Simulizi : Chozi La Mwisho
Sehemu Ya Tano (5)
majaliwa ya Mungu. Mwenye uwezo katika familia yangu nilikuwa mimi peke yangu na ndiye niliye kuwa tegemeo lao.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Si kwa mke wangu na mwanagu tu hata wazazi wangu nilijua nao watateseka. Hawakuwa na nguvu tena za kutafuta na tegemeo lao lilikuwa kwangu.Katika familia yetu tulikuwa wengi zaidi ya watano mimi nikiwa wa nne kuzaliwa, lakini wote ndugu zangu wanaishi maisha ya kubahatisha.
Labda dada yangu ambaye kidogo mumewe alikuwa na uwezo kiasi, lakini na yeye alikuwa na familia kubwa inayokuwa ikimtegemea.
Kwa hiyo msaada wa dada ulikuwa mdogo sana kwenye familia, wengine walio bakia kazi zao zilikuwa mama lishe wenye mtaji wa kuuza kilo mbili, si kwamba dada yangu simjali pesa, zake nyingi anazimalizia kwenye mapambo kama hereni, cheni na pete za dhahabu mwisho wake anakula mpaka mtaji.
Nilikuwa nimeisha msaidia mtaji zaidi ya mara tano lakini alikuwa habebeki. Kibaya zaidi kila sherehe alikuwa hakosi yupo radhi kulaza biashara kwa ajili ya sherehe. Mwingine ni kaka yangu yeye kazi zake akipata mia tano inatosha anakwenda kwenye vibanda vya pombe za kienyeji maisha yake hayana nyuma wala mbele.
Nina imani umeona mzigo uliokuwa unanikabili, kama nitahukumiwa kunyongwa au kufungwa maisha nani atakaye itunza familia yanguna wazazi
wangu, kila nikifikia hapo hujikuta nikibubujikwa machozi. Nikiwa nimeegemea ukuta wa gereza nilisilia sauti ikiniita.
"Anderson," mara ya kwanza sikusikia mpaka aliporudia mara tatu.
"Naam nipo hapa."
"Kuna mgeni wako," askari magereza alinieleza.
Nilijinyanyua toka pale chini nilipokuwa nimekaa na kumfuata askari magereza. Alinipeleka mpaka sehemu ya wageni na kunitambulisha kwa msichana mtanashati aliye kuwa amevalia suti yake ya bluu na ndani alivalia shati jeupe.
"Huyu ndio mgeni wako?"
"Eeh! Ndiyo," alijibu yule msichana mrembo ambaye alikuwa mgeni machoni mwangu nilijikuta nikijiuliza ni nani huyu ambaye kila nikijaribu kurudisha kumbukumbu nilitoka patupu.
"Habari yako shemeji?"
"Nzuri tu."
"Pole na matatizo."
"Asante...sijui mwenzagu wewe ni nani?" Nilimuuliza.
"Mimi naitwa Mihayo," mmh! Jina lilikuwa geni kwangu nilijiuliza ananiita shemeji kwa minajili gani, nikiwa sijapata jibu aliendelea kujitambulisha.
"Nina
imani hunijui."
"Ni kweli."
"Mimi na mkeo Minza tumecheza pamoja na tumesoma shule moja, nilimuacha Minza kwa madarasa manne lakini tulikuwa tunakaa jirani...Hata siku ya harusi yenu nilikuwepo lakini hatukuwahi kutambulishana kutokana na mimi kuwahi kuondoka.
"Hata kwako nimeisha wahi kufika wakati mkeo alipojifungu vile vile hatubahatika kuonana…. Shemeji ni hivi majuzi nimepata simu kutoka kwa mkeo kuwa una matatizo ambayo yanahitaji msaada utaoambatana na pesa.
"Nilimueleza kuwa japo huu ni mwaka wangu wa mwisho kuchukua sheria nilisema nitajaribu kukusaidia bila malipo yoyote. Hata kama itakuwa nzito wapo wa juu yangu nina imani tutajitahidi kuhakikisha tunakusaidia."
"Siakuelewa wewe ni nani?" Nilimsikia lakini sikumuelewa.
"Mimi shemeji ni Mwanasheria ninaye somea shahada ya sheria chuo
kikuu na huu ni mwaka wangu wa mwisho."CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kauli ile ilinirudishia matumaini nusu japo nilijua kazi ni nzito, lakini kama itafuatwa haki sina kesi ya mauaji.
"Sasa shemeji utanisaidiaje?"
"Kwanza naomba unipe ukweli ili tujue tutakusaidia vipi maana mkeo amenipa kauli mbili, sijui ipi ya kweli."
Nilimuelezea yote bila kuacha hata moja kwa kujua wakili ili aweze kukusaidia usimfiche neno. Baada ya kunisikiliza aliniuliza swali:
"Shemu naomba urudie uliyonieleza.
Nilirudia kama nilivyomueleza mwanzo bila kupunguza wala kuzidisha neno.
"Hukumpiga?"
"Shemeji hata kumsukuma labda kitandani aliponilazimisha kutenda uchafu. Lakini sidhani kama kufanya mapenzi kunaweza kumtoa uhai mtu tena ndiyo tulikuwa tunaanza tendo."
"Mbona nasikia umeanza naye mapenzi kitambo na kufikia kumpa mimba na alipo kujulisha ana ujauzito wako ulimlazisha kuutoa na alipokataa ndipo ulipompiga mpaka alipopoteza uhai, kuna ukweli juu ya hilo?"
"Shemeji kama vipimo vya hospitali vinasema kweli wamchunguze waone kama kuna sehemu nimempiga, suala la mimba kwa kweli silijui kama alikuwa nayo ni ya mumewe au kama ni tabia yake kulazisha mapenzi ya mtu mwingine siyo mimi."
"Basi shemeji nimekuelewa ila nakuomba jambo moja unapotoa maelezo yako suala la kusema tatizo lilitokea wakati mkianza mapenzi ndipo tumbo lilipo mshtuka linaweza kukutia matatizoni. Hata kama usipokutwa na kesi ya mauaji nina imani huna kesi ya mauaji nitafuatilia vipimo kama ni kweli.
"Unapotoa maelezo yako sema alipogonga na kufungulia mlango hata kabla hajasema shida yake alianza kusema tumbo linamuuma ndipo ulipo kimbilia dawa na uliporudi ulimkuta amefariki...nina imani tumeelewana."
"Sawa shemeji nitafuata maelekezo yako..nakutegemea shemeji uhai wangu na familia yangu upo mikononi mwenu."
"Tutajitahidi kwa uwezo wa Mungu utatoka salama."
Shemeji yangu aliye jitambulisha kwa jina la Mihayo aliondoka na kuniacha na mawazo mengi na kuona mke wangu pamoja na hasira zake bado ananithamini kwa kumwita rafiki yake toka chuoni Dar mpaka Mwanza tena kaja kwa ndege.
Kweli ukiwa na mtu wa kukusimamia kesi yako inasikilizwa upesi. Kesi yangu ilianza kusikilizwa mara moja. Mimi nikiwa mshtakiwa ninaye simamiwa na wakili Mihayo rafiki wa Minza mke wangu.
Nilipotaka nijieleze mahakama ilikuwaje, nilielezea mwanzo hadi mwisho hapo ndipo wakili wa serikali aliponihoji maswali:
"Ndugu Anderson umeiambia mahakama kuhusiana na kifo cha marehemu Sabina mke wa jirani yako, nikisema ni uongo kutokana na maelezo yako utasemaje?"
"Nitasema si kweli yote niliyoyaongea ni kweli tupu."
"Unamfahamu marehemu?"
"Ndiyo."
"Una mfahamu vipi?"
"Kama jirani yangu."
"Nikiieleza mahakama unamfaham zaidi ya ujirani nitakuwa ninasema uongo."
"Ndiyo muheshimiwa."
"Unataka kuieleza mahakama ile mimba kwa nini uliitaka aitoe?"
"Mimba gani hiyo?"
"Unaniuliza mimi tena badala ya kujibu."
"Muheshimiwa mimba hiyo siijui."
"Lakini bwana Anderson nina imani unajua ni kosa kufanya mapenzi
na mke wa mtu?"
"Ndiyo najua."CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kwa nini ulikubali kufanya mapenzi na mke wa jirani yako."
"Sikuwahi kufanya naye hata mara moja."
"Nikiiambia mahakama kuwa wewe ulipanga kumuondoa mke wako ili ufanye uchafu wako nitakuwa nasema uongo?"
"Ndiyo."
"Unajua kuua ni dhambi?"
"Ndiyo."
"Baada ya kufanya dhambi ya kuzini hukuona inatosha umeongezea ya kuua na kuamua kumzika kabisa."
"Sikuzini naye wala sikumuua kama amechukuliwa vipimo nina imani ni ushahidi tosha."
"Kama hukumuua kwa nini ulimzika na usitoe taarifa polisi?"
Jibu lilikuwa mbali nilibakia kimya ndipo wakili wa serekali
aliposema:
"Sina ziada muheshimiwa hakimu," aliinama na kugeuka, mahaka
yote ilikuwa kimya ilikuwa imejaa mpaka pomoni wengi walikuja
kushudia nitakapo hukumiwa kunyongwa.
Wakili anaye nitetea Mihayo alisimama na kuja mbele yangu akiwa na kalatasi mkononi.
“Mr Anderson,” aliniita.
“Naam,” niliitikia.
"Mr Anderson umesema ulikuwa unamfahamu marehemu kama jirani yako, je, alikuwa na mazoea ya kuja ndani wakati mkeo akiwepo?"
"Ndiyo, mara nyingi na alikuwa rafiki wa mke wangu."
"Unasema alikulazimisha mapenzi je, ni mara ya ngapi kufanya vile?"
"Kwa kweli siku ile ya tukio ndiyo mara yake ya kwanza."
"Hebu ieleze mahakama ilijisikiaje alipokutamkia kuwa anakutaka kimapenzi?"
"Kwa kweli nilishtuka sana hasa tukizingatia ni mtu tuliyekuwa tunaheshimiana sana."
“Mr Anderson,” alilitaja jina langu.
“Naam.”
"Ulimjibu nini?"
"Sipo tayari kufanya uchafu ule."
"Nini kilichoendelea?"
"Alinisogelea ili anivamie nilirudi nyuma hapo ndipo nilipomuona
akijishika tumbo na kuomba msaada huku akisema, mama nakufa."
"Nikisema wakati anakuvamia ulimsukuma nitakuwa nasema uongo?"
"Ndiyo muheshimiwa."
"Ni nini kitachotuthibitishia hukumuua bali amekufa kwa ugonjwa?"
"Nina imani kama alichukuliwa vipimo ndivyo vitakavyo toa ukweli."
"Je nikitoa ushahidi wa vipimo utakuwa tayari kuupokea?"
"Ndiyo muheshimiwa."
Wakili Mihayo alimgeukia mheshimiwa hakimu na kusema:
"Muheshimiwa huu ndiyo ushahidi ya kitaalamu uliopatikana hospitali ya rufaa unaoelezea sababu ya kifo cha Sabina naomba uupokee."
Alimpa hakimu bahasha ambayo alisema ndiyo ilikuwa na ushahidi wa kitaalamu kama alivyosema wakili wangu na kuzipokea. Baada ya kumpa alisema:
"Muheshimiwa hakimu sina la zaidi,” Wakili Mihayo alirudi kukaa na kumuacha hakimu akipitia zile kalatasi baada ya kuzisoma aliahirisha mahakama wa wiki mbili ndipo hukumu itakapo tolewa.
Nilirudishwa mahabusu huku nikimuona mke wangu Minza akilia kitu kilichozidi kunipa machungu moyoni. Hali ya mke wangu ilikuwa inasikitisha nilimuona wakili Mihayo akimbembeleza mke wangu wakati huo nilikuwa napandishwa kwenye kalandinga tayari kurudishwa Butimba gerezani kusuburi
siku ya hukumu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mke wangu hakuchoka kuja kunipa moyo kutokana na maneno aliyopewa na shoga yake wakili Mihayo kutokana na vipimo kuonyesha marehemu amekufa kwa shinikizo la damu na mwili wake haukukutwa na jeraha lolote vilevile hata zile habari kuwa alikuwa na mimba zilionyesha ni uongo baada ya vipimo kuonyesha hakuwa na ujauzito wowote.
Kidogo mke wangu alianza kurudhisha imani kwangu kutokana na maelezo ya shoga yake na ushahidi niliotoa mahakamani. Mke wangu aliniahidi kuniendelea kuniombea dua kuhakikisha natoka salama katika janga lile.

***
Baada
ya wiki mbili siku iliwadia ya kujua mbivu na mbichi siku ya kusomewa hukumu
iliwadia siku ambayo mahakama alijaa mpaka barabarani. Wapo walionionea huruma
pia walikuwepo waliosubiri kusherehekea kifungo au kunyongwa
kwangu.
Miongoni mwa wabaya zangu alikuwepo mzee Masanyiwa na aliye kuwa rafiki yangu kipenzi Mathayo mume wa marehemu Sabina ambaye baada ya tukio lile aligeuka kuwa adui yangu mkubwa. Aliyeapa hata nikifungwa atahakikisha ananipoteza kupitia njia za miti shamba.
Mahakama yote ilikuwa kimya ikimsubiri muheshimiwa hakimu atoe hukumu. Baada ya kupitia vitu muhimu, Hakimu Maisha Kimburu alikohoa ili kuweka sauti katika hali nzuri kisha alisema:
"Natumaini wote mu wazima kama siku zote zilizopita, leo ndiyo siku ya kutoa hukumu ya kifo cha bi Sabina kilichomuhusisha bwana Anderson. Baada kupitia nyaraka zote za pande mbili za upande wa mashitaka na upande wa utetezi.
“Mahakama nimeridhika na maelezo ya pande zote mbili kwa upande wa mashtaka umemtia hatiani mtuhumiwa kwa kumpiga marehemu na kusababisha kifo na baada ya kumuua mshitakiwa alitaka kumzika
kwa siri na kwa bahati nzuri jirani yake aliyemuona akichimba usiku na kushindwa kujua mlalamikiwa anataka kufukia nini usiku wa manane.
”Kutokana na mgogoro wa kiwanja alijua wazi kuwa jirani yake anataka kumroga japo serikali haitambui mambo ya uchawi. Kutokana na wasiwasi wake ilisababisha awataarifu polisi ambao walimuwahi kabla hajafukia kitu ndipo walipogundua alikuwa anataka kuzika mwili wa mtu ambaye alitambulika kama mke wa jirani yake bwana Mathayo.
“Hapo ndipo alipokamatwa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji. Upande wa pili wa utetezi ulisikiliza maneno ya mtuhumiwa kuwa marehemu hakumpiga wala hakuwahi kufanya naye mapenzi kama taarifa zingine zilizosema kuwa mtuhumiwa alikuwa na mahusiano ya muda mrefu na marehemu iliyosababisha kumpa ujauzito.
“Upande wa mashahidi ulisema walishuhudia kwa masikio yao mtuhumiwa akimlazimisha marehemu autoe ujauzitoa, ubishani ulisababisha mtuhumiwa kumpiga marehemu na kumsababishia maumivu yaliyopelekea umauti.
Upande wa utetezi ulimsikiliza mtuhumiwa na kukanusha yote kwa kusema kuwa hakuwahi kufanya mapenzi wala kuwa na mahusiano yoyote na marehemu na kuomba ushahidi wa kitaalamu utumike kuchunguza kifo cha marehemu na kutoa hukumu ya kweli.
Upande wa utetezi ulifuatilia vipimo alivyo chukuliwa marehemu baada ya kufikishwa hospitali ambavyo vilisomeka kama hivi:
Marehemu Sabina aliyefariki siku ya jumapili saa tano na dakika arobaini na tano usiku siku ya tarehe 22 mwezi wa pili mwaka. Vipimo vya dakitari vilivyotibitishwa na madaktari bingwa watano vinasomeka kama hivi:
Marehemu Sabina hakuuawa kama taarifa za awali zinavyosema bali marehemu amekutwa na tatizo la ugonjwa wa moyo yaani shinikizo la damu. Pia hakuwa na ujauzito wowote kutokana na maelezo ya upande wa utetezi. Vile vile vipimo zaidi vimeonyesha kuwa marehemu hakuwa majeraha yoyote mwilini mwake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mahakama imeridhika na ushahidi wa utetezi ila unatoa onyo kali kwa mtuhumiwa kuwa kitendo cha kinyama cha kutaka kumzika marehemu kwa siri kisirudiwe tena. Kutokana na maelezo yote ya pande mbili Mahakama imeridhika na maelezo upande ushahidi na kumuona mtuhumiwa hana kosa hivyo Mahakama inamuachia huru mtuhumiwa Anderson."
Sikuamini masikio yangu mke wangu alifurahi mpaka machozi yakamtoka nilipiga magoti kumshukuru Mungu kwa kuuona ukweli. Wapo waliofurahi kuachiwa kwangu lakini wabaya wangu walibakia midomo wazi.
Nilitoka kizimbani nikiwa nabubujikwa machozi kwa furaha kilipanua mikono niilaki familia yangu pamoja na wakili wangu aliyepigania haki yangu Mihayo. Nikiwa nawakaribia huku nikiwa nimechanua mikono machozi yakinibubujika kama maji yanayo toka juu ya chemchem inayotililika mlimani kwenda chini na
kutengeneza vijito na mabwawa ambayo huwa kiburudisho kwa viumbe hai na mimea.
Nilipoikaribia familia yangu nilisikia sauti ya mtu akipayuka toka katikati ya watu akisema:
"Sikubari ...haiwezekani....haiwezekani," alitokea katikati ya watu, alikuwa mume wa marehemu Sabina akiwa ameshikilia bastora mkononi kila mmoja alilala chini kwa uoga mimi nilikuwa bado nimepigwa na butwaa. Mathayo alisema huku jasho likimtoka na macho ameyatoa pima akiwa amenielekezea mdomo wa bastora kifuani.
"Haiwezekani umuue mke wangu uachiwe hivi hivi, kama Mahakama imeshindwa kukuhukumu ninakuhukumu kwa mkono wangu."
"Tafadhari Mathayo usiniue mimi siyo niliye...." sikumaliza
Sikumalizia kujitetea risasi mfurulizo zilitua kifuani na zingine tumboni
zilizonirusha kwa nyuma. Baada ya kunipiga risasi alikimbilia nje wakati huo wote walikuwa wamelala chini kwa woga.
Baada ya kuanguka chini nilishuhudia matumbo yangu yakiwa nje. Pale nilipokuwa nimeangukia palitapakaa damu na kuniweka kwenye dimbwi la damu. Macho yakiwa na nuru hafifu yaliweza kumuona mke wangu akiangua kilio huku akija kuukumbatia mwili wangu uliokuwa umetapakaa damu na kuharibiwa vibaya na risasi.
Nilimuona wakili Mihayo naye akilia akimtoa Minza kwenye dimbwi la damu niliyokuwa nimelilalia. Walipokuwa wakimtoa kwenye mwili wangu ambao taratibu ulikuwa ukupoteza uwezo wa kuendelea kuishi. Nilishangazwa na machozi ya mke wangu alipokuwa akilia yalinidondokea juu ya paji la uso yalikuwa ya baridi sana tofauti na machozi mengi huwa ya moto.
Mmh! nilishtuka kwenye usingizi mzito na kuanza kuhema huku nikitetemeka na kujiuliza ndoto ile ina maana gani. Ilikuwa kweli jana nilimsindikiza mke wangu ambaye alikwenda kumuona mama yake aliyekuwa anaumwa lakini si kwa kupigiwa simu bali taarifa zilikuja wiki moja.
Wakati huo nje mvua nje ilikuwa ikiendelea kunyesha, kumbe sehemu niliyokuwa nimelala kulikuwa kunavunja na matone ya maji yalikuwa yakinipiga kwenye paji la uso na kuona ni machozi ya mke wangu yaliyokuwa ya baridi.
Baada ya kugundua machozi ya baridi yaliwa matone ya mvua ambayo ilikuwa ndiyo ikikatika, nilijikuta nikicheka mwenyewe. Machozi ya baridi ilikuwa matone ya mvua lakini maana nzima ya ndoto ilikuwa ikimaanisha nini. Nikiwa katikati ya mawazo nilishtushwa na sauti iliyokuwa ukigongwa mlango. Nilijinyanyua kitandani na kutoka hadi sebuleni na kwenda moja kwa moja kufungua mlango. Baada ya kufungua aligeuka na kurudi kwenye makochi
"Karibu"nilisema bila kugeuka.
"Za asubuhi jirani," sauti ile ilinishtua na kugeuka kuangalia.
Ha! alikuwa ni yule mke wa jirani yangu niliyemuota usiku tena akiwa kwenye vazi moja la kanga. Nilijikuta na patwa na mshtuko na kuanguka chini kilichoendelea sikujua. Niliposhtuka nilijikuta hospital nikiwa nimetundikiwa drip.
Nilirudisha mawazo nyuma kutaka kujua nini kilichonisibu baada ya jana kulala salama usalimini. Baada ya muda kumbukumbu zilijirudia na kukumbuka ndoto ya kutisha na tukio lililonitokea asubuhi. Nilijiuliza ndoto na vitu vyote vina maana gani.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

MWISHO
0 comments:
Post a Comment