Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

KIFO CHA MTU ASIYE NA HATIA - 1

 







    IMEANDIKWA NA : ERICK SHIGONGO



    *********************************************************************************



    Simulizi : Kifo Cha Mtu Asiye Na Hatia

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    ILIKUWA ni siku ya Desemba 23, tena siku mbili tu kabla ya Christmas, dunia nzima ilijawa na shamrashamra za Sikukuu hiyo ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, maduka mengi jijini Dar yalijaa watu wakinunua nguo na vitu mbalimbali kwa ajili ya sikukuu.

    Magari mengi yalisongamana barabarani na kufanya usafiri wa magari kuwa mgumu, sehemu ya kuendesha kwa dakika moja yalikwenda kwa dakika thelathini! Madereva wengi waliyaacha magari yao na kutembea kwa miguu.

    “Mary’s boy child Jesus Christ was born on Christmas day, up now here the Angel sing the king was born to day, a man will live forever more because of Christmas day!....” Nyimbo za Chrismas zilitawala kila kona ya jiji la Dar es Salaam.

    Siku hiyo Belinda alikuwa ndani ya daladala la kuelekea Segerea akiwa na mtoto wake wa miaka mitano, Alicia! Alikuwa mtoto mzuri mno na mwenye sura ya kumvutia kila aliyemwangalia, wengi walisema alichukua sura ya baba yake! Kila mtu ndani ya basi hilo alitamani kumbeba Alicia lakini Alicia mwenyewe alikataa na kubaki mikononi mwa Belinda mama yake.

    Pamoja na uzuri wote huo wa mtoto Alicia alikuwa na kasoro katika mwili wake, hakupitisha hata wiki mbili bila kuugua! Homa na kikohozi hazikumpa nafasi katika maisha yake, Belinda alishatafuta tiba sehemu mbalimbali lakini hakufanikiwa kupata tiba kamili ya mtoto wake.

    “Mom what are we going to do for Christmas? Are you going to buy me new clothes? My friends are going shopping with their parents? Mom are you going to take me shopping too? (Mama sisi tutafanya nini Christmas? Je, utaninunulia nguo mpya? Rafiki zangu wanakwenda madukani kununua nguo mpya na wazazi wao, utanipeleka na mimi kununua nguo?) Alicia alimuuliza mama yake huku akimpigapiga mgongoni.

    Belinda alijifanya kutosikia maswali ya mwanae hii ni kwa sababu hakuwa na pesa wala jibu la kumpa mtoto wake ambaye kwa umri wake alikuwa hajaambiwa na mtu yeyote juu ya kilichoendelea katika maisha yao! Kwake kila kitu kilikuwa sawa.

    “Mummy! Please answer my question!” (mama tafadhali jibu swali langu!)

    “What have you said my dear daughter, I didn’t hear you! (Umesemaje kweli  binti yangu mpendwa? Sikukusikia).

    “Are you going to buy me new clothes this Christmas?” (utaninunulia nguo mpya Chrismas hii?”) Alicia aliuliza tena lakini bado mama yake aliendelea kukaa kimya, ni kweli hakuwa na jibu la swali hilo, hakuwa na pesa za kumnunulia mtoto wake nguo mpya! Si nguo tu bali hata pesa ya chakula cha siku ya Christmas hakuwa nayo!

    Siku hiyo asubuhi walikuwa ndani ya daladala wakielekea kwenye gereza la Segerea kupitia Tabata, ilikuwa ni siku ya mwisho kwenda kuonana na mumewe Prosper aliyekuwa amekaa gerezani kwa muda wa miaka minane baada ya kuhukumiwa kifo kwa kosa la kumuua baba yake mzazi kwa kumpiga na mchi usoni.

    Kwa kutumia mawakili Belinda alijitahidi kwa kila alichokuwa nacho kuhakikisha mume wake anatoka gerezani au kufungwa kifungo cha maisha lakini haikuwezekana, Prosper alikaa gerezani muda wote wa miaka minane akisubiri  siku ya kunyongwa.

    Ni siku iliyofuata ndiyo Prosper alitegemea kufa kwa kupigwa sindano ya sumu aina ya Digoxmait ili kumwondoa kabisa duniani, Prosper hakuwahi kuua kabla lakini kwa kosa hilo moja alihukumiwa kifo! Ni siku hiyo ya Desemba 23 ndiyo Belinda alitegemea kupewa nafasi ya mwisho kuongea na mumewe kabla ya kifo chake! Ilikuwa ni siku ya huzuni kubwa mno katika maisha yake na kila alipomfikiria mume wake roho ilimuuma sana na kufanya aanze kulia!

    Hakuna mtu aliyewahi kumwambia Alicia kuwa baba yake asingerudi tena nyumbani na angenyongwa na kufa! Kila siku walipomtembelea gerezani, ili kumuondolea huzuni Alicia aliyeonekana kumpenda mno baba yake, Prosper alimwambia mwanaye Alicia kuwa angetoka gerezani siku si nyingi, jibu hilo ndilo mtoto aliliweka kichwani, hakuwahi kufahamu kabisa kuwa baba yake tayari alishahukumiwa kifo na alikuwa akisubiri siku yake.

    “Mum! Mummy! Dad told me he is going to be with us during Christmas dont you remember? (Mama! Mama! Baba aliniambia atakuja nyumbani Christmas hii? Haukumbuki?) alipaza sauti Alicia mpaka watu ndani ya gari wakageuza shingo zao kumwangalia.

    Belinda alishindwa kumjibu kitu chochote badala yake machozi yalianza kumtoka! Maneno ya mwanae yalimuumiza sana moyo alielewa wazi mtoto wake alikuwa  haelewi chochote na asingeweza kumwambia ukweli kuwa baba yake alikuwa anakufa siku iliyofuata na walikuwa safarini kwenda gerezani kuagana naye kwa mara ya mwisho! Belinda aliendelea kulia kichinichini.

    “Haya Segerea gerezani hapa, wa kushuka sogeeni mlangoni upesi msilete urembo wenu hapa” Alisema kondakta wa daladala na Belinda alisimama na kumshika Alicia mkono wakaanza kusogea mlangoni.

    “Shusha hapo gerezani!” kondakta alipiga kelele na dereva akakanyaga breki na Belinda na mtoto wake wakateremka na kuanza kutembea kuelekea gereza la Segerea lililokuwa umbali wa kama mita mia tatu kutoka kituo cha basi.

     Walipofika gerezani walionyeshwa chumba maalumu kilichoandaliwa kwa ajili yao kuongea na Prosper, Belinda aliketi chumbani humo akiwa amembeba mtoto wake miguuni, muda wote machozi yaliendelea kumbubujika na kufanya azilowanishe nguo zake.

    “Mom stop crying, what are we doing here? Let’s go and see dady!”(Mama acha kulia, tunafanya nini hapa twende tukamwone baba!) Alicia aliendelea kumwambia mama yake.

    Kabla Belinda hajatoa neno lolote mara mlango uliokuwa pembeni yao ulifunguliwa akajitokeza askari jela mmoja akiwa na bunduki mkononi mwake na baadaye aliingia mtu akiwa amevaa nguo nyeupe juu hadi chini na akiwa amefungwa kitambaa cheusi usoni, Belinda alipomwangalia mtu huyo alimtambua alikuwa ni mume wake Prosper. Alinyanyuka kitini na kuanza kumfuata.

    “We mama hebu kaa chini usubiri utaratibu wa gereza kwanza, usituletee mambo ya uraiani, hapa ni gerezani kuna sheria zake vinginevyo na wewe utajikuta unanyea ndoo!” Askari alimfokea Belinda.

    Bila ubishi Belinda alirudi kinyumenyume na kuketi kitini kwake akatulia akisubiri taratibu zote za gereza zimalizike. Prosper alikalishwa chini na kufunguliwa kitambaa usoni, alipowaona mke wake na mwanae alitokwa na machozi, huruma ilimshika kwani alijua kuwa hiyo ndiyo ilikuwa siku yake ya mwisho kuonana na familia yake.

    “Mama una saa moja tu na nusu ya kuongea sisi tunaondoka tukirudi tutamchukua mumewe, utumieni vizuri muda mliopewa na mpange mambo vizuri! Hii ni nafasi ya mwisho kuonana na mumeo duniani!” Alisema askari mmoja na baadaye kutoka nje na kufunga mlango nyuma yake.

    “Belinda umekuja mama mtoto wangu?”

    “Ndiyo Prosper!”

    “Hebu kabla ya yote na tupige magoti tumwombe Mungu kwani hii ni siku yetu ya mwisho katika dunia hii kuwa pamoja!” Prosper alimwambia mkewe na wote watatu walipiga magoti chini, Prosper akiwa na pingu zake mikononi na miguuni.

    “Father in the name of Jesus and the mighty power of holly spirit, I thank you for every thing that happened in my life! Father you know how innocent I’m in this case, you know I didn’t kill anybody! But the entire world knows I’m a killer, tomorrow I’m dying leaving my wonderful wife and daughter behind me, protect them Lord,   make me meet them in heaven! Father you know how much I Love my wife and how much I love my daughter Alicia too. It haunts me badly inside to learn that this is my last moment with them! I’m dying and leaving my Alicia and Belinda alone, but I know with you they will never be alone..... (Baba katika jina la Yesu na uwezo wa Roho Mtakatifu ninakushukuru kwa kila kitu kilichotokea katika maisha yangu, baba ninajua ni kiasi gani unaelewa sina hatia katika suala hili, unajua wazi sikuua lakini dunia nzima inanijua mimi ni muuaji. Kesho ninakufa nakuwaacha mke wangu mzuri na mwanangu nyuma yangu, baba uwalinde, nifanye nikutane nao Mbinguni, baba unajua ni kiasi gani ninampenda mke wangu na ni kiasi gani ninampenda binti yangu Alicia. Inaniumiza vibaya kujua kuwa huu ni wakati wangu wa mwisho kuwa nao, ninajua ninakufa na kuwaacha Belinda na Alicia peke yao lakini ninafahamu wakiwa na wewe hawatakuwa wapweke milele.....) Alipofika hapo Prosper alishindwa kuendelea na kuanza kulia.

    “Daddy what’s going to kill you? But you said you will be home this Christmas!” (Baba nini kitakuua, lakini si ulisema utakuwa nyumbani Christmas hii!”) Alicia aliuliza kwa mshangao ilikuwa ni mara ya kwanza kwake kusikia kuwa baba yake angekufa.

    “My daughter Alicia let me reveal the truth to you today, the truth that even you mother never knew about!”(Mwanangu Alicia acha nikuonyesha ukweli wote leo, ukweli ambao hata mama yako hakuwahi kuufahamu!)

    Baada ya kusema hayo huku Belinda na Alicia wakiendelea kulia, Prosper alisimulia kila kitu kilichotokea katika maisha yake na nini kilichopelekea awe gerezani, Belinda alionekana kufungua mdomo wake kwa mshangao wakati Prosper akielezea kilichotokea, siku zote alielewa kitu tofauti kabisa.

    “Kwa hiyo hukumuua baba yako!”

    “I didn’t kill him but my mom did!) (Sikumuua baba ni mama yangu aliyemuua baba)

    “Why are you in Prison then? (Sasa kwanini upo gerezani).

    “Nilimpenda sana mama yangu, sikutaka kitu kibaya kimtoe maana nikasema ni mimi ndiye niliyemuua baba ili tu mama yangu aachiwe huru na mimi nikawekwa gerezani, sikuwahi kukueleza hili Belinda lakini leo ni lazima nikuambie ukweli, nakufa sababu ya mama yangu ingawa naye hivi sasa ni marehemu, nitaonana naye ahera kesho! Nakupenda sana Belinda na kuomba umtunze sana mtoto wetu ingawa naye ni mgonjwa mara kwa mara lakini mpeleke hospitali ipo siku atapona!”

    Hawakuongea kitu tena zaidi ya kuendelea kulia kwa pamoja muda mrefu  mpaka askari walipokuja na kumfunga Prosper kwa kitambaa cheusi tena usoni, Belinda na Alicia walimkumbatia na kumbusu usoni kwa mara ya mwisho akaanza kuvutwa kutolewa chumbani.

    “I love you Belinda! I love you Alicia! I will love you forever, see you in Heaven! (Nakupenda Belinda! Nakupenda Alicia, nitawapenda milele, tutaonana mbinguni!) alisema Prosper huku akivutwa na maaskari kutolewa chumbani.

    Walipotoka chumbani huku wakilia Belinda na mtoto wake walinyoosha moja kwa moja hadi kituo cha basi, habari aliyoisikia siku hiyo kwa Prosper ilimsikitisha sana Belinda, alikuwa ameamua kwenda kufanya kila lililowezekana kumwona Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kumsimulia juu ya jambo hilo, alipita ofisini kwa wakili wake na kumweleza na wote walinyoosha hadi ofisini kwa Mwanasheria Mkuu!

                  *********

    “Nasikitika leo hamuwezi kumwona ana kazi nyingi sana!” alisema Katibu Muhtasi wake!”

    “Hapana dada ni jambo muhimu sana linalohusu kifo, tusipomuona leo kesho mtu ananyongwa na ana uwezo wa kuzuia!” alijibu Belinda huku akilia machozi.

    “Hebu subirini nimuulize?” alisema Katibu huyo na kunyanyua simu iliyokuwa mezani kwake, alisikika akiongea na mtu na alipoweka simu chini alimgeukia Belinda.

    “Dada nakuhurumia ila sina jinsi ya kukusaidia, Mwanasheria amesema mje kesho saa nne kamili ataonana nanyi!”

    “Mume wangu ananyongwa saa 4.30 tu dada!”

    “Siwezi kulazimisha awaone kwa kweli huyo ni bosi wangu!”

    Belinda na mwanaye waliondoka pale wakilia machozi na kwenda nyumbani kwao ambako Belinda chakula hakikulika wala usingizi haumwijia alikesha usiku mzima akisali kumwomba Mungu afanye miujiza yake.

                            ******

    Siku iliyofuata asubuhi na mapema Prosper alianza kuandaliwa kwa ajili ya kifo! Alipewa muda wa masaa mawili kusali na kusoma Biblia ili kutubu dhambi zake, ilipofika saa nne kamili alitolewa chumbani kwake akiwa amefungwa kitambaa cheusi usoni na kupelekwa katika chumba maalum cha kunyongea, kilichoitwa Death room, ambako alilazwa katika kitanda maalum tayari kwa kifo.

    Mtaalam wa kuua aliyeitwa bwana Nyonganyonga ambaye kwake kutoa roho za watu ndio ilikuwa kazi yake, alisimama pembeni mwa kitanda cha kifo akimwangalia Prosper kwa huruma ni kwa mara ya kwanza katika kazi yake aliyoifanya kwa miaka 15 alijisikia kumwonea mtu huruma kiasi hicho!

    “Kweli uliua?” Alimuuliza Prosper

    “Sikuua?”

    “Ila?”

    “Ni mama yangu aliyeua mimi nilisema nimeua ili kumwokoa mama asife!”

    “Kwa hiyo wewe upo tayari kufa kwa ajili ya mama yako?”

    “Ni sawa tu!”

    “Mama yako hivi sasa yupo wapi?”

    “Alifariki kwa Kifua Kikuu muda mfupi baada ya kutoka gerezani!”

    “Kwa hiyo upo tayari kufa?”

    “Sawa tu!”

    Bwana Nyonganyonga alikuwa tayari na sindano yake ya dawa ya Digoxmait Tayari kwa kumchoma Prosper ikitimia saa 4.30 juu ya alama!, sumu hiyo iliua  kwa kuusimamisha moyo kusukuma damu.

    Wakati huo tayari ilikuwa ni saa 4.20! Prosper alilala pale akisubiri kifo, zilikuwa zimebaki dakika kumi tu achomwe sindano ya sumu, alijaribu kukifikiria kifo na kushindwa kukielewa.

    “Hivi inakuwaje mtu akifa, kweli nitawasahau Belinda na Alicia?” alijiuliza Prosper na picha ya mke na mtoto wake ilimwijia kichwani akasikia huzuni kubwa sana moyoni mwake! Alipotupa macho ukutani tayari ilikuwa saa 4.25 zilikuwa zimebaki dakika tano afe!

    “Nichome hiyo sindano, nataka kufa unasubiri nini?” Prosper alisema katika hali ya kukata tamaa.

    *******

    BELINDA SAA 4. KAMILI OFISINI KWA MWANASHERIA

    “Karibuni Mwanasheria anawasubiri!” Katibu Muhtasi aliwakaribisha

    Belinda, Alicia na wakili Joseph Mziray waliingia ofisini na kwenda moja kwa moja hadi mbele ya meza yake, Mwanasheria alikuwa mzee wa makamo mwenye umri kati ya miaka 50-55, kichwa chake kilijaa mvi nyingi sana na alivuta kiko!

    “Shikamoo mzee” Belinda na wakili walimwamkia

    “Marahaba!”

    “Niwasaidie nini?”

    Belinda alianza kusimulia kila kitu kilichotokea huku machozi yakimtoka, Alicia pia alilia machozi akiliita jina la baba yake! Maneno ya Belinda yalimwingia Mwanasheria akajikuta akinyanyua simu na kuanza kubonyeza namba fulanifulani.

    “Shikamoo Mheshimiwa Rais!” kuna habari ya kusikitisha sana hapa juu ya yule kijana anayenyongwa leo!”Mwanasheria alisimulia kila kitu katika simu alipokata simu alichukua kalamu na karatasi na kuanza kuandika kitu fulani.

    “Rais ameamua kusitisha adhabu ya kifo kwanza mpaka uchunguzi ufanyike!” Alisema mwanasheria mkuu.

    “Haleluya!”Belinda aliruka juu na kushangilia.

    “Chukueni hii barua muikimbize gerezani haraka iwezekanavyo!”

    “Hivi sasa ni saa 4.10 Mheshimiwa tuna dakika ishirini tu, hatuwezi kuwahi lazima tutakuta amenyongwa!”

    “Hizo zinatosha! Gari linawasubiri hapo chini!”

    Waliteremsha ngazi kwa haraka hadi chini ambako walikuta gari aina ya Ladrover 110 likiwasubiri tayari kwa safari ya kuelekea Segerea, wote waliingia na kwa kasi ya gari lilianza kuondoka wakati wanafika gerezani ilikuwa tayari saa 4:29:30, zilikuwa zimebaki sekunde 30 tu! Belinda aliruka na kuanza kukimbia hadi kwenye lango la kuingilia gerezani ambako alianza kupiga kelele.

    “Jamani msimuue mume wangu! Barua hii hapa kutoka kwa Mwanasheria, aliwakabidhi maaskari waliokuwa getini walipoiangalia ilikuwa na muhuri wa Mwanasheria Mkuu na iliandikwa neno ‘URGENT’ ikimaanisha ‘HARAKA’

    “Mungu wangu mbona zimebaki sekunde 15 tutawahi kweli?” alisema askari mmoja baada ya kuangalia saa yake na palepale alitoka mbio kwenda ndani kujaribu kuokoa maisha ya Prosper, Belinda, Alicia na wakili walibaki nje wakisubiri jibu! Waliendelea kulia machozi waliomba muujiza utokee!

    Jua lilikuwa bado halijaanza kuchomoa vizuri, hivyo hali ilikuwa bado ya ubaridi asubuhi ya siku hiyo, msichana alitembea kandokando ya barabara akielekea shuleni baada ya kuteremshwa na gari la nyumbani kwao, alivaa vizuri na kuufanya uzuri wake uongezeke maradufu!

    Katika umri wa miaka 16 tu msichana huyo alikuwa msichana mrembo mno! Kwanza alikuwa mrefu, mwembamba mwenye macho ya kulegea, alikuwa na nywele ndefu, miguu minene iliyomfanya avutie zaidi.

    Hapakuwa na msichana mzuri kama yeye katika shule yao ya St. Magreth jambo lililofanya atamaniwe na kila kijana shuleni hapo mpaka walimu wake, mpaka wakati huo alishasababisha walimu wawili kufukuzwa kazi baada ya majaribio ya  kumbaka ofisini! Wengi walimwita kwa jina la queen ingawa jina lake halisi lilikuwa Belinda.

    Alizaliwa katika familia yenye kila kitu, familia tajiri, baba yake alimiliki majumba mengi ya kifahari jijini Dar es Salaam, meli nyingi za kusafirisha mizigo katika bahari ya Hindi na maduka mengi makubwa karibu kila mkoa nchini Tanzania.

    Familia ya msichana huyu ilikuwa ya watoto watatu, ndugu zake wawili David na John wakiwa wa mama mmoja na yeye alizaliwa peke yake kabla baba yake hajafunga ndoa na mama yao David na John, Angelina Kapinga.

    Baba yake Thomson Komba alimpenda sana Belinda pengine kuliko hata David na John na alimpa kila kitu, lakini mama yake wa kambo hakumpenda Belinda hata kidogo! Alimfanyia kila aina ya manyanyaso na kuyafanya maisha yake kuwa ya shida na huzuni kubwa .

    Mbegu ya chuki ilipandikizwa hadi ndani ya mioyo ya kaka zake David na John! Walimchukia Belinda kupita kiasi, baba yao alijitahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha upendo unakuwepo kati ya watoto wake lakini haikuwezekana kwa sababu mbegu ya chuki baina ya watoto ilitoka kwa mama aliyekaa na watoto muda mwingi.

    MzeeThomson alikuwa mtu wa safari nyingi kupita kiasi, katika mwezi ni wiki moja tu aliyokaa nyumbani, wiki nyingine tatu zote alizimaliza katika safari zake za kibiashara, ni katika muda huo ndio Belinda alipata mateso makali kutoka kwa mama yake wa kambo, alinyimwa chakula! Alipigwa na kupewa kazi ngumu kila alipotoka shuleni.

    Baba yake aliporudi kutoka safari Belinda hakudiriki hata siku moja kufungua mdomo wake kueleza yaliyompata kwa kumwogopa mama yake wa kambo, maisha yake yalijaa huzuni na muda wote alikuwa mnyonge na hata kupungua uzito.

    Baba yake aliligundua hilo na ili kumuepushia matatizo zaidi aliamua  kumhamishia Belinda katika shule ya St. Magreth iliyokuwa ya bweni ambako aliendelea na masomo yake vizuri na kufaulu mtihani wake wa kidato cha nne akachaguliwa kuendelea na kidato cha tano na sita katika shule hiyo hiyo.

            ********

    “Fungua mlango wee kenge!”

    Hiyo ndiyo ilikuwa kauli ya mzee Kabaka kila aliporejea kutoka ulevini saa 8:30 usiku kila siku! Prosper aliyelala chumba cha karibu na mlango wa kuingilia ndani waa kibanda chao kidogo cha vyumba viwili alinyanyuka na kwenda kumfungulia baba yake mlango!

    “Weee! Unafungua mlango wewe ndiyo mke wangu?” Ndilo swali ambalo mzee Kabaka alimuuliza Prosper.

    “Hapana baba mama amelala!”

    “Niniiii? Funga huo mlango upesi kabla sijakuvunja mbavu na kimbia upesi ukamuamshe mama yako aje anifungulie mlango!”

    Bila ubishi sababu aliyesema ni baba yake Prosper aliufunga mlango na kwenda chumbani kumwamsha mama yake.

    “Mama! Mama! Mama! Baba amekuja amka ukamfungulie!”

    “Mfungulie tu wewe mwanangu mimi atanipiga!”

    “Amekataa mimi kumfungulia!”

    Baada ya jibu hilo mama yake Prosper, Kalunde Katunzi alisikia dirisha la chumbani likipondwa na jiwe kubwa akashtuka na kuchukua shuka alilokuwa amejifunika na kufunga kifuani.

    “Wee kenge hivi hutaki kunifungulia? Nikiingia humo ndani hakyanani leo nakutoa roho, nilishakukata sikio moja hujasikia eh?” Alisema mzee Kabaka.

    “Nakuja mume wangu!” Alijibu mama yake Prosper huku akitetemeka na kuanza kukimbia kwenda kufungua mlango, alimgonga Prosper aliyekuwa amesimama njiani wakati akikimbia.

    Alimuogopa sana mume wake na alijua siku hiyo angepata kipigo kikubwa mno, Prosper mtoto mkubwa wa mama huyo akifuatiwa na wadogo zake Nyamizi na Kasanda, alimfuata mama yake nyuma alijua angepigwa na alitaka kumsaidia.

    Alipoingia tu ndani baada ya kufunguliwa mlango baba yake aliyekuwa kipande cha mtu cha miraba minne, mwanajeshi aliyepigana vita vya Kagera lakini aliporudi akaasi jeshi na kuamua kufanya biashara zake, alimdaka mke wake na kumpiga ngumi mdomoni, meno kama matatu hivi yakadondoka chini! Damu nyingi zikatapakaa sakafuni, hakumwachia hapo alimfuata na kumpiga teke tumboni akaanguka chini.

    “Prosper! Prosper! Prosper! Mshike baba yako ataniua!” Alisema mama huyo na baadaye kukaa kimya huku akiendelea kutoka damu, hiyo ndiyo ilikuwa kawaida mama huyo aliishi kwa mateso jambo lililomkera sana Prosper na dada zake.

    “Baba mwache mama! Kwanini unampiga hivyo si keshakufungulia mlango?”

    “Wee unanishika unataka kunichangia na mama yako siyo?”

    “Sitaki kukupiga baba lakini naomba usimpige mama kiasi hicho hana kosa!”

    Wakati Prosper akiongea maneno hayo tayari Kasanda na Nyamizi walishafika na kumnyanyua mama yao aliyekuwa amelala chini akiwa amepoteza fahamu huku damu nyingi zikimtoka mdomoni, midomo yake ya juu na chini ilikuwa imevimba kwa ngumi aliyopigwa na mume wake, wakambeba na kumpeleka chumbani kwao ambako walimmwagia maji akarejewa na fahamu.

    “Mama twende polisi!” Kasanda alimshauri mama yake.

    “Hapana watoto wangu tukienda polisi baba yenu atafungwa! isitoshe sisi Wanyamwezi hatutakiwi kabisa kushtaki polisi tunapopigwa na waume zetu”

    Watu wote katika kijiji cha Tutuo barabara ya kwenda Sikonge walikoishi Prosper na wazazi wake walitambua ukorofi wa mzee Kabaka na hakuna mtu aliyediriki kumkemea, kila mtu alimuogopa.

    Kama ungefanikiwa kukutana na mama Kalunde, sio siri machozi yangekutoka, alikuwa ni mama wa makamo, mrefu mwenye umbile la kitutsi,rangi ya ngozi yake ilikuwa nyeusi lakini iliyojaa makovu mengi, kwa kumwangalia ungegundua kabisa kuwa mama huyo aliwahi kuwa tishio wakati wa ujana wake!

    Alikuwa ni mama mwenye mateso, alipigwa karibu kila siku na mume wake,hakuwa na sikio moja  tayari lilishakatwa na mumewe! Jicho lake  la kulia lilikuwa chongo baada ya kupasuliwa na mume wake wakati wa kupigwa miaka miwili kabla ya siku hiyo! Alikuwa ni mama aliyepata mateso makubwa mno katika maisha yake ya ndoa.

    Wakati hayo yote yakitokea Prosper alikuwa  na umri wa miaka 17 akimalizia kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Sikonge, pamoja na matatizo aliyokuwa nayo alifanikiwa kuchaguliwa kuendelea na kidato cha tano katika shule ya sekondari ya St.Magreth ilikuwa ni shule ya bweni,  na ilikuwa ni lazima aende  kuishi bwenini akiwaacha dada zake Kasanda na Nyamizi pamoja na wazazi wake.

    “Prosper tutaweza kweli kumhimili baba akimpiga mama?”

    “Mungu atawasaidia dada zangu sina budi kwenda shule ili niwasaidie baadaye!” Prosper aliwaeleza dada zake wakati wa kuagana, akaondoka kwenda zake  Moshi shuleni.

    Alipofika shuleni kwa mara  ya kwanza alikuwa amechelewa na kilichomchelewesha zaidi ilikuwa ni ada, mama yake  Kalunde  alilazimika kufanya  vibarua katika mashamba ya watu ili aweze kupata pesa za kumwezesha Prosper kwenda shule! Baba yake hakujali kabisa.

    “Prosper mwanangu usifanye michezo shuleni, si unaona maisha yetu yalivyo na unaona nilivyohangaika? Baba yako hana msaada wowote, yeye ni pombe  kila siku na kunipiga mimi tu, familia nzima tunakutegemea wewe uje kuwa mkombozi wetu kajitahidi mwanangu!”

    “Sitakuangusha mama nakuahidi! “

    “Sawa mwanangu!”

    Darasa lao lilikuwa na wafunzi hamsini na mbili kati yao wasichana wakiwa kumi na saba! Ni Prosper peke yake aliyeonekana kuwa na uwezo mdogo kifedha na watu wengi walimdharau, alikuwa na nguo zilizochanika na madaftari yake yalikuwa ni ya kurasa shirini na nne ambayo hayakutumiwa na wanafunzi wengi shuleni hapo! Yalidaiwa kuwa ya watoto wa shule za msingi.

    Pamoja na umasikini wake Prosper alijitahidi sana na masomo kama alivyomuahidi mama yake na hiyo ni kwa sababu aliifahamu familia yake, alitaka asome ili apate uwezo wa kuwakomboa ndugu zake, barua zilizokuja kutoka nyumbani kwao zilimweleza juu ya kipigo alichopata mama yake na Prosper alilia.

    Wanafunzi wengi walimtenga sababu ya umasikini wake isipokuwa msichana mmoja tu aliyeitwa Belinda!Msichana huyo alimsaidia Prosper kwa vitu vingi shuleni ikiwemo Sabuni, mafuta na hata sukari na wakatokea kuwa marafiki wakubwa.

    Katika mtihani wa mwisho wa muhula aliwashangaza wengi pale alipoibuka na kushika namba ya kwanza kati ya wafunzi wote! Ni matokeo hayo ndiyo yalianza kumpa heshima na marafiki wengi shuleni.

                 ******

    Shule zilipofungwa  kwa sababu Prosper hakuwa na nauli ya kumrudisha hadi nyumbani kwao Tabora, ilibidi abaki shuleni peke yake akijisomea! Alimkumbuka sana mama yake na alitaka kwenda nyumbani lakini kwa sababu hakuwa na nauli alilazimika kubaki peke yake shule nzima.

    Shule zilipofunguliwa wanafunzi wote walirejea shuleni  na yeye na  Belinda msichana aliyeonekana kutoka familia tajiri jijini Dar es Salaam, walisoma  na kufanya  kila kitu pamoja Belinda alikuwa miongoni mwa wasichana wagumu kuelewa masomo yao, lakini Prosper alitumia muda wake mwingi kumfundisha hatimaye akawa miongoni mwa wasichana waliofanya vizuri katika mitihani yao.

    Mwisho wa muhula wa pili Prosper alishika tena namba ya kwanza darasani kwake na Belinda aliibuka katika kumi bora! Kila mtu mpaka walimu wake walishangaa,hilo liliukomaza zaidi uhusiano wao.

    “Prosper utakwenda Tabora likizo hii?”

    “Mimi? Mimi? Hapana sitakwenda!”

    “Kwanini?”

    “Sina nauli ya kunipeleka nyumbani nendeni tu mtanikuta!”

    “Hapana Prosper this time ni lazima uende!”

    “Nitakwenda na nini sina nauli Belinda?”

    “Nitakupa nauli ya kukupeleka na kukurudisha!” Alisema Belinda.

    Prosper hakuamini aligeuka na kumwangalia Belinda usoni, wote wawili walijikuta wakitabasamu na baadaye kukumbatiana na kuanza kupigana mabusu usoni, Belinda alijaribu kuupenyeza ulimi wake kuuingiza mdomoni kwa Prosper lakini Prosper aliuma meno yake kuonyesha hakupenda kitu hicho kitokee!

    “Belinda unataka kufanya nini?”

    “Nakupenda Prosper  tafadhali tunyonyane ndimi!”

    “Nitatapika  Belinda sijawahi kufanya kitu kama hicho hata siku moja!”

    Belinda alishindwa kuendelea lakini alijua ni kwanini Prosper alisema hivyo, alimwachia na wakaendelea na safari yao kuelekea mabwenini kujipumzisha wakisubiri siku inayofuata.

    Asubuhi  kitu cha kwanza alichofanya Belinda ni kumkabidhi Prosper kiasi cha shilingi 50,000 kwa ajili ya nauli ya kumpeleka Tabora na kumrudisha shuleni.

    “Belinda mbona pesa hizi ni nyingi sana!”

    “Zitakazobaki utawanunulia wazazi na ndugu zako zawadi!”

    “Ahsante  Belinda, sikutegemea!”

    “Ahsante wewe kwani bila wewe mimi nisingefanikiwa kimasomo? Isitoshe nakupenda  Prosper huwezi kupata taabu wakati mimi nina kitu!”

    “Belinda mzazi wako ni nani hasa hapa nchini?” Ilibidi Prosper aulize, sababu alishangazwa na msichana mdogo kama Belinda kuwa na kiasi kile chapesa.

    Belinda alimweleza kila kitu kilichokuwepo katika maisha yake, alieleza pia juu ya utajiri wa baba yake na jinsi baba yake alivyompenda sababu alikuwa mtoto pekee wa kike! Hakuacha kumweleza juu ya mama yake wa kambo.

    “Nina kila kitu nyumbani isipokuwa upendo wa mama, mama yangu wa kambo ananitesa sana, hanipendi amewafanya hata kaka zangu wa kambo pia wanichukie!”

    “Unafikiri ni kwanini?”

    “Kwa sababu wanajua baba ananipenda na kuna uwezekano wa kupata sehemu kubwa sana ya mali yake akifa, hiyo nafikiri ndiyo sababu kubwa!”

    “Pole!”

    “Ahsante, lakini nataka   uelewe nakupenda na tukirudi kutoka likizo safari hii nataka kila mtu aelewe jambo hapa shuleni  ili wavulana waache kunisumbua!”

    “Huogopi kuchekwa Belinda!”

    “Kwanini?”

    “Sababu mimi ni masikini!”

    “Nakupenda kwa jinsi ulivyo Prosper!”

    Ni kweli Prosper alikuwa na sura ya kumvutia kila mwanamke kilichomsumbua kilikuwa ni umasikini.

                 ******************

    Prosper alikata tiketi ya treni na kusafiri hadi  Tabora mjini ambako alipanda mabasi ya kumpeleka hadi nyumbani kwao Tutuo, kiasi cha  kilometa   sabini hivi kutoka Tabora mjini, njia nzima alimfikiria mama yake  alitaka sana kumwona! Ulikuwa umepita muda mrefu   bila kuonane naye! Mawazo juu ya dada zake na  baba yake hayakumuumiza kichwa  sana, alimuwazia mama yake zaidi,  alimpenda sana na hapakuwa na mtu mwingine kama mama maishani kwake!

    Aliposhushwa na basi kituoni kitu cha kwanza alichofanya ni kukimbia dukani na kununua vitenge doti  tatu kwa ajili ya mama yake na pia alinunua magauni mawili  kwa ajili ya dada zake, Nyamizi na Kasanda!  Hakusahau kumnunulia baba yake suruali nzuri! Moyo wake ulijaa furaha, alikuwa na hamu kubwa mno ya kuiona familia yake tena.

    Baada ya manunuzi hayo alinyoosha moja kwa moja kwenda nyumbani kwao,njiani akiwa amebeba begi lake alishangaa jinsi ambavyo watu walimwangalia na kuonyesha masikitiko.

    Alipofika nyumbani kwao  hakuna mtu aliyejitokeza kumpokea, mlango wa nyumba ulikuwa wazi, ilibidi aingie hadi  ndani akiliita jina la mama yake, lakini  hakuitikiwa, mwisho alianza   kuita majina la dada zake lakini bado ilikuwa kimya.

    Wakati  bado akijiuliza maswali kichwani mwake   alitokea rafiki yake mkubwa aliyeitwa Kategile na kusimama mbele yake.

    “Pole sana Prosper bahati mbaya umechelewa mazishi!”

    “Ya nani?” Aliuliza kwa mshangao Prosper.

    “Baba yako!”

    “Baba?”



    Wakati  bado akijiuliza maswali kichwani mwake   alitokea rafiki yake mkubwa aliyeitwa Kategile na kusimama mbele yake.

    “Pole sana Prosper bahati mbaya umechelewa mazishi!”

    “Ya nani?” Aliuliza kwa mshangao Prosper.

    “Baba yako!”

    “Baba?”

    “Ndiyo!”

    “Baba kafariki lini?”

    “Wiki iliyopita!”

    Prosper alianza kulia na majirani wengine zaidi walifika na kuanza kumpa pole, walishangaa kuwa hakuwa na taarifa hizo!”

    “Sasa mama na ndugu zangu wapo wapi?”

    “Wapo kituo cha polisi kati mjini Tabora”

    “Wamefanya nini?”

    “Ni wao ndio walimpiga baba yako na kumuua!”

    Siku iliyofuata  asubuhi Prosper alikwenda moja kwa moja kituo cha polisi kati kuwaona ndugu zake pamoja na mama yake, alilia machozi alipomwona mama yake akiwa mahabusu, aliomba kuongea naye akaruhusiwa na wakapewa chumba yeye na mama yake pamoja na dada zake waongee.

    “Mama kweli mlimuua baba?”

    “Mwanangu nililazimika kufanya hivyo kwani alichukua kisu na kunikata sikio langu la  pili…..”Mama yake Prosper alianza kulia.

    “Alilitoa?”

    “Halipo mwanangu, nimepoteza masikini yangu yote mawili baba yako alikuwa katili mno alistahili kufa na ninakiri nimemuua!”

    “Ulimuua na nini?”

    “Nilimpiga na mchi kichwani akaanguka na kufa! Huo ndio ukweli mwanangu!”

    “Mama ulishindwa kweli kufuata ushauri wangu?”

    “Nisamehe mwanangu!”

    “Mama hautafia gerezani ni heri nifungwe mimi na kunyongwa lakini wewe uwe huru nakupenda mno mama!” Alisema Prosper huku akilia.

    Baada ya maongezi Prosper alirejea mjini ambako alikwenda moja kwa moja kituo cha polisi kati mjini Tabora.

    “Naomba kuonana na mkuu wa kituo!”

    “Wewe nani na una shida gani?”

    “Nina maongezi   marefu kidogo siwezi kukueleza wewe!”

     Alionyeshwa ofisi ya mkuu wa kituo na kuingia.

    “Shikamoo mzee!”

    “Marahaba nikusaidie nini kijana!”

    “Mzee unakumbuka mzee Kabaka aliyeuawa  siku chache zilizopita?”

    “Ndiyo si yule aliyeuawa na mke wake?”

    “Ndiyo! Yule ni baba yangu na aliyemuua si mama yangu ni mimi! Nilitoroka baada ya kitendo hicho na ninakueleza wazi kuwa  nimerudi ili mama yangu aachiwe mimi ndiye niwekwe rumande!”

    “Kweli?”

    “Huo ndio ukweli ni mimi niliyempiga baba na mchi kichwani akafa!”

    “Kwanini?”

    “Kwa sababu alikuwa anamtesa mama yetu!”

    “Mungu wangu!Afande Charles!”

    “Naam Afande!”

    “Hebu njoo hapa mara moja!”

    Sekunde tano tu tayari askari alisimama mbele ya meza ya mkuu wa kituo.

    “Ndiyo afande!”

    “Mchukue  huyu kijana umpeleke rumande, kumbe ndiye aliyemuua baba yake kule Tutuo na sisi tukawakamata mama yake na dada zake  sasa amejileta mwenyewe! Peleka mahabusu haraka na mama yake na dada zake waachiwe mara moja?”

    “Sawa afande!”

    Askari alimnyanyua Prosper na kumzaba vibao kadhaa usoni, kisha akamchukua na kupelekwa chumba cha mahabusu, muda mfupi baadaye  alishuhudia mama yake na dada zake wakitoka mahabusu  wakati wanatoka kituoni walisikia sauti ya Prosper ikiita kutoka mahabusu.

    “Mama!Mama! Acha mimi nife huku lakini wewe uwe huru baba alikutesa mno na ulikuwa na haki ya ku....!”

    “Masikini mwanangu, umefanya nini tena?” Aliuliza mama yake Prosper huku akilia.













    Hakuna mtu aliyekuwa tayari kuamini yaliyotokea 
yalikuwa kweli , Prosper alikuwa ameyatoa maisha yake kwa ajili ya mama yake! Ulikuwa ni upendo mkubwa mno kwa binadamu  kuonyesha,  wengi waliamini ni Yesu peke yake aliyeweza kulifanya hilo, Prosper alikuwa ameudhihirishia ulimwengu kuwa hata binadamu anaweza kuutoa uhai wake kwa ajili ya mwenzake.

    “Namhurumia sana Prosper sikupenda ajiingize katika suala hili ni heri ningenyongwa   kwa sababu ndiyo niliyemuua baba yenu! Nitafanya nini mimi Ili Prosper atoke mahabusu?” Alihoji mama Angelina huku akilia.

    Alilia usiku na mchana kwa siku   tatu na hakula chakula kabisa zaidi ya maji  katika siku zote hizo, Nyamizi na Kasanda walimbembeleza  mama yao lakini hakukubali, alikonda na kupoteza uzito mwingi  sana mwilini mwake, sababu ya kumlilia Prosper.

           *********************

    Mahabusu:

    Prosper alikuwa amekaa ndani ya chumba kidogo cha mahabusu mjini Tabora,  kilichotoa harufu kali na mbaya ya mikojo! Tangu aingie ndani ya mahabusu hiyo siku mbili kabla alikuwa hajaongea na mtu yeyote kati ya watu wote waliokuwemo. Alikaa peke yake kwenye moja ya kona za mahabusu hiyo akiwa na mawazo mengi kichwani mwake.

    “Acha nife mimi si mama yangu!” Aliongea kwa sauti kubwa Prosper na mzee aliyekuwa karibu yake aligutuka na kumgeukia.

    “Kijana mbona unaongea peke yako?”

    “Mh! Hapana mzee! Unajua? Mimi!......” Prosper aliongea maneno mengi yaliyochanganyika ambayo hayakutoa jibu la moja kwa moja kwa swali aliloulizwa!

    “Niambie kijana ni kitu gani kimekufanya uje hapa mahabusu?”

    “Shikamoo mzee!” Prosper aliamkia.

    “Marahaba, hebusasa nieleze tatizo lililokufanya uje humu!”

    “NIMEUA!”

    “Umeua? Watu wangapi?”

    “Mtu mmoja tena ni  baba yangu!”

    “Kha! Hilo ndilo linakufanya ulie? Mbona mimi nimeua watu hamsini na mbili na  nimetulia tu!”

    “Watu hamsini! Umewanyonga?”

    “Hapana, nilizamisha mtumbwi tuliokuwa tukisafiria na watu wote wakafa mimi tu nikaokoka!”

    “Kwanini ulifanya hivyo?”

    “Nilitaka kuiba pesa zao, wote walikuwa ni wafanyabiashara wakitokea Burundi kuja Kigoma, baada ya mtumbwi kuzama nilichukua mifuko yao ya pesa na kuogelea  nayo hadi ufukweni ambako nilikodisha gari likanileta hadi hapa Tabora lakini nilipoingia tu mjini nikakamatwa na ninajua nitahukumiwa kunyongwa lakini  bado silii sasa wewe unalia kitu gani na umeua mtu mmoja tu? Nyamaza bwana usitupigie kelele usikigeuze chumba hiki kliniki, humu wanakaa wanaume bwana!”

    “Sawa mzee!”

    “Una miaka mingapi kijana?”

    “Nina miaka 19!”

    “Unaitwa nani?”

    “Ninaitwa Prosper! Wewe unaitwa nani?”

    “Ninaitwa Savimbi, ulimuuaje baba yako?”

    “Nilimpiga na mtwangio kichwani!”

    “Kwanini?”

    “Sababu alikuwa akimtesa sana mama yangu!”

    “Unasoma?”

    “Ndiyo!”

    “Shule gani?”

    “St Magreth huko Moshi nipo kidato cha tano!”

    “Sasa hivi shule tena basi! Maisha yako yatakuwa ya gerezani ambako kuna mateso makubwa sana lakini kwa sababu unakwenda na mimi usiwe na wasiwasi nitakusidia, utakula chakula kizuri, utalala mahali pazuri, unavuta sigara?”

    “Hapana!”

    “Bangi?”

    “Hapana!”

    “Sawa, lakini kila kitu nitakupatia, utakuwa lakini unalala karibu na mimi sawa?”

    “Sawa nitashukuru sana!”

    “Umeshaota ndevu?” Jambazi alimuuliza.

    “ Zimeanza kuota kidogokidogo!”

    “Aisee hebu nione!” Jambazi ali anza kumpapasa Prosper kidevu, ilikuwa kizani hakuna mtu aliyeona kitendo hicho kikiendelea.

    “Mzee unafanya  kitu gani hicho?”

    Ghafla mlango wa mahabusu ulifunguliwa na majina ya watu kadha yakaanza kutajwa, waliosikia majina yao walitoka mmoja baada ya mwingine hadi nje ambako walikuta maaskari wawili wenye bunduki wakiwasubiri na kuwalinda.

    “Haya wa mwisho ni Savimbi  Mfugambwa,hebu toka nje upesi muuaji mkubwa wee!”

    Prosper alipolisikia  jina la Mfugambwa alielewa  ni nani aliyekuwa amekaa naye mahabusu!  Halikuwa jina geni kabisa kwake masikioni kwake, alishalisikia jina hilo mara nyingi tu tangu akiwa mtoto mdogo, Mfugambwa alikuwa jambazi aliyejulikana sana mikoa ya Tabora,Mwanza, Shinyanga na Kigoma ni yeye aliyeteka  mabasi  na treni za  abiria na kuwanyanganya   mali zao!

     Alidaiwa  kuwa na madawa yaliyomsaidia kushinda kesi aliyoyapata kutoka nchini Zaire, alishakamatwa mara nyingi kwa makosa  hayo lakini alishinda kesi zote  kiajabu ajabu na kuwa huru. Sekunde chache baadaye Prosper alisikia jina lake likitajwa na kutembea hadi mlangoni ambako  alifungwa pingu mikononi na  mlango wa mahabusu ukafungwa.

    “Tangulieni nje nyie wauaji”

    “Kwani kuua ni kitu cha ajabu bwana, usitunyanyase!” Savimbi alimjibu askari bila woga kwa jibu hilo alipokea kipigo cha kitako cha bunduki na kupasuka usoni,damu zikamtoka lakini bado hakuacha kutoa matusi.

     Walipandishwa ndani ya gari la polisi  na ulinzi mkali wa msafara wa magari kama matano hivi uliongoza safari kwenda mahakamani. Mahakamani waliteremshwa na kuanza kusukumwa kuelekezwa katika mahabusu iliyokuwepo nje ya mahakama, Prosper alipotupa macho   pembeni alimwona mama yake akilia, machozi huku akiwa  ameshikiliwa na dada zake.

    Alionekana  akijaribu kujitoa mikononi mwao  ili asogee mbele lakini alishindwa, mdomo wake ulifunikwa na viganja vya binti zake  ili maneno aliyokuwa akiyatoa yasisikike, lakini bado Prospe alisikia kilichosemwa na mama yake!

    “Niachieni! Niende kwa mwanangu nikawaeleze polisi ukweli ili wamwachie”

    Prosper  aliposikia maneno hayo alimkonyeza mama yake lakini bado aliendelea kupiga kelele, jambo lililofanya dada zake waamue kumwondoa mahakamani haraka iwezekanavyo.

    Prosper na Savimbi walisomewa mashtaka yao tofauti na kurudishwa  mahabusu, hawakutakiwa kujibu kitu chochote sababu kesi zao zilikuwa za mauaji.

                 ****************

    Walipotoka mahakamani hawakurudishwa tena polisi bali walipelekwa moja kwa moja gereza la Isanga ambako waliwekwa mahabusu, huo ndio ukawa mwanzo wa Prosper kuishi gerezani  na kila mwezi alipelekwa mahakamani ambako kesi yake ilitajwa tu!

    Kila siku iliyokwenda kwa Mungu Prosper alikuwa na mawazo mengi  juu ya maisha yake, lakini mawazo yaliyomsumbua zaidi ni juu ya msichana Belinda,  alikaa na Belinda kwa muda mfupi shuleni na kumzoea na ni wazi alimpenda, kila alipoikumbuka siku   waliyoachana shuleni baada ya Belinda kumpa   nauli za kumpeleka likizo, roho ilimuuma sana Prosper!

    Alikuwa na mapenzi makubwa sana kwa msichana huyo  na aliamini hata yeye  alimpenda na alimkubali pamoja na umasiki aliokuwa nao!  Alishindwa kuelewa Belinda angepata vipi taarifa juu ya matatizo yaliyomkuta, kumbukumbu juu ya Belinda    zilimtia simanzi zaidi.

              ********************

    Belinda Dar es Salaam, Julai:

    Siku chache kabla ya shule kufunguliwa kwa pesa aliyopewa na baba yake Belinda alimnunulia Prosper zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, viatu na hata vitabu vizuri kwa ajili ya masomo yao.

    “Prosper atafurahi sana kupokea zawadi hizi na ndio ataamini kuwa kweli ninampenda!” Aliwaza Belinda wakati akipakia mabegi yake katika gari tayari kwa kuondoka kwenda shule.

    Belinda alikuwa na hamu kubwa ya kukutana na Prosper na aliona gari halifiki Moshi, alipofika shuleni hakumkuta na alikaa kwa  mwezi mzima shule bila kumwona   alianza kupata wasiwasi mkubwa moyoni mwake, alihisi pengine alikuwa amekosa pesa ya ada! Aliamua kumwandikia barua haraka  na kumwomba aje shule na  kama tatizo lilikuwa ada basi   yeye angemlipia.

    Kwa miezi miwili mfululizo haikujibiwa akaamua kuandika tena barua nyingine, lakini nayo  pia haikupata majibu, Belinda akazidi kuchanganyikiwa hakuelewa ni kitu gani kilimpata Prosper!

    Maisha ya shuleni yalikuwa magumu sana  bila Prosper ! Kila siku  alilia akiomba  Prosper aje tena shule waendelee na maisha yao lakini haikuwa hivyo kwani hadi mwisho wa  muhula Prosper alikuwa bado hajaripoti shuleni.

                 ****************

    Miaka mitatu baadaye:

    Belinda alisoma  kwa mateso bila kumwona Prosper tena, roho yake ilimuuma kila siku na mpaka anamaliza kidato cha sita alikuwa ni mtu wa kumlilia Prosper tu! Wanafunzi wenzake walimcheka,  alipomaliza kidato cha sita alijiunga na Chuo Kikuu cha  Dar es Salaam kwa masomo ya sheria, mawazo yake yalikuwab bado kwa Prosper!

    Likizo yake ya kwanza aliamua kusafiri  bila kuwataarifu wazazi wake kwenda  Tabora,  Belinda alidandia treni lililompeleka hadi Tabora mjini ambako alipanda tena basi la Sabena lililokwenda hadi Mbeya, basi hilo lilimshusha kijijini kwao na Prosper Tutuo kilometa kama thelathini kutoka Tabora mjini.

    Aliingia Tutuo saa saba mchana na kuulizia nyumbani kwa akina Prosper akaonyeshwa, kila mtu kijijini alimshangaa kwa mavazi aliyovaa!   Alishangazwa na hali aliyoikuta nyumbani kwao na Prosper ilikuwa ni nyumba ndogo mno iliyokandikwa kwa udongo na ilianguka upande mmoja. Alipobisha hodi  alipokelewa na mama mmoja aliyevaa nguo zilizochanika na alionekana  kuwa mgonjwa  alikohoa kila baada  ya kuongea sentensi moja! Mama huyo alifanana sana na Prosper.

    “Karibu binti!” Alisema mama huyo na kumpokea Belinda begi lake na mmoja wa wasichana alilipeleka ndani,  akavuta kigoda kilichokuwa karibu na kumpa Belinda akikalie, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Belinda aliyezaliwa katika familia ya kitajiri kuwa katika familia ya aina ile na alielewa ni kwanini Prosper aliishi maisha duni shuleni.

    Baada ya salamu Belinda hakusita kueleza sababu ya safari yake! Wasichana   wawili waliovaa magauni yaliyochakaa walikaa pembeni ya mwanamke huyo wakisikiliza.

    “Mama mimi naitwa Belinda!”

    “Wewe ndiye Belinda? Uliyeandika barua hapa miaka miwili na nusu iliyopita?” Uliyekuwa ukisoma na prosper Moshi?” Angelina mama  yake Prosper alilipokea jina la Belinda kwa mshangao.

    “Ndiyo mama na madhumuni ya safari yangu ni kujua aliko Prosper kwa sasa, sababu ni miaka miwili na nusu   sijamwona! Roho inaniuma sana kumpoteza kwani ninampenda!”

    Badala  ya kujibu ombi la Belinda mama yake Prosper aliangua kilio na hata wasichana waliokaa karibu yake nao walianza kulia machozi. Belinda alishindwa kujizuia na kujikuta nae akilia ingawa hakujua sababu ya wao kulia ilikuwa ni ipi!

    “Niambieni basi ili nifahamu Prosper yupo wapi hasa?”

    “Yupo gerezani!”

    “Alifanya nini Prosper?”

    “Alimuua baba yake!” Mama yake Prosper alishindwa kuueleza ukweli!

    Belinda alianguka chini na kuanza kugalagala akilia kwa uchungu   walijaribu kumbembeleza lakini hakusikia, alipotulia swali lake lilikuwa moja tu!

    “Ni kwanini alimuua baba yake masikini Prosper?”

    “Unaniona mimi nilivyo mwanangu?”

    “Ndiyo!”

    “Sikuzaliwa hivi  unavyoniona yote hii ni kazi ya baba yake prosper, alinitesa sana  kwa kunipiga kila siku na kunitoa viungo vyangu kwa kisu, Prosper alimuua baba yake kwa bahati mbaya akijaribu kunisidia mimi!” Alisema mama huku pia akilia machozi.

    “Nahitaji kumwona Prosper mama hata huko gerezani mnipeleke!” Alisema Belinda.

    “Prosper  yupo gereza la Isanga lakini siku ya kumwona ni Jumapili pekee!”

    Jumapili ilikuwa siku sita mbele yao, Belinda hakuwa na njia nyingine  kumwona Prosper  zaidi ya kusubiri  mpaka siku hiyo ifike! Maisha yalikuwa magumu sana kwake kuendelea kusubiri lakini hakuwa na la kufanya   aliishi nyumbani kwao Prosper akifanya kazi zote za nyumbani na alitumia pesa alizokuwa nazo kutatua baadhi ya matatizo katika familia hiyo.

    Ni yeye alimpeleka mama yake Prosper hospitali ya Kitete mjini Tabora kupimwa,  daktari aliamua kumpima makohozi, baada ya kuhisi alikuwa na kifua kikuu  na alipigwa  X-ray  ya kifua na kuonekana mapafu yake yalikuwa yameharibika kabisa.

    Makohozi  yake yalipopimwa kwa muda wa siku tatu yaligungulika  kuwa na wadudu wa  kifua kikuu na kuanzishiwa matibabu!Angelina alimshukuru Belinda kupita kiasi.

    Siku ya Jumapili ilipofika wote waliondoka kwenda gerezani Isanga, moyo wa Belinda ulikuwa ukidunda kwa nguvu na hakujua nini kingetokea baada ya kukutana na Prosper  alishindwa kupata picha halisi ya Prosper kwa wakati huo lakini aliamini bado alikuwa ni kijana mwenye sura nzuri kama alivyokuwa awali. Walipofika gerezani waliandikisha majini yao na watu waliotaka kuwatembelea, taratibu zote hizo kwa Belinda zilikuwa ni kumchelewesha kumwona Prosper! Baada ya kujiandikisha walionyeshwa  chumba maalum cha kumsubiri Prosper aje na kuongea naye!

    Dakika kumi   baadaye wakiwa wamekaa, Belinda alishuhudia kijana mmoja mwembamba mrefu akiingia chumbani humo, urefu wake ulikuwa sawa na Prosper lakini  unene wa mwili na ngozi yake  vilikuwa tofauti,alijaa ukurutu mwili mzima! Aliingia  chumba akiongozana na mtu mmoja mwenye mwili mkubwa na ndevu nyingi.

    Kijana huyo alipotupa macho chumbani akiwaangalia watu waliokuwepo,  ghafla aliruka na kukimbia moja kwa moja kuelekea mahali alipokuwa amekaa Belinda! Alipomfikia ndipo Belinda aligundua kijana huyo alikuwa Prosper lakini katika hali mbaya.

    “Belinda umefikaje huku?”

    “Prosper ni wewe? Umekuwaje hivi mpenzi wangu?”

    Waliangushana  hadi chini na kuanza kulia,  Angelina pamoja na binti zake Nyamizi na Kasanda walishindwa kujizuia na kujikuta wakiangua kilio, mwanaume  aliyeambatana na Prosper    alikwenda  na kumvuta Prosper na kumtoa mikononi mwa Belinda.

    “Ha! Hebu achianeni!” Alisema mwanaume huyo ambaye baadaye Belinda alimtambua kwa jina la Savimbi.

    “Kwanini?” Prosper aliuliza.

    “Kwani huyu msichana ni nani?”

    “Huyu ni mpenzi wangu!”

    “Nani amekuambia unatakiwa uwe na mpenzi?”

    “Savimbi mimi sitakii,niachie bwana niongee na Belinda wangu!”

    Sura ya Savimbi ilibadilika  na ghafla   bila hata kuuliza alimnyanyua Prosper na kuanza kumvuta kumrudisha ndani ya gereza, Belinda alilia na kushindwa kabisa kuelewa kilichokuwepo  kati ya Savimbi na Prosper  wote walibaki wameangaliana bila kujua la kufanya!



    Belinda hakuamini 
alichokiona alishangaa 
ni kwanini mwanaume huyo  amchukue Prosper  kabla hajamaliza kiu ya maongezi naye, alifikiria sana na kujikuta akilia.

    Alishindwa kuelewa ni kitu gani kiliendelea kati ya Prosper na mwanaume aliyemchukua kwa nguvu ukumbini na Prosper alionekana kutokuwa na sauti kabisa mbele ya mwanaume huyo.

    Kichwa cha Belinda kilihisi kitu fulani lakini hakuwa na uhakika  nacho sana na  alishindwa kupitisha moja kwa moja kuwa kulikuwa na uhusiano wa kishoga kati ya Prosper na mwanaume huyo!

    “Haiwezekani Prosper ninavyomfahamu hawezi kufanya hivyo!” Aliwaza Belinda!

    Hapakuwa na sababu ya wao kuendelea kubaki gerezani siku hiyo, walilazimika kuondoka   kwenda hadi stendi   ambako walipanda  basi na kurudi tena kijijini Tutuo!

    Njiani Belinda  aliwaza mambo mengi sana juu ya kifo cha baba yake Prosper na alishindwa kuelewa ilikuwaje mpaka Prosper akafikia uamuzi huo wa kikatili, mama yake Prosper ilibidi aeleze kila kitu kuhusu ukatili aliofanyiwa na mumewe na hatua aliyoichukua prosper kumkingia mama yake.

    “kwanini hamkwenda mahakamani mama?”

    “Mwanamke wa Kinyamwezi hatakiwi kumshtaki mume wake hata kama akipigwa mwanangu!”

    “Hivi mama yule mwanaume aliyekuja na Prosper pale gerezani ni nani?”

    “Ni rafiki mkubwa wa Prosper anaitwa Savimbi kila mara tukienda gerezani huwa anakuja naye!”

    “Mh! Mbona jina lake linatisha?”

    “Hivyo ndivyo anavyoitwa!”

    Walifika kijijini saa tisa mchana na Belinda aliendelea kuishi kijijini kwa wiki nyingine zaidi akisubiri Jumapili ifike ili aende gerezani kumwona tena Prosper,  siku ilipofika walikwenda tena gerezani    siku hiyo mama yake Prosper hakwenda kwa sababu hali yake haikuwa nzuri kifua kilimbana sana na alikuwa ameshindwa hata kuhema.

    Walikwenda Belinda  na dada zake Prosper peke yao na walifanikiwa kuonana na Prosper lakini siku hiyo alikuja peke yake bila Savimbi na kusalimiana nao, dada zake walionekana kushangaa.

    “Leo Savimbi yupo wapi?” Nyamizi alimuuliza Prosper.

    “Alipigana na Mnyapara jana!”

    “Kwanini?”

    “Kwa sababu Mnyapara alinipa ugali mkubwa na mboga yenye mafuta!”

    “Ndio wakapigana?”

    “Ndiyo!”

    Belinda alizidi kuyaamini mawazo yake, ilikuwa si rahisi watu wapigane sababu ya  Prosper kupewa ugali!Roho ya Belinda iliumia sana na kujikuta akilia alitaka kusema kitu lakini alishindwa sababu dada zake walikuwa pale.

    “Wifi zangu  mnaweza kunipa nafasi kidogo tu niongee na kaka yenu faragha?”

    “hakuna shida wifi!” Walijibu na wote wakatoka nje wakiwaacha prosper na Belinda peke yao chumbani, kilikuwa ni chumba chenye mwanga mdogo.

    “Prosper pamoja na matatizo yote yaliyokupata bado nakupenda!”

    “Hata mimi nakupenda pia Belinda na sasa ninaamini   hunidanganyi  penzi lako kwangu ni kweli tupu ingawa nasikitika kuwa nitafia gerezani,bila hivyo tungeoana na kuzaa watoto wetu Belinda!”

    “Usiwe na wasiwasi Prosper bado nina uhakika tutaoana!”

    “Tutaoanaje wakati mimi tayari nilishahukumiwa kunyongwa?”

    “Usijali muujiza wa Mungu utatokea na nikirudi nyumbani nitamshawishi baba yangu anipe pesa ili   nikutafutie wakili ajaribu kukutoa gerezani!”

    “Baba yako atakubali kweli?”

    “Nina uhakika baba atakubali wala usiwe na wasiwasi mpenzi!”

    Wote wawili waliangaliana na kujikuta wakitokwa na machozi ya uchungu! Kumbukumbu kubwa sana juu ya maisha yao ilikuja vichwani mwao, mambo mengi waliyoyafanya shuleni na kufurahia maisha yalirejea akilini mwao, Belinda alihisi mapenzi makali sana yakiutwaa tena moyoni mwake! Kweli alimpenda Prosper kuliko kitu kingine chochote, ni wanaume wengi walishamfuata kumtaka mapenzi lakini hakuwakubali moyo wake ulimpenda Prosper kijana masikini  tena aliyekuwa gerezani wakati huo.

    Kitu kama sumaku kilijitokeza katikati yao na kujikuta wamekumbatiana na kuanza kupapasana miili yao! Kwa mara ya kwanza katika maisha yao tangu wafahamiane walijikuta wakitamaniana kimwili na  mambo yaliyofuata katika muda wa dakika tano ndani ya chumba hicho hayaandikiki wala kuelezeka  ila ilikuwa ni raha ambayo wote wawili waliipata kwa mara ya kwanza maishani mwao.

    “Proper ahsante! Ninakupenda sana Prosper na sijui nitaishije bila wewe!” Alisema Belinda huku akilia machozi.

    “Nakupenda pia Belinda  na kama nilivyokueleza bila  haya matatizo tungeoana na kuwa mke na mume!”

    “Usiwe na wasiwasi Prosper tutaoana tu!” Belinda aliendelea kusisitiza alichokisema awali.

    “Hivi sasa unasoma wapi?’

    “Mimi?”

    “Ndiyo!”

    “Baada ya kumaliza kidato cha sita nilijiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam ambako ninasoma Sheria!”

    “Kweli?”

    “Ndiyo!”

    “Unataka kuwa mwanasheria Belinda?”

    “Ndiyo!”

    “Soma sana uje utusaidie!”

    Dakika tano baadaye kengele ililia ndani ya gereza na Prosper alinyanyuka na kumkumbatia Belinda walipigana mabusu na kuagana! Mwili wa Prosper ulikuwa  mchafu kupita kiasi  alihisi Belinda angemwonea kinyaa lakini haikuwa hivyo, Belinda hakujali wala kuonyesha kushangazwa na hali hiyo alizidi kumkumbatia.

    “Belinda ni lazima niende sasa muda wa kuongea na wewe umekwisha!”

    “Sawa darling lakini jaribu kuwa mwangalifu sana na Savimbi siipendi tabia yake!”

    Prosper hakujibu kitu alizidi kuinamisha kichwa chake chini kwa aibu jambo lililomfanya Belinda aendelee kupata uhakika kuwa kulikuwa na jambo kati yao!

    Baada ya kuagana Belinda alitoka nje ya gereza na kuungana na wifi zake na safari ya kwenda stendi kupanda basi la kuwarudisha nyumbani ilianza, njia nzima Belinda alikuwa ni mwenye mawazo  alifika akiwa amechoka na kujitupa kitandani ambako aliendelea kumlilia Prosper!

                  ***************

    Alikaa Tabora kwa wiki tatu  bila wazazi wake kufahamu mahali alikokuwa, baba mzazi yake alishamtafuta kila mahali  bila kumpata mpaka kukata tamaa! Alitangaza katika vyombo mbalimbali vya habari lakini bado hakufanikiwa kumpata binti yake, wengi walihisi Belinda alikufa lakini baba yake hakuliamini hilo.

    Hatimaye mzee Thomson Komba baba yake Belinda aliamua kutangaza zawadi nono ya shilingi milioni kumi kwa mtu yeyote ambaye angefanikisha kupatikana kwa Belinda,  wanakijiji wawili wa kijiji cha Tutuo walijitokeza na kwenda kutoa taarifa moja kwa moja kituo cha polisi Belinda akawa amekamatwa.

    Siku aliyokamatwa aliiacha familia  ya akina Prosper katika majonzi makubwa kwa sababu kwao mkombozi alikuwa ameondoka! Kukaa kwa Belinda katika familia hiyo kulipunguza sana shida zao za maisha, pesa yote aliyokuwa nayo aliitumia katika matumizi ya nyumbani na ni yeye pia aliyenunua dawa za mama yake Prosper.

    Alichokifanya Belinda wakati wa kuondoka ni  kumtupia Nyamizi dada yake Prosper shilingi elfu hamsini alizokuwa nazo katika mfuko wa suruali ili  ziwasaidie.

    “Wifi!Pesa hizo zitawasaidia!”

    ITAENDELEA  

0 comments:

Post a Comment

Blog