Simulizi : Duwa La Kuku
Sehemu Ya Tano (5)
‘Basi sina hili na lile siku moja nilikuwa nimetoka maana kuna mambo mengine ilibiaidi nisafiri kama alivyotaka huyo mtaalamu, nikawa nimesafiri kufuatilia vifaa fulani, niliporudi, mke wangu akasema alimpeleka kijana hospitalini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Eti nini…kwanini umefanya hivyo, si nilikuambia dawa hizo alizopewa, hazitakiwi kuchanganya na madawa ya hospitalini, sasa utakuwa umemuharibu mtoto..’nikasena nikiwa nahaha sasa…
Na kiukweli, hali ya kijana sasa ikazidi kuwa mbaya zaidi ya hapo, akawa kama kachanganyikiwa kila mara anapiga makelele, wakati mwingine anakimbia na kupotea, tunamtafuta anarudi, akawa sasa ni mtu wa kufunga kamba ndani…anatoa ulimi nje kama mbwa anavyofanya, mtoto akawa sio mtoto bali ni kama dalili za mnyama anavyokuwa…’hapo akatulia.
‘Je hamkuwasiliana na huyo mtaalamu wako ili muone jinsi gani ya kumsaidia…?’ akaulizwa.
‘Tulifanya hivyo yeye,alisema hiyo hali itakwenda na itakuja kutulia baadae, ila sisi tumeharibu kwa kumpeleka mtoto huyo hospitalini,…
Basi muda ukafika akatulia, na wakati huo yale matendo ya kuhamisha zile nguvu kutoka kwake, zikawa zimafanyika na mimi nikawa na nguvu …nguvu za ajabu, ikawa ni shida sasa, yale aliyokuwa akiyafanya kijana yakahamia kwangu, japokuwa mimi nilikuwa nikiyafanya ki utu uzima zaidi.
‘Ukawa unacheza kamari..?’ akaulizwa
‘Ndio, unajua pesa za kishetani hupatikana kwenye njia za kishetani pia, kwenye kamari ndio ilikuwa sehemu ya kukusanya mali, na kila ukicheza hukosi, na hiyo hali ya kupata pesa inakuvutia kucheza zaidi na zaidi, na huko ulevi, umalaya ndio sterehe yenyewe,…na kiukweli kwa mapesa hayo, ni lazima ufanye mambo ya kujionyesha, ndio nikaanza kujenga majumba, unakumbuka mke wangu alilalamika kuwa nina nyumba mahali,..ndio hizo pesa, lakini utajiri wake haudumu, unajenga nyumba nzuri ikiisha unauza, au unahonga kwa wanawake…ni utajiri wa shida tu, na muda huo hujitambui, akili inakuwa na kumuhe muhe cha kufanya machafu, starehe, ‘akasema
‘Kwahiyo hata wewe ulikuwa ukiwachukua mabinti wadogo…?’ akaulizwa
‘Ndio..maana ndio makafara ya hao watu wa mtaalamu, ni lazima hayo yafanyike kila akiwahitajia, na mimi usiku kama wamekuja ni lazima nishirikie, kuwepo,, …’akasema.
‘Kwahiyo kumbe ndio wewe ulimpa ujauzito huyo mdada aliyetoa mimba…?’ akaulizwa
‘Hapana, sio mimi, pamoja na mengine pamoja na hata kumtamani huyo binti, kufanya hivyo, sikuweza kwasababu ukumbuke huyo binti ni msichana aliyekuwa akitakiwa na huyo mtaalamu, ni mtu wake, ila alitaka kumfundisha adabu, na akatumia watu wake wengine kumzalilisha…’akasema.
‘Wakina nani hao…?’ akaulizwa
‘Mimi siwajui, ila anasema ana vijana wake, ana watu wake ambao hutembea naye usiku na hao ndio wanatumiwa kushiriki na hao mabinti wakichukua makafara yao…’akasema.
‘Kwahiyo tuseme kuwa kwa upande wako hao mabinti wa usiku ulikuwa huhusikani nao, hao ni kwa ajili ya hao wachawi ….?’ Akaulizwa
‘Ndio….’akasema
‘Je si hayo mambo ya kutuma mabinti na kuhamisha nyota yalishakamilika kwanini sasa muendelee kuwazalilisha watoto wa watu usiku ..?’ akaulizwa.
‘Hayo mambo ya muda wake kila mara kuna namna ya kuyaweka yawe yanafanya kazi, kwa hiyo mara kwa mara wao walikuwa wakija, na kunichukua ili kuwezesha nguvu ziendelee kuwemo, kwahiyo vitendo hivyo vilikuwepo lakini sio kama awali, ni mara moja labda kwa mwezi, au mara mbili hivi…’akasema.
‘Wewe hayo yakitokea ni lazima ujue..?’ akaulizwa
‘Wakitaka kuja wananiarifu kuwa watakuja, ..kama wanakuja kwa kushitukizia ujue wamekuja kwa mambo yao mengine..ambayo mimi sihusiki…’akasema
‘Kijana wako ikawaje..?’ akaulizwa
‘Kijana japokuwa alikuwa kapona kinamna…, lakini hakuwa na nguvu zake, …na hali hiyo ikaanza kumtesa kimawazo, si unajua tena…ikabidi hata aniambia mimi kuwa na hali fulani inamkera…akaniambia ukweli alivyo, na ikabidi sasa nimshauri twende hospitalini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Si uliambiw usiende huko hospitalini…?’ akaulizwa
‘Hio ilikuwa ni awali, kwasasa haikuwa na shida, mimi najua ni kwanini, ila kwa kumuaminisha kijana ikabidi nimshauri hivyo,..twende akapimwe,..na kupimwa ndio ikagundulikana ana magonjwa kama yangu, kisukari ..na shinikizo la damu..yaani yale yale niliyokuwa naumwa mimi ndio sasa anaumwa mtoto wangu, nikajua ni hizo nguvu ndio zimesababisha hayo…
‘Oh, kwahiyo wewe ukawa radhi na hali hiyo ya kijana wako ateseke wewe, uwe kijogoo..au sio…?’ akaulizwa
‘Kiukweli, kwa muda huo sikujali kabisa, niliona ni sawa tu, atulie nyumbani, ilimradi nafahamu ni kwanini, na utajiri ukipatikana itakuwa kwa manufaa ya familia, sio kama ilivyokuwa yeye, utajiri ulikuwa kwa ajili yake tu, na hakutaka kuulizwa…’akasema.
.
‘Kwahiyo kumbe ni kweli, kuwa ukifanya hayo mambo unapata utajiri, japokuwa ni wa kichawi..?’ akaulizwa
‘Ukweli ndio huo kuwa unapata utajiri, lakin kwa kupitia njia za kishetani..unafanya mambo mabaya sana..mengine siwezi hata kusimulia, na mbaya zaidi huwezi kufaidi huo utajiri maana unaumiza wengine, unaumiza hata familia yako, na wakati wote huna amani, kila muda una mawazo kuwa huenda nikajulikana huenda watu wananiona huenda…halafu shughuli unazozofanya kwa jamii, ni za kukuzaraulisha tu japokuwa mwenyewe unajifanya hujali…’akasema
‘ Sasa ikawaje kwa kijana wako….?’ Akaulizwa.
.
‘Nilianza kukaa naye kumshauri, na nilimuahidi kuwa kila anachotaka nitampa, lakini hakuwa na raha kabisa,..unajua tena hali ya kibindamu ilivyo, ulikuwa hivi, mwanume sasa unajiona tofauti, huna kazi, alizoea kubadili mabinti sasa akiwaleta anaishia kuabika tu…, na taarifa zikawa zinazagaa kuwa kijana hana nguvu tena..ikawa ni aibu na ikawa inamtesa sana kisaikolojia…’akasema
‘Mungu wangu ikawaje sasa…?’ akaulizwa
‘Ndio hapo akaanza kutumia pombe zaidi kupitiliza,…, na hakutosheka na hilo, akaanza kutumia madawa ya kulevya
‘Mungu wangu, kwanini, na wewe ulijua hilo…?’ akaulizwa
‘Mimi nilijua, ila mama yake alikuwa hajui kuwa kijana wake kaanza kutumia madawa ya kulevya, nikawa namtetea na kuificha hiyo hali, na nikawa najaribu kumshauri kijana wangu aachane na madawa kwani ni mabaya zaidi…
‘Sasa kwanini uifiche wakati unajua kijana anaharibika kwasababu yako…?’ akaulizwa
‘Mtaalamu aliniambia nisimzuie kwa yale anayoyafanya , maana yatakuja kuisha kwa muda muafaka,… ni mambo ya muda tu, lakini hayo hayakuwa kweli..nikaona kama huyu mtu hamtakii mema kijana wangu…’akasema
‘Kwanini sio kweli..?’ akaulizwa
‘Kwasababu kipindi kile kijana wangu akiwa kijogoo, yule binti wa awali alishafika, huyu mtaalamu kume aligundua kuwa kijana wangu kampenda huyo binti, na akagundua kuwa wana mahusiano ya siri…’akasema
‘Kwa vipi sasa kijana nguvu zake ulishazichukua..au ilikuwa bado…hapo unatuchanganya?’akaambiwa
‘ Huyo binti alikuja muda, ..na muda aliofika niikuwa bado zitazichukua, hizo nguvu kutoka kwa kijana,..na nilikuja kugundua baadae kuwa kumbe huyo mtaalamu alifanya hivyo kumuadhibu kijana wangu, pamoja na mengine …’akasema.
‘Ikawaje sasa,….je huyo mtaalamu hakutaka kumsamehe huyo kijana wako…?’ akaulizwa
Ghafla ndio huyo mtaalamu akaanza kuzidiwa zaidi,…tatizo lake likazidi kuwa kubwa zaidi, awali sikujua ni tatizo gani, hadi alipofika kuniambia kuwa kagundulika ana ugonjwa mbaya, ila anahisi kuwa mbaya wake ndiye kamfanyia hivyo.
‘Lakini wewe si ulikuwa na pesa kwanini sasa alikimbilia kuomba kwa akina mama, au kipndi hicho alichokuja kuomba pesa ilikuwa bado,…?’ akaulizwa
‘Kipindi hicho, ilikuwa bado, kipindi anakuja kuomba pesa, ni kipindi hali imebadilika hata kwangu….’akasema
‘Ehee, endelea…..’akaambiwa
‘Kukawa kunakuja taarifa kuwa kwa wakwe zangu hali yao ni mbaya, kiuchumi,
‘Kwahiyo kumbe kweli nyota iliondoka kule kwao na kuja huko kwenu au sio…?’ akaulizwa
‘Hapo mimi sijui, ila kiukweli, wazazi wa mke wangu walikuwa na hali mbaya, na mimi nikitaka kuwasaidia lakini wao walikataa kabisa, waliniambi wazi wazi kuwa wao hawataki pesa za kishetani….
‘Oh, ina maana wao walishajua kuwa pesa zako ni za kishetani…?’ akaulizwa
‘Wao waliniambia hivyo, na sikuwa na muda wa kuwafuatilia kwa nini wanasema hivyo, ila walikuja kumuita mke wangu wakamkanya kunihusu mimi, na kipindi hicho ndio mke wangu akaanza kunifuatilia kwa karibu, …’akatulia.
‘Haya sasa tuambie kuhusu yaliyotokea kwa hao mabinti wawili….maana naona umefikia kipindi chao, ilikuwaje maana mama alisema kuna mambo mabaya mliwafanyia wao..?’ Akaulizwa
‘Kama nilivyosema binti wa mwanzo nisingeliweza kumgusa, japokuwa nilifanya juhudi hizo mara kwa mara, na wakati mwingine naamua kwenda kwake usiku,lakini kila nilipojaribu nilijikuta nikikutana na huyo mtaalamu.
‘Unakutana naye kwa vipi, yeye si anakuja humuoni,…?’ akaulizwa
‘Simuoni ila ananifanyia mambo yanayo-onyesha kuwa yupo….’akasema
‘Sasa yeye anajuaje kuwa wewe unakuja kwa huyo binti…?’ akaulizwa
.
‘Sijui anajuaje, sio kila siku, ila siku ambazo, navutika kwenda kwa huyo binti, ndio siku nakutana naye, na yeye, ananiuliza nimefuta nini kwa mke wake…na hata kesho yake lazima atanipigia simu kuniuliza na kunikanya, kuwa nisipoacha hiyo tabia atanifanya kitu kibaya sana….’akasema.
‘Mke wake!!!..kwanini anamuita mke wake…?’ akaulizwa
‘Yeye anadai alishamuoa kimzimu, kwahiyo ni mke wake kihivyo…’akasema.
‘Kwahiyo yawezekana mimba iliyotolewa ya huyo binti ni ya huyo mzee..au sio…?’ akaulizwa.
‘Hapo mimi sijui….maana siku ilipotolewa, huyo mjamaa alikasirika sana kuwa huyo binti kamfanyia kitu kibaya, na zaidi kajiunga na adui yake kummaliza yeye, na kwahiyo anafanya kila njia kuhakikisha huyo binti anamrejea yeye.
‘Oh, sasa ikawaje…?’ akaulizwa
‘Muda huo ndio vita ikapamba moto, kati ya hao watu wawli....mimi muda huo sina hili wala lile kumbe wajamaa wanapambana usiku na mchana, na ndio ikaja huyo binti mpya…huyu hapa…’akasema
‘Je hayo ya kumleta huyu binti mpya ilitokea kwa amri ya huyo mjamaa, kuwa huyo binti aondoke hapo, mlete mwingine au ni wewe na mke wako mlipanga hivyo…?’ akaulizwa
‘Ni amri ya huyo jamaa aliniambia hapo nyumbani kwangu mambo yanaanza kuwa mabaya, tumeingiliwa, kwahiyo tutafuta makao mapya ya kufanyia shughuli zetu, na huyo binti aliyepo humo aondolewe, tutafuta binti mwingine, na ndipo nikamshauri mke wangu atafute binti mwingine, na alipokwenda huko kijijini ndio akaja na huyo binti …’akasema.
‘Shughuli gani hizo zilihitajika kufanyika kwingine..?’akaulizwa
‘Si nimekuambia, hayo mambo yalihitajia kuyaongezea nguvu ili yaweze kufanyaa kazi, yana-expire, kwahiyo yanahitajia kuwa activiwa…labda niseme hivyo kwa kiingereza…’akasema.
‘Kwahiyo mkafanyaje…?’ akaulizwa
‘Huyo binti akaondoka pale, na kuhamia huko kwa rafiki wa mke wangu, na huko ndio hao wachawi wakaweka makao mapya,..lakini haikuwa rahisi kihivyo, …’akasema
‘Kwanini…?’ akaulizwa.
‘Huyo binti alishajiunga na huyo adui wa jamaa, akawa kapata namna ya kujilinda, na huko kwenye hiyo nyumba alipokwenda wenyeji wake ni wacha mungu, hawaingiliki ovyo…ndio akaja na hoja ile ya kuondoa makafara…nia yake ni kuweza kuweka mambo yake…lakini kama mlivyoona haikuwa kazi rahisi, na yeye hali yake kiafya ikazidi kuwa mbaya, akawa sasa analemewa na adui yake…’akasema
‘Kwahiyo na wewe ikawaje…?’ akulizwa
‘Sasa kwa vile hayo mambo hayafanyiki tena, madawa na zile nguvu za kishetani zikawa zinaisha nguvu, mimi nikawa naanza kuishiwa nguvu, mambo yakaanza kuwa mabaya, madeni,..kamari, ukicheza hushindi, unaishia kukopa, kulipa siwezi, nikaishia kunyang’anywa nyumba, magari…hali ikaanza kuwa mbaya sasa …’akasemaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Na siku moja kijana wangu akanitaka tuongee, kipindi hicho naanza kuchanganyikiwa, jamaa mtaalamu hapatikani na akipatikana analalamika hali mbaya anahitajia pesa za matibabu, hana pesa, nimsaidie au nitaishia kubaya, na leo kijana wangu ananiita, sikutaka kabisa kuongea naye…
‘Mliongea naye, ..alikuambia nini…?’ akaulizwa
‘Baba nimegundua kuwa matatizo haya niliyo nayo sababu kubwa ni wewe, umenifanyia hivi ili nifirisike ili nisiwe tajiri, umenipa madawa ya kuniharibia nguvu zangu za kiume,… ili nisiwe natembea na wasichana warembo umenionea wivu na kunifanya..hivi sasa nakupa wiki moja tu, unirejeshee hali yangu la sivyo , nitamuambia mama haya yanayoendelea humu ndani….’akaniambia hivyo na kuondoka.
‘Sasa ilikuwaje….?’ Aakulizwa
‘Nikawasaliana na mtaalamu, na mtaalamu akasema dawa ipo hapo hapo nyumbani, …huyo binti mpya ndiye kafara, kwani ana sifa zote…nisiwe na wasiwsi atayamaliza hayo, ila mimi hali yangu itawa vigumu kuirejeshwa kwani mambo yameharibika, na kijana ili afanyiwe hivyo, kuna mambo makubwa yanatakiwa kufanyika, nitafute mbwa..…’akasema mzee sasa akiona aibu kuniangalia mimi machoni.
‘Mbwa wa nini…?’ akaulizwa
NB: Mbwa wa nini….tutakuja kusikia sehemu ijayo..
WAZO LA LEO: Utajiri wa kishetani hata kama utaupata lakini ukumbuke mwisho wake ni mbaya sana,..wengi waliofanya hivyo, wameishia kubaya sana, na kama itatokea ukafariki kabla hujatubu , kifo cha mtu kama huyo kinakuwa kibaya sana, wengine wanafikia kuoza wakiwa wazima, na mambo mengi mabaya hutokea kwa watu hawa hata kabla ya kukata roho, jamani tumuogope mola wetu, kwani hayo tunayoyataka ya utajiri ni vitu tu vya kupita, na mwisho wake tutarejea kwa yule aliyetuumba, je unajuaje kuwa utaupata huo utajiri na kuendelea kuutumia, hukumbuki kuwa siku ya kufa ni siri ya mola pekee…tutubie na tuache…
Baba nimegundua kuwa matatizo haya niliyo nayo sababu kubwa ni wewe,….’kijana alimuambia baba yake
‘Nani kakuambia hayo, ni nani …?’ baba akamuuliza kijana wake akiwa kama kapigwa kofi usoni.
‘Nimeshajua kila kitu baba…, unachonifanyia mimi,..na nakupa siku saba, baba mimi nakupenda sana, nawapenda sana wazazi wangu, ...lakini kwanini unifanyie hivi, kwanini baba, sasa baba, japokuwa, nawapenda, japokuwa nyie ni wazazi wangu, lakini kwa hili umevuka mpaka, ..baba,..nakuomba, ... usiporejesha hali yangu, nitamuambia mama yoote, mbele ya babu na bibi, unasikia mbele yao, …’kijana akasema na kuondoka..
'Mwanangu sikiliza kwanza...we....'alikuwa ameshaondoka.
Ndio nikaamua kuongea na mtaalamu akasema hiyo ni kazi ndogo kwake, na kwa vile humo ndani kuna binti ambaye anaweza kulifanikisha hilo, basi atakuja...lakini pamoja na hayo anahitajika mbwa.
Mbwa…ndio mbwa….!!!
‘Mbwa , mbwa wa nini…?’ nikamuuliza
Tuendelee na kisa chetu…..
****************************
‘Nilimuuliza swali hilo, lakini hakunijibu hapo kwa hapo, akasema tutajua huko usiku ukifika,…’akasema
‘Kwahiyo huyo mbwa alitoka wapi..ni wewe ulimtafuta, au…?’ akaulizwa
‘Yeye aliniambia tunahitajika kutafuta mbwa, na hakusema nimtafute mimi, lakini cha ajabu kulipopambazuka nikasikia mke wangu akilalamika kuwa kuna mbwa yupo hapo nje na hataki kuondoka, nikakumbuka maneno ya mtaalamu kuwa hilo kafara la usiku linahitajia mbwa…basi ili kulificha hilo, nikamwambia mke wangu.
‘Huyo ni mbwa nimepewa na rafiki yangu, atatusaidia kwenye kazi ya ulinzi wa hapa nyumbani..
‘Mimi sitaki mbwa, mimi na mbwa tofauiti,…na kwanini mpaka tutafute mbwa, nani kakuambia kuna tatizo la wezi hapa nyumbani kwetu…’akalalamika mke wangu.
‘Ni kuwa huyo rafiki yangu kasafiri, na huyu mbwa wake hana sehemu ya kumweka, basi nikaona nimchukue tu mimi maana ni mbwa aliyefunzwa vyema…, akirudi atamchukua mbwa wake, tatizo lipo wapi mke wangu…’nikasema na mke wangu akaondoka bila mabishano zaidi , na huyo mbwa akawa hapo kwetu, sikujua anatakiwa kufanyiwa nini kwa muda huo,….na sikuwa na uhakika kuwa huyo mbwa ndiye aliyeletwa na huyo mtaalamu au la…’akasema
‘Ina maana hukumuuliza huyo mtaalamu wako….?’ Akaulizwa
‘Sikukumbuka hili hutaamini, mpaka usiku ukafika….ghafla wakati naingia ndani kutoka kwenye shughuli zangu nasikia mnguromo wa mbwa, nikashtuka, na nilipochunguza vyema nikamuona huyo mbwa kalala pembeni mwa nyuma karibu na dirisha la mdada….’akasema.
****************
‘Endelea, ehe mbwa huyo alifanya nini maana hapo unatutisha…na mbwa tena….’akasema mama Ntilie.
Mimi alipomtaja huyo mbwa, ndio nikamkumbuka vyema, mbwa huyo nilimuona alipokuja, siku hiyo nilikuwa nafanya usafi, mara nikaona mbwa kasimama karibu na geti, mlango wa geti ulikuwa wazi, nikajua katokea nje, nikamfukuza kwa mawe, ili atoke nje, hakuondoka, badala yake akaja kusimama karibu na mlango, na akawa ananitizama ninvyofanya usafi...
Basi mimi nikamuacha nikaendelea na shughuli zangu, na mama mwenye nyumba alipomuona akaniuliza huyo mbwa katokea wapi, mimi nikamwambia sijui...basi akajaribu kumfukuza lakini hakuweza maana huyo mbwa alikuwa akikimbia kuzunguka nyumba, hatoki nje, na alipochoka kumfukuza akamuacha na kumuuliza mumewe kumuhusu huyo mbwa, na sijui waliongea nini.
Cha ajabu cha huyo mbwa, akawa karibu na mimi sana siku ile, na mimi kwa huruma nikampa chakula mchana ule, na usiku akalala nje, karibu na dirisha langu, nakumbuka kweli, usiku alikuwa akitoa mngurumo wa ajabu, kama analia wakati mwingine kama mtoto, au..kama sauti ya mtu hivi analia.....sikumjali sana, maana mimi nimetokea kijijini, milio ya mbwa, paka, ni kitu cha kawaida huko kijijini.
Ila cha ajabu kingine ninachokikumbuka ni kuwa usiku ile niliota ndoto, kuwa huyo mbwa, kaja kulala na mimi, hiyo ni ndoto lakini,...nikajaribu kumfukuza lakini hakutoka, na nikamuacha akalala ubavuni mwangu..ndivyo nilivyokumbuka na mengine yalikuwa yale ya kukabwa, na nakumbuka huyo mbwa ndiye alikuwa akinisaidia, hadi nilipokuwa sikumbuki tena kilichotokea hadi asubuhi,
Kulipopambuzuka huyo mbwa alikuwa hayupo....!
************
Huyo mzee akawa anaendelea kusimulia,...
‘Usiku sikuwa na raha kwanza kuhusu kijana wangu, nilijiuliza kajuaje,…maana yanayotokea usiku inakuwa sisi tumelala,na hatuyaoni….na labda kuna mtu kamuambia, atakuwa ni nan…nikawa najiuliza bila kupata hjibu.
Na nikakumbuka kuwa kuna kauli ya wakwe zangu kwa pesa zangu ni za kishetani, na wao wameshanipa muda nijikoshe, kwa kusema ukweli hayo ninayoyafanya, la sivyo wao wataingilia kati, hawawezi kuona mtoto wao yupo kwenye maattizo wao wakae kimia,..na pia wao wamesema wameshagundua ninafanya mambo ya kishirikina, na kwa hilo watahakikisha nazalilika, hilo sikulijali sana, maana vitisho vyao sio kwa mara ya kwanza, lakini hili la mtoto wangu lilinifanya nisiwe na raha kabisa.
Mke wangu siku hiyo alisema atachelewa maana mke wangu kwa shughuli humtoi, na hakujua kuwa shughuli zake ndizo hawa watu walitumia kufanikisha mambo yao…’akasema.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Kwa vipi, kwani zinawasaidiaje..?’ akaulizwa
‘Mara nyingi mke wangu akirudi kwenye shughuli huwa kachoka, hana muda wa ibada, yeye ni kukimbilia kulala, na hao jamaa ndio wanatumia mwanya huo kufanya mambo yao, sijui wanajuaje kuwa mke wangu leo ana shughuli na ndio wakati wao muafaka wa kufika…’akasema.
‘Kwahiyo usiku huo, wakafika, niliwahisi kama kawaida, na kipindi hicho sikuwa nalala kitanda kimoja na mke wangu, tulikuwa hatuivani kila mtu na kitanda chake, …’akatikisa kichwa kusikitika.
‘Kwahiyo mke wako alikuwa hajui kuwa hali yako imerejea kama kawaida, …?’ akaulizwa
‘Sijui, nahisi hakuwa anajua na aliona nikiwa na wasichana ni kama kujipotezea pesa tu, ndio maana hakujali sana….’akasema.
‘Basi nikawa nasubiri nione mtaalamu atakavyonisaidia,…kumbe alikuwa yupo dar, alikuwja kufuatilia matibabu yake,, ….alikuwa anahangaika na hospitali, na kwa kipindi hicho alikuwa kaandikiwa kwenda Muhimbili. Kwahiyo haikuwa ile safari ya kutoka huko mikoani, ….’akasema
‘Ulijuaje…?’ akaulizwa
‘Alikuja kuniambia baadae….’akasema
Usiku wakafika na kikosi chake, na nilihisi kuwa wapo kamili, kuna hali niliihisi hivyo, na na ile hali yangu ya kuishiwa nguvu ikanijia, na nakumbuka wakati hali hiyo inatokea, nikaona mke wangu akihangaika, akipambana pale kitandani, na hata kabla sijapotezaa fahamu zangu kabisa, nilimuona mke wangu akiinuka kitandani, ana akawa anatoka nje, ….nikajua itashindikana..na hapo hapo mimi nikazama kwenye giza…
***************
Mimi sikujua kilichotokea ule usiku, …ila asubuhi mke wangu alkuwa hayupo, nikaulizia, wakasema mke wangu aliondoka usiku huo hukalala hapa nyumbani…nikampigia simu, na akasema;
‘Nipo kwetu,….’akasema
‘Kwanini…?’ nikamuuliza
‘Sikuweza kulala usiku, mbwa, alikuwa akitoa mngurumo wa ajabu, kuna milio kama ya bundi…kuna hali nahsi kuna watu wanaifanyia mabaya, nikaona humo ndani hakulaliki, ndio nikaondoka…’akasema
‘Sasa mbona mimi nimebakia humu ndani, kwanini hukuniamuisha…?’ akaulizwa
‘Nilikuaga, lakini hakusema kitu,…ulikuwa kama unaweweseka weweseka, nikajua ni dharau zako tu…, nikaondoka zangu, na wakati napita kwa huyo binti nilisikia makelele fulani , nikajua ni kawaida yake ya kuota , sikutaka kusubiria, nyumba ilikuwa inatisha muda huo, ajabu nilipotoka nje sikumuona huyo mbwa, wakati nikiwa ndani nilisikia sauti ya mngurumo kama wa mbwa…’akaniambia.
‘Huyo mbwa atakuwa alienda wapi, au alikuwa katoka nje…?’ nikamuuliza
‘Mimi sijui alienda wapi , sikutaka kujua, nikaondoka zangu…’akasema
‘Ni kijana wetu je, hukutaka kumuangalia, ulijijali mwenyewe…?’ nikamuuliza mke wangu.
‘Kwanini nisimjali, nilipotoka nilikwenda chumba chake, na kugonga, hakukuwa na mtu ndani, nikajua hakulala humo ndani…’akasema mke wangu.
‘Atakuwa alienda wapi usiku huo..?’ nikamuuliza mke wangu.
‘Labda alikwenda kulala kwa marafiki zake, alinilalamika kuwa kuna jambo linaendelea humu ndani, linampa shida, usiku analala kwa shida, na hali yake imekuwa mbaya sana anahisi tatizo linatokea humu ndani, sikutaka kumuuliza sana mambo hayo, maana sitaki mambo ya kishirikina,…kwahiyo kuanzia sasa kaamua,kuwa hatalala hapa nyumbani siku zote…’akasema
‘Atakwenda kulala wapi, na kwanini hajaniambia mimi mmwenyewe…?’ nikauliza
‘Kasema anakuja kulala huku kwa babu yake, na hilo la kwanini hajakuambia sio kweli, kasema kuwa keshakuambia, na kakupa wiki moja umpatie jibu….’akasema
‘Kaniambia nini, wiki moja ya nini,…kasema hivyo, anataka jibu gani..?’ nikamuuliza, nikijifanya kushangaa
‘Kasema wewe unajua ni kitu gani, na kaapa kuwa usipompa jibu atakachokifanya humu ndani tutakuja kumsikia kwenye vyombo vya habari, sasa labda nikuulize wewe kuna nini kinachoendelea humo nyumbani kwetu, nisingelipenda kusikia yanayosemwa na wazazi wangu lakini hali iliyopo inanilazimisha kuamini hayo…’akasema
‘Kwani wewe hajakuambia ni kitu gani…?’ akaniuliza
‘Kaniambi wewe unajua kila kitu, sasa ukiniuliza mimi nakushangaa, hamjaongea naye…?’akasema na kuniuliza
‘Oh, haya ngoja nitaongea naye..’nikasema
‘Mim sitarudi hapo nyumbani kwa leo, nitakuwa narudi mara moja moja kuna kazi naifanya kwanza, …huyo binti atakusaidia saidia kazi za hapo nyumbani,..ila nakuonya huyo binti wa watu, kama kuna lolote unalomfanyia, sitakusamehe kabisa…muogope mungu…’akasema.
‘Nimfanyie nini mimi huyo binti,…., si unanijua nilivyo, hali yangu si unaijua, ukiniona nastarehe, ni kujipooza tu , ili kuondoa mawazo…’nikasema.
‘Ulivyo eeeh, unanifanya mimi mtoto mdogo, sioni kinachoendelea, unakumbuka uliniambia kuwa unajiona umepona, je ulipona nini…kwako wewe kupona imekuwa kama ng’ombe wa ndani kufunguliwa nje, unaparamia kila mtu, haya endelea na tabia yako hiyo mbaya, unachokitaka utakuja kukipata, …’akasema.
‘Mke wangu hayo umeyapatia wapi, hali sasa mbaya, wewe huoni, …?’ akaniuliza
‘Umenisikia bara bara, na kwa vile hata mtoto wako kakufahamu ulivyo..basi itakuwa rahisi kwangu, kuchukua hatua muda ukifika, usije kusema sikukuambia,..nasubiria watoto wengine wakija watoto ndipo kila kitu kitawekwa bayana,, sasa hivi naogopa kumuumiza kijana wangu…’akasema
‘Ndio maana umekwenda kwenu, kumbe umeshaanza kuwafuata wazazi wako wanavyotaka au sio, sas ahuko unafuata nini wakati wazazi wako hali zao ni mbaya…?’ nikamuuliza
‘Nilikuwa sina sehemu nyingine ya kwenda usiku huo, mimi siwezi kuchukua haya mambo kiharaka hivyo, ninajua sheria za ndoa, na mimi ni mtu mnzima…muda utafika utapata nafsi ya kufanya hayo unayoyataka, siku hizi si una nyumba, una pesa, au…’akasema
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Mke wangu, si nimeshakuambia, sasa hivi hali imekuwa mbaya, kuna mambo yamekwenda tofauti kabisa.. hali imeharibika nyumba , magari yamechukuliwa kulipia madeni…’nikamwambia mke wangu.
‘Kwanini leo unaniambia hayo mambo yako…?’ akaniuliza
‘Wewe ni mke wangu lazima nikuambie mambo yetu ya famalia, nilishakuambia kuwa hali ni mbaya, hukutaka kuniamini, na…na… haya yote nilikuwa nikifanya kwa ajili ya familia yetu…’nikasema.
‘Yatakushinda, ila nakuonya, kama kuna kitu unachokifanya kwa ajili ya wazazi wangu, utakachokipata utakuja kujuta, hawa ni wazazi wangu, na sijui kwanini unashindana nao…’akasema
‘Nani kakuambia hayo mke wangu, hayo ni mawazo yao, kama wameishiwa wameishiwa kwa mambo yao wasinisingizie mimi…’nikasema.
‘Sio swala la kuishiwa, kwani kuishiwa imeanza leo, wazazi wangu wamekuwa wakikutana na mitihani kama hiyo mara kwa mara, na wanakuja kuinuka tena, biashara ndivyo zilivyo, wao hawafanyi mambo ya kishirikina, kama ya kwako..’akasema,
‘Mambo gani hayo ya kishirikina mke wangu mbona huniamini, kama ningelikuwa nafanya hivyo si ungeliniona,..?’ akauliza.
‘Kuna mtu alikutwa nyumbani kwa wazee akiwa uchi, ..anafanya mambo ya ajabu alipobanwa sana akasema katumwa kuchukua vitu humu kwa wazazi wangu na wewe…’akasema
‘What!!…na mimi kwa vipi, …’nikauliza huku miguu ikiniishia nguvu.
‘Ndio hivyo huyo mtu kachukuliwa na polisi kupelekwa kituoni,…’akasema
‘Kituo gani hicho, nitakwenda kumuona maana mimi sijui kitu kama hicho,…’nikasema
‘Kumuona wapi,…maana hapo walipokuwa wamemfungia, hawakukuta mtu, walikuta mbwa, na huyo mbwa sawa na huyo niliyemuona hapo nyumbani, sasa najiuliza iweje, mtu ageuke kuwa mbwa, wewe mwanaume niambie ukweli kuna kitu gani kinachoendelea hapo nyumbani kwangu…’akasema mke wangu.
‘Mungu wangu, mi-mi….sijui kitu mke wngu na huyo mtu ni muongo mnafiki tu, usiwasikilize hao watu, na uwe unaniuliza mimi kwanza…’nikasema kumuambia mke wangu.
‘Siku zenu sinahesabika, najua kuna jambo unalifanya, ... ila jingine tena la muhimu, ni kuhusu huyo binti wa watu, hajui kujitetea, hataki kunieleza ukweli, ila najua kuna kitu mnamfanyia, ...nakuonya tena kuhusu huyo binti wa watu ogopeni hao watu, mayatima,..masikini, hivi hamna huruma nyie watu....sawa ngoja tuone mnachokitaka kitaishia wapi, utakuja kujuta kwa hilo…..’akasema
'Mke wangu achana na mambo hayo ya kishirikina...'akasema
'Na je huyo mbwa bado yupo hapo nyumbani..?' akaniuliza
'Ina maana ndiye unamuogopa, mimi sijamuona hapo nje...'nikasema na yeye akakata simu.
Kiukweli kauli hiyo ilinichoma moyoni, nilijaribu kuvuta hisia,...nikijaribu kuona ni kitu gani hao watu walimfanyia huyo binti...lakini baadae nikapotezea, kujipa matumaini...sio mimi niliofanya hayo japokuwa ni mshiriki, .., shauri lake huyo mtaalamu, na watu wake...hata hivyo sikuwa na raha...niliona mambo yanazidi kuongezeka, ndio nikatoka nje kuhakikisha kama huyo mbwa hayupo kweli,..hakuwepo
'Huyu mbwa kaenda wapi...?' nikauliza lakini hakukuwa na mtu wa kunipatia jibu, binti alikuwa anafanya usafi huko jikoni na sikutaka kuonana naye, nafasi inanisuta...
Baadae ndio nikasema;
'Ngoja nimpigia Mtaalamu simu yeye atanisaidia kwa haya mambo maana naona hali inazidi kuwa mbaya...'nikasema na kuchukua simu yangu kumpigia huyo jamaa
****************
Nikampigia simu mtaalamu..nikapiga simu ikawa inaita tu, haipokelewi, nikajaribu tena na tena, na nilipotaka kukata tamaa baadae ikawa hewani, na alipopokea sauti niliyosikia ilikuwa ya mgonjwa aliyezidiwa sana.
‘Mtaalamu vipi, mbona simu hupokei..?’ nikamuuliza
‘Oh,… mimi naumwa sana hali imekuwa mbaya ghafla, tokea nirudi jana usiku, mambo hayaendi vyema, nahisi adui yangu huyo…’akawa anaongea sauti ya mgonjwa ambaye hata kuongea ni shida,
‘Unaumwa nini….?’ Nikamuuliza
‘Si nilikuambia naumwa, nimekuja hapa Dar, kwa matibabu, na…hali inazidi kuwa mbaya, hiyo jana usiku nilifika kwa nguvu za mizimu na kilichonipata huko kimenizididshia matatizo….’akasema.
‘Kwahiyo, jana hukufanikiwa , nitamuambiaje kijana wangu sasa , …?’ nikamuuliza
‘Nitakuambia subiria nipate dawa hali ni mbaya sana…yule mbwa, wamemkamata…na yeye ndiye ooh, kijana wako, ngoja nitakuambia, su-su--aaah….’simu ikakatika.
NB: Naishia hapa kwa leo, kuna mambo naweka sawa kuhusu sehemu hiyo inayokuja...ili tuweze kuhitimisha hiki kisa bila maswali megi....
WAZO LA LEO: Ukiishi kwa kutegemea dhuluma, ukawa unafanya mambo ya kishetani, kula yako, kipato chako, maendeleo yako, mienendo yako,..hakika wewe ni shetani kimatendo, na kwahiyo wewe unakuwa adui wa mwenyezimungu, tubia ewe mwana –wa adamu kabla milango ya toba haijafungwa,…
Siku hiyo sikuwa na raha kabisa,…na tofauti na siku nyingine ambayo nilipenda kumfuata fuata huyo bint kwa siri, nikimuangalia alifanya usafi, siku hiyo nilijaribu kumkwepa, na hata alipotaka kufanya usafi ndani kwangu, sikutaka anikute hapo, nakumbuka siku moja alipotaka kufanya usafi, nilidhamiria kumshika kwa nguvu, lakini nilipomkaribia tu, nikahis kichomi kikali tumboni, nikanywea na kwa haraka nikarudi nyuma…
Kwa huyu binti, kila nilipojaribu kumfanya chochote ilikuwa ni kama kuna mtu anamlinda, kama ilivyokuwa kwa yule binti wa awali, nikakumbuka maonyo, kuwa huyu binti naye ana mtu wake, na yule halikadhalika alikuwa na mtu wake, na wote hao ni hao wachawi…
Basi nikatoka hapo nyumbani, baada ya kuhakikisha kuwa kweli huyo mbwa hayupo, na kwenda kwenye shughuli zangu na baadae nikampigia simu huyo mtaalamu nia ni kumuulizia kuhusu kijana wangu na je kulifanyika nini huo usiku na je kilichofanyika kimeweza, au kitaweza kumsaidia kijana wangu.
Nilipiga simu ikaita kwa muda baadae akawapokea na kuwa hewani,, nikajitambulisha kwake, akasema ameshanitambua mimi ni nani,...na sauti aliyotoa ilionekana ina uhai, nikamuuliza
‘Vipi mtaalamu ulifanikiwa…?’ nikamuuliza
‘Nusu nusu, kama nilivyokuambia, mkeo aliondoka mapema, na kijana wako pia..kwahiyo..mambo mengi yakashindikana kufanyika,..tukajaribu kumtuma mbwa wetu usiku huo, akaone alipokwenda huyo mkeo, na tuone kama tunaweza kufika huko angalau kwa muda, lakini kilichotokea huko ikawa ni mkosi wa siku …’akasema
'Mkosi !....mkosi wa nini...?' nikauliza
‘ Jamaa alinaswa....'akasema
'Alinaswa na nani sasa…?’ nikauliza
‘Hao wakwe zako naona safari hii wamejiimarisha, jamaa alifika vyema na alipojaribu kufanya vitu vyake, akajikuta anaonekana...nguvu zake za kinga zikawa hazifanyi kazi, na hakuwa na jinsi, akapatikana,...na alaichukuliwa kwenda polisi na hata hivyo watayaona maajabu yake…’akasema
‘Maajabu gani…?’ nikamuuliza kama sijui
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Tuyaache hayo,…ila mbwa wanaye bado, nimeacha abakia huko kidogo, atatusadia mambo mengine ya huko, na usiku atawatoroka, huyo hana shida, hawamuwezi…’akasema.
‘Atawasaidia nini huko polisi, huyo mbwa…?’ nikamuuliza
‘Tatizo lako hunijui mimi…lazima nijue wamepanga nini huko baada ya hilo tukio….’akasema
‘Sawa nimekuelewa…’nikasema hivyo, nikasikia akipiga miayo halafu akasema;
‘Haya niambie unataka kujua nini zaidi, hayo mazungumzo mengine tuyaache kwanza…’akasema.
‘Sawa mimi usiku huo mlipofanya hayo mambo unajua siwezi kuona yanayotendeka ila wewe ndio unanisimulia, je hmlifanya nini..na je mlifanikisha hayo mambo maana siku alizo nipa kijana wangu ndio hizo zinakwisha…’nikasema.
‘Nashangaa leo unataka kuyafahamu mwenyewe tofauti na siku nyingine,….’akasema
‘Ndio wewe huoni hali ilivyokaa sasa hivi…..’nikasema.
‘Japokuwa mke wako alikimbia na kijana wako, lakini tuliweza kufanya baadhi ya mambo yetu, hasa mambo yetu ya kujilinda, na huyo adui yetu, sasa yaliyotukwamisha ni mambo yako, lakini mambo yetu yamekamilika….’akasema.
‘Mambo yenu yapi sasa, na kama ni mambo yenu kwanini mje kuyafanyia hapa kwangu, hamuoni mnanifanya niwe kwenye wakati mgumu, …na,…na…mke wangu…?’ nikamuuliza na nilipotaka kuongea zaidi akanikatisha na kusema;
‘Nilikuambia kitu, huyo binti hapo ndani ametufaa sana, kuanzia sasa kachukua nafasi ya yule binti wa awali japokuwa sijakata tamaa, maana huyu hatanifaa mimi , kama mimi,…yule binti mwingine alikuwa ni mke wangu, huyu sio wa kwangu…ila tumemtumia sana,…na mambo mengi yamefanikiwa, na kijana wako, kama angelikuwepo hali yake ingelijirudia kama kawaida…’akasema
‘Sasa kwanini kwani ni mpaka awepo ndio hayo mambo yafanikiwe…?’ nikauliza
‘Sasa tutamfanyia vipi ili kuhakikisha karejea kwenye hali yake, ilitakiwa yale matendo ya awali yafanyike, mkabidhiane tena, na …hilo litasubiria, utajua mwenyewe jinsi ya kumweka sawa, ukitaka tumnyamizishe tunaweza lakin hamtapendezewa na hiyo hali hasa mke wako…’akasema
‘Na, na yuleo mbwa wenu atarudi tena hapo nyumbani…?’ nikamuuliza
‘Huyo mbwa , keshamaliza kazi yake kama mbwa…, kuna kazi alitakiwa kuifanya hapo ndani ya kafara maalumu la kuunda silaha mpya, kombora litakalomumaliza kabisa huyo adui yangu…na limefanikiwa,….’akasema
‘Kwa vipi huyo ni mbwa au sio…mumemfanyia nini na huyo binti wa watu…?’ nikauliza
‘Hahaha..huyo ni mbwa kwa uoni wenu wa macho, huyo ni shetani wetu , yeye anaweza kujigeuza mbwa, paka, nk…na tumemtumia kwenye mambo hayo makusudi ili kuficha ukweli…, na yeye kwa hivi sasa ndiye bwana wa huyo binti ….’akasema
‘Bwana wa huyo binti, binti yupi…una maana gani kusema hivyo?’ nikauliza nikiwa na mashaka.
‘Binti yupi tena si huyo hapo nyumbani kwenu, yeye katunukiwa na huyo shetani-mbwa wetu..kwahiyo hana budi kumtumia huyo binti, na kupitia kwake tutafanikisha mambo mengi sana nyota yake ina nguvu sana kwenye makafara yetu…usiku huo tulimchukua huyo binti hadi kuzimuni, akachezewa huko kuwafurahisha hao mashetani ..’akasema.
‘Mungu wangu, kwanini mumefanya hivyo, huyo binti wa watu ni masikini tena yatima, sio vizuri jamani…’nikawaambia
‘Sisi hatuangalii huko, mambo yetu ni kishetani, na yanafuata mkonodo huo…wewe ulitaka utajiri hukuupata,unafikiri uliupataje, ni njia hizo hizo…..sasa umetaka mengine…haya tufanyeje…ni lazima mambo hayo yafanyike ili mambo yetu yafanikiwa, ukiwa na huruma hiyo hawezi kufanikiwa….’akasema
‘Hapana, hilo mimi sipo na nyie kabisa…’nikasema
‘Hupo na sie k, kwahiyo unataka kijana wako aendelee kuwa hivyo, maana bila hayo yaliyofanyika kijana wako hataweza kurejea kwenye hali yake, huyo ndiye atatusaidia kila hatua,… si ndio unataka hivyo…mtoto wako arejee kwenye hali yake, au unataka nini…?’akauliza.
‘Kwa-kwa-hiyo mumefanikisha kuhusu mtoto maana hapo sijakuelewa…?’ nikauliza nikiwa sina hamu maana kila hatua najikuta naingia kwenye mambo mabaya zaidi,..
‘Tutawezaje kuanikisha wakatu wahsuika wakuu hawakuwepo, mke wako, haya kijana wako, ..tulijaribu kuwafuatilia, mtumishi wangu ndio akanaswa huko,..unajua nikuambie kitu, .sio kila mahali tunaweza kuingia, …’akasema.
‘Kwahiyo lini tena, maana siku zimekwisha unajua sitaki kijana wangu anifikiri vibaya, hivi sasa anaonekana kujua kila kitu sijui ni nani kamuambia…’nikasema.
‘Ndio maana tunatakiwa kumnyamazisha hadi haya mambo yakamilike…’akasema.
‘Una maana gani kumnyamazisha…?’ nikauliza.
‘Anakuwa kama zezeta, hawezi kufikiri wala kuongea , …ni swala la muda mfupi tu…vinginevyo hiyo hali inaweza ikakujia wewe, na ikikujia wewe ndio basi tena, kwahiyo ni bora kuifanya hivi sasa kwa kijana wako ili iwe rahisi kwetu kufanikisha haya mambo, asitusumbue…’akasema
‘Hapana….kwa kijana wangu sitaki tena, sitaki muiguse familia yangu tena, imetosha…’nikasema
‘
‘Hahaha hapo ulipofikia huwezi kurudi nyuma . kama nilivyokuambia kuachana na haya mambo ni mmoja wenu afe….hilo sitanii ndugu yangu…na hivi huoni kuwa ile nyota imeshaanza kurudi kwa wenyewe…wenzako pia wanahangaika kivyao, usipojitahidi, sio kwamba tu utafirisika kabisa, lakini pia unaweza kuwa kichaa, na ikitokea hivyo umekwisha..…’akasema.
‘Oh…..mtaalamu, fany aufanyavyo, kijana wangu arudie hali yake, usijali kuhusu mimi…na mke wangu arudi nyumbani, …lakini kwa hivi sasa usifanyie nyumbani kwangu…’akasema.
‘Kwangu hatuwezi kupaacha, labda umuhamishe huyo binti kwenda sehemu nyingine ambayo tunaweza kumpata kiraisi…umenisikia…’akasema na kukata simu.
Mimi …pale nilipokuwa nimekaa nilianza kujisikia vibaya, ina maana mimi nimeolewa na mbwa-shetani, na usiku walinipeleka makaburini,maneno hayo yalinichefua zaidi na zaidi hapo sikutaka hata kumuangalia huyo mzee, maana hata mimi nilishaanza kujihisi kama huyo mama, moyo wangu ulishaanza kumchukia huyo mzee, lakini sikusema neno.
Nikasogea hadi dirishani kupata hewa, naona wote wakageuka kuniangalia mimi.
‘Upo sawa…?’ akaniuliza mama Ntilie.
‘Nipo sawa..hewa ilikuwa nzito…’nikasema
*********************
‘Tuendelee…?’ akauliza huyo mzee, alipoona mimi nahangaika…
‘Endelea lakini naomba uongee mengine sio hayo ya kunihusu mimi…’nikasema nikijaribu kutafuta hewa, maana nilikuwa kama nakabwa, pumzi ilikuwa ndogo.
‘Muache aendelee ni vyema ukajua walichokufanyia, ili ujue ni kwanini mimi nakataa kumsamehe huyu mtu, tamaa zake ndio zitufanye tuzalilishwe, unajua ni mangapi waliyokuwa wakiyafanya kwako na kwangu, na hujui ni nini hatim,a ya iyo mimba yako , …’akasema.
‘Kwangu mimi inatosha…’nikasema nikitikisa kichwa nilitaka nitoke nje kabisa
‘Ni mengi yalifanyika, baadae wakikutumia wewe, na kipaba zaidi licha ya mimi kugoma kuwa wasifanye hayo mambo yao hapo nyumbani kwangu, lakini waliendelea kuja, na bado walinitumia nikisimamia …’akasema.
‘Ina maana kuna mambo mengine yaliendelea kufanywa kwa huyo binti…?’ akaulizwa.
‘Wanasema walikuwa wakitengeza shetani ambaye atakuwa mlinzi wa kupambana na hayo yanayoendelea kati yake na huyo adui yake, na wamegundua kuwa huyu binti ana damu itayowezesha hayo,..kwahiyo waliendelea naye kila hatua, kwani walihitajia shetani ambalo litazalishwa kupitia kwenye tumbo la huyu binti….’akasema.
‘Oh….’nikajitizama tumboni, na kuhisi tumbo likianza kuniuma, nikahisi kizungu zungu, kutaka kutapika…
‘Ina maana kilichopo tumboni ndio hayo mambo yao..?’ akauliza mama Ntiliye
‘Mimi kiukweli yaliyokuwa yakifanyika baadae sikutaka kujua, nilishaanza kuogopa, mambo yalishaanza kuniwia magumu kwangu, na kijana wangu tukawa hatuonani akija anaongea na hyu binti anaondoka, na mama yake akija anaongea na huyu binti anaondoka zake kwahiyo, ili niwasiliane nao ni kwa kupitia huyu binti, mimi nikawa kama nimetengwa
‘Hawakukuambia kitu gani kinaweza kupatikana kwa huyu binti, kuwa atazaaje ….?’ Akaulizwa
‘Hawakuniambia. Ila walisema iwapo atapata ujauzito kuna mambo alitakiwa kufanyiwa kabla hajajifungua….’akasema.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Je aliwahi kufanyiwa hayo mambo…?’ akaulizwa.
‘Mhh..hapana kwa jinsi nijuavyo mimi…’akasema.
‘Ikawaje sasa..maana ulisema kuwa kijana wako alikupa muda wa kumrejeshea hali yake..au nguvu zake, iliwezekana au ilikuwaje, kijana wako alipokuja kwako, uliwezaje kuliweka hilo sawa, na je hajaweza kurejewa na nguvu zake mpaka sasa…?’ akaulizwa.
‘Haikuwezekana , maana baada ya hapo, huyu mtaalamu alisema mwenzake kaharibu kila kitu chake alichokuwa nacho, na sasa iliyobakia ni kuweka mitego yake anayoijua yeye mwenyewe, ili kumnasa huyo adui yake, na hiyo mitego inahitajika kuwekwa kwenye nyumba ambazo huyo adui wake huwa anapita mara kwa mara wakiwindana…ndio maana akawa anawaomba hao akina mama, kwa kusingizia kuwa kuna mazindiko na kitu kama hicho,…’akasema.
‘Kumbwe hakukuwa na mazindiko kama alivyotuambia sisi, sasa kulikuwa na kitu gani …?’ akauliza mke.
‘Hakukuwa na mazindiko, yeye ndio alitaka kuyaweka hayo mazindiko kwa ajili ya kupambana na adui yake, na kama mlivyoona hakufanikiwa, mwenzake alimuwahi…kipindi hicho yupo huko Ocean road, na huko ndio mlikutana naye…yaliyotokea huko mnayafahamu zaidi kuliko mimi.’akasema.
‘Sasa swali, je ina maana hii mimba ya huyu binti ndio huyo shetani wa kupambana na huyo adui yake na ina maana ni mimba ya huyo mbwa -shetani…?’ akaulizwa.
‘Hapo mimi sijui, lakini kwa mara ya mwisho kuongea na huyo jamaa aliniambia hivyo, kuwa ni moja ya silaha zao za kupambana na huyo adui wake, sasa zaidi ya hapo, mimi sijui, na wala sikuwahi kuongea naye kuhusui kuwa hiyo mimba ni ya nani, zaidi ya kauli hiyo, kwa kipindi hicho nilikuwa na mawazo jinsi gani nitaongea na kijana wangu…’akasema.
‘Kwa kifupi unataka kusema kuwa hii mimba sio ya kawaida, mtoto aliyepo tumboni sio wa kawaida, atajifungua kioja au sio…?’ akaulizwa.
‘Mimi hapo siwezi kujua, naomba mnielewe hivyo, siwezi kudanganya, maana sikupata muda huo wa kuongea na huyo mtaalamu tena…baada ya tukio lililotokea….’akasema.
‘Kwahiyo hapa tunabakia na mambo mawili makubwa, la kwaza ni hilo la mimba ya huyu binti….,je atasaidiwaje maana hapo alipofikia hakuna jinsi ni lazima ajifungue, na hatujui atajifungua kitu gani, je hakuna jinsi gani nyingine ya kumsaidia,…hiyo ni kazi yako wewe uliyesababsiha hili..au sio jamani….’akauliza mke wake.
‘Ni kweli, wao ndio sababu na wao ndio wanatakiwa wajue jinsi gani ya kumsaidia huyu binti…’akasema mama Ntilie, mimi nikawa kimia tu, sikuwa na nguvu ya kuongea kabisa.
‘Lakini la pili ni kuhusu kijana wako, je alikuambiaje mlipokutana baada ya siku saba kupita, na yeye utamsaidiaje kurejesha hali yake,…?’ akaulizwa.
‘Ni kweli siku saba zilikuwa zimeshapita, maana hapo kulipita siku mbili tatu hivi baada ya jamaa kusema mwenzake kamuwahi kaharibu kila kitu chake, na ilitokea kabla haijafika hiyo siku ya saba.,..’akatulia.
‘Kijana muda wote huo alikuwa haki hapo nyumbani kama nilivyosema, alikuwa akikaa na babu yake, na huko hawakuwa hivi hivi, walikuwa wakimuhangaikia, kwa namna wanayoijua wao,kwani alimuelezea babu yake kuwa kapatwa na mambo ambayo hayafahamu na yamemuathiri..wakakimbilia kumuambia labda ni sababu ya madawa ya kulevya..
‘Babu sio madawa ya kulevya, …’akasema
‘Sasa unahisi ni nini…?’ akaulizwa
‘Babu nimepimwa haospitalini, wanasema eti kwa umri huo nina martatizo ya kisukari…mara shinikizo la damu, ni kweli babu, hayo sio magonjwa ya wazee…?’ akauliza.
‘Hahaha, mjukuu nikuambie kitu, sasa hivi ni wewe unajiumiza, kwanini unatumia vilevi, madawa ya kulevya, hujui athari zake ndio hizo…’akaambiwa
‘Babu mimi sikupenda iwe hivyo..ni hali ya hapo nyumbani …wazazi wangu nawapenda sana, lakini yanayotokea hapo yananipa mawazo sana, naamua kutumia hivyo vilevi…’alimuambia babu yake hivyo.
‘Hayo mazungumzo, niliyapata kutoka kwa huyu mama yake hapa….nashukuru kuwa wao hawakuweza kukimbilia kusema kuwa kijana kafanyiwa mabaya, kwahiyo ilikuwa ni swali gumu kwangu, nikijiuliza je kijana wangu aliambiwa na nani hayo mambo…
Nilikuwa na wakati mgumu sana na siku saba zikapita bila mchezo,…na kijana hajapona, na aliahidi kama asipopona, atamwambia mama yake na atamwambia mbele ya babu na bibi yake,…
Ilikuwa siku ya saba nikiwa nipo kwangu, siku hiyo sikuweza hata kutoka kwenda kwenye shughuli zangu, siku hiyo mke alikuwa hayupo , na kipindi hicho hata huyu binti hayupo, maana kuna kikao kilifanyika nyuma ikashauriwa huyo binti aondoke, ni kipindi hicho hicho, nahangaika….na nashukuri kuwa hata kwenye hicho kikao kijana wangu hakuweza kuliongelea hilo,
Sasa safari hii sizani kuwa atanisamehe…na nitamuambia nini, ili anielewe, hapo nipo mimi mwenyewe nawaza na kuwazua, mtaalamu anaumwa hawezi kunisaidia tena, je akifa kabla hajamsaidia kijana wangu itakuwaje, nitakwenda kwa nani, ..nikawa najiuliza maswali mengi kichwa …na.mara nikasikia mlango ukigongwa, maana kwa usalama nilikuwa nimefunga milango, nikajua ni mke wangu.
Nikakimbilia kufungua mlango, na mlango ulipofunguka …moyo ukanilipuka utafiri nimeona kitu gani,...nilibaki nimeduwaa, ….CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
NB: Ngoja niishie hapa kwanza
WAZO LA LEO: Familia hujengwa na mshikamano wa wanafamilia, wote wawe kitu kimoja na lengo moja, kusiwepo na sintofahamu ya kila mtu anakuwa na jambo lake binafsi, kwa kufanya hivyo ni kumpa nafsi shetani, ambaye raha yake ni kuhakikisha ndoa hazisimami, ndugu kwa ndugu hawaelewani….
Ni nani hao waliingia …mbona huwataji?’ akaulizwa mama Ntilie akiwa na hamasa ya kujua kilichotokea, lakini mume wa mtu hakujibu swali hilo kwa haraka, ….kama vile anaogopa, kama vile tukio hilo lipo mbele yake.
‘Unajua siku ile nilitarajia kuwa kijana wangu atakuja, kama alivyopanga,..kuwa ikipita siku saba, hajapona basi atamwambia mama yake, na sio mama yake pia na babu yake,…mimi sikutarajia kuwa kijana atakuja mapemda hivyo,…. namfahamu sana kijana wangu, pamoja na hayo yakliyotokea, lakini yeye, ana mapenzi sana kwa wazazi wake.
'Baba naona umegoma kuniondolea hilo tatizo ,ambalo nina uhakika ni wewe uliyelisababisha….’kijana wangu akaanza kuongea, tulipokaa kwenye viti, huyo mwanamke mwengine alikuwa bado nje akiongea na simu. Nilimtupia jicho huyo mgeni, ambaye sikuwa nimemtambua vyema, na sikupenda mambo hayo yaongelewe mbele ya mtu mwingine.
'Subiri kijana wangu tutaongea mambo hayo baadae, huoni kuna mgeni hapa…..'nikisema nikiwa na maana asiongee hayo mambo mbele ya huyo mgeni , lakini ilikuwa kama nampandisha jaziba za kuongea zaidi.
'Mzee hili halina kusubiria, maana nipo kwenye hali mbaya, natamani ninywe sumu tu, kuliko hii aibu ninayokumbana nayo ambayo wewe ndiye chanzo chake….’akasema kijana wangu.
'Kwanini unasema hivyo mwanangu, mimi sikupenda yakukute hayo…na hata mimi linaniumiza sana, lakini bado nalihangaikia hilo swala, tatizo mama yako haamini mambo haya ya kienyeji, kama angetoa ushiriakiano wa kutosha tungeshalimaliza kabisa hili tatizo…, wewe hujui tu…’nikasema
'Najua , usijaribu kukwepesha ukweli, najua haya yote yametokea kwasababu ya kuutaka utajiri…’akasema
‘Mwanangu nielewe hapo..mimi sifanyi mamabo kwa masilahi yangu mwenyewe…kama nilifanya jambo ujue ni kwa ajili ya familia yetu..kama ni utajiri, lakini uwe kwa familia yetu…’nikasema.
‘Ina maana baba kweli unathamini utajiri kuliko mimi mwanao, upo tayari kuizalilisha familia yako, ili tu utajirike, upo tayari kumfanyia mama mambo mabaya ili…..’hapo kijana akashika kichwa kwa kusikitika.
'Wewe unaongea nini mambo hayo, kwanini,…huoni kuna watu hapa hawafai kusikia mambo ya kifamilia, ….’nikasema na kijana bado alikuwa kashikilia kichwa na kuinamisha kichwa kabisa, hataka kuniangalia.
'Huyu anajua kila kitu, bila ya yeye nisingeliweza kuyajua haya yanayoendelea humu ndani, nimemuamini kwa vile kila alichonielezea kimetokea humu ndani, ninavyoteseka usiku na zaidi ni kuwa huyo mtu anayemuelezea kuwa ni adui yake nimeshamuona mara nyingi mkiongea naye, na simuamini huyo mtu kamwe…hata yule mdada wa kwanza alinisimulia kuhusu habari zake…’akasema huyo kijana.
'Ni nani huyu kwani…?’ nikauliza sasa nikianza kuingiwa na mashaka naye, nikamtupia jicho, na yeye akawa kanikazia macho, ..mimi nikagwaya na kuangalia pembeni.
'Baba usitake nifanye kitu kibaya, na kabla ya kukifanya hicho kitu, nitahakikisha mama ameyafahamu hayo yote uliyoyafanya humu ndani, najua ana wakati mgumu na yeye najua na yeye anahangaika kujua humu ndani tumeingiliwa na kitu gani..hajui kuwa adui anayemtafuta wanaishi naye chumba kimoja…’akasema
'Sikiliza kijana wangu, hawa watu ndio wachonganishi,usiwasikilize, hawa ndio wanaovunja ndoa za watu, hawa ndio waoingia kwenye familia na kuzifanya zisiwe kitu kimoja, usiwasikilize kamwe..’nikamwambia kijana na kijana ni kama hakunisikia akasema;
'Baba sio swala la kuambiwa, kwani hali halisi haijionyeshi, kwani mimi sina matatizo, je haya matatizo yametokea wapi, hebu niambie wewe baba, si nilikuja nikakuambia nina matatizo hayo, umenisaidia nini mimi, zaidi ya kuhangaikia utajiri wako unaoutaka …kama ni utajiri sawa, utafute kwa njia zako, kwanini unaniumiza na mimi, kwanini unamutesa na mama, kwanini unawatesa watu wengine baki…binti wa watu kawakosea nini…’kijana akasema.
'Hayo matatizo yako nitayashughulikia, kuna mtu namuamini sana, tutayamaliza, usiwe na wasiwasi ,haina haja ya kutefuta watu wa pembeni, watu ambao hawana huruma na familia yako..haya yataisha, nakuahidi mwanangu..’nikasema
'Huyo mtu unayemuamini ndio huyo mchawi wako wa usiku…’kijana akauliza na kunifanya nishtuke, na kumtupia jicho huyo jamaa, huyo jamaa alikuwa habandui macho kwangu, unafikiri ana kitu hataki akikose kwangu.
Hapo, hapo nikahisi kuwa huenda huyo jamaa ndiye kamuambia kila kitu huyo kijana yawezekana ni mganga wa kienyeji,..au hata sijui ni nani,niliiona ni sura ngeni kwangu, sikuweza kuvumilia, nikasema;
‘Hebu kwanza tutambulishane huyu ni nani, na huyo huko nje anayeongea na simu muda wote huo ni nani…?’ nikaulizai
'Baba kwanza tumalizane na hili langu, nilikupa siku saba, na siku saba zimekwisha, sioni mabadiliko yoyote,…niambie unataka nini kwangu, unataka nijiue…au………?’ kijana akauliza
'Samahanini kidogo, naombeni niwakatize kidogo, samahan sana mzee mwenzangu, unajua kijana kakimbilia kukulalamikia badla ya kunitambulisha mimi kuwa ni nani..ndio utaratibu ulivyo, lakini naona matatizo aliyo nayo yanamnyima amani…’akasema huyo mgeni.
'Wewe ndiye umemdanganya kijana wangu kuhusu hayo anayoongea…?’ nikamuuliza sasa nikiwa nimekunja sura ya hasira.
'Nimemdanganya au ni kweli, hayo aliyoongea ni kweli tupu, niambie uwongo wa hayo aliyoyaongea ni upi,…yeye, alikuja kwangu akiwa na shida zake, kaelekezwa kwangu, kwanza tuliwasiliana kwa simu, nikamwambi akarubuni nitakuja huko….na nikawa nimefika..’akatulia kidogo.
‘Basi nilipofika hapa nikawasiliana naye, nikamwambia aje tukutane, akaja akanisimulia matatizo yake, na kwa bahati nzuri, alikuja sehemu sahihi, kwasababu huyo mtu anayekusaidia hadi mkaingia kwenye matatizo hayo, mimi namfahamu sana….’akasema
'Sina mtu anayenifanyia mambo yoyote kama aliyoyaongea huyu kijana, hizo ni hisia zake tu,..na wewe ndiye umemjaza maneno yenu ya kiganga ya uwongo…’nikasema.
'Huyo mtu unaye…sio kwamba na kisia, au ramli au nini…huyo namfahamu ilivyo maana alikuwa mwanafunzi wangu , aliletwa kwangu nimfundishe mambo ya uganga,… akaasi, akaniibia hata mikoba yangu ya uganga…, na kwenda kujihusisha na mambo ya kichawi badala ya kufuata yale niliyomfundisha,…huyo ndiye anayekutumia, lengo lake sio zuri, anawatumia kwa masilahi yake binafsi….’akasema.
'Tafadhali, hayo unayoyaongea ni uwongo, na sijui yametokea wapi, nakuomba tafadhali tena sana, usimpoteze kijana wangu kwa mambo yenu hayo ya kishirikina, …’nikasema.
'Sio mimi ninayempoteza kijana wako…, tatizo wewe umeshatekwa akili, na huyo mtu, wewe ndiye unayempoteza kijana wako kwa kumharibia maisha yake… na usipofanya juhudi utakuja kujuta, utakuja kumuharibu kijana wako kabisa kabisa…, na maisha yake ya baadae yatakuwa ni ya giza…atakuwa punguani…, na pia umeiharibu familia yako mwenyewe, , kwa kutumiwa na huyo mtu, huyo mtu hana wema kwenu, akimaliza kuwatumia, atarudi kijini kwake na ukimtafuta ataishia kuwazidishia mavumba ya kuwaharibu kabisa…’akasema.
'Sasa wewe unataka nifanye nini…maana naona umeshamuhadaa kijana wangu na amekuamini kuliko hata mimi baba yake..umefanya vibaya sana, fikiria kama angelikuwa kijana wako kakufnyia hivyo ungelijisikiaje…na ni nini lengo lako,…, unataka mimi nifanye nini …?’ nikauliza.
'Huyo mtu.unayeshirikiana naye haaminiki, anachojali ni masilahi yake, anawaharibu mabint za wenzake, ..uchawi wake unategemea sana kuwatumia mabinti, kweli si kweli…kila siku mabinti wanaokuja hapa wanatumiwa kwenye mambo yao ya kishirikina ya usiku, na mashetani na wachawi wenzake, hebu fikiria hilo kama mzazi…’akasema hyo mzee.
'Mimi sijui unachokiongea…’nikasema nikiangalia pembeni, lakini moyoni nilishaona kuwa sasa nimepatikana.
'Kijana, kama nilivyokuambia, huyu baba yako keshalishwa kiapo hawezi kusema ukweli, na usipofanya kama nilivyokuambia, hutaweza kuokoka na hilo tatizo ulilo nalo, hili tatizo lako asili yake ni kutoka kwa baba yako, wewe mpigie simu mama yako, aje na babu yako apa, kabla muda haujakwisha, hao ndio watakaoweza kukusaidia kutoka kwenye hili tatizo, huyu hataweza kukusaidia…’kijana akaambiwa.
Kijana akamuangalia baba yake kwa amcho yaliyojaa hasira huku akitoa simu yake kwenye mfuko wake, nikajua sasa keshatekwa na huyo jamaa, anamsikiliza yeye kuliko mimi na nisipojitahidi kulizuia hili mapemaa, basi mimi nitafukuzwa kwenye nyumba hii kama mbwa…
'Wewe mwanangu ina maana umefikia hatua hiyo ya kumuamini mtu wa nje kuliko hata mimi baba yako, unataka kumuua mama yako kwa shinikizo la damu, maana akisikia haya mambo ya kizushi ataishia kudondoka, kwa shinikizo la damu, unajua jinsi alivyo…’nikamwambia huyo kijana wangu.
‘Baba wewe ndiye unataka kumuua mama kwa shinikizo la damu, nimegundua kuwa wewe hutujali tena…kwahiyo ngoja nimuite mama, maana yeye ana uchungui na familia yake, yeye hawezi kuniumiza mimi kwa masilahi ya utajiri, au ubinafsi…’akasema sasa akiwa anaanza kubonyesha simu yake kutafuta namba ya mama yake. Na huyu mzee akawa ananiangalia mimi usoni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Subiri kwanza mwaanagu, niongee naa huyu mchonganishi…’nikasema, nikimuangalia huyo jamaa machine, na huyu jamaa akawa ananiangalia bila kupepesa macho..
‘Wewe mtu wewe….hebu niambie unataka mimi nifanye nini, maana hujaniambia unachokitaka, zaidi y kuziei kutaka kuiangamiza familia yangu….’nikamwambia huyo jamaa. Na kuwa muda huo kijana akswa kaishikilia simu yake tayari kumpigia mama yake. Niliangalia kuhakikisha kuwa simu hiyo haipo hewani.
'Lengo la kuja hapa ni kutaka kumsaidia kijana wako, aondokane na hilo tatizo alilo nalo, ukiangalaia utagunduaa tatizo hilo ndilo ulikuwa nalo wewe, sasa limehamia kwa mtoto, iweje matatizo yako ya kizee, yahamie kwa kijana mdogo kama huyu, kama sio hayo mliyoyafanya wewe na huyo mwenzako…’akasema huyo jamaa.
‘Sasa mimi nimekuja kumuokoa huyu kijana na kuikoa hii familia kutoka kwenye mikono ya huyo mchawi ambaye anajifanya kuwa anakusaidia kumbe anakutumia tu….’akasema.
'Kumsaidia kijana wangu, safi kabisa, kama ni hivyo basi kwani kuna tatizo gani hapo, mimi sijakukutaza, sikuelewa dhjumuni lenu, haya niambia mimi nifanye nini,…ila kwa maoni yangu, tatizo hili la kijana ni letu tu hapa, tusimuhusishe mama yake kwanzaa, huyo mama yake kwa hivi sasa yupo kwenye matatizo makubwa…, ukimuongezea na hili utamuua kabla muda sio wake…wewe humjui mke wangu …………….’nikasema.
'Ni hivi ili niweze kumsaidia huyu kijana, natakiwa nipambane na huyo mchawi, nim-malize kabisa, ili niweze kuchukua mikoba yangu ya uganga wangu ambao aliniibia na humo ndio nitapata mwongozo wa kuweza kumtibia huyu kijana, hayo ni mambo ya kimizimu, yanahitajia kibali cha huo mkobwa, na hilo tatizo limefungwa kwenye huo mkoba, huwezi kwenda kokote, ukatibiwa, …’akasema.
'Kwahiyo kumbe, nimekuelewa wewe lengo lako ni kutaka kumtumia mtoto wangu kufanikisha mambo yako…wewe unautaka huo mkoba wako, lakini hwezi kuupata mpaka umtumie mtoto wangu, kwanini unafany ahivyo…’nikasema kumuambia huyo mzee.
‘Mambo gani, ya kunifanikisha mimi, hapana, wewe sasa unataka kupotza muda,..mimi nayafahamu sana hayo mambo, najua kabisa, wewe ulishalishwa amini kuwa usiseme kitu…., ni sawa kwa mfumo huo, lakini amini uliyokula ni ya ulaghai,haita fanya kazi, muhimu kwa sasa ni familia yako, usipoijali familia yako ukajali mali, ukajali nafsi yako, wewe sio mzazi mwema…’akasema.
‘Wewe ni mchonganishi, wewe ni mchawi kuliko hao wachawi unaowasema wewe…’nikasema kwa hasira
'Kijana piga simu kwa mama yako, kwa haraka, muda unakwisha….usipoteze muda zaidi,…huyu mtu haelewi ninachotaka kukufanya, na haelewi ugumu na hatari ya hilo jambo, unavyozi kuchelewa huyo jamaa huko alipo anazidi kuficha makucha yake..tatizo linazidi kuwa kubwa, sasa hivi keshagundua kuwa anakaribia kushindwa, nimeshamzunguka, ukichelewa ataficha kila kitu, mimi sitaweza kukusaidia baada ya hapo….’akasema huyo mzee, na kijana akawa anataka kubonyesha kitufe cha kuita kwenye simu.
Nilipoona kijana anataka kupiga simu nikamzuia…na kumshika ule mkono alioshika simu, na mzee akataka kusogea kunizuia, hapo nikasema kwa haraka;
'Sikilizeni kwanza niwaambie, mwanagu usipige simu, kama kweli unampenda mama yako, kama huyu mtu kaja kwa nia ya kukusaidia kweli , hata mimi nitafurahi, nitatoa ushirikiani wote kuhakikisha wewe unapona,..lakini haya mambo akiyasikia mama yako utamchanganya kabisa, mimi namjali sana mama yako huyu hamjali, hata akipatwa na matatizo…’nikasema
'Kijana piga simu, muda unakwenda sijaja hapa kupoteza muda wangu, nina mambo mengi ya kufanya, kama hupigi mimi naondoka, na usije kujilaumu kwa hilo,….’akasema huyo jamaa na kijanaa sasa akabonyesha kitufe cha kuita simu.
Mimi kwa haraka nikaibetua hiyo simu mkononi mwa kijana, na ile simu ikadondoka chini,..na nikasikia sauti ya mama yake akisema;
‘Halloh, unasemaje, mbona huongei….’ Na simu ikatulia.
Kijana akawa anainama kutaka kuichukua, nikasema;
‘Izime hiyo simu tuongee,… maana mama yako alisema atakwenda hospitalini, huenda sasa hivi yupo na docta, na wewe unataka kumsumbua, tusitake kumchanganya kichwa, niambia wewe mchonganishi ulitaka mimi nifanye nini, nipo tayari kutoa ushirikiano…’nikasema.
‘Kwanza mkaribisheni huyo mama huko nje, yeye atatusaidia sana kwa hili jambo…’akasema
*************
Aliingia mama mmoja na kusalimia, nikamkaribisha kiti, na alionekana kuwa na wasiwasi kweli, akawa anaangalia huku na kule, na yule mzee akasema;
‘Huyu ni mke aliyatalikiwa na huyo mchawi anayekutumia, huyu anamfahamu huyo mtu kuliko mwingine yoyote, aliishi na huyo mchawi kwa muda, na kipindi kirefu amekuwa akiona alichokuwa akikifanya huyo mtu, yeye akajaribu kumvumilia, kwa tabia zake mbaya, lakini baadae alipoanza kutaka kumuingiza na yeye kwenye uchawi wake, ndio akaamua kuondoka….’akasema na mimi nikamkagua huyo mwanamke kwa makini,
‘Sasa mbona unapoteza muda tena, unaona ulivyo muongo….’nikasema
‘Sio muongo, huyu ndiye anaweza kukitafiti hicho kitu tunachokitafuta kwa maana yeye anakijua wapi kilipo kutokana na mizimu ilivyo…tutaweza kukipata…?’ akamuuliza huyo mwanamke, na huyo mwanamke akawa ananusua nusa kwa pua…baadae akasema;
‘Hapa kuna kitu…’huyo mwanamke akasema sasa akiangalia muelekeo wa chumba anacholala yule mfanyakazi wa ndani.
‘Huko ndani au…?’ huyo mzee akauliza na huyo mwanamke akakubali kwa kichwa…na mzee huyo akasema;
‘Yaonekana huko ndipo mambo yalikwua yakifanyika, …sasa ndugu yangu tusipoteze muda, kuna kitu tunakitafuta, kakiacha humu ndani, tukikipata hicho, tutaweza kupambana na huyu mtu kirahisi tu, na hatimaye nitapata mkoba wa kuweza kumtibia mwanao…’akasema.
‘Kitu gani mbona mimi sikijui…’nikasema nilimuangalia huyo mzee na hatimaye huyo mwanamke.
‘Unaweza usikijue, lakini kumbuka siku ya kwanza alikuambia anataka kufanya nini ndani ya hii nyumba….mimi nimeshaanza kujua wapi kilipo, lakini wewe mwenye nyumba, unaweza kuturahisishia kazi…’akaambiwa, na mimi nikakumbuka huyo jamaa alichimba shimbo nyuma ya nyumba, na huko chumbani anapolala mdada kuna kitu alikipandikiza..juu ya kona ya chumba,…
‘Huku ndani ni chumba cha msichana wa kazi,sasa hivio hayupo…’nikasema na mama akatikisa kichwa kukubali, na huyo mzee akatoa kitu chake kwenye mkoba, kama pembe ya mnyama, akawa anakiielekeza huko,
‘Unaturuhusu kuingia huko ndani..?’ akauliza
‘Sawa ingineni, mimi sijui kitu…’nikasema
Wawili hao wakaingia ndani, na baadae wakatoka, na kusema;
‘Kuna vingine havipo humu ndani, vitakuwa nje….’akasema na wakatoka nje baadae wakarudi, na kusema;
‘Kuna sehemu mbili hazipo kabisa humu ndani, kwenye eneo lako, kuna sehemu kaziweka,…sasa ni hivi, hapa tupo kwenye mapambano, huyo jamaa siku zake zinahesabika, sijui, kama ataweza…ngoja kwanza tuvitafute hivyo vitu vingine kabla hajavificha, tunakwenda na muda,..’akasema na wao wawili wakatoka.
‘Sawa fanyeni muwezavyo, ila mimi sijui kitu…’nikasema
Wakatoka na baadae huyo jamaa akarudi na kusema;
‘Wewe kijana ngoja tutafute hivyo vitu vingine, sisi tunaondoka ubakie hapa na baba yako, usiondoke,..hakikisha baba yako hatumii simu, maana anaweza kumpa taarifa ya kinachoendelea, akaharibu kila kitu,… kama tukifanikiwa tutarudi, ukituona kimia ujue bado tupo kwenye mapambano…’akasema na wawili hao wakatoka mimi nikabakia na kijana wangu.
Tulikaa kimia, bila kusema neno baadae nikasema;
‘Kijana wangu usiwaamini sana hao watu, kama wana nia ya kukusaidia kweli…., sawa, mimi sina tatizo na hilo, ila hilo la kusema mimi nahusika, sikubaliani nalo kabisa, ni waongo na lengo lao ni kuisambaratisha familia yetu….’nikamwambia kijana na yeye akabakia kimia tu, nikataka kutoka nje , hapo akasema.
‘Umesikia walivyosema, tusitoke humu ndani…, kuna mambo wanayafanya, usitake wakaharibu hayo matibabu, mimi hapa nilipo sina raha, nateseka,..hivi wewe baba hunionei huruma, nimefikia kutumia madawa ya kulevya, bila kupenda, ili kuondoa mawazo, kumbe ndio yamezidi kuniharibu, baba unataka nini, unataka mimi nife kwanza nio urizike,..kama hili halitafanikiwa, sina budu nitafanya hivyo unavyotaka wewe…’kijana akaongea huku akitaka kulia.
‘Mwanangu unataka nikuambie nini ili unielewe, hivi nikuulize kipindi kile unatumia utajiri, unafurahi, ulijua huo utajiri umetokea wapi..mbona muda ule hukuja kuniuliza, hujui ni vipi nateseka kwa ajili yah ii familia, tatizo wewe unamsikiliza huyo mtu bika kuataka kunisikiliza mimi…niamini mimi, mimi ni baba yako siwezi kufanya jambo baya kwa mtoto wangu mwenyewe…umenielewa…?’ nikasema na kumuuliza.
‘Najua ni wewe ulifanya hayo mambo ya kishetani, ukaniwekea mimi, na mimi sikujau, sikuwa na akili yakuyatambua hayo, lakini baadae ndio ukaamua kuyachukua hayo mambo , ili utajiri uhamie kwako, hayo nayafahamu yote, …ila ulichokosea ni kuchukua na hali yangu,….unanifanya mimi niadhirike, nionekane sina maana , mabinti wengi sasa wananidharau, mchumba wangu kani….’akashika kichwa.
‘Sikiliza kijana, hayo mimi nitahakikisha yanakwisha, hilo nakuahidi ilimradi uhai uwepo, mimi nitakusaidia utapona, hata kama ni kuchukua sehemu ya viungo vyangu, hata kama ni mimi kuharibikiwa, hata kama tutakuwa masikini, mimi ni baba yako mimi ni mzazi wako,…lakini tuwe na subira..maana haya mambo sina uwezo nayo mimi, ila yupo mtu ambaye ananisaidia…’nikasema.
‘Huyo mtu si ndio huyo mchawi , huyo anayekutumia, huyo mchawi kawaharibu wasichana wa watu, wewe hujiulizi, kama anawatumiwa watoto wa wenzake, anawaharibu bila kuwajali, huoni jinsi gani alivyo mnyama,.. ..hata huyo mdada alikuwa akikaa humu ndani kamfanyia mambo mabaya sana…’akasema
‘Mambo gani..ambayo unayajua wewe aliyomfanyia huyo mdada, usiamini mambo hayo, ..au ni nani kakuambia hayo mambo..unaona ilivyo, …keshakuingiza kwenye mambo ya kishirikina, …ni mangapi kakuambia, hebu niambie..?’ nikamuuliza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Huyo mjaamaa ni adui wa huyo mchawi, wamekuwa wakiwindana tokea huko kijijini, na wamefukuzana hadi hapa, na kaniambia huyo mdada aliyekuwa hapa kapandikiziwa shetani,…’akasema
‘Kapandikiziwa kwa vipi…uwongo huo…’nikasema
‘Sio uwongo baba,..hayo ya kupandikiza shetani, hayakuanza leo,…wamekuwa wakimfanya huyo mdada mambo mengi mabaya…hiyo mimba ya huyo mdada akikua, na hayo mambo yao yanakuwa, yanamuingia huyo mdada, na huyo mtoto akizaliwa hatakuwa na hali ya kawaida…’akasema
‘Unataka kusema nini , kuwa huyo mdada, ohoo, nimegundua, kumbe wewe ulimpachika huyo mdada mimba na lengo lenu ni kuiharibu au sio, niambie ukweli, mimi baba yako nitakusaidia…’nikatulia.
‘Ukweli upi baba, mwenyewe unajua, sina uwezo huo…labda ni wewe, labda ni wao, …ila nijuavyo, kwa jinsi alivyoniambia, huyo mdada ni mke wa shetani –mbwa, na wamekuwa wakimfanyia mambo mengi, wewe ukihusishwa PIA….’akasema.
‘Na wewe pia…’nikasema halafu nikashtuka kuwa nimeropoka, nikasema
‘Na wewe ukiamuamini…Ina maana kakuambia hayo, kwanini akuambie wewe, sije kuniambia mimi,……?’ nikauliza
‘Akuambie wewe wakati wewe unashirikiana na adui yake…..’akasema
‘Muongo huyo anataka kukutumia wewe ili kupambana na adui yake, tunatakiwa hapa tuwe makini…’nikasema
‘Baba huelewi, naona wewe hutaki mimi nipone, kwa hivi sasa nipo tayari kufanya lolote lile, ili nipone, najua wewe unachofanya ni kujiangalia hali yako, lakini ukumbuke mimi sikuwa na matatizo, matatizo yako umehamishia kwangu, uone baba ulivyo, kwanini unichague mimi, kwanini unanichukia hivyo,…’akasema
‘Nikuchukie kwanini nikuchukie, hapana usifikirie hivyo mwanangu,na wala usije kuliongea hilo, hakuna mzazi anayewachukia wanae…’ akasema.
‘Unaweza kusema hivyo usoni kwa watu, lakini moyoni ikawa tofauti na ikipatikana nafasi kama hii huwezi kusita kufany akama ulivyonifanyia mimi, lakini baba, hata kama wewe hunipendi, lakini mimi nawapenda sana wazazi wangu, nimejitahidi sana kuombea nyie na mama muishi kwa amani, na upendo, lakini sijui kwanini, na hili sasa limetokea, yaonyesha kuwa wewe ndiye una matatizo baba….’akasema.
‘Kijana wangu haya ni mambo ya kikubwa hutakiwi kuyaingilia,…utaumia muda sio wako, nisikilize, mimi na mama yako tumekuwa hivi, ..kuna kukosana , badae tunapatana, ni hali ya kawaida ya ndoa, hilo lisikuumize kichwa kabisa, unajua nimekuelewa, mawazo hayo ndiyo yamekufanya upatwe na matatizo hayo uliyo nayo, sio hayo anakudanganya huyo mtu,…umenielewa hapo…?’ nikauliza
‘Baba mimi sijui…usitake kunificha …mimi ninachotaka nipone, kama huwezi kunisaidia wewe, najua mama atanisaidia, …..’akasema
‘Hilo mwanangu lipo mikononi mwangu haya ni mambo ya wanaume,mama yako hawezi kuyafahamu, ngoja tuaone huyo mtu wako atafanya nini, akishindwa mimi nitalifuatilia mpaka utapona, yatakwisha tu….’akasema
‘Kwahiyo baba, kama nisipopona hili tatizo ina maana mimi sitaweza kuoa tena…?’ kijana wangu akaniuliza
‘Kwanini usipone, ..tatizo huyo mtu kakuvuruga akili tu…mimi najua hayo mambo yapo na yanapona,…niamini mimi utapona,…mimi nitahangaika kumtafuta bingwa wa hayo mambo, tutayamaliza, kitu muhimu, iwe siri kati yangu mimi na wewe..hakikisha mama yako halijui hili…’nikasema
‘Babu nilimuambia ..kuwa nahisi kuwa nina tatizo la namna hiyo sikumfafanulia jinisi ilivyo, akasema ni sababu ya madawa na ulevi, niache nitapona, lakini sio kweli, najua kuna tatizo zaidi ya hilo, na huyo mtu ndiye kanifichulia ukweli,……’akasema.
‘Hata mimi naamini ni kwasababu ya madawa na ulevi,…muhimu wewe na subiria tu,…niamini mimi haya mambo, nitayamaliza mimi mwenyewe…’nikasema huku moyoni nawaza nifanye nini kumthibitishia kijana wangu kuwa mimi namjali kama mzazi wake, je ni yupi nimuamini kati ya hao watu wawili, huyo mtaalamu wangu au huyo adui yake.
‘Baba mimi nakuahidi hapa, kama hili tatizo halitatafutiwa ufumbuzi mimi nitafanya jambo…mtakuja kujuta wenyewe, lakini kabla ya kulifanya hilo jambo, nitahakikisha familia nzima inafahamu kila kitu kilichowahi kutokea hapa kwenye hii nyumba nitakiweka wazi,,…kuanzia yule binti wa awali, hadi huyu wa sasa…kuwa wewe ndiye unayehusika, hilo baba sikufichi, …’akasema.
‘Kwanini mwanangu unasema hivyo…kwanini huaniamini mimi….’akasema
Kabla hatujaendelea na maongezi, mara simu ikalia, ilikuwa simu yangu nikaichukua, alikuwa anapiga mke wangu,…
‘Halloh,…?’ nikaita na kusikiliza kwa makini…
‘Unasema nini…kwani wewe upo wapi, hospiatalini …mmh, nakusikiliza…?’ nikauliza kwa mshangao huku jicho limenitoka…..nikawa namsikiliza huku namuangalia kijana wangu ambaye naye alivutika kusikia hicho ninachoambiwa na mama yake, lakini asingeliweza kusikia kile mama yake anachokiongea.
NB: Ni kitu gani kitakachoendelea.
WAZO LA LEO: Usimuombee mwenzako ubaya hata kama ni adui yako, maana huwezi kujua , huenda huo ubaya anaokufanyia wewe unaweza ukawa ni neema ambayo mola wako kakukadria kukupa huko mbeleni, muhimu ni kuvuta subira na kuendelea kutenda mema.
‘Unasema yaonakena kuwa amefariki, ina maana huna uhakika bado…?’ akauliza kwenye simu na kuendelea kusikiliza
Baba mtu aliuliza huku akijaribu kuangalia pembeni ili kijana wake asisikie anachoongea…, baadae akasikiliza kidogo, halafu alipomaliza kuongea na simu akamgeukia mtoto wake na kusema;.
‘Oh….sasa sijui itakuwaje…’akasema
‘Ni nani amefariki..?’ kijana akauliza na baba yake aliposikia hivyo akajua kijana wake kamsikia, hakutaka ayajue hayo kwanza, akasema;
Tuendelee na kisa chetu...
************************
Nilitulia kwanza nikiwa sina nguvu,...unajua kuishiwa na nguvu..nikajikuta nimesema tu...
‘Bado hawana uhakika…, yule mtu ana roho kama ya paka, nasikia kuna kipindi ilitokea hivyo, wakawa wameshajua kafariki, baada ya muda akazindukana..ngoja tusubirie…’akasema akiangalia pembeni, na kijana wake akamsogelea na kuuliza;
‘Lakini ni nani huyo..?’ akauliza kijana, na mara simu ikaita , ilikuwa simu ya kijana, na kijana kwa haraka akataka kuisikiliza....na baba mtu akataka kumzuia kijana asiipokee, lakini kijana alikuwa ameshaiweka hewani, akawa anasikiliza….
‘Ndio unasema, kuwa…taarifa,… taarifa gani hiyo, sijasikia taarifa yoyote..kwani imekuwaje, hakuna nilichosikia bado, sawa nasubiria…kwani…!’ kijana akasema, na kukatiza, yaonekana mpigaji alishakata simu. Kijana akageuka kumuangalia baba yake, baba yake alikuwa karibu akijaribu kusikiliza hayo maongezi.
‘Ni nani huyo…?’ baba akauliza akimuangalia kijana wake,na kijana wake akawa anageuka wasiangaliane na baba yake, akasema;
‘Ni rafiki yangu tu…’akamdanganya baba yake, na baba yake akageuka akiwa anataka kuondoka, kijana akageuka na kumuona baba yake keshafika mlangoni, akamuuliza;
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Sasa baba mbona unaondoka, unakwenda wapi..?’ akauliza kijana akitembea kutaka kumzuia baba yake asiondoke , lakini baba yake alishafika mlangoni..
‘Lazima niende huko hospitalini nikaonane na huyo mtu akifariki kabla hajamalizana na sisi unajua itakuwaje,…yaani ni muhimu sana nionane naye vinginevyo, hatutaweza ..oh, ngoja niondoke mwanangu, sijui itakuwaje…’akasema baba mtu, akionyesha kuchanganyikiwa.
‘Kwani ni nani huyo… mbona sikuelewi…baba, niambie..mbona unaondoka…’kijana akasema na baba yake akawa ameshatoka nje, na kwa haraka kijana akachukua simu na kupiga namba na alipopokelewa, akasema;
‘Mzee kaondoka sasa nifanye nini..?’ akauliza na alipojibiwa akasogea kwenye sofa akakaa, na kuinamisha kichwa chini, alibakia pale kwa muda, baadae akasimama, …akatembea huku na kule kwa muda bila kutuilia, baadaye akashikwa kichwa na kujikuna kwa mara nyingi, alikuwa kama anawashwa, akawa anahangaika kwa muda, baadaye huyo akatoka nje
Wakati anatoka simu yake ikawa inaita, yeye hakutaka kuipokea, akawa anatembea kuelekea kituo cha mabasi hadi sehemu wanapokaa vijana na kuongea na mmojawapo, wakasogea pembeni akapewa kitu mkononi, akatoa pesa na baadaye akaondoka pale na kuelekea sehemu nyingine…
****************
‘Umemaliza….’akaulizwa na mkewe na hapo akashika kichwa, na baadae akasema;
‘Hayo ndio maelezo ninayoweza kuwasimulia, kwani baada ya hapo ndio ikaja taarifa kuwa yule mzee mtaalamu amefariki kiukweli, na taarifa hizo nilizipata nikiwa nimeshafika hospitalini, nikiwa nahangaika kuonana naye…
‘Ina maana siku ile ulikuwa upo hospitalini muda, wakati tunakutafuta kwenye simu…?’ akauliza mkewe.
‘Ndio, sikutaka kupokea simu zenu maana ningeliwajibu kitu mshindwe kunielewa,…nilifika hapo hospitalini muda, nia kuonana na huyo mtu, ili nimuwahi aniambie cha kufanya, maana kijana ataponaje, wakati alikuwa hajamaliza hayo mambo yake…’akasema.
‘Sasa ikawaje….?’ Akaulizwa.
‘Yaani pale nilikuwa kama sio mimi….nilitaka hata kwenda kuiona hiyo maiti yake, nilikuwa siamini kuwa huyo mtu ni marehemu..., lakini hao wahusika wa hapo hospitalini walinikatalia kuiona hata hiyo maiti.. , basi nikahangaika pale, baadae wazo likanijia, nimpigie simu huyu adui yake, lakini sikuwa na namba yake ya simu, nikampigia kijana wangu simu;
‘Unaweza kunipatia namba ya huyo mganga wako…?’ nikamuuliza huyo kijana hata bila ya kusema haloo.
‘Mganga wangu, yupi….baba…sipo vizuri kwa sasa, nipigie baadae…’kijana akakata simu, nikahamaki nikampigia tena na tena, baadae nikasikia,
‘Simu unayopiga haipatikani…’hapo nikajua mambo yameharibika.
Nilibakia pale hospitalini kwa muda, na baadae ndio nikapokea simu ya mke wangu akiniarifu kuwa taarifa kamili zimekuja huyo mtu keshafariki, na wao, hawawezi kuondoka hapo, hospitalini …mimi sikutaka hata kuuliza kwanini hawataki kuondoka hapo hospitalini, nilikata simu.
Kiukweli kuwa muda huo ungeliniona ungelinihurumia, kuna muda, ninalia, kuna muda ninaongea peke yangu , hata sijielewi,.....baadae nikaona watu wanafika, nikamuona mume wa rafiki wa mke wangu ambaye ni askari akifika, mimi nikaona niondoke tu...
‘Kwanini sasa na ulitakiwa uwepo hapo na mkeo ili kujua kinachoendelea…?’ akauliza mama Ntilie.
‘Hapo kichwa hakikuwa changu, na sikuwa nafahamu kinachoendelea kati ya mke wangu na huyo marehemu kuwa walikuwa huko hospitalini kwa dhumuni gani, hilo sikuwa nalifahamu,..na muda huo akili yangu ilikuwa inawaza mengi, nawazia jinsi gani nitaweza kumsaidia kijana, nawazia hatima ya yoe hayo, ina maana baada ya hilo, kijana atamwambia mama yake, na babu yake, kwahiyo itakuwaje, ndoa itavunjika.
Nilitoka hapo nikawa nimepanga sasa niende kwa rafiki yangu mmoja, rafiki yangu huyo ndiye yule aliniunganishia na huyo marehemu, nikijua yeye anaweza kunisaidia kimawazo, nilipofika kwake, hakutaka hata kuniona, kisa nilipofanikiwa sikumjali, ni kweli kipindi hicho, sikutaka hata kumsikiliza matatizo yake, ..
‘Sikiliza kwanza, kipindi kile nilikuwa nimechanganyikiwa…’nikasema kumwambia, hakutaka hata kunikaribisha ndani, mimi nikaingia kama kulazimisha tu..
‘Unachanganyikiwa ukiwa na hali nzuri, hiyo hali nzuri ungeipataje kama sio mimi kukushauri uende kwa huyo jamaa, sasa naona umefirisika, au sio,.sasa unataka nini kwangu…?’ akaniuliza.
‘Nina shida, umepata taarifa…’nikamwambia
‘Taarifa gani…?’ akaniuliza akiniangalia kwa uso wa kutaka kujua.
‘Yule mtaalamu kafariki…’nikasema na jamaa akashikwa na butwaa kwa muda,….halafu akasema
‘Oh, kumbe ni kweli, usiku nililiona hilo...ooh, sasa eeh...mungu wangu, mambo yameharibika…’akasema.
‘Sasa ndio hivyo nimekuja kwako, unipe ushauri…si unajua...’nikasema
'Najua...najua...oh..hapana, sijui kitu, ondoka, ondoka...'akasema hivyo, na baadae akakaa kimia, hasemi kitu ni kama ana jambo limemgusa zaidi ya huo msiba..akashika kichwa, akataka kutembea kuingia chumbani, lakini akagundua kuwa kunma mgeni, akasimama.
‘Unasikia, bora uende, maana mambo yameharibika….’akasema
‘Ni kweli yameharibika, kijana wangu nitamfanyaje...'nikasema
'Kijana wako....?' akaniuliza akiniangalia kwa mshangao.
'Ndio, alikuwa hajamalizana naye...ndio nimekuja kwako unipe ushauri, maana yeye ndiye aliyenifanyia mambo mengi, sasa yanamuathiri kijana wangu, nifanyeje sasa…’jamaa akauliza.
‘Wewe unafikiria kijana wako tu, hujui mimi nina majanga kiasi gani,..yeye ndio alikuwa kiongozi wetu, tunakula kwa kupitia mgongo wake, sasa kandoka, kukiwa na mambo mengi hayajakamilika, hata mimi familia yangu ipo hatarini, bora uondoke tu…kila mtu afe kivyake, ...'akasema
'Sijakuelewa ina maana na wewe alikufanyia mambo hayo kama mimi...?' nikamuuliza
'Yaani we acha tu,...lakini mimi sio kama wewe...ila sikiliza, mungu wangu sijui utafanyaje, maana kama mlikuwa hamjamalizana, imekula kwako, jiandae kuwa tahira, vinginevyo, wewe au mkeo, au mtoto wako akatolewe kafara,…’akasema akinisukuma jamaa niondoke.
'Akatolewe kafara la nini na nani...?' nikauliza
'Inabidi ufunge safari...mmh, kamuulize yule binti...'akasema
'Binti gani huyo...?' nikamuuliza
'Yule mfanyakazi wako wa kwanza...atakusaidia..mimi sijui zaidi ya hapo, nina mambo yangu mengi kichwani, sijui. maana kila kitu alikuwa nacho yeye, mambo ya usiku, ...mmh, sasa hili balaa...vitu vyangu vitakuwa wapi...'akasema akishika kichwa.
‘Kwahiyo ina maana gani hapo mbona sikuelewi, au,… wewe ndio miongoni mwa watu mliokuwa mkishirikiana naye usiku…?' nikamuuliza
'Wewe ondoka bwana usinichanganye..ondoka ondoka....'akasema kwa ukali.
'Wewe ndiye ulinielekeza kwake, wewe ndiye unayemfahamu, na sasa yaonyesha wewe ndiye mlikuwa mkishirikiana naye,...'nikasema
'Sikiliza sasa hivi tupo hatarini,...jamaa kazidiwa na adui yake, na kama ni hivyo wote washirika wake wapo matatani,hapo ni mmoja baada ya mwingine, bila kufanya jambo, tumekwisha...'akasema
'Kufanya jambo gani sasa...?' nikamuuliza
'Mimi sijui...mpaka nihangaike, sijui...wewe ondoka tu, siwezi kukusaidia kwa hilo...'akasema
'Sasa tusaidiane ..maana kama ni hivyo...'nikasema
'Nimekuambia uondoke nyumbani kwangu, usiniongezee matatizo..,..au nikuitie mwizi,..hebu ondoka, jamaa akazidi kunisukuma niondoke , alikuwa kachanganyikiwa kweli, na mimi nikaona hapo sitasaidiwa kitu ikabidi niondoke
**************
‘Ina maana huyo mtaalamu alifariki kutokana na mapigano ya mambo yao na adui yake…?’ akaulizwa baada ya kupita kitambo, kwani alikuwa kama hajisikii vyema, ikabidi atulie kwanza.
‘Yawezekana,…kwani huyo mama ambaye aliongozana na huyo adui wa mpinzani wa mtaalamu wangu, alitumwa kwenda huko hospitalini na huyo mpinzani, sijui alitumwa nini,…maana nilisikia, alipofika tu ndio huyo marehemu akapiga ukelele,…kwahiyo kuna namna ilifanyika hapo…’akasema.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Namna ipi hiyo….?’ Akaulizwa.
‘Huyo adui yake alikuwa natafuta mwanya wa kumuingia huyo adui yake,…na akaona njia ni kumtumia huyo mwanamke, ..ni kama vile yeye alijificha nyuma ya huyo mwanamke, na huyo mwanamke alipoingia tu, yeye akarusha hilo kombora lake,..au yeye, alibakia sehemu akiangalia huo mwenendo, au huyo mama alipewa kitu akifanye akifika huko hospitalini…’akasema.
‘Wewe ni nani alikuambia hayo…kuwa huenda ilifanyika hivyo?’ kaulizwa.
‘Nahisi hivyo tu…, maana baada ya hapo sikuweza kuonana na yoyote kati yao, zaidi ya huyo jamaa niliyekwenda kwake akanifukuza..na huyo jamaa akatoweka siku kadhaa alirudi baada ya mazishi, sijui alikwenda wapi, na hata aliporudi na yeye akawa anaumwa sana..’akasema.
‘Sasa ikawaje..?’ akaulizwa.
‘Basi mimi nikarudi nyumbani, nikidhamiria kuonana na kijana wangu , na kijana hakurudi mpaka kesho yake, na aliporudi nikamwambia kuwa huyo mtu kafariki, na kijana hakutaka kusema na mimi akawa kimia tu, ndio nikamwambia naomba namba ya huyo mganga wake, akanipa…’akatulia.
‘Ukampigia huyo mganga wake..?’ akaulizwa.
‘Ndio nilimpigia,…na alipopatikana akasema anaumwa, hataweza kuongea na mimi kwenye simu…hali yake sio nzuri…na nikamuomba anielekeze hapo anapoishi, akasema nimuulize kijana wangu atanielekeza, na nikamuuliza kijana wangu akanielekeza.
Nikajipanaga kwenda kuonana na huyo jamaa nikijua sasa yeye ndiyo wa kutusaidia, kijana akawa haongei zaidi ya kile unachomuuliza, anakujibu kwa mkato tu, akawa hana raha, kama mgonjwa.
Basi siku iliyofuata nikaamua kwenda kuonana na huyo mtu, nilitoka mapema kabisa, nilipofika nikakuta watu wamejazana, nikauliza kulikoni, nasikia kuna msiba,..msiba wa nani, nikaambiwa ni mzee mmoja alifika hapo, ni mgeni, na nilipodadisi sana, nikagundua kuwa ni huyo niliyemfuata..hapo sikukaa tena nikarudi nyumbani.
Baadae kijana akaja, akiwa anatetemeka, hali yake ni mbaya, nikajaribu kumdadisi ndio akanipa taarifa kuwa huyo mganga wake naye kafariki,…na sasa hajui ataponaje,..basi ikabidi nimliwaze kuwa nitamtafutia mtu mwingine asijali, lakini moyoni nilikuwa sijui ni nani wakutusaidie, nilishakata tamaa.
‘Sasa kijana wako ataponaje, au mlifanya juhudi gani …?’ akaulizwa
‘Kiukweli kuanzia hapo, na mimi nikaanza kujisikia vibaya, kichwa kinauma kupitiliza, nikawa kama naanza kuchanganyikiwa, nahisi vitu vingi kichwani,…’akasema
‘Sawa ikawaje..?’ akauliza
‘Sasa ikawaje…hahaha..hapo nikajua sina changu, sina familia, sina ….basi nikaanza kuongea peke yangu kama mtu aliyechanganyikiwa.
****************
Kesho yake nipo nipo tu..mara kijana akaja, na kunikabidhi bahasha, na hakusema kitu akaondoka,…nilipoifungua hiyo bahasha ndio nikakuta kanda ya video,..cd
‘Video ya nini…?’ akaulizwa
‘Sikujua ya nini, maana ilikuwa haijaandikwa kitu juu yake, ila mimi nikaamua kwenda kuitizama ina ujumbe gani ndani yake,..akilini nilishaanza kuingiwa na mashaka, ukumbuke mimi muda huo nipo nipo tu, ila hamasa ya kuiangalia hiyo video, ilinijia tu…nikaenda kuiangalia..mamamama..ni aheri nisingeiangalia…
‘Ilikuwa na nini…?’ akaulizwa
‘Kila kitu kama alichosema kijana..kila kitu, na mwishoni ..ooh, hapo nikaitoa……nilichofanya hapo, ni kuitoa na kuiharibu, nikahakikisha hakuna hata salio limebakia, nikatoka humo ndani na kuanza kukimbia, …
‘Kukimbia…unakimbia kuelekea wapi…?’ akaulizwa
'Kumtafuta mwanagu ,kumuwahi kabla....hapana sikuwa na akili hapo, karibu ngongwe na magari...
‘NB: Haya, jamaa ndio hivyo, je haya yaliendaje…maana baada ya hapa, mke anaanza kuingilia kati..ilikuwaje kuhusu huyu jamaa na je ni nini hatima ya kijana , je kwenye hiyo video kulikuwa na nini hasa….tutaendelea seehmu ijayo
WAZO LA LEO: Chuki ni tabia ya shetani, na yeye kazi yake kupandikiza chuki kwenye nafsi zetu ili tukosane, ili kusiwe na upendo kati yetu, nia ni kufarakanisha ndoa, udugu, na mshikamano. Tunatakiwa tulishinde hili, na kulishinda hili n kujenga upendo, kuhurumiana, kusameheana. Ukijiona wewe unawachukia wenzako, kwasababu mbali mbali ujue unatawaliwa na shetani. Mpende jirani yako, mpende hata adui yako, utaweza kumshinda shetani.
‘Kwanini ulikimbia kwani hiyo video ilionyesha nini…?’ akaulizwa na hapo akatulia kama anawaza jambo, akaniangalia mimi, na alipoona namuangalia akageuza uso kuangalia kwingine, halafu akasema;
'Hiyo video, ilionyesha karibu kila kitu, ….’akasema na kutulia
Tuendelee na kisa chetu
***************
‘Kila kitu , ...hya tuambie vitu gani hivyo, mbona unakuwa kama unaogopa kuviongea hivyo vitu, ukumbuke kuwa haya tunayafanya kwasababu yako, sasa usitupotezee muda hapa…’akasema mke
'Unajua hapa natafakari mengi...sawa nitaongea tu, usiwe na shaka...'akasema
'Kwenye hiyo video, ilipoanza, ilikuwa inaonyesha kijana wangu, kakaa kashika shavu, kainamisha kichwa chini, baadae akainua kichwa, usoni kukaonekana machozi..kuashiria kuwa alikuwa analia..ndivyo ilivyoanza hivyo...baadae ikaonyesha anaongea, ...alikuwa anaongea mengi tu, lakini mimi nitaelezea yale yanayohusu hili tatizo.
'Ndugu walengwa, sikupenda kulifanya hili,...maana najua madhara yake, nawaheshimu sana wazazi wangu na kuwapenda sana, na najua baada ya kuuona huu ukweli, mtahakikisha kuwa video hii mumeiharibu, nisinelipenda hili likaenda zaidi ya nyie niliowalenga...'akalisema hivyo kwenye hiyo video.
'Mimi sina ubaya na mama, maana pamoja na ya kuwa awali nilihisi yeye ndiye mbaya kwa baba, lakini baada ya uchunguzi huu, nikagundua kuwa kumbe baba ndiye yupo nyumba ya haya mabaya yote kwa ushahidi wa haya mtakayoyaona...nampenda sana baba yangu, niliomba kila siku abadilike, niliomba kila siku ..ampende mama, niliomba kila siku hali yetu iwe kama zamani, lakini kila siku ilikuwa afadhali ya jana...
Basi hapo akaonyesha picha za wazazi wake, wakati wa ndoa, jinsi walivyokuwa wakipenda, na baadae akaonyesha kitu kama mpasuko...na kuweka ngurumo kwa radi, halafu akaanza kuongea...
‘Siku za baadaye hali ikaanza kubadilika, baba akawa kama hamjali mama, kukawa na mabishani hata kwa kitu kidogo, baadae nikahisi labda ni kutokana na hali za kiuchumi, maana kuna muda hali ilikuwa mbaya, maisha yalikuwa magumu, nikasikia mara kwa mara baba akisema ipo siku nitakuwa tajiri kama baba yako na wewe na wazazi wako mtakuja kuniheshimu.
Kijana alielezea mengi kwa jinsi alivyoona yeye....'hapo akatulia kuongea na mama Ntilie akamuuliza
‘Sema ukweli wako, ni nani chanzo cha mabadiliko ya ndoa yenu, ni kitu gani kiliwafanya nyie wawili msielewane…?’ akaulizwa.
‘Ukiuliza hivyo utanifanya nijitetee nafsi yangu, mimi niliona kama mke wangu hanijali, kila nichomuambia hanisikilizi, anajiamulia anavyotaka yeye, vikao, shughuli, ..yaani hakuna kushirikishwa...na hilo likanifanya nihisi ni kwa vile mimi sikuwa na mali kama wazazi wake, kwahiyo uinabidi nitafute mali niwe kama wazazi wake …ndivyo nilivyoona hivyo…’akasema.
‘Ni kweli kuwa mke wako alifanya hivyo, kwa vile wewe hukuwa na mali kama wazazi wake..?’ akaulizwa.
‘Kwa muda huo nilifikiria hivyo, lakini baada ya haya yote niligundua kitu, kuwa ni udhaifu wangu tu, unajua tena sisi wanaume tulivyo,...ukiona huna kitu , mke ndiye mtendaji kuna hali ya...kujisikia vibaya fulani...kwahyo nikaona nitafuta namna ya kujionyesha kuwa mimi ni mwanaume...
Mara kwa mara kulikuwa na vikao vya watu fulani, unajua kwenye jami kuna makundi ya namna hivyo, wenye uwezo wanakutana kwenye mahoteli,..au vikao vya ..namna kwa namna, mimi ilifika sehemu siwezi kuhudhuria...sikuwa na kitu, na nikifika,..oh, labda michango , wenzangu wanatoa bila kusita, mimi, kwanza najiuliza..ni hali yangu ..lakini iliniuma sana..'akatulia
'Kwahiyo kwa hali hiyo, ikanivuta nifanye jambo...nikaanza kutafiti, wenzangu wamefanya nini..kwa bahati mbaya nikakutana na marafiki wa namna ambayo isingelinisaidia, na nikajikuta nimetekwa na mawazo yao zaidi, sikujali elimu yangu tena...'akatulia.
'Ni kwamba ilishafika mahali nahitajia mambo kwa haraka bila kufikiria mbele, na hao niliowauliza ndio wakanisimulia utajiri wa kupitia huko kwa shetani ….…’akasema.
Haya tuache hayo tuelezee kuhusu hiyo video...'akaambiwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Kwenye hiyo video alielezea kuwa ile hali ya sisi wazazi kutokuelewana ilikuwa ikimkera sana , akawa anatafuta jinsi gani ya kuwasuluhisha wazazi wake, jinsi gani hata yeye anaweza kuleta utajiri, ili wazazi wake wawe na raha.. lakini hakuweza, hakujua, kwani hata elimu yake aliyopata japokuwa alifaulu vyema, lakini alikuw ahajapata kazi, kazi zimekuwa ni adimu...
'Kuna muda akavutika na biashara haramu....'hapo akatulia
''Biashara gani...?' akaulizwa
'Hakusema, ila alisema hivyo, kuwa alitaka atafuta njia ya kupata utajiri, huenda ukawafanya wazazi wake wakajirudi na kuwa kitu kimoja...hapo akawa anaonyesha jinsi wazazi wake wanavyogombana, kumbe tukigombana , alikuwa akatuchukua kwenye video yake.
Alielezea mengi tu, na hata kuwatupia lawama babu na bibi kwa jinsi walivywatenga watoto wao, anasema kwamba kama babu na bibi wangeliwachukua watoto wao walivyo, wakawawezesha kuliko kuwatenga , eti kwa vile bint yao hakukubaliana na wao, huenda mengine yasingelitokea...
Sasa ndio akaja sehamu ya pili, sehemu hii akawa anaonyesha, mabadiliko ya baba...
Akaelezea alivyoanza kuona mambo ya ajabu
‘Kiukweli nimevumilia sana, na sijui hata nianzie wapi..ila ninachoweza kuwa na uhakika nacho ni kuwa mambo yalianza kuwa mabaya pale baba aliporudi kutoka safari ya mikoani…ninaweza kushuhudia hilo, maana mimi nipo karibu sana na baba yangu.
'Siku hiyo aliporudi , usiku wake nilimuona akichimba shimbo upande wa mbele wa nyumba, na nikajua labda kuna kitu kichafu anakifukia, lakini kilichonishangaza, ni ile hali ya baba alikuwa hajavaa nguo, na ilikuwa ni usiku sana, na kuna matukio kama hayo yaliendelea kutokea. hapo akaonyesha kwa mbali picha ya mimi nikifanya jambo..nikiwa sina nguo..
Akaendelea...
'Mara nikaanza kuhisi kama kuna watu wanakuja usiku lakini siwaoni, na wakati mwingine nahisi kama kukabwa, hali hii ilikuja hata kutokea kwa mabinti wa kazi waliokuja hapo nyumbani, na kuna siku nilijaribu kumuuliza baba lakini hakutaka kuliongelea hilo nikahisi kuna kitu ananificha, aliniambia ni mambo ya kawaida ya watu wazima nisiwe na wasiwasi nayo…
Mimi napenda kudadisi, nikavutika sana nikawa nachunguza kinachoendelea usiku, na kawaida yangu nimejenga tabia hii ya kuhifadhi kumbukumbu nyingi kwenye video…basi nikaona hili la baba nitalichukua kwenye kumbukumbu zangu, ili baadae nije kumuonyesha..
Uchunguzi huu ulinifanya nigundue mambo ya kutisha zaidi...maana usiku nilioweza kuamuka, na kufuatilia, niliweza kumuona baba akifanya mambo ya ajabu ajabu...na cha ajabu kuna usiku mwingine nilikuwa siwezi hata kualala, maana nikilala najikuta naota ndoto mbaya, au nahisi watu wanakuja kunisumbua, japokuwa hata nikijitahidi kuna muda nazidiwa nguvu najiukuta nimelala…hali hii ikwa inanipa mashaka, nikaogopa hata kulala humo ndani.
Hata hivyo niliweza kuchukua baadhi ya video, zikimuonyesha baba akiamuka usiku, na kilichonita mashaka ni jinsi baba alivyokuwa akitembea...anakuwa kaam sio yeye...ndio maana hata niliposikua habari kuwa baba ana ugonjwa wa kuota kwamatendo nikakubaliana na hilo.
Lakini baada ya kuchunuza sana nikagundua sivyo hivyo wanavyosema kutokana na matukio haya nitakayoyaonyesha hapa ...hapo akaanza kuonyesha baba yake anavyotoka usiku...na kuna muda kama anaongozwa na mtu , mtu aiyeonakena...
Ikawa inaonyesha video mbali mbali, nyingine baba yake akitioka usiku na kutembea kama roboti akielekea chumba cha msichana wa ndani, baadae anatoka, ..na vitendo kama hivyo vilikuwa vingi, lakini ambayo ilionyesha mambo ya ajabu
Baadae nikasikia kuwa mama katengeneza video ya kuchukua matukio humo ndani, nikachunguza mpaka nikaigundua ilipo, nikawa naifuatilia hiyo, na siku mama alipoipeleka kwa huyo mtu wake, mimi nikaifuatilia na kuiba, ...baada ya kukamlisha kazi aliyopewa,..huyo mtu namfahamu sana.
Na nilipoona hiyo video ndio nikaamini kuwa baba hakuwa na matatizo kama alivyosema docta kuwa baba anaota ndoto kwa vitendo, maana ….ndani ya video hiyo walioekana watu waliojificha kwenye kitu kama giza, na huyo mtaalamu akakuza, na kuwaonyesha watu wa ajabu,..wachawi waliokuwa wakimuongoza baba, na mambo ya ya ucafu waliyokuwa wakifanya...
Video hiyo ikaonyesha kila kitu...inatisha , hata mie ambaye sikuwa na ufahamu wa hayo, niliogopa, na kiukweli nilijuata kwanini niliuangana na hao watu..sitaki hata kuelezea zaidi ya hayo niliyoyaona kwenye hiyo video, kwani baada ya kuiona nilihsii vibaya sana,…’akasema
‘Ina maana ni kweli hizo taswira za hao wachawi ziliweza kuonekana kwenye hiyo video…?’ akaulizwa.
‘Unajua kijana alichukua hiyo video akatoa nakala kama nne, hivi, moja akaniletea mimi, nyingine kwa mama yake nyingine kwa babu yake, nyingine sijui alataka kumpa nani, na ujumbe kuwa anakwenda na hatagemei kurudi, kurudi kwake labda apone, lakini kaba hajafanya hivyo, anataka wanafamilia wajua kinachoendelea ndani ya hiyo nyumba. Na alichogundua kuwa nyumba hiyo ilishatekwa na wachawi, na aliyesababisha hayo ni baba yake, na video hiyo ndio ushahidi...kiukweli ilionyesha kila kitu, hakuna ubishi...'akasema
Jamani dunia hii , usiku wengine wamelala, wengine wanafanya mambo ya ajabu kabisa,..nilipoona video ile, nikahisi kichwa kinauma, nililia, nikalia…maana kweli kila kitu kilionena kiu-wazi, jinsi gani hao wanga walivyokuwa wakiingia na kufanya mambo, yao, ilikuwa kama unaangalia video ya kuigiza, kumbe ni matukio ya kweli, na mimi ni muhusika…sijui huyo jamaa aliwezaje kuzifichua hizo taswira za kichawi…’akasema.
‘Unasema ulilia sana, kwanini sasa ulilia, wakati ulipenda wewe mwenyewe..?’ akaulizwa.
‘Nyie hamjui jinsi gani nilivyokuwa nampenda huyo mtoto wangu, .jinsi gani nampenda mke wangu, hamjui ndani ya nafsi yangu kulivyo..lakini ningeliwezaje kulionyesha hilo, wakati akili imeshaona kuwa ili upendwe, ili uonekane ni bab bora ni mpaka uwe na mali...
Kiukweli kijana wangu ambaye nilishibana naye sana alikuwa huru kunielezea matatizo yake na mimi yake niliyoyaona anastahiki kuelezewa nilikuwa namuelezea, yeye alikuwa karibu na mimi kuliko, alivyokuwa kwa mama yake, muulizeni hata mama yake hapa analijua hilo…’akasema.
‘Sasa kwanini ulimfanyia hayo uliyomfanyia..mbona sisi hapo hatukuelewi...?’ akaulizwa.
‘Kama umenielewa vyema maelezo yangu tokea awali, mimi sikudhamiria kuyafanya hayo mabaya kwa nia ya kuiumiza familia yangu.., lengo langu ilikuwa kutafuta hali nzuri ya maisha, kwa masilahi ya familia yangu …na ujue shetani alivyo na nguvu nilijua hayo mambo ni ya muda mfupi tu, nitapata nitafikia kileleni kama hao ninaowaona, na maisha yataendelea, sikujua kuwa mambo hayo ni ya muda tu..yana mitihani yake…’akasema.
‘Sasa ikawaje…?’ akaulizwa.
‘Nilitoka kumtafuta, mtoto wangu, kwa marafiki zake, na sijui ilikuwaje siku kwa maana kwa, kila rafiki yake niliyemuendea, nikifika kwake anasemaa ametoka sasa hivi, ni kama alitaka kuwapitia marafiki zake kama anawaaga vile..mpaka usiku sikuweza kumpata , na nilipochoka ndio nikakumbuka kuhusu hizo video nyingine alizowatumia hao watu…
‘Ulijuaje kuwa kawatumia hao watu wengine na ni akina nani..?’ akaulizwa.
‘Kwenye hiyo video aliyonitumia mimi aliandika nakala kwa…mama, babu..na mtu mwingine hakumtaja…
‘Sasa ulikuwa una uhakika gani kuwa kweli kaituma kwa hao watu na kwa njia gani?’ akaulizwa
‘Hapo sikujua, nikaanza kumtafuta mke wangu, nijue wapi alipo, nikajua kama kamtumia mke wangu itakuwa humo humo ndani, nikatafuta sikuipata, nikamtafuta mtu wa karibu na baba mkwe ajaribu kuona kama kutakuwa na mzigo wowote uliotumwa huko, sikuweza kupata taarifa yoyote…kwani baba mkwe hakuwepo nyumbani.
‘Hayupo nyumbani, nakuomba uhakikishe kama kuna mzigo utafika hapo unaupokea na mimi nitakulipa pesa nyingi, si unanifahamu nilivyo,…sawa..’nikamwambia huyo mlinzi wa hapo nyumbani kwa baba mkwe, mlinzi huyu niliahi kumfanyia jambo kubwa, kiasi kwamba aliahidi kuwa hataniangusha.
‘Hamna shida bro…’akaniambia, kwahiyo hapo nikawa sina shida napo sawa, lakini ni swala la kubahatisha tu.
‘Mtu anayeweza kukusaidia ni yule bint…’nilipokumbuka hilo ndio nikaanza kumtafuta huyo binti, nilijua wapi naweza kumpata, nikaenda nyumbani hapo anapofanyia kazi, na nilipokutana naye hakutaka hata kuongea name.
‘Umekuja kufanya nini hapa, unataka kunigombanisha na mke wako au sio, kama ulivyofanya huko nyumbani mapaka nikafukuzwa kazi…hayo uliyonifanyia hayatoshi, nakuheshimu sana baba, nakuomba uondoke…’akasema
‘Nimekufanyia nini, kwanini unasema hivyo, unajua nimekuja hapa kufanya nini,..…?’ nikamuuliza sasa kwa hasira na sauti hiyo ikamfanya anywee na kutulia.
‘Unafikiri mimi sijui mlichonifanyia na huyo mchawi wako, nayajua yote, na najua kilichokuleta hapa ni hicho, mnanitakia nini nyie watu, tumewakosea nini,…’akasema kwa sauti ya huzuni.
‘Sijui unaongea nini, wenyewe hawapo humu…?’nikajifanya sijui kitu, ni kama vile nimekuja kukutana na wenye nyumba.
‘Wewe na huyo mchawi mpo kitu kimoja japokuwa unajifanya wewe hujui kinachoendelea, na unajua fika muda kam huu wenyewe wanakuwa kazini, …’akasema akiendelea na shughuli za usafi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Sikiliza nikuambie kitu,…yule mzee mbaya wako amefariki, huna taarifa hiyo…’nikasema na yeye akashtuka kidogo, halafu akasema, kama kuuliza
‘Mzee gani…?’ akaniuliza, sasa akiwa kasimama na kuniangalia, uso wake ulijaa hamasa au wasiwasi fulani.
‘Yule mbaya wako wa kijini kwenu aliyetaka kukuoa…’nikamwambia
‘Nimesikia hivyo, na kifo chake nasikia ni kibaya kweli, alikuwa kipiga kelele kama anaumia,anaomba msamaha…mmmh, mpaka nikakufuru na kusema,..kumbe na yeye anakufaga, au ndio huko kuigiza kwake, maana kuna kipindi walisema hivyo, kesho yake tunaambiwa yupo hai…siwezi kuamini mpaka afikishwe kaburini, yule mzee alikuwa tishio…lakini ndio hivyo hakuna atakaye ishi milele…’akasema
‘Ndio keshafariki, usiwe na mashaka naye tena….’nikasema
‘Ndio umekuja kutoa taarifa au…?’ akauliza.
‘Hapana, najua watu wameshafahamu,..ila huu mguu ni wa kwako…nimekuja kwako unisaidie jambo moja..’nikasema na hapo akageuka kuendelea na shughuli zake, akasema
‘Nilijua tu…unajifanya umekuja kwa wenyeji hapa….haya niambie ni jambo gani, mimi sina uhusiano na huyo mtu, zaidi ya kuwa alitaka kunioa,nikamkatalia…kama ni mambo yenu ya kichawi, mimi sijui, na wala sijahusika kupambana na huyo mtu….’akasema
‘Sawa,…nisikilize kwanza,…mbona unakuwa na maneno mengi,… wewe unajua huko anapotokea, ni nani anaweza kunisaidia…unajua wewe unafahamu fika jinsi gani alivyopaharibu pale ndani kwangu, na nilishaongea naye akasema atayaondoa mambo yake, sasa ndio huyo ameshafariki, ninataka nyumba yangu iwe safi, ni nani anaweza kunisaidia..?’ akaniuliza
‘Ni yule yule adui yake, yeye alikuwa ni mwalimu wake, nenda ukaonane naye, huyo ataweza kukusaidia…’akasema
‘Oh..mbona hata yeye kafariki pia….’nikasema na hapo huyo binti akadondosha ufagio aliokuwa kaushika kumbe alikuwa hajapata hiyo taarifa ya kifo cha huyo mzee mwingine.
‘Hapana ..ina maana hata yeye kafariki, unajua wale watu, nasikia kipindi cha nyuma walikuwa marafiki, mwalimu na mwanafunzi wake,..ghafla wakaja kukosana, wakaanza kupigana vita ..niliposikia huyo marehemu kaja hapa Dar, nikajua na huyo mwenzake atakuja tu, maana wanawindana kweli..oh, sasa, mimi sijui nikusaidieje…’akasema
‘Sasa baada ya hao ni nani mwingine anayeweza kunisaidia,maana haya mambo yamekuwa makubwa kwangu…’nikamuuliza
‘Mimi sijui..huko kijijini kwenyewe nimekuja kupaelewa baada ya matatizo yaliyotokea huko kwako…zaidi ya hayo mimi sitaki hata kurudi tena huko kijijini…, lakin kama hao watu wawili wamekufa, nahisi kijiji sasa kitakuwa na amani…’akasema
‘Mhh…sasa nitafanyaje…’nikabakia kushika kichwa
‘Sasa umekuja kwangu ukijua mimi nitakusaidia, hahaha, sikiliza baba,..mambo kama hayo ulitakiwa uende kuwauliza wazee wa huko huko, kijijini…na kuna watu wlifika hapa karibu, niliwaona, wnatokea huko kijijini, wao ni watu wa dini, hao wanaweza kukusaidia, kuliko njio hiyo ya kutafuta waganga wa kienyeji…’akasema
‘Nitawapataje hao watu…?’ nikamuuliza.
‘Niliwaona tu mara moja, sijui wapo wapi…jaribu kuulizia watuu…na jingine ni hilo la kwenda kuwaona wazee wa huko kijijini…’, aliniambia,
‘Lakini kuna mtu kasema wewe unaweza kunisaidia….’nikasema
‘Mimi nitakusaidia kwa vipi sasa, na kwanini asema hivyo, anahusika na hao watu nini,, anatokea huko kijijini au,..?….mimi kwa udadisi wangu niliwahi kuwauliza wazee, waliniambia matatizo mengine kama hayo yako, ambayo yanaingiliana na dhuluma,…wewe si umefanya mabaya, kwa watu , si ndio hivyo, kinachotakiwa ni kuwaendea hao uliowakosea uwaombe msamaha, hakuna njia nyingine…’akaniambia
‘Oh, basi mimi naanza kwako wewe…kukuomba msamaha….’nikasema
‘Kwani mimi umenikosea nin…si unakumbuka nilikulilia hali kukupigia magoti wakati nafukuzwa pale nyumbani kwenu.., ukasema wewe hujui lolote, ukanisaidi kuitoa ile mimba, huku ukidai sio ya kwako…uliniambia kabisa wewe, huna makosa mimi nakusingizia tu…’akasema
‘Kiukweli mimi hata sijui kitu,..ila nahisi kuwa nimekukosea sana, nakuomba unisamehe…’nikasema huku nikienda kumpigia magoti, yeye akabakia kushangaa tu.
‘Wewe mbamba, mna nini leo, …mimi sijui kitu…kama ulinikosea ni haki yangu kufahamu ulichonifanyia, niambie ulinifanyia nini, la sivyo sitaweza kukusamehe..nikuulize tena je ni wewe ulinipa hiyo mimba..?’ akaniuliza
‘Sina uhakika na hilo,…sio mimi…mi-mi-sijui…ndio maana nakuomba unisamehe, maana yaliyokuwa yakifanyika mimi sina uhakika nayo, si unajua ilivyo kuwa…’nikasema
‘Kama huna uhakika nayo, basi huna kosa, nenda kwa hao uliowakosea, hasa kijana wako, mimi niache niendelee na kazi za watu, usije kunifukuzisha kazi..…’akasema akiendelea na shughuli zake.
‘Kijana wangu nitampata wapi sasa…?’ nikamuuliza
‘Alikuja hapa akaniomba nimsamehe..na anaonekana kachanganyikiwa kabisa, nikamuuliza kosa langu akasema hana uhakika, kama ulivyosema wewe, akanipigia magoti huku analia, anataka nimsamehe, anadai kuwa kaambiwa ili apone awaombe msamaha wale wote aliowakosea, kwahiyo kaja kwangu,.., nikamwambia mimi sijui kosa langu kwake…akawa analia, hajijui,…mmh, nikamuonea sana huruma…’akasema
‘Oh, jamani kijana wangu, sijui nitawezaje kumsaidia, sasa wewe utanisaidiaje mimi…?’ nikamuuliza
‘Unajua nyie watu wawili mna nini sijui, hayo unayoniambia sasa hivi kijana wako kaniambia hivyo hivyo…na nilipomuuliza ana matatizo gani akasema…, lakini nikamuambia mimi siwezi kujua matatizo yake, wewe bab yake ndiye unaweza kuyafahamu…ndio akasema, wewe yaonekana hutaki kumsaidia kwa hiyo atakachokifanya anakijua yeye mwenyewe, ….’akatulia kama vile kasikia sauti
******************
‘Kuna nini..?’ nikamuuliza.
‘Bosi atakuwa kafika, nimesikia mngurumo wa gari lake…naomba tafadhali uondoke humu ndani haraka, isije kulete picha mbaya, yaliyopita bado yapo kichwani mwa watu, na mim sitaki kuzalilika tena…’akasema.
‘Usiwe na wasiwasi nitaongea na huyo bosi wako, mimi sina matatizo na hii familia, wananifahamu vyema…usijali kwa hilo…..’nikasema na haikupita muda, akaingia mama mwenye hiyo nyumba, aliponiona akaonyesha uso wa kushangaa, nikasalimiana naye na kumuambia nilikuja kuangalia kama mke wangu yupo hapa
‘Mke wako!!!….hapana, hayupo hapa, japokuwa ndio nafika…’ akasema huku akimuangalia mfanyakazi wake kwa mashaka, halafu akasema.
‘Nilihisi yupo hapa napiga simu yake haipatikani…’nikadanganya hivyo.
‘Mhh….mke wako aje hapa wewe usijue,… mke wako si yupo polisi…’akasema huku akimtupia tena jicho huyo mfanyakazi wake , ambaye kwa muda huo alikuwa akipanga panga vitu kwenye kabati.
‘Polisi…!!!? Kufanya nini huko…?’ nikamuuliza na yeye akashikwa na butwa, akiniangalia kwa mshangao.
‘Ok…yupo huko, kuhusu maswala ya huyo marehemu, kuna mambo anahojiwa, sasa shemeji, nikuulize tu, kwanini wewe hukufika siku ile hospitalini, wenzako wote walikuja, kasoro wewe, hata hivyo tumemalizana, na keshazikwa..mmh, ndio hivyo tena…yaani we yasikie tu…karibu shemeji mboana upo wima wima…’akasemaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Kwanini azikiwe hapa, si anatakiwa kupelekwa huko kijijini kwao au..?’ akaulizwa
‘Yaani inatisha..japokuwa mwili uliwekwa kwenye majokofu, lakini umeoza, na kuanza kujaa mafunza..inatisha huwezi hata kuangalia…kwa hali iliyopo, wakaona ni bora tu kuzika hapa hapa kwenye makaburi ya city…’akasema
‘Mungu wangu…’nikasema
‘Sasa vipi kuhusu kijana wako, maana mke wako anasema kijana alikuwa akimitafuta kwenye simu, na alipotaka kumpigia tena akawa hapatikani, kwenye simu alikuwa akiongea huku kama analia, alivyosema mama yake, inaonekana hayupo vizuri, ….’akasema
‘Analia, analia nini, mbona ….’akataka kusema jambo halafu akakatisha.
‘Zaidi alisema ana mzigo muhimu sana kwa mama yake, alikuwa akitaka kumpatia mkono kwa mkono kwani anasafiri, kwani anasafiri kwenda wapi..?’ akauliza
‘Sijui kama anasafiri, lakini vijana wana shughuli zao nyingi, kama anasafiri ataniambia,…hata hivyo, hata mimi namtafuta, nilijua mke wangu yupo hapa , maana simu ya kijana nilipompigia alikuwa hayupo hewani..’nikasema
‘Mhh..huyo kijana mu8angalie sana, nahisi ana matataizo makubwa, …’akasema
‘Kwanini unasema hivyo…kwani unamuonaje wewe?’ nikauliza
‘Mke wako anadai kijana wake siku hizi hayupo sawa, na yeye anahisi huenda ni kunatokana na nyie wenyewe wazazi, ..’akasema
‘Kasema hivyo mke wangu, mmhh, siamini, kwanini asema hivyo…!?’nikaguna nikihisi huenda wameongea mengi kuhusu familia yake, kitu ambacho siki-kipendelea.
‘Ni katika kuongea tu, lakini mke wako hakutaka kusema zaidi, sasa kwa ushauri wangu mtafuteni kijana wenu mkae naye pamoja, muone mtamsaidiaje, hilo linaweza kuwa suluhisho, …kwani shemeji kuna tatizi gani, maana yule ni rafikiyangu lakini sio kila kitu anakiongea, hasa kuhusu mambo ya familia yake, namuona hana raha siku hizi…?’akaniuliza
‘Hamna kitu shemeji ni mambo ya kawaida tu,…sawa shemeji,nashukuru, kama takuwa hewani nitampigia simu, na kama ukimuona, basi mwambie namtafuta, au huenda sasa yupo nyumbani..nikasema na kuanza kuondoka, na wakati nipo nje….simu yangu ikaita…, alikuwa mke wangu.
‘Halloh..’nikasema
‘Sikiliza wewe mwanaume, kama kuna kitu kitatokea kwa mtoto wangu, nitakachokufanyia hutaamini, utakwenda kuozea jela..nakuhakikishia kwa hilo…’akasema
‘Kwanini unasema hivyo, kwani kuna nini kimetokea, na wewe upo wapi..?’ nikamuuliza
‘Nipo polisi, ndio naondoka huku, nikitoka hapa napitia kwa baba, nataka tuje naye huko nyumbani…’akasema, hapo nikahis labda ameshauona huo mkanda...na ukiona ilivyo, utahisi mimi ni mchawi...
‘Kuhusu nini…ni kuhusu huyo marehemu kwanini nyie muende polisi..?’ nikamuuliza
‘Kuna jingine ndilo limenichelewesha, askari wa kitengo cha madawa ya kulevya, alitaka kuongea na mimi , anadai kuwa kijana wetu anatumia madawa ya kulevya, na wana wasiwasi kuwa anafanya biashara hiyo,…’akasema
‘Kwa ushahidi gani,…?’ akauliza.
‘Wanasema kuna kipindi ghafla hali yake ilikuwa nzuri, maisha ya juu sana, hana shughuli ya maana inayojulikana pesa alipatia wapi…na ameshaonekana akiwa kalewa hayo madawa….’akasema
‘Sio kweli, sasa umelimalizaje hilo, ngoja nitaongea na mume wa rafiki yako, tuone atavyoweza kutusaidia au unasemaje mke wangu….?’ Nikauliza na kusema
‘Usitake kusema hujui, hayo umeyasababisha wewe...'akasema hapo moyo ukanilipuka pwaah
'Kwanini unasema hivyo mke wangu, una ushaidi...'nikataka kusema hivyo bahato yeye akanikatiza kwa kusema
'Kwenye simu nilimuuliza ana matatizo gani akasema nikuulize wewe, na kuna huo mzigo anataka kunipatia, una kila kitu..nikamuuliza kitu gani, akakata simu, huku analia,…sasa nataka nikifika nyumbani unieleze ni nini kinachoendelea, na hata baba anataka kuja kuongea na wewe, na anaonekana kakasirika sana, mimi nimechoka..…’akasema na kukata simu.
‘Mungu wangu….’nikasema hivyo huku nakimbia..nakimbia kuuwahi huo mzigo kabla haujafika mikononi mwa mke wangu…na wakati nakimbia simu yangu ikaita tena nilipoangalia, nikaona ni namba ya yule mlinzi wa kule kwa baba mkwe
‘Halloh..’ nikaita na mara simu ikazima, kuangalia imejizima, nikaiwasha, kumbe chaji imekwisha, hapo hapo nikatafuta bajaji, sasa safari ikawa huko kwa baba mkwe, nikakutane na huyo mlinzi, huenda ndio huo mzigo...yaani hiyo video haifai kabisa waione wakwe zangu, najua wakiiona itakuwa ni ushahid wa kile wakilichokuwa wakikisema, na sizani kama kutakuwa na mjadala hapo...
Bajaji ilienda kwa kasi, kama nilivyomuomba huyo muendeshaji, na nikakaribia hapo kwa baba mkwe, sikutaka nionekane kwa mbali nikamuona huyo mlinzi kasimama mlangoni, na gari la baba mkwe linaingia…na nilimuona yule mlinzi kashika kitu...ni bahasha…nikajua ni huo mzigo wa video...
‘Hapa nikumuwahi tu…’nikasema na kushuka kwenye bajaji mbio mbio kuelekea nyumbani kwa baba mkwe...
‘Pesa yangu mzee….’mwenye najaji akaniuliza, na mimi sikuwa na muda wa kumsikiliza mbio mbio kuelekea kumuwahi huyo mlinzi, nyuma yangu bajaji inakuja kwa kazi
'Mzee pesa yangu...
WAZO LA LEO: Tusione kuwa kuongea, kutumia ulimi, kuandika mambo ya kiuzushi, ni jambo la kawaida tu, haya mambo ambayo yanaumiza wengine, yanasababisha madhara kwa jamii, ni dhuluma, na madhambi yake ni makubwa, maana hujui ukumbwa wa hayo madhara kwa wengine, hujui kiasi gani mtu mwingine anaumia na huo uzushi…, na je kuumia huko kunaishia wapi…na je hayo uliyoongea, au kuandika yana ukweli, yanasaidia jamii, tujiulize kwanza kabla ya kuandika, au kuzua,..
Hala hala jamani...tuweni makini sana na ulimi, tuweni makini sana kalamu..tusione ni jambo rahisi tu,..Uzushi waweza kusababisha vita, na vita havina macho, watu wanauwana, na wamakufa watu wasio na hatia, watoto wadogo, wazee, akina mama,… je huoni kuwa wewe ulizua, ukachonganisha ndio wewe uliyewaua, …kwanini twajifanya wacha mungu , lakini matendo yetu ni ya kumcha shetani….
Tumuombe mwenyezimungu azisafishe nyoyo zetu, tupendane, tusaidiane,…ili dunia iwe ya amani na upendo.
Nilifika getini kwa baba mkwe wakati huo nilimuona yule mlinzi akiwa bado kaishikilia ile bahasha mkononi , nikajua ndio hiyo video ambayo mtoto wangu kaileta hapo kwa babu yake,…mimi pale nikawa najiuliza nifanye nini, ..sikutaka kusubiria nikakimbilia kwenye mlango wa geti, labla lile geti halijafungwa, nia ni kumuwahi huyo mlinzi asije kumpatia huyo baba mkwe…na huku nyuma bajaji inafukuza, kwa wakati huo sikujua inanifukuza mimi..
Nilipofika getini, nikaita jina la yule mlinzi kwa sauti kubwa, na wkati huo yule mlinzi anaongea na bosi wake, akiwa bado ndani ya, na yule mlinzi aliposikia jina lake, jina la utani tunaitana mimi na yeye, akageuka akaniona mimi nikamuonyeshea ishara kuwa hiyo bahasha ndio naihitajia, yeye ni askari akanielewa kwa haraka
‘Kuna mzigo wangu wowote…’nikasikia bosi wake akimuuliza hapo nikahisi mapigoa ya moyo yakiongezeka
‘Mzigo upi mzee, ukiwepo nitakueletea, bosi…’akasema.
‘Na hiyo bahasha ni ya nini..?’ akaulizwa
‘Kuna mtu kaacha huu mzigo nimpatie jamaa yangu mmoja….’akasema.
'Sawa sitakawia kama kuna mzigo wowote niletee ndani...'akasema na kuingia na gari la geti lkafungwa.
Nikasubiria kwa nje, nikiwa naomba asije kumpelekea kabla hajaonana na mimi, na mlinzi alipohakikisha bosi wake kaingia ndani, haraka akanifuata na ile bahasha mkononi, na kusema.
‘Bosi unaniweka pabaya…’akasema
‘Kwa vipi…?’ nikamuuliza
‘Huu mzigo nimeambiwa nimpatie huyo mzee akiingia, na aliyeuleta hapa ni kijana wako, alikuwa na haraka sana, anaonekana hayupo vizuri, na alipoulizia kuwa babu yake yupo, nikamwambia hajafika, akasema huu mzigo nihakikishe umefika mikononi mwa babu yake, sasa niambie, una nini..?’ akauliza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Una mambo fulani ya kifamilia, tulikuwa tunataka kumshirikisha babu yake, nikamtuma aulete, sasa kuna mambo ya kurekebishwa kabla huyo mzee hajauona, nimejaribu kumpigia huyo kijana simu, lakini hapatikani, …ndio maana nikaamua kuja mwenyewe, …’nikasema.
‘Basi kumbe sio tatizo, mimi nitampatia mzee na wewe ukiwemo umuelezee tatizo lipo wapi, unajua mimi ni mlinzi siwezi kukiuka masharti ya kazi yangu japokuwa tunaelewana kihivyo…’akasema.
‘Aaah, usitake kuharibu, …haitakiwi kufika kwa huyo mzee kwanza unielewe hapo, huyo ni baba mkwe wangu kuna mambo sitakiwi kuharibu...nataka nilete mambo yakiwa hayana makosa, ni muhimu sana, sutakiwi nikuambie kila kitu…’nikasema.
‘Hapana, nahisi kuna jambo, mzee..bosi, sikiliza mimi nitakaa na hii bahasha, wewe wasiliana na kijana wako kwanza, ili niwe katika usalama zaidi, nahisi kuna jambo, na huyo mwenye bajaji anasemaje..’akasema na hapo ndio nikakumbuka nikageuka na kumuona mwenye bajaji yupo nyuma yangu.
‘Hujanilipa pesa yangu mzee…’akasema huyo mwenye bajaji
‘Oh, samahani sana…’nikasema na kumpatia pesa yake, na mara nikasikia mzee ndani akimuita huyo mlinzi, na mlinzi akasimama na kukimbilia ndani, nikamfuatilia, na alichofanya yeye, akaicha ile bahasha kwenye droo za meza hakujua nimemfuatilia hadi ndani,.
Hapo nikasema, mungu akupe nini, sikuwa na uvumilivu tena, nikaivuta ile droo na kuichukua ile bahasha kwa haraka na nilihakikisha ina jina la huyo mzee hapo, ilikuwa ni ile ile bahasha aliyokuwa kashikilia yule mlinzi,,,,nikatoka mle kwenye kibanda cha mlinzi na kumuwahi mwenye bajaji
‘Twende, narudi huko nilipotoka…’nikasema, sikutaka hata kugeuka nyuma, najua huyo mlinzi akitoka huko atakutana na mashangao, nitakuja kumweka sawa nikikutana naye, nakama alishamuambia bosi wake kuwa kuna bahasha alitakiwa ampatie. basi atajua mwenyewe cha kusema.
‘Hukujua kilichotokea huko kwa mlinzi na bosi wake…?’ akaulizwa
‘Kwa muda hapana, mimi nilikuwa na haraka za kwenda kumuwahi mke wangu, kabla hajapatiwa hiyo bahasha nyingine na kijana wangu.
‘Ehee, ilikuwaje..?’
*************
Nilipofika nyumbani nilisikia kijana akiongea na mama yake, nikajua tayari mambo yameshaharibika,…nikaingia kwa haraka na kuwakuta mama na mwanae wanaongea, na mkononi mwa kijana niliona bahasha kama ile niliyoiona kule kwa baba mkwe..
‘Naona nimewaingilia, lakini nina haraka kidogo naweza kuongea na kijana wangu kwanza…?’ nikauliza
‘Kitu gani cha kuongea wewe na yeye ambacho mimi sitakiwi nikisikie…?’ akauliza mke wangu.
‘Leo hii unasema hivyo mke wangu…ajabu kabisa, siku zote matatizo ya huyu kijana akitaka kukuambia unamwambie kamwambie baba yako, hayo ni matatizo ya kiume…, sasa leo nataka kuongea naye mambo ya kiume, unaingilia kati…’nikasema na mama akamuangalia kijana wake, na kusema;
‘Ni kweli kuna mambo mnataka kuyaongea wewe na baba yako ambayo , mimi sitakiwi kuwepo…?’ akauliza
‘Mimi sijui baba anataka kusema nini, hata hivyo, nilikuwa na mzigo wako mama..kama nilivyokupigia simu, nimekuwa nikikutafuta siku nzima ya leo..nataka uupokee mkono kwa mkono…nataka hili lifanyike kabla sijaenda kuongea na baba…sijui anataka kuniambia jambo gani jipya, …’akasema sasa akinyosha mkono kutaka kumkabidhi mama yake hiyo bahasha..
‘Mama, naomba uichukue, utaona kilichopo ndani, na kila kitu kitajieleza, nashindwa kuvumilia tena, haya mambo yamenishinda, sina maana tena, mama.. …’akasema akijizuia kulia.
‘Kijana, wewe ni mwanaume kwanini unajilegeza hivyo, nilishakuambia haya mambo nitayamaliza mimi, ukideka kwa mama yako unafikiri ataweza kukusaidia kwa hilo, na hiyo bahasha unayompa mama yako ina nini, kuna nin ikipya wakati tulishaongea, huo ni udhaifu mwanaume hatakiwi kuwa hivyo,.unasikia au unataka kumuua mama yako…?’ nikamuuliza
‘Kama nilivyokuambia baba, muda umekwisha na mimi ni lazima nitimiza nadhiri yangu…’akasema na muda huo bado bahasha ipo mikononi mwake, nikavutika kutumia nguvu kuichukua lakini nikaona nisifanye hivyo, namfahamu mke wangu namfahamu kijana wangu,..najua jinsi gani ya kuwaweka sawa.
‘Sikiliza kijana wangu ndio maana nimefika kwa haraka nikitoka hapa kuna sehemu tutakwenda, tutayamaliza hayo matatizo yako …nimeshapata ufumbuzi wake, wewe achana na mama yako, mama yako kwa hivi sasa ana mambo mengi yakufuatilia, usimzidishie presha…’nikasema.
Mke wangu kwa muda huo alikuwa akiweka kitambaa kwenye meza vizuri, huku katega sikio, hakutaka kuingilia moja kwa moja, na mimi namfahamu mke wangu alivyo, sio mtu wa papara, nikaona nichukue nafasi hiyo kuyaweka haya mambo sawa, nikasema.
‘Mke wangu kijana wetu ana matatizo, lakini kama nilivyokuambia kuna matatizo mengine ya kiume, na mimi nimeshajua jinsi gani ya kumsaidia,..lakini naona kama haamini, unajua vijana walivyo, wanataka kila kitu kiende kwa haraka..sio vitu vyote vinakwenda hivyo,.. na njia anayotumia yeye itazidi kumuharibu…’nikasema na mama yake akasimama na kumuangala kijana wake, akasema.
‘Ni kweli anayosema baba yako..?’ akamuuliza, na kijana akawa anaangalia pembeni, huku akijipiga piga na ile bahasha mguuni.
‘Mimi sijui baba ana maanisha nini, lakini kwa vyovyote iwaavyo, mimi najua baba anachotaka ni nini, na keshashindwa kwenye mambo yake, lakini hataki kuukubali ukweli…mimi nitahangaika kivyangu, ikishindikana, basi maamuzi yangu hayatakuwa tofauti na wengine….sitakuwa mtu wa kwanza kulifanya hilo…’akasema hivyo, na mama yake hapo akageuka sura na kusema.
‘Kwani ni kitu gani kinachoendelea hapa, nimekuuliza mara nyingi, una tatizo gani hutaki kusema, mwishowe unasema baba anajua una tatizo gani, haya baba yako kaja anasema kapata namna ya kukusaidia, unasema sio kweli, ..haya niambie tatizo ni lipi ili na mimi niweze kukusaidia…’akasema.
‘Mama utayajua tu….’akasema akiiangalia ile bahasha.
‘Nitajua kwa vipi, unajua polis wanakuchunguza, nimeambiwa unatumia madawa la kulevya, wewe unakana,…na hilo baba yako anakutetea, kuwa hutumii, nyie watu wawili mna nini, mbona mnataka kuniua kwa shinikizo la damu…’akasema mama mtu.
‘Mke wangu hili swala la kijana wetu niachie mimi mwenyewe, nitalimaliza…sema yeye hataki kunielewa,..nimeshamuambia kuna mambo mengine ni ya kiume zaidi, mama yako hataweza kukusaidia, mimi peke yake ndiye naweza kukusaidia,..kijana wangu niamini mimi, na acha mawazo yako ya haraka haraka, unachofikiria kukifanya…, sijui ni kitu gani, lakini nakuambia, hakitakusaidia, mimi ni baba yako niamini…’nikasema.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kijana akageuka kuniangalia na kusema;
‘Uliyemtegemea kukusaidia ameshafariki, na niliyetegemea kunisaidia mimi na yeye ameshafariki, najau siku nzima ya leo umekuwa ukinifuatili nyendo zangu, kila sehemu ulipopitia nimepigiwa simu, sasa sikiliza baba, hatua hii ilipofikia, sizani kama una loloye jipya la kunisaidia,..’akasema
‘Ninalo la kukusaidia, unajua mimi nimetokea wapi…?’ nikamuuliza
‘Ulitokea kwa yule binti alikuwa akifanya kazi hapa, ukaenda kwa babu…’akasema
‘Kwa yule binti kufanya nini…?’mke wangu akauliza na mim sikujali swali la mke wangu, nikasema
'Huko nilikuwa nakutafuta wewe ili kukuelezea hatua niliyofikia kuwa nimeshampata mtu wa kukusaidia...'nikajitetea hivyo.
‘Mama yote utayaona humo, baba anachoongea ni kutafauta njia ya kupoteza muda, najua yameshashindikiana, …ngoja mimi nikajaribu bahati yangu huko ninapokwenda, mkiniona kimia, basi mjue mambo yameharibika…lakini kama nilivyoahidi, kabla ya kuondoka, nataka kila kitu wewe mama ukijue…’akasema sasa akinyosha mkono kumkabidhi mama yake ile bahasha.
Sikutaka kuchukua papara , japokuwa kiukweli bahasha hiyo akija kuiona mke wangu akaona yaliyomo humo, najua atazidi kunichukia, na itakwua ushahidii wa kuvuinja ndoa yetu....mimi hapo nikatabasamu na kusema;
‘Vizuri kijana, hata mimi nilikuwa nataka mama yako ayaelewe hayo mambo yote.. kama yana ukweli,..lakini ukumbuke mimi ni baba yako nimeiona dunia kabla yako,..na siku zote nimekuambia, unapokutana na matatizo usikimbilie kuona kuwa watu watakusaidia, kwanza fikiria jinsi gani ya kujisaidia wewe mwenyewe kwanza.., halafu ukihitajia msaada angalia mtu ambaye anaweza akawa keshakutana na tatizo kama hilo, na sio wote watakaoweza kukusaidia…’nikasema nikionyesha sina wasiwasi.
Muda huo mama yake alikuwa anasita kuipokea ile bahasha, namfahamu mama yake alivyo, yeye sio mtu wa papara, aliona huenda akiichukua hiyo bahasha bila kujua undani wake anaweza kuharibu kabisa akasema;
‘Hebuni kwanza nyote wawili…, kijana wangu, hiyo bahasha unayotaka kunipa ina kitu gani…?’ akauliza mama
‘Ukweli wote kuhusu mambo ya humu ndani…’akasema akinitupia jicho mimi.
‘Mambo gani, sikiliza wewe mtoto, usifanye mambo ya kijinga, ukatoa siri za humu ndani kwa vyovyote vile, mpaka unatengeneza vitu kama hivyo ina maana ulipeleka mahali wa kutengenezee,…sikiliza mwanangu usione mimi nipo hivi nimekutana na matatizo mengi sana, kati yangu mimi na baba yako,.. lakini siwezi kamwe kutoa siri za humu ndani, maana hujui ni nani adui yako…’akasema mama yake
‘Unaona kijana wangu…sisi ni watu wazima tuna hekima zetu…wewe unachokifanya ni utoto….msikilize vyema mama yako…’nikasema
‘Mimi mama sijatoa siri za humu ndani, nalifahamu hilo sana na kama ningelitaka kufanya hivyo ningelikuwa nimeshafanya hivyo mapema tu…, ndio maana haya mambo ya humu ndani ambayo najua kwa hivi sasa yamefikia kubaya, yanahitajia msaada wa mtu baki ambaye sio mbaya ,..ndio maana nikamshirikisha na babu, sijampa mtu mwingine wa nje…’akasema
‘Unasema nini wewe mtoto ina maana humo kuna mambo ya humu ndani, na umempelekea babu yako, una akili kweli wewe..babu yako muda wote anataka nitengane na baba yako, ndivyo unavyotaka wewe..sii kila siku siku wewe unataka mimi na baba yako tuwe na furaha..nafahamu hilo halitawezekana tena, lakini..sio kwa jinsi unavyotaka wewe, wewe ni kijana mdogo sana..’mama yake akasema kwa ukali
‘Mama nisikilize na mimi, huenda kuna mambo ambayo nashindwa kukuelezea kwa moja kwa moja ndio maana nimetumia njia hiyo, kuna mambo ambayo hata wewe huyafahamu ndio maana nimetumia njia hii,kuna mambo ambayo kiukweli yakiachiwa yatakuja kuleta matatizi makubwa kwenye familia hii ndio maana nimetumia njia hii..kuna mambo ambayo yananitesa,…..ndio…’akatulia, maana simu yangu ilikuwa inaita, nikasema
‘Sasa sikiliza, wewe si unataka mama yako ayaona yote hayo, haya mpe hiyo bahasha tuone atakavyokusaidi, kama hutakuja kujuta..utamuua mama yako kwa shinikizo la damu, halafu utajuta ukiwa umeshachelewa…unasikia, na likitokea hilo, ndio hapo utaona ni nani kama wazazi wako..’nikasema na hapo kidogo akahisi jambo, sasa akawa karudisha ule mkono uliokuwa umeshika hiyo bahasha, na mimi nikapokea simu
‘Halloh ni nani wewe..?’ nikauliza
‘Ni mimi bosi…’ilikuwa sauti ya yule mlinzi kwa baba mkwe
‘Unasemaje..?’ nikauliza
‘Umeshaangalia hiyo bahasha uliyochukua, kwanini umefanya hivyo bosi…?’ akaniuliza na muda huo ile bahasha niliweka kwenye koti langu , koti langu ni kubwa tu, nikasema.
‘Bado kwani kuna tatizi gani..?’ nikauliza
‘Mzee, kumbe huniamini…’akasema
‘Kwanini..nakuamini sana, ila kuna mambo yanahitajia haraka wewe hujui nilichotaka kukuelezea, lakini usijali sana, kwani kuna tatizo?’ nikamuuliza.
‘Usingelifanya hivyo bosi..., ulichokifanya kimenifanya nikufikirie vibaya, kuwa kumbe hata wewe hunitakii mema, hivi huyo mzee akiligundua hili, mimi nitakuja kusema nini…’akasema.
‘Usiwe na shaka, aliyekupa hiyo bahasha ninaye hapa, nimeshayamaliza, ni kijana wangu na ni mambo ya kifamilia, usiwe na shaka na hilo..’nikasema.
‘Lakini hayajaisha kwangu bado, kwani huyo kijana wako alimpigia babu yake simu kuhakikisha kuwa keshaupata huo mzigo na babu yake akaniuliza kuna mzigo ambao nimepewa na huyo kijana, ..ulitaka mimi nisema nini hapo..?’ akauliza
‘Sikiliza mimi nipo na huyu kijana, tunayaongelea hayo mambo, nitakupigia nikimalizana na yeye usiwe na wasiwasi..unasikia, hebu niache kidogo ,….’nikasema.
‘Sikiliza bosi nayaongea haya kwa vile bosi anasubiria hiyo bahasha, na ….’akasema nikataka kukata simu
‘Usikate simu bosi,..maana sitaki kupoteza kazi yangu..mimi nitampa hiyo bahasha kulinda kitumbua changu,…’akasema
‘Utampa bahasha ipi tena,..sikia, nimeshakuambia …?’ nikauliza nikishika pale kwenye koti langu kuhakikisha kama ile bahasha ipo.
‘Hiyo aliyonipa kijana wako, ni lazima niifikishe kwa bosi maana ameshapigiwa simu na anajua ipo kwangu…’akasemaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Usiwe na wasiwasi na hilo, nitaongea na bosi wako, nitayamaliza…’nikasema.
‘Sawa wewe ongea naye tu, ila mimi ndio hivyo nataka kumpelekea bosi ndani...'akasema
'Utampelekea vipi bosi wkati bahasha hiyo ninayo..'nikasema
'Hahaha bosi, usifikirie mimi ni mtoto mdogo bosi, bahasha hiyo bado ninayo hapa, nilitaka kukujua unanithamini vipi, hebu iangalie hiyo bahasha ina nini...'akasema na kabla sijajibu kitu akaongezea kwa kusma
'Na kama una lolote utampigia bosi mwenyewe ..mimi nakwenda kumpa..’akasema hapo, nikahisi mwili ukinicheza cheza, ikabidi niitoe ile bahasha niliyokuwa nayo bila kujali kitu na nilipotoa na kuifungua ndani nikakuta kadi ya mualiko wa harusi..
NB: Ndivyo ilivyokuwa siku hiyo, je kuliendelea nini, tukutane kwenye sehemiu ijayo
WAZO LA LEO: Wengi wetu tunapenda kujiangalia wenyewe kwanza, ndivyo asili yetu ilivyo, mtu upo tayari kudanganya au kufanya lolote ili upate wewe kwanza, na mwenzako akose, hata kama unajua haki ni ya mwenzako. Ubinafsi wa namna hiyo ndio unaipeleka dunia kubaya, uhasama, chuki, propoganda, ilimradi mtu au taifa linataka kumiliki hata ikiwezekana kila kitu. Mola wetu katuambia, tukitaka tuwe na imani sahihi ya kumuabudu yeye, basi ni mpaka pale itakapofikia mtu yupo radhi mwenzake apate yeye akose, au yupo tayari kumpendelea jirani yake zaidi yake yeye...je imani hiyo tunayo.
Kabla hujaendelea mbele naona muda unakwisha, nauliza maana mpaka hapo ulipofikia, sijasikia kuwa ni nani mwenye huu mzigo, hiyo mimba ni ya nani,...’alikuwa mama Ntilie akinionyeshea mimi kidole tumboni, na hapo akili ya kufuatilia hiki kisa ikapotea na kurejea kwenye hali yangu,…
Mzee mzima akageuka na kuniangalia, akatikisa kichwa na kusema;
‘Yaani sijui nisemeje…kama nilivyoelezea awali mambo ya usiku mimi nilikuwa siwezi kuyaona, sasa siwezi kudanganya, …’akasema.
‘Yawezekana ni yako..ndio maana unavuta vuta muda…’akasema mama Ntilia
‘Mhh..hebu kwanza tuendelee na muendelezo, kama kuna swali mtakuja kuuliza baadae maana huko mbele ndio tutapata ufumbuzi, wa swali lako…na mimi nitawaambia maamuzi yangu ambayo yamenifanya nifike hapa hii leo, najua wengi watanishangaa lakini haina budi…’akasema mke wa jamaa
Yule mbaba akamuangalia mke wake kwa macho ya huruma, na alipoona kuwa yeye ndio anasubiriwa kuendelea kuongea, kwanza akakohoa…
Tuendelee na kisa chetu.
********
‘Baada ya kupokea simu hiyo kutokwa kwa yule mlinzi nilichanganyikiwa, kumbe sikuchukua ile bahasha yenyewe, nilikuwa nimechukua bajasha nyingine, lakini pale nilipoichukua bahasha hiyo hakukuwa na bahasha nyingine, labda hiyo yenye video alikuwa kaiweka kwingine,…Ilichobakia hapa ni kuchukua hatua…
Kwanza nikageuka kumwangalia mke wangu, yeye alikuwa kainamisha kichwa chini, nikageuka kumuangalia kijana, kijana alikuwa akinitazama mimi na ile bahasha bado ipo mikononi mwake, alipoona namuangalia akheuka kumuangalia mama yake hapo akafanya kosa, mimi kwa haraka nikatembea kwa kasi na kumkabili kijana, na kubakua ile bahasha mkononi mwa kijana, yaonekana hakulitegemea hilo, na kabla hajasema kitu,.nikisema kwa hasira.
‘Sasa unaona …babu yako keshajua kila kitu, haya nikutokana na mambo yako ya kitoto, nilikuambia uniamini mimi, haya nenda kwa babu yako akusaidie na huu mkanda ndio unataka mama yako akauangalia, haya ngoja nimpe akaangalia yaliyomo , tuone matokea yake yatakuwaje..’nikasema na kutembea kuelekea kwa mke wangu nikimkabidhi huo mkanda, lakini mke wangu hakuinua mkono kuipokea hiyo bahasha.
‘Chukua sasa uangalie kilichopo, ambacho ndicho huyo kijana wako kampalekea baba yako…’nikasema moyoni nikiomba ujanja wangu ufanye kazi, ni ujanja wa kuwajulia hawa watu tabia zao..nilijua kabisa mke wangu hawezi kuchukua kwa haraka hivyo.
‘Kwanza ni nini kipo ndani ya hiyo bahasha…aah, hayo ni mambo yenu sitaki hata kuyaona…’akasema na moyoni nikasema bao moja tayari, nikageuka kumuangalia kijana na kusema.
‘Haya unasemaje sasa….?’ Nikamuuliza
‘Baba, …huko kwa babu …’kabla hajasema kitu, mara simu ya mke wangu ikalia, na mke wangu akaipokea na kusikiliza;
‘Unasemaje baba…?’ akauliza.
‘Mjukuu wako nipo naye hapa, kuna nini..?’ akauliza
‘Mzigo gani..?’ akauliza
‘Kwahiyo unataka kusema nini…?’ akauliza
‘Ok, sawa atakuja muonane naye…’akasema na kugeuka kumuangalia kijana, na kusema;
‘Babu yako anasema uende mkaonane naye…’akasema
‘Huo mzigo keshaupata..?’ nikauliza lakini mke wangu hakujibu kitu, akawa anamuangalia kijana wake kwa makini,
‘Hebu sasa niambie una tatizo gani mpaka uende, na….na kitu gani hicho ulichompelekea babu yako..?’ akamuuliza.
‘Mama kila kitu kimejielezea humo, sikutaka kuongea, sikutaka hii hali ya kuulizwa ulizwa maswali, mimi sipendi kuulizwa ulizwa maswali,…na…’akasema sasa akimuangalia baba yake ambaye alikuwa kashikilia hiyo bahasha.
‘Huyu mtoto wako hana akili, hajui alivyoharibu, anatuvizia na kutupiga picha tukiwa tunagombana,..kila tukio analiweka kwenye video, hiyo ni tabia gani …sasa ndio kaamua kumpelekea baba yako ili aone jinsi gani hatupo sawa, nia yake ni nini kuvunja ndoa yetu,…’nikasema na sasa nikitaka njia ya kutoka humo ndani.
‘Basi kama ni hivyo, basi, ngoja tuone kilichomo, halafu nitajua la kufanya…’akasema mke wangu akiangalia ile bahasha niliyo nayo mkononi.
‘Hakuna cha maana hapa, hivi sio vitu vya kuweka, maana vikitua kwa watu wabaya tutapata shida sana…tatizo ni hiyo aliyoipeleka kwa baba yako,..sijui itakuwaje…’nikasena sasa nikiiweka ile bahasga kwenye koti langu.
‘Kama ni hayo uliyoyaelezea sizani kama kuna tatizo, labda kuwe na jamabo jingine ambalio wewe hutaki kulisema, eti kijana wangu niambie ukweli…’akasema mama.
Kijana akawa katulia tu, …na mara simu ya mke wangu ikaita;
‘Nini tena baba, mara ya pili unanipigia simu..nipo kwenye kikao…, ndio..tupo wote hapa kuna nini kwani baba…?’ mke wangu akauliza.
‘Unasema unataka kuja huku, eeh, kuhusu nini…?’ akauliza na kusikiliza.
‘Bahasha gani hiyo, kutoka kwa kijana wangu, ya nini..?’ akauliza na kutulia kimia akisikiliza
‘Hapana, sina habari yoyote..’akasema mke wangu huku akimuangalia kijana, na kijana akageuka kutaka kuondoka na mama akamuashiria kwa mkono asiondoke.
Na alipomaliza kuongea na simu akamuambia kijana…
‘Unakwenda wapi subiri babu yako anakuulizia, …’ akasema
‘Hapana mama mimi nataka kuondoka,…sitaki tena kukaa humu ndani…’akasema sasa akitoka kwa kasi humo ndani, kama anakimbia..
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mimi nikawa namuangalia mke wangu kutaka kujua atasemaje , lakini hicho cha babu yake kuja hapa, kama kauona huo mkanda nafahamu kabisa ni nini kitakachoendelea, na kama keshauona huo mkanda ni bora nisikutane naye kabisa,, ili kuwa na uhakika nikauliza;
‘Baba yako anasemaje..?’ nikauliza
‘Anataka kuja hapa nyumbani, na anataka sote tuwepo,…’akasema.
‘Sote tuwepo…! Na wakati kijana ndio huyo kakimbia, kagundua upuuzi alioufanya hauna maana, kwani baba kasemaje kuhusu hicho kikao ni kuhusu nini hasa…?’ nikauliza
‘Hajasema, ngoja….’
Baadae mke wangu akaamua kumpigia baba yake kuwa kikao hicho anachokitaka yeye kwa leo hakitawezekana..
*************
Nilibakia na mke wangu, nikisubiria amalize kuongea na simu, na wakati anaongea na baba yake mara simu yangu ikalia..nikaipokea kwa haraka;
‘Nani mwenzangu..?’ nikauliza,na huyo mtu akaongea kwa sauti kama ya kuigiza, mimi moja kwa moja nikajua ni yule mlinzi
‘Unataka nini, si umefanya ulichotaka, sawa bwana, najua malipo ya wema wangu kwako ndio hayo, sasa umepata faida gani…?’ nikamuuliza na kusikiliza alichokuwa akiongea, sikuamini kuwa mtu huyo anaweza kunifanyia hivyo.
‘Unasema nini…?’ nikasikiliza kwa makini anachokiongea
‘Unasema unataka nikulipe niini…acha uhuni wewe mtu…wewe kama haja yako ni pesa, sio lazoma utumie njia hiyo, unasikia,…aah, hapana hatuendi hivyo,…hebu jiulize, je nikiamua kumwambia bosi wako kuwa, huoni utapoteza kazi yako, au unasemaje nimwambie…’nikasema na simu ikakata.
Huyu mlinzi anasema kuwa ile bahasha hajaipeleka, kapeleka bahasha nyingine tu, na hiyo bahasha anayo yeye mkononi, na amegundua kuwa ndani ya ile bahasha kuna video, video ambayo ni hatari ikiingia mikononi mwa watu hasa watu wa mitandani na magazeti, na pia ikifika kwa mzee, baba mkwe wangu, kwahiyo kwa hivi sasa anayo hiyo video, kama nitaka yeye anahitajia pesa nyingi tu, hakusema kiasii gani, vinginevyo atamkabidhi bosi wake, na kumuomba msamaha …’akakata simu.
Niliwaza sana hilo, na wakati nawaza hayo nikawa namuangali mke wangu, sikutaka kabisa ajue hicho kinachoendelea kati yangu na mlinzi wa baba yake,….na baadae mke wangu akamaliza kuongea na simu, akaja na kuniangalia usoni…
‘Mzee anasema tuhakikishe leo tunakutana na yeye, atakuja yeye mwenyewe …’akasema
‘Kwani hilo lina tatizo, tatizo ni kijana wako, je tunaweza kumpata..?’ mume akauliza
‘Hilo sio tatizo, baba keshaongea naye, na kakubali kuwa atakuwepo kwenye hicho kikao, kwani yeye ana mengi ya kuelezea,...na anao huo ushahidi wa hicho anachotaka kukisema…’akasema
‘Oh, kwahiyo kumbe bado hajanielewa..’mume mtu akasema na kutizima nje, akilini akijua ana majanga mawili tayari, sijui aanze lipi kwanza.
‘Akuelewe vipi, baba gani wewe, mwenye tabia ya ajabu, hata ingelikuwa mimi, ningelifanya hivyo hivyo..sasa ujiandae, nafahamu maamuzi ya baba, na nikuambie ukweli safari hii, tutasigishana,..ya kuwa mimi nitakuwa pamoja na wazazi wangu, vinginevyo…’akatulia
‘Vinginevyo nini…?’ nikauliza
‘Vinginevyo, …nitayaongea hayo kwenye kikao,….na najua hicho kitakuwa kikao cha mwisho baada ya hapo sitaki tena kikao na wewe…’akasema na kuanza kuondoka
‘Je kikao kitafanyika saa ngapi mbona unaondoka…?’ nikauliza lakini mke wangu hakujibu akawa keshaondoka, na mimi nikabakia peke yangu nikijiandaa kwenda kukabiliana na huyo mlinzi.
*******************
Wakati hayo yakiendelea, mbaba akiendelea kusimulia yaliyomsibu,
Mimi ghafala akili ikahama, nikawa nawaza mengine tofauti, ikafika muda hata sisikii hicho wanachokiongelea sijui kwanini mawazo hayo yaliteka akili yangu…
Nilijiuliza ni kwanini mimi ndiye yanikute hayo yote….mimi nimezaliwa masikini, wazazi wangu walikuwa omba omba, kula yetu na maisha yetu yalitegemea kile tutakachopewa na wasamaria wema,..na kwa bahati ndio nikapata hiyo kazi ya ufanyakazi wa ndani,…lakini badala ya kupata kile nilichotegemea ndio nikazidi kuingie kwenye mtihani mkubwa.
Mama yangu niliyemuacha huko kijijini, akisubiria angalau jasho la binti yake, akaishia, kuangamizwa kwa kuchomewa banda lake na yeye kufariki kutokana na majeraha ya huo moto, je ana kosa gani, je walifanya hivyo ili iweje,..
Nasikia kumbe lile kundi la uharamia, la vijana hao waliotelekeza dhuluma hiyo lilikuwa likisimamiwa na huyo huyo marehemu, nia na lengo lake ilikuwa kupora ardhi ,lakini hata baada ya adhima yake hiyo kutekelezwa, akajikuta bado anagombea eneo hilo na hasimu wake.
Hayo nilikuja kusimuliwa na wale watu wa dini waliokuja kunitembelea wakinitafuta mumiliki halali wa eneo hilo, na hilo lilikuja kukubaliwa baada ya watu kushindwa kulimiliki. Kwani hao waliotaka kulimiliki kwa dhuluma, hawakuweza hata kujenga nyumba, kila walichofanya kilishia kibaya.
Lakini hayo hayakunisumbua sana, kilichonisumbua sana akilini ni mawazo ya hatima yangu, tumboni nina kiumbe, je ni mtoto kweli,...na kama sio mtoto itakuwa ni nini...na huenda akawa ni mtoto, atakuwaje nikijifungua, na mpaka hapo , maelezo yote ya huyo mbaba, hakuna sehemu inayofichua ukweli wa hii mimba, ni nani anahusika, sio hoja kwangu, hoja ni je atazaliwa kiumbe wa namna gani
Nikawa najiuliza sana hilo swali, lakini hata nikijiuliza ni nani atafahamu, hapo nikaona nimuachie mola mwenyewe,, ..kila nilichowaza hapo hakikuwa na ufumbuzi, ..nikiisia kujiuliza tu, kwanini mimi…kwanini mimi nizalilishwe hivyo, kwanini mimi yanitokee hayo yote, nimekosa nini jamani…’hapo machozi yakawa yanazidi kunitoka kwa wingi.
Sasa nikaona mawazo hayo hayatanisaidia, ndio nikazama kwenye imani ..nikawa sasa namuomba mola wangu nikisema kimoyo moyo…
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
.
'Ewe mola wangu, nisamehe kwa dhambi hii, mimi sijui nimetenda madhambi gani hadi haya yanikute, wewe peke yake ndiye unaye ujua ukweli wa haya yote, mimi ni kiumbe dhaifu tu,..uwezo wa kuyabeba haya kwa hivi sasa sina tena.., kama kweli wapo watu wenye uwezo wao waliamua kuyafanya haya, wewe unawajua, na sipendi kusikia tena walitaka nini kwangu, na hata hivyo, mimi sina nia ya kuwaombea mabaya,...wasamehe tu... na sina lengo la kulipiza kisasi, ninachokuomba uwasamehe tu hilo kwangu ni faraja…’nikapandisha viganga vyangu usoni na kuyafuta machozi.
‘Nakuomba mola wangu uwasamehe, hususani huyu baba hapa, nawatambua hawa kama walezi wangu, najua walichokifanya ni kibaya, lakini ni katika kuhangaika kwao, walijua wakifanya hivyo labda watafanikiwa lakini ni shetani tu kawazidi nguvu, mimi nakuomba uwasamehe, na nitajua kuwa umewasamehe kama nilivyowasamehe mimi, nikisikia wamesameheana na kurejeana kama mke na mume....' hapo ni machozi tu yanatoka,..hata nilipojitahidi kuyazuia sikuweza.
‘Nakuomba ewe mola wangu, na huyo kijana wao, apone, aondokane na mitihani inayomakabili arudi na kuungana na wazazi wake..hili kwangu litakuwa ni faraja kubwa sana, na huyo binti naye aachiwe awe huru, kwani na yeye ni miongoni mwa waathirika wa mitihani hii ambayo, wewe peke yake ndiye unajua ni kwanini ilifanyika kwetu, huyo binti kadhulumiwa na yeye, lakini najua na yeye atasamehe , na kusamehewa,..nakuomba ewe mola wangu wangu unitimizie maombi yangu hayo, ..sijui nifanye nini ili unitekelezee hayo maombi yangu…’nikainua viganja vyangu na kufuta machozi yangu tena.
Hapo nikahisi hicho kiumbe tumboni kikinikwangua, nilihisi maumivu na baadae yakapoa, nikaendelea na mawazo yangu sasa yakiwa ya kuomba tu.....
‘Pamoja na hilo, …nakuomba mola wangu, kinyume na imani za hao watu walionifanyia hivyo, nakuomba tena na tena hii mimba, huu, uja uzito uwe ni faraja, kwangu, nimzae mtoto aje kunifuta haya machozi, zaidi ya wewe sina wa kumtegemea, zaidi ya huyo mtoto hakuna wa kunifuta haya machozi.....’hapo sikuweza kuvumilia nilijikuta nikilia kilio cha kwikwi , na muda huo ndio watu wote mle ndani walikuwa wamenigeukia..mimi....hapo sijijui nimezama kwenye duwa, kwenye maombi kwa mola wangu
Kumbe wawili hawa wapo mbele yangu wamepiga magoti mimi sijui...ao wanajua nalia kutokana na hayo yaliyotokea, wao wananibembeleza ili niwasamehe..sijui ...na ndipo akili ikafunguka,, na kutoka kule kwenye imani, na mawazo niliyokuwa nayo yakapotea na kuwaona wawili hao wamenipigia magoti baba na mama mfadhili.
‘Kwanini…mnafanya hivyo…?’ nikauliza, huku nikihangaika kujifuta machozi...
‘Kwanini wewe unalia, ina maana muda wote ulikuwa kwenye mawazo, na hata hujui tulichokuwa tunaongea..?’ akauliza mama Ntilie
‘Oh, kwakweli, nilipotea, nisameheni sana, ila…mimi sina kinyongo na nyie wazee wangu naombeni msimame, msifanye hivyo, mimi sio mtu wa kupigiwa magoti, hamuniamini kuwa mimi nilishawasamehe nyote, mimi nawauliza tu, je nyie wawili mumeshasameheana..?’ nikawauliza
Wote mle ndani wakashikwa na mshangao, na mama Ntilie akasema
'Inaonekana hukuwepo humu ndani kabisa...'akasema mama Ntilie.
Na wawili hao wakaangaliana, na tabasamu likatawala kwenye midomo yao, na kwa pamoja wakasema
‘Ndio….kwa ajili ya familia, kwa ajili yako, na kwa ajili ya mola wetu tumesameheana…’wakasema, hapo kiukweli nilijikuta machozi yakitoka tena lakini sasa kwa furaha, kilichoendelea hapo ni furaha, .....na baadae tukaongea kidogo wao wakaaga kuondoka kwani walikuwa wakisubiriwa na familia zao, na kabla hawajaondoka simu ikapigwa, kijana wao kaachiwa, yupo huru, ila yule binti bado kashikiliwa, hata hivyo, hata yeye atachiwa baadae.
Mambo hayo yalitokea siki hiyo hiyo...
Kwahiyo familia hiyo ikaondoka ikiwa na furaha...na hakuna aliyefikiria kuniuliza vipi hatima yangu itakuwaje,..hilo sikujali, moyoni nilijua, kama hayo yametokea, ina maana duwa langu kwa muumba limeshapokelewa, ...najua hata mimi mambo yangu yatakuwa mazuri,..mungu hamtupi mja wake...imani yangu ilisema hivyo
‘Siamini,...ina maana hao watu wamesameheana, kiukweli.. kwani ilikuwaje…, unajua mimi nilipotea, nikazama kwenye mawazo ilikuwaje, hebu niambie jamani...?’ Hayo nilimuuliza mama Ntilie, wakati wawili hao wameshaondoka..
Muda wa kunisimulia hayo haukupatikana, wageni, wateja..ikawa kazi siku hiyo ikapita, na kesho yake ukaingia ugeni...
NB: Tutakutana kwenye hitimisho
WAZO LA LEO: Tujiepushe sana na tabia ya kiburi, hasa ukijaliwa mali, nguvu, cheo au na neema yoyote ile, usijione wewe umefika, usijione kuwa umevipata hivyo kwa ujanja wako, jiulize wangapi wenye uwezo kama wako, walikuwa na akili sana madarasani, walikuwa na namna nyingi sana, lakini hawajapata kama ulivyopata wewe, sio kwamba wao ni wajinga hawaju njia za kupata kama ulivyopata wewe, ..ni neema za mola ambaye humpa mja wake kwa kadri aonavyo ni sawa, basi ukipata mshukuru mola wako, na saidia wenye kutaka msaada, na shukuru na kuwaombea wasio nacho wapate kama wewe au zaidi yako.
Kwa vile kuna kipindi nilizama kwenye mawazo, nikapotea kabisa kifikra, sikusikilia alichokuwa akisimulia yule mbaba, kwahiyo nikamuuliza mama Ntilie anihadithie walichokiongea, hadi wawili hao wakafikia kusameheana mtu na mke wake,… lakini haikuwezekana kwa muda huo yeye kunisimulia kwani walifika wateja wakihitajia huduma na siku hiyo ikapita, na siku ya pili ikawa hakuna kazi nyingi sana, na tulipopata muda na ndio nikaweza kuelezewa na mama Ntilie, kabla hatujaingiliwa na ugeni mnzito….
Tuendelee na hitimisho la kisa hiki….
**********
Ni siku ya pili yake baada ya hicho kikao changu na baba na mama , wafadhili wangu ambao waliondoka baada ya mimi kuhakikishiwa kuwa kweli wamesameheana, nashukuru mungu kuwa kweli, kwa hali ilivyojionyesha watu hao sasa ni mke na mume wema.
Kila muda nilikuwa najiuliza nilipitwa na nini hapo kati, maana sikumbuki jinsi walivyofikia hapo, ndio ikafikia muda nikamuuliza mama Ntilie..
‘Hebu niambie ilikuwaje siku ile..?’ nikamuuliza mama Ntilie.
Mama Ntilie akasema;…
‘Unajua nilikuona ukiwa umezama kwenye mawazo, sikutaka kukusumbua, nikakuacha tu, nikawa mimi nasimama badala yako, wakikuuliza swali nakujibia, na ndipo ikafika ile hatua ya wao kuja kukupigia magoti, nikawaambia…CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Mngelijua moyo wa huyo binti ulivyo, hapo yupo kwenye imani na mungu wake, hapo yupo na mola wake, mimi naona msijisumbue kumpigia magoti, ni nyie tu, kwanza mumuhakikishie kuwa mumeshasameheana, vinginevyo hataweza kuwa na amani, na kama mlivyosema hatima yenu itategemeana na huyo binti kwa vile yote yalitokea kutokana na hayo aliyofanyiwa,…’nikawaambia hivyo.
‘Oh….ina maana ni hivyo tu…?’ nikaguna na kuuliza.
‘Ndio nakuanzia, sijui wewe ulianza kupotea wapi, ila nikirudia hapo, baada ya kuwaambia hivyo, mume mtu akauliza
‘Ina maana mke wangu asiponisamehe, na yeye msamaha wake hauna maana au sio, sasa mke wangu muambie kilichopo moyoni mwako, je umenisamehe kiukweli…’akasema.
‘Ndio, aliniambia kuwa msipofanya hivyo, yeye atamlilia mola wake mpaka musamaheane na hapo anamlilia mola wake, mimi namfahamu sana…’nikasema wakati huo moyo wangu una mashaka, ni kwanini upo hivyo, unalia, huongei….’akasema.
‘Mke wangu unasikia…’akasema mbaba.
‘Mhh, wewe tatizo lako hunielewi, isingelikuwa ni wazazi wangu sijui kama ningelikusamehe, lakini nimekusamehe, kwa ajili ya familia yangu…’akasema.
‘Sasa tumuonyeshe binti yetu,…lakini kwanini anaendelea kulia tu…’akauliza huyo mbaba akiniangalia mimi, na hao nikasema;
‘Tumpe muda bado yupo kwenye kumlilia mola wake….’nikasema
‘Unajua mama Ntilie, tangia tunafika hapa, nilishafikia uamuzi fulani,..maana huko nilipotoka ilikuwa shughuli kubwa, mimi nilikutana na wazazi wangu, nikiwa nataka ndoa ivunjwe, lakini cha ajabu sasa wazazi wangu hawataki ndoa nivunje …’akasema mke mtu.
‘Kwanini…?’ nikamuuliza wakati huo wewe upo kama ulivyokuwa machozi, huongei…
‘Wazazi wangu wamasema wao sasa wanakiri kuwa wamefanya makosa, na mitihani wanayokutana nayo kwa hivi sasa inaweza ikawa inatokana na wao kuwa mbali na watoto wao, hususani mimi na mume wangu…’ akasema.
‘Kiukweli niliwaonea huruma sana wazazi wangu..na nikawaza sana, nikaona kweli inabidi tusahau yaliyopita tugange yajayo, ni vigumu lakini utafanyaje…ndio ikabidi nimtafute huyu mwanaume, sikumuambia nilichoongea na wazazi wangu..nilitaka nisikie kauli yake ya sasa na ukweli wote,na kama angelificha safari hii,…, nisingelimsamehe, safari hii alikiri yote tofauti na yaliyotokea kipindi kile kabla hajachanganyikiwa…’akasema.
‘Kwani kipindi mlipoitwa na baba yako ilikuwaje…?’ akaulizwa.
‘Siku ile niliumia sana, kwani alipokuja baba, baba akiwa kajiandaa kumsamehe, yeye aliendelea kuficha ukweli, mbele ya kijana wetu ambaye alikuwa anafahamu kila kitu, siku ile…baba alikuja, akatuuliza kuna tatizo gani kwa kijana wetu mbona kuna kitu kinamsumbua.
‘Kijana huyu achana naye, nitamalizana naye, ni tatizo dogo tu... Nilishaongea naye, tatizo hanielewi, unajua watoto wa siku hizi walivyo, …’akasema mume mtu.
‘Eti kijana kuna tatizo gani…?’ akaulizwa, na kijana sasa alionekana kuwa na wasiwasi, akawa kidogo anamuangalia baba yake kwa mashaka na mara nyingi anaangalia chini. Halafu alipoona anasubiriwa yeye kuongea akasema;
‘Mimi nataka baba aongee yeye mwenyewe, kama hataki kuongea …mimi siwezi kuongea tena…nimeamua bora yaishe …nitajua la kufanya mwenyewe…’akasema.
‘Kwanini,… si ulisema utaongea kila kitu…sasa hiki kikao kina maana gani…’akaambiwa.
‘Hapana nimewaza sana, nikaona ..baba ndiye angelipaswa aongee au seme ukweli..lakini kama hataki kuusema ukweli,… basi, mimi nitaamua la kufanya mimi mwenyewe…’akasema
‘Auseme ukweli gani sasa…ina maana sisi tumekuja hapa kupoteza muda wetu, tukitarajia kusikia hilo jambo, ambalo lilikupeleka hadi kwa babu yako, ..na hiyo bahasha yenye ujumbe ipo wapi..?’ akauliza huyo mzee.
‘Mhh..mimi sijui…’akasema akimuangalia baba yake.
‘Haya baba mtu hebu tuambie kuna tatizo gani hapa nyumbani kwako…?’ akaulizwa na baba mkwe.
‘Hakuna tatizo mzee, matatizo ni ya kawaida, kama ujuavyo maisha yalivyo, kunatokea mitihani ya hapa na pale, sasa haikuwa na lazima wewe uje, kama ingebidi hivyo, sisi wakubwa tungekuita rasmi,…, unajua vijana siku hizi wamepata simu, wana mitandao, wanahisi kila kitu ni kupiga video, hawajui madhara yake,…nimeongea naye najua keshajirudi..’akasema baba mtu.
`
‘Una uhakika huna cha kuongea…?’ mama mtu akamuuliza kijana wake, na kijana akainua uso kumuangalia baba yake halafu akasema;
‘Baba kama hataki basi…’kijana akasema.
Mimi hapo nilikuwa na ajenda yangu kichwani sikutaka kusema lolote, nilijua nikisema kitu baba atachukua hatua mara moja, sikujua baba ana kitu gani moyoni,..na pia nilitaka kusikia mume wangu atasema kitu gani, hakujua kuwa mimi nilishagundua ukweli wote…’akasema mke mtu.
‘Ukweli wote uliupataje huo ukweli..?’ akaulizwa na mama Ntilie.
‘Mimi nilishaupata huo mkanda wa kijana wangu, na ni ule alioupeleka kule kwa babu yake…’akasema na kila mtu akashikwa na mshangao
‘Kwa vipi…ina maana muda wote huo ulikuwa nao…?’ akaulizwa.
‘Siku ile wakati huo mkanda unaletwa kule nyumbani kwa wazazi wangu, nilikuwepo, nilifika kule kwa mambo yangu, na wakati kijana anaingia na kuonana na mlinzi nilikuwa dirishani namuangalia, sijui waliongea nini na mlinzi, ila niliona kijana akimkabidhi huyo mlinzi bahasha,….kwa muda ule nikajua labda mlinzi alipomuambia kuwa mimi nipo ndani, kijana akaona aondoke, labda alikuwa akinikwepa, lakini kumbe mlinzi hakumuambia mimi nipo humo ndani…
Nilitaka nitoke nje kwa haraka nimuite huyo kijana tuongee naye, lakini hakusubiria, hata wakati natoka nje alikuwa keshaondoka,..alikuwa anaendesha piki piki lake…na muda huo mlinzi alikuwa kashika hiyo bahasha wakati natoka, kwahiyo mlinzi hakupata muda wa kuikagua vyema…mimi kwa haraka nikaona jina la baba juu ya ile bahasha…sikuwa na shaka nilijua ni mzigo wa baba,..lakini nikajiuliza ni kwanini aulete huyo kijana…na kabla sijamuuliza mlinzi , yeye akasema;
‘Kijana wako kaleta bahasha hapa, kaniambia nimpatie babu yake mkono kwa mkono, lakini mume wako alisema kama kuna mzigo utaletwa hapa na kijana au mtu mwingine yoyote, nisimpatie baba yako, kwani una makosa, inahitajiak urejeshwe nyumbani, alinisisitizia sana, je ndio huu, au kuna mwingine…?’ akaniuliza
‘Ni kweli, wewe nipe nitampatia, kama ndio wenyewe…’nikasema akilini mwangu nikihisi kuna jambo, kwanini kijana alete huo mzigo, na kwanini baba yake asema hivyo, akili ikachanganua na kuhisi kuna jambo, na hapo hamasa ya kuchunguza hiyo bahasha ikanijia…’akasema
‘Unajua nimekumbuka kuna kazi nilimuachia mume wangu, nahisi ndio hii, ngoja nione kama kuna cha kubadili nitafanya hivyo, haina haja mpaka yeye aje kuuchukua, ngoja, nitaongea naye kwenye simu..’nikamwambia huyo mlinzi
‘Lakini mume wako…’akalalamika
‘Nitampigia kwani una wasiwasi gani, kwani alikuambia nini kuhusu huu mzigo…?’ nikamuuliza
‘Alinisihi nisimpe mtu mwingine mpaka yeye aje kuuona mwenyewe….’akasema
‘Alikuambia huo mzigo ni kwake unakuja hapa kwa baba, atauleta huyu kijana..?’ nikamuuliza
‘Ndio….’akasemaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Basi haina shida..nitaongea naye ikibidi nitamsubiria, huenda yupo njiani anakuja, tutakutana naye hapa…’nikasena na yeye akakubali shingo upande, na hali hiyo ikazidi kunipa hamasa, nahisi kuna jambo kati ya mume wangu na kijana wangu, na kuna kitu nyuma ya pazia. Nikaingia na hiyo bahasha ndani, nikaichunguza ndio nikagundua kuwa video.
Kwa haraka nikaenda kwenye deki,, bila kujali kuwa huenda ni mzigo wa baba, huenda ni kazi fulani kijana alipewa kuifanya na baba, …nikaona kwanza niondoe mashaka moyoni mwangu, nikaiweka kwenye deki na kuanza kuiangalia, kiukweli nilihamaki..nilikasirika, na kama …sio subira…nashukuru hata baba hakuwepo..’akasema.
Basi nikawaza sana, nikaona ngoja kwanza nione huu mchezo mwisho wake ni nini, ndio nikatoka nje nikamsomesha mlinzi anisaidia jambo moja, na hayo aliyoyafanya mlinzi ni yale niliyomuelekeza mimi..na wakati huo nikapata muda wa kuatafakari haya mambo vyema, na mpaka hapo nikawa nimejua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea ndani ya nyumba yangu.
Kiukweli hadi hapo nikawa nimeazimia uwe mwisho wangu na huyu mwanaume, tuachane tu kwani hayo niliyoyaona sio ya mtu wa kawaida, hayo ni ya mchawi…na nitaishije ndani na mchawi, ndio, kuna namna inaonyesha kuwa sio dhamira ya huyu mwanaume kufanya hivyo, lakini kwanini..kama ni tatizo kwanini asiniambie…na nilipoona ile sehemu ambayo niliipeleka kule kwa yule mtu anichunguzie, ndio hapo nikazidi kutishika zaidi, kuwa kumbe naishi na shetani ndani ya nyumba….sasa sina jinsi, kwani ushahidi ninao, lakini moyoni, nikasema ngoja nimpatie nafasi ya mwisho huyu mtu, unajue tena mumeshazaa naye, watoto wakubwa, kuna mambo yanakusuta…’akasema mke mtu..
‘Ndio ikaja hicho kikao chako na baba yako au sio…?’ akauliza mama Ntilie
‘Ndio, lakini hicho kikao sikuitisha mimi, hicho kikao ni cha kijana kutaka kusema jambo na alishaongea na babu yake kuwa ana jamabo la kutaka kuongea, na nilion ajabu ni kwanini tena kijana akaghairi, na sizani kama aliongea na baba yake akatishiwa, nahisi kuna kitu aliogopa, na sikuwahi kumuuliza..…na cha ajabu mume wangu hakutaka kusema ukweli, hapo nikajua kweli huyu mwanaume ana tatizo…’ akasema
‘Ni kwanini hakukubali kusema ukweli, ni ili hali hakuwa na uhakika kuwa hiyo bahasha iliyotumwa huko kwa baba ipo kwa mlinzi, au baba yake ameshaipata…?’ akaulizwa
‘Hakukubali, akijua kuwa siri hiyo haijajulikana, yeye alikuwa na uhakika bahasha hiyo bado anayo mlinzi, na nilimuambia mlinzi amuambie hiyo bahsha bado anayo,… na walishapanga na mlinzi kuwa alipe kitu kidogo, apewe hiyo bahasha, kwahiyo akajiona yeye bado yupo salama, …
‘Unajua mtu kama huyu mpaka mabaya yamkute ndio anaweza kukubali ukweli..sasa utaona yaliyotokea baadae, ambayo yalimpa fundisho, hebu atuelezee mwenyewe ilivyokuja kutokea adhabu kutoka kwa mola mwenyewe…’ mkewe akamgeukia mumewe.
*****************
Hapo ndio mume mtu akaanza kuelezea ilivyokuja kutokea baadae….
‘Ni kweli, tulikuja kukutana na baba mkwe akiwemo kijana…na nilishangaa mzee alipokuja alikuwa na sura tofauti na siku nyingine,…alinisalimia kwa unyenyekevu, badala ya mimi kuanza kumsalimia, ..mzee huyo ni mkali, hana utani kwa watoto,
‘Watoto wangu nisameheni sana,..nahisi nimekuwa mkaidi kwenu….na naona sasa nahatarisha ndoa yenu mpaka kijana anakuwa hana raha…na nimegundua bila ya mimi kutoa idhini yangu kwenu hamtaweza kuishi kwa amani, nimeliwazia hilo sana, kwahiyo kuanzia sasa nipo radhi na nyie, nimeikubali ndoa yenu, lakini kabla ya hilo nataka jambo moja kutoka kwa huyu mkwe wangu..je upo tayari kubadilika na tabia yako hiyo mbaya…?’ akasema
‘Tabia mbaya, baba nina tabia gani mbaya,..sawa labda mimi nina kiburi, labda…basi kama ni hivyo mimi nikubali nitabadilika, nipo tayari kubadilika….!’nikasema hivyo.
‘Je upo tayari kubadilika, na kuacha hayo mambo unayoyafanya yasiompendezesha mungu na ndoa yako..?’ nikaulizwa na mke wangu.
‘Mke wangu mambo gani yasiyompendezesha mungu…ambayo mimi nayafanya..?’ nikauliza kwa mshangao.
‘Mume wangu…unajua hapa yupo baba, hapa yupo kijana, na kijana ana mambo anataka kuyasema …ambayo yamekuwa yakimkera, ana ushahidi, bado wewe unaendelea kusema huna tatizo, je huo ushahidi ukitolewa utakuja kusema nini…?’ nikauliza
‘Ushahidi gani jamani..eti kijana wangu una ushahidi gani kuwa mimi nina tabia mbaya, nimefanya kitu gani, sema ..au utoe huo ushahidi wako…mmi nipo tayari…na sijui kwanini haya yote mimi sina tatizo, sijamkosea mtu yoyote na kama nimemkosea basi..nisamaheeni…’akasema huku nikiwa na mashaka mashaka.
‘Umesikia binti, huyu mume wako hajabadilika..umesikia mwenyewe, nilikuambia kama kweli kabadilika basi mimi nitakwua radhi na nyie, lakini kwa hili, bado…bado, sikiliza binti yangu, mimi nipo tayari kuwapa idhini yangu, lakini nahisi bado, siwezi kukutelekeza binti yangu kwa mtu ambaye ninajua ana matatizo, kama utaniamini haya, kama hutaniamini haya,..sisi tutazidi kumuomba mungu, kama upo ukweli wa haya aje autoe, sina zaidi, labda tumsikia kijana atasema nini…’akasema baba, na mke angu hakukata tamaa akaniuliza tena..
‘Mume wangu kwanini unanilazimisha nifanye nisicho kipenda, kwanini hutaki kutubu, ukajirudi, tukapata baraka za wazazi wetu..mume wangu wewe hadi kijana kasema una mambo unayoyafanya usiku, sasa unafanya nini, tuambie tukusaidie, kwanini upo hivyo…?’ mke wangu akaniuliza.
‘Nani mimi..oh,…hahaha, hivi mke wangu hayo yametoka wapi,..hivi wazazi wangu wangelikuwepo hapa wakayasikia haya, wangehisije, kuwa mim kijana wao ni mchawi, au si hivyo unavyotaka kusema...sio vizuri jamani, mnanifanya nijishi mpweke baba na binti yake mnanisingizia mambo ambayo sio kweli…’nikasema
‘Na kama ni kweli, ujue utapata mabaya makubwa sana, maana sisi tunamuomba mola atusaidie, awasaidie na nyie muondakane na hayo yanayowasumbua, na kama upo ukweli, aje audhihirishe, utakuja kuumbuka mkwe,…’akasema baba mkwe
‘Nasema ukweli hakuna kitu kama hicho, mimi sijawahi kufanya hayo unayoyasema baba, au mke wangu kijan huyu hapa aseme mwenyewe, ..hao waliotaka kufanya hivyo ndio hao wamelipiliziwa mimi wala sijui walikuwa wakitaka nini…wamekufa , wangekuwepo mungeliwauliza wenyewe…’nikasema na baba alipoona sijabadilika akasimama kutaka kuondoka, kijana wangu akasema;CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Baba kwanini hutaki kusema ukweli..?’ aliponiuliza kijana hivyo, hapo nikashtuka…nikajua sasa kijana anataka kuusema ukweli. Nikamwangalia kwa kumkazia macho, kijana wangu toka utotoni anajua sura yangu ikiwa vipi nipo na hasira hapo anakuwa makini na hata kuogopa kuongea, naona hadi sasa kawa mkubwa anajua hulka yangu,
‘Sikiliza kijana hujui haya…nilikuambiaje mambo ya wakubwa usiyaingilie litakalotokea utakuja kujuta mwenyewe.., kaa pembeni,…usipende kuingilia mambo ya watu wakubwa, wewe tabia yako ya unga ndio imekuharibu, acha tabia hiyo,… mimi sijafanya hayo unayoyafikiria wewe, wewe ni mzushi, ni unga wako unakupeleka kubaya, na tabia yako hiyo mbaya, uiache mara moja, unasikia, sitaki tena kusikia kijana wangu anatumia unga, iwe mwisho leo……’nikasema kwa ukali…
Kijana alitulia kwa muda, machozi yakawa yanamlenga lenga…kijana wangu sio mdogo, angeliamua la kufanya hapo angelifanya, lakini nahisi kuna kitu kilimpata au kuna mtu kamshauri akaona awe hivyo.
‘Basi mimi naondoka kwenye hii nyumba, maana sasa naonekana kuwa mimi nii mzushi, maana sasa kila mtu ananionyeshea kidole mimi kuwa nilitunga uwongo, na mambo yangu yote niliyoyaweka kama ushahidi umeyaharibu, sasa…naonekana mimi kama mzushi, na hata huku kuumwa nazusha tu…, haya, mimi naondoka zangu, nitajua mwenyewe la kufanya….’akasema na kuanza kuondoka. Hakuna aliyemzuia…
Kijana hakuonekana tena hapo nyumbani, na hata huko kwa babu yake hakufika tena, siku zikapita…na mpaka tuliposikia taarifa hiyo ya kukamatwa kwake…
Sasa baada ya kikao kile,…yaliyofuatia hapo kwangu ilikuwa ni mawazo , mawazo….nahisi kabisa sipo sawa…namuwazia kijana wangu nawazia hayo niliyoyaona kwenye hiyo video, nawazia….yaani sielewi..
Nikawa sasa najilaumu, kwanini nilifanya hayo, kwanini sikukubali kusema ukweli, kwanini sikukubali kuwa hayo yaliyotokea usiku nilikuwa nahusika, nikaungama mbele ya familia yangu, na je nitafanyaje ili kijana wangu apone…mawazo hayo hayakuniacha, mara siku moja nikahisi sauti nyingi zikizizima kichwani mwangu, yaani ikawa kama kichwa na watu wanaopiga kelele…na haikupita muda nikawa sijitambui, nikatoka mbio mbio huku niki-ita…jina la kijana wangu!
‘Kijana wangu njooo..nitasema kila kitu, nimekosa kijana wangu…’ilikuwa sauti yangu ya kila siku nikawa sasa ni mtu wa kushikwa, nataka kukimbia…nikiuliza ni nini shida, kauli ni hiyo,..namtafuta kijana wangu…na hata kijana wangu alipopatikana nikawa simtambui tena, nahisi kama sio yeye, ikawa ni kazi hadi nikafikishwa muhimbili wodi ya wenye matatizo ya akili, baadae nikarejeshwa nyumbani, ikafika muda sijijui kabisa..
Masiku, miezi ,.nipo hivyo..na kuna wakati hali inajirudi, lakini sio kwa kujielewa sana, mke na wanafamilia walijitahidi kila aina ya matibabu,..mwishowe nikawakimbia,..hayo mimi siyajui, nasema sasa kama nilivyokuja kuambiwa…na ndio nikaja kukutana na nyie..
‘Kwahiyo safari zote hizo ni za kumtafuta kijana wako…?’ akaulizwa
‘Ndivyo ilivyoanzia hivyo, na nilipo-potelewa kabisa, akili iliyokuja baadae ni ya kumtafuta huyo binti…anisamehe...’akasema
‘Jamani hicho ndicho kisa changu…
***************
Na alipofikia hapo ndio akageuka kukuangalia wewe, akashanga kukuona anabubujikwa na machozi, hapo, akashtuka, na ile hali ye yeye kushutuka, ikawafanya na wengine wote kugeuka kukuangalia, mimi nilishakuona ulivyo…tokea awali nilikuwa nimetulia tu, ndio mama mtu akasema;
‘Oh, binti..usilie, mimi nimeshakubali haya yaishe, na japokuwa kwa shingo upande, nimekubali kumsamehe mume wangu,na wewe sasa tunakuomba utusamehe…..’ilikuwa kauli ya mama huyo
‘Hayo ndiyo yalitokea ukiwa umezama kwenye duwa sijui,..ulikuwa unaomba …si ndio hivyo, mmmh na maombi yako sio mchezo, yakajibu…’akasema mama Ntilie.
******************
Siku zikapita na siku moja, ukafika ugeni, ni ugeni ule wa awali, wa wale watu walikuja kutaka kununua lile eneo la urithi huko kijijini, sasa wakisema wamekamlika, kwahiyo mimi na wao tuongozane hadi benki ambapo huko ndio malipo yatafanyikia, mama Ntilie akasema kwa siku hiyo yeye hawezi kuacha shughuli zake mimi niende peke yangu tu.
‘Usijali hawa ni watu wema hawawezi kukudhulumu…’akasema na mimi nikaondoka na hao watu hadi benki ambapo nilishafungua akaunti yangu, nikalipwa hizo pesa, tukaandikishana na hao watu, na kila kitu kakamilika kwa mara ya kwanza nikawa na milioni kadhaa benki,
Sasa wakati tunatoka hapo benki, tupo nje ya korido la benki,…mmojawapo akaniuliza;
‘Dasa samahani wewe una matatizo gani yanayokusumbua…?’ akaniuliza na kunifanya nishikwe na mshangao, nikamuuliza hivi
‘Nina matatizo!!...nina matatizo gani!..., kwanini unaniuliza hivyo…?’ nikauliza na mwingine akasema;
‘Huyo hapa mwenzetu ni mtu aliyejaliwa kipaji cha kusaidia watu wenye matatizo, anaweza kukuangalia hivi tu akatambua matatizo yako, na jinsi ganii ya kukusaidia, huwa anajiwa na vitu kama njozi…na tukuambie ukweli, siku ile tulipofika awali alipokuona tu, yeye akagundia kuwa una matatizo makubwa sana…ambayo yanahitajia msaada wa haraka, kabla hujajifungua…’akasema.
‘Mhh…mimi naona hayo hayana umuhimu kwangu, na sihitaji mtu wa kunisaidia,..najua mungu pekee ndiye wa kunisaidia, kama nina matatizo nimeshayafikisha kwa mwenyewe, nasubiria matokeo tu, vyovyote itakavyotokea najua ni kwa matakwa yake…’nikasema.
‘Hapana hakuna malipo yoyote utalipa kwetu, ..sio kwamba tunafanya hivyo kwa vile una pesa, hapana..kamwe hatutaki hata senti moja yako….na sisi hatuwezi kuondoka bila kukuambia hilo na kama utahitajia kusaidiwa, ..na si kusaidiwa, sisi tunachofanya ni kumuomba mola wetu…yeye, huyu mwenzetu kasema hataweza kuishi kwa amani akiondoka bila kukusaidia, na yeye anamtegemea mungu wake,…yeye atakuombea tu, na mengine tutamuachia mungu, utuelewe, sisi ni watu wa imani…’akasema
‘Wapi sasa, hapa hapa, au …?’ nikajikuta nimesema hivyo, niikiwa siamini maneno yao…, sikuwa na mawazo hayo tena kuwa mimi nina tatizo. Nilijua nimeshamkabidhi mola wangu…
‘Vyema turudi kule nyumbani unapofanyia shughuli zako, ili tupate nafasi kuliko hapa, ila ni kama wewe upo radhi, na kama haupo radhi basi, sisi tutakuacha, ila mwenzetu huyu kajaliwa kipaji cha namna hiyo na amewasaidia watu wengi sana tena bure…’akasema huyo kiongozi wao.
Basi mimi sikuwa a kipingamizi tukarudi nyumbani, nilikuwa nimechukua kiasi fulani cha pesa kwa ajili ya kuongezea biashara na mama Ntilie.. Tulipofika, hakukuwa a wateja wengi , nikamuelezea huyo mama kilichofanyika na hayo wanayotaka kuyafanya hao watu,..huyo mama akaniita pembeni.
‘Unawaamini hao watu wasije wakafanya hivyo kesho na kesho kutwa unakuta pesa yote imekwisha huko benki…’akasema
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Wao ndio wamenilipa, wao ndio wamefanya juhudi yote hiyo, wao ni watu wa dini, mimi nimewaamin, na najua mungu atanilinda, huenda ikawa ndiyo sababu ya kuondolewa hii mitihani, tumuachie mungu anajua zaidi …’nikasema
‘Sawa….kama umewaamini mimi sina shaka…’akasema na basi wale watu wakaniombea na yule mmojawapo ambaye ndiye mwenye hicho kipaji akasema nilale tumbo juu, nikafanya hivyo, yeye akaweka kiganja chake tumboni,i kwangu, nilihisi tumbo likitetemeka kama mtu aliyeshikwa na umeme, iliendelea hivyo kwa muda, badaye likatulia.
‘Pole sana…natumai sasa utajifungua salama…’akasema huyo mtu wa dini.
‘Kwani ni kitu gani umekigundua …?’ akauliza mama Ntilia
‘Inaonekana huo uja uzito una maagano ya shiriki ndani yake, ..lakini yamekwisha, muhimu ukijifungua tu hakikisha unatimiza wajibu wote wa mtoto,…kumuomba mola wako, ..na kamwe usije kumshirikisha mtoto huyu na mambo ya kishirikina…yeye anahitajia imani tahabiti ya dini, ndiyo itakayomsaidia, na ianzie kwako wewe,… hakikisha unamfanyia mambo yote yanayostahiki kwa mtoto, itamsaidia sana yeye huko mbeleni kwenye maisha yake…na kama kutatokea tatizo usisite kutupigia simu..’akasema na wakaaga kuondoka.
‘Lakini lazima niwape kitu kidogo…’nikataka kuwapa pesa, wakakataa, na kusema;
‘Sisi tunarudi huko kijijini, na kuanza kazi za ujenzi, tunashukuru sana, kwani pamoja na hizo pesa tulizokulipa kwa ajili ya hicho kiwanja, lakini fadhila zitakazopatikana kwa ajili ya nyumba hiyo ya ibada zitakusaidia hata wewe na familia yako huko mbele…ukumbuke ukitoa kwa jili ya mwenyezimungu utarajie malipo makubwa sana, hiyo ni akiba yako endelevu, hata ukiwa haupo hai… na hebu fikiria hiyo nyumba ya ibada itadumu muda gani,..na kila siku utakuwa unapata fadhila kiasi gani…umefanya jambo la maana sana…’wakasema
‘Nashukuruni sana, nawashukuruni sijui niwalipe nini, chukue hii sadaka yangu basi…’nikasema, na wao wakasema sio kwa wakati huu kwani itakuwa nimetoa kwa ajili ya hayo waliyoyafanya
‘Usijali…kwani hutakiwi utulipe chochote, ..sisi kazi yetu ndio hii ya kuitangaza dini, na kwa hili umetusaidia sana kwani tutakuwa na sehemu yetu ya kudumu…kwa ajili ya ibada na ofisi ya mambo ya kidini…’wakasema na baadae wakaaga na kuondoka.
Hutaamini baada ya tendo hilo , nilihisi kamaa nimepunguziwa mzigo tumboni, awali nilikuwa kama nimebeba mzigo mzito ambao unahisi unataka kudondoka, lakini baada ya hapo, japokuwa nina kitu tumboni lakini sio kama vile awali, na ile hali ya kusikia vibaya, ikawa imekwisha kabisa,..
Baada ya miezi kutimia nilifikishwa hospitalini, nasema nilifikishwa kwa maana hali hiyo ilinianzia nikiwa nyumbani, na kiukweli, nilipofika hospitalini haikuchukua muda, nikajifungua salama, japokuwa mtoto alitoka akiwa sehemu kubwa ya mwili haina ngozi, ni kama mtu aliyeungua, docta wakasema ni udhaifu tu wa ngozi tu itaisha…
Basi mimi nikafuatilia masharti yote ya jinsi mtoto akizaliwa anatakiwa kufanyiwa kidini, na siku baada ya siku,..hali ya mtoto ikawa inakuwa vyema, ngozi inarejea, kunabakia makovu ya kawaida tu..namshukuru mungu sana, kwani hadi sasa kama unavyomuona ngozi yake inakuwa kama ya kawaida, ni alama alama zinabakia tu.., na mtoto mwenyewe ndio huyu hapa..’akasema huku akinionyeshea mtoto wake.
‘Mhh..hongera..tena mtoto ana afya nzuri kabisa, sijui kwanini walisema hivyo, kuwa atakuwa sio kiumbe wa kawaida, mbona ni mtoto mnzuri kabisa, imani za shirkiii mbaya sana…’nikasema na hakunijibu hiyo hongera yeye akasema;
‘ Unajua nilijiuliza sana , nilijiuliza tu,…hivi kweli duwa la kuku halimpati mwewe..’akasema
‘Kwanini ukajiuliza hivyo…na wewe umeliona hilo kivitendo.au sio…wale waliojifanya wao ni zaidi ya wengine, wanaweza kuingia majumba ya watu wakafanya wapendavyo, mbona wameshindwa kupambana na hayo yaliyowakuta…kwahiyo hiyo kauli ilikuwa ya kuwaasa hao watu au sio..?’ nikasema
‘Mhh…kiukweli, mimi sijui, ila najua kuwa msemo huo ulitolewa kwa maana fulani maana wazee wetu walikuwa an hekima sana…ila nimeamini kuwa, masikini silaha yake kubwa ni duwaa, ni maombi kwa mola wake, na muhimu wakati unafanya hivyo uwe na moyo safi, usiwe na hasira za visasi, chuki kwa wengine…mimi hilo nimelithibitisha kwa vitendo..’akasema.
‘Hata hivyo,..kila hali ina mitihani yake, umasikini una mitihani yake mingi tu..kama ulivyo utajiri, na ili uweze kuishinda hiyo mitihani,…yabidi uikubali hiyo hali, lakini usijipweteke, upambane na mazingira, utafute hukio ukiwa huna kinyongo na mtu, na hata ukitendewa mabaya, usikimbilie kulipiza kisasi, kwa njia za uovu, …’akawa anasimama kutaka kuondoka.
‘Ni kweli, lakini kwa walimwengu, sizani kama atakubali atendewe ovu akae kimia tu…wengi tunakimbilia visasi tena wati mwingine hata huna uhakika na hilo jambo…ndio hulka zetu…’nikasema
‘Kwa ushauri wangu, kama wewe ni mnyonge utafanyaje sasa,..kuliko kuingia kwenye shiriki, kwanini tusimuombe mola wetu atusaidie…na wakati unafanya hivyo usiwalipizie maombo mabaya hayo waovu wako, moyoni wasamehe na ufanye hivyo kwa imani thabiti…imani hiyo thabiti ndio inageuka kuwa silaha ya mnyonge… hutaamini hapa nipo hivi, unaniona bado nipo kama hohe hahe, lakini sio kwamba mimi ni masikini tena,..hapana..’akatabasamu kidogo.
‘Umepata utajiri, kutokana na kile kiwanja au…?’ nikamuuliza
‘Hiyo ilikuwa miongoni mwa neema alizokuja kunipatia mola wangu,…hapa najibana tu, ili niweze kujiajiri, kuna mipango inakamilika,…maana nilikutana na wataalamu wa ujasiriamali wakanielekeza na kunisaidia jinsi gani ya kuwekeza, kile nilichojaliwa nacho, na ikibid nichukue mkopo kidogo niongezee, nimefanya hivyo,…
‘Na..ni… hatua kwa hatua, lakini najua sio kazi rahisi, inabidi nipambane kweli, maana mtoto huyu anakua, atahitajia kusoma, sitaki itokee sababu, watu waseme uliambiwa…ni staki nirudie makosa ya nyuma, siwalaumu wazazi wangu, lakini sitaki niwe kama wao..na sitaki mtoto wangu aishie kama mimi nataka yeye awe zaidi ya mimi, na, elimi ndiyo itakayomuokoa huyu mtoto…. nina imani baada ya hapa nitaweza kumiliki duka la vifaa..mbali mbali, na huyu mtoto atakuja kuyafuta machozi yangu….’akasema akitabasamu.
‘Mashallah…hongera sana, nakuombea kila la heri….’nikasema na sasa akawa anataka kuondoka, nikakumbuka kitu na kumuuliza
‘Vipi kuhusu ile familia ya wafadhili wako..iliishia wapi?’ nikamuuliza
‘Ile familia ya wafadhili wangu sasa hivi imeshakuwa kitu kimoja, baada ya wazazi wao kuwapatia idhini, sasa wana mabadiliko makubwa sana,..ndio hapo nimeamini kuwa wazazi ni kitu kingine…na hutaamini, kijana na baba yake wote walipona, hebu utajua mwenyewe waliponaje, …mola kawafungulia njia…nashukuru sana kwa hilo, na mimi wamenifanya kama mwanafamilia wao, ila sikutaka kuwa karibu sana na wao, nimeamua kuhangaika kivyangu, japo mwanzo mgumu…, ila kila mara nikipata muda nakwenda kuwatembelea…naomba niishie hapa, natumai nimewakilisha..’akasema
NB: Huu ndio mwisho wa kisa hiki. Nawashukuru mliokifuatilia, najua wengi walitaka kiishe haraka wengine kivile, lakini hivi ndivyo ilikuwa ,…tuzidi kuwa pamoja, na mwisho wa kisa hiki ni mwanzo wa kisa kingine,….CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MWISHO
WAZO LA LEO: Hivi kweli duwa la kuku halimpati mwewe, hii ni kauli ya kuwaasa wale wenye uwezo, wale waliopo kwenye madaraka na hawafuati maadili ya uongozi, wale ambao wanajiona wanaweza kufanya wapendavyo, kwa wengine, wao ni taifa kubwa, wanaweza kuwadhibiti wengine na wengine hawana nafasi , hata wakionewa, hawawezi kufanyiwa jambo lolote, ndio wao kwa kiburi wanasema duwa la kuku halimpati mwewe….hivi ni kweli halimpati mwewe?..., duwa la mnyonge huenda moja kwa moja kwa muumba, na malipizo yake yanaweza yasiwe ya haraka, mola mwenyewe anajua ni kwa vipi…
0 comments:
Post a Comment