IMEANDIKWA NA : NYEMO CHILONGANI
*********************************************************************************
Sehemu Ya Kwanza (1)
Mwenyekiti wa Chama cha Vijana cha Casfeta (Christian Ambassador Students Fellowship Tanzania), Samuel Mpelele alikuwa akiendelea kuhubiri katika mkutano wa Injili uliokuwa ukifanyika katika Uwanja wa mpira wa Chekereni.
Huo ulikuwa mkutano wa Injili ulioandaliwa na vijana waliookoka mkoani Kilimanjaro. Watu walikuwa kimya uwanjani hapo huku wakimsikiliza Samuel ambaye alikuwa akitiririka jasho jingi huku akiendelea kuhubiri mahali pale.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kila mtu alikuwa akiingiwa na maneno yale ambayo alikuwa akiyaongea katika mkutano ule kwa kutumia kipaza sauti kilichoonganishwa na spika kadhaa zilizokuwa katika uwanja huo. Samuel alionekana kujawa na nguvu za Mungu, kadiri alivyokuwa akihubiri na ndivyo ambavyo watu walizidi kupiga makofi huku wengine wakianza kulia.
Huo ulikuwa ni mkutano wa pili kuandaliwa na wanafunzi wa Chama cha Casfeta mkoani Kilimanjaro, mkutano ambao ulikuwa ukiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho mkoani hapo, Samuel Mpelele, mwanafunzi aliyekuwa akisoma katika shule ya Uhuru hapo Kilimanjaro. Watu waliokuwa wakimsikiliza ambao hawakuwa wameokoka, siku hiyo wakaokoka kwani maneno ambayo alikuwa akiongea mahali pale yalionekana kumgusa kila mmoja.
Samuel Mpelele alikuwa mtoto wa mchungaji Christopher Mpelele wa Kanisa la Praise and Worship lililokuwa Mwenge jijini Dar es Salaam. Kwa sababu alizaliwa katika familia iliyomjua Mungu, familia iliyomcha Mungu, Samuel akajikuta akimuabudu Mungu maishani mwake huku wazazi wake wakiwa muongozo mkubwa katika maisha yake.
Mara nyingi Samuel alikuwa akielekea kanisani na kumuona baba yake akihubiri, moyoni alifurahi kupita kawaida, nae akaanza kujisikia msukumo wa kufanya kama ambavyo baba yake alivyokuwa akifanya kila alipokuwa madhabahuni. Katika kipindi hicho, kumuona mtu akiwa anahubiri ndicho kilikuwa kitu ambacho kilikuwa kikimfurahisha mno maishani mwake.
Maisha ya Samuel yakawa ni kwenda kanisani na kumuomba Mungu aweze kuonekana katika maisha yake tu. Moyoni mwake alikuwa akijisikia wito kabisa kwamba nae alitakiwa kuwa kama baba yake kuhubiri madhabauni.
Mchungaji Mpelele tayari aliiona karama ya uhubiri aliyokuwa nayo mtoto wake, alichokifanya ni kuanza kumpa ushirikiano katika kila kitu juu ya karama ambayo alikuwa nayo.
Huo ulikuwa ni wakati ambao Samuel alikuwa darasa la saba, alipomaliza shule, matokeo yake hayakuwa mazuri na hivyo kupelekwa katika shule ya Sekondari ya Uhuru iliyokuwa mkoani Kilimanjaro. Huko, Samuel akajiunga katika Kikundi cha Casfeta, kikundi kilichoanza kumuweka karibu na watu wengi ambao walikuwa wakimuabudu Mungu katika maisha yao shuleni pale.
Shule hiyo ilikuwa ni ya mchanganyiko, kulikuwa na wanafunzi ambao hawakwenda kanisa na wala hawakujua makanisa yalikuwa sehemu gani, kuna wanafunzi wengine ambao walikuwa wakielekea kanisani kila siku katika maisha yao lakini hawakuweza kubadilika, bado walikuwa wakiendelea kuvuta sigara na kunywa pombe pamoja na kufanya starehe za aina mbalimbali.
Ukiachana na hao, kulikuwa na Waislamu ambao wengi wao hawakuwa wakienda msikitini, tena mbaya zaidi wengine wakiwa watoto wa maustadhi wakubwa katika mikoa waliyotoka.
Wao pamoja na watoto wa wachungaji na viongozi wa makanisa mengine ndiyo waliokuwa wakiongoza kwa fujo na tabia chafu shuleni hapo.
Ukiachana na hao, kulikuwa na wanafunzi wengine waliokuwa Waislamu safi. Walikuwa wakielekea misikitini kuswali swala tano. Maisha yao yalikuwa tofauti na maisha ya watu wengine, walikuwa wakiishi kipole sana, hawakuwa wagomvi, walimheshimu kila mtu, kila wakati, walikuwa wakiongea maneno ya dini huku wakiwataka hata watu wengine wabadilike na kumuabudu Allah.
Kwa kifupi, shule ile ilikuwa na watu waliochanganyika ila kwa watoto wa wachungaji na maustadhi ndio ambao walikuwa wakiongoza kwa maovu shuleni pale.
Wao hawakupenda dini, walijiona kuzaliwa katika familia ambazo zilikuwa zikiijua dini, hivyo nao wakajiona kuwa hata kama wasingekwenda kanisani au msikitini, maisha yao yalikuwa na ulinzi wa kutosha.
Walimu hawakuyapenda maisha waliyokuwa wakiishi vijana hao, mara kwa mara walijitahidi sana kuwarekebisha lakini maneno yao hayakusaidia chochote kile, bado vijana hao waliendelea kuwa hivyohivyo.
Shule nzima, watoto wa viongozi wa dini ndio waliokuwa wakitenda yale waliyotakiwa kuyatenda kama wazazi wao. Kwa upande wa dini ya kikristo alikuwepo Samuel au Sam kama alivyojulikana, mtoto wa mchungaji wa Kanisa la Praise and Worship lililokuwa Mwenge jijini Dar es Salaam pamoja na Sadiki Hamidu, mtoto wa Ustadhi Hamidu ambaye alikuwa imamu katika msikiti wa kichangani uliokuwa Magomeni jijini Dar es salaam.
Wawili hao ndiyo waliokuwa mifano mizuri ya kuigwa shuleni hapo huku walimu wakiwataka wanafunzi wote kuishi maisha kama jinsi watu hao wawili walivyokuwa wakiishi. Wanafunzi hawakuonekana kuelewa, kila siku walikuwa wakivuta bangi huku matendo ya ngono yakiwa ya hali ya juu kupita kawaida.
“Inasikitisha sana Sadiki kila ninapowaona vijana wenzangu wa Kikristo wakiwa wanafanya matendo machafu kama wafanyayo,” Samuel alimwambia Sadiki huku akionekana kuwa na huzuni.
“Wewe ni kama mimi Samuel. Waislamu tunatakiwa kuswali swala tano kwa siku na kufuata nguzo tano za Kiislamu lakini wenzangu hawataki kufuata kama Allah anavyotaka tufanye. Inaniuma sana Samuel,” Sadiki alimwambia Samuel kwa sauti ya unyonge.
Wawili hao walikuwa pamoja japokuwa walikuwa viongozi wa dini tofauti. Wao ndio waliokuwa chachu kubwa ya kuwafanya watu waliokuwa na dini tofauti kuwa pamoja zaidi.
Shuleni hapo hakukuwa na mitafaruku ya kidini, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akiidharau dini ya mwenzake, kila mtu alijiona sawa na mwenzake mbele za Mungu
Bado Samuel alikuwa akiendelea kuhubiri, watu walionekana kumkubali kupita kawaida, kila wakati watu walikuwa wakitikisa vichwa vyao kuonyesha ni jinsi gani walikuwa wakimkubali Samuel aliyekuwa akiendelea kuhubiri. Mara baada ya mkutano kumalizika, akawaita watu ambao walitaka kufanyiwa maombezi, akawafanyia maombezi na mkutano kufungwa.
Hayo ndio yalikuwa maisha yake shuleni hapo. Kila siku alikuwa akimuabudu Mungu na kumuomba usiku na mchana, alimtegemea Mungu zaidi ya alivyowategemea wazazi wake katika maisha yake.
Taaluma yake darasani wala haikuwa mbaya, ilikuwa ikiridhisha sana kiasi kilichomfanya kuwa miongoni mwa wanafunzi kumi ambao walikuwa wakifanya vizuri shuleni hapo.
“Unapaswa kubadilisha maisha yako na kumfuata Yesu Kristo Catherine,” Samuel alimwambia Catherine, msichana aliyekuwa akimuoneshea hisia za kimapenzi toka zamani shuleni hapo.
“Nimeshindwa mchungaji. Nimeshindwa kabisa,” Catherine alimwambia Samuel kwa sauti ya chini iliyosikika kimahaba.
“Kwa nguvu zako kamwe hautoweza. Muache Mungu ayabadilishe maisha yako. Unapoelekea si sehemu ambayo Yeye anataka wewe uende,” Samuel alimwambia Catherine.
“Kwa hiyo nifanye nini mchungaji?”
“Muombe sana Mungu akubadilishe.”
“Na kama nikishindwa kubadilika?”
“Mungu ashindwi kitu au labda uwe haujaamua moyoni mwako. Ukiamua, Mungu ashindwi kitu chochote katika maisha yako,” Samuel alimwambia Catherine.
Hayo ndio yalikuwa maneno ambayo kila siku Samuel alikuwa akimwambia Catherine juu ya maisha yake. Catherine alikuwa akijitahidi sana kuishi katika maisha ya kutotenda dhambi lakini bila kulazimishwa, mara kwa mara alijikuta akitenda dhambi.
Kuna kipindi kikafika, Catherine akajiona kushindwa kabisa kuuzuia moyo wake hasa pale ulipoamua kumuingiza Samuel. Akazidi kumpenda mvulana huyo na kumhitaji kupita kawaida.
Japokuwa Catherine alikuwa akijua fika kwamba alikuwa akimpenda Samuel lakini aliogopa kumfuata na kumwambia ukweli juu ya mapenzi aliyokuwa nayo juu yake, hivyo akaamua kubaki na dukuduku moyoni mwake.
Siku zikaendelea kukatika mpaka kufika kipindi ambacho Catherine akajiona kushindwa kujizuia kabisa, akaona hakuwa na jinsi na wala asingeendelea kubaki kimya, hivyo akaamua kumfuata Samuel kwa lengo la kumwambia ukweli bila kujali Samuel angemchukuliaje.
“Unasemaje?” Samuel aliuliza huku akionekana kutokuamini.
“Ninakupenda mchungaji.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndio maana kila siku nakwambia muombe sana Mungu kama unataka ayabadilisha maisha yako. Bila Yesu ni kazi bure maishani mwako Catherine,” Samuel alimwambia Catherine.
“Nakupenda Samuel.”
“Hilo ni pepo. Njoo kwenye ibada yetu ya maombezi saa kumi jioni uje uombewe. Hilo ni pepo la uzinzi,” alisema Samuel, muda huo walikuwa darasani.
Samuel hakuridhika, alichokifanya ni kumfanyia maombi Catherine. Hiyo wala haikubadilisha kitu chochote kile, bado moyo wa msichana huyo ulikuwa kwenye mapenzi kwa Samuel.
“Ninashindwa Samuel,” alisema Catherine baada ya maombi.
“Unashindwa nini?”
“Kuacha kukupenda.”
“Haiwezekani. Haujataka kumruhusu Yesu kuingia moyoni mwako Catherine.”
“Nimemruhusu ila bado ninakupenda. Kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele nazidi kukupenda Samuel,” Catherine alimwambia Samuel kwa sauti ya chini iliyojaa mahaba.
“Ngoja niendelee kukufanyia maombi” Samuel alisema huku akisimama.
“Ila usiniguse tena. Nifanyie maombi hivi hivi bila kunigusa” alisema Catherine, Samuel akashangaa.
“Kwa nini?”
“Unaponigusa......”
“Kuna nini?”
“Nasikia vijidudu vikinitembelea mwilini mwangu. Mwisho wa siku napata tabu hasa niwapo kitandani peke yangu usiku,” alisema Catherine.
Samuel akanyamaza kwa muda na kuanza kumwangalia Catherine usoni, uso wa Samuel ukaonekana kubadilika kama mtu ambaye alikuwa akimuona kiumbe fulani cha ajabu machoni mwake. Alichokifanya ni kuanza kumfanyia maombi Catherine bila kumgusa kama ambavyo alivyotaka iwe.
Hayo ndio yalikuwa maisha ambayo yaliendelea shuleni hapo, bado Catherine alionekana kuwa karibu na Samuel, kila siku alikuwa akitaka kufanyiwa maombi na Samuel lakini kamwe hakuweza kubadilika. Moyo wake ulionekana kuwa mgumu kubadilika, hakumruhusu Mungu kuubadili moyo wake, mapenzi yalikuwa yakimtesa kupita kawaida.
“Vipi mchungaji?” Sadiki alimuuliza Samuel katika kipindi ambacho alikuwa akionekana kuwa na mawazo.
“Mungu anahitajika sana kuyabadilisha maisha ya wanafunzi shuleni hapa. Kuna wengine wanatumiwa na shetani katika kutujaribu watumishi wa Mungu. Ila kamwe tutasimama imara” Samuel alimwambia Sadiki.
“Umekwishajaribiwa?” Sadiki alimuuliza.
“Ndio. Kuna yule msichana Catherine huwa kila siku anakuja, ishu yake ileile, nimfanyie maombi ila moyo wake hajauweka tayari kumpokea Yesu” Samuel alimwambia Sadiki.
“Pole sana ndugu yangu ila maisha yako hayatofautiani na mimi,” Sadiki alimwambia Samuel.
“Kwa nini?”
“Unamjua yule Mariamu msichana tunayesoma nae kidato cha tatu?” Sadiki aliuliza.
“Mariamu yupi? Wapo watatu darasani.”
“Yule mweupe.”
“Ninamfahamu.”
“Huwa kila siku ananitaka, mara kwa mara ananiandikia barua za kimapenzi,” Sadiki alimwambia Samuel.
“Mungu wangu!”
“Ndio hivyo. Jana tu alikwenda kuninunulia kanzu mpya pamoja na kofia kama zawadi” Sadiki alimwambia Samuel.
“Haya ni majaribu na inapaswa tuyashinde. Mungu wetu hashindwi” Samuel alimwambia Sadiki.
“Ndio hivyo. Ninapenda niendelee kumcha Allah katika maisha yangu. Sipendi kumpa ibilisi ruhusa ya kuyachezea maisha yangu. Namcha Allah si kwa sababu wazazi wangu wanamcha Allah, hapana, ninamcha Allah kwa sababu ninatakiwa kumcha Allah kwani Yeye ndiye muongozo wa maisha yangu” Sadiki alimwambia Samuel.
Hayo ndio yalikuwa majaribu yao ya kila siku. Mara kwa mara wasichana hao walionekana kama kutumwa na shetani kwa ajili ya kuwajaribu katika maisha yao.
Japokuwa walikuwa wakiwaepuka sana lakini kila siku walimuomba Mungu aweze kuwashindia katika vita hivyo ambavyo kwao vilionekana kuwa vigumu sana, walihitaji msaada wa Mungu kuyashinda majaribu hayo ambayo kwao yalionekana kuwa makubwa zaidi ya uwezo wao.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya
Uhuru wakazidi kubadilika kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele. Vilevi vilikuwa
vikiingizwa shuleni hapo kinyemela pasipo uongozi wa shule kufahamu kitu
chochote kile.
Kutokana na asilimia kubwa ya wanafunzi waliokuwa
wakisoma shuleni hapo kuwa wa kutwa waliokuwa wakiishi nyumbani, mara nyingi
waliwachukua wenzao wa bweni na kuwapeleka katika kumbi za starehe nyakati za
usiku.
Idadi kubwa ya wanafunzi walikuwa wakiondoka usiku na kwenda
katika kumbi za starehe, hakukuwa na mwalimu yeyote ambaye alikuwa akifahamu
kile kilichokuwa kikiendelea mahali hapo kutokana na walimu wawili tu waliokuwa
wakibaki shuleni hapo kulala mapema sana.
Walinzi ndio waliokuwa
wakicheza mchezo mzima ambao ulikuwa ukifayika kwa wanafunzi. Wao ndio waliokuwa
wakiwaruhusu wanafunzi kutoroka shuleni hapo na kuingia mitaani huku wakihongwa
kiasi fulani cha fedha.
Wanafunzi wa kike hawakuweza kujizuia, huko
walipokwenda walikuwa wakifanya ufuska na hata wakati mwingine kujiuza kutokana
na kutokuwa na fedha za kutumia shuleni.
Kadiri siku zilivyozidi
kwenda mbele na ndivyo ambavyo shule ile ilivyozidi kuharibika kiasi ambacho
hata wazazi wengi ambao watoto wao walikuwa shuleni pale kuanza kuingiwa na
hofu. Taaluma za wanafunzi zilishuka chini kila siku jambo lililowashangaza hata
walimu wenyewe.
Hapo ndipo walimu walipoonekana kugundua kitu.
Kiranja, John Gilipa ambaye alionekana kuwa mnoko shuleni hapo akaenda kuwaambia
walimu juu ya kile ambacho kilikuwa kikiendelea nyakati za
usiku.
Hatua ya kwanza ambayo ilichukua uongozi wa shule ni kumkamata
mlinzi na kumfikisha katika kituo cha polisi kwa yale aliyokuwa akiyafanya,
kupokea fedha na kuwaruhusu wanafunzi usiku kwenda katika kumbi za starehe
zilizokuwa mitaani.
“Unasema ilikuwaje jana usiku?” Mwalimu wa zamu
alimuuliza Kiranja mkuu, John ambaye alikuwa ameleta kesi ofisini
hapo.
“Kitanda changu kilimwagiwa maji, tena nahisi ndoo zaidi ya
tatu,” John Gilipa alijibu huku akionekana kuwa na hasira.
“Nani
aliyefanya hivyo?” Mwalimu wa zamu, Salumu Issa
aliuliza.
“Sijui.”
“Wewe unamuhisi
nani?”
“Simuhisi mtu yeyote. Ila nadhani bweni zima linahusika,”
alisema John.
Siku hiyo ikaonekana kuwa mbaya kwa wanafunzi ambao
walikuwa wakiishi katika bweni alilokuwa akiishi kiranja mkuu, John. Mchana wote
walikuwa wakipewa adhabu huku wakichapwa fimbo za uhakika na kutakiwa kuwataja
watu ambao walikuwa wamehusika katika kulimwagia maji godoro la John lakini
hakukuwa na mtu aliyesema kitu chochote kile.
Visa havikuisha, mara
baada ya adhabu ile wanafunzi wakaonekana kumkasirikia John kitendo ambacho
wengi hawakutaka kuongea nae. John akaonekana kuwa mpweke, wavulana wa shule
nzima walikuwa wamemtenga, ni Samuel na Sadiki tu ndio ambao walikuwa wakiongea
naye. Aliishi shuleni pale kama mkimbizi, mtu ambaye hakuwa na amani yoyote
ile.
Kila siku godoro lake lilikuwa likimwagiwa maji jambo
lililomfanya kulipeleka godoro lake ofisini kwa walimu, asubuhi alikuwa
akilipeleka ofisini na usiku alikuwa akilichukua na kwenda nalo bwenini kulala.
Shuleni, aliendelea kuwa na maisha ya unyonge jambo lililoishusha kiwango chake
katika taaluma.
“Hata kama dunia nzima itakutenga, hata kama wazazi
wako na ndugu zako watakutenga, jua kwamba kamwe Mungu hawezi kukutenga endapo
utamtumikia,” Samuel alimwambia John ambaye alionekana kuhitaji
msaada.
“Najiona kuwa katika wakati mgumu sana mchungaji. Wakati
mwingine natamani kujiua” John alimwambia Samuel.
“Kujiua! Unadhani
hilo litakuwa suluhisho la tatizo lako? Unadhani kujiua kutakufanya kupumzika
kwa amani? Ukijiua utakuwa umeua na adhabu yako itakuwa ni moto wa milele.
Hautakiwi kufanya kitendo kama hicho. Muachie Mungu” Samuel alimwambia
John.
“Sawa. Ila kwanza nataka kuokoka. Nataka kumpa Mungu maisha
yangu” John alimwambia Samuel.
“Hakuna tatizo” Samuel alimwambia John
na kisha kuanza kumuongoza sala ya toba.
****
Kila siku
Sadiki alikuwa mtu wa kushinda na kitabu kitakatifu cha Qur-an akijisomea
bwenini kwake juu ya kitanda huku mkononi akiwa na Tasbihi yake ambayo
ilionekana kumpa nguvu ya kuendelea kusoma kitabu kile. Maishani mwake, hakukuwa
na kitu ambacho alikuwa akikipenda kukifanya kama kuswali.
Kila siku
alikuwa akifanya ibada bwenini au hata msikitini. Sadiki hakuonekana kuwa radhi
kupita muda wa swala bila kuswali. Kufanya swala ndio ilikuwa sehemu ya maisha
yake shuleni hapo, kila alipokuwa akihitajika kufanya swala alikuwa akifanya
kama kawaida.
Wanafunzi wa dini ya Kiislamu ambao walikuwa wakitaka
kuyabadilisha maisha yao, Sadiki ndiye alikuwa mtu pekee ambaye alikuwa akiwapa
mafunzo mbalimbali kuhusiana na dini ya Kiislamu pamoja na mambo mengi mema
ambayo alikuwa amefanya Mtume Muhammad S.A.W.
Kwa sababu maisha yake
yalionekana kuwa matakatifu, hata wanafunzi ambao walikuwa wakiyapokea
mafundisho yake nao walikuwa wakijitahidi kuishi maisha kama aliyokuwa akiishi
Sadiki. Muda mwingi, mavazi ya Sadiki yalikuwa ni kanzu nyeupe zilionekana
kung’aa sana katika kila kipindi ambacho alikuwa akizivaa.
“Jumaa
Qareem,” Sadiki aliwaambia wanafunzi wenzake waliokuwa wamekaa nje ya bweni
wakipiga stori.
Kila mmoja akakunja uso, mtu kama Sadiki au Samuel
hawakuwa watu ambao walihitajika katika shule hiyo, wanafunzi shuleni hapo
walionekana kutamani kuendelea kuishi maisha ambayo walikuwa wakiyaishi, maisha
ya uchafu ambayo hayakupendeza hata machoni mwa mwanadamu.
Kitendo
cha Sadiki na Samuel kuzipenda dini zao na kupenda sana kuabudu vilikuwa vitu
pekee ambavyo vilikuwa vikiwakasirisha wanafunzi wengi mahali
hapo.
“Ananikera huyu jamaa,” alisema mwanafunzi mmoja aliyekuwa
akijulikana kwa fujo shuleni hapo, Chepuo.
“Hahaha! “ Wenzake wote
wakaanza kucheka.
“Yaani kuna huyu jamaa na yule mwenzake, wananikera
sana, kila ninapowaona natamani kuwaua,” Chepuo aliwaambia
wenzake.
“Wapotezee tu. Hawana jipya hao.”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Haiwezekani. Acha
leo niende kuyamwagia maji magodoro yao,” alisema Chepuo huku uso wake
ukionekana kuwa na hasira juu ya watu hao.
Chepuo alikuwa mwanafunzi
wa kidato cha tatu, mwanafunzi aliyekuwa na fujo kuliko wanafunzi wote shuleni
hapo. Kwake, hakuwahi kushika Biblia wala Qur-an , alikuwa akizichukia dini zote
kupita kawaida.
Alijijua kabisa kwamba wanafunzi wengi wa shuleni
hapo walikuwa wakimuogopa, hivyo alitaka kuigawa shule hiyo. Alitamani wanafunzi
wengi wawe katika kundi lake ambalo angeliongoza kuleta fujo za mara kwa mara
shuleni hapo pamoja na migomo isiyokuwa na sababu yoyote ile.
Kutokana
na kutopenda dini yoyote ile, ikawa sababu kubwa ya kuwachukia Samuel na Sadiki
shuleni hapo. Kila alipokuwa akiwaona, hasira za waziwazi zilikuwa zikimkaba
kooni mwake huku kila siku maombi yake yakiwa ni kumtaka Mungu awaue watu hao
ambao walionekana kuwa chukizo mbele za uso wake zake.
Usiku ukaingia,
wanafunzi wakaanza kwenda darasani kusoma kama ambavyo ratiba ilivyokuwa
ikisema. Katika kipindi hicho, Chepuo alikuwa darasani pamoja na marafiki zake.
Kama kawaida, hakuwa akisoma zaidi ya kupiga stori za mitaani na wenzake ambao
walikuwa wamemzunguka.
Maisha, kwake yakaonekana kuwa si lolote lile,
elimu ambayo alitakiwa kuipata mahali hapo haikuonekana kuwa na faida yoyote ile
katika maisha yake ya mbele.
Hakujali kitu chochote kile, yeye ndiye
aliyekuwa akiwaongoza wanafunzi wengi kufanya maovu mpaka kuanzisha kikundi
chake kilichokuwa na wanafunzi ishirini ambacho alikuwa akikiita ‘Black
Ninja’.
Black Ninja ndilo lilikuwa kundi la kihuni ambalo kazi yake
kubwa lilikuwa ni kufanya fujo shuleni hapo. Kila siku walikuwa wakiwafanyia
fujo wanafunzi wengine na hata katika kipindi kingine kutoka na kwenda katika
shule ya Majengo, Northern Highland, Majengo na shule mbalimbali kufanya
fujo.
Wanafunzi ambao walikuwa katika kundi hilo walionekana kuwa
wachochezi wakubwa katika kuifanya shule hiyo kutawaliwa na mambo ya
ajabuajabu.
Chepuo ndiye alikuwa kiongozi wao ambaye kila siku kazi
yake ilikuwa ni kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawa. Hakuonekana
kuridhika na idadi ya wanafunzi ambao walikuwa katika kundi hilo, akazidi
kuwaongeza wanafunzi wa kiume na wa kike huku muonekano wao ulionekana kuwa kama
watu waliopinda.
“Niandalieni ndoo mbili kubwa za maji. Nataka vitanda
vyao usiku wa leo viwe mabwawa ya kuogelea,”Chepuo aliwaambia
wenzake.
Kwa haraka sana bila kupoteza muda vijana wawili wakasimama
na kisha kuelekea nje ya darasa lile kwenda kuandaa ndoo mbili kubwa ambazo
zilitakiwa kuwa na maji. Baada ya dakika ishirini, vijana wale wakarudi darasani
mule.
“Vipi?” Chepuo
aliwauliza.
“Tayari.”
“Mmeziweka wapi?” Chepuo
aliuliza
“Katika mlango wa kuingilia bwenini.”
“Bweni lipo
wazi?”
“Hapana. Limefungwa.”
Hapohapo Chepuo akasimama na
kisha kutoka nje. Safari yake ikaishia katika darasa la kidato cha tatu B na
kumwambia kiranja wa bweni kumpa ufunguo wa bweni lile. Japokuwa hakuwa
akitakiwa kumpa mwanafunzi yeyote ufunguo wa mlango wa bweni lakini kwa Chepuo,
kiranja yule akajikuta akimgawia.
Chepuo akatoka darasani humo na moja
kwa moja kuelekea bwenini. Alipozikuta ndoo zile mlangoni, akaufungua mlango na
kisha kuzibeba na kuingia nazo ndani. Alichokifanya ni kuchukua ndoo moja na
kumwagia katika kitanda cha Samuel na ndoo nyingine kumwagia katika kitanda cha
Sadiki.
“Leo watalala chini mbwa hawa” Chepuo alisema na kisha
kuondoka bwenini hapo huku akimrudishia ufunguo ule kiranja wa
bweni.
Ilipofika saa 4:00 usiku, kengele ikagongwa na hivyo wanafunzi
kutakiwa kwenda mabwenini mwao. Kama kawaida yao, Samuel na Sadiki wakaanza
kuelekea bwenini huku wakiongea kwa furaha bila kujua kwamba magodoro yao
yalikuwa yameloanishwa maji dakika kumi zilizopita.
Chepuo hakuonekana
kuwa na wasiwasi, muda wote alionekana kuwa na furaha juu ya kile ambacho
alikuwa amekifanya bwenini. Yeye na wenzake wakaanza kuelekea bwenini. Macho
yake hayakutoka kwa Samuel na Sadiki ambao walionekana kutokuwa na wasiwasi
wowote ule.
Mpaka wanaingia bwenini, Chepuo alikuwa akiwaangalia huku
wenzake wakiona ni kitu gani kingetokea mara baada ya watu hao kugundua kwamba
magodoro yao yalikuwa yameloanishwa na maji. Walibaki wakiwaangalia, Samuel na
Sadiki wakapanda katika vitanda vyao na kisha kulala.
Chepuo hakuamini
kile ambacho alikuwa amekiona, hakuamini kama kulikuwa na watu ambao wangeweza
kulala huku magodoro yakiwa yameloanishwa maji. Alichokifanya ni kumtuma kijana
mmoja ambaye alikuwa mmoja wa wanachama wa kundi lake la Black Ninja kwa ajili
ya kwenda kuhakikisha.
“Hebu kaangalie kama bado yameloa,” Chepuo
alimwambia kijana yule ambaye alikwenda na baada ya sekunde kadhaa
kurudi.
“Vipi?” Chepuo aliuliza.
“Mbona hayana
maji.”
“Unasemaje?” Chepuo aliuliza huku akionekana
kushtuka.
“Hayajaloa hata kidogo” Kijana yule
alijibu.
Chepuo hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kwenda
kuhakikisha yeye mwenyewe kujionea kama kile alichoongea kijana yule kilikuwa
cha kweli au uongo.
Akafika katika kitanda cha Samuel, alipoligusa
godoro, lilikuwa kavu kabisa. Hakuishia hapo, akaelekea mpaka katika kitanda cha
Sadiki na kisha kuligusa godoro, nalo lilikuwa kavu kabisa jambo lililomfanya
kupiga kelele ambazo ziliwashtua watu wote.
“Uwiiiiiii...kuna watu
wachawi humu sijapata kuona,” Chepuo alisema kwa sauti kubwa na
kuendelea:
“Kuna watu wachawi humu...kuna watu wachawi humu bwenini,”
Chepuo alisema.
Tukio lile likaonekana kumchanganya mno, hakuamini
kama magodoro yale hayakuwa yameloana na wakati yeye ndiye alikwenda na
kuyamwagia maji usiku huo.
Akili yake kwa wakati huo haikuonekana
kuwa sawa, ule ulionekana kuwa muujiza mkubwa. Alichokifanya ni kuanza kuelekea
katika kitanda chake, alipoligusa godoro lake, lilikuwa limeloanishwa na maji
mengi.
“Nani amemwagia maji godoro langu?” Chepuo aliuliza kwa
hasira.
“Hata sisi hatujui kwani magodoro yetu pia yamemwagiwa maji,”
Kijana mmoja alisema baadhi ya vijana wa kundi la Black Ninja ambao walikuwa
humo wakiwa wamesimama kutokana na magodoro yao kuloanishwa na
maji.
Mpaka kufikia hatua hiyo Chepuo alichanganyikiwa zaidi, godoro
la Samuel na Sadiki hayakuwa yameloanishwa na maji na wakati alikuwa ameyamwagia
maji.
Godoro lake pamoja na magodoro ya vijana wenzake waliokuwa
katika kundi la Black Ninja yalikuwa yameloanishwa maji. Haikutokea kwa Black
Ninja ambao walikuwa katika bweni lile tu, bali hata wale waliokuwa katika
mabweni mengine, nao magodoro yao yalikuwa yamemwagiwa maji, mmwagaji wa maji
yale katika magodoro yale hakujulikana kwani katika kipindi ambacho walikuwa
wakijisomea darasani, mabweni yalikuwa yamefungwa na
funguo.
Asubuhi ya siku iliyofuata,
kila mtu aliyesikia taarifa kuhusiana na kile ambacho Chepuo alikuwa amekifanya
bwenini cha kuloanisha maji magodoro ya Samuel na Sadiki lakini hayakuwa
yameloana zaidi ya godoro lake pamona na vijana wake,walikuwa wakicheka.
Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akiamini kama kile kitu kweli kilikuwa kimetokea
au Chepuo alikuwa ametunga tu.
Asilimia kubwa waliamini kwamba kweli
kile kitu kilikuwa kimetokea kutokana na muonekano ambao alikuwa nao Chepuo
katika kila kipindi alichokuwa akiwangalia Samuel na Sadiki.
Baadhi
ya wanafunzi wakawaogopa, tayari walijua fika kwamba katika kila hatua ambayo
watu hao walikuwa wakiishi shuleni hapo, Mungu alikuwa akiwaangalia katika
maisha yao.
Kwa upande mwingine, kasi ya Catherine na Mariamu wala
haikuweza kupungua, kila siku walikuwa wakijiona kuwa na uhitaji wa kuwa na
wavulana hao waliokuwa wamesimama imara katika misingi ya dini
zao.
Kila mmoja alikuwa akimfuata mtu wake kwa nyakati tofauti,
katika vipindi ambavyo walikuwa wakikaa darasani kujisomea na hata wakati wa
kula chakula.
Walikuwa na wakati mgumu, Samuel na Sadiki walionekana
kuwa na misimamo imara katika dini zao. Wanafunzi wengi walikuwa wakitamani
kuishi maisha kama ya watu hao wawili waliyokuwa wakiishi lakini hiyo ikaonekana
kuwa ngumu katika maisha yao.
Kuishi maisha kama ambayo Samuel na
Sadiki walivyokuwa wakiishi ilimaanisha kwamba ilitakiwa uache kila kitu kichafu
ambacho kilikuwa kikiendelea katika maisha yako.
Kama wewe ulikuwa
mtu wa wanawake au wanaume basi katika ulitakiwa kuachana nao na hata kama wewe
ulikuwa mtu wa kutoroka usiku na kuelekea disko pia ulitakiwa kuachana na mambo
hayo yaliyokuwa magumu kuachika kwa baadhi ya wanafunzi ambao walikuwa shuleni
hapo.
“Nataka nikununulie vitafunio leo,” Ilisikika sauti ya Mariamu
akimwambia Sadiki.
“Inshallah...! Mwenyezi Mungu akujalie....nashukuru
sana. Ila naomba ninunue mimi mwenyewe,” Sadiki alimwambia Mariamu aliyekuwa
akimwangalia macho yaliyojaa mahaba.
Mariamu hakuishia hapo, alijua
fika kwamba Sadiki alikuwa amemkatalia kumnunulia vitafunio hivyo kitu
alichotaka kufanya ni kumlazimisha kufanya kile alichokuwa akikitaka mahali
hapo. Alipoona Sadiki amechukua chapati, kwa haraka haraka akatoa kiasi cha
fedha cha chapati tatu na kisha kumgawia muuzaji.
Sadiki alitaka
kuzuia jambo hilo lakini kwake ikaonekana kuwa ngumu kwani tayari Mariamu
alikuwa amekwishamuwahi. Siku hiyo, Sadiki hakuonekana kuwa na amani, kila
alipokuwa akimwangalia Mariamu, binti huyo mrembo naye alikuwa akimwangalia
jambo ambalo liliyafanya macho yao kugongana kila wakati.
Kwa wote
wawili, kitendo kile kikaonekana kuwa na madhara fulani, moyo wa Sadiki ukaanza
kuyumba kidogo lakini akajitahidi sana kuuweka sawa ili kusiweze kuharibika kitu
chochote kile. Kwake, tayari alijiona kama kutaka kuangukia dhambini jambo
ambalo kamwe hakutaka kuliona likitokea katika maisha yake.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Huyu ibilisi naona
anataka kunizidi nguvu” Sadiki alijisemea macho yake yalipogongana na macho ya
Mariamu, macho mazuri mithili ya mwanamke aliyekula kungu.
Tayari
Sadiki akaanza kujiona wa tofauti, alichokifanya ni kuinuka na kisha kuelekea
bwenini. Alipofika huko, hatua ya kwanza ilikuwa ni kuchukua kitabu Kitakatifu
cha Qur-an na kuanza kukisoma.
Japokuwa alikuwa ameanza kukisoma
kitabu hicho mahali hapo, mawazo yake yalikuwa yakimletea picha ya Mariamu
katika kipindi ambacho alikuwa akiangaliana nae.
Ukiachilia vitu
hivyo, naye shetani akaanza kumuingizia picha za ajabu ajabu kichwani mwake.
Mara taswira yake ikaanza kumuona Mariamu akiwa amesimama mbele yake huku
akimchekea, mara akaonekana akivua nguo zake na kubakia na nguo ya ndani tu.
Mawazo hayo hayakuishia hapo, ghafla yakabadilika na kujikuta yupo chumbani na
Mariamu huku wote wakiwa watupu.
Mpaka kufikia hatua hiyo, Sadiki
akashtuka kutoka katika lindi la mawazo hayo machafu na kisha kuchukua Tasbihi
na kuivaa shingoni. Japokuwa akili yake ilimfanya kuhisi kwamba kufanya kitu
kama kile kingeweza kumsaidia lakini hakuambulia kitu, bado shetani alikuwa
akiendelea kumletea taswira za ajabuajabu kichwani mwake.
Kadri siku
zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo hali yake ilivyozidi kubadilika zaidi
na zaidi. Katika kipindi cha kwanza kila mawazo machafu yalipokuwa yakimjia
alikuwa akijitahidi sana kujizuia lakini baadae akajikuta akishindwa kufanya
hivyo.
Japokuwa hakutaka kumpa nafasi moyoni mwake, akashangaa kuona
akianza kuyaruhusu mawazo juu ya Mariamu, mawazo yale ambayo yalikuwa
yakimuonyeshea kuwa kitandani pamoja na Mariamu ndio ambayo yalikuwa yameanza
kumtawala katika kipindi hicho. Baada ya mwezi mmoja, nguvu za Mungu ambazo
alikuwa nazo Sadiki zikatoweka kabisa mwilini mwake.
Akamruhusu
shetani kuzichezea hisia zake na mwisho wa siku akajikuta akihitaji kusoma na
Mariamu katika darasa la kidato cha nne hasa katika kipindi ambacho wanafunzi wa
kidato cha nne walikuwa wamemaliza shule mahali hapo. Kusoma kwao wawili huko
ndipo ambapo kukaanzisha mambo mengine.
Mikono ya Sadiki ikaanza
kuwasha, ikaanza kuhitaji kuushika mwili wa Mariamu, na bila hiyana yoyote, mtu
ambaye alikuwa akijuliakana kama Ustadhi shuleni hapo, Sadiki akaanza kuyachezea
mapaja ya Mariamu jambo lililomuweka kwenye hali nzuri ambayo hakuwahi kuipata
kabla.
Hapo ndipo akili yake ilipofunguka kwa kuona kwamba kila siku
alikuwa akijitahidi kutofanya kitu kile na wakati kilikuwa kizuri. Aliendelea
kuyachezea mapaja ya Mariamu mpaka akaanza kuuhisi mwili wake ukianza
kutembelewa na vidudu fulani, Sadiki akashindwa kujizuia.
“Sasa
unataka kufanya nini? Mbona unafungua mkanda wa suruali yako?” Mariamu aliuliza
huku akijifanya kutokujua kitu kinachotaka kutokea.
“Hakuna mtu,
darasa zima tupo peke yetu, tatizo nini?” Sadiki aliuliza huku akiendelea
kuufungua mkanda kwa kasi ya ajabu, tayari hamu ya kufanya mapenzi ikawa
imekwishamuingia.
“Hapana Sadiki. Hapa darasani, siwezi kufanya
hivyo,” Mariamu alimwambia Sadiki ambaye akaonekana
kunyong’onyea.
“Kwa nini sasa? Mbona mahali hapa pako salama kabisa,”
Sadiki alimwambia Mariamu.
“Sehemu hii si salama Sadiki. Muda wowote
wanafunzi wanaweza kuja.”
“Waje huku! Kufanya nini?”
“Kwani
huku wanafunzi huwa hawaji?”
“Mara mojamoja sana. Form four
washamaliza shule na kuondoka,” Sadiki alimwambia Mariamu.
“Hata kama.
Hii skendo ustadhi.”
“Hilo si tatizo. Skendo si kitu cha kushangaza.
Ni jambo la kawaida tu kama kumchungulia mwanamke bafuni,” Sadiki alimwambia
Mariamu.
Sadiki alimuona Mariamu kama anamchelewesha, alichokifanya ni
kuanza kumshikashika mapaja yake kwa mara nyingine tena. Katika kipindi hicho,
Sadiki alionekana kusahau kwamba shuleni pale alikuwa akiheshimika sana kutokana
na ushika dini ambao alikuwa nao, alionekana kusahau kabisa kama mwezi mmoja
uliopita alikuwa mtu wa kuswali swala tano, kitu ambacho alikuwa akikitaka
mahali hapo ni kufanya ngono na Mariamu ambaye kwa kipindi kirefu sana alikuwa
akijipendekeza kwake.
“Siwezi....” Mariamu alisema na kisha kuifunika
sketi yake na kuanza kutoka nje.
Sadiki akaonekana kushtuka, hakuamini
kama Mariamu angeweza kuondoka darasani mule na kumuacha akiwa katika hali ile.
Sadiki akainuka na kusimama, akajikuta akirudi tena kitini na kutulia kwani
tayari alionekana kuwa tofauti.
“Mungu nisamehe,” Sadiki alisema kwa
sauti ya chini.
Hiyo ndiyo ilikuwa siku ya kwanza kwa Sadiki kumuacha
Mungu kimatendo, kuanzia hapo akaanza kumnyemelea Mariamu na hatimae mwisho wa
siku kufanikiwa kutoroka nae na kwenda nje ya shule. Huko, wakafanya sana ngono,
Sadiki akalipizia mara zote ambazo alikuwa akijifanya mtakatifu mbele za
Mungu.
Huo ndio ukawa mchezo wao, mara kwa mara walikuwa wakiendelea
kwenda huko na kuuufanya mchezo ule. Unafiki mbele za macho ya binadamu
ukaendelea kufanyika.
Hakuacha kuvaa kanzu, hakuacha kuvaa kofia ya
Kiislamu, hakuacha kutembea na Tasbihi, kila siku alikuwa akivaa mavazi hayo
lakini moyoni alikuwa mzinifu mkubwa.
Kasi zake za kwenda msikitini
zikaonekana kuanza kupungua. Kila alipokuwa akiulizwa, sababu ilikuwa ni
kujiandaa na mitihani ya mwisho wa mwaka kumbe ukweli ulikuwa ni kwamba alikuwa
ameanguka dhambini.
Mara kwa mara alikuwa akijitahidi kuomba msamaha
kwa Mungu juu ya kile ambacho alikuwa akikifanya lakini kesho yake alikuwa
akimchezea mapaja Mariamu na hatimae kufanya mapenzi.
Kila kilichokuwa
kikiendelea kilionekana kuwa siri kubwa, Sadiki hakutaka mtu yeyote afahamu kile
kilichokuwa kikiendelea kati yake na Mariamu.
Kufanya ngono
kulipozidi sana, baadhi ya wanafunzi waliokuwa kwenye kundi la Black Ninja
wakaonekana kufahamu hasa mara baada ya mara kadhaa kumfuma Sadiki akiwa na
Mariamu wakitoka nje ya shule na kutokomea kusipojulikana.
“Lazima
niwaharibie. Halafu nasikia hata Samuel ndio zake hizo kwa yule Catherine.
Lazima niwaharibie” Chepuo, kiongozi wa kundi la Black Ninja aliwaambia
wenzake.
****
Mabadiliko ambayo yalikuwa yakitokea kwa
Sadiki pia yakaanza kutokea mpaka kwa Samuel. Naye, taratibu akaanza kupiga
stori sana na Catherine kitu ambacho wakati mwingine kilikuwa kikimsahaulisha na
muda ambao alikuwa ameupanga wa kufanya maombi binafsi.
Catherine
akaanza kuuteka moyo wake, naye, akaanza kujiona akikosa nguvu katika kumtumia
Mungu. Muda wa kwenda kwenye maombi binafsi alikuwa akijisikia uchovu mwingi
mpaka wakati mwingine kulala. Mara kwa mara usiku alikuwa akiota ndoto za mbaya,
alikuwa akiota akifanya mapenzi na Catherine, msichana ambaye alikuwa akimhitaji
toka zamani.
Taratibu, nao mchezo wao ukaanzia katika kipindi ambacho
walikuwa wakila chakula cha mchana. Mguu wa Samuel ulipougusa mguu wa Catherine
bahati mbaya, kijotojoto alichokipata jumlisha na baridi lile la Kilimanjaro,
akajihisi kabisa kuwa mtu wa tofauti.
Alichokifanya, mara kwa mara
akawa anaugusisha tena mguu wake miguuni mwa Catherine huku akiupandisha juu
jambo ambalo likamfanya baadae kuanza kuupandisha zaidi na zaidi mpaka kufika
mapajani.
Kwa sababu kulikuwa na meza katikati yao, hakukuwa na
mwanafunzi ambaye alishtukia mchezo ambao ulikuwa ukifanyika kwa wawili hao
kwani walionekana kuwa katika hali ya utulivu sana.
Mguu ule ukafika
katika mapaja ya Catherine na hatimae kupitiliza kabisa. Shetani akaonekana
kumshinda nguvu kwa wakati huo. Yule shetani ambaye mara kwa mara alikuwa
akimkemea, katika kipindi hicho alionekana kuwa mjanja zaidi yake. Huo nao ukawa
mwanzo wa kila kitu katika maisha ya wawili hao, kuchezeana ndio ikawa sehemu ya
maisha yao shuleni hapo.
Kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele,
ulinzi wa Mungu hakuwa nao tena maishani mwake, aliamua kumuacha Mungu, nae
Mungu akamuacha.
Hapo ndipo maisha ya ngono yalipofunguliwa zaidi.
Samuel akaanza kutoka sana nje ya shule pamoja na Catherine na kisha huko
kufanya ngono.
Huko ndipo ambapo wakakutana na Sadiki ambaye alikuwa
pamoja na Mariamu, wakaungana pamoja na kuwa watu wanne. Toka walipozaliwa hicho
ndicho kikawa kipindi chao cha kwanza kuwa na wanawake, hivyo wakatokea
kuwapenda sana Mariamu na Catherine.
Wakawa wakitoka na kuelekea mjini
na kisha kununua vinywaji mbalimbali isipokuwa pombe na kuanza kunywa. Kutokana
na Catherine kuwa mnywaji mzuri wa pombe, akaanza kuwafundisha wenzake namna ya
kunywa pombe hizo.
Kwa siku za kwanza zilionekana kuwa chungu lakini
kadri walivyokuwa wakiendelea kunywa, uchungu ule ukaanza
kupotea.
Wazazi wao walikuwa wakiwaamini kupita kiasi, kila mwezi
walikuwa wakiwatumia fedha za matumizi lakini kwa bahati mbaya, fedha zile
zilikuwa zikiishia kwenye ulevi wa siri ambao ulikuwa ukiendelea maishani mwao.
Walimu hawakujua kile ambacho kilikuwa kikiendelea kwa watu hao, kila siku
walikuwa wakiwaamini kupita kawaida.
Hata katika kipindi ambacho
Samuel alikuwa akiomba ruhusa kwa walimu ya kubaki usiku na wanamaombi kwa ajili
ya kuomba, walikuwa wakimkubalia.
Alikuwa akibaki nao na kufanya nao
maombi, ila walipokuwa wakimaliza, wanafunzi wengine ambao walikuwa wanamaombi
walipokuwa wakiondoka kwenda kulala, alikuwa akibaki na Catherine japo kwa
dakika thelathini na kisha kufanya ngono darasani.
“Siku hizi kidogo
unajitahidi nami naanza kufika ninapopahitaji,” Catherine alimwambia Samuel mara
baada ya kufanya mapenzi.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Usijali. Kuna
kipindi kitakuja nitatumia hata saa moja,” Samuel alimwambia
Catherine.
“Ila hivi itakuwaje kama walimu watajua?” Catherine
aliuliza.
“Watajuaje sasa?”
“Si unajua dunia haina
siri?”
“Najua. Dunia haina siri ila shule ina siri,” Samuel alimwambia
Catherine.
“Mmmh! Unajiamini sana mpenzi.”
“Hilo usijali.
Hakuna kitakachoharibika hapa,” Samuel alisema kwa kujiamini.
Watu
ambao walikuwa wakiaminiwa kuwa wacha Mungu shuleni hapo nao wakawa
wameharibika. Sadiki hakuwa mtu wa kuswali tena, hakuwa mtu wa kuvaa kanzu mara
kwa mara, msikitini alikuwa akipitiliza hata wiki mbili bila kwenda
huko.
Maisha yake, shetani alikuwa akizidi kuyatawala, alimruhusu
shetani kuchukua nafasi katika moyo wake, akamuachana Mungu, nae Mungu hakuwa na
shaka, akamuacha.
Kilichotokea kwa Sadiki ndicho kile kile ambacho
kilikuwa kimetokea kwa Samuel. Kwenda ibadani na kufanya maombi ikawa ni kwa
mazoea, hakufanya kwa sababu alikuwa na msukumo wa kufanya hivyo bali alifanya
kwa sababu alikuwa amekwishazoea kufanya ibada na maombi.
Mapenzi
ndicho kitu ambacho walikuwa wakikifikiria sana kwa wakati huo, hawakujali kitu
chochote kile, hawakujali kama baadae kuna mambo mabaya ambayo yangeweza kutokea
katika maisha yao, kitu ambacho walikuwa wakikijali katika kipindi hicho ni
kufanya kile ambacho mioyo yao ilikuwa ikiwataka
wafanye.
Chepuo akaonekana kuwa na
hasira. Alijua kwamba shule nzima ilikuwa ikiwaamini watu hao ambao kwao
walionekana kuwa watakatifu kuliko wanafunzi wote shuleni hapo. Chepuo alikuwa
akikasirikiwa na walimu kutokana na tabia zake mbaya zilizoonekana kuwachosha
walimu hao. Kitendo cha kuambiwa kila siku kwamba ailitakiwa aige tabia kama za
Samuel au Sadiki kilionekana kumkasirisha sana.
Moyo wake ulikuwa na
chuki kubwa kwa watu hao kiasi ambacho hata kuwaona tu alikuwa akijisikia
vibaya. Kwa kipindi kirefu sana alikuwa akitamani kitu kimoja, alijua fika
kwamba walimu walikuwa wakiwaamini sana watu hao wawili, sasa alitaka
kuwaharibia kwa walimu ili wasiweze kuaminika tena.
Katika kipindi
ambacho aliletewa taarifa kwamba hata Samuel na Sadiki walikuwa wakitoka boda
hakuonekana kuamini kabisa, kwake, kitu kama kile kilionekana kutokuwezekana
hata mara moja.
Japokuwa alikuwa hawapendi kabisa watu hao lakini kila
siku moyoni mwake alikuwa akiwakubali, utakatifu ambao watu hao walikuwa nao
hata yeye mwenyewe kuna kipindi kingine alikuwa
akiwaogopa.
“Unasemaje?” Chepuo aliuliza huku akionekana
kutokuamini.
“Ndio hivyo. Yaani hata mchungaji na ustadhi nao wanatoka
boda kama sisi,” Mrisho, mwanafunzi aliyekuwa kwenye Kundi la Black Ninja
alimwambia Chepuo.
“Kwanza unapoongea na mimi kuhusu hao mbwa hebu
usiwaite hayo majina uliyowaita,” Chepuo alimwambia
Mrisho.
“Sawa.”
“Hebu nieleze juu ya jambo hili. Inawezekana
vipi?” Chepuo aliuliza.
“Huo ndio ukweli kiongozi. Samuel na Sadiki
nao wameanza kwenda boda,” Mrisho alisema.
Chepuo hakutaka kuamini
moja kwa moja, kama ambavyo Mrisho alivyoona basi nae alitaka kuhakikisha juu ya
kile ambacho kilikuwa kinaendelea katika maisha ya watu hao
wawili.
Siku ambayo wanafunzi walikuwa wakipendelea kwenda nje ya
shule ikawaida, kama kawaida Chepuo na wenzake wakaanza kuelekea katika njia za
kutokea nje ya shule, sehemu ambayo asilimia kubwa ya wavulana walikuwa
wakiitumia.
Chepuo akatoka mpaka nje ya shule na kisha kwenda sehemu
kujificha. Katika usiku huo alitaka kuona kile ambacho Mrisho alikuwa amemwambia
kuhusiana na Samuel pamoja na mwenzake, Sadiki kuanza tabia za kwenda nje ya
shule huku wakiwa na wasichana.
Chepuo aliendelea kujificha, siku hiyo
hakuwa radhi kwenda disko mpaka pale ambapo angepata ukweli juu ya kile ambacho
alikuwa ameambiwa.
Saa 6:20 usiku, akaanza kuwaona Samuel na Sadiki
wakitoka katika uzio wa shule kwa kuruka ukuta kama walivyokuwa wakifanya
wanafunzi wengine na kuanza kuelekea katika upande mwingine huku wakiwa na
wasichana wawili.
Chepuo hakuamini kile ambacho alikuwa akikiona
mahali hapo, hakuamini kama hata Samuel na Sadiki nao walikuwa wameanza tabia za
kutoka nje ya shule kama wanafunzi wengine.
Huo ukaonekana kuwa
ushahidi tosha kwa Chepuo kwamba hata katika kipindi ambacho angeamua kuwachafua
basi asingepata kazi kubwa.
Siku iliyofuata, asubuhi na mapema Chepuo
akaanza kuwaambia vijana ambao walikuwa katika kundi la Black Ninja juu ya kile
alichokuwa amekiona usiku uliopita. Wanafunzi wengi hawakuamini, bado Samuel na
Sadiki waliendelea kuonekana watakatifu katika macho yao.
Hata jambo
hilo lilipofikishwa kwa walimu, kwanza wanafunzi ambao walipeleka jambo hilo
ofisini wakaadhibiwa kwa kuwa walionekana kupeleka taarifa za uongo kwa ajili ya
kuwachafua watu ambao walikuwa wakijuliakana kwa utakatifu shuleni
hapo.
Tetesi hizo hazikuishia hapo, bado zilikuwa zikiendelea kusikika
zaidi na zaidi kiasi ambacho walimu nao wakataka kuhakikisha kile ambacho
kilikuwa kikiendelea.
Muda ulionekana kuisha katika kipindi hicho.
Mitihani ya mwisho wa mwaka ikawa imekwishafika na hivyo Samuel na Sadiki
kutulia na kuanza kujisomea huku wakiacha tabia za kwenda boda.
Walimu
wakajitahidi kuwaweka wapelelezi wao kwa ajili ya kuwafanyia kazi ya
kuwapeleleza watu hao lakini mwisho wa siku Samuel na Sadiki wakaonekana
kusingiziwa.
“Nimejua tu kwamba hizi zitakuwa tetesi za kutaka
kuwachafua watumishi wa Mungu,” Mwalimu mkuu, Massawe aliwaambia walimu
wenzake.
“Unajua mara ya kwanza niliposikia uzushi huu nilishtuka
sana. Niliuhisi mwili wangu ukitetemeka sana,” Mwalimu Agness aliwambia walimu
wenzake.
Mpaka shule inafungwa, bado Samuel na Sadiki walionekana
watakatifu kupita kawaida. Katika siku ya kuondoka kuelekea nyumbani, Samuel na
Sadiki wakaanza kuleta visingizio kwamba walitakiwa kwenda kwa ndugu zao hapo
Moshi jambo ambalo wala halikuonekana kuwatia wasiwasi walimu.
Kwa
Mariamu na Catherine, wao wakajifanya wanakwenda Arusha kwa ndugu zao huku
malengo yao yakiwa ni kukutana sehemu na kisha kutumia usiku mzima pamoja katika
hoteli yoyote ile.
Kila kitu walichokuwa wamekipanga kikaonekana
kukamilika bila matatizo yoyote yale. Wakakutana Moshi mjini na kuelekea
Kibororoni ambapo huko wakachukua vyumba katika hoteli na kulala na wasichana
wao.
“Nashangaa kwa nini nilikuwa nikipitwa na mambo haya,” Samuel
alimwambia Catherine.
“Mambo gani?” Catherine aliuliza huku akiwa
amemlalia Samuel kifuani.
“Haya ya kulaliwa kifuani na binti mrembo
kama wewe. Yaani sijui nilikuwa nachelewa vipi kuyajua,” Samuel alimwambia
Catherine.
“Tatizo ulijifanya kuwa mtu wa dini sana.”
“Hilo
ndilo kosa lenyewe. Unajua baba yangu ni mchungaji, mama yangu nae kiongozi wa
kanisa, basi tabu tupu. Raha kama hizi unafikiri ningezitoa
wapi?”
“Mmmh! Pole yako.”
“Asante sana.”
Usiku huo
hawakulala, walikuwa wakifanya mapenzi tu. Kilichokuwa kikitokea kwa Samuel na
ndicho kilichotokea kwa Sadiki katika chumba cha pili.
Kila mtu katika
alikuwa na msichana wake, hawakutaka mambo ya kuingiliana. Japokuwa katika
kipindi cha zamani muda wa kuondoka shuleni walikuwa wakiondoka na vitabu vyao
vya dini kama Qur-an na Biblia, katika kipindi hicho walikuwa wameziacha
shuleni.
Kwa wakati huo dini ikaonekana kuwaendea kushoto, hakukuwa na
mtu yeyote ambaye alikuwa akikumbuka kwamba alikuwa ametoka katika familia
ambazo zilikuwa na msimamo mkubwa wa dini, vitu ambavyo walikuwa wakivijali ni
kula raha na wasichana hao tu.
Walikaa katika hoteli hiyo kwa siku
moja na ndipo walipoamua kuanza safari ya kuelekea Dar es Salaam. Ndani ya basi,
kila mmoja alikuwa amekaa na msichana wake, walikuwa wakibusiana na kushikana
hapa na pale.
Mioyo yao kwa wakati huo ilikuwa imejaa dhambi,
walionekana kumsahau Mungu ambaye aliwapa bahati ya kuzaliwa katika familia
ambazo zilikuwa zimewapa misingi ya dini maishani mwao.
“Tukifika Dar
es Salaam ndiyo itakuwa mwisho wa kuonana Sadiki?” Mariamu alimuuliza
Sadiki.
“Yaani huko ndipo ambapo mapenzi yatazaliwa upya. Itatupasa
kufanya kitu kimoja,” Sadiki alimwambia Mariamu.
“Kitu
gani?”
“Tuanze kwenda tuisheni kule Mchikichini ili tuwe tunaonana
kila siku,” Sadiki alimwambia Mariamu.
“Hakuna tatizo. Ungemwambia
Samuel na Catherine basi ili tuwe wote,” Mariamu alimwambia
Sadiki.
Kwa haraka bila kuchelewa Sadiki akamuita Samuel na kumpa
taarifa juu ya kile walichokuwa wamekipanga na Mariamu ambacho kilitakiwa
kufanyika mara watakapofika jijini Dar es salaam. Hakukuwa na mtu aliyepinga,
jambo lile likakubaliwa na kila mtu kwa sababu waliona kwamba lingewafanya kuwa
karibu zaidi.
****
Maisha yao yalikuwa yamekwishabadilika
kabisa, kitu ambacho walikuwa wakikifikiria katika kipindi hicho ni kufanya
mapenzi na wapenzi wao tu. Nyumbani hawakutulia, mara kwa mara walikuwa
wakionana na wapenzi wao ambao walikuwa wakiwavutia kila aliyekuwa
akiwaangalia.
Kasi zao za kwenda msikitini na kanisani hawakuwa nazo
tena, walikuwa wakimtumikia shetani bila kujitambua. Wazazi wao wala hawakuwa na
wasiwasi, bado walikuwa wakiendelea kuwaamini watoto wao kwa kuona kwamba ni
masomo ndio ambayo yalikuwa yamewaweka bize kwa wakati huo mpaka kutokwenda
katika nyumba za dini.
Kila mwisho wa wiki walikuwa wakielekea
ufukweni kwa ajili ya kula raha na wapenzi wao hao. Katika kipindi hicho,
walikuwa wakichukia ibada kupita kawaida. Hayo ndio maisha ambayo waliamua
kuishi katika, kupenda starehe ndogondogo za hapa na
pale.
“Umebadilika sana Samuel. Tatizo nini mtoto wangu?” bi Magreth
alimuuliza mtoto wake, Samuel.
“Nimebadilika! Nimekuwaje mama? Mbona
najiona kuwa kawaida tu,” Samuel alimwambia mama yake.
“Hapana Samuel.
Kipindi cha nyuma haukuwa hivi. Siku hizi hata kanisani hautaki kwenda. Kwa
nini?” bi Magreth alimuuliza Samuel.
“Huwa ninakwenda tuisheni mama,
sasa hivi ninaingia kidato cha nne, nisiposoma sana, nitafeli,” Samuel
alimwambia mama yake, Bi Magreth.
“Tuisheni mpaka jumapili muda wa
ibada?” bi Magreth aliuliza kwa mshangao.
“Ndio mama. Masomo yamekuwa
mengi sana na magumu,” Samuel alimwambia mama yake.
Mabadiliko ambayo
alikuwa nayo Samuel yakashindwa kujificha, bado yalikuwa yakionekana waziwazi
machoni mwa wazazi wake ambao kila siku walikuwa wakiendelea kumsisitizia
kuelekea kanisani na kusali. Kutokana na kuingia katika maisha ya kumtumikia
shetani, hata ibadani kulionekana kuwa kugumu kwenda jambo ambalo lilimfanya
baba yake, mchungaji Mpelele kumuita na kumuweka kikao mara kwa
mara.
“Umeanza kumtumikia shetani?” Mchungaji Mpelele alimuuliza
Samuel huku akionekana kuwa na hasira.
“Hapana baba.”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kumbe unamtumikia
nani siku hizi?”
“Namtumikia Mungu.”
“Mungu huyu huyu wa
Ibrahim, Isaka na Yakobo au mungu mwingine?” Mchungaji Mpelele alimuuliza
Samuel.
“Huyu huyu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo.”
“Hapana.
Kama unamtumikia Mungu huyu, utakuwa umekosea sana, Mungu huyu tunayemtumikia
huwa hatumikiwi kama ambavyo unamtumikia Samuel,” mchungaji Mpelele alimwambia
Samuel.
“Ninamtumikia Mungu huyuhuyu,” Samuel alimwambia baba yake,
mchungaji Mpelele.
“Kwanza siku hizi kanisani hauendi. Kweli au
uongo?” Mchungaji Mpelele aliuliza.
“Kweli.”
“Kwa
nini?”
“Naingia kidato cha nne baba, nakuwa bize na masomo,” Samuel
alimwambia baba yake, mchungaji Mpelele.
“Usitake kunitania. Hivi
Mungu na masomo nani bora?”
“Mungu.”
“Nisikilize Samuel.
Utaweza kusoma usiku na mchana, ukakesha katika maisha yako yote ukisoma, ila
kumbuka kwamba bila Mungu, unakesha bure mwanangu. Kusoma sana si kufaulu,
unaweza ukasoma sana na usifaulu ila ukimtumikia Mungu hata usiposoma sana,
utafaulu kwani yeye anajua kila kitu, atakufanya usome muda mchache lakini vile
ambavyo utavisoma ndivyo ambavyo vitakavyotoka katika mtihani yako,” Mchungaji
Mpelele alimwambia Samuel.
“Naomba unisamehe
baba.”
“Haujanikosea mimi, umemkosea Mungu muumba Mbingu na Nchi.
Nenda mbele zake na umuombe msamaha,” Mchungaji Mpelele alimwambia
Samuel.
Japokuwa mchungaji Mpelele alikuwa ameongea maneno mengi kwa
kijana wake, Samuel lakini wala hakuweza kubadilika kabisa, maisha ya anasa
yakaonekana kumteka kabisa. Kila siku alikuwa akionana na Catherine na kuendelea
na maisha yao kama kawaida yao, maisha ya kwenda ufukweni na sehemu nyingine za
starehe.
Maisha ambayo alikuwa akiishi Samuel yalikuwa ni sawa na
maisha ambayo alikuwa akiishi Sadiki. Katika kipindi hiki mapenzi yakaonekana
kumteka Sadiki, hakutaka kabisa kwenda katika nyumba ya ibada, msikitini
kuswali.
Ile kasi yake ya kwenda msikitini kila siku katika kipindi
cha nyuma, kwa wakati huo ikaonekana kupungua kabisa mpaka kufikia kipindi
kutoweka kabisa.
Sadiki akachukia ibada za msikitini, msikiti kwake
ukaonekana kama jela, sehemu ambayo ilionekana kuwa si nzuri kwa kijana kama
yeye. Kanzu nyingi ambazo alikuwa akipenda sana kuzivaa katika kipindi hicho
alikuwa amezifungia kabatini na kuanza kuvaa majinzi pamoja na fulana ambazo
aliziona kuwa nzuri.
Baba yake, Ustadhi Hamidu alijitahidi sana
kuongea nae lakini hakuonekana kuelekea kabisa. Kila siku alikuwa akitoka na
kujifanya kuelekea tuisheni kumbe alikuwa akienda kuonana na Mariamu wake ambaye
alikuwa akitumia muda mwingi kuwa pamoja nae.
Maisha yake yakaonekana
kuzidi kuharibika kadri siku zilivyozidi kwenda mbele, hofu ya Mungu ikaonekana
kutoweka moyoni mwake, alikuwa akijifanyia vitu ambavyo alikuwa akitaka
kuvifanya kwa wakati huo, vitu ambavyo havikuwa vikitakiwa kufanyika na mtu
aliyekuwa akimcha Mungu.
“Maisha yako yamebadilika sana Sadiki,
umeanza kuwa firauni sasa,” Ustadhi Hamidu, Imamu wa msikiti wa Kichangani
alimwambia mtoto wake, Sadiki.
“Hapana baba, mbona naishi maisha kama
zamani,” Sadiki alimwambia baba yake, Ustadhi Hamidu.
“Usinidanganye.
Siku hizi hata msikitini hautaki kwenda. Ijumaa iliyopita nilikwambia twende
kwenye Maulidi, ukanipiga piga chenga weee ukanipotea,” Ustadhi Hamidu
alimwambia sadiki.
“Nilikwenda baba ila sikuongozana
nawe.”
“Usitake kunidanganya. Hivi wewe mtoto siku hizi una nini? Kwa
nini hautaki kumuabudu Allah? Hivi kuna nani ambaye unamuabudu zaidi ya Allah?”
Ustadhi Hamidu alimuuliza Sadiki.
“Namuabudu Allah.”
“Labda
Allah mwingine lakini si Allah ninayemfahamu mimi, labda si Allah ambaye
alimuongoza Mtume wetu, Mohammad S.A.W katika kila njia njema maishani mwake.
Kwa sasa umekuwa kama Firauni Sadiki. Badilisha maisha yako, usipobadilisha,
utapotea,” Ustadhi Hamidu alimwambia Sadiki.
Wazazi wote wa pande zote
mbili walionekana kuumia, mabadiliko mabaya ambayo walikuwa nayo watoto wao
yalionekana kuwaumiza kupita kawaida.
Walijua fika kwamba watoto wao
walikuwa wamebadilika na kuziacha njia ambazo walitakiwa kuzifuata, walionekana
kuvutiwa na dunia pamoja na mambo yake ya anasa ambayo yakaonekana kuwapoteza
zaidi endapo wangeendelea
kuyatumikia.
Siku ziliendelea kukatika
mpaka siku ambayo wanafunzi walitakiwa kurudi shuleni. Kila mmoja alionekana
kukasirika kwani walijua fika kwamba kila kitu ambacho walikuwa wakikifanya
nyumbani basi kingeweza kufanyika kisiri shuleni ili kuwazuia wanafunzi wengine
wasijue kile ambacho kilikuwa kikiendelea katika maisha yao.
Samuel na
Sadiki walikuwa wamezoeana sana na wapenzi wao kiasi ambacho kilionekana kuwa
ngumu kuwatenganisha, kuwakataza wasikae pamoja katika kipindi cha kujisomea au
kula.
Ukaribu wao ule ndio ambao ukawafanya wanafunzi wengine
kugundua kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kikiendelea kwa wanafunzi
hao.
Kwa kuwa shule ilikuwa ikitumia umeme, nyakati za usiku ambazo
umeme ulikuwa ukikatika, walikuwa wakishikana sana huku wakibadilishana mate kwa
kipindi kirefu. Mpaka jenereta linawashwa, tayari walikuwa wamechezeana vya
kutosha jambo ambalo liliifanya miili yao kushikwa chachu kubwa ya kufanya
mapenzi.
Kutoroka hakukukoma, mara kwa mara walikuwa wakitoroka pamoja
kuelekea nje ya shule ambapo huko kama kawaida yao walikuwa wakifanya vitu vyao
vingi vya ngono na mambo mengine. Kwa sababu walikuwa wamejifunza kunywa pombe,
wakajikuta wakinunua vilevi hivyo siku za mwisho wa wiki na kunywa
taratibu.
Walimu walipopelekewa kile ambacho kilikuwa kikiendelea
katika maisha ya wanafunzi hao, bado waliendelea kutokuamini kabisa kwani watu
hao waliendelea kuwa watakatifu katika macho yao kutokana na unafiki ambao
walikuwa wakiwaonyeshea kila walipokuwa wakijua wanaangaliwa na walimu
hao.
“Astaghafilullah! Yaani mimi nitembee na msichana?” Sadiki
aliuliza huku akijifanya kushtuka mara alipoitwa ofisini na kuulizwa juu ya
Mariamu.
“Ndio. Tumeletewa kesi kwamba unatembea na Mariamu tena
wakati mwingine mnaruka ukuta na kwenda boda,” Mwalimu Michael, mwalimu wa
nidhamu alimwambia Sadiki.
“Hii ni kashfa nzito sana kwangu mwalimu.
Siwezi kuongea neno lolote baya kwa watu ambao wanaeneza habari hiyo.
Ninachotaka kusema ni kimoja tu kwamba Allah ninayemuabudu anayaona maumivu
ninayoyasikia moyoni mwangu. Atanilipia tu,” Sadiki alimwambia mwalimu
Michael.
Maneno yake pamoja na mshangao mkubwa wa kinafiki ambao
alikuwa ameuonyesha mahali pale ukawafanya walimu kuendelea kuamini kwamba yale
yalikuwa ni maneno ambayo yalikuwa yameanzishwa na wanafunzi ambao walionekana
kuwa na chuki juu ya Sadiki na walifanya hivyo kwa kuwa walitaka kumuharibia kwa
sababu alikuwa mtumishi wa Mungu.
Walimu hawakuishia hapo,
walichokifanya ni kumuita Samuel na kumuuliza kuhusu tetesi ambazo walikuwa
wamezisikia kuhusiana na Catherine, kama ilivyokuwa kwa Sadiki, nae Samuel
akajifanya kushtuka kupita kawaida kana kwamba alikuwa ameambiwa taarifa nzito
ya uongo masikioni mwake.
“Yesu wangu! Mimi nifanye hivyo? Sasa
kutakuwa na maana gani ya kuwa Mwenyekiti wa Casfeta mkoani Kilimanjaro?
Kutakuwa na umuhimu gani wa kumuomba Mungu nyakati za usiku, kutakuwa na umuhimu
gani wa kwenda kanisani?” Samuel aliuliza maswali mfululizo.
Hakukuwa
na mwalimu ambaye alionekana kuuamini uvumi ule kutokana na wahusika kuruka
kupita kawaida. Kadri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo uvumi ule
ulivyozidi kusikika zaidi na zaidi jambo ambalo liliwafanya baadhi ya walimu
kuanza kufuatilia wao wenyewe ili kuhakikisha kwamba ulikuwa ni uvumi au
kweli.
****
“Mkitaka kufuatilia ninyi wenyewe hamuwezi
kuwaona,” Chepuo alikuwa akiwaambia walimu ofisini.
“Kwa nini
tusiweze?”
“Kama wanaondoka saa saba za usiku, mtaweza kuwaona?”
Chepuo aliuliza.
“Kwa hiyo tufanye nini ili tuweze
kuwaona?’
“Nipeni simu.”
“Eeeh! Sasa simu ya nini
tena?”
“Si ili nikiwaona niwapigie mje
kuhakikisha.”
“Mmmh!”
“Nini tena?”
“Hatukuamini
Chepuo. Usije ukaiuza hata simu yenyewe. Mtu mwenyewe dakika moja mbele wewe,”
mwalimu Michael alimwambia.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Basi milele
hamtoweza kuujua ukweli. Huu ni mwezi wa nane kumbukeni, miezi miwili baadae
wanafanya pepa halafu wanasepa,” Chepuo aliwaambia walimu.
“Sawa.
Ngoja tukupe simu halafu utuambie wakiondoka usiku,” mwalimu mkuu, Massawe
alimwambia Chepuo na kumkabidhi simu ambayo hakuwa akiitumia.
Katika
kipindi hicho, walimu walikuwa wamejaribu kwa kiasi kikubwa kufuatilia lakini
hawakuweza kufanikiwa mpaka pale ambapo wakaonekana kuhitaji msaada kutoka kwa
Chepuo, mwanafunzi ambaye alionekana kutokuwa na nidhamu shuleni
pale.
Kutokana na chuki kubwa ambayo ilijengeka moyoni mwa Chepuo juu
ya Samuel na Sadiki, moja kwa moja akaomba kupewa kazi ya kuwahakikishia walimu
juu ya zile tetesi ambazo zimekuwa zikiendelea kusikika kwa zaidi ya miezi
saba.
Walimu hawakuwa na jinsi, katika kipindi hicho walikuwa wakitaka
kujua ukweli juu ya kile ambacho kilikuwa kikiendelea katika maisha ya Samuel na
Sadiki, walitaka kuufahamu ukweli kwamba wawili hao walikuwa wakitoroka shuleni
hapo na wasichana au la.
Chepuo akapewa kazi hiyo, akapewa simu ndogo
ya Nokia Obama kwa ajili ya kumpigia mwalimu Michael ambaye alikuwa akilala
shuleni hapo katika kipindi ambacho angewaona Samuel na Sadiki wakitoka nje ya
shule pamoja na wasichana hao.
Chepuo akaonekana kufurahia, hakuamini
kama kwa wakati huo walimu walikuwa wamemuamini mpaka kumpa kazi hiyo. Kwanza
alipofika bwenini, hakutaka kumwambia mwanafunzi yeyote juu ya simu ambayo
alikuwa amepewa, alitaka kufanya kila kitu kimyakimya kwani alijua fika kwamba
kama angeamua kuwaambia wanafunzi wengine ambao walikuwa katika kundi lake la
Black Ninja basi siri ingeweza kuvuja.
Siku ya Jumamosi usiku wa saa
saba, kama kawaida yake Chepuo akainuka kutoka kitandani na moja kwa moja
kuelekea katika kitanda cha Samuel huku wanafunzi wakiwa wamelala. Akaanza
kupapasa kitandani pale, hakukuwa na mtu yeyote. Chepuo hakuishia hapo,
alichokifanya ni kuelekea katika kitanda cha Sadiki, nae hakuwepo kitandani
hapo.
Moja kwa moja akili yake ikamwambia kwamba wawili hao tayari
walikuwa wametoka bwenini na kuelekea boda kama kawaida yao. Kwa kasi ya ajabu
akaanza kuvaa nguo zake na kisha kuelekea nje ya bweni hilo. Hakutaka kuchelewa,
akaanza kuelekea sehemu ambayo wanafunzi walikuwa wakiitumia sana kutorokea
kwenda nje ya shule.
“Wewe nani?” Ilisikika sauti ya mlinzi nyuma
yake. Chepuo akageuka.
“Haaaaa! Kumbe mwana. Inakuwaje?” Mlinzi
alimwambia Chepuo mara baada ya kumgundua.
“Poa. Hivi Samuel na Sadiki
wametoka leo?” Chepuo aliuliza.
“Yeah! Kama kawaida wametoka na malaya
wao. Mbona umewaulizia hivyo?” Mlinzi aliwauliza huku tayari akiwa amekwishapewa
fedha kama kutunza siri ya watorokaji shuleni hapo.
“Watumishi wa
Mungu wale,” Chepuo alimwambia mlinzi.
“Acha utani.”
“Kweli
tena. Yule Samuel ni mchungaji na Sadiki ni ustadhi wa shule,” Chepuo alimwambia
mlinzi ambaye alionekana kushangaa.
“Kama na wewe unataka kwenda boda
nenda tu ila si kuniambia maneno mengi ya uongo,” mlinzi alimwambia
Chepuo.
“Kweli tena mpwa. Unafikiri nakudanganya! Uliza shule
nzima.”
“Duuh! Kama ni kweli kumbe hata mimi naweza kuwa Ustadhi
mwamba,” mlinzi alimwambia Chepuo.
“Ndio hivyo. Umewaona wameelekea
wapi?”
“Wamekwenda upande wa kulia bila shaka watakuwa wakielekea kule
kwenye Ukumbi wa Manyasa”
“Basi poa. Cha msingi toka maeneo haya. Muda
wowote ule ticha anaweza kuja,” Chepuo alimwambia mlinzi.
“Poa poa.
Usijali.”
“Aminia. Nipe gwala,” Chepuo alisema na kisha kugongeshana
mikono na mlinzi na kuondoka mahali hapo huku simu aliyopewa na walimu ikiwa
mfukoni mwake.
Kwa harakaharaka Chepuo akapita katika uwazi mkubwa
ambao ulikuwa umetengenezwa na wanafunzi kwa ajili ya kutorokea na kutokea nje
ya shule ile.
Hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuanza
kuelekea katika ukumbi wa muziki ambao wanafunzi wa shule mbalimbali walikuwa
wakipenda sana kukutania usiku ambao walikuwa wakitoroka shuleni
kwao.
Siku hiyo, Chepuo hakujisikia kwenda nje ya shule kwa ajili ya
kufanya mambo yake, siku hiyo alijisikia kuelekea huko kwa sababu alitaka
kuwahakikishia walimu kwamba wale watu waliokuwa wakiwaamini hawakuwa watakatifu
kama ambavyo mioyo yao ilivyokuwa ikifikiria juu yao.
Ukumbi wa
Manyasa uliokuwa Moshi mjini uliendelea kutoa burudani ya muziki kwa kiingilio
cha shilingi elfu tatu tu. Watu walikuwa wamejazana ndani ya ukumbi huo,
wanafunzi kutoka katika shule mbalimbali kama Majengo, Huru, Northern Highland
pamoja na shule nyingine walikuwa wakifika ndani ya ukumbi huo kwa wingi
sana.
Burudani ya muziki bado ilikuwa ikiendelea ndani ya ukumbi huo
huku asilimia kubwa ya watu ambao walikuwa ndani ya ukumbi huo wakiwa wanafunzi
wa shule mbalimbali hapo Moshi Mjini.
Wanawake ambao walikuwa
wakijiuza hawakukosa mahali hapo, biashara yao bado ilikuwa ikiendelea kama
kawaida. Wateja walikuwa wakifika kwa wingi, walikuwa wakiwanunua na kisha
kufanya nao ngono katika vyoo vya ukumbi huo au hata katika sehemu ambazo
zilikuwa na giza.
Chepuo akafika katika ukumbi huo, siku hiyo hakutaka
kuongea na mtu yeyote yule jambo ambalo lilimfanya kuvua fulana yake na
kukifunika kichwa chake huku akibaki na kaoshi pamoja na suruali mwilini mwake.
Alipofika mlangoni, akatoa kiasi ambacho kilikuwa kikihitajika na kisha kuingia
ndani ya ukumbi ule wa Manyasa.
Macho ya Chepuo hayakutulia sehemu
moja, yalikuwa yakiangalia huku na kule, alikuwa akiwatafuta wabaya wake ndani
ya ukumbi ule. Watu walikuwa wakicheza kifujofujo, Chepuo akaanza kupiga hatua
kuelekea katika sehemu ambayo ilikuwa na kigiza, sehemu ambayo watu ambao
hawakutaka kujulikana walikuwa wakiitumia sana kukaa na wasichana
wao.
Alipofika karibu na sehemu ile, akaanza kuangalia katika vikochi
kadhaa ambavyo vilikuwa mahali pale. Macho yake yakatua nyusoni mwa watu ambao
alikuwa na uhakika kwamba walikuwa wabaya wake. Chepuo hakutaka kuonekana kuwa
na presha, alichokifanya ni kusogea na kuanza kuwaangalia
vizuri.
“Ndio wenyewe,” Chepuo alisema huku akiachia tabasamu
pana.
Mpaka kufika kipindi hicho akawa na uhakika kwamba watu ambao
walikuwa wamemfanya kufika katika ukumbi ule alikuwa amekwishawaona jambo ambalo
lilimfanya kuanza kuwafuatilia kwa karibu sana, hakutaka awapoteze machoni
mwake.
Samuel na Sadiki walionekana kutokuwa na habari kabisa,
walikuwa wakishikanashikana na wapenzi wao, Catherine na Mariamu bila kujua
kwamba Chepuo alikuwa ndani ya ukumbi ule akiwaangalia tu.
Matendo ya
kimalavidavi yalionekana kuwatawala mahali pale, walikuwa wakinyonyana mate huku
wakishikana katika maungo yao ya siri. Kutokana na kofia ambazo walikuwa
wamezivaa vichwani mwao ili kuwafanya kutokugundulika na watu mbalimbali ndizo
ambazo zilionekana kuwa ulinzi kwao machoni mwa watu wengine.
Watu
ambao walikuwa wakijulikana kama watumishi wa Mungu kwa walimu wao, watu ambao
walikuwa wakiaminika kwamba ni watakatifu kwa walimu wao, katika kipindi hicho
walikuwa ndani ya ukumbi wa Manyasa, ukumbi mkubwa ambao ulikuwa ukisifika kwa
kutoa burudani kabambe ndani ya mkoa wa Kilimanjaro.
Saa 9:17 usiku
ndio ulikuwa muda ambao Samuel na wenzake wakainuka mahali pale kwa ajili ya
kuondoka ukumbini hapo. Chepuo alivyoona hivyo, kwa haraka sana akatoka nje ya
ukumbi na kisha kwenda kujibanza sehemu huku macho yake yakiwa katika mlango wa
kutokea katika ukumbi ule.
Akawaona Samuel, Sadiki, Catherine na
Mariamu wakiwa wanatoka nje ya ukumbi ule. Kwa haraka sana akaanza kuelekea
katika sehemu ambazo zilikuwa na bodaboda na kisha kuchukua moja ambayo
ilimpeleka mpaka nje ya shule yao. Akamlipa dereva na kisha kuchukua simu yake
na kisha kuanza kumpigia mwalimu Michael.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Pokea simu basi
kabla hawajafika,” Chepuo alijisemea mara simu ilipoanza kuita. Simu iliendelea
kuita mpaka kukata, Chepuo akaamua kupiga tena, simu ile ikaanza kuita mpaka
ikapokelewa.
“Hallow....” Sauti ya mwalimu Michael ilisikika
kichovu.
“Ticha unalala utafikiri umekufa,” Chepuo alimwambia mwalimu
Michael.
“Kuna nini? Mbona usiku sana?”
“Toka nje basi uje
kuhakikisha kwa macho yako.”
“Kuhakikisha nini?”
“Kwamba
watumishi wa Mungu nao wamekwenda kwenye klabu ya usiku” Chepuo alimwambia
mwalimu Michael.
“Watumishi gani?”
“Samuel Mpelele na Sadiki
Hamidu,” Chepuo alijibu.
“Upo wapi wewe?”
“Njoo huku nyuma
ya jiko la shule.”
“Sawa.”
Simu ikakatwa, tabasamu pana
likaanza kuonekana usoni mwa Chepuo kwa kuona kwamba siku hiyo ndio ingekuwa
siku ambayo kila kitu kingekwenda kujulikana kwa kila mtu kwamba Samuel na
Sadiki walikuwa wakitoka usiku na kwenda katika klabu za starehe pamoja na
wasichana.
Ndani ya dakika tatu, mwalimu Michael akatokea sehemu ile
huku akiwa amevaa bukta na koti kubwa. Macho yake yalipomuona Chepuo amesimama
karibu na tundu kubwa la ukuta, akaanza kumfuata.
“Wapo wapi?” Mwalimu
Michael aliuliza.
“Usiwe na presha ticha, wewe subiri tu utawaona,”
Chepuo alimwambia mwalimu Michael.
Ndani ya dakika ishirini, baadhi ya
wanafunzi wengine wakaonekana wakianza kuingia ndani ya eneo la shule hiyo
akitokea katika ukumbi wa starehe wa Manyara. Kila mwanafunzi ambaye alikuwa
akitokea mahali hapo, alikuwa akiwekwa pembeni kwa ajili ya kuandikwa majina na
baadae kupewa adhabu.
Waliendelea kusubiri zaidi na zaidi lakini watu
ambao walikuwa wakiwasubiria mahali hapo wala hawakutokea jambo ambalo
lilimshangaza sana Chepuo.
Ilipofika saa 10:15 alfajiri, mwalimu
Michael akaonekana kuchoka kuvumilia, hapohapo akaamua kwenda katika bweni
ambalo Samuel na Sadiki walikuwa wakilitumia, alipoingia ndani, moja kwa moja
akaelekea katika vitanda ambavyo walikuwa wakilalia, akawakuta wakiwa wamelala
usingizi mzito.
“Mmmh! Sasa mbona wapo humu?” mwalimu Michael
alijiuliza huku akionekana kushangaa.
Hakutaka kubaki mahali hapo,
alichokifanya ni kuanza kuondoka kuelekea nje ya bweni lile na kisha kumfuata
Chepuo kule alipokuwa pamoja na wanafunzi wengine. Alimpomfikia, akamuita
pembeni na kisha kuanza kuongea nae.
“Una uhakika kwamba Samuel na
Sadiki walitoka nje ya shule usiku huu?” Mwalimu Michael alimuuliza
Chepuo.
“Nina uhakika. Nimewaona mimi mwenyewe kwa macho yangu ndani
ya ukumbi wa Manyasa,” Chepuo alisema huku akiapa.
“Unavyoona watakuwa
wamerudi au watakuwa bado nje ya shule?” Mwalimu Michael
alimuuliza.
“Bado watakuwa nje ya shule, hawajapitia hapa,” Chepuo
alijibu.
“Sawa. Ila kwa nini kila siku umekuwa mtu wa kuongea mambo ya
uongo juu ya watumishi wa Mungu?” Mwalimu Michael alimuuliza
Chepuo.
“Uongo gani tena ticha?”
“Kwamba watu hawa wameanza
kwenda kwenye kumbi za starehe.”
“Ila kweli wamekwenda kwenye kumbi
za starehe.”
“Mbona nimewaona bwenini wamelala,” mwalimu Michael
alimwambia Chepuo maneno ambayo yalionekana kumshtua.
“Unasemaje?”
Chepuo aliuliza huku akionekana kushtuka.
“Nimewakuta bwenini
wamelala.”
“Haiwezekani. Hawajapita hapa, utakuwa umechanganya vitanda
ticha,” Chepuo alimwambia mwalimu Michael huku akionekana
kutokuamini.
Hapo hapo wakaanza kuondoka kuelekea katika bweni lile na
kisha kuingia ndani. Wakaanza kuelekea katika vitanda vile na kumuonyeshea
Chepuo kwamba Samuel na Sadiki walikuwa wamelala. Ili kuhakikisha juu ya kile
ambacho alikuwa akimwambia, akawaamsha, ni kweli walikuwa wenyewe ambao
walionekana kuwa na usingizi mzito.
“Umeamini?” mwalimu Michael
alimuuliza Chepuo.
“Imekuwaje? Mbona pale hawakupita?” Samuel aliuliza
huku akionekana kushangaa.
“Wewe ni muongo. Asubuhi nitakuadhibu kwa
adhabu ya kuchimba shimo la takataka. Kosa lako kubwa ni kuwasingizia watumishi
wa Mungu ili wafukuzwe shule, kosa lako la pili ni kuniamsha wakati nikiwa naota
njozi nzuri,” mwalimu Michael alimwambia Chepuo ambaye alikuwa amebaki na
mshangao mkubwa huku swali likibakia kichwani mwake, walipitia wapi watu wale
kuingia shuleni.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment