Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

CHOKORAA - 3

 





    Simulizi : Chokoraa

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Wakati Emma anaingia mtaani. Kuna kiumbe mwingine naye baada ya kuguswa na maneno ya Mwanaidi aliamua



    kuingia mtaani kumsaka mtoto huyo ambaye alionyesha kuwa amekata tama na maisha. Japo alikuwa mwanaume



    aliyeyapitia mengi, bwana Kindo alitokwa machozi kutokana na maneno ya Mwanaidi.

    Bahati ya maajabu wote wakajikuta wakianzia feri, mwanasheria akimtafuta Masha ili apate pa kuanzia, Emma



    akimtafuta Mwanaidi moja kwa moja.

    Hakuna aliyejua mwenzake anawaza nini kichwani



    Mtaa ukajikuta ukihangaishwa na watu wawili wakiwa na nia tofauti. Mmoja akimtetea chokoraa huku mwingine



    akitaka kumgandamiza.

    Siri aliyoigundua Mwanaidi inamtesa Emmanuel, Emmanuel anaamini kuwa yupo bega kwa bega na mwanasheria



    Kindo, kumbe tayari amesalitiwa.

    Sasa kila mmoja yupo ha lake mtaani!!



    Wakati wawili hawa wakihangaika kumsaka kiumbe mmoja asiyekuwa na silaha kubwa zaidi ya siri. Msakwa



    mwenyewe alikuwa ananyemelea mahali. Akalifikia geti akatazama kushoto na kulia, akajihisi unyonge kuibofya



    kengere ili waliopo ndani waweze kuufungua mlango. Akatumia sekunde chache tu kufanya tafakari kasha



    akakikumbuka kisu chake alichokificha mahali ambapo ni yeye pekee anaweza kupafikia kwa urahisi. Akajenga ujasiri



    kasha akajinong’oneza.

    Mimi ndo Mwanaidi aisee!!

    Akabofya kengere!!



    Baada ya dakika takribani tatu geti likafunguliwa katika kitundu kidogo.

    “Nani?” akaulizwa. Hakujibu.

    Geti likafunguliwa. Mtoto amabye angeweza kujiona kuwa yu mtu mzima kutokana na kuwa na mwili mkubwa



    alitokezea kwa nje akiwa amevaa fulana iliyomkaa vyema.

    Alikuwa amenuna, ni kama alikuwa ametoka usingizini.

    Wakatazamana na Mwanaidi nani aanze kuzungumza?

    “Naitwa Mwanaharusi ni mgeni wa bwana Emma.”

    “Hayupo…” alijibu kwa shari bila kuuliza zaidi. Mwanaidi akamtazama vyema akamkazia macho makali yaliyozoea



    kutazamana na mgambo wa jiji. Yule mvulana akainama chini.

    “Je mama?” aliongeza swali.

    “Subiri!!” alimalizia hivyo.

    Akalifunga geti akatoweka. Hakurejea tena badala yake akafika mama mtu mzima. Mrembo wa haja ambaye enzi za



    usichana wake halikuwa jambo la kushangaza kwa mwanaume kupiga magoti kubembeleza apate penzi



    Akamtazama Mwanaidi kwa jicho lililoonyesha kuwa hajawahi kumuona hapo kabla au iwapo aliwahi kumuona basi



    tayari amemsahau.

    “Shkamoo mama…naitwa Mwanaidi.”

    “Mwanaidi? Mwanaharusi?” aliuliza yule mama. Mwanaidi tayari alikuwa amesahau kuwa mwanzoni alijitambulisha



    kama Mwanaharusi kwa yule aliyekuja awali kumsikiliza.

    Mwanaidi hakujibu!!

    “Haya unasemaje?”

    Mwanaidi alimtazama yule mama ambaye hapakuwa na haja ya kujiuliza kama ni mama mwenye nyumba ama la.

    Mwanaidi akajiegesha katika mlango wa kuingilia. Yule mama akaagiza kuletewa viti viwili. Upesi vikaletwa.

    Sasa mazungumzo yakaanza!!

    Mwanaidi alifumba macho yake, kuna jazba alikuwa anaizuia. Sasa akaanza kuzungumza.

    “Mama, mama yangu mzazi. Bila shaka u mke wa bwana Emma.” Alianza Mwanaidi kasha akayafumbua macho



    akamtazama yule mama aliyekiri kwa kunyanyua na kushusha kichwa kwamba kweli ni mke wa Emma.

    “Nimejileta peke yangu bila kulazimishwa mama. Nimejileta kwako unihukumu kama ni sahihi…” alianzia hapo



    Mwanaidi, akayafumba macho na kusimulia kuanzia mwanzo wa maisha yake hadi hapo alipofikia huku akimuelezea



    juu ya George na utata uliopo kwa mama yake mzazi kutelekezwa na bwana Emma miaka mingi iliyopita.

    “Mama, mimi simjui mama yangu sijui kama naye alitendwa hivi, sijui kama yupo hai nimeishi uyatima miaka yangu



    yote, nimekuwa chokoraa, nimetendwa na dunia bila kikomo. Naamini u mwanamke mwenye uchungu, uchungu wa



    kunizaa mimi, uchungu ambao hata mimi nitaupata ndio uchungu ulionileta hapa. Nateseka mama, nab ado nasakwa



    niuwawe, watoto wako wengine wapo rumande hadi sasa. Amewaweka bwana Emma. Unyama alioutenda miaka mingi



    iliyopita haujamtosha sasa ananyanyasa yatima kwa kuwa yu hai.”

    Mwanaidi alizungumza sasa wazimu ukiwa umempanda, uchungu uliopitiliza ukayaruhusu machozi kuendelea



    kububujika. Kilio cha kwikwi nacho kikatawala. Sasa alikuwa analia na hakuweza kuzungumza.

    Alipojaribu kuyafumbua macho yake. Mama mwenye nyumba alikuwa anatiririka jasho. Na alikuwa ametulia tuli.

    Mwanaidi akajiweka sawa kitini. Akamuita mama, hakujibu. Akaita tena na tena bado hakujibiwa!!

    Machale yakamcheza, ule ujasiri ukatoweka.

    Akatazama kushoto na kulia. Geti likamuita, akachomoka upesi.

    Sasa alikuwa anaogopa tena!!



    *******



    UNAPOKUWA katika tatizo la aina yoyote ile, lazima unakuwa mtu wa kujishtukia. Kila kitu kwako kinakuwa ni



    adui. Hautakuwa na amani moyoni mwako na imani kwa kila mtu inapooza.

    Ni hali hii ilikuwa inamkabili bwana Emma. Huku akiwa na taarifa kuwa Mwanaidi alikuwa huru, huku akijua fika



    kuna siri nzito anaimiliki moyoni mwake, hakutaka kumuamini mtu yeyote kwani aliamini kila mmoja ni adui na kwa



    namna moja au nyingine anaweza kuwa anashirikiana na polisi kuweza kumkamata. Jambo ambalo hakutaka kabisa



    litokee.

    Umakini huu alifika nao feri, hakutaka kukurupuka na kuanza kumsaka Mwanaidi. Aliamua kuwa kimya na



    muangalifu ili aweze kufanya msako wa hayawani!!

    Utulivu wake ukampa majibu mapema.

    Alipoiona pajero nyeupe ikitafuta mahali pa kuegesha alisita kushuka garini. Kupitia vioo vilivyowekewa utepe



    mweusi wa kuzuia aliyeko nje asione ndani. Emma aliweza kushuhudia namba za gari alizokuwa anazifahamu.



    Zilikuwa namba za Mwanasheria.

    Emma alivuta subira na hatimaye aliyekuwa ndani akashuka. Hakika alikuwa mwanasheria kindo.

    Baada ya mwanasheria kutembea hatua kadhaa. Emma naye alishuka.

    Akaanza kumfuatilia. Alikuwa makini asionekane kama anayefuatilia jambo.

    Aliweza kumuona akiongea na watoto kadhaa waliopo maeneo ya feri na hatimaye alikutanishwa na mtu mwingine.



    Huyu walionekana kufahamiana. Baada ya mazungumzo marefu wakaongozana hadi wakaifikia gari wakaingia ndani.



    Gari ikawasha injini na kuanza kuondoka.

    Emma alijipongeza kwa kutumia gari ambayo haikuwa ikijulikana sana na watu hivyo hata alipoamua kumfungia tela



    bwana Kindo hakuwa na mashaka kabisa.

    Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kwa kawaida huwa haina msongamano mkubwa wa magari na isitoshe siku hii ilikuwa



    ya mapumziko.

    Hivyo Emma hakupata tabu kumfuatilia Kindo ili ajue mwisho wake.

    Safari ya waliomtangulia ikaishia Kinondoni kituo cha Studio, wakaingia upande wa kulia na kupaki gari. Emma



    akawapita kidogo naye akapaki kwa mbele zaidi. Alikuwa anatumia kioo cha pembeni kutazama wawili hawa



    walipokuwa wanaelekea.

    Aliamini kabisa kuwa mwanasheria alikuwa amemgeuka. Na kama ni hivyo basi kwa namna yoyote alikuwa



    anafahamu wapi yupo Mwanaidi.

    Emma alipotelemka garini aliingia dukani akanunua miwani kubwa. Akaiweka machoni. Kasha upesi akaanza



    kuwafuatilia wawili hawa bila wao kujijua.

    Waliposimama na kuanza kuelekezana pia alikuwa makini kuwatazama. Kasha mwanasheria akatoa kiasi cha pesa na



    kumkabidhi yule kijana. Akatoweka.

    Wakati anaondoka alipishana na Emma.



    Hatua kwa hatua hatimaye wakaifikia nyumba ya kulala wageni yenye hadhi ya kawaida. Kindo akaingia. Emma anaye



    kwa ukaribu akaingia. Akajiweka mapokezi isiyokuwa na wahusika kisha kwa makini kabisa akatega sikio na



    kusikiliza hatua za Kindo zinaishia wapi.

    Mahesabu sahihi kabisa, chumba namba kumi na nane (18) !!

    Alisimama mlangoni kwa dakika kadhaa akasikia mazungumzo kati ya mwanaume na mwanamke mwenye wasiwasi



    wa hali ya juu.

    Ngoja ngoja yaumiza matumbo!! Alijisemea Emma, kisha akaufungua mlango akaingia ndani, ana kwa ana na



    mwanasheria Kindo.



    Kati ya jambo ambalo mwanasheria hakulitegemea ni kufungiwa tela na Emma bila kujijua. Mshtuko alioupata



    alitamani iwe ndoto lakini haikuwa.

    Emma alikuwa katika munkari ya kufanya lolote ilimradi aweze kuitetea heshima yake mtaani. Hata kuua kwake



    ilikuwa sahihi kwa wakati ule. Alipotembea na kisu hakuwa amefanya bahati mbaya.

    “Umekuja kufanya nini huku?” aliuliza Emma huku akiwa anatetemeka.

    Kosa alilofanya mwanasheria bila kutegemea ni kuamini kuwa anaweza kutumia maneno yake ya kisheria kumhadaa



    Emma.

    “Bwana Emma unamfahamu vipi huyu mama hapa kitandani na yule binti..ambaye…” kabla hajamalizia. Bwana



    Emma akachomoa kile kisu kutoka katika kiuno chake.

    Mwanasheria akatumbua macho.

    “Ulikuja kufanya nini na Mwanaidi yupo wapi?” aliulizwa.

    Jibu lilipoonekana kuwa mbali sana. Emma aliamua kujichagulia jibu.

    Akamrukia. Kisu kikazama alipohitaji. Yule mama pale kitandani akapiga kelele mara moja na kupoteza fahamu damu



    iliporuka juu ikitokea katika kifua cha Kindo, aliyekuwa mwanasheria kabla ya haya mauti.

    Simu ya mkononi ndiyo iliyomgutusha Emma aliyekuwa ameganda kana kwamba hakutegemea kama anaweza kufanya



    jambo kama lile.

    “Nani Mama Jenny amekuwaje….” Aliuliza, akathibitishiwa kilichotokea nyumbani.

    Ilikuwa ni taarifa kuhusu mkewe ambaye alikuwa epooza upande mwa mwili, baada ya kuwa amepewa taarifa ya



    mauzauza na Mwanaidi.

    Hakika alikuwa anmpenda sana mke wake.

    Alisahau yote aliyokuwa anayatetea sasa akauwaza uhai wa mkewe. Akatupa kile kisu bila hata kusafisha alama za



    vidole, akatoka ndani. Akakimbilia garini, akaondoa kwa mwendo mkali sana huku akimkosakosa msichana aliyevuka



    bila uangalifu barabarani.



    *******



    Mwanaidi aligeuka na kuitazama gari iliyomkosa kiduchu kumgonga. Akafanya ishara ya dua, akaisindikiza kwa



    macho hadi ilipotokomea.

    “Kuna watu wanaendesha hovyo..au ni mimi mawazo yangu!!” alijiuliza. Kisha akapuuzia akaendelea na safari yake,



    moyo ukiwa bado unamdunda. Kwanza kwa hali iliyomkuta mama Emma kule nyumba kisha kukoswakoswa na gari



    sentimeta chache.

    Akaingia hadi ndani. Akapigwa na mshtuko tena. Mlango wa chumba chake ulikuwa wazi.

    Nani ameufungua!! Alijiuliza huku akiingia kwa umakini mkubwa.



    Maajabu mengine makubwa kubebeka.

    Picha ya mama Emma akiwa anatokwa jasho, kukoswakoswa na gari, mlango kwa wazi na sasa anashuhudia damu.

    Alitokwa na yowe moja kubwa kisha akazirai.

    Aliporejewa na fahamu alikuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.

    Mauaji ya mwanasheria aliyeheshimika sana yalikuwa yanamuhusu.

    Mwanaidi alijikuta akikata tama na kuamini sasa harakati zake zimefikia kikomo. Yote aliyoyahangaikia yameishia



    hapa alipofikia.

    Hakuna wa kumpigania mtaani. Ni nani atakayemtetea.

    Pingu zikaiunganisha mikono yake. Akapandishwa katika gari ya polisi.

    Safari ya kuelekea rumande!!

    Harakati za chokoraa zikaingia doa. Mkono wa dola ukamnasa.





    *****



    Emmanuel aliwasili hospitali saa moja baadaye akiwa amepita njia za uchochoro hapa na pale kuweza kuikwepa foleni



    ambayo haikuwa ya kutisha sana. Mwanzoni hakufahamu iwapo mkewe alikuwa amefikishwa hospitali, taarifa hiyo



    aliipata baada ya kufika nyumbani.

    Aliambiwa msaidizi wa kazi za ndani.



    Sasa alikuwa hospitali na kama alivyoambiwa awali kuwa mkewe yupo hoi. Kweli alikuwa hoi. Tena aliyepooza.

    Emma alichanganywa na habari hii. Alijaribu kuuliza huku na kule hatimaye mwanaye wa kumzaa alimueleza juu ya



    ujio wa binti aliyeitwa Mwanaharusi.

    “Sasa alimfanya nini hadi akawa hivi.” Emma aliuliza swali la kijinga wakati tayari alikuwa ameelezwa kuwa hakuna



    aliyeshuhudia tukio hili moja kwa moja. Bali wamemkuta mgonjwa katika hali mbaya zaidi ya hiyo aliyokuwa nayo



    wakati ule. Hakupata jibu.

    Akahaha huku na huko. Bado hali haikuwa shwari.

    Hospitali aliyolazwa mama Emma haikuwa mbali sana ana alipolazwa George asiyejitambua.

    Huduma za madaktari ziliendelea kwa kasi ili kuokoa uhai huu.



    Muda ulikwenda upesi sana. Msongo wa mawazo ukiwa umekijaza kichwa cha Emma. Siri na hatia kubwa



    aliyoandamana nayo ikaanza kumzidia. Alitamani kumshirikisha mtu lakini alikuwa amechelewa sana. Alikuwa ameua



    tayari!!.

    Emma alikumbuka kuiangalia saa yake baadaye sana. Akagutuka ilikuwa saa tatu usiku!!

    Akili ikafyatuka. Ikakimbia maili mia nyuma. Akakumbuka kitu!!

    Sharti!!

    Sharti alilopewa na mganga wa kienyeji. Muda ulikuwa unakaribia!!



    Hakuna kitu kibaya kama kumtegemea mwanadamu katika jambo lolote lile na kumkabidhi maisha yako akuongoze.



    Kosa hili lilifanywa na mtu mzima huyu aliyehitimu chuo kikuu kasha kuwa mzembe katika kuisaka ajira hatimaye



    akajiingiza katika vitendo vya kishirikina.

    Sasa ule utajiri wa kupewa na mwanadamu ukaanza kumtafuna.

    Emma akaanza kulia. Waliomtazama walidhani anamlilia mkewe, lakini akilini alikuwa analia kilio cha majuto



    ambaye sasa anadeka kama mjukuu. Majuto ambaye hakutambuliwa wakati safari inaanza amejitokeza wakati huu



    mbaya.

    Alikuwa na masaa matatu tu!!

    Kuuondoa uhai wa mama George, kasha baada ya hapo atakuwa huru.

    Atampatia wapi sasa mama George?? Hilo lilikuwa swali.



    Emma akasimama wima kama mwendawazimu. Akaifikia gari yake. Akaingia ndani na kuiwasha kasha kwa mwendo



    wa kasi akaanza kuitafuta barabara ya Bagamoyo. Aweze kumuwahi mganga na kumwomba amuongezee muda. Hali



    ilikuwa tete.

    Safari ilianza vyema sana. Lakini siku ya kufa nyani, miti yote huteleza. Na vita ya ardhini haiwezi.

    Polisi wa usalama barabarani wenye njaa kali walimsimamisha.

    Lahaula!! Alikuwa hajatembea na leseni wala kadi gari. Na kibaya zaidi alikuwa na kiasi kidogo sana cha pesa ambacho



    kisingewatosheleza askari wale kupeleka mboga nyumbani kwa ajili ya siku inayofuata.

    Maneno matupu hayavunji mfupa!! Alibembeleza sana.

    Walimwachia baada ya kuwaachia simu yake kama dhamana.

    Dakika thelathini zikatokomea.



    Sasa aliweza kuondoka.

    Wakati Emma anaondoka. Kitanda kilichotulia kwa muda mrefu sasa kiliweza kuchezacheza kwa kiasi Fulani. Kasha



    kikacheza sana. Macho yakafunguka.

    “George…..George yupo wapi.” Mwanamke aliyepooza upande mmoja aliuliza. Nesi wa zamu akatabasamu!!



    Mwanamke akaendelea kuuliza.

    Hapo sasa akaitwa ndugu yake!! Swali lilikuwa lile lile.

    “Namuhitaji hapa sasa hivi.” Aliamrisha.

    Yule mtoto akatoweka na kwenda katika hospitali aliyokuwa amelazwa George.

    Ilikuwa saa tano kamili usiku. George akashtuka kutoka katika usingizi wake wa kifo. Akaangaza huku na huku. Ile



    akili yake iliyofungwa na mwanadamu, ikawa huru.

    Binadamu aliyeahidi kumuachia George akamuachia kweli baada ya muda wa masharti kupita.

    Lile gogo pale kitandani. Likakaa kitako.

    Hapakuwa na mtu chumbani. Na hakuna aliyetegemea gogo lile ipo siku litazinduka.

    Aliyeagizwa akakumbana na maajabu haya.

    George hakuwa chumbani!!

    Nesi wa zamu na daktari aliyekabidhiwa jukumu la kulinda gogo lile kwa siri wakapigwa butwaa.

    Daktari akajaribu kumpigia simu Emmanuel ili kumpa taarifa hii ya maajabu. Hakumpata hewani.

    Hofu!!





    *******



    Mimi ni chokoraa!! Ni neno la kwanza alilokiri baada ya kuingia mtaani. Akili yake ilikuwa nyepesi sana. Tofauti na



    awali.

    Mambo yote aliyoayaishi akiwa katika usingizi mzito lakini akinyanyaswa na sura ya Emmanuel ilimpatia picha ya



    yeye ni nani.

    Emmanuel hakuwa mtu mzuri. Alikuwa ni shetani.



    George akiwa ananuka madawa ya hospitali anaingia mtaani. Mtaa ambao alikuwa ni nia kubwa ya kuuokoa sasa



    anaingia akiwa anahitaji kuokolewa.

    Frida, Isha, na Mwanaidi. Hili likawa wazo la kwanza juu ya wapi pa kuanzia aweze kupata hifadhi na kuusema ukweli



    wote anaoufahamu. Alihitaji kuusema ukweli huu ili amtie hatiani Emma aliyekuwa akimnyanyasa katika kijiji cha



    maajabu asichokijua.

    Simulizi za akina Frida zilimbeba sana na kujua jinsi gani ya kuishi na watoto wa mitaani ili wasikuone kuwa u mgeni



    sana eneo lao. George hakutaka kujulikana kama yule George mtoto wa kitajiri. Hakutaka kuheshimika mtaani, alitaka



    kuishi alivyotakiwa kuishi.

    Alitaka kuishi kichokoraa na afe akiwa chokoraa. Kama alivyozaliwa na kuamini kuwa alitupwa.

    Usiku huu ukawa mwanzo wa safari ya George kuishi kichokoraa, ile hali ya kulala kitandani muda mrefu, kukosa



    chakula bora mtaani. Mabega yakapanda juu, macho yakabonyea ndani.

    Watoto wa mtaani wakampachika jina jipya kabisa. Bonge!! Ikiwa ni utani wa waziwazi.

    Bonge alikuwa mcheshi, asiyependa makuu, mkarimu. Na alionekana kama wa maajabu kwa jinsi alivyokuwa tayari



    kuwatetea wenzake hata mbele ya mgambo wa jiji. Alikuwa na majibu ambayo yaliburudisha masikio ya mgambo wa



    jiji na kushusha hasira zao.

    Bonge alikuwa ni mtunzi wa hadithi na aliyajua maneno ya kuiteka hadhira yake.



    Ni nadra sana kwa watoto wa mtaani kuheshimiana, lakini katika kempu hii ya Kariakoo mtaa wa gerezani heshima



    ilikuwepo. Kila mmoja kwa wakati wake alijikuta akimuheshimu mwenzake kutokana na nasaha za George ambaye



    alizoeleka kama Bonge.

    Bonge aliyafurahia haya maisha.



    Bonge naye ni mwanaume, tena mwenye hisia, japo moyo wake mkubwa uliwahi kumsumbua na kuingilia kipaji chake



    cha kucheza soka. Hii haikuwa na maana moyo ule ulipigwa ganzi katika suala la hisia.

    Usiku huu palikuwa na baridi kali haswa. Handaki dogo walilokuwa wamejihifadhi watoto hawa wasiokuwa na kwao,



    lilipenyeza upepeo uliozidi kuwasulubisha. Bonge alikuwa kimya sana tofauti na kawaida yake ya kuwa msema mengi



    ili kuwaliwaza chokoraa wenzake.

    Akiwa ametulia tuli. Alivamiwa na pepeo la maajabu, akahisi upweke na kujiona kuwa kuna kitu alikuwa anahitaji.



    Alihitaji joto.

    Pepo la ngono likampanda bila kutarajia. Tena katika mzingira ya kustaajabisha.

    “Kelvin…Kelv…” Bonge aliita kwa kunong’ona. Kelvin aliyekuwa anahangaika kuusaka usingizi aligeuka bila



    kusema lolote.

    “Hivi Regina analala chimbo lile la ng’ambo bado.”

    “Mh!! Analala palepale vipi kwani.”

    “Aaah!! Basi tu..lala” alisema Bonge.

    Kelvin hakujali akaendelea kuusaka usingizi.

    Bonge akasimama kimya kimya. Akatoweka, hadi ng’ambo. Akamshtua Regina. Regina akaitikia wito.

    Bonge akajielezea dhahiri kuwa amezidiwa. Regina akacheka sana kwa sauti ya chini. Hakuamini kama Bonge ana



    uhitaji huo.

    “Namaanisha Regina kama una kiumbe nisaidie lakini usiambie mtu.” Alisihi Bonge.

    “Nisubiri pale ‘chemba’ Bonge la bwana.” Aliongeza nakshi katika lile jina. Wote wakacheka.

    “Regy…..asiwe ananijua…” alitoa maelekezo Bonge.



    Kisha akachukua nafasi katika chemba aliyoelekezwa. Baada ya muda akasikia hatua zikijongea eneo lile.

    Mapigo ya moyo ya Bonge yakaongezeka huku tamaa nayo ikichukua nafasi.



    *******





    Mcha Mungu kamwe hawezi kumficha mwovu.

    Licha ya kukosa nafasi ya kuzungumza na George baada ya kuwa amerejewa na fahamu. Hakusita kuuelezea umma juu



    ya kilichojiri, hasahasa polisi ambao walichukulia hili jambo uzito.

    Emma alitoweka kwa siku tatu. Siku zisizokuwa na mafanikio.

    Alirejea nyumbani kisirisiri ili kuchukua pesa katika amana zake ili aweze kumpatia mganga waendelee na zoezi la



    kumsaka George ambaye alikuwa ameachwa huru.

    Siku aliyorejea kwake ikawa siku ya mwisho kuwa huru mtaani.

    Mama mcha Mungu. Akauweka uongo kando akayatua mapenzi ya kupendana na mfuasi wa shetani. Akatoa taarifa



    polisi.

    Bwana Emma akakamatwa.

    Ikiwa ni mara yake ya kwanza kulala rumande tangu azaliwe.



    Maswali mawili matatu ya mitego. Akanasa.

    Makofi mawili matatu. Akausema ukweli.

    Kipigo kitakatifu akakiri kuwa alimuua Mwanasheria Kindo.



    Salamu za kushangaza tena za wakati muafaka zikawafikia wale wanaoonewa gerezani. Mwanaidi, Frida na Isha. Wote



    wakaachiwa huru. Aliyetakiwa amepatikana. Chokoraa wasiokuwa na hatia wakarejea mtaani. Bado hakuwepo wa



    kuwapokea, ni mtaa uleule usiobadilika ukawasabahi.

    Kila mmoja alitolewa kwa wakati wake.

    Mwanaidi kivyake lakini Frida na Isha walioshtakiwa kwa kosa moja waliachiwa pamoja.

    Ilikuwa majira ya mchana. Wakaingia tena mtaani wakiwa hoi. Lakini huru.

    Mtaa mmoja baada ya mwingine, hatimaye mguu wao wa mwisho unaishia mtaa wa Kariakoo gerezani.

    Ni hapa waliamini wanaweza kujihifadhi na wenzao.

    Usingizi wa mang’amung’amu unakatizwa na amri kutoka kwa dada mkubwa wa kempu.

    Frida akiwa amesinzia, Isha anaamshwa na kuamriwa afunge tela amfuate dada mkubwa.

    Safari yao inaishia katika chemba yenye giza.



    Anasukumiwa ndani, anapokelewa na mikono kakamavu ya kiume. Hakuna mazungumzo

    Anajua nini kinachoendelea binti huyu analia kwa kusihi, “Kondomu…kondomu….” Kinga pekee ndiyo msaada



    anaoamini anaweza kufanyiwa lakini sio chokoraa kusamehewa katika kubakwa. Ni kawaida yao kubakwa.



    Wanaonewa.

    Mwanaume anasita kwa muda anafanya tafakari kilio kile cha mwanamke. Tamaa inazidi nguvu maamuzi.



    Anamkumbatia yule msichana aliyekondeana.



    “Bonge kuna UKIMWI…kuna kisonono, kuna fangasi…Bonge…Bonge!! Shauri zako.” Sauti ilimwambia katika nafsi



    yake. Akatamani kuacha lakini alikuwa ametamanika tayari!! Angefanya nini.

    Akaitawanya kanga ya yule binti. Akaanguka naye chini. Badala ya kutua chini wakatua katika kitu kingine.



    Kikaunguruma.

    Wakatulia. Bonge suruali magotini, binti kanga pembeni.

    Kikaunguruma tena.

    Hapa sasa Bonge akawa mwanariadha mzuri, huku Isha akimfuatia kwa kasi.

    Walienda pande mbili tofauti.

    Dada mkubwa Regina naye alishtushwa na hali hii. Chokoraa hana ngojangoja. Naye akatimua mbio.

    Walifurahisha kuwatazama.







    Bonge hakugeuka nyuma, japo zilikuwa njia za kubumba lakini aliweza kufika katika handaki bila kukosea. Alikuwa



    anathema juu juu, wakati wa kuondoka hakuaga mtu lakini mwanasoka huyu wa zamani baada ya matatizo haya sasa



    anamkurupua Kelvin.

    Anamtoa nje ya handaki na kumsimulia mkasa wote. Hapa akiwa ameikamata vyema suruali yake kiunoni isiweze



    kudondoka. Miguuni palikuwa patupu, viatu vyake alivisahau maksudi kutokana na kashkash aliyokumbana nayo huko



    alipotoka. NDIYO, asingeweza kujiuliza mara mbilimbili iwapo achukue kwanza viatu ama atimue mbio kuokoa uhai



    wake.

    Kelvin alikuwa akicheka tangu simulizi ile inaanza kuhadithiwa. Hadi Bonge alipoweka kituo cha mwisho. Hapakuwa



    na la kushauriana zaidi ya kungoja asubuhi waende kutazama kulikoni.

    Wakarejea ndani ya handaki waweze kulala tena.

    Baada ya dakika chache walikuwa wanakoroma.

    Wakati chokoraa hawa wanakoroma na kuota ndoto mbalimbali za utajiri siku za usoni, kuna watu walikuwa



    wanaamka na kuingia katika shughuli zao. Na wengine hawakuwa wamelala kabisa.

    ****

    Huyu alitamani kulala lakini usingizi ulizidiwa nguvu na maumivu ya ajabu aliyokuwa anayapata katika sehemu zake



    za siri. Alikuwa anajikuna kwa jitihada zote lakini bado hali ilikuwa tete.

    Akaanza kutetemeka, alitokwa machozi hakuwepo wa kuyafuta. Alikuwa peke yake nje ya chumba cha hospitali ya



    Mwananyamala jijini Dar. Hapakuwa na dalili yoyote ya kuhudumiwa. Kwani yeye nani?

    Wamelia wanawake wengi miaka nenda rudi. Yeye kilio chake kina tofauti gani?

    Mbaya zaidi hana pesa. Ilimuumiza.

    Muwasho ulizidi kukua na kusambaa. Mwili nao ukashikwa ganzi.

    Ni kama alikuwa anaumwa uchungu.

    Hali hii ya kuwashwa kwa siku hii ilikuwa imezidi siku mbili zilizopita alipoanza kuwashwa akiwa katika chumba cha



    mahabusu akingoja kesi yake kuanza kusikilizwa.

    Hakuwahi kuyajua magonjwa ya zinaa zaidi ya kusikia mara moja moja katika vyombo vya habari na kwa kutumia



    elimu yake ndogo ya shule ya msingi.

    Sasa alikuwa anadhani ni muwasho wa kawaida, lakini muwasho huu sasa unamtesa.

    “Umefanya ngono lini? Na nani?” daktari alimuuliza.

    “Sikumbuki..” alijibu huku akitetemeka kwa uchungu unaomkabiri.

    Daktari akakerwa na jibu hilo akamtupia tusi la nguoni, akimtukania ukoo wake mzima.

    Binti hakusema lolote.

    Daktari aliendelea na yake baada ya kuwa amemchukua vipimo na kupata majibu kuwa binti huyu alikuwa na kisonono



    kilichokomaa ndani kwa ndani kutokana na kukosa tiba ya upesi.

    Dawa kwa ajili ya kisonono kilichokomaa ilikuwa inagharimu pesa ambayo kwa namna yoyote yule binti asingeweza



    kuipata kwa wakati ule.

    “Mwanaidi nakupatia dawa ya kutuliza muwasho kwa masaa. Nenda ukatafute pesa kwa ajili ya dawa. Msaada wangu



    wa mwisho umekuwa huo mdogo wangu. Hakikisha unaipata hiyo pesa vinginevyo hautaweza kutibika tena ugonjwa



    huo” Daktari alijieleza kwa utulivu. Mwanaidi akatikisa kichwa kukubali. Alikuwa ana hofu!!

    Daktari akaandika madawa kisha akamsogelea na kunong’ona, “Ukipona mwambie awe anatumia kinga….”

    Mwanaidi akakubali yaishe!! Hakujua hata huyo mtu anayezungumziwa ni nani. Je ni yule askari aliyembaka siku mbili



    zilizopita wakiwa rumande ama ni yule mwanaume aliyelala naye kabla ya kutiwa mikononi mwa polisi.

    Akapatiwa dawa na kuimeza pale pale.

    “Unaishi wapi.” Daktari huyu aliyekuwa na matusi alimuuliza.

    “Magomeni Mikumi.” Alijibu huku akijua kuwa anaishi mitaani katika jamii yake ya chokoraa.

    Daktari akampatia shilingi elfu mbili. Akaondoka na kujituliza nje katika viti.

    Dawa ikafanya kazi, muwasho ukapungua hatimaye ukapoa.

    Mwanaidi akatoweka. Akaenda katika mtaa aliouzoea akajichanganya hapa na pale akapata mahali akajilaza.

    Saa kumi na moja alfajiri alikuwa macho tayari. Wima anajiuliza aanzie wapi, kuitafuta pesa ya madawa.

    Kama ilivyokuwa ngumu kupata jibu la aanzie wapi kuipata pesa. Ndivyo ilivyokuwa ngumu kwa upande wa pili kwa



    chokoraa mwingine.



    Isha naye alikuwa wima akijiuliza arejee kuifuata kanga yake aliyoisahau kule chemba alipotakiwa kubakwa, ama



    atimue mbio kuelekea atakapojua yeye.

    Kutimua mbio halikuwa jibu la swali lake. Akaamua kumuamsha Frida.

    Wakajikongoja pembeni ambapo hawakuweza kusikiwa na mtu. Isha akahadithia kilichotokea.

    Frida alikuwa na asili ya uoga. Hakukubaliana na suala la kurejea tena kule katika chemba kutazama nini



    kilichokoroma na kuwashtua wawili hawa.

    “Hapa tuondoke mwenzangu…bora hata posta.” Frida alishauri.

    Saa kumi na mbili hawakuwa eneo lile.

    Walitoroka.



    ****



    Upande wa Mwanaidi naye alikuwa amepata jawabu baada ya kujizungusha hapa na pale, jua likachomoza, akatafuta



    kibanda cha hadhi ya chini kabisa cha mama n’tilie, akaingia kuitibu njaa yake. Kisha akapanda gari.

    Safari ya kwenda nyumbani kwa Emma ambaye alikuwa mikononi mwa polisi. Nia ya Mwanaidi ilikuwa kuonana na



    yule mama.

    Aliamini anaweza kupata msaada. Walau wa pesa ndogo.

    Alifika akiwa na tumaini kubwa sana la kuitatua shida yake tena huenda ni zaidi ya hapo anapofikiri.

    Aliamini huruma ya yule mama hasahasa baada ya kuujua ukweli itakuwa juu yake na atamsaidia maradufu.

    Imetamkwa kuwa ‘baada ya dhiki ni faraja’ lakini kwa Mwanaidi dhiki moja inapanda juu ya dhiki mwingine na kuzua



    dhiki maradufu.

    Mama Emma na familia yake hawakuwepo, nyumba ilikuwa kama haijawahi kukaliwa na watu.

    Geti lilikuwa limefungwa.

    Mwanaidi akajikongoja kichwa chini mikono nyuma. Akarejea katika kituo cha mabasi alichotoka.

    Akapanda basi bila kujua atashuka kituo gani.

    Maskini, hakuwa na kwao msichana huyu!!

    “Kipati!! Wakushuka Kipati!!” kondakta akapiga kelele. Mwanaidi akakurupuka kutoka katika mawazo yake. Akasema



    ashushwe!!

    Kondakta akatii akamshusha!!

    Kwanza hakuwahi kutegemea kuwa ipo siku atarejea katika kituo alichowahi kufukuzwa kwa kufanyiwa njama. Lakini



    sasa anarejea kutokana na shida inayomkabili.

    Anarejea katika kituo cha watoto yatima. Alipolitazama geti la kuingilia akaanza kumkumbuka rafiki yake mpenzi



    Frida!!

    Akayakumbuka mabaya aliyotendewa na mkuu wa kituo. Alivyobakwa kwa ahadi kwamba ataishi kituoni milele.

    Mawazo yake yakakatishwa na honi kubwa ya gari.

    Alipotazama pembeni kuna sura ilikuwa inatabasamu. Sura hii ilizibwa na miwani nyeusi ya jua.

    Miwani ilipotolewa.

    Mkuu wa kituo akaonekana.

    Mwanaidi akamsalimia kwa heshima ya uoga. Moyoni alimchukia.

    Akajieleza kwa ufupi kuwa alikuwa anamtafuta yeye.

    Akaamuriwa kupanda ndani ya gari. Akapanda gari likatoweka.

    Mbagala Kuu, Kijichi. Nje ya jiji la Dar es salaam huku ndipo gari lilisimama.

    Wakashuka na kuingia katika nyumba ambayo ilikuwa mpya kabisa.

    “Nyumba yangu hii…nimemaliza kuijenga mwezi uliopita naishi mwenyewe….vipi nzuri eeh!” alizungumza kwa



    majivuno, Mwanaidi akamuunga mkono. Moyoni akilaani sana jinsi watu hawa wanavyotumia misaada inayotumwa



    kwa yatima kujinufaisha wao na matumbo yao.

    Hata kabla Mwanaidi ajajieleza shida yake tayari yule bwana mwenye tamaa akaanza kumgusa. Mara amtoe uchafu



    katika nywele mara amfute shavuni.

    Ni kweli Mwanaidi alikuwa anavutia. Hakuwa amekaa rumande siku nyingi. Bado alikuwa Mwanaidi yuleyule. Lakini



    huyu bwana aliwahi sana kuonyesha tamaa kwa yatima huyu.

    Mwanaidi mwenye shida alikuwa annakubali kila jambo lakini moja tu alilojiwekea moyoni ni kwamba.



    Udhalilishwaji wa Frida ulikuwa unatosha sana. Kwake itakuwa uzembe kudhalilishwa.

    Bwana mpenda sifa akajitapa zaidi ili kumvuta Mwanaidi. Akaonyesha pesa zake nyingi, mara aongee na simu



    kuhusiana na biashara mara awapigie watu anaowadai. Mwana akajichekesha.

    Akajifanya naye ni mwepesi kama wasichana wa mjini mbele ya pesa.

    Chumba kikawapokea kwa furaha. Mashuka meupe yakachukia kuvurugwa na viumbe hawa.

    Bwana matamaa, akawasha kiyoyozi. Kisha akasaula nguo zake moja baada ya nyingine. Mwanaidi aliyeanzia bafuni



    kwanza aliporejea alimkuta bwana huyu akiwa mtupu. Alichukiza kumtazama….

    Mwanaidi akamtazama huku mengi yakipita kichwani mwake.

    Nani atajua huenda alikuwa anamchagulia aina ya kifo ambacho kitamfaa….au…au….hakika ilikuwa hivyo.

    Papara za dakika mbili tu zilitosha kuyafanya mashuka yashangae kulikoni huyu bwana amebaki peke yake kitandani



    halafu hata hachezichezi. Mashuka yakakosa jawabu.

    Alipoanza kuharibika tena mashuka yakajiuliza kulikoni huyu bwana hanyanyuki na anazidi kutoa harufu na



    kutuchafua?

    Hapakuwa na jibu, lakini safari hii swali lao lilipata jibu.

    Mkuu wa kituo cha watoto yatima anagundulika kuaga dunia baada ya kugandamizwa na mto wa kulalia na kukosa



    pumzi hadi umauti ulipomkuta.

    Marehemu alikuwa mtu wa watu!, alikuwa mkarimu, mwenye upendo, aliyejitolea kwa ajili ya yatima na wasiojiweza.



    Mungu amlaze pema pepeoni.

    Wasiojua maovu yake wakajibu Amin!.

    Akazikwa na kusahaulika.



    ****



    Viwiliwili viwili vya vilikuwa vinafuatilia tukio moja katika nyakati na umbali tofauti.

    Kiwiliwili cha kiume kilikuwa kinanyata huku kingaa ili kupata uhakika kama kinachoshuhudia ni sahihi ama la.

    Kile cha kike kilikuwa kimepata uhakika kabisa na jambo lile.

    Kikatimua mbio na kumsimamisha mwanamke wa makamo aliyekuwa katika mizunguko yake isiyokuwa na uelekeo



    rasmi.

    “Kanga yangu hii umeitoa wapi.” Aliuliza kwa shari huku akiwa na furushi lake la chupa tupu za plastiki.

    Mwanamke badala ya kujibu alitoa tabasamu. Kisha kicheko.

    “Huyu vipi? Hivi viatu vyangu ujue.” sauti ya kiume iliuliza katika kuhamaki na kushangaa.

    “Kanga yangu hii…namwam…..” alishindwa kuendelea kuzungumza akamtazama mwanaume aliyekondeana. Mabega



    juu kama mgonjwa wa Ukimwi.

    Mwanaume akadondosha zigo lake la machuma.

    “Isha!!” aliita.

    Msichana akazidi kuduwaa, alikuwa hajapata uhakika kama yule ndiye ama siye.

    Alipomuita jina akaamini alikuwa ni George.

    George mkombozi wa yatima na chokoraa.

    George ambaye sasa anaitwa Bonge!!



    Mwanamke waliyemshutumu kuwa ana vitu vyao alikuwa anawatazama kama anayeyafuatilia maongezi yao na



    kuyapenda.

    Mara akawasogelea. Isha akajisogeza kwa George,



    ****



    Yule mwanamke aliyeonekana kama hana akili timamu baada ya kuachwa mbali na akina Isha, alianza kuwacheka pasi



    na kikomo. Alicheka sana mwisho akaanza kujigalagaza chini.

    George akaelekea kule alipokuwa Isha. Wakakumbatiana viumbe hawa wasiokuwa na afya. Kila mmoja akalihisi joto



    la mwenzake, wakajikuta wanatokwa na machozi. George akawa wa kwanza kumbembeleza Isha.

    Baada ya mazungumzo marefu huku kila mmoja akiogopa kuyaanzisha maongezi yanayohusu jaribio la kubakwa Isha,



    walitembea hadi ambapo mwanadada Frida alikuwa katika harakati zake za utafutaji. Ni katika mgahawa mmoja wa



    kimasikini sana. Alikuwa anaosha masufuria kwa ujira wa chakula cha mchana na usiku.

    Kwanza Frida hakumtambua George upesi. Lakini baada ya kukaribia sana alimtambua. Vyombo alivyokuwa anaosha



    vikakosa umuhimu. Akatimua mbio akamfikia akamrukia, George asiyekuwa na afya akakosa muhimili. Akayumba



    lakini hakuanguka. Matusi aliyokuwa anayatoa mama muuza genge aliyempa ajira Frida hayakuathiri masikio ya



    watoto hawa watatu.

    Kwa pamoja wakakumbatiana, kama machozi yao yalivyolowanisha kile chumba ambacho George alikuwa



    amewapangia wasichana hawa ndivyo sasa yalidondoka katika ardhi kavu inayowazomea wenye shida.

    Tofauti ya kilio cha kwanza ambapo walikuwa wamenawiri na kunukia marashi, hivi sasa walikuwa wamekonda na



    walikuwa wakinuka jasho.





    Tofauti hii haikupunguza furaha yao hata chembe.

    Siku ikamalizika kwa furaha ya maajabu. Isha na George walipita tena jioni wakati Frida amemaliza kazi. Walitaka



    kuondoka naye lakini kauli hiyo ikamfanya apoteze furaha, kuna jambo lilikuwa linamchanganya kichwani. Alijaribu



    kujiweka katika uchangamfu lakini haikuwezekana.

    Alikuwa amekula vya watu. Kuna mwanaume alikuwa amemnunulia pedi na kumpatia kiasi fulani cha pesa. Sasa



    alikuwa anahitaji malipo. Alihitaji malipo ya ngono na Frida alikuwa tayari kwa hilo japo hakuwahi kufurahia.

    Frida alishindwa aanze vipi kumwelezea George juu ya deni analotakiwa kulipa, akaona ni nafuu kumueleza msichana



    mwenzake. Akamvuta Isha pembeni akamueleza, Isha aliumia lakini hakuwa na ujanja wowote. Akamkubalia.

    George akapigwa changa la macho akaridhika kuwa, Frida anatakiwa kulala pale katika lile genge hadi maharage



    ambayo bado hayajawekwa jikoni yaive.

    Isha akaondoka na George kuelekea mahali watakapoweka migongo yao.

    Safari yao ya usiku ikaishia katika uchochoro. Wakakaa kidogo bila kujua kwa nini wanakaa, hawakuliogopa giza.



    Giza lilikuwa halina mamlaka ya kuogopesha nafsi zao. Kwani walikuwa wanaishi katika giza.

    George akayaanzisha maongezi ambayo kila mmoja aliyatambua. Japo alikuwa mzito kusema, lakini alilazimika.



    Akauzungumzia usiku ule wa jaribio la kubaka.

    Alikuwa anongea kwa sauti ya chini sana lakini iliyosikika vyema katika masikio ya Isha. Kwa kiasi kikubwa George



    alikuwa kama anayesihi jambo fulani. Na alikuwa na dalili zote za kuomba msamaha.

    Kiupepo kutoka baharini kiliwapuliza wakati maongezi yanaendelea. Isha akalalamika baridi.

    George akavua shati lake akampatia, japo hata yeye baridi ilikuwa inamsumbua lakini aliweza kuhimili kwani hata



    angelalamika isingesaidia kitu.

    Mvulana mvulana tu!!

    Maongezi yakaendelea. Mwisho jibu likapatikana kuwa hakika ni Isha na George walikuwa pamoja usiku ule. Isha



    hakumlaumu George, alimuelewa na kumsisitiza kuwa lile ni jambo la kawaida tu mtaani.

    Katika kushukuru, George akamkumbatia Isha. Hapa miili yao ikasafiri.

    Miili yao ikabadilishana joto. Zile hisia zilizomkabili George usiku ule na kujikuta anahitaji msichana sasa ziliamka



    tena, huku hizi za sasa zikiwa kali zaidi. Na sasa walikuwa huru.

    Akamkumbatia kwa muda mrefu. Isha naye akahama kimawazo akalihisi joto la kiume likitambaa mwilini. Nguo



    zilizochanika zikaruhusu miili yao kugusana. Mipapaso isiyokuwa ya kitaalamu ikachukua nafasi.

    Hili likawa kosa kubwa sana. Akili za kujitambua zikapaa. Wakajikuta wanafikiria kuhalalisha lililopo mbele yao.

    Giza likawafichia siri. Wakajuana palepale.



    ****



    Wakati Isha na George wakizidiwa na kujikuta wakifanya wasilotarajia. Frida alikuwa amepambana sasa alikuwa



    amezidiwa. Bwana aliyemchukua alikuwa anamlazimisha kufanya mapenzi pasipo kutumia kinga.

    Ni kweli alikuwa amemtunza kipindi akiwa katika magonjwa ya kike ya kila mwezi. Lakini malipo yake yalikuwa



    makubwa sana. Ngono!!

    Frida hakupata hisia zozote kwa yule bwana. Lakini alilazimishwa.

    Mwanaume ni mwanaume tu.

    Asubuhi wakati anatoka pale mwanaume alikuwa ameridhika. Alikuwa amekidhi haja zake.

    Walipokutana na Isha, hakumueleza kilichotokea, naye Isha hakusema alichofanya na George usiku kichakani. Kila



    mmoja akaishi na siri yake.

    George kwa mara ya kwanza katika maisha yake akagundua amefanya tendo kutokana na msukumo wa kimwili.



    Akajilaumu sana kimyakimya, hakutaka kuyaonyesha majuto yake waziwazi..

    Hapana siri chini ya jua. Kila mmoja akaendelea na maisha haya.

    George akachakarika akapanga chumba kisichokuwa na umeme. Kilichowagharimu shilingi elfu kumi kila mwezi.



    Akawachukua Frida na Isha.

    Ni huku ambapo mzozo mkubwa ulitokea. Mzozo ambao ulimuhitaji mwanaume kufanya kazi mara mia ya awali ili



    kuubeba mzigo huu.

    Isha alikuwa mjamzito.

    Hapa George akarukwa na akili kuwa Frida atamfikiriaje.

    Wakati George akimuwazia Frida atamfikiriaje kwa kitendo cha kufanya mapenzi na Isha hadi kupata ujauzito. Frida



    naye alikuwa hoi kimawazo akifikiria ni kwa jinsi gani atamueleza George kuwa yu mjamzito, ujauzito aliopewa na



    mtu asiyemfahamu ambaye alikuwa akimfadhili wakati wa shida ndogo ndogo. Alimuonea huruma sana kwa



    majukumu aliyonayo kama kaka mkubwa wa familia hiyo duni.

    Frida aliamini kabisa kuwa yule bwana aliyemnunulia pedi ndiye muhusika wa hiyo mimba lakini alitambua kuwa



    yupo katika ndoa na kamwe asingeweza kuikubali mimba ile. Frida aliutambua ukorofi wa Yule bwana, alielerwa



    kabisa kuwa akithubutu kuunyanyua mdomo wake kumsema kwa lolote basi ni kujitafutia matatikzo. Matatizo



    ambayo yanaweza kutambaa na kuendelea hadi kwa wenzake.

    Sasa kikawa kizaazaa. Mimba mbili katika nyumba moja. Tena ziliingia katika usiku mmoja.

    Mimba za chokoraa.

    George anaitambua moja tu ya Isha.

    Isha anaitambua moja tu, yak wake.

    Frida naye anaitambua moja tu, iliyopo katika tumbo lake.   

    Kizungumkuti!!.



    ****



    Aliwakumbuka sana chokoraa wenzake, hasahasa alioishi nao kwa muda mrefu na kushirikiana katika harakati za hapa



    na pale. Ugonjwa pekee ndio ulimuweka kitandani na kumfanya ashindwe kuwatafuta.

    Kisonono kilichokomaa!!

    Alikuwa anajitibu huku akiwa amelala katika godoro lake alilonunua ndani ya chumba alichokuwa amepanga.

    Sindano zilikuwa zinampelekesha sana na alishauriwa kuwa mvumilivu hadi hapo atakapopona vizuri.

    Pesa ilikuwepo ya kutosha. Hakuwa na papara. Alitulia kama alivyoagizwa. Tiba ikaendelea. Vidonge, sindano pamoja



    na kula vizuri.

    Hatimaye akarejea vyema katika hali yake ya kawaida. Mwezi mmoja na siku kadhaa za kulala kitandani na kula.



    Akawa amenenepa.

    Hakujali kuwa zile pesa amezipata kwa kuondoa uhai wa mtu. Na kwanini ajali iwapo yeye hayupo hata mmoja wa



    kumjali?

    Alipokumbuka kuhusu kutokuwepo mtu wa kumjali akakumbuka kuwa ana mama katika dunia hii aliyewahi kuishi



    naye kwa siku kadhaa. Akamkumbuka mama George. Yule alikuwa ana hadhi zote za kuwa mama wa chokoraa.

    Kumbukumbu za kumuona mara ya mwisho ilikuwa ni katika chumba kimojawapo katika nyumba ya kulala wageni



    akiwa amezimia…

    Ama alikuwa amekufa? Alijiuliza huku akikaa kitako. Macho kayakodoa bila kujua anachokiangalia kwa wakati ule.



    Mbele palikuwa na vitu kadhaa lakini hakuweza kuvitambua. Alikuwa kama zezeta.

    Hofu ikatanda. Akajishangaa na kwa mara ya kwanza akauhisi uchungu unaopatikana kwa kifo cha mtu unayempenda.



    Hakuwahi kuumia kwa kukisikia kifo cha yule bwana mnene katika nyumba ya kulala wageni, wala mama mweupe



    mmiliki wa danguro hakuishtua nafsi yake huku bwana matamaa kiongozi wa kituo cha watoto yatima naye



    hakumhuzunisha.

    Kwanini mama George? Alijiuliza.

    Upendo wa dhati!! Alipata jawabu la kinachomsumbua hadi kuumizwa na msiba huu. Aliamini kuwa alikuwa



    amempenda yule mama kwa dhati. Na alikuwa amemfanya kuwa mama yake wa kumzaa kwa kipindi kifupi.

    Uchungu ukapitiliza. Macho yakapoteza uwezo wa kuona. Yakazibwa na machozi. Mwanaidi akaomboleza.

    Aliomboleza kwa muda lakini akaona kuwa bado si suluhisho.

    George hawezi kumuelewa kuwa kweli mama yake alikuwa anaishi kwa kipindi chote cha kukua kwake.

    Au George tayari anajua? Kama hajui itakuwaje? Maswali yakawa mengi sana. Akafikiria kuhusu kupata ushahidi



    wowote utakaothibitisha kuwa yule mama anayedhaniwa kuwa mfu aliwahi kuishi.

    Hapa Mwanaidi akaamini kuwa kama alikufa bila shaka alizikwa na jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Akawaza



    kukutana na yule askari aliyemgeuza mke kwa siku mbili tatu rumande.

    Aliamini kuwa ni huyu anaweza kumsaidia kujua walau alizikwa wapi, halafu baada ya hapo atajua ni adhabu gani ya



    kumpa kwa kiushiriki katika kumuambukiza kisonono.

    Kulingana na maelezo ya daktari. Askari huyu hakuwa akihusika katika kumuambukiza kisonono kilichokomaa. Lakini



    ‘mkamatwa na ngozi ndiye aliyekula nyama’, Mwanaidi akamuuzia kesi askari yule mwenye cheo cha chini.

    Siku iliyofuiata Mwanaidi akiwa katika mavazi mapya yaliyovutia. Macho yake yakiwa yamezibwa na miwani



    nyekundu ya kisasa. Viatu vya kiuanamitindo vikistahi visigino vyake alikuwa anakatiza mitaa miwili mitatu, alijisikia



    mpya kabisa kimwili lakini kiroho akiwa na madeni mengi.

    Alijitazama vyema. Akagundua alikuwa amependeza sana. Akawatazama wavuja jasho wanavyozigombania daladala.



    Akatabasamu na kugundua kuwa kwa siku hiyo alikuwa katika hadhi tofauti.

    Akaabiri Bajaji. Dereva akatii amri.

    Safari aliyoipanga ikaanzia hapo.

    Kama kawaida katika kiuno chake kuna silaha ilihifadhiwa kwa kujihami iwapo yeyote atajaribu kumsumbua.

    Ilikuwa kama bahati iliyokuja katika wakati muafaka, Mwanaidi hata kabla hajakifikia kituo cha polisi alimuona yule



    askari barabarani. Alikuwa amenyong’onyea na sura yake ilitangaza matatizo tupu.

    “Dogo upo…..” askari alimsalimia Mwanaidi.

    “Shkamoo…” alijibu.

    Akamkaribia wakapeana mawili matatu bila kuzungumzia uhusiano wao wa kulazimishana kule rumande. Mwanaidi



    akajielezea shida yake. Bahati nzuri yule askari alikuwa mpenda kujua mengi ‘kiherehere’ hizo taarifa alikuwanazo.

    “Mbona alitolewa mapema tu yule.” Alianza kujielezea, akaelezea kila kitu alichokuwa anakifahamu kuhusu mama



    mlemavu.

    “Sasa alitoka vipi mwenyewe wakati hawezi kutembea au mlimtupa jamani.” Alilalamika mwanaidi.

    “Hapana hakutupwa lakini aliwekwa mahali akaachwa kama alivyo. Ndiyo serikali yetu ilivyo.” Alimaliza.

    Kisha akamuaga Mwanaidi na kutaka kuondoka.

    “Mbona umenywea hivyo lakini.”

    “Matatizo mdogo wangu…”

    “Nini tena.”

    “Wifi yako anaumwa na mtoto wake mchanga dah we acha tu.” Alijibu yule askari.

    Mwanaidi akamtazama huku akimuwazia mawili matatu. Lakini kubwa lililotawala kichwa chake ni kuhusu mama



    George ambaye alielekezwa ni wapi alipotelekezwa.

    Akatoweka eneo lile.

    Majira ya saa moja usiku alikuwa maeneo ya Kariakoo gerezani ambapo alielekezwa kuwa upo uwezekano wa



    kumkuta anayemtafuta.

    Alikuwa makini akitazama huku na huko, kabla ya kuvamiwa na kundi la machokoraa waliomuhoji ni kipi anatafuta



    eneo lile.

    Chokoraa walidhani ile ni bahati yao usiku ule aidha wanaweza kumuibia alichonacho. Hawakujua kama ni mwenzao.

    Mwanaidi alijitetea kuwa kuna mtu anamtafuta. Hakika alikuwa hafananii na kuwa chokoraa alikuwa amependeza sana



    siku hiyo.

    Sauti nyingi zikauizidi sauti yake. Wakadhani ni polisi.

    “Njagu, Njagu!!” kelele zilianza wakimaanisha polisi.

    Kama wasivyowapenda mgambo wa jiji ni hivyohivyo kwa askari polisi wasivyopendwa na chokoraa. Kwao ni kama



    sumu.

    Wakati mgambo huwasumbua chokoraa mchana, askari polisi katika doria zao huwasumbua viumbe hawa usiku.



    Hakuna anayewapa chokoraa nafasi ya kupumzika walau kidogo!!

    Sasa Mwanaidi anaonekana kufanana nao. Nywele zake fupi na mavazi yake yanamuingiza matatani. Sauti hizi



    zikawavuta wengine.

    Wakajisogeza eneo la tukio ili kujua nini kinatokea.

    George aliwazuia Isha na Frida kusogea eneo hilo la kelele. Yeye akajongea kushuhudia kuna nini.



    Heleni ikavutwa na kulichana sikio la Mwanaidi. Akapiga yowe la uchungu. Yowe kubwa sana. Yowe lililotetemesha



    ngoma za sikio la George. Akakaza mwendo na kufika eneo lile.

    Akapenyeza katikati akafika mbele. Kila aliyemuona George alijua kuna suluhu. Japo kwa muda alikuwa amehamia



    nyumba ya kupanga lakini bado mara kwa mara alikuwa akirejea kambini. Na siku hii pia alikuwa bado kambini hapo.

    Kila mtu akasubiri uamuzi wa George.

    “We ni nani?” akauliza kwa jazba, mkononi akiwa amekamata fimbo.

    “Naitwa Mwanaidi.” Alijibu yule binti huku akiwa amekaa chini akiugulia maumivu ya sikio lililokuwa linavuja



    damu.

    Jina hilo likamshtua George akainama na kumtazama.

    Hilo likawa kosa kubwa sana kwa chokoraa huyu mwenye uzoefu wa kutosha mtaani. Ule upenyo uliotumika



    kumwachia njia George apite akautumia kama nafasi ya wazi ya kufunga goli.

    George alikuwa amemshika mkono kumdhibiti asiweze kutoroka. Mwanaidi akajichezesha kidogo na kujidai



    anajikuna akachomoka na alichokihitaji. Kisu kidogo kikali cha kutahiria kilichohifadhiwa katika pindo la nguo yake.

    Ama kwa hakika ilikuwa ni lazima kwa namna yoyote binti huyu ajaribu kujihami. Chokoraa wanaweza kukuua bila



    kujuta. Wana hasira na maisha yao magumu, hawakuyapata malezi bora ya wazazi wala walezi na hata watu wazima



    wanaoitwa walimwengu hawakuweza kuwafunza lolote la kimaadili. Huenda angeendelea kulaza damu, angebakwa na



    kuibiwa kila kitu. Alipokumbuka kuwa ana jukunu la kumtafuta mama George, akili ikamchemka.

    Akamuweka katika rada huyu mwanaume mwembamba aliyemshika mkono.



    George ambaye hakujua nini kinaweza kutokea na kamwe asingeweza kutegemea. Alishtushwa na ubaridi fulani wenye



    ladha tamu isiyosimulika, lakini ladha ambayo haikudumu kwa muda mrefu ikageuka kuwa maumivu makali. Yowe



    kubwa likamtoka Bonge. Waliomzunguka wakasogea mbali naye bila kujua nini kimetokea.

    Hili likawa kosa la mwisho ambalo Mwanaidi alilisubiria. Chokoraa wakiwa katika taharuki ya ajabu kabisa.



    Chokoraa mwingine alitabasamu, na kisha kikafuata kitendo.

    Waliishia kubaki na viatu vyake pekee.

    Mwanaidi alitoka mbio za ajabu. Hakuna aliyeweza kumfikia.

    Laiti kama angejua kuwa yule muulizaji ni George ambaye asingeweza kumdhuru hata kama angekuwa upande wa



    makosa, basi angeweza kubaki. Lakini hakuyajua haya yote. Sasa alikuwa amemfyeka vyema mkono na kisu chake



    kikali. Amakweli usilolijua…..



    ****



    ****



    IKAWA kazi pevu ya Isha na Frida kumuuguza George ambaye alikuwa ana jeraha mkononi. Walitumia tiba za



    kuungaunga hapa na pale. Ilimradi aweze kupona.

    Licha ya kuwa na jeraha George aliendelea kuhangaika huku na huko. Na asubuhi iliyofuata majira ya saa mbili



    asubuhi alikuwa katika geti kubwa jeusi akiwa na rafiki yake wa mtaani. Alikuwa amempeleka mahali alipokuwa



    anafanya kazi. Alihitaji kazi hii pia

    Ndoo ikatolewa, ilikuwa na vinywaji mbalimbali baridi vilivyotolewa katika jokofu.

    “Utamuelekeza mwenzako inavyokuwa.” Mwanaume wa kiarabu alimuambia kijana aliyeambatana na George



    aliyejifunga kitambaa katika mkono wake.

    Baada ya kuvipanga vinywaji katika mkebe mdogo. Waliaga na kuingia mjini. Huku sasa ikawa shughuli ya kukimbilia



    magari ya abiria na kuwasihi wanunue vinywaji aidha maji ama juisi. Ilikuwa shughuli pevu hasahasa kwa George



    ambaye alikuwa anaianza.

    Alikuwa ana aibu kukariri sauti na maneno ‘Maji, sayona, Azam Cola, azam Mango’. Rafiki akaigundua aibu



    iliyomtwaa George. Akamvuta pembeni.

    “George wewe ni chokoraa, hauna thamani yoyote na hauna ndugu anayekutazama hapa duniani…usimuonee mtu



    yeyote aibu, pigana pigana kaka….aibu yako itakufanya ulale njaa kaka.” Yule rafiki yake alimwambia huku jasho



    likiwa linamtiririka usoni kutokana na jua kali sana kuwapiga. George alikuwa mnyonge sana huku kapu lake likiwa



    bado lina vinywaji vingi huku mwenzake akiwa anakaribia kumaliza.

    Jasho lililokuwa linamtiririka Roja lilikuwa funzo tosha kwa George. Akaukumbuka ule usemi katika maandiko



    ukisema mwanaume atakula kwa jasho.

    Ni kweli alikuwa amewahi kuokota vyuma, kuokota makopo tupu ya plastiki lakini sasa alikuwa katika kulitoa jasho



    jingine.

    George hakusema neno. Alitikisa kichwa na kuyakariri kichwani maneno ya Roja. “George wewe ni chokoraa, hauna



    thamani yoyote na hauna ndugu anayekutazama hapa duniani…usimuonee mtu yeyote aibu, pigana pigana kaka….aibu



    yako itakufanya ulale njaa kaka.”

    Yakamkaa vyema kichwani. Akayafanyia kazi.

    Baada ya siku mbili alikuwa mzoefu zaidi ya wengine. Ni kama alikuwa katika kazi hiyo kwa miaka miwili nyuma.

    George alijitoa ufahamu. Akasahau kabisa juu ya elimu aliyoipata ya chuo kikuu. Hata kama angeiwazia angevipata



    wapi vyeti vyake tena?? Aliamini kuwa aliyekuwa na mamlaka yote ni Emanuel na hakutaka kuonana naye tena.

    Mimi ni chokoraa natakiwa kuishi na chokoraa. Lilikuwa neno lake mara kwa mara. Neno hili likamjaza kiburi na



    ujasiri zaidi.

    Kilichosikitisha ni malipo. Unalipwa kadri ya mapato utakayoyawasilisha jioni kwa bosi. Mapato yakiwa kidogo na



    malipo yanakuwa kiduchu.

    Sala na maombi yote kwao waliendelea kulitaka jua zaidi kuliko mvua. Maana siku za mvua……wanajua wao.



    ****



    SIRI haiwezi kudumu milele.

    Mimba nayo haina dogo. Isipokuvimbisha tumbo upesi basi lazima tu itakuletea balaa jingine. Aidha kichefuchefu ama



    chuki juu ya kitu fulani.

    Kwa Frida ilikuwa afadhali yake tumbo lilikuwa kama hana siri sirini lakini kwa Isha mambo yalikuwa vingine.

    Tumbo lake liliwahi sana.

    Isha alipogundua hilo alizungumza na George kuhusu Frida. Itakuwaje akigundua kuwa ana mimba yake.

    Wakakubaliana asimtaje yeye bali asingizie lolote lile, ikiwezekana hata aisingizie kubakwa. Uongo huu ukabarikiwa.

    Siku iliyofuata, Isha akamuweka chokoraa mwenzake kitako.

    Akamueleza juu ya mimba aliyonayo. Frida akataharuki tofauti na mategemeo ya Isha.

    “Lakini ni ya nanii huyu….yaani sijui hata ni nani kwakweli..” alijikanyaga Isha. Frida akabaki kuwa kimya. Mshangao



    ukiendelea kumtafuna.

    Ilimchukua dakika mbili Frida kusema neno.

    “Mwenzangu..sasa itakuwaje hapo. Maana nashindwa hata nisemeje. Kwani ina miezi mingapi hadi sasa.”

    “Itakuwa miwili au..ni miwili.”

    Frida akashtuka tena, safari hii sasa akaamini kuwa huenda Isha alikuwa akiongea kwa niaba yake, maana kila kitu



    kilifanana.

    “We Isha jamani….yaani sijui hata nikuambiaje labda.”

    “Yaani we acha tu…mi mwenyewe sielewi hapa patakalikaje.”

    “Isha nina mimba pia.” Hatimaye Frida alisema kwa sauti ya chini sana.

    Ikawa zamu ya Isha kushtuka sasa. Kidogo atapike akajizuia kwa kipande cha limao.

    Lakini si kama ilivyokuwa kwa Frida. Waliendelea kuzungumza mengi huku kila mmoja akidai anahofia George akijua



    itakuwaje.

    Isha aliunga mkono hoja kinafiki. Maana George alikuwa anajua tayari kuhusu mimba yake na alikuwa ndiye



    muhusika mkuu.



    ****



    Mwanaidi alikuwa ndani ya chumba chake, akijisafisha sikio lake ambalo lilikuwa limejeruhiwa siku kadhaa nyuma.



    Wakati anakitazama kioo kilichokuwa kikimsaidia kuliona sikio lake, alirejewa na kumbukumbu juu ya mwanamke



    ambaye alimsaidia kuongeza kasi yake ya kukimbia baada ya kuwa amechoka.

    Anakumbuka kuwa aliwahi kumuona mahali.

    Feri? Posta? Kigogo? Koko Beach? Hayo yalikuwa maswali makuu aliyokuwa anajiuliza. Hakupata jawabu. Japo



    ulikuwa ni usiku bado aliweza kumuona kiasi kidogo.

    Akakuna kichwa chake na kuachana na jinamizi hilo linalomkabili.

    Maajabu, bado aliendelea kuhangaishwa na sura hiyo.

    Akajilaza katika godoro lake sakafuni akaanza tena kufikiria upya.

    Sasa akaijenga picha kisha akatabasamu.

    “Kumbe namuwaza mama yake George?” alisema kisha akacheka. Ile sura aliyodhani ameiona gizani ilikuwa ni ya



    mama George.

    Akaendelea na shughuli zake huku akipuuzia mawazo yale.

    Laiti kama angekuwa mlemavu hapo sawa. Yule mwanamke anakimbia balaa, sijui alikuwa anataka nini kwangu au



    kichaa yule? Alijiuliza Mwanaidi.

    Lakini amenisaidia kukimbia kwakweli. Alikiri.

    Usiku huu ambao Mwanaidi alikuwa akiwaza haya.

    Mjeruhiwa wa kisu kile alikuwa akilitazama jeraha lake lililokosa huduma bora. Wakati analitazama akawa anawaza



    juu ya maongezi yake na Isha juu ya kutoa mimba.

    Alijiuliza yule msichana atayachukulia vipi maamuzi haya magumu. Je atakubaliana na hali hiyo ama ataweka ngumu?



    Hayo yalikuwa maswali.

    George alikiri moyoni kuwa alikuwa akimuhitaji sana mtoto lakini atamtunza vipi? Hilo lilikuwa tatizo.

    Japo ilimuuma sana, akaamua kuheshimu ule usemi wa ‘Heri nusu shari kuliko shari kamili’. Akaamua kuchukua



    maamuzi na usiku huu aliamua kwa namna yoyote ile kumshawishi Isha akubali wafanye mpango wa kuitoa mimba.

    Sasa alikuwa mlangoni, moyo ukawa mzito sana kwa maamuzi yale lakini hakuwa na namna ya kujizuia.

    George aliingia hatimaye, akapokelewa na ukimya mkubwa. Frida na Isha walikuwa hoi kwa usingizi.

    Alitamani amuamshe Isha ili waweze kuongea kuhusu jambo alilokuwa amefikiria. Lakini akahofia kumsumbua na pia



    akahisi kuwa hatakuwa na umakini mkubwa wa kuelewa kutokana na kuelemewa na usingizi.

    George akalala, kutokana na mawazo mengi yaliyohitaji maamuzi yake, alijikuta akilala fofofo.

    Alipokuja kushtuka alikutana na miale ya jua ikimaanisha ni muda umepita tangu mapambazuko yaingie.

    Akayapikicha macho yake aweze kuona mbele vyema. Akakutana na kiwiliwili kimoja kikiwa bado kimelala. Alikuwa



    ni Isha.

    Akamuamsha ili aweze kuzungumza naye kabla Frida hajarejea kutoka popote alipoelekea.

    Isha akaamka huku akisumbuliwa na mang’amung’amu ya usingizi.

    George akalazimisha tabasamu. Isha akalipokea.

    “Nahitaji tuzungumze Isha.” George alimwambia kwa sauti ya upole. Isha akajiweka sawa katika mkeka aweze



    kumsikiliza vizuri.

    “Frida yupo wapi?” aliuliza Isha, baada ya kujiweka vyema.

    “Nikuulize wewe hapo uliyelala naye.”

    Isha hakuwa na cha kujibu na mazungumzo hayo yakasahaulika.

    George akaingiza mada zake. Akajizungusha mbali sana akiweka busara anazojua yeye ilimradi kuhalalisha



    visivyokuwa halali.

    Akafikia lengo lake hatimaye. Akamueleza Isha juu ya kuitoa ile mimba. Hapo Isha akasimama wima mtoto huyu wa



    kizaramo, akashika kiuno. Akaanza kuwaka, George akajaribu kumpooza hakufanikiwa kitu.

    Isha akazungumza mengi sana huku akimlaumu George kuwa ni mgandamizaji tena muonevu mkubwa.

    Katika kulalamika huko hasira ikapanda sana, ule ubaya wa kauli ya ‘hasira hasara’ ukachukua nafasi. Hasara ikaingia



    kati. Isha akajikuta akimtaja Frida katika mazungumzo yake, akafichua siri ya Frida kuwa na mimba bila yeye



    mwenyewe kujua kama amefichua siri.

    George akashtushwa na kauli hiyo.

    “Frida ana mimba??” aliuliza, hakujibiwa badala yake wote wakajikuta wapo kimya.

    George aliwahi kujifunza kidogo juu ya saikolojia ya mwanadamu alipokuwa katika masomo yake chuoni. Upesi



    alimsoma Isha akagundua kuwa alikuwa katika kujutia alichosema na sasa alikuwa anajaribu kukificha.

    George akakazania swali lake. Isha hakuwa na jinsi akamueleza George ukweli kuwa Frida ni mjamzito.

    Hapo sasa, kwa pamoja wakajiuliza.

    “Yupo wapi?” hakuna aliyemjibu mwenzake.



    ****



    Wakati wawili hawa wakilumbana na hatimaye kufikia kumwongelea Frida. Muongelewa alikuwa katika kuwania



    kupanda pantoni ambalo lilikuwa linapiga honi za mwisho za kuondoka kivukoni.

    Bahati nzuri aliliwahi pantoni lile.

    Hakuwa na uhakika sana ni wapi alikuwa anataka kwenda lakini alijikuta tu anaelekea katika pantoni.

    Ndani ya pantoni lile Frida alikuwa akijiuliza mengi sana.

    Alijihakikishia kuwa yupo sawa kabisa kuamua kuondoka katika makazi yale bila kuaga.

    Aliamini kwa namna yoyote ile Isha atamshirikisha George juu ya mimba yake.

    Frida aliamini fika George atajisikia vibaya sana akigundua jambo hilo na kama hiyo haitoshi atakuwa amebebeshwa



    mzigo mkubwa sana.

    Mzigo wa kulea mimba mbili.

    Uamuzi wa kuondoka bila kuaga akaubariki.

    Lakini hakujua anaelekea wapi hilo lilikuwa tatizo.

    Baadaye akakumbuka zile tenda za kuwafulia wanafunzi nguo. Hapo akili ikasogeleana na kukumbuka nia yake.

    Alikuwa ameamua kujipatia kipato kama alivyokuwa anafanya awali.

    Pantoni ndio kwanza lilikuwa limeanza kuondoka, mahali alipokuwa amekaa Frida palikuwa na familia ambayo kwa



    mtazamo wa haraka ilikuwa inaelekea aidha ufukweni ama katika sherehe fulani.

    Frida alivutiwa na mtoto mdogo aliyekuwa amesimama huku akicheza kwa furaha nawenzake. Frida akajifananisha na



    mtoto huyo mwenye malezi ya wazazi wawili. Akamshika mkono akawa anauchezea huku akivuta picha nyuma,



    ikajijenga picha ya kuzaliwa gerezani, mama yake anakufa akiwa katika kifungo, anasoma akiwa anaishi kwa mkuu wa



    gereza.

    Anafukuzwa pasipo na makosa, anageuzwa mtumwa wa ngono na mkuu wa kituo cha yatima, anabebeshwa mimba,



    anaitoa kwa uchungu mkub wa, mara mbili anawekwa rumande na kisha kuachiwa, anabakwa hovyo. Anadharaulika na



    sasa ana mimba tena.

    Kilio cha yule mtoto mdogo kinamshtua, anajarib u kuyafunua macho yake yanashindwa kuona mbele. Sasa akagundua



    kumbe yule mtoto alikuwa analia baada ya yeye kuanza kulia.

    Mara yule mtoto akanyakuliwa kutoka katika mikono yake na wazazi wake. Frida akauhisi upweke wa hali ya juu.



    Akajipa jibu moja kuwa vikwazo alivyokuwa anapitia ni njia ya kumuonyesha kuwa hakustahili kuishi katika



    ulimwengu huu. Basi tu alikuja kwa bahati mbaya. Walioletwa kwa maksudi mazuri walikuwa wanaishi maisha ya



    kupendeza.

    Hasira, chuki na mfadhaiko. Vyote vikamuelemea Frida.

    Pepo la kukata tamaa likamnyanyua juu juu. Yule pepo wa umauti akafanya msaada wa ajabu wa kumpatia Frida



    nguvu. Akajitoa pale alipo akajirusha majini kabla pantoni halijakimaliza kivuko.

    Kila mtu mdomo wazi wakati anatapatapa kwenye maji ili kukamilisha ule usemi wa mfa maji haishi kutapatapa.

    Nani ajirushe ndani ya maji haya kumuokoa yatima huyu?

    Hakuna hata mmoja. Akina mama waliishia kupiga kelele, kelele zisizokuwa na manufaa.

    Hata wanaume nao walitulia tuli bila kufanya jitihada zozote.



    Frida akapanda juu kwa mara ya kwanza, akazama akaibuka tena kwa mara ya pili.

    Hapo sasa likatokea tukio la maajabu mengine. Kiwiliwili kilichokuwa ndani ya nguo mpya zilizong’ara. Kilijichomoa



    katika kundi la watu kisha kikapaa hewani na kutua katika maji.

    Filamu ya kushangaza.

    Waliofika upande wa pili wa kivuko. Walingoja sana kumshuhudia huyo aliyekuwa amejirusha katika maji ni nani na



    huyo aliyejirusha kwa mara ya pili ni nani.

    Hawakutokea.





    ****



    Mwanaidi alikuwa anaufurahia mchezo aliokuwa anaufanya kwa rafiki yake wa mtaani. Alifurahi sana kumfuatilia bila



    kumpoteza, kila mara alitaka kumshtua lakini akaendelea kuvuta subira.

    Moyoni alikuwa na furaha sana kwa ushuhuda huu, hakutegemea kuonana naye kwa wepesi hivyo.

    Sasa alikuwa anapiga hatua nyuma yake bila mlengwa kuelewa nini kinaendelea.

    Walianzia Kariakoo, kwa miguu hadi Posta, bado kamchezo kakaendelea wakafika feri. Wakakata tiketi wakaingia



    katika ukumbi mpana wa kungoja pantone kutoka ng’ambo ya pili. Wakajituliza hapa, Mwanaidi bado alikuwa makini



    sana kumfuatilia rafiki yake huyu. Hakutaka kumpoteza. Na pia hakutaka ajulikane kama anamfuatilia.

    Sasa aliamini kumfuatilia huku kulikuwa kumetosha na alijiahidi kuwa wakati wa kushuka katika pantoni atawahi



    kushuka chini ili aweze kumshangaza mwenzake.

    Wakiwa ndani ya pantoni alimwangalia kwa kuibia ibia rafiki yake hadi pale alipoanza kulia kwa uchungu.

    Mwanaidi alitambua kuwa huu ulikuwa uchungu wa maisha magumu ya kutengwa. Maisha ya uchokoraa.

    “Leo ni mwisho wa kilio hiki ee Mungu tutazame wanao.” Mwanaidi alifanya dua hiyo fupi.

    Kisha akairefusha zaidi, na yeye machozi yalikuwa yanamtoka sasa, alikuwa akijisitiri na kitambaa cha mkononi.



    Alikuwa katika uchungu mkuu.

    Alipomaliza sala yake ya kuwaombea yatima. Akayafumbua macho yake kwa tabu. Kelele za akina mama zilimshtua,



    akadhani pantoni linazama, mara akadhani kuna mtu amekufa.

    Mara akaona macho yote yakitazama majini, na yeye akatazama lakini hakuona kitu.

    Akiwa bado anashangashangaa mara alisukumwa kwa kishindo kikubwa akaanguka chini. Yule mtu aliyemsukuma



    kama mwendawazimu vile akajirusha majini.

    Mwanaidi kuja kusimama tena hakupata nafasi ya kuangalia majini.

    Akaangaza huku na huko. Hakumuona Frida.

    Akajaribu kutelemsha ngazi za pantoni. Bado hakumuona Frida wala mtu anayefanana naye, wasiwasi ukatanda



    akajiuliza amekwenda wapi? Ule utani wake ukaanza kumtafuna. Akajuta kuchelewa kumkabili Frida.

    Mwanaidi akawahi kuwa wa kwanza kushuka katika pantoni kisha akakaa katika mlango wa kutokea akawa makini



    kutazama wanaotoka. Umakini wake mkubwa haukusaidia kitu hakumuona Frida.

    “Kwani nini kimetokea?” hatimaye aliwauliza watu waliokuwa wanashangaa majini.

    “Kuna dada amejirusha ndani maji. Sijui kama amepona.”

    “He, mdada yukoje?”

    “Nenda majini ukamtafute labda.” Alijibiwa jibu lililojaa sanifu.

    Mwanaidi anachanganyikiwa. Hajui nini cha kufanya. Hisia kuwa kile kilio alichotoa Frida kilikuwa cha mwisho



    katika ulimwengu huu zilimshambulia na hakutaka kudumu katika hilo wazo.

    Akili ikashindwa kufanya kazi ipasavyo.

    Hakuwa na mwingine wa kumlilia aweze kumsaidia kimawazo.

    Kama alivyobarikiwa kipaji cha kufikiri upesi, akafanya maamuzi. Akawafikia chokoraa wa feri ambao hutumia muda



    wao mwingi kuogelea katika bahari ya hindi.

    Pesa ikaongea akawasihi warejee na yule binti.

    Vijana wanne wakazama majini, kama samaki, wakaibukia mbali.

    Pesa iliwasukuma.



    ****



    Jitihada zilizofanywa na wale vijana waliokuwa wamekubaliana bei na Mwanaidi, hazikuzaa matunda, hapa sasa



    Mwanaidi akazidi kuhamanika, alijiona yu katika hatia ya waziwazi kwa kosa la kumchezea shere Frida hadi



    kumwingiza katika mauti hayo.

    Mchelea mwana kulia hakika hulia mwenyewe. Sasa Mwanaidi alikuwa katika majuto makuu. Alikuwa ameichezea



    nafasi ya kuonana na Frida.

    Alisubiri sana walau aweze kuuona mwili wa Frida, lakini hata harakati za kumuibua kutoka majini hazikufanyika.



    Alikuwa na jina gani hadi ashtue vichwa vya watu, waache kazi zao na kuja kumtafuta??

    Hakuwa na lolote, hata roho yake pia haikuwa na lolote lile.

    Majira ya saa moja usiku, Mwanaidi aliyashika maji ya bahari. Kwa imani yake ndogo akamuombea alazwe pema



    peponi.

    Machozi yake yakachukuliwa na bahari ile ambayo aliamini ilikuwa imemmeza rafiki yake. Bahari isiyokuwa na



    huruma, inameza hadi machokoraa.



    ****



    Wakati Mwanaidi analia na bahari, Isha na George walikuwa wamegeuziana migongo, kila mmoja akiwaza lake.



    Walikuwa wamezunguka sana bila kupata walau tetesi za Frida kuonekana.

    Isha alikuwa ameuvuta mdomo wake baada ya George kuwa amemlaumu sana kwa kuchelewa kumweleza juu ya Frida



    kuwa mjamzito. Licha ya Isha kujitetea kuwa hakuwa akijua lolote hadi Frida alipomweleza mwenyewe bado George



    aliendelea kulalamika, sasa Isha ambaye alikuwa amebeba mtoto wa George tumboni alifikia hatua ya kununa.

    George ambaye alikuwa anamuwaza Frida hakuwa tayari kumwomba msamaha Isha. Mtafaruku!!

    Usiku ukapita huku kila mmoja akijiona yupo sahihi.

    Palipokucha, zile baraka walizopewa wanawake wachache zikajionyesha kwa Isha. Akajishusha na kumchangamkia



    George. George akashindwa kuendelea kuwa kimya. akazungumza

    Amani ikarejea!!

    Sasa waliweza kuzungumza tena!.

    Juma zima likakatika bila Frida kuonekana. Walijadiliana kwenda kutoa taarifa polisi lakini hata kabla ya kukubaliana



    wakatambua kuwa hawatapata msaada wowote huko. Waliamini kuwa hawakuwa wakithaminiwa na jamii. Hizo ndizo



    hisia halisi za Chokoraa, hata siku moja haamini kama ana usawa na wanadamu wengine. Wao huamini kuwa wapo



    katika dunia yao ya kipekee. Dunia iliyojaa mateso, dhiki na manyanyaso.

    Hawakwenda kutoa taarifa!

    Walisubiri muujiza.



    ****



    UPARA wake kichwani haukutangaza umasikini, bali utajiri wa hali ya juu. Tumbo lake liliunda mfano wa kijimlima



    kidogo, kilichonakishiwa kwa jina la kitambi. Alikuwa akilikuna tumbo hilo kwa ujivuni wa hali ya juu.

    Mlango ulipogongwa alikuwa anatazama taarifa ya habari ya asubuhi.

    “Nani?” aliuliza. Badala ya kujibiwa, magazeti mbalimbali ya siku hiyo yalipitishwa chini ya mlango.

    “Karume za asubuhi bwana!” alisalimia mzee huyu, alitambua tayari ni nani aliyeugonga mlango huo.

    Mkewe alipopita pale sebuleni alimuagiza amchukulie yale magazeti.



    Siasa ilikuwa imemkaa kichwani na kwa siku za usoni alikuwa amefikilia kugombea udiwani ama ubunge kama



    ikiwezekana.

    Kama ilivyo kawaida magazeti ya udaku ambayo ni magazeti pendwa kwa mkewe na mwanaye wa kike akayaweka



    kando. Akapekua yale ya siasa. Akaanza kuyapitia moja baada ya jingine.

    Huyu Kasuku ana nini leo! Alijiuliza mzee Mathias huku akifanya tabasamu hafifu, akajiweka sawa katika sofa



    akaiweka sawa miwani yake.

    Kila mara alipoliona hilo jina alikuwa akimfikiria Kasuku wake ambaye kila asubuhi alikuwa akimuamsha kwa



    kumuita ‘bosi’.

    Kasuku huyu wa gazetini yeye alikuwa akimuamsha akili yake kwa kumfungua mengi yanayotokea katika jamii na



    yeye hayatambui.

    “MTANZAGIZA GIZANI, MWONYESHE NJIA EWE MWENYE MACHO” Kilisomeka hivyo kichwa cha habari.



    Mathiasi akacheka kwa sauti ya juu kidogo, kisha akajisemea “Kuna watu wabunifu…sasa hapa lazima mtu usome



    utake usitake…ama kweli kasuku huyu.”

    Makala iliyoanza kwa kichwa cha habari chenye mashiko, ilianza kutiririka. Makala hii ilimzungumzia binti aliyekata



    tamaa na kuilaumu serikali kwa kutowajali yatima, binti huyu aliyejiita mtanzagiza bila kutaja jina lake halisi alizidi



    kulaumu wale wote wenye uwezo wa kuwasaidia watoto yatima lakini wanawafumbia macho na kuwatukana kisha



    kuwanyayasa kila siku.

    “Sijawahi kucheka kwa furaha, sijui mama yangu aliikosea nini Tanzania. Kwa nini wananifumbia macho, kila mahali



    sikubaliki, ama kwa kuwa katika jina langu kuna nyongeza ya majina mengine mawili, yatima na chokoraa? Ama kwa



    kuwa si msomi na siwezi kusimama mbele ya watu kuzungumza?

    Tanzania inaninyanyasa.

    Mimba yangu ilipatikana mama yangu akiwa huru, ikakua akiwa gerezani. Nimezaliwa na kuwa mtoto wa gereza.



    Mtoto huru bila kosa anayelelewa na gereza. Mama yangu alidhalilishwa nikishuhudia kwa jicho langu. Nilipokuwa na



    kuufikisha umri wa shule nilisomea shule iliyopo jirani na mwalimu alikuwa akiniita mtoto wa gereza pale



    nilipomkosea.

    Mama yule anayetumikia kifungo cha miaka mingi aliugua!! Nilishuhudia huduma mbovu alizokuwa anapewa!!



    Hakuna aliyemjali hatimaye akaaga dunia huku akiita CHOKORAA!!

    Mkuu wa gereza akanitwaa na kunilea nikiwa mmoja wa familia yake!! Watoto wake walinitenga, walinitukana



    walivyotaka!! Nilinyimwa chakula na hakuna aliyejali!! Nilipojaribu kulalamika nilipigwa sana kichwani. Hata chanzo



    cha kufeli masomo yangu ni mateso haya!!

    Walitafuta mbinu ya kunifukuza licha ya kuwanyenyekea!!

    Hatimaye wakaipata sababu!! Ni mimba mimba!!! Mimba aliyopata mtoto wa mkuu wa gereza!! Nikaambiwa nahusika



    nayo!!

    Kwa amri yake nikawekwa gerezani. Chumba kile ambacho marehemu mama aliishi!! Baada ya miezi sita nikaachiwa



    huru!!

    Sasa baada ya miaka kadhaa nikaingia mtaani. Mtaa nisioufahamu. Mtaa ambao haunifahamu pia!! Bila ndugu bila



    rafiki nikaingia mtaani!!!

    Niliyakumbuka maneno ya mama yangu!! Aliniita CHOKORAA. Sasa nikawa chokoraa rasmi lakini CHOKORAA



    MWENYE CHUKI, KISASI NA ALIYEKATA TAMAA!!

    Maneno haya makali yakamgusa Mathiasi, lile tabasamu lake likafutika kabisa, mawazo juu ya kumfananisha



    mwandishi na kasuku wake yakafutika mara moja. Akashtushwa na matone yaliyodondoka katika ile kurasa.

    Mathiasi alikuwa analia!!

    Akashangaa, haijawahi kutokea katika ukubwa wake kutokwa na machozi. Hata misibani alikuwa anavaa uso wa



    huzuni lakini kamwe sio kutokwa machozi.

    Iweje leo analizwa na makala hii. Akajikuta akihisi amewahi kumuona huyu binti aliyemsoma. Ni wapi lakini amewahi



    kumuona sasa?

    Akakumbuka ni katika vituo vya watoto yatima ambavyo huwa anaenda kwa ajili ya kutoa misaada huku moyoni



    akijua huo msaada malipo yake ni yapi.

    Mathiasi alikuwa akichukua watoto yatima wenye vipaji kwa ajili ya kuwasomesha nje ya nchi lakini kamwe



    hawakurejea. Na ni nani wa kuuliza wapi walipo watoto hao?

    Walikufa na kutupwa kama mizoga huko wanapopelekwa kwa danganya toto ya kusomeshwa.

    Mathias alikuwa ni ‘zungu la unga’ na alikuwa akiwatumia watoto yatima na machokoraa katika kusafirisha madawa



    ya kulevya. Hakuwa na huruma kwao, alichoangalia yeye ni masilahi yake.

    Sasa alikuwa na pesa nyingi sana na alikuwa anaendelea na biashara ile haramu. Biashara iliyokuwa inaondoka na roho



    za watoto wasio na hatia. Watoto wanaotumikia dhambi ya wazazi wao. Watoto wasioelezeka kwa neno moja. Walitia



    huruma!!



    Iweje sasa leo anatoa machozi kwa maneno ya mtu ambaye hajawahi kumuona hapo kabla. Mtu amabye hayajui



    matendo yake maovu? Aliduwaa.

    Akatamani kujificha. Ni kama yule mwandishi na muhusika wa hiyo makala walikuwa wanamtazama. Mathiasi



    akajihisi kupatwa na hofu. Hofu akiwa katika himaya yake, himaya iliyojengwa kwa damu ya yatima na chokoraa.



    Mzee huyu akapatwa na ubaridi wa hali ya juu.

    Mara akajikuta akinakiri namba ya Kasuku, akabonyeza kitufe cha kupiga simu ikaita. Ikapokelewa upesi wakati



    Mathias hajajiandaa nini cha kusema.

    “Bwana Mathiasi naongea…..hongera kwa makala yako nzuri bwana Kasuku.”

    “Asante sana, Mathiasi….”

    “Mtanzagiza ndo nani natamani kuonana naye sana.”

    “Upo maeneo gani?” iliuliza sauti ya Kasuku.

    “Mbweni Masaiti lakini mara kwa mara nakuwa Kariakoo….hata hapo ofisini kwenu huwa nafika. Kuna sijui



    umewahi kuniona?” alizungumza bila kituo bwana Mathias.

    “Hapana sijawahi kwani unafanya kazi hapa.”

    “Hapana nilikuja kwa ajili ya mahojiano…kuhusu watoto yatima.”

    “Ohoooo!! Bwana Mathiasi Dembele!! Bila shaka.”

    “Ewalaaa!! Ndio mimi, ni wapi naweza kumpata mtanzagiza?”

    “Nipo naye maeneo ya huku Tandika ndio nyumbani kwangu. Karibu bwana Dembele karibu sana.”

    Waliagana baada ya kupeana ahadi ya kuonana.

    Simu ilipokatika. Upande wa Mathias alishusha pumzi kwa nguvu huku akiwa bado hajajielewa nia yake.



    Upande wa bwana Kasuku, alichanua tabasamu pana.

    Frida aliyekuwa pembeni yake alimtazama kwa macho ya kitafiti.

    “Nilikwambia..haooo wameanza kupiga simu…ile simulizi yako lazima kwa mwanadamu mwenye nyama aguswe



    ipasavyo. Huyu aliyepiga simu ni mmoja kati ya wadau wakubwa hapa nchini kwa kuwezesha yatima.” Alisema bwana



    Kasuku huku akinyanyua mabega yake juu.

    “Anakuja kesho jioni utamuona. Usimuogope kuwa muwazi. Atakusaidia amini Frida amini kuwa bado unao



    umuhimu mkubwa sana katika hii jamii. Jiamini kuwa Tanzania inakuhitaji sana.” Kasuku alisisitiza.

    Frida alijenga tumaini jipya baada ya kusikia kuwa atakutanishwa na muwezeshaji wa yatima na watoto wasiokuwa na



    makazi.







    Muda mwingi Frida alikuwa akizungumza na Kasuku mambo mbalimbali ambayo yalimjenga tena kisaikolojia.

    “Frida..hutakiwi kuwa mtu wa kukata tamaa, ni kweli maisha ya mtaani yana kero kubwa lakini jiulize, mfano sasa u



    mjamzito. Ulitaka kukiua hicho kiumbe bila kosa. Ni upendo gani unao wewe hadi kufikia kuiua damu yako?? Lazima



    ujifikirie na iwapo ni sahihi basi wasilaumiwe wale waliowatupa watoto wao, asilaumiwe mama aliyekuzaa akiwa



    gerezani na hata mkuu wa gereza, mkuu wa kituo cha watoto yatima wote wasilaumiwe. Wapo sawa.” Maneno haya



    makali na yenye kuuweka ukweli wazi yalimgusa sana Frida. Sasa akajutia kitendo chake cha kujaribu kujitosa majini



    ili aweze kufa.

    “Hivi ulijifikiria nini na wewe ukajirusha baharini. Ungekufa je?” hatimaye alimuuliza huku akitabasamu, kana



    kwamba haamini kabisa kuwa inawezekana mwanadamu wa kawaida kujitosa majini kwa ajili ya kumwokoa mtu.

    “Ni kiherehere changu tu, naitwa Kasuku napenda kujua mengi hata yasiyonihusu.” Alijibu kwa sauti iliyojaa utani.



    Wakacheka kisha kugonganisha mikono.

    Wakati wakifanya hayo, jicho kali sana liliwatazama bila wao kujua kama wametazamwa. Jicho hili likafanya tafsiri ya



    kuchezewa shere ama kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa. Wivu ukatambaa na kuusulubisha moyo wake wa



    nyama.

    Furaha ya Kasuku na Frida haikumpendeza.

    Akakimbilia chumbani, kukiwahi kilio chake kisiweze kusikiwa na wengi.

    Akiwa chumbani binti huyu alijikuta akiilaani kazi aliyokuwa anaifanya Kasuku, kazi ya uandishi wa habari. Kwani



    kazi hii ilimfanya kukutana na wanawake wengi tena wenye mvuto kumshinda yeye.

    “Emiliana amka amka umelala..” aliongea maneno hayo huku akijipigapiga kichwa chake. Hakika alikuwa amelala.



    Analetewa mwanamke nyumbani kwake!!

    Hisia potofu zikamtuma kuwa Frida na Kasuku wana mahusiano na wanatumia kigezo cha uandishi wa makala



    kuficha maovu yao.

    Emiliana alikuwa na haki ya kulalamika, alikuwa na haki ya kuwa na wivu. Mara ya kwanza alimkuta Kasuku akiwa



    anambembeleza yule binti tena akiwa amemlaza mapajani.

    Mara ya pili akaenda naye kumfanyia manunuzi ya nguo. Tena nzurinzuri zilizoufanya urembo wake uanze kuonekana.



    Na zile nywele zenye asili ya kiarabu kwa mbali zikang’ara.

    Sasa amewafumania wakicheka kisha wakagonga mikono.

    Hata!! Wanafahamiana hawa, tena siku nyingi. Alipitisha jibu hilo binti huyu ambaye ndio kwanza alikuwa anakaribia



    kufunga ndoa na Kasuku. Mwandishi wa habari na makala katika magazeti.

    Leo namweleza kila kitu!!

    Ulipofika wakati wa chakula cha mchana, Emmy akiwa analazimisha tabasamu usoni alimwandalia mumewe



    mtarajiwa chakula chumbani badala ya meza ya kulia kama ilivyo kawaida.

    Meza kuu akasalia Frida peke yake. Hilo halikumuumiza kichwa.

    Huko chumbani Emmy akautua uchungu wake!!

    “Kwa hiyo kuna mawili Kasuku, aidha niondoke ama huyo hawara yako aiache nyumba hii. Msaada uliompatia



    imetosha. Iam not mtoto mdogo ujue.” Alipandisha jazba, Kasuku akaamua kuyatatua haya kwa busara. Alijua yale ni



    mapenzi tu na si kwamba Emmy ana roho mbaya.

    “Ataondoka mpenzi usijali!!” alikubali yaishe.

    “Lini?”

    “Nimekwambia usijali.” Alizungumza kwa hasira kiasi, hakupendezwa na yale maswali ya mahakamani.

    Chakula hakikulika tena.

    Kasuku aliporejea mezani ili kuzungumza na Frida. Tayari muda wa kumpokea mgeni ulikuwa umefika.

    Ni kama alikuwa mzungu mwenye ngozi nyeusi bwana Mathias.

    Alifika kwa wakati. Akapokelewa.

    Furaha ya Kasuku ikarejea kiasi fulani.

    Walifika nyumbani na kuingia moja kwa moja katika mazungumzo.

    Walizungumza mengi sana. Mathias Dembele akionekana kuguswa sana na yaliyomtokea Frida.

    Kwa kumtazama mbele yake hakuamini kama kweli yule ni chokoraa. Alikuwa amependeza tena kwa hizo siku kadhaa



    alizoishi kwa Kasuku.

    Baadaye Kasuku ili kupata ushauri aliamua kumuelezea Mathiasi juu ya tatizo la mchumba wake.

    “Hiyo ni kawaida ya wanawake. Ila anyway usijali, naweza kukusaidia bwana Kasuku. Nitampeleka mahali kama



    utaniruhusu. Nimeguswa sana.” Mathias alitoa kauli ambayo ilimpa ahueni Kasuku.

    Wakati wa kuondoka waliandamana na Frida.

    Akahakikishiwa kuwa yu katika mikono salama.

    Mikono ya Mathias Dembele.



    ****



    Nyumba kubwa ya kifahari iliyozungushiwa uzio unaodhibitiwa na umeme ilimshangaza mwanadada Frida. Nyumba



    hizi alizoea kuziona mandhari yake ya nje tu maeneo ya posta na kwingineko Kariakoo.

    Baada ya kengele kubonyezwa geti lilifunguliwa.

    Gari ikazama ndani!! Injini ikazimwa. Wakashuka.

    Kimya kikubwa kilikuwa kimetanda, ndege aina ya kasuku akawapokea kwa shangwe. Mathias akachekelea kuitwa



    bosi na yule kasuku.

    Akamshika kichwa kasuku akajichekesha. Frida naye akacheka.

    Maajabu haya ndege anaongea!!

    Mlango ulikuwa wazi, akakaribishwa, ndani aliwakuta watu wawili wanaume. Wakatoa tabasamu na kumkaribisha



    kwa Kiswahili kibovu. Baada ya hapo hakujua linaloendelea maana walikuwa wakiongea lugha ya kigeni.

    Frida akawa mgeni katika hili.



    Kisha mathias akamvuta kando wakanong’ona kidogo. Mathias akatoweka, Frida akabaki na wenyeji wasioelewa



    Kiswahili.

    Frida akatamani kuwa mtaani alale nje usiku kuliko kuishi mahali pazuri bila kuwa na amani.



    ****



    Mwanaidi baada ya kuwa amempoteza Frida katika mazingira ya kustaajabisha. Sasa aliikumbuka furaha yake nyingine



    iliyosahaulika.

    Alimkumbuka mama yake George. Ile sura aliyokutana nayo usiku ule ikamkimbiza haikutaka kutoweka katika



    ubongo wake. Akajiuliza kwa nini iwe hivyo.

    Kwa mara nyingine akaamua kurejea katika maeneo yale. Sasa alikuwa anaulizia kwa kila namna aliyoweza.

    Kuhusu mama mlemavu hapo hakuambulia kitu.

    Lakini mama kichaa, hapa majibu kadhaa yalikuwepo.

    “Yule si ndo aliyechukuliwa na Dembele au?” alijibu bwana mmoja kwa njia ya kuwauliza wenzake.

    Wote wakakubaliana kuwa ni kweli. Frida akawalipa pesa kwa malipo ya kuuliza na kujibiwa.

    Hapo ndiyo Dar es salaam!! Kila kitu ni biashara.

    Malipo yaliyofuata ni kupelekwa nyumbani kwa Dembele.

    Mwanaidi akapatazama siku hiyo lakini hakuingia nia yake ilikuwa kumfahamu kwanza Dembele.

    Alikuwa maarufu haikumchukua muda kumfahamu baada tu ya kupita na gari lake.

    Kama ilivyo kawaida yake, hakurupuki anafanya mambo kwa hatua.

    Alianza rasmi kuzifuatilia nyendo za Dembele. Hatimaye akapata nafasi ya kuingia kwake kama msichana anayetafuta



    kazi. Aliingia akiwa anatambua fika kuwa Dembele hayupo nyumbani.

    Japo hakupata kazi. Hata huyo mama anayesadikiwa kuchukuliwa na Dembele hakuweza kumuona pia.

    Duniani hakuna siri, katika harakati zake za kumfuatilia bwana huyu alizipata habari za juu juu kuwa bwana Mathias



    ni ‘zungu la unga’. Tetesi hizi zikamkuna. Akahisi kuna jambo.

    Hatua iliyofuata ni kuonana moja kwa moja na Mathiasi Dembele, lakini katika njia ya siri sana.

    Subira yavuta heri. Siku ikawadia aliyoingoja Mwanaidi.

    Mathias Dembele alikuwa analewa na rafiki zake.

    Mwanaidi akaivaa fani ya uigizaji, akayaigiza maisha yake halisi ya uchokoraa. Akamvamia Dembele huku akiwa na



    huzuni, akamlilia sana akalia akiuhitaji msaada wake. Kwa kilio chake hata walevi walishikwa na huruma.

    Mathias Dembele akauvaa mkenge.

    Akakatisha shughuli ya kujiongezea ulevi kichwani.

    Akamchukua Mwanaidi hadi garini.

    Akaaga na kuondoka naye. Mwanaidi akaombea mahesabu yake yaende sawa. Alikuwa na ile silaha yake ya kila siku ya



    kujilinda.

    Kisu!!



    ****



    Suala la Frida kuwa mjamzito na mzigo mkubwa uliokuwepo kwa ajili ya kusafirishwa kuelekea ughaibuni



    lilimuumiza kichwa Mathiasi. Ni kweli aliguswa sana na maisha aliyopitia Frida lakini baada ya kumweka katika



    himaya yake ile huruma ikatoweka akawa Mathias yuleyule.

    Alijiuliza ni wapi anaweza kupata mtu wa upesiupesi kuubeba mzigo ule. Sasa bahati ikajileta mbele yake.

    Akakutana na binti aliyepevuka katika kilabu cha walevi.

    Mwanaidi!!

    Kwa umbo lake komavu aliamini kuwa anaweza kubeba kete kadhaa za madawa ya kulevya bila wasiwasi.

    Kisha hiyo inakuwa safari yake ya mwisho maana akirejea Tanzania atazua tafrani.

    Mbebaji aliyeruhusiwa kwenda Tanzania na kurudi alikuwa ni mmoja tu. Mwanamke mnene asiyekuwa na akili



    timamu. Huyu hata akiachiwa kuingia mitaani bado hataweza kusema lolote.

    Nani wa kumuamini?



    Mathiasi aliamua kumfikisha Mwanaidi moja kwa moja katika machinjio yake. Nyumba inayomwaga damu za yatima



    na chokoraa.

    Kwa mtazamo wan je alimchukulia Mwanaidi kama chokoraa wengine dhaifu wa kike waliobakwa sana na hatimaye



    kuwa legelege wanaokubali kusukumwa hovyo.

    Akamfikisha katika jumba lile akamkabidhi kwa wale wanaume wasiojua kishwahili vizuri.

    Akaagana naye kwa ahadi kama alizompa Frida siku tano zilizopita.



    Kisha akatoweka na gari lake akiamini kila kitu kitaenda barabara.

    Alipofika nyumbani alipokelewa na magazeti. Akafunua ukurasa wa kasuku.

    “MATHIAS DEMBELE: Mwanadamu mmoja kati ya mamilioni ya watu!!” ilikuwa makala ya kumpongeza kwa moyo



    wake wa kujitolea na kufanikisha ndoto za Yatima wengi.

    Mathias akatabasamu.

    Wajinga ndio waliwao!!

    Alidhihaki!!

    Kisha akalala akitegemea kila kitu kitaenda kama alivyopanga.

    Mzigo ulitarajiwa kuondoka alfajiri sana!!



    ****



    ***MWANAIDI, FRIDA MAMA GEORGE katika domo la mamba.....sasa ni mpango kabambe wa kusaafirisha



    madawa ya kulevya.....JE WATAPONA????



    ***DEMBELE je ataishia wapi???



    ***ISHA NA GEORGE pia...



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog