Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

DUWA LA KUKU - 3

 







    Simulizi : Duwa La Kuku

    Sehemu Ya Pili (2)



    Wewe binti uliwahi kuniona nikiingia chumbani kwako usiku…?’



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Hapana….’ akasema



    Binti wa nyumbani akaulizwa na kuambiwa aseme ukweli, yeye akasema hakuwahi kumuona baba mwenye nyumba akiingia ndani , maana yeye huwa anakuwa na usingizi mnzito, japokuwa anakabwa na majinamizi….



    Ushahidi huo ukaonekana hauna mshiko…na baba mwenye nyumba akapendekeza yule binti mwingine aitwe, ili atoe ushahidi, mimi niliona ni ajabu , kwanini baba mwenye nyumba awe anajiamini hivyo, inawezekana kweli hahusiki na hizo shutuma, lakini mama mwenye nyumba anadai ana video inayoonyesha tukio zima.



    Tuendelee na kisa chetu….



    ***************

    ‘Huyu binti mwingine kakataa kuja, lakini sio kitu, tunaweza kuangalia shahidi mwingine, eti mke wangu.. tumuulize nani tena…au, labda kijana wetu , kama na yeye anaweza kuwa shahidi wako…’akasema baba mwenye nyumba,



    ‘Hapana, ….’akasema mama mwenye nyumba, na kuwafanya watu pale kushikwa na mshangao.



    ‘Kwanini hutaji kijana wako akahojiwa, yeye aliwahi kuingia ndani, au sio, yeye alikuwa karibu na huyu binti, na huyo aliyekuwepo hapa kabla, basi huenda kuna jambo analifahamu ,…’akasema kiongozi wa dini.



    ‘Sitaki kumuingiza mtoto wangu kwenye maswala haya ya kikubwa, nina uhakika hahusiki ni ujanja ujanja wa baba yake tu….’akasema mama mwenye nyumba.



    ‘Basi ngoja nihakiki jambo kwa huyu binti wa sasa kwanza, nataka nikuulize maswali tena machache…’akasema kiongozi wa dini akimuangalia huyo binti….na baadae akaanza kumuhoji…

    .

    'Mama amesema kuna siku alikukuta umepoteza faham chumbani kwake, ulikuwa ukifanya usafi au sio…?’ akaulizwa,



    'Ndio…nilikuwa nfanya usafi nikagundua barua, nilipoisoma ndio nikapoteza fahamu…’akasema.



    'Baba mwenye nyumba anasema alikufanyia huduma ya kwanza, ambayo ndio ilimfanya mama mwenye nyumba amuhisi mumewe vibaya…kwa maelezo niliyopewa, je kwa muda wote wakati baba mwenye nyumba anakufanyia huduma ya kwanza ulikuwa huelewi hicho anachokufanyia..?’ akaulizwa.



    'Ndio, nilikuwa sielewi kabisa..…wala sijui alinifanyia nini,….’akasema.



    'Sasa kwanini ulipozindukana ukakimbia…?’ akaulizwa



    'Nilihisi anataka kunizalilisha..kwa vile …hata sijui, unajua mwanaume awe amekukalia juu hivi.., …inatisha, ndio maana nikakimbia….’akasema.



    'Alikukalia juu kwa vipi…?’ akaulizwa



    ‘Alikuwa kapiga magoti, na kuniinamia, uso wake ulikuwa karibu na uso wangu, …ndivyo nilivyoona hivyo, na sikuelewa anataka kufanya nini, ..wazo lililonijia haraka ni labda alikuwa anataka kunifanyia kitu kibaya….’akasema.



    ‘Sasa kwanini uhisi hivyo, wakati huyo ni baba yako, ni sawa na baba yako…?’ akaulizwa.



    'Kwa jinsi alivyokuwa kaniinamia…siweza kuwazia jambo jingine zaidi ya hilo, hata sijui kwanini niliwazia hivyo….’akasema.



    'Yaonyesha humuamini baba yako, ..au kuna kitu kiliwahi kukutokea mpaka ukaogopa au?’ akaulizwa.



    'Wanaume wote mimi siwaamini, mama aliniusia hivyo..anasema nisipende kuwa karibu nao kihivyo, maana ibilisi ni mkali ukiwa nao karibu na wao hawawezi kujizuia, kuingiwa na ushawishi mbaya…’akasema.



    'Sio kwasababu ya hayo yaliyotokea humo ndani, au kuna jambo liliwahi kukutokea, la kukutia mashaka..?’ akaulizwa.



    'Zaidi ni hayo majinamizi tu ..mmh, hakuna jambo lilinitokea,…mmmh, mimi sikumbuki zaidi….., ni hisia zilinijia tu hivyo…’akasema.



    'Unahisi labda kuna mtu humu ndani anaweza kuhusika na hayo majinamizi au unaamini ni ndoto tu, au kuna mashetani…?’ akaulizwa.



    'Hapana, sitakiwi kumuhisi mtu vibaya, na sijui nini, mashetani, hapan, mimi siyajui hayo, …kiukweli mimi sijawahi kutokea na vitu kama hivyo, nasikiaga kuna ndoto za majinamizi ,na dalili zake ni kama hizo, ..hivyo tu…’akasema.



    'Chumba chako kipo karibu na kijana, na kijana anasema, mara nyingi amekusikia ukipiga kelele, je na yeye hujawahi kumuona akiingia chumbani kwako  usiku ukiwa umelala..?’ akaulizwa.



    'Mhh, hapana, ..awali nilipofika kwenye nyumba hii, ndio yeye alikuwa akinielekeza mambo mengi ya humu ndani, kazi nk…ndio aliwahi kufika siku usiku siku za awali nilipoanza kazi… , nilipofungua macho, nikamuuliza nini kimetokea, amefuata nini ….akasema kanisikia nikipiga kelele, lakini haijatokea tena mimi kumuona akiingia ndani usiku…’akasema.



    'Huhisi kuwa anaweza kuwa ndio yeye anayekufanyia hivyo usiku…?’ akauliza.



    'Siwezi kumuhisi mtu yoyote vibaya, kama hajanifanyia, na kuhakikisha kuwa ndio yeye, kwangu mimi hayo yote nayaona kama ilikuwa ni ndoto tu…’akasema.



    'Sasa ikitokea baya mfano umepata mimba utasemaje..nasema hili kwa vile umesikia mwenzako aliyekuwa hapa awali ilimtokea kama hivyo, akajikuta ana mimba…?’ akaulizwa.



    'Mimba!... nitapataje hiyo mimba, hapana kwani ndoto  inaweza kumpatisha mtu mimba!, mmhh, mimi hata sijui...mimba mungu wangu! , iingiaje hiyo mimba....hata sijui…’nikasema sasa nikionyesha mashaka.



     'Ndio hivyo, usiposema ukweli, usije kumlaumu mtu , utafukuzwa humu ndani, na hakuna wa kukusaidia tena….’akaambiwa



    'Sasa mlitaka mimi niseme nini zaidi, maana hivyo nilivyosema ndivyo nijuavyo, kama kuna zaidi mimi  namuachia mungu.

    ***************



    ‘Ngoja nimjaribu tena huyu binti mwingine labda aliogopa kupokea simu kwa vile yupo na mabosi wake….’akasema baba mwenye nyumba na kuanza kupiga simu tena, na safari hii binti akapokea na wakaanza kuongea na baba mwenye nyumba. Baba mwenye nyumba akaweka spika ya nje ili kila mtu asikie anachoongea na huyo binti, hakutaka ionekane kampanga huyo binti aje kuongea atakavyo yeye.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ‘Samahani unaweza kufika hapa nyumbani mara moja…?’ akasema.



    ‘Nije kufanya nini, mizigo yangu nimeshaichukua, mimi siwezi kufika hapo nyumbani kwenu tena…’akasema.



     ‘Kwanini, ..hakuna tatizo lolote baya,  muhimu kuna kitu tunataka kukuuliza, tunakuomba tafadhali…’akasema na huyo binti hakujibu kitu akakata simu.



    ‘Siwezi kuja,….kwanza bosi wangu hataki niwe ninatoka toka ovyo, …’akasema



    ‘Basi tuongee hapa kwenye simu , tukuulize maswali mawili matatu utusadie….’akaambiwa



    ‘Hapana hata hivyo nimetoka nje kidogo simu ilipoita…, nasubiriwa ndani kuna kazi nafanya, kwaheri….’akakata simu.



    ‘Huyu bint naona hatuwezi kumpata kwa hivi sasa, nilitaka na yeye aje hapa ili aweze kuthibitisha hili, kwa kauli yake, ili tuyamalize haya mambo kwa amani, nitafurahi turejee maisha yetu ya kawaida, …’akasema baba mwenye nyumba.



    ‘Kwa hali kama hii sizani kama hilo litawezekana tena….’akasema mama mwenye nyumba.



    ‘Kwanini mke wangu, mbona hujaamini hilo, niamini mke wangu…unajua wewe ni hisia zako tu, lakini kiukweli sivyo hivyo kabisa, je uliwahi kuingia ndani ukaniona nikifanya lolote baya,..hujawahi, na mengine yote ni hisia zako tu….’akasema.



    ‘Tatizo lako, unajifanya mjanja sana, unaniona mimi sina akili, mimi sijui hawa mbinti umewapa nini,…hata sijui…na huyu binti angelisema ukweli, lakini nahisi kuna kitu umewafanyia, mpaka wanaogopa kusema ukweli,na huo usiku kuna kitu unawafanyia mpaka wanashindwa kuamuka,…’akasema mkewe.



    ‘Sasa huko nikunisingiziana uchawi, mimi nifawafanyie nini, na kwa ajili gani, kuna raha gani hapo…mke wangu, hivi na umri huu ninaweza kuanya kitu kama hicho…’akasema.



    ‘Sio uchawi, sio lazima uchawi, ila kuna jambo uliwafanyia hawa mabinti, haiwezekani itokee siku zote washindwe kuzindukana, na mimi mwenyewe nilikuona ukiingia huko chumbani kwao, …’akasema mama mwenye nyumba na kiongozi wao wa dini, akasema;



    ‘In maana uliwahi kumfuatilia, akienda huko chumbani kwa hao mabinti, hebu hapo kidogo, tuelezee ulivyomfuatilia na kumuona akiingia huko chumbani kwao na je ilitokea hivyo kwa mabinti wote wawili..?’ akaulizwa.



    ‘Siku ya kwanza, nilipoanza kumshuku, …’akasema huku akimuangalia mume wake.

    ************

    ‘Ilikuwa ni usiku, ghafla nikashtuka kutoka usingizi, nikajiona nipo peke yangu, nikajua mwenzangu labda kaenda kujisaidia, nikasubiria kama nusu saa sikumuona mwenzangu akitokea, nikaamuka na kuanza kumtafuta chooni, alikuwa hayupo, hapo nikaingiwa na mshaka, huyu mtu kaenda wapi..sikuwa na wazo jingine zaidi ya kuwa, labda katoka nje kuna tatizo.



    ‘Nikataka kuelekea nje, lakini wazo likanijia huenda kuna tatizo chumbani kwa huyo binti, maana tatizo hilo nilishalisikia kutoka kwa mtoto wangu, kuwa huyo binti huwa anapiga kelele usiku,…wazo hilo liliponijia nikaelekea huko chumbani kwa huyo binti….’akatulia



    ‘Wakati natoka sasa kuelekea huko, nikamuona mume wangu akitokea chumbani kwa huyo binti, na mimi kwa haraka nikajificha na kumuacha apite,..hakuniona, aknipita  na aliponipita tu mimi nikamfuata kwa nyuma hadi chumbani, yeye akapanda kitandani kulala, na kuanza kukoroma, kama vile hakujatokea kitu…’akasema.



    ‘Hukumuuliza kwa muda huo..?’ akaulizwa.



    ‘Hapana, sikumuuliza usiku huo, nilimuuliza asubuhi yake, na nikashangaa, akikataa kuwa hakutenda hivyo, nikaona ajabu sana, kwanini akatae, nilipombana sana, akasema, huenda alisikia sauti, maana huyo binti wakati mwingine huwa anapiga makelele, na aliposikia sauti za ukelele,ndio akaenda huko, kuangalia kuna nini,,….’akasema.



    ‘Sasa kwanini nimekuuliza mara ya kwanza ukakataa kuwa hukufanya hivyo…?’ nikamuuliza.



    ‘Aaah, unajua kichwa changu kina mambo mengi, nikiamuaka asubuhi huwa nawazia mambo ya kazini, nisamehe tu mke wangu….’akaniambia hivyo.



    Kiongozi wa dini, akauliza swali jingine;

    ‘Na huyo binti ulipomuuliza na yeye  alisema nini..?’ akaulizwa.



    ‘Alisema hajui…maana alikuwa amelala, ila ni kweli yeye aliendelea kuota kukabwa,….na hajui zaidi…basi kwa vile sikuwa na mashaka sana siki hiyo,  sikutaka kudadisi zaidi, na hiyo ilikuwa siku ya kwanza kugundua hayo mambo kutoka kwa mume wangu, kuwa huwa usiku ana tabia ya kuelekea huko kwenye chumba cha mabinti…’akasema.



    ‘Je kuna siku nyingine ilitokea hivyo, na ilitokeaje, maana umesema hukuwa na wasiwasi na tukio hilo…?’ akaulizwa.



    ‘Kiukweli japokuwa sikuwa na wasi wasi na tukio hilo , lakini siku zilizofuatia niliamua kulala kwa kuvizia ili kama nitamuona mume wangu akitoka nimfuatie, au nikisikia kelele kwa huyo binti, mimi sasa ndio niende huko badala ya mume wangu…, lakini hutaamini, nikawa nashikwa na usingizi mnzito, najikuta nazindukana kukiwa ni asubuhi….’akasema.



    ‘Kwahiyo hukuwahi kumfuatilia na kumfumania mumeo wako, kama ni hivyo kumbe hisia zako ni za kuhisi tu, sio kweli kuwa uliwahi kumfamania mume wako..?’ akaulizwa.



    ‘Ipo siku moja, nilizindukana kama hivyo hivyo tena,…na nikakuta mume wangu hayupo kitandani, nikasema sasa nitaweza kuhakiki jambo hilo , kama sijachelewa…akilini sio kwamba nilikuwa simuamini mume angu, lakini kutokana na kisa cha mfanyakazi wa awali na yaliyotokea kwake, na tukio hilo lililotokea humo ndani kipindi hiki, nikawa naanza kujenga hisia hizo,…’akatulia.



    ‘Basi kwa haraka nikaamuka na kuelekea huko chumbani kwa binti, ni kweli kumbe alikuwa keshaingia huko ndani, ..nilipofika mlangoni, nikasikia kelele za kulalamika….’akatulia.



    ‘Sauti ya nani anayelalamika….?’ Akaulizwa



    ‘Nahisi ilikuwa ni ya binti,..sikuwa na uhakika sana… ni kama mtu anayeongea akiwa usingizi, ..’sitaki, mimi sitaki…niach, sitaki,…’.vitu kama hivyo…niliposikia sauti kama hiyo nguvu zikaniishia,…nikataka kufungua mlango,…nithibitishe huo ukweli, maana hapo akili ilikuwa kama sio yangu tena,..kwanini asema sitaki, niache, …ina maana kuna mtu kweli anataka kufanya kitu kibaya kwa huyo binti,na ni nani zaidi ya mume wangu…kwa haraka kwa hasira nikataka kufungua mlango,  na ile nashika kitasa, cha mlango, mlango ukafunguliwa kwa haraka…akatokea mtu…’akatulia .



    ‘Ni nani…mume wako…?’ akauliza.



    ‘Hapana alikuwa ni kijana wangu…!’akasema, na watu wakaonyesha uso wa mshangao.



    ‘Oh, kijana wako tena….?’ Akaulizwa na huyo kiongozi.



    ‘Ndio, kijana wangu, na aliponiona akanishika mkono na kuvuta pembeni, akaniambia…’



    ‘Huyo binti anapiga ukelele, na baba yupo ndani, anajaribu kumsaidia….’akasema.



    ‘Oh, mimi nikataka kwenda huko, ili nikasaidie, lakini kwa mshangao  kijana wangu akanizuia na kusema;



    ‘Hapana mama usiende huko, baba aliwahi kuniambia awali, kuwa mtu akiota ndoto kama hizo haitakiwi kumshtua, na akizindukana akiona watu ni wengi wamemjalia, mtu kam huyo anaweza kushikwa na presha, ..basi mimi nilipomuona baba yupo huko ndani, sikutaka kuwasumbua hata baba hajui kuwa nimefika huko na kuwaona, ….’akasema.



    ‘Umewaonaje..?’ nikamuuliza hivyo tu.



    ‘Baba alikuwa akijaribu kumtikisa kidogo huyo binti ili aweze kuamuke, lakini huyo binti alikuwa bado anaendelea kupiga kelele, anagala gala tu,…’akasema.



    ‘Kelele gani..?’ nikamuulizaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Kama anakabwa, anasema sitaki, niachie,…lakini sauti haitoki vizuri, ..kama yakujiuma uma …’akasema, na wakati tunaongea mara mume wangu akatokea huko ndani, na kuelekea chumbani, mimi nikamfuatilia hadi chumbani, na kumkuta ameshalala fofo…, ..kiukweli siku hiyo sikuwa na amani, kwasababu kumbe hata kijana wangu analijua hilo.



    ‘Ulipomuuliza kesho yake alisemaje?



    ‘Kama kawaida yake alidai kama ni kweli basi alikwenda huko, aliposikia kelele, na madhumuni ni kuangalia kuna nini kinachomfanya huyo binti apige makelele,…’akasema.



    ‘Alitamka  hivyo….’kama ni kweli,…’ kwanini asema hivyo, kama ni kweli….?’ Akaulizwa.



    ‘Ndio alitamka hivyo…, hata mimi nikajiuliza kwanini anasema hivyo, kama ni kweli, ina maana hakumbuki, ina maana gani, nikawa najiuliza sana, ndio nikajiwa na wazo hilo la kuweka video ya kurekodi matukio huko chumbani, nione ni nini kinachotokea maana kufuatilia usiku ilishindikana,kwasababu ya usingizi,..huwa mara zote nilizopanga nifuatilie, najikuta nimelala usingizi mnzito…’akasema.



    ‘Ukafanikiwa kufanya hivyo….?’ Akaulizwa.



    ‘Ndio..nilifanikiwa video ilichukua picha vizuri sana…japokuwa, ..kuna …mapungufu fulani, lakini nilichotaka kukiona nilikiona, kwa uwazi zaidi hawezi kukataa akiiona hii video….’akasema.



    ‘Muongo, …hiyo kanda ya video, itakuwa imetengezwa huko mitaani, sio kweli kabisa, je ilionyesha nini, kuwa mimi ndiye ninayewakaba hao mabint…?’ akauliza.



    ‘Ni zaidi ya kuwakaba,……ulikuwa unawazalilisha hao mabinti, kwa ushahid huu hapa…’akasema mama mwenye nyumba,a kionyesha hiyo kanda ya video alioyokuwa nayo.



    ‘Sikubaliani na hilo kabisa, na kwasabau hiyo itabidi uionyeshe hiyo kanda ya video, tuhakikishe, …siwezi kufanya lolote zaidi ya kuwakagua na kumtikisa tikisa ili azindukane….’akasema.



    ‘Sio kweli..nimeona kwa macho yangu ulichokifanya kwa huyo binti…, ni aibu mume wangu, sikupenda kulisema hili, au kulionyesha,  lakini sasa umenichefua, unataka nionekane mimi ni muongo, mbele ya wazazi wangu hawa,  wakati ni kweli….’akasema.



    ‘Mimi nipo tayari niione hiyo video,…ionyeshe….’akasema mume wake na mkewe akamuangalia kwa uso wa mshangao, na kusema;



    ‘Wewe…unataka nionyeshe huo uchafu wako mbele ya wazazi hawa,….’akasema mke wake.



    ‘Mimi najua hakuna kitu kama hicho ndio maana nataka uionyeshe, sijwahi kufanya kama anavyotamka yeye, ni uwongo mtupu,….’ Akasema.



    ‘Una uhakika kuwa kanda hiyo ya video inaonyesha kila kitu, ambacho kinadhihirisha kuwa mume wako ndiye anayafanya hayo…?’ akaulizwa



    ‘Ndio…niliiangalia mimi mwenyewe, nikarududia tena na tena….kiukweli baada ya kuiona hiyo kanda ya video, nikasema basi, ….yale mapenzi niliyokuwa nayo kwake, yakaondoka, na ikabakia chuki, nasema ukweli huo,chuki, sasa haivi namchukia huyu mwanaume …sizani kama hali hiyo ya zamani itarejea tena, sizani….’akasema.



    ‘Aonyeshe, …kama anavyodai ni kweli, aonyeshe, maana mimi sijafanya hivyo…, lini jamani, …hapana, huo ni uwongo,mke wangu una uhakika na hilo…usiseme kwa kujifurahisha, na usije ukadanganywa na mashoga kuwa utengeze kitu kama hicho ili kunizalilisha, …samahani sana, mke wangu kwa hilo mimi sikuamini….’akasema na wajumbe pale wakaangaliana, na ilikuwa kama hawakupendelea hilo tendo lifanyike, na mkuu wa dini, akauliza.



    ‘Je kama ikionekana ni kweli, utasemaje ..?’ akaulizwa baba mwenye nyumba.



    ‘Hakuna kitu kama hicho….sio kweli,…labda iwe ni ya kugushi, lakini kama ni kweli, ilichukua matukio ya ndani, mimi nina uhakika sikuwahi kufanya kitu kama hicho, …jamani mimi nimechanganyikiwa, hapana, mke wangu, tafadhali sema ukweli….’akasema jamaa.



     ‘Wewe unampenda mke wako?’ akaulizwa na kwanza akamuangalia mkuu huyo kwa mshangao, halafu akasema;



    ‘Sana tu, nampenda sana mke wangu, ni yeye tu na dhana zake potofu…’akasema na wazee na mkuu wa dini wakaangaliana na mkuu wa dini akamuuliza mke mtu.



    ‘Wewe unampenda mume wako..?’ akamuuliza.



    ‘Nimeshasema awali, mume wangu nilimpenda sana, na ningeendelea kumpenda, kama angekiri kuwa ana tatizo, lililomsukuma hadi kufanya tendo hilo, maana hata ukiangalia hiyo video, ni kama analazimishwa, …anakuwa kama sio yeye….’akasema

    ‘Mimi kwa uni wangu, naona sio vizuri kuonyesha kitu kama hicho mbele ya watu, lakini kama mume mtu unazidi kukataa, na mke unaona huo ndio ushahidi wako, basi hatuna jinsi, ila kwa ushauri wangu,..baba mkwe utuwie radhi, mimi na baba yake tutaangalia, na kama ni kweli tutakuthibitishieni huo ukweli…’akasema hivyo.



    ‘Sawa, ni vyema…’akasema baba mkwe.



    ‘Aaah, kwanini, mimi nataka wote tuone, ili tubainishe uwongo, mimi najua jinsi gani watu wanavyogushi video, wanachukua mapicha ya watu wengine wanawekeza vichwa, kwenye mapicha hayo,…nataka nije kumuumbua mke wangu,…’akasema baba mtu kwa kujiamini.



    ‘Hapana, ….mimi na huyu mfanyakazi wenu wa kazi za ndani tutatoka nje…’akasema na wakati wanajiandaa kutoka, mara mlango ukagongwa, na aliyeingia alikuwa yule bint wa kazi wa zamani



    ‘Mimi nimekuja kufuata muito wenu….’akasema



    ‘Oh karibu lakini tunakuomba usibirie nje kidogo…’akaambiwa.



    ‘Hapana mimi sina muda zaidi, ila nataka niseme ukweli, nimeona siwi na amani…’akasema.



    ‘Ukweli gani..?’ akaulizwa



    NB: Bint anataka kumwaga radhi, au kuna jingine





    WAZO LA LEO: Mwanadamu ana staha zake, ndio maana sehemu zake nyingine zinaitwa za siri, sio vyema kudhihirisha viungo hivyo vya siri kwa kila mtu, kwa kufanya hivyo unakiuka haki za binadamu. Wengi wamekuwa wakipiga picha za wengine na kuzituma mitandaoni, sio vizuri jamani,…Mwenyezimungu katuwekea mipaka, ya maumbile yetu..kuwa ni nani na nani wanatakiwa kuonana maumbile yao ya siri. Na kuyadhihirisha maumbile ya siri ya watu wengine huko ni kuzalilishana ni dhambi kubwa sana, tutakuja kuulizwa madhambi hayo siku hiyo ya hukumu, kwa kuwakosea wanadamu wenzetu…. Tuweni makini jamani.



    ‘Najua mumekusanyika hapa kuhusu yanayotokea humu ndani, najua nyote mtakuwa mumeninyoshea kidole mimi, kutokana na tuhuma za huyo mtoto wenu kuwa mimi ni …mchawi au namini ushirikina, najua kuna mengo mnataka kusikia kutoka kwangu…’akaanza kuongea huyo binti.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Tunachokitaka kutoka kwako ni ukweli, je hayo yanayosemwa ni kweli…?’ akaulizwa



    ‘Yapi hayo....kuwa mimi ni mshirikina, kuwa labda nimemfanyia kitu mtu humu ndani, au si ndio hivyo,..?’ akauliza.



    ‘Hapana sisi hatuna maana hiyo, labda utulie tukuulize maswali utujibu kwa ukweli unavyoujua wewe…’akaambiwa.



    ‘Mimi nimekuja kuusema ukweli... ili niwahi kazini kwangu, najua labda itakuwa ni hatari kwangu, lakini sina jinsi, kutokana na wema niliotendewa na hawa watu,...na.. labda nikiri kuwa kweli haya yanayotokea humu chanzo ni mimi…’akasema na watu wakamkodolea macho.



    ‘Tuelezee kwa vipi?



    ‘Ehee….ngoja nianze tokea awali ili mnielewe vyema japokuwa naogopa nitachelewa huko kwa mabosi zangu….’akasema.



    ‘Sawa endelea, kwa haraka kidogo, ili usichelewe….’akaambiwa.



    ‘Mimi nilifika kwenye nyumba hii, nikitokea mitaani,..' akaanza hivyo.



    'Huyu baba, ndiye alinikuta siku moja nikiwa na hali mbaya sana, nina njaa, naumwa, akanionea huruma, bada ya kunihoji hoji, …akaninunulia chakula na kunipeleka hospitalini. Huko nikalazwa,…nililazwa wiki hivi, na yeye alikuwa akija kunijilia hali na hata kuniletea chahakula…kiukweli niingiwa na faraja, na badala ya kufurahi nikawa nalia…’akatulia kidogo.



    ‘Kwanini sasa ulie..wakati mtu kajitolea kukusaidia…?’ akaulizwa.



    ‘Unajua huwezi kuelewa haya mpaka yakukute, nililia kwasababu nilijiuliza hivi sisi tulikosa nini, …ina maana na mimi nilitakiwa niwe na baba kama huyu, je yupo wapi huyo baba yangu, haya mama alifariki, lakini …..aah, sitaki nikumbuke, nililia kwakweli, na…namshukuru mungu…japokuwa sikuelelewa kwenye mazingira ya dini, lakini najua mungu yupo….’akatulia.



    ‘Ehe ikawaje…?’ akaulizwa.



    ‘Baada ya wiki hivi nikaambiwa nimepona, hapo nilitamani niwadanganye pale hospitalini kuwa sijapona ili niendelee kubakia hapo, ili niweze kupata chakula cha kupikwa sio cha kuokota majalalani…ili nilale kitandani, sio kulala kwenye maboksi, huku mbu ndio marafiki zako…ili..jamani msiombee maisha haya, nyie mliojaliwa kuwa na wazazi, mshukuru sana….’hapo akageuka kuangalia huku na kule kama anamtafuta mtu, na watu walibakia kimia.



    ‘Je utakwenda wapi ukitoka hapa..?’ akaniuliza huyu mfadhili wangu, alipofika na kusikia kuwa natakiwa kuruhusiwa nimeshapona.



    ‘Mimi sijui pa kwenda, sina wazazi, sina ndugu, …nyumbani kwangu ni mitaani tu…’nikasema na huyu mfadhili akaniangalia kwa jicho la huruma akasema;



    ‘Oh,… basi ngoja nitaongea na mke wangu tutaona jinsi gani ya kukusaidia…’akasema na aliondoka siku hiyo, akijua nitaruhusiwa, lakini nahisi alishindwa kunichukua moja kwa moja mpaka akaongee na mke wake…mimi nilibakia pale nikisubiria taratibu za hospitalini, ili niweze kuondoka na kurejea mitaani, na haikupita muda docta akaja akaniambia nipo huru kuondoka.



    ‘Nikiwa nimekata tamaa,…nikijua sasa ndio maisha yangu tena yameanza, mara nikaona gari likija, muda huo nimeshatoka nipo nje, napiga plani za wapi nianzie maana maisha yetu ilikuwa kuomba omba, …kutukunwa, na usiku ku…zalilishwa, tulishazoea hivyo.



    Gari likasimama, kumbe ni huyu baba wa watu, sasa alikuwa kaja na mke wake, wakaniuliza nimeambiwaje, nikawaambia, wao wakaenda kuongea na docta, kuona kuwa kila kitu kipo sawa, kama kuna dawa, au gharama yoyote, walipomalizana huko, wakaniambia niingie kwenye gari.



    Basi ndio wakanichukua kwenye gari lao hadi nyumbani kwao, ndio nikanza maisha ya kuishi kwenye nyumba, sisi makazi yetu yalikuwa mitaani, vichochoroni,…..mara ya kwanza naingia kwenye nyumba nzuri, bila kutukunwa, kwa kukaribishwa na kuulizwa nitakula nini..kwanini machozi yasinitoke, nililia sana..nililia mpaka wenyeji wangu wakashangaa, wakaniuliza nalilia nini tena.., na mimi niliwajibu tu;



    ‘Nyie acheni tu…nalia, nimemkumbuka mama yangu, ….’nilisema hivyo, wakajua ni hivyo, lakini sikuwa nalia kwasababu hiyo tu, nilikuwa nalia, nikijiuliza maswali mengi,…na sikuamini kuwa hata siku moja nitakuja kupata fadhila kama hizo, mungu awazidishie watu kama hawa wenye moyo wa upendo….’akasema na aliyeitikia amina alikuwa kiongozi wa dini.



    ‘Kiukweli nilifika kwa watu hawa nikiwa sina mbele wala nyuma, nilifika hapa mchafu sijui hata kuoga, nikaambiwa nikaoge, nikapewa nguo za kubadilisha,..nikafundishwa mambo mengi tu ya maisha,…japokuwa kiukweli mimi sio mvivu, kazi za ndani, kuosha vyombo kufagia, nilifundishwa na mama yangu, navijua sana, lakini yale maisha ya watu wenye uwezo, umeme…na vitu vya kisasa, nilikuwa sijui kuvitumia.



    Kwa haraka sana nikazoea maisha hayo mazuri, na unajua tena, ukitoka kwenye shida ukapata raha, mwili hubadilika kwa haraka sana…nikawa binti mrembo, watu , hasa wanaume wakawa wakiniangalia kwa macho ya tamaa,…sisemi haya nia mbaya, lakini ndivyo ilivyokuwa, hata wafadhili wangu waliniambia hivyo, kuwa mimi ni binti mrembo sana…mimi sijui…’akatulia.



    Kuna kipindi niliona mabadiliko kwa wafadhili wangu hasa kijana..hahaha, hivi yupo wapi, samahani kwa hilo, ila inabidi niseme tu, nilivyoona mimi, labda nimekosea lakini ndivyo ilivyokuwa, sio kama ilivyokuwa awali, nikaona macho ya aina yake, kwangu mimi niligundua ni macho ya namna gani,…maana mitaani, na maisha niliyoishi nilijifunza mambo mengi bado nikiwa na umri mdogo….’akatulia.



    ‘Ningelipenda huyu kijana wa humu ndani awepo ili nisije kuonekana mimi ni muongo maana mengi anayafahamu na aje kuyathibitisha haya nitakayoyasema, na ili baadae litakolotokea, maana ndicho kilichonisukuma hadi kuja hapa,…ili nisije kulaumiwa…’akasema.



     ‘Ehee, hebu muiteni huyo kijana…una maana huyu kijana wa humu ndani…?’ akaulizwa.



    ‘Ndio namuita kijana japokuwa kwa umri tupo sawa, tulizoea kumuita hivyo …’akasema huyo binti, na Kijana akaitwa, na huyo kijana alipoingia tu na kumuona huyo binti, akashikwa na mshtuko kidogo, halafu akasema.



    ‘Huyu mdada msimuamini kabisa, huyu mshikirina huyu…atawadanganya na kubadili badili maneno, mimi simuamini kamwe…’akasema huyo kijana.



    ‘Ndio maana nimekuja unionyeshe huo ushirikina wangu, hiyo kauli yako mimi siipendi, nakuambia kabisa……na nitaongea ukweli wote leo, …uukane sasa, hata yale uliyosema nisiseme nitasema yote,….mimi sio mshirikina kama unavyohisi wewe…,na kama unadai kuwa mimi ni mshirikina nataka unionyeshe huo ushirikina wangu la sivyo tutafikisha kubaya….’akasema huyo binti.



    ‘Aaah, wewe tulia, hayo hayana nafasi hapa endelea kuelezea historia yako ya kuishi humu ndani, ilitokea nini, unasema ulipoanza kupendeza kijana akaanza kukutamani, kwani humu ndani alikuwepo kijana peke yake wa kukutamani,  hebu tuambie hapo una maana gani…?’ akaulizwa.



    ‘Ni kweli, kwasababu kijana ndiye tulikuwa naye wakati mwingi, wengine walikuwa wakija na kuondoka, na hata baba alikuwa anaonekana usiku tu na siku za wikiendi, kwahiyo mtu niliyekuwa naye karibu alikuwa huyu kijana…kwani nadanganya, aseme yeye mwenyewe, huyu kijana maana yeye ndiye aliyenianza kunitongoza, nikamkatalia, akaanza kunifanyia vitimbwi, aseme ukweli…’akasema



    Kijana akawa kimia tu, hakusemi neno hapo, ila mama yake aliniangalia kwa macho ya hasira, akitaka kusema neno, lakini mdada huyo hakumpa nafasi akaendelea kuongea.

    .

    ‘Kijana huyu akaanza kunisemea kwa wazazi wake kuwa mimi usiku natoka kwenda kufanya uhawara, au huo ushirikina anaousema,..wakati hata siku moja sijawahi kufanya hivyo, kisa nimemkatalia.., …kwanini niende nje wakati wanaume wapo humu ndani,…eti, tena wenye pesa, lakini nikavumilia, na siku moja kijana akaanza visa vyake, muulizeni alinifanyia nini…’akasema.



    ‘Wewe elezea, alikufanyia nini…?’ akaulizwa



    ‘Alitaka kunibaka, nikapiga ukelele…’akasema



    ‘Mwongo huyu, …ananisingizia, hata siku moja sijawahi kufanya hivyo, yeye usiku alikuwa akifanya madawa yake, nikamfuma, akiwa nje uchi…si umetaka niseme ….na…siku anayosema nilitaka kumbaka alikuwa akipiga kelele, nikawa namshika, maana alikwua akigonga gonga,…’akasema kijana.



    ‘Hahaha…eti nikiwa nje uchi, wakati ni mambo yenu humu ndani,…. ndio yalinifanya nitoke nje, nikiwa sijitambui,…nimejikuta niko nje uchi,….na kama ningeliendelea kubakia humu , bila ya kwenda kuhangaikiwa sijui ingelikuwaje,…labda ningekuwa kichaa...kuna kitu kilikuwa kikiniingia kichwani nakuwa kama nimechanganyikiwa, navutwa kufanya mambo nisiyoweza kuyafanya nikiwa na akili zangu, nilikuwa sio mimi…’akasema.



    ‘Oh, kwahiyo…sio huyu kijana ni kitu kingine kilitokea kwako, ?’ akaulizwa.



    ‘Huyu kijana ana yake, lakini kiukweli mimi niliambiwa matatizo hayo yametoka huko kwetu, kuna watu wananitaka nirudi nyumbani…nikaolewe huko, kuna mjamaa mmoja anaogopewa sana huko, eti aliniona akanipenda, kipindi fulani nilikwenda huko, …wakati nimeshapendeza, nilipata ruhusa , na kwenda kuona asili yetu, nikiwa na rafiki yangu mmoja wa kutokea huko kijijini walipotokea wazazi wangu...’akatulia.



    ‘Akamuambia huyu rafiki yangu aniambie kuwa yeye anataka kunioa, mimi nikamkatalia, kwanza nilikuwa mdogo, japokuwa umbo langu, lipo hivi, naonekana mkubwa lakini sio sawa na umri wangu…’hapoa akatulia kwa muda kidogo.



    ‘Sasa ikawaje, ?’ akaulizwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ‘Nilimkataa, na ndipo akasema atanikomoa…na huyo rafiki yangu alinisihi nikubali, kwani nispokubali, huyo mtu anaweza kunifanyia vituko…mimi nikamwambia sitaki, na huko sitarudi tena, bai huyo jamaa akamwambia huyo rafiki yangu, atanifanyia mambo mpaka nitakubali, na huko ninapoishi wote watakoma ubishi, mpaka wanifukuze.



    ‘Mimi …nilikuja nikawaambia humu ndani, ndio wakaanza kuniita mimi mshirikina, hasa huyu kijana, mama aliniambia kama nina tabia hiyo ya kishirikina niache kabisa, lakini ujumbe niliufikisha…’akasema.



    ‘Kwahiyo ulimwambia mama kuhusu huyu mzee….?’ akaulizwa.



    ‘Kwanza nilimuambia huyu kijana maana ndiye nilikuwa karibu naye…’akasema



    ‘Kwanini ulikuwa karibu naye..?’ akaulizwa.



    ‘Nilianza kusema awali, kuwa nilianza kupendeza, na huyu kijana akawa aknitongoza, kila siku, kiukweli kama …isingelikuwa ni tofauti za hali, ningelisema nikubali, si nitaolewa kwenye nyumba ya watu wanaojiweza, lakini nafsi ilinisuta, nikamkatalai kata kata…sasa nilipopata taarifa hiyo ya huyo mzee, nikamwambia kijana.



    ‘Umenikataa mimi, sasa nenda kaolewa na wazee wa kijijini….’akaniambia.



    ‘Mimi siwezi kuolewa huko, na wala sitaki kuolewa,…’nikamwambia.



    ‘Ila kuna kitu nataka umwambie mama, huyo jamaa kasema nisipokubali kuolewa na yeye atanifanyaia kitu kibaya, na hata nyumba hii mtafanyiwa hivyo hivyo…’nilimuambia hivyo, na yeye akasema, huyo mzee hawezi, hayo ni mambo ya kishirikina, na neno hilo lilianzia hapo.



    ‘Na haikupita muda, huyo jamaa akanitembea usiku, nikiwa usingizini sijijui…’akasema.



    ‘Una maana gani hapo, kukutembea usiku, kwa vipi..?’ akaulizwa.



    ‘Kutokana na nilivyoambiwa, huyu jamaa ni mchawi, huko kijijini wanamfahamu sana, na akitaka jambo lake ni lazima alipate, kwahiyo alivyonitaka mimi na kukataa, ndio akawa anakuja usiku, humu ndani…’akatulia.



    ‘Unamuona..?’ akaulizwa.



    ‘Siku ya kwanza nilimuona, …lakini ni kama njozi, na akaniambia ..sasa nimekuja, wewe si hunitaki, sasa nitakufanyia mambo mabaya, mpaka ujute kuzaliwa….nikawa sijui nifanyeje, na akasema, yeye, nia yake ni kunioa, ila kwa vile sitaki, basi atawatumia watu wa humu ndani kunizalilisha….’akatulia.



    ‘Watu gani…?’ akaulizwa.



    ‘Baba na kijana…’akasema na watu hapo wakahema.



    ‘Ni kweli alifanya hivyo…?’ akaulizwa.



    ‘Hahaha, hivi hamuamini hayo…muulizeni mama aliona nini, aliniambia alimuona baba akija chumbani kwangu, mimi nilimkatalia kwasababu yaliyokuja kutokea baadae, mimi nilikuwa sioni, nakuwa kama nipo kwenye njozi,…siwezi kufanya lolote zaidi ya ufanyiwa hayo anayoyataka huyo mzee….’akasema.



    ‘Lakini uliambiwa, hujawahi kuona kwa macho yako…?’ akaulizwa.



    ‘Kiukweli hivyo vitendo, nafanyiwa, ila wanaonifanyia siwaoni, maana ninakuwa usingizini…’akasema.



    ‘Na sikuyajua hayo, mpaka nilipokuja kuambiwa…ila siku ya kwanza huyo mzee nilimuona kwenye njozi zangu, akiniambia kuwa atakuwa anakuja kila siku kunifanyia vitendo vibaya, na atawatumia watu wa humu ndani, kunizalilisha, huku yeye akiniangalia, na kunikaba….’akasema.



    ‘Kwahiyo ni kweli kuwa baba mwenye nyumba na kijana huwa wanakuja usiku na kukufanyia hivyo, bila hata yaw ewe kujua, …kuwaona..kujua unajua kwa vile uliambiwa, sio ila wanapokuja huwaoni kwa sura si ndio hivyo..?’ akaulizwa.



    ‘Ndio wanakuja, muulizeni hata mama aliwahi kwuafuatilia akawaona, anasema ana ushahidi wa kuonyesha hayo, mimi kiukweli sijawahi kuwaona ila nakabwa, ..na kuhisi nazalilishwa, na watu nikiwa kwenye ndoto..ni kama ndoto…’akasema



     ‘Unasema nini wewe…?’ aliyeuliza sasa ni baba mwenye nyumba.



    ‘Nasema nilivyoambiwa, na yanayonikuta,…huyo jamaa lengo lake ni kunikomoa, unielewe hapa, ndio maana nimesema sasa nataka kuufichua ukweli, sasa iwe ni kazi kwenu…kama mtahangaika sawa, kama mtakaa kimia sawa, ila kama msipohangaika ndoa yenu itakuwa matatani, ndivyo alivyoahidi kwani alitaka kunioa na nyie mlinishauri nikatae…’akasema.



    ‘Kwani wewe ulimwambi ahivyo, kuwa umeshauriwa na wafadhili wako usikubali....?' akaulizwa



    'Hata, sijaongea naye, unajua yeye mara nyingi alikuwa akiongea na huyo rafiki yangu sio mimi, sasa sijui alifahamuje hivyo...siwezi kujua,...'akasema



    'Kwahiyo kwa kifupi, haya yote yanayotokea humu ndani kumbe kisa ni wewe?’ akulizwa.



    ‘Kisa ni mimi ndio, kama nilivyoambiwa,….ndio maana nimekuja kuwaambia, ili isje kujulikana baadae mkaniona mimi ni mbaya, au kama anavyoniita huyo kijana kuwa mimi ni mshirikina,…na nilimuambia mama, yeye hakuniamini, na wakafanya mbinu niondoke humu, wakijua nikiondoka huenda mambo hayo yataisha,… lakini huyu mtu alishasema atawakomoa na nyie mlionishauri nisiolewe na yeye…’akasema.



    ‘Sasa hebu tueleze inakuwaje, yaani huyu jamaa si anaishi huko kwenu mbali kabisa anawezaje kufika huku usiku, na anawezaje kumchukua huyu baba mwenye nyumba atoke naye waingie kwako na kuanza kukusumbua, si ndio hivyo, yeye anasafiri na nini hadi huku..?’ akaulizwa.



    ‘Ina maana hamuamini hayo mambo, mimi pia nilikuwa siamini, lakini anakuja kweli, ananifanyia hayo wanayofanya, na je kweli mama hajawahi kumuona baba akiingia chumbani kwangu susiku….?’ Akauliza akimuangalia mama.



    ‘Wewe ndio utuambie…’akaambiwa.



    ‘Huyu jamaa ana njia zake za kusafiri , niliambiwa anasafiri kwa njia za kichawi, usiku, na kila mara anafika hapa,…sasa anasafirije mimi sijui,….’akatulia.



    ‘Na eti wewe mdada, haya mambo hayayajakutokea na wewe…maana alisema na yoyote atakayeingia humu naye atakumbana na matatizo hayo, na hasa baada ya mimi kutibiwa nasikia alisema keshapata badili yangu, ..lakini hao watu waliosababisha yote hayo, ataendelea kuwasumbua mpaka wakome ubishi…’akasema.



    ‘Haya hebu tuambie ukweli, katika siku zote ina maana hukuwahi kumuona baba mwenye nyumba akiingia chumbani kwako usiku,..?’ akaulizwa.



    ‘Tatizo ni kuwa huyo jamaa, anapokuja nyumbani kwako, wewe mlengwa huwezi kumuona labda uwe umezindikwa,..au una imani safi ya dini, wapo wenye imani za dini mungu anawalinda, hawezi kufanyiwa mambo hayo, lakini wengi wetu imani zetu ni haba, kama mimi sikuwahi kufundishwa dini, nikamjua mungu, nikajua kujilinda kwa kupita kwa mwenyezimungu….’akasema.



    ‘Sasa akija anaingia ndani, sote tumelala, hakuna anayweza kumuona, na wanafanya mambo yao, unachohisi ni kama kukabwa, maana wanakuzuia usije kuzindukana,..na wakimaliza kazi yao wanaondoka huku nyuma ukizindukana usingizi unahisi athari hizo,…alinifanyia hivyo, lakini kwa kupitia kwa baba mwenye nyumba na kijana wake…’akasema.



    ‘Hatujakuelewa hapo…’akaambiwa.



    ‘Ni hivi nia yake ni kunikomoa mimi…, kwahiyo anachofanya akija, anawavuta wawili hao wakiwa usingizini, wanakuja kwangu, wananizalilisha, huku yeye akiniangalia na kunikebehi,…’akasema.



    ‘Sasa akifanya hivyo, wewe huoni, na wala hujui, huwaoni hao wanaokufanyia hivyo, sasa yeye anapata  faida gani..?



    ‘Si ndio hivyo,…mimi silali kwa raha, nahsi nakabwa, ni yeye ananikaba,…huku hao wawili wananizalilisha, yeye anafurahia hivyo,…mimi naona kama hamuniamini, sasa ni hivi mkitaka muamini kama hamtaki shauri lenu, mimi naondoka…’akasema.



    ‘Ngoja kwanza..’akasema kiongozi wa dini pale huyo msichana alipotaka kuondoka.



    ‘Ningoje nini tena hapa,  huo ndio ukweli wenyewe hangaikeni …’akasema.



    ‘Nasikia wewe uliwahi kupata mimba, ni kweli si kweli..?’ akaulizwa.



    ‘Ndio nina mimba mpaka sasa, ila yeye alinifanya nisiione hiyo mimba, nikaenda kuangaikiwa, nikapona na huyo mzee akasalimu amri baada ya mimi kuhangaikiwa, na akaja kuniachia, sasa yupo kwa wengine sio mimi tena, labda kwa huyu mdada hapa, kama haamini basi,…ila mimba nilikuwa nayo ikapotea, ….’akasema.



    ‘Kwa vipi? Akaulizwa.



    ‘Nilitaka kuitoa, kwasababu nilimbiwa nitazaa kioja sio mtoto kamili anaweza akawa shetani, huyo mzee kaniwekezea shetani tumboni…, ndio nikaona niwaambie hapa wanisaidie tuitoe, tukaitoa, kumbe yote ilikuwa kiini macho tu, ikaonekana nimeharibu hata kizazi, kumbe ni huyo mzee ananichezea, hata hospitalini waliona kizazi kimeharibika, lakini wiki iliyopita baada ya kutibiwa, nimeenda kupimwa , tatizo hilo halipo tena,…’akatulia.



    ‘Kwahiyo bado una mimba?’ akaulizwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Ndivyo walivyosema hospitalini kuwa bado nina mimba, haikutoka…’akasema.



    ‘Sasa mimba hiyo mimba ni ya nani..?’ akaulizwa.



    ‘Hapo mimi sijui…’akasema.



    ‘Kwa vipi, maana kama ni hiyo ya awali ilitoka sasa hiyo uliyo nayo, utakuwa umeipatia wapi..?’

    ‘Nasema mimi sijui tusubirie nizae, kiumbe kikitoka tutakipima na ukweli utajulikana ni mimba ya nani…na safari hii siitoi, …sitaki kuja kuharibu kizazi changu….’akasema.



    ‘Hebu kwanza naona unataka kuharibu ukweli, nataka unijibu kwa uwazi,..je mume wangu aliwahi kuingia ndani kwako mkafanya uchafu wenu..?’ aliyeuliza hivyo ni mama mwenye nyumba.



    ‘Mimi sikuwahi kumuona, unielewe hapo, nilikuja kuambiwa kuwa wawili hao, wanakuja kwangu, kwa kuongozwa na huyo mzee, wakiwa hawajijui, na kunifanya wanachoamrishwa kukifanya, sasa kama waliingia , hawakuingia, mimi sijui, niliambiwa hivyo, kama huamini shauri lako….’akasema.



    ‘Usitake kunitania wewe,  sema ukweli wako, kwanza umeanza kusema mume wangu na kijana walianza kukutamani, hiyo kauli inaashiria kuwa wewe ulikuwa na njama nao, sasa nataka useme ukweli la sivyo, nitakuitia polisi kuwa wewe unakuja kwenye majumba ya watu na kuharibu ndoa za watu..’aliyesema hivyo ni mama mwenye nyumba.



    ‘Waite hapo polisi,..nenda kawaita na mimi nitawaambi ahuo ukweli wote,… kama wataweza kukusaidia haya,….hivi mimi kuamua kuwaambia huu ukweli ndio nimekuwa mbaya, sawa, waite nikafungwe, nyie si mna pesa zenu, ila nazidi kuwatahadharisha, humu ndani hakuna usalama, huyo mzee keshafanya humu ndani ndio makao yake …hangaikeni …’akasema sasa akitaka kuondoka.



    ‘Kijana wewe unasema ulimuona huyu mdada akifanya mambo ya kishirikina akiwa uchi, sawa si sawa ?’ akaulizwa kijana.



    ‘Ni kweli nilimuona usiku akiwa uchi,…na sio mara moja, aliniambia kuhusu huyu mjamaa huko kijijini, mimi sikuamini, na hilo la kuwa tunakwenda usiku kwake, niliona ni mambo ya kishirikina, ila, yalinipa mawazo sana, sikupenda kuwasumbua wazazi wangu…’akasema.



    ‘Ulipomuona ulifanya nini..?’ akaulizwa.



    ‘Nilishindwa kufanya lolote, nilitaka kupiga kelele au kumuendea lakini sikuweza kabisa, ilikuwa kama nimenatishwa,…’akasema.



    ‘Je wewe ulishawahi kuingia chumbani kwake usiku ?’ akaulizwa.



    ‘Ndio, nilitaka kuhakikisha kuwa kweli huyo mtu ni mshirikina au la…na siku zote nilipoingia nilimkuta ndani kalala…’akasema.



    ‘Ila uliwahi kumuona nje, akiwa uchi..?’ akaulizwa.



    ‘Ndio..?’



    ‘Alikuwa akifanya nini..?’akaulizwa.



    ‘Kasimama tu, au kachuchumaa, au anatembea tembea, ni kama anasubiria kitu…lakini sikuweza kufanya lolote, maana nilikwua kama nimegandishwa….’akasema.



    ‘Oh…sasa hili ni tatizo…’akasema mzee mmojawapo.



    ‘Wazee, huyu binti ni muongo, nahisi kuna kitu anatuficha….’akasema mama mwenye nyumba.



    ‘Kama ni muongo, au ni mkweli, sisi tutakuja kumjua tu,….watu kama hawa hawawezi kushindana na mungu, sisi hatutakwenda huko kwa waganga wa kienyeji, sis tunafanya yetu kwa kumtegemea mungu, na yote haya yatakwisha…ila tunachotaka ni nyie wawili mkubaliane, muwe kitu kimoja, maana shetani lengo lake ni kuharibu ndoa za watu, na ndio matokea yake haya, niliwaambi awali kuna kitu nimegundua, sasa kimejitokeza, na haya yataisha kama mtaungana na kuelekeza nguvu zenu kwenye imani ya kweli…’akasema kiongozi wa dini.



    ‘Sasa mimi nakwenda…’akasema huyo binti.



    ‘Sawa unaweza kuondoka, ila tutakihitajia tena,…’akaambiwa.



    ‘Hahaha, kama hamjaamini, subirini mtakachokiona huyo mzee akijua mumemfahamu atakuja kuwafanyia baya zaidi ya hilo…’akasema.



    ‘Atafanya nini acha kutisha watu hapa…’akasema kiongozi wa dini.



    ‘Sawa mimi nawatisha,..lakini jiulizeni mangapi yamefanyika humu ndani na hamkuweza kuyazuia…jamaa huyo alikuwa anakuja kwangu usiku, wewe mama uliweza kumzuia…hujaweza kumzuia,…na nani anapata shida, ndio mimi nimepata shida, lakini hata nyie, …..mimi nimejitolea kuja kuusema ukweli kwa vile mumenisaidia sana…’akasema.



    ‘Ila tunakuonya kama wewe upo nyuma ya haya mambo utakuja kupata shida …’akaambiwa na hao wazee.



    ‘Wazee wangu, ..ndio maana nimekuja, nimeona nateseka kwa kuiweka hii siri moyoni mwangu, hawa watu walinipokea wakanilea, wakanihifadhi, na haya yanatokea kwasababu yangu mimi, ..kwanini nikae kimia, hapana, ..mungu mwenyewe anajua ila nimetimiza wajibu wangu, sasa iliyobakia ipo mikononi mwenu kwaherini…..’akaaga, na alipofika mlangoni, akageuka na kusema



    ‘Na wewe binti mdada mwenzangu, uwe makini, kwani yaliyonipata mimi , huenda ndio hayo yanayokupata na wewe, siku ile nilikuona unalia, huenda hayo yameanza kwako, …sasa ni juu yako kuhangaika au kukaa kimia na kusema,..’mimi sijui….’haya endelea kutokujua, …kwaherini…’binti akasema na kuondoka.



    NB Tuendee…. hapana tusubirie sehemu ijayo.





    WAZO ZA LEO: Mwenyezimungu alitujua sisi wanadamu tulivyo, kuwa kuna wengine nafsini mwao ni zaidi ya mnyama, roho mbaya, na wengine wanyonge, ndio maana akatuambia vyovyote iwavyo, yeye yupo karibu nasi kuliko mshipa wa damu uliopo mwilini wetu, tumuombe yeye, tumtegemee yeye, lakini ukweli wa kumuamini, na sio kwa kinafiki au kwa kumshirikisha. Tumuombe mola wety atupe imani thabiti ya kumuamini yeye, na kumtegemea yeye..Aamin.



    Yule mdada alipoondoka, kwanza kulipita ukimia fulani, kama vile watu wameambiwa watulie, na baadae kiongozi wa dini akasema;



    ‘Kuna mambo mengine yakitokea unajiuliza ni kweli au sio kweli, ..lakini kwenye hii dunia lisemwalo lipo, na uchawi upo, hata kwenye vitabu vya dini vimesema hivyo, na tatizo ni jinsi gani ya kupambana nao, au kujikinga nao, wengi hukimbilia kwenye shirki, badala ya kumuendea yule aliyewaumba. Ndugu zanguni, niliwaambia awali nimehisi hapa kuna tatizo, na hata kabla ya kuja huyo mdada, nikahisi kuna kitu zaidi ya maelezo…’akatulia



    ‘Unataka kusema umeamini hicho alichoongea huyo mdada..?’ akauliza mama mwenye nyumba.



    ‘Kuamini au kutokuamini, ni nyie wawili, ambao mumeyashuhudia hayo, na mnapata mitihani hiyo, ukijua kuwa yote hayo ni mitihani, lakini vyovyote iwavyo nimewashauri jambo moja kubwa ni kujirudi, na kuwa kitu kimoja, ili muweze kupambana na hilo tatizo mkiwa na nguvu moja, maana nyie ni kitu kimoja mke na mume na familia kwa ujumla,…’akatulia.



    ‘Mara nyingi adui ili ashinde hupenda kuwagawa, kutenganisha, kuwagombanisha…na hiyo ndio kazi ya shetani…kujenga fitina,..ili wanandoa wakosane, wanandugu wafarakane, majirani wasielewane…huyo ni adui yetu tupambane naye, lakini kwa njia sahihi….’akatulia, na mama mwenye nyumba akachukua nafasi hiyo na kuanza kuongea;



    ‘Mimi nilisema kuwa mume wangu anakwenda kwa huyo binti na nilisema nina video yenye ushahidi huo…lakini mume wangu akanikatalia,..sasa tumuulize yeye anasemaje ..?’ akasema mama mwenye nyumba na mume akabakia kimia, alikuwa kama kamwagiwa maji, hakusema kitu…hakumuangalia mke wake alionekana kuwa mbali kimawazo.



    ‘Huna cha kuongea…’akasema baba yake.



    ‘Nitaongea nini tena baba hapo…, haya yamenikuta, na kiukweli bila ya huyo mdada kuyasema hayo, nilikuwa siamini, …hata mpaka sasa bado sijaamini, lakini nifanyeje, nitajitetea vipi,..kama ni kweli, basi ni kweli…’akasema.



    ‘Kwahiyo unasemaje?’ akaulizwa.



    ‘Niseme nini hapo…kwasasa mimi namsikiliza mke wangu ..maana kiukweli itakuwa imemuumiza sana, najaribu kufikiria kama mimi ndio yeye,…lakini kiukweli mimi sijui hayo mambo, na kama kweli nilikuwa nafanya hivyo, ooh, mbona ni mtihani huu, yaani mimi kiukweli sijaamini bado…’akasema.



    ‘Nikuulize kitu, hali kama hiyo ilishawahi kukutokea kabla?’ akauliza kiongozi wa dini na kuwafanya watu sasa wamuangalia kiongozi huyo wakijiuliza ana maana gani.



    ‘Hali hiyo ya …..hapana, au una maana gani kiongozi, umesikia alivyosema, na hili kwangu ni jipya, yaani ningebisha mpaka kesho…hata hivyo, bado, jamani, yaani nitoke hivi hivi, mguu kwa mguu nisijitambue, hivi kweli nyie mnaamini hayo…!’akasema kama anauliza lakini akionyesha uso wa kutahayari.



    ‘Kwanini unauliza hivyo mkuu..?’ sasa akauliza mzee mmojawapo.



    ‘Mimi mawazo yangu, hayakuwa mbali na hilo aliloliongea huyo bint, ni kweli yanaweza kuwa ni ya ukweli kwa mtizamo wa huyo binti, kama nilivyosema awali , uchawi upo…, lakini pia, tusikimbilie huko moja kwa moja , kwa vile bado kuna utaalamu wa kihospitalini….’akasema



    ‘Hayo mambo yana matibabu hospitalini…?’ akauliza mzee.



    ‘Kuna jambo jingine nilitaka kuliongea kabla, na japokuwa nilikuwa na walakini mbili, sasa…hili limetokea likanifanya nijiuliza mara mbili, je ni mambo ya shirki, au ni tatizo la ugonjwa..’akasema kiongozi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Kwani kuna ugonjwa kama huo, mimi naona ni mambo ya nguvu za giza, na hospitalini kamwe hawawezi kuyaamini hayo au una taka kusema nini kiongozi wa imani…?’ akauliza mzee.





    ‘Ndio, lakini hao wanatibia, madocta nk, ni wanadamu kama sisi, na hata wao wanakumbana na matatizo kama haya, je hamjawahi kuhangaika na mgonjwa wenu ikafikia sehemu huyo docta anakushauri ujaribu njia mbadala….?’ akauliza.



    ‘Ipo sana…..’akasema mzee.



    ‘Unajua mimi ni kiongozi wa dini wa eneo hili, lakini kabla ya hapo nilisomea udakitari, kuna tatizo linaitwa ‘somna-mbulism’ sijui kama nimelitamka sawa…ni neno la kitaalamu, wanajua wenyewe wazungu kwanini wakatumia neno hilo…’akatulia akiwaangalia kila mtu kwa waakti wake.



    ‘Ni nini hiyo…ni..ok, nimewahi kusikia kitu kama hicho, ….’akasema mzee mwingine.



    ‘Yaani… mtu anaota na kutenda, huku akiwa usingizi, ….na mara nyingi anachofanya hakikumbuki, anaweza akaota, akaenda kuchota maji, au kufanya kazi, na baadae akarudi akalala..bila kujijua….ndio maana nikamuuliza baba mwenye nyumba hii ni mara yake ya kwanza kumtokea hivyo…?’ akauliza kiongozi huyo wa dini.



    ‘Mhh…uajua umeonga jambo, ukanikumbusha kitu….’aliyesema hivyo ni mke mtu, akawa kama anawaza jambo, na kiongozi wa imani akamuuliza.



    ‘Kitu gani, tuambie ndio maana nilitaka mfunguke, muelezee kila kitu, huenda ikajileta yenyewe, ni kitu gani, umekikumbuka…?’ akauliza.



    ‘Mume wangu unakumbuka,…’ akageuka kumuangalia mume wake, ambaye bado alionekana kuwa mbali kimawazo.



    ‘Nini….hapana, sikumbuki….’akasema akitikisa kichwa



    ‘Kuna kipindi fulani humu ndani kulikuwa kunatokea maajabu, ..nilikuwa nikiamuka asubuhi, nakuta vyombo vyote vimeoshwa, kumefagiliwa kumepigwa deki, na kila kitu kimepangwa vyema kabisa, hatukuwa na mtu mwingine humu ndani, nikamuuliza mume wangu, ni nani kafanya hivyo, hata yeye akawa anashnga tu, na ilitokea mara kwa mara kipindi hicho,…’akasema.



    ‘Unakumbuka kwanini ilitokea hivyo..?’ akaulizwa.



    ‘Kipindi hicho, nilikuwa nalalamika kazi zimekuwa nyingi, na tukiongea na mume wangu anasema tuwe na subira maana hali sio nzuri kiuchumi, basi, nikawa sina raha, na hayo yakaanza kutokea, unajua, nilijua ni mume wangu anafanya kuni-shtukizia, lakini yeye akawa anashangaa, na kuniuliza, …’akasema mke mtu.



    ‘Mhh…nakumbuka, lakini …sio mimi, niliyekuwa nafanya hivyo..inawezekana ulikuwa ni wewe…ulipitiwa tu, maana ule usafi na jinsi ya vitu vilivyokuwa vinapangwa ni utaalamu wa aina yake, na anayeweza hivyo ni mwanamke…’akasema.



     ‘Yah, ulikataa hivyo hivyo, kama ulivyokataa hili….na sasa unajiuma uma…inawezekana ni wewe, inabidi kweli tumtafute docta,…ndio sasa naanza kukumbuka, inawezekana, sasa huyo docta tutampataje kiongozi wetu wa imani..?’ akauliza mama mwenye nyumba.



    ‘Lakini sioni kwamba hilo lina ukweli ndani…na hata kama lipo,  mimi sina  tatizo hilo…’akasema baba mwenye nyumba akizidi kujitetea.



    ‘Kama huna tatizo hilo, ina maana ulifanya makusudi,…kama ulikusudia tuambie tujua, utubu dhambi zako…’akasema mama mwenye nyumba, na baba mwenyenyumba akabakia kimia.



    ‘Sasa kabla ya kufikia maamuzi hayo, kuna mambo mawili ya kufanya, kwanza, nyie wawili mshuke chini, muombeane msamaha, maana mola hukubali toba za yule alietubia madhambi yake, akawa hana kinyonga na mtu, akasamehe ili na yeye aweze kusamehewa, na la pili, ndio hapo tutamkabidli yeye muumba, tutaomba kwa pamoja, ili tupate radhi zake, ulizi wake, na kama kuna jambo la shiriki, basi mwenyezi mungu aliondoe, na kuweka ulinzi wake, …sawa..?’akasema kiongozi wa imani akiwaangalia wanandoa hao.



    ‘Sawa kabisa…’wakasema wazee wale wawili na kijana akawa wa kwanza kusimama akiwasubiria wazazi wake, kwa uso wenye furaha.



    ‘Unasemaje baba mwenye nyumba, bado una mashaka na hilo..?’ akaulizwa na wazee



    ‘Mimi nilitaka nione hiyo video kwanza, nihakikishe kwa macho yangu maana mimi sijaamini hilo…’akasema

    ‘Kama ni kuiona hiyo video, basi mtaiona mkiwa nyie wawili, kama ni muhimu kwenu…, ila mimi ningelishauri muiharibu kabisa hiyo video…, isje kuleta chuki nyingine…’akasema kiongozi wa dini.



    ‘Ni kweli, hebu ilete hapa tuiharibu…’akasema mzee akimuangalia mama mwenye nyumba.



    ‘Hapana siwezi kuiharibu kwa sasa… bado nataka kuifanyia kazi…’akasema mama mwenye nyumba.



    ‘Kazi gani tena..?’ akauliza baba mwenye nyumba akimuangalia mke wake.



    ‘Nataka kuhakiki kama alichosema huyo mdada ni cha u- kweli,…’akasema



    ‘Kwa vipi..?’ akauliza mumewe.



    ‘Kuna mtaalamu mmoja, yeye kasomea, mambo ya mitandao, lakini pia ana utaalamu wa nguvu za giza, anasema yeye anapambana na hayo mambo, yeye, hatai kuitwa mganga wa kienyeji, bali anapendelea akiitwa mtaalamu, maana hapigi ramli, au…sijui tunguli, hapana, yeye anatumia mitandao…alisema yeye anaweza kupiga picha, na kwenye picha kunaweza kukawa na mtu zaidi ya mmoja,..labda, nikamuuliza kwa vipi.



    ‘Akasema, duniani kuna viumbe vingine havionekani, kama majini mashetani, na usiku kuna wachawi, sasa unaweza ukapiga picha bila kujua kuwa viumbe hao wapo karibu yako,..kwenye picha hawataonekana, lakini yeye akiingalia, akaweka kwenye vipimo vyake anaweza kuona vitu kama hivyo…’akasema



    ‘Kwanini alikuambia hayo…?’ akauliza mumewe



    ‘Ilitokea tu, wakati tunaongea, rafiki yangu alinitambulisha kwake, …ni mumewe….’akasema



    ‘Ok….kama ni hivyo sawa…’akasema baba mwenye nyumba.



    ‘Lakini huo ndio mwanzo wa kuamini mambo hayo, au unataka uhakikishe kitu gani sasa..?’ akaulizwa

    ‘Kama alichosema huyo mdada ni kweli, ina maana mume wangu alipokuwa huko chumbani, alikuwa pamoja na huyo mtu mwingine lakini, huyo mtu mwingine alikuwa haonekani, kwa kauli yake au sio…sasa kama haonekani, kwa ujuzi wa huyo mtu atamuona, kwahiyo tutagundua ukweli wa maneno ya huyo mdada, kama kweli hatudanganyi…’akasema mama mwenye nyumba.



    ‘Unajua ukianza kupekenyua, pekenyua hayo mambo,.. ndio mwanzo wa kujiingiza kwenye shirki, kitu ambacho ndicho tunakikwepa hapa, au sio jamani wazee wangu…’akasema kiongizi wa dini.



    ‘Mimi siwezi kuingia kwenye shirki hata siku moja… imani yangu ni thabiti, ndio maana hata hao mnaowaita wachawi sijui, hawajaweza kunichezea mimi,…hilo la mume wangu kufanya hayo, akilini mwangu kuwa ni uchawi sijaliafiki,…ila nilishagundua kuwa kuna tatizo kwa mume wangu,sasa sikuwa na uhakika ni tatizo gani,…kama alivyosema kiongozi wa dini, kuwa kuna hali hiyo ya kutembea kwenye ndoto, hapo naweza kuamini kidogo,…sasa mimi nahitajia muda, kuyachunguza haya…’akasema.



    ‘Kwahiyo bado huniamini mimi…?’ akauliza mume wake.



    ‘Kukuamini au kutokuamini, kunahitajia mambo mengi, na mojawapo ninalotaka kulifanya ni hilo, la pili…ni hilo la kumtafuta dakitari, na la tatu ni kumuelekea mwenyezimungu, mimi hayo yote nayapitisha, ila hilo la uchawi, bado sijaliamini, labda huyo mtu anionyeshe huyo mchawi kwenye hizo picha, …’akasema.



    ‘Atakuonyeshaje sasa..?’ akaulizwa.



    ‘Hilo niachieni mimi..sio kwamba nitaamini, lakini kama kasema anaweza kumgundua mchawi hata kama kajificha ,basi ataligundua na hilo..alisema hata picha kama kuna kitu kisichoonekana lakini kimechukuliwa na picha atakiona, alinionyesha pich alizopiga usiku akiwa piga wachawi, lakini ukiziangalia hivi huoni kitu, yeye anakiona hicho kitu,…na ana namna ya kusafisha hizo picha kwa utaalamu wake, na hizo sura za wachawi zikaonekana kabisa…..’akasema.



    ‘Oh, unaamini hayo..? akaulizwa na mumewe.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Kuamini au kutokuamini kutakuja baada ya ugunduzi huo..mimi tabia yangu ni kufanya utafiti kwanza, ndio maana nilikwenda shule…, na nikigundua basi, nitakuwa nimegundua jambo ambalo nilikuwa silijui, akili yangu itaongeza ujuzi huo, japokuwa kwangu mimi bado nayaona mambo hayo kama nguvu za giza tu, mambo ambayo hayahitajiki kwetu sisi wanadamu…’akasema.



    ‘Sawa, sasa mnasemaje..mpo tayari kushikana mikono na kuyamaliza haya mambo..?’ akauliza kiongozi wa dini.



    ‘Samahanini wazee wangu…..nisema ukweli wangu, hata kama nitakubali hapa, kuwa nimesamehe, nimshike mkono, utakuwa ni unafiki tu,  bado mimi sijawa na imani …sijakubaliana na hili jambo kuwa ni kweli, mume wangu alikuwa hajui mambo yote hayo, kuwa hakuna kitu kwenye moyo wa mume wangu, kumtamani huyo binti, …hawa mabinti, maana hata huyu kasema hay ohayo yamekuwa yakimtokea, sijafuatilia hili, ila nilishaanza kufuatilia…’akasema.



    ‘Sasa unataka kusema nini..?’ akaulizwa.



    ‘Nasema hivi, nahitajia muda wa kulifanyia kazi hili na..nikijirizisha basi , nitawaambia, lakini sio kwamba,..nimekasirika au nina nia yoyote mbaya,..naomba mnielewe hivyo, kwasababu,..nilipoona hiyo video, moyo wangu ulikufa ganzi, na mimi sio jiwe,  penzi nililokuwa nalo moyoni, silioni tena…aah, nisameheni tu, na mwenyezimungu anisamehe pia…’akasema.



    ‘Oh…lakini mwenyezimungu katuambia, kamwe tusiweke kinyongo moyoni, au tusiwe na kisasi au chuki moyoni, maana umauti ukikukuta ukiwa bado na kinyongo hicho, au chuki hizo,..kuuona ufalme wa mbingu, kuingia peponi kwako itakuwa ni mtihani, na mwenyezimungu anajua zaidi..ni bora msameheane,..hata kama moyoni bado una hasira, ile kusamehe,..huku unamuomba mungu, mungu mwenye atailanisha nafsi yako, nahasira na chuki hizo, zitayeyuka kidogo kidogo,…muhimu ni kumuomba mwenyezi mungu awasaidie, maana haya mambo bila muongozo wa mola wetu bado yatakuwa ni mazito kwetu,…’akasema.



    ‘Kiongozi,..hata kama moyoni, au kwenye nafsi yangu bado sijarizika, nikubali tu…hapana mimi bado  nina ..duku duku,…kwani jamani, siruhusiwi kujirizisha kwanza.niongoze kiongozi wangu, mimi ninachotaka ni kufany autafiti, nijirizishe, maana mume niliyemjua sio huyu tena….’akasema.



    ‘Hata hivyo,…mimi niliona ni vyema mkasameheana kwa leo, huku mkiendelea na michakato mingine kama nilivyosema, huku mnamuomba mungu awasaidie, maana haya yote sio kwa ujanja wetu, na hatjui ya kesho, hatujui uhai wetu upo kiasi gani….ni muhimu tukalitambua hilo…’akasema kiongozi wa imani.



    Basi wote wakakubaliana tukaanza ibada ya kumuomba mwenyezimungu na kuomba hayo yote yaliyopo humo kwenye nyumba kama ni ya kibinadamu au kama ni ya kishetani..yaondoke na nyumba ibakie kwenye amani…na tuliomba mwenyezimungu atupe kinga yake, na kutuongoza kwenye njia sahihi, baada ya hapo wanandoa hao wakashikana mikono, na kijana alionekana kufurahi sana.



    ‘Kabla hatujaondoka nina ombi jingine na hili sitaki likataliwe, na sitarudi nyuma tena,  kwa uamuzi huo…’akasema mama mwenye nyumba.





    ‘Ombi gani tena..?’ akauliza mume mtu akionekana kuwa na mashaka zaidi.



    ‘Ni kuhusu huyu mfanyakazi wa ndani tuliye naye sasa…’akasema.



    ‘Ehe, unatakaje au naye ana nini..?’ akaulizwa.



     Huyo mama hakutaka hata kuniangalia machoni, akasema…



    ‘Mume wangu, ..hili ninataka wewe ulifanyie kazi, ..utajua wewe mwenyewe kwa jinsi gani, …’akatulia.



    ‘Niambie mke wangu nipo tayari, kukubalia lolote lile, najua nimekukosea sana, na sitaki niendelee kukukosea, nataka nikuonyesha kuwa mimi ninakupenda sana mke wangu...’akasema baba mwenye nyumba akitamani hata kupiga magoti.



    ‘Najua kwasasa utasema hivyo, siwezi kukulaumu..nimekuzoea…, ila hili, nimeliwazia sana nikaona ni bora iwe hivyo, hata kama watu wataniona mimi ni mtu wa ajabu sana…’akasema mama mwenye nyumba.



    ‘Sawa uamuzi ni wako, kama mnataka muongee wawili basi mturuhusu sisi tuondoke…’akasema kiongozi wao wa imani.



    ‘Hapana hili nitaka niliongee hapa hapa ili kila mtu alisikie na lifanyiwe kazi , ….’akasema sasa akimuangalia mume wake machoni, halafu akageuka kuniangalia mimi, na hapo moyo wangu ukaanza kudunda, nikahisi kuna jambo kubwa linakuja,..lakini siweza kubahatisha ni jambo gani!



    NB: Hatimaye nimefanikiwa kuandika sehemu hiyo hivyo….kama nilivyosimuliwa na mwenyewe, tusihie hapa kwa leo.



    WAZO LA LEO: Riziki haigombewi, kwani kila mja ana fungu lake.

                               Lakini pia riziki haupewi, ukilala na kusubiri fanI zake.

    Jibidishe kwa amali hata kupiga kiwi, ufanye ibada na kila kitu kwa mahala pake.



     Mola ni mwingi wa rehema, atampa kila mja fungu lililo lake.





    Niambie mke wangu nipo tayari, kukubalia lolote lile, najua nimekukosea sana mke wangu..., na sitaki niendelee kukukosea, nataka nikuonyesha kuwa mimi ninakupenda sana mke wangu...’akasema baba mwenye nyumba akitamani hata kupiga magoti.



    Na mke wake ndio akaanza kuongea....





    Tuendelee na kisa chetu...





    'Wazee wangu, ni kweli mume wangu ana huruma sana, nilimpenda tokea awali kwa tabia hiyo ya huruma na upole, kwasababu hata mimi sipo mbali na yeye, na tabia hiyo ya huruma niliyokuwa nayo mimi  ndiyo iliyonifanya niwe mbali na wazazi wangu !





    Kwanini nasema hivyo, …kwasababu sijui ni kwanini, wao kwa mtizamo wao, na siwezi kuwalaumu, ndio kawaida ya kibinadamu, wao wanaamini madaraja ya maisha yapo kuwa kuna watu wa hali ya juu na wa hali ya chini…na kwamba wao kwa vile wapo juu, kwa jinsi wanavyojiona wao hivyo, marafiki wao wa kweli ni wale walio sawa na wao, na wale watakao-oa kwao wawe ni watu wanaojiweza kama wao walivyo…





    Kiukweli, sijui ni kwanini tupo hivyo,… kwangu mimi hilo sikulipenda, hasa nikikutana na watu ambao hwakujaliwa kuwa na uwezo, najua wengi sio kwa dhamira yao,…kiukweli mimi nikikutana na masikini, mayatima watoto wa mitaani, naingiwa na moyo wa huruma, najiuliza ni kwanini wao wanateseka hivyo, wakati kuna watu wana mali, wana uwezo uliopitiliza, …sijisifu ila kwetu kwa wazazi wangu tuna kila kitu, tunakula na kusaza, wakati huo huo kuna watu wanateseka…’akasema kwa uchungu.





    Hapana mimi sikulifurahia hilo, kwanini tumwage chakula, kwanini tubadilishe magari kama nguo, kwanini, tunaishi maisha ya raha sana, wakati dunia hii ni ya kupita tu, sikupenda hiyo hali, mimi nikawa kila siku naleta watoto wa mitaani, hapo nyumbani kwetu..nawapa chakula nguo..nawasaidia,…, na hilo liliwakera sana wazazi wangu…sio kwamba nawateta wazazi wangu, lakini wengi wenye uwezo wapo hivyo. Isjui kama nakosea!





    Mimi nilipokutana na mume wangu, tukawa marafiki, akanielezea maisha yake, nilijawa na huruma na mapenzi yakaanzia hapo, …nilijua huyu ndiye wangu wa kufa na kuzikana, nilitamani kuwa na mume wa namna hiyo, mwenye huruma na upendo, ambaye anawapedna wale wasiojaliwa kupata upendo kwasababu ambazo zipo nje ya uwezo wao, kama mayatima na watoto wa mitaani, tulikuwa mimi na yeye tunalijadili hili mara kwa mara….



    Sasa haya yanatokea usoni mwangu,…yamenipa fundisho fulani, kuwa sio vyote ving’aavyo ni dhahabu, sio kwamba wengine wote wanaoteseka wana miyo mizuri, wengine ni kwasababu tu hawajaipata hiyo nafasi,… mtu akipata hubadilika, huwezi kuamini kua ndio yule wa zamani…mimi sitaki maisha hayo….’akasema





    ‘Lakini mke wangu mimi sijabadilika,…mbona wanasingizia mambo ambayo sio ya kweli….’akajitetea mume wake,lakini yeye hakumsikiliza, akaendelea kuongea kwa kusema;





    'Ndio maana,  sasa hivi nataka nipate muda wa kuyatafakari haya yote, nahitajia muda wa kujipima wapi nilikosea, lakini pia, sitaki kumkwaza mtu, sitaki kumuumiza mtu, sitaki mtu anione kuwa nafanya haya kwa vile, hapana, maana sitaki nifanye mambo yenye kumkasirisha mola wangu.





    'Ninajua maagizo ya mola wetu ni kusaidiana, kutendeana wema, kujenga udugu wa kiukweli nk..lakini mitihan ikizidi sana mtu hukengeuka, hujikuta akiingia kwenye dhambi bila kupenda, lakini pia sio vyema kujilegeza na kusema nimeshindwa,..hapana mimi bado sijajishindwa, naji….ninajibidisha ndio maana nikafikia maamuzi hayo ambayo nitayateleza ili name nipate muda wa kujijongeza kwenye uhalisia.





    Baada ya kuyasema haya, nataka niwaambie nini maamuzi yangu, mume wangu hata kama una matatizo ya kiafya,…labda kama ipo hivyo, siwezi kukubali tu, maana mimi sina kipaji hicho… au hata kama ulilogezewa kama alivyodai huyo mdada maana wengi tunapenda kukimbilia huko, hata kama sio …hata kama kuna njia mbadala, na njia sahihi nyingine, …mimi naamini kuwa mola wetu anatujua sana sisi tulivyo…, ndio maana akatuelekeza njia hiyo, lakini ….hapa nilipofika nasita, na inabidi tufanye hivyo….CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/







    Mume wngu, nimeipima nafsi yako, japokuwa sina uwezi huo, ila kwa kile kidogo nilichojaliwa nacho nimekiona kuhusu wewe ulivyo, japokuwa utapinga,… nafsi yako haijatulia, ina muwashawasha wa tamaa za kimwili, kama walivyo wanaume wengi, nyie mnakuwa wa kwanza kutuchoka sisi wanawake, hasa tukianza kuchujuka, ukubali usikubali ndio hivyo…’akasema pale alipoona mume wake anataka kusema neno.





    ‘Ni kweli nyie wanaume hamzeeki, sisi wanawake tunazeeka mapema, ule urembo wetu unatoweka, lakini kwani hayo ni mapenzi yetu, kwanini mungu alifanya hivyo…najiuliza sana tu, na sio kwamba namlaumu mola wetu,lakini majibu yapo, ndio maana nitachukua maamuzi hayo, na mtu asije kuniona mimi ni mtu wa ajabu sana, hapana na mimi ni mwanadamu..







    Nataka unielewe hapo mume wangu…, hata kama utapinga na kujitetea vipi, hili nitakalo kushauri ulifanyie kazi, nilishalifanyia kazi mimi akilini mwangu kwa uoni wangu, na nipo tayari kulibeba hili , japokuwa moyoni nitaumia, sikupendelea iwe hivyo,… lakini mimi nayafanya haya kwa vile nakupenda sana mum ewangu…’akatulia kidogo.





    Mimi nayafanya haya kwa vile ninataka wewe uzidi kuwa na furaha, lakini pia furaha yako isiwaumize wengine… sasa ni juu yako kulifanya au kuliacha, nimefikia mamuzi hayo baada ya kupiti utafiti mmoja ya wa njozi, mtu huyo kwa fikira zake na utafiti wake, yeye alisema, ndoto nyingi tunazoota usiku, ni zile hisia zetu za matamanio yetu ya kila siku, kila mtu anatamani kuwa hivi kupata kile hata kama uwezo huo hana,….





    Mimi sio …mshirikina, na sipendi imani hizo, ila….kuna mengine unayaona kuwa ni kweli hata bila kupitia huko,

    Mtu anataka awe tajiri, au amuoe bint wa sultan ili hali yeye ni masikini, ataota nini hapo , ni lazima usiku ataota ndoto zake, kuwa kafanya hivi na vile akafanikiwa, hata kama haitawezekana kuwa hivyo..maana mipangilio ya mweneyzimungu ina hekima zake, japokuwa sisi hatulioni hilo.





    Sasa kuna kitu nilikiwazia sana,  ndoto kama alizosema kiongozi wetu wa dini , kuwa zipo …ndoto za matendo, ya kuwa uliwazalo mchana utakuja kuliota kwa matendo usiku, hata kama mchana ulishindwa kulifanya, basi usiku unaweza kulifanikisha kwa njia ya njozi, na unatenda kwa matendo, hii ni hatari eti…kwa mfano , nachukulia tu kama mfano,…je ukimchukia mtu hadi kutamani afe, usiku utafanyaje,..najiuliza tu  ni nini hatima yake, lakini mungu ni waajabu sana huwalinda waja wake, na haijatokea watu kama hao wakafanya mabaya kiasi hicho cha kuua,… ila wanaweza kufanya madhambi kama hayo aliyoyafanya mume wangu, hahaha hapo unajiwekea alama ya kuuliza…’akasema





    Naombeni mnivumilie kwa maneno mengi, lakini nina maana yangu hapo, ili kwa maamuzi yangu msije kuniona nimegeuka kuwa jiwe….





    Mume mtu kusikia hivyo, akanyosha mkono kutaka kupata ruhusu ya kuongea, na mkewe akamuangalia bila kusema neno, na yeye akasema;





    ‘Mke wangu, usfikie kunuhukumu kihivyo,…yawezekana nilifanya ndio, maana ushahidi si unao,…, yawezekana nina matatizo hayo,mimi sijui....lakini ukizidi kuninyanyapaa, ujue nasikia vibaya sana, najiuliza hta mimi, kwanini iwe hivyo, kwanini…hizi kwanini zinaumiza mke wangu…kama tulishakubaliana yaishe, basi, yamekwisha, tuyasahau, na mimi nitajitahidi kujirekebisha…’akasema.





    ‘Sikunynyapai, lakini ukweli lazima usemwe, na ukisemwa kama hivi utakuwekea kumbukumbu ya kujihami kila ukikusudia kufanya mabaya, ukikumbuka kikao kama hiki, maneno kama hayo, utaogopa,..ndio maana tumeusiwa kukatazana mabaya na kuamrishana mema, nia ni nini, sio kuhukumu mtu hapo, sio kujikweza, nia ni kujengeana kumbukumbu za kujihami…unielewe hapo, mimi nimesomea ualimu na najua ni vipi niwafundishe watu…’akasema mkewe.





    ‘Ok, sawa, sasa unaonaje ukalisema hilo ulilokusudia kulisema kwasababu kwa jinsi unavyorefusha maneno unanipa shikizo la moyo, nashindwa kujua nini dhamira yako unaanza kuniogopesha hata mimi….’akasema





    ‘Ni kweli, hata mimi nilipata sana shida kulifikiria hilo…na ni maamuzi magumu kama hayo kwangu mimi, kwa mtu kama mimi, lakini sina jinsi, na…binti ataelewe tu, na ipo siku atakuja kunielewa kwa hili, sasa hivi…itakuwa vigumu na huenda akaniona mtu wa ajabu sana.





    ‘Baada ya kuyawaza hayo yote, nimefikia maamuzi haya, kuwa hivi sasa, nataka wewe mume wangu, umtafutia huyu binti, sehemu ya kuishi, umtafutie chumba chake, kwa namna utakavyoweza wewe, umuwekezee mradi kwa namna utakavyoweza wewe, na hata ukitaka mfunge ndoa, ili uweze kwenda kwake kwa nafasi, bila kujiiba, si ulimtamani, si ulimpenda, sasa nataka hilo usilifanye kwa kificho na mimi nipo radhi…’aliposema hivyo, mimi nilishtuka, nikatoa macho ya kuogopa.





    ‘Unasema nini mke wangu, unataka kufanya nini, kunifukuza humu ndani au.?’ Akauliza mume mtu akisimama.





    ‘Mume wangu mimi sijatamka hilo, na hata siku moja, japokua niliwahi kutamka kwa hasira, kuwa utaondoka humu ndani, lakini mimi sijafikia maamuzi ya kuwa tuachane kwa talaka, kutamka kuwa utaondoka humu ni namna ya kukujenga uelewe wajibu wako, ninachotaka kwa hivi sasa ni wewe usiwe mnafiki, uweze kuifurahisha nafsi na matamanio yako kwa uwazi,…sijui kama  bado sijaeleweka hapo, maana huyo unayemfanyia hivyo yeye ni mwanadamu, kwanini umzalilishe na wakati ipo njia halali, kwanini mfanye kwa siri wakati mnaweza kuifanya kwa dhahiri kwa halali…’akasema.





    ‘Mimi sijafikiria huko na siwezi kufanya hivyo…’akasema mume mtu.







    ‘Hili nimelipanga hivyo, kwasababu gani, huyu binti nilikabidhiwa mimi, na yupo mikononi mwangu, na mama yake keshafariki, ni masikini na ni mjane, …na haya yametokea ndani ya nyumba yangu, ndani ya mamlaka yangu, na mimi wakati mwingine ndiye wa kulaumiwa, huenda nimeshindwa kumshibisha mume wangu, huenda…sasa hizi huenda….hapana, na zaidi waliomtendea hayo  ni familia yangu, tunahitajika kuwajibika kwa hilo, lakini pia tunahitajika kuchukua tahadhari..ili yasije kutokea tena makubwa zaidi ya hilo, maana chuki zinakuja kutokea, na chuki, hahaha, zinaweza kuotwa usiku tukaja kuuana humu ndani….’akasema.





    ‘Kwahiyo, mume wangu kaa ufikirie hilo.., ila kwa huyu binti kuanzia leo, naomba baba, wewe ndio tegemea langu, wewe mara nyingi umekuwa ukinielewa, haya yakiendelea kufanyika, tukiendelea kumpa muda mume wangu kuyafanikisha hayo, kwa jinsi yeye atakavyoona ni sahihi, ninaomba huyu binti aje akae kwako..sikutupii mzigo, mimi bado nitaendelea kumsaidia kwa kadri niwezavyo,..ila hili saa ni jukumu la mume wangu, sio mimi nitamsaidia, ila nitahakikisha misaada hiyo inamfikia mlengwa…’akatulia.





    ‘Hapana mimi siwezi kulifanya hilo, kama humtaki mtoto wa watu umrudishe huko ulipomchukulia, mimi huyu sijamleta mimi, …’akasema baba mwenye nyumba.





    ‘Mume wangu uliahidi kuwa nitakachokisema utakitekeleza, ahadi ni deni, sasa kazi ni kwako….’mke mtu akasimama.





    ‘Mke wangu unataka kwenda wapi hili hatujakubaliana nalo, japokuwa nilikuahidi hivyo….’mume akaanza kulalamika.





    ‘Mimi nimemaliza, binti fungasha kile kilicho chako, mtaondoka na baba yangu hii leo....nilishaongea naye hili kabla japokuwa sikujua haya yatakuja kuwa hivi,…nimuomba kama kutatokea lolote kama hili, niliwazia hivyo tu, basi huyu binti sio wa kutelekezwa, anahitajia njia nyingine ya kumsaidia, na njia nyingine ndio hiyo..mume wangu usijivunge, huyu  binti umempenda…’akasema na watu humo ndani wakataka kucheka,



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Hapana mke wangu huko umefika siko…hapana, …hayo ni mawazo yako…’akasema





    ‘Sisi tutaendelea kulijadi kama mke na mume, lakini maamuzi yangu ni hayo, leo hii huyu binti ataondoka na baba, na ni lazima wewe umtafutie njia ya kujikimu huyu bint, ndio ni mimi nimleta, lakini sikumleta hapa li mumuzalilishe, na adhabu ya kuzalilisha watoto wa watu ni nini…au hujui kuwa huyu naye ni mtoto wa watu…uwajibike kwa hilo..Baba nakuomba unisaidie, sikutupii mzigo, naomba unielewe hivyo, tutazidi kuliongea hili na kulifanyia kazi..’akasema akimuomba baba yake.





    ‘Aaah, mimi sina tatizo, kuna nafasi kubwa kule kwangu, atakaa ila naomba iwe ni kwa muda, kama ulivyosema, mume wako anahitajika kuwajibika, basi atawajibika, au sio mzee mwenzangu..?’ akasema huyo mzee akimuangalia mzee mwenzake.





    ‘Eeeeh, yeye atajifunza kwa kupitia njia hiyo, lakin hilo la kuoa, aah, sijui ni yeye mwenyewe, hapo kuna mtego, lakini kama hajatulia, tutamsaidia vipi,..ila la kuoa bado sijaliafiki, ila kumuhudumia huyo binti ni kazi yako mwanangu, na ushukuru kwa hilo, ni wapi utampata mke mwenye hekima kama huyu…ila usije kulichukulia hili jambo kijuu juu, ikawa ndio umepata nyumba ndogo,..huu ni mtihani kwako..kama ni kuoa uoe, sio nyumba ndogo, …’akasema huyo mzee.





    ‘Nyumba ndogo hata mimi ndio siikubali, ndio maana nimempa nafasi hiyo, kama anataka kumuoa, amuoe, tujue moja, na kama hataki anajivunga huku nafsi inatamani, lazima huduma zimfikie huyu binti,, ni dhamana tuliyokabidhiwa,..ichukulie hii kama ni adhabu kwako kwa kumzalilisha binti wa watu, na jiulize je kama ulipana begu zikaota, itakuwaje, hapo iliwazie kwa makini …huyu binti wa watu ana kosa gani, mim inaniuma sana kuchukua hatua kama hii, lakini najihami, ..hili ni tatizo ..mume wangu hajijuai tu..na kwa hili hata akija ndugu yangu wa kike humu ndani,, itabidi nifikirie mara mbili tatu…’akasema.





    ‘Mke wangu umefikia huko, huniamini tena…’akalalamika.



    ‘Sio swala la kuaminiana hapa, imetokea mara ngapi, huyu ni binti wa pili unamfanyia hivyo, huo sasa ni  ugonjwa, ni tatizo ulilo nalo, je akija mdogo wangu wa kike na yeye ukimtamani, usiku itakuwaje, ….hahaha, sio kwamba nacheka kwa furaha, lakini hili ni tatizo, na naomba mungu atujali tuwe kulipatia ufumbuzi wake, bila kufanya makosa ….naogopa sana, tukitoka hapa tunakwenda kumtafuta dakitari, na …jingine .nitafanya uchunguzi  wangu, mungu akipenda, nitakuja kuwapa matokea yake kama ni lazima…’akasema .





    ‘Mimi naona hapo tumemaliza…’akasema kiongozi wa dini.





    ‘Tunakusikiliza wewe…’akasema mzee na baba mwenye nyumba akamuangalia kiongozi huyo wa dini, kama vile anasubiria hekima zake za kumuokoa kwa hilo.





    ‘Unajau hakuna kitu kigumu na rahisi kama kutatua kesi ya wanandoa, lakini ugumu wake na urahisi wake unategemea na wanandoa wenyewe,…mara nyingi, sisi tunatakiwa kuwasikiliza wanandoa, na ni muhimu kila mmoja ukampa nafsi yake, mimi nimependa maamuzi ya huyu mama wa nyumbani...'akasema



    'Japokuwa baba wa nyumbani anaona ni gumu sana kwake.., lakini hebu jaribu kulifanya kwanza kama mlivyokubalina hapa ili uone matokea yake, huenda ni heri kwenu, na tumuombe mungu iwe hivyo, mimi naona utafanikiwa tu,,maana binti wa watu akiendelea kukaa hapa, na haya yakiendelea kutendeka, ni dhambi kubwa sana, kazi iliyobakia ni nyie watekelezaji, mzee, ondoka na huyo binti, ili ulete amani kwenye hii ndoa, na..mambo yakikaa sawa, anaweza kurudi tena, …’akasema kiongozi wa dini.





    ‘Lakini wazee wangu, mimi naliona hili kuwa halijakaa sawa, naona kama mke wangu ananitega…’akasema mume wa familia.





    ‘Ni kazi yako sasa kuweka sawa hilo wewe ni mume…liweke sawa lisiwe ni mtego kwako, uwe na hekima za kuitunza ndoa yako, na hapo hapo,….uhakikishe huwaumizi wasio na hatia kama huyu binti wa watu, inasikitisha sana kwa haya yaliyotokea, hili sasa lipo mikononi mwako….’akasema kiongozi wa dini sasa akianza kuondoka.





    ‘Sawa, sina jinsi, nitafanya kama alivyotaka mke wangu, lakini sio kwa kuoa,..mimi bado nampenda mke wangu, haya yaliyotokea najua  ni mtihani kwangu,…nitaanza kuhangaika kumtafutia huyu binti sehemu ili aje kuishi na aanze maisha yake, nitajitahidi kufanya hivyo, nab ado tutaendelea kulijadili hili mimi na mke wangu, nawashukuruni sana wazee wangu…’akasema.



    *****************



    Mimi pale nikabakia nimeduwaa, sikujua ni nini kipo mbele yangu, sikujua ni nini hatima yangu, sikujua naenda kukabiliana na maisha gani huko mbele, lakini nikaona ni heri tu ,…maana kama hayo yaliyosemwa ni kweli, kuwa na mimi kumbe ilikuwa sio ndoto, ..hapo nikajihisi kama nimepakwa kinyesi, nilitamani nitoke pale nikaoge,…





    Lakini pia nikaona ni heri niondoke hapo, maana chuki zilishaanza kunijaa, kwa huyo baba mwenye nyumba, japokuwa kama walivyosema sio dhamira yake, pia chuki kwa kijana wake, aliyejifanya mwema kwangu kumbe usiku wananizalilisha,..





    Moyoni nilimuomba mungu anisaidie, kama kuna kosa kwangu, mimi sijui, ..namuomba mungu aniongoze kwenye njia sahihi, nisiwe sehemu ya mitihani kwa watu…nikajikuta nalia, nililia lakini kwa kujificha, na aliyenishtua ni baba wa mama mwenye nyumba.





    ‘Binti kajiendae tuondoke…’akaniambia, na nilipoinua kichwa nilijikuta nipo na huyo mzee, wengine walikuwa nje wakiagana,





     Baada ya hapo nikafungansha kile kilicho changu, na tukaondoka na baba mkubwa wa mama mwenye nyumba, machozi yalitoka sana nilipokuwa naagana na hawa watu, kwangu mimi pamoja na haya yote, niliwaona kama wazazi wangu…





    Mama mwenye nyumba akasema wakati naagana naye,…





    ‘Unaondoka, sio kwamba nakufukuza, lakini pia iwe ni fundisho kwako, najua kuna kitu umenificha, sasa ni juu yako, kama uliona mume wangu ni mbora kwako, ukamtetea, badala ya kusema ukweli wote, sasa utakuja kuona ukweli wa kusema ukweli, sikuombei mabaya, ila inatakiwa na wewe ukaayanze maisha, ili ujue maisha yalivyo na changamoto zake, na najua, hakuna baya lolote linaweza kutokea huko mbele.., ila likitokea usisite kuniambia, ila lisiwe kuhusu mume wangu au kijana wangu, kwasababu mwenyewe umekiri kuwa hawajakutendea mabaya,..sawa..kwaheri..



    Sikuweza hata kumuangalia baba mwenye nyumba machoni au kijana wake, sikuweza hata kuwasemesha, nilipitiliza hadi kwa mzee, ambaye sasa ndiye atakuwa mafadhili wangu, na safari nyingine ya maisha ikaanzia hapo…







    NB: Tukutana kwenye sehem uijayo, je itakuwa hitimisho la kisa hiki, au kuna muendelezo wake, ngoja nimuulize msimuliaji je huko kulitokea nini…kwani wakati ananihadithia hilo, alikuwa kambeba huyo mtoto, je huyo mtoto ni wa nani



    WAZO LA LEO: Dhambi ni dhambi tu, hata ukitenda kwa siri, ni dhambi!!



    Iweje tuwaogope wanadamu wenzetu, kwa kuchelea kuonekana tukitenda madhambi yetu…, tukidhulumu, tukiwanyanyasa, na kuwadhulumu haki zao mayatima na masikini…, tukiwanyanyapaa wasiojiweza na wazee kwa maneno ya kejeli kama vile na sisi hatutakuwa hivyo, ..tukiwadhulumu wafanyakazi haki zao, kwa vile sisi ni wamiliki au ni vingozi tuliopewa mamlaka hayo...nk

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



     Tunasahau kuwa yule aliyetuumba anatuona, hata kama tumejificha tukitenda  hayo madhambi , tukumbuke yeye aliyetuumba hana mapungufu tuliyo nayo sisi viumbe wake, anayabaini yote, ya siri na ya dhahiri.





     Tumuombe mola wetu atusamehe makosa yetu na atuongoze njia iliyonyooka





    Nilifika nyumbani kwa huyu mzee, ikiwa ni  makao mapya, niliyoambiwa yatakuwa ni y amuda, na humo nikakutana na familia nyingine, ikiwa ya watu wengi kwani mzee huyu alikuwa na watoto wengi tu, na wengi wao alikuwa akiishi nao, hawajaolewa…



     Ukaribisho wangu hapo ulikuwa wa maswali mengi, na yalianzia kwa mke wa huyo mzee, kumbe mama mwenye nyumba wa hapo, hakuwa na taarifa na ujioa wangu, na hata kama alikuw anao, huenda hakukubaliana nao,..na kauli yake ya kwanza naikumbuka sana ilikuwa hivi;



    'Naona umeniletea mke mwenza, maana nyie waume hamzeeki…’akasema mke wake akiwa kashika kiuno. Alikuwa mwanamke aliyejaliwa mwili, kwa unene, na huyu akikushika hupurukuti..tofauti na mume wake.



     'Mke wangu, ukisikia kisa na maisha ya huyu binti utamuonea huruma, hapa alipo ni yatima, na mbaya zaidi, tokea anakuwa mkubwa maisha yao yeye na mama yake ni ya umasikini, ya kuomba-omba,  mabarabarani, haya hilo lisitoshe, yule aliyemtegemea,kama mama yake alifariki dunia, kwa kuchomwa moto na wezi..inasikititsiha kwa kweli…’akasema



     'Mhh, na ukaona hapa ndio kituo cha kulelea mayatima au sio, sikatai, hilo ni heri, kama ningelijua mapema, na nikuulize tu,  na huko alipokuwa awali ilikuwaje, si ulisema yupo kwa yule bint yako unayemdekeza, kila anachosema unamkubalia tu…na hata hili nalo umemkubalia, hata bila ya kuomba ushauri wangu…’akasema



    'Mke wangu, huko kumetokea mtihani, ndio maana nimeamua kumleta hapa, na ni kwa muda tu, sikujua kuwa leo ninaweza kuja naye hapa….’akajitetea mume mtu.



    'Na iwe kwa muda,kweli, maana kama huko wamemshindwa, kwa jinsi nimjuavyo yule bint, basi kuna tatizo, huyu binti anaweza kuwa na …haya ngoja nisiseme mengi nikaja kuonekana nina gubu…’akasema mke wake.



     'Kwa huyu kiukweli hana tatizo, ila yaliyotokea huko ni mambo juu y auwezo wao, hayana haja kuyaselezea zaidi, tupo mbioni kulitatua hilo, najua litaisha na likiisha huyu binti atarejea huko, au tutamtafutia njia mbadala za kumuzesha, ili awe na maisha yake ya kujitegemea..’akasema



    ‘Hahaha unanichekesha kweli, wewe una watoto hapa, hawana kazi, umeshindwa kuwatafutia njia mabadla za kujiwezesha, leo hii uje kumtafutia huyu..mimi sijui, lakini ipo siri ndani yake, na itakuja kujulikana tu, nawafahamu sana nyie wanaume…’akasema mama huyo.



    ‘Mke wangu niamini…mkaribishe mgeni, hayo mengine tutaongea wenyewe..hiyo sio tabia nzuri ya kukaribsiha wageni…’akasema mzee huyo.



    'Mhh,..haya karibu mgeni samahani kwa lugha yangu, inabidi unizoee, kuwa mimi sina mzaha kwenye wajibu wangu, ukikosea, nitakupasha, na ikibidi nakutimua…na mume wangu, jingine ulisikie kabisa, mimi sitaki kufanyiwa majaribio, maisha yenyewe haya ya kuunga unga, kama umesema ni wa muda, na iwe hivyo,..sio kniletea mizigo humu ndani,mimi nimempokea mgeni kwa vile wewe ni kichwa cha familia, vinginevyo, …haya karibu mgeni…’akasema na kunipokea mzigo wangu.



     Basi nikakaribishwa kama ada, na kuanza kutambulishwa kwa wenyeji wangu, humo kulikuwepo na wasichana wa rika langu, niliwaona wengine wakiniangalia kwa macho ya kininyali, mpaka nikahisi vibaya, lakini niliona ni jambo la kawaida tu , kwani maisha yangu yamekuwa hivyo toka utotoni, kudharauliwa kukashifiwa, kunyanyapaliwa,…nikavumilia tu.



    Ila mimi nilijua hali kama hizo ni kwa watu wasiokuwa na uwezo, kumbe hata hawa watu wana tabia hizo,,…nilivumilia tu.., japokuwa kulikuwa na visa vya hapa na pale, vya mauzi, hata wakati mwingine nasingiziw vitu ambavyo sijavifanya mimi, niliendelea kuvumilia tu, nilijua mvumilivu hula mbivu, mpaka wakaanza kuchoka wenyewe, na baadae ikageuka kusifiwa tu.

    Nilishangaa tangu nifike hapo ile hali ya kuota ndoto mbaya za kukabwa, au majinamizi sikuwahi kuipata tena nikahisi huenda ni ile duwa na maombi tuliyoyafanya siku ile kabla sijaondoka pale nyumbani, na hata yule binti wa awali aliyetuambia mambo hayo, sikuwahi kuwasiliana naye tena, hali yangu ilirejea kama kawaida, nikawa nalala kwa amani, hilo lilinipa faraja sana…ila mara chache nilikuwa nikimuota mama yangu akinisihi nizidi kuwa na uvumlivu kwani mambo bado magumu, …

    ‘Mambo gani magumu mama, naona sasa nina amani licha ya hali ya hapa nyumbani, najitahidi kufany akama ulivyonielekeza…’nikamwambia kwenye ndoto.



    ‘Najua hilo, lakini mitihan yako ni mingi, uvumilivu wako ndio utakupandisha daraja, …usije kuhadaika maana mengi yanayokutokea sio dhamira yako,…ina maana yake…’akaniambia na nilipotaka kumuuliza swali jingine mara nikazindukana ikawa asubuhi, na asubuhi kwangu ni mchaka mchaka wa kazi, nasahau kila kitu kazi ni nyingi, lakini sikupenda kuziacha,…



    ‘Huyu mgeni ni mchapakazi kweli, hana muda wa kuongea au kubisna na mtu, ukimuambia kitu anakubali tu, na wakati mwingine anasingiziwa ubaya, yeye anakubali tu hata kama sio yeye aliyefanya, na kuomba msamaha…...mmh, kweli kajaliwa ..’wengine wakaanza kusema hivyo



    ‘Hata hivyo muwe makini naye…’mama yao akawaasa hivyo.

    **************m

    Siku moja nikiwa sokoni na wenyeji wangu mara nikahisi mtu ananishika bega, kugeuka namuona ni yule binti wa kule nilipotoka, akaniambia kwa ishara ni mfuate, nilishapigwa marufuku nisiwe na huyo binti, hata wakati natoka kule, lakini kwa hapo, nikaona nimfuate nisikie anataka kusema nini…

    ‘Unasemaje maana siruhusiwi kuongea na mtu…’nikasema

    ‘Hata mimi, najua tu…wameshachukia sana, lakini ukweli niwapasha,…sasa sikiliza unajua yule mjinga yupo hapa Dar…’akasema

    ‘Mjinga gani..?’ nikamuuliza

    ‘Si yule mchawi…..’akasema

    ‘Huyo aliyetaka kukuoa, au…?’ nikauliza

    ‘Ndio huyo huyo, kaja anaumwa kweli, sasa najiuliza vipi mchawi naye akaumwa…’akasema



    ‘Anaumwa nini…?’ nikauliza.



    ‘Mguu umevimba, utafikiri ana matege…’akasema.



    ‘Oh, maradhi hayo, ndio umeniitia hicho,…?’ nikamuuliza.



    ‘Hivi hilo waliona dogo  hata kama anaumwa, hashindwi kupaa usiku na kukujia, ila kuna kitu nataka kukuambia,..’akasema.



    ‘Kitu gani..?’ nikamuuliza.



    ‘Nilikwenda sehemu,..nikaambiwa wewe upo kwenye hatari kubwa sana,  unajua na nilipokutana naye kasema  wewe ipo siku utamtafuta, upende usipende….’akasema.



    ‘Hatari gani,..?’ nikauliza.



    ‘Na huyo mtaalamu kasema ukisubiria mpaka uanze kuumwa, ndio basi tena, utakwenda na maji…fanya juu chini uje tuonane kabla mambo hayajaharibika,...’akasema.



    ‘Ni hatari gani hiyo…?’ nikauliza na mara nikasikia nikiitwa, na yule mwenzangu akainama chini na kupotea kwenye makundi ya watu waliopo humo sokoni,hakutaka hao jamaa zangu wamuone, na mimi nikaguka na kuwafuta wenzangu.



    ‘Ulikuwa unaongea na nani..?’ nikaulizwa.



    ‘Yule ni msichana mmoja nilisoma naye…’nikadanganya hivyo kitu ambacho sikipendi, nilijisikia vibaya sana kudanganya hivyo nikawa natubu kimoyo moyo.



    ‘Achana nao, hao watakupoteza, na ukipotea utafute pa kwenda na nakuasa siku nikisikia umeharibikiwa, wala usisubirie kauli yangu, fungasha ondoka..maana nitakuumbua mpaka mitaa yote watafahamu…’akasema mama mwenyeji wangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    *************



     Siku zikaenda mwezi sasa unapita…, sikusikia lolote kutoka kwa huyo aliyekuwa mfadhili wangu wa awali, mama mwenye nyumba awali alikuwa kilalamika lakini siku zilivyokwenda akawa ananizoea maana niligeuka kuwa mfanyakazi wa ndani, kila kazi naifanya mimi, tena bila kulalamika au kulipwa chochote.



    Nilianza kutokujisia vyema, japokuwa nilijitahidi kuficha hiyo hali,..ilikuwa kama kitu kigeni kuingia mwilini mwangu, sikuzoea kuumwa umwa, na nikiwa nyumbani na mama mara nyingi nikijisia kuumwa mama alikuwa akinipatia miti shamba, natafuna, hali inapotea, lakini hii hali ilikuwa ngeni kwangu, sijawahi kujisikia hivyo kabla,.. siku zilivyozidi kwenda hali ikazidi kuwa mbaya, nikaanza kuzidiwa, najisikia vibaya, siwi na hamu ya kula, kizunguzungu…mpaka siku moja nikadondoka na kupoteza fahamu..



    Nilipozindukana, wakawa wanajiuliza



    ‘Au ni hiyo hali aliyokuwa nayo ya kuota majinamizi..?’ wakaulizana



    ‘Tumpeleke tena hospitalini..?’ wakaulizana



    ‘Hapo kuna mawili, …nina wasi wasi na huyu mtu, hivi hamuoni anavyonawiri,..kunenepa gani huko, …’sauti ikasema

    ‘Wasi wasi wako mama, ….mimi naona …’akasita aliponiona najitingisha, kuashiria nimezindukana, na wakanisaidia nikaa vyema, wakaniuliza najisikiaje, niwajibu sasa nina nafuu, ni kichwa tu kinauma, wakanipatia dawa za mauimvu ya kichwa. Baadae hali ikawa nzuri tu.



    Baadae baba mwenye nyumba akafika wakamuelezea hali iliyonitokea na yeye akauliza kwanini sikupelekwa hospitalini…



    ‘Kwasababu alipozindukana, akasema hajambo, na mpaka sasa anaendelea vyema, haina haja ya kumpeleka hospitali tena, kwani bado yupo kwenye dozi, dawa za awali bado hajazimaliza…’wakasema



    ‘Sawa hebu muangalieni, kama hali hiyo ikitokea tena, basi ni muhimu tumuwahishe hospitalini…’akasema baba mwenye nyumba.

    **************

    Siku zilivyozidi kwenda nikawa sasa ni mgonjwa kweli…

    .

     Kuumwa kukawa tatizo sasa, hata nilivyojaribu kujificha nisionyeshe hiyo hali, lakini ilifikia mahali sasa nashindwa, nikifanya kazi kidogo kizunguzungu,  najisikia vibaya-vibaya tu, kula inakuwa ni shida, kutapika kukaanza, nikawa sasa mtu wa kitandani hapo nikaanza kuonekana ni  mzigo.



    'Mama huyu mgeni nahisi sasa ni mzigo kwetu, kwanini haponi, mlimpima magonjwa yote..?’ akauliza binti mmoja akiongea na mama yake, na waliongea baadae baba mwenye nyumba alipokuja mama akalifikisha kwake, na mazungumzo yakawa hivi…



    ‘Huyu binti kuumwa kwake kumezidi….’akasema mama mwenye nyumba.



     'Anaumwa kama binadamu wengine au sio, binadamu  yoyote kuumwa ni kawaida au…’akanitetea baba mwenye nyumba.



     'Hapana hii hali sio ya kawaida, mimi ni mwanamke na mtu mnzima, huyu bint tunatakiwa tumuhoji vyema kuna jambo …’akasema huyo mama mtu mnzima.



    'Kwani unahisi ana nini, nakumbuka ulishaanza kumsifia kuwa ni mfanyakazi mnzuri wa hapa nyumbani ana Tabia nzuri tofauti na ulivyofikiria awali, sasa imekuwaje, au watu kama hawa hawatakiwi kuumwa, mke wangu tuwe makini na wanadamu wenzetu…’akasema baba mwenye nyumba hiyo.



    'Sio swala la kuumwa tu, na siwezi kusema hisi zangu kwa sasa, hebu jaribu kuongea naye, umuulize ana tatizo gani, labda mimi nikimuuliza zaidi atasema ninamuonea,…jana nimejaribu kumdadisi, lakini majibu aliyonipatia, nahisi hajielewi,..huu ni mzigo na mtihani, na mimi msimamo wangu upo pale pale…’akasema mama huyo



    ‘Kwani una mashaka gani na huyo binti mke wangu, tumempa dawa,..si alipima akaonekana ana malaria wengi tu, ana UTI, ana…typhoid, magonjwa yote hayo yameonekana mwilini mwake,…sasa ngojeni amalize dozi tuone matokeo yake kwanza, tukikimbilia hospitalini atazidi kupewa madawa mengine…’akasema baba mwenye nyumba.



    'Hata akimaliza dozi, tatizo hilo halitakwisha, ndio maana awali  nilikuuliza huko alipotoka, aliondokaje huko au kuna kitu unanificha mume wangu..?’ akauliza mama mwenye nyumba.



     'Kwani kuna nini unahisi kwanini huaniambii, mimi nitakuficha nini, huko alipotoka tatizo ni kuwa likuwa ikifika usiku anaota ndoto mbaya,  za majinamizi, watu usiku hawalali, ndio wakaona tumlete hapa tuone kama hiyo hali itarudia au tatizo ni nini, na baadae mambo yakikaa sawa tutamrejesha huko…’akasema.



     'Una uhakika na unachoniambia au ni mbinu za kufiachia uovu wenu, kuna nini kilitokea huko alipotokea, mkwe wako alifanya nini,..niambie ukweli mume wangu , maana ukinilazimisha nikagundua ukweli kwa njia nyingine kiukweli hatutaelewana humu ndani, mimi sitkauwa na subira tena, ataondoka humu ndani, hata kama ni usiku…’akasema huyo mama kwa ukali.



    ‘Mke wangu kwani kuna nini, kwanini wewe huaniambii, una hisia gani kwa huyo binti, kwani ukiniambia mimi kutakuwa na tatizo gani…kwani ulipompeleka hospitalini walimpima ni na nini..?’ akaulizwa.



    ‘Niliwaambia wampime magonjwa  ya kawaida tu, kama malaria na hayo mengine, kwasababu nilimuhoji kwanza, nijua kama anaweza kuambukizwa magonjwa mengine  aliniambia hana uhusiani na wanaume, mimi nilimuamini kwa vile ulivyosema, kuwa ni mkweli na muaminifu,…kwahiyo mimi sikuwa na mawazo ya tatizo jingine lolote…’akasema

    ‘Kwahiyo kwa vile katumia dawa haponi, unahisi kaambukizwa magonjwa mabaya,kwa muda mfupi namna hiyo unaanza kumuhisi hivyo, kwani sisi hatujawahi kuumwa zaidi ya mwezi, na baadae tukapona, mke wangu acha hisia mbaya hizo..?’ akauliza baba mwenye nyumba.



    ‘Kwa hali aliyo nayo naweza kuhisi hivyo na vinginevyo…, mimi sijui lakini, muhimu ni vipimo vitasema, na nakuona una kwepesha kwepesha ukweli, haya kesho tumpeleke hospitali, ukweli utagundulikana huko…’akasema huyo mama mwenye nyumba.



    ‘Basi wewe umpeleke tu, utaniambia majibu yamekuwaje,..na hata hao madakitari watakushangaa, ndio katoka kupimwa, akaonekana ana malaria, sasa wamrejesha tena,…sawa kwa vile unataka kumjua afya yake zaidi sio mbaya, kwanza kipimo hicho siku hizi ni bura tu…’akasema mume mtu.



    ‘Mume wangu, na umri huo hujanielewa nina maani gani…, basi kesho inabidi tuongozane, maana naona hutaniamini, hata nikija kukuambia, hahaha, wanaume bwana mnaogopa kuumbuka eeh, hapo hapoo mtakuja kujieleza, ni nani, …’akasema mke mtu…



    ‘Kwanini tuongozane mimi na wewe, ..kwani mkienda wewe na yeye kuna ubaya gani..au hata kaam unaona anaweza kuzidiwa unaweza kuondoka nab into yako mmoja au unasemaje?’ akauliza.



    ‘Nataka uwepo wewe mwenyewe, umuwakilisho huyo anayehusika, au kama ni wewe, au mkwe wako, au yoyote, uweze kumuelezea vyema atakavyosema docta, maana mimi sitaweza kuwa naye tena..kama ni hivyo na nin auhakika ni hivyo, sisi tukitoka huko anakuja kufungasha virago vyake kwaheri ya kuonana…’akasema mama mwenye nyumba.



    ‘Mke wangu mbona sikuelewi…’akasema.



    ‘Utanielewa tu hiyo kesho…, mimi sitaki mzigo hapa nyumbani, .., unaona hawa mabinti, nilishawapa somo, na wakiona tumelikubali hilo kwa huyi binti, wataona kumbe eeh, ni kawaida tu…, wataambukizwa, na matokea yake tutakuwa na mizigo mingi humu nyumbani,..tuna bahati yamabinti sasa isiwe kugeuka badala ya neema ikawa ni …aah,.. hilo mimi silitaki, nilishawaambia atakaye fanya uchafu wake huko nje.., asije kuniletea matatizo humu ndani, unakumbuka kila siku tunawaasa mabint zetu,  …sasa wewe unataka kulianzisha, hivi utaweza kuibeba hiyo mizigo…’akasema.



    ‘Mizigo gani mke wangu… atapona tu huyu, hizo ni hisia zako tu, huyu binti kwa maelezo yake hana hata tabia chafu kama hizo..labda awe kaambukizwa na sindano…vinginevyo, sijui…maana huwezi kumsemea mwanadamu mwingine,..ila mimi nina uhakika ni maradhi tu ya kawaida, atapona...sizani kama wamemuambukiza hao…’akasema.



    ‘Hao akina nani..?’ akauliza mke mtu.



    ‘Maana mle ndani alikuwa hata kutembea hana tabia hiyo, alisema hana hata rafiki mmoja wa kiume, sasa ataambukizwa magonjwa hayo na akina nani…au unataka kusema nini, kuwa ndugu zetu hao wana maradhi ya kumuambukiza huyu binti, hapana wale ni watu safi kabisa…’akasema.



    ‘Unafikiria hayo tu eeh, maana unataka kumtetea mkwe wako au sio..au yule kijana wao, maana yule kijana wao naye, siku hizi kabadilika sana, suruwali zinavuka tu..hajisumbui kuzipandisha, anatuonyesha chupi yake, hizi tabia nyingine za kuiga, hazina hata maana, wenzao wanafanya biashara za kutangaza chupi, na mauchafu yao yaliharamishwa, wao wanaona ni fasheni…, ile ni tabia mbobu kabisa, ..mimi humu ndani sitaki mchezo huo, wakiniletea wanaume kama hao nitafukuza…’akasema na mara nikatokea, wakanyamaza.



    ‘Mhh..lakini mbona ana mwili wake tu, hajakonda..’baba mwenye nyuma akasema nilipopita.



    ‘Kesho utalijua hilo vyema, mimi sikosei,…hali hiyo ishajionyesha haina kificho tena… huyo binti kaukwaa, na …kama ni zezeta, hatajua wapi alipoubebea huo mzigo…’akasema mama mtu na baba mtu sasa akainama kama anawaza jambo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Usiwaze sana,…kama na wewe ulipitia kidogo, usubirie haki yako… maana baada ya vipimo, siwezi kukufanya uwe unawaza hivyo zaidi, nataka mume wangu uwe na raha, tuwe na maisha yetu na watoto wetu, huo ndio mzigo wetu halali, ..sio kubebeshwa mizigo mingine  ambayo haipo kwenye bajeti yetu, unasikia sasa kama ni mzigo wako, utajua mahali pa kuupeleka…’akasema.



    ‘Sawa kesho tutakwenda huko hospitalini kupima, maana kwa hivi hatutaelewana…, lakini nilikuwa na mipangilio yangu mingine, unajua kesho ndio i siku ya kwenda kuonana na huyo mkwe na binti yetu kule alipotoka huyu binti…nataka , nijua kama wamefikia wapi, kwasababu wamekuwa kimia, ..sijui wana mipangilio gani, lakini sio tatizo..tutakwenda na nikitoka huko nitapitia huko mara moja.,…’akasema.



    ‘Utapitia au utakwenda naye…?’ akasema kama anauliza.



    ‘Hapana itakuwa sio vizuri, kwa vile anaumwa, hapan, huyu mpaka apone, na kama wameshamtafutia sehemu, bado atakaa hapa mpaka apone, ndio ubinadamu…’akasema mume mtu.



    ‘Sasa hapo utaamua moja, mimi niondoke au huyo hawara wenu aondoke…hilo sina mjadala nalo, kwetu bado kupo, unasikia, kama ulinileta mke mwenza, umtafutie sehemu yake mpaka hapo kitakapojulikana, unasikia, mzee wewe, utaumbuka kweli,..haya wewe jifanye msiri…’akasema mke mtu na mara simu yam zee ikalia, na alipoangalia akasema.



    ‘Haya, hao wananipigia simu, nahisi wameshapata sehemu au wameamua kumchukua tena akakae nao, subiri niongee nao…’akasema akiweka simu hewani.



    ‘Hahaha ..mnajidanganya wenyewe



    WAZO LA LEO: Katika maisha jitahidi sana kupende wengine, chuki iwe mwiko kwako,  usisubiri wewe kupendwa, kwani yupo anayekupenda kwa vyovyote uwavyo, yeye kakubariki neema zote ulizo nao.



     Jitahidi kusaidia wengine kwa kadri uwezavyo, hata kama una kidogo tu..na usitegemee wewe kuisaidiwa na wengine, kwani ukisaidia wewe hata kidogo,… mola wako atakuzishia barak..na utazidi kupata na kuzidi kusaidia zaidi. Kwani usiposaidia, itafika muda utakuwa hunacho kabisa, na hapo utakosa wa kukusaidia kabisa.



     Jitahidi kusamehe hata kama wewe ndiye uliyefanyiwa ubaya, kwani kusamehe, kunavuta heri nyingi, kamwe wewe usisubiri kusamehewa kwa wale wliokukosea, ..ukumbuke ukisamehe, yupo yule ambaye atakusamehe, siku ambayo msamaha ni kwake tu.





     Tumuombe mola atupe iman thabit ya kumcha mola wa kweli, na kuwa mbali na unafiki, kwani unafiki ni mbaya zaidi ya ubaya.





    ‘Sasa hapo utaamua moja, mimi niondoke au huyo hawara wenu aondoke, kama ikigundulikana kama ninavyofikiria mimi, basi utachagua moja kati ya hayo mawili... unasikia, mzee wewe,...'ilikuwa kauli ya mama mwenyeji akimuambi mume wake kabla hatujafika hopsitalini.



     Tuendelee na kisa chetu..



                                                               ***********



    Waliongea wenyewe huko bila kujua ni nini kimekubaliwa, ila subuhi ndio nikaambiwa nijiandae kwasababu nitakiwa kuepekwa hospitalini,…’nikaambiwa.



    ‘Na kule kwa wafadhili wako wa awali, wamepiga simu na kusema kuwa bado mambo hayajakaa sawa, kwahiyo wameomba niendelee kukaa na wewe hapa hadi muafaka utakapopatikana…’akasema mzee wa hapo



    ‘Lakini mimi siumwi kwasasa najisikia nafuu kwa sasa..na kwa vile zile dawa nilizopewa awali bado zipo, naona ni bora niendelee kuzitumia,, sioni ni kwanini twende huko hospitalini nikapewe madawa mengine zaidi…’nikasema.



    ‘Hapana inabidi tukupeleke ukachunguzwe vizuri afya yako, huenda kuna tatizo jingine limejificha, huko kuanguka-anguka sio kuzuri, unajua kizungu zungu, kinaweza kuwa ni sababu ya matatizo mengi, sasa ni tatizo gani, hatuwezi kulijua mpaka ukapimwe, …na vipimo ndio vitasema,…’akasema mzee.



    ‘Sawa, lakini mimi sikuona sababu ya kwenda huko, na mara nyingi mimi nikiumwa natumia dawa za miti shamba na zinanisaidia, hazi dawa za hospitalini zinaniongezea matatizo tu…mimi najua dawa zangu, kama tukienda kwa wauza madawa ya kienyeji nitawaonyesha…’nikasema



    ‘Hapana hayo matatizo, kama malaria, huenda una upungufu wa damu, au shinikizo la moyo, halihitajii madawa ya kienyeji, usiwe kama wazee, wao walifanya hivyo kwa vile hakukuwa na hospitali, au hospitali zipo mbali, hapa hospitali zipo….’akaambiwa



    ‘Sawa mimi nawasikiliza nyie, kama siwatii hasara, basi, mimi nipo tayari twendeni…’nikakubali tu kwa shingo upande.



    Tuliondoka hapo nyumbani mimi na baba na mke wake,…namuita hivyo baba kama wenzangu walivyozoea kumuita,…na hatukuchelewa tukafika hospitalini, wao wakongea na docta na nikachukuliwa vipimo vya damu , choo na mkojo, na tukaambiwa tusubiria nje, na tulipokuwa tunasubiria mama akamuona rafiki yake mmojwa, wakawa wanaongea, na baadae wakasema wao wanakwenda kumuona mgonjwa aliyelazwa hapo, kama nikiitwa kabla hajarudi tuende mimi na baba, basi mimi nikabakia na huyo mzee tukisubiria majibu ya vipimo.



    ‘Usiwe na wasiwasi kabisa…, kama ulivyoniambia ni kweli, basi hakuna jambo la kuhofia…au sio, kama ni kweli lakini, nilikuambia awali, usinifiche kitu, nichukulie mimi kama baba yako,…unasikia,..na kuja kwtu hapa ni utaratbu wa kawaida tu wa kujirizisha, ni muhimu ukaijua afya yako, sawa, kwahiyo usiwe na mawazo na wasiwasi…’akasema.



    ‘Kwani mnataka kujua ni nini zaidi baba..kuwa labda nina..tatizo gani..?’ nikauliza



    ‘Hapana, sio kwamba tunahisi kuna tatizo kubwa,lakini ni vyema upimwe, hakitaharibika kitu ukipimwa, …’akasema



    ‘Sawa baba, basi Itakuwa vizuri, ili mjirizishe nafsi zenu, maana naona mna wasiwasi sana na mimi, na kiukweli hata mimi naona iwe hivyo, maana sijawahi kujisikia hivi kabla, ..’nikasema.



    ‘Umeona eeh, sasa vipimo ndivyo vitasema ukweli, …nikuulize tena,..umesema hujawahi kuwa na rafiki yoyote wa kiume, niambie ukweli, hili ni mimi na wewe, kama yupo wewe usiwe na wasiwasi na mimi nitajua jinsi gani ya kukulinda..?’ akaniuliza.



    ‘Sijawahi kuwa na rafiki yoyote wa kiume mzee wangu, niamini kweli kabisa, kama angelikuwepo ningelikuambia wewe nakuamini sasa kama baba yangu,…mimi sina tabia hiyo,  mama alinikataza kabisa alipokuwa hai, na siwezi kuvunja ahadi ya mama yangu..’nikajitetea.



    ‘Basi kama ni hivyo itakuwa vizuri sana, mimi nimemuambia mke wangu haina haja ya kuwa na wasiwasi, wewe ni binti mwema kabisa,nimechukua dhamana kwako, ..na nikuulize kitu kingine labda kuhusu zile ndoto, si ulisema hujaota tena, tangia uje hapa kwangu, au sio… je kule ulipokuwepo, una uhakika ilikuwa ni ndoto tu, maana hapa unatakiwa useme ukweli wote, docta takuuliza yote hayo, kama kutatokea tatizo lolote, japokuwa kama ulivyoniambia ni kweli hakuna tatizo,....’akasema huyo mzee.



    ‘Kweli kwa vipi baba…, ilikuwa ni ndoto tu, kama kuna jingine mimi sijui, na kwa vipi, kwani ndoto inaweza kuwa kweli baba, maana haya sasa yananitia mashaka..?’ nikauliza.



    ‘Unajua bint  nyie wanawake mna mitihani mingi, …sasa ukiwa msiri sana, unaweza ukaficha tatizo likaja kuwa kubwa,…mkiumwa maradhi kama hayo,…, kuna mambo mengi sisi kama wazazi tunayafikiria, lakini usijali, kipimo kitasema ukweli, nia ni kuondoa mashaka , hasa kwa mama yako, mimi nina imani hauna tatizo lolote jingine…’akasema.



    ‘Tatizo kama lipi, analonifikiria yeye, naona kanihoji maswala mengi akinihisi labda mimi ni wanaume, baba mimi sina tabia hiyo kabisa, na wala siyajui mambo hayo, sijui anataka kujua nini..?’ akaniuliza na mara tukaitwa, kuwa vipimo vipo tayari na mama mwenyenyumba alikuwa hajarudi,ikabidi tuingie na huyo mzee, na docta alipotuona tupo wawili , akamuuliza mzee.



    ‘Huyu ni nani wako?’ akauliza



    ‘Mimi ni baba yake mlezi….’akasema, sijui kwanini hakusema babu, lakini ndio hivyo, hata mimi nimezoea kumita baba

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Je huyu binti ameolewa..?’ akauliza docta, hapo nikahisi mwili ukinisisimuka, maana haya maswali ya kuolewa, mchumba, mbona yanazidi kuwa mengi.



    ‘Bado hajaolewa, na wala hana hata mchumba, kwani kuna nini umegundua docta…?’akasema na kuuliza.



    ‘Je ana rafiki yoyote wa kiume…anayetambulikana..?’ akauliza na hapo mzee nikamuona sura ikimbadilika, na haraka akasema;



    ‘Hapana, hana, nimekuambia huyu binti hana rafiki wala mchumba, hana tabia hiyo kabisa…kama vipimo vyenu vinasema kweli hamtagundua jambo lolote la mahusiano…’akasema mzee na docta akaniangalia usoni, halafu akamgeukia mzee, na kusema;



    ‘Kwasababu hiyo mzee, mimi nakuomba utupe nafasi kidogo, nataka kuongea na huyu binti peke yake, tafadhali ….’akasema docta.



    ‘Lakini mimi ndio mlezi wake, nilitaka kufahamu ana tatizo gani, yeye kasema hana tatizo, …..ndio maana nikajitolea kumleta mimi na mke wangu, sasa ukisema unataka kuongea na yeye tu , basi tungelimuambia aje peke yake..’akasema mzee.



    ‘Sawa naelewa hilo…, lakini kuna mambo ya kitaalamu zaidi nataka kuongea na huyu binti akiwa peke yake, kuna maswali naweza kumuuliza akashindwa kuyajibu kwa vile wewe upo hapa….’akasema na mzee  akaelewa na kusimama ili atoke nje, nikamuona kama anasita sita, halafu akasema;



    ‘Basi ngoja nimuite mama yake aje… kama ni mambo ya akina mama zaidi…’akasema mzee akiharakisha kutoka nje.



    ‘Usijali mzee, haina haja kumita yeye,…, nitawaita wote nikimalizana na binti, ni bora niongee na yeye tu kwanza, sio tatizo kubwa..ni jambo jema tu, usiwe na wasiwasi mzee.’akasema na mzee akaondoka, na mlango ukafungwa.



    ***********

     .

    Docta akasimama na kusindika mlango vizuri, mimi pale nikawa na wasiwasi, kukaa chumba na mwanaume halafu ndio kafunga mlango kabisa, moyo ukaanza kunienda mbio, najiuliza huyu mtu anataka kunifanya nini, nilishajipanga kupiga ukelele, kama lolote litatokea,…docta akahisi nina wasiwasi. Kwanza akarudi kwenye kiti chake na kukaa, halafu akaichukua ile karatasi ya vipimo, akawa kama anaisoma, halafu akasema;



    ‘Afya yako haina matatizo, huna maambukizi yoyote, ni uchafu kidogo tu kwenye mkojo, itabidi uendelee na hizo dawa ulizopewa awali, si bado unaendelea kuzitumia hizo..?’ akaniuliza, akiongea kwa lugha nyepesi kuniweka sawa.



    ‘Ndio bado naendelea kuzitumia, niliwaambia haina haja ya mimi kuja huku, lakini sijui wana wasiwasi gani…’nikasema.



    ‘Lakini hawajafanya vibaya, unajua ukipatwa na tatizo, hata kama huna tatizo ni vyema ukajenga tabia ya kuchunguza afya yako, yaonekana wazazi wako ni watu wema sana….’akasema



    ‘Nashukuru sana kwa kupata walezi kama hao….’nikasema



    ‘Mhh…unajua umri , ukienda, mwili nao unabadilika, na tabia ilivyo, kuna mambo yanakuja kujitokeza kwa kadri tunavyokuwa, hiyo ni kawaida,  kuna maswali machache nataka kukuuliza ili usije kupata matatizo kama hayo tena,…’akasema



    ‘Sawa niulize tu….’nikasema.



    ‘Mimi ni docta, na madocta ni wasiri wakubwa , kwa wagonjwa wao, usipomuamini docta basi wewe hutaki afya yako iwe njema, …nataka uniamini sawa, …’akasema



    ‘Sawa mimi nakuamini docta….’nikasema.



    ‘Niambie ukweli, unajua nilipokuwa shule, nilikuwa na rafiki wa siri, watu walikuwa hawalijui hilo, na wengi wanakuwa hivyo, na wakati mwingine kuna ule mchezo wa baba na mwana, tunajificha..na hata tunajikuta tunaanya mambo bila kutegemea…’akasema.



    ‘Mhh, mimi hata siku moja sijawahi kucheza hiyo michezo ya baba na mama…, docta maisha yangu na mama ni ya shida, sisi tulikuwa wakuhangaika barabarani kuomba, hatuna shamba, ni kibanda kidogo tu,hatuna jamaa , tulizaraulika....basi ni shdia, namshukuru mungu kuwa nimepata hawa wafadhili, na niliposikia kuwa mama kafariki, nilijua basi hata mimi nitakuja kumfuta tu…’nikasema.



    ‘Hapana wewe ni kijana na maisha yapo mbele yako, kamwe usikubali kushindwa, na matatizo iwe ni sehemu ya changamoto ya kupiga hatua mbele…, inatakiwa ufike mahali ujipange upate kitu cha kufanya ambacho kitakuingizia kipato, kama hivyo upo na walezi kama hao, wanakujali.. watumie, ujifunze jambo, ufundi, au kazi yoyote ya kuzalisha, ambayo itakufanya usimame kwa miguu yako mwenyewe, usikate tamaa kabisa…’akasema docta.



    ‘Sawa nitafuata ushauri wako docta…’nikasema.



    ‘Na kama nilivyokuambia, uniamini, kuna jambo nataka unifunulie kidogo, sio bay asana…, nataka uniambie kitu, kwasababu sote tumepitia huko, nata uniambie ni nani huyo rafiki yako wa siri..usiseme huna rafiki, kila mtu anaye…, hata awe siri,… unajua kuna jambo hapa, linatakiwa wewe nay eye mtibiwe pamoja, tunaweza kupanga mimi na wewe jinsi gani ya kumuita, hata watu wengine wasijue…najua unaye rafiki wa kiume, kwahiyo nilipenda tusaidiane kwa hilo, unasemaje…? Akasema.



    ‘Mhh docta, ina maana huaniamini, mimi sina rafiki hata mmoja wa kiume, na ..kwanini tena.., si umesema sina tatizo…au?’ nikauliza.



    ‘Ni kweli huna tatizo kabisa..umesema huna rafiki wa kiume, au mchumba, lakin inaweza kutokea, ujana una mambo mengi mimi naelewa, labda, nikuulize hujawahi kukutana na mwanaume, au kwa kulazimishwa au kwa namna yoyote ukakutana naye kimwili,..inaweza ikawa ni kwa bahati mbaya.?’ Akaniuliza.



    ‘Kukutana na mwanaume kwa vipi..hapana haijawahi kutokea, hapana wee, mama akijua hilo, yaani sio kwa ajili ya mama tu, mimi mwenyewe nimeahidi sitaki mwanaume, hadi hapo mungu atakaponiongoza, sitaki na sijawahi kuwa na rafiki mwanaume,..na hakuna, ..hata kushikwa kwa nguvu. Haijawahi kutokea kabisa, mimi sijawahi kukutana  na mwanume, sijawahi niamini docta..kwani kuna nini mbona kama kuna tatizo, niambie kama kuna tatizo?’ nikauliza.



    ‘Huwa inatokea kwa umri wenu, wenu, na ni vyema ukasema ukweli , maana ni vizuri sana hili swala likajulikana na wazazi wakajua, ndio maana nikata tuongee uniambie ukweli, ukificha, itakuwa vigumu kwako kusaidiwa, na mtu wa kukusaidia ni mimi, unajua sisi madocta kisheria tunatambulikana sana, pia mimi nipo kitendo cha kuwasaidia wanawake walio kwenye mazingira magumu, lakini siwezi kumsaidia mtu kama hasemi ukweli..’akasema



    ‘Docta unataka ukweli gani…?’ nikamuuliza



    ‘Unajua ukinificha, haitasaidia kitu, maana mimi naweza kukupima kuona kama kweli hujawahi kukutana na mwanaume, na itabidi nifanye hivyo kama utaendelea kunificha, bora useme ukweli ili tuanze sura nyingine, na ukificha, nitawaachia wazee wafanye kazi yao…’akasema.



    ‘Docta niambie ukweli, kwani mimi  nina tatizo gani, usinizungushe zungushe…’nikasema.



    ‘Una mimba…na kwa maelezo yako na vipimo, una mimba ya miezi miwili na kitu hivi hongera sana, lakini unanistajaabisha ukisema hujakutana na mwanaume unaona hapo, unajidanganya mwenyewe, sasa iambie ukweli ili niweze kukusaidia…’akasema.



    ‘Hongera, docta, unanitania, mimi mimba nitaipataje..’nikasema kwa hasira

    ‘Binti, usifiche, hili swala sasa sio la kuficha, unanielewe, inabidi umtambulishe huyo mwenzako ili muona jinsi gani ya kuliweka sawa, ukiendelea kuficha, wazee watakuelewa vibaya, kwa ushauri wangu umsema mapema, mimi nitakusaidi kuliweka sawa nikiongea na wazee wako…’akasema



    *************



    Docta aliponiambia hivyo, kwanza sikuamini, lkn jambo lililonijia akilini ni kuhakikisha kuwa wafadhili wangu hao hawaipati hiyo taarifa, na hata wakiipta niwe mbali kabisa na wao, wasije kuniona tena..



    'Tafadhal docta, nakuomba nipo chini ya miguu, unisitir na hii aibu…kama ni kweli..maana mpaka sasa mimi siamini….’nikasema.



    'Kwann unasema hivyo, kwani huna mume, huna mchumba, mimba hii umeipataje…haiwezekani, sema ukweli tu…’akasema.



    'Docta mimi sijui nakuambi aukweli mimi sijui… na ndio maana siamini, mimi sijawahi kukutana na mwanaume yoyote, nitapataje mimba, kwani mimba unaweza kuipata hata kwa kupitia kwenye ndoto..sio kweli docta…’nikasema



    'Docta kwanza akasita, halafu akauliza;



    'Unasema wewe hujawahi kukutana na mwanaume ila uliwahi kuota kuwa umekutana na mwanaume, na ukawa na dalili hizo za kukutana na mwanaume au sio niambie ukweli..?’ docta akauliza akionyesha uso wa kushangaa na kutokuamini maneno ya huyo binti.



    'Ndio docta,…huwaga naota hivyo, lakini sio hapo kwa sasa,  tena zilikuwa ni  ndoto za majinamiz hata sura ya huyo mtu sikuwahi kuiona, ni ndoto tu na sio kweli, mtu ananikaba, halafu nazalilishwa, ni ndoto na sio kweli…’nikasema.



    'Mhh, hili la ajabu eeh,… kwani awali ulikuwa unaishi wapi, na ulikuwa ukiishi na nani..?’ akaniuliza docta

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     "Ni hadith ndefu docta , ukitaka kuifuatilia historia ya maisha yangu utachoka....muhim, usiwaambie hao jamaa zangu, nakuomba tafadhali sana docta, nipo chini ya miguu yako, nitaumbuka mimi, na wala sina kosa, sijui ni nini hiki jamani, hivi mimi nina tatizo gani, jamani..mungu wangu nisaidie na mitihani hii…’nikasema nikiashiria kuomba kwa kuweka mikono kifuani na docta akawa ananiangalia kwa uso wa kushangaa kidogo.

    'Kwani hao jamaa zako ni nani kwako hasa….?’  Docta sasa akawa ana mashaka na mimi.



    'Ni wafadhili wangu tu, mimi sina baba wala mama, sina hata ndugu wa karibu, wao wamejitolea kunifadhili, na…awali sikuwa na wao, na baya zaidi ni kuwa hawa wafadhili wangu wakilifahamu hili, watanifukuza kama mbwa….nisaidia sana docta…’nikasema.



     'Sasa mimi sielewi, wewe ulitaka niwaambie unaumwa nini, maana kukusaidia kwangu ni kuwaambia hao jamaa zao jinsi gani ya kuhakikisha afya yako inakuwa salam, hadi muda wa kujifungua ukifika, sasa ukisema nisiwaambie, nitakuwa nafanya vibaya …’akasema docta.



    'Uwaambie ugonjwa mwingine wowote lakini sio kwamba mimi nina mimba, kwasababu hata mimi simini kuwa nina mimba, ni mimba ya nani wakati mimi sijawahi kukutana na mwanaume..’nikasema.



     Docta, akatikisa kichwa kutokukubalina na mimi lakin baadae akasema;



    ‘Sikiliza wewe nenda nje, waite hao jamaa zako waingine na mimi nitajua jinsi gani y akuongea na wao, na wala usiwe na wasiwasi, hakuna baya litatokea dhidi yako, niamini mimi..’akasema docta, na mimi nikawa sina la kufanya,nikatoka, na wakati natoka, nikagundua kuwa mama mwenye nyumba alikuwa hapo mlangoni, nahisi alikuwa akijaribu kuona kama atasikia ni nini tulikuwa tunaongea huko ndani.



    'Ehe tuambie ukweli, kulikoni masaa yote hayo…?’ akauliza mama mwenye nyumba

    'Amesema muende, atawaambia mwenyewe tatizo ni langu ni nini….’nikasema sasa nikikwepa hata kuwaangalia usoni.



    'Kwahiyo kumbe una tatizo, mbona baba yako kasema huna tatizo, ni mazungumzo ya kawaida ya kimalezi tu, kwa vile umekuwa, ..ooh, nilijua tu, una kitu wewe…’akasema baba mwenye nyumba.



    ‘Hakuna kitu mama, yote ni mitihani ya mungu tu..’nikasema kwa sauti ya kutaka kulia, nilijitahidi sana nislie nisje kuharibu , na baba mwenye nyumba, alikuwa mbali,akawa anakuja ili waungane na mkewe kuingia kwa docta, akanitupia jicho, lakini mimi sikuweza kumuangalia usoni.



    ‘Kwahiyo docta kasema twende ndani, mumemalizana kuongea…najua hakuna tatizo au sio, mama yako ana wasiwasi bure tu…’akasema baba mwenye nyumba.



    ‘Hahaha, eti hakuna tatizo, wewe unajidanganya bure, kuna tatizo, humuoni huyo binti alivyo….huyo ana tatizo, na ole wake, nigundue kuwa ni hivyo ninavyofikiria mimi, sizani kama kutakalika, sizani kama nitaweza kuishi naye tena, unasikia wewe mwanaume, huyo utamtafutia makazi ambapo mtaenda kukutana wawili sio nyumbani kwangu…’akasema huyo mama



    ‘Mke wangu kwani umesikia nini..mbona unanitia aibu…’akasema mume wake



    ‘Mimi nakutia aibu au nyie ndio mnatutia aibu sisi, familia yetu haina doa, tunahitajia kuijenga familaia yetu kwenye maadili safi, sasa wewe unataka kuleta doa, kwa kuleta watu wenye tabia mbaya..huyo bint ana mimba asitudanganey hapa…’akasema mke wake.



    ‘Eti nini, hapana hili sio kweli na haliwezekani, umasikia wapi hayo, kakuambia huyu binti…?’ baba mtu akauliza kwa mshangao, na jicho likamtoka kama kasikia jambo la kutisha



    ‘Unajifanya hujuiee,..wewe a utu uzima wako wote huwezi kuliona hili, mimi nilitaka tuje huku, il uhakikishiwe kitaalamu,wewe si unapenda hivyo, haya  twende huko ndani ukasikie mwenyewe, kwa octa, mtaalamu unayemuamini….’akasema na kufungua mlango.

    Baba mtu akawa kasimama, kaduwaa, hakuniangalia, akakatikisa kichwa, halafu akamfuata mke wangu huko ndani kwa docta. Na mimi nikatulia kidogo, halafu nikasimama, nikaanza kutembea kwa haraka kuelekea kitu cha boda boda, akili hapo ilikuwa sio yangu,..



    NB: Mdada anazidi kuingia kwenye mitihani, tuone jinsi gani watu wanavyoteseka,…

    WAZO LA LEO: Ukiona kwako kuna fuka moshi ujue kuna kwingine kunawaka moto.. Ukiona wewe una shida, una matatizo yanakuandama kila kukicha,…, ujue kuna mwingine shida hizo na matatizo ni zaidi maradufu ya matatizo uliyo nayo wewe. Wapo wengine hawaijui raha duniani, wapo wengine hawajui watakula nini,..wapo wengine kila siku ya mungu wanalia kwa mauimivu ya mwili na akili, ….



    Je hayo matatizo uliyo nayo ndio unafikia kukata tamaa…





    Ndugu yangu…usikate tamaa ya maisha ilimradi unapumua,.., mkabidhi mola wako matatizo yako, huku ukitafuta njia rahisi ya kufanikisha mambo yako, lakini iwe ni njia ya halali…tatizo wengine wanatafuta njia za haramu, ukitumia njia hizo, utakuwa unajipalia makaa..hutafanikiwa na ukifanikiwa itakuwa ni kwa muda tu. Tukumbuke wakati wote kuwa Mungu hamtupi mja wake, na kila mja ana riziki yake, ni namna tu ya kuitafuta riziki hiyo ,lakini iwe sababu ya halali. Tumuombe mola wetu atufanikishie malengo yetu halali na atujalie tuipate riziki ya halali, bila kuingie kwenye dhuluma..Aamin.



    Hutaamini wakati haya yanatokea hadi nafika hosp, na kuambiwa tatizo hilo, nilikuwa nimesahau kabisa yale aliyokuwa kaniambia yule mdada siku ile kule sokoni…, na baada ya tukio hilo, baada ya kutoka kwa dakitari, ndio kumbukumbu hizo zikanijia, kama vile mtu fulani ananikumbusha; …



    'Unatakiwa uwahi kabla hujaanza kuumwa, ukianza kuumwa, utakwenda na maji..’maneno hayo yakaanza kunirejea akilini, lakini nilishaanza kuumwa, je kuumwa huku ndiko alikomaanisha huyo mdada, nikawa najiuliza



    'Oh, kama ndio huko basi ...nimeshachelewa, ..'nikasema kwa sauti.



    ‘Hapana sijachelewa…hapana sijachelewa…’nikasema na kwa haraka nikasimama, sikutaka hata kusubiria tena.., sikutaka kuwasubiria wafadhili wangu hao, nilijua wakitoka humo, itakuwa kuumbuliwa, kwani huyo nikasimama alishaniambia;



     Kwa muda huo wafadhili walikuwa wakiongea na docta, na ilionekana walikuwa wakivutana huko ndani,



     'Bint, hili niachie nitajua jins gani ya kuongea nao, na watakusaidia tu, vinginevyo itabidi waeleze walichokufanyia



    'Docta, hawa wazee wa watu hawahusiki lolote na haya, walinichukua kutoka kwa wafadhili wa awali, ambapo labda ndio chanzo cha tatizo hili



     'Lakini hawa ndio watasaidia haki yako ipatikane, hawa ndio nitawatumia, upate huduma zote stahiki, hilo niachie mimi



     Nilijua sitaweza kumshawishi docta zaidi, ndio nikatoka na kuwaambia wazee wanaitwa ndani



    Tuendelee na kisa chetu.



    *****************



     Nilimuambia mwenye bajaji nataka kwenda wapi, akanitajia gharama, sikutaka hadi kujadiliana naye zaidi, nilikuwa na akiba ya pesa zangu, nikamwambia anipeleke huko kwa haraka sana, na yeye bila ajizi akaanza kuiendesha bajaji yake kwa mwendo kasi, hapo sikujali kama anaendesha kupitiliza mwendo wa kawaida..



     Njiani niliwazia ni nini nifanye, kiukweli akili ilikuwa haijakubali kuwa kweli mimi nina mimba, sikuamini hilo kabisa lakini ndio hivyo, vipimo vimesema mimi nina mimba, tena ya karibu miezi miwili…



     'Au ndio hiyo  hatari aliyosema yule mdada, labda sio mimba halisi, labda kuna kitu kingine tumboni..labda, oh sasa iliingiaje, ina maana wale watu walikuwa ni kweli, oh, mungu wangu..nitafanyaje mie…’nikawa naongea kwa suti ya chini kwa chiini…



     Niliwazia hivyo, na jinsi nilivyozidi kuwaza ndivyo nilivyozidi kujenga hofu akilini mwangu, mpaka nafika eneo hilo ambapo mdada huyo alinielekeza siku moja, nilikuwa nawazia jinsi gani nimeipata hiyo mimba, na mpaka hapo nilikuwa hata sijui nafanya nini au nitafanya nini, akili yangu niwahi, ….niwahi nini sasa, wakati kama nikuumwa nimeshaanza kuumwa, lakini kuumwa nini…



     'Tumefika dada yangu, si ndio hapa….?’ Akasema na kuuliza.



    'Sawa..'nikasema na kumpa pesa yake, na alipoanza kuniuliza maswali kuwa nina shida gani, mbona ninalia,  mimi sikumsikiliza nikaanza kutembea nikifuatilia ramani niliyoelekezwa na yule mdada, sijawahi kufika maeneo hayo kabla, ila mimi ni mwepesi sana wa kugundua maeneo ukinielekeza vizuri.







     Nilifika eneo hilo…ilikuwa sio sehemu iliyojificha, nikaona hiyo bara bara inayoingia kuelekea kwenye hiyo nyumba, na kwa mbele yangu nikaiona,….





    Ni  jumba la maana, nikajua ni wale wale…sio kwamba nawachukia hao watu, ila nazichukia tabia zao tu, wana uwezo lakini hawana huruma na watu kama sisi,.. ndivyo akili yangu ilivyonituma hivyo.





    Ilikuwa nyumba kubwa ni kama ili nyumba ya mfadhili wangu wa kwanza…, kuashiria kuwa ni mtu anayejiweza pia, moyoni nikasema;





    ‘Hawa watu sasa nitaachana nao, nitarudi mitaani tena…sijui itakuwaje, maana ni nani atanichukua tena na mimi nina mimba…oh …’nikajisema hivyo.

    .



    Nikafika mlangoni, na kabla sijagoonga nikajiuliza, hivi akitokeza mwenye nyumba, nitamuambiaje,…wakati najiuliza huku mkono upo hewani nikitaka kugonga mlango wa geti..huku akili bado inajilaumu kwa namna nyingine kuwa ni, kwanini nimefanya haraka kuchukua hatua hiyo, kwanini sikusubiria kwanza, huenda docta angeliwashawishi hao wafadhili wangu na kuafiki kunisaidia.





    ‘Hapana sio kwa yule mama, nahisi nikikutana naye atanitapia maneno mabaya…bora nitoweke kabisa na nisikutane no kabisa…’nikajisema hivyo,





    Ndio ile nataka kugonga geti, mara geti likaanza kufunguka, kwanza nilishtuka kuwa huenda ukilishika hilo geti hujifungua lenyewe, kumbe…. hapana, kuna mtu alikuwa anafungua kwa ndani, kwa haraka nikachepuka pembeni kujificha.. ili mtu wa huko ndani asinione.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Kumbe kulikuwa na gari linataka kutoka nje, hapo nikajiingiza pembeni mwa hiyo nyumba kulikuwa na barabara inayotengenisha geti la  nyumba hiyo na geti la nyumba nyingine,..kulikuwa na miba ya miti ya michongoma, lakini nikajilazimisha hivyo hivyo na kujikuta ninachomwa na hiyo miba, sikujali, ..





    Nilisubiria hadi lile gari likaanza kuondoka, na kabla halijaondoka,  nikasikia sauti ya kutoka kwenye gari, ilikuwa ni sauti ya kike, ikisema,…



    ‘Huenda jioni nikafika na rafiki yangu, hakikisha kila kitu kipo kama nilivyokuelekeza, sasa uanze kutanga tanga mitaani, au kuleta watu humu ndani….sitaki tabia hiyo,..unanisikia..na, nikute hujafanya hivyo nilivyokuelekeza, itakuwa ndio siku yako ya mwisho kukaa humu ndani, umenielewa….’sauti ya kike nzito ikasema, akiwa yupo ndani ya gari lake la bei mbaya.





    ‘Nimekusikia madamu…’sauti nyingine ikasema kutoka huko ndani ya geti,..sikumuona kwa vile nipo nyumma ya huo ukuta , ila nilihisi kutoakana na ile sauti atakuwa ni yule mdada niliyemfuata humo. Kumbe anamuita bosi wake madamu, nikatabasamu mawazoni, mimi kwangu nilizoea kuwaita mabosi wangu mama au baba.





    Nilisubiria kidogo,hadi lile gari likaondoka…. halafu nikagonga mlango wa geti, kukawa kimia, nikagonga tena, baadae mlango ukafunguliwa,..na mdada akajitokeza aliponiona akashtuka, halafu akaangalia kwa ndani na kusema;





    'Wewe umekuja huku, hata bila kuniarifu, hukusikia madamu alivyosema, huyo mama ni mkali kweli ungenipigia simu kwanza, ooh, halafu `sir…’  bado hajatoka, sasa wewe fanya hivi, kaa nje kidogo, ukiona gari limetoka ndio uje….unasikia, haya nenda….’akasema na mimi nikachepuka hadi sehemu nyingine inayoangaliana na hiyo nyumba, nikasubiria.





    Na haikuchukua muda, gari likatoka, na nikasubiria kidogo kidogo, gari likatoka na likapit akaribu yangu, na sijui ilikuwaje, mara likasimama, na kiyoo kikashushwa, hapo nikahisi mwili kunicheza, jamaa akatokeza kichwa na kuniangalia, hakusema kitu, akapandidha kiyoo, na kuendelea na safari yake,





    Alikuwa na maana gani, au aliniona wakati naongea na mdada pale getini, …nikajiuliza lakini sikuwa na muda wa kupoteza, muhimu nionane na huyo mdada, mengine yatafuta baadae.





    Nikatembea hadi kwenye geti nikagonga mlango na mdada akafungua geti, akaniambia…





    ‘Kumbe yule sir,… kakuona, alichungulia kwa kupitia dirishani, haya madirisha ya viyoo ukiwa ndani unaona nje, ila ukiwa njehuwezi kuona huko ndani…’akasema.





    ‘Sasa,..’nikauliza nikionyesha wasiwasi





    ‘Yule mbaba, hana tatizo, nimemuambia wewe ni rafiki yangu ulikuwa unapita tu, ukaona unisalimie,  na hakuniambia kitu, zaidi ya kusema niwe makini ….hana tatizo huyo mbaba wa watu, mwenye shida ni mama, akikuona humu ndani, atakutoa kama mbwa…’akasema.





    ‘Sasa…’nikasema tena hivyo





    ‘Niambie, kwanini hukufika mapema kama nilivyokuambia…’akasema.





    ‘Kwani ilitakiwa nifike haraka, mimi sikukuelewa siku ile, hata hivyo si unajua hizi kazi zetu, huwezi kupata mwanya wa kutoka, labda utumwe, na huko ndio ujiibe, na …ghfala nikaanza kuumwa…’nikasema.





    ‘Mungu wangu, lakini nilikuambia…uwahi kuniona kabla hujaanza kuumwa…’akasema akionyesha uso wa wasiwasi.





    ‘Kwani tatizo ni nini, haya mfani ndio ningewahi ungelifanya nini…?’ nikauliza.





    'Oh hebu twende ndani tuongee haraka, mabosi zangu wakitoka, kurudi ni jioni , labda kutokee dharura, lakini kuna kazi nyingi za kufanya ndani, tutaongea huku nachakarika, ..si unajue tena, mjibi hapa….na kuliko kukaa tu, wewe utanisaidia zile unazoweza au sio, lakini sio kwamba nakulazimisha, wewe ni mgeni wangu… ‘akasema akianza kufagia.





    ‘Mimi naumwa hata kukusaidia siwezi, we acha tu…’nikasema





    ‘Usijali, niambie sasa  imekuwaje, na umekuja kufanya nini, maana tuulizane mapema,  kama umeshaumwa mimi sina la kufanya, hilo nilikuambia mapema, usije kunilaumu…’akasema.





    'Mimi hata sijui nifanyeje hapo, ulivyoniambia mimi sikuamini ..unajua mimi siamini mambo ya kishirikina, mama alinikataza,…na sasa hapa nilipo nimechanganyikiwa… huko kwenyewe nimetoroka…’nikasema.





    ‘Mungu wangu, umetoroka, kwanini umetoroka,…wewewe… unataka kufanya nini, hawa watu ndio wanaotufanya tuishi hapa mjini..tusiishie mitaani na kuzalilika,…, ukitoroka huko utakwenda kuishi wapi, mimi siwezi kukupokea,, ulisikia madamu alivyosema,…sasa wewe lengo lako ni nini,…unataka kuishi tena mitaani, utapaweza na sura yako hiyo, labda kama unataka kujiuza….’akasema.





    'Wewe siku ile uliniambia nini, ni kutafute, sasa si ndio nimefanya hivyo….’nikasema





     'Sawa naelewa, nilikuambia hivyo… ujitahidi unione, lakini sio kwa kutoroka, maana ulivyofanya utajichongea, na kuniharibia hata mimi kazi yangu, na mimi sikubali kwa hilo..nayajua maisha ya mjini, sasa hivi hanidanganyi mtu, usipokuwa na kazi, huna kazi..utazalilika…, pili nilikupa tahdhari kuwa unione kabla hujaanza kuumwa, sasa umeshaumwa,..si ndio hivyo… na huenda ulipoteza fahamu au sio….’akasema.







    'Sawa sasa wewe niambie, ulitaka nikuone ili iweje, kuna maagizo, au  uliambiwa nina hatari gani itakayonipata…na kuumwa huko ni kupi, yawezekana nina tatizo ambalo halihusiania na hilo….’nikasema.







    'Umeumwa, una dalili za mimba, umedondoka na kupoteza fahamu, kama ni hivyo hilo ndilo tatizo lenyewe,…..’akasema.







    'Ndio nimeumwa, nikapoteza fahamu na sasa hivi natokea hospitalini, nimewatoroka mabosi zangu, huenda sasa hivi huko wananitafuta kama kweli wana nia njema na mimi , ila nijuavyo mimi, kwa kauli ya huyo mama mimi sitakwi tena kwenye hiyo nyumban, labda itokee miujiza, kwa baba kumshawishi mke wake…, hivi kwanini hawa akina mama matajiri wanatuchukia hivi…’nikasema







    'Kama ni hivyo umechelewa, hatuwezi kufanya lolote, ndivyo nilivyoambiwa,na sitakiw kukuambia la kufanya ndio miiko yenyewe,…’akasema





    ‘Oh, kwahiyo kumbe nimepoteza muda wangu bure kuja hapa…na wewe unaaminije hayo, ..miiko miiko…niambie nilitakiwa nifenyeje, mfano ningelikuja mapema…?’ nikauliza





    ‘Wewe huamini miiko, eeh, .wewe hujiulizi huyo mtu kajuaje yote hayo hata kabla hayajatokea, eti umeuliza nini, kuwa kwanini hao akina mama wanatuchukia, … hata kama ingelikuwa ni wewe, analetwa kimwana umependeza kama wewe, unafikiri yeye hawezi kuona wivu, ni wivu kwa vile wanahisi utawaibia waume zao, na waume wengine ndio hivyo, tamaa mbele…’akasema







    'Sasa nifanyeje…nitafanya nini mimi jamani, nitakwenda wapi masikin ya mungu, hivi nimewakosea nini hawa walimwengu jaman, kwanini wasiwafuate watu wenye uwezo wao, wanatusumbua sisi masikini ya mungu, kwani mimi nitawasaidia nini jamani, basi waniue kabisa, kama walivyomuua mama yangu…’nikaanza kulia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    'Kwani vipi….wewe unalia, mimi nililia sana tu..sasa wewe lia ukimaliza tutaendelea kuongea…’akasema





    ‘Inatia uchungu, kwanini ….’nikasema





    ‘Sasa nikuulize ,kuacha matatizo hayo kwani kuna tatizo jingine zaidi,…kama umekwenda hospitalini kutibiwa na sasa upo na afadhali, basi,…nikushauri kitu,  wewe ukitoka hapa rudi kwa mabosi zako, ukawaombe msamaha, uendelee na maisha, kwani pale wanakupia shilingi ngapi…?’ akaniuliza.





    ‘Hapo kwasasa silipwi kitu zaidi ya kula na kuwafanyia kazi tu….’nikasema





    ‘Hapo pagumu, lazima utafuta kazi ya kulipwa, ili usiishie kuomba omba, waambie wakutafutia kazi, kama wao hawataki kukulipa…’akasema.





    ‘Ni nani atanipokea na hali hii tena…’nikasema





    ‘Hali gani tena, si umesema umeshatibiwa, tatizo lipo wapi tena,…labda ilikuwa ni matatizo ya kawaida, na wewe huamini mambo ya kishirikina….’akasema





    'Nimeambiwa nina mimba…’nikasema na hapo akadondosha chombo alichokuwa kakishikila, na kunitolea jicho la kuogopa, akahema, halafu akasema





    'Mimba, wee..unasema ukweli…. ya nani hiyo mimba, unajua mimi nilipoambiwa nina mimba nilitafauta kile njia nisijulikane, na nashukuru, sasa nipo salama…sasa hebu niambie, …maana mimi niliambiwa utahisi dalili za mimba lakini sijaambiwa utakuwa na mimba, sasa hapo hata mimi sielewi kitu…’akasema





    'Mimi sijui ya nani..hapa nimechanganyikiwa, hata sielewi nifanye nini mimi ndio maana nimekuja huku , nilijua labda ndio hicho ulitaka kuniambia, na hata hivyo mimi sijaamini kuwa nina mimba, kwani…hiyo mimba imetoka wapi, wakati mimi simjui mwanaume….’nikasema





    'Yale yale..kama yaliyonikuta mimi, …sasa unajua..kama ni hivyo,…oh, kwako wewe iakwu ani ngumu,..mmh,  lakini inategemea na wewe mwenyewe..kwa hivi sasa mimi sina zaidi la kukusaidia, wakati mwingine inabidi ule matapishi yako, kwasababu aliyefanya hayo yupoo humu jijini, basi inabidi uende kwake…’akasema.





    ‘Kwa nani…?’ nikauliza nikionyesha uso wa mshangao.





    ‘Huyo mwanga, aliyekusababishia haya yote, umuone kabla hajaondoka, kama keshatibiwa…’akasema





    ‘Kabla hajatibiwa kwani na wao wanatibiwaga hospitalini, wao si wachawi,…?’ nikamuuliza akajifanya kama hajanisiakia, akasema;





    ‘Hebu nikuulize kwanza,…una uhakika kweli hujakutana na mwanaume mwingine,..usinifiche maana mtu anayeweza kukusaidia ni mimi, kama nitaujua huo ukweli wote, nitajua cha kufanya, au cha kukushauri…je hujakutana na mwanaume mwingine uwe na uhakika, maana kama umewahi kukutana na mwanaume mwingine na iwe ni mimba yake, hapo kuna mawili, kuonana na huyo mwanaume au jingine….una uhakika..?’ akaniuliza





    'Uhakika gani …mimi sina mwanaume, sijawahi kukutana na mwanaume yoyote, hilo nina uhakika nalo, ndio maana siamini kuwa nina mimba kweli, huenda labda kama ulivyosema…’nikasema.





    'Mhh, sasa unaanza kuamini eeh, eti kama nilivyosema, …hahaha, … sasa hapo ni tatizo, yawezekana yule jamaa kakufanyizia hivyo, ..hilo hakuwahi kuniambia,…hata hivyo kwa maelezo yake, maana ilibidi nimtoe kwa nguvu, yeye alisema utakuwa na  dalili za mimba, sasa kama umepimwa una mimba,hicho ni kitu kingine, sikuweza kumuuliza zaidi..’akasema.





    'Unasema labda kanifanyizia, kanifanyizia nini sasa…?’ nikauliza na yeye akaendelea kuongea bila kujali swali langu.





    'Au ni wale watu wawili mle ndani, inawezekana eeh, labda mmojawapo ndiye mimba yake hiyo,au ..hebu niambie ukweli, maana yule kijana naye, mmh, usipokuwa makini  …’akasema na kuniangalia machoni.





    'Unataka kusema nini…hapana mimi likuwa ni ndoto tu, sijawahi kutembea na yoyote mle ndani, hilo sio kweli, ndio maana akilini mwangu naamini kuwa mimi sina mimba, huenda ni hayo mambo ya huyo mjamaa wako….’nikasema





    'Ina maana nilichowaambia siku ile wewe hukuniamini, na huyo sio mjamaa wangu huyo ni adui yangu….’akasema.





    'Mimi siwezi kuyaamini hayo kwasababu mimi nilikuwa naota tu…haiwezekani ikawa ni kweli…’nikasema





    ‘Hahaha, hiyo sio ndoto ile ni kweli na sababu inaweza ikawa kweli ni huyo mjamaa kuhusiana na hizo ndoto, sio kuhusiana na hiyo mimba , maana lengo lake sio ubebe mimba ya watu wengine, alikuwa makini kwa hilo, ila uzalilike tu… alichokuwa akifanya  yeye ni vile vile kama nilivyowaambia, pale baba na mtoto walikuwa wakiletwa kwako usiku, ….wanakuzalilisha, wakati huo, hata wao wenyewe hawajijui…’akasema.





    ‘Una uhakika gani na hilo, ….?’ Nikauliza





     ‘Jamaa alininisimuliza yote alivyokuwa akifanya…’akasema





    ‘Mlikutana naye..?’ akaniuliza





    ‘Nitakusimulia tu  , usiwe na wasiwasi chukua chai hapo jipimie kiasi chako, na vitafunio hapo kwenye kabati, ukimaliza tutaongea, ….saa hizi hakuna chakula,  sijapika…nitapika chakula maalumu cha mgeni, madamu kasema leo ana mgeni wake humu ndani, sijui ni nani….’akasema.





    ‘Hapana mimi sina hamu ya kula chochote…’nikasema.





    ‘Utakufa wewe, kula kama una mimba basi..hiyo mimba itakusumbua, jilazimishe kula wakati kipo, hujui huko mbeleni itakuwaje…’akasema





    ‘Sina mimba mimi jamani….’nikasema





    ‘Hahaha, unalo hilo, nakuonea huruma sana, lakini …pambana, usikate tamaa, tatizo je ni ya nani…’akasema





    ‘Nimeshakuambia mimi sina mimba, imetokwa wapi hiyo mimba, mimi sijaamini bado….’nikasema





    ‘Eti huna mimba, wewe si ndio umeniambia hivyo, kuwa umepimwa na vipimo vimeonyesha kuwa una mimba au,…?’ akaniuliza





    ‘Inawezekana ni huyo mjamaa  kaniwekezea mambo yake humu tumboni kunifanya nizalilike tu …’nikasema





    ‘Basi kama ni hivyo, dawa ni kuonana naye, …’akasema





    ‘Kwa vipi, mimi sitaki hata kumuona huyo mtu, nahisi siku nikionana naye,  nita….nita-mfanyia kitu kibaya, nitamuua…’nikasema

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ‘Hahaha, unakuwa kama mimi, niliapa kuwa nikikutana naye, nitamfanya  hivyo, lakini nilipokutana naye safari hii , nikagwaya…’akasema





    ‘Ulikutana naye safari hii, kumbe umeonana naye uso kwa uso…?’ nikamuuliza





    ‘Tatizo wewe umechanganyikiwa….nimekuambia nilionana naye…’akasema





    ‘Wapi, au usiku ..?’ akauliza





    ‘Alikuja hapa kwenye hii nyumba,…, karibu anifukuzishe kazi…’akasema.





    ‘Alijuaje upo hapa, au ulimuelekeza wewe aje hapa….?’ Nikamuuliza.





    ‘Hahaha, hivi hujanielewa, jamaa yule ni mchawi, usiku anatembelea majumba ya watu, hasa kwa watu wake aliowafanyizia, kama balozi wa nyumba kumi, ila hapa kashindwa…na aliposhindwa ndio, ikabidi sasa aje mguu kwa mguu kuonana na mimi….’akasema.





    ‘Oh….kwanini…?’ nikaguna na kuuliza.





    ‘Wewe subiria, niitakuelezea kila kitu, alivyokuja na mambo yake,.. alivyonielezea alivyokufanyia wewe na..mengine mengi ndio utaona kuwa wewe matatizo yako sio bure ni huyo huyu jamaa, lakini kisa kilianzia kwangu…wewe subiria kidogo nimalize usafi…’akasema na kuelekea nje.





    Mara ghafla akaja mbio mbio akiwa kashikilia simu mkononi….akasema





    ‘Fanya uondoke….’akasema





    ‘Kwani vipi, kuna nini...…?’ nikauliza



    'Huu sio muda wa kuuliza,....ukikutwa humu, ....utanifukuzisha kazi, na madamu anakuja na mtu ambaye hutapenda kukutana na yeye,....fanya haraka katafute sehemu, nikipata nafasi nitakuita, au nikipata mwanya nitatoka tuongee...lakini sijui kwa vipi,....'akasema sasa akinishika mkono kabisa kuhakikisha natoka nje, na wakati tunatoka nje, mara geti likagongwa, gari lilikuwa limesimama nje ya geti.





    NB: Itakuwaje tena..









    WAZO LA LEO: Kuna watu wanachukua dhamana za watu, wanachukua watoto wa wenza wao, iwe wa ndugu au jamaa ili waishi nao, lakini watu hao, wanakuja kuwafanyia mabaya hao watoto, wakisahau kuwa watoto hao ni sawa na watoto wao, na ya kuwa, na wao watakuja kulipiziwa kwa watoto wao. Adahabu nyingine huanzia hapa duniani. Tuweni makini sana, kama kweli tunazipenda familia zetu, basi na tuzipende familia za watu wengine.



    Tulifika mlangoni na muda huo ndio geti likawa linafunguliwa, ina maana walipogonga geti hawakusibiria kuja kufunguliwa mama mwenye nyumba mwenyewe, alishuka kwenye gari lake, na kuingia ndani kwa kupitia mlango mdogo ambao, ulikuwa haujafungwa,  akafungua geti mwenyewe, na kuwakaribnisha wageni wake..



    Wakati huo mimi na mdada tupo ndani hatuna habari, na kugongwa huko mdada alikusikia, lakini alijua ni watu wa nje wasumbufu tu, hakutoka kwa haraka, ila ilipolia honi ya gari, akajua ni wenye nyumba, anaangalia getini anaona magari yanaingia yaliongozana magari matatu…

    Ndio akaja kule nilipo,



    ‘Fanya uondoke….’akasema





    ‘Kwani vipi, kuna nini kwani...…?’ nikauliza





    ‘Madamu kaja na wageni wake, na hao wageni usingelipenda wakuone….’





    Tuendelee na kisa chetu…





    ************



    ‘Mungu wangu sasa ni nani hao, wageni gani, itakuwaje sasa..?’ nikauliza nikianza kutembea kuelekea nje.





    ‘Fanya haraka ni mwenye nyumba, kaja na wageni wake, hakuniambia watawahi kufika, sasa katafute sehemu ukajifiche…, nikipata nafasi nitakuita, au nikipata mwanya nitatoka nje tuongee vizuri, lakini sasa kama wameshaingia getinni, utapitia wapi, ....'akasema sasa akinishika mkono kabisa kuhakikisha natoka nje.





    Tunafila mlangoni, ile tunafungua mlango , ndio muda huo geti limeshafunguliwa magari matatu yanaingizana…la madamu likiwa la mwisho…yalikuwa ni magari matatu, yaliyoingia, likiwemo hio la madamu…hapo mdada akawa anahaha, na kusema;





    ‘Madamu na wageni wake….sijui itakuwaje leo, umeniharibia kazi yangu, nilijua tu hili litatokea na wewe ndiye utaniharibia maisha yangu, …mungu wangu eeh…, najua wameshakuona, sijui tufanyeje…’akasema sasa akijaribu kujituliza.





    Mimi nilikuwa kwa ndani, nilijirudisha haraka pale nilipoona magari hayo yanaingia,…





    ‘Sikiliza, mimi nitatoka kwa haraka wakati wanapaki magari yao, hawakuwa na muda wa kuniangalia, au unasemaje, hao wengine hawanifahamu mimi ni nani…’nikasema





    ‘Hivi unaelewa hayo magari mngine ni ya akina nani, umeshayasahau..?’ akaniuliza na mimi ndio nikatokeza kichwa na kuyaangalia, ndio nikayagundua ni magari ya akina nani, japokuwa magari yanafanana, lakini kwa fikira za haraka nikawazia hao ni akina nani…





    ‘Mungu wangu wamefuata nini huku…?’ nikauliza huku nikirudi ndani na kuangalia huku na kule..





    ‘Unataka kufanya nini sasa, kujificha humu ndani, ..haiwezekani wewe toka nje, ujifanye hivyo hivyo, kama ulivyosema ulikuja kuomba maji, inamisha kichwa chako chini  wasikuone…’akasema na nikataka kufanya hivyo, lakini haikusaidia





    ‘Wewe ni nani na unataka kwenda wapi…?’ ilikuwa sauti ya mama mwenye nyumba kumbe yeye alishatoka tayari kwenye gari lake, na wenzake ndio walikuwa wanatoka taratibu.





    ‘Hahaha et anajifanya kuinama chini kuwa hatutamtambua..’ilikuwa sauti ya mama mwingine ambaye naye tayari alishatoka kwenye gari, wakawa wote wananiangalia mimi. Nilimuona mdada kwa ndani, akiwa kashikilia kichwa, …keshachanganyikiwa.





    ‘Mnafiki mkubwa huyu, hakujua kuwa tunajua huku leo hii, kumbe huko ndipo alipokimbilia, hahaha,…hahaha, haya tuambie ulikuwa unakimbilia wapi sasa si ulikuja kujificha huku au…’.ilikuwa sauti ya mama mwingine, nikasimama nikiwa nimeduwaa.





    ‘Kwani ni nani huyu unamfahamu…?’ akauliza madamu…





    **************

    Wakina mama wale wakakaribishana ndani, na mimi nikabakia pale nje nimesimama tu, na mwenzangu akawa anafanya kazi ya kuwaandalia hao wageni, na mara sauti ikasema;



    ‘Mwambie huyo mwenzako akusaidia, au bado anaumwa…’ilikuwa sauti ya mmojawapo wa wale wamama wengine wawili.



    ‘Anasema anajisikia vibaya,…’akanitetea, lakini sikujali kunitetea kwake, nikaungana naye na kuanza kusaidia kazi za kuwaandalia, mpaka zilipokwisha na wakawa wanakula wakijadili mambo yao ya kibiashara, na mimi nikawa na mdada, alikuwa hataki hata kuongea maana nimeshamuharibia kazi yake,..na baadae tukaitwa;



    ‘Haya nyie marafiki wawili njooni hapa…’ilikuwa ni sauti ya mwenye hiyo nyumba, na kwa aibu tukafika mbele yao na kusimama, nikijaribu kujificha nyuma ya mwenzangu.



    ‘Hebu kaeni msije kutuangukia hapa, na wewe unajificha nini, hahaha, unaogopa madhambi yako, hapa umeshafika, na hukumu yako ni mara moja tu,hatuhitajii kuwaita polisi, maana umekuja umeingia kweney nyumba za watu bila kukaribishwa, wewe ni sawa na mwizi tu..’akasema mwenye nyumba, na tukakaa , unakaa kwenye sofa upande upande, kwa kuogopa.



    ‘Haya tuambieni lengo lenu ni nini, maana mlipata muda wa kuongea, tuanze na wewe mwenyeji, tuambie mwenzako ulimuita au alikuja mwenyewe, au…?’ akauliza mama mwenye nyumba, na tukabakia kimia



    ‘Nilipotoka hapa, niligundua kuna mtu kajificha pembeni mwa nyumba yangu, niliingiwa na mashaka sana, nikampigia simu mume wangu, akaniambia amekuona umeshaingia ndani na unaongea na mfanyakazi wangu wa ndani, na umetoka nje… lakini sikuamini…nikajua huenda ni nyumba ndogo za mume wangu, …’akasema akiwaangalia wenzake.



    ‘Nyumba ndogo…waume zetu hawa…’akasema mwingine.



    ‘Basi nikamtuma mtu wangu mmoja kuja kuchunguza…aliingia hadi huku ndani, hamukumuona muone jinsi gani unavyojisahau,na siku nikiibiwa humu ndani najua ni wewe, ni kwa vile huna muda humu tena…’akasema na kauli hii ilimfanya mwanzangu awe kama anatetemeka.



    ‘Nilishakuvumilia sana, na nilikuwa natafuta mwanya wa kukufukuza humu ndani, sasa nimeupata, lakini kabla hujaondoka, nataka kusikie ukweli,…’akasema mama mwenye nyumba, na wote tukabakia kimia.



    ‘Haya na wewe tuambie,…umetokea wapi na kwanini umekuja hapa nyumbani kwangu,…?’ akaniuliza akiniangalia kwa dharau. Na mimi nikakaa kimia



    ‘Huyu namfahamu, alikuwa kule kwangu…na hutaamini,  alinitoroka hospitalini, nikawa najiuliza amekwenda wapi, na ulipokuja kuniambia kuna mtu kajificha pembeni mwa nyumba yako, na ulivyoelezea jinsi alivyovaa, nikajua ni yeye, lakini hakuwa ameva hivi, kabadilisha nguo…’akasema



    ‘Ni kweli, nilivyomuona awali hakuwa amevaa hivi…’akasema mwenye hiyo nyumba.



    ‘Sasa wapendwa, mtuambie mumepanga kufanya nini, au mlikutana kupanga mikakati ya kutumalizia ndoa zetu..?’ akauliza yule mwingine ambaye muda mwingi alikuwa kimia, akiandika kitu kwenye simu yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Ngoja mimi niwasaidie kidogo, maana wote wawili wamefanyia kazi nyumbani kwangu, na huyu wa kwanza, ndiye kasababisha yote haya, ..sio mbaya, siwezi kusema yeye ni mbaya kihivyo, kutokana na uchunguzi wangu, ila tunataka kuwaambia kuwa sasa muda wenu wa kuishi kwenye jiji hili umekwisha, kwa usalama wenu, itabidi mrudi makwenu, au sio wenzangu…’akasema huyo mama mwingine, na wenzake wakakubali.



    ‘Jamani kwanini mumeamua hivyo, wakati mnafahamu kuwa haya yote yanayotokea sio kwa makusdio yetu..’akasema mdada na mimi nikabakia kimia.



    ‘Tatizo wewe unajifanya ni mjanja sana,…na ujanja wako unawafundisha na wengine, unajua kutunga maneno na kuwhdaa watu wengine, lakini sio hapa kwangu, unasikia,..nilikukanya sana, …’akasema mama mwenye nyumba.



    ‘Lakini mimi sijawahi kufanya kitu chochote kibaya humu ndani, …’akajitetea



    ‘Nilikuambia nini kila siku, nikiondoka usilete wageni humu ndani, maana sio wageni wote wana nia nzuri, huyu ni nani…?’ akauliza mama mwenye hiyo nyumba.



    ‘Huyu kaja ghafla, wala sikujua kuwa atafika humu, na nilikuwa namfukuza aondoke, unajua ilivyo mtu kaja kwako, na sikutakiwa ni mfukuze kama mwizi..’akajitetea.



    ‘Usijifanye mjanja, haya unayoyafanya hujayaanza leo, umekuwa ukirudia kila mara na mimi nakusamehe.., na wasiwasi wangu huyu kwa mambo yake haya, na hao wanafunzi wake, wakiendelea kubakia hapa jijini mtawatia waume wetu wazimu, maana kila siku mazungumzo ni hayo hayo, kwanini tumefanya hivi kwanini , kwanini..kwani nyie ni nani …eeh, tuambieni, wema wetu ndio imekuwa adhabu kwetu, hapana inabidi muondoke tu…’akasema.



    ‘Lakini kabla hamjaondoka, ili msije kuona sisi ni wabaya kihivyo, sisi sio wabaya kama mnavyofikiria nyie, sisi tunawajali sana, tunawaonea huruma sana kwa maisha mliyopitia ndio maana tuliwakubali,  lakini kama kuna mdudu ambaye ataambukiza maradhi mabaya ndani ya mwili, dawa yake ni nini, eti dawa yake ni nini, tukitumia dawa ya kumuua kuna makosa, lakini sisi hatutaki kuwaaua, tunataka mrudi makwenu…’akasema.



    Hapo nikaona ni bora na mimi niongee, nikanyosha kidole kama darasani kuomba ruhusa, na mwenye nyumba akasema;



    ‘Haya sasa ongea naona umeguswa sasa….’akasema



    ‘Mimi naombeni jambo moja, sawa kama mnataka turudi makwetu….ni sawa tu, kwasababu hatuna haki kwenu, ..hamuwezi mkahisi maisha yetu kwasababu hamukuwahi kuyaishi kabla…lakini tungelipenda tupate muda, kwasababu kurudi huko nyumbani ni kama mnatupeleka kuuwawa, kama huko kwetu watu wanauwawa ovyo, sasa tunawaombeni sana mtupe muda…’nikasema



    ‘Unajua kwanini anasema hivyo…’akasema mama mmojawapo, yule aliyenipeleka hospitalini.

    ‘Kwanini anasema hivyo..?’ akauliza mama mwenye nyumba.



    ‘Ana mimba…sasa huenda anataka njia ya kwenda kwa huyo bwana wake…’akasema huyo mama.



    ‘What!…..! unasema ukweli..?’ akauliza yule mama aliyekuwa mfadhili wangu wa kwanza..



    ‘Nilimgundua kutokana na dalili alizokuwa nazo, mimi na mume wangu tukaamua kumpeleka hospitalini, akapimwa, na docta akagundua hilo tatizo, docta naye akajifanya kumtetea, nikamwambia wewe si una huruma, sasa tunaenda kumchukua akakae kwako….unajua alisema nini…?’ akawauliza wenzako

    ‘Tuambie….’wakasema



    ‘Siwezi kumchukua maana sio  mimi niliyemtoa huko kijijini, na huyo aliyempa huo uja uzito anatakiwa akapatikane ili akawajibike, nikamwambia, haya mtafute huyo mtu, sisi hatumjui…, ukimpata mlete, …na umemuuliza huyo binti ni nani alimbaka, ni nani alitembea naye…ni nani aliyempa hiyo mimba, kakuambia nini…’akatulia.



    ‘Alisema ni nani kafanya hivyo..?’ akaulizwa na wenzake.



    ‘Kasema huyo binti anadai yeye aliota tu, …hahaha’ akacheka na wote wakacheka kwa pamoja.



    ‘Hapo sasa…wewe si docta, kama yeye anadai kuwa aliota tu, na hakuna mtu aliyewahi kutembea naye, basi docta utusaidie kumtafuta huyo mtu, hapo docta akagwaya, akasema tumuite huyo binti ili tusaidiane, yeye anaweza kutusaidia tukampata huyo mtu..tukasema haya, ..mimi natoka nje kumuita ..hakuna mtu, keshakimbia…’akasema.



    Docta kwanza hakuamini, akatoka yeye mwenye nje kumtafuta, baadae anarudi anasema,…



    ‘Kweli huyo binti ni tatizo….’



    Hapo ndio docta akajua huyo binti ni muongo na tapeli, kama angelikuwa mkweli angelisubiria tumalize mazungumzo, tuone muafaka wake utafikia wapi, kwanini akakimbia, basi docta akanyosha mikono.



    Sisi tukamsihi docta, kuwa yeye si anataka haki itendeke, basi aende mahakamani, yeye si anajifanya mtetezi wa wanyonge, mtetezi wa wanawae wanaonyanyaswa, basi afanye hiyo kazi na sisi tutaitwa, kujieleza, huyo binti amtaje aliyemfanyia hivyo, ni nani…’akasema.



    ‘Hahaha, atamuona wapi na yeye aliota tu…’akasema huyo mama mwingine na wakaangua kicheko tena.



    ‘Sasa ndugu zanguni, wadada warembo, wanaowachengua waume zetu, sisi hatuna lengo baya na nyie, lakini tunachotaka ni kuzilinda ndoa zetu,..tunakwepa sana mambo hayo ya kishirikina, tunakwepa sana kuingiza mambo mabaya kwenye familia zetu, …mfano sasa wewe una mimba, hatujui umaipatia wapi, ni nini kitatoka baada ya hapo, .humjui aliyekupa hiyo miba au sio…, ina maana gani hapo, familia zetu zitaingia matatani kwa mambo yenu mliokuja nayo…’akatulia.



    ‘Unajua niwaambie kitu, sisi tulishakubaliana huyu mdada atafutiwe chumba, na biashara, ajiwekeze, maana akikaa kwenye nyumba za watu mambo kama haya yatajitokeza kwa wengine, basi awe na kwake, ajihangaikie, tulipanga kumtafutia mtaji..kuna mambo bado hatujakubaliana na mume wangu, lakini tulishafika hatua ya mwisho, sasa kama kuna hili la mimba tena,..mmh, sijui itakuwaje…’akasema mama mmojawapo.



    ‘Kwahiyo mume wako ataambiwa ni yeye au ni kijana wako, ..si ndio hivyo, kuwa wao ndio walimpa mimba au itakuwaje hapo, ndio maana watu kama hawa watakiwa warejeshwe huko walipotoka…’akauliza mama wa hiyo nyumba



    ‘Kama sasa ana mimba tunachohitajia ni yeye atoe ushahidi, kama kweli kapachikwa na mtu wa familia yangu, lakini yeye, tangia awali nilimuuliza kama kweli aliwahi kuwa na mahusiano na mume wangu , akasema hana na hajawahi kumuona mume wangu akiingia chumbani kwake…



    ‘Mhh…kwahiyo kumbe hakuna lolote la kuwashinikiza familia yako kaa itafika mahakamani, maana wanaweza kwenda kushawishiwa na watu fanyeni hivi, nendeni mahakamani, sasa waende, waone watavyoumbuka,…’akasema mama mwenye myuma.



    ‘Mimi nilihsjitolea kumsaidia huyu binti, kama kweli angelikuwa mkweli, ningelimsaidia kwa namna niliyoona ni bora kwake, lakini akawa muongo, akanificha ukweli,…sasa atajijua mwenyewe, …’akasema.



    ‘Je kama kweli ni mimba ya mwanafamilia yako itakuwaje…?’ akauliza mama mwenye myumba.



    ‘Muhimu ni ushahidi, ..kama aliota ni nani atamshika, ..kama anaficha ukweli ni nani atamsaidia, naona dunia ikamfundishe, hakuna jinsi hapa,…asije akaja kutuletea watoto balaa kwenye familia zetu…’akasema



    ‘Mimi naona tuliongelee hili sisi wenyewe kwanza maana linaleta picha mbaya, tukifikia muafaka tutachukua hatua, haina haja ya kuwashirikisha waume zetu..sasa nyie mabint nendeni huko ndani au huko nje, mkaongee, mtafute njia gani, sisi tunaweza kuwasaidia, mje na wazo lenye maana, na sisi mtuache tuongee, lakini mkae mkijiandaa na safari ya kurudi huko kijijini kwenu, sawa…’tukaambiwa,



    ‘Lakini mimi nina kosa gani..?’ akauliza yule mdada



    ‘Na wewe ndio chanzo cha yote hayo, unauliza una kosa gani, tukuulize bila ya wewe haya yote yangelitokeaje, wewe ndiye chanzo, na kwahiyo wewe ndiye mkosaji mkuu, unastahili adhabu kubwa sana, na adhabu yako ni kurejeshwa huko makwenu,…’akajibiwa na yule mama, mfadhili wangu wa kwanza.



    ‘Lakini nilishawaambia kisa na sababu …nilijitolea kuja kuusema ukweli, ili mjua kinachoendelea hivyo mimi nilifanya kosa,…’akajitetea.



    ‘Ndio maana tunataka nyie make waili muongee, mtafuta njia nzuri ya kulimaliza hili, kama mtahitajia msaada wetu, sawa, na sisi tutaliongelea kivyetu, tuna mambo yetu mengi tunayaongea hii leo, na hili limekuja tu, litatupotezea malengo yetu ya maendeleo,..kwahiyo nendeni mkaongee huko…’akasema yule mama mfadhili wa kwanza.



    ‘Na mimi nawapa ofa, kwa leo, na kesho na kesho kuwa mtakaa  humu ndani kwangu , mtakaa humu, mtakula, lakini mtanisaidia kazi, huku nikitafuta mfanyakazi mwingine, huku mkijifungasha virago vyenu tayari kwa kuondoka, na kama kuna lolote la ziadi, tutaangalia, mimi ndiye kiongozi wa kundi letu na maamuzi yangu ni mwisho, nendeni…’akasema mama mwenye nyumba.



    ‘Au mimi niulize tu, maana nyie mnawajulia zaidi hawa mabinti wawili zaidi yangu, huyu bint, ailetwa kwangu, na mume wangu na sikutakiwa kuuliza, kwa vile ni mgeni, ..nilikubali nilijua njia ya mnafiki ni fupi…niliambiwa kaja kwa muda, mara naona mwezi huo, mara kumbe mgeni kaja na mzigo tumboni, sasa nauliza, huyu anasema sio kusudio lake, kuna mtu kasababisha hivyo, wao si wanamfahamu, sasa watuelekeze sisi tutawasaidia kupambana na huyo mtu, kama ni kisheria, au vyovyote inavyowezekana,..’akasema yule mama aliyenipeleka hospitalini.



    ‘Wanadai ni mchawi mmoja kutoka huko kijijini kwao…’akasema mama fadhili wa kwanza



    ‘Mchawi tena ni yale yale niliyoyapiga marufuku hapa nyumbani kwangu, huyu binti alikuja na hadithi ndefu, kuwa kuna mchawi anaweza kuingia usiku akafanya hivi na vile, nikamwambia wee, ishia hapo hapo, hapa nyumbani kwangu kuna ulinzi , mchai hawezi kuingiza mguu wake humu….’akasema



    ‘Je hakuwahi kupiga kelele za kuota usiku…?’ akaulizwa mama mwenye nyumba.



    ‘Thibutu, angepiga ningemuonyesha kazi, hakuna cha uchawi au shetani anaingia humu ndani kwangu ninajua nikwanini….nilimpiga marufu, na nilimuambia kama ataleta mtu wa namna hiyo, yeye, na huyo mtu wake, watakwenda jela..’akasema mama mwenye nyumba.

    ‘Kumbe wachawi wanaogopa jela…’akasema yule mama mlezi wa kwanza..



    ‘Hebu tuambie, ni nani huyo mchawi aliyewafanyia hivyo, je ndiye aliyemfanyia mwenzako hivyo, na huenda ndiye alimpa mimba, ili wasingiziwe wanafamilia…’akasema yule mama aliyenipeleka hopsitalini.



    ‘Atuambie huyo mdada wa kwanza…’akasema yule mama mfadhili wa kwanza.



    ‘Ndi-ndi- ndio yeye, aliyesababisha yote hayo, lakini sina uhakika na hiyo mimba ya huyu…’akasema

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘Na awali ulikuwa na dalili ya mimba ulipofika hapa kwangu, ilikwenda wapi hiyo mimba…?’ akaulizwa



    ‘Mimi sijui, ilipoteaje..’akasema na akina mama hao wakaangaliana huku wakionyesha uso wa kushangaa.



    ‘Mimba imepotea, hahaha, kwa vile nilimuambia kama ana mimba basi afungashe, kwani kidogo alianza kunisumbua, anaumwa, ..nikahangaika,..baada ya kutoa hivyo vitisho, aah, akajirudi, lakini kwa hili sasa simtaki tena…’akasema

    ‘Sasa huyo mtu wenu, unayemuita mchawi, yupo wapi..?’ akaulizwa



    ‘Alikuja hapa dar, akasema anakwenda kutibiwa…’akasema



    ‘Mlionana naye wapi…?’ akaulizwa



    ‘Ali-ali-kuja hapa nyumbani…akasema huyo mdada kwa mashaka.



    ‘Ni yupi huyo,..lini, ooh,.. ni yule jamaa alikuja akasema wewe ni ndugu yake, kumbe familia yenu ni wachawi eeh,…’akasema mama mwenye nyumba.



    ‘Hapana sio ndugu yangu yule, alisema hivyo tu, ili aweze kuongea na mimi….’akasema



    ‘Unaoan jinsi ulivyo muongo, siku ili ulituambia nini mimi na mume wangu kuwa huyo mtu ni nani wako…’akasema mama mwenye nyumba



    ‘Niliogopa kusema ukweli maana hata mimi sikutaka aendelee kunisumbua, ndio nikamfukuza, …’akasema



    ‘Je tutampataje huyo mtu, kwa kuwasaidia, ili wajibike, kama mimba ni yake ahakikishe anamtunza mwenzako tutampataje..?’ wakauliza



    ‘Alisema kaja kutibiwa, sasa sijui kama kaondoka au la…’akasema mdada



    ‘Anaumwa nini, huna namba yake ya simu..?’ akaulizwa



    ‘Anasema anaumwa mguu umevimba, kaja kutibiwa, namba yake nilikuwa nayo nikaifuta, sikutaka kuwa na mawasiliano naye …’akasema mdada.



    ‘Ni kweli nakumbuka huyo jamaa alipofika hapa, alikuwa anachechemea, na ilionyesha wazi mguu mmoja umevimba, kama ana tege, la mguu mmoja, na ulikuwa unatoa harufu , au..ilikua ni harufu ya nini sijui, sikukumbuka kulifuatilia hilo,…’akasema



    ‘Mimi sijui kama ulikuwa ukitoa harufu, ila alisema anahitajika kutibiwa na kama nina pesa nimkopeshe…’mdada akasema



    ‘Hahaha, ndio huyo aliyetaka kukuoa, na sasa anataka kukukopa mmh, una pesa nyingi wewe, utuambie umezipatia wapi…?’ akaulizwa



    ‘Simtaki kabisa,..nilimkataa,na kumkataa ndio chanzo cha yote hayo. Na sikuwahi kumpa pesa nilimfukuza…’akasema.



    ‘Sawa, sasa nyie kayaongeeni yote hayo..ila msimamo wetu ndio huo huo, …lazima muhame huu mji, maana mkindelea kubakia hapa,  mtawatia wazimu waume zetu, wanaojifanya kuwajali sana…mnasikia, kaongeeni muone sisi tutawasaidiaje na mkitaka tunaweza kukutana na huyo mtu mnayesema ni mchawi, sisi tutapambana naye, hatuogopi uchawi…’wakasema wakigongeana mikono.



    Mara simu ya mama mwenye nyumba ikalia, na akaipokea, na kuuliza



    ‘Wewe ni nani..?’ akauliza na kusikiliza



    ‘Unataka nini..?’ akauliza



    ‘Unamtaka aje hospitalini, wapi,…?’ akauliza



    ‘Ocean road, kwani wewe ni nani kwake..?’ akauliza na kusikiliza



    ‘Aaah, ndio wewe eeh, ulikuja hapa siku ile, aheri umepiga simu, tunakutafuta sana, sasa sikiliza tutakuja huko hospitalini, tuna maongezii na wewe, wewe si mchawi, au sio…’akauliza na kusiliza.



    ‘Hahaha, ulikuwa mchawi na sasa umeacha, kwanini umeacha, uchawi wa kurithi utauachaje,…?’ akaulizwa



    ‘Nini…usamehewe, mbona wewe hukuwasamehe uliokuwa ukiwatendea hayo maovu yako..?’ akaulizwa



    ‘Kwahiyo wewe unataka nini sasa…, msaada wa kutibiwa, mchawi anaumwaga.. ..huyu mdada atapatia wapi pesa, anikopeshe mimi, haaa, mimi ni benki wa kukopesha watu… na atazirudishaje,..hahaha, wewe kweli umepagawa kwa mshahara gani alio nao yeye,  na kwanini yeye akugharamie hivyo, wakati wewe ….nini, unataka kuwaondolea nini,…mazindiko ndio nini…mmh, haya ..subiri nitakupigia…’akakata simu



    ‘Mumesikia jamani, nilikuwa naongea na mchawi mwenyewe…hahaha’akasema na wale wengine wakatulia.

    ‘Anasemaje..?’ akaulizwa.



    ‘Anasema anahitajia msaada wa kipesa, anahitajia pesa kwa ajili ya matibabu, anatakiwa pesa nyingi tu, milioni kadhaa, sasa anataka huyu mdada akope kwangu,..watu wa ajabu sana hawa…’akasema



    ‘Akope kwako kwa vipi…?’ akauliza



    ‘Anasema yeye anajua kwa vipi maana asipofanya hivyo hatakubali kuyaondoa, ..mazindiko, kitu kaam hicho….’akasema



    ‘Oooh, kumbe, sasa kayawekaje ..?’ wakaulizana.



    ‘Labda tumuulize mpenzi wake…’akasema mama mwenye nyumba.



    ‘Huyo sio mpenzi wangu jamani, huyo ni adui yangu…’akasema.



    ‘Ndio ananitishia mimi kuwa eti nisipokubali kutoa huo mkopo, hataweza kuyaondoa hayo mazindiko, kwa wote aliowawekea, na hapa kwangu ameshakamlisha kazi hiyo tutaanza kupata shida…’akasema.



    ‘Hahaha…hawa watu wanachekesha, halafu anatishia, kwa kujiamini kabisa, mtu anaumwa, badala ya kuongea vizuri anatishia, hivi..eeh yupoje huyo mtu..?’ akauliza yule mama aliyenipeleka hospitalini.

    ‘Sio mtu mzima sana, nashangaa kwanini kajiingiza kwenye mambo kama hayo…’akasema mama mwenye hiyo nyumba.



    ‘Mimi naona,…tukakutane na huyo mchawi, maana kwanza kama kwli ni yeye aliingia kwenye nyumba yangu akafany ahayo aliyoyafanya , nahitajia kuonana naye , na atanitambua, ..kuna ushahudi ninao, .. waonyesha kweli aliingia, …sikutaka kuliingilia sana hili, maana nitakuwa naamini mambo ya kishirikina, lakini kwa vile keshaanza kututushia amani, basi kesho twendeni huko, hata leo ikiwezekana…’akasema yule mama mfadhili wa kwanza



    ‘Na wewe kama hiyo mimba ni kwake, basi tukifika pale sisi tunakubidhisha kwake, mtajuana wewe nay eye, unasikia, sasa hili limefika kubaya, mtu anayetishia amani mwenzake, anakuwa katenda kosa, sasa atapambana na polisi…’akasema yule mfadhili wa kwanza



    ‘Ngojeni kwanza niwasiliane na mume wangu, hajui kuwa mume wangu ni polisi, eeh, ngoja, hapa sasa inabidi tuwashikirishe waume zetu, atanyea jela…’akasema mke wa hiyo nyumba.



    WAZO LA LEO:  Kuna watu wengine wanaona ufahari kushindana kwenye kesi, ugomvi, malumabano hata kama kuna njia nyingine mbadala, kila jambo wao wanalijenga ligi ya ushindani,  hata kama ni jambo la kusameheana tu,..ugomvi, shutuma, visasi na uhasama imekuwa ni hulka zao. Kusameheana ni jambo lenye kuleta heri, na maridhiano ya kujenga mshikamano ndio njia ya salama ya kuleta amani. Tusikimbilie kuonyeshana ubabe, ubabe hauabna heri kamwe, bali tuwe na tabia njema ya kusameheana, kusaidiana na kuhurumiana, na mola ataleta heri zake.



    Mimi naona,…tukakutane na huyo mchawi huko huko hospitalini, kwanini anatutishia amano...'alisema huyo mama mwenye nyumba



    'Sawa mimi naona iwe hivyo, kwa maana kwanza kama ni kweli yeye aliingia nyumbani kwangu akafanya hayo aliyoyafanya..akaharibu familia yangu na kutia fitina,..mimi mwenyewe , nahitajia kuonana naye...'akasema mama mfadhili wangu wa kwanza.



    'Hilo jambo jema,, tuhakikishe tumelimaliza hili ili tuishe kwenye familia zetu kwa amani, maana leo kwako kesho kwangu, kama huyu binti kaja kwangu na mzigo, na huenda huo mzigo ni wake, si lazima atakuja kunisumbua na mimi,...huyu na mwenzake tuwakabidhishe kwake, na huyo mtu, apate kipigo, ajifunze...'akasema yule mama aliyenipeleka hospitalini.



    Kiukweli sikuwa na amani, nikajua sasa maisha yangu yanakwenda kuharibiwa kabisa, bado nina mzigo, na simjui baba yake ni nani, na....haya yanayokwenda kutokea huko sijui yatatufikisha wapi, kama akina mama hawa wataamua kufany hayo yaliyopo kwenye nfasi zao



    Tuendelee na kisa chetu...



    ****************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wale akina mama watatu wakakubaliana hivyo ikawa ni muda wa kusubiria simu ambayo ilikuwa inapigwa kwa mume wa mmojawapo hapo, na wengine wakaamua na wao watumie muda huo kuwasiliana na waume zao, ili wajulikane wapi  walipo na wanataka kwenda kufanya nini huko.



    Kiukweli waume walikubaliana na maamuzi yao, ila waliwatahadharisha kutokuchukua maamuzi ya haraka na kuchukua hatua mikononi mwao, muhimu wafike huko wamuulize wasikie huyo mtu atasema nini, kwasababu mambo ya kichawi, mara nyingi huwa hayana ushahidi wa moja kwa moja.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog