Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

ADHABU YA PENZI LAKO - 5

 





    Simulizi : Adhabu Ya Penzi Lako

    Sehemu Ya Tano (5)





    Umetimia mwaka Sasa tangu Anthony apotee, lakini ni miaka miwil na miezi mitatu tangu ajali itokee, nilishaamini kuwa Anthony amekufa kwani hata kama ni mateka si rahisi wamteke siku zote hizo, nilitupilia mbali habari za Anthony na kuanza upya mikakati ya kumshambulia Gabriel Kwan tayari amerudi toka India, ila sikuweza kujua alipo ni wapi na pia haikuwa rahisi kuonana nae sababu kwa maelezo ya daktari bado hajaweza kutembelea, kusikia wala kuongea anachoweza kufanya ni kuona, na kufanya kujigusa ishara yuko hai ila kuoga, kuvaa, kula na mengineyo alisaidiwa na Jackline ambae aligeuka kuwa mama wa nyumbani, majukumu yote ya kazi alimuachia Mary ambae tayari alikuwa kama ndo ndugu yake na walipendana sana na kusaidiana kwa kila jambo. Na waliishi vizuri tu bila kuoneshana tofauti yoyote hali ya kuwa si ndugu. Jambo lile lilinikera na kunizidishia hasira nikiapa kuwasambaratisha milele

    ***

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Victor nae, mambo yalibadilika, aliitegemea sana mali za Gabriel akiamini atazipata ivo alijikuta akiingia kwenye mikopo mingi kiasi cha kushindwa kuzilipa, mambo yalipokuwa magumu akajikuta anadaiwa na taasisi za kipesa fedha nyingi sana, matumaini ya kupata pesa za Gabriel zilikwama ukizingatia hatujui documents zile zilipo kwenda, siku ya siku nyumba zake pamoja na magari yake yalipigwa mnada akajikuta Hana chochote tena, Hana nyumba wala gari wala biashara tena, akarudi kulelewa na mimi na kuishi kwangu akila na kunywa kwa pesa yangu, kwa sababu nilimpenda na pia namtumia kama mshauri wangu sikuona shida kuishi nae, basi habari zilipowafikia Jackline na Mary, walifurahi sana na kuamini kuwa mwanzo wa ushindi umekaribia, Victor alilazimika kuwa karibu yangu na kunisaidia mambo yangu Kwan alijua wazi nikichukia nitamfukuza,

    Mikakati ilianza na mara nyingi tulikuwa tunafanyia mikutano yetu kwangu, mimi, Victor pamoja na vijana wangu, walio kama sita, wataalamu wa bastola zisizotoa sauti na wauaji waliosomea na wenye ujuzi wa kutosha katika kupambana na adui, wenye uwezo wa kukuua bila ya kukuvamia, niliwategemea sana na kuwaamini sana, Basi tulianza mazungumzo yetu na kila mmoja alitoa mawazo yake na kuchangia, "Ili tuweze kujua wapi alipo Gabriel ni Lazima tuwafatilie popote waendapo na tuwe na mawasiliano ya karibu karibia kila siku naamin tutajua," mmoja alisema "iyo itasaidia ila Lazima tufanye kila liwezekanalo tumkamate mtoto wa Jackline kisha atueleze Gabriel aliko, najua atasema tu akiona mwanae tunae" Yan kabla hajamaliza kusema wote tulipiga makofi ishara ya kukubali, "vizuri basi tufanye haraka iwezekanavo kesho tuchore ramani alafu kesho kutwa kazi ianze" Nilisema na wote tulitawanyika kila mmoja kwenye majukumu yake,

    Siku ya tukio iliwadia, tulijipanga haswa, mimi nilibaki nyumbani kumsubiri mtoto wa Jackline aletwe kwangu, nilikuwa mimi pamoja na Victor, "Dada! Dada!" nilimsikia Wema akiita huku akilia, "shida nini wewe," nilishtuka kwani alikuwa anaumwa sana na jasho linamtoka, nilipomtazama vizuri alikuwa anatapika, haraka nilimwita dereva Ili ampeleke hospital, nae aliingia na kumbeba hadi hospital, wakiwa garini Wema alimshika dereva huyo ambapo alimpaka dawa Ili alewe na kama sekunde chache alilewa kabisa na kupoteza fahamu ndipo Wema alipomsogeza pembeni na kuendesha gari lile hadi mahali ambapo kundi lake lipo, "upo fasta sana vizuri," wote walijiandaa na kuchukua pikipiki zao mbili wakiwa wamebebana, "mwangalie huyo si tunakuja" Wema alisema na kuondoka wakiwa watano wavulana watatu na wasichana wawili. Pikipiki zao ni zile kubwa na zenye mwendo kasi pia zisizo na kelele, ni miongoni mwa pikipiki chache ambazo unaweza hata usizione barabarani zikipita kwani ni ghali kununua ila wao wanazo, walitumia dakika kumi kufika wanakotaka kufika ambapo kwa pikipiki zingine wangetumia dakika hata thelathini. Walipofika walijificha mahali, kwa kuwa ni usiku ilikuwa rahisi kujificha, kundi langu liliingia ndani na kuanza kufanya fujo, walitegea siku ambayo Jackline na Mary wapo pamoja na watu wanaoishi nao, "lete mtoto hapa" kwa nguvu Jackline alinyanganywa mtoto huku akiambulia kichapo cha maana yeye pamoja na Mary, Ghafla bin vuu! Vijana watatu waliovalia nguo nyeusi zenye kitambaa cha leather, hawacheki, wanajiamini na wana vimiili vembamba wastani ila wakakamavu, wameficha nyuso zao na si rahisi kuwajua japo kundi langu lilienda kawaida sababu walijua haitakuwa shida na hata walipoingia waliingia kwa kujua hawatapata kizuizi "rudisha mtoto kwa mama yake" mmoja alisema "hahaha nyie kama nani" aliuza wa kwangu kabla hajajibiwa alishtukia kitu kikitua kwenye mkono wake alioshikia bastola ambayo ilidondoka chini kwa maumivu makali alitaka kumwachia mtoto ila kutokana na umakini wao walimuwahi mtoto ndipo hapo fujo zilianza wote wakionesheana bastola, kundi langu lilidhani watu hao wapo watatu ila watano, kidogo waliona mlango umefunguliwa na wawili wa kwangu waliopo nje wameingizwa kwangu wakiwa tayari marehemu. Duuuu! Hofu ilitawala ila wale wengine wapo kawaida hawacheki wala kupoteza muda, waliobaki walitii amri "mpigie simu bosi wenu" amri ilitolewa nao walitii "oya mmefanikiwa" niliuliza ila kabla ya kujibiwa nilisikia sauti ya mtu ambayo sikuzoea "popote mlivo na sisi tupo" kisha simu ilikatwa "ondokeni La sivyo tutasambaratisha ubongo" amri ilitolewa nao waliondoka bila ya kipingamizi, walipoondoka nao walikabidhi mtoto na kutaka kuondoka "hey subirini, nyie akina nani" Jackline kwa woga aliuliza "tutaonana tena mtatujua ila msiogope" Wema alijibu na kuondoka zao



    Baada ya mashambulizi Yale Wema na wenzie waliondoka hali wameacha maiti mle kwa Jackline, hakuna aliyeaminika kile kilichotokea "mbona Ile sauti ni ya Rose" Jackline kwa kutahamaki aliuliza, "Ina maana Rose kanitumia majambazi" alizidi kujiuliza hali hajiwezi kwa kukosa nguvu, Mary nae alikosa ujasiri akajikuta amejitupa sofani Hana nguvu za kusimama kwa yale waliyoyaona, Ile nyumba ghafla iligeuka kuzimu baada ya kuona maiti zile mbili zikivuja damu tena wamelaliana, mfanya kazi alipiga simu polisi Ili waje kushuhudia matukio Yale na ukizingatia ilikuwa usiku wa saa kama sita ivi, polisi walipofika hawakuamini, kama kawaida ya waandishi hasa kwa watu wenye pesa kama Jackline huwa hawapitwi na matukio, usiku ule ule habari zikasambaa, Lakin hakuna aliyejua upande wa pili ni nani aliyewasaidia, Ni kwel Jackline alisikia saut yangu ila aliamua kunyamaza kana kwamba hajui chochote, hawakuwa na uhakika kweli kama ni mimi japo sauti yangu,

    Mimi na mi huku sikuamini kusikia eti vijana wangu wawili wameuawa alafu wengine wamenusurika, "ni nani mhusika wa haya matukio" nilijiuliza maswali ambayo sikupata jibu, sikuwa na adui mwingine zaidi ya Jackline Sasa huyo mwingine sikujua katokea wapi, "nadhani huyo ndo atakuwa amemchukua mwanangu" niliwaza "lakini wamejuaje kama leo tulipanga kwenda kwa Jackline" niliwaza tena "kutakuwa na mtu ananisaliti miongoni mwetu" nilipo waza vile ghafla niliamini yupo anaenisaliti, hisia zikanijia ni Victor "au anataka kurudiana na Mary" maswali yangu mengi hayakuwa na jibu zaidi yalizidisha hali ya sinto fahamu kwangu. Kwakuwa ni usiku niliamua kulala bila ya kuwatafuta wale vijana na nikapanga kuonana nao baada ya siku moja

    Palipokucha hali ikawa si shwari kabisa, vyombo vya habari ndo vilipamba moto, hili "MAJAMBAZI WATUNISHIANA MISULI KWENYE NYUMBA YA JACKLINE" lingine "JACKLINE ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUSAIDIWA NA WATU ASIOWAFAHAMU" na hili "MIUJIZA YATENDEKA KWENYE NYUMBA YA JACKLINE" lakini pia waandishi hawakutaka kulichukulia juu juu swala hili waliamua kumtafuta Jackline na kumhoji "kiukwel mpaka sasa sijui ilikuaje ila nachojua walitaka mtoto wangu" alisema "lakini watu wengine walinisaidia na nilipotaka kuwajua walinijibu nitaonana nao tena" alisisitiza kuwa hajui chochote kile na hamfahamu yoyote Kati ya wale, Polisi nao walifanya uchunguzi wao na kubaini majambazi hao wanaonekana ni wataalamu wa silaha hasa za moto na kupigana kwani walipochunguza miili ya marehemu walibaini kwanza waliuliwa na mkono alafu risasi ikafuata lakini pia risasi hazikuweza kusikia kwani walitumia bastola za kisasa zisizotoa sauti, cha kushangaza ni kundi lililomsaidia Jackline lina wadada Yan iliwachanganya sana polisi kubaini ni nani "hakuna mtu yeyote unayemhisia ni adui yako?" Jackline aliulizwa swali lililo kuwa gumu kwake, ukizingatia alisikia sauti yangu ivo Lazima angenitaja ila alikwepa na kudai Hana. Nadhani alikataa sababu Kuna roho ya undugu bado ilikuwa moyoni mwake, Mary alimshangaa sana "huu ndo muda muafaka wa kumkamata Rose" kwa ukali alisema ila Jackline hakuwa tayari kunishitaki na alizidi kusisitiza Hana uadui na mtu yeyote

    Wema nae baada ya kumaliza kazi yake alimchukua dereva yule na kwenda nae hadi hospital ambapo alipofika hospital aliomba kitanda alale pia mkononi alikatwa na kisu wakati anapambana na adui ivo aliomba walau alale pale kama mgonjwa Ili kuficha ushahidi wa alipo kuwa, alihudumiwa na kushonwa pale na uzuri alifahamiana na daktari wa pale, "najua umetoka kwenye kazi zako ila angalia utakamatwa siku moja" daktari aliyemfahamu fika Wema alimweleza huku wakicheka, "ndo zinatufanya tunaishi mjini" Wema alijibu kisha alipumzika na alikaa siku mbili hospital Ili kuficha maovu

    ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kama wiki kuisha, habari za ujambazi ule zilianza kupungua, na kuisha kabisa, Wema alirudi nyumbani na kuendelea na kazi zake bila ya yeyote kumshtukia, kidonda chake cha mkono kilikuwa kikubwa ila hakuna mtu yeyote aliyejua kama aliumia maana alivaa nguo zenye mikono mrefu. Siku moja akiwa anafanya usafi wake yuko peke yake alijivalia vesti tu na kufanya kazi, ghafla aliingia moja ya wale vijana wangu na kumkuta, walipokutana macho kwa macho wote wawili wakasomana machoni kila mmoja kwa tafsiri yake, kisha Kaka yule akatupa macho yake kwenye mkono "hapo umefanyaje?" kwa sauti ya kibabe aliuliza "Juzi wakati napika niliungua" Wema alijibu kwa ujasiri tena bila ya hofu, kijana yule aliguna tu kisha akachukua kilicho mleta na kutaka kuondoka ila moyo ukasita, alirudi ndani na kumkuta wema bado anafanya kazi zake, "Wema ebu njoo" alimwita na kumsubiri, Wema alipofika alibaini tatizo na akishajua ameshtukiwa, "ivi karibuni uliondoka usiku ulienda wapi" swali lile lilimfanya Wema ajue wazi kashashtukiwa, japo alimjibu ila bado hakuridhika, punde si punde alimtolea bastola na kumtaka asemae ukweli, yule kijana alimjua kwani yeye ndiye aliyeona wakati Wema akiwa ameshikilia sehemu aliyokatwa usiku ule "kumbe wewe ndo miongoni" kwa hasira alisema huku akimtaka waende nae chumbani kwake kukagua, Wema nae tayari alishajua hayupo salama ivo akawa hana ujanja wowote, walipofika kijana yule alipekua na kuona bastola pamoja na simu vitu vingi vilivyo ashiria kweli Wema Wema alihusika siku ile, kijana yule alijawa na jazba pia alijua wazi Wema ni hatari, alimrudisha sebuleni Ili awapigie simu wenzake, looh! Haikuwa rahisi kiivo kwani Wema alibahatika kushika silaha bila ya kijana yule kujua, Wema alikuwa mwembamba alafu mwepesi sana pia ndiye aliyetegemewa katika kulenga shabaha, basi alifanikiwa kushika kisu kidogo ambacho hicho hutembea kwenye kiuno, namna alivoichukua haikujulikana na jinsi alivokirusha hatimae kutupa bastola chini haikujulikana pia kisha alijirusha hadi alipo na kumnyanganya simu Ile, kijana alimshika na kumpiga ngumi aliyoikwepa ila ya pili ilimbahatisha puani ndipo Wema alipopata wenge na kuyumba japo akili haikuwa tayari kushindwa kujua namna ya kumshinda, alisimama kwanza kuelewa mchezo kisha alipambana nae sana, kijana yule alimzidi nguvu na kumpiga sana, kwa bahati alipopigwa aliangukia sehemu bastola ipo kwa hasira na maumivu makali Wema alimtukana kisha alifyatua bastola na kumuua, alipoona kashamuua alichukua bastola Ile na kuiweka karibu yake alafu yeye akalala pale chini bila ya kutoa taarifa popote.... Ndipo mimi na kundi lake lilirudi nyumbani na kukuta matukio hayo..."whaaaaaaaat "kwa tahamaki nilisema Wema yuko hoi alafu mwingine maiti" wamemuua Kaka " kwa sauti ya chini Wema alisema kupoteza ushahidi na kweli ukizingatia Wema alipokea kipigo cha maana ndo kabisa tuliamini amevamiwa ndipo tulipompeleka hospital kwa matibabu zaidi Ili apate unafuu aweze kutueleza ilikuaje, ingawa yeye hakuzidiwa sana ila alijifanya hajui chochote, tulipomfikisha hospital mimi nilirudi nyumbani kwa ajili ya kushirikiana na polisi Kuhusu maiti Ile, nilipoingia chumbani kwa Wema Ili nichukue kanga sikuamini kabisa macho yangu kwani nilikutana na bastola pamoja na simu nilipopekua nilikutana na ujumbe zilizoniashiri wazi Wema anahusika na uvamizi ule uliofanyika wakati vijana wangu wanaenda kwa Jackline





    Sikuamin kama wema hakuwa mfanyakazi wa ndani bali mpelelezi wangu. Nilijawa na hasira huku jasho jembamba likinitoka hali sijui alikuwa akimfanyia nani kazi. Niliwaza kwenda polisi kushitaki ila wazo langu lilionekana kama halina maana sababu niliogopa huenda binti yule anajua mengi ya kwangu. Kwakuwa najuana na baadhi ya watu wa kituo cha polisi basi nilienda kuongea nao kwa kuomba ulinzi kama hospital ili asiondoke. Wema alifungwa pingu pale pale kitandani kama muhalifu kisha polisi waliwekwa mlangoni kuhakikisha usalama.

    Kama siku mbili ivi wema alipata unafuu na alipojitambua aligundua amefungwa pingu pale kitandani. Akili ilimcheza haraka japokuwa ni mgonjwa, aliwaza atatokaje ukizingatia wenzake hawana taarifa, akiwa kwenye dimbwi la mawazo aliingia nesi kwa ajili ya kumtazama alipomwona alimtazama kwa makini sana kisha alimuuliza swali, "doctor vene yuko wapi.?" Nesi bila hiyana alijibu kisha wema aliomba aitwe "ok, ila usizoee sababu haturuhhusiwi kukusikiliza kwa lolote " alisema na kuelekea aliko doctor vene. Kama dakika chache ivi aliingia na kumkuta wema ametoa macho kama anataka kufa. Alimweleza yote na alihitaji msaada wake wa hali na mali. Vene aliogopa kumsaidia ila wema alisisitiza lazima atoke pale hospitali haraka iwezekanavo "nisaidie kuwatafuta wenzangu wape taarifa ivi wajue" wema aliomba Kwan hakuwa na ujanja wowote. Alichofanya vene ni kuwajulisha wenzie wema. Kwakuwa hakuruhusiwa kuingia mtu yeyote mle ndani basi walilazimika kutumia simu kufanya mawasiliano ndipo vene alipopewa mbinu za kumtorosha wema.

    Ilipofika asubuhi ya siku iliyofuata vene hakuingia kazini. Ila kuna mtu alivaa nguo za kidaktari na kuingia kazini kama doctor. Alipofika alichukua file kana kwamba analikagua kisha alipokuwa akitembea daktari mwingine alimfata na kuanza kuongea "naona hali yake si mbaya japo saiv nguvu ndo hana" alisema mwenzake huku wakizidi kuelekea kwenye chumba alichomo wema. Walipofika mlangoni pale walisimama na kuzidi kuonesha wako makini sana na kazi yao, mwingine alijidai kupiga chafya sana "wewe umekuaje" aliulizwa ila alizidi kupiga chafya "afande ebu nisaidie kushika hili file kwanza" nae afande alichukua na kuendelea kumtazama Yule daktari nae afande mwingine alizidi kutoa pole nyingi. "Asante sana" ndipo alipotulia na kujiweka sawa alitabasamu na kuondoka zake huku mwenzie akiingia kwenye chumba alichomo wema. Alitumia dakika kama tano kisha alitoka.

    Baada ya dakika kumi tangu Yule daktari apige chafya ., wale askari waliaanza kusinzia hatimae walilala. Bila ya kupoteza muda wema alitolewa mle ndani na kuondoka zake bila ya mtu yeyote kujua. Kilichowashtua watu ni jinsi wale askari walivokuwa wamelala. Waliposhtuliwa walionekana kuchoka sana. Daktari aliyewashtua alipowaona alibaini walipuliziwa dawa za kulevya na walipofungua chumba cha wema hawakumkuta mtu yeyote. "Heeè wale hawakuwa daktari. Daaaa tumekwisha" askari wale walinywea kama kuku aliyenyeshewa mvua. Nilipopewa taarifa nilichanganyikiwa sana. Sikuamini kama wema aliwazidi ujanja hadi polisi. Sikuelewa nani anahusika na haya. Hofu ilinivaa wakati siyo kawaida yangu. Sikuweza kutoa taarifa yeyote kwa mtu yeyote kwani nilihofia mengi kunipata. Nilinyamaza kana kwamba sihusiki na chochote japo moyo bado uliamini yote hayo yanafanywa na Jack au Mary.

    *****

    Hali ya Gabriel ilizidi kuimarika siku hadi siku hatimae alipona majeraha ila alipoteza kimbukumbu zake zote hata jina lake hakuwa analijua. Alirudi Tanzania kwa matibabu ya kawaida kwani Yale ya ulazima sana aliyamaliza. Alirudi kimya kimya bila ya mtu yeyote kujua.

    Sikumoja Gabriel akiwa kwenye matibabu yake, mwanasheria wake alimuona "Dada Rose nimemwona Gabriel nadhani amerudi matibabuni" nilivosikia vile moyo ulipasuka paaaa! Sikuamin kabisa. Kwakuwa mwanasheria yule alishakuwa upande wangu basi alianza kunipa mikakati ya chakufanya kumpata Gabriel. Nilitabasamu sana na kukubaliana nae.

    Ndani ya siku tatu tangu nipewe mikakati na mwanasheria huwezi amini nilipokea taarifa kuwa mwanasheria yule ameuwawa akiwa ofisini kwake na muuaji ameacha karatasi ULIPO NIPO. Daaa! Sikuelewa kinachoendelea wala sikujua nani anahusika na haya. Akili ilianza kupambana kujua nani anahusika lakini haikuwa rahisi kiivo kubaini.

    Victor nae alizidi kuhangaika namna ya kunipokonya mali zangu. Haikuwa rahisi sana sababu wote wawili hatuna hati halisi ya mali za Gabriel na akisema kuhusu zangu isingekuwa rahisi zaidi sababu hajui hati zangu ziko wapi. Alianza kuonesha mapenzi moto moto kwangu na kunihoji sana kuhusu mali zangu. Kiukweli kwa kipindi kile sikuwa tena na ushamba wa mapenzi ivo haikuwa rahisi kwake kujua habari zangu. Siku moja nilimpima kwa kumtajia zilipo. Nae bila kufikiria aliridhika na kuweka mipango ya kuchukua kumbe mimi niliweka hati feki. Alipofika nilipomwelekeza alichukua bahasha Ile na kuondoka zake. Sikutegemea kama kweli Victor yuko kimaslahi kwangu. Nilimchukia na sikutaka hata kuhoji chochote kutoka kwake. Niliandaa timu yangu tayari kwa uangamivu wa Victor

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilimpigia simu Victor ili tuonane lakini hakupokea simu yangu, hasira zilinivaa sana kuona Victor ameamua kunisaliti. Tangu nazaliwa mpaka sasa sikuwahi kuchukia au kujawa na hasira kama ilivyo leo. Kadiri navomtafuta alafu hapatikani ndivo na hasira ilizidi. Nilichukua gari langu na kuondoka hadi ofisini kwake. "Ametoka sasa ivi kaenda kikaoni " Secretary alijibu bila ya kunitazama machoni. Niligundua kuna tatizo na nilihisi yeye na Victor kuna kitu wananificha. Nilimtazama binti Yule bila ya kusema kitu nikajidai nataka kuondoka ile nimegeuka kumpa mgongo nilitoa bastola na kumgeukia hali sicheki wala sitabasamu pia sauti ilibadilika. "Victor yuko wapi" maneno machache Ila yenye vitisho. Binti yule aliogopa sana tena alikosa hadi nguvu "yuko ofisini kwake amesema ukija niseme hayupo " daaa! Bora binti yule asingenipa maelezo yale ila kwa maelezo yale nilijua wazi lengo la Victor . Niliingia ofisini kwake nikiongozana na kijana wangu. Victor aliponiona alishtuka sana kiasi cha kuogopa. Niliingia na kuketi kitini. "Vipi mke wangu mbona mapema leo"alijidai hajui chochote tena haelewi kitu. Sikutaka kubishana nae nilifungua pochi yangu na kutoa bahasha ya kaki iliyojaa makaratasi ndani."asa nini hizi mke wangu" aliuliza na ukumbuke sikuhoji kwanini hataki kuonana nami. Aliivuta na kuikagua "vile vitu ulivyokuwa unavitaka na ulivovichukua ndo hivyo hapo " nilisema "ulivyonavyo si orijino ila ulivyovishika hapo ndo vyenyewe nimekuletea" nilisema kwa kujiamini sana tena sikuwa na mapenzi na yeye siku hiyo. Alitabasamu tabasamu la aibu huku akiogopa kwani alinijua sina mzaha. "Nifuate niendako" nilisimama na kuondoka naye Victor alinifuata "na wewe nifuate"nilimweleza secretary. Niliwapakiza gari chini ya ulinzi mkali sana hadi nje kidogo ya mji. Tulipofika nilishuka garini nao walishushwa. Sikuwa na maneno mengi juu yake. Wala sikutaka kujieleza au yeye ajieleze nilichofanya ni kutoa ishara kwa vijana wangu ambao waliwafunga pamoja "waueni kifo cha taratibu kisicho na haraka" victo kusikia vile alilia sana "Rose please nisikilize" alisema kwa kuhangaika sana "nisamehe Rose ngoja nikueleze jambo usilolijua" alihangaika sana ila sijumjali "Rose nooooo!" Victor alilia hasa pale risasi ya kifua upande wa kulia ilipopenya. Nae yule dada alifyatuliwa risasi iliyosababisha kifo chake pale pale. Wote wawili walidondoka upande mmoja na sisi tuliondoka zetu.

    Nikiwa kwenye gari nililia sana tena sikutaka mtu yeyote anisemeshe. Kufika nyumbani niliingia chumbani kwangu na kujifungia. Nilimpenda sana Victor na Victor alijua siri zangu nyingi. Kulikuwa na ulazima wa yeye kuuawa sababu alionesha kunigeuka. Nilikumbuka mambo mengi yamhusuyo na jinsi alivyokuwa akinishauri na nilipiga hatua kubwa sana sababu yake. Haikuwa rahisi kumsahau japo ilibidi. "Kama nimeweza kumuua mwanaume niliyempenda basi sitashindwa kumuua Jackline na Gabriel " nilijisemea hayo na kuhakikisha nawaua wote. Nilikunywa pombe sana hadi kupoteza fahamu.

    Nikiwa usingizini nilianza kuota vitu vya ajabu. Kwa ghafla nilimwona mama yangu akitoa machozi akiwa amevaa nguo nyeupeeè yenye kung'aa sana. Nilipomtazama kwa makini napo ghafla alibadilika na kuwa joka kubwa lililotaka kunimeza ile ananimeza nilishtuka sana. Niligundua ni ndoto tu nikapuuza.

    *****

    Maisha ya jackline, Mary na Gabriel yalizidi kusonga mbele. Ni muda mrefu hawakubambana na mimi kwaiyo kidogo walijisahau. Gabriel alianza kurudisha kumbukumbu taratibu sana. Katika kitu anachokumbuka ni jina Rose kila mtu alimwita Rose na hakuweza kujua huyo rose ni nani. Hawakuwa na haraka sana za kumfanya arudie hali yake.

    Wiki kama tatu kupita taarifa ya habari ilitoka kwamba wapita njia wameokota mwili wa binti ukiwa marehemu. Katika uchunguzi ulibainika kuwa ni mfanyakazi wa Victor. Walipofika ofisini kwa Victor nae Victor hakuonekana, waliponiuliza nilitoa ushirikiano ulionifanya nionekane sina hatia. Mawazo yalinijia mwili wa Victor umekwenda wapi. Taarifa hizo ziliwachanganya sana watu hasa Mary . "Noooo Victor itakuwa ameuawa" Mary alilia sana na aliamini mimi nahusika kwa kifo chake. Alinifata siku moja ofisini kwangu na kuanza kunitishia "najua unahusika na kifo chake wewe ndo umemuua" alisema kwa jazba hali mimi sina habari nae "lazima unahusika sababu Victor alitaka kukufilisi na hicho not chanzo cha mimi na yeye kugombana" aliposema vile niliacha kile nifanyacho ili nimsikilize "nahisi umegundua hilo ndo maana umemuua" Mary alikuwa anaongea mambo ambayo utadhani alikuwepo ."huu ni muda wangu wa kulipiza kisasi Rose nitakuua kwa mkono wangu mwenyewe labda uniwahi" aliposema vile aliondoka zake kwa hasira. Niliposikia yale maneno nilichukia sana kiasi cha kutamani kumuua muda ule. Alipoondoka nilipiga simu kutoa agizo la kumfatilia Mary popote aendapo.

    Mary alikosa raha baada ya Victor kukosekana. Alianza kuhangaika huku na kule kujua Victor yuko wapi lakini haikuwa rahisi. Sikumoja alikuwa anatokea ofisini kwake kuelekea nyumbani alipofungua mlango wa gari ili aingie garini alishtukia mtu akimtolea bastola "fata nisemayo ili nisikudhuru" Mary kusikia vile aliogopa sana na kutii amri. "Washa gari na uendeshe kwa maelekezo yangu" kijana yule alisema nae alitii "pita kushoto alafu endesha mpaka kwenye mti yule pale alafu park gari mbele ya kale kajumba" Mary alitii na kufanya kama alivoambiwa. "Shuka kwenye gari ukiwa huna chochote hasa simu" Mary aliogopa sana na alijua mwisho wake umefika. Alipiga moyo konde na kuelekea kule alikoelekezwa. Alipofika hakuona mtu yeyote wala hapakuwa na kitu chochote. Kwakuwa ni nyumba iliyoharibika na chakavu na ina vyumba vingi alianza kupita kila chumba. Aliingia cha kwanza hakuna kitu, cha pili hadi cha tatu Ile anatazama chumba ambacho ni kama stoo aliona mtu amelala chini. Alishtuka sana alitamani kukimbia ila alijikaza na kuanza kusogelea kile chumba . "Munguuuu weeeee!" Mary aliangua kilio kikuu ambacho nahisi kama kuna aliyekuwa anapita karibu na jengo hilo alisikia. " nooòoo!!!" Alisikika akilia. Alikuwa ni Victor aliyelala pale chini hajitambui ila anapumua....



    Mary aliyekuwa amevaa gauni refu sana pamoja na viatu vya kisigino alijikuta akivua vile viatu na kushikilia gauni lile ili limpe uwepesi wa kupiga hatua kubwa kubwa kumfikia Victor aliyelala pale chini. Aliangua kilio kikubwa sana baada ya kuufikia ule mwili na kuukumbatia. Aliubusu kwa huba na majonzi makubwa. Kiuhalisia Mary alimpenda sana Victor japo awali halikuwa chaguo lake Ila kadiri walivyoishi pamoja walijikuta wakipenda sana. Mary kutengana na Victor haikuwa kazi rahis kwa yeye kumsahau na kila mara alisali Victor amrudie. Binti yule aliuchukua mwili wa mume wake na kuulaza kifuani pale na kuupapasa kwani hakuwa na jinsi. "Mume wangu umekumbwa na nini baba " machozi hayakuisha machoni mwake "nilikwambia Rose siyo mtu mzuri hukuniamini" Mary alilia sana "nani kakuleta huku jamani" aliuuliza mwili ambao haukuwa ukisikia chochote. "Mimi ndo nimeuleta huku " ilisikika sauti ya mwanaume na alipogeuka alimwona yule aliyemleta huko."kwanini usimpeleke hospital kwanini unamtesa mume wangu" Mary bila ya kujua chochote alianza kugomba Ila kaka yule hakuonesha kumjali wala kuyajali maneno yake. Alielekea kwenye kabati lililochakaa sana na kutoa embe na kuanza kumenya taratibu na kisu chake ili ale. Mary alishindwa kuelewa kijana yule ni nani. Bila ya kusemeshana kwa muda yule kaka alizidi kumenya embe na kula. "Naitwa Jose na najua wewe ni Mary " alijitambulisha na kuendelea kula embe. Alionekana hana haraka na mtu yeyote pale wala hakuwa na la kujali. Alipomaliza kula alivuta kiti na kukiweka karibu yake kisha alimtaka Mary akae. "Unataka kujua ilikuaje" aliuliza ndipo Mary aliitikia na kusubiri kuelezwa jambo.

    "Victor ni kama kaka yangu. Yeye ndiye aliyenipeleka kwa Rose kufanya kazi kama jambazi. Mimi na wenzangu ndiyo tuliyokuja kuwavamia usiku ule. Pia ndiye tunayemsaidia Rose kufanya uhalifu mwingi akitutegemea sisi. Victor alitakiwa afe na mimi ndiye niliyempiga risasi kwa agizo la Rose. Sikutaka kumuua kwani Victor amenisaidia mambo mengi kifedha na hata ushauri. Victor ni kama kaka yangu wa damu hivyo sikuona sababu za kumuua. Nilipompiga risasi tulirudi nyumbani ila Mimi sikufika nyumbani nilirudi kama nusu saa kupita na kukuta kavuja damu nyingi sana. Sikutaka kumpeleka hospital kwani kufanya ivyo kungepelekea kuuawa kirahisi maana Rose anafahamiana na watu wengi hospital, polisi na sehemu zinginezo kwaiyo isingekuwa msaada kwake. Nilichofanya ni kumwita daktari awe anakuja kumtibia huku kwa siri na kwa kificho kukubwa. Na ndo maana hali yake inaendelea vizuri. Kilichonifanya nikulete huku ni kwa sababu Victor anakupenda sana tena sana. Kila mara alisema mambo yake yakikubali lazima aje kukufata muishi kama zamani. Kila mara alikutaja na kukusifia kuwa mwanamke shujaa na mwenye mapenzi ya dhati. Nadhani mambo aliyokuwa anayazungumzia ni kumfilisi Rose japo alikosea kitu kimoja kumshirikisha moja Kati ya vijana wa Rose akiamini atasaidiwa kumbe haikuwa ivo kwani kijana yule alienda kumweleza Rose. Ndiyo maana Victor alikamatwa na kutendwa hayo. Nilipojua atauawa nililazimika kumwambia Rose kuwa nitamuua mimi ili nisije kumlenga risasi itakayo sababisha kifo pale pale. Hayo ndiyo yaliyomkuta mumeo"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Jose alipokuwa akiongea yale Mary alizidi kulia kwani hakuamini. "Rose nitalipiza na nitahakikisha nakuua mikononi mwangu" Mary alisema kwa kuapa kabisa "siyo rahisi kwa wewe kutimiza lengo lako kwani Rose amejipanga na ana ulinzi mkubwa sana" Jose alimkatisha tamaa na kumuonya asijaribu kushindana na mimi sababu mpaka hapa nilipofika nina majeshi mengi. "Tungeshawaua wote hasa Gabriel ila mshukuruni Victor kwa upendo wake kwako alikuwa akimzuia Rose ila kama kuwasambaratisha tungesha wasambaratisha" Jose alizidi kumtisha Mary ambae alianza kuniogopa. "Onyo!!! Ni marufuku mtu yeyote kujua kama Victor yuko hapa ukijaribu nitamuua mbele yako pamoja na wewe" Jose alisema bila ya kuonesha kicheko "kwanini unamfanyia kazi Rose tena kazi za kinyama ivi" Mary alihoji swali lililomchekesha sana Jose. "Siyo kwamba napenda. Nilisomea maswala ya mitandao INFORMATION TECHNOLOGY maisha yakawa magumu nikakosa msaada, familia yangu yakimasikini mimi ndo tegemezi tangu nimekuwa kwa Rose nimebadilisha maisha ya kwetu na nina maisha mazuri sana. Nina nyumba, gari na ndugu zangu wanasoma vizuri. Kwaiyo siko tayari kutoka kwa Rose." Jose alisema na kumtaka Mary amweke vizuri Victor kisha aondoke "kuja huku mpaka nikuruhusu ukija bila Mimi kujua hutaniona nikicheka wala kuongea kwa upole ivi" alisema na kumruhusu aondoke zake.

    Mary hakuamini kile alichokiona na kusikia. Akiwa garini aliwaza mengi sana ambayo hakuwa na majibu nayo. Pamoja na vitisho vyote bado aliahidi kuniua kwa mikono yake. "Sitoacha kufanya kazi kwa Rose na nitafata maelekezo yake" maneno ya Jose yalimchanganya sana binti Yule. "Victor ndo alikuwa anazuia tusiwazuru kwa sababu yako" maneno yalizidi mchanganya sana Mary kiasi cha kushindwa afanye nini. "Onyo mtu yeyote asijue kama Victor yuko hai " maneno yale ndo yalizidi kumchosha akili Mary . Alikubali kuwa mkimya mpaka pale Jose atakapomruhusu kumweleza yeyote.

    Siku nenda siku rudi Mary alizidi kuwa msiri tena hakutaka mtu yeyote kujua habari ile. Japo alitamani kumweleza jackline.

    ****

    Mimi nami ndo nilizidi kuwa katili. Mtu yeyote akinichezea sichelewi kumfanyia unyama. Tangu nimfanyie unyama Victor nilishamuua dada mmoja na kumfilisi kaka mmoja aliyejaribu kunitoroka na mali zangu . Kilichobaki ni kumuua Gabriel na mtoto wa jackline sababu kuishi kwao kutanifanya nirudishe Mali za Gabriel wakati mimi sitaki kupunguza mali nilizo nazo. Japo wakati mwingine niliwaza sana nani amenichukulia document pamoja na Anthony wangu. Kuna wakati roho ya umama inanijia na kumkumbuka sana mwanangu ila wakati mwingine hata simuwazi.

    Ilikuwa siku ya alhamisi saa tano asubuhi natoka nyumbani kuelekea kazini kwangu. Sikuiyo niliamka mchovu mno. Nikiwa kwenye gari langu kuelekea kazini nilianza kujiona kama siyo mimi, nilipofika sehemu trafiki alinisimamisha ili watu wapite, "whaaat?" Nilishtuka baada ya kumwona mtu ninaemfahamu akivuka barabara. Nilipomtazama vizuri niliogopa sana baada ya kumwona mama yangu akivuka barabara "mbona huyu ni mama yangu na mama si ameshafariki miaka kadhaa iliyopita" nilijiwazia huku nikisahau kuwa niko barabarani na kumbe honi zilikuwa zikipigwa ili niondoe gari ila sikusikia. Kaka mmoja alishuka garini na kunifata aliponifikia alinipiga kibao taaasssss!!! Kibao hicho kilinishtua kwenye mduwao Ule "pumbavu sana umelewa nini ebu endesha gari" kutokana na hali ile sikuwa na uwezo wa kubishana nae zaidi niliendesha gari hadi kazini kwangu najiuliza kwanini namwona marehemu mama yangu. Nilipofika tu ivi ofisini naona moto kwenye jengo langu kwani nilinunua jengo lenye ghorofa tano mjini, huwezi amini lilikuwa linateketea kwa moto kwa kasi ya ajabu ndani ya jengo hilo ofisi zangu zilikuwa kama saba na wengine waliopanga ofisi kama ishirini na zaidi. Nilipofika tu pale nilibaki kuduwaa. Zima moto walijitahidi lakini wapi haikusaidia Ile nageuka upande mwingine kutazama huku na kule nilimwona tena mama akilia. Nilipotazama vizuri nilijua ni yeye basi kuna roho iliyonituma nimfate ukizingatia alikuwa upande mwingine wa barabara. Ile naenda kumfata nilivuka barabara bila ya kutazama magari ndipo kuna gari lililokuwa linakuja kwa kasi lilinichota vuuuupppp na kunitupa upande mwingine wa barabara. Kabla sijafunga macho yangu nilimwona mama akinifata na kunitazama hali akitoa machozi ndipo nilipodondoka chini..............



    Ndipo nilipofumbua macho yangu na kuona watu wengi wamenizunguka. Nilipotazama huku na kule niliweza kubaini baadhi ya watu akiwemo jackline na Gabriel. Sikuweza kukumbuka chochote ila kumbukumbu za kuwajua ni akina nani nilikuwa nazo. Wote kwa pamoja walionesha kunikarimu na kunijali. Jackline alipoona nimezinduka alikimbia haraka kumwita daktari. "Docta njoo Rose ameamka" nilisikia akisema kwa furaha na upendo. Alipoingia daktari alinikagua na kunipima vipimo vilivyohusika kwa muda ule. "Naona amepona damu mliyomuwekea imemsaidia sana" niliposikia damu nilishtuka "damu ya nini" bado akili haikurudi kuwa nilipata ajali. Nilipotaka kunyanyuka nilisikia maumivu makali sana ya kichwa huku wengine wakinizuia nisiamke. "Pumzika kwanza Rose hujapona vizuri" Jackline alinirudisha nilale kisha alichukua supu na kuninywesha. "Kwani niko wapi" niliuliza "upo hospitali umelazwa ulipata ajali ya gari" Jackline alisema huku akinipapasa nywele zangu. Niliwaza sana ajali kivipi tena nilijiuliza waza kwanini nilipata ajali. Kwakuwa haikuwa rahisi kukumbuka niliamua kutulia. Nilipojitazama vizuri nilibaini kuna tatizo. Nilipotaka kusogeza mguu wangu niliona uzito mguuni. Nilishtuka na kuogopa. "Mbona mguu wangu hausogei" kwa tahamaki niliuliza ila Jackline hakunijibu kitu. Nilizidi kusisitiza kuna nini ila Jackline alibaki akilia na kuogopa kusema. "Baada ya ajali ulivunjika mguu ambapo haukuwezekana kuurudisha katika hali yake hivyo ulikatwa" Jackline kusema tu vile niliangua kilio kikubwa sana. Uvumilivu ulinishinda kiasi cha kulia kwa kupiga ukunga kama mwanamke anaejifungua. "Mguu wangu mimi nitatembeaje kwanini mmeukata mguu wangu." Nililia sana Jackline alijitahidi sana kunituliza ila haikuwa rahisi. Kumbuka hapo sikuwa na kumbukumbu zozote kuhusiana na Jackline au Gabriel. Katika machozi yale ghafla nilikumbuka kuwa mimi na Jackline hatuelewani. Ikawa kukosa kwa mguu changanya na ugomvi wetu ndo hasira zilizidi. "Umetaka nikatwe mguu ili niwe kilema naomba uondoke hapa" maneno yangu yaliwashangaza watu walioko pale "naomba uondoke muuaji mkubwa wewe" nilisema huku watu wakijaribu kunielewesha. " umelazwa huu ni mwezi wa nne, aliyekuwa anakuhudumia ni Jackline leo hii umepona unamfukuza" walisema "hakuna mtu hata mmoja aliyeweza kukutolea damu ila Jackline na alikutolea si kwa kupenda ila tulimwomba sana" walizidi kusema maneno ambayo ndo kabisa yalinizidishia chuki. Ni bora hata asingenisaidia ila kitendo cha yeye kunisaidia kilinifanya nijione kuwa Jackline kanizidi akili. "Tokaaaaaa sikutaki" nilitupa vitu vyote viliyokuwa karibu yangu kwa kumtupia Jackline aondoke. Muda huo wote Jackline alikuwa akilia sana. Akikumbuka alivyopoteza fahamu baada ya kutoa damu ile pia jinsi alivyokuwa mgumu kunisaidia na watu walivomshawishi sana aliishia kulia bila ya kuongea chochote. "Na ukumbuke neno hili lazima nilipize kisasi wewe ndo umetaka nikatwe mguu" kila mtu aliyesikia maneno yale alishangaa sana na kunisikitikia. Muda huo wote Gabriel alikuwa mkimya. Hakuwa anaelewa chochote sababu hana kumbukumbu zozote za kwangu. Ye alijua wazi labda ni ndugu tu wanagombana ila hakujua chanzo cha ugomvi ni yeye. Jackline na Gabriel waliondoka zao na kuniacha pale hospitali. Na baadhi ya watu walikereka kwa kitendo kile kiasi cha kuondoka na wao. Masikini mimi nilibaki peke yangu pale nikitafakari jinsi mguu wangu ulivyokatwa. Nililia mno na kijuta kwanini imekuwa vile. Tangu siku hiyo hakuna mtu aliyekuja kunisalimia tena pale hospitali zaidi ya vijana wangu.

    *****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Stori za mimi kumfukuza Jackline zilisambaa na kila mtu alinichukia. Hakuna aliyenisema kwa mazuri. "Ivi kumbe Rose ana roho ya ukatili kiasi kile" hakuna aliyenipenda tena na jamii ilinisimanga kwa kila namna. Mimi kupata taarifa hizo sikujali wala kuogopa. Chuki yangu na ndugu zangu ndo ilizidi mara dufu.

    Jackline aliumizwa sana na kitendo kile ila hakuwahi kuniwazia mabaya. Kila mara alikuwa akikaa na familia yake hakuacha kusisitiza kuwa hana kinyongo na mimi. Maneno yale ya Jackline ya kila siku yalimfanya hata Mary kutoa kinyongo na kukiri kunisamehe na hana mpango wa kulipiza kisasi. " nilazima nifanye jitihada za kurudisha undugu Kati yangu na Rose" Jackline alisema "ni kweli kwani ugomvi hauna maana" Mary alidakia "Rose! Rose!" Ghafla gabriel alisema. "Hili jina si geni kwangu " wote kusikia vile walianza kushtuka wakijua kumbukumbu zinaanza kurudi. Aliposema tu vile alisimama na kuanza kupiga hatua moja hadi nyingine taratibu "kuna kitu anakumbuka" Mary alisema ivo wote wakawa kimya ikawa kuna kitu anakumbuka na akitaka kukisema ghafla anasahau."ivi jackline si anatakiwa kuwekewa damu" Hali ile ilimsumbua kama dakika nyingi. " Rose, Anthony...aahhh shiiit" akitaka kusema jambo analisahau. Aliamua kuingia chumbani kwake na kuanza kupekua vitu. Jackline alipomfuata alikuta vitu vimepanguliwa hiki like hiki hapa. "Unatafuta nini" Jackline aliuliza ila Gabriel hakusema kitu ghafla alianza kushika kichwa na kujikunyata kana kwamba kuna kitu chakutisha amekiona. Bila kutarajia alijikuta akipiga kelele kubwa sana. "Nooooooo gari hilo linakujaaaaaaa" alijikuta akijitupa upande mwingine na kudondoka chini. Alibaki ameduwaa bila ya kuongea na mtu yeyote. Walimpigia simu daktari wao na muda mfupi aliwasili. "Msijali nadhani kumbukumbu zimeanza kurudi." Alisema na kuanza kumsemesha taratibu. Alimhoji maswali mengi sana, aliyajibu vizuri na kuyaelezea kwa undani. "Asante Mungu umepona" wote walifurahi na kushukuru sana. "Mke wangu Rose yuko wapi" Gabriel aliuliza. "Na mbona tunaishi hapa" hakuna aliyeweza kuyajibu maswali yale kwa muda ule. Alipozidi kuhoji Mary alianza kumwelezea yote. Alipomweleza kila kitu Gabriel alikaa kimya hakusema kitu wala hakuonesha ishara yoyote zaidi aliamua kuingia ndani hatimae alijifungia ndani.....





    Kumbukumbu za Gabriel zilianza kurudi kwa kasi sana tena kikubwa alichokuwa anakumbuka ni jinsi mimi na yeye tulivyoishi. Alikumbuka jinsi ambavyo alipanga kunioa ila hakukumbuka kilichomfanya asinioe. Lakini pia alikumbuka kuwa alitembea na Jackline na muda mfupi Jackline akadai mjamzito. Maswali mengi alikuwa akijiuliza ila hayakuwa na jibu. "Kwanini naishi na Jackline na si Rose" aliwaza bila ya kupata jibu. Muda huo wote alikuwa chumbani kajifungia. Jackline na wenzie waliogopa wakihofia anaweza kufanya kitu kibaya baada ya kuelezwa yale. Walimsihi sana afungue mlango ila alizidi kuwa mkimya "nitafungua kwa muda wangu" bila kutegemea aliwajibu kwa mkato tofauti na walivotegemea. Waliamua kukaa kimya bila ya kumsumbua na hata ilipowadia usiku bado hakufungua mlango wala kutaka kula chakula cha usiku. Kiukwel hofu kubwa iliwavaa na kukosa kujua kipi wafanye. "Anyway ebu tumuache kwanza maana huenda akili yake ina mambo mengi ya kukumbuka" Mary alisema na wote walimuacha na kuelekea kulala.

    Jackline hakupata usingizi kabisa tena aliingiwa na hofu sana juu ya kipenzi chake Gabriel. Nae alianza kuwa mnyonge kwani alijua wazi Gabriel ananipenda na hayuko tayari kuamini kama mimi ni mbaya na ukizingatia kabla ya ajali nilijifanya kujirudi na kuwa mtu mwema. Moyo wa Jackline ulikuwa ukikosa mwelekeo kwani mapigo ya moyo yalikuwa yakibadilika kila mara. Alijikuta akitoa machozi ya woga na mashaka sababu alijua hana tena chake. "Mdogo wangu ebu kalale unawaza nini" Mary alimfuata sebuleni na kumbembeleza " najua mwisho wa furaha yangu umewadia hasa pale Gabriel akikutana na Rose" alisema "nakiri kumpenda sana Gabriel ila siku atakayoniacha itakuwa fedheha sana kwangu na majuto makubwa" alizidi kueleza hisia zake "Rose ni bingwa wa kushawishi na ivi hana kumbukumbu vizuri sijui itakuaje" kila akijikaza asilie basi ndo machozi yalibubujika kama mvua ama mto utiririshao maji kuelekea baharini. " kila mara nakufundisha kuishi kulingana na unayoyapitia" Mary alimsogelea akamshika mkono na kumtuliza. "Hata Mungu anaujua ukweli wako hivyo hawezi kukuaibisha" alisema " huenda Gabriel si chaguo lako atakuja aliyewako ivo usilie mdogo wangu" alimbembeleza sana "Mungu alikubariki tangu awali ivyo ataendelea kukubariki" alimshika na kumsogeza kifuani kwake na kumbembeleza hatimae walienda kulala.

    *****

    Sikuamini kama kweli sina mguu, sikutaka kuamini kama moja ya kitega uchumi changu kimeteketea ambacho kilikuwa kinaniingizia utajiri kwa 40% wakati nasikilizia maumivu ya mguu pia maumivu ya jengo langu lile. "Kwanini mama yangu hunitokea mara kwa mara" nilijiuliza ila sikupata jibu. Niliishia kiguna tu. Kutokana na uwezo wa kuficha maumivu yangu , kila aliyeniona aliamini niko sawa ila asikwambie mtu nilikuwa mtu niliyejaa hofu, mashaka, woga, ukiwa na hata kutokujiamini. Moyo wangu haukutulia kabisa wala akili yangu ila nilijilazimisha kabisa kuhakikisha hakuna mtu anaetambua yanisibuyo. Nikiwa pale kitandani bado sijaruhusiwa kutoka ghafla bin vuu! Namwona Gabriel akifungua mlango wa chumba changu na kuingia. Macho yalinitoka, moyo ulipasuka paaa! Mapigo ya moyo yakawa yakienda kasi dudududu! Mwili uliloa jasho kisha moyoni nilijisemea "leo nimepatikana lazima anajua kila kitu" nilijikaza na kumtazama tu anavyoingia " habari mke wangu " kusikia vile ndo mashaka yalizidi "atawezaje kuniita mke wake wakati kuna mabaya mengi nimemfanyia" niliwaza "nzuri Gabriel mzima wewe" niliitikia hali sijiamini. Aliketi na kunitazama tu machoni. Sikuweza kuwa jasiri kwa kweli ila nilijikaza. "Pole sana kwa matatizo siamini kama huna mguu" alisema hayo jambo lililonishtua na kuhisi hajui kitu. Pale pale nilitengeneza machozi "tangu upate ajali nimekuwa mtu wa matatizo tu, kila mtu ananisema vibaya kibaya zaidi umeamua kunisaliti na kutembea na Jackline siamini kabisa" nililia japo moyoni nilikuwa nikitafakari ule usemi wa "KUKU WA KWAKO MANATI YA NINI" Gabriel kusikia vile alikuwa mpole sana "nisamehe mke wangu nimepitiwa tu nisamehe wewe ndo mke wangu halali" weeee mmhh! Kusikia vile nilitabasamu nikajua kazi iliyobaki ni ndogo sana. Nilizidi kuonesha msimamo ili na yeye azidi kujishusha nikafanikiwa. Gabriel alijieleza sana "wananiambia ulikataa kuja kunisalimia pia ulitaka kuniua" aliposema vile niliia sana "tumeishi wote miaka mingi pia umenisaidia mambo mengi iweje leo nitake kukuua" nilijitetea kwa Gabriel acha kabisa hatimae aliingia kati na kukubali ya kwangu. Yote aliyokuwa akiyaamini kwa kuambiwa niliyabadili na kugeuza kuwa Jackline ndo alikusudia hayo. Pale pale Gabriel alibadilisha mwelekeo na kumchukia Jackline mwanamke aliyemsaidia na kumwokoa kwenye hatari nyingi. Bila kujiuliza mara mbili Gabriel alimkana hadi mwanae kisa mimi na akidai hakuwahi kumpa mimba Jackline ila kweli alitembea nae. Kusikia vile nilitabasamu sana na kuamini nimeshinda. Aliniahidi hatorudi kwa Jackline atarudi nyumbani kuishi kama tulivyoishi tangu zamani.

    Jackline alipopata habari ile alipata mshtuko kiasi cha kutaka kufa. "Gabriel hana kosa ila Rose" alisema huku akilia hapo inapata siku kama tano Gabriel hajarudi nyumbani. Katika siku ambazo Jackline alilia kwa uchungu ni siku iyo. "Eeh Mungu naomba ukawe hakimu katika hili tena na usichelewe kuhukumu maana wanao tunatamani kuona haki ikitendeka" siku hiyo hadi Mary aligundua wazi maumivu ya Jackline.waliamua kumuachia Mungu yote. "Nakuja saivi kuna mtu nataka kwenda kumuona" Mary aliondoka pale ofisini na kuelekea kule aliko Victor ambae alikwisha kupona. Mary alimweleza kila kitu. "Mmhh Gabriel katekwa akili si bure" Victor alijikuta akicheka kwakuwa si kawaida ya mwanaume kushindwa kujua nani ni nani. "Rose nimeishi nae na ninajua mambo yake mengi ivyo kumwangamiza ni jambo rahisi sana" Victor alisema hayo na aliongea akijiamini sana. "Unajua Rose asijifanye mjanja wakati me nimemzidi ujanja" alizidi kusema "kuna mkataba nilimshawishi ausaini na aliukubali bila ya kujua ni kampuni yangu ye alidhani ya mtu mwingine ila ni kampuni yangu halali" Victor aliposema vile Mary alikodoa macho sana. "Lakini katika mkataba ule

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kuna vipengele ambavyo sikumwonesha yeye na hajui kama vipo kwakuwa aliniamini alisaini tu bila ya kusoma" alizidi kusema "moja ya kipengele ni kwamba yeyote atakayetaka kujiondoa halipwi faida yoyote wala riba wala chochote kile atajiondoa kama yeye binafsi." Alisistiza "lakini pia kampuni ikifilisika hakuna kudaiana chochote" Victor alisema vipo vipengele vingi sana ambavyo vinanibana mimi. "Na mpaka sasa tuko katika mchakato wa kumtoa kwenye mkataba japo yeye aliwekeza pesa nyingi sana" alizidi kumpa habari Mary aliyeduwaa. " ivi unajua Rose anahusika na madawa ya kulevya?" Alimweleza Mary "Na amewekeza pesa nyingi sana na wale vijana ambao wako nae ndo anaowatumia japo kama wawili ni marafiki zangu" alidokeza. "Rose anawasumbua akili nyie msiye mjua ila si mimi na ndo maana alikimbilia kuniua sababu anajua wazi sina mchezo na nimemzidi akili" aliposema vile alibadilisha mada na kumgeukia Mary "unajua sikutegemea kama kweli ungeweza kuniokoa pamoja na kipigo kile ila leo umekuwa msaada wangu" Victor alisema "nisamehe mke wangu na nakuahidi kukupenda milele" alimbusu na kumsogezakaribu yake huku akimpa mabusu moto moto. Walisahau kama wako kwenye lijengo chakavu basi walijikuta wakisasambua nguo moja moja hatimae kama walivozaliwa mwisho walikumbushana jinsi walivyokuwa wakiburudisha kwa mapenzi moto moto. Mary alijikuta akipokea penzi lile kwa hamu kubwa sababu tangu waachane na Victor hakuwahi kujihusisha na mapenzi tena..."mbona leo nimejisikia tofauti sana" Mary alisema "hata mimi na nahisi kuna kitakachotokea" Victor alisema huku akimbusu maungo yake. Alivaa nguo zake na kujiweka sawa kisha alitaka kuondoka "hata mimi jioni nitaondoka mahali hapa na kuhamia nyumbani kwangu" Victor alisema ndipo walipoagana Mary akaelekea nyumbani



    MWISHO





0 comments:

Post a Comment

Blog