Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

MIMI NI MWENYE DHAMBI NISAMEHE MUNGU - 4

 





    Simulizi : Mimi Ni Mwenye Dhambi Nisamehe Mungu

    Sehemu Ya Nne (4)



    Mitihani ya kidato cha sita ikafanyika huku Catherine na Edmund wakiwa kwenye mapenzi ya dhati. Katika kipindi hicho wote wawili walionekana kuwa na furaha sana kwa sababu ndio kwanza mapenzi yao yalikuwa machanga na hivyo walikuwa na mambo mengi ambayo walikuwa wameyabakiza kuyafanya katika maisha yao ya mahusiano ya kimapenzi.

    Mpaka mitihani inakwisha, mapenzi yao hayakuishia shuleni tu bali yaliendelea mpaka nyumbani. Kichwani mwa Catherine, hakumkumbuka tena Samuel, mwanaume ambaye alikuwa pamoja nae katika miaka miwili iliyopita. Katika kipindi hicho alijiona kuanza upya maisha ya mahusiano pamoja na Edmund ambaye alionekana kuwa na mapenzi ya dhati kwake.

    Edmund akaona kama anachelewa jambo ambalo lilimfanya kuwaambia wazazi wake juu ya Catherine ambaye kadri siku zilivyozidi kwenda mbele alikuwa akizidi kuvutia zaidi na zaidi machoni mwa kila mwanaume ambaye alikuwa akimwangalia. Ile figa ambayo alikuwa nayo katika kipindi cha nyuma ikaonekana kuongezeka, figa nzuri ambayo ilimdatisha kila mwanaume ndio ambayo ilikuwa ikiupendezesha zaidi mwili wake mpaka kufikia hatua ya kila mwanaume ambaye alikuwa akimwangalia kumkazia macho.

    “Mnapendana?” Baba yake Edmund, mzee Zilikana aliwauliza.

    “Tunapendana sana” Edmund alijibu na wote kuachia tabasamu.

    “Malengo yenu ya baadae ni kufikia ndoa au ni mahusiano ya kupita tu?” Mzee Zilikana aliwauliza.

    “Hii ni moja kwa moja mpaka ndoa” Edmund alijibu.

    “Ila mbona kila swali unajibu wewe tu Edmund, hebu mpe nafasi Catherine nae tuisikie sauti yake ikijibu swali” Mzee Zilikana alimwambia Edmund.

    “Nitampenda mpaka pale kifo kitakapotutenganisha” Catherine alimwambia Edmund.

    “Vizuri. Kuweni makini katika maisha yenu, magonjwa mengi kwa sasa, hamtakiwi kuwa na tamaa ya vitu vidogo vidogo” Mzee Zilikana aliwaambia.

    “Hilo si tatizo”

    “Ila kuna kingine amesahau kuwaambia” Mama yake Edmund, Bi Elizabeth aliwaambia.

    “Kipi tena?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mnatakiwa kwenda kupima kwanza mjue afya zenu kabla ya mambo mengine kuendelea” Bi Elizabeth aliwaambia.

    Maneno yale hawakutakiwa kuyapuuzia hata mara moja, kila mtu alikuwa akijiamini kwamba hakuwa ameathirika lakini kwa sababu wazazi wao waliwataka kwenda kupimwa damu zao, wakaamua kwenda kupima na majibu yalipotoka walionekana kuwa wazima kabisa. Majibu hayo yakawa furaha kwao, japokuwa hapo kabla walikuwa wakihofia lakini kwa kiasi fulani walikuwa na uhakika kwamba kila kitu kilikuwa salama kabisa.

    Siku zikakatika na wiki kusogea mpaka kufika kipindi ambacho matokeo ya kidato cha sita yalipotoka. Kwa wote wawili walikuwa wamefanya vizuri jambo lililowapelekea kuchaguliwa kujiunga na chuo Kikuu cha Dar es salaam huku Edmund akichaguliwa kujiunga na chuo cha Dodoma.

    Kwa kiasi fulani hiyo ikaonekana kuwanyong’onyeza sana, hawakutaka kutengana kwa umbali mkubwa kiasi hicho, kila siku walikuwa wakitaka kuwa pamoja zaidi na zaidi ili uhusiano wao uendelee kukua zaidi na zaidi. Hali ambayo ilikuwa imetokea hawakuwa na jinsi nayo, walichokifanya ni kutengana na kila mtu kuendelea na masomo kama kawaida.

    Kwa Catherine maisha hayakuonekana kuwa na furaha hata mara moja, kitendo cha kuishi mbali na mpenzi wake alikiona kuwa ni mateso makubwa, mateso ambayo hakuwa akitamani yamfikie hata siku moja katika maisha yake. Kwa kiasi fulani mawasiliano hayo yakawafanya kujiona wapo karibu sana. Kila siku walikuwa wakizungumzia kuhusu mahusiano yao, hawakutaka kukaa muda mrefu bila kuzungumza. Mara kwa mara usiku Catherine alikuwa akijifunika shuka kitandani na kisha kuanza kuwasiliana na mpenzi wake huyo ambaye kwake alimuona kuwa mtu muhimu katika maisha yake.

    “Leo ningetaka unionyeshee ni kwa jinsi gani unanipenda” Sauti ya Catherine ilisikika.

    “Ungependa nifanye nini kwa ajili yako?” Edmund aliuliza.

    “Unibusu”

    “Nikubusu wapi?”

    “Popote pale”

    “Sawa, hakuna tatizo. Ngoja nikubusu kwenye unyayo wako” Edmund alimwambia Catherine huku akiachia tabasamu kana kwamba Catherine alikuwa mbele yake.

    “Mmmh! Jamaniiiii”

    “Nini tena mpenzi?”

    “Unibusu kwenye unyayo?”

    “Yeah! Si umekataa kuniambia nikubusu wapi”

    “Naomba unibusu kwenye lipsi zangu” Catherine alimwambia Edmund.

    “Umenikumbusha mbali sana mpenzi”

    “Wapi?”

    “Siku ya kwanza nilipoanza kuzibusu. Zilinipa msisimko wa ajabu sana, miguu ilinilegea kabisa, mapigo ya moyo yalikuwa yakidunda sana. Bado nusu nife” Edmund alimwambia Catherine kwa sauti ya chini.

    “Mmh! Basi usifanye hivyo tena, sitaki kukupoteza mpenzi wangu”

    “Hapana. Usifanye hivyo. Acha niendelee kama kawaida. Hivi inamaana mpaka mwezi wa sita ndio tutaonana?” Edmund alimuuliza Catherine.

    “Yeah!”

    “Hivi kwa nini vyuo vilianzishwa hapa duniani? Yaani huyu aliyeanzisha mambo ya vyuo bora asingezaliwa tu” Edmund alimwambia Catherine.

    “Kwa nini?”

    “Amenifanya nitengane na mpenzi wangu, barafu wa moyo wangu, mwanamke ninayempenda sana” Edmund alimwambia Catherine.

    Katika usiku huo walikuwa wakiongea mambo mengi sana. Kwa mtu mwingine endapo angeyasikia yalionekana kuwa maneno ya kawaida na kijinga sana lakini kwa wao wawili walikuwa wakiyafurahia kupita kawaida. Kila wakati walikuwa wakicheka cheka tu, kila mmoja alikuwa akijisikia raha sana kuongea na mpenzi wake katika usiku huyo.

    Katika chuo Kikuu cha Dar es Salaam, msichana Catherine alikuwa akionekana kuwa mrembo miongoni mwa wasichana wengi ambao walikuwa wakisifika kwa urembo chuoni hapo. Umbo lake zuri pamoja na macho yake yaliyotafsiriwa na wavulana kuwa macho ya kuita vilikuwa miongoni mwa vitu ambavyo vilikuwa vikiwavutia wanaume wengi kutamani kuwa nae.

    Kiuno chake kizuri ambacho kilikuwa kimejigawa vilivyo, kifua chake kidogo kilichoitwa cha saa sita pamoja na sura yake nyembamba navyo vilikuwa miongoni mwa vitu ambavyo vilionekana kuwatoa udenda wanaume wengi chuoni hapo. Idadi kubwa ya wanaume walikuwa wakitaka kuwa na Catherine ambaye alionekana kutokuwa na mpango na mwanaume yeyote zaidi ya mwanaume wake ambaye alikuwa akimpenda kwa moyo mmoja, Edmund ambaye alikuwa akisoma katika chuo kikuu cha Dodoma, UDOM.

    Japokuwa Catherine alikuwa akiwakatalia wanaume wengi chuoni hapo lakini wanaume hawakuonekana kukoma kabisa, kila siku walikuwa wakimfuata Catherine kwa maneno matamu na ya kuchombeza lakini kwa Catherine hakuonekana kujali kwa sababu maneno yale wala hayakuwa mageni masikioni mwake.

    Hapo ndipo ambapo wanaume wale wakaamua kutafuta mbinu nyingine ili mladi msichana huyo aweze kuingia katika mikono yao. Wakaanza kufungua pochi kwa kuamini kwamba msichana huyo angezitetemekea fedha zao lakini hali haikuonekana kuwa kama walivyotarajia, mapenzi ya dhati na uaminifu wake kwa mpenzi wake vilikuwa ni zaidi ya fedha ambazo walikuwa wakija nazo wanaume kama chambo ya kumakatia.

    Wanaume hawakujua ni kwa jinsi gani wangeweza kumuingiza msichana huyo katika mikono yao, kila njia ambazo walikuwa wakizitumia zikaonekana kugonga mwamba jambo ambalo liliwakatisha tamaa wanaume wengi. Catherine akaonekana kuwa msichana wa tofauti sana katika chuo kile, wasichana wengi wazuri ambao walikuwa wakisoma chuoni hapo walionekana kuwa radhi kuzipandisha juu sketi zao kwa wanaume katika kipindi ambacho walikuwa wakionyeshewa fedha lakini kwa Catherine hali ilionekana kuwa tofauti sana.

    Hakuwa akienda katika pati yoyote ya usiku ambazo marafiki zake walikuwa wakimtaka kwenda pamoja nae, hakuwa akienda disko kwa ajili ya kuiburudisha nafsi yake katika kipindi ambacho marafiki zake walikuwa wakienda huko, yeye, alikuwa akipenda kushinda katika chumba alichokuwa akiishi pamoja na marafiki zake hapo hapo chuo.

    “Au huyu msichana ameokoka?” Msichana mmoja alimuuliza mwenzake kuhusiana na Catherine.

    “Wala hajaokoka. Kwanza sijawahi kumuona akienda kanisani, cd zake ambazo mara nyingi huwa anazikiliza ni zile zilizojaa nyimbo za kidunia. Wala hajaokoka kabisa” Msichana mwingine alijibu.

    “Sasa mbona amekuwa hivi?”

    “Nadhani kwa sababu ya msimamo wake tu”

    Hiyo ndivyo ilivyokuwa chuoni hapo, wasichana wengi walikuwa wakifikiri kwamba Catherine alikuwa ameokoka kutokana na aina ya maisha ambayo alikuwa akiishi chuoni hapo kumbe hali ilikuwa tofauti kabisa. Katika kipindi chote toka amalize kidato cha nne hakuwahi kwenda kanisa, katika siku ambazo alianza kufanya mapenzi na Samuel shuleni ndicho kilikuwa kipindi cha mwisho kukanyaga miguu yake kanisa.

    Msimamo wake mkubwa ambao alikuwa amejiwekea katika maisha yake ndio uliwafanya watu wengi kujua kwamba msichana huyo alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wameokoka, watu ambao hawakutaka kabisa kufanya dhambi. Kwa mtazamo, Catherine alionekana kuwa mtu wa dini japokuwa ukweli ulikuwa ni kwamba dini aliyokuwa nayo ilikuwa imempitia kushoto kabisa.

    “Leo kuna sherehe ya kuzaliwa ya Pedeshee Sam” Jamala alimwambia Susan, msichana ambaye alikuwa akiishi ndani ya chumba alichokuwa akiishi Catherine.

    “Mmmh! Sipati picha huko jinsi mambo yatakavyokuwa. Itafanikia katika jumba lake lile lile la kifahari?” Susan aliuliza huku akionekana kushtuka.

    “Kama kawaida. Kutakuwa na mambo mengi sana usiku wa leo. Kama vipi twende, kiingilio hakuna, ni bure kabisa” Jamala alimwambia Susan.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Lazima niende, nadhani naweza nikapata hata fedha kidogo za kusogeza siku. Wewe vipi Catherine?” Susan alisema na kisha kumgeukia Catherine ambaye alikuwa kitandani na kumuuliza.

    “Kuhusu nini?”

    “Kwenda kusherehekea na Pedeshee sam. Au hautaki?” Susan alimjibu na kumuuliza.

    “Hapana. Siwezi” Catherine alitoa jibu lililomfanya Susan kupiga hatua kukisogelea kitanda alichokuwa amelalia.

    “Mbona unakuwa hivyo Catherine? Yaani kila siku umekuwa mtu wa kukaa ndani tuuu na hautaki hata kutoka kwenda sehemu mbalimbali. Usifanye hivyo, wakati mwingine uwe unatoka, yaani hata kutupa kampani sisi wenzako. Urafiki gani huo, kila siku unataka kututenga. Wewe unapotuambia twende na wewe sehemu yoyote ile tunakwenda nawe, haijalishi iwe nzuri au mbaya, ila wewe tukikwambia uongozane nasi, hautaki, sasa urafiki gani huo? Kwani ukienda huko tutakupa mwanaume? Kwani ukienda huko tutakulazimisha unywe pombe? Kwani tukienda huko tutakulazimisha ucheze muziki? Hapana, tutachohitaji ni kampani yako tu, nasi tujue kwamba tuna rafiki ambaye anatujali na kutusikiliza kama sisi tunavyomsikiliza” Susan alimwambia Catherine.

    Susan hakuishia hapo, aliendelea kuongea maneno mengi ambayo yalimaanisha kumpa lawama Catherine kwa kile ambacho alikuwa akiwafanyia. Maneno yale yakaonekana kuwa mwiba moyoni mwa Catherine ambaye baada ya dakika kadhaa akakubaliana nao kwenda katika sherehe ya kuzaliwa ya huyo mtu ambaye alikuwa akijiita Pedeshee Sam, mwanaume ambaye alijulikana kuwa na fedha nyingi katika wakati huo, mwanaume ambaye alikuwa kivutio kwa wanawake wengi, hasa wanavyuo.

    ****

    Katika mwezi huo wa nane, nchi ya Malaysia ilikuwa yenye baridi kali, watu wengi ambao walikuwa wametoka katika nchi mbalimbali barani Afrika katika kipindi hicho walikuwa wakivaa makoti mazito au masweta ambayo yalikuwa na uwezo wa kuzuia baridi lile. Walipoteremka kutoka katika ndege ile, moja kwa moja wakaanza kupiga hatua kuelekea katika jengo la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur uliokuwa katika jiji hilo kubwa la Kuala Lumpur.

    Mpaka katika kipindi hicho walichoanza kupiga hatua katika ardhi ya nchi ya Malaysia hawakujua ni kitu gani ambacho walitakiwa kukifanya kwa kuona kwamba kama wangeendelea kwenda na abiria wale basi wangeishia katika sehemu ya kuchunguzia mabegi na hatimae madawa yao ya kulevya kukamatwa na hivyo kuingia matatizoni.

    Huku wakiwa wamebakiza hatua kumi kabla ya kuingia katika mlango wa kutokea katika sehemu ambayo wangetakiwa kuyaacha mabegi yao madogo kuungana na makubwa na kisha kuchunguzwa, wakatolewa katika mstari wa abiria wale na watu ambao wala hawakuwa wakiwafahamu na kisha kupelekwa pembeni.

    “Are you Samuel and Sadiki (Nyie ni Samuel na Sadiki)” Mwanaume mmoja kati ya wanaume watatu ambao waliwavuta pembeni waliwauliza huku wakiwaangalia.

    “Yeah” Samuel alijibu.

    “Lets go this way (Twendeni njia hii)” Mwanaume huyo aliwaambia na kisha kuanza kuondoka nao. Wakaingia ndani ya jengo la uwanja wa ndege na kutokea katika sehemu iliyokuwa na mlango wa V.I.P na kisha kupitishwa.

    Kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea kilionekana kuwa katika mchongo mkubwa ambao ulikuwa umechezwa na matajiri tu ambao walikuwa wakihusika na uuzaji wa madawa ya kulevya. Khaled alionekana kuwa mwanaume ambaye alikuwa na mtandao mkubwa, mtandao ambao ulimfanya kupanga mbinu mbalimbali na wakuu wa nchi nyingi nje ya Afrika. Mara baada ya kufanikiwa kuvuka salama, wakachukuliwa mpaka katika gari na safari kuanza.

    Wote walionekana kushangaa, hawakuamini kama kulikuwa na kazi sana kuvuka katika uwanja wa ndege namna ile, ndani ya mioyo yao waliona kwamba kama wangeanza biashara hiyo basi wangefanikiwa kuifanya kwa wepesi kupita kawaida. Ndani ya gari, wote walikuwa kimya, mabegi yao hawakutaka kumwachia mtu yeyote ayashike, walikuwa wameyashika vilivyo na hawakutakiwa kuyaachia.

    Huku safari ikiendele, macho yao walikuwa wameyaelekeza nje huku wakiangalia mandhari mazuri ya jji la Kuala Lumpur kwa jinsi ulivyokuwa ukionekana. Idadi kubwa ya watu ambao walionekana kuwa bize kufanya mambo yao ilikuwa ikionekana kuwashangaza sana. Katika barabara hiyo ya Mupush 23 kulionekana kuwa na idadi kubwa ya watu ambao walionekana kuwa kama kwenye maandamano kiasi ambacho magari ambayo yalikuwa yakitumia barabara hiyo kutembea kwa mwendo wa taratibu sana.

    Barabara hiyo ilikuwa ikielekea mpaka Kajang, sehemu ambayo watu waliokuwa wakiishi huko walikuwa matajiri wakubwa. Kutoka uwanja wa ndege mpaka Kajang walichukua zaidi ya dakika arobaini na tano na ndipo wakaweza kuingia ndani ya jumba moja kubwa na la kifahari ambalo lilionekana kukamilika kwa kila kitu. Kulikuwa na bwawa kubwa la kuogelea, kamera nyingi za CCTV pamoja na walinzi ambao walikuwa wamezagaa katika kila pembe ya nyumba hiyo huku mikononi mwao wakiwa na bunduki.

    Kwa mtazamo tu, tayari walikwishafahamu kwamba mtu ambaye alikuwa anamiliki jumba lile alikuwa mtu mwenye fedha ambaye alikuwa akiuza sana madawa ya kulevya na alionekana kutokuwa mtu mwenye huruma hata kidogo. Bunduki ambazo zilishikwa na walinzi wale zilionekana kuwatisha kupita kawaida.

    Wakaingia hadi ndani ya jengo la nyumba ile kubwa na kisha kutulia. Macho yao hayakutulia sehemu moja, yalikuwa yakiangalia katika kila kona ya sebule ile walipokuwa. Muonekano mzuri wa sebule ile ukaonekana kumvutia kila mtu mahali pale kiasi ambacho mioyo yao ikatamani sana na wao kuanza kuuza madawa yao wenyewe na si kuwa wafanyakazi wa Khaled.

    Baada ya dakika kadhaa, mwanaume mmoja ambaye alikuwa na ndevu nyingi akatokea mahali hapo. Kwa heshima wakasimama na kisha kumsalimia. Mwanaume yule alionekana kuwa mwenye furaha tele, hakuamini kama mfanyabiashara mwenzake, Khaled angeweza kukamilisha ishu yote kuhusiana na biashara ya madawa ya kulevya.

    Kitu alichokifanya mzee yule ni kujitambulisha kwao kwamba alikuwa ni mzee Carlos, mtu ambaye alikuwa akisifika sana nchini Malaysia kwa kufanya biashara nyingi za magendo kwa kuwa viongozi wengi wa serikali walikuwa mikononi mwake.

    Mzee Carlos alikuwa tajiri mkubwa sana nchini Malaysia, tajiri ambaye alikuwa akisifika sana kutokana na wema wake wa kuwasaidia watu waliokuwa katika matatizo mbalimbali. Mzee huyu alikuwa akimiliki kampuni nyingi ambazo zilikuwa zikimuingizia fedha nyingi, ukiachana na kampuni hizo, pia alikuwa na viwanda vingi ambavyo vilikuwa vikitengeneza pombe pamoja na vinywaji vingine.

    Kuhusiana na kilimo, mzee Carlos alikuwa akimiliki mashamba mengi ya mpunga pamoja na mazao mengine ambayo kila siku yalikuwa yakiendelea kumuingizia kiasi kikubwa cha fedha. Mzee Carlos hakuishia hapo, yeye ndiye alikuwa mtu pekee ambaye alikuwa akimiliki zaidi ya hoteli saba ndani ya nchi ya Malaysia, Mongoria, China na Indonesia.

    Jina la mzee Carlos lilikuwa kubwa ndani ya nchi ya Malaysia, kila raia wa nchi hiyo alikuwa akimfahamu mzee huyo ambaye kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo alivyokuwa akizidi kupata utajiri zaidi na zaidi. Heshima yake ikaongezeka. Alichokuwa akikifanya kila siku ni kuongeza biashara zake nyingine ambazo zilionekana kumuingizia kiasi kikubwa cha fedha na kuzidi kuweka heshima.

    Japokuwa mzee Carlos alikuwa akifanya biashara nyingi za kihalali lakini katika upande wa pili alikuwa na biashara nyingine ambayo ilikuwa ikimuingizia kiasi kikubwa zaidi, biashara hii ilikuwa ni madawa ya kulevya. Mara kwa mara mzee Carlos alikuwa akinunua madawa ya kulevya kutoka kwa wafanyabiiashara wengi kutoka katika nchi nyingine, wauzaji ambao alikuwa akiwalipa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kilimfanya kuvutiwa na kila mfanyabiashara wa madawa yale.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alifahamiana na Khaled katika kipindi kirefu cha nyuma, kipindi ambacho alikuwa nchini Iraq na kisha nae kuomba kufanya nae biashara ambayo aliamini ingezidi kumuingizia kupita kawaida. Kwa Khaled hilo wala halikuonekana kuwa tatizo kabisa, kwake kufanya biashara na wafanyabiashara mbalimbali duniani kulionekana kumuingizia kiasi cha fedha kupita kawaida.

    Mara kwa mara Khaled alikuwa akiyapata madawa yake ya kulevya kutoka Brazil na Mexico ambayo kila alipokuwa akija nayo Tanzania, nae alikuwa akiyasafirisha kwa watu wengine. Katika kipindi cha kuyasafirisha madawa ya kulevya kutoka katika nchi hizo hakuwa akitumia ndege kwa sababu alikuwa akichukua mzigo mkubwa, usafiri pekee ambao alikuwa akiutumia ulikuwa ni meli.

    Ukaribu wao ukaongezeka na kuwa wafanyabiashara ambao walikuwa wakiuziana madawa ya kulevya kiasi ambacho wakaonekana kuaminiana kupita kawaida. Vijana wengi ambao walikuwa wakifanya kazi kwa Khaled walikuwa wakifahamiana na mzee Carlos ambaye hakutaka kusikia wala kuambiwa kuhusiana na Khaled ambaye alikuwa amefanya nae biashara kwa zaidi ya miaka mitano.

    Siku hiyo alikuwa amekutana na vijana wengine, vijana ambao walikuwa wametumwa na Khaled kumpelekea madawa ya kulevya, vijana ambao kwa kuwaangalia tu walionekana kuwa wajanja. Muda mwingi mzee Carlos alikuwa akitabasamu, kila alipokuwa akiwaangalia alikuwa akijisikia uhuru na amani kwa kuona kwamba vijana wale wangeweza kuendesha biashara ya Khaled kama alivyokuwa akisisitiza.

    “Khaled aliniambia kuhusu ninyi, mnaonekana kuwa vijana hodari ambao hamuonekani kuwa wazi kumtaja bosi wenu. Vizuri sana” Mzee Carlos aliwaambia huku akitoa tabasamu.

    “Hakuna haja ya kumtaja hata kama tutakuwa katika hali ipi. Yeye ndiye ambaye anatufanya tuwe hivi tulivyo, tumejitoa kufanya kazi kwa asilimia mia moja” Samuel alimwambia mzee Carlos ambaye alionekana kufarijika.

    “Vijana wengine huwa wapumbavu sana, yaani wakibanwa kidogo tu, wanazungumza kila kitu. Watu kama hao hawafai kufanya biashara hii” Mzee carlos aliwaambia huku bado tabasamu lake likiendelea kubaki usoni mwake.

    “Kamwe hatuwezi kumtaja wala kumsaliti. Yeye ni bosi wetu na milele atakuwa bosi wetu” Sadiki alisema huku akionekana kumaanisha kile alichokuwa akikisema.

    Hiyo ndio ilikuwa safari yao ya kwanza kutoka nje ya bara la Afrika kwa ajili ya kuuza madawa ya kulevya. Kuanzia hapo, wakaanza kupewa safari mbalimbali za kusafirisha madawa. Katika kila safari ambayo walikuwa wakizifanya, walikuwa wakitumia muda mwingi kuzoeana na wateja mbalimbali ambao walikuwa wakifanya biashara na Khaled.

    Ndani ya miezi nane, walikuwa wamekwishazoeana na wafanyabiashara wengi ambao walikuwa wakihitaji madawa ya kulevya. Majina yao yakaanza kuzoeleka katika masikio ya wanunuaji wa madawa ya kulevya. Samuel na Sadiki hawakuonekana kuwa na haraka, katika kipindi hicho walikuwa wakiendelea kuwazoea watu mbalimbali.

    Katika safari zote za nchini Brazil na Mexico ambako walikuwa wakienda kwa ajili ya kuchukua madawa ya kulevya, Samuel na Sadiki walikuwa wakiendelea kufahamiana na watu mbalimbali huku lengo lao katika kipindi hicho likiwa ni lile lile, kuzijua njia zote ambazo walitakiwa kuzitumia katika kipindi ambacho wangeanza kazi ya kuuza madawa katika nchi mbalimbali duniani.

    Samuel na Sadiki wakajikuta wakizidi kupata jina hata zaidi ya bosi wao ambaye alikuwa akiwatuma kila mwezi, wakafanikiwa kusafiri katika nchi nyingi duniani, ulinzi ambao walikuwa wakiwekewa katika viwanja mbalimbali vya ndege ulionekana kuwatosha sana, kwao, walijiona kuwa kama wafalme ambao walitakiwa kuheshimika katika kila sehemu ambazo walikuwa wakikanyaga.

    “Mwaka umepita. Yaani bado tu tunatakiwa kusubiri zaidi?” Sadiki alimuuliza Samuel.

    “Wewe unaonaje?”

    “Nahisi kama tutachelewa vile. Kwa nini tusikamilishe kila kitu kwa kipindi hiki?”

    “Kumbuka kwamba hatutakiwi kuwa na haraka hata kidogo. Hii ishu inakuwa mdogo mdogo mpaka kinaeleweka” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Kwa hiyo tuendelee kusibiri zaidi?”

    “Hapana. Kama kusubiri tumekwishasubiri. Tukifika, tuhakikishe tunakamilisha kila kitu” Samuel alimwambia sadiki.

    “Sasa tumuue kwa kifo gani?”

    “Tutajua huko huko tukirudi Tanzania” Samuel alimwambia Sadiki.

    Huo ndio ulikuwa mpango ambao walikuwa wameupanga kwa wakati huo, kitu ambacho walikuwa wakikihitaji ni kumuua Khaled na kisha kuiweka biashara ile chini ya mikono yao. Kitendio cha kuagizwaagizwa sana na Khaled kilionekana kuwachosha kupita kawaida, mbaya zaidi walikuwa wamekwishagundua kwamba Khaled alikuwa akiingiza kiasi kikubwa sana kupitia biashara zile ambazo alikuwa akiwatuma kupeleka au kuchukua madaya ya kulevya.

    Katika kipindi hicho wakaonekana kuchoka, hawakutaka tena kusafirisha madawa kwenda katika nchi yoyote ile, kitu ambacho walikuwa wakikitaka katika kipindi hicho ni kumuua Khaled na wao wawe mabosi wa biashara ile ambayo ilikuwa ikiingiza sana fedha. Wakaweka makubaliano juu ya mpango wao huo ambao ulikuwepo vichwani mwao toka zamani kwamba ilikuwa ni lazima wamuue Khaled na mambo mengine kufuata. Kwa wakati huu hakukuwa na mtu ambaye alilipinga hilo kwani kama kutumika chini ya mikono ya Khaled walikuwa wametumika vya kutosha na sasa waliona kuwa muda wao wa ukombozi.

    Waliposhuka katika ndege ya Qatar wakitoea nchini Urusi kupeleka madawa, moja kwa moja wakaingia katika gari la Khaled ambalo liliika mahali hapo na kuwachukua huku kukiwa na dereva ambaye walikuwa wakifahamiana nae sana. Ndani ya gari, hawakuongea kitu chochote kile, muda wote walikuwa kimya huku kila mmoja akifikiria lake. Vichwa vyao vilikuwa vikifikiria mauaji ambayo walitakiwa kuyafanya katika kipindi ambacho wangekuwa nchini Tanzania, mauaji ambayo yangewafanya kupanda daraja la juu zaidi, badala ya kuitwa wafanyakazi basi wangeweza kuitwa mabosi.



    Vichwa vyao vilikuwa vikifikiria kufanya mauaji tu, hawakutaka kuendelea kuwa chini ya Khaled ambaye alikuwa akiwatumia kusafirisha madawa ya kulevya kwenda sehemu mbalimbali duniani, kitu ambacho walikuwa wakikitaka ni kufanya biashara wenyewe na kujiingizia fedha nyingi kwani walikwishaona kwamba kama wangeendelea kuwa chini ya Khaled kamwe wasingeweza kupata fedha nyingi kama walivyokuwa wakizihitaji.

    Mipango yao ilikuwa ikiendelea na katika siku hii ya Jumanne ndio ilikuwa siku ambayo walipanga kukamilisha kila kitu. Walitaka kumuua Khaled katika kifo ambacho kilionekana kama ni ajali lakini ukweli ni kwamba haikuwa ajali bali kila kitu kilikuwa kwenye mipango yao. Kwa sababu siku hiyo ndio ilikuwa siku yenyewe, walichokifanya ni kuelekea katika sehemu walizokuwa wakichinjia ng’ombe na kisha kununua lita tano za damu ya ng’ombe na kisha kurudi na kidumu kile mpaka nyumbani.

    Mauaji ambayo walikuwa wameyapanga katika kipindi hicho ni kumuua Khaled kwa kumhusisha na ajali kitu ambacho kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angefahamu kama ajali hiyo ilikuwa ni ya kupangwa. Kila kitu kilipokuwa tayari wakajiweka vizuri kwa ajili ya kumuua Khaled ndani ya nyumba hiyo na kisha kufanya kile ambacho walikuwa wakitaka kukifanya.

    Siku hii ya leo hawakutaka kuelekea katika nyumba ambayo walikuwa wamepangiwa, walikuwa wakikaa tu kwa Khaled kana kwamba hawakutakiwa kuelekea nyumbani kwao. Hiyo wala haikuonekana kumshangaza Khaled kwa kuchukulia kwamba kila kitu kuwa ni cha kawaida tu kwani hata kama wangetaka kulala ndani ya nyumba hiyo, walikuwa wakiruhusiwa bila kuulizwa swali lolote lile.

    Katika siku zote za nyuma Khaled alikuwa akijitahidi kuishi nao kama ndugu zake ambao alikuwa amezaliwa nao tumbo moja. Alikuwa akiwajali sana kwa sababu wao ndio walikuwa watu pekee ambao walikuwa wakiifanya kazi yake kwa ukamilifu bila longolongo yoyote ile. Katika kipindi chote ambacho alikuwa akiwaonyeshea upendo wa dhati lakini mioyoni mwa vijana hao kulikuwa na kitu cha tofauti sana, kumuua na kisha kumdhulumu biashara ambayo alikuwa akiifanya.

    Samuel na Sadiki walijua fika kwamba Khaled alikuwa na mtandao mkubwa sana, mtandao wa madawa ya kulevya na pia alikuwa akishirikiana na watu wengi katika uuzaji wa madawa hayo ya kulevya jambo ambalo kama wangemuua katika kifo cha kawaida basi wangeweza kuuawa na wafanyabiashara wenzake wakubwa ambao walikuwa ndani ya jiji la Dar es Salaam.

    Kati ya wafanyabiashara wakubwa ambao Khaled alikuwa akifanya nao kazi kulikuwa na Bwana Marko, mzee tajiri ambaye alikuwa akipenda sana kuwa karibu na Khaled katika kila kitu kilichokuwa kikihusu biashara. Kila walipokuwa wakimfikiria mzee Marko, kwa jinsi alivyokuwa akionekana kuwa na roho mbaya na kwa jinsi alivyokuwa akimpenda sana Khaled waliona kwamba kulikuwa na kila sababu ya kumuua Khaled katika hali ambayo ingeonyesha kwamba alikuwa amepata ajali.

    “Uliwasiliana na yule jamaa mwenye lori la mchanga?” Samuel alimuuliza Sadiki.

    “Yeah! Niliwasiliana nae” Sadiki alijibu.

    “Alihitaji kiasi gani kwa kazi ya usiku mmoja tu?”

    “Laki saba”

    “Ulimpa?”

    “Ndio. Nilimpa laki saba taslimu”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Na vipi kuhusu kwenda kulichukua hilo lori?”

    “Amesema nikutane nae baadae pale Magomeni Mikumi. Kuhusu lori hilo si tatizo. Tatizo ni jinsi ya kumuua huyu mpumbavu” Sadiki alimwambia Samuel.

    “Hata hili si tatizo. Mtu mmoja hawezi kutushinda” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Kwa hiyo tumuue vipi? Tumchome kisu?” Sadiki aliuliza.

    “Hapana. Ukimchoma kisu ishu itajulikana kwani dokta akiangalia ataona mwili una jeraha la kisu. Cha msingi tumuue kwa kumkaba tu, unaonaje?” Samuel alimwambia Sadiki na kumuuliza.

    “Mmmh! Hatotuzidi nguvu?”

    “Hawezi. Watu wawili hatuwezi kushindwa nguvu na yeye”

    Katika kipindi chote ambacho walikuwa wakipanga yote walikuwa sebuleni huku Khaled akiwa chumbani kwake. Mipago yao ilikuwa ni kutaka kummaliza Khaled na kisha kuendelea na maisha yao huku wakiwa wamiliki wakubwa wa biashara ya madawa ya kulevya. Mpaka inafika saa sita, bado walikuwa ndani ya nyumba ile ambapo wakaamua kumuita Khaled pale sebuleni huku wakijifanya kuwa na tatizo.

    “Kuna nini tena?” Khaled aliwauliza.

    “Kuna tatizo”

    “Tatizo gani? La kifedha? Mnataka kiasi gani?” Khaled aliuliza maswali matatu mfululizo.

    “Tatizo ambalo litatupasa sisi watatu tukae chini na kuongea” Samuel alimwambia Khaled.

    “Mbona mnanitisha! Kuna nini tena?” Khaled aliuliza huku akionekana kutokuelewa.

    “Kuna karatasi ambayo tuliipata getini leo asubuhi, karatasi ambayo ilikuwa imeandikwa maneno mengi ambayo hayakuwa yakieleweka” Samuel alimwambia Khaled.

    “Maneno gani?”

    “Kwamba ni lazima sisi watatu tufikishwe mbele ya vyombo vya dola kwa biashara hii tunayoifanya” Samuel alimwambia Khaled.

    Katika kipindi chote hicho Khaled alikuwa amesimama huku Samuel na Sadiki wakiwa wamekaa kwenye kochi. Kitu ambacho walikuwa wakikitaka ni kumkaba Khaled lakini hawakuwa wameona ni kwa namna gani wangeweza kusimama na hatimae kumkaba kwa nguvu na kisha kumuua. Katika maneno yote hayo ambayo alikuwa akiongea Samuel, alikuwa akitafuta sababu ambayo ingemfanya kuinuka mahali pale na hatimae kumsogelea Khaled na kisha kwa kasi kumkaba.

    “Yaani hapa tumechanganyikiwa na ndio maana leo hii mpaka muda huu tupo mahali hapa” Samuel alimwambia Khaled.

    “Usichanganyikiwe. Nyuma yangu kuna watu wengi sana. Karatasi yenyewe iko wapi?” Khaled alimwaambia na kisha kuuliza kuhusiana na karatasi hiyo.

    Hiyo ndio ikaonekana kuwa nafasi ambayo walikuwa wakiitaka. Samuel akasimama na kisha kuingiza mkono wake mfukoni, akatoa karatasi na kisha kuanza kumsogelea Khaled huku akionekana kuwa na lengo la kumgawia karatasi ile. Khaled akaichukua na kisha kuifungua. Machoni mwake hakuonekana kuwa na wasiwasi wowote ule, akili yake iliamini katika kila kitu ambacho Samuel alikuwa akikiongea.

    Alipoifungua karatasi ile, alikutana na maneno madogo madogo ambayo yalimfanya kuisogeza karatasi ile karibu na uso wake huku Samuel akiwa amesimama mbele yake. Alichokifanya Samuel ni kuanza kuzuga kwa kutembea pembeni mwa Khaled, alipoona amesimama katika eneo zuri, kwa kasi akajisogeza nyuma ya Khaled na kisha kuanza kumkaba roba kali.

    Khaled akashtushwa na roba ile, alionekana kama kupigwa butwaa lakini hapo akagundua kwamba kama angebaki akiwa ametulia bila kuleta kipingamizi chochote kile angeweza kufa. Alichokifanya ni kuanza kujitetetea kwa kutaka kuitoa roba ile. Sadiki ambaye alikuwa kwenye kochi, kwa kasi ya ajabu akasimama na kisha kuanza kuwasogelea, alipowafikia akaanza kumpiga Khaled ngumi nzito za mbavu kwa lengo la kumchosha.

    Zilikuwa ni ngumi nzito zilizokuwa zikipigwa kwa mfululizo, ngumi zile nzito za mbavu ndizo zilizomchosha Khaled na kujikuta akilegea mwili mzima. Samuel hakutaka kumuachia, aliendelea kumkaba roba zaidi na zaidi huku Sadiki akiendelea kumpiga ngumi mfululizo za mbavu. Ni ndani ya dakika moja na nusu tu, damu zikaanza kutoka puani mwa Khaled, mwili ukamlegea, miguu yote ikalegea na pumzi kukata.

    Samuel hakutaka kumuachia, bado alikuwa akiendelea kumkaba zaidi na zaidi. Mpaka pale alipohakikisha kwamba Khaled alikuwa amekwishakufa hapo ndipo ambapo akaonekana kuridhika, akaachia roba ile, Khaled akaanguka kama mzigo. Hicho ndicho kitu ambacho walikuwa wakikihitaji mahali hapo, tayari walikwishaona kwamba walimuua Khaled na hivyo kulikuwa na kazi moja ambayo ilikuwa imebakia, kazi ambayo ilitakiwa kufanyika usiku huo huo.

    “Nenda kwa mlinzi” Samuel alimwambia sadiki.

    “Kufanya nini tena?”

    “Kamwambie afungue geti kwani bosi anataka kutoka, katika kipindi ambacho nitakuwa nambeba wewe kuwa bize kuongea nae. Nitapitia nae mlango wa nyuma ili asiweze kuniona katika kipindi ambacho namuingiza ndani ya gari” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Hakuna noma” Sadiki alimwambia Samuel.

    “Na kile kidumu cha damu ya ng’ombe kipo wapi?”

    “Kwenye gari letu”

    “Ok! Hakuna noma. Tunaondoka na magari yote. Wewe endesha gari letu mimi nitaendesha gari la huyu marehemu” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Hakuna noma”

    Sadiki akatoka ndani ya nyumba ile na kisha kuelekea nje. Hakutaka kuonekana kuwa na wasiwasi au uharaka wowote ule kwa kuamini kwamba kama angekuwa vile basi angeweza kushtukiwa na mlinzi. Alichokifanya ni kuwa katika hali ya kawaida na kisha kumfuata mlinzi na kumwambia kwamba Khaled alikuwa akitaka kutoka na hivyo alipaswa kufugua gari.

    Ndani ya nyumba ile, Samuel hakutaka kuchelewa, kitu ambacho alikuwa akikifanya mahali hapo ni kuubeba mwili wa Khaled na kisha kuanza kuelekea nao jikoni na kutoka nje kwa kupitia mlango wa nyuma. Akaanza kupiga hatua huku mwili wa Khaled ukiwa begani mwake, alipolifikia gari la Khaled, akaupandisha mwili ndani, akafunga vioo vya gari lile ambavyo vilikuwa na tinted na kisha yeye mwenyewe kuingia na kuondoka mahali hapo.

    Mpaka gari linatolewa ndani ya eneo lile, mlinzi hakuonekana kugundua kitu chochote kile kutokana na vioo vya tinted ambavyo vilikuwa vimefungwa hivyo kutokuona ndani. Magari yote mawili yalipotoka, safari yao ikaanza.

    Katika muda huo walikuwa wakielekea Magomeni Morocco, sehemu ambayo walikuwa wamepanga kufanya mikakati ya ajali ile. Njiani wakasimamisha magari yao na kisha Sadiki kumpelekea Samuel kidumu kile kilichokuwa na damu na kisha kuendelea na safari zao.

    Kutoka Kijitonyama wala hawakutumia muda mrefu mpaka kufika Magomeni, ni ndani ya dakika chache wakawa wamekwishafika sehemu hiyo huku ikiwa ni saa sita na robo usiku. Walipofika magomeni Morocco, Sadiki akakata kona kulia, alikuwa akielekea Magomeni Mikumi kwa ajili ya kuongea na dereva wa lori la mchanga huku Samuel akikata kona kulia na kuanza kuelekea Kinondoni Mkwajuni lengo likiwa ni kufika huko na kisha kukata kona na kuchukua barabara ya kuja Magomeni.

    Huo ndio mpango ambao walikuwa wameupanga, ulikuwa ni mpango kabambe ambao ulionekana kufaa kwa kila mtu bila watu wengine kufahamu kile ambacho kilikuwa kikitaka kutokea mahali hapo. Ndani ya dakika tano, Samuel alikuwa amekwishageuza gari na kufika pale Magomeni Morocco kutokea Mkwajuni na kujifanya kama alikuwa akitaka kuingia katika barabara nyingine. Alipolifikisha gari mahali hapo, Samuel akachukua kidumu kile na kuanza kumwaga damu ndani ya gari lile na kisha akateremka, akaacha indiketa za gari lile kama dereva ambaye alikuwa akitaka kukata kona na kuingia katika barabara nyingine

    Samuel hakutaka kubaki mahali, hapo, akaondoka huku kidumu kikiwa mkononi mwake, akaelekea katika kituo cha daladala na kutulia huku akitaka kuona mchezo mzima ambao ulikuwa ukitarajiwa kufanyika mahali hapo.

    “Kila kitu tayari huku” Samuel alimwambia Sadiki simuni.

    “Tunakuja” Sadiki alimwambia Samuel na kisha kukata simu.

    ****

    Mara baada ya kukata kona ya kulia, moja kwa moja Sadiki akaanza kuelekea Magomeni Mikumi huku lengo lake kubwa likiwa ni kuonana na dereva wa lori ambaye alikuwa amemwambia kuhusiana na gari hilo kwa lengo la kulikodi na kisha kulitumia na ndani ya dakika arobaini lingekuwa tena mikononi mwake.

    Katika kipindi alichokuwa akiambiwa, dereva alionekana kutokukubali lakini mara baada ya kupewa kiasi cha shilingi laki saba, moyo wake ukalainika na kukubaliana na Sadiki juu ya kile ambacho alikuwa amemwambia, kumkodisha gari lile huku dereva yule akiwa pambeni.

    “Ila kila kitu kitatakiwa kuwa siri kama tulivyokubaliana mchana, tumeelewana?” Sadiki alimwambia dereva yule.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tumeelewana. Hakuna tatizo” Dereva yule aliyejitambulisha kama Athumani alimwambia sadiki.

    Sadiki hakutaka kuchelewa, akaanza kulifuata lori lile huku akiwa pamoja na dereva yule, walipolifikia, wakaingia ndani na kutulia. Katika kipindi hicho Sadiki alikuwa akisubiria simu kutoka kwa Samuel, simu ambayo ingemtaarifu kwamba kila kitu kilikuwa tayari. Wala hazikupita dakika nyingi, simu yake ya mkononi ikaanza kuita, kwa haraka akaichukua na kisha kuipeleka sikioni.

    “Tunakuja” Sadiki alisema na kisha kuikata simu ile.

    Kilichofuata baada ya hapo ni kuliwasha roli lile na kisha kuanza safari. Kutokana na usiku kwenda sana, barabarani hakukuwa na magari mengi, hivyo ilikuwa haina budi kwa Sadiki kuendesha gari lile kwa mwendo wa kasi kidogo. Athumani hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea, yeye alikuwa amekaa pembeni huku mfukoni akiwa na fedha ambazo alipewa kama malipo.

    Gari lile lilipofika Magomeni Hospitalini, likaendelea mbele kana kwamba lilikuwa likielekea Mkwajuni. Lilipofika maeneo ya Magomeni Morocco, Sadiki akaiona ile gari ya Khaled ikiwa imepakiwa katika sehemu ambayo gari lililokuwa likitaka kuingia barabara nyingine lingeweza kuingia. Sadiki akaongeza kasi zaidi, kwa kiasi fulani dereva yule akaonekana kuwa na wasiwasi lakini Sadiki hakuonekana kujali.

    Watu ambao walikuwa pembeni ya barabara ile ambao wengi walikuwa ni walevi waliokuwa wametoka katika baa mbalimbali wakabaki wakilishangaa lori lile ambalo lilikwenda moja kwa moja na kuligonga gari lile la Khaled ambalo lilikuwa limepakiwa katikati ya sehemu iliyokuwa na maunganiko ya barabara mbili za upande tofauti.

    Gari la Khaled likabamizwa, mlio mkubwa ukasikika mahali hapo, kutokana na lori kuwa na uzito mkubwa, gari lile likapelekwa pembeni na kuanza kubimbilika. Athumani alipigwa na mshangao, hakuamini kama mtu yule ambaye alikuwa amempa lori lile aliendeshe alikuwa amesababisha ajali ambayo ilionekana kuwa ya kijinga sana. Sadiki hakuonekana kujali, alichokifanya baada ya kuona gari la Khaled limebimbirika ni kupiga gia na kisha kuondoka mahali hapo huku watu wakianza kukusanyika mahali pale.

    Ile ikaonekana kuwa ajali mbaya ambayo ilitokea mahali hapo, mlio ule mkubwa ambao ulisikika ndio uliosababisha watu wengi kuanza kukusanyika mahali pale. Walichokifanya wanaume wenye nguvu ambao walifika ndani ya eneo hilo ni kuanza kulifuata gari lile na kisha kusaidiana kuliweka sawa, kutokana na kuwa kiubavu ubavu.

    “Kuna mtu?” Jamaa mmoja aliyeonekana kuwa mlinzi wa mahali fulani aliuliza huku akiwasha tochi yake na kuangalia ndani.

    “Hebu cheki” Jamaa mwingine alimwambia mwanaume yule ambaye akaanza kumulika kwa tochi.

    “Mmmh! Kumbe kuna mtu. Tusaidiane kumtoa na tumpeleke hospitali” Mwanaume yule aliyekuwa mlinzi aliwaambia wenzake ambao wakaanza kuufungua mmoja wa milango iliyokuwa mbele.

    Hilo wala halikuwa zoezi kubwa, ni ndani ya sekunde kadhaa walifanikiwa kuufungua mlango na kisha kuutoa mwili wa Khaled ambao ulionekana kuharibika vibaya, damu ile ya ngombe ilionekana kutapakaa mwilini mwake jambo ambalo lilionyesha kwamba alikuwa ameumia viabaya sana. Wingi wa damu ndani ya gari lile ukaonekana kuwaogiopesha watu wengi waliofika mahali pale na kwa sababu ya kujigonga huku na kule mwili ule uliweza kuchanika chanika, kichwa kilikuwa kimebondeka kidogo kutokana na kujigongagonga katika vyuma ndani ya gari lile.

    Mwili ulipotolewa, wakasimamisha gari jingine na kisha kuupakiza na safari ya kuelekea katika hospitali ya Muhimbili kuanza huku kukiwa hakuna hata mtu moja aliyekuwa akijua kama ajali ile ambayo ilikuwa imetokea ilikuwa ni ajali ambayo ilipangwa na vijana waliokuwa wakiuza madawa ya kulevya.

    “Hivi ilikuwaje Ally?” Jamaa mmoja alimuuliza mwenzake.

    “Hizi ajali nyingine za kizembe sanaaaaa” Ally alisema maneno ambayo yakawafanya baadhi ya watu kuanza kumsogelea kwa kutaka kujua ni kitu gani kilitokea.

    “Kivipi?”

    “Huyu dereva wa hii gari ndogo nae alikuwa mzembe sana” Ally aliwaambia.

    “Kivipi tena?”

    “Yeye alikuja kusimamisha gari lake hapa kana kwamba alikuwa akitaka kuingia katika hii barabara nyingine kwani indiketa za gari zilikuwa zikiwaka kuonyesha kwamba alikuwa akitaka kuingia ndani ya barabara hii nyingine” Ally aliwaambia huku kila mmoja akiwa kimya kumsikiliza, akaendelea.

    “Alikaa mahali hapa kwa muda mrefu sana, kama dakika saba hivi. Mimi nilifikiri alikuwa akitaka kuvuka na kuingia katika barabara hii nyingine. Kila nilipokuwa nikiangalia, hakuwa akiingia. Baada ya muda, ghafla nikaliona lile lori likija, sijui nae dereva wa lori alikuwa amelewa, akaanza kuelekea katika sehemu ambayo kulikuwa na gari lile, akaligonga, gari likabimbirika. Dereva wa lori alivyoona vile, hakukaa, akapiga gia na kusepa zake” Ally aliwaambia.

    “Kwa hiyo nani alikuwa mzembe?”

    “Wote wawili, ila kuhusu kifo, dereva wa gari ndogo alijitakia” Ally alisema.

    Kila mmoja mahali hapo akaonekana kuridhika, mara baada ya Ally kuelezea kile ambacho kilikuwa kimetokea. Kwa maelezo ya Ally, dereva wa gari dogo alionekana kuwa mzembe sana kwa kulisimamisha gari lake eneo moja huku akitaka kuingia katika barabara ya pili lakini hakufanya hivyo mpaka pale gari lake lilipokuja kugongwa na lori lile.

    “Mipango kabambe hii hufanywa na watu wajanja kama sisi” Sadiki alimwambia Samuel katika kipindi ambacho walikuwa wakiongea ndani ya nyumba yao, kila kitu walichokuwa wakitaka kifanyike, kilikuwa kimekwishafanyika.

    “Nini kinachofuatia kwa sasa?” Samuel aliuliza huku akimimina pombe katika glasi yake.

    “Ni kusherehekea tu” Sadiki alimwambia Samuel na kisha kugongesheana glasi zao bila kujua kwamba ni kitu gani kingeweza kutokea katika maisha yao ya baadae, hawakuonekana kukumbuka kwamba damu ya mtu inaweza ikawafanya kutokuwa na amani.



    Kila kitu ambacho walikuwa wakitamani kuwa nacho katika kipindi hicho walikuwa nacho kupitia mauaji na dhuluma ambayo walikuwa wameifanya. Kwao, fedha zikaonekana kuwa kila kitu, biashara ya madawa ya kulevya ambayo walikuwa wakitaka kuimiliki ikaonekana kuanza kuwa yao. Wafanyabiashara wengi ambao walikuwa wakishirikiana na Khaled katika kuuza madawa ya kulevya wakaonekana kuwa na huzuni kupita kawaida, hawakuamini kama mtu wao ambaye walikuwa wakifanya nae biashara alikuwa amekufa katika ajali ya gari, ajali ambayo ilionekana kuwa ya kizembe kupita kawaida.

    Kwa kuwa Khaled hakuwa na ndugu, Samuel na Sadiki ndio ambao wakawa wamiliki wa biashara hiyo na kila kitu ambacho Khaled alikuwa akimiliki. Kama alivyowafanyia Khaled, nao wakatafuta vijana ambao walikuwa tayari kuwafanyia biashara ile kwa kuwasafirishia katika nchi nyingine. Kuwapata wala haikuwa kazi kubwa kutokana na vijana wengi kupenda kufanya kazi haramu na kuingiza fedha za haraka haraka, wakawapata vijana wawili, Joram na Ignas ambao walijitolea kufanya biashara pamoja nao.

    Hao ndio vijana ambao walikuwa wakiwasafirisha kuelekea katika nchi nyingine na kisha kufanya biashara ya madawa ya kulevya ambayo waliamini kwamba ingewaingizia fedha nyingi kupita kawaida. Vijana wale wakawafundisha mambo mengi juu ya kusafirisha madawa ya kulevya katika nchi nyingine huku wakiwaahidi kuwa nyuma yao kwa kuwatengenezea mazingira yote mazuri ya kufanyia kazi.

    Biashara haikusimama, kila siku walikuwa watu wa kuwa bize kuwasiliana na wafanyabiashara wenzao kutoka katika nchi mbalimbali. Katika kipindi hiki ndicho ambacho waliamua kuongeza matawi zaidi ya kusafirishia biashara yao kwa kutambua makosa ambayo Khaled alikuwa akiyafanya, wao wakaamua kuyatatua makosa yale jambo ambalo liliwafanya kuendelea zaidi katika biashara hiyo.

    Kila kitu ambacho walikuwa wakikihitaji walikuwa wamekwishakipata, ndani ya miezi minne tayari walikuwa na fedha nyingi na bado walikuwa wakiendelea kuingiza fedha kama kawaida yao. Wakawa wanaishi maisha ya starehe, maisha ambayo yalikuwa yakijumusiha kwenda kwenye viwanja vya starehe pamoja na kulala na wasichana huku kila mmoja akiwa makini kutumia kinga.

    Maisha yakawa yamebadilika, Samuel na Sadiki hawakuwa watu wa kulala chumba kimoja kama ilivyokuwa zamani kabla ya kuwa wafanyakazi wa Khaled, katika kipindi hiki kila mmoja alikuwa na maisha yao. Nyumba ambayo alikuwa akiishi Khaled wakaamua kuiuza na kila mtu kununua nyumba yake ya kifahari pamoja na magari.

    Biashara ile haramu ikaonekana kuwaingizia fedha nyingi jambo ambalo liliwafanya kutajirika kila siku. Hakukuwa na aliyekuwa akikumbuka kwamba katika kipindi cha nyuma walikuwa watu wa dini kupita kawaida, watu ambao wazazi wao walikuwa wakitamani wawe viongozi wa dini katika nyumba za ibada. Maisha ya starehe yakawateka na kuwapoteza kabisa, hawakuzipenda nyumba za ibada hata mara moja, kwa kifupi ni kwamba walichukia kila kitu ambacho kilikuwa kikikufanya kumsifu Mungu.

    Siku zikaendelea kukatika mpaka kufika kipindi ambacho wakaamua kujitegemea katika biashara zao. Kwa kuwa walikuwa wamekwishapata mafanikio makubwa, wakagawana na kisha kuanza kufanya biashara kila mtu kivyake. Mafanikio yakazidi kuongezeka, majina yao yakaanza kusikika masikioni mwa watu kwamba walikuwa wakiingiza kiasi kikubwa cha fedha na walikuwa miongoni mwa watu waliokuwa na fedha nyingi nchini Tanzania huku wakiwa na umri mdogo, chini ya miaka ishirini na tano.

    Ili kutaka kuwapa upofu watu wengine hasa serikali, wakaamua kuanzisha biashara mbalimbali kama kufungua maduka mengi ya nguo pamoja na kufungua kampuni nyingi ambazo waliamini kwamba zingekuwa zikiwaingizia kiasi kikubwa cha fedha. Watu wakapigwa upofu, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akijua kwamba watu hao walikuwa wakifanya biashara ya madawa ya kulevya, biashara ambayo walikuwa wameanza nayo kitambo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baadhi ya watu ambao walikuwa na vyeo vikubwa wakawa katika upande wao kiasi ambacho wala halikuwa suala kubwa kuhusu kusafirisha madawa ya kulevya kwenda katika nchi nyingine. Kwa Sadiki ndiye ambaye alionekana kuchanganyikiwa zaidi katika kipindi hicho, wanawake wakaonekana kumlevya hata zaidi ya Samuel ambaye kipindi cha nyuma alikuwa mtu wa wasichana kupita kawaida.

    Kwa kila msichana mrembo ambaye alikuwa akipita mbele yake, Sadiki alikuwa akitembea nae. Katika kipindi hicho alichokuwa na fedha wala hakumuogopa msichana yeyote yule, fedha ikamfanya kujiamini kupita kawaida kiasi ambacho hakuonekana kujali itu chochote kile. Alihakikisha kwamba analala na wanavyuo mbalimbali ambao walikuwa wakivuma sana, alihakikisha analala na wanawake ambao walikuwa wakizipenda sana fedha katika maisha yao, kuhusu kugawa fedha kwa wanawake, Sadiki hakuwa mchoyo, mara kwa mara alikuwa akimwaga fedha alivyotaka.

    “Utakufa” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Hata wewe utakufa” Sadiki alimwambia Samuel.

    “Nipo serious Sadiki, utakufa, wanawake hawafai kabisa. Huu ugonjwa unaousikiasikia unaweza kukupata na kuyaona maisha machungu” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Unazungumzia UKIMWI? Hahaha! Hakuna kitu kama hicho, huu ugonjwa ni wa kutunga tu, wala haupo” Sadiki alimwambia Samuel ikiwa mwaka 2003.

    “Sikiliza Sadiki, hakuna kitu cha kudanganya kuhusu ugonjwa huu”

    “Hivi toka umetangazwa umekwishawahi kumuona mtu yeyote akiugua ugonjwa huu?” Sadiki alimuuliza Samuel ambaye akabaki kimya kwa muda.

    “Mbona wapo wengi tu”

    “Hakuna kitu kama hicho”

    “Usipuuzie Sadiki”

    “Najua. Ila usiamini kitu usichowahi kukiona. Ona na ndio uamini”

    “Hayo ni makosa. Hatutakiwi kuishi hivyo”

    “Kwani tatizo lipo wapi? Wewe una fedha zako, mimi nina fedha zangu, kuna tatizo hapo?” Sadiki alimuuliza Samuel.

    “Fedha si kila kitu Sadiki”

    “Umeanza. Kwa hiyo unataka kuniambia nini sasa? Au unataka kuanza kurudi tena kanisani na kisha uanze kuhubiri kama baba yako?” Sadiki alimiiliza Samuel huku akionekana kumshangaa.

    “Hapa sizungumzii kuhusu kanisa, sizungumzii kuhusu kuhubiri, hapa ninazungumzia kuhusu UKIMWI” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Ok! Nimekuelewa baba mchungaji. Nitaacha tabia hii” Sadiki alimwambia Samuel na kisha kusimama, akachukua chupa iliyokuwa na pombe na kuanza kunywa.

    Sadiki hakuishia hapo, bado alikuwa akiendelea na tabia yake ya kuchukua kila mwanamke ambaye alikuwa akimuona kumfaa. Samuel alijitahidi kuongea sana lakini mwisho wa siku akaonekana kuchoka jambo ambalo lilimfanya kubaki kimya na kutaka kuona ni kitu gani ambacho kingetokea katika maisha ya baadae.

    Bado fedha zilikuwa zikiwasumbua, walikuwa na fedha nyingi sana kiasi ambacho wakaamua kufanya sherehe mbalimbali na kisha kuwaita watu na kusherehekea pamoja nao huku wakimwaga fedha kila wakati. Warembo wakaonekana kuwanyenyekea, fedha walizokuwa nazo zikaonekana kuwa ulimbo kwa wasichana wengi, hasa wanavyuo.

    Kwa Samuel hakuonekana kupenda wanawake katika kipindi hicho, kama wanawake alikuwa amekwishatembea na wanawake wengi lakini mwisho wa siku hakuona kama kulikuwa na utofauti wowote ule. Ukiachana na hilo, ugonjwa wa UKIMWI ambao ulikuwa ukuvuma kila siku ndio ambao ulionekana kumuogopesha kupita kawaida. Taarifa mbalimbali za habari ambazo zilikuwa zikitangaza kuhusiana na ugonjwa huo zikaonekana kumuogopesha, akatokea kuwahofia wanawake japokuwa alijua kwamba kulikuwa na mipira ya kinga.

    “Kesho ni sikukuu yangu ya kuzaliwa. Nahitaji watu wengi wa kuwa mahali hapa” Samuel alimwambia Sadiki.

    “Mbona ghafla hivyo?”

    “Nilisahau kama ni kesho, nimekuwa bize sana katika kipindi hiki. Naomba unitafutie watu wengi wa kuja kuhudhuria” Samuel alimwambia Sadiki ambaye akachukua simu yake na kisha kuanza kuwasiliana na watu mbalimbali hasa wasichana wengi huku akiwataka kufika katika nyumba ya Samuel iliyokuwa Mbezi Beach, Africana kwa ajili ya kusherehekea katika siku yake ya kuzaliwa pamoja na kuwaita marafiki zao mbalimbali.

    “Itakuwa asubuhi, mchana au usiku?” Sauti ya msichana mmoja iliuliza,

    “Ile ni sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mtu mzima na si ya mtoto. Itafanyika usiku, watoto ndio wanaofanya asubuhi na mchana” Sadiki alimwambia msichana huyo.

    Kuhusu kuwaita watu mbalimbali halikuwa tatizo, Sadiki alikuwa akijitahidi kadri ya uwezo wake kuwaita watu mbalimbali katika sherehe ile ambayo ikawafanya watu wengi kufahamu kile kilichokuwa kikienda kutokea siku ya kesho.

    “Kama kawaida. Warembo watakuwa wa kumwaga” Sadiki alimwambia Samuel.

    “Hakuna noma. Itakuwa poa sana”

    “Kila siku nakwambia lakini unanibishia, vitu vingine bila warembo havipendezi kaka” Sadiki alimwambia Samuel ambaye akakubaliana nae.

    Siku ya sherehe ya kuzaliwa kwa Samuel ikawadia, watu wakajazana katika uwanja wa nyumba yake kubwa na ya kifahari, wasichana wengi kutoka vyuoni walikuwa ndani ya eneo la nyumba hiyo huku kila mmoja akiwa amejaribu kuvaa na kupendeza kupita wengine. Wapo ambao walikuwa wamevaa sketi fupi ambazo ziliachia mapaja yao nje, wapo ambao walikuwa wamevaa sketi ndefu lakini vifua vyao havikuwa vimestiliwa vilivyo na ukiachana na hao, wapo pia ambao walikuwa wamevaa suruali za jinsi, kila msichana katika kipindi hicho alikuwa amejitahidi kuvaa na kupendeza zaidi ya mwenzake.

    Wanaume hawakukosa, nao walikuwepo mahali hapo huku wakiwa wamefika kwa ajili ya kusherehekea pamoja na Samuel ambaye alionekana kuwa na furaha kila wakati. Sadiki alikuwa bize, kila wakati alikuwa akijiweka karibu na wanawake, hayo ndio maisha ambayo aliamua kuishi kwa kipindi hicho, kupenda wanawake kama mchungaji anavyopenda kwenda kanisani.

    Muziki ulikuwa ukisikika kwa sauti ya juu huku kila mmoja akiwa bize na vinywaji mikono mwao. Wale ambao walikuwa wakitaka kula, siku hiyo walikuwa huru kula mpaka kusaza, wale ambao walikuwa wakitaka kunywa, bia na soda zilikuwepo mahali hapo, walikunywa mpaka kuacha na hakuna kilichopungua hata kidogo.

    Watu waliendelea kuburudika mpaka katika kipindi ambacho Samuel akasimama na kisha kuanza kuongea, maneno ambayo alikuwa akiyaongea mahali hapo yalikuwa ni ya kuwashukuru watu tisini ambao walikuwa wameruhusiwa kuingia ndani ya eneo la nyumba hiyo ya kifahari. Kila alipokuwa akiongea, tabasamu lake pana lilikuwa likionekana usoni mwake.

    “Endeleeni kuburudika, mkihitaji vinywaji zaidi, vipo na havitokwisha, mkihitaji vyakula, navyo vipo. Na hata wale ambao watataka kulala mahali hapo, vyumba vipo vya kutosha.” Samuel aliwaambia na kisha kuruhusu sherehe kuendelea zaidi huku watu wakizidi kufurahia kwa shangwe.

    Mara kwa mara watu walikuwa wakimsogelea Samuel na kumpongeza kwa kutimiza miaka ishirini na nne. Alionekana kuwa kijana mdogo lakini mwenye fedha nyingi sana, fedha ambazo hakudhani kama ingetokea siku yoyote na fedha zile kumuisha. Kila alipokuwa akipongezwa, Samuel alikuwa akitoa shukrani huku katika mkono wake wa kulia akiwa ameshika chupa moja ya pombe ya John Walker.

    “Samuel....” Samuel aliisikia sauti ya msichana ikimuita, akageuka nyuma na kunza kumwangalia.

    “Samuel...” Msichana yule aliita huku Samuel akibaki amesimama kwa kutaka kumuona msichana huyo karibu zaidi kwani alikuwa kwa mbali kidogo na mwanga haukuwa mkubwa.

    “Catherine...” Samuel alijikuta akiita kwa mshtuko.

    Kila mmoja akabaki akiwa ameduwaa, Samuel akabaki akimwangalia Catherine mara mbili mbili huku akionekana kutokuamini kama mtu ambaye alikuwa amesimama mbele yake alikuwa Catherine, msichana ambaye alikuwa akitembea nae katika kipindi alichokuwa shuleni. Samuel akashindwa kuvumilia, akajikuta akimsogelea Catherine na kisha wote kukumbatiana.

    “Umebadilika Samuel” Catherine alimwambia Samuel.

    “Nimekuaje?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Umenenepa na umekuwa na mwili, kumbe mpaka jina umebadilisha?”

    “Hapana. Bado naitwa Samuel”

    “Mbona nimesikia wakikuita kwa jina la Pedeshee Sam?”

    “Fedha Catherine. Zote fedha hizi” Samuel alimwambia Catherine.

    Moyo wa Samuel ukaonekana kufarijika kupita kawaida. Ni kweli alikuwa ametembea na wanawake wengi katika kipindi cha nyuma lakini kwa msichana Catherine kwake alionekana kuwa msichana wa tofauti sana, kila alipokuwa akimwangalia Catherine, Samuel alikuwa akijisikia amani moyoni mwake, mapenzi juu ya Catherine ambayo yalikuwa yamesahaulika yakaanza kurudi moyoni mwake, tena kwa kasi kubwa sana.

    “Umeolewa?” Samuel alimuuliza Catherine.

    “Hapana. Wewe umeoa?”

    “Hapana. Nisingeweza kuoa na wakati wewe haukuwepo” Samuel alimwambia Catherine.

    “Lakini nasikia una fedha nyingi sana, kwa nini usioe?” Catherine alimuuliza Samuel.

    “Hapana, sikuwahi kumuona mwanamke aliyekuwa sahihi katika maisha yangu zaidi yako Catherine. Wewe ndiye mwanamke ambaye uliniingiza katika mapenzi, thamani yako bado kubwa moyoni mwangu” Samuel alimwambia Catherine.

    “Kwani bado unanipenda?”

    “Nadhani kwa sasa hivi ni zaidi ya nilivyokuwa nakupenda” Samuel alimwambia Catherine.

    “Ila umechelewa”

    “Kwa nini?”

    “Nina mpenzi ambaye anajulikana nyumbani” Catherine alimwambia Samuel.

    “Unafikiri inaweza kubadilisha chochote kile?”

    “Ananipenda na yupo tayari kufanya chochote kwa ajili yangu” Catherine alimwambia Samuel.

    “Ila sidhani kama anakupenda kama ninavyokupenda. Kama nilikupoteza miaka mitatu ya nyuma, kwa sasa hivi sitotaka kukupoteza tena, nitataka kukushikilia vilivyo” Samuel alimwambia Catherine.

    “Please Samuel...umechelewa”

    “Hapana. Nimekuja muda sahihi. Kama ningekuwa nimechelewa, moja ya kidole chako kingekuwa na pete. Ukiona hauna pete, jua kwamba sijachelewa bali nimekuja muda muafaka” Samuel alimwambia Catherine.

    “Ila Samuel nil......”

    “Naomba nikuulize kitu. Unanipenda?”

    “Samuel...Samuel naom.......”

    “Haujanijibu”

    “Lakini ni laz.......”

    “Naomba uniangalie machoni mwangu” Samuel alimwambia Catherine ambaye akaunyanua kidogo uso wake na kumwangalia Samuel machoni.

    “Unanipenda?” Samuel alilirudia swali lake.

    “Nina mpenzi Samuel....ananipenda”

    “Hilo si jibu Catherine. Unanipenda?” Samuel alilirudia swali lake.

    Swali lile likatengeneza kitu cha tofauti moyoni mwa Catherine, hapo hapo akaanza kukumbuka maisha yake ya nyuma ambayo alikuwa ameishi pamoja na Samuel, maisha ambayo yaliwafanya kuwa huru ya kupendana kupita kawaida. Kumbukumbu zile ndicho kilikuwa zaidi ya vitu vyote ambavyo vilimfanya Catherine kuona kwamba kutokuwa na Samuel katika kipindi chote hicho kulikuwa na kitu ambacho alikuwa amekikosa moyoni mwake, kitu ambacho aliamini kwamba hata Edmund hakuwa nacho.

    “Unanipenda?” Samuel aliuliza swali ambalo likamfanya Catherine kushtuka kutoka katika lindi la mawazo, alipomwangalia Samuel machoni kwa mara nyingine, hakuongea kitu, akahisi kama kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kikimtamanisha kufanya kitu kimoja mahali hapo, kubadilishana mate na Samuel. Bila kutarajia, huku kichwa chake kikiendelea kukumbuka mambo ya nyuma, akakikuta kinywa chake kikianza kubadilishana mate na Samuel, hiyo ikawa mara ya kwanza kumsaliti Edmund, mwanaume ambaye alikuwa akimpenda kuliko mwanamke yeyote katika dunia hii.

    “Nakupenda Samuel” Catherine alimwambia Samuel ambaye alionekana kuwa kwenye furaha kubwa, kwake,

    Catherine ndiye alikuwa msichana ambaye alikuwa akimpenda na kumhitaji kuliko wasichana wengine. Alitembea na wanawake wengi ila kwa Catherine, thamani yake haikupungua, bado alikuwa akimpenda kupita kawaida na katika kipindi hicho alijiahidi kumpenda zaidi ya alivyokuwa akimpenda katika kipindi cha nyuma huku akiwa hajui kama katika kipindi hicho msichana huyo alikuwa na kijana Edmund na ndio maana alikuwa akimwambia kwamba alichelewa.



    Catherine akaonekana kubadilika, moyo wake ukaanza kuingiza kitu cha tofauti sana, kitu ambacho alikuwa nacho miaka mitatu iliyopita na katika kipindi hicho kilikuwa kimerudi tena, mapenzi ya Samuel. Catherine alijua fika kwamba katika kipindi hicho alikuwa na mwanaume mwingine ambaye alikuwa akijulikana sana mpaka nyumbani kwao lakini kwa Samuel alijiona kuwa tayari kwa kila kitu.

    Moyo wake ulikuwa umegawanyika pande mbili, kulikuwa na upande ambao ulimhitaji sana Edmund lakini kulikuwa na upande mwingine ambao ulikuwa ukimhitaji sana Samuel, upande huo ndio ambao ulikuwa na nguvu sana moyoni mwake. Kwa Samuel, hakupenda fedha zake, kitu ambacho alikuwa akikitaka ni mapenzi ambayo yalionekana kupotea katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

    Catherine akaonekana kuwa na furaha zaidi, kitendo chake cha kuwa na Samuel kilionekana kumfurahisha kupita kawaida. Kwa Edmund kukaanza kubadilika, mara kwa mara alipokuwa akipigiwa simu Catherine alionekana kukasirika kupita kawaida, mapenzi yake juu ya Edmund yakaonekana kuanza kupungua kabisa kitu ambacho kilionekana kuwa kama maumivu kwa Edmund.

    Catherine alipokuwa akiiona simu ya Edmund ikiingia, alikuwa akiikata na hata wakati mwingine alipokuwa akijisikia kuipokea, aliipokea na kuanza kuongea kwa hasira kwamba asimsumbue kwa sababu alikuwa bize sana katika kipindi hicho. Maneno yale yalionekana kuwa kama msumali wa moto moyoni mwa Edmund, hakuamini kama mpenzi wake wa kipindi kirefu, Catherine, msichana ambaye alikuwa akijulikana mpaka kwao ndiye ambaye alikuwa akimfanyia mambo yale.

    Mkoani Dodoma, Edmund hakusoma kwa raha, kila siku alikuwa na mawazo juu ya mpenzi wake, Catherine ambaye katika kipindi hicho alikuwa katika mapenzi ya dhati kwa Samuel, mwanaume ambaye alikuwa wa kwanza kwake kuutoa usichana wake katika kipindi ambacho walikuwa shuleni miaka mitatu iliyopita.

    Edmund hakutaka kukata tamaa, kila alipokuwa akiisikia sauti ikimwambia kwamba kulikuwa na uwezekano wa Catherine kuwa na mwanaume mwingine, kwake akaonekana kulipinga hilo kwa nguvu zote. Alimjua vilivyo Catherine, alimjua vilivyo jinsi alivyokuwa akimpenda na kumthamini kuliko mwanaume yeyote yule katika dunia hii.

    Hali ile ikaendelea zaidi na zaidi, moyo wake ukaonekana kuungua katika maumivu makali sana lakini Edmund aliendelea kuvumilia tu huku akiamini kwamba mpenzi wake alikuwa bize na hivyo hakuhitaji usumbufu wowote ule. Edmund alipoona kwamba maumivu yanaendelea zaidi moyoni mwake, hapo ndipo ambapo akaamua kuwaambia wazazi wake, Bwana Zilikana na mama yake, Bi Elizabeth.

    Kwanza wazazi hao hawakuamini kama Catherine alikuwa amefikia hatua ya kubadilika namna hiyo kiasi ambacho hawakutaka kuyaamini maneno ya mtoto wao, Edmund na kumtaka kuchunguza zaidi na zaidi juu ya mabadiliko ya Catherine. Edmund hakutaka kujali sana, akaufuata ushauri wa wazazi wake lakini hali haikuonekana kubadilika kwa Catherine, aliendelea kuwa vile vile, mapenzi yalikuwa yamepungua moyoni mwake.

    Hapo ndipo wazazi hao wakaamua kuanza kuelekea nyumbani kwa wazazi wa Catherine na kuamua kuwaambia kile ambacho kilikuwa kikiendelea katika kipindi hicho. Masikoni mwa Bwana Mushi na Bi Maria kitu kile kilionekana kutokuaminika hata ara moja, hawakuamini kama binti yao angeweza kufanya kama vile ambavyo maneno ya wazazi wale wa Edmund yalivyokuwa yakisema.

    “Haiwezekani kabisa” Bwana Mushi aliwaambia huku machoni akionekana dhahiri kutokuamini.

    “Huo ndio ukweli” Bwana Zilikana alimwambia.

    “Hivi mnayafahamu vilivyo mapenzi ambayo watoto wetu walikuwa nayo juu ya mahusiano yao au mnaongea tu?” Bwana Mushi aliuliza.

    “Edmund alipotuambia, na sisi hatukuamini kabisa, ila alipoendelea kutuambia zaidi na zaidi, tukaonekana kumuamini kwa asilimia mia moja” Bwana Zilikana aliwaambia.

    Bado mioyo yao ilikuwa migumu kuamini kile ambacho kilikuwa kinaendelea katika kipindi hicho, hakukuwa na mtu ambaye aliamini kwamba Catherine angeweza kubadilika namna ile. Japokuwa Bwana Mushi na mkewa, Bi Maria walikuwa wakimfahamu Samuel lakini kwa wakati huo hakukuwa na mtu ambaye aliamini kwamba Samuel huyo ndiye ambaye alikuwa amesababisha hayo yote.

    Kilichofanyika mahali hapo ni kumpigia simu Catherine ambaye alihitajika nyumbani hapo kwa ajili ya wazazi kutaka kufahamu kile ambacho kilikuwa kikiendelea katika mahusiano yao. Ndani ya dakika arobaini baada ya kuongea na Catherine, akafika nyumbani hapo na kisha kuwasalimia wote na kukaa kochini huku kichwani akionekana kufahamu kile ambacho alikuwa ameitiwa mahali pale kutokana na uwepo uliokuwepo ndani ya nyumba ile.

    “Nini kinaendelea?” Bwana Mushi alimuuliza binti yake.

    “Wapi?” Catherine aliuliza.

    “Katika mahusiano yenu” Bwana Mushi alimjibu Catherine.

    “Hakuna kinachoendelea”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Usitudanganye Catherine, mbona mwenzako amekuwa akilalamika kwamba umebadilika sana na si kama zamani?” Bwana Mushi aliuliza.

    “Mwenzangu nani?”

    “Hivi Catherine unataka kujifanya mtoto kwamba haufahamu kitu chochote kile na ni nani tunayemzungumzia mahali hapa?” Bwana Mushi aliuliza huku kwa mbali akionekana kubadilika.

    “Unaniambia kwa mafumbo sana baba kiasi ambacho naonekana kutokuelewa” Catherine alimwambia baba yake.

    “Tunaongea kuhusu wewe na Edmund” Bi Vaness akaingilia.

    “Hakuna kilichobadilika, mambo yapo kama zamani” Catherine alijibu.

    “Hapana. Hebu tuambie kinachoendelea”

    “Hakuna kitu baba. Kila kitu kipo kama kawaida” Catherine alimwambia baba yake.

    Kila alipokuwa akiulizwa juu ya kitu kilichokuwa kikiendelea Catherine alionekana kutokuwa tayari kuongea hali halisi, macho yake yakaonekana kujaa uongo. Kila alipokuwa akiulizwa zaidi hakuonekana kuwa radhi kuzungumzia kitu chochote kuhusiana na ukweli ambao ulikuwa ukiendelea katika maisha yake ya kimapenzi pamoja na Edmund. Wazazi wakaonekana kugundua kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kinaendelea lakini Catherine hakuonekana kuwa radhi kusema ukweli.

    “Unajua kwamba dunia haina siri hii?” Bwana Mushi alimuuliza binti yake.

    “Nafahamu baba. Na ninafahamu kwamba kila chenye mwanzo kina mwisho” Catherine alimwambia baba yake.

    “Umemaanisha nini?”

    “Hakuna kitu baba. Nadhani natakiwa kuondoka kurudi chuo” Catherine aliwaambia.

    Catherine akaonekana kubadilika, hakuonekana kuwa kama alivyokuwa katika kipindi cha nyuma, majibu yake pamoja na muonekano wake vilionekana kuwa vitu viwili ambavyo vilikuwa tofauti kabisa na jinsi alivyokuwa katika kipindi cha nyuma. Wote wakajua kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilimtokea Catherine ambaye hakuonekana kuweza kuyaficha mabadiliko ambayo alikuwa nayo. Hawakutaka kumzuia, wakamuacha kuondoka mahali hapo.

    “Mmegundua nini?” Bwana Zilikana, baba yake Edmund aliuliza.

    “Catherine amebadilika sana” Bwana Mushi alijibu huku akionekana kuwa na mshangao.

    “Kuna nini? Waligombana au?” Bi Elizabeth aliuliza.

    “Sijui. Yaani sijui ni kitu gani kinachoendelea mpaka hali kuwa hivi...Catherine amebadilika, tena mabadiliko makubwa” Bi Maria alisema.

    Huo ndio ukweli uliopo, Catherine alikuwa amebadilika kupita kawaida, mabadiliko yake hayakuweza kujificha, yalikuwa yakijionyesha waziwazi mbele ya wazazi wake kitu ambacho kilionekana kumtia wasiwasi kila aliyekuwa akimwangalia pasipo kujua kwamba katika kipindi hicho Catherine alikuwa katika mahusiano na mwanaume ambaye alikuwa nae katika kipindi cha nyuma, mwanaume ambaye aliutoa usichana wake, Samuel.

    Maisha yaliendelea kusonga mbele, Catherine na Samuel wakaonekana kuwa pamoja zaidi, mara kwa mara Samuel alikuwa akiondoka nyumbani kwake Mbezi Beach na kuelekea chuo kikuu cha Dar es salaam kwa ajili ya kumuona mpenzi wak e ambaye alikuwa akimthamini sana, Catherine. Chuoni, kila msichana ambaye alikuwa akimuona Samuel, alimuonea wivu Catherine kwa kuwa na mwanaume kama Samuel, mwanaume ambaye alikuwa akijulikana kuwa na fedha nyingi katika kipindi hicho.

    Catherine hakuwa mtu wa kukaa sana chuoni, mara kwa mara alikuwa akiondoka chuoni hapo na kisha kwenda kulala nyumbani kwa Samuel. Maisha yale yaliendelea, wakaanza kuishi kama mume na mke, kila siku walikuwa pamoja nyumbani huku wakifanya kila kitu ambacho mke na mume walitakiwa kukifanya.

    “Nataka tuoane” Catherine alimwambia Samuel.

    “Wewe unataka lini?”

    “Nikimaliza chuo”

    “Chuo utamaliza mwaka gani?”

    “Bado miaka miwili mbele”

    “Duh! Mbona mbali sana?”

    “Ndio hivyo, inatubidi tuvumiliane mpenzi” Catherine alimwambia Samuel.

    “Hakuna tatizo mpenzi” Samuel alimwambia Catherine.

    Kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo mapenzi yao yalizidi kuongezeka zaidi na zaidi. Walipendana mpaka kufikia hatua ambayo iliwashangaza hata watu ambao walikuwa wakiwaangalia. Hayo ndio mapenzi yalivyokuwa, katika kipindi cha kufurahi, unayafurahia mapenzi na kujiona kama malkia au mfalme, ila wakati yanapoamua kubadilika, moyo unanyong’onyea na kuumia, katika hilo, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akilifikiri, kila mmoja aliona kama wangeendelea kuwa pamoja mpaka kifo kiwatenganishe kumbe mambo yalikuwa tofauti na mategemeo yao.

    ****

    Mzee Hamidu akaonekana kuchanganyikiwa, mpaka katika kipindi hicho hakujua mtoto wake, Sadiki alikuwa mahali gani. Kila siku alikuwa mtu wa majonzi pamoja na mke wake, Bi Aisha ambaye wala hakuweza kuficha hisia zake juu ya kutoonekana kwa mtoto wao ambaye katika kipindi cha nyuma waliamini kwamba angekuwa Imamu kama alivyokuwa baba yake, ustaadhi Hamidu.

    Maisha katika kipindi hicho yalikuwa yamebadilika kabisa, furaha zikapotea mioyoni mwao, hawakuamini kama Sadiki hakuwa ameonekana kwa takribani miezi mitatu. Kitu ambacho walikiona kufaa ni kuwasiliana na mchungaji Mpelele na kisha kuhitaji ushirikiano wao. Familia mbili zikaungana na hatimae kuanza kuwatafuta watoto wao.

    Hawakujua ni mahali gani wangeweza kuwapata lakini walikuwa wakitaka kuiridhisha mioyo yao kwamba nao walijaribu kuwatafuta. Wakaanza kuwaulizia kwa marafiki zao lakini huko wala hawakuweza kupata taarifa juu ya mahali ambapo watoto wao walipokuwa jambo ambalo wakati mwingine liliwafanya kuona kama watoto wao walikuwa wamefariki.

    Siku zikaendelea kukatika, mwaka wa kwanza ukakatika na mwaka wa pili kuingia, bado hawakuweza kufahamu sehemu ambayo watoto wao walipokuwa mbaya zaidi hata tetesi hawakuweza kuzisikia. Mioyo yao ikanyong’onyea kupita kawaida, hawakuamini kama watoto wao hawakuwa wameonekana machoni mwao kwa muda wa miaka miwili.

    Miezi ikakatika na hatimae mwaka wa tatu kuingia, huku ikiwa imebaki miezi minne kabla ya mwaka wa tatu kumalizika, hapo ndipo walipoweza kuwaona watoto wao. Kwanza hawakuamini ila kutokana na picha ambazo walikuwa wakiziona kwenye magazeti hasa ya udaku, wakakubaliana nazo.

    Watoto wao walikuwa wamejijengea majina makubwa na kuwa wafanyabiashara ambao walikuwa wanaingiza kiasi kikubwa cha fedha. Hawakuyaamini macho yao, hali ile ikaonekana kuwatia hofu kupita kawaida. Walichokifanya ni kuitana na kisha kukaa chini na kuanza kuyazungumzia mabadiliko waliyokuwa nayo watoto wao.

    “Hapana. Nina wasiwasi” Mchungaji Mpelele alisema huku uso wake ukionekana kuwa na wasiwasi.

    “Hata mimi mchungaji nina wasiwasi. Usiku ninaota ndoto fulani fulani kuhusiana na mtoto wangu na huo utajiri wake” Ustadhi Hamidu alimwambia Mchungaji Mpelele.

    “Kuna kitu, nahisi watakuwa wameingia kwenye dini inayomuabudu shetani” Mchungaji Mpelele alimwambia ustadhi Hamidu ambaye akaonekana kukubaliana nae.

    “Kwa hiyo tufanye nini?” Mchungaji Mpelele aliuliza.

    “Cha msingi tuonane nao kwanza” Ustadh Hamidu alimwambia mchungaji Mpelele.

    Hicho ndicho kilichofanyika, kwa haraka sana wakaanza kwenda katika kampuni moja ya magazeti ya udaku na kisha kuulizia mahali ambapo Samuel na Sadiki walipokuwa wakiishi. Kutokana na majina yao kuwa makubwa ndani ya jiji la Dar es Salaam, wakafanikiwa kuelekezwa mahali ambapo walipokuwa wakiishi na kisha kuwafuata.

    Kila mmoja katika kipindi hicho alikuwa na hamu ya kumuona mtoto wake, vichwani mwao hawakuwa na hamu ya kuziona mali ambazo walikuwa nazo, wao walichokuwa wakikitaka ni kuwaona tu ili mioyo yao ifurahi na kuwa na amani. Hawakuchukua muda mrefu mpaka kufika Mbezi Beach ambapo wakaanza kuelekea katika sehemu iliyokuwa na nyumba ya Samuel. Wakajitambulisha kwa walinzi na kisha kuingia ndani.

    Samuel alipowaona, kwanza akashtuka, hakuamini kile ambacho alikuwa akikiona, hakuamini kwamba wazazi wake walikuwa wamemuona mara baada ya kuondoka kipindi kirefu kilichopita. Bi Magreth hakuonekana kuvumilia, alichokifanya ni kupiga hatua na kumfuata Samuel, alipomfikia, akamkumbatia huku akianza kutokwa na machozi.

    “Samuel....” Bi Magreth aliita huku akionekana kutokuamini macho yake kwamba siku hiyo alikuwa amekutana na mtoto wake.

    “Nipo hapa. Usilie mama” Samuel alimwambia mama yake, Bi Magreth.

    Samuel hakuwa na jinsi, japokuwa hakuwa akitaka wazazi wake wafahamu mahali alipokuwa akiishi lakini katika kipindi hicho kila kitu kilikuwa wazi kabisa. Alipoona kwamba hata ustadhi Hamidu alikuwa mahali hapo, akampigia simu Sadiki ambaye ndani ya dakika kumi, akawa mahali hapo huku muonekano wake tu ukionekana kuwa na fedha.

    Kama alivyofanya Bi Magreth, Bi Aisha akajikuta akisimama na kwa furaha kumkumbatia mtoto wake. Machoni mwake, Sadiki alionekana kuwa mpya, alionekana kubadilika kupita kawaida. Nae machozi yakaanza kumtoka na kujiona kama alikuwa ndotoni ambapo baada ya dakika chache angeshtuka na kujikuta yupo kitandani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hatimae nimekuona tena” Bi Aisha alimwambia Sadiki huku akiwa amemkumbatia.

    “Hata nami nashukuru kukuona mama” Sadiki alimwambia mama yake, Bi Aisha.

    Hapo ndipo kikao kikawekwa, familia mbili zikaanza kuzungumzia kile kilichokuwa kimetokea. Kitu cha kwanza kabisa, Samuel na Sadiki wakaanza kuomba msamaha kwa kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea kwa kisingizio kwamba hawakupenda kile kilichotokea kitokee katika kipindi cha nyuma. Wazazi wao wakaonekana kuwa waelewa, wakawasamehe kwa moyo mmoja.

    “Na vipi kuhusu utajiri huu” Mchungaji Mpelele aliuliza.

    “Ni habari ndefu sana baba”

    “Ni ndefu ambayo haisimuliki Samuel?” Ustaadhi Hamidu aliuliza.

    “Si kwamba haisimuliki ila kwa kifupi ni kwamba tulikuwa tukifanya kazi mgodini kule Arusha” Samuel aliwaambia.

    “Ikawaje sasa?”

    “Ni habari ndefu sana” Samuel aliwaambia.

    “Hebu Sadiki tuelezee wewe” Mchungaji Mpelele alimwambia Sadiki.

    “Ngoja aelezee yeye” Sadiki alisema kwa kuona kwamba stori yake na Samuel zingeweza kutofautiana.

    “Kuna siku tuliingia mpaka kwenye mgodi kama wachimbaji, tulipofika humo, kifusi kikajifukia. Watu kumi na mbili ambao walikuwa pamoja nasi wakafariki dunia” Samuel aliwaambia stori ya uongo ambayo ilikuwa ikianza kuaminika .

    “Ikawaje?”

    “Kwa sababu tulikuwa tumepata madini, kule chini tukayachukua madini na kuyaweka mdomoni mwa maiti moja” Samuel aliendelea kuwaambia habari ya uongo.

    “Ilikuwaje hapo? Nyie mbona hamkufa?”

    “Kule chini mashimo huwa hutofautiana sana. Shimo la mgodi wetu lilikuwa limekwenda chini kama kilometa moja na kisha kuanzishwa mashimo mengine humo humo, mashimo ambayo yalikuwa upande wa kulia au wa kushoto. Katika kipindi ambacho kifusi kilikuwa kinafukia shimo lile, bahati yetu tulikuwa katika mashimo yale ya pembeni, tukanusurika japokuwa nasi tungekufa kutokana na hewa kuwa nzito” Samuel aliwaambia na kuendelea:

    “Kwa sababu tulikuwa na tochi, tukaanza kufukua mchanga na hatimae kukutana na maiti zile ambapo tukayachukua madini na kisha kuwawekea midomoni mwao. Ilikuwa inahitaji ujasiri wa hali ya juu lakini kwa sababu tulikuwa tukitafuta fedha, tukajivika ujasiri na hatimae kufanikiwa” Samuel aliwaambia.

    “Mmmh! Sasa hayo madini hayakuonekana?”

    “Hapana. Sisi tulikuwa majeruhi na tulikuwa tukiangalia kila kilichokuwa kikiendelea” Samuel aliwaambia.

    Japokuwa uongo ule ulikuwa ni wa kitoto sana lakini uso wa kinafiki ambao alikuwa akiuonyesha Samuel ndio ambao ukawafanya wazazi kuwaamini kwa asilimia mia moja. Wote wakaonekana kuridhika kabisa, mioyo yao ikaonekana kukubaliana nao bila kuwa na maswali yoyote vichwani mwao.

    “Na vipi kuhusu kwenda katika nyumba za ibada? Mnakwenda?” Mchungaji Mpelele aliwauliza.

    “Baba ni rahisi sana kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia Ufalme wa Mbinguni” Samuel alimwambia baba yake.

    “Kwa nini?”

    “Unapokuwa na fedha unahitaji nini tena? Wakati mwingine ninaona kwamba watu wengi humwabudu Mungu kwa kuwa hawana fedha” Samuel alimwambia baba yake ambaye akaonekana kutokuamini kile alichokisikia.

    “Na vipi kuhusu wewe Sadiki?” Ustaadhi Hamidu alimuuliza Sadiki.

    “Kama alivyosema Samuel ndio hivyo hivyo” Sadiki alisema huku akiwa ameuinamisha uso wake chini kwa aibu.

    “Mnakosea watoto wetu, mnakosea kabisa. Fedha si kila kitu, umaarufu ambao mmekuwa nao si kila kitu katika maisha yenu, hivi vyote ni ubatili tu, unapokufa hauzikwi na fedha zako wala mali zako. Mungu ndiye kila kitu” Mchungaji Kipelele aliwaambia.

    “Nadhani niliongea nawe mengi sana Sadiki. Kama ni fedha umekwishapata, huu ndio muda wako wa kumrudia Allah, hakuna muda ulio maalumu, muda wako ni sasa” Ustaadhi hamidu alimwambia Sadiki.

    “Ni ngumu baba”

    “Kwa nini?”

    “Sitaki kuwa mnafiki katika maisha yangu” Sadiki alimwambia baba yake.

    “Unatakiwa kumrudia Allah na kumuomba msamaha. Mtume Mohammad S.A.W alitufundisha mengi sana ikiwa pamoja na kumuabudu Allah kwani Yeye ndiye kila kitu. Wakati wako ni huu Sadiki. Saidia watu wenye matatizo mbalimbali, mtolee Allah sadaka kwani hivyo ndivyo Qur-an inavyoagiza” Ustaadhi Hamidu alimwambia Sadiki ambaye hakuonekana kuelewa hata mara moja.

    Samuel na Sadiki walionekana kubadilika kabisa, hawakutaka kwenda katika nyumba za ibada kwani waliamini kwamba kama wangeanza kwenda katika nyumba zile za ibada basi iliwalazimu waache kabisa kufanya biashara zao za madawa ya kulevya kitu ambacho wala hawakutaka kuachana nacho. Bado walikuwa wakihitaji fedha zaidi, hawakutaka kabisa kubadilika na kuwa watu wa dini kama ilivyokuwa zamani.

    Wazazi wao hawakuwa na jinsi, japokuwa walikuwa wamejitahidi sana kuwaambia maneno mengi kuhusu Mungu lakini mioyo yao ilionekana kuwa migumu sana. Walikaa katika nyumba ile kwa muda wa masaa mawili huku wakiongea hili na lile na kisha kuondoka kuelekea katika nyumba ya Sadiki ambayo wala haikuwa mbali kutoka mahali hapo.

    Kama ilivyokuwa kwa Samuel, Sadiki nae alikuwa na nyumba kubwa ya kifahari, nyumba ambayo ilikuwa na kila kitu ndani. Wazazi wake wakaonekana kufurahia lakini maisha ambayo alikuwa akiishi mtoto wao yakaonekana kutia doa furaha ambayo walikuwa nayo mioyoni mwao.

    “Mali bila Allah! Hakuna kitu” Ustaadhi Hamidu alimwambia mtoto wake, maneno mbayo aliamini hata kama atakwenda wapi, kuna siku angeyakumbuka tu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog