Simulizi : Kwa Nini Mimi?
Sehemu Ya Pili (2)
ILIPOISHIA…..
Basi ndugu walifanya mipango ya mazishi, wakausafirisha mwili wa Baba mpaka Iringa tukampumzisha Baba katika nyumba yake ya milele.
Baada ya kukaa kikao cha familia yakafanyika makubaliano mimi niende nikakae kwa Baba mdogo na kaka zangu waendelee kukaa katika nyumba yetu,kwa kuwa mimi nilikuwa mtoto wa kike hivyo haikuwa vizuri kukaa na watoto wa kiume.Kikao cha famila ndio kiliamua hivyo.Hatimaye nikaondoka kwetu huku nikiwaacha kaka zangu wakiendelea kuishi kwenye nyumba yetu,na huku wakisimamia baadhi ya biashara za marehemu Baba wakisaidiwa na Baba mdogo.Nilipokelewa vizuri na mke wa Baba mdogo wakawa wananilea vizuri kwa upendo sawa na watoto wao…..
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ENDELEA…
……MAPENZI SIYO JAMBO LA KUTUMIA NGUVU AU KUMLAZIMISHA MTU MPAKA KUFIKIA HATUA YA KUMBAKA.ILIPOISHIA…..
Hatimaye maisha yakaendelea mbali na kwetu nikiwa naishi na familia ya Baba mdogo.
Niliendelea kuishi vizuri na familia ya Baba mdogo mpaka nikafanikiwa kumaliza kidato cha nne, baada ya kumaliza mitihani, Baba mdogo aliumwa sana na mama mdogo na familia walijitahidi kumtibia.Kila hospital walienda na kila dawa walitumia mpaka miti shamba lakini haikusaidia.
Mwishoni mwa mwezi wa kumi na mbili,Baba Mdogo aliaga dunia, hapo ndipo shida zilipoanza.
Nikaacha kumsimulia Thomas,n ilibanwa na pumzi na iliyonifanya kuanza kulia huku nikitamka maneno makali na kwa uchungu,
" Kwanini mimi jamani?,eti Thomas hivi kwa nini mimi, eeh?".Chozi lilitirika shavuni mwangu, Thomas ikawa kazi yake kunibembeleza mpaka nikalala akaniacha akaendelea na shughuli zake.Nilikuja kushtuka baada ya masaa mawili nikakuta ameniandikia ujumbe kwenye karatasi kuwa ameenda mjini atarudi jioni.
Nilikwenda jikoni nikakuta chakula tayari, nilikula chakula nikakosha vyombo nikatoka nje kwenda kuangalia mazingira. Hapo niliiona nyumba vizuri tofauti na jana usiku nilivyofika kwa Thomas. Nilijiuliza maswali mengi likiwepo, kwanini Thomas aishi mwenyewe pasipo kuwa na mfanyakazi na wala ndugu lakini sikupata
.Basi nikaamua kurudi ndani nikaendelea kupumzika. Jioni ilipofika Thomas alirudi na mboga tukasaidiana kupika tukala.Halafu nikamuomba Thomas akae niendelee kumsimulia historia ya maisha yangu.
ANNE ANAENDELEA KUSIMULIA.
Tulifanikiwa kumaliza msiba vizuri, nikaendelea kuishi na mama mdogo na matokeo ya mitihani niliyofanya yalivyotoka nilikuwa nimefaulu vizuri. Hapo ndipo mama mdogo alipoanza kubadilika na kuniambia hana hela ya kunisomesha, akaanza kunifanyia vituko mbalimbali mpaka nikaanza kuogopa. Marehemu baba mdogo alikuwa ameninunulia nguo nzuri,lakini mama mdogo alininyang'anya zile nguo, nilikuwa nalala sehemu nzuri, akanihamishia kwenye banda la kuku. Nililia sana lakini sikuwa na jinsi. Nikawa kijakazi wa pale nyumbani yaani kazi zote nikawa nazifanya mimi,nikawa wa mwisho kulala lakini wa kwanza kuamka.Nilikuwa nawasubiria wale chakula kwanza halafu chakula kilichobaki ndicho nilikuwa nakula, kikikosekana chakula ujue siku hiyo nalala njaa.
Siku moja nilimuomba jirani simu nikampigia Kaka John na kumuelezea kila kitu.Kaka John alinihaidi kuja kunichukua, alisikitia sana alivyosikia kuwa mdogo wake napata shida.Hali yangu ilibadilika ghafla, ule uzuri wangu wote niliokuwa nao uliondoka, sikuwa yule Anne ambaye nilikuwa nikifahamika vizuri kama mlimbwende.
Nakumbuka kulikuwa na mama moja ambaye alikuwa ni jirani yetu. Alikuwa akijulikana kama mama Benja, yeye alikuwa ni mtu mwenye huruma sana.Mama mdogo alipokuwa hayupo alikuwa akiniita na kunipa chakula kwa kificho, hata hivyo baadae mama Benja alifariki, MUNGU amlaze mahali pema peponi mama yule.
Siku moja alikuja mdogo wake mama mdogo, alikuwa akiitwa Moses. Moses alikuwa akinisifia kila akiniona kuwa mimi ni mzuri.Basi usiku moja Moses alikuja kunigongea mlango nilipofungua tu mlango aliingia na kufunga mlango na kuanza kuniingilia kimwili yaani kunibaka. Niliumia sana na yeye ndiye aliyenibikiri, kiukweli nililia sana nikakosa nguvu mpaka nikapoteza fahamu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikuja kushtuka siku ya tatu nikiwa nipo hospitali, pembeni yangu alikuwa amekaa kaka yangu John. Mwanzoni sikuelewa kwanini niko pale, kaka John akanipa pole.Nilivyokumbuka sababu ya kuwa pale nililia sana. John akanimbembeleza,lakini ghafla mlango ukafunguliwa akaingia mama mdogo huku akinipa pole,nilimjibu
"Sitaki pole yako ya kinafiki".Mama mdogo ilibidi atoke nje, kisha nikamuuliza kaka John aliko Moses, akaniambia ametoroka na anatafutwa. Nilipatwa na hasira kali sana utafikiri simba mwenye njaa anayetamani kula hata nyasi sababu kakosa nyama,hiyo ni baada ya kusikia kutoweka kwa Moses.
Nilikaa hospital kwa muda wa wiki moja, daktari alinishauri baada ya miezi mitatu niende hospital yoyote kupima afya.Nilipotoka hospital niligoma kurudi kwa mama mdogo,hivyo kaka John alinichukua na kunipeleka nyumbani.Nilipofika nyumbani nilimkuta kaka John akiwa anaishi na mwanamke.Akanitambulisha na kuniambia kwamba huyo ndiye wifi yangu, nimuheshimu kama ninavyomuheshimu yeye.
Maisha yalikuwa mazuri, niliishi vizuri sana na wifi yangu yule. Baada ya miezi miwili walikuja wadogo zake na wifi,walitafutiwa shule wakawa wanasoma huku mimi nikiwa nakaa tu nyumbani.
Nikimuuliza kaka John vipi mimi kuhusu shule.Alichonijibu hakikueleweka na kipindi hicho hata wifi alipunguza mapenzi kwangu, alikuwa akitoka mjini ananiletea zawadi mbalimbali kama vile nguo na viatu, lakini sasa akawa haniletei tena.
Nikamuuliza kaka John alipo kaka yangu Zakaria akaniambia yupo Dar-es-salaam.Ghafla moyoni nikapanga kutoroka kuja Dar kumtafuta kaka yangu Zakaria.Sikuwa na nauri, ila nilipanga kutafuta kwa mbinu zote ninazozijua mimi ilimradi tu nipate nauri.
Nilimuomba Kaka John namba ya simu ya kaka Zakaria alinipa,halafu nikamuomba elfu ishirini akanipatia elfu thelathini nazo nikazichukuwa nikazibana huku hajui nitazifanyia nini.
{SAFARI YA KUELEKEA DAR-ES-SALAAM}
Nakumbuka ilikuwa ni alfajiri niliamka mapema sana, nikatafuta peni na karatasi nikaandika barua kwa kaka John nikamwambia, asinitafute nimeelekea dar kwa kaka Zakaria.Sababu kuu ni kuwa yeye hanijali. Niliifunga vizuri kwenye bahasha na kuiweka sebuleni kwenye meza,nikatafuta pesa bahati nzuri nilikuta noti ya elfu tano juu ya meza nikaichukua.Nilitoka taratibu kwa kunyata, nilifunga mlango nikatoka nikatembea kama hatua tano kisha nikageuka kuiangalia nyumba yetu tulioachiwa na wazazi.
Huku nikilia nikasema "kwaheri nyumbani tutaonana tena MUNGU akipenda".Hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kuiona nyumba yetu. Baada ya hapo nilikimbia sana huku nikaelekea stendi. Nilipofika stendi kujisachi mfukoni nikawa na elfu ishirini na tano. Sikukumbuka elfu kumi nyingine nilikuwa nimeiweka wapi. Nikajifikiria nitafanya nini,nauri ya basi efu kumi na tano, bado sijala wala huko nitakapofika sijui nitalala wapi kama kaka nisipo mpata, na nyumbani sitaki kurudi.
Mara nililiona basi la Nyagawa na watu walikuwa wakikatiwa tiketi huku wakiingia ndani ya basi.Hapo nikajiwa na wazo la kuingia kwenye boneti. Nilizunguka nyuma ya gari kisha nikaingia kwenye boneti, nikajilaza na kupitiwa na usingizi. Nilikuja kushtushwa na kelele za konda, konda alisimama mbele yangu huku akipiga kelele.
"jamani njooni muone maajabu huku chini ya boneti kuna mtu"abiria walishuka na kuja kuniangalia, nguo na mwili wangu ulikuwa umejaa mavumbi kupita kiasi. Nikaanza kutetemeka huku nikilia na kujilaumu pia kwa nini nilichuka hatua ya kuingia ndani ya boneti.
KUSAIDIANA NI VIZURI KULIKO KUSAIDIWA NA NDUGU INAWAPASA KUPENDANA NA KUWA NA UPENDO WA KWELI USIPOMPENDA NDUGU YAKO UNAFIKIRI ATAPENDWA NA NANI MWINGINE?.
Abiria walikuwa wamekwisha shuka kutoka ndani ya basi na wote walikuwa wakiniangalia. Konda alikuwa amenishikilia kwa nguvu huku amenikwida blauzi yangu.Akawaambia abiria huyu ni mwizi lazima tumpeleke polisi. Lakini kwa bahati nzuri kulikuwa na baba mmoja ambaye baadaye nilikuja kugundua kuwa alikuwa ni polisi.
Alimwambia yule konda aniache yeye atanilipia nauli mpaka Dar. Kwa kweli nilishukuru sana mpaka nikampigia magoti yule baba, akaniambia wa kumshukuru ni MUNGU na si yeye.Basi nikaingia ndani ya basi na kupewa siti. Kufika kitonga yule baba alininunulia chakula nikala, nikamshukuru tena.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hatimaye baada ya mwendo wa masaa kama nane tukawa tumeingia Dar-es-Salaam.Kufika Ubungo nilikuwa nikishangaa tu, ndipo yule baba aliniuliza nimefika Dar kufanya nini? Nikamuelezea kila kitu,akaniambia twende kwangu nitakusaidia kumtafuta kaka yako. Kufika kwake akaniingiza sebuleni kwake, akaniambia hapo ndipo kutakuwa chumbani kwangu. Baba yule alikuwa amepanga chumba na sebule.
Akaenda kununua chipsi na maji akanikaribisha. Baada ya kula akanielekeza bafuni, nikaenda kuoga. Nakumbuka mtaa huo ulikuwa unaitwa Tandale Kwa Mtogole.Akanipa mashuka nikajifunika na kulala usingizi. Nikiwa usingizini katikati ya usiku nilishangaa nikipapaswa, nilivyogeuka nikazibwa mdomo na yule baba ambaye nilimtambua kwa jina la Abdalah. Aliniingilia kimwili,ambapo nililia sana, sikuwa na jinsi, nikawa mtumwa wa ngono kwa mara nyingine.
Abdalah au Dullah hakupiga simu kwa kaka yangu badala yake alinigeuza mkewe, alifanya mapenzi na mimi muda wowote aliohitaji, na nikikataa au kumwambia nimechoka nilikuwa napokea kipondo kitakatifu.Niliendelea kuishi na Dullah hadi siku moja nilipoiba simu yake na kumpigia kaka Zakaria. Alipokea simu na kuniambia anaishi maeneo ya Ubungo Kibangu.
Nilifurahi sana. Nikapanga kuondoka kwa Dullah kwa kutoroka kwenda maeneo ya Ubungo Kibangu kumtembelea kaka.Siku hiyo Dullah alirudi mapema sana, nikamuandalia chakula na kumwambia nataka nimtafute kaka yangu, aliniambia ninyamaze,kama makazi nimepata hivyo haina gaja ya kumtafuta kaka yangu ,nikawa sina jinsi.
Tulivyomaliza kula nikamuaga Dullah kuwa nataka kwenda kulala, akaniambia sijamuhudumia.Akanivuta kwa nguvu na kuanza kuniingilia kimwili, licha ya hiyo haikumtosha, ghafla akanigeuza na kuanza kuniingilia kinyume na maumbile. Nilipiga kelele lakini aliniziba mdomo,niliishiwa na nguvu aliniingilia mpaka alipojisikia amechoka ndipo aliniacha.
Nilimvizia amelala usingizi nikampekua nikakuta kwenye waleti yake kuna shilingi sitini elfu.Nilizichukua zile hela na kuondoka pale nyumbani kwa Dullah usiku ule ule, nilienda kulala kwenye lodge. Asubuhi nikaanza mchakato wa kumtafuta kaka Zakaria.
Ilikuwa ni asubuhi na mapema ndipo niliingia mtaani kumtafuta kaka yangu.Nilipanda daladala mpaka Ubungo, nikaingia kwenye kibanda cha simu na kumpigia simu kaka yangu. Nikamuelekeza nilipo na akahaidi kuja kunichukua.Nilikaa kama nusu saa, ghafla nikashangaa naitwa kugeuka nyuma nikamuona kaka yangu Zakaria nilibaki nimepigwa na butwaa nikiwa nimeganda mithili ya barafu iliyoko juu ya mlima Kilimanjaro .
Kaka Zakaria alikuwa amebadilika sana, hakuwa yule ambaye nilikuwa ninamjua mimi, alikuwa amekonda na hata rangi yake ya mwili ilikuwa imebadilika.
Tulisalimiana vizuri na akanisaidia kubeba begi langu dogo, safari ya kwenda kwake ikaanza. Kufika nyumbani kwake aliniambia amepanga chumba kimoja,na akasema nitaishi hapo na yeye atakuwa akilala kwa rafiki zake wakati akiangalia ustaarabu mwingine.Basi niliishi hapo, kaka yangu Zakaria alikuwa akija na rafiki zake, na kuniambia nitoke nje kwa sababu ana maongezi na rafiki zake. Walichokuwa wanakifanya humo ndani nilikuwa sikijui.
Nilikaa kwa kaka Zakaria kwa muda wa miezi miwili.
Kulikuwa na dada moja tulikuwa tumemzoeana sana, naye alikuwa amepanga hapo anapokaa kaka Zakaria. Yule dada alikuwa akiitwa Agness. Siku hiyo aliniuliza kama ninajua kazi anayoifanya kaka yangu Zakaria na nikamjibu siijui.Akanieleza kuwa kaka yangu anauza madawa ya kulevya na pia ni mtumiaji mzuri sana wa hayo madawa. Kwa kweli sikuamini kabisa kama kaka yangu anafanya kazi hiyo.Nikapanga kufanya upelelezi wa siri ili nijue kazi anayofanya kaka yangu.
Siku hiyo ilikuwa ni jioni, nikamuuliza kaka Zakaria anafanya kazi gani. Kaka Zakaria alinibadilikia akafura kwa hasira na kuniuliza
"kwani huli chakula?,unavyokaa hapa sikupi matumizi au haki zako za msingi?.Tafadhali usiniulize tena hayo maswari yako yasiyo na kichwa wala miguu".Kaka Zakaria akaondoka akiwa amekasirika sana.Alivyotoka tu nje niliamua kumfuatilia kwa siri anakwenda wapi, alivyokuwa anageuka nyuma nilikuwa ninajificha.Alipanda gari la kuelekea Makoka, na mimi nilichukua boda boda nikamuambia dereva nipo tayari kulipia hela yoyote atakayohitaji alifuatilie gari alilopanda Kaka Zakaria bila ya yeye kujulikana kuwa analifuatilia hilo gari.
Tulilifuatilia hilo gari kwa ustadi mkubwa, Kaka Zakaria alishuka kwenye gari na mimi nikashuka nikamlipa bodaboda akaondoka.Mimi nilikuwa najificha.Nilimuona kaka Zakaria akiingia kwenye kichochoro,na mimi mikawa nimejibanza sehemu nikichungulia. Niliona kundi likiwa limekaa, kuna wengine walikuwa wanajidunga sindano yaani mateja, wamelewa huku wakitiririsha udenda na wengine wakibwia unga,huku wengine wakifunga vifuko vilivyokuwa na unga mweupe.Kwa kweli nilivyoona vile nilishtuka na nikajawa na hofu nikashindwa kuamini.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kaka Zakaria alifika pale akasalimiana na wenzie akawaambia"oyaa dogo leo amenibana eti ananiuliza ninafanya kazi gani kwa kweli nimemuwakia sana,hawezi akanifuatilia kaka yake ninafanya ishu gani"
Akachota unga akabwia nikamsikia teja mmoja akisema, achana naye bwana tuendelee na ya kwetu.Niliyashuhudia hayo yote kwa macho yangu. Nilitoka pale kwa kukimbia nikarudi pale nilipokuwa naishi.Nikamuambia Agnes mimi naondoka pale nyumbani, kaka yangu anafanya biashara ya madawa ya kulevya. Agnes alinionea huruma akanipa elfu thelathini.
Niliondoka pale nyumbani na kwenda kulala stendi ya Ubungo huku hela nikiwa nimezificha jirani na nguo yangu ya ndani,nikiwa nimezifunga kwa ustadi mkubwa maana nilishasikia sifa ya Ubungo. Hivyo nililala salama huku nikitafakuri nitakwenda wapi?.Asubuhi na mapema nilidamka na kuchukua uamuzi wa kurudi kwetu Iringa, hivyo nilipanda basi la upendo na kuanza safari ya kwenda Iringa.
Thomas alishtuka baada ya kuangalia saa akaniambia
"we Anne huna njaa? Mbona umeongea kwa muda mrefu bila kula? Twende tukale kwanza,halafu tutaendelea".Aliongea Thomas na bahati nzuri Thomas alikuwa amepika chakula mpaka cha jioni, tukala chakula halafu nikaendelea kumsimulia.
ITAENDELEA…
0 comments:
Post a Comment