Simulizi : I Fail To Forget You
Sehemu Ya Pili (2)
Akili yake ya kuwaza masomo darasani ilianza kubadilika na sasa akawa anawaza mapenzi, alijikuta akiutumia muda wake mwingi katika kumuwaza Herieth msichana ambaye hakuwa amemwambia lolote lile kuhusu hisia zake. Alipokuwa akuimuona darasani amekaa alijisikia furaha sana hasa kwa kumtazama msichana huyo ambaye alikuwa akitumia muda wake mwingi katika kuishi naye maisha ya ndotoni. Kila alipokuwa akimkumbuka alihisi kama anamuona na walikuwa wakizungumza mpaka kufikia hatua ya kukumbatiana.
“Nakupenda sana Herieth,” alijisemea siku moja majira ya usiku wakati aliopokuwa kitandani amejilaza.
Kuna kipindi alipokuwa chumbani kwake aliamua kujifungia na kuichukua simu yake kisha akawa anasikiliza nyimbo za kimapenzi, aliamini zilikuwa zikimliwaza hasa pale alipokuwa akimkumbuka Herieth.
Nyimbo yake kubwa aliyokuwa akiipenda kuisikiliza nyakati za usiku ilikuwa ni “Queen of My Heart” (Malkia wa Moyo Wangu). Nyimbo iliyoimbwa na kundi lililokuwa likijulikana kwa jina ‘Westlife’. Westlife lilikuwa ni kundi kutoka nchini Ireland, lililoundwa tarehe 3 Machi mwaka 1998. Asili ya kundi hili linajumuisha wanamuziki kama vile Nicky Byrne, Kian Egan, Mark Feehily,Shane Filan na Brian Mcfadden ambapo waliweza kuimba nyimbo nyingi zilizowapa umaarufu mkubwa dunia.
SONG:Queen Of My Heart
[Kiana:]
So here we stand In our secret place With a Sound of the crowd So far away And you take my hand And it feels like home We both understand It’s where we belong
[Bryan:]
So how do I say? Do I say goodbye? We both wanna fly So let’s take tonight To carry us through The Lonely times
‘CHORUS’ [All:]
I’ll always look back As I walk away This memory Will last for eternity And all of our tears Will be lost in the rain When be lost in the rain When I’ve found my way Back to your arms again But until that day You know you are The Queen of My Heart
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
(KWA KISWAHILI)
NYIMBO: Malkia wa Moyo Wangu.
[Kian:]
Kwa hiyo hapa tunasimama Katika nafasi yetu ya siri Kwa sauti ya umati Mbali sana Na wewe ushike japo mokono wangu Na uhisi kama tupo nyumbani Sisi wote tunaelewa Ndipo mahali ambapo mimi na wewe tulipo.
[Bryan:]
Kwahiyo nasemaje? Je, niseme kwaheri? Sisi sote tuna ndoto zetu Sisi wote tunataka kuruka Basi hebu tuchukue usiku wa leo Ili kutubeba kupitia nyakati za upweke.
‘CHORUS’ [Wote:}
Mimi daima kuangalia nyuma Ninapoondoka Kumbukumbu hii itandelea milele Na machozi yetu yote Itapotea katika mvua Wakati nimepata njia yangu Rudi mikono yako tena Lakini hadi siku hiyo Unajua wewe ni Malkia wa Moyo Wangu.”
Hii ndiyo nyimbo kubwa aliyokuwa akiipenda kuisikiliza sana, kila alipokuwa akiisikiliza alihisi kuwa na mapenzi ya dhati kwa Herieth lakini katika hali ya kushangaza alishangaa kuona ule ukaribu uliyoanza kati yake na Herieth ukianza kupungua taratibu, hakujua ni nini kilikuwa chanzo, hilo lilizidi kumpa wakati mgumu sana.
Herieth alikuwa ni msichana mrembo sana aliyejaaliwa kila aina ya sifa ambayo iliwavutia wanafunzi wa kiume pale shuleni, kila mmoja alikua akitamani kuwa naye kimapenzi.
Alizaliwa katika familia ya kitajiri sana, Baba yake mzee Thomas alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa wa madini Arusha aliyekuwa amewekeza sana katika biashara mbalimbali ambazo zilikuwa zikimuingizia pesa nyingi sana, alikuwa ni miongoni mwa matajiri wakubwa ambao walikuwa wakitamba mkoani Kilimanjaro, alikuwa akijulikana sana hasa kutokana na utajiri aliyokuwa nao. Mama yake Herieth aliyejulikana kwa jina la Mary alikuwa akimsaidia Mume wake katika kuziendesha biashara mbalimbali alizokuwa akizimiliki. Alikuwa ni Mama aliyekuwa akiipenda familia yake ambapo alibahatika kuwa na watoto wawili tu! wa kwanza kuzaliwa katika familia hiyo alijulikana kwa jina la Jackline Thomas ambaye alibahatika kusoma mpaka chuo kikuu cha Daresalaam, alikuwa akisomea masomo ya sheria ambapo baadae aliweza kupata bahati ya kwenda kusomea masomo ya sheria nchini Uingereza katika chuo kikuu cha Oxford. Mtoto wa pili na wa mwisho kuzaliwa katika familia hiyo alijulikana kama Herieth Thomas. Alikuwa ni mtoto aliyekuwa akipendwa sana na Baba yake Mzee Thomas. Hakutaka kuona mtoto wake akipata shida yoyote ile katika maisha yake, kila kitu alichokuwa akikihitaji aliamua kumtimizia kwa wakati, aliamini katika mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa mtoto wake ambaye alikuwa akimthamini kupita kawaida, katika kipindi cha miaka mitatu alikuwa akimuhamisha mtoto wake shule kutokana na sababu alizokuwa akishtakiwa na binti yake. Hakujali lolote na alichokuwa anaangalia ni utajiri aliyokuwa nao, aliamini kutimiza kila kitu na kama alivyokuwa akiamini ndivyo ambavyo aliweza kutimiza, kila shule ambayo mtoto wake hakuipenda aliamua kumuhamisha.
“Baba ile shule hata siipendi,” alisema Herieth, wakati huo alikuwa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Majengo.
“Kwanini malkia wangu?” aliuliza Mzee Thomas huku akimtazama Herieth ambaye alikuwa ameukunja uso wake.
“Basi tu mimi siipendi Baba,” alisema Herieth.
“Kuna mtu amekukorofisha?”
“Hapana.”
“Sasa nini tatizo.”
“Hakuna kitu baba ila mimi siipendi tu!”
“Unataka nikupeleke shule gani nyingine?”
“Saint Mary Goreti”
“Oooh! Usijali mwanangu lazima nikupeleke huko, nataka uishi katika ndoto zako.”
“Nitafurahi baba.”
“Usijali Mwanangu,” alisema Mzee Thomas.
Alichoamua kukifanya Mzee Thomas ni kufuata taratibu zote za kumuhamisha mtoto wake shule na hatimaye Herieth akawa mwanafunzi wa Sain Mary Goreti.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya miaka miwili Herieth alidai kuomba kuhamishwa shule kwani hakuwa ameipenda hata kidogo na kama ilivyokuwa kawaida ya Baba yake aliamua kumtimizia kile kitu ambacho mtoto wake alikuwa akikihitaji.
“Kuna nini tena?” aliuliza Mzee Thomas.
“Baba hii shule hata sijui ikoje, halafu kwanza kuna uchawi kila siku wanafunzi wanalogana,” alisema Herieth maneno yaliyokuwa na uwongo, alikuwa amechoka kuishi maisha katika shule ile hivyo alikuwa akitafuta sababu za kutaka kuhamishwa.
“Uchawi!” aliuliza Mzee Thomas huku akionekana kushangaa.
“Ndiyo Baba.”
“Lakini ile shule mbona ni ya dini?”
“Baba mimi siipendi sasa,” alisema Herieth huku akijidekeza.
Mzee Thomas hakutaka kuwaza mara mbilimbili, alichoamua kukifanya ni kumuhamisha kama ilivyokuwa kawaida yake.
Shule aliyoamua kumuhamishia ilikuwa ni Wazalendo, aliipenda sana shule hii hasa kutokana na Mkuu wa shule hiyo aliyejulikana kwa jina la Dr. David alikuwa ni rafiki yake.
“Ni shule nzuri sana naamini utaipenda Mwanangu.”
“Kweli Baba.”
“Ndiyo.”
“Inaitwaje?”
“Wazalendo High School.”
Herieth alianza kusoma katika shule hiyo ya Wazalendo, alikuwa ni msichana mrembo ambaye alitokea kupendwa na kila mtu, wanafunzi wavulana walianza kumtamani, hakukuwa na mvulana ambaye hakuacha kumzungumzia msichana huyo ambaye alionekana kuwa mrembo kupita wasichana wengine.
“Aisee mtoto mkali yule,” alisema Mwanafunzi mmoja ambaye alikuwa kidato cha pili.
“Yupi?” aliuliza mwanafunzi mwenzake.
“Yule mgeni.”
“Sasa wewe upo kidato cha pili hivi unafikiri utamuweza yule halafu anaonekana kwao maisha safi.”
“Inamaana kuwa kidato cha pili ndiyo sababu?”
“We jipe moyo utashinda,” alijibu yule mwanafunzi mwingine.
Kila mvulana pale shuleni alikuwa akitamani kuwa na Herieth kimapenzi, tamaa ya mapenzi haikuwaingia wao tu bali hata baadhi ya walimu walianza kumpenda, alitazamiwa kwa macho ya tamaa ya kimapenzi na kila mtu.
Agustino Magede huyu alikuwa ni mwalimu wa somo la Kiswahili ambaye alikuwa akimpenda sana Herieth, alivutiwa sana kuwa naye tangu siku ya kwanza alipoweza kumuona msichana huyo mrembo. Alikuwa ni Baba wa familia ambapo katika maisha yake alibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume.
Alikuwa ni Baba ambaye hakuwa akiijali familia yake, starehe yake kubwa ilikuwa ni wanawake. Alikuwa akiutumia muda wake mwingi katika kuwatongoza wanafunzi ambapo alikuwa akiwarubuni na mwisho wa siku kufanya nao mapenzi.
Alitembea na wasichana wengi sana pale shuleni na kila mwanafunzi ambaye aliyewahi kutembea naye na kuweza kushika ujauzito wake alikuwa akiwalazimisha watoe ili kuendelea kufanya ibaki kuwa siri yao.
Moyo wake ulimtamani Herieth, kitu kikubwa kilichomjia katika akili yake ni kuhakikisha anafanikiwa kumpata na hatimaye anafanya naye mapenzi, hiyo ndiyo ilikuwa starehe yake kubwa, alikuwa akipenda kufunua sketi za wasichana sana.
“Unaitwa nani?”
“Herieth.”
“Herieth?”
“Ndiyo.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Una jina zuri sana kama ulivyokuwa wewe.”
“Asante.”
“Halafu hongera, umefanya vizuri sana katika somo langu.”
“Asante.”
“Unaishi na nani?”
“Wazazi wangu.”
“Una simu?”
“Ndiyo ila huwa natumia siku za weekend.”
“Sawa unaweza kunipatia namba yako?”
“Ndiyo.”
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Mwalimu Agustino na Herieth. Herieth aliamua kumpa namba ya simu Mwalimu wake huyo ambaye alionekana kuwa na uchu wa kuwa naye kimapenzi na kitu kilichoendelea ni kuchat na kuzungumza kila siku za weekend ambapo waliweza kuongea mambo mengi sana.
Ilikuwa ni siri kati yao na hawakutaka kila mtu afahamu kile kilichokuwa kikiendelea. Licha ya utajiri aliyokuwa nao Baba yake kama vile kutembelea magari ya kifahari, kumili hoteli kubwa za kitalii, nyumba nzuri, kuwekeza katika biashara mbalimbali lakini bado Herieth aliendelea kudanganyika na ahadi za Mwalimu huyo ambaye alimuahidi kumuoa.
“Unanidanganya.”
“Kweli niamini lazima nikuoe, wewe ndiyo mwanamke wa ndoto yangu.”
“Kweli?”
“Wewe niamini na tena nitakufanyia mpango ili mtihani wako wa mwisho wa Taifa uweze kufaulu.”
Hilo ndilo lililokuwa kosa kubwa ambalo alilifanya mwalimu Agustino kwa Herieth, kitendo cha kumuahidi kuwa angeweza kumuoa na kumfanyia mpango ili aweze kufaulu katika mtihani wake wa Taifa hakika kilimchanganya sana Herieth. Kwa muda mfupi aliyoweza kuhamia pale shuleni akajikuta akizama katika dimbwi la kimapenzi na Mwalimu wake. Alikuwa akimpenda sana katika moyo wake na wala hakutaka kila mtu aweze kufahamu hilo, ilibaki kuwa ni siri ya moyo wake.
Hakukuwa na mwanafunzi aliyekuwa akifahamu mahusiano kati ya Herieth na mwalimu Agustino, kila mtu alifahamu kuwa Herieth alikuwa peke yake, hakuwa akijihusisha katika mtandao wa kimapenzi na mwanafunzi yoyote yule. Uzuri wake ulifanya wengi waamini kuwa ilikuwa ni vigumu kwa yeye kuweza kumkubalia mtu kirahisi, alionekana kuwa msichana aliyetokea katika familia ya kitajiri sana na hilo ndilo lililozidi kuwafanya wanafunzi waliyokuwa wakimtamani washindwe kuchukua hatua katika kuziwasilisha hisia zao.
Katika kipindi hicho Selestine alizidi kujiaminisha kuwa Herieth angeweza kuwa wake, alizidi kuamini hilo hasa baada kumuona Herieth akiutumia muda mwingi kukaa na wasichana wenzake, hakuwa akijichanganyachanganya na wavulana jambo ambalo Selestine lilizidi kumpa matumaini ya kuweza kumpata.
Alikuwa tayari ameshamueleza hisia za moyo wake na kwa jinsi alivyokuwa akimpenda kuliko msichana yoyote pale shuleni. Aliutumia muda wake mwingi katika kumshawishi Herieth ili aweze kumkubalia ombi lake ambapo baada ya kumueleza Herieth aliomba aweze kupewa muda ili afikirie.
“Mbona inachukua muda hivyo?” aliuliza Selestine, wakati huo ilikuwa ni majira ya jioni, wanafunzi walikuwa tayari wamesharuhusiwa kurejea nyumbani.
“Kwani unataka nini?” aliuliza Herieth.
“Nataka kujua jibu langu Herieth nakupenda sana.”
“Ndiyo nafahamu lakini kwanini usisubiri?”
“Nisubiri nini Herieth.”
“Kuwa mvumilivu nitakujibu,” alisema Herieth.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kitendo cha Herieth kushindwa kumjibu Selestine katika wakati ambao alikuwa akiuhitaji kilizidi kumuweka katika wakati wa mawazo. Hakujua ni nini kilichokuwa kipo nyuma ya pazia mpaka Herieth ashindwe kumjibu jibu ambalo alikuwa akilisubiria kwa hamu kubwa sana. Moyo wake haukuacha kumfikiria msichana huyo na kila alipokuwa akimuona au hata wakati mwingine kuzungumza naye alijikuta akizidi kumpenda kana kwamba alikuwa tayari ameshapewa jibu lake.
“Kwanini hataki kunipa jibu langu?” alijiuliza Selestine alipokuwa nyumbani kwao kisha kichwani yakamjia mawazo kuwa Andrew ndiyo chanzo cha yote hayo, alikuwa ndiye mtu ambaye alisababisha yote hayo hata kitendo cha kuchelewa kupewa jibu lake pia aliweza kuhusika.
“Andrew!” aliita Selestine kwa ghadhabu huku akiwa amekunja ngumu kisha akaipiga pembezoni mwa kitanda, alihisi maumivu makali mno lakini aliyavumilia.
Wazo lililomjia kichwani mwake ni kuhakikisha anamfanyia chochote Andrew ili mradi aweze kukaa mbali na Herieth, aliamini yeye ndiye alikuwa sababu ya yote yale kutokea jambo ambalo halikuwa kweli.
****
Andrew alianza kuwa mpenzi wa kusoma riwaya mbalimbali za kimapenzi, alikuwa akipenda sana kusikiliza nyimbo za kimapenzi pamoja na kutazama filamu za kimapenzi.
Chumbani kwake kulitawaliwa na majarida mengi yaliyokuwa yakihusu mapenzi. Hakukuwa na kitu alichokuwa akitaka kujifunza kwa wakati huo zaidi ya mapenzi. Mbali na kuutumia muda wake katika kusoma riwaya za kimapenzi, kusikiliza nyimbo pamoja na kutazama filamu za kimapenzi lakini hakuacha kutilia mkazo katika masomo yake. Alikuwa akijitahidi sana kuwekeza akili nyingi katika masomo yake japo mapenzi yalikuwa yakimuendesha lakini hakuacha kusoma kwa bidii, alizaliwa katika familia iliyokuwa na maisha ya kawaida sana hivyo aliamini elimu ndiyo ngao pekee ambayo ingeweza kumsaidia katika maisha yake.
Kuna kipindi alikuwa akitazama filamu za kimapenzi halafu akawa anajaribu kukariri yale maneno waliyokuwa wakiyazungumza wale waigizaji kwa lengo la kwenda kumwambia Herieth lakini alipofika shuleni na kumuona maneno yote yaliweza kumpotea, hakujua ni nini alitakiwa afanye kwa msichana huyo aliyetokea kumpenda sana. Katika maisha yake hakuwahi kujihusisha na mahusiano na msichana yoyote. Herieth ndiye msichana pekee ambaye alitokea kumpenda. Hisia za mapenzi juu yake hakujua zilitokea wapi.
Ama kwa hakika mapenzi ni majani huota popote, hivi ndiyo ilivyotokea kwa Andrew, alikuwa akimpenda msichana katika mazingira ambayo hakutegemea kabisa.
“Mwambie ukweli usimfiche.”
“Sasa nitamueleza nini?”
“Kuhusu hisia zako.”
“Nitaanzia wapi?”
“Ina maana hujui kutongoza?”
“Hapana ila naogopa.”
“Sasa unaogopa nini?”
“Hawezi kunichukia?”
“Hawezi wewe nenda kamwambie.”
“Mh!”
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Martha na Andrew. Martha alikuwa ni rafiki yake na Andrew, kwa muda ambao wanafunzi wenzake walikuwa wakimtukana na kumsema kuwa Andrew alikuwa ni shoga, Martha kitendo hicho hakuweza kupendezewa nacho kabisa, aliamua kuwa na ukaribu na Andrew, ukaribu wake uliweza kuletwa na uwezo mkubwa aliyokuwa nao Andrew darasani, alikuwa akiongoza katika kila mtihani waliyokuwa wakifanya.
Maneno ya Martha yaliweza kukaa vyema kichwani mwa Andrew, alitakiwa kuuvunja ukimya na kwenda kumueleza ukweli Herieth kuwa alikuwa akimpenda sana. Hakujua alitakiwa aanzie wapi kuzifikisha hisia zake na hiyo ndiyo ilikuwa kazi kubwa ambayo ilimkabili kiasi kwamba kuna muda alihisi kushindwa lakini kila alipoyakumbuka maneno ya Martha alijikuta akipata tumaini jipya na akadhamiria kwenda kumueleza ukweli Herieth.
Alianza na kuandika barua ya kimapenzi ambayo hata katika uandishi wake uliweza kumpa tabu. Aliandika hivi;
Mpendwa Herieth,
Natumaini u mzima wa afya kabisa, binafsi mimi ni mzima wa afya na ninayofuraha kukuandikia barua hii yenye kubeba kila aina ya hisia zilizotawala moyoni mwangu.
Dhumuni la kuandika barua hii ni kukujulisha kuwa nakupenda sana kwani wewe ndiye mwanamke wa maisha yangu, ndoto yangu ni wewe. Wewe ndiyo uliyeuteka moyo wangu wa mapenzi. Hisia zangu zipo kwako, wewe ndiye unayezimiliki. Usiku silali kutwa mawazo juu yako. Mzimu wa mapenzi unaniendesha vibaya unanituma nikufate wewe. Nakupenda sana Herieth.
Nimeona ni bora nikuandikie katika maandishi ili ufahamu hisia zangu, nakupenda sana na nipo tayari kuwa na wewe.
Ni mimi wako Andrew.
Aliiandika barua hiyo majira ya usiku alipokuwa chumbani kwake na alipanga siku iliyofuata aweze kumpelekea Herieth msichana aliyeamini aliumbwa kwa ajili yake. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku iliyofuata aliamua kumpa barua hiyo Martha ili aweze kumpelekea Herieth, aliamini kwa maandishi aliyokuwa ameyaandika katika barua hiyo ni lazima yangeweza kumshawishi Herieth mpaka akakubali kuwa wake. Alizidi kujipa matumaini katika hilo na kila wakati alionekana kuwa mwenye furaha.
“Kwanini hutaki kumpa wewe mwenyewe?” aliuliza Martha.
“Naomba unisaidie Martha, najua nikimpelekea mwenyewe ataikataa,” alijibu Andrew.
“Mmh!” aliguna Martha kisha akaipokea barua hiyo ilikuwa imewekwa kwenye bahasha ambayo kwa juu ilikuwa imeandikwa kwa maandishi makubwa “KWAKO MPENDWA HERIETH.”
Martha aliamua kuipokea barua hiyo na kufanya kama alivyoambiwa. Hakutaka kupindisha chochote, alimfuata Herieth na kumwambia kuwa alikuwa na ujumbe wake hivyo alitakiwa kumpatia.
“Ujumbe wangu?” aliuliza Herieth huku akionekana kushangaa.
“Ndiyo,” alijbu Martha.
“Ujumbe wangu kutoka kwa nani?”
“Upokee kwanza kisha utafahamu ukishausoma.”
“Kwani ukiniambia aliyekupa unahisi utapungukiwa nini?”
“Pokea kwanza,” alisema Martha.
Herieth aliamua kuipokea barua hiyo, alionekana kuwa mwenye shahuku ya kutaka kujua kilichokuwa kimeandikwa ndani. Aliyasoma yale maandishi yaliyokuwa yameandikwa juu ya bahasha, yalizidi kumfanya atamani kuisoma, kila wakati alikuwa akitamani kuisoma.
Aliporudi nyumbani siku hiyo hakukuwa na kazi yoyote aliyotamani kuifanya, alijifungia chumbani kwake akaifungua bahasha ile kisha akaitoa barua, akaanza kuisoma na baada ya kumaliza kusoma alianza kubadilika, uso wake ulitawaliwa na hasira.
Hakutaka kuamini kile alichokuwa akikisoma kuwa kilikuwa kimetoka kwa Andrew, alimchukua sana mvulana huyo kutokana na tabia zake alizokuwa ameambiwa za ushoga. Kitendo cha kumuandikia barua ya kimapenzi halafu akaamua kumtumia alikiona kuwa ni kitendo cha kumdharau.
“Hivi huyu shoga ananitafutia nini mimi?” hili ndiyo swali kubwa lililomjia kwa wakati huo alipomaliza kuisoma barua. Moyoni hakutaka kumuhifadhi Andrew mvulana aliyeamini alikuwa na tabia za ushoga.
****
Alipokuwa shuleni aliamua kuitumia nafasi ile katika kumtangaza Andrew kwa kitendo alichokuwa amekifanya cha kumuandikia barua ya kimapenzi. Hilo lilizidi kumfanya Andrew achekwe na kila mwanafunzi na kuonekana alikuwa limbukeni katika swala zima la kimapenzi na ni hapa ambapo wale waliyoamini alikuwa ni shoga walizidi kumchukia kupitiliza. Alionekana kuwa domo zege.
“Hivi nitaanzaje kumpenda shoga?”aliuliza Herieth alipokuwa na rafiki zake ambao muda wote walikuwa wakicheka.
Hakukuwa na neno zuri walilokuwa wakilitumia katika kumtaja Andrew, kila mtu alimtaja kwa ubaya na hii ndiyo sababu iliyomfanya azidi kuchukiwa na kila mtu.
****
“Oya umesikia habari mpya?”
“Habari gani?”
“Kuhusu Andrew.”
“Kafanyaje tena huyo shoga?”
“Nasikia amemuandikia barua Herieth eti! Anampenda.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Acha utani wewe.”
“Sasa niache utani upi nenda kule kwa mademu wakakusimulie.”
“Unasema kweli?”
“Sasa nikudanganye ile iweje?”
“Duh!” alisema Selestine.
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Derick na Selestine, muda huo ulikuwa ni wa mapumziko. Selestine hakutaka kuamini kirahisi kile alichokuwa akiambiwa na Derick, alichoamua kukifanya ni kwenda kwa wasichana na kuwauliza kile kilichokuwa kimetokea na waliweza kumsimuliwa kila kitu. Alibaki katika mshangao mkubwa baada ya kusikia kuwa Andrew alikuwa amemuandikia barua ya kimapenzi Herieth msichana aliyekuwa akimpenda sana na tayari alikuwa ameshamueleza ukweli huo.
Alihisi Andrew alikuwa akimzibia riziki yake, kitendo cha kumuandikia barua Herieth alikiona kama alikuwa amemdharau kwa wakati ule na ni hapa ambapo alikuwa tayari ameingia katika anga zake za kumfuatilia msichana aliyekuwa akimpenda.
Hakutaka kupoteza muda kwa wakati huo aliamua kumfuata Andrew alipokuwa darasani kisha akaanza kumpiga ngumi, mateke huku akimsindikiza na matusi lukuki ya nguoni. Alihisi kwa kipigo kile alichokuwa akimpiga Andrew hakikutosha na sasa akaamua kuchukua kiti na kuamua kumpiga nacho kichwani na hapohapo Andrew aliweza kuanguka chini na kupoteza fahamu, damu zikaanza kuchirizika mahali pale. Selestine hakutaka kupoteza muda aliamua kutoka nje ya darasa na kukimbia kusikojulikana.
Hatimaye muda wa mapumziko ulipoisha Wanafunzi walianza kuingia darasani.
LAHAULA!
Walikutakana na mwili wa Andrew ukiwa chini huku damu zikiendelea kuchirizika kutokea maeneo ya kichwani.
Kitendo cha kuukuta mwili wa Andrew ukiwa chini huku damu zikiendelea kuvuja sehemu za kichwani hakika kilimuogopesha kila mwanafunzi aliyemtazama. Sauti za kelele pamoja na hali ya sintofahamu ndiyo iliyowagubika wanafunzi.
“Amekufaa!” zilisikika sauti za Wanafunzi zikisema katika hali ya mshangao.
Hakukuwa na mwanafunzi aliyetaka kuamini kuwa Andrew alipoteza maisha tena alikuwa amefia darasani, tukio hilo liliwafanya wazidi kuingiwa na hofu, wakazidi kujiwa na maswali yaliyokosa majibu.
Waliamua kwenda kumuita Mwalimu wa darasa aliyejulikana kwa jina la Jane, alipofika macho yake yalikutana na mwili wa Andrew ukiwa chini huku ukiendelea kuvuja damu sehemu za kichwani. Aliusogelea mwili wa Andrew kisha akajaribu kumuita kwa jina akidhani angeweza kuamka lakini haikuwa hivyo, Andrew alikuwa amepoteza fahamu, hilo lilimfanya Mwalimu Jane aingiwe na hofu.
“Kwani amefanyaje?” aliwauliza Wanafunzi wake waliyokuwa wamemzunguka kwa wakati huo.
“Hatujui Mwalimu sisi tumemkuta ameanguka hapo chini,” alijibu mwanafunzi mmoja wa kike.
”Una uhakika kuwa hajafanya kitu?”
“Ndiyo Mwalimu,” alijibu yule Mwanafunzi.
Jibu hilo halikumuingia Mwalimu Jane kichwani, kwa akili ya haraka haraka alianza kuingiwa na wasiwasi, hakutaka kuamini kirahisi kuwa hakukuwa na tatizo lolote lililokuwa limetokea.
Alichoamua kukifanya ni kuanza kumpatia huduma ya kwanza Andrew huku akisaidiana na baadhi ya wanafunzi ambao walionekana kuguswa na tukio lile. Baada ya kumaliza kumpa huduma ya kwanza haraka taratibu za kumpeleka hospitali zilifuata, Mwalimu Jane aliondoka na wanafunzi watatu ambao mmoja wao alikuwa ni Martha rafiki yake na Andrew.
****CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Shuleni hakukuwa na mada nyingine iliyozungumziwa zaidi ya tukio lile lililokuwa limetokea, kila mwanafunzi alikuwa akisema lake. Wapo baadhi ya wanafunzi waliyosikika wakisema kuwa Andrew aliamua kujipiga na kitu kizito kichwani kwasababu ya jina lake kuzidi kuchafuliwa lakini katika hali hiyohiyo alikuwepo mwanafunzi mmoja wa kike wa kidato cha nne ambaye alisikika akisema kuwa wivu wa kimapenzi ndiyo uliyosababisha mpaka Andrew akapigwa kiasi kile. Alionekana kuwa mmbeya wa darasa, wanafunzi wote wakawa kimya kumsikiliza kwa wakati huo.
“Andrew amepigwa kisa wivu wa kimapenzi,” alisema.
“Embu acha kutudanganya wewe Shoga tangu lini akapenda?” alisema mwanafunzi mmoja mvulana ambaye alionekana kutoamini kabisa.
“Sasa hutaki kuamini nini?”
“Andrew ni shoga yani hata huyo msichana aliyependwa na shoga basi atakuwa hajielewi,” alisema yule mwanafunzi mvulana aliyeonekana kutoamini kabisa.
“Ni nani sasa atakuwa amempiga?” alidakia mwanafunzi mwingine msichana kwa kuuliza swali.
“Ina maana humfahamu?”
“Kama ningemfahamu ningekuuliza jamani?”
“Ni Selestine,” alijibu msichana huyo na kuwaacha wanafunzi wote wakibaki katika hali ya mshangao.
Kwa muda huo Selestine hakuwa darasani, hilo lilianza kuwafanya waanze kuamini maneno hayo kuwa alihusika kwa namna moja ama nyingine lakini hawakujua ni msichana gani ambaye alisababisha mpaka Andrew akapigwa kiasi kile. Hilo lilikuwa ni swali ambalo kila mwanafunzi alikuwa akijiuliza lakini kutokana na umbeya wa yule mwanafunzi aliyesema kuwa Andrew alipigwa kisa wivu wa kimapenzi hakutaka kulifumbia macho hilo, aliamua kusema ukweli kwani kila kitu kilichokuwa kikiendelea alikuwa akikifahamu.
“Msichana mwenyewe aliyesababisha ni Herieth,” alisema maneno yaliyowafanya wanafunzi wote washikwe na bumbuwazi, wakamtazama Herieth ambaye kwa muda wote huo alionekana kuwa mkimya, hakutaka kuzungumza lolote lile, macho yake alikuwa ameyaelekezea chini.
Hakukuwa na Mwanafunzi aliyetaka kuamini kuwa Herieth ndiye alikuwa msichana aliyesababisha mpaka Andrew akapigwa kiasi kile, uzuri wa msichana huyo uliwafanya wasiamini kama kweli Andrew alidiriki japo kumwambia neno nakupenda, walimdharau kwa kila kitu, wengi hawakutaka kukubaliana na ukweli huo ambao walikuwa wakielezwa.
****
Hatimaye waliweza kufika katika hospitali ya Mkoa iliyojulikana kwa jina la KILIMANJARO CHRISTIAN MEDICAL CENTER (KCMC), Andrew akaweza kupokelewa na kuingizwa moja kwa moja katika chumba cha upasuaji “Theatre” na huko madaktari walikwenda kuianza kazi yao ya kujaribu kuyaokoa maisha yake ambapo mpaka kufikia wakati huo alikuwa bado amepoteza fahamu.
Mwalimu Jane aliamua kumpigia simu Mama yake Andrew na kumueleza tatizo lililokuwa limetokea kwa mwanaye.
“Mwanangu amefanyaje tena?” aliuliza Mama Andrew kwa sauti iliyogubikwa na mshangao, wakati huo alikuwa akizungumza kwenye simu na Mwalimu Jane. Mwalimu wa darasa ambaye alimkabidhi mwanaye.
Hakutaka kupoteza tena muda baada ya kusikia kuwa mwanaye alikuwa amepoteza fahamu na kwa wakati huo alikuwa hospitali ya Mkoa, alichoamua kukifanya ni kutoka na kuanza kuelekea huko hospitalini alipokuwa mwanaye.
Alipokuwa kwenye daladala hakuwa akiwaza kitu kingine zaidi ya mwanaye, Kila alipokuwa akimkumbuka na kwa jinsi alivyokuwa akimpenda alihisi kuchanganyikiwa, alikuwa ndiye mtoto wa pekee katika maisha yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akili yake bado iliendelea kumfikiria mwanaye ambaye alitamani kumuona kwa wakati huo, kuna kipindi alihisi kama dereva wa daladala alikuwa akitembea mwendo wa polepole, alitamani kumwambia akimbize lakini yote yalikuwa ni mawazo yake tu! alionekana kutokuwa sawa kwa wakati huo.
Alipofika hospitalini aliongoza moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha upasuaji na kumkuta Mwalimu Jane pamoja na wanafunzi wake wakiwa nje, walikuwa katika hali ya sintofahamu huku nyuso zao zikitawaliwa na huzuni.
Alipowaona wakiwa katika hali hiyo alianza kulia huku akilitaja jina la mtoto wake Andrew, alikuwa akiomboleza kana kwamba kulikuwa kumetokea msiba eneo lile. Machozi aliyokuwa akiyatoa yalimfanya kila mtu aanze kutokwa na machozi, walikuwa wakimlilia Andrew ambaye mpaka kufikia wakati huo hali yake ilikuwa si nzuri.
Kwa upande wa pili Jopo la madaktari waliendelea na kazi yao, walikuwa makini katika kuyaokoa maisha ya Andrew. Kila mmoja alionekana kuwa makini kwa nafasi yake. Dokta Masawwe huyu ndiyo alikuwa Daktari bingwa ambaye alikuwa amebobea katika kitengo cha upasuaji. Alikuwa amehusika kuanzia mwanzo mpaka mwisho katika upasuaji wa Andrew na kuhakikisha kila kitu kilikuwa kikienda sawa.
“Koh! Koh!” alikohoa mara baada ya kumaliza kushona sehemu za majera aliyoyapa Andrew sehemu za kichwani.
“Nini tena?” aliuliza Nesi huku akimtazama Dokta Masawwe ambaye alikuwa Kama kuna kitu alikigundua.
“Kuna tatizo limempata,” alisema Dokta Masawwe huku akionekana kumaanisha kauli yake.
“Tatizo gani?” aliuliza Nesi.
“Amepata mtikisiko katika ubongo wake, tatizo hili tunaliita Concussion pia mishipa yake ya fahamu imeshtuka hivyo imepoteza mawasiliano na uti wa mgongo kwa kifupi amepooza,” alisema Dokta.
“Amepooza?” aliuliza Nesi yule kwa mshangao, alionekana kumuonea huruma Andrew hasa pamoja na umri aliyoonekana kuwa nao, alionekana kuwa mwanafunzi ambaye bado alikuwa akipigania ndoto za maisha yake.
“Ndiyo hataweza tena kuamka kitandani,” alisema Dokta Masawwe.
“Kweli?” aliuliza Nesi.
“Ndiyo hataweza tena kuamka kitandani, maisha yake yote yatakuwa ni ya kitandani,” alisema Dokta Masawwe.
“Amepoteza kumbukumbu?”
“Ndiyo,” alijibu Dokta Masawwe.
Yalikuwa ni maneno madogo yaliyozungumzwa lakini yalibeba uzito mkubwa ambao ulichanganyika na maumivu ya hali ya juu. Kwanza Andrew alikuwa ni miongoni kati ya watahiniwa ambao walikuwa wakitarajiwa kufanya mitihani yao ya kumaliza kidato cha nne kwa mwaka huo pili alikuwa amepooza na kupoteza kumbukumbu.
Maneno ya Dokta Masawwe yalimaanisha kuwa Andrew hakutakiwa tena kuendelea na shule, maisha yake yalibadilika na kuwa ya kitandani tena kibaya zaidi alikuwa amepoteza kumbukumbu, hakuwa akikumbuka kitu chochote kile kilichowahi kutokea katika maisha yake.
Ilikuwa ni taarifa mbaya sana ambayo haikutegemewa na kila mtu, hakukuwa na mtu aliyetaka kuamini ukweli wa kile ambacho Dokta Masawwe alikuwa akikizungumza. Tukio la kupooza Andrew na kupoteza kumbukumbu lilikwenda kumuumiza kila mtu.
“Dokta unasema mwanangu amefanyaje, amepooza?” aliuliza Mama Andrew ambaye alionekana kutoamini kile alichokuwa akiambiwa na Dokta, macho yake yalikuwa yamejaa machozi kwa wakati huo.
Kila kitu alichokuwa akiambiwa kuhusu mwanaye kilikuwa ni maumivu, alihisi maumivu makali sana katika moyo wake, maumivu ambayo alishindwa kuyavumilia mwisho akabaki akilia machozi ya uchungu wa mwanaye. Hakutaka kuamini kuwa Andrew alikuwa amepooza tena alipoteza kumbukumbu zote.
“Mwanangu….mwanangu amka usinyamaze…mwanangu amka….amka….amka mwanangu,” alisema Mama Andrew kwa sauti iliyochanganyika na kilio.
Sauti ya kilio chake ilikwenda kumuumiza kila mtu hata kwa upande wa mwalimu Jane na wanafunzi walianza kulia lakini sauti ya vilio vyao vilifunikwa na sauti ya kilio cha Mama yake Andrew ambaye alionekana kuwa na uchungu uliopitiliza.
Alimpenda sana mtoto wake kwani ndiye alikuwa mtoto wa pekee aliyebahatika kumpata katika maisha yake. Alikuwa ni Mama mjane ambaye aliishi maisha ya kuhangaika usiku na mchana ili mtoto wake aweze kusoma ana baadae aje kuwa mkombozi wa maisha yake. Aliamini katika elimu na ndiyo sababu risala kubwa aliyokuwa akimwambia mtoto wake. Alibahatika kuwa na mtoto mwenye akili sana darasani na hilo ndilo lililozidi kumpa matumaini ya kuwa kuna siku angeweza kuyafahaidi matunda ya mtoto wake.
****
Ndoto zake zote zilizimwa na ugonjwa alioupata wa kupooza mwili pamoja na kupoteza kumbukumbu. Alipopata fahamu alijikuta amelazwa kitandani, hakujua pale alikuwa wapi wala hakujua lolote lile lililokuwa likiendelea katika maisha yake, alipoteza kumbukumbu, hakukumbuka kitu chochote kilichowahi kutokea hapo kabla hata Mama yake alipokuja alipata wakati mgumu wa kuweza kumtambua. Alibaki kuwa Andrew kijina.
“Mwanangu,” aliita Mama Andrew alipoingia kumuona mwanaye mara baada ya kuambiwa kuwa alikuwa ameshapata fahamu lakini Andrew hakujibu lolote alibaki akiwa amenyamaza huku akimtazama Mwanamke aliyekuwa mbele yake, hakujua kama alikuwa ni Mama yake mzazi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Machozi ndiyo yaliyotawala katika uso wa Mama yake Andrew, muda wote alikuwa akilia machozi ya uchungu wa mwananye ambaye aliteseka naye sana tangu alipowez kumpoteza mume wake baada ya kuangukiwa na kifusi cha udongo alipokuwa mgodini Arusha na tangu siku hiyo jukumu la kumlea Andrew likabaki mikononi mwake.
****
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment