Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

CHOKORAA - 2

 





    Simulizi : Chokoraa

    Sehemu Ya Pili (2)



    SIKU hii ya jumapili Frida alikuja pekee kufua nguo. Isha alibakia katika makazi yao waliyokuwa wamepanga na



    kulipia shilingi elfu tano kila mwezi. Haikuwa nyumba bali kibanda tu ambacho wangeweza kujilaza walau kwa amani



    kiasi fulani.

    Kibanda hiki walipewa kwa minajiri ya kuwa walinzi wa nyumba kubwa iliyokuwa inajengwa isiweze kuingiliwa na



    watoto na watu wazima wasiojiheshimu na kuibadili matumizi kuwa choo.

    Licha ya ulinzi huu lakini bado walimlipa mwenye nyumba kiasi hicho cha pesa. Unyanyasaji!

    Isha alikuwa anasumbuliwa na matatizo yanayowakabili wanawake kila mwezi na tumbo lilikuwa linamuuma sana



    hivyo hakuweza kwenda katika majukumu hayo. Frida akaenda.



    Siku hii yule bwana waliyezoea kumfulia nguo alikuwa ametembelewa na rafiki yake wa kike hivyo aliyatimiza



    majukumu yote ya kumfulia na shughuli nyingine za usafi.

    Riziki ya akina Isha na Frida ikawa imezibwa.

    “Kaka, samahani..hakuna rafiki yako ambaye naweza kumfulia hata kwa nusu bei. Rafiki yangu anaumwa. Anahitaji



    dawa.” Frida alimueleza yule kijana. Ambaye alimtazama huku akijikuna tumbo lake kubwa lenye vinyweleo vingi.

    Njoo huku! Alimuita.

    Akaenda hadi mlango wa tatu kutoka chumba chake. Akabisha hodi akafunguliwa. Akanong’ona jambo na yule bwana.



    Kisha wakageuka kumtazama yule binti. Macho ya yule bwana yakagongana na yule binti. Yakaganda kwa muda, binti



    akawahi kuinama chini.

    Bwana mnene akaondoka, huku akimfanyia yule binti ishara kuwa sasa anaweza kuzungumza na yule kijana mrefu.

    “Za saa hizi” alisalimia akajibiwa. Kisha akajieleza

    “Nilikuwa nimemwambia yule kaka kuwa kama una nguo nikufulie hata kwa nusu bei..nipate pesa kidogo, rafiki



    yangu anaumwa.”

    “Usijali amenieleza kila kitu. Sawa eeh!”

    “Bei zenu ni shilingi ngapi?” aliulizwa akazitaja bei kwa mpangilio maalumu kama alivyofunzwa na Isha.

    Yule bwana akaingia ndani mwake. Akarejea na shati mbili ambazo hazikuwa na uchafu wowote na suruali moja.



    Nguo hizi kwa nusu bei zilikuwa zinagharimu shilingi mia tatu. Hii haitoshi hata kununulia pedi.

    Frida akafua kwa moyo mkunjufu akazianika.

    Akarejesha ndoo na sabuni iliyobakia.

    Safari hii hakuishia nje. Alikaribishwa mpaka ndani.

    Akaingia akiwa na uoga. Nguo zake zilikuwa na hali fulani ya uchafu kutokana na kuvaliwa mara kwa mara.

    “Naitwa George, nawe waitwa nani?”

    “Frida Ge..” hakumalizia jina lake.

    “Naitwa Frida.” Alirudia. Macho yake yalikuwa yamepepesa hapa na pale na kutambua vitu vingi vya thamani katika



    kasri ile ndogo.

    “Yule ni mama yangu!! Marehemu lakini” George alieleza huku akimwonyesha Frida picha kubwa ukutani ya



    mwanamke akiwa anatabasamu.

    Frida akataka kutoa pole lakini George akaendelea na mazungumzo ya hapa na pale. Kisha akamkabidhi Frida noti ya



    shilingi elfu kumi. Wakaagana.

    “Uwe unakuja kunifulia.” George alimwambia Frida. Frida akamtoa wasiwasi.

    Siku ikapendeza. Noti ya shilingi elfu kumi kwa nguo tatu. Bahati iliyoje.

    Fridah akanunua mahitaji ya msingi. Akarejea nyumbani akiwa na furaha tele. Isha ambaye hali ilikuwa kidogo inatia



    matumaini alimpokea Frida akiwa na jiko la mkaa.

    Ukawa mwisho wa kuumia na moto wa kuni!

    Isha alishangazwa na ukarimu wa yule bwana!! Kila mmoja kwa imani yake akamshukuru Mungu.



    *****



    SIKU nne zilipita. Isha akarejea katika hali ya kawaida. Lile jiko wakalitumia kujiingizia kipato. Kwa mtindo wa



    kuazima azima vifaa hatimaye wakaanzisha biashara ya kukaanga mihogo na kuuza majira ya asubuhi na jioni.

    Maisha yao walau yakabadilika kwa kiasi fulani. Japo waliendelea kuishi katika kijumba kile lakini uhakika wa kula



    ulikuwepo asubuhi na usiku.

    Mihogo haikuwa na faida sana lakini walau ule utembezi wa kutafuta makopo tupu ya plastiki kwa ajili ya kuuza



    ukakoma.

    Si kila mwanadamu anaridhika akiona mwenzake anapiga hatua ya kimaendeleo. Licha ya yatima hawa kujibunia



    mbinu hii ya kujiingizia kipato. Wapo binadamu wenye roho za unyama hawakujiweka mbali.

    Usiku wa saa tatu. Mlango wa kuegesha ulisukumwa ukaachia. Wanaume watatu wakavamia ndani. Mmoja akamziba



    mdomo Frida na mwingine akamziba Isha. Yule mwingine akaanza kupekua hadi akaipata akiba yao ya shilingi elfu



    thelathini. Akabeba na jiko lao. Akatoka nje. Wale wengine wakakosa kingine cha kuchukua. Wakabahatika kupata



    mihogo ya kukaanga iliyosalia jioni hiyo. Wakaitwaa.

    Huruma ipo wapi!!

    Msichana msichana tu! Wawili hawa hawakuweza kupiga kelele. Kila mmoja alikuwa anatetemeka. Isha alikuwa



    amejikojolea tayari. Frida alikuwa anatokwa machozi.

    Roho ziliwauma. Pesa ya jasho lao ilikuwa imebebwa na vibaka. Wakamlilia Mungu kwa lawama zote.

    “Mungu upo wapi? Mbona watuacha yatima tunanyanyasika, kwani tulipenda kuachwa na wazazi Mungu, kwani



    tulipenda kuzaliwa sisi Mungu, kwanini adhabu za wazazi wetu waziacha ziishi nasi. Mbona dunia imetutenga nawe



    hautupiganii!! Ni kosa gani tulifanya katika matumbo ya mama zetu baba!! Zitwae roho zetu sasa kama hatuhitajiki



    dunianai na kama ulituumba ili tuteseke baba nasema imetosha baba tumekuwa funzo kwa wengine imetosha baba



    zitwae hizi roho sasa” Frida alikuwa analaani. Alikuwa analia kwa uchungu. Isha akasimama akamkumbatia huku na



    yeye akilia sana.

    Vilio vya watu wawili vikageuka kuwa vya watu watatu lakini huyu mmoja hakutoa sauti kabisa japo machozi



    yalikuwa yanamtiririka.



    ****



    GEORGE EMMANUEL, hakuridhika na mazungumzo aliyoyafanya na Frida siku yao ya kwanza kukutana. Japo



    walizungumza kwa ufupi lakini maisha ya Frida yalimgusa kwa namna ya kipekee. Hayakumtesa kwa namna ya



    ulimwengu wa huruma tu! Bali alitambua kuwa lile jicho la Frida lilipomtazama liliutetemesha moyo wake.

    Akatambua kuwa kuna kitu alihitaji kukijua zaidi.

    Walipoagana na Frida. Alifanya kitendo cha upesi cha kubadilisha njia ya kupita. Lakini lengo likiwa kuelekea kule



    anapoelekea Frida.

    Wakajikuta wapo ndani ya Pantoni pamoja. Bila Frida kujua lolote.

    Waliongozana tena hadi katika daladala. Bado Frida hakujua lolote.

    Kituo cha Davis Corner Tandika alichoshuka Frida na George naye akatelemka. Frida akaanza kwenda kwa miguu.



    George naye akiwa mamini kabisa na miwani yake usoni aliendelea kumfuatilia Frida. Ulikuwa umbali mrefu lakini



    hakuchoka. Frida alipoingia dukani yeye alijiweka mita kadhaa mbali naye.

    Hatimaye wakafika katika jumba ambalo halijakamilika maeneo ya Abiola. Hapa akatokea dada mmoja kuja kumpokea



    Frida. Chumba walichoingia kikakaririwa na George. Kisha akatoweka huku akijuta kumpatia Frida shilingi elfu



    kumi. Kwani haikukidhi kabisa haja yake.



    Aliondoka pale akidhani atangoja mpaka mwisho wa juma Frida atakapokuja kumfulia nguo. Lakini alipofika



    nyumbani kwake tu akagundua kuwa alikuwa anatamani kumuona ama kumsikia Frida mara kwa mara.

    Alitamani kumsikia kwa sababu aliamini kuwa atajifunza mengi ambayo yatamsaidia katika fani yake ya uandishi wa



    simulizi. Hasahasa simulizi za maisha halisi ya mwanadamu wa daraja la chini.

    “Lakini mbona nimekutana na wengi sana na sikujali kama nionavyomjali huyu?” George alijiuliza. Hakupata jawabu.

    Siku ya pili aliendesha gari yake tofauti na awali alivyokuja kwa miguu. Akaiegesha mbali na kujipitisha jirani na ile



    nyumba aliyomuona Frida akiingia. Akawamkuta Frida akiwa amejikita katika kuuza mihogo. George akashangaa



    sana. Hakutegemea.

    Ile hali ya kutaka kumjua zaidi Frida ikaongezeka.

    Muda wa kufunga gege ulikuwa ni saa mbili usiku.

    Baada ya siku kadhaa George aliwasili pale usiku zaidi.

    Kama kawaida aliiegesha gari yake mbali na ile nyumba.

    Akajongea kwa mguu. Kundi la watu watatu likampita. Akalipuuzia lakini kisha akalitilia maanani baada ya kuwaona



    wakifanya mnyato kuelekea nyumbani kwa akina Frida.

    George akajiweka katika kigiza na kutulia tuli huku nguo zake nyeusi zikimfanya asionekane.

    Alishuhudia kila kitu kilichotokea. Sasa alikuwa jirani kabisa na nyumba ile. Kilio cha Frida kilichoambatana na



    maneno ya kumlaumu muumba mbingu na nchi yakamgusa. Funda kubwa likajifinyanga kooni. Alipojaribu kulilegeza



    halikulegea. Alipomeza mate akawa ameyaruhusu machozi kumtoka.

    Watu watatu wakawa katika kilio kikuu!!!

    Akiwa amejisahau kuwa hakuwa amefanya ugeni rasmi.

    Mara kimya kikatanda. Kisha likatokea jambo la ajabu asilolitegemea.

    Jambo lililoifanya siku hii ibaki kuwa ya kukumbukwa.



    *****



    Frida alikuwa amejuta sana na kugundua kuwa majuto yake hayana maana kwani anayemlaumu hatoi majibu kama



    wanadamu tunavyotaka. Yeye ni Mungu aliye karibu wala si Mungu aliye mbali.

    Frida alibakia kuwa katika kilio cha kwikwi akisaidiana na Isha. Macho yake yaliyokuwa yamevikwa ukungu yaliweza



    kuona kwa mbali mfano wa kivuli kikitikisika. Akatulia tuli akiwa bado amekumbatiana na Isha. Hakuweza kuyasikia



    maneno ya ziada ambayo Isha alikuwa anamueleza. Akili yake ikamtuma mbali sana. Hasira ikampanda na ule



    uwazimu wa kimbwamwitu aliourithi bila kujua kutoka kwa mama yake mzazi ukampanda. Hakutaka kuwaza zaidi.



    Harufu ya kifo ikamtawala.

    Bora nife! Akawaza! Akamsukuma Isha kisha akafanya tukio la ghafla akapiga hatua mbili kubwa akatoka nje.

    Kelele alizozitoa zilitosha kumwamsha mtoto mchanga aliyelala fofofo na hata mlevi wa gongo lazima ashtuke.

    Mwiziiiii!!1 Mwiziii!! Alipiga kelele. Hakika alikuwa sahihi kile kivuli kilikuwa ni mtu na sasa kikaanza kukimbia!!

    Kosa kubwa! Kivuli kile hakikujua kama Frida amepandwa na mashetani makali sana yaliyochoka kunyanyaswa!!

    Zile kelele sasa zikawa maradufu! Isha ambaye hakujua lolote linaloendelea na yeye aliunga mkono mbio hizi



    zisizokuwa na umbali maalumu dhidi ya mwizi huyo.

    Bahati ilikuwa mbaya kwa yule mwizi! Siku hiyo palikuwa na mechi ya mpira wa miguu. Na sasa ilikuwa imemalizika



    na masgabiki wanarejea katika familia zao. Walioshinda wakiwa wanashangilia sana huku wale wanyonge timu zao



    zikiwa zimefungwa.

    Hawa wanyonge walikuwa wa kwanza kumuona mwizi yule!! Hasira ya kufungwa ikahamia kwa mwizi huyu.

    Mara alikuwa ardhini akihangaika kujibizana na sauti za watu wengi. Kila mmoja akisema la kwake.

    Frida alifika katika kundi lile huku roho ya kuua ikiwa imemuandama. Hasira kali zikiwa zimemjaa kichwani.

    Pishaaaaa!!! Sauti kali ya kike ilisikika kutokea nyuma. Wadau wa kumpiga mwizi walipogeuka walikumbana na



    mwanamke akiwa kasi na jiwe kubwa mkononi. Wakampisha afanye alilokusudia. Huku kimya cha ghafla kikitanda!



    Ulikuwa mshtuko hakuna aliyeweza kudhania mwanamke anaweza kuwa jasiri kiasi kile.

    Mwizi yule alinyanyua mkono wake akijaribu kumsihi yule anayekuja na jiwe. Alijaribu kupaza sauti lakini sauti



    haikutoka.

    “Friiiidaa!!” jiwe lililotua katika mguu wake wa kuume lililainisha koo. Akatoa sauti kuu ya mwisho!!

    Kisha kimya kikatanda. Damu ikichuruzika kwa fujo.

    Frida na Isha walishangazwa na hali hii. Ni nani yule aliyemtambua Frida kwa jina.

    Kundi moja baada ya jingine lilianza kutoweka eneo la tukio baada ya mwizi kunyooka na kukaa kimya. Kila mmoja



    akatambua kuwa ni maiti.

    Hatimaye akabaki Frida, Isha na wanaume wawili.

    Frida akainama ili kumtambua yule mwizi. Japo alikuwa ameumuka usoni lakini kuna kitu alikiona. Mwanya!

    Ule mwanya ukamrudisha nyuma siku kadhaa. Akatazama vyema zaidi. Akamtambua kuwa huyu mwizi alikuwa ni



    George Emmanuel wa kigamboni!!

    Maajabu!!

    Frida alimueleza Isha kwa ufupi!! Wote wakataharuki.

    Watafanya nini? Hilo likawa swali.

    Usiku ulikuwa umeenda.

    Ukarimu wa George na tukio hili la wizi wa shilingi elfu thelathini havikuendana hata kidogo. Alikuja kufanya nini



    sasa?

    Swali jingine!!



    Frida akafanya maamuzi, akaingiza mikono katika nguo za mwili huu unaopumua kwa shida.

    Pesa nyingi zikajaza mikono ya Frida. Zilikuwa ni mara kumi ya ile pesa iliyoibiwa. Hapana huyu sio mwizi!!



    Isha akakimbia na kutafuta teksi.

    Safari ya kuelekea hospitali ya Temeke.



    *******



    Majira ya saa nane usiku baada ya kuongezewa maji ya ‘insuline’ chupa mbili. Fahamu zikarejea katika mwili wa



    George. Frida na Isha walikuwa pembeni yake. Jicho lake likakutana tena na jicho la Frida. Akatabasamu! Frida naye



    akajibu tabasamu lile.

    Huu ukawa mwanzo wa rejeo la tumaini lililokaribia kupotea!

    Mguu ulifungwa bandeji ngumu (P.O.P), bahati nzuri haukuwa umevunjika. Frida aitumia pesa ya George kwa ajili ya



    matibabu!

    Iliyosalia alimkabidhi! George hakusema neno bado alitabasamu.



    Siku hiyo wawili hawa walikesha na mgonjwa hadi asubuhi.



    “Gari yangu ipo salama kweli.” George alimuuliza Frida. Frida hakuwa na la kujibu maana hakujua lolote kuhusu gari



    ya George.

    George aliwapa maelekezo kadhaa juu ya wapi aliiegesha gari hiyo.

    Maelekezo sahihi kabisa yakawafikisha wawili hawa eneo lilipoegeshwa gari lile. George alikuwa amewaomba



    wamchukulie pia simu mbili alizozihifadhi garini. Wakafanya hivyo!

    Wakarejea hospitali. George bado alikuwa kitandani. Alipokea zile simu na kupiga simu mbili tatu. Alizungumza kwa



    lugha ya kigeni hakuna aliyemuelewa aidha nesi, ama machokoraa hawa. Kilichoonekana ni kuwa mazungumzo hayo



    yalikuwa na mvutano kiasi fulani.



    Siku hiyo aliwapatia kiasi fulani cha pesa huku akiwashukuru sana kwa kuuokoa uhai wake. Alikiri kuwa bila Frida



    huenda angekuwa mfu tayari. Walijikuta wote wakitokwa machozi.



    Siku iliyofuata walipofika hospitali hapo. George hakuwepo tena.

    Manesi hawakuwa na majibu iwapo ameruhusiwa ama la! Madaktari nao hawakutoa maelekezo kwa Frida na Isha.



    Ng’ombe wa masikini hazai. Wahenga walisema! Wakati Frida wakiwa katika maswali mengi juu ya kutoweka ghafla



    kwa George, likazuka jingine.

    Walikuwa njiani kuelekea nyumbani. Siku hii walipanda daladala mara mbili. Yaani kutoka Temeke na pia kuelekea



    Abiola.

    Isha alitangaza hisia zake juu ya kifo cha George, Frida hakukubaliana naye japo pia hakuwa na jibu sahihi ni kipi



    kimemsibu kijana huyu ambaye hawajui nivipi alipajua nyumbani kwao na hatimaye kukumbwa na maswaibu ya



    kupigiwa kelele za mwizi na mwisho kuvunjwa mguu.

    “Jumapili twende kule wanapoishi lazima rafiki zake watakuwa wanajua alipo….” Frida alitoa wazo. Isha akaliunga



    mkono lakini akiongezea na maneno yake mengine ya kujishangaa kwa nini wamfuatilie George iwapo hakuna



    analowahusu.

    Wakati Frida anataka kujibu. Akaona kitu! Kitu kama mkeka. Mkeka wenye rangi mithiri ya ule ambao wawili hawa



    walikuwa wameununua katika siku chache nyuma kwa ajili ya kulalia.

    Mkeka huu ulikuwa juani na juu yake kulikuwa na kisufuria kidogo, vikombe viwili, ndoo ndogo ya maji na sahani



    kadhaa zikiwa zimechanganyika na vibakuli.

    Kabla hajamshirikisha Isha naye aliona tukio hilo. Wawili hawa wakaongeza mwendokasi, kisha wakaupunguza baada



    ya kumuona baba mwenye jengo. Alikuwa amevaa msuli na alikuwa anapiga mluzi usiokuwa rasmi.

    Wakamfikia na kumsalimia. Hakujibu!! Akawatazama kuanzia juu mpaka chini.

    “Chukueni virago vyenu na huo umalaya mkaufanyie mlipokuwa mnaufanyia awali.” Alizungumza kwa sauti nzito.

    Hakuongea tena. Alimaanisha anachosema.

    Nguvu zikawaishia. Wakauliza hawakujibiwa. Safari hii hawakulia. Huenda waliamini kuwa wameumbwa kwa ajili ya



    kuja kuteseka duniani.

    Mchana kweupe wakavitwaa virago vyao. Wakatoweka kimya kimya. Mahali ilipokuwa gari iliyosadikika kuwa ni ya



    George hapakuwa na kitu tena!



    Wakarejea mtaani!



    ******



    Moshi wa sigara ulipepea juu kwa fujo. Kikohozi kikasikia kikitokea eneo lile. Mvutaji hakuwa mzoefu!

    Mara likapita kundi la wanaume wawili. Mmoja akajongea hadi eneo lile. Baada ya dakika kadhaa akajongea eneo la



    siri na msichana ambaye alionekana kuwa muoga sana.

    Licha ya kupiga kelele za maumivu lakini kilichotakiwa kilifanyika.

    Huyu alikuwa ni mteja wa kwanza.

    Biashara ikazidi kukolea alipofika tena mteja wa pili na wa tatu. Msichana mdogo akahisi kuchoka lakini yule mpokea



    pesa alimbembeleza kuwa asichoke!

    Yalikuwa ni maeneo ya Buguruni jijini Dar es salaam. Majira ya usiku eneo ambalo wasichana huuza miili yao.

    Huenda hawa wengine kwa hiari yao wenyewe walifika eneo lile. Lakini huyu mmoja alikuwa analazimishwa na



    ilikuwa siku ya nne.

    Alilazimika kukubaliana na hali kutokana na makubaliano baina yake na yule mama. Makubaliano ambayo sasa



    yalikuwa yanamtesa.

    Hakuwa na wa kumtetea kwa sababu alikuwa yatima. Tena chokoraa mzoefu!

    Pesa aliyoingiza ilitumika kumnunulia nguo zinazomuacha uchi mwili wake, nguo maalumu kwa ajili ya biashara ya



    kujiuza.



    “Unaitwa nani mpenzi!” mwanaume ambaye kwa umri alikuwa analingana kabisa na mzazi asiyejulikana wa mtoto



    huyu alimuita kimapenzi wakiwa garini. Huyu alikuwa amelipia huduma ya kulala na mtoto huyu hadi asubuhi popote



    atakapo na vyovyote awezavyo ilimradi amelipia itakiwavyo.

    Yule msichana hakujibu!! Alikuwa katika majonzi!

    Mwanaume asiyekuwa na aibu akanyoosha mkono usiokuwa na nidhamu akamminya chuchu. Mapigo ya moyo



    yakaenda kasi kwa hasira.



    Hatimaye gari ikapaki katika hoteli ya kifahari!

    Chumba kilikuwa kimelipiwa tayari. Mtoto na baba yake wakaingia chumbani kama mtu na mpenzi wake.

    Walianzia kuoga. Hapa binti alivumilia japo hakupendezwa na biashara hii isiyomfaidisha yeye.

    Walipotoka kuoga chakula kilichoagizwa kwa njia ya simu kilikuwa tayari pia. Wakaanza kula huku yule mwanaume



    mwenye tumbo kubwa akijaribu kutabasamu kila mara.

    Ukafika wakati wa kuzima taa. Giza likaambatana na mambo ya giza. Mwanaume akaanza kumpapasa mtoto. Mara



    amfinye huku mara kule. Chokoraa akawa ametulia tuli. Hakuwa na jinsi.

    Akafikia hatua aliyotaka akatimiza haja zake mara nyingi awezavyo. Binti akavumilia adhabu hii.

    Kilichotokea baada ya hapa ndio kilibadili hali ya hewa na historia ya huyu binti.

    Yule mwanaume akaanza kumlazimisha kufanya jambo ambalo yule binti kwa elimu yake ndogo alikuwa anafahamu



    madhara yake. Yule mwanaume asiyekuwa na staha wala huruma sasa alikuwa akimtaka mapenzi kinyume na



    maumbile.

    Haikuwa ombi bali lazima.

    Hapa zikaibuka zile kumbukumbu zote chafu tena za kuumiza za vituko wanavyofanyiwa chokoraa. Kila chokoraa ni



    chokoraa. Analotendwa chokoraa huyu basi na kwa mwenzake linaleta uchungu.

    Mimba za kubakwa, vifo kwa sababu ya njaa, matusi kutoka kwa watoto wenye wazazi, ulawiti kwa watoto wa kiume.



    Aliyakumbuka hayo yote kisha akamkumbuka rafiki yake wa muda mfupi lakini uliojaa mengi mtaani.

    Frida!

    Alipokumbuka jina hilo, akashambuliwa na hisia kuwa huenda Frida alikufa kwa mateso kama haya anayotaka kupewa



    yeye.

    Akapingana na roho ya mauti, akajisikia ujasiri.

    “Sifi kabla ya kukulipia kisasi Frida. Popote ulipo wewe na machokoraa wengine na damu hii iwe juu yangu kwa



    kuwatetea ninyi!” alijisemea kimoyomoyo huku akijaribu kupambana na yule bwana aliyekuwa anakaribia kufanikisha



    uovu ule kwa nguvu!

    Nguvu za ajabu zikauvaa mwili wake. Udhaifu ukaondoka bila kuaga, akazikumbuka mishemishe zote za kufukuzana



    na polisi mitaani, kupigana na machokoraa wakorofi. Akajisikia ni shujaa wa kike na anatakiwa kuthibitisha ushujaa



    wake.

    Hakuwa tayari kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

    Kama risasi akajichomoa mikononi mwa yule mwanaume. Aliposhuka kitandani akaikanyaga sahani waliyotumia kulia



    chakula.

    Ule mlio wa kisu na uma ukawa kama umemuita. Akarejea akainama akaokota vyote viwili. Kisu upande wa kulia na



    uma upande wa kushoto.

    Maumivu aliyoyapata huyu bwana pendapenda. Ni heri angeuwawa kwa risasi. Hayasimuliki.

    Mwanadada huyu chokoraa aliyegeuzwa kitega uchumi alichoma popote alipoweza. Palikuwa na giza. Aliporidhika



    akachukua nguo zake akavaa. Bila akajifuta mikono yake. Kisha akawasha taa. Hakutaka kuona kiumbe



    kinachokoroma kitandani.

    Akahakikisha hana damu mikononi. Akaufungua mlango. Kama vile mzuka akatoka nje akimpita mlinzi kama kivuli.

    Pale nje akawakuta chokoraa wawili wakiwa wamelalia mkeka. Alitamani kuwasogelea ili ajue kama ni wa kike ama



    kiume lakini akahofia kushtukiwa alichofanya ndani.

    “Nimefanya kwa ajili yenu!” alisema kwa sauti ya chini.

    “Ewe mzazi wa Mwanaidi, mwanao nimefanya jaribio la kujiokoa sijui kama nimeua!” alizungumza akizitazama



    mbingu.

    Laiti kama Mwanaidi angepata ujasiri wa kuwajulia hali chokoraa wale. Angekutana na rafiki yake mpenzi. Frida!!



    Lakini hakufanya hivyo!!!



    Siku iliyofuata mauaji haya yakapamba vichwa vya magazeti!





    ****

    TABASAMU pana lilijitengeneza katika uso wa mwanamama Diana, alifurahia kuhesabu pesa alizokuwa



    amejikusanyia usiku uliopita. Ilikuwa biashara nzuri sana yenye faida kubwa bila kutokwa jasho. Alichokifurahia



    katika biashara hii ni kwamba walioteseka na kuumia ni watoto wa wengine sio wa kwake.

    Hakubahatika kupata mtoto! Hivyo uchungu wa mwana hakuujua.

    Mfanyakazi wake mpya alikuwa akimuingizia kipato kizuri sana. Alifurahia kuwa naye na hakujuta kumchukua usiku



    ule alipokuwa na hali mbaya ya kukimbilia mauti maeneo ya posta jijini Dar es salaam.

    Haikuwa bahati mbaya kwa mama huyu. Hiyo ilikuwa kawaida yake kuzurura usiku na kuwatafuta watoto wa mitaani



    jinsia ya kike kwa ajili ya biashara yake inayomuweka mjini. Biashara ya kuuza miiili ya wasichana.

    Alipomaliza kuhesabu pesa zake ndipo akakumbuka kuwa Mwanaidi hakuwa amrejea hadi muda huo. Hakushtuka



    sana, aliujua usumbufu wa wateja hasahasa waliolipia huduma kwa pesa nyingi.

    Ngoja ngoja huumiza matumbo!!! Subira ikamshinda ilipotimu saa nne asubuhi. Akaamua kumpigia mteja wake simu.



    Simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Alipiga mara ya pili. Haikupokelewa pia.

    Akaamua aendelee kusubiri.

    Akiwa katika kusubiri alipokea mgeni. Akajiandaa kwa kunawa uso wake akajitia vipodozi bila hata ya kuingia bafuni.



    Akatoka!!

    Mzungu!!!

    Biashara nyingine nzuri.

    Huyu alikuwa ni mmoja kati ya wateja wake wakongwe. Katika mazungumzo, huyu mzungu naye alikuwa anahitaji



    huduma za Mwanaidi. Diana akafanya tabasamu huku akiendelea kujisifia kwa kumsaidia Mwanaidi sasa anatoa



    matunda!!

    Mzungu alilipa kwa dola huku akiahidi kurejea majira ya usiku kumchukua Mwanaidi.



    Masaa yakasogea hatimaye jua likazama, hapakuwa na dalili ya Mwanaidi kuonekana. Pesa za watu zikaanza kumtokea



    puani Diana. Akajiuliza kulikoni hadi muda huo Mwanaidi hajarejea wala mteja hajapokea simu!!!

    Halafu sipajui kwake dah! Alifanya majuto Diana. Si kwa kumuonea huruma Mwanaidi bali kulilia pesa alizopokea



    kutoka kwa mzungu zisije zikapeperuka.

    Hofu ya jambo hili ilimfanya Diana ashindwe hata kuwakagua vyema watoto wanne wageni walioletwa kwa danganya



    toto ya kufanya kazi za ndani wakati ukweli ukiwa ni kugeuzwa biashara katika danguro hilo ambalo mchana huwezi



    kudhania kuna uchafu huo ndani. Na hata usiku usipokuwa mwenyeji utaambulia patupu.

    Majira ya saa mbili usiku, hapa ndipo simu ya Diana huanza kuwa bize. Na siku hii kama kawaida simu zilianza



    kuingia. Mmoja kati ya wateja wake alikuwa ni Saimon, huyu alimweleza kuwa yeye ni mgeni na anahitaji kuonana



    naye. Alitumia lugha za kiujanja ujanja hatimaye Diana akampa maelekezo yote. Jinsi ya kumfikia anapopatikana.

    Magomeni Mapipa!!

    Wakakubaliana kuonana baada ya masaa kadhaa!!



    *****

    MWANADAMU ni mnyama lakini ana utofauti mkubwa sana na wanyama wengine. Binadamu ana damu ya ajabu.



    Damu ambayo ukiimwaga basi inakukaa kichwani.

    Hali hii ilimtokea Mwanaidi baada ya kuondoa uhai wa bwana mnene aliyetaka kumdhalilisha kijinsia. Akili yake



    ikamruka na ikagoma kutulia. Alikuwa na hasira siku nzima. Alijiona yu tofauti na wanadamu wengine alikuwa na



    chuki huku ujasiri ukiwa umemtawala.

    Alikuwa anatamani damu nyingine tena na tena!!



    Usiku huo alimalizia safari yake katika sehemu maarufu kwa kuwa na machokoraa wenye hasira na wakorofi.

    Feri!!

    Mwanaidi hakuwa katika hali ya msichana dhaifu bali alikuwa jasiori sana. Ni kama alikuwa ameuvaa uanaume katika



    mwili wake wa ndani.

    Wavulana aliowakuta pale walitaka kumsumbua lakini hakuonekana kutetereka na alithibitisha kuwa alikuwa na



    uenyeji wa mahali hapo miezi mingi iliyopita.

    Mwanaume mmoja akamvuta Mwanaidi pembeni. Mwanaidi akamueleza shida yake.

    Akataja neno ambalo linachukiwa na machokoraa wote na yatima popote pale. UONEVU!!

    Mwanaidi akadai kuwa kuna mtu anamuonea.

    Unataka kuijua hasira ya chokoraa!! Muonee mwenzao mmoja wakujeruhi wote kwa pamoja!! Hivi ndivyo



    ilivyokuwa.

    Machokoraa sita, Mwanaidi akiwa mmoja wao. Waliusubiri usiku. Wakati Mwanaidio akiwaza kumuadabisha Diana,



    wengine waliwaza na kingine cha ziada. Kuadabisha na kuiba!!! Maisha yalikuwa yamewabadili watoto hawa na



    kujikuta katika mkumbo huu.



    Majira ya saa mbili usiku. Danguro likiwa kimya kabisa. Kichwa kimoja kiliingia ndani. Vingine viwili vikingojea kwa



    makini. Nyumba ilikuwa imezungukwa kimya kimya.

    “Mwanaidi mwanangu jamanii…..yaani nilikuwa nimechanganyikiwa.” Diana alimkumbatia Mwanaidi baada ya kuwa



    ameingia ndani. Mwanaidi naye alimkumbatia kinafiki huku hasira ikizidi kumkaa kooni.

    Walizungumza mawili matatu. Katikati ya maongezi Mwanaidi akapaliwa. Akaanza kukohoa kwa sauti ya juu sana.



    Diana akaanza kumpigapiga mgongo. Wakati akiendelea na shughuli hiyo aliguswa mgongoni. Alipogeuka alikutana na



    sura za kitoto lakini zilizokomaa.

    Alipojaribu kupiga kelele. Aliwahi kuzibwa mdomo.

    Baada ya dakika chache. Mwili wake ulitua chini ukiwa haujiweza kunyanyuka tena milele. Na mahali pale hapakuwa



    sahihi yake. Alitakiwa kuhifadhiwa mochwari!!

    Simu yake ilikuwa inaita wakati kiumbe huyu anaaga dunia!! Bila shaka na dhambi yake ilimfuata.



    Viumbe wale wakatoka nje!!

    Walipokuwa wanatoka gari dogo lilipaki nje ya ile nyumba!!!

    Hawakujali. Wakapotelea gizani.

    Wawili waliompekua Diana walikuwa na pesa kadhaa mifukoni.

    “Dili kama hizi ndo tunataka. Safi sana komando.” Walimpongeza Mwanaidi. Ambaye bado hakuwa akijielewa elewa.



    ****



    GARI dogo lililopaki nje ya danguro lilikuwa la Saimoni. Alikuwa amechukua ruhusa kazini kwenda kutimiza wajibu



    wa kuipeleleza kesi ya mauaji ya mwanaume katika hoteli. Alizitazama namba zilizokuwa zikimpigia mara kwa mara



    na kuzihifadhi namba zolizokuwa zinampigia marehemu. Namba ya Diana ikawa inapiga mara nyingi zaidi.

    Akaamua kufuatilia. Kwa mbinu za kikachero akafanikiwa kuiteka akili ya Diana. Hatimaye wakakubaliana kuonana



    usiku.

    Kwa maelekezo ya Diana, mkongwe huyu wa jiji la Dar asingeweza kupotea.



    Maajabu! Baada ya kufika eneo lile simu zikaacha kupokelewa. Alipiga zaidi ya mara mbili nab ado hali ilikuwa ile ile.

    Saimon akaamua kuingia ndani, baada ya kugonga mlango bila kujibiwa. Nyumba ilikuwa imejigawanyagawanya



    katika vyumba vingi.

    Akausikia mlio wa simu akaamini huko patakuwa na mwenyeji. Akajongea. Kila simu anayopiga ilivyoanza kuita na



    mlio wa simu ndani ya nyumba uliitika.

    Upesi akavamia kile chumba kwa tahadhari.

    Kimya!! Akawasha tochi. Akakutana na mwili wa mwanamke mnene ukiwa umejikunyata ardhini na damu zikiwa



    zinamtiririka.

    Tatizo!!

    Simu ikapigwa kituoni.

    Baada ya muda nyumba ikazungukwa.

    Msako mkali ukapitishwa pale ndani.

    Wakakutwa watoto wanne. Walilia kuwa hawajui lolote. Lakini kilio chao hakikuwasaidia kitu.

    Frida na Isha walikuwa kati ya watoto hawa!!!

    Ilikuwa ni siku yao ya kwanza katika kazi hii waliyoipata. Kazi ya ndani!! Na ni siku hii hii walipigwa makofi na



    kuambulia kulala katika kituo cha polisi magomeni Usalama.

    Walitakiwa kusaidia upelelezi!

    Hawakurundikwa katika chumba kimoja.

    Walitengwa!! Frida kivyake na Isha kivyake.

    Matatizo juu ya matatizo.

    Sasa wanakabiliwa na kesi ya mauaji wasiyoyajua.



    Siku waliyoulizwa kuhusu uwepo wa wazazi wao. Wakadai kuwa hawana wazazi wao ni watoto wa mitaani ndipo



    uzito wa kesi hii uliongezeka.

    Kila mtu aliamini kuwa watoto wa mitaani hawana utu! Wanauwezo wa kuua na kujeruhi bila wasiwasi.

    Mahakamani hawakupata dhamana!!

    Ukikosa dhamana mahakamani ukiwa umetokea rumande ya kituo cha polisi. Unahamishiwa mahabusu katika gereza!!

    Frida akatupwa Segerea.

    Isha makazi yake yakawa gereza la Keko!



    Nani wa kuwatetea watoto hawa!! Hawakuwa na mtetezi. Hivyo mtu wa kufanya msukumo wa kesi yao kutajwa



    hakuwepo. Wakaendfelea kusota gerezani, kula mlo mmoja kwa siku.

    Kulala kwa tabu! Yalikuwa mateso ambayo hawakuyatarajia.

    Dunia ilikuwa kimya ikitazama yote haya.

    Bila kutoa msaada!



    Mwanaidi aliipata taarifa hiyo ya chokoraa kutuhumiwa kumuua mwajiri wao, kupitia magazeti. Picha za wale



    machokoraa waliovimba kutokana na kipigo hazikuonekana vyema sana. Lakini kuna jambo Mwanaidi aliliona. Na



    kumfananisha mmoja wao na mtu ambaye wamewahi kuonana hapo kabla.

    Ni Frida huyu ama mwingine!! Alijiuliza baada ya kuyasoma majina ya chokoraa hawa.

    Akapanga siku aende kuwapelekea chakula!



    Jumamosi!! Hii siku ikafika akajiunga na watanzania wengine kwenda kusalimia wafungwa na mahabusu!





    Kila mtu aliamini kuwa watoto wa mitaani hawana utu! Wanauwezo wa kuua na kujeruhi bila wasiwasi.

    Mahakamani hawakupata dhamana!!

    Ukikosa dhamana mahakamani ukiwa umetokea rumande ya kituo cha polisi. Unahamishiwa mahabusu katika gereza!!

    Frida akatupwa Segerea.

    Isha makazi yake yakawa gereza la Keko!



    Nani wa kuwatetea watoto hawa!! Hawakuwa na mtetezi. Hivyo mtu wa kufanya msukumo wa kesi yao kutajwa



    hakuwepo. Wakaendfelea kusota gerezani, kula mlo mmoja kwa siku.

    Kulala kwa tabu! Yalikuwa mateso ambayo hawakuyatarajia.

    Dunia ilikuwa kimya ikitazama yote haya.

    Bila kutoa msaada!



    ******

    MIEZI minne baadaye baada ya Frida na Isha kusota rumande hatimaye waliachiwa rasmi baada ya kuonekana wanajaza



    selo ilhali hawana kubwa linalowakabiri.

    Mwanaidi aliwapokea mtaani ambapo aliwaambia kuwa ni pachungu kulio huko jela walipokuwa.

    Wote wakajihisi wana laana!!!

    Majira ya saa kumi na moja jioni. Mwanaidi alitoa wazo la kuvamia shrehe ambayo yatima wamealikwa kwa ajili ya



    chakula cha mchana na usiku. Hawakuwa na ujanja wa kupata chakula kwa siku hiyo. Njia ya kuingia katika sherehe



    hiyo ikawa pekee kwa ajili yao.

    Wakajikongoja hadi katika viwanja vya Biafra kinondoni ambapo paliandaliwa kwa ajili ya jambo hili.

    Watoto walikusanyika. Wote walitangaza jambo moja katika nyuso. Huzuni!! Hakuna aliyekuwa na furaha ya moja



    kwa moja.

    Majira ya saa moja usiku nao wakawa kati ya kundi kubwa la watoto.

    Na ulikuwa muda muafaka kwa ajili ya kupata chakula.

    Utaratibu maalumu ulifuatwa bila mtafaruku, mambo yote yakaenda sahihi.

    Walipomaliza kula ukafuata wakati wa vinywaji. Hapa sasa aliyeandaa sherehe hii alizungumza mengi huku akiwasihi



    watoto hawa yatima na machokoraa kutokata tamaa katika maisha yao.

    Katika kunogesha maongezi yake aliwasimulia stori kuhusu chokoraa. Ilikuwa inasisimua sana huku ikiwatoa watu



    machozi.

    Frida aliyekuwa amesafiri maili mia kwa mawazo aliguswa na simulizi hii. Mara akatajwa jina lake!!

    Aliponyanyua uso wake. Alidondosha chupa yake ya soda!!!

    Mshtuko!!!



    ****



    Burudani pekee iliyosalia katika maisha yake ilikuwa kuandika hadithi na mashairi ya muziki baada ya kile



    alichokoipenda maishani kuingia doa. Fani yake ya kucheza mpira iliingiliwa kati na matatizo ya moyo. Moyo wake



    ulikuwa umetanuka.

    Majibu ya daktari yalimuweka katika kipindi kigumu cha maisha yake!! Hakutakiwa kucheza mpira wala kufanya kazi



    zozote ngumu!!

    Haya akayaweza, mara nyingine figo yake ikajaa michanga. Aligundua matatizo haya baada ya kuwa anaumia kila



    akinywa maji ya kunywa. Tatizo lilikuwa limefikia pabaya sana wakati linagundulika.

    Laiti kama walezi wake wasingekuwa na pesa na kazi nzuri pia kuishi vizuri na majirani huenda angekuwa amegeuka



    chakula cha funza zamani sana. Lakini hadi sasa anaishi baada ya kupelekwa nchini India ambapo alifanyiwa upasuaji



    na kuondolewa michanga hiyo. Akarejea Tanzania akiwa mzima wa afya.

    Walezi wake walimpenda sana. Licha ya kwamba walimuokota akiwa ametupwa jalalani na mama yake wa kumzaa.



    Walimtunza kama mtoto wao.

    Familia nzima ilimpenda na alikua na kukomaa akiwa mtoto wa familia ile ya watoto sita na yeye akihesabiwa kuwa



    damu ya mzee Emmanuel Magembe na mkewe Emelensiana .

    Na haikustaajabisha alipopewa jina lenye ubini wa familia hiyo.

    Akakua hadi kufikia utu uzima akiitwa George Emmanuel.

    Wazazi hawa walimueleza juu ya uhusiano wake katika familia hiyo. Alimlaumu sana mama yake na baba yake wa



    kumzaa kwa kitendo hicho cha kikatili. Lakini lawama zikaishia hewani wazazi wake hawakuwa wakimtambua na yeye



    hakuwahi kuwatambua tena.

    Mapendo makubwa kutoka katika familia hii yalimfanya ajisikie amani kila mara. Alipoingia shuleni ndipo alianza



    kukutana na watoto wasiokuwa na wazazi na wanaishi katika mazingira magumu. Huu ukawa mwanzo wa George



    kujiuliza ni kipi afanye kwa ajili ya yatima wenzake.

    Alipoanza kuandika. Akagundua si tu kipaji cha kucheza mpira kilichokuwa ndani ya damu yake bali pia kipaji cha



    utunzi na uandishi wa simulizi mbalimbali.

    Alianza na simulizi za mapenzi, mara za kichawi. Zote hazikudumu sana. Ni hapo alipoanza kuandika maisha halisi ya



    yatima anaopata kukutana nao.

    Alikuwa chuo mwaka wa tatu wakati anakutana na Frida.

    Alijifunza vitu kadhaa kwa Frida lakini hakupata muda wa kumuhoji zaidi akapatwa na maswahibu ya kuitwa mwizi



    kisha kupokea kipigo kikuu.

    Akiwa hospitali ya wilaya ya Temeke, familia yake inamuhamisha na kumkimbiza nje ya nchi.

    Pesa iliongea!!!

    Matibabu yalipokamilika na yeye kupata nafuu. Walirejea tena Tanzania.

    George alikuwa anapendwa sana. Na kupitia familia hii alijifunza mambo mengi sana. Kubwa zaidi likiwa kumcha



    Mungu!!!

    Upendo maradufu aliopewa alitamani sana siku moja atoe zawadi kwa familia hii. Mwanzoni alitegemea kutoa zawadi



    kipindi atakapokuwa mchezaji katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania. Ndoto zikakatishwa na upana wa moyo



    wake.

    Alipoanza kuandika, akapata zawadi nyingine kubwa ya kuizawadia familia yake.

    Kitabu cha simulizi za kweli kuhusu watoto wa mitaani!! Na yatima. Alikiandika kimyakimya bila kumshirikisha mtu



    yeyote!!

    Alipokutana na Frida akazidi kutanuka kimawazo. Na kuamini kuwa ataandika kazi nzuri mno.

    Kumpoteza Frida lilikuwa pengo kubwa kwake. Baada ya kumkosa kule alipokuwa anaishi zamani. Aliungoja muujiza



    wa Mungu kumkutanisha tena na chokoraa huyu wa kike.

    Alingoja sana lakini bado hakukutanishwa na Frida.



    Alipomaliza elimu yake ya chuo kikuu miezi kadhaa baadaye, badala ya kuwazawadia wazazi wake kitabu kisichokuwa



    kamilifu aliamua kuandaa sherehe ili aweze kula kunywa na kufurahi na yatima wenzake.

    Alizungumza nao mambo mengi sana. Sasa ukafika ule wakati wa kugonga chupa na watoto wote waliofika katika



    mualiko ule.

    Ilikuwa shughuli pevu kuwafikia watoto wote. Hivyo wale wa karibu walipata nafasi hiyo.

    Baada ya pale wakafanya sala ya pamoja kisha wakaagana huku George akilia. Alilia sana kwa kuwa wenzake



    walikuwa wanarejea mitaani kuhangaika na mbu wakali wasiokuwa na huruma.

    Misukosuko ya vijana wakorofi na mengine mengi!! Yeye alikuwa anarejea kulala katika kitanda cha futi sita kwa sita



    huku ndani pakiwa na kila kitu.

    Mawazo yake yaliyomtoa machozi yalikatishwa na sauti kali iliyomuita!!

    Ni kweli alijitambulisha jina lake hapo kabla. Lakini hii sauti ilimkaa vyema masikioni. Akasita kupanda katika gari



    akageuka. Akakutana na mikono mingi ikimpungia.

    Akasita kuondoka lakini akawa anajiuliza huyo anayepunga ni yupi?? Hakupata jawabu.

    Alitaka kuendelea mbele ile sauti ikaita tena!! Sasa zilikuwa nyingi zikisaidiana. Akatazama kwa makini akawaona



    wasichana watatu wakipenya kundi kubwa. Akawasubiri huku akijifanya hazisikii sauti za walezi waliokuwa



    wakimsihi apande garini.



    Uso wake ulikuwa umechakaa sana lakini sauti yake yenye mikwaruzo bado ilikuwa inasikika vyema.

    “Frida!!” alishangaa George, kisha akachomoka kwa nguvu akamkumbatia Frida!! Mwanaidi na Isha wakawa



    watazamaji.

    George alimvuta Frida pembeni kidogo. Mshtuko alioupata hakujua hata aulize kipi na kipi asiulize.

    Frida alijilazimisha kutabasamu.

    “George, nipo na rafiki zangu. Tumetokea rumande..bila kosa tumefungiwa miezi mingi. Najihisi naumwa sana,



    naumwa. Imekuwa kama bahati kukutana nawe. Iwapo ni vyema tafadhali tusaidie chochote kitu. Kesho niweze



    kwenda hospitali na walau leo niweze kulala mahali penye unafuu. Nahisi mgongo wangu umeoza..najua naumwa



    vingi lakini kama I sahihi kwako naomba unisaidie nateseka!!!” alijieleza Frida. George akapepesa macho na kujizuia



    machozi yasimdondoke. Jicho la kuume likakosa subira likakubali kulia, na la kushoto likapatwa na tamaa likaiga



    maisha ya jicho la kuume likalia. Koo likajibana, kwikwi ikatoka mfululizo.

    Hatimaye George akawa analia kama mtoto huku akimtazama binti aliyechujika ngozi yake, nywele chafu kama kichaa,



    macho yaliyobonyea kuingia ndani na mabega yaliyopanda juu. Sahau kuhusu mavazi yasiyostahili kuitwa mavazi.

    Frida alijisikia vibaya. Kila jicho lilikuwa linamuangalia yeye!!!



    George alitumia dakika tatu akaingia garini. Akarejea na bahasha, akamnong’oneza kitu Frida kisha akampatia.



    Wakaagana akarejea garini na kutoweka.

    Mwanaidi na Isha wakamwekea ulinzi Frida. Wakatoweka eneo lile.

    Shilingi laki moja za kitanzania na simu ya mkononi!!

    Hivyo ndo vitu walivyovikuta katika bahasha. Frida akalia sana kilio cha furaha huku akimwombea George kwa



    Mungu amjalie Baraka zaidi. Isha na Mwanaid wakaitikia ‘Amen’. Kisha wakajicheka maana hata kanisa wala msikiti



    hawakujua vilipo!!

    “Amesema kesho nimtafute!!” hatimaye Frida aliwaambia wenzake!! Huku akichukua namba ya simu



    iliyoambatanishwa katika simu iliyopo ndani ya bahasha.

    Siku hii walilala nyumba ya kulala wageni na siku iiyofuata asubuhi. Frida na Isha walimtembelea daktari kwa ajili ya



    matibabu!!



    ****



    Frida na Isha walisikilizwa na daktari, wakafanyiwa vipimo kisha wakapatiwa dawa za bei ya kawaida. Wakatoweka.

    Wakati wanatoka hospitali walipishana na mtu ambaye alisababisha Frida na Mwanaidi wote watazamane na kugundua



    kuwa wameona kitu cha kufanana. Mwanaidi aliukunja uso wake kwa hasira.

    “Mungu atatulipia..” Alisema Frida. Mwanaidi hakutaka kukubaliana na hilo ombi.

    Roho mbaya ikamuingia. Roho isiyokuwa na uoga.

    Akaitamani tena roho ya mwanadamu!!

    Hyu alikuwa ni mkuu wa kituo cha kulea yatima kule Mbagala. Aliyemnyanyasa Frida kisha akamtelekeza akiwa na



    mimba.

    Sasa anaingizwa hospitali. Wawili hawa wanamuona.

    Frida anaweka ubinadamu mbele.

    Mwanaidi anauvaa unyama!!!

    Hawashirikishi lolote akina Isha na Frida lakini anawaza juu ya kumuadabisha yule mwanaume asiyekuwa na utu.





    Baada ya kutoka pale hospitali. Frida alimpigia simu George ambaye alikuwa amejiweka tayari akiisubiri simu hiyo!

    Wakapanga wakutane mchana wa siku hiyo. Akiwa na rafiki zake wawili.

    Ni mkutaniko huu ulioharibu mipango ya Mwanaidi kumuadabisha yule mkuu wa kituo cha watoto yatima. Lakini



    moyoni alijipa ahadi kuwa atamsaka hadi ampate na kumtimizia anachostahili.



    George alikuwa muongeaji mkuu katika mkutaniko huu. Frida, Isha na Mwanaidi wakiwa wasikilizaji.

    Sauti ya utulivu ya kijana George pekee ilileta faraja na kuangusha ngome za majonzi kwa muda. Kila nukta



    aliyoweka, ilistahili kuwekwa. Na alivuta pumzi kisha akaendelea tena kuzungumza.

    George aliwatamkia wazi kuwa anawahitaji katika harakati zake za kumtetea yatima mwenzake anayeteseka mtaani.



    Aliamini kuwa kwa kuwa na watatu wale ambao wanaujua mtaa vyema anaweza kuzianzisha harakati zake.

    Hapakuwa na maswali zaidi. George akawapakia katika gari lake. Wakaanzia katika maduka ya nguo. Hapa kila mmoja



    akajichagulia nguo anayodhani inampendeza.

    Wakarejea garini. Likafuata suala la kutafuta nyumba ya kuishi. Hili nalo halikuwa tatizo. Nyumba ikapatikana maeneo



    ya Magomeni Mikumi. George akalipia vyumba viwili.

    Siku hiyo hawakuhamia katika nyumba ile, walilala nyumba za kulipia tena. Siku iliyofuata walikutana tena na George,

    Kwa siku hii, hata kama una elimu ya kiwango cha uprofesa usingeweza kubashiri kuwa watatu hawa wanaonata



    katika barabara walikuwa yatima, tena walioishi maisha ya kichokoraa.

    Frida hakuwa amerejewa afya yake vyema, japo alipendeza Mwanaidi aling’ara kupita wote. Kwa mara ya kwanza



    wakatokwa na tabasamu la moja kwa moja kutoka mioyoni mwao.

    Wakakutana eneo la Best Bite, mazungumzo yakasindikizwa na chakula. Kisha wakatoweka tena. Siku hii vitu vya



    msingi vinavyofaa kuwa ndani ya nyumba vilinunuliwa. Kitanda, godoro, vyombo, mashuka na vingine vingi bila



    kusahau burudani ya muziki. Nyumba ikapendeza. Frida akaangua kilio kikubwa kwa ukarimu huu wa kijana huyu wa



    maajabu!!

    Kilio cha Frida kikaungwa mkono na Mwanaidi kisha Isha, George naye akashindwa kujizuia.

    Watatu hawa wakakumbatiana huku wakilia sana. Machozi ya yatima yakaifungua rasmi nyumba hii!!



    Ndani ya mwezi mmoja, ile picha ambayo Frida, Mwanaidi ama Isha ambayo angepiga akiwa chokoraa isingefanana



    hata kidogo na hii ya sasa. Walikuwa watu wengine kabisa.

    Ofisi aliyofungua George kwa kupewa ufadhili na walezi wake ilikuwa inahusika na mambo ya kijamii zaidi, hasahasa



    kusaidia na kutoa elimu kwa watoto wa mitaani na yatima. Jitihada kamilifu zilizofanywa na George akishirikiana na



    akina Frida ziliisimamisha imara kampuni hiyo. Kila mmoja alifanya kazi kwa moyo mmoja akiamini kuwa



    anawasaidia ndugu zake mitaani.



    ****



    ILIKUWA siku ya kupendeza kama zilivyokuwa siku nyingine katika juma hilo la aina yake. Chokoraa wanne



    walikuwa chumbani wakibadilishana mawazo. Walikuwa wakijadili juu ya mikakati yao kemkem ya kuhakikisha



    yatima na chokoraa wanaishi walau kwa tumaini.

    Siku hiyo walikuwa wakishangilia baada ya kumpata mdhamini kwa ajili ya kujenga kituo cha watoto yatima. Lazima



    wafurahie maana hii kwao ilikuwa ndoto ya muda mrefu.

    Ule utani wa hapa na pale ulioinogesha furaha yao mara ukaingia doa baada ya George kuanza kukohoa. Mwanzoni



    walikichukulia kama kikohozi cha kawaida ambacho kinaweza kumkumba mtu yeyote yule na kasha kutoweka bila



    kuleta madhara yoyote. Kwa ajili ya kutunza ustaarabu wake alijaribu kujizuia asiweze kuendelea kukohoa lakini



    haikuwezekana.

    Alikohoa sana mara akaanza kutema damu. Macho yakaanza kuupoteza uangavu wake yakawa mekundu sana.



    Hakuweza kuongea alifanya ishara ambazo hakuna ambaye alizielewa. Frida alikimbia na kurejea na maji ya kunywa



    lakini George alikataa kwa ishara huku sasa akiwa anakoroma tu bila kukohoa.

    Baada ya muda akajinyoosha chini akatulia tuli.

    Wasichana hawa wakapiga mayowe! Majirani wakafika. Damu ilikuwa imetapakaa mle ndani. Hakuna aliyediriki



    kumgusa George.

    Hofu ikatanda!! Frida akawapigia simu walezi wa kijana huyu. Aliwaelezea kwa ufupi juu ya tukio lililojitokeza.

    Baada ya muda baba mtu akawasili akiwa na gari yake binafsi, na daktari binafsi.

    George akabebwa na kuingizwa garini upesi. Gari ikatoweka bila kujulikana inaelekea hospitali gani. Akina Frida



    hawakuambiwa lolote juu ya nini kinafuata baada ya hapo….hali hii iliwafadhaisha sana

    Furaha ikatoweka, taharuki ikatawala. Hakuna aliyejua nini tatizo hadi jambo hili likatokea.

    Walisafisha zile damu.

    Wakalala wakiwa na maswali kedekede!! Hakuwepo wa kuwajibia. Mwanaidi hakulala hapo siku hiyo.

    Palipokucha, waliamshwa na mlango uliokuwa unagongwa kwa nguvu sana. Walipofungua walikuwa ni askari.

    Frida na Isha walitakiwa kituoni kwa ajili ya kusaidia upelelezi. Juu ya aliyemnywesha sumu George.

    Taarifa hiyo iliwashtua sana! Hawakutegemea wanaweza kuwa washukiwa wa kwanza kabisa. Lakini ilikuwa hivi!!

    Kilio chao hakikuwasumbua askari. Pesa ya bwana Emmanuel tayari ilikuwa imewatembelea mifukoni na ilikuwa



    lazima ajulikane aliyeyafanya haya kwa mtoto wake.





    Kwa mara nyingine tena Frida Gereza na Isha wakarejeshwa mahabusu. Kwa kesi ya kumnywesha George sumu, lengo



    likiwa kumuua.



    Mwanaidi aliipata taarifa hii kupitia kwa majirani. Hata kabla hajaingia ndani. Akapatwa na mshtuko mkubwa, lakini



    hakutaka mtu yeyote ajue kuhusu hili.

    Dakika mbili baadaye hakuwa tena eneo lile akashtukia kuwa kuna hila zimefanywa na wabaya wao lengo likiwa



    kuwarudisha kwenye msoto mwingine.

    Hasira zikamfukuta kichwani. Akaelekea katika vibanda vinavyotoa huduma ya kuweka na kutoa pesa akatoa kiasi



    kidogo alichokuwanacho, kisha akatafuta nyumba ya kulala wageni akajihifadhi.

    “Kabla hawajanitafuta..ninawatafuta!” alijiapiza. Zile hasira na chuki za uchokoraani zikarejea maradufu kifuani



    mwake. Akakumbuka chanzo cha haya yote. Ile damu ya yule mwanaume mnene katika nyumba ya kulala wageni



    ikasimama tena katika akili yake.



    Siku iliyofuata Mwanaidi akiwa amejitanda baibui, huku akiacha macho pekee yakitazama. Alitembea kiujasiri hadi



    katika hospitali ambayo vyombo vya habari vilitangaza kuwa George alikuwa amelazwa na bado akiwa hajarejewa na



    fahamu zake. Alipofika mlangoni, alisikia sauti ikimuita a kuomba msaada wake.

    Akageuka na kutazama

    Alikuwa ni mwanamke ambaye alikuwa amezeeka sana na alikuwa mlemavu alitembea kwa kujivuta chini, nguo zake



    zilikuwa chafu sana. Mwanaidi akarejea na kumsikiliza, alikuwa anaandaa kutoa chochote kitu katika pochi yake.



    Alijua yule mwanamke anataka pesa.

    Lakini haikuwa hivyo. Mwanaidi akamsogelea na kumtazama machoni.

    Katika macho haya aliona kitu cha ajabu, ilikuwa inashangaza sana lakini bado hakuwa na uhakika kama ni kweli ama



    la! Alivutiwa akachuchumaa aweze kumsikiliza.

    Baada ya kumsalimia alitega sikio kumsikiliza.

    Yule mama alianza kuzungumza mazungumzo ambayo yalimpa hamasa Mwanaidi ya kuendelea kusikiliza zaidi na



    zaidi.



    ******



    Ilikuwa ni simulizi ya miaka mingi sana iliyopita lakini ilisisimua sana kama vile imejitokeza siku mbili zilizopita.



    Ilikuwa inaliza na kustaajabisha.

    Mwanamke masikini asiyeijua kesho yake. Wazazi maskini walioshindwa kumsomesha huenda ndiyo chanzo



    chamaisha yake kuwa magumu kiasi kile. Wazazi walioshindwa kumpatia elimu ya darasani wakashindwa walau



    kumpatia elimu ya duniani hasahasa ya uzazi.

    Alipokomaa hakujua nini kinafuata baada ya hapo.

    Hakupajua mjini ipasavyo. Alipoingia kwa mara ya kwanza mjini Morogoro kwa nia ya kufanya kazi za ndani ndipo



    alipokutana na kizaazaa ambacho kiliyahamisha maisha yake kutoka hatua ya kuwa mabaya na kuwa mabaya zaidi.

    Aligundua ana mimba akiwa amechelewa sana. Kwani yule bwana aliyempa hiyo mimba alikuwa ametoweka mjini



    tayari.

    Bosi wake naye hakuwa tayari kulea watu wawili. Akamtimua!

    Je? Arejeshe aibu hiyo kwa wazazi? Hapana!! Ndio jawabu alilolipata. Akaamua kubaki mjini.

    Bila rafiki wala ndugu!!



    Akiwa katika kuhangaika huko na huku anakutana na bwana mwenye huruma. Alikuwa masikini kama yeye lakini



    walau alikuwa na mahala pa kujihifadhi kidogo.

    Waliishi vizuri kama mume na mke hadi pale alipojifungua, mtoto alipofikisha miezi saba ndipo yakatokea ya kutokea.

    Mwanamke akapooza!! Bwana alishtuka sana lakini kinyume na matarajio ya yule mwanamkea kuwa yule bwana



    atampa huduma zote za msingi. Haikuwa hivyo japo maisha yalibadilika.

    Yule mwanaume akapata pesa akaanza kung’ara, akaanza majivuno.

    Kisha kama vile filamu akatoweka kimauzauza na yule mtoto mdogo waliyemuita jina la Matatizo. Mwanamke



    aliyepooza miguu akabaki mwenyewe katika kijumba kibovu.

    Mateso yakaanza upya. Ofisi ya kata haikuwa na lolote la kumsaidia kwani hata wenyewe walikuwa na matatizo yao na



    walihitaji msaada kutoka serikali kuu.

    Miaka ikaanza kukatiza. Huyu mama akaungana na ombaomba wengine katika stendi ya msamvu na maeneo ya mjini



    kati.

    Maisha yake yakabadilika kuwa hayo.

    Akayazoea na hatimaye miaka mingi ikapita akiwa mzoefu wa shida.

    Siku moja katika mazingira ya kuomba omba alijiburuza akaingia sehemu ya hoteli kuomba chakula.

    Huku alipatiwa msaada wa sahani ya chakula akaanz kuisasambua upesi.

    Wakati anakula alishtushwa na habari katika luninga. Habari hii ilimuhusisha mtu ambaye alimjua kabisa.

    Alitamani kumuuliza mtu yeyote pale ndani lakini hawakuwa wakifahamu analojua yeye.

    Alikuwa amemuona baba aliyekimbia na mtoto wake.

    Uchungu wa miaka mingi alioupitia aliamini iwapo atampata mtoto wake basi walau anaweza kumsaidia.

    Mama ni mama tu..sura ya mwanaye hata ifinyangwe vipi lazima ataibaini. Ndivyo ilivyokuwa kwa mama huyu wakati



    George Emmanuel anayedhaniwa kuwa amepewa sumu afe. Alivyoonyeshwa katika taarifa ya habari.

    Mama huyu hakutaka kulaza damu.



    Shughuli ya kuomba omba ilikuwa imempatia kipato cha kuweza kusafiri hadi jijini Dar es salaam. Akafanya maamuzi



    akasafiri!!!

    Japo alipata bughudha na mahangaiko makubwa kutoka katika kituo cha mabasi ubungo lakini sasa alikuwa mbele ya



    ile hospitali ambayo ilitangazwa kuwa George Emmanuel alihifadhiwa akiwa hajitambui.

    Mwanaidi anavutiwa naye anamsikiliza na sasa anapata jambo jipya kabisa ambalo ni wachache wanalitambua



    ulimwenguni!!!!

    SIRI KUU!!! Siri inayoweza kuwaokoa Frida na Isha, siri ambayo itamuweka mwenye haki mahala pake na yule



    mkosefu katika sawa yake!!!







    Mwanaidi sasa aliamini alichokiona katika macho ya yule mwanamke mlemavu! Alikuwa ameiona sura ya George



    katika macho yale, hivyo hakuwa na maswali mengi kwani alikuwa amekubaliana na ukweli hata kabla ya maongezi.

    Alijiuliza maswali mengi sana kichwani hasahasa kuhusu maisha ya George, alijiuliza kwanini mlezi wake alifanya



    unyama kama huo? Hakupata jawabu.

    Mwanaidi akatumia kama dakika sita kufikiri kisha akapata maamuzi ya kufanya. Kwanza alikodi teksi upesi yule



    mama akachukuliwa pamoja naye hadi katika nyumba ya kulala wageni aliyokuwa amefikia. Alimuhifadhi mama huyu



    ili aweze kuwa huru zaidi katika kufanya maamuzi thabiti.

    Mama hakuwa na kipingamizi baada ya kuthibitishiwa kuwa kila jambo litaenda sawasawa.

    Alipotoka pale akiwa na baibui kama awali, alirejea kule hospitali. Kikubwa alichokifuata pale ni kumjua ipasavyo



    baba mlezi wa George. Wapi anapoishi? Lilikuwa jambo kubwa zaidi.

    Kwa mazungumzo ya watu wawili watatu akapata kuyajua majibu hayo.

    Akatoweka!!



    *****



    Kikundi kikubwa kilikuwa kinamsikiliza msichana ambaye alikuwa na umbo kubwa kiasi. Ukorofi wao ulikuwa



    kando kabisa. Kilichosimuliwa kiliyagusa maisha yao kiundani, lazima watulie.

    Mwanaidi alikuwa amewakusanya machokoraa wengi wa kempu ya feri, aliwaeleza juu ya kisa cha George, wengi wao



    walikuwa wanamjua kutokana na harakati zake za kuwasaidia kutoka katika hali hiyo ngumu. Wengine waliacha



    kutumia madawa ya kulevya kutokana na harakati zake, tumaini jipya likajijenga katika mioyo yao.

    Mtu anayekupa chakula wakati unakihitaji ni vigumu sana kumsahau. Ndivyo ilivyokuwa kwa hawa! Walikikumbuka



    chakula cha kule Biafra.

    Suala la George kunyweshwa sumu liliwashangaza mno na kwa pamoja wakakiri kuwa mtukufu yule hakustahili



    adhabu hiyo kwa mema anayoyatenda.

    Lakini kubwa zaidi lililowaacha katika kizungumkuti ni simulizi juu ya kupatikana kwa mama yake. Mama mlemavu



    anayeishi maisha ya shida. Shida zilizosababishwa na mlezi wa George.

    Sasa hapa matusi ya kila namna yalimwagika. Kila chokoraa akamtamani huyo mlezi wa maajabu kwa ajili ya



    kumwadabisha. Mwanaidi akawatuliza kwa maneno yote wakatulia.

    “Yule ana pesa sana tunahitaji kujipanga kwa ajili ya kuwaokoa ndugu zetu waliopo gerezani bila makosa, pia



    kumuokoa mkombozi wetu. George!” alisema kwa sauti kuu. Kila mtu kimya!!

    Kijana mmoja ambaye alikuwa muathirika wa madawa ya kulevya kabla ya harakati za George hazijaanza alitoa wazo



    la kutafuta msaada wa kisheria. Hili aliomba aachiwe yeye kwani kuna watu waliokuwa wakimpa tiba hapo nyuma



    wanayafahamu mambo haya.

    Akakabidhiwa jukumu hilo!!



    ****

    Pesa zilikuwa tatizo jipya lilijitokeza katika harakati hizi za ukombozi wa mwenye haki na hukumu kwa mwenye



    stahili hiyo. Kwa ujasiri usiku wa kutisha kabisa mwanadada Mwanaidi alinyata akamuacha yule mama chumbani



    akiwa anakoroma, akatoka na kuelekea ‘club Ambians’ maeneo ya Sinza Afrikasana, shughuli zinazofanyika hapa



    asilimia kubwa ni za kuuza vyakula, burudani ya muziki na biashara ya kuuza miili ya akina dada.

    Mwanaidi hakwenda tena kwa kulazimishwa bali safari hii alifanya kwa hiari yake lengo likiwa kupata pesa kwa ajili



    ya kufanikisha harakati zake za kuwakomboa waliostahili. Alifika pale alipohitaji akiwa katika mavazi ya kulalia.



    Alikuwa nusu uchi! Huku akiwa makini kabisa na kifaa chake alichokihifadhi katika nguo yake kisiweze kuonekana.



    Kisu kidogo!!

    Hadi majira ya saa saba usiku alikuwa ameingia mara mbili katika huduma na alikuwa ana kiasi kidogo tu cha pesa.



    Alitamani kuondoka kwa kuona kuwa biashara ni mbovu lakini machale yake ya siku zote yalikuwa yanamshawishi



    abaki.

    Laiti kama angeendelea kusoma zaidi na zaidi huenda angekuwa mpelelezi mashuhuri sana. Alikuwa anayaheshimu



    sana machale pale yanapomcheza. Hali hii imekuwa ikimsaidia mara kwa mara, hata siku ambayo George anapatwa na



    haya maswahibu yeye alijikuta bila sababu anaondoka na kulala alipojua yeye.

    Hata baada ya kuwaeleza chokoraa wa feri kuhusu jambo linalowakabili. Hakujiaminisha sana kuwa usalama upo wa



    kutosha. Aliendelea kujiweka katika wasiwasi na kuheshimu kila hisia inayokatiza mbele yake.



    Kwa siku nyingine tena machale yake yalimbeba binti huyu. Aliishuhudia sura aliyoifahamu fika katika mawindo ya



    kusaka machangudoa. Alikuwa peke yake na ni kama alikuwa muoga na mgeni sana eneo lile.

    Huyu alikuwa ni Emmanuel baba mlezi wa George!!

    Au ananitafuta!! Alijiuliza Mwanaidi huku akijificha kwa kutumia kitambaa cha mkononi.



    Tofauti na Mwanaidi alivyodhani kuwa anatafutwa, kichwani mwa Emmanuel jambo lilikuwa jingine kabisa alikuwa



    katika kutafuta changudoa ili aweze kutimiza masharti magumu aliyopewa na mganga wa jadi kwa ajili ya kuimarisha



    utajiri wake dhidi ya wapinzani ambao muda wowote siri ikifichuka mambo yatakuwa mabaya kwa upande wake.

    Baada ya kudumu imara miaka mingi bila ya kujutia uamuzi wake wa kujipatia utajiri kwa njia za kishirikina, kwa



    kumtoa kafara mwanamke masikini asiye na kosa kisha kumweka mtoto wa mwanamke huyo kama ngao, sasa alikuwa



    ana hangaika. Ilikuwa ni lazima afanye uzinzi na changudoa usiku huo kabla ya kuendelea n masharti mengine.

    George hakutakiwa kuwa mkarimu kiasi kile, alitakiwa kuwa na roho mbaya ili katika urithi wa mikoba ya kichawi ya



    kumshikia utajiri mzee Emmanuel asiweze kuogopa.

    Emmanuel alijifanya kuwa mcha Mungu sana. Lakini haya yote aliyafanya kwa ajili ya kujiweka katika kivuli



    kitakachomlinda na watu wabaya wanaoweza kutilia mashaka utajiri wake.

    Sasa George anaonekana dhahiri kuwa katika upande usiowapendeza wale waliompatia utajiri Emmanuel.

    Hivyo anatakiwa kufata masharti yote. Sharti la kwanza likiwa kumlaza kitandani George asiendelee na jambo lolote



    lile katika maisha hadi masharti yatimie. Aharibiwe akili yake na kuanza kupelekeshwa wanavyotaka wao.

    Sasa George yupo kitandani na serikali inaamini amenyweshwa sumu. Daktari aliyezoea rushwa amechukua pesa



    kutoka kwa Emma na sasa anasema kile bosi wake anataka.

    Frida na Isha wanatupiwa mzigo huu!! Emma aliamini kabisa kwa mchezo huu hakuna wa kuweza kumshtukia.



    Mwanaidi aliendelea kumfuatilia Emma hadi alipomuona anasemezana na msichana aliyekuwa eneo lile kibiashara.



    Maelewano yakawa mazuri wakaelekea sehemu ya tukio.



    Baada ya kutoka pale mzee Emma alizengea huku na kule kisha akaanza kuelekea alipopajua yeye mwenyewe.

    Mwanaidi chokoraa mzoefu asiyeogopa jua, mvua, giza wala mwanga aliendelea kumfuatilia kwa tahadhari kubwa



    sana. Hadi alipofika katika mtaro na kuibuka na kifurushi fulani.

    Bado Mwanaidi hakuchoka akaendelea kufuatilia nyendo za tajiri huyu wa mchana.

    Bila kujua kama anafuatiliwa bwana Emma alipoifikia njia panda alitazama kushoto na kulia kisha akazamisha mkono



    wake katika ule mfuko akaibuka na nazi. Akanong’ona maneno machache kisha akaivunja.

    Haya yote Mwanaidi aliyashuhudia bila kuogopa. Kwani kwa maisha yake ya uchokoraa ni mengi ameyashuhudia ya



    kutisha na kushangaza zaidi ya hayo.

    Upelelezi huu kwa kiasi fulani ukawa umemtosheleza!!

    Akachukua hamsini zake!! Akimwacha mzee Emma akiendelea na safari zake.

    Kumbe ni mshirikina!! Alipata jawabu Mwanaidi.



    *****



    Ule wakati ambao Mwanaidi anaamua kuachana na Emma na kuendelea na mambo yake ndio wakati ambao Emma



    anapokea simu kutoka kwa rafiki yake ambaye ni mwanasheria. Mwanasheria huyu anamsihi na kumsihi bwana Emma



    kuwa siku inayofuata mapema sana waweze kuonana kuna tatizo linalotakiwa kusawazishwa kabla mambo hayajawa



    mabaya.

    Mwanasheria hakutaka kumueleza lolote juu ya tatizo hilo maana lilikuwa gumu sana kuelezeka.

    Emmanuel aliahidi kuwa siku inayofuata mapema kabisa atakuwa pale.



    Siku iliyofuata asubuhi wakat Emma akiwa katika gari lake kuelekea kwa huyo mwanasheria. Na Mwanaidi naye



    alikuwa pamoja na yule kijana aliyeagizwa kumsaka mwanasheria wakielekea kwa huyo mwanasheria kumuelezea juu



    ya tukio la bwana Emma kuonekana usiku akiwa na changudoa kisha akafumaniwa bila kujua akivunja nazi njia panda.



    Mwanaidi aliamini ni yeye anayeweza kukielezea kisa hicho vizuri sana hakuna mwingine!!

    Sasa wanaelekea katika ofisi ambayo mbaya wao naye anaenda kwa ajili ya kuvujishiwa siri.



    ****







    Kwa kuwa Emma alikuwa anatumia usafiri wake binafsi ilikuwa ni lazima awe wa kwanza kufika katika ofisi ya



    mwanasheria.

    Baada ya maongezi ya dakika kadhaa, jasho lilianza kumtoka Emmanuel. Alikuwa kama mtoto mdogo asijue nini cha



    kufanya kwa wakati ule. Kwa mwanasheria hili halikuwa jambo kubwa la kwanza kusikia jambo kwa kiasi fulani



    lilimshangaza na kumfanya ile heshima aliyokuwa nayo kwa bwana Emmanuel ishuke kwa kiasi fulani.

    Sauti yenye kitetemeshi na iliyokosa utulivu ya bwana Emma ilipenya katika mlango na kumfikia Mwanaidi aliyekuwa



    pamoja na yule kijana aliyeileta taarifa kwa mwanasheria. Sauti hizo zilikuja katika mithili ya miungurumo hivyo



    ilikuwa ngumu sana kutambua neno linalosemwa. Hakuitilia maanani sana aliendelea kuvuta subira ili mteja



    anayehudumiwa aweze kumaliziwa shida zake na wao waweze kusikilizwa.

    Dakika zikasogea hatimaye zikafiki sitini. Saa moja

    Masaa mengine mawili yakapita, ndipovikasikika viti vikiburuzwa ishara ya mtu kusimama. Tendo hilo nalo likatwaa



    dakika tano ndipo mlango ukafunguliwa. Wakati mlango unafunguliwa Mwanaidi alikuwa anayapikicha macho yake ili



    aweze kuona mbele sawasawa baada ya kuwa amesinzia kwa kitambo fulani pale alipokuwa amekaa.

    Macho yake yaliyotandwa na ukungu yaliweza kuona kitu. Alimuona Emma, yule mlezi wa George. Mwanaidi



    aliganda kama picha katika luninga. Akatulia tuli mapigo yake ya moyo ndo kitu pekee kilichojitahidi kwenda kasi.

    “Ingia we dada watu tuna haraka” sauti za makaripio ndio zilimrudisha katika uhai wa kufikiri, akaingia katika ofisi ya



    mwanasheria.

    Kijana waliyekuwa naye akabaki nje, alikuwa amesinzia! !.



    Mwanasheria huyu aitwaye Kindo alimkaribisha mteja wake kwa tabasamu hafifu. Uso wake ulikuwa kama una hatia



    inayojaribu kujificha, sura ya mwanadada huyu nayo haikufanya makosa ikajibu tabasamu la bandia. Mwanasheria



    akajichekesha. Sarafi hii Mwanaidi hakutabasamu wala hakucheka.

    “Naitwa Suzan.” Alijitambulisha bila kuulizwa huku akiiegemea meza. Kabla hajaendelea zaidi mlango ulisukumwa



    akaingia mteja mwingine lakini kwa shida ile ile. Huyu alikuwa ni kijana ambaye Mwanaidi alikuwa amefika naye



    eneo lile. Sasa alikuwa ameamka kutoka usingizini.

    “Ohoo. Masha, karibu sana.” Alizungumza mwanasheria.

    Masha akatoa salamu kisha akakaa.

    “Nipo na huyu dada.” Masha alijielezea. Mwanasheria akaonyesha ishara ya mikono kuwa wanaweza kuongea.

    Mwanaid ambaye alikuwa ameshtuka kutokana na uoga aliouonyesha mwanasheria huyu alikuwa hana nguvu kabisa za



    kuweza kusema jambo. Lakini alijikaza na kutaka kuanza kuzungumza.

    Kabla mazungumzo hayajakolea simu ya mwanasheria iliita.

    Akawataka radhi akatoka nje.

    Mwanaidi alitamani sana kumweleza Masha kuwa huenda siri yao imevuja tayari na hakuna msaada wowote kwa



    bwana huyu, lakini alihofia kumchanganya kijana huyu na kumsababisha daktari awashtukie.

    Mwanadada wa kizaramo, yatima na chokoraa mzoefu akakaa kimya.

    Baada ya dakika kadhaa mwanasheria akarejea, akiwa anaukuna upara wake na kuiweka sawa suti yake mwilini.

    “Ndio nakusikiliza. Mmesema mpo wote?” aliuliza.

    Wakatikisa vichwa kukubali.

    Mwanaidi akajivika tena ujasiri lakini safari hii hakuweza kuendelea zaidi. Na yeye akasingizia udhuru kuwa anhitaji



    kuzungumza na Masha kando.



    Walipotoka hawakurejea!



    Mwanaidi alimueleza Masha kwa kifupi juu ya wasiwasi wake. Masha akamuelewa kabisa. Wakarejea kule



    walipomwacha mama George. Masha hakufika hadi eneo husika, aliondoka kuelekea feri.

    Jioni kwa kupitia taarifa ya chokoraa wenye nia njema, Mwanaidi aliipata taarifa ya kuwa anatafutwa na mtu



    wasiyemfahamu anadai kuwa ni ndugu yake.

    Mwanaidi hakudanganyika kirahisi. Aliyasikia maneno haya na kuyafanyia kzi upesi. Akili yake komavu ikayachambua



    na kugundua kuwa anawindwa sana na alijua pia Emma tayari ameambiwa juu ya uwepo hai wa mama yake George.



    Akafanya tabasamu la kujilazimisha!



    *****

    George aliendelea kuwa kama gogo katika kitanda cha hospitali. Jambo la maajabu ni kwamba alikuwa anapumua bila



    shida. Lakini alilazimika kulishwa kwa kutumia mipira.



    Pesa nyingi alizozichukua daktari kwa ajili ya kuuficha umma juu ya ukweli uliojificha ziliendelea kumfanya awe



    jasiri. Manesi walikuwa wakimsikitikia George. Lakini ukweli ni kwamba kijana huyu asiye na hatia alikuwa mbali



    kabisa. Alikuwa katika kuwatumikia watu wabaya.

    Pale kitandani, walikuwa wanahudumia gogo bila kujua.

    Nguvu za maajabu walitunukiwa hawa wachawi!

    Juma zima lilikatika. Hali ya George ilikuwa tete sana. Mke wa Emmanuel alishangazwa sana na hatua hii ya



    kuendelea kumuacha mgonjwa huyu katika hospitali hii kwa muda mrefu wakati uwezo wa kumpeleka nje ya nchi



    ulikuwepo.

    Siri kuu ikasalia kichwani mwa bwana Emma aliyekuwa amemtoa kafara Mama yake George na mwanaye ili aupate



    utajiri, na mwingine aliyejua walau kidogo ni daktari aliyempima George na kugundua kuwa hana ugonjwa wowote.

    Frida na Isha wakaendelea kusota rumande kwa kosa wasilolifahamu! Uonevu uliokithiri.



    Bwana Emmanuel alikuwa amebadilika sana, hakuwa na furaha tena, alikondeana ndani ya siku chache. Mkewe



    hakujua nini tatizo na aliogopa sana kumuuliza kwa sababu ya hasira za ajabu ajabu alizokuwanazo. Mabadiliko haya



    yalikuwa wazi hata kwa watoto wake wa kuzaa, hali hii iliwashangaza.

    Lakini siri aliijua yeye na nafsi yake. Tatizo lilikuwa kubwa.

    Mali za lelemama zilikuwa zinampeleka puta. Suala la kuambiwa na mwanasheria juu ya uwepo wa mama



    anayemtuhumu kuwa alimuibia mtoto, ni jambo ambalo lilimchanganya sana. Akiwa hajakaa sawa huku akitegemea



    kumpata kirahisi mwenye siri hiyo.

    Simu anayopokea kutoka kwa mwanasheria kuwa wale wenye siri wapo naye kisha anapofika anaambiwa wametoweka



    bila kuaga inamchanganya zaidi. Sasa ameagiza vijana watatu maalumu kwa ajili ya operesheni sana Mwanaidi ama



    kwa jina la uficho Suzan.

    Alitegemea kuwa shughuli hii itakuwa nyepesi lakini sasa inakuwa ngumu sana. Hapati anachokihitaji na muda unazidi



    kwenda huku aibu nayo ikijongea kwa kasi.

    Alitia huruma mzee huyu, lakini alistahili kuaibika!



    *****



    Mwanaidi alijiweka mbali tena na wale machokoraa wa feri nap engine popote pale. Viwanja vya kuuza mwili wake



    pia alibadili. Ni katika kukwepana na watu wa Emma ambao aliamini usiku na mchana wanamsaka ili awaeleze ni



    wapi yule mama yupo waweze kumuua afe na siri yake kifuani. Afe na ushahidi ambao utawaweka wengi huru.

    Mwanaidi hakuwa tayari!

    Gharama za kuendesha maisha ya pale hotelini zikaanza kumzidia. Kurejea kule walipokuwa wanaishi ili aweze



    kuchukua chochote na kuuza haikuwezekana alihofia usalama wake.

    Hakuwa na mbinu nyingine ya ziada zaidi ya kuuza mwili wake kwa jitihada. Kilichopatikana alimuhudumia yule



    mwanamke.

    Kibaya zaidi hakujali tena iwapo kinga inatumika ama la. Akawa makini kuikwepa mimba kuliko kuvikwepa virusi.

    Mpaka lini? Alijiuliza Mwanaidi ikiwa zimepita siku saba tangu amuhifadhi yule mama huku rafiki zake wakisota



    rumande kusubiri kesi yao iliyokuwa katika upelelezi wa kitaalamu. Mtaalamu mwenyewe ni daktari ambaye tayari



    amenunuliwa na kuusema uongo ukisikika kama ukweli.

    Ilikuwa siku ya jumatatu asubuhi. Mwanaidi hakuwa sawa kiafya, alisumbuliwa na mafua na kichwa kilikuwa



    kinamuuma. Hii ilitokana na kunywa pombe kwa mara ya kwanza.

    Angefanya nini wakati mteja wake ndicho alichohitaji!

    Hakika alimlipa pesa nzuri lakini alimuathiri.

    Mwanaidi alimtazama yule mama aliye katika usingizi, uzo wake wenye makunyanzi ukijionyesha dhahiri shahiri kuwa



    tegemezi lake hapo mjini ni Mwanaidi pekee. Uso huu ulimsikitisha sana Mwanaidi.

    Akahamishia macho yake katika miguu isiyoweza kutembea bali kujiburuza. Akachukua kiganja chake na kulifuta



    chozi lake lililokuwa linatiririka kutoka katika jicho la kuume.

    Mwanaidi akasikia kifua chake kikijawa na kitu ambacho hakikufanana na hasira lakini kilipasha joto kifua chake.



    Akasimama akijisikia ana ujasiri wa hali ya juu.

    Akaingia maliwatoni akausafisha mwili wake. Akatoka bila kuaga.

    Safari yake hii ya kutatanisha alikuwa anenda pia eneo la kutatanisha lisilokuwa na amani.

    Alimfuata mwanasheria!

    Yuleyule ambaye walimtoroka siku kadhaa nyuma.

    Bahati nzuri siku hiyo hakumkuta na watu kabisa. Akaingia ndani. Wakagonnganisha macho, Mwanaidi akapatwa na



    mshtuko akajisahau hata kutoa salamu.

    Akajiruhusu mwenyewe kuchukua nafasi katika kiti.

    Mwanasheria kabla hajamuuliza binti huyu anahitaji nini, Mwanaidi alianza kuzungumza. Bila kumpa nafasi



    mwanasheria kusema lolote.

    “Nimejileta mwenyewe baba, najua ninasakwa sana kuliko thamani yangu ilivyo, ni heri angekuwa ananisaka mama



    yangu ili anirudishe tumboni nisiishi tena duniani. Sina hadhi ya kuwa katika dunia hii. Huenda nilikuja kimakoda,



    mwenyezi mungu aliwaumbia ninyi wenye elimu dunia hii iwe makazi yenu. Unao watoto kama mimi. Unajisikiaje



    mwanao akichelewa kurudi nyumbani, unajisikiaje ukisikia ana mahusiano na mwanaume fulani. Sasa huyo mtoto



    mfanye awe mimi, nimezaliwa katika tabu na ninaishi katika hizo tabu, nimenyanyasika, sijawahi kuwa na amani, ni



    kitu gani mimi cha udhalilishwaji mwanaume hajanifanyia, ni tusi gani sijatukanwa! Na sasa ninasakwa kwa ajili ya



    kutetea haki. Ewe mwanasheria mimi sijasoma na wala siwezi kukukosoa, mimi ni uchafu tu ambaye wanadamu



    wanazidi kunibebesha uchafu wao. Sina wa kunitetea mimi, hebu kuwa nasi watoto yatima kuwa nasi japo kidogo



    watoto wa mitaani na mwenyezi Mungu atakubariki.

    Kwanini uwatetee hao watesaji, Emmanuel anamtesa mwanamke ambaye analingana na mke wako, anaweza pia kuwa



    mama yako, unatetea mama yako kunyanyaswa, unaweza kutabasamu iwapo mkeo amevunjwa miguu maksudi?”



    Mwanaidi hakuweza kuongea zaidi, kilio kilikuwa kimemshinda. Akainama chini kwa muda kisha akayasema maneno



    haya ya mwisho, “Mikono yangu hii hapa, sina silaha, nifunge kamba umwite anikamate na kunifanya anavyotaka na



    amani iwe nanyi!.

    Hapa sasa mwanasheria aliusikia mgongo wake ukilowana. Alikuwa amepigwa na shambulio kali asiloweza



    kulielezea. Alijaribu kumbembeleza Mwanaidi lakini haikuwa kazi nyepesi.

    Picha za matukio machafu yote aliyotendewa zilipita kichwani, akajiona afai tena kuishi. Akajisalimisha.

    Mwanaidi alipoona kuwa mwanasheria hakuwa na la kufanya na kuna wateja wengine walihitaji kuingia katika



    chumba chake cha ofisi, alisimama wima akatoka bila kuaga.

    Uso wa mwanasheria ukashikwa na soni!

    *****



    Mkuu wa shule alikuwa makini sana kumsikiliza dada huyu ambaye kabla ya kutoweka alikuwa ni kiongozi mkuu pale



    shuleni. Dada huyu alimuelezea mikasa yote aliyoipitia hadi kufikia hatua hiyo aliyopo.

    Alielezea maisha ya uchokoraa na kunyanyaswa jinsi yalivyopoteza uelekeo wa maisha yake.

    Kilio cha Mwanaidi kikapokelewa kikamilifu na mkuu huyu wa shule ya msingi aliyokuwa anasoma hapo awali.

    Hii ikawa safari yake ya pili kwa siku hiyo.

    Umoja wa shule za msingi unaweza kuwa ni umoja kamilifu kupita aina nyingine za umoja. Wakiandama



    wanaandamana wote. Wakipiga kelele ni wote wanapiga kelele.

    Walipoelezwa jambo hili. Wengi wao walilia sana.

    Mwanaidi alikuwa anapendeka sana pale shuleni!

    Vilio vyao viliambatana na ahadi kemkem, kuwa siku ya mahakama watakwenda kuwatetea watoto waliofungwa



    pasipo makosa.

    Kuwatetea watoto wa mitaani!



    Tofauti na utendaji wao kuanza siku ya mahakama, hali ilianza siku hii wakati Mwanaidi anatoweka eneo lile.

    Kilio chake kikali cha mara moja katika uchochoro kiliwashtua wengi. Wakawahi kukimbilia kilipotokea. Waliokuwa



    wanataka kumteka Mweanaidi hawakuhitaji kusali sala zao za mwisho ili waingie katika safari ya milele. Walikuwa



    watatu. Na dakika hizo hizo tatu ziliwatosha kuwa nyang’anyang’a. na dakika kumi baadaye walikuwa maiti.

    Bahati mbaya hawakusema ni nani aliyewatuma!

    Mwanaidi pekee alijua kuwa hiyo ni mipango ya bwana Emma kumkamata ili aifiche siri yake.



    Kelele za wanafunzi na tukio walilolifanya liliifikia serikali.

    Kwa kuwa kuna roho tatu zimetoweka. Jambo hili halikufumbiwa macho.

    Akasakwa aliyeshukiwa kutekwa! Jina la Mwanaidi likawekwa katika orodha kuu. Sawali likawa ni wapi pa



    kumpata??.



    Kupatikana kwa Mwanaidi ilikuwa sawa na taarifa ya msiba kwa Emmanuel ambaye alitegemea vijana wake



    aliowaagiza watamleta binti huyo mikononi mwake. Lakini badala yake wameuwawa kinyama kwa kupigwa na



    wanafunzi.

    Hali hii ilizidisha ugumu kwa upande wake. Alijiuliza itakuwaje endapo mkewe atagundua maasi haya ya miaka mingi



    iliyopita. Itakuwa vipi akigundulika na jamii kuwa yu mshirikina??



    ****

    Emmanuel akajaribu kucheza karata ya mwisho kwa kuingia mtaani kumsaka Mwanaidi ambaye alimjua sura yake kwa



    mbali sana. Emma akaamua kuwawahi polisi katika kuwania kuificha siri yake.

    Wakati Emma anaingia mtaani. Kuna kiumbe mwingine naye baada ya kuguswa na maneno ya Mwanaidi aliamua



    kuingia mtaani kumsaka mtoto huyo ambaye alionyesha kuwa amekata tama na maisha. Japo alikuwa mwanaume



    aliyeyapitia mengi, bwana Kindo alitokwa machozi kutokana na maneno ya Mwanaidi.

    Bahati ya maajabu wote wakajikuta wakianzia feri, mwanasheria akimtafuta Masha ili apate pa kuanzia, Emma



    akimtafuta Mwanaidi moja kwa moja.

    Hakuna aliyejua mwenzake anawaza nini kichwani



    ***HARAKATI ZA UKOMBOZI WA CHOKORAA NA YATIMA. Je watafanikiwa……..nini hatma ya FRIDA na ISHA Gerezani…..



    ITAENDELEA.



0 comments:

Post a Comment

Blog