Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

JAMANI MCHUNGAJI !! - 5

 





    Simulizi : Jamani Mchungaji !!

    Sehemu Ya Tano (5)



    Giza la ghafla limetokea katika mkutano wa injili majira ya saa tano usiku,sauti ya mchungaji Marko iliendelea kutetema kwa mbali hata bila kutumia kipaza sauti aliweza kuendelea na mahubiri yaliyowavutia wengi. Ghafla amani inatoweka na kila aliyekuwa eneo lile alianza kuitafuta amani yake,jukwaa lilikuwa limetapakaa damu
    ENDELEA

    Roho mbaya iliyokuwa imemwingia Timoth ndiyo hiyo iliyomtuma kutenda uovu huu,silaha yake kubwa ilikuwa ni mshale wake aliokuwa nao ndani ni huu pekee aliamini ungeweza kuwa dawa ya mchungaji Marko kwa tabia yake ya kuchukua wake za watu

    Timoth kwa mara nyingine aliingia katika vita lakini safari hii alikuwa peke yake bila ushirikiano kutoka kwa Deo.
    “mambo vipi Timoth habari za siku nyingi rafiki yangu yaani umekuwa kimya mpaka naogopa” sauti ya Deo ilisikika pale Timoth alipopokea simu yake.
    “majukumu mengi tu rafiki yangu,mi mzima nipo tu!!!” alijibu kinyonge Timoth.
    “nina ujumbe wako bwana amakweli we mwanaume wa shoka ndugu yangu” alianza kuongea Deo kwa mshawasha mkubwa lakini Timoth hakusikika kuwa na furaha yoyote ile na badala ya kujibu alikata simu kasha akaizima kabisa.

    Majira ya saa nne nne usiku tayari alikuwa eneo la tukio pamoja na silaha zake tayari kwa mapambano makubwa yaliyomkabili mbele yake. Hakuna aliyemtambua alijificha mbali kidogo na kundi la watu,kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo watu walivyozidi kusogea eneo la tukio kutokana na kuvutiwa sana na mahubiri motomoto ya mchungaji Marko,lakini tofauti na hisia za wengine siku hiyo kwa Timoth ilikuwa tofauti sana kwani kadri mchungaji alivyozidi kuhubiri hasira zake zilizidi kupanda na chuki ikaongezeka dhidi ya mchungaji yule.

    lilipowadia somo la ndoa ndio Timoth hasira zake zilipanda maradufu kwani aliamini mchungaji anaurubuni umati wote ule uliokuwa pale.
    “……..utasikia mwingine anasema eti nahisi naibiwa mke wangu,tena mbele ya wanaume ambao wametulia na ndoa zao salama kabisa zikiwa na amani tele,anashangaa kwa nini wenzake wanafurahia ndoa zao jibu ni rahisi sana wamezikabidhi ndoa zao kwake mweza wa yote naye si mwingine ni mwenyezi Mungu” sauti nene ya mchungaji Marko ilikuwa inarindima kwa kishindo,Timoth kwa mara ya kwanza akajikuta anashindwa kuzuia hasira zake,sehemu aliyokuwa amejificha ilikuwa jirani na chumba ambacho umeme ulivutwa kutoka pale,kwa mwendo wa kunyata alisogea mpaka katika chumba kile na kuuchomoa waya uliokuwa unatoa umeme pale,giza lililotokea lilimkosesha ramani ya kumwona vizuri mbaya wake.

    Hakuna kosa kubwa alilofanya mchungaji kama kuendelea kupaza sauti yake wakati tatizo la umeme likiendelea kushughulikiwa na watu waliowekwa kwa ajili hiyo. Timothy kwa ujasiri alitumia mwanya huo mbio mbio akapanda jukwaani akiwa na mkuki wake mkononi moja kwa moja katika mgongo wa mchungaji hakusubiri kujua nini kitaendelea aliruka kutoka pale jukwaani na kutua chini akimwacha mchungaji Marko akigalagala kwa uchungu pale jukwaani na maumivu hayo yakifuatiwa na kilio kikali sana,harufu ya damu iliyotapakaa eneo lile ndiyo ilikimbiza watu hapa na pale wakijua kuna hali kubwa ya hatari mbele yao. Mkuki ulikuwa umemuingia vyema mchungaji katika mgongo wake kama Timoth alivyokuwa amepanga. Hakuna aliyegundua harakaharaka aliyetenda ukatili ule kwa mchungaji wa kanisa ambaye mamia kwa mamia walimpenda sana kutokana na moyo wake wa kujitolea kwa sababu ya kanisa na wafuasi wake. Mahubiri yake ya siku hiyo ndiyo yaliwavuta wengi zaidi kuamini kuwa mchungaji Marko alikuwa akiifanya kazi ile ya utumishi kutokea moyoni,hakuogopa kusema ukweli hata siku moja.
    Sasa alikuwa ameanguka chini damu zilikuwa zinamvuja kwa kasi na alikuwa ameuma meno yake kwa uchungu lakini bado kilio cha maumivu kilisikia. Hadi umeme ulipoweza kuwaka tena baada ya marekebisho madogo yaliyofanywa na wataalamu mchungaji hakuweza kusema neon zaidi ya kunyoosha mkono wake kama vile anaomba kitu huku mkono mwingine ukiwa kama unauzuia mkuki usitoke pale ulipokuwa umejichimbia kwenye mwili wake,hakuwepo mama mchungaji eneo lile kumwangalia mumewe,watumishi walikuwa kama vichaa kwani waligongana hapa na pale bila kufanya lolote la maana hadi waliposhuhudia mchungaji anatulia tuli bila kusema neno lolote.

    *****
    Kila mtu aliyeshuhudia kilichomtokea mchungaji pale jukwaani na hali iliyojionyesha dhahiri ya kutulia ghafla pale pale alipokuwa huku mkuki ukiwa umezama katika mgongo wake,watu waliamini tayari mtumishi huyu alikuwa maiti na hakuna cha kuzuia jambo hilo hata ilipopatikana gari kwa ajili ya kumpeleka hospitali lilifanywa jambo hilo kama kutimiza wajibu tu!
    “maskini sijui hata amewakosea nini bwana huyu,kifo chake ni cha uchungu sana yaani kinasikitisha” alisema maneno hayo mtumishi wa Mungu aliyeshuhudia gari likitimua vumbi kuliacha eneo hilo na kwenda hospitali kwa ajili ya kujaribu kuokoa maisha ya mchungaji Marko. Mkuki aliokuwa nao uliendelea kubaki eneo lilelile mwilini kwani alishauriwa kubaki hivyo hivyo kitendo cha kuthubutu kuun’goa pale ilikuwa ni kukamilisha mauti ambayo walisubiri daktari aweze kuyathibitisha kwani macho yao tayari yalikuwa na majibu kuwa mchungaji amefariki dunia,jambo lakushangaza hadi wanafika hospitali bado mke wa mchungaji alikuwa hajaonekana. Noela ndiye alikuwa kama mke wa mchungaji kwani katika kila hatua alikuwepo akiwa pamoja na msaidizi wake katika kazi (Oscar). Uchungu aliokuwanao Noela kila mmoja aliutambua kwa wale waliomshuhudia akihangahika huku na kule baada ya mchungaji kupatwa jambo hilo la kusikitisha na kuhuzunisha sana
    Timoth baada ya ukatili ule alioufanya kwa mchungaji wa kanisa lake aliondoka kwa kasi ya ajabu hadi nyumbani kwake bila kutambuliwa na mtu yeyote kuwa huenda anahusika,lilikuwa tukio lake la kwanza kutoa mtu damu lakini hakuwa na uoga wowote aliona amefanya jambo sawa kabisa na lilikuwa halitoshi kuuridhisha moyo wake.

    “huo ni mwanzo naamini atakoma sasa kuchezea wake wa watu wakati nayeye ana wa kwake,halafu asivyokuwa na adabu anahubiri kuwa sisi tunaolia kuibiwa hatuna akili haya ameziona akili zetu huo ni ujumbe tosha” aliongea peke yake Timoth wakati akivua nguo alizozitumia kwenye tukio na kuvaa nyingine kasha akajilaza kitandani na kupitiwa na usingizi fofofo uliotokana na uchovu wa kukimbia kwa kasi hadi kwake hadi alipokuja kushtuka asubuhi ya siku iliyofuata.
    Katika hospitali ya taifa ya Muhimbili,mchungaji Marko alifikishwa huku sala za waumini zikilipeleka jina lake katika uso wa bwana aweze kumuepusha na janga la kifo lililokuwa linanukia mbele yake,sala hizo ziliweza kumfikisha akiwa hai katika kitanda cha wagonjwa mahututi mbele ya daktari bingwa wa magonjwa yahusuyo mwili wa mwanadamu aliyefahamika kwa jina la dokta Mpejiwa mzaliwa wa Kahama katika mkoa wa Shinyanga. Katika uzoefu wake wa kazi kamwe hakupenda kupoteza maisha ya mwanadamu katika huduma zote za kiafya zinazoletwa mbele yake. Na sasa alikuwa katika mtihani mwingine ambapo mchungaji mkuu wa kanisa lake alikuwa katika hali mbaya sana iliyokuwa inakatisha tama sana na dakika yoyote ingesababisha vilio kwa waumini na watu wote waliomfahamu au kuzisikia sifa kemkemu alizomwagiwa mchungaji huyu. Kwa madaktari wengine mtihani huu ulionekana kuwa mgumu lakini yeye alijiaminisha kuwa ilimradi mchungaji badoanapumua basi ataendelea kupumua tena hadi anavyoondolewa pale hospitalini. Kiujasiri kabisa Dokta Mpejiwa aliingia kijasiri sana katika chumba alichoingizwa mchungaji akiongozana na wauguzi watatu tayari kwa kukumbana na mtihani huo mbele yake.
    Mapigo ya moyo ya mchungaji yalikuwa mbali sana hali iliyopunguza asilimia chache za matumaini ka daktari huyu na kidogo kuanza kuhisi huenda mchungaji alikuwa katika hatua za mwisho za kuvuta hewa chafu ya dunia hii dhaifu. Mashine za kupumulia alizovalishwa zilimsaidia sana kuweza kuongeza dakika za kuishi lakini ubaridi katika mwili wake ulimaanisha mzunguko wa damu ulikuwa katika kasi ya chini sana ambayo ingesimama wakati wowote ule na kulibadili jina lake kuwa maiti halafu marehemu
    Ilianza siku ya kwanza,ya pili,ya tatu hadi ya saba bila hali ilikuwa ile ile ya awali mchungaji alikuwa hajafumbua macho wala kusema neno yaani alikuwa hajazinduka bado kutoka katika safari ya usingizi aliyoianza ghafla usiku wa mwisho wa mahubiri ya huduma za kiroho. Hali sasa ilikuwa tata,waumini hawakukoma kufunga na kusali kwa ajili ya kumuombea mchungaji wao aliyekuwa katika usingizi wa kifo,daktari Mpejiwa naye hakukata tamaa aliendelea na jitihada zote za kujaribu kokoa uhai wa mtumishi huyu wa Mungu.
    Baada ya kuwa amekaa kimya kwa muda wa siku thelathini sasa mtumishi wa Mungu,mchungaji Marko alikuwa ameweza kupata fahamu zake tena,japo alikuwa ameperaraizi upande mmoja wa mwili wake lakini ule uwezo wake wa kuongea japo kwa sauti ya chini ilikuwa furaha tosha kwa waumini wake na wasiokuwa waumini lakini kwa daktari Mpejiwa ulikuwa ni ushindi na kumbukumbu nzuri katika maisha yake kwani ni yeye alikuwa ameshikilia furaha ya maelfu ya watu,ni yeye aliyekuwa na uamuzi wa kuleta vicheko au vilio na sasa aliamini ameleta tabasamu pana kwa watu.
    “unatakiwa uendelee kuwa hapa hospitali hadi hapo utakapopona kabisa” daktari Mpejiwa alimwambia mchungaji Marko masaa machache baada ya kuwa ameshtuka kutoka usingizini.
    “hapana hapana,Mungu amenituma kuihubiri injili yake na wakati ndio huu,kwa nini nilale?” alijibu mchungaji huku akishangaa kwa nini yuko pale. Daktari akishirikiana na wauguzi pamoja na wanakanisa wengine walijaribu kumueleza kila kitu kilichotokea na ni kwa muda gani alikuwa kama maiti pale kitandani akilishwa kwa kutumia mipira.
    “mwezi mzima??? Yaani sijatoa huduma mwezi mzima hapana ni uzembe wa hali ya juu” alijibu Mchungaji kwa sauti ya chini alijibu. Baada ya maongezi marefu mchungaji Marko akiwa tayari amepooza upande wa kulia wa mwili wake alipata ruhusa ya kwenda kufanya mkutano alioahidi kuwa kuna mengi sana ya kuwaeleza wananchi kuhusu injili. Kanisa bila hiana likaandaa mkutano huo wa hadhara kama alivyohitaji mchungaji Marko.




    Ulikuwa mkutano mkubwa sana uliohudhuriwa na mamia ya watu,hata wasiokuwa wahusika rasmi wa kanisa hilo siku hiyo walihudhuria katika tukio hili lililovuta hisia za waumini na wasiokuwa waumini,muda uliokuwa umepangwa kwa ajili ya shughuli hii ulikuwa ni saa nne na nusu asubuh

    i lakini kufikia saa mbili asubuhi kiwanja kilikuwa kimefurika watu wa kila rika watoto,wakubwa,wazee kwa vijana na wanaume na wanawake wote walikuwa na shauku kubwa ya tukio lililokuwa limekonga nyoyo zao viti tayari vilikuwa vimejaa na watu wazima hawakuona ajabu kukaa chini huku wengine wakithubutu kukaa chini kabisa ilimradi tu waweze kuwa miongoni mwa mashuhuda wa tukio hili. Kwaya kutoka mikoa mbalimbali zilialikwa kutoa burudani yenye ujumbe ndani yake kwa watakaobahatika kuwasikia.
    ****
    Timothy alikuwa mtu mwenye furaha sana tangu tukio lile la kusikitisha lilipotokea,kinyume kabisa na Noela pamoja na Oscar waliokuwa na simanzi japo waliilazimisha furaha wakati mwingine,hawakuamini mchungaji yule aliyekuja pale usiku akiwa na afya tele leo hii yupo hoi kitandani hajiwezi kwa lolote na hata chakula pia analishwa. Waliamini furaha ya Timoth ilitokana na Noela kuwa mjamzito na kwa sababu ulikuwa wa kwanza basi lazima furaha kila siku,mapenzi kwa mkewe Noela yalikuwa yameongezeka maradufu kwani kitendo cha Noela kutulia nyumbani muda wote bila kumwongea mchungaji lilimhakikishia adui yake ameisha makali. Lakini uhakika huo uliisha makali yake usiku mmoja uliopita baada ya kushuhudia kwa macho yake tena masikio yake yakiwa makini kusikiliza kilichokuwa kinatokea katika chumba cha Oscar maneno aliyoyasikia yalikuwa yanazunguka kwa kasi katika kichwa chake bila kuwa jasiri angeweza kufanya kitendo kingine kichafu mara ya pili katika mwezi mmoja na mara ya tatu ndani ya miezi miwili.
    Mchungaji Marko alifikishwa pale kwa shangwe kubwa lakini aliposhushwa akiwa katika kiti cha kutembelea wagonjwa furaha za watu zikageuka vilio sasa,alikuwa ndani ya suti ya suti yake nyeusi ambayo haikuweza kuutosha mwili wake vyema kutokana na kukondeana sana. Mkononi aliishikiria kwa ujasiri biblia yake,moja kwa moja hadi jukwaani ambapo aliwekwa mbele kabisa na kukabidhiwa kipaza sauti ili aweze kuanzisha mkutano ule kasha yeye arejee hospitali kwani kwa hali yake hakuweza kukaa kwa muda mrefu eneo lile.
    “bwana asifiwee watu wa Mungu” alianza mchungaji Marko kwa sauti iliyokwaruza kwaruza.
    “ameeeeeen!!!!” walijibu kwa sauti ya juu mamia ya waliofika eneo lile huku wengine wakishindwa kabisa kuzuia vilio vyao muda wote.
    “bwana ni mwema na mwenye huruma,hakuna mwenye haki atakayeaibika akiwa naye moyoni mwake……..hayo ndiyo bwana amenitendea,sala zenu zimenifikisha hapa nilipo,nilitakiwa kuwa nimezikwa zamani sana lakini bado ni hai bwana asifiwe!!.....hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kuukatisha uhai wa kiumbe ambaye bado bwana anahitaji huduma zake katika hii dunia,ulemavu wa mwili sio sawa na ulemavu wa akili,ilimradi naweza kusema na nikasikika basi amani ya bwana iwe naye aliyeunyanyua mkuki na kunichoma nao katika mgongo wake,hata yeye ni mwanadamu aliyeumbwa na Mungu aliyeniumba mimi basi kama yupo hapa mimi namwambia nampenda sana na nimemsamehe zamani sana kwani lazima ana sababu zake zakufanya hivi kwani mimi ni nani hata nisitendwe hivi??? Hakika mimi si kitu na wala sijakamilika” alizungumza mchungaji maneno ambayo yaliwagusa wengi sana,ukimya ulikuwa wa hali ya juu kwikwi za hapa na pale zilitawala kwa walioshindwa kujizuia kulia.
    “najua nitaumia sana kwani nilipenda kumchezea bwana kwa shangwe katika viwanja hivi lakini kamwe sitajutia kwani hata walemavu wanaweza pia kucheza kwa mbinu zao ambazo hivi karibuni nitajifunza na kuzielewa……” aliendelea mchungaji kabla ya kukatishwa kidogo na mtumishi aliyekuja kumnon’goneza.
    “hamna shida mwambie aje tena ajisikie huru!!” alijibu mchungaji baada ya kuambiwa ujumbe flani na mtumishi.
    “karibu karibu sana” alikaribishwa jukwaani kijana huyu mtanashati ambaye alikuwa hana uoga wowote na macho yake mekundu kutokana na kulia muda mrefu yalielezea uchungu aliokuwa nao.
    “katika maisha ya kila siku ushuhuda ni kitu ambacho kinaongeza imani na kwangu mimi,ushuhuda ni zaidi ya mahubiri ya kawaida sasa wakati napumzika kidogo kuna ushuhuda tunatakiwa kuusikiliza kutoka kwa mmoja wa waumini wetu” alisema mchungaji kisha akamkabidhi kipaza sauti mtumishi mwingine.
    “kabla sijazungumza lolote ningependa familia yangu pia iwe hapa kwani hawa ndio mashahidi wangu,na kama nawe pia ni shahidi wa hili nitakalosema tafadhali usisite kupanda jukwaani” alianza kijana huyo,hakuwa mwingine bali Timoth ambapo Noela na Oscar kwa furaha walipanda jukwaani.

    “maisha ya ndoa niliyaogopa kuanzia mwanzo sikutarajia kuoa mapema lakini jitihada za mchungaji Marko pamoja na mama yangu mzazi hatimaye nikamuoa mke wangu huyu kipenzi anaitwa Noela ni mwanakwaya wetu pia,nimefurahia mengi katika uhusiano wangu huu lakini leo kwa uchungu na kwa msukumo wa moyo wangu nachukua nafasi hii kuyazungumza machungu niliyoishi nayo kwa muda mrefu sana,hisia potofu zilivyoyumbisha maisha yangu na kuivuruga kabisa akili yangu. Sitaficha lolote nitauelezea umma ukweli wote atakayeumia na aumie kwani ni kwa muda mrefu naumia mwenyewe” alisisitiza Timoth na kuzidi kuvuta umakini wa watu pale ambao taratibu walianza kusahau kuhusu mchungaji Marko na sasa macho yao yalikuwa kwa Timoth
    Sitaficha lolote nitauelezea umma ukweli wote atakayeumia na aumie kwani ni kwa muda mrefu naumia mwenyewe” alisisitiza Timoth na kuzidi kuvuta umakini wa watu pale ambao taratibu walianza kusahau kuhusu mchungaji Marko na sasa macho yao yalikuwa kwa Timoth.

    “Sipo hapa kwa ubaya bali wema tupu,na nia yangu ni kuitafuta amani iliyokuwa imetoweka moyoni mwangu siku nyingi. Hasira zangu na chanzo cha hayo yote ni moyo wangu uliopondeka na hatimaye kukubali kupokea hisia chafu sana hisia za kwamba mke wangu wa ndoa ananisaliti pamoja na mchungaji mkuu wa kanisa langu!!”
    “aaaaaaaah!!!!” watu wote waliguna kwa mshtuko kusikia hivyo,hata waliokuwa wamekaa pale jukwaani walishangaa.
    “hizo zilikuwa ni hisia na wala sio uhakika hata kidogo,lakini kwa binadamu wa kawaida ile hali ilikuwa inaleta mawazo mabaya,kila mara mke wangu aliongea kuhusu mchungaji,ni mara nyingi walikuwa naye na mbaya zaidi hata ndoto zake alitaja neon mchungaji,niliumia sana ndugu zangu niliumia mno……….hiyo haitoshi nikawaona siku moja wanatoka maeneo yaliyokuwa karibu na nyumba ya kulala wageni,ndugu zangu kabla hamjanipa hukumu yoyote hebu fikiri ungekuwa wewe ungefikiriaje??? Ni mengi sana niliyoshuhudia ambayo yaizidi kunithibitishia kuwa mchungaji ana uhusiano wa kimapenzi na mke wangu mimi lakini kamwe sikuwahi kumuuliza mke wangu kwani sikuwa na uhakika lakini mambo yalivyoniwia magumu nilithubutu kumshirikisha rafiki yangu kipenzi anaitwa Deo nadhani yeye aliumia kuliko mimi na ni huyo aliyenishauri kuwa tulipize kisasi kwa mchungaji huyu kwa tabia yake hiyo mbaya,kisasi chenyewe kilikuwa kumtendea kama yeye anavyowatendea wenzake. Mpango mzima wa kumuingiza majaribuni mama mchungaji ulipangwa na ukafanikiwa kwa kiasi kikubwa,na hatimaye mimi Timoth nikazini na mama mchungaji ili kupunguza maumivu niliyokuwa nayapata kwa kuibiwa mke wangu………najua mama mchungaji hakuniona sura yangu lakini nilimtambua kuwa ni yeye. Niisema maneno yangu yanaweza kuumiza wengi lakini huo ndio ukweli naomba watu tuwe watulivu na wavumilivu ili niweze kumaliza dukuduku langu moyoni” alizungumza Timoth huku umati ukiwa kimya na kutawaliwa na mshangao mkubwa sana kwa maneno aliyokuwa anazungumza Timoth,kwa ufupi ilikuwa kama sinema ya kusadikika na ngumu kuaminika. Mama mchungaji alikuwa kama amemwagiwa maji ya baridi tena amevuliwa nguo zote hadharani na wakwe zake wakiwepo mbele yake,ni kama alitamani apate uwezo wa kugeuka upepo na apotee pale mara moja lakini haikuwezekana hata kidogo aibu ilikuwa juu yake. Noela na Oscar hawakuweza kuangaliana usoni kwani waliamini zamu yao sasa inakuja ndani ya muda mfupi walitamani itokee mvua ya ghafla ili mkutano uvunjike lakini ndio kwanza miale ya jua ilizidi kuchanua eneo lile. Mchungaji alikuwa ametulia tuli hakuwa na papara zozote zile.
    “ni usiku uleule niliporudi nyumbani kwangu naye mchungaji alikuja kwangu kwa tatizo moja kuwa mke wake (mama mchungaji) alikuwa haonekani pale nyumbani na milango ilikuwa imefungwa,kwa mara ya kwanza katika maisha yangu niliweza kupoteza fahamu kutokana na mvutano wa mawazo kuwa aidha mchungaji alikuwa na tabia ya kuja kumchukua mke wangu kwa staili ile au ilikuwa imegundulika kuwa nimelala na mkewe siku ile na sasa alikuwa amekuja kumueleza mke wangu,hata nilivyopata fahamu na kujua nini kinaendelea sikuwa tayari kwenda kwa mchungaji kumsaidia katika tatizo lililomkabiri kwani nilikuwa naujua ukweli moyoni kuhusu mama mchungaji. Nilimwomba aongozane na huyu kijana Oscar pamoja na mke wangu Noela ili mimi niweze kupumzika kwani kichwa kilikuwa kinaniuma,…….sikuweza kukaa muda mrefu pale ndani hisia zikanivuta kuwa kuna janja nimechezewa na wawili hawa hivyo baadae kidogo nikaamua kufuata nyayo hadi nikafika kwa mchungaji,kama nilivyokuwa nawaza katika chumba kimoja pale nilishuhudia yaleyale tena na jina la mchungaji likitajwa pale chumbani,hasira zilinishika nikataka kufanya fumanizi lakini kabla hata sijafanya lolote niliona kuna mwanga mkali unaelekea pale nilipokuwa,kwa kuhofia kupigiwa kelele za mwizi niliamua kutoweka tena kwa mbio kali nilianguka na kuumia mkono wangu huku nikichubuka kwenye goti
    “Sipo hapa kwa ubaya bali wema tupu,na nia yangu ni kuitafuta amani iliyokuwa imetoweka moyoni mwangu siku nyingi. Hasira zangu na chanzo cha hayo yote ni moyo wangu uliopondeka na hatimaye kukubali kupokea hisia chafu sana hisia za kwamba mke wangu wa ndoa ananisaliti pamoja na mchungaji mkuu wa kanisa langu!!”
    “aaaaaaaah!!!!” watu wote waliguna kwa mshtuko kusikia hivyo,hata waliokuwa wamekaa pale jukwaani walishangaa.
    “Mungu wanguuuuu!!!!!” umati ulipiga kelele kusikia taarifa hiyo inayoshtua na kuaibisha sana kanisa. Timothy hakuwa na hofu kwani kilichokuwa mbele yake alikitambua.

    Kabla hajaendelea Timoth alishuhudia kundi la watu wakimzuia mtu ambaye alimtambua vizuri

    “tafadhali mwacheni aje ana mengi ya kuwaeleza” Timoth aliwaomba wale watu waliodhani kijana yule alitaka kuleta fujo,alikuwa ni Deo mbele ya jukwaa sasa,mapigo ya moyo ya mama mchungaji yaligonga kwa kasi sana alipomuona kijana huyu pale mbele alijua longolongo aliyopanga kujitetea nayo imefika ukingoni.
    “tafadhali mwacheni aje ana mengi ya kuwaeleza” Timoth aliwaomba wale watu waliodhani kijana yule alitaka kuleta fujo,alikuwa ni Deo mbele ya jukwaa sasa,mapigo ya moyo ya mama mchungaji yaligonga kwa kasi sana alipomuona kijana huyu pale mbele alijua longolongo aliyopanga kujitetea nayo imefika ukingoni.




    DEO

    “Mama mchungaji sikutegemea kama kweli yuko kama nilivyodhani, mavazi yake ya nje ni mazuri sana lakini ni kahaba mzoefu,nasikitika kusema mbele ya umati huu kwamba ni kweli nilipanga mpango huu ili kumsaidia rafiki yangu kipenzi katika kulipa kisasi kwa mchungaji na ndio maana mama mchungaji hakupata nafasi ya kumuona Timoth kutokana na giza la pale ndani. Lakini kabla ya Timoth mambo hayakuwa mepesi mama mchungaji kwa maksudi mazima aliniingiza majaribuni kwa mavazi aliyokuwa amevaa na vitendo alivyokuwa anafanya kwa hayo niliyosema ni kwamba hatimaye nilizini na mama mchungaji na hiyo mamba aliyonayo ni ya kwangu wala sio ya Timoth kama anavyodhania lakini kikubwa ni kwamba mama mchungaji ni kahaba.” Alimaliza Deo a kuongeza hamu ya watu kusikiliza nini maana ya haya yote,Timoth alishikwa na mshtuko lakini kwa sababu alikuwa amejiandaa kushuhudia haya aliweza kuchukua kipaza sauti na kuendelea.

    “ni jana usiku niliposhtuka usiku kutoka usingizini ndipo nilipata jibu la machungu yangu ya siku nyingi …..sikumkuta mke wangu pembeni yangu nikahisi ameenda chooni lakini kadri alivyochelewa ndivyo wasiwasi ulivyozidi kunitawala nikaamua kufatilia hadi katika chumba cha Oscar ambaye ni msaidizi wa kazi pale nyumbani nitanukuu niliyoyasikia japo kwa ufupi na wenye watoto mnisamehe hii ni hali halisi kabisa na kama nikipunguza maneno sana nitaupotosha ukweli” alisema Timoth na kuanza kunukuu kama ifuatavyo

    NOELA: Mchungaji jamani,ni siku nyingi ujue tafadhali fanya haraka niende kulala nimemuacha yule boya amelala fofofo

    OSCAR: Nawewe ulivyozoea kuniita mchungaji jamani au unanifananisha na mchungaji wako wa kanisa

    NOELA:Mh! Yaani wewe ufanane na yule mzee na likipara lake nimpeleke wapi au unataka anifie chumbani nipate mada kesi??(wau wote wakacheka pale aliposema hivyo)

    OSCAR:Dah! Na mimi siku moja utaanza kuniponda eeh!!

    “maneno hayo yalinitosha kabisa kwani nilihisi wanaweza wakaanza kunitusi na mimi nikose uvumilivu na kufanya vibaya palepale,aliporudi aliniambia eti ametoka kuoga sio siri niliumia sana kushuhudia eti Oscar kijana niliyekuwa namwamini nayeye akawa kati ya watu waliouumiza moyo wangu kwa juhudi zote”

    “maskiniiiiii!!!!!!” kina mama walimsikitikia Timoth kwa hilo lililomtokea,Noela na Oscar walikuwa kimya na aibu kuu mbele yao.

    “nampa nafasi ya kuongea japo kidogo mheshimiwa Oscar najua nayeye ana mengine msiyoyafahamu” alisema Timoth huku akimkabidhi Oscar kipaza sauti.

    OSCAR
    “Kwanza naomba msamaha kwa yote yaliyotokea lakini sio kusudio langu bali ni msukumokutoka kwa Noela,alitumia mbinu zote kunilaghai na hata vitisho pia alitumia,kwa mara ya kwanza naweza kusema alinibaka likini kwa siku nyingine sina la kujitetea kwani tulifanya tena kwa hiari yetu wenyewe hasahasa wakati kaka Timoth……….”
    “aaaaaaa mimi sio kaka yako labda unite mume mwenzako” aliingilia maongezi hayo Timoth.

    Oscar akaendelea

    “alipokuwa amesafiri ndio tulikuwa kama mtu na mkewe,tuliendekeza sana tabia hii hadi ikawa mazoea nasikitika kuwa hayawi hayawi hatimaye yakawa Noela aka….aka…..akapata ujauzito lakini akaniahidi atamsingizia Timoth na hiyo ndio hali halisi hadi sasa,mimba aliyonayo Noela ni ya kwangu sio ya Timoth kama anavyodhani” alimaliza Oscar wakati huo Timoth alikuwa anatetemeka kwa hasira kubwa kwa kugundua kuwa mimba zote zilikuwa hazimuhusu hata kidogo.

    “ni hayo ndugu zangu yaliyonisukuma mimi Timoth kuchukua hatua mbaya sana hatua ya kutoka kwangu nikiamini mchungaji ndiye adui yangu namba moja katika hii dunia kumbe nilisahau kuwa kuna wachungaji wa aina mbili mwingine ni mchungaji wa mali za watu wakati mchungaji mwingine kazi yake ni kuongoza watu katika njia ya uzima,kumbe siku zote zile Mchungaji aliyekuwa anakuja katika ndoto za mke wangu,mchungaji alifanya zinaa na mke wangu katika sehemu tofauti hakuwa mchungaji huyu aliyekuwa katika usingizi kwa mwezi mzima bila kosa lolote lile lakini mchungaji halisi ni mchungaji Oscar. Kwa mdomo wangu natoa laana kwa mkono wangu wa kuume ulio….ulioshika mkuki na kumchoma mchungaji Marko na kumsababishia kupooza.” Kwa kusema neno hilo kelele nyingi sana na palizuka fujo kubwa ya ghafla mno,watu walikuwa na hasira juu ya mtu aliyemtenda vibaya mchungaji huyu na huyo mtu sasa alikuwa mbele yao akijitangaza hadharani,wengine walimwonea imani Timoth kutokana na alivyojieleza na chanzo chote cha maasi hayo.Yalijengeka makundi mawili yanayomtetea Timoth na yale yanayompinga vikali.
    Kuona dalili za fujo kubwa inataka kutokea na hapakuwa na chombo chochote cha usalama eneo lile mtumishi mmoja aliamua kumpa kipaza sauti mchungaji Marko aliamini sauti yake ingerudisha amani eneo lile.

    Mchungaji alipopewa kipaza sauti hakukipokea japo alionekana kama vile alikuwa anakiona tena vizuri sana,mtumishi alijaribu kumsisitiza mchungaji lakini hakupokea jibu hata la vitendo,mchungaji alikuwa ametulia tulii katika kiti chake cha wagonjwa alicholetwa nacho pale jukwaani.

    ****

    Kadri alivyokuwa anasikia maneno yale makali kutoka kwa Timoth,mchungaji Marko alikuwa anapatwa mshtuko uliokuwa unaathiri ubongo wake kwa kasi ya ajabu,na hasa hasa aliposikia habari kuhusu mkewe na tabia mbovu za usaliti alizofanya tena hadi kufikia hatua ya kupata mimba ni palepale neno hilo lilipelekea kupoteza fahamu zake akiwa ametulia tuli macho yake yakiwa wazi kama vile anaona kinachoendelea,hata mtumishi alipokuwa anampa kipaza sauti ili aweze kutuliza ghasia iliyotaka kuzuka pale yeye (mchungaji) alikuwa katika ulimwengu mwingine kabisa. Ilimchukua mtumishi dakika tano kuweza kugundua kuwa pale ulikuwepo mwili wa mchungaji na sio mchungaji mwenyewe. Haraka haraka alitoa taarifa hiyo kwa wenzake na kumkimbiza katika gari la wagonjwa lililokuwa jirani. Timoth kwa kuhofia usalama wake alitimua mbio kuelekea katika kituo cha polisi kilichokuwa jirani huku mam mchungaji akiungana na Noela pamoja Oscar katika kuibeba aibu iliyowakumba watu waliwazomea sana na hawakuwa na la kujibu kwa umati ule.

    Mchungaji alikuwa ameathirika sana katika ubongo wake uliosababisha kupararaizi upande wa pili uliokuwa umebaki hivyo kusababisha mwili wote kupoteza hisia zake na haikuwepo njia yoyote ya kumsaidia kitaalam zaidi ya daktari Mpejiwa kutoa ushauri wa kurejeshwa nyumbani ambapo angemaliza maisha yake yaliyobaki kitandani au kusubiri muujiza kutoka kwa Mungu.

    Kwa upande wa Timoth alihukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kufanya jaribio la kutaka kuua,na hakusikitishwa na adhabu hii kwani ilikuwa haki yake kabisa. Noela na mama mchungaji hawakusubiri talaka zao walijiongeza wenyewe kutoweka katika jiji hilo la Dar kwa aibu kubwa huku Oscar akirejea kijijinini kwao kujipanga upya kwa maisha mengine na kusahau kabisa kuhusu yaliyotokea kwa Noela.

    Mchungaji alibakia katika hali ile ngumu ya maisha huku akiendelea kumtukuza Mungu kwa kuendelea kumpa uhai hasahasa uweza wa kuendelea kuzungumza vyema kwa mdomo wake ili aendelee kuihubiri injili yake. Waumini waliendele kuwa karibu yake huku imani yao ikiwa bado thabiti kwa mtumishi huyo wa Mungu lakini kila walipokumbuka enzi za uzima wa mchungaji huyu na sasa walipoangalia mateso anayoyapata mchungaji Marko walibaki na neno moja tu “AH! JAMANI MCHUNGAJI!!!!”
    ***************MWISHO************

0 comments:

Post a Comment

Blog