Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

JAMANI MCHUNGAJI !! - 3

 





    Simulizi : Jamani Mchungaji !!

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Mama mchungaji anaingilia ugomvi anaohisi kama unamuhusu,anauvua umama mchungaji na kuivaa shari.

    Oscar na Noela wamenogewa na penzi la kiwiziwizi wanalomwibia Timoth aliyetoweka jijini Dar na kwenda Mwanza kikazi lakini Noel anahofia kupata mimba

    E N D E L E A.

    "aah! Noela kwani wewe siku zako hujui zinavyokwenda?" Oscar alihoji.

    "najua lakini huwa nakosea siku nyingine mfano pale kwenye zizi la n'gombe siku ile usiku nilikuwa vibaya lakini ulivyoniteka mtoto wa kiume ukaweza kufanya" alijibu Noela huku akianza kumsugua mgongo Oscar ambaye alikuwa anajiamini kama vile ile nyumba ni ya kwake sembuse chumba.

    "usijali baby hatutafanya makosa tena! Sawa eeh!" alijibu kwa upole Oscar na Noela akamuunga mkono.

    Akiwa Mwanza Timoth aliendelea kuwa katika dimbwi kubwa la mawazo juu ya mkewe kila siku usiku alipokuwa kitandani amelala peke yake imani yake ilimwambia kwamba mkewe yupo na mchungaji kitandani,msimamo wake katika dini ulikuwa umefifia sana

    "kama hawa wanaoitwa wachungaji ndio wanaochukua wake zetu na kuwafanya wa kwao nini maana ya kwenda kuabudu kanisa linaloongozwa na mnafiki mkubwa...jibu ni fupi sana ni heri kuacha kusali kabisa" alijisemea Timoth kwa sauti iliyokwaruzika kwa hasira huku akikanyagakanyaga kitanda alicholalia kwa nguvu akitumia miguu yake. "dawa ya moto ni moto aliniambia Deo nitakuwa mjinga nikipuuzia,we ngoja nikirudi Dar...yaani ngoja nirudi nasema" alishindwa kuzuia kilio chake Timoth akalia kwa uchungu wote na kutamani hizo wiki tatu zikatike upesi aweze kwenda kulipa kisasi.

    Akiwa ndio anakausha machozi kwa kutumia shuka ya kujifunika simu yake iliita hakuwa mwingine bali mkewe.

    "huyu mshenzi ananipigia simu wakati yupo na jianaume hapo yaani naumia mimi...naumia jamani nyie niacheni" alizungumza kama anahadithia watu huku akiitizama ile simu.

    "hellow mpenzi umelala? Nini mbona simu imeita sana" upande wa pili sauti ya Noela ilimuuliza Timoth.

    "hapana nilikuwa naoga,mimi mzima namshukuru Mungu kwa ulinzi wake,nyie huko wazima?"

    "sisi wazima sana tu japo Oscar aliugua kidogo mafua"

    "ooh! Mpe pole,nitamletea dawa nzuri za kienyeji kutoka Mwanza,bado siku nne nimalize hizo wiki tatu huku"

    "karibu sana mume wangu nimekumis sana"

    "nimekumis pia mpenzi wangu,usiku mwema mamaa"

    "na wewe pia babaa" alimalizia Noela kisha akakata simu.

    "mh! Amesema bado siku nne arudi,tumalizie malizie kwa usongo lakini salama " Noela alimwambia Oscar aliyekuwa kifuani pake akimchezea chezea anavyotaka.

    "dah! Siku nne chache jamani sasa inabidi dozi iwe alfajiri,asubuhi,mchana,adhuhuri,jioni na usiku eti eeh!" alijibu Oscar kwa kibesi.

    ***

    Kama vile watoto wake wa kuwazaa mama mchungaji alifika na kuwafinyangafinyanga wawili hawa waliokuwa wanapigana

    "Mtanieleza leo,mkipenda hapa hapa hadharani na mkiamua mwaweza kufanya hivyo majumbani kwenu" mama mchungaji aliwaambia wawili hao wakati huo mtandio ulikuwa umeanguka tena na kubaki wazi kichwani na usoni.

    "he! Rehema jamani ni wewe kumbe kulikoni tena" Zinduna ndiye aliyekuwa wa kwanza kumtambua akasema hayo.

    "ha! Da Rehema jamani kulikoni" alidakia Ashura ambaye tayari alikuwa amechubuka usoni. Umati uliongezeka kwani burudani ilikuwa imeongezwa ladha na ujio wa mama mchungaji ambae jina lake halisi ni Rehema.

    "jamani Rehema twende basi nyumbani tunaaibika hapa dada Rehema" kwa sauti ya chini Ashura alimwambia mama mchungaji naye akamuelewa taratibu bila kuhoji akawaachia wakaongoza njia kuelekea nyumbani kwao maeneo hayo hayo ya uswahilini.

    "he! Kumbe wanajuana jamani" washakunaku waliokuwa eneo hilo kushuhudia mpambano huo. Kila mmoja alibaki mdomo wazi wakati mama mchungaji,Zinduna na Ashura walivyokuwa wanatoweka ghafla tena kirafiki

    "ni lini mmeniomba pesa nikawanyima? Mara ngapi mmetuma please recharge me nikajikausha eeh! Nawauliza nyie vibwengo msokuwa na haya hata kidogo" mama mchungaji alianza kuongea hayo baada ya kuingia katika kijumba kidogo walichoishi Ashura na Zinduna,midomo yake ilikuwa inatetemeka sana na macho yalikuwa mekundu.

    "ujue shoga hatukuelewi hata kidogo" walisema kwa pamoja Ashura na Zinduna.

    "ambacho hamuelewi ni nini hapo nyie wanafiki mlidhani sitajua?...haya ni shida gani mlipata hadi mkaziuza zile picha chafu nilizopiga wakati ule Maisha club,na Masai club na zile nyingine siku zile kwenye kitchen party Lango la jiji Magomeni" alijaribu kujieleza kwa sauti ya chini kidogo mama mchungaji ili aweze kueleweka mbele ya wawili hawa waliokuwa wanashangaa tu jinsi mama huyu alivyokuwa anapepeta mdomo.

    "jamani jamani jamani,nani huyo anataka kutuchonganisha? Nani huyo anataka kuuvuruga urafiki wetu? Nani nauliza" Ashura alistukia na tayari akawa ameamka kutoka alipokuwa amekaa na kujishika nyonga zake.

    Lilikuwa ni jambo la kushangaza sana na kwa jinsi walivyojieleza hatimaye mama mchungaji akaamini kuwa huenda kweli hawajui lolote.

    "lakini ndo hivyo mwenzenu maji ya shingo tayari yamenifika huyo kijana aliyeleta hiyo barua ametoa maneno makali na kuwa ataisambaza picha yangu mbaya sasa hapo nitafanya nini mnadhani kama sio aibu ya mwaka,ni nyie tu mnaonifahamu kama Rehema huko pote naheshimika kama mama mchungaji hebu jenga picha ya hiyo aibu jamani" aliongea akiwa amekata tamaa kabisa mama mchungaji.

    "wasikutishe sana hao Rehema,cha msingi we onana nao na uwafanyie yale yaliyomsababisha yule diwani amwache mkewe unakuwaje wewe mbona mwoga? Au ndo dini imekukaa kichwani tayari?" alichombeza Zinduna aliyekuwa kimya muda mwingi.

    "kwa hiyo Zinduna una maanisha ni....."

    "ndio namaanisha hivyohivyo" alijibu Zinduna hata kabla mama mchungaji hajamalizia

    "na tena inabidi iwe fasta fasta maana uzito wa hiyo aibu nina imani huwezi kuubeba,utaishia kujiua na sie bado tunakupenda shoga yetu,kuliko kujiua ni bora urudie enzi zako tu" alielezea Zinduna.

    "mh! Kweli nitaweza jamani,imepita miaka kumbukeni" alijitetea mama mchungaji.

    "utaweza tu ujuzi hauzeeki kamwe!!" alisisitiza Ashura.

    ***

    "Nina mimba Oscar" ndio maneno mafupi lakini makali yaliyopenya katika sikio la Oscar kutoka kwa Noela,na ilikuwa imebaki siku moja mwenye mali (Timoth) aweze kurejea tena Dar-es-salaam.

    Hakuweza kuficha hata nukta moja uoga wake wa waziwazi,

    "Noela sasa itakuwaje,au unatania?" aliongea Oscar akiwa amekaa kitako katika kitanda.

    "ndio maana nimekwambia ili tushauriane ehe! Niambie tunafanyaje sasa mpenzi wangu" alijieleza Noela.

    "sina hata jibu moja la kutoa mbele ya suala zito kama hilo isitoshe wewe ni mke wa mtu" alizidi kujikanyagakanyaga Oscar wakati huo yupo mbali kidogo na Noela



    Mama mchungaji anapata ushauri kutoka kwa shoga zake wa zamani wakati hajaolewa juu ya nini cha kufanya ili kujiokoa na skendo iliyokuwa inakuja mbele yake.

    Noela ana ujauzito anaodai ni wa mtunza mifugo wake (Oscar). Wasiwasi mkubwa unampata kijana Oscar kwani bado siku mbili mwenye mali (Timoth) anarejea kutoka Mwanza.

    ENDELEA.

    "kwa hiyo Noela nitafanyaje mimi hapo unadhani...eh! nitafanyaje?" Oscar alimuuliza Noela kwa sauti iliyotetemeka kwa uoga.

    "kwa kweli hatuhitaji kukurupuka katika hili inabidi tujipange sawasawa" alijibu Noela.

    "tujipange? Huo muda wa kujipanga uko wapi? Timoth anarudi sijui keshokutwa utamficha kwa staili gani?"

    "haya we hilo niachie mimi na hofu ondoa cha msingi uwe thabiti sana na utoe ushirikiano" alijieleza Noela huku akitabasamu kwa mbali,Oscar hakumwelewa.

    "sasa si uniambie huo ushirikiano nijue mapema kwa sababu Timoth akija sitapata muda wa kuongea na wewe kama ninavyofanya hapa"

    "ushirikiano wenyewe ni ujiandae kulea mwanao!" alijibu Noela.Ni kama vile jibu lile lilimtia ganzi Oscar,aliamini kama Noela alikuwa hana utani basi labda hakumsikia vizuri.

    "yeye ni bosi wangu,sina hata chumba cha kupanga,kamshahara kote natuma nyumbani,sasa nitaanzia wapi mie kuhudumia mtoto,nimekwisha mie Oscar na tamaa zangu,ah! Lakini mimi sikutamani si alinilazimisha kufanya ah! Ona sasa" alisema kimoyomoyo Oscar huku uso wake ukiwa umejawa na simanzi,haikuwepo furaha hata kwa mbali.

    "Noela hivi unanipenda kweli?"

    "ningekuwa sikupendi ningekubebea huu mzigo"

    "he! Kumbe umefanya maksudi Noela jamani sasa ndio nini hicho?" alilaumu Oscar.

    "nimebeba bahati mbaya lakini nitailea maksudi Oscar nimekwambia ondoa hofu" alizidi kusisitiza Noela hakujua ni jinsi gani Oscar alikuwa amejawa uoga kwa tukio la kumpa mimba bosi wake ambaye alikuwa kwenye ndoa tayari.

    "najua atatoka huko Mwanza na mahamu yake na mimi bila hiyana nampa hivyo hivyo,akijichanganya tu hii kitu inakuwa ya kwake kwa muda lakini ni yako milele" Noela alimwambia jambo hilo Oscar,ambapo kwa upande fulani lilisaidia kurejesha furaha japo kidogo.

    "ngo ngo ngo ngo" ulisikika mlio huo kutokea sebuleni wakati Noela akiwa amekumbatiana na Oscar.

    "he! Nani tena huyo" Noela alijiuliza haikuwepo kawaida ya kupata wageni katika nyumba yao tena ilisikika hodi iliyorudiwa rudiwa kuonyesha msisitizo.

    ***

    Mama mchungaji aliondoka mitaa ya Temeke akiwa bado mwingi wa mawazo,mawazo yaliyohitaji umakini mkubwa katika kuyatatua. Katika mkoba wake alibeba kifurushi cha zana za kazi alizopewa na shoga zake Zinduna na Ashura,alikuwa hata hajafungua kuangalia kulikoni humo ndani.

    Majira ya saa kumi jioni mama mchungaji alikuwa tayari amerejea kwake.

    "sina njia ya ziada lazima nifanye kama walivyonishauri wenzangu labda ndio ponea yangu" mama mchungaji alijisemea wakati anaitua pochi yake kubwa kitandani.

    "ngoja niwapigie waheshimiwa" taratibu mama mchungaji akachukua simu yake iliyosalia na kupiga namba alizopewa na Desmund siku ile kanisani.

    "halo,nani mwenzangu" upande wa pili ulipokea na kuhoji. Mama mchungaji hofu ikamtanda akashindwa kujitambulisha.

    "we nani tafadhali namba yako ni mpya huku kwangu" sauti iliendelea kuhoji.

    "ha ha ha ha ha ok! Hata kama hutaki kujitambulisha najua wewe ni mama mchungaji" kicheko na maelezo kutoka upande wa pili vilimshtua mama mchungaji.

    "Mungu wangu amenijuaje!!" alijikuta akisema baada ya kukata simu kwa mshtuko.

    Deo ama Desmund kama alivyojitambulisha kwa mama mchungaji alikuwa amejiandaa ipasavyo na aliamini janja yake itamleta mama mchungaji katika mstari anaoutaka yeye. Namba ya simu aliyoiandika katika kibarua kifupi alichokipeleka kwa mama mchungaji ilikuwa ni mpya kabisa na hakuna hata mtu mmoja aliyeitambua zaidi ya yeye (Deo) na mama mchungaji. Siku zilikatika bila mama mchungaji kupiga simu ile,Deo akaanza kuhisi huenda alikosea kuandika namba katika ile karatasi. Zilipita siku tatu matumaini yakizidi kufifia kuwa huenda mama mchungaji ameushtukia mchezo ndipo majira ya jioni ile simu ambayo alikuwa ameweka lain ya tigo anayoitambua mama mchungaji,mara simu iliita.Deo hakukurupuka kuipokea taratibu akainyanyua na kuhakikisha kuwa mpigaji wa hiyo simu alikuwa habip bali anapiga. Kwa uzoefu wa harakaharaka baada ya kupokea alizisikia pumzi za upande wa pili zilivyopishana kwa kasi."bila shaka ni yeye" alifanya utabiri wake kisha akaongea kwa kujiamini kama vile anamfahamu fika alizepiga hiyo simu.

    Punde tu baada ya kufanya ubashiri wake alishtukia simu imekatwa,akiwa bado anajiuliza nini tatizo hadi simu imekatwa kwa mara nyingine tena iliita simu yake.

    "samahani simu imekatika bahati mbaya"

    "usijali hata kidogo una shida gani" alihoji Deo.

    "mimi ni yule mama wa siku....." alianza kujieleza mama mchungaji lakini kabla hajamaliza alikatishwa

    "nakufahamu vizuri sana,kwa nini umepuuzia maagizo niliyokutumia au ulidhani ni maigizo?" alihoji Deo kwa sauti iliyojaa hasira za kuigiza.

    "samahani baba,nisamehe sasa lini nikutafute,nisamehe baba yangu" alijitetea mama mchungaji

    "baada ya siku tatu nipigie simu nikueleze wapi pa kunikuta,ole wako upuuzie au utoe taarifa yoyote" alitoa karipio Deo.

    "sitapuuzia mheshimiwa tafadhali nioneeni huruma hizo picha mimi nitajificha wapi?" kwa sauti iliyojaa majonzi na iliyobembeleza mama mchungaji alimjibu Deo.

    "utanipa maelezo hayo siku tukikutana" alijibu Deo kisha akakata simu.

    ***

    "Oscar hiyo hodi ni kama ya mume wangu mh! Ingia uvunguni haraka tafadhali ukijidanganya tu kutoka tu,kwisha habari yetu" Noela alimwambia Oscar kwa sauti ya chini,jasho lilikuwa linawatoka kwa sana,kila mmoja alikuwa mdogo kama pilton,hakuna aliyekuwa mjanja mbele ya mwenzake.

    Oscar hakupinga haraka akajiviringisha na kutosha chini ya uvungu wa kitanda walichokuwa wamelalia. Huku hodi ikiwa imetulia sasa,Noela alichukua haraka nguo yake ya kulalia akaivaa na kisha kwa mwendo wa kuigiza kuwa ametoka usingizini alianza kwenda sebuleni ambapo ndio hodi imetokea. Huku uvunguni,Oscar alikuwa hasumbuliwi hata kidogo na vumbi lililojihifadhi uvunguni,uoga uliziba pua zake na kuhisi hilo vumbi halikuwepo hata kidogo.

    "eeh! Mungu niepushe na janga hili mbele yangu" Oscar alijikuta akimkumbuka muumba wake wakati wa matatizo.

    Hatua za kurejea chumbani kwa kunyata zilizidi kumwogopesha Oscar maeneo ya uvunguni alipokuwa."huwa nasoma kwenye magazeti ya udaku juu ya mafumanizi sasa leo ni la kwangu nitakoma" aliwaza Oscar huku akijizuia kuzitoa pumzi zake kwa nguvu.

    "Oscar bora uje mwenyewe tumegundulika tayari mi nilikukataza usije chumbani ukalazimisha" sauti iliyosindikizwa na kilio cha kwikwi ilisikika vyema katika masikio ya Oscar pale alipokuwa,alitamani iwe ndoto lakini ni kweli alikuwa chini ya kitanda cha mke wa mtu.

    "siamini Noela amenisaliti yaani mimi ndio nilimlazimisha!! Dah! Nauwawa leo" aliwaza huku akiwa ameuma meno yake kwa hasira,mikono haikuwa na nguvu tena huku tumbo la kuhara likiwa limemshika tayari.

    "huyu hapa yuko humo humo uvunguni amejificha" ilisikika tena sauti ya Noela kana kwamba kuna mtu pembeni anamwambia. Bila kujizuia papo hapo haja ndogo ikaanza kuchuruzika katika kaptula ya Oscar

    Pensi yake ikiwa imelowana mkojo tayari Oscar alikuwa ameamua kutoka pale uvunguni ili akutane na adhabu aliyotakiwa kupewa na mwenye mali. Macho yake yalikutana na jambo asilolitegemea uso wa Noela ulikuwa umezibwa na kalenda kubwa kiasi ambayo kwenye moja ya tarehe ilikuwa imezungushiwa alama ilikuwa ni tarehe 17 mwezi wa 11. Oscar hakuelewa haraka maana ya tarehe ile hadi Noela alipotoa kalenda usoni huku akijizuia kucheka japo macho yake mekundu yalidhihirisha kwamba ametoka kucheka muda si mrefu.

    "kuna nini Noela"

    "happy birthday to you" alijibiwa

    "kuna nini?" aliendelea kuhoji Oscar.

    "ni siku yako ya kuzaliwa" alijibu Noela na kuangua kicheko kikubwa.

    "na aliyekuwa anagonga mlango ni nani?"

    "ni mlio nilioweka kwenye simu yangu hakuna mtu humu ndani"

    "umeniweza Noela,yaani hadi nimejikojolea mwenzako" kwa sauti ya kinyonge alijibu Oscar huku akijitizama katika bukta yake jinsi alivyoilowanisha,wakati huo Noela alikuwa hacheki tena bali alimwonea huruma Oscar.



    Mama mchungaji ameomba aelekezwe kilipo choo kwani amebanwa na haja ndogo hivyo alihitaji kwenda msalani,bila kusita Deo anamwonyesha choo kilipo,akiwa anajongea kukifuata choo,khanga aliyokuwa amevaa inadondoka huku nyuma Deo anashuhudia shanga,cheni na kiuno kilichosindikizwa na michirizi ya uhondo.

    ENDELEA.

    Deo alijikuta hisia za mapenzi zilizokuwa zinamtawala tangu aone paja la mama mchungaji zilizidi ghafla akajikuta yuko wima akimkabili mama mchungaji aliyekuwa ameinama taratibu akichukua kanga yake,uoga ulikuwa kwa mbali na akajikuta tayari amekikamata kiuno cha mama mchungaji ambaye badala ya kushtuka aligeuka na kuikutanisha midomo yake na ya Deo,kighza tayari kilikuwa kimeanza kutawala pale ndani hivyo kilichangia wawili hawa kutokwa na uoga na aibu. Deo tayari alikwisha sahau mpango kabambe uliokuwa mbele yake hivyo aliamini alichotaka kufanya ni halali yake kabisa. Mikono yake tayari ilikuwa imezunguka katika kiuno cha Mama mchungaji,mapigo ya moyo ya Deo yalikuwa kasi sana joto la mama mchungaji lilikuwa limemchanganya Deo.

    ***

    Kelele za hapa na pale kutoka chumbani zilimvuta Timoth kutaka kujua kulikoni na nini kinatokea humo ndani,giza lililokuwa mbele yake halikumtia hofu sana na aliamini hatua zake za miguu zitakuwa zitakuwa sawa kabisa hadi atakapoufikia mlango wa chumba kile.

    "kuuuu!!!! Kaaaaa!!" ulisika mlio pale chumbani Timoth mbio mbio aliondoka kwa mshtuko mkubwa hakujua ni nini kinatokea pale ndani ulikuwa mlio mkubwa sana.

    "puuu!"ulifuata mlio mwingine na safari hii alikuwa ni Timoth akiwa anasalimia na sakafu baada ya kujikwaa kwenye kochi lililokuwa limepangwa vibaya pale sebuleni. Maumivu makali aliyoyapata yalimsababishia kilio cha kimya kimya,licha ya kujikaza sana ilishindikana alikuwa ameumia sana goti lake pamoja na kifua chake. Akiwa bado anagumia kwa maumivu makali pale chini mara mlango aliokuwa anaufuata kwa ajili ya kujua kulikoni ulifunguliwa baada ya kimya kirefu kuwa kimetawala na hatua za binadamu zikaanza kusikika kuanzia mbali na sasa zilizidi kusikika kusogea eneo ambalo alikuwa ameanguka. Timoth alijaribu kuinuka lakini maumivu yalizidi kumweka pale chini.

    "Timo vipi kaka mbona upo hapa eeh!"

    "kiajali kidogo kaka!" alijibu kwa sauti iliyojaa maumivu baada ya kugundua aliyekuwa anauliza swali lile ni Deo.

    "Pole sana kaka lakini jikaze sasa uamke mambo tayari huko ndani,ebwana! Unasubiriwa wewe tu kuamua mwisho wa mchezo huu" alizungumza Deo kwa sauti ya kunon'goneza,maneno yale ni kama yalitibu majeraha na maumivu ya Timoth japo yaliongeza hasira zaidi kwa mama huyo ambaye aliamini mume wake ndiye anayefaidi mwili wa mkewe (Noela). Kama vile amepigwa shoti ya umeme aliinuka pale na kukaa kitako.

    "hebu ongeza sauti ya redio nikupe mchakato sasa" Deo alimwambia tena Timoth ambaye tayari hamu zilikuwa zimempanda juu ya kulipiza kisasi. Timoth haraka haraka akaongeza sauti ya redio na kusababisha lugha ya kunon'gonezana ikome na kuwapa uhuru mkubwa wa kuongea.

    "nimemwacha yupo pale kitandani sasa ni wewe kwenda kumtoa pale na kumweka chini sakafuni kwa sababu kitanda kile ni kibovu. Umenielewa" alitoa maelekezo Deo yaliyoeleweka vizuri kwa Timoth,kwa mujibu wa saa zao ilikuwa saa tano usiku.

    "mimi hata bafuni sawa tu,nia yangu ni kulipiza kisasi" alijibu Timoth huku tayari akiwa wima.

    "hakuna kuongea neno we ukifika ni shughuli tu sawa" alisisitiza Deo

    "haina tatizo"

    ***

    Deo hakuchukua muda mrefu kuingia katika majaribu joto la mama mchungaji lilimmaliza kabisa akajikuta palepale waliposimama akithubutu kuibanjua amri ya sita,mara wakahamia sakafuni,ujuzi wa mama huyu ulikuwa wa hali ya juu

    "huyu kweli mama mchungaji au mama mfundaji? Mh!" alijiuliza Deo wakati mama mchungaji anamuongoza kuelekea bafuni walipouendeleza mchezo huo,walipotoka bafuni ndipo walipohamia kitandani,Deo sasa naye aliamua kuonyesha ufundi wake katika mambo hayo ili watoe baraka njema katika kitanda kile. Mama mchungaji akiwa amepagawa kabisa na Deo akiwa anajiandaa kumrukia mara kitanda walichokuwa wamelalia kikapata anguko kubwa baada ya chaga za kitandaka kushindwa kubeba uzito ule,mlio mkubwa ulisikika na kumkurupua Timoth aliyekuwa pale mlangoni akitega kusikiliza kinachoendelea. Ilikuwa aibu kubwa kwa Deo lakini mlio aliousikia tena nje ndio ulimshangaza. Mama mchungaji yeye hakuwa na habari alikuwa ametulia tuli akiwa katika ulimwengu mwingine na hata Deo alipotoka nje hakuweza kusikia

    Mama mchungaji hakutegemea shughuli ingekuwa pevu hadi kufikia kiasi cha yeye kupagawishwa kiasi hicho,ama kweli ule usemi kuwa jasiri aachi asili ni kweli tupu isiyokuwa na uongo,mama mchungaji alikuwa amekosa vitu vingi tangu aingie katika ndoa na mchungaji yule. Mapenzi aliyopewa na mchungaji yalikuwa ya heshima tele,hapakuwa na kukuru kakara za hapa na pale,kila walipohitaji kuwa faragha mama mchungaji alikuwa anatakiwa kujitanguliza chini halafu taratibu mchungaji anafuata kwa juu na stori inaishia hapo lakini usiku huu alikuwa ametenda bafuni,sakafuni na kitandani lakini sio kwa staili zile za mchungaji.

    "mh! jamani mie nimeyamis mambo haya kwa nini mchungaji hanipi lakini mwanaume yule?" Mama mchungaji alikuwa anajiuliza wakati akiwa amejilaza palepale katika kitanda kibovu,hakuwa hata na kumbukumbu kuwa bikini yake ilikuwa imechanwa na tayari shanga mbili zilikuwa zimetawanyika kutokana na shughuli pevu. Akiwa bado hajiwezi pale kitandani alisikia mlango unafunguliwa na hatua zikasikika zikijongea pale kitandani. Mama mchungaji aliamini alikuwa ni Desmund (Deo). "please come darling!" alitamka kwa sauti ya kimahaba sana. Bila kupata jibu lolote alishtukia yanatokea mambo kama yanayowatokea wacheza mieleka.

    Alikuwa ni Timoth amewasili ndani ya kile chumba alichoamini kimeandaliwa kwa ajili yake kulipiza kisasi,sauti ya mama mchungaji ilimsaidia kuelewa ni wapi anapatikana kwa kufuata sauti ile alivamia pale kitandani na kumnyanyua,giza lilimpa sapoti kubwa kwani bila hilo huenda angemwonea aibu mama mchungaji . Joto lilipenya katika mikono yake na kusambaa mwili wote. Ulaini wa ngozi ya mama mchungaji ulisababisha mchezo kuanza mapema sana,Timoth hakupoteza muda kuleta longolongo za hapa na pale kwani nia yake ilikuwa kulipa kisasi. "aaai jamani mchungaji!" sauti ya mkewe (Noela) usiku ule alipokuwa anaota ilimjia kichwani mwake na kuleta hasira kali sana iliyomchochea Timoth kumweka mama mchungaji chini kabisa tayari kwa shuguli,bila kusita wala kuleta heshima ya mama mchungaji Timoth alivamia milki ya mama mchungaji na kuanza kufanya mauaji tena ya kinyama sana yale ya kukomesha.

    "umenipa mimba jamani umenipa mimba mie nipo kwenye siku mbaya unaniua jamani mchungaji wangu hana uwezo wa kuzaa jamani nitaumbuka mie aaah! Aaaash!" alipiga kelele mama mchungaji lakini Timoth hakujali kwani aliamini hizo zilikuwa kelele tu za furaha.

    "ntalea mtoto" alijikuta Timoth akitamka bila hata kujua alisemalo,tofauti na mwanzo alivyotegemea kufanya kwa kukomoa ili kulipa kisasi sasa alikuwa akipima ujuzi wa mama mchungaji na mkewe (Noela) katika fani husika ya kitandani."mama mchungaji alikuwa kiboko" hilo ndio lilikuwa jibu.

    ***

    Oscar kama alivyoahidiana na Noela kweli ratiba ilifuatwa vyema kila mara walikuwa katika mahaba mazito zaidi ya asilimia 50 ya maisha yao waliyatumia kitandani katika starehe yao ya kuiba.

    Oscar hakuwa na raha kama mwanzo suala la Noela kuwa na mimba lilimchanganya sana kichwa chake hakuamini kama litakuwa jepesi kama yeye (Noela) alivyochukulia. Oscar aliamini kuwa anacheza katika mdomo wa simba mwenye njaa.

    Licha ya kutokuwa na raha lakini suala la mapenzi yao lilibaki palepale japo sio kwa fujo kama awali.

    "Noela una uhakika utafanikiwa kumficha Timoth kuhusu ujauzito?" Oscar alimuuliza Noela usiku wao wa mwisho kabla ya Timoth kurejea.

    "asilimia zote!!" alitoa uhakika Noela kwa kujiamini kabisa.

    Majira ya saa kumi jioni siku iliyofuata Timoth alirejea tena nyumbani kwake kama alivyokuwa amemwahidi mkewe.

    Alikuwa na furaha kubwa sana kurejea nyumbani kwake lakini furaha yake kubwa zaidi ilikuwa kwa yote aliyoyatenda usiku uliopita jambo la kulipa kisasi lilikuwa sawa na ushindi mkubwa sana kwake.

    "karibu laazizi wangu wa moyoni karibu sana" Noela kwa madaha makubwa huku akimkumbatia mumewe alimkaribisha.

    "asante sana mamaa" alijibu Timoth kwa furaha pia.

    Nyumba ilitawaliwa na utani wa hapa na pale siku hiyo hadi majira ya saa mbili usiku utani ulipohamia pande za chumbani,hakuwa Oscar kwa upande wa Noela wala mama mchungaji kwake yeye bwana Timoth. Leo walikuwa ni mtu na mkewe katika anga za usiku wa mahaba ya kukamiana kwani ni wiki tatu walikuwa hawajaonana,kila mmoja alimwambia mwenzake eti 'amemmisi sana'

    "jamani tangu uondoke napigwa baridi tu hapa nyumbani afadhali umekuja walau na joto litausabahi mwili wangu" alidanganya Noela kwa sauti ya kijasiri wakati huo akiwa anapapasa kifua cha Timoth.

    "mi mwenyewe huko Mwanza palinyesha mvua kwelikweli hadi nikakukumbuka mke wangu kwa hilo baridi lililotanda ndani ya jiji lile" alijibu Timoth na kumpiga kibusu kidogo shavuni.

    Maneno maneno hatimaye taratibu waliyaacha maneno na kuingia katika vitendo. Timoth alikuwa mwingne leo katika kuta za kitanda chao,alimchosha Noela hadi akatoa malalamiko yote na hatimaye kilugha cha kwao.

    "game over" alijisemea kwa sauti ya chini Noela baada ya kugundua iwe isiwe lazima Timoth afanye atakalo yeye (Noela)

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog