Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

CHOKORAA - 5

 





    Simulizi : Chokoraa

    Sehemu Ya Tano (5)





    Mwanaidi matatani!!

    George stareheni!!

    Isha na Mama George hawafahamiani. Hawajui kuwa watu wanaowasubiri wapo katika wakati gani huko walipo.

    Harakati zinamchukua na kumtesa Mwanaidi, starehe zinamtwaa na kumpelekesha George.

    Kizungumkuti!!



    ****

    Ilikuwa kama bahati tu. Bahati ya mtende kuotea jangwani pasi na maji.

    Siku nyingine, mahali pengine George anaingia katika mtego wa maajabu. Mtego ambao hakujua autegue vipi. Na kwa



    nini awaze kuhusu kuutegua wakati aliufurahia mchezo huo?

    Akiwa anatokea kufundisha darasa la jioni pale mchikichini anakutana na kiumbe ambaye alikuwa ameyahifadhi



    macho yake nyuma ya vioo vwa miwani nyekundu ambayo ilikuwa kubwa sawasawa na uso wake. Walikutana katika



    namna tofauti, George akiwa anatembea kwa miguu wakati kiumbe mwingine alikuwa katika gari.

    George hakuamini kama ni yeye alikuwa anaitwa hata sauti ilivyoita mara mbili, akageuka nyuma kutazama kama kuna



    mtu zaidi yake.

    Hapakuwa na mtu!! Akaitikia wito.

    Aliposogea karibu na ile gari akaanza kuitambua kwa mbali ile sura. Hakika ilikuwa yenyewe.

    “Shkamoo mama.” Alisalimia kwa nidhamu kubwa. Lakini kama ilivyokuwa siku ya kwanza hakujibiwa tena. Safari



    hii hakujali

    Wakachangamkiana kwa michapo ya hapa na pale.

    Akaombwa apande garini. Akabweteka akapanda.

    Gari ikaanza kuondoka. George akiwa ametilia maanani kuchungulia paja lililoachwa wazi la yule mwanamama, paja



    lile liliachwa wazi aidha kusudi ama kwa bahati mbaya. Hakujali ni wapi anapelekwa. Kwanza alikuwa ameshikwa na



    matamanio tayari.

    Geti likafunguliwa wakaingia ndani.

    Nyumba ilikuwa tulivu sana tofauti na awali ambavyo ilizoeleka.

    “Vipi hawapo nini?” aliuliza George.

    “Yap wametoka na baba yao”

    Alijibu yule mwanamke huku akikishika kiganja cha George na kukiminyaminya. Joto likapenya na kumsisimua.

    George akapagawa!!



    Alikuwa ndani ya nyumba ya bwana Dembele na alikuwa mikononi mwa mke wa Dembele. Mama sakina!!

    Mama wa kiarabu.

    Ni kipindi kirefu wakati anamfundisha Sakina mama huyu alikuwa akimtazama kwa jicho la matamanio. George



    alielewa jambo lile lakini akawa anajificha asitambulike kung’amua chochote. Lakini siku hii ilikuwa nyingine na



    matendo yalikuwa mengine.



    Hapa hawakudumu sana, yule mama wa kiarabu akachukua alichohitaji kutoka chumbani, kisha akarejea garini



    wakatoweka tena.

    Mama Sakina alikuwa amechoshwa na tabia za mume wake za kumnyima haki yake ya ndoa. Ulikuwa umekatika



    mwezi mzima tangu mume asitishe huduma hiyo. Na hakutoa sababu yoyote ya kuwa katika hali hii. Siri alibaki nayo



    pekee moyoni akijua ni kipi kinachomkabili. Alikuwa na msongo wa mawazo juu ya siri yake kuvuja. Mama Sakina



    alikuwa ana uenyeji wa Pwani, kukosa penzi kwake ulikuwa mtihani mkubwa sana, isitoshe hali hiyo ilikuja ghafla na



    kuendelea kudumu siku hadi siku.

    Ujio wa George kama mwalimu wa mwanaye ulimfanya ajikute katika kumtamani kijana huyu. Kila alipojaribu



    kutafuta upenyo wa kumueleza, alikuwa na mtoto wake na mbaya zaidi hawakuruhusiwa kutoka nje familia nzima



    hivyo alikuwa anaikosa nafasi.

    Ilikuwa jambo la kushangaza siku ambayo Dembele alibadilika na kuwa kama yule wa zamani. Akaichukua familia



    nzima kasoro mkewe ambaye alidai hayupo sawa kiafya. Hiyo ilikuwa janja yake tu kumkomoa mume wake huyo kwa



    ubinafsi aliokuwa amemfanyia kwa mwezi mzima.

    Familia nzima ilipotoweka. Mama Sakina aliingia garini naye akatoweka pia.

    Alikuwa na nia ya kwenda kumtembelea rafiki yake kwa lengo la kunywa naye pombe kwa kufuru na furaha ya kuwa



    huru tena.

    Safari yake ikaishia pale alipomuona George. Sasa amemchukua garini wamefika na kuondoka nyumbani kwa



    Dembele.

    Mwisho wa safari yao ukawa katika hoteli yenye hadhi ya juu sana. Chumba kikubwa kabisa kinachojumuisha sebule.



    Ni humu walifikia.

    George ametamanika japo hawezi kusema.

    Mama Sakina anagundua madhaifu hayo.

    Hakuna mazungumzo.

    Wakajibwaga sebuleni. Mama na mwana katika penzi zito.

    Hakuna aliyejali kwa mara nyingine kuhusu kinga.

    George akafurahia penzi la mama mtu mzima. Mke wa Dembele.

    George hakuwa anatambua ni katika hatari kubwa kiasi gani anajiweka.



    Majira ya saa sita usiku, mama wa kiarabu anaitazama saa yake na kumsihi George waondoke kwani hawezi kulala nje



    ya nyumba yake bila mumewe kupewa taarifa. George hana kipingamizi.

    Wanajiandaa na kukiacha chumba hicho katika upweke mkubwa sana. George anaelekea upande ambao mama Sakina



    haelekei, hivyo wanaagana huku yule mama akimpatia George kiasi cha pesa kwa ajili ya nauli. George aliipokea huku



    akitabasamu kwani hakuwa katika uhitaji wa ile pesa.

    George alibaki kusimama akitafakari aelekee upande upi.

    Hospitali!!

    Akakumbuka kuwa Isha alitakiwa kutoka hospitali siku hiyo.

    Japo hakushtuka sana lakini alihisi hatia ikimtafuna. Sasa akaangaza uwezekano wa kupata usafiri aweze kufika



    hospitali.

    Aliamini kuwa Isha atakuwa amekasirika lakini atamsamehe kwa namna yoyote.

    Akapata teksi!! Safari ya kuelekea hospitali ikaanza.



    Wakati George anaanza safari ya kuelekea hospitali, jemedari wa kike alikuwa amepokea kipigo kitakatifu hatimaye



    akajikuta anaimba kwa kurudiarudia kuhusu kutambua walipo Frida na yule mama George.

    Dembele akiwa amechemkwa na hasira baada ya kufurahishwa na wimbo huo wa Mwanaidi alimchukua katika gari



    lake kisha wakaelekea mahali alipopataja kuwa Frida na Mama George wanapatikana.

    Hospitali. Hapa ndipo walipoanzia.

    Hapakuwa na mtu aliyetajwa na Mwanaidi. Dembele akachukia kudanganywa. Akataka kumpa kipigo kingine



    Mwanaidi lakini akajirudi na kumuhoji zaidi.

    Sasa walitakiwa kwenda kumchukua Frida.



    ****



    Isha licha ya kumkasirikia George kwa kuchelewa kufika eneo la hospitali kumchukua. Alikuwa na sharti la



    kumsamehe.

    “Kuna mama tunaondoka naye…”

    “Mama yupi?” George aliuliza.

    Isha akamuelezea yule mama ambaye mwenyeji wake hadi wakati huo alikuwa hajafika. George hakutaka kumkera Isha



    na aliuhitaji msamaha ili kujivua hatia iliyokuwa inamkabili. Akakubali!!

    George alimchukua Isha pamoja na yule mama. Wakaingia katika taksi aliyokodi.

    Muda wote yule mama ambaye awali alikuwa mchangamfu sana sasa alikuwa kimya na kama anafanya tafakari ya



    jambo zito.

    Isha alijitahidi kumsemesha lakini hakuonyesha ushirikiano.

    “Mama ulikuwa unaumwa nini?” hatimaye George alianzisha mazungumzo.

    “Oparesheni mwanangu…ilikuwa inanisumbua walinishona vibaya.”

    “Ohoo!! Pole sana mama.” Alijibu George huku akiliona jicho la kuibia ibia kutoka kwa yule mwanamke.

    George hakupendezwa na kitendo hicho cha kuangaliwa kiwiziwizi. Alimhisi vibaya yule mama lakini hakuwa na la



    kufanya kwa kuwa Isha alikuwa amependekeza waondoke naye.

    Walifika nyumbani usiku sana. Isha akalala kitandani na yule mama. George akajiegesha chini kwenye mkeka.

    George akiwa katika mawazo yake mbalimbali yaliyohangaisha kichwa chake alikatishwa na maongezi yaliyonoga



    kutoka kwa Isha na yule mama kitandani.

    Mazungumzo haya yalikuwa mfano wa filamu ambayo George aliwahi aidha kuhadithiwa hapo kabla ama aliwahi



    kuiona.

    Ilikuwa ni filamu juu ya bwana ambaye anahusishwa na usafirishaji na uuzaji wa madawa ya kulevya. Yule mama



    alikuwa anasimulia sio tu kwa kuwa anaifahamu bali naye alikuwa muhusika mkuu katika filamu ile.

    George hakuamini kama amelala chumba kimoja na muhusika wa filamu anayoifahamu.

    “Kuna binti huyo…..yaani sijui nisemeje tulikutana naye hapahapa Dar, kisha tukapoteana baadaye ndiye aliyekuja



    kuniokoa. Wale watu wangeniua, halafu sikuwa peke yangu kuna binti mwingine walimleta ana mimba huyo. Iliniuma



    sana kutambua kwamba na yeye atafanyishwa kazi kama mimi. Sikuwa na la kumsaidia. Lakini huyo binti aliyekuja



    kutuokoa sijui hata nimuelezeeje sijui ni malaika?” mama aliendelea kutiririka. Isha alikuwa anasikiliza huku



    anasisimka mwili.

    “We hili tumbo unaona lipo sawa sasa hivi. Lilikuwa halitamaniki mbona. Walikuwa wanafungua na kufunga,



    wanafungua na kufunga.” Simulizi iliendelea.

    George akakosa ustahimilivu. Akaamua kujumuika katika mazungumzo.

    “Mama!!” George akaita. Yule mama akasisimka ghafla kusikia lile jina. Akaketi.

    Ama kwa hakika damu ni nzito kuliko maji. Na mama kamwe hawezi kumsahau mwanaye. Mama akamuita George,



    kijana akamsogelea. Isha akawa mtazamaji.

    Mama akamshika sura yake kisha akaiminyaminya.

    Akamshika mikono.

    George akashangaa na kutaka kujitoa katika mikono ile.

    “Wewe ni mwanangu.” Alisema yule mama bila kusita. George akashangaa tena bila kusema neno lolote. Mara maneno



    ya kusikitisha yakaanza kumtoka yule mama, akaanza kumueleza George juu ya maisha yake ya utotoni.



    Akiyazungumza hayo alikuwa amemkumbatia mwanaye.

    George akajisikia yupo katika mikono salama.



    “Alinifanya mimi kilema. Akatoroka na wewe.” Alimaliza kuzungumza akaanza kulia. George aliamini yale maneno



    kwa asilimia hamsini na nyingine hamsini hakuamini. Lakini alipogusiwa juu ya Mwanaidi, Frida pamoja na mama



    huyu kuwahi kufika mahali alipokuwa anaishi alianza kuamini.

    Alipoulizia juu ya Mwanaidi na kuelezwa juu ya kutoonekana kwake. George akajishtukia kuwa ile siri aliyoiuza kwa



    bwana Dembele alikuwa amemuuza pia chokoraa mwenzake. Mwanaidi!!

    Hali ikawa tete!! Usingizi ukapaa.

    Hasira ya mama yake kufanyishwa kazi haramu ya kusafirisha madawa. Ukatili wa bwana Dembele kunyanyasa yatima



    ikarudisha upya moyo wake uliokuwa umeyumba.

    Uchungu ukamshika.

    Jemedari wa kiume akauvaa u-George wake wa awali akaingia vitani.

    Alihitaji usiku huohuo kuonana na Mwanaidi pamoja na Frida. Lengo likiwa kumtia hatiani bwana Dembele siku



    inayofuata kwa kosa la kunyanyasa na kuua.

    Safari ya usiku ule ikashindikana kutokana na Isha kugoma kubaki peke yake nyumbani. Wakaamua kufanya kila kitu



    siku inayofuata.

    Laiti kama wangejua kuwa bwana Dembele naye yupo katika mawindo. Wangeiendesha oparesheni yao usiku huohuo.



    Kwani ni usiku huohuo, Frida alitiwa mikononi mwa mashetani hawa.

    Dembele alitamani kuziondoa roho hizi lakini alihofia kuwa kubaki kwa ile roho ya mama George kungemletea



    matatizo na angekabiliwa na hatia nyingine kubwa zaidi iwapo mama huyu atafanikiwa kutoa ushahidi.

    Frida ambaye hakuwa amejeruhiwa akahifadhiwa mahali asipopajua akiwa ametenganishwa na Mwanaidi ambaye



    alikuwa hoi.





    Asubuhi George na jopo lake hawakukuta mtu nyumbani kwa Mwanaidi. Mlango ulikuwa umerudishiwa na chumba



    kilikuwa tulivu.

    Na Frida naye hakuwepo!!hili likawa tatizo jingine jipya.

    Mama yake George akaanza kuomboleza kana kwamba tayari Mwanaidi alikuwa mfu tayari, Isha naye machozi



    yakamlenga lakini akakabiliana nayo yasiweze kumwagika. Aliamini kuwa kwa kuyaruhusu machozi yamtoke ni ishara



    tosha ya kukata tamaa jambo ambalo hakuwa tayari kulifanya japo moyoni alikiri kuwa hali si njema hata kidogo na



    hatari inawaita tena.

    Hali ya wanawake hawa kuwa katika simanzi nzito ilikuwa kama shambulizi kali kwa George ambaye kwa namna



    moja au nyingine alikuwa amehusika japo hakutaka kukiri hilo wazi. Yeye na Suzi waliuza siri isiyokuwa siri tena kwa



    bwana Dembele.

    George akawa anasumbuliwa na hatia ya kuwauza chokoraa wenzake, lakini ni hatia ya bila kujua nini anafanya,



    aliwauza akiwa katika harakati za ukombozi vile vile japo baada ya pesa zile alijiingiza katika uasherati badala ya



    ukombozi. Hakujua aanze vipi kujieleza mbele ya jopo lake ili aweze kueleweka. Akaamua kukaa kimya.

    Mgogoro wa nafsi ukamtawala, ilikuwa ni lazima afanya jambo ili kukabiliana na mgogoro huo. George akaamua



    kuchukua maamuzi binafsi. Maamuzi ya kupambana na Dembele. Alihitaji kumkabili ili aweze kumweleza ni wapi na



    ni kitu gani amekitenda kwa Mwanaidi.

    George aliamini fika kuwa Dembele ni bwege tu ambaye hana lolote la kumtisha, hizo habari za kuuza madawa ya



    kulevya hakuzitilia maanani, wakati huu alichokitazama zaidi ni usalama wa chokoraa wenzake.

    Alitaka kufika na kumkabili ana kwa ana, hakujua Dembele ana hatari kiasi gani.



    Akaondoka bila kuaga akitegemea kurudi na matumaini tele. Akitumia usafiri wa teksi alifika nyumbani kwa Dembele,



    safari hii hakuwa amefuata mapenzi ama kumfuata Sakina kwa ajili ya kumfundisha somo la hesabu. Wakati huu



    George alikuwa ameenda kimapambano. Nia alikuwa nayo na aliamini kuwa uwezo pia anao.

    Akafika nyumbani kwa Dembele, George akatulia kwanza getini bila kuugusa kufanya tendo lolote, akaweka umakini



    kusikiliza kwanza ni nani alikuwa jirani na geti. Akasikia mazungumzo kati ya watoto wa mzee Dembele na mama yao,



    walikuwa wanasimuliana huku wakilaumu juu yam zee wao kuwaacha solemba baada ya kuwatoa kwa ajili ya chakula



    na burudani nyingine. Alimsikia mdogo wake Sakina akilalamika zaidi kuwa baada ya kutoweka aliwapa taarifa kwa



    njia ya simu kuwa hatarejea.

    “Ndo mjue wanangu kuwa yupo mama yenu mdogo” alijibu kinyonge mama Sakina.

    Wanawake wana wivu sana! George aliwaza kisha akagonga geti, aliyefungua alikuwa ni Yule mama ambaye masaa



    kadhaa nyuma walikuwa wamekumbatiana wakipeana raha za dunia. Akapokelewa na mama yake Sakina aliyemtazama



    kwa jicho la huba lakini lililojawa na haya.

    George akamuulizia bwana Dembele, swali hili likamyumbisha mama Sakina akahisi kuwa George amekuja



    kumuumbua baada ya kufanya naye uzinifu. George akaligundua hili akawahi kuliweka sawa.

    “Sio kwa ishu ya jana wala.” Alitoa kauli hiyo. Kauli waliyoielewa wao wawili tu. Hofu ikapungua akakaribishwa



    sebuleni ili aweze kumngoja bwana Dembele.

    Baada ya muda mfupi alikuwa anatazamana ana kwa ana na Dembele. Macho ya Dembele yalionyesha hofu kiasi



    fulani, lakini aliwahi kukabiliana nayo kwa kumpa salamu George, salamu isiyokuwa na utawala ndani yake. Dembele



    alikuwa amepooza sana. Akaketi katika mojawapo ya jozi ya sofa katika sebule yake kubwa ya kisasa.



    “Mwanaidi yuko wapi?” George aliuliza na kuliyeyusha tabasamu bandia la Dembele katika uso wake. Dembele



    alitaka kusema neno lakini mkewe alifika na kukatisha mazungumzo baada ya kumuuliza George anatumia kinywaji



    gani.



    “Usijali mama mi si mkaaji.” George akamjibu huku akionyesha waziwazi kuwa anamaanisha analosema. Mama



    George akatoweka bila kuongeza neno.

    “Mzee nadhani umenisikia vyema. Mwanaidi yupo wapi?” alitilia mkazo.

    “Mwanaidi nd’o nani?” aliuliza kama mpumbavu bwana Dembele.

    “Dadangu!” alijibu huku akionyesha wazi wazi hasira ikiwa imechanua usoni. Dembele akakumbwa na hofu, hakujua



    kijana Yule alijiamini nini hadi kumkaribia na kumkoromea hadharani.

    “Samahani kijana tunaweza kuzungumzia haya mambo nje kidogo maana ni kama sielewi hivi. Na sina uhuru sana wa



    kuzungumza nikiwa hapa. Juzi tu kuna tukio kama hili limetokea hapa nimetembelewa na mtu akimuulizia kaka yake,



    na mwaka juzi pia. Nahisi kuna Dembele mwingine ama kuna mtu anafanya ujinga na kutumia jina langu ili anichafue



    kisiasa….sikubaliani na hili kwa sasa. George please kijana wangu nakuomba tukazungumze. Unaweza kuwa msaada



    mkubwa sana kwangu” Sasa bwana Dembele alizungumza kwa makini sana ili aweze kucheza na akili ya George.



    Akaufinyanga uongo ukafanana na ukweli. George ambaye hakuwa na taarifa yakinifu kuhusiana na Dembele alijikuta



    anadanganyika. Akahisi mama yake alikuwa anazungumza kitu ambacho hakuwa akikifahamu, alifika mbali na kuhisia



    huenda hata zilikuwa ni ndoto za mchana.

    Lakini vipi nyumbani kwa Mwanaidi? Mbona ni kweli Mwanaidi hakuwepo? Kabla hajapata jibu la swali lake



    alikatishwa na harufu kali ya marashi. Aliponyanyua kichwa alikutana na mzee Dembele akiwa ndani ya suti ya bei



    ghali. Akamwonyesha ishara wakasimama na kuondoka. Wakati anapita kulifuata geti aligonganisha macho na mama



    Sakina. Mwanamke Yule alikuwa na hofu waziwazi, George akajaribu kutabasamu lakini tabasamu hilo halikuondoa



    ile hofu usoni mwa mama yule wa kiarabu.

    George akajiahidi moyoni kuwa jambo hili likipita atakutana tena na mama huyo na kisha atamtania juu ya uoga wake



    wa kitoto.



    Hiyo siku aliyoingoja George haikuweza kutimia kirahisikwani amani yake ilitoweka dakika kumi tu baada ya kupanda



    ndani ya gari. Kimya kilitanda tangu safari ilipoanza lakini maongezi yalianza baada ya mlango wa nyuma wa gari lile



    kufunguliwa. George alishtuka lakini Dembele alijua nini kinaendelea.

    Akaingia kijana mmoja mwembamba kwa mtazamo lakini nadhifu na alionekana kuwa mpole sana. Hata



    alivyomsalimia bwana Dembele sauti yake ilikuwa inabembeleza badala ya kushtua na kuogopesha. Hili likampa



    ujasiri upya George.

    “Dogo..” ile sauti ya upole ikamwita George. Hilo lilikuwa mojawapo ya jina ambalo hakuwa akilipenda maishani.



    Akatamani kubwatuka lakini akajikaza na hakusema neno.

    Kama alitarajia yule kijana atamwita kwa mara ya pili alikuwa amekosea sana. Ghafla alihisi kitu kama nyundo



    kimetua katika bega lake, akapiga yowe kubwa. Alipotazama vyema akakutana na kiganja cha yule kijana mwenye sauti



    ya upole.

    Hapa ndipo mkasa ulipoingia doa tena….



    George alifungwa kitambaa cheusi usoni, akafungwa na kifaa kinachofanana na pingu, kisha akadidimizwa katika



    uvungu wa viti. Alilia kwa kugugumia bila sauti kutoka kwani alionyeshwa mtutu wa bunduki na iwapo angethubutu



    kutoa kilio basi roho yake ilikuwa halali ya sauti ya upole.

    Lilikuwa ni shambulizi ambalo halikutegemewa hata kidogo na George.



    Baada ya dakika nyingine nyingi za ukimya hatimaye mlango ulifunguliwa George akachukuliwa msobemsobe hadi



    katika chumba, akarushwa kama kiroba cha mahindi. Upesi akafunguliwa kitambaa usoni na zile pingu mikononi.

    Ana kwa ana na sauti ya upole.

    “Dogo..” aliita tena, safari hii George aliitika upesi.

    “Mama mwendawazimu yupo wapi?” aliuliza kama hana haja ya kujibiwa.

    “Sifahamu..”alijibu huku akitetemeka George. Ni kweli hakuwa akifahamu lakini yule kijana angemwamini vipi?

    Kama George alitegemea kuwa yule kijana atarudia swali lake hapa napo alikuwa amekosea. Yule kijana mwembamba



    alikuwa wa aina yake. Harudii swali.

    “Wasichana wakitoboa masikio huwa wanaitaje kwa lugha za kitaalamu?” swali jingine tena ambalo lilionekana



    kutokuwa na maana.

    “Kutoga.” Alijibu upesi. Laiti kama angejua yule kijana ana maanisha nini basi ni heri na swali hilo asingelijibu.

    Ghafla alivamiwa na kile kiwiliwili, teke moja la mbavuni likamfanya atokwe na yowse kali huku akiegemea upande



    mmoja. Mikono yake ikazungushwa kwa nyuma kisha akafungwa na zile pingu.

    Kilichofuata baada ya hapo hakifai kufanywa kwa mwanadamu yeyote yule. Ulikuwa ni ukatiri wa aina yake.

    Sauti ya upole akachukua sindano ya kushonea nguo. Akalikamata sikio moja la George, hakuyasikiliza mayowe ya



    George. Na mbaya zaidi hakuuliza swali lolote, akaizamisha katika kinyama cha sikio ambacho wanawake wengi



    hukitumia kuvaa hereni. Yowe kuu likamtoka George. Ni kama zile kelele hazikumaanisha kitu kwa yule kijana.



    Akahamia sikio na pili, kabla hajamtoga na sikio hilo Dembele akafika na kukutana na ile dhahama. Damu ilikuwa



    imeruka na kuchafua ukuta. Dembele akashtuka sana hakutegemea kama adhabu zingeanza mapema kiasi kile.

    “Imba kila kitu unachokijua kuhusu huyo Mwanaidi, mahali ulipotoka na ulipanga na nani mchezo huu wa kuigiza.”



    Sauti ileile ya upole ilisema tena.

    George alikuwa ni ‘mtoto wa mama’ licha ya kupitia msoto wa uchokoraa lakini asili yake ni familia yenye maisha



    bora isiyojua nini maana ya shida. Hakuweza kuvumilia tena kipigo kile alichokipata kilimfanya awataje Isha na mama



    yake mahali walipo. Kwa kuonyesha uoga wake alimtaja hadi Suzi. Yule binti ambaye ana mahusiano na diwani.

    Faida kwa Dembele. Mwanaharamu huyu akauona ushindi ukija mezani kwake.



    Nikishawachukua hawa naua!! alijiapiza huku akiandaa safari ya kwenda kuwakamata.

    “Wanawake hutoga pua, midomo, kitovu, macho na wengine wapumbavu hutoga hadi mikono…..nadhani unanielewa



    tukifika na tusiwakute kitakachokutokea.” Sauti ya upole alisema na George. Hakusubiri jibu akaondoka akiongozana



    na Dembele.

    Huku nyuma wakimwacha George akiwa hoi kwa suluba aliyoipata. Hakuwa akiamini kuwa ni ndani ya masaa



    machache hali yake imegeuka kuwa mbaya kiasi kile.

    George alisdhindwa kuelewa ni sdala ipi aweze kufanya, je ni kuombea mama yake pamoja na Isha wasikamatwe ili



    yeye aweze kubeba mzigo wa kutobolea pua, mdomo na kitovu chake? Ama wakamatwe ili waangamie pamoja maana



    hapakuwa na dalili yoyote ya msamaha. Na isitoshe hakuwa akifahamu fika mahali alipo ni wapi maana aliingizwa



    akiwa amefungwa kitambaa cheusi usoni.

    Hali ilikuwa tete sana hakika.





    *****



    FRIDA alikitambua kwa uzuri kabisa chumba ambacho alikuwa amehifadhiwa. Haikuwa mara yake ya kwanza



    kuhifadhiwa katika chumba hicho cha ajabu ambacho kina hewa safi lakini hakina madirisha na mlango wake



    usiokuwa na kitasa, ni katika chumba hicho hicho alihifadhiwa baada ya kutekwa mara ya kwanza bila kujijua huku



    akiwa anadhani amepata msaada baada ya habari yake kutangazwa gazetini. Maombi yake yalikuwa kwa mtu mmoja tu,



    aliamini kuwa ni huyo pekee ambaye angeweza kuwaokoa kutoka katika janga hilo. Lakini hakuamini kama atawaokoa



    kwa wakati, huenda anaweza kufika wakiwa wamepasuliwa matumbo yao na kujazwa madawa ya kulevya, ama



    anaweza kufika wakiwa wafu! Hii nayo haikuwa na maana. Frida alitazama tumbo lake, akatokwa na machozi, na



    jitihada zote za kuilea ile mimba isiyokuwa na baba anayetambulika. Leo hii anatakiwa kupasuliwa na huyo kiumbe



    aangamizwe kisha awekewe zigo la madawa ya kulevya. Ilimuumiza sana akili.

    Frida akamlilia Mungu huku akihofia huenda kile chumba kilizuia hata sala zake kuweza kupenya na kufika nje



    hatimaye kutazamwa na Mungu kwa jicho la huruma.

    Kilio cha Frida kikaishia ndani ya chumba kile.



    MWANAIDI yeye kwa upande wake alikuwa mgeni kabisa na hakujua kabisa pale alipo ni mtaa gani katika jiji la Dar



    es salaam ama popote Tanzania. Alikuwa akishangaa tu kile chumba kikubwa kisichokuwa na mwanga wa kutosha



    lakini hewa safi ikitawala. Akili yake ilikuwa imefikia ukomo na hakujua anaweza vipi kujikomboa yeye kisha ndugu



    zake. Alijiuliza maswali mengi bila kupata jawabu. Akajaribu kujilaza hakuweza kupata usingizi….alihangaika



    kutafuta mlango wa kutokea lakini haikuwa rahisi hata kidogo. Mwanaidi aliwahi kukaa rumande kwa siku kadhaa



    kipindi cha nyuma, akajiaminisha kuwa rumande ni sehemu mbaya sana kupita zote kwa sababu hakuna uhuru



    wowote….lakini sasa alikiri kuwa ni heri rumande hakuna uhuru lakini unatazamana na marafiki na wanadamu



    wengine wanaoishi. Lakini hapa alipokuwa ni mfano wa jehanamu yenye hewa safi.



    ****



    KWA mara ya kwanza baada ya huzuni ya muda mrefu uhatimaye uso wake ulichanua na kutoa tabasamu japo hafifu.



    Tabasamu hilo liliambatana na maumivu ya kutoneshwa kidonda ambacho hakikuwa kimepona vizuri japo kilikuwa



    katika hatua hizo.

    Aliimaliza siku hiyo huku akijiona mwepesi sana. Kichwa chake ambacho kilikuwa kinazidi kuwa kizito kadri siku



    zilivyosonga mbele na ukweli aliouhitaji kuzidi kuota mbawa sasa kilipata ahueni.

    Mateso ya nafsi aliyokuwa anayapata yalimdhihirishia wazi kuwa alikuwa katika dimbwi la mapenzi na kiumbe yule



    ambaye alizikwa akiwa na kovu kubwa kabisa la kisu mgongoni.



    Emiliana, mchumba wake ambaye walikuwa wanahesabu siku kadhaa waweze kuoana. Ndoto ikayeyuka baada ya binti



    huyu kukutwa ametupwa mtaroni akiwa mfu.

    Wazazi wa upande wa mwanamke hawakuisha kumwaga lawama. Walimlaumu sana Kasuku kwa kushindwa



    kuwafichua wauaji wa mpenzi wake. Maneno hayakuishia hapo ilifikia wakati mama mkwe akamlaumu Kasuku kuwa



    huenda anawajua wauaji lakini anawaficha kwa kuwa amenufaika na mauaji hayo.

    Sasa kijana huyu alikuwa amerejewa kidogo na ari. Kwa sababu aliamini ni wakati wa kumsaka muuaji kisha amfichue



    na wakwe zake wawe na amani…..

    Haikuwa kazi nyepesi kuirejesha furaha yake na tumaini jipya kama asingeupata ugeni huu…ugeni kutoka kwa



    msichana…..



    ilikuwa jioni ya aina yake kwa bwana Kasuku. Jioni ambayo hakutarajia kilichotokea, kitu kilichoirejesha furaha yake



    tena furaha iliyokuwa imetoweka moja kwa moja.

    Furaha yake kidogo iliweza kurejea, kwanza kwa kuweza kuonana na mtu ambaye siku nyingi zilipita bila kuonana na



    hakujua kama yu hai ama amekufa tayari. Alikuwa mtu wa maajabu ambaye wameweza kuonana kwa kipindi kifupi



    wakazoeana sana kisha akatoweka machoni pake kwa mategemeo ya kuonana baada ya siku kadhaa lakini haikuwa



    hivyo hadi walipoweza kuonana katika hali ambayo Kasuku hakuitarajia

    Wote walitabasamu huku wakikumbatiana, nyumba ilikuwa na upweke sana na binti aliyewasili hapo aliiona hali hiyo,



    mwenyeji wake alikuwa amekonda na alikuwa na uso wenye huzuni japo ulitabasamu. Tabasamu hafifu sana ambalo



    halikuweza kuificha huzuni iliyokuwa moyoni mwake.

    Binti akauliza kulikoni kimya kikubwa. Majibu aliyopewa yalimsikitisha na kumfanya awe na huzuni kuliko mwenyeji



    wake.

    Emiliana amekufa? aliuliza kwa sauti ya chini.

    “Yaah wamemuua…….” alimalizia Kasuku huku akikwepesha macho yake yasitazamane na yale ya yule binti.



    Taarifa ya kifo cha mama mwenye nyumba hiyo ilimsikitisha sana Frida ambaye aliamua kuja kumtembelea bwana



    Kasuku baada ya Mwanaidi kukawia sana kurejea nyumbani na uwepo wa mama yao hospitali.

    Kasuku hakupenda sana kukizungumzia kifo cha mkewe tena kwani aliamini kimejaa sintofahamu nyingi sana



    zisizokuwa na utatuzi, kimya kilipotanda Frida akaamua kuvunja ukimya, hakutaka naye kuzungumzia kifo cha mke



    wa bwana huyu bali akazungumzia yaliyomsibu katika mikono ya bwana Dembele. Alianza kusimulia akiwa



    anatabasamu kama kwamba anasimulia kisa cha kuchekesha. Lakini kadri alivyozidi kusimulia ndipo sauti ikazidi



    kwenda chini, hatimaye kwikwi. Frida akaanza kulia.

    Ilikuwa lazima alie, tena kilio kikali. Unyama aliokuwa anaufanya bwana Dembele haukuwa wa kuchekesha wala



    kumshawishi mwanadamu yeyote yule kukenua meno. Frida alijieleza kwa uchungu mkubwa unyama anaoufanya



    bwana Dembele, unyanyasaji wa watoto na akina mama. Roho nyingi zinavyopotea kwa kumnufaisha yeye na familia



    yake.

    Frida aliendelea kumsimulia Kasuku jinsi walivyookolewa na Mwanaidi. Ujasiri wa binti yule ulivyowaweka huru.

    “Asingekuwa Mwanaidi, ningekuwa mfu tayari. Alitaka kunipasua tumbo nikalia sana nikimwambia kuwa mimi ni



    mjamzito. Kidogo akanielewa lakini kinyume na hapo……”

    Frida alisimulia kila kitu. Kasuku akawa msikilizaji. Simulizi hii ilimgusa kwa kiasi kikubwa bwana Kasuku.



    Mazingira yaliyozungumzwa na Frida wakati wa kutoroka katika ngome ile yalifanana kabisa na kifo cha mkewe. Gari



    walilolikuta nje ya nyumba lilikuwa lilelile ambalo lilikutwa barabarani na marehemu Emiliana ambaye ni mkewe



    kukutwa mtaroni.

    “Kwa hiyo Dembele alimtaka mke wangu pia…” alijiuliza huku hasira kali zikimchemka kichwani.

    Kasuku hakutaka kuonyesha wazi kuwa ana hasira juu ya Dembele, alijivika hali hiyo ili Frida awe huru kuzungumza.

    Majira ya saa kumi na mbili jioni Frida alihitaji kuondoka, tofauti na awali ambapo alikuja kwa usafiri wa daladala



    sasa Kasuku alimpakia Frida katika gari lake akamrudisha nyumbani huku akiahidi kufika tena siku inayofuata ili



    aweze kuzungumza na mama George pamoja na Mwanaidi kisha zifanyike harakati za kuwapata George na Isha popote



    pale walipo. Kasuku alikuwa amerejea katika ari ya kufanya kazi, japo mkewe asingeweza kurudi kamwe, lakini kisasi



    kwa kumfikisha bwana Dembele katika mikono ya sheria lilikuwa jambo kubwa ambalo lingezidisha amani yake.



    “Bro…tunakutegemea sana……tupiganie….kama nilivyokueleza. Tunayo haki lakini nani wa kuitetea haki hiyo



    tuipate?? Kuwa sauti yetu kaka naamini kama ulivyoandika makala ile bado unao uwezo zaidi wa kutupigania. Lazima



    atakuwa anatusaka na lazima atafanikiwa kutupata maana sisi ni chokoraa na mtaa ndiyo makazi yetu. Atatuua.” Frida



    alizungumza kwa hisia kali. Hisia zilizomgusa Kasuku. Wakaagana kwa kukumbatiana. Kasuku kwa mara ya kwanza



    akadondosha chozi. Jinsi Frida alivyomkumbatia hakika alionyesha ni jinsi gani hawana msaada mwingine zaidi yake



    yeye pekee.

    Usiku huu baada ya kuachana na Frida. Bwana Kasuku alipita katika baa moja akajikita katika ulevi ili aweze



    kupunguza anachomuwazia Dembele. Tuhuma zote alizopewa kuwa anahusika na kifo cha mkewe alizihamishia kwa



    Dembele, kisha akamuona kuwa stahiki yake ni kifo. Tena kifo ambacho atajua wazi kwa nini anakufa. Kifo mbele ya



    sheria.



    Akiwa kitandani alitamani ufike wakati unaoitwa asubuhi aweze kufunga safari na kukutana na huyo msichana wa



    ajabu anayeitwa Mwanaidi na huyo mama wa kipekee anayesadikiwa kuwa mama wa chokoraa. Kasuku alimini kuwa



    palikuwa na jambo zito la kuunganisha matukio ili aweze kujua pa kuanzia katika kumkamata Dembele na kumfikisha



    mbele ya sheria. Aliwaza mengi sana hadi pale usingizi ulipompitia.

    Siku iliyofuata Kasuku aliwahi katika nyumba ambayo Frida alimueleza kuwa ndipo wanapoishi pamoja na Mwanaidi



    na yule mama ambaye alikuwa msafirishaji wa madawa ya kulevya bila hiari yake.

    Maajabu, asubuhi yote ile hapakuwa na mmoja kati yao na majirani hawakuwa na taarifa yoyote. Kasuku



    aliyejiaminisha kuwa alikuwa amewahi sana kupita mtu yeyote Yule atakayeingia katika nyumba ile akafadhaika….

    Kasuku akahisi huenda Frida alimdanganya na wala si pale wanapoishi. Lakini kwanini amdanganye? alijiuliza bila



    kupata jawabu.

    Akaiacha siku hiyo ipite. Na siku iliyofuata akajaribu tena, tatizo likawa lilelile, mlango umeegeshwa na hakuna mtu



    wala dalili ya kiumbe hai katika chumba kile.

    Kasuku akachezwa na machale. Kuna jambo baya linawakabili watu hawa. Kasuku akajihisi kuwa analala tena na



    kama akilala na kuukosa ushahidi wa kumwadhibu Dembele basi lawama kutoka ukweni zitamfuata mpaka siku



    atakayofukiwa kaburini. Kasuku akaamua kujishughulisha. Kama Frida alivyomwezesha kwa kumpa habari ile naye



    akaamua kuwapigania chokoraa. Alijua wanamuhitaji sana.

    Yale maneno aliyozungumza Frida, mara ya mwisho walipokuwa wakiagana yalimgusa na kumweka katika deni.

    Wakati Kasuku akihangaika huku na huko katika kuwasaka viumbe hawa. Tayari walikuwa mikononi mwa watu



    wabaya…..walikuwa mikononi mwa Dembele.

    Ile sauti ya Frida ikaendelea kujirudia katika kichwa chake kama ishara ya kumkumbusha kuwa wanamtegemea



    Kasuku akajisikia vibaya na hakuona dalili yoyote ya sauti ile kutoweka pasina kufanya jitihada.

    Kasuku akaamua kuhangaika



    *****



    MWANAMKE NA MKE ni viumbe wawili tofauti sana katika kufikiri na mfumo wa maisha wanaoishi. Mke huwa



    anahofia sana kuivunja ndoa yake tofauti na mwanamke ambavyo hajali sana akiachana na mpenzi wake.

    Zainabu alikuwa mmoja kati ya wake wanaoihofia aibu ya kutazamwa mtaani kama walioshindwa kuzitunza ndoa zao.



    Na alikuwa tayari kugharamika kwa aina yoyote ilimradi tu awaridhishe walimwengu. Jambo hili lilikuwa



    linamgharimu mara kwa mara na bado hakulitupa mkono. Alifanya hivi akiwa na sababu, sababu hii ilikuwa ni ukiwa.



    Hakuwa na ndugu anayeweza kukimbilia kwake baada ya ndoa yake kuvunjika. Pande zote zilikuwa zimemtenga tena



    hawakutaka kumsikia kabisa kutokana na kosa la kuolewa na mtu mweusi tena mswahili, wakati yeye alikuwa ni



    mwarabu asilia.

    Jambo hili lilikuwa na uzito sana kwa asili yao na hivyo akawa ametengwa rasmi. Hii hali ilimsababisha amuone



    mumewe kuwa ni kila kitu kwake, hata watoto wake hawakuwajua ndugu zao zaidi ya ule upande wa mume.

    Utengwaji ule ukamtia hasira kali na kuhisi ni uvunjaji wa haki za binadamu….akafanya malipizi, akabadili jina lake



    kutoka kuwa Zaituni Baraghash akajipa ubin wa mumewe akabadilika kuwa Zaituni Dembele.

    Hili nalo likazidisha uhasama, mwanzoni walikuwa wamemtenga tu, sasa wakaongeza adhabu nyingine.



    Wakamchukia!!!

    Katika matukio yote ya kuipendezesha ndoa yake hakuwahi kukutana na pepo mchafu wa kumlaghai kufanya mapenzi



    nje ya ndoa, kama asingekuwa George kupewa nafasi ya kumfundisha mwanaye mpenzi Sakina basi huenda asingeweza



    kukabiliwa na mwanaume yeyote mtaani.

    Walikuwa wanamuhofia!



    Kile kitendo cha kufanya uzinzi na George kisha George anaonekana akiwa na Dembele waklizungumza kisha



    wanatoweka kilimtia katika mashaka makubwa sana. Alihisi George ‘anamuuza’. Akapagawa sana na kuhisi ile aibu ya



    kutupiwa virago nje imewadia, na kama angeendelea kutulia basi ajiandae kupewa talaka.

    Mke wa Dembele akajiapiza kuwa lazima afanye kitu lasivyo anaumbuka.

    Ni hapa alipomkumbuka SULEIMAN MEJA.

    Msaada pekee katika tatizo hili…..kama huyu akishindwa basi atakaa kuisubiria talaka na aibu tele.



    Jawabu la kusubiri kufadhaika hakutaka kabisa litawale kichwa chake lakini hakuwa na budi kukubaliana nalo iwapo



    itabidi. Jitihada zikigonga mwamba ni hicho kitakachofuata.



    Zai alimfahamu vyema baba yake mzazi mzee Barghash jinsi alivyokuwa mkorofi na alivyowachunga tangu wakiwa



    watoto wadogo akimtumia kijana wake asiyezeeka akili. Mwarabu mweusi. Akili ikamshtuka kwa kumkumbuka



    mwanaume huyu wa aina yake.



    Huyu alikuwa ni mtu wa aina yake ambaye alikuwa na uwezo wa kuyafuatilia matukio yote ya watoto wa mzee



    Barghash na kisha kutoa ripoti ya aina yake iliyomfurahisha mzee wao kila siku.

    Kadri umri ulivyozidi kwenda na wao walizidi kujijengea hofu, sasa wakawa wanajiuliza baba yao anapata vipi habari



    zao wakati wanafanya kwa siri. Wakaanza kuhisi huenda mzee wao kukna nitu amewachanjia hivyo anawaona lolote



    watakalojaribu kulifanya. Hisia za ushirikina zikawatawala na kuwajengea hofu. Kila mmoja kwa namna yake



    akaamua kujiepusha na mtego huu wa mzee Barghash

    Hawakumfahamu kabisa kinara wa haya yote. Na hata kumwekea hisia kuwa anaweza kuwa yeye lilikuwa jambo gumu



    sana.

    Walimchukulia kama kibaraka wa mzee Barghash ambaye amepewa ajira ya kuwa anaiweka bustani katika hali ya usafi



    na kuhakikisha nyumba ipo katika utaratibu maalum hasahasa eneo la nje. Hawakuwa wamezoeana naye sana zaidi ya



    salamu ya asubuhi tena si kila siku.

    Kwa mtazamo wan je alionekana mshamba tu asiyeujua mji hata kidogo na alitakiwa kuvushwa barabara kama



    akitakiwa kutoka. Naye alizidi kujiweka hivyo kwa sababu maalum.



    Walifahamishwa haya baada ya miaka mingi kupita kila mmoja akiwa anajitambua……iliwashangaza sana na



    hakufanania.

    Ilikuwa siku ya mahafali ya kumaliza elimu ya chuo kikuu kwa watoto wawili wa mzee Barghash, walishangaa kusikia



    kuwa katika meza ya wageni wa heshima ataambatanishwa Suleiman Meja, walichukulia jambo lile kama utani lakini



    siku ilipowadia Meja alikuwa meza kuu. Alikuwa amejihifadhi katika vazi maridadi la suti nyeusi. Hapakuwa na



    mengi ya kumwelezea lakini alipendeza vilivyo na alikuwa kijana haswaa.

    Katika utambulisho wa heshima Meja akatajwa kuwa amewaongoza kwa kiasi kikubwa katika njia njema watoto wa



    mzee Barghash hadi hapo walipofikia. Watoto walimshangaa baba yao kwa maneno yale lakini ni siku hiyo aliyovunja



    siri ya miaka kadhaa. Akamtambulisha Meja kuwa ndiye aliyekuwa anafuatilia nyendo zao.

    Kila mtu akapigwa na butwaa. Meja akafanya tabasamu jepesi.

    Ni siku hiyo ambapo kila aliyekuwa anamchukulia juu juu Meja alibadili mtazamo wake na kumtazama kwa jicho la



    tatu.

    Zainabu akiwa mmoja wapo.



    Zai akiwa na kumbukumbu hiyo kichwani upesi akapekua simu yake upesi akakutana na jina Anko Meja. Akakimbilia



    chumbani akapiga simu.

    “Nani mwenzangu..” sauti tulivu iliuliza.

    “Zai hapa…Zai wa mzee Barghash…” alijitambulisha kwa papara.

    “Asalamaleykum mwana mpotevu..”

    “Sikiliza Meja nina tatizo tafadhali, naamini haunichukii kama wanavyofanya ndugu zangu.”

    “Nikuchukie kwa lipi Yakhee…yale n’maamuzi yako ati..” alimjibu kwa utulivu uleule.

    Zai akajituliza kisha akamueleza juu ya jambo linalotokea, hakusema kama alifanya uzinzi na George bali alimwambia



    anataka kujua wapi wamekwenda na ikiwezekana ni kitu gani watazungumza iwapo itabidi.

    “N’tumie ya mafuta kwanza mambo mengi tutamalizana sie kwa sie..” alijibu bila kuuliza zaidi.

    “Kisha u’ntumie namba za gari, na barabara waliyopita mumeo namtambua vizuri hakuna haja ya kunikumbusha sura



    yake Yule mswahili na midevu yake ka ya kwangu na misharubu yake ile ama ameiondosha..”

    “Hapana yupo hivyo hivyo, nisaidie tafadhali.” Alijibu kwa uoga mkubwa. Akatoa namba ya gari na barabara



    aliyoamini kuwa wamepita.



    Baada ya dakika kadhaa Meja alipokea pesa kutoka kwa Zainabu, akajaza mafuta gari yake kisha akaingia mzigoni.

    Akaingia katika kazi alizozizoea, kazi ambayo ilimkutanisha na mzee Barghashi nchini Sudani na kufikia hatua ya



    kurejea naye nchini Tanzania. Miaka mingi iliyopita. Na sasa ni mtanzania.



    *****



    TAARIFA ambayo Zai aliipokea usiku ule ilimyumbisha kidogo. Hakutegemea kuwa n’do yanaweza kuwa majibu



    sahihi ya hofu yake.

    Kijana amepigwa sana anavuja damu, amefungwa kamba, kuna mtu ana bunduki. Ameingizwa katika nyumba nyeupe



    pembeni ya jiji la Dar es salaam, mzee Dembele amekasirika sana. Kuna dalili ya kitu kibaya sana.

    Hayo yalikuwa majibu kutoka kwa Meja, majibu ambayo hata yeye mwenyewe mtoaji yalimshangaza wakati akiyatoa.

    Zai akashukuru kwanza kisha kujipa muda wa kufanya tathmini ya kitu gani kinaendelea.

    Au jamaa alituona? Alijiuliza. Lakini kama ni hivyo mbona hajaanza kunihukumu mimi?

    Hapo hapo akakumbuka kitu….

    “Zakiaaaaaa!!!!” akaita kwa sauti ya juu sana. Mtoto wake aliyekuwa nje akaitika.

    “Jana unasema baba yako aliondoka na kuwaacha…ilikuwa saa ngapi?” aliuliza kwa utulivu na hakutaka kumtazama



    mwanaye usoni aliogopa kuwa atamgundua kuwa hayupo sawa.

    “Yaani mama mimi baba kaniboa na nitamwambia akija yaani hata hakukaa sana akaondoka yaani baba…” alilalamika



    yule msichana.

    “Na ulisema kuna daftari Sakina alikuachia umpe mwalimu eeh..”

    “Eeh mama aliniachia basi mi simpi mpaka nimalize kusoma ile hadithi yaani mama ni nzuri hiyo weee!” Zakia alijibu



    kwa furaha huku akimchezea nywele mama yake.

    “Hebu kalilete mara moja hiloo daftari kwanza. Hadithi hadithi…..aaargh!!” alitoa karipio bila kutarajia. Zakia



    akapigwa butwaa.

    Kwa mara ya kwanza wakatazamana usoni. Mama sakina akainama.

    “Nenda ukalilete hapa mwanangu.” Alisema kwa sauti ya chini, Zakia akatoweka.



    “Yaani kama kweli aliniona nikiwa na George nasema kuna daftari lake nilikuja kumpa full stop…tena uzuri daftari



    lenyewe lipo kweli na Zakia anajua….” Alijipa moyo mke wa Dembele.

    Lakini ndo hadi bunduki ashikiwe, afungwe kamba na kupigwa sana.!!! Alijihoji kichwani mwake. Mara Zakia akafika



    na kumkabidhi daftari.



    ****



    Dembele alijisikia fahari sana kuwamiliki wabaya wake ambao maneno yao na uwepo wao katika maisha huru ilikuwa



    kikwazo cha usalama wake.

    Mwanzoni baada ya kuwakamata alikuwa na ari ya kuziondoa roho hizi kwa mkono wake ilimradi tu awe huru bila



    hatia ya waziwazi. Lakini sasa akajikuta akiwaza mengine.

    Mzigo wake. mzigo uliotakiwa kusafirishwa kuelekea ughaibuni.

    Tatizo lilikuwa watu wa kubebeshwa mzigo huu. Dembele akaiona nafasi iliyopo mbele yake ni ya kipekee sana.



    Alikuwa na Mwanaidi, Isha, Frida, George, Suzi na mama George. Hakika alikuwa na matumbo mengi ya kupasua na



    kuweka mizigo yake bila kujali kama aliyepasuliwa ataendelea kuwa hai ama la. Cha msingi Punda afe lakini mzigo



    ufike.

    Mzigo wa madawa ya kulevya.

    Wazo hilo likamkatisha mipango yake ya kuwaua viumbe hawa. Kwanza aliona ni heri wakafie ughaibuni asipate



    ugumu katika kuwafukia ama kuwatupa baharini.



    Dembele akaamua kuvuta subira bila kutambua kuwa kuna nyakati subira huvuta shubiri.

    Wakati akivuta subira roho nyingine ziliendelea kujiuliza maswali, mama George alikuwa akimlaumu Mwanaidi kwa



    kuchelewa kuja kumfuata hospitali hatimaye akaondoka na Isha akafanikiwa kukutana na George lakini huyo George



    akatoweka na hatimaye wakiwa hawajui hili wala lile wakapata ugeni. Ugeni wa maajabu.

    Wakatekwa na mtu yuleyule ambaye alikuwa akimtumia awali kusafirisha madawa ya kulevya. Kipigo alichopokea



    Isha baada ya kufanya jaribio la kutoroka kilimwogofya mama huyu na kujikuta akilaani kuzaliwa na kuishi kwa miaka



    mingi katika dunia isiyokuwa na usawa hata kidogo.



    Alikuwa hajapona vidonda vyake vizuri, n’do kwanza alikuwa ameanza upatiwa huduma hospitali, n’do kwanza



    alikuwa amekutana na mwanaye wa kumzaa, n’do kwanza alikuwa anaanza kuipata furaha ghafla anapokonywa furaha



    yake na kujikuta matatani.

    Akalitazama lile tumbo lililomuhifadhi George kwa miezi tisa,

    akajitazama kifua kilichomnyonyesha George kwa miezi tisa.

    Akajilaani kuitwa mwanadamu!!!!



    Isha alikuwa amerejewa na fahamu baada ya kupokea kipigo kitakatifu kutoka kwa wafuasi wawili wa Dembele ambao



    walikuwa wamelewa. Walimpiga sana kisha kuna vitu walimtishia akiwa hajapoteza fahamu…haikuwa kumtishia tu



    anakumbuka kama…..kama…..

    Walimwambia wata….wata..

    Ghafla akafunua nguo yake aliyokuwa amevaa, hakuhitaji kuthibitisha zaidi wale watu wabaya walikuwa wamembaka.

    Maumivu yakasafiri kutoka katikati ya mapaja yake, yakasafiri kwa kasi ya ajabu na kuacha makovu kila mahali kisha



    yakatua katika moyo mpweke!! Yakaukoa bila huruma.

    Machozi yakamtoka alipojikuta yu peke yake katika chumba asichokijua, mbaya zaidi kwa kosa asilolijua amepigwa



    sana na kubakwa juu. Alisononeka, kilio cha kimya kimya kikaanza kumshinda, akatanua mdomo wake aweze kutoa



    yowe kubwa, sauti haikutoka koo lilikuwa limemkau haswaa. Alikuwa na kiu ya maji.

    Kilio kikaishia pale, ule moyo mpweke ukaendelea kuisononekea dunia juu ya maonevu haya.



    “Ewe Mungu wa Chokoraa uliyesinzia, amka sasa wanao tunanyanyasika. Amka ufanye muujiza mmoja tu uziponye



    roho hizi ama uzitupilie mbali na uso wa dunia tupumzike eeh mwenyezi Mungu” maneno haya yalimtoka bila kujua



    mwanadada Isha. Kisha akajilaza chali kama anayengoja majibu kutoka huko alipoomba.





    Wakati Dembele akihangaika kupitisha maamuzi sahihi kichwani mwake, Mama George akilia na kulaumu kila kitu,



    Isha naye akimtupia lawama muumba wake.

    Binti shujaa na jemedari wa vita hii alikuwa katika mahangaiko ya aina yake. Ni siku nyingi sana zilikuwa zimepita



    bila kukumbwa na tatizo hili ambalo lilimsababisha apotezane na Frida maeneo ya posta huku akiwa nusu mfu na nusu



    hai.

    Mwanaidi aliwaza ni kifo gani ambacho bwana Dembele atawachagulia. Mawazo hayo yakapandisha shinikizo la



    damu. Shinikizo hili likaambatana na ugonjwa wake wa tangu kuzaliwa.

    Pumu.

    Mwanaidi akaanza kuikosa hewa murua kifuani mwake. Akaanza kuhangaika huku na kule. Dawa yake ya kupuliza



    ilikuwa katika pochi yake.

    Alijaribu kuita akiomba msaada lakini hakuna aliyesikia. Aliita kwa juhudi zote lakini ilikuwa sawa na bure.

    Alijaribu tena na tena. Nguvu zikaanza kumuisha, akaanza kutapatapa. huku akipepesuka. Macho akiwa ameyakodoa.

    Roho ikalazimisha kuuaga mwili. Mwanaidi hakuwa radhi kuondoka. Hakutaka kuondoka kwa sababu aliamini



    alikuwa binti mdogo sana kupumzika wakati ana harakati kubwa za kufanya ili kuwakomboa wenzake.

    Mwanaidi hakutaka kufa wakati anazo mbio ndefu za kuwapigania Chokoraa. Alimwomba Mungu amuache walau



    kidogo lakini alipangalo mola………

    Mwanaidi shujaa wa machokoraa, Mwanaharakati aliyepigana kwa nguvu zake zote. Sasa alianguka chini, kiza



    kikatanda. Akatulia tuli.

    Macho yakakutana na mkoba wake, mkoba wenye kile kichupa cha dawa yake ya kupulizia, ambayo humpa ahueni kila



    anapokuwa katika hali hii. Akili ikakiri kuwa ndani ya ule mkoba ipo dawa lakini haiwezi kutoka bila kutolewa. Nani



    wa kuusogeza ule mkoba? nani wa kuiokoa roho hii??



    Viungo vyote vikasita kufanya kazi, yakabakia macho yaliyokodolewa kuelekea ulipo mkoba na masikio ambayo



    yalisikia vishindo vya miguu kuelekea katika chumba kile. Vishindo hivyo vikaambatana na sauti zinazovuma mithili



    ya kelele. Mwanaidi hakuweza kutikisika.

    Picha mbalimbali zikaanza kumpitia katika akili yake. Anazaliwa, anakulia mitaani, anachukuliwa na mjomba wake,



    anafukuzwa kwa kumsaidia Frida.

    Anarudi kituo cha watoto yatima, anafukuzwa akiwa na Frida, anamsaidia Frida kutoa mimba, anakaribia kupoteza



    uhai kwa ugonjwa wa pumu, anaokolewa na mama mbaya muuza miili ya wasichana, anauzwa kwa mwanaume



    anayetaka kumlawiti, kwa mara ya kwanza anafanya mauaji, mara picha ya mama muuza miili akiuwawa nayo



    ikampitia, anakutana tena na Frida na Isha, wanaunganika na George, George anawekewa sumu, Frida na Isha



    wanakamatwa, anakutana na mama yake George akiwa mlemavu.

    picha zinaendelea kwa kasi ya ajabu. Mara anamuua mkuu wa kituo, anapata pesa za damu, anawakomboa bila



    kutarajia Mama George na Frida…anaua tena…..kisha …kisha….picha zikaanza kufifia….

    Mwili unapatwa joto kali sana.

    Jasho linatiririka.

    Kiza kinazidi kutanda.

    ni KIZAAZAA!!!



    ****



    Isha alikuwa amemlilia Mungu pasina kupata dalili zozote za majibu ya upesi, hali ya upweke ilimkosesa amani kabisa



    na alipofikiria juu ya kubakwa akazidi kufadhaika.

    Aliyafikiria maisha yake yalivyozongwa na sintofahamu ndani ya juma moja tu. Tayari alikuwa amesalitiwa katika



    mapenzi, katika kuifuatilia haki yake hiyo anakumbana na kimbembe cha kupigwa na wasichana watatu. Anapoteza



    fahamu, anapozinduka anapokea taarifa kuwa mimba yake iliharibika kutokana na kipigo kile. Anabaki hospitali kwa



    matibabu, anapopata ruhusa ya kurejea nyumbani hata bila kutulia zaidi anakutana na balaa la kutekwa na sasa yu



    mpweke katika chumba kipweke.

    Ghafla akaijiwa na wazo tena lililomghafirisha, Isha akayakumbuka maneno mazito kutoka kwa mama George usiku



    ule wa kwanza na wa mwisho kuwa pamoja. Mama Yule alizungumzia juu ya bwana huyu ambaye anahusika katika



    kusafirisha madawa ya kulevya.

    Kumbe ametuteka ili atutumie kusafirisha madawa!! Isha alijiuliza na kujikuta akiwa anapingana na ukweli.

    Lakini atafanya nini? Hili likabakia kuwa swali zito na la aina yake.

    Kifo!! Hili likasafiri katika akili yake. Isha akaamini kuwa ni heri kufa kuliko kufanyishwa kazi zile zilizoliharibu



    kabisa tumbo la mama George. Isha hakuwa tayari kukabiliana na maumivu yale.

    Sasa atakufa vipi? Hili nalo likaingia katika mfululizo wa maswali aliyokuwa anajiuliza, akatamani itokee sumu



    aweze kunywa lakini muujiza huo haukuwa mwepesi, akatamani walau kijitokeze kisu, ama kamba ajinyonge. Bado



    haikuwezekana.

    Macho yaliyokata tamaa yakainuka na kukutana na ule ukuta mweupe katika kile chumba. Wazo la ujasiri usiokuwa



    kifani likaandamana katika fikra zake, akasimama wima na kuamua kujiua katika namna ya ajabu namna



    isiyotamanisha kusimulia.

    Isha aliyebakwa akaamua kuuvamia ukuta ule kwa kutumia kichwa chake, lengo likiwa moja tu kukikutanisha kichwa



    chake na ule ukuta ili aweze kutokewa na lolote ambalo litatokea. Aidha kifo ama lolote lile.



    Ni heri kukumbwa na wazimu kuliko kukutana na yule mwanaharamu kwa jina Dembele. Ambebeshe madawa ya



    kulevya kisha amuue, ama la wale wabakaji waendelee na ile tabia yao katika mwili wake…..

    Wakati akitegemea kukutana na kishindo kikubwa kwa kichwa chake kukutana na ukuta, hali haikuwa hivyo. Ule



    mwendo wake akajikuta amesukuma kitu ambacho kilizidiwa uzito na kuachana Isha akapenya.

    Lahaula! Hakuwa amekufa wala kurukwa na akili……alipofumbua macho alikuwa katika chumba kingine….aliona



    tundu la mahali ambapo alikuwa amepenya, kumbe ule haukuwa ukuta kama alivyodhania awali.

    Mara akahisi kitu kingine tena, hakuwa peke yake katika kile chumba. Wazo likamjia kuwa yu katika chumba kimoja



    na wale wabakaji wasiokuwa na huruma hata kidogo. Akageuza shingo yake taratibu aweze kukabiliana na ukweli,



    maajabu mengine alikutana na macho yakiwa yamekodolewa katika namna ambayo hakuwahi kuona hapo kabla,



    hakuhitaji dakika ya ziada kuhisi jambo. Hapana hazikuwa hisia ilikuwa ni kweli…..alikuwa yeye……

    Mwanaidi shujaa wa kike asiyeogopa lolote alikuwa taabani. Alikuwa anahangaika, alikuwa amenyoosha mkono wake



    bila kutikisika, midomo ilikuwa wazi kabisa na jicho lilikuwa limekodolewa kuelekea mahali…..kulikuwa kuna kitu.



    Ni hapa Isha alipoikumbuka ile siku ambayo alikutana na Frida maeneo ya posta akiwa amepotea, alimueleza kuwa



    rafiki yake aitwaye Mwanaidi alikuwa amekumbwa na ugonjwa wa ajabu alipoenda kumtafutia dawa akapotea. Kwa



    wakati ule hakuwa na mahali pa kwenda. Ni siku hiyo Isha alivyoanza kuishi rasmi na Frida.



    Sasa anakutana na Mwanaidi akiwa na ugonjwa uleule ambao Frida aliwahi kumweleza. Ugonjwa wa Pumu.

    Kumbe mtu akitaka kufa n’do anafanania hivi!!! Alijisemea Isha katika namna ya kustaajabu. Lakini hakutaka mfano



    wa mtu kufa mbele yake uwe Mwanaidi….

    Upesi Isha akatazama tena jicho la Mwanaidi, lilikuwa limekodoa kutazama mahali, akalifuatisha na kukutana na kitu



    mfano wa mkoba mdogo.

    Kwa nini anautazama mkoba huo. Isha hakutaka kumuuliza yeyote maana alijua hatakuwepo wa kumjibu. Kwa mara



    ya kwanza akashukuru kwa hali ile aliyokuwa nayo, laiti kama angekuwa mjamzito huenda asingeweza kuthubutu



    kujirusha namna ile. Isha alizirukia mbao moja baada ya nyingine hadi akaufikia mkoba ambao ulitupwa kule juu



    wakati Mwanaidi anasulubiwa. Ulikuwa mkoba mdogo ambao Mwanaidi hutembea nao mara kwa mara, Isha akajivuta



    zaidi na sasa alikuwa akitembea katika ‘kenchi’ kwa kunyata…….

    Ni huku alipokutana na jambo ambalo lilimfanya afanye kitendo ambacho hakutarajia na mwisho kuleta mikikimikiki.



    ****



    BADALA ya kumtumia pesa yote kwa njia ya simu, Zainabu aliamua kukutana na Meja faragha kidogo ili waweze



    kuzungumza zaidi japo hakumweka wazi anahitaji wazungumze jambo gani jingine. Meja aliendesha gari upesi



    kuelekea nyumbani kwa Mama Sakina kama ambavyo alikuwa ameelekezwa.

    Baada ya saa zima walikuwa wakizungumza juu ya tukio ambalo Meja alikuwa amelishuhudia. Hapakuwa na neno



    jipya lililoongezeka katika maongezi yale, maswali ya Zainabu na maelezo yake n’do yalimuweka Meja mdomo wazi.



    Hakutegemea hata kidogo Yule mama wa kiislamu anaweza kufanya kitendo alichokifanya na kijana George wakati



    yupo ndani ya ndoa….

    “Meja nilijikuta tu nafanya hivyo usinilaumu…”

    “Ona sasa umemtakia balaa mwenzio..mtoto mdogo Yule umemuingiza katika kash kash kama hiyo. Utamtoaje sasa



    pale.” Alilaumu Meja.

    “N’do maana nipo na wewe hapa nahitaji msaada zaidi, nahitaji kufahamu kwa nini anampa vitisho hivyo na pia



    nahitaji kujua huko ndani anafanywa nini na pia Meja anampango gani na mimi.” Alizidi kuelezea. Meja akatikisa



    kichwa kumaanisha kuwa amemuelewa.

    Zainabu akatoa kiasi cha pesa bila kuhesabu, “Ukimaliza hiyo kazi nitakuongezea” akasindikiza na maneno hayo.

    Meja akazipokea bila kusema lolote. Wakaagana.



    ****



    MEJA alianzia upesi eneo la Mchikichini, huko akafanya upelelezi wa haraka sana na kugundua ni wapi George



    alikuwa anaishi. Bila kuhitaji kusindikizwa yule mwarabu akatuliza akili na kufahamu fika mahali ambapo George



    alikuwa anaishi. Huku akakutana na neno la ziada kuwa George alikuwa anaishi na mwanamke aitwaye Isha, pia



    akafahamu kuwa George alikuwa Chokoraa ambaye n’do kwanza anaanza kujikwamua kimaisha…..

    Kama hiyo haitoshi Meja anasimuliwa mkasa wa kuonekana kwa mama mmoja akiwa na mkewe George wakihangaika



    kumtafuta George bila mafanikio kisha katika hali ya kushangaza nyumbani kwa George wakatokea wageni wa ajabu,



    wageni ambao waliwalazimisha yule mama pamoja na mke wa George kuondoka nao.

    Huo ukawa mwisho wa kuwaona hadi wakati ule waliokuwa wanazungumza na Meja.

    “He! Wamempeleka wapi tena ticha wangu dah!! Ujue nasoma elimu ya watu wazima….siu unajua mambo ya elimu



    tena hizi…” akasita huku akijichekesha kama ambaye ameona aibu kusema jambo lile la kuwa yeye ni mwanafunzi.

    “…kwa hiyo n’do ananipiga msasa kidogo.” Meja akamalizia kuteka akili za majirani wawili waliokuwa wamechotwa



    akili zao bila kujua.



    Hata alipoondoka tayari alikuwa na jambo la ziada. Kumbe George ni yatima na mke wake naye ni yatima, na huyo



    mama ni nani haswa? Na kwa nini watoweke baada ya George kutoweka.

    Hapa kuna jambo la ziada huenda ambalo hata mama Sakina halijui na halimuhusu!! Meja alijisemea kwa sauti ya juu



    kidogo huku akiingiza gia katika gari na kutoweka.

    Alipoyafikia mataa, aliyatazama kwa makini kisha katika yale mataa ya barabarani alijikuta akirejea akili zake nyuma



    miaka mingi sana ya msoto nchini Sudani, alipoishi maisha ya kutomjua baba wala mama, aghalabu hata ndugu



    mmoja. Wote hakuwajua.

    Maisha yaliyomkutanisha na wasaliti na vizingiti…akaishi kila aina ya maisha magumu na kujikuta akiwa na mi8aka



    kumi na tatu akijua vyema matumizi ya bunduki.

    Alishikishwa bunduki huku akisisitizwa kuwa ni vyema akamate mtutu na kulipiza kisasi kwa watu waliowaua wazazi



    wake, ile sumu ikamwingia yatima yule akatenda waasi walivyotaka….

    Kadri alivyozidi kuwasiliana na wenzake ndivyo alivyozidi kubaini kuwa ule mtutu aliokuwa anaushika ni kwa



    manufaa ya watu kadhaa na si kwa kulipa kisasi., akaamua kuitupa Bunduki na kurejea mtaani akiwa yatima vilevile



    kama awali.

    Huku akakutana na vijana wengine waliomwonyesha njia na kumwingiza katika biashara haramu ya kuiba silaha na



    kuuza kwa kwa wageni wanaotembelea nchi hiyo kwa sababu zao binafsi. Ni huku alipokutana na mzee Barghash,



    mwarabu kutoka Tanzania. Wakaanza urafiki, mara ya kwanza wakiuziana silaha, mara ya pili akimsaidia kuijua mitaa



    kadhaa ya Sudan na mipaka na namna ya kupenya kwa njia za panya. Ilikuwa rahisi kwa wawili hawa kuwasiliana kwa



    sababu msudani huyu alikuwa anafahamu baadhi ya maneno ya Kiswahili.

    Damu zao zikaendana na hatimaye siku moja akaamua kurejea Tanzania akiambatana naye…..huu ukawa mwanzo wa



    kuitambua maana ya amani isiyokamilika…amani inayokosa watu muhimu wa kuifanya iitwe amani.

    Amani bila ndugu wa damu yako hasahasa wazazi, inakosa maana.

    Honi za magari mengine zilimfumbua macho na kugundua kuwa mataa ya kijani yalikuwa yamewaka. Akarejesha akili



    yake barabarani na kukanyaga mafuta. Gari ikapepea kuelekea kule alipokuwa anaenda.



    Mawazo yaliyopenya katika kichwa chake kwa kipindi kifupi yakamfanya ajengeke kihisia fulani. Akahisia anatakiwa



    kujua jambo kutoka kwa yatima wenzake. Japokuwa umri ulikuwa umeenda wa kujiita yatima lakini bado alikuwa ana



    kumbukumbu ya kuzaliwa yatima na kuishi kiyatima.

    Gari lake akaliegesha katika baa fulani mita nyingi kidogo kutoka katika nyumba ya Dembele. Akaagiza mchemsho wa



    kuku, akaanza kujilia taratibu huku akitegea muda fulani ufike aweze kufanya kile alichotakiwa kufanya.

    Saa mbili usiku akajikongoja kwa mwendo wa miguu, umri wake wa miaka 40 haukufanania hata kidogo na umbo



    lake, alikuwa amekomaa na haikushangazwa kama ungeweza kumkadiria kuwa na miaka 28. Alikuwa mkakamvu sana.

    Alilifikia geti la ile nyumba. Akabofya kengere ya mlango akangoja kwa dakika tano mlango ukafunguliwa.

    Jambo la kwanza Meja akawahi kumtazama mtu aliyefungua geti. Hakuwa mlinzi na ni mtu ambaye alionekana kuwa



    na wasiwasi na hakutarajia ujio wa mtu yeyote katika nyumba ile.

    “Samahani eti Ndesamburo yupo…” aliuliza kwa kitetemeshi kana kwamba anahofia umaridadi wa yule kijana.

    “Hakuna mtu kama huyo hapa aisee….” Alijibu kwa ghadhabu kisha akafunga geti kwa nguvu. Meja akajifanya



    kuduwaa, wakati alikuwa anatafuta sababu ya kuweza kuchungulia nini kinaendelea ndani.

    Kupitia tundu dogo akamwona yule kijana akirejea ndani.

    Hapakuwa na mlinzi!! Meja akapata jibu. Akajipapasa kiunoni mwake akakisikia kitu kigumu ambacho huwa



    hakitumii mara kwa mara isipokuwa kwa shughuli nyeti tu anazofanya na mzee Barghash. Mafia asiyejitangaza



    hadharani….



    Kwa wepesi akasogea nyuma biula kupoteza muda, alijua kuwa kwa muda ule kama kuna watu wengine ndani basi



    watakuwa wakisimuliana juu ya ujio wake katika himaya n ile. Jambo ambalo litawapumbaza na kushindwa kutilia



    maanani jambo jingine geni. Meja akanyata na kuona kipande cha ukuta ambacho kilikuwa kirefu lakini kikipokelewa



    na mti wa mwembe uliochungulia nje. Meja akafaya tabasamu hafifu. Kisha akarudi hatua kadhaa nyuma na kujirusha



    akanasa alipotaka, akajitutumua hadi akafika juu, kwa uangalifu kabisa akanasa katika ule mwembe.

    Akatulia kwa sekunde kadhaa kisha akaanza kushuka. Wakati anashuka akakutana na kitu kilichomtia faraja nyingine.



    Akaliona tundu……vioo vya kuingia katiuka choo cha ndani vilikuwa wazi, Meja akashuka hadi chini kisha akasogea



    hadi katika kile choo, akatulia kama kivuli kusubiri matokeo yoyote. Hakikutokea kitu.



    Akajirusha na kutua ndani ya kile choo kama aliyepita kimiujiza tu na kuwa pale ndani. Akaangaza huku na kule, kisha



    akajituliza kiakili kwanza. Akataka kuufunga mlango wa chooni ndipo aliposikia hatuazikisogea kuelekea katika choo



    hicho.

    “Oya mi nalala kabisa nyie mafala endeleeni na filamu yenu hiyo.” Sauti ilisikika, haikuwa mara yake ya kwanza



    kuisikia. Na hakuhangaika sana kutambua kuwa ni yule bwana aliyemfungulia geti na kumjibu kwa dharau.

    Meja akaendelea kutulia vile vile akamsikia akipiga mluzi, bila shaka kabla ya kulala alihitaji kuanzia chooni. Maana



    mluzi ulielekea sana kule.

    Hakika ilikuwa hivyo. Mlango ukatikiswa, Meja akajiweka nyuma ya mlango ule. Yule kijana akiwa uchi wa myama



    akaingia bila shaka alikuja kwa ajili ya kuoga. Akiwa kama bwege alianza kupiga miluzi huku akikata viuno. Mara



    akaanza kuongea mwenyewe.

    “Lile bwege kwenye ile filamu linapiga aisee, yaani mfano pale hivi ndo ningekuwa mimi daah yule demu simuachi,



    yaani nimemsaidia vile halafu nimwachie aah wapi….halafu karembo aisee…..wanafaidi sana hawa jamaa. Hapo ukute



    baada ya filamu wanaenda kumalizana aah….kudadeki usiku namzamia yule demu chumbani kwake nambaka kama



    hataki kwani atanifanyaje….halafu siwaambii hawa mabwege maana watakomaa tupige wote….” Kadri alivyozidi



    kuzungumza ndivyo maungo yake yalizidi kuwa magumu kisha yakasimama wima……



    Mara akachezwa na kitu kama machale kuwa nyuma yake kuna mtu anamtazama. Alitaka kugeuka lakini akahisi kuwa



    ni mawazo yake hafifu tu. Akabaki kujitazama jinsi maungo yake ya uzazi yalivyokakamaa. Hakika jamaa alikuwa



    kwenye uhitaji.

    Na wazo alilokuwa nalo ni kwenda kumbaka tena Isha.

    Machale yalivyomcheza kwa mara ya pili, alifungua bomba linalotoa maji kwa juu. Yalipoanza kummwagikia



    akageuka aweze kutwaa sabuni, ni hapo alipokuta na kituko.

    Yule mgeni mshamba aliyemwacha solemba getini. Sasa alikuwa pale bafuni.

    Uume ukasinyaa ghafla kana kwamba haukuwahi kuwa wima hapo kabla.

    Akataka kupiga mayowe. Meja akamuwahi kooni.



    Akamnyanyua juu juu. Akahakikisha kuwa analegea vilivyo.

    “Ni maelezo yako pekee yanaweza kukutoa huru humu ndani ili ukafanye huo ubakaji wako kwa amani kijana.”



    Mwarabu mweusi alizungumza kwa utulivu na kwa sauti ya chini sana.

    Yule kijana sasa akajikuta akitokwa na kojo lisilotarajiwa. Ni kama alikuwa anaona mauzauza ya ajabu sana.

    “Wewe ni nani na unafanya nini katika jumba hili la bwana mdogo.” Alimuuliza huku akiwa amemdhibiti kiuhakika.

    “Sikwambii chochote.” Alijaribu kuweka jeuri lakini Meja alikuwa jeuri wa majeuri.

    Akamnyanyua juu kisha akakunja mguu wake na kuliweka goti katika hatamu. Akaanza kumpiga na goti lile tumboni.



    Mapigo matatu pekee. Kisha Meja akakiachia kichwa chake kikubwa kilichokomaa kikatua katika paji lake la uso huku



    akiwa amemkaba koo asiweze kutoa kelele zozote.

    . .E bwana eee! Palepale haja kubwa ikamtoka yule bwege……na kuanzia pale akasema kila kitu alichokuwa anajua.

    Kumbe alikuwa ni daktari kabisa aliyeajiriwa na serikali na anapokea mshahara mkubwa tu lakini nje ya hapo alikuwa



    anapasua matumbo ya raia wema na kutia madawa ya kulevya ndani yake. Na pale ndani walikuwa wanangojea



    kuwapasua wanawake wane na mwanaume mmoja. Usiku huo walitarajiwa kumtoa mimba muhusika mmoja ili zoezi



    liweze kwenda kama lilivyopangwa.

    Huyu muhusika aliitwa Frida. Frida Gereza.



    Kujieleza huku kukamkera zaidi na kumtia hasira kuu mzee Meja. Akaghafirika na kutokwa na tusi zito la nguoni kwa



    lugha ya kiarabu.

    Kisha akafanya kitendo ambacho hapo zamani kwake ilikuwa kawaida sana kukifanya hasahasa akikasirika.

    Akaikama shingo ya yule daktari muuaji. Akaizungusha kwa nguvu, akatulia hivyo kwa sekunde kadhaa.

    Ile zawadi ya uhai ambayo daktari alikuwa amepewa na mwenyezi Mungu ikaondoka zake hata kabla hajajisafisha



    kutokana na tendo la kutokwa na haja kubwa na ndogo kwa pamoja.

    “We fala ndo kuoga huko au unapiga masterbation…” ilisikika sauti kutoka nje ikiuliza lakini haikutilia maanani



    kuhusu jibu.

    Meja akacheka kwa sauti ya chini kidogo ili azidi kuwahadaa kabla ya kuwavamia kiaina nyingine.



    BAADA ya kuhakikisha pametulia tena alipanda juu kidogo akasukuma kiubao kilichokuwa kinaziba tundu ambalo



    nyumba inatumia kupumua. Ni hapa alielekezwa kuwa pana njia ya kuingia katika dari.

    Alipohakikisha kuwa hakudanganywa. Alishuka tena akaufunga vyema mlango wa choo kile kisha akapanda juu. Kwa



    ustadi wa hali ya juu akaanza kutambaa akivitafuta vyumba ambavyo wamehifadhiwa binadamu waendao kwa majina



    ya George, mama George, Isha,Mwanaidi, na Frida.

    Meja alikiri kauli yake ya awali kuwa anaenda kukutana na jambo ambalo hata Mama Sakina pekee halijui. Hii ilikuwa



    zaidi ya wazo lake kuwa amefumaniwa. Hii ilikuwa kivingine kabisa.

    Ulikuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

    Alipitisha mawazo hayo huku akinyata kwa umakini wa hali ya juu sana. Mara akakutana na tukio la ajabu zaidi na



    lililomshtua na kufikia hatua ya kutoa bunduki yake aweze kuitumia.

    Ana kwa ana na kiumbe kama paka mkubwa wa kutisha akiwa anahaha kutembea katika dari. Upesi akatoa bunduki



    yake kiunoni. Mara ghafla yule paka akapiga kelele akisema ‘mamaaaa’ hii ilishangaza sana paka anasema mama? Haya



    yalikuwa maajabu ya pekee.

    Haiwezekani……



    Kishindo kikasikika! Meja akataka kukimbia kurejea chooni lakini akajipa imani kuwa bunduki yake ipo kumpa ulinzi.

    Akanyata tena hatua kadhaa kisha akatazama chini, huku sasa akawaona wanadamu wawili.

    “He! Ina maana yule paka amegeuka kuwa mwanadamu ama sikuona vizuri. Tena msichana tazama…” Meja aliyasema



    haya huku akimtazama Isha na Mwanaidi waliokuwa wametulia tuli sakafuni.







    Usilolijua ni sawa na usiku wa kiza kinene. Hali hii ilimkabili bwana Dembele pia, baada ya kuwa amewamiliki



    mateka hawa katika himaya yake ya siri akafikiri sasa yupo huru, hakutambua kuwa hakuna siri inayodumu milele, na



    sasa siri yake ilikuwa imetapakaa, na alikuwa ananuka hatia. Hatia mbaya zaidi ya ambavyo angeweza kudhani.

    Tamaa zikamponza.

    Amakweli mshika mbili moja humponyoka.

    Dembele alikuwa anatamani kuua na wakati huohuo akatamani kuwatumia wale wafu watarajiwa katika biashara yake



    ya madawa ya kulevya.

    Ngoja ngoja hii ikamponza. Hakuwa na mtu wa kumshauri, akahisi pombe pekee inaweza kuwa suluhu ya matatizo



    yake. Dembele akahamia katika baa iliyopo jirani na nyumbani kwake.

    Chupa moja baada ya nyingine zikazidi kusalia chupa tupu mezani. Na ulevi nao ukaingia kichwani.

    Katika meza yake awali alikuwa peke yake lakini sasa akaanza kuona kama wapo watatu hadi wanne lakini cha ajabu



    kila akiwashika anaambulia hewa.

    Alitambua kuwa sasa amelewa. Akafanya tabasamu dogo. Kisha akamimina kilevi zaidi katika glasi yake. Kasha



    akaitwaa simu yake akapiga namba Fulani.

    “Fanyeni kazi yenu usiku huu..hakikisha mzigo wote unaondoka kesho kutwa asubuhi…..yule mwenye mimba naye



    ahusishwe hakuna kubakiza hata mmoja. Nimemaliza!!!” alizungumza huku akitokwa na matemate hovyo. Dalili tosha



    ya ulevi. Akaitua simu yake kisha akaitwaa tena pombe yake. Akagida mfululizo kabla ya kuitua chini chupa tupu.

    Akatikisa chupa nyingine ambayo ilikuwa imefunguliwa tayari akataka kuifanyia ukatili ibaki tupu kama ile nyingine.



    Alipoanza kunywa mara wale watu aliowahisi mwanzo kisha akawashika na kuambulia patupu wakaongezeka tena.



    Akajaribu kuwashika kama awali.



    Maajabu. Mara hii walikuwepo kweli. Wakamkamata mkono. Akajaribu kufurukuta akaona wanaonyesha



    vitambulisho.

    Ulevi mwingi uliokuwa umemkabili hakuweza kusoma maandishi. Akahisi ni wezi wanataka kumuibia.

    Akajaribu kufurukuta akakumbana na pigo kali katika shavu lake. Bia kadhaa alizokunywa zikatoweka mwilini kwa



    kasi ya ajabu.

    Alipoongezwa mapigo mengine mawili fahamu zikamrejea vyema. Ikabakia harufu tu mdomoni.

    Aliweza kuvisoma vile vitambulisho.

    Walikuwa ni askari!! Askari wa jeshi la polisiTanzania.

    Alhamdulilah!!

    Dembele akapagawa. Wakamvuta pembeni, wakamuuliza iwapo alikuja na gari lake. Akasema hapana!!

    Wakaingia naye katika magari yao.

    Vumbi likatimka. Ving’ora vikipiga mayowe.

    Dembele akasindikizwa kituoni. Hapo akiwa hajaulizwa kitu chochote kile.

    Wakati anashuka, suruali yake ilikuwa tepetepe kwa mikojo, jicho likiwa limemtoka pima zaidi ya mjusi aliyebanwa na



    mlango.

    Askari mmoja akamcheka.

    Moja kwa moja katika chumba cha mahojiano. Mwanzoni Dembele alijifanya mbishi, askari wakawa wabishi zaidi



    yake.

    Lile tipwatipwa lilipominywa kidogo likatiririka mistari zaidi ya George alivyofanya baada ya kutogwa sikio.

    Dembele akasema kila kitu anachofahamu.

    Kwa uoga aliokuwanao akakiri kuwa ni yeye aliyemuua mke wa Kasuku. Maajabu!! Hakuna aliyetarajia taarifa ile hata



    kidogo.

    Kumbe hayawani anahusika!!!



    Maelezo yake ya awali yalitosheleza kwa askari hawa wazoefu.

    Upesi sana wakatoweka wakiwa wameambatana na Kasuku hadi nyumbani kwa Dembele.

    Msako ukaanza.

    Msako wa ukombozi.

    Chumba hadi chumba.

    Kamata mke wa Dembele, kamata watoto. Wote wakatupwa katika kalandinga.

    Msako ukaendelea katika vyumba vya siri. Hakuna kilichopatikana huko.

    Wakayakumbuka maneno ya Dembele kuwa mateka walikuwa katika nyumba yake nyingine, Kasuku alikuwqa



    anaifahamu akawaongoza maaskari katika jambo hilo.

    Huku kikazuka kitimtim kingine cha aina yake ambacho kilinyamazisha mtaa kwa muda mrefu.

    Hali ilikuwa imetulia kama kwamba eneo lile hakuna mtu hata mmoja. Askari hawakubabaika kutokana na hali ile



    wakaweka umakini katika kuendesha ule msako. Wakiwa na nguo zao za kiraia wakaizingira nyumba ile waweze



    kupenya.

    Kupitia katika ukuta jicho moja kali ajabu kutokea katika eneo lisilofikirika liliona kiwiliwili kikihangaika kumalizia



    kupanda ule ukuta. Bunduki makini ikiwa katika kiwambo cha kuzuia sauti ilifyatuka na kutua katika chemba ya moyo



    barabara.

    Yowe la hofu likasikika kutokea nje, mshambuliaji alikuwa na uhakika kuwa hajaikosa shabaha ile hivyo bila shaka



    kuna maaduio wengine walikuwa wamemtanguliza mwenzao kama chambo sasa ametua kama maiti. Muuaji akaweka



    hadhari ya hali ya juu. Macho yake yakafanya mzunguko mwingine mkali, akakutana na kichwa kikimangamanga huku



    na kule. Mara macho yao yakagongana, yule askari alikuwa hajategemea kukutana na macho yale gizani. Akatokwa na



    yowe la hofu lakini hilo lilikuwa neno lake la mwisho kusema kabla hajasukumwa kwa nguvu kurudi nyuma mapande



    ya damu yakaruka huku na kule.

    Alikuwa amekufa.



    Mshambuliajni akiwa makini kabisa alididimia chini tena kwa uangalifu akarejea mahali ambapo alimwacha msichana



    mwingine akimuhudumia mwenzake…akiwa katika hatua za kunyata mithili ya paka anayewinda panya, aliendelea



    kutembea katika ‘kenchi’ ile hadi akafikia kile chumba.

    Jicho lake likakutana na kitu cha ajabu kingine. Mwanaume mmoja alikuwa akimuhangaisha msichana ambaye muda



    mfupi uliopita walikutana katiuka dari kisha akaporomoka na kuanguka chini. Huyu alikuwa ni Isha na mwanaume



    alikuwa katika jaribio la kumbaka.

    Macho ya Isha yaliyokuwa yamekata tamaa kutokana na kubanwa vilivyo na yule mwanaume yalikutana ana kwa ana



    na macho angavu ya Meja. Tumaini likarejea upya, japo hakutambua yule mwanaume ni nani lakini alifarijika



    kutambua kuwa alikuwa upande wao.



    Ni mwanaume huyu ambaye alifanikiwa kuitoa ile dawa ya kupuliza katika mkoba wa Mwanaidi na kuurejesha uhai



    wake tena. Na ni huyu ambaye alikuwa anatazamiwa kutoa msaada baada ya sekunde kadhaa.

    Wakati Isha akijiuliza ni wakati gani atatoa msaada Alishangaa mwanaume yule mweusi lakini mwarabu akijiachoa



    kutoa juu.

    Akatua mgongo ukiwa umejikunja. Kishindo kikatoka.

    Isha alitarajia kuwa mtu yule asiyekuwa na jina atafanya papara, haikuwa hivyo yule mwarabu alitua kama vile



    ameanguka bahati mbaya. Mara ghafla chumba kikawa na watu wanne. Yule mbakaji ambaye alikuwa amevua nguo



    zake tayari alitaharuki akajaribu kujirusha pembeni lakini Isha alikuwa habari nyingine. Mnyanyase akiwa peke yake



    lakin kuna mwanaume pembeni yake…usithubutu.

    Upesi akamdaka yule mwanaume kama ambaye anamsihi aendelee na zoezi la kujaribu kumbaka. Mwarabu mweusi



    bado alikuwa wima kama anayesubiri kitu fulani kitokee. Jinsi alivyosimama alifanania na mwendawazimu ambaye



    hata ule wazimu hana tena ni kama roboti linalopumua tu lakini akili haiku pale. Yule mbakaji ambaye alikuwa



    ametaharuki akaanza kushangaa kiumbe kile, sasa alitaka kujing’atua kutoka kwa Isha. Isha alipozidi kumng’ang’ania



    akamshushia ngumi nzito tumboni.

    Binti akatokwa na yowe…yowe kali lililosafiri katika masikio ya Meja na kumkumbusha juu ya vifo vya wanawake



    katika vita walikuwa wanalia lakini hakuna wa kuwasaidia.

    Mara akaunganisha meno yake kwa ghadhabu. Hata wakati akifanya hivi yule mwanaume alikuwa amesimama.

    Akiwa hajajua afanye nini na kile kiumbe mara, kiligeuka na kumpa mgongo.



    Mwendawazimu kamili!! Isha na yule mbakaji ambaye pia ni daktari walifikiria hivyo. Lakini mara miguu ya yule



    mwendawazimu ikarushwa katika mtindo wa sarakasi ya aina yake ya kuzunguka.

    Lile korodani lisilokuwa na nguo likakutana na dhahama ya ajabu mguu wa kuume ukalitandika kwa uzito wa ajabu.



    Yowe kubwa likatoka na halikuweza kutoka tena Suleiman Meja alikuwa amegeuka na kumkaba tena shingo yake.

    Kama alivyomjaza mateke yule marehemu wa bafuni sasa alikuwa anamshambulia huyu mbakaji mwingine…..

    Ni kama jamaa alikuwa mwendawazimu kweli, alimrukia katita staili hii mara akaruka huku na kumng;ata sikio yule



    mbakaji mara akamtwisha ngumi nzito, kisha akamwangusha chini na kuzidi kuthibitisha kuwa yeye ni mwehu.



    Akaanza kumkanyaga kanyaga pasipo na utaratibu maalumu hadi pale kiliposikia king’ora cha polisi na matangazo yao



    yakisihi kila mmoja atoke ndani ya nyumba hiyo.

    “Mpo wangapi?” kwa mara ya kwanza mwarabu alizungumza.

    “Wapi? Aah wawili lakini…..na wengine wapo lakini…sij…” kabla hajamaliza yule mwarabu aliruka juu na kukwea



    kurejea darini.



    Akina Kasuku waliendelea kungoja na kusihi kuwa kila aliye hai katika chumba kile ajitokeze nje. Kimya hakuna



    aliyejitokeza.

    Tangazo lilirudiwa tena na tena. Na kimya kikaendelea kutanda. Askari wawili walikuwa wamepoteza roho zao. Bila



    shaka mtandao wa Dembele ulikuwa mkubwa na hatari sana.



    Tangazo lililotolewa nje n’do lilimshtua akili Meja na kutambua kuwa badala ya kupambana na maadui alikuwa



    amepambana na maaskari na kwa jinsi alivyokuwa akiiamini bunduki yake hakuwa na shaka kuwa kuna roho alikuwa



    amezitawanya tayari. Sasa alihitaji kufanya namna yoyote ile kuwasaidia maaskari katika kazi iliyopo mbele yao.

    Akiwa darini alitambaa huku na kule kwa umakini kabisa bila kufanya vurugu yoyote ile. Alipita chumba kwa chumba



    kwa umakini. Alitambua fika kuwa watu wale wabaya kwa kusikia tangazo lile kutoka kwa maaskari lazima watafanya



    namna ya kufuta ushahidi wa mchakato mzima. Na ushahidi huu ulikuwa unatoka kwa hawahawa wahanga.

    Meja alikuwa hajaridhika kabisa kutoiona sura ya yatima ambaye alimtia hasira na chuki na kumfanya achukue



    maamuzi haya bila kumshirikisha mtu yeyote. George! Bado alikuwa hajaonekana.

    Meja akazidi kutambaa kwa kasi na hatimaye akafikia chumba kingine……

    Wazo lake lilikuwa sahihi kabisa, sasa aliweza kumuona mama mtu mzima!!

    Mama George huyu. Alijisemea……mama huyu alikuwa amekodoa macho yake huku kijana mwenye jaketi jeupe



    akiwa anajiandaa kumdfunga sindano. Kijana huyu alionekana kufanya jambo hili kwa haraka kupita kawaida.

    Meja mwarabu mweusi mzoefu wa mapambano ya aina mbalimbali na sehemu za kila aina akatambua kuwa yule



    mama alikuwa katika dakika za mwisho za uhai wake. Ni heri angemkuta amedungwa sindano tayari angesikitika tu na



    kusahau, lakini kumkuta akiwa katikia mchakato wa kudungwa sindano na yeye ashuhudie hakika asingeweza kusahau



    maishani na angejiweka katika kundi la wauaji.

    Wakati huu hakutaka kupoteza muda kushuka chini na kukabiliana naye, japo aliamini kuwa anaweza. Akaitoa bunduki



    yake na kuiweka vyema mkononi. Akajikohoza kidogo, yule daktari akasita, akajikohoza tena. Daktari akatazama juu.

    Hapakuwa na nafasi ya kuulizwa alikuwa anataka kufanya nini. Risasi ikapenya mahali palipostahili. Daktari



    akarushwa kwa nguvu kuelekea ukutani…..maajabu ule ukuta ukabomoka.

    Lilifanana na tukio la Isha aliyedhani kuwa ule ni ukuta.

    Chumba kilichofuatia alikuwemo Frida.

    George akashuka upesi, hakusema neon na yule mama. Akajirusha kwa nguvu kuvamia chumba kingine, humo



    akamkuta George Emmanuel. Alikuwa na majeruhi ya kipigo kikali. Akawatazama jinsi walivyotaharuki, akaamua



    kusema nao neno.

    “Mkiulizwa semeni kuna yatima mwenzetu, yatima wa kiarabu alikuja kutukomboa.” Kila mmoja alimsikia. Lakini



    hakuna aliyeelewa kwa wakati ule.

    Aliporuka darini tena. Huo ukawa mwisho wa kumuona mazingira yale.



    *****



    Askari walifanikiwa kupenya na kuingia ndani bila kukutana na kikwazo kipya, ulinzi ulikuwa umeimarishwa vyema



    sana na yule mshambuliaji alikuwa hashambulii tena. Jambo hili liliwaduwaza askari. Waliweka tahadhari ya aina yake



    tahadhari kubwa sana…..

    Ndani walikutana na miili mitatu ikiwa haina uhai tena, maiti moja ikiwa na kovu la risasi huku nyingine zikiuwawa



    katika namna ya kustaajabisha zikiwa uchi wa mnyama.



    Walifanikiwa kuwatoa watoto na mama yao. Huku Mwanaidi akiwa bado na hali tete. Licha ya Meja kufanikiwa



    kumpulizia ile dawa yake ya pumu lakini mambo yalikuwa bado.

    Wakambeba katika gari ya wazi, akakimbizwa hospitali.

    Wale wengine wakafikishwa katika kituo cha polisi kwa usalama wao.

    Walihifadhiwa pale hadi majira ya saa kumi na moja jioni siku iliyofuata wakiwa chini ya ulinzi maalum.

    Kila mmoja akiwa ametoa maelezo yake juu ya chochote alichokuwa anafahamu kuhusiana na maovu ya Dembele. Pia



    walifafanua juu ya mwanaume mweusi wa kiarabu jinsi alivyowafikia kama muujiza na kuwakomboa, George, mama



    yake pamoja na Frida kwa pamoja waliyakariri maneno aliyosema nao kabla hajatoweka na wasiweze kumuona tena.

    Katika maelezo yao akapewa jina la ‘Mwarabu wa kuchovya’ kwa sababu hakuna aliyemtambua jina lake.

    Walitarajia pia kumuhoji mke wa Dembele ambaye naye alikuwa mahabusu waweze kutambua kama anajua lolote juu



    ya maasi ya mumewe ama kwa namna moja au nyingine wanashirikiana.



    Majira ya saa mbili usiku yule diwani aliyenunua taarifa juu ya Dembele naye alikuwa mahabusu, kuingia kwake



    mahabusu kukaambatana na taarifa mbaya kupita zote katika riwaya ya CHOKORAA.

    Yule mwanaharakati kijana kabisa, tena wa kike. Alikuwa amejaribu kuupigania uhai wake kwa namna zote lakini



    madaktari bingwa wakakiri kuwa hali si shwari na muda wowote anaweza kuiaga dunia. Ama la Mungu aweke mkono



    wake muujiza utendeke.

    Kila mmoja aliumia kwa namna yake. Frida aliangua kilio.

    Kwikwi ikamshika mama George.

    George akaugulia kiume!!

    Wote wakaomba kwa namna zao. Mwanaidi asipotee kirahisi hivyo katika uso wa dunia.

    Kimya kikatandaaa....



    Makala maalumu ya Kasuku ilifanya vizuri sana katika magazeti mbalimbali.Watu walioisoma walibaki midomo wazi.



    Kwa wote waliomfahamu Dembele walibaki wakijiuliza? Maswali yasiyo na majibu. Hakuna aliyetegemea anaweza



    kuwa bwana mbaya namna ile.

    Lakini ilibaki kuwa hivyo, kila aliyemsoma mwanadada jasiri, yatima na chokoraa aliyewapigania wenzake. Bila kuwa



    na mhimili wa kuegemea na kisha kuishinda vita hii, alitamani kumuona.

    Umri wa Mwanaidi uliwashangaza wengi. Haukuendana na harakati alizokuwa anafanya.

    Harakati zile zilihitaji mtu msomi, mwenye pesa na nguvu kimapambano. Mwanaidi hakuonekana na vyote hivyo.

    Mwanaidi akasubiriwa anyanyuke kutoka kitandani aweze kupewa heshima yake. Lakini hakuamka mapema kama



    wanavyotaka wengi.



    Hadi usiku fulani ambapo Frida alikuwa amelala. Alishtuliwa na ndoto mbaya. Ndoto ya maajabu. Alishtuka na



    kujikuta akiwa anatokwa jasho lakini jasho pekee halikuwa linamtia kero, kuna kitu alikuwa anahisi kinamtokea kwa



    mara ya kwanza katika maisha yake.

    Maumivu !! maumivu makali sana. Frida akajikaza lakini yaliongezeka, akapiga kelele kubwa, kelele ikavuka mipaka



    ikawafikia walengwa waliopewa kazi ya kumtunza.

    Wakafika na kugundua kuwa binti huyu alikuwa ameshikwa na uchungu.

    Upesi zikachukuliwa hatua.

    Baada ya masaa kadhaa Frida alikuwa hoi huku macho yake yaliyolegea yakimtazama mtoto wake. Mtoto asiyekuwa



    na baba.

    Japokuwa alikuwa amechoka sana aliweza kuwasikia manesi wakimpa hongera ya kujifungua mtoto wa kike.

    “Mwana….Mwanaiiiidi.” alijitutumua akakiita kitoto kile jina hilo.

    Kikalipuka kwa kilio cha kitoto.

    Jina kubwa!! Mwanaidi.

    Kisha Frida akapoteza fahamu….



    Kwa sababu Frida alikuwa bado kitandani hata alipozinduka hakupewa taarifa yoyote mpya juu ya maendeleo ya



    Mwanaidi aliyekuwa anapumulia mipira.

    Lakini ndoto yake ya kuota kuwa anajifungua mtoto anayefanana na Mwanaidi huenda ilikuwa sahihi. Alikuwa



    amejifungua Mwanaidi mpya na kumbatiza jina hilohilo.

    Wakati akiota ndoto hiyo tayari simanzi ilikuwa imetanda kwa wale waliomjua ama kutomjua Mwanaidi, yule malaika



    mbaya anayesadikika kuwa na kazi moja tu duniani ya kutoa roho alikuwa ameshikilia msimamo wake, licha ya



    wananchi wengi kumsihi amwache hai walau atazame jinsi jamii ilivyompa heshima kuu…malaika akagoma. Akampa



    dakika ya mwisho kupumua Mwanaidi huku wakati huo huo akimpa ndoto Frida. Ndoto ya kuagana na kumpokea



    Mwanaidi mpya.

    Yule msichana mashuhuri kabisa, mpambanaji wa kweli ambaye hakuwahi kukata tamaa, aliyewajali yatima na



    kuamini kuwa siku moja wataishi kwa umoja na furaha, yule mwanajeshi asiyekuwa na gwanda wala nyota begani.



    Akavuta pumzi kwa usongo wote ndani kisha akazitoa tena kwa nguvu na asiweze kuzivuta tena.

    Madaktari wakatazamana na kukiri kuwa hatimaye jitihada zilikuwa zimegonga mwamba.

    Mwanaidi akatoweka!!!

    Wangeweza kusema amekufa kijasiri, wangeweza kumuita shujaa lakini hii haikupunguza uchungu wa kifo kile.



    Mwanaidi alikuwa amekufa!!!!

    Yule shujaa wa mapambano, asiyeogopa kufa wala asiyehofu kuua, ugonjwa wa pumu ukatwaa uhai wake.

    Alikufa akiwa anapambana, hakuwahi kupumzika kamwe.

    Kwa kifo chake akawaokoa wengi!!



    Frida alipopewa taarifa juu ya umauti uliomkumba Mwanaidi, alifanya tabasamu hafifu kisha akasema.

    “Ili itimie ile ndoto. Ndoto ya Mwanaidi kuishi maisha mapya ya furaha akiwa na mzazi wake ambaye ni mimi. Ni



    muda wa kumtunza aliyenitunza na kuniokoa. Alinipigania muda wote wa maisha yake, rafiki wa kweli asiyekuwa na



    unafiki hata kidogo….rafiki anayetambua thamani halisi ya urafiki.” Maneno yale yaliamsha hisia, George akawa wa



    kwanza kudondosha chozi. Frida akalipuka na kilio kisichozuilika. Alikuwa anamlilia Mwanaidi.

    Kisha Frida akaomba aletewe kile kichanga mbele yake. Hakika kikaletwa. Akakitazama kisha akiwa amelala vile vile



    akaanza kuzungumza.

    “Wewe ni shujaa ambaye hukufaidi utoto wala ujana wako, Mungu aliyekuleta wewe kwangu na kunionyesha njia



    ndiye huyu amekuleta tena kwangu nikuhudumie, uishi kwa raha na amani ukilipata joto la mama ambalo ulilikosa



    hapo awali. Kwa mkono wangu na uhai atakaonipa Mungu nitakupigania kama ulivyonipigania, nitakuweka mbali na



    watu wabaya walisababisha mauti haya. Mwanaidi unaishi katika moyo wangu, utaendelea kuishi milele katika moyo



    huu.” Alimaliza kauli hii na hakufumbua macho yake tena. Akaamua kusinzia.

    Hakuna aliyemsemesha. Kila mmoja alikuwa na uchungu wake, Isha katika wodi aliyokuwa amelazwa kwa uchunguzi



    zaidi baada ya kubakwa na watu wabaya naye alikuwa akisina huku kwikwi nazo zikimwandama. Alikuwa kwenye



    uchungu mkubwa baada ya kupata taarifa za kifo cha Mwanaidi.







    ****



    Makala ya Kasuku ikazidi kupenya anga zote hatimaye kila jicho likaingoja serikali ifanye maamuzi juu ya



    wanaharakati wale vijana tena yatima.



    Bwana Dembele akasomewa mashtaka kadhaa yakiwemo ya kuhusika na vifo vya askari wawili usiku ule jambo



    ambalo Dembele alilikataa kata kata. Lakini sheria ilimbana zaidi hatimaye hukumu ikatolewa.

    Dembele alihukumiwa kifungo cha maisha jela. Mkewe na watoto wake nd’o viumbe pekee waliotokwa na machozi na



    kuumizwa na jambo lile lakini hawakuwa na la kubadilisha hali ile.



    Mali haramu za bwana Dembele zilitaifishwa baada ya kuwa amehukumiwa kumalizia maisha yake yote jela huku



    akisindikizwa na diwani ambaye alivuliwa madaraka kutokana na kuficha siri kubwa kama ile baada ya kuuziwa na



    hayati Mwanaidi kisha kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela, mali zile zikawekwa mnadani. Zilikuwa mali nyingi



    sana. Mauzo yake yakawezesha kujengwa kituo kikubwa cha watoto yatima. Ili kuenzi harakati za mapambano yale ya



    siku nyingi. Kwa heshima ya yule mtoto aliyekufa akipigania watoto kituo kile kikaitwa jina lake ‘MWANA’. Jina hilo



    likisimama badala ya jina la hayati Mwanaidi ambaye alizikwa kwa heshima zote.



    Ilikuwa huzuni wakati wa kukifungua kituo hicho. Hapakuwa na burudani ya muziki wala kelele za kushangilia tukio



    lile. Umati mkubwa sana ulihudhuria ufunguzi ule. George, Isha, Frida, Suzi na mama George wote walivaa nadhifu



    mavazi yaliyofanana huku fulana zao kwa nyuma zikiwa na na jina Mwanaidi Shupavu huku mbele ikipambwa picha



    ya Mwanaidi. Picha ambayo ilitolewa katika kituo cha watoto yatima. Kituo ambacho Frida alitendewa unyama na



    mkuu wa kituo hadi akapata mimba na kisha kuitoa. Alisaidiwa na Mwanaidi kuitoa mimba ile.

    Katika picha ile Mwanaidi alikuwa katika hali ya kulazimisha tabasamu ilhali huzuni ikimtawala zaidi.

    Hatua kwa hatua mkuu wa mkoa akiongoza msafara huu, kuelekea katika mlango wa kuingilia katika kituo kile kipya.

    Binti aliyekuwa amejitanda kichwa chake alikuwa anatembea kwa kusuasua huku pembeni yake akiwepo binti



    mwingine aliyemshika mkono…….

    Hatimaye akasimama alipotakiwa kusimama, pembeni yake akiwepo mkuu wa kituo.

    Akaomba kipaza sauti, akapewa alihitaji kusema neon kwa jamii.

    Kila kinywa kilikuwa kimya. Ni kama mahali pale ulipigwa wimbo wa taifa.

    “Ni siku ambayo laiti kama angekuwa hai…kwa mara ya kwanza angecheza na kurukaruka…..kwa niaba yake popote



    alipo najua anatutazama….Mwanaidi huko ulipo huyu motto mikononi mwangu ni wewe, naamini ni wewe. Naye



    anaitwa Mwanaidi. Kwa upendo usiohesabika, kwa heshima zisizoandikika, nakusihi kifungue kituo hiki. Kwa ajili ya



    kutimiza zile harakati zako za muda mrefu….harakati za ukombozi.”

    Frida alizungumza kwa sauti ya kusihi kisha akakikabidhi kile kitoto kilichokuwa na takribani miezi minne kisu,



    akakisogeza katika ule utepe. Akakisaidia kukaza mkono….utepe ukakatika.

    Makofi, vigelegele vikasikika kwa sauti ya juu sana.,

    Hatimaye kile kitoto cha Frida kilichoitwa Mwanaidi kikacheka kwa furaha.

    “Hakika Mwanaidi anaishi!!!” George na Isha walinong’onezana.

    Sherehe zikaendelea kwa hotuba ya mkuu wa mkoa. Kisha zikamalizika kwa uongozi wa kituo kuchaguliwa….

    George kutokana na kuwa na elimu ya juu sana kupita wote akapewa jukumu la kukiongoza kituo kile.

    George akawa mkuu wa kituo……

    Frida akamkimbilia na kumkumbatia huku akimnon’goneza, “Usiwe kama wale wakuu wengi hakika utalaaniwa



    ukifanya yale.”

    “Sitawaangusha!!” George alijibu kwa sauti hafifu.

    Wakati wawili hawa wakipongezana kuna jicho lilikuwa likiwatazama kwa makini sana. Jicho ambalo lilikuwa na



    mashaka na kitu fulani lakini halikutaka mdomo useme chochote.

    Jicho la ajabu, jicho ambalo halikuwa likipepesa huku na kule.

    Hakuna hata mtu mmoja katika ya wanaomfahamu walioweza kumtambua kwa jinsi alivyokuwa amejiweka.

    Jicho hili halikuishia kuangali hapa tu…..

    Liliendelea zaidi na zaidi kwa umakini….





    ****



    MIAKA ilikatika kituo cha Mwana kikiwa kituo bora na kimbilio sahihi kwa watoto wa mitaani na yatima. Kituo



    kilikuwa na huduma bora sana kimaadili na pia kimarazi.

    George hakuisha kuchukua tunzo kadha wa kadha kutoka kwa washika dau jambo ambalo lilijenga jina lake Tanzania.



    Mzee Emmanuel kutoka gerezani aliamriwaq kutoa maelezo juu ya wapi vyeti vya Georege vinapatikana. Akatii…ile



    elimu ya George ikarejeshwa tena mikononi mwake.

    Alipozipata sifa kwa mara ya kwanza za kuwa mwalimu mzuri wa somo la hisabati katika kituo cha masomo ya ziada



    cha Mchikichini, George alisukumwa na sifa mwishoe akajikuta katika mkondo asioujua na kuangukia dhambini. Sasa



    amekutana na sifa maradufu kuliko za awali, sifa zilizompelekea kuitwa Ikulu akala chakula cha jioni na familia ya



    raisi. Picha zikasambaa magazetini.

    George akaanza kutafutwa. Ni jambo hili lilihofiwa na lile jicho. Yule mtazamaji wa siku ya ufunguzi wa kituo kile



    alijipongeza kwa jicho lake kumpa machale ya uhakika. Akafanya tabasamu japo moyoni alihofia sana uhakika ule,



    kwani aliamini kuwa kijana yule atatafutwa na watu wazuri na wabaya kitu ambacho kitaleta madhara makubwa iwapo



    atadanganyika. Na mbaya zaidi litazuka fukuto.

    Lakin kwa siku ile ni kama vile hakuwa na la kufanya kuzuia hali ile.



    Hakika muonja asali haonji mara moja. Akiwa safari za kikazi nje ya jiji la Dar es salaam George alijikuta majaribuni,



    akashiriki tendo la ngono na msichana kutoka Mwanza. Ile ladha ikaanza kuishi naye na kumtawala…..aliporejea jijini



    Dar es salaam akaanza pupa za awali akiwa chokoraa.

    George Emmanuel. Alikuwa muonja asali, na ladha ya shubiri hakuitambua. Suluba walizopitia wenzake yeye alikuwa



    hajazipitia kwa kiasi kikubwa hivyo. Hakuwa mwanamke akumbuke kubakwa wala kutoa mimba. Alichokumbuka



    zaidi ni kulala bila kula, jambo ambalo husahaulika pindi chakula kinapokuwa kingi tena.

    Starehe alizoendekeza baada ya kuwa amepata pesa za bwana Dembele enzi za uchokoraa akaendelea nazo tena baada



    ya kupata kazi katika kituo kile cha watoto yatima cha MWANA..

    Starehe yake aliyoendekeza zaidi ilikuwa wanawake.

    Ukiyaendekeza mapenzi lazima uupoteze uelekeo, George aliyaendekeza huku akiisaka ile ladha aliyoipata kwa yule



    binti wa kitanga aliyemuingiza katika ulimwengu huu. Na ile ya mrembo kutoka Mwanza,

    Alijisahau kuwa aliwahi kuwa chokoraa, alisahau kila kitu akavimba kichwa kutokana na heshima aliyoipata katika



    jamii.

    Machoni pa watu alijionyesha kuwa yu mwema sana tena mkarimu lakini ndani alificha mengi. Alikuwa zaidi ya



    mchafu.



    Frida na Isha walijaribu kumshauri, aliwasikiliza kwa makini na kuahidi kubadilika lakini kamwe haikuwa hivyo.

    Kila yatima aliyekuja katika kituo cha MWANA ilimradi alikuwa ni mrembo George alifanya juu chini ili aweze



    kushiriki naye mapenzi.

    Yote haya yalifanyika kimyakimya. Bila mtu yeyote kutambua.

    George alitumia pesa!!

    Kweli pesa mwanaharamu.

    George alijisahau kuwa aliyekifungua kituo kile ni Mwanaidi, askari makini bila gwanda mwilini mwake.



    Tabia hii ilizidi kukomaa huku ikiwa siri ya watu wachache tu…siri iliyoendelea kumwacha akiwa na nguvu ya



    kuishawishi jamii yake, nguvu ya kusema neno na kuaminika kwa asilimia zote.

    Tabia hii ingeweza kudumu kwa kipindi kirefu sana tena bila jamii kutambua iwapo tu usingefika usiku huu, usiku wa



    aina yake. Ulikuwa mrefu kuliko giza lolote lile ambalo George amewahi kuliishi.

    USIKU huu George akapata mgeni wa maajabu mgeni ambaye hakuwa na ahadi ya kumtembelea lakini akafika usiku



    mnene….

    Alikuwa na lake jambo…..jambo lililozua mjadala mkubwa kisha kubadilika na kuwa utata….





    *****



    George alijilazimisha kufumbua macho yake kwa ukubwa ambao hajawahi kufumbua ili aweze kubaini iwapo yu



    ndotoni ama la! Lakini aliona hali halisi, ile sura ni kama aliwahi kuiona mahali lakini hakujua yule mtu anaitwa nani.



    Alitaka kumuita lakini sauti haikutoka, na bila kukaribishwa yule mtu ama kiumbe akaketi katika upande mmoja wa



    kiti. Kisha akafanya mfano wa tabasamu….George akaduwaa.

    “Haujambo mheshimiwa!!.” Hatimaye yule mgeni alimsemesha. George akashindwa kujibu akabaki kuduwaa. Mgeni



    wake hakujishughulisha na mshangao uliomkumba bwana George, aliendelea na shughuli zake ambazo kwa utashi



    wake anaamini ndizo zilimleta pale ndani, alifunua huku na kule akiwa anatafuta anachojua yeye mwenyewe hatimaye



    akakipata kipande cha karatasi, akaipata na kalamu. Akaandika maneno fulani katika mweandiko mbovu kabisa kisha



    akampatia George aweze kuangusha saini yake. George akasita, yule mtu akamuangalia kwa macho makali sana.



    Macho yaliyosisitiza amri. George akaweka sahihi. Yule mgeni akatabasamu, kisha akafungua matambala aliyokuwa



    ameyabeba. Akatoa mzigo ambao ulionekana wazi kukusudiwa kuachwa nyumbani kwa George.



    George akaendelea kushangaa lakini safari hii alijikuta akiuliza, “Wewe ni nani na…na unataka nini?” yule mgeni



    akasita alichokuwa anafanya, akamgeukia Georgekwa macho ya utulivu kabisa. Akafanya tabasamu kisha



    akajitambulisha kwa ufasaha.

    Jina geni kabisa masikioni mwa George, alitaka kuuliza zaidi lakini yule mtu alikuwa na mzigo mkononi akamkabidhi



    George.

    George akapokea pasina ubishi. Yule mgeni bila kuaga alifungua mlango akaondoka zake, mara kiza kikatanda baada



    ya George kubaini mzigo aliokuwa ameachiwa. Kiza kilekile ambacho George hakuwahi kukiishi kamwe. Kiza kizito



    tena kilichotanda ukimya wa hali ya juu.

    Simu yake ya mkononi iliita ndipo aliposhtuka, akapapasa kisha akabofya hovyo bila kutambua iwapo alipokea au



    alikuwa ameikata. Akaendelea kuuchapa usingizi, mara ikaanza kuita tena.

    “Aaargh mamtu mengine bwanaa….” Alilalama huku akifanya juhudi za kufumbua macho. Akaoitazama simu



    zilikuwa ni namba za Isha.i Aaaargh usumbufu tena Isha, si tumeshakubaliana kuwa hatuwezi kuwa wapenzi tena au?



    Nishamwambia kabisa dini haziruhusu…hanidai wala simdai. Aah mi sipokei…..alizidi kughafirika George. Simu



    ikakatika.

    Akapiga kite cha ghadhabu, mara ikaanza kuita tena. Akataka kuipokea kwa pupa na kumjibu hovyo Isha, lakini



    akakutana na jina la Suzi.

    “He! Inamaana wanaambizana kunipigia au?” alijiuliza George…..

    Sasa sipokei zote pumbavu kabisa!!! Akasema kwa sauti ya juu. Usingizi ulikuwa umekatika tayari. Akasimama wima



    huku akiwalaani wasichana hao kwa kuukatisha usingizi wake mtamu kupita yote aliyowahi kulala.

    Alipofika sebuleni akakuta ustaarabu ukiwa umevurugwa, alishangaa kidogo na kujilaani kwa kuanza kuwa na tabia ya



    uzembe wa kutopanga chumba chake kama ilivyokuwa zamani. Akajilaumu zaidi kwa kumwajiri yule msichana wa



    kazi.

    “Monicaaaa!!!! Weee mwanahizayaaa!!” aliita kwa ghadhabu. Sauti ya msichana kutoka nje ikaitika kwa ustaarabu….

    Simu yake ikaita tena kutoka chumbani.

    Sasa naenda kutukana mtoto wa mtu haki ya nani!!! Alisema kwa sauti ya juu yenye kutawaliwa na kitetemeshi cha



    hasira.

    Aliifikia simu akiamini kuwa ni aidha Isha ama mwenzake Suzi.

    Wakati anafika chumbani, Monica naye alikuwa amefika sebuleni akishangaa ni kitu gani bosi wake anatafuta hadi



    afanye vurugu kubwa kiasi kile.

    Mpiga simu alikuwa ni Frida wakati huu. Hapa George akatuliza akili na kufikiri mara mbili, akaamini palikuwa na



    tatizo huenda tofauti kabisa na mawazo yake.

    Akaipokea simu ile.

    Frida badala ya kuongea alikuwa analia….kwikwi ilisikika na kuonyesha kuwa yule mtu alikuwa amezidiwa na kilio.

    “Vipi? Amepokea!!! Eeeh!!” ilisikika sauti ya Isha pembeni…..George alizidi kusema ‘halooo’ bila kupata majibu.



    Mara ile simu ikahamia katika sikio jingine.

    “Kaka George kuna tatizo huku, tafadhali njoo tupo hapa chumbani kwa Frida njoo tafadhali….”

    “Tatizo? Tatizo gani?” alihoji.

    Isha kutoka upande wa pili hakuwa tayari kusema tatizo ni nini akamsihi afike.

    George hakukumbuka kusafisha mwili wala kinywa chake, alikwapua suruali yake kutoka katika kiambaza cha



    mlango, akajivika na fulana aliyovaa siku iliyopita….akashika viatu mkononi, akaanza kutimua mbio akimpita Monica



    akiduwaa pale sebuleni bila kumsemesha lolote hadi alipofika nje.

    “We mwanamke wewe yaani unalipwa mshahara halafu naniii….ngoja nikirudi…” aliropokwa haya akiwa nje tayari.

    Akaita taksi na kuamuru apelekwe Kinondoni Studio.

    Upesi gari ikaondolewa, George alikuwa kimya kabisa. Baada ya nusu saa walikuwa eneo alilokuwa anahitaji kufika.



    Akafanya malipo upesi na kuendelea kutimua mbio kuifikia nyumba.

    Hakika palikuwa na tatizo maana hata majirani walikuwa wapo katika mchanganyiko wa majonzi na hamaniko kama si



    mshangao.

    Mungu wangu Mwanaidi!!! George alianza kuweka hisia zake kuwa mtoto wa Frida alikuwa matatani, ama la sivyo



    basi mama yake mzazi alikuwa matatizoni.

    Jibu la kwanza lilikuwa sahihi. Mwanaidi alikuwa matatizoni. Na ingekuwa heri zaidi kama angekuwa matatizoni na



    anaonekana pale ili aweze kupatiwa huduma ya kuliondosha hilo tatizo. Ilishangaza kwamba mtoto Mwanaidi hakuwa



    mahali pale.

    Mwanaidi alikuwa ametoweka katika mazingira ya kutatanisha sana. Alikuwa na miezi sita tu tangu azaliwe siku



    ambayo wajina wake alikuwa anaiaga dunia, sasa haonekani tena kama wajina wake.

    “Nimelala saa sita na nusu, kuna tamthilia nilikuwa naangalia na mama Mwana, wakati huo Mwana alikuwa amesinzia



    tayari…..kwa kweli hadi sasa ni maajabu ninaamka mama Mwana ananiambia eti mtoto hayupo kitandani….” Mama



    mmoja ambaye alikuwa anaishi ujirani mwema na akina Frida alielezea. Mama George naye akadakia, “Na ni mimi



    niliyeenda kumlaza, Mama Mwana alikuwa amejikita katika tamthilia mimi nikamchukua mtoto nikamlaza kisha



    nikaenda kujilalia huko. Yaani mbona kazi?”

    “nilimkuta mwanangu kitandani jamaniii….niliangusha kioo akashtuka na kuanza kulia jamanii….kwa mikono yangu



    nikambeba nikampa titi anyone, aliponyonya akanyamaza tukaanza kucheza na mwanangu jamaniii uuuuuwi…..mamaa



    weeeeee!! Asubuhi naamka naikuta midoli tu uwiiiii mwanangu jamaniiiii nisaidieni mimiii Mwananidi wangu weeee”



    Maneno ya Frida na kilio chake yakaamsha msiba wa ajabu msiba usiokuwa na maiti.

    Mara Frida alipokaribia kunyamaza, vikasikika vilio vingine kutokea njea vilianza taratibu kisha vikazidi kuvuma na



    kufika ndani, walikuwa akina dada wawili. Isha na Suzi. Hawa walikuwa wameenda kutoa taarifa polisi juu ya tukio



    hilo, huko wakaambiwa hakuna taarifa yoyote juu ya mtoto kupotea.

    E bwana ee!! Kuna watu hawanyamazishwi wakifungulia kilio. Isha na Suzi walikuwa wanaongoza.

    Kila aliyejaribu kumtuliza kama asipoambulia tusi zito basi angeweza hata kung’atwa meno.

    Frida naye akaanza kulia, mama George akafunga orodha sasa akimlilia mjukuu wake. Huyu alilia hadi akapoteza



    fahamu.

    Ilikuwa imetimia saa tatu asubuhi.

    George akaaga kuwa anatoka mara moja kuangalia kipi kinaweza kufanyika, aliongozana na Isha ambaye alikuwa



    amejituliza mwenyewe. Wakaingia ndani ya taksi. Safari ya kuelekea nyumbani kwa George.

    George alipokumbuka juu ya wapi wanaelekea akakumbuka juu ya mpangilio mbovu aliouacha pale sebuleni.



    Alijiuliza iwapo Monica atakuwa ameuweka sawa ama la anaenda kuabika na wageni wake….

    Kuukumbuka mpangilio ule mara George akakumbuka kuwa usiku uliopita ni yeye alikuwa wa mwisho kukaa pale



    sebuleni pakiwa katika mpangilio mzuri kabisa. Lakini akakumbuka kuwa kuna muda alirejea tena pale na kuna jambo



    alikuwa anafanya na akamwona yule mtu aliyevuruga sebule yake, hakuwa Monica alikuwa ni kiumbe mwingine



    kabisa. Tena alijitambulisha jina, na kuna jambo la ziada alifanya..kuna mzigo alimpa naye akaupokea…..

    Ni kama kiumbe hai ….alipewa kiumbe hai. Akajaribu kuikumbuka sura yake lakini likatokea giza, hakika giza



    lilitokea hata kabla hajatabua sura ya kiumbe kile….

    “Mungu wangu weeee!!” George alipayuka ghafla. Isha akamtazama kwa masikitiko bila kusema lolote.

    George alitangulia mbele na Isha akafuata, wakaingia sebuleni. Monica alikuwa ameiweka sawa sebule na



    haikuonyesha dalili yoyote ya kashkash! Isha akaanza kuona mwenzake anakaribia kupandwa na wazimu, alimwona



    George akiishangaa sebule yake mwewnyewe.

    “Ehee alikuwa hapa hivi amesimama.”

    “Nani tena?” Isha aliuliza ndipo George akagutuka kumbe mambo aliyokuwa anayawaza kichwani aliyasema kwa



    sauti.

    “Aaah hapana basi tu kwani….nani…karibu Isha.” Alijiumauma.

    “Upo sawa G.” Isha aliuliza kwa sauti ya kinyonge.

    “Aaah mimi?” aliuliza swali la kipumbavu bila kutarajia.

    Isha akamtazama bila kusema lolote. George akasimama na kuingia ndani chumbani mwake …Isha akamsindikiza kwa



    macho.

    Macho yaliyomsanifu kijana yule kama kwamba anaukaribisha uchizi kichwani mwake bila kujua.

    “Unadhani nina tatizo basi mimi…hamna basi tu ujue…yaani..” alitokwa na maneno hayo wakati anaingia chumbani



    huku akirusha mikono huku na kule na tabasamu la kujilazimisha midomoni.

    Isha hakutia neno akabaki kumtazama tu. Hadi alipotokomea kabisa.

    Kimya kilitanda kwa sekunde kadhaa Isha akiwa anatafakari jambo lilitokea alfajiri ya siku hiyo kama mkosi ambao



    unawafuata kwa nyuma.

    Mtoto mwenye umri wa miaka mitatu kutoweka katika mazingira ya kutatanisha tena akiwa mikononi mwa mama



    yake. Ilistaajabisha hakika.

    Mara mawazo yake yalikoma baada ya kusikia purukushani ikitokea katika chumba cha George, ni kama alikuwa



    akipambana na mdudu ama chochote kile ambacho kilikuwa chumbani mwake kimakosa. Isha aliendelea kuzisikiliza



    zile purukushani za uhakika, mara kianguke hiki mara kianguke kile.

    “We ni nani..unataka nini hapa eeh….Sikujui toka…” sauti ya George iliyokuwa inasota ilisikika ikihangaika. Isha



    akastaajabu, akavamiwa na hisia kuwa George alikuwa ameanza kuishi katika uchizi rasmi. Alifanya tabasamu la



    karaha kisha akajisemea ‘mzimu wa majanga unaandamana nasi bado’.

    Neno lake la mwisho ‘bado’ liliambatana na kishindo kikubwa baada ya yowe kubwa kutoka chumbani kwa George.



    Hapa sasa hakuendelea kukaa. Akasimama wima akakimbilia chumbani kwa George.

    Macho yake yakakutana na mwili wa George ukitiririkwa jasho chumba kikiwa katika hali ya utulivu sana lakini



    kilichovurugika sana.

    George alikuwa hajitambui

    Isha akapagawa, hakuamini kilichokuwa kinatokea mbele yake, ulikuwa muendelezo wa ile filamu ya alfajiri ya



    kutoweka mtoto wa Frida katika mazingira tatanishi na sasa ilikuwa zamu ya George kupoteza fahamu katika



    mazingira ya kutatanisha vilevile.

    Upesi akaitwaa simu yake akampigia Suzi. Simu ikapokelewa akamwomba afanye upesi akiongoza na wanaume



    kadhaa wafike nyumbani kwa George.

    “Vipi Mwanaidi ameonekana?” Suzi aliuliza kwa kihoro.

    Isha akamsisitiza afike upesi.



    ****



    George alikurupuka kutoka katika usingizi mzito uliozigandamiza fahamu zake na kujikuta akiwa katika kitanda cha



    hospitali ya Mazengo katikati ya jiji.

    Alijitazama huku na kule na kujikuta amezungukwa na watu kadhaa. Pole mfululizo zikafuata baada ya kujitambua.

    “George ni nani ulikuwa unajibizana naye ndani.” Isha alimuuliza wakiwa wamekaa.

    “Mimi? Mimi nikajibizana na mtu.” George aliuliza huku akijielekezea kidole kifuani kwake. “Sijazungumza na mtu



    hata mmoja wala.” Alimalizia sentensi ile.

    “Niliwaambia jamani….” Isha aliwatazama Suzi na wale vijana wengine ambao aliwaambia kuwa ana mashaka



    kupotea kwa mtoto Mwanaidi kunaelekea kumpa wazimu George. Suzi akainama chini na kufanya ishara ya msalaba



    kuombea lisitokee hilo linalodhaniwa na Isha.

    Ilikuwa tafrani hakika.



    Wakati haya yakiendelea huku hospitali kuna jicho lilikuwa likiyatazama yote haya huku uso wake ukitabasamu kwa



    matumaini makubwa sana. Alikuwa analifanikisha lengo lake taratibu lakini kwa umakini mkubwa sana….hakuna



    aliyejua kuwa kuna jicho linawatazama kutokea katika kona moja ya kile chumba.



    George alikuwa mtulivu sana, akitafakari juu ya tukio lililotokea chumbani kwake. Alitamani sana kuwashirikisha



    watu waliomzunguka lakini akayakumbuka masharti yaliyotajwa na mtu yule wa ajabu…..kingine kilichomtia uzito



    katika jambo hili ni ile hali ya kukumbuka kuwa kile kitu alichokabidhiwa katika ile hali aliyodhani kuwa ni ndoto



    sasa alitambua fika kuwa alikabidhiwa mtoto mdogo ambaye alikuwa anamjua kwa sura na historia pia.

    Lakini hakulitambua jina lake kwa wakati ule.



    George angeweza kuelezea juu ya ndoto hiyo lakini nani angeamini kama asingetimiza masharti aliyopewa na yule mtu



    wa ajabu ambaye hisia zake zinakiri kuwa hapo kabla aliwahi kumuona. Alipomuona ni wapi? Hilo lilikuwa swali



    gumu zaidi.

    Kichwa kikawaka moto zaidi ya kawaida. Huu ulikuwa mtihani mkubwa sana kuupata maishani. Yale maneno ya



    mwisho ya yule kiumbe ndo yalimfadhaisha zaidi, kuna jambo zito alitakiwa kuliweka bayana mbele ya jamii. Jambo



    ambalo George alitaka libaki siri milele.

    Lakini kama angesimamia msimamo wake basi kuna shauri jingine ambalo lilikuwa zito zaidi na iwapo lisipotimizwa



    basi kinazuka kizaazaa kisichokuwa na mfanowe.

    Ni heri yale maisha ya uchokoraa ya kulala katika vichochoro bila kupata chakula. Ni heri kukimbizana na mgambo wa



    jiji kuliko kukumbana na kizaazaa. Na ilikuwa heri zaidi kuishi jela miaka yote kuliko kuishi katika dunia huru



    inayotawaliwa na kizaazaa.

    Kizaazaa kinazuliwa na George bila chokoraa wale kufahamu, lakini kinasambaa na kuwakumba wote, lakini wakati



    huu anaongezeka mtu mwingine matata kabisa anayeondoka kwa jina la Suleiman Meja.



    ****

    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog