Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

JAMANI MCHUNGAJI !! - 4

 





    Simulizi : Jamani Mchungaji !!

    Sehemu Ya Nne (4)



    ILIPOISHIA

    "Game over!" ndivyo alivyosema Noela moyoni mwake baada ya kuhakikisha kuwa Timoth lazima atafanya yeye (Noela) alivyokusudia. Na bila utata ilikuwa kama alivyodhani Timoth alimtenda hivyo.

    ENDELEA.

    Timoth baada ya kuwa amemaliza hasira na hamu zake zote kwa mama mchungaji alitoweka pale chumbani na kwenda kumpa taarifa Deo.

    "nimemaliza kaka,shughuli sio ya kitoto dah! Yule ni mama mchungaji kweli?"

    "ni yeye kwani vipi,ni bwege tu au vipi?" alizuga Deo.

    "hee! Bwege? Nani kasema bwege yaani ni hatari tupu,sijui hata alijifunzia wapi yote haya....tuachane na hayo kaka mimi naingia kulala sasa wewe mwondoe hapa asije kutuletea matatizo bure" alijieleza Timoth kwa sauti iliyokoroma koroma ishara ya usingizi.

    "poa poa ngoja mimi nimtoe sasa we tulia tuli humu ndani" alijibu Deo huku akimpisha Timoth aingie khtandani wakati yeye anatoka.

    Deo alimkuta mama mchungaji akiwa tayari ameingia bafuni na kujimwagia maji,hakuwa na wigi tena kichwani na mavazi aliyabadilisha kutoka katika mkoba aliokuja nao alijitanda kitenge na chini pia palikuwa na kitenge,alikuwa amekuwa tofauti sana na yule aliyeingia mwanzoni. Deo aliyashuhudia hayo yo e baada ya kuiwasha taa ya chumbani.

    "chukua hii upande taksi uende pia kuhusu picha kamwe hatutazitangaza kama awali tulivyoahidi cha msingi uje wiki ijayo uzichukue,lakini kabla ya kuja unitafute kwenye simu" Deo alimkabidhi mama mchungaji pesa taslimu shilingi elfu kumi ikisindikizwa na maneno hayo yaliyorejesha kwa kiasi fulani imani ya mama mchungaji na kuamini ameshinda mtihani uliokuwa unamkabili.

    ***

    Majira ya saa nane na nusu usiku,Noela akiwa chumbani kwake pamoja na mumewe (Timoth) wakiwa hoi kwa shughuli pevu waliyokuwa nayo kila mmoja alikuwa akimwangalia mwenzake anavyohema na kuvuja jasho. Hodi iliyosikika getini iliwashangaza sana ule ulikuwa ni usiku wa katikati kabisa na lilikuwa jambo la kushangaza kupata mgeni wakati ule labda mpita njia aliyepotea.

    "Mh! Noela atakuwa nani tena huyo usiku huu mke wangu?" Timoth alihoji huku akimtazama mkewe kwa mshangao.

    "na mimi nikuulize wewe maana wote tuko hapa ndani tumejifungia" alijibu Noela

    "twende tukamfungulie tujue ni nani labda" alishauri Noela huku akijifunika khanga na Timoth akavaa bukta yake wakaanza kujongea taratibu kuelekea lilipo geti lao iliposikika hiyo hodi.

    "ah! Mchungaji!! Bwana asifiwe sana" Noela alimkaribisha mgeni yule,alikuwa ni Mchungaji Marko,mchungaji wa kanisa lao. Usoni alitawaliwa na hofu kubwa,kijasho chembamba kilikuwa kinamtiririka,dhahiri kuna jambo kubwa na gumu lilikuwa linamkabili. Hofu aliyokuwa nayo mchungaji ilimshtua sana Timoth "Mungu wangu au tayari amegundua nilikuwa na mkewe ooh! My goodness naomba isiwe hivyo....au ndio tabia yao na mke wangu kukutana mida hii?" alijiuliza Timoth,mawazo haya mawili yalifanya kichwa chake kiume sana,na ule muonekano wa mchungaji Marko kujin'gatan'gata na kushindwa kuzungumza ulimtia hasira na kuhisi huenda alikuja hapo kwa ajili ya kufanya uovu na mkewe.

    "aah! Bwana Timoth mbona unarejea kimya kimya bila hata taarifa?" aliuliza mchungaji.

    "ilikuwa bahati tu kufika leo,nilitarajia nitafika kesho hapa lakini niliahidi nitarudi baada ya wiki tatu na ndio hizo zimetimia" alijibu Timoth huku akijaribu kujilinda hasira pamoja na hofu yake isionekane dhahiri.

    "jamani kuna tatizo kubwa limenileta hapa nalo si jingine ni...yaani sijui pa kuanzia lakini kiufupi linashangaza na ni vigumu kuamini....ni mama mchungaji" alijieleza mchungaji Marko. Akiwa bado hajapata jibu alishtukia Timoth analegea na kuanguka chini kama gunia la mahindi

    Baridi kali lililotokana na kimvua kidogo kidogo cha manyunyu kilisabababisha ugumu sana kwa mchungaji Marko kuendelea na shughuli ya kuihubiri injili,nguo zake nyepesi ziliruhusu ile baridi kupenya hadi katika mifupa yake.

    "Mchungaji Isaya tafadhali endelea kuhubiri mimi nitumie pikipiki yako mara moja niende nyumbani nikachukue koti langu,hali yangu sio nzuri" mchungaji Marko alimweleza mchungaji mwenzake huku meno yakigongana kinywani kwa sababu ya baridi.

    "ooh! Pole sana mtu wa Mungu,pole sana,funguo za pikipiki hizi hapa nakutakia safari njema na Mungu akutangulie huko njiani" mchungaji Isaya alimjibu mchungaji Marko huku akimkabidhi funguo za pikipiki.

    Haraka haraka ili kwenda na muda mchungaji alitembea upesi akikatiza katika kundi la waumini waliokuwa katika mkesha huo,hadi akaifikia pikipiki na kuipanda tayari kwa safari. Kwa mwendo wa wastani ulio salama kabisa mchungaji aliendesha hadi akaifikia nyumba yake mlangoni kabisa na kwa kuepusha usumbufu kwa mkewe hakupiga honi bali alijongea hadi dirishani na kuanza kuita kwa sauti ya chini."mama,mama,mama,mama" alijaribu kuita mara nyingi lakini hakupata jibu ndipo akaamua kuanza kugonga dirisha taratibu hadi akachoka mkono.

    "mh! Anausingizi gani leo huyu mtu wa Mungu" mchungaji alijiuliza bila kupata jibu lenye uhakika. Akaamua kutumia honi ya pikipiki lakini bado hakupata jibu,alijaribu kutikisa mlango lakini bado hakupata jibu lolote.

    Wasiwasi ulimpata na alipojaribu kuchungulia ndani aliweza kuona pale kitandani kama kuna uwepo wa mkewe,kwa akili iliyofanya kazia aliamini kulikuwa na tatizo kubwa linamsibu mkewe mle ndani. Haraka aliiwasha pikipiki na safari ikaanza kwenda kwa Noela ambapo aliamini ndio wapendwa waliopo jirani naye wanaoweza kumpa msaada kwa tatizo hilo. Kwa wakati huu mwendo uliongezeka kidogo,na alipishana na teksi ikiwa imepaki hakujali hata kidogo wazo na lengo lake lilikuwa kufika haraka nyumbani kwa Noela na kuona kama anaweza kupata msaada wowote.

    Mama mchungaji akiwa ndani ya teksi aliyokuwa ameikodisha kuweza kumfikisha nyumbani kwake aliweza kushuhudia ule mwanga wa taa ya pikipiki hivyo kwa tahadhari kubwa alimsihi yule dereva kusimamisha mara moja gari yake hadi pale atakapomruhusu tena. Kwa jicho lake alitumia sekunde chache sana kutambua umbo la mwanaume aliyeshuka katika pikipiki kuwa ni mumewe yaani mchungaji Marko. Roho ilimdunda sana,harufu ya fumanizi ilianza kunukia kwa ukaribu kabisa "Yesu wangu,anaenda kuchungulia!" mama mchungaji alijikuta kwa sauti iliyosikiwa na dereva akisema hayo.

    "kwani vipi mama?" alihoji dereva.

    "mh! Wala hamna kitu eeh! Amna kitu" alijibu mama mchungaji kwa hali ambayo hata mtoto mdogo angejua anadanganywa.

    "au unamfahamu huyo mtu!" aliongeza swali yule dereva.

    "nimekwambia hamna kitu,hivi wewe wajibu wako ni kunifikisha ninapotaka au kujua ninachofuata,mbona adabu zinakushuka we mtoto" alifoka mama mchungaji na yule kijana akatulia tuli baada ya kuomba msamaha.

    "yaani umenin'gan'gania kama kupe,looh! Huna haya we mwanaume yaani kama vile mpelelezi kah! Hukawii kuniuliza kama nimezaa au bado we kiumbe" aliendelea kumwaga maneno mama mchungaji huku jicho lake likiwa makini kumtazama mchungaji anachofanya pale nyumbani.

    "nisamehe mama yangu! Nimepitiwa" aliomba radhi tena.

    "we we we we! Nitake radhi tena nitake radhi kabisa,nani mama yako hapa nani mama yako nauliza eeh!" aliongeza sauti mama huyu kwa ghadhabu ambazo hata dereva hakuelewa chanzo chake kwani muda wote walizungumza vizuri hadi hapo walipofika.

    Jitihada za mchungaji zilipogonga mwamba,mama mchungaji alimshuhudia akipanda pikipiki na kuanza kusogea pale walipo,kama vile mchezaji wa mchezo maarufu Afrika kusini,India na Uingereza mchezo wa 'rugby' mama mchungaji alijirusha jini ya siti za nyuma akiachia miguu juu juu. Dereva alibaki ameduwaa alìhisi kuwa yule mama amechanganyikiwa.

    "mwanangu hiyo pikipiki imepita?" kwa sauti kama vile ameinamia kwenye mtungi mama mchungaji aliuliza.

    "nani mtoto wako hapa we mama wewe si umekataa kuitwa mama hebu shuka garini kama umefika" alijibu kwa jeuri yule kijana wakati huu.

    "samahani jamani,nisaidie akikuuliza mwambie mi mgonjwa au...." alijieleza mama mchungaji lakini hakumalizia kauli yake ndio yule dereva akamwambia tayari pikipiki imepita. Mama mchungaji kwa tahadhari kubwa akakaa kitako na kumruhusu dereva amfungulie mlango aweze kushuka,mlango ulipofunguliwa mama mchungaji alilipa pesa iliyokuwa inahitajika na kama vile mzoefu wa kukimbia riadha akafyatuka hadi karibia na mlango lakini mara akarudi tena mbio hadi katika teksi ambayo bado mlango ulikuwa wazi na kuchukua funguo kisha kwa kasi ile ile akarejea pale nyumbani akimwacha dereva mdomo wazi.

    "aah! Dunia ina mambo na sisi madereva ndio tunaona" alijiongelea yule dereva huku akifunga milango na kugeuza gari kisha akatoweka.

    ***

    "Oscar,Oscar njoo utusaidie,njoo haraka jamani" alipiga kelele Noela baada ya Timoth kuwa ameanguka pale chini,Oscar alikuwa macho muda wote tangu mchungaji anaingia pale ndani masikio yake yalikuwa wima kusikia na kutaka kujua kulikoni mida ile hodi pale nyumbani. Aliposikia jina lake alikurupuka kutoka katika chumba chake na kumfuata Noela.

    Oscar alitii sauti kuu ya Noela iliyokuwa inamuita kutoka nje,ndani ya sekunde chache tayari alikuwa mbele ya Noela na mchungaji Marko. Mchungaji Marko alikuwa kama chizi kwani alikuwa hana la kufanya na wote walikuwa wanamuangalia Timoth pale chini kama vile luninga.

    "jamani kuna nini?" alihoji Oscar.

    "ameanguka tu hata hatujui tatizo" alijibu Noela. Oscar hakusubiri kuuliza tena alitimua mbio hadi katika pipa la maji akateka ndoo moja na kuja nayo kasi "pwaaa!" akamwagia Timoth na palepale akasimama na kuanza kuzungusha macho huku na kule kama vile ametoka usingizini.

    "jamani mume wangu nini tatizo kipenzi,mchungaji hamwoni mkewe nyumbani na mlango umefungwa wewe tena wataka kutuongezea tatizo darling tatizo ni chakula au?" alihoji Noela akiwa amepiga magoti mbele ya mumewe aliyekuwa amekaa chini.

    Timoth aliposikia neno kuwa tatizo kuwa ni mama mchungaji hakuwepo nyumbani walau hofu ikapungua kwani mawazo yake ya mwanzo kuwa huenda mambo yote hadharani ndio chanzo cha kuzimia kwake. Taratibu Timoth akasimama wima bila kuzungumza neno.

    "wajionaje na hali sasa" aliuliza mchungaji ambaye muda wote tangu Timoth azinduke alikuwa katika maombi mazito ya kumshukuru Mungu kwa muujiza wake wa kumnyanyua tena Timoth juu.

    "bwana ni mwema,najisikia vyema" alijibu Timoth kwa sauti ya chini.

    "ok! Basi mimi nadhani kama wajisikia vyema sote tuongozane mkanisaidie kutatua tatizo linalonisibu pale kwangu" alipendekeza mchungaji.

    "mh! Itakuwa vipi tukifika halafu na mama mchungaji afike,hivi imekuwaje Deo amechelewa hivyo kumrudisha? Na mimi siamini kabisa kale kagiza pale ndani eti hawezi kuwa aliniona sura mh! naweza kujitafutia matatizo hapa" aliwaza Timoth badala ya kujibu.

    "jamani mimi kwa kweli sidhani kama nitafika nahisi kizunguzungu kwa mbali,naomba muongozane na Oscar pamoja na Noela naamini halitaharibika jambo" alitoa pendekezo Timoth ambalo lilikubalika mara moja,Noela akaingia ndani akajitanda vitenge na Oscar akavaa sweta pamoja na suruali ya jeans wakaondoka huku mchungaji kwa mara ya kwanza akikiuka sheria na kupakiza watu wawili nyuma kama wafanyavyo 'boda boda' wa pikipiki katika miji.

    Ndani ya dakika kumi tayari walikuwa mbele ya nyumba yake,hali ya utulivu ilikuwa ileile,Oscar na Noela walijaribu kufanya kama alivyofanya awali mchungaji,waligonga dirishani na kuita mama mchungaji lakini hawakupata jibu lolote. Wakiwa wamekata tamaa na kuamini kuwa aidha mama mchungaji hakuwa ndani ya nyumba au amekumbwa na maswaibu makubwa humo humo ndani.

    "inabidi tuvunje mlango!" alitoa hoja mchungaji mbele ya Noela kwani Oscar bado alikuwa anahaha hapa na pale kutafuta ufumbuzi.

    "huyu hapa,yumo yumo nadhani anaumwa!" alipiga kelele Oscar akitokea katika upande mmoja wa nyumba,mbio mbio Noela na mchungaji walifuata kwa nyumba,ni kweli macho yao yalimshuhudia binadamu akiwa sakafuni akiwa na mahangaiko fulani na alikuwa akijigalagaza chini. Wakati huu mchungaji hakutaka ushauri aliuvamia mlango na kuupiga teke moja palepale kitasa cha ndani kikakubali kuachia wote wakaingia.

    "mama mama mama umekuaje ni nini lakini?" alihoji mchungaji huku akijaribu kumzoazoa mama mchungaji kutoka pale chini.

    "naumwa! naumwa nipeleke hospitali" alilalamika kwa sauti ambayo ilimsikitisha kila mtu na kuamini kuwa maumivu aliyokuwa nayo mama mchungaji yalikuwa makali sana.



    Timoth imani yake bado ilikuwa ndogo na ilimwambia kuwa huenda mchungaji ametumia ile janja kupata nafasi tele ya kujiachia na mkewe.

    "ngoja nifanye fumanizi leo,yani kila siku nayasoma gazetini" aliongea Timoth huku akishuka kutoka pale kitandani alipokuwa amejilaza bila kupata hata lepe la usingizi. Kwa ujasiri uliotiwa hamasa na wivu uliokithiri Timoth hakuogopa kitu alipiga hatua kwa hatua hadi akaifikia nyumba ya mchungaji.

    "wakiniuliza jibu lipo tayari,nimekuja kuangalia hali zenu na hali ya mama mchungaji" aliwaza Timoth.

    Masikio yake na macho havikumdanganya hata kidogo,macho yalishuhudia vivuli vya watu wawili wakiwa wamekumbatiana huku masikio yakisikia miguno ya kimahaba.

    Moyo uliumia sana,hasira zilimpanda ilikuwa ni sauti ya mkewe akilalama kitandani,kwa sasa haikuwa ndoto tena aliamini kabisa alikuwa ni mkewe wa ndoa tena akiwa na mwanaume kitandani.

    Alisahau kuwa ndani ya muda mfupi uliopita naye alikuwa anatenda hayo hayo kwa mke wa mchungaji.

    "mchungaji una utani wewe jamani" alisikika Noela akizungumza kutokea pale chumbani maneno yale yaliuchoma sana moyo wa Timoth. Alitamani sana kuingia kufanya fumanizi palepale lakini roho ilisita sana kufanya hivyo.

    Akiwa bado anasumbuliwa na kizungumkuti aliona kwa mbali sana mwanga kama unaelekea pale kwa mchungaji,kama haukuwa wa pikipiki basi ilikuwa baiskeli au kama ni gari basi ilikuwa ina tatizo la taa moja kuwa mbovu,Timoth kwa kuepusha kujulikana alikuwa pale alijikongoja kwa kupitia njia ya nyuma akatoweka eneo lile huku akiupa nafasi ule mwanga kuzidi kuchukua uhuru wa kutawala eneo lile,jambo lililompa uhakika kuwa safari ya kifaa kile kilichokuwa kinatoa mwanga ilikuwa inaishia pale kwa mchungaji.

    ***

    Hali ya mama mchungaji ilionekana kuwa mbaya sana,hakuna aliyekuwa na wazo yale yote yanayotokea pale ni mchezo wa kuigiza uliotungwa haraka haraka kitaalam zaidi na mama mchungaji na kufanikiwa kuwateka akili viumbe wote waliomzunguka pale.

    Mama mchungaji aliingia kama mwizi ndani ya nyumba yake mwenyewe na suluhisho la yote aliyoyashuhudia kuwa mchungaji Marko alikuwa amerejea na kushuhudia kwamba hapakuwa na mtu pale ndani basi mama mchungaji alipoingia alizidi kuutumia uzoefu wake wa miaka mingi iliyopita alipokuwa anafanya biashara ya kuuza mwili,mama mchungaji alikumbuka jinsi alivyokuwa na uwezo wa kujiundia ugonjwa na kunywea kiasi kwamba buzi analokuwa nalo siku hiyo linachunika bila hata kupata nafasi ya kutumia mwili wake,ni mbinu hiyo hiyo mama mchungaji aliitumia siku hiyo ili kulinda heshima ya ndoa yake aliyofunga kanisani mbele ya waumini wengi wenye imani naye.

    Mchungaji,Noela pamoja na Oscar wote hawakushtukia mchezo huo kila mmoja alisikitika kwa hali mbaya aliyokuwa nayo mama huyo. Mwili wake ulikuwa unatetemeka sana na kila alipoguswa alilia akidai anahisi maumivu. Pikipiki moja isingeweza kuwatosha watu wote hawa kumsindikiza mama mchungaji hospitali basi kwa busara za mchungaji aliamua kuwaacha nyuma Oscar na Noela walinde nyumba kwani mlango ulikuwa umebomoka na yeye akaongozana na mama mchungaji hadi kwenye pikipiki akamsaidia kupanda kisha akaondoa kwa mwendo wa wastani kwenda katika zahanati ambayo wangeipata kilometa kadhaa mbele.

    Kwa Noela na Oscar kuachiwa nyumba ilikuwa nafasi nyingine ya kipekee sana na ambayo hawakutakiwa kuichezea.

    "mh! Afadhali jamani Nilikuwa nimekumis tayari mwenzio dah!" Noela alianza kumchokonoa Oscar wakiwa pale sebuleni baada ya mchungaji kuondoka.

    "Noela lakini hii nyumba ni ya mtu wa Mungu hauogopi? " alihoji Oscar.

    "mi siogopi bwana wee! Tatizo lako unawazia tu ile mimba,usijali kuhusu hilo tena nimerekebisha mambo yote tayari usijali sio yako tena" Noela alimjibu Oscar jibu ambalo kwa Oscar lilimaanisha mengi lakini furaha yake ikiwa kumalizika kwa utata wa ile mimba,taratibu akajisogeza kwa Noela,wakaanzia sebuleni palepale bila haya lakini mwisho wa yote wakajikuta wakiangukia chumbani

    Kwa hatua aliyokuwa amefikia Noela japo zilikuwa ni siku 21 tu katika uhusiano lakini yeye (Noela) alikuwa amenogewa tayari na alikuwa hajiwezi mbele ya Oscar.

    "yaani Oscar laiti ningekutana na wewe mapema ni mimi ambaye ningekutongoza wala nisingesubiria unianze kwa jinsi ambavyo nahisi raha kuwa na wewe mh! ni mwili wangu tu unaoweza kuelezea furaha hiyo" Noela alikuwa anajieleza mbele ya Oscar huku jicho lake likiwa limelegea mpaka linataka kufumba,kwa Oscar haukuwepo ujanja wowote ule alimwangalia tu Noela kwa matamanio kisha akamvagaa na kuendelea kukichafua chumba cha mchungaji kwa dhambi yao hiyo waliyoigeuza kuwa haki kwa sheria waliyoitunga wao bila kumshirikisha bwana Timoth ambaye ndiye mmiliki halali wa mali ile. Mwanga wa taa uliomulika pale ndani ndio uliwakurupua wawili hawa na kukimbilia sebuleni walipokuwa.

    "hodi hodi hodi watu wa Mungu" ilisikika sauti mlangoni.

    "Karibu karibu mpaka ndani" alijibu Noela na yule aliyekuwa nje akausukuma mlango ule mbovu uliokuwa umeegeshwa na kuingia ndani.

    "bwana asifiwe wapendwa" alisalimia mgeni yule ambaye baada ya muda mfupi alitambulika mbele ya Noela japo kwa sura kuwa ni mpendwa ndani ya kanisa analosali yeye na Timoth.

    "amina mpendwa karibu tupo sisi"

    "poleni sana kwa matatizo mchungaji amenipa taarifa na akaniomba nije hapa kuwapa kampani kwani mpo peke yenu na wote ni wageni" alijieleza yule mgeni.

    "mh! Hapana amekusumbua tu bure hatuna hofu yoyote hapa na hata akirudi asubuhi sisi atatukuta

    tu tena bila hata uoga" alijibu Noela na Oscar akamuunga mkono kwa kutikisa kichwa juu na chini.

    "aah! Basi kama ni hivyo basi ni vyema nadhani mimi nisikae sana ngoja ninyonge baiskeli yangu nirejee nyumbani,nyie mbaki salama na Mungu awabariki" aliaga yule mgeni,kwa mawazo yake alidhani uwepo wake unahitajika pale lakini kwa Oscar na Noela alikuwa ni kero kubwa tena aliwachukiza kwani alikuwa amewaharibia mipango yao yote katika starehe.

    Punde tu baada ya kutokomea wawili hawa wasio na aibu pia wasiokuwa na heshima mbele ya nyumba ya mchungaji walivutana wakarejea chumbani tena kitandani.

    ***

    "kweli mchungaji amenizidi ujanja yaani amekuja kumchukua mke wangu hapa nyumbani kwangu dah! Kwa karata hiyo sio siri amecheza" Timoth akiwa kitandani kwake nyumbani kwa uchungu alikuwa anawaza jinsi alivyomsikia mkewe kwa masikio yake mwenyewe akiongea na mwanaume,ambaye Timoth aliendelea kuamini ni mchungaji Marko wa kanisa lake.

    "sasa ina maana wiki zote hizo hajaridhika tu kwa mke wangu au ndio maksudi hayo?" aliendelea kujiuliza Timoth. Usingizi ulikuwa umepaa kabisa na jasho kali lilivuja kutoka mwilini mwake.

    "Deo aliniambia kulipa kisasi ndio suluhisho lakini mimi siamini hata kidogo,mbona ndio nazidi kuumia moyo? Mh! Nadhani natakiwa kutafuta dawa nyingine ikishindikana ni heri kumfukuza huyu mwanamke kabisa" kwa hasira Timoth aliendelea kuzungumza peke yake kabla hajakatishwa na sauti ya mkewe akigonga hodi sebuleni.

    "vipi mpenzi wangu wa pekee umerejea jamani" Timoth alimwambia Noela baada ya kumfungulia mlango,badala ya kujibu Noela alimwangukia Timoth begani huku akiwa amemkumbatia na kumwambia "nimekumis jamani kipetito" neno hilo lilipandisha hasira za Timoth maradufu

    "vipi mpenzi wangu wa pekee umerejea jamani" Timoth alimwambia Noela baada ya kumfungulia mlango,badala ya kujibu Noela alimwangukia Timoth begani huku akiwa amemkumbatia na kumwambia "nimekumis jamani kipetito" neno hilo lilipandisha hasira za Timoth maradufu.

    Alihisi ule uoga wa mkono wake kila siku kushindwa kumwadhibu mkewe kila anapokosea alikuwa unamtoka kuepusha hayo aliamua kuingia ndani haraka asiweze kumuangalia Noela usoni kwani kufanya hivyo ilikuwa ni sawa na kukumbushia uchafu uliokuwa unafanywa na mkewe muda mfupi uliopita katika nyumba ya mchungaji,ama kweli waanaume huwahi sana kusahau makosa yao na kuwashutumu wake zao huku wakijihalalishia makosa yao kuwa halali na hata kwa Timoth ilikuwa vilevile kosa la mkewe alilichukulia kubwa sana wakati ni yeye huyohuyo alikuwa ametoka kuvuja jasho juu hya kifua cha mama mchungaji kwa furaha na baadae akatoa sifa kedekede kuwa mama Yule ni mjuzi sana wa mambo hayo. Akiwa amefanyiwa hivyo hivyo mkewe (Noela) kwa Timoth ilikuwa pigo kubwa,hakika mkuki kwa Nguruwe kwa mwanadamu mchungu sana.

    Noela alifuata baadae kidogo na kumuelezea Timoth kila kilichotokea baada ya kuwa wameachana wakati wanamsindikiza mchungaji kwenda kuangalia ni nini kinamsibu mkewe ndani ya nyumba yake,Timoth hakutaka kujibu neno lolote kwani aliamini dawa ya hasira ni kukaa kimya ili usiweze kutenda jambo baya bila kujitambua.

    “mke wangu ninahisi usingizi naomba unisimulie kesho asubuhi lakini nina imani kila jambo limeenda vizuri” alisema Timoth huku akiwa amemugeuzia Noela mgongo wake.

    “ni kweli hakuna kilichoharibika mume wangu tumempata mama mchungaji ila hali yake haikuwa nzuri sana” alijibu Noela

    “haya we lala mimi naenda kuoga nimejichokea mie” alisema Noela baada ya kutopata jibu lolote kutoka kwa Timoth,kauli ya Noela illimkera sana Timoth kwani aliamini tena ni mchungaji aliyemchosha mkewe hadi kuwa katika hali ile.

    “enough is enough sasa kwa kweli ewe pepo wa huruma naomba unitoke nawe pepo wa uvumilivu hebu ondoka kichwani mwangu,karibu pepo wa kiburi,ukorofi na maasi yote ya dunia unisaidie katika mtihani huu mgumu. Hakika nikiendekeza upumbavu huu siku moja watakuja kufanya mbele yangu,….au tayari waliwahi kufanya wakati mimi sipo??” alikuwa anafanya mjadala huo na kichwa chake wakati mkewe akiwa bafuni anaoga.

    *****

    Mchungaji alimfikisha mkewe hospitali,hali aliyokuwa nayo ilimshangaza kila aliyemuona alikuwa kama mtu ambaye dakika yoyote ile angeweza kutoa pumzi yake ya mwisho na kuiaga dunia.

    “mheshimiwa tunasikitika kuwa……”

    “tafadhali isiwe kuwa mke wangu amekufa,daktari sema yote isipokuwa hilo peke yake,haiwezekani kuwa mke wangu amekufa,haiwezekani nasema!!!” mchungaji alimkatisha daktari ambaye alikuwa anataka kutoa taarifa Fulani aliyoamini kuwa ilikuwa mbaya sana kwake. Wakati huo tayari waumini mbalimbali wa kanisa lake walikuwa wamewasili kutoa ushirikiano wa hapa na pale.

    “sio kama uzaniavyo mheshimiwa,mkeo hata hajawa wa kufa na hizo dalili hazipo hata kwa mbali labda itokee miujiza ya maanani ndio tutashuhudia tukio hilo lakini suala ni kuwa mkeo hana tatizo lolote lile kiafya ndo jambo linalotushangaza hata sisi waganga wa hospitali hii kwa hali aliyokuja nayo haikuwa sawa hata kidogo asipatwe na chembechembe za ugonjwa wowote” alijibu daktari huku akizungusha macho yake hapa na pale.

    “ashindwe shetani huyo aletaye magonjwa,nakwenda kinyume na nguvu za giza kama zimezungushwa kwa mama huyu asiyekuwa na hatia nazikemea na pepo zote chafu zilizofungamana ndani yake ili kuzuia kazi ya Mungu isichukue nafasi yake,kwa mamlaka niliyopewa ya kukupondaponda ewe shetani nasema toka ndani yake” alianza kuomba mchungaji na kumfungua akili Yule daktari kujua kwamba mteja wake alikuwa muumini wa kanisa Fulani ambao wamezoeleka kama walokole.

    “najisikia vizuri sana nina imani neno la Mungu limeuchoma mwili wangu na kupondaponda ugonjwa wa ghafla ulionijia na kutaka kunijaribu imani yangu” Mama mchungaji alikuwa akiwaeleza waumini waliofika chumbani kwake kumpa pole asubuhi palipokucha baada ya kusikia matatizo yaliyokuwa yamemfika. Wote kwa pamoja walitoa ombi la kumshukuru Mungu kwa neema zake huku wakishirikiana na mama mchungaji ambaye yeye ndiye aliyeujua ukweli wote,hakuwa na jinsi ya kufanya huo pekee ndio ulikuwa ujanja wake wa mwisho alioweza kuutumia ili kuiokoa ndoa yake iliyokuwa katika hatihati za kubomoka tena kwa aibu kubwa sana ambayo ingeweza kudumu kwa muda mrefu sana.

    “pole sana mke wangu yaani……”

    “tafadhali usiniambie yote yaliyotokea,tumuachie Mungu ndiye muweza wa yote na tayari amenipigania!!!” aliwahi kuingilia maongezi mama mchungaji kabla hata mchungaji ajakamilisha alichotaka kuanza kuzungumza.

    “usijali mama yangu,tuachane na hayo ni heri umepona,tuwahi nyumbani ili Noela na Yule msaidizi wa kazi waweze kwenda nyumbani kwani wamekaa muda mrefu sana”

    “aah!! Kumbe walikuja maskini Mungu awabariki sana,uliwaacha peke yao!!” aliuliza kwa mshangao mama mchungaji.

    “niliwatumia mtumishi mmoja akakae pamoja nao lakini walidai kuwa watakuwa salama bin salmini basi naye akawa amerejea kuwa nasi hapa” alijibu mchungaji

    “wabarikiwe sana” alisema mama mchungaji

    Iliwachukua kama dakika ishirini kwa mwendo wa pikipiki ileile kuweza kufika nyumbani kwao ambapo waliwakuta Noela na Oscar wakiwa sebuleni wanapiga stori za hapa na pale,baada ya shukrani za hapa na pale Noela aliaga kwa niaba ya Oscar wakimuacha mchungaji akiwa anafanya mpango wa kutafuta fundi aweze kurekebisha ule mlango uliovunjwa katika harakati za kuangalia kinachomsibu mama mchungaji usiku ule.



    Ilimchukua mama mchungaji wiki moja tu kuweza kujitambua kwamba tayari ameushika ujauzito kutokana na tendo alilofanya na kijana Deo au Desmund kama yeye alivyomtambua.

    Ilimchukua mama mchungaji wiki moja tu kuweza kujitambua kwamba tayari ameushika ujauzito kutokana na tendo alilofanya na kijana Deo au Desmund kama yeye alivyomtambua.

    “nilijua tu!! Tayari balaa jingine hili hapa mbele yangu nitafanyaje mie Rehema??” alijiuliza mama mchungaji kwa hofu tele baada ya siku zake za kwenda mwezini kupita bila dalili zozote za hedhi.

    “nimekwisha safari hii siujui ujanja wa kuniepusha na hili” aliendelea kujiuliza mama mchungaji.

    “mwanangu Rehema,kamwe usije kuwa kama dada yako mkubwa,nilimueleza kuwa ukoo wetu hairuhusiwi kabisa kutoa mimba,yeye akaleta ujuaji na mwisho wa siku tukamzika,narudia tena kwako mwanangu jihadhari sana na wanaume lakini kama ikitokea bahati mbaya ukapata ujauzito japo sitegemei kitu kama hicho kamwe usithubutu kutoa mimba UTAKUFA Rehema,utakufa!!!!!!” Rehema alikaa akakumbuka maneno ya marehemu baba yake aliyomwambia katika msiba wa marehemu dada yake aliyekufa katika jaribio la kutoa mimba baada ya Yule aliyekuwa amempa mimba hiyo kuikataa,damu nyingi iliyovuja ilipelekea mauti yake na hivyo kutimiza neno alilolisema baba yake hata kabla hajapata mimba “ukitoa mimba hakika utakufa”

    “nitafanya nini mimi jamani,sipo tayari kufa hapana hapana siwezi kufa nasema nataka kuishi bado……..vipi sasa hii mimba,mchungaji kwa mdomo wake amenieleza kuwa hawezi kuzaa na ni suala ambalo kila siku tumekuwa tukimwomba Mungu kila siku bila dalili yoyote mh! Leo hii nina mimba je? Ataamini kuwa ni majibu kutoka kwa Mungu au? Na hata kama akiamini je? Motto nitakayezaa hawezi kuzua utata? Nimelikoroga “ mama mchungaji alizidi kuumia kichwa asijue nini cha kufanya.

    “nadhani cha msingi ni kuwafata hao wanaohusika na ujauzito huu huenda watanishauri kitu cha kufanya sina la kufanya kwa kweli mimi hadi hapa nilipo” aliamua kufikia hatua hiyo mama mchungaji

    ****

    Shughuli za huduma ya kiroho zilikuwa zinaendelea kama kawaida na safari hii mchungaji tayari alikuwa amejifunza kitu kamwe hakumwacha mke wake nyuma tena,alikuwa anaongozana naye hadi eneo husika na kama ikitokea siku ambayo hawezi kuongozana naye basi waliagizwa watumishi kadhaa waweze kukaa naye pale nyumbani.

    Ilikuwa siku ya mwisho kabisa ya mkutano huu wa injili uliokuwa na kauli mbiu ya “kesheni mkiomba”. Mchungaji Marko aliongozana na mkewe katika kuliongoza kundi kubwa la waumini waliohudhuria siku hiyo ya kipekee. Shangwe za hapa na pale zilitawala eneo lile huku watoto wadogo wakifurahia kuangalia sinema mbalimbali zenye mafunzo mengi sana katika maisha yao ya baadae.

    Noela,Oscar nao pia walikuwa kati ya watu walioongeza idadi ya waumini;Noela alikuwa katika mstari wa mbele kabisa wa kwaya kuu ya kanisa lake wakiwaburudisha mamia ya waumini eneo lile,Oscar yeye alikuwa akiburudika tu kumwangalia Noela alivyokuwa anan’gaa na kuzidi kuipendezesha kwaya ile,sauti yake haikuwa ya kujiuliza mara mbilimbili kama ni bora au sio bora,sauti ya Noela ilikuwa ya kipekee na madaha yake katika kuimba yalisababisha watu wengi hasahasa wanaume kumuonea wivu Timoth.

    Siku hiyo Timoth aliamka akiwa na mawazo mengi sana na kwa alichokuwa anawaza aliamini ombi lake lilikuwa limepokelewa na lilikuwa limefanyiwa kazi na majibu alikuwa amepewa,roho mbaya na ya kikatili kwa mara ya kwanza yaliumbika kichwani mwake.hakujua yametoka wapi lakini aliamini yalikuwa mawazo sawa kabisa yanayotakiwa kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo. Chuki kuu ilikuwa imejengeka dhidi ya mchungaji wa kanisa lake,matatizo na visanga vyote alivyopitia aliamini ni kwa sababu ya huyo huyo mchungaji.

    “ni adui wangu namba moja” alisema kwa hasira Timoth wakati akiwaza nini cha kumfanyia mchungaji ili nafsi yake ilizike

    “kufanya mapenzi na mke wake tena kwa siri bila kujulikana haitoshi hata kidogo nitakuwa mpumbavu nikijipa kichwa kuwa hicho ni kisasi” aliendelea kuongea peke yake Timoth wakati akifikiria nini cha kufanya.

    Jioni ilipofika hakutaka kuongozana na mkewe pamoja na Oscar kuelekea kanisani katika siku ya mwisho ya mkutano ule mkubwa wa injili.

    “nyie tangulieni mimi namsubiri rafiki yangu nitakuja nae,si unakumbuka mchungaji alisema kila mmoja alete mggeni!!! We tayari umemchukua Timoth basi na mimi nataka kuja na wangu” alijibu Timoth huku akitawaliwa na tabasamu pana usoni kwake.

    “mh!! Nimekuwahi mimi mjanja zaidi yako” alitania Noela huku akiondoka pamoja na Oscar. Timothy alitabasamu na kurejea ndani.

    Hakuna aliyejua kichwani mwakeTimoth alikuwa anawaza nini.

    *****

    Giza lilitokea ghafla eneo lote lililokuwa linafanyiwa mkutano huo,tayari ilikuwa majira ya saa sita usiku

    “aaaaaaaah!” ndio kelele zilizosikika kutoka kwa watu baada ya giza kuchukua nafasi eneo lile la mkutano wakati mahubiri ya mchungaji Marko yakizidi kunoga na kukonga nyoyo za mamia waliohudhuria eneo lile.

    “hata pasipo na umeme nina sadiki kuwa sauti yangu itafika hapo ulipo,bwana Mungu alinipa sauti kuu niweze kuipaza mbele yenu na bila kujalisha umbali neno hili litakufikia na ujumbe wake utakuingiaaaaaaa!!! Haleluyaaaaa!!!!!!!!” ilisikika sauti ya mchungaji Marko ikisambaa eneo lile na kusisimua umati.

    “ameeeeeeen!!!!” umati ulijibu kwa shangwe kubwa zilizozizima hadi miji ya jirani.

    Kelele za furaha kabla hazijaisha vizuri msukumano wa hapa na pale ulianza pale katika umati ule kila mmoja alikuwa anajaribu kutafuta pa kukimbilia,kelele zilitokea jukwaani alipokuwa anahubiri mchungaji Marko,haikusikika tena sauti ile kuu iliyosisimua umati ule kwa shangwe tele. Giza totoro lililotanda pale lilisababisha watu wakanyagane na kugongana hapa na pale vilio vya watoto vilisikika huku mama zao wakipaza sauti kuu wakitaja majina ya watoto wao hao.

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog