Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

SHIDA - 1

 





    IMEANDIKWA NA :  GADYSON BAITA



    ********************************************************************************



    Simulizi : Shida

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Shida alikuwa na furaha isiyo na kipimo,Baada ya shida nyingi kama jina lake alizopitia katika maisha yake ya kawaida na kimapenzi hatimaye sasa alikuwa anakalibia kwenye pumziko kuu na la milele

    "Ndoa.....ndoa.... Hatimaye Mungu hamtupi mja wake,kesho na mimi naolewa jaman! Rafiki zangu hatimaye naolewa" aliwaambia rafiki zake usiku huu wakiwa chumbani kwake akiwa anajiandaa na sherehe yake ya kuolewa na kijana Kolumba kesho yake..CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya mapenzi ya muda wa miezi saba kati yao,huku Kolumba akimuonesha mapenzi ya dhati, akimpa chochote alichohitaji ili kuikamilisha furaha ya msichana huyu aliyepitia shida nyingi sana katika maisha yake.

    "I was always crying, why me? But now there is somebody to weap my tears"nimekuwa nikilia kila marakwamba kwa nini mimi?? Ila sasa yupo wa kuyafuta machozi yangu" alendelea kuwaambia rafiki zake

    "Usijali best, amini Mungu amesikia kilio chako cha muda mrefu na sasa unaenda kupata faraja maishani, tunakutaman mwenzetu, sisi hatujui kama tutaolewa" akasema Amina mpambe wake mkuu katika harusi hii.

    "Usijali Amina utaolewa, wewe umetoka familia bora tofauti na sie kapuku na wewe ni mzuri sana,utaolewa tena na mdosi balaa" akasema shida.

    "I wish siku moja na mimi itanitokea, by the way matroni alisemaje juu ya ile shela? Itapunguzwa?"akauliza Amina

    "Hivi sijakwambia best? Mbona ishapunguzwa na nimejaribu imefiti balaa, nakwambia kesho! Ntaringaje? Ndani ya shela na Mr ndani ya suti, we subiri" akaendelea Shida

    Laiti binadamu tungepewa macho ya kujua yatakayojili mbele yetu,nafikiri Shida angelia usiku kucha akiombolezea maisha yake



    Kolumba kijana mdogo anayemiliki kampuni ya kusambaza sola vijijini ila makao makuu ya kampuni yakiwa Dar, alimpenda Shida siku aliyomwona akiwa kaenda kuomba kazi ofisini kwake, hakuwa na papara, alimwajiri na katika ufanyaji wa kazi ndipo wakaangukia katika penzi hili tamu ambalo hitimisho lake lilikuwa kesho asubuhi kanisani Njiro huko mkoani Arusha.





    Asubuhi ya siku ilofuata





    Maandalizi ya ndoa hii yalikuwa moto moto,kila aliyehusika kwa namna moja au nyingine alikuwa busy kuhakikisha kitengo anachosimamia kinakaa sawa kabla harusi haijakamilika



    Shida akiwa na mpambe wake walifuatwa na gari maalumu na kupelekwa saloon , huko wakapambwa na kupambika haswaaa.

    Shida alipendeza sana, ule uzuri wake wa asili akachanganya na madoido kidogo, hakika alionekana mrembo sana hasa katika siku hii muhimu sana kwake

    Walitoka saloon saa mbili ikielekea saa tatu na moja kwa moja wakarudi nyumbani

    Shida hakutaka kitu zaidi ya maji ya kunywa kwa kuogopa kuchafua tumbo

    "Best, nimetoka ukumbini muda si mrefu, pamependeza balaa, yaani nimetamani harusi ingekuwa yangu" aliongea Rose, rafiki mwingine wa Shida

    "Kweli eee?" akauliza Shida.

    "Nakwambia! Dah! Kuna watu wanapamba, wee acha tu" akajibu.

    "Natamani mama yangu angekuwepo leo hii kushuhudia tukio hili muhimu kabisa katika maisha yangu" aliongea shida huku machozi yakianza kumtoka

    Ikabid rafiki zake waanze kumbembeleza.





    Kanisani saa 11.00 asubuhi





    Baada ya watu wote kuingia kanisani na kuketi, mchungaji Jafari aliingia katika madhabahu na kuanza zoezi hili muhimu la kufungisha ndoa hii.

    "Wakati mliokuwa mkiusubiri sasa umefika, nawaomba maharusi na wazazi wao waje hapa mbele" akaongea Mchungaji.

    Kanisa zima likalindima vigelegele. Wakasogea mpaka pale mbele na mchungaji akaanza taratibu zote zinazohusika na ufungishaji wa ndoa.

    Baada ya kuapa kikafika kipindi ambacho Kolumba alikuwa akikiogopa kuliko vyote

    Kipindi cha kuulizia kama kuna pingamizi.

    "Kabla sijaifungisha ndoa hii rasmi, kuna yeyote mwenye pingamizi?" akauliza mchingaji.

    Kanisa lote kimya,akarudia mara ya pili kimya!

    "Mara ya tatu na ya mwisho na mkumbuke mkikaa kimya basi mkae kimya milele, je; Kuna yeyote mwenye pingamizi?" aliuliza mara ya tatu mchungaji.

    Mara ghafla nyuma ya kanisa akasimama mdada wa saizi kiasi cha kukadilia umri wa miaka thelathini na ushee,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nina pingamizi mchungaji" akasema

    Kolumba akatetemeka mpaka nikashangaa!!

    Yule dada alipoanza kuondoka kuja mbele nyuma yake wakafata watoto wawili wadogo,

    Wakatokea poa mzee na mkewe na wakaanza kuongozana kuja mbele na walipofika

    "Nina pingamizi mchungaji, huyu kolumba ni mme wangu halali na cheti cha ndoa ninacho, amenitoroka na kuja kufungia ndoa huku Arusha na kimada wake, hawa unaowaona hapa ni wazazi wake halisi na sio hao, lakini kinachoniumiza ni kuwa mimi na Kolumba ni waathirika, badala ya mwenzangu kukaa tujadiliane jinsi ya kumwandalia maisha mwanetu yeye anafikiria kuambukiza wengine" aliongea kwa uchungu sana

    Puuuuuu!!! Kikatokea kishindo kanisani.

    Shida akawa kaanguka na kuzimia pale pale!!!

    Baada ya Shida kuanguka chini watu walianza kulia na kelele pale kanisani hali iliyoleta tafrani ya aina yake.

    Kolumba yeye aliinama na kuanza kumwamsha Shida aliyekuwa amepoteza fahamu

    "Shida....Shida......shida....tafadhali amka Shida, jaman iteni gari haraka tumuwahishe hospitali" aliongea kwa woga baada ya kuona kama anazalisha tatizo lingine.



    "Nani aite gari kwa ajili ya malaya wako huyu, mwanaizaya wewe huna hata aibu? Kazi kuua watoto wa watu, umeniletea UKIMWI hauridhiki unaanza kuwaambukiza watoto wa watu wasio na hatia unawadangaya" aliongea mkewe kwa hasira.

    "He!he!he!he! Jaman acheni malumbano, mzee mwenzangu wapeleke hawa ofisi ya mchungaji, acha mimi nishughulike na huyu mgonjwa nitakuja tuyamalize huko" mchungaji alimwambia mzee wa kanisa.

    "Jaman tunaomba utulivu kidogo" aliongea mchungaji kwenye kipaza sauti cha kanisa lile na watu wakatulia huku vijana wakimtoa nje Shida na kumweka sehemu yenye upepo ili apate hewa ya kutosha.

    "Kila mtu ni shuhuda wa kilichotokea, na uhakika hakuna baya linaloenda kumtokea mwanetu na muumini wetu Shida, nawaomba muwe watulivu wakati tukifanya majadiliano na wazee huko ofisini ndipo tutaleta kwenu kinachopaswa kufanyika, namuomba shemasi wa kiume na kike na wazee wa Baraza la kanisa waingie hapo ofisini mara moja" aliongea mchungaji.



    Kule nje wale vijana walitoa mashati yao na kumpepea Shida kwa muda wa dakika tano akawa amerudiwa na fahamu zake.

    "Mmmmh! Niko wapi jaman?..............au.....Kolumba...kwa nini mimi? Eee Mungu nimekukosea nini mimi mja wako?" alivuta kumbukumbu baada ya kuamka na kuanza kulia

    "Shida usilie wala usijute kwa hili, kwanza tupate ukweli juu ya hili ndipo tujue cha kufanya, nakuomba twende kwenye kikao kama unajisikia nafuu ili tukapate ukweli" alimwambia mzee mmojawapo wa kanisa hili aliyebaki naye pale nje.

    Shida aliamka taratibu kutokana na kutokuwa na nguvu za kutosha na akashikiliwa na mzee huyu moja kwa moja mpaka ndani,

    Waliingia na kukuta kikao hakiajaanza kwani walikuwa wakimsubilia yeye,akaenda moja kwa moja na kukaa pembeni ya mchungaji na mzee wa kanisa.

    "Unajisikiaje mwanangu?" akauliza mchungaji.

    "Najisikia vizur baba mchungaji" alijibu na kumwangalia yule dada aliyedai ni mke wa kolumba,yule dada alimpandisha juu chini na kusonya.

    "Jaman, hapa ndani hatujaja kwa ajili ya ugomvi hivyo naomba tupunguze hasira ili kikao kiishe kwa amani ya Bwana" aliongea mchungaji na kuendelea



    "Nishukuru kwa aliyeleta pingamizi hili kwa sababu amelileta muda muafaka kabisa, kwani angechelewa mpaka ndoa ikafungwa asingepata nafasi ya kusikilizwa....aaaaaa..... Sijui nianze na nani?... Nafikiri mwenye pingamizi ndiye angepata nafasi ya kuongea...mama kwanza jitambulishe kisha uendelee" akaongea mchungaji

    Akakohoa kidogo kurekebisha sauti kisha akaanza kueleza





    ***************





    akaenda moja kwa moja na kukaa pembeni ya mchungaji na mzee wa kanisa.

    "Unajisikiaje mwanangu?" akauliza mchungaji.

    "Najisikia vizur baba mchungaji" alijibu na kumwangalia yule dada aliyedai ni mke wa kolumba,yule dada alimpandisha juu chini na kusonya.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mimi naitwa Lydia Kolumba, ni mke halali wa bwana Kolumba, tumefunga ndoa yetu miaka mitano iliyopita, tuna watoto wawili, na hawa hapa nyuma ni wazazi halisi wa Kolumba....Mimi na mme wangu tulizaa mtoto huyu wa kwanza tukiwa wazima wa afya ila baada ya kumzaa huyu mwenzangu akaanza tabia ya uhuni sana, hali iliyosababisha tuanze kuugua mara kwa mara na ikabidi twende kufanya vipimo ndipo tukagundulika kuwa tumeathilika.....tukaanza kutumia vidonge ndipo afya zetu zikawa angalau,vyeti vya ndoa hivi hapa.....na vya UKIMWI pia hivi hapa.........Nilishtuliwa na mtu nisiyemjua kuwa mwenzangu anakuja kufunga ndoa huku,nikaweka mtego na ndipo akaniaga kuwa anasafili kikazi kwa mwezi mzima, nikawafuatilia mpaka hapa kanisani" aliongea huk akikabidhi vyeti vyote kama ushahidi.



    Mchungaji alivipitia kimoja baada ya kingine na alipohakikisha ni vyeti halali akamgeukia Kolumba

    "Bwana Kolumba je anayoongea mwenzako hapo ni kweli??"

    "Ndiyo baba Mchungaji"

    Shida alihisi dunia yooote inamwangukia yeye!!

    "Why me?.......why me..........kwa nini mimi jaman???" alilia kwa uchungu "Why me???.........Why me??.... Kwa nini mimi lakini?" Aliongea kwa majonzi makubwa sana.

    "Kolumba kwa nini umemfanyia hivi huyu binti?" Akauliza Mchungaji.

    Kolumba hakuwa na jibu lolote la kutoa, aliinama chini na kuanza kuomba msamaha!

    "Sina cha kujitetea, najuta kwa nilichokifanya najuta, Shida nisamehe! Nimekosa sana, mke wangu nisamehe! Mchungaji nisamehe na wazazi wangu pia"

    Kila mtu alinyamaza pale na hawakuongea chochote!

    "Nawaomba ninyi mmchukue kijana wenu mwende mkamalizie mambo yenu huko kwenu, acha sisi tutajua cha kufanya" alongea mchungaji.

    "Lakini mchungaji mi......." alijalibu kuongea Baba yake Kolumba ila Mchungaji akamkatisha

    "Nafikiri sitawapa nafasi ya kujadili chochote, kwa sababu mmeshaona alichokifanya sasa msimuongezee machungu binti yetu naomba muondoke" Aliongea kwa hasira mchungaji.

    Hawakuwa na namna yoyote ile ilibidi waondoke na watoto wao pale kanisani

    Baada ya kuondoka Mchungaji alimgeukia Shida na kuanza kumbembeleza

    "Shida maisha yana safari ndefu sana, usichanganyikiwe kwa kilichotokea, amini wapo wagonjwa wengi sana ila wana maisha yao na wanaishi vizuri, kuathirika sio kufa bado kuna maisha tena marefu sana inahtaji ukubaliane na hali halisi na pia mrudie Mungu, samehe saba mara sabini na anza upya mwanangu" alijalibu Kumweka sawa.

    "Mchungaji nimekuelewa kwa kila ulichoongea, sitalia tena nakuahidi, ila kuna kazi moja ambayo niliamua nisiifanye baada ya kupata faraja kutoka kwa Kolumba sasa inabidi niifanye kwani naamini nina haki ya kuifanya" akaongea kwa ujasiri Shida



    "Kazi?..... Kazi gani hiyo mwanangu?" aliuliza Mchungaji.

    "Naitwa Shida hiyo inaonesha nimepitia shida sana, maisha yangu yamekuwa ya shida sana na shida hizo zimesababishwa na wanaume, niliwachukia sana wanaume ila Kolumba alitaka kuibadili akili yangu niwapende ila naona kaniongezea chuki dhidi yao, wamenitesa sana, wamenifanyia vitendo vibaya sana ambavyo siwezi kuvisahau, sasa ni wakati wangu wa kulipa kisasi! NITAWAUA WOTE walioyafanya maisha yangu yawe ya shida sana" aliongea Shida

    "Unasema !? Unataka kuwaua wanaume? Walikufanya nini?" akauliza tena Mchungaji.

    "Maisha ya tabu yalianzia kwa mama yangu mpaka kwangu, elewa ninahitaji kulipa kisasi, roho yangu imebadilika na sasa imekuwa kama ya mnyama, nahitaji kulipa kisasi, haya ni MAPENZI, USALITI, CHUKI na KISASI sasa naanza kisasi kwa kila mmoja aliyeleta Shida katika maisha yangu, siri ya mimi kuanza kufanya mauaji unaijua wewe peke yako, nawachukia wanamme, na wewe ni mwanamme sasa ukijaribu kutoa siri hii na wewe utaingia kwenye msafala!

    Nitakuwa naua kisha nakuja nakusimulia kwa nini nimemuua kila mmoja mpaka wataisha, nafikiri umenielewa" alihitimisha Shida

    "Mmmmmmh! Nakuomba mwanangu, Mungu anasema samehe saba mara sabini" alijaribu kushawishi mchungaji

    "Sina msamaha, mbona wao hawakunisamehe? Wamenitesa, wameninyanyasa, nimeishi kwa shida maisha yangu yote kwa sababu yao, kwa heri" akaaga na kuondoka kanisani.



    * * * * * *

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Asubuhi ya siku iliyofata ilimkuta Shida katikati ya mji wa Dodoma, akaelekea mtaa wa Uwanja wa Ndege na kuchukua chumba katika Hotel moja ya kawaida sana, akajipumzisha, akaanza kuwaza namna atakavyoikamilisha kazi ya kulipa kisasi kwa wote waliomfanyia maisha yake kuwa ya Shida!

    Alilala mpaka mchana na kuchukua tax na kuelekea moja kwa moja Benki na kutoa kiasi kikubwa sana cha pesa ambacho aliamin kitaweza kumsaidia kuikamilisha kazi yake

    Baada ya hapo akarudi hotelini

    "Inabidi kabla ya kuua niwe namfahamisha mchungaji ni nani nayeenda kumuua na kwa nini?" aliwaza

    Akachukua simu yake na kubinyeza namba za mchungaji, simu ikaita.

    MCHUNGAJI : haloo..... Nani anaongea??

    SHIDA . Ni mimi Shida mchungaji

    MCHUNGAJI : ooooh! Shida?...... Uko wapi mama?

    SHIDA : siwezi kukwambia ila nipo kwenye mkakati wangu, sasa naelekea kwenye mauaji ya mtu wa kwanza

    MCHUNGAJI : haaaa! Ni nani huyo?

    SHIDA : naelekea kumuua baba yangu mzazi! Baadae ntaenda kumuua baba yangu mlezi!

    MCHUNGAJI : haaa!!!!

    MCHUNGAJI : naomba kitu kimoja binti yangu?

    SHIDA : omba mchungaji, ilimradi kisizuie kazi yangu.

    MCHUNGAJI : sawa, basi naomba kabla hujaenda kutekeleza kusudio lako uniambie walichokufanyia watu hao, kwa sababu tangu nimezaliwa sijawahi kusikia mtu anamuua baba yake mzazi na pia mlezi, walikufanyia nini mamangu?

    SHIDA : unataka kujua?

    MCHUNGAJI : ndio nahitaji kujua,niambie tafadhali!

    SHIDA : haina shida nisikilize kwa makin, matatizo yalianzia kwa mama yangu aitwaye Amina!!



    Shida anasimulia

    MIAKA ISHIRINI NA SITA ILIYOPITA



    Amina mtoto wa kigogo aliyezaliwa huko Chamwino mkoan Dodoma aliingia Dodoma mjini kwa minajili ya kutafuta kazi,hiyo ni baada ya kumaliza kidato cha nne huko kijijini kwao

    Aliamin badala ya kuishi pale kijijini akihangaika na kilimo ni bora aende mjini akatafute kibarua kidogo cha kumwingizia kipato aweze kuwasaidia wadogo zake waendelee na masomo na pia aweze kujikimu na yeye.

    Alifikia kwa mjomba wake anayeishi Area C ambaye kidogo alikuwa na ka uwezo kutokana na kumiliki stationary maeneo ya karibu na Chuo kikuu cha Mtakatifu John!

    Amina alianza kufanya kazi katika Stationary hiyo ya mjomba wake huku akilipwa pesa kidogo ambazo zilimuwezesha kujikimu na kumsaidia mdogo wake aliyekuwa kaingia kidato cha kwanza kule kijijini kwao.

    Baada ya muda wa miezi mitano Amina akawa na uwezo wa kupanga chumba na kujitegemea mwenyewe

    Kazini kwake alikuwa akiwahudumia wanachuo wa chuo cha Mtakatifu John

    Kila binadamu ana hisia hali iliyomsababisha Amina ajikute katika mazoea na kijana mmoja kwa jina la Filbet kutoka chuo hicho

    "Amina, viip leo nikikutoa dinner?" aliuliza Folbert

    "Hahahahaha! Haya bana ila isiwe usiku sana " akajibu Amina!

    Jioni ilipofika Filbet alimfata Amina na wakaenda Hotel iliyotulia na kupata chakula cha usiku

    "Unayaonaje mazingira haya? Na chakula kwa ujumla?" aliuliza Filbet

    "Mazingira yako poa na chakula ni kitamu sana, ila nimepapenda sana, ahsante Fil kwanini umeamua kunileta hapa?" akauliza

    "Unataka kujua Amina?" akauliza Fil

    "Yes, nataka best angu" akajibu

    "Amina, tangu nilipokuona pale kazini kwenu nilivutiwa sana na wewe, nilihisi moyo wangu ukipiga paaaa! Pale pale nikahisi wewe ndiye mke wa maisha yangu, nakupenda, nakupenda kutoka ndani ya moyo wangu naomba ukubali kuwa wangu tafadhali" akamaliza mashairi yake Fil

    "Mmmmh! Unanidanganya Fil, na chuo huwaoni? Mbona kuna warembo balaa? Oa hao?" akauliza

    "Amina sio kila mwanamke anafaa kuwa mke wa mtu, wengine ni wa kupita tu na wewe ndiye unafaa kuwa wangu wa maisha nakuomba tafadhali" akaomba Filbet

    "Mmmmh! Nipe nafsi ya kufikilia tafadhali" akajibu Amina

    Walikula na wakanywa baadae wakatoka na Filbet akampeleka mpaka nyumbani kwake kisha akarudi hostel



    *************



    Baada ya miezi mitatu uhusiano kati ya Filbet na Amina ulikuwa mkubwa sana, walipendana kwa dhati na hakuna aliyekuwa hajui hilo

    "Nakupenda sana Amina,sitajuta kukupenda na wewe hutajuta,wewe ni mke wangu " aliongea Filbet

    "Nakupenda pia Filbet, tena sana, wewe ndiye mwanamme wa maisha yangu, ntakupenda milele" akajibu Amina.

    Mapenzi kabla ya wakati ni dhambi kwa mwenyezi Mungu ila binadamu ila wengi wetu tumekuwa hatutambui hilo. Na siku zote dhambi inazaa,

    Baada ya mapenzi moto moto kati ya Filbet na Amina mwisho matokeo yakaonekana

    "Baby samahani kwa hili, sijielewi! Mwezi huu nimepitisha siku zangu na mara kwa mara sijisikii kula chakula, sijui nina nini mimi?" akaongea Amina

    "Acha msikhara wewe, una mimba?" akajibu Filbet

    "Sijui mme wangu mtarajiwa, labda ila sina uhakika" akaongea Amina

    "Mmmmmmmmh! Makubwa haya sasa" akaongea taratibu Filbet

    Filbert alishtuka kutokana na kile alichokisikia kutoka kwa Amina, hakutarajia na pia hakuwa tayali kubeba majukumu ya ubaba kwa wakati huo

    "Baby, naomba kujua uko tayari kuwa mama kwa sasa? Au umejiandaa kuwa mzazi kwa sasa?" akamuuliza.

    Amina alifikilia sana kabla ya kujibu swali hilo, alishaona mwenzie alivyombadilikia hivyo alijua lile swali ni la mtegoCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sijajua unauliza ukiwa na maana gani?" akajibu

    “Sijaeleweka kivipi?, nimeuliza uko tayari kuzaa kwa sasa?" akauliza tena Fil

    "Umri wangu hauniruhusu kuwa mzazi ila pia siwezi kuua kiumbe kisicho na hatia" alijibu kwa kujiamin

    Filbert aliinama chini na kufikiria kwa muda kabla ya kuamua aongee nini.

    "Unanipenda kiasi gani? " akauliza Fil

    "Nakupenda zaidi ya kitu chochote kile" akajibu kwa kujiamini.

    "Basi kama unanipenda na unataka nije kuwa mmeo, lazima utoe mimba hiyo" akaongea Filbet kwa kujiamin

    "Heee! We mwanamme una wazimu? Hata hatujapima kujua kama kweli nina ujauzito ushaanza kuleta habari za kutoa, umerogwa?" akaongea kwa hasira sana Amina

    Yakaibuka malumbano makubwa sana ambayo ilibidi kila mmoja aondoke kivyake kama hawakuja pamoja pale.

    Asubuhi ya siku iliyofata Amina kabla hajaamka Filbet alifika pale na kuanza kumbembeleza kwenda kupima

    Wakaondoka na kwenda kupima na kwa bahati mbaya majibu yalipotoka yakaonesha kuwa ni kweli Amina ana ujauzito wa wiki saba yaani mwezi mmoja na wiki mbili na nusu.

    Njiani hakuna aliyemuongelesha mwenzake chochote

    Kila mmoja alikuwa akiwaza cha kufanya ili kukabiliana na tatizo lililojitokeza

    Huku Filbet kwenye akili yake akiwaza namna ya kumrubuni Amina aitoe ile mimba

    Upande wa Amina yeye alikuwa akiwaza namna ya kukabilian na Filbet ambaye ameshaonesha nia ya kutaka ile mimba itolewe

    "Mwanangu, katika maisha yako yote usije kujaribu kufanya kosa la kutoa mimba, nimekutaarifu mapema ili huko mjini uendako uwe makini, Babu yake baba yako alilaani hicho kitendo na pia ni dhambi kwa Mungu, yeyote aliyejaribu kufanya hivyo alifariki, nafikiri ulishasikia kilichompata Shangazi yako yulee marehemu, alijaribu kutoa akafa" maneno mazito kutoka kwa mama yake yalijirudia kwenye akili yake kila mara.

    Walipofika chumba anachoishi walikaa kidogo kisha Filbet akatoka na kwenda kumnunulia Chipsi akamletea akala na kisha akaaga na kuondoka akiahidi kurudi tena!

    Jioni ya siku hiyo Filbet alirudi na wakati huu alikuwa mbogo sana, alitaka iwe isiwe Amina lazima atoe ule ujauzito

    "Narudia kukwambia kuwa kukupenda isiwe sababu ya kuhatarisha maisha yangu, Babu yetu alishalaani hicho kitendo, nikitoa lazima nitakufa na siko tayali" alilalama Amina.

    "Hayo ni maneno tu, huyo babu yako mwenyewe alishakufa sasa maneno yake ndiyo tuyaogope, na kumbuka hii ni dunia iliyoendelea hatuwezi kuendelea kukumbatia mila na imani za kipuuzi kama hizo, hii mimba lazima itolewe" akalazimisha Folbet

    Amina alibaki analia sana.

    "Ngoja nikuulize, hivi Amina unanipenda kwa dhati na uko tayali kwa lolote kwa ajili yangu?" akauliza

    "Nakupenda tena zaidi ya sana, na niko tayari kwa lolote kwa ajili yako ila si kwa ajili ya uhai wangu" akajibu

    Jibu hilo lilimuudhi sana Filbet na kwa sababu ya hasira akajikuta akianza kumpiga Amina,

    Alimpiga sana tena sana mpaka amina akawa anavuja damu

    "Amina umeumia? Nisamehe mpenzi ni hasira tu jaman" aliongea Fil

    "Fil kweli unataka kuniua, kaninunulie dawa hali yangu sio nzuri ndipo unipeleke, hospital" akajibu

    Hii ndiyo nafasi pekee aliyoisubilia Filbet akambembeleza sana Amina na kisha akatoka kwenda kununua dawa, akiwa njiani akapiga simu

    "Oyaaa..... Tayari....ninunue dawa gani?......poa" akakata simu na kwenda kununua dawa anazozijua

    Aliporudi akampa Amina dawa ameze

    Baada ya kumeza dakika tano baadae tumbo likaanza kumuuma sana!

    "Te teh teh teh! Ulijiona mjanja Amina sasa mimba inatoka" aliongea kwa kejeli!

    Maumivu yalizidi kiuwa makubwa sana kwa Amina,alijalibu kumbembeleza sana Filbet ampeleke hospitali ila Fil akakataa

    "Ngoja nikwambie Amina, ukweli mimi siwezi baba sasa hivi, na siyo hivyo tu, nimetoka familia tajiri sana ambayo haiwezi kuniruhusu kuoa msichana maskini kama wewe, pia kiwango chetu cha elimu ni tofauti, baba yangu alishaniambia nisioe familia maskini kwa sababu sitakuwa nimeoa mke peke yake bali na matatizo ya ukoo mzima, kwa sababu hiyo sitaendelea, nitabaki kuwa nazalisha kwa ajili ya ukoo wenu huo wa kimaskini, nimekupiga makusudi ili uniombe dawa na nimekuletea dawa ya kutoa mimba, we tulia tu mpaka mimba itoke" alimaliza Filbet



    Amina aliendelea kulia huku damu zikianza kumtoka ukeni kwake,hali iliyoongeza maumivu makali sana tumboni kwake.

    Baada ya kupita saa nzima aliamini kuwa tayali mimba itakuwa imetoka,Filbet alimchukua moja kwa moja mpaka kwa daktari wake ambayae huwa anamsaidia katika shuguli zake hizo za kutoa mabinti mimba!

    Alipomfikisha walimuingiza kwenye chumba cha kazi.

    "Nilifanya kama ulivyoniagiza,na yametoka mabonge mengi sana,na uhakika itakuwa imetoka" Filbet alimwambia Dokta James

    "Kama umeyaona basi tayari itakuwa imetoka, cha msingi tumuweke hapa siku chache mpaka apone kisha utaondoka naye" akajibu Dokta James

    Filbet alimuacha pale Amina akipewa matibabu na kusafishwa!

    Matibabu yake hayakughalimu pesa nyingi na siku chache baadae alipewa ruhusa ya kumchukua Amina kutoka pale.

    Filbet alimchukua amina kwenye gari lake na moja kwa moja akampeleka kwenye nyumba yake ya siri

    "Hujapona vizuri, itabidi ukae hapa kwa siku chache mpaka utakapokuwa sawa ndipo nitakuruhusu urudi kwako" alimwambia Amina

    Amina alikaa katika nyumba ile ambayo hakuruhusiwa kutoka nje hata mara moja kwa muda wa siku tatu akiwa analetewa chakula na Filbet

    "Nafikili utakuwa umepona, mimi nina hamu ya kufanya mapenzi bana" akaongea

    "Fil sijapona vizuri, lakin nakumbuka ulinambia huwezi kuwa na mimi hivyo naomba uniache nirudi kwangu niendelee na maisha yangu" akajibu Amina

    "Sikukwambia sikutaki, nilichosema ni kuwa siwezi kukuoa kutokana na wewe kuwa maskin, wewe ni mpenzi wangu,nimetumia pesa yangu kwako haiwezi kupotea bure" akaongea kwa kujiamin.

    Amina alipotaka kuleta ubishi Filbert akatumia nguvu na kumwingilia kimwili

    Amina aliumia sana wakati wa tendo lenyewe ila hakuwa na jinsi kwani Filbet alitimiza alichokitaka

    Baada ya kumaliza kitendo cha kumbaka Amina,

    Amina alianza kutokwa na damu ukeni, alishangaaa sana na si yeye peke yake bali hata Filbet naye akashangaaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ikambidi ampigie simu daktari wake na kumweleza kinachoendelea,daktari akashauli ampeleke pale aone kinachoendelea.

    Walipofika pale alifanyiwa vipimo na uchunguzi kidogo kisha akaruhusiwa kurudi naye nyumbani huku daktari akimwambia kuwa ni damu ya mzunguko wa mwezi ndiyo inayotoka, kosa moja walilofanya ni kutokupima kama mimba ilitoka kweli

    Maisha yalianza kubadilika kwa Amina pale aliporudi nyumbani aliendelea kutokwa na damu kwa siku kadhaaa

    Kitendo cha kutokwa na damu kilimkela sana Filbet na ndipo alianza kuwa mnyama sana kwake

    "Amina mimi nina hamu ya kufanya mapenzi, sasa tufanyeje?” akauliza

    "Fil lakini si unaona hali yangu jaman, sa tutafanyaje?" akajibu Amina

    "Itabidi unipe nyuma bwana" akajibu kwa kujiamin Fil



    *************







    Mshangao mkubwa ukamkumba Amina, hakuwahi kutarajia kitu kama hicho katika maisha yake,kwanza alipokuwa akisikia alidhani watu wanatunga,ila sasa yeye ndiye aliyetakiwa kufanya hivyo.

    Pamoja na jitihada kubwa za kupinga alizoonesha ila hakuweza kupambana na Filbet,alifanikisha azma yake kwa binti huyu

    Mchezo haukuhishia siku hiyo uliendelea kila siku huku akinyimwa ruhusa ya kutoka ndani na damu nayo iliendelea kutoka!

    Cha ajabu baada ya miezi mitatu, siku moja Filbet alimkuta Amina akiwa anaoga pale ndani, alishangazwa na alichokiona.

    "Amina, mbona tumbo lako ni kubwa? Ina maana mimba haikutoka?" aliuliza kwa mshangao!!!!!

    Filbet alihamaki sana kwa kile alichokishuhudia kwani hakutegemea kukiona tena! Aliamin ile mimba ilitoka kwani alithibitishiwa na daktari kuwa ilitoka sasa anashangaa kuiona tena!

    "Ina maana bado una mimba Amina?" akauliza

    "Mimi sijui ila hata mimi najishangaa kwani tumbo linazidi kuwa kubwa na kuwa gumu" akajibu Amina

    Filbet alizubaa kwa muda akimtazama Amina, alishindwa afanye nini, kwani tayali alikuwa na mchumba aliyekuwa nje ya nchi kimasomo na hakutaka kutia doa uchumba ule kwa sababu ya huyu binti,alitafakari mwishowe akapata wazo

    "Amina naomba ukojoe mkojo wako unipatie tafadhali" akaomba

    Amina alifanya kama alivyoagizwa na Filbet kisha akamkabidhi,na Yeye akaondoka nao moja kwa moja mpaka kwa yule daktari wake na kumweleza mkasa mzima ulivyo

    "Sasa dokta,inakuwaje hili liwe hivi?" akauliza

    "Ningekuomba uwe mtulivu mpaka niupime huu mkojo" akajibu Dokta

    Dokta alichukua ule mkojo na kwenda moja kwa moja mpaka maabara na kuupima, baada ya muda mfupi alirudi na majibu

    "Dah! Kijana, siamini ninachokiona hapa, huyu binti ile mimba haikutoka, na sasa hali si shwari" akasema Dokta

    "Inawezekana vip dokta? Na hali mbaya kivip?" akajibu Fil

    "Unajua kwa kumbukumbu zangu nahisi kuna kosa moja tulifanya, hatukumpima kipindi kile ili kuhakikisha kuwa mimba ametoka, na sasa hali iliyopo ni mbaya, mimba ina miezi mitano, kumbuka kipindi kile ilikuwa na wiki saba na imepita miezi mitatu na kwangu mimi nisikudanganye siwezi kujalibu mchezo wa kutoa mimba kubwa hivyo" akahitimisha dokta



    Walibishana kwa muda mrefu bila maelewano juu ya swala la kufanya juu ya ule ujauzito, Filibet alilazimisha utolewe huku dokta akimsihi asijalibu kufanya hivyo kwani ni hatari kubwa



    "Sikia dokta siko tayali kumpoteza Lily wangu kisa huyu demu fala,9iko tayali kwa lolote,nakupamuda mfupi sana nitakupa majibu" akajibu kwa jeuri kisha akaondoka

    Filbet aliondoka pale akiwa na hasira kubwa sana alijua alichotaka kukifanya hivyo alipofika nyumbani hakumwambia Amina kilichotokea huko, Alichokifanya ni kuanzisha ugomvi usio na sababu.

    "Hivi wewe ni mwanamke wa aina gan? Huna kazi unafanya hapa kazi kukaa tuu na kutoka dami?" akaanzisha maongezi ya kishari shari

    Amina hakujua kinachotokea hivyo alijibu kiungwana tu na hapo ndipo alipopataka Filbet

    "Unanijib? Nani kakwambia mwanamke ana haki ya kumjibu mmewe?"

    Na pale pale akaanza kumshushia Amina kipigo kikali sana, alikuwa akijua anachokifanya hivyo hata upigaji wake ulienda sehemu husika

    Tumbo, hapo ndipo lilipokuwa lengo lake halisi,alimpiga Amina ngumi na mateke mengi sana tumboni mpaka Amina akaanza kutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili wake.

    Kipigo kilizidi mpaka Amina akapoteza fahamu huku damu zikizidi kumtoka ukeni kwa wingi, Filbet alipohakikisha kuwa kazi aliyofanya ni nzuri na italeta majibu anayoyataka alitoka nje na kufunga mlango

    "Hakikisha huyo malaya hatoki humo ndani mpaka nikirudi" alimuamrisha Alex mlinzi wake wa getini

    Sio kila mwanamme ana roho mbaya na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Alex mlinzi wa Filbet

    Tangu yule mwanamke aletwe pale alijua yatakayomkuta ni makubwa kwani haikuwa mara ya kwanza kwa Filbet kuleta mwanamke pale ndani na kumtesa kisha kumtelekeza

    Kwa huyu hali ikawa tofauti alionekana binti mdogo sana na mwenye shida kubwa, moyo wa huruma ukamwingia, akapanga kumsaidia, kila alipojaribu alishindwa kwani funguo zilifichwa na bosi wake,

    Hapo ndipo alipoanza kumchunguza bosi wake ili ajue pale funguo zinapofichwa, alifuatilia sana na siku ya tukio la Amina kupigwa sana ndipo akaona zikiwa zinafichwa

    Filbet alipoondoka pale ndani Alex akaenda na kuchukua zile funguo na kuingia ndani

    Alimkuta Amina katika hali mbaya sana,alipoweka mkono wake kwenye kifua chake akakuta mapigo ya moyo yamesimama!!



    Alex alihangaika kumpulizia pumzi kutoka katika mdomo wake Amina,na kwa muda mtefu hatimaye alisikia mapigo yake ya moyo yakipiga kwa mbali,alichokifanya ni kumeba mzima mzima na kuondoka naye katika mazingira yale,

    Alipofika nje alitafuta tax na kupanda moja kwa moja akaelekea mtaa aliokuwa kapanga wa airport

    Alipofika alimuingiza ndani na kuchukua maji akayapasha na kuanza kumkanda sehemu mbali mbali za mwili wake na alipoona vidonda vina angalau alienda kwenye duka la dawa za binadamu na kununua dawa ya kukausha vidonda akaja na kumpaka seemu zote zenye vidonda!

    Alex alikaa na kufikiria kwa makini, akaona kajiingiza kwenye vita kubwa sana, alimjua Filbet alivyokuwa katili na pia alijua baba yake alivyokuwa na pesa ambazo angeweza kufanya chochote kwa ajili ya mwanae, akaona uwezekano wa yeye kuendelea kuishi pale Dodoma mjini ni mgumu



    "Hawa wameniajiri kwa kukutana hapa hapa mjini, hawanijui kwa namna yeyote ile, nikajifiche kule kwetu mpaka haya mambo yatulie na huyu binti apone ndipo nitajua cha kufanya" alipitisha uamuzi.

    Na moja kwa moja akachukua akiba aliyokuwa amejiwekea pale mjini na akakabidhi chumba kwa mama mwenye nyumba kisha akaaga na kuondoka na Amina kuelekea kijijini kwao huko Hombolo nje kidogo ya mji huu wa dodoma.

    Alifika kwao jioni sana ili watu wasimuone yule binti na kuleta maneno pale kijijini, alipokelewa na mama yake na baadhi ya ndugu zake waliokuwepo na moja kwa moja akampeleka Amina kwenye nyumba yake ( kwa sababu vijijini kila kijana huwa ana nyumba yake anayolala) akamlaza kitandani pake na kutoka kwenda kumwona mama yakeCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Vip baba? Huko kwema kweli? Naona na mkwelima juu" akauliza mama yake

    "Huko ni kwema na pia si kwema,huyu binti ana matatizo ingawa siyajui kiundani ila nimeona nimsaidie" akajibu na kuanza kumweleza mkasa ule kwa jinsi anavyoujua mwanzo mpaka mwisho

    "Jaman! Kuna watu wana roho mbaya sana,kama ndiyo hivyo acha nikamwone mtaalamu aje aone namna ya kumsaidia baba" akashauru mama na wote wakakubaliana na wazo lile

    Baada ya muda wakati usiku ulishaanza kuwa mkubwa mama yake Alex alirudi na mganga na kumpeleka ndani kumona yule binti

    Mtaalamu alitengeneza dawa za kuponya maumivu ya ndani ya mwili na kuondoa uvimbe na damu iliyogandiana pale pale na wakamnywesha kwa nguvu Amina ambaye hakuwa na fahamu kwa wakati huo.

    Asubuhi ya siku iliyofata mganga alifika tena na kuendelea na matibabu yake, kwa sababu mwanga ulikuwepo tofauti na usiku uliopita aliweza kugundua maeneo aliyoumia zidi na kumpatia matibabu vizuri

    Mchana wa siku hiyo wakiwa wanakula Alex yeye alikuwa pembeni ya kitanda cha Amina kumwangalia maendeleo yake,ndipo aliposhangaa Amina akipiga chafya mara tatu kisha akaamka na kukaa

    "Mama.....mama....kaamka...njoeni" alipiga kelele kwa furaha. Mama yake na ndugu zake wakaingia na kila mmoja akaonesha furaha yake pale

    "Niko wapi? Na nyie ni nan?" aliuliza

    "Tulia binti, sisi ni msaada kwako, tuko hapa kukusaidia, hivyo usijali, uko katika mikono salama" akamwambia Alex.

    Waliondoka na kwenda kumwita mganga na baada ya muda mfupi akafika na kuanza kumpa matibabu kidogo kisha Amina akaonesha nafuu ambayo aliweza kuongea mwenyewe

    Mganga akamuulizia kilichomtokea na sehemu yeyote yenye shida aweze kusaidia,ndipo Amina alipoeleza kisa chote kilichomtokea mwanzo mpaka mwisho,alipomaliza wenye moyo mwepesi walilia ila wakampa pole na kuwahidi kusaidia

    Ikabidi na yeye aulize imekuwaje awe pale na pale ni wapi?

    Alex akabeba jukumu la kumwelewesha kila kitu kilichotokea mwanzo mpaka mwisho

    "Nashukuru sana Alex, wewe ni binadamu wa pekee, sina cha kukulipa ila elewa umeokoa maisha yangu, nakushukulu sana" alitoa shukrani zake.







    *************







    :: Unavyodhani nini kitaendelea?



    :: Hii ni mojawapo ya riwaya kali sana kutoka kwa mwandishi chipukizi hapa uwanja wa simulizi.



    :: Onesha ushirikiano wako katika kumpa sapoti mwandishi wa riwaya hii kwa ku LIKE, ku SHARE na hata ku COMMENT kuhusiana na hii riwaya hapo chini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog