IMEANDIKWA NA : AGNESS MATIMBA
*********************************************************************************
Simulizi : Kwa Nini Mimi?
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*****RIWAYA HII NI MAALUM KWA WOTE WALIOPITIA SHIDA MBALIMBALI HAIJALISHI SHIDA NI YA AINA GANI, ILIMRADI NI SHIDA.*****
*****SASA TWENDE NAYO.*****
ILIKUWA ni alfajiri ya asubuhi na mapema nilipoamshwa na kelele za makuli mbalimbali wakiwa wamebebelea mizigo yao kupeleka katika soko la kariakoo. Nilikuwa nimelala kwenye varanda la duka la wahindi la pale Mtaa wa Kongo.
Japo palikuwa ni nje nilipokuwa nimelala lakini nilikuwa nafanya malipo kidogo, na malipo yenyewe ilikuwa ni shilingi elfu moja kwa walinzi waliokuwa wanalinda pale. Siku niliyokuwa nakosa hela yao, sikuwa na jinsi ilinibidi niwape mwili wangu wauchezee wanavyotaka.
Hayo ndio yalikuwa maisha yangu. Basi niliamka nikachukua yale maboksi niliyoyalalia nikayakunja na nikayaweka vizuri kwa kuyabana pembeni ya tofali kisha nikachukua chupa ya uhai iliyokuwa na maji kidogo nikakamata mswaki na jivu kidogo la mkaa nikasukutua na fundo moja la maji kisha nikayatema fyuu!
Hakika nikikumbuka nilikotoka mimi Anne, nilikuwa naishi vizuri nakula vizuri,leo hii nipo kariakoo tena mtaani.Basi nilijikokota taratibu nikaelekea kwenye magenge ya kinamama waliokuwa wakipika vyakula wakijulikana kama MAMA NTILIE.
Wakati naelekea vibandani nilikuwa napigana vikumbo na watu mbali mbali kama kawaida ya jiji la Dar,ni jiji la hekaheka wengine walikuwa wamebeba matenga yenye bidhaa mbalimbali kama vile nyanya,mboga za majani,vitunguu na bidhaa nyingine, nilikwenda kwenye banda la mama Hadija.
Mama Hadija aliniamini sana na kunipenda alikuwa akiniagiza mzigo popote na nilikuwa naufikisha.Hivyo nilivyofika pale bandani kwa mama Hadija alinipa kazi ya kuandaa vikombe na kukaanga chapati kwa ajili ya wateja.Wakati naendelea kuandaa ndipo alipokuja mtoto wake Hadija kuja kuchukua nauli ya shule,hapo kumbukumbu zangu zikarudi nyuma nikiwa Iringa nyumbani nilikuwa nasoma vizuri, huku nikidekezwa,kitu gani ambacho nilikuwa nahitaji nikakosa? Nilikuwa napata mahitaji yote, na haki zote kama binti wa pekee wa mzee Mkanyagasi.
Baba yetu alitupenda akatupa haki sawa. Leo hii mimi nimekuwa binti wa mtaani!? Na mtaa umenibeba umekuwa Baba na Mama, wakati nawaza huku nimejishika tama.Kumbe mama Hadija alikuwa akiniita na mimi sikuwa nasikia,
"Anne,Anne" mpaka akaja kunitingisha na hapo ndio nikashtuka.Akaniuliza, "Uunawaza nini mwanangu?Au unapoishi wanakutesa?nilishakuambia njoo uishi nami".Masikini nilimdanganya mama Hadija naishi na shangazi yangu kumbe nilikuwa naishi mtaani tu, sikutaka kuishi na watu nilikuwa nimenyanyasika na nimejifunza mengi kutokana na kuishi na watu mbalimbali.Nikamtazama kisha nikamjibu,
"hapana mama nimepakumbuka nyumbani tu".Basi mama Hadija akaridhika na jibu lile na kunipa moyo. Kisha akaniagiza kwenda mtaa wa pili kufuata mafuta ya kupikia huku akanipa shilingi elfu ishirini mkononi.Wakati ananipa zile hela pembeni yangu walikuwa wamesimama vijana wawili nikapokea zile hela na kuanza kuondoka,wakati naondoka wale vijana wakanifuata huku moja wao akiniambia
"dada tukusindikize maana mtaa huu umejaa vibaka".Mimi sikuwa na hofu yoyote nikawakubalia na kuanza kuondoka.Tulitembea kwa muda wa nusu saa ghafla mmoja wao akageuka na kuniambia dada kwa usalama wako tupe hizo hela nilipigwa na mshtuko! nikashindwa kuongea.Ghafla wakanitolea kisu kisha wakasema.
"Tupatie hizo hela unatuchelewesha ikabidi niwape hizo hela.Wakazipokea halafu wakaanza kupiga kelele mwizi!mwizi huyo! Hakika nilianza kuogopa na kutetemeka leo mimi nimeanza kuitwa mwizi! Rundo la vijana likajitokeza aliyeshika tofali mwenye jiwe wakanikamata mmoja wao akasema mnamchelewesha nini?.Vibaka kama hawa tunahitaji tuwafunze adabu akanyanyua tofali na kutaka kuniponda nilifumba macho na kuanza kumuomba MUNGU anikutanishe na wazazi wangu.Ghafla tofali zito likanidondokea nikaona giza huku nikiziona taswira za wazazi wangu.
Kilichoendelea hapo sikukijua bali nilijikuta nikielea kisha nikajikuta nipo kwenye sehemu nzuri sana, kwa mbali nilimuona mama yangu akilia,huku akiniambia
"mwanangu umekuja huku kufanya nini? Tafadhali rudi, ndugu zako umewaacha peke yao".Halafu nikajikuta nimeshikwa mkono na mtu moja aliyevaa mavazi meupe kama theluji, huo weupe wake sijapata kuona hapa duniani,akaniambia huku akiwa na tabasamu.
"Binti tafadhali rudi duniani bado haujamaliza kazi yako".Hapo hapo nikashtuka kutoka kwenye usingizi mzito, nikamuona mtu amevaa mavazi meupe amekaa pembeni yangu.Nikamuuliza huku nikiongea kwa sauti ya chini sana,
"hapa nipo wapi?"akanijibu
"hospitali" nikaanza kuvuta kumbukumbu nimefikaje pale.Ghafla nikaanza kupiga kelele,
“wananiua jamani!” huku nikichomoa dripu na kushuka kwenye kitanda.Yule mtu alinishika kwa nguvu na kuanza kumuita dokta,basi dokta alifika pale kisha akaita wahudumu wawili wakaja, kisha wakaendelea kunishika kwa nguvu halafu Dokta akanichoma sindano,kilichoendelea hapo sikukitambua. Nikalala usingizi mzito. Walikuwa wamenichoma sindano ya usingizi na niliposhtuka kwa mara za pili sikuwa na vurugu tena kama mara ya kwanza.Pembeni yangu alikuwa ameketi mtu mwenye mavazi meupe ambeye baadae nilikuja kugundaua alikua ni nesi aliyeagizwa akae karibu na mimi.
Aliponiona nimeamka, yule muuguzi alifurahi kisha akamwita dokta, dokta alivyofika aliniangalia halafu akaniuliza
"unaendeleaje binti?" nikamjibu ninaendelea vizuri na kumtupia swari dokta la kwani pale nipo wapi? Akaniambia
"hapa ni kwenye hospitali yangu ya binafsi" kisha akaniuliza jina langu nikamwambia naitwa Anne Mkanyagasi.Dokta akawa ananitania
"jina lako zuri kama wewe mwenyewe ulivyo mzuri, nikatabasamu kisha nikamuuliza dokta nimefikaje pale.Yule dokta akaanza kunisimulia kila kitu, ambapo baadae nilikuja kugundua anaitwa Dokta Hans.
DOKTA HANS ANASIMULIA.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa ni jumatano mida ya saa nane mchana uliletwa hapa na rafiki yangu ambaye alikukuta katika hali mbaya ukiwa umelazwa barabarani.Na kila gari lililokuwa likipita lilikuwa likikukwepa rafiki yangu ni mtu mwenye huruma sana, yeye aliamua kukuchukua na kukuleta kwenye hospital yangu na alilipia gharama zote za matibabu. Dokta Hans akasema Anne ulikuwa upo kwenye hali mbaya sana,nilimshauri rafiki yangu aende polisi kwanza lakini yeye alikataa hivyo niliamua kukutibia hivyo hivyo.
Baada ya maelezo yale,nikamuuliza Dokta Hans,
"kwani leo ni lini?"akanijibu
"Jumapili"nilipigwa na butwaa ila nikasema ahsante MUNGU kwa kuniokoa,kisha nikajaribu kuamka miguu yangu haikuwa na nguvu. Dokta Hans akaniambia
"tulia umeumia sana maeneo ya miguuni na kichwani".Nilianza kulia akanimbembeleza kwa utaratibu, lakini ghafla akaingia kaka moja amebeba mfuko wenye vyakula akaniuliza
"dada unaendeleaje?" nikamjibu
"naendelea vizuri"Basi dokta Hans akanitambulisha kwa yule kaka kuwa anaitwa Thomas ndiye alieniokota kule barabarani. Kwa kweli nilimshukuru sana Thomas kwa ukarimu wake na kumwambia sina cha kumlipa.
Nilikula chakula alicholeta Thomas, baada ya hapo Dokta akamwambia Thomas aniache nipumzike. Kumbe nilivyozinduka dokta Hans alimpigia simu Thomas akamwambia aandae chakula na baada ya Thomas kuondoka nililala huku nikifikiria je! Nikitoka hospital nitakwenda wapi? Na nitakuwa mgeni wa nani?
VIZURI UISHI VIZURI NA WATU HAPA DUNIANI,ILI UJIPATIE THAWABU MBINGUNI. KUSAIDIANA NI JAMBO LA BUSARA NA UNAPOMSAIDIA MTU JITOE KWA MOYO MMOJA NA UPENDO WA KWELI. KWANI VITABU VITAKATIFU VYA DINI VIMEANDIKWA.MALIPO YAKO YAPO MBINGUNI
Nilikaa pale hospital kwa muda wa wiki moja ,na Thomas siku zote alikuwa anakuja kunitembelea huku akiniletea chakula na huduma nyingine muhimu, hata nguo alininunualia maana siku niliyopelekwa hospital nguo zangu zilikuwa hazitamaniki kwa kupigwa.Basi muda ukaenda na hatimaye niliruhusiwa, lakini Dokta Hans akaniuliza
"Anne unaishi wapi? Nikipata nafasi nije kukutembelea?".Ndugu msomaji sikufichi nilijawa na donge kwenye koo, machozi yakaanza kunitoka.Kipindi hicho Thomas alikuwa ametoka kuninunulia dawa kwenye duka la hapo hospitali,na hapo ndipo Thomas aliponikuta nikiwa nalia.Nikamwambia dokta Hans
"Sina pa kwenda, mama Khadija aliyekuwa ananisaidia, toka siku ile nikutane na vibaka sikuenda anaweza akajua nilimwibia. Hapo Thomas akadakia kwa kuniambia
"Anne usijari,tutaondoka wote utaenda kuishi kwangu".Nilijikuta uso wangu ukichanua kwa tabasamu huku vishimo viwili vya kwenye mashavu yangu vikibonyea kisha nikamuambia Thomas
"Ahsante sana, sina cha kukulipa ila MUNGU ndiye anayejua atakupa nini"Thomas akasema usijali tupo pamoja Anne. Nilimshukuru Dokta Hans kwa huduma zake nzuri alizonipa.Dokta Hans akahaidi kuja kunitembelea mara kwa mara, halafu nikaondoka na Thomas.Nilivyotoka nje Thomas akanipakiza kwenye gari lake kisha akakanyaga mafuta huku Dokta Hans akitupungia mikono.
Tulifika salama nyumbani kwa Thomas,na sikuamini kama Thomas alikuwa akimiliki nyumba kubwa kama ile na yenye uzio mpana, na kulindwa na mitambo ya kisasa ya umeme, huku bado kukiwa na mlinzi wa kawaida aliyekuwa akilinda hiyo nyumba. Alinikabisha ndani kwake, lakini nyumba yake ilikuwa kimya sana. Akaniambia
"Usiogope Anne, hapa naishi mwenyewe ila yupo mtu anayenifanyia usafi wa ndani ya nyumba yangu na kuondoka".Thomas alinikaribisha vizuri akanionyesha chumba changu,kisha nikaingia chumbani nqa kupitiwa na usingizi ambapo baadaye nilishituka kwa mlango wangu kugongwa.Ni Thomas alikuwa ananigongea huku akiniambia
"Anne hutaki kula? Chakula tayari mumy",nilijivuta taratibu nikiwa na mang'amung'amu ya usingizi kisha nikaijongea meza. Kumbe nilivyolala Thomas aliingia jikoni na kuandaa chakula.Chakula kile kilikuwa kitamu sana, nikamtania
"unajua kupika, siku mke wako akikupikia chakula kibichi utamuumbua vibaya"Thomas akacheka sana halafu akaniambia,
"usijali kadri siku zinavyokwenda tutajuana vizuri".Tulivyomaliza kula Thomas akaniambia yupo tayari kunisaidia kama nina shida yoyote,akaomba nimsimulie kilichonikuta, na hivi ndivyo nilivyoanza kusimulia
ANNE ANASIMULIA..
Naitwa Anne Mkanyagasi, wazazi wangu walikuwa ni wenyeji wa Iringa. Katika familia yetu tulibahatika kuzaliwa watoto watatu, mimi nikiwa binti wa pekee na wa mwisho. Wa kwanza ni John na mwingine ni Zakaria. Tulilelewa kwenye maadili ya dini, na wazazi wangu walikuwa wacha MUNGU. Nakumbuka mama yangu alikuwa akiitwa Damaris na baba yangu ni Lawrence, kipindi hicho kaka zangu walikuwa shule za bweni wakiendelea na masomo ya sekondari,huku mimi ndio kwanza nilikuwa darasa la saba. Katikati ya darasa la saba Mama yangu alianza kuugua ghafla, miguu yake ilikuwa inajaa maji na kuvimba. Ikabidi niwe naacha kwenda shule na muda mwingi nilikuwa nautumia kumwangalia mama maana Baba alikuwa ni mfanyabiashara,muda mwingi aliutumia safarini na kaka zangu walikuwa shule za bweni.
Kwa kweli baba yangu alikuwa na vitega uchumi vingi sana ila watu ni wabaya sana mpaka najilaumu kwanini niliumbwa binadamu. Niliongea hayohuku nikianza kulia.Thomas alinibembeleza huku akiniambia.
"Anne acha kumkufuru MUNGU, MUNGU anamakusudi yake nyamaza acha kulia tafadhali".
Nikanyamaza na nikaendelea kusimulia.Tulikuwa tunaishi vizuri hatukupata shida katika masuala ya kubadilisha chakula, nguo na hata mahitaji mbalimbali, kwa upande wa darasani nilikuwa naongoza lakini ghafla nikaanza kushuka, na muda wa mtihani wa mwisho ulikuwa umekaribia huku nikimuuguza mama yangu. Huwezi amini Thomas, nilifanya vibaya mtihani na matokeo yalivyotoka nilikuwa nimefeli sana. Baba hakuchoka, akanipeleka shule ya binafsi ya kutwa, nikaanza kidato cha kwanza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sitasahau katikati ya mwezi wa sita ilikuwa ni tarehe 16/6/2000,Mama yangu mpendwa alipoiga dunia akiwa mikononi mwangu.Nikiwa nimempakata mama yangu huku machozi yananitoka kwa uchungu,mama alinihusia kwa kusema,
“Anne waheshimu kaka zako na Baba yako umsikilize, yeye ndiye Mungu wa pili”. Nilianza kulia huku nikimpa Thomas kazi ya kunibembeleza.
Nikamuomba Thomas kwa kumwambia kuwa nitaendelea kumsimulia kesho.Thomas alinisikiliza na akanibembeleza mpaka nikalala.Asubuhi nilivyoamka nilimkuta Thomas ameshapika chai,mimi nilimsaidia kuiandaa mezani chai ile, na baada ya hapo kwa vile ilikuwa ni wikiend, Thomas alikuwa haendi kazini aliniomba niendelee kumsimulia historia ya maisha yangu.
{ANNE ANAENDELEA KUSIMULIA}
Baada ya msiba nikaendelea kusoma, ila daima sikusahau kwenda kulitembelea kaburi la Mama kila tarehe aliyofariki.Nilikuwa nikifarijika sana hasa pale ninapo lifagilia kaburi lake,nilikuwa nahisi bado yupo nami na wala hajaondoka duniani.Baba alijitahidi kututoa ‘out’ watoto wake ili tusahau na tugange yajayo, pia alikuwa akitupa ushauri lakini kwangu mimi hakuwezekana.
Mwaka uliyofuata pigo jingine likatokea katika familia,na hapo ndipo matatizo yalipoanza kuniandama mimi,
“oh!oh! kwanini mimi jamani”.Nikaanza kulia, Thomas alichukua mkono wake akanipiga piga begani huku akiniambia
"jikaze Anne tafadhali".
"Why yote yameniandama mimi, kwa nini mimi?" niliongea kwa uchungu huku nikimkumbatia Thomas na machozi mengi yakishuka kwenye mashavu yangu.Nilinyamaza baada ya kubembelezwa sana, kisha nikaendelea.
Nakumbuka nilikuwa kidato cha pili, ilikuwa ni mwezi wa tatu tukikaribia mitihani ya kufungia shule kwa ajili ya pasaka,Baba alikuwa amesafiri akiwa ameelekea nchini Kenya kwaajili ya kufuatilia mali mpya.Alikuwa amepanda basi la Akamba, ghafla Kaka yangu John akapokea simu ya Baba huku mpigaji akiwa siyo Baba.Simu ile ilimtaarifu kuwa mwenye hiyo simu amepata ajali na amefariki dunia, na hiyo ajali imetokea Same halafu akakata simu,
John alichanganyikiwa, alivyoipiga tena namba ya Baba ikawa haipatikani Kabisa.Mpigaji alishaiba simu ya Baba. John alimpigia simu Baba mdogo na kumweleza,Baba mdogo na ndugu wengine wakakaa kikao na kuanza kufuatilia.Ni kweli Baba yangu alifariki dunia, inasemekana tairi la mbele lilipasuka na basi lilikosa muelekeo na kupinduka.
Ndugu msomaji nillia, na kifo cha Baba kiliniuma sana kwa vile Baba yangu hakuumwa, aliondoka nyumbani akiwa mzima wa afya tele.
Basi ndugu walifanya mipango ya mazishi, wakausafirisha mwili wa Baba mpaka Iringa tukampumzisha Baba katika nyumba yake ya milele.
Baada ya kukaa kikao cha familia yakafanyika makubaliano mimi niende nikakae kwa Baba mdogo na kaka zangu waendelee kukaa katika nyumba yetu,kwa kuwa mimi nilikuwa mtoto wa kike hivyo haikuwa vizuri kukaa na watoto wa kiume.Kikao cha famila ndio kiliamua hivyo.Hatimaye nikaondoka kwetu huku nikiwaacha kaka zangu wakiendelea kuishi kwenye nyumba yetu,na huku wakisimamia baadhi ya biashara za marehemu Baba wakisaidiwa na Baba mdogo.Nilipokelewa vizuri na mke wa Baba mdogo wakawa wananilea vizuri kwa upendo sawa na watoto wao…..
JE ANNE ALIISHI VIZURI NA FAMILIA YA BABA YAKE MDOGO DAIMA? VIPI UPANDE WA KAKAZAKE? MAJIBU YOTE HAYO TUKUTANE SEHEMU IJAYO.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment