Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

PAINFUL MEMORIES - 5

 





    Simulizi : Painful Memories

    Sehemu Ya Tano (5)



    Moyo wa Rahman ulikuwa na hasira kupita kawaida. Hakuonekana kuwa na furaha kabisa kumuona msichana ambaye alikuwa akimpenda akiolewa na mwanaume mwingine tofaut na yeye. Hakumjua mwanamke ambaye alitarajia kumuoa Uki, ila kitu ambacho alikuwa akikitaka kufanya mahali hapo ni kitu kimoja tu ambacho kitawafanya wao wote kukosa.

    Hapo ndipo wazo la kusababisha ajali lilipomjia kichwani mwake. Hakutaka kumuacha Uki hai, alitaka kumuua kwa kifo ambacho kisingemfanya mtu yeyote kujua kwamba yeye ndiye aliyehusika katika kifo hicho. Akawandaa vijana wake wawili, kitu alichotaka kufanya mahali hapo ni kulegeza breki za gari ambalo alikuwa akilitumia Uki.

    Rahman akasafiri kutoka nchini Afrika Kusini na kuja Tanzania na kisha kukutana na hao vijana ambao walikuwa wamejiandaa vilivyo huku wakijua mambo mengi kuhusiana na magari. Kitu alichokifanya Rahman ni kuwapa kiasi cha shilingi milioni tano kama kianzio cha kazi hiyo.

    “Mkikamilisha nitawamalizia na milioni tatu” Rahman aliwaambia.

    Fedha ndizo zilionekana kuwa kila kitu kwa wakati huo, vijana wale wawili, Iddi na John wakajiandaa kwa ajili ya kufanya kazi ambayo walikuwa wameagizwa kuifanya. Ujauzito wa Uki ulikuwa ukitangazwa sana katika vyombo vya habari, kwa wakati huo kitu ambacho walikuwa wakikitaka ni kuifuatilia ratiba yake ya wiki nzima likiwa lile suala la kwenda kliniki.

    Wala haikuwa kazi kubwa sana kwa upande wao, kwanza wakaifahamu hospitali ambayo Uki alikuwa akielekea mara kwa mara kama huduma zake za kliniki na hata muda ambao alikuwa akielekea huko wakaufahamu. Waliporudi katika chumba ambacho walipanga, wakaanza kupanga mipango yao ya namna ya kusababisha ajali ambayo ilionekana kuwa kitu kizuri kufanyika.

    Mipango ikapangwa na baada ya hapo, wakaelekea katika duka la vifaa vya gari na kununua vifaa vyote ambavyo vilikuwa vikihitajika katika kazi yao ya kulegeza breki ya gari. Walipopewa kila kitu, wakarudi katika chumba ambacho walikuwa wamepanga na siku iliyofuatia, walikuwa karibu na nyumba ya Edmund kwa ajili ya kumfuatilia Uki ambaye siku hiyo alikuwa na ratiba ya kuelekea kliniki katika hospitali ya Ocean Road.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walilifuatilia gari lile mpaka pale ambapo likaingia katika eneo la hospitali ile. Walipoliona limepaki na Uki kutoka gari pamoja na Uki, nao wakaanza kupiga hatua kuingia ndani ya eneo la hospitali ile na kisha kuanza kuangalia huku na kule kuona kama kulikuwa na watu walikuwa wakiwafuatilia, hakukuonekana kuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa na habari nao..

    Kwa haraka sana Iddi akaelekea upande wa pili wa gari na kisha kujifanya kufunga kamba za viatu na kuingia chini ya uvungu wa gari lile. Akachukua vifaa vyake na kuanza kuifanya kazi yake kwa umakini mkubwa sana. Alitumia dakika chache akawa amekwishakamilisha kazi ile na kutoka.

    “Vipi?” John aliuliza.

    “Nimeilegeza breki” Iddi alijibu.

    “Kwa hiyo inabidi tuifuatilie mpaka pale ambapo itakapopata ajali”

    “Nina uhakika na kazi yangu. Wewe tuondoke tu na wala tusipoteze muda” Iddi alisema.

    Walchokifanya mahali hapo ni kuondoka na kurudi katika chumba ambacho walikuwa wamepanga katika hoteli ya La Vista Inn iliyokuwa Magomeni. Saa mbili kamili, taarifa ya habari ikatangazwa na habari juu ya ajali mbaya ambayo ilitokea maeneo ya daraja la Salender ndio ilikuwa ya kwanza. Iddi na John wakafurahia sana kwa kuona kwamba mpango wao wote ulikuwa umekamilika.

    Walichokifanya kwa wakati huo ni kumtaarifu Rahman ambaye akafika ndani ya chumba kile huku akionekana kuwa na furaha na kisha kuwalipa kiasi ambacho kilikuwa kimebaki. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na wasiwasi kabisa, kwa jinsi ajali ilivyokuwa ikitangazwa, kila mtu alijua kwamba ni lazima Uki angekufa tu huko huko hospitalini.

    Baada ya kukaa siku mbili nchini Tanzania baada ya ajali ile, Rahman akaamua kurudi nchini Afrika Kusini kuendelea na maisha yake huku moyo wake ukiwa na matumaini makubwa sana kwamba Uki angekufa huko huko hospitalini.

    ****

    Miezi iliendelea kukatika zaidi na zaidi huku Rahman akijitahidi sana kufuatilia kila wakati hai ambayo alikuwa akiendelea nayo Uki hospitalini. Baada ya miezi sita, hali ya Uki ikaanza kurejea kama zamani. Ile ikaonekana kuwa taarifa mbaya sana kwa Rahman lakini kwa wakati huo hakutaka kufanya kitu chochote, akajifanya kusahau huku akijiapiza kurudi tena na kumuua yeye pamoja na watoto ambao wangzaliwa.

    Mwaka wa kwanza ukapita, wa pili, wa tatu mpaka kufikika mwaka wa tano hapo ndipo Rahman alikuwa akitaka kufanya kile ambacho alikuwa amekipanga. Japokuwa kilikuwa kimepita kipindi kirefu sana lakini bado hasira zake zilikuwa juu ya Uki ambaye aimuona kama kumsaliti. Kwa wakati huu alikuwa amepanga mipango kabambe sana ambayo aliamini kwamba kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angepona.

    Alichokifanya ni kusafiri tena na kurudi nchini Tanzania kisiri na kisha kuonana na kundi jingine la uuaji ambalo lilikuwa likijiita Black Mask lililokuwa na makzi yake Temeke Mikoroshini. Mara baada ya kuonana nao, akapanga nao mipango ya kuwateketeza watoto wake hata kabla ya kumuua yeye mwenyewe.

    Kutokana na kubobea sana katika kufanya mauaji mbalimbali nchini Tanzania, kaziile kwao wala haikuonekana kuwa kubwa. Baada ya siku kadhaa kupita huku malipo makubwa yakiwa yamekwishafanyika, wakaliandaa lori lao ambalo lilitakiwa kuligonga gari lililokuwa likitumiwa na Eric na Erica kuelekea shuleni.

    Mwanaue mmoja alikaa maeneo ya Bamaga, njia panda ya kuelekea ubarozi wa Marekani huku lori lile likiwa limepakiwa kituo cha Macho, njia panda ya kuelekea katika ukumbi wa Maisha Club. Mara baada ya gari lile kuonekana Bamaga, simu ikapigwa na hivyo dereva wa lori kujiandaa kuliendesha lori lile.

    Ukiachilia mbali vijana hao, pia kulikuwa na vijana watatu ambao walikuwa wamekaa pamoja na gari lao katika kituo cha General Tyre, kituo ambacho walipanga gari lile ligongwe na kitu kingine kuendelea. 

    Dereva wa lori lile ambalo lilikuwa limebeba matofali akaanza kuliendesha lori lile kwa mwendo wa kasi kama gari ambalo lilikosa breki. Akaliendesha zaidi na zaidi mpaka alipokaribia katia kituo cha General Tyre, gari walilokuwa wakilitumia Eric na Erica kuelekea shuleni kuonekana mbele yake. 

    Dereva akaongeza kasi zaidi na zaidi na kisha kuanza kulifuata gari lile. Derev akajitahidi kulirudiaha gari nyuma ili lori lile lisiligonge gari lile lakini ikashindikana kutokana na kuwa na gari jingine kwa nyuma. Lori lile likaja na kuligonga gari lile, huku watu wakishikwa na mshangao, dereva wa lori akafungua mlango na kukimbia.

    Kwa haraka sana vijana ambao walikuwa wamelipaki gari lao pale kituoni, Genera Tyre, wakasogea karibu na gari lile na kisha kumtoa Eric na kumpakiza garini mwao huku wakijifanya kumsaidia. Gari likaondoka mahali hapo huku watu wakiwana kuwa wasamalia wema.

    “Kuna kikaratasi bosi alisema nimuwekee huyu mtoto mfukoni mwake” Kijana mmoja alisema huku akikitoa kikaratasi kile.

    “Kikaratasi gani?”

    “Mmmh! Wala sijui. Kimeandika BINADAMU” 

    “Poa. Fanya kama alivyotaka” 

    Hapo hapo, huku Eric akirusha mikono yake huku na kule, kijana yule akamuwekea kile kikaratasi katika mfuko wa shati lile. Walipofika katika hospitaliya Muhimbili, moja kwa moja Eric akapakizwa ndani ya machela na kisha kuanza kuskumwa kuelekea ndani ya hospitali ile.

    ******

    Mpaka Eric anakuja kusafirishwa na kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi, Rahman akaonekana kukasirika, kwa jinsi alivyojua matibabu makubwa ya India yangemfanya Eric kurudiwa na afya yake. Kwa kipindi hiki akataka kuwaua huko huko nchini India.

    Alichokifanya akasafiri kuelekea nchini India pamoja na vijana wake wanne. Akaanza kupeleleza hospitali ambayo Eric alikuwa amepelekwa na kisha kuanza kufanya mishemishe ya kumuua. Vijana wawili wakajifanya kuwa madaktari ambao mara kwa mara walikuwa wakifka hospitalni pale kwa ajili ya kuangalia njia ambazo wangeweza kuzitumia kufanikisha kile ambacho walitaka kukifanya kwa wakati huo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    Miezi iliendelea kukatika mpaka pale ambapo waliona kwamba hali ilikuwa shwari kufanya kile ambacho walitakiwa kukifanya. Usiku mmoja, huku vijana wake wakiwa wamevalia makoti makubwa na marefu ya kidaktari wakaanza kuingia ndani ya hospitali ile. Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa na wasiwasi nao, kutokana na hospitali ile kuwa kubwa sana, hata baadhi ya madaktari hawakuwa wakifahamiana.

    Moja kwa moja wakaanza kuelekea katika chumba ambacho alikuwa amelazwa Eric na kisha kutaka kuingia. Ndani kulikuwa na daktari mmoja pamoja na manesi wawili ambao walikuwa wakiendelea kumhudumia Eric ambaye alikuwa amepata nafuu. Wakasubiri mpaka yule daktari na nesi walipotoka na kisha wao kuingia ndani.

    Walichokifanya humo ndani ni kumuua Eric kwa kumchoma visu viwili kifuani na kisha kutoka ndani ya chumba kile na kuandika neno lililosomeka ‘BINADAMU’ mlangoni. Kila kitu ambacho walikuwa wakmekipanga kufanyika kwa mafanikio makubwa, hapo hapo wakaanza kutoka nje na kisha kumpigia simu Rahman ambaye alikuwa amejiandaa kumpigia simu Edmund.

    Rahman alipomaliza kuongea na vijana wake na kupewa taarifa ya mauaji ambayo yalikuwa yamefanyika, akaanza kuelekea katika hoteli ile aliyopanga Edmund na Uki na kisha kuelekea mapokezini.

    “Can I help you? (Naweza kukusaidia?)” Msichana wa mapokezi alimuuliza Rahman.

    “Yeah! You can. I want to make a call to my brother (Ndiyo! Unaweza. Nataka kumpigia simu kaka yangu)” Rahman alijibu.

    “Where is he? (Yupo wapi?)” Dada yule alimuuliza.

    “Room number 56 (Chumba namba 56)” Rahman alijibu.

    Hapo hapo yule dada wa mapokezi akachukua simu yake na kisha kuanza kupiga simu ya chumba kile alichokitaja Rahman. Alipoona simu imeanza kuita tu, hapo hapo akamgawia mkonga wa simu ile Rahman. Simu iliendelea kuita zaidi na zaidi na kisha kupokelewa.

    “ERIC” Rahman alisema na kisha kukata simu.

    Rahman hakutaka kubaki mahali hapo, akaanza kuelekea katika makochi ambay yalikuwa pembeni na kisha kutuia huku vijana wake ambao walikuwa wamevalia suti wakiwa mahali pale. Haikupita hata dakika moja, Edmund akaonekana akianza kushuka ngazi huku akiwa na haraka sana na kisha kutoka nje.

    Rahman hakutaka kusubiri, alichokifanya yeye na vijana wake ni kuchukua lifti na kisha kuelekea katia ghorofa namba tano na kisha kuanza kukitafuta chumba hicho ambacho mara baada ya kukiona, wakaingia ndani na kumkuta Uki akiwa amekaa kitandani huku akionekana kutokuelewa mume wake aliambiwa nini simuni.

    “Uki” Ilikuwa ni sauti ya Rahman ambayo ilimuita.

    Uki akashtuka kupita kawaida. Rahman akawasha taa na kisha kuanza kumuangalia Uki ambaye hakujua afanye kitu gani mahali hapo. Rahman akaanza kuongea maneno ya kumkejeri, Uki alionekana kukasirika sana kiasi ambacho kilimfanya kutaka kupiana na Rahman.

    “Nitakuua” Rahman alimwambia Uki na kuendelea.

    “Tena nitakuua kwa mkono wangu mwenyewe kwa kile ambacho ulinifanyia kwa kuniona sifai kukuoa” Rahman alimwambia Uki na kisha vijana wake kumfuata na kisha kumshika mikono na kumlaza kitandani. Alichokifanya Rahman wakati huo ni kuchukua kisu chake na kisha kuelekea kitandani pale. Bila kuonekana kuwa na hata chembe ya huruma, akaanza kumchoma Uki visu mfululizo tumboni mpaka kufa pale pale.

    Hawakutaka kuendelea kubaki mahali pale, wote wakaondoka na kuelekea katika hoteli ambayo walikuwa wamepanga. Huku Rahman akiwa ameandika neno lililosomeka ‘BINADAMU’ katika mlango wa kuingia ndani ya chumba kile. Kila kitu ambacho kilikuwa kimeendelea kilionekana kumpa amani moyoni mwake. 

    Mara baada ya siku tatu kupita, akawapigia simu vijana wake nchini Tanzania na kisha kuwaambia kumuua Erica na kisha kuandika maneno yale yale getini. Vijana wale wakafanya kama walivyoambia, siku hiyo hiyo ambayo Edmund alikuwa akirudi nyumbani kwake, nao wakawa wamekwishamuua Erica huku wakiwa wamemfunga kamba mlinzi katika kibanda chake.

    “Kazi nzuri” Rahman alisema mara baada ya kupewa taarifa kila kitu kilikuwa kimefanyika na baada ya siku kadhaa kurudi tena AfrikaKusini kuendelea na maisha kama kawaida huku moyoni akijisikia amani ya kukamilisha kazi ile.



    Edmund alionekana kuchanganyikiwa kupita kawaida, hakuamini kama yue Rahman mtoto wa tajiri Adamu ndiye ambaye alikuwa nyuma ya matokio yote ambayo yalikuwa yamehusika katikafamilia yake. Akauhisi mwili wake ukitetemeka kwa hasira huku kijasho chemba mba kikianza kumtoka.

    Hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, taarifa ambayo alikuwa amepewa ilionekana kumchanganya kupita kawaida. Akaondoka nyumbani hapo na moja kwa moja kuingia garini na safari ya kuelekea nyumbani kwa Bwana Msantu kuanza. Njiani alionekana kuwa na mawazo mengi kupita kawaida, ni kitu kimoja tu ndicho ambacho alikuwa akitaka kukifanya kwa wakati huo, kumuua Rahman.

    Haijalishi mtu huyu angekuwa anakaa katika sehemu gani ya dunia, kitu ambacho alikuwa akitamani kwa wakati huo ni kumfuata popote pale na kisha kumuua kwa kifo kilichojaa maumivu. Alichukuadakika kadhaa mpaka kufika kwa Bwana Msantu ambako akapiga honi na kisha geti kufunguliwa na kuliingiza gari lake.

    Moja kwa moja akateremka na kuanza kuelekea ndani ya nyumba ile. Alipoufikia mlango akaingia ndani na kupokewa na mfanyakazi wa ndani ambaye alikwenda kumuita Bwana Msantu ambaye akafika mahali hapo akiwa na mkewa, Bi Nasra.

    Wakasalimiana na kisha kutulia kitini huku wakianza kuongea mambo mbalimbali mpaka pale ambapo Edmund akaaza kuongea kile ambacho kilikuwa kimemleta mahali pale. Kila mmoja alionekana kutokuamini kile ambacho Edmund alikuwa akikisema kwa kipindi kile, walibaki wakimwangalia kwa mshangao.

    “Unamaanisha huyu Rahman mtoto wa mzee Adamu?” Bwana Msantu aliuliza huku akionekana kutokuamini.

    “Ndiye huyo huyo. Ameiangamiza familia yangu yote, hakutaka kumuacha mtu yeyote mikononi mwangu. NI LAZIMA nimuue” Edmund alisema huku kichwa chake kikichukua nafasi ya kuvuta picha ya marehemu mke wake pamoja na watoto wake ambao walikuwa wameuawa kinyama.

    “Anaishi hapa hapa Dar kwa sasa hivi? Kwa sababu kimepita kipindi kirefu sijasikia chochote kuhusu yeye” Bwana Msantu aliuliza.

    “Hayupo hapa kwa sasa. Anaishi nchini Afrika Kusini” Edmund alijibu.

    “Kwa hiyo unataka kumfuata?”

    “Hilo ndilo lengo langu kubwa”

    “Unajua ni mahali gani anakaa nchini Afrika Kusini?” Bwana Msantu aliuliza.

    “Sipafahamu. Ila kama nitachukua wiki moja ya kupeleleza zaidi nitajua tu” Edmund aliwaambia.

    Siku hiyo Edmund hakutaka kukaa sana ndani ya nyumba hiyo, alichokifanya ni kutoka nje na kisha kuelekea nyumbani kwake. Suala aliloongea Bwana Msantu likaonekana kuwa na maana sana, alijua fika kwamba Rahman alikuwa nchini Afrika Kusini lakini tatizo lililojitokeza ni kwamba hakujua ni sehemu gani ambayo alikuwa akiishi nchini Afrika Kusini.

    Kitu cha muhimu ambacho alikiona kwamba ni lazima akifanye kwa wakati huo ni upelelezi tu. Alihitaji kila jambo ambalo angekwenda kulifanya kwa wakati huo liwe rahisi na wala lisimpe tabu sana. Kila alipofikiria namna ambayo alitakiwa kufanya ili afahamu sehemu alipokuwa akiishi Rahman, jambo hilo lilikuwa gumu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nifanye nini sasa? Au niende nikamuulize baba yake? Hapana, hilo gumu” Edmund alijiuliza na kujijibu.

    “Au niende halafu nianze kumtafuta kila kona? Hapana. Afrika Kusini nayo kubwa, nitasumbuka sana bila mafanikio” Kila kitu ambacho Edmund alikuwa akijiuliza mahali hapo kichwa chake kilikuwa na majibu ya uhakika. Alibaki akifikiria kwa kipindi fulani na ndipo wazo moja likamjia kichwani mwake, kitu ambacho alitakiwa kufanya kwa wakati huo ni kumtumia mwandishi wa habari yeyote yule.

    Wazo hilo likaonekana kupita kichwani mwake, alichokifanya ni kuanza kuelekea katika ofisi ya gazeti la PEKEE na kisha kutaka kuonana na mhariri mkuu wa gazeti hilo, Bwana Ramadhani. Ramadhani alipotoka nje ya ofisi ile, akaamua kumchukua na kuelekea nae katika mghahawa mmoja uliokuwa pembeni ya ofisi ile.

    “Kitambo sana Edmund. Unaendeleaje?” Ramadhani alimuuliza Edmund.

    “Naendelea vizuri sana. Kidogo naanza kurudi katika hali yangu japokuwa mambo yale ni magumu sana kusahaulika kichwani mwangu” Edmund alimwambia Ramadhani.

    Edmund hakutaka kuingia katika lengo lake moja kwa moja, alichokifanya ni kuanza kuongea nae kuhusu mambo mengine huku akijaribu kumteka na kumuingiza ndani ya himaya yake. Stori za hapa na pale ziikuwa zikiendelea kama kawaida huku wakiendelea kupata vinywaji vilivyokuwa vimeletwa mezani pale.

    “Kuna kitu nataka unisaidie” Edmund alimwambia Ramadhani.

    “Kitu gani?” Ramadhani aliuliza.

    “Nataka unisaidie kumtafuta mtu fulani, najua ninyi waandishi wa habari mtakuwa mkifahamu mengi” Edmund alimwambia Ramadhani.

    “Mtu gani?”

    “Unamkumbuka Rahman Adamu?” Edmund aliuliza.

    “Mmmh! Ndiye nani huyo?”

    “Yule mtoto wa tajiri Adamu anayemiliki visima kadhaa vya mafuta” 

    “Yeah! Namkumbuka. SI yule dogo ambaye alikimbilia Afrika Kusini?” Ramadhani aliuliza.

    “Ndiye huyo huyo” Edmund alimwambia.

    “Sasa unataka nikusaidie nini hapo?”

    “Jinsi ya kumpata kule Afrika Kusini. Hivi anaishi sehemu gani?” Edmund aliuliza.

    “Mmmh! Hapo wala sifahamu. Au nikamuulize Magreth atakuwa akifahamu kwa sababu miezi minne iliyopita alikuwa ameandika mengi kuhusu yeye” Ramadhani alimwambia Edmund.

    “Magreth ndiye nani?”

    “Mwandishi wenzangu wa habari”

    “Sawa. Kamuulize ila usiseme kama mimi ndiye nimekutuma. Si unajua wanawake walivyo, isije ofisi nzima ikajua” Edmund alimwambia Ramadhani.

    “Nawajua vilivyo. Usijali juu ya hilo” Rahman alimwambia Edmund.

    Edmund hakutaka kulaza damu, hapo hapo akauchukua mfuko wa kaki ambao alikuwa nao na kisha kumgawia Ramadhani ambaye akaufungua na macho yake kukutana na noti kadhaa za shili elfu kumi kitu ambacho kilikuwa kamahamasa ya kumfanya kufanya kazi ile kwa nguvu.

    “Hapo imetulia” Ramadhani alimwambia Edmund na kisha kuanza kuondoka mahali hapo.

    “Kwa hiyo nikusubiri au utamuuliza kimya kimya kwa siku kadhaa?” Edmund alimuuliza Ramadhani.

    “Nipe siku ya leo tu, nitakufanyia kila kitu” Ramadhani alimwambia Edmund na kisha kuondoka mahali hapo huku akiwa na furaha kana kwamba alikuwa ameshinda bingo.

    Edmund akaondoka mahali hapo na kisha kuelekea nyumbani kwake. Moyo wake ulikuwa na shauku ya kutakakufahamu mahali ambapo Rahman alikuwa akiishi nchini Afrika Kusini. Usiku wa saa nne, Ramadhani akampigia simu na kumwambia mambo mengi kuhusu Rahman.

    “Anakaa katika jiji la Pretoria mtaa wa Mandela barabara ya 48 karibu kabisa na nyumba anayokaa balozi wa Tanzania nchini humo” Ramadhani alimwambia Edmund.

    “Safi sana. Kuna kingine cha zaidi alichokwambia?” Edmund aliuliza.

    “Yeah! Amesema kwamba kwa sasa kumpata Rahman nyumbani kwake inakuwa ngumu sana kwa sababu yeye ni mtu wa starehe sana, hivyo kumpata kwa urahisi ni katika kumbi nyingi za starehe hasa nyakati za usiku” Ramadhani alimwambia Edmund ambaye alionekana kufurahi zaidi.

    “Ni kumbi gani ambazo huwa anapenda kwenda?”

    “Kuna ukumbi mmoja uitwao Cambodia ambao upo katika jiji la Cape Town” Ramadhani alimwambia Edmund.

    “Sawa. Nimekupata. Kuna kingine cha zaidi?” Edmund alimuuliza Ramadhani.

    “Nadhani hakuna”

    “OK! Nashukuru sana. Nitakupitishia mzigo mwingine kama shukrani kesho asubuhi” Edmund alimwambia Ramadhani na kisha kukata simu.

    *******

    Mipango ya safari ya kuelekea Afrika Kusini ikaanza kufanyika, kitu ambacho alikuwa akikitaka Edmund katika kipindi hicho ni kumuua Rahman kwa mikono yake mwenyewe kisasi cha kuuawa kwa familia yake. Akaanza kushughulikia kila kitu ambacho kilikuwa kikihitajika na kisha kujiandaa kwa safari hiyo ambayo ilihitajika kufanyika baada ya siku mbili.

    Alichokifanya mara baada ya kuona kwamba amekamilisha kila kitu ilikuwa ni kwenda nyumbani kwa Bwana Msantu kwa lengo la kuwaaga hata kabla hajaianza safari hiyo ambayo aliiona kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

    “Ninaelekea Afrika Kusini” Edmund alimwambia Bwana Msantu.

    “Wamesema anaishi wapi?” Bwana Msantu aliuliza.

    “Anaishi Pretoria. Nitakwenda huko na kumtafuta mpaka pale ambapo nitakamilisha kila kitu ambacho kikitakiwa kufanywa kwa mikono yangu” Edmund alimwambia.

    Mara baada ya siku ya safari kufikia, Edmund akaanza kuelekea nchini Afrika Kusini huku kichwa chake kwa wakati huo kikifikiria kufanya kitu kimoja tu, mauaji. Aliiona ndege kwenda katika kasi ndogo, kitu ambacho alikuwa akikitamani kwa wakati huo ni kufika Afrika Kusini na kisha kukamilisha kile ambacho kilikuwa kimempeleka kule.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baaada ya masaa matano ndege ikaanza kutua katika uwanja wa ndege wa Nelson Mandela uliokuwa katika jiji kuu la Johannesburg na kisha kuchukua teksi ambayo ilimpeleka mpaka katika hoteli kubwa ya nyota tano iliyokuwa nje kidogo mwa jiji hilo iliyoitwa St’ Patricia. 

    Mara baada ya kufika katika hoteli hiyo akachukua chumba na kisha kupumzika. Siku hiyo hakutaka kujishughulisha na kitu ambacho kilikuwa kimemleta ndani ya nchi ile. Akapumzika huku akianza kuipanga mipango yake juu ya namna ambayo angeweza kuanza kazi ile kwa umakini mkubwa ambao usingewafanya watanzania kugundua.

    Siku hiyo hakulala, kila wakati alipokuwa akifikiria kwamba alikuwa kwenye nchi ambayo muuaji wa familia yake alipokuwa ilionekana kumuumiza kupita kawaida. Siku iliyofuata ndio siku ambayo akaamua kusafiri mpaka katika jiji la Pretoria, sehemu ambayo Rahman alikuwa akiishi. Kwa sababu alikuwa amempa maelekezo dereva wa teksi, akapelekwa mpaka nje ya nyumba hiyo, alipoiona, akaridhika na hivyo kuondoka na kwenda kuchukua chumba kingine katika hoteli nyingine hapo Pretoria.

    Kila kitu ambacho alikuwa akijitahidi kukifanya mahali hapo alijitahidi kukifanya kwa makini sana, hakutaka kuonekana na Rrahman kwamba katika kipindi hicho alikuwa nchini Afrika Kusini kwani alijua fika kwamba kama mtu huyo angejua basi hali ingeweza kuwa mbaya zaidi na hivyo kumfanya Rahman kujificha.

    Alibaki chumbani ndani ya hoteli hiyo huku wazo moja kwa wakati huo ndio ambalo lilikuwa likimjia kichwani mwake. Ni kweli kwamba alikuwa akitaka kumuua Rahman lakini hakujua ni kwa namna gani angeweza kumuua mtu huyo. Kwa wakati huo hakuwa na bunduki au silaha yoyote ile, kama angekosa vitu hivyo basi ingekuwa ni vigumu sana kuweza kumuua Rahman.

    Akaanza kujiona kuwa na kila sababu za kuweza kutafuta bunduki kwa wakati huo. Alichokifanya ni kuanza kutafuta bunduki na aliona kusingekuwa na uwezekano wa kupata bunduki kama asingeweza kukutana na watu ambao wangeweza kumuuzia bunduki. Hapo ndipo kichwa chake kilipoanza kufikiria upya mpaka pale ambapo alipata wazo la kwenda katika mtaa wa uswahilini wa Soweto.

    Imani yake ilimtuma kwamba kama angekwenda Soweto basi ilikuwa ni lazima kupata kile ambacho alikuwa akikihitaji kwa wakati huo. Hakutaka kuendelea kubaki ndani ya hoteli ile kwa wakati huo, akatoka ndani na kisha kuanza kuelekea katika mtaa wa Soweto. Mweto haukuwa wa masaa mengi akawa amekwishafika katika mtaa huo na kisha kumlipa dereva kiasi cha Rand kumi ambacho alikuwa akikihitaji.

    “Nataka unisaidie kitu” Edmund alimwambia dereva yule.

    “Kitu gani?”

    “Nataka kununua bunduki”

    “Unataka kununua bunduki? Ya kazi gani?”

    “Hebu acha swali la kitoto bwana. Nadhani kazi ya bunduki unaifahamu. Naweza kumpata mtu ambaye anaweza kuniuzia bunduki hiyo?” Edmund alimuuliza dereva yule.

    Dereva hakujibu kitu chochote kile, alibaki kimya huku akianza kufikiria kwa muda fulani. Edmund alitulia akimwangalia tu, mara baada ya sekunde kadhaa, tabasamu pana likaanza kuonekana usoni mwa dereva yule.

    “Inamaanisha kwamba unataka kumuua mtu fulani?” Dereva aliuliza.

    “Ndio lengo langu hilo” Edmund alijibu.

    “Umekwishawahi kuua hata siku moja?”

    “Hapana”

    “Je kumtoa mtu damu?”

    “Bado”

    “Kwa staili hiyo, hautoweza kuua kweli?” Dereva yule alimwambia Edmund.

    “Kwa hiyo ninaweza kuipata bunduki hiyo na kununua?” Edmund aliuliza.

    “Ndio. Ila naona kama ningekushauri kitu kimoja hivi”

    “Kitu gani?”

    “Kwa nini usiwaandae watu fulani kwa ajili ya kufanya mauaji hayo?” Dereva yule alimuuliza.

    “Hapa Afrika Kusini simjui mtu yeyote zaidi ya huyo ninayetaka kumuua” Edmund alijibu.

    “Uko tayari kutoa ajira kwa vijana wakufanyie kazi hiyo?” Dereva aliuliza.

    “Itakuwa vizuri zaidi” Edmund alijibu.

    “Sawa. Twende ila kabla hatujafika nipe Randi elfu moja kwa kazi kama dalali” Dereva yule alimwambia Edmund na bila hiyana Edmund akamgawia kiasi kile cha fedha na kisha safari ya kuelekea huko kuanza.

    Gari likaingia zaidi katika mitaa ya Soweto, nyumba zilikuwa zimekaa shaghalabhagha, watoto walionekana kuwa wengi wakicheza mitaani huku kelele za hapa na pale zikiwa zinasikika kwa juu kila eneo. Watu wa hapo Soweto hawakuonekana kuogopa kitu chochote kile, wengi walikuwa wamekaa nje huku wakizisafisha bunduki zao na wengine wakivuta bangi pamoja na madawa ya kulevya hadharani kabisa bila kubughudhiwa na mtu yeyote yule.

    Mambo mengi ambayo Edmund alikuwa akiyaona yalikuwa mageni kwake. Japokuwa alikuwa ameishi sana katika mtaa wa uswahilini wa Tandale lakini kwa kila kitu ambacho alikuwa akikiona katika mtaa ule wa Soweto kilikuwa kigeni machoni mwake. Gari liliendelea kwenda zaidi na zaidi mbpaka kusimama nje ya nyumba moja ambapo kulikuwa na vijana wengi mahali hapo.

    Dereva akateremka na kumtaka Edmund abaki ndani ya gari na kisha yeye kuteremka na kwenda kuongea na kijana mmoja ambaye alikuwa ameshika bunduki. Mara baada ya kuongea nae kwa muda fulani, akamwangalia Edmund na kisha kuteremka na kuanza kuwafuata.

    Wote watatu wakaingia ndani na kisha kukaa katika viti vilivyokuwa vimewekwa pale sebuleni na kisha kuanza kuongea. Edmund akawaeleza dhamira yake ambayo ilikuwa imemleta nchini Afrika Kusini. Vijana zaidi ya watano walikuwa wakimsikiliza kwa makini sana mahali pale.

    “Una kiasi gani tukufanyie kazi yako?” Kijana mmoja, Masumbuko alimuuliza.

    “Sijajua ninyi mnahitaji kiasi gani”

    “Una randi elfu kumi na tano?” Masumbuko alimuuliza.

    “Hilo si tatizo kabisa. Nitawapeni kiasi hicho cha fedha hasa mara baada ya kutoka hapa” Edmund aliwaambia.

    “Sawa. Tutaifanya kazi yako kwa usalama mkubwa sana na kisha kufanya kila kitu ambacho utahitaji tukifanye. Utataka tumuue au tumteke?” Masumbuko alimuuliza.

    “Msimuue. Nataka mumteke na kisha nionane nae”

    “Sawa. Unapajua sehemu yoyote ambayo tutaweza kumpata?” Masumbuko aliuliza.

    “Ndio. Mara nyingi huwa anapatikana katika ukumbi wa Cambodia jijini Cape town” Edmund alijibu.

    “Sawa. Tutakwenda huko. Kila kitu kitakuwa kwenye mipango yote” Masumbuko alimwambia Edmund na kisha kumtaka kuwa pamoja nao katika kipindi ambacho wangekwenda katika ukumbi ule nyakati za usiku huku wakiwa wamekwishaweka sawa bunduki zao kwa ajili ya kwenda na kumteka tu Rahman na kisha kumleta mbele ya Edmund.

    ***

    *******

    Usiku Edmund alikuwa akimfikiria Rahman tu, katika kipindi hicho alikuwa na hasira nae kupita kawaida. Kila wakati alikuwa akitembea tembea ndani ya chumba kile huku akiipiga mikono yake kwa hasira. Kwa wakati huo alikuwa akikumbuka mambo mengi sana hasa mauaji ya familia yake ambayo yalikuwa yametokea katika miezi ya nyuma iliyopita.

    Hakukuwa akikitaka kitu chochote kutoka kwa Rahman zaidi ya uhai wake tu. Rahman ndiye ambaye alikuwa amemsababishia kumbukumbu nyingi zenye kuumiza, hakutaka kumuacha hai mtu huyo, alikuwa radhi kutumia kila kitu alichokuwa nacho mpaka kuhakikisha kwamba anamuua tena kwa mkono wake mwenyewe kwa kutuia aina ya kifo ambacho kingemfanya kujiona kwamba ankufa.

    Saa nne kamili simu ya mezani ndani ya chumba kile ikaanza kuita, kwa haraka akaifuata na kisha kuipokea na kuanza kuongea na mtu ambaye alikuwa akimhitaji sehemu ya mapokezi. Hakutaka kuchelewa, tayari alijua fika kwamba mtu huyo alikuwa ni dereva ambaye alikuwa ameonekana kuwa msaada mkubwa kwake katika harakati zote za kumpata Rahman. 

    Akaanza kuvaa nguo zake na kisha kutoka nje ya chumba kile, akashusha ngazi mpaka sehemu ya mapokezi. Hisia zake zilikuwa kweli kabisa, alikuwa ni dereva teksi ambaye akahitaji amfuate mpaka nje ya hoteli ile na macho yake kutua kwa vijana ambao walikuwa wamevaa suti nyeusi, vijana ambao walikuwa tayari kufanya kile ambacho alikuwa amewaagiza.

    Akaanza kuongea nao na kisha kumwambia aingie ndani ya gari kwani katika kipindi hicho ndicho ambacho walikuwa wakitaka kuondoka na kuelekea Cape Town kwa ajili ya kumteka Rahman tu. Hapo ndipo safari ilipoanza rasmi, kwa sababu wakati huo ulikuwa ni wa usiku na gari ambalo walikuwa lilikuwa na uwezo mkubwa wa kutembea kwa mwendo wa kasi, wakajikuta wakitumia masaa mawili mpaka kuingia katika jiji la Cape Town.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hawakuwa na muda wa kupoteza mahali hapo, walichokifanya ni kuanza kuelekea katika ukumbi wa starehe wa Cambodia ambao ulipatikana katikati ya jiji hilo na kisha kulipia kiingilio. Hakukuwa na mlinzi yeyote ambaye alikuwa na waiwasi nao, kwao walionekana kuwa watu wazuri ambao hawakuwa na uwezo wa kufanya fujo zozote kutokana na suti ambazo walikuwa wamezivaa.

    Wakaingia mpaka ndani. Watu walikuwa wamejazana kupita kawaida huku wakiwa wamegawanyika katika makundi mawili. Kuna wale ambao walikuwa wakicheza kila muziki ambao ulikuwa ukipigwa lakini pia kuna wale ambao walikuwa wamekaa katika makochi huku wakiwa wamezungukwa na wasichana ambao walikuwa wamevaa nusu uchi na bia za kila aina tena zile zilizokuwa za gharama zikiwa mezani.

    Ukiachilia ukumbi huo wa muziki, katika mlango mwingine ambao ulikuwa ukiingia ulikuwa ukitokea katika ukumbi wa cassino moja kubwa. Kila mwanamke ambaye alikuwa ndani ya Cassino hiyo alikuwa kama alivyozaliwa. Wengine walikuwa wakicheza muziki huku wakizionyesha nyeti zao kwa wanaume mbalimbali ambao kazi yao ilikuwa ni kuwatunza fedha kwa kile walichokuwa wakikiona.

    Ukiachana na hao, pia kulikuwa na sehemu ambayo ilikuwa na michezo mbalimbali ya kamari. Watu walikuwa wakiwekeana madau makubwa sana, kila mtu ambaye aliliwa katika kipindi hicho, alikuwa mpole. Kama zilivyokuwa Cassino nyingine kama ya Las Vegas ya jijini Dar es Salaam ndivyo ilivyokuwa Cassino hiyo, wanawake walikuwa wakicheza utupu huku kukiwa hakuna kiti hata kimoja katika ukumbi huo.

    Edmund akaanza kupitisha macho yake kwa watu ambao walikuwa wamekaa katika makochi huku lengo lake likiwa ni kumtafuta Rahman lakini mtu huyo hakuonekana kitu ambacho kiliwafanya kuingilia mlango ule na kisha kutokea katika ukumbi wa Cassino. 

    Wakaanza kuyapitisha macho yao huku na kule na kisha kumuona Rahman akimtunza fedha msichana ambaye muda mwingi alikuwa akimuonyeshea nyeti zake. Moja kwa moja Edmund akamnyooshea kidole Rahman na hivyo vijana wale kuanza kumfuata na kisha kumchukua huku wakiwa wamemuonyeshea bunduki kisiri.

    Uwepo wa bunduki zae ndizo zilizoonekana kumtia wasiwasi Rahman na kumfanya kutulia. Akatolewa nje ya ukumbi ule huku kukiwa hakuna hata mtu mmoja ambaye alikuwa akifahamu kile kilichokuwa kikiendelea, wakampakiza ndani ya gari. Muda wote Rahman alikuwa akiuliza maswali lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye aliyajibu maswali yale, na hata hakupewa nafasi ya kukutanisha macho yake na Edmund. 

    “Tukupelekee wapi mtu wako?” Kijana mmoja aliuliza.

    “Baharini” Rahman alijibu.

    Safari ya kuelekea baharini ikaanza, kwa wakati huo vijana wale walikuwa wakifanya kila kitu ambacho Edmund alikuwa akiwaambia kufanya, kiasi cha fedha ambacho alikuwa amekitoa kilikuwa kikubwa sana, alihitaji kuheshimika. Wala hawakuchukua muda mrefu wakawa wamekwishafika ufukweni.

    “Kingine bosi?”

    “Hatuwezi kupata mtumbwi?” Edmund aliuliza.

    “Kuna mitumbwi mingi hapa. Ngoja tuchukue mmoja” Kijana mmoja alisema na kisha kuanza kuufuata mtumbwi ule ambapo akamkuta mwenyewe akiwa amejilaza mtumbwini. Alichokifanya mahali hapo ni kuongea nae na kisha kumuazima mtumbwi ule kwa kiasi cha rand mia tano.

    “Kingine?”

    “Kuna kamba?”

    “Hilo si tatizo”

    “Sawa. Kuna chumba chochote kizito?”

    “Nafikiri kitakuwa garini. Chuma cha taili si linafaa?”

    “Linafaa sana” Edmund alimwambia.

    Hapo hapo kijana yule akaelekea garini na kuvileta vitu vile na kisha kuvipakiza garini na safari ya kuelekea kwenye kina kirefu baharini mule kuanza. Tayari Rahman alionekana kushikwa na wasiwasi zaidi, watu wale wakaonekana kuwa si watu salama machoni mwake. Alikuwa akiogea maneno mengi ya kuomba msamaha na kuwaahidi kuwapa kiasi kikubwa cha fedha kama wangemwacha lakini hakukuwa na mtu aliyemsikiliza.

    Baada ya kufika umbali wa mita elfu moja, wakasimamisha mtumbwi ule na kuanza kumwangalia Edmund. Alichokifanya Edmund ni kuanza kumwangalia Rahman usoni mwake huku tayari machozi yakitiririka mashavuni mwa Edmund.

    “Unanikumbuka?” Edmund alimuuliza rahman ambaye alibaki akimwangalia Edmnd usoni.

    “Hapana ila hauna ugeni machoni mwangu” Rahman alijibu huku akiwa na wasiwasi.

    “Unamkumbuka Eric? Unamkumbuka Erica?” Edmund alimuuliza.

    “Hapana” Rahman alijibu huku akitetemeka.

    “Na vipi kuhusu Uki? Unamkumbuka?” Edmund aliuliza swali ambalo likamfanya Rahman kumkumbuka Edmund.

    Rahman akauinamisha uso wake chini, akaanza kulia kama mtoto mdogo jambo ambalo likawafanya hata wale vijana kumshangaa. Hawakuelewa ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha ya watu hao wawili zaidi ya wao kuifanya kazi ambayo bosi wao alikuwa amewaelekeza tu.

    “Naomba unisamehe kwa kila nilichokufanyia” Rahman alisema huku akijaribu kupiga magoti mtumwini pale.

    “Umechelewa mno. Umechelewa Rahman. Ni lazima nikuue, nitakuua kwa kifo kilichojaa maumivu, kifo ambacho utakuwa ukijua kwamba unakwenda kufa” Edmund alimwambia Rahman na kisha kuwataka vijana wale kumfunga kamba pamoja na lile chuma kiunoni.

    “Nitakapokupiga risasi za miguuni na kukutupa baharini, kamwe hautoweza kuogelea, kwa jinsi ambavyo chuma kilivyokuwa kizito, kamwe hautoweza kuja juu. Utabaki chini ya maji, hautoweza kurudi juu, mbaya zaidi, hata mwili wako hautoonekana milele kwani utakuwa chakula cha samaki wa humu baharini” Edmund alimwambia Rahman huku akiwa amemnyooshea bunduki.

    Katika kipindi chote ambacho Edmund alipokuwa akiongea maneno yale, moyo wake ulikuwa ukimuuma kupita kawaida. Alikuwa akiifikiria familia yake tu, aliwakumbuka watoto wake, Erick na Erica ambao walikuwa wameuawa kinyama na Rahman, kila alipokuwa akifikiria hayo, hakuona sababu ya kumsamehe Rahman.

    ****

    Maisha ya raha bado yalikuwa yakiendelea kwa Rahman, mara baada ya kumaliza kufanya mauaji yote ndipo alipoamua kurudi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuendelea na maisha yake kama kawaida huku moyo wake ukiwa na amani kupita kawaida. Alionekana kuridhika, aliliridhika kwa kila kitu ambacho alikuwa amekifanya.

    Kitendo alichokifanya cha kumuua Uki pamoja na watoto wake mapacha wawili kilionekana kuwa kitendo cha kujivunia sana katika maisha yake. Kwa wakati huo alijiona kuwa mshindi hata zaidi ya washindi wote duniani, kila wakati alikuwa akizidi kujipongeza. Hakuona sababu ya kumuua Edmund, mume wa Uki kwa kuona kwamba mtu huyo hakuwa na makosa yoyote ambayo alikuwa amemfanyia.

    Baada ya kufika Afrika Kusini, maisha ya starehe yakaanza upya. Aliendelea kutanua na fedha za baba yake kama kawaida. Hakuona hasara kutumia zaidi ya rand elfu ishirini kwa siku. Fedha kwake halikuwa tatizo lolote kwa sababu baba yake, Bwana Adamu alikuwa akimjali sana.

    Ukumbi wa Cambodia ambao ulikuwa Cape Town ndio ulikuwa ukumbi wake wa kutanulia kipindi hicho. Aliupenda ukumbi huo kwa sababu ulikuwa umegawanyika sehemu mbili, sehemu za kucheza muziki na sehemu ya Cassino. Wasichana wazuri wa Kizulu ambao mara nyingi walikuwa wakija katika ukumbi huo ndio ilikuwa chachu kubwa ya kuacha kumbi zote na kuja mahali hapo.

    Alitumia nao fedha alivyotaka, alilala na wasichana tofauti, katika maisha yake alijiona kupata kila kitu. Siku zikaendelea kwenda mbele mpaka kufikia siku ambayo alichukuliwa na vijana watatu na kisha kupelekwa katika gari ambalo liliishia ufukweni na kisha kupandishwa kwenye mtumbwi. Alikuja kumjua mtu ambaye alikuwa nyuma ya tukio lie mara alipopewa ruhusa ya kumuona, tena akiwa mbele yake akiongea.

    Aliikumbuka sura hii lakini hakuwa na uhakka ni sehemu gani alipowahi kumuona ila alipoongea na kumtajia majina ya watu aliowahi kuwaua ndio akamkumbuka, alikuwa Edmund, mwanaume ambaye alikuwa amemuoa mwanamke aliyekuwa akimuhitaji.

    *****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bado Rahman alikuwa akiendelea kuomba msamaha lakini Edmund hakuonekana kumuelewa. Machozi yalikuwa yakitiririka mashavuni mwake. Kadri alivyokuwa akimwangalia Rahman na ndivyo ambavyo kumbukumbu za familia yake zilivyokuwa zikizidi kumiminika kichwani mwake. Rahman alikuwa amepiga magoti huku vijana wote mahali pale wakiwa kimya wakiwaangalia.

    “Paaaaa” Ulisikika mlio wa risasi mahali hapo, Rahman alikuwa akilalamikia maumivu ya mguu wake. Risasi ilikuwa imepenya katika mguu wake wa kushoto.

    “Paaaaaa” Risasi nyingine ikasikika, Rahman akaushika mguu wake wa kulia huku akilia kama mtoto. 

    Hakuwa na nguvu za kusimama, miguu yote ilikuwa imepigwa risasi. Kilio chake kwa wakati huo kilikuwa kikubwa kupita kawaida. Alilia sana lakini kilio kile hakikuonekana kumsaidia kwa kitu chochote kile. Edmund akawaambia vijana wale wambebe na kisha kumtosa baharini huku chuma kizito cha taili kikiwa kiunoni mwake.

    “Ninakuua kifo cha kukutesa, utazama majini, utakosa pumzi kwa sekunde kadhaa, utatapatapa lakini hautoweza kuibuka juu,” alisema Rahman huku akitoa tabasamu lililoonesha ni kwa jinsi gani alikuwa na maumivu moyoni.

    “Naomba unisamehe, naomba unisamehe Edmund,” alisema Rahman huku akilia.

    “Nitaanza vipi kukusamehe? Umeimaliza familia yangu, umenisababishia maumivu makali moyoni mwangu, ulifikiri sitokupata, unashangaa kuona nimekupata. Uliandika BINADAMU kwa kuona kwamba nisingekugundua, umekwisha Rahman, ninakumaliza kwa kukuua kifo chenye mateso ndani yake,” alisema Edmund na kuwaambia vijana wake wamtupe Rahman baharini.

    “Mwili wako utakuwa chakula cha samaki,” alimalizia Edmund.

    Rahman akatoswa majini, alijitahidi kutapatapa ndani ya maji lakini haikusaidia, chuma kile kilizidi kumzamisha chini. Hicho ndicho kilikuwa kifo kilichojaa maumivu, alikuwa akifa taratibu huku akijiona. Macho yake yakajaa giza, ndani ya dakika moja, Rahman akafa ndani ya maji na kisha Edmund na vijana wale kuondoka mahali hapo.

    Edmund hakutaka kukaa sana nchini Afrika Kusini, alichokifanya ni kuwaongezea fedha zaidi vijana wale na kisha kurudi nchini Tanzania na kuandaa sherehe kubwa ya kufurahia kifo cha Rahman bila wahudhuriaji kujua walikuwa wakisherehekia nini.

    “Nilimpata na kumuua” Edmund alimwambia Bwana Msantu na mkewe, Bi Nasra.

    “Safi sana” Bwana Msantu alimsifia.

    Huo ndio ulikuwa mwisho wa kila kitu. Ingawa Rahman alikuwa amefanikiwa kumuua bila mwili wake kuonekana lakini bado KUMBUKUMBU ZENYE KUUMIZA ziliendelea kuwa moyoni mwake. 

    Baada ya mwaka mmoja kupita, Edmund akamuoa Ester huku sababu kubwa ikiwa ni kumkumbuka Uki katika kila wakati ambao atakuwa akimwangalia Ester ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa marehemu mke wake. 

    Biashara zake ziliendelea kama kawaida, hakukuwa na kipingamizi chochote kile. Ulinzi mkubwa ukawekwa na kitengo cha ulinzi cha Ultmate Security nyumbani kwake. Rahman hakutakiwa kuguswa na wabaya, kwa fedha ambazo alikuwa akiziingiza katika kipindi hicho kupitia biashara zake mbalimbali ziliingizia serikali kiasi kikubwa cha fedha.

    Maisha yaliendelea zaidi na zaidi, mwaka ukakatika na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye walimpa jina la Baraka, jina ambalo lilikuwa kama kumbukumbuku ya rafiki yake, Baraka Kyomo ambaye aliwahi kusoma nae mkoani Shinyanga katika kipindi alichokuwa kidato cha pili.



    Hii ni hadithi yangu ya mwaka 2012, imejaa makosa kinoma, uandishi wa zamani lakini, napo kipindi hicho nilionekana nipo vizuri.

    Asanteni kwa kuifuatilia mwanzo mwisho, japo ina makosa, si nzuri kihivo, mpangilio mbaya, naamini mmeipenda kimtindo

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog