Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

CHOKORAA - 1

 





    IMEANDIKWA NA : GEORGE IRON MOSENYA





    *********************************************************************************



    Simulizi : Chokoraa

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Moshi mweusi uliokuwa unatoka katika jalala lililokuwa linachomwa ulifanya mfano wa ukungu usiopendeza



    machoni.

    Wapita njia waliongeza mwendokasi walivyokaribia eneo lile. Wengine waliziba pua zao kwa kutumia viganja vya



    mikono yao kuepukana na hewa hiyo chafu.

    Baadhi yao walijiziba na magazeti, wengine kwa bahasha zao. Ilikuwa ni jioni na kila mmoja alikuwa anarejea kutoka



    katika mizunguko yake.

    Kwa jinsi watu walivyokuwa wametingwa na mambo vichwani mwao hawakuweza kulishuhudia kundi la viumbe hai



    ambalo halikubabaishwa na moshi huo mzito. Na hata kama wangeona wasingekuwa na la kusaidia zaidi ya kupata la



    kuongea na kujisahaulisha suluba ya siku nzima huko walipotoka.

    Ardhi iliyobeba uchafu wa kila aina iliyopewa jina la jalala ilikuwa katika mahangahiko ikifukuliwa kwa fujo na



    watoto wanne wa rika moja huku mkubwa akikadiriwa kuwa na miaka kumi na mitano

    Macho yao yalikuwa mekundu, matambala ambayo zamani yaliitwa nguo yalifunika miili yao.

    Wengine walikuwa wameinama wengine wakiwa wamepiga magoti, mikono yao ikiwa 'bize' kuchimba ardhi na kutoka



    na vyuma chakavu.

    Matambala waliyovaa yaliwafanya wote wafanane, na ilikuwa ngumu kutambua iwapo wana jinsia tofauti.

    Hakuna aliyezungumza na mwenzake, nyuso zao zilizotiririka jasho zilitangaza njaa kali na chuki.

    Mtoto mmoja alivyojiridhisha kuwa eneo lile vyuma vilikuwa vimekwisha alinyanyuka na mfuko wake wa



    chumvichumvi, akachukua mkono wake mchafu akajipangusa jasho. Tambala alilokuwa amevaa lilisomeka kwa shida



    maandishi 'I LOVE TANZANIA', lilikuwa kubwa kumpita na lilikuwa limetatuka na kuruhusu matiti yake yaliyokuwa



    yameanza kujifunza kusimama yachungulie nje. Huyu pekee alikuwa mkubwa kupita wenzake.

    Alijikongoja na fuko lake hadi akalifikia jalala jingine. Hapo pia alipapasa bila kupata chochote. Akasimama wima



    akiwa amekata tamaa. Alipopiga hatua nne kuliacha jalala macho yake yalivutiwa na kifurushi cha uchafu wa siku



    nyingi, akatua tena fuko lake akachukua kimti kigumu akaliendea lile furushi na kuanza kupekenyua.

    Lahaula! Tabasamu pana likachanua usöni mwake, akayapongeza macho yake kwa kuvutiwa na furushi lile. Akavuta



    kwa nguvu, akatoka na jembe chakavu.

    Biashara nzuri kwa siku hiyo!

    Wakati anasimama kuliendea fuko lake, akasita kabla ya kupiga hatua. Hakuwa peke yake!

    "Siso yangu hiyo!" sauti ya kiume ilikoroma. Binti akamtazama yule chokoraa mwenye nywele zinazotaka kufanana na



    mwarabu, ngozi nyeusi yenye ukurutu unaotiririka jasho.

    "Siso yangu hiyo uliyoshika" sauti ya mvulana haikuwa na mzaha. Alimaanisha!

    Yule binti akashtuka na kulitazama lile jembe mkononi kana kwamba hakutambua kama amelishikilia.

    Kisha akapuuzia akapiga hatua kadhaa kuliendea fuko lake, yule kijana akamfanyia shambulizi la kushtukiza,



    akamnyakua lile jembe. Alipotaka kukimbia yule binti akawa mwepesi akakamata shati chakavu la yule kijana. Kama



    vile wembe mkali unavyokutana na karatasi laini ndivyo lilivyoachana tambala lile.

    "Mamaa! Umenichania shati we malaya!"

    "Nani malaya? Malaya mama yako aliyekuzaa akakutupa jalalani mwanahizaya mkubwa nipatie jembe langu!" binti



    naye alijibu mapigo kwa sauti kali.

    Pasipokutegemea alivamiwa na kuchabangwa teke tumboni kwa nguvu, akajipindua na kuanza kuugulia maumivu.



    Tambala lililokuwa linamuhifadhi likakosa umakini, chupi yake ambayo zamani ilikuwa nyeupe lakini sasa ikiwa kama



    ina kutu ilichungulia nje. Mbavu zake zilizohesabika kutokana na wembamba zilitokeza nje.

    Yule mhanga wa kuchaniwa shati akiwa hajaridhika na pigo lile alimrukia tena akamchabanga teke kali katika zile



    mbavu zilizokuwa nje kimakosa, sasa binti akanyoosha mikono kuomba msamaha huku maumivu yakiukunja uso



    wake.

    Hakuupata msamaha bali kukaribisha kipigo kingine. Tumboni tena!

    "Mariaa! Mariaa!" sauti ilisikika kutokea katika ule moshi mzito.

    Maria aliyekuwa amekumbatia uchafu wa jalalani alisikia lakini hakuweza kugeuka. Mbavu zilikuwa zinamuuma na



    alipumua kwa shida sana.

    Vishindo vya miguu vikafika karibu yake.

    "Kwanini unampiga?

    "Kwanini unampiga?" sauti ya kitoto ililalamika kwa uchungu.

    "Kwani na wewe dogo unasemaje?" alijibu kwa ubabe na jeuri yule mhanga wa kuchaniwa shati.

    Maria alisikia kila kitu lakini hakuweza kuongea. Alitamani yule mtoto angekuwa mtu mzima huenda angemsaidia.

    Yule kijana ambaye alikuwa kama amepandwa na mori ya kimasai, alijitazama tena shati lake lililoachana, hasira



    ikapanda upya!

    Akampuuzia yule mtoto. Akamrukia Maria. Sasa aliamua kutumia mikono.

    "Utalipa shati langu utalipa we malaya." maneno hayo hayakutoka bure, yalisindikizwa na mdundo wa mapigo ya



    ngumi na vibao katika uso wa Maria, ambaye naye tambala lake lilikuwa limeuacha mwili. Matiti mawili madogo



    yakitazamana na mbingu za bluu.

    Hapa likatokea tukio lisirotarajiwa na wote mpiga na mpigwa.

    Yule mtoto mwenye umri wa miaka tisa aliyekulia katika kundi maarufu na hatari jijini Mwanza la 'watoto wa



    wakoma' alichomoka mbiombio akamfikia mpigaji.

    Kitendo cha sekunde tatu hali ikabadilika. Maria akabaki huru, yule mpigaji akatua chini akiwa anagalagala, damu



    ikiruka kwa fujo mgongoni mwake. Mtoto wa wakoma alikuwa anatoweka kuelekea mashariki.

    Wembe wenye makali ulikuwa umepenya katikati ya mgongo wa yule mpigaji.

    ****

    Chumvi chumvi ilipenya katika koo lake alivyojaribu kumeza mate. Akatambua kuwa midomo ilikuwa imepasuka.



    Mbavu zilikuwa zinauma sana lakini hakuwa na budi kusimama. Akaunganisha tambala lake, kidogo likamstiri. Yule



    mpigaji hakuwepo tena eneo lile. Zilisalia damu nzito pale ardhini.

    Maria alibaki katika sintofahamu, hakujua ni kwa namna gani yule mtoto alimuokoa. Sasa alikuwa amesimama wima,



    mwili wote ukiwa unauma na giza lilikuwa limeanza kutanda.

    Upepo uliokuwa unavuma kutokea jalalani, jaa maarufu la 'mchafu kuoga' jijini Mwanza. Uliileta harufu mbaya katika



    pua zake.

    Kwa mara ya kwanza katika maisha yake akajuta kuzaliwa. Akaupata ukiwa maradufu, ukiwa wa kutengwa na dunia

    Taswira ya mama yake mzazi ikakimeza kichwa chake, japo alilelewa naye kwa kipindi kifupi lakini anakumbuka



    amani aliyokuwanayo kwa kuyapata malezi yale bora.

    Akiwa na miaka tisa pekee, mama yake (Mama Maria) baada ya kutoka masomoni katika chuo cha Kigurunyembe



    Morogoro anapatwa na maswaibu ya kuchekesha, baada ya kuyakwepa magari mjini Morogoro na jijini Dar es salaam



    alipokwenda katika mafunzo ya vitendo. Anakuja kugongwa na baiskeli mjini Singida. Aliyemgonga ni mwanamke.



    Badala ya kukasirika mama Maria alicheka.

    Alicheka maana hakuumia!

    Hata alivyomsimulia mumewe na mtoto wao wa pekee Maria. Wote walimcheka na kumtania!!

    Siku iliyofuata hakuweza kuamka!

    Mguu ulikuwa umevimba! Mguu ule uliogongwa na baiskeli.

    Baba Maria alishangaa. Maria alikuwa shuleni wakati huo!

    Kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo mguu ulizidi kuvimba!

    Huduma za hospitali zikahitajika.

    Akakimbizwa upesi.

    Ile tamthilia ya kuchekesha iliyoanzia kwa kugongwa na baiskeli, ikamalizikia kwa huzuni kuu. Mama Maria akaaga



    dunia hata kabla hajafika hospitali.

    Maria alimngojea mama yake aende kumchukua shuleni lakini hakutokea! Siku hiyo akajiunga na rafiki zake wakarejea



    nyumbani ambapo alikuta kundi la watu

    Wengi wakiwa wameizunguka nyumba yao. Ulikuwa msiba!

    Maria akiwa na miaka kumi na tatu akabakiwa na malezi ya baba pekee baada ya kuwa amerusha udongo kumfukia



    mama yake kaburini.

    Mzee Paul alivyorejea katika biashara zake. Yule mama aliyemgonga marehemu Mama Maria na hatimaye kupoteza



    uhai kimaajabu akawa haishi kufika pale nyumbani. Wakati mwingine alikuwa akimpeleka Maria shuleni, anampikia



    chakula.

    Baada ya miezi sita, Maria akatambulishwa rasmi kuwa yule ni mama yake mpya.

    Muuaji wa mama yake sasa anakuwa mama yake!

    Angefanya nini angali ni mdogo!

    Akakubali!

    Mambo yakabadilika, yule mwanamke akaanza manyanyaso kwa Maria. Akamfanyisha kazi nzito kumzidi.

    Cha ajabu mzee Paul hakujali.

    Baada ya kuyazoea yale manyanyaso. Miaka miwili baadaye alikuja mgeni ambaye Maria alitmbulishwa kama kaka



    yake.

    Hili nalo hakupinga wala hakuuliza!

    Ule ukaka ukawa na utata ndani yake.

    Mara leo anamtekenya, mara amkumbatie.

    Maria hakuwa na pa kulalamika.

    Siku moja walipobaki wawili nyumbani yule kaka akambaka! Kisha akatoweka.

    Siku aliyomweleza mama yake wa kambo ndiyo siku aliyofukuzwa nyumbani.

    Maajabu! Baba akabariki uamuzi huo!

    Maria akiwa na miaka kumi na tano anapokelewa na mtaa wenye ndugu wachache wasiojali.

    Mapokeo hayo mabovu kutoka kwa ndugu anaowafahamu yanamfadhaisha!

    Baadaye akiwa kwa shangazi yake anagundulika kuwa ni mjamzito. Hakuna aliyetaka kumsikiliza, akalazimishwa



    kurudi nyumbani kwa baba yake.

    Akarejea kwa shingo upande. Siku hiyo aliyofika hakukuta mtu lakini funguo ulikuwa juu ya mlango. Maria



    akafungua na kuzama ndani!

    Akapokelewa na fungu la pesa katika meza ya kulia chakula. Akili ikakimbia maili mia mbele. Akawaza juu ya kutoa



    mimba, alihitaji pesa, kama vile kunguru anyakuapo vifaranga ndiyo naye alivyonyakua zile pesa zilizokuwa



    zimeigandamiza karatasi, yenye maandishi.

    Laiti kama angefikiria walau kuisoma ile barua, angegundua kuwa baba yake amejirudi anamtafta yeye (Maria) kwa



    udi na uvumba na barua ile ilikuwa ya kumfukuza yule mwanamke mwenye roho mbaya!

    Na zile zilikuwa pesa kwa ajili yake.

    Maria hakuisoma

    Laiti angeisoma asingefikia pale ambapo alifikia!!





    ***



    Doreen alilipokea tatizo la Maria kama la kwake. Ni msichana huyu pekee ambaye Maria alikuwa anamuamini kati ya



    rafiki zake. Kwa kuwa pesa likuwepo kila kitu kingewezekana.

    Vyuma vikapenya katikati ya miguu ya Maria, matusi ya nguoni mfululizo kutoka kwa daktari mwenye kipara ambaye



    tayari alikuwa amepokea shilingi elfu hamsini kwa ajili ya kufanya dhambi hii ya utoaji mimba. Hatimaye mabonge



    mabonge ya damu yaliyoanza kujikusanya katika mji wa uzazi wa Maria yakaharibiwa maksudi, mimba ikawa



    imetolewa kwa uchungu mkubwa.



    Ni Doreen aliyemshawishi Maria kukimbilia jiji la Mwanza kutafuta maisha. Maria hakufikiri mara mbili akakubali.

    Huku akapokelewa na mtaa, mtaaukamsulubu na sasa amepigwa vibaya na chokoraa wa kiarabu, amevimba usoni.

    Anamkumbuka mama yake mzazi.

    Anamkumbuka mama Maria.

    Nani kama mama???



    *******

    Baridi kali iliyoambatana na upepo mkali ilimuhangaisha sana binti ambaye alikuwa akishangaa huku na kule



    kuthibitisha kuwa ni mgeni katika jiji hil ambalo lna baridi kali likiambatana na jiji la Arusha.

    Mama aliyekuwa anamuongoza alikuwa amejikita katika mazungumzo na mwanamke mwenzake, waliongea



    kinyakyusa huku wakigongesha mikono yao kuonesha kuwa ni marafiki wa siku nyingi.

    “Maria!” aliita kwa sauti ya juu kidogo yule mama.

    “He! Kumbe anaitwa Maria!! Jina la mama yangu hilo.”

    Maria akiwa anasulubiwa na baridi alijongea huku akiwa anatetemeka.

    “Shkamoo mama.” Alisalimia kwa nidhamu lakini hakujibiwa.

    “Maria! Huyu ndiye bosi wako sawa. Nimekutoa Dar kwa ajili ya kufanya kazi sawa!! Usilete mchezo kabisa.”



    Mwenyeji wa Maria alimpa mawaidha mbele ya yule mama wa kinyakyusa aliyefahamika kwa jina la mama Atuganile



    na ofisi yake iliitwa ‘mama Atu mgahawa’.

    Maria kwa mara ya kwanza akawa pekee tena katika jiji la Mbeya. Maeneo ya Sai.

    Alimshukuru yule mama aliyempeleka Mbeya baada ya kumpa hifadhi ya muda jijini Dar es salaam baada ya mkasa wa



    kupigwa na mtoto chokoraa wa kiarabu.

    Maria alimchukulia yule mama kama Mungu wake wa hapa duniani!!

    Hakujua siri iliyopo sirini!!



    Siku hiyo alionyeshwa mahala pake pa kulala.

    Alistaajabu lakini hakusema.

    Ilikuwa ni lazima angoje mpaka shughuli za mgahawa zimalizike ndipo apangue mabenchi yaliyopo pale ndani ndipo



    aweze kulala. Alistaajabu kidogo kwa kuwa aliwahi kulala nje mara kwa mara jijini Mwanza akiwa chokoraa.



    Alinyeshewa mvua na kuumwa mbu.

    Kilichomstaajabisha kwa huko Mbeya ni ile hali ya hewa ya ubaridi kisha anakabidhiwa upande wa kanga kwa ajili ya



    kujifunika.

    Laiti mama yangu angekuwa hai…!!! Aliwaza Maria. Maisha yakaendelea.

    Shughuli za mgahawani zilikuwa na suluba lakini haikuwa tatizo kwa Maria maana mwili wake uliyazoea maisha yale.



    Ilikuwa siku ya jumapili usiku wa saa mbili! Kwa kawaida siku kama hii mama Atuganile huwa na kawaida ya



    kutofungua mgahawa. Kwani ni siku yake ya kuabudu. Siku ya jumapili hutumika kwa ajili ya maandalizi.

    “Unapafahamu Uyole?” mama Atu alimuuliza Maria. Akapata jawabu kuwa Maria hapafahamu.

    Mama Atu akamuelekeza Maria magari ya kupanda na wapi ashuke ili aweze kufikisha mzigo atakaompa. Maria alitaka



    kupingana na mama yule kisa ni usiku lakini akakumbuka kuwa pale hayupo kwa mama yake mzazi. Akatii!!

    Akapewa maelekezo pamoja na bahasha!! Akatoweka.

    Ndani ya dakika ishirini tayari kipanya kilikuwa kimezima injini maeneo ya Uyole.

    Kama alivyoelekezwa akiwa na bahasha yake mkononi alivuka barabara na kulifikia duka. Hapo akapokelewa na mtoto



    wa kiume. Huyu ndiye aliyempeleka huko panapotakiwa.

    Akaingia mlango ukafungwa!!!

    Mwanaume mwenye umri wa miaka zaidi ya thelathini akaachia tabasamu hafifu. Maria akashangaa na kumsalimia.



    Hakujibiwa!

    Akampatia ile bahasha, ikapokelewa.

    Hata haikusomwa sana. Ikawekwa chini.

    “Karibu!.” Sauti ikamtoka yule bwana, sauti nyembamba tofauti na umbo lake.

    “Mama amenituma nikuletee hiyo.” Alijibu kwa hofu huku machale yakianza kumcheza.

    Yule bwana badala ya kujibu. Akachukua simu yake akabonyeza namba kadhaa kisha akasikiliza.

    “Nipo naye tayari amefika. Umemueleza kila kitu?”

    Akatulia upande wa pili ukajibu kwa kirefu. Kisha akakata simu na kuirejesha mezani.

    Kwa hatua za kunyemelea akaanza kumsogelea Maria. Maria akaanza kurudi nyuma lakini chumba kilikuwa kidogo.



    Akaufikia ukuta. Akagota hapo. Akanyoosha mikono kama anataka kumzuia.

    Lishe haikuwa nzuri na Maria alikuwa amedhoofu. Hivyo alijikuta katika mikono imara ya dude nene lenye sauti



    nyembamba.

    Maria akabakwa kwa mara ya pili!!

    Tena siku hii hadi asubuhi!!

    Kilio kikawa ndugu yake Maria. Akatamani asirudi kwa mama Atu lakini ni huyo pekee aliyekuwa ndugu yake. Maria



    binti mdogo kabisa akafunika kombe ili mwanaharamu apite. Akarejea kwa mama Atu.

    Yule bwana alimpatia shilingi elfu tano kama ujira alioupunguza makali nakumwambia Maria ile ilikuwa nauli. Pia



    alimnunulia nguo mpya. Wakati anamuaga alimuita ‘mpenzi.

    Maria akajisikia kupasuka!!

    Miaka kumi na mitano, suluba zaidi ya maelezo!!



    Aliporejea kwa yule mama hakusema neno. Akaingia kazini moja kwa moja. Akili ikiwa haijui ni maamuzi gani sahihi



    yanahitajika.

    Kabla akili fupi na changa ya Maria haijajua nini cha kufanya. Lile tukio lilijirudia. Safari hii alinunuliwa viatu.

    Bwana alikuwa yuleyule. Siku hii wakiwa wanakunywa supu alimtamkia kuwa alikuwa anataka kumuoa.

    Kero nyingine!! Maria akachukizwa na unyanyasaji huo.

    Katika jiji geni masikioni mwake. Maria akatamani kurejea maisha ya uchokoraa kupambana na watoto wenzake



    katika soko la kuuza vyuma chakavu kuliko kudhalilika namna hii.

    Wazo lake likawa limekuja wakati muafaka. Yule mama mbaya aliyemuuza kwa bwana mnene mwenye sauti ya kike



    alijisahau siku hii akaacha kiboksi chake cha kutunzia pesa akawapelekea chakula mafundi waliokuwa wanajenga



    kanisa maeneo ya Ilomba jirani na Sai jijini Mbeya.

    Akili ya Maria ikamkumbusha lile fungu alilolitwaa nyumbani kwa baba yake. Akafanya kama alivyofanya mjini



    Singida.

    Akaibuka na pesa zote zilizokuwa katika kisanduku kile.

    Siku iliyofuata akiwa ndani ya gari ndipo aihesabu na kugundua alikuwa ameondoka na shilingi elfu tisini za mama



    mbaya.

    Mama Atuganile!!



    *****



    Aliupita mji uliomlea wa Singida kama vile hauoni. Hakutaka hata kushuka wala kula chochote kinachouzwa pale.



    Alikuwa ameuchukia mji huo.

    Aliendelea kuwa mtulivu hadi jiji lilipompokea tena. Jiji la Mwanza.

    Siku aliyofika alilala nymba za kulala wageni. Kwa mara ya kwanza pia.

    Asubuhi aliamka akijisikia amani sana. Akamkumbuka Douglasi ambaye walizoea kumuita dogolasi. Huyu ni yule



    mtoto ambaye alimsaidia kwa kumchana na wembe yule chokoraa wa kiarabu ambaye alikuwa anampiga pasipokuwa



    na makosa.

    Alijua wapi pa kumpata na hakika alimpata.

    Baridi la Mbeya na makombo ya chakula cha mama Atu kiasi yalikuwa yamembadili Maria na kumng’arisha lakini



    bado alibakia kuwa chokoraa.

    Dogolasi alikuwa dhaifu sana, ni kama hakuwa amepata chakula kwa siku mbili au tatu. Midomo yake ilikuwa



    imepauka na mwili ukiwa umelegea. Maria alimnyemelea akamfumba macho.

    Dogolasi alitamani kuongea lakini koo lilikuwa limekauka.

    Maria akamwachia dogolasi akageuka.

    Maria akamkumbatia kwa nguvu dogolasi. Wakajikuta wote wanalia.

    “Da Maria sijala tangu juzi….halafu walinipiga wenzangu…da Mariaa….” Dogolasi alishindwa kuendelea kuongea



    donge la uchungu likamkaba kooni. Akalia kwa uchungu. Maria naye akalia. Kilio cha Dogolasi kilimkumbusha siku



    ile ananyanyaswa na yule mwarabu, Dogolasi alilia kwa sauti kama anayoisikia hapa. Ilimuuma!!

    Laiti mama yangu angekuwepo ningemwambia amchukue huyu awe mdogo wangu!! Alijiwazia Maria. Akamchukulia



    Dogolasi kama mdogo wake!!

    Baada ya wote kumaliza kuyafuta machozi yao. Maria alimshika mkono Dogolasi wakaenda gengeni kupata chakula.



    Walau sasa yule mtoto mdogo ambaye hajulikani kama alitupwa na mamaye ama alizaliwa na mtaa aliweza



    kutabasamu.



    Kile kilio alicholia Douglas kilikuwa na mengi ndani yake. Haikuwa njaa tu bali yalikuwemo na mengine.

    Japokuwa ulikuwa umepita mwezi tangu amchane yule mwarabu koko na wembe. Kuna jambo lilikuwa linaendelea.

    Yule mwarabu alimsaka na kumkamata yule mtoto wa wakoma. Safari hii hakupata nafasi ya kutumia wembe wake



    tena. Adhabu yake ikawa adhabu asiyostahili kuibeba mwanadamu wa kawaida aliyezaliwa na mwanamke anayeshika



    uchungu.

    Adhabu ambayo ilitendwa na wengine na sasa wanatumikia kifungo cha maisha jela.

    Ulawiti!!

    Yule mwarabu na kundi lake walifanya kisasi cha namna hii kwa yule mtoto aliyemchana na wembe ili kumuokoa



    Maria.

    “Mpaka umlete yule Malaya ndipo tunaacha!!” alitoa karipio hilo yule mwarabu baada ya kumaliza kumtesa yule



    mtoto.

    Adhabu ile ilichangia kumuathiri Douglas.

    Walimfanyie vile mara kwa mara. Angeshtaki wapi wakati mtaa ndiyo mzazi wake na mzazi huyu haongei!!

    Angefanya nini chokoraa huyu!!!



    Sasa amekutana na Maria. Douglass aanachukua maamuzi magumu. Akiwa na miaka tisa anaamua kuitetea nafsi yake.

    Anakusudia kumtoa muhanga Maria ili waache kumlawiti!!

    Anaamua kufanya usaliti huu usiku!!

    Majira ya saa nne Douglass moyo ukimuuma kabisa anawasili katika kijiwe cha akina mwarabu koko. Anajisikia



    mdomo mzito kusema lakini anajikaza. Anajaribu tena machozi yanamtoka. Picha ya Maria akinyanyaswa na wahuni



    hao inajijenga usoni pake!!







    Dogolasi hatimaye aliweza kutamka. Akawaeleza juu ya uwepo wa Maria.

    “Ole wako uwe unatudanganya!”

    “Siwadanganyi yupo amelala pale nyuma.”

    Wanaume watatu wakasimama wakiongozana na Douglasi.

    “Ni pale hivi sitaki anione mimi.” Alitoa maelekezo huku HATIA ikimshambulia kwa hatua ya kumuuza Maria.



    Alikuwa anbatetemeka na kujihisi msaliti.

    Akayakumbuka mafundisho aliyokuwa anayapata kanisani wakati akiutafuta ubatizo wake. Akamkumbuka Yuda



    Iskalioti yule aliyemsaliti Yesu. Douglasi akajiinamia na kuanza kulia baada ya kumsikia Maria akipiga mayowe ya



    kuomba msaada na baada ya muda akawa kimya.

    Wanamuua!! Aliwaza Douglasi na ghafla akajikuta akipandwa na maruhani ya maajabu. Akajisikia ana nguvu sana.



    Akazamisha mkono wake katika pindo la nguo yake. Akachomoka na kisu ambacho ni maalumu kwa ajili ya tohara ya



    wanaume. Akazama katika kaputula yake akaibuka na wembe mpya.

    Akatimua mbio, akiruka mashimo mawili matatu. Akalifikia eneo la tukio.

    Akakuta tukio likiwa linaendelea. Maria alikuwa mikononi mwa wanaume watatu. Wawili wamemshika kikamilifu na



    kumziba mdomo. Mwingine mmoja alikuwa anambaka. Na wale wengine walikuwa watupu katika maandalizi ya



    kumbaka tena na tena Maria.

    Hakujali kama yeye ni mdogo. Akaruka akatua kwa yule aliyekuwa juu ya Maria. Kisu cha kutahiria kikakwangua



    sikio lake akaruka maili kadhaa mbele akabiringita mbali na mwili wa Maria.

    Mmoja aliyekuwa anashangaa bila kujua nini kinaendelea aligutushwa na na ubaridi usoni pake. Halafu yakafuata



    maumivu makali. Akapiga yowe. Alikuwa amechanwa na wembe mkali usoni.

    Mwanaume wa tatu akawa mwepesi akajirusha pembeni. Kisha akamvaa Douglasi akampiga teke. Katoto haka kadogo



    kakaanguka mbali huku kanalia.

    Yule aliyechanwa sikio akamalizia filamu hii ya mapigano. Wanaume watatu waliobalehe dhidi ya mtoto mdogo kabisa



    anayehitaji malezi ya baba na mama na jamii kwa ujumla.



    Maria alirejewa na fahamu majira ya saa kumi na moja alfajiri akiwa na maumivu makali sana katika mwili mzima.



    Alikumbuka kuwa alibakwa na wanaume wengi hakumbuki walijirudia mara ngapi ngapi. Akauma meno yake kwa



    hasira! Akasimama akashangaa watu wale hawakuchukua pesa yake . Maajabu!!

    Akajikongoja baada ya kujifuta damu kidogo iliyokuwa inatiririka.

    Douglass!! Jina hilo lilishambulia kichwa chake kama vile lilingoja asimame!!

    Maria akajiuliza huyu mtoto mdogo yupo wapi. Na alikuwa wapi wakati anatendewa unyama ule. Hakupata jawabu



    hilo hadi asubuhi inavyosambaa taarifa ya chokoraa aliyekutwa amekufa katika jalala.

    Maria aliyaunganisha meno yake alipomtambua Douglas akiwa ni maiti. Huku akiwa amejeruhiwa sana. Zaidi ya



    kipigo alichopokea alikuwa amelawitiwa pia.

    Machozi yakamtoka!!

    Douglas akaiaga dunia akiwa chokoraa, alikufa akijaribu kumuokoa Maria. Anakufa bila kuwa na ndugu.

    Halmashauri ya wilaya ya Ilemela ikachukua jukumu la kuuzika mwili katika namna ya kuufukia na kuusahau.

    Hakuna hatua zozote za upelelezi zilizochukuliwa. Douglas akasahaulika rasmi katika mlolongo wa machokoraa,



    Douglas akafuta katika simulizi yetu.



    Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!

    Msemo huu ulichukua nafasi katika nafsi ya Mariam. Punde tu baada ya mwili wa Douglas kupatikana akiwa mfu.



    Mnyonge huyu hakuwa amepewa haki yake hata kidogo.

    Hata mimi sitatendewa haki yangu! Hata mimi naonewa na nitakufa nitazikwa kama mzoga wa mbwa!

    Hasira zikamkaba Maria. Akaamua kuwa kama atazikwa kama mbwa basi lazima aishi kama mbwa. Tena mbwa



    mwenye ukichaa.



    Baada ya wiki moja. Maria mwenye hasira na chuki. Aliyeamua kuwa mbwa.

    Anakutana na chokoraa wanaojaribu kuishi kama wafalme katika ngome ya uchokoraa. Waliomchukulia yeye kuwa



    swala ambaye huonewa na wanyama pori wote.

    Ilikuwa saa nane usiku. Akasikia ubaridi ukipenya katika mapaja yake. Kisha akazibwa mdomo.

    Maria aliyekuwa amejifika umbwa kichaa. Akaijiwa na fahamu. Akafumbua macho. Akakuta nguo yake inamaliza



    kutolewa.

    Akapandisha kichaa chake cha kupinga unyanyasaji.

    Hatimaye ile siku ya kufanya umbwa kichaa kwa vitendo ikawa imewadia.

    Akapapasa bila kuleta vurugu. Akakikamata kisu kikali ambacho tangu kinolewe hakikuwahi kufanya kazi.

    Sura iliyokuwa gizani ikamsogelea. Akasikia anapapaswa zaidi. Walikuwa watatu!!!

    “Tulia hivyo hivyo ukileta fujo tunakufanya kama mdogo wako.” Sauti ilimuamrisha.

    Akamkumbuka Douglas. Kumbe aliuwawa na watu hawa! Basi ni hawa walinibaka! Aliwaza Maria. Hasira



    zikamchemka kichwani.

    Hasira zikampanda zikiambatana na kichaa cha mbwa alichojipandikiza makusudi.

    Yule aliyemtishia kisu alikuwa wima, mbali na yeye.

    Hivyo hakumtisha. Yule mwarabu koko alipoanza kumbaka. Alijikuta akipiga kelele kuu.

    Kelele ya kutisha. Jisu kubwa kali. Lilipennya katika kitovu chake. Kisha likachomoka kama vile halikuwa limetenda



    jambo lolote. Ile rangi ya kung’aa haikuwepo lilikuwa jekundu.

    Mbwa huyu mwenye kichaa bila uoga akamrukia yule bwana mwenye kisu kidogo. Jisu lililokuwa na damu likapenya



    sehemu zake za siri barabara. Akapiga kelele moja kuu akaanguka chini.

    Mmoja akafanikiwa kukimbia lakini mbwa mwenye kichaa anayeitwa Maria alikuwa nyuma yake. Alipojikwaa tu.



    Mbwa akawa juu yake. Mbwa akaanza kushambulia kwa kisu. Picha ya Douglas akiwa mfu jalalani ikamjia Maria



    akazidi kuchoma na kuchomoa.

    Ilikuwa afadhali kwa wale wawili wa awali huenda walipoteza uhai katika namna ya maumivu ya mara moja.

    Huyu wa mwisho roho yake huenda hata haikuweza kuzifikia mbingu salama.

    Jisu lilizama na kuchomoka, likazama tena na kuchomoka.

    Hadi wote wawili walipotulia.



    Maiti tatu asubuhi na muhusika mwingine aliyedhaniwa amekufa anazinduka akiwa na pingu, hospitali.

    Huyu alikuwa ni mbwa mwenye kichaa cha chuki. Chokoraa wa kike, Maria!!

    Alilala akiwa na chuki na kisasi na sasa anaamka akikabiliwa na kesi ya mauaji. Mauaji ya watu wanne. Akashangaa!!

    Watatu kwa usiku mmoja na akarushiwa kesi ya kumuua Douglas.

    Vipi kuhusu kumlawiti sasa? Au na ulawiti alifanya Maria!!! Kichekesho lakini serikali ikajifanya haijui kujibu



    maswali. Ikasema sheria itachukua mkondo wake.



    Hawakuwepo wazazi wala ndugu wa marehemu hawa wanne kusikiliza kesi. Hivyo Maria akawa ameshtakiwa na



    jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Bila kuwa na mtetezi.

    “Bi. Maria Paul. Mwenye umri wa miaka ishirini na moja anahukumiwa ……..” kimya kikali kikatawala kisha yule jaji



    bila kumtazama Maria usoni alivunja KALAMU NYEKUNDU.

    Hii ikimaanisha kuwa amehukumiwa hukumu ya kunyongwa ama maisha yake yote kumalizikia gerezani. Labda



    utokee msamaha wa raisi. Lakini msamaha wa raisi hauendi kwa yatima kama yeye. Na wenyewe pia mpaka kujuana.

    Alitamani kujitetea kuwa alikuwa na miaka kumi na tano lakini vifungu vya sheria asivyovijua vikambana. Akawa



    kimya. Hadi mahakama ilipohairishwa na yeye kutupwa gerezani.

    Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!! Alisikia kauli hizi kutoka kwa baadhi ya watu waliohudhuria



    mahakamani. Akainama chini akadondosha chozi.







    ******



    Katika uzio huu wanawake wenye nguo tofauti kabisa na wengine walikuwa wamejikita katika kumzongazonga



    mwenzao ambaye zile nguo zilikuwa zimempwaya, alivutwa mithili ya mwivi anayekaribia kuadhibiwa. Baadaye



    alitokeza mwanamke mmoj mnene aliyekuwa anatembea kifua mbele kama mwanaume anayefanya mazoezi ya



    kunyanyua vyuma. Taratibu lile kundi likamuachia yule msichana.

    Mama mnene akafika akamchukua. Haya yote yalikuwa yanatokea gerezani na Maria kwa mara ya kwanza alikuwa



    ameupoteza uhuru wake.

    Gereza la Keko jijini Dar es salaam liliukwapua uhuru wake.

    Wafungwa wanaohukumiwa kifungo cha kunyongwa wawapo gerezani huishi peke yao kwa kutengwa, hwajichanganyi



    na wafungwa wengine. Wafungwa hawa ambao wanangojea kitanzi hawafanyishwi kazi ngumu. Kazi kubwa



    wanazofanya ni kusafisha mahali pao pa kulala. Kwa upande wa wanaume waliona bila kujali lolote maana walikuwa



    wafu watarajiwa na walijua kuwa ni lazima watakufa.

    Kila mahali kuna mtemi gerezani. Na upande huu wa wanawake wanaongoja kitanzi alikuwepo Mamamia, huyu ndiye



    alikuwa anatetemesha selo nzima ya wanawake wanaongojea kitanzi. Ni huyu ambaye bila kusema neno alipotokea tu



    kila mtu akakaa mbali na Maria.

    Waliufahamu undava wa mwanamama huyo. Na pia walijua kuwa kila mgeni anayepokelewa pale gerezani alikuwa



    haki ya Mamamia kumfanya mke.

    Ilikuwa hivyo pia kwa Maria. Mamamia aliondoka naye hadi katika chumba kizuri. Akakaribishwa.

    Maisha yakaanzia hapo!! Kule kubakwa mtaani kukahamia huku gerezani. Lakini huku alifanywa mke wa mwanamke



    mwenzake.

    Hapo sasa hakuwa na ujanja japo alikuwa anaumizwa sana na hali ile lakini wakati mwingine alijipa moyo kuwa muda



    wowote ule atakufa hivyo hakuna harakati zaidi anaweza kufanya kujitoa katika janga hilo.

    Baada ya mwezi mzima afya yake ikabadilika. Mume wake wa gerezani alikuwa wa kwanza kugundua.

    Mamamia alikuwa mtulivu sana siku hii, alimuita Maria baada ya kuwa wamepata chakula. Maria akadhani kuna



    mahali amefanya makosa, maana Mamamia alikuwa ana wivu sana kwa wafungwa wenzake.

    “Una miaka mingapi Maria.”

    “Kumi na tano mama nakaribia kumi na sita.” Alijibu kwa upole.

    “Ulikuwaje ukafika huku mbona u mdogo sana.”

    Maria akaweka kimya kirefu kisha akajieleza kwa urefu huku akiwa ameinama. Machozi yakiwa yanamtoka na kilio



    cha kwikwi kikiyaingilia maongezi yake.

    Alipomaliza na kuunyanyua uso wake. Alimkuta yule mama analia kwa uchungu. Wakakumbatiana!! Bila kusema



    lolote kisha wakaachiana.

    “Maria ulipobakwa mara ya pili wamekupa mimba tena.” Mamamia alimwambia Maria. Maria akakodoa macho yake



    kumtazama Mamamia. Hakuamini alichokisikia, lakini Mamamia alimaanisha alichokiongea.

    Mama huyu mnene alisimama tena akamsogelea Maria akamgongagonga mgongoni. Akamtia moyo.

    Kuanzia siku hiyo Mamamia akaacha rasmi suala la kujifanya mume wa Maria na badala yake akauvaa umama Maria.

    Akaanza kumpa huduma zote Maria anazoweza kumpatia.

    Zilizoshindikana akawa anamshirikisha mkuu wa gereza ambaye alikuwa anawatembelea mara kwa mara.

    Miezi mitano ikakatika. Maria akiendelea kuitunza mimba yake kwa uangalizi wa Mamamia.

    Asubuhi moja Maria alipokea ujumbe kutoka kwa mwanamke mmoja kati ya ishirini waliokuwa wanangoja kitanzi.



    Mamamia alikuwa anamuhitaji. Ujumbe ule ulimshangaza. Ni kwanini Mamamia anaagiza mtu amuite wakati anajua



    kuwa anaumwa tumbo? Hakuleta ubishi alisimama na kuelekea eneo husika.

    Nondo zikawatenganisha. Mamamia alikuwa anatokwa jasho jingi na alikuwa anatetemeka.

    “Maria mwanangu! Naenda kanisani.” Alianza kujieleza Mamamia. Maria hakuelewa, kanisa liliwezaje kumtoa jasho



    na kumfanya atetemeke.

    Mamamia alipoona Maria haelewi aliendelea. “Naenda kujikabidhi kwa Mungu aliyetuumba mimi, wewe na wao,



    akawapa madaraka wanadamu watutawale. Kisha akawaweka na wengine watuonee, halafu wengine wakayachukua



    mamlaka ya kujiweka kuwa miungu watu, wakajipa mamlaka ya kuzitwaa roho. Naenda kuungama dhambi zangu



    niingie katika kitanzi. Nilitamani kuwa nawe hadi nimuone mjukuu wangu lakini wakati umefika.” Alizungumza kwa



    sauti yenye kitetemeshi cha uoga. Maria akatetemeka sana kusikia kitanzi. Tumbo likazidi kumuuma. Akatolewa pale.



    Akageuka akamwona Mamamia akijilazimisha kutabasamu, kisha akafanya ishara ya msalaba.

    Huo ukawa mwisho wa Maria kumtia machoni Mamamia. Mama aliyempokea vibaya kwa kumfanya mke lakini



    baadaye akageuka kuwa mama mzuri mwenye upendo. Huu ukawa mwanzo wa kuishi maisha ya hofu tena!



    Miezi iliyobakia pale gerezani ikamfanya awe kama mpira wa kona. Anawaniwa na kila mmoja. Leo huyu kesho yule.



    Wote wanamminyaminya hovyo. Hawakuijali mimba yake.

    Hata kabla mwezi wa tisa haujatimia vizuri aliushika uchungu.

    Wafungwa wakapiga kelele! Msaada ukaletwa!

    Maria akaingia kwa mara ya kwanza katika chumba cha wazazi kwa ajili ya kujifungua.

    Akiwa na miaka kumi na sita anageuka kuwa mzazi.

    Ilikuwa siku ya ijumaa. Akamuita mtoto wake Friday akiamini kuwa ni wa kiume. Akili ilipotulia kapunguza herufi



    moja.

    Mtoto yule wa kike akapewa jina la Frida. Cheti cha kuzaliwa hakikuwa na jina la baba!!

    Maria aliishi kwa muda wa siku kumi akimlea Frida.

    Kisha akarejea rasmi gerezani. Huko akaendelea kuolewa mara kwa mara na wenzake waliojifanya wababe.

    Maria aliruhusiwa kumnyonyesha mwanaye, ambaye sasa alikuwa chumba cha jirani. Wakati mwingine Frida alikuwa



    analia sana lakini Maria hakuruhusiwa kumuona.



    Maisha haya yalienda kwa miaka miwili. Frida akahamishiwa gerezani. Chumba maalumu akawa anaishi na mama



    yake.

    Frida asiyekuwa na kosa lolote akatumikia kifungo na mama yake!!

    Alikula alichokula mama yake, alishuhudia jinsi mama yake alivyokuwa akinyanyaswa. Hakuwa na la kufanya mtoto



    huyu.

    Neno lake la kwanza kutamka lilikuwa ‘baba’. Maria alilia sana siku hiyo maana hata hakuwahi kumjua baba mzazi wa



    mtoto wake. Lakini ule mchanganyiko wa rangi aliokuwanao Frida ulimfanya amuhisi yule mwarabu koko kuwa



    anahusika!! Lakini haikusaidia kitu kwani alikuwa marehemu tayari.

    Wakati akiwa na miaka miwili na nusu Frida. Mama yake aliugua ugonjwa wa ajabu ulimshambulia sehemu za siri.



    Gereza halikujali.

    Aliendelea kuugua huku akiishia kupewa dawa za kutuliza maumivu tu!! Hali ikazidi kuwa mbaya ndipo akapelekwa



    hospitali.

    Kama Mamamia alivyomuita na kumuaga wakati anaelekea kunyongwa ndivyo naye alivyoomba Frida apelekwe



    hospitali aliyokuwa naugulia.

    “Frida hata wewe utakuwa chokoraa kama mama yako.” Maria alimwambia mwanaye ambaye hakuwa anaelewa nini



    kinaendelea.

    Siku iliyofuata mapazia yenye rangi za kijani yalizungushwa katika kitanda cha mtoto huyu mwenye mtoto. Hatimaye



    roho ya Maria ikapumzishwa!!!

    Baada ya msoto wa miaka kadhaa na tabu za mtaani kisha mateso ya gerezani hatimaye Maria akafa kishujaa akiwa



    ameuachia mtaa damu yake!!!

    Frida!! Mtoto wa gerezani asiyekuwa na hatia!!



    Baada ya mwili wa Frida kufukiwa, hatimaye Frida akachukuliwa na familia ya mkuu wa gereza. Huku akaanzishwa



    shule ya awali.



    Frida hakuwa na marafiki wa karibu. Alikuwa ni mkimya sana. Hakuifurahia shule. Na hakuwa na amani nyumbani



    alipokuwa anaishi.

    Watoto wenzake walimuonea sana. Licha ya kuonewa lakini bado aliadhibiwa kila mara.

    Hii ilitokana na yule mkuu wa gereza ambaye walau alikuwa ana huruma kwake kuhamishwa gereza. Sasa alikuwa



    anakuja nyumbani mara chache. Hakutaka uhamisho wa mapema wa familia yake hivyo waliendelea kuishi palepale.

    Mke wa mkuu wa gereza na watoto wake wawili walifanana kimatendo hivyo Frida hakuwa na wa kumtetea.

    Akanyanyasika huku anasoma.

    Mkuu wa gereza aliporudishwa katika gereza lile tena walau Frida akaanza kuipata amani.

    Miaka ikapita. Frida akasoma shule ya jirani katika elimu ya msingi. Frida hakuwa na baba na walizoea kumtania Frida



    gereza. Hakujali.

    Alipomaliza darasa la saba. Tayari alikuwa na miaka kumi na sita.

    Mkuu wa gereza mara kwa mara alikuwa anakaa na Frida na kumueleza juu ya maisha ya mama yake ambayo



    aliyafahamu kwa kumsikiliza mara kwa mara. Alimsisitiza juu ya kusoma kuwa huo ndio ukombozi wake pekee.

    Frida aliyasikiliza kwa umakini maneno yale mazito kutoka kwa mkuu wa gereza. Akajikuna kichwa chake na



    kuyaruhusu yamkae vyema.

    Unyanyapaa aliofanyiwa na watoto wa familia ile ya mkuu wa gereza, wanafunzi shuleni. Ilimfanya ajihisi anafanana



    na marehemu mama yake. Akajiweka makini asije kufa kama mama yake.

    Hivyo licha ya kujitambua kuwa kifua chake chenye chuchu ndogo kilikuwa kinawatamanisha wanaume wengi.



    Hakujiweka karibu nao na hakutaka kuwasikiliza walipojaribu kumtaka kimapenzi.

    Wakatio Frida anajilinda na mambo haya. Nyumbani kikazuka kizaazaa.

    Mkuu wa gereza alikuwa amesafiri lilipojitokeza jambo hili.

    Mtoto wake wa pili na wa mwisho alikuwa amegundulika kuwa ana ujauzito. Ilikuwa ni aibu kubwa kwa mama yule



    aliyewadekeza watoto wake.

    Sasa yalikuwa yamemrudi!!

    Frida alizidi kujifunza kupitia tukio hili. Lakini hakujifunza sana kabla kesi haijamgeukia. Mama mwenye nyumb



    alijua ni jinsi gani mume wake alikuwa mkali sana, alihofia kesi hii inaweza kuhatarisha ndoa ama maisha yake.



    Akatafuta wa kumuuzia kesi hii akaumiza kichwa. Kisha akajikuta katika orodha likijitokeza jina moja tu. Frida



    Gereza.

    Mama alimuita kwa sauti ya juu. Alipofika akapokelewa na kibao kizito akayumba lakini akawahi kupata muhimili



    kwa kushika ukuta.

    “Nani amempa mimba Jesca?” aliulizwa. Akashangazwa na swali hilo. Akashangaa. Akapokea tena ngumi nzito ya



    mgongo akapiga kelele.

    Hapo sasa akawa amebariki kipigo. Akaanza kushughulikiwa. Kisha akafukuzwa nyumbani pale majira ya saa mbili



    usiku akiwa anafua nguo zake za shule. Alipewa shilingi elfu mbili aende anapojua.

    Frida angeweza vipi kung’ang’ania makazi yasiyokuwa ya kwake? Akaondoka binti huyu ambaye ana kumbukumbu



    nzuri ya kuambiwa kuwa yeye ni chokoraa na marehemu mama yake.

    Sasa akayaamini maneno ya marehemu!! Akaingia katika mtaa ambao hajauzoea na wala hakuwahi kuingia kabla.

    Tofauti na mama yake. Frida aliingia akiwa na chuki iliyopitiliza!!

    Kisasi kikiwa kimemkaba koo!!

    Machozi yakamtoka Frida akalia kwa uchungu sana na kutengeneza picha inayopamba ukurasa wa mbele kabisa wa



    kitabu cha CHOKORAA.







    ******



    Alipita njia za uchochoro akiwa haoni mbele vizuri. Machozi mazito yalikuwa yameuziba uso wake, alikuwa kama



    kipofu asiyekuwa na mkongojo wa kumuelekeza vikwazo vilivyopo katika njia.

    Alitokea kituo cha mabasi. Hakuwa na uhakika ni wapi anatakiwa kwenda. Mkononi alikuwa na shilingi elfu mbili



    alizopewa na mama, huku mfukoni akiwa na shilingi mia tano na hamsini iliyosalia kama chenji baada ya kuwa



    ameagizwa dukani muda mfupi kabla ya kutimuliwa.

    Daladala ikapita akajikuta yu ndani tayari.

    “Frida Gereza.” Alisikia sauti ya kike ikimuita.

    Alipogeuka alikutanisha macho na msichana aliyekuwa anatabasamu. Lakini ghafla akakoma kutabasamu baada ya



    kuyaona macho ya Frida. Mekundu na michirizi ya machozi mashavuni.

    Wote walikuwa wamesimama baada ya kukosa nafasi ya kukaa katika basi hili liendalo Mwenge.

    “Frida ni nini kibaya.” Aliuliza kwa upole. Frida hakumjibu dada huyu ambaye alikuwa ni kiongozi pale shuleni



    akifahamika zaidi kama ‘dada mkuu’.

    Frida hakuweza kujibu. Badala yake machozi yakamtoka maradufu.

    “Usilie Frida…haya sikia nikwambie, unashukia wapi mamii”

    “Siju…sijuii” alijibu huku analia.

    Dada mkuu akatumia busara ambazo zilimuwezesha kuchaguliwa kushika kitengo hicho katika shule hiyo ya msingi.



    Akachukua kitambaa akamfuta Frida machozi kisha akamnong’oneza jambo. Frida akatulia tuli na hapakuwa na



    maongezi tena.

    Walikuwepo wazazi wa kiume na wa kike katika daladala ile lakini hakuna hata mmoja aliyerjikita katika kulifuatilia



    tukio hili. Kwa jiji la Dar es salaam hii ni kawaida kabisa, wao wanasema ‘mtoto mtoto wako, mtoto wa mwenzio si



    wako.’ Hivyo Frida Gereza hakuwa akiwahusu hata kidogo.

    “Tuache Mwananyamala hospitali.” Dda mkuu alimkumbusha kondakta. Kisha akatoa nauli, “kata wawili. Wote wa



    kusoma.” Alipepeta mdomo upesi akatoa nauli na kulipa. Akarejeshewa baki yake.

    Gari iliposimama dada mkuu akamvuta mkono Frida aliyekuwa amesinzia huku amesimama. Wakashuka!!

    Dada mkuu akatazama pochi yake . kisha akamwongoza Frida katika banda la mama ntilie wa Mwananyamala A karibu



    na kituo cha polisi.

    Akaagiza chakula, wakachangia sahani moja. Pesa yao iliwaruhusu kula hivyo.

    Wakagida na maji yasiyochemshwa kisha wakatembea na kupata nafasi ya kukaa katika uwanja ule.

    “Haya niambie umekuwaje Gereza?” alianzisha maongezi dada mkuu.

    Frida mtoto wa Gereza akavuta pumzi akatazama juu mbinguni kama anayesubiri kushukiwa na roho mtakatifu.

    Umbo lake kubwa tofauti na umri wake mdogo lilikuwa limehifadhiwa katika kanga zilizowekwa katika mfumo wa



    kutanda. Kama mwanamke akiwa msibani.

    Kwa sauti ya kunong’oneza akaanza kujieleza. Moja baada ya jingine. Mwanadada jasiri kabisa aliyepewa jina la



    Mwanaidi alipozaliwa na sasa ni dada mkuu katika shule ya msingi akawa anamsikiliza.

    Hatimaye akamaliza!! Mwanaidi akajikuta anatokwa na jasho! Hakujua kama Frida ni yatima tena aliyezaliwa gerezani



    akizaliwa na mama anayesubiri kunyongwa. Na hatimaye mama huyo akaaga dunia kabla ya kuhukumiwa!!

    “Kwa hiyo haujui unapokwenda.”

    Frida akatikisa kichwa kuashiria anakubali!

    “Sasa Frida…kuhusu kulala…..aah! hebu ngoja.” Dada mkuu akagundua akili ya Frida bado ilikuwa fupi. Akaamua



    kumsaidia kufikiri.

    “Ubaki hapahapa…nakuja.”



    Mwanaidi akatoweka. Frida akabaki mpweke na shilingi elfu mbili yake. Alikuwa hana analofikiri zaidi ya kujutia



    kuzaliwa.

    Kwanini mama aliua watu wengi hivyo!! Halafu wanaume!! Frida alijiuliza baada ya kujikuta akimuwazia marehemu



    Maria. Hakupata majibu mpaka alipoguswa begani.

    Mwanaidi alikuwa amerejea.

    Akamwongoza hadi katika nyumba ya kiwango cha kawaida. Bati lenye kutu likionekana kwa kumulikwa na taa za



    nyumba ya jirani. Pale hapakuwa na umeme.

    “Utaweza kupanda hapa dirishani!!” alimuuliza Frida kwa sauti ya kunong’oneza.

    Frida akakubali kwa kichwa. Mwanaidi akamtazama kwa huruma akidhani Frida ni mtoto wa mama. Kufumba na



    kufumbua Frida alikuwa amenata katika nondo akingojea maelekezo.

    “Ingia taratibu kabisa!!” alinong’ona tena dada mkuu.

    Frida akatua ndani kama paka. Hakuna aliyesikia.

    Mwanaidi naye akafanya kama Frida. Wakajikuta ndani.

    “Frida mdogo wangu leo ulale hapa, kesho tutajua cha kufanya nitakupeleka shuleni sawa.” Mwanaidi akawa



    anabembeleza.

    “Mwanaidiii!! Sauti kali iliita.

    “Shhhh!! Mama huyo.” Mwanaidi alimwambia Frida lakini akiwa anaogopa.

    “Frida ingia uvunguni!!”

    Frida akazama uvunguni na kukumbana na vumbi kali. Akajikaza.

    Mara ghafla mlango wa chumba cha Mwanaidi ukafunguliwa.

    “Tangu nikutume ni saa ngapi.” Sauti iliuliza kwa shari sana.

    “Mama usafiri ulikuwa tatizo!!” alijibu Mwanaidi.

    “Malaya wewe….usafiri ulikuwa tatizo..” aliongea kwa kubana pua mwanamke huyo.

    Ghafla akamvamia na kuanza kumnasa vibao.

    “Joooohn!! Niletee huo mkanda…” alitoa amri kwa sauti kuu.

    “Mama nisamehe!!”

    Mkanda ukafikishwa na mtoto mdogo. Kichapo kitakatifu kikaanza kushuka. Frida akawa anayasikilizia maumivu



    huku akiwa uvunguni.

    Kosa alilofanya Mwanaidi ni kujaribu kujificha kwa kurukia kitandani. Yule mama mweupe aliyeiharibu ngozi yake



    kwa mikorogo akamrukia akiwa na nia ya kumkwangua na makucha yake marefu yasiyopendeza.

    Kitanda kilichotengenezwa na fundi asiyekuwa makini na kazi yake ama aliyeletewa mbao za kiwango cha chini,



    kikaitika ‘kaaa!!!’ chaga mbili zenye uzito wa ziada zikatua juu ya mwili wa Frida. Hakika aliweza kulivumilia vumbi



    lakini uzito huu hata ungekuwa wewe msomaji!!

    Yowe likatoka!! Yowe kubwa sana. Mwanaidi akaukunja uso wake kuonyesha kuwa amekata tamaa tayari mpango



    umekuwa batili!! Yule mama wa mikorogo akadhania ni jini ndani ya chumba akatimua mbio, lile giza hakujua



    anapoelekea akakutana na ukuta. Puu! Akajibamiza akatowa yowe.

    Mwanaidi akacheza akili ya upesi akanyanyua chaga Frida aweze kutoka. Akafanikiwa. Lakini aliyeharibu filamu hii na



    kuirudisha katika majonzi ya awali ni yule mtoto mdogo aliyeagizwa mkanda wa kumuadhibia Mwanaidi.

    Aliingia pale chumbani na tochi. Akamulika bila kutarajia. Mama wa mikorogo akaona kitu. Akamuona Frida pale



    chumbani.

    Kanga yake ilikuwa imemtoka na ndani akasalia na kinguo kifupi alichoondoka nacho nyumbani.

    Yowe jingine likamtoka!! Sasa baba mwenye nyumba akafika eneo la tukio. Akathibitishiwa kuwa Mwanaidi ni Malaya



    na siku hiyo alikuwa ammleta Malaya mwenzake ndani.



    Baada ya dakika thelathini, Mwanaidi alikuwa akizurura usiku bila kujua wapi yeye na Frida watalala. Alikuwa



    amefukuzwa.

    Upole wake kumsaidia maskini mwenzake umemponza yatima huyu aliyekuwa anafanya kazi za ndani wakati huo huo



    akisoma shule ya msingi na kupewa wadhifa wa dada mkuu!!

    Mwanaidi na Frida matatani!!

    Usiku mrefu kwa watoto hawa!!



    Lile eneo walilokaa kusimuliana juu ya mkasa wa Frida ndipo hapo walikaa kujadili pia upande wa pili wa Mwanaidi.

    Mwisho wa maongezi wakajikuta wote ni wamoja.

    “Huwa ananipiga sana..anasema mimi nina mahusiano na mume wake..wakati mwingine anadai mimi nawaroga



    watotowake..Frida mimi hata sijui uchawi ni nini leo hii naambiwa mimi nawaroga watoto wake. Kila kitu



    ninachofanya kwake kibaya. Ananifanyisha kazi ngumu. Sijawahi kulalamika. Pesa yangu silipwi. Mume wake



    akijaribu kunitetea kesho yake napigwa eti nafanya naye mapenzi mumewe. Si ulisikia na leo alipojaribu kunitetea.



    Mume wake ni mtu mzuri lakini yule mwanamke ni shetani. Tazama sasa amechoma hadi nguo zangu” alishindwa



    kuendelea kuzungumza ikawa zamu ya Frida kubembeleza.

    Ilikuwa simanzi kwa yeyote yule mwenye moyo wa nyama. Hakika iliumiza.

    Wawili hawa wakalala palepale.

    Siku iliyofuata. Wakafunga safari kuelekea kituo cha kulea watoto yatima. Kigogo jijini Dar es salaam,



    kinachojulikana kama ‘Dogodogo Center’. Ni huku Mwanaidi alilelewa baada ya kutelekezwa na mama yake.

    Sasa anarudi akiwa na mtoto mwingine yatima. Frida!!!





    *****



    Miaka ilikuwa imepita utaratibu nao ukawa umebadilika. Kituo cha ‘Dogodogo center’ alichokulia Mwanaidi sasa



    kilikuwa na utaratibu mpya kabisa. Kilikuwa maalumu kwa ajili ya watoto wa kiume pekee.

    Wingu zito la mimba za yatima kwa yatima lilikuwa limetawala hivyo wakawekwa mbalimbali ili kupunguza kidogo



    hali hiyo. Dogodo center ikawa kwa ajili ya wavulana pekee.

    Mwanaidi na Frida wakapewa maelekezoi juu ya kituo cha kulea yatima kilichopo maeneo ya Kipati nje kidogo ya jiji



    la Mbagala.

    Ilikuwa bahati kuwa walikuta watoto wengine wa kike wakiwa katika taratibu za kupelekwa kule Mbagala Kipati.



    Wakapata kuondoka nao.



    Wakasajiliwa baada ya kuulizwa maswali mawili matatu!!

    Wawili hawa wakaungana na watoto wengine pale kituoni!!



    Maisha ya kulelewa yakaanza rasmi.

    Shule waliyokuwa wanasoma ilikuwa mbali na kituo cha kulelea yatima hivyo neno la mwisho waliloambiwa ni



    kwamba taratibu za kutafuta uhamisho zinafanyika.

    Walidumu na kauli hiyo vichwani kwa muda mfupi tu ikasahaulika.



    Maisha ya pale kituoni hayakuwa mabaya, waliishi vizuri tu. Wakipata mahitaji yao ya msingi. Wababe walikuwepo



    kama ilivyo ada! Mwanaidi na Frida walikuwa wanyonge. Lakini hawakunyanyasika sana!!



    *****



    Kiubaridi cha siku hiyo kiliwafanya watoto wengi wajikute wakiwa na masweta ya misaada kutoka taasisi isiyokuwa



    ya kiserikali. Kila mmoja alikuwa amejikita katika linalomuhusu. Wengine walikuwa na marafiki zao wakicheza.



    Wengine walikuwa wanasukana nywele na baadhi walikuwa vitandani tayari.

    Frida na Mwanaidi walikuwa chini ya mti wakiwa katika mazungumzo. Muongeaji mkuu alikuwa ni Mwanaidi. Frida



    alikuwa anasikiliza tu.

    Kabla ya wawili hawa kukaa na kuzungumza. Siku hii Mwanaidi alikuwa mjini kwa siku nzima baada ya kupata



    ruhusa kutoka kituoni. Kuna jambo zito alitoka nalo huko mjini.

    “Frida!!”

    “Bee!”

    “Unajua kuwa kuna umri wa mwisho kukaa hapa kituoni.”

    “Hapana sijui.”

    “Ndio ujue na ninadhani tumebakiza miezi michache tutaambiwa tuondoke.” Alizungumza huku akiangalia anga. Frida



    akakumbwa na taharuki!!!

    “Tunarejea mtaani tena. Una chochote cha kufanya mtaani..jibu ni hauna na mimi sina.”

    Mwanaidi aliendelea kuzungumza mengi hatimaye akalifikisha jambo gumu kwa Frida. Mkuu wa kituo alikuwa



    akimuhitaji Frida kimapenzi ili aweze kuwaongezea miaka ya kuishi pale kituoni.

    Miaka waliyoandikiwa katika fomu walizojaza siku ya kuingia ni miaka kumi na saba na miezi mitatu kwa Frida na



    miaka kumi na saba na miezi tisa kwa Mwanaidi jambo ambalo halikuwa kweli hata kidogo.

    Na sheria na kanuni ziliwataka wakifikisha miaka kumi na nane kuingia mtaani kama watu wazima.

    Wakuu hawa wa vituo walifanya hivi ili kuepuka gharama za kuwatunza watoto wengi. Wadhamini wao walijitoa kwa



    moyo lakini wanadamu hawa wenye roho mbaya waliweka ujanja ujanja na kuwagandamiza watoto hawa.

    Kibaya zaidi waliofanya haya wote walikuwa wanazungumza Kiswahili na waliowanyanyasa pia walizungumza



    Kiswahili. Yule muwezeshaji mwenye huruma alikuwa anazungumza kiingereza safi huku akijua maneno mawili tu ya



    Kiswahili ‘NAWAPENDA SANA’

    Mwezeshaji alikuwa ni mzungu mwenye upendo huku akiwaacha waswahili wakinyanyasana wao wao. Pesa za



    muwezeshaji wanazipigia mahesabu ya kuezeka na kupaua nyumba zao. Mawazo batili ya muafrika!!!



    Kwanza Frida hakumuelewa Mwanaidi alitaka kumaanisha nini kwa kauli yake ile ya kumtaka Frida awe na uhusiano



    wa usiku mmoja na msimamizi wa kituo ili waweze kudumu pale.

    Lakini baada ya maelezo marefu Frida alielewa na kupinga vikali. Hakuwa tayari kwa wazo la Mwanaidi.

    Jeuri yake ilikatika baada ya Mwanaidi kumweleza kuwa mahali hapo walipo lile sio ombi bali lazima!! Hapo sasa



    Frida akashusha pumzi kwa nguvu. Akakosa la kusema.

    Mwanaidi akambembeleza sana rafiki yake huyu, akatumia kila aina ya ushawishi hatimaye Frida akakubali japo kwa



    shingo upande.

    Angeshtaki wapi unyanyaswaji huu iwapo aliyemnyanyasa ni mkuu wa kituo.

    Usiku wa makubaliano ukafika. Mwanaidi akamtwaa Frida hadi nyumba ya kulala wageni maeneo ya Mbagala



    Kizuiani. Frida alikuwa anatetemeka wakiwa wanaingia chumbani. Hakuwa amewahi kufanya mapenzi hapo kabla.



    Maisha ya kuishi gerezani na kisha katika nyumba za magereza yalimbana sana na kamwe hakuwahi kushiriki mchezo



    huu mchafu. Sasa anatakiwa kufanya kwa lazima.

    Sayansi aliyosoma darasa la tano ilimkumbusha jambo moja tu. Mimba!! Na ikamdokezea kuhusu matumizi ya kinga



    kuizuia isiingie katika mji wa uzazi.

    Saa nne usiku mlango ukagongwa. Likafanyika tendo moja tu!! Mwanaidi nje, mnyanyasaji anayesimamia kituo ndani!!

    Hapakuwa na maongezi sana!! Frida akabakwa kwa hiari yake mwenyewe. Kwa ajili ya kujipigania aweze kuendelea



    kuishi kituoni.

    Saa kumi na moja alfajiri Mwanaidi akaingia na kuondoka na Frida kama walivyoingia awali!



    *****



    Muonja asali haonji mara moja!

    Mnyanyasaji akataka tena!! Tofauti na makubaliano ya awali kuwa angefanya mara moja na kuwaongezea miaka ya



    kuishi pale kituoni.

    Frida kiroho upande akaingia tena katika adhabu hii aliyorithishwa na mama yake mzazi aliyefia gerezani. Mnyanyasaji



    akaendelea kunogewa zaidi na zaidi!!

    Mbaya kupindukia hakuwahi kutumia kinga!!!

    Frida alilazimika kuvumilia japo hakupenda!!

    Idadi ya mialiko ya kwenda nyumba za kulala wageni ilipozidi. Frida akakumbuka jambo!! Akamkumbuka mama yake



    mzazi. Akamkumbuka marehemu Maria Paul.

    Akakumbuka kuwa alihukumiwa kunyongwa baada ya kuua wanaume watatu.

    Au walimfanya kama wanavyonifanya!! Mbona aliua wanaume peke yao? Frida alijiuliza sana. Kifo cha mama yake



    kikamshtua akili yake. Akajiona ni mjinga ambaye hajijui kama ni mjinga.

    Mawio na machweo yakapita. Ikafika siku ya kutembelewa na muwezeshaji kutoka nchi za mbali. Huyu alikuwa ni



    yule mzungu mwenye upendo wa dhati kwa watoto wasiokuwa wa nchi yake.

    Frida hakuwa anajua kiingereza. Alitamani sana kumweleza yule mzungu juu ya unyanyasaji anaofanyiwa na



    msimamizi mkuu wa kituo chao. Siku moja kabla hajafika yule msimamizi aliufanya tena mwaliko. Kama kawaida



    akamadhibu bila makosa na kumfanya mtumwa wa ngono.

    Asubuhi ya mwezeshaji kufika kituo kilipendeza sana baada ya usafi yakinifu!!

    Mwezeshaji alifika na zawadi nyingi. Watoto wenyeji walimchangamkia sana na nyuso zao zilionyesha



    matumaini.hakika alikuwa ana upendo unaoonekana machoni waziwazi.

    Alikuwa analia na watoto akiona wapo katika majonzi. ‘NAKUPENDA SANA’ ndilo neno aliloweza kusema.



    Majira ya mchana watoto wote waliitwa katika holi la kulia chakula. Mbele yao walikuwepo wanaume wawili na



    wanawake watatu. Walitambulishwa mbele yao kama madaktari na washauri.

    Walizungumza nao mengi na kuwaeleza kuwa walikuwa wamefika pale kwa ajili ya kutazama kama watoto hao



    wanaweza kuwa wameathirika na ugonjwa wa Malaria.

    Zoezi la uchukuaji damu lilichukua muda mfupi. Kisha watoto wakaruhusiwa kuendelea na shughuli zao wakati



    wataalamu hao wakiendelea na utafiti.

    Ni wachache sana walioelewa nini kinaendelea. Wazoefu walijua kuwa wanapimwa mimba!! Mwanaidi akiwa mmoja



    kati ya waliokuwa wanafahamu. Akamtonya Frida juu ya jambo hilo. Frida hakushtuka hata kidogo. Alikumbuka kuwa



    shuleni alifundishwa kuwa dalili za mimba ni kichefuchefu!! Naye hakuwahi kukipata hapo kabla.



    ****



    Majibu yalimuumiza sana kichwa mzungu!! Alizunguka huku na huko. Alimkaripia sana mkuu wa kituo. Chumba



    kilikuwa na kiyoyozi lakini mzungu alikuwa anatokwa jasho. Hakutaka kuamini kabisa inawezekana vipi kituo kilicho



    na ulinzi imara kama ule mtoto anabeba mimba. Mkuu wa kituo alijaribu kujitetea lakini mzungu hakumuelewa.

    Maneno mengi hayavunji mfupa. Mzungu akatoa kauli. Kwa nini mate yatumike kuandika angali kuna wino?

    “Her name is Fridah! I need her right now!” (Anaitwa Frida, namuhitaji hapa sasa hivi!) alikoroma mzungu!

    Mkuu wa kituo akatoka nje akiwa anatetemeka!!

    Ndio. Lazima atetemeke maana kwa namna yoyote Frida lazima atamtaja kuwa yeye ndiye muhusika wa mimba ile!!



    Kibarua kitaota majani!!

    Hofu ikatanda sana!! Hadi anafika nje hakujua afanye nini!!!



    Wakati mnyanyasaji huyu akiwa katika hofu kuu. Frida alikuwa katika mawazo ya ataweza vipi kuzungumza na yule



    mzungu mwenye upendo wa hakli ya juu. Alihitaji kutoa shtaka lake dhidi ya mkuu wa kituo. Uamuzi huu



    hakumshirikisha Mwanaidi. Aliuhifadhi moyoni.

    Mara akiwa katika mawazo hayo mazito. Akasikia akiitwa jina lake kwa mbali. Akageuka!! Alikuwa mkuu wa kituo!!

    Moyo ukamwenda mbio Frida. Na ilikuwa kawaida kila alipomuona mwanaume huyu alimchukulia kama mnyama



    mkali.





    *****



    Hakuna kitu kinachokera nakuumiza kichwa kama kutafuta kazi na hakuna kingine kibaya kama kuipoteza kazi



    uliyoitafuta kwa kutumia nguvu nyingi.

    Ni fedheha hii ilimkumba msimamizi mkuu wa kituo. Ni kweli alifurahia kujistarehesha na Frida kwa kutumia



    mamlaka aliyokuwa nayo lakini hakutaka huyo Frida awe chanzo cha yeye kupoteza kazi yake.

    Akiwa amehamaki sana huku akiwa ameogofyeka na ukali wa mzungu yule. Mwanaume huyu katili asiyekuwa na



    upendo hata kidogo alitoka nje. Alipoagizwa kumuita Frida

    Akazurura huku na huko! Akamuona aliyetaka kumuona. Frida!

    Akamuita! Hakutegemea kama tukio hilo linaweza kutokea. Aligeuka mtu asiyemtegemea japo huyo ndiye



    aliyehitajika.

    “Sio wewe!” alimwambia kwa sauti ya kuamuru!!

    “Frida!” aliita tena, sasa yule aliyemtaka akageuka. Akapunga mkono kuashiria amfuate.

    Alipomfikia akamtaka amfuate anapoelekea. Yule binti mrefu mwembamba akamfuata akinyata kama hataki.



    Hawakuzungumza lolote wakaingia katika kile chumba alichokuwa mzungu.

    Binti akaendelea kusimama wima, nywele zake ndefu kiasi fulani zikiwa zimemziba jicho moja. Akazirusha nyuma na



    kushindwa kutoa salamu kwa mzungu kwa sababu ya kutojua lugha.

    Mzungu hakuwa na papara. Na aliujua ujanjaujanja wa wa afrika. Hakumuaga mtu pale chumbani akatoka na kurejea



    baada ya dakika chache akiwa ameongozana na muhusika mwingine wa kile kituo.

    “I want you to translate! (Nahitaji ufanye tafsiri)” aliamuru huku uso wake ukiwa umeiva kwa hasira.

    “What’s you are real name! (Jina lako halisi ni nani)”

    “Winifrida…” alijibu bila wasiwasi.

    “Famous name! (Jina maarufu)”

    “Frida..” akatoa jibu ambalo mkuu wa kituo alikuwa analingojea kwa hamu.

    Mahojiano yakaendelea kwa hatua ndogondogo. Hadi wakaifikia nia yao. Mimba!

    Hapo huyu binti akaruka maili mia. Akakataa katakata.

    Mzungu akabadili tena mtu wa kumtafasiria. Alifanya hivyo ili kuepukana na wabongo hawa waliomzunguka wasije



    kucheza dili ili kumdanganya.

    Hali ikawa ile ile.

    “Tunaweza kukupima tena??” aliulizwa. Hakungoja kujifikiria akakubali kuwa yu tayari tena mbele ya watu wote.

    Vipimo vikafanywa tena, majibu yakatoka. Hayakuwekwa hadharani. Wakapima tena. Frida hakuwa na mimba!!!

    Hapa sasa madaktari walioaminiwa na yule mzungu aibu ikawa juu yao. Mzungu akahamishia hasira zake kwao.



    Hawakuwa na cha kujibu. Heshima kwa mkuu wa kituo ikarejea maradufu. Akamwomba msamaha kwa lugha za ukali



    alizotumia dhidi yake.

    Maskini bwana huyu hakujua kuwa mkuu wa kituo ni mbongo halisi, tayari alikuwa amemchezea mchezo. Aliyeletwa



    mbele yake alikuwa ni mtu mwingine kabisa. Huyu alikuwa ni Winifrida na wala sio Frida yule chokoraa kutoka



    gerezani.



    Mzungu akiwa na hasira tele, kipara chake kikitokwa jasho. Hakutaka tena kuzungumza na mtu na hata mtoto mnene



    kiasi, mwenye sura inayotangaza msiba huku macho yake yakiwa mekundu. Alimkimbilia. Alikuwa ana haja ya



    kuonana naye kwaajili ya kumueleza kitu kizito sana.

    Alimfikia akamkumbatia. Mzungu akamkumbatiakisha akawaambia waliokuwa pembeni yake, “Tell her that I will be



    back (Mwambie nitarejea).

    “Yuko bize siku nyingine” mbongo akafanya tafsiri anayojua yeye.

    Huyu binti alikuwa ni Frida Gereza. Akawa ameikosa nafasi ya kuzungumza na mzungu huyo.



    Kwa pona pona aliyoipata mkuu wa kituo. Hakutaka tena kucheza karata hizi mbovu. Hata kabla huyo mzungu



    hajarudi tena tayari alikuwa ameweka mambo sawa. Mwanaidi na Frida walikuwa maeneo ya Posta wakitafuta mahali



    pa kulala. Makazi ya usiku ya chokoraa!!

    Walikuwa wamefukuzwa kimyakimya!!

    Mkuu wa kituo akabaki na tabasamu usoni huku akijisifu kuwa yu mshindi katika vita kuu. Hakuiwaza tena mimba ya



    Frida.

    Dada mkuu yule w zamani katika shule ya msingi alikuwa na akili ya kuzaliwa. Kitendo cha wawaili hawa kufukuzwa



    mapema baada tu ya mzungu kuwatembelea na kuwapima mimba kilimtia mashaka. Uhusiano wa Winifrida kuitwa na



    kutuhumiwa kuwa ana ujauzito kisha kupimwa na kukutwa salama pia kulimshtua. Hakutaka kumweleza Frida



    mapema. Lakini baada ya muda kidogo alifanya maamuzi. Kwa senti chache alizokuwanazo alinunu Pregnant Tester



    (PT). Hiki ni kifaa binafsi cha kupimia ujauzito kwa njia ya mkojo.

    Frida akaamriwa kukikojolea. Akafanya hivyo.

    Machale na hisia sahihi kabisa. Frida alikuwa ana mimba!!!

    Msichana huyu alichanganyikiwa kusikia hivyo. Lakini bado Mwanaidi alikuwa jasiri. Alimshauri kuwa kuamua



    kubaki nayo ni kujiua kwa mateso kabla ya wakati.

    “Kwa hiyo nitafanyaje mimi.”

    “Usijali!! Lala hapa nakuja.”

    Mwanaidi akatoweka tena na kutafuta duka la madawa lililokuwa wazi usioku ule. Akanunua madawa aliyoyajua yeye.



    Akafanikiwa kupata na maji ya kunywa ya bei chee. Frida akapewa sharti akatii. Akanywa yale madawa. Kisha akalala.



    Mambo yakaanza kubadilika baada ya masaa machache. Ule usiku ukageuka kuwa usiku wa uchungu mtakatifu.

    Tumbo likamsokota Frida. Mwanzoni alijikaza lakini uvumilivu ukamshinda akaanza kupiga kelele. Akalia sana



    Mwanaidi kazi yake kumbembeleza.

    Damu ikaanza kumtoka. Hatimaye uchungu uliopitiliza ukaondoka na fahamu zake. Alipoamka alfajiri hakuwa



    mjamzito tena.

    Mungu alikuwa pamoja naye! Njia hii hatarishi ingeweza kuondoka na uhai wake.



    ****



    Hakuna kipindi watoto wa mitaani wananyanyasika kama kipindi cha masika. Mvua hizi za masika huvuruga kabisa



    makazi yao ya kulala. Watoto hukesha kama popo. Sehemu zao za kulala zote huwa majimaji na magunia yao ambayo



    ni vitandavyenye thamani huwa chepechepe.

    Usiku huu ulikuwa usiku wa namna yake kwa Mwanaidi na Frida. Hawakuitegemea hali hii lakini sasa ilikuwa



    imewakumba. Walizurura huku na huko bila kuupata muafaka wa watalala vipi. Baridi kali iliwapuliza na manyunyu



    yaliyoambatana na upepo mkali yaliilowanisha miili yao.

    Baada ya kuzurura sana!! Mwanaidi akaanza kupunguza mwendo na hatimaye akasimama. Frida aliyekuwa



    ametangulia akageuza na kurudi nyuma kutazama nini kimemsibu rafiki yake.

    “Frida…” Mwanaidi aliita huku midomo yake ikichezacheza na meno yakigongana mdomoni.

    “Naumwa!! Naumwa sana” Mwanaidi alimweleza. Kifua kilikuwa kinambana. Frida alibaki anashangaa, mtu ambaye



    anamtegemea. Sasa anaumwa. Na ni yeye aliyekuwa mwalimu wake mtaani.

    “Kaninunulie dawa. Dawa ya kupuliza naanza kukosa hewa.” Alizidi kujieleza Mwanaidi huku sasa akiwa amekaa



    chini.

    Hali tete!! Hakika palikuwa na tatizo.

    “Inaitwaje…na hela sasa.” Aliuliza Frida huku akiwa na hofu kubwa.

    “Nenda watakuelewa waambie siwezi kupumua. Nitakufa Fri…Fri…” Sauti ikazidi kupotea.

    Ilikuwa saa tatu usiku. Mitaa ya posta haikuwa imejikita vyema katika akili ya Frida. Alijaribu kukata huku na kule.



    Hatimaye akalipata duka.

    Akawaeleza kama Mwanaidi alivyomuelezea. Akawalilia akalia sana chokoraa huyu. Hatimaye akaeleweka.

    Akapewa bure dawa ile ambayo hata aliyempa aliamini kuwa hawezi kuwa na nia mbaya na dawa ile ya kupuliza



    ambayo hutumiwa hasahasa na wagonjwa wa pumu.

    Frida akatimua mbio aweze kumuwahi Mwanaidi.

    Unapajua Posta unapasikia?

    Hilo swali alilijibu Frida kwa vitendo. Mtaa huu na mtaa ule inafanana. Jingo hili na lile la awali yanalingana urefu.



    Kila mahali panafanana na ikulu ya Tanzania. Frida akwa amepotea.

    Alijaribu kuituliza akili yake. Akapunguza mwendo aweze kuwa makini lakini bado hali ikawa ileile.

    Alitaka kuwauliza watu lakini hakujua atawauliza wamuelekeze wapi maana hata pahali alipokuwa awali na Mwanaidi



    hakupajua vizuri.

    Frida akaanza kulia. Mvua kubwa ikayatwaa machozi yake na kuyasafirisha mbali. Nguo zikanata katika mwili.

    Sasa Frida alikuwa anaomboleza kana kwamba Mwanaidi amekufa tayari. Usiku huu ukapita. Asubuhi anakuja



    kugundua alilala nyuma ya jingo ambalo Mwanaidi alikuwa akimngojea. Dawa yake mkononi ndiyo ilimgutusha



    akamkumbuka. Mwanaidi.

    Akaangalia sehemu zote hapakuwa na kiumbe anayeishi!

    Mwanaidi alikuwa ametoweka!

    Kilio kikaanza upya kwa yatima huyu. Aliugulia maumivu sana.

    Ile hali ya kumfikiria Mwanaidi kuwa amekufa kwa kusombwa na maji ikamfanya ajisikie kitu kama chuki kikitambaa



    katika mtima wake. Chuki dhidi ya wanaume. Akamuweka katika orodha mkuu wa kituo kama muhusika namba moja



    wa kifo cha Mwanaidi.



    Waarabu wa pemba hujuana kwa vilemba. Na hata yatima na machokoraa hujuana kwa vilio vyao. Chokoraa mmoja



    akafahamu kuwa Frida alikuwa katika majonzi. Kwanza alimgawia kipande cha muhogo alichokuwa anatafuna. Frida



    akapokea.

    “Unaonekana mgeni maeneo haya. We ni wa kempu ipi?”

    “Kempu ni nini?” aliuliza Frida.

    Yule msichana aliyejitambulisha kwa jina la Isha akatabasamu. Hakuendelea kuuliza maswali. Frida akajiumauma



    akaelezea juu ya kupotea kwa Mwanaidi.

    “Hiyo ni kawaida, wengine hubakwa na wengine huchunwa ngozi. Sijui watakuwa wameenda naye wapi.” Alijibiwa



    kwa tahadhari.

    “Mama yangu alichukuliwa mikononi mwangu. Mimi wakanibaka yeye aliondoka nao moja kwa moja hadi leo.



    Majangili na wanyang’anyi ni watu wabaya.”



    Isha aliongozana na Frida. Wakaelekea feri. Huko wakapanda pantoni. Iliyowavusha ng’ambo ya pili. Isha akiwa



    kiongozi wa Frida walizifikia nyumba nyingi walizokuwa wanaishi wanafunzi wa chuo kikuu cha IFM.

    “Huwa tunawafulia nguo. Nifuate!”

    Walianzia mlango wa kwanza. Wenyewe hawakuwepo. Mlango wa pili hawakuhitaji huduma. Mlango wa tatu bahati



    ikawa upande wao. Kijana mnene aliyenukia raha, akawakabidhi lundo la nguo.

    “Jinsi mia tatu, suruali na shati mia mbili, soksi na fulana huwa tunafanya mia mia.” Isha alimtajia bei.

    Yule kijana akawapatia ndoo na sabuni. Akawaelekeza bomba lilipo. Wakaanza kufua. Frida alikuwa mwepesi zaidi



    kuliko Isha na hakuonekana kuchoka. Isha hakuitegemea hali hiyo.

    Mchana wakapokea ujira wao na kuondoka.



    Urafiki wao ukaanzia hapa. Mwanaidi akaanza kusahaulika ili kutimiza ule usemi usemao ‘mavi ya kale hayanuki!’

    Kila mwisho wa juma walikuja na kutafuta kibarua cha kufua nguo za wanafunzi. Kwa siku za kawaida waliokota



    makopo tupu ya maji na soda na kuyauza kwa kilo katika viwanda vya wahindi na waarabu.

    Maisha yakaendelea!!

    Ni huku Kigamboni ambapo Frida alikutana na maajabu!!



    ***MAAJABU gani FRIDA anakutana nayo Kigamboni!!

    ***MWANAIDI na ugonjwa wake wa PUMU….ameishia wapi.

    **JE MKUU WA KITUO ataishi milele na roho yake mbaya.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog