unamuona..kakondoa tu kwasababu ya matatizo, lakini …atarejea hali yake hivi karibuni…’akasema huyo jamaa.



    ‘Mke wangu huyu ni mama Ntilie amenifaa sana, chai nzuri,…na chakula, lakini mara nyingi niliwa sili chakula hapa, maana nilikuwa natimiza wajibu wa kuzunguka kuwatafuta niliowakosea,..na sikupenda kula mchana,…huwa nilikuwa nakunywa chai ya nguvu, nikishiba mpaka kesho tena,..kwangu mimi, kiukweli ulikuwa mchana wa toba, wa kuomboleza, ndivyo maisha yangu yalikuwa hivyo, baada ya kuwakimbia, hayo nakumbuka sana….’akasema huyo mbaba.



    ‘Oh, nashukuru sana, mama Ntilie, kama alivyokuita mume wangu maana tumehangaika sana kumtafuta huyu mtu, mpaka ikafikia muda, tukasema basi huenda huyu mtu hayupo tena duniani, jana tu tulikuwa kwenye kikao cha wanandugu kuamua hatima yake, unajua tena mtu akipotea siku nyingi wengine hufikiria vibaya, na leo ilikuwa kutoa maamuzi,…bahati ndio nikapata hiyo simu, sikuamini….’akasema huyo mwanamke.



    ‘Walijua nimekufa ee, watakufa wao kwanza…watu wengine bwana wanakimbilia kuona wenzao wamekufa….walifurahi nimechanganyikiwa hawachakoma, sasa wanazua nimekufa, wajinga sana hao watu…sasa nipo hai, na nkuja kivingine,…hivi hapa kuna slooni karibu..eeh, ngoja…’jamaa akasema sasa akishika shika maywele yake akihis vibaya



    ‘Sio hivyo wewe mwanaume, ilikuwa, ni…ni namna ya kutafuta njia ya kuhakikisha upo wapi na je upo salama…wewe fikiria umepotea muda gani, hujulikani wapi ulipo,…hivi hata ingelikuwa wewe unaglifikiriaje,..na yote umayataka wewe mwenyewe…’akasema huyo mwanamke.



    ‘Sawa, mke wngu… mimi nipo salama kama unavyonioana na ni kwa mara ya kwanza leo nimeweza kujitambua, waulize hawa watu ambao walikuwa wakiniona kwa siku chache nilizoweza kufika hapa,…siku nyingine zote ilikuwa kama nipo gizani, sijijui sijui nipo wapi,…na najua huku kupona sio bure , ni baada ya huyo mdada kukubali kunisamehe, vinginevyo sijui ingekuwaje…’akasema.



    ‘Mdada yupi huyo maana na wewe ulikuwa mwingi sana, umewakosea mabinti wa watu wengi tu, sijui wangapi, kiukweli inatakiwa uwaendee wote mmoja baada ya mwingine, maana bila hivyo…utakuwa bado, hujafanikiwa,..na ni kweli haya yote yaliyokupata ni sababu ya uzandiki wako,, na tatizo ni kwamba madhara yake yametukumba na sisi tusio husika na madhambi yako, yupo wapi huyo binti jamani natamani nimuone …’akasema huyo mama akiangalia huku na kule.



    ‘Anakuja…’akasema huyo mama na mimi ndio nikatokea..



    **************

    Unajua ni maajabu sana, wakati natokea huyo mama mgeni alikuwa kageukia mlango mwingine, akijua huko ndio nitatokea,  sasa mimi nikatokea mlango mwingine uliopa nyuma yake, aliposikia sauti ya nyayo zangu, ndio akageuka, macho yake yakakutana na yangu…hata mimi mwenyewe nilipigwa na butwaa, kuachia yeye ambaye, akabakia mdomo wazi, na macho kayatoa, ananiangalia tu…na kuniangalia, akawa hanimalizi…



    ‘Ndio wewe ….mungu wangu, ni wewe au ..hapana siamini…’akasema sasa akishika kichwa, na hakuishi ahapo akapiga magoti, akasimama, akasogea , ikawa kama anatafuta hewa, au siju anataka kukimbia…



    ‘Hata mimi ilikuwa hivyo hivyo mke wanguu nilipomuona huyu binti…sikuamini kuwa ni yeye….kabadilika eeh…lakini sura haipotei, unamuona alivyo, na nasikia….’akasema mume wake, na kabla hajamaliza mke wake akamkatili na kusema;



    ‘Mungu wangu,..ooh, unajua hii dunia, …samahani sana binti…niliambiwa huyu binti kafariki…’akasema na akawa anatikisa kichwa, sasa akimuangalia huyo mama Ntilia. Na kauli hiyo ikanifanya hata mimi nishutuke.



    ‘Nani alizuia hivyo…unaona watu walivyo, mimi wanafikiria nimekufa, na huyo binti naye walimzulia kuwa amekufa, kwanini wao hawajifikirii kuwa wamekufa…watu wabaya kweli…ni nani huyo alikuambia hivyo…?’akaulizwa na mume wake.



    ‘Yaani, akili hapa haipo sawa, na unajua aliyesema hivyo ni nani, alikuwa yule rafiki yake, yule binti mwingine aliyeiba na kutoroka…na yeye anasema kasikia kwa watu…’akasema



    ‘Kwani keshapatikana..?’ akauliza mume wake sasa akimuangalia muke wake kwa macho ya hamasa.



    ‘Unacheza na serikali wewe..na hata hivyo za mwizi ni arubaini, walitegwa wakanaswa, utaiba utatumia zitakwisha, lazima utatoka tu…na cha wizi hakidumu, kamwe,…’akasema huyo mama.



    ‘Oh afadhali …kama wamepatikana eeh, sasa wataenda kunyea debe, si wameshafungwa au….?’akasema mume wake, na kuuliza.



    ‘Basi huyo binti aliniambia hivyo, nilipokwenda kuwaona, wakiwa jela …yeye sijui alisikia wapi, akaniambia ana masikitiko sana, kwani kapata taaarifa kuwa rafiki yake, yule binti aliyekuwa kwangu, akaondoka, kafariki,, aliumwa sana akalazwa na kutokana na yale mazindiko, na masharti aliyopewa ambayo aliyapuuzia, akaacha kuyafuatilia, yalianza kumpatiliza…’akasema huyo mama.



    ‘Waongo hao…’akasema huyo baba.



    ‘Sasa sikiliza …,  basi huyo binti alipokuwa huko hospitalini, alizidwa sana, uamuazi ukawa afanyiwe upasuaji, na kabla hawajafanya hivyo, akafariki, na mtoto alifarikia tumboni…na alipopasuliwa kumtoa mtoto, akatokea kiumbe wa ajabu sana…’akasema huyo mama.



    ‘Mungu wangu ni nani huyo alitengeneza huo uzushi..?’ akauliza huyu mama Ntilia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Aaah, tuyaache hayo, mungu akupe maisha marefu binti….na kiukjweli, huyu mwanaume kanieleza mengi hapo nje, kuwa kakuomba msamaha, na mimi sitakuwa mbali na yeye na mimi nakuomba unisamehe sana, najua mengi yaliyotokea…eeh,…’akawa ananisogelea kunipigia magoti.



    ‘Mama usifanye hivyo, hustahiki kunipiga magoti mimi, wewe hujanikosea kabisa hata huyu baba, mimi sijui kanikosea nini, mpaka sasa hajatuambia nilichomkosea, nashangaa tu kaja anasema nimsamehe, nimsahemeh anini sasa, hata hivyo mimi nishamsamehe, kama kuna lolote alinifanyia, mungu amsamehe tu maana yeye ni sawa na mzazi, …’nikasema, na huyo mama akaniangalia kwa macho ya kushangaa na huruma



    ‘Kakukosea sana tu…na ni kwa vile hakujakusimulia….’akasema huyo mama, na akashika kichwa kama anawaza jambo, na kama vile kakumbuka kitu akasema



    ‘Unajua, ...usije kumdharau mtu katika hii dunia, hata kama unacho, una uwezo, lakini hujui ni kitu gani kamtunuku mja wake, ambacho wewe huna…huyu binti mungu kamtunuku jambo ambalo wengi hawana,…hata wakijifanya wanalo, lakini ni gumu sana kuwa nalo….’akasema



    ‘Nakushukuru sana binti yangu,…maana kwa uoni wangu, mimi najua nimekukosea sana, hivi sasa ndio naanza kulitambua hilo, lakini muda ule ambao nilikuwa na uwezo wangu, maisha mazuri, nilikuwa silioni hilo kabisa…kwa muda ule ilikuwa rahisi kuchukua maamuzi ya haraka, hasira, dharau, vilinitawala sana, njia rahisi ni kufukuza, si nitapata mfanyakazi mwingine,..nilijiona nimesoma, pesa ninazo,  watu kama hawa hawawezi kunibabaisha,…sasa mitihani iliponizidi, nikaanza kuchanganyikiwa, vyote nilivyokuwa navyo havikuweza kunisaidia…’akasema.



    Nilimuangalia huyu mama akiwa anaongea na akilini nikawa nawaza sana maisha ya mwanadamu yalivyo, jinsi gani mwanadamu anavyoweza kubadilika kwa muda mfupi, maana huyu mama alikuwa kibonge siku zile, mwenye nazo, anajiamini , leo hii anaonekana kakonda,kazidi kuzeeka, ..mvi zinameta meta, kichwani, anaoenakan hana raha kabisa, ni kwa muda mfupi tu,….moyoni nilimuonea huruma sana.



     ‘Najua utanisamehe, lakini moyo unanisuta kwa maana ni mimi ndiye nilikutoa kijijini nikaahidi kuwa nitakutunza, nikachukua dhamana hiyo kwa mama yako, na hadi anafariki alijua mtoto wake yupo mahali salama, lakini sikuikumbuka dhamana hiyo na adhabu zote zimenishukia mimi,…adhabu za familia nimezibeba mimi, kila nikiwazia hilo, naona nimekukosea sana, unajua niliwahi kumuota mama yako alinilaumu, ananiambia saa umefany anini..hivyo, sasa nimefanya nini, ina maana ananisuta, ananilaumu….’akasema.



    ‘Mama kiukweli mimi sina kinyongo na wewe, najua hata ingelikuwa mimi nipo kwenye hiyo sehemu yako labda ningelifanya hivyo hivyo,..na una maana huyu baba ndiye yule mume wako, mbona kabadilika hivi, .?.’nikasema na kuuliza



    ‘Ndio yeye, ni hiyo midevu na hali ngumu, ndivyo vimemfanya usimkumbuke,  ndiye yule aliyekusababishia hayo yote, huku sasa akinichunguza tumboni na mimi nikajitahidi kujiminya kwa ndani ili ile mimba isionekane kwa vile nimevaa dera, lakini haikuwezekana, yeye akasema



    ‘Ina maana hiyo mimba ndio imekuwa hivyo, jamani watu waongo, hata siwezi kumuamini mtu tena, ..hapana…’akasema sasa akificha uso wake na mikono.



    ‘Ndio hivyo mama,  nasubiria kudra za mungu, nina imani mimi nitajifungua salama na mtoto wangu atakuwa mwema tu, sizani kama yale waliyoongea watu yanaweza kuwa ni ya ukweli, hata asipokuwa na baba, mimi sijali, nitamlea kama mtoto wangu….’nikasema

    ‘Safi kabisa, utazaa na utazaa mtoto mwema kabisa, hiyo ndiyo imani sahihi, nikuambie ukweli kwenye matatizo unakutana na vishawishi vingi, mimi walikuja watu wakanishawishi niende kwa waganga wa kienyeji kwa matatizo ya huyu mwanaume….’akasema nilishangaa kwa nini hasemi mume wangu kama zamani,



    ‘Ilibidi nikubali tu maana nipo na mtoto wa watu, ni mume wangu, ningefanya nini, lakini kwa bahato nzuri sijui ilikuwaje mwanaume huyu akatoroka, na akapotoea hadi leo ndio tunampata…sasa kumbe ndio alikuwa akikutafuta wewe…’akasema



    ‘Mimi sijui kama alikuwa akinitafuta mimi..’nikasema nikimtupia jicho huyo mzee, yeye alikuwa kainamisha kichwa chini, …



    ‘Hisia ndizo zilikuwa zinamtuma hivyo, nakumbuka alipoanza kuchanganyikiwa ni pale nilipokuwa namuuliza, je atakuja kusema nini mbele ya mungu kwa  hayo aliyokufanyia wewe..baada ya kuanza kuugundua ukweli,.. unajua nimekuja kugundua mengi yaliyokuwa yakitendekea pale ndani, na kumbe kisa ni huyu mzee,…’akatulia akimuangalia mume wake.



    ‘Waambie tu, ukweli mke wangu mimi nipo tayari, maana  nilitaka wewe uje uyaseme yote, maana nikisema mimi watafikiria bado nimechanganyikiwa, waambie ukweli wote kunihusu mimi..ila sasa aujue na akisamehe ajue ni kwanini nimehangaika hivi na kwanini namuomba huo msamaha…’akasema.



    ‘Nina imani nikisema kila kitu huyu bint hataweza kukusamehe kamwe…’akasema huyo mama



    ‘Hapana mwambie tu…nipo tayari ..’akasema huyo mzee



    ‘Kwani ni lazima kuniambia…kama mnaona kuna utata, na huenda nika…lakini mimi vyovyote iwavyo, siwezi kuwa mbaya kiasi hicho, furaha yangu ni kuona nyie wawili mnarejeana kama mlivyokuwa awali,…familia yenu iwe na furaha…’nikasema.



    ‘Kiukweli…ni ngumu,…’akasema.



    ‘Ina maana mlifikia hatua hiyo, mpaka wewe na yeye mkataka kuachana,au mumeshaachana tayari…?’ nikauliza



    ‘Hatujaachana…’akasema huyo mzee



    ‘Sasa tatizo ni nini hapo….?’ akauliza mama Ntilie



    ‘Sijaachana na yeye kisheria, mnielewe hapo, lakini upendo wa kweli ni kutoka moyoni, huwezi ukaishi na mtu mpo mpo tu…ni kama unafuga nyoka,…maana mtu kama alifikia hapo, akayafanya mambo mabaya kiasi hicho, ni sawa na nyoka tu, siku yoyote angeliweza kuniua,…ohooo, hapana nyie hamjayasikia aliyoyafanya….’akasema.



    ‘Sasa mimi na kushangaa..ina maana wewe hukutaka mume wako apone au..?’ akauliza huyo mama



    ‘Kupna ni kitu kingine,.sawa nimefurahi kapona, kama binadamu maana hakuna binadamu eliyekamilika anayeweza kumuombea mwingine mabaya, akitokea hivyo, huyo ni shetani,..mimi sio shetani…ila moyoni, nikiyawazia yaliyotokea, nilivyoteseka, na walivyoteseka wengine unaaambiwa chanzo ni mtu mnayeishi naye,….’akasema



    ‘Na ni kweli ….?’ Akauliza huyo mama Ntilie



    ‘Ni kweli si huyu hapa, …muulizeni…..’akasema



    ‘Lakini hata hivyo, kupona kwake, ni kupona kwa familia, na haya yakiisha ni mafamikioa ya familia yenu au sio…sasa kama wewe upo hivyo, mnatarajia nini kwa huyu binti, kama wewe umeshindwa kumsamehe mume wako, huyu binti afanyeje sasa…?’ akauliza huyo mama Ntilie.



    ‘Hapana, yeye, ni kwa utashi wake,hilo siwezi kumuingilia na nashukuru kwa moyo wake huo, ni mtu wa pekee katika hii dunia,na sijui labda nahisi ni kwa vile hajausikia ukweli wote, kuhusu alichofanyiwa na huyu mwanaume…sijui kwanini watu kama hawa ..wanaoa…’akasema akimuangalia mume wake kwa hasira.



    ‘Lakini mama, mimi sioni kosa, kukosea kupo, ina maana wewe hujamkosea mtu, akakusamehe…?’ nikamuuliza



    ‘Si kama hivyo nilikukosea wewe, na umenisamehe lakini sio kama hayo aliyonifanyia huyu mtu…’akasema



    ‘Lakini mimi nimekusamehe sijaona kosa kubwa ulilonifanyia yeye, ..muhimu, nionavyo mimi,  ni kuliona kosa lolote ni kosa tu la kibinadamu, na wanadamu tunateleza, ten asana, muhimu ni kusameheana,na mimi nimemsamehe kwa lolote lile alilonifanyia nimemsamehe…’nikasema.



    ‘Hapana kabla hujasikia hayo aliyokufanyia, usiseme hivyo kuwa umemsamehe, nafsi itakuja kukusuta baadae, subiria kwanza, ngoja nikusimulia tu… na ukiyasikia ukimsamehe na mimi , labda…nitaweza kuingiwa na nguvu hiyo labda na mimi mungu atanijalia niwe na moyo kama wa kwako, ili niweze kumsamehe…’akasema.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Oh, kama unaona ni lazima kunisimulia, lakini…sawa,  ….lakini mimi vyovyote iwavyo, nimeshamsamehe huyu baba, yeye ni baba yangu, na alichukua jukumu hilo, kama baba yangu, na wewe ni mama yangu ulinichukua kijijini kwa wema wako, yaliyotokea ni mapito tu, …’nikasema.



    ‘Huyu ndio binti yangu, natamani ningelikuzaa mimi…’akasema mama Ntilie



    ‘Hata kama hujanizaa nakuona sawa na mama yangu, sitakusahau maisha mwangu …’nikasema kumuambia huyo mama Ntilia, na huyo mam Ntilia akainua mkono juu wa ushindi.



    ‘Haya tuambie hayo ambayo huyu mbaba alimfanyia huyu binti…..’akasema huyo mama Ntilie,na huyo mama akamgeukia mume wake na kusema.



    ‘Upo tayari mume wangu niyaseme madhambi yako yote…?’ akaulizwa



    ‘Ndio maana nilisubira uje uyasema yote wayasikia,usifiche kitu hata kimoja..nipo tayari…’akasema



    NB: Haya yale maswali yote yatajibiwa humo…





    WAZO LA LEO: Tukikoseana ni wajibu wetu kusameheana, ni mangapi tunawafanyia wengine, mabaya zaidi, lakini tunasamehewa, ni mangapi tunamkosea mola wetu anatusamehe, tunaiba maofisini, njiani ..kwa dhahiri na kwa kificho, tunafanya makosa mbali mbali, pasi na kuonekana, lakini tukitendewa sisi ni wepesi, kutumia mikono yetu hata kuua,..chuki zipo mbele kuliko upendo,  je ingelikuwa hivyo, tunafanyiwa sisi, tungelikuwa hai……tusamehe ili na sisi tuje kusamehewa.



    Mnajua kuna vitu vingine ukivisikia kwa watu utasema wanazusha, huwezi kuamini, kuwa binadamu anawezaje kudanganyika na kufanya mambo mabaya bila kufikiria athari zake baadae, bila kujali familia yake, bila kujali watu wengine, lakini zaidi bila kujali damu yake mwenyewe ..mimi sikuamini hilo kabla…’akasema huyo mama



    Yule mzee pale akawa kainama huku kashika shavu, akiashiria kuhuzunika sana

    Mimi na mume wangu tulioana bila ridhaa ya wazazi wangu, labda hilo naweza kusema linaweza kuwa ni sababu sikuwa na radhi ya wazazi wangu,labda,…imefikia kila likitokea baya wanasema tulikuambia,sasa ubebe mzigo wako mwenyewe, wanadai walishamchunguza mume wangu na kugundua kuwa hataweza kubadilika, na mimi sasa nimeliamini hilo…



    ‘Sio kweli….’akasema mume wake kwa sauti ya unyonge.



    Kumbe mume wangu baada ya kuona hilo kuwa wazazi wangu hawamtaki, yeye akaenda mbali zaidi na kufikiria kuwa anafanyiwa hivyo kwa vile anatokea kwenye familia masikini, kakulia kwenye mazingira ya kimasikini..ndio maana hathaminiki, kwahiyo alichofanya yeye ni kutafuta njia ya kulipiza kisasi,..nakumbuka siku moja tulipokwenda kusema sisi tutaoana mume wangu wakati anajibishana na wazee aliwaambia



    ‘Wazee wangu, mimi sikupenda niwe masikini au familia yangu iwe masikini, yote ni maisha tu, na huwezi kujua, ipo siku naweza kuwa kama nyie, na mkawa mnanitegemea mimi…’aliwaambia wazee wangu.



    ‘Sawa lakini hatutaki wewe umuoe binti yetu, maana wapo wengi tu, unaweza kuwaoa, mnaoendana nao, sisi tunajiuliza ni kwanini huyu, sisi tuna kujua wewe vilivyo.., tumepeleleza nyendo za kizazi chako na hata wewe mwenyewe ulivyokulia, hutaweza kutulia wewe, una tamaa, japokuwa hapo ulipo hauna kitu, ukipata utabadilika,…sisi ni waze tunajua mengi….’wakasema.



    ‘Wazee ipo siku mtanishangaa, ipo siku na mimi nitakuwa kama nyie na nyie mtakuwa hamna kitu, hilo nawahakikishia,.mimi nawajali na nitawasaidia kama wazazi wangu….’akasema



    ‘Utafanyaje wewe…?’ akaulizwa na wazee wangu



    ‘Katika dunia hii hakishindwi kitu ukiwa na nia, mimi nina nia ya kufikia hapo mlipo,  na ipo siku nitafanikiwa tu wazee wangu, na huwezi jua, ipo siku na nyie mtahitajia uwepo wangu, tuombeeni tu mungu, ipo siku mtajijutia, na siku ya leo iwepo kama kumbukumbu…’akasema.



    ‘Kwanini unasema hivyo…hamna haja ya kubishana na wazazi wangu nimeshakuambia nitasimamiwa ndoa na baba mkubwa, inatosha, sipendi hayo maongezi yako..?’ mimi nikamwambi ili tuondoke hapo.



    ‘Wewe huoni wanatufanyia hivi kwa vile wao wana utajiri, utajiri wao ni nini si mali tu, mali si inatafutwa, na sisi tutaitafuta kwa njia yoyote ile,..na huenda hata hiyo mali yao hawakuipata kwa halali, ngoja na mimi nitaitafuta wewe ngoja tu…’akasema .



    ‘Kiukweli kipindi hicho nilijua kwa vile anasoma , kwa vile ana juhudi ya kutafuta basi atafanikiwa kwa wivu huo wa maendeleo kumbe mwenzangu alikuwa ana ajenda yake kichwani, ana wivu wa kishetani, lengo lake ni kujitajirisha kwa haraka, kwa njia za kishetani..



    ‘Sijui alikutana na nani akamdanganya, pamoja na usomi wake wote huo, akakubali kujiingiza kwenye mambo ya kishirikina, akaenda kwa waganga wa kienyeji, akadanganywa…sijui elimu yake ilikuwa na maana gani sijui, labda ni kweli kama walivyosema wazazi wangu….’akasema.



    ‘Sikutaka kuyaongea haya tena….maana jinsi ninavyozidi kuyaongea ndivyo hasira zinazidi kunijaa …nilishaamua basi bora nibakie mwenyewe na hayo yaliyopita yapite tu,….’akaashiria mikono ya kukata tamaa.



    Sasa kilichofanyika kipindi hicho ni kuwa,Mume wangu akawa ananiaga kuwa anakwenda safari za kikazi,mikoani, kumbe safari hizo zilikuwa sio za kikazi hasa, niliulizia kazini kwao, wakasema hawajawahi kumtuma huko kwenye huo mkoa, haya niliyafanya kabla sijafunuliwa huo ukweli, kumbe yeye alikuwa akienda kwa mganga mmoja ambaye wanasema anaaminika kwa mambo hayo….’akatulia.



    ‘Sasa huko ndio wakamdanganya, kuwa akifanya hiki na kile atafanikwia atakuwa tajiri, kama wazazi wangu, na zaidi ya wazazi wangu muhimu ajitahidi aibe nyota ya wazazi wangu,..sasa sijui nyota za mtu zinaibiwaje, …wenyewe wanajua walichokifanya, ila alitakiwa afanye mambo kadha wa kaadha, kama alivyoelekezwa,..hakuwa peke yake mwenye ndoto hizo za ajabu, alikuwa na wenzake na wote hao wameishia kubaya kama alivyoishia huyu mwanaume hapa….’akasema



    ‘Huyo mtu waliyemuendea alitaka kuwakomoa, yeye naye alikuwa na visasi vyake akaona atumie mwanya huo kufanikisha mambo yake, sijui kwanini wanadamu tunachukiana, wajinga hawa wakaingia kwenye anga za huyo mtu….’akatulia.



    ‘Aliporudi nikamuona mwenzangu kabadilika, kipindi hicho sikuwa nafahamu lolote, maana nishapenda tena, namuamini sana muda huo, haniambi mtu kuhusu yeye,  kuna mambo alinifanyia mengi mabaya lakini kwa muda huo nilikuwa siyaoni, akawa ananitumia kinamna nisiyojua kuiumiza familia yangu…’akatikisa kichwa kwa kusikitika.



    Ni mambo mengi mabaya ,na sikupenda kuyaongelea,…na mengi aliyanifanyia aliyafanya nikiwa usingizini, kama alivyoelekezwa, na huyo mtaalamu wao …mimi nikawa napata shida sana, nikawa naumwa, nasumbuliwa na mambo ya ajabu ajabu, nikaenda hospitalini, nikapimwa,…nikawa na magonjwa ambayo sikuyaratajia,…nikatibiwa lakini yakawa yanajirudia rudia….mpaka madocta wakanitilia mashaka…ikafika sehemu mimi mwenyewe nikawa sipendi kabisa wajibu wangu wa ndoa…’akatikisa kichwa.



    ‘Yote hayo nilifanyiwa ili nyota ya mali ya wazazi wangu ije ihamie kutoka kwenye familia ya wazazi wangu iende kwa huyu mtu…mimi natumiwa kama chambo…huyu ni mtu kweli au ni shetani…hivi angelifanyiwa kwa wazazi wake hivyo angelifurahi, na kwanini ufanye hivyo..ina maana gani ya kwenda shule…’akasema

    Jamaa akatikisa kichwa kusikitika…



    Kwa kipindi hicho nisingeliweza kuyafahamu hayo,..maana huwezi kuamini kuwa mume wako anaweza kukufanyia mambo kama hayo, baadae akasafiri tena aliporudi, sasa ikawa kazi ya kuchukua wafanyakazi wa ndani,…alikuwepo mfanyakazi wa ndani hapa mama mtu mnzima akamfukuza anasema yeye hafai, haendi na wakati kumbe waligundua kuwa huyo mama akiendelea kuwepo hapo , wao hawataweza kufanya madawa yao ya uzandiki….’akasema akitikisa kichwa.



    ‘Yeye akaanza kuleta dogo dogo, na basi alete wasichana wakubwa, hapana analeta watoto, vibinti vya watu hata kujielewa bado, …inasikitisha sana nikiwazia hilo, ina maana hata wazazi wa hao mabinti walikuja kugundua hayo na kuiona familia yangu ni kichawi..kuna mama mmoja alikuja kwangu akanisuta kweli, niligombana naye karibu nimfunge jela,..kwa kuniita mimi mchawi, na mume wangu, nilikuwa sijui hayo..kumbe naishi na shetani ndani ya nyumba…’akasema huyo mama.



    ‘Ndugu zanguni nayasema haya kutoka moyoni mwangu mkitaka kuoa au kuolewa chunguzeni sana, huyo mtu anapotokea… mkiona mtu anamuelekeo wa mambo ya kishirikina familia yao ipo hivyo achana naye, wapo wengi wazuri, ukumbuke familia yako inajengwa kuanzia hapo..kwenye ndoa yako, ukikosea hapo umeharibu kizazi chako, mshirikina sio mtu kabisa…’akasema.



    ‘Lakini mke wangu mimi sio mshirikina ni ibilisi tu alinipitia, na hata wazazi wangu sikumbuki kama walikuwa na tabia hiyo, hayo mengine walizuliwa tu, sio kweli….’akajitetea.



    ‘Si umesema nieleze kila kitu, sasa kwanini walalamika, au niache kuelezea….?’ Akaulizwa



    ‘Hapana endelea tatizo unahitimisha kuwa mimi sifai,..mshirikina na tabia hiyo ipo kwenye damu, hapana hiyo tabia ilikuwa ya kughilibiwa tu, mimi naweza kubadilika na nakuhakikishia nitabadilika hilo nakuahidi na ikitokea tena niua,..tuachane kabisa,…’akasema.



    ‘Mimi sio muuaji, mimi sina roho mbaya kihivyo, yaliyotokea hadi kuja kuwafukuza hawa mabinti ni kutokana na wewe…mimi sipo hivyo kabisa, nawapenda wote bila kujali huyu ni nani, ila sipatani na matendo mabaya hasa ya kishetani, …’akasema huyo mama.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Sawa endelea mpendwa, samahani kwa kukukatili…..’akasema



    ‘Kumbe kuwaleta hao mabinti wadogo ni moja ya masharti waliyopewa na huyo mganga wa kienyeji, mabinti wadogo ambao hawajaguswa na mwanaume, eti ndio wanaofaa kwenye hizo dawa zao za kishirikina ambazo eti  ndio hizo zitakazowaletea utajiri, ni ujinga, elimu ndogo ya kufikiri,, na nashukuru sikuwahi kuzaa mabinti maana wangelikuwepo kwa jinsi nilivyosikia,ungewatumia hao hao…’akamuangalia mume wake kwa hasira..

    ‘Kwani walikuwa wakifanyiwa nini …?’ akaulizwa na huyo mama Ntilia.



    ‘Mambo mabaya, wanazalilishwa, eti ile damu yao ichukuliwe na hao wachawi, wakachanganye na makafara yao, ni watu wa ajabu kabisa, ….sasa hebu niambie huyu sio mwanga mchawi, mimi niishi na mwanaume mchawi, jamani hamnitakii mema nyie, leo kanifanyia hivyo kesho itakuwaje,….’akatikisa kichwa kukataa.



    ‘Mke wangu usiseme hivyo…’akasema mume wake.



    ‘Wanadai dawa hizo zilikua zikifanyika kwa awamu ,eti awamu ya kwanza ni kuhamisha nyota ya wazazi wangu ije kwenye familia yetu, lakini kwanza ipitie kwangu, kama mrithi,…halafu sasa itoke kwangu iingie kwa huyu mwanaume..mimi hapo ndio natumika, usiku nafanyiwa mambo mabaya..ni mabaya kweli..sitaki hata kuyasemna.



    Sasa baya zaidi, kwa laana , mwenyezimungu ni mwingi wa rehama akampiga kiboko huyu mume akashikwa na ugonjwa wa kisukari, si unajua tena kisukari, alikuwa hana tatizo hilo ghafala akaanza kuhisi hali fulani mwilini, jogoo hawiki, na kazi anayotakiwa inatakiwa jogoo awike, …kuona hivyo akaingiwa na mashaka, hapo akaniambia

    ‘Mkee wangu, nahisi nina tatizo…’akaniambia



    ‘Tatizo gani…?’ nikamuuliza hapo na mimi nilishahangaika na hali yangu mengine nilikuwa hata simuambii, sikutaka kuyaongea, nimeyaongea baada ya kupata uhakika huo, na alipotka hapo nje na kumuuliza baadhi ya maswali ambayo bado nilikuwa sia uhakika nayo, akakiri kuwa ni kweli, basi…nikajua huyu mtuu sio mtu…’akasema.



    ‘Watu hawa walifikia kula nyama za wafu..hawa si wanga hawa…, wachawi wakubwa…, mnakula nyama za watu waliokufa..hahaha, hapana sio mimi, nasema sio mimi..siwezi kuishi na mchawi ndani ya nyumba yangu…’akasema.



    ‘Lakini mke wangu nilidanganywa tu, ndio maana nilikuambia yote hayo,…kama ningelikuwa mchawi eeh, ningewezaje kukubali hayo, nilidanganywa tu,…ni shetani alinipitia, nikijua nitakuwa tajiri kama wazazi wako….’akasema .



    ‘Sasa tatizo likaanza mwilini mwake, alipoenda kupimwa akaonekana ana kisukari ndio sababu, jogoo hawezi kuwika hapo jasho likaanza kumtoka maana ili dawa hizo zifanye kazi anahitajika kuwazalilisha mabinti wa watu wadogo,..na alipewa muda fulani , baada ya hapo ataanza kuupata utajiri,…sasa tatizo limetokea kabla hajamaliza hiyo kazi, masharti yakaanza kumshinda…, shetani ana mbinu, lakini hawajui kuwa mungu yupo, mungu humlinda mja wake, kwa namna ambayo huwezi kutegemea.

    .

    ‘Kuna kipindi mama aliniita, akaniambia je kweli nyumbani kwangu kuna usalama,…nilishangaa mama alijuaje kuwa nipo kwenye matatizo,…mimi kwa kujivunga nikasema, hakuna kitu kinanisumbua, sikumuelewa kipindi hicho, nikajua ni zile chuki zao, kumbe wao walishaona,..unajua tena wazee wana njozi zao, mama akaniambia, huyo mume wako hakufai, uwe makini,..mimi sitaki muachane naye, ila bidisha ibada na umuombe sana mungu wako akulinde..bila hivyo mtaangamia, …



    ‘Kwangu mimi  nikafuata kama alivyoniagiza mama, na mambo yangu yakaisha na ndio mume akaanza kulalamika kuwa ana matatizo, ..yeye aliporudi kwa huyo mtaalamu wao, akaambiwa kwa hivi sasa hawezi kumsaidia, ila itakuja kuisha hiyo hali akapewa, dawa, lakini akaambiwa dozi haitakiwi kukatizwa, kwahiyo inatakiwa kutafutwa njia nyingine mbadala ya haraka,…’akasema.



    ‘Njia gani maana hali yangu ndio hivyo, yaani sina raha…’akasema mume wangu.



     ‘Kuna njia mbili ya kwanza, ambayo ndio naiona ni nzuri kwako maana hatutawaruhudu mashetani watusaidie..ni wewe kumtumia  mtoto wako badala yako..’akaambiwa



    ‘Mtoto wangu, hapana mtaalamu usiingize mtoto wangu kwenye mambo haya…’akalalamika.



    ‘Ndio nja rahisi nyingine itakuwa ngumu sana kwako, makafara yake ni mabaya zaidi, na ukumbuke umeshaanza huwei kuacha, huoni umeshaanza kuneemeka, hali imebadilika au nadanganya…’akaambiwa



    ‘Ni kweli mtaalamu…’akasema



    ‘Na kwa mtoto wako ndio itauwa bora zaidi, ..kwasababu ni mtoto wako na mambo kama tunavyoyafanya kwako, kwani tukifika kwako unatuona, hutuoni, ila tunakuchukua wewe tunafanya yetu tunaondoka, au sio,…na tutafanya hivyo hivyo kwa mtoto wako, lakini ni lazima muwe naye sambamba, na ukubali kwa utashi wako,…wewe au yeye hamuwezi kuona, wakati hayo yanafanyika… inafanyika usiku watu wamelala,…hata nyie mnakuwa kama magoigoi tu, mnafanyizwa bila kujijua, asubuhi utaona dalili tu…’akasema.



    ‘Kwa vipi sasa…?’ akauliza maana ni kweli hali ya kimaisha ilishaanza kushamiri, uone mungu anavyo mpima mwanadamu unataka utajiri kwa njia hiyo anakujaribu kwa kukupa kidogo tu, kupima imani yako…wewe unazidi kusahau, …shetani anashangilia,…’akatulia.



    ‘Kama ilivyokuwa awali,…ina maana sasa mtoto wako ndiye atashika usukani wako, …ila wewe na yeye mtakuwa pamoja, yeye anatekeleza majukumu wewe unamshikilia mkono ili iwe kitu kimoja, iwe ni kama wewe unafanya ili kafara likamilike …’akaambiwa



    ‘Sawa kama ni hivyo hakuna shida…’akasema



    ‘Lakini ili huo usukani yeye , mtoto wako aweze kuushika ni lazima awe kama wewe, ina maana ile hali yako inahamia kwa mtoto wako, unanielewa hapo…’akaambiwa



    ‘Kwa vipi…sasa hapo…?’ akauliza



    ‘Ina mtoto anakuiwa ni wewe, si ndio hivyo..sasa takuwaje ni wewe, ina maana kuna mambo anatakiwa kuyafanya ili awe ni wewe,…’akaambiwa ..hapa nilichoka, siku nilipoambiwa hivyo, nilidondoka nikazimia, kwa hilo achilia mbali hayo yaliyopita, kunizalilisha nikiwa nimelala, kula nyama za wafu, lakini hili, haniambii mtu hapa, sitaki sitaki, ni bora niishe bila ndoa, sitaki….’akasema na akawa kama anajisikia vibaya.



    ‘Vipi …huwezi kuendelea?’ akaulizwa na mama Ntilie.



    Huyo mama alibakia vile vile ..huku anatikisika kwa hasira…, kumbe alikuwa analia, alipoinua kichwa, usoni kulijaa machozi.



    ‘Niacheni jamani, siwezi,…nimesema siwezi, kama ndoa ndio hivi sitaweza, wazee wamenishi sana, lakini hapana,.. sitamki huyu mtu tena nyumbani kwangu….’akasimama akitaka kuondoka



    ‘Lakini ulishanisamehe….’akalalamika



    ‘Kukusamehe sawa nimekusamehe, hilo halina shaka, lakini sio  kwa wewe kuwa mume wangu tena, tutafanya taratibu za kuachana, na nitakupa kila ukitakacho, ukitaka nyumba, nitakupa, lakini wewe ….hapana….’akasema



    ‘Mama mbona unaniacha njia panda, nimesikia yote hayo, najua ni makosa makubwa sana, lakini yanaweza kusameheka,..’nikasema



    ‘Hujasikia hilo kubwa lao,hujasikia walivyokuwa wakija kwako usiku, walivyokuwa wakikufanyia…..hapana…ndio utaona kuwa huyu sio mtu wa kuishi naye…’akasema



    ‘Lakini nakumbuka yule marehemu alisema…hawa walikuwa wanafanyiwa na wachawi, na sio kwa dhamira yao…’nikasema.



    ‘Hivyo ndivyo walipanga , huyo mtaalamu aliwaambia najua jinsi gani y akutuweka sawa, ukumbuke zile nyumba tatu, yaani ya kwangu na marafiki zangu wawli zilifanywa ndio makao ya watu hao kukutana, na walishahisi kuwa wamegundulikana, kwahiyo ili wajilinde wakabuni uwongo huo, ….’akasema.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ‘Mungu wangu ni kweli baba…?’ nikamuuliza.



    ‘ Ni kweli ndio maana nilitaka yeye aongee ili ….muone kuwa nimekosa na nimetubu madhambi hayo yote , sitarudia tena…’akasema.



    ‘Sasa wakati tunahangaika kumbe ulikuwa ukitusanifu baba, kwanini ulifanya hivyo….’nikasema.



    ‘Ni shetani tu,..nilitaka niwe tajiri kama wazazi wake mke wangu ili nisisanifike…na sijui kwanini akili yangu ilikuwa haiwezi kutafakari, kumbe yote yalikuwa ni viini macho huyo mjaa alikuwa akitutumia kwa masilahi yake…’akasema .



    ‘ Ni nani huyo…?’ nikauliza



    ‘Ni marehemu…’akasema



    ‘Ina maana kumbe ni yule yule aliyekuja kutuambia kuwa yeye atatusaidia, ….oh, sasa yule rafiki yangu alihusikinaje , mbona alimtumia yeye…?’ nikauliza



    ‘Yule ni binti wa adui yake mkubwa,…na binti huyo aliamua kutoroka kwao baada ya kugundua kuwa baba yake huyo ana tabia hizo chafu, na hapo hapo, alitakiwa kuolewa na huyu marehemu ambaye ndiye alikuwa mganga wa huyu mwanaume hapa, umenielewa hapo,..…lakini hakutakiwa kumuambia mtu yoyote yule…, akisema tu, atadhurika, kwa imani zao, ndio maana hata siku moja hataweza kukubali hilo…’akaambiwa



    ‘Ina maana anayajua yote hayo, kuwa…..’nikauliza



    ‘Hajui..haya ya kuwa mume wangu anahusika, hajui kabisa, haya tumekuja kuyafahamu kipindi hiki mume wangu alivyoanza kuchanganyikiwa, mume wangu alianza kutuelezea yote huku akiomba msamaha akijua sasa anakufa, kwa jinsi alivyokuwa akiteseka…, na tulijua anatania, labda ni kwa vile kachanganyikiwa, lakini nilipofika hapa leo , akiwa na akili yake vyema,  kumuuliza akasema yote aliyotuambia na kuniambia mimi mwenyewe yalikuwa ni yya kweli…kwakweli nilichoka, ndio maana nilibakia nje nikilia, …’akasema.



    ‘Sasa mama ina maana huwezi kumsamehe kwa hayo,..je ukifanya hivyo mimi nifanyeje…najua kakosea hata hivyo ili ajirudi na kujisikia kasamehewa, kiukweli, ni wewe kumkubali na mrejeee kwenye maisha yenu ya kawaida, na najua hatarudia tena, mimi nipo tayari kumsamehe, na nimeshamsamehe , na sina kinyongo naye japokuwa inauma sana na sasa kuna uhakika labda hii mimba haina uhusiani na yeye au shetani….’nikasema.



    ‘Hapana, kumsamehe sawa,… sio shida, maana yaliyofanyika yamefanyika, mimi nimeshamsamehe, lakini kutokana na hayo aliyokuja kumfanyia mtoto wangu, ..siwezi kumrejea, nitasemaje kwa mtoto wangu, nitamuangaliaje mtoto wangu…mtoto wangu sasa hivi anaozea jela, mimi nikae na mtoto niamuambie nilimsamehe baba yako kwa hayo aliyosababisha hadi upo hivyo….nitakuwa na akili kweli…’akasema.



    ‘Lakini mtoto si hajui hayo..?’ nikamuuliza.



    ‘Nitakuelezea sehemu nyingine ndio utagundua ukweli wa chuki yangu, na nikimaliza tutaagana,..maana inaumiza sana…’akasema.



    ‘Tumalizie basi mama….lakini umsamehe tu …au sio mama.’nikasema nikiwa na hamasa ya kusikia zaidi, lakini pale nilipo moyo wangu ulishaanza kudunda, sikuamini hayo, ina maana basi huyu mtoto anaweza kuwa ni mtoto wa huyo mtoto wake,…niligeuka na kumuangalia yule mbaba, alikuwa kainama, kama analia,..lakini kuna kitu kilianza kunijaa, kama hasira, kwanini huyu mtu akafanya hivyo, kwanini…nilijaribu kujizuia, lakini ...



    ‘Mke wangu kama hutanisamehe, …kama ulikuwa unanidanganya, kama..basi mimi sina maana ni bora nirejee kwenye huo ukichaa, au nikajinyonge tu…wewe unajua sikufanya makusudi , wewe unajua yote nilikuwa nataka niwe kama wazazi wako ili wasitunyanyase, niliyafanya kwa ajili yetu,…ndio nilikosea, na…yule marehemu alinitega mpaka nikaweza kumweka mtoto wetu, iliniuma hata mimi….nakuomba nipo chini ya miguu yako…’akasma sasa akimuendea mkewe,



    Mkewe akamkwepa na akawa kama anamsukuma ili asimsogelee..jamaa akazidi kumuendea..niliona huyu mama akishika kichwa nahis alikuwa ana maumivu ya kichwa, au…



    Mara yule mama akawa anayumba …mimi nilikuwa karibu yake nikamdaka, kabla hajadondoka chini,  na wakati huo mimi nikawa sijihisi vizuri, sijui ni kwanini, nikahisi ghafla giza likitanda usoni, mimi na huyo mama sote tukaserereka na kudondoka sakafuni…na jamaa alipoona hivyo haraka akasimama na kumsogelea mke wake.



    Na muda huo huo simu ya huyo mama ikawa inaita, nani ataipokea wakati mama hajiwezi, na mama Ntilia akaichukua na kusikiliza

    ‘Halloh nani mwenzangu, eeh,…. polisi… ……mimi sio mwenye simu…..’



    NB: Ngoja niishie hapa kwa muda, tutaendelea baadae, maana inauma,..binadamu sio wazuri, kwanini..



    WAZO  LA LEO: Jinsi utandawazi unavyozidi na kuwa huru zaidi, ndivyo mwanadamu anavyozidi kutakabari, sasa ivi Mwanadamu kafikia hatua mbaya sana, anafanya mambo ambayo hata shetani atakuja kutushangaa, yanayotendeka kwa hivi sasa ni ya aibu na yamezidi hata hayo tuliyowahi kusimuliwa kwenye vitabu vitakatifu, watu wanafanya mambo zaidi ya mnyama, jamani, jamani tunatafuta nini, wakati dunia hii ni ya kupita tu, wangapi wangapi walikuwepo sasa hawapo, ina maana wao hawakutaj kuishi…tujirudi jamani, tuache, tutubu, turejee kwenye njia sahihi.





     Tumuombe mola wetu atulindie vizazi vyetu na atuwezeshe kuyashinda majaribu haya yanayotuzunguka kwa sasa, vijana wetu wanakulia kwenye mitihani mikubwa bila ya msaada wa mola wetu hawataweza. Ewe mola wetu tusaidie na utuongoze kwenye njia sahihi…..



    Ilichukua muda, kabla huyo mama hajazindukana, mimi sikuwa nimepoteza fahamu kabisa ilikuwa ni kizunguzungu tu, ndicho kilinifanya nidondoke na huyo mama, nikawa nimekaa nikisubiria hali irejee vyema, na mama Ntilie akaniuliza naendeleaje nikasema;



    ‘Mimi nipo sawa, tuendelee…’nikasema hivyo.



    ‘Polisi walikuwa wanataka kuongea na huyu mama, …wanamuhitajia kituoni leo hii..nilishindwa kuwapa majibu ya haraka …sasa sijui huko kuna nini…’akasema.



    ‘Tusubirie ikibidi nitaenda mimi mwenyewe…’akasema huyo mzee



    ‘Na hiyo hali , ni nani atakuelewa huko…’akasema mama Ntilie



    Na muda huo ndio huyo mama akazindukana, na akawa anajaribu kuituliza ile hali, kwa kujinyosha nyosha na kutikisa kichwa, na alipoulizwa hali na kama inawezekana apelekwe hospitali akasema;



    ‘Hapana mimi nipo ok…sijui ni kitu gani kimenipata….ila nataka kuondoka…’akasema

    ‘Polisi walipiga simu, walikuwa wanataka kuongea na wewe…’akaambiwa

    ‘Oh, basi mimi nakwenda huko huko najua labda ni kuhusu shauri la mwanangu,…’akasema sasa akitaka kuondoka



    ‘Lakini kwa hali hiyo utaweza kwenda huko…?’ akaulizwa



    ‘Ndio nitaweza hakuna jinsi,  japokuwa, mpaka sasa sijajua la kufanya ili kwanza atoke,..lakini yeye anahitaji maelezo kujua ni nini kilimtokea, anasema anahis mimi kama mama au baba tunafahamu tatizo alilo nalo,…kwani huyo binti aliye naye kamwambia eti sisi wazazi wake tunahusika,…sasa mimi nitamuambiaje….’akasema mama



    ‘Mimi nitamuambia kila kitu….na ni bora nikafungwe mimi mwenyewe…’akasema yule mzee.



    ‘Usije kuthibutu kumwambia kitu, mpaka nihakikishe nimeshindwa kumtibia, nina uhakika tatizo hilo litakwisha, lakini sijajuia ni nani wa kulitatua hilo…’akasema huyo mama



    ‘Mama mimi nina imani litakwisha tu….na kwisha kwake inatokana na nyie wawili…’nikajikuta nikisema hivyo, na sijui kwanini nilisema hivyo



    ‘Sawa nitarudi tuyamalize haya mazungumzo, lakini sio leo tena…’akasema akijiandaa kuondoka

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Ngoja tuongozane…’yule mzee akasema.



    ‘Na nani, …hapana, wewe bakia hapa hapa,…’akaambiwa na huyo mama akaondoka



    Tuendelee na kisa chetu



    ************************



    ‘Natabakiaje hapa kwani hapa ni nyumbani kwangu…’akasema yule mzee na kuanza kuondoka kumfuata mkewe, na sisi tukabakiwa tukiwa na maswali mengi kichwani. Huku mama Ntilie akisema;



    ‘Huyu mzee bado akili haijakaa sawa, na shukuru kuwa hiyo mimba sio ya kwake….’akasema



    ‘Hata kama ingelikuwa ni ya kwake nisngelikubali anihudumie, sitaki kabisa…’nikasema



    ‘Kwahiyo sasa hiyo mimba itakuwa ya nani…?’ akaniuliza mama ntilie



    ‘Kiukweli mpaka sasa siwezi kujua ni ya nani…na sina haja ya kutaka kujua…’nikasema



    ‘Kwa maelezo ya mwanzo ya huyo mama nilijua labda itakuwa ya huyo mzee, lakini sasa anasema mumewe alianza kuumwa, akawa hana nguvu tena…je alianza kuumwa wakati umeshafika au kabla…hapo mimi sijaelewa…?’ akauliza.



    ‘Mimi sijui, maana ndio nimeanza kuyasikia hayo hapa kwa huyu mama, japokuwa kuna maelezo yalitolewa awali kuwa huyu baba na kijana wake wanahusika,….lakini haya ya sasa yanazidi kunichanganya,..ina maana kuna namna nyingine ilifanyika, ….hata sijui tuyaache tu…’nikasema.

    ‘Namna nyingine kwa vipi, kuwa ulipandikiza mbegu ..kama ng’ombe hahaha..hapana kati ya hao wawili kuna mmoja anahusika, sasa baba katoka, kabakia kijana, …haya jiandae kama ni kijana ..inabidi akuoe, au sio…?’ akauliza



    ‘Sitaki na simtaki kabisa…huyo wanaendana na yule binti, rafiki yangu, huoni mpaka wamefungwa, kumbe walikuwa na jambo lao la pamoja…wanafaana hao…’nikasema



    ‘Mhhh….hapo sasa, unalo, huyo mtoto ni wako, na huna jinsi utamzaa, bila ya kujua baba yake ni nani, lakini mimi nashindwa kuelewa, ilikuwaje, watu waingie ndani usiku, wakufanyia waliyokufanyia wewe umelala tu kama gogo,…ndio naamini kuwa ni lazima kulikuwa na mtu wa ndani alikuwa anahusika….umeona eeh…’akasema.



    ‘Kama ulivyosikia, wao wanakufanyia madawa unakuwa hujijui,…ndio hivyo ilivyofanyika…, kiukweli mimi sijui..naona ni mtihani tu umenikuta…’nikasema.



    ‘Ingelikuwa ni mimi, ningeliwaganda hao hao, maana sababu kubwa ni wao, lakini utamgandaje mtu kama huyo, mtu kachanganyikiwa,…maana bado hapo naona hajakaa vyema, akili bado haijatulia, hata hivyo, wao wanastahiki kubeba gharama zote…ngoja kama tutaendelea kuwa pamoja nitakusaidia kupambana na hao watu hadi kieleweke…’akasema.



    ‘Haina haja, nilishaamua nitapambana mwenyewe na maisha yangu, nimegundua kuwa ili nikae salama, basi nitafute njia ya kusimama kwa miguu yangu mwenyewe,…na muhimu nimeshamkabidhi mwenyezi mungu yote yaliyotoea, mungu…’nikasema.



    ***********



    Ilikuwa siku nyingine huyo mama alikuja pale tunapofanyia biashara, mumewe hakuwepo, kwani alipoondoka hapo kwenda polisi na mumewe alimfuata huko, sasa hatukuwa tumejua ni nini kitokea huko, tukawa na hamasa ya kusikia kutoka kwa huyo mama.



    ‘Mumeo yupo wapi…?’ tukamuuliza



    ‘Hata sijui huko alipo, siku ile alinifuata huko polisi, hakuwaelewana, ikabidi polisi wamfukuze, wakijua yeye bado kachanganyikiwa, na nilimuambia wazi atafute sehemu nyingine ya kuishi hadi hapo matatizo haya yatakapomalizika.



    ‘Kwahiyo mama uamuzi wako ni upi…?’ nikamuuliza



    ‘Nimeshaamua sirudi nyuma,….hilo hakuna wakunishauri …..nasubiria watoto angu waje, niwaelezee maamuzi yangu na wao watajua la kufanya, ila, sio wao au wazazi wangu watakaoweza kulimaliza hili, ni mimi mwenyewe ndiye nitalimaliza…’akasema.



    ‘Na vipi kuhusu mtoto…?’ tukamuuliza.



    ‘Kulikuwa na makubaliano yafanyike kati ya walioibiwa na hao wezi, yaani yule binti na mwanangu, tukaishia kulumbana tu…, wao wanataka walipwe kila kitu…, nikawaambia kulipwa, itachukua muda, na kulipwa ina maana ni mimi sasa nibebe mzigo huo…mimi nina kosa gani…sitaweza kulipa kwa hivi sasa, na aliyeiba ni huyo binti, mtoto wangu anasema hakumshauri binti aibe, yeye alimpigia simu kuwa kafanya hivyo, wakati ameshaiba na kutoroka

    ‘Aliniambia mimi nina matatizo, ambayo yeye anajua jinsi gani ya kutibiwa…’akasema kijana wangu.



    ‘Matatizo gani…?’ akaulizwa.



    ‘Ya kiafya, nisingelipenda kuyaongelea hapa maana yatanizalilisha….’akasema



    ‘Utayaongea tu, maana hapa unatakiwa uongee kila kitu,…sasa kwahiyo wewe ukaenda huko ..kwa huyo binti?’ akaulizwa.



    ‘Ndio nikaenda kama alivyonielekeza….’akasema

    ‘Ndio ulipofika akakuambiaje…?’ akaulizwa



    ‘Akaniambia kafanya jambo baya sana, hakujua wakati analifanya, kuna kitu kilimsukuma afanye hivyo, kuna kitu kila siku kilikuwa kikimshawishi afanye hivyo, na ikafikia hatua kikamuambia haya muda ndio huu fanya, usipofanya sasa hutaweza tena, na utaendelea kuwa masikini maisha yako yote…akafanya na , sasa kaanza kujuta na hajui atafanyaje kujirudi na kuliongelea hilo kwa hao aliowafanyia…’akaniambia.



    ‘Kwahiyo mpaka unafika kwake ulijkuwa bado hujajua kuwa kaiba…?’ akaulizwa.



    ‘Kiukweli mimi nilikuwa bado sijajua hilo, nashangaa watu wanadai kuwa nimeshirikiana naye, mimi nilikuwa sipo, niliafiri kidogo, niliporudi sijakaa vyema ndio napata hiyo simu…’akasema.

    ‘Ulisafiri kwenda wapi…?’ akaulizwa



    ‘Kuna sehemu nilielekezwa kuwa kuna mtaalamu wa kusaidia matatizo yangu ya kiafya ndio nilisafiri kwenda kwake…’akasema.



    ‘Ulisafiri kwenda wapi, maana tunahitajia kuhakiki ukweli wako….?’ Akaulizwa



    ‘Tanga….’akasema



    ‘Sasa ulijua muda gani kuwa huyo mdada kaiba..?’ akaulizwa.



    ‘Aliniambia yeye mwenyewe nilipofika, aliniambia alitoroka pale alipokuwa akifanyia kazi, na pesa nyingi, akiwa na maana atakwenda sehemu azifanyie biashara, akizalisha atazirejesha kwa wenyewe…’akasema.



    ‘Nikamwambia azirejeshe haraka kwa wenyewe….’akasema



    ‘Akasemaje…?’ akaulizwa na polisi



    ‘Kaibiwa zote, walikuja majambazi na bunduki wakamvamia na kumpora kila kitu, nahapo alipo hana hata pesa ya kula na anaogopa akitoka atakamatwa na polisi…kwahiyo ananiomba msaada wa pesa, na mimi nikamwambia sina pesa, mwenyewe nahitaji pesa ,wazazi wangu hawataki kunipa pesa tena…’akasema



    ‘Kwanini sasa hukutoa taarifa polisi kwa haraka ulipoonana naye, mpaka tulipoonza kukufuatilia, na kuwakamata…?’ akaulizwa na polisi.



    ‘Muda huo nilikuwa sipo vyema, akili yangu ilishavurugika, nina matatizo yangu, nina shida zangu, na nilijua anataka kunisaidia kumbe anataka mimi nimsadie…’akasema.



    ‘Kwasababu ya madawa ya kulevya au sio…?’ akaulizwa



    Hapo akatulia kimia, na aliposhinikizwa ndio akakubali kuwa alihitajia madawa na pesa hana, na alihitajia msaada wa huyo binti kwa vile kasema kuna namna ya kumsaidia hilo tatizo liishe…’akasema.



    Alipofikia hapo ndio mama Ntilie akamuuliza huyo mama.



    ‘Ina maana kumbe mtoto wako anatumia madawa ya kulevya…?’



    ‘Si ndio nawaambia mume wangu kanifanya kitu kibaya kiasi kwamba nashindwa kumsamehe,,,’akasema



    ‘Lakini sio yeye aliyemfundisha mtoto, au sio…?’ akaulizwa



    ‘Sio yeye, na hata yeye alikuwa hajui kuwa mtoto kajiingiza huko…’akasema



    ‘Sasa kwanini unamshutumu kwa kuharibika kwa mtoto…?’ tukamuuliza



    ‘Ni hivi…..’akatulia akiangalia simu yake kuna ujumbe was auto uliingia, na akajibu , halafu akasema;CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ‘Huyo mwanaume anakuja….’akasema



    ‘Anakuja hapa…?’ nikauliza.



    ‘Ndio maana alisema tuje kwako tuhakikishe tumeliweka hili jambo vyema, nilimuambia yeye anshitajika kuhakikisha wewe upo katika hali nzuri, maana wewe kumsamehe ni pamoja na kukulipa gharama zote, unakumbuka kuna kikao tulifanya nikamuambia hivyo…’akasema



    ‘Lakini mama mimi sihitaji msaada wake…nisingelipenda kumuingiza mtu kwenye haya matatizo tena…nyie wawili mnatakiwa msameheane kwangu itakuwa ni faraja…’nikasema



    ‘Hilo halina hiari….maana yote yalifanyika ndani ya nyumba yangu na waliofanya ni familia yangu, japokuwa hatuna uhakika ni nani mwenye huo mzigo, lakini wawili hao watawajibika,...na huyo mwanaume sio mtoto…mtoto aliingizwa bila hata kujua,…’akasema



    ‘Kwahiyo hata wewe hujajua ni nani ambaye tunaweza kusema ndio mwenye mtoto…?’ mama Ntilia akauliza.



    ‘Yaani sio rahisi….maana mume wangu alianza matatizo kabla hata huyu binti hajafika,….’akasema



    ‘Kwahiyo basi itakuwa ni kijana wako…’akaambiwa



    ‘Mhh…ni kwa vile sijawahadithia ilivyokuwa baadae….’akasema na kukatisha baada ya kusikia hodi, tulijua ni wateja, kumbe sio wateja.



    Waliofika walikuwa wale wanunuzi wa kiwanja wakasema ninatakiwa mimi nikafungue akaunti benki kabla ya kuanza kazi ya malipo, na walisema kwa vile bado wapo kwenye michakao ya kukusanya pesa, na haijakamilika kwanza, wao wamekuja na kiasi kidogo tu cha kufungulia akaunti, na malipo kamili yatakuja baadae, mimi nikakualiana na wao,



    Niliondoka na wao nikaenda kufungua akaunti benki, na wakati nataka kuachana nao , yule kiongozi akaniuliza



    ‘Binti, samahani kwa hili, wewe huna matatizo yoyote…?’ akaniuliza



    ‘Matatizo gani…?’ nikamuuliza



    ‘Huyu hapa ni mmoja wa wanafunzi wangu, kajaliwa kipaji cha ajabu, anaweza kukuangalia hivi tu akajua wewe una matatizo, yeye kajua wewe una matatizo …’akasema



    ‘Hapana mimi sina matatizo…’nikasema



    Yule anayeambiwa ana kiaji hicho, akanisogelea na kuniangalia usoni kwa muda halafu akawa ananitizama taratubu kushuka hadi tumboni halafu akasema;



    ‘Hiyo mimba uliyo nayo sio ya kawaida…’akasema



    ‘Mhh, kwanini unasema hivyo…?’ nikamuuliza



    ‘Mimi sijui, ila nilivyokuona nikahisi kuna uchafu mwilini mwako,…na kwa vile tunajua wapi ulipotokea maisha yako, na sasa tunagundua haya tukaona tukusaidie tu, kupambana na hili tatizo, hatuhitaji malipo yoyote, usiwe na shaka na hilo…’wakasema



    ‘Mhh..’nikaguna tu



    ‘Siku tukija kukulipa tutakuja tukiwa tumejiandaa, ni kisomo kidogo tu cha kumuomba mwenyezimungu na mengine tutamuachia yeye, na hili linatakiwa , kabla hujajifungua…’akasema



    ‘Lakini nitajifundua salama…?’ nikauliza



    ‘Baada ya maombi hayo, ya kumuomba mwenyezimungu kwa uwezo wake, utajifundua salama maana hayo waliyokufanyia ni mambo ya kishetani, na shetani hatakiwi awe mwilini mwa watu, akiwa mwilini atakusumbua sana, na mtoto atakuwa akisumbuliwa sana,…sasa kabla hujajifungua tutalifukuza hilo shetani mwilini mwako,..’akasema



    ‘Mimi hata sijui mnaongea nini…’nikasema



    ‘Tukija utajua…’wakasema na kuondoka.



    ****************.



    Siku nyingine  wakaja yule mama , sasa akiwa na yule mzee, nilifurahi kuwaona wakiwa wote sambamba…na mama akaanza moja kwa moja kuhadithia mambo ya nyumbani kwake ambayo yanamfanya asiweze kumsamehe mume wake…



    ‘Nimekuja naye kaniomba tuje kuyaongea yale tuliyotaka kuyaongea, kwa msemo wake anataka wewe, ambaye kukosea ujue alichokukosea, na pili, tuone jinsi gani ya kukusaidia, yeye, kukusaidia…’akasema



    ‘Sisi hamu yetu ni kutaka kujua, kama kuna yoyote kati ya hao wawili, yaani mume wako na kijana ambaye anahusikana na huo ujauzito,..au sio binti…?’ akasema mama Ntilie.



    ‘Ni sawa..mimi sikuona haja ya kuyafanya haya mambo yawe makubwa, yaliyopita yamepita, …ila nilitaka kujua zaidi kuhusu huyo kijana wako, imekuwaje hadi kufikia hiyo hali,…?’ nikauliza.



    ‘Ni vyema nikaelezea yote kutokea pale nilipoachia, ndio utajua jinsi gani hayo yaliyotokea yalivyoiathiri familia yangu…na kwa vile yeye mwenyewe karuhus hilo, basi ngoja niwaelezee tu, na tukitoka hapa kila mtu atajua hamsini yake..’akasema huyo mama.



    ‘Tutasameheana kiukweli…’mimi nikasema na nikijaribu kutabasamu lakini huyo mama hakutoa tabasamu akasema;



    ‘Mnajua mlipokuja nyiee mabinti wawili, yule wa kwanza,ambaye yupo jela kwa hivi sasa na wewe ndio mliowezesha haya mambo kuanza kuonekana kwa uwazi, mabinti wengine walifanyiwa mabaya lakini, labda nisema ni kwasababu ya utoto wao, sikuweza kugundua kinachoendelea, au labda kutokana na mazindiko ya kichawi hata sielewi…’akaanza kuelezea.



    Yule binti wa kwanza alifanyiwa na kushika mimba,  akaja kuitoa hiyo mimba, na ..yaliyotokea yanajulikana kwa huyu binti, sasa kwa huyu, ndio nikaamua kufanya uchunguzi wakwa kuweka vifaa maalumu chumbani kwa huyu binti, na lengo langu ilikuwa kubaini yale niyowahi kusikia , na kwa vile kuna mtu alishaniambia kweli wachawi wanaweza kuingia usiku usiwaone, lakini yeye ana vifaa vya kuwezesha kuwapiga picha,au kama picha imepigwa na karibu yake yupo mchawi au shetani anaweza kuisafisha na kuona kilichojificha.



    ‘Ndio nikawekeza hivyo vifaa….’akasema akimuangalia mume wake.



    ‘Yule jamaa aliweza kufanya hayo na siku nataka kwenda kuonana naye, akaptawa na dharura akasafiri, na kabla hajarudi ndio akaja huyo marehemu na maelezo yake ambayo, tulikuja kuyaamini kuwa huenda ndio sahihi, na kwasababu hiyo ikanifanya nisihangaike tena na huyo jamaa yangu, na mambo mengi yakawa yametokea hapa kati kati..kwahiyo hilo likasahaulika.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     ‘Ina maana mume wako na huyo mtaalamu wako, ndio waliweka hayo mazindiko aliyokuwa akiyasema yule marehemu…?’ akaulizwa.



    ‘Ndio, na hayo ndiyo yalimfanya huyo jamaa yao, kuweza kutuona hata akiwa huko kwake, na kuweza kuja usiku kwa mbinzu zao za kichawi na kufanya mamboyao bila kujulikana..na walitafuta sehemu nyingine zaidi, ndio huko kwa wale marafiki zangu, ..kote huko waliweka ili kila ninapokwenda ijulikane ninafanya nini…’akasema.



    ‘Mhh…mbona hatari…’akasema mama Ntilie.



     ‘Kama nilivyosema awali, nilipogundua hayo, nilitaka ndoa yetu ivunjwe mara moja, nikahangaika kisheria,lakini wazee wakagoma, wakanishauri sana, na kunisihi sana, hasa bab yangu mkubwa, wazazi wangu kama kawaida yao walishasema huo ni mzigi wangu wa kujitakia,..basi nikafuata ushauri wa baba mkubwa kuwa siwezi kumuacha mume akiwa kwenye hiyo hali anaumwa, nihangaike naye mpaka apone kwanza,…unajua inauma ikizingatiwa kuwa alimuingiza hata kijana wangu kwenye  mambo yake ..iliniuma sana…’akasema.



    ‘Hapo sasa tuambie kijana wako aliingizwaje…?’ akauliza Mama Ntilie



    *************



    Kama nilivyosema awali, mume wangu alikuja kuathirika akawa hana nguvu tena kama mwanaume na dawa zao za kishirikina zilihitajia hivyo, kufanya uchafu wao kwa watoto wa watu wasio na hatia, wakihitajia damu..ni mambo ya ajabu kabisa,…basi mume wangu alipoona hivyo ndio akamuendea huyo mtaalamu wao,huyo mtaalamu wao, akamwambia;



    ‘Dozi ya dawa haikatwishi,..kwahiyo ni lazima kutafutwa namna na namna ni kumtumia mtoto wako, awe kama wewe, afanye majukumu yako..mume wangu hakukubaliana na hilo awali, baadae akakubakubali akiwa hajui mtego uliwekwa hapo.



    ‘Kwahiyo ili mwanao awe wewe ni lazima afanye kazi zako, kama wewe , kama mume…ashiriki matendo yote tuliyokuwa tunayafanya, …’akaambiwa.



    ‘Nini,…hebu hapo, una maana gani hapo…, matendo yapi maana mnapokuja usiku mimi sijiuu nimelala..au sio…?’ akauliza.



    ‘Lakini nilikuambia tunafanya nini, au sio,…tukifika kwanza ni lazima wewe ufanye mambo kwa mkeo kupata baraka zake..huku tunashuhudia, ili zindiko lifanye kazi, ukishamaliza kwa mkeo ndio tunakuchukua hadi kwa mwanawali, na huko tunakwenda kutafuta damu ya mizimu, ambayo itawafurahisha na kuwezesha kuhamisha nyota ya utajiri kutoka milki ya vizaz vile na kuhamia kuja hapo kwenu…’akasema.



    ‘Oh, hapo..hata sielewi, maana sijawahi kuona ila nahisi kuna kitu kinafanyika..na bora mfanya hivyo hivyo, nisijue kinachofanyika,…kwani naweza kuchanganyikiwa, unajua sipendi, ila nafanya hayo kwa ajili ya kutaka huo utajiri, vinginevyo nisingelifanya,..yule baba mkwe ananikera sana, moyoni mwangu…’akasema.



    ‘Hapana ni lazima uelewe kinachofanyika ili ifanikiwe uwe wewe unafanya jambo ambalo upo huru nalo, hatuna haja ya kukuweka wazi ulione ila kibali chako ndicho tunakihitajia…’akaambiwa.



    ‘Ehe niambie..mimi inakuwaje..maana ndio hivyo, na kama kijana wangu ndio anatakiwa afanye, tafadhali, naomba asije kujua au kuwa na fununu hiyo….’yeye akaomba hivyo.



    ‘Ni hivyo, kwa vile wewe hufanyi kazi, kijana wako atachukua nafsi yako, atafanya kazi zako, ina mama , yeye atashiriki na mkeo ili kuipata baraka kama ulivyokuwa unafanya wewe kabla hatujawaendea hao wanawali….’akasema



    ‘What!!!..Una maana gani hapo…ina maana, wewe hapana, huyo ni mtoto haiwezekani…..’mume alisema kwa ukali



    ‘Kama hutaki utajiri basi,..na hilo ni lazima lifanyike kwanza,..huwezi kupata baraka za huyo mwenye nyota bila ya kuptia kwake, na unapitia kwake kwa njia hiyo, na unakwenda kwa wanawali kuiongzea nguvu, mizumu inafurahi,…muhimu ni kuwa  mkeo hajui,..yanayofanyika nyote hamuyaoni, wewe na kijana wako mnakuwa kama magogo tu, kinachowasukuma ni mizimu inatembea na nyie,…tusipoteze muda, maana hapo hakuna kurudi nyuma tena, ukitaka kukatiza haya mambo kafara lake ni damu ya mtu, ina maana mmoja wenu anakufa..’akasema.



    ‘Oh, hapana, sitaki hilo litokee, sitaki mtu afe…’akasema



    ‘Chagua unaendelea au unakatiza…ukikatiza kijana wako au mkeo, au hata wewe kesho unazikwa, na maisha yanaendelea…’akaambiwa,



    ‘Hapo umeniweka njia panda…’akasema



    ‘Kesho tutakuja kama kawaida na kijana wako atachukuliwa na yeye ataanza kazi zako,na hakikisha binti mpya analetwa kama kawaida, mtumie huyo kijana wako awe anawaleta mabinti, usiku watapitiwa na usingizi tutachagua mmojawapo, kazi inaendelea mpaka tumalize hili zoezi, baada ya hapo nyota inahamia kweko, wewe utaanza kujaa utajiri, …unaelewa…’akaambiwa.



    Jamaa alivyo mjinga,… hakuwa na jinsi ikabidi akubali hivyo hivyo..bila hata kufiria athari zake.



    ‘Sasa hao mabinti walipatikanaje..?’ akaulizwa na mama Ntilie.



    ‘Kama nilivyosema awali mwanzoni alikuwa akichukua wafanyakazi wa ndani, wa muda, leo huyu anakaa siku mbili tatu, anaondoka kesho mwingine, yeye akijifanya anawasaidia mabinti wasiojiweza, alikuwa akienda hata vituo vya kulelea mayatima kule anamchagua yoyote kuwa aje afanye kazi kwa muda…mmi sijui, kwangu mimi niliona ni jambo la neema kuwasaidia waliopo kwenye mazingira magumu, kumbe mwenzangu ana ajenda yake ya siri.



    ‘Sasa akaja kuongea na kijana wake kuwa afanye paty, awaalike mabinti, ..yeye alimsisitizia mabinti, na kijana akawa anajiuliza ni kwanini baba anataka jambo kama hilo, kahisi labda ni kavile baba anataka yeye aoe, kwahiyo kati ya hao mabinti atamchagulia anayemfaa, kwahiyo yeye akafanya juhudi ya kuwachukua mabinti wazuri anaowafahamu , akawaalika na mabinti wengi wakakubali …



    ***************



    Siku hiyo ya kijana kukabidhiwa mikoba ya baba yake ikafika, usiku mabinti walioalikuwa wakafika,…na hao wachawi wakawa safarini kuja huku,..wanajua wenyewe walivyosafiri, na mimi nikapangiwa madawa ya kufanyiziwa ili niendelee kulala kama siku nyingine..ili kijana wangu mwenyewe wa kumzaa aje afanye kazi ya baba yake,..’ hapo huyo mama akanyamaza kwa muda, akiwa kainamisha kichwa chini, baadae akainua kichwa huku machozi yanamtoka akasema;



    ‘Hebu jamani niambieni hapo hata ingelikuwa wewe unasikia jambo kama hilo limekuja kufanyika kwako, na anafanyiziwa mtoto wako, utajisikiaje, je utakuwa radhi kumsamehe mtu kama huyu..?’ akaniuliza



    Nilibakia kimia, sikuweza kutoa jibu,…hapo hapo , akili ilikuwa imganda siamini kuwa ni kweli…



    ‘Hebu niambie kama ni wewe ungelikuwa umefanyiwa wewe hivyo na mumeo, ungelifanyaje, ungemsamehe tu, yaishe, je una uhakika gani kama hatakuja kurudia tena, je una uhakika gani kuwa hatafanya mengine makubwa zaidi ya hayo, je utamuelezaje kijana wako….maana mpaka sasa mtoto wangu ana matatizo makubwa yaliyotokana na vitendo hivyo..na kisa ni baba yao…



    ‘Huyu hapa shetani mkubwa,…’akasema akimnyoshea kidole.



    ‘Kwahiyo hebu kwanza hapo, huyo kijana wako kwa hivi sasa ana atatizo gani ni hayo ya kutumia madawa kama ulivyosema au kuna mengine…?’ nikauliza.



    ‘Huko kutumia madawa, imetokana na madhara ya hayo aliyofanyiwa, na alianza kutumia baadae,kwanza alianza kuvuta sigara, akaja pombe na baadae madawa…nitakuelezea hatua kwa hatua ili uelewe vyema…..na kukuelezea huko sio kwamba umchukia huyu mtu, …hapana, ni ili uelewe pia kuwa kijana wangu hana hatia na mambo hayo, hata kama yeye alikufanyia,..na …’kabla hajamaliza smu ya huyu mama ikaita, akaangalia ujumbe wa maandishi,



    ‘Wazazi wangu wananipigia simu natakiwa nikitoka hapa nikakutane nao, najua moja ya maswala ya kuongelea ni hili, je nipo tayari kuwa nao, au kuwa na huyo mwanaume…’akasema.



    ‘Mke wangu …’mumewe akataka kuongea jambo lakini yeye hakumruhusu akasema;



    ‘Ulitaka niyahadithie yote subiria nimalize , nikimaliza hawa ndio watakuhukumu na hukumu hiyo ni jinsi gani wewe uadhibiwe, na wakati huo huo, wewe ujue jinsi gani ya kubeba huu mzigo wa huyu binti..na huwezi kujitetea kuwa hutaweza, kazi bado unayo, hujaachishwa… ila kwangu, sahau….’akasema.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ‘Mama…’mimi nikasema



    ‘Unataka niendelee au niache…?’ akaniuliza mimi



    ‘Endelea….’nikasema



    Na  huyo mama akaendelea kumalizia sehemu iliyobakia…



    NB: Tutakuja kuiona sehemu iliyobakia ambayo, ndio iliyomfanya huyo mama akatae kabisa kurudiana na mumewe.





    WAZO LA LEO: Hutaamini kuna watu wamefikia hadi kuwaumiza watoto wao wa kuzaa, kwa ajili ya kuutafuta utajiri, wanaenda kwa waganga wanadanganywa wafanye hivi na vile, ..kuna wengine kweli wanaupata, utajiri wa kishetani, , ikiwa ni mtihani kwao, lakini hebu wachunguze kama wana raha maisha mwao, watakuwaje na raha wakati wanamuona mtoto wao akiwa hivyo, zezeta, hajiwezi,, na wachunguzeni kwenye vifo vyao wanakuwaje, maana madhambi kam hayo adhabu yake huanzia hapa hapa duniani,..…hivi jamani tumefikia hapo…INATISHA!





    Nilipokuja kuambiwa haya yote, kweli nikaikumbuka hiyo siku, nakumbuka sana siku ile nilikimbilia kulala bila kufanya ibada yoyote, nilikuwa nimechoka sana, nilikwenda kwenye sughuli za harusi za jamaa zetu, kwahiyo niliporudi nyumbani, nikajibwaga kitandani.., bila hata kumuomba mola anilinde, maana usiku ni safari ya nusu kifo. Ni muhimu jaman kabla ya kulala, kufanya ibada, kumuomba mola wetu atulinde, maana usiku una masaa mengi ambayo huoni kinachoendelea mbele yako, usiku kama huo, wengine wamelala, wengine kwao ni masaa ya kazi, kuna viumbe vingine usiku ndio vinafanya shughuli zao, kwa wema na kwa ubaya, kwao ndio kumekucha, yanayotokea ukiwa usingizini mola ndiye mlinzi wetu, sasa kwanini tunalala bila kumuomba… Siku hiyo nilipitiwa….. Nilikuja kuikumbuka sana siku ile, kwani ilikuwa siku ambayo nilipata mateso sana, zaidi ya siku nyingine. Kiukweli siku nyingine mambo kama hayo yalikuwa yakitokea, sawa ila siku hiyo yalizidi,…unajua hata hawa mabint walipokuwa wakilalamika kuwa wanaota ndoto za majinamizi, mimi niliwahi kuwaambia hata mimi naotaga lakini kwangu mimi nilichukulia kuwa ni ndoto tu, ila moyoni





    nilishaanza kuingiwa na wasisi, …..ni kwanini itokee hivyo karibu kila siku… Ndio maana niliamua kufanya uchunguzi wa kisayansi wa kuweka vyombo vya kunasa matukio, baada ya kusikia kuwa kuna mtu wa namna hiyo ambaye ana uwezo wa kuyagundua mambo yaliyofichika kwa kutumia, picha, au video,…na siku akielezea niliona ni kama uwongo wa kutafuta pesa, ila baada ya kufikia sehemu akaelezea kuwa kuna watu wanaingia majumbani usiku hatuwaoni, ukiweka video, ukapiga matukio ya usiku, yeye anaweza kusafisha vile video ukawaona hao watu wanakuja kwako usiku. 'Hiyo ni kweli,…yawezekana kweli, mmh… je kweli uliona hivyo…?’ akauliza mama Ntilia na kabla huyo mama hajajibu na mimi nikauliza hapo kwa hapo… ‘Kwani huko kwa huyo mtu aliyekuambia anaweza kuona hivyo vitu kwa kusafisha picha hukuweza kumpata tena? ‘Kwa bahati mbaya sikuweza kumpata…hayupo tena hapa nchini, kasafiri nchi za nje….’akasema ‘Kwahiyo ilikuwaje maana tuna hamu ya kuusikia usiku huo ulivyokuwa….’akasema huyo mama Ntilie. 'Tukirudi kwenye huo usiku, kiukweli nilipambana sana,….ukiwa na imani ya dini, inasaidia sana, lakini kwa kujisahu kwangu kufanya ibada siku ile, na kuomba, …mmh, yakanikuta makubwa, japokuwa nilijitahidi sana…na mengine hutokea ili iwe mitihani kwetu, naweza kusema hivyo tu… nakumbuka hata nilipoamuka, mwili mnzima ulikuwa unauma, na kiukweli, ndani ya ndoto, niliwaona watu ninao wafahamu,…’akatulia ‘Nani hao…?’ nikajikuta nimeuliza ‘Mume wangu na kijana wangu,…’akasema na sisi tukageuka kumuangalia huyo mzee. ‘Mume wangu alionekana akiwa anamlazimisha kitu kijana watu, huku kijana wangu analia hataki,…







    lakini mume wangu akishirikiana na watu wengine wakawa wanamlazimisha, na kitendo hicho kilionekana ni kibaya kwangu, na sikuweza kukitambua hicho kitendo,…maana niliona mambo mengi ya kutisha, huku nimekabwa, nahangaika huku na kule, yaliyotokea usiku huo itaweza kuyasahau na mengine siwezi kuyahadithia…’akasema ‘Hao watu wengine ni akina nani, hukuweza kuwakumbuka…?’ akaulizwa ‘ Nakumbuka siku nilipomuona yule marehemu pale hosp, tulipokwenda kumuona, nikajiuliza huyu mtu niliwahi kumuona wapi,…akili yangu ilikuwa ikinituma kuwa niliwahi kumuona mahali,.. baada ya kupata huu ukweli, ndio nikakumbuka, nilimuona kwenye ile ndoto mbaya….’akasema 'Naona unazunguka mama, je waliweza kufanikiwa kukufanyia kama walivyotaka…?’ akauliza mama Ntilie. 'Mimi sijui,…kama nilivyosema mengine yatabakia moyoni mwangu, siwezi kuyahadithia, lakini kwa ufupi kwa hicho walichotaka kukifanikisha walikifanikisha, maana bila kupitia kwangu, kama walivyoelekezwa na huyo mchawi, wasingeliweza kufanya mambo mengine…na hayo mambo mengine yalikuwa ni muhimu kwao…’akasema huyo mama kwa huzuni, akitamani kulia. 'Lakini wewe si uliwauliza …ulimuuliza huyo aliyekuhadithia kuwa walifanya hivyo, au ilikuwaje…?’ akauliza mama Ntilie. 'Kuwauliza akina nani sasa…, haya ninayoongea aliyenisimulia ni huyu mume wangu, sasa aseme ukweli, je haya ninayoyaongea ni uwongo, na je siku ile akinihadithia aliongea tu , akiwa kachanganyikiwa. Hayana ukweli ndani yake…’akasema huyo mama akimuangalia mumewe. Basi sisi tukamgeukia huyo mzee tusikilize jibu lake, naye kwanza alitulia kama anawaza jambo, aliopnekana kuchoka, hana raha, hata uso wake ulikuwa umesawajika…., baadae akasema; 'Hata nikidanganya kua sio kweli, namdanganya nani,..hata niki…unajua naona kama ndoto ya kulazimishwa, sijui ilikuwaje mpaka nikaghilibiwa kiasi hicho,…hapana isiwe ni…naombea iwe ni ndito tu….’akasema akishika kichwa. ‘Swali je ni kweli au si kweli..hata mimi natamani isiwe ni kweli, sema ukweli wako…?’ akauliza mke wake. ‘Yote ni kweli, siwezi kuwaficha hayo, na





    hata mimi usiku ule nilipata shida sana, maana nilijipanga kukataa, nilimuomba mungu sana ili aniepushie na hao watu, wakija isifanikiwe, kwa namna yoyote ile, kwahiyo hata walipokuja nilijaribu kuonyesha kukataa, lakini nilijikuta kama kawaida mwili wote unaisha unaisha nguvu, na unazama kwenye giza ambalo hajui kinachoendelea…’akasema ‘Kwahiyo kumbe wakija usiku wewe unaowaona…?’ akaulizwa ‘Siwaoni, ila inakuja hali fulani, unahisi mabadiliko...kitu kama njozi fulani hivi, na mwili unalegea kabisa, unakuwa huna nguvu kabisa,..ni kama njozi,…njozi ambayo huwezi kukumbuka ulichokifanya, ila unahisi kuna kitu ulikifanya, na ukiamuka asubuhi, kuna hali unaihsi kuwa kuna kitu umekifanya , lakini hukumbuki ni kitu gani,...'akasema 'Wakija, unahisi, unalegea au sio..una kabwa...kama sisi au sio...?' nikamuuliza 'Hukabwi,..nyie mnaotendewa hivyo ndio mnafanyiwa hivyo,...mnajiona mnakabwa, hasa mkileta kiburi...ila kwa upande wangu nilikua nahisi wamefika, sasa …na hapo sasa unakwua sio mtu wa kawaida,...na kinachoendelea huko mbele mimi huwa sikijui, mpaka narudi kulala….’akasema ‘Kwahiyo kume wewe unaamuka kiukweli, kimwili na kiroho…?’ akaulizwa ‘Ndio hivyo, utatendaje bila mwili…’akasema 'Sasa kwanini wao wakija hawaonekani, lakini nyie mnaonekana mkifanya hayo mambo, kwasababu wewe ulionekana ukitoka chumbani kwako na mkeo....au sio...?' nikauliza 'Wao ni wachawi, lakini sisi sio wachawi, sisi tuanatumika tu...kwahiyo, wao wa namna ya kujificha wasionekane , namna ambayo hawawezi kutufanyia sisi...mpaka na sisi tuwe wachawi kama wao...'akasema ‘Sasa unasema ulipambana nao kwa vipi sasa…?’ akaulizwa ‘Nilikuwa sitaki, siku nyingine nakuwa huru, kukubali, lakini siku hiyo , nikijua ni kitu gani kinakwenda kufanyika sikuweza kukubali kwa haraka, ila wao wanajua jinsi gani ya kunifanya nikubali tu,….’akatulia. 'Kwahiyo kwa uoni wako, au ulivyokuja kuambiwa, …Je hilo tendo lilifanyika la kumkabidhi mtoto wako hayo mambo yako…?’ akaulizwa 'Ndio lilifanyika…jamaa kesho yake alinipigia simu, akanielezea lilivyofanyika akaniambia walifanikiwa lakini ni kwa shida sana, na ilibakia kipindi kifupi…mke wangu alikuw amgumu sana, lakini mwisho wake walimshinda, kwahiyo nikiona mke wangu hayupo vyema leo,





    nijua kuwa ni hayo mapambano, ila makafara ya kimizimu yameshakamilika, na sasa kazi itakuwa mikononi mwa kijana wangu…’akasema ‘Mungu wangu ina maana wewe ulikubali kijana wako awe ….mume, awe ..hapana, una akili wewe….’nikasema nikimuangalia huyo mzee bila kum-maliza. ‘Ningefanyaje muda kama huo, muda huo shetani alishaniteka, nikijua kama nisipokubali mke wangu, au kijana wangu wanakuwa marehemu ili kuzima hasira za mizimu hiyo…ndio badili yake, je hapo ningelifanyaje…’akasema ‘Kwani wao ni mungu anajua kumuua mtu, na kujua ….?’ Nikauliza na kushindwa kumalizia. ‘Binti, hayo mambo yasikie hivi hivi, kwenye kujiingiza kwenye mambo hayo nilijifunza mambo mengi, usiku una maajabu, usiku una vitisho…kuna kipindi huyo mtu alimua kunionyesha mambo wanayoyafanya…wanavyokwenda makaburini, wanavyokula nyama za wafu…inatisha, kuua kwao ni kutu rahisi tu….’akasema ‘Kwahiyo na nyie mliwahi kula nyama za wafu…?’ akaulizwa ‘Kipindi cha awali ili kuja kuanza huo mchakato, tuliambiwa ni lazima tule nyama za wafu..tunywe damu za watu…kesho yake nilipoyakumbuka hayo nilitapika sana, nikawa sitaki kula nyama, hata mke wangu alishangaa sana, maana mimi nilikuwa mpenzi wa nyama,…lakini kila nikiona nyama nakumbukia hizo nyama za wafu…’akasema 'Sasa j mlifanikiwa….?’ akaulizwa 'Kwa lipi sasa hapo…?’ akaulizwa 'Hilo la nyota ya utajir kuhamia kwako…?’ akaulizwa 'Halikuwezekana, kwasababu mbali mbali…, kulikuwa na vita kati ya huyo mtaalamu wangu na mwenzake, ikawa wanapambana wao wenyewe kwa wenyewe mwenzako akitaka yeye ndio alifanikishe hilo…kutokana na kuwa yeye ndiye aliyekuwa na huo mkoba wa uganga…na kuna mambo mengine makubwa tu….’akasema 'Mambo gani hayo, hatuwezi kuyafahamu…?’ akaulizwa 'Kuna mambo yao mengine ya kugombea maeneo yao, ardhi….huko kwao ugomvi wa ardhi ni mkubwa sana, na wengi wanauana kwasababu ya ardhi….’akasema ‘Kwahiyo hilo la kuwa alitaka kumuoa binti akamkatalai sio kweli…?’ akaulizwa ‘Hilo pia ni moja wapo,





    lilijitokeza katika mapambano yao, ..na huyo binti alikuwa na kitu wanachokitaka, wana..mambo yao ya kuamini nyota ya bahati…huyo binti alikuwa nayo…na hata hivyo huyu mtaalamu akatokea kumpenda huyo binti, baada ya kuachana na mke wake, na alisema angelimpata mambo yake mengi yangelifanikiwa…’akasema ‘Sasa ilikuwaje…?’ akaulizwa ‘Kumbe huyo binti ni mtoto wa nje wa adui yake, adui yake akaligundua hilo, kukawa na vita vya kupambana, na kilichotokea ni kuwa huyo binti akaenda kwa mganga, kumbe huyo mganga ni kati ya wafuasi wa huyo adui wa huyo mtaalamu, kwahiyo ikajengwa hoja, ya kuhakikisha huyo mtaalamu hawezi kumuoa huyo binti….’akasema. ‘Je huyo binti anayafahamu hayo, kuwa baba yake alikuwa huyo adui wa huyo mtaalamu wenu…?’ akaulizwa ‘Hafahamu….maana huyo mama yake aliyepewa huo ujauzito alifukuzwa kwa wazazi wake akahamia mbali na hicho kijiji, na huku yalitokea mengi hadi huyo mtoto wake akachukuliwa huku mjini, na …akapotea kwenye mazingira ya ajabu, amekuja kuonekana akiwa mkubwa tu….ila hao wazee walikuja kumtambua kuwa ndio yeye…’akasema 'Kwahiyo ikawaje sasa…?’ akaulizwa 'Ikawa jamaa haji tena mara kwa mara…, anatuma watu wake, …na mambo mengi yakawa hayakamiliki, maana watu wake wakija wanashindwa kumuingia mke wangu, wanaishia kukimbia,….na ghafla nikasikia jamaa anaumwa, alidondoka kwenye safari zao akaumia, na anadai chanzo ni huyo rafiki yake, katupiwa mzinga,…kwahiyo vita vyao vikawa ni kipaumbele…’akasema 'Kwahiyo hukuweza kufanikiwa….?’



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Akaulizwa ‘Kwa jinsi ilivyotakiwa haikufanikiwa, lakini jamaa alisema anakuja mwenyewe kumalizia sehemu iliyobakia, ila alidai nyota tayari ipo nyumbani kwetu, sasa imehamia kwa mtoto….’akasema ‘Kwahiyo mtoto wenu akaanza kuwa tajiri…?’ akaulizwa ‘Utajiriri...hahaha, alianza ...lakini, ooh, yakaanza kutokea matatizo kwa mtoto, akaanza kupatwa na maradhi kama yangu….na...na....’akasema na kushindwa kuendelea kuongea zaidi. ‘Maradhi gani….?’ Akaulizwa na hapo akainamisha kichwa chini, na mke akasema ‘Ulisema tuhadithie yote, sasa elezea kila kitu…..mtoto alipatwa na maradhi gani, kama yako….?’ Mkewe akamuliza kwa hasira, na jamaa akashikwa kichwa, na kuanza kulia…. ‘Kulia hakutasaidia kitu,..., si umesema ili upone matatizo yako watakiwa kufunguka, kuyaelezea yote kwa uliowakosea, unakumbuka,…?' akaulizwa 'Nakumbuka sana mke wangu....'akasema kwa unyonge. 'Na mpaka nafika hapa na wewe uliniomba sana, ukasema kutokana na hayo, kujitolea kutubu, kuanza kuongea yote kwa watu uliowakosea umeshaanza kupona ni kweli si kweli...?' akaulizwa 'Ni kweli mke wangu....'akasema 'Sasa ni kipi kinakufanya ushindwe kuongea mwenyewe,ili na mimi haya yaishe vyema moyoni mwangu, na sijui yataishaje..'akasema huyo mama 'Yatakwisha tu mke wangu mimi nina uhakika na hilo....'akasema 'Kama una uhakika na hilo,...basi ongea, ulivyofanya,....'akaambiwa 'Sio mimi niliyefanya, alifanya huyo mtu kwa kunitumia mimi....'akasema 'Ehee....hapo hapo, alikutumiaje, maana usione mimi naongea hivi ukahisi kuwa mimi nina moyo wa jiwe, je na huyu binti ambaye anahitajia maelezo yako jinsi gani ilitokea kwake, au umesahau kuwa kisa cha kuja hapa ni kuelezea yaliyotokea kwake, ili akusamehe vyema kiukweli kutoka moyoni, isije akaja kuyasikia kwa mtu mwingine akaumia,





     na kusema kwanini hukuyasema hayo…..’akaambiwa. ‘Lakini mke wangu unanifahamu nilivyo, kwenye kuongea wewe upo bora zaidi, mimi siwezi kuyaelezea kama utakavyoelezea wewe, hapa nilipo…naumia sana…tafadhali nakuomba elezea nimekuruhusu , elezea kila kitu usiogope...’akasema ‘Wewe leo unaumia eeh., wakati unautafuta utajiri, hukuliona hilo au sio...?' akaulizwa 'Mke wangu, hayo yameshapita,...'akasema 'Kama yamepita na kweli unataka yapite, sasa ongea, au unanionaje mimi, .., je mimi ambaye pamoja na hayo mliniumiza, mlinifanyia mambo ambayo hayatakiwa kufanyika kwenye ustaarabu wa kibinadamu, na mbaya zaidi kwa mtoto wangu mwenyewe, halafu naambiwa nikusamehe, labda sio mimi …'akataka kulia. 'Lakini mke wangu, ina maana hutaki mtoto wetu apone, ....'akasema 'Ndio unanitega kwa hilo....'akasema mkewe 'Wewe mwenyewe umeota ndoto kuwa usiposamehe haya mtoto wetu hatapona, je tuyaache hivi hivi, sawa, mimi nitaenda mitaani, au nitaenda kujinyonga, ...maana kiukweli usiponisamehe wewe, sina haja ya kuishi tena...'akasema 'Unanitishia, jiue tu..kwani ukijua unaniongezea au kunipunguzia nini, wangapo wajane wapo na wanaishi....'akasema mke wake 'Sio sababu hiyo, ni sababu ya mtoto wetu,...mimi nina imani kuwa ukiyasameeh haya, tukawa kitu kimoja na mimi nimeshatubu, mtoto wetu atapona, na...wote waliohusika hapa, akiwemo huyu binti, mambo yake yatakuwa sawa, atajifungua salama..si ndio hivyo,...?' akauliza Mkewe akabakia kimia akiwa kashi 'Mke wangu....'jamaa akalalamika. 'Kwani mama, hayo anayosema baba kuwa ukimsamehe, ndio itakuwa sababu ya matatizo haya kuisha ni nani kayaongea, au yametokea wapi....?' akaulizwa 'Yalitokea kwangu usiku, niliota ndoto ya namna hiyo, ndio ikabidi nimtafute huyu mwanaume ili tuje tuyamalize hapa, ..ni ndoto, lakini ndoto zangu za namna hiyo mara nyingi huwa ni kweli....lakini siwezi...'akasema



     'Mama mbona hata mimi naamini hivyo, haya yote yatakwisha, lakin kuisha kwake ni wewe na bab msameheane, kwangu mimi haina shida, nimeshawasamehe....'akasema 'Hujasikia yaliyotokea kwako bado...'akasema huyo mama 'Yapi hayo,..mimi naona umeshayaelezea, na yalitokea kwa muongozo wa huyo marahemu au sio...?' akaulizwa 'Mengine ni kutokana na huyo marehemu lakini mengine ni kutokana na yeye mwenyewe...'akasema 'Kwa vipi wakati yeye umesema alikuwa anaumwa, na hakuwa na uwezi tena...?' nikauliza 'Unajua mengine nikiongea mimi watu wataona kama natilia chumvi, hata huyu mwanaume kuna muda nikiongea unanikatiza...sasa kwa vile yeye mwenyewe yupo na ndiye alikuwa mtendaji, basi aelezee kila kitu....'akasema na kumgeukia mumewe 'Haya…tuambie sisi sote, mimi nimefikia pale mliponifanyia uchafu wenu, mkahamisha uwezo wako kwa kijana wetu....ilikuwaje sasa kwake,...na kwa vipi akaanza kubadilika, na ni kwa vipi akaanza kuumwa kama wewe, ..na aliumwa nini, ambacho unasema ni kama wewe, na je mlifanikiwa kwenye mipango yenu hiyo, …hayo ni maswali yanahitaji majibu kutoka kwako?’ akaulizwa. 'Sawa....'akasema na kuanza sasa kuelezea yeye mwenyewe. NB: Inasikitisha,….je mpo tayari tuelezee yaliyotokea kwa mtoto hadi akafikia hapo alipo,…au tumalizie kisa chetu..? WAZO LA LEO: Matatizo mengine ya watu yanayotokea ukubwani yameanzia utotoni,, kumbe yalianzia kutoka kwa wazazi au walezi, kuna watoto wamekuja kuathirika na maradhi mbali mbali, au kuja kuiga tabia fulani, au kuja kuwa kasoro fulani, kisa ni kutokana na wazazi au walezi waliowalea. Wazazi jamani tuweni makini sana kwa watoto wetu, na hasa pale wanapokuja wageni, mnawalaza na watoto je mnawafahamu hao watu tabia zao. Tujenge tabia ya kuhakikisha watoto wetu wanakuwa na vyumba vyao ambavyo, wageni hawaruhusiwi kulala nao... Nayasema haya sio kwa kukataa wageni, lakini kua mengi yametokea ya kuharibu watoto, na matokea yake wanakuja kuharibika ukubwani, kisa ni mgeni, tena ndugu wa akribu tu, kisa ni mlezi, kisa ni wafanyakazi wa ndani, au kisa ni hata mzazi wenyewe. Tumuombe mungu atulindie vizazi vyetu, na atuepueshie na mitihani mingine ambayo sio dhamira yetu…Aamin.



    ‘Kiukweli inabidi nielezee, ila nakuomba sana mke wangu uniongoze, najua wewe unaweza kuniuliza maswali ya kuniongoza….’nikamwambia mke wangu, na yeye akabakia kimia.



    ‘Wewe ongea bwana, wewe si mwanaume,….’akasema mke wake kwa hasira.



    ‘Sawa, nitaelezea tu, ila hamuwezi kuamini, inaniuma sana ikizingatiwa kuwa mimi nilishawishika kijinga na kuyafanya hayo yote, lakini kama ungelinifunua moyo wangu ukauona ulivyo ungeniamini haya ninayowaambia, hii ni familia yangu, na nilitaka kufanya hivyo nikijua…’akawa anataka kuongea zaidi, lakini mke wake, akamkatiza kwa kusema



    ‘Wewe ongea hayo ya muhimu, hayo ya kujidai kuwa unaijali fanulia yako yataonekana kwenye maelezo yako…’ akaambiwa



    ‘Inabidi nijitetee kwa hili kuwa nilifanya hadi hapo, licha ya kuwa nilishaona kuna madhara, ila kwa hatua niliofikia hadi hapo sikuweza kuacha, kwa masharti hayo, kuwa nikiacha kuendelea kuyafanya kama yalivyotakiwa ili yawezekane, basi kafara lake ni mmoja wa ninaowapenda afe…awawe kama kafara la hiyo mizimu.



    ‘Sawa hapo tumekuelewa na imani zenu za kishirikina,…..endelea ….’akasema mke wake naona alishakubalia kumuongoza kwa maswali.



    ‘Basi, baada ya tendo lile la kuhamisha nguvu za uwezo wangu kama mume wa familia, …na kuhamishiwa kwa kijana wangu,…,ikawa mimi kazi yangu ni kuwa msindikizaji tu, ila kila anachofanya kijana nilitakiwa niwepo, na niwe nimemshika mkono, inakuwa nguvu zetu zipo pamoja,….hayo yanafanyika mimi sijijui..na hata kijana wetu hajijui..’akasema



    ‘Kwahiyo kila mkienda kwenye hizo shughuli za usiku, ilikuwa ni lazima kijana wako, apitie kwa mama yake afanye yale uliyotakiwa wewe uyafanye kwa mama yake..?’ akaulizwa sasa na mama Ntilie.



    ‘Nahisi ndio hivyo, ili dawa hizo zifanye kazi, …’akasema



    ‘Kwahiyo unahisi huna uhakika….hakuwahi kukuambia kuwa ndivyo ilivyokuwa inafanyika...?’ akaulizwa na mke wake.



    ‘Aliniambia, ndio kawaida ….kila safari ikifanyika huniambia kilichofanyika, ila mimi nilimuomba hayo ya kijana wangu asiwe ananiambia, lakini akasisitiza kuwa ni lazima nijue kila kinachotendela kabla ya kutenda na baada ya kutenda ndivyo masharti yalivyo hivyo, ….’akasema.



    ‘Kwahiyo hiyo safari ya kijana wako kuchukua nafasi yako na kufany akila ulichokuwa ukikifanya wewe kama mume wa familia, ni zaidi ya mara moja…’akaulizwa.



    ‘Ndio..mimi siwezi kuwa na uhakika ilikuwa mara ngapi, lakini ni zaidi ya mara moja, na baadae huyo mtu akasema tayari nguvu zimeshahamia kwa kijana na nyota imeshaanza kuonyesha uhai, iliyobakia ni matendo mengine sasa ya kuihamisha kutoka kwa kijana kuja kwangu, lakini hiyo si lazima kwa sasa, ilimradi nyota sasa ipo ndani ya familia yetu….’akasema.



    ‘Kwahiyo utajiri ulianza kuonekana ..au?’ akulizwa



    ‘Kijana alianza kubadilika, ..ghafla akanunua gari la kifahari tu… nakumbuka tuliulizana na mke wangu kijana kapatia wapi pesa kiasi hicho cha kuweza kununua gari la gharama hivyo, mimi akilini najua ni kitu gani, mke wangu akawa hajui, kwahiyo yeye akataka tumuulize kijana, na mimi nikamwambia ni juhudi za kijana wetu tusipende kumuingilia maisha yake…’akatulia akisubiria kuulizwa maswali.



    ‘Ehe, endelea sio lazima nikuulize maswali wewe si unaendelea kuelezea tu…..’akasema mke wake.



    ‘Kijana akaanza kubadilika, akawa hata nyumbani haonekani mara kwa mara , kitu ambacho sio kawaida yake, ukimpigia simu anakuambia, nipo kwenye mishe mishe zangu, ninalala hotelini, na anaongezea kwa kusema, sasa atanunua nyumba yake ili tusiwe tunamuulizia ulizia, kuwa yupo wapi…’



    ‘Kununua nyumba  au kupanga nyumba?’ akaulizwa



    ‘Yeye alisema anataka kununua nyumba ..tukamuuliza pesa kapatia wapi, yeye alisema kwenye dili zake za hapa na pale, ikabidi mama yake amuwekee watu wakufuatilia nyendo zake, na akagundua kuwa pamoja na mengine kijana, alikuwa akicheza kamari, na alikuwa akipata pesa nyingi sana, na ndio hizo anazichezea hivyo…mimi nilijua ni hiyo nyota sasa inafanya kazi,…lakini sikuwa na raha na hali iliyokuwa ikiendelea maana sio mimi naonekana mwenye utajiri, na mimi nilitaka nionekane mimi ni tajiri kwa ajili ya kumuonyesha baba mkwe.



    Mama yake hakuwa na raha na mabadiliko hayo ya kijana wake, akashangaa kuniona mimi namtetea, sitaki kumfuatilia, …na akataka tumuite huyo kijana kwenye kikao, na kijana alipokuja akawa anatujibu kijeuri, kuwa kama ni pesa anazitafuta kwa akili zake, kwahiyo tusimfuate fuate…ilikuwa kwa mara ya  kwanza kijana wetu anatujibu hivyo, hakuwa na tabia hiyo kabisa,…’akatulia.



    ‘Unaona kijana wako alivyobadilika, wewe unakaa kimia tu…sasa mke wangu akaanza kuniandama mimi, mimi sikupenda kubishana na mke wangu maana nilijua ni nini kinachoendelea..



    Na mara nyingine namjibu, hivi;

    ‘Atatulia tu, nina imani akioa, mambo yatakuwa safi…ndio maana nafurahi akiwaleta mabinti ili niweze kuwachunguza ni nani anafaa…’nikamwambia mke wangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Katika mambo yake aliyokuwa akifanya, zaidi ilikuwa ulevi, kubadilishana mabinti, na siku nyingine anakuja na mabinti wa watu zaidi ya watano, kustarehe nao, kwangu nilijua ni kwasababu gani, na ni mimi nilimshauri afanye  hivyo awali, na nilimuambi ahakikishe anachagua wazuri…hakujua usiku hao mabinti wanachukuliwa kufanyiwa mambo na hao wachawi…



    ‘Basi ikawa sasa ni kero hata mimi nikawa sina raha, maana mama yake alikuwa haachi kunisemesha kuhusu mtoto, na hata ndugu zake achilia mbali wazazi wake,…nikaona sasa ni bora nitafuta njia ya kulituliza hili, nikawasaliana na huyo mtaalamu, ndio akaniambia japokuwa yupo kwenye matatizo na huyo mpinzani wake, lakini yeye anatarajia kuja huku hivi karibuni, na akija huku atahakikisha analimaliza hilo tatizo…



    Kweli haikupita muda, akafika huku Dar, tukaongea naye, akaniambia ni nini cha kufanya…na hapo nikazidi kuingia matatani…lakini sikuwa na jinsi…’akasema



    ‘Uliambiwa ufanye nini…?’ akaulizwa



    ‘Ili tulimalize hilo, inabidi turejeshe hizo nguvu alizo nazo kijana kwangu mimi, kwani hizi sasa inawezekana kufanya hivyo, awali ilikuwa haiwezekani, ilitakiwa muda fulani upite…na muda huo ulishapita…’akasema.



    ‘Ina maana ukizirejesha hizo nguvu kwangu, hali yangu itakuwa kama awali, na kijana atakuwaje..?’ nikamuuliza



    ‘Ndio, hali yako itakuwa bora, kama kijana wako… ila kijana wako yeye, anaweza akawa kama wewe…’akaniambia hivyo..na kunifanya nishtuke.



    ‘Kwa vipi…awe kama mimi?’ nikamuuliza.



    ‘Ujue hizo nguvu utakazozipata sio zile za kwako za asili, hizo ni nguvu za kupandikizwa, lakini zinafanya kazi kama kawaida,, ….’akaniambia



    ‘Ina maana mimi sitaweza kuwa na nguvu zangu za asaili…?’ nikamuuliza



    ‘Hilo hatujui, maana mizimu ndio inayokumiliki, na hatuwezi kuilazimisha,…kwahiyo kwa hivi sasa tunatakiwa kufanya yale wanayotaka wao kwanza, …ila ukiona umechoka na hizo nguvu, kwa kipindi fulani mtakwua mkibadilishana na kijana wako, ukitaka lakini…’akasema.



    ‘Lakini yeye bado kijana anazihitajia sana kuliko mimi…’nikamwambia



    ‘Sasa ni wewe mwenyewe kuchagua, kama unataka kijana wako aendelee kuwa hivyo, na hatari yake ni kama mnavyoona, yeye ni kjana hajui kujizuia, hana busara, atawaletea keshi humu ndani, bora umnyamazishe kwa hivyo kwanza, na baadae akirejeshewa atajirudi…’akanishauri hivyo.



    Basi nikaongea na mama yake nikamwambia kuna dawa natakiwa nimfanyia kijana ili atulie, aachane na mambo hayo.



    ‘Dawa, kwanini dawa, kwani huwezi kumshauri tu hivi hivi akatulia…?’ akaniuliza.



    ‘Tumemuita mara ngapi, mke wangu….na tumemkanya mara ngapi…, umeona majibu yake, sasa uamue mwenyewe , tumueche hivyo hivyo au tumtafutie hizo dawa, maana ni wewe unanisumbua kuhusu yeye…’nikasema na mke wangu akasema;



    ‘Hizo dawa unazitafutia wapi…?’ akaniuliza kwa mashaka.



    ‘Wewe niruhusu tu, nitazipata, kuna mtu kaniambia zipo dawa za kumdhibiti mtu wa namna hiyo, vinginevyo atazidi kuharibika na hata kuchanganyikiwa, wewe huoni imekuwa ni tatizo sasa…uso wetu tutauweka wapi….au wewe unasemaje mke wangu…’nikamwambia mke wangu nikiwa kama muungwa anayetaka kushirikiana mambo na mke wake, lakini hakujua kuwa mimi ni ndumila kuwili…’akasema akitabasamu ile ya kuumia.



    ‘Basi sawa ilimradi zisiwe za kishirikina..’mke wangu akasema hivyo

    Mimi nikawasiliana na huyo mtaalamu, na kuwa muda huo bado yupo hapa Dar, akiwa na shughuli zake, akaniambia tujiandae usiku, atakuja na watu wake….



    ‘Na ujue zoezi lilivyo, ni kama lile la siku ile,…sasa sijui mke wako kajiandaaje, lakini tumeshamjulia madhaifu yake hawezi kutushinda,..ila kuna kazi ya ziada, kuna mambo yatakiwa kufanyika kuzimuni…’akaniambia hivyo.



    ‘Kuzimu ndio wapi..?’ nikamuuliza



    ‘Makaburini, na huko wewe unatakiwa kuona, utachukuliwa hujijui, ila ukifika huko utarejeshewa fahamu zako, na  utaona yatakayofanyika, ila kijana wako atanyamazishwa…kama ilivyo kawaida yake….’nikaambiwa



    ‘Kwani ni lazima niyaone hayo mambo yenu ya kichawi…?’ nikamuuliza



    ‘Ndio kwasababu hayo ni dhidi yako na kijana wako, …inakuwa ni wewe unamfanyia kijana wako..’nikaambiwa



    ‘Na mama yake je…?’ nikauliza



    ‘Kawaida njiayetu nikupitia kwa mama yake, atafanya yote kama kawaida, na tukishamaliza mambo ya huko kuzumuni ukirudi wewe ndio utashika usukani, na ukitoka kwa mkeo, ni lazima kuwe na mabinti kama kawaida, hao mabinti ni wa kuwafurahisha vijana wangu,…unanielewa…’nikaambiwa.



     ‘Na itakuwaje kwa mtoto wangu baada ya hapo…?’ nikauliza



    ‘Itakuwaje kwa vipi, si unataka mtoto wako atulie, atatulia kama awali…’akasema



    ‘Sawa…’mimi nikakubalia, nikijua kwua kijana wangu atakuwa kama zamani, sikujua kuwa kuna jambo linguine litamtokea….’akasema.



    ‘Basi usiku hiyo ikafanyika hivyo, nakumbuka kijana sijui ilikuwaje, wakati tupo huko makaburini, ghafla akazindukana na kuanza kukimbia, …na ikawa kazi ya kumtafuta, …lakini alipatikana na kazi ikafanyika kama kawaida…’akasema…



     ‘Asubuhi yake ikawaje…?’ akaulizwa



    ‘Kijana akawa mgonjwa hatoki kitandani, hatoki nje yeye na ndani tu, …sasa ikawa kuhangaika mimi na mama yake, maana inabid nifanye hivyo, ili mama yake asijuei kinachoendelea,…kijana akawa habadiliki, mpaka mama yake akaanza kukata tamaa..



    ‘Hivi kijana wangu kawaje tena…?’ akaniuliza



    ‘Mimi sijui labda ni hizo dawa ndio zimemfanya hivyo…’nikasema



    ‘Dawa gani ulimpa mtoto wangu…?’ akaniuliza kwa ukali



    ‘Ni dawa za kumzuia mtu mlevi, aache pombe, na huyo mganga alisema, hali hiyo itatokea lakini itakwisha taratibu taratibu, kwahiyo tusubiria tu mke wangu…’nikasema.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Na kama umemfanyia mtoto wangu mambo ya kishirikina hatutaelewana, sizani kama nitaweza kukusamehe kwa hilo, maana wewe mtu sasa sikuelewi elewi…’akaniambia hivyo, na ninachoshukuru ni kuwa mke wangu alikuwa haamini mambo hayo zaidi ya kuhimiza tumpeleke mtoto wetu hospitalini, lakini mimi nikawa nazuia kinamna.



    ‘Kwanini hukutaka apelekwe hospitalini…?’ nikaulizwa



    ‘Haikutakiwa kupelekwa hospitalini, vinginevyo angeliharibika kabisa….ndivyo nilivyoambiwa na huyo mtaalamu…’akasema





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog