Simulizi : Ndoa Ilivyoteteresha Imani Yangu
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
NILIONA CK NI MWANAUME MWENYE UPENDO KWANGU, NISINGEMUELEZA UKWELI INGENIHARIBIA MAHUSIANO YANGU, HIVYO SASA NILIAMUA KUMUELEZA UKWELI,
Fransis Haki ya Mungu sijawahi kwenda kwa mganga ila ni mama Kely alinishauri na kuniambia nikasafishe nyota, na nikiwa na wewe nivae hiyo pete na nikiwa siko na wewe nisivae.
Fransis alinitazama na kuniambie ndio hiyo pete umeivaa kwa vile uko na mimi?
Ndio nilijibu. Kisha akaniambia Flora mimi siamini uchawi na uchawi hauna kazi kwangu na leo nitakuhakikishia na kukkudhihirishia kwamba waganga ni waongo, na kama ni wa kweli kwa wanaoogopa ila sio kwa wasio ogopa.. mimi namuamini sana Mungu flora.
ALisema hayo huku akiwa kama anahasira lakini anazizuia…
Kisha akaniambie enhe, ni nini uliwahikunifanyia ulichoabiwa na mganga?
Hakuna nilijibu.
Enhe na kuhusu mimba mbona huelezei mama?
Nilianza,, kweli Fransis nilitoa mimba kwa kuogopa tu, lakini sio kwa sababu ya uchawi.
Fransis alinitazama na kutingisha kichwa chake. Na huku akigonga gonga kalamu mezani kwako
Aliniambia Flora huna Mungu wewe, kweli unatoa mimba, sasa uliibeba ya nini? Ningekuea natka mtoto si ningekuwambia? Na hata kama ungeniambia una mimba ningetumia akili yangu ya kiume mptka huyo mtoto umzae na ingewezekana,, ila wewe ni muuaji..
Alisimama kwa hasira na kusema Devil! Wewe ni shetani,,, Aliniuliza funguo zangu za gari ziko wapi? Nilikuwa nimeziweka mezani pamoja na wallet yangu pembeni ya glass ile ya juice, alichukua ile glass na kupigiza ukutani kisha akasema Shit all women are Devil.. Aliniambia sasa ili ujue kwamba siogopi uchawi na uchawi hauna nguvu,, nakuacha na pete yako mkononi,, san asana utanipa hiyo yangu, niliyokupa,, haya vua,, alichukua mkono wangu na kuvua ile pete yake.. kisha akaniambia give me my CAR KEY,,, OPEN THE DOOR GO.. YOU DEVO. .. NILIJARIBU KUUA SUA NA AKANIAMBIA NIMEKUWAMBIA TOKA SHETANI WEWE,, NILIANZAKUMUOMBA MSAMAHA, ALINIZABA KIBAO CHA USONI NA KILINIINGIA HASWA NAKUAMUA KUJIONDOKEA MAANA NISINGEWEZA KUNDELEA KUKAAA,
ALINIAMBIA MAMA KELY NI MWANAMKE MZURI NA ANA ROHO NZURI ALINISHAURI VYEMA,, KUMBE MUMEO ANALEWA KWA AJII YA UCHAWI WAKO ILI UWE NA MIMI.. NA NITAMPA ZAWADI YAKE HII NZURI NA AUTAMUONA KAIVAA SOON.. KWENDA SHETANI WEWE..
NILITOKA NIKILIA SANAKWA UCHUNGU.. SIKUJUA NIENDE WAPI,,, OFCN AMA NYUMBANI AMA WAPI,, NILIJIULIZA NANI ATANISAIDIA? RAFIKI GANI NINAYE?
MARAFIKI WA KANISANI NILISHAWAACHA,, NIKAONA MARAFIKI WENGINE NDIO WA MAANA,, KILINIUMA,, NILIAMUA KWENDA OFCN KUMUONA BIBI KWANI NDIYE ALIKUWA FARAJA YANGU PEKEE.
NILIFIKA NA NILIPOMUONA NILIANGUKA NA KUANZA KULIA MOJA NA KUHISI KUISHIWA NGUVU,, TAYARI NILIKUWA NA LOW PRESSURE,, NILIANZA KUKOSA NGUVU NA KULEGEA.
888888888
BIBI ALNIWASHIA FENI OFCN KWAKE NA ALINIHURUMIA SANA,, ALNIPETI PETI NA KUNIAMBIA COOL DOWN MAMBO YATAKUWA SAWA..
SIKUWA NAONA MAMBO YAKIWA SAWA HATA KIDOGO, CK ALINIDHALILISHA SANA,, NILIUMIA SANA,
ILIKUWA NIMAJIRA YA SAA KUMI NA NUSU, WAFANYAKAZI WENGINE WALIKUWA WAMESHAANZA KUTOKA NA MIMI NA BIBI TULIUWA OFCN,, SARA ALIKUJA NA KUGONGA MLANGO,, KISHA AKASEMA DA FLORA SHIKAMOO NAOMBA USINICHUKIE MIMI NAKUPENDA NA NDIO MAANA NILIUAMBIA ILA UMENIANGUSHA KUNISEMELEA,,,
BIBI ALIMWAMBIA HEMBU TUPISHE KWANZA HUONI MWENZAKO ANAVYOLIA HAPA UNA NINI WEWE BINTI,,, SARA ALITOKA NA KUONDOKA,, KISHA ALIKUJA NA SPEED YA AJABU NA KUTUAMBIA MAMA KELY ANAKUJA.
BIBI ALITUAMBIA TUONDOKE… TULISIMAMA NA KUJIANDAA KUONDOKA.
MARA MAMAKELY ALIWASILI NA KUTUSUBIRI NJE YA GETI LA KAZINI, HAPO HUWA KUNA MGAHAWA NA WATU HUPENDELEA KUKAA HAPO ILI WANYWE CHAI NA KAHAWA MIDA YA JIONI.
ALIPOTUONA ALIANGUA KICHEKO,,,
Hahahahaha! Halaaaa.. hivi wewe Flora nini unawashwa na mimi mwanaizaya wee,, wmanamke usokkuwa na haya wala adabu.. mimi ni wa kutoka na bwana wako,, nakuuliza mimi ni wa kutoka na bwana wako? Hivi unanionaje mimi wee kahaba mzee? Alinisogelea na kunichoma mavidole ya usoni,, kisha pembeni nikasikia watu wakisema mpashe huyo mgeni wa mapenzi.. mshamba huyo…. … anasahaulishwa mume na hawara
HAPO NDIPO NILIJUA KUMBE WATU WALIKUWA WANAJUA.. SIKUJUA BIBI ALIPITIA WAPI,, ILA NILISIKIA BIBI AKIAMBIWA MAMA UNAJIAIBISHA KUWA NA HUYU KAHABA…
NILIPATA AIBU YA MWAKA,,
Kisha akaanza unanizodoa amimi natoka na ck,, ck ni mumeo? Nakuuliza wewe shuwain,,, Fransisi ni bwana wangu mii ama ni bwana wako kikuume nikitoka naye/ kawafuate kina mwenge ambao wanakuchukulia bwana ila sio mimi,, mwanamke huna shukrani nimekufadhili kwa lift siku zile huna lolote leo umepata gari la kuhongwa ndo unajioona umefikaaa… hahaha halaaa,,haya hilo gari liko wapi? Nakuuliza gari liko wapi?
NA UTATEMBELEA VISIGINNO MPAKA VIOTE SUGU,, SHETANI WEE USOKUWA NA HAYA..
Eti unaomba haya omba sasa basi omba…
Alikuja mama mmoja sijui alitoka wapi alimsukuma mama kely na kumwambia hata wewe ni Malaya tu, umejuaje haya yake yote, nani asokujua mama kely wewe Malaya mzoefu,, muache mtoto wa watu,, na huyo mama akaniambia haya na wewe panda taxi hiyo ondoka..
NILIONA YULE MAMA NI KAMA MALAIKA,,, NILIPATA AIBU AMBAYO SIWEZI KUIELEZEA,, NILIMWAMBIA DEREVA TAXI ANIPELEKE KWA BIBI KWANI NILIOGOPA HATA KWENDA NYUMBANI,, NLIJUA MUME ATAZIPATA HABARI HIZO,, DEREVA ALINIPELEKA KWA BIBI NIKIWA SIFAI KWA KILIO NA KWIKI,, NILITAMANI KUFA,, NILITAMANI ARIDHI IPASUKE NIINGIE NDANI,, NILIUMIA KULIKO SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
888888
MAMA NISAIDIE NIFANYE NINI NISAIDIA MAMAYANGU,
BIBI ALINITAZAMA NA KUNIAMBIA NIKUSAIDIE NINI MWANANGU? NIKIPI CHA KUKUSAIDIA SASA HIVI/
UMESHACHELEWA MWANANGU MGUU UMEOTA TENDE HUO,, TUFANYEJE SASA?
SANA SANA NITAKUSHAURI UWE TU MPOLE MAANA SASA HIVI MUMEO AKIPATA HIZI HABARI HUNA NDOA,,, NA MIMI HATA NIKIJIDANI KUKUSAIDIA NITAKUWA NAKUDANGANYA MAANA MARAFIKI ZAO WANAOKUJUA FIKA WANAHABARI ZAKO ZOTE, MWISHO WA SIKU NITAONEKANA MWANAMKE MPUMBAVU KAMA WEWE MWANANGU,, NIKUSHAURI WEWE UTULIE NA KUKUBALIANA NA MATOKEEO,, HIVI LAKINI FLORA NI SHETANI GANI ALIKUINGIA MWANANGU? AGH? BIBI ALIKARIKIRAK GHAFLA NA KUSEMA SASA AUMEMTUKANISHA MAMA YAKO MASKINI, ATOONEKANA TABIA ZAKO UMEZITOA KWAKE KUMBE MASKINI WALA HAJUI ULIPO NA UNACHOFANYA.
BIBIALIONGEA KWA UCHUNGU KISHA AKANIAMBIA SASA HIVI AFYA YAKO SIYO NZURI HATA KIDOGO,,, SIONI SABABU YA WEWE KUSUMBUKA TENA, HEMBU TULIA USIJE KUFA NA KIHORO MAMA. TULIA KABISA JIFANYE HAMNAZO MAMBO HAYA YATAPITA,, MBONA MENGI YAMEPITA,, NA HILI MAMA LITAPITA, ILA NDO UTULIE SASA.
BIBI ALINIFARIJI KIDOGO,,KISHA AKANISINDIKIZA MPAKA NYUMBANI NA KUNIACHA,, NILIINGIA NDANI NA KUAMUULIZA DADA KAMA BABA ALIKUJA, DADA ALINIAMBAI BABA HAJARUDI BADO,, NILIINGIA BAFFUNI NA KUOGA,, KISHA NIKAJITUPIA KITANDANI,, NILIKUWA NAUMWA SANA KICHWA NA KUJISIKIA DHAIFU..
NILIKUWA NIMEAMUA LIWALO NA LIWE KAMA NI MUME KUNIKUTA NA KUNIPIGA ACHA ANIPIGE NIFIE NDANI KWAKE ILA NILSEMA SITAONDOKA KABLA YA KUJUA LOLOTE TOKA KWA MUME.
NILIKUMBUKA WNAWAKE WA KANISANI, NILIKUMBUKA NILIVYOPENDWA N A KUPEWA HESHIMA,, NILIUMA SANA, NILIJIONA SIFAI KABISA NA KUTAMANI HATA SIJUI KUJIUA.. NILIANZA KUPATA PICHA NIEMEKUFA NA WANAANGU WANAVYOLIA, KISHA NIKASEMA SITAJIUA ACHA DUNIA INICHEKE LAKINI SIJUUI NG’O.
NILIAMKA NA KUANZA KUANGALIA JIKONI KAMA DADA KAPIKA VYEMA… KISHA NILIONA CHAKULA KIZURI, NILIKAA SEBULENI NIKITAFAKARI PICHA NZIMA YA SIKU HIYO,, KUANZIA KWENYE GIVE ME MY CAR KEY NA GO YOU DEVIL… NILIUMA NILIONA YOTE YAMENISTAHILI,, NILIMKUMBUKA MAMA KELY NA KUAPIZA KULIPIZA KISASI NILIJIULIZA KISASIKIPI KINAFAA?
NILISEMA AIZA NIKAPIGANE NAYE,, AMA LA NITOKE NA BWANA WAKE NA YEYE AUJUE KAMA KUFA ACHA NIFE LAKINI NITALIPIZA KISASI.
MUME ALIREJEA NANILIJIKAUSHA KAMA SIO MIMI, NILITAKA KUMSIKIA KASIKIA NINI?
SIJUI ILIKUWAJE AMA HAKUSIKIA AMA ALISIKIA NA KUJIKAUSHA LAKINI HAKUNISEMESHA LOLOTE LILE, ALILALA TU, NA ASBH PALIKUCHA ILI NIENDE KAZINI.
NILIJIANDAA NA KUDANDIA DALA DALA, MAMA KELY ALINIPITA NA GARI NA KUACHIA CHEKO,, KIINIKERA NA HASIRA ILINIPANDA NA KUSEMA MOYONI NITAMUUA.
NILIFIKA OFCN NA NILISHANGAA SANA KUKUTA BOSS AKINISUBIRI.
NILIITWA OFCN KWA BOSS AKIWEPO BOSS, CHIEF ACCOUNTANT NA MENEJA UAJIRI NA BIBI. WOTE WALIKUWA WNANISUBIRI.. ROHO YANGU ILINIPASUKA PWAAAA…
NISIJUE NI NINI NIMEITIWA,
Je ni nini Flora kaitiwa? Tutaona katika muendelezo huu wa kisa hiki cha ukweli kabisa lakini cha kutufndisha sana sisi wengine.
Usikose kufuatilia hapa hapa…
88888
MOYO ULINISHTUKA. HARAKA NILIJUA KOSA LANGU NI KUSHUTUMIWA KUTUKANANA HADHARANI. KWANI MARA ZOTE UKIITWA NA WATU HAO BASI NI KUPEWA ONYO KALI. NILIINGIA NDANI NA KUKAA KWENYE ROUND TABLE. ALIANZA KUZUNGUMZA BOSS NA KUNIAMBIA.
Flora kuma shutuma nzito sana zinakuhusu wewe. Sijui kimetokea nini hadi mama kuwa katika hali hii lakini shutuma hizo zinakuhusu moja kwa moja.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alidakia mhasibu mkuu na kusema..
Boss naona tusipoteze muda kwani ni dhahiri analigahamu hili.
Nikiwa katika kutafakari … muajiri alisema..
Flora kukosa nidhamu kazini ni kosa kubwa sana. Na ni kuaibisha shirika letu. Hivyo haitakuwa na sababu ya kujadili jambo lililoko mbele ila ni kupokea adhabu yako ambayo ni aiza… kusimamishwa kazi kwa muda ama kugukuzwa kabisa kwani kosa ni kubwa sana na la aibu.
Bibi aliitizama na kuniambia…Flora kufukuzwa kazi wewe mimi sinhependelea. Na hakuna umachohitaji wewe kujieleza isipokuwa tu kuomba msamaha. Ama una lolote uwezalo kusema?Nilushauri mwanangu..Tekla atakapokuja hapa uwe mkweli. Muombe msamaha yaishe. Kwani anavyo vizibiti vyote. Na atakapoamua kufikisha jambo hili kwa mumeo ni hatari.Tecla akiingia jishushe na uwe mpole sana.
Moyo ulinilipuka niliposikia Tecla. Nilijiuliza tecla ni nani?Na maralango uligongwa na aliingia msichana mrembo ambaye sijawahi kumuona popote. Nilianza kusikia kiu na Bibi aloniambia usiogope. Huyu ndo teclA
8888
Boss alisema karibu Tecla. Karibu sana. Tecla alisogeza kiti na kuketi. Ni msichana mdogo sana kwangu. Naweza kumzidi miaka 6 mpaka 8 hivi. ALIWASALIMIA WOTE KWA MIKONO kasoro mimi. Kisha aliambiwa je huyu ndiye uliyekuja kumshtakia? Binti huyo aliitika ndio haswaa ndo huyu mwanamke mshenzi..
Hapana binti usitumie lugha chafu. Jaribu kuzuia jazba.
Kisha boss alinitazama na kuniuliza unamfahamu binti huyu?
Hapana nilijibu.
Boss aliniangalia na kusema huyu anaitwa Tecla. Alikuja kushtakia kwamba una mahusiano na mchumba wake ili hali wewe una ndoa na akashangaa kwa nini ufanye hivyo?
Sijui nini kilitokea nikaanza kujieleza…
Mimi Fransis hakuniambia ama mchumba..
Binti yule aligonga meza na kusema shit! Fuck you ana shame on you. Huoni haya kusema hakukuambia ana mchumba!una laana mama ama?wewe si mke wa mtu wewe ?
Tecla alisimama kama mwenye hasira sana. Akili yangu ilimivurugika. Mambo yamekuwa mengi. Kazi lazima sina. Sasa nasikiliza nini na kukitetea nini?nilisema endapo huyo binti atanigusa nitamalizia hasira zangu hapo na liwalo na liwe kama kuaibika nimeshaaibika vilivyo.
Nilimwambia binti usinikaripie ongea pole pole.
Aliendelea kung’aka..
Kisha akatulizwa.
Na boss kunigeukia na kunieleza…
88888
Flora hembu tulia kwanza. Tunataka kufanya suluhu. Vingimevyo tusingewaita hapa.
Tecla hebu eleza tumalize mambo haya.
Tecla alianza.
Fransis ni mchumba wangu na ananisesha urusi. Ananilipia ada yeye na kila kitu. Huu ni mwaka wa tatu wa masomo yangu. Na huwa ninawadiliana naye kama mke na mume kwani hata wazazi wanalifahamu hilo.
Hapo nyuma nilipata taarifa za mahusiano ya flora na fransis. Kilimiuma sana. Na ndipo nikapanga kuja bila kumjulisha Fransis ili niweze kufumania na kama uchumba kufa ufe kwani nilielezwa kila kitu kuhusu mwanamke huyu na mambo amfanyayo na mcbumba wangu. Nashangaa anawezaje kufanya hivi ili hali ana mume.
Hivi wewe mwanamke huna hata aibu jamani?
Muajiri alimuuliza tecla umemaliza?tecla alisema siwezi kumaliza kirahisi. Nimeingia gharama ambazo ni kubwa sana. Ticket ya ndege na hotel niliyolala. Lakini pia nimepoteza muda wangu kuja kulihakiki hili. Ninachotaka ni gharama zangu yaishe. Sinaninachotaka kwake zaidi ya ticket ya ndege nirudi chuoni.
Kila mmoja alionekana kushangazwa na madai ya tecla.
Boss alimuambia lakini unaminije watu waliokuambia?swala la sisi kukubali une hapa ni kuweka mambo sawa na sio kulipishana.
Tecla alicheka kwa kejeli na kusema.
Mh.. ha ha ha… hamnijui bila shaka. Sijashindwa kwenda hata polisi. Ninao ushahidi. Ama sijashindwa kwenda kwa mumewe. Ninatumia tu busara mpaka sasa kwani najua ninyi no waajiri wake mnaweza ku mdispline.
Haya niambieni mnataka nini?
Kwanza mapoteza muda tu hapa.
Niliwaza sana nifanye nini sasa?.. nikiwa katika kuwaza… Tecla alitoa mfuko wa malboro chini ya meza na kunipiga nao na kusema mshenzi wewe… nini hiii….. nini hii unajidai kununulia wachumba za watu nguo…
888888
Mfuko ule ulikuwa na ile kadi niliyoanfika… keki iliyorojeka chupa ya champagne na shati na suruali. Alikasirika sana akasema….. huku akimuangalia boss wangu..
Haya abishe sasa… nasema huyu mwanamke hajitambui…
Kisha tecla aliendelea kuzungumza…
Baada ya kupewa taarifa za flora na fransis na walionipenda niliamua kuja kwa siri. Lakini sikutala mpenzi wangu ajue kwamba ninakuja kumfumania kwani nilishaelezwa kila kiti juu yao mpaka flora kuishi mule ndani. Kitu nilivhojiuliza kwa nini huyu mwanamke aishi kwa mchumba ili hali ama mume? Hapo nilipoambiwa anaishi ndipo nilisema lazima nije. Yamkini sio mke wa mtu na huenda fransis anataka kuoa. Na ndio maana nikaja.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilifika kwa siri sana bila yeyote kutambua. Nilijua kama ni wapenzi laxima watajivinjari siku ya kuzaliwa kwa fransis na ndio maana nikaja siku hiyo ili kumsuprise fransis. Na isimgekuwa na maswali.
Nilifika mapema sana. Na kwa bahati nilichelewa kidogo tu. Ningewahi lazima ningekutana na huyu mmbwa.. Tecla alininyoshea mkono kwa dharau alinetua midomo yale aliposema huyi mmbwa…
Kisha alaendelea kwa jazba kuongea…
Nilipofika tu uwanjani nilichukua taxii na kukimbia hadi nyumbani na kukuta gari haipo. Nikajua hawako. Nikaenda ofcn kwani niliam iwa huwa hukaa huko. Nilikuta gari huko na sasa niliamua kufanya fanizi kwani ilikuwa ni usiku.
Nilipofika niliona kuna purukushani na hili limwanamke liliondoka kwa kasi na gari yake akakimbia akiwa kajifunga funga maushungi.
Ofcn walikuwa wakifanya mapenzi.
Mh…Aliposema maushungi nikajua tu huyo ni mama kely
.. sikutaka kujitetea kwani hakuna ambaye angeamini…
Aliendelea..
Baada ya hapo mimi na mpenzi tulielekea nyumbani. Nilikuwa na hasira sana. Na nilipofika ndipo nikaona hizi zawadi zake.
Sasa bado unabisha?
Nikiachana ma fransis nitaonekana mimi mbaya kwani ananisomesha… lakini flora umetia doa na domda mahusiano yangu. Heri ungekuwa msichana.. mke wa mtu.. loooo?
Kisha alianza kulia.
Bibi alinitazama.. kisha akasema…
Tumesikia yote tecla.
Maji yameshamwagika… hapa unahitaji kutoa msamaha tu basi.
Tecla alisema nitakacho ni nauli yangu basi. Mimi sina shida naye.
Nimeumia bya kutosha. Ni mfanyakazi wenu naomba nauli tu basi.
Aliulizwa ni bei gani akasema ni laki nane. Kwa wakati huo.
Mimi mshahara wangu ulikuwa ni laki mbili kwa mwezi.
Mh..
Mhasibu mkuu alisema haya flora sema tumpe?
Dah… nilikuwa naumia…
Bibi alisema flora kubali yaishe. Muombe msamaha yaishe.
Dah… nilijitosa kimaso maso.
Sikuwa na la kufanya.
Nilisogeza kiti. Nilienda mpaka alipo binti yule.
Nilipiga magoti chini na kumuomba msamaha.
Aliniambia simama yameisha.
Kisha alianfikiwa cheki yake na akaondoka.
Na kikao kikaisha.
Nilikuwa na mawazo tu.
Baada ya muda wa kazi kwisha nilipewa barua.
Nilienda kuifungulia chooni.
Barua ya lunisimamisha kazi mpaka watakapoamua kuniita.
Dah…. nililia chooni sana.
Nilitoka na kurlekea nyumbani.
Moyo wangu ukiwa na majeraha mengj ya kujitakia.
Moyo mzito sana. Unauma sana.
Nilijitupa kitandani na kulia sana.
Nikijiuliza je Deus analifahamu hili?akilifahamu itakuwaje?
Kisasi kikazidi kukomaa.
Nikawa napanga kisasi cha malipizi ya haja. Na kuyatekeleza mapema sana.
Hivi ndivyo niliamua na nikawa nasubiri pakuche NitEkeleze nilichopanga.
88888
Mume alikuja. Maisha yetu yalikuwa ya kupuuzana. Tuliishi mradi salama.
Nilisema hivi haya mume hayajui ama?ni kweli ama?kama mama yake anajua ina maana mume hajui?nilijiuliza sana. Ilikuwa ni saa nne usiku. Nilisema ngoja nimueleze kuhusu kusimamishwa kazi.
Nilimpatia barua akasoma. Kisha akasema pole. Na akalala. Hakuongea sana.
Mh.. nilijiuliza kulikoni?
Asbh aliondoka. Nilimuomba pesa kidogo ya nauli.
Aligeuka na kuniambia.nauli ya nini.?gari iko wapi?
Na fransis je hawezi kukupa pesa?
Usione nimenyamaza Flora… naogopa lawama kwa wazazi wako…. naogopa laana ya mama yako nikikutaliki. Ishi utakavyo naishi nitakavyo. Kama kuondoka ondoka wewe.aibu uliyonipa inatosha
Usitake nifanya maajabu nikafungwa maisha.
Najua kila lako wewe shetani. Tena niache.
Deusi machozi yalimdondoka na akaondoka.
Mh…. nilijiuliza kumbe anajua kanyamaza?
Looo.. nifanyeje sasa? Nikahisi akirudi usiku nauwawa. Nikaanza kifungasha kila kilicho changu na kutoa kidogo dogo. Na kupeleka kwa bibi mpaka nikamaliza mizigo yooote.
8888
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
NILIKUWA NIMESHAFUNGASHA KILA KITU CHANGU. NILIWACHUKUA WATOTO NA MSICHANA WANGU WA KAZI. NILIENDA KWA BIBI. FUNGUO TULIZIACHA KWA JIRANI. NILIONA NI LAZIMA NAAMUE MAMBO MENGINE ILI MAISHA YAENDELEE. NI KAMA NILIKUWA NIMECHAMGANYIKIWA SANA. TULIFIKA KWA BIBI NA KUPUMZIKA HUKO. BIBI ALIKUJA NA NILIMUELEZA AZMA YANGU. NA LWA NINI NIMEAMUA KUONDOKA LIWALO NA LIWE. ALINIAMBIA KWA VILE MUME ANAJUA NI HATARI VINGINEVYO WAZAZI WAKAE KUSULUHISHA.
ALINIULIZA UMAENDA WAPI?NILIMUELEZA NASAFIRI MKOANI KWA KAKA YANGU. NILIMPENDA SANA KAKA YANGU. JAPO SIKUWAHI KUMSHIRIKISHA LOLOTE LILE LAKINI NILPENDA SANA.
BIBI ALONITAKIA SAFARI NJEMA NA NILIENDA KWA KAKA.
KARIBU NJIANI KUFIKA KWA KAKA MACHOZI YALINITOKA MENGI. NILILIA SANA. WOTE KWENYE BASI WALIJUA NIMEFIWA.
NILIFIKA KWA KAKA WIFI AKANIPOKEA. SIKUWEZA KUMUELEZA CHOCHOTE. NILINYAMAZA.
JIONI KAKA ALIFIKA NA KUNIONA. ALIJUA NINA MAWAZO TELE. NILIMUELEZA KILA KITU PEKE YAKE. MWANZO MPAKA MWISHO. NA KILA KILICHOTOKEA.
KAKA ALINIHURUMIA.
ALIMUITA MKEWE NA TUKAWA NA KIKAO CHA PAMOJA.
MKE WA KAKA mama dina alisema hivi….
Flora pole na kwa kila jambo. Imeshatokea. Huwezi kubadilisha kitu. Ila lazima uanze maisha mapya. Isipokuwa tukikaa na wewe bila kuwapa taarifa wazazi kwamba uko hapa haitaleta picha nzuri. TutawaeleA wazazi wa pande zote uko hapa. Na utakaa hapa. Mpaka akili yako iwe nzuri. Wewe kwa sasa sio wa kawaida. Kichwa chako kimelemewa na mambo mengi. Tulia flora. Tutakusaidia.
Mama dina alichukua upande wa kanga na kufuta machozi na kupenga makamasi. Kisha alimtazama kaka yangu na kumwambia Baba dina wewe unaonaje ushauri wangu?
Kaka alimtazama Mkewe na kusema umenena vyema mke wangu. Asante sana kuliona hilo.
Mama dina alisimama na kwenda kumiandalia mahali pa kulala. Aliwachukua wanangu na kuwaogesha mwenyewe. Na kisha kutuita mezani kwa chakula.
Tulikula. Walifanya sala na kisha kusoma neno na tulienda kulala. Nilisikia lidogo ka ahueni.
88888
ASBH HABARI ZILIFIKA KOTE JUU YA JAMBO LANGU. WAZAZI WA DEUSI WALIFIKA WA KWANZA. KISHA BABA YANGU NAYE ALIFIKA. WADHAMINI NAO WALIFIKA. WALIFIKA WAMECHOKA. NILIPOWAONA MOYO ULILIPUKA SANA.
Mama Dina alinifuata na kusema Usijali flora. Usijali
Makosa yameshatokea. Kukulaumu sio suluhu. Ila kukuonya na kukufungua ndiyo suluhu.
Nililia na kumwambia hivi nitafanyaje?
Mama dina aliniambia usijali. Niko kwa ajili yako.
Aliniambia kaa tulia wala usichoshe akili yako hata kidogo. Relax mamii. Uko mahali salama. Wakikuambia kujieleza wewe sema tu UMEONDOKA KWA KUONA HAKUNA MAELEWANO KWENYE NDOA YAKO. ALAFU KUANZIA HAPO TUTAONA KAMA KUNA SABABU YA KUELEZA HAYO MENGINE.
Nilifarijika sana. Nilimpenda sana wifi yangu. Sikuwahi kumuwazia ana roho nzuri hivi. Aliniambia valia vizuri kikao kitaanza punde.
KISHA ALIKUJA KUNIITA NA KUNIAMBIA KIKAO KINAANZA.
WAKATI HUO DEUS HAKUWA KAFIKA.
kIkao walikianza kwa sala.
Kisha akaanza kuongea kaka yangu. Alisema hivi.
NIMEWAITA HAPA KWA JAMBO LILILOPO MBELE YETU. FLORA KAJA KASEMA KAAMUA KUONDOKA KWAKE KWA SABABU AMBAZO ATAZIELEZA MWENYEWE NINI KIMEMUONDOA.
Kisha kaka akanigeukia na kuniambia eleza nini kimekuondoa kwako.
Mh… ilikuwa ni kazi ngumu kuanza.
Nilisita kidogo.
Kisha wifi akanitazama na kusema elwza tu usiogope. Hakuna siri.
SIJUI NILITOA WAPI UJASIRI KISHA NIKASEMA Nimeondoka kwa kuona hakuna maelewano kwenye ndoa yangu. Baada ya kumaliza kusema.. kaka alisema kuna mwenye swali ama nyongeza?
88888
Baba mkwe aliuliza ni kukosekana kwa maelewano gani?
Kisha nikasema mume ananipuuza. Hanijali ananipiga na kutonisikiliza.
Baba mkwe akauliza je uliwahi kusema popote hayo?
Nilisema ndo ninasema sasa.
Baba mkwe akauliza kwa nini ukimbilie huku na usikimbilie kwangu ama kwa wadhamini?
Hapo nilikosa jibu nikawa nimenyamaza. Kisha mama mkwe akadaikia Ni ametudharau.
Ana dharau sana huyu.
Wifi yangu alimkatiza na kumwambia mama tafadhali usikasirike. Zamu yako itafika utamhoji wala usijali.
Wakati huo deus aliwasili. Kisha akaingia na kuketi.
Baada ya dakika kazaa aliambiwa tunaomba kwanza ukae nje kisha tutakuita.
Deusi alitii na kutoka nje.
Baada ya hapo aliulizwa mwingine je kuna mwenye swali?na hutakiwi kumuuliza swali lililokwishwa kuulizwa. Maana majibu tayari.
Mama mkwe alisema kwa nini hakuja kwetu na kakimbilia kwako? Ina maana hatuamini ama ni anaficha madhambi yake?CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Palitokea kutoelewana na ndipo mama mkwe akaambiwa nyamaza.
Kisha nilatakiwa kujibu kwa kaka kirudia swali.
Nilishindwa kuwa na jibu ila nikasema sikujua kama utaratibu ni kwenda lwa wakwe ama wapi.
Mama mkwe aliguna… mh….
Kisha ikafikia wakati wa Baba kuzungumza.
Baba hakuwa na maneno mengi. Alisema tu mimi naomba swali langu ni hili.
Pamoja na wewe kuamua kuka kushtaki je unataka nini haswa?
Tukigundua una kosa ama huna osa nini unahitaji ili isiwe tunakaa hapa kuzungumza na mtu ambaye Mwisho wa jambo anaujua. Je unahitaji nini haswa?
NILISHTUKA KIDOGO KWA SWALI ZITO.
Na nilipoanza kuongea aliniambia…
Kile unachokitaka ndicho kitatufanya tuendelee kukuhoji ama tuache. Emhe….
Dah… nikawaza.. je nikisema nataka kurudi kwenye ndoa itakuwaje?je nikisema sitaki itakuwaje?
Nilikosa jibu.
Baba alisema mimi nimeshauliza. Kama kuna mwenye swali aendelee.
Dah. Mdhamink wa kiume alisema swali la baba lijibiwe kwanza ndipo aendelee.
Nilishindwa kuwa na maamuzi. Nikakosa jibu.
Kisha mdhamini wa kike akasema Unampenda mumeo ama humpendi?
Haraka nilijibu nampenda. Sikuona sababu ya kuchelewa kujibu hilo. Kisha mdhamini wa kike akasema baba jibu lako limekibiwa. Kasema anampenda mumewe. Bila shaka hapa anahitaji usuluhisho ili warudiane. Kwa maana hiyo anataka ndoa yake.
Kila mmoja alisema ahaaaa. Safi sana.
NILISHANGAA KWA NAMNA AMBAVYO KESI HIYO ILIKUWA IKIENDESHWA. KWA UTAALAMU WA HALI YA JUU.
Mama mkwe alionekana kukasirika sana. Lakini aliambiwa mama usiulize lolote mpaka tukupe nafasi.
Ulushamaliza kuuliza.
Kisha waliniambia haya waweza kwenda na wakamuita Deusi.
Nikiwa chumbani nilisogea karibu kabisa na mlango ili nisikie kila kitu.
888888
Deus aliingia. Alionekana kuchoka sana. Alivaa nguo mbaya sana. Alionekana kuwa na hang over na alikuwa akitafuna bublish na chupa ya maji.
Baba yake alimwambia tema unachokula. Alitema na kutupa nje.
Kisha kabla hajaanza kujieleza baba yake alidakia mpumbavu sana wewe funga zipu yako hiyo…
Deus alifunga zipu yake iliyokuwa iko wazi na kufanya nguo yake ya ndani ionekane.
Kisha kaka alimtazama Deus na akatabasamu.
Na kumwambia Deus… hapa utajibu maswali ya kila mmoja. Unachotakiwa kufanya ni kuwa mpole na mtilivu tu. Kuwa huru kusema lolote maana sisi wote no wana familia. Aibu yenu ni aibu yetu. Ila mkieleA ukweli tutawasaidia sana na kuficha aibu.
Deus aliitika na kusema sawa bro. Alimuita kaka yangu bro siku zote.
Kisha kaka akasema haya mwenye swali?
Wifi yangu aliuliza.
Mkeo alikuka hapa akidai kwamba nyumbani hakuna maelewano. Je alikuaga anakuja huku?
Deus alianza. .. hapana hakuniaga.
Kisha wifibakamuuliza tena.. kama hakukuaga na ulipogundua hayupo ulitoa taarifa wapi kumuulizia?Deus alicheka kwa kejeli na kusema sikumuilizia maana nilijua kaenda kwa hawara yake Fransis.
NILIWA CHUMBANI MOYO UKIFANYA PWAAAAAAA….
Na ndipo sasa mdhamini wabkiume akauliza fransis ni nani?
Deus akajibu ni hawara yake.
Tena huyu mwanamke kanikera sana. Amenidhalilisha sana.. ni aibu ya mwaka kaniachia.
Kaka alimnyamazisha na kumwambia jibu tu swali. Usikasirike. Tunaelewa. Ukishasema ni Hawara yake tunaelewa ni Aibu ya namna gani tumepata wote. Na sio wewe peke yako.
Baba yangu alionekana kuchoka na akawa kama anataka kutoka nje.
Kaka alimwambia hsitoke mzee.
Mafanikio yao tuliyafurahia. Acha na hii aibu tuibebe. Yamkini tukajua tatixo lilipo tuwaokoe hawa.
Mama mkwe alidakia na kusema muache aseme. Usimkatize.. usimkate kauli muache aseme.
Kaka alimwambia mama mkwe.. mama akishasema hawara nini kimefichika hapo? Acha tuokoe muda.
Kisha akatakiwa mwingine aseme.
Mama yake akapokea na kusema… Kwa nini unakubali kuishi na mwanamke kahaba?kwa nini?
Mdhamini wa kike aliangusha mavho yake chini.. kisha deus akasema mama niache. Unanichanganya. Wewe mwenyewe uliniambia habari za flora nikakuambia acha nizifanyie kazi. Sasa ulitaka nifanyeje?
Mama mkwe alinyamaza kidogo.. kisha baba mkwe akamgeukia mkewe na kusema Uliyajua haya?Aibu gani hii sasa?
Kaka aliwaambia Baba una swali?baba mkwe aliuliza huyo fransis ni nani?kwa nini ujue na unyamaze?wewe ni mwwnaume kweli?mzembe wewe… Deus alidakia na kusema mimi sikujua haya baba. Mama ndiye alinieleza. Na sikuweza luwashika wala kuona. Mpaka rafiki yake Flora alipokuja kunieleza habari ya flora na fransis nakununuliwa gari. Bite alinieleza kwa uhakika. Ila sikujua na sikuona na ndo maana sikuachana na mke wangu.
Dah.. mdhamini wa kiume alikuna kichwa kisha akasema..Deus je kuna lolote ambalo unaweza kumshtakia mkeo hapa licha ya swala la fransis?
Ndio mengi sana.
Flora kabafilika sana. Anavaa uchi. Anakunywa pombe. Hanisikii. Hakai nyumbani na ana marafiki wa kishenzi. Kuna li mwanamke hapo mtaani linaitwa mama kely ndo shoga yake mkuu.
Mdhamini wa kike aliguna na kusema ba amuuulize Deus swali kisha nitauliza.
BABA YANGU MZAZI ALIULIZA SWALI LILE LILE ALILONIULIZA.
Je nini muafaka wa kikao hichi? Haijalishi mmmekoeseana kwa kiwango kikubwa namna hiyo. Je nini unqchokihitaji?CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Deusobalijibu kwa hasira… Sitaki mwwnamke malaya. Simtaki mwanao baba.
BABA YANGU aliangalia chini.. na kama alilia.
Mama mkwe alisema… usije mlaani mwanangi mzee… unalia nini sasa?
Kaka alisema jamani kila mmoja atumie nafasi yake.
Kisha baba mkwe akasema… mzee mwenzangu aibu sio yako. Aibu ni yangu. Mwanaume akishindwa kuwa rijali mwanamke anamkimbia. Hii ndiyo maana yake. Sio wewe wa kulia. Wa kulia ni mimi. Kisha baba mkwe naye machozi yakamtoka.
Na kaka akasema sasa mkilia nini maana yake?ninyi ni wazee wa hekima ma busara. Mkilia nyie sisi tufanyeje?
Kaka alimueleza mdhamini wa kike je unalo swali tumalize?
Mdhamini wa kike alimuuliza Deus.. je umewahi kuwa na mahusiano na mwanamke yeyoye mkeo akajua na kukuliza?
Ndio… mwennge ni alikuwa mpenzi wangu. Na bite pia. Bite alinieleza mambo ya flora nilampenda. Na bite nitamuoa. Ana mimba yangu. Hilo mlielewe kabisa. Sitaki vikao mara ingine. Kama hajui ajue sasa.
DAH… NILIPATA BARIDI HUKO NDANI. kisha kaka akasema haya tumemaliza.
Mtuache kidogo tujadili tuwarudie.
Wazee walianza kutoka nje na kuongea. Kisha wakapewa chai na kunywa. Na kisha wakaitwa tena. Nikiwa bado chumbani tumbo likinikata. Deus alitoka na kwenda kukaa kwa gari lake.
Kisha wazee wakarudi kukaa tena.
888888
NIKIWA CHUMBANI NILIENDELEA KUSIKILIZA KWA MAKINI WANACHOKIJADILI. NDOA NILIITAMANI SASA. LAKINI NARUDIJE?DEUSI ATANIAMINI TENA?NILIWAZA. NILITAMANI MAMA DINA AJE KWA DAKIKA CHACHE TUZUMGUMZE.
Kisha waliendelea na kikao.
Kaka alisema.
JAMANI TUMEWASIKIA WOTE. AIBU TUMEPATA WOTE. WOTE WAMEKOSEA. JE MNATAKA TUFANYEJE?TUWASHAURI KURUDIANA AMA KUACHANA?NA KAMA TULIWASHAURI KURUDIANA TITAKUWA TAUARI KUWASAIDIA MA KUWAKUMBATIA KWA UPENDO BILA KUWASUMANGA MANKUWAKOSOA KILA LEO?
NA KAMA TULIWASHAURI KUACHANA TUKO TAYARI KUPOKEA FAMILIA NYINGINE YA FLORA AMA DEUS?
kaka yangu aliuliza swali zito. Aliongea kwa hekima ya hali ya juu kisha akasema kila mmoja aongee jambo lake.
BABA MKWE ALIANZA;
wote wamekosea. Ni lazima tufikirie tuwaganyeje. Kama deus akiwa hamtaki flora kulazimisha ni kumkandamiza flora. Lakini kama flora hataki kumlazimisha ni kumkandamiza deus. Wataumizana huko ndani sisi tukiwa na amani. Tuwaulize watakacho. Ila tusilazimishe.
Kisha Mama mkwe akasema;
Mimi naona tuwaonye wote. Na kila mmoja aombe msamaha. Warudiane.
MDHAMINI WA KIKE AKASEMA;
mimi naona tuwakutanishe. Tusijadili makosa yao wawapo pamoja ila tuwaulize kama wanaweza kuishi pamoja.
MDHAMINI WA KIUME AKASEMA;
Dhumuni la kikao hiki ni kuwapatanisha. Ni lazima sisi kama kikao tuwape masharti yetu tumeamua nini. Kwani najua wanaweza kataana. Lakini kwa msimamo wetu wakasaidika.
BABA MZAZI AKASEMA;
Mimi naona kwa vile wana hasira wote wawili. Flora arudi kwa wakwe zake. Akakae pale. Na kama miezi sita itaisha bila mume kumhitaji kwa upendo basi tuchukue hatua zingine. Ila akae pale kwa wakwe wakimuangalia tabia zake na kumuonya. Na Deus akiona wazazi mnamhitaji flora anaqeza kurejeza nafsi. Ila la basi tutakaa tena.
WIFI AKASEMA;
Baba hapana. Asikae kwa wakwe…
Kisha Kaka akadakia na kumwambia mkewe… usipinge hoja ya mwingine ula toa hoja yako mama Dina.
Ma dina aliachia tabasamu na kila mmoja akacheka.
Kisha yeye akasema tena;
MIMI NAONA FLORA NA MUMEWE WAPATANISHWE LEO LEO MA WARUDI KWAO. TUKIANZA KUWAVUTIA MUDA NA KUWAPA NAFASI WANAZIDI KUKARIBISHA MAADUI.
Kaka aliwaambia sasa naona ni wakati muafaka kuwaita wote na kuwadukiliza nink watakacho.
Walimaliza hivyo na tukaitwa.
8888
Tuliitwa wote. Kisha baba mkwe akaanza kwa kuongea.
WANANGU MMETUAIBISHA SANA. WOTE WAWILI. NA MMETUSONONESHA SANA. KWANZANAPASWA KUTUOMBA RADHI KWA AIBU YENU HII KUBWA. NA KILA MOJA APIGE MAGOTI AOMBE MSAMAHA. ILA KAMA UNAONA HUJAKOSEA ACHA USIOMBE MSAMAHA.
Dah..Baba alimaliza.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilianza luomba msamaha kwa kupiga magoti. Niliona jinsi nimeaibisha vichwa vya mvi. Niliamza kwa baba mkwe.. kisha baba.. kisha mama mkwe… kisha wadhamini na kwa kaka na wifi. Tena nikilia ma kutembea kwa magoti.Wifi alinikumbatia na kusema Umepona. Msamaha ni dawa tosha.
Baada ya kumaliza Deus naye aliomba msamaha hivyo hivyo. Ila kwa kusimama tu na kushika kila mmoja mkono.
Kisha baba akasema nitaongea badae. Mwenye neno aseme.
Kimya kilitawala kisha kaka akasema hivi;
DEUS NA FLORA. NDOA YENU MNAIVUNJA WENYEWE. NA MTADAIWA. HAO KINA FRANSIS SIJUI MWENGE SIJUI BITE MMEWARUHUSU NINYI WENYEWE. SASA HAO SISI HATUNA NENO NAO
NA SIO WABOMOAJI WA NDOA YENU NA WALA MSIWASINGIZIE. ALICHOKIUNGANISHA MUNGU MWANADAMU ASIKITENGANISHE. SASA MTUAMBIE HAPA JE MNATAKA KUYENGENISHA NDOA YENU AMA MNATAKA NINI?
Kaka alimaliza kuongea kisha wakatusikiliza. Kila mmoja alikuwa kainamisha kichwa chake chini.
Zilipita dakika 5 bila jibu. Na mdhamini wa kiume akasema jamani muda muda..
Ilikuwa ni saaa saba na robo usiku.
Kaka alisema hapa mpaka pakuche. Na hata ikibidi kukaa tutakaa tena.
Mdhamini wa kiume alisema je mnahitajiana ama?
Hakuna aliyejibu ndio ama hapana.
Deus aliulizwa je unamhitaji Flora?alisema simhitaji kabisa. Simtaki.
Kisha nikaulizwa je unamhitaji Deus?
Nilisema ndio namhitaji.
Niliulizwa kwa nini unamhitaji?nilisema mi mume wangu. Nilipata uchungu. Ni kama akili ilifunguka wakati ule. Nilianguka kwa magoti na kumlilia mume wangu anisamehe. Nilimuomba msamaha sana na kumueleza sitaki kuwa sababu ya kulaumiwa kuvunja ndoa. Nililia sana. Lakini Deus alinisukuma na kusema sitaki unafiki. Mwanamke mbaya sana wewe. Mama ndhamini na wifi walilia na mimi.
Baba yangu aliniambia simama mama. Simama.
Nilisimama. Kisha baba mkwe akasema Deus hutaki kumsamehe mkeo?mbona huwezi mhurumia?
Deus alisema siwezi.
Baba mkwe alisema mama uko huru mwali wangu. Hakuna wa kukudai.
Mama mkwe alisema baba deus unamlaani deus ama?si uache aamue mwenyewe? Ni mtu mzima.
Baba mkwe alimwambia mkewe… unaona ni sawa asiposamehe?na je tukifunga kwa sala hapa Deus atasema sala ya baba yet ama hatasema?
Mama mkwe alisema ni kweli deus. Ninkweli. Msamehe mwenzako yaishe mwanangu.
Deus alisema namsamehe lla simhitaji.
Wifi alisema ni hatua nzuri
Haina neno msamehe tu
Deus alisema nimemsamehe.
Kisha wakakaa na wakawa wanajadili nini kifuate.
KAKA ALISEMA SASA NI KUMSIKILIZA DEUS ANATAKA NINI. NA DEUSI ATUAMBIE SISI TUTATEKELEZA.
Ilikuwa yapata saa tisa na robo alfajiri. Asbh sana. Kumetulia. Wifi aliba ruhusa kidogo. Kisha tuliambiwa na siso tunaweza kutoka nje na kuimgia ndani tena.Kaka yangu aliniita na kuniambia Flora Mungu anakupenda. Hata Sauli alifanya makubwa mabaya…Lakini mwisho wake ulikuwa mzuri.Usijali. Mungu anakupenda.
Nikaka wa pekee. Aliyebeba aibu yangu. Asinilaumu wala kunitenga. Nilimuuliza wifi yuko wapi?aliniambia atakuwa chumbani. Nilienda na kuingia. Nilikuta wifi kapiga magoti kwenye kona akisali. Nilipata wivu. Nilikumbuka zamani. Moyo uliniuma.
Wifi alikuwa akiomba kwa unyenyekevu wa hali ya juu.
Nilimsikia akisema..
Mungu Nakushukuru kwa amani.. furaha na upendo pamoja na familia yangu. Si kwa jihudi zangu wala akilinzangu ila mibkwa Nea yako tuCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nijalie kutambua haya. Mope kuona umuhimu wa amani siku zote za maisha yangu. Niitafute amani kwa bidii na kuilinda. Msaidir flora na deusi. Wape kujua umuhimu wa amani yako Mungu. Nilihisi anamaliza kuomba kisha nikanyata na kuondoka.
Baada ya dakima kadhaa kikao kikaendelea.
Deus aliulizwa unataka nini?
Deus alisema hawezi kuishi na Mimi tena. Hanihitaji kama mke. Ila kama mzazi mwenzake. Alisema hawezi kuishi ili hali anajua fransis alikuwa ma mimi. Hivyo alisema hanihitaji kabisa na ana mambo yake na taratibu zake aachwe.
Alisema wtoto atalea hilo halina tatizo.
Alikataa kata kata hata alipobembelezwa. Kisha akasema anamkabidhi rasmi mimi kwa kaka na baba yangu. Asije kudaiwa lolote na hajanidhuru.
Dah. Niliumia. Alaliza hivyo na kikao kikafungwa rasmi kiloja akiwa anajua muafaka.
88888888NILIHISI KUPUMUA. JAPO MOYO ULIMIUMA MNO SANA. NILIENDA KITANDANI MOJA KWA MOJA. UGENI ULIONDOKA WOTE. BABA ALIBAKI. SIKUAMSHWA ILA NILIACHWA NILALE.
KAJUA KALIKUWA KAKALI KAKAPENYA KWENYE DIRISHA NA KUONA MWANGA WA JUA. NILIAMKA NA KUSHTUKA SANA. NILILIA MNO TENA NA TENA. WIFI ALIKUJA NA KUNIKUTA NALIA.
ALINIAMBIA KULIA HAKUSAIDII. ISIPOKUA KUJIPANGA NA KUANZA MAISHA MAPYA.
Sikia flora. Mungu humrudi ampendaye. Mungu anakupenda na ndio maana haya yakakupata. Ni bora kurudiwa ma Mungu ili urekebike. Kuliko unheishia huko na kupotea.
Mimi sioni sababu ya Wewe kulia tena. Omba Mungu akupe tena kuinuka. Omba Mungu akupe tena hatua ingine.
Mungu wetu ni muaminifu sana. Haangalii kama wanadamu waangaliavyo. Mungu huangalia moyo. Tubu kwa kumaanisha na anza upya. Aziungamaye dhambi zake na kuziacha atapata rehema. Hili ndilo unalolihitaji mama.
Haya amka uoge. Umywe chai. Uchangamke. Wala usijali.
Dah… ni pendo la ajabu kwa wifi yangu. Watu husema wake za kaka ni wabaya ila ubaya hapa sikuuona. Mwema.. mfariji… na mwenye upendo wa dhati. Nilifarijika.
Baba alikuja naye akanitia moyo. INGEKUWA NI WAKATI HUU NINGEIMBA ULE WIMBO WA MISULI YA IMANI USEMAO SIJAONA UPENDO KAMA HUU…haijalishi maovu yangu lakini walikuwa pamoja na mimi. Aibu yangu waliivaaa. Wangapi wanatengwa na kukataliwa?wanabezwa na kufukuzwa… wanaambiwa maneno makali na kejeli?Si kwa mama dina na baba dina na baba yangu mzazi. Walinipenda mno ma maovu yangu.
888888
Jioni kikao kilikaa cha kwetu. Kaka yangu. Wifi yangu na Baba. Tulikaa wenyewe. Kaka alisema..
Baba tumeongea na mke wangu. Tumeona kwamba Flora hatakuwa na mahali salama pa kukaa zaidi ya hapa kwetu. Tutaishi naye na wanawe. Tutamtia moyo. Tutamfundisha na kumuelekeza vyema anapaswa kuganyaje. Hatutamuacha kamwe.
Baba alidondosha machozi na kusema Pendo la ndugu na lidumu.
Wote wanne tulikumbatiana na kuimba wimbo wa Mahali ni pazuri ndugu wanapokaaa.. wakipatana vyeeeema na wakipendana.
Tulilia sana.
Baba yangu alimaliza kwa kumshukuru sana Kaka na mkewe.
Kisha mkewe akasema.
Baba nafurahi kwa namna ulivyowalea wanao kwa upendo na kumjua Mungu. Natamani na wanangu wawe kama wanao.
Wote tulifurahiana na kaka akasema..TAZAMA YA KALE YAMEPITA YAMEKUWA MAPYA.
Kisha wifi akainipeleka chumbani na tukalala.
Niliwaza kazi… niliwaza ugumu wa maisha kukaa kwa watu. Dah… ilikuwa kazi haswa. Wifi alinifundisha mambo mengi mno na kumielekeza. Alinifundisha kusamehe kwa kumaanisha. Pole pole nilianza kutoa misamaha. Kwa bite… mwenge…. ck… tecla… mama kely.. haikuwa rahisi lakini pole pole nilianza kutoa misamaha.
Kisha mama dina akaniambia sasa utaenda kusalimia wakwe zako. Na wala usijali. Ni babu wa wanao. Dah. Ilikuwa ngumu. Akaniambia utaenda. Nilijikaza. Akanipatia sukari mchele na mafuta. Na nilaenda kusalimia. Mama mkwe alioneka a kufurahia na kusema kumbe unatukumbuka eee. Nilisema ndio. Baba mkwe alikuwa mwema sana. Na jogoo alituchinjia. Nilikaa siku tatu kwa wakwe. Kisha Deus alikuja na kunikuta huko. Tuliongea kwa upendo na Deus. Lakini alioneka a bado ana kinyongo na kuumia sana moyoni.Sikuendelea kuongea naye. Ila nilimuaga naondoka. Alinipatia nauli na niliondoka.
Nilifika na kumuelezea mama dina kila kitu. Mama dina aliniambia ni hatua nzuri. Usijali.
Nilikaa kwa kaka kwa muda wa miezi 6. Kisha nikaitiwa barua ya kufukuzwa kazi kabisa. Niliumia sana.
Nilikaa kwa mawazo. Mama dina aliniambia kila mapito yana ufunguo wake. Kikubwa kujinyenyekeza mbele za Mungu tu basi.
Nilifanya hivyo kwa kumaanisha. Nilianza kusali kanisani kwa wifi. Nilipata saport kubwa sana kwa kaka ma wifi.
Niliendelea kuwa muaminifu sasa.
Mwaka uliisha. Kisha kaka akasafiri na wanawe na wanangu kwa x mass. Niliwaambia waniache mimi sitaenda mahali ili nitengeneze na Mungu wangu. Niliomba usiku na mchana. Nililia usiku na mchana.Nikamwambia Mungu sitanyamaza mpaka unibariki.
Nilianza kuandika barua za kuomba kazi sehemu sehemu. Niliandika nyingi sana.
Na mwisho wa siku nikaitwa kwa interview.
Asbh ya Interview Wifi aliniambia tuombe pamoja. Tuliomba na kufunga.
Kisha nikaenda. Kulikuwa na watu wengi sana.
Na nilipogikia zamu yangu ni kama nilikata tamaa.
Nikamaliza interview na kuondoka tukaambiwa saa nne ya jumatano twende tukaone matokeo.
Nilifika na nilishangaa kuona jina langu. Ilikuwa ni muujiza wa pekee.
Nililia kwa furaha.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilirudi nyumbani na amani tele.
Nilifika nyumbani tulifurahia kwa pamoja. NA KUJIANDAA KUANZA KAZI MAPEMA. Mama Dina aliniambia sasa utaenda kuwaeleza wazazi umepata kazi. Nilimtii na kwenda. Niliwaeleza wazazi wakwe nimepata kazi naomba baraka zao. Kisha wakafurahia sana. Na nikaondoka.
Nilimuuliza mama dina kwa nini alinituma kuganya vile?aliniambia Mungu anapenda shukrani. Kuwaeleza unaofikiri hawakupendi mafanikio yako ni sifa kwa Mumgu. Na Mungu anapenda na kukaa kati kati ya sifa. Anaona unashkrani. Nilimuelewa sana.
Muda ulipita nikiwa kazini.
Nilifanya kazi kwenye shirika kubwa sana la kimataifa. Nilionekana kwenye mitandao mara kwa mara nikisoma report.
Mama Dina aliniambiq MUNGU AKIAMUA KUKUBARIKI ANAKUBARIKI HASWA NA KUWASETA WATESI WAKO.
Mambo yalikuwa mazuri mno na mafanikio mazuri mnooo.
Nilikuwa nina heshima iliyokithiri.
Niliogopa dhambi kama ukoma.
Nje ya nchi naenda kikazi kama nipendavyo.
Vishawishi havina nafasi kwangu tena. Hata angekuja mwanaume wa aina gani kunitongoza nilimuona kama mavi mapya.
YOTE NILIYAONA KAMA MAVI KWA AJILI YA KRISTO NA MSAMAHA ALIONIPA.Deus alioa. Na hakumuoa Bite. Japo alizaa na Bite. Tunawasiliana vyema na Deus kama mzazi mwenzangu.
Ninamtumikia Mungu na nimeahidi kusimama vilivyo. Mwaka wa 8 huu Ninamtumikia Mungu. Nafanya kazi na maishanyanaenda.Nina amani Tele
Nina furaha tele.
Ninaishi kwangu kama ikulu. Na baraka kede kede za Kumtukuza Mungu.Deus huja na kuwaangalia watoto. Na huwa analala na kuonhea na wanawe.Sina kinyongo sina kisasi.NASUBIRI KUFA KATIKA KRISTO IKIMPENDEZA MUNGU KUISHI NAISHI KWA KUMTUKUZA YEYE.
……The End…………….MWISHO
0 comments:
Post a Comment