Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

IPO SIKU TU - 2

 







    Simulizi : Ipo Siku Tu

    Sehemu Ya Pili (2)





    Wakiwa ndani ya gari, siku hii Dk.Anthony alionekana kuwa mtulivu sana mpaka Angel alikuwa akimshangaa maana alishamzoea muda mwingi ni mtu mwenye utani.

    " Anko Anthony."

    "Ndio Angel."CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Naona umekuwa mpole kweli, ngoja nikuulize swali moja ili uchangamke."

    "Hahaha, haya niulize." Alijikuta akiangua kicheko Dk.Anthony kutokana na udadisi mkubwa aliokuwa nao Angel.

    "Hivi mama yangu ni nani na yuko wapi kwa sasa?" Lilikuwa ni swali kutoka kinywani mwa Angel na kumuuliza Dk.Anthony.

    Swali hili liliweza kutikisa vilivyo katika masikio ya Dk.Anthony mpaka akajikuta akishika breki ya gari ghafla.



    "Hilo ni swali zuri sana Angel, ila nakuahidi nitakupa jibu lako siku nyingine."

    "Kwanini Anko usiniambie leo!, kwani wewe humjui mama yangu!?"

    "Mimi simjui ila nikimuona nitakuonyesha."

    "Basi leo Anko, nimekutana na mama." Alizungumza Angel na kumfanya Dk.Anthony atanasamu na kuongeza umakini wa kumsikiliza.

    "Mh!, umekutana na mama yako wapi!?"

    "Pale hospitali Anko.nimemuahidi kuanzia leo yule mama mgonjwa atakuwa mama yangu kwakuwa nilimsikia yule shangazi aliyekuja pale akimwambia kuwa hatoweza kuwa na mtoto katika maisha yake daima.Pia Anko naomba kila nikitoka shule, unipeleke nikamsalimie yule mama halafu ndio nirudi nyumbani."

    Maneno yaliyojaa weredi kutoka kwa mtoto Angel, yalimgusa sana Dk.Anthony na moyoni mwake binafsi akawa anajieleza kuwa wahenga waliosema msemo usemao 'Damu ni nzito kuliko maji' hawakukosea hata kidogo maana Angel anampenda mtu ambaye bila hata ya kumtambua kuwa ni mama yake mzazi.Dk.Anthony hakuweza kumnyima nafasi ile Angel, zaidi akamuahidi kila siku atakuwa anamfikisha hospitali kwa ajili ya kumsalimu Janet.



    "Jesca mke wangu, kila kitu ulichokuwa unakihitaji kipo mikononi mwako sasa, kwanini usimuache naye mwenzako akaishi kwa amani ukizingatia na hali aliyokuwa nayo!?"

    "Nadhani huelewi chochote Baba Beatrace kwanini mimi nahitaji kuyafanya haya, hivyo naomba suala hili liache kama lilivyo."

    "Hapana mama Beatrice!, hivi unafikiri nafsi ngapi zitakulilia kwa haya unayoyafanya?, jitahidi kurudi kwenye mstari mke wangu ili tumuongoze mtoto wetu katika mstari unaofaa."

    "Imetosha Nelson!!, haya ni maamuzi yangu mimi na ni lazima Janet afe ili amani iendelee kutawala katika maisha yetu.Tayari nimeshazungumza na daktari na muda si mrefu kila kitu kitakuwa kimeisha." Yalikuwa ni maongezi baina ya Jesca pamoja na mume wake.

    Nelson alionekana kutoweza kukubaliana kabisa na kile alichoelezwa na mkewe hivyo akawa anajitahidi kupingina nae vikari na kumbembeleza asilifanye lile alilokusudia kulitenda.



    Urafiki mkubwa kati ya Angel pamoja na Beatrice, ulianza kati yao huku kila mmoja akifurahi kuwa pamoja na mwenzake.Tangu wanafika darasa la nne mpaka kufikia kuhitimu darasa la saba, wote wawili walikuwa na wastani mzuri wa ufaulu na walibahatika kupangiwa shule moja katika kwenda kuanza kidato cha kwanza.

    Katika kipindi chote hicho Dk.Anthony hakusita kumpeleka Angel kwenda kumuona Janet hospitalini kila alipohitaji kwenda kumsabahi, na hii ilimpelekea Janet kufarijika sana maana alitokea kumpenda sana Angel mithili kama alikuwa akitambua yule ni binti yake wa kumzaa.



    Siku hii Angel akiwa ameambatana na rafiki yake ampendaye, wakaelekea hospitali kwa ajili ya kwenda kumsalimu mama yake Angel.Hii ilikuwa ndio mara yake ya kwanza Beatrice kwenda kumsalimu mama wa rafiki yake.Baada kufika hospitali, kwanza wakaenda kusalimiana na Dk.Anthony kisha wakatoka na kuelekea katika chumba alichokuwepo Janet.Kitendo tu cha kumuona Angel akiingia pale, Janet alitabasamu na moyo wake kulipuka kwa furaha maana hakuna mtoto aliyekuwa akimpenda kama Angel.

    Angel akamkimbilia mama yake kwa furaha na kumkumbatia, kisha wakasalimina na kuzungumza nae.

    "Mama, naomba umfahamu rafiki yangu nimpendaye, jina lake anaitwa Beatrice." Angel alimtambulisha rafiki yake kwa mama yake naye mama akatikisa kichwa na kumkaribisha Beatrice mahali pale.

    "Kiufupi mama, Beatrice ni kama dada yangu pekee ninayemuona katika dunia hii hivyo kuanzia sasa usihesabu kama una mtoto mmoja bali tupo wawili." Alizungumza Angel na kumfanya mama azidi kutabasamu.

    Wakati wakiendelea na mazungumzo na kuendelea kutaniana na mama, mara Beatrice aliuliza swali ambalo lilikatiza furaha yote aliyokuwa nayo Janet kutokana na uzito wa swali lile.

    "Samahani mama, hivi ulikuwa huna uwezo wa kuzungumza tangu kuzaliwa kwako au kuna kitu chochote kilichotokea mpaka kukupelekea sauti yako isisikike tena." Ni swali ambalo aliuliza Beatrice.

    Swali hili lilimpelekea Janet akumbuke maisha aliyoishi zamani akiwa pamoja na marehemu mume wake, huzuni ilizidi kumtawala hasa zaidi pale alipokumbuka siku ambayo Brian anafariki dunia kutokana na ajali mbaya ya gari waliyoipata.Pia alikumbuka vyema kuwa ajali ile waliyoipata ndio ilikuwa chanzo cha matatizo yale aliyonayo sasa kumsibu.

    Hakuwa na jibu lolote lile la kuweza kumjibu Beatrice zaidi alikamata mikono ya Beatrice huku akitikisa kichwa chake kama kumpa ishara fulani.Beatrice hakuweza kumuelewa mama anachomaanisha lakini kwakuwa Angel alikuwepo pale, basi akaweza kumuelezea na kumfafanulia kile alichokuwa anakieleza mama.

    "Mama amesema umemuliza swali zuri, ila leo hatoweza kukujibu labda utakapokuja siku nyingine ndipo atakueleza." Aliongea Angel na kumueleza Beatrice yale aliyoyasema mama.

    Baada ya kuzungumza machache na Beatrice kuweza kumfahamu mama wa rafiki yake, walimuaga mama na kuelekea ofisini kwa Dk.Anthony, kisha wakaagana nae na kutoka pale hospitali kwa ajili ya kuelekea katika matembezi yao ya kawaida.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya Angel pamoja na Beatrice kutoka pale hospitali, haikupita muda, Jesca ambaye ni mama yake mzazi Beatrice akawasili pale hospitalini.Siku hii Jesca alifika hospitali si katika hali ya kiungwana bali alifika hospotali kishari zaidi huku akihitaji kumuonya vikali Dk.Anthony kwa kushindwa kumfanyia kazi yake.

    Alifika ofisini kwa Dk.Anthony, naye Dk.Anthony bila hiyana yoyote, akamkaribisha ili waweze kuzungumza.

    "Karibu dada Jesca, habari za siku nyingi tena?"

    "Kamsalimie mama yako kama hiyo salamu yako unaiona ni ya thamani." Alijibu Jesca kwa dharau mpaka akamfanya Dk.Anthony aduwae maana hakutarajia kupata jibu kama lile.

    "Mbona hivyo dada, embu jaribu kuwa mstaarabu kidogo."

    "Shetani mkubwa wee!, 'Eti kuwa mstaaraabu!' ungekuwa mstaarabu ungevunja makubaliano yetu?.Ni muda gani umepita tangu ushindwe kuikamilisha kazi hii!, sasa nakupa siku mbili tu za kuondoa maisha ya Janet la sivyo nitakufanya kitu kibaya sana."

    "Nyamazaa!!,Imetosha, nimesema imetosha Jesca!." Aliongea Dk.Anthony kwa hasira sana huku akifoka kwa hasira.

    "Hivi wewe umezaliwa na mwanamke kweli!?, kwanini unapenda muda wote mwanamke mwenzako atendewe unyama!, mtoto wake ulishamuua ila kwa hili sitoweza kukuvumilia."

    "Unanigeuka!, nakuuliza wewe Dk.Anthony, unanigeuka!?, sasa nasema kuanzia leo ama zako ama zangu na lazima utanitambua vizuri kuwa mimi ni nani." Aliongea Jesca huku akipigiza mikono yake kwa nguvu katika meza iliyokuwepo pale ofisini, kisha akainuka na kuondoka kwa hasira.

    Huu ulikuwa mtihani mzito sana kwa Dk.Anthony, lakini pamoja na yote dhamira yake ya kumsaidia Janet pamoja na mtoto wake ilibaki palepale huku tegemezi lake aliloliona katika kukabiliana na yale, ni Mungu pekee.

    Siku hii ilikuwa ni siku ya mawazo sana kwa Dk.Anthony hasa zaidi kila alipokumbuka maneno ya Jesca pamoja na vitisho alivyokuwa anavitoa.Alipotoka ofisini Dk.Anthony, akaona ni vyema amchukue Angel na kutafuta sehemu waende maana kuna mambo machache alihitaji kuzungumza nae.



    "Angel, binti yangu." Aliita Dk.Anthony wakati wakiwa wapo kwenye mazungumzo na Angel

    "Ndio Anko."

    "Leo kuna mambo machache nahitaji kukueleza, hivyo naomba uwe makini kunisikiliza na kuyazingatia sana haya nitakayokueleza."

    "Sawa Anko." Aliitika Angel na kuongeza umakini wa kumsikiliza Dk.Anthony.

    "Si kila mtu umwonaye katika dunia hii atakuwa mwema upande wako, binafsi kwasasa nahisi siku za kuendelea kuwa pamoja nawe zimebaki chache." Aliongea Dk.Anthony na kumshangaza Angel kwa maneno haya.

    "Kwanini Anko unasema hivyo!, ina maana utasafiri na kuniacha mimi na mama peke yetu!?"

    "Usijali binti yangu, hata kama mimi nitakuwa mbali nawe lakini haitakuwa kikwazo cha wewe kuweza kuzikamilisha ndoto zako maana nahikikisha nakutengenezea msingi mzuri ili usije ukakwamia njiani." Yalikuwa ni maneno kutoka kwa Dk.Anthony ambayo alikuwa akiyazungumza katika hali ya uchungu sana.

    "Unamaanisha nini kusema hivyo Anko!?" Aliuliza Angel kwa sauti ya upole huku akiwa na hofu ndani yake.

    "Angel binti yangu?"

    "Ndio Anko"

    "Yule mama mgonjwa aliye pale hospitali, leo hii nimemuahimisha na kumpeleka sehemu moja ya siri ambayo nitakupeleka hivi punde ili ukaione, ila naomba sana usije kumpeleka wala kumueleza mtu yoyote mahali alipo na pia naomba uendelee kumpa heshima ya mama maana yule kwako ni mtu muhimu sana na atakusaidia katika mengi."

    Maneno yaliyojaa wosia ndani yake, yalizidi kumchanganya Angel maana hakuelewa kwanini Dk.Anthony alikuwa akimueleza yale.

    Dk.Anthony aliamua kumueleza maneno yale binti yake, maana aliona maisha yake yapo hatarini sana kutokana na vita kubwa aliyonayo.

    Dk.Anthony aliendelea kumueleza mengi Angel na kubwa zaidi kumbe tayari alishatafuta mdhamini ambaye anaishi nchini Uingereza, ili amdhamini Angel katika masomo yake mpaka atakapomaliza.

    Baada ya kumaliza maongezi, Dk.Anthony akamchukua Angel na kumpeleka hadi katika sehemu ambayo alikwenda kumuhifadhi Janet kwa ajili ya usalama wake zaidi.



    Jambo lile la Dk.Anthony kushindwa kumfanyia kazi yake lilimuumiza na kumpandisha hasira Jesca, na aliamua kuandaa mpango maalumu kwa ajili ya kuhakikisha anamfanyia jambo Dk.Anthony ambalo hatoweza kulisahau katika maisha yake.



    Yakiwa majira ya asubui, Jesca akiwa nyumbani mara nyingi akawa anawasiliana na watu wake ambao aliwaandaa kwa ajili ya kumtendea ubaya Dk.Anthony ili kuhakikisha mpango wao unaenda kama walivyoupanga.

    Wakati Jesca akiendelea kufanya mawasiliano yale ya siri na watu wake, kwa bahati njema au mbaya Nelson, ambaye ni mume wake, akaweza kusikia na kugundua mpango wa mke wake japo hakuelewa ni nani anayekwenda kutendewa ubaya.

    Akili ya haraka ambayo ilimjia Nelson kichwani mwake, alihisi moja kwa moja lipo jambo baya analokwenda kutendewa Janet.Bila kumuuliza chochote mke wake, Nelson akatoka pale nyumbani na kuanza kuelekea hospitali haraka iwezekanavyo ili aweze kwenda kumsaidia Janet.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ikiwa ni siku tulivu, asubui na mapema, kama ilivyo ada na akiwa hana ile wala lile, Dk.Anthony akaanza safari ya kutoka nyumbani na kuelekea katika majukumu yake ya kila siku.Akiwa karibu kufika na hospitali ambapo ndipo sehemu anapofanyia kazi, mara gari yake inapata hitilafu ghafla na kuzima kabisa.Baada ya kujaribu mara kadhaa kuiwasha bila mafanikio yoyote ya gari kuwaka, ndipo Dk.Anthony ikamlazimu ashuke ndani ya gari ili aweze kuangalia tatizo.

    Kitendo cha yeye kushuka tu ndani ya gari, ghafla kuna gari moja aina ya Alterza ambayo ilikuwa imeinawiri kwa rangi nyeusi, ilikuwa inakuja upande alipokuwepo yeye kwa kasi kubwa mno.Dk.Anthony alibaki ameduwaa na kuitazama gari ile ambayo ilikuwa imeshamkaribia kwa kiasi kikubwa, ikamchota na kumrusha juu mithili ya maji yalukavyo kutoka katika bomba lililopasuka.Baada ya kusababisha ajali, gari ile haikusimama badala yake iliongeza mwendo zaidi kwa ajili ya kuondoka eneo la tukio.



    Nelson ambaye alikuwepo karibu na eneo lile, ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuweza kushuhudia ajali ile ya kutisha ambayo hakuwahi kuishuhudia kabla.Licha ya haraka aliyonayo lakini Nelson akaona ni vyema asogee eneo la tukio lilipotokea ili akajue hali ya mtu aliyesababishiwa ajali ile, ambaye kwa muda huo alikuwa amelala chini huku sehemu mbalimbali za mwili wake zikivuja damu.Muda wote huo, Nelson alikuwa hajafahamu kuwa mtu aliyepata ile ajali, alikuwa ni Dk.Anthony.





    Nelson alisogea hadi sehemu alipoangukia Dk.Anthony.Jinsi mwili ulivyokua umeharibika hasa zaidi katika sehemu ya kichwa, ilikuwa ni ngumu kumtazama Dk.Anthony mara mbili lakini Nelson akaweza kukaza roho ili aone kama anaweza kutoa msaada wowote wa haraka.Aliposogea zaidi na kumpindua muhanga wa ajali ile ili aweze kumtazama usoni kama ataweza kumtambua, hapo ndipo Nelson alipochoka mwili na roho.Alishindwa kuamini baada ya kutupa macho yake kumtazama vizuri na kugundua mtu amwonaye pale ni Dk.Anthony.Alijaribu kumuita huku akimtikisa kwa nguvu kwa lengo la kumuamsha lakini Dk.Anthony alionekana kuwa kimya pale chini huku mapigo yake ya moyo yakiwa yamezima na mwili wake ukiwa umepoa kabisa.Baadhi ya watu ambao nao walikuwa karibu na eneo lile, waliweza kusogea eneo la tukio ili kuweza kushuhudia yaliyojiri.

    Kwakuwa hospitali haikuwa mbali sana na eneo lile, haikuchukua muda mrefu gari ya kubebea wagonjwa ikaweza kufika na kuchukua mwili wa Dk.Anthony kwa ajili ya kuupeleka hospitali.



    Akiwa ameambatana na Beatrice, rafiki yake wa karibu sana, Angel aliweza kufika hospitali mapema kama alivyoelezwa na Dk.Anthony siku iliyopita ili aweze kumkamilishia baadhi ya vipengele kwa ajili ya udhamini wake.

    Baada ya kufika pale hospitali na kuelezwa kuwa Dk.Anthony alikuwa bado hajawasili pale hospitali iliwalazimu Angel pamoja na Beatrice waketi sehemu ya mapokezi na kumsibiri.Wakiwa hawana hili wala lile na wakiendelea na mazungumzo yao ya kawaida, mara kinapitishwa kitanda ambacho juu yake kulikua na mwili uliofunikwa kwa shuka jeupe, ambalo lilikuwa limelowana na damu mno.Ilikuwa ni ngumu kwa Angel pamoja na Beatice kuweza kuugundua mwili uliokuwa unapitishwa pale kwasababu ulikuwa unefunikwa wote, lakini kumbe ndio ulikuwa mwili wa Dk.Anthony ambao ulikuwa unapelekwa kwenda kuhifadhiwa katika sehemu husika.

    Wakiwa katika mshagao na kuyashuhudia hayo yaliyokuwa yanaendelea pale, mara Beatrice alipotazama katika mlango wa kuingilia pale hospitali, akamuona baba yake akiingia eneo lile.Alijiuliza na kupata hofu Beatrice maana alihisi pengine baba yake atakuwa ni mgonjwa au ana tatizo lolote lililompelekea afika pale hospitali, wakatoka na kwenda kuzungumza nae.

    "Shikamoo Anko Nea." Angel alimsalimu Nelson.

    "Marahaba mjomba, habari ya asubui tena?"

    "Nzuri Anko."

    "Mnafanya nini hapa hospitali?"

    "Nimekuja kumuona Anko Anthony hivyo nilimuomba Beatrice anisindikize." Alijibu Angel na kumueleza Nelson.

    Moyoni mwake Nelson alihisi kupata huzuni sana baada ya kusikia kauli ile kkutoka kwa Angel maana alitambua Dk.Anthony ndio alikuwa tegemezi lake na hayupo tena katika ulimwengu huu.

    "Ooh, basi sawa mabinti zangu ila wakati nakuja huku niliwasiliana na Dk.Anthony na alinieleza leo hatoweza kufika ofisini maana kuna dharura kidogo ameipata." Aliongea Nelson ili Angel asielewe chochote juu ya kile kichotokea.

    "Mh! mbona jana hakuniambia kama leo hatakuwepo na zaidi alinisisitiza sana nifike hapa asubui!?"

    "Hili ninalokueleza ni la kweli Angel, pia naomba tutoke nje kuna jambo moja nahitaji kuueleza." Alizungumza Nelson na kuhitaji kumtoa nje Angel ili akamueleze yale yote yaliyotokea kwa Dk.Anthony maana aliona pale sio sehemu sahihi ya kumieleza.

    Kabla ya kutoka ya nje, Nelson akahitaji kulikamilisha kwanza jambo lililomleta hivyo akafika mapokezi na kuulizia jina la chumba ambacho alikuwa amelazwa Janet.Kitendo cha kutaja jina na kumuulizia Janet pale mapokezi ilimfanya Angel ashtuke kidogo maana alifahamu yule mama ambaye yeye binafsi amezoea kumuita mama yake, ndiye aliyekuwa na jina lile.Japo hakuwa na uhakika kama mama yake ndiye anayeuliziwa na Anko Nelson pale mapokezi lakini Angel alibaki kimya na kutohitaji kuuliza wala kuongea lolote kuhusiana na lile.

    Wahudumu wa pale mapokezi, walumueleza Nelson kuwa hawana kumbukumbu zozote kuhusiana na mgonjwa anayemuulizia na wala pale hospitali hakuna mgonjwa mwenye jina la Janet.Lilikuwa ni jambo la kushangaza sana kwa Nelson na akaanza kuingiwa hofu na kuhisi pengine zile zitakuwa ni njama za mkewe za kuweza kumuangamiza Janet.Nelson hakuhitaji Kuendelea kuhoji sana zaidi aliona atakapofika nyumbani majibu yote ya maswali anayojiuliza atayapata kwa mkewe.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Taarifa za kifo cha Dk.Anthony zilikua zimetikisa vilivyo katika nchi kutokana na kazi yake nzuri aliyokuwa anaifanya.Watu wengi sana walionekana kuguswa na msiba ule maana Dk.Anthony alikuwa ni daktari bingwa wa magonjwa ya kike na moyo hivyo watu wengi walimtambua kutokana na umaridadi mkubwa wa kazi yake.

    Japokuwa watu wengi walionekana kuguswa na msiba ule lakini kifo cha Dk.Anthony, hili lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa binti Angel ambaye yeye siku zote aliishi kwa kumtegemea Dk.Anthony.Muda wote Angel alikuwa ni mtu wa kulia na kuomboleza tu huku akilalamika, "'Uko wapi Anko Anthony!, nitaishi na nani mimi Anko!, naomba urudi Anko!, usiniache peke yangu mimi Anko Anthony.!?".Huzuni hii haikuwa kwa Angel pekee bali hata kwa mama yake ambapo taarifa zilimfikia kule mahali alipo.

    Baada ya vyombo vya sheria kufanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa ile ilikuwa ni ajali ya kawaida tu kama zinavyotokea barabarani, ndipo ruhusa ya kuzika mwili wa marehemu ikatolewa.Watu wengi sana wakiwemo ndugu, jamaa, madaktari wenzake na baadhi ya viongozi wa kiserikali ambao walikuwa wakimfahamu Dk.Anthony, waliweza kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika safari ya kumsindikiza Dk.Anthony katika makao yake ya milele.Huzuni ilikuwa imetanda kila kona huku kila mmoja aliyekuwa akimfahamu Dk.Anthony, alibaki kusikitika tu na kumuombea safari njema katika maisha ya sayari nyingine tofauti na ya kwetu, nayokwenda kuyaanza.

    Baada ya maziko ya Dk.Anthony kukamilika, Nelson akaona ni vyema aweze kumchukua Angel na kumpeleka nyumbani ili wakaishi nae maana Angel hakuwa na msaada wowote tena aliokuwa anautegemea kuupata baada ya Dk.Anthony kufa.



    "Enhe binti, umesema jina lako ni nani!?" Jesca alimuuliza Angel baada ya kufikishwa pale nyumbani na Nelson.

    "Kama alivyokwambia Anko Nea, jina langu naitwa Angel."

    "Je tushawi kuonana mahali!?" Aliuliza Jesca maana kila alipomtazama Angel, alihisi kama kuna mahali alishawahi kumuona na kukutana nae mahali.wakati Angel akijiandaa kulijibu swali lile aliloulizwa, Nelson akaamu kudakia na Kulijibu yeye.

    "Imetosha Jesca na wala haina haja ya kumuhoji maswali mengi binti huyu zaidi naomba aishi nasi hapa maana huyu ni rafiki wa mtoto wetu na kwasasa hana mtu yoyote wa kumlea kutokana na matatizo yaliyompata."

    Jibu hili lilimfanya Jesca abakie kuguna na kuinuka kwa ajili ya kuondoka pale sebuleni huku akimtazama sana Angel.

    "Usijali Angel, kuanzia sasa utaishi pamoja nasi hapa nyumbani na nitajitahidi kukutimizia mahitaji yako yote muhimu unayostahili kuyapata."

    "Asante Anko Nea, lakini ni kweli sitoweza kumuona Anko Anthony tena katika maisha yangu!?, kwanini ameniacha peke yangu mimi." Alizungumza Angel kwa uchungu sana nae Anko nea akasogea karibu yake na kuanza kumtuliza huku akimueleza maneno ya kumtia moyo na kumfariji.

    Wakati hayo yakiwa yanendelea pale sebuleni, mara kikasikika kicheko kikubwa kutokea upande wa ndani ambapo alikuwepo Jesca.Nelson alipandwa na hasira mno ila alijitahidi kujizuia maana kuna jambo fulani alihitaji kulififanya kwanza juu ya mkewe.



    Licha ya kupata msaada ule Angel, lakini fikra zake siku zote hazikuacha kumfikiria na kumkumbuka Dk.Anthony huku akiona kama yale yote yalioyotokea yalikuwa ni kama ndoto kwake, lakini ile ndio ilikuwa ni hali halisi iliyojitokeza.



    Baada ya kufanikisha kusudio lake la kwanza, Jesca aliendeleza jitihada zake za kuhakikisha anayaondoa maisha ya Janet pia na baada ya kumkosa hospitali na kutojua ni wapi alipopelekwa, Jesca alikuwa na wakati mgumu sana wa kuweza kujua ni sehemu gani Janet alipo.Mtu pekee ambaye alikuwa anafahamu sehemu alipohifadhiwa Janet na marehemu Dk.Anthony, alikuwa ni Angel na yeye licha ya kuwa moja ya mwanafamilia wa pale lakini hakuthubutu hata siku moja kufungua mdomo wake na kumueleza mtu mahali alipo Janet, ambaye yeye alikuwa akimchukulia kama mama yake.



    "'Janet mke wangu, naomba kuwa mwangalifu sana na binti yetu, yupo katika wakati mgumu sasa na maisha yake yapo hatarini sana, tafadhali..tafadhali mke wangu naomba jitahidi katika hilo.!"'

    Alikurupuka Janet na kuamka kutoka usingizini huku akihema kwa nguvu sana baada kuota ndoto hii.Akiwa ndotoni, janet alimuona mume wake akiwa amevalia mavazi meupi na kumueleza maneno haya kwa msisitizo sana.Katika hali ile ya kukurupuka kutoka usingizini akajikuta akidondoka kutoka kwenye kitanda alichokuwa amelala mpaka chini.Machozi yakawa yanamtoka Janet huku akijitahidi kuita jina la Brian lakini kwa bahati mbaya ilikuwa ni ngumu sauti yake kuweza kutoka na kusikika.Akiwa katika hali hiyo mara Angel naye anafika mahali pale na kumkuta mama yake akiwa anataabika pale chini kwa ajili ya kujiinua kuweza kurudi kitandani.



    Akiwa na binti yake pekee nyumbani, mara Jesca anapata mgeni ambaye alijitambulisha sehemu alipotoka na kueleza dhumuni la yeye kuweza kufika pale.

    " Habari ya hapa mama?" Alisalimia yule mgeni baada ya kukaribishwa ndani.

    "Nzuri kaka, tukusaidie nini?"

    "Kwa majini naitwa Steven Dawson.Samahani mama, hapa ndipo mahali anapoishi binti aitwaye Angel?" Aliuliza yule mgeni na kumfanya Jesca au mama Beatrice ashtuke na kujiuliza kidogo maana hakuelewa kwanini yule mgeni anamuulizia Angel.



    "Bila shaka kaka, hapa ndipo mahali anapoishi huyo binti unayemuulizia."

    "Asante dada, mimi ni daktari ambaye nilikuwa nafanya kazi na marehemu Dk.anthony sehemu moja, hivyo nimefika hapa kwasababu kuna fomu ambazo zililetwa pale hospitali kutoka nchini Uingereza kwa ajili ya binti aitwae Angel kuhusiana na udhamini wake."

    "Udhamini!, samahani kaka naomba unifahamishe kidogo, huo ni udhamini wa nini!?"

    "Huu ni udhamini wa masomo ambapo marehemu Dk.Anthony alimtafutia Angel kwa ajili ya kumsaidia katika kusoma kwake.Hivyo fomu hii anatakiwa aijaze vizuri, yakiwemo majina yake kwa usahihi pamoja na kuweka picha yake kisha hapo chini ya fomu kuna maelekezo jinsi ya kuituma kupitia mtandao."

    "Ooh!, basi sawa kaka na pia nashukuru sana maana naamini ufadhili huu ni msaada mkubwa kwa binti yetu Angel katika kuweza kukamilisha ndoto zake siku zijazo kupitia elimu." Huku akiwa antabasamu, alizungumza Jesca na kumueleza yule mgeni.Muda wote wakati mazungumzo hayo yakiwa yanaendelea, Beatrice yeye alikuwa amekaa pembeni ya mama yake akishuhudia.

    Maneno aliyokuwa anayatoa kinywani kwake Jesca yalikuwa hayaendani kabisa na dhamira aliyokuwa nayo moyoni mwake, ila alizungumza vile ili kumridhisha yule daktari aliyeleta taarifa ile.Baada ya Dk.Steven Dawson kuweza kufikisha ujumbe ule na kuondoka, Jesca akaichukua ile fomu na kuijaza majina ya mtoto wake mpaka Beatrice akabaki anashangaa maana hakuelewa kusudio la mama yake kuamua kufanya vile.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kila alipomkumbuka marehemu Dk.Anthony, huzuni ilizidi kumtawala Janet na kibwa zaidi lililokuwa linamuumiza vilivyo moyoni mwake, Dk.Anthony amekufa bila ya hata kumueleza ni wapi alipo mtoto wake na ukizingatia amebahatika kukaa nae wiki mbili tu baada ya kumzaa.Kila alipoyakumbuka haya na maneno ya marehemu mume wake yaliyokuwa yanamjia ndotoni mara kwa mara, machozi yalizidi kububujika kutoka machoni mwake.

    "Nahuzunika sana mama ninapokuona katika hali hii kila wakati, mimi natumaini Ipo Siku Tu mungu ataweza kukuangaza na wewe, naomba usilie mama yangu." Alizungumza Angel kwa sauti ya upole na kumueleza mama yake, Janet nae akamkumbatia Angel kuonyesha anakubaliana na maneno anayoambiwa na binti yake.

    "Japokuwa Anko Anthony alinieleza kuwa nisimwambie mtu yoyote mahali ulipo wewe, ila mama nimeona ni heri nikamueleza Anko mmoja ambaye amenisaidia mimi baada ya Dk.Anthony kuondoka ili aweze kukusaidia na wewe pia.Naomba mama ugeuke kutazama kule mlangoni ili uweze kumtambua Anko Nea ambaye ameniahidi atatusaidia mimi pamoja na wewe kama vile alivyokuwa anafanya Anko Anthony." Alizungumza Angel kwa umaridadi mkubwa na kumueleza mama yake, Janet naye akageuka kutazama katika mlango wa kuingilia pale ndani ambapo kwa muda huo kulikuwa na mtu akiingia mahali pale.Alipigwa na butwaa na kushangaa sana baada ya kumshuhudia mume wa wifi yake ndiyo aliyekuwa anaingia pale.Nelson akasogea hadi karibu na kitanda alichokuwa ameketi Janet pamoja na Angel huku akishindwa kuamini kama ni kweli leo ameweza kumuona shemeji yake kwa mara nyingine.Akamsalimia kwa kumpa mkono huku imani ikimuingia moyoni mwake kutokana na hali aliyokuwa anamuona nayo.

    "Shemeji!, kumbe ni kweli bado upo hai!?" Aliuliza Nelson kwa mshangao maana akilini mwake alikuwa akidhani kuwa Janet hayupo tena katika ulimwengu huu baada ya kumtafuta sana bila mafanikio ya kumuona wala kumpata.Janet hakuwa na jibu lolote zaidi alibaki akiendele kulia tu.

    "Pole sana shemeji yangu kwa wakati huu mgumu unaoupitia ila kwakuwa upo hai, mimi nakuahidi nitajitahidi kukusaidia kadri ya uwezo wangu ili siku moja nawe uweze kuipata furaha yako." Alizungumza Nelson na kumueleza Janet.

    Kwakuwa hakuwa na uwezo wa kujibu kwa kuongea, Janet akachukua karatasi nyeupe na kuandika ujumbe ambao alimkabidhi Nelson ili aweze kuusoma.

    "'Sina muda mrefu nami nitamfuata mume wangu kule alipoenda, lakini naomba shemeji kabla ya ilo kutokea, nikutanishe na mwanangu ili niweze kumuona hata sura yake tu.Huo ndio msaada pekee naomba unisaidie"' ulikuwa ni ujumbe ulioandikwa katika karatasi.Baada ya kusoma ujumbe huu, Nelson alihuzunika sana moyoni mwake na kumuonea huruma Janet maana alionekana kukata tamaa kabisa ya yeye kuendelea kuishi.

    " Hukuna haja ya kukata tamaa kwa haya yote unayoyapitia maana Mungu ni wetu sote na amini shemeji yangu Ipo Siku Tu huruma yake itakuangukia na wewe pia." Aliongea Nelson kwa lengo la kumfariji na kumtia moyo Janet.

    Muda wote huo Angel alikuwa metulia kimya tu huku akishangaa na kujiuliza mbona kama mama yake pamoja na Anko Nea wanafahamiana.



    "Mbona mama unaandika jina langu katika hiyo fomu ya Angel, si anatakiwa yeye ndiyo aijaze!?" Beatrice alimuuliza mama yake kwa mshangao mkubwa baada ya kumshuhudia mama yake akijaza majina yake fomu ya udhamini aliyoletewa Angel.

    "Hii bahati ni ya kwako wewe mwanangu na sio ya Angel, hivyo mwanangu wewe ndiye utakayekwenda kusoma katika shule hii kubwa na usije kumwambia mtu yoyote jambo hili." Aliongea Jesca kwa msisitizo mkubwa na kumueleza binti yake.

    "Hapana mama!, hiyo ni kwa ajili ya Angel sasa inakuwaje mimi ndio niende wakati mwenyewe yupo!?"

    "Kelele wewe mtoto!, yote haya nayafanya kwa ajili ya faida yako, sasa ole wako nikusikie unafungua mdomo wako na kumueleza mtu yeyote kuhusiana na ili!" Alizungumza Jesca na kumfokea kwa ukari binti yake baada ya kumuhoji maswali kutokana na lile alilokuwa analifanya.



    Ikiwa ni siku nyingine tulivu, Nelson akiwa nyumbani aliendelea kufikiria hali aliyomuona nayo shemeji yake na kubwa zaidi ambalo lilikuwa linaumiza ufahamu wake vilivyo, ni lile ombi ambalo Janet alimuomba amsaidie kumtafutia mtoto wake.

    Alifikiri sana Nelson maana yeye alikuwa akifahamu kuwa mtoto wa Janet alikufa mara tu baada ya kuzaliwa, sasa iweje Janet amuombe msaada wa kumsaidia kumtafuta na kumkutanisha na mtoto wake, kila alipoyafikiri hayo ndipo Nelsoni alipozidi kujiuliza maswali mengi zaidi.

    "Anko!, Anko Nea!..Anko Nelson!?"

    "M..mm!, ndio Angel!" Alijibu Nelson kwa mshtuko kidogo baada ya kuitwa na Angel zaidi ya mara moja bila ya kusikia kutokana na kuwa mbali kimawazo.

    "Inaelekea fikra zako zipo mbali sana Anko, unifikiri kuhusu nini!?"

    "Hahaha!, hakika unanifurahisha sana Angel, yani sijawai kuona binti mdadisi kama wewe." Alijibu Nelson huku akitabasamu na kuzidi kufurahi.

    "Kweli Anko, kila ninapokutazama nakuona haupo sawa kabisa siku ya leo, je una tatizo lolote linalokusumbua Anko?"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Oooh!, ni kweli binti yangu, kuna jambo moja muhimu sana nalifikiria."

    "Jambo gani ilo Anko?, pengine naweza nikakusaidia kimawazo."Alizungumza Angel, naye Nelson akawa tayari kumshirikisha jambo linalomtatiza.

    "Wakati jana tukiwa pale hospitali, yule mama yako aliniomba nimsaidie jambo ambalo ni gumu sana upande wangu.Shemeji Janet ameniomba nimkutanishe na mtoto wake wakati mimi nafahamu mwanae alifariki mara tu baada ya yeye kumzaa."

    "Hapana Anko, amekueleza hivyo kwakuwa anatambua mtoto wake hajafa.Pia fikra zake ni za kweli kwakuwa hata mimi natumbua mtoto wake ni mzima." Alisema Angel na kumueleza mjomba ake.

    Nelson alishtuka sana baada ya kusikia jibu ili kutika kwa Angel, akamtazama vizuri usoni ili aweze kuona kama aliyokuwa anayaongea alikuwa anamaanisha au anatania lakini Angel alieleza yale kwa utulivu mkubwa kwakuwa alikuwa akiyafahamu anayoyaongea.Nelson akahitaji kumuhoji zaidi Angel kuhusiana na lile, lakini kabla hajauliza chochote mara Beatrice akiwa ameambatana pamoja na mama yake wanaingia pale ndani.Nelson akakatisha maongezi yale kisha akamkaribisha mkewe pamoja na binti yake.

    "Nimerudi muda mrefu sana lakini ni Angel pekee niliyemkuta hapa nyumbani, mlienda wapi?" Nelson aliwauliza Beatrice pamoja na mama yake baada ya kusalimiana nao.

    "Nadhani hili nitakalokueleza utarifurahia sana mume mume wangu, binti yetu Beatrice ameweza kupata wadhamini watakaomfadhili katika masomo yake mpaka atakapomaliza hivyo tulienda kwa ajili ya kulifuatilia hilo na tumshukuru Mungu maana kila kitu kimeenda sawa."

    "Waooo!, hongera dada Beatrice hilo ni jambo jema sana na zaidi tumshukuru Mungu maana hata mimi kesho naelekea kumuona Dk.Steven ili nikafuatilie fomu za udhamini wangu alionitafutia marehemu Anko Anthony kama zitakuwa zimeshatumwa." Aliongea Angel kwa furaha na kumpongeza Beatrice kwa kuweza kupata udhamini katika masomo yake.

    Alipozungumza na kugusia kwenda kuonana na Dk.Steven, Beatrice pamoja na mama yake wakatazamana maana walikuwa wakifahamu kuwa Dk.Steven alishakuja pale nyumbani na kuzileta fomu zake.Baada ya kumaliza maongezi yale, Mama Beatrice akamchukua mtoto wake na kwenda nae maeneo ya jikoni ambapo kulikuwa hakuna mtu yoyote sehemu hiyo na kumueleza kitu cha kufanya ili aweze kumzuia Angel asifanikiwe kuonana na Dk.Steven.



    Maneno aliyoelezwa na Angel, yalimfanya Nelson afarijike ndani ya moyo wake maana alihisi kama kweli mtoto wa Janet atakuwa yupo hai, basi Angel pekee anaweza akamueleza sehemu alipo.

    Nelson alitafuta nafasi na kumvuta Angel chemba kidogo ili aweze kumuuliza ni wapi alipo mtoto wa Janet.Angel naye alipoulizwa hakuona sababu ya kumficha lolote Anko Nea na akamueleza ukweli wote anaoufahamu kuhusiana na lile.Angel alimueleza Anko Nelson kuwa siku moja wakati akizungumza na marehemu Dk.Anthony, alishawahi kumueleza kuwa Janet anaye mtoto ila hakuhitaji kumfahamisha kwa wakati ule kwasababu alikuwa akihofia usalama wa Janet pamoja na huyo mtoto wake.

    Baada ya kufahamishwa na kuelezwa hili, Nelson akabaki ameduwaa sana huku akimtazama Angel usoni vilivyo maana alishaanza kuhisi pengine Angel ndiye anaweza akawa ndiye mtoto mwenyewe anamyemtafuta huku akijieleza yawezekana ndio maana siku zote marehemu Dk.Anthony alikuwa akimchukulia uangalifu mkubwa sana.

    Nelson hakuhitaji kumuuliza zaidi Angel kuhusiana na lile zaidi akilini mwake aliona ni vyema siku inayofuata ataelekea hospitali ili akaonane na daktari ambaye alikuwa ni rafiki wa karibu sana na marehemu Dk.Anthony akihisi pengine anaweza kumthibitishia lile analolifikiri.



    Baada ya kufahamu mahali alipohifadhiwa shemeji yake, kila wakati alipopata nafasi Nelson alijitahidi kwenda kumtembelea huku jambo lile yeye pamoja na Angel wakilifanya kuwa siri yao bila ya mtu yoyote kutambua.

    "Habari shemeji, wajionaje na hali tena?" Nelson alimsalimia Janet huku siku hii akiwa na furaha sana moyoni mwake.Janet naye akamshika mkono shemeji yake kuonesha ameipokea salamu ile.

    "Ahsante shemeji.Leo nina furaha sana kwasababu kuna habari njema ambayo nimekuja kukueleza, naamini hutoamini kwa hili nitakalokueleza." Aliongea Nelson na kumfanya shemeji yake awe na shauku ya kutaka kuisikia habari hiyo njema aliyoletewa.



    Alifika hospitali Angel na kusalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa pale hospitali maana wengi walikuwa wakimfahamu kama mtoto wa marehemu Dk.Anthony kutokana na ukaribu uliokuwepo hapo awali kati yao, wakati Dk.Anthony angali bado akiwa hai.Baada ya kusalimiana na baadhi ya wafanyakazi na watu mbalimbali, Angel akaelekea hadi katika ofisi ya Dk.Steven Dawson, daktari ambaye alikuwa ni rafiki mkubwa wa marehemu Dk.Anthony.Alipofika pale ofisini na kufungua mlango, kitu ambacho alikishuhudia kilimshangaza na kumduwaza sana Angel maana hakutegemea kama ataweza kuona kile anachokiona pale ofisini kwa Dk.Steven.



    >>> HAPO SASA ..Mimi sina mengi zaidi napenda kukusihi usikose sehemu ijayo maana yapo mengi yanoyokuja kupitia riwaya hii.

    Kwa wale wanaohitaji kuipata simulizi hii yote kwa mara moja, unaweza kuwasiliana nami kupitia mawasiliano yangu ya hapo chini ili nikupe utaratibu wa kuipata.



    Alishangaa sana Angel pale alipotua kutazama macho yake na kumshuhudia Beatrice pamoja na shangazi yake wakiwa wapo pale ofisini kwa Dk.Steven.

    "Karibu binti yangu, mbona umeishia kusimama hapo mlangoni?, njoo huku maana ujio wetu hapa ni kwa ajili yako." Alizungumza Jesca kinafiki na kumtaka Angel asogee mahali walipoketi wao.

    "Yani sasa hivi tu nilikuwa nakuwaza binti yangu, heri umefika hapa muda muafaka maana ujio huu tuliojia hapa ni kwa ajili ya kufuatilia udhamini wako ambao dada yako hapa alishanieleza kila kitu." Aliendelea kuzungumza Mama Beatrice.

    "Asante shangazi kwa mema yote haya unayonifanyia hakika Mungu akuzidishie sana katika maisha yako." Aliongea Angel kwa hekima ya hali ya juu na kumueleza shangazi yake.

    "Karibu sana Angel, na umefika muda muafaka maana muda si punde nilikuwa nazungumza na shangazi yako hapo kuhusiana na udhamini wako.Tangu juzi mpaka kufikia siku ya leo asubui nilikuwa najitahidi kuwasiliana na wafadhili wako lakini nasikitika kukwambia kuwa wale wafadhili wameamua kusitisha ufadhili wao na hii ni kwasababu kuna taarifa za kwako ambazo marehemu Dk.Anthony alikuwa bado hajazituma kwao." Dk.Steven alimtaarifu Angel yaliyojiri kuhusiana na udhamini wake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zilikuwa ni taarifa za simanzi sana kwa Angel na ambazo hakutarajia kuzikuta mahali pale.

    "Hapana Dk.Steven!, nakumbuka mara ya mwisho nilipozungumza na Dk.Anthony, aliniambia kila kitu alikuwa ameshakikamilisha na ilibaki atumiwe fomu tu ambazo ilinipasa mimi pamoja na yeye tuzijaze, sasa iweje leo wasitishe ghafla namna hiyo!?" Alizungumza Angel kwa uchungu sana huku macho yake yakianza kudondosha machozi.

    "Kweli binti yangu, jambo hili limetuumiza sisi sote lakini haina jinsi zaidi tukakabiliana nayo na tumuombe Mungu pengine ataweza kukufungulia mlango mwingine wa mafanikio." Alizungumza mama Beatrice huku akimkumbatia Angel kwa ajili ya kumtuliza.

    Jinsi Angel alivyokuwa anahuzunika na kulia, Dk.Steven alishindwa hata kumtazama usoni maana hata yeye aliguswa sana na lile japokuwa ilikuwa ni ngumu kwake kuweza kukataa kiasi kikubwa cha fedha ambacho alikabidhiwa na mama Beatrice kuweza kufanya mabadilisho yale aliyoyafanya.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog