Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

CHOKORAA - 4

 





    Simulizi : Chokoraa

    Sehemu Ya Nne (4)



    Mathiasi aliamua kumfikisha Mwanaidi moja kwa moja katika machinjio yake. Nyumba inayomwaga damu za yatima



    na chokoraa.

    Kwa mtazamo wan je alimchukulia Mwanaidi kama chokoraa wengine dhaifu wa kike waliobakwa sana na hatimaye



    kuwa legelege wanaokubali kusukumwa hovyo.

    Akamfikisha katika jumba lile akamkabidhi kwa wale wanaume wasiojua kishwahili vizuri.

    Akaagana naye kwa ahadi kama alizompa Frida siku tano zilizopita.



    Kisha akatoweka na gari lake akiamini kila kitu kitaenda barabara.

    Alipofika nyumbani alipokelewa na magazeti. Akafunua ukurasa wa kasuku.

    “MATHIAS DEMBELE: Mwanadamu mmoja kati ya mamilioni ya watu!!” ilikuwa makala ya kumpongeza kwa moyo



    wake wa kujitolea na kufanikisha ndoto za Yatima wengi.

    Mathias akatabasamu.

    Wajinga ndio waliwao!!

    Alidhihaki!!

    Kisha akalala akitegemea kila kitu kitaenda kama alivyopanga.

    Mzigo ulitarajiwa kuondoka alfajiri sana!!



    ****



    Chokoraa asipoonekana mtaani kwa siku zaidi ya tano. Fikra ambazo huibuka ni aidha amekamatwa na doria ya usiku



    ama ameamua kuhama kambi kwa sababu zake mwenyewe. Kama alikuwa ni mtumiaji wa mabaya ya kulevya huisiwa



    kuwa amekamatwa kijiweni. Mara chache sana huisiwa kuwa amekufa.

    Licha ya kuwa na maisha magumu. Chokoraa huishi miaka mingi sana. Wakihangaika huku na kule. Hali hii ya kuishi



    muda mrefu katika maisha yaliyojaa mateso huwafanya waamini kuwa wamesahauliwa na Mungu.

    Hali hii iliwakumba pia George na Isha. Baada ya harakati za kumtafuta Frida kugonga mwamba waliamua kuendelea



    na maisha yao ya upweke.

    George akakubaliana na Isha wakasimamisha zoezi la kuitoa mimba ile. Litakalokuwa na liwe…walikubaliana.

    Maisha yakaendelea. Chokoraa akijiandaa kuwa baba mtarajiwa, mwenzake naye akijiandaa kuwa mama. Hawakujua



    watamlea vipi kiumbe huyo lakini pia hawakuwa tayari kumuua maksudi.



    George alikulia maisha ya kudekezwa sana alipewa kila kitu alichokuwa anakihitaji wakati akiishi katika utumwa bila



    kujua yu utumwani kwa bwana Emmanuel. Kwa Kiswahili Swahili aliitwa ‘mtoto wa mama’ na alikuwa mtoto wa



    mama haswa. Akili yake ilikuwa imejifunga asiweze kuyatambua yanayotokea katika upande wa pili wa dunia.

    Sasa akili yake ilikuwa imefunguka na mambo mengi kwake yalikuwa mageni. Lakini alikuwa ameyazoea baada ya



    muda mfupi sana.

    Hali ya kuwa baba mtarajiwa ilimuogopesha sana, hakuamini kama aulikuwa wakati muafaka wa kubeba majukumu



    hayo. Jukumu la kujilisha na kulisha familia. Mtihani mkubwa….

    Shilingi mbili alizokuwa akizipata kwa kusota mtaani kufanya kibarua hiki na kile hazikutosheleza kabisa gharama za



    kwenda kliniki, ama dharula iwapo Isha ataugua. Hili lilikuwa tatizo.

    Siku zote hakuwahi kuwaza kuwa anaweza kufanya jambo jingine tofauti na kuzurura mtaani akiokota hiki na kile na



    kufanya vibarua kadhaa, hadi ilipofika siku. Siku ya aina yake. Siku iliyobadili mtazamo wake….



    Siku alipokutana na tangazo linalohusu kuhitajika mwalimu wa somo la hesabu kwa ajili ya masomo ya ziada



    (Tution). Alivutika na kujihisi kuwa anaweza kuipata nafasi hiyo. Japo hakuwa na vyeti lakini alijikuta akivuta



    kujitosa katika usaili.

    Visenti alivyokuwa navyo alivitumia kununua suruali ya bei chee pamoja na shati. Hakuweza kununua viatu. Akaamua



    kuvipeleka kwa fundi vile vibovu alivyokuwanavyo. Vilikarabatiwa lakini havikuleta mvuto.



    Utumwa huu wa kuwa chokoraa ulianza kumkinai na kujihisi kuwa hajitendei haki yeye na chokoraa wengine.

    Aliamini kuwa ni lazima waonyeshe njia huenda na serikali itawasikia. George akaamua kuwa mfano hai.

    Siku ya usaili, George alikuwa mmoja wao.

    Isha alimsindikiza. Kama mkewe….kama mzazi mwenzake. Alipomfikisha George eneo la tukio alifanya kumtazama



    usoni, macho yao yakagongana. George akatambua kuwa Isha alikuwa ana hofu na huenda hakuamini kama anaweza



    walau kufundisha watoto wadogo.

    Akabaki chini ya mti wakati mwalimu mmoja baada ya mwingine wakiingia. “Mungu akubariki.” Ndo neno



    alilojisemea japo George hakulisikia.

    Mwalimu mmoja baada ya mwingine wakaingia na kutoka, walipigiwa makofi na vigelegele kwa chati.

    Ilipofika zamu ya George wanafunzi walipiga kelele sana. Walikuwa wanamfahamu. Alikuwa muokota makopo tupu



    na vyuma chakavu. Hata katika uvaaji wake alionyesha kuwa amejilazimisha kuwa vile.

    Suruali haikumkaa vyema kiunoni ilisaidiwa na mkanda uliochakaa kuizuia isianguke. Na shati lilikuwa kubwa



    lilimvaa badala ya yeye kulivaa. Mbaya zaidi nguo zake hazikuwa zimenyoshwa. Mtazamo wake ulikuwa mojawapo ya



    sababu ya kumfanya mtu atabasamu.

    George alijua hizo kelele ni juu yake.

    Isha naye alijua hilo. Akainama chini, akaomba dua huku akiwa anajipa matumaini kidogo sana kuwa George anaweza



    kufanya vizuri. Japo alimuamini vyema linapokuja suala la kutumia busara. Hapa alikuwa na wasiwasi.

    Wanafunzi walipotulia, George alikuwa mbele yao hakuwatazama usoni. Na aliunda tabasamu la kulazimisha.

    Chokoraa anaijaribu bahati yake.

    Mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda kasi akiwa mbele ya wanafunzi, ule ujasiri aliokuwanao taratibu ukaanza kupotea,



    George akagundua jambo jipya kabisa kuwa alikuwa anatetemeka japo si kwa kiasi kikubwa. Wanafunzi walikuwa



    kimya lakini ilisikika minong’ono. Minong’ono hiyo haikuwa na jingine zai

    “Mi sifundishwi na choko aisee.” Mwanafunzi mmoja aliyeonekana kutokea familia bora kutokana na mavazi yake ya



    kifahari aliyasema hayo huku akijivuta na kutoka nje.

    Macho yake yakatazamana na George. George akainama chini kwa uchungu na aibu….kisha akajikuta akisema na mtu



    asiyeonekana.

    Uliniumba niwe chokoraa, umenipa mzigo huu wa adhabu nimeukubali, ulimuumba mama yangu awe na roho mbaya



    ya kunitupa yote hayo nimeyabeba, na baba ukamfanya asinithamini bado ninakupenda bwana, ukanitupia katika



    familia ya kitajiri, bado haukupooza machungu yangu bali kuyaongeza. Najua unanijaribu baba.

    Kwani nipo peke yangu baba hadi unipe adhabu nyingine ya aibu mbele ya viumbe hawa wasiokuwa wastahimilivu.



    Mbona sikuwahi kumdharau mtu katika maisha yangu? Mbona nidharauliwe. Ni nani nilimdhulumu hadi nilipwe kwa



    ubaya huu….

    Nitue mzigo huu baba nakiri kuwa, nimeelemewa.

    Naamini leo utanitetea!!!leo utakuwa upande wangu baba…ni siku nyingi umekuwa mbali nasi hebu geuza shingo



    yako, geuka tutazamane uuone uchungu nilionao hapa.. George alitumia nusu dakika kuzungumza na Mungu wake.



    Mungu anayejibu kila aina ya ombi.

    Alipoyafumbua macho msaili alikuwa akimngoja aanze somo.

    “Simameni mmsalimie mwalimu!!” aliamuru msimamizi. Ili kuijenga tena saikolojia ya George ambayo ilikuwa



    pabaya.

    Robo ya darasa walisimama, robo tatu hawakusimama.

    Na hata waliosimama, wachache walimaanisha. Wengi wao walikejeli.

    George akauma meno kwa nguvu, akaizuia hasira iliyotaka kumtawala. Akaijibu salamu iliyotolewa.



    Akauendea mkebe uliokuwa na chaki za kutosha. Akatwaa mbili akautazama ubao kisha akawageukia wanafunzi.



    Akakutana na nyuso zisizokuwa na imani naye, mavazi yao yalikuwa ya kushindana, kila mmoja aliamini amevaa



    vizuri kuliko mwenzake.

    Twisheni za mjini zina mambo!!

    Somo likaanza kwa sauti ya chini, licha ya kuwa alipendelea kuwa mtunzi wa hadithi lakini bado alikuwa mzuri sana



    katika somo la hesabu. Na mada aliyopangiwa kuwafundisha wanafunzi wale wa kidato cha nne ilikuwa mada



    iliyoganda vyema katika kichwa chake.

    Matrix!!

    George akapandwa na mizuka. Dakika thelathini zikapotea kama upepo.

    Alipoambiwa muda umekwisha wanafunzi wakapiga kelele kuwa aendelee. Kelele za sasa hazikuwa na kejeli ndani



    yake. Zilikuwa kelele za uhitaji. Wanafunzi walimuhitaji George.

    Ama kwa hakika Mungu hujibu pale unapokiri kuwa unauhitaji msaada wake!! George alikiri kumuhitaji Mungu.

    Japokuwa George aliwashangaza wamiliki wa kituo kile kwa kutokuwa na vyeti. Lakini nani angejali hilo wakati kwa



    matendo ameonyesha kuwa anaweza.

    Kwanza vyeti vya nini wakati ni masomo ya ziada na ni ajira ya muda? Havina maana.

    Usiku wa siku hii. Isha na George walikuwa wamekumbatiana katika kajumba kao. Mkeka ukiwatazama. Walikuwa



    wanalia kilio cha furaha.

    George alikuwa amepita katika usaili. Chokoraa alikuwa amepata ajira ya muda. Ajira ambayo hawakuitarajia.

    Usiku huu wenye furaha ya kwanza kabisa kwa chokoraa hawa baada ya muda mrefu kupita.

    Joto la Isha likaamsha hisia za George, baada ya kilio cha furaha wakajikita katika kubembelezana, huyu akimshika



    mwenzake hapa huyu anamtekenya hivi…..wakajikuta katika uhitaji kila mmoja akimuhitaji mwenzake kwa dhati.

    Mshumaa ukazimishwa, giza likatanda.,

    Usiku huu wawili hawa wakashiriki kufanya mapenzi.



    Wakati Isha na George wakifurahisha miili yao Chokoraa wengine walikuwa katika kuipigania haki ya zao.

    Mwanaidi alikuwa katika kuitetea nafsi yake na kutoka na majibu aliyoyahitaji. Dembele je? Ni kweli anayoyafanya?



    Mama George je? Yupo hai? Na je? yeye atatoka hapo akiwa hai.

    Alipokelewa vyema. Akaishi kwa tahadhari ndani ya chumba hicho cha kifahari alichokaribishwa na watu hawa



    wasiojua Kiswahili.

    Hakuhitaji kunywa chochote kile cha kuandaliwa na watu wale. Kila walipoandaa chakula ama chochote. Mwanaidi



    aliwasemesha kwa Kiswahili, hawakuelewa. Walipompigia Dembele simu. Mwanaidi alimueleza kuwa ameshiba na



    hana uhitaji wa chochote.

    Hawa wanaume huenda walikuwa makini sana na kazi yao. Lakini kosa moja huzaa goli moja. Nao walifanya kosa…

    Ndo kilichowagharimu wanaume hawa weusi.

    Walijisahau kuwa walimuandalia maji ya matunda Mwanaidi.

    Baada ya kuyakataa wakasahau palepale mezani.

    Mtu mweusi mwingine akajongea mezani akiwa na maji ya machungwa kama ya Mwanaidi, lengo likiwa kumhadaa ili



    aweze kunywa. Mwanaidi akajikita yupo makini na luninga.

    “Me take water drink.” Ghafla Mwanaidi, alimwambia yule mtu mweusi kwa kiingereza kisichokuwepo katika



    ulimwengu huu. Akaeleweka ilhali neon maji limesikika vyema.

    Yule bwana akafanya kosa la kukurupuka.

    Chokoraa makini kabisa na mwepesi akamwongezea juisi kwa kumimina ile ya kwake ambayo hata hajaionja.

    Mtu mweusi alirejea akiwa anatabasamu. Mwanaidi akayapokea maji.

    Akayashikilia bila kunywa huku akiendelea kutazama luninga.

    Mtu mweusi naye akafanya kuwa hajali kuhusu Mwanaidi. Akaigida juisi yake kwa fujo.

    Dakika kumi na tano zilikuwa nyingi sana yule bwana kugeuka mzoga unaopumua.

    Hapa sasa Mwanaidi akajipongeza kwa machale yaliyomcheza. Watu wale walikuwa wamemwekea madawa katika



    juisi.

    Hasira zikachemka kichwani. Akakitoa kisu chake na kukikamata vyema.

    Alijua kuwa yule mwenzake ni lazima tu atarejea muda wowote. Na akimkuta mwenzake katika hali ile lazima



    achukue hatua mbaya kwa Mwanaidi.

    Hapo sasa akajiweka makini maradufu.

    Sikio lake likanasa mawimbi ya sauti ya mwanamke akipiga kelele.

    Akaanza kufuatilia sauti huku akijiapiza atakayekutana naye aidha afe yeye ama huyo mtu lakini sio kufungwa kamba



    na kuwekwa mateka.

    “Maicon….Maicon…..Maicon”…sauti ya kiume sasa ilipaza ikiita kwa namna ya kuomba msaada. Ilikuwa sauti ile



    iliyobakia isiyojua Kiswahili.

    Mwanaidi akakaza mwendo zaidi. Mara jicho lake likakutana na jambo la kuvutia.

    Kisu kikubwa, tena chenye makali. Ukubwa wake ulikaribiana na panga. Akatabasamu akahifadhi kile kisu kidogo



    akatwaa panga.

    Damu nyingi amewahi kumwaga tayari. Hakuna alichoogopa.

    Kukurukakara zikazidi kumuweka katika tahadhari kubwa. Mara vikafuata vishindo.

    Hapa mwanadada akalikamata jisu lile kwa mikono miwili.

    Mara akapigwa kikumbo. Akayumba kidogo kisu kikiwa mkononi. Akataka kumfuata aliyempiga kikumbo lakini



    akasita yule mtu asiyeongea Kiswahili naye akaonekana akiwa katika mbio.

    Hapa haisimuliki ni ujasiri wa namna gani na pia hayaelezeki maumivu aliyoyapata bwana huyu.

    Kisu kikapenya katikati ya tumbo lake.

    Kwa Mwanaid lilikuwa jambo la kawaida.

    Akasonga mbele kwenda kukutana na maajabu mengine.

    Damu ikiwa imetapakaa.

    Damu kila mahali.

    Kisha akamuona mtu. Naye alikuwa anavuja damu vilevile.

    Akasita kuingia katika chumba hicho.

    Akiwa bado hajajua nini cha kufanya. Sasa alikuwa na kisu chake kidogo, bila kutilia maanani, mshangao ukamtwaa.

    Ghafla kisu chini, miguu ikaanza kunyanyuka juu ikilifuata shingo lililokabwa.

    Alijaribu kupiga kelele. Sauti haikutoka alikuwa amekabwa haswa.

    Akafurukuta. Bado hakufanikiwa kukitoa kilichomkaba shingo.

    Akazidi kukabwa na uwezo wa kupumua ukizidi kwenda likizo.

    Hali ya hatari. Mwanaidi akauona mwisho wake ukiwa unakuja kwa kasi. Kiza kikaanza kutanda....sura za watu tofauti



    tofauti zikaanza kupita mbele yake....alitamani kuita lakini hakuweza. Kiza kikazidi kutanda....

    Hakuwa tayari kufa lakini dalili zilimaanisha



    kifo….



    Roho ya mwanadamu si nyepesi kupotea, uhangaika sana kabla haijakubali kuuacha mwili, hata mwanadamu awe



    dhaifu kiasi gani hupigana kufa na kupona kabla ya kuikubalia roho iondoke. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Mwanaidi.



    Aliruka huku na huko kujitoa katika ile kabali huku fahamu zikimweleza waziwazi kuwa anaelekea katika kufa.

    Katika kujirusha rusha alifanikiwa kugeukia upande mwingine lakini roba ikiwa palepale.

    Ilisikitisha lakini hakuupata ule uwezo walau kufanya sala yake ya mwisho. Alikumbuka kuwa enzi zake shuleni



    aliikariri vyema sana ya ‘kusahadia’ sala inayosadikika kuwa ni maalumu ukikikaribia kifo.

    Kwanza hata angeipata nafasi ile bado asingeweza kuitendea haki. Alijiona mkosaji mwenye dhambi nyingi sana.



    Aliamini kushahadia kusingemsaidia kitu.

    Mwanaidi akaukubali kwa shingo upande mwaliko wa Israel yule malaika maarufu kama mtoa roho.

    Mwanaidi akatambua kuwa amempata mjanja wake siku hiyo na iwe isiwe lazima afe.

    Anakufa bila kutimiza azma yake. Lakini anakufa akiwa amejaribu sana.

    Anakufa kijasiri. Japo kifo ni kifo tu.



    Wakati anamngojea yule mtoa roho mwenye tamaa achukue kilicho chake kwa wakati anaoutaka yeye. Likatokea tukio



    la ghafla na kustaajabisha, Mwanaidi akajikuta yu sakafuni tena kwa kishindo kikubwa sana. Alikuwa anatapika huku



    akiivuta hewa kwa kasi ya ajabu. Uhai ulikuwa unarejea tena.

    Fahamu zilizoanza kupotea zikarejeshwa na hewa mwanana ya kiyoyozi iliyopenyeza katika pua zake na koromeo.

    Jambo lililofuata ni kufufuka kutoka katika wafu. Mwanaidi akayafunua macho yake hakika alikuwa hai.

    Mbele yake palikuwa na kioo, jambo la kwanza kuona baada ya kufumbua macho ni kujiona yeye mwenyewe.

    Tatizo hakuwa peke yake!

    Nyuma yake alikuwepo kiumbe mwingine. Huyu alionekana miguu pekee katika kile kioo.

    Mwanaidi akatazama kushoto na kulia, kisu chake kilikuwa kimedondoka mbali naye.

    Hakuwa na silaha nyingine. Alitaka kujihami lakini hakujua adui yake ana silaha gani hapo alipo.

    Akaamua kutulia!

    Dakika mbili zikapita, adui bado alikuwa ametulia bila kusema lolote.

    Uvumilivu ukamshinda Mwanaidi akaamua kuvunja ukimya.

    "Wewe ni nani?" akauliza kwa hofu.

    hakujibiwa.

    Akauliza tena, bado hakujibiwa.

    Akajitoa muhanga binti huyu akageuka kukabiliana na adui yake.

    Maajabu! Mdomo wazi!Hakuwa adui bali...bali...alikuwa mtu anayemfahamu…

    Picha ikajengeka katika vichwa viwili wakati huyu akikumbuka siku ya balaa la kukoswakoswa kujeruhiwa na



    chokoraa wenzake, muhusika mwingine alijikuta katika kumbukumbu asizozitarajia. Aliukumbuka ukaribu wa binti



    aliyepo mbele yake. Akaikumbuka mara ya mwisho alikuwa yu katika nyumba ya kulala wageni. Akitegemea



    kukutanishwa na mtoto wake.

    Ahadi haikutimia, yakatokea maajabu ndani ya chumba kile, marehemu bwana Emanuel akavamia na kufanya mauaji.



    Tangu alipozimia na tangu alipozinduka sasa mwanamke huyu anamwona Mwanaidi mbele yake.

    Mwanaidi yu katika sintofahamu, huyu mama ndiye ama siye?

    "Mwanaidi...Mwanaidi..." mara yule mama alianza kusema kwa kurudia rudia jina la Mwanaidi kama anayejaribu



    kukumbuka kitu.

    "Mama!" Mwanaidi alijikaza akajibu.

    Yule mwanamke akaanza kumsogelea aweze kumkumbatia.

    Hapa sasa Mwanaidi na ushujaa wake hakuna kitu alikuwa anahofia katika maisha yake kama ushirikina na mauzauza.

    Hivi mizimu huwa inakuwa hivi? Alijiuliza huku akitetemeka. Kile kiwiliwili kikaendelea kumsogelea.

    Alitamani kukimbia lakini miguu ikawa mizito. Mara akajikuta katika mikono ya yule mama aliyeaminika kuwa mama



    yake George.

    Joto la upendo likapenya katika mwili wake baada ya kumbatio lile, Mwanaidi akaupoteza uoga wake! Akamkumbatia



    yule mama kwa nguvu zaidi.

    Mzimu uliokuwa unamsumbua siku zote sasa ulikuwa mbele yake. Mama George alikuwa na Mwanaidi

    Sasa aliweza kutembea mwenyewe, yale masharti aliyoshindwa kuyatekeleza bwana Emmanuel yakawa faida kwa



    mama huyu aliyekuwa amefungwa kwa muda mrefu. Ile miguu iliyopooza kwa roho mbaya ya bwana Emanuel, roho



    ya tamaa ya utajiri sasa ilikuwa thabiti.

    Aliweza kusimama tena. Alikuwa mzima.

    Kifo cha Mwanasheria Kindo mbele yake kilimvuruga kabisa, aliporejewa fahamu hakuwa sawasawa. Sasa alikuwa



    timamu na alimtambua Mwanaidi. Lakini hakuweza kuongea sana.

    Walipoachana mama huyu alifunua tumbo lake, Mwanaidi akapatwa na msisimko wa ajabu ambao hajawahi kuupata



    hapo kabla.

    Alisisimka kwa kile alichokiona. Mishono isiyokuwa ya kitaalamu sana na vidonda vibichi katika tumbo la yule mama.



    Mwanaidi akahisi kwa mbali joto kali zaidi. Kisha jasho likachuruzika, katika mfereji wa uti wa mgongo wake.

    Alikuwa amesisimka. Yule mama hakusema neno lolote lakini alijiumauma kama anayelalamika na kulaani.

    Mwanaidi akatoa chozi.

    Zile soga zilizozagaa mtaani kuwa bwana huyu anajihusisha na madawa ya kulevya sasa zikaanza kuwa katika vitendo,



    mwanaidi hakuwa na utaalamu lakini mambo haya amewahi kuyasikia mtaani.

    Mama huyu ambaye aliitwa mwendawazimu alikuwa akitumikishwa na Dembele katika biashara yake.

    Biashara haramu ya madawa ya kulevya.

    Inakera!! Inaumiza. Kupasua tumbo la mama aliyekuzaa na kumrundikia madawa ya kulevya.



    Mwanaidi alikuwa amezizima kwa hofu na msisimko.

    Alimwona mama huyu kama ambaye muda wowote ule anaweza kuupoteza uhai.

    Mama alizidi kulalamika katika sauti za chini, sasa alionyesha mkono wake kuelekea katika chumba kimoja. Mwanaidi



    hakuelewa ana maana gani hadi yule mama akiwa bado hajafunika tumbo alipomshika mkono na kumvuta kuelekea



    anapomaanisha. Wakakifikia chumba, mama akakifungua Mwanaidi akakutana na mshangao mwingine lakini huu



    haukudumu sana akakumbuka kuwa yupo eneo hatarishi.

    Akazivamia kamba na kuzifungua, hazikuwa zimekazwa sana.

    Frida Gereza chokoraa aliyezaliwa gerezani akawa huru.

    Mwanaidi akajipongeza kimyakimya kuwa ameua ndege wawili kwa jiwe moja.

    Honi ya gari ikasikika nje. ikawashtua!!

    Ikaendelea kupigwa kwa fujo. Wote wakabaki katika bumbuwazi.

    Hofu ikatawala tena wakakata tama ya kutoka humo ndani wakiwa hai…



    ****



    WIVU WA MAPENZI huteketeza nafsi nyingi chini ya jua. Wivu huja ukipata wasiwasi juu ya mwenzako. Mbaya zaidi



    moyo wako ukiwa unampenda kwa dhati.

    Kila anapoenda unahisi anakusaliti. Kila akipigiwa simu unahisi hawala amempigia. Hata akitabasamu baada ya



    kusoma ujumbe katika simu unahisi ametumiwa na mwanamke wa nje.

    Tena akirejea nyumbani huku ana hasira, ndio mbaya kabisa unaweza kuamini kuwa yule msaidizi wake wa kazi



    amemkasirisha baada ya kumkatalia penzi. Wivu huja ili kuonyesha kuwa mapenzi yasiyoonekana kwa macho yapo na



    yanaishi ndani yetu…..

    Hali hii ilikuwa inampeleka puta mwanadada aliyelala katika kitanda cha futi tano kwa sita alichoamini kuwa ni



    kikubwa kumzidi.

    Usingizi uligoma kabisa kumchukua tangu mume wake mtarajiwa amuage kuwa amepata dharula kuna mahali



    anakwenda.

    Hofu yake kuu ilikuwa kauli ya mume wake huyo kuwa anampenda sana msichana fulani aliyeishi nao kwa siku



    kadhaa.

    Kivipi aseme anampenda? Au ni hawala….

    Wivu ukampiga kikumbo akayumba.

    Hali ya hewa ya jijini Dar es salaam siku hiyo ilikuwa ya ubaridi.

    Akashtuka !!

    Akahisi vibaya kuwa mume wake huyo amekwenda kulitafuta joto mahali.

    Akafanya tabasamu la karaha kisha akasimama. Akiwa na nguo zake hizo hizo za kulalia. Akajitazama katika kioo



    baada ya kuwasha taa, alikuwa mwekundu sana.

    Hasira !!

    Akatembea hadi nje. Akawaza kwenda kufumania.

    Akajipa uhakika kuwa anapotegemea kuwa mume wake yupo basi atakuwa hapohapo.

    Hivi hanijui huyu mwanaume eeh!! leo atanikoma na hicho kisichana chake.

    Akaliendea gari lililoachwa na mumewe. Akatazama lilikuwa na mafuta ya kutosha.

    Akawasha injini akatoweka kwa makini kabisa huku akijipongeza kwa uamuzi wa kumfuatilia Kasuku ambaye



    alikuwa akimfuatilia Dembele siku aliyomwondoa Frida na kumkabidhi kwa Dembele kwa ajili ya msaada zaidi…

    Kasuku hakutegemea kama mke wake alimfuatilia siku ile lakini ilikuwa hivyo na sasa mke anafurahia matunda.



    Kasuku alitambua kuwa ni yeye pekee aliyekuwa anatambua wapi Frida anapelekwa na Dembele hakujua kama mkewe



    yu katika msafara….

    Mwanamke huyu aliamini kuwa Kasuku alikuwa ameenda kukutana na Frida. Yule binti ambaye mumewe alidai kuwa



    alimuokoa baharini…jambo ambalo halikumuingia akilini.

    Huyu mwanamke anayepelekeshwa na wivu alikuwa ni Emiliana mke mtarajiwa wa bwana Kasuku.

    Kwa kuwa alifahamu mahali ambapo Frida alipelekwa siku hiyo hakuhangaika sana kumfuatilia usiku huu. Alimini



    fika kuwa Kasuku ameelekea huko…



    Alifika katika nyumba ile majira ya saa tisa usiku.

    Akiwa amepagawa kabisa alibonyeza kengele baada ya kupiga honi bila ya geti kufunguliwa. Bila kujali bughudha



    anazowaletea wamiliki wa nyumba ile.

    Mapenzi bana!! Acha yaitwe mapenzi. Hayo hakujali.

    Alibonyeza mara kadhaa bila kujibiwa.

    Wakati akihangaika kubofya ile kengele, viumbe wawili walikuwa katika hofu huku yule wa tatu akiwa hajui lolote.

    Frida na mwanaidi walikuwa wametaharuki.

    “Ni yeye amekuja huyo.” Frida alimwambia Mwanaidi huku akitetemeka.

    Mwanaidi akamtazama mama George aliyekuwa anacheka bila sababu. Akakutanisha macho na lile tumbo lililoshonwa



    hovyohovyo.

    Damu ikachemka kwa uchungu hakuwa tayari kupasuliwa na kushonwa kama huyo mama. Akatazama nyuma yake



    akakutana na ule mwili aliousulubu kwa kisu kikali.

    Akauendea akiwa amepandwa na mizimu asiyoijua asili yake akachomoa kile kisu kwa fujo kikatoka na matone



    mazito ya damu.

    Frida akapiga kelele ya hofu.

    Mwanaidi akaondoka bila kuaga mtu yeyote.

    “Mwanaidi…Mwana….” Aliita kwa kunong’ona Frida. Mwanaidi hakugeuka. Hakutaka kusikiliza lolote aliamua



    kufanya analotambua yeye.

    Akapiga hatua hadi akalifikia geti lililokuwa linagongwa.

    Uoga ukamshika lakini hakusita. Aliamini mpinzani wake hakuwa amejiandaa kikamilifu na kamwe asingetegemea



    pigo kama lile kukumbana naye.

    Mwanaidi akalitazama geti akashika kitasa bila kuuliza lolote akafungua. Akili yake ilikuwa kwamba ni heri apambane



    kisha auwawe kuliko kujituliza ndani kisha kufumaniwa kama kifaranga cha kuku na kisha kutumikishwa biashara ile



    haramu. Japo alikuwa na kisu pekee Mwanaidi aliamini kuwa pigo moja tu litatosha kumpooza hata kama watamuua.

    Binti akalifungua geti…

    Kiwiliwili kilichojaa shari kikaingia kichwa kichwa.

    Mwanaidi asiyekuwa na akili zake timamu akatii kiu yake. Akaamini kuwa aliyempa mgongo ni Dembele. Wazo lake la



    pigo moja likafanya kazi.

    Kisu chenye urefu wa mita kadhaa kikazama katika mgongo huu laini. Kikatoka kilio kikali cha mwanamke. Kisha



    kikatua chini.

    Wivu ukawa umemponza Emiliana na sasa alikuwa katika kuipigania roho yake pasipo mafanikio. Damu ilikuwa



    inaruka kama bomba la maji lililopasuka. Emiliana alikuwa anagalala, hiyo hali ya kugalagala ikasababisha kisu kizidi



    kuzama ndani zaidi

    Mwanaidi akashtuka lakini hakutaka kujua yule ni nani akamuwahi ili asipige kelele nyingi. Akamziba mdomo.

    Baada ya dakika chache akasimama. Hakutaka kufuatilia iwapo amepoteza fahamu ama amekufa.

    Roho ya paka ilikuwa imemkaa kifuani.

    Huenda ni mke wa huyu mwanaharamu…..

    Hakujua kama mwanamke aliyemsulubisha alikuwa na matatizo yake ya wivu na hakujua lolote kuhusu Dembele…..

    Wivu huponza na usiombe kuwa mfano wa aliyeponzwa na wivu. Emiliana alikuwa mfano tayari….



    Upesi akaingia ndani, ile hali ya kuliona geti wazi ikampa wazimu aliamini kuwa hiyo ilikuwa nafasi yao ya mwisho



    kutoweka kwa amani…hakutegemea kama ingekuwa rahisi kiasi kile..

    Baada ya dakika tano. Majira ya usiku mnene unaoikaribia alfajiri. Mwanaidi, mama George na Frida walikuwa katika



    jitihada ya kutokomea kuelekea popote pale wanapojua wao. Walijikokota taratibu kwa sababu ya uzito wa mama



    George na pia vidonda vyake vibichi havikuhitaji kukutana na baridi. Alilia kama mtoto mdogo lakini hapakuwa na



    namna ilimlazimi kutembea ili watoweke eneo lile hali ilikuwa tete. Mwanaidi aliumia sana kuliona chozi la mtu



    mzima. Kuna wakati alishindwa kutembea kabisa akawa anakaa chini na kuanza kulia kilio kama mtoto mdogo.

    “Mwanaharamu amemuhukumu mama yangu kabla Mungu hajaamua kumuhukumu, mshenzi sana huyu mshenzi



    kupindukia. Naamini kwamba ni Mungu ametutoa salama katika janga hili na ni Mungu huyu huyu atamsulubisha



    mwanaharamu huyu..” Mwanaidi aliongea peke yake Frida akiwa msikilizaji.

    Safari ikaendelea kiongozi akiwa Mwanaidi.



    *****



    Taharuki ilimkumba bwana Dembele Mathias, alipikicha macho yake aweze kuhakikisha anachokiona na akagundua



    kuwa haikuwa ndoto kuna ukweli mbele yake, geti la nyumba anayoitumia kwa maasi yake lilikuwa wazi, wakati



    anatafakari ni kwa namna gani geti linakuwa wazi mara jicho lake likakutana na jambo jingine la kutisha na



    kufadhaisha gari la mwandishi mpekunuzi wa mambo lilikuwa limeegeshwa kwa nje.

    Gari la bwana Kasuku. Na bila shaka ndani yake hapakuwa na mtu.

    Ilikuwa saa kumi na moja alfajiri.

    Mshenzi amenigundua!! Aliwaza Dembele.

    Akarejea katika gari lake upesi akapapasa huku na kule akatoka na mfuko mdgo akachomoa alivyovihitaji akarejea na



    pilipili ya kupulizia na dawa ya usingizi.

    Aliamini kwa kumkabili kwake bwana Kasuku huu utakuwa ushindi mkubwa kwake kuukwepa mkono wa sheria



    lakini vinginevyo alikuwa anatakiwa kujiandaa kusoma makala mbaya zaidi kati ya zote ambazo amewahi kusoma.



    Makala itakayomvua nguo na kumwacha uchi. Kisha kujikuta akisimama mahakamani kujibu mashtaka zaidi ya kumi



    yatakayokuwa yanamkabili.

    Aliingia ndani huku akihemea juu juu. Kile kitambi chake kikaanza kuwa mzigo mzito.

    Ile anaanza tu kuingia ndani akakutana na mwili ukiwa umetulia sakafuni. Mwili wa mwanamke. Akausukuma kwa



    mguu, ulikuwa mzito sana. Mwili ulikuwa katika dimbwi la damu, nguo nyepesi ya kulalia iliufunika mwili ule ambao



    haukuwa ukipumua tena. Mauaji yamefanyika katika nyumba yake na gari la Kasuku lipo nje.

    Akatamani kukimbia lakini hiyo haikuwa njia ya kulikimbia tatizo.

    Akasonga mbele hadi akaifikia sebule. Hapa akamkuta msaidizi wake mweusi asiyejua Kiswahili akiwa amelala



    fofofo.

    Akamtandika kofi la nguvu akitegemea atakurupuka kutoka usingizini ajabu na kweli hakutetereka wala hakulalamika.



    Lakini alikuwa anakoroma.

    Akaachana naye.

    Hatua kadhaa mbele akakutana na maiti nyingine. Na damu zikiwa zimetapakaa. Hii ilikuwa imetoa ulimi nje, utumbo



    nao ulikuwa nje bila shaka muuaji alimaanisha kuua na si kujaribu kuua. Muuaji alikuwa mtu wa hatari na hakuwa wa



    kupambana naye kwa kutumia pilipili ya kupuliza na dawa ya usingizi. Dembele akaona dalili ya yeye kuuwawa pia



    kwa kuchomwa kisu…..hofu!!!

    Hapa sasa shinikizo la damu likaanza kupanda.

    Ujasiri ukakosa nafasi.

    Akalainika. Akasalimiana na sakafu bila kutarajia.

    Cha kuchekesha alidhani kuwa atapoteza fahamu kisha aibuke kutoka ndotoni. La alibaki akiwa anaona



    kinachoendelea. Hakuwa ndotoni.

    Dembele matatani!!

    ****



    George Emmanuel alishangazwa na jinsi darasa lilivyojaa likimsubiri kwa ajili ya kuwafundisha. Alipoingia kila



    mmoja alisimama na kumsalimia kwa heshima zote. Kimoyomoyo akamshukuru Mungu.

    Katika msafara wa mamba hata kenge hujiweka humo bila kujulikana. Ndivyo ilivyokuwa pale sauti ya mwanafunzi



    mmoja ilipomsalimia kwa kesema ‘Shkamoo mwalimu Choko’ sauti hii ilitokea katika madawati yaliyokuwa nyuma



    sana…..wanafunzi wachache walicheka huku wengine wakichukizwa waziwazi na neno hilo.

    Ubaya wa wanafunzi huwa ni wagumu kumtaja anayekuwa amefanya kosa fulani hata kama wanamfahamu fika. Hata



    huyu hakutajwa. Japokuwa walimtambua.

    “Popote ulipo uliyediriki kuniita mimi hivyo, endelea kuniita hivyo sana bila kuchoka kabla Mungu muweza wa yote



    hajauchukua uhai wa wazazi wako, kabla dunia haijawa adui kwako, kabla haujawa takataka inayotakiwa kuzikwa na



    wanadamu unaowatukana. Jisifu sana, lakini ujue kuwa si mimi wala wewe anayeyapanga haya. Sisemi haya ili



    uniheshimu la! Lakini itafikia kipindi dunia itakufunza. Hongera kwa kusifiwa na wanadamu kwa maneno yako juu



    yangu. Nilizaliwa Chokoraa na nitakufa chokoraa nafurahia kuwa chokoraa maana si lazima kila mmoja aishi kwa raha



    kama uishivyo wewe….”

    Neno likamfikia mlengwa akainama kwa aibu. Hatia ikaanza kuishi naye. Chozi likamlengalenga akajikaza asilie,



    akafanikiwa kukizuia kilio cha nje lakini moyoni akabaki kuugulia. Neno lilikuwa limemchoma ipasavyo…

    George hakujali!!

    Kabla ya kuanza kufundisha alifanya sala fupi kisha akaukabili ubao.

    Hali ilikuwa zaidi ya awali.

    Alipotoka darasani wanafunzi wakamzunguka. Kila mmoja alitaka huduma zake za masomo ya ziada kwa malipo.

    George alikuwa na shida na pesa hakukataa hata ofa moja.

    Baada ya wiki mbili alikuwa katika mabadiliko.

    Siku waalimu walipopewa pesa yao ya awali ‘advance’. George akawa na pesa inayohesabika na kushikika walau. Kwa



    mara ya kwanza katika maisha yake ya uchokoraa alikuwa amepokea pesa nyingi.

    Ni nani haupendi umeme. Nani asiyependa kuishi katika nyumba yenye uhai kidogo wa kuitwa nyumba, nani hapendi



    nyumba yenye choo kizuri na bafu pia huduma za maji? Bila shaka hakuna ambaye hapendi.

    Hata chokoraa pia alihitaji hivi vitu. George akiwa mmoja wao. Tatizo huwa ni pesa tu ndo maana wengi huvikosa



    vitu hivyo…

    George akiwa na Isha walihama katika nyumba ile , wakahamia nyumba yenye umeme, choo na huduma ya maji



    ilikuwa jirani.

    Historia ya kulalia mkeka ikafutika. Ukabaki kuwa kwa ajili ya kukalia na kulia chakula. Godoro ndani ya nyumba.

    Tabasamu likachukua nafasi.

    Isha na mimba yake wakajikuta wakiishi maisha yenye ahueni kidogo. Hakika walikuwa na haki ya kutabasamu.



    Mungu alikuwa ametenda muujiza.

    ****

    Kichwa kilikuwa kinamuuma sana Kasuku. Kifo cha mpenzi wake na mkewe mtarajiwa kilikuwa kimemchanganya



    sana. Hakuweza kukielezea kwa marefu na mapana kama anavyofanya pindi aandikapo habari. Hili lilikuwa jambo zito



    sana na lisilohadithika.

    Gari lake lilikutwa limeegeshwa katika hoteli, mwili wa marehemu ukakutwa katika mtaro mkubwa ukiwa na mpini



    wa kisu uliozama ipasavyo katika mgongo wake.

    Kifo hiki sio kwamba kiliishia kumsisimua na kumuumiza Kasuku lakini kilimtia wazimu kabisa. Alijiuliza maswali



    mengi. Hakupata jawabu. Nani amemuua mkewe kifedhuli kiasi kile?

    Huzuni!! Huzuni ikawa rafiki yake.

    Akachukua likizo isiyokuwa na malipo aweze kuipumzisha akili yake.

    KASUKU alizoea kufuatilia matukio ya hapa na pale yasiyomuhusu, haya yalikuwa mepesi na alikuwa anafurahia



    kuyafuatilia kisha kuyaandika. Matukio aliyokuwa anayafuatilia na kuyaandika yalikuwa makubwa sana. Tena ya



    kushangaza. Cha kushangaza tukio hili la kifo cha mkewe hakujua ni wapi ataanzia. Hakujua atafuatilia vipi aweze



    kupata jibu.

    Gari limekutwa barabarani, mwili umekutwa mtaloni.

    Ataanzia wapi kupeleleza.

    Alama za vidole zilizokutwa katika mwili wa marehemu zilikuwa za mwanamke. Mwanamke ameua? Likawa swali.

    Usukani haukukutwa na alama zozote zile. Hii inamaanisha muuaji alikuwa makini sana na kazi yake. Hakukubali



    kuacha ushahidi kirahisi.

    Hapa kila aliyeufuatilia mlolongo huu alichanganyikiwa na kupoteza tumaini la kumpata muuaji. Ama kwa hakika



    muuaji alikuwa mtu hatari sana. Kasuku alikiri katika nafsi yake.



    Kasuku alikumbwa na fedheha kubwa sana. Simu kutoka katika ukoo wa mwanamke kila siku kumuuliza ni wapi



    amefikia zilimkwaza sana lakini hakuwa na jeuri ya kukataa kupokea simu yao wala kujibu maswali yoyote



    watakayouliza.

    Ilikuwa bahati kuwa alikuwa amejaaliwa mwili mwembamba. Hata alivyopungua haikushangaza sana tofauti kama



    angekuwa na mwili mkubwa. Maana kila mtu angejua kuwa Kasuku amefikwa safari hii.



    Mwenzake aliyekuwa na mwili mkubwa alikongoroka kwa kasi kubwa sana. Kitambi kikaanza kufutika. Mali



    alizokuwanazo zikakosa maana. Akawa mkali katika familia yake, kila mara anamgombeza mkewe, mara apige watoto



    wake bila sababu ya msingi.

    Alikuwa kama amechanganyikiwa.

    Siri kubwa ilikuwa inamtesa. Atamshirikisha nani? Hakuwepo wa kumshirikisha.

    Habari za upelelezi unaendelea zilikuwa zinamchanganya mzee Dembele. Kila alipozisikia jitihada hizi zinaendelea



    aliona namna anavyokaribia kuumbuka.

    Mbaya zaidi hakuwa anafahamu ni wapi Frida na Mwanaidi pamoja na yule mama mwendawazimu walikimbilia. Hili



    ndilo lilikuwa kubwa kupita yote. Atawapata wapi?

    Akili ilikuwa imechoka kujiuliza ilikuwaje mkewe Kasuku akakutwa amekufa katika nyumba yake ya siri. Mwanamke



    Yule alifuata nini pale iwapo Kasuku mwenyewe anaomboleza kifo chake bila kujua alikufa kwa sababu gani. Nani



    alimpeleka katika nyumba ile?

    Alizihitaji roho zao ili kujiweka mahali salama. Ni roho hizi pekee ambazo zingetoa jawabu kwake.

    Uhuru wake ulikuwa matatani. Na laiti kama ingefahamika kuwa alikuwa anajihusisha na na uuzaji wa madawa ya



    kulevya kwa njia ya kutoa misaada kwa yatima maisha yake yangemalizikia katika kitanzi.

    Alikuwa muuaji!!

    Siku zilizidi kukatika bila bwana Dembele kugusiwa lolote juu ya kuhusika kwake katika katika kifo cha mke wa



    Kasuku.

    Wasiwasi wake haukupungua kamwe. Aliamini bado alikuwa katika wakati mgumu sana. Hakuwa na la kufanya



    akaungoja wakati uzungumze!!

    Ni wakati pekee ambao ungeweza kumpa hukumu….





    ****



    Mwanaidi hakuwa na mamilioni ya pesa kuweza kuwahifadhi watu hawa wawili. Mama George na Frida. Lakini



    alijitahidi kadri ya uwezo wake kuwahifadhi wawili hawa kwa kidogo alichokuwa nacho.

    Pesa aliyoipata kwa kumwibia marehemu mkuu wa kituo cha watoto yatima isingeweza kudumu kamwe. Hasahasa



    ikiwa inatumika pasi kujizungusha. Mwanaidi aliamini kuwa akifikia uamuzi wa kumpeleka mama hospitali basi pesa



    itaishia hapohapo.

    Baada ya siku takribani tano za mapumziko katika chumba alichokuwa amepanga Mwanaidi sasa likaibuka wazo la



    kutazama nini cha kufanya ili maisha yaweze kuendelea.

    Mwanaidi hakutaka kurejea tena katika maisha ya uchokoraa.

    Kwanza kwanini arejee?? Wakati sasa anaye mama anayemwona kama mzazi kwake?

    Hapakuwa na haja ya kujiita yatima tena.

    Alikuwa na dada aliyeitwa Frida na bado mwingine anayeitwa Isha na kaka anayeitwa George. Hapa alipungua mzazi



    wa kiume pekee kuweza kuikamilisha familia hii ya maajabu.

    Mwanaume? Mwanaume wa nini George ndo mwanaume pekee ninayemuamini duniani!! Mwanaidi alisema na nafsi



    yake.

    Mwanaidi alipofikiria na kujitoa katika uyatima akagundua kuwa amefanya ubinafsi wa hali ya juu sana. Kummiliki



    yule mama ilhali kuna yatima wengi mtaani. Akajikuta katika kujishangaa tabia hiyo ya ubinafsi ameianza lini?



    Hakupata jibu sahihi maana hakuwahi kuwa hivyo…..

    Atakuwa mama wa wasiokuwa na mama mtaani!! Alipitisha kauli hiyo katika ubongo wake.

    Kila neno lahitaji kitendo liweze kuonekana.

    Mwanaidi akafikiria cha kufanya ili neno lake liweze kuishi katika matendo. Frida na yule mama walikuwa wamelala



    bado, akawatazama kwa jicho la huruma.

    Moyo wake ukakiri kuwa alikuwa anawapenda sana!!

    Mwanaidi alingoja baada ya siku tatu. Sasa akawa amefikiria nini cha kufanya.

    Katika hili alihitaji sana kumpata mtu mwenye taaluma kidogo anayeweza kuzungumza na msomi. Mwanaidi



    alimuhitaji mtu wa kuweza kuyafichua maovu ya Dembele kisheria moja kwa moja. Aliamini kwa kufichua siri nzito



    kama hiyo basi atakuwa amejiweka katika nafasi ya kuwakomboa mayatima wengi. Zawadi nono itatolewa….aliamini



    hivyo.

    Atampata wapi huyo mtu? Alijiuliza. Mara akapata wazo.

    “Frida!!” aliita.

    “Sema kamanda.” Alijibu kwa utani huku akiwa analamba kipande chake cha limao kukata kichefuchefu cha mimba.

    “Ulisema kuwa unapafahamu nyumbani kwa George.”

    Frida akatikisa kichwa juu na chini kuashiria kukubali.

    Mwanaidi akaelezea nia yake ya kutaka kuonana na George.

    Frida aliposikia jina George na mpango wa kuonana naye alifadhaika sana kutokana na mzigo alioubeba tumboni.

    Hakusita kumueleza ukweli Mwanaidi. Mwana akamuelewa.

    Wakazungumza kuwa, kwa kuwa tumbo bado halijachungulia sana basi George hataelezwa ukweli. Mwanaidi



    aliongezea kumweleza Frida kuwa yule mwanamke ni mama yake George hivyo wanampelekea zawadi kwa ukarimu



    wote aliowahi kuwatendea.

    Kwa kusikia hivyo, Frida akasahau yote yaliyopita akakubaliana na Mwanaidi. Frida aliamini kwa zawadi



    watakayompa George bila shaka atasahau kila kitu kuhusu ujauzito na maisha yataendelea……

    Laiti angejua George ni baba mtarajiwa kamwe asingejishuku……lakini hakulijua hilo.

    Wakamuacha mama nyumbani.



    Kadri walivyoikaribia nyumba anayoishi George ndivyo Frida alizidi kupatwa hofu, hakujua kwanini ana hofu lakini



    alitambua kuwa huenda ni hofu yenye raha ndani yake. Raha ya kukutana tena upya na Isha na George..kisha kuunda



    upya umoja wao. Wakaifikia nyumba, wakaulizia kulikoni mbona nyumba wazi.

    Kisichokuwa ridhiki hakiliki!! Alipokuwa anaishi George hakuwepo tena. Na hapakuwa na taarifa yoyote ya wapi



    alipohamia.

    Chokoraa hana makazi ya kudumu. Mwanaidi akafadhaika.

    Lakini hawakuwa na jinsi wakaamua kurejea walipotokea.



    ****



    ****



    SIASA ni mchezo mchafu. Lakini mchezo huu hauchezeki bila pesa, pesa nyingi si pesa kidogo. Pesa hunogesha



    mchezo huu. Na iwapo hauna pesa ni vyema usijiingize kabisa katika mchezo huu. Mchezo wa maajabu mchezo wa



    kuchafuana kwa kila namna.

    Wakati ikiaminika kuwa bila pesa mchezo huu hauchezeki, cha kushangaza bwana Seba Sebastian aliingia katika



    mchezo huu bila pesa na akaweza kuucheza. Ilishangaza.

    Wengi walijaribu kumuiga njia yake ya maneno matupu lakini hawakufanikiwa kitu zaidi ya kuangukia pua na



    kusahaulika katika ulingo huu wa siasa.

    Msimu huu wa kuelekea uchaguzi hali haikuwa kama zamani.

    Mgombea wa chama alitakiwa kuteuliwa kwa kura za wajumbe wa chama. Hapa sasa pesa haikuwa na budi kutumika.

    Seba alikuwa bahili sana, hakuwa tayari kutumia pesa nyingi kununua nafasi ya uongozi.

    Sasa anafanya nini kuwashawishi wajumbe wakati ukifika wamchague tena? Hili lilikuwa linamuumiza kichwa.



    Alitakiwa kuwa na pesa nyingi sana kuweza kumkabili mpinzani wake mtarajiwa, kwani alikuwa na pesa nyingi tena za



    kutisha. Jambo hili lilimuumiza kichwa kwa mara ya kwanza tangu awe kiongozi, hakutamani kuyaachia madaraka



    lakini kila dalili ya kuyaachia kinguvu ilinukia.

    Mawazo haya yakaitwaa akili yake na kuisafirisha mbali, alikuwa kimwili ofisini lakini kiakili alikuwa maili nyingi



    sana mbali kutoka hapo.

    Mlango wa ofisi ya diwani wa kata ulipogongwa hakuusikia vyema mpaka ulipogongwa tena ndipo akili ikarejea



    sawasawa. Akajinyoosha viungo. Akamruhusu aliyegonga. Akaingia.

    “Shkamoo.”

    “Marahaba binti karibu” alijibu kichovu bwana huyu.

    Binti akaketi. Bwana Seba kwa kumtazama yule binti akaanza kuweka ubashiri wa nini kimeletwa mbele yake. Aidha



    amefaulu anataka kuchangiwa ada ama ana matatizo na familia yake amekuja kutoa taarifa. Hakupenda taarifa ziwe



    hizi lakini angefanya nini??

    Udiwani nao una kero zake!! Aliwaza.



    “Nakusikiliza msichana.”

    Binti akajiweka sawa katika kiti. Akamtazama diwani. Akakohoa kuweka koo sawa.

    “Naitwa Mwanaidi.” Alijitambulisha bila chembe ya wasiwasi.

    “Nakusikiliza binti zungumza.” Alisema kwa hasira.

    “Nimekuja hapa mimi na wewe tusaidiane, iwapo tutashindwana naweza kwenda kwa mwingine japo wewe itakusaidia



    sana.” Alianza kuzungumza chokoraa huyu aliyekuwa ngazi ya cheo cha dada mkuu kabla ya kushindwa kuendelea na



    shule.

    Diwani akatoa miwani yake akaifuta kisha akamtazama tena yule binti mdogo kiumri. Alihisia kama hakumsikia vizuri



    lakini hakutaka kumwambia arudie tena alichokitaja.

    Hakusema neno. Akaendelea kumsikiliza.

    “Ni kuhusu Dembele…Mathias Dembele.”

    Diwani akashtuka. Binti mdogo kama huyu ana nini cha kuzungumza juu ya Dembele. Akastaajabu bila kusema lolote.



    Ni kama alikuwa anatazama filamu.

    “Upo tayari.” Badala ya kumruhusu diwani amalize kushangaa Mwanaidi akamtupia swali.

    Diwani akaduwaa, hakujua nini cha kumuuliza yule binti. Midomo ikawa kama inataka kusema lakini inashindwa



    kuendelea kusema, ikawa inatetemeka.

    “Umesema unaitwa nani?” akauliza bila kutarajia, hapa sasa alikuwa ameuona umuhimu wa jina la binti yule.

    “Upo tayari tusaidiane?” Mwanaidi hakumwambia jina lake tena. Na wala hakuonyesha kumwogopa diwani.

    Ule uoga aliokuwanao awali ulikuwa umetoweka na hakuona maana ya kuwa na uhitaji wa msomi kuweza kufanya



    jambo hili. Aliamua kufanya mwenyewe.

    “Nipo tayari, ni nini kwani?”

    “Kuna jambo unatakiwa kujua kuhusu jamaa.” Mwanaidi akazungumza kwa sauti ya chini.

    “Jambo gani?”

    “Ndo nahitaji tusaidiane.”

    “Kivipi?”

    “Nataka nikwambie na wewe unilipe kidogo tu.”

    Diwani akakuna kichwa. Ubahili ukamwandama.

    “Kwani kuniambia mpaka nikulipe?” Seba akaingiza ubahili wake wa kuzaliwa.

    “Jamaa zungu la unga.” Alisema huku akitabasamu. Karata ikawekwa mezani barabara sasa ilitakiwa kuchezwa.

    Diwani akashtuka kusikia habari hiyo. Akatoa miwani tena akaisafisha na kuivaa tena.

    “Kivipi? Nani kakwambia?” alipagawa.

    “Unapenda kuuliza hupendi kulipia. Naondoka wapo wengi tu wa kuilipia siri hii.” Alinung’unika Mwanaidi huku



    akisimama aweze kuondoka.

    “Hapana sikiliza..sikia wewe niambie kisha nakulipa.”

    “Naomba niondoke.”

    “Haya bei gani.”

    “Mshahara wako wa mwaka mzima. Halafu faida yako wewe itakuwa mara mia. Kwanza utaupata tena udiwani, na



    serikali itakulipa kwa kumfichua jamaa.” Mwanaidi aliongea kwa kujiamini sana, maneno hayo hakuyapanga hapo



    awali. Alijikuta tu akitokwa na maneno ya ajabu ajabu

    “He!! Nini, nipishe nipishe.” Bahili alipagawa kusikia mshahara wa mwaka mzima uishie kumpa binti yule mdogo.

    Mwanaidi akasukuma kiti nyuma akasimama. Akaufungua mlango akimuacha diwani bahili akitukana matusi yote



    anayojua.

    Diwani alijikuta akiwa kimya ghafla. Akayakumbuka maneno ya Mwanaidi, akamfikiria na Dembele ambaye ndiye



    alikuwa mpinzani wake mtarajiwa katika kiti hicho cha udiwani. Akaitazama ofisi yake na kukitazama kiti



    alichokikalia, kama akishindwa uchaguzi hakitatakuwa chake tena. Hapa sasa akataharuki, akagundua kuwa hakuwa



    tayari kumwachia mtu yeyote kiti chake cha udiwani. Akasimama wima mbiombio akatoka nje ya ofisi. Kimya kimya



    hadi akamfikia Mwanaidi akamsihi warejee ofisini.

    “Tunaenda kumalizana ama..sitaki maneno kuna mahali naipeleka habari hii na nitalipwa mara moja.” Alikoroma sasa



    chokoraa. Tayari alikwishaugundua udhaifu wa diwani na uhitaji wake mkubwa katika habari ile.

    Diwani akaubali yaishe. Alikuwa anaupenda udiwani na pesa pia alikuwa anaipenda.

    Wakarejea ofisini.

    Mwanaidi akauza habari. Mauaji ya mke wa Kasuku akamuuzia bwana Dembele. Kila uozo ukawa juu yake. Akampa



    diwani vithibitisho vyote. Wakaenda hadi katika ile nyumba ambayo bwana Dembele hufanyia maasi yake.

    Wakati akizungumza haya alikuwa na milioni nyingi katika mkoba wake, pesa iliyotoka katika akiba ya diwani bahili,



    Mkoba ulikuwa na kisu chake iwapo kuna ujanja wowote unaoweza kufanyika.

    Mwisho wa biashara!!



    Mwanaidi akarejea nyumbani akiwa ndani teksi. Hakuamini kama alikuwa amefanya jambo hilo kwa wepesi kiasi kile.

    Sasa alikuwa na jeuri ya kusema kuwa alikuwa na pesa ya kuweza kufanya jambo.

    Nani kama Mwanaidi??

    ****

    MCHIKICHINI almaarufu kama ‘Mchikidown’. Mwanafunzi gani wa jijini Dar es salaam mwenye nia ya kufaulu na



    shule anayosoma haina waalimu bora halijui eneo hili?

    Hapa kuna vibanda vingi sana vinavyofundisha masomo ya ziada kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.

    Ni eneo maarufu ambalo huchangia wanafunzi wengi wasihudhurie vipindi vya kawaida shuleni na badala yake



    hujikita Mchikichini kwa ajili ya masomo ya ziada.

    Cha kufurahisha. Mchikichini mwanafunzi unalipa kwa siku kupata huduma. Hapana masuala ya malipo kwa mwezi.

    Jina George likatambaa kama upepo likafika Mchikichini.

    Huduma zake zikahitajika.

    Hesabu ugonjwa wa taifa. Daktari kapatikana.



    George alikuwa ana utaratibu wa kurejea nyumbani mapema baada ya kumaliza vipindi vyake mahali alipoajiriwa.

    Alipohitajika Mchikichini mambo yakaanza kuwa tofauti.

    Pesa huenda pale penye pesa. George alivyoanza kuikamata pesa ndogo na nyingine ndogo iliongezeka na kuwa kubwa.



    Pesa ikazidi kutiririka.

    Furaha kwa chokoraa huyu.

    Thamani yake ikapanda.

    Akatingwa haswa. Na akapokea pesa murua.

    George hakuwasahau watoto wa mitaani. Kila mara alipopata nafasi alifanya kitu alichoweza kwao.



    Kuna vitu kadhaa ambavyo humfanya mwanadamu anukie, sahau kuhusu marashi. Kuna umaarufu, kipaji, na kingine



    ni pesa.

    Pesa ikikuzoea hukufanya unukie, ukishanukia kuna viumbe wataisikia ile harufu, wakiisikia wataanza kukumendea ili



    wakunuse vizuri. Ole wako wakunuse!!

    George alianza kunukia.

    Akinadada wakatamani kumnusa. Akawakwepa kwa jitihada zote akafanikiwa kwa awamu kadhaa.

    Huo haukuwa mwisho wa mchezo.

    Mwanamke ni sumu, huua pale anapotaka. Lakini hukuua kama ukishawishika. Na hakuna jambo gumu kama



    kuikwepa sumu hii.

    Sumu iliyommaliza Adam na kujikuta akila lile tunda.



    George akapokea simu kutoka mahali asipopajua.

    Sauti ya mwanamke. Akajitambulisha kama mama Sakina.

    Akazungumza na George kuhusu kibarua cha kumfundisha mwanaye anayejiandaa na mitihani ya kidato cha sita.

    Sharti ni kwamba alitakiwa kumfundishia nyumbani.

    George hakuwa ameikinai pesa. Akakikubali kibarua.

    Malipo yalikuwa mazuri.

    George alikuwa na muda usiku pekee. Hivyo majira ya saa mbili alikuwa anafika katika nyumba hii kutimiza wajibu



    baada ya malipo.

    Alaaniwe binti yule aliyeubadili uelekeo wa kijana George.



    ****

    Nyumba nzuri ya kuvutia. Hii haikumshangaza George maana awali kabla ya kurejea katika dunia ya uchokoraa



    aliwahi kuishi.

    Gari nzuri za kifahari. Hata hizi pia aliwahi kuishi mahali zinapobadilishwa kila siku.

    Kwa bwana Emmanuel ambaye alikuwa baba yake mlezi.

    Hakushangaa!! Akapokelewa ndani.

    Akapelekwa mahali akajibweteka, akapewa huduma ya kinywaji alichoagiza. Baada ya kuulizwa.

    Mazingira yalikuwa mazuri sana.

    Wakati akiendelea kufanya utafiti na ukaguzi wa macho katika yale mazingira. Mara alikatishwa na hatua zilizojongea



    kwa kunyata.

    Kwa jicho la kuibiaibia alianza kumtazama. Akaugundua utofauti wake. Nywele zake zilitaka kufanana na za Frida,



    tofauti kati yao ilikuwa ni hizi anazoziona zilikuwa zinang’ara sana.

    Na hazikuwa fupi. Zilianguka hadi mgongoni.

    Alitembea kwa madaha sana. Na macho yake yalikuwa yamefunikwa na vioo vya mawani aliyokuwa amevaa. Alijongea



    hadi akamfikia George. Akaondoa ile miwani.

    “George!!...”

    “Shkamoo.”

    “Karibu mwalimu.” Alikwepa kujibu ile shkamoo.

    Yule mwanamke akaketi pembeni ya George. Marashi makali yakapenya katika pua ya kijana huyu. Hayakumkera zaidi



    ya kumburudisha.

    Mazungumzo yalipoanza George alibaini kuwa ile sauti haikuwa mara ya kwanza kuisikia. Alikuwa ni

    Yule mama aliyejitambulisha katika simu.

    Mazungumzo ya sasa yalikuwa juu ya lini somo linaanza.

    Baada ya kukubaliana kuwa lianze siku inayofuata. Sasa ikafuata zamu ya mwalimu kukutana na mwanafunzi wake.

    George alikuwa na uzoefu wa kukutana na wasichana walimbwende wakati yupo chuoni na kama hii haitoshi baada ya



    kuingia mtaani katika zunguka zunguka za huku na kule usiku wa manane aliweza kukutana na machangudoa. Hata



    hawa walikuwa warembo pia.

    Sasa mbele yake alikuwepo mwanadada anayefanana na wasichana hawa maarufu kwa biashara za usiku.

    “Naitwa Sakina.”

    “Mwalimu George ndio jina langu.” Alijitambulisha George.

    Mwanadada akabetua midomo yake.

    “We ndo umetumwa uje kunilinda.”

    George alishtushwa na kauli hiyo, akashindwa kujibu chochote akajichekesha.

    “Nimekuuliza mbona unajichekesha ndugu.” Aliongezea yule binti.

    Majibu ya yule binti yalimfadhaisha George, hakujua ni kwanini anamletea dharau hivyo. Kwa sababu haikuwa mara



    ya kwanza kudharauliwa alipuuzia. Na kumuona huyu naye ni wale wale.

    “Tutaanza na topic gani?” George aliuliza.

    “Yoyote unayojua.”

    George alibaki kushangaa!!

    Hakujua aegemee upande gani kimtazamo kuhusu binti huyu, ni jeuri ya pesa ama kuna jingine la kumfanya amjibu



    vile.

    Baada ya binti. Mtu wa mwisho kukutana na George alikuwa ni mzee ambaye haukuhitaji maelezo yoyote kumtambua



    kama mwenye nyumba hiyo. George akamsalimia kwa heshima zote.

    Mazungumzo yalikuwa juu ya mshahara na hatua za kulipana.



    ****



    MKEWE alidhani mume wake huenda amerogwa kutokana na uamuzi wake wa kujiingiza katika kinyang’anyiro cha



    kuwania udiwani. Ama la laana ya ndugu zake inamshambulia, laana ya kudiriki kuoa mwanamke wa dini nyingine kwa



    ndoa ya kiserikali badala ya kuoa mwanamke wa dini na mabila yao.

    Hofu ikatawala.

    Hali ilikuwa tete. Mume hakamatiki wala hashikiki, ukithubutu kumshauri anabwatuka matusi mazito. Tena mbele ya



    watoto bila kujali lolote.

    Kama hii haitoshi, baba mwenye nyumba akaibuka na mengine.

    Watoto wake waliokuwa likizo, kama ilivyo kawaida hujikita katika masomo ya ziada. Wakazuiliwa kutoka nje ya geti.

    Hakuna sababu yoyote waliyopewa kuwa ni chanzo cha maamuzi hayo lakini waliamrishwa wakatii.

    Sakina. Binti aliyekuwa kidato cha tano alikerwa sana na kitendo hiki cha mzee wake kupiga marufuku wao kutoka nje



    ya uzio. Lakini angefanya nini.

    Kimbilio lake likawa kwa mama. Nani kama mama? Hata tatizo liwe kubwa vipi anaaminika kuwa anaweza kulitatua.

    Sakina alihitaji kusoma somo la hesabu kwani hakuwa mzuri sana katika somo hilo na alikuwa amekaribia mitihani



    yake.

    Mama Sakina, mama wa kiarabu aliyeolewa na Dembele kwa sababu tu ana pesa akafanya aliloombwa na mwanaye.



    Dembele na kichaa chake cha hofu akajibu kwa hofu pia.

    Akamuagiza yule mama wa kiarabu atafute mwalimu mzuri wa kuja kumfundishia Sakina nyumbani. Hilo halikuwa



    wazo bali amri.

    Ikapitishwa.

    Dembele alikuwa katika mbio za sakafuni ambazo kwa namna yoyote ile huishia ukingoni. Yeye hakuamini kuwa kuna



    ukingo japo matumaini yalikuwa yanapotea kwa kasi.

    Kuizuia familia yake isionekane nje ya nyumba aliamini kuwa anawazuia wasiifikie siri ambayo hataki waitambue. Siri



    ya kuuza madawa ya kulevya.

    Sasa ameagiza mwalimu aletwe. Mama sakina anapata mawasiliano ya mwalimu ambaye anasifika sana kwa



    kufundisha somo la hisabati.

    Nani mwingine kama sio George?

    George anatangaziwa dau kubwa. Anavutika!!

    Baada ya kuelekezwa nyumba ilipo. Anaingia rasmi katika himaya ya bwana Mathias Dembele.

    Mwanaume anayesumbuliwa na siri kubwa moyoni siri inayomtesa.

    Ni mwanaume huyu aliyechanachana tumbo la mama yake mzazi George, akatia madawa ya kulevya mara nyingi



    awezavyo kwa manufaa yake. Akajitajirisha na sasa ile pesa chafu, anategemea kumlipa George kwa kumfundisha



    mwanaye, Sakina.

    Sasa mwalimu George na Dembele ana kwa na wakizungumza juu ya namna ya kupeana malipo.

    George anapendekeza kulipwa nusu kwanza na nusu nyingine baadaye.

    Wanaafikiana.

    George anaondoka, kwa makubaliano ya kuanza kazi usiku wa siku inayofuata.





    ****



    TAA iliendelea kuwaka hadi majira ya saa nane usiku.

    Haikuwa kawaida kwa kiumbe huyu kujisomea kwa muda mrefu kiasi hicho. Lakini siku hii alikuwa mzito sana



    kuzima taa.

    Kila alipojipa moyo kuwa anamalizia ukurasa mmoja kisha anazimisha taa, alitamani tena ukurasa mwingine. Sasa



    ilikuwa imetimia saa nane usiku na bado alitamani kuendelea kusoma. Hakuwa na usingizi bali alifanya kazi ya



    kupangusa machozi mara kwa mara.

    Kuna muda alifunika daftari lile na kujilaumu kuwa yeye ni mjinga aliyepitiliza. Analia kwa maandishi!!

    Maajabu na kweli!! Maandishi yasiyokuwa hai yanamtoa machozi

    Akajitia ujasiri akaendelea kusoma tena. Sasa kidogo alitabasamu, alichokisoma kidogo kiilimfariji.

    Ghafla giza!! Umeme ulikuwa umekatika.

    Akatoa tusi zito la kiingereza akiwatukana wahusika wa Nyanja hiyo ya serikali. Kisha akajibweteka kitandani, akaanza



    kumjengea picha mwandishi wa simulizi ile ya ajabu.

    Hakika ni mwandishi wa ajabu, maana binti huyu hakuwahi kuwa na kawaida ya kusoma makala yoyote ndefu.



    Aliamini kila makala ndefu ni siasa ama michezo, na hakuwahi kuvutiwa na vitu hivi. Hata alivyosikia baba yake



    anajiingiza katika mambo hayo alilaani kuwa mtoto wa mwanasiasa lakini angefanya nini wakati mzee nd’o ameamua



    tayari.

    Lakini sasa amesoma makala ndefu na ameburudika. Zaidi amejifunza kitu.

    “Alimaanisha nini sasa UKURASA ULIOSAHAULIKA!!” Alijiuliza yule binti. Akilinukuu jina la riwaya hiyo



    iliyoandikwa kwa mkono moja kwa moja lakini mwandiko ulionyooka vyema.

    Akiwa katika kufikiria ni kwa nini simulizi ile ambayo hajaimaliza bado ilimtoa machozi, akakumbuka kuwa kuna



    mistari mingi ilimshambulia moja kwa moja. Simulizi ile ilikuwa inamjenga mwandishi katika upande wa



    mlalamikaji, alilalamika kuhusu mengi sana ambayo kwa yeyote ambaye anaweza kufikiria lazima achukue hatua.

    Akakumbuka majibu yake aliyoyatoa kwa mwalimu wake mtarajiwa. Akajikuta katika HATIA huku aibu ikimsindikiza.

    Akazilaza nywele zake za kiarabu. Akajifunika shuka.

    Sakina akasinzia huku akijiwekea ahadi ya kumwomba msamaha George siku inayofuata.



    ****



    George alipopanda ndani ya gari aligundua kupungukiwa kitu. Alijipekua huku na kule lakini hakupata jibu.



    Akajituliza kwa sekunde kadhaa akapata jibu.

    Daftari lake lenye umuhimu huenda kupita yote. Daftari analolitumia kuandika simulizi.

    Licha ya kupitia magumu ya mtaani. Bado alipenda kuandika kila anachokipitia na chochote anachoona kinafaa



    kuandika.

    Aliihangaisha sana akili yake kupata kujua ni wapi alikuwa na daftari hilo kwa mara ya mwisho. Akili iliyochoka



    ikagoma kutoa majibu.

    George akafika nyumbani akiwa mpweke. Isha akaigundua hali hiyo.

    Akamuuliza George, kwa simanzi George akajielezea.

    Isha ambaye hakuona umuhimu wowote wa simulizi hizo aliishia tu kumpa pole isiyo na msaada zaidi.

    Akamuandalia maji bafuni, akaingia kuoga.

    Wakapata chakula pamoja. Kisha wakaingia kulala. Isha akamtoa George katika msiba ule wa kimawazo kwa



    kumkumbatia na kumwimbia nyimbo kadha wa kadha. George akasinzia.

    Siku ikamalizika.



    ****



    HAKUNA somo lenye washabiki wachache kama hisabati, licha ya kuonekana kuwa gumu upande wa wasichana,



    lakini hata wanaume huangaika nalo kimya kimya bila kulia hadharani kama wsasichana ambao ipo wazi kuwa jitihada



    zimeshindikana kujikwamua katika somo hilo..

    Ukipewa talanta ya kulifahamu vyema somo hili basi nafasi yako katika jamii inakuwa kubwa na ya kuheshimika.

    George alikuwa analifahamu vyema somo hili. Akageuka daktari wa hisabati.

    Wagonjwa wake wengi wakawa wasichana.

    Wasichana wa vidato kuanzia cha tatu hadi cha sita, kwa mjini hawa ni wasichana wakubwa na wengine wanawatunza



    wazee umri wa baba zao.

    George hakuwahi kukutana na dhahama hii ya usumbufu. Lakini huu ulikuwa usumbufu wa maajabu, usumbufu



    usiokuwa na maneno ndani yake.

    Usumbufu wa vitendo!!.

    Mara huyu avae hivi mara yule arembue jicho. Ilimradi shaghalabaghala.

    Mwanaume akajikaza!!

    Lakini atajikaza mara ngapi iwapo usiku ule uvumilivu ulimshinda akataka kumbaka Isha??

    Hata kama hakumbaka sasa ana ujauzito.

    Hata George ni mwanadamu!!





    ****



    MAJI ukiyavulia nguo sharti uyaoge. Mwanaidi alikuwa ameamua kupigana kwa ajili ya watoto yatima na wasiokuwa



    na makazi. Watoto ambao wameugeuza mtaa kuwa makazi yao. Watoto waliobandikwa jina nchini Kenya wakiitwa



    ‘chokoraa’ jina ambalo linatumika sasa afrika mashariki kwa ujumla.

    Kadri mwanaidi alivyoikamata pesa ndivyo alivyoona kuwa haitoshi katika harakati zake. Alitakiwa kufikiri zaidi



    anapata vipi pesa nyingi zaidi ili aweze kutimiza alichonuia katika akili yake.

    Sasa alikuwa amefanikiwa kuikamata akili ya diwani na alikuwa amechota pesa nyingi.

    Jambo la kwanza lilikuwa kumpeleka mama George katika huduma ya afya.

    Huku aligharamika kiasi kikubwa cha pesa ikiwemo ya kuwahonga madaktari ili wasipeleleze zaidi alikumbwa na nini



    hadi kufanyiwa upasuaji mbovu namna ile.

    Kwa hili alifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

    Jambo jingine alilolifikiria kwa wakati uliopita na sasa alilitendea kazi ni kuhusu kutafuta nyumba kubwa.

    Madalali wa mjini wakachukua pesa yao na nyumba ikapatikana.

    Nyumba ya vyumba viwili pamoja na sebule.

    Maisha mapya!!



    Frida akaanzishwa kliniki. Kwa ajili ya ile mimba yake isiyokuwa na baba.

    Mwanaidi akawa mlezi rasmi wa familia.

    Familia yenye muunganiko wa damu tofauti tofauti ambazo kiini chake kikuu ni mtaa.

    Maisha yakaendelea.



    ****



    WIVU wa mapenzi. Hauchagui kaliba yoyote katika jamii. Maskini anao, tajiri anao vilevile.

    Usiombe wivu ukauteka moyo wako. Waweza kujikuta unafanya mambo ambayo mjukuu wako akisimuliwa atakiri



    kuwa bibi ama babu yake alikuwa na wazimu. Si bure!!

    Huwezi kutambua kama una wivu, wivu humfanya mtu awe mjingamjinga na kujiona anayofanya ni sahihi.

    Ule wivu ulioiondoa roho ya mwanadada Emiliana. Sasa ulikuwa unashambulia na kuigalagaza roho nyingine katika



    mazingira mengine.

    Huyu alikuwa anahangaika muda mrefu lakini hakuweza kulalamika popote kwa kuwa tu hakuwa na ushahidi wa



    kumpa uhuru wa kuongea.

    Je? Ushahidi unajileta wenyewe? Jibu ni hapana. Ushahidi hutafutwa.

    Binti huyu akalazimika kuutafuta ushahidi, kimya kimya kama alivyofanya marehemu Emiliana kwa mume wake



    mtarajiwa Kasuku.

    Mitego aliyokuwa ameitega ili imnase ushahidi sasa ilikuwa imetoa majibu aliyoyasubiri. Majibu yaliyomkera na



    kumfanya ajute kufanya upelelezi ule.

    Kichefuchefu kikamshika. Akatamani kutapika lakini hakutapika.

    Akawahi limao lake akakikabiri.

    Njiani aliona maluweluwe. Hakuamini alichokiona, lakini alijilaumu kwa nini alikitafuta.

    Hakuitikia salamu ya mtu yeyote yule. Alitembea akiyumba huku na kule, akaufikia mlango wa chumba chake



    akaufungua. Akajitupa kitandani. Akamngoja adui yake aweze kurejea amkabili.

    Mwanzoni hakuhisi usingizi kabisa lakini alikuja kushtuka asubuhi.

    Adui alikuwa anamalizia kufunga mkanda wa suruali yake aende kazini.

    Alitaka kumzuia lakini akajikuta anaagwa. Hakujibu!!



    Subira yavuta heri endapo yule hasira ambaye majibu yakle ni hasara atakuwa likizo.

    Lakini siku hii hasira alikuwa amejikunyata katika moyo wa mwanadada huyu. Hivyo subira akawa ameondoka zake.

    Hakuweza kuikabili hasira hii.

    Aliona yule bwana wake anachelewa kurejea akaamua kutoka mwenyewe aweze kumfuata. Alitegea mida ile ya siku



    iliyopita, alitegemea kumuumbua.

    Akiwa njiani anakutana na kundi la akina dada.

    Alikuwa anawafahamu wawili kati yao.

    Hasira zikachachamaa. Akawakabili. Akawasimamisha.

    “We malaya George ni nani yako?”

    “Malaya? Nani Malaya..na George yupi?” alijibu kwa kiburi binti mnene mfupi.

    “Nakuuliza George ni nani yako. Yule mwalimu.” Alitoa maelezo ya ziada.

    “Mwalimu wangu kwani vipi? Unataka namba yake? Kakujaza mimba nini?” alijibu kwa dharau. Wenzake wakacheka.

    Sasa akakumbwa na msukumo wa hasira isiyosimulika. Akamvamia yule aliyetoa majibu yale. Akaanguka naye chini.



    Akaanza kumshambulia na makucha.

    Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Wale wasichana wawili wakajiunga kumtetea mwenzao.

    Kibao kikamgeukia yule binti. Ambaye alijuta kuzaliwa chokoraa na kisha kuitwa Isha. Akaijutia ile mimba aliyopewa



    na George.

    Majuto hayo yakawa na thamani yake.

    Akaupata msaada.



    ****

    George, akiwa darasani siku hii alikuwa anawaza juu ya msichana wa kitanga ambaye alikuwa katika wakati mgumu



    sana kukabiliana na hisia hizi. Hisia za ajabu.

    Alikuwa anajiuliza aliwahi lini kukumbana na hisia hizi.

    Alipoumiza kichwa sana akamkumbuka Frida. Siku ya kwanza walipoonana wakati anasoma chuo kikuu.

    Upendo!!

    Aliamini alikuwa anampenda.

    Lakini kikwazo kikubwa kilikuwa ni Isha. George alitambua kuwa licha ya kwamba anaishi na Isha bila kuwa na



    mipango yoyote ya mbeleni. Lakini alikuwa amembebea mtoto wake.

    George aliogopa kujihusisha na msichana mwingine kwa kuhofia kumjaza msichana mwingine mimba kisha kuongeza



    wimbi la watoto wa mitaani.

    Hakutaka kabisa kuhusika katika tatizo hili. Kwani yeye alikuwa katika harakati za kulipunguza tatizo na si



    kulitawanya kama hivi anavyowaza.

    Binti huyu wa kitanga aliyekuwa kidato cha tano. Alikuwa na kila kigezo cha kuitwa mrembo. Lakini hili halikuwa na



    maana kubwa kwa George. Na alilipuuzia mpaka siku ambayo alichelewa kutoka kazini baada ya mabinti watatu



    kumsihi awasaidie maswali kadhaa ya somo la hesabu.

    Kati ya mabinti hawa alikuwemo binti wa kitanga.

    Baada ya kumaliza kufundishana, mabinti na mwalimu waliongozana njia moja.

    Marafiki wawili wakapeana ishara. Mara George na Lisa wakabaki peke yao. Marafiki wawili wakifuata kwa nyuma.

    Aliyesema mapenzi yalizaliwa Tanga huenda hakukosea.

    Lisa akaanza kufanya yale aliyoyajua. Ilimradi tu kumtega bwana George.

    George ni mwanaume na macho yake hayana pazia. Kilicho chema machoni naye kwake pia kilikuwa chema.

    Akajisahau kama ni mwalimu. Akauvaa ujana.

    Yaliyotokea, yaliwafanya waonekane kama wapenzi wa siku nyingi.

    Wakati yanatokea. Lilikuwepo jicho la mwanadada mjamzito Isha likifuatilia kwa ukaribu.

    Isha hakutaka kuwavamia kwa wakati ule.

    Akaachana nao akawahi nyumbani.



    George alipoachana na Lisa alijutia alichokifanya. Japo hakikuwa na madhara yoyote, sawa lakini ni kosa kukamata



    kiuno cha msichana hadharani. Walionitazama watanionaje? Hata Isha angenifikiriaje?

    Mimi ni mwanaharakati. Sitakiwi kuwa dhaifu!!

    Nikirudi nyumbani nitamshirikisha Isha juu ya jambo hili. Najua atanishauri vizuri. Alijisemea George.

    Hapo alikuwa katika basi akielekea nyumbani kwa akina Sakina. Kwa ajili ya somo la usiku.

    Ilikuwa bora huku alipotoka kuliko hapa anapoelekea maana mitihani ilikuwa inamkabili.



    Usiku aliporejea Isha alikuwa amesinzia fofofo.

    Hayakufanyika mazungumzo yoyote yale.

    Asubuhi kama ilivyo ada alitakiwa kuwahi kazini.

    Alimuaga Isha. Lakini hakujibiwa.

    Hakujali, aliamini ni mang’amung’amu ya usingizi.



    Sasa ni jioni anakumbwa na mshtuko. Yule binti aliyemuacha kitandani. Akiwa katika lindi la usingizi.

    Anakutana naye akiwa hana fahamu. Amezungukwa na wanafunzi wakimshangaa tumbo lake kubwa likiwa nje.

    George anapigwa na butwaa kukutana na Isha katika hali ile.

    Hapakuwa na haja ya kujiuliza maswali mara mbimbili. Hakuwepo wa kuyajibu.

    Zikachukuliwa hatua.

    Isha akapelekwa katika kituo cha afya kilichokuwa jirani.

    George badala ya kwenda nyumbani kwa akina Sakina, aliandamana na gari la walilokodi kumpeleka Isha hospitali.

    Hali tete!!





    ****



    Seba Sebastian, diwani aliyekuwa na nia ya kuwania tena kiti cha udiwani alikuwa anafurahia kila hatua aliyokuwa



    anapitia kwa wakati huu. Habari aliyoinunua kwa bei mbaya sasa ilikuwa inampa faraja. Lazima afarijike maana habari



    ile ni kama majibu ya uchaguzi uliotarajiwa kufanyika, uchaguzi uliokuwa ukimuumiza kichwa.

    Katika pitapita zake huku na kule aliweza kuzisikia tetesi juu ya bwana Dembele na shughuli zake za kuuza madawa.



    Lakini kati ya hawa wote hakuna hata mmoja ambaye alikuwa na uhakika juu ya anachokizungumza.

    Hali hii ilimpa faraja Seba na kujiamini kabisa kuwa ni yeye pekee anayehodhi habari ile kiukamilifu. Jambo hili



    lilimpa faraja zaidi na kujikuta akimshukuru Mwanaidi kwa biashara waliyofanya.

    Alihitaji sasa kuifanyia kazi habari hiyo. Asingeweza kwenda peke yake kufanya maamuzi haya. Yule mwanamke wake



    mbichi kabisa ambaye alikuwa anamuandaa kuwa mke wake baadaye ilikuwa lazima ashirikishwe. Ni huyu alikuwa na



    mawazo ya kisasa na msomi.

    Seba alikuwa na mke na watoto lakini bado alikiuka maadali ya dini yake akaweka nyumba ndogo. Nyumba ndogo hii



    aliitunza tangu ikiwa shuleni. Alimlipia ada na kumgharamia kila kitu na sasa alikuwa amemaliza chuo kikuu.



    Alimchukulia Seba kama baba yake wa kumzaa, wazazi wake wote walifariki kitambo na hakuwahi kuwatambua.

    Walipishana sana umri kwa kiasi kikubwa lakini angefanya nini binti yule iwapo alikuwa anahitaji huduma za mzee



    Seba?

    Hakuwa na ujanja. Akafunika kombe mwanaharamu apite.

    Kwa kuwa Seba alikuwa na elimu duni. Alikumbwa na kihoro akaketi meza moja na mtoto wake huyu ambaye



    anamuandaa kuwa mke wa pili. Akamfungukia kila kitu juu ya habari aliyoinunua.

    Habari kuhusu Dembele.

    Binti alisikiliza kwa makini sana. Kisha akachukua nafasi ya kutoa ushauri baada ya kushukuru kwa kushirikishwa.

    Akamshauri avute subira kidogo, uchaguzi ukikaribia ndipo amuumbue bwana yule.

    “Yule mtoto hawezi kuiuza tena habari hii?” Seba aliuliza.

    “Akiiuza bado itamchafua bwana Dembele na atakuachia kiti..tena hiyo itakusaidia sana maana hautakuwa na hatia



    yoyote na hawezi kukuwekea kisasi.” Alijibu kwa utulivu, usomi ukichukua nafasi.

    Seba akakolea.

    “Sikukosea kukuchagua.” Alisifia mzee huyu kisha akamkumbatia na kumbusu shavuni. Suzi naye akambusu katika



    paji la uso kisha akampapasa huku na kule katika namna ambayo anajua kuwa ilimpendeza bwana huyo….

    Mzee seba alilala katika nyumba aliyompangia binti huyu.

    Asubuhi akaondoka na kuiacha ile siri ikiwa sio siri tena.

    Alijisahau kuwa hakuna siri ya watu wawili.

    Kitita cha pesa kiliachwa mezani kama sumaku ya penzi. Asidanganyike na wajanja wa jiji akamsaliti.



    ****



    MAPENZI ni kitu cha ajabu sana, mapenzi kati ya watu wawili huletwa na hisia. Na mara hisia zisipokuwepo basi



    mmoja kati ya wahusika anatakiwa kuleta ushawishi ambao utasababisha hisia kuibuka..

    Mwalimu wa kike hakuwa na amani hata kidogo moyoni. Mshawasha wake wa kumuona George ulikuwa



    unamwadhibu.

    Siku hiyo alitambua kuwa lazima itakuwa siku ya kipekee kwake.

    Siku ya kumshawishi kitu George.

    Maajabu George kuchelewa kazini.

    Dakika, masaa yakakatika. Bado George hakuonekana na hapakuwa na taarifa yoyote ile. Kibaya zaidi hakuna aliyejua



    nyumbani kwake.

    Suzi akakosa amani. Jambo alilobeba moyoni lilikuwa linamsumbua sana.

    Jioni ikafika, bado George hakuonekana.

    Suzi akamlaani George kimoyomoyo kwa kutomiliki simu ya mkononi wakati uwezo alikuwanao. Akaikumbuka tabia



    ya George kupenda kuazima simu kila mara anavyohitaji kuzungumza na watu wake, hata siku ya kuzungumza na



    mama Sakina alitumia simu ya rafiki yake. Namba ambayo alikuwa anaitambulisha kama yake kwa waliohitaji.

    Suzi hakuamini kabisa kama ataweza kupata usingizi katika hali hii ya mawazo. Lakini angefanya nini? Akaamua



    kuondoka huku amani ikizidi kumkimbia. Alimuhitaji sana George.



    Wakati Suzi akihangaika kumuwaza George. Wakati huo George alikuwa akihangaika huku na huko kulipia pesa za



    matibabu.

    Hakuwa na pesa ya kutosha kutokana na kuwaazimisha waalimu wenzake pesa pamoja na kulipia kodi ya nyumba.



    Sasa pesa ilihitajika huenda kuliko vipindi vyote alivyokuwa anapitia.

    Si kwamba hakuwa na akiba ya pesa nyingine la!!

    Pesa ilikuwepo lakini anayefahamu pesa zilipo alikuwa amepoteza fahamu.

    Isha alikuwa mtunzaji wa pesa nyingine katika njia ya kibubu, ambacho alifahamu mwenyewe ni wapi anakihifadhi.



    Mwanaume alitakiwa kuchukua maamuzi. Akafikiria kukimbilia katika familia ya Dembele, moyo ukasita. Alihofia



    kujibiwa vibaya maana Sakina hakuwa anatabirika. Akapiga kite cha hasira na kumwangushia lawama muumba mbingu



    na nchi kwa kumuumba katika tabaka la kimasikini.

    Suzi !!

    Jina hilo likashambulia kichwa cha George. Akamkumbuka binti huyo mhitimu wa chuo kikuu ambaye kwa muda huo



    wa kutafuta kazi alikuwa anafundisha masomo ya ziada pia. George aliminini kuwa ni huyu ambaye anaweza



    kumsaidia bila kuuliza mara mbilimbili….George alikuwa na sababu ya kuamini hivyo

    Suzi licha ya kuwa mwalimu na yeye alikuwa katika mpambano na wanafunzi wengine wengi wanaomuwinda George



    kimapenzi.

    Aliwahi kumkaribisha George nyumbani kwake mara mbili lakini hakufanikiwa kumteka kimapenzi.

    Suzi alikuwa akimuhitaji sana George. Lakini mazungumzo kati yao yalileta huzuni kubwa. Japokuwa maisha ya Suzi



    yalikuwa vyema kutokana na kutunzwa na diwani. Bado alibakia kuwa yatima, aliyepata adha ya uyatima utotoni



    pekee.

    Historia ya George na mipangilio kabambe aliyokuwanayo katika kuwaokoa yatima na chokoraa ilimkosha Suzi na



    kuahidi kuwanaye bega kwa bega

    Walihitaji pesa kufanikisha harakati hizi.

    Pesa hiyo ilikuwa kikwazo na sasa pesa hiyo inayohitajika inamsukuma George kwenda kwa Suzi.

    Suzi hakutegemea ujio wa George. Akiwa na kanga moja pekee alimkumbatia George kwa nguvu. Na ghafla



    akambusu. George akajilazimisha kutabasamu.

    MAPENZI KITOVU CHA UZEMBE. George alianza kuyaendekeza.

    Mchezo wa kulala leo na huyu kesho na yule alianza kuufurahia huku akiamini ni kati ya starehe aliyokuwa anajinyima



    kwa muda mrefu. Hakupenda kujionyesha waziwazi kuwa upande wake wa pili ni mtu wa namna ile. Alivaa sura ya



    mwanaharakati ambaye anafundisha pia somo la hesabu.

    Wanafunzi wa kike waliojigonga kwa mwalimu huyu hawakucheleweshwa walishughulikiwa ipasavyo kisha



    kusahaulika.

    Isha alikuwa ametoa msamaha wake tayari kwa George na sasa waliendelea na maisha kama awali.

    ****

    Suzi akaketi hovyo mbele ya George ambaye hakuwa na furaha.

    “Una nini Gee”

    “ Acha tu…..Suzi kuna tatizo. Dada yangu mmoja amefikwa na tatizo. Yupo hospitali mi sina kitu nahitaji sana msaada



    wako we fanya kuniazima..halafu…”

    “Mimi na wewe hatuazimani. Shilingi ngapi inahitajika. Pole sana G najua ni kiasi gani una upendo wa dhati kwa



    chokoraa na yatima”

    George akataja kiwango cha chini kabisa. Akapewa mara mbili yake.

    “George ukitoka huko hospitali pliiiz usiache kuja kuna jambo zito kwa faida yangu na yako. Usiache hata kama ni



    usiku vipi?” Suzi alimsisitiza George wakati anatoka.

    George akakubali.

    Akatoweka upesi kuwahi hospitali. Hakuamini ingekuwa rahisi kiasi hicho kukomba pesa kwa Suzi.

    Kichwani aliamini kuwa Suzi alimhitaji usiku huo kwa ajili ya mapenzi tu hapakuwa na jipya lolote.

    “Ameninunua tayari sina ujanja.” Alikiri kwa sauti ya chini akiwa peke yake.

    Aliwasili hospitali na hali ya Isha ilikuwa vyema tofauti na awali lakini daktari hakuwa na furaha na mafanikio haya ya



    kumrejesha Isha katika hali ya awali.

    George alipowasili alikaribishwa kuonana na daktari.

    “Naona ameamka!!” George aliongea huku akimtazama daktari aliyelilazimisha tabasamu.

    Daktari alimpa maelezo ya kitaalamu George huku akimsisita kuwa na jasiri. Kauli ya kutakiwa kuwa jasiri ilimshtua



    George lakini hakutia neno.

    “Mgonjwa wetu anatakiwa kufanyiwa upasuaji….upasuaji wa haraka sana. Hivyo hapo zinahitajika pesa kiasi.



    Mwenyewe hajui kuhusu hilo. Ana furaha na tusingeweza kumwambia chochote. Mtoto aliyembeba amefia tumboni,



    na tumejaribu kumchoma sindano ya maji ya uchungu haijafanya kazi na kama isipofanya kazi masaa ishirini na nne



    mbele hakuna ujanja zaidi ya kumfanyia upasuaji. Na masaa ndo haya yanayoyoma.” Daktari alijieleza kwa marefu na



    mapana. George alikuwa amekodoa macho, hakujua lolote kuhusu maji ya uchungu, alichotambua pale ni kuwa damu



    yake si hai tena. Imetoweka.

    Hakuweza kuzungumza. Daktari aliendelea kuwa muongeaji mkuu.

    Hitimisho likawa kumfanyia upasuaji Isha.

    Kwa kuwa ilikuwa hospitali binafsi, huduma hii ililipiwa. Tatizo la pesa halikuwepo.

    Asubuhi Isha hakuwa yule Isha mwenye tumbo kubwa tena. Hakuwa na mimba. Kisu kilipenya na mtoto ambaye



    hajatimiza siku zake akatolewa akiwa mfu.

    Aliomboleza kwa muda, akabembelezwa akatulia.

    Aliendelea kubaki palepale hospitali kwa ajili ya kufanya mazoezi mepesimepesi ya kumrejesha katika hali ya kawaida.



    ****



    Msongo wa mawazo ulimhangaisha George. Hakutamani kulala katika kitanda alichokuwa analala na Isha.

    Alijiona ni mtu mwenye mikosi kila siku. Alizaliwa katika mazingira na ajabu akakulia katika raha yenye mashaka.

    Alimpoteza Frida na sasa Isha yu matatizoni.

    Siku hii akaenda kuimalizia nyumbani kwa Suzi.

    Huku aliamini wanaweza kubadilishana mawazo.

    Alimkuta Suzi anaandaa chakula jikoni. Wakasalimiana kisha akaketi kumngojea Suzi amalize kupika.

    Wakati chakula kikiwa mezani mazungumzo yaliendelea. Tofauti na George alivyodhania kuwa Suzi yupo kimapenzi



    tu.

    Hali ilikuwa tofauti. Suzi akamueleza George kuwa pesa imepatikana. Pesa ya kufanya harakati za kumkomboa



    chokoraa na yatima.

    George akaweka umakini na kumsikiliza Suzi. Naye bila hiana akazungumza yote aliyoambiwa na hawara yake ambaye



    ni diwani.

    “Kwa hiyo?” George aliuliza.

    “Tunatakiwa kumuuzia huyo Dembele habari hii kwa bei mbaya.” Suzi alimwambia George. Kisha akaongezea “Kwa



    kuwa anahitaji sana kuheshimika katika jamii na hakuna apendaye kwenda jela. Basi lazima ainunue taarifa hiyo



    ambayo ni ya muhimu kwake kuliko sisi.”

    Suzi akaeleweka. Wakapanga mikakati ya siku gani wakutane na Dembele.

    Suzi asingeweza kwenda kuonana na Dembele, walifanya hivyo ili kumpoteza diwani asijue ni nani aliyeiuza siri hiyo.

    Wakakubaliana hiyo siku iwe baada ya siku mbili.



    Mtafutaji hachoki na akishachoka ujue kapata. Usemi huu ulitenda kazi siku ambayo Dembele alimkabidhi George



    kitita. Hawakuwa katika mazungumzo juu ya masomo ya ziada anayosoma Sakina ama lolote lile kuhusiana na mambo



    ya elimu hapa walikuwa katika biashara ya kuuziana siri. Dembele hakutaka kuwa mbishi alifanya hivyo upesi kwani



    George alitishia kuwa iwapo atagoma kuinunua basi atawaruhusu wanaoimiliki taarifa hiyo waitumie wanavyotaka.

    Mwanzoni Dembele alitaraji kumpatia pesa George kisha kumfuatilia na kumwondoa duniani lakini baada ya kusikia



    kuwa wapo watu ambao wapo nyuma yake alifadhaika na kumuacha kama alivyo.

    Lakini alijiweka makini sana naye.

    Alitulia akitunga sheria ya ni kwa jinsi gani atazitwaa roho zilizohifadhi siri hii.

    Baada ya siku kadhaa Sakina alirejea shuleni na huu ukawa mwisho wa George kufika katika nyumba ile mara kwa



    mara.



    ****

    PESA mwanaharamu, George hakutegemea kuzikamata kwa uwingi kiasi kile. Uwingi ule ukampagawisha.

    Kwa akili ya kibinadamu akamsahau Isha kwa muda. Na ilikuwa ngumu kumkumbuka iwapo hana ujuzi kama watoto



    wa mjini.

    Akiwa mtaani mara akalikumbuka kumbatizi la mtoto wa kitanga, Lisa. Hakika lilikuwa kumbatizi maridhawa ambalo



    hajawahi kulipata. Kucha za bandia zilizojipenyeza na kumfinyafinya zilimpatia hisia fulani ya ajabu.

    Akaitamani tena ile hisia ijirudie. Na itajirudia vipi kama sio kumtafuta Lisa?

    George akaingia kinyemela eneo la Mchikichini, akafanikiwa kumpata Lisa mtoto wa kitanga.

    Akasahau kabisa kuwa anaye mgonjwa hospitali.

    Alihitaji kukumbatiwa, lakini hakutaka iwe hadharani.

    Akajikongoja akalipia chumba katika nyumba ya kulala wageni.

    Lisa ambaye alikuwa anamtamani George siku nyingi akaiona nafasi hiyo ni ya kipekee kwake kutimiza haja zake.

    Wawili ndani ya chumba. Uwezo wao wa kufikiri ukiwa umesahauliwa majumbani kwao, hapa vichwa vilikuwa wazi



    kabisa.

    Walichokifanya, wanakijua wao. Na hawakujutia maana kiliwafurahisha.

    Mtoto wa kitanga aliyefunzwa kisha akauongezea ufundi binafsi, akamnyanyasa George ipasavyo.



    Waliagana asubuhi ya siku iliyofuata. George hakukumbuka hata kumuuliza yule binti ni kwa nini hajarejea nyumbani



    kwao angali hakuaga.

    Asubuhi hii George akiwa na zigo la pesa alifika nyumbani kwa Suzi ambaye alikuwa amemuuza rasmi diwani bila



    kujali lolote baya litakalomtokea.

    Furaha yao ya kuzipata zile pesa nayo ikaishia pabaya.

    Suzi akaitumia fursa hiyo kumshawishi George.

    George akashawishika, japo alikuwa amechoka sana lakini akajikaza kisabuni akajivinjari na binti huyu.

    Katika haya yote hakuna aliyejali kama wametumia kinga ama la.

    George akaanza kujisahau kama yeye ni mwanaharakati.

    Akamsahau na Isha!!





    ****



    MWANAIDI alikuwa amejiegesha katika kitanda cha futi sita kwa tano kilichopo katika nyumba ya kulala wageni



    maeneo ya Magomeni jijini Dar es salaam. Mara hii si kwa lengo la kumsubiri mwanaume wapate kustarehe kwa



    malipo maalum la! Hakuwa na shida na pesa ya mwanaume tena sasa alikuwa anaweza kusimama yeye kama yeye huku



    akitumia mbinu nyingine mbadala, mbinu hizi zilikuwa zinamuingizia pesa nyingi, na zilimpa matumaini ya kuweza



    kutimiza kile ambacho anakiota kila siku. Kwanza Mwanaidi aliweza kuuondoa uhai wa mkuu wa kituo na kutwaa



    pesa, pili alimshawishi diwani na kuondoka na pesa lakini hizo hazikumtosha kuna pesa ya ziada aliihitaji ili aweze



    kutulia na kupanga mambo mengine ya msingi hasahasa ni kwa namna gani anawakomboa watoto wengine na



    kuirejesha furaha yao tena.

    Sasa alikuwa akihesabu masaa ili aweze kupata taarifa juu ya jambo ambalo alikuwa amelifanya kwa uangalifu



    mkubwa sana. Huenda kupita majaribio yote aliyoyafanya kipindi cha nyuma.



    Tabasamu lilikuwa linachanua katika midomo yake huku akiona kila jambo likienda sawia, alikuwa amejiegesha katika



    kitanda huku akiuegemea mto mweupe mkubwa uliokificha kichwa chake cha mviringo, alijipakata kichwa chake kwa



    viganja vya mikono yake macho yake yakilitazama pangaboi lilivyokuwa linazunguka, alijiuliza ilikuwaje akawa



    anapata mawazo ya kupata pesa na kufanikiwa kwa wepesi namna ile lakini hakupata majibu.

    Yawezekana ni Mungu anatenda maajabu! Alijiuliza, lakini Mungu gani huyu anayejibu wakati mimi ni muovu?



    Alijiuliza na safari hii alifanya tabasamu dogo kisha akapiga mbewe.



    Mwanaidi alikuwa na haki ya kushangaa kisha kujiuliza inakuwa vipi anayaweza yote haya kwa umri wake mdogo.



    Lakini alijikatisha kujiumiza kichwa na maswali yasiyokuwa na msingi. Alifurahia kumiliki pesa nyingi na alikuwa



    anafurahia kijana aliyemuagiza mahali kwa ajili ya kwenda kuchukua pesa nyingine, nyingi zaidi kwa nini asiendelee



    kufurahi?

    Huyu kijana aliyeagizwa alimuamini sana na hivyo Mwanaidi hakuwa na mashaka kabisa. Aliamini kuwa hapatakuwa



    na jambo lolote la kuzuia mkakati huu zaidi kwa jinsi alivyoupanga.

    Muda ulizidi kwenda bila majibu yoyote. Mwanaidi akachukua simu yake aweze kumpigia na kumuuliza kulikoni,



    akaanza kupekua alimuhifadhi kwa jina gani, ghafla akatokwa na msonyo mrefu kisha akaitupa simu kitandani,



    alikumbuka kuwa kijana Yule hakuwa na simu kwa siku hiyo. Huyu alikuwa ni aina ya kijana ambaye akiwa na simu



    leo kisha akapatikana mteja. Anaiuza siku hiyohiyo huku mfukoni akibaki na kadi yake pekee na maisha yanaendelea.



    Mwanaidi akajikuta akilaani tabia hiyo vikali kwa sababu tu amejikuta akiwa muhanga.



    Taratibu Mwanaidi alianza kuingiwa na hofu bila sababu, mapigo ya moyo yaliongeza kasi yake bila kushtushwa na



    chochote, bila shaka kuna roho ilikuwa inazungumza naye, haikuwa mara ya kwanza hali hii kumtokea enzi za



    uchokoraa alikutana nayo mara kwa mara na kila alivyoshtuka na kukimbia alijikuta akiikwepa dhahama aidha ya



    mgambo wa jiji ama vibaka wasiokuwa na huruma lakini kwa mara ya kwanza katika maisha yake akaipuuzia hofu



    hiyo. Akayapuuzia machale yaliyokuwa yakimcheza kuwa huenda kuna jambo lilikuwa limeharibika. Alipuuzia



    kutokana na misingi thabiti aliyokuwa ameiweka na mbinu aliyokuwa ametumia kufanya jambo hili.



    Chumba kikaanza kuonekana kidogo kupita ule ukubwa wa awali, kijasho kikaanza kumtoka Mwanaidi, kila



    alivyojaribu kupuuzia ndipo hali iulizidi kuwa mbaya moyoni. Mapigo ya moyo yalizidi kukimbia kwa kasi, alitamani



    kuondoka lakini akajiuliza je? Akiondoka kisha Yule kijana awasili itakuwaje? Na je akihamia sehemu nyingine wakati



    Yule kijana amemuelekeza tayari kuwa atakuwa katika chumba kile nini kitajiri? Bila shaka ni kupoteza pesa zake



    kiurahisi kwa kijana huyu kutokomea nazo……

    Lakini sipo katika hali ya kawaida jamani!! Alisema kwa sauti yua juu Mwanaidi. Ni kama roho ilikuwa inazungumza



    naye sasa kwa sauti ya juu. Mwanaidi akajisikia vibaya sana kuyapuuzia machale yake.

    Au ni joto jamani? Akajiuliza…..lakini mbona feni linapuliza kwa nguvu sana akasikia kama anajibiwa….lakini



    alikuwa anajipa jibu mwenyewe. Hofu ikaendelea kutanda.

    Kati ya kuheshimu machale na kungoja pesa kipi muhimu? Alisikia kama swali katika masaikio yake…….Mwanaidi



    akajikuta anajibu kuwa ni kuheshimu machale yake…lakini alikuwa anahitaji pesa…

    Hilo likawa kosa kubwa kati ya makosa yote yaliyowahi kufanywa na Mwanaidiu hakika lilikuwa kosa kubwa sana!!

    Ndio ni kosa kubwa sana lililofanywa na Mwanaidi. Ni heri angeyaheshimu machale yake. Huenda hili lisingetokea.



    Jambo la kufedhehesha kupita yote.



    ….Mlango wa chumba chake uligongwa kwa utaratibu. Akauliza nani mgongaji, sauti ya kiume ikajibu kwa upole



    sana.

    Mwanaidi akacheka kidogo. Alicheka huku akiyalaumu yale machale kuwa yalitaka kumpoteza kwa siku ile.



    Akauendea mlango na kuufungua bila chembe ya wasiwasi huku akijiahidi kumlaumu Yule kijana kwa tabia ya kuuza



    simu hovyo, akajiapiza pia kuwa atamnunulia simu nyingine upesi ili waendelee kuwasiliana.

    Hakutegemea kama ingekuwa rahisi kiasi hicho wala kuwa ngumu kiasi hicho kilichotokea. Yule kijana hakuwa kijana



    pekee, lilikuwa ni kundi la watu. Mwanaidi alitaka kupiga kelee kuomba msaada lakini moyo ukaongea bila mdomo



    kusaidia lolote. Hakuna aliyeweza kusikia.



    Mara akasukumwa ndani, kundi lote likaingia. Akataka kufurukuta akakutana na pigo maridadi mgongoni akatulia.

    Mwanaidi bila silaha yoyote anatiwa mikononi mwa wanaume wawili. Kisha mmoja anamtazama kwa macho makali



    yaliyojaa chuki. Macho yasioyokuwa na huruma hata kidogo japo midomo ilitabasamu

    Mwanaidi ana kwa ana na bwana Dembele!!

    Yule mnyanyasaji aliyemteka kwa nia ya kumtumikisha biashara ya madawa ya kulevya. Mwanaharamu aliyepasua



    tumbo la mama George na kurundika madawa ya kulevya, hayawani asiyekuwa na huruma.



    Mwanaidi alipojaribu kufurukuta alikutana na mkono imara, ukalisalimia shavu lake. Ni kama alikuwa amepigwa na



    kipande cha ubapa wa panga, akaona nyota nyota kisha giza, Maumivu yakatambaa chozi likamtoka. Alipopata nuru



    aligundua kuwa Dembele alikuwa amemchapa kofi.

    Dembele akatabasamu. Mwanaidi akatukana kwa kikabila chao tusi zito la nguoni. Dembele hakuelewa maana.

    Mwanadada jasiri na mwanaharakati wa ukweli sasa yu mikononi mwa watu wabaya. Hana silaha, na hawezi



    kujinasua. Utata mkubwa tena fedheha.

    Bwana Dembele aliyekuwa amevaa suti iliyomkaa vyema mwilini aliingiza mkono ndani ya mfuko wa ndani wa suti



    kisha akachomoa bastola akamuonesha Mwanaidi.



    “Ukileta fujo tu nasambaratisha hicho kichwa chako. Chenye akili ndogo” Onyo likatolewa, Mwanaidi akahisi ubaridi



    baada ya kuiona ile silaha. Mkojo ulikuwa unapenya.

    Kama vile hakuna chochote kinachoendelea. Mwanaidi akiwa na yule kijana aliyemuagiza kwa bwana Dembele



    kumuuzia siri walipitishwa mapokezi na safari yao ikaishia katika gari aina ya Pajero, ilikuwa na vioo vyenye utando



    mweusi.

    Mwanaidi matatani!!



    Umahiri wake katika kuchepuka kutoka mazingira magumu ukawa katika kikomo. Alitamani sana iwe ndoto lakini



    hapakuwa na ndoto katika mazingira yale kila kiliichoonekana kilikuwa halisi halisia.

    Moyo wake ulishikwa na ganzi na akatamani kufa kuliko manyanyaso haya. Harakati zilizokuwa zimeanza kupata nuru



    sasa zimeingia doa tena. Donge la hasira likamshika akajikaza asilie tena mbele ya maadui zake.

    Asingeweza kulizuia zaidi chozi lake, kwa pale aliweza lakini safari ilipoanza na kuyafikia mataa watoto wa mitaani



    walifikia lile gari na kuanza kuomba omba, walikuwa wadogo sana hakika, walistahili kukumbatiwa na mama zao



    huku wakilifaidi lile joto tamu la mama, joto la upendo wa dhati. Joto linaloibua matumaini hata pale pasipokuwa na



    dalili ya matumaini. Lakini sasa wanarandaranda mitaani.



    Mtoto mmoja akaanza kuosha kioo cha gari la Dembele bila ruhusa, Mwanaidi akamtazama Dembele jinsi alivyokuwa



    akimtazama kijana yule kwa jicho baya. Jicho lenye chuki lisilokuwa na huruma.

    Yule kijana alipomaliza kuosha kioo cha gari aliomba pesa.

    “Mpumbavu mkubwa nenda ukamuombe mama yako nyumbani. Shenzi kabisa. Bastard!!” alitoa tusi hilo Dembele



    japo halikumfikia muhusika. Kisha wakaondoa gari.

    Mwanaidi akainama chini akaanza kutiririkwa na machozi. Machozi mazito, machozi ya uchungu. Alijikaza asitokwe



    na sauti ya juu wakati analia lakini ilishindikana, Mwanaidi akaangua kilio kikubwa.



    Hakuwa anajililia yeye bali alikuwa anawalilia chokoraa anaowaacha bila msaada. Akamkumbuka na mama aliye



    hospitali alitakiwa kwernda kumuona baada ya kupokea pesa zile lakini sasa ni ndoto.

    “Atakufa mama yangu..” alisema mwanaidi kwa sauti ya juu katika kilio chake.

    “Atazikwa na serikali Malaya mwenzako. Malaya wote serikali huwa ina…..hivi nilisema kuzikwa …hapana huwa



    wanafukiwa na serikali na yeye atafukiwa.” Dembele alizungumza kwa hasira kali. Jibu hili likawa pigo jingine kali



    kwa Mwanaidi.



    Safari yao ikafikia kikomo mahali asipopajua Mwanaidi.

    Usiku huo wakajikuta katika vyumba viwili tofauti. Mwanaidi chumba chake na yule mjumbe chumba chake.

    Mwanaidi alitakiwa kufanya jambo moja tu kwa ajili ya uhai wake.

    Kumuelekeza bwana Dembele mahali alipo mama George na Frida.

    Kupatikana kwa watu hawa kisha kuondolewa uhai ilikuwa njia pekee ya bwana dembele kujiweka mbali na hatia ya



    kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya. Kinyume na hapo ni lazima angekuwa hatiani na jina lake lingechafuka



    sana.

    Mwanaidi matatani….



    ****



    Isha alikuwa anafanya mazoezi ya mwisho na mgonjwa mwenzake ambaye walikutana siku hiyo hapohapo hospitali.



    Kitu kilichowafanya wazoeane kwa siku moja ni kwamba kila mmoja alikuwa amefanyiwa upasuaji na kila mmoja



    alikuwa anatolewa siku hiyo. Mama na mwana walikuwa wamechoka na sasa walikuwa wanapiga soga za hapa na



    pale.

    Wote walikutana wakiwa waongeaji sana. Hakika walikuwa wamekutana

    Waliongea sana baada ya mazoezi huku kila mmoja akimngojea ndugu yake aweze kuja kumchukua.

    Maongezi yakaisha na muda ukazidi kwenda kasi. Mmoja akasdinzia na kuamka na mwingine akasinzia vile vile…



    bado hakuna aliyemwona ndugu yake.

    Sasa kigiza kilianza kuingia, Isha akashangazwa sana na ukimya wa George na huyu mama naye akalalamika kuwa



    mwanaye amekawia sana kuja kumchukua.

    Majira ya saa mbili usiku hali bado ilikuwa vile vile hakuna ndugu aliyejitokeza.



    Wakati Isha anawaza George kuja kumchukua, George alikuwa katika gari la mama mtu mzima akielekea anapopajua



    yeye mwenyewe, wakati huo mama huyu aliyekuwa akimngojea Mwanaidi aje kumchukua…binti shupavu alikuwa



    matatani na ni kauli yake pekee inatakiwa ili awe huru ama aangamie peke yake.

    Mwanaidi anatakiwa kuwafichua Frida na mama George ili uhai wake uende mbele kwa dakika kadhaa.

    Mwanaidi matatani!!

    George stareheni!!

    Isha na Mama George hawafahamiani. Hawajui kuwa watu wanaowasubiri wapo katika wakati gani huko walipo.

    Harakati zinamchukua na kumtesa Mwanaidi, starehe zinamtwaa na kumpelekesha George.

    Kizungumkuti!!



    ****



    ***UTATA….UTATA…MWANAIDI matatani……je atawachoma wenzake? Kumbuka kuwa ni neno lake pekee



    litakalomwokoa…..anafahamu kuwa Frida yupo nyumbani na mama George yupo hospitalini

    ***GEORGE yupo na mama yupi tena? Amesahau kuwa Isha yupo hospitali na anatakiwa kumchukua…….HALI



    TETE….

    ***FRIDA naye hajui nini kinaendelea….

    **ISHA na MAMA G….watatoka vipi? Ama ndo wanangoja hukumu





    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog