Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

JAMANI MCHUNGAJI !! - 2

 



    Simulizi : Jamani Mchungaji !!

    Sehemu Ya Pili (2)



    Mikono yake ilikuwa inatetemeka sana wakati anashika kitasa cha mlango wake,hakuwa tayari kushuhudia kitu alichokuwa anawaza,taratibu alianza kujutia maamuzi yake ya kuoa,alijiuliza ni kwa nini alikubaliana na maamuzi ya mchungaji na mama yake mzazi juu ya kuoa.

    “jamani mchungaji!! Aah!! Usinitende hivyo tafadhali nitakufa” malalamiko yaliendelea mle ndani,moyo wa Timoth ukasita tena baada ya kusikia jina la mchungaji mle ndani “nitamuangalia vipi mimi huyo mchungaji jamani eeh!!” alijiuliza Timoth uoga ulikuwa unaanza kumtawala sasa alijisikia aibu sana kuonana na Mchungaji hakuamini kama ni mchungaji huyo huyo anayetangaza habari za uzima kanisani na sasa alikuwa kwenye kitanda cha sita kwa sita akieneza uzinzi kwa kuivunja amri ya sita na mkewe tena mkewe wa ndoa ambaye yeye huyo huyo mchungaji aliwabariki na kuwatakia mema yeye na mkewe(Noela) katika ndoa yao.

    “liwalo na liwe sasa” aliamua moja Timoth na kuufungua mlango kisha akaingia ndani . Noela alikuwa anajigalagaza kitandani alikuwa ameinyanyua nguo yake juu kabisa na alikuwa uchi wa mnyama sasa,vidole vyake vyote viwili vilikuwa vimezama katika maungo yake ya uzazi,jasho lilikuwa linamtoka kwa wingi. Alikuwa peke yake Noela kitandani ilikuwa ni katika ulimwengu wa ndoto,jina la mchungaji lilitawala katika mdomo wake halikuwa suala la kujiuliza mara mbilimbili kuwa alikuwa anaota ndoto iliyohusisha suala zima la mapenzi ilikuwa ni ndoto pevu.

    Pumzi zilimshuka kwa kasi Timoth walau alipatwa na ahueni lakini bado lilikuja swali kwa nini anamuota mchungaji tena si kwa ndoto za kiroho bali za kidunia.

    Kwa hatua za kurudi nyuma Timoth alirudi hadi jikoni tena akarudisha silaha zake na kurudi tena chumbani.

    “koh! Koh! Koh!” alikohoa Timoth na Noela akakurupuka kutoka usingizini.

    “mh! Mchungaji aah! Mhhh! Honey umerudi” Noela alianza kuongea huku akipikicha macho yake ili aone mbele vizuri. Hasira zilimtetemesha sana Timoth,lakini alishindwa kuuliza swali hilo.

    * * *

    “wanawake wote baada ya ibada hii mnatakiwa kubaki kuna jambo tunatakiwa kuzungumza kidogo kina baba mnaweza kurejea majumbani” sauti ya mchungaji Marko iliwatangazia waumini wakati wa matangazo mwisho wa ibada.

    “leo lazima nijue kuna nini hapa” aliamua Timoth katika halmashauri ya kichwa chake na kuamua kutafuta mbinu za kumfumania mkewe.

    “mimi naenda mke wangu tutaonana nyumbani” Timoth alimuaga mkewe kasha akatoweka eneo lile.

    * * *

    Kupitia kitundu kidogo katika mabanzi ya ukumbi mdogo wa mikutano Timoth alikuwa makini kabisa kuchungulia kuna nini kinaendelea pale,hakuna mtu ambaye angeweza kumuona pale kwani ilikuwa ni njia ya kupitisha maji machafu alipojiweka Timoth akiwa na suti yake.

    Baada ya dakika kumi tangu awe pale macho ya Timoth yalishuhudia jambo ambalo alitamani lisiwe kweli,akili yake ilijaribu kufikiri nini cha kufanya na hakikuonekana. Mapigo ya moyo yakaanza kupishana kwa kasi katika kifua chake,macho yakamtoka kama mwanamama aliyechanikiwa na nguo katika daladala.

    Walikuwa ni mbwa wawili saizi ya ndama kwa kasi kubwa bila kubweka walijongea alipokuwa amejibanza Timoth ili kuufatilia ukweli juu ya nini kipo kati yake na Mchungaji. Bila kujali heshima ya suti yake aliyokuwa amevaa Timoth alianza kutimua mbio huku kiatu kimoja kikimtoka mguuni. “ni heri aibu kuliko dhahama inayokuja mbele yangu” hivyo ndio aliwaza Tim huku anatimua mbio. Miiba iliyokuwa imewekwa maeneo yale ili kuziba njia ambayo zamani ilikuwa ikitumiwa na watu kupenya pale haikuwa chochote mbele ya Timoth aliruka kama Swala na hiyo ndio ilikuwa ponapona yake kwani wale mbwa hawakuendelea kumkimbiza bila shaka walikuwa wamefunzwa hivyo.

    “samahani kandambili unauzaje” huku jasho jingi likimtoka Timoth alimuuliza mwenye duka

    “he!! We huoni kama na sisi tunasubiri huduma au wewe ndo wa muhimu zaidi ya wenzako!!!” sauti kali iliyojaa hasira ya mwanamama ilimjia juu Timoth.

    “samahani mama yangu samahani sana sijafanya kusudi” alijitetea Peter na kwa sauti yake ya upole alieleweka kwa yule mteja,baada ya waliokuwa wametangulia kupewa huduma ndio hapo sasa Timoth alipata nafasi ya kupewa huduma. Tai shingoni,suti kali halafu chini ndala ndivyo alionekana Timoth kwa kweli alipatwa na mfadhaiko wa hali ya juu sana kwa tukio lile. Machoni kwa watu alionekana kituko tena kikubwa sana

    “pipiiiii!!!” honi kali ya gari pamoja na breki kali ndio zilifungua akili yake na kugundua alikuwa katika hatari kubwa sana ya kuweza kugongwa na gari.

    “we vipi wewe bwana hauangalii mbele ala!! Mawazo ya familia yako unaleta barabarani utakufa wewe.

    “samahani ndugu samahani sana sikusikia aah!! Sikuona unajua aah!! Eeh!!” alianza kujiumauma Timoth kabla dereva hajaondoa gari lake kwa ghadhabu kali sana.

    “shiit!! Nimetoa sadaka pesa yote niliyokuwa nayo mh!! Hapana haiwezekani hata kidogo mbona nilikuwa na 2700 nimetoa 1700 hiyo nyingine itakuwa wapi sasa” alijiuliza Timoth huku akijisachi hata sehemu zisizohusika.

    “wewee Mbagala kilwa road unaenda bosi!!” kondakta wa basi aliuza maneno kwa Timoth akatamani kupanda kwani ndio gari hilo lililokuwa linamfikisha kwake lakini hakuwa na nauli mfukoni.

    “kutembea hadi nyumbani!!! Oooh!! Mungu wangu” alivuta pumzi Timoth baada ya kufikiria umbali uliokuwepo kutoka alipokuwa hadi nyumbani kwake. Hakuwa na jinsi alilazimika kutembea kwani ujanja wake haukuwepo ilikuwa jumapili mbaya sana kwake yeye Timoth.

    “haya yote ni mapenzi siamini yaani bila Noela yasingenikuta haya,yaani kweli mchungaji ndio chanzo cha haya yote loh!! Kwa nini lakini ananifanyia hivi wakati ana mke nyumbani kwake tena tunamuita kwa heshima kubwa eti mama mchungaji hapana nimezidi kuwa mpumbavu lazima nishtuke sasa mambo yanapoelekea nitakuwa mwehu kwasababu ya kujifanya nina heshima sana na ni mtu wa kupeleleza sana kabla ya kutoa maamuzi. Tazama sasa huu upelelezi unaponipeleka Imetosha sasa” alilalama peke yake Timoth huku akikaza mwendo kuelekea nyumbani kwake. Ghadhabu ilimfanya ajisikie kupasuka mwili wote ulitetemeka

    “atajuta kuolewa na mimi huyu mwanamke yaani nimeishi maisha yangu yote vizuri leo hii ananiingiza kwenye aibu kama hii hapana nasema hana mtoto wangu na kama ana mimba najua sio ya kwangu huo ni uhakika sihitaji tena kupata uhakika mwingine.” Timoth aliendelea kuweka foleni ya maamuzi katika kichwa chake ambacho kilikuwa kimezidiwa tayari.

    “aah!! Timoth yani kufungwa kwa Yanga ndio sisi wa Simba tunakusalimu haujibu mh!! Ushabiki gani huo kaka” alishtuliwa Timoth na sauti ya rafiki yake aitwaye Deo;walipatana yote na Deo lakini lilipokuja suala la ushabiki wa mpira walikuwa maadui wakubwa Timoth akiwa ni mnazi wa klabu ya Yanga wakati Deo yeye ulikuwa humwambii lolote kuhusu timu ya Simba hata kama ingefungwa ngapi yeye angetoa vigezo vyake na kuhalalisha ushinda wakati tayari wamefungwa.

    Timoth hakusikia aliposalimiwa na Deo kutokana na msongo wa mawazo lakini Deo hakuligundua hilo akahusisha na uhasama wao katika michezo.

    “sikukusikia Deo wala sio maksudi mimi kunyamaza kama ni kufungwa tayari tumekubali lakini niliyonayo we acha tu!!!” alijieleza Timoth.

    “kulikoni tena huko mguuni ndala au viatu umeacha kwa fundi anakun’garishia kidogo”

    “bora vingekuwa kwa fundi ndugu yangu yaani ningekuwa mtoto wa kike ningeangua kilio lakini mimi ni mwanaume ngoja nijikaze japo inauma kwa hili lililonitokea” alijibu kwa sauti ya chini iliyojaa simanzi tele

    “vipi umekabwa!!....wapi hapo??” aliuliza kwa ghadhabu Deo.

    “sijakabwa ndugu yangu ni siku nyingi nimevumilia nisiseme lakini leo ngoja nikuelezee wewe mzoefu huenda leo ndio mwisho wa matatizo yangu,na huwezi jua ya Mungu mengi labda ndio maana tumekutana hapa muda muafaka kama huu”

    “kitu gani hicho swahiba ambacho tunakutana kila siku hauniambii mimi ndugu yako”

    “ningeweza kumwambia kila mtu lakini ni jambo Fulani linalotia aibu kulizungumza hasa hasa kwa mwanaume aliyekamilika”

    “usiseme hivyo Timoth hebu zungumza tusije tukapewa lawama sisi siku moja kwamba hatukukushauri” alijibu Deo huku dhahiri akionekana kuwa na hamu ya kutaka kusikia kitu kutoka kwa Timoth.

    “mkeo yupo mida hii!!” aliuliza Timoth

    “hapana kajiendea sokoni tayari” alijibu Deo.

    “basi tukae kwako japo kidogo nikuelezee na wewe ndio wa kwanza kuyasikia haya” alisema Timoth huku kiuvivu uvivu akijivuta na kandambili zake kuelekea nyumbani kwa Deo.

    “bwana Deo sina haja ya kuzunguka sana lakini napenda kukujuza kwamba nina asilimia 99 za uhakika kwamba mke wangu mpendwa ananisaliti na mchungaji wa kanisa langu” alieleza kwa kifupi Timoth.

    “unamaanisha mkeo na mchungaji Marko wanauhusiano??”

    “asilimia 99” alijibu Timoth.

    “Mungu wangu!!!!! Yaani mchungaji ana…yaani kweli hapana” Huku jasho likianza kumtoka kwa mshtuko Deo alijikuta anashindwa kuongea lolote.

    “usishtuke sana ndio aibu hiyo niliyokuwa nakwambia tangu nigundue ni mwezi na kama ni mimba basi imezoea nyumba ya uzazi na hiyo mimba sio yangu ni ya huyo mchungaji mwenyewe” kwa uchungu alitamka Timoth.

    “umewahi kuwashuhudia lakini au unatabiri tu,isjekuwa umeambiwa na wewe!!” aliuliza Deo

    “nimeshuhudia zaidi ya mara mbili kwa macho yangu,yaani ndio maana nilikuwa sitaki kuoa mimi mkawa mnanisema ona sasa ninavyotendwa leo hali hii unayoniona nayo ni kwa sababu yake” maneno ya Timoth yalimuumiza sana Deon a kuhisi hayo yote anatendewa yeye.

    “dawa ya moto ni moto sasa na sisi tuuheshimu usemi huo wa wahenga” akasema Deo.

    “una maana gani Deo!!!”

    “kwa sababu amekutia uchungu na aibu hii kubwa huku nay eye akiwa na mke sasa nay eye tutamfanya ausikie uchungu wa mke wa ndoa kama yeye anavyofanya kwa wengine hilo ndio somo pekee” alisema Deo kwa kujiamini na hasira ya waziwazi. Timothy alibaki anashangaa asijue mpango thabiti aliokuwa nao Deo hadi ajasema vile.



    Hasira na uchungu alioupata Deo ulimtuma moja kwa moja kulipiza kisasi cha moja kwa moja kwa huyo mchungaji anayeiharibu ndoa ya rafiki yake kipenzi (Timoth).

    "sasa tutaanza vipi huo mpango,yule ni mtu wa Mungu na ameshika dini,tutafanyaje?" aliuliza Timoth.

    "Mtu wa Mungu!!! Nani kasema we ngoja uone" alijibu Deo huku ameyakodoa macho yake kumuelekea Timoth.

    ***

    "karibu Mume wangu,karibu sana mbona umechelewa kurudi sana" Noela alimkaribisha mumewe kwa furaha kubwa sana.

    "ah! Nilipitia kidogo kwa swahiba wangu mmoja mtaa wa tatu" alidanganya Timoth.

    "darling jamani na viatu ulivyovaa asubuhi mbona ah...ah!"

    "ah! Vile viatu vimebanduka Sole dah! Nashukuru nilikuwa nimekaribia kwa huyo swahiba akanipatia hizi kandambili namshukuru sana" aliendelea kudanganya Timoth na kueleweka kwa mkewe.

    "mh! Kikao chenyewe kilikuwa kirefu kweli,na baada ya kikao mchungaji alinihitaji faragha kidogo nimsaidie katika....."

    "Oscar yuko wapi?" aliingilia kati Timoth ilimradi tu asisikie habari za Mchungaji.

    "yupo huko chumba cha nje amepumzika,karibu ndani" alijibu Noela kwa upole.

    ***

    "honey mbona umenyon'gonyea sana leo au ndio overtime zinakuchosha" Noela alimuuliza nume wake siku moja aliporejea kutoka kazini majira ya saa kumi na moja jioni.

    "nimepata majukumu nje ya mji kitu ambacho nilikuwa naomba kila siku kisitokee sipendi kuwa mbali na familia yangu" alijieleza Timoti kwa sauti iliyojawa majonzi.

    "ooh! Mungu wangu,pole sana mpenzi na ni jambo la kusikitisha sana japo ni moja ya majukumu ya kikazi na mkataba unasema hivyo" Noela naye alimjibu huku akionekana dhahiri kushtushwa na taarifa hiyo.

    "kibaya zaidi ni wiki tatu yaani siku ishirini na moja" aliendelea kueleza Timoth na kumsikisha sana mkewe (Noela). Lakini haikuwepo namna yoyote ya kukwepa jambo hili ilikuwa ni lazima Timoth aende Mwanza kama kampuni yake ilivyomtaka kufanya mara moja.

    Ulikuwa usiku wa pili kwa Noela kulala peke yake bila uwepo wa mumewe,lilikuwa jambo gumu sana na alikuwa hajazoea hata kwa mbali,nyumba nzima alikuwa yeye na Oscar aliyekuwa ameajiriwa rasmi kuwa msimamizi wa mifugo yote pale nyumbani katika chakula,usafi na hata katika magonjwa ya hapa na pale.

    Majira ya saa tano usiku usingizi ulikuwa umemkosa kabisa Noela aliyekuwa amelala kuanzia majira ya saa mbili usiku.

    "sijui kama nitakuwa jasiri lakini ngoja nijaribu kwa leo siwezi kuvumilia zaidi" Noela alikuwa akijiongelea mwenyewe kwa sauti ya chini huku akiwa amekaa kitako kitandani kwake akiwa na khanga moja huku kichwani akiwa amevaa mfuko mweusi wa plastiki kuzuia nywele zake kuvurugika kichwani.

    Kwa mkono wake wa kulia aliichukua simu yake ya mkono na kuiweka vyema katika kiganja chake.

    "nitume meseji au nipige!!..." alijiuliza Noela.

    "mh! Nikipiga kweli nitaweza kuongea mie...tangu utotoni naogopa mie hadi leo miaka 25 hapana ngoja nijaribu" alijipatia jibu mwenyewe.

    Akiwa bado anatafakari joto lile kali mbele yake alishtukia mikono laini ya Noela ikizunguka katika mgongo wake na kumng'an'gania kwa nguvu kabisa. Oscar hakujua lengo la Noela alidhani ni uoga wa giza lakini haikuwa hivyo Noela alizidi kumkumbatia kwa nguvu zote,akiwa anakifahamu vyema chumba chake alimzungusha taratibu hadi usawa wa kitanda na kisha akamwangusha pale na yeye kutua juu yake.

    "Os..ah! Os...Mchungaji please..." alianza kulalamika Noela juu ya Oscar,ndoto zilizokuwa zinamsumbua kila siku sasa haikuwa ndoto tena Noela alikuwa mbele ya Oscar,uwepo wake pale kitandani ulimchanganya kabisa,japo Oscar alikuwa anatapatapa kujiondoa mikononi mwake lakini kwa nguvu zote alijitahidi kumdhibiti katika himaya yake.

    "Noela niachie,niachie jamani kaka atanifikiriaje akinikuta humu unadhani,niache da Noela nikafate mshumaa niwashe giza liondoke" alijitetea Oscar.

    "Timoth hayupo jamani tafadhali usiondoke..usiondoke mchungaji" alijibu Noela huku akionekana kutojitambua hata kidogo.

    Akili ya Oscar ilifanya kazi haraka akaitambua hatari iliyokuwa mbele yake,hatari hiyo ilikuwa ni kama nusu kifo kama Timoth angerejea muda huo na kumkuta ndani ya chumba chake anachokitumia na mkewe tena alikuwa amevuka mipaka na alikuwa kitandani mbaya zaidi alikuwa na mwanamke mwenye pete ya ndoa katika kidole chake cha shahada.

    ***

    Hadi kufikia kutoa kiapo cha kulipa kisasi kwa mchungaji wa kanisa kwa kitendo kibaya anachoendelea kumfanyia rafiki yake mpendwa (Timoth) Deo alikuwa anajua wapi pa kuanzia na aliamini lazima atafanikiwa.

    Deo aliwahi kumsikia Adelah ambaye ni muimba kwaya kanisani lakini pia ni rafiki mkubwa wa mkewe,katika maongezi yao siku moja aliwahi kumsikia akitoa habari fulani ambayo ilikuwa ya kustaajabisha lakini waliichukulia kama tetesi,eti kwamba mke wa mchungaji Marko ametulia baada ya kuolewa na Mchungaji lakini kabla ya hapo alikuwa ni kiruka njia sana."hapo hapo ndio nitaanzia kama kweli ni kiruka njia basi kazi itakuwa nyepesi sana" Deo alifikiria wakati akijiandaa kuanza rasmi kutimiza ahadi aliyokuwa amempa rafiki yake (Timoth) ahadi ya kumlipia kisasi kwa uovu ambao mchungaji anautenda kwa mke wake (Noela)

    "mama mchungaji bwana Yesu asifiwe!! Samahani kuna kijana mmoja anakuhitaji hapo nje" sauti tulivu ya mmoja wa watumishi wa Mungu katika kanisa ilimnon'goneza mama mchungaji au mama Marco kama walivyomwita wengine kutokan na mumewe kuitwa hivyo. Ilikuwa ni katika sherehe ya kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka ambapo kanisa lilifanya pamoja na waumini wake.

    "eeh! Nani tena huyo ambaye ameshindwa kuingia ndani au hakulipia sherehe halafu anataka kuingia" alitania mama mchungaji huku akiweka vyema mkoba wake begani tayari kwa kuamka.

    "hapana anadai kwamba eti alikupa mchango wewe halafu hukumpa kadi ya mwaliko" alijibu mtumishi yule kwa sauti ya juu kidogo.

    "nilijua tu! Tayari ndio yale yale,nani huyo mi amenipa mchango halafu sikumpa kadi?" alijiuliza mama huyu mnene kiasi akiwa amevalia nguo za kitenge pamoja na kitambaa kichwani cha kitenge.

    "twende ukaongee nae mimi na yeye tumeshindana kabisa!" alijibu mtumishi wakati wakizidi kuukaribia mlango wa kuingilia.

    "bwana asifiwe mpendwa" alisalimia kwa upendo na nidhamu mwanamama huyu.

    "amen" alijibiwa na kijana aliyekuwa amevaa suruali ya kitambaa na shati ya mikono mirefu iliyochomekewa vyema katika suruali hiyo na chini kiatu cheusi cha ngozi kilikuwa kinan'gara vyema kuruhusu staili ya "O" Aliyoitumia kunyoa ndevu zake kuchukua nafasi yake kuongeza utanashati.

    "eeh! Ngoja mimi niwaache sasa nirudi katika majukumu mkielewana utanieleza" aliaga yule mtumishi na kuwaachia wawili hawa uwanja mpana wa maongezi.

    "samahani sana mama mchungaji kwa kukutoa katika starehe zako muda huu lakini ilikuwa ni lazima kwani ni muhimu.Naitwa Desmund wa Desmund nina ujumbe wako ambao utaelewa ukishafungua ni hatari sana ukishawishika kuujua sasa hivi na ni mbaya sana kama utaupuuzia" aliongea kijana huyu huku akiwa jirani kabisa na mama mchungaji ili asiweze kusikia mtu yeyote yule.

    "mbona sikuelewi mpendwa?"

    "utanielewaje wakati ujumbe upo katika maandishi? Ukishasoma na usielewe ndio utaniambia kuwa hujaelewa nikueleweshe!" alijibu Kijana yule aliyejitambulisha kwa jina Desmund.

    "haya baba naomba ujumbe huo nina imani hauna madhara katika jina la bwana!" alisema mama mchungaji huku akichukua bahasha ndogo ya kaki kutoka kwa Desmund.

    "naona mmemalizana,vipi alikuwa mzamiaji au vipi labda!" alihoji mtumishi aliyeenda kumwita mama mchungaji ndani.

    "aah! Nimemaliza tatizo lake ameenda kuichukua kadi kuna mtu nilimpa ampelekee" alidanganya mama mchungaji.

    Uvumilivu wa kukaa na ujumbe asioufahamu dhamira yake ulikuwa umemshinda sasa,akiwa katika meza ya chakula taratibu alizama katika mkoba wake na kuanza kuchungulia kiwiziwizi kama wafanyavyo watoto wadogo wakipewa ripoti za matokeo kuwapelekea wazazi.

    Uso ulilegea ghafla,raha zikamwisha,haja ndogo ilimbana na tumbo la kuhara lilikuwa limemshika,sio kisa ubovu wa vyakula ila maneno machache aliyoweza kuyasoma. Kichefuchefu kilimtawala na kuondoka na raha zote alizokuwa nazo hapo awali.

    "kimbelembele kimeniponza mie,eeh! Mungu badili uhalisia huu kuwa ndoto tena ndoto ya mchana kabisa" aliomba mama mchungaji.

    "na sasa tumkaribishe mama mchungaji kwa ajili ya kushukuru kwa chakula alichotupatia bwana Mungu,bwana wa miujiza" Mc wa sherehe hiyo alipaza sauti kuyasema hayo kisha akajibiwa kwa vigelegele na shangwe kutoka kwa waumini waliohudhuria sherehe hizo.

    "naumbuka mimi leo!" alijihakikishia mama mchungaji

    "samahani sitaweza kutoa sala ya shukrani ninasumbuliwa na kizunguzungu cha ghafla" alijitetea kinafiki mama mchungaji na kuwatia simanzi watu wengi waliohudhuria tafrija ile iliyofana. Ilikuwa ni kama saa moja limepita tangu mama mchungaji aimbe wimbo wa "Nipishe Nipite" wa Rose Muhando lakini sasa alikuwa mgonjwa.

    "mtumishi mwongoze nje akapigwe na upepo kidogo humu ndani kuna joto" alitoa wazo hilo mchungaji Marko na kwa utaratibu kabisa akatii yule mtumishi na kumwongoza mama mchungaji nje,kwa jinsi alivyokuwa amelegea ni dhahiri alionekana kuzidiwa na hicho kizunguzungu.

    ***

    "ubabe wa Oscar kujitoa katika mwili wa Noela ulififia baada ya Noela kuipandisha juu nguo yake ya kulalia na kufanya paja lake kugusana na la Oscar,hisia zilizotiwa hamasa na giza lililotanda pale ndani lilimfanya Oscar ajenge picha ya mpenzi wake aliyemwacha kijijini Kigoma na kumfanya asimwogope tena,yaliyotokea hayasimuliki japo ilikuwa nusu saa tu mashuka yalilowanishwa ipasavyo,kwa Noela ilikuwa shangwe kwani ile ndoto yake ilikuwa imetimia sasa lakini kwa Oscar licha ya kupata raha lakini uoga mkubwa sana ulimzunguka na kujiona msaliti namba moja duniani. Kimya kimya bila kusema neno alitoweka pale chumbani na kurejea katika chumba chake akimwacha Noela pale khtandani hoi.

    ***

    Deo alikuwa amenuia kweli kulipiza kisasi kwa moyo wa kijasiri aliandika kibarua kifupi kikimuelezea mama mchungaji juu ya ulokole wake feki na alitakiwa kuonana nao haraka kwani wana picha zake nyingi chafu alizopigwa enzi hizo kabla ya kuingia katika huo ulokole,japo Deo alifanya kwa kubahatisha lakini alijiamini sana kuwa ataiweza vita hiyo. Uoga ulimtanda wakati mama mchungaji ameenda kuitwa ndani,alipofika mama huyo mavazi ya heshima aliyoyavaa na heshima aliyopewa na waumini ilimwongezea uoga lakini Deo ambaye alijitambulisha kama Desmund hakujali na alijikaza akaufikisha ujumbe kisha akatoweka na kusubiri utendaji.

    "kama ni kweli alikuwa kiruka njia lazima akili imruke" alisema Deo kwa sauti ya chini wakati anaondoka eneo lile



    "wamejuaje niliyokuwa nafanya zamani mimi,mbona wanataka kuniharibia hawa na ndo hivyo wamesema nisipowatafuta wananitangaza kwa kila mtu,dah! Watanichafulia jina mie mama mchungaji nitaficha wapi sura yangu sasa,hivi hizo picha ni wakati ule Maisha club?? Au itakuwa Billicana....mh! Isijekuwa ni kwenye kitchen part ya Mwajuma nitaumbuka mimi yale mashanga na kanga moja nitajificha wapi?" Mama mchungaji alikuwa akijiuliza hayo punde baada ya kuwasili kwake na kujitupia kitandani,alikuwa ameusoma zaidi ya mara tatu ujumbe ule aliopewa na huyo mtu aliyejiita Desmund na yalikuwa ni maneno yaleyale hapakuwa na ndoto kati yake.

    "hebu ngoja nipige hizi namba zao"

    "07152870.....mh! Ninavyowapigia sasa nitawaambia nini? Nadhani kabla ya kupiga nijifikirie cha kuwajibu wakinipiga maswali" alisita kumalizia zile namba mama mchungaji na badala yake akaamua kutuliza akili kabla ya kukurupuka kupiga simu. Akili yake ilikuwa imevurugika sana hofu ya kuaibika ilikuwa inambughuzi akili yake,ulikuwa ni mshtuko mkubwa sana na jaribio la kipekee katika maisha yake.

    ***

    Dini ya uislamu ilikuwa imetawala sana maeneo ya Temeke lakini uvaaji wa baibui linaloziba sura kwa wanawake lilipingwa vikali kwani kuna vibaka,wezi na majambazi sugu walikuwa wanajivika vazi hilo na kuingia katika kazi zao hizo haramu katika jamii. Siku hii ya jumatatu asubuhi ya saa tano alishuka mwanamama huyu katika daladala za kutoka Mwenge kwenda Temeke akiwa na mavazi yaleyale yanayopingwa vikali na wananchi wa Temeke jijini Dar-es-salaam. Alikuwa hajiamini hata kidogo aligeuka huku na huko na wakati mwingine alijikwaa,hali hiyo ya kutojiamini iliwatia wasiwasi vijana wanaopatikana eneo lile.

    "mh! Huyu dume huyu washkaji" alisema kwa sauti ya juu kijana huyo aliyekuwa amevalia jinsi iliyojaa viraka na kiunoni ikiwa imefungwa kwa kamba ya katani alionekana kuwa mtu wa shari ambaye maisha yalikuwa yamempiga ipasavyo.

    "tumwanzishie huyu kibaka huyu huenda hata ndio waliovunja juzi kwa mama Hasan" aliendelea kusisitiza kijana huyu kwa hasira na chuki ya waziwazi. Taratibu sauti yake ikawaingia wenzake na wakaanza kuyaamini maneno ya kijana yule,alianza mmoja wakawa wawili hatimaye watano sauti zao zikageuka kuwa kelele kumuelekea yule mama.

    ***

    Siku ya jumapili usiku ulikuwa mrefu sana kutokana na mawazo mengi ambayo yalimtawala akilini. Alijifichaficha mumewe ambaye ni mchungaji asitambue matatizo aliyokuwa nayo,usoni alijichekeshajekesha na kwa ujanja huo alifanikiwa kumfunga macho mchungaji. Siku iliyofuata mchungaji aliwahi kwenda katika shughuli za kikanisa katika wilaya jirani ya Kibaha,mama mchungaji alidai kwamba bado ana kizunguzungu asingeweza kuongozana nae katika shughuli hizo "haya mwenyezi Mungu akubariki sana na hali yako irejee kama awali nakemea pepo hilo la magonjwa" mchungaji alitoa ombi fupi kisha akamuaga mkewe na kuondoka zake akiwa na biblia mkononi.

    Mama mchungaji alitumia upenyo huo kuangalia ni kitu gani atafanya kujiepusha na aibu iliyokuwa inamjia mbele yake.

    Haraka haraka alikuwa amefanya maamuzi aliyoamini kwake yeye ni sahihi tayari alikuwa amejitanda khanga iliyoziba nywele pamoja na uso wake almaarufu kama 'ninja' mama mchungaji alikuwa ndani ya daladala inayotoka Mwenge kwenda Temeke,alilipa nauli yake mapema kukwepa maongezi na usumbufu wa kondakta baadae.

    Ndani ya dakika 45,gari lilifika kituo cha mwisho,mama mchungaji ndani ya mavazi yake alikuwa wa tatu kushuka toka kwenye gari,kwa mwendo wa haraka haraka alianza kupiga hatua kuelekea mbele,ugeni wake katika vazi hili ulimfanya ashindwe kutembea vizuri na kuna wakati alijikwaa hovyo hovyo.

    "mh! Kuna nini tena hapa mbona kelele au..." alijiuliza mama mchungaji aliposikia makelele na miluzi nyuma yake,kelele zile zilizidi kumfuata kwa kasi na kabla hajajipa jibu tayari alikuwa amezungukwa na kuzongwa zongwa na kundi lile la watu

    Mama mchungaji hakuamini kuwa kundi lote lile la watu lilikuwa limemaliza safari yao mbele yake,mapigo ya moyo yaliongeza kasi sana aliukamata mkoba wake kwa nguvu mno kwani kwa upande mwingine alidhani wale pale ni wezi wanataka kumwibia kwa staili ya kumzingira.

    "nini? Nini?" kwa uoga mama mchungaji alianza kujitetea mbele ya kundi lile,ile sukumwa sukumwa ya hapa na pale ilipelekea kuanguka kwake,lakini kabla hajafika chini tayari ile kanga aliyokuwa amejitanda kichwani ilikuwa imetolewa na kumwacha uso na kichwa wazi.

    "ana bahati kumbe mwanamke kweli" alisema mmoja kati ya waliokuwa kwenye lile kundi kisha kila mmoja akatoweka na kumwacha mama mchungaji peke yake eneo lile. Juhudi zake za kuubana mkoba wake zilikwisha wakati anapepesuka kuelekea chini ni katika kipindi hicho hicho mikono ya kijanja ya kijana mmoja ilizama na kutoka na simu moja ya mama mchungaji.

    "Mungu wangu na simu wamechukua maskini wee nitafanyaje sasa mimi" alijiuliza mama mchungaji huku akitazamwa na wananchi wengine kana kwamba ni mwendawazimu fulani aliyetoroka hospitali,mwili wake ulijaa vumbi na nywele zake zilikuwa zimevurugwa sana na wale vijana wakati wa varangati lile.

    "eeh! Mwenyezi Mungu nisaidie waumini wa kanisa wasiwepo mitaa hii" huku akitetemeka alizungumza na wakati huo huo akijaribu kurudishia khanga yake kichwani na usoni. Kwa kuelewa kwamba heshima yake imeshuka tayari eneo lile mama huyu hakutaka kuongeleshana na mtu yeyote badala yake hatua kwa hatua akajitoa eneo lile kuelekea katika mitaa iliyochangamka zaidi kutokana na wingi wa nyumba zilizojengwa pale na kusababisha msongamano wa watu.

    "sijui ni njia hii hapa sijui ni kule,mama yangu leo napotea hapa na sijui itakuwaje sasa..kwaheri ndoa yangu" alijisemea kwa upole na sauti ya chini mama mchungaji huku akitazama pete aliyovishwa na mchungaji siku walipofunga ndoa takatifu kanisani.

    "Zinduna..nasema niachie we m¥€&** tena malaya mkubwa,niachie nisije nikakuchania blauzi yako huo mtindi ukabaki nje sasa hivi"

    "umchanie nani blauzi,unaijua thamani yake wewe,nakuuliza bwana yako anaweza kununua? Ashura nitakukun'guta mpaka uione dunia chungu"

    ulikuwa ni ugomvi kati ya wanawake wawili ambao kwa hali na matusi ya nguoni waliyotukanana walionekana kuwa katika mtafaruku mkubwa wa kugombea bwana,umati uliowazunguka haukuwa hata na wazo la kuwatenganisha katika ugomvi wao,zilikuwepo pande mbili na kila mmoja akishabikia mtu wake ili aweze kushinda.

    Mama mchungaji alipita jirani kabisa na eneo hilo macho yake yalivutia kwenda kutazama visa alivyovikosa kwa siku nyingi tangu aolewe na mchungaji.

    "he! Sio zinduna yule...ha! Na yule pale mbona ni Ashura" alisema kimoyomoyo mama mchungaji alipofika eneo lile

    "au nawafananisha jamani" alizidi kuwaza.

    "hapana ni hawahawa wabaya wangu yaani kweli wamegawa picha zangu zile mbaya na chafu ili waniharibie ndoa yangu nasema hivi UMAMA MCHUNGAJI Pembeni ngoja niwaonyeshe nadhani wamenisahau" alijiapiza huku hasira zikimpanda kwa kasi kubwa. Taratibu alianza kuwapangua watazamaji mmoja baada ya mwingine hadi macho yake yakawaona maadui wake ana kwa ana.

    "ni wenyewe ku*%$%" alitoa tusi mama mchungaji kisha kama nyati akatimua mbio kuwafuata wawili hawa kwa kasi.

    ***

    Mwonja asali haonji mara moja na haba na haba hujaza kibaba,ni misemo hii iliyotumika kuendeleza maasi baina ya Oscar mfanyakazi katika mabanda ya mifugo na Noela ambaye ni bosi wake. Licha ya kuoneana aibu siku iliyofuata baada ya kuibanjua amri ya sita katika kitanda anachotumia Noela na mumewe Timoth ambaye alikuwa safarini kikazi,sasa Noela na Oscar walibadili na kuhalalisha wizi wao kuwa kitu halali,mara leo bafuni,kesho sebuleni,mara waoge wote. Kwa kifupi hazikuwepo aibu tena na kila mmoja alifurahia uchafu na usaliti huo mkubwa na usiofaa kuigwa hata kidogo.

    "Oscar unajua tumekuwa tukijisahau sana?"

    "mbona unasema hivyo Noela,kipenzi changu" alijibu kwa njia ya swali Oscar wakati wakienda kuoga na Noela katika bafu la mumewe (Timoth).

    "hatujawahi kutumia kinga na leo ni mara kama sikosei ya tisa tunafanya mapenzi"

    "ni mara ya kumi na moja mimi huwa nahesabu" Oscar alimkosoa Noela kwa takwimu zake alizotoa.

    "mimi katika uwanja huu kwa takwimu zake Magufuli chamtoto,yaani hadi lita nilizokunywa kwako nakumbuka ni lita themanini point sita" alitania Oscar wakajikuta wote wanacheka.

    "we shauri zako uje unipe mimba!" alilalamika Noela



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog