Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

MIMI NI MWENYE DHAMBI NISAMEHE MUNGU - 2

 





    Simulizi : Mimi Ni Mwenye Dhambi Nisamehe Mungu

    Sehemu Ya Pili (2)



    Bado Samuel na Sadiki walikuwa wakiendelea kuleta unafiki mbele ya macho ya walimu. Muda mwingi walikuwa wakionekana wakiwa na vitabu vyao vya dini jambo ambalo liliwafanya walimu kujua kwamba bado watu wale walikuwa watakatifu kama katika kipindi cha nyuma.

    Kutokwenda sana kanisani na msikitini kukaonekana kuanza kuwatia hofu walimu lakini mara baada ya Samuel na Sadiki kuligundua hilo, wakajirudi na kuendelea kufanya kama kile ambacho walikuwa wakikifanya katika siku za nyuma.

    Mara kwa mara Samuel alikuwa akionekana ameshika Biblia huku akiisoma kwa muda mwingi. Usiku, kama kawaida alikuwa akifanya maombi na hata wale wanafunzi ambao walikuwa wakisumbuliwa na magonjwa mbalimbali shuleni hapo alikuwa akiwafanyia maombezi.

    Matukio hayo na mangine yakaongeza upofu machoni mwa walimu, waliweza kuwaficha kabisa juu ya kile ambacho kilikuwa kikiendelea mioyoni mwao, Kwa Sadiki, kama kawaida yake alikuwa akivaa kanzu, muda mwingi alikuwa akishika Tasbih na kujifanya Shekhe mkubwa ambaye alikuwa akimtumikia Mungu.

    Kilemba kikubwa kilikuwa kichwani mwake, alikuwa akionekana kama mtu ambaye alikuwa akimuabudu Mungu kwa moyo mmoja. Katika swala zote tano za siku, Sadiki alikuwa akihudhuria lakini bado mambo yake machafu yalikuwa yakiendelea katika maisha yao.

    Siku zikaendelea kukatika huku maisha yale yakiendelea zaidi na zaidi. Kikafika kipindi, kipindi ambacho Mungu hakutaka kuona watu hao wakiendelea kufanya vitu kwa kujificha na kuleta unafiki mbele za walimu ambao walikuwa wakiwaona kuwa watakatifu, watu waliokuwa wakimuabudu Mungu kwa moyo mmoja.

    Siku ya jumamosi ya tarehe 7 mwezi wa 9 ikaonekana kuwa mbaya kwao hasa mara baada ya ukaguzi kufanyika katika mabegi ya wanafunzi wote kwa lengo la kutaka kuwatambua wanafunzi ambao walikuwa na simu katika shule hiyo.

    “Kuna wengine wanatumia simu shuleni hapa. Kama mnavyojua haturuhusu kitu hicho ndani ya shule hii, tena sio hii tu bali hata shule nyingine za Serikali,” Mwalimu mkuu aliwaambia walimu katika moja ya vikao vya walimu shuleni hapo.

    “Nini kifanyike mkuu, tuweke wapelelezi?” Mwalimu Mkuu msaidizi aliuliza.

    “Hakuna. Kamwe hatutakiwi kuwaamini wanafunzi kuwapeleleza wanafunzi wenzao, hiyo ngumu. Jumamosi hii ya leo ndio tutataka tufanye upekuzi katika mabegi yao yote bwenini, tutagundua tu,” Mwalimu mkuu aliwaambia walimu wezake.

    Kile ambacho kilikuwa kimezungumziwa mahali pale ndicho ambacho kilitakiwa kufanyika tena kwa haraka sana. Ilipofika saa 10:00 jioni, kengele ikagongwa, wanafunzi wote wakahitajika kwenda sehemu ya kukutania.

    Kila mwanafunzi alibaki akijiuliza juu ya kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea. Uwepo wa walimu ndani ya shule hiyo hasa katika siku ya Jumamosi ilionekana kuwashangaza sana, mbaya zaidi walikuwa wametumia zaidi ya saa moja kuwa katika kikao chao ofisini.

    Siku hiyo, mwalimu mkuu hakuonekana kuwa katika hali ya kawaida, ndita zilikuwa zikionekana usoni mwake. Wanafunzi wakajipanga mstalini na walimu kufika mahali hapo. Kitu cha kwanza, mwalimu mkuu akachukua fimbo na kisha kuelekea mbele kabisa ya wanafunzi wale.

    Hata kabla hajaongea kitu chochote kile akaanza kuwaangalia wanafunzi waliokuwepo mahali pale, wanafunzi walionekana kuhofia sana kwani mwalimu mkuu hakuonekana kuwa katika hali ya kawaida kabisa.

    “Tumechoka,” Ilisikika sauti ya mwalimu mkuu, sauti iliyojaa utetemo fulani, sauti ambayo ilizidi kuongeza hofu mioyoni mwa wanafunzi wale.

    “Wanafunzi wote wapo hapa?” Mwalimu mkuu alimuuliza kaka mkuu, John Gilipa.

    Kwa haraka haraka John akaanza kuwaangalia wanafunzi mahali hapo, alipoona kila mwanafunzi mtukutu ambao walikuwa wakijificha wapo mahali pale, akamuangalia mwalimu mkuu ambaye bado alionekana kuwa katika hali isiyo ya kawaida.

    “Ndiyo.”

    “Una uhakika?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Labda niangalie katika mabweni mwalimu,” John alimjibu mwalimu mkuu na kisha kuanza kuelekea katika mabweni yale na baada ya dakika moja kuja na wanafunzi ambao walikuwa mabwenini ambao asilimia kubwa walikuwa viongozi, wakatakiwa kujumuika na wanafunzi wengine.

    “Kuna nini tena? Moyo wangu umejawa na hofu sana,” Samuel alimuuliza Sadiki kwa sauti ya chini.

    “Mmmh! Sijui. Hata mimi sina amani kabisa. Ngoja tuwasikilize,” Sadiki alimwambia Samuel huku akiwa amevaa kanzu pamoja na kilemba kichwani.

    “Kuna watu leo hii tunakwenda kuwaandikia barua za kurudi nyumbani kwao kama adhabu na baada ya wiki mbili kuja na wazazi wao,” Mwalimu mkuu aliwaambia wanafunzi ambao bado walionekana kuwa na hofu na kisha kuendelea:

    “Hatujui ni wangapi. Inawezekana akawa mmoja au inawezekana wakawa mia moja, hatujui,” Mwalimu mkuu alisema na kuendelea.

    “Kuna watu wanatumia simu kificho, kuna watu wanatumia pombe kificho, leo hii tutakwenda kuwafahamu tu. Tutaanza kupekua katika kila begi la mwanafunzi na sehemu nyingine, ukikuta umeitwa katika bweni lako, nenda kwa haraka sana” Mwalimu mkuu aliwaambia wanafunzi ambao idadi kubwa walionekana kuwa na wasiwasi.

    “Mungu wangu!” Sadiki alisema huku akionekana kushtuka.

    “Nini?”

    “Kuna pombe.”

    “Wapi?”

    “Kwenye begi langu na lako.”

    “Unasemaje?”

    “Jana nilinunua viroba, nimeviweka kwenye begi langu na kifuko kimoja kukuwekea katika begi lako kama ulivyoniambia” Sadiki alimwambia Samuel.

    “Unasemaje?”

    “Ndio hivyo.”

    “Hapana. Uliweka kwenye begi?”

    “Ndio.”

    “Kwa nini usingeweka ndani ya magodoro kama tunavyofanya kila siku?”

    “Sijui kwa nini sikufanya hivyo,” Sadiki alimwambia Samuel.

    “Kwa hiyo tufanye nini?”

    “Sijajua. Ila ngoja tuwasikilizie. Mungu tusaidie sisi watumishi wako,” Sadiki alisema huku kijasho chembamba kikianza kumtoka.

    Walimu wakaingia katika mabweni na kisha upekuzi kuanza. Wanafunzi walionekana kutokuwa na amani kabisa, wengi wao walionekana kuwa na wasiwasi mwingi nyusoni mwao. Kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wengine na ndivyo ilivyokuwa kwa Samuel pamoja na Sadiki ambao walikuwa wakitokwa na vijasho vyembamba nyusoni mwao.

    Tayari waliona kwamba siku hiyo ndio ilikuwa siku ambayo kila mwanafunzi angekwenda kufahamu ukweli kuhusiana na tetesi zile ambazo kila siku zilikuwa zikisikika masikioni mwao. Macho yao yalipotua nyusoni mwa Mariamu na Catherine, nao walionekana kutokujiamini kabisa.

    Baada ya dakika tano, mwanafunzi mmoja baada ya mwingine akaanza kuitwa bwenini jambo ambalo liliwaongezea hofu kupita kawaida. Walimu walichukua muda wa saa moja kuangalia mabegi ya wanafunzi shuleni hapo huku zaidi ya wanafunzi themanini wakiwa wameitwa mabwenini mwao.

    Mpaka upekuzi unamalizika, tayari walimu walikuwa wamekuta pombe kali, sigara, simu pamoja na vitu vingine ambavyo havikutakiwa kuingizwa shuleni hapo. Kitu cha ajabu ambacho kiliwafanya Samuel na Sadiki kushtuka, hawakuwa wameitwa bwenini jambo ambalo liliwafanya kuona kwamba kila kitu kilikuwa fresh.

    “Mbona hatujaitwa! Au ulivificha sana?” Samuel alimuuliza Sadiki.

    “Sijajua kwa nini. Ila nafikiri Mungu bado yupo pamoja nasi. Yaani kama tukisalimika leo hii, hakika nitamrudia Allah kwa kuona kwamba bado ananipenda,” Sadiki alimwambia Samuel.

    Mara baada ya wanafunzi ambao walikuwa na vitu ambavyo havikuwa vikiruhusiwa kuingizwa shuleni kupelekwa ofisini, wengine wakaruhusiwa kuondoka mahali hapo. Kitu cha kwanza ambacho walikifanya Samuel na Sadiki ni kuelekea katika bweni lao na kisha kufungua mabegi yao, Pombe hazikuwepo.

    Kila mmoja akabaki kuwa na wasiwasi, ilikuwaje pombe zikosekane ndani ya mabegi yao huku wakiwa hawajaitwa na walimu? Kila mmoja alikosa jibu jambo ambalo liliwafanya kutulia kuona ni kitu gani ambacho kingeendelea mahali hapo.

    Saa mbili usiku, wakaitwa ofisini, tayari wakajua kwamba pombe zile zilikuwa zimeonekana na hivyo kuchukuliwa. Moja kwa moja wakaelekea katika ofisi ya mwalimu mkuu ambaye mpaka katika kipindi hicho siku hiyo bado alikuwa shuleni hapo.

    “Funga mlango,” Mwalimu mkuu, Massawe alimwambia Sadiki ambaye alikuwa wa mwisho kuingia.

    Wakamsalimia mwalimu mkuu lakini wala hakuitikia salamu zile, alibaki akiwaangalia kwa muda na kisha kuingiza mkono katika kidroo kidogo cha meza yake na kisha kutoa viroba vya Konyagi na kisha kuweka juu ya meza yake. Sadiki na Samuel wakaonekana kuwa na wasiwasi zaidi, tayari wakaonekana kugundua kwamba walimu walikuwa wamekwishagundua kilichokuwa kikiendelea.

    “Hivi nani ana ujasiri wa kuniambia kwamba yeye ni Mtumishi wa Mungu?” lilikuwa swali la kwanza aliloliuliza mwalimu mkuu, swali ambalo halikupatiwa jibu lolote lile.

    “Swali gumu. Samuel, wewe ni mtumishi wa Mungu? Unaishi kama Yesu alivyotaka tuishi?” mwalimu mkuu alimuuliza Samuel ambaye alibaki kimya, akayageuza macho yake usoni mwa Sadiki.

    “Sadiki, wewe ni mtumishi wa Mungu? Unaishi kama Mtume Muhammad alivyotutaka tuishi?” mwalimu mkuu alimuuliza Sadiki ambaye wala hakujibu kitu chochote kile.

    Siri ya kipindi kirefu ambayo ilikuwa imefichika siku hiyo ikaonekana kugundulika. Kuanzia siku hiyo, maisha yao yakawa ya unyonge sana jambo ambalo likawapelekea kutokusoma kabisa. Hakukuwa na siri tena, wanafunzi wakajua ni kitu gani ambacho kilikuwa kimeendelea katika maisha yao, wakaanza kudharauliwa kwa kuonekana kwamba walikuwa wakileta unafiki shuleni hapo.

    Kila walipokuwa wakipita walikuwa wakidhihakiwa, walikuwa wakikasirika lakini hawakuwa na la kufanya. Uongozi wa shule haukutaka kuwarudisha nyumbani kwani waliona kwamba kilikuwa kimebakia kipindi kichache sana kabla ya wanafunzi wa kidato cha nne kufanya mitihani yao ya mwisho.

    Mpaka kipindi cha mitihani kinafika, wote walikuwa katika hali mbaya. Kutokana na kutosoma, wakajikuta wakiiona mitihani ile kuwa migumu kupita kawaida. Wiki mbili za mitihani zilipomalizika, wakaondoka shuleni hapo huku wakiwa wamemaliza shule na aibu kubwa.

    “Tumemtenda Mungu dhambi,” Samuel alimwambia Sadiki katika kipindi ambacho walikuwa ndani ya basi wakirudi Dar es Salaam.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Najua Samuel. Kuna kipindi kingine nabaki nikijuta kwa nini nilimruhusu shetani kunitawala maishani mwangu, sijui kingetokea kitu gani kama baba na mama wangejua kilichoendelea,” Sadiki alimwambia Samuel kwa sauti ya unyonge.

    “Nitamrudia Mungu kwa mara nyingine tena, naamini nitasimama” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Sijui kama nitaweza. Moyo wangu umefadhaika sana, moyo wangu umekuwa na unyonge mkubwa kupita kawaida na sidhani kama nitakuwa na nguvu ya kumrudia Allah. Siwezi Samuel,” Sadiki alimwambia Samuel ambaye alikuwa akimwangalia tu kwa mshangao.

    “Mungu anasamehe Sadiki,” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Najua. Mungu anasamehe sana lakini najiona kutokuwa na nguvu ya kumrudia, moyo wangu umekata tamaa kwa kila kitu maishani mwangu,” Sadiki alimwambia Samuel huku uso wake ukionekana kukata tamaa.

    “Kwa hiyo unataka kumtumikia shetani?”

    “Hapana. Sijamaanisha hivyo.”

    “Kumbe umemaanisha nini?”

    “Kuishi kivyanguvyangu.”

    “Sikiliza Sadiki. Katika maisha yetu kuna mambo mawili tu katika kutumika. Kama ukishindwa kumtumikia shetani basi ni lazima utamtumikia Mungu na kama ukishindwa kumtumikia Mungu basi ni lazima utamtumikia shetani. Hauwezi kuishi kivyako vyako kama unavyosema. Utamtumikia shetani tu,” Samuel alimwambia Sadiki.

    Siku hiyo ndani ya basi walikuwa wakiongea mengi sana. Kila mmoja alionekana kuwa mnyonge, mioyo yao ilikuwa ikiwasuta juu ya yale ambayo walikuwa wameyafanya katika maisha yao. Kitendo chao cha kuacha kumtumikia Mungu kikaonekana kuwaharibia kabisa taswira ya maisha yao ya mbele.

    Waliona kila kitu kikiwa kimeharibika maishani mwao. Japokuwa walikuwa wamefanya mitihani ya Taifa ya kidato cha nne lakini walikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwamba wangekwenda kufeli mitihani ile kutokana na kutumia muda mwingi kufanya starehe na wasichana wao ambao walikuwa wamepanda basi tofauti na hilo.

    “Nimeshafeli mtihani Samuel,” Sadiki alimwambia Samuel.

    “Wewe ni kama mimi tu. Nimefeli pia. Tena nilifeli hata kabla mitihani haijafanyika,” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Tuangalie mbele yetu, naomba tusahau yaliyopita,” Sadiki alimwambia Samuel.

    “Unavyoona tufanye nini tena?”

    “Tutafute shule mapema za kuendelea na elimu ya kidato cha tano na sita,” Sadiki alimwambia Samuel.

    “Itakuwa safi kama tutasoma shule moja Sadiki. Wewe ni rafiki yangu wa karibu sana, ningependa tuendelee kuwa pamoja zaidi na zaidi,” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Usijali. Nadhani shule ambazo tunatakiwa kwenda ni za mikoani tu,” Sadiki alimwambia Samuel.

    “Hapana. Huko tutapotea sana Sadiki. Ni bora tusome shule za Dar es Salaam tu ili tuwe karibu na uangalizi wa wazazi wetu,” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Sitaki kuwa karibu na wazazi wangu Samuel.”

    “Kwa nini?”

    “Watakuwa wakinilazimisha kwenda msikitini.”

    “Sasa hautaki kwenda tena msikitini?”

    “Nimekwishakwambia kwamba sitaki kumtumikia Allah tena. Bora niishi na maisha yangu,” Sadiki alimwambia Samuel.

    “Hapana Sadiki, unachokisema si sahihi kabisa. Maisha bila Mungu hayana kitu kabisa. Kumbuka kwamba hata Mtume Mohammad asingekuwa anamtumikia Mungu asingefika pale alipofika. Alifika pale kwa sababu alikuwa akimtumikia Mungu katika maisha yake na Mungu akaamua kumuinua. Unaposema kwamba hautaki kumtumikia tena Mungu unakosea sana Sadiki,” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Nimekata tamaa Samuel,” Sadiki alimwambia Samuel kinyonge.

    “Huu ndio muda ambao Mungu anataka tumrudie ili aweze kutuinua tena,” Samuel alimwambia Sadiki.

    Safari nzima walikuwa wakiyazungumzia maisha yao. Walijua fika kwamba walikuwa wamefanya mambo mengi sana ambayo hayakuwa yakimpa Mungu Utukufu na hivyo walijiona kuwa na sababu ya kuomba msamaha na hatimae kuishi kama zamani.

    Kwao, Mungu akaonekana kuwaaibisha sana. Kwao, Mungu alionekana kutopenda wao kuishi maisha ya kinafiki na hivyo alitaka shule nzima ijue kile kilichokuwa kikiendelea katika maisha yao ili iwe hata fundisho kwa wanafunzi wengine ambao walikuwa wakibaki shuleni pale.

    “Mungu ameamua kutuaibisha,” Sadiki alimwambia Samuel.

    “Hii ni kwa sababu tulikuwa tukileta unafiki. Mungu hapendi unafiki, Mungu hapendi tusimame mguu moja kwake mmoja kwa shetani, anataka tusimame miguu yote kwake tu au kwa shetani na si kusimama katika falme mbili tofauti. Kupitia aibu tuliyoipata shuleni, Mungu ametaka tujifundishe kitu kimoja,” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Kitu gani?”

    “Kwamba Yeye ndiye Muweza wa kila kitu na kipindi chote alikuwa akichukia maisha ambayo tulikuwa tukiyaishi. Katika maisha yangu yote sitoweza kuisahau aibu ambayo imetukuta shuleni katika kipindi hiki Sadiki. Nitaendelea kukumbuka maishani mwangu mpaka nakufa,” Samuel alimwambia Sadiki.

    Basi lilichukua masaa nane mpaka kuingia jijini Dar es Salaam ambapo wakakodi bajaji ambayo ilianza kumfikisha Samuel Mwenge na kisha kumpeleka Sadiki Magomeni alipokuwa akiishi.

    Samuel alionekana kuwa mnyonge. Katika kipindi ambacho alikuwa akifungua geti la nyumbani kwao, moyo wake ukaongezeka upweke, maneno ya mistari mingi ya Biblia ambayo ilikuwa imeandikwa mlangoni ikaonekana kumchoma kupita kawaida.

    Akaufuata mlango na kisha kusimama. Hakutaka kuingia, akabaki mlangoni pale na kisha kuanza kufikiria maisha yake ya shule na aibu ambayo alikuwa amekumbana nayo. Moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali, kwa wakati huo alikuwa akijuta kwa kuubadilisha moyo wake na kumtumikia shetani kwa nguvu zote.

    Alisimama mlangoni pale kwa muda wa dakika mbili nzima na ndipo akaufungua mlango. Ghafla katika hali ambayo hakuitegemea akakutana na wazazi wake pamoja na ndugu zake wengine ambao walikuwa wameshika maua na kisha kuanza kumwagia huku wakiwa katika nyuso za furaha.

    “Supriseeeeeee,” Wote walisikika wakisema kwa sauti ya juu iliyomshtua Samuel.

    Samuel alionekana kushtuka sana, badala ya kufurahia kile ambacho alikuwa amekutana nacho mahali hapo, bado uso wake ukaonekana kuwa na huzuni jambo ambalo likawafanya wazazi wake, mchungaji Mpelele pamoja na mama yake, Bi Magreth kumsogelea huku wakionekana kushangaa.

    “Kuna nini tena?” Mchungaji Mpelele alimuuliza Samuel ambaye akaliweka begi lake chini na kisha kuanza kulia.

    Kila mmoja akaonekana kushtuka, hawakuelewa ni kitu gani ambacho kilimfanya Samuel kuanza kulia. Hapo ndipo walipoanza kumbembeleza na kisha kuanza kumfanyia maombezi ambayo yalichukua kwa zaidi ya dakika tano.

    “Kuna nini Samuel?” Mchungaji Mpelele alimuuliza Samuel.

    “Nimemtenda Mungu dhambi,” Samuel alijibu.

    “Umemtenda Mungu dhambi?”

    “Ndio baba. Nimekuwa nikimtumikia shetani shuleni,” Samuel aliwaambia.

    “Hebu subiri kwanza. Imekuwaje?” Mchungaji Mpelele alimuuliza kijana wake, Samuel ambaye akaanza kuelezea mengi ambayo yalitokea shuleni.

    Kila mmoja alionekana kushtuka, hawakuamini kama Samuel angeweza kufanya kile ambacho alikuwa amewaelezea mahali hapo. Ilikuwa ni stori ambayo ilimgusa kila mmoja, Samuel, kijana ambaye alikuwa akitarajiwa kuwa mtumishi mzuri wa Mungu hapo baadae tayari alikuwa ameanguka dhambini, dhambi ya uzinzi ilikuwa imemwelemea.

    “Mungu anasamehe kama tu utaomba msamaha kwa kila ulichokifanya. Mungu wetu ni mwingi wa rehema,” Mchungaji Mpelele alimwambia Samuel na kisha kuanza kumuongoza sala ya toba.





    Sadiki akaonekana kukata tamaa, tayari moyo wake ulikuwa umenyong’onyea kupita kawaida, alijiona kutokuwa na nguvu kuwa kama katika kipindi kilichopita. Maisha ambayo alikuwa ameishi shuleni kificho, maisha ya kumtumikia shetani yakaonekana kumuumiza kupita kawaida, aibu ambayo alikutana nayo shule ndio ambayo ilionekana kumdhoofisha kupita kawaida.
    Katika kipindi hicho hakufikiria kuwa mtu wa dini kama alivyokuwa zamani, alitamani kuishi maisha ya peke yake, maisha ya kutokumuabudu Allah na maisha ya kutokumtumikia shetani. Kila wakati Sadiki alikuwa akionekana kuwa mnyonge. Baba yake, ustadhi Hamadi hakupenda kumuona mtoto wake akiwa katika hali hiyo jambo ambalo mara kwa mara alikuwa akimuuliza lakini Sadiki akaonekana kuficha.
    Msikitini hakuwa akienda tena, hakuwa akivaa kanzu tena na wala hakupoteza muda wake wowote kusoma kitabu kitakatifu cha Qur-an . Aliamua kwa moyo mmoja kuishi maisha yake, kwake, mambo ya dini yakaonekana kumuendea kushoto. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Kadri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo chuki kubwa na msikiti ilipokuwa ikimuingia. Hakupenda kuuona msikiti wowote ule, hakupenda kuwaona waislamu wenzake wakiwa wamevaa kanzu na kuelekea msikitini. Maisha ambayo alikuwa akiishi kwa wakati huo yalikuwa ni maisha ya tofauti kabisa.
    “Umebadilika. Umebadilika Sadiki, hata msikitini hautaki kwenda. Kwa nini?” Mzee Hamidu almuuliza Sadiki ambaye alibaki kimya kwa muda.
    Swali hilo likayarudisha mawazo yake nyuma kabisa katika kipindi ambacho alikuwa shuleni, kipindi ambacho alikuwa akileta unafiki mbele ya macho ya watu kwa kujifanya mtu wa dini na wakati alikuwa akifanya mambo mengi gizani yakiwepo ulevi pamoja na uzinzi.
    “Sipendi kwenda msikitini” Sadiki alimwambia baba yake, ustaadhi Hamidu ambaye alionekana kushtuka.
    Kwanza akaanza kumwangalia mtoto wake mara mbili mbili huku akionekana kutokuamini kile ambacho alikuwa amekisikia kutoka kwake. Hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea kwa mtoto wake mpaka kuamua kusema maneno yale huku akionekana kuwa na ujasiri mkubwa kiasi kile. 
    “Unasemaje?” Ustaadhi Hamidu aliuliza huku akionekana kushtuka.
    “Sitaki kwenda msikitini” Sadiki alijibu kwa kujiamini.
    “Kwa nini?
    “Sitaki kutumia falme mbili tofauti. Mimi ni mwenye dhambi baba, sitaki kuwa mnafiki kwa mara nyingine tena” Sadiki alimwambia baba yake ambaye alionekana kutokumuelewa.
    “Kuna kitu gani kimetokea?”
    “Nimekuwa nikiishi maisha ya kumtumikia shetani kwa kipindi kirefu baba, naomba nipumzike, sitaki kuwa mnafiki maishani mwangu. Nimeshindwa kumuabudu Allah” Sadiki alimwambia baba yake, ustadhi Hamidu.
    Maneno yakaonekana kuwa kama mwiba mkali moyoni mwa Ustadhi Hamidu, hakuamini kama kijana wake angeweza kutamka maneno yale kwa kujiamini kiasi kile. Akabaki akimwangalia mara mbili mbili huku akijiona kama mtu ambaye alikuwa akiota.
    Katika maisha yake yote ustadhi Hamidu alikuwa akijitahidi kumlea mtoto wake, Sadiki katika maisha ya kumcha Allah ili baadae aje na kuwa ustaadhi mkubwa kama ambavyo alivyokuwa. Katika kipindi cha nyuma aliona kila kitu kikienda kama alivyokuwa akitaka kiwe hasa mara baada ya Sadiki kuhudhuria mafundisho mengi ya Kiislamu ambayo yalikuwa yakimhusu Mtume Muhammad S.A.W.
    Kwa wakati huo Sadiki akaonekana kubadilika, hakuonekana kuipenda tena dini, hakuonekana kumpenda Allah, alionekana kumsaliti mtume Muhammad S.A.W na wakati katika kipindi cha nyuma aliahidi kwamba kamwe asingeweza kuishi maisha ya dhambi kwani lengo lake kubwa lilikuwa ni kuja kuwa Mufti nchini Tanzania.
    Maisha ya dhambi ambayo alikuwa ameishi shuleni yalionekana kubadilisha kila kitu katika kipindi hicho, alikuwa akiichukia sana dini, hakutaka kujihusisha nayo hata mara moja. Ustaadhi Hamidu bado alikuwa amechanganyikiwa kupita kawaida, maneno ambayo alikuwa ameongea mtoto wake yalionekana kumchanganya kupita kawaida.
    “Umeingiliwa na nini Sadiki? Kwa nini umekuwa hivyo?” Ustaadhi Hamidu alimuuliza mtoto wake, Sadiki.
    “Kwa nini niwe mnafiki baba? Kwa nini nimtumikie Allah na shetani kwa wakati mmoja baba. Haiwezekani, haiwezekani kabisa” Sadiki alimwambia baba yake.
    Huo ndio uamuzi ambao Sadiki alikuwa ameupanga kwa wakati huo, hakutaka kutumikia falme mbili kwa wakati mmoja kwani kwa kufanya hivyo alikuwa akijiona kufanya kitu kibaya katika maisha yake. Maisha ya kumtumikia shetani yakaanza rasmi. Sadiki hakutaka kwenda msikitini kuswali hata mara moja, vitabu vyote vitakatifu vya Qur-an ambavyo vilikuwa chumbani kwake akavitoa na kuviweka katika chumba cha wazazi wake.
    Picha mbalimbali zilikuwa na jumbe nyingi za kumtukuza Allah ambazo alikuwa amezibandika katika ukuta chumbani kwake akazitoa na kisha kuzipeleka chumbani kwa wazazi wake. Katika kipindi hicho hakutaka kujihusisha na kitu chochote cha dini maishani mwake, alitaka kuishi maisha mapya, maisha ambayo hakutakiwa kwenda msikitini au kujihusisha na kitu chochote kuhusiana na dini
    “Ni heri niwe hivi kuliko kuwa mnafiki” Sadiki alijisemea bila kujua kwamba katika kipindi ambacho unapoamua kumuacha Mungu maishani mwako nae hukuacha ili uendelee na maisha yako.
    ****
    Siku ziliendelea kukatika kama kawaida. Mara kwa mara Samuel alikuwa akionana na Sadiki ambaye alionekana kukata tamaa kuhusiana na kumrudia Mungu na kutengeneza mambo yake kama ilivyokuwa katika kipindi cha nyuma. Wazazi wake wakaonekana kukata tamaa lakini kamwe hawakusita kuomba dua kwamba siku moja Sadiki arudi kule alipotoka.
    Katika kipindi hicho, bado hakuwa akielekea msikitini, madrasa ambayo alikuwa amekabidhiwa katika kipindi cha nyuma akaamua kuachana nayo. Maisha ya kuishi bila kufanya ibada au kusoma kitabu chochote cha dini ndio yalikuwa maisha ambayo alikuwa ameamua kuishi kwa wakati huo.
    Moyo wake haukujuta kabisa kutokana na hatua ambayo alikuwa ameichukua katika maisha yake, moyoni mwake, aliona kila kitu kuwa sahihi kabisa. Ustadhi Hamidu hakutaka kukata tamaa kwa mtoto wake, mara kwa mara alikuwa akimsisitiza kumrudia Mungu lakini jambo hilo bado lilionekana kuwa gumu kwa Sadiki ambaye alionekana kuzidi kubadilika.
    Kutokana na kupita kipindi kirefu cha mwezi mmoja bila kunywa pombe, Sadiki akaanza tena kunywa pombe kwa kujificha kwani hakutaka wazazi wake wamgundue kwamba alikuwa ameingia katika ulevi wa pombe. Mara kwa mara alikuwa akijificha sehemu na kisha kunywa kiasi fulani cha pombe na kusha kutafuna Big G ambazo zilikuwa zikimletea harufu fulani mdomoni mwake na kuipoteza harufu ya pombe ile.
    Sadiki hakuishia hapo, bado aliendelea kubadilika zaidi na zaidi mpaka pale ambapo akaanza kutumia mirungi. Kila siku alikuwa akikusanya mirungi mingi ambayo alikuwa akiletewa na rafiki wake wa Kiarabu na kuanza kuitafuna kama mbuzi huku akisindikizia na Big G. Kadri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo Sadiki alizidi kubadilika zaidi na zaidi na kuwa mtu wa tofauti na jinsi alivyokuwa kabla.
    “Mmmh! Mbona unatafuna majani kama mbuzi?” Mama yake, Bi Aisha alimuuliza katika kipindi ambacho alimkuta akila mirungi.
    “Hapana mama” Sadiki alisema.
    “Sasa hiyo ni nini? Au ndio hiyo mibangi yenu?” Bi Aisha alimuuliza Sadiki ambaye wala hakujibu kitu zaidi ya kuondoka mahali hapo.
    Bi Aisha akaonekana kushindwa kuvumilia, alichokifanya mara baada ya mumewe, ustadhi Hamidu aliporudi kutoka msikitini kuswalisha akampa taarifa kuhusiana na majani ambayo alikuwa akiyala Sadiki. 
    Ustadhi Hamidu akaonekana kufahamu dhahiri kwamba majani ambayo mke wake alikuwa akiyazungumzia ilikuwa ni mirungi. Alichokifanya huku akionekana kuwa na hasira, akaanza kuelekea katika chumba cha Sadiki.
    “Umeanza kula mirungi ndani ya nyumba yangu” Ustadhi Hamidu alimwambia Sadiki huku akionekana kuwa na hasira.
    “Yaani unafanya upumbavu wako mwingi unaonekana kutokutosheka mpaka kuja kula mirungi ndani ya nyumba yangu. Yaani mimi baba yako ni Imamu mkubwa hapa Magomeni halafu eti leo ndani ya nyumba yangu unaingiza mirungi. Sadiki...Sadiki....” Ustadhi Hamidu alimwambia Sadiki.
    Moyo wa Ustadhi Hamidu ulikuwa kwenye maumivu makali kupita kawaida. Mabadiliko ambayo alikuwa ameyaonyesha mtoto wake, Hamidu katika kipindi kichache yalionekana kumuumiza kupita kawaida. Kwake, aliyachukulia hayo kuwa sehemu ya majaribu kwa kuona kwamba Mungu alitaka kumjaribu kupitia mtoto wake na hivyo kupunguza kufanya mambo ya ibada.
    “Tatizo nini baba?” Sadiki alimuuliza baba yake huku akiendelea kula mirungi ile.
    “Unaniuliza tatizo nini! Tatizo haulioni Sadiki? Hauoni wewe kula mirungi ni tatizo kubwa?” Ustadhi Hamidu alimuuliza Sadiki.
    “Mbona unanilalamikia sana baba kana kwamba nimekuchukulia mkeo?” Sadiki alimuuliza baba yake swali ambalo lilionekana kumkasirisha sana ustadhi Hamidu.
    “Unasemaje?”
    “Umenisikia vizuri sana. Kila mtu na stimu zake bwana, kama wewe stimu zako kuswali sisi wengine stimu zetu kula mirungi na kunywa pombe” Sadiki alimwambia baba yake.
    “Unanijibu majibu yako ya kipumbavu!!!!”
    “Sikiliza baba, kula mirungi siyo tatizo na ndiyo maana Mungu kauweka mmea huu uendelee kukua. Kama ingekuwa ni tatizo, Mungu asingeruhusu mmea huu ukue, nashangaa unavyonimaindi, ungekuwa wewe ndiye Mungu, nadhani hata ngano usingeiotesha kwa kudai kwamba zinatengenezwa pombe,” alisema Sadiki, maneno hayo yakamkasirisha zaidi baba yake.
    Ni kweli katika maisha yake ustadhi Hamidu alikwishawahi kudharauliwa mara nyingi na vijana wengi lakini kwa dharau ambazo alizionyesha mtoto wake mwenyewe, Sadiki siku hiyo zilionekana kuwa dharau kubwa ambazo hakuweza kuamini. Ustadhi Hamidu hakusema kitu, alichokifanya ni kutoka ndani ya chumba kile huku machozi yakianza kumlenga machoni mwake.
    Moyoni alijisikia akihukumiwa kutokana na kushindwa kumdhibiti Sadiki kutokana na tabia ambayo alikuwa ameianza ya kula mirungi. Hilo likaonekana kuwa pigo kubwa moyoni mwake, kila alipokuwa akielekea msikitini kuswalisha, moyoni mwake kulikuwa kukija sauti ambayo ilikuwa ikimdhihaki kwa kitendo cha kushindwa kumzuia mtoto wake kutumia vilevi mbalimbali.
    Baada ya kipindi fulani, mtaa wa Magomeni mapipa wakafahamu kwamba Sadiki alikuwa amebadilika. Watu wengi wakaonekana kushtuka, kitendo cha Sadiki kubadilika na kuwa namna ile kilionekana kumshtua kila aliyekuwa akisikia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Hawakuamini kama mtoto wa Imamu wa msikiti mkubwa wa Kichangani alikuwa amebadilika na kuwa vile alivyokuwa, hawakuamini kama mwalimu wa Madrasa ya Nur- Munira Sanoor iliyokuwa Magomeni alikuwa amebadilika na kuwa mlevi. Watu wengi wakaanza kuamini kwamba ushirikina ndio ambao ulikuwa umesababisha mpaka Sadiki kuingia katika maisha yale.
    Watu wengi wakaanza kumfuata ustadhi Hamidu na kumshauri kwamba ilikuwa ni lazima aende akaonane na mganga yeyote mkubwa kwa ajili ya tatizo lile lakini ustadhi Hamidu hakutaka kukubaliana nao kabisa. Katika maisha yake hakutaka kumwamini mganga zaidi ya Allah, katika maisha yake hakutaka kuweka tumaini lake kwa mwanadamu yeyote yule.
    Siku zikaendelea kukatika mpaka kufikia kipindi ambacho matokeo ya kidato cha nne yalipotoka. Kama ambavyo walivyotarajia ndivyo ambavyo ilivyokuwa. Samuel na Sadiki walikuwa wamepata sifuri katika mitihani yao jambo ambalo likaonekana kuwa aibu kwa wazazi wao ambao walikuwa ni watu wa ngazi za juu ambao walikuwa wakiheshimika katika dini zao.
    “Umefeli sana. Yaani umefeli sana Sadiki” Ustadhi Hamidu alimwambia Sadiki kwa sauti ya majonzi.
    “Kawaida tu mzee” Sadiki alijibu.
    “Kawaida?”
    “Ndio. Kwani Tanzania nzima nimefeli peke yangu? Halafu kufeli hakumaanishi kwamba sikuwa nikisoma, upepo tu haukuvumia kwangu” Sadiki alimwambia baba yake, ustadhi Hamidu.
    “Badilika Sadiki. Allah si binadamu mpaka umchezee namna hiyo” Ustadhi Hamidu alimwambia Sadiki.
    “Nibadilike! Nitabadilika vipi na nibadilike kuwa nani?” Sadiki aliuliza.
    “Kuwa mtu mwema kama zamani”
    “Kwani sasa hivi mimi sio mtu mwema? Kwani nimeua? Kwani nimebaka? Kitu gani kinakufanya kusema mimi si mtu mwema?” Sadiki aliuliza huku akimwangalia baba yake usoni.
    “Kuwa kama zamani. Acha ulevi Sadiki”
    “Baba unaonekana kuwa si muelewa kabisa. Kama pombe zingekuwa zinamfanya mtu kuwa mbaya basi serikali ingepiga marufuku uuzaji wa pombe hapa nchini, na kama mirungi inamfanya binadamu kuonekana kuwa mbaya basi natumaini hata Mungu asingeweza kuiotesha ardhini hapa duniani. Nadhani vitu hivi vinaonekana kuwa bora na ndio maana serikali imeacha kampuni mbalimbali zitengeneze pombe na hata Mungu kaacha mimiea hii ya mirungi iendelee kuota kwa ajili ya kutufaidisha” Sadiki alimwambia baba yake.
    Katika kipindi cha miezi kadhaa toka Sadiki arudi kutoka shuleni alikuwa amebadilika na kuwa mtu mbaya sana. Muda mwingi alikuwa akijifungia chumbani kwake akitafuna mirungi pamoja na kunywa pombe. Ustadhi Hamidu alikuwa amezungumza nae mpaka kuchoka lakini Sadiki hakuonekana kubadilika kabisa.
    “Ni lazima aende shule tena” Ustadhi Hamidu alimwambia mkewe, Bi Aisha.
    “Mmmh!” Bi Aisha aliguna.
    “Unaguna nini tena mke wangu?”
    “Ataweza kusoma huyu?”
    “Kwa jinsi alivyo, kusoma ngumu sana” Ustadhi Hamidu alimwambia mke wake.
    “Kama hatoweza kusoma, kwa nini tumpleke shule?” Bi Aisha aliuliza.
    “Kwa sababu atoke maeneo ya nyumbani. Ninaamini atakapokuwa huko ataweza kuchana hata kutafuna mirungi yake na kunywa pombe. Cha msingi tumtafutie shule ya bweni ambayo itakuwa na ulinzi mkali” Ustadhi Hamidu alimwambia mke wake.
    Huo ndio uamuzi ambao ulikuwa umefikiwa. Mara baada ya Sadiki kuona kwamba alikuwa akitarajiwa kurudishwa shuleni hapo ndipo alipoanza kuwasiliana na rafiki yake, Samuel na kuanza kuongea nae ili kama ingewezekana basi waende kusoma shule moja.
    “Ila mimi nimebadilika Sadiki, namshukuru Mungu kwa kunibadilisha” Samuel alimwambia Sadiki.
    “Sikiliza Samuel, tunachokiongea hapa si mabadiliko, tunaloongea hapa ni kwenda kusoma shule moja. Mabadiliko yako hayanihusu” Sadiki alimwambia Samuel.
    “Najua ila natakiwa kukuambia ukweli Sadiki”
    “Sawa. Nimekuelewa. Niambie, itawezekana au manake wote tushafeli” Sadiki alimuuliza Samuel.
    “Hakuna tatizo” Samuel alijibu.
    Kama walivyokuwa wamepanga na ndivyo ambavyo ilivyokuwa. Baada ya miezi kadhaa, wakaanza kusoma kwa ajili ya kurudia mitihani yao katika shule ya Makongo huku wote wakiwa wamelilia kutaka kuweka katika hosteli za wanafunzi wa vyuo mbalimbali zilizokuwa Kinondoni. 
    Kitendo cha kuruhusiwa kwenda kusoma katika shule hiyo pamoja na kukaa hosteli yalionekana kuwa makosa makubwa sana. Katika kipindi cha kwanza Samuel alionekana kuwa na msimamo mkali sana kwa kudhani kwamba tayari alikuwa amemrudia Mungu na hivyo alikuwa akiishi Kitakatifu. 
    Katika kipindi cha wiki moja tu cha kukaa na Sadiki tayari kiu ya mambo yale ambayo alikuwa amewaambia wazazi wake kwamba alikuwa ameachana nayo ikaanza kumkaba. Kila alipokuwa akimuona Sadiki akinywa pombe huku akimtambia kwamba alikuwa akikosa utamu na radha iliyo bora duniani, akajikuta akitamani kunywa pombe kwa mara nyingine tena.
    Maisha ambayo alikuwa akiishi zamani ambayo alisema kwamba alikuwa ameachana nayo yakaanza kurudi tena, Samuel akarudia kunywa pombe na kisha kufundishwa namna ya kutafuna mirungi kitu ambacho alipokizoea kilionekana kumpa stimu zaidi na zaidi. 
    Katika maisha yao ndani ya hosteli ile yakaonekana kuwashangaza hata wanachuo ambao walikuwepo ndani ya hosteli ile. Samuel na Sadiki wakaonekana kupenda sana starehe kuliko vitu vingine mahali hapo. Sadiki akawa mtu wa kunywa pombe kwa sana na mirungi huku Samuel akiingia katika tabia nyingine, kutembea na wanawake mbalimbali shuleni.
    Matendo yao yakaonekana kuwashangaza hata walimu, wanafunzi hao ambao walikuwa wameletwa shuleni hapo kwa ajili ya kusoma na mwisho wa siku kurudia mitihani yao ya kidato cha nne walionekana kuwa na maisha ya ajabu ambayo yalikuwa yakimshangaza kila mtu.
    Si kila siku walikuwa wakifika shuleni pale, mara nyingi walikuwa wakikaa chumbani wakinywa na kuvuta sigara mfululizo pamoja na kutafuna mirungi ambayo walikuwa wakiletewa na waarabu ambao waliwafanya kuwa kama wateja wao wakubwa.
    “Badilikeni bwana...mnatuzingua na maisha yenu” Cosmas, kijana ambaye walikuwa wakiishi nae ndani ya chumba kimoja aliwaambia.
    “Tuweje sasa?” Samuel alimuuliza Cosmas.
    “Kama watu wengine mahali hapa. Yaani kwa tabia zenu kila mtu anawashangaa na ndio kwanza mpo sekondari” Cosmas aliwaambia huku akionekana kukasirika.
    “Mbona wewe hubadiliki”
    “Nibadilike kwa lipi?”
    “Kwa kumvua sketi Halima” Samuel alimwambia Cosmas.
    “Hivi unafikiri mapenzi nayashobokea sana kama wewe unavyoyashobokea kwa kutembea na mademu wengi, hiyo sio sifa, mademu ni watu wa kupita tu na kamwe siwezi kuwashobokea. Siwezi kubadilisha kama nguo, mmoja ananitosha na si kama wewe” Cosmas alimwambia Samuel.
    “Nisikilize Cosmas. Ishu si kuwa na demu mmojammoja tu, ishu ni kuwa muaminifu. Unaweza wewe kuwa muaminifu halafu demu unayempata sio mwaminifu” Samuel alimwambia Cosmas.
    “Mimi ni mwaminifu na hata Halima ni mwaminifu pia. Hatuna matatizo katika mahusiano yetu” Cosmas alimwambia Samuel.
    “Usiusemee moyo. Una uhakika Halima ni mwaminifu? Unajiamini kwa kumuwekea dhamana demu? Toka lini demu akawekewa dhamana?”
    “Nina uhakika. Halima ni msichana anayejitambua sana, ni msichana ambaye anaelewa mapenzi ni nini na si kama wasichana wako unaowachukua ambao unawatoa Uwanja wa Fisi” Samuel alimwambia Cosmas.
    “Sasa hizo dharau Cosmas” Sadiki alimwambia Cosmas ambaye alionekana kama mtu mwenye hasira.
    “Ukweli ndio huo. Mademu anaowachukua rafiki yako wote wachafuwachafu tu” Cosmas alimwambia Sadiki na kisha kuinuka mahali hapo na kuondoka.
    Samuel alibaki kimya huku akionekana kuwa na hasira. Hakujua ni kitu gani ambacho alitaka kuongea mahali hapo, baada ya sekunde chache, akasimama na kisha kuanza kutembea tembea ndani ya chumba kile huku akionekana kutokuamini kama maneno yale ambayo yalisikikika masikioni mwake yalikuwa yametoka mdomoni mwa Cosmas.
    “Watu hawa dawa yao moja tu” Samuel alimwambia Sadiki.
    “Ipi?”
    “Kutembea na demu wake na kisha kujipiga picha kadhaa” Samuel alimwambia Sadiki.
    “Hahaha! Hayo mambo nakuachia wewe player...sisi wengine mademu zetu pombe na mirungi tu” Sadiki alimwambia Samuel huku akitafuna mirungi.
    “Ngoja nimuonyeshee jinsi mchezo unavyokuwa” Samuel alimwambia Sadiki.
    “Shida ni kutembea na Halima tu?”
    “Ndio maana yake. Nataka nitembee nae na kisha nimuonyeshee picha ili aache dharau”
    “Utaanzaje kutembea nae?”
    “Kazi ndogo tu. Halima udhaifu wake upo sehemu moja tu” Samuel alimwambia Sadiki.
    “Sehemu gani?”
    “Pombe. Anapenda sana pombe. Ngoja nimuonyeshee kazi” Samuel alimwambia Sadiki huku akionekana kupania kile ambacho alikuwa amekiongea mahali pale.
    “Ila Halima si anakujua?” Sadiki aliuliza.
    “Hanifahamu wala nini, hajawahi kuniona japo sisi tumekuwa tukimuona kila siku” Samuel alimwambia Sadiki.
    “Sasa umjuaje kama anapenda pombe?”
    “Si huwa unamsikia bwana wake anavyosema kwamba demu wake mnywaji mzuri wa pombe, wewe niachie mimi kaka” Samuel alimwambia Sadiki.


    Samuel alikuwa amedhamiria kufanya kile alichokuwa akitaka kukifanya. Shauri mbalimbali ambazo walikuwa wakipewa na Cosmas pamoja na kumsifia msichana wake, Halima kwamba alikuwa mwaminifu vilikuwa ni vitu vilivyomuumiza sana moyoni mwake na kutamani kumuoneshea Cosmas kwamba msichana hakutaka kupewa uaminifu wa asilimia mia moja wala kumsifia kama alivyokuwa akifanya.
    Siku ambayo alikuwa amepanga kuanza kazi kwa Halima ikafika. Cosmas alipokuwa akielekea bafuni kuoga ndicho kikawa kipindi ambacho Samuel akaichukua simu ya Cosmas na kisha kuchukua namba ya Halima na kuihifadhi katika simu yake. 
    B4 Tayari alijiona kukamilisha kila kitu, kitendo cha kupata namba ya simu ya Halima kilionekana kuwa nusu ya ushindi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Walikuwa wakimfahamu sana Halima, udhaifu wake wa kupenda pombe ndio uliowapa uhakika kwamba Samuel angeweza kukamilisha kufanya kile ambacho alikuwa akitaka kukifanya kutokana na kuwa na fedha za kutosha huku nae akipenda sana kunywa pombe.
    “Wewe ni nani?” Ilisikika sauti ya Halima simuni ikimuuliza Samuel ambaye alimpigia simu.
    “Unaongea na Paul,” Samuel alimjibu Halima.
    “Paul, ndiye nani?” Halima aliuliza simuni.
    “Mvulana anayesoma CBE.”
    “Umeipata wapi namba yangu?” Halima aliuliza.
    “Nimeinunua. Nimetoa kiasi cha shilingi elfu kumi na tano kwa ajili ya namba yako tu. Nahitaji kukuona, itawezekana Halima?” Samuel alimuuliza Halima.
    “Haiwezekani,” Halima alisema na kukata simu.
    Samuel akaonekana kusikitika sana, hakuamini kama msichana huyo angeweza kukata simu bila kumsikiliza shida yake. Tayari jambo lile ambalo alikuwa amelipanga pamoja na rafiki yake, Sadiki likaonekana kuwa gumu kufanyika, wote kwa pamoja walikuwa na hamu kubwa ya kuumiza moyo wa Cosmas ambaye alikuwa akimuamini sana msichana wake.
    Samuel hakuishi hapo, kila siku alikuwa akipata kazi kubwa ya kumpigia simu Halima. Mara nyingi simu ilikuwa ikiita bila kupokelewa na kama ilitokea kupokelewa, basi alikuwa akipokea msonyo mmoja na kisha simu kukatwa.
    Samuel hakutaka kukata tamaa, kila siku ndoto yake ilikuwa ile ile tu, kutaka kumuingiza Halima katika mikono yake ili apate nafasi ya kumuumiza Cosmas na kumuonyeshea kwamba wanawake hawakutakiwa kuonyeshewa uaminifu wa hali ya juu kama alivyokuwa akifanya kwa msichana Halima.
    Siku zikaendelea kukatika, Samuel hakukoma kumpigia simu Halima. Mara kwa mara tena kila siku alikuwa akimpigia simu Halima lakini hali ilikuwa ile ile. Hapo ndipo Samuel akapata wazo jipya, wazo ambalo aliliona kufaa sana, akaanza kuandika meseji nyingi na kumtumia. 
    Samuel alijua fika kwamba meseji zote zile ambazo alikuwa akizituma Halima alikuwa akizipokea na kuzisoma. Hata kama alikuwa akizifuta lakini bado alikuwa amekwishazisoma na kujua ni uhitaji gani ambao Samuel alikuwa akiutaka kutoka kwake.
    Mwezi mzima Samuel alikuwa akiendelea kumtafuta Halima na kumuingiza katika himaya yake. Kwa kiasi fulani meseji ambazo alikuwa akimtumia zikaonekana kuanza kumbadilisha Halima. Kwa sababu zilikuwa ni kati ya meseji zenye kugusa moyo na zilizoonyesha uhitaji mkubwa, Halima akaonekana kuanza kubadilika kwa kuanza kupokea simu na kumsikiliza Samuel alikuwa na shida gani.
    “Kwa nini unataka kuonana nami Paul?” Halima aliuliza.
    “Ninataka kuongea nawe Halima. Kuna tatizo hapo?” Samuel alimuuliza.
    “Ndio. Kuna tatizo.”
    “Tatizo gani?”
    “Tena sio tatizo, kuna matatizo.”
    “Matatizo gani?”
    “Sina muda.”
    “Hilo siyo tatizo. Naomba uniambie tatizo Halima” Samuel alimwambia Halima.
    “Huwa sipendi kukutana na watu nisiowafahamu.”
    “Kwa sababu gani?”
    “Basi tu huwa sipendi.”
    “Acha uoga Halima. Kukutana na watu usiowafahamu ndio mwanzo wa kuwafahamu. Nadhani marafiki zako wote ambao uliwahi kukutana nao kwa mara ya kwanza haukuwa ukiwafahamu, si ndio hivyo?” Samuel alimuuliza halima.
    “Yeah!”
    “Na baadae ukaja kuwafahamu, si ndio hivyo?”
    “Yeah!”
    “Basi nadhani hilo si tatizo, hata nami utakwenda kunifahamu tu.” Samuel alimwambia Halima.
    Japokuwa Samuel alikuwa akitumia sana vilevi lakini akili yake katika kufanya mazungumzo ilikuwa na uwezo mkubwa sana. Ushawishi wake mkubwa ambao alikuwa nao maishani mwake ulikuwa na uhakika wa asilimia kubwa ya kubadilisha mambo mengi sana katika akili ya mtu. Kitendo cha Halima kukubali kumsikiliza Samuel kwa muda wa dakika mbili tu, tayari akaonekana kuwa mtu ambaye hakuwa na tatizo lolote lile.
    “Lakini kwa nini unataka kuonana nami Paul?” Halima alimuuliza Paul.
    “Nahitaji kukufahamu zaidi. Nimejaribu kukutafuta kwa muda wa mwezi mzima Halima, hivi kama nisingekuwa na umuhimu wa kuonana nawe si ningeachana nawe Halima. Hebu wakati mwingine naomba uuthamini uvumulivu wangu ambao nimejiwekea juu yako, mwezi mzima halafu bado unataka kunikatalia! Hiyo ni dhambi Halima” Samuel alimwambia Halima.
    Katika kila neno ambalo alikuwa akiongea mahali hapo lilikuwa likiubadilisha moyo wa Halima na kumfanya kukubaliana nae. Tayari kwa maneno yake ambayo alikuwa akiyaongea, kwa majibu yake ambayo alikuwa akiyajibu, moyo wa Halima ukaonekana kubadilika, kiu ya kutaka kuonana na mvulana huyo na kuongea nae ikaonekana kuanza kumshika.
    “Ok! Tutaonana nikimaliza mitihani,” Halima alimwambia Samuel.
    “Mnaanza lini hiyo mitihani?”
    “Wiki ijayo.”
    “Mbona mbali sana Halima. Yaani unataka kuniweka na presha wiki nzima na wakati nilikuwa na kiu ya kuonana nawe kwa mwezi mzima. Tafadhali Halima naomba usinifanyie hivi,” Samuel alimwambia Halima kwa sauti ya kipole.
    “Nina mitihani Paul.”
    “Najua. Ila sidhani kama kuonana nawe kwa dakika ishirini kutakufanya kufeli au kutosoma. Naomba tuonane hata kesho,” Samuel alimwambia Halima.
    “Kesho?”
    “Ndio. Kwani kuna tatizo hapo?”
    “Yeah! Kesho nitakuwa bize sana.”
    “Masaa ishirini na nne?”
    “Bado sijajua.”
    “Naomba unisikilize Halima. Kwenye masaa ishirini na nne ambayo ni sawa na dakika 1440 ninahitaji dakika 20 tu za kukutana nawe na kuongea. Nakuomba Halima,” Samuel alimwambia halima huku akijaribu kuiweka sauti yake katika huruma.
    “Sawa. Dakika ishirini tu,” Halima alimwambia Samuel.
    “Nitakuwa mwaminifu katika hilo,” Samuel alimwambia Halima.
    Hapo ndipo walipopanga kuonania. Kwa Samuel hakutaka kuonana na Halima katika sehemu tofauti na baa kwa kuamini kwamba kama wangeonana katika sehemu hiyo basi ilikuwa ni lazima kwa Halima kunywa pombe jambo ambalo lingempa urahisi wa kutaka kufanya kile alichokuwa akitaka kukifanya.
    “Nakwenda kuonana naye pale Kijitonyama Bar usiku wa leo” Samuel alimwambia Sadiki.
    “Acha utani.”
    “Siwezi kukutania. Huyu mjinga atalia na kunichukia milele,” Samuel alimwambia Sadiki.
    Samuel hakutaka kuchelewa, kwa sababu walikuwa wamepanga saa mbili ndio muda wa kuonana na kuongea, akajitahidi kufika kabla ya muda husika. Saa moja na nusu tayari alikuwa katika baa hiyo ambapo akaagiza pombe na kisha kuanza kunywa taratibu huku akimsubiria Halima.
    Saa 2:17 usiku, Halima akaonekana kusimama pembeni mwa baa ile huku akiangalia huku na kule. Samuel akaiwasha simu yake na kisha kuuinua mkono wake ulioshika simu na mwanga kuelekea kule alipokuwa Halima, Halima alipouona mwanga huo, akaanza kusogea mahali pale. Samuel akasimama.
    “Karibu Halima,” Samuel alimkaribisha Halima huku akimvutia kiti na kutulia.
    “Asante. Samahani Paul, sina muda mrefu wa kukaa hapa,” Halima alimwambia Samuel.
    “Usijali, sitochukua muda wako mrefu,” Samuel alimwambia Halima. 
    Hapo hapo bila kupoteza muda wowote ule Samuel akamuita mhudumu na kisha kumtaka kumsikiliza Halima alihitaji kinywaji gani. Mhudumu akafika mahali pale na kutakiwa kumsikiliza halima.
    “Naomba Fanta,” Halima alimwambia mhudumu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Unakunywa soda? Acha utani Halima. Hebu agiza vinywaji vya watu wazima bwana. Toka lini mtu mzima akanywa soda,” Samuel alimwambia Halima huku akijichekesha. 
    “Naomba Kilimanjaro,” Halima alimwambia mhudumu huku akitoa tabasamu.
    “Tunahitaji nyama ya kuchoma pia” Samuel alimwambia mhudumu yule ambaye aliondoka mahali hapo.
    Wote wakabaki wakiangaliana mahali hapo, hakukuwa na mtu ambaye aliongea jambo lolote lile, macho yao yalionekana kama kutamaniana. Alichokifanya Samuel ni kuchukua chupa yake na kisha kupiga fundo moja na kukiweka vizuri kiti chake.
    “Nashukuru kwa kuja,” Samuel alimwambia Halima.
    “Usijali,” Halima alimwambia Samuel.
    Huo ndio ukawa mwanzo wa mazungumzo yao, katika kipindi chote hicho walikuwa wakiongea mambo mengi. Halima hakuonekana kumfahamu Samuel japokuwa Samuel alikuwa akimfahamu Halima kutokana na kumuona mara kadhaa akiwa pamoja na Cosmas.
    Ndani ya dakika kumi ya mazungumzo yao wakaonekana kuzoeana sana kana kwamba walikuwa wamefahamiana kwa zaidi ya mwaka mzima. Kila mmoja akajitahidi kuonyesha uchangamfu kwa mwenzake, kila mtu akajitahidi kumuonyeshea mwenzake kwamba alikuwa akijali sana ukaribu wao huo.
    “Unaongea sana Paul,” Halima alimwambia Samuel
    “Hahaha! Ila sikushindi wewe. Natumaini utakuja kuwa mwanasiasa baadae,” Samuel alimwambia halima.
    “Hapana. Sipendi kuwa mwanasiasa.”
    “Basi utakuwa mwandishi wa habar,i” Samuel alimwambia Halima na kisha wote kuanza kucheka.
    Wakazidi kuongea zaidi, wakala na kunywa mahali hapo. Kwa kipindi fulani Halima akaonekana kujisahau kabisa, akasahau kwamba alikuwa na mpenzi wake. 
    Japokuwa alikuwa amemwambia Samuel kwamba wangetumia muda wa dakika ishirini tu kuongea lakini wakajikuta wakitumia muda zaidi na zaidi mahali hapo.
    Samuel hakutaka kuishia hapo, chupa ya pombe ya Halima ilipokuwa ikiishia, aliagiza nyingine na kuendelea kunywa. Waliendelea kuyafurahia maisha mpaka katika kipindi ambacho Halima akaonekana kutokujiweza, chupa kadhaa za pombe ambazo alikuwa amekunywa zikaonekana kumlewesha kupita kawaida. 
    “Umelewa?” Samuel alimuuliza Halima huku akimshika mkono.
    “Sijalewa,” Halima alijibu huku akijifanya kuwa imara.
    “Hahaha! Kama haujalewa basi tuendelee,” Samuel alimwambia Halima na kisha kuendelea kuhitaji pombe zaidi.
    Katika kipindi chote hicho Samuel alionekana kuwa makini, alikuwa akiagiza pombe lakini hakuwa akinywa kama alivyokuwa akinywa siku nyingine. Taiming yake muda wote ilikuwa ni kumvizia halima alewe na kisha kufanya kile ambacho alikuwa akitaka kukifanya. Ilipofika saa tano usiku, Halima akaonekana kutokujiweza, mwili wake ukakosa nguvu kabisa. 
    Alichokifanya Samuel ni kumchukua na kisha kuondoka nae mahali hapo huku akiwa amemshikilia kiuno. Akaita bajaji na kisha kuondoka katika eneo la baa hiyo huku Halima akionekana kutokujielewa kabisa.
    “Wapi braza?” Dereva wa bajaji alimuuliza Samuel.
    “La Vista Inn.”
    “Ile ya Magomeni au Sinza?”
    “Twende ya Magomeni,” Samuel alimwambia dereva wa bajaji.
    Hapo hapo safari ya kuelekea katika hoteli hiyo ikaanza. Moyoni mwa Samuel alikuwa akijiona kuwa na uharaka mkubwa sana wa kukamilisha kile ambacho alikuwa amekipanga kwa wakati huo. Kitendo cha Cosmas kumtambia kila siku kwamba msichana wake, Halima alikuwa mwaminifu sana kilionekana kumkera kupita kawaida.
    Walichukua dakika kumi mpaka kufika katika hoteli hiyo ambapo Samuel akalipa fedha na kisha kukabidhiwa ufunguo wa chumba namba 23. Akaanza kuondoka na Halima kupanda ngazi mpaka kufika kwenye korido ambayo ilikuwa na chumba hicho. 
    Katika kipindi chote hicho Halima hakuwa akijitambua, kiasi kikubwa cha pombe ambacho alikuwa amekunywa kilionekana kumlewesha kupita kawaida.
    Walipofika chumbani, Samuel akamlaza Halima kitandani na kisha kuanza kumvua nguo moja baada ya nyingine huku Halima akiwa ametulia tu. Alimvua nguo zote mpaka kumuacha mtupu na ndipo nae akaanza kuvua nguo zake. Alipojiona amekuwa mtupu, akachukua simu yake ambayo ilikuwa na uwezo mkubwa wa kupiga picha na kisha kuanza kumpiga picha Halima.
    Kwa kuwa hakuwa akijitambua kitandani pale, hata picha mfululizo ambazo alikuwa akipigwa huku akigeuzwa huku na kule hakuonekana kutambua chochote kile. Samuel hakuridhika, alichokifanya ni kumpigia simu Sadiki na kisha kumpa kile kilichokuwa kikiendelea chumbani pale.
    “Umefikia wapi?”
    “Hahaha! Chezea pombe wewe. Pombe sio chai kaka,” Samuel alimwambia Sadiki.
    “Unanitia presha. Umefikia wapi?” Sauti ya Sadiki ilisikika simuni.
    “Yupo hoi kitandani. Ngoja nikutumie picha zaidi ya themanini kupitia whatsApp,” Samuel alimwambia Sadiki na kisha kuanza kumtumia sadiki picha alizokuwa amempiga halima kitandani pale.
    Siku hiyo hiyo ndio ilikuwa siku ambayo Samuel akafanya sana mapenzi na Halima kitandani pale huku bado akiwa amelewa kupita kawaida. Alijipiga picha mbalimbali huku akiwa kifuani mwa Halima. 
    Japokuwa kitendo kile kilionekana kuwa kama udharirishaji kwa mwanamke lakini kwake yeye wala hakuonekana kulijali hilo, kitu ambacho alikuwa akikifanya mahali hapo kama kumuonyeshea Cosmas kwamba alikuwa na uwezo wa kulala na mwanamke yeyote ambaye alikuwa akimtaka bila wasiwasi wowote ule. Mara baada ya kufanya nae mapenzi zaidi ya dakika themanini, akalala pembeni ya Halima.
    Asubuhi ilipofika, Samuel akaamka na kisha kuelekea bafuni. Akaagiza supu iletwe ndani ya chumba kile pamoja na chai, vyote vikaletwa. Baada ya muda fulani, Halima akaamka kutoka usingizini. 
    Kitu cha kwanza, akaanza kushangaa mahali ambapo alipokuwa katika, akaanza kuangalia huku na kule, hakuonekana kupafahamu mahali hapo. Alipoangalia pembeni, macho yake yakatua usoni mwa Samuel.
    Hapo ndipo Halima alipoonekana kurudiwa na kumbukumbu. Hata kabla hajauliza kitu chochote kile, akajifunua shuka lake, alikuwa mtupu. Akashtuka kupita kawaida, hakutaka kubaki hapo, akauchukua mkono wake na kuuingiza sehemu zake za siri, akagundua kwamba alikuwa amefanya mapenzi jambo ambalo lilionekana kumshtua.
    “Paul,” Halima aliita huku akionekana kubadilika.
    “Naam mpenzi.”
    “Tumefanya mapenzi?”
    “Ndio mpenzi. Kuna tatizo?” Samuel alijibu na kisha kuinuka na kuanza kusogea kitandani pale.
    Uso wa Halima tayari ukaanza kubadilika mahali pale, akaonekana kuanza kuingiwa na chuki moyoni mwake juu ya Samuel ambaye alionekana kutokuwa na wasiwasi hata kidogo. 
    Hapo ndipo Halima alipoonekana kujutia hatua ambayo aliichukua ya kunywa pombe kupita kiasi katika kipindi ambacho alikutana na Samuel.
    “Kwa nini tumefanya mapenzi? Kwa nini tumefanya mapenzi Paul?” Halima aliuliza huku akionekana kuwa na hasira.
    “Kwa sababu ninakupenda Halima. Umekuwa msichana muhimu sana katika maisha yangu. Mara kwa mara nimekuwa mtu wa kukuhitaji sana. Nilikuwa radhi kupoteza muda mwingi kwa ajili yako Halima, nilikuwa naisubiria nafasi hii katika kipindi kirefu sana kilichopita: 
    “Leo imeonekana kuwa nafasi kubwa sana kwangu. Nakupenda Halima” Samuel alimwambia Halima huku tayari akiwa amekwishafika kitandani pale na kumkumbatia.
    Maneno ambayo mara kwa mara Samuel alikuwa akiongea mahali hapo yalionekana kuwa faraja sana kwa Halima ambaye alikuwa akiyasikiliza. Kwake, tayari alimuona Samuel kuwa mtu ambaye alikuwa na mapenzi ya dhati, mtu ambaye alikuwa tayari kufanya kitu chochote kwa ajili yake katika maisha yake.
    Japokuwa katika kipindi cha sekunde chache kilichopita alikuwa na hasira lakini akajikuta hasira zote zikianza kutoweka, maneno matamu ambayo alikuwa akizidi kuyaongea Samuel mahali hapo yalionekana kuipoteza hasira yote ambayo alikuwa nayo moyoni mwake dhidi yake.
    “Sikufanya makusudi baby, nilikuwa nimevutiwa nawe toka kitambo. Jana usiku tulilewa sana, nikashindwa kuzizuia hisia zangu juu yako hasa mara baada ya kuuona uzuri wa umbo lako. Kama nimefanya makosa naomba unisamehe,” Samuel alimwambia Halima.
    Japokuwa ilikuwa ni siku ya kwanza kwa Halima kulala na Samuel lakini akaonekana kuanza kumuamini mwanaume huyo. Hata jina lake halisi hakuwa akilifahamu lakini kwa sababu Samuel alikuwa mtu wa maneno mengi, akajikuta akikubaliana nae. 
    Wakakumbatiana kitandani hapo huku Halima akiendelea kutokwa na machozi, kilichotokea, wakaanza kunyonyana ndimi zao na mwisho wa siku kuanza kufanya mapenzi kwa mara nyingine tena.
    Kwa Samuel jambo lile likaonekana kuwa kama ushindi moyoni mwake. Kufanikiwa kufanya mapenzi na Halima mahali pale kilionekana kitendo cha ushindi ambacho alikuwa akikitaka sana kifanikiwe katika maisha yake. Lengo lake kubwa si kwamba alikuwa amevutiwa sana na Halima, hapana, lengo lake lilikuwa ni kutaka kumuumiza sana Cosmas kwa kumuonyeshea kwamba kama mwanaume haukutakiwa kumuamini sana mwanamke.
    Kitendo kile kilichukua zaidi ya saa moja na ndipo wakanywa chai. Hawakutaka kutoka chumbani humo siku hiyo, walikuwa wakiongea mengi huku wakifanya mapenzi mara kwa mara. 
    Kwa Samuel, hakutaka kuwa mkweli hata mara moja, kwa sauti ya unyenyekevu ambayo alikuwa akiitumia masikioni mwa Halima ilionekana kuuficha ubaya ambao alikuwa nao.
    “Una mpenzi?” Lilikuwa swali ambalo lilitoka mdomoni mwa Samuel.
    “Yeah! Ninaye,” Halima alijibu huku wote wakiwa watupu kitandani pale.
    “Unampenda kama unavyonipenda?” Samuel alimuuliza.
    “Sijui nijibu nini.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Kwa nini?”
    “Sijui mpenzi.”
    “Mpenzi wako anaitwa nani?” Samuel alimuuliza.
    “Anaitwa Issa,” Halima alitoa jibu ambalo lilionekana kumshtua Samuel.
    “Anaitwa nani?”
    “Anaitwa Issa. Ninampenda sana na ninaamini nae ananipenda pia,” Halima alimwambia Samuel.
    Hapo Samuel akaonekana kugundua kitu. Akagundua kwamba Halima hakuwa mwaminifu kwa Cosmas japokuwa Cosmas alikuwa akitamba sana kila siku. Halima hakuwa msichana mwenye mpenzi mmoja, hata Cosmas ambaye mara nyingi alikuwa akitamba kwamba alikuwa peke yake kumbe nae alikuwa ni mwanaume wa pembeni tu.
    Samuel akaonekana kuwa na uhakika zaidi kwamba mwanamke hakutakiwa kuaminiwa hata mara moja. Kwa Halima, tayari alionekana kuwa mtu ambaye alimfanya kuwa na uhakika juu ya kile ambacho alikuwa akifikiria siku zote. Huo haukuwa mwisho wake, aliendelea kufanya mapenzi zaidi na zaidi.
    “Na wewe una mpenzi?” Halima alimuuliza Samuel mara baada ya kufanya tena mapenzi.
    “Sina. Demu wangu alikuwa pombe tu,” Samuel alimwambia Halima.
    “Kwa nini hukutafuta msichana?”
    “Basi tu. Unajua hapo kabla nilikuwa na msichana, aliniumiza sana na kuahidi kwamba nisingeweza kuwa na msichana tena. Kuanzia hapo, demu wangu akawa pombe, tukawa tunapenda, tunalala wote au wakati mwingine namuweka kwenye friji alale peke yake. Tunapenda mpaka sasa,” Samuel alimdanganya Halima uongo ambao ulimfanya kuanza kucheka.
    “Nimekuelewa,” Halima alimwambia Samuel.
    “Kwa hiyo inamaanisha kwamba kuanzia leo sisi ni wapenzi?” Samuel alimuuliza Halima.
    “Wewe unaonaje?”
    “Mbona unaniuliza kimitego sana. Unatakiwa kunijibu Halima,” Samuel alimwambia halima.
    “Nadhani. Sisi ni wapenzi ila ni wapenzi wa siri. Nina mpenzi wangu, Issa, sitaki siku ajue kwamba nina mvulana mwingine,” Halima alimwambia Samuel ambaye akaonekana kuelewa.
    Siku hiyo ndio ilikuwa siku ambayo Samuel akaanzisha uhusiano wa siri na Halima. Kila mmoja kwa kipindi hicho alimuahidi mwenzake kwamba angempenda siku zote. Kwa Samuel, maneno yote ambayo alikuwa akimwambia Halima wala hakuwa akimaanisha hata kidogo, alikuwa amedanganya sana.
    Hakuwa na mapenzi yoyote kwa Halima, kitu ambacho alikuwa akikitaka kutoka kwa msichana huyo ni kufanya nae mapenzi na kisha kujipiga picha na mwisho wa siku kumuonyeshea Cosmas ambaye alikuwa akimuamini sana Halima. 
    Waliendelea kukaa ndani ya chumba kile mpaka ilipofika jioni muda ambao wakaagana kwa mapenzi motomoto huku wakipeana mabusu mfululizo na kisha kuondoka kila mtu kuelekea alipokuwa akiishi huku wakiahidiana kuendelea kuwasiliana zaidi.


    “Nisikilize,” Samuel alimwambia Sadiki ambaye alikuwa akimsikiliza.
    “Niambie ilikuwaje.”
    “Yule demu anaabudu sana pombe.”
    “Kwa hiyo ikawaje?”
    “Nikamnywesha sana pombe mpaka akawa hajiwezi.”
    “Duuh!”
    “Yeah. Baada ya hapo nikampeleka katika hoteli yetu ile.”
    “Ipi? La Vista Inn?”
    “Kama kawa. Baada ya hapo, kilichoendelea ndio nikakituma kwa simu yako,” Samuel alimwambia Sadiki.
    “Wewe noma kaka.”
    “Ndio hivyo. Ninachokitafuta ni heshima tu. Nataka kifike kipindi watu tuanze kuheshimiana,” Samuel alimwambia Sadiki.
    Muda wote Samuel alikuwa akijisifia kwa Sadiki mara baada ya kutoka kufanya mapenzi na Halima. Kwake, alijiona kuwa mshindi kwa kutekeleza kile ambacho alikuwa amekipanga kukitekeleza katika kipindi cha nyuma.
    Kitendo cha Cosmas kujitamba kwao kwamba mpenzi wake alikuwa mwaminifu na asiyeyebabaika na vitu vidogovidogo kama wasichana ambao alikuwa akiwachukua Samuel ndicho kitu ambacho kilimfanya Samuel kutumia mwezi mzima kumtafuta Halima mpaka pale ambapo alifanikiwa kumpata na kufanya nae mapenzi huku ushahidi akiwa nao simuni.
    “Ila kuna kitu kingine nimekijua,” Samuel alimwambia Sadiki.
    “Kitu gani?”
    “Demu ana jamaa yake mwingine anaitwa Issa,” Samuel alimwambua halima.
    “Umejuaje?”
    “Aliniambia.”
    “Kwa hiyo hata Cosmas nae anachunwa tu?”
    “Hiyo ndio maana yake.”
    Wote wakabaki wakicheka. Kila mmoja alionekana kuwa na furaha kupita kawaida, kitendo cha Samuel kufanikisha kutembea na Halima kilionekana kumfurahisha kila mmoja mahali hapo. Walikuwa wakipiga strori wakicheka na kugongesheana mikono. Hata katika kipindi ambacho Cosmas aliingia ndani ya chumba kile, bado walikuwa wakicheka tu.
    “Karibu mgeni,” Samuel alimkaribisha Cosmas huku akicheka jambo ambalo lilionekana kumkasirisha Cosmas.
    “Kuwa na nidhamu basi Samuel. Wakati mwingine ujinga unakuwa sio ishu,” Cosmas alimwambia Samuel ambaye bado alikuwa akiendelea kucheka.
    “Tatizo lake anapenda kuchukua wanawake wachafu huyu ndio maana anaonekana kuwa hana nidhamu,” Sadiki alimwambia Cosmas.
    Katika kila kipindi ambacho walikuwa wakimwangalia Cosmas walikuwa wakicheka tu. Kitendo kile cha kutembea na Halima kiliwafanya kumdharau sana Cosmas kiasi ambacho walimuona kuwa si lolote lile. Thamani yake kwao ikashuka sana, wakamuona kama mtu mshamba ambaye alikuwa akimuwekea dhamana msichana kwa asilimia mia moja.
    Hayo ndio yalikuwa maisha yao ya kila siku. Japokuwa wazazi wao walikuwa viongozi wa dini lakini wao walikuwa wakiishi maisha ya tofauti sana. Bado walikuwa wakilewa sana jambo ambalo liliwafanya hata wanachuo waliokuwa wakiishi katika hosteli hiyo kuwalalamikia sana na mwisho wa siku kuamua kuwafukuza katika hosteli hiyo.
    Hawakubadilika hata kidogo, walichokifanya baada ya hapo ni kwenda kupanga chumba mitaani na kufanikiwa kupata chumba kilichokuwa mtaa wa Tandale Kwa Mtogole. Huko, maisha yao yakaonekana kubadilika zaidi, wakakutana na watu wengi ambao walikuwa wakitumia pombe, watu ambao walikuwa wakivuta bangi kwa wingi, nao wakaingia katika mfumo huo.
    Maisha yao yakazidi kubadilika zaidi na zaidi, hawakutaka tena shule japokuwa kila siku wazazi wao walikuwa wakijitahidi sana kuwatumia fedha kwa kuamini kwamba watu hao walikuwa wakiendelea kusoma. Tabia zao wakaambukizana. Sadiki akamfundisha Samuel kutumia mirungi huku Samuel akimfundisha Sadiki namna ya kuwachukua wanawake mbalimbali mtaani.
    Wote wakaanza kubadilisha wanawake. Kwa sababu walikuwa na fedha nyingi ambazo walikuwa wakitumiwa mara kwa mara na wazazi wao, wanawake wakaanza kuwababaikia na kisha kuanza kufanya nao mapenzi. Maisha kwao yakaonekana kuwa kitu kingine kabisa, hawakutaka kujithamini kabisa, walikuwa wakifanya vile ambavyo waliviona kustahili kuvifanya kwa wakati huo.
    Huko Tandale ndipo ambapo wakampata mtu mmoja ambaye alikuja kuwa rafiki yao sana, huyu alikuwa Tenende. Tenende alikuwa mmoja wa vijana ambao walikuwa wakisifika sana katika mtaa wa Tandale kutokana na tabia chafu mbalimbali kama uporaji, uvutaji bangi pamoja na vitu vingine. Watu wengi waliokuwa wakiishi Tandale walikuwa wakimhofia Tenende ambaye maisha yake yalikuwa yakitawaliwa na uchafu mwingi.
    Huyo ndiye ambaye alikuja kuwa rafiki yao wa karibu, Tenende ndiye ambaye walikuwa wakimtumia katika kuwanunulia bangi na kuwaonganisha kwa watu wengine ambao walikuwa watumiaji wazuri wa vilevi kama bangi na madawa ya kulevya. Japokuwa walikuwa wakivuta bangi na hata kutumia vilevi vingine lakini Samuel na Sadiki walikuwa wakionekana kuwa wasafi muda wote, walikuwa wakivaa vizuri huku wakijitunza kadri walivyoweza jambo ambalo lilikuwa liwavutia wasichana wengi kwao.
    “Kuna UKIMWI,” Sadiki alimwambia Samuel.
    “Nakumbuka. Kwani wewe ulishasahau hilo?”
    “Hapana. Tunatakiwa kujikumbusha mara kwa mara kuhusiana na jambo hilo kwamba UKIMWI upo na unaua,” Sadiki alimwambia Samuel.
    “Nafahamu. Siwezi kusahau hilo. Mtoto Joah vipi?” Samuel alimuuliza Sadiki.
    “Yupo freshi. Jana mama yake alizingua lakini natumaini leo atakuja kama kawaida,” Sadiki alimwambia Samuel.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Kila kitu ambacho kilikuwa kimepita katika maisha yao ya nyuma kwa wakati huo kilikuwa kimesahaulika, Wakaonekana kusahau kwamba wazazi wao walikuwa wamewaandaa kwa kipindi kirefu sana na kuja kumtumikia Mungu kama ambavyo wao walivyofanya.
    Anasa za dunia zikawateka, hawakukumbuka kitu chochote kwa wakati huo, kile ambacho walikuwa wakikikumbuka ni kuendelea kutumia vilevi kadri walivyoweza.
    Wazazi wao walikuwa wakiendelea kuwatumia fedha kwa kujua kwamba watoto wao walikuwa wakiendelea kwenda shule kama kawaida. Matendo ambayo walikuwa wakiyafanya hayakuwa yakitambulika na wazazi wao. Japokuwa hawakuwa wakiwaamini sana lakini kwa kitendo cha kuwaachia waende kupanga katika hosteli kilionekana kama kuwapoteza kabisa.
    “Kuna bonge la mchongo,” Tenende aliwaambia katika kipindi ambacho aliwaletea bangi.
    “Mchongo gani?”
    “Khaled amerudi jana.”
    “Khaled! Ndiye nani?”
    “Jamaa ambaye anafanya kazi na mabosi wakubwa hapa Tanzania,” Tenende aliwaambia.
    “Mabosi gani?”
    “Kumbe mlikuwa hamjui! Kuna jamaa anaiwa Khaled, jamaa ana fedha chafu, yaani ana fedha mpaka anapagawa,” Tenende aliwaambia.
    “Unazidi kutuchanganya. Ndiye nani huyo?” Sadiki aliuliza.
    “Jamaa ambaye anachukua mizigo hapa anaipeleka huko bara la Asia,” Tenende aliwaambia.
    “Bado unatuchanganya,” Samuel alimwambia Tenende.
    “Dah! Naona kama hamnielewi. Ishu ipo hivi, jamaa anatengeneza sana fedha kwa kupeleka poda barani Asia. Alitaka nami nijiunge nae, nilipokwenda kwa wakubwa zake, wakanitoa nduki,” Tenende aliwaambia.
    “Poda ndio nini?” Samuel alimuuliza Tenende.
    “Poda ni madawa ya kulevya Samuel,” Sadiki alimwambia Samuel.
    “Kwa hiyo Khaled amepata fedha kijingajinga. Hivi sasa anatengeneza sana fedha huwezi amini. Alipeleka mizigo kadhaa tu, nae sasa hivi kawa bosi,” Tenende aliwaambia huku akionekana kuwa na shauku ya watu hao kuingia katika uuzaji huo.
    “Ok! Vizuri,” Sadiki alimwambia Tenende.
    “Sasa nyie vipi? Hamtaki kupata fedha?” Tenende aliwauliza.
    “Kwa njia hii ya uuzaji?”
    “Yeah! Unatengeneza fedha sana.”
    “Sasa kwa nini usingetengeza wewe?”
    “Mabosi wake walinikataa.”
    “Kwa nini walikukataa.”
    “Eti ningekimbia na mizigo yao kwani waliniona kuwa mlevi sana,” Tenende aliwaambia.
    Muda mwingi Tenende alikuwa akiongea kuhusiana na Khaled huku lengo lake likiwa ni kuwataka Sadiki na Samuel wakubaliane nae na hatimae waingie katika uuzaji wa madawa ya kulevya na kisha kujiingizia fedha kwa kuamini kwamba kama watu hao wangeingia na kupata fedha basi hata yeye pia angeweza kupata fedha.
    Kutokana na Tenende kuongea sana kuhusiana na Khaled tena ikiwa mara kwa mara, hapo ndipo walipokubaliana kwamba kulikuwa na umuhimu wa kukutana na Khaled na kisha kuanza kuzungumza nae. Tayari maneno mengi ya Tenende pamoja na sifa ambazo alikuwa akizitoa kuhusiana na Khaled zilionekana kuwaingia vilivyo mioyoni mwao.
    Hiyo ikaonekana kuwa furaha kwa Tenende, hakutarajia kama watu hao wangeweza kukubaliana nae na hatimae kutaka kuonana na Khaled ambaye alikuwa akisifika kwa fedha katika kipindi hicho. Walichokifanya ni kutaka kuonana nae kwa haraka sana kwani nao pia walikuwa wakitamani kuwa na fedha za kutosha kwa ajili ya kufanya mambo yao mengine ikiwa pamoja na kufungua biashara kubwa.
    Hapo ndipo safari ya kuelekea Kijitonyama kuanza. Muda mwingi Tenende alikuwa akiongea kuhusiana na Khaled, kwake kwa wakati huo alikuwa akitumia muda mwingi kumlemba mtu huyo. Samuel na Sadiki wakawa na hamu ya kuonana na Khaled ambaye sifa zake zilikuwa zimemwagwa sana mdomoni mwa Tenende. Hawakuchukua muda mrefu sana, wakafika katika nyumba moja kubwa ya ghorofa ambayo ilikuwa na mlinzi nje na kisha kuanza kumuulizia Khaled.
    “Yupo. Mna shida gani?” Mlinzi aliwauliza huku akiwaangalia kwa zamu.
    “Tuna maongezi nae,” Tenende alijibu.
    “Haiwezekani,” Mlinzi aliwaambia.
    “Kwa nini bosi?”
    “Hawa wengine wanaweza kuingia, ila wewe itakupasa ubaki hapa,” Mlinzi alimwambia tenende.
    “Kwa nini mimi nibaki?”
    “Muonekano wako. Unaonekana unaweza kuiba hata vijiko humu ndani,” Mlinzi aliwaambia huku akifungua geti na kuwaambia Samuel na Sadiki kuingia ndani.
    “Sasa bro mimi ndio niliowaleta hao wana kuja kuonana mpwa wangu. Inakuwaje unanizuia?” Tenende alimuuliza mlinzi ambaye alikuwa akijiandaa kufunga geti.
    “Hiyo ndio ilivyo kaka.”
    “Ila mimi ndio mshika ramani. Hao watafikaje?” Tenende aliuliza.
    “Bro, huyo ndiye mtu muhimu sana kwetu. Yeye ndiye alitumwa kutuita,” Samuel alimwambia mlinzi.
    “Ila si mnaona jinsi alivyokuwa. Watu kama hawa hawahitajiki ndani ya nyumba hii,” Mlinzi aliwaambia Samuel na Sadiki kuhusu Tenende ambaye alikuwa akionekana vibaya kutokana na bangi kumharibu na kumuweka katika hali ya uchafu.
    Baada ya kuongea sana na mlinzi mahali hapo ndipo alipokubali kumruhusu Tenende kuingia ndani ya nyumba hiyo. Muonekano wake bado haukuwa mzuri kabisa. Mlinzi akawaambia wasubiri mahali hapo karibu na mlango wa kuingilia sebuleni na kisha yeye kuelekea ndani na kumpa taarifa Khaled kuhusiana na ugeni ambao ulikuwa umefika mahali hapo.
    Mlinzi akarudi na kisha kuwakaribisha ndani mpaka sebuleni. Nyumba ilionekana kuwa na thamani sana katika macho yao. Ilionekana kuwa moja ya nyumba ya kisasa ambayo kweli alitakiwa kuishi mtu ambaye alikuwa na kiasi kikubwa cha fedha. Macho yao yalikuwa yakiashangaa tu mandhari ya nyumba ile, walikuwa hawaamini kama kungekuwa na binadamu ambaye angekuwa akiishi ndani ya nyumba ile ambayo ilionekana kuwa na mvuto mkubwa.
    Wakatulia kwenye makochi makubwa. Macho yao hayakutulia hata kidogo, walikuwa wakiangalia huku na kule. Zuria kubwa la manyoya liliwafanya kujisikia vizuri kabisa miguuni mwao. Walitulia katika makochi yale sebuleni pale mpaka katika kipindi ambacho Khaled akafika sebuleni hapo.
    Kitu cha kwanza akaanza kuwaangalia watu ambao walikuwa wamefika mahali hapo. Vijana wawili walionekana kuwa wageni wakubwa machoni mwake, ni Tenende tu ndiye ambaye alikuwa akimfahamu mahali hapo. Khaled hakuonekana kujali, alichokifanya ni kuwasalimia na kisha kukaa katika kochi jingine.
    “Nimewaleta hawa,” Tenende alianzisha mazungumzo.
    “Wakina nani?”
    “Washikaji zangu pande za kitaa,” Tenende alimjibu Khaled.
    “Ok! Umewaleta wa kazi gani?”
    “Mambo yetu yale.”
    “Mambo gani?”
    “Yale ya kupaa paa na ndege.”
    “Sijakuelewa Tenende.”
    “Si yale ya unga wa sembe mkuu,” Tenende alimwambia Khaled ambaye hakuonekana kujisikia vizuri katika hilo.
    “Ok! Nimekuelewa. Hebu njoo huku mara moja,” Khaled alimwambia Tenende na kisha kumtaka kumfuata kule alipokuwa ameelekea ukumbini.
    “Mbona unaonekana kuwa kama mtoto wewe,” Khaled alimwambia Tenende huku akionekana kubadilika.
    “Kivipi?”
    “Sasa hawa ndio wakina nani?”
    “Washikaji nao wanataka kufanya biashara ya madawa,” Tenende alimwambia Khaled.
    “Huu ni upumbavu Tenende. Unajua unaweza kuwaita polisi na kuniletea matatizo.”
    “Lakini bosi si.....”
    “Hakuna cha lakini. Hili linaweza kuwa tatizo kwangu. Je wakiwa polisi unafikiri itakuwaje?”
    “Hawa sio polisi. Ni wana ambao kila siku nipo nao kitaa tunafanya yetu.”
    “Umeanza kufahamiana nao kipindi gani?”
    “Huu mwezi wa tatu sasa.”
    “Bado muda ni mfupi sana. Angalia Tenende na mambo yako naomba usiyafanyie mbele ya macho yangu. Umesikia?”
    “Nimesikia bosi.”
    “Na hata watu wako iwe mwanzo na mwisho kuwaleta watu nisiowajua ndani ya nyumba hii. Tumeelewana?”
    “Tumeelewana.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Khaled akaondoka mahali pale na kisha kuelekea sebuleni. Hakutaka kuongea kitu chochote kile, alichokifanya ni kuchukua chupa ya maji ambayo alikuwa ameiacha sebuleni pale na kisha kuondoka mahali hapo na kuelekea chumbani kwake. Samuel na Sadiki nao hawakuongea kitu chochote kile, walibaki wakimwangalia Khaled ambaye alikuwa akiondoka mahali hapo.
    Huku akionekana kuchoka, Tenende akarudi na kisha kukaa kwenye kochi. Hakuonekana kuwa na furaha kana kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kimetokea kule ambapo aliitwa na Khaled.
    “Vipi?” Samuel aliuliza.
    “Amekaza.”
    “Kivipi?”
    “Twendeni tu,” Tenende aliwaambia huku akisimama.
    Hakukuwa na mtu ambaye alibaki mahali hapo, tayari waliona kwamba kile kitu ambacho walikuwa wamekifuata mahali pale kikiwa kimeshindikana kabisa. Pamoja na hayo yote kila mmoja alitaka kufahamu ni kitu gani ambacho Khaled alikuwa ameongea na Tenende kule alipokuwa amemuita.
    “Hebu tuambie amesemaje,” Sadiki alimwambia Tenende walipokuwa njiani wakirudi.
    “Nimeongea nae.”
    “Tunajua. Amesemaje?”
    “Amezingua kinoma.”
    “Kivipi?”
    “Amesema nisiwalete watu tena ndani ya nyumba yake kwani anajua kwamba inawezekana ninyi mkawa polisi,” Tenende aliwaambia.
    “Dah! Kwa hiyo ishu imebuma?” Samuel alimuuliza.
    “Yeah!” Tenende alijibu.
    Kila mmoja akaonekana kunyong’onyea mahali pale. Kitendo cha Khaled kukataa kufanya kazi pamoja nao kilionekana akuwakata maini kabisa. Wakawa wakirudi nyumbani lakini hawakuonekana kuwa na amani. Katika kipindi hicho, kila moja alikuwa na kiu ya kufanya biashara ile ambayo ilionekana kulipa kupita kawaida, kila mmoja katika kipindi hicho alikuwa na hamu ya kupata fedha nyingi katika kipindi kichache.
    “Kwa hiyo ndio basi tena?” Sadiki aliuliza.
    “Nadhani.”
    Ile kwao ikaonekana kuwa bahati ambayo ilikuwa imefutika machoni mwao. Kitendo cha kuiona nyumba ambayo alikuwa akiishi Khaled pamoja na magari ambayo yalikuwa yameegeshwa katika eneo la nyumba yake tayari wakajua kwamba biashara ile ya kuuza madawa ya kulevya ilikuwa ikilipa sana. Kiu kubwa ya kufanya biashara ile ikawa imewashika lakini hawakujua ni kwa namna gani wangeweza kufanya biashara ile.
    Kwa sababu Khaled hakuwa ameonekana kuwakubali, walipofika nyumbani maisha yao yakaendelea kama kawaida. Mara kwa mara walikuwa watu wa kuingiza wanawake ndani na kufanya nao mapenzi, maisha ya anasa yalizidi kuwatawala kila siku. Walikuwa wakinywa pombe na kuvuta bangi huku kila siku wakila mirungi kama kawa yao.
    Samuel hakutaka kuachana na Halima, mara kwa mara msichana huyo alikuwa akija nyumbani hapo na kisha kufanya nae mapenzi kiasi ambacho kikafika kipindi akachoka kabisa, akahitaji kumuacha kwani kama angeendelea nae kila siku ingeweza kuwa tatizo hapo baadae.
    “Kwa hiyo utamuacha vipi?” Sadiki alimuuliza.
    “Kazi rahisi sana. Ni kama kumsukuma mlevi katika mteremko wa mlima,” Samuel alimwambia Sadiki.
    “Kivipi sasa?”
    “Ngoja nimtumie bwana wake zile picha.”
    “Nani? Issa?”
    “Hapana. Issa simjui. Nataka nimtumie Cosmas.”
    “Unadhani hiyo itasaidia?”
    “Sana tu. Asilimia mia moja,” Samuel alijibu.
    Samuel hakutaka kuchelewa, alichokifanya siku hiyo ni kumtumia Cosmas picha kadhaa ambazo zilimuonyesha akifanya mapenzi na Halima. Samuel hakuonekana kujali kwamba Cosmas angejisikiaje katika kipindi hicho, kitu ambacho alikuwa akikijali zaidi ni yeye kuachana na Halima tu.
    Picha zile zilionekana kumuumiza Cosmas kiasi ambacho kikamfanya kumtafuta Samuel na kisha kuonana nae Tandale. Ugomvi mkubwa ukatokea, Cosmas alionekana kuwa na hasira kupita kawaida, hakuonekana kuamini kama Samuel angeweza kufanya kitu kama kile hasa kwa msichana ambaye alikuwa akimpenda.
    “Tatizo nini sasa? Demu wako malaya na nilikwambia usimwamini mwanamke. Umeona?” Samuel alimwambia Cosmas ambaye alikuwa ameshikwa na wanaume kadhaa kutokana na fujo ambazo alikuwa amezileta mahali hapo.
    “Nitakuua,” Cosmas alisema kwa hasira.
    “Sikiliza Cosmas. Demu wako mchafu sana na ndio maana nimeamua kuachana nae. Ulikuwa unatamba sana kwamba demu wako mwaminifu, ana uaminifu gani sasa, yaani nilimpata kirahisi sana kama kumsukuma mlevi kwenye mteremko,” Samuel alizidi kuongea maneno ambayo yalmfanya Cosmas kupata hasira zaidi.
    “Nimesema nitakuua.”
    “Unataka kumuua msela kisa demu? Wewe wa wapi?” Sadiki aliuliza huku akicheka kidhihaka.
    “Achana nae bwana. Demu mwenyewe demu basiii, demu mwenyewe mchafu tu,” Samuel alimwambia Sadiki huku akiingia ndani.
    Maneno yale yakaonekana kumtia hasira Cosmas ambaye alikuwa akitamani kuachiwa na watu ambao walikuwa wamemshika mahali hapo na kisha kumfuata Samuel ambaye aliingia chumbani pamoja na Sadiki. Watu ambao walikuwa wamemshika mahali hapo wakaanza kumpoza huku wakimwambia aondoke mahali hapo.
    Idadi kubwa ya watu tayari ilikuwa imekusanyika mahali hapo huku kila mmoja akitamani kushuhudia watu hao wakipigana. Cosmas hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka huku akionekana kuwa na hasira kali moyoni mwake kwani kitendo cha Samuel kutembea na msichana wake, Halima kilionekana kumuumiza kupita kawaida.
    Kidogo lile likaonekana kuwa suluhisho, mara baada ya siku kadhaa, Halima akafika nyumbani hapo na kisha kuamua kuachana na Samuel kwa madai ya kumdhalilisha. Hicho ndicho kitu ambacho alikuwa akikitaka sana Samuel, hakubisha wala kugoma, akamkubalia Halima kwamba huo ndio ulikuwa mwisho wa uhusiano wao wa siri.
    Maisha hayakubadilika hata mara moja, bado yalikuwa yakiendelea kama kawaida. Kila siku walikuwa wakiendelea kuvuta bangi ambazo walikuwa wakimtuma Tenende kwenda kuzinunua kwa watu ambao walikuwa wakiziuza pamoja na mirungi ambayo ilikuwa ikiuzwa na watu wachache ambao walikuwa wakitoka Manzese kuja Tandale.
    Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akikumbuka ibada kwa wakati huo. Maisha yao yalionekana kubadilika kwa asilimia mia moja. Hawakutaka kwenda kanisani wala msikitini, hawakutaka kusoma Biblia wala Qur-an , kitu ambacho walikuwa wakikitaka katika muda huo ni kuendelea kuishi katika maisha yale kama kawaida.
    Siku ziliendelea kukatika huku nazo wiki zikiendelea kusonga mbele mpaka katika kipindi ambacho Tenende akawaletea habari ambayo kwao ikaonekana kuwa njema kwamba Khaled alitaka kuwaona siku ya kesho. Kila mmoja hakuonekana kuamini, tayari waliona kwamba walikuwa wamepata nafasi ambayo walikuwa wakiitaka katika kipindi hicho, kitendo cha Khaled kutaka kuwaona tayari kikawapa uhakika kwamba wangeweza kuingizwa katika mtandao wa uuzaji wa madawa ya kulevya na hivyo nao kupata fedha kama ilivyokuwa kwa Khaled.
    “Kitu kimetiki,” Samuel alimwambia Sadiki huku akionekana kuwa na furaha.
    “Bado kwanza. Tutasema kimetiki mpaka tutakapokabidhiwa mzigo,” Sadiki alimwambia Samuel.
    “Lakini si umeona mawingu! Au umezisahau dalili za mvua?” Samuel alimuuliza Sadiki.
    “Najua. Ngoja kwanza mpaka tuanze kupeleka mzigo,” Sadiki alimwambia Samuel.
    Siku iliyofuta, wakaanza kuelekea nyumbani kwa Khaled. Hawakutaka kuelekea huko pamoja na Tenende kutokana na kuambiwa kwamba walitakiwa kufika mahali hapo peke yao. Njiani, kila mmoja alionekana kuwa na furaha, tayari wakaanza kuona utajiri ukinukia katika maisha yao. Mara baada ya kufika getini, wakaruhusiwa kuingia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Ni kweli mnataka kufanya biashara hii?” Khaled aliwauliza huku akivuta sigara kubwa.
    “Ndio.”
    “Sidhani,” Khaled aliwambia.
    “Kweli. Tunataka kuifanya biashara hii,” Samuel alimwambia Khaled.
    “Kitu gani kimewavutia katika biashara hii ambayo inaonekana kuwa na majanga makubwa na ambayo polisi wanaitolea macho sana?” Khaled aliwauliza.
    “Tumependezwa nayo kuifanya kwa sababu tumegundua nyuma yake kuna mafanikio makubwa,” Samuel alimjibu Khaled.
    “Kwa hiyo mnaamini kwamba mtapata fedha na kuwa matajiri?” Khaled aliwauliza.
    “Ndio.”
    “Msipopata?”
    “Tutaendelea kupigana nayo mpaka tupate,” Sadiki alitoa jibu lililowafanya wote kucheka.
    “Nisikilizeni kwa makini. Biashara hii ni biashara ya hatari sana ambayo kila mtu anatamani sana kuifanya. Ukiwa serious katika biashara hii utaingiza fedha sana lakini ukiwa upo upo tu haueleweki, hautofanikiwa, mbaya zaidi utakamatwa na kufikishwa polisi,” Khaled aliwaambia.
    “Kwa hiyo umakini ndio unaohitajika?”
    “Hiyo ndio maana yangu. Ukiwa makini utapata kile unachokitaka lakini usipokuwa makini utaweza kuingizwa hata gerezani,” Khaled aliwaambia huku akinywa juisi.
    “Tutakuwa makini,” Samuel alimwambia.
    “Kila mmoja anapotaka kuanza kufanya biashara hii husema hivyo lakini mara anapoanza kuifanya, anasahau kile alichokisema kabla ya kuanza biashara hii” Khaled aliwaambia.
    “Kuna kingine zaidi?” Samuel aliuliza.
    “Ndio. Tamaa.”
    “Kivipi?”
    “Vijana wengi hukimbia na mizigo kwa kujiona kwamba watafanikiwa lakini mwisho wa siku tunawapata na kuwaua huku maiti zao tukisafirishia madawa hapa hapa Afrika,” Khaled aliwaambia.
    “Tumekuelewa.”
    “Sawa. Kuna mengi nitakuwa nikiwaambia kuhusiana na biashara hii kabla ya ninyi kuanza biasha hii chini yangu. Ninyi mtakuwa wafanyakazi wangu. Nyie ndio mtakuwa mkisafirisha mizigo kwenda mikoani na hata nchi nyingine hapa hapa Afrika,” Khaled aliwaambia.
    “Hilo sio tatizo. Inawezekana tukafika mpaka Ulaya,” Sadiki aliuliza.
    “Ulaya! Ulaya ni kama Kariako mara unapoanza kufanya biashara hii. Kote huko mtafika, ila kwa sababu bado hamjafahamu jinsi ya kuifanya biashara hii, tuanze hapa hapa Afrika, mkiwa makamanda wa kuaminika, mtaanza kwenda Ulaya. Ninawahakikishia, safari zenu kumi za kwenda Ulaya, msipotajirika, basi mtakuwa mmerogwa,” Khaled aliwaambia.
    “Tutatajirika vipi na wakati sisi tutakuwa wafanyakazi wako?” Sadiki aliuliza.
    “Mtanifanyia kazi kwa kipindi fulani ila katika wakati huo nanyi inawapasa kufahamu njia mbalimbali, msitegemee kunifanyia kazi milele. Nanyi pia mnaweza kutajirika na kisha sisi kwa sisi tukawa tunafanyiana biashara. Hamuoni kama hiyo ni hatua mojawapo ya maendeleo?”Khaled aliwauliza.
    “Kweli.”
    “Hiyo ndio inavyokuwa. Mimi nilikuwa na mfanyakazi fulani anajiita Zinja. Alinifanyia biashara hii kwa uaminifu mkubwa na baada ya miezi kadhaa akaanzisha biashara yake, ninafanya biashara pamoja na yeye, yaani tunauziana. Hivi ndivyo biashara inavyokuwa,” Khaled aliwaambia.
    “Ok! Tumekuelewa.”
    “Sawa. Cha mwisho sasa.”
    “Kipi?”
    “Siri. Hamtakiwi kuonyesha mabadiliko yoyote mitaani. Kuweni wasiri sana kwa watu wote hasa hasa wanawake,” Khaled aliwaambia.
    “Hasa wanawake,” Sadiki alisema huku akicheka.
    “Yeah! Najua udhaifu wa vijana. Sketi zinatufanya kutokuwa wasiri sana na ndio maana hata polisi huwatumia wanawake. Kuweni makini katika hilo. Nadhani mwezi ujao tutaanza kazi,” Khaled aliwaambia.
    “Hakuna tatizo.”
    “Ila yawapasa kufika mahali hapa mara kwa mara kwa ajili ya kuweka ukaribu sana kati yangu na nyie,” Khaled aliwaambia.
    “Hakuna tatizo.”
    “Basi sawa,” Khaled aliwambia.
    Hawakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, walichokifanya ni kuondoka huku kila mmoja akionekana kuwa na furaha. Tayari wakayaona maisha yao yakianza kubadilika na kuwa vile ambavyo walitaka yawe. Kila wakati walikuwa wakicheka kwa furaha, tayari wakajiona kuwa matajiri hata kabla biashara ambayo waliambiwa kwamba waifanye hawajaaza kuifanya.
    Katika kipindi hicho, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akijua kwamba bado shetani alikuwa akiendelea kuwateka na kuwapoteza zaidi na zaidi, hakutaka kabisa vijana hao wakumbuke kule walipotoka, nguvu zake nyingi katika kipindi hicho alikuwa ameziweka kwa vijana hao ambao alikuwa na kiu kubwa ya kutaka kuendelea kupoteza zaidi na zaidi.


    Khaled alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakifanya biashara ya magendo ya madawa ya kulevya nchini Tanzania. Hata kabla hajapata nafasi ya kufanya biashara zake yeye kama yeye, Khaled alikuwa akifanya biashara chini ya muuzaji mkubwa wa madawa ya kulevya, mzee Othman ambaye alikuwa akipenda kujiita kwa jina la Zungu kutokana na weupe wake aliokuwa nao.
    Kazi kubwa ya Khaled ilikuwa ni kusafirisha madawa kuelekea katika nchi mbalimbali duniani. Hata kabla hajaanza kuyasafirisha madawa katika nchi za Ulaya na Asia, Khaled akaanza na kuyasafirisha madawa hayo ndani ya nchi ya Tanzania pamoja na nchi kadhaa katika bara la Afrika. 
    Khaled akafahamiana na watu wengi, yeye ndiye ambaye alikuwa akiongea na madaktari na kisha kuwalipa kiasi fulani cha fedha na kuwapa maiti ambazo walikuwa wakizipasua tumboni na kisha kuziwekea madawa ya kulevya na kuanza kuyasafirisha katika nchi nyingi hapa Afrika. Katika kipindi hicho cha zamani, polisi hawakuweza kugundua kitu chochote kile, kila maiti ambayo ilikuwa ikisafirishwa ilionekana kuwa maiti ambayo wala haikuwa na matatizo kabisa.
    Baada ya kuweka mizizi mikubwa barani Afrika hapo ndipo ambapo alipoanza kutumwa kuelekea katika nchi mbalimbali Ulaya na barani Asia. Uwezo wake wa kusafirisha madawa ulikuwa mkubwa sana na ilikuwa ngumu kugundulika. Katika kipindi hicho kila kitu kilionekana kuwa chepesi, hakukuwa na ulinzi mkubwa sana jambo ambalo lilimfanya Khaled kutokupata tatizo lolote lile.
    Malipo makubwa yalikuwa yakifanyika huku yeye akilipwa fedha kidogo mno. Malipo hayo madogo ndio yakaonekana kumkasirisha Khaled. Kwanza alijiona anayahatarisha maisha yake kwa ajili ya mtu mwingine halafu anapewa kiasi kidogo, hapo ndipo alipoamua kuiba baadhi ya madawa na kisha kuyauza yeye mwenyewe.
    Mzee Othman hakuweza kugundua kama Khaled alikuwa akiiba baadhi ya pakti za madawa na kisha kuuza kwa manufaa yake mwenyewe. Mpaka katika kipindi ambacho mzee Othman anakuja kugundua, tayari Khaled alikuwa amekwishachuma fedha za kutosha.
    “Nitamuua,” alijisemea mzee Othman kwa hasira.
    Kwa sababu Khaled alikuwa amekwishaacha kufanya kazi kwake huku akiwa amechukua fedha nyingi kupitia biashara ile hapo ndipo mzee Othman alipotaka kumuua Khaled. 
    Kila siku alikuwa akiwatuma vijana wake kwa ajili ya kukamilisha kila kitu alichotaka kikamilishwe lakini mwisho wa siku vijana wale wakashindwa kutekeleza kile ambacho walikuwa wameagizwa.
    “Mmeshindwa wapi?” mzee Othman aliwauliza huku akionekana kuwa na hasira.
    “Kila tunapokwenda tunamkosa bosi. Yaani ni kama ana hirizi,” kijana mmoja alimwambia mzee Othman.
    “Yaani nashindwa kuelewa mnashindwa sehemu gani. Mbona kazi inaonekana rahisi sana.”
    “Huwa anatupotea sana. Sijui inakuwaje.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Ninawapeni wiki moja tu nataka mtu huyu auawe,” mzee Othaman aliwaambia.
    Bado akili ya mzee Othman ilikuwa imechanganyikiwa. Hakutaka kabisa kumuona Khaled akiendelea kuvuta pumzi ya dunia hii na wakati alikuwa amemfanyia mambo mengi ya wizi wa madawa yake. Katika kipindi hicho alikuwa akihitaji kukiona kitu kimoja tu, kumuona Khaled anauawa na vijana wake.
    Siku ziliendelea kukatika lakini wala hakukuwa na taarifa yoyote ile kutoka kwa vijana wake kuusiana na kifo cha Khaled. Huku ikiwa imebakia siku moja kabla ya kutimiza wiki ambayo alikuwa amewapa vijana wake, akajikuta akivamiwa ndani ya nyumba yake na watu kadhaa, aliwaangalia, mmoja alikuwa Khaled.
    “Khaled,” mzee Othman aliita huku akionekana kutokuamini.
    “Kwa sababu umeshindwa kuniua, nakukuua wewe,” Khaled alimwambia mzee Othman.
    Siku hiyo ndio ilikuwa siku ya mwisho ya mzee Othman kuvuta pumzi ya dunia hii, akauawa ndani ya nyumba yake na kisha vijana wale akiwepo Khaled kuchukua kiasi kikubwa cha fedha ambacho alikuwa amekificha na kisha kuondoka mahali hapo.
    Kuanzia hapo, Khaled akaanza kufanya biashara kwa amani na ndani ya mwezi mmoja tu tayari alikuwa amepata kiasi kikubwa cha fedha. Khaled hakuishia hapo, akaanza kutafuta vijana zaidi wa kumfanyia kazi ya kusafirisha madawa katika nchi mbalimbali. Zoezi lake lilikuwa gumu kwani kila kijana ambaye alikuwa akimpata alikuwa akikamatwa kirahisi na polisi na mizigo yake kupotea kizembe.
    Khaled hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, hakujua sababu ambayo iliwafanya vijana wake kukamatwa kizembe namna ile. Alipokaa kwa muda huku akiwa hajui ni kitu gani kilikuwa kikitokea hapo ndipo alipopata jibu ambalo alikuwa na uhakika nalo kwamba ndilo lililosababisha vijana wake wengi kukamatwa kirahisi.
    Vijana ambao alikuwa akiwatumia, asilimia kubwa walikuwa watumiaji wa madawa ya kulevya kiasi ambacho katika sehemu za kukagulia uwanja wa ndege walikuwa wakikamatwa kirahisi sana. Hiyo ndio ilikuwa sababu kubwa ya Khaled kuachana na vijana hao na kisha kuanza kuwatafuta vijana ambao wala hawakuwa wakitumia madawa ya kulevya.
    Kuwapata vijana wa namna hiyo halikuwa jambo jepesi hata mara moja, kila siku alikuwa akihangaika lakini mwisho wa siku hakuwa akimpata mtu yeyote yule. 
    Hakukata tamaa, kila siku alikuwa mtu wa uvumilivu. Alipoona siku zinasogea bila kuwapata vijana hao ndipo akaamua kuwasiliana na Tenende kwa kuamini kwamba mitaani kulikuwa na vijana ambao wangeweza kuyatoa maisha yao kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
    Kitu cha kwanza Tenende akataka kufanya kazi hiyo yeye kama yeye lakini Khaled hakuonekana kukubali, kwa Tenende, alionekana kuwa kama vijana wengine ambao walikuwa wakikamatwa kirahisi sana katika viwanja vya ndege. Alihitaji vijana wengine ambao wangeonekana kuwa wasafi na ambao hawajawahi kutumia madawa ya kulevya.
    Baada ya wiki kadhaa ndipo Tenende akawaleta Sadiki na Samuel ndani ya nyumba yake. Hali ile haikuonekana kumfurahisha kwani alitaka kuonana na vijana hao nje ya nyumba yake kwa sababu ya usalama zaidi. Japokuwa alimkoromea sana Tenende lakini mwisho wa siku alipowaangalia Samuel na Sadiki kwake wakaonekana kufaa sana katika kuifanya biashara ile ambayo kwa kiasi fulani ilikuwa imekwishaanza kuzorota.
    “Ninawahitaji. Waambie waje lakini waje peke yao,” Khaled alimwambia Tenende katika kipindi ambacho alikwenda Tandale.
    “Unataka kuwaona lini?” Tenende alimuuliza.
    “Hata kesho mchana itakuwa poa sana,” Khaled alijibu huku wote wawili wakiwa ndani ya gari lake.
    “Hakuna noma. Tutakuja muda huo.”
    “Hapana. Waambie waje peke yao.”
    “Unamaanisha mimi nisije?”
    “Ndio. Ninawahitaji wao peke yao.”
    “Ila bosi unanitenga kweli siku hizi.”
    “Hakuna tatizo Tenende. Wewe ni mtu wangu wa karibu. Kwanza chukua hii,” Khaled alimwambia Tenende huku akiwa amefungua pochi yake na kumkabidhi kiasi cha shilingi elfu hamsini.
    “Shwari. Nitawaambia waje,” Tenende alisema na kisha Khaled kuondoka mahali hapo.
    *****
    Samuel na Sadiki tayari walikwishajiingiza katika biashara ya uuzaji wa madawa ya kulevya huku wakiwa chini ya Khaled ambaye alikuwa bosi wao. Kitu ambacho kilifanyika kwa wakati huo kilikuwa ni kuanza kupewa ramani pamoja na kila njia ambayo biashara ilitakiwa kufanyika 
    Katika kipindi hicho kila mtu alikuwa na ndoto za kuwa milionea, kila mtu alikuwa akitaka kumiliki kiasi kikubwa cha fedha. Kujiingiza na kuwa miongoni mwa wafanyakazi wa Khaled kwao wala halikuonekana kuwa tatizo hata mara moja, kitu ambacho walikuwa wakikihangalia kwa wakati huo ni fedha tu.
    Alichokifanya Khaled ni kuanza kuwatafutia passport. Kitu ambacho alikijua ni kwamba kama angekamilisha suala zima la passport ingekuwa rahisi sana kwao kuanza kusafiri kuelekea katika nchi mbalimbali kwa ajili ya kupeleka madawa hayo ambayo katika kipindi hicho yalikuwa yakiuzwa sana huku njia kali za kukamata wasafirishaji zikiwa bado hazijaboreshwa duniani.
    Kila kitu kilipokuwa tayari, baada ya mwezi mmoja Khaled akawapa mzigo wa kilo moja kwa ajili ya kuusafirsha mkoani Arusha uliokuwa ukihitajika kupita kawaida. Kwa sababu walikuwa marafiki ambao walikuwa wamezoeana sana hata zaidi ya ndugu, wakaanza kuelekea huko Arusha huku wakiwa na gari aina ya Prado ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Khaled.
    “Kazi imeanza,” Sadiki alimwambia Samuel.
    “Yeah! Kinachohitajika ni uvumilivu tu katika kazi hii na mafanikio yatajileta,” Samuel alimwambia Sadiki ambaye alikuwa akiendesha gari.
    “Alisema tuchukue kiasi gani?”
    “Milioni mbili kama mzigo utafika salama. Yaani kitendo cha kutoka Dar es Salaam kuja Arusha tayari tuna milioni moja kila mmoja. Hauoni kama huu ni utajiri unatunyemelea?” Sadiki aliuliza huku akiendelea kuendesha gari.
    “Huu ni utajiri dhahiri. Umri mdogo unaanza kukamata mamilioni, mitaani watanitafuta ubaya,” Samuel alimwambia Sadiki.
    “Hahaha! Bila shaka unamaanisha sketi.”
    “Hiyo ndio maana yangu. Ili uonekane una fedha, haina budi kulala na wakina Salome, Christina na mademu wote wakali,” Samuel alimwambia Sadiki.
    Bado safari ilikuwa ikiendelea kama kawaida, kila mtu katika kipindi hicho alikuwa akifikiria fedha. Kiasi cha shilingi milioni moja kwa kila mmoja ambacho walikuwa wamepewa kama malipo ya kupeleka mzigo wa madawa ya kulevya Arusha kilikuwa kiasi kikubwa katika maisha yao kutokana na umri wao kuwa mdogo.
    Katika safari nzima, kila askari wa barabarani ambaye alikuwa akiwasimamisha walikuwa wakimpa fedha, hawakutaka gari lao lipekuliwe kabisa, walitaka kusafiri kwa amani mpaka wanaingia mkoani Arusha.
    “Nimewaambia wote teremkeni garini?” ilisikika sauti ya polisi mmoja wa barabarani akiwaambia huku akionekana kumaanisha alichokuwa akikiongea.
    “Ila bosi naomba utuelewe, tunawahi msibani,” Samuel alimwambia askari yule ambaye hakuonekana kuelewa kabisa.
    Maaskari wa barabarani wengine ambao walikuwa pembeni ya barabara wakaanza kusogea kule gari alilokuwa Samuel na Sadiki lilipokuwa. Tayari waliona kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kikiendelea mahali hapo. Askari yule wa barabarani alikuwa akiendelea kusisitiza kwamba Samuel na Sadiki wateremke kutoka garini lakini wao hawakuonekana kuelewa kabisa.
    “Kuna nini tena?” askari mmoja ambaye alionekana kuwa kiongozi aliuliza mara baada ya kufika mahali pale.
    “Hili gari nina wasiwasi nalo. Nadhani watakuwa wamebeba mirungi hawa,” askari yule alimjibu bosi wake ambaye alifika hapo na kisha kuanza kuwaangalia Samuel na Sadiki ambao walikuwa ndani ya gari lile.
    “Hamjambo!” askari yule kiongozi aliwasalimia.
    “Hatujambo. Shikamoo,” wote walimsalimia.
    “Mmebeba nini garini?” askari yule aliuliza kwa sauti ya upole.
    “Hakuna kitu. Tunaelekea katika msiba wa mjomba wetu Marangu Kilimanjaro,” Samuel alijibu huku akimkazia macho askari yule.
    “Hamjabeba mirungi nyie?”
    “Hapana mzee. Hebu tuangalie kwa macho yako mzee, hivi tunaonekana sisi ni watumiaji wa mirungi?” Samuel alimuuliza askari yule.
    “Sasa kwa nini mnashindwa kumuelewa anaposema kwamba mteremke kutoka garini?”
    “Kumuelewa tumemuelewa ila tulitaka kuongea nae kiutu uzima. Unajua vitu vingine inabidi tuongee kiutu uzima ili tusimcheleweshe na majukumu yake na hata sisi tusichelewe kuwahi msibani,” Samuel alimwambia askari yule.
    “Hebu njoo huku tuongee kidogo. Wewe kijana unaonekana kuwa muelewa,” askari yule alimwambia Samuel ambaye akateremka na kisha kumfuata.
    Mpaka kufikia hatua hiyo tayari wakajiona kwamba kusingekuwa na kitu chochote ambacho kingeharibika mahali hapo. Kitendo cha askari yule kumuita Samuel pembeni kilionekana kwamba kuwa ushindi kwao. Samuel na askari yule wakaelekea pembeni kabisa ya barabara na kisha kuanza kuongea.
    “Mlisema mnaelekea wapi?” askari yule alimuuliza.
    “Tunaelekea Marangu Kilimanjaro kwenye msiba,” Samuel alijibu.
    “Nani amefariki?”
    “Mjomba wetu.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Sasa mbona mlikuwa mkimbishia kijana wangu kuteremka kutoka garini?”
    “Tatizo muda bosi. Unajua kuna vitu vingine inabidi tumalizane kimyakimya,” Samuel alimwambia askari yule.
    “Sasa kwa nini mmebeba mirungi?”
    “Hatujabeba mirungi bosi. Hivi kwa kutuangalia jinsi tulivyo nadhifu tunaweza kuwa wala mirungi kweli?”
    “Ok! Naona tunapoteza muda wa bure. Tumalizane basi ili muwahi,” Askari yule alimwambia Samuel.
    Samuel hakutaka kuremba, aliiona ile ndio kuwa nafasi yenyewe, alichokifanya ni kuuingiza mkono mfukoni na kisha kutoa noti mbili za shilingi elfu kumi na kisha kumgawia. Kwa kasi ya ajabu askari yule akazichukua noti zile na kisha kuziweka mfukoni.
    “Nendeni ila kuweni makini barabarani,” askari yule aliwaambia.
    Samuel hakutaka kuchelewa, kitu alichokifanya ni kuondoka mahali hapo na kisha kuingia garini na kisha safari ikiendelea. Kila wakati walikuwa wakicheka tu, fedha ambazo alikuwa amempa askari yule kilikuwa kiasi kikubwa cha fedha, fedha ambazo kwa askari yeyote katika kipindi kile asingeweza kuziacha.
    “Fedha ni shetani,” Sadiki alimwambia samuel.
    “Tena shetani baba lao aisee.”
    Safari iliendelea zaidi na zaidi. Mpaka wanaingia Arusha saa tisa alasiri kila mmoja alionekana kuchoka. Walichokifanya ni kwenda kwenye moja ya hoteli na kisha kula chakula, walipomaliza, wakaondoka na kuelekea mjini. Huko, ndani ya hoteli ya Jumanji ndipo walipokutana na bwana Pawasa ambaye alikuwa ameagiza mzigo huo. 
    Malipo yakafanyika katika benki ya CRDB, kiasi cha fedha cha zaidi ya milioni mia moja na hamsini kikaingizwa ndani ya kaunti ya Khaled na kisha Samuel na Sadiki kuondoka mahali hapo huku mzee Pawasa akimgawia kila mmoja kiasi cha shilingi laki tano.
    “Haya ndio maisha tuliyokuwa tukiyataka,” Sadiki alimwambia Samuel.
    “Ukiwa na uhakika wa kuingiza kiasi cha fedha namna hii, kuna nini tena? Unataka Mungu akupe nini tena?” Samuel alimwambia Sadiki
    “Hakuna cha zaidi. Ila bado nina majonzi” Sadiki alisema huku uso wake ukipoteza tabasamu ghafla.
    “Majonzi gani tena?” Samuel aliuliza.
    “Unajua kama tunayahatarisha maisha yetu?”
    “Najua.”
    “Unajua kwamba tunamchezea rais Benjamin Mkapa sharubu?”
    “Najua.”
    “Hivi kama mtu anaingiza zaidi ya milioni mia moja na hamsini, kweli sisi ni wa kutulipa milioni moja kila mmoja! Hivi kuna uwiano hapo?” Sadiki aliuliza.
    “Mmmh! Hilo uliloongea nalo neno. Hakuna uwiano.”
    “Kwa hiyo jamaa anaingiza sana fedha halafu sisi tunaoyaatarisha maisha yetu tunapata kiasi kidogo. Hapana. Ni lazima tufanye kitu,” Sadiki alimwambia Samuel.
    “Kitu gani?”
    “Unaonaje kama tukampindua?”
    “Kwa sasa hivi, hilo ni wazo baya sana.”
    “Wazo baya! Kivipi?”
    “Kumpindua ngumu kwa sababu hatujajua njia ya kuuzia madawa Ulaya. Kwanza acha tujue njia za huko kisha tunampindua. Au unaonaje?”
    “Sawa. Hakuna tatizo. Ila kitu hiki kimeniuma sana.”
    “Usijali. Tuendelee kuwa wafanyakazi. Tutakapokamilisha kila kitu, tunampindua na kisha sisi kushika uongozi wa biashara hii. Unaonaje hapo?”
    “Hakuna tatizo.”
    Tayari katika kipindi hicho mioyo yao ikaanza kuingiwa na tamaa ya kuhitaji fedha nyingi. Walikwishaona kwamba biashara ile ilikuwa inalipa kupita kawaida na hivyo waliona lingekuwa jambo jema kama biashara ile wangeifanya wao wenyewe. Kitu ambacho walishauriana, ilikuwa ni lazima wampindue Khaled na kisha wao kushikilia uongozi wa biashara ile.
    Hakukuwa na mtu ambaye alijali kama wangeweza kumwaga damu mpaka kumpindua, kitu ambacho wao walikiona kufaa kwa wakati huo ni kumpindua tu Khaled na kisha wao kuwa viongozi wa biashara ile. 
    Hawakuishia hapo, bado Khaled alikuwa akiwatuma katika sehemu mbalimbali nchini Tanzania kwa ajili ya kusafirisha madawa ya kulevya huku akijiingizia kiasi kikubwa cha fedha huku wao wakiingiza kiasi kidogo sana cha fedha.
    Kila siku jambo lile lilikuwa likiwaumiza sana mioyo yao, hawakuamini kama kweli Khaled asingeweza kuwaongezea kiasi kikubwa zaidi kwa sababu walikuwa wakiyahatarisha maisha yao. 
    Wakavumilia kila siku, tayari wateja wakubwa wa madawa ya kulevya nchini Tanzania walikuwa wamekwishawajua, kwa sasa walikuwa wakitaka kuwafahamu wateja na mabosi kutoka katika nchi za Ulaya, hasa katika bara la Asia ili baada ya hapo, basi waweze kumuua Khaled na kuchukua uongozi wa kuuza madawa ya kulevya.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog